Worcester Now | Next Draft Plan Flyer - Swahili

Page 1

Fahamu Worcester Now | Mpango wa Jiji Zima wa Next! Katika kipindi cha miaka miwili, mchakato wa Worcester Now | Next uliwashirikisha wanajamii mbalimbali katika uundaji wa pamoja wa mpango wa kipindi kirefu katika kiwango cha jiji zima ambao unaonyesha ndoto na mahitaji ya jamii ya Worcester sasa, na kutoa mfumo wa kuongoza jinsi tunavyowekeza na kupanga jiji letu katika miaka 10 ijayo, hasa kuhusiana na maendeleo ya majengo na miundombinu ya Worcester. Changanua msimbo huu wa QR au utembelee now-next.worcesterma.gov ili upate maelezo zaidi kuhusu mpango na utoe maoni yako kuhusu hati ya Mpango wa Rasimu, ambayo inapatikana kwa maoni ya umma hadi tarehe 25 Februari. Maono Katika karne ya nne ya Worcester, tunatazamia kupata jiji bunifu la majirani wanaothamini ujumuishaji na wanaoheshimu uwepo wa tofauti. Tutainua jiji letu kwa kuwekeza kwa usawa kwenye jamii zetu, kuunganisha mitaa yetu na fursa, na kutoa kipaumbele kwa ukuaji endelevu unaowezesha ubora wa maisha ulioimarika kwa wote.

Vichwa vya Mpango Vichwa vitatu vikuu vya mpango viliibuka kutoka kwa majadiliano ya kina na uchambuzi uliofanywa kupitia mchakato huu wa kupanga. Vichwa hivi vinawakilisha msingi wa kile ambacho Mpango huu unahusu, na jinsi unavyoelekeza Jiji kuchukua hatua katika miaka michache ijayo. Mfumo unaozingatia maadili kwa ukuaji unaonufaisha wanajamii wote wa Worcester Uwekezaji wenye usawa na endelevu wa umma katika mitaa ya Worcester. Jiji lililounganishwa na linalofikika zaidi kwa wote

Vipaumbele vya Utekelezaji Vipengee vifuatavyo vya utekelezaji wa mapema vyenye kipaumbele cha juu vitakuwa lengo kuu la utekelezaji wa mpango huu katika miaka 3 - 5 ijayo. Vingi tayari vinaendelea kwa njia fulani.

Angalia ukurasa unaofuata ili upate maelezo zaidi kuhusu Mfumo wa Ukuaji ambao utaongoza upangaji wa mitaa katika siku zijazo, ugawanyaji upya wa maeneo, na uwekezaji wa miundombinu!

1. K ubuni na kutekeleza Mpango wa Utekelezaji wa Usafiri (Mobility Action Plan, MAP) 2. Kutekeleza mabadiliko yafuatayo (marekebisho ya awali) ya ugawanyaji wa maeneo: a. Kuhalalisha nyumba ndogo za ziada (ADUs) zinazotimiza kanuni katika jiji zima b. Kupunguza masharti ya kuegesha magari katika maegesho yaliyo mbali na barabara za umma c. Kurekebisha masharti ya ulinzi wa miti 3. Kubuni Mpango wa Kujenga na Kukarabati Nyumba 4. Kuunga mkono kukuza na kupata rasilimali za utekelezaji (uwezo wa wafanyakazi na ufadhili) 5. Kufanya tathmini za uwezo wa miundombinu na mahitaji 6. Kuanzisha marakebisho ya kina ya ugawanyaji wa maeneo katika jiji zima


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.