The Bournemouth Protocol on Mass Grave Protection and Investigation - Swahili translation

Page 14

D. Utambulisho Kanuni za kimataifa Kifungu cha 15 cha CED kinasema: ‘Washirika wa taifa watashirikiana pamoja na kupeana viwango vikubwa zaidi vya usaidizi kwa nia ya kusaidia waathiriwa wa upoteaji unaotokana na mamlaka, na katika kutafuta, kupata na kuachilia watu waliopotea na, iwapo kifo, kufukua na kuwatambua na kurudisha mabaki yao’ (mkazo umeongezwa). Maelezo pia yanahitaji kufahamishwa kwa watu walio na nia halali ya maelezo kama hayo, kama vile jamaa (ibid, Kifungu cha 18). Na kifungu cha 24(3) cha CED kinahitaji kurejeshwa kwa mabaki ya binadamu. Mataifa yamo chini ya wajibu wa kutoa maelezo ya kumbukumbu kuhusu mtu aliyekufa51 na kutenga rasilimali muhimu kwa uchimbaji wa maeneo ya mazishi ikiwa ni pamoja na ukusanyaji, uhifadhi na utambuzi wa mabaki ya binadamu.52 Utoaji wa cheti cha kifo ni muhimu sana.53 Kwa kuongezea, katika kesi ya Pueblo Bello Massacre v Colombia Mahakama ya Kimarekani ilipendekeza kuwa Taifa linapaswa kuhimiza umma kujitokeza na maelezo ambayo inaweza kusaidia kuwatambua waathiriwa.54 Thamani ya uchambuzi wa DNA kama njia ya msingi ya utambulisho inatambuliwa (Kanuni za ICMP Paris, Kanuni ya 6).55 Sheria ya kitamaduni ya kibinadamu ya kimataifa inaeleza kwamba wahusika kwenye mgogoro (iwe wa kimataifa au sio wa kimataifa) warudishe mabaki ya wafu baada ya kuombwa (Kanuni ya 114 ya CIHL) Kwa kuongezea, ‘[k]ila mshirika kwenye mgogoro lazima achukue hatua zote zinazowezekana kuwajibikia watu waliopotea kutokana na vita na anapaswa kuwapa wanafamilia wao maelezo yoyote inayohusu hatima yao’ (CIHL Kanuni ya 117). ICRC inapanua nafasi hii: ‘Mara tu hatima ya mtu aliyepotea inapobainishwa kuwa kifo, njia zote zinazopatikana lazima zifanyike ili kuhakikisha urejeshaji wa mwili na vifaa vyovyote vya kibinafsi’ (Sheria ya Mfano ya ICRC kuhusu Waliopotea, Kifungu 19). Sheria pia zinahusu mazishi

yanayotakiwa, ufukuaji na mazoea ya ukumbusho na jinsi ya kushughulikia mabaki ya binadamu ambayo hayajatambuliwa, zikiomba rekodi zihifadhiwe, juhudi za utambulisho ziendelee na familia ijulishwe. Ingawa utambulisho unaunda sehemu muhimu ya uchunguzi na utambuzi wa haki, inaeleweka kama jukumu la njia.56 Utambulisho wa mabaki ya binadamu ni sharti la kurudishwa kwa mabaki kwa familia ili kuwezesha mazoea ya ukumbusho lakini pia kwa familia kupokea cheti cha kifo.57 Mahitaji ya ndani ya eneo: Urejeshaji, kurekodi na kuhifadhi mabaki ya binadamu na ushahidi husika unapaswa kuzingatia masharti yaliyoainishwa katika sehemu ya uchunguzi. Jitihada za nje ya eneo: Uchunguzi wa baada ya kufa58 na ushahidi husika unafanywa katika chumba cha kuhifadhia maiti. Kazi kama hii kwa kawaida inahitaji upangaji mahususi na utengaji wa rasilimali zaidi. Kwa kuongeza, yafuatayo yanahitajika: • Udumishaji wa mfululizo wazi wa kumbukumbu wa michakato ya utambulisho na uwajibikaji; • Vifaa vya kutosha vya uhifadhi na udumishaji wa mabaki ya binadamu; na • Uwezo wa familia zinazotembelea chumba cha kuhifadhi maiti wa kutambua na/au kuona ushahidi husika. Ukusanyaji wa data ya watu waliopotea ikiwa ni pamoja na sampuli za marejeleo ya DNA ya familia zinahitajika kutoa maelezo ili kuwezesha utambulisho. Data hii lazima ikusanywe kwa njia nyeti ambayo inalinda haki za manusura na marehemu. Mazoea kama haya yanayohusiana na data ya kibinafsi, maelezo ya jeni na uhifadhi wa maelezo kama hayo lazima yazingatie sheria za ndani za data na yatambue viwango vya kimataifa.

The Massacres of El Mozote and other Places v El Salvador, Hukumu kuhusu Ustahili, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 252 (25 Oktoba 2012) aya ya 334. 52 Aslakhanova and others v Russia, Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 2944/06 na 8300/07, 50184/07, 332/08, 42509/10 (18 Disemba 2012) yaa ya 226. 53 Utoaji na uchakataji wa vyeti vya kifo ulikuwa kiini cha Mkataba wa UN kuhusu Azimio la Vifo vya Watu Waliopotea baada ya Vita vya Kidunia vya II (1939-1945) ambalo lilitumika hadi 1972. Sheria ya Mfano ya ICRC kuhusu Kupotea inaelezea katika muhtasari wake wa Kifungu cha 4 ‘Katika tukio la kifo, kuna jukumu la kutoa cheti cha kifo, kushughulikia mabaki ya binadamu kwa heshima na utu, na vile vile kurudisha mwili kwa familia na/au kuhakikisha mazishi’ (katika ukurasa wa 12) na yanapaswa kufanywa na mamlaka adilifu (katika ukurasa wa 44). Zaidi ya hayo, vyeti vya kifo vinatambuliwa katika Usimamizi wa Miili ya Wafu baada ya Majanga wa ICRC: Mwongozo wa Eneo la Kazi kwa Wahudumu wa Kwanza, kwa mfano, kwenye ukurasa wa 30; na Utambulisho cha Waathirika wa Majanga wa Interpol, katika 5.4. Awamu ya 4: Upatanisho, kwenye ukurasa wa 17. 54 Pueblo Bello Massacre Colombia, Hukumu kuhusu Ustahiki, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 140 (31 Januari 2006) aya ya 272. 55 Tume ya Kimataifa ya Watu Waliopotea (2019), Kanuni za ICMP Paris, Toleo Lililofafanuliwa, ICMP.DG.468.1.W.doc. 56 Ingawa Mwongozo wa Utambulisho wa Waathiriwa wa Majanga wa Interpol unaonyesha mbinu mahususi zaidi kupitia kusema: ‘Waathiriwa wana haki ya utambulisho baada ya kifo chao’ (Sehemu ya B, Kiambatisho cha 2, Ripoti Rasmi - DVI). 57 Hali maalum ni kwa sheria ya Ajentina Nambari 14,321 ya 11 Mei 1994 ambayo inaunda aina ya waliotoweka kwa nguvu kama sawa kisheria na kifo kwa madhumuni ya raia. Inaruhusu familia kushughulikia wosia, kushughulikia mali ya vitu vya aliyepotea na maswala ya urithi, lakini uwezekano wa ‘kupatikana tena’ kwa mtu huyo unabaki wazi. Azimio kama hilo kwa linakubali kwa uwazi kuhusika kwa Taifa au jukumu la kifo cha mtu huyo (tofauti na cheti cha kifo tu). 58 Kwa mfano, kulingana na Miongozo ya Minnesota kuhusu Uchunguzi wa Baada ya Kifo inayotoa mwongozo kuhusu uchunguzi wa maiti, uchunguzi wa meno na uchambuzi wa anthropolojia wa mabaki ya mifupa, kama ilivyo kwenye Mwongozo wa E kwenye kurasa za 49-51 na vile vile Viambatisho vya 1-5, kurasa za 57-87 zinazotoa kanuni. Hizi zinaweza kufanyika katika vituo salama vya muda vya kuhifadhi maiti. 51

12


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.