
9 minute read
D. Utambuzi
Kanuni za kimataifa
Kifungu cha 15 cha CED kinasema: ‘Washirika wa taifa watashirikiana pamoja na kupeana viwango vikubwa zaidi vya usaidizi kwa nia ya kusaidia waathiriwa wa upoteaji unaotokana na mamlaka, na katika kutafuta, kupata na kuachilia watu waliopotea na, iwapo kifo, kufukua na kuwatambua na kurudisha mabaki yao’ (mkazo umeongezwa). Maelezo pia yanahitaji kufahamishwa kwa watu walio na nia halali ya maelezo kama hayo, kama vile jamaa (ibid, Kifungu cha 18). Na kifungu cha 24(3) cha CED kinahitaji kurejeshwa kwa mabaki ya binadamu. Mataifa yamo chini ya wajibu wa kutoa maelezo ya kumbukumbu kuhusu mtu aliyekufa51 na kutenga rasilimali muhimu kwa uchimbaji wa maeneo ya mazishi ikiwa ni pamoja na ukusanyaji, uhifadhi na utambuzi wa mabaki ya binadamu.52 Utoaji wa cheti cha kifo ni muhimu sana.53 Kwa kuongezea, katika kesi ya Pueblo Bello Massacre v Colombia Mahakama ya Kimarekani ilipendekeza kuwa Taifa linapaswa kuhimiza umma kujitokeza na maelezo ambayo inaweza kusaidia kuwatambua waathiriwa.54 Thamani ya uchambuzi wa DNA kama njia ya msingi ya utambulisho inatambuliwa (Kanuni za ICMP Paris, Kanuni ya 6).55 Sheria ya kitamaduni ya kibinadamu ya kimataifa inaeleza kwamba wahusika kwenye mgogoro (iwe wa kimataifa au sio wa kimataifa) warudishe mabaki ya wafu baada ya kuombwa (Kanuni ya 114 ya CIHL) Kwa kuongezea, ‘[k]ila mshirika kwenye mgogoro lazima achukue hatua zote zinazowezekana kuwajibikia watu waliopotea kutokana na vita na anapaswa kuwapa wanafamilia wao maelezo yoyote inayohusu hatima yao’ (CIHL Kanuni ya 117). ICRC inapanua nafasi hii: ‘Mara tu hatima ya mtu aliyepotea inapobainishwa kuwa kifo, njia zote zinazopatikana lazima zifanyike ili kuhakikisha urejeshaji wa mwili na vifaa vyovyote vya kibinafsi’ (Sheria ya Mfano ya ICRC kuhusu Waliopotea, Kifungu 19). Sheria pia zinahusu mazishi yanayotakiwa, ufukuaji na mazoea ya ukumbusho na jinsi ya kushughulikia mabaki ya binadamu ambayo hayajatambuliwa, zikiomba rekodi zihifadhiwe, juhudi za utambulisho ziendelee na familia ijulishwe.
Ingawa utambulisho unaunda sehemu muhimu ya uchunguzi na utambuzi wa haki, inaeleweka kama jukumu la njia.56 Utambulisho wa mabaki ya binadamu ni sharti la kurudishwa kwa mabaki kwa familia ili kuwezesha mazoea ya ukumbusho lakini pia kwa familia kupokea cheti cha kifo.57
Mahitaji ya ndani ya eneo:
Urejeshaji, kurekodi na kuhifadhi mabaki ya binadamu na ushahidi husika unapaswa kuzingatia masharti yaliyoainishwa katika sehemu ya uchunguzi.
Jitihada za nje ya eneo:
Uchunguzi wa baada ya kufa58 na ushahidi husika unafanywa katika chumba cha kuhifadhia maiti. Kazi kama hii kwa kawaida inahitaji upangaji mahususi na utengaji wa rasilimali zaidi. Kwa kuongeza, yafuatayo yanahitajika: • Udumishaji wa mfululizo wazi wa kumbukumbu wa michakato ya utambulisho na uwajibikaji; • Vifaa vya kutosha vya uhifadhi na udumishaji wa mabaki ya binadamu; na • Uwezo wa familia zinazotembelea chumba cha kuhifadhi maiti wa kutambua na/au kuona ushahidi husika.
Ukusanyaji wa data ya watu waliopotea ikiwa ni pamoja
na sampuli za marejeleo ya DNA ya familia zinahitajika kutoa maelezo ili kuwezesha utambulisho. Data hii lazima ikusanywe kwa njia nyeti ambayo inalinda haki za manusura na marehemu. Mazoea kama haya yanayohusiana na data ya kibinafsi, maelezo ya jeni na uhifadhi wa maelezo kama hayo lazima yazingatie sheria za ndani za data na yatambue viwango vya kimataifa.
51 The Massacres of El Mozote and other Places v El Salvador, Hukumu kuhusu Ustahili, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu
Mfululizo wa C Nambari 252 (25 Oktoba 2012) aya ya 334. 52 Aslakhanova and others v Russia, Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 2944/06 na 8300/07, 50184/07, 332/08, 42509/10 (18 Disemba 2012) yaa ya 226. 53 Utoaji na uchakataji wa vyeti vya kifo ulikuwa kiini cha Mkataba wa UN kuhusu Azimio la Vifo vya Watu Waliopotea baada ya Vita vya Kidunia vya II (1939-1945) ambalo lilitumika hadi 1972. Sheria ya Mfano ya ICRC kuhusu Kupotea inaelezea katika muhtasari wake wa Kifungu cha 4 ‘Katika tukio la kifo, kuna jukumu la kutoa cheti cha kifo, kushughulikia mabaki ya binadamu kwa heshima na utu, na vile vile kurudisha mwili kwa familia na/au kuhakikisha mazishi’ (katika ukurasa wa 12) na yanapaswa kufanywa na mamlaka adilifu (katika ukurasa wa 44). Zaidi ya hayo, vyeti vya kifo vinatambuliwa katika
Usimamizi wa Miili ya Wafu baada ya Majanga wa ICRC: Mwongozo wa Eneo la Kazi kwa Wahudumu wa Kwanza, kwa mfano, kwenye ukurasa wa 30; na Utambulisho cha Waathirika wa Majanga wa Interpol, katika 5.4. Awamu ya 4: Upatanisho, kwenye ukurasa wa 17. 54 Pueblo Bello Massacre Colombia, Hukumu kuhusu Ustahiki, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 140 (31 Januari 2006) aya ya 272. 55 Tume ya Kimataifa ya Watu Waliopotea (2019), Kanuni za ICMP Paris, Toleo Lililofafanuliwa, ICMP.DG.468.1.W.doc. 56 Ingawa Mwongozo wa Utambulisho wa Waathiriwa wa Majanga wa Interpol unaonyesha mbinu mahususi zaidi kupitia kusema: ‘Waathiriwa wana haki ya utambulisho baada ya kifo chao’ (Sehemu ya B, Kiambatisho cha 2, Ripoti Rasmi - DVI). 57 Hali maalum ni kwa sheria ya Ajentina Nambari 14,321 ya 11 Mei 1994 ambayo inaunda aina ya waliotoweka kwa nguvu kama sawa kisheria na kifo kwa madhumuni ya raia. Inaruhusu familia kushughulikia wosia, kushughulikia mali ya vitu vya aliyepotea na maswala ya urithi, lakini uwezekano wa ‘kupatikana tena’ kwa mtu huyo unabaki wazi. Azimio kama hilo kwa linakubali kwa uwazi kuhusika kwa Taifa au jukumu la kifo cha mtu huyo (tofauti na cheti cha kifo tu). 58 Kwa mfano, kulingana na Miongozo ya Minnesota kuhusu Uchunguzi wa Baada ya Kifo inayotoa mwongozo kuhusu uchunguzi wa maiti, uchunguzi wa meno na uchambuzi wa anthropolojia wa mabaki ya mifupa, kama ilivyo kwenye Mwongozo wa E kwenye kurasa za 49-51 na vile vile Viambatisho vya 1-5, kurasa za 57-87 zinazotoa kanuni. Hizi zinaweza kufanyika katika vituo salama vya muda vya kuhifadhi maiti.
Mfumo wa usimamizi wa data unaolingana na nyanja zote za ukusanyaji na uchambuzi wa data pia ni hitaji ya nje ya eneo ili kuwezesha utambulisho. Kama kiwango cha chini, hii itajumuisha: • Usajili wa watu waliopotea na maelezo husika; • Maelezo ikiwa ni pamoja na sampuli za marejeleo ya
DNA ya familia za waliopotea; • Data kuhusu shughuli za uchunguzi wa akiolojia na urejesho wa mabaki ya binadamu na ushahidi husika; • Uchunguzi wa anthropolojia na orodha ya kesi; • Michakato ya maabara ya DNA; • Hifadhidata ya wasifu wa DNA; na • Kulinganisha DNA. Uwezo wa kuchakata DNA hauhitaji kuwepo nchini kwa sababu unaweza kupatikana kupitia mashirika ya watu wengine yanayoweza kutoa usaidizi wa upimaji wa DNA kwa kiwango kikubwa. Mkakati wa mawasiliano utawezesha: • Ufafanuzi wa michakato na wakati wa utambulisho na uchakataji wa data kwa wanafamilia na jamii kwa ujumla ili kuwezesha kukubalika; • Kuzijulisha familia kuhusu maamuzi kuhusiana na uchunguzi wa baada ya kufa, na matokeo ya uchunguzi kama huo. Hii inapaswa kujumuisha maelezo kuhusu usaidizi wa familia na chaguo za rufaa; • Mawasiliano bora na mashirika ambayo yanaweza kuhifadhi na kutoa maelezo ya ziada; • Mawasiliano bora na vyombo vya habari ambayo inaheshimu haki za faragha za familia zilizoathiriwa, hutambua unyeti wa familia na haki ya kujua matokeo kabla ya mawasiliano na vyombo vya habari.
Matokeo yanayowezekana ya juhudi za utambulisho
(1) Utambulisho chanya: inagundulika ambapo kuna udhabiti kati ya data ya mtu aliyepotea na kabla ya kufa na baada ya kufa na hakuna tofauti ambazo haziwezi kuelezewa. Mbinu za utambulisho za kuaminika za kisayansi ikiwa ni pamoja na alama za vidole, uchunguzi wa meno, wasifu wa kibaolojia kupitia uchunguzi wa anthropolojia ambapo mabaki yanapangwa kwa mifupa, na uchambuzi wa DNA unapaswa kutumika. Utambuzi wa kuona (ikiwa ni pamoja na picha), maelezo ya kibinafsi, tatoo, mali na mavazi yanayopatikana mwilini na vile vile matokeo ya kimatibabu yanaweza kusaidia utambulisho lakini hayapaswi kutumika kama kitambulishi pekee.59 Ambapo utambulisho umebainika, mamlaka inayofaa inapaswa kutoa cheti cha kifo60 . (2) Utambulisho haujabainika: ambapo, kwa mfano, ushahidi unaunga mkono kutengwa kwa nadharia fulani kuhusu utambulisho wa mabaki ya binadamu, au ambapo hakuna hitimisho kuhusu utambulisho wa mabaki ya binadamu.61 Rekodi inapaswa kuhifadhiwa kikamilifu ili kuruhusu utambulisho wa baadaye na arifa inayofuata kwa jamaa na wahusika, ikiwa ni pamoja na mamlaka ya serikali. Udumishaji na hatua za uhifadhi wa muda mrefu zinahitajika kulinda matarajio ya utambulisho cha baadaye. Ambapo hatua za udumishaji na uhifadhi hazipatikani au hazifai, mabaki ya binadamu ambayo hayajatambuliwa yanaweza kuzikwa katika makaburi yaliyotiwa alama kulingana na mila na desturi zinazofaa za kidini za marehemu.62 Ili kuhakikisha uwezekano wa utambulisho wa baadaye, uteketezaji wa mwili unapaswa kuepukwa kila inapowezekana. Ufuatiliaji wa mabaki unapaswa kuhakikishwa kupitia mbinu kama vile: • Uwekaji wa kumbukumbu na kuambatisha eneo, ikiwa ni pamoja na kuambatisha eneo la miili ya kibinafsi ndani ya eneo; • Kuweka nambari na alama kwa kila mwili na mfuko/ jeneza kwa kurejelea nambari ya sampuli ya DNA na uhifadhi; • Matumizi ya ishara ili kuweka alama kwenye eneo; • Uhifadhi salama wa maelezo ili kuhakikisha usalama wake. (3) Utambulisha usio sahihi: ambapo kuna hitilafu katika kutoa utambulisho kwa mabaki ya binadamu. Utambulisho kama huo usio sahihi utakuwa na athari mbaya kwa seti mbili za familia zinazohusika na vile vile uchunguzi. Ugunduzi wa hililafu kama hiyo unapaswa kuchochea ushirikiano unaofaa na usaidizi wa kifamilia na vile vile hatua ya kurekebisha kulingana na Taratibu za Kawaida za Uendeshaji.
Haki za familia katika kisa cha kutotambuliwa
Katika hali ya kutotambuliwa, wanafamilia waliobaki hata hivyo wanaweza kuhitaji baadhi ya vyeti ili kuthibitisha kutokuwepo kwa wapendwa wao na kuwawezesha kudai haki zingine au kuendelea na uuzaji wa mali, urithi, kuoa tena n.k. Hali au cheti kisichokuwepo kinapaswa kutolewa ili kulinda haki za familia.63
59 Angalia Mbinu za Utambulisho (Msingi na za Pili) kama sehemu ya Mwongozo wa Utambulisho wa Waathiriwa wa Majanga wa Interpol kwenye ukurasa wa 18; Mwongozo wa Utambulisho cha Waathiriwa wa Majanga wa Interpol Kiambatisho cha 12 kuhusu Mbinu za Utambulisho na Itifaki ya Minnesota, sehemu ya E kuhusu Utambulishi wa Miili iliyokufa, kurasa za 21-24. 60 Kama, kwa mfano, Cheti cha mfano cha kifo katika Kiambatisho 2 cha ICRC/Sheria ya Mfano kuhusu Waliopotea. 61 Angalia Itifaki ya Minnesota, sehemu E kuhusu Utambulisho wa Miili iliyokufa, ukurasa wa 24. 62 Mazishi kama hayo ya mabaki ambayo hayajadaiwa na ambayo haijatambuliwa yanachukuliwa kuwa sahihi na Azimio la Mytilini linalohusika na utunzaji wa heshima wa watu waliopotea na waliokufa na familia zao kama matokeo ya safari za wahamiaji (Azimio la Mytilini la Utunzaji wa Utunzaji wa Heshima wa
Watu Wote Waliopotea na Waliokufa na Familia zao kama Matokeo ya Safari za Wahamiaji (2018) katika Kifungu cha 16). Sheria ya Mfano ya ICRC kuhusu
Waliopotea katika ufafanuzi wake wa Kifungu cha 22 (Mazishi na ufukuaji wa maiti) inasema ‘[u]teketaji unapaswa kuepukwa, isipokuwa pale inapobidi (kwa mfano kwa sababu ya afya ya umma) na rekodi ya sababu hio kuhifadhiwa, ikiwa ni pamoja na majivu’ (katika ukurasa wa 48). 63 Sawa na aina ya Watu Waliopotea katika Ajentina na Sheria ya Kolombia ya 1531 kuhusu Azimio la Kutokuwepo kwa Watu Waliopotea, 2012, Kifungu cha 7.
Chini ya sheria za kimataifa hali ya kisheria ya mtu aliyepotea na jamaa zao haidhibitiwi lakini CED inatoa katika Kifungu cha 24(6) ‘Bila kuathiri jukumu la kuendelea na uchunguzi hadi hatima ya mtu aliyepotea itakapofafanuliwa, kila Mshirika wa Taifa atachukua hatua stahiki kwa kuzingatia hali ya kisheria ya watu waliopotea ambao hatima yao haijafafanuliwa na ile ya jamaa zao, katika nyanja kama vile ustawi wa jamii, maswala ya kifedha, sheria ya familia na haki za mali.‘