4 minute read

F. Haki

Kanuni za kimataifa a. Utoaji wa maelezo:

Haki ya ukweli imejikita katika Vifungu vya 32 na 33 vya Itifaki I ya Ziada ya Mikataba ya Geneva, iliyojumuishwa katika mkutano wa haki za binadamu (Dibaji ya CED na Kifungu cha 24 (2)), maarifa ya sheria67 na kufafanuliwa katika sheria zisizoshurutisha. Haki inajumuisha hitaji la waathiriwa, familia na jamii ya kujua ukweli kuhusu matukio ya zamani, ikiwa ni pamoja na hali na sababu ambazo zilisababisha kutekelezwa kwa uhalifu huo (Kanuni za Orentlicher, Kanuni ya 2). Katika kisa cha kifo au upoteaji unaotokana na mamlaka, haki ya ukweli ni pamoja na haki ya familia kujua hatima na mahali walipo wapendwa wao. Ujifunzaji na maarifa ya majii pia yanajumuisha jukumu kwa Taifa kuhifadhi kumbukumbu ya pamoja ya tukio (Kanuni za Orentlicher, Kanuni ya 3).

b. Suluhisho:

Kwa waathiriwa na familia zao, sheria za kimataifa kupitia Kanuni na Miongozo ya Msingi ya 2005 na CED (kwenye Vifungu vya 24(4) na 24(5)) hutoa suluhisho kadhaa zinazowezekana: • Fidia; • Marejesho; • Urekebishaji; • Kuridhika (ikiwa ni pamoja na uthibitisho wa ukweli na/au utafutaji, urejeshaji, utambulisho na mazishi) na; • Dhamana za kutorudia (kupitia, kwa mfano, kanuni za maadili, elimu na mafunzo).68 Katika kutafuta suluhisho69 waathiriwa wana haki ya: • Ufikiaji sawa na fanisi wa haki; • Fidia ya kutosha, inayofaa na ya haraka kwa madhara yaliyopatikana, ikiwa ni pamoja na utunzaji wa kisaikolojia kwa jamaa wa karibu70; na • Ufikiaji wa maelezo muhimu kuhusu ukiukaji na mbinu za kufidia. Hii imepata kuelezwa katika kisa cha mauaji ya Mapiripán: ‘wakati wa michakato ya uchunguzi na kimahakama, waathiriwa wa ukiukaji wa haki za binadamu, au ndugu zao wa karibu, wanapaswa kuwa na fursa za kutosha kushiriki na kusikilizwa, zote kuhusiana na ufafanuzi wa ukweli na adhabu ya wale waliohusika, na katika kutafuta fidia ya haki’.71

c. Katazo na adhabu au uhamishaji:

Mauaji ya halaiki, ukiukaji mkubwa wa Mikataba ya Geneva, mateso na upoteaji unaotokana na mamlaka umepigwa marufuku na mkataba, na Washirika wa Mataifa wanahitajika kutunga sheria ya ndani ili kutoa adhabu madhubuti pale ambapo ukiukwaji unatokea (tazama Kifungu cha 5 cha Mkataba wa Mauaji ya Halaiki; Kifungu cha 49 cha GC I; Kifungu cha 50 cha GC II; Kifungu cha 129 cha GC III; Kifungu cha 146 cha GC IV; Kifungu cha 2 na 4 cha UNCAT; Kifungu cha 6 cha CED; na Kifungu cha 6 cha ICCPR kuhusiana na mauaji ya halaiki). Kufuatia kunyimwa kwa haki ya kuishi, jukumu la kuchunguza linajumuisha ‘utambulisho na, ikiwa inafaa, adhabu ya wale waliohusika’.72 Kanuni za Kuongoza za CED zinabainisha kuwa ‘utafutaji wa mtu aliyepotea na uchunguzi wa jinai wa watu wanaohusika na kutoweka kunapaswa kuimarishana ‘(Kanuni ya 13(1)). Mikataba ya Geneva inahitaji Washirika wa Mataifa kuwatafuta kikamilifu wahusika wanaodaiwa ili wawafikishe mahakamani kwa mashataka (Kifungu cha 49 cha GC I; Kifungu cha 50 cha GC II; Kifungu cha 129 cha GC III; Kifungu cha 146 cha GC IV).

d. Utangazaji rasmi:

Sambamba na haki za ziada za waathiriwa, kama matarajio ya haki ya jamii ya kidemokrasia na kama hatua ya kuimarisha heshima kwa sheria, matokeo ya uchunguzi wowote yanapaswa kutangazwa rasmi kikamilifu.73

Ugunduzi na uchunguzi wa eneo la kaburi la halaiki unaweza kutokea ndani ya muktadha mpana wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu au ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu. Katika hali kama hizo, mahitaji ya haki ya watu binafsi, jamii, Mataifa na jamii ya kimataifa yanaweza kuwa ya kuongezeka na ya kupingana. hitaji la na/au haki ya urekebishaji wa pamoja na upataji nafuu, uwajibikaji, mshikamano wa jamii, uaminifu na upatanisho.

67 Kwa uamuzi wa mapema angalia Velásquez Rodríguez v Honduras, Hukumu kuhusu Ustahiki, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu C Nambari 4 (29 Julai 1988), aya ya 177. Haki ya ukweli inahitaji uchunguzi wenye mamlaka juu ya unyanyasaji wa haki za binadamu pamoja na muktadha wa kijamii na kisiasa unaosababisha unyanyasaji; unajumuisha hatua ya ushiriki wa waathiriwa katika mchakato na utangazaji rasmi wa matokeo ya uchunguzi ili kufaidi jamii na mtu binafsi. 68 Kama ilivyoainishwa katika UNGA, Kanuni na Miongozo ya Msingi kuhusu Haki ya Suluhisho na Malipo kwa Waathiriwa wa Ukiukaji Mkubwa wa Sheria za

Kimataifa za Haki za Binadamu na Ukiukaji Mkubwa wa Sheria ya Kimataifa ya Kibinadamu, Kanuni za 19-23. 69 Kanuni za Msingi, Kanuni ya 11. 70 Pueblo Bello Massacre v Colombia, Hukumu kuhusu Ustahiki, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 140 (31 Januari 2006) aya ya 274. 71 Mapiripán Massacre v Colombia, Hukumu ya Ustahiki, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 134 (15 Septemba 2005), aya ya 219. 72 Kukhalashvili and others v Georgia, Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 8938/07 na 41891/07 (2 Mei 2020), aya ya 129. Angalia pia Pueblo Bello Massacre v

Colombia, Hukumu kuhusu Ustahiki, Malipo na Gharama, Mahakama ya Kimarekani ya Haki za Binadamu Mfululizo wa C Nambari 140 (31 Januari 2006) aya za 265-269 kuhusu wajibu wa Taifa katika kuchunguza ukweli wa kesi na, inapobidi, kutambua, kushtaki na kuadhibisha waliohusika. 73 ‘Las Dos Erres’ Massacre v Guatemala, Hukumu ya Mapingamizi ya Awali, Ustahiki, Malipo na Gharama, IACtHR Mfululizo wa C Nambari 211 (24 Novemba 2009) vifungu vya 256-264 na El-Masri v the Former Yugloslav Republic of Macedonia,Hukumu ya Baraza Kuu la Hukumu, Maombi ya ECtHR Nambari 39630/09 (13 Disemba 2012), aya ya 192 na Maoni ya Pamoja ya Maamuzi ya Majaji Tulkens, Spielmann, Sicilianos na Keller.

This article is from: