ZAMU YANGU MAGAZINE - WASANII KUNUFAIKA NA COSOTA

Page 1

Sina chakula, sina kodi, mnionavyo nje sio halisi Uk. 07.

Alhamis 16-31 Julai, 2020 | Habakuki 2:1-2

MICHEZO : YANGA YAISHUSHA AZAM FC NAFASI YA PILI BAADA YA KUIGALAGAZA SINGIDA UNITED 3-1.

COSOTA YAPEWA SAA 24 KUWASILISHA MKAKATI UTAKAOWANUFAISHA WASANII, MONALISA, KALA JEREMIAH WAZUNGUMZA UK. 04

Pichani ni Viongozi wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo na Wizara ya Viwanda na Biashara wakikabidhiana nyaraka za COSOTA kufuatia agizo la Rais Dr. John Pombe Magufuli la kuhamishia kitengo cha COSOTA katika Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo jana jijini Dar es Salaam.

NAIROBI, KENYA

Pasta Burale aruhusiwa baada ya kupata nafuu

M

hubiri maarufu wa jijini Nairobi nchini Kenya, Robert Burale amepona corona na kuruhusiwa kuondoka hospitali alipokuwa amelazwa. Burale alikuwa hospitali kwa kipindi cha wiki moja alipofikishwa na kuwekwa katika

chumba cha wagonjwa mahututi mara ya kwanza. Vyanzo vya habari vinasema Alikuwa akirekodi video akiwa hadi katika chumba cha wagonjwa mahututi na kurusha kwenye mitandao Wakenya wakahofia kuhusu ugonjwa wake.

Makala ya Wanaume Uk. 08

Mapambano dhidi ya Corona yanaendelea, chukua tahadhari PROUDLY SPONSORED BY:- RADIO 5 | EVG MINISTRY | FOUNTAIN RADIO | M!SA RICE | SHALOM RADIO & TANGANYIKA PRODUCTION

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


Kitabu / Vitabu

alhamis JULAI 16-31, 2020

2

Uchambuzi wa Kitabu cha MUNGU ANAPATIKANA WAPI?

SURA YA PILI - WEWE NI MWANA

Kuwa Mwana (mtoto)

NA HELLEN SOGIA, PWANI.

M

penzi msomaji wetu Bwana Yesu asifiwe, asante kwa kuendelea kuwa pamoja nasi katika sehemu ya kwanza ya kitabu chetu cha Mungu anapatikana wapi. Leo tunamalizia sehemu ya kwanza na kuingia sehemu ya pili ya kitabu chetu, endelea kuwa nasi. Ruhusu Nira iliyokufunga ifunguliwe kwako, ili uweze kurudi sayuni. Mtu akifunguliwa nira iliyomfunga, hapo ndipo mtu anaweza sasa kujifunga NIRA ya Bwana Yesu, na hapo ndipo mtu ataweza kujifunza kutoka kwa Bwana Yesu kama Neno linavyosema. Mt. 11:29. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni pole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Hapo ndipo mtu atafikia mahali pa kumjua Bwana na ndipo ushirika wa kweli utaanza kuumbika kati ya mtu na Mungu, na utukufu wake Mungu utaonekana kwa udhahiri lwa mtu. Ushauri: Ukiona kuwa uko katika hali ya mateso kutokana na haya yaliyoandikwa humu, au una hali yeyote ambayo inafanana na ulivyosoma, chukua hatua hizizufuatazo. Orodhesha zile vitu unavyoona vinakutesa, iwe ni, tabia, au roho chafu, hata kama hazijaandikwa humu, ukimshirikisha Roho Mtakatifu akukumbushe na yale uliyoyasahau na akuonyeshe yale usiyoyajua. Yoh. 16:9.a) Omba rehema kwa Mungu, ukiungama makosa yako yote, tafuta maandiko ya kusimamia. 1 Yoh.

1:8-9. b) Tumia damu ya Yesu, kujifunika, na kufunika familia, mali na vyote vinavyokuhusu. 1Petro 1:2, Ebra 9:22(c) Mfanyie Mungu ibada fupi, ukimwambia anaweza. Anza kukataa kila roho, ukizitamka na ukijitenga nazo tafuta andiko la kusimamia. Yak. 4:7. Anza kung’oa, bomoa, haribu, na kuangamiza kila roho kwa majina, jitenge na hizo roho, uwe na andiko la kusimamia. Efe. 6:13, Yer. 1:10, Waamuzi. 6:25, Yer 1:10,a. Anza kujenga na kupanda kwa upya, ukijitabiria mambo mema na ushirika na Mungu. Uwe na andiko la kusimamia. Eze. 37:2-10, Yer 1:10,b Jiwekee ulinzi wa Damu ya Yesu na kujizungushia uzio. uwe na andiko la kusimamia. Zab 91:4b, Ufu. 12:11. Mshukuru Mungu kwa kukufungua. uwe na andiko la kusimamia. 1 Kor ; 15-57, 2 Kor. 9:15 / Zab. 107:

SEHEMU YA PILI

WEWE NI MWANA Kuwa mwana (mtoto).

Yohana 1:12. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. Inapofikia mahali mtoto anaposhindwa kujitambua kuwa yeye ni nani katika familia aliyotoka, kuna hatari ya mtoto huyo kusababisha uharibifu katika familia yake kwa namna moja au nyingine Katika familia yeyote ile, mtoto

anatakiwa kuwa huru na kuwa karibu na Baba yake; kama mwana, kuna mambo mengine, na mahitaji mengin kutoka kwa baba yake, ndio aweze kupewa, La hasha! Yako mahitaji ambayo ni ya lazima, na pia ni wajibu wa baba kumtimizia mtoto wake; maana, kuna uhalali na haki kwa mtoto huyo kuyapata; Kwamba inabidi avipate kawa sababu yeye ni mwana katika familia hiyo, inapofikia mahali ambapo, inakuwa ni sharti mtoto afanye fujo, ndio aweze kupewa chakula, mavazi, na huduma nyingine zinazomstahili, in maana, hapo kuna tatizo!! Pia ni jambo la kuchekesha na la kuhuzunisha wakati mtoto wa mfalme anapokuwa hajitambui kuwa yeye ni mwana wa mfalme. Katika ufalme wowote ule mtoto wa mfalme huwa anafundishwa nidhamu ya kifalme na utawala wa kifalme, ikiwa ni sehemu ya kumwandaa, kwa ajili ya kuja kutawala baadae, na pia ili aweze kujitambua kuwa yeye ni nani katika ufalme huo, mtoto huyu huwa na mwenendo na tabia, tofauti na watoto wengine, maana, katika mafunzo hayo anayopewa,

yanamjengea nidhamu, na kumfanya awe mtu mwenye hesima, kwa jamii inayomzunguka ya kifalme, na kwa watu wote kwa ujumla. Pia mtoto huyu huishi kwa kuzingatia sheria zilizowekwa na ufalme huo akiwa kama kielelezo kwa wengine. Tatizo limetokea kwa wana wa Mungu, badhi ya watu, wanaokiri kuwa wameshayakabidhi maisha yao kwa Yesu, ni kwamba engi wameshindwa kujitambua, na wengine wamekataa kufundishika, na wamekuwa wagumu kutembea kulingana na sheria za ufalme wa Mungu, ufalme wanaoukiri kuwa ni wa Baba yao, Mungu, hivyo basi wamekuwa wakisababisha uharibifu kwenye ufalme, kwa sababu ya kukosa kujitambua kwao. Kwa msaada na ushauri, maombi, tafadhali wasiliana na Mtumishi wa Mungu,

Apostle Hellen Sogia

THE OAK MISSION MINISTRY. P.o Box 30838. Kibaha Tanzania Simu.

+255 (0) 753 351 048 au +255 (0) 716 711 867

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


Wasifu / Habari

alhamis JULAI 16-31, 2020

hawa ndio zablon singers, wanatoka ukoo mmoja, ALBAMU YA KWANZA ILITOKA 2012. NA MWANDISHI WETU

M

ambo vipi rafiki yangu na msomaji wa gazeti lako pendwa la Zamu Yangu. Leo bwana nakuletea historia fupi ya waimbaji wa nyimbo za injili kutoka Shinyanga nchini Tanzania, waliojikita katika mji wa Kahama. Kiongozi wao yaani Japhet Zabron anatueleza kwa nini wakaitwa Zabron Singers. Karibu ujiosemee. “Kundi letu linaitwa Zabron Singers kwa sababu wote ni watoto wa familia moja, mzee Zabron alikuwa ni kiongozi wetu mkubwa kwenye ukoo wetu hivyo tukaamua kuendelea kumuenzi. Sote tunaimba tukitoka kwenye mashina yetu wenyewe hivyo hili kundi limeanzishwa ndani ya familia hali inayofanya iwe ngumu kutengeneza matabaka ndani ya kundi letu. Kundi letu limeanzishwa mwaka 2006 makao makuu ni mkoa wa Shinyanga, wilayani Kahama tupo chini ya kanisa la wasabato linaitwa Kahama Central SDA na mlezi wetu ni Benedict Burash. Kundi letu lina jumla ya waimbaji 15 ambao tunafanya nao kazi kwa kushirikiana ila bado tuna amini litakuwa kubwa hapo baadaye kwa kuwa ukoo wetu ni mkubwa. Tumeanza kuongeza pia kwa kuwafundisha wengine ambao wapo nje ya Zabron pia kupitia kujitoa kwetu kwa jamii hii inafanya tuwe ni familia kubwa bila kujali dini wala kabila.

Wazo la MKONO WA BWANA lilikuja baada ya mengi ambayo Bwana alikuwa anatutendea nyuma hata sasa amekuwa akitutendea ni mkono wake hali iliyofanya tukaandika wimbo huo. “Ilikuwa ni wakati ambao tunaongea na Bwana na kutaka aongee na watu wake wote bila kujali aina ya dini, kabila wala rangi ndipo tukauona Mkono wa Bwana’’ Wengi wanaweza kujiuliza kama kweli tumeona matokeo mazuri katika wimbo wetu MKONO WA BWANA ila kwa uhakika mkono wa Bwana tumeuona, namna ambavyo tumegusa hisia za mashabiki na kubadilisha mienendo yao inabadilika na kutenda matendo mema hivyo kwetu ni faraja na tunaamini wengi wanauona mkono kutokana na namna shabiki zetu walivyoupokea wimbo huu hivyo ni imani yetu kuwa mkono wa Bwana unagusa wengi. Kwa sasa tuna jumla ya albamu tatu ambapo albamu yetu ya kwanza inaitwa Nawakumbuka ilitoka mwaka 2012 ina jumla ya nyimbo 11, albamu ya pili inaitwa Mkono wa Bwana mwaka 2015 na albamu ya tatu inaitwa Sio Bure ina nyimbo 9 imetoka mwaka 2018. Kitu gani kilifanya Mkono wa Bwana ikapendwa zaidi 2016? “Wakati wa Bwana ukifika hakuna anayeweza kuuzuia, tulitunga wimbo mwaka 2013 tukarekodi mwaka 2014 tukauachia mwaka 2015 ukaja kupokelewa vizuri 2016 na mpaka leo bado unasikilizwa na kupendwa.

“Tulimwomba Mungu aweze kutushika mkono na akatuonyesha njia mpaka tukafanikiwa kuandika nyimbo hii, haikuwa kazi rahisi kwa kuwa wengi walikuwa hawaamini kama tunaweza kufanya kitu kikubwa kulingana na jinsi tulivyo na ndio maana mpaka sasa wimbo ni mkubwa kuliko sisi tulivyo. Changamoto kwenye huduma ilikuwa wapi? “Kukubalika na kupewa nafasi, mengi yalikuwa magumu kwetu kwani hatukuwa tukipewa muda wa kusikilizwa kazi zetu, ni mapito ambayo tumeyapitia na kikubwa tuliamini kwamba ni lazima tuuone mkono wa Bwana na imetokea. Tutarajie nini kutoka kwenu? “Kumtumikia Mungu na kufanya kazi nyingine bora zaidi ya mkono wa Bwana na ndio maana kwa sasa tupo kwenye

mpango wa kutengeneza albamu ya nne ambayo itakuwa ni moto wa kuotea mbali zaidi ya Mkono wa Bwana. “Kufanya Zabron iwe taasisi kubwa ya kusaidia jamii na kuinua vipaji vya wengi ambao wamekata tamaa ili kuendelea kupambana. “Kufanya kazi na wasanii wengine nje ya kundi letu ili kuendeleza huduma na kuwafikia watu wengi zaidi. Sema neno na wapenzi wa muziki wa injili duniani. “Kazi ya Bwana yatupasa tuitende kwa moyo hivyo sapoti yao ni jambo la msingi kila siku na ndio maana tunafanya kwa ajili yao hivyo wakati wa Bwana ni siku zote, kama ambavyo nasi tulikuwa na subira mpaka muda wa Bwana ulipofika nao pia wanapaswa wawe na subira kutafuta mafanikio,” Mwalimu Japhet Zabron.

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE

3


Habari / Makala

alhamis JULAI 16-31, 2020

4

COSOTA YAPEWA SAA 24 KUWASILISHA MKAKATI UTAKAOWANUFAISHA WASANII

familia ya marehemu Steven kanumba kutoka katika kampuni ambazo ziliingia mikataba na Wasanii hao.

NA MWANDISHI WETU, DAR

K

atibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hasaan Abbasi ametoa saa 24 kwa Bodi na Menejimenti ya Chama cha Hakimiliki na Haki Shirikikishi Tanzania (COSOTA) kuwasilisha mkakati wa namna Wasanii watakavyonufaika kupitia Taasisi hiyo. Katibu Mkuu ametoa agizo hilo jana Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya makabidhiano ya chama hicho kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara kwenda Wizara anayoisimamia. “Tumshukuru Rais John Magufuli kwa sababu mjadala wa kwa nini COSOTA ipo Wizara ya Viwanda na Biashara umekuwa mrefu, lakini ndani ya saa 24 tangu Julai 12, 2020 Rais aliweza kusaini Waraka wa kuihamishia Wizarani kwetu�, Dkt. Abbasi.

Naye Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe ameutaka uongozi wa taasisi hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Habari katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

hiyo inatakiwa kuhakikisha kuwa inawasaidia wasanii katika kusimamia haki zao ili kuondokana na umaskini na kufikia malengo waliyojiwekea katika kazi zao za Sanaa kwani ni jukumu la taasisi hiyo kuhakikisha kuwa inamsaidia msanii kutoka kuwa msanii maarufu maskini na kuwa msanii maarufu tajiri.

jukumu ya kila siku ya Idara ya Maendeleo ya Sanaa kwa kuhakikisha wasanii wanapata huduma kwa wakati na chini ya mwamvuli mmoja.

KWAYA ZONE FESTIVAL SEASON TWO

Dkt. Abbasi alieleza kuwa kwa sasa kuna mabadiliko na mafaniko mengi katika sekta ya Sanaa ambapo Juni 26, 2020 Wizara ilifanikiwa kutangaza Kanuni za Filamu na Michezo ya Kuigiza kupitia gazeti la Serikali namba 488 ambapo kuna manufaa mengi kwa wasanii ikiwemo kupungua kwa tozo za filamu kutoka shilingi 500,000/= hadi shilingi 50,000/= lengo ikiwa ni kuwawezesha kutengeneza filamu zenye ubora.

TAREHE 2 AGOSTI 2020 SAA 8 MCHANA TABATA SEGEREA KWA PASTOR KATEMBO

Vile vile faida nyingine ya kanuni hizo ni kuwepo kwa kamati ya kutetea haki za wasanii ambapo Serikali imefanikiwa kurejesha kiasi cha milioni 200 ambapo kati ya hizo, shilingi milioni 65 zilirejeshwa kwa familia ya marehemu Mzee Majuto pamoja na kiasi cha milioni 20 zilirejeshwa kwa

Aliongeza kuwa taasisi

Aidha, Dkt. Abbasi aliongeza kuwa taasisi hiyo kuhamia Wizara ya Habari ni jambo jema katika kutekeleza ma-

Kwa upande wa Afisa Mtendaji wa COSOTA, Doreen Sinare ameahidi kusimamia kwa ufanisi majukumu ya taaasisi hiyo inayosimamia haki miliki pamoja na kusajili wabunifu kukusanya na kugawa mirabaha na kusuluhisha mogogoro inayohusianana haki miliki pamoja na kutoa ushauri. Nao baadhi ya wasanii walitoa maoni yao kuhusiana na makabidhiano haya ambapo Msanii wa Filamu na Michezo ya kuigiza, Vyonne Cherrie (Monalisa) ameeleza kufurahishwa na uamuzi wa kuhamishwa kwa taasisi ya COSOTA kwenda Wizara ya Habari kwani imeepusha milolongo mingi ya ufuatiliaji wa kazi za filamu na sanaa. Huku Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Kala Jeremiah alisema kuwa ulinzi na ulezi wa sanaa unatakiwa kwenda pamoja hivyo ni jambo jema kwa COSOTA kuhamia Wizara ya Habari ili waweze kufanya kazi kwa ushrikiano na BASATA. Chanzo: Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


afya YA MWANAMKE 5

alhamis JULAI 16-31, 2020

MADHARA MATANO YA UGONJWA WA FANGASI ZA SEHEMU ZA SIRI NA NJIA MBILI ZA KUTIBU HARAKA FEMININE WASH Hii huwa inafahamika kama mkombozi wa wanawake kwa maambukizi ya sehemu za siri. Imeandaliwa maalum kwa ajili ya wanawake.

NA MSHAURI BABRA.

M

aambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na uwepo wa fangasi wanaojulikana kitaalamu kama Candida albicans. Maambukizi haya pia hujulikana kama yeast infection au thrush.

Imetengenezwa kwa vyakula,mimea na madini na viua sumu mwilini. Inamadini yanayohuisha uke na kuwa na ulinzi asilia,inaviua sumu vinavyozuia uke kuzeeka(mashavu),uke uliolegea, Ina mafuta mazuri yanaitwa essential oil kwa ajili ya kufanya uke urudishe mnato wake wa asili.

VISABABISHI •

• • • • •

• • • • • • • • • •

Kutumia sana dawa za detergents sehemu za siri au douches (vifaa vya kusafishia uke kwa kutumia maji na siki) Kutumia madawa ya antibiotics na steroids Mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini Ujauzito (kutokana na kubadilika kwa mfumo wa homoni mwilini na kupungua kwa kinga ya mwili) Matumizi ya dawa za kupanga uzazi (vidonge vya majira) Upungufu wa kinga mwilini kutokana na magonjwa sugu kama kisukari, saratani aina yoyote ile, ugonjwa aina ya mononucleosis Ugonjwa wa ukimwi (HIV/AIDS) Matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy) kutokana na sababu mbalimbali Matibabu ya kusaidia kushika mimba kwa wale wenye matatizo ya uzazi (infertility treatment) Msongo wa mawazo (stress) Utapia mlo (malnutrition) Kuvaa nguo au mavazi yanayoleta joto sana sehemu za siri Kujamiana kwa njia ya kawaida mara tu baada ya kujamiana kupitia njia ya haja kubwa Kuvimba kwa tezi la koo (goiter) Saratani ya tezi la koo (thyroid cancer) Wanawake wenye umri wa miaka kati ya ishirini na thelathini wapo kwenye hatari.

DALILI NA VIASHIRIA • Kuwashwa sehemu za siri (kwenye tupu ya mwanamke)Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri (burning sensa

• • • • • •

tion) Kufanya kama vidonda katika sehemu za siri (soreness) Maumivu wakati wa kujamiana (superficial dyspareunia) Maumivu au usumbufu wakati wa kujisaidia haja ndogo (wakati mtu anakojoa) Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwa mdomo wa nje wa tupu ya mwanamke (labia minora) Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au nyeupe kijivu, unaoweza kuwa mwepesi, majimaji au mzito na ambao umefanana na jibini.

MADHARA YA FANGASI 1. Muwasho usiostahimilika 2. Husababisha magonjwa ya hormonal imbalance 3. Huathiri utungaji wa mimba/ na kutoka kwa mimba 4. Maumivu wakati wa kujamiina na kuondoa ladha ya tendo 5. Maumivu wakati wa kujisaidia 6. Ugumba 7. Kutokwa na uchafu sehemu za siri. NJIA MBILI ZA MATIBABU YA FANGASI 1. Tumia kitunguu Swaumu: Menya punje tatu Meza au Kiponde loweka usiku kucha asubuhi unywe. 2. Kutumia feminine wash; ni njia ambayo ni rahisi isiyokuwa na maandalizi mengi.

Licha ya kukutibu tatizo la fangasi pia itakusaidia kukulinda dhidi ya maradhi mengine kwa mwanamke kwa kufanya kazi zifuatazo;• Huondoa harufu mbaya ukeni • Huondoa bacteria wabaya na kuzuia U.T.I • Huondoa tatizo la miwasho ukeni • Hurudisha size nzuri ya uke • Huondoa maji maji yatokayo ukeni yenye Harufu mbaya • Huondoa maumivu wakati wa tendo la ndoa • Hufanya mwanamke kujiamini muda wote • Huzibua mirija ya uzazi hivyo kusaidia wenye shida ya kutoshika mimba • Huondoa uchafu kama maziwa mtindi • Huondoa vipele na vidonda ukeni • Humkinga mwanamke na maambukizi mabaya hasa u.t.i kwenye vyoo,kemikali za swimming pool, maambukizi Mabaya kutoka kwa mwanaume. JE, UNA TATIZO LA FANGASI SUGU? • Kama ni NDIYO una tatizo hili na umeshindwa kulipatia ufumbuzi, wasiliana nasi kupata elimu zaidi, ushauri na tiba. Tunapatikana Mikocheni, Dar Es salaam, na pia huduma zetu zinafika mikoa yote Tanzania na nje ya nchi. Kwa mahitaji huduma (Ushauri) Wasiliana nasi +255 757 519 313

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


MSANII WETU

alhamis JULAI 16-31, 2020

6

Mungu amenipa kibali ila chuki, kusemwa vibaya na uongo haviishi

NA MWANDISHI WETU, DODOMA

B

wana Yesu asifiwe sana mpenzi msomaji wangu, mambo vipi? natumaini uko vema kabisa. Eeh bana leo nimepiga stori na Bighton Mundah kijana mdogo mwenye kibali kikubwa sana. Karibu twende sote tukasome alichokisema...

Naitwa Emmanuel Isaya Mundah maarufu kama Brighton Mundah, ni muimbaji wa nyimbo za injili kutoka Tanzania pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) nilianza kuimba kutoka katika vikundi vya kwaya katika makanisa ya pentekoste na kwa sasa naabudu kanisa la FPCT Morogoro kwa mch Aloyce Kalega, mwaka 2015/2016 nilishirikishwa katika album ya mwimbaji mmoja kutoka Morogoro na kwa baadhi ya nyimbo. Mwaka 2018 ndio nilifanikiwa kufanya wimbo wangu wa kwanza unaoitwa Faraja ya Moyo, namshukuru Mungu kuwa wimbo huo ulipokelewa vizuri na watu wengi kitu hicho kikanitia moyo sana. Mwaka 2019 nikafanya nyimbo nyingine nilifanikiwa kuingia mkataba na kampuni moja ya kenya kunisambazia kazi zangu zote na kwa sasa kuna wimbo wangu mpya ninaoufanyia video, naomba watanzania na watu wote wanaofuatilia huduma yangu na nyimbo zangu wawe tayari kuupokea. Changamoto ninazokutana nazo katika huduma hii ya uimbaji ni pamoja na ukosefu wa fedha za kutosha za kukamilisha kazi zangu za uimbaji pamoja na chuki kutoka kwa waimbaji wengine pale tu Mungu anapoleta kibali juu yangu, kukubalika na watu, kusemwa vibaya ikiwepo na watu kuzusha mambo ya uongo na yasiyokuwepo kuhusiana na huduma yangu. Ushauri wangu juu ya waimbaji wote tupendane na tuombeane haina haja ya kuchukiana sisi kwa sisi, maana mwisho wa siku ni huduma tu, asante abarikiwe kila mmoja. Kama nilivyosema hapo juu kuwa sasa hivi nipo katika maandalizi ya video yangu mpya hivyo naomba wapendwa wote wawe tayari kwa yanayokuja yenye Baraka na upako wa kiMungu. Alieleza Brighton Mundah.

USHAIRI WA INJILI

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


Habari / MAHOJIANO 7

alhamis JULAI 16-31, 2020

Sina chakula, sina kodi, mnionavyo nje sio halisi NA MIKE SAMA, ARUSHA Ablenty ni nani? Mimi ni MC (mshereheshaji) kwa kupenda kabisa na huwa nikifanya nafurahi sana maana hakuna kitu napenda kama kufanya mtu afurahi na zaidi huwa napenda sana kuifanya picha kuwa halisi. So nimejikita sana na harusi, Sendoff, events za gospel na events za kijamii na makampuni kadhaa. Nafanya kuanzia planning ya tukio mpaka tukio nzima yaani management cause nina team nafanya nayo so sisi ni full package. Na sasa nafanya kazi official maana kuna usajili nimeshamaliza, nawakaribisha watu wote hakika hutojutia kufanya kazi na MC ABLENTY Je? wakati gani uliwahi kufanya kazi ikakuvunja moyo? Wakati naanza hii kazi, kuna wakati nilishafanyaga kazi nyingi sana bure na kuna nyingine niliumia na nyingine nilikuwa poa sana na hasa kilichokuwa kinaniumiza, ni picha wanayoniona nayo watu njee haikuwa halisi, sina chakula, sina kodi mpaka nikafukuzwa nyumba nilipokuwa naishi ila unaenda kwenye kazi watu wanakupongeza lakini hata kuthamini kuwa unatakiwa uishi hakuna na sababu unataka kukua inabidi ukaushe tuu maisha yaende na wakikuita tena unaenda. Hivyo maumivu yameshawahi kuwa mengi sana cause hata nyumbani walikuwa hawanielewi na picha ya mimi Leo nilibaki nayo mwenyewe, Ilikuwa inaniumiza na kutaka kukata tamaa kabisa. Mimi na wewe Tuongee na kusaidia watoto yatima bado vinafanyika? Yeah hicho kitu nilianza na sababu ilikuwa napenda kuona mtu akifurahi so nikaanzaga kitu inaitwa Mimi na wewe Tuongee na tuna hatua ila ilisimama kidogo sababu zikiwa nyingi japo wengi wanadhani sababu nimekuwa MC.

Kwanza misingi niliyoanza nayo haikuwa imara, pia vita yake ilikuwa kubwa maana kuna watu walizani ni issue ya kisiasa so ikaanza kuleta shida na ukakasi na vitu kuwa vingi nikaona itulie kidogo ila moyo wangu kufanya kwa jamii bado naendelea na pia ile programme inarudi soon na kwa ubora zaidi cause lazima tuguse maisha ya watu maana sijaumbwa kwaajili yangu ni kwaajili ya watu au mtu Fulani. Tunaona kazi mpya ya Review Session kila jumatano, hii iko vipi? Review Session ni kitu kipya kabisa nilichoanza hivi karibuni na kama hujawahi kukiona ni kila Jumatano katika YouTube channel yangu MC Ablenty. Sababu kubwa napenda ninachokipenda na huwa naamini kuna mtu kinaweza mjenga na kumpa hatua hivyo napenda movies na hapa naongelea movies zinazoweza kutujenga kwa namna moja ama nyingine. Kuna mengi sana yanakuja hivi karibuni na bora sana Hivi karibuni pia tunafungua ofisi ya MC Ablenty entertainment. Pia tunaanza kipindi bora sana cha gospel jina nalitoa hivi karibuni na maelezo mara tu kitakapoonekana. Wanaonifuatilia wanajua mwaka jana msimu wa Christmas tulikuwa na tukio so this time linaenda kuwa kubwa na zuri zaidi. Mambo ni motoooo, Alimaliza MC Ablenty. Kwa shughuli mbalimbali za MC tafadhali wasiliana naye kwa namba +255 652 861 961, anapatikana jijini Arusha na yupo tayari kufanya kazi mahali popote ndani na nje ya nchi.

TUNAPOKEA MATANGAZO NA KUYATANGAZA BURE KUPITIA GAZETI LETU. KARIBU SANA ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


WANAUME KAZINI

alhamis JULAI 16-31, 2020

8

YAJUE MAJERAHA YA WANAUME NA MWANDISHI WETU

T

akwimu zinaonesha kuwa Wanaume ndio wanaoongoza kupoteza maisha kwa kazi zaidi ukilinganisha na Wanawake. Zipo sababu nyingi sana zinazopelekea vifo vingi vya Wanaume. Wanaume kuhusika mstari wa mbele vitani, kutokujali sana mambo yanayohusu Afya, Kutokuwa makini Barabarani na kutochukulia mambo kwa mzigo wake ni maadui ya sababu zinazochochea vifo vingi vya Wanaume.

na wanadhani endapo Lakini sababu kubwa in- wakimwaga hisia zao ayochochea vifo vingi vya za kuumizwa basi wataWanaume ni MAJERAHA onekana dhaifu. Japo waya ndani. Wanaume wen- naume wanapokea manegi wameumizwa hisia zako no makali ya kuwakatisha na kusababisha fikra na tamaa, lawama, na mamtazamo wao kuathiriwa juto ya kufeli mitihani vibaya. Mbaya zaidi MA- mbalimbali ya kimaisha; JERAHA haya yamekua ya- bado wanaona ni Bora kisababishwa na watu wa wafe kiume kuliko kukubKaribu kama familia, mke, ali kimaisha machozi na watoto, ndugu wa Karibu kuachilia. n.k. MAJERAHA mengi huWanaume wengi wamesababishwa pia na Baba kataliwa na Baba zao; zao. wametelekezwa na Mama Wanaume ni watu wa- zao; wamesalitiwa na naoshikilia sana maumi- wenza wao; wamejeruhivu ya moyo, chuki na ku- wa na wafanyakazi wenlipiza kisasi na hawawezi zao na marafiki wa Karikuyaachilia wala hawako bu. Hii inawafanya kuhisi tayari kuyahadithia maa- kuwa hawana thamani tena ya kuishi na wengine

kujenga kisasi na kutokumuamini mtu. Mambo haya yanasababisha wanaume kufa ghafla kwa mshtuko na msongo wa mawazo.

MAJERAHA hayo; familia na makini yake huwa ni marehemu wa kwanza na kisha yeye hufuata.

Ndio maana ni muhimu sana kufuatilia DARASA LA Vifo vya Wanaume hawa WANAUME linaloendeshhaviishii tu kwenye mai- wa na Taasisi ya Wanasha yao Bali yanaende- ume Tanzania - MEN AT lea kupata athari kubwa WORK GLOBAL ili kuweza kwenye familia na jamii kujua mbinu za kuponya ya wanaume hao. Hivyo, MAJERAHA hayo kwa ajili kabla mwanaume aliyeje- ya MUNGU, FAMILIA NA ruhiwa hajafa; asipotibu TAIFA.

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


makala/ Habari

alhamis JULAI 16-31, 2020

9

NINI KILICHO MBELE YAKO.

MAJIRA NA NYAKATI - SEHEMU YA NNE za Ahadi zake kwetu, Mara nyingi tumekwa kusudi la kukakuwa tunashindwa milisha alichokusudia NA HELLEN SOGIA, PWANI kufahamu kilicho mbele kufanya kwako. yetu kutokana na hali aada ya kupita hiyo, tumekuwa na Yako mambo mengi, katika mambo taswira ya kuona kuwa ambayo hupita katikati matatu, katika Mungu yuko naye atahapo, hadi utekelezaji Makala zetu za nyuma;fanya, tukawa wavivu wake uweze kutokea. 1. WAKATI. na tukadhania kuwa Na katika kipindi hicho, 2. MAJIRA YALIYOANyale uliyoyaona kwenye mtu huwa anatakiDALIWA. ndoto, maono nk, vita- wa kusimama katika 3. MAJIRA KWA NYAmaombi ili kutengeza KATI ULIOAMRIWA. fanyika tu. Tukasahau kuwa yuko mpinzani. njia kwa ajili ya jambo hilo liweze na kuwekea Leo tunatazama eneo Katika kila tunaulinzi pia. Bila ya kufanla nne, ambalo ni;chokitegemea kutende- ya hivyo, kuna mambo ka katika maisha yetu, mengi hutokea hapo NINI KILICHO MBELE katika yale yalioko, katikati. YAKO. ambayo, kwa hayo, tuShetani hutega Kilicho mbele yako ni natazamia kuona hatma yetu katika yale ambayo mitego yake hapo, mambo yameandaliwa Mungu alikuwa ametuambayo mitego hiyo, na Mungu kwa ajili wekea, inaweza kusababisha yako, ambapo katika Kuna hatua ambayo sisi kuharibika kwa mimmambo hayo ndiko iliko tunahitajika kufanya ili ba ya vilivyokusudiwa hatma ya maisha yako. • Mengine yanakuwa jambo hilo liweze kuto- kwako, mimba ya kea, katika uhalisia wa udhihirisho wa baraka bado yamefichwa ulimwengu wa damu na zako, mimba ambayo kwako. nyama. ilikwisha kutungwa. • Mengine yakuwa

B

yamefunuliwa kwako kwa njia ya ndoto au maono ya waziwazi kwako. • Mengine Mungu anakuwa amesema nawe kwa waziwazi kwa njia ya sauti au ujumbe kutoka kwa mtumishi wake pia. • Mengine anakuwa amekupa kwa njia ya wewe kuyasoma kwenye Biblia ukakutana na ujumbe wako hapo. Yote haya yanakuwa yamehusu mambo yatakayotokea kwako baadae.

Mungu husimama katika uaminifu wake katika kutimiza yale:• Alilokuwekea. • Alilosema. • Alilokuonyesha.

Yohana 10:10. Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu, mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

Kumbukumbu 7: 9. Basi jueni ya kuwa Bwana Mungu wenu, ndiye Mungu, Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.

Shetani amekuwa akizuia, na kuharibu mipango ya maisha ya watu, kwa kuingilia kati kile ambacho hakijafunuliwa kwetu, kwenye ulimwengu wako wa damu na nyama. Yeye hukifuata katika ulimwengu wa rohoni na kuzuia kabla hakijafunuliwa katika ulimwengu wa damu na nyama.

Mungu ni mwaminifu, ni kwa huo uaminifu wake, Yeye husimama kikamilifu katika kutimi-

Baba na Mama Mchungaji Massawe wa Mlima wa Moto wakiwa na mtoto wao katika picha ya pamoja.

Familia yapitishwa kwenye magumu, wamshukuru Mungu kuwaokoa Na mwandishi wetu.

J

umapili iliyopita katika kanisa la Mlima wa Moto Kerai lililopo jijini Arusha, kulifanyika ibada ya shukrani iliyoihusisha familia ya Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Mchungaji Massawe na waumini wote wa kanisa hilo la Mlima wa Moto. Ibada ilikuwa nzuri sana, waimbaji, wachungaji na Askofu pamoja na watumishi mbalimbali walikuwepo. Ibada hii ililenga hasa matendo makuu aliyotendewa mama mchungaji Lilian Masawe kupitishwa kwenye magumu ambayo bila Mungu asingeweza kuyapita. Aidha neno la shukrani lilitoka Yeremia 30 : 19 “Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao, nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache, tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge.” “Ninamshukuru sana Mungu kwa matendo yake makuu aliyonitendea, hakika nimepitia magumu yaliyoniumiza sana moyo na kunikatisha tamaa kiasi cha kufa, ila nilikiri kwa Mungu kuwa sitakufa bali nitaishi na nilisimama na Mungu bila kuchoka, akanirudishia afya yangu na leo ninamshukuru kwa yote, mume wangu, familia, watumishi na kanisa la Mlima wa Moto ninawashukuru mno kwa kusimama nami katika maombi. Mungu awabariki sana.” Alisema Mchungaji Lilian Massawe

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


MAHOJIANO / NYOTA

alhamis JULAI 16-31, 2020

10

MAOMBI NA UFAHAMU WA NENO LA MUNGU NDIO NA MWANDISHI WETU DAWA YA KIBURI - EZEKIEL

B

SWALI: Kitu gani hukipendi kwa waimbaji wa injili? EZEKIEL: Sipendi muimbaji ambaye hajiamini kwenye kile anachokifanya, sijui nitaweza, sauti yangu mbaya, hua ninapofundisha hata kwaya sitakagi kusikia hizo kauli kabisa maana kama umeamua kumtumikia Mungu amini kwamba wewe ni wa thamani sana ndio maana akakupa kazi maalum. Hivyo hupaswi kujidharau au kujilinganisha na watu wengine.

wana Yesu asifiwe ndugu mnaofuatilia ukurasa huu makini sana wa “NYOTA WA SIKU� Tunatambua kila mtu ni nyota na ana nyota yake inayomuangazia zaidi kufikia mafanikio yake. Wiki hii tulipata wasaa wa kuzungumza na Ezekiel Makililo kutoka Kigoma mwisho wa reli. Anasema yeye ni mtoto wa 10 kati ya watoto 12 wa mzee Makililo, ni mshirika wa kanisa la FPCT ingawa tulifanya naye mahojiano haya akiwa Shinyanga Tanzania SWALI: Kaka nini kiu yako kwenye huduma uliyopewa? EZEKIEL: Kiu yangu ni kumtumikia Mungu kwa nguvu zangu zote na kuitimiza ahadi yake aliyonipa mpaka aridhike. SWALI: Kitu gani kinakupatia kipato cha kuendesha huduma? EZEKIEL: Ni mjasiriamali ila pia ni mwalimu wa kwaya na huduma za kusifu na kuabudu. SWALI: Wewe upo katika kundi la msanii au muimbaji wa injili? EZEKIEL: Ni mwimbaji ila kama uimbaji unatokana na sanaa basi na mimi nimo, kwa sababu ninapopata melodi, ninapojua kupangila uzani wa sauti, ninapojua tempo, key na vinginevyo nakuwa nimeshaingia kwenye sanaa, kwa hiyo nafanya sanaa kwa kumtumikia Mungu. Ila ukiniita msanii kama kazi yangu inatokana na sanaa ni hivyo.

MR &

NYOTA WA LEO - EZEKIEL MAKILILO

toka uanze huduma? EZEKIEL: Tangu nianze kufanya huduma nimepata vingi sana, maana maisha yangu yamebebwa sana na huduma, Mungu amekuwa akinifadhili sana, ninamshukuru sana Mungu.

SWALI: Umeshawahi kukutana na ugumu gani kwenye uimbaji? EZEKIEL: Ugumu au changamoto niliyowahi kukutana nayo katika uimbaji ni kushindwa kuaminiwa na kukosa fedha ila bado Mungu ni mwema.

SWALI: Kitu gani hutaweza kukisahau katika huduma? EZEKIEL: Sitaweza kusahau siku nilipoitwa kuhudumu jukwaani kwenye mkutano, nilitaka niimbe mubashara kwa sababu sikua na flash, kiongozi wa mkutano aliniita ili nikahudumu ila wakati mpiga kinanda anajiandaa ili niimbe yule kiongozi aliyeniita akapokea oda kutoka madhabahuni kuwa nishuke kwenye jukwaa apande mwingine. Ilinifedhehesha sana.

SWALI: Faida gani umeona

SWALI: Ni nini kinachochochea

MRS

huduma mtu aliyopewa na Mungu? EZEKIEL: Ili huduma ikue, tafadhali msikilize yule aliyekutuma, kama una huduma lazima umsikilize yule aliyekutuma kama vile anavyotaka. Ukimsikiliza Roho Mtakatifu aliyekutuma lazima huduma yako ikue tu. SWALI: Unanufaika vipi na mitandao ya kijamii, hususani Youtube, BBM na WE CHAT EZEKIEL: Kwa sasa nanufaika kwa kile Mungu alichoweka ndani yangu kinapenya na kuwafikia watu wengi zaidi ila kipesa bado sijaanza, faida kubwa ni muziki wangu ukipenya na kuwafikia watu wengi zaidi. Faida nyingine zitakuja kwa sababu ni ahadi ya Mungu kukutumikisha kisha mwisho atatupa ujira wa kile tulichokitenda.

SWALI: Zungumza neno na walioinuliwa wakawa na kiburi. EZEKIEL: Kaini aliambiwa dhambi inakutamani, lakini yakupasa uishinde. Kumbuka unapokuwa na Kristo na Neno likikaa kwa wingi, shetani hakai mbali anakaa pembeni na anakutafutia dhambi, na kiburi ni chanzo cha uwazi, Sasa ili kuishinda dhambi lazima tuwe ufahamu wa neno la Mungu, maombi na kutenda mema, tofauti na hapo hutoweza kushinda kiburi bali maarifa ya kiMungu na maombi tu. SWALI: Una ushauri gani kwa waimbaji wanaoianza huduma? EZEKIEL: Ushauri wangu kwa wanaoanza huduma ni kuwa waondoe kabisa mawazo kumtegemea mtu kukuvuta mahali fulani, hayo mawazo toa kabisa, lakini kitu unachotakiwa kujua ni kwamba Mungu aliyekuita atakufikisha mahali ambapo anataka wewe ufike. Yaani usitegemee mtu kabisa kukusaidia kufikia ndoto zako lakini ukimtegemea Mungu zaidi atakuinulia mtu yeyote na utaweza kufika anapotaka kufika. Pia fanya ile kazi ya Mungu kwa uaminifu kabisa maana ukifanya kwa uaminifu Mungu atakuinua ila ukifanya ili uinuliwe yawezekana ukachelewa sana.

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


Makala M0t0 Ulao

alhamis JULAI 16-31, 2020

11

MAMBO YA MTU NA MKEWE - 2

EV. IMANI O. KATANA

H

aleluyaaa! Atukuzwe MUNGU juu Mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. Mpendwa msomaji wangu tar 30.6 nilitimiza miaka kadhaa ya ndoa yangu, tumeifurahia na mke wangu na kukumbushana mengi. Karibu tuendelee mbele. Kama kuna kitu naweza kuwashauri vijana mnaotarajia kuingia kwenye ndoa ni kuwasihi kwamba jitunze kataa kabisa kuzini. Usitegemee kwamba ukichuma embe na kula likiwa bichi huwezi kuja kifurahia lililoiva. Ujana na fahari yake yote Mungu hajakuzuia kufanya chochote lakini amekataza na kusema usizini. Ninakuandikia makala hii kwamba mimi ninamshukuru MUNGU sijawahi kuzini.Ujana wangu nimemtumikia Mungu na niliweka agano kubwa na baba kwamba ni afadhali kufa kuliko kuzini. Maombi yangu kwa Yesu yalikuwa kuliko kuz-

ini, kwamba Kama itatokea nimeshindwa na jaribu hilo kuliko kuanguka dhambini bora niondoke katika dunia hii nikakae na BWANA.

bawanga hawauzi mabinti zao, Bali wanakupa binti kwa mahari inayolipika.Makabila mengine tujifunze kwa wakwe zangu.

Wakaka wazuri na wadada wazuri imeanikwa kwamba usizini Kut 20:14 yako madhara mengi ya kuzini kwa usitawi wa ndoa yako, tutaelekezana huko mbele katika mfululizo wa makala hii, ngoja niendelee na simulizi.

Mambo ya sijui ngambako laki tano, Ng’ombe 3 laki 4, Ulughoje Kali ifhikingi, laki2 sijui mablanket , mkaja wa mama, hapo bado mashangazi hawajakutoa upepo.Jamani msituonee kwa sababu tumeokoka tunafuata utaratibu.Unakuta baba wa bibi harusi na kaka za Bibi harusi wote walikwapua hawajafunga ndoa ukifika kijana wanakudunga mahari mpaka unajutaa, acheni hizo wapendwa wapigeni vijana mahari zinazolipika wakaendeleze zoezi la kuijaza nchi.

Sasa kama unavyojua Mungu anakupa mtu wa kufanana naye , nilipompata huyu malkia wangu tukakubaliana kwamba hakuna kuanguka katika dhambi ya kuzini Jambo ambalo tuliweza kulifanya kwa ushindi. Sasa ikatokea kwamba nataka kuoa , mazingira ya uchumi yalikuwa sio mazuri.Wapendwa walinishauri kwamba ningesubiri kwanza nijipange lakini msukumo wa kuoa ukawa mkubwa sana ndani yangu, nikakumbuka kwamba maandiko yanasema umfurahie mke wa ujana wako .Nikajua kuoa ni wakati wa ujana. Sitasahau nilienda kwa kaka yangu mmoja aliekuwa ametoka kuoa akaniambia “hatuoi kwa sababu tumejipanga, tunaoa kwa sababu muda umefika” kauli hii ilinitia nguvu Sana. Nikafanya mchakato wa Mahari, mke wangu ni mtu wa Sumbawanga, aisee watu hawa ni waungwana sana mahari zao ni rafiki sio Kama za kabila langu. Nakumbuka nilihangaika tu kupata jembe chapa jogoo hahaha hapo hakuna kupokea pesa lazima jembe. Waoaji karibu Sum-

Nitumie fursa hii, uwapo Dar es salaam kuabudu pamoja nasi kila siku ya Alhamis na jumapili saa KUMI Hadi KUMI NA MBILI JIONI. Na kila siku Ijumaa tuna Mkesha wa Maombi hapa hapa Moto ulao fellowship, Georgious House, MABIBO Makutano. Kwa MAOMBI, MAOMBEZI na SADAKA waweza kutuma kwa namba ya mpesa 0752 352 116. Mungu awabariki sana. Mwinjilist Imani O. Katana Whatsapp +255 752 352 116 katanaimani@gmail.com

Baada ya mahari mipango ya ndoa ikaanza kimbelembele nikataka harusi iwe tarehe yangu ya kuzaliwa yaan tar 16.5 wakongwe wakaniita upenuni wakaniambia tarehe ya ndoa anapanga Bibi harusi ama kweli kuishi kwingi nikuona mengi na kweli bibi harusi akapiga tarehe ya harusi 30.6 na kweli hekima za wahenga zilisaidia. Sikutaka kufuata Mkumbo, nilifahamu kipato changu niliamua kwamba ndoa itafungwa kanisani Kisha tutarudi nyumbani watu wachane majani ya migomba wapige wali, wapige maraine kumila imibhaghala hahaha halafu niwe nimeoa. Hakika nilioa kiinjilisti, fuatana nami wiki lijalo kujua jinsi ambavyo mambo ya mtu na mkewe hayapaswi kukupasua kichwa barikiwa.

TUNAPOKEA HABARI NA MATANGAZO MBALIMBALI, WASILIANA NASI KWA FAIDA YA WENGI ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


HABAKUKI 2:1-2

SOKA LA BONGO

ISSN 2714-2108: Toleo Na.009. Jumatano Julai 01-15, 2020

TETESI ZA USAJILI SOKA LA ULAYA

Real Madrid inaamini kuwa mshambuliaji Kylian Mbappe ,21, atakuwa na mazungumzo nao kuhusu uhamisho kutoka Paris St-Germain. Barcelona inamuuza kiungo mchezeshaji wa Brazil Philippe Coutinho, 28, kwa Arsenal na Newcastle huku wakijaribu kutafuta fedha za kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22.

YANGA YAISHUSHA AZAM FC NAFASI YA PILI BAADA YA KUIGALAGAZA SINGIDA UNITED 3-1. NA MWANDISHI WETU

P

AUL Godfrey, beki wa kulia leo ameifungia timu yake bao la kwanza ndani ya msimu wa 2019/20 ndani ya Ligi Kuu Bara wakati wakishinda mabao 3-1 mbele ya Singida United. Mchezo huo wa ligi ulichezwa leo Julai 15 Uwanja wa

Taifa na kuwafanya Yanga wasepe na pointi tatu. Bao la pili lilipachikwa na Mrisho Ngassa alipachika bao la pili dakika ya 37 akimalizia pasi kutoka kwa Deus Kaseke. Mwili jumba dakika ya 68 Ikpe Gnamien alipachika bao la tatu baada ya kumpiga chenga kipa wa Singida United na kuwafanya Yanga

waifunge jumla ya mabao 3-1 Singida United. Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Liti, Yanga ilishinda kwa mabao 3-1 ambayo yamejirudia tena Uwanja wa Taifa. Ushindi huo unaifanya Yanga kujikita nafasi ya pili ikiwa na pointi 67 baada ya Azam FC kupoteza mbele ya Mtib-

Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 28, anataka kurudi Barcelona, na Paris St-Germain wanapiga hesabu za thamani yake huku akiwa amesalia na kandarasi ya miaka miwili katika mkataba wake Manchester United itakosa malipo ya £25m kutoka kwa wafadhili iwapo watafeli kufuzu katika michuano ya kombe la klabu bingwa Ulaya. Inter Milan wanafikiria kumnunua kiungo wa kati, Mfaransa N’Golo Kante huku Blues wakiwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kumuuza mchezaji huyo wa Ufaransa, 29. wa Sugar kwa kufungwa bao 1-0. Azam FC inashushwa mpaka nafasi ya tatu ikiwa na pointi zake 67 kibindoni. Singida United ipo nafasi ya 20 ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi 35 ambapo bao la kufutia machozi lilifungwa na Stephen Sey 45.

TANGAZA NASI MATANGAZO MBALIMBALI UONE FAIDA NA NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook

Articles inside

Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.