JARIDA LA ZAMU YANGU OKTOBA 01-15,2021

Page 1

Jarida huru pendwa la mtandaoni la Kikristo linalotoka tarehe 01 na 16 kila mwezi.

eekklesiatz@gmail.com

I

ZaMuYaNgu ISSN 2714-2108 Uk.04

Glory Kadeghe

MOYO WANGU

Uk.11

TOLEO NA. 38, IJUMAA OKTOBA 01-15, 2021

Askofu David Oyedepo ni nani? Uk.03

YALIYOMO

UK 09

MWANAMKE KAMA UMEOLEWA NA UNA DALILI HIZI 10, Uk.09 NDOA YAKO IPO MATATANI.

Mambo matano yenye faida kuliko fedha Bondia mlokole Manny Pacquiao astaafu Ndondi

UK 08

UK 12

HABARI . MAKALA . NENO . HISTORIA . AFYA . VITABU . TANGAZO . MICHEZO PROUDLY SPONSORED BY:- RADIO 5 | EVG MINISTRY | FOUNTAIN RADIO | M!SA RICE | SHALOM RADIO & TANGANYIKA PRODUCTION

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE


ZaMuYaNgu Oktoba 01-15, 2021.

Ibada Chumbani MUNGU ANAPATIKANA WAPI?

Uchambuzi wa kitabu

kuomba hivi ni muhimu kwetu).

NA AP. HELLEN SOGIA.

SURA YA SABA. Ziko nyimbo zinazoweza kumuingiza mahali pa Ibada.

Tenzi 50. YESU NAKUPENDA U MALI YANGU. 1. Yesu nakupenda, u mali yangu, Anasa na dhambi sitaki tena, Na mwokozi aliyeniokoa, Sasa nakupenda, kuzidi pia. 2. Moyo umejaa, mapenzi tele, Kwa vile ulivyonipenda mbele, Uhai wako ukanitolea, Sasa nakupenda, kuzidi pia. 3. Ulipoangikwa msalabani, Tusamehewe tulio dhambini; Taji ya miiba uliyoivaa, Sasa nakupenda, kuziidi pia. 4. Niwapo hai, niwapo maiti, Kupendana nawe kamwe siachi; Hari za kifo zikinienea, Sasa nakupenda, kuzidi pia. 5. Mawanda mazuri na masikani, Niyatazamapo huko mbinguni, Tasema na taji nitakayovaa, Sasa nakupenda, Kuzidi pia. Tenzi 114. BWANA MUNGU NASHANGAA KABISA.

1. Bwana Mungu, nashangaa kabisa, Nikitazama jinsi ulivyo, Nyota, ngurumo, vitu vingi vyote, Viumbwavyo kwa uwezo wako, Roho yangu na ikuimbie, Jinsi wewe ulivyo mkuu, Roho yangu na ikuimbie, Jinsi wewe ulivyo mkuu. 2. Roho yangu na ikuim-

bie, Jinsi wew ulivyo mkuu, Roho yangu na ikuimbie,Jinsi wewe ulivyo mkuu. 3. Nikikumbuka kama wewe Mungu, Ulivyompeleka mwanao, Afe azichukue dhambi zetu, Kuyatambua ni vigumu mno. 4. Yesu mwokozi utakaporudi, Kunichukua kwenda mbinguni, Nitashukuru na kwimba milele, Wote wajue jinsi ulivyo.

Kuingia chumba cha ndani na Bwana, ina maana kujiachilia kwake muda wote, kwa hiari yako mwenyewe, na sio kwa kushurutishwa wala kujilazimisha. Hapo ni mahali pna unakuwa kwenye uwepo wake Bwana masaa yote, na uwapo popote pale, na katika mazingira yeyote yale; Utamsikia akisema nawe, napokuwa kazini, barabarani, jikoni ukipika, kwenye sherehe, mahali popote pale, na anaweza akasema na wewe mahali popote, katika mazingira yeyote, hatachagua ni wapi pa kusema nawe, maana hata wewe hutachagua ni wapi na wakati gani useme nae, haitakulazimu kujitenga, au kufunga kwa maombi, ndipo umsikie Bwana akisema, (sina maana tusifunge wala

Uwepo unaomfunika mtu unaotokana na ushirika wa Ibada; Ni tofauti na uwepo unaoshuka wakati nguvu za Roho Mtakatifu zinaposhuka wakati yuko kazini akifanya kitu kwa mtu, hasa wakati mtu yuko kwenye kusanyiko. Roho Mtakatifu huwa anaelekeza nguvu hizo kwenye kusudi maalum la wakati huo; Inawezekana ni kwa ajili ya kuponya, au kugawa vipawa, n.k. wakati wa huduma hii ya Roho Mtakatifu, mtu ukajikuta naogelea kwenye uwepo uliojaa nguvu, na wengine utakuta ni kwa ajili ya msisimko tu, unaotokana na nguvu ya Roho Mtakatifu inaotembea mahali hapo kwa wakati huo, mtu akishatoka mahali hapo, au baada ya muda Fulani, au baada ya siku chache, mtu anajikuta anarudia hali yake ile ile ya kawaida.

Uwepo unaotokana na mtu kuwa na Ibada na Mungu, ni uwepo unaoambatana na mtu siku zote, kila saa, na kila dakika. Popote aendapo, usiku na mchana; uwepo huu unatokana na mapenzi kati ya mtu na Bwana wake, kama ilivyo mapenzi kati ya wawili wapendanao (mume na mke)

KANISA.

Kanisa la Kristo leo, limefikia mahali pa kutojielewa na limefikia mahali pa kupoteza mwelekeo, (confussed). Kwa sababu limepoteza mapenzi yake kwa Bwana Yesu. Halijataka kuingia kuwa na muda wa utulivu katika chumba cha ndani na Yesu; Laiti tungelifahamu, na kukubali

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE

7

2

kuingia, lingefunuliwa siri nyingi zilizojificha, na hii ingeondoa maswali maswali tuliyonayo leo; Kwa maana, ingekuwa rahisi sana kwetu kupokea majibu yetu, na kujulishwa mambo ya sirini tukiwa chumbani; Siri huwa hazianikwi barabarani, wala haziongelewi barazani, wala sebuleni; bali mahali pa siri, kama ilivyo siri, na si mahali pengine popote, ila kwenye chumba cha ndani; Sisi kama kanisa hatupashwi kumzuilia Yesu kitu chochote, kwa sababu sisi na mali zetu, sote ni mali ya Bwana.

Kanisa leo limeshindwa kumpa Yesu Mpenzi wake zawadi, na hata kama litampatia; Lakini baadae hugeuka na kumdai tena, arudishe hiyo zawadi aliyoipokea tena kwa matusi na mateke. (mtu anatowa kitu kanisani na kurudi tena kudai kwa ugomvi). Kanisa limegeuka kuwa mwizi, kumwibia mpenzi wake fungu la kumi, bila kujali laana itakayomlaani. Ni lazima kanisa lifahamu kuwa kanisa ni mali ya Mungu; Na ili linatakiwa liache kuishi kikahaba na Yesu wake. Sio sahihi kanisa kujichanganya na uovu, maana haiwezekani kanisa kuwa na ibada na Bwana, huku likiwa na matendo ya ukahaba, kujichanganya na uovu.

ITAENDELEA KATIKA TOLEO LIJALO __________________________________ Apostle Hellen Sogia

THE OAK MISSION MINISTRY. P.o Box 30838. Kibaha Pwani.

Simu: 0753 351 048 au 0716 711 867

_____________________________________


ZaMuYaNgu Oktoba 01-15, 2021.

ASKOFU DAVID OYEDEPO NI NANI?

Historia

NA MWANDISHI WETU

S

eptemba 27, 1954 alizaliwa Mhubiri wa Neno la Mungu, Mwandishi wa vitabu vya Kikristo, Mfanyabiashara, Mhandisi wa ujenzi na mwanzilishi wa Kanisa la Faith Tabernacle lililopo

Ota katika jimbo la Ogun nchini Nigeria na mwanzilishi wa Huduma ya Living Faith Worldwide maarufu Winners Chapel International Bishop David Oyedepo. Alizaliwa mjini Osogbo nchini Nigeria. Jina lake halisi ni David Olaniyi

Oyedepo. Oyedepo alikulia katika familia ya kidini. Baba yake alikuwa mwislamu, mama yake aliyefahamika Dorcas alikuwa muumini wa kanisa la Holy Order of Cherubim and Seraphim Movement tawi la Aladura huko nchini Nigeria. Oyedepo alikulia kwa bibi yake mjini Osogbo ambaye alimfundisha mambo mengi kuhusu Mungu. Oyedepo aliokoka mwaka 1969 wakati huo akiwa na miaka 15 kutokana na msukumo alioupata kutoka kwa mwalimu wake aliyefahamika kwa jina la Betty Lasher. Alisomea masomo ya Usanifu wa Majengo katika Chuo cha Kwara State Polytechnic. Pia aliwahi kufanya kazi katika Wizara ya Nyumba mjini Ilorin kabla ya kuacha na kuendelea na wito wake wa kimisheni.

3

Alipata shahada ya uzamivu nchini Marekani katika Chuo Kikuu cha Honolulu, Hawaii. Oyedepo aliwahi kusema alipokea upako na maono kutoka kwa Mungu ambaye alizungumza naye kwa saa 18 mnamo Mei 1981. Maono hayo yalikuwa kwa ajili ya watu wanaokandamizwa na Ibilisi. Maono hayo ndiyo yaliyosababisha kuanzishwa kwa huduma ya Winners Chapels International.

Mnamo mwaka 2011 Jarida la Forbes lilimtaja Oyedepo kuwa ni Mchungaji mwenye Utajiri mkubwa nchini Nigeria. Oyedepo amekuwa akitoa huduma kupitia Winners Chapel zaidi ya miji 300 duniani kote ambapo barani Afrika yupo katika nchi 45. Pia ameenda hadi Dubai, Uingereza na Marekani. Mbali ya kuwa ni mtumishi wa Bwana kwa sasa ni Kansela katika Chuo Kikuu cha Covenant na Landmark vilivyopo nchini Nigeria.

BADO UNA NAFASI TENA. NA MWANDISHI WETU

D

audi Kweka Ni Mtumishi Wa Mungu katika uimbaji wa nyimbo za Injili hapa Tanzania, Ameachia kazi nzuri kama HODARI, JINA YESU Na UNANIPENDA SANA. Hivi karibuni aliachia kazi mpya inayoitwa JIBU. Kwanini JIBU?

“Jibu ni ujumbe ambao umebeba maisha ya kila mmoja na maisha yana changamoto katika uchumi, mahusiano, familia na hata biashara. Na kuna wakati watu tunakata tamaa na KUSHINDWA kuendelea mbele lakini yote katika yote TUKUMBUKE kwamba bado JIBU lipo na yupo MUNGU anayeweza kuleta MAJIBU ya maswali yetu. Hivyo BADO UNA

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE

NAFASI TENA, USIRUDI NYUMA” Mpenzi msomaji wetu, kazi yake Daud Kweka sasa inapatikana Youtube na kwa jina la Daud Kweka. Pia anapatikana katiks mitandao yote ya kijamii. Karibu sana usaidiane na Daud kueneza injili kupitia huduma yake ya uimbaji.


ZaMuYaNgu Oktoba 01-15, 2021. HABARI. Kibonzo

Na Kissabella Michael

B

wana Yesu asifiwe. Naitwa Hope Mwende Mwende ni mzaliwa wa Kenya, County ya Makueni, Emali, ninaishi Mombasa ni Muimbaji wa nyimbo za injili, namshukuru Mungu kwa kipaji na kibali cha kumtumikia kwa njia ya uimbaji tangu mdogo nikiwa darasa la tano. Nimefanikiwa kutoa albamu tatu ambazo natarajia kuzin-

Askari Polisi apiga tatu kwa mpigo Kenya.

dua zote tarehe 6/11/2021 pia kuwekwa wakfu huduma iliyoko ndani yangu ya uimbaji.

Mbali na uimbaji mimi nafanya kazi na Serikali ya Kenya kama Polisi na namshukuru Mungu sababu ya nafasi hiyo ya kuhudumia Wakenya kwa upande wa usalama na pia Kwa kuihubiri injili kupitia uimbaji wangu. Kuna changamoto zozote katika huduma au kazi unayofanya?

Changamoto hazikosi kwanza ukiangalia kazi ninayoifanya ambapo ni ngumu mtu kuamini kuwa unaweza kuwa Polisi ambaye ameokoka cha ukweli, Jambo ambalo hufanya wengi kutoamini uimbaji wangu ukilinganisha na tabia zinazoambatanishwa na Polisi, lakini naishukuru sana kwanza familia yangu wameniamini na wanajua nimeokoka na Mungu ananitumia sana tu, pili niwashukuru pia wachungaji niliopitia mikononi mwao hawakuangalia ubaya unaozungumzwa kuhusu

4

maana ndio imekuwa daraja la kunisogeza mbele huku nikiwa ni mwanafunzi wa Chuo kwa wakati mmoja. Inakua ni ngumu saa nyingine kupangilia mambo yote lakini neema ya Mungu yanitosha na kuniwezesha. Suala zima la ndoa vipi? Umeolewa? Kwa upande wa ndoa mimi bado ni msichana ila siku moja nitawaalika katika harusi yangu. Ninachoomba Mungu kila wakati ni kunipa kunyenyekea tu sababu mara nyingi sisi waimbaji tunapoinuliwa huingiwa na kiburi na jeuri mpaka tunatoka katika malengo tuliyoitiwa kama waimbaji wa nyimbo za injili. Vipi kuhusu kolabo na waimbaji wenzako? Nimekua nikishawishiwa kufanya kollabo na waimbaji wengine lakini jambo hili bado sijapata wepesi wake mpaka pale Mungu atanielekeza tu.

Polisi bali waliona Mungu mkuu aliye ndani yangu na wakanipokea vizuri sana tu. Changamoto nyingine ni mtu kunichukia tu sababu ya kazi yangu na hilo kufanya hata asiupokee muziki wangu lakini kufikia sasa hivi naona wengi wamenielewa vizuri na wanaendelea kuniamini na kuamini kazi yangu ya uimbaji ambapo wimbo wangu mpya Ee Mungu unaendelea kufanya vizuri. Changamoto ingine ni kupata mda mzuri wa kuweza kuhudumu kwa sehemu tofauti sababu ya kazi yangu ambayo pia naiheshimu sana

Unawashauri nini waimbaji wenzako wa injili? Ushauri wangu Kwa waimbaji wote tuongozwe na Roho wa Mungu, tupendane, tutulie makanisani chini ya neema ya wachungaji wetu hata kama tunatoka kuieneza injili na zaidi ya yote tusiimbe tukilenga pesa, tuimbe tukilenga wito wa kugusa mioyo ya watu. Wacha Mungu awabariki sana na muendelee kunisaidia huduma yangu ya uimbaji. Napatikana YouTube kwa jina Mwende Mwende. Asanteni sana na Karibuni wote kwenye Uzinduzi tarehe 6/11/2021 Temple of grace redeemed Magongo. Kwa Rev. Dr. Joseph Maweu.

TANGAZA NASI

+255 766 231 717

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE


ZaMuYaNgu Oktoba 01-15, 2021. Neno la Mungu Mahubiri

5

FAIDA ZA MAOMBI YA KUFUNGA

NA MCH. M. KABALAMA

B

wana Yesu Kristo asifiwe sana mpendwa wangu katika Yesu Kristo. Nakukaribisha katika somo hili la siku ya leo. Kabla hujachukua jukumu la kuomba ni lazima kwanza uamini kwamba Mungu anatenda, anajibu. Marko 9:23; • Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. Kwa hiyo inakupasa uamini ndipo utaona mambo yanawezekana. Hata hilo ambalo unaona ni gumu, ukiamini linawezekana maana hakuna jambo lililo gumu kwa Mungu. Yeremia 32:27. • Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza? Kuna wakati ambao unapaswa uombe kwa kufunga kwa kuwa maombi ya kufunga ni mhimu sana kwa kila aliyeokoka. Faida za maombi ya kufunga. Hapa nitaweka baadhi ya faida za kufunga. (i). Ni kuimarisha wito na uteule wetu. 2 Petro 1:10; • Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. Pasipo kufunga na kuomba tunaweza kujikwaa katika wito wetu, hivyo zinahitajika juhudi na nguvu ili kutufanya tusijikwae. Katika biblia kuna bibi, kikongwe wa miaka 84 aliyekuwa ni mjane, lakini alikuwa anafunga na kuomba.

Luka 2:37; • Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.

di kumpenda Mungu. Kupitia fundisho hili leo uamue ndani yako kuweza kufunga na kuomba, nakwambia kama vile Mungu aishivyo atakwenda kukuhudumia.

Hii ni ajabu sana, katika umri huu siyo rahisi kuweza kufunga na kuomba, lakini huyu alifanya. Leo kuna we wenye umri mdogo kabisa, chini ya miaka 40 wanashindwa kufunga na kuomba, hivi kweli utakuwa na cha kukitetea mbele za Mungu? Kumbuka kuwa maombi yanapaswa kuwa maisha ya mkristo, maombi yanapaswa kuwa mkono wa kupokea kutoka kwa Mungu kwa kila hitaji.

(iv). Unapofunga na kuomba unamruhusu Roho Mtakatifu kukuongoza na kukutumia.

(ii). Maombi ya kufunga hukufanya uwe na nguvu za Mungu. Mathayo 11:12; • Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. Ufalme wa Mungu hutekwa na wale wenye nguvu tu, pasipo nguvu za Mungu huwezi kuuteka ufalme wa Mungu. Wakati ambao mawakala wa shetani wanawinda maisha yako,unahitajika kuwa na nguvu za Mungu ili kuwashinda. Kwa njia ya maombi ya kufunga, unapata nguvu za rohoni ili kuweza kushinda vita na magumu yote. (iii). Kwa njia ya Maombi ya kufunga, hukufanya uongezeka kiimani. Mathayo 17:21; Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga. Ikiwa kuna mambo ambayo hayatatoka ila kwa kusali na kuomba, ni wazi kwamba pale utakapofunga na kuomba juu ya jambo fulani na ukapokea majibu ya maombi yako basi imani yako itaongezeka na utazi-

inawezekana Mungu kusema na wewe ikiwa utaamua kufunga na kuomba.

1 Wakorintho 12:11; • Lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. Kuna watu wana huduma lakini huduma hizo hazifanyi kazi kwa sababu ya kutokuomba. Kumbuka kuwa Yesu alisema, ”Mengine yatawezekana kufunga na kuomba.” Unapofunga na kuomba unamruhusu Roho Mtakatifu akutumie kwa kuwa wakati huo unakuwa umeimimina roho yako na umejinyenyekesha kwa Mungu. (v). Maombi ya kufunga na kuomba yanaweza kukufungulia njia ya kuitwa. Matendo ya Mitume 13:2-3; 2 Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. • 3 Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.

Kama kwa njia ya maombi ya kufunga Mungu anazungumza na watumishi wake hawa, hata kwako

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE

Maombi ya kufunga yana faida nyingi sana, hizo hapo juu nimekuwekea baadhi tu hivyo sasa unalo jukumu la kuhakikisha kwamba unaomba.

Ni mimi, Mch. Kabalama M. M. +255 753 305 957.


ZaMuYaNgu Oktoba 01-15, 2021. NYIMBO MPYA Tangazo

Kazi zilizoingia Youtube wiki hii.

6

Doreen Tito Atafanya Njia

Boaz Danken Uongezeke Yesu

Glory Kadeghe

MOYO WANGU

Sam Yonna x Upendo Mwanri - Hossana

JE UNA WEWE NI MUIMBAJI, MUHUBIRI, MWALIMU, MSANII AU UNA HABARI, BIDHAA, TANGAZO NA UNGEPENDA KUTANGAZA NASI? WASILIANA NASI SASA KUPITIA +255 766 231 717. WHATSAPP / SMS / CALL ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE


7

ZaMuYaNgu Oktoba 01-15, 2021. Shairi Tatu za wiki

Sarah Magesa - Nakungoja

WASANII WA INJILI

Bado bado nakungoja hata kama nonalia Baba Bado bado nakungoja hata watu wote waniache. Niko hapa mwanao bado nakungoja. Nakusubiri wewe mwenye majibu yangu. Niko hapa mwanao bado nakungoja. Nakusubiri wewe mwenye hatima yangu.

Bado bado nakungoja niko hapa Yesu. Bado bado nakungoja niko hapa Baba. Bado nakutazama wewe Yesu, Niko hapa mwanao bado nakungoja. Niko hapa Yesu, niko hapa mwanao, Bado nakungoja nalia machozi lakini nakusubiri wewe Baba Kuna mtu mmoja aliyeitwa ayubu. Maisha yake ya mwanzo yalikuwa mazuri sana. Lakini mwisho maisha ya ayubu, yaliku wa mabaya Lakini mwisho maisha ya ayubu, yaliku wa mabaya. Alikuwa na mali nyingi mungu alimbabriki. Alikuwa na familia uzuri Mungu alimbariki. Alikuwa na maisha mazuri tena ya kifahari Alikuwa na kila kitu ayubu Mungu alimbariki Lakini mwisho wa siku ayubu alibaki masikini,

ZY GOSPEL Top3

3.

NEEMA CIZUNGU - SEMA NAMI

2.

IRENE ROBERT - MABILIONI

1.

KANYE WEST - DONDA

B.

SARAH MAGESA - NAKUNGOJA

Tena pamoja na umasikini alioza mwili mzima. Tena pamoja na yote alikuwa ni mtu wa shida nyingi,

Alilia lia lia kila wakati ayubu. Aliteseka kwa mawazo ayubu, Lakini moyo wa ayubu ulimtumainia Bwana, Lakini ayubu alimngoja Yesu Lakini ayubu alimsubiri Bwana. Mwisho wa siku mambo ya ayubu yakabadikali, Aliyekuwa han akitu akawa mwenye utoshelevu Ayubu alikungoja bwana Ayubu alikusubiri. Bado bado nakungoja, hata waniache peke yangu. Nipo hapa mwana bado nakungoja. Nipo hapa mwana bado nakungoja, Bado bado nakungoja, bado nakusubiri Baba, Bado nakuangalia wewe, bado nakutumainia wewe, Nipo hapa mwana bado nakungoja. Nipo hapa mwana bado nakungoja Baba niko hapa. Kama ni kusoma nimesomu sana eehe. Nilikuwa na kazi nzuri sana. Kama ni elimu niilikuwa na elimu nzuri, Ya duniani hapa. Hata familia nilikuwa na familia nzuri sana, Nilikuwa na watoto, nilikuwa na mali nyingi

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE

sana Lakini vyota wimeondoka Yesu. Lakini vyota wimeondoka Bwana, Nimebaki sina mbele wala nyuma mungu wangu, Nimekuwa mtu wa kuomba omba kila siku, Nimeachishwa kazi nimefutwa kazi.

Sina mbele wala nyuma, Nimefukuzwa kazi sijui Bwana mimi ninaishije, Ila moyo wangu bado unakusubiri, Ila moyo wangu bado unakungoja, Ila moyo wangu bado unakutazama wewe, Lakini ayubu alimsubiri Bwana, Mwisho wa siku mambo ya ayubu yakabadilika, Aliyekuwa hana kitu akawa mwenye utoshelevu, Na mimi ninakungoja Bwana, Na mimi niko hapa Baba ninakusubiri. Bado bado nakungoja, Bado Yesu bado nakusubiri wewe, Nipo hapa mwana bado nakungoja, Nipo hapa mwana bado nakungoja, Bado bado nakungoja, Bado Yesu bado nakusubiri wewe. Uliyebeba hatima ya maisha yangu, Nipo hapa mwana bado nakungoja, Nipo hapa mwana bado nakungoja, Nakungoja Yesu wangu.


ZaMuYaNgu Oktoba 01-15, 2021. MOTO ULAO MAKALA

MAMBO MATANO YENYE THAMANI KULIKO FEDHA. ki kwa kutupa pesa na akili, tukitumia akili na afya basi twaweza kufikia malengo yetu.Hivi unajua wako watu wanagaharamia mamilioni ya pesa ili kuiendelea kuishi, sikiliza uzima unathamani kubwa kuliko pesa.

NA MCH. IMANI O. KATANA

M

pendwa msomaji wa gazet letu pendwa la zamu yangu ni wakati mwingine tena ninakusalimu katika jina kuu la Yesu Kristo, MUNGU amekuwa mwema tena kutufikisha jumapili ya leo. Tayari nimeeleza mambo manne ikiwa pamoja na hekima, jina jema, kibali cha MUNGU na Karama za MUNGU leo namalizia jambo la tano. Kusema ukweli mpendwa wangu vitu vyenye thamani kubwa wala hata havina gharama, mathalani hewa ya oxyegeni ambayo ndio hewa inayoleta uhai kwetu, ni bure kabisa.Ni ukweli usiopingika kwamba ukikosa hewa kwa dakika tano, basi afya yako itakuwa matatani kuelekea kifoni, lakini pamoja na umuhimu wa hewa hii lakini bado ni bure. Kadhalika maji ni kitu cha muhimu sana katika miili yetu lakini , ukiondoa huku mijini maji ni bure kwa asili yake, ila maswala ya uchafuzi wa mazingira yamekuwa kikwazo kikubwa kufanya watu watumie maji ya bure kwa kuhofia maambukizi. Katika kitabu cha Luka 12:15 imeandikwa “Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo. Leo nazungumzia suala zima la uzima wa mtu ni bora mara nyingi kulikom pesa. Watu wengi wanafikiri pesa ni bora ndio maana kuna wanaodiriki kuuza figo zao ili wapate pesa. Lakini sikiliza hekima hiii

uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu alivyonavyo. Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi;lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa. Luka 10:41-42. Huyo ni BWANA wetu Yesu mwenyewe anamwambia Martha kwamba kinachotakiwa ni kitu kimoja kukaa miguuni kwa MUNGU na kujifunza kwakwe. Watu wengi wanafikiri wakipata pesa ndipo watakuwa wenye furaha tele na Amani tele lakini kumbe sivyo, pesa haina uwezo wa kununua furaha, inashangaza kuona mamilione kama Peter Duff, Rei Jane Huai, Howard Worthington ni miongoni mwa orodha kubwa ya watu matajiri waliojinyonga na kukatisha Maisha yao. Watu wana pesa lakini wana kansa, hawana tena furaha na Maisha yao. Mimi nataka kukushauri mpendwa msomaji wangu , wakati mwingine tunakuwa na pilika za kuomba baraka , tukimaanisha pesa kumbe MUNGU tayari ametubali-

Mtu Tajiri kuliko wote waliowahi kuishi, yaani Sulemani mwana wa Daudi, yeye ndiye anaongoza kwa kuandika kuwa mambo yote ni ubatili chini ya jua, anatushauri kwa kusema “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.” Mhubiri 12:1314. Kutokana na uwezo mkubwa wa kifedha aliokuwa na Sulemani alijaribu kila kitu alichokitamani katika moyo wake kukifanya , lakini mwisho wake akagundua kuwa ni ubatili.Napenda kukushauri mpendwa msomaji wangu kwamba Uhai ulio nao ni wa thamani sana kuliko pesa, usikubali kuhatarisha uhai wako kwa sababu ya pesa, ndio maana watu husema pesa zinatafutwa. Lakini uhai wenyewe hauwezi kutafutwa, tumepewa kuishi mara moja.Tuthamini uzima wetu kuliko pesa Ndiposa Yesu alisema Math 16:26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya

TUNAPOKEA MAKALA NA SHUHUDA MBALIMBALI KUPITIA NAMBA YA WHATSAPP 0766231717 ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE

5

8

nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Itakufaidia nini kama utapata mabilioni ya shilingi na ukapoteza nafsi au uhai wako.Kumbuka ni mwili ndio unaokupa haki ya kukaa katika dunia hii bila mwili, huwezi ukaishi duniani, Ndio maana huwa inanishangaza kuona mtu, hauoni muujiza wa uhai ambao MUNGU amempa anang’ang’ana kununua vitambaa na mafuta ya upako ili abarikiwe. Eti kwenda ulaya ni muujiza mimi nasema muuujiza sio kwenda ulaya muuujiza ni kwenda mbinguni Yesu atakapo kuja. Ni heri mtu yule asiyeyatia mavazi yake uchafu kwasababu ya pesa. Uwe miongoni mwao. Mpendwa msomaji nakushukuru kwakuwa msomaji mzuri wa Makala hizi , na wiki lijalo nakuletea mfululizo mwingine mzuri sana, ambao utakupa nguvu mpya na Amani tele katika kutafuta Usowa MUNGU. Barikiwa ni mimi nikupendaye Imani Oscar Katana. Mpendwa msomaji unaweza kuwa sehemu ya baraka kwa kuweka alama katika ujenzi wa kanisa unaondelea hapa kanisani bado tunahitaji matofali na mabati.Tofali moja ni sh 1000 na bati moja ni sh 20000/= Karibu sana tuijenge nyumba ya BWANA.


ZaMuYaNgu Oktoba 01-15, 2021. MAHUSIANO NDOA

MWANAMKE KAMA UMEOLEWA NA UNA DALILI HIZI 10, NDOA YAKO IPO MATATANI.

NA MWANDISHI WETU

W

anawake wote sio sawa kifikra kuna namna baadhi ya wanawake wanaweza kuwa wanatenda mambo ambavyo kwa namna yao hiyo ya kimienendo ikakusaidia ukiwa kama mwanaume kutambua upumbavu wake. Labda unataka kufahamu upumbavu ni nini? Upumbavu kwa muktadha huu ni hali ya kukosa utimamu kifikra na hivyo hali hiyo kumfanya mwanamke ama mtu mwingine kutenda mambo ya ajabu yasiyo ya kistaarabu ama mambo ya aibu. 1. Analala pasipo kumjali mumewe. Hali hii ipo kwa wanandoa wanaoishi pamoja. Ndoa huwa na mitihani yake na moja wapo ya mtihani mgumu ni wanandoa kuendelea kuwa na hisia na mwenzi kuelekeana hata baada ya kuwa wameishi pamoja kwa muda wote wa ndoa. Sasa katika ndoa hiyo suala la mwanamke kulala mapema ama kufanya mambo yake pasipo kujali hali ya mumewe kama kala ama kumuandalia mahitaji mengine ya nyumbani. 2. Ni mbishi Mwanamke mpumbavu huwa na sifa ya kubishana na mumewe kila mara, yeye hujihisi kuonewa au kila wakati yupo sahihi na

hivyo kutopendelea kusikia upande wa kimaamuzi wa mume wake. Mpumbavu hupendelea kubishana hata katika mambo madogo ambayo angeweza kuyasuluhisha na mume wake. 3. Anapenda kumnyima mume wake unyumba. Mwanamke mpumbavu anapenda kumyima mume wake unyumba na anadhani akimnyima ni amemkomoa. Pasipo kujua kwamba kufanya hivyo kuna hatarisha hali ya ndoa yake, kwani kitendo hicho kinaweza kumfanya mwanaume achepuke ili kutosheleza tamaa yake ya kingono.

4. Anapenda kuzungumzia mafanikio ya familia za watu. Mwanamke huyu anapenda kuzungumzia mafanikio ya watu aliofahamiana nao kwa muda mrefu, anawasifia hata muda mwingine anaonesha wazi kutoridhishwa na hali ya nyumbani kwake. Badala ya kuweka mipango ya kuboresha kipato cha familia yeye anakuwa bize na maisha ya watu.

nyumbani wanahitaji hela, mara deni au wanapaswa kuboresha nyumba na mengineyo.

6. Ni msengenyaji Mkiwa pamoja tu anaanza kuwasema vibaya majirani na watu wengine ambao ni marafiki zake. Mwanamke wa hivi ni hatari, haishangazi kwamba inawezekana hata muda mwingine yeye hukusema anapokuwa vijiweni uwapo kazini. 7. Hataki kufuatiliwa mambo yake. Mwanamke wa hivi huwa ni mbinafsi, hapendi ufahamu mambo yake, hataki ujue ni kiwango gani cha pesa anatengeneza kwa siku kupitia biashara yake. Hata ikiwa ataamua kukujulisha basi atakudanganya ila inapotokea amekwama mahali atahitaji msaada kutoka kwa mwanaume.

5. Anapenda kujenga kwao. Maandiko matakatifu yanasema mwanamke ataiacha familia ya kwao na kwenda kuishi na mumewe kujenga familia yao. Lakini mwanamke mpumbavu mara zote yeye anawaza kuwasaidia wa kwao. Sio vibaya kuwasaidia kwani wazazi ni muhimu lakini kwa kiwango hiki yeye kufanya ilivyo pitiliza. Kila muda atagusia kwamba

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE

9

8. Anaona tabu kupangiwa na mumewe. Hapendi kabisa mumewe ampangie mambo fulani ya kimkakati ya kifamilia. Anachotaka ni kwamba yeye awe muamuzi wa kila jambo, kwa lugha nyingine ndio kusema hana heshima kwa mumewe. 9. Hatosheki na sifa anazopewa na mumewe. Mwanamke huyu hatosheki kabisa mumewe kuona uzuri alionao, anaenda mbali zaidi kujipamba ili asifiwe na wanaume ama vijana wengine huko mtaani. Anachohitaji yeye ni sifa tu. 10. Ni mzururaji. Muda wote yeye anapendelea kuzurura na ni mtu wa shughuli zisizo rasmi. Anapendelea kusafiri kwenda kuwatembelea zaidi kwao kuliko muda anaotumia pamoja na familia yake na mume wake.


ZaMuYaNgu Oktoba 01-15, 2021. Makala Tangazo

NA AP, HELLEN SOGIA

K

ujitunza, kunamwelekezea mtu kwenye usafi wa moyo. Moyo wa mtu unapokuwa mafia, ndipo mtu huyu anaweza akamwona Bwana, katika maisha yake, pia anakuwa yuko kwenye njia sahihi, ya safari yake ya wokovu.

KISU CHA MAKALI MAWILI. kufanya kwenye maisha ya mtu huyu, basi! Itakuwa rahisi kwake kufahamu, na kuchukua hatua hiyo.

• ²⁴ Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele.

Kwa mtu kuishi bila kujikagua, kunamtengenezea mtu huyu hatari ya kuingizwa kwenye kifungo cha Adui, au kuangamizwa na Adui. Maana, atakuwa akihalalisha anayoyafanya, na kujichukulia haki kati hayo anayoyafanya.

Mambo yasiyofaa, huonekana kuwa na sura ya mteremko, na wepesi katika kutenda kwake, lakini! Mara nyingi Unakuta kuna madhara ambayo huja kujitokeza baadae, aidha kutakuwa na garama ya kulipa baadaye, ambayo itakuja kumgharimu mtu huyu, ama mtu ataingizwa kwenye uharibifu, ambao utamfanya Aumizwe yeye, au aumize mtu mwingine.

Mathayo 5:8. • Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. Kujitunza, ni silaha kubwa sana, ya kumkinga mtu, dhidi ya mashambulizi ya adui, Ibilisi anaporusha mishale yake dhidi yako, ili kukushambulia. Mtu anapojitunza, huwa anatoa nafasi kwa malaika aweze kumsaidia mtu huyu aweze kuyashinda majaribu, na mashambulizi yanapomjilia. Kujitunza kunazuia kasi ya mashambulizi yanayotoka kwa adui. 3. KUJIKAGUA Kujikagua kunampa mtu kuijua hali aliyonayo kwa wakati huo. Na hii humpa mtu nafasi ya kurekebisha maisha yake, na endapo kutakuwa na matengenezo yoyote ya

Bila kuyapima na Neno. Hii nayo, inaweza kumwondolea thamani mtu huyu. Zaburi 139:23-24 • ²³ Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu;

Mtu huyu pia, anakuwa amebeba kisu chenye makali yakatayo kuwili, pole pole kisu hiki humjeruhi na kumkata yeye mwenyewe. Na jinsi kisu hicho kinavyoendelea kusababisha majeraha, ndivyo thamani ya mtu huyu inavyoendelea kushuka.

KISU CHA MAKALI MAWILI NI NINI:

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE

THAMANI YAKO 22

10

Kisu ni tabia, mwenendo, maneno, nk. 1. Tabia yeyote inayokwaza na kuchukiza watu wengine, ni kisu ambacho kinamkata mtu mwingine kwa kutumia upande mmoja, na upande mwingine unakukata wewe. 2. Maneno unayomtamkia mtu mwingine yakamuumiza, ni kisu kimetumika upande mmoja na kumkata, na upande mwingine ikakukata wewe. Kisu hiki huumana pande zote, sababu chochote umtendeacho mtu mwingine, ni DHAMBI kwa MUNGU. Luka 3:13-14. • ¹³Akawaambia, Msitoze kitu zaidi kuliko mlivyoamriwa. • ¹⁴Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu. ITAENDELEA... __________________________________ Apostle Hellen Sogia

THE OAK MISSION MINISTRY. P.o Box 30838. Kibaha Pwani.

Simu: 0753 351 048 au 0716 711 867 __________________________________


ZaMuYaNgu Oktoba 01-15, 2021. MAHOJIANO SANAA

11

Vurugu au Vibe la Mkutanoni sio nguvu za Mungu

NA MWANDISHI WETU,

B

wana Yesu asifiwe, natumaini mnaendelea vema kabisa na majukumu ya kila siku. Kwa neema ya Mungu wiki mbili zilizopita Zamu Yangu na Nyota Shine zilipata muda mzuri sana wa kuzungumza na Ambwene Mwasongwe na alifunguka kuhusu mengi yanayohusu injili na waimbaji.

MWANDISHI: Kitu gani hakikupendezi kwa waimbaji wenzako? AMBWENE: Vipo vitu vingi lakini kikubwa sana ni kutokuwa na hela na kiukweli inaniuma, yaani kama kuna kitu kinaniuma Tanzania ni waimbaji kutokuwa na hela. Na dalili zinaonyesha huko mbele tunapoelekea tunaweza tusiwe na hela zaidi (aki(akitabasamu)) Kutokuwa na tabasamu hela ndiko kulikotufanya tuwe na mambo mengi magumu na meusi, naomba Mungu atupe neema na ninaamini tukiwa na fedha za kuendesha huduma zetu hata hizi kesi zisizo na mashiko zitaisha kwa sababu migogoro mingi inasababishwa na uchungu wa kukosa hela. Wakati mwingine tunafikia mahali tunamtafuta wa kumlaumu na tukimkosa tunaanza kulaumiana wenyewe na kuanza kuhisi sina hela kwa sababu ya fulani. Hicho ndicho ninachokiona tatizo Mungu atukumbuke na ainue uchumi wetu. Kama ningeweza kuingia

katika moyo wa kila muimbaji natamani tungekuwa na kampuni kuubwa ya waimbaji nchi nzima. Tutafute biashara tuendeshe kwa sababu tukiendelea kuwa na hii hali tutakuwa na hali ngumu sana maana wachungaji wetu tunataka kuwakamua fedha ambazo hata wao hawana, lakini najua sio kwamba tunapenda sababu nakuja kwenye kanisa lako halafu nahitaji milioni 2 au 3 na ukizingatia hiyo pesa katika kanisa hilo wanaweza kuipata baada ya miezi sita wewe unazitaka jumapiili moja. Sio kwamba tunapenda pesa au hatuwahitaji wazee wetu lakini mahitaji ya kuendesha huduma ni makubwa na magumu, sasa kama hicho ndio chanzo chetu ni kwamba tunafeli. Jamani waimbaji Mungu atupe helaa sababu njaa ikiondoka hayo mengine yote yanaondoka. MWANDISHI: Mbali na huduma, unajishughulisha na nini? AMBWENE: Mbali na huduma nina vitu vyangu vidogodogo navifanya ambavyo ni binafsi sana siwezi kuvitaja lakini huwa napenda kujishughulisha na vitu vidogovidogo ambavyo vinaongezea kipato changu yaani ujasiriamali mdogo mdogo. MWANDISHI: Je ulitegemea Misuli ya Imani ingekupeleka kwenye viwango ilivyokupeleka? AMBWENE: Kila albam ninayofanya matarajio yangu ya kwanza ni albam

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE

ifanye vizuri kuliko iliyopita kwa sababu naamini katika Utukufu hadi Utukufu na ninaamini katika ukuaji. Huwa napenda kujichunguza mwenyewe yaani eneo gani ambalo nilifanya vizuri na eneo gani ambalo sikufanya vizuri. Nitazingatia eneo nililofanya vizuri na kuliboresha zaidi lakini pia nitarekebisha pale ambapo sikufanya vizuri, na ndio maana huwa naamini albamu inayofuata lazima nifanye vizuri zaidi ya ile iliyopita. Ukiangalia Misuli ya imani nimeifanya na Producer wanne katika studio nne tofauti kama ambavyo nimefanya albam ya Moyo wa Ibada. MWANDISHI: Unawashauri nini wachungaji wanaoandaa semina na mikutano na kuhitaji/kualika waimbaji wenye nyimbo zenye midundo ya haraka haraka tu? AMBWENE: Waimbaji tusijaribike bali imba vile ulivyo, mfano hivi leo mimi niimbe wimbo wa kukimbia , naweza nikajaza watu, kitu ambacho kinaweza kikawa kizuri kwa waandaji, unajua kuna watu wakiona lile vurugu/vibe wanahisi ndio nguvu za Mungu zimeshuka kitu ambacho si cha kweli, Imba vile ulivyo na mimi sina mpango wa kufanya kile ambacho mimi siwezi kufanya.

Nitakuwa Ambwene ninayefanya kitu ambacho ninaweza kufanya na hicho ndicho nilichoridhika nacho. Mungu akinipa zaidi nitafanya lakini siwezi kulazimisha ambavyo mimi siwezi kwa sababu sitaki kuwa kituko. Natamani kuchangamka kwetu kuwe na nguvu ya Mungu ndani yetu na waandaaji wajue hilo.


ZaMuYaNgu Ijumaa Oktoba 01-15, 2021.

Michezo na Burudani NA MWANDISHI WETU,

ISSN 2714-2108 Habakuki 2:1-2 Toleo Na.038

B

ondia wa Ufilipino Manny Pacquiao ametangaza kustaafu mchezo huo ili kuangazia kazi yake ya siasa.

TETESI ZA USAJILI

Bondia Mlokole Manny Pacquiao astaafu ndondi

Bondia huyo anayeshikilia mataji ya uzani tofauti ni seneta nchini humo na tayari ametangaza nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2022. Katika pigano lake la mwisho bondia huyu mwenye umri wa miaka 42-alishindwa na bondia wa Cuba Yordenis Ugas mjini Las Vegas mwezi uliopita. “Nilisikia kengele ya mwisho tu. Mchezo ulikua umeisha,” alisema Pacquiao. Katika video iliyowekwa katika mitandao ya kijamii, Pacquiao alielezea kustaafu kwake kama

“uamuzi mgumu” katika Maisha yake, akiongeza kuwa ndondi ilimpatia “nafasi ya kupigana na umaskini” na “ujasiri wa kubadilisha maisha zaidi”. Pia aliwashukuru mashabiki wake, marafiki na wale wote waliomuunga mkono katika mchezo huo,hususan Mkufunzi wake wa muda mrefu Freddie Roach, ambaye alimtaja kama “familia yangu, kaka na rafiki”. “Sitasahau kile nilichofanya na kufanikisha maishani mwangu,” alisema. Pacquiao anatambulika kama bondia bora wa kulipwa duniani, akishinda mataji 12 katika mikanda minane tofauti na ni bondia wa pekee kushikilia ubingwa wa dunia kwa miongo minne.

KMC NGUVU ZOTE SASA MKWAKWANI KWA COASTAL UNION NA MWANDISHI WETU

B

AADA ya kupoteza pointi tatu kwenye mchezo wao wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara, Klabu ya KMC nguvu zake zote sasa ni kuelekea kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Coastal Union. Jumatano iliyopita ikiwa

Uwanja wa Karatu, ilishuhudia ubao ukisoma Polisi Tanzania 2-0 KMC jambo lililowafanya wapoteze furaha kwa kuziacha pointi tatu mazima. Ni mabao ya Vitalis Mayanga ambaye aliwahi pia kuwa ndani ya KMC aliwatungua dakika ya 3 na 20 kipindi cha

kwanza huku kipindi cha pili jitahada za washambuliaji wa KMC kuweka mzani sawa zilikwama pale Uwanja wa Karatu.

di ya Coastal Union ya Tanga ambayo imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wao wa ufunguzi.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wamepoteza mchezo wao wa kwanza mbele ya Polisi Tanzania hivyo nguvu zao wanazipeleka kwenye mchezo ujao.

Ikumbukwe kwamba kabla ya mchezo wa KMC kukamilika kuchezwa Uwanja wa Karatu ulibadilishwa viwanja mara mbili ambapo awali ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ushirika kisha ukapelekwa Uwanja wa Sheik Amri Abeid kisha ukaibukia Karatu.

Itakuwa ni Oktoba 2, pale Uwanja wa Mkwakwani dhi-

ZAMU YANGU PROJECT & MAGAZINE


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.