GAZETI ZAMU YANGU AGOSTI 01 | 2020

Page 1

2

UK.0

Uchambuzi wa kitabu cha Mungu anapatikana wapi. habakuki 2:1-2

UK. 06

Habakuki 2:1-2

UNAJIO NGELEAJE? #MIRIAM LUKINDO

Jumamosi Agosti 01-15, 2020 ISSN 2714-2108 Na.011 KAMATI YA MAADILI YA YANGA KUTOA MAAMUZI DHIDI YA BERNARD MORISSON. HABARI UK.12

USHUHUDA | UGUMU ILIKUWA . UK KUTOKA KWENYE MIZIMU NA 10 UGANGA, NI MKASA MKUBWA.

Kila hatua ya maisha yako, itahitaji utofauti wako

YALIYOMO

Kila hatua ya maisha yako itaitaji utofauti wako. Ni hatari sana kujaribu kupanda ngazi ya kwenda hatua nyingine bila kubadilisha mtazamo au fikra za jana” Elly David

INAMUHITAJI MWANAUME KUMFUNZA MWANAUME KUWA MWANAUME BORA - HABARI UK.08

MAAMBUKIZI YA FANGASI SUGU NA INAYOJIRUDIA RUDIA, VYANZO NA KINGA - HABARI UK.05

Mwamba Jessica Honore BM MPYA INAPATIKANA BOOMPLAY

Historia ya Mchungaji Chris Oyakhilome maisha, huduma na uponyaji - HABARI UK. 03

UK. 03

Mapambano dhidi ya Corona yanaendelea, chukua tahadhari PROUDLY SPONSORED BY:- RADIO 5 | EVG MINISTRY | FOUNTAIN RADIO | M!SA RICE | SHALOM RADIO & TANGANYIKA PRODUCTION

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


Kitabu / Vitabu

JUMAMOSI AGOSTI 01-15, 2020

2

Uchambuzi wa Kitabu cha MUNGU ANAPATIKANA WAPI?

SURA YA PILI - WEWE NI MWANA

Kuwa Mwana oto

NA HELLEN SOGIA, PWANI.

W

engine wamefika mahali pa kujiweka kwenaye nafasi ya wajakazi (mtumwa). Wameiondoa haki yao ya msingi, ambayo tuliipokea siku ile tulipoma Bwana wetu Yesu Kristo maisha yetu, Yeye ayamiliki, ambapo mbele za Baba yetu sisi ni wana, lakini, wao wamejiona kuwa ni watu duni, na hawafai, wakajiwekea namna ya kukosa ujasiri wa kumsogelea Baba yao wanapotaka kumsogelea au wanapotakiwa kuzungumza na Baba, wao hutumia mtu wa kati ( c/o) kuwazungumzia mambo yao, Wamejiweka kwamba wao wameruhusiwa tu kuishi katika jumba la ufalme lakini wao sio sehemu ya umiliki. Hata wanapotakiwa kumtolea baba yao, huwa wanatoa kwa uchoyo, na si kwa moyo, ni vyema tukafahamu na kanisa litambue kuwa sisi ni warithi pamoja na Kristo Yesu; na vyote vinavyohusu ufalme wa Mungu, sisi ni warithi pamoja nae. WAZAZI. Sisi kama watoto wa Mungu tunatakiwa tuwe tunaishi nyumbani kwetu (ufalme) kama watoto na sio kama wageni, au watumwa, wala hatutakiwi tuukose uhuru wetu tunapokuwa nyumbani kwetu, hali hii hutokea endapo kama baba yetu amekuwa ni dictator! Mungu wetu hayuko hivyo. Ni mzazi pekee ndio awezaye kumpa motto wake MAPENZI ya kweli, Mtoto anapomtambua baba yake ni nani, ndipo anapoweza kufurahia mapenzi ya baba yake, watoto wengini wamekuwa hawajaelekezwa

Mt

mioyo yao kwa mzazi (Baba), mlezi huwa anatumia muda wake kumfanya mtoto huyu amtambue yeye mlezi, zaidi ya baba yake, ambaye ni Mungu, Hali hii imesababisha watoto wengi kufanya makosa na wao kukosa mapenzi ya kweli na faraja ya moyo, kutoka kwa baba yao Elohim. Jambo hili limeathiri sana wana wa Mungu, maana, imewasababishia wengine kuingia mitaani na kuwa wazururaji, wakitangatanga huku na kule wakitafuta ushirika na Baba yao Mungu, hali hii, ikaondoa ibada ya kweli, na katika roho ndani yao, wakakosa uhuru wa kuabudu; baada ya kukosa jinsi ya kuelekeza mioyo yao kwa Bwana, aliye Muumba wao; Na matokeo yake, ndani ya moyo, kunakuwa nafasi ya utupu (vaccum) nafasi hii hutoa upenyo, na kuingiza hewa chafu ndani ya moyo wa mwana wa Mungu, ambayo huemtu anapofika katika hatua hii, sifa na kuabudu kwake inakuwa ni mzigo, na ibada ya sifa na kuabudu ndani hutoweka, mtu hujisikia udhia, kufanya kitu kwa ajili ya Mungu; watu wa aina hii inabidi wapigiwe kelele na kiongozi wa sifa au maombi na kuwahamasisha Ruka! Cheza! Simama! Mtolee Mungu! Piga makofi, magoti! Nk. Ibada ya kweli, inaanzia rohoni, na kupokewa moyoni, kama ndani ya mtu hakuna Ibadaa, inakuwa ngumu, kwa mtu huyu kudhihirisha ibada kwa nje, Yote hii hutokea kwa sababu ya muunganiko wa kiungu wa kiibada (divine connection of true worship) ambayo ingemwezesha mtu huyu kuyafanya haya yote kwa uhuru bila kushurutiswa, hau-

ko; hapo unakuta watu wengine pia, wakisifu (imba sifa) sana lakini si katika roho na kweli, bali katika msisimko wa hisia tu; Muunganiko huu wa kiungu pia huwa unamwepusha mtu na kuizoelea dhambi, maana hofu ya Mungu inakuwa imepata makao ndani yake. Watu wengi wamejikuta wakiingia mahali pabaya na kujitumbukiza kwenye mateso, na magonjwa yasiyotibika kwa maombi ya aina yeyote ile, ila kwa kumrudia Mungu tu. Wako watu walioathirika na hali hii kwa sababu ya kukosa kuwa na baba wa kiroho (spiritual father) 1 Kor 4:15 – 16. kwa kuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika kristo Yesu kwa njia ya injil Basi nawasihi mnifuate mimi. Kanisa linahitaji kuwa na baba wa kiroho maana hata kama mtoto amesoma kuliko baba lakini anamhitaji baba, maana kuna vitu vingine huwezi kuvipata popote ila kwa baba, ushauri bora na wenye hekima unapatikana kwa baba. Shetani alitambua kuwa haiwezekani mtoto akamdharau baba yake, na kisha akafanikiwa, ndio maana alifanikiwa kuwafanya watoto wengi wawe wanazurura huku na kule kama vile wamekosa makao. Kazi kubwa ya hofu ni kufanya NEEMA ya Mungu isitende kazi ndani ya mtu pia

mtu kuwa na jitihada nyingi za kibinafsi kwa kutaka kumpendeza Mungu, kwa kufanya hivi husababisha mtu kukosa uhuru wa kweli ambao mtu aliupata alipompokea Yesu kristu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake. Pia hofu huzuia KWELI ya Mungu isifanye kazi ndani ya mtu na mwisho hum tia mtu kifungoni bila kujijua. Hapo ndipo mtu hujihisi kuwa hawezi kufanya kitu chochote kile na pia hujihisi kushindwa wakati anapokuwa na watu wengine hofu humsababisha mtu ajihisi kutoweza kufanya kitu, bali mwingine ndio anayeweza, mtu huyu huvamiwa na roho ya wivu itakayomsababisha aingie kwenye mashindano na baadae kukaribisha roho ya chuki kuingia ndani yake na kumfanya mtu huyu awe anachukia anapomwona mwenzake akiinuliwa au akifanya kitu kizuri au anapoingia kwenye mafanikio, moyo wake husononeka na kuugua ndani kwa ndani kimya kimya. Kwa msaada na ushauri, maombi, au kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako tafadhali wasiliana na Mtumishi wa Mungu,

Apostle Hellen Sogia

THE OAK MISSION MINISTRY. P.o Box 30838. Kibaha Tanzania Simu. +255 (0) 753 351 048 au +255 (0) 716 711 867

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


Wasifu / Habari

JUMAMOSI AGOSTI 01-15, 2020

Historia ya Mchungaji Chris Oyakhilome maisha | huduma na uponyaji NA MWANDISHI WETU

CHRIS NI NANI? Chris Oyakhilome (maarufu kama “Mchungaji Chris”; alizaliwa Edo, Nigeria, 7 Desemba 1963) ni “televangelist” na rais mwanzilishi wa Believers’ LoveWorld Incorporated ama “Christ Embassy”, ambalo ni shirika la Kikristo, makao yake makuu yakiwa jijini Lagos, Nigeria.

MAISHA Mchungaji Chris alilelewa katika familia ya Kikristo na aliokoka akiwa na umri wa miaka 9. Akiwa kijana alianzisha huduma yake kwa Wakristo kama kijana katika Chuo kikuu cha Bendel State ambacho kwa sasa kinajulikana kama Chuo kikuu cha Ambrose Alli” aliposomea ujenzi. Mnamo mwaka 1991 alimuoa Anita Oyakhilome ambapo walijaliwa kupata watoto wa kike wawili. Anita alikuwa Mkurugenzi wa ofisi ya kimataifa ya Christ Embassy na mchungaji katika makanisa ya Christ Embassy huko Uingereza, Embassy Docklands

katika North Woolwich London. Pia alikuwa Mkurugenzi-mshiriki wa “Loveworld Christian Network”. Mnamo mwaka wa 2016, Mchungaji Chris na Anita walitalikiana baada ya kuishi pamoja kwa miaka 25.

HUDUMA NA UPONYAJI Chris Oyakhilome ni mwandishi wa vitabu kadhaa vilivyonunuliwa kwa wingi sana, kimojawapo kikiwa “Rhapdsody of Realities” ambacho alikiandika pamoja na mkewe Anita. Mafundisho yake yanapatikana pia katika mfumo wa sauti na video. Moja ya kitabu chake pendwa ni “How to receive your miracle and retain it?” ambacho kinaonyesha maisha ya Mkristo, mamlaka yake kama muumini, na mali yote katika ufalme wa Mungu kuwa ni ya kila muumini.

wa shirika kubwa Afrika, Yeye husimamia mafundisho na uponyaji mkubwa na makutano ya watu zaidi ya milioni 3.5 katika tukio la usiku mmoja. Mwaka 2003, alianzisha mtandao wa kwanza wa kikristo barani Afrika kwa dunia nzima ambao unajulikana kama LoveWorld Christian Network. Yeye pia

ni mwenyeji wa mpango wa programu ya televisheni iitwayo “Atmosphere for Miracles”, ambayo huwa ni kuhusu uponyaji wa magonjwa ya kimwili na kiroho na hutangazwa katika mitandao na televisheni kubwa duniani kote. Mchungaji Chris pia ana Shule ya Uponyaji kama sehemu ya huduma yake.

Mbali na kuongoza mtandao mkubwa wa makanisa ya Christ Embassy na waumini katika mabara yote matano, Chris huwa pia ni mchungaji

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE

3


Habari / Makala

JUMAMOSI AGOSTI 01-15, 2020

4

GEL yawaunganisha wanafunzi wa Tanzania na yawafunda wanafunzi wa kidato cha sita. Yawaasa ni vyuo vya nje ya nchi. “Kwanza kwa maslahi yao na Taifa zima. Mkurugenzi mtendaji bwana Abdulmalik (pichani kushoto) awaomba wasizamie huko na kusahau maslahi ya Taifa.”

yani lazima watambue hilo na likae vichwani mwao” alisema bwana Mollel. Amesisitiza kwamba, wanafunzi wanaokwenda nje ya nchi kusoma, ni hazina ya Taifa kielimu, na elimu wanayoipata lazima iwe na faida yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

NA MWANDISHI WETU, DAR

W

ahitimu wa kidato cha sita 2020, wametakiwa kutambua kuwa, Elimu waliyoipata ni kwa faida yao na Taifa kwa ujumla. Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Education Link, bwana Abdulmalik Mollel, amefafanua kuhusu Adhma ya Taasisi hiyo katika

kuwaunganisha wanafunzi wa Tanzania na vyuo vya nje ya nchi. “Pamoja na kwamba GEL inawaunganisha wanafunzi wa hapa nyumbani na vyuo vikuu nje ya nchi, lazima vijana wetu wajue kwamba wanaenda kusoma ili kuliletea Taifa letu heshima na maendeleo kutokana na elimu wanayoipata huko,

“Maendeleo ya Tanzania yanaanza na Watanzania wenyewe, na kwa kulitambulia hilo tumejikita katika kuandaa Rasilimali watu yenye ustadi na uweledi wa hali ya juu, ndio maana tunawasikiliza na kuwashauri vijana wetu kuhusu fani na baadaye vyuo wanavyotaka kwenda kusoma nje ya nchi, hususani katika fani ya Afya, Biashara,

Uhandisi ama Sanaa, hivyo ni Imani yetu kuwa tunaisaidia Serikali kuzalisha Wataalamu wengi watakaoliletea maendeleo Taifa letu.” alisisitiza bwana Mollel. Ameongeza kuwa, hakuna mtu anayeelimishwa kwa faida binafsi bali mtu hupewa ujuzi na maarifa ili aweze kuwatumikia wenzake katika fani aliyohitimu na watu wa kwanza wa kuwatumikia ni Watanzania hivyo amewaasa wanafunzi hao kwamba, pindi watakapo maliza elimu yao ya juu nje ya nchi wasizamie katika Mataifa mengine bali warudi nyumbani watumie elimu yao kwa faida ya Tanzania. Global Education Link ambao ni mawakala wa vyuo vikuu nje ya nchi wamejipambanua katika kukuza na kuboresha elimu hapa nchini kwa kuwaunganisha wanafunzi na vyuo vikuu bora duniani zaidi ya nchi 200.

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


afya YA MWANAMKE 5

JUMAMOSI AGOSTI 01-15, 2020

MAAMBUKIZI YA FANGASI SUGU NA INAYOJIRUDIA RUDIA - VYANZO NA KINGA. NA MSHAURI BABRA. Fangasi Inasababishwa na jamii ya fungi anaitwa CANDIDA. Seli za fangasi na bacteria wazuri huishi ukeni bila tatizo lolote. Tatizo linakuja endapo ukuaji wa fangasi hawa ukeni watakuwa wengi kushinda wazuri. Basi hapo ndio inapotokea ugonjwa wa fangas na miwasho mingi. Kama unapata maambukizi ya fangasi zaidi ya mara nne kwa mwaka basi kitaalamu hali hii hiyo hujulikana kama vulvovaginal candidiasis (fangasi sugu au inayojirudia rudia). Na ni hatari sana Kama ukichelewa kuipatia matibabu sahihi mapema kwani upelekea tatizo la PID ambalo nalo upelekea tatizo la ugumba Kwa wanawake wengi asa kwa sasa. VYANZO VYA FANGASI SUGU / INAYOJIRUDIARUDIA Zipo sababu kadhaa zinazoweza kupelekea fangasi kuwa sugu/kujirudia rudia. Sababu hizo ni:1. Vitu vinavyoweza kusababisha mvurugiko wa homoni kama ujauzito, dawa za uzazi wa mpango, na matibabu ya estrogen. 2. Matumizi ya mara kwa mara ya antibiotic ambazo huondoa bakteria ambao husaidia kupunguza idadi ya candida. 3. Magonjwa yanayoshambulia kinga ya mwili kama VVU (HIV) 4. Unene, unaoweza kusababisha joto na unyevu mazingira yanayofanya candida kuongezeka kwa wingi. 5. Nguo za kubana na zisizo za pamba zinazofanya maeneo ya via vya uzazi kuwa na joto na unyevunyevu. Mazingira ya joto hii inamaanisha nguo ambazo tu-

6. 7.

8.

9.

natakiwa kuvaa kama vile chupi za cotton hasa kwa wanawake, hazihitaji joto sababu bacteria wabaya wanakuwa wengi sana na kusababisha miwasho na FANGASI. Maambukizi kutoka kwa mtu unaeshirikiana nae tendo la ndoa. Kukosa usingizi stress, vidonda sehemu za siri,matumizi ya antibiotics, kuweka marashi sehemu za siri. Watu wanaougua kisukari ambao hawawezi kudhibiti kwa kutumia dawa za kisukari, inakuwa kwenye damu na hicho kisukari ndiyo chakula kikuu cha hao fangasi. Hata wanawake ambao wanapenda kula vyakula vya sukari nyingi kama vile chocolates, soda, na vingine vyenye sukari nyingi ambavyo ni chakula cha fangasi.

DALILI ZA FANGASI SUGU. Kuna dalili nyingi zinazoonyesha kuwa una dalili za kua na fangasi ukeni kama zifuatazo; • Kuwa na miwasho sehemu za siri mara kwa mara. • Vipele vidogo vidogo ukeni. • Vidonda au kuwa na michubuko ukeni. • Kutokwa na harufu mbaya ukeni. • Kupatwa na maumivu makali wakati wa tendo la ndoa. • Kuvimba au kuwa mwekundu katika mdomo wa nje ya uke. • Kuwaka moto ndani na nje ya uke. • Maumivu ya misuli na tumbo hasa chini ya kitovu. • Maumivu ya kiuno. • Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri baada ya tendo la ndoa. • Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa mwepesi au mzito au majimaji.

MADHARA MAKUBWA YA FANGASI Kuwa na Fangasi sugu kwa muda mrefu ambayo inajirudia mara kwa mara bila kupata matibabu sahihi upelekea Kupatwa na ugonjwa wa Pelvic Inflammatory Disease (PID) maambukizi katika via za uzazi na kupelekea kuwa mgumba, ndio maana wanawake wengi ni wagumba. Pamoja na kuwa na muwasho wa kudumu sehemu za siri inayosababisha kukosa raha na Uhuru wakati wote. JINSI YA KUJIKINGA DHIDI YA MAAMBUKIZI YA FANGASI YANAYOJIRUDIARUDIA. 1. Vaa nguo za ndani zilizotengenezwa na pamba. 2. Epuka nguo za kubana. 3. Jisafishe kutoka mbele kwenda nyuma baada ya kujisaidia haja kubwa. 4. Tumia antibiotics pale tu unaposhauriwa na daktari. 5. Epuka kujisafisha kwa kuingiza vidole kwenye via vya uzazi. 6. Epuka kufanya mapenzi hadi utakapopona maambukizi ya fangasi. Itaendelea toleo lijalo...

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


MSANII WETU

JUMAMOSI AGOSTI 01-15, 2020

UNAJIO NGELEAJE?

#MiriamLukindowaMauki #MsaniiWetuLeoZamuYangu

NA MWANDISHI WETU

B

adili vile unavyojiongelea. Kuna maneno ambayo siyo mazuri umekuwa ukijitamkia, na yamekuwa kama kitanzi katika maisha yako. Badilisha unavyojiongelea, au unavyo jitazama. Usiwe mtu wakushikilia

watu moyoni. Wasamee watu wote waliokukosea. Ukiwa mtu wa msamaha unaifungua milango ya baraka.

mawazo mgando, wavivu, wasio kubali maonyo. Na tabia hii ukufanya upoteze marafiki na hata fursa mbali mbali.

Usiwe mtu wa kulalamika. Watu wengi wenye tabia za kulalamika si watendaji, niwatu wenye

Tafuta mtu unayemuamini ongea naye kwa yale mambo magumu unayopitia ili kupara ushauri.

USHAIRI WA INJILI

Lakini kuwa makini sana ni nani unamwambia mambo yako. Kwakuwa wapo wanao tamani kukuona unaishia njiani na wapo wanao tamani kukuona unasogea mbele zaidi. Alisema Miriam Lukindo wa Mauki.

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE

6


Habari / MAHOJIANO 7

JUMAMOSI AGOSTI 01-15, 2020

NA MWANDISHI WETU, DAR

M

tangazaji wa miaka mingi Daniel Mngoma Maarufu kama Dcom, amekiri kuondoka N.Y.U Radio na GD TV za Arusha.

MTANGAZAJI DCOM AIKIMBIA N.Y.U RADIO NA TV, AIELEZA ZY KILICHOMKIMBIZA...

Akizungumza na Gazeti Hili, Lililotaka kujua Kwanini Yupo kimya tofauti na Alivyozoeleka kwenye Media, Dcom amesema kwamba haikua rahisi lakini imebidi, yote ikiwa ni katika utafutaji. Aidha amesema kua ameamua kufanya hivyo ikiwa ni kwa hiari yake, huku akimshukuru Nabii Mkuu Mh Dr GeorDavie, Radio na huduma ya Ngurumo Ya Upako kwa ujumla, kwa malezi, upendo na ushirikiano uliodumu miongoni mwao kwa zaidi ya miaka 9.. “Nabii mkuu ni mlezi mwema wa vipawa na karama mbali mbali za vijana, nilienda N.Y.U nikiwa kijana mdogo ila mwenye elimu ya habari na utangazaji, Nabii mkuu aliniamini katika umri wangu huo na kunikabidhi kazi na tukaiendesha radio kwa kushirikiana na wenzangu had hapo unapoiona Leo radio...Hivyo sina ucheche wa shukrani kwa mema hayo, na tutaendelea kushirikiana...Nimeandika barua Kwa uongozi wa juu hivyo naamini imepokelewa na Nina baraka zote za kufanya kazi ya taaluma yangu popote”. Aidha Dcom hajasema ni media gani atakayoifanyia kazi kwa sasa ila amesisitiza atakua Mwandishi wa kujitegemea. “Sijaitwa na media yoyote, wala sijaomba kazi kwenye media yoyote, Na pia Sipo Arusha kwa sasa nafanya project binafsi, nadhani soon nitazitambulisha. Kikubwa nawapenda sana wasikilizaji wangu wote tuliokua pamoja najua tutamisiana sana maana Utangazaji ni maisha yangu, hivyo sitakaa kimya sana mtanisikia tu” Alisema Daniel Mngoma.

JOEL LWAGA AWAFOKEA SHABIKI ZAKE INSTAGRAM

TUNAPOKEA MATANGAZO NA KUYATANGAZA BURE KUPITIA GAZETI LETU. KARIBU SANA ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


MAKALA YA WANAUME 8

JUMAMOSI AGOSTI 01-15, 2020

Pichani ni Rais wa Men @ work Ndg. Maxwel Chaila akimkumbatia mmoja wa vijana aliowatengeneza katika moja ya mafunzo yanayofanywa na taasisi hiyo ya Men @work Global.

INAMUHITAJI MWANAUME KUMFUNZA MWANAUME KUWA MWANAUME BORA NA BROWN MANUKATO, ARUSHA

M

oja kati ya maumivu ambayo wanayo WANAUME wengi ni kitendo cha Baba zao kutowatambulisha, kutowapa muda, kutowasikiliza, kutowafundisha, kutowaonesha njia na kutojali hisia na mawazo yao. Hali hii imeongeza idadi ya wanaume wenye majeraha na madhara yake wanayahamisha kuwa maumivu kwa watoto wao, wake zao, jamii na Taifa.

Wanaume wengi hawajui gharama za kuwa mwanaume bora. Wengi ni wagumu kujifunza. Wanadhani wakishazaliwa na jinsia ya kiume Basi inatosha kuwa mwanaume. Na hii inatokana na ukweli kwamba wengi wamekosa malezi ya Baba ambaye ni mwanaume anayehitajika kumtambulisha na kumuonesha njia sahihi ya kuwa mwanaume bora. Ukweli

ni

pamoja na kuwa Wanaume wengi wamewaachia wanawake suala zima la malezi hasa kwa mtoto wa kiume lakini inamhitaji mwanaume kumfunza mwanaume kuwa mwanaume bora.

anachokifanya Baba au mwanaume Mwenye nafasi ya Baba kwenye maisha yake.

Waingereza wanasema “ It takes a man to teach a man to be a man�. Kama ambavyo haiwezekani suMwanaume ni kocha, ala kumfunza simba mtoni mwalimu na Kiongozi. to kuwa simba ndivyo Ushawishi wa mwanau- ilivyo kwa mwanaume. me ni pale anapomfun- Mwanaume anafunzza kijana wake wa kiume wa na mwanaume kuwa kwa vitendo kwa sababu mwanaume bora. Hakuna wavulana hujifunza mengi mbadala. kwamba; na kwa haraka kwa kuona

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


makala/ Habari

JUMAMOSI AGOSTI 01-15, 2020

9

SAULI APOTEZA UFALME wake KABLA YA KUTAWALA NA HELLEN SOGIA, PWANI MAJIRA NA NYAKATI - SEHEMU YA TANO Katika nyakati nne tulizozipitia hapo nyuma ni;1. WAKATI. 2. MAJIRA YALIYOAMRIWA. 3. MAJIRA KWA WAKATI ULIOAMRIWA 4. NINI KILICHO MBELE YAKO. Hizi ni nyakati ambazo, ni muhimu mtu kuzitambua, katika maisha ya mwanadamu; Ni nyakati ambazo, mtu anapokuwa sio makini, anaweza akapoteza thamani ya maisha yake; Na kupata hasara katika kuishi kwake hapa duniani, Pia anaweza akapoteza faida ya umilele wake. Maisha ya mwanadamu baada ya kuishi hapa duniani, yanategemea majira na Nyakati hizi nne kwamba ni:1. Jinsi gani mtu atakavyotembea katika hayo. 2. Kumaanisha katika kila majira na wakati, chini ya jua, mtundio hutengeneza mwisho mzuri au mwisho mbaya wa mtu 3. Mtu anatakiwa kuishinda ile nguvu inayomshikilia na kumzuia asiweze kutembea na kuvuka salama katika kipindi hicho chote. Adui Shetani, ameweka mitego yake katika kila majira na Nyakati. Wakati mwingine hugeuza ufahamu wa mtu katika kuyaelewa majira yaliyopo kwake sasa, na kwa kufanya hivyo, inakuwa sio rahisi kwa mtu kufahamu kama amecheleweshwa au kuzuiliwa kwenye majira ya wakati wake. Shetani anaweza pia kumhamisha mtu na kumpotezea NJIA YAKE, na jinsi YA kutenda katika wakati wake uliojiri. Hivyo ndivyo mtu anaweza akapoteza kile alichokuwa ameandaliwa na Bwana na akashindwa kukipokea. Sauli alitiwa mafuta na Samweli kuwa mfalme WA Israeli.

kushindwa hadi mwisho wa utawala wake.

1 Samweli 10:1. “Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! Bwana hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa Bwana, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa Bwana amekutia mafuta] Lakini! baada ya kupakwa mafuta, Sauli alipoteza ufalme wake, kabla ya kuanza kutawala, alipomtangulia Mungu, naye akaingia kwenye utendaji na kutangaza vita kabla ya kuwekwa wakfu, na kutolewa kwa sadaka SADAKA YA BWANA. 1 Samweli 13:2. Naye Sauli alijichagulia watu elfu tatu wa Israeli; ambao katika hao, elfu mbili walikuwa pamoja na Sauli katika Mikmashi, na katika mlima wa Betheli na elfu moja pamoja na Yonathani katika Gibea ya Benyamini, nao wale watu waliosalia akawaruhusu waende kila mtu hemani kwake. Sauli alianza kazi mwenyewe, alishindwa kuyatambua MAJIRA YA wakati ule kwake, yalimtaka afanye nini. Badala yake, Sauli akatangaza vita, na Aliposhindwa kufata agizo la Samweli. Vita ya Sauli YA kwanza aliyotangaza akashindwa na katika utawala wake, akatawala kwa

1 SAMWELI 13:10-14. Hata mara alipokwisha kuitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, kumbe! Samweli akatokea. Naye Sauli akatoka kwenda kumlaki na kumsalimu. Samweli akasema, Umefanya nini? Naye Sauli akasema, Ni kwa sababu naliona ya kuwa watu wanatawanyika mbali nami na wewe hukuja siku zile zilizonenwa, nao Wafilisti wamekusanyika pamoja huko Mikmashi, basi nikasema, Wafilisti watanishukia sasa mpaka Gilgali, kabla sijaomba fadhili za Bwana, kwa hiyo nalijishurutisha, nikatoa sadaka ya kuteketezwa. Naye Samweli akamwambia Sauli, Umefanya upumbavu, hukuishika amri ya Bwana Mungu wako aliyokuamuru, kwa maana Bwana angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele. Lakini sasa ufalme wako hautadumu, Bwana amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye Bwana amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika neno lile Bwana alilokuamuru Lakini! Katika kupoteza kwake dira, Haikuwa rahisi kwa watu kufahamu, kuwa Sauli alikuwa tayari ameshapoteza ule uliokuwa ni “WAKATI” wake wa kutawala. Pamoja na kuwa, Sauli aliendelea kutawala Israeli.

kama mfalme wa Israeli, lakini! Ukweli ni kwamba, mbele za Mungu alikuwa ni kivuli cha mfalme. Mungu alimtambua Daudi kama mfalme wa Israeli, baada ya Daudi alipopakwa mafuta na Samweli. Daudi akachukuwa nafasi ya “WAKATI” wa utawala wa Sauli, na hii ikampa Sauli kuishi maisha ya hofu, akimwogopa Daudi maana Daudi alikuwa ameshika “ WAKATI” mkononi mwake. Sauli alipoteza “WAKATI” Bila ya yeye kufahamu kuwa wakati wake umekwisha kumwacha. Kwa Sauli kuendelea kuwa mfalme haikuwa tatizo, Tatizo ilikuwa ni Sauli kupoteza nguvu ya utawala juu ya Israeli. Nguvu na mamlaka ya utawala inapopotea mtu hupoteza nguvu ya “WAKATI “. WAKATI ni majira ambayo mtu hupewa NGUVU NA MAMLAKA juu ya kitu, watu au nchi, na nguvu hii ya kiutendaji, anapaswa mtu kuitumia kwa kipindi cha wakati huo aliopewa. Baada ya wakati huo kupita, au MTU anapopoteza “ WAKATI” huo, MAMLAKA hiyo haitakuwa na NGUVU tena juu yako.

Ni mara nyingi kwetu sisi wanadamu, tunakuwa tumeshapoteza dira za maisha yetu kwa jinsi ya tuliyokusudiwa na BWANA, tukaenda katika mitazamo yetu Sisi ya kibinadamu, kwa kile tunachokiona kwa macho yetu ya damu na nyama, nayo yakatuondoa kwenye “WAKATI” wetu WA sasa.

MFANO. Raisi aliye madarakani, sheria ndio humpatia raisi huyu mamlaka ya kutawala nchi hiyo kisheria, pia hupewa nguvu ya kisheria, kutoa amri, agizo na maamuzi ya utekelezwaji. Inapotokea raisi huyu akashindwa kuitumia mamlaka ya cheo chake vizuri kwa wakati huo anapokuwa raisi, Punde atakapoondolewa kwenye nafasi hiyo atapoteza hiyo mamlaka ya uraisi na hatakuwa na nguvu tena ya KIUTENDAJI tena kiraisi raisi kwa sababu “WAKATI” wake umepita.

Sauli aliendelea kuonekana kwa macho ya kibinadamu

Mpendwa msomaji itaendelea katika toleo lijalo, Usikose!!

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


MAHOJIANO / NYOTA

JUMAMOSI AGOSTI 01-15, 2020

10

USHUHUDA | UGUMU ILIKUWA KUTOKA KWENYE MIZIMU NA UGANGA, NI MKASA MKUBWA. NA MWANDISHI WETU

B

wana Yesu asifiwe ndugu mnaofuatilia ukurasa huu makini sana wa “NYOTA WA SIKU� Tunatambua kila mtu ni nyota na ana nyota yake inayomuangazia zaidi kufikia mafanikio yake. Wiki hii tulipata wasaa wa kuzungumza na Atlucky Njovu mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Mbeya mwenye asili ya Songea Tanzania. Ni kijana aliyepatwa na mikasa mingi ya mizimu. Karibu tusome wote na kufahamu mambo tusiyoyafahamu.

mazuri

bia na wenyewe wamejionea na hasa mama yangu aliamua kuchukua hatua na kuokoka baada ya kuona nimepona kabisa. Nampenda sana mama yangu.

SWALI: Je nini kilikusukuma kuanza kumtumikia Mungu kiuimbaji? ATLUCKY: Kiukweli ni ushuhuda mrefu kidogo kutokana na Mungu aliponitoa maana nilikuwa muamini wa dini nyingine. SWALI: Kitu gani ambacho umekiona tangu uanze huduma hii ya uimbaji na sio kizuri kwako? ATLUCKY: Aisee ni namna waimbaji wanavyochukuliwa sasa hivi kuwa hawawezi kudumu katika ndoa zao kutokana na baadhi yao kushindwa kufanya hivyo. Jambo lingine ni waimbaji kuhudumu na kuondoka bila kusikiliza neno kana kwamba haliwahusu. SWALI: Je ndugu zako wamepokeaje wewe kubadili dini na huduma uliyonayo, kuna namna wanakusapoti? ATLUCKY: Kiukweli changamoto ni nyingi sana katika familia yangu hakuna anayeniunga mkono katika hili zaidi ya mama yangu kuniombea basi. Wanaoniunga mkono ni watu wa mbali ila hapa nilipo hakuna anayekubaliana na suala langu la kubadili dini. SWALI: Maisha ya wokovu unayaonaje ukilinganisha na dini uliyotoka? ATLUCKY: Maisha ya wokovu ni

sana kulinganisha na chochote yaani maana kila ninachoomba napata. Namshukuru sana Mungu kwa kweli. SWALI: Ni ugumu gani umekutana nao katika kazi aidha kwa watayarishaji wa muziki au directors? ATLUCKY: Hapa mimi niliwahi kumpa director kazi yangu na pesa yote aliyohitaji, ilipofika siku ya kurekodi alinisumbua sana, kuna watu niliwaita wakaanza kuondoka kumbe director hakuwepo kabisa. Alinikwaza sana na huo ndio ugumu naukumbuka wakati naanza huduma. Prodyuza huwa nawalipa pesa kamili hivyo hawanisumbui. SWALI: Hebu tuambie ulikuwa katika dini gani ili wasomaji wetu watambue pia. ATLUCKY: Mimi nilikuwa ni muislam kabisa na nilikuwa naagua watu kwa sababu nilikuwa na mizimu yaani nilikua mganga kabisa wa kiimani.

SWALI: Yepi malengo yako ya mbeleni? ATLUCKY: Lengo kubwa nililonalo sasa hivi ni kuendelea kuimba ingawa yaani hii ilitokea tu nikaimba lakini baadae na moyo wangu unapiga kelele ni kuwa Mchungaji. SWALI: Kutoka uislam mpaka kuokoka, kuna changamoto kubwa sana kwa familia na wakuu wa dini na anga, upande wako ilikuwaje? ATLUCKY: (akahema kwanza kwa nguvu) yaani kutoka uislamu haikuwa ngumu, ugumu ulikuwa kutoka katika hali ile ya mizimu, uganga yaani hali niliyokuwa nayo ndio ilikuwa ngumu kutoka mpaka kuwa kuwa hali ya kawaida lakini kwa Yesu kila kitu kinawezekana na kwangu ameniokoa. SWALI: Vipi kuhusu kuwahubiria ndugu zako habari za Yesu? ATLUCKY: Nilishawahi kuwaam-

SWALI: Ili ufanikiwe kihuduma ni lazima uwe na baba wa kiroho, Je kazi aliyofanya Yesu nani alikuwa baba yake wa kiroho? Pili ili baba wa kiroho ajulikane anatakiwa afanye nini ili watu wajue huyu ni baba yako wa kiroho? ATLUCKY: Ninavyofahamu ni kwamba huwezi kufanikiwa bila baba wa kiroho, lakini ujue pia kuwa Mungu humtumia mtu kumuinua mtu. Mfano Mungu alimtumia Musa kuwatoa wana Israel utumwani, Musa aliuvaa uhusika wa baba wa kiroho. Pili naomba utambue Yesu ni Mungu na tunajua Mungu ni roho hivyo Yesu alivikwa mwili huu wa damu na nyama tu lakini kilichokuwa ndani yake ni Mungu mwenyewe. SWALI: Je wakitaka kukurudisha ulipotoka utarudi? ATLUCKY: (akahema kwa nguvu)Ni heri uniue kuliko kurudi kule nilikotoka kwa kweli, sirudi, sirudi kwa sababu mimi ndio najua nilikuwa nateseka kiasi gani. SWALI: Unadhani kwa nini ndoa nyingi zinavunjika sana nyakati hizi? ATLUCKY: Siwezi zungumzia sana kwa sababu sina uzoefu lakini kwa kusikia ni kwamba wengi huwa tunakurupuka sana kuoa na kuolewa, tunaomba Mungu atupatie mchumba wakati kwenye akili yako umeshafikiria mchumba ni nani, afu unajijibu Mungu ameshakujibu wakati wewe ulishamtangulia Mungu na ndio maana mtu anaoa/olewa na mtu ambaye sio chaguo kwa sababu alishajichagulia. TUKUTANE TOLEO LIJALO...

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


Makala M0t0 Ulao

JUMAMOSI AGOSTI 01-15, 2020

11

WAKUFUNZI MUOGOPENI MUNGU.

â–Ş Tunaomba msitoe mitihani siku ya Jumapili, kwa niaba ya wanafunzi wote

kuwatisha wanafunzi waje kuabudu test unayotoa badala ya kwenda kumuabudu MUNGU. Rafiki yangu tutorial assistance, Dr, Prof huo mchezo unaoufanya ni hatari kwa afya yako huwezi ukachukua nafasi ya MUNGU aliye hai , MUNGU wetu ni mwenye wivu utukufu wake hatampa mtu mwingine.

EV. IMANI O. KATANA Wakufunzi, maarufu kama malekchara (lecturers) salamu nyingi ziwafikie hapo mlipo. Nachukua nafasi hii kukupongeza kwa majukumu mazito mnayoyafanya kuwajenga vijana wetu katika elimu ya juu. Hakika kazi yenu ni njema sana. Nimelazimika kuandika makala hii haswa kwa sababu ya tabia ambayo imejitokeza kwa baadhi yenu katika siku za hivi karibuni.Tabia ya kutoa mitihani siku ya Jumapili. Inashangaza kwamba mnazo siku tano za kazi, lakini hizo mnaona kama hazitoshi mpaka kutangaza mitihani siku ya ibada.Unatumia nafasi yako

Kanisani tunawahitaji vijana utasikia tuna test! Jumapili? kwa nini oooh Prof kasema twende .Prof huo ni uwakala wa shetani bila kujua huwezi kuingilia uhuru wa kuabudu wa vijana wetu kwa sababu ya Mambo yako mengi uliyonayo siku ya vijana kuwa nyumbani mwa Mungu wakawa kwenye madarasa ya vyuoni kufanya test yako.Hizo ni dharau kwa MUNGU waziwazi . Heko tume ya uchaguzi imeliona hili na kuondoa uchaguzi siku ya Jumapili, tuige mfano huo ndugu zangu wakufunzi. Jumapili ni siku ya BWANA, ambapo vijana wanapaswa kukaa makanisani na kuadibishwa kufundishwa maadili badala ya kuwa na vijana wasio na hofu ya MUNGU.

Waraka huu uwafikie katika vyuo vyote tuheshimu ibada za wanafunzi wetu.Yesu alisema ole wake anayemkwaza mmoja kati ya wadogo hawa atafaa afungiwe jiwe kubwa la kusagia akatupwe baharini. Imeandikwa katika Marko 9:42 na yeyote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio,afadhali afungiwe jiwe kusagia shongoni mwake , na kutupwa baharini. Wakufunzi kwa kutangaza test jumapili mnatikwaza mno.Hao vijana mnaodhani ni wapagani wapo wacha MUNGU tunawategemea kwa huduma kanisani wengine kupiga vyombo vya muziki, uimbaji na Huduma za madhabahuni .Halafu unaambiwa eti chuoni kuna test jumapili. Ninaendelea kuwahubiri vijana waisimamie imani. Nawapenda vijana Wasabato hawa hawataki huu upuuzi ukiwatangazia test jumamosi utafanya mwenyewe.Hawa vijana wa jumapili ngoja tuwasaidie kuwasemea. Sasa iko hivi, wakufunzi msipobadilika na hii tabia tutawashitaki kwa MUNGU anayejua kuwanyoosha wajeuri.Na kuanzia sasa kila test

Itakayofanyika jumapili tutachukua jina la mtoa test huyu ili tumshtaki kwa MUNGU. Nimefanya kazi na vijana, ukweli ni kwamba bila imani hakuna maadili.Vijana wanaomuamini MUNGU wanakuwa na hofu ya kuwajali na kuwatumikia watu wa jamii zao msiwanyime vijana nafasi ya kuabudu. Wengine mnasema nitatoa mtihani,baada ya kusali.Jambo hili haliwezekani kijana hawezi kuabudu kwa raha wakati kuna mtihani.Lakini hata hivyo jumapili ni siku ya mapumziko kwa wanaosali siku hiyo.Maana ndiyo siku iliyowekwa ya kupumzika kwao, kuwaambia waje kufanya mtihani ni ukatili. Ni imani yetu kama kanisa kwamba ujumbe huu utamfikia kila mkufunzi na ataiheshimu siku ya Jumapili na hatatoa mtihani siku hiyo. Kwa MAOMBI, MAOMBEZI na SADAKA waweza kutuma kwa namba ya mpesa 0752 352 116. Mungu awabariki sana. Mwinjilist Imani O. Katana Whatsapp +255 752 352 116 katanaimani@gmail.com

TUNAPOKEA HABARI NA MATANGAZO MBALIMBALI, WASILIANA NASI KWA FAIDA YA WENGI ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


HABAKUKI 2:1-2

SOKA LA BONGO

ISSN 2714-2108: Toleo Na.011. Jumamosi Agosti 01-15, 2020

TETESI ZA USAJILI SOKA LA ULAYA

Uhamisho unaokisiwa wa Jadon Sancho kwenda Manchester United uko karibuni kufikiwa, wakati Borussia Dortmund wakiwa tayari kukubali ada ya awali ya pauni milioni 60 kwa ajili ya winga huyo, 20.

JAMES KOTEI KUTAMBULISHWA AGOSTI 9 NA YANGA AKIWA NA NYOTA WENGINE 9.

KAMATI YA MAADILI YA YANGA KUTOA MAAMUZI DHIDI YA BERNARD MORISSON NA MWANDISHI WETU KAIMU Katibu Mkuu wa Yanga, Patrick Simon amesema kutokana na matukio ya Bernard Morrison ya utovu wa nidhamu amepelekwa kwenye Kamati ya Maadili. Morrison hajajiunga na timu kwa sasa ambapo mara ya mwisho kuonekana akiwa na Yanga ilikuwa ni Julai 12, Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba. Baada ya mchezo huo ambapo Morrison alitolewa dakika ya 64 na nafasi yake kuchukuliwa na Patrick Sibomana aliondoka jumla uwanjani na kwa sasa amekuwa akionekana akicheza mechi za mtaani huku akieleza kuwa anahofia

kupigwa ikiwa anakwenda mazoezini. “Kwanza nimeshachoka habari za Morrison lakini ni kwamba kuna kamati ya maadili ya Yanga inashughulikia suala lake muda si mrefu watalitolea maamuzi kwa sababu yametokea matendo ya kujirudia, ilibidi tumpeleke kwenye kamati ya maadili ambayo ni huru mimi sipo kwenye hiyo kamati.

Chelsea imeweka mezani ofa kwa ajili ya mlinda mlango wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen, 28. Gareth Bale, 31, amemwambia kocha wa Wales Ryan Giggs kuwa ana dhamira ya kusalia Real Madrid msimu ujao. hata kama kukosa michezo kutaathiri kipato chake. Chelsea na Manchester City ni miongoni mwa vilabu vinavyoongoza ambavyo vinafuatilia kama mchezaji David Alaba, 28, atasaini mkataba mpya na Bayern Munich. Inter Milan wanatarajiwa kukubali dili kumsajili Mshambuliaji Alexis Sanchez,31 kutoka Manchester United kwa mkataba wa kudumu msimu huu.

“Kwa hiyo wanafanya taratibu zao wameshamwalika kumsikiliza na kufanya taratibu zao halafu watatoa uamuzi wao, sisi tunawasubiri wao pamoja na TFF watuambie maamuzi yao juu ya kesi yake. “ alisema Patrick.

TANGAZA NASI MATANGAZO MBALIMBALI UONE FAIDA NA NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.