JARIDA ZAMU YANGU SEPTEMBER 01-15, 2021

Page 1

Jarida huru pendwa la mtandaoni la Kikristo linalotoka tarehe 01 na 16 kila mwezi.

eekklesiatz@gmail.com

I

ZaMuYaNgu ISSN 2714-2108 Uk.10

Donda

Uk.06

Uk.03

TOLEO NA. 36, JUMATANO SEPTEMBA 01-15, 2021

Aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania, Askofu mkuu Luigi Pezzuto ang’atuka madarakani. Uk.04

NA MWANDISHI WETU,

YALIYOMO UK 02

IBADA YA SANAMU

UK 11

UKISHAONJA HIYO ASALI.. RONALDO ATUMA UJUMBE KWA SIR ALEX

UK 12

UK 02

UK 08

A

skofu mkuu Luigi Pezzuto alizaliwa kunako tarehe 30 Aprili 1946 huko Squinzano, Kusini mwa Italia. Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 27 Septemba 1971. Tarehe 6 Januari 1997 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu mkuu. Amewahili kuwa Balozi: DRC, Gabon, Tanzania, El Salvador, Beliza, Antilles na mwishoni alikuwa huko nchini Bosnia-Herzegovina na Montenegro. Inaendelea ukurasa wa nne (4)

UK 11

UK 12

MAMBO MATANO YENYE THAMANI KULIKO FEDHA

HABARI . MAKALA . NENO . HISTORIA . AFYA . VITABU . TANGAZO . MICHEZO PROUDLY SPONSORED BY:- RADIO 5 | EVG MINISTRY | FOUNTAIN RADIO | M!SA RICE | SHALOM RADIO & TANGANYIKA PRODUCTION

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE


ZaMuYaNgu Septemba 01-15, 2021.

IBADA YA SANAMU MUNGU ANAPATIKANA WAPI?

Uchambuzi wa kitabu

wone na kumtambua, aliendelea kusema; Mimi ndiye Mungu nayatenda yasiyowezekana, ni Mimi, niliyelisha taifa la Israeli Mana jangwani, ninaweza kuyatenda yasiyowezekana, tambua, Mimi ni Mungu, sina njia moja ya kutenda, NILIFANYA, NINAFANYA, NITAFANYA.

NA AP. HELLEN SOGIA.

SURA YA SITA.

MATUNDA

M

tu anaweza kuangamizwa kwa sababu ya kukosa maarifa ya kiMungu ndani yake. Hos 4:6.

Uko mchezo aliouleta Ibilisi, wa kurudisha kanisa la Kristo nyuma, badala ya kwenda mbele. Watu wa Mungu wanarudi kwa mwendo wa kinyumenyume huku wakitazama mbele, wakidhani wanaenda mbele.

Kuna mtu anakuwa amelenga shabaha zake kubwa kwa kumtafuta shetani, na mapepo yake waliko ili apigane nao, Ukweli ni kwamba adui lazima tumbonde, lakini ni vyema kuchukua tahadhari katika kila anachokifanya mtu, kwa sababu, hali ya namna hii inapoendelea na mtu asipokuwa mwangalifu, baada ya muda fulani mtu anajikuta ule moto wa kumpenda Mungu unaanza kupoa, kwa sababu mtu huyu alikuwa na muda mwingi wa vita, akasahau ushirika wake na Mungu. Wakati mwingine mtu hufanya hivi kwa ajili ya kutafuta maisha ya kujistarehesha nafsi yake mwenyewe, na si kwa ajili ya Bwana, bila ya kujitambua wako watu ambao wamekamatiwa hapo, kwa kukosa muda wa kutafuta kuwa na ushirika na

Mungu; Hali hii imeliingiza kanisa la Kristo jangwani; Ni vyema mambo haya mawili yawe kwenye uwiano mzuri. 1. Mapepo yashughulikiwe, 2. Ushirika na Mungu pia uzingatiwe vizuri.

Yak 4:7–8. • Basi mtiini Mungu. Mpingeni shetani naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yen, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Siku moja Bwana akanionya na kusema; Nyumba yangu za Ibada imekuwa kama jengo la sinema, watu wangu hawaji tena ili kukutana nami na kuniabudu mimi, bali wanakuja kutazama sarakasi, wamekuwa wakichagua ni jengo gani linaonyesha picha nzuri zaidi ya nyingine.

Fahamuni hili basi! Kuwa shetani amewafungia watu wangu kamba kiunoni, na kuwavuta kwa nyuma, akiwarudisha nyuma kwa kunyumenyume, ili wasim-

Zama hizi za leo, Mungu ametufunulia mambo ambayo yamekuwa yakitutesa, pamoja na visababisho vyake, na jinsi ya kuviondoa kwa kutumia uweza wake wa kiungu, kupitia huduma ya UKOMBOZI NA UPONYAJI. Mungu ameweka mambo yote wazi kwetu, amemfunua shetani kwa uwazi, amefunuwa mambo yake, kazi zake zote, na jinsi ya utendaji wake, mambo yote hayo, yamewekwa bayana. Lakini! Pamoja na watu kumjua Mungu katika uweza wake wa kiungu, wenye nguvu na mafunuo, na ukombozi unaomkomboa mwanadamu, hawakumtukuza Mungu wala kumshukuru badala yake wamepotea kwenye uzushi na ujinga, na mioyo yao ikawa mijinga na kutiwa giza, ile nuru iliyokuwemo ikiwamulikia watu na kuwajulisha Mungu wao ni nani, ikaendelea kufifia siku hadi siku na mioyo ikaendelea kwenye nguvu za Mungu tu na sio kwa Mungu mwenyewe.

Wanadamu wakabaki wakitafuta nguvu na miujiza yake Mungu, wakasahau kuwa Mungu ndio hiyo nguvu yenyewe na ndio huo Muujiza wenyewe.

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE

6

2

IBADA YA SANAMU.

Yakobo alipokuwa anamkimbia ndugu yake Esau, alifika mahali akawa amechoka,jua likawa limezama, Yakobo alichukuwa jiwe akalala pale mahali, usiku akaota ndoto na Bwana akasema naye, akampa ahadi, ndipo Yakobo akapaita pahali pale Bethel. Yakobo anaonekana akiendelea na safari yake, baada ya ahadi alizopewa na Mungu hakubakia Betheli. Mwa 28:10-22. Kuna watu ambao bado wako Betheli, wameamua kubakia hapo wakisubiri muujiza wao hapo, kumbe muujiza wao uko Padan-Aram, wengi bado wamelalia jiwe pale Betheli, na kulifanya jiwe hilo kuwa Mungu wao. Betheli sio mahali pa kukamilishia ndoto wala malengo ya mtu, bali ni mahali pa kupokelea tu. Mtu anapobakia betheli akilalia jiwe ataishi kwa ndoto na maono yasiyokamilika, na sio katika uhalisi wake (Reality). Uhalisi unapatikana ndani ya Ibada na Bwana. Ukishapokea ujumbe wako, ndoto yako, unabii wako; unapashwa kuingia kazini na kutendea neno hilo kazi, ili, neno hilo lipate kuwa halisi katika matendo, usibakie na simulizi la hayo uliyopokea kwenye kinywa chako kila siku. ITAENDELEA

__________________________________ Apostle Hellen Sogia

THE OAK MISSION MINISTRY. P.o Box 30838. Kibaha Pwani.

Simu: 0753 351 048 au 0716 711 867

_____________________________________


ZaMuYaNgu Septemba 01-15, 2021.

Historia

Huyu ndiye Sarah Wayne

aliecheza filamu ya Prison Break.

NA MWANDISHI WETU

S

arah Wayne Callies (Sarah Anne Callies amezaliwa tar. 1 Juni 1977 huko La Grange Illinois) ni mwigizaji filamu na tamthiliya wa Kimarekani, anayejulikana vizuri baada ya kuigiza kama Dr. Sara Tancredi katika misimu miwili ya kwanza ya tamthilia ya Kimarekani Prison Break. Miasha ya Awali Callies na familia yake walihamia Honolulu, Hawaii. Kipindi hicho alikuwa na umri wa mwaka mmoja. Alianza kujionyesha mapema kuwa mapenzi yake ni kuigiza kwa kushiriki katika maigizo kadha wa kadha ya shuleni hapo Punahou School. Wazazi wake wakiwa ni maprofesa katika chuo cha Hawaii kilichopo Manoa, Callies hakufuata nyayo zao kabisa. Badala yake, alichagua kujiingiza moja kwa moja kwenye Uigizaji. Alipohitimu elimu ya sekondari, alijiunga na chuo cha Dartmouth kilichopo Hanover, New Hampshire. Pamoja na kuwa na masomo, aliendelea kujihusisha kwenye maigizo.[1] Aliendeleza elimu yake hapo Denver’s National Theatre

Conservatory alipojipatia Shahada ya Sanaa ya Maigizo hapo 2002.

Sanaa Callies’s alionekana mara ya kwanza kwenye luninga kama Kate O’Malley, uhusika wa mara kwa mara kwenye Queens Supreme. Aliigiza nafasi ya nyota kwa mara ya kwanza kama Jane Porter kwenye tamthiliya ya Tarzan, iliyorushwa na Warner Bros. Baada ya kushirikishwa kwenye Law & Order. Special Victim Unit, Dragnet na NUMB3RS, Callies alikamata nafasi ya nyota kwenye Prison Break ya FOX kama Dr. Sara Tancredi. Pia aliigiza kama nyota kwenye filamu za Universal Picture za Whisper na The Celestine Prophecy. Maisha Binafsi Mnamo Juni 21, 2002, Callies alifunga ndoa na Josh Winterhalt, aliyekutana nae katika chuo cha Dartmouth. Winterhalt ni mwalimu wa sanaa. Ilipofika Januari 23, 2007, msemaje wake alitangaza kuwa wawili hao walikuwa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza. Julai 2007, Callies na mume wake walimkaribisha mtoto wao wa kike, Keala Winterhalt(Kay-AH-lah).

TUNAPOKEA USHUHUDA, TAFAKARI, MAKALA, MATANGAZO NA MASOMO MBALIMBALI ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE

3


4

ZaMuYaNgu Septemba 01-15, 2021. HABARI KIMATAIFA. Kibonzo

Askofu mkuu Luigi Pezzuto ang’atuka madarakani. NA MWANDISHI WETU.

B

aba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la Askofu mkuu Luigi Pezzuto la kutaka kung’atuka kutoka madarakani kama Balozi wa Vatican. Askofu mkuu Pezzuto amewahi kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Monaco, Bosnia, Erzegovina na Montenegro. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Pezzuto alizaliwa kunako tarehe 30 Aprili 1946 huko Squinzano, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapewa

Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 27 Septemba 1971.

Tarehe 6 Januari 1997 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu mkuu. Tangu wakati huo amekwisha tekeleza dhamana na utume wake wa kidiplomasia nchini DRC, Gabon, Tanzania, El Salvador, Beliza, Antilles na mwishoni aliteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Bosnia-Herzegovina na Montenegro.

TANGAZA NASI +255 766 231 717

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE


ZaMuYaNgu Septemba 01-15, 2021. Neno la Mungu Mahubiri NA MCH. KABALAMA SINGIDA

B

wana Yesu Kristo asifiwe mpendwa wangu katika Yesu Kristo. Nakukaribisha katika somo la siku ya leo. Mungu ametuita tuwe milki yake ili tuweze kuzitangaza fadhili zake na tutoke gizani. Imeandikwa 1Petro 2:9; • “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu,mpate kuzitangaza kazi zake yeye aliyewaita mtoke mtoke gizani makingie katika nuru yake ya ajabu”. Tunayo nafasi kubwa sana mbele za Mungu. Tunayo thamani kubwa sana mbele za Mungu. Thamani hii kubwa ililetwa na Yesu Kristo pale alipokubali kuzaliwa na kuishi kama mwanadamu na hatimaye kufa ili ulimwengu wote ukombolewe kutolewa katika giza la dhambi na kuletwa katika nuru yake Mungu iliyo ya ajabu. Mungu anakupenda sana wala usije ukajidharau kwa sababu watu wamekudharau, usije ukajidharau sababu mwenza wako amekudharau, hakuthamini wala kukujali; Mungu anakuthamini na kukujali mno. Wewe ni wa thamani sana kwa Mungu na ndiyo maana amegharamia maisha yako, amegharamia roho yako usipotee milele katika giza bali

ONDOA VIZUIZI ILI MUNGU AKUHUDUMIE ukombolewe na kuwekwa huru. Gharama zote hizi Mungu amezitimiza kwa kumtoa mwanawe pekee Yesu Kristo. Hivyo Mungu anakupenda na anataka akuhudumie, anataka ahudumie maisha yako na kukuinua kukutoa katika kilio, kukutoa katika kudharauliwa na wanadamu.Ili Mungu akuhudumie huna budi kushughulika kwa juhudi zote ili kujitenga na vizuizi vifuatavyo:(i). Dhambi. Dhambi ni chukizo kwa BWANA, dhambi ni zuio la mema kutoka kwa BWANA. “Maovu yenu yameyageuza haya, na dhambi zenu zimewazuilia mema msiyapate”. Yeremia 5:25. Hata kama umemwomba Mungu na akasikia, lakini kabla ya majibu kuja ukatenda dhambi, nataka nikwambie majibu yanazuiliwa mara moja. Dhambi zinazuia mema usiyapate. Wako wakristo wanaishi maisha ya dhambi kana kwamba hawajui wanamchukiza Mungu.Kama unaishi maisha ya dhambi, hakika unamchukiza Mungu na unamfanya Yesu Kristo kuonekana si kitu chochote na kwamba mateso na kifo chake msalabani ni upuzi. Dhambi ni kizuizi kikubwa sana cha kuhudumiwa na Mungu kwa maana yeye Mungu hawasikii wenye dhambi hata kidogo. Yohana 9: 31. • “Twajua ya kuwa Mungu hawasiki wenye dhambi bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo”.

5

Ni heri utubu leo dhambi zako na Mungu atakusamehe na kuzifuta zote kabisa. (ii). Kutokutoa sadaka kwa usahihi. 2Wakorintho 9:6-7; • “Lakini nasema neno hili, apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu”. Kutokutoa sadaka kwa usahihi pia ni kizuizi cha kutokuhudumiwa na BWANA. Wako wakristo ambao wamekuwa na roho ya uchoyo ambao wao wanaona kwamba wakitoa sadaka na mafungu ya kumi kwa usahihi ni kumshibisha Mchungaji na nyumba yake. Wakristo wa namna hii huchukia sana wanapoona Mchungaji amefanya maendeleo, mioyo yao huwa kama wanataka kupasuka. Wakristo wa namna hii wako tayari hata kutengeneza makundi ndani ya kanisa ili kuwashawishi watu wasitoe sadaka. Na ukichunguza maisha yao mara nyingi huwa hawana maisha mazuri sana, wanakuwa na maisha ya tabu na hofu kila siku. Ukweli ni kwamba tukiamua kuanza kutoa sadaka kwa usahihi tena kwa kumpenda Mungu utaona maisha yetu yanabadilika maana yatahudumiwa na Mungu mwenyewe.

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE

(iii). Nguvu za giza. Nguvu za giza pia ni kizuizi katika maisha yetu. Maisha ya watu wengi yameteswa na kuonewa na nguvu za giza kiasi cha kupinga maendeleo yao. 1Wakorintho 16: 9; • “Kwa maana nimefunguliwa mlango wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao”. Mlango ni nafasi ya uwazi katika nyumba inayokuwezesha kupita ili kuingia ndani au kutoka nje ya nyumba. Mlango ni mpenyo. Ili uweze kuendelea kimaisha ni lazima iwepo nafasi ya wazi itakayokuwezesha kupenya kuyafikia maendeleo unayotaka. Watu wengi sana wamepingwa kuelekea katika maendeleo ambayo Mungu amewawekea. Leo kwa jina la Yesu Kristo kubali kuondoa vizuizi vyote ili Mungu akuhudumie.

Ni mimi, Mch. Kabalama M. M. +255 753 305 957.


ZaMuYaNgu Septemba 01-15, 2021. Mahojiano Tangazo

Sisi ni The Survivors Gospel kwaya.

6

NA MWANDISHI WETU, DAR

B

wana Yesu asifiwe, natumaini mnaendelea vema kabisa na majukumu ya kila siku. Kwa neema ya Mungu wiki iliyopita Zamu Yangu ilipata muda mzuri sana wa kuzungumza na viongozi wa kundi linakuja juu sana la The Survivors Gospel Choir. Fuatana nasi kwa karibu sana ujue kilichoendelea katika sehemu ya kwanza na kwaya hii, karibu.

SURVIVORS: Tunafahamika Kama The Survivors Gospel Choir tunapatikana Dar es salaam Tabata Chang’ombe, kwaya Ina jumla ya watu 48, na mpaka Sasa tumeachia nyimbo sita (6) video ambazo zipo YouTube nyimbo hizo ni Kihome home tuliomshirikisha Joel Lwaga ,Nami nimo, Amka uende, Sio mwisho, One day pamoja na wimbo mpya wa Nami nimo remix ambao tumewashirikisha Zabron singers. MWANDISHI: Mnasali kanisa gani na kundi lenu lipo chini ya kanisa gani? SURVIVORS: Hatupo chini ya kanisa lolote ni kundi linalojitegemea.

MWANDISHI: Kundi lenu lina miaka mingapi Sasa? SURVIVORS: Kundi Lina miaka mitatu. MWANDISHI: Mmewezaje kudumu muda WOTE huo bila kuwa na kanisa linalowasimamia? SURVIVORS: Ni kwasababu tunafanya kazi ya Mungu hivyo Mungu anatusimamia nasi tunasonga mbele kwa msaada wake. MWANDISHI: Mkiwa kama viongozi wa kundi Kuna changamoto gani mnapitia ngumu katika kuliendesha kundi? SURVIVORS: Changamoto tunazozipata Kama viongozi kwanza Kama unavyojua vijana wanakua na mambo mengi lakini pia kila mmoja anakua na tabia zake hivyo ku

waweka wote pamoja na wakaweza kufanya Jambo moja Kuna ugumu wake, pia vijana wengi tulionao no wanafunzi hivyo kwa Jambo linalohusisha fedha linakua gumu kutekelezeka kwa wakati maana wengi wao ni tegemezi. MWANDISHI: Je bado mnapokea waimbaji wengine ama idadi imetimia? SURVIVORS: Bado tunawakaribisha wengine wajiunge nasi.. MWANDISHI: Mnatarajia kuwa na idadi ya waimbaji wangapi kwenye kundi lenu? SURVIVORS: Hatuna idadi ya mwisho Kila anaejisikia wito wa kumtumikia Mungu amoja nasi anakaribishwa.

MWANDISHI: Vigezo vyenu mnavyozingatia mtu kujiunga nanyi ni kipi? SURVIVORS: Awe ni mtu mwenye nia ya kumtumikia Mungu, lakini tunazo kanuni ambazo mtu akiwa ndani ya kundi anatakiwa azifuate. MWANDISHI: Mlipata ugumu gani kumshawishi Joel Lwaga kufanya naye kazi mpaka akakubali ukizingatia mlikua mnaanSURVIVORS: za huduma?SURVIVORS: Hatukupata ugumu wowote maana Joel ni moja Kati ya waanzilishi wa hili kundi kabla hatujawa the Survivors tulikua nae na alikua ni makamu mwenyekiti wa kwanza wa hili kundi hivyo ilikua ni rahisi kwa Yeye kuja kufanya kazi nasi.

Itaendelea toleo lijalo...

JE UNA WEWE NI MUIMBAJI, MUHUBIRI, MWALIMU, MSANII AU UNA HABARI, BIDHAA, TANGAZO NA UNGEPENDA KUTANGAZA NASI? WASILIANA NASI SASA KUPITIA +255 766 231 717. WHATSAPP / SMS / CALL ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE


7

ZaMuYaNgu Septemba 01-15, 2021. Shairi Tatu za wiki

Kanye West - Donda (feat. Stalone & The World Famous Tony Williams)

WASANII WA INJILI

Forever, yeah Can you hear me? Yeah Forever, yeah Forever, forever, no Oh yeah, glory, glory, glory Glory, glory, glory, glory It feels good to be home And to all of you, I thank you so much for your support For your support of me for so many years And more importantly, for the work you continue to do. What do you want me to talk about? Well, he said something that was a little bit dangerous He told me I could talk about anything I wanted to.

ZY GOSPEL Top3

3.

PAMMY RAMZ - MWEMA

2.

FLORENCE MACKENZI - NIMEBARIKIWA

1.

KANYE WEST - DONDA

B.

DAUDI NYIGO - UNIONGOZE

And you know, I am my son’s mother The man I describe in the introduction as being so decidedly different My son (When you’re runnin’ outta time and you’re not outta time) And what made the project extra special to me is I got a chance to share not only what he has meant to me But what he has meant to a generation (Change the time) As one writer said, we came from somewhere Not just from the wombs of our mothers and the seeds of our fathers But from a long line

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE

of generations who came before us It’s the kingdom (It’s the kingdom) And the power (And the power) And the glory (And the glory) Forever (Forever) It’s the kingdom (It’s the kingdom) And the power (And the power) And the glory (And the glory) Forever (Forever) Forever, yeah Forever, yeah Forever, forever, no Oh yeah, glory, glory, glory What did I teach him? (Glory) And why Kanye ain’t scared?


ZaMuYaNgu Septemba 01-15, 2021. MOTO ULAO MAKALA

MAMBO MATANO YENYE THAMANI KULIKO FEDHA.

ya maua na bila shaka vipepeo watakuja kwenye maua nawe utawakamata kwa urahisi.

NA MCH. IMANI O. KATANA

Kibali cha MUNGU huvunja mapingo, unaweza ukawa hauna pesa lakini kibali kinakupa kununua bila pesa, tafuta kibali kwa MUNGU ili uweze kuwa na uwezo wa kununua bila pesa. Na kuna njia kumi za kimaandiko unazoweza kuzitumia kupata kibali . Unaweza kupata kibali kwa kutenda mema

A

tukuzwe Mungu juu mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia .Ndugu yangu mpendwa unayefuatilia Makala hii,nakusalimu kwa jina la YESU tayari nimeelezea mambo mawili ambayo yanathamani kubwa kulikom pesa.Nimeeleza habari ya jina jema kwamba lina thamani kubwa kuliko pesa, Lakini pia nimeeleza kwamba hekima inathamani kuliko pesa. Leo tunaingia katika jambo la tatu karibu.. Kibali cha MUNGU kina thamni kuliko pesa, mtu mwenye kibali anaweza kununua bila pesa, hapo ndipo utajua maana ya kibali.Wapo watu waliofanya mambo makubwa ukiwauliza sio kwamba walikuwa na pesa nyingi la hasha! Walikuwa na kibali cha MUNGU. Kibali (favour) ni hali ya kupata upendeleo wa kiungu, yaani popote unapokuwa unaenda MUNGU anakujalia kukubalika na kupendwa watu wanakuwa tayari kukusaidia.Watu wanajitoa Maisha yao kwa ajili yako, popote unapokwenda

3

8

unajikuta watu wanakufadhili na kukujali. Yusufu alipata kibali kwa Potifa na kwa mkuu wa gereza lakini si hivyo tu hata kwa wazazi wake maana mzee Yakobo alikuwa anampedna sana Yusufu. Mwanzo 39:21. Mtu mwenye kibali cha MUNGU hawezi kubaki chini, namfananisha na mpira uliojazwa upepo ambao hauwezi kuzamishwa kamwe , unaweza ukapiga mbizi nao mpaka chini ya bahari lakini jambo moja ni dhahiri utaachiwa na utarudi juu na kuelea.Ndio maana

mtu kama Yusufu walimtupa kwenye shimo lakini kibali cha MUNGU kikamtoa shimoni akapelekwa kwa Potifa, Alipotupwa gerezani bado huko na kibali cha MUNGU kikamtoa akajikuta ni miongoni mwa wakuu wan chi ya Misri. Mpendwa ukiambiwa kukamata vipepeo, kama utaaamua kukimbiza kimoja kimoja na kukamata ni kweli utakamata lakini itakuwa ni kwa taabu sana. Kwani utatumia nguvu nyingi kukamata kwa njia hii lakini njia rahisi ni kupanda bustani

TUNAPOKEA MAKALA NA SHUHUDA MBALIMBALI KUPITIA NAMBA YA WHATSAPP 0766231717

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE

Sawa na Mungu alivyomuambia Kaini katika kitabu cha mwanzo 4;7 kwamba ukitenda mema utapata kibali. Mpendwa wangu Yesu ni nuru ya ulimwengu ukipoea na akakaa ndani yako uwe na uhakika kwamba utapata kibali na kibali hicho kitakuletea fedha unazozihiitaji. Yesu alisema I mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya kilima .Ukitenda mema na kusimama katika kutimiza kusudi la BWANA uwe na uhakika kwamba utakuwa mtu aliyejaa kibali. Rafiki yangu na msomaji wangu naomba nikukaribishe sana madhabahu ya MOTO ULAO hapa Dege aaKigamboni hakika utakutana waziwazi na MUNGU wetu ambaye ni MOTO ULAO sawa na WAebrania 12:29.KARIBU SANAAAAA


ZaMuYaNgu Septemba 01-15, 2021. MAONI YA WASOMAJI

Walichozungumza wadau baada ya Zamu Yangu kutimiza miaka mitatu ya huduma.

9

K

wa machache haya, kati mengi. Kwa “Gazeti zamu yamu”, nimeona moyo wa ushujaa, kuitangaza injili ya Yesu Kristo, kwa mataifa, naiona nuru ikiwafikia miisho ya nchi, kupitia gazeti zamu yangu, endelea kupasua mawimbi kuifikia ndoto yako. “Gazeti zamu yangu, ni mtenda kazi mwenzangu katika Bwana” Ap Hellen Sogia.

M

imi niwapongeze tu kwa huduma nzuri na ya kisasa Robert.

B

inafsi niwashukuru sana kwa jarida la Zamu Yangu maana mmekuwa bega kwa bega kwetu na wasomaji wamekuwa wakilipenda sana hususani sisi kama Nyota Shine Every Where kutokana na kipindi kinachopendwa cha Nyota wa leo, kiukweli kama C.E.O wa Nyota Shine every where niwapongeze maana mmekuwa sababisho kujulikana na wengi kwa kipindi hicho, na niwatie moyo tu kufika mbali na kuwafikia wengi zaidi ya hapa. Asante Bahati Simwiche C.E.O ©Nyota Shine Every Where

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE


ZaMuYaNgu Septemba 01-15, 2021. Makala Tangazo

ZINGATIA VITU HIVI VITATU MUHIMU.

10 THAMANI YAKO - 20

1. Kutazama maisha yako NA AP, HELLEN SOGIA

M

wanadamu, ishi kwa kuyafuatilia maisha yako, uone kama yanalingana na Neno lake Mungu, pia unatakiwa ufahamu kuwa, Wewe ndio askari wa maisha yako mwenyewe, kama jinsi Mungu alivyotuumba, na kutuwekea nguvu ya maamuzi ndani yetu, ili tuwe waamuzi juu ya maisha yetu wenyewe, ndivyo hivyo tunavyopaswa kuyafuatilia maisha yetu kabla Roho Mtakatifu hajaingilia kati. Kila mwanadamu katika maisha yake yote, anapaswa kuwa makini na vitu muhimu vitatu (3), ambavyo ndio kioo cha dira ya maisha yake kila iitwapo leo na katika kuishi kwake hapa duniani. Kumbuka tunaishi leo kwa ajili ya kuishi kesho na kwa jinsi ya kuishi kwetu leo ndio itategemea wapi tutaishi kesho. Vitu vitatu vya kuzingatia katika kuishi kwetu:1. Kujihoji. 2. Kujitunza. 3. Kujikagua. Nini maana ya kujihoji. Kujihoji ni kujitazama,

Wafilipi 2:15. • “Mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu.” 2. Kutazama mwenendo wako uko vipi mbele zake BWANA YESU. Tito 2:12. • Nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa. 3. Kutazama tabia zako zilivyo, mbele za Mungu, na wanadamu. 1 Wathesalonike 2:4. • Bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu. Warumi 12:1. • Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili

• yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. 4. Tazama maneno ya kinywa chako. Je yanapata kibali mbele za Mungu? Au la! Mathayo 12:36. • ³⁶Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. • ³⁷Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.

Kuihoji nafsi yako, kila siku, itakusaidia kuona wapi uliteleza na itakutengenezea mazingira mazuri ya kujikung’uta na kurejea tena kwenye mstari sahihi. Utakuwa umepata nafasi ya kuilinda thamani yako.

__________________________________ Apostle Hellen Sogia

THE OAK MISSION MINISTRY. P.o Box 30838. Kibaha Pwani.

Simu: 0753 351 048 au 0716 711 867 __________________________________

USIKOSE MUENDELEZO WA MAKALA HII KATIKA TOLEO LIJALO.

Tuweke pembeni utashi wetu

M

iaka ya 199798 kilio changu nilitamani kuona muziki wa injili unakua juu zaidi kuliko muziki aina yeyote, namshukuru

Mungu kwa sasa Muziki huu unazidi kukua hapa Tanzania, napenda kuwashauri waimbaji wenzangu tuweke pembeni utashi wetu ili

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE

Mungu aonekane katika uimbaji wetu - Askofu Ephraimu Mwansasu Lala salama Askofu uliona mbali sana #RIP


ZaMuYaNgu Septemba 01-15, 2021. HABARI MAHOJIANO

Ukishaonja hiyo asali utaelewa kwa nini huwa wanachaji - Ambwene Mwasongwe

NA, MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

S

halom Shalom, naitwa Ambwene Obadia Mwasongwe, ni mtumishi wa Mungu kwa njia ya uimbaji, nashukuru sana kwa kunikaribisha na kunipa heshima ya kuwa nyota wa leo, niko tayari kushirikiana nanyi kwa kile ambacho Mungu amenipa. SWALI: Umeachia kazi mpya ya Unikumbuke, ilikuwaje? AMBWENE: Unikumbuke ni wimbo wa ushuhuda wa jamaa mmoja aliyefungwa kwa miaka tisa kwa tuhuma za ujambazi na mauaji angali alikuwa akifanya kazi katika taasisi nyeti sana nchini. Aliyetuhumiwa kwa kosa la ujambazi ambalo hakulifanya kwa sababu tu ya maisha aliyokuwa anaishi ya bata. SWALI: Je una mpango wa kuwa Mchungaji siku za mbeleni? AMBWENE: Uchungaji ni wito na anayeita ni Kristo na kama akiniita, mimi ni mtumishi tu na nimeitwa kwa kusudi lake na nitaitika, lakini kwa sasa siwezi kupanga japokuwa unaweza kutamani kitu kama Biblia inavyosema “tamanini kuwa na karama zilizo kuu” Kwa sasa mimi sijatamani wala kupanga ila kama nitaitwa na Mungu mwenyewe nakusikia wito huo basi nitaitika. Lolote laweza kutokea kwa sababu tupo kwa ajili ya kumtumikia Mungu. SWALI: Baadhi ya waimbaji hufanya kiki kisha kuachia wimbo na tunaona wewe hunaga kiki bali ukiachia kazi zinafika kwa wengi, Je unaamini kiki inasadia kumpandisha au kumshusha

muimbaji? AMBWENE: Siamini katika kiki na sidhani kama tuna kitu cha kiki sababu hatukuitwa kufanya kiki, ukipewa wimbo wa kumuhudumia mtu mmoja unatosha, kwa nini uangaike na kiki? labda endapo unatafuta mambo yako mengine ambayo siamini kwa muimbaji wa injili anaweza kufanya hivyo. SWALI: Kufikia sasa una albam ngapi? AMBWENE: Nina albam tatu rasmi, Majaribu ni mtaji, Heshima ya mrefu ni mfupi na Misuli ya imani na kwa sasa ndio nafanya mchakato wa albam ya nne ya Moyo wa ibada ambayo ndiyo imebeba wimbo wa unikumbuke na mwaka huu naiachia albam hiyo. SWALI: Unahisi kwa nini makampuni makubwa hayajajikita kuwekeza au kufanya biashara na waimbaji wa injili hapa Tanzania? Angali wadhamini siku zote mtaji wao ni watu na ukiangalia waimbaji wanafuatiliwa na watu wengi lakini wawekezaji hakuna. AMBWENE: Jambo la kwanza utambue kuwa kampuni zinafanya biashara na zipo kutengeneza faida, hazipo tayari. Niliwahi kwenda CRDB na kuuliza hili swali lakini yule Meneja aliniambia waimbaji wa injili hawajawa na muunganiko. Mfano leo ukija na wazo la kuwakusanya waimbaji wa injili, hawatakuja ila ukiwaambia mje na baadae kutakuwa na bahasha ndio watakuja, lakini mawazo ya kuungana na kufanya vitu vikubwa ni tatizo na kampuni hizi zinahitaji uhakika na anuani kwamba hawa watu tunaohitaji kuwapa pesa wana umoja kiasi gani. Jambo la pili, Sera za nchi yetu nyingi hazijihusishi na

ZAMUYANGU PROJECT & MAGAZINE

masuala ya dini yaani sera zinazoongoza makampuni na mashirika hazihusiki na masuala ya dini, leo hii nikijiuliza waimbaji wangapi wamesajili Brela ambazo zinaweza kufanya kazi katika kampuni mbalimbali wanaweza wasizidi kumi na inawezekana hawana elimu ya namna gani ya kufanya hizo kazi kitaalamu, ila kama tutaendelea namna hii basi tusahau udhamini wa namna yeyote, sababu usije kutegemea eti tigo watakufuata wewe eti sababu una wanaokufuatilia wengi. hicho sio kigezo tu. nafikiri tunatakiwa kukaa chini na kufikiria njia gani tunaweza kufanya ili tupate ushauri wa kitaalamu ambao unaweza kusukuma mziki wa injili tukaja kuwa zaidi fiesta, wasafi festival nasi tuwe na matamasha makubwa ambayo yana wadhamini na kampuni kubwa ambazo zipo tayari kuwekeza. SWALI: Kwa nini waimbaji mashuhuri huwalipisha waimbaji wachanga fedha wanapohitaji kufanya kolabo? Je ni sahihi? AMBWENE: Wapo sahihi kwa sababu, wewe unataka kolabo ya nini? yamkini umeona ana faida kwako sababu asingekuwa na faida kwako usiongeomba kolabo. Labda umeona ana watu wengi na kwake wale watu ni mtaji na yawezekana anafahamu thamani ya nyimbo. Hivyo mimi nikifanya na wewe halafu nikagundua kuwa huo wimbo waweza kukuingizia milioni mia kwani nikikudai milioni tano kwa nini usikitike? Wakati mwingine

11

tuache malalamiko ya hovyo na ni moja ya kitu kinachoturudisha nyuma, hivyo umeenda kumchokoza mtu kuomba kolabo, akikuchaji kama unaweza lipa kama huwezi acha, na sio suala la kulalamika kwa sababu

haikusaidii kitu na ninaamini siku ukija kuomba kolabo pia kama utakuwa umeshaonja hiyo asali utaelewa kwa nini wanachaji, tunatakiwa kuwaza nje ya box na kukaza misuli yetu ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana bila kunung’unikiana na kulaumiana kwa sababu ambazo hazina msingi. SWALI: Unajishughulisha na nini nje ya huduma? AMBWENE: Nina vitu vyangu vidogovidogo ambavyo ni binafsi na ujasiriamali mdogomdogo unaoongezea kipato changu. Mungu akubariki. Itaendelea Mahojiano haya pia yataanza kupatikana kwenye Youtube katika chaneli ya ZAMU YANGU.

TUNAPOKEA NA KUTANGAZA MATANGAZO YA HUDUMA, RATIBA ZA IBADA, TAMASHA NA MAKANISANI, UJASIRIAMALI NA VIPINDI VYA RADIO, TV NA BIASHARA HALALI.


ZaMuYaNgu Jumatano Septemba 01-15, 2021. ISSN 2714-2108 Habakuki 2:1-2 Toleo Na.036

MICHEZO NA BURUDANI RONALDO ATUMA UJUMBE KWA SIR ALEX FURGASON

TETESI ZA USAJILI

NA MWANDISHI WETU,

K

ila mtu anayenijua, anajua juu ya mapenzi yangu yasiyokwisha kwa Manchester United. Miaka niliyotumia kwenye kilabu hiki ambapo ya kushangaza kabisa na njia ambayo tumefanya pamoja imeandikwa kwa herufi za dhahabu katika historia ya taasisi hii nzuri na ya kushangaza.

MANNY PACQUIAO AWASHUKURU MASHABIKI ZAKE BAADA YA KUCHEZEA KICHAPO CHA UGAS. NA MWANDISHI WETU

N

inataka kumshukuru Mungu kwa kunipa nguvu ya kupigana. Ninashukuru familia yangu kwa kusimama karibu nami kila wakati. Ninataka kumpongeza Ugas na timu yake. Ingawa, nilitarajia matokeo tofauti, ninamtakia kila la heri.

JE UNA TANGAZO AU HABARI? ITUME KWENDA NAMBA +255 766 231717 BURE KABISA.

Asante kwa mashabiki kote ulimwenguni ambao walikuwa wakitazama. Asante kwa kila Mfilipino ambaye amewahi kuniunga mkono. Ninajivunia kuwakilisha nchi yangu. Samahani sikuweza kukupa ushindi, lakini nimefanya bidii yangu yote. Kutoka kwa moyo wangu wote, ASANTE! Mungu awabariki ninyi nyote! - MANNY PACQUIAO.

TETESI ZA USAJILI

V

Siwezi hata kuanza kuelezea hisia zangu hivi sasa, kwani naona kurudi kwangu Old Trafford kutangazwa ulimwenguni. Ni kama ndoto imetimia, baada ya nyakati zote ambazo nilirudi kucheza dhidi ya Mtu. Umoja, na hata kama mpinzani, kila wakati nilihisi upendo kama huo na heshima kutoka kwa wafuasi katika viunga. Hii ni 100% kabisa mambo ambayo ndoto hufanywa! Ligi yangu ya kwanza ya ndani, Kombe langu la kwanza, wito wangu wa kwanza kwa timu ya Kireno ya Ureno, Ligi ya Mabingwa yangu ya kwanza, Kiatu changu cha kwanza cha Dhahabu na Ballon d’Or yangu ya kwanza, vyote vilizaliwa kutokana na uhusiano huu maalum kati yangu na Mashetani Wekundu. Historia imeandikwa huko nyuma na historia itaandikwa mara nyingine tena! Una neno langu!

ilabu za Ligi Kuu ya Primia zimetumia pauni milioni 962 katika uhamisho wa wachezaji hadi sasa, ikimaanisha kwamba kutakuwa na haja ya kuongeza kiwango kikubwa tu cha fedha kufikia kile kilichotumika mwaka

ZAMU YANGU PROJECT & MAGAZINE

katika kipindi cha dirisha la usajili cha Pauni bilioni 1.3. Dirisha la uhamisho kwa Ligi Kuu ya Primia, Ligi ya Soka ya Uingereza na Uskochi yaani Scotland limefungwa Jumanne, Agosti 31, saa 23:00 BST.


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.