ZAMU YANGU MAGAZINE, AUGUST 15-31,2020

Page 1

Je unajitambua kama wewe ni mwana?

2

UK.0

Habakuki 2:1-2 Sio mapenzi ya Mungu kukuona unataabika miaka yote - Uk. 06

UK. 06

#ANGELBENARD

Jumapili Agosti 16-31, 2020

ISSN 2714-2108 Na.012

HASSAN MWAKINYO BINGWA WA NDONDI mkanda wa Dunia wa WBF. HABARI UK.12

IRENE ROBERT ATINGA NA SIDONDOKI. Ni wimbo mpya alioachia wiki hii na umetokea kupendwa sana, kutokana na ubora wa video yenyewe. Kazi ipo youtube na karibu kuitazama

MWL MWAKASEGE NA ASKOFU GWAJIMA WAFUNGA 9 0 . BAADHI YA AKAUNTI ZA K U YOUTUBE ZENYE MASOMO YAO. WAMILIKI WALIA, TUMEFUTA VIDEO ZENU ZOTE, MTUSAMEHE!

MACHO YAKO NI MLANGO

KANUNI YA MWANAUME MWENYE HOFU YA MUNGU NA ATAKAYEFANIKIWA LAZIMA ACHUNGE MACHO YAKE. ALICHOKIPENDA ADAM NDICHO KILICHOMPA UPOFU SAMSONI NA KUMUANGUSHA SULEIMANI - ELLY DAVID WAY MAKER YA SINACH KWENYE VIPENGELE VITATU TUZO ZA DOVE MAREKANI- HABARI UK.03

YALIYOMO EVERLYN WANJIRU APAGAWISHWA NA BOOMPLAY YA KENYA- HABARI UK. 07

Mapambano dhidi ya Corona yanaendelea, chukua tahadhari PROUDLY SPONSORED BY:- RADIO 5 | EVG MINISTRY | FOUNTAIN RADIO | M!SA RICE | SHALOM RADIO & TANGANYIKA PRODUCTION

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


Kitabu / Vitabu

JUMApili AGOSTI 16-31, 2020

2

Uchambuzi wa Kitabu / VITABU

KITABU CHA MUNGU ANAPATIKANA WAPI? SURA YA PILI - WEWE NI MWANA

Je unajitambua kama wewe ni mwana?

W

mahali pa KUZINGATIA.

NA HELLEN SOGIA, PWANI.

atumishi wa Mungu wanaojichanganya na dhambi wamewafanya watoto waliokabidhiwa kuwalea (watu wanaowaongoza) kutowaelewa na wanawafanya watu kutokuwa na uhakika kuwa baba yao hasa ni nani, je ni MUNGU au ni Shetani? Wakati mtumishi wa Mungu anaposhindwa kuthibitisha ushuhuda wake mbele za watu na mbele za Mungu inakuwa haipendezi, unakuta wakati mwingine wamejibadilisha hata kuwafanya watu wasiwatambue, leo wamekuwa chui kesho kondoo, asubuhi wako rangi ya bluu jioni nyeusi, wamewafanya watu wakose kuwa na matumaini na msimamo waelewe lipi au waamini nini. Baba wa kweli atamfundisha mwana wake afanane na yeye. (like the father like the son), baba mzuri hutumia neno kumfundisha nalo mwanae, na kwa neno hilo hukemea, huonya, hukaripia pia. 2 Tim. 3:13-17. lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea,na kuzidi kwa uovu, wakidanganya na kudanganyika, lakini wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ulijifunza kwa; naku

wa tangu zamani uliyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imaniiliyo katika Kristo Yesu, kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho, na kwa kuonya watu makosa yao,ns kuwaongoza na kuwaadibisha katika hak. Ili mtu wa Mungu awe kamili amekamilishwa apate kuutenda kila tendo jema. Swali; Je unajitambua kama wewe ni mwana? Kama umejisahau basi geuka haraka utafute kwenu ni wapi urudi! ili uwe na uhuru wa kweli nyumbani kwenu, Babsa yetu wa mbinguni yuko tayari anakusubiri ufanye MAAMUZI ya kurudi nyumbani ili akupokee na akukumbatie.Bwana Yesu alishamaliza kazi ya kurudisha uumbaji wa mungu katika nafasi yake, kilichobakia ni wewe kufikia

Mwana mpotevu alipoona amefikia mahali pa kula makombo ya nguruwe, alizingatia, alitia moyo wake ufahamu, akageuka akarudi nyumbani kwao, hata wewe japo umekawia uko nje, lakini! Kumbuka upendo wa Mun gu bado unakuita na baraka zake ziko kwa ajili yako, WEWE RUDI NYUMBANI. Luka 15:15-32. Bwana Yesu akapiga kelele akasema njooni!! Mwenye kiu na aje anywe maji, kwangu ndio yanapatikana maji ya uzima; aliendelea kusema mtu akishakunywa hayo maji ya uzima yapatikanayo kwangu, mtu huyu atabadilishwa, na ndani yake kutaumbika mto ambao utakuwa na mifereji ambayo itakuwa na uwezo wa kupitisha maji hayo yakaweza pia kuwafikia watu wengine hata kuweza kuwasaidia na kuwaponya, kwa sababu maji anayokunywa mtu ni maji yaliyo na uzima ndani yake, maji yaliyonauwezo wa kuondoa matatizo, magonjwa, mapepo na

kumpa mtu ushindi na uzima tele. Mtu anapokunywa maji yasiyotoka kwa Yesu huwa yakosa uwezo wa kumzuia mtu huyo asitende dhambi wala kuishi katika uovu, na kwa uovu huo mtu huendelea huendelea kuambukiza wengine uovu huo maana uovu ni roho. Yoh; 7:37-38. hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akasema, mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Cha ajabu ni, kumbe ndani ya mwanadamu kuna mifereji ya maji!! Pia katika mwili wa mtu kuna milango inayotumika kupitisha maji (neno la Mungu) au maji machafu (uovu) kutoka kwa shetani, milango hii ni macho, masikio, pua, mdomo, mikono, miguu, akili. Kwa msaada na ushauri, maombi, au kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako tafadhali wasiliana na Mtumishi wa Mungu, Apostle Hellen Sogia THE OAK MISSION MINISTRY. P.o Box 30838. Kibaha Tanzania Simu. +255 (0) 753 351 048 au +255 (0) 716 711 867

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


Wasifu / HISTORIA

JUMApili AGOSTI 16-31, 2020

HISTORIA, MKATABA, DOLA NA SERIKALI YA VATIKANI ROMA.

Jumba la Vatikani anaLOISHI Papa

Uwanja wa Mt. Petro

ROMA, ITALIA

HISTORIA

M

ji wa Vatikani ni mabaki ya Dola la Papa lililotawala sehemu kubwa ya Italia ya Kati kwa karne nyingi hadi 1870. Tangu 1860 baadhi ya maeneo hayo yalitwaliwa na Ufalme mpya wa Italia uliolenga kuunganisha sehemu zote za peninsula ya Italia. Utawala wa Papa juu ya mji na mkoa wa Roma ulilindwa na Ufaransa hadi 1870.

Vita ya 1870 kati ya Ujerumani na Ufaransa ililazimisha Ufaransa kuondoa jeshi lake Roma, ambao hivyo ulitekwa na jeshi la Italia tarehe 20 Septemba 1870. Wakati huo serikali ya Italia ilitaka kumuachia Papa Pius IX sehemu ya mji wa Roma kama eneo lake lakini Papa alikataa akitumaini Wakatoliki wa Italia na nchi nyingine duniani watalazimisha serikali ya Italia kumrudishia mji wote. Kwa miaka 57 Mapapa walijifungia ndani ya jumba la Vatikani.

Makumbusho ya Vatikani

Mkataba wa Laterani 1929. Mwaka 1929 serikali ya Benito Mussolini ilitafuta amani na Papa Pius XI aliyekuwa tayari kukubali mabadiliko. Mkataba wa Laterani wa 11 Februari 1929 ukampa Papa mamlaka na madaraka ya nchi huru juu ya basilika la Mt. Petro pamoja na maeneo mengine.

Serikali Mkuu wa Dola ni Papa mwenyewe, kwa sasa Papa Fransisko (Jorge Mario Ber-

goglio). Nafasi yake ni kama mfalme wa kuchaguliwa asiyebanwa na katiba au masharti yoyote. Mambo ya utawala yako mkononi mwa gavana anayeteuliwa na Papa pia. Vatikani ina uhusiano wa kibalozi na nchi 180 duniani kote kupitia Ukulu Mtakatifu. Vatikani ina jeshi dogo kabisa lakini lenye historia ndefu kabisa duniani. Ni kikosi cha Walinzi Waswisi ambacho kipo tangu mwaka 1506 na chenye wanajeshi 100 hivi. Wote ni Wakatoliki raia wa Uswisi kwa kuzaliwa. Vatikani ina Posta pia, ikitoa stempu na hata sarafu za euro.

WAY MAKER KWENYE VIPENGELE VITATU TUZO ZA DOVE LAGOS, NIGERIA Way maker ni wimbo uliotungwa na kuimbwa na muimbaji wa muziki wa injili kutoka nigeria Sinach umechaguliwa kuwania tuzo katika vipengele vitatu kwenye tuzo za Dove awards 2020 huko nchini marekani. Vipengele ambavyo wimbo wa “WAY MAKER “ umechagulia kuwania tuzo ni ‘Song Of The Year’, Spanish language recorded song of the year (as recorded by Priscilla Bueno), na Worship recorded song of

the year (as recorded by Leeland).

Dove awards ni moja t u z o kubwa za muziki wa injili duniani ambazo huandaliwa na jumuiya ya muziki wa injili marekani (GMA). Ikiwa ni mara ya kwanza kwa wimbo

kuandikwa na muimbaji wa injili kutoka Nigeria kuwania tuzo za Dove, Sinach amesema uteuzi huo umekuja kupitia roho wa Mungu na sio mwanadamu “Kama nilivyosema hapo awali,wimbo huu ulizaliwa kutoka kwa roho ni wa wakati huu,ninashukuru kwa kila mtu ambaye ameniunga mkono, makanisa na watumishi ambao wameupeleka wimbo huu katika miisho ya dunia na

kwa watu wote na umeendelea kuwa baraka kwao.” Tangu kutolewa kwa wimbo huu sept 30,2015 “WAY MAKER”waimbaji kutoka mataifa mbalimbali wameurudia wimbo huu (covered) baadhi yao ni kama Michael .W. Smith, Christafari, Passion Worship Bank,Maranda Curtis na Bethel Music. Tuzo za 51 GMA Dove awards zitatolewa ijumaa ya Oct 30 live kupitia Tritinity Broadcasting Network (TBN).

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE

3


Habari

JUMApili AGOSTI 16-31, 2020

4

BARAZA LA MAASKOFU T.A.G WAMTUNUKU RAIS JPM TUZO YA MAPAMBANO DHIDI YA CORONA. NA MWANDISHI WETU.

B

araza Kuu la Kanisa la Tanzania Assemblies of God limemtunukia tuzo ya heshima Rais John Magufuli ya kutambua mchango wake katika uongozi imara kwa taifa na kwa imani kwa Mungu katika kuliongoza taifa kupambana na janga la Corona.

Askofu Mtakambali amesema kuwa uamuzi wa Rais Magufuli kutokufungia wananchi ndani wakati wa janga la Corona na kuelekeza katika kumtegemea Mungu umeliweka Taifa kwenye nafasi ya kipekee.

ho na pia kuliwezesha Taifa kutoyumba kiuchumi jambo hili limegusa sana baraza hili tunaomba Mungu akubariki sana na sana kwa kumtanguliza yeye katika uongozi wa taifa letu”amesema Askofu Mtakambali. Aidha kwenye hotuba ya Rais Magufuli, aliwaasa T.A.G kutengeneza viwanda badala ya kubaki tu kwenye shule maana hapatakuwepo

mwizi wa misumari maana atakemewa na kuanguka. Pia aliwashukuru sana kumpa tuzo ingawa Rais anasema haikumstahili yeye. “Hii Tuzo ambayo Baraza Kuu la TAG mmenipa haikunisitahili mimi, ni ya Mungu aliyetujalia kutokomeza corona baada ya Watanzania wote kumuomba, palipo Mungu hakuna kinachoshindikana, ila kiukweli nashukuru kwa zawadi hii na imeni-

gusa sana” Alisema JPM. “Nilipopata mwaliko wa kuja kuzungumza kwenye Baraza Kuu la TAG kiukweli nilijiuliza sana, nikasema mimi ni nani?, nilitaka kuwa Padri nikashindwa leo nitaongea nini mbele ya Maaskofu,lakini nilimuomba Mungu nipate cha kusema na nimepata kitabu cha historia ya Kanisa hili TZ” Aliongeza Rais JPM

”Uamuzi wako wa kutowafungua watu ndani na badala yake kuwaelekeza wafanye kazi na wamtafute Mungu wao kwa bidii ambaye ndiyo jawabu la kweli la mambo yote umeliweka Taifa katika nafasi ya peke sana duniani” amesema Askofu Mtakambali ”Katika kumtegemea Mungu kwenye medani za kiro-

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


afya YA MWANAMKE 5

JUMApili AGOSTI 16-31, 2020

MAAMBUKIZI YA FANGASI SUGU NA INAYOJIRUDIA RUDIA - VYANZO NA KINGA - SEHEMU YA PILI NA MSHAURI BABRA.

MATIBABU YA FANGASI SUGU NA MUWASHO SEHEMU ZA SIRI.

SULUHISHO LA WENGI. Watu wengi wanapokuwa na Fangasi Sugu huenda hospital au duka la dawa na kupewa antibiotics ambazo uwa kawaida upelekea kutuliza tatizo na Siyo kutibu na hatimaye huenda kuua bakteria wazuri na matokeo yake baada ya muda upelekea tatizo kubwa zaidi ambalo ni PID ( maambukizi Kwenye via vya Uzazi). Na ikifika hatua hii upelekea Mirija ya uzazi kujaa Maji au kuziba, matatizo ya hormones, na mwisho upelekea tatizo la UGUMBA, Kama utakuwa umechelewa kupata Tiba sahihi mapema. Na ndio sababu kubwa moja wapo ya wanawake wengi kwa sasa kupata tatizo la ugumba.

ININE WASH. FEMININE WASH Hii huwa inafahamika kama mkombozi wa wanawake kwa maambukizi ya sehemu za siri. Imeandaliwa maalum kwa ajili ya wanawake Imetengenezwa kwa vyakula,mimea na madini na viua sumu mwilini. Inamadini yanayohuisha uke na kuwa na ulinzi asilia,inaviua sumu vinavyozuia uke kuzeeka(mashavu),uke uliolegea, Ina mafuta mazuri yanaitwa essential oil kwa ajili ya kufanya uke urudishe mnato wake wa asili.

Faida ambazo Mwanamke anazipata unapotumia FEMININEWASH ni:• Huondoa harufu mbaya ukeni • Huondoa bacteria wabaya na kuzuia U.T.I SULUHISHO LA KUDUMU. • Huondoa fangasi na miwasho ukeni Kama una tatizo la fangasi inayojirudia mara kwa mara njia ambayo • Hurudisha size nzuri ya uke itakusaidia na ni ambayo imekuwa • Huondoa maji maji yatokayo ukeni yenye Harufu mbaya mkombozi na msaada mkubwa • Huondoa maumivu wakati wa kwa wanawake wengi ni kupitia tendo la ndoa SUPPLEMENT,Hii ni njia ya asili ya • Hufanya mwanamke kujiamini kutibu tatizo ili la fangasi sugu na muda wote muwasho ukeni na kuondokana na • Huzibua mirija ya uzazi hivyo tatizo ili kabisa, haijalishi tatizo lina kusaidia wenye shida ya kutomuda gani, na pia ni njia ambayo shika mimba haina kemikali yoyote ndani yake • Humkinga mwanamke na na hivyo ni njia salama zaidi kiafya maambukizi mabaya hasa U.T.I ambayo ninakushauri. kwenye vyoo, kemikali za swimming pool, maambukizi MabaMambo ya muhimu kufahamu ya kutoka kwa mwanaume. n.k kuhusiana na Tiba lishe hii ya FEM-

Mwisho kabisa napenda kushauri wanawake wote uwe unaumwa au huumwi hii supplement ni vizuri kuwa nayo ndani itakusaidia kwenye mazingira usiotegemea.

USHAURI. Unapaswa mwanamke usijioshee ndani ya uke wako kwa kutumia vidole vyenye kucha ndefu na kutoweka marashi au sabuni za chemical kwa ajili ya kuondoa harufu mbaya ukeni, maana kwa kufanya hivyo zaidi huuwa bacteria wazuri na kuwaacha wale wabaya. Na pia kutumia dawa bila ushauri kutoka kwa daktari ni hatari kwa afya yako pia kwani kuna wengine wanatumia dawa za kuweka ukeni na baada ya muda ujikuta uchafu unaanza kutoka na mwisho wa siku tatizo uwa kubwa zaidi na ndipo pia kupata PID Tunapatikana Mikocheni , Dar Es salaam Tanzania, na Kama upo mkoani unaweza kupata huduma zetu kwa kuwasiliana nasi kupitia namba zetu za simu/ WhatsApp +255 757 519 313 ili kupata ushauri na msaada zaidi. Karibuni sana.

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


MSANII WETU

JUMApili AGOSTI 16-31, 2020

NA MWANDISHI WETU Ni mara ngapi, tumeweka macho kwa watu wenye nguvu, nafasi, upako, ujuzi, elimu n.k na kusahau hao wote, mwisho wa siku wanamtegemea Mungu yule yule tunaemtumainia? Nielewe Jambo Moja Huruma za Mungu zitatupata pale tulipo, yaani hivyohivyo hata Kama ndio upo kwenye kifungo, una mapungufu, unataabika, u mgonjwa au unashindana na umasikini.

6

Sio mapenzi ya Mungu kukuona unataabika miaka yote

Hapo hapo ulipo Mungu anaweza kukutana na wewe kupitia njia yoyote Ile. Nakusihi ondoa macho katika njia, wengine wanafanikiwa, muangalie Mungu Yeye ana mpango kazi kwa ajili ya kila mmoja kwa jinsi alivyo. Macho yetu yasipokuwa katika mambo sahihi, tunacheleweshwa, tunakwamishwa, tunaibiwa, tunaonewa na hilo sio fungu letu. Zinduka tafadhali, mwambie Mungu leo natoa macho katika hayo yote. Daudi akasema, Nitainua macho yangu nitazame Milima, Msaada wangu u katika Bwana aliyeziumba mbingu na Nchi. Daudi aliijua siri, Watu wanakuja na kuondoka, vitu vinakuja na kuondoka , hata watoto tulionao siku moja na wao wataanza maisha yao. Lakini Mungu! Milele na milele yupo na sisi. Karibu kuliko hata nguo tulizovaa. Geuza macho tafadhali. YESU ALIPOONGEA na aliepooza akaanza kutoa maelezo ya jinsi ambavyo imekuwa tangu awe hapo. Masikini ya Mungu, adui akampofusha hata asijue yupo na nani. Nakuombea Leo kwa huruma za Mungu, kwamba inawezekana umepooza kimaombi, kiimani, kihuduma, kimahusiano, malezi, kazi na kwa kuwa umepitia Jambo Fulani kwa muda mrefu ambalo limesimama Kama mwiba maishani. Roho wa Mungu leo akupe nguvu ya kugeuka. Geuka kabisa kabisa na umwangalie Mungu anakuelekeza nini ili usiendelee kuwa hapo.

SIO MAPENZI YA MUNGU KUKUONA UNATAABIKA MIAKA YOTE. Kwa Kila Jambo Kuna majira na nyakati, taabu huwa zinaisha, ikikaa Sana, Kuna sababu, Muulize Mungu maswali. Amesema

MSANII WA INJILI

#AngelBenardwaGodsave #MsaniiWetuLeoZamuYangu

njooni tusemezane. Na ukisikia majibu usifanye ujinga wa kuanza mijadala, piga hatua. Mungu hajashindwa kutenda, na anaweza kukukuta ulipo. Ondoa macho kwenye lolote lile, weka kwa Mungu. Na ukielekezwa. Tii kwa

uaminifu. Uponyaji wako unaweza usiwe kwa kutumbukia kwenye birika kama wengine. Majibu yako yanaweza kuwa kinywani mwa anaekuuliza, Kwa Nini upo hapa? Usimdharau mtu, hujui aliekubebea muujiza wako.

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


Habari/TANGAZO 7

JUMApili AGOSTI 16-31, 2020

NA MWANDISHI WETU, NAIROBI

B

wana Yesu asifiwe mpendwa msomaji wetu, wiki hii mwanzoni kabisa mwimbaji wa muziki wa injili nchini Kenya Evelyn Wanjiru alipata furaha ambayo hakuitegemea baada ya mashabiki wake kumfikishia wapendwa lakini tano katika albamu yake ya MUNGU MKUU. Alifurahi sana maana hakutegemea na Boomplay Kenya walimkaribisha katika ofisi zao zilizopo jijini Nairobi kwenda kujinyakulia zawadi yake. Kutoka moyoni mwake aliyasema haya...

EVELYN WANJIRU APAGAWISHWA NA BOOMPLAY KENYA.

Asanteni marafiki kwa kuniamini na zawadi hii Mungu aliyoweka ndani yangu na kwa MUNGU MKUU ALBAMU, 500,000k na wanaonifuatilia kwa Boomplay. Upendo wenu ni wa ajabu sana. Asanteni sana BoomplayKe pia record label yangu Bwenieve na uongozi wote kwa kazi nzuri pamoja nami. Mungu awabariki sana, endeleeni kufanya zaidi. Alisema Everlyn

NYOTA SHINE EVERYWHERE WAKATA KEKI KIBABE

NA MWANDISHI WETU UIMBAJI wa nyimbo za injili nchini Tanzania Bahati Simwiche, ambaye pia ni muanzilishi wa brand ya Nyota Shine Everywhere anatarajia kufanya maadhimisho ya kumbukumbu ya kuanzishwa kwa brand yake ya Nyota Shine.

M

Mbali na brand iliyoanzishwa pia mkali huyo wa injili ana kundi kubwa la Whatsapp ambalo limekuwa msaada kwa waimbaji na wahubiri wengi

ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Sherehe hizi zitafanyika tarehe 30 agosti mwaka huu katika kanisa la Calvary Celebration Center, lililopo Tabata Segerea katika kituo cha Chama au kwa Mchungaji Bahati Bukuku. Ibada itaanza saa 3 asubuhi mpaka saa 12 jioni. Waimbaji nguli wa muziki wa injili watakuwepo kumtukuza Mungu siku hiyo. Wote mnakaribishwa

TUNAPOKEA MATANGAZO NA KUYATANGAZA BURE KUPITIA GAZETI LETU. KARIBU SANA ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


MAKALA YA WANAUME 8

JUMApili AGOSTI 16-31, 2020

NONDO TANO ZA KIUME KUTOKA MEN AT WORK GLOBAL

NA BROWN M. ARUSHA

awake hujiweka wazi zaidi ili kusababisha akili ya Mwanaume ifikiri na itake Ngono. Ngono ni mtumishi mwema lakini ni bwana mharibifu. Uamuzi wa Mwanaume juu ya namna anavyoshiriki Ngono ndio huamua iwe Mtumishi mwema au kuwa bwana 2. Akili na Macho ya mharibifu. Mwanaume ni viungo vikubwa sana vya 3. Mwanaume bora ni Baba anayetambua Ngono. Wanaume huvutiwa kwa kile waumuhimu wa kucheza nachokiona na wanna watoto wake. Ha1. Wanaume wengi tumetekwa na maadui ambao ni tabia zetu za uvivu, ubabe, ubinafsi na majivuno. Na ndio maana ushujaa wetu hauonekani wala hausemwi sana na watoto wetu, familia na jamii.

ovunjika”. Baba ni mtu chezi kama Baba mtu muhimu sana katika mzima bali anacheza kama mtoto na anajua maisha ya mwanaume kwani anapaswa mbinu ya kuruhusu watoto washinde ili kurithisha #Uanaume kuwaongezea watoto kwenda kwa mwanae wa kiume. wake ujasiri wa kushinda vikwazo mbalimbali kwenye maisha 5. Mwanaume Bora anayao. jua kuwa kutunza mahusiano yake na watu wake, familia na jamii 4. Mwandishi Ken Canfield anaandika “Wani gharama ambayo ana wajibu wa kuhakinaume, walioharibiwa na Baba zao, wanakisha anayalinda kwa gharama zozote zile. warithisha wana wao wa kiume pembe iliy-

MASOMO ZAIDI YA WANAUME YANAPTIKANA KATIKA AKAUNTI YETU YA YOUTUBE YA MEN AT WORK GLOBAL. KARIBU SANA, PIA TUNAOMBA MJULISHE MWANAUME. ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


makala/ Habari

JUMApili AGOSTI 16-31, 2020

MAJIRA NA NYAKATI - 8 MWL MWAKASEGE,

ASKOFU GWAJIMA WAFUNGA BAADHI YA AKAUNTI ZA YOUTUBE ZENYE MASOMO YAO.

NA HELLEN SOGIA, PWANI 1. WAKATI. 2. MAJIRA YALIYOAMRIWA. 3. MAJIRA KWA WAKATI ULIOAMRIWA 4. NINI KILICHO MBELE YAKO. Nyakati zote hizi nne ni muhimu katika maisha yetu sisi, ambao bado tunaishi hapa duniani, Ili kumpatia mtu urahisi wa kutambua mwendo wake, katika kuishi na kutenda, anapokuwa akingali kuishi hapa duniani. Hii itamsaidia mtu kuweza kutambua, nini afanye na wakati gani afanye nini. Majira na Nyakati inapompita mtu kimaisha bila ya yeye kutambua, ndipo hapo hubeba kikapu kwenda shambani kwa ajili ya kuvuna hali wakati huo ni majira ya kulima. Mhubiri 3:2-8. • Wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa. Wakati wa kupanda na wakati wa kung’oa yaliyopandwa. • Wakati wa kuua na wakati wa kupoza. Wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga. • Wakati wa kulia na wakati wa kucheka. Wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza. • Wakati wa kutupa mawe na wakati wa kukusanya mawe. Wakati wa kukumbatia na wakati wa kutokumbatia. • Wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza. Wakati wa kuweka na wakati wa kutupa • Wakati wa kurarua na wakati wa kushona. Wakati wa kunyamaza na wakati wa kunena. • Wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia. Wakati wa vita na wakati wa amani. Kufanya kitu chochote kinyume na majira ya kitu hicho.Hii humletea mtu mate

“WAMILIKI WALIA, TUMEFUTA VIDEO ZENU ZOTE, MTUSAMEHE”

NA MWANDISHI WETU

gemeo hewa. Hapa ndio pale mtu hutumia nguvu nyingi katika kufanya jambo bila ya kupata matokeo mazuri. Hili limekuwa ni tatizo kubwa sana Leo hii, katika maisha ya watu wengi, pia hali hii imetukumba wengi na kutusababisha tukabaki katika eneo moja, tukifanya kitu kile kile kimoja kwa muda mrefu sana (tunapiga mark time) bila kuona matokeo mazuri, au bila kuona matokeo yeyote ile. Majira ya Mungu kwa mwanadamu ndio sawa kwetu, Majira ya kibinadamu humpotezea mtu muda na kumtoa mtu kwenye kusudi la kuumbwa kwake, na ukweli ni kwamba, mwanadamu anapokuwa nje ya mpango wa Mungu juu ya maisha yake, Kamwe hataweza kufika kwenye hatma yake iliyo ndani ya mpango wake Mungu katika lile kusudi, la kuumbwa Kwake. Pamoja na kwamba utaonekana katika macho ya kibinadamu, hapa duniani mtu anaweza kuonekana amefanikiwa sana. Ukweli ni kwamba, kusudi lililobeba hatma ya maisha yetu, kipimo chake hakipo kwenye mafanikio ya kimwili. Mtu anaweza akawa amefanikiwa nje ya mpango wa Mungu, maana shetani pia, humfanikisha mtu, lakini! Mtu huyu, akaikosa hatma yake. Mpendwa msomaji itaendelea katika toleo lijalo, Usikose!!

W

amiliki wa akaunti za Youtube ambao walikuwa na kawaida ya kuwawekea wapendwa wao masomo mbalimbali ya Mwl Mwakasege au ya Askofu Gwajima, sasa hawana amani kutokana na doria kubwa sana inayoendeshwa na IT wa viongozi hawa, kuhakikisha masomo yaliyopo katika mitandao ni yale yenye uhakika na ubora wa kimataifa tu. Mwezi mei mwaka huu katika Mwl Mwakasege katika moja ya semina zake alizokuwa anafanya kila mwisho wa mwezi, alisikika akiwaeleza wale wote ambao wamefungua vikundi vya facebook kwa jina la Diana & Christopher Mwakasege (MANA) wavifute, kwa sababu yeye binafsi havitambui. Aliweza kumtaja mmoja wa viongozi wa group mojawapo (jina tunalihifadhi) na kusema alimpigia simu akaongea naye kwa ufasaha kabisa ili afute na asiendelee kuwaaminisha watu kuwa hilo group ni la MANA. Aidha alisema kuwa anataka kila mmoja ambaye anahitaji kufanya jambo lolote linalohusu huduma za Mwl C. Mwakasege afuate utaratibu uliopo ili awe huru kufanya kile anachotakiwa kufanya kwa utaratibu mzuri. Tukigeukia upande wa Youtube watendakazi pamoja nao wameanza kufanya kazi ya ku-

toa masomo yote yanayowahusu kwa kuwataarifu youtube kuwa wenye hati miliki ni wao. (Strikes Copyright) Chaneli nyingi sana kufikia leo zimefungwa na nyingine zitafungwa, cha muhimu ni kufuta video zote ambazo hazikuhusu na hiyo ndio itakuwa salama yako. Moja kati chaneli zilizoathirika kiasi ni DMENDTV ambao baada ya kuona hilo walifuta video zao zote na kubaki na Copyright strikes ambayo itaisha muda wake baada ya miezi mitatu. “Tunaomba mtusaidie kufuta copyright strike katika chaneli yetu ya dmend tv. Lengo letu sio baya ilikua ni nia njema, kama isemavyo injili tuhubiri popote na kulitangaza neno la Bwana. Kama mtumishi unavyo fahamu kuwa Youtube ni mtandao wenye matumizi tofauti hata kueneza injili unasaidia. Wala si mtandao unao mnufaisha sana mtu awekapo nakala zake, bali kwa mapenzi mema tuliweka moja ya video zenye sauti na picha za Mwl Mwakasege ili kusambaza injili wala sio kuuza injili na tunakiri kosa sababu mlikua hamjafungua rasmi channel ili kuwafikia watu wengi zaidi, hivyo tulipata nafasi ya kuhudhuria semina zenu tukarekodi kama waandishi na kuziweka Youtube. Pia tumesha futa video zote na tunaomba msaada zaidi kufuta copyright strike katika chaneli yetu.” Dmendtv

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE

9


MAHOJIANO / NYOTA

JUMApili AGOSTI 16-31, 2020

10

MIMI NI DARASA LA SABA FELIA | MSANII WA BONGO MUVI KIMLOLA KIMLOLA. NA MWANDISHI WETU

S

halom ndugu zetu mnaofuatilia ukurasa huu makini sana wa “NYOTA WA SIKU” Leo tupo na Kimlola Ahmad KImlola msanii wa nyimbo za injili na filamu za bongo. Karibu usikie machache kutoka kwake. Amezaliwa katika familia ya kiislam na kikristo, Baba akiwa muislam na mama akiwa mkristo. Anaishi Dar ila wazazi wake wapo Mpwapwa Dodoma. Twende pamoja sasa. SWALI: Una kiwango gani cha elimu? KIMLOLA: Mimi ni darasa la saba falia, first selection na second selection sikuwepo.

SWALI: Ilikuwaje wewe ukafuata upande wa mama kidini? KIMLOLA: Kiukweli niliamua binafsi kuokoka lakini zamani nilikuwa napelekwa madrasa au misingi ya kiislamu sikuwahi kuvielewa ila nilipokutana na watumishi wa Mungu nilijikuta naokoka tu.

wewe kuona umefeli shule? KIMLOLA: Baada ya mimi kufeli na kwa sababu nilikuwa naishi na mjomba wangu, maisha yalibadilika hivyo tukatawanyika, mimi nilienda kuishi na dada yangu ambaye alikuwa amepanga chumba kimoja vingunguti na ikatulazimu tuishi mimi, dada, mume wa dada na mtoto wao chumba kimoja. Baadae nilipata kazi kwa mtu tena kazi za ndani (Houseboy) huku naishi kwa dada yangu ambayo nilikuwa nalipwa elfu 15. SWALI: Ulifikaje katika sanaa ya uigizaji? KIMLOLA: Nimepitia sehemu nyingi ila KAOLE SANAA GROUP ndipo paliponitoa na niliunganishwa na mwandishi wa habari aliyekuwa anafanya kazi ITV, ndugu Alfred Mtoyi ambaye alifia Uingereza.

SWALI: Muimbaji gani alikuwa anakuvutia sana katika injili? KIMLOLA: Waimbaji niliokuwa nawapenda sana, sio mmoja ni Ambwene Mwasongwe, Chidumule na Bony Mwaitege nilikuwa nawapenda sana kabla sijaanza kuimba. SWALI: Mbali na uimbaji, sanaa ya bongo nini kingine unachojishughulisha nacho? KIMLOLA: Mimi ni muhubiri, nilikuwa naona mapepo yanavyotesa watu na wanavyopata shida ndipo nilipojua kuwa Mungu ananipitisha katika uimbaji ila lengo ni kuhubiri. Nilipofahamu hilo, nilimuomba Mungu anipe eneo la kufanyia kilicho ndani yangu na mwaka 2017 Mungu alinipa eneo kubwa sana karibia heka nzima, ningekuwa na haraka ningekuwa nimeshafungua huduma lakini ilinibidi niende kuongeza

ufahamu zaidi na kuendelea kunyenyekea ili nipate mafuta zaidi, ndio maana nikaamua kwenda kuchukua certificate, diploma na sasa natarajia kupata digrii ya kwanza ya uchungaji mwezi novemba jijini Arusha. SWALI: Kuna muimbaji mmoja nilimtafuta tuende kwenye huduma akaniuliza wanatoa kiasi gani, je wewe huwa unachaji kiasi gani? KIMLOLA: Ukishaona muimbaji anaalikwa mahali kisha anaweka fedha mbele na kukusumbua umtumie hiyo fedha, ujue kabisa wito wa huyo muimbaji ni wa mashaka. Biblia inasema “Vya kwangu nimetoa bure, na ewe nenda katoe bure” hivyo kwenye upande wa huduma nenda katumike utakachopewa pokea, usiweke kiasi cha fedha. TUKUTANE TOLEO LIJALO...

SWALI: Ugumu gani huwa unaupata katika huduma yako? KIMLOLA: Kiukweli changamoto ni nyingi, mfano unaweza kualikwa kwenye huduma ila unapoamka asubuhi ukakuta gari haina mafuta hivyo unaenda ukitarajia unaweza pata chochote lakini mchungaji anakuambia UBARIKIWE SANA MTUMISHI, kitu kinachopelekea kuanza kutafuta msaada kwa ndugu, jamaa na marafiki. SWALI: Maisha ya wokovu yalikuwaje baada ya kuokoka na upande wa familia je? KIMLOLA: Tangu niamue kuokoka katika familia yangu hakukuwa na ugumu wowote kitu kilichopelekea mpaka kufikia sasa watu wanne wameokoka kupitia mimi katika familia yetu, hivyo mimi nimekuwa lango la wao pia kuokoka. SWALI: Ilikuwaje baada ya

ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


Makala M0t0 Ulao

JUMApili AGOSTI 16-31, 2020

11

YUPO YESU MTULIZA DHORUBA

NA MCH. IMANI O. KATANA

M

pendwa msomaji wangu ninakusalimu katika Jina la YESU ,karibu sana katika Makala ya wi ki hili, fungua pamoja nami kitabu cha Marko 4:39 • “Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari”

Tukianzia mstari wa 36 tunaona wanafunzi wakianza safari pamoja na YESU baada ya siku nzima ya huduma na miujiza mikuu wanaanza safari ya kuvuka. Lakini ghafla dhoruba kubwa inapiga chombo na kutishia maisha ya wanafunzi na wanaanza kuogopa. HAPA LAZIMA UJUE KWAMBA WAKATI WOWOTE UN-

APOAMUA KUVUKA LAZIMA UKUTANE NA DHORUBA, NA PIA SIO KWAMBA UNAPOKUWA NA YESU DHORUBA HAZITAKUPIGA. Dhoruba zitapiga chombo chako ila habari njema ni kwamba hautaangamia kwa maana imeandikwa ili kila mtu amwaminiye asipotee bai awe na uzima wa milele na tena. Isaya 43:2 Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.Kila aaminiye lazima ajue uwapo na YESU YUKO SALAMA.

Biblia inasema lakini YEYE alikuwa amelala usingizi wakati kukiwa na dhoruba kubwa. Hapa inatujulisha kuwa kama ukimuamini MUNGU wakati wa dhoruba hutakiwi kukosa usingizi bali uwe kama mtoto mdogo ambaye akirushwa juu na wazazi wake anacheka maana anajua lazima watanidaka tena. Lakini wengi wanakuwa na wasiwasi wakijua kuwa MUNGU hawaoni wanaanza kulaumu Mbona mimi natoa fungu la kumi lakini dhoruba inanipiga, usilalamike yakupasa kuiga mfano wake YESU yeye wakati kuna dho-

ruba kali alikuwa analala.

MUNGU ANAPOKUWA KIMYA SIO KAMA HAKUONI! Wakati wa dhoruba MUNGU huwa anakuwa kimya, ndio maana ni muhimu sana kujaa NENO LA MUNGU ili liweze kuwa msaada unapokuwa unapitia wakati wa dhoruba. Wakolosai 3:16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Hili NENO likijaa ndani yako litakusaidia uweze kushinda na kuvuka salama wakati wa dhoruba yako. Jamani unapokuwa na shida kwenda kwa mtu kuomba akusaidie baada ya kumaliza kumuambia anakuwa amekaa kimya, hicho kimya chake hakina maana amedaharau akini yamkini anatafakari namna ya kukusaidia na akiisha kutafakari atakupa jibu na msaada unaouhitaji. Ni suala la muda tu, muda ulipofika maandiko yanasema akainuka akaukemea upepo, na upepo ukakaoma kukawa

na shwari kuu. Wakahamaki kwa sababu walijua YESU anaweza kwa magonjwa na kufufua tu hawakuwahi kuwaza kwamba hata upepo na dhoruba vyaweza kumtiii. Napenda kukupa moyo kwamba YESU ANAWEZA YOTE HATA KATIKA DHORUBA UNAYOPITIA YESU ANAWEZA, dhoruba ya kukosa kazi, kutenda dhambi, magonjwa, kuonewa, kusingiziwa, kukataliwa, kunyanyaswa, kunenewa vibaya NASEMA KWA JINA LA YESU NAIKEMEA DHORUBA HIYO NA IWE SHWARI KUU KATIKA MAISHA YAKO. Karibu moto ulao online church ,Mchungaji Katana nitakufundisha na kukulea kiroho. Kupitia Whatsapp, tuma neno moto ulao kwenda namba 0752352116 utatumiwa fomu ya kujaza ili kuwa msharika wa Madhabahu ya Moto Ulao. Kwa MAOMBI, MAOMBEZI na SADAKA waweza kutuma kwa namba ya mpesa 0752 352 116. Mungu awabariki sana. Mwinjilist Imani O. Katana Whatsapp +255 752 352 116 katanaimani@gmail.com

TUNAPOKEA HABARI NA MATANGAZO MBALIMBALI, WASILIANA NASI KWA FAIDA YA WENGI ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


HABAKUKI 2:1-2

MCHEZO WA NDONDI

ISSN 2714-2108: Toleo Na.011. Jumapili Agosti 16-31, 2020

TETESI ZA USAJILI SOKA LA ULAYA Manchester United iko tayari kutoa ofa kwa kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, 25, anayesemekana kuwa thamani yake ni pauni milioni 70 ya mkataba wa muda mrefu wa pauni 150,000 kwa wiki ili kumsajili mchezaji huyo kutoka Atletico Madrid msimu huu.

HASSAN MWAKINYO BINGWA NDONDI WA mkanda wa Dunia wa WBF. NA MWANDISHI WETU

H

ASSAN Mwakinyo, bondia wa ngumi za kulipwa Mtanzania anayeipeperusha vema Bendera ya Taifa kwenye ndondi, usiku wa kuamkia jumamosi amemnyoosha kwa pointi Tshibangu Kayembe raia wa DRCongo. Mwakinyo ameshinda kwa pointi pambano hilo la raundi 12 la uzito wa Super Welter katika kuwania mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBF. Mabondia hao walionekana kukamiana na kushushiana makwenzi mazito na makali katika

pambano hilo lililofanyika Ukumbi wa Mlimani City Dar na kuhudhuriwa na wadau wengi. Baada ya ushindi huo mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza alimvalisha Mwakinyo mkanda huo na kumtawaza Ubingwa mpya wa mkanda huo wa WBF.

Mlinda lango wa Arsenal Emiliano Martinez anasema vilabu 10 Ulaya vimeonesha nia ya kumsajili baada ya mchezaji huyo, 27, raia wa Argentine kuonesha mchezo wa kuridhisha kuelekea mwisho wa msimu Matumaini ya Chelsea kumsajili mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak, 27, yameimarika huku klabu ya La Liga ikisemekana kuwa makini kutafuta mbadala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Slovenia. Lille imekataa ofa ya euro milioni 20 euro kutoka kwa Everton kwa ajili ya mlinzi Gabriel, 22, kwasababu wana makubaliano ya kumuuza mchezaji huyo kwa Napoli, licha ya Arsenal na Manchester United pia kuonesha nia ya kutaka kumsajili raia huyo wa Brazil.

Waziri Shonza amesema anampongeza Mwakinyo kwa kuutetea mkanda huo uliopambaniwa nyumbani na kuiletea nchi sifa.

TANGAZA NASI MATANGAZO MBALIMBALI UONE FAIDA NA NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII ZAMU YANGU PROJECT / ZAMUYANGU MAGAZINE


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.