SIMULIZI: AMIGERY (I FALL FOR YOU)
MTUNZI: SIMULIZI ZA SUMMY
WHATSAPP: 0624853116
SEHEMU YA: 01-35
Sehemu ya 01
Msisahau mwandishi halali wa simulizi
hii ni Sumaiya Mwendo, Simulizi za
Summy . Epuka matapelii.
Utangulizi…..
Maisha halisi ya binadamu yanajengwa
na binadamu mwenyewe, Maisha mazuri
yanajengwa na uzuri wenyewe, nguvu
pamoja na mafanikio ya mtu Ni juhudi
zake mwenyewe. Dahh!! Sijui nawaza nini? Njaa hii’
Ok mmekuja hapa kwa ajiri ya kumfahamu mengi juu ya AMIGERY.
Kwa nini AMIGERY labda?. Yaani kirefu
cha AMIGERY nitawafahamisha mapema au baadae, na kwa nini aseme I fall for you? Ni juu yenu Sasa kua pamoja
nami. Ila acha nijitambulishe kwenza.
Kwa jina naitwa Amina, watu wengi
Sana wanapenda kuniita Ami yaani ndo
hivyo wanapenda kuniita Ami. Leo
nimeamua kuwaletea mkasa wangu wa
Maisha ambao najua kabisa
utawafurahisha. Utawahuzunisha na
kuwasisimua sanaaaa. Ila kubwa zaidi
utawafunza vya kutosha. Tena kwa
sababu kalamu namkabidhi rafiki yangu
mwenyewe, Chanda na kidole, ayaa!! Eti
Chanda na kidole? Ni chanda na Pete
#Simulizi za Sumaiya. Natumai Sana
mtainjoi. Sitawaambia Ni kitu gani
kimesababisha Hadi nimeamua kukaa
nae chini niwaeleze mkasa wangu. Ila tu
kila mmoja atege sikio na akili Yake
aielekeze kwangu msimuliaji, huku
umakini akimpatia MWANDISHI wake
#Simulizi za Sumaiya.
Anza……
Ni miaka kadhaa nyuma imepita, nilikua
kidato Cha sita, katika mkoa wa
morogoro. Nilikua nasoma shule ya
wasichana tupu. Siku moja Majira ya saa nne na nusu siku ya jumamosi
kengele ya kantini iligonga ishara
wanafunzi wote tujikusanye kwa ajiri ya
kupata chai. Siku hiyo haikua siku ya
chai uliandaliwa uji kwa ajiri yetu. Kwa
kweli maishani mwangu Mimi sipendi uji
kabisa yaani.
“ Twende Basi” rafiki yangu Miracle
aliniambia kwa msisitizo tukapate uji
huo ambao kwenye moyo wangu ulikua
chukizo kila nilipouwaza.
“ Mmh hapana, Mira, mi sipendi huko
unajua kabisa Mimi na uji mbalimbali”
nilimwambia akatamani anichambe
maana Mira kwa machambo hajambo.
Ila siku hiyo sijui roho ya kiungu
ilimshukia, aliweza tu kutikisa kichwa
kwa masikitiko makubwa Kisha
akaondoka zake.
Nilishukuru Mungu na kuendelea kukaa
kwenye gogo lililokua limeanguka muda
mrefu’. Punde baada ya wanafunzi wote
kuelekea kantini, nilijikuta pekee yangu
kwenye maeneo ya nje. Daahh!! “
Kruuol” mhh! Tumbo liliunguruma ishara
Ni kwamba Hali yangu ni tete na sio
mchezo. Nina hisia njaa. Nifanye nini
Sasa? Kwa kweli uji haupo akili.
Niliweza kukumbuka Jambo wakati huo
huo. Nilipokumbuka Mara moja na
haraka niliinuka kutoka chini Kisha
mapema Sana nikawahi kwenda nyuma ya madarasa yetu ambayo tulikua
tukisomea. Huko kulikua na uwazi
ambao wasichana wapenda disco na kulala nje ya shule walizoea kupita, mtoto wa kike na Mimi siku hiyo nikajitosa na kupita eneo Hilo nikiwa na wasiwasi hatari sijawahi kutoroka
mwenzenu Mimi! Na ilikua weekend, imagine watu hutoroka siku za shule na kurejea Ila Mimi natoroka mchana na sio siku ya shule Ila naogopa hatari.
Hatimae nikifanikiwa kuoenya kwenye
fensi ya wavu bila kukamatwa na mlinzi
yeyote. Taratiiibu nikawa natembea
kuelekea kutafuta chochote kitu ili Nile
Ami wenu. Huko nilikutana na watoto
Wana kula icecream nikawa
nawatamania tu. Mara nikaona watu
wanauza ndizi. Eee! Sio Nile ndizi
nipoze njaa’ nikawasimamiaha wakatua
beseni la ndizi mbele yangu. “Shing ngap? “ Niliwahoji wauzaji
“ Mia Mia tu” walipotaja hiyo Bei wee, mtoto wa watu na njaa yangu
nikachuiua ndizi mbili na kumenya Kisha
nikaanza kula. Daah Maisha haya
wakati wote huo najua kabisa nina pesa
kwenye mfuko wa sketi. Baada ya kula
Sasa nikashika mfukoni niwapatie pesa
Yao.
‘ la haula, Sina hela’ nilishtuka
mwenzenu, Sasa hapa ntafanya nini?
Nitawaambia nini Hawa wauza ndizi?
“ Dada Kama unalipia lipia tuendelee na biashara jua Kali” muuza ndizi ambae
nilichukua ndizi kwake akaniambia
nikabaki hoi! Sijui nifanye nini? Hata
sikumbuki pesa nilikua nimeweka wapi
mwenzenu?
“ Dada vipi?” Yule mwenzake pia
akauliza.
“ Usitake kusema huna hela, Maisha
yenyewe haya umetusimamisha hapa
muda mrefu’ Sana, alafu usitume pesa
na ndizi umekula kwa kweli
patachimbika” niliekula ndizi zake
akachachamaa. Ningefanya nini zaidi ya kuwatolea macho ya huruma.
“ We wa kusoma umewahi kupigwa wewe?” Haa Mambo ya kupigana Tena.
“ Jamani mnisamehe sio Kama sikua na hela nilikua nayo kabisa elfu moja, Ila nashangaa siioni humu, sijui nimeiweka wapi?” Nilianza kuhanya mtoto wa kike.
“ Usituigizie, yaani hapa hamna anae
kuelewa pesa utatoa tu” nikajikuta
tayari nimekamatwa Kora mwenzenu, nikaanza kuomba samahani, daah! Ni
bahati mbaya iliyoje ndo siku yangu ya
kwanza kutoroka na kutana na bahati
mbaya Mungu angesikia kilio changu
angemsaidia nisiumbuke Mimi?.
“ Jamani naombeni mnisamehe Ni
bahati mbaya Ila Kama hamtajari
naombeni muda niwaendelezee pesa yenu Kisha niwakute hapa hapa”
“ Ahaha, huyu dada ana wazimu, hivi upo form ngapi wewe?” Kwa Hilo swali
Ni kana kwamba walinidharau Sana.
Nilishindwa la kusema.
“ Jamani naombeni niwaletee”
“Unatuona sisi Ni wajinga Sana”
nilikosea la kusema.
“ Yaani utuache hapa tukae tusubiri
ukituchoresha eti utufatie pesa, ili
uende jumla, umechanganyikiwa wewe”
“ Jamani hamna mimi”
“ Paah!” Kofi lilitua kwenye uso wangu
nikajikuta nachanganyikiwa. Ile
wanajiandaa kunizaba Kofi jingine
niliinamisha uso wangu kwa huzuni mno, uso wenyewe huu mdogo masikini ya
Mungu. Nikiwa nimeinama ghafla
nikahisi kimya kimechukua nafasi Yake.
Nikashangaa na kufungua macho yangu
taratibu nijue nini tatizo mbona
nimenusurika.
“ Hamuoni aibu kumpiga msichana
mwenzenu, Tena mwanafunzi
barabarani, kwa sababu gani kubwa Hadi mfanye uonevu huu??” Sauti ya
kiume ulinifanya niinue uso wangu
kutazama Ni malaika gani huyo
alietumwa na Mungu kuja kuninusuru?
Maana nilikua kwenye hatua mbaya
Sana ya Maisha, kwa Hali ilivyokua
ilibaki kidogo tu nijichimbie kaburi
mwenyewe.
Nilipoinua uso wangu nikakutana na sura ya kijana ambae kamwe sikuwahi, Wala
sikua nimewahi kumuona popote pale
hapa ulimwengu, ilikua Mara yangu ya
kwanza kumuona huyo Kaka, alikua
amevaa suruali ya kitambaa ya rangi ya
kaki imemkaa vizuri Sana na Shati la mikono mirefu la dark blue, alionekana
Kama kijana anaejijari na kujitunza kwa
ujumla, usoni alivaa miwani. Kwa kweli
alionekana wa kuvutia kwa jinsi
alivyokua. Ana weupe flani hivi, yaani
sio mweupe Sanaa Ila Ni mweupe,
aliongea kwa hasira lakini Ni Kama
alikua akitabasamu. Nilimuwekea macho ya huruma akiwa kaniangalia Kisha
akarejesha macho Yake kwa wale wasichana.
“ Mmefanya nini? Hamuoni Kama nyie
Ni wakubwa Sana kushinda yeye, amewaomba awaletee pesa yenu Ila
mmefanya kumpa adhabu isiyostahili”
alifoka hapo nikapata mwanya wa
kuwaponyoka wale wasichana na kujificha nyuma Yake.
Sehemu ya 02
” Usijar” aligeuka pembeni kidogo
alipotamka hilo neno. Daah nilihisi raha
kuona angalau nimepata shahrukhan wa kibongo.” Kaka tafadhari huyu dada
katufanyia kitu ambacho sio, ndizi shing
Mia Mia Ila ameshindwa kutupa pesa yetu eti Hana.”
“ Kwani nyie mnamdai sh ngap?”
Wakataja pesa Yao huyo Kaka akazama
akatoka na noti ya 2000 wakakata
pesa yao Kisha wakarejesha chenchi.
Wale wadada wakaniangalia na Mimi
nikawakodolea macho Kisha
nikawazomea kisiri Siri. Ahaha mi
mkorofi nyie acheni tu. Wale wadada
wakaishia kuniangalia bila neno. Baada ya hao dada wawili kuondoka kijana wa
watu ndo anigeukie Sasa. Uwiii material
yote ambayo nimesoma asubuhi hiyo
yalinitoka nik akili yangu. Yaani ki ufupi
kijana alijua kunivutia kana kwamba
aliungwa na mimi! Aibu hii mniache mie, ndo akili imehama hivyo.” Upo sawa”
aliniuliza kwa upole huku akisogeza
miwani yake’ vizuri. Nilitabazamu na kumjibu. “ Ndio, nipo sawa” nikatoa
sauti ya madeko kana kwamba nilikua
karibu kudondoka. “ Usijari kila kitu
kitakua sawa, waweza enda shule”
aliniambia hivyo nikajikuta nakumbuka
sijakula hata, nikatia sura yangu ya
huruma. Na wakati huo huo tumbo
likakoroma akajikuta amecheka mwenyewe. Anacheka kivivu mwenyewe.
Mi hoi.. jamani wa kusoma mnisamehe
mapenzi hayana mwanafunzi. “ Twende
ukale, alafu usirudie kutoroka shule
sawa mtoto mzuri” alipotamka hiyo kauli
nilipagawa mwenzenu, kweli Mimi Ni
mtoto mzuri? Nilimfata bhana uroho huu, mtu simjui nimekutana nae njiani tu. “ Mi Ni mgeni hapa, sio mwenyeji Sanaa, unaweza niongoza njia sehemu ambayo utakula?” Aliniuliza nikajikuta nainamisha macho yangu chini huku nikitabasamu. “ Ndio, nifate Mimi”
utadhani yeye ndo alikua na shida.
Bhana alinifata taratiibu mwendo mdogomdogo tukazama mgahawani
kabisaa. Aliingia mgahawani akiwa Kama
hajisikii Uhuru, Ila Mimi nilikua na tabasamu, nikaanza na kuchangamka hapo hapo. “ Mimi natamani kula
chapati na chai niagize?” Nilimwangalia
na macho yangu makubwa na mazuri, akabaki ameganda aliniangalia mwisho
akatabasamu kwa uvivu sana nikapata
aibu, kiukweli akitabasamu kivivu mi ananiacha hoi, anafanya nijione Kajol. “
Usijari, we agiza kila unachotaka kula”
aliposema hivyo mwenzenu nika faall in love jamani, kwa neno niagize
nachotaka. Kwani maneno hayo
nimezoea kuyasikia kwenye movie. Za
wakorea jamani ‘Oppa’ aii nimesemaje
Mimi? Sina aibu kabisa “ Mbona Kama
unaongea Mambo mengi Sana kwenye
kichwa Chako?” Aliniuliza swali la ukweli
kana kwamba aliisoma akili yangu vilivyo
nilikua na serikali kubwa Sana kwenye
kichwa changu.’ Ahaha’” Agiza uwahi
kurudi shule, alafu usiwe unatoroka”
aliniambia hivyo nikaishiwa tabasamu
kabisaa, ningefanya nini zaidi ya kupata
aibu na kuagiza zangu chapati mbili na
kikombe Cha chai jumla Mia tano. Kwani chapati ziliuzwa moja Mia mbili, alafu chai kikombe Mia moja.
Nikaletewa mtoto wa kike kwa namna
nilikua na njaa nilikaa sawa sawa
kwanza kabla ya yote. Na hapo ndo
kuanza kula. “ We huagizi chochote?”
Nilimtumbulia macho akabaki kaniangalia
Tena. Sijui alijenga kitu gani kwenye
ufahamu wake, nikainamisha macho
yangu. Na kuendelea kula zangu mdogo
mdogo. Mpaka nikamaliza. “ Asante
Kaka mkubwa” nilipomuita hivyo
akaniangalia tu bila kujibu kitu kwa
muda.” Naitwa Gerald” aliponambia Hilo
jina nikatabasamu “ sawa Kaka Gerald”
mjinga Mimi hata sijui kujiongeza,
potelea mbali kwani yeye sio sawa na
Kaka yangu tu!. “ Niite Gery, itapendeza “ aliposema hivyo nikajikuta
nacheka kwa sauti, sikuweza kusubiri
kucheka. “Ahahaha”” Unacheka nini?” “
Hamna, najiuliza kwa nini imebidi
nikuite Gery, au nikuite Jery, napenda
Sana Ile katuni” alicheka pia Ila cheka
yake Sasa. Hapigi hata kelel yaani Ni
Kama amelazimishwa acheke. “Ahaa, aa…” Nilimuona wa ajabu. Labda
anacheka kitajiri. “ Usicheke bhana, naitwa hivyo hivyo, we niite unachotaka iwe Gery, iwe Jerry, Ni sawa Ila isiwe
Kaka Gerald “ hapo ndo nikaelewa
hakutaka nimuite Kaka. Hata hivyo
yeye sio Kaka yangu. “ Ok nitakuita,
Gery nikijisikia, na nitakuita Jery
nikitaka, ok”
nikamwambia hapo ndo
akaelewa Mimi Ni mtu asiejua kuficha tabia yake, yaani naongea mno. “ Sawa
wewe je? Nikuite Nani? Tom au mpenda chapati” “ Haa! Kumbe unajua kutania?”
Nilishangaa” Kwani naonekana sirias Sana?” “ Hapana nilihisi wewe ni mtu asie na maneno mengi “ nilipomwambia
hivyo aliinuka na kuhakikisha kalipia
Kisha nikafatana nae. “ Ni kweli upo sahihi, Ila Mimi naishi kulingana na mazingira, wewe ni mchangamfu Sana kwa nini na Mimi nisichangamke?”
Nilifurahi kusikia hivyo na hapo
nikakumbuka kumpa jibu juu ya jina langu. “ Naitwa Amina “ “ Amina?”
Alitabasamu kidogo Kisha akaongea.”
Ndo maana una akili za kuku” ‘chiii huyu
mwanaume ni nyau mkubwa, mi na akili
za kuku!’ niliuma meno yangu ye mwenye
akagundua Hilo na kucheka kwa uvivu
Tena. “ Haraka nenda shule, usije ukakutana na watu uliowadhulumu kwa
Mara nyingine, ukinimiss Sana juma
mosi ya wiki ijayo mida Kama hii, utanisubiri hapo kwenye huo mgahawa
sawa?” Aliniambia na kujiweka sawa
daah!! Kijana huyu? Nisiseme mengi, sema Ni mwembamba ahaha! Unahisi
nini kitafata hapo????Kikubwa zaidi
usiache ku like na kudondosha comment
yako hapo chini. Na ki share. #Simulizi
za Sumaiya#Summy stories# Simulizi
za Summy. Huku Ni kuinjoi tu. Usiache
ku download App yangu ya Simulizi za
Summy au Summy stories. Kuzidi
kuburudika zaidi.
Sehemu ya 03
Nilimuaga akaondoka zake taratiibu
nikiwa namuangalia kwa nyuma tu.
Taratibu na Mimi nikageuka na kuifata
njia ya kurejea shuleni, akili yangu
ilichangamka kwa kuukumbuka wakati
mfupi uliopita, Gery, alikua akiitwa
hivyo. Daahh ki ufupi nilivutiwa nae sio
tu jina lake la mvuto Ila hata yeye
mwenyewe kwa ukamilifu anaonekana
kua smart Sana. Hatimae nilifanikiwa
kuingia shuleni Tena.
“ Ulikua wapi? Nimekutafuta kila Kona ya hapa” Mira alinikaribisha na maneno ya uongo, najua hakufanya hivyo kabisa.
“ Kwani? Nimefanya nini hadi nitafutwe shule nzima?”
“ Ni Jambo la kuuliza, umefanya nini kweli? Ami, hujanywa uji, na pesa yako
niliitumia kununua vitafunio japo
sikukwambia, Ila ki ufupi umenikwaza mpaka nimegawa kila kitu”
“ Nini?” Niliweka mikono kichwani kwanza. “ Aaaaa haaaa, Mira naomba pesa yangu, ungejua nimekumbwa na
mangapi huko usingenikwapua hiyo hela mpuuzi wewe!! Nilimtukana hapo huku
machozi yakinilenga kwa nini alinifanyia hivyo mwenzie?
“ Amiii… We hukujiongeza nilipokuomba tukanywe uji hukuinuka nikakuacha tu, nilijua ungeshuku kumbe we kichwa Maji tu!” Duh leo hii yamenikuta. Nimetoka kuambiwa Nina akili za kuku muda si mrefu bado Kuna mtu anao ujasiri wa kuniita Mimi kichwa Maji?
Bora wa kuniita akili za kuku, maana
yeye hajaniweka matatizoni.
“ Miracle we mshenzi” nilimlaumu hapo
na kumfata nyuma haiwezekani jamani
pesa yangu yote ameitumia bila Shaka
tutakutana.
Majira ya usiku tukiwa tumelala, hatulali kitanda kimoja Ila vitanda
vyetu vimekaribiana Sana. Nikaanza
kumpa ubuyu kuhusu yaliyojiri siku ya leo. Miracle Ni shoga yangu, Siri yake’
Siri yangu.
“ Wee kwa hiyo leo Ami wangu kala
chapati na chai. Jamani sio poa mbona
hukunisanua juu yake” miracle kwa
uroho ahaa alitaka tufatane ili mi
nisipewe ofa. Siku nyingine kuachana na
rafiki yako ukaenda safari zako’ Kuna
fahida yake’ bhana we kuweza!
Niongozane nae ili nikose vitamu.
“ Aahh jamani, si ndo nimebahatisha leo, ningejuaje Sasa wakati sikuwahi
kuonana nae Leo ndo nimekutana nae?”
Nilimtania hapo akabaki kutikisa kichwa najua tu akilini mwake aliwaza namna
nilivyoinjoi kula chapati zangu mbili bila
kumletea chochote.
“ Mbona hukuniletea hata kidogo”
hatimae alitumbua jipu kifuani kwake.
“ Mmh Sasa ningeleta vipi Mimi, kikubwa nimeshiba, hata hivyo we
mwenyewe umetumia hela yangu fanya
unirejeshee”
Nilipomwambia hivyo akavuta na blanket kabisa. “ Mwanamke usiefaa wewe hebu
ulale huko, umuote huyo Deri wako sijui
Geri, potelea mbali kwanza mbaya”
aliongea kana kwamba alikua akimjua?.
Ahaha atakoma bhana.
Nkajifunika pia nikiwa naiwaza taswira
Yake hakika Gery alinivutia. Usiku
aliiteka akili yangu yote. Nilijikuta
nakumbuka namna alivyokua
akitabasamu, akili yangu ikanituma
labda hiyo midomo iliyokua ikitabasamu
ingeenda mbele zaidi na akainama
kunibusu. Aii kwa aibu nilificha macho yangu kwa mikono.
“ Jamani Ami lala pleeaaaaaass” da!
Ilibidi nijiombee kulala. Lakini taswira
Yake haikufutika. Bila Shaka kichwa yangu imeoza. Niliwazaa kumuona anavyotembea na kunikumbatia huku akinitania. .
“ Ami amka unywe chai na chapati”
ayaaa yalikua mawazo yangu bhana, yaani kitanda hakikulalika siku hiyo, mbona niliamka na kukaa tu.
Hatimae weekend iliisha tukaanza
masomo Tena. Nasoma huku nahesabu
siku ni lini zitaenda mbona zinachelewa
hivi jamani. Lengo juma mosi iwahi
kufika ili nikaonane na Gerald nyie nyie.
Mimi nachokitafuta hakika nitakipata.
Badala nitumie akili yangu kusoma na
kupambana nipo kumwaza Gerald tu.
Hatimae bhana hayawi hayawi mwisho
huwa Jumamosi ikafika. Hiyo siku
niliamka mapema Sana na kujiandaa
vizuri, na kujiweka fresh baada ya
kufua nguo zangu Kisha nikaweka
mazingira Safi nikisubiri muda usogee
sogee.
“ Tunaenda ama? Na Leo unaniacha? “
Mira nae sijui kwa nini hakunipa nafasi ya kupata Uhuru nikiwa na Gery wangu nilihisi kulia alikua Gery wangu toka lini hiyo ?
“ Sawa siendi hata hivyo Mimi na safari zangu, nataka tu tuvuke pamoja njia ya Siri Kisha utaenda kuonana na huyo mwenda wazimu wako”
“ Wee kaa kimya usimuite Gery mwenda
wazimu, mi ndo namjua” nilimkanya wakati nilimuona Gerald kwa masaa tu dah?!
“ Sawa bi kipotabo umeeleweka” baada ya mazungumzo ya muda kidogo hatimae
tulikubalina na mwisho tukaongozana
moja kwa moja mpaka kwenye njia yetu ya magendo na hatimae tukafanikiwa
kutoka nje ya fensi. Duh! Yaani sisi!
Baada ya kufika nje mwenzangu
akajipakia kwenye boda mi ndo
nikaongoza njia kuelekea mgahawahani.
Inashangaza niliwazaa labda nikifika
ntalizimika kumsubiri Gerald Ila
mwenzangu kumbe alifika zake mapema
kabla yangu. “ Hi Ami” alinisalimia
Mara baada ya kuniona. Nilitabasamu
Kisha nikamfata huko alipokua amekaa.
“ Gery umewahi kabla yangu”
nilitabasamu.
“ Hakika ilinilazimu kuwahi” aliponambia hivyo alijtengeneza vymea miwani yake’.
Siku hiyo pia alipendeza jamani, alivaa
Shati jeupe la mikono mirefu Ila alikua
ameikunja mikononi, na suruali ya
kijivu, ki ukweli alionekana Kama afisa
mikop. Alibaki kunitazama Mimi ambae
nilivaa vazi la siku Ile sema limefuliwa tu juzi juzi.
“ Tusikae hapa, sio sehemu nzuri kwa
Mimi kuonekana na mwanafunzi”
aliniambia nikapata uoga pia Ni kweli
haileti picha nzuri. Alichukua chapati
zangu mbili maana alihisi nitatumia
baadae nilitabasamu kwani alikua
akinijari. Kisha tukaondoka kuelekea
anakojua yeye.
Nyie nahisi Mimi Ni wazimu, hivi
umewahi kumuamini mtu kwa kumuona
siku moja tu? Ndo yalinikuta Mimi
Sasa, utadhani labda ndo nipo hivyo
lakini Wala. Ni Hali ambayo ilinitokea
ghafla baada ya kukutana na Gerald.
Nilimfata huyu kuelekea anakokwenda
mwenzenu hata sikua na hisia hasi juu
Yake hata kidogo.
Sehemu ya 04
Nilimfata Gerald ambae alisimamisha taxi ya kulipia tukaingia mi na yeye.
Hapo ndo nikakumbuka kumuuliza
tunaenda wapi? “ Gery, tnaelekea
wapi?.usije ikawa unaniteka mwenzako?”
“ Ndo.mpango huo Ami wangu, nakuteka
kimya kimya” alijibu hivyo nikabaki
kutabasamu mwenzenu, eti natekwa?
Ahaha! Hata hivyo Ni sawa tu.
“ We ni teke tu sio kwa ubaya lakini”
nilimwambia akacheka.
“ Umewahi kuona mtekaji anaeteka mtu
kwa uzuri Ami”
“ Nahisi ndo wewe utakua wa kwanza, Ni furaha yangu kukutana na mtekaji
wewe hapo”
“ Mimi je? Ninafuraha zaidi kukutana na mateka mwenye akili za kuku Kama
wewe Ami, hakika umejua
kuichangamsha akili yangu hivi karibuni, kila muda nakuwaza wewe tu”
aliniangalia machoni yaani tukawa
tunatizamana face to face. Mi nilihisi
aibu maana Gery aliongea kwa hisia
kubwa kwa wakati huo.
“ Usinionee aibu, napenda Sana
kutazama macho yako yenye mvuto”
nilijikuta nainama kabisa sitaweza
kusikia kila neno toka kwake.
Nilipojiinamia alipitisha mkono wake
nyuma yangu na kuangushia kiunoni kwa kusudi. Nilishtuka nyie baada ya kuhisi
msisimko. Yaani Ni Kama vile Moto
uliwaka kwenye mwili wangu mapigo ya moyo wangu yakaanza kwenda mbio.
Hivi? Nilikua na mtu wa aina gani
wakati huo? Ni mwanaume eti hakua
mwanamke mwenzangu, mbona
nimejisahau Sana? Niliwazaa hivyo Ila
shetani akanirejea Tena.
‘Gery hawezi fanya chochote’ nilijiwazia
hayo, hakika Mimi Ni wazimu kabisa
Nina uhakika gani wa kuamini kwamba
Very hanifanyi kitu. Ila Sasa daah!!
Anazo chapati zangu. Nilitulia kimya
baada ya kuwaza Hilo.
“ Tumefika” gari ilisimama baada ya Gerald kumwambia dereva hivyo. Na
huo ndo wakati ambao aliondoa mkono
wake kwenye kiuno changu nikapata
ujasiri wa kuinua uso wangu. Aligeuza
macho kuningalia nikashangaa
mwenzangu anatabasamu.
“ Kwa kwa nini unanicheka?” Nilimuuliza
maana Ni kama.kuna kitu kilitokea”
“ Uso wako umekua mwekundu, umetawaliwa na hisia” ayaa kwa nini
Sasa aliniambia hayo maneno sio
angenyamaza tu? Hakika Gerald Ni
mwanaume asie na tabia ya kunyamazia
Jambo nilihisi hivyo. Hatimae
tuliteremka kwenye gari akalipia Kisha
dereva taxi akaondoka zake.
Baada ya taxi kuondoka alinishika
mkono tuvuke barabara nikafatana nae,
nyie wakati huo nilikua na share zangu
za shule. Mbele yetu kulikua na nyumba
ambayo ilizingirwa na fensi alafu
pembeni.kuna nyumba nyingine za aina
Ile, Wala sikua na wakati wa kujiuliza
Sana isipokua tu nilimfata Gerald
anakokwenda. Alisogelea nyumba ya geti moja kubwa akafungua mlango
mdogo yeye akatangulia nikafata nyuma
Yake.
Tulipoingia ndani geti ikajilock. Kisha
nikatupa macho mbele kulikua na
nyumba moja ndogo tu. Akanikaribisha
mwenzenu nikaingia mpaka ndani.
Nilitupa macho mbele na kuona mkate
mkubwa huo kwenye meza ya chakula
blueband, cocoa butter. Asali sema
sikua pale jamani. Gerald aliniomba
nikae sebureni nikakaa nyie nyumba
nzuri Ila sijui Ni ya Nani hata. Ila
ndani kulikua na ukimya. Gerald
aliniacha sebureni nikibung’aa macho
kwa kutalii hiyo Sebure. Daah! Ni
kijana mdogo tu Sasa hapa Ni kwake
ama amepanga? Nikiwa nawaza hayo
Kuna mwanaume akatokea ghafla huku akiongea.
“ Gery mbona umechelewa kurejea wakati leo juma mosi?” Nilishtuka nikagandisha macho yangu mbele
kumwangalia. Uwiii.. alikua mwanaume.
Mrefu’ mweusi mnene kidogo, hakua
hata amevaa Shati na kwenye kifua
chake alichafuka na vinyweleo sijui ndo
wanaitaga garden love. Watajua wao
bhana. Aliponiona akabaki kutabasamu na kuanza kuniita shemu.
“ Ahaha Shem karibu sana, jisikie huru, jisikie umefika” wee nilipagawa
nakujihisi Mimi ndo mama la mama kuitwa shemu. Nilitabasamu na kujibu kwa upole.
“ Ahaha mi sio shemeji yako, mi na Gerald Ni marafiki tu.”
“ Ohoo, sikugundua Hilo, sema Gery
alisema atamleta Shem wangu Ila Cha
ajabu ameamua kua singo tu”
alitabasamu na kuondoka kimya.
“ Labda ataletwa Ila haitakua Mimi”
nilicheka yule bwana akapotelea.
Baadae nikiwa sebureni nilimuona huyo
mwanaume mweusi akiishia getini baada ya Mimi kumchungulia dirishani.
Nikiwa pale Gery akaja na vikombe viwili wakati huo, na vyote vilikua na chai TAMU aiyaaaa, alinifata Kisha
akanipatia kimoja. Na kunipa chapati zangu.
“ Your favorite” aliniambia hivyo lakini daah! Nilimuonea aibu wakati huo maana
kwanza alikua kavaa bukta ya karoti
alafu juu yupo kifua wazi nyie. Maksudi haya alikua nayo Gerald. Nilikua nakula
kwa wasiwasi hakuna kuongea kabisa.
Alisogea karibu yangu na kuchukua
laptop yake’ Kisha akawasha na kuweka movie ya kihindi.
“ Hupendi movie za wahindi?” Aliniuuliza kana kwamba alikua alikua akinitega.
“ Naachaje Sasa kupenda?” Nilimjibu na kuendelea kula chapati Kisha
akaniangalia. Nyie huyu Kaka
anamaksudi Sana. “Naomba nilishe
kidogo”. Aliniambia nikabaki hoi
mwenzenu aibu.
“ Naanzaje kukulisha Sasa? Nilijikataa kimya kimya.
“ Kwa mdomo” duhh. Ilibidi nigeuze
macho yangu ili kumtazama wewe!!
Nilijuta kwani wakati huo sijui
mwenzangu Ni saa ngapi alinishika kiuno
changu kwa nguvu na kuanza kunibusu
mdomo.wangu!. Sikua nafahamu lengo
lake wallahi Tena.
Sehemu ya 05
Nyie nyie, Mimi nilijuta mpaka hapo
nilihisi Kama kichwa changu
kimeelemewa yaani sikua najikumbuka
jamani, kwanza Ile it was my first kiss for sure. Japo na machachari yangu yote niliyonayo Mimi sikua kua na mahusiano. Kwa hiyo haya Mambo
bhana ndo Kama vileee nayaanza.
Gerald alinibusu hapo bila Mimi
kutarajia, kwa muda wote aliokua
akinibusu sikua najikumbuka hata kwani
nilishindwa kumfanya chochote, lakini
hatimae nilikumbuka kabisa sio sahihi
kuhusu kinachoendelea, haraka Sana
nilimsukuma kwa nguvu akawa kaniachia.
“ Samahani samahani Ami, sijui niseme nini? Ila kiufupi we unanivutia Sana, sio tu macho yako, nikikaa karibu yako,
kweli Tena nahisi kupagawa natamani nifanye chochote kwako”. Shenzi
kabisa’ huyu aliongea bila kutumia akili
hata kidogo kwamba mi sijui alikua na
tabia za kihuni nilijikuta nakosa cha
kusema nikabaki tu nimeshika midomo
yangu. Na sura yangu ikabadilika
kabisaa kuashiria kwamba sijapendaa
alichokifanya. Ila moyoni nilikua na
msisimko usio jidhihirisha, actually
nilifaa kulia lakini Ni Kama vile moyo
wangu ulikua ukishangiria juu ya
kilichotokea. It was an amazing feelings, kwani ilikuaje Hadi akanibusu nilitamani afanye hivyo Tena.
“ Sorry, Ami naomba unywe chai yako”
aliniambia hivyo Kisha aka consecrate na movie ilikua kwenye laptop. Alikua karibu yangu Sana kiasi kwamba
nilishindwa hata kutumia chapati zangu vizuri.
“ Ami “ aliniita
“ Abee” niliitika kwa upole na kwa aibu
Sana.
“ Please naomba ule, sitaki niwe
kikwazo kwenye hisia zako’ kwa hivi
sasa” nyie mkisikia mtu ana sauti
TAMU ndo huyu Kaka, alikua akitumia sauti flani hivi kana kwamba aliongea na mtoto wake. Hatimae nilijikuta namjibu
kijasiri ili asihofu kuhusu Mimi.
“ Usijari Gery, ki ufupi sio kosa, kua na hisia na mtu hakuna anae chagua”
nilimpa jibu kana kwamba nilikua na mtu
wa maana daah! Ningejua Mimi hata
nisingemwambia hayo maneno.
“Kweli?” Aliniuuliza akiwa kanitazama, kwa muda huu nilimuibia macho kidogo
sikutaka tuangaliane muda mrefu’, hatimae niliitikia kwa kichwa. Akawa
ametulia.
Muda kidogo ukasonga nikawa
nimemaliza kunywa chai yangu na yeye
kamaliza yake’, niliinuka na kumuacha
nikapeleka vyombo vichache tulivyotumia
jikoni. Nilipofika jikoni nikaona Karo ya
kuoshea vyombo nikaanza kuosha.
Karibu na karo kulikua na kioo ghafla
nikajiona kwenye kioo wee si nikaona
lips zangu. ‘aiii Mungu wangu alinibusu’
niliwazaa Hilo haraka Sana nikaziba
macho yangu na mikono siamini Hilo, yaani hiyo busu haikua ikinipa hata
sekunde tano za kupumua. Lazima
niikumbuke. Nikiwazaa hayo nilishtuka
kiuno changu kinasongwa na mikono ya
mtu mzima.
‘ mamaaa’ kumbuka Gery hakua amevaa nguo tofauti na Bukta. Nyie huo mwili
wake tu ulinipa usumbufu nilishindwa kumuelewa kwa nini yupo haraka Sana.
“ Gery unafanya nini?” Nilimjibu bila kusubiri.
“ Ami kiukweli mi nakupenda Sana”
neno nakupenda lilikua neno TAMU Sana
ambalo, nilitamani kusikia toka kwake
lakini sio haraka hivyo, nilitamani
nisikie Hilo neno hata baadae lakini
nimesikia wakati huo huo, ndo kwanza siku mbili tu.
“ Ami najua unaweza ukaniona mi muhuni au kicheche sitajari Ni vipi
utaniona Ila huo ndo ukweli uliopo, I fall for you” nilikaa kimya wakati huo
moyo wangu unadunda Sana hauwezi
hata kutulia yaani Gerald nyau huyu
alijua kuniweza. Kikubwa alichofanya
huyu mpuuzi alinigeuza taratiibu upande wake akaushika uso wangu mdogo usio
na hatia akabaki kunitazama nami
nikawa namwangalia. Kweli Gerald alikua na macho ya ushawishi kiasi kwamba
nilikua siwezi kumwangalia hata kwa
dakika moja. Sekunde Saba zilitosha
kumtazama huyo jamaa.
“ Please, nahitaji nafasi katika moyo wako, najua unasoma sitamani
kukuharibia Maisha yako Wala masomo
yako lakini moyo wangu umeshindwa
kudhibiti hisia zinazonijia bila kusubiri
tafadhari. Naomba usinikatae” ki ufupi
sikua na jibu la kumpatia lakini
alichoweza kufanya mjinga huyu Ni
kunibusu Mimi kwa Mara nyingine, hapo
mwanzo nilikua Kama namzuia zuia lakini
baadae daah! Nilitulia mwenyewe ogopa
Sana first love feelings, inatia kiwingu.
Sikua najiweza kwa lolote.
Kwa busu iliyochukua muda mrefu’ Kati
yetu ilimfanya Gerald asafiri kutoa
hatua moja ya mwili wangu kwenda
hatua nyingine, katika sekunde za
kufumba na kufumbua nilijikuta Sina
nguo Ami Mimi, nyie nilikua naogopa
nilikua na aibu nilikua natetemeka vyote
kwa pamoja. Sikua na utulivu maana Ni
Kama sijui nilikua naenda kutenda
dhambi gani nisiyoijua?
Gerald aliweza kunibeba nikiwa nimebaki
kwenye taiti tu, na Pichu ndani Yake.
Ki ufupi sikua kwenye fahamu zangu.
Hatimae tulifika kwenye mlango wa
chumba ambao aliufungua bila kusubiri
akanishusha na kuanza kunbusu upya
mtoto wa kike Mimi, siku hiyo naanzaje
kuisahau. Maisha yangu yaligeuka
ghafla kutoka kwenye utoto na kujiunga
na watu wazima kwenye ulimwengu wa mapenzi.
Sehemu ya 06
Baadae Sana nilijikuta nalia tu mwenyewe, nilijilaumu kwa kufanya
maamuzi bila kufikiria, yaani ilikua kana
kwamba akili yangu ilishikiliwa. Hivi
mimi ni wa kufanya mapenzi na mtu ambae sikua na mfahamu vyema.
Nilikua nimetulia zangu kitandani hapo
huku nalia. Gerald alikua pembeni yangu
akinibembeleza kwa maneno mazuri kua
nisijari.
“ Tafadhari Ami, najua nimekukosea
sikufaa kua na haraka hivi lakini
unanivutia Sana, na kingine mi sikujua
Kama wewe ni bikra, ningejuaje Sasa?”
“ Gerald sitaki uniongeleshe chochote, kwako Mimi naonekana Malaya ndo
maana umenifanyia hivi, sio makosa
yako lakini Mimi ni mjinga” nililia hapo
Gerald akahuzunika kidogo.
“ Hapana Ami, we sio mjinga, ki ufupi
Ni makosa yangu, sikufaa kufanya hivyo
kwako nilifaa kua mtulivu, angalau
ungenipa muda “
“ Nyamaza Gerald kwa hiki
ulichonifanyia, hakika naaoa
sitakusamehe, sitakusamehe mbwa
wewe” nilimsukuma hapo nikainuka na
shuka kwani sikua na nguo mle chumbani
hatimae nikaingia bafuni huku nalia,
haraka Sana nikaoga huku. Nawaza
Mambo mengi Sana.
‘ hivi ntamwambia nini mama yangu
Mimi?mama wa watu anahangaika
kuwahamasisha watoto wake wa kiume
waweze kunisomesha nihitimu vyema mi nimekuja kufanya ujinga, kwa kweli
sikufaa kufanya hivi, huu Ni usaliti
mkubwa Sana nimemfanyia mama yangu, sikufaa kumfanyia hivi jamani’ nililia
hapo mpaka macho ya kavimba. Baadae
hatimae nilisikia sauti ya Gerald akiwa
mlangoni ananigongea.
“ Ami please open the door Sina amani mwenzako” shenzi kabisa’ kwa nini
akose amani wakati tayari
kashanichukulia usichana wangu.
Sikumjibu kitu zaidi ya kuinuka na
kufungua mlango nikiwa na taulo,
nilimpita na kuelekea jikoni kuchukua
nguo zangu. Lakini wakati huo nilikua
naumia japo sio Sana kwani Gerald
hakutumia fosi kunitoa usichana wangu
alifanya taratiibu na Asante Mungu
sikua na maumivu makali. Japo
yalikuwepo kiasi chake. Nilivaa nguo
zangu na kutaka kuondoka Gerald akanizuia.
“ Hapana Ami, sitaki uondoke hivi”
alinizuia nikashindwa Cha kumfanya,
sijui nimmeze, ki ufupi nilimchukia ghafla yaani.
“ Gerald niachie” nilitoka hapo
akaniachia akiwa na macho ya huzuni
Kama mtoto alienyimwa pipi.
“ Hivi unajiona Nani labda? Unaweza
kusimamisha dunia nzima mikononi
mwako. Tena ikibidi usinizoee”
nilimwambia hivyo nikafungua na mlango.
Wakati huo tayari Ni saa Saba
inaelekea saa nane kabisa. Duhh Mimi
lakini?.
Hatimae nilifika nje na kuanza
kutembea taratibu nikielekea nishuleni
ghafla mkono wangu ukashikiliwa, daah!
Katika hii dunia Kuna watu ving’ang’anizi
nyie wa kwanza alikua Gerald
“ Ami huwezi kwenda hivi, angalia na Hali yako, ona unavyohangaika
kutembea mpaka ufike shuleni kwenu
kila mtu ataelewa wewe umetoka
kutolewa usichana wako, yaani itakua
aibu Tena Kuna uwezekano damu
ikaanza kutoka Tena” aliponambia hivyo
nilihisi kupagawa hivi hayo Ni ya kweli.
Nilitulia tuli, kwani pale kitandani
mbona hakukua na damu kama watu
wanavyosemaga Sasa yeye damu kaiona wapi?
“ Hiyo damu we una undugu nayo, hebu achana na Mimi, watu huwa wanasema
kua bikra ikitolewa basi mtu hutoa
damu nyingi mbona mi sikuona, itaanza vipi kuchuruzika wakati haijatoka”
.” Ami usijifanye mjuaji Sana, mi
mwenyewe Dr hapa najua nachokueleza, ambao husema wanatokwa damu nyingi
Ni kwa sababu huwa wanafanya mapenzi
kabla ya umri wao kuruhusu, au
wanaume wao hutumia nguvu kubwa
Sana wakati wa tendo lakini Mimi
sikufanya Hilo, sikutaka nikuumize ndo
sababu hukuona damu, la sivyo
ningejuaje Kama wewe ni bikra iwapo
nisingeona utandu wa damu kwenye
‘naniliu’ yangu, licha ya utandu tu,
nimekugundua mara punde nilipoanza
kuingiza naniliu yangu kwako kwa hiyo
kua muelewa. “ Niliusukuma mkono wake
Ila akanifata na kunishika kwa nguvu
Kisha akasimamisha taxi na hapo ndo
tuliweza kuingia ndani ya taxi kwa
lazima.
Bahati mbaya Sana taxi alietuleta ndo
taxi tuliepatana nae Mara ya pili.
“ Jomba tumekutana Tena, kwa kweli
riziki yangu ya Leo iliandikwa mikononi
mwako”
“ Yawezekana mzee baba” Gerald
alijibu hapo nikiwa nimenuna mwenzenu
sitaki hata kuongeleshana na mtu.
Hatimae tuliwasili sehemu ambayo
tulipanda tax mwanzo. Nikateremka na
kutembea kuelekea kwenye mlango wa
Siri bila hata kumuaga huyo nyau huyo.
Sikugeuka hata nyuma kumwangalia.
Niliweza kuingia shuleni kimya kimya
Kisha nikaelekea bwenini, nilikuta
wanafunzi wenzangu wapo wanakula,
kwa Hali niliyokua nayo sikutamani hata
kuutazama huo ugari mgumu wa dona na
maharage ya bila kuungwa. Nilimpita
moja kwa moja mpaka bwenini.
Nikajitupia kitandani, bahati nzuri nilikuta Mira karejea.
“ We Leo vipi? Mbona hoi?” Alinihoji nimakosa Cha kusema.
“ Em sogea huko kwanza nikupe ubuyu”
“ Aiiii” nilipiga kelel za maumivu maana alinisukuma ghafla alafu Sasa
nikajitonyesha, daah siku hiyo nilipata
kidonda Cha ghafla yaani bila kutarajia.
Kwa hiyo maumivu niliyokua nayo sio ya nchi hii. Mira aliniangalia kwa jicho
Fulani hivi la ‘ Hadi wewe?’.
Sehemu ya 07
“ Wewe! Ami! Ume umefanya?” Alinihoji
kana kwamba yalikua maajabu mapya ya
dunia, Ila ki ufupi ilikua Ni aibu kubwa
Sana iwapo nitamjibu kua ndio nilifanya
hivi nawezaje kumjibu kua nilifanya?
Naona aibu Sana Mimi.
“ Ami nieleze ukweli huna rafiki
mwingine hapa shuleni mi ndo ndugu
yako wa pekee na anaeweza kukusaidia”
aliniambia nikamkanusha haraka.
“ Hamna sikufanya unavyowaza sema
ilibaki kidogo tu yanitokee ya
kunitokea” nilimwambia akanikumbatia
haraka ki ukweli alipata hisia
mchanganyiko juu yangu, ki ufupi Mira
alihisi kabisa kunionea huruma ila angefanya nini Sasa.
“ Ami umekula?”
“ Miracle mwenzio sili maugali yenu, nimechafukwa”
“ Sawa hata Mimi siwezi kula ugali ilhali nilitoka nje ya shule leo.” Alifungua tranka moja ambalo tulishaligeuza
tranka la maakuli pamoja na vipodozi
yakiwemo mafuta ya kupakaa na sabuni za kuogea na kufulia. Alitoa mifuko
miwili iliyotuna. Wee harufu tamu nayo ipenda kupita kiasi ikasikika.
“ Mira hakia Mungu Tena nasikia njaa”
nilimwambia.
aliponambia hivyo nilijikuta natamani
kulia yaani mwenzake nililiwa siku hiyo
Tena kwa chapati za Mia nne na chai
ya Mia tu. Mi Sina aibu jamani.
“ Usipoteze sura yako nzuri kwa kuwaza
mabaya em kula kwanza “ nilitabasamu na kuanza kula hapo chips na kuku
alivyonipatia pamoja na peps big yangu
hapo, sijui niseme nini, Kuna watu
wanajua kuwapendelea wapenzi wao
nyie. ‘Lakini li Gerald limeweza tu
kunifanya na halijanipa hata Mia mbwa
yule.’ Nilimtukana Gerald kimoyomoyo.
Nikaendelea kula.
“ Shenzi kabisa’, najua Sana umekula vinono huko alafu hujaniletea”
“ Mira ki ufupi Ni kwamba wewe ni rafiki mkubwa tu na Mimi hapa siwezi
kukuficha Jambo, yaani ukweli Ni hivi, tumalize kula nikupe hadithi juu ya
yaliyojiri huko nakwambia sio mchezo”
nilidumkiza nyama ya kuku nakuitafuna
haraka huku nashushia peps taratiibu.
“ Ok natumai Ni salama” tulikula hapo
wenyewe, vilikua vingi Sana kiasi
kwamba tulishindwa kumaliza tukatunza
kwanza vilivyobaki tutakula na usiku, siku hiyo ilikua siku njema kwenye
upande wa misosi hatimae tulijitupia
kitandani nilimuomba Mira aje karibu
yangu sikutaka visokorokwinyo wasikie
hata kwa bahati mbaya juu ya
kilichonikuta.
“ Haya nambie ndugu yangu kipi
kimekutokea huko?”
“ Mira mwenzako sio bikra Tena”
nilianza kulia na kumhadithia kila kitu,
Mira akabaki kunionea huruma huku
akiiambia nisikhofu Ni bikra tu Kama
sikua nampenda Gerald Ni pole yangu
Ila Kama nilikua nampenda Basi nafaa
kujipongeza kwani sio kila mwanamke
hupata bahati ya kutolewa usichana na mtu anae mpenda.
“ Acha kuongea ujinga yule sio mume
wangu”
“ Vipi Kama akiwa hapo baadae, hata hivyo unaonekana kumuelewa Sana, hata
usimkasirikie juu Yake, kikubwa kwa
Sasa ni.kuangalia afya yako kabisa na kujitunza, kwanza huyo Gerald
anafanya kazi gani?”
“ Mi sijui” nilijibu hivyo Mira
akaniangalia wakati huo huo
nikakumbuka alisema yeye ni daktari, daah ningeonekana mjinga kupita kiasi.
“ Ni daktari mwaya” Mira alitabasamu angalau nimekutana na mtu anae jielewa kwani tayari alikua amesha Anza
majukumu yake ya kikazi.
Siku zilisogea bhana tukiwa shuleni
weekend iliyofata sikuweza kutoka nje
ya shule kabisa eti nikaonane na Gerald. Ki ufupi sikua tayari yanikute
Kama yaliyonikuta Mimi. Kwa Mara
nyingine.
Wiki nyingine Tena siku ya Jumamosi
ikafika Mira akanuliza iwapo natoka
nikamkatalia, yeye akatoka mwenzangu
mi sikuthubutu. Jumapili ya kesho Yake
tukiwa darsani mi na Mira
tunajisomea..nilitwa na matroni.
Nilishtuka kwani nilifanya nini? Mira
hakuweza kujizuia kunifata nyuma kwani
alipata mashaka dhidi yangu.
Tuliongozana Hadi kwenye ofisi ya
matroni tukiwa pamoja.
“ Ona Hawa nimeita mtu mmoja
wamekuja wawili, haya sawa Amina leo
kuna mgeni wako amekuja kukuona”
matron aliniambia nikabaki kumshangaa
‘mgeni? Ilisikika ki ajabu haikua hata
visiting day siku hiyo, licha ya visiting day sikuwahi kutembelewa na mtu
yeyote Mimi kwani ndugu zangu wapo
mbali Sana.
“ Mbona umeduwaa? Hutaki kuonana
nae?” Matron alinihoji.
“ Hapana bila Shaka ntaonana nae”
nilimjibu na hapo nikaongozana na Mira
kwenda kuonana na huyo mgeni aliekuja
kunitembelea.
.” Mmhh shost atakua Nani Tena
huyo?” Mira alinihoji nikabaki kimya
kwani hata Mimi hapa sikua najua
chochote. Ila ikabidi tufatane mpaka
kwenye jukwaa dogo la makutano.
“ Mambo Ami” aiiihh sauti hii Ni sauti
ambayo yaani ki ufupi niliifahamu.vyema
Sana japo sikua nimeishi.nayo kwa muda
mrefu Ila ndo hivyo tayari niliifahamu.
‘” Gerald umekuja kufanya nini hapa?”
Nilihoji akabaki kunichekea wakati huo
miracle ndo akaelewa kua huyo ndo
Gerald ki.ufupi alianza mkagua jinsi
alivyo na hatua alizokua akipiga
kutufata eneo tulilopo.
Sehemu ya 08
“ Mambo” hakuweza kunijibu kwanza alisalimiana na Mira ambae alitabasamu baada ya kumkagua vya kutosha.
“ Poa vipi?”
“ Safi tu, hamjambo hapa shule?”
Alituhoji kwa pamoja Ila aliejibu alikua Mira pekee Yake.
“ Hatujambo we ndo Gerald?” Mira alimpa mkono na hapo Gerald akaitikia salamu yake nikiwa nawaangalia tu.
“ Ndio Ami alikwambia?”
“ Ndio Mimi ni rafiki yake’ wa karibu, kwa hiyo atanieleza kila kizuri na kibaya dhidi Yake Mimi hufanya hivyo pia”
“ Waoo mna bond nzuri Sana, mpaka
nawaonea wivu” alitania hapo mi namzoom tu mpuuzi huyo sijui kaletwa nini hapo? Aahh Ni miguu Ila sababu
kuu ya yeye kuja kuniona sikua naijua.
“ Ami mbona huitikii salamu yangu?”
Alinihoji hapo kwa huzuni.
“ Kwa nini niitikie kwani Kuna ulazima?
Alafu kwa nini umemdanganya Matron
kua wewe ni mgeni wangu? Kwani we ndugu yangu?”
“ Ami tuliza mdomo utajaza watu, alafu kingine matron hajui Kama huyu Ni
mpenzi wako fikiria watu wakitambua
Hilo taarifa zikazagaa si utakua
umejidharirisha mwenyewe.” Nilikaa
kimya baada ya Mira kuniambia hivyo.
Gerald alisogea na kuushika mkono
wangu Kisha akanikalisha kwenye
benchi. “ Mpenzi nisamehe lakini ki
ufupi nimekumiss Sana, siwezi kutulia
bila maelewano na wewe, nakuahidi
kabisa sirudii kufanya nilichokufanyia sawa.”
“ Sawa nimekuelewa unaweza ukaenda”
sikutaka kukaa nae muda mrefu’ hata
hivyo.
“ Nawezaje kwenda Sasa. Unajua
nakupenda so ndio. Ndo maana nimekuja
tuongee mwenzako Mimi, wiki ijayo siku ya Alhamisi naondoka zangu.
Nimemaliza field yangu” aliponambia
hivyo ndo nikaelewa kumbe alikua bado anasoma.
“ Kwa hiyo nifanye nini?” Nilimjibu short and clear sikutaka kuongea Sana.
“ Ok, najua hutamani hata kunisikia
Wala kuniona, Ila sitamani kuondoka
bila kua na mawasiliano na wewe, tafadhari iwapo utapata nafasi naomba
unitafute please” alinikabidhi karatasi ya namba iliyokua juu ya bahasha
nikabaki kushika tu Kisha akainuka.
Ki ufupi nilijifanya mkavu Ila moyoni nilipata simanzi inamaana alikua
akiondoka, amirejea masomoni, alafu na Mimi nabaki bila kumuona kabisa niliwaza kidogo.
.” Nakuomba usiache nitafuta, nitaisubiri simu yako milele, nakuomba
Sana, usiache kunitafuta” alinisisitiza
kana kwamba angekufa iwapo asingetafuwa na Mimi.
“ Gerald” nilimuita kwa uzuri akasimama nami nikamfata. Nilipomfikia akabaki
amenitazma tu.
“ Unaenda masomoni sehemu gani? Na itachukua muda gani?” Nilihoji hapo
akaelewa kabisa hata Mimi nawaza juu
Yake.
“ Aahh, nasomea muhimbili, Ila nipo mwaka wa mwisho” aliniambia hivyo nikabaki mwenye huzuni kidogo.
“ Uwe na masomo mema sawa Ami, usome kabisa usiwahi kupata Gery
mwingine tena zaidi yangu sawa”
aliongea kwa umakini huku
nikibembelezwa daa!! Gery nyie
niachieni tu. Aliondoka nikabaki mwenye
huzuni hapo mwenyewe. Mira alikuja
akasimama kando yangu na kuichukua
Ile bahasha ambayo ilitangulia na karatasi la namba za simu yake.
Akafungua ndani kuangalia wee, alikutana na cheque ya hela.
“ Uuuuuuwwe Ami” alipiga kelele
akanishtua kutoka kwenye msongo wa
mawazo jamani niliogopa kelele zake?.
“ Pesa zote hizi, Ni za kweli ama?”
Ndo nami nikatupa jicho nakutana na
hiyo cheque, ohh my God laki tano yote
hiyo, na Mimi mwanafunzi ya nini ?
Macho yalinitoka ya pesa tamaa
ikaniangaza. Kwani tulikua karibu
kufunga shule. Niliwaza kufanya Mambo
mengi wakati huo huo..
“ Gerald Ni daktari wa Figo au moyo, pesa zote hizo akuachie” Mira aliongea
kana kwamba hakuwahi kuona pesa
inaitwa laki tano. Nilimtazama kwanza
Kisha nikamjibu. ..
“ Hajawa daktari kabisa bado. Alikua field tu” hapo ndo miracle akapagawa
Sasa Kama Ni field tu na tayari
nimepewa laki tano vipi kuhusu
akiajiriwa kabisa.
“ Ami ntakua mgeni wako kila Mara
pindi Gerald akikuoa” Mira shenzi
kabisa alinikumbatia kwa furaha
nikabaki kucheka kajuaje kama atanioa?
Siku zilisogea wakati huo hakuna Gerald
Wala nani zaidi yangu Mimi na Mira.
Tulikazana Sana kujisomea na kufanya
mazoezi kwa wingi. Siku zilikata
hatimae wiki, hatimae miezi tukafanya
mitihani yetu. Na Kisha tukafunga
shule.
Kwa likizo hiyo sikutaka kwenda
nyumbani kwani nilibakisha muhura
mmoja tu nimalize masomo yangu.
Tulitafuta chumba tukapanga mim na
miracle tukaanza Maisha mapya. Pesa
ilikuwepo jamani. Alafu tukanunua simu moja ambayo tuliitumia pamoja.
Niliweka namba za Gerald hiyo siku kwa kusita sita nikawa natamani kumpigia
Ila moyo unasita. “ Mpigie bhana mbona hivyo” Mira akinipa moyo Ila moyo.wangu ukawa unadunda.
“ Mira mi naogopa, dunia mwisho, hivi umewahi kuongea na mtu unaempenda kwa Mara ya kwanza kwenye simu”
“ Acha hizo Basi mpigie” Mira alishika simu na kupiga namba ambayo tayari
iliseviwa My Gery. Simu iliita haikuchukua muda ikapokelewa.
“ Hallo, Gerald yupo anaoga” weee moyo wangu ulisimama ghafla sauti
iliyotumika Kutamka neno anaoga, ilikua sauti ya kike, nilihisi kupagawa inamaana Gerald alikua na mwanamke mwingine wakati huo?.
Sehemu ya 09
Tulipigwa na butwaa kwa pamoja, yaani
Mimi na Mira tulijikuta tukiangaliana bila kumaliza yaani. Alikua mwanamke?
“ Uu wewe ni.
Nilimkatisha baada ya kumnyakua simu na kuikata. Sikutaka kuuliza mengi juu ya hiyo simu, ki ufupi Gerald Ni
kicheche hawezi kua kawaida huyo hata iweje.
“ Umefanya nini Sasa Ami? Tulifaa
kumjua kwa nini yeye mwanamke ndo
kapokea simu ya Gerald na Gerald ni mtu wako”
“ Aah! Em Mira achana nae, una hakika
gani Kama Gery Ni mtu wangu, mtu
mwenyewe huyo tulikutana tu bahati
mbaya sidhani Kama
chochote”
nalazimika kumhoji
.” Ami acha ujinga hili Ni penzi lako la kwanza pambania na ujivunie”
“ Nahisi kujuta kukubali kumvulia nguo
mwanaume Mimi katika Maisha yangu
sipo tayari kugombania mwanaume hata
siku moja, hata Kama nimepoteza
usichana wangu, bado sijapoteza utu
wangu acha nijifunze”
“ Ami wewe” Mira alinionea huruma ki
ufupi nilipata machungu kwani moyo
wangu ulisongwa na huzuni kubwa Sana
nikajikuta nalia, ki ukweli Tena tayari
nilimpenda Gerald nilimpenda Sana. Kwa
muda mfupi tu lakini napiga simu yake
usiku anapokea mwanamke tena
anaongea bila khofu kua Gerald yupo
bafuni. Nililia Sana mwenzenu.
“ Gerald kwa nini alinifanya nimpende, sikutarajia kuumizwa hivi, alisema mwenyewe nimpigie, alisema ataisubiri simu yangu milele lakini kaishia kuniliza
Mira nifanye nini Sasa”
Mira hakua na njia ya kunibembeleza
zaidi ya kuanza kulia na yeye tulikua
kana kwamba tulikua na msiba, kwa nini
Gerald katufanya tulie sisi wawili
hakika Mira alivunjika moyo kwani
tayari alikua kamuamini.
“ Sikujua Kama Gerald atakufanyia hivi
Ami, ametufanya sisi watoto wadogo
Sana, aaaaaaaaa” nyie hiyo siku siwezi kuisahau yaani Mimi na rafiki yangu
tulikua Kama machizi.
“ Kama ungejua hili mapema usingekubali kumpa bikra yako kwa chai ya Mia na chapati za Mia nne, ungehakikisha unaondoka na sikio lake” badala ya kulia tulijikuta tukicheka pia
japo inauma Sana.
“ Mira inaniuma Bora hata ningemtia
meno ingependeza zaidi, kinachosikitisha sikumuacha hata na
kovu mwenzako nimefeli Mimi, miraaaaa” nilizidisha kilio.
“ Amiiiii tumepoteza shilingi sisi, huenda sisi Ni wajinga kabisaaa” daah
Angepita mtu karibu bila Shaka
Angekufa kwa kicheko maana sio kwa kilio hicho tulichokua nacho wenzenu.
Siku hiyo ikapita bhana maana haikua
vyema kabisa. Wazo la kuipiga tena
namba ya Gerald likanijia asubuhi, wee
haraka Sana nilimlaani shetani, lisitokee Jambo Kama Hilo kwangu.
Tulifanya shughuri zetu za hapa na pale
Mira baadae akaniaga anaenda sokoni
kufanya manunuzi nami nikabaki
nyumbani, hiyo siku nilijisikia kuchora
nikawa nachora Ile nachora nikajikuta
nachora lips, ghafla nikakumbuka kiss
ya Gery, kwa nini Gery aitawale akili
yangu Mimi jamani? Hivi ana haki gani
kwenye Maisha yangu? Aaahh!
Nilikasirika.
Mara simu ikaita iliyokua pembeni. “ My Gery” nikasahau Kama nilikua na hasira
haraka sana na Gerald nikapoke na
kuongea kwa shahuku. “ Hallo” baada
ya kusikia sauti yake ndo nikakumbuka
kua usiku wa Jana alipokea mwanamke
simu Yake. Nikapoteza furaha nikajuta
kwa nini nilipokea simu yake wakati huo.
“ Wao Ami, kumbe Ni wewe kipenzi changu” alipoongea hivyo nilijikuta natoa msonyo mrefuuu usiostahili kabisa katika jamii.
“ Ami kwani nimefanya nini?”
“ Anyi nyinyi nyinyenyanya nyinyi.. nyoko wewe? Umefanya nini kwani
hujui? Jana usiku nakupigia simu
anapokea mwanamke wako, si ungesema tu kua una mwanamke wako nisikusmbue”
“ Ami yule sio mwanamke wangu, yaani ungejua kua unanitukana kwa ajiri ya
Nani hakika ungepiga magoti kuniomba
msamaha”
“ Gerald nadhani ushaniokota katika
watu wa kuokotwa sindio, hata Kama
Sina akili angalau nione kwa Ile kidogo
tu niliyojaaliwa na Mungu, hivi wewe
hapo kweli kabisa wa kuniongopea Mimi, usiku wa saa nne, Maji yanasikika
yakitiririka bafuni, alafu mwanamke
anapokea simu yako, Kuna haja ya
kuuliza kua wewe ni Nani yake Gerald “
“ Amina ulifaa kuuliza kabla, yule Mimi
Ni dada yangu huo ndo ukweli”
alipoongea hivyo sikutaka hata
kumsikiliza zaidi kikubwa nilichofanya
Mimi Ni kukata simu Yake kabisa.
Nilikaa kwa kutulia ghafla simu ikaita kwa Mara ya pili nikaimute, sikutaka
kusikia mikelele hata kidogo. Akapiga
Tena duuh! Sikua na njia nyingine zaidi ya kuipokea ikiwezekana nimtukane kabisa.
“ Ami najua huwezi nielewa Ila huo ndo
ukweli, naomba usikate simu nataka
kukwambia Jambo” niliguna ghafla na hapo ndo akaanza kuongea.
“ Ki ukweli Ami, Mimi Ni kijana ambae
huwezi nifikiria kwa mazuri kulingana na Hali niliyotengeneza kwako Ila ki
ukweli.kabisa elewa moja kwa moja
Mimi Ni wakwako na naempenda Ni
wewe tu, nimeangukia kwako”
Sehemu ya 10
“ Gerald nimechoshwa na mashairi yako ya uwongo, ulinikuta mtoto wa watu
Sina tabia za kihuni Ila tayari
umenifungulia UKURASA acha niiishi
Maisha yangu nayo ona Ni sawa”
nilimwambia akanifokea kana kwamba
amenioa.
“ Ami ole wako nikukute na mtu yeyote
Yule utanitambua, hivi una akili timamu
wewe? Unajisahau Sana, yaani
unajisahau kabisa Kama bado wewe ni
mwanafunzi. Hapo ulipo kaa ukijua wewe ni wa Gerald. “
Hee! Ananifokea? Ahaa! Bila Shaka ana wazimu, kwani mi sijui kua Ni
mwanafunzi? “ Baba unikome, hunijui
sikujui tumekutana bahati mbaya tu, kwa chai yako ya Mia tano usifanye
Kama wewe ndo mmiliki wangu, endelea na Maisha yako. Mi ligi ya mapenzi
siiwezi alafu kwanza___”
“ Ami usifanye nipande gari kuja huko
Sasa hivi unadhani sijui unapokaa, jichanganywa uwe na mtu yeyote utajua
Kama Gerald aliwahi kula Dona au la”
“ Ahaha! Unanitisha unadhani
nakuogopa, sikuogopi kwa lolote, na
usifatilie Maisha yangu, hata Kama
uweke walinzi kumi kunifatilia bado
ntabaki kufanya nachoamua kwani
muamuzi wa mwisho wa Maisha yangu Ni
Mimi mwenyewe umenielewa”
“ Ilikua hivyo zamani kabla hujakutana na Mimi, usifanye nivuruge mustakabari
mzima wa Maisha yako Amina, nimekupenda wewe imetosha nimechoka
kubembeleza Sasa hivi ntakuendesha vile unavyotaka nifanye”
“ Gerald we ni mshenzi mi bado binti
wa form six lakini ulisex na Mimi kwa
njama zako’ za kilagahai nakuchukia
kushinda dunia nzima” nilimwambia kwa
hasira nyie kwa namna tulitupiana maneno kwenye simu laiti Kama
tungekua karibu karibu hakika Kuna
mmoja angebaki bila jicho.
“ Nichukie usinichukie hiyo Ni juu yako
Ami, nitahakikisha unanipenda kuliko hata uhai wako labda Mimi sio Gerald.
Mwana wa Tantalila” aii shenzi huyu.
“ Nakuchukia, nakuchukia, nakuchukia na usipige Tena simu, nakulaani kabisa nisiwahi kutana na wewe Maisha yangu yote na leo hii lazima nipate mtu mpya”
“ Keleleee”” miracle alifika hata sikua najua.
“ Ami usinivuruge najua ni utoto tu bado unakusumbua Ila tambua wewe ni wa kwangu na Gerald anakupenda” alikata simu baada ya kusema hivyo, nilijikuta nakaa ghafla. “ Uuufff”
nilishusha pumzi ndefu haikua kazi rahisi kudeal na huyu mpuuzi Gery.
“ Daahh natokea kule, sijakaribia hata mlangoni nasikia sauti yako nikahisi mwenzangu kavamiwa kumbe upo kupigizana kelele na mpenzi wako”
“ Wewe acha hivi unajua Gerald Ni mshenzi, actually namchukia eti tayari
anajua tunakaa wapi? Aliemtuma anifatilie Ni Nani?”
“ Kwa kweli Gerald Kama anapajua hapa
bila shaka anakupenda Sana hataki
kuona ukiteseka kabisa.”
“ Mira una akili timamu, yaani Mimi
nifatiliwe eti hairuhusiwi
Mimi.kutongozwa, eti nusijichanganye akanikuta na mtu, aha! Kichaa’ kabisa
yeye ana mtu wake ana Maisha Yake
alafu niwe single daima anikome”
“ Najua unampenda, na huyo mtu
mwingine Nani wakati tangu nikujue mtu
pekee uliempaparikia Ni yeye tu, labda
dunia ipinduke ardhi ya juu’ iwe chini na ya chini iwe juu “
“ Mira achana na laana za Gery nahisi
njaa umenunua nini?” Nilivamia kapu
aliloleta kutoka sokoni nikaanza kukagua
yaliyomo sikuchelewa kuanza kupika
haraka Sana. Nikiwa jikoni najipikilisha
nilijikuta nacheka ghafla kwa
kuyakumbuka maneno ya Gerald ‘ahaha
we, eti mi Ni wake bila Shaka
anawazimu’ ahahaah’ nilicheka kwa sauti
kubwa Mira aliekua akichat aligeuka
kuniangalia.
“ Ami una wazimu hivi karibuni” alihisi
kuvurugwa na tabia zangu mpya.
“ Mwenzangu, najikuta nacheka kila
nikimkumbuka Gerald eti mi Ni wake, nisijichanganye nikawa na mtu mwingine
hakika yule Ni kichaa’ Tena sio kidogo.”
“ Khaaa hata wewe ni kichaa’”
aliendelea kuongea na simu mi nikabinua
midomo na kuendelea kupika hatimae
nilitenga mezani ugali na samaki mtamu
aina ya sato.toka mwanza. Tulikula kwa
kushangiria huku tukipiga story tulijadili
Mambo mengi Sana kuhusu graduation
yetu itakavyo kua. Yaani hata hivyo
bado muda mchache tu tumalize alafu
tulikua likizo ya mwisho kabisa wewe
Mambo yatakua fire.
“ Sijui tutavaa sare gani? Natamani
kila mtu aende na nguo zake Mambo ya
kufanana fanana Kama maparachichi
kwa kweli hainogi” Mira Ni wazimu Sasa
tusipovaa sare wanafunzi watakua kina
Nani na wageni waalikwa watakua kina
Nani?
“ Huna akili” nilimwambia
“ We ndo huna akili, ushaambiwa utulize kiuno ndani usionekane na mtu
Sasa ole wako”
“ Unampa Nani onyo? Hivi mi nikutane na hensam boy huko nje nishindwe
kumkubalia kisa yule binadamu
mwembamba kama skeleton… Ahaha sahau kabisa”
“ Alafu mwenzio sio mwembamba yule
usimdharirishe. Ana mwili mzuri tu ndo
maana hukuweza kumshinda”
“ Aa wapi?” Nilikunja midomo yangu
nikiwa sitaki sifa yoyote impate Gerald
nyie alinikera ilikua kila nikikumbuka
vipindi vizuri ambavyo tumeshare mi
na yeye lazima Kuna ka shetani
katanikumbusha kuhusu simu aliyopokea
mwanamke, Gerald my foot!! Kichwa
yangu muda wote ilimuwaza yeye tu.
Hakika nilitamani kulia.
Sio tu kutamani kwa jinsi moyo ambavyo
ulianza kuuma ghafla nilijikuta naanza
kulia Tena. “ Gerald shenzi kabisaa
nakuchukia wewe mwanaume kuliko
navyowachukia maadui zangu, umeniliza
mtoto wa mama yangu, nakuchukia Sana
Gery, kwa nini moyo ulimpenda mtu
Kama Gerald “ nililia Tena mwenzenu.
Daah huyu Gery huyu?
Sehemu ya 11
Mira alipata tabu kunibembeleza upya
maana anajua kifuatacho Ni kulia Tena, akaona Bora ampigie simu huyo Gerald
anaetunyima amani.
“ Ami hatimae umenitafuta mwenyewe”
maneno ya kwanza kutoka kwa Gery
hakujua hata anaeongea nae Ni Nani?.
“ Anaachaje kukutafuta kwa mfano, nilikuamini kupita kiasi na kujua labda
utamthaminisha kabisa rafiki yangu Ila
mwisho wa siku umefanya nini? Kila
muda analia tu, nahisi kukutukana sema
unanizidi umri natamani nikuheshimu Ila
umenivunja moyo nifanye nini Sasa?”
Mira alivurugwa yaani akajikuta
anaongea kila kilichotoka moyoni mwake.
“ Sikua Shem, yule mwanmke mlieongea nae Jana alikua dada yangu, najua ni vigumu kuamini, Ila Mimi wiki ijayo
ntakua free juma mosi nakuja huko, ntamchukua Ami namleta huku aje
kuonana nae! Siwezi kuhangaishwa na fikra zenu mbaya juu yangu” alimjibu
Mira ambae sikumpa nafasi ya kuongea tena.
“ Gery acha uongo vipi Kama ukimtafuta mtu mwingine na kumpanga, kwa kweli
mi nahisi kukuchukia nimefanya maamuzi
yangu mwenyewe na hata hivyo sijawahi
kukwambia Kama nakupenda”
nilimwambia kwa sauti huku nalia Mira
aliona Bora tu anipatie simu moja kwa
moja.kisha akatoka zake nje
“ Ami mama…” Dah sauti aliyotumia
kuniita uwiii ilininyamazisha kwa muda.
“ Usiniite hivyo”
“ Usikasirike mama angu mi nawezaje
kukufanyia hivyo, mi naempenda Ni
wewe tu”
“ Sikupendi Gerald hata hivyo sijawahi
Kiri Hilo kwako acha kujichosha nafsi
yako” nilizidi kulia Ila kimya kimya.
“ Ami Gery anakupenda Sana wewe, Hana mwingine kabisa niamini Mimi”
“ Gery nawezaje Sasa wakati alipokea simu yako mwanamke na kusema upo bafuni Maji yalikua yakitiririka
utamdanganya Nani? Gerald labda mtoto mdogo”.
“ Ami wewe sio mtoto mdogo we ni mwanamke wangu na ninakuheshimu Sana tafadhari “ niliguna.
“ Gery utafanya kitu gani kunifanya nikuamini”
“ Ami ntafanya chochote kile kuliweka salama Penzi letu”
“ Gery Ni kwamba unamaanisha?”
“ Kwani Ami we hunipendi?” Swali lake
lilinipa kimya.
“ Ami….” Aliniita nikaitikia kidogo.
“ Najua huna jibu kwangu ila mwenzako kweli Tena nakupenda Sana” nilikaa
kimya Tena na ye akawa kimya.
Tulibaki kusikiliza mapigo ya moyo ya kila mmoja wetu ahaha.
“ Ami… Mi nakata simu, Ila katika moyo na fikra zako’ kaaa ukijua na kuamini
hakuna mtu anaekupenda Sana hapa
duniani zaidi ya Gerald sawa”
“ Gery Mimi…. Ki ukweli sidhani Kama
nafaa kua kwenye mahusiano wakati
huu” nilimwambia hivyo Ila ukweli moyo
wangu ulikua tayari kua na mahusiano
Tena sio tu mahusiano kua kwenye
mahusiano na Gerald ki ufupi moyo
wangu upo tayari sema mdomo unakana
“ Ami Ni sawa, lakini mi nakupenda, actually I run all the world in love, but now I fall for you” aliponambia hivyo
nikasahau Kama tuligombana mchana
huo huo. Na machozi yangu yote kwisha
nikawa kimya nyie Kuna watu wanajua
kubembeleza ndo maana alinidanganya
nikawa mrahisi Hadi kuvua nguo zangu
aiii! Gery huyu.
“ Gerald mi kwa Sasa na kazi, tutaongea baadae bhana” nilimuaga Ila
bado nilitaka kumsikiliza
“ Sawa mrembo wangu, unaendesha
moyo wangu kwa usukani Sina njia
mbadala ya kuishi bila uwepo wako
kwenye haya Maisha , alafu imetokea
ghafla tu” nililainika kweli wasichana
tuna danganyika mapema Sana.
Haya bhana alinipa maneno matamu
hapo mwishowe nikajikuta nabadili kila
aina ya pozi kwa kumsikiliza yeye tu,
kila sifa aliyokua akinipa nilikua navimba
bichwa mtoto wa kike. Gerald ana laana
huyu hakuona mwanamke mwingine wa
kumzuzua zaidi yangu kweli. Hatimae alikata simu nikabaki natabasamu tu.
Mira alifika akakuta nacheka cheka wakati aliniacha na kilio Cha Hali ya juu’.
“ Kwa hiyo nyie wawili tayari? Tofauti zimeisha kabisa”
“ Ndio Mira hata sielewi kwa nini nipo
mdhaifu kushinda kila kitu”
“ Because your in love with him. Your Gery your own Gery.”
Baadae majira ya jioni kabisa tulitoka na kwenda kwenye mizunguko yetu ya
uzurulaji si unajua Tena mtu kukaa tu
nayo haivutii kabisa. Tulitembea tembea huku tunakula miguu ya kuku.
Na vikachori tulikua na ka pesa kiasi
Fulani kwenye mikono yetu.
Wakati tunarejea nyumbani Kuna kijana
ghafla majira ya saa moja akaziba njia yetu, Mira akanitazama Nami nikabaki
kumwangalia kwa sio mimi Wala yeye
tulimfahamu huyo kaka.
“ We Kaka vipi?” Nilihoj kaka
“ Samahani sister naomba tuongee”
aliniambia Mimi nikajisontea kidole
kuhakiki.iwapo Ni Mimi ama?”.
“ Ndio Ni wewe, hakika natamani Sana
kuzungumza Jambo na wewe sio kwa
ubaya lakini tafadhari Kama hutojari. “
Nilimwangalia Mira ambae alitingisha
kichwa chake kuashiria nikubali tu.
Hata hivyo Ni maongezi tu na sio kingine.
Tulisogea pembeni kidogo na Mira yule
kijana alionekana mrefu’ kiasi hakuweza
kumfikia hata Gery wangu.
“ Mambo naitwa Abel. Dada ujue hii ni siku ya tatu tangu nianze kukufatilia
sema wewe unapenda Sana kushinda
ndani?” haya Sasa Kuna kina Abel Tena
hapa ngoja nimsikie, nilitega sikio langu
kwa Makini.
Sehemu ya 12
“ Haya nakusikiliza” nilimwambia.
“ Najua unanisikiliza Ila naomba pia unielewe ki ufupi, nimevutiwa na wewe”
“Mmhh” nilitumbua macho nyie acheni tu.
“ Ni kweli sijui hata jina lako
unaitwa.nani lakini natamani
kufahamiana Zaid na wewe”
“ Hapana sipo tayari Nina Mambo mengi
Sana hivi Sasa, nao fahamiana nao
wananitosha” nilimjibu bila huruma
nikaanza kuondoka akaushika mkono
wangu.
“ Hapana dada yangu, siwezi ruhusu uende hivi hivi naomba hata namba yako
ya simu “ aliongea kinyooonge nikawa namkwepa.
“ Simu Mimi Sina unaweza kunipa nafasi
nijiondokee ndugu yangu”
“ Tafadhari” akaung’ang’ania mkono wangu, Mira akaona hapa tunaweza
maliza masaa matatu akaja
akauachanisha mkono wangu na huyo kijana Kisha akamwambia.
“ Usijari, nambaa hii hapa, utatutafuta” alimpa simu aandike namba
Yake kwenye simu yetu. Nilimtolea Mira
macho kuashiria sipo tayari kabisa
akanikonyeza nikatulia kwani sikuelewa maana yake.
“ Asante Sana dada yangu, sema rafiki
yako mkali hataki hata ukaribu na
Mimi” alijipigia na namba yetu ikaingia
kwenye simu Yake. Kisha akaondoka
huku anachekelea. Nilipagawa na
kumwangalia Mira baada ya yule Kaka
kuishia zake.
“ Usiniangalie hivyo Nina mpango wangu”
Mira alitabasamu nikamuacha
Baada ya siku mbili yule Kaka tayari
nilikua nawasiliana nae hakua
amenitongoza Kama nilivyofikiri hapo
mwanzo aliomba urafiki tu. Sikua na njia ya kumkataa kwani Mira aliniambia
mpango wake. Alitaka kuamini iwapo
kweli Gerald ananifatilia.
“ Kwa hiyo leo tunaenda mtoko wa Abel?”
“ Naanzaje kukosa ofa Kama hiyo, huyo
Gery atakoma nataka nione atafanya
nini si alinitisha kua atanitafuna nyama
iwapo akiniona na mtu Sasa tuone
atafanya nini?.”
Tulijiandaa na kutoka mtoko wa ghafla
siku hiyo. Tukiwa tumekaa kwenye baa
moja Mimi na Miracle tuliagiza vinywaji
laini pamoja na chips kuku. Jamani
tulijua kuitumia vibaya pesa niliyopewa
na Gery. Tulikua tukila tunavyotaka
wakati huo tunajua likizo ikiisha
tunarudi kwenye Dona letu Kama
kawaida.
“ Umelipia ?”
“ Awee, hebu kua na akili, naanzaje
kulipia wakati tupo na mwanaume hapa”
haa! Miracle mshenzi nikajua tuliitumia
pesa ya Gerald kumbe walaa. Ndo
kwanza tulimchuna Abel. Abel wakati huo alikua washroom kabla hajaturejea.
“ Huyu Kaka anajifanya Kama anataka
tu urafiki na wewe Ila ukweli
usiopingika Ni kwamba anakupenda
waziwazi” Mira aliniambia huku
akimwangalia Abel aliekua akirejea.
Nilitulia macho yangu kwake na kubaki nimemtazama.
“ Hata mi naona” nilijibu nikiwa bado
namwangalia. Kwa kweli alikua kijana mtanashati anaevutia alikua na
tabasamu Fulani la kipekee na weusi wa mfano, nikisema weusi wa mfano
nadhani naeleweka yaani ana weusi flani
hivi amazing waweza sema Ni brown
kala yaani ngozi yake inatreza. Alafu
alikua na lips za ‘M’
“ Mbona umeniangalia Sana” alinihoji
akitabasamu baada ya kufika upande
wangu.
“ Aahh labda anashangaa uzuri
ulioumbiwa, si unajua yeye kazoea
kujifungia ndani”
“ Mira acha utani, ningekua wa
kujifungia ndani angeniona vipi? Alafu
sikua nimekuuliza uliniona vip we Kaka?”
“ Nilikuona ulikua ukianika nguo”
“ Ooh! Safi Sana” nilimjibu na
kuendelea kula paja la kuku nikijiamini.
Baadae nikashika glass nimimine peps
yangu ninywe nikaweka glass mdomo
funda la kwanza. Nikatulia nakuendelea
kupiga story. Ile naweka mdomoni kwa
Mara ya pili nilijikuta natema soda bila kutarajia.
“ Vipi?” Miracle alinihoji nikabaki Sina hata nguvu za kuongea.
“ Amina upo sawa” Abel aliinuka kwenye kiti alichokua amekaa akaja kuanza
kunipiga piga mgongoni Kama ntakua na
tatizo labda nimepaliwa Basi nitulie.
Mwenzao sikua hata na hizo shida zote
isipokua tu daah! Niseme nini Sasa?
Nilishindwa Cha kuongea na kuishia kupata kwikwi za ghafla.
“ Ujue sikuelewi?” Miracle
alichanganyikiwa na Mimi akinitumbulia macho jamani nyie. Nilimpa ishara kwa
Macho yangu ya kungu ishara afatishe macho yangu yalipokodolea.
Alifanya hivyo weee!! Hee Miracle aligeuza shingo Yake na ghafla
akairejesha kuniangalia Mimi niliekua
nabembelezwa na Abel kua nitulie.
Maana aliamini nimepata mshtuko. Ni
kweli nilikua na mshtuko sikuweza
kupindisha macho yangu na yalipokua
yamegeukia.
Mbele yangu kulikua na meza ambayo alikaa mwanaume mrefu’ mwembamba
kiasi mweupe na alivaa miwani.
Alikumbatia kiti na kuangalia upande
ambao tulikaa sisi. Hakukwepesha
macho yake yaani muda wote
alinitazama Mimi. Wee nilihisi
kupagawa.
“ Abel Asante Asante naomba niende
washroom” ilinilazimu kuaga nisingeweza
kuangaliana na huyo jinamizi aliekua
mbele yangu masaa yote. Bora
nimkwepe tu. Nikainuka na kuondoka
zangu.
“ Kua Makini Amina “ aliniambia Abel
nikatamani kuzimia huo umakini nautoa
wapi Sasa? Nilifika washroom na
kuanza kuzunguka zunguka bila Cha
kufanya. “ Ukimaliza kuzunguka na
kuvuta harufu yote ya huku uje hapa
tuzungumze” sauti ya kiume ilisikika
kutokea mlangoni nikabaki hoi.
“ Gerald umekuja vipi hapa? Huoni
mlangoni pameandikwa ladies au hujui
kusoma kiingereza, Basi angalia mdoli
uliopo kwenye mchoro Ni jinsia ya kike”
nilimkumbusha huyo mpuuzi aliekua
akiniangalia. Aliweza tu kunijibu jibu
moja “ sawa” Kisha akaingia kabisa mle
ndani na kuushika mkono wangu
nimfate.
“ Gery niache, unanipeleka wapi?”
Sikutaka anipelekeshe.
“ Ukileta ubishi nakupiga makofi hapa
hapa huoni aibu kushikwa shikwa na wanaume baa!” Gery alinifokea nyie
nikahisi kupauka nikiwa nimeganda
nimeshikwa shikwa saa NGAPI Mimi?.
Aliweza tu kunivuta mkono wangu
nikajikuta namfata bila kutegemea.
Sehemu ya 13
Tulitembea mpaka nje ya baa kwa
kupitia mlango tofauti na aliokuepo
Mira. Wakati huo Ni majira ya saa
moja mwenzenu tayari nilimuogopa
Gerald Ila sikujizuia kumfata. Tulifika
parking Kuna gari moja ilisogea karibu
yetu, alikuwepo yule mwanaume ambae
nilimuona siku ya kwanza kabisa
nimeenda na Gerald kwenye nyumba
ambayo siwezi isahau Kisha akampatia
Gery funguo. Mlango wa gari
ulifunguliwa nikakalishwa kwenye siti
kwa nguvu jamani nilitamani kulia.
“ Gerald kwa nini unanifanyia hivi?
Unahisi unanipeleka wapi labda ntapiga
kelele unaniteka” nilimwambia huku
nikitoa sauti ya huzuni Wala hakunijari
huyo mtu mzima hovyo. Hata sielewi
Mimi amefika huku saa NGAPI? Si
alikua dar huyu? Au kwa kua dar na Moro sio mbali hiyo ndo sababu kuu.
Alifungua mlango wa gari akakaa
kwenye siti ya dereva akaanza
kuendesha, aliendesha gari pale
taratiibu kutoka hapo mpaka barabarani
nikawa na muwaza zangu Mira Sasa
atajua wapi nipo? Nikiwa namuwazia
simu ya Gerald ikaita. Sikujua Nani
kapiga ila nilitupiwa simu utadhani
alilazimishwa anipatie.
“ Mmh” niliishia kuguna bila kufanya
lolote.
“ Mwambie tumeondoka, na leo hurudi nyumbani”
“ Nini?” Nilishtuka sirudi nyumbani hiyo inamaana gani? Naenda kulala na yeye
au hapana kwa kweli sipo tayari
kufanya Hilo. Sura yangu ilibadirika nikatamani.kumla nyama mbichi.
“ Hutaki kupokea” alinifokea nikajikuta
naanza kulia. “ Gerald nakuchukia
unanichukulia Mimi Kama toy lako la kufanya uhasherati siwezi kulala na wewe Tena. Nimenyamaza kimya.muda
wote kwa sababu nilikumiss natamani
kupata muda wa kuongea na wewe pia
Ila wewe umekuja kwa Kasi ya ajabu
Sana na unanifanyia makusudi
yasiyostahili” nililia hapo simu iliyokua
ikiita ilikata na kuita Tena. Aliekua
akipiga alikua Mira. Gerald hakunijibu
kitu licha ya kilio changu aliokota simu na kuipokea.
“ Gerald upo na?”
“ Ndio nipo nae na harudi nyumbani
usiku wa leo unaweza kurudi pekee yako
usiku wa leo tafadhari” Gerald Gerald
Gerald nilijikuta namuita Mara tatu kwa
Nini anifanyie hivyo?. Nilianza kulia.
Mira akasikia.
“ Sasa kwa Nini analia?”
“ Amina yupo salama mi si mpenzi wake ama?”
“ Sawa lakini kulingana na Hali yake.
“ We jitahidi kuwahi kurudi nyumbani”
Gerald alikata simu hakutaka kuongea
zaidi na Miracle nilichukia na.kuzidi
kulia. Baadae hatimae gari iliwasili
kwenye nyumba ileile ambayo nilipoteza
usichana wangu siwezi sahau hiyo
kumbukumbu mbaya kabisa.
Alifungua mlango wa gari baada ya kuingiza gari ndani, Kisha akazunguka upande wangu kunifungulia mlango.
“ Shuka” aliniambia nikabaki nimekaa bila kumjari.
“ Shuka Ami” sikumjibu akaona suluhisho Ni kunishusha kwa nguvu.
Alinibeba kwa nguvu kunitoa humo nikawa napiga kelele.
“ Kwa Nini Gerald unifanyie hivi? Kwani
Mimi sio mke wako sio dada yako, sio
yeyote kwako lakini unanifanyia Mambo
ambayo hayatakiwi”
“ Wewe ni Ami wangu, Amina wa Gerald ukisema sio yeyote kwako hiyo ni juu yako kwa nini nikuone karibu na mwanaume mwingine alafu nikae kimya, sikukuzuia wewe kwamba sitaki kukuona na mtu lakini ukaenda kinyume”
“Haa! Hilo nalo kosa, hiyo inamaanisha
hata ndugu zangu wa kiume Sina ruksa ya kua nao karibu. Tena ukome
kunifatilia Maisha yangu, kwa Nini
ulitokea kwenye Maisha yangu we upepo wa kisurisuri.” Nilimlaani wakati huo
tayari tumefika ndani mwenzenu
nilitupwa kwenye sofa.
“Funga mdomo wako” aliniambia Kisha
akaniacha hapo na kulock milango vizuri
hakutaka nitoroke kabisa.
“ Gerald usiku huu kwa Nini umenileta
hapa?” Nilimfata nyuma nikiwa na hasira nae, Ni usiku Sana alafu nipo na mwanaume. Nilijikuta namkumbuka
mama yangu jamani.
Mimi Ni mtoto wa kike wa pekee kabisa
nyumbani kwetu waliobaki wote wa kiume japo ninae mdogo wangu wa kiume Ila mi nilikua Kama mtoto wa mwisho.
Kaka zangu walikua na familia zao Ila
walihangaika kunisomesha alafu litoto la mtu linafanya Kama limenioa nimekua
mke wake.. “ nakulaani Gery” nilipiga
kelele kwa Gerald aliekua jikoni anapika
Nikiwa nimesimama pembeni yake namwangalia kwa hasira.
“ Ni sawa Ami Ila Gery anakupenda
Sana kila siku nakwambia na ntabaki kukwambia kabisa uelewe Hilo.
Anaekupenda wewe ni Gery”
“ Funga mdomo wako, kwani wewe hukuona mwanamke mwingine zaidi
yangu katika hii dunia??” Nilipiga kelele sema hakukua na watu wengine mle ndani na Hilo lilinitishia amani kabisa.
“ Na wewe ulikosa mtu wa kumpa
usichana wako zaidi yangu Mimi? Sio
kosa langu kukufanya uwe bikra mpaka
nilipokuanza Mimi” aliongea kwa ujasiri
kana kwamba alikua kwenye haki
nilipata aibu jamani ? Kwa Nini Gerald
alizaliwa kwenye hii dunia. Uso wangu
uliwaka kwa hasira na maumivu wakati
mmoja. Nilianza kulia bila kujari uwepo wake.
Sehemu ya 14
Nilijikuta nakaa kwenye kiti kilichokua
karibu na alipo yeye huyo mpishi aliekua
anapika ndizi za kichaga. Alisogeza kiti
baada ya kunawa mikono yake na kukaa
mbele yangu nikiwa bado nalia. Aliishika
mikono yangu na kuiweka kifuani kwake.
Nilihisi kuyasikia mapigo ya moyo wake
nikajikuta nakaa kimya ili nijue shida yake.
“ Ami wangu. Ki ufupi Gery, anakupenda
Sana, unapokua karibu yangu moyo
wangu unasikika hivyo sio tu kukupenda
yaani Ni kwamba kwako nipo mzima.
Najua wewe ni mwanafunzi lakini siogopi
Sheria yoyote itakayonihukumu kwa
kukuchukua Kama mke kwa muda wa wiki moja nisamehe mama angu””
Nini?? Aahaa? Huyu Gery wenu bila
Shaka alikua akipata kichaa alipanga
kunifanya mke wake kwa muda wa wiki nzima. Hapana bila Shaka alikua
alitania sikua na Imani na Hilo kabisa
labda alitania jamani? Hakua serious mi sikua mtu wa aina hiyo! Wakati huo uso
wangu uliganda kumwangalia huyo
mwanaume asie na aibu kabisa.
nikiwa
nadondosha machozi mwenzenu nilikua
mgeni kabisa kwenye ulimwengu wa
mapenzi hebu angetokea mtu jamani
akaniambia kabisa. Ami mapenzi huwa
hayaendi hivyo mapenzi ni kukubaliana
na kueleweshana
“ I love you” aliniambia
“ Usiwaze Sana. Nenda chumbani
kaoge, Kuna baadhi ya nguo nilikuletea wakati nakuja”
“ Siingii kwenye chumba Cha mwanaume
nisie mfahamu” nilimjibu kwa jeuri na kuzidi kukaa. Aliniangalia kwa jicho la dhihaka akiwa na mfarakano moyoni
mwake, kwani aliwaza nini dhidi yangu
kwenye kichwa chake. “ Potelea mbali , sijari kabisa kuhusu sura yako
isiyoeleweka” nilimwambia hakuweza
kujibu chochote.
Hatimae alimaliza kupika na kuandaa
mezani akaniita nile. Sawa nilikua na
shida dhidi yake sikua na shida na
chakula hata hivyo mi Ni mpenda kula
japo huwa sinenepi Ila napenda vitamu
Sana ahaha! Hata Summy ananielewa
vyema. Aahh! Alafu sijawaambia
Summy Ni Nani? Summy Ni Sumaiya
rafiki yangu yaani rafiki yangu kabisa..
Kuanzia kidato tuko pamoja. Ule
urafiki wa kugombana na kununiana na
kusameheana tumeupitia wenzenu.
Pamoja na Miracle. Ila wakati huo yeye
hakua na sisi katika shule moja. Alikua
akisoma chuo huko Moshi. Na sisi
tulibahatika kwenda shule moja.
Tukiunganisha akili zetu Mimi na
Miracle tukijumlisha summy unaweza
pata mwendawazimu mmoja
alieshindikana. Kwa Sasa ukitaka
kumpata Sumaiya. Ingia Facebook
andika #Simulizi za Sumaiya utampata
huko utakutana na visa na Mikasa
motomoto kutoka kwenye kichwa Cha
huyo mtoto wa kike ambae Ni rafiki
yangu. Mimi na ndo mwandishi halali wa mkasa wangu. Acha niendelee kuwapa
story Sasa kuhusu Mimi na Gery.
Haya bhana baada ya kula sikujisumbua
kuinuka eti nitoe vyombo nikaoshe hee!
Nani kasema mi mtumishi wake kwani?
Alifanya mwenyewe nikiwa nimekaa bila
Cha kufanya hapo. Hatimae alinirejea
akasimama nyuma yangu. Nilitetemeka
kwa uwoga mwenzenu nikabaki Sina Cha
kufanya zaidi ya kupumua kwa nguvu.
“ Mmhhff” nilivyopumua hivyo akanihoji.
“Nakusisimua Sana?” Swali lake lilikua
rahisi iwapo ningekua na ujasiri wa
Kutamka neno ‘sana’ Ila Sasa ujasiri
wangu ulikua sifuri kumjibu vizuri. Ila
kwa kumsema navyojisikia sikua na uwoga kabisa. “ Unanitia kichefuchefu”
sikua namuona kwani alikua nyuma yangu
Ila najua Sana kua sura Yake
ilibadirika rangi maana nilihisi kifua
chake kikipanda na kushuka.
“ Ami “ nilishtuka maana sauti na pumzi
Yake vilisikika kwa ukaribu zaidi
masikioni mwangu. Ki ufupi nilihisi
kusisimkwa zaid kila nilipopata
kumbukumbu juu ya siku aliyonitoa
usichana wangu.
“ Toka hapa” niliinuka na kutaka
kusogea sebureni akaushika mkono
wangu na kunivuta kifuani kwake. Nyie
mwenzenu mwili uliwaka Kama
transfoma ya umeme. Ilikua hisia ya aina gani hii? “Nakupenda” aliongea
Hilo neno kila wakati kana kwamba
alizoea kuongea hivyo. Nilikua kimya
kwani ningesema Nini zaidi.
“ Kaoge, haraka Sana, nenda chumbani ukaoge” aliniambia baada ya kumuachia mwenzenu wakati huo nilihisi unyevu nyevu maeneo fulani.
“ Mwanzo nilikwambia kabisa siingii
kwenye chumba Cha mwanaume nisiemfahamu” nilisubiri jibu lake hata
kwa mwonekano. Alitabasamu na
kunisogelea. Alinishika vyema kiunoni na kuanza kunibusu. Kwa nguvu nikawa
nahangaika hapo aniachie kwa Nini
anifanyie haya nilianza kumsukuma kwa
nguvu.
“ Unafanya nini?” Niliongea baada ya kupata upenyo Ila hakuniacha muda
mrefu’ aliudaka Tena mdomo wangu na kuanza kunibusu.. alinibusu’ karibu nusu
saa nzima jamani mdomo wangu Ni
Kama vile ulichemshwa Maji ya Moto, ndipo akaniachia. Nilipumua kwa nguvu
kwani tayari nilikosa pumzi.
“ Kwa Nini upo Kama mzimu?”
Nilimwambia.
“ Nataka nikukumbushe kua unanifahamu Tena sio kidogo” aliniambia
sikuelewa maana yake. Najuta kwa Nini
nilizaliwa na umbile dogo kwani Gery
alinichukulia anavyotaka. Alinivuta na kuninyanyua mikononi mwake mpaka
chumbani. Kisha akanitupia kitandani
“ Gerald unataka kufanya nini? Sipo
tayari kwa Hilo” niliogopa Ila yeye
hakua ananijari, alianza kuvua nguo
zake nyepesi na kunisogelea nilipata
uwoga kadri alivyofanya Hilo jambo.
Kwa nini alikua mkatili Sana kwangu?
Nililia mwanzo Ila baada ya yeye
kuanza alichokidhamiria hatimae
nilijikuta napata uzoefu na kutamani
aendelee na asiache japo sura yangu
haikumuonyesha Hilo.
Sehemu ya 15
Daah asikwambie mtu nilitulia baada ya
Gery kufanya nizoee tukio Hilo kwa
muda japo nilipata maumivu kwani sikua
nimezoea, Ila alikua akitumia trick za
kufanya nitulie na sisikie maumivu
makali Sana.
Hatimae baadae tulimaliza tulichokianza
ukweli nilijifanya kununa japo
nilifurahia. Mwenzenu nilisahau Kama
nasoma nilisahau kabisa Kama Mimi Ni
mwanafunzi. Nilijikuta mke wa Gery
kwa wakati huo. Gery aliutazama uso
wangu ulioonekana kuvurugwa kwa
kilichotokea sikutaka aonyeshe unafiki
wake wa kujari kwa hiyo niliusukuma
mkono wake mbali na alipokua akitaka
kuuweka. Hatimae niliinuka na kwenda
bafuni kuoga. Baada ya kuoga nilivaa
nguo huko huko sikutaka Mambo ya
kuoneana hapa hata Kama ameninaniliuu
lakini hainamaana anichungulie
anavyotaka. Kisha nikatoka bafuni
nikiwa na vazi la kulalia la hariri hakika
lilinikaa vilivyo. Kisha nikaelekea
mlangoni nitoke nje wakati huo yeye
alikua bafuni. Sikutaka kumsemesha
hata yeye alijua Hilo.
Nilijaribu kufungua mlango ili nitoke nje ya hicho chumba. Aiyaa mlango
ulifungwa. “ Gery umefunga mlango
Mara hii”
“ Unapiga kelele kwa Nini?” Alinihoji.
Nilisogea Hadi kwenye mlango wa bafu na kuanza kuupiga kwa nguvu
ikiwezekana atoke nje kabisa kwa Nini
afunge mlango .
“ Ujue nilipo Sina nguo”
“ Kwa hiyo nikusaidie Nini? Naomba
funguo sitaki kuishi nyumba moja na
wewe hata kwa dakika sembuse chumba
kimoja.” Nililalamika. Gery akafungua
mlango jumla na kutoka nje ya bafu
akiwa Hana nguo kweli.
“ Gerald!!” MAPIGO ya moyo wangu
yaliruka Kasi kwa kumuona hatimae
nikaziba uso wangu kwa viganja vya
mikono yangu.
“ Usijari huu mwili Ni wako siku zote”
aliniambia nikahisi kulia hakua
mwanaume mwenye mshipa wa aibu hata
kidogo. Hatimae alinikumbatia akiwa
Ameloa Maji mwili mzima.
“ Gerald unafanya nini wewe? Sii tu Kama hukuvaa nguo wakati unatoka nje
lakini bado unaoujasiri wa kunikumbatia.
Nililalamika dhidi Yake.
.” Kwa sababu ulinimiss kwa dakika
kadhaa baada yaa.. kwa hiyo
sitaruhusu hilo Tena”
Hatimae nilijikuta bafuni Tena kwa
Gery. Nyie mapenzi haya Ni upofu
kabisa mtoto wa kike nilijisahau Mimi
na bado mwanafunzi nilikua Kama
kimdoli Cha Gery. Kisha tulilala kimya
baada ya Mambo mengi kufanyika usiku
huo.
Kesho yake kulipambazuka yule
mwanaume ambae sikujua Ni Nani yake
Gerald aliwasili nikiwa ndo nimemaliza
kufanya usafi. Ukweli Ni kwamba
nilimwambia Gerald siwezi kukaa nae
hata kwa dakika moja Ila ki ufupi
nilikaa kwa kuridhika.
“ Shem habari za asubuhi?” Alinisalimia
huyo mwanaume nikajikuta Sina njia
zaidi ya kuitikia tu.
“ Safi tu, karibu” nilitabasamu.
“ Usijari shemeji nimekaribia” alipita
moja kwa moja mpaka chumba Cha pili
ambacho kilifungwa na kwanzia nifike
hapo sikuwahi ingia. Alichukua baadhi
ya vitu Kisha akatoka akiwa anaongea na Gery wakati huo nimekaa nje kwenye bustani napungwa hewa.
“ Haya Shem mi naenda” aliniaga hapo
sikua na kinyongo kumuitikia.
“ Hapana huwezi ondoka wakati
sikuwahi kamilisha utambulisho kwa
pamoja” Gery aliongea na wakasogea
karibu yangu niliinuka bila kutaka na
kusalimiana na huyo mwanaume. Na siku
hiyo ndo nikajua jina lake aliitwa.
Brighton.
“ Ami yeye ni rafiki yangu na mmiliki wa hii nyumba, yaani sio tu Kama Ni
Kaka yangu, Mimi Bali ni rafiki yangu
ambae tumeamua kuutenga mbali undugu na kua marafiki wa kawaida”
“ Mmh nashukuru kukufahamu Brighton” nilimpa mkono wa Salam Kisha Gery
akanitambulisha kwake. Japo Brighton
alionekana kunifahamu tangu mwanzo.
Alitabasamu Kisha akaonyesha
uchangamfu kwa kufahamiana. Na hapo
aliweza tu kuondoka zake.
Siku zilisogea nikiishi na Gery ambae
alikua akimpigia simu Mira kila siku na kumpanga kua ntaenda kesho. Hatimae
wiki ilikata nikiwa kwake na mwisho
baada ya wiki kuisha ndo nikarejea
kwetu na Mira. Alinirejesha Gery
mwenyewe na kunipa onyo kadhaa kabla
sijashuka kwenye gari na kwenda ndani.
..” hakikisha haujichanganyi na mwanaume yeyote Yule bila uwepo wangu”.
“ Mmhh, nilijua tu huwezi badilika”
nilimwambia na kwenda zangu ndani
taratibu akaushika mkono wangu.
“ Ami namaanisha nachokwambia kwa
sababu hivi karibuni huenda tukapokea
taarifa za kushangaza kwa hiyo sitaki
unifikirie kwa ubaya, jiweke mbali na
wanaume wasiofaa. Jiweke chonjo na vishawishi ambavyo vitanitia mashaka”
baada ya yeye kuniambia hivyo sikua na haja ya kumsikiliza Tena kwani
niliezoea. Nilimsukumia huko na kuingia
zangu ndani baada ya kumuaga kwa
lugha nyepesi Sana.
“ Kwa heri, ashukuriwe Mungu
umeniacha huru” nilimwambia Hilo
akabaki kaniangalia mpaka naingia ndani.
“ Mwanampotevu hatimae umenikumbuka
rafiki yako , tayari nilikata tamaa juu
yako na ilibaki kidogo nimpigie simu
mama yako, sikua na imani Tena na
Gery. Na hapa nimemwambia jioni
ntampigia Kuna Jambo la msingi
namtaarifu.” Nilihisi kumwagiwa Maji
kichwani. Nini? Inamaana Mira aliwaza
Hadi Hilo Jambo.
Sehemu ya 16
“ Usishtuke bhana sijafanya kitu Kama
hicho na sikuwaza kufanya hivyo, Ila
nilipanga kuja hukohuko ulipo” aliniambia
nikashusha pumzi ndefu bila kutegemea.
“ Ami umekua mlaini Sana kana kwamba
ulikua ukioshwa maziwa na kupakwa
siagi kila siku” ki ufupi nilipata
mabadiliko kiasi mwilini mwangu kwani
kwa Gery nilikua Kama mwali.
“Mira we acha tu, nilikua kifungoni, Gery hakunipa hata nafasi ya kupumua
kwa amani, najua Ni ngumu kuelewa
hisia zangu, Ila ki ufupi nimepitia
wakati mgumu Sana kwa kukaa na
Gerald “ moyo wangu ulionyesha
kunisuta kwa nachokiongea Ni kweli
kabisa Kuna wakati alinikatisha tamaa
Ila ki ufupi atanielewa kua sikua na furaha.
“ Mmh! Sawa fanya Kama nimekuamini”
alipoongea hivyo nikaelewa kabisa Kama
kajua namdanganya. Huyo ndo Mimi na Mira mmoja akidanganya mwingine
anaelewa Bora kua muwazi tu.
“ Nikwambie vipi Sasa uniamini?”
Nilishuhsha sura yangu akabaki
ananiangalia kwa hatia.
“ Sawa Basi acha nikwambie tu” sikua na namna zaidi ya kumpa hadithi na mkasa wote ulionitokea juu yangu na
Gerald ki ufupi ilikua ya kuaibisha lakini
Sasa ningefanya Nini? Ndo hivyo siwezi
badili wakati nimejikuta nampenda Kama
kichaa’.
“
Ami usiniambie Kama umesahahu wewe ni Nani? Au wewe ni mwanafunzi bado?”
Alinipa onyo.
“ Mira nasahau vipi Sasa?”
Nilimwambia.
“ Mjinga Sana wewe umeishia kula
kuamka kushinda na kulala nyumba moja na mwanaume kwa wiki nzima alafu
bado unajiita binadamu wa kike ambae
Ni mwanafunzi kweli” alikasirika kiasi
kwamba alinitupia mto.
“ Mira ningefanya Nini sikua na njia nyingine tofauti na hiyo”
“ Kwa hiyo unataka kusema kulikua na ulazima wa kua mrahisi Sana kwake
ilhali alikuchukua kwa nguvu, ulifaa
kukataa na kukataa mpaka pale ambapo
nafsi zenu zingekubaliana moja kwa moja.”
“ Mira ki ufupi Mimi nampenda Sana
Gerald. Nimegundua hilo baada ya
kuishi nae kwa mudaa huu, japo mwanzo
nilimuona anakera ila kwa Sasa najikuta
sijari kuhusu matokeo yatakayonikuta”
Mira aliniangalia kwa huruma akabaki
kusikitika. “ Sio Kama nakuonea wivu
Ila nakuonea huruma Ami, Ni Mara
yako ya kwanza kuangukia kwa mtu
kimapenzi alafu umempa moyo wako
wote pamoja na mapenzi ndani ya muda
mfupi. Ki ukweli mtu kama huyo
akitokea kukuacha atakufanyia dharau
za hela yote. Ulifaa kua mgumu kwake”
Mira alikua sahihi kabisa kulingana na
maneno Yake alafu isitoshe aliwahi
kusalitiwa kabla lakini sikuamini Hilo
kuhusu Gerald. Niliamini hayupo Kama
wanaume wengine kabisa.
Siku zilisogea taratiibu huku nikizidi
kuonana na Abel huku nikiongea na
Gerald lakini sielewi kwa nini Gerald
alikua akigundua iwapo nimetoka na
Abel na alikua akinisema.
‘kwa Nini leo ulienda beach na
Fulani……nakwa nini ulivaa nguo fupi
Sana kwenda kwenye mkutano wa hadhara… Kwa Nini uliambatana na
Miracle kuzurura usiku…. Kwa Nini
ulienda sokoni ukiongozana na mwanaume…….’ Hakika hakuna chochote
ambacho nilifanya asijue ki ufupi alikua
akinifatilia Sana mpaka nikajikuta
namtukana kwa Nini aliamua kuniwekea
spy wa kunipeleleza kila wakati.
“ Umesikia wewe Kaka hebu fanya
ufate Maisha yako, kwa Sasa bado
tupo kama wapenzi tu hata mguu wako
kwetu hautambuliki Ila bado unataka
kuyaendesha Maisha yangu vile
utakavyo, nisahau na Mimi siwezi
kufikiria hata kidogo juu yako… Nina
mambo mengi Sana dah!” Nilimkatia
simu siku hiyo baada ya kumtolea uvivu.
Kwa kua nilizoea huwa anatabia ya
kunipigia simu hata nikipaniki tunaanza
kujibizana Basi siku hiyo ikapita.
Hatimae kulipambazuka bila kupokea
ujumbe Wala simu kutoka kwa Gerald.
Kesho Yake Tena. Siku tatu hatimae
wiki.
.duhh Ilibidi nimpigie Mimi alipokea
simu yangu na kunipa jibu ambalo
lilinikatisha tamaa ya kumpigia tena.
“ Nina kazi, Sina muda wa kuongea na binti mchafu Kama wewe” haaa! Nini?
Na baada ya hapo hakuongea Tena na Mimi alikata simu. Nilijikuta nakosa
nguvu mwili mzima. Nili nilikua Nini?
“ Eti Mimi nilikua mchafu?” Nilijikuta naongea. Nilikua mchafu, au Mira
alikua sahihi kua Penzi la kwanza sio la kuzamia mzima kwa sababu Lina umiza zaidi. Nilijikuta nalia bila kunyamaza.
Niliitwa mchafu na Gerald kwa sababu gani au kwa ajiri ipi labda mpaka
nikawa mchafu kwake? Kwani nilikosea.
Sehemu ya 17
Nilijiuliza Sana juu ya Hilo nikakosa
jibu. Kwa maana ipi labda Gery
kanambia hivyo au labda Nina kasoro?
Au Kuna kitu nimemkosea. Kwani
kumjibu kwa jeuri na kiburi siku Ile ndo
imekua sababu ya yeye kuniona Mimi
mchafu?
Sikua na jibu zaidi ya kupata maumivu
kimya kimya. Mara hii sikuthubutu kulia
hata kidogo Wala sikua na ujasiri wa
kumwambia Mira juu ya kilichotokea
kwangu. Sikua na furaha lakini
nililazimika kua na furaha japo kwa
kuigiza. Mira alikua akinipigisha story
na Mimi namjibu vile vyema zaidi ya alivyotaka lakini ukweli moyoni sikua
sawa hata kidogo. Ki ufupi nilikua
mrahisi Sana kwa Gerald ndo maana
kapata sababu ya kunitukana na kunisema kadri alivyojisikia. Hakika
niliweza kujidharau mwenyewe.
Siku zilienda Kasi hatimae tulifungua
shule tukarejea kumalizia masomo.
Daahh haikua kazi rahisi. Mwezi wa kwanza wa pili. Hatimae tulibakiza miezi michache zaidi.
Lakini wakati huo mwenzenu Kuna
mabadiliko ya ghafla Sana ambayo
yalinitokea Mimi. Yaani ki ufupi
nilinenepa kiasi. Nilibadirika Mimi Ni
mtu mwenye umbile dogo lakini ki ufupi
nilijihisi kabisa Nina ujauzito. Kwani
niliimaliza miezi kadhaa bila kuona siku
zangu, japo huwa inatokea lakini hii
Sasa ilikua too much.
‘ sitaki kuamini Kama Ni kweli ninao
ujauzito’ Ni hivyo yaani sikutaka
kuamini Hilo niliipinga nafsi yangu
isiwaze kua Nina ujauzito. Hata Kama
kwa dalili za nje iliniaminisha hivyo Ila
sikutaka kuamini Hilo.
“ Ami huonekani kua sawa. Kwa Sasa
umekua na makalio makubwa zaidi ya
mwanzo kifua chako kimejaa. Umbo
lako limejikata isivyoelezeka, uso wako
umekua na mng’ao Safi zaidi kupita
kawaida kana kwamba umeanza
kujichubua” Mira aliniambia nikabaki
kimya. Hayo yote yalikua kweli lakini
vipi ntasema kwamba najihisi mjamzito.
Bila Shaka Mira atang’ang’ana nipime na
Ni kitu ambacho siko tayari kabisa
kinihusishe.
“ Hata mimi najishangaa nahisi Ni kwa
sababu nimezoea mazingira ndo maana
nimekua na mwili wa kunenepa”
nilimwambia Mira aliebaki na Shaka
dhidi yangu Ila hakuthubutu kunihoji.
Ki ufupi nilijiweka bize Sana na masomo
sikutaka kufikiria juu ya Hali yangu
japo sirika ya kibinadamu haikunipa
nafasi, nilitamani Sana kuziona siku
zangu lakini haikuwezekana. Mwisho
mwezi wa tatu ukakata sijaona siku
zangu, wakati huo tunakaribia mitihani na hatimae nilipata mawazo zaidi
nilijaribu kusoma kwa bidii Ila ilikua
ngumu kwangu kusoma ki ufupi nilikua
kwenye wakati mgumu Sana nilio
sababishiwa na Gery.
Usiku mmoja AMBAO siwezi kuusahau
kabisa kwenye Maisha yangu nilikua
nimekaa kitandani namalizia kupanga
nguo niweze kulala. Alikuja Mira na
kukaa kando yangu aliniangalia kwa
Makini Sana nikajikuta nashindwa
kuuzuia mdomo wangu na kumhoji.
“ Kwa Nini unaniangalia hivyo Mira?”
“ Nimejikuta nakuonea huruma Sana
Ami. Najua huwezi kusema kwa sababu
unajitahidi kujiaminisha kua fikra zako
sio sahihi Ila wewe ndo upo sahihi lakini
unafanya makosa. Bora kuwahi kuliko
kuchelewa. Siwezi Kukuacha mwenyewe
katika hili ntaandamana na wewe kama
tulivyokua hapo mwanzo tukiwa O level.
Nakujua vyema unanijua vyema. Kwa
Nini nikutenge”
“ Sielewi maana yako bado” nilimtolea macho na kujiweka sawa kitandani.
Nilichukua blanket nijifunike akalitoa na kuliweka pembeni kabisa.
“ Miraaa… Nataka “ Sawa utalala, lakini sio kwa usiku huu” alinishika
mkono na Kisha akatoka nje na Mimi.
Nikajua labda alitaka tuongee mbali na wanafunzi wengine lakini haikua rahisi
hivyo. Kwa hiyo kitu alochokifanya Ni kunipeleka moja kwa moja mpaka chooni.
“ Kwani nilikwambia nataka kukojoa
mbona una kimuhemuhe wewe”
nilimsema.
“ Hukuniambia lakini ndo lengo langu mpenzi. Naomba mkojo wako hata Kama
hutaki”
“ Miraaa usiseme kua na wewe Ni sawa na wanafunzi wengine ya kwamba
unanishuku???.. nilipata hofu dhidi yake.
“ Sio Kama nakushuku Ami ninao
uhakika kabisa juu ya wanalosema watu.
Kweli wewe niii……, Ah sitaki kuongea
naomba tu mkojo wako hakuna mtu
huku” Mira alinifosi kwa kweli Mimi na yeye tulitoka mbali Sana tulichukuliana
zaidi ya ndugu yaani Ni marafiki
AMBAO tulishibana sana alikua kama
dada kwangu nilikua Kama dada kwake.
Hivyo niliweza tu kukojoa bila kujua
kusudio lake. Nilimpatia mkojo wangu
nikiwa na hofu kupindukia mwenzenu
Kisha akachukua kipimo Cha kwanza Cha
ujauzito nikabaki hoi…… “ inamaana
aliandaa” nilipata wasiwasi.
Alichomeka vipimo vitatu kwenye mkojo
kwa wakati mmoja. Mungu wangu!!!
Alivichukua baada ya kufanya upimaji
huo bila kunionyesha akavikagua
mwenyewe kwanza. Alipomaliza
kuvikagua akabaki amejishika shingo
yake Kisha akavitupa chooni na
kumwaga Maji kabisa.
“ Mira hiyo inamaana gani? Mimi ni ni mjamzito??? Nilimuuliza kwa shahuku ya kujua iwapo kweli ntakua mjamzito basi nizimie kabisa. Aliniangalia akiwa na khofu kidogo Kisha akanipa jibu moja kwa moja. “ Ami actually upo safe kabisaaaa.. kua na Amani, puuza juu ya
maneno Yao” aliniambia hivyo nikahisi
moyo wangu ukipasuka kwa furaha.. hivi kweli alimaanisha? Aisee siamini.
Huenda Ni kweli.
Sehemu ya 18
“ Kwa Sasa unafaa kutuliza akili yako na kujiweka moja kwa moja kwenye
masomo, hufai kuwaza kabisa juu ya
Maneno au mabadiliko uliyonayo hivi
Sasa, sahau KUHUSU Gery sahau
KUHUSU kidudu penzi kilichojitokeza
hivi karibuni, waza masomo Kisha
tusonge pamoja” aliniambia point
ambayo iliniingia akilini sio Siri.
Mira Ni rafiki yangu jamani rafiki wa kweli rafiki wa dhati, sijui niseme Nini?
Sio tu katika hadithi Bali Maisha halisi, Ni rafiki ambae hakuwahi kutuacha
nyuma rafiki zake, kwa kweli Mira
alijaaliwa upeo wa fikra na maneno
mazuri juu ya sisi, tunalingana ki umri
lakini utakuta tunamchukulia Kama dada
yetu, ki ufupi kila mkubwa anamkubwa
wake hata kwenye kundi la wadogo
wenzake. Nilijikuta namkumbatia bila
kutoa kauli kwani alinimaliza wasiwasi japo haikua Sana.
Nilijiweka bize na masomo.mwenzenu.
hatimae mitihiani iliwadia tukafanya
mitihani kwa pamoja kwa muda
uliopangwa. Nilijikita Sana katika
kufanya mitihani Ila afya yangu ilikua
isiyoeleweka hivyo ilinisumbua. Hatimae
ulibaki mtihani mmoja kabisa au tuseme
mtihani wa mwisho kabisa.
Siku hiyo nililala usingizi ambao kiufupi, sikua nimewahi kulala usingizi Kama ule
tangu niwepo shuleni. Tulikua na mtihani mchana, hiyo ndo ilikua bahati yangu.
Mira aliniamsha kadri alivyoweza, Ila niliweza tu kuitikia bila kuamka.
maswali kibao kwenye vichwa vya watu’
Mira alikua na khofu juu yangu Ila Mimi
niliishia kumsikia na kujaribu kujitahidi
kuinuka lakini ikashindikana sikua na jinsi zaidi ya kuchagua kulala zaidi.
Nyie acheni tu….
Nilikuja kuamka Bado nusu saa tuingie
kwenye mtihani, watu wote waliniangalia
“ Amii,, ulalaji wako wa Leo utaacha
Mimi na kubaki na sintofahamu kwenye
vichwa vyao. Nilishika mswaki na
kujifunga vyema khanga yangu kifuani, daah nikaiona nzito haraka Sana
nikaifunga kiunoni na kuacha kifua
kikiwa wazi, hata hivyo Ni hostel ya wasichana. Nikaanza kutembea
kuelekea bafuni nikapige mswaki nioge na kuoga. Nilipofika bafuni nikaingia
chumba moja wapo kwa ajiri ya kujipa
huduma, nikiwa bafuni nikaanza kusikia minong’ono ya watu.
“ Kabla hatujaanza mitihani, Jamila
aliwavizia Mira na Ami bafuni kujua
Nini kitaendelea lakini Ni Kama Ami
hakua na mimba ! Au Jamila alisikia
vibaya?” Sauti hiyo ilikua sauti ya mwanafunzi niliemfahamu kabisa.
“ Ni kweli hata Mimi nahisi Kuna Jambo halipo sawa,, ulalaji wa Ami, ukiachana na mabadiliko mwilini mwake huwezi
kuangalia hata chuchu zake, zimekua kubwa na nyeusiiii,,, sidhani Kama Hana
ujauzito yule dada”
“ Baahati iliyoje? Angalau anamaliza zake mtihani anaondoka na Kuondoka,
matamanio ningepata fursa Kama hiyo,”
“ Hivi we una akili wewe, huyo Ami
unadhani kwao wanachochote, hapo
alipo anategemea kusomeshwa na ndugu
zake, usichukulia life kua easy, najua atasota”
Mmhh waliendelea kunijadili vyema
kwelikweli, ikabidi kwanza nikague
chuchu zangu ambazo zilikua zikiwasha
na kuuma kwa wakati mmoja Hadi
khanga nilihisi Kama inanisumbua, alafu
zilikua nyeusiiiii… Ki ufupi nilihisi kupata
uhakika wa hisia zangu potovu, niliamni
kabla kua mimi sikua mjamzito kwa
sababu sikutaka kuupokea ukweli, lakini
katika dunia hakuna ukweli mbaya kama
mimba, Ni haijifichi nyie Ni tobo la
kuvuja.
“ Hapana hapana Mira alisema Sina na kweli Sina, Mira hawezi kua muongo”
nilijipa Imani Ile Ile Kisha nikajiweka
sawa baada ya kuoga. Kizuri Ni kwamba
tumbo langu halikua likichomoza. Baada ya kujiandaa na kuvaa kisawa sawa
hatimae tuliingia kwenye chumba Cha
mtihani na kufata utaratibu Kama
kawaida.
Nikiwa nafanya mtihani nilijikuta
nafikiria Mambo mengi Sana, niliwaza
iwapo kweli Mimi ni mjamzito?
Nitasema Nini nyumbani? Nitawaambia
Nini kaka zangu? Nitafanya nini kwa
mama yangu kwa aibu hii niliyomtia?
Nikizingatia wakati huo Gerald hataki
hata hata MAWASILIANO na Mimi?
Aliniita Mimi mchafu?? Daahh!!
Nilishindwa kuyazuia machozi ambayo
yalidondokea kwenye booklet niliyotumia
kufanya mtihani.
Lakini hatimae nilimaliza mtihani, ambao niliufanya kwa machungu mengi Sana.
Muda haukua umeisha nikalazimika
kuusubiri muda, mwenzenu nililia kwenye
chumba Cha mtihani nikiwa nasubiri
muda uishe, hatimae Kuna msimamizi
mmoja aliniona akaja nilipokua Mimi?.
“ Vipi mwanafunzi? Mbona unalia
kwenye chumba Cha mtihani ? Hujui
Kama unavunja Sheria?” Alinihoji huyo
msimamizi wa kike nikashindwa kumjibu zaidi ya kufuta machozi.
“ Nimekuuliza?” Alifoka
“ Samahani madam, ki ukweli sipo vizuri kiakili na na kichwani nawaza mengi
Sana haswa juu ya baba yangu
marehemu, ukizingatia siku kama ya Leo ndio siku alifariki mikononi mwangu”
nyie ilinilazimu kutumia uongo ili
kujisaidia kwa wakati huo. Masikini ya Mungu msimamizi wa watu aliguswa na kilio changu.
“ Jamani pole, umemaliza kufanya
mtihani wako au bado ?”
“ Nimemaliza madam”
Unaweza kwenda
mama alifaa kua mlezi wa watoto na sio mwalimu. Alinisindikiza mpaka nje
kabisaaa. Akaniacha huko.
Nilipofika nje akili yangu ilikua moja tu kipimo Cha mimba. Kwa kua pesa kiasi
nilikua nayo, sikuchelewa kuongoza njia
kwenda kununua sikutaka kumngoja
miracle Tena, kwani tayari nilihisi
kanidanganya. Atimae nilikipata
nikajipima mwenyewe. ‘uuwii! Nilikua
m ja m zi to’
“
nje, Ila kua Makini usijipe stress zaidi sawa” daah yule
Sehemu ya 19
Nilishtuka nyie na kuhisi huenda labda
kipimo kinaniongopea, nikalazimika
kutumia kipimo kingine kwani nilinunua
vitatu. Na Kama bahati nilikua pekee
yangu mle Dom, kwani wanafunzi wa
junior class walikua kwenye Madarasa
yao wakijisomea huku senior wakiwa
kwenye mtihani. Nilipima Tena
mwenzenu.
Ilikua positive nyie mistari miwili
nyekundu ilisoma Mimi Ni mjamzito, nilipagawa nilipagawa na kwenda
kuvidumkiza chooni vile vipimo.
Nilibakisha kimoja Cha kuja kumalizia
hasira yangu kwa miracle. Kwa Nini
anidanganye, nilianza kulia Sana nililia
Mimi.
“ Kwa Nini imekua hivi? Kwa Nini
Maisha yangu ya furaha na matamu
yameingia kisukari. Yote kwa sababu ya
Nini? Kwa sababu ya Gerald “ nilihisi
kumtapika huyo Gerald. Ila moyo wangu
uliuma kila nilipomkumbuka Gerald.
Gerald alikua mwanaume wa kwanza
kuingia moyoni mwangu, Ila mwisho wa siku amekuja Kasi na kuishia kunichezea tu. Ameniharibia Maisha yangu huyu.
Nililia bila mpozaji na mwisho nikaishia
kulala usingizi Tena nikiwa na majonzi
ilikua saa nane wakati nalala. Lakini
nilikuja kushtuka tayari jua linaenda kupotea mawinguni, it means ilikua saa
11, Mira alikua amekaa pembeni yangu tayari ashapakia kila kitu
kuashiria tupo mbioni kuondoka.
“ Mm Mira mbona__”
“ Huna haja ya kuongea! Najua una maswali mengi juu yangu Ila sio Sasa”
alinikatisha nyau huyu aliogopa kabisa ntamsema.
“ Mira wewe Ni rafiki wa aina gani??”
Nilisikitika jamani kua na rafiki Kama
yeye, kwa Nini aliniongopea.
“ Ami Mimi Ni huyo huyo, umesikia
sasa, gradu wiki ijayo Kama ilivyo
ratiba hivyo Basi kwa Sasa tunafaa
kuondoka na kwenda nyumbani kwetu
mpaka Gradu iishe ndio Turudi mkoani kwetu”
Mira hakua akichukulia uzito suhara la
Mimi kua mjamzito, niliweza kutoa
kipimo mkobani Ila akaona na kukikandamizia ndani! Sikuelewa kwa
Nini hayupo tayari kushuhudia?.
“ Ami ntakuzabua em kua mkubwa”
alipandisha macho Yake juu hapo ndo
nikaelewa kua kitanda Cha juu alilala
mtu, na alielala alikua Jamila, mdada
mmbea huyo nikashusha pumzi zangu.
“ Daah kwa hiyo tunaenda”
“ Mapema Sana hata hivyo tayari
nshaleta bajaji kuja kubeba mizigo
yetu, acha nianze kutoa, kanawe uso wako umejaa makunyanzi” nilipatwa
hasira nilikua na makunyanzi. Nilienda
kunawa uso kweli. Ila wakati naenda nje nikakutana na jovina.
“ Mmhh Ami siku hizi unalala wewe!
Hadi netball hukucheza leo” nilijua
kabisa ananidhihaki anatamani kujua
kuhusu Mimi.
“ Napumzisha akili hata hivyo sisi
vichwa Maji hutumia muda mwingi
kujisomea wakati wa mitihani” nilimjibu Kama alivyouliza.
“ Mmh hiyo ni sahihi, alafu huwa tunafeli”
“ Kabisaa, na yote hutokana na kufatilia Sana Maisha ya watu,, jovina mwenzio nahitaji kureport unaweza niacha” nilitabasamu kwa kejeri na kufinya macho yangu ndani.
“ Sawa kila la kheri Ami namuona dada
yako hataki mlale humu ndani Leo na
tayari kashatoa kila kitu nje”
alipindisha midomo Yake wadada Hawa khaa!
“ Ndo maana nakwambia, kufeli kwa
Maisha husababishwa na kujiweka bize
na Maisha ya watu kuliko ya kwako!!”
Nilimpa vyeke hapo Kisha huyo, nikachomoka zangu na kwenda bafuni.
Ki ufupi maneno ya watu nilihisi
kuyazoea kwa kipindi hicho, kwani mtu
pekee aliekua akizungumziwa siku hiyo
Ni Mimi na namna nilivyowahi kuondoka
kwenye chumba Cha mtihani. Watu
waliweka green mark ( tiki ya kijani
)kabisa kua Mimi ntakua mjamzito.
Anyway hata Kama ninao Sasa wao
inawahusu Nini?
Majira ya saa mbili za usiku Mimi na
Mira tulikua na mjadala mzito Sana
kwenye chumba chetu. Mira alinieleza
ukweli kabisa.
“ Ami Mimi niligundua mapema Sana kua
wewe ni mjamzito, nilipata mawazo
mengi Sana juu yako nilikua na khofu Ni
vipi utaukaburi ukweli huo na tayari
tunakaribia mitihani. Sikua na Budi
zaidi ya kukujenga ki saikolojia ili
ugundue ya kua wewe si mjamzito Kama
ulivyotamani, ili angalau urejee katika
ufahamu wako wa darasani uwaze juu
ya mtihani, kwani niliamini kabisa laiti
ungejua kabla kwa hakika hakuna kitu
kingefanyika.
“ Mira wewe! Unajua kabisa nilivyo Bora
ungenambia mapema nisingepata maumivu haya ya leo”
“ Imagine ndio ningekwambia bado
hatujafanya mtihani bila Shaka hata
huo mtihani usingeweza kuufanya, Ni
mwili wako na taarifa za madiliko
ulizipata Ila hukutaka kukubali, vipi mtu
angekuthibitishia kabisa kua wewe ni
mjamzito, bila Shaka ungezimia”
Daah! Maneno Yake yalikua na maana
hakika ningekufa kidogo na kurudi
baadae, sikua tayari mpaka muda huo
vipi kuhusu ningepewa hiyo taarifa
nikiwa kwenye mtihani wa kwanza, bila
Shaka ningepanic na kutamani kuharibu
kila kitu. Wakati huo tu akili haikua
yangu.
“ Kwa Sasa unawaza kufanya nini?”
Mira alinihoji swali Kama Hilo lakini
tayari nilikua na suluhu ambalo.kamwe
katika Maisha yangu sikuwahi
kumuwazia mtu kufanya. “ Mira Sina
jinsi lazima nitoe!!”
Sehemu ya 20
Mira alihisi Kama nimempiga shoti
kwenye masikio yake’, yaani Mimi ndo wa kumwambia hivyo kweli? Sijui lakini
sidhani Kama hata aliwahi kulala akaota
namwambia maneno Kama hayo, yaani
Mimi Ni wa kuwaza kutoa mimba hata
Kama imeingia bahati mbaya sikufaa
kuiwazia mabaya.
“ Ami umewaza kweli?” Alinihoji swali la kutatanisha lakini mwenzie tayari
nilichanganyikiwa. Nifanye nini Sasa?
Sina jinsi.
“ Miracle nifanye nini Mimi? Mama yangu anahangaika na Mimi kila siku!
Kaka zangu walijitoa kwa ajiri yangu, wanahangaika kudunduliza ada kidogo
kwa ajiri yangu alafu mtu mmoja aje
apoteze matumaini yangu ya miaka mingi? Ki ufupi Sina namna sikuwahi
kuwaza juu ya Hilo, hata hivyo Sina
ujanja Mimi na Gerald Ni Kama tushaachana”
“ Ami ni Sawa lakini vipi kuhusu yeye?
Anajua kuhusu ujauzito wako?”
“ Hapana Mira, hata Sina haja ya
kumwambia kuhusu hili, hujui Ni jinsi
gani nilihisi kufa nilipopata uhakika kua
Ni mjamzito Mimi, nitaitoa” nilishika
kichwa changu kwa kuchanganyikiwa zaidi.
“ Ami kumbuka tumetoka wapi? Just imagine Kuna watu wanatamani kupata
hata watoto wa kusingiziwa tu, Ila
hawapati kumbuka tumetoka kwenye familia gani? Bahati mbaya sisi sote
mama zetu walianza kwa kushika
ujauzito ndo wakapata vibali vya
kuolewa tukajikuta tumezaliwa katika
ndoa salama, kwa ajiri ya vibali vya
ujauzito, Sasa wewe unataka kutoa
Ami, una mawazo gani? Hata Kama
unawaogopa ndugu zako’, kumbuka
baadae utakua na Maisha yako bila
wao, kubali ku kabiriana na changamoto
zote utazokutana nazo, Ila usifanye
dhambi Kama hiyo”
Mira alikua sahihi lakini kwa kweli
siwezi Mimi? Siwezi kukaa nayo hii
mimba, labda anaongea tu kwa sababu
haijamkuta yeye.
“ Ami mwambie kwanza Gerald “ hapo
ndo alikua akinimaliza kabisaaa. Yaani
Gerald huyo mwanaharamu nimwambie
eehhee mtu mwenyewe simjui vyema
sema Basi tu nimeishia hivi kwa ajiri
Yake? Ila aliniita mchafu.
“ Hapana Mira sitamwambia, sitaki kua
mnyonge na mdhaifu mbele Yake, hata
ikitokea ujauzito wangu umekua acha
ukue wenyewe Ila sitamwambia Gerald kuhusu Hilo”
“ Haufanyi sawa, huwezi jua Gerald anakuwazia Nini? Unachojari Ni fikra mbaya tu juu Yake? Kwa Sasa hujui anapitia wakati gani bila kuwasiliana na wewe?”. Mira Ni Kama alikua na undugu na Gerald mbona anamtetea hivi?
“ Mira sitaki? Sipo tayari kujihusisha na Gerald hakiya Mungu, Gerald sio mwema kwangu”
“ Nisikilize kwa Mara ya mwisho, mtafute umwambie ukweli kuhusu wewe na ujauzito wako, iwapo ataukana na kukutolea nje, nakuahidi kipenzi changu, ntakua bega kwa bega na wewe katika
kila maamuzi” nyie huyu Mira nilipewa
pekee yangu Kama rafiki ama? Mbona
wengine hawana bahati.
“ Nahisi kabisa Gerald atanikataa Mira”
nilikua na mawazo Sana, ki ukweli
nilijiona Sina bahati Kama mwanamke, yaani ndo mpenzi wa kwanza maishani
mwangu lakini sijaweza kudumu nae
hata kwa nusu mwaka, bahati mbaya
iliyoje?
Hatimae usiku huo tulilala japo nilikua
na mawazo chungu nzima, nilikua
nawaza Hadi nikakumbuka kuhusu story
zangu na Gerald. Siku moja nikiwa
kwake alikua akifua huku Mimi
nikimsaidia. Alikua mvivu Sana wa kufua mjinga huyo.
“ Mi sipendi kufua kwa mikono inachosha akili na mwili” alilalamika.
“ Mwanaume gani unakua mvivu
kupindukia, nahisi umeachika kwa
wanawake kwa sababu hiyo” nilimwambia akanimwagia Maji ya mapovu.
“ Gery unanitafuta la rohoni?”
Nilimfokea bila kusita akanimwagia tena
Kama kutaniana. Nilihisi kuvurugwa
nilijikuta nabeba beseni Zima la mapovu ya sabuni na kummwagia akaloana kwa
mshtuko, nikaanzaa kumcheka. Gery
alinitazama kwa hasira nikaogopa na kuinuka haraka. “ Ami ume__” kabla
hajainuka anikamate nikaanzaa kukimbia mbio.
“ Simama hapo” tulianza kukimbizana hapo uani tulipoanika nguo Gery
hakuniacha mwenyewe, alinikimbiza
nikawa najificha kwenye mashuka yaliyoanikwa. Ghafla nikashtuka
nimenaswa kwenye mikono Yake ambayo
ilizunguka kwenye kiuno changu.
“ Ami wewe Ni wangu unawezaje
kunipotea” aliongea kwa sauti ya
mahaba kwenye masikio yangu nikawa
mtulivu, Ila tayari alinilowesha na Maji
kutokana na alivyokua kaloana.
“ Gerald mwenzio baridi huoni
umeloana” nilimwambia kimadeko.
“ Usijari kipenzi, upo kwa ajiri yangu, nipo kwa ajiri yako my love”
alinizungusha kwa nguvu mpaka nikahisi
wivu Kama aliwahi kua namtu mwingine inamaana alikua na Raha Kama hizi pia.
“Usiulize juu ya Mambo yaliyopita sio
muhimu, hudhorotesha afya ya mahusiano “ alinipa onyo nkatulia
sikumuuliza Tena. Alinibusu’ jamani na kumbukumbu yangu ikaishia hapo.
Hatimae nililala baada ya kumbukumbu
hiyo nzuri.
Asubuhi majira ya saa tatu ndo niliweza
kuamka, nilinawa uso na kupiga mswaki
bila kuoga. Kitu Cha kwanza ambacho
niliwaza Ni kumpigia Gerald.
Nilichukua simu nikiwa na hofu na
mashaka kibao. Ila niliweza kuipiga
namba iliyoseviwa My Gery. Simu iliita
muda mrefu’ kidogo mpaka nikahisi
itakatika yenyewe ndipo ikapokelewa.
“ Hallo” moyo wangu ulidunda hatari, moyo ulikua juujuu kwa sauti aliyoitoa
Gery, Ni sauti ileile niliyokua nimeizoea
wakati tupo wawili Mimi na yeye. Ni
sauti ileile iliyozoea kuupa moyo wangu
msisimko.
“ Mbona upo kimya?” Aliniuuliza baada ya kuona kimya nikaogopa kuongea Ila
nilijikuta natetemeka mwenzenu.
“ Sema unashida gani?” Nilihisi kulia
Gerald hata salamu hakuna kashaulizia
shida. Na Mimi nikahisi kua na jeuri
sikua tayari kujishusha nikaenda moja
kwa moja kwenye point. “ Gerald mi Ni mjamzito, ki ufupi Nina mimba yako”
nilimwambia.
“ Una uhakika hujakosea mtu wa
kumwambia maneno hayo” aii umewahi
kumwagiwa Maji ya ukoko ukijiandaa
kuhudhuria interview kwa suti ya kuazima. Ndo kilinikuta Mimi Sasa
jamani. “ Gerald wewe?? Ni Kama vile hunifahamu kabisa”
“ Hebu fanya utafiti sahihi wa kumtafuta huyo muhusika wa mimba ndo unitafute, useme kwa Nini unipakazie kesi isiyonihusu” daah! Kwa uwoga ambao niliupata sikuweza kusubiri akate simu niliikata mwenyeweeee.
Sehemu ya 21
Baada ya kukata simu nilijikuta
naidondosha bila kujua, yaani nilihisi
Kama natamani kufa kufa hivi kweli
alikua yeye? Alikua Gerald ambae
nilimchukulia Kama mpenzi wa Maisha
yangu? Vipi kuhusu Yale mapenzi na
wivu aliokua akinionyesha hapo mwanzo?
Yote Yale alikua akijifanya tu?
Sikuweza kuamini Hilo. Niliwaza Sana
nililia Sana kila nilipomkumbuka huyo
mwenda wazimu Gerald. Kila
nilipoukumbuka uwongo wake jamani
wanawake kwa Nini tuliumbiwa
kudanganywa. Nililia Sana Hadi macho
yangu yakawa mekundu. Wakati huo
Mira hakuwepo, alienda kufanya
manunuzi kwa ajiri ya graduation yetu,
Ila ki ukweli kwangu Mimi akili ya graduation haikuwepo hata kidogo.
Nililala Tena baadae ndo nikaja kuamka
na kujikuta nakumbuka mazungumzo
yangu na Gerald . Sijui ilikua saa
ngapi? Kwani hata simu ilipodondoka
ilizima moja kwa moja na Mimi sikujua
kuhusu Hilo hivyo sikuangalia saa.
Nilitamani kupata pesa na kwenda kutoa
huo ujauzito wakati huo huo? Akili
yangu haikuweza kusimama yenyewe
mwenzenu nilitembea taratiibu kuelekea
mpaka duka la dawa. Nilifika duka la
dawa bila kufikiria na kumkuta huyo
dada ambae sikua namazoea nae Sana nikamsalimia.
namna nilivyokua
nimechanganyikiwa alihisi kabisa naumwa
Sana kiasi Cha kumfia.
“ Dada shikamoo” kwa
“ Dada punguza presha ndo uongee, utapoteza direction” aliniambia hata
kumuelewa sikuweza. Yaani mawazo
yangu yote yalikua Gerald Gerald kwa
nini alinifanya hivi?
“ Una tatizo gani dada yangu?” Alinihoji
huku akinipatia kiti na Maji ya kunywa
kwanza. Maji yalikua nusu Lita lakini
niliyapiga yote.
“ Acha papara dada hii ndo dunia” yule
dada muuza dawa alikua mwema Sana, aliongea na Mimi kirafiki kana kwamba
alinijua, nyie Mira alikua sahihi
kunificha Jambo hili wakati wa mitihani
kwa Hali niliyokua nayo sidhani Kama
mtihani ningefanya. Hakika nilichanganyikiwa.
“ Samahani dada, unaweza kuniambia kidonge Cha kutoa mimba kinauzwa Bei gani?” Nilimpatia kikombe alichonipea
Maji ya kunywa. Alipokea akiwa na mshtuko mkubwa Sana kwenye uso wake akiniangalia.
“ Dada tafadhari naomba unielewe, unaweza nifikiria unavyotaka Ila baada ya kunijibu mwenzio nimeteleza kabisa”
nilimwambia akakaa kuniangalia tu.
“ Dada yangu nipo chini ya miguu yako”
nilishuka kwenye kiti na kupiga magoti
mbele Yake, kitu pekee alichoweza Ni kuniinua pale akiwa na uwoga wa kufa
mtu kwenye uso wake Kisha akaniingiza ndani ya duka lake.
“ Samahani hadithi yako sio ya kuongelea nje, hii Ni jinai kubwa Sana kutoa mimba ! watu wakigundulika huwa
wanafungwa kabisa, ni kosa kubwa
Sana” aliponambia hivyo nikaona daah!
Mjinga Sana Mimi mbona sikua najua.
“ Sawa unaweza kuniambia Ni shingapi?”
“ Ni kweli naweza Ila inabidi kwanza
nitambue ujauzito wako una muda gani?”
“ Dada yangu hata sijui, kiufupi Mimi
nimepima Mara kadhaa na kugundua
kabisa Mimi Ni mjamzito Ila sijui Ina muda gani nachotaka Mimi Ni kutoa”
nilimwambia bila kufikiri.
“ Unajua kuhusu madhara ya kutoa ujauzito dada yangu?”
“ Acha kuwaza juu ya Mimi? Waza tu kuhusu kunisaidia nikikaa nayo Ni madhara zaidi”
“ Ok sawa Ni elfu 50” mmhh Bei hiyo
ilinishinda kwani kwa wakati huo Mimi
sikua na pesa kabisa. Na tayari
nilitamani kutoa hiyo mimba sikua tayari
kua nayo kwa Nini niwe na mimba ya mtoto asie na baba?.
“ Dada yangu naomba unipe siku mbili tu tayari nakuja na pesa unipe hizo dawa” sijui hata nilikua naenda kutafutia wapi? Kikubwa niliamini kuipata.
“ Sawa Ila itabidi upime kwanza ujue huo ujauzito una muda gani?” Aliniambia nikaondoka zangu. Sikutaka risala zake
hata hivyo hakuonekana kua tayari na Hilo. Niliondoka zangu nikiwa sina raha zaidi na hiyo Hali.
“ Umeondoka Ami umeacha mlango wazi, simu umezima. Kila kitu kipo hovyohovyo kwa Nini unaniweka kwenye khofu” Mira
alinipokea na maneno chungu nzima kweli nilipoondoka sikua hata na wazo la kufunga mlango.
“ Mira naomba uniache kwanza, sipo
sawa kabisa” nilimwambia na kuingia ndani nikajitupia kwenye godoro letu la bila kitanda.
“ Ami Kuna nini kwani? Nimefika
nikawasha simu hapa, nimekutana na meseji za Gerald Kama sita na kasisitiza anataka kuongea na wewe?”
Aliponambia kuhusu Gerald sikutaka hata kumjibu niliweza kujilaza tu kitandani na kulia Sana.
“ Najua hutaki kuongea nae Wala
kuongea kuhusu yeye, Ila ukweli
kwanzia nimewasha simu mtu pekee
anaepiga simu hii Ni yeye Ami” Mira
alikua na matatizo gani? Kwa Nini
amegeuka kumtetea Gerald mimi ndo
napitia changamoto kubwa wakati huu
Kama rafiki yake’ alifaa kuungana na
Mimi kunisaidia Ila mdomoni kauli kubwa
Ni Gerald.
“ Nipe simu” nilimwambia kwa kumpa
mkono wangu hewani akanipatia.
Nilitafuta namba ya Gerald nikaipiga
kwani inasemekana yeye ndo amepiga
Sana. Simu iliita kidogo tu na
kupokelewa. “ Ami naomba unisamehe
nimeenda mbali” yalikua maneno ya kwanza kutoka kwa Gerald. Sikua na jibu zuri la kumpa zaidi ya. “ Nisaidie ikiwezekana nikopeshe shilingi elfu 50, nikatoe ujauzito huu”
Sehemu ya 22
Nilihisi ukimya kutoka upande wa pili wa simu, sijui alikua na reaction gani huko
alipokua Ila nahisi aliridhia kabisa
maana alinipa jibu ambalo nilitarajia.
“ Sawa nakutumia Leo hii” mmhh moyoni
niliumia na kuona Ni jinsi gani? Ni jinsi
gani mwanaume huyu hakufaa kua na Mimi kabisa.
“ Sawa sidhani Kama Kuna kingine
kimebakia” nilimwambia na kukata simu.
Nilimrejeshea simu miracle ambae
alibaki kwenye mshtuko akiwa haelewi
aanze na Nani Kati yangu na Gerald ki
ufupi tulimvuruga Sana. Akiwa
kasimama Kama mlingoti huku Mimi nalia
Sana na kujutia maamuzi yangu na
utoto wangu wa kipuuzi ulioniletea
madhara, simu kwenye mikono ya Mira iliita. Mira alinambia. “ Gerald amepiga
simu”
“ Mpokelee mwambie Kama hawezi
kutuma hiyo pesa aache ntatafuta kwa
mpango wangu mwenyewe” Mira alikosa
usemi alipokea simu na kutoka nje ya chumba kabisa. Sijui Ni kipi waliongea
Ila majira ya jioni Mira aliniamsha
maana nilikua mpenda kulala hovyo.
“ Vipi Sasa, mbona upo hivyo, Mimi ndo
mwenye tatizo “ nilimwambia.
“ Ami kweli wewe na Gerald hamkufaa
kuishia hivi, Gery katuma pesa” alitoa
kibunda Cha elfu sabini akanipatia.
“ Akipiga tena mwambie Amina anashukuru Sana, na hatokaa
amsumbue” nilikua na Majibu hayo kwa
Mira Kisha nikainuka na kuelekea kule
kule duka la dawa kwenda kuchukua
vidonge nitoe huo ujauzito.
“ Dada nimeona siku mbili zitakua
nyingi, nikaamua kudunduliza hatimae leo ndo siku yenyewe, naomba mzigo
wangu” nilimwambia baada ya
kusalimiana nae kabisa.
“ Sawa lakini mmhh!!” Dada wa watu
aliguna kwanza akanipatia vidonge, kiufupi sikua najua Ni vidonge vya aina
gani Ila niliamini kabisa vinatoa
ujauzito. Akaniambia Kuna vya kunywa na vingine vya kuweka chini… Na
maelekezo kamili akanipatia. Niliondoka
hapo kimya na kurejea nyumbani nikiwa
nimebakiwa na elfu ishirini tu.
“ Ami ki ufupi inaniuma, naogopa Kama
litakutokea tatizo bora usifanye hivyo”
alinisisitiza kabisa nikaona Mira
anaogopa labda nitamfia apate kesi.
Nikachukua kalamu na karatasi
nakuandika hapo ujumbe mrefu’, ili
ikitokea nimekufa Basi asipate tabu.
“ Ami sidhanii kufa kwako Ila nahofia
kukupoteza, kwa madhara
yatakayojitokeza” aliniambia sikuweza
kumjari, niliweka kidonge kimoja
mdomoni huku machozi yakinitoka, Kisha
nikanywa kabisa. Alafu nikaelekea
bafuni na kupachika kingine Kama
nilivyoelekezwa Kisha nikarejea
chumbani na kuandaa beseni nikisubiri
matokeo… Mira hakutaka kuondoka
karibu yangu kwani alikua na khofu.
“ Mira jiondokee zako’, utakoma iwapo nitakufa watakukamata”
“ Sijari kuhusu kukamatwa nachojari
Mimi Ni uzima wako tu, kwa nini Ami unalazimisha kufanya hivi?” Ki ufupi
Mira alihisi kukata tamaa na kuishia
kushika kichwa chake kwa majuto.
Mimi sikujari Hilo Bali nilisubiri tu matokeo ya mimba kutoka. Nilisubiri
karibu nusu saa nzima Ila sikusikia hata
dalili ya kijusi kushtuka.
“ Mira mbona sipati matokeo yoyote mwenzako?” Nilihoji.
“ Sijui labda muda bado” alinijibu Kama
hakua anafahamu’ kitu pia.
“ Mira ki ufupi sitaki hii mimba
inigomee kutoka nataka itoke nje, sipo tayari kua na mtoto wa Gerald kwenye tumbo langu” nilimwambia Mira kana
kwamba alikua na uwezo wa kuiamuru
hiyo mimba kutoka nje.
“ Tuendelee kungoja” Mira alijibu
utadhani hata yeye alikua tayari
kushiriki dhambi moja na Mimi.
Masaa mawili yakakatika wapi? Mmhh !
Nikapata khofu! Isiwe huyu muuza dawa
amenipiga na kitu kizito kichwani?
Nikazidi kungoja. Mpaka hiyo siku
ikapita bhana. Hadi kunapambazuka
mwenzenu sijatokewa na hata dalili za
kijusi kuvuruga Wala kuhisi kutapika
kwa kutoa mimba.
Asubuhi hiyo Gerald akapiga simu,
mbwa huyu kwa kua alihisi mimba
imetoka ndo maana kupiga simu. Mira
alipokea Kisha akanipatia simu.
“ Ami hujambo mama angu” mabadiliko
yake’ ya lugha yalinichoma nikajikuta
namtukana.
“ Unawezaje kujifanya hata katika umri
huu?, Gerald Mimi na wewe hatujuani
lakini maumivu uliyonipatia Ni kiboko,
unataka nikwambie sijambo wakati unajua sipo sawa ki afya, Ni Nani
alikuchagua uwe daktari mbwa wewe!”
Nilimtukana bhana.
“ Ami punguza ukali, natamani kuongea vizuri na wewe, ki ufupi Mimi sipo tayari kuachana na wewe, natamani kujua kuhusu afya yako, na kuhusu kile
ulichodhamiria kufanya umefanikiwa??”
Aliniuuliza akiwa na maana gani? Akiwa na shahuku ya kujua iwapo nimetoa
ujauzito? Ahaha! Kweli nilifeli Maisha
kua na Gerald Kama mpenzi wangu?
“ Gerald naomba nikuombe kitu, niongezee Elfu thelathini nikanunue
vidonge vingine kwani vya kwanza
havijasaidia, nahitaji kubadili mtu wa kuniuzia” nilimwambia.
“ Hivi Ami upo serious kabisa unataka kumuua mtoto wangu?” Gerald alifoka
kwa sauti hapo ndo nikashtuka kua
huenda hata hii ya mimba kugoma
kutoka Ni kwa ajiri Yake. Kwani nini
kilitokea? Niliyatua macho yangu kwa
Mira alieshindwa kunitazama kwa aibu.
Sehemu ya 23
Mira aliniangalia kwa macho ya khofu
Kisha akatoka nje baada ya kushindwa
kunikabiri, ki ufupi alinivunja moyo kwa
hiyo alishirikiana na Gerald kuzuia
mimba isitoke ?
“ Ami, najua nilikukosea ila nilikua
nakutest, nilikua nakujaribu uvumilivu
wako! Sikufaa kufanya hivyo kwako, lakini tafadhari naomba usimuue mtoto
wangu, ntakuja huko hivi karibuni”
aliniambia nikahisi hasira nikahisi
kumuua Gerald.
“ Gerald wewe unajisikia unachoongea
kweli? Hivi hujui Kama umeyavuruga
Maisha yangu kiujumla “ nilimwambia
nakuanza kulia upya.
“ Kwa Sasa sitaki chochote Gerald
nahitaji kutoa huu ujauzito sipo tayari
kua na wewe, sipo tayari kuzaa na
wewe sipo tayari kubaki na huyu mtoto
kwenye tumbo langu”
“ Ami nisamehe Mimi, Mimi ndo mwenye
makosa na sio mtoto wangu, tafadhari
Sana” aliniambia nikawa simuelewi nikamkatia simu. Kisha nikaandika
ujumbe mrefu’.
[ Nilikua muungwana Sana hata
kukufahamisha kua Nina ujauzito wako,
Ila unasema nitafute wa kumpakazia, Sasa Basi naenda kumtafuta na
ntahakikisha ananipatia pesa ya kutoa
ujauzito huu ili Maisha yaendelee]
nilibonyeza kitufe Cha kuruhusu ujumbe
nikawa nimeutuma kabisa. Haikupita
muda mrefu’ nikaona meseji kutoka kwa
Gerald.
[ Ami Ni kweli kabisa umedhamiria
kumuua mtoto wangu, sawa nimejaribu
kumuokoa Mara ya kwanza lakini
inaonekana wazi kabisa hayupo kwenye
hifadhi salama, Sina Budi kutumia pesa
nyingine ukatafute dawa kwa watu unao
waamini wakusaidie kumtoa huyo mtoto]
nilipomaliza tu kusoma ujumbe ambao
kiasi Fulani ulinigusa Ila sikutaka kujari
Sana. Meseji ya muhamara ilifika.
Ilikua laki moja kabisaaa.
Nilihisi kucheka na kumuona Gerald Ni
mnafiki Sana anajifanya anamlinda
mtoto asife alafu anatuma pesa za
kumuua, ili ionekane Mimi ndo mwenye
dhambi pekee yangu.
Siku hiyo ilipita, kesho Yake asubuhi
tulienda shuleni Mimi na Mira kwa ajiri
ya hili na lile maana graduation ilikua
mbioni, sikuweza kumwambia Mira Kama
Gerald alituma pesa Tena ili nikatoe
ujauzito, kwani nilijua anaweza
kuzunguka Tena na kumsaidia Gerald
yule mnafiki.
Wakati tukiwa shuleni nilienda kwa nesi
wa shule alikua rafiki yangu Sana,
nikajaribu kumshirikisha matatizo yangu na yeye akasema nisijari atanipatia
dawa kikubwa niwe na pesa. Kweli
bhana sikua na shida juu ya Hilo
nilimpatia pesa. Baada ya kumpa pesa
akanipa dawa.
aliniambia akitabasamu kwa hamu zote.
Nikatoka mpaka nje ya shule
nikawaacha wenzangu wanajimwaya
mwaya na graduation. Inayokuja hapo
mbele
Nilifika nyumbani na kuandaa vidonge
ambavyo vilikua na maelekezo sawa
sawa na Yale ya kwanza. Ki ufupi siwezi
“ Asante nesi”
“ Usijari Ami, mi ndo nakujua zaidi”
kua mnafiki, nilikua nafanya hayo yote huku moyo wangu unauma Sana.
Nilijiona shetani kwa muda mfupi?
Wakati huo Sasa dalili tayari zilikua
kubwa na nilikua naziona live. Hata
tumbo langu lilikua na msitari mweusi ambao ulijichora. Inamaana kweli nilikua na kiumbe kwenye tumbo langu. Kiumbe
ambae nililazimika kumtoa kwa sababu ya kujipenda mwenyewe. Mimi sifai
kuitwa mama katika huu ulimwengu.
Niliwaza hayo nikaanda Maji ili nimeze
kidonge. Wakati najiandaa kumeza simu
ikaita, nikasita kwanza na kuangalia
mpigaji. Mmhh’ alikua Gerald huyu
baba anamachare Sana. Nilimpokelea
nikiwa tayari nimedumkiza kidonge
mdomoni paomja na Maji.
“ Ami usiniambie umekunywa vidonge tayari??” Ndo yalikua maneno Yake ya kwanza baada ya Mimi kupokea simu.
“ Kwani we unatakaje?” Nilimwambia.
“ Nina uhakika kabisa ya kwamba wewe ni mwanamke mwenye moyo wa tofauti
Sana Ami, sidhani Kama utakua tayari
kumuua mtoto wako mwenyewe” aliniambia.
“ Gerald nimeamua, nahitaji kua salama
pia, hata hivyo siioni future nzuri
katika sisi, sitaki kua single mama hapo
baadae” nilikata simu baada ya kumwambia hivyo. Alinitumia ujumbe
mrefu’ Sana baada ya Mimi kumkatia simu.
[ Ami najua Sana Mimi Ni Kama tatizo
kwako, Ila nakuomba Sana Ami wangu
usifanye makosa ya kibinadamu kwa
kukubali kumuua mtoto wako mwenyewe,
jiwazie pia iwapo mama yako angekutoa
Nini kingetokea usingenijua Wala mimi
kukujua wewe, kubaliana na karaha
pamoja na dhiki utakazopitia kwa
kusemwa na kudhihakiwa na watu hata
iweje sitakuacha mwenyewe, nitakua
sambamba na wewe Ami wangu, naomba
unipe Imani yako hata punje au
theluthi, tafadhari Sana huyu Gerald
unaemuona Kama mlaghai, Ni kweli
yawezekana ikawa hivyo, Ila huyu Ni
Gerald ambae amengukia kwako Amina.
Ni kweli huwezi nipa moyo na Imani
yako Ila Imani yangu inaniambia kabisa
kua hakuna mwingine alieangukiwa na
Gerald zaidi yako wewe. Ami I really I
FALL FOR YOU, naomba unikubali na
umuache salama mtoto wetu ili tujenge
familia, japo haiwezi kua rahisi
kulingana na wakati huu Ila kubali ya
kwamba kesho yako ipo mikononi kwa
mwanaume mmoja tu ambae ni Gerald
Tantalila ]
Nilihisi Kama ananiambia upuuzi, kwani tayari ibilisi wa kumtoa huyo mtoto
tumboni mwangu alikua amenikamata vilivyo. Nilifata maelekezo Tena na tena.
Sehemu ya 24
Majira yalisogea nikajikuta napata usingizi mrefu’ Sana, sielewi Kama hiyo ndo ilikua dalili moja wapo ya ujauzito
kutoka Ila ndo hivyo yaani nilijikuta
nalala usingizi mrefu’ mpaka pale ambapo nilihisi midomo yangu ilikua na kitu.
Nilihangaika ili kutoa hicho kitu
nisichokielewa kwenye midomo yangu
lakini wapi? Ghafla nikahisi kama
napata Raha kwa msongamano huo, hivi
nilikua naota au? Ni kweli labda nilikua
naota? Nilihisi kama mtu ananibusu
Tena busu yake’ ilikua TAMU Sana na
tulivu nilijikuta namkumbatia mtu huyo
baada ya kufungua macho yangu na
kuona taswira ya Gerald.
Niliamini Ni ndoto kabisa.
Nilikandamiza midomo yangu kwake na
yeye akafanya hivyo baada ya
kunikumbatia kwa nguvu, shida ikaja
kwangu hivi hii ndoto ya aina gani ya
vitendo halisi. Nilijaribu kung’ata
midomo Yake iwapo ataumia nijue sipo
ndotoni. Ila hakushtuka. Nikaamini
kabisa ni ndoto, kwani naona Hadi damu
ikimtoka. Ghafla harufu ya damu
ikatawala kwenye pua zangu. Mmhh’
inamaana alikua Gerald kweli nilitumbua
macho kana kwamba Kuna mtu alisema
zinduka. Haraka Sana nikamsukuma
huko Kisha nikakaa.
“ Uu wewe?!” Nilifoka na kuanza
kutema mate yenye damu kwenye
beseni, ndo nikajiuliza beseni lile
liliandaliwa kwa ajiri gani? Nikakumbuka
kabisa nilikunywa dawa nyingine kwa
ajiri ya kutoa mimba. Na Gerald kafika
vipi hapa?
“ Gerald wewe??” Sikua hata na neno la kumwambia nikajikuta nafunua nguo
kujiangalia iwapo mimba imetoka au la.
Khaaa!! Haikua imetoka sikua na dalili yoyote Ile ya mimba kutoka.
“ Usijisumbue Ami, mtoto wangu hawezi kufa kirahisi anadamu ya baba yake’”
aliniambia hivyo nikapata hasira
inamaana nimechezewa mchezo Tena?.
Nilikunja uso wangu ukakunjamana
vilivyo. Kwa Nini niliishia kujuana na mtu huyu katika uzao mwingine ?
Nilikata tamaa.
“ Gery umethubutu vipi kunifanyia hivi?”
“ Mimi Ni baba nasimama kama baba na mume kwa ajiri ya mtoto na mke
wangu” nilisimama bila kupenda. ‘ehe!
Eti mke’ eti baba’ khaa!
“ Gerald kwa nini ulizaliwa katika hii
dunia. Tayari nilikua nimeridhika na Maisha yangu lakini haikua na tatizo
kunipa wewe Kama mleta shida maishani
mwangu” nililalamika Gerald akabaki
kuniangalia kwa huzuni.
“ Usinitumbulie macho yako ya kulegea, Bora uvae miwani siwezi kuivumilia sura yako unanitia kichefu chefu”
alitabasamu Kisha akainuka na kunikumbatia.
“ Inasemekana wanawake wakiwa
wajawazito huwa wakali na wachachu
Kama limao na pilipili” alipotamka hayo
maneno mwenzenu nilipata uchu muda
huo huo, nikahisi njaa, ghafla
nikatamani kula chips kavu za pilipili
nyingi pamoja na limao. Gerald
akajitupa kitandani na kuniacha
nimesimama.
“ Gerald nifanyie hisani nahisi njaa,
naomba unipikie chips kavu, japo Sina
hakika Kama wewe ni Gerald “ Gerald
alitabasamu Kisha akaniambia.
“ Nilimwambia rafiki yako kua nakuja
Leo hivyo awe Makini na wewe usije toa
mtoto wangu, Kisha nikamueleza ya kwamba nimekutumia pesa lazima
utatafuta mtu unaemuamini ili akusaidie
kutoa mimba, na kweli ulifanya hivyo, bahati nzuri Miracle alikuwahi aliongea na nesi wa shuleni kwenu kabla yako.
Ami acha kumsumbua mtoto wangu
kisaikolojia, ana miezi mitatu Sasa
anaelewa “ Nilichoka jamani! Kumbe
Mira yupo pamoja na Gerald
kuniteketeza kimya kimya, hajui tu Ni
changamoto gani ntapata mwenzie
nikirudi nyumbani na hii mimba!
Iliniumiza sana. Kisha nikakumbuka
Gerald katamka miezi mitatu! Hee!
Kumbe ilikua kubwa hivyo?
“ Gerald umesema Nini? Miezi mitatu?”
Nilihoji kwa kumpa sura ya sintofahamu.
Aliniinulia macho Yake yaliyolegea Kama
anataka kufa kwa hisia,, aa wee Bora
awe na miwani Maisha Yake yote! Hivi
alistahili kuniangalia hivyo! Bila miwani
mi siwezi. Midomo Yake ilisambaa kwa
tabasamu murua Kisha akanijibu “
mitatu, binti yangu atakua amekua
Sana “ aahh! Nilihisi kulia ndo kwanza
najua mtu aliekotumboni mwangu atakua
na miezi mitatu Kisha natajiwa jinsia
huyu karogwa Nini?
“ Gerald usinichanganye kwanza ondoka hapa, sitaki kukuona” nilimwambia kwa hasira nikakumbuka sio siku nyingi Sana aliniita Mimi mchafu.
“ Gerald wewe sio mwanaume anaestahili kua na Mimi, ki ufupi Mimi sio wa hadhi yako Mimi Ni binti wa hadhi ya chini Sana, Tena sio ya chini
mimi ni masikini Sana, mbali na umasiikini, Mimi ninae mama tu katika
hii dunia, alafu nalelewa na kusomeshwa na Kaka zangu, we unadhani mi nikirejea nyumbani na hii mimba
ntapokelewa na Nani? Naomba tu uniache mwenyewe na Maisha yangu”
nilimwambia akabaki kunitumbulia macho
alijikunja pale alipokua amelala
akauvuta mkono wangu nikadondokea kitandani.
“ Gerald sipo kwenye Hali ya kutaniana!” Niliweka sura ya huruma
akanikandamiza kitandani. “ Najua kwa
Sasa hauna Hali yoyote ya usawa, Ila
usijari Ami, hata iweje hata itokee
ndugu zako wakutenge, litakua suhara
la muda tu, naomba uvumilie, nakuahidi
ntakulinda, hata hivyo Sina hakika
Kama watakufanyia hivyo, kikubwa
amini na uelewe kua Gerald yupo upande
wako sawa” aliniambia akiwa amenishika
vyema sura yangu ndogo na kuibusu
midomo yangu kwa Mara nyingine.
Mimi ki ufupi nilikua nampenda Gerald.
Hivyo haikua rahisi kumuwekea kinyongo
rohoni. Haikua rahisi kabisa. Nilijikuta
namsamehe kila dakika. Hata busu
yake’ ilitumika Kama fimbo ya
kunituliza. Na kufuta kila kumbukumbu
mbaya dhidi Yake.
Sehemu ya 25
Baada ya kiss kunoga mtoto wa kike
nilitulia hapo na tukajikuta tunazama
kwenye ulimwengu mwingine kabisa,,,,
ulimwengu mpya wa mahaba, Kama
serikali ingeweza jamani ingeingilia Kati
hili swala. Mimi na Gery tulikua Kama
Wenda wazimu wawili tusio na aibu hata
kidogo. Nilisahau Kama nilikua najiliza
kutoa ujauzito, lakini akinitaka
simkatai. ‘aah mapenzi Ni konyo, nahisi
kuumia kila nikiyawaza’
Baadae kabisa mida ya usiku Gery
alikua kaondoka muda huo nilikua na
Mira nyumbani. Akiwa anaandaa mavazi ya gradu huku Mimi naongea na mama
yangu nikimueleza kua narejea nyumbani
siku gani? Mama alifurahi na kushukuru
Mungu akiamini nimemaliza shule
salama.
“ Mama kwani ulihisi siwezi kua
salama?” Nilihoji inamaana kwa Nini
alikua akiwaza kupita kiasi.
“ Sijamaanisha vibaya. Ila maana yangu
Ni kwamba, sio kila mtu katika hii
dunia anaebinti wa kujitambua Kama
binti yangu, hivi hujui Kama Eliza mtoto
wa mama yako mkubwa Ni mjamzito hivi
Sasa, si huyo hapo, form four pekee
imemshinda” daahh! Mama Kama
Angejua Bora asingemsema mtoto wa mama mkubwa.
“ Wee mama ! Eliza ana mimba, na
upole wake wote?” Nilishika midomo
yangu huku nikimwangalia miracle ambae
aligeuka kunitazama. Sina hakika Ila
najua Sana alinisema kimoyomoyo kua ‘
usimcheke mwenzako ikiwa hujui ya
kwako’.
“ Ndio binti yangu, watu Hawa
walinisema Sana, Sasa itabidi urejee
kwa Sasa najua umekonda nikupe vya
Moto unenepe, wajue ulikua kusoma, we
msomi bhana wasikufananishe “ mama
yangu alipenda Sana kuweka kifua
mbele linapokuja suhara langu, Ila
kiufupi nilimuonea huruma maana daah!
‘ nisamehe mama, nimeivunja Imani
yako, nilijitahidi Sana kujitunza ili
kukuheshimisha walinisema Sana
kutokana na uchangamfu wangu uliopita
kiasi, Ila kwa Sasa, nimegundua zaidi
uchangamfu wangu Ni udhaifu wangu, kwa Sasa Mimi Ni mjamzito’ nilishtuka
baada ya kuongea hayo kimoyo moyo, nilihisi kana kwamba labda mama
angenisikia sijui ingekuaje?
Usiku huo ulipita, hatimae siku ya graduation iliwadia na watu
wakasherehekea, Mimi pia nilisherekea na picha nikapiga, Wala sikua na tatizo lolote mbele ya alaiki. Hatimae Sasa
ilikua siku yangu kuondoka nirejee
nyumbani. Kabla sijaondoka, Gerald
akanipatia notebook moja hivi ambayo
sikuelewa maana yake.
“ Ya Nini hii?”
“ Ni kwa ajiri yako mpenzi, humo Kuna
namba zangu nyingi, uendako huko sijui
utakumbana na changamoto gani? Ila
kumbuka Gerald ndo kimbilio lako la mwisho hivi Sasa, sawa! “ Alinipandishia
nyusi akiashiria kusisitiza.
“ Gerald!” Nilimkumbatia hakika nilikua na bahati, japo Sina uhakika na niendako, lakini kwa hapa daah! Sio
rahisi mwanaume kukupa mimba
akakwambia usiitoe, japo kanipitisha
kwenye kipindi kigumu Cha mawazo Ila
daah! Alikua tofauti Sana.
“ Usiogope, Mimi kwa Sasa namalizia masomo yangu, Kisha niangalie
utaratibu mwingine umekaaje sawa , hakika Mimi nakuhitaji wewe tu kwenye
Maisha yangu, na ujio wa mtoto wetu, niliuandaa haikua bahati mbaya, nilitaka uwe wa kwangu, ndo maana
nilikuzunguka Ami” aliniambia hiyo kauli nikatamani kulia na kucheka kwa wakati
mmoja mwisho nikabaki na sura
isiyoeleweka. Inamaana alikua
alimtafuta mtoto kwangu ilhali alijua
nasoma.
Hatimae tuliagana, mimi na miracle
tulipanda Basi moja japo yeye alikua
akishukia Tabora, Mimi niliendelea na safari, kwani kwetu Ni Geita. Geita
mjini ndo nyumbani kwetu nilipozaliwa
Mimi, japo sio msukuma.
Nilifika stand majira ya saa nane usiku
kulingana na mlolongo mrefu’ wa safari
nilichoka Sana nikashindwa kwenda
nyumbani, kulingana na Hali niliyokua
nayo nilijikuta nahisi kuzimia kwa safari
ndefu, nilipata maumivu ya tumbo
ghafla hiyo ilitokana na safari kua
ndefu . Nilichukua chumba nikapumzika
kwanza. Hadi kukacha. Na hapo ndo
niliweza kuchukua pikipiki nikiwa na
mizigo yangu kwenda nyumbani.
Majira ya saa mbili niliwasili kwenye
nyumba yetu ambayo iliachwa na
marehemu baba yangu ndo jasho pekee
alilopigania baba yangu wakati wa uhai
wake. Mlio wa pikipiki ulimtoa
mwanamke mmoja mnene kidogo mweupe
mweupe, ukimuangalia tu Kisha
ukinitazama mimi unapata jibu moja kwa
moja kua Nina taswira halisi ya mama
yangu.
“ Jamani Amina wangu huyoo” mama
yangu alitamani kulia baada ya kuniona.
Mwenye pikipiki alimaliza kushusha
mizigo kwa kua nilimlipa pesa tayari, aliweza kuondoka zake.
“ Mamaaa” nilimkumbatia mama yangu
kwa shangwe aliekua na tabasamu la
kwenda kabisa yaani tabasamu ambalo lilimtoka moyoni.
“ Ami binti yangu wa pekee za masomo mama angu?” Aliniuuliza akidhihirisha
furaha Yake Kisha nikatoa mtandio
uliokua ukinizonga. Ili niingize mizigo ndani.
“ Mama masomo ndo hivyo, tumeyatamatisha” nilimjibu huku navuta begi kuliingiza ndani, ghafla nikashtuka
baada ya kusikia sauti Kali na nzito
ambayo sikuwahi kuisikia ilitoka kwenye
kinywa Cha mama yangu tangu nizaliwe.
“ Kama ulivyowasili hapa na mizigo
yako, yote yote, iwe hivyo hivyo, uondoke hapa kwangu, ukatulize maisha
yako kwa huyo uliemtegea kiuno mpaka
ukapata ujauzito” uuuuff! Nini? Nilihisi
kurukwa na akili kwani nilipauka kwa
maneno ya mama yangu mzazi.
Sehemu ya 26
“ Mmamaa… U naongea Nini?” Niliongea
kwa sauti ya chini kabisa na upole
usioeleweka nikimwangalia mama yangu.
“ Unathubutu kuniuuliza!!!! Mama alifoka
nikajikuta nakaa kimya Sana.
Mama alishika kichwa chake na mikono
miwili kana kwamba alihisi kua chizi,
Kisha akashusha mikono Yake na
kufunga kitenge vyema… Mama yangu
alipagawa kwa taarifa yangu ya ghafla.
“ Amina… Yaani Amina una mimba?”
Alinihoji kana kwamba Mimi ndo nilimpa hiyo habari.
“ Kwa Nini umekuja hapa na ujauzito, huyo mwenye huo ujauzito wako kwao wapi?” Mungu wangu swali la mama
yangu liliniacha hoi. Mimi na Gerald tulipata muda mzuri wa kufanya Mambo
yetu kwa wingi lakini hakuna ambae
aliweza kumuuliza mwenzie kuhusu
kwao, huo ulikua upendo wa aina gani?
“ Nakuuliza wewe mwanaharamu” kwa
maneno makali ya mama yangu ambayo
sikuwahi kuyaambulia nilianza kulia kwa
sauti na kwikwi huku nikiogopa
kufukuzwa nyumbani. Nikakumbuka siku
moja katika story za juu juu Gerald
alisema kwao Ni iringa.
“ Mama kwao kwao Ni iringa” nilimjibu
mama ambae hakuweza kuniacha zaidi ya kunishushia kibao Cha haswaaaa.
Nilishika shavu langu na kuzidi kulia. Ni makosa yangu hata hivyo.
“ Mama naomba unisamehe, nilipitiwa
mama yangu, Ila nahuakidi mama
matokeo yangu yatakuja yakiwa vizuri na ntasoma mama yangu”
“ Shenzi unadhani Kuna mtu wa kukusomesha Tena. Fanya haraka uondoke hapa sitaki kukuona Amina. “
Mama yangu aliongea Kama vile yupo serious
“ Mama Mimi Ni binti yako”
“ Ulivyokua unatega kiuno kupokea
mtoto mwingine ulinikumbuka mama yako? Uliwaza hata Mara moja kua
ntakua kwenye Hali gani nikipata
taarifa hii?” Mama yangu aliniwakia
kiasi kwamba nikashindwa kuvumilia.
Nilimbembeleza Sana anisamehe Ila
mwisho wa siku alinifukuza kabisa.
Sikua na sehemu ya kwenda wakati huo
hivyo nilivuta mizigo yangu mpaka kwa
jirani kabisa. Nilifika kwa jirani na
kuanza kumtafuta Gerald ili nimueleze
Ila sikuweza kumpata kwenye simu mwenzenu mimi niliumbiwa mikosi eti.
." Umempata?" Jirani aliniuliza nikakosa
jibu zaidi ya kulia tu.
“ Amina binti yangu, sio Kama
nakufukuza Ila tambua ya kwamba Mimi na mama yako Ni watu ambao
tumeshibana Sana na tumetokea mbali,
kwa kosa kubwa ambalo umefanya
kwake naomba usiwe sababu ya kunikosanisha nae’”
Kwa maneno hayo tu nilikua mtu mzima
tayari Sasa kwa Nini nisimuelewe Mimi.
Niliweza tu kuinuka na haraka Sana
nikachukua vitu vyangu na kufunga
safari mpaka kwa dada yangu ambae
alipatikana mjini hapo hapo Ila eneo
tofauti kabisa na nyumbani kwetu.
Majira ya saa 10 nilikua kwa dada yangu Da froza.
“ Ami mbona umekuja ghafla Sana alafu hata taarifa hukutoa mi natoka sokoni
napokelewa na Daniella ananieleza
mamdogo kaja vipi kwani?” Alinihoji.
Da froza Ni mtoto wa shangazi yangu,
Ni dada ambae tulitokea kushibana kabisa.
“ Dada wee acha tu mdogo wako Nina magumu hapa, sijui nifanye Nini Mimi?”
Nilimwambia kwa kuweka sura ya huruma nikiwa naongea nae simu Yake ikaita akaipokea na kuanza na neno “
hallo shangazi Tausi”
Wee! Huyo shangazi tausi Ni mama
yangu Mimi? Na hapo ndo nikajua
kabisa moja kwa moja Sina pa kukaa.
“ Wee aunt, kwa hiyo Ami ana ujauzito?” Da froza alifoka nikajikuta
nainamisha uso wangu mwenyewe.
“ Sawa aunt nimekuelewa, hakika
nitamtafuta kwa Hali na Mali niongee
nae, kwa Nini Amina ameishia kututia
aibu hivi?” Sidhani Kama mama yangu
alitambua hata Niko wapi? Kwa kweli
nisingerudi nyumbani kwa jinsi
alivyonifukuza sio Siri nilimuwekea
kinyongo moja kwa moja. Baada ya
muda kidogo da froza alikata simu Yake na kuniangalia kwa Makini.
“ Aminaaa!!!” Sauti yake’ ya msisitizo
ilimaanisha kabisa yaliyomo.
“ Da froza hakika mama kakwambia
ukweli, sio Siri Mimi Ni mjamzito, lakini haikua kusudi nili___”
“ Em kaa kimya” da froza hakutaka
hata kunisikiliza.
“ Amina, kwa Sasa Ni jioni na hivi Sasa
muda umekwenda Sana, hifadhi yako
hapa Ni moja tu, kulala usiku mmoja
kesho asubuhi urejee nyumbani kwenu, najua aunt Tausi atakupokea tu”
“ Dada ukweli siwezi kurudi nyumbani, mama anahasira na Mimi kiufupi wakina
Kaka wataniua naomba unisaidie “
“ Hivi wewe ni kichaa’, hao Kaka zako’
sio Kaka zangu Mimi? Inamaana hapa
huwa hawafiki si ndio?” Dada alinifokea
nikakaa kimya na kuanza kulia.
“ Sijali kuhusu kilio Chako Ila unafaa
ujiandae kwenda popote ambapo unajua
patakufaa sio hapa kwangu, usinigombanishe na ndugu zangu Amina “
sikuweza kusema kitu. Hata hivyo Ni
ujinga wangu Mimi. Nilijiachia Sana kwa
Gerald.
Majira ya usiku baada ya chakula
ambacho nilikula Basi tu kikubwa nisife
na njaa, Ila Radha yake haikuweza
kupenya hata kidogo kwenye kinywa
changu. Nilielekea chumbani kulala.
Bahati mbaya Sana simu ambayo nilikua
naitegemea ghafla sikuweza kuiona.
Niliitafuta Sana kwenye mizigo niliyokua
nayo Ila sikuipata kabisa. Ndipo
nikakumbuka wakati nashuka kwenye
Basi nilikua na hekaheka za kushusha
mizigo na Kuna mtu nilimkabidhi anishikie.
Wakati huo nilikua nikija kwa Da froza
“ Mungu wangu, Mungu wangu, nilipoteza simu kwa uzembe wangu
Mimi” nilianza kulia upya. Kwa kipindi
hicho Cha siku moja nilihisi Kama dunia ilikua na miguu. Na niliibeba kichwani
kwangu.
Sehemu ya 27
Nilichanganyikiwa baada ya kukosa
simu, nikajikuta najuta kwa Nini
sikuweza kutoa ujauzito ule. Yote yalikua makosa yangu Sasa kwa Nini
niliwasikiliza watu ambao hawakuelewa machungu niliyokua nayapitia Mimi wakati huo.
Usingizi haukuweza kupita kwa wakati
huo. Asubuhi na mapema majira ya saa kumi na mbili alfajiri dada alikuja
kuniamsha na wakati huo ndo nilikua nimelala.
“ Amina amka sasa hivi uende nyumbani
mdogo wangu, naimani mama yako
kashaisuuza nafsi Yake siwezi Kukuacha
hapa na Sasa nataka kuwahi kazini”
aliniambia nikahisi kupagawa dada alikua
akinifukuza. Kwa kweli niliinuka na nguo ambayo nilivaa nikaingia bafuni kuoga
nikamaliza kuoga na kuvaa. Kisha, nikachukua vitabu vichache Sana notebook aliyonipatia Gery, moyo wa kwenda nyumbani haukuwepo kabisa.
“ Fanya haraka” alinisisitiza nikajua kabisa hataki uwepo wangu pale nyumbani. Kitu pekee ambacho nilihitaji toka kwake ilikua msaada wa simu Yake tu.
“ Niazime simu yako dada” nilimwambia hakua na shida alinipatia simu, nikafungua notebook niliyokua nayo.
Nikaanzaa na namba moja baada ya nyingine, ki ufupi namba za Gerald
nilizokua nimezoea hazikupatikana
kabisaa. Nikaangalia kwenye notebook.
Nikakutana na namba iliandikwa (office)
hiyo ndo niliitumia kumpigia Gerald
namba Ile iliita kwa muda kidogo ikapokelewa.
“ Hallo “ sauti ambayo sikuifahamu
kabisa kwenye ngome ya masikio yangu ilisikika.
“ Samahani naweza kuongea na Gerald
Tantalila” nilipoongea hivyo, sikua na matumaini kabisa.
.” Dr Gerald yupo kwenye chumba Cha
upasuaji, subiri Kama masaa mawili
baadae Kisha umtafute kwenye simu
Yake ya kawaida” mmhh nilishtuka Sana
masaa mawili Tena?
“ Samahani Kaka yangu, nilikua nashida nae kubwa sijui naweza kumpata”
“ Dada samahani, yupo anapambana na uhai wa mtu, unaweza kungoja kidogo.
Masaa mawili sio marefu Kama
kupambana na roho inayoning’inia”
Majibu ya huyo Kaka yalimtoka kwa
upole Ila Ni Kama nilitupiwa mawe
kwenye masikio. Hatimae niliweza
kungoja. Baada ya kukata simu na kumpatia dada.
“ Unaenda Sasa?” Alinihoji.
“ Ndio dada naenda” nilimjibu bila shida.
“ Hakikisha unafika nyumbani na sio
kufanya Jambo la kipuuzi” aliniambia
hata hivyo alikua ndugu yangu khofu
lazima iwepo. Ukizingatia alikua
akinipenda Sana hapo awali japo kwa
hili hakua na msaada Ila Da Froza
siwezi msema vibaya.
Baada ya dada kuondoka nami
nilisimama nje ya nyumba Yake Kwani
alifunga mlango kabisa. Sikuchukua
chochote zaidi ya vitu vichache
vilivyotoshea kwenye mkoba wangu.
Majira ya saa tatu, tayari Yale masaa
mawili yalikua yamepita, hakika nilikua
tayari nilikua nimewaza kujifia iwapo
Gerald atakosekana, nilikumbuka kauli
yake kua yeye ndo kimbilio langu la
mwisho. Sikua na wa wa kumuamini zaidi yake.
Niliazima simu kwenye kibanda Cha
jirani yake dada aliekua akiuza matunda na mboga mboga (genge) aliniazima huyo
dada nikaweka namba ambayo ilinipa
muda wa kupiga. Nilipiga Ile simu
ikaita. Na haikuchukua muda
ikapokelewa.
." Halo" nilianza kuongea.
“ Naongea na Nani?” Sauti iliyoufanya
moyo wangu kusisimka nakujihisi kupona
baada ya mbio za muda mrefu’
niliisikia, mwenzenu nilianza na kilio kabisa.
“ Ami,,, tafadhari usilie” aliongea Gery kwa mshtuko niliokua nao nilihisi kabisa
amenielewa nipo kwenye Hali gani?.
“ Gerald kwa sasa suluhu langu Ni moja
tu, kufa” nilimwambia nikiwa
namaanisha yaani, niliamua kuchagua kifo baada ya yote.
“ Ami naomba utafute sehemu ya
utulivu ukae, nakupigia saa hii, kwenye
namba yangu ya kawaida sawa, sawa
mama angu, acha kulia kipenzi changu
nipo Gery wako.” Gerald alinijibu hivyo
na kunipa faraja kidogo angalau nilihisi
kupata pa kuegemea. Kisha simu
ilikatwa na Mimi nikafanya Kama
alivyosema, muda huo huo simu
niliyoshika iliita nikabaki kushtuka na
kushindwa kuipokea. Nilikaa sekunde
kadhaa mpaka simu ikakaribia kukata
ndio nikapokea.
“ Geryy,,, mmhhi hii” kilio changu ilikua neno la kwanza kwa Gery .
“ Ami tafadhari nisikilize kipenzi
changu, nakuomba usilie, mm sawa
mama, usilie na unisikie, si unakumbuka
nilikuahidi kua kimbilio lako la mwisho?”
“ Gery Sasa utawezaje wakati upo mbali, na bado upo mafunzoni? Sitaki
wote tuharibikiwe, kwa Sasa jipambanie”
“ Itakua na maana gani iwapo
nitapambana alafu akosekane wa kutumia kile nachopambania Ami
wangu,, mpenzi napambana kwa ajiri
yako na mtoto wetu, haya nisikie kwa
Makini si upo Geita?” Aliniambia na kunihoji kwa pamoja. Kwa ujinga nikaitikia kwa kichwa utadhani ananiona.
“ Ami nijibu tafadhari”
“ Gery nimekujibu ndio, naishi geita”
aah’ Gery alihisi nimechanganyikiwa kabisa.
“ Ok una shingapi hapo ?” Alinihoji nikabaki kujiuma Uma.
“ Nina elf thelethini na tano. “
Nilimjibu ukweli.
“ Hiyo Ni nyingi Sana Ami, Sasa sikia, nataka uende nyumbani kwetu, uende
nyumbani kwetu, wanapopatikana wazazi pamoja na familia iliyonileta ulimwenguni” mmhh nilishtuka. Inamaana nilikua naenda kwao Gerald.
“ Gerald kwenu sio iringa??” Nilihoji
kwani nilijua hivyo.
“ Nilikua nakutania hapo kabla kwani
sikua nayachukulia serious mahusiano yetu, wazazi wangu wapo chato origin yao Ni Kenya. Ila wanaishi chato.
Unafaa kwenda huko kwa utambulisho ninaokupatia sawa”
“ Sawa” sikua na Budi kumsikiliza
maelekezo yote aliyonipa.. Kuna wakati
nilipingana nae kutokana na mbinu
aliyonipatia Ila sikua na Budi kumsikiliza
kwani nilikua nashida zaidi.
Sehemu ya 28
Niliyasikia vyema maelezo ya Gery na kilichofata ilikua kutenda. Ki ufupi
ilikua mtihani Sana kwangu lakini sikua na namna, maana hakuna
kilichowezekana. Nilienda mpaka stand ya magari na kukata ticket tokea Geita
mjini kwenda Chato. Nauli haikua
kubwa Sana kwani Ni karibu tu.
Hatimae gari iliwashwa na dereva
akaiongoza kufatia barabara
inayoelekea huko Chato.
Majira ya saa Saba mchana gari
iliwasili katika mji mdogo na maarufu
zaidi Geita uitwao Chato. Madereva
boda boda Kama ilivyo kawaida Yao
iwapo Wataona gari ikiwasili stendi Basi
haraka wataiwahi ili kuwania abiria
waliopo ndani ya gari niliteremka kwa
uangalifu Sana nikiwa sitaki kusumbuana na watu pamoja na wapiga debe
wanaohitaji abiria kwenda sehemu nyingine mbalimbali.
“ Dada Mambo” Bodaboda mmoja
aliwahi kunisalimia. Nilimwangalia na kuelewa Nia yake hata hivyo.
“ Poa”nilimjibu kwa kumdadisi.
“ Twaweza enda usafiri upo, popote
ndani ya Chato Ni buku tu” aliongea
kibiashara zaidi.
“ Sawa nipeleke kwa mchungaji Tanta”
sikuweza kumalizia jina linaloendelea
Kwani sikua nimekalili.
“ Oohh’ sister hesabu umefika, we utakua mteja wa sita kumpelekea kwa
pastor Tantalila leo” aliniambia Kisha
akaanza kuongoza njia kuifata pikipiki
yake. Nilipanda pikipiki hiyo na
kupelekwa mahala nisipopajua . ‘ dah!
Huyu mchungaji Tanta ambae Ni baba
yake’ Gery atakua maarufu kiasi gani?
Yaani umtaje Mara moja tu mbele ya mabodaboda na tayari mtu apajue.’
Niliwaza tu na kukata kimya
TARATIBU.
Mdogo mdogo hatimae pikipiki iliwasili
nje ya ngome moja ambayo ilikua na geti jeusi lililofunguliwa na kuachwa wazi, kitendo Cha kuingiza pikipiki
ndani, nilishtuka KWANZA. Kulikua na watu karibu ukumbi mzima uliokua mbele yangu.
“ Sister, naona leo mnamaombi ya kanisa” yule dereva Bodaboda alitania sijui kwa Nini aliniambia hivyo
mwenzake, nilimrejeshea tabasamu na kumlipa pesa yake tu Kisha huyo akaondoka zake.
“ Unangoja Nini hapo? Beba ndoo ya Maji tukanawishe wanaume ndani” Kuna
mwanamama mmoja alikuja nilipokua
nimesimama Mimi Kisha akanikabidhi
ndoo la Maji mengi kiasi. Nikashangaa
khaa! Ilikua ajabu. Hata hivyo
nilipoangalia Hali ya hewa nikagundua
kabisa kutakua na ugeni hapo kwenye
hiyo nyumba. Japo nimewasili wasaa
huo huo, tayari nimeanza kufanyishwa
kazi.
Jamani simjui yeyote wakati huo, sio
Cha mchungaji Tanta mwenyewe Wala
Nani? Ila ndo kufika nafikia majukumu
makubwa. Nilimfata huyo mwanamke na
kuanza kunawisha wanaume Maji. Ki
ufupi wanaume waliokuwemo ndani ya
Sebure nzuri ya kupendeza iliyosheheni
mapambo na samani za gharama
walikua watu wazima.
Baada ya kunawisha nikaanza kugawiwa
sahani ambazo kwa mikono yangu mimi
nilisafirisha mpaka kwenye mikono ya
hao kina baba na kuhakikisha kila
mmoja amepata sahani yake na tayari
wapo wakila.
Baada ya hapo wanawake wengine
wadogowadogo ambao nililazimika
kujichanganya nao ili nipate kula kwani
tayari nilihisi njaa. Niliambatana nao
kwa ajiri ya chakula, hadithi zao zote
ilikua juu ya masuhara ya kanisani.
Mwenzao kwenye suhala la ibada nilikua
nyuma Sana, hata sikumbuki kabisa kua
Ni lini nilienda kanisani?.
Baada ya kula watu wote walikusanyika
katika ukumbi ulioandaliwa na kuanza
kupeana mahubiri. Mwanaume mmoja
nadhifu’ na alieonekana mrefu kiasi
Fulani na mwenye kitambi japo sio
Sana. Mweupe mweupe Kama Gery tu alikua msitari wa mbele kuhubiri. Yangu
yalikua macho tu na masikio nikisikiliza
neno la Mungu. Baada ya yeye kuongea
kwa muda mrefu alisimama mwanamke
mmoja aliejaa tabasamu Kama la Gery, wee bila kuambiwa nilijua kabisa huyo
Ni mama Yake Gery kwa Nini alikoswa
aibu na kuchukua sura ya mama Yake
alafu akawa na tabia za hovyo!, Daah!
Ningefanya Nini zaidi ya kutazama tu.
Hatimae majira ya saa 11:30 watu
walitoweka na kuacha mazingira yakiwa
Safi kabisa. Watu walipoondoka
tukabaki watu wachache Sana pale.
Wazazi wa Gery, kijana mmoja mdogo
mdogo tu, alionekana kua na umri wa miaka 21 hivi, binti mmoja mdodogo wa miaka 18 pamoja na Mimi.
Mwenzao sikua nimeondoka na Hilo
liliwashangaza watu pale. Yule kijana
alishindwa kuvumilia kuniona bila
kuondoka akaamua kunifata nilipokua nimekaa.
“ Dada samahani” alivuta kiti na kukaa
pembeni yangu nikiwa nimejiinamia tu.
“ Aah’ kwani we ni Nani? Mbona
hujaondoka?” Swali lake liliniacha hoi, daah! Nilifaa kuondoka kweli?.
“ Mi siondoki, ndo nimefika” nilijikuta
Nampa Hilo jibu bila aibu, akanitaza
kwa Makini.
“ Inamaana gani? Muda umeenda hivi
sasa Kama mtoto wa kike unafaa kuwahi
nyumbani kwenu” mmh! Eti nyumbani
kwetu, shenzi kabisa kwa ajiri ya Kaka
yako mama yangu alinifukuza nyumbani
utadhani labda hakunizaa, ndugu
wamenikataa alafu unasema maswala ya nyumbani kwetu?. Nilimkodolea macho nikiwa namtukana kimoyo moyo.
“ Mbona kimya?”
“ Ndio nipo kimya kwa sababu Mimi
siondoki. Nimekuja hapa kwa sababu Sina sehemu nyingine ya kwenda” Kaka
wa watu alivurugwa akajikuta
akitabasamu bila kuelewa maana yangu.
“ Kaka yangu, Mimi Ni mjamzito, na
muhusika wa ujauzito wangu sijui Kama
Ni Kaka yako Ila anaitwa Gerald”
nilipotamka Hilo jina kijana wa watu
alishtuka na kubaki kanitazama tu.
Nilijua tu nimemuacha na maswali mengi kwenye ubongo wake.
“ Wewe Gerald umekutana nae wapi?”
Aliniuliza kwa mshtuko nikabaki kumtazama.
“ Ningetamka vipi jina lake iwapo simjui, nimekutana nae morogoro, nilikua masomoni pia, kwa ajiri Yake
kila kitu kimevurugika, ki ufupi Nina ujauzito wake” nilimjibu kwa huzuni na kuanza kulia juu.
Sehemu ya 29
Kijana wa watu alibaki kutoa macho bila
kuamini Ila haikua sababu ya Mimi
kushindwa kuongea. Ni kweli kabisa
ulikua ujauzito wa Gerald.
“ Sister subiri kwanza, acha niwape hii
taarifa mjomba na shangazi watajua
namna ya kukupa sikio Lao” hapo ndo
nikajua kumbe alikua binamu.yake Gery.
Aliinuka kwenye kiti na kujikongoja
mdogomdogo Hadi alipokua kasimama
mwanaume na mwanamke wakiwa na
maongezi matamu kwani walionekana
kutabasamu kila wakati.
Nilikua mbali nao hivyo sikusikia
walichokiongea ki ujumla, Ila niliona
wakija taratibu mahali nilipokua Mimi.
Kwa pamoja walivuta viti vyao nikabaki
na aibu, bila kusita niliinuka taratiibu
na kuwasalimia upya. Wakati huo
tayari Ni majira ya saa 12:15
“ Usijari mama, amani ya bwana iwe
nawe” mwanaume yule alijibu nikaitikia.
Pamoja na mwanamke wa pembeni Yake.
“ Eti binti? Taarifa alizotupatia Gerson
Ni sahihi?” Nikabaki kimya bila kujibu
maana ilikua aibu, kwanza kabisa
nimepata ujauzito pili, nimejipeleka
mwenyewe nyumbani kwao mwanaume
wangu. Aibu hii! Niliinamisha uso wangu na kujikuta natoa machozi tu.
“ Ongea kipenzi, huu Ni wakati wa kua huru kimaongezi ili uhakika wa kusaidiwa upatikane” yule mama
aliongea kwa lugha laini nikashindwa kujizuia kuongea.
“ Nnndio, Ni sahihi” nilisita kwanza na kuinua uso wangu kwa aibu. “ Mimi Ni mjamzito, na ujauzito huu Ni wa
Gerald, nilikutana nae morogoro mjini
nikiwa masomoni, na yeye alikuja kwa ajiri ya field “ nilijibu hapo kwa
kutetemeka.
“ Una uhakika Ni Gerald Tantalila?”
Mchungaji alinihoji.
“ Baba samahani lakini Ni yeye, alikua akiishi na mwanaume mmoja aitwae
Brighton, nawezaje kumsingizia!”
Nilianza kulia hapo ili nisihojiwe zaidi.
Kwa Nini hawakuniamini moja kwa moja
mpaka wanihoji?
“ Usilie ngoja kwanza tumpigie simu
Gerald, kijana mshenzi huyu anathubutu vipi kunitia aibu,, ameenda kusoma au ameenda kuharibu Maisha ya watoto wa watu??” Mwanaume yule alivuta uso
wake ndita zikakunjamana huku akitoa
simu kwenye mfuko wa Shati lake.
Nilipata uoga Mimi ki ufupi mwili ulikua
pale lakini roho ilikua mbio maili 20
kabisa kuiacha nyumba hiyo.
Simu iliita muda mrefu’ mwisho ikakata
bila kupokelewa, hatimae mwanaume yule alipiga Tena.
“ Kwa hiyo ujauzito wako una miezi mingapi?” Mwanamama alinihoji huku
mume wake akihangaika na simu ya
Gery .
“ Mitatu” nilijibu kwa aibu.
“ Mmhh! Miezi mitatu Ni mingi Sana
masikini binti wa watu, kwa hiyo hata
masomo hukuweza kuhitimu. “ Kabla
sijampa jibu lake tayari Gerald alipokea simu.
“ Hallo mzee” simu iliwekwa sauti ya juu’ kila mtu asikie hivyo nilimsikia
kabisa. Walisalimiana hapo ki imani nikashangaa Gerald kumbe Ni mlokole mzuri tu, imekaa kushangaza.
“ Gerald unamfahamu binti aitwae
Amina Iddi” nilibaki kimya kwa kutajwa jina langu.
“ Samahani baba Amina ndo Nani?”
Duhh nilishtuka hatari, kwamba Gerald hakua akinijua?
“ Unafanya Kama humjui Amina si ndio, amekuja binti mmoja hapa, kasema
kwao Ni Geita mjini, alipo kwa Sasa
kwao amefukuzwa amekuja moja kwa
moja hapa nyumbani, na kibaya zaidi
Ni mjamzito, humfahamu.huyo binti?”
“ Mmhh baba hebu muulize vizuri, siku
hizi wanawake wengi Ni matapeli, nawezaje kumjua alafu nimkane mi simjui”
Aiiii nilihisi kunyeshewa na mvua ya
mawe, kweli Gerald wakuniona mi
tapeli, ajabu na aibu iliyoje mbele ya
wazazi wake. Nikabaki na mtazamo
usiyoeleweka shenzi kabisa Gerald,
wewe ni kuku wa kizungu, nakuchukia
wewe na mipango yako ya mchongo’
niliwaza kumtukana zaidi Ila
nikakumbuka nafaa kung’ang’ania point yangu. Nilishuka chini kwenye magoti ya
yule mzee na kuanza kulia kwa sauti ya
juu’
“ Gery usijifanye umenisahau, nadhani
unanikumbuka vyema kabisa, Mimi Ni
Amina, Amina Iddi ulikutana na Mimi
nikiwa likizo, hukumbuki vyema hata
Kama ilikua Mara mbili tu, lakini
ilitosha mimi kua mjamzito, naomba
usinikane ntaishi wapi Mimi?” Nililia
hapo kwa uchungu huku nikiwa na aibu
Sana kujidharirisha.
“ Gerald kweli katika masikio yako hiyo
sauti hukuwahi kuisikia, binti wa watu
anaonekana asie na hatia, kwa Nini
umeharibu Maisha Yake huku yako
yakisonga mbele, ntakuachisha
masomo.sasa hivi na dhamiri yako
isitimie shenzi wewe” angalau
alipatikana mtu wa kumtukana Gerald
mbwa huyu, ananikana?
“ Baba samahani Sana mzee wangu
najua ntakukwaza Ila sina Budi kusema ya kwamba, mwanamke huyo ni.kama
namfahamu vile, nilikutana nae Mara
mbili tu, sidhani Kama ilitosha kwake
kua mjamzito, hata hivyo hatukua na
uhusiano wa karibu ki hivyo mpaka awe na mimba.”
“ Nyamaza kimya, na bado unajiita daktari shenzi kabisa wewe!!” Baba
yake alikasirika kiasi Cha kwamba
Angekua karibu angempiga mangumi ya kutosha tu, kimoyo moyo nilihisi furaha.
“ Sawa baba, kwa kua mnahisi hivyo, na kwa vile anasema Ni ujauzito wangu, samahani niliteleza naomba unikubalie
ombi langu, naomba Sana akae hapo na kutunzwa kwa chochote kiasi
ntakachopata, ili.tuangalie pindi
akijifungua iwapo mtoto atakua wa kwangu?” Yaani Gerald alikomaa akikana
kama vile hakua mtoto wake. Wakati
alipigana nisimtoe.
“ Unaongea kana kwamba sisi hatuwezi
kumtunza mwanamke aliebeba mjukuu
wetu kwenye tumbo lake, potelea mbali
huna maana kabisa na haufai hata
kidogo” mama Yake Gerald aliwaka kwa
hasira juu Yake. Na baba yake’ Gerald
akawa amekata simu.
“ Mama karibu ndani! Mpaka hapo
tumekuamini japo kwa asilimia nusu, Ila
tuombe Radhi Sana kwa kuharibiwa
mustakabari wako na huyu kijana
tuliemzaa bila manufaa” wee nilihisi
kucheka kimya kimya, Gerald hakua na manufaa. Hatimae nilipokelewa kibabe.
Sehemu ya 30
Nilianza Maisha mapya nyumbani kwao
Gerald, nyie nilikua tu mjamzito lakini
niliishi Kama malkia. Ki ufupi mipango
ya Gerald kujifanya ananikana ilinikera
japo sikua na njia zaidi ya kukubari
kujidharirisha. Ila hata hivyo ilikua ya msaada Kati yangu na yeye. Baba yake
alionekana mtu mzuri katika
kuwahifadhi wengine Ila mkali Sana kwa watoto wake.
Kwa kua nilienda huko bila nguo, kesho
Yake yule binti pamoja na mama Yake
Gerald. Walienda kuninunulia nguo za
kutosha nikabaki kushangaa, kila aina
ya nguo kwa kua wakati huo mimba
ilikua changa nilikua naweza kuvaa nguo yoyote.
Niliangalia yale mavazi nikakutana Ni
viwalo vizuri vizuri nikabaki kushangaa
Hawa Ni walokole na wachungaji bila
Shaka ningefaa kuletewa nguo za
kichungaji lakini nimeletewa nguo za
kwenda na fashion. Amazing.
“ Usijari una mwili mzuri Sana, hufai
kuvaa manguo ya kukuzeesha mkwe
wangu” mama mkwe huyo jamani, bahati
iliyoje alinikubali moja kwa moja. Ki
ufupi nilimmiss Mira, nilitamani
kumhadithia majanga yote
yaliyonikumba Ila ningempata vipi Sasa?
Sikua na simu.
Majira ya jioni, baba mkwe alirejea
kutoka kwenye majukumu yake’
tulimpokea hapo, akiwa anaongea na
mke wake kwa wingi huku wakicheka ki
ufupi walijaaliwa kupendana Sana kwa
namna walikua wakitaniana. Baada ya
muda baba mkwe aliingia chumbani
kwake. Na mama mkwe akaniita.
“ Amina njoo” nilimfata bila kusita.
“ Shika hapa, Gerald amekutumia simu
na tayari kakusajilia laini, kua huru
kuongea nae wakati wowote” wee
nilishangaa, mwanzo nilikua natumia
kiswaswadu lakini hivi Sasa ilikua simu
janja Tena ya kisasa zaidi nilihisi
kuvurugwa mwenzenu, huyu Gerald Kuna
wakati anakaa Kama mtu jamani.
“ Mama asante, Asante Sana mama”
nilimshukuru Sana jamani.
“ Sii Mimi wa kushukuriwa, mshukuru
Sana mumeo, na uhakikishe unamtunza
vyema mjukuu wangu” mmh! Kila Mara
mama huyu angenikumbusha suhara la mjukuu wake. Nilifanya Kama alivyotaka
hata hivyo ilikua Raha Sana kununuliwa
kitu na mtu unaempenda hata Kama
unakila kitu, ila zawadi yake ndogo tu Ni tabasamu Tosha moyoni mwako.
Usiku baada ya chakula changu, maana
nilikua nikiandaliwa chakula special
kabisa na mama mkwe akidai Mimi Ni
mjamzito sifai kula kula kila kitu
haitakua afya kwa mtoto alietumboni
mwangu. Hivyo alikua akinipikia
mwenyewe. Niliingia chumbani kwangu
chumba ambacho kiliandaliwa maalumu
kwa ajiri yangu kilipambwa
inavyotakikana na kuhakikisha kinavutia
macho yangu, nilikaribishwa na Mwalu, alikua binti yule wa miaka 18 alikua
mfanyakazi katika nyumba hiyo.
“ Asante” nilimwambia kwani alijituma
Sana kuniandalia chumba hicho.
“ Mmhh sio lazima useme Asante wifi yangu, wewe ni mke wa Kaka Gerald. “ Alitabasamu na kutoka nje, nikabaki
mwenyewe na kufunga mlango kwanza, Kisha nikaoga na kujitupia kitandani na kushika simu yangu mpya iliyokua na
laini bando mpaka salio, nikajaza namba
za Miracle kwani nilikua nazo pamoja na namba za Gerald, na namba za
wanafunzi wenzangu sikuweka namba ya ndugu yangu hata mmoja.
Nilitaka nimpigie Gerald kwanza ili
nimshukuru Ila nikaona haina haja kwani
Gerald si yupo tu, mtu wa kwanza
kumpigia alikua Mira. Simu yake iliita sekunde kadhaa hatimae. Ikapokelewa.
“ Hallo” aliongea akiwa wa kwanza.
“ Patia unaongea na Nani bi mdogo!”
Sauti.yangu tu ilimtosha kuguna.
“ Kwamba nimekua kiziwi Hadi nisijue sauti yako, hujambo kwanza ? mbona
una namba mpya? Na kwa Nini simu
yako haipatikani ?”
“ Daahh ndo kupokea na maswaaali, anyway nilikutana na majanga kibao hivi
Sasa ndo nimetulia mwenzako, najuta
Sana kukutana na watu wawili katika
dunia ambae Ni wewe na Gerald”
“ Ami chunga bakuli lako” alinikanya.
“ Mira unajua nimepitia kipindi gani
mwenzako?” Nilijigeuza hapo kitandani na kuanza kumsimulia jinsi ilivyokua, alibaki kusikitika Ila mwishoni alifurahi
kusikia nimepokelwa vyema Sana.
Nikiwa naongea na Mira simu yangu
ikaita yaani ikaingiliwa na simu nyingine,
ikabidi niangalie mpigaji ni Nani? ‘
owner of my heart’ (mmiliki wa moyo wangu) haa!! Huyu Ni wazimu, niliweka tu namba Yake sikua nimeisevu kumbe aliisevu kwa jina baya Kama Hilo, bila
Shaka ana wazimu.
“ Ami mbona najiongolesha pekee yangu” Mira alinishtua upande wa pili nikawa Sina Budi kumuaga.
“ Mira samahani naomba ukate
ntakutafuta, acha kwanza niongee na Gerald” nilimwambia hivyo akanijibu haraka.
“ Haa;! Mimi Tena, linapokuja swala la AmiGery huwa Sina usemi” alikata
haraka nikabaki kucheka . AMIGERY
alimaanisha kuunganisha jina langu na Gerald kua pahala pamoja. Nilipokea simu ya Gerald nikiwa nawaza hayo.
“ Unawaza Nini? Kwa Nini nipige simu
yako iite muda mrefu’ bila kupokelewa?”
Lilikua swali lake la kwanza.
“ Nilikua naongea na Mira, hata hivyo
nilimmis na sikua na sehemu ya kuipeleka hadithi yangu ya majonzi zaidi ya kwake Gery”
“ Kwa hiyo Mira na Mimi. Mimi kwako
Ni wa mwisho si ndio? Anyway Ni vyema zaidi ikiwa hivyo” aliniambia
nikajua Sana ametumia lugha ya kunisimanga inamaana nilimkosea tayari.
Potelea mbali asinichanganye kwanza.
Sehemu ya 31
“ Gery na wewe huishi lawama, unaendeleaje kwanza?” Nilimuuliza
kwani kwanzia nipate misukosuko
hatujawahi hata kujuliana Hali.
“ Naendelea vizuri kipenzi changu, lakini nimekumiss Sana, nakutamani kila wakati, nawaza ungekua Moro Ni karibu
Sana bila Shaka ningewasili kuja
kuondoa missing zangu kwako”
aliniambia nikajua Sana uzinzi
unamsumbua mbwa huyu.
“ Ami ki ufupi nakupenda sana, yaani
Hadi moyo wangu huwa unaruka ruka
ukiliwaza jina lako tu “ aliniambia
“ Gery unaweza kuacha siasa, kwa Sasa
Mimi ni mtu mzima sio wa kudanganywa
danganywa”
“ Ami namaanisha, nadhani unanielewa zaidi ya kila mtu hapo ulipo,, naomba
Sana ujitahidi kumtunza binti yangu, natumai Sana mama yangu anakutunza vyema”
“ Gerald kwa kweli sijui niseme Nini?
Wazazi wako Ni watu wenye
moyo.mzuri na laini Sana Kama theluji, ki ufupi wanajari Sana najivunia
kukutana nao katika kipindi hiki kigumu, wananifanya nimkumbuke mama yangu”
“ Usijari, najua hakuna mzazi mwenye
hasira daima na mtoto wake, bila
Shaka Mimi nikija huko ntaenda na wewe nyumbani nikaombe na samahani, sio kwa makosa makubwa niliyotenda
kwa ndugu zako’, najua inaumiza Sana
wamehangaika kukusomesha alafu
msenge mmoja ambae Ni Mimi, nimevuruga samahani Sana Ami”
“ Gerald sio tu kosa lako Ni kosa langu pia, nilikua mwepesi Sana kwako Hadi
unaweza ukahisi Mimi Ni Malaya” nilihisi kulia baada ya kujisema vibaya.
“ Kwa Nini Ami ujiite hivyo?, Hizo Ni hisia tu, Ni ngumu Sana kuzuia
unapokutana na mtu unaempenda,
ulinipenda Mimi Mara moja tu baada ya
kuniona ndo maana hukua na shida
kuniamini moja kwa moja Kama mtoto alipotea njia”
“ Gerald” nilimuita kwa utamu
“ Nambie kipenzi changu”
“ Nakupenda Sana “ kwa Mara yangu ya kwanza Kutamka neno Hilo kwa Gerald ambae sikuweza kusikia sauti yake’ zaidi ya ukimya wa muda kidogo, ki
ufupi Mimi mwenyewe nilipata aibu na kufunika uso wangu. Nikiwa nasikilizia atasema Nini?
“ Ami…” Nilishtuka baada ya kuitwa moyo wangu ukawa unaenda mbio mbio.
“ Naomba uwe unamaanisha, umaanishe
kabisa ukitamka neno Hilo, na usiwahi
waza kunisaliti hata itokee vipi Kati
yetu sawa” aliniambia Kama
anamfundisha mtoto wa darasa la kwanza kuelewa utofauti wa ‘a’ na ‘ q’
“ Namaanisha Gery, Sina mwingine
kwenye moyo wangu. “
“ Nakuamini zaidi Ami wangu, nakupenda Sana, yaani sijui niseme
Nini? Ki ufupi nakupenda Sana .”
Maneno ya kupendana kwa dhati yalikua
mengi Sana, niliongea na Gerald muda
mrefu’ hatimae nikajikuta napata
usingizi kabisa na kuanza kusinzia simu
ikiwa sikioni, Gery alikua na sauti ya
kubembeleza mpaka nikasinzia
mwenzenu.
Majira ya saa tatu asubuhi nilikuja
kushtuka baada ya kuamshwa na mama
mkwe. “ Mama amka ukaoge kipenzi
changu unafaa kua msafi kwa ajiri ya
mjukuu wangu” daahh! Hatimae mama
mkwe anamjua mjukuu wake wa thamani
kwenye tumbo langu. Niliingia bafuni na
kukutana na Maji Safi laini na vugu
vugu, shampoo ilikua tayari imeandaliwa
yaani kila kitu kilikua bomba Sana.
Baada ya kuoga nilipewa nguo maalum na mama mkwe akaniingoza kuelekea
kliniki nikaenda kufungua kadi kwa ajiri ya mahudhurio na maendeleo ya afya
ya mtoto tumboni mwangu.
Maisha yakasonga, miezi ikasogea
nikilelewa Kama binti wa kifalme pale
ukweni, ki ukweli nilikua nammiss Sana
mama yangu wakati wote huo, Kuna
wakati nilikua Hadi naweka namba yake’
ili nimpigie lakini nasita kwa uwoga
ntamwambia Nini Sasa? Kwamba naishi
wapi na kwa Nani?.
Kadri siku zilivyozidi kwenda ndo tumbo
lilizidi kukua kubwa, Ila halikua kubwa
Sana. Nyie kulea ujauzito ilikua kazi
ngumu Sana. Ukizingatia nilipata
kwenye umri mdogo wa miaka 20 tu. Ila
nilikua na mama mkwe pembeni yangu wa kunifariji wakati wote, nilikua na
Gery kwenye simu yangu muda wote
angenipigia simu kunipa maneno mazuri ya faraja tele.
Nilipotimiza miezi nane walikuja dada
zake wawili na Gerald, mmoja aliitwa
Zena mwingine aliitwa Cynthia .
Walikua wadada warembo kupindukia, kiufupi walivutia Sana macho yangu, alafu kikubwa zaidi walikua
wachangamfu kupita kiasi. Kwa ujumla
Gerald alikua mtoto wa kiume wa pekee
kwa mchungaji Tanta, wengine wote
walikua wa kike. Majira ya jioni wifi
zangu wangenipeleka mazoezini na kudai
hawataki niwe mzembe.
“ Yaani wifi tunavyohangaika hivi, alafu
atokee mtoto sio wa kwetu, haki Tena
nakuroga, hujui tu Ni jinsi gani
nilifurahi nikiwa chuo baada ya mama
kuniambia Gerald anatarajia mtoto”
alikua wifi yangu Zena alienipa onyo
Kali akiwa na maana yake.
“ Huna haja ya kufanya mazoezi Sana
unafaa kula matunda ili mtoto azidi
kuhisi msisimko wa kukua mkubwa” nyie
Kuna watu tunazaliwa na bahati
kichwani, sijui ningemtoa huyu mtoto
tumboni mwangu hii care ningeipata wapi?.
‘ wanawake wenzangu, msiwe mnapaniki
mkiwa wajawazito bila kutarajia, Bora
uwe mvumilivu tu haijalishi Ni vipi? Au
wapi utapitia, lakini huwezi jua huyo
mtoto ameandaliwa aje awe tulizo
Tosha la moyo wako. Ki ufupi kila
mtoto huwa anakuja na rizki yake.’
Sehemu ya 32
Baada ya mazoezi walikua wakinirejesha
nyumbani, na asubuhi wangeamka kunipa
mazoezi ya kutosha. Maji ya kuoga
waliniandalia wao kwa wakati huo, chakula chochote ambacho
kingenichefua Basi waliacha kutumia ili wasimuudhi mtoto tumboni mwangu.
Nyie ilikua ya kuchekesha kiasi fulani.
Nilijikuta nahisi kupagawa nikiwaza
mfano hiyo mimba isingekua ya Gerald
ningepata aibu kubwa na laana juu.
Asante Mungu nilikua mtulivu na uhakika
kabisa ya kwamba huyu mtoto Ni wa
Gerald.
Maisha yalisogea. Na hatimae ilifika
miezi Tisa nikiwa pale. Siku ya kusubiri
kwa muda mrefu iliwadia nyie nyie
asikwambie mtu, sikua najua Kama ndo
uchungu ule. Siku hiyo nakumbuka
vyema yaani, alikuja wifi Cynthia
kuniamsha chumbani twende mazoezini
nikabaki kumwangalia. Kwanza sikua
nimelala usiku mzima.
“ Mke wetu, twende mazoezini
ukamchangamshe huyo dogo dogo, hatutaki awe mdhaifu” aliongea hivyo
nikabaki kumwangalia kwa macho ya
maumivu, kwani hawezi kuelewa Hali
yangu mpaka nimwambie?
“ Vipi unaumwa?” Alinihoji nikaitikia kwa
kichwa, sikua na sababu ya kumuelezea
kwa mdomo.
“ Jamani kipenzi pole, Basi lala tu ngoja nikuabdalie Maji ya kuoga na kiamsha kinywa sawa mamy wangu”
aliniambia kwa utamu lakini haikua na
maana kwani wakati huo sikua mtu wa shukrani Kama walivyonizoea.
Niliendelea kulala. Baada ya muda
alikuja wifi Zena, akaniamsha nikaoge, nilitamani kuamka ili kumridhisha lakini
kiburi Cha nafsi kilinizuia kabisa
nikabaki kulala, niliona kulala Ni Bora
zaidi kuliko kuamka. Nikageukia upande wa pili.
“ Ami, una uhakika upo sawa kabisa mdogo wangu” ilibidi anifanye mdogo
wake wakati huo wakati nilikua wifi Yake.
“ Nahisi maumivu kidogo tu, wifi sijisikii kuamka, unaweza kuniacha angalau nilale tu.” Nilimwambia kwa huruma na macho yangu yalilegea.
“ Mmhh sawa wifi we lala, lakini angalau ungepiga mswaki, ngoja nikuletee beseni hapa hapa upige mswaki sawa” afadhari alikua na akili, ananiletea hapa hapa Sina haja ya
kuingia bafuni.
Alifanya hivyo Hadi mswaki akaniandalia
akaniambia niinuke nikawa nahisi Kama
miguu yangu imekufa ganzi, nilipojaribu kuikanyagia iliniuma nikajikuta naguna
mwenzenu.
“ Mmh!’’ Zena alinitazama kwa Makini na kuhisi kabisa sipo sawa. “Wifi
samahani naomba nikupigishe mswaki
mwenyewe” kweli alikua na Nia Ila Mimi
sikua tayari kudeka kiasi hicho.
“ Hapana wifi, nitaifanya mwenyewe”
nilimkatalia na kujaribu kupiga mswaki, nikajikuta nimeweka mswaki mdomoni na
kuganda bila kufanya kitu, daahh!!
Maisha haya, anaemdharau mama Yake
kwa kweli! Mungu anamuona.
“ Mama unaumwa Nini?” Mama mkwe
aliingia ndani akiwa kaongozana na Cynthia sikuweza hata kumsalimia aliponiangalia tu nilisikia sauti yake’
kumuelekea Zena.
“ Unasubiri Nini? Mpigishe mswaki haraka” mama mkwe alitoa amri na Zena akamfatisha.
“ Cynthia kalete usafiri, fanya haraka
Sana” Cynthia aliondoka hapo chapu
chapu. Mama mkwe niliona anaanza
kuvuta vifaa vyote ambavyo vilihusika
mahususi kwa ajiri ya mtu kujifungua.
“ Mwalu andaa chai iwe na majani mengi kiasi” mama mkwe siku hiyo alikua na maagizo kibao. Baada ya wifi Zena kunipigisha mswaki. Mama alianza
kunivisha. Nyie nilikua sijiwezi kwa kila kitu.
“ Ami mama angu, jitahidi usimame usiwe mlegevu kiasi hicho, kule hautakua na sisi utakutana na manesi wa kila rangi sawa mpenzi” alinipa
maneno matamu nikajaribu kuinuka. Ki ufupi miguu yangu ilikufa ganzi tangu
usiku wa Jana Yake, ningewezaje
kuinuka.
“ Jitahidi hivyo hivyo mama angu” wee mama.mkwe aliamua nikajikuta siwezi
kuvumilia namna anavyonibembeleza
alafu nimfelishe nilijitahidi hatimae nikainuka.
“ Haya Zena haraka Toa vifaa nje
Cynthia amefika” Zena alifanya Kama
alivyoambiwa. Mama mkwe alinipeleka
bafuni kukojoa. Akaniambia. “ Kojoa
Mara ya mwisho kwenye choo, kwani
baada ya hapa hautatumia Tena choo
zaidi ya beseni mama yangu” kweli huyu
mwanamke alifaa kuheshimiwa na watu
wengi alijua kubembeleza.
Hatimae tuliingia kwenye gari na safari
ikaanza kuelekea hospitalini. Nilikua
naumia huku sitoi sauti kabisa kwani
mama mkwe aliniambia iwapo nitatoa
sauti kwa uzazi wa kwanza na kupiga
makelele, basi nitazaa hivyo kwa vizazi vyangu vyote. Niliogopa mwenzenu
nikajikaza nikataka kushika kichwa.
“ Mpenzi usishike kichwa Chako hiyo
inamaanisha kukata tamaa Kama
mwanamke, na ukikata tamaa baada ya kujifungua nywele zako’ zitakatika
katika. “ Daah! Huyu mama alikua
mtamu kila wakati lakini saa hii hakuna
kinachokua kizuri nikifanya. Nilijikuta
natamani kulia.
“ Usilie kabisa maana utakua mwanamke wa kushindwa, kitu pekee unafaa
kufanya nikupiga maombi Hadi
kieleweke, Tena sio kwa makelele piga
maombi kimya kimya, omba baraka za
wazazi wako wote sawa” aliniambia
huku naingizwa kwenye wodi ya wazazi.
Ilikua ngumu kujifungua maana hata
masaa yalisogea Sana, nilishikilia kauli
ya mama mkwe wangu kua nisipige
mikelele japo wengine walipiga nisilie
nafaa kujikaza, Kisha nisishike shike
nywele zangu. Nyie yalikua masharti
magumu Ila nilijitahidi kuyafata.
Masaa yalisogea wakati huo nafanya
mazoezi Kama Nini? Baada ya muda
kwenda mama mkwe aliingia ndani nikiwa
nimechanganyikiwa. “ Amina mama
angu, namba za mama yako mbona hakuna humu kwenye simu?” Alinihoji
Hilo swali nikajikuta namjibu vibaya masikini. Uchungu huu?
“ Mama tafadhari naomba uniache, huu sio wakati wa kuulizana maswali juu ya watu fulani, nyie tafuteni mtapata”
mama yangu? Mama mkwe aliishia tu kuniangalia na kutabasamu Kisha akatoka nje! Aah’ potelea mbali!
Mwenzenu niliwaza hivyo yaani sikuweza kumjari.
Sehemu ya 33
Sijui walifanya Nini mpaka wakaipata
namba ya mama yangu, nilishangaa
mama.mkwe anaingia ndani ya wodi
Tena nikiwa nimejikatia tamaa kwani
tayari ilikua saa Saba. Akanipatia simu.
“ Mpenzi salimiana na mama yako, amesema ana Jambo la kukwambia”
alipotamka neno mama ilibaki kidogo
nimwage machozi lakini nikajitahidi
kuyazuia kwani aliniambia nisilie lie.
“ Mama amepatikana ?” Nilihoji kwa
upole na kuweka simu sikioni.
“ Mama” nilijitahidi kumuita kwa maumivu.
“ Ami binti yangu, usife moyo sawa, unafaa kushukuru Mungu kwa kua
umekuza ujauzito wako salama, usiogope
sawa mwanangu” aliongea maneno Yake
nikahisi kufarijika kidogo. Nilijikuta
nasahau Kama vile alinifukuza.
“ Kua mwanamke na ujitahidi Sana
hakika utajifungua salama sawa binti
yangu, mama yako nilikua jasiri Sana
wakati nawazaa nyie” aliniambia kwa
maumivu Hadi nikahisi Kama alikua
akilia. Ni mama.yangu namjua vyema
nashindwa vipi kuelewa kua analia hata
akijifanya kua sawa.
“ Sawa mama hakika ntajitahidi na ntakua jasiri” nilimjibu hivyo na kurejesha simu kwa mama mkwe.
“ Usiogope sawa kipenzi changu, sisi Ni
wanawake wenye nguvu, kwa uwezo
wake Mungu, baba wa mbinguni Alie
hai, naamini na kua na hakika kabisa
binti mkwe wangu atajifungua salama
kabisa” aliniambia hivyo nikatabasamu.
Hatimae alitoka nje. Tabasamu langu
lilififia baada ya kuhisi maumivu yakija
kwa Kasi kuelekea chini. Nyie mama
yangu ndo alikua kanishika nisizae Nini?
Mbona uchungu umekuja kwa haraka
hivyo?
mleteni huku” nilisikia sauti ya nesi
mmoja akizuia nisijifungilie wodini.
Kitanda changu kilivutwa nikahamishiwa
kwenye kitanda Cha magurudumu huku
naaandaliwa kujifungua, Mara moja
nikapelekwa kwenye chumba Cha
{Deriverly Unit }. Haikuchukua masaa
hata kidogo nilijifungua mtoto ambae
sikujua Ni jinsia gani Ila nilisikia sauti
yake’ akilia kwa utamu, nilihisi kupumua
baada ya kushusha mzigo mzito tumboni
mwangu. Nilisafishwa vyema Sana na kubaki mwepesiii. ‘ jamani mwenzenu, hatimae nimekua mama’
“ Usijifungulie hapo haraka Sana
Sikupoteza fahamu Bali nilijikuta nalia
kwa furaha, mtoto huyu alikua Kama
zawadi iliyokuja ghafla kwenye Maisha
yangu, nilianza kumuomba samahani
wakati huo huo kwa kujaribu kumtoa
Mara kadhaa hapo mwanzo.
” Usilie dada, binti yako atalaumu kwa
Nini amekuudhi kwa kuzaliwa” nesi
alisema hivyo huku akimaliza kumvisha
vyema baada ya kumsafisha.
“ Hee! Kumbe kweli Ni wa kike?”
tabasamu langu lilienea zaidi kwa
sababu Gerald alitabiri Hilo mwanzoni
Sana.
“ Ndio Ni wa kike kwani ulikua ukijua?,,
Aa ulipiga picha kuangalia jinsia?” Nesi
alienisadia kujifungua alinihoji nikatikisa
kichwa kupinga.
“ Hapana Kaka, sikua Mimi alikua baba yake’, alitamani Sana kupata binti” nilitabasamu
“ Hakika una bahati Sana, na ninao
uhakika kua mume wako sio msukuma
hata kidogo, maana Ni wanaume
wachache Sana wa kisukuma
wanaopenda watoto wa kike, hujivunia
Sana wakipata watoto wa kiume”
“ Mmh Kaka yangu, kwa dunia hii” nyie
mzazi aliekua amechanganyikiwa na
uchungu nilijikuta naimiliki leba kwa
kuongea kupita kiasi. Nahisi Kama
nilikua mfungwa Sasa nimefunguliwa.
Yule kijana alisaidiana na wenzake
wakaniweka kwenye kitanda Cha
magurudumu Kisha nikapelekwa wodini.
Nilipewa chumba changu binafsi kutokana na maagizo ya mama mkwe
wangu. Walinipokea vyema huku akili
Yao ikiwa imemuelekea mtoto. Nilikua
nimechoka Sana kiasi kwamba sura
yangu ilishuka na kua ndogo zaidi.
Sikuweza kupiga story sana Ila
nilicheka baada ya kumsikia wifi Zena
akisema.
“ Daah mrembo, sio poa katika vyote
nilivyokua navyo vizuri ukaamua
kuchukua bichwa langu” kila mtu
aliangua kicheko hatari.
“ Acheni kumkagua mke mwenzangu, ana sura ya kutisha kwa sababu Ni mdogo, Ila kosa lake kubwa Ni kubeba macho
yaliyolegea Kama Abby na Gerald “
mmhh nilishangaa huyo Abby hata sikua
namjua. Zaidi ya yote yeye ndo alizuia
wasimkague Ila kusema macho
yaliyolegea Kama Abby hiyo
inamaanisha hata yeye anamkagua pia.
Nilicheka kwa Siri.
“ Mama kwa Nini hajafata hata shepu langu zuri??” Cynthia alitia aibu mtoto
hajakamilisha hata siku tayari alifaa
kua na shepu? Nyie Hawa watu.
Mara simu ikaita wakati huo sijamshika hata mtoto Mimi niliemzaa. “ Simu yako
inaita, baba mtoto anapiga kaeni kimya”
mama mkwe alipokea simu na kuweka laudspeaker.
yaani hata kabla watu hatujaongea kitu
tayari ameshalia kwa sauti. Tulijikuta
tunaangua kicheko kwa pamoja.
“ Ng’aaa” hee mtoto mbeya kupita kiasi
“ Mama yangu, kwa Nini mnamliza Gift wangu?” Lilikua swali la kwanza la Gerald.
“ Haa! We Gery wewe hatujatoka hata hospital tayari mtoto anajina?” Zena
alishindwa kuvumilia.
“ Niliandaa jina kabla hata sijampata
mama Yake” watu walibaki hoi Mimi pia, Gery alitamani Sana binti, hatimae kampata.
“ Ulisema tusubiri ajifungue ili tuhakiki
iwapo Ni wa kwako au sio wako
wanawake Ni matapeli, hakika Kaka
Gery, Gift sio binti yako kwani
hafanani na sisi hata kidogo.” Cynthia aliekua mdogo kwa Gery alimtania.
kwangu, hamjui tu namna gani
nilipambana kumpata huyo mtoto”
nilipata aibu kwani nilienda kwao kwa
mipango yake’ mwenyewe. Mama mkwe
alinikata jicho nikainama haraka Sana.
Akaishia kutabasamu.
Sehemu ya 34
“ Ahaa kumbe mlitufanya sisi watoto
wenzenu?” Mama mkwe alimfokea
Gerald.
“ Ahaha’ najua Sana kua Ni wa
“ Mama yaliyopita si ndwele, hapo ujue Sasa mwanao ndo kashaleta mkwe na mjukuu kwa wakati mmoja. Naombeni kuongea na mke wangu kwanza pamoja na binti yangu” aliongea kwa sauti wakakosa usemi.
“ Sawa baba mkwe tunatoka, Ami mama tupo hapa karibu, unafaa ule kwa Sana
usiongee Sana na Gerald sawa?” Mama mkwe aliongea huku Gery akisikia.
“ Mama acha kumfunza tabia mbaya, Ami wangu nimtiifu” hee ! Anajifanya kunisahau. Niliwaza kimoyo moyo.
Hatimae walitoka nje na mlango
ukafungwa nikapata hata nafasi ya
kumshika binti yangu, hakika nilitamani
kua wa kwanza kumshika Ila sikupata nafasi.
“ Ami, upo kwenye dimbwi zito la hisia kipenzi changu, nishukuru Mimi hatimae
umeitwa mama” alinitania nikajikuta
nacheka ningeweza ningemtukana lakini
nilikua kwenye hisia chanya ya kumiliki
mtoto wangu pia.
“ Gery nyamaza, kwanza nataka
kumfeel binti yangu, haikua kazi
rahisi, Gery Ni ngumu Sana kua mama, Ila kwa Sasa sikumbuki Kama niliumia
muda mchache uliopita” nilimwambia kwa
uchangamfu akajikuta anatabasamu kivivu.
“ Aha’ AAA” mmh ! Hilo tabasamu lake ndo lililo nizuzua hapo awali mpaka
kumpata huyu mtoto Sasa, kwa hiyo ndo kaanza mitego yake mapema tu.
“ Gerald acha kujichekesha usije niboa bure”
“ Najua, Ila kiufupi, nakushukuru Sana
Ami, hakika wewe ni bingwa, umeweza
kuniheshimisha katika hii dunia kwa kuniletea binti”
“ Gerald kwa Nini ulitamani Sana binti
ilhali kwenu wa kiume umezaliwa pekee
yako, inaonekana kushangaza!”
Nilimwambia, “ Kwa sababu hiyo ndo
maana nilitamani Sana binti, hakika
nimeishi vyema Sana na dada zangu,
wameumbwa na mioyo mizuri Kama
alivyo mama yangu, hivyo nikaamini
nikiwa na binti atakua sawa na wao. Ila
zaidi nilitamani kua na binti kwa sababu
inasemekana mtoto wa kike humpenda
Sana baba yake’. Maana Mimi Ni
kipenzi Cha mama Gerald na hiyo Ni
kweli na dada zangu wanapendelewa
Sana na baba yangu”
Sababu zake zote, sababu ya kwanza
ndo ilikua sababu ya maana. “ Potea
huna manufaa mama yako alisema”
nilimkumbusha.
“ Upo sahihi, kwa sababu nilikuvurugia
mipango yako, ndo maana mama Gerald
alichukia, Ila Ami nashukuru Sana kwa
kuniheshimisha, na Sasa Gerald anaitwa
baba Gift, acha nikutumie pesa
usherehekee kwani na Mimi Ni siku
yangu ya kusherekea kwa nguvu” sikua
karibu nae lakini hakika niligundua zaidi
kua anayofuraha isiyokua na mwisho.
“ Ami, nakupenda Sana, usinikatie tamaa” aliniambia hivyo nikawa tayari
nimemuelewa na wakati huo Gerald alikua tayari kaajiriwa. Na hakua Dar
Tena, Bali alikua mbeya.
“ Gery kwa Sasa acha kwanza nilee
mtoto wangu” nilimwambia mapema na
maongezi mengine machache yalifata ghafla mama akaingia ndani kwa nguvu baada kusikia maongezi yamekua marefu.
“ We kijana , hebu muache mtoto wa watu ale, mwenzio Ni mzazi huyu, hujui uchungu ulivyo na hutawahi kuujua”
alimwambia kwa sauti Gerald akacheka tu na kunikatia simu bila kuaga.
Nilitabasamu na kukabidhiwa bakuli la supu ya nyama ya ng’ombe nitumie.
Ndani Yake kulikua na ndizi Kama nne hivi. Mama mkwe alimchukus Gift na kumbeba, hakika alikua na furaha isiyokwisha kila alipomtazama.
Baada ya kula sana hatimae nilifaa
kupumzika, wakati huo mama mkwe
aliongea na mama yangu. Niliwasikia
wakipeana pongezi kana kwamba walikua
wakifahamiana. Nikakausha hata hivyo
nitaongea nae nikiwa sawa, Nina mengi ya kumuelezea nafaa kumuomba
msamaha pia. Nilimkosea Sana mama yangu.
Majira ya usiku alikuja Dr kuniangalia
akatoa maagizo kadhaa kwa mama Kisha
akaondoka zake. Mama alisogea kwangu na kunikazania Nile kwanza. Yaani
nilikua nakula huku nimesimamiwa na kuambiwa nimalize kila kitu, wakati huo
tumbo limefungwa kwa kukazwa nikiwa
sielewi. Ilibidi usiku huo niulize.
“ Mama Sasa kwa Nini unahimiza nile
wakati tumbo langu umelifunga, huoni
Kama naumizwa na chakula?”
Nilimwambia.
.” Hakuna kitu Kama hicho, huwezi
kuumia. Ikitokea nikafungua tumbo
lako, utahutaji kupakia kila kitu na
hautajihisi kushiba kabisaa, maana kwa
Sasa tumbo lako lipo wazi, yaani lipo
wazi kwa ukubwa zaidi, Ila kwa
kulifunga inasaidia kuzuia kutamani kila
kitu. Na nafasi zilizoachwa wazi
kujivuta zenyewe taratibu. “
“ Aahh! Sikua najua, kwa hiyo nisipolifunga baadae ntakua na tumbo
kubwa Sana”
“ Kama turbo, ahahaha!” Mama mkwe
wangu alikua na vituko. Hatimae nililala
baada ya kukandwa Maji ya Moto na mtoto kunyonya. Mwenzenu sikua
najiweza kwenye kulala. Kwanza nilikua
mlalafi, nalala vibaya nisipokua Makini
mtoto nilikua namuwekea miguu.
Afadhari mama mkwe alikua makini, hata mtoto alipolia usiku sikuweza
kumsikia eti niamke kumnyonyesha.
Hiyo kazi aliifanya mama mkwe kwa
ugumu Sana.
“
Amina amka mtoto analia unafaa
kumnyonyesha” yalikua majira ya saa
kumi alafu naamshwa kumnyonyesha
mtoto, nilijitahidi kuvuta chuchu
nimuwekee mdomoni Ila mwisho wa siku
usingizi ukawa na nguvu zaidi yangu,, wee mama mkwe aliniacha nilale akaja
akasaidia kukamua maziwa na kumsaidia
mtoto kunyonya, la sivyo kangekoma hako ka Gift.
Sehemu ya 35
Hatimae kesho Yake tulipewa ruhusa ya
kuondoka kurejea nyumbani. Baba mkwe
alinifata na gari Yake pamoja na maua ya zawadi akinipongeza kwa safari
ndefu ya kupata mtoto. Tena binti
alimpokea akimsemea maneno mazuri eti
mke wake. Kisha akampiga maombi hapo.
Daah! Gift alikuja na baraka tele.
Gerson alinikaribisha kwenye gari huku
akiwa kanishushia mwamvuli jamani
nilikua kama malkia anaependelewa
mwenzenu.
“ Kipenzi usihofu, wewe kwa Sasa Ni
Mrs Gerald Tantalila mkwe pekee wa
familia hii, Tena shukuru Sana mungu
Gerald kwa Sasa ameajiriwa tayari,
hapa Ni sisi tu kujiandaa na ndoa yenu”
nilitumbua macho hivi nilifaa kuolewa
hivi karibuni? Hapana hapana haikua
sawa? Kuzaa sio kuolewa? Sitaki
kumtumia binti yangu Kama kibali Cha
kupata ndoa? Nililaani hayo maamuzi ya watu wengine kabisa.
“ Mbona Kama hujafurahishwa na maneno yangu, samahani Kama nimeenda mbali” Cynthia alijishtukia.
“ Hapana wifi hujakosea, lakini nahitaji muda kuwazia Hilo” nilimpa tabasamu
hafifu akaelewa maana yangu, hata
hivyo wao walikua wakubwa kwangu japo
nimewahi kuzaa kabla Yao. Hata Zena
alinielewa ki ukweli walionekana
kuvunjika moyo kwa mawazo yangu.
“ Ki ufupi natamani Sana uwe mkwe
wangu, sitaki kijana wangu aruke ruke
na wanawake wengine wakati tayari
nimeshaonja utamu wa kua na wewe
Kama mkwe na mjukuu umeniletea,
naomba usiikwepe hii nafasi” mama
mkwe aliniambia nikapiga kimya.
Hatimae tuliwasili nyumbani nikaanza
kuhudumiwa Kama mzazi Sasa. Nilikua
natumikia kifungo changu Cha uzazi kwa
uangalizi wa Hali ya juu’, Kwa kua sikua
najiweza kumwangalia mtoto ilimlazimu
mama mkwe ahamie chumbani kwangu,
usiku kucha angetutunza Mimi pamoja na mtoto haswaa. Siku zilisogea
hatimae mwezi mmoja hukupatikana.
Mwezi wa pili nilianza kuzoea pia na
mwili wangu ukaanza kurejea katika
Hali Yake ya kawaida nikawa mzuri
zaidi ya mwanzo, hiyo ilitokana na
sababu ya kua chini ya uangalizi mzuri
kupindukia. Ki ufupi nilitunzwa vyema
Sana. Mama yangu alikuja kunitembelea
pale kwa machungu Sana akiniomba samahani.
“ Hapana mama, Mimi ndo wa kuomba
samahani kwako mpaka kufa kwangu
nilikuvunja moyo mama yangu”
nilimwambia.
“ Hapana mwanangu nilifeli pakubwa
Sana Kama mzazi, kwa Nini nilikufukuza
nilishindwa kutumia akili na kujiuliza
iwapo Mimi ningefukuzwa nyumbani ningeishije?”
“ Mamaaa.. mzazi hakosei, hakika
nilifanya makosa kwa kufata kiburi
changu, siku hiyo sikufaa kuondoka
nyumbani nilifaa kuelewa ya kwamba
hasira za mzazi huwa hazidumu”
“ Ni kweli binti yangu, jioni ya siku hiyo
nilienda kwa mama shera kukuulizia
akaniambia haupo, nilichanganyikiwa
kwani nilihisi labda umechukua maamuzi ya kwenda kujiua. Nikampigia Froza na kumuelezea wewe ni mjamzito angalau
akutafute popote muongee akasema
atakutafuta. Ila mwishowe kumbe hukupatikana hata kwake”
Niilikumbuka vyema hiyo siku kwani
dada aliongea mbele yangu nikiwa
namsikia. Hakika ilikua siku ambayo
dunia ilikua kichwani kwangu.
“ Mama tufanye yamepita, bahati nzuri
mwanaume alienipa ujauzito alikuwepo
kwa ajiri yangu, alikua msitari wa
kwanza kunisaidia we usijari binti yako nipo salama. “
“ Amina wangu, hongera Sana, kwanza unayo bahati huko mwenzako Eliza
kakataliwa kabisa”
“ Mama usiongee habari zao, hata hivyo, unakumbuka kabisa
wanavyotuchukulia hao watu” sikutaka
mama yangu ajari kuhusu watu
wasiotujali.
“ Usijari binti yangu, hata hivyo kwa
Sasa Ni muda wa kulea wajukuu”
alimbeba Gift na kumchezesha. Siku
hiyo tulishinda pamoja na mama yangu
mpaka jioni, nilitamani alale hata hivyo
Ila alikataa akasema sio sheria kwa
yeye kulala ukweni kwao na binti Yake.
Usiku wa siku hiyo Gery alinipigia simu
na kuniambia yupo mbioni kuja, sijui Ni
vipi lakini nilihisi Kama moyo wangu
ulipata ahueni, kweli alikua akija?
Maana tayari nilikata tamaa kumuona.
Kesho Yake asubuhi mama mkwe aliingia
chumbani kwangu kuchukua nguo za Gift
nilizombadili usiku pamoja na nguo zangu
chafu akafue. Aliniangalia baada ya
kusalimiana namna nilikua na furaha
akaanza kuniambia.
“ Nakuona ulivyo na furaha Mrs Gerald , Sasa wewe neng’eneka hapo umrudishe nyuma mtoto wako asikue kwa afya!”
Mmhh! Nilishtuka kwanza. Alikua na maana gani? “ Mama sijakuelewa kabisa, kwani Kuna kitu kibaya?”
Nilipata wasiwasi kidogo.
“ Hapana maana yangu Ni kwamba, huwajui vizuri wanaume, acha Sasa
nikwambie Gerald anakuja.. Gerald anafanya Nini?” Aliniangalia “Anakuja”
nilimjibu nikimwangalia.
“ Eeh! Unajua kumbe, Sasa Basi, sahau kuhusu huyo Gerald kitu muhimu
Ni kwamba unafaa kua Makini na binti
yako, amini usiamini wanaume
wanapenda Sana kufanya tendo la ndoa, Sasa wewe jichanganye umpe kila siku
we bado Ni mzazi na haujawa salama ki
afya, na kuhusu Gift bado anahitaji
hewa Safi, we unajuaje huko aliko kua
Gerald hakua na michepuko? Kua Makini na binti yako, nakuonya”
Aii! Nilipata aibu mama mkwe aliamua
kutomuamini kabisa Gerald, hata hivyo
alikua sahihi Gerald sio wa kuaminika
Kuna siku nilimpigia simu akapokea
mwanamke alafu yeye akiwa bafuni,
hiyo Ni ishara tosha anao wanawake wengine. nilipata wivu tayari na kutamani kulia.
Unahisi nini kitafuata hapo?
Tukutane sehemu ya 36