waandishi ebook 1688283182.2797718

Page 1

supu ya mawe!

supu ya mawe!

kikosi cha waandazi:

mtunzi na mchoraji wa mkasa huu

shauri kati

mchoraji wa jalada marco tibasima

mchapaji wa maandishi grace majo

usanifu wa kurasa

simon marco

mchana huu unawakuta bandibu na nyang’au wakiwa kijiweni. mwanangu, kuna mali iko nje nje mitaa flani hapo kati, halafu siye tunalia ukenenge kizembe zembe tu hapa!

mali gani hiyo mwanangu, na iko pande zipi watu tuingie msambweni sasa hivi?

mitaa ya kati hapo keinyama kuna fremu inapangishwa, halafu fremu zinazofuata zina mazagazaga kama yote, mijismati-foni macho matatu ya kumwaga, maduka mengine suti za kishua kibwena, hiyo mikwaju ya kidon ndiyo usiongee, duka jingine wanauza vipodozi, yaani full unyunyu askari wangu!

acha bwana!

1

mzee nikajiongeza

kimuvi muvi… yaani pale tunaichukua ile fremu halafu

tunaweka ofisi ya kukata bima!

ofisi yenyewe haitafunguliwa hata wiki, maana ndani ya siku tatu tu itakuwa imefungwa, shughuli imeisha!

kivipi?

tukishafungua ofisi siku ya kwanza, siku ya pili usiku mimi wakati nafunga ofisi, nakufungia wewe ofisini! enhe!

halafu mimi na wewe tunakuwa tunawasiliana kwa sms, maduka mengine yakishafungwa nakutonya ili uanze kutoboa ukuta kwa ukuta, fremu kwa fremu, hata nisipokutonya ikifika mishale ya saa saba we unaanza kutindua! duh!

kila fremu unayoingia unahakikisha unakomba kila kitu, simu, viatu, nguo, vipodozi, vyote unatia ndani ya mifuko yetu ile ya kazi, halafu unavipaki kwenye fremu yetu, unanicheki hewani, natimba na gari, tunakomba mzigo, tunapotelea kusikojulikana! kwani sehemu yenyewe hakuna mlinzi?

2

duh! we noma mwanangu, mchoro si wa kitoto huo!

yupo, ila kachoka choka kama anaenda kufa! na mchongo ulivyo sasa…nisikilize kwa makini. kabla haujaanza kutindua kule ndani…

sema nini bandidu…

nambie mwanangu!

hapo lazima tuwe na mpunga wa kuweka mambo flani sawa kwa jinsi mchoro

ulivyo, kama kulipia hiyo kodi ya fremu na mengine... itakuwaje?

usiwaze mwanangu, yuko

mama la mama mmoja

nammudu, atasimamia

shoo!

3

bandidu na nyang’au hawakulaza damu. fasta wakaelekea ofisini kwa madam brenda.

mama la mama, madam brenda mwenyewe!

nambie bandidu, naona leo umeniletea mgeni!

huyu anaitwa nyang’au, a.k.a mwalimu wa zamu, mtu mbaya! ukiniona naye huyu ujue tuna jambo letu, kuna mchongo mnene!

haya niambie mmekuja na mchongo gani leo?

kwanza awali ya yote… hongereni sana wamama! maana mnaongelea kileleni sasa hivi! mko juu kama mvinje!

umeona eeh! sasa weka mpango ubaoni!

4

ok, mchongo wenyewe ni kuwa… kuna mali iko sehemu ila inahitaji mkwanja tu wa kupush ili kuifikia, akili tayari imeishatumika madam!

wakampa

mpango mzima ulivyo…

shusha data!

plani iko vizuri, pesa nitawapa, ila hakikisheni inarudi mara mbili yake ndani ya mwezi! na mnajua vizuri kuwa sifanyagi kazi ya hasara!

imepita hiyo madam!

baada ya kupewa kitita na madam brenda…

haina mbambamba!

hapa cha kwanza kabisa ni kwenda kutupia kiofisi halafu tukalipie ile fremu kabla hajailipia mtu mwingine!

5
sure
mwanangu!

wakaonana na mwenye fremu…

mnataka kuweka biashara gani?

wakala wa bima! tunashughulika na ukataji bima, hasa za vyombo vya moto!

hiyo sawa, nilidhani grosare au biashara zingine za kijinga-jinga!

baada ya kulipa na kusaini mkataba wa pango…

funguo zenu hizi hapa, muwe huru, mnaweza kuendelea na mambo mengine sasa!

sawa mkuu, tunashukuru kwa ushirikiano wako!

walipoachana na mwenye fremu…

sasa mwanangu hapa mwake! kinachofuata pale ni kuweka mazingira fresh watu tufanye yetu!

sana tu, kazi iendelee!

6

siku ya tatu ofisi ilikuwa imekamilika ‘kimagumashi’.

sasa mwanangu leo tumefungua hapa, lakini kesho hatupo hapa, kazi inapigwa leo leo usiku!

tutakula kwa urefu wa kamba zetu, haina kuremba!

poa, ngoja mimi niingie kariakoo nikachukue vitendea kazi, nipite nikampange dereva wa kirikuu pamoja na zabibu!

punde si punde bandidu alipanda daladala kuelekea kariakoo.

poa, mi navimba hapa hapa, utanikuta askari wako!

kesho wamiliki wa zile fremu lazima waamkie icu, presha pomoni!

7

baada ya daladala kukatiza mitaa kadhaa, hatimae bandidu akafika kariakoo...

duh! kila siku kariakoo kumejaa watu hata pa kukanyaga ishu! mwanangu chanx aliwahi kusema unaweza kudhania wote ni watu kumbe vingine vijini, ukitaka kuamini tembea unaangalia chini, wengine wana kwato!

weee mama mwenye mtoto mgongoni, weee dada mwenye mimba, weee shangazi lake uliyevaa dera, kamata dera mali mpya, dera la 5g, lina ‘blututh’, dera limeunganishwa na gb3 mwezi mzima kwa bei ya supu na chapati!

oyaaa za leoleo!

za leoleo! jerojero tu unasusiwaa!

8

ya bonyokwa, china au ya uturuki?

akaingia duka la vifaa vya ujenzi…

tunaingiza nyimbo kwenye simu, flash, cd na kaseti, pia mikoani tunatumaa!

nigee madera kumi fasta!

yoyote, mradi yasiwe modo tu!

nipatie nyundo mbili, tindo mbili na kudu mbili!

shopping ikaendelea…

pimamaji hauchukui?

ninayo!

nigee barakoa mbili!

za rangi gani?

ya kinyonga!

9

mh! rangi ya kinyonga!! hizo sina!

lete barakoa wewe, acha kumbwela!

baada ya shopping pale kariakoo kukamilika, bandidu akaenda mchikichini kwenye pub ya anti moza ili kuyajenga na zabibu, mkwanja upo zabibu! kamata chako hiki, ila ujue ukizingua nakuzingua!

yaani kazi yako siyo kubwa wala nini, ni kupiga kelele za kuomba msaada kuwa unakabwa, mlinzi akijipendekeza kuja kukusaidia… nikikuachia unatakiwa upotee mazima, na ‘sini’ yako inakuwa imeishia hapo!

kazi ubwabwa kabisa hiyo, naifanya fasta tu! ila nipe changu kabisa tusije kuzinguana baadae!

baridda!

10
imeisha hiyo!

kisha akaenda kuonana na dereva wa usafiri

kwa hiyo wewe kaa ‘stendi bai’, nikikupigia ulete chombo, usiuweke usiku mwanangu, amsha fasta!

ghafla…

mama weeeghhh… jamani

mwiziiighhh…

naomba

msaadaaaghhh… msaadaaghhh…

hebu tulia wewe!

uskonde bandidu, kiswaswadu changu kiko full chaji kusubiri mwongozo wako spika!

huko,

11
saa saba usiku maduka yote yalikuwa yamefungwa na mtaa ulikuwa umetulia, mlinzi akiwa amebana kwenye chimbo lake kama ilivyo kawaida yake.
he!
ngoja nikatoe msaada mtu asije kufia kwenye lindo langu ikawa tabu!

alipotokeza tu akakutana na nondo, akaiona!

he! jama! vuuuuuu! ha! nimemkosa!

kwetu waungwana salamu ni lazima, hebu

salamu kwanza hiyo!

kazi yangu

imeishia hapo, watajuana wenyewe huko!

mama yooooh!! amenipiga na radi!!

duh! yule siyo mtu aisee, kwanza sijui nimemkosaje ile nondo! halafu badala ya kupiga ngumi ye anapiga radi! kanipiga radi mbili za uso!!

waaape salaaam!!! mimi ndiye naitwa mikono ya radi, mzee wa kugawa supu ya mawe! tumbaf!

12
pokea zabibu alipopata upenyo akachomoka. ama baada ya salamu, kiroho safi huwa tunakunywa supu ya mawe, ipokee ukagawane na ukoo wako!

kan’tia sumbwi za maana! kule sirudi tena aisee!

ngoja nimpigie nyang’au nimwambie asitishe zoezi kwanza!

muda huo huo...

hamadi! cha kuokota si cha kuiba...

he! simu iko wapi tena, mbona siioni?

jamaa lina roho mbaya sana hata yule putin mi’naona wanamsingizia tu... ngumi gani zile?

aiya weee… nimepoteza kiswaswadu changu! sasa askari wangu nyang’au mule ndani itakuwaje?

13

si ataona nimemtoa kafara!? itabidi nifanye jambo.

muda huo...

hili joto litaniua humu ndani, ngoja nimtumie meseji bandidu kuwa mi naanza kutindua ukuta, maana mida yenyewe ndiyo hii!

mh!

oya! mi nalianzisha singeli huku ndani, mida ndiyo hii!

mh! ukuta wenyewe mgumu utasema umejengwa na wana wa izraeli!

kwa medani za kiintelijensia, hii meseji inaashiria kuna tukio la kihalifu linaenda kufanyika mahali fulani!!

14
meseji ikaingia kwenye simu ya bandidu..

oya ras uchebe, fungua mlango mwanangu!

nani?

he! huo uso vepe, kuna usalama kweli?

bandidu!

usalama gani? wa taifa!? au wa raia na mali zake!? hebu acha umbeya mtoto wa kiume wewe! amsha chombo tukafanye uokozi...

kuna askari wa miguu amenasa kwenye mtego huko! rasta gani unakuwa mmbeya!!

muda huo nyang’au kule ndani…

nyang’au!

nani kanasa?

yes! kihunzi cha kwanza tayari, ngoja nichome ndani!

15

akaibukia duka la simu, akawasha taa.

mwemwereee!!! zigo kama lote! ngoja niupakie kabisa mzigo halafu nianze kutindua, nizame duka linalofuata kiulainii kama kutafuna biskuti!

kwa spidi ya hamorapa nyang’au akaanza kuzipakia simu ndani ya dera!

waswahili walivyo washamba sasa, wanajua madera ni kwa ajili ya kuvaa tu, kumbe yana kazi nyingine kibao, ubunifu wako tu!

duka la kwanza tayari, hapa wana wakija ni kupakia garini na kusepetuka! ngoja niendelee na ukuta mwingine... yaani ni kamserereko tu!

16

mh! halafu muda mrefu nasikia sauti kama kitu kinagonga gonga mahali halafu kinatulia!

mh! mbona hizo sauti za kugonga gonga zinatokea humu ndani!? ngoja!

pole kwa kukatisha usingizi wako boss!

fanya uje sasa hivi, maana kuna kitu sikielewi kinaendelea ndani ya hizi fremu!

kuna tatizo gani?

kuna mtu anagonga gonga kwenye maduka humo ndani, wapigie wenye maduka waje wafungue tuone kuna nini kinaendelea humo!

aisee, fanya fasta uje mara moja

hapa kwenye duka lako, uje na ufunguo!

he! ha!

17
akampigia mwenye fremu... muda si mrefu mwenye fremu akafika. mwenye fremu akawapigia wenye yale maduka. lakini alipompigia bandidu…

he! vipi mlinzi? mbona sielewi? inakuwaje simu ya mwenye fremu ya wakala wa bima unayo wewe?

aisee… kuuumbe!!!

nahisi kuna mchezo mchafu.

vipi? kuna nini kinaendelea hapa mkono wa radi?

ngoja wenye haya maduka waje wafungue, utanielewa boss!

muda si mrefu... vipi mkuu, kuna tatizo gani?

aisee… na huyu mwenzetu wakala wa bima mbona hajafika? umempigia?

fungueni maduka yenu, kuna mtu anagonga gonga huko ndani!

huko ndani…

kuhusu huyo tutajua muda si mrefu!

mh! machale katikati ya jicho la kushoto yananicheza.... nasikia zogo huko nje? ngoja!

kitendo bila kuchelewa...

mbwa kala mbwa!

18

haa! kazima taa! fungueni haraka tum’sandwichi’ humo humo ndani!

jama, wengine wazunguke nyuma ya fremu asije akafumua ukuta huko akatuacha!!

huko niachieni mimi!

walifungua fremu

leo nd’o atajua hajui!

mama weeh!! nimeibiwa!!

huyu atakuwa na phd ya uhalifu!

walipoibukia ndani ya flemu ya ‘wazee wa bima’… he! na haya madela vipi tena?

atakuwa ni komando kipensi huyu!

itakuwa ndiyo wamepakia mali zetu humo!

duh! hawa jamaa mikosi! walikuwa wamevaa smati walipokuja kulipia fremu, lakini nilikuwa na mashaka na kile kiremba kichwani na kibalaghashia kilivyovaliwa! halafu wanajifanya mawakala wa bima, bima yenyewe ndiyo hii!!?

19
moja na kuingia ndani…

nyang’au akaibukia juu ya bati.

acha wapige stori na madera huko ndani, mi nasanzuka juu kwa juu!

wakitoka humo ndani wakatafute maana ya nyang’au!

yaani ghafla tu!

mamaaa weee! nimepigwa na shoti ya umemeee!

karibu supu ya mawe ewe mzee wa bima!

mara bandidu na ras uchebe wanawasili...

nyang’au tuondoke! atakuua huyo! ana radi mikononi!!

kweli aisee, huyu siyo mtu mwema, ataniua huyu jamaa!

he! we bima, rudi hapa!

hizo radi zako nenda kapige mawe huko malampaka, hapa hupati kitu! KWAHERi!

20 mwisho

Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.