waandishi ebook 1688377772.3657446

Page 1

#030 Jumatatu Jumatano ijumaa

Kikamerachetu...

1

ya mtunzi: ally mbetu mchoraji: aloys mabina

2 39 sehemu

Salma anashtuka usingizi na kutulia akiwaza huku mume wake akizuga kama amelala..

He! Kumbe kumekucha!

Simshtui kama nimesikia, lazima nifanye upelelezi ili nijue huyo Mti Mkavu ni nani.

Japo penzi la ndotoni lakini lilikuwa tamu ambalo toka nivunje ungo sijakutana na mwanaume shababi kama

Mti Mkavu. ingekuwa kweli mbona ningefaidi! ni huu ugwadu mmh!.

Hii ndoto ina maana gani mbona inafanana na ile niliyoiota siku nilipolala kwa Mti Mkavu. Halafu chini pamevurugika kama kumetumika.

Japo ni ndoto lakini nimechoka sana isingekuwa leo siku ya peresheni ya kwenda kwa mwana haramu Mti Mkavu ningeomba Sick sheet ya ugonjwa ili nilale siku nzima.

3

Yaani na huu ugwadu kutokana na jogoo wa mume wangu kupinda mdomo ingekuwa ndiyo mume wangu angenishika vile ningeinjoi mtoto wa kike.

Mmmwaaa, nakupenda sana mume wangu.

Siamini! yaani kutompa haki yake ya msingi kwa siku chache tu mke wangu amekosa uvumilivu mpaka kunisaliti na huyo sijui nani Mti nini, loh, wanawake!

Asante, kazi njema.

4

itakuwaje?

Siamini kama mke wangu amenisaliti, nilikuwa namuamini sana.

Hivi hizi ndoto za kufanana zinatokana na nini, kwa utamu wa penzi la ndotoni nilitamani kila siku zijirudie mpaka tatizo la mume wangu liishe.

naona kikosi kiko vizuri, leo atajuta yule kizee!

5
endelea kufuatilia mkasa huu kwenye jarida hili la alkasus kila siku za jumatatu, jumatano na ijumaa. Salma akikagua na kikosi maalumu kabla ya kuvamia kwa Mti Mkavu.
6 sehemu ya 13 mtunzi/ mchoraji

walipofika wakakuta mwili wa mwanamke ukiwa umetapakaa damu na kuliwa sehemu kubwa ya mguu wa kushoto na mkono wa kulia ukiwa umenyofolewa na yule mbwa koko kisha akakimbia nao ..maskini alikuwa ni dorice!

mungu wangu, yuko hai kweli huyu!!?

sidhani aiseee !!

aisee !!

wakampakia ndani ya gari waliyokuwa wanaitumia kwa kufanyia doria na kuondoka naye kuelekea muhimbili hospitali.

itakuwa kabakwa na beach boys mpaka kufa kisha wakaja kuutelekeza mwili hapo!!

yaah maana anaonekana ana damu mapajani …. au ametoa mimba nini..!!?

yote yanawezekana maana siku hizi dunia iko kwenye maonyesho !!

7
mh!!

huku nako…. mona baada ya kutoka polisi akaenda muhimbili hospitali. dada naomba nikamuone daktari wa watoto huyu mtoto kazaliwa njiani na hajapata huduma mpaka sasa!

aisee! nenda dada yangu muwahishe! ok !!

mara…

we mona, dorice yuko wapi?

nani tena huyo !!?

8

alikuwa yule mama mwenye nyumba! ah! kumbe wewe! unamuulizia kama nani? anakuhusu nini?

kama mwenye nyumba wake na ndiye niliyetoka naye nyumbani !! yuko wapi?

inahusu !!? anajua mwenyewe alipo !!

inahusu ndiyo !!

anajua mwenyewe alipo kivipi wakati wewe ndiyo umeondoka naye tabata pamoja na mtoto??

utasema tu leo!!

9 itaendelea toleo lijalo...

Binti wa RAIS - 30

mchoraji

10
mtunzi - fortunatus ndilla - aloyce jacob

enhe… kwa hiyo nini mpango wa serikali?

sikia, anytime from tomorrow, interpol, sijui fbi, cia wataingia nchini kwa ajili ya kumchukua nyeke under escort hadi katika mahakama zao za umoja wa mataifa.

baada ya taratibu zote kukamilika, rais atatia saini na kuwakabidhi mtuhumiwa wao, kama sheria za umoja wa mataifa zinavyosema.

11

kwa hiyo unataka kuniambiaje, nijiandae kupambana na fbi na cia kumuokoa nyeke? come on kisoka, you must be joking!

hapana zombi, simaanishi mkapambane na fbi, kwani itakuwa ni sawa na kukimbiza ndege kwa baiskeli. namaanisha cheza na chief!

chief? yes…. chief, yaani rais. yeye ndiye mwenye maamuzi ya mwisho kumkabidhi mtuhumiwa au kumwachia.

12

kisoka sasa umenichoka, yaani nimfuate rais nimwambie…... aaa si nitakuwa mwendawazimu!?

sikia zombi, simaanishi umfuate rais umhonge au umbembeleze amwachie nyeke, ila namaanisha ukiwa unamshikilia mateka binti yake pekee na kipenzi, iwe isiwe atamwacha tu!

yeah, kisoka kweli we ni jiniasi. sasa hebu niambie, tutampataje huyo binti wa rais?

aaah... sasa usiwe na papara, binti mwenyewe hayupo nchini kwa sasa. yupo chuo huko washington marekani, lakini sasa wamefunga chuo na ijumaa usiku ataingia na swiss air. hapo ndo pakuchangamka!

13 itaendelea
toleo lijalo...

Kifungashio...

ADELA alijiliza utadhani kweli kaguswa kwenyewe, Mzee Kuyu kama kawaida alijua binti huyu anajaribu kumuuzia mbuzi kwenye gunia lakini alijua muda si mrefu atalia kilio cha kweli. Binti hakujua mzee aliyekutana naye ni mtoto wa mjini unayekula fedha yake kihalali.

Adela binti mdogo lakini kahaba mzoefu aliyekuwa na mbinu za kuwaibia wanaume kwa ujanja wa kujiliza kama kagusika kumbe uongo hajaguswa, kelele tu.

Aliamini kwa umri na umbile lile la Mzee Kuyu na umri wake

14
1

lazima mtu mzima angechemsha katikati ya safari. Adela

aliendelea kutatalika kama chumvi ya mawe kwenye moto huku

akimwaga sifa za uongo kwa Mzee Kuyu ambaye hakuonyesha papara kwa kutwanga taratibu bila wasi, akiamini mchicha haujakolea nazi.

“Babuuu hakuna kama wewe, jamani babu ulikuwa wapi mzee wewe, unajua kumpa raha mjukuu wako kamua babuuu.”

Pamoja na sifa zote Mzee Kuyu au kama vijana wapendavyo kumwita Mkali Kuyu, hakujibu chochote zaidi ya kutandaza soka safi kama kijana aliyebalehe juzi kwa nguvu na uwezo aliokuwa nao.

Muda wote alijua binti anampa penzi ‘kanyaboya’, kwa umri wake binti yule alikuwa sawa na mjukuu wake. Lakini kama ujuavyo mambo ya utandawazi kiatu kikikutosha usiulize watakucheka, wee vaa tu.

Pia alizingatia nidhamu ya chakula, kutafuna karanga huku anapiga mruzi ni kitu kisichowezekana. Siku zote ukitaka kufaidi karanga usipige mruzi na ukitaka kumfaidi mwizi wako asipigwe na watu wengi, mkimbize kimya kimya.

Sifa zote za uongo alizopewa na Adela alijua bado binti hajaguswa ikulu akiguswa angesema mwenyewe. Kila muda ulivyozidi kwenda ndivyo mtoto wa kike alipogundua mti aliokuwa akichimba ni mti mkavu usiochimbwa dawa.

Alijikuta akilia kilio cha kweli kweli aliguswa akagusika baada ya kwenda marikiti zaidi ya mara nne.

“Jamani babu bado tu?”

“Kwani vipi?”

“Maliza babu au umeninywea pombe kali ili unikomoe.”

“Binti niombe radhi, toka nizaliwe sijui kitu pombe.”

“Kama si pombe kali ni nini? Mwenzio nina nne wewe hata moja bado.”

15

“Tatizo nini?”

“Nimechoka.”

Baada ya Adela kujisalimisha polisi, mkali Kuyu aliamini fedha alizompa binti huyo zimekwenda kihalali. Alishusha mzigo na kumfanya binti aheme kama kamaliza mbio ndefu.

“Vipi?” Mzee Kuyu alimuuliza huku akitabasamu.

“Babu lazima utakuwa umekula dawa.”

“Kwa nini?”

“Kwa umri kama wako huwezi kwenda mwendo mrefu kama huu bila kuchoka na ‘netiweki’ bado inasoma.”

“Ni mtazamo tu binti, nani alikuambia panga la zamani halikati?”

“Babu kama hutumii vumbi la kongo basi unatumia viagra au Supershaft.”

“Binti mbona maneno mengi kama umepoteza nauli? Ulifikiri hapa kuna fedha za bure! Hapa ni Kisemvule hakuna kitu cha bure, lazima uneng’emule ndiyo ule.”

“Pamoja na shughuli niliyopata lakini leo nimeinjoi japo umenichosha.”

“Sasa mbona unalalamika?”

“Mmh! Uliniganda kama ruba, pia sikutarajia muziki mnene, nilijua ngoma ya kitoto.”

“Basi binti leo umekula kihalali.”

“Wacha nikaoge niondoke.”

“Hakuna tatizo, nikikuhitaji nitakutafuta mambo unayaweza.”

“Hakuna tatizo babu basi niongeze hata fedha ya nauli nichukue bajaji.”

“Nitakuongezea usiwe na wasi.”

16

Adela baada ya kuoga aliagana na Mzee Kuyu kisha aliingia mtaani akiwa amechoka na kuamua siku ile kwenda kulala baada ya mzee huyo kumharibia siku yake kutokana na mbinu zake za kujiliza kwa wanaume ambao siku zote walionekana watu wazima walikuwa kama madume ya bata, safari moja walikuwa wapo hoi.

Kwa mtindo ule, kila siku alikuwa akikutana na wanaume zaidi ya watatu na kutengeneza fedha ya maana. Hata shoga yake, Mariam ambaye anamfupisha kwa kumuita Mamu alipompitia jioni alimweleza hawezi kutoka.

“Vipi shoga leo mbona upo kitandani hutoki?”

“Babu wee leo mbona nimepatikana.”

“Kivipi?”

“Nilipata tenda ya asubuhi asubuhi nikajua biashara imeanza mapema.”

“Ehe, tenda gani tena hiyo shoga?”

“ Kuna mtu wangu mpambe wa pedejee mmoja alinipigia simu kuwa jamaa yao huwatumia watoto wazuri kuburudika nao. Ili kukupa dili lazima mnapatana cha juu chake.”

“Ehe! Lete utamu?”

“Basi J4 kwa muonekano wangu aliona akimwambia bosi wake natokea Mlimani (chuo kikuu) atakubali, basi mtoto nikajiandaa tofauti na mitoko yetu ya usiku nikaenda kisomi kweli. Si unajua mtoto navunja mayai kama sina akili nzuri. J4 alinieleza babu dau lake kuanzia laki.”

“Wacha!” Mamu alishtuka.

“Sikiliza, mbona haraka hebu tulia nikupashe.”

“Haya mwari nipashe nipashike, nakuona umechoka kama umevuta mambo yetu.”

17 ****

“Kama nilivyokueleza J4, alivyonieleza dau la chini la yule mzee ni laki, alinieleza ni mimi kujua kuzungumza vizuri dau linaweza kupanda. Ila chake cha juu alitaka elfu 30.”

“He! Mbona nyingi kazi ufanye wewe umpe kiasi chote hicho?”

“Dada hata hizo sabini kama angetaka kumpa mwingine si ningekosa.”

“Haya, ikawaje?”

“Basi nikaenda kuonana na mzee mmoja wa haja mwenye fedha zake, pedejee wa ukweli.”

“Usiniambie!”

“Katika makubaliano nilimzuga mimi ni mtoto wa mbunge, nilimtaja mbunge jina lake lililokuja mdomoni, nipo Mlimani mwaka wa tatu nasomea sheria.”

“Wacha weee kama nakuona!”

“Basi katika makubaliano nilianza laki tano.”

“Mtumeee! Mbona nyingi sana?”

“Kumbe mzee mwenyewe wa mjini, alisema zaidi ya laki niondoke.”

“Mmh! Makubwa, ikawaje?”

“Nami nikamwambia mwisho laki mbili kama akishindwa naondoka.”

“Patamu hapo, ikawaje?”

“Mzee akafika laki na nusu.”

“Yaani kama nawaona, nipe raha, ukamjibu nini?”

“Nikaona si pabaya kwani huwa tunaliwa na mbu kama siku hali siyo nzuri na kuambulia elfu tano tu za chap chap.”

“Kwa hiyo ukakubali?”

18

“Nisikubali? Nani apige teke fuko la fedha.”

“Baada ya hapo?”

“Mwari si tukaenda kwenye hoteli ya nguvu ndani ya usafiri wa heshima ‘full’ kiyoyozi. Nilipomwangalia mwili mkubwa mtu wa makamo nikajua maji ya kisigino.”

“Ehe!”

“Mwana temea chini, hebu subiri kwanza,naona J4 anapiga.”

Adela alisitisha mazungumzo baada ya simu yake kuita na kuona jina la J4.

“Haloo J4, lete stori mtu wangu.”

“Upo wapi?”

“Home.”

“Vipi mmemalizana?”

“Tayari.”

“Hukuniangusha?”

“Mmh! Sikukuangusha, lakini pamechimbika.”

“Vipi alitaka kukataa kukulipa?”

“Walaa.”

“Sasa pamechimbika vipi?”

“Mmh! Babu mzima.”

“Kivipi?”

“Aah, J4 kwani we mtoto? Ulinipeleka nikaimbe taarabu?”

“Ooh, nimekuelewa kweli yule anajiita babu wa Kisemvule.”

“Na kweli nimeneng’emuka ndipo nilipokula.”

19

“Wachaaa! Kwa hiyo?”

“Njoo uchukue chako.”

“Ok, nakuja.”

Baada ya kukata simu, alimgeukia shoga yake aliyekuwa na shauku ya kujua kilichoendelea.”

“Unaniambia nitemee chini kulikoni?”

“Wee acha, yule babu si bure lazima anatumia dawa za kuongeza nguvu.”

“Kwa nini?”

“Yaani, mzee alipopanda juu nilijua atachemsha, mwari nimechemsha mimi, Mwenzake nimelia mara nne yeye hata mara moja.”

“Wacha!”

“Nakwambia bila kuomba msaada mbona pangewaka moto.”

“Au alikunywea pombe kali?”

“Walaa, hatumii kinywaji kikali chochote.”

“Basi atakuwa anatumia dawa za kuongeza nguvu.”

“Hata hilo alilikataa amesema dawa yake ni kula vizuri na mazoezi.”

“Ikawaje?”

“Mpaka ananiachia nipo hoi, japo fedha nimepata lakini cha moto nimekiona.”

Mara mlango iligongwa, alikuwa J4.

“Karibu J4.”

“Mbona tena kitandani?”

“Unauliza jibu, kumbe mtu wenu mnamjua hukuniambia nilijua

2020

‘wazee bata’ kimoja tu yupo hoi, tena akiguswa kidogo anawahi kufika. Lakini leo mwanangu umeniingiza chaka la nyani mashavu yote yamewaka moto.”

“Nimekwambia anaitwa Babu wa Kisemvule.”

“Kweli, leo nimeneng’emuka ile mbaya, kidogo gwaride linishinde.”

“Lakini mvuvi haogopi dhoruba, Adela sina muda nipe changu nitambae.” Adela alimpa elfu 30.

J4 baada ya kupata cha juu alitambaa zake, lakini kabla ya kuondoka, Mamu shoga wa Adela naye aliomba shavu la kukutana na Babu wa Kisemvule.

“ J4, nipe na mimi shavu kwa babu.”

“Wewe tu dada yangu, maelezo yote atakupa Adela, ukiafiki utanipigia.”

“Nimeishayapata nipo tayari.”

“Poa, nipe namba yako ya simu ishu ikitiki nikutwangie,” Mamu alimpa J4 namba ya simu.

“Basi kati ya siku mbili nitakutwangia dada angu.”

“Poa.”

J4 aliwaaga na kuwaacha wakiendelea kupiga stori za kalinye kalinye la Babu wa Kisemvule.

Baada ya kuondoka Adela alimgeukia Mamu aliyekuwa akisubiri kwa hamu kusikia habari za Babu wa Kisemvule.

“Mhu, Mwari.”

“Temea chini, babu ukimwangalia kwa umbile hata mkononi hajai, lakini mambo anayaweza, uzeeni yupo vile ujanani alikuwaje?”

“Babu wee, inawezekana umepungua uwezo na hayo madawa yako ya kujidunga, subiri auingie moto huu kama hajanifia kifuani!”

Inaendelea toleo lijalo la Alkasus

21

Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.