waandishi ebook 1686148482.5697222

Page 1

STORY………...LISA

KURASA……..26-50

SURA YA 26

Saa kumi na moja asubuhi Pamela

alifika kwa haraka pale hospitalini. Alipomwona Lisa, hasira zilimpanda.

“Bado sisi ni marafiki? Hata hukunifahamisha kuhusu jambo hili zito.

Isingekuwa mimi kuuliza namba za Harrison, nisingegundua kuwa upo hospitalini.”

"Nilidondosha simu yangu, na sijabadilisha SIM kadi nyingine." Lisa

alimwambia kwa upole.

Uso wa Pamela ulionyesha wasiwasi

alipoushika mkono wa Lisa. “Ni nini

hasa kiliendelea jana usiku? Kweli

ulikua wakala wa siri wa polisi?"

Lisa mara moja akagundua. Inavyoonekana, polisi walikuwa wametoa tangazo rasmi. "Ni nini kinachozunguka kwa sasa?"

Pamela aliyazuia macho yake ambayo yalikuwa yakimetameta. "Watu wengine wanaamini, wakati wengine hawaamini."

“Hiyo ni kawaida. Watu wengi wamekuwa wakingojea nyakati zangu za aibu kwa muda mrefu.” Lisa alimweleza kwa kifupi Pamela kilichotokea wakati wa mchakato wa zabuni jana yake.

Pamela alikasirika sana na kusema kwa

uchungu. “Ethan ni mwanaharamu. Huo ni upuuzi gani aliokufanyia? Hivi yeye ni binaamu kweli? Mbona zamani

alikuthamini sana na sasa amebadilika

kabisa? Lina alimroga vipi hadi akupige?”

“Labda alinipenda zamani kwa kuwa

alijua mimi ndiye ningekuwa mrithi. Lakini sasa upepo umebadilika na yeye

kabadilika, anampenda tu mwanamke mrithi wa familia tajiri ya Masawe.

Kwake, haijalishi yeye ni nani cha muhimu ni urithi tu alionao.”

Lisa aliongea kwa uchungu sana..

“Habari nilizozisoma asubuhi ya leo ziliripoti kwamba Mzee Kamote na bodi

inayosimamia Kituo cha Utamaduni na Teknolojia cha Taifa walihusika mara

kwa mara katika kupokea hongo, kwa hivyo anasimamishwa kazi na kuchunguzwa. Tukio la zabuni la jana pia limebatilishwa. Kulingana na maoni

yaliyotolewa mtandaoni, wengi

wanadhani kuwa Kibo Group ilimpa

Mzee Kamote rushwa ambayo

ilichangia Kibo Group kupata matokeo ya zabuni hiyo hapo jana.

Lisa alipigwa na butwaa. “Hii inawezekanaje?”

“Kwa nini nikudanganye? Ngoja nikuonyeshe habari hiyo.”

Pamela aliwasha simu yake haraka na kutafuta tovuti ya habari hiyo ili kumuonyesha Lisa. Lisa alishangaa kabisa. Alihisi kuwa kuna jambo geni kuhusu sadfa hiyo.

"Yajayo yanafurahisha!"

Pamela alisema kwa furaha kubwa, "Unaona, makampuni mengi makubwa ya tasnia ya ujenzi yalishiriki katika zabuni jana, na walitumia muda mrefu na rasilimali nyingi za wafanyakazi na nyenzo katika maandalizi ya tukio hilo. Juhudi zao zote

zimeishia bure sasa. Nadhani kituo

kimemchukiza kila mtu.”

Lisa aliamini hivyo baada ya kuwaza. Hata hivyo, ilikuja kama habari njema

kwake kwamba juhudi za Lina

hazikufaulu.

•••

Ndani ya ofisi za Kibo Building Design Group, Jones Masawe, mkurugenzi

mkuu, alikuwa amekasirika sana hivi

kwamba kifua chake kilikuwa hatarini

kupasuka muda wowote. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Lina kumuona

baba yake akivimba kwa hasira. Akiwa

ameinama upande mmoja, hakuthubutu

kusogea hata kidogo.

Siku moja tu nyuma, wasimamizi wakuu wa kampuni walikuwa wamesherehekea

mafanikio ya zabuni ya Kituo Cha

Teknolojia Na Utamaduni Cha Taifa, lakini kesho yake furaha hiyo ilianza

kuyeyuka taratibu baada ya kusikia

kuwa Mzee Kamote alikuwa

amekamatwa na TAKUKURU. Je, angefanya nini ikiwa kuhusika kwa

Mzee Kamote katika hongo

kungefichuliwa?

“Mama…” Lina alimwangalia mama yake, kwa wasiwasi. Mama Masawe

alimpiga bega na kumfariji. “Usijali. Kwa kuzingatia hali ya baba yako kwa miaka

mingi, ataweza kusuluhisha hili tatizo.”

"Hata kama naweza kusuluhisha, sifa ya Kibo Group itaathiriwa kwa kiasi

kikubwa," Jones Masawe alijibu kwa hasira.

Mama Masawe alimkodolea macho

mumewe. "Hii sio kazi ya Lina.

Amefanya kwa kadri yake. Yeyote

kutoka kwa kampuni ambaye

angejihusisha nayo angekumbana na hali kama hii. Kwa kweli, kuna mtu

alipanga kumdanganya Mzee Kamote.

hata Jones Masawe hajamaliza

sentensi yake, meneja mkuu ghafla

akaingia ndani na kusema, “Bw.

“Sina maana ya kumlaumu…” Kabla

Masawe, kuhusu mpango wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa klabu ya Simba, mratibu alitupigia simu hivi punde na kutufahamisha kwamba hawatafanya kazi na sisi tena. Pia, Hoteli ya

Kimataifa ya Holmes ilisema kwamba hawatafikiria kufanya kazi nasi.”

Jones Mwasawe alihisi kizunguzungu

huku akiwa amefura kwa hasira. Hii ndiyo miradi miwili mikubwa ambayo

Kibo Group ilikuwa ikilenga kwa muda wa miaka miwili iliyopita na ilikuwa

karibu kuipata.

Meneja mkuu kisha akaongeza, “Mbali na hayo, kampuni yetu ilituma maombi ya kutembelea maonyesho ya dunia

katika nchini ya India mapema, lakini

sasa wametukataa moja kwa moja. Bw.

Masawe, je kampuni yetu imemkosea

nani? Ni wazi kuna mtu anayeichafua

Kibo Group nyuma ya mgongo wetu.”

Jones alianza kutetemeka. Yeye ndiye

alikuwa ameongoza Kibo Group kwa

juhudi na kwa miaka mingi na hakuwahi

kugombana na mtu. "Siku zote

nimekuwa nikifanya kwa uangalifu

katika tasnia hii kwa miongo kadhaa.

Sijawahi kumuudhi mtu yeyote.”

“Inaweza kuwa… Lisa ?” Lina aliongea

kwa kusitasita. “Usinielewe vibaya.

Sijaribu kumsema vibaya. Haikuwa

suala kubwa wakati Lisa aliponikokota

nje ya Mgahawa wa Grapefruit wakati

huo. Lakini, Janet na Cindy walikuwa

wamekasirika sana wakati huo.

Walisema kwamba wangefanya jambo

kuhusu hilo. Wote hawa wanatoka

kwenye familia za matajiri wenye

ushawishi mkubwa. Huoni kwamba

tatizo linaweza kuwa lilianzia hapo?”

"Hakika inahusiana na Lisa!” Mama

Masawe alinguruma.

“Mwambie arudi.” Usemi wa Jones

uligeuka kuwa wa kusikitisha.

"Bw. Masawe, kuna jambo moja ambalo huenda hulijui…” Meneja mkuu alisita

kabla ya kusema, “Video ya moja kwa moja kwenye chaneli moja ya yotube

ilionyesha matukio machache ya aibu jana usiku, na Lisa akatokea kuwa

mhusika wa kike. Hata hivyo, video hiyo ilizimwa wakati polisi walipoingia na kuwakamata watu hao. Baada ya tukio hilo, polisi waliondoa video zote

zilizosambazwa mtandaoni na kutangaza kwamba Lisa alikuwa wakala wa siri wa polisi!”

Lina alishangaa kwa kufoka, “Hiyo ilikuwa hatari! Yeye hata hajapitia

mafunzo ya upolisi, sasa amekuwaje wakala wa siri?”

Mama Masawe aliuma meno. “Ni

wakala gani wa siri? Kuna uwezekano

mkubwa alijifanya kuwa wakala wa polisi baada ya kupata matatizo. Ni lazima polisi ndio waliomuokoa. Ni aibu iliyoje.”

Meneja mkuu akasema, “Ndiyo. Hicho ndicho kimekuwa kikienea katika

mtandao. Inajadiliwa sana kuwa maisha ya Lisa ni ya fedheha. Sifa yake

imeharibiwa sana.”

“Ni kiumbe mbaya sana. Kwa sababu yake, sifa ya familia ya Masawe imeharibiwa.” Akiwa amekasirika kwa hasira, Jones Masawe alichukua

chombo kwenye meza na kukitupa. “Tafuteni njia ya kumrudisha. Sitaki abaki nje na kuendelea kuwa fedheha kwa familia.”

SURA YA 27

Lisa aliruhusiwa kutoka hospitali baada ya siku mbili. Alvin binafsi aliendesha

gari hadi hospitali kumchukua.

Akikumbuka jinsi alivyotendewa kwa ukarimu isivyo kawaida, Lisa alijisikia

faraja sana. Akiwa anaendesha gari kurejea nyumbani, Alvin alipitia kwenye

maduka kufanya shopping kwanza.

"Charlie amekuwa mbaguzi sana wa chakula wakati haukuwa karibu naye

kumpikia siku chache zilizopita. Nunua viungo zaidi na umtayarishie kitu kizuri.”

Alvin alimwambia Lisa.

Akiwa anautazama uso wake wa kifahari, Lisa alijiuliza sana ikiwa ni Charlie au ni Alvin ambaye alikuwa mbaguzi wa chakula.

"Unasubiri nini? Harakisha." Alvin alimkurupua. Alikuwa amechoshwa na

vyakula visivyopendeza ambavyo Hans

alimletea kwa siku mbili zilizopita.

“Oh.” Lisa alifungua mkanda na kushuka kwenye gari. Kwa kuwa

alikuwa amemfanyia wema na hisani

kubwa wakati huo, alipanga

kumwandalia chakula kizuri ili

kuonyesha kuwa anajali fadhila zake.

Alipokuwa akiingia kwenye jengo la maduka, zaidi ya aina kumi ya mapishi ya Charlie yalimwangazia akilini mwake.

Kulikuwa na viungo vingi sana alihitaji

kununua. Pia alikusudia kupata mtindi, maziwa mabichi, matunda, na vyakula

vingine.

Baada ya duru moja ya ununuzi, aligundua kuwa mkokoteni ulikuwa

tayari umejaa. Hakika ilikuwa ni shida

kwake kubeba vitu vyote peke yake.

Baada ya kufikiria kidogo, alimtumia

Alvin ujumbe kwenye WhatsApp.

[Alvlisa, nimenunua vitu vingi, na sidhani kama naweza kubeba kila kitu.

Unaweza kunisaidia kubeba mifuko michache?] Baada ya kutuma ujumbe huo, hakusikia kutoka kwake kwa muda wa dakika tano. Alipumua na kuacha kuwa na matarajio makubwa kwake na kufikiria kubeba mwenyewe mizigo ile. Akiwa katikati ya mawazo yake, ghafla aliona kivuli kikubwa cha mtu kikiibuka. Alipoinua kichwa chake, umbo refu na wima la Alvin likatokea mbele yake.

"Nilitaka tu ununue viungo vya Charlie, lakini umekuja kununua duka zima."

Alvin alimkejeli Lisa baada ya kuona lundo la vitu alivyokuwa amenunua.

Lisa alieleza haraka, “Nilikuwa nikifikiri

kwamba wewe na Charlie hamjaweza

kula chakula chochote kinachofaa siku

chache zilizopita, kwa hivyo nimenunua zaidi…”

Alvin aliinua mkono wake na kumkatisha kwa kukunja uso, “Nilikula vizuri. Alikuwa Charlie ambaye hakula vizuri, usijumuishe na mimi. Mimi si mbaguzi wa chakula.”

“Una uhakika?”

"Ndio, Charlie hakula vizuri." Alvin alihakiki usemi wake.

Ili kumwokoa asipoteze heshima yake, Lisa aliitikia kwa kichwa na kueleza

kwa fikira, “Vitu ninavyonunua vyote ni vya lazima. Unahitaji kula mtindi, maziwa freshi, na matunda kila siku ili mwili wako upate lishe ya kutosha.

Huenda ukaonekana mzima sasa, lakini unafanya kazi kwa bidii kila siku na hata kunywa pombe kwa nyakati fulani. Kwa

hiyo, ni lazima utunze mwili wako na kula mlo kamili unapokuwa nyumbani.”

Alvin aliposikia hivyo alipigwa na butwaa. Macho yake yalifichua hisia zinazokinzana.

Kabla ya hii, hakuna mtu aliyejali kuhusu lishe yake. Watu wengine

walichojali zaidi ni uwezo wake wa kuleta manufaa kwa familia ya Kimaro na kama alikuwa ametimiza mahitaji ya familia ya Kimaro.

Lisa kisha akaongeza, “Ninahitaji

viungo hivi katika upishi wangu. Pia

nilinunua hizi tambi ili nikupikie

ukichelewa kutoka kazini. Tunahitaji

toilet papers na sabuni za maji kwa ajiliya usafi pia.”

Wakati huo, Alvin alikuwa chini ya hisia

kwamba mwanamke huyu alipaswa

kuwa mke wake, kutokana na kwamba

alikuwa anajali sana kila kitu ndani ya nyumba.

Akionyesha kisanduku cha karatasi, Lisa aliendelea, “…hii tishu itawekwa kwenye gari lako. Kwa hiyo si mara zote utalazimika kutumia karatasi ya tishu iliyotolewa kwenye kituo cha mafuta. Aina hii ya tishu ni nafuu sana…”

"Tangu lini ninatumia karatasi ya tishu iliyotolewa bure kwenye kituo cha mafuta?"

“Ipo kwenye gari lako. Bado ipo.” Kwa kuogopa kwamba alikuwa na wasiwasi juu ya kuokoa heshima yake, Lisa alijifanya kuwa alipenda vitu alivyotumia Alvin. “Haijalishi. Ninapenda kwa kuwa unatumia vitu visivyo na bei sana. Nimefurahi kukutana na mwanamume ambaye anaishi maisha ya kujali matumizi mazuri ya pesa.

Wewe ni mfano wa mwanaume kamili

ninayependa kuishi naye."

Akiwa amezidiwa na pongezi hizo za

ghafla, Alvin aliinamisha kichwa chini. Jinsi alivyotazama juu na kumwangalia

kwa macho angavu ilimkumbusha mara ya kwanza walipokutana. Ikilinganishwa na mwonekano wake mbaya siku mbili zilizopita, sura yake isiyo na aibu sasa

hivi ilimfanya ajisikie vizuri.

"Haupaswi kufanya kazi kama mbunifu. Unapaswa kuwa mama wa nyumbani."

Alvin alimtania.

Lisa alicheka. "Nataka tu kuwa mama wa nyumbani na chumbani pia."

"Nenda ulipe bili sasa." Alvin alimwambia kwa kupotezea.

Muuzaji mwenye shauku ambaye

alikuwa akitangaza bidhaa fulani

aliharakisha hadi kwenye kaunta ya

kulipia na kuwazuia wawili hao. “Halo

bwana na bibie. Je! ninyi mnataka

kununua Durex? Tuna promosheni

ianyoendelea ambapo unanunua moja na kupata moja bila malipo. Ni kweli inaokoa pesa.”

Lisa aliona haya kuona kisanduku kidogo cha kondomu mkononi mwa muuzaji. “Hapana… Hakuna haja. Hatuhitaji.”

“Ohhh. Nyote wawili ni watu waliooana

hivi karibuni, kwa hiyo mnapanga kupata mtoto?” Muuzaji aliuliza bila

kujua lolote.

“Ndiyo.” Akiogopa kwamba muuzaji angeendelea kuwasumbua

Lisa alinong'ona kitu na kisha akamvuta

Alvin mbele.

"Nani kasema anataka kupata mtoto?"

Alvin alimtazama Lisa kwa jicho kali.

“Nilikuwa namdanganya tu aende zake, au unataka kuzinunua?" Lisa aliuliza kwa kawaida.

“Acha kuota. Hata kama ningenunua, sitaitumia na wewe.” Licha ya maneno yake ya kikatili, sura ya Lisa ilitabasamu kwa furaha.

Baada ya wao kuondoka kwenye maduka, Alvin aliendesha gari kurudi

nyumbani Walipofika nyumbani, Lisa

aliingia moja kwa moja jikoni kuandaa

chakula. Mwanzoni Lisa alifikiri

kwamba alikuwa ameandaa chakula

kingi sana. Mara tu Alvin alipoanza kula, alifikiri chakula kisingetosha. Alionekana

kuwa na njaa ya siku mbili. Chakula

kiliisha kwa muda mfupi. Baada ya

chakula cha mchana, Alvin na Charlie

walilala kwenye kochi kwa uvivu, akijipumzisha kidogo ili chakula kishuke

taratibu.

“Unapanga kufanya nini baadaye?

Utaendelea kutafuta kazi?” Alvin alimuuliza Lisa

“Tulizungumzie hilo baadaye. Nitaenda kusajili laini ya simu kwanza.” Lisa ajibu.

“Usijali kuhusu hilo. Ikiwa huwezi kupata kazi, kaa tu nyumbani unipikie. Kama

una shida ya pesa nitakupatia kiasi chochote muda wowote unaotaka.”

Alvin alimwambia huku akitoka.

Lisa alipigwa na butwaa kwa muda.

“Unakwenda kazini sasa hivi?”

"Ndio, bado nina kazi nyingi ya kushughulikia." Mara baada ya kuondoka, Lisa alitupia macho muda

huo ambao ulionyesha ni saa saba

mchana. Kwa kweli alimuonea huruma

kwani kuwa bosi haikuwa rahisi.

Hakuwa na hata mapumziko baada ya

chakula cha mchana. Pengine alikuwa

ameiba tu muda nje ya ratiba yake

yenye shughuli nyingi ili kumchukua hospitali.

SURA YA28

Baada ya Lisa kusajili laini ya simu

mchana huo, simu yake ilionyesha zaidi ya simu kumi ambazo hazikupokelewa.

Alikuwa amerudisha namba yake ileile ya zamani. Simu hizo zilipigwa na

Pamela Masanja, Jones Masawe, na

Mama Masawe, na watu wengine

wengi. Je, inawezekana kwamba walikuwa na wasiwasi juu yake baada ya kujua kilichomtokea? Bila kujali

sababu, alimpigia simu mama yake.

“Mama…”

“Hatimaye umenipigia simu tena.” Sauti ya hasira ya Mama Masawe ilisikika.

“Unakusudia kukaa nje hadi lini? Njoo

nyumbani sasa hivi.”

Ule msemo 'njoo nyumbani' ulimfanya Lisa ahisi uchungu ndani kabisa, akauliza kwa hasira. “Hapo bado ni nyumbani kwangu?”

“Lisa, ikiwa hautarudi sasa, usirudi

milele. Huhitaji tena kumtambua baba yako na mimi pia.” Mama Masawe

alikata simu mara baada ya kumaliza kuongea.

Baada ya kusitasita, hatimaye

Lisa aliamua kurudi nyumbani. Kwani, Jones na Mama Masawe ndio

waliomzaa na kumlea. Pia alitaka

kuwapelekea rekodi iliyo na maneno ya Juma Masudi nyumbani na waisikie ili

wajue rangi halisi za Lina.

Saa moja baadaye, aliendesha gari hadi

kwenye jumba la kifahari la familia ya Masawe. Ingawa ilikuwa imepita zaidi ya mwezi mmoja tu tangu aondoke

nyumbani hapo, alihisi kwamba watu

wanaoishi hapo walikuwa wageni kabisa kwake. Baada ya kuegesha gari lake aliingia ndani. Jones, Mama Masawe, na Lina wote walikuwa sebuleni. Mara tu Lisa alipoona sura ya Lina, chuki iliwaka ndani yake. “Baba, Mama, unajua kwamba Lina aliiba mpango wangu, na yeye—”

“Lisa, sijali kunishtaki nje, lakini

unawezaje kuthubutu kunirushia matope hapa?” Tabasamu la uchungu lilienea

kwenye uso wa Lina. "Tayari nimesema sijafanya."

Mama Masawe alivuta uso mrefu pia.

“Kwa nini unamwakia tu dada yako kwa

maneno makali kila unapomwona?”

“Nina ushahidi.” Lisa mara moja akatoa

simu yake na kucheza rekodi ya Juma

Masudi. Mara tu Lina aliposikia sauti ya Juma, sura yake ilibadilika kidogo. Hata hivyo, upesi alipata utulivu na kusema

kwa huzuni, “Ulimpata wapi mtu huyu wa kumlaghai kurekodi haya? Juma ni nani? Hata simfahamu.”

Lisa aligeuka na kumtazama baba yake kwa macho mekundu kidogo. “Baba, Lina alihamisha mamilioni ya pesa kwenye akaunti ya Juma ambayo

unaweza kuangalia mwenyewe. Alikulia kijijini na alijifunza kubuni tu baada ya wewe kumkubali. Kwa kuzingatia kwamba alijifunza kwa muda mfupi tu, angewezaje kutokeza na muundo mzuri kama huo?”

"Baba na mama, sikufanya hivyo."

Machozi yalitiririka usoni mwa Lina.

Mama Masawe alikunja uso na kunyoosha mkono wake. "Lisa , nionyeshe hiyo rekodi." Akiwa na moyo

mpole kidogo, Lisa akamkabidhi simu

kwa utiifu. Mama Masawe alifungua faili ya kurekodi na kulifuta mara moja.

"Mama, wewe ... kwanini?"

Lisa alishangaa kwa kitendo cha hicho cha mama yake, lakini alivyotaka

kumpokonya simu yake, alikuwa ameshachelewa.

Mtazamo wa Mama Masawe

ulidhihirisha ukatili wake kwa mara nyingine tena. “Siwezi kukuacha uharibu

sifa na mustakabali wa dada yako kwa rekodi hii ambayo inaweza kuwa ya uwongo. Afadhali kuifutilia mbali.”

Lisa alichanganyikiwa sana hivi

kwamba alitetemeka. Mara moja, alitoa kicheko kisicho na maana. “Sasa

naona. Ninyi nyote hata hamjali ikiwa

rekodi ni ya kweli au la. Mnachojali ni kumkingia kifua Lina tu. Unawezaje

kuwa mkatili hivyo? Mimi pia ni binti yako.”

Jones alipiga meza na kusimama.

“Kama ningejua mapema kwamba

ungekuwa mtu hatari sana, ningalikuacha wakati huo. Angalia

mambo ya ajabu ambayo umefanya. Umepoteza sifa yako kwa kufanya

jambo la aibu tena hadhahari na kurekodwa kwenye video. Je, mtu

yeyote mwenye heshima angependa kukuoa katika siku zijazo? Pili, ni nani

aliyekukosea hadi ukatufanya kupoteza miradi mikubwa michache?”

"Sijui unazungumza nini." Lisa akatikisa kichwa huku akilia. “Kama wazazi

wangu, hamna wasiwasi nami tangu

mlipoona nimekutana na matatizo kama

hayo?”

“Hicho ndicho unachostahili,” Mama

Masawe alizungumza kwa njia ya

dharau, “Si ajabu Ethan alikutupa kwa

sababu haujitambui kabisa.”

Lisa alishindwa kabisa kusema. Hata wazo dogo la matarajio ndani yake

lilikatishwa tamaa. Alijiona mjinga sana. Hakupaswa kurudi. Ukweli haukuwajali baba yake wala mama yake hata kidogo. Muhimu zaidi alikuwa ni Lina.

Akiwa amehuzunika, Lisa alinyoosha

mkono wake kwa mama yake.

“Nirudishie simu yangu mama, nitaondoka. Mtu mwenye aibu kama mimi hastahili kurudi. Sistahili kuwa na uhusiano na ninyi nyote pia.”

"Unapanga kuendelea kuzurura mitaani na kuleta aibu kwa familia yetu sivyo?"

Jones alicheka. “Afadhali ukae

nyumbani na kutafakari matendo yako.

Ukiamua kusema ukweli, nitafikiria

kukurudisha kwenye kampuni.”

Mara Jones alipomaliza kuzungumza, alipiga makofi. Walinzi wachache

walitoka kwenye mlango na kumkamata

Lisa mara moja.

“Nyie mnajaribu kufanya nini?

Mnaniteka nyara, huh?” Lisa alikasirika.

Kamwe katika ndoto zake kali hakuwahi

kufikiria kuwa familia yake ingewahi

kumfanyia kitendo kama hicho.

“Ninamfundisha tu binti yangu somo. Mleteni juu na kumfungia chumbani.”

Jones Masawe alisema.

Lina akashauri haraka, “Usifanye hivi baba. Baada ya yote, Lisa bado ni mdogo na hajakomaa. Zaidi ya hayo, daima kuna wageni wanaokuja

kututembelea hapa. Haitakuwa nzuri

ikiwa atapiga mayowe kutoka juu.

Jones alishtuka. “Uko sahihi. Kwanini…

Hebu tumpeleke mbali kabisa

tukamfungie katika nyumba ya Old

Moshi.”

Lisa alianza kuingiwa na hofu. Katika

miaka michache iliyopita, alikuwa

amerudi huko kijijini kwao Mbokomu, Moshi vijijini mara moja tu kwa ajili ya

shughuli za matambiko. Nyumba hiyo

ilikuwa imejengwa na ukoo wa Masawe

miaka mingi sana iliyopita. Ingawa sehemu ya nyuma ya nyumba ilikuwa

imerekebishwa kidogo, eneo jirani

lilikuwa ukiwa na la kutisha. Hatimaye

Lisa alielewa ni kwanini Lina

alimuombea apelekwe huko. “Lina, wewe ni mtu mbaya sana—”

Mama Masawe alimpiga Lisa kofi

usoni. "Nyamaza! Dada yako anajaribu

kukuombea, kumbe unamtukana.

Hakika wewe ni mbaya sana!”

mkono wake. Akiwa amechanganyikiwa

"Mpelekeni sasa hivi." Jones alipunga

na mabadiliko ya tabia ya Lisa , alijiuliza

ni kitu gani kilimfanya awe mbaya kiasi kile. Akiwa amepitiwa na usingizi, Lisa hakujua safari ya gari iliendelea kwa muda gani. Aliachwa moja kwa

moja kwenye nyumba ya zamani ya kijijini baada ya hapo.

Walinzi wachache wakafunga mlango

mkuu mara moja. Hata madirisha

yalifungwa kwa misumari. Mbaya zaidi

hakukuwa na umeme wala maji. Hata

blanketi hakupewa, na ukizingatia baridi

la milima ya old Moshi kipindi hicho, Lisa alihisi kuganda. Kwa vile simu yake

ilikuwa kwa Mama Masawe, hakujua

muda huo ulikuwa ni saa ngapi.

Nyumba hiyo kubwa ya zamani ilikuwa

imejengwa kwenye eneo kubwa, ikiwa

imezungushiwa na ukuta mkubwa

yapata mzunguko wa kiwanja cha

mpira. Ndani yake kulijaa pori la

migomba na miti ya miparachichi na mifenesi hivyo kuifanya nyumba ile kubwa kuwa ya kutisha sana ndani

yake. Upepo ulivuma na hivyo kugonga mlango na madirisha, sauti ya kutisha ya popo waliokimbizana pia ilisikika. Lisa karibu awe mwendawazimu.

Akajikunja juu ya kitanda kwa uwoga mkubwa, hakuthubutu kusogea hata

kidogo. Aliogopa giza. Aliogopa sana. Mara tu alipogundua kuwa dirisha limefunguliwa, alikimbilia huko. Bibi mzee aliweka bakuli la wali kupitia

dirishani. Mara Lisa alimshika mkono na kumsihi, “Bibi naomba uniache niende. Ikiwa hilo haliwezekani, angalau washa taa na unipe kitanda na blanketi, tafadhali.”

"Hapana. Hili ni agizo kutoka kwa bwana na bibi Masawe" Bibi kizee

alijitenga na mikono yake kikatili. Kisha, kulikuwa na kishindo kwenye dirisha likifungwa.

Akiwa amesimama gizani, Lisa alikuwa anaumia sana hivi kwamba alishindwa

kupumua. Alikuwa amefanya nini hasa? Kwanini kila mtu alimtenda hivi? Alikuwa amevuliwa utu wake. Hata uhuru na maisha yake ulichukuliwa pia.

Alimchukia Lina, Bw. Masawe, Bi. Masawe, na Ethan kabisa. Hata hivyo, hakuweza kukata tamaa. Alitaka kubaki hai na kulipiza kisasi. Alijaza wali mdomoni. Hakukuwa na kitu kingine zaidi ya wali. Mbaya zaidi mchele ulikuwa umevunda. Machozi yalimwagika usoni mwake. Ikiwa hakuna mtu angekuja kumwokoa, labda asingeweza kutoka nje ya nyumba hiyo akiwa hai.

Bibi kizee alitoa simu kwa mbali kidogo na mlango mkuu. "Lina, nimefanya kila kitu kulingana na maagizo yako."

“Usijali. Kwa mwonekano wa mambo, hakika hataweza kuishi kwa zaidi ya siku nne.”

SURA YA 29 Baada ya Alvin kutoka kazini, alienda moja kwa moja kwenye mkutano kuhusu kesi ya kimataifa ya kifedha usiku. Akiwa amekunywa pombe wakati wa mkutano, alihisi kizunguzungu kidogo. Mara baada mkutano

kumalizika, alirejea nyumbani. Hali ya nyumba ilikuwa tulivu na kimya. Baada

kuingia ndani ya nyumba hiyo na kuwasha taa, Charlie alimkimbilia.

Aliendelea kulia ‘mieww…mieww..’ huku

akikumbatia mguu wake.

"Charlie, unataka

huh?" Alvin akatikisa kichwa chake taratibu. Baada

“Sawa. Anza kupunguza halijoto kesho.
Natumai ... atafia nyumbani."
nini,

ya muda kidogo, aliona kitu kibaya kwa

Charlie ambacho hakuweza kufahamu hadi alipoisugua pua yake kwenye

bakuli tupu. Charlie alikuwa na njaa. Je, Lisa hakumlisha? Mara moja

akammiminia chakula cha paka Charlie ambaye alionekana kuwa na njaa kali.

Alvin alikwenda chumbani kumtafuta

Lisa, na kugundua kuwa alikuwa

hajarudi. Uso wake ukajawa simanzi ghafla.

Mwanamke huyu amekuwa

akisababisha matatizo yasiyoisha. Hapo awali alilazwa hospitalini, na sasa kwa

kuwa hatimaye alikuwa amerudi

nyumbani kwake, alimwacha Charlie

katika hali kama hiyo. Bado alikuwa

hajarudi ingawa tayari ilikuwa ni usiku

sana. Akatoa simu yake ili ampigie, lakini simu yake ilikuwa imezimwa. Je, kuna jambo jingine lililomtokea?

Baada ya kuitoa simu yake, Alvin

alifuatilia mahali alipo Lisa. Kwa bahati nzuri, alipomkabidhi simu siku hiyo,

alikuwa amewasha ufuatiliaji wa eneo (gps) kwa kuhofia matukio mabaya

yangeweza kumtokea tena. Baada ya kufuatilia eneo lake, Alvin alimtumia ujumbe Hans. [Niangalizie eneo hili.]

Dakika moja baadaye, Hans alipiga simu, “Hii ni nyumba ya familia ya Masawe ambapo wazazi wa Lisa wanaishi.”

"Nimeelewa." Alvin alikata simu kwa hasira. Alvin alishindwa kabisa kumtafakari

Lisa. Alikuwa tu akionyesha ladha ya fadhila baada ya yeye kumtendea

wema. Sasa alikuwa ameenda

nyumbani kwao bila kumpigia hata simu kwanza. Mbaya zaidi alikuwa amezima

simu yake. Alikuwa na maana gani?

Je, hakuwa na mpango wa kurudi nyumbani kwake baada ya kusamehewa na familia ya Masawe?

“Afadhali asirudi milele” Alvin alijiapiza moyoni. Asingemjali tena hata kama

angekuwa na matatizo. Kamwe asingetarajia kwamba Lisa angekuwa hana moyo kiasi hicho.

Hakukuwa na habari juu yake kwa siku

tatu zaidi. Hakujibu hata simu zake.

Kilichomshusha moyo zaidi Alvin ni kwamba hakula vizuri katika siku hizo

tatu. Hata alitembelea mgahawa ambao

ulitoa chakula kitamu zaidi kama

ilivyopendekezwa na Sam, lakini aliona chakula hicho hakikupendeza.

Wakati fulani, alishuku kwamba jambo

fulani linaweza kuwa limetokea kwa

Lisa. Hata hivyo, kila alipowasha simu

yake kuangalia mahali alipo, mara zote

ilimuonyesha yupo kwenye nyumba ya familia ya akina Masawe. Wazazi wake wa kumzaa wasingeweza kumdhuru, aliamini hivyo. Ni wazi kwamba alikuwa ameamua kumsahau na kumpuuza kwa makusudi.

Katika siku tatu mfululizo alikuwa amepooza sana ofisini. Muda wa kutoka

kazini ulipofika, mara moja alifungasha vitu vyake na kuondoka. Kisha

akagongana na Sam mlangoni.

“Unaenda nyumbani kumtunza Charlie?

Lisa bado hajarudi?"

"Usimtaje tena mwanamke huyu." Alvin aliendelea mbele akionekana kutokujali.

Sam alishtuka. “Sikuwa na jinsi zaidi ya

kukuuliza kwani Pamela aliniomba kujua

kuhusu Lisa. Alisema hajaweza

kuwasiliana naye, hivyo ana wasiwasi

kwamba kuna jambo limempata.”

"Siku zote hizi amekuwa katika nyumba ya familia ya Masawe, sivyo?" Alvin alisimama akiwa ameganda palepale.

Ilieleweka kuwa Lisa hakumpigia tena simu kwani wote wawili walikuwa

wamekutana tu muda si mrefu, lakini

Pamela alikuwa rafiki yake mkubwa.

“Ngoja nimpigie simu tena.” Sam

alijaribu kupiga simu.

Alvin alishuka kwa kutumia lifti bila kumsubiri. Akiwa njiani kuelekea

nyumbani, alihisi mambo yanazidi kuwa

mengi huku akiwaza. Hata hivyo,

aliogopa kwamba huenda akawa

anawaza kupita kiasi juu ya Lisa wakati

Lisa mwenyewe hata hamfikirii kabisa.

Bila kutarajia, Alvin alipokea simu

kutoka kwa Sam mara baada ya kufika nyumbani kwake.

“Hilo haliwezekani kabisa. Sasa hivi

Pamela aliniambia kwamba alitembelea

familia ya Masawe. Wakamwambia

Lisa ameenda nje ya nchi kupumzika, lakini hawakumpa namba yake ya mawasiliano. Damn, kuna kitu kinaweza kuwa kimemtokea?"

Alvin alikunja uso. “Sifikirii hivyo. Baada ya yote, yeye ni binti wa damu kabisa wa familia ya Masawe.

“Labda sivyo. Pamela alisema kuwa

familia ya Masawe ina upendeleo sana kwa Lina na inambagua Lisa.

“Sawa. Nitaifuatilia hiyo.” Alvin alisema.

Akiwa na hasira, Alvin kisha akampigia

Hans simu. "Tafuta ni wapi

Lisa alionekana mara ya mwisho."

Saa moja baadaye, Hans alimletea

habari fulani. “Lisa alienda kwenye

nyumba ya familia ya Masawe siku tatu

zilizopita. Muda mfupi baada ya kuingia

ndani ya nyumba hiyo, familia ya Masawe ilielekea kwenye nyumba ya zamani iliyoko Moshi kwa kutumia gari

lao. Pengine atakuwa yupo huko.”

“Unamaanisha kuwa anaweza kuwa kafungiwa?”

"Uwezekano mkubwa sana. Familia ya Masawe haingeenda huko isipokuwa kwa matambiko yao ya familia wakati wa mapumziko ya mwisho wa mwaka. Isitoshe, mahali hapo ni mbali sana.”

Alvin aliishika simu yake kwa nguvu.

“Fanya uchunguzi ujue mahali nyumba hiyo ilipo kisha unichukue. Nitatembelea nyumba hiyo mimi mwenyewe."

SURA YA 30

Kwa kuzingatia kwamba Moshi iko mbali

sana kutokea Dar es Salaam, Hans

aliendesha gari kwa saa sita kabla ya

kufika huko. Tayari ilikuwa ni saa sita

usiku walipofika. Nyumba ya ukoo wa Masawe ilikuwa katika kijiji cha

Mbokomu wilaya ya Mosh vijijini. Alvin aliposhuka tu ndani ya gari ndipo

alipogundua kuwa mahali hapo palikuwa na ukiwa wa kutisha.

Palizungukwa na ukuta mkubwa wenye eneo sawa na uwanja wa mpira.

Migomba mingi na miti mikubwa ya miparachichi pamoja na mifenesi

ilizunguka jumba hilo na kuliweka katikati. Hakuna mtu aliyeishi humo kwa

wakati wote. Jumba hilo lilitumika

sanasana kwa ajili ya wanaukoo wa Masawe kukutana mwisho wa mwaka.

Kutoka kwa mlango mkuu, ilionekana

kuwa nyumba hiyo ilikuwa ya miaka ya sabini au themanini hivi.

Alvin aligonga mlango, lakini hakukuwa na majibu. Kwa hivyo, mara moja

alipanda juu ya ukuta. Dakika

alipokanyaga chini, miale ya mwanga

ilimulika. "Wewe ni nani? Mbona unaingia ndani ya nyumba usiku wa manane?”

Alvin aligeuka nyuma na kumuona bibi kizee aliyekuwa ameshika tochi.

“Natafuta mtu. Niligonga mlango sasa hivi, lakini hukufunguliwa.”

“Mimi pekee ndiye ninayeishi hapa. Ondoka sasa hivi.” Bibi kizee

alimsukuma. Alvin alimsukuma tu yule bibi kizee akarudi nyuma. Alichukua

tochi na kuelekea kwenye ile nyumba ya ghorofa moja. Alipotazama huku na kule, akapata mshtuko. Aligundua kuwa madirisha yote yalikuwa yamefungwa

kwenye sakafu zote mbili huku mlango

nao ukiwa umefungwa.

"Fanya haraka uondoke sasa, au nitaita polisi." Kwa hofu, bibi kizee alimsukuma

Alvin kwa nguvu zaidi.

“Afadhali upige simu polisi waje

wakukamate kwa kosa la kumfunga mtu kinyume cha sheria.” Usemi wake

ulithibitisha zaidi dhana yake. Yule bibi kizee akaogopa mara moja.

Alvin akapiga hatua kubwa mbele, kisha

akaupiga teke mlango kwa nguvu. Hata baada ya kuupiga kwa muda mrefu, bado alishindwa kuuvunja ule mlango.

Alipoona shoka pembeni ya nyumba, alivunja dirisha moja kwa kutumia shoka hilo na kuruka ndani ya nyumba.

Harufu mbaya ikajaa puani mwake. Kwa

kuwa nyumba hiyo haikuwa na umeme, ilimbidi kumtafuta Lisa chumba kwa

chumba. Hatimaye, alimkuta amejikunja

kwenye kona ya kitanda cha mbao.

Bado alikuwa amevalia nguo ile ile

ambayo aliiona kabla ya kuondoka mchana ule. Kulikuwa na baridi kali

kwenye milima ile ya Old moshi. Hata

hivyo, hakukuwa na blanketi na mito

kwenye kitanda alichokuwa amelalia

Lisa. Hakukuwa na hata na tandiko la kitanda. Alipomkaribia, aliweza kuhisi harufu

iliyokuwa ikitoka mwilini mwake. Hata

hivyo, hakuweza kuwa na kinyaa juu ya harufu hiyo. Alimkimbilia na kumtikisa

kwa nguvu, lakini hakuonyesha kushtuka. Mwili wake ulikuwa wa baridi

kama barafu, huku uso wake ukiwa mweupe kama kipande cha muhogo.

Kwa bahati nzuri, aligundua kutoka

kwenye ncha ya pua yake kwamba

bado alikuwa akipumua kwa shida, au angefikiria kuwa amekufa. Alvin

akambeba na kukimbilia mlango mkuu.

Bibi kizee aliyekuwa amejificha nyuma ya mlango aliingiwa na hofu baada ya

kutambua hali ya Lisa . Kwa kuogopa

kukaa tena, mara moja alikimbia kwa

kutumia mlango wa nyuma. Alvin

hakuwa na muda wa kumkimbilia

kumshika. Ikiwa asingempeleka

Lisa hospitalini muda huo, bila shaka angeweza kufa.

Wakiwa njiani kuelekea hospitalini, Lisa

alibaki ametulia mikononi mwa Alvin.

Alvin aliinamisha kichwa chake huku

akimtazama usoni. Mashavu

yake yalikuwa yamekonda, huku

midomo yake kama jeli ilikuwa mikavu na yenye kupasuka. Alivin hakuamini

hakuamini kabisa baada ya kujionea tukio hilo. Lisa alikuwa binti wa damu wa familia ya Masawe lakini walimfanyia

unyama kama ule. Walikuwa wabaya

sana! Ndani kabisa, Lisa alielemewa na kufadhaika na mateso. Alvin alimuonea

huruma mwanamke huyo. Wakati huo

huo, alijilaumu tena kwa kutomtafuta

mapema.

Alvin alimpeleka Lisa katika hospitali ya Mawenzi. Alvin alikosa utulivu wakati

akisubiri nje ya chumba cha dharura. Karibu nusu saa baadaye, daktari

alitoka kwenye chumba cha dharura na kusema, "Ikiwa mngechelewa kufika

hapa kwa saa moja baadaye, tusingeweza kumwokoa.”

“Amezinduka?” Alvin alipumua kwa huzuni. Hatimaye uzito ulikuwa umeondolewa moyoni mwake.

"Ndio, lakini mwili wake umedhoofika

sana. Pia, ana homa ya nimonia.” Akiwa amemkazia uso Alvin, daktari aliongeza, “Hajapata maji ya kunywa kwa angalau

siku tatu, na pengine hakula chakula

cha kutosha pia ama chakula alichokula kilikuwa hakifai. Inawezekana

itamchukua nusu mwezi hivi kupona.”

Sio tu kwamba Alvin alishtuka, bali pia

Hans alipigwa na butwaa. "Je, akina Masawe wana chembe ya ubinadamu kweli?" Uso wa Alvin ukaanguka. "Itume habari yote kwenye mitandao, eleza kila kitu kilichotokea leo ili ulimwengu ujue rangi halisi za familia ya Jones Masawe."

“Sawa.” Hans akakubali.

Baada ya Lisa kupata huduma ya kwanza, kesho yake safari yakurejea Dar ikaanza. Lisa aliota ndoto ambapo

alikuwa karibu kufa. Hata hivyo, alipokea kumbatio la uchangamfu

kutoka kwa mtu aliyesitasita kumwacha aende zake. Ikaja akilini mwake

kwamba alikuwa kweli ... bado yuko hai!

Hili ndilo wazo lililompata Lisa mara ya kwanza alipofumbua macho yake.

Wakati huo, mwili wake ulikuwa

umefunikwa na blanketi ya joto. Kulikuwa na taa ndogo inayowasha

wodini, na kiyoyozi kilikuwa kimewashwa. Hakuwa katika nyumba ya zamani ya giza. Hii ilikuwa ni baada ya kufika Dar es Salaam ambapo Alvin alimpeleka kwenye hospital binafsi ya Premier Care clinic, Masaki.

"Lisa , hatimaye umeamka, mwanamke aliyelaaniwa!" Pamela alimrukia kwa macho mekundu na kusema kwa sauti ya kilio, "Unaendelea kulazwa hospitali baada ya hospitali, na kila wakati hali ni mbaya zaidi kuliko hapo awali. Umenitisha sana.”

“Ni wewe uliyeniokoa?” Lisa aliuliza kwa mshangao. Alikumbuka tu kwamba

alihisi kizunguzungu na alionekana

kuwaka. Tumbo pia lilikuwa likimuuma

sana. Kwa kweli alifikiri kwamba

angekufa kwa vile aliteswa sana na

njaa, baridi na kiu.

“Hapana, ni Alvin ndiye aliyekuokoa.”

Pamela alimwambia. “Nilikuwa

nimeenda nyumbani kwenu kukutafuta, lakini haukuwepo. Nilisikia ulipelekwa

Moshi na kufungiwa kwenye jumba lenu la ukoo. Mara moja niliwasiliana na

Alvin, na akaenda kukuokoa usiku huo.

Hapo awali, ulikuwa katika hospitali ya

Mawenzi kwa matibabu. Umekuwa

katika hali nzuri tangu jana, kwa hivyo

Alvin alikuhamisha hadi Hospitali hii.

Hajalala vizuri kaka wa watu kwa siku

chache zilizopita kwani alikuwa

akikutunza kila wakati. Nimemuomba

aende nyumbani akapumzike.”

"Ni yeye …?" Lisa alinong'ona kwa kutokuamini, macho yake yakiwa mekundu.

Kinyume na matarajio yake, alikuwa

amemwokoa kutoka kwenye matatizo

tena na tena. Kwa kweli, hakuwa

amemfanyia kitu kingine chochote kando na kumpikia yeye na Charlie mara chache. Alikuwa na deni kubwa kwake.

"Hapo zamani, ulidai kwamba yeye ni mtu asiyejali. Nadhani yeye ni mzuri sana, pamoja na kasoro zake ndogondogo." Pamela aliongeza, “Hata aliviambia vyombo vya habari habari

kuhusu wewe kufungwa na kunyanyaswa na familia ya Masawe.

Hisa za Kibo Group zimekuwa zikishuka

tangu jana, na wengi wanawakosoa

baba na mama yako mtandaoni.

Hutapingana na wazo lake, sivyo?

“Sitathubutu!” Kwa kutajwa kwa familia ya Masawe, macho ya Lisa yalionyesha

hisia kubwa ya chuki. “Kwa vile

walipanga kuniua, sitawaacha salama.

Nitalipiza kisasi kwao hivi karibuni au baadaye!

Pamela alipumua. “Usijali, Kibo group imeumizwa sana safari hii. Thamani

yake ya soko imeshuka kwa angalau dola milioni kadhaa.

Lisa alisema bila kujali, "Pamela, nitawafanya wale wote walionidhulumu walipe gharama siku moja."

Pamela alipigwa na butwaa alipohisi

mabadiliko ya mtazamo wa Lisa . “Kwa kweli, unaweza kumwomba Alvin akusaidie. Hufikirii… ameanguka kwa ajili yako?”

SURA YA31

Alvin na Sam walingia hospitalini pale

mida ya jioni. Sam aliweka kikapu cha matunda kwenye meza ya kahawa, kisha akamsalimia Lisa kwa tabasamu.

"Shemeji, unajisikia vizuri?"

"Vizuri zaidi." Lisa kwa siri alitazama

pembeni kwa Alvin aliyekuwa kasimama kimya. Lisa alipepesa macho yake kwa

utii. "Samahani kwa kukuletea shida tena." “Ni vyema kama umelitambua hilo.

Nilidhani wewe ni mjinga tu.” Alvin alikasirika bila sababu kumuona

Lisa akiwa amekonda mithili ya mfuko wa mifupa. Maneno makali yakamtoka

kinywani mwake. “Sijapata amani hata siku moja tangu nikuoe. Sitaki kuhojiwa

na polisi ukiwa umekufa siku moja.

Unaelewa?" "Haitatokea tena wakati ujao." Lisa

aliuma mdomo wake uliopauka kuzuia

machozi yasiendelee kuchuruzika

mashavuni mwake.

Upepo wa kufadhaika ulimpitia. Alvin

hakutaka kuendelea kumfundisha, lakini

alihitaji aache kufanya makosa ya

kipumbavu namna hii. “Simu

niliyokununulia iko wapi? Kwa nini

iliachwa nyumbani kwa akina Masawe?”

"Mama yangu alinidpokonya na kuikatalia."

"Kweli wewe ni nguruwe." Alvin alifoka.

“Uko sahihi. Tafadhali niite Nguruwe Masawe kuanzia sasa.”

Mapovu ya kicheko kilichoshindwa

kuzuilika yalitoka kwenye midomo ya Sam, na kulainisha hali ya wasiwasi katika wodi ya hospitali. “Sawa, Alvin, acha kumponda. Hakuna mtu ambaye

angetarajia ukatili kama huo kutoka kwa wazazi wake waliomzaa.”

Lisa alitetemeka. Baada ya kuona

hivyo, Alvin aligeuza macho yake kwa

Lisa na kumuonya. "Kaa mbali na familia hiyo ikiwa unataka kubaki hai."

"Hiyo ni sawa." Sam aliitikia kwa kichwa. “Zingatia tu kumwandalia rafiki yangu chakula. Tazama jinsi amekuwa na hasira baada ya kutoweza kufurahia milo yako iliyopikwa nyumbani katika siku chache zilizopita.”

“Sam Harrison.” Alvin akatupa jicho la hatari upande wake.

Sam aliacha kusema mara moja. Lisa hakuweza kupinga tabasamu usoni mwake. “Nitapona hivi karibuni na nianze kukupikia tena.”

"Kaa kimya na uzingatie kupona." Sauti ya Alvin ilikuwa ya ukali kama kawaida, lakini maneno yake yalileta uchangamfu moyoni mwake.

“Alvin, asante, kweli.” Lisa alishukuru kwa dhati.

•••

Siku mbili baadaye, Ethan akiwa

kwenye ofisi za kampuni yao, ‘Lowe Enterprises’, alikutana na habari ya Lisa

mtandaoni iliyosambazwa pamoja na cheti cha matibabu kilichotolewa na Dk Johnson. Ethan alishtushwa sana. Mara moja, aliingia kwenye gari na kukimbilia

kwenye makazi ya akina Masawe.

Alipofika, aliwahoji wanandoa hao wazee huku akijaribu sana kuzuia

hasira yake. “Mjomba Jones na Shangazi Masawe, ni kweli mlimfungia

Lisa kwenye makazi ya zamani

ambapo mlikataa kumpa maji na kumlisha chakula kibovu?”

“Upuuzi gani huu Ethan. Ulikua na sisi muda wote. Unafikiri tunaweza kufanya

hivyo?" Johes Masawe alikasirika na kufadhaika kwa wakati mmoja. “Kwa

kweli, nilimweka kwenye makazi ya

zamani lakini alitunzwa vizuri na

watumishi kwa chakula kitamu kila siku.

Yeye ni binti yangu wa kuzaliwa, hata hivyo. Ningewezaje kuwa mkatili hivyo?”

"Lakini inaenea mtandaoni kwamba ..."

Lina alimkatisha kwa huzuni, "Zote ni habari za uwongo. Sielewi kwa nini

Lisa angeidharau familia yake kama hivi baada ya kuondoka kwenye makazi ya zamani na marafiki zake. Mama na Baba wana wasiwasi sana juu yake.

Walimweka tu katika makao ya zamani ili asichangamane na watu wabaya na kuharibu sifa yake huko mitaani tena.”

Hilo lilimshangaza Ethan. Maneno magumu yalienea usoni mwake baada ya kukumbuka uvumi aliosikia muda si mrefu uliopita. Sasa, alielewa uamuzi wa familia ya Masawe. “Samahani, sikuwaelewa nyote.”

Mama Masawe aliweka mkono juu ya kifua chake kwa huzuni. "Sijali maoni ya

watu juu yetu mtandaoni kwani

tumeshindwa kama wazazi. Lakini Kibo Group ambayo tumetumia muda mwingi na juhudi kuijenga iliharibiwa mara moja. Hisa za kampuni ziko chini kabisa kwa siku kadhaa zilizopita na thamani yake ya soko ilipungua kwa zaidi ya dola milioni. Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba kila mtu mtandaoni anaisusia

Kibo Group sasa. Mambo yatakuwa mabaya sana ikiwa hii itaendelea."

Ethan alikatishwa tamaa na

alichokisikia. Kufaulu au kutofaulu kwa kampuni ya Kibo Group kulimuathiri sana yeye mwenyewe. "Tunahitaji

kudhibitisha kwa umma kuwa familia ya

Masawe iko kwenye uhusiano mzuri na

Lisa. Kisha, tunaweza kuajiri kundi la

watu kutangaza hili mtandaoni ili kufuta uvumi huo.”

“Ni wazo zuri.” Johes alikubali kwa

kichwa. "Tarehe ya sherehe yako ya

uchumba inakaribia. Vyombo vya habari

pia vitakuwepo. Tunahitaji tu Lisa kujitokeza ili kubadilisha taswira ya kampuni.”

“Atajitokeza kweli?” Lina alimtazama Ethan kwa wasiwasi. “Ujue bado anakupenda. Sidhani kama anaweza akaja."

“Nitafikiria jambo fulani la kumshawishi

Lisa ahudhurie.” John Masawe alisema. •••

Lisa alilazwa hospitalini kwa siku tatu kabla ya kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Aliporudi nyumbani alishangaa kuona

kwamba Charlie alikuwa ameongezeka unene. Alifikiri kwamba paka huyo

angekuwa dhaifu kwa kukosa mtu wa

kumtunza ipasavyo siku chache

zilizopita.

Alvin alipofika nyumbani baadaye usiku

huo, alimsikia Lisa akinung'unika wakati

akimlisha paka. “Charlie, inabidi uache

kula sana. Angalia ukubwa wa tumbo lako. Ni kana kwamba una mimba ya

kujifungua!”

Tumbo la mimba la Charlie lilikuwa likiongezeka kadiri siku zilivyopita. Alvin

asingeweza kuweka siri hiyo kwa muda mrefu zaidi. Hata hivyo, bado ilikuwa

bora kuwa na mtu wa kumhudumia nyumbani. Alvin alitokea tena akiwa

amevaa nguo za kawaida za mapumziko. Lisa alikuwa tayari

ameshaandaa meza ya chakula.

Lisa alimwandalia Alvin meza ya

shukrani iliyojumuisha aina zake zote za vyakula anavyopenda. Macho ya

Alvin yaliwaka kwa furaha baada ya

kuvitazama vyakula

vilivyotapakaa mezani. “Nimechoshwa na kula vyakula vilivyochomwa na kukaangwa. Tengeneza hata supu au

kitoweo wakati mwingine,” Alvin

alijivungisha kama kawaida yake huku

akivishambulia.

Baada ya chakula cha jioni, Alvin alirudi

kwenye chumba cha maktaba

kuendelea na kazi. Alvin aliendelea na kazi hadi karibu saa sita usiku.

Lisa alitayarisha kahawa na kumpelekea. Alvin alikuwa ameketi

kwenye dawati, akichanganua hati zilizo

chini ya mwanga mkali huku akirejelea

kompyuta ya mkononi kwa wakati

mmoja. Jozi ya miwani yenye fremu za

dhahabu ilikaa kimya kwenye daraja la pua yake.

"Utaendelea kutazama hadi lini?" Lisa

alimuuliza Alvin wakati akimkaribisha

kikombe cha uji wa ulezi.

Alvin akafunga laptop yake na kugeuka

kumwangalia kwa utulivu kisha

akapokea kikombe cha kahawa.

“Sijawahi kukuona umevaa miwani hapo

awali. Nilikaribia kuzimia kwa sababu ya haiba yako ya kuvutia,”Lisa alisema huku akitabasamu.

“Bado hujaacha maneno yako?”

Lisa akaguna. Hatimaye, muda mfupi baadaye, alizungumza tena, “Mwonekano wako mzuri hunivutia kwa njia tofauti kila siku. Kadiri

ninavyokutazama, ndivyo ninavyozidi kuvutiwa nawe. Haichoshi…”

Kabla Lisa hajamaliza sentensi yake, ghafla mkono mkubwa ulionekana kumziba mdomo. Mkono wa Alvin ulinuka kama msonobari mkavu. Harufu hafifu ilimtuliza kwa kushangaza.

Muhimu zaidi, mkono wake ulikuwa na

joto sana!

"Nyamaza." Macho ya Alvin yalipepesa chini ya lenzi za miwani yake.

Alihisi mashavu yake yakiungua pia.

Baada ya kuondoa mkono wake,

aliweka kikombe cha kahawa kwenye meza. "Ninahisi lazima uwe umechoka

kufanya kazi usiku kucha. Kikombe cha kahawa kitakuchangamsha kidogo."

Alvin aliitazama ile kahawa iliyochanganywa kwenye mazima.

Hakika ilionekana kumvutia.

"Lisa , unajaribu kunifanya nishindwe kulala, hujui kahawa kufukuza usingizi?"

"Hapana, kahawa haifukuzi usingizi."

Alimshawishi. “Itakuchangamsha tu na kukufanya ujisikie na nguvu mpya kimwili na kiakili."

Alvin aimtazama huku pembe za mdomo wake zikicheza kwa dharau.

"Sawa. nitakunywa. Ila nikikosa usingizi ujue tutakesha wote hapa.”

“Usijali. Hata ukisema tulale pamoja

hadi asubuhi, nitafanya.” aliahidi.

“Sithubutu kutegemea hilo. Ninaweza

kufa kabla hata halijatokea.” Alvin alijibu

huku akijinywea kahawa yake.

Lisa ambaye alikuwa ametoka tu kudhihakiwa, alitoka nje ya maktaba

akiwa ameudhika. Aliapa kumthibitishia kuwa ipo siku angemtaka tu!.

SURA YA32

Saa saba usiku Lisa alishtushwa na

ndoto zake mbaya, ndipo akagundua

kuwa alikuwa anatokwa na jasho

kwenye paji la uso wake. Mara moja

akawasha taa. Utulivu ulikuja juu ya

mwili wake taratibu huku mwanga

ukitawala giza.

Alikuwa ameota juu ya kufungiwa ndani ya nyumba ile yenye giza tena. Sehemu

hiyo ilijaa kila aina ya kelele za kutisha

usiku. Kwa hofu, alijikunja ndani ya shuka. Ilikuwa ni shida kwake kulala peke yake sasa. Baada ya muda wa kufikiria, alijifunika blanketi na kubisha hodi kwenye mlango wa chumba cha kulala cha Alvin.

“Nani huko?” Alvin, ambaye alikuwa amekereka kwa kuamshwa usiku wa

manane, aliuliza kwa sauti iliyojaa hasira. “Ni mimi.” Lisa aliitikia kwa hofu. Nusu

dakika ikapita kimya kabisa. Alipotaka kukata tamaa, mlango ulifunguliwa

ghafla kutoka ndani. Alvin akatokea upande wa pili wa mlango. Nywele zake

zilikuwa zimevurugika na macho yake

meusi yalionekana kuogopesha.

"Afadhali uwe na sababu nzuri ya kunisumbua."

“Naogopa kulala peke yangu…” Lisa alitetemeka. Alivin aliinua macho yake taratibu.

Jasho lilikuwa likimvuja Lisa usoni kwa sababu ya hofu. Hata hivyo, alishangazwa na blanketi alilokuwa ameshikilia mikononi mwake.

"Hii ni mbinu yako nyingine ya kunitongoza?" Alvin alikiri moyoni mwake kuwa karibuni uzalendo ungemshinda. Hata hivyo, alikuwa amechoka sana na kazi za kutwa nzima

na bado alihitajika kuamka mapema

kwa ajili ya kesi mahakamani kesho

yake. “Ni usiku sana. Nahitaji kulala

hata kama wewe huna haja ya kulala.”

"Sio hivyo." Lisa hakutaka kubaki peke

yake chumbani kwake. Aliongeza nguvu

na kuvuta kona ya mkono wake. “Tangu

nifungiwe kwenye nyumba ya giza kijijini

naogopa kulala peke yangu usiku.

Ninasumbuliwa na jinamizi la kutisha. Tafadhali niruhusu nilale japo kwenye

sakafu ya chumba chako. Niko serious.”

“Si ulikuwa umelala vizuri hospitalini?”

"Nilikuwa na mlezi wakati huo." Lisa alijitetea huku akitetemeka.

Ni Alvin ambaye alikuwa amemuokoa

kutoka kwenye nyumba hiyo ya zamani. Mahali hapo palikuwa kimya sana na giza muda wote kama usiku. Hata

mwanaume angepatwa na kiwewe

baada ya kufungiwa mle ndani kwa siku tatu. Lisa aliona kusita kwake kama kukubali, na akatoa ahadi haraka. "Naapa sitakusumbua."

“Kumbuka ahadi yako.” Alvin alirudi

kitandani kwake bila wasiwasi.

Baada ya kupata kibali chake, Lisa haraka akaweka blanketi kwenye

sakafu karibu na kitanda chake. Alvin alikaa makini kwa muda mfupi lakini

punde akapitiwa na usingizi. Hata hivyo muda fulani baadaye, kilio cha Lisa kilimwamsha tena.

“Fungua mlango… Tafadhali… ni baridi… giza sana… ninaogopa.”

Alvin akajiinua kutoka kitandani.

Mwangaza wa mbalamwezi

uliomiminika kupitia dirishani ulimulika

kivuli chini. Lisa aliyekuwa amejikunja

ndani ya blanketi alikuwa ameziba

masikio yake kwa nguvu. Mwili wake

wote ulikuwa ukitetemeka kwa hofu.

“Lisa amka. Ni ndoto tu.” Alvin alitoka

kitandani ili kumvuta mikono. Lakini, Lisa alikuwa kazama kabisa katika

ndoto hiyo mbaya. Uso wake wa hofu

ulikuwa umepauka kama kauzu. Akiwa

hana njia nyingine, akamvutia kifuani

kwake na kumpigapiga mgongoni

taratibu. "Ni sawa. Uko salama sasa…” Sauti ya Alvin ilikuwa na athari ya kutuliza

ambayo polepole ililegeza mkazo

mwilini mwake.

Uso wake mdogo ulisukumwa kifuani

mwake. Nywele zake za giza

zinazong'aa zilikuwa zimening'inia

mabegani mwake huku nyuzi kadhaa

zikiwa zimepigwa plasta kwenye ukingo

wa uso wake wa kusikitisha lakini mzuri.

Pia alitoa harufu hafifu ya kutuliza. Hii

haikuwa harufu ya manukato, badala yake, ilikuwa harufu ya shampoo yake.

Hakuwahi kutambua jinsi shampoo yake

ilinukia vizuri hadi wakati huu. Harufu

hiyo ilimfunika taratibu hadi akafumba

macho hatimaye. Aliwaza kumwachia

mara baada ya kutulia kabisa. Hata

hivyo, ilikuwa tayari asubuhi iliyofuata

alipofungua tena macho yake.

Wawili hao walijikuta wakitumia kitanda kimoja, shuka moja na mto mmoja.

Mkono wake wa kushoto na mguu wa kushoto ulikuwa umewekwa juu ya mwili

mwake. Kulikuwa na tabasamu la

kudumu kwenye pembe za midomo

yake. Ilionekana alikuwa na usingizi mzuri. Alvin pia hakujisikia raha. Alihisi hata

kwa sekunde ya haraka kwamba

walikuwa kama wanandoa wapya. Alvin

aliwaza bila kufikiria kwa sekunde

chache kabla ya kunyanyua blanketi

kwa uangalifu ili asimame. Bila

kutarajia, mtazamo chini ya blanketi

ulimshangaza. Karibu vifungo vyote vya

pajama za Lisa vilitenguliwa. Wakati

huo Lisa naye alifungua macho yake

polepole. Macho yao yalikutana na

mboni zake zlipanuka polepole.

Alipiga kelele kwa mshtuko sekunde tu alipogundua kuwa alikuwa amelala

mikononi mwa Alvin. Lisa alinyanyuka kwa haraka na kujiweka mbali na mwanaume huyo. "Kwa nini ... kwa nini umenileta kitandani kwako?"

Alvin alidhihaki kwa kutoamini.

“Ulinizunguka huku ukilia wakati ukiota ndoto mbaya jana usiku. Nilikuwa nikikufariji na kukutuliza…”

“Umenifariji?” Aliona jambo hili kuwa gumu kuamini. Uso wa Alvin ukajaa hasira. “Unajaribu kusema nini? Lisa, sema kweli sasa

hivi. Je, jana usiku kilikuwa ni kitendo cha makusudi? Ulikuja chumbani

kwangu ili kunitega, huh?"

“Sijui unazungumza nini. Nililala vizuri sana.” Alikumbuka bila kufafanua kuwa

alipata ndoto mbaya mwanzoni, lakini

alihisi amani wakati sauti ya upole ilinong'ona masikioni mwake. Subiri, sauti hiyo ya upole ilikuwa ya Alvin?

Alvin alimtazama kwa macho makali wakati anainuka na kusimama. "Kabla hujaendelea kuongea, angalia hali ya nguo zako za kulalia."

Akiwa amechanganyikiwa, Lisa

alishusha macho yake. Sura ya mshtuko na aibu ilimwangazia usoni mwake alipojiona alivyokuwa kifuani.

Mikono yake iliruka kukifunika kifua

chake mara moja.

Alvin akafoka. “Uigizaji mzuri. Nina hakika ulifungua vifungo hivyo kwa siri ili kunitega.”

“Sina haja ya kufanya hivyo.” Lisa

alijisikia kulia wakati huu. “Vifungo

vilifunguka vyenyewe. Si kosa langu

kuwa na matiti makubwa.”

"Kwa hivyo kama una matiti makubwa ndiyo uyaache waziwazi? Sema tu

ukweli kuwa unajaribu kunitega." Alvin

alisema huku akimtazama Lisa kwa

dharau. “Ndiyo! Um… Ninaweza kueleza hili. Ni kwa sababu mimi…nakupenda kupita

kiasi,” Lisa alisema kwa sauti iliyotiwa chumvi. Akiwa amechanganyikiwa, alisonga mbele na kuishika shingo ya Alvin. Kwa kweli, Alvin alishtushwa na kitendo chake cha ghafla na ambacho hakuwa amekitarajia.

‘Je, mwanamke huyu alikuwa akijaribu

kumlazimisha busu?’ Alvin alijiuliza

huku picha ya midomo yake nyororo

ikaingia akilini mwake. Alisita kwa

sekunde kadhaa kabla ya kusikia

maumivu makali mashavuni mwake.

Lisa alikuwa amempiga Lovebite!. Alvin alimsukuma Lisa kwa nguvu huku

mkono wake ukiruka kufunika sehemu aliyong’atwa.

“Lisa, unathubutu vipi? Usifikiri sitakuadhibu kwa hili.” Macho ya Alvin yalikuwa kama miali ya moto.

Lisa akacheka tu kwa mzaha huo na kumwambia. “Kwani hujawahi kuiona kwenye sinema za kihindi? Waigizaji wakuu huwa wanamng’ata mtu wanayempenda sana. Nilikuwa najaribu tu kuacha alama kwako.”

Alvin akapiga hatua kadhaa mbele, huku akiwa ameuma meno kwa hasira.

"Unanichukulia kama mjinga sivyo?"

"Sawa, unaweza kuning’ata na wewe kulipiza kisasi." Lisa alijikaza na kuinamisha uso wake karibu na Alvin.

"Ning’ate kwa nguvu kadri uwezavyo.

Ukining’ata kwa nguvu zaidi nitajua unanipenda zaidi.”

Bila hata kujiuliza, Alvin alikiweka

kichwa cha Lisa katikati ya viganja vyake na kumng'ata kwa nguvu kwenye shavu. Shavu nene la Lisa lilikuwa nyororo na laini kama jeli. Hakutaka kusogeza midomo yake mbali.

“Loo!” Lisa alipiga kelele kwa uchungu.

Hatimaye, Alvin baada ya kuona meno yakiwa yameganda kwenye mashavu yake yaliyonenepa, alimwachia.

"Kumbuka adhabu hii."

Lisa alijifanya mwenye haya licha ya maumivu. "Hapana, hii siyo adhabu, huu ni uthibitisho wa upendo wako."

"Endelea kuota." Alvin alicheka kwa

kejeli kabla ya kuingia bafuni na

kufunga mlango kwa nguvu. Taswira

kwenye kioo ilionyesha alama za meno kwenye shavu lake mwenyewe. Alihisi

kukimbilia mlangoni ili kumchana mwanamke huyo vipande vipande.

Ilimbidi awe mahakamani siku hiyo kwa

hiyo ilimbidi aende akiwa amevalia barakoa. Akiwa amekasirika, Alvin

alipata tu kifungua kinywa kidogo kabla ya kuondoka nyumbani.

Saa tatu asubuhi Alvin aliwasili ofisini

kwao. Sam alimpokea kwa swali, “kwa nini umevaa barakoa? Unaumwa?"

Alvin alikataa kujibu. "Eh, ni vizuri kuwa unajali na kuvaa barakoa ili kuzuia

kueneza korona. ” Sam alimpongeza

baada ya kumuona yupo kimya.

Baada ya kukamilisha taratibu kadhaa

za kiofisi, walielekea katika mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusimamia kesi.

Dakika kumi baada ya kuwasili kwao,

kesi ilikuwa karibu kuanza. Sam nusura

aangue kicheko hadharani wakati Alvin alipotoa barakoa yake na kufichua

alama za meno kwenye shavu lake.

"Ni nini …?"

"Nimeng’atwa na mbwa." Sauti kali ya Alvin ilisikika kwa vitisho. Aliingia ndani ya chumba cha mahakama kwa hatua kubwa.

Sam hakuweza kujizuia tena kuangua

kicheko. Alvin alifikiri angeweza kumpumbaza? Mwanamume huyo

alikuwa ameng’atwa na mwanamke.

Hakuwahi kumuona Alvin akiona aibu

vile. Kwa hiyo alimpiga picha kwa siri na kuituma kwenye group lao la whatsapp.

SURA YA 33

Lisa alipumzika nyumbani kwa siku

kadhaa, akisubiri alama za meno

shavuni kwake kutoweka kabla ya kwenda kutafuta kazi mpya. Lakini, kila alikotuma maombi ya kazi, alipokea maoni hasi tu.

"Bi Jones, samahani lakini hatuajiri waizi wa kazi za wangine."

"Bi Jones, kashfa yako imekuwa habari ya kawaida katika sekta ya ujenzi.

Hakuna mtu anayethubutu kukuajiri tena.”

"Bi Jones, familia ya Jones Masawe imetangaza kwenye mtandao wa sekta nzima kwa siri kwamba mtu yeyote ambaye atathubutu kukuajiri atakuwa anawadharau waziwazi."

Lisa alikutana na majibu kama hayo

kwenye mahojiano ya kazi na makampuni kadhaa aliyotuma maombi.

Alikatishwa tamaa kabisa na kupandwa

hasira kwani alikuwa ametumia muda

mwingi na bidii katika elimu yake lakini

bado hakuweza kupata kazi.

“Pipiii…” Mara akagutushwa na sauti ya honi. Gari lililokuwa karibu naye lilipiga

honi mara kadhaa. Hakutambua kama mtu huyo alimkusudia yeye hadi alipomwita jina lake. "Lisa !"

Lisa alitazama kwenye gari hilo na kuona uso mzuri ukichungulia nyuma ya dirisha la Range Rover. “Joseph? Unafanya nini hapa?" Lisa alipatwa na mshangao wa furaha baada kumuona mwandamizi wake kutoka Chuo Kikuu

cha New South Wales alikokuwa ameenda kusoma.

“Nina ofisi katika jengo hili. Nilikuona ukitoka nje nikashangaa unafanya nini hapa." Joseph aliegesha gari lake

pembeni na kumpa ishara aingie ndani.

Lisa alipoingia ndani ya gari alijibu kwa

kinyonge, “Nimekuja kwa mahojiano ya kazi, lakini sijafanikiwa.”

“Hata wewe hukuweza kufanikiwa na sifa zako?” Joseph aliona jambo hilo

kuwa gumu kuamini.

“Nimekosana na familia yangu na wananichafua kwenye mtandao mzima wa sekta ya ujenzi. Sifa yangu yote

inazidi kuporomoka!” Lisa alimwambia

Joseph kwa huzuni na kumweleza kila kitu kwa undani wake.

“Siamini kwamba unaweza kuiba kazi

za wengine. Inapaswa kuwa kinyume chake." Tabasamu likatanda usoni mwa

Joseph. "Sawa, nimeanzisha kampuni mpya hapa Dar es Salaam na bado sina

wafanyikazi wa kutosha. Njoo ujiunge na timu yangu."

Lisa alishtuka na kuguswa wakati huo

huo. “Huna shaka nami hata kidogo?”

"Najua wewe ni mtu mzuri wa tabia na ninafahamu vyema vipaji vyako.

Nilikuwa nimekupendekezea hapo awali kwamba tuanzishe biashara pamoja

huko Uganda baada ya kuhitimu, lakini ulisisitiza kusaidia biashara ya familia na kukaa karibu na mpenzi wako. Vipi umeolewa sasa hivi?" Joseph aliuliza.

Lisa akainamisha kichwa kwa aibu na kujibu. "Tuliachana."

Joseph alionekana kushangaa lakini haraka akamfariji kwa upole. "Ni sawa.

Bado wewe ni kijana na mrembo. Nina hakika unaweza kupata mtu bora zaidi.”

"Inatosha kuzungumza juu yangu.” Lisa akahamisha mada. “Unafanya vizuri

sana kwenye kazi. Nilisikia umekuwa

mbunifu watatu bora zaidi huko Uganda

na hata kuchapisha vitabu kadhaa.” Lisa alitania huku

akitabasamu. "Na sasa unajaribu

kushindana hapa Bongo pia?"

"Jiunge na kampuni yangu ikiwa unadhani nina uwezo. Ninahitaji watu

wenye talanta kama wewe,” Joseph alimshawishi kwa bidii, “naweza kukupa mshahara mkubwa. Unaweza pia kuwa mwanahisa biashara itakapoingia sokoni.”

"Sawa, nitakuandalia chakula cha jioni leo ili kusherehekea kuwa bosi wangu."

Lisa hakika hakutarajia mshangao huu wa kupendeza. Alimpigia simu Alvin na kumwambia. “Sitakuwa nyumbani kuandaa chakula cha jioni. Panga mwenyewe."

Alvin alikasirika sana siku hiyo kwa

sababu wengine walikuwa wakimdhihaki

kwa siri kutokana na alama za meno

kwenye shavu lake. “Nini tena muda

huu? Usifanye ujinga wako ukidhani

nitakuokoa tena. Sina muda.” Alvin

alimjibu kwa hasira.

Lisa alimwambia kwa upole. "Ninaenda tu kula chakula cha jioni na rafiki yangu

niliyekutana naye nikiwa nasoma nje ya nchi."

Alvin alicheka kwa kejeli. "Loo, kwa hivyo ni rafiki kutoka chuo kikuu wakati huu. Usisahau jinsi ulivyotekwa hotelini na rafiki yako wa shule ya sekondari mara ya mwisho.”

"Nilikuwa nakupa taarifa tu. Kwaheri.”

Lisa alikata simu kwa papara.

Hali ya kukatishwa tamaa iliangaza machoni pa Joseph alipouona uso wake wenye hasira. “Mpenzi mpya? Au mume?”

Alitoa macho kwa mshtuko. "Hapana. Ni

mwenzangu tu… Housemate.” Lisa

hakuwa amekosea hata hivyo kwa

kujibu vile. Ingawa Alvin alikuwa mume wake halali wa ndoa, mwanamume

huyo alikataa kukiri hilo. Kwa hivyo, uhusiano wao ulikuwa wa maonyesho tu. Joseph alitoa tabasamu hafifu.

"Ilionekana kama unazungumza na mpenzi wako."

“Um… Kweli?” Lisa alihisi mapigo ya moyo yakirukaruka. Hivi ndivyo

alivyokuwa akitangamana na Alvin. Labda ilisikika tu kwa sababu walikuwa

wakiishi katika nyumba moja.

Ilikuwa ni muda mrefu sana tangu

alipokutana na Joseph huko Marekani.

Wawili hao walifurahia jioni pamoja na

chakula cha jioni kilidumu hadi saa tatu

usiku. Alimpa lifti na kumpeleka hadi

nyumbani kwani siku hiyo Lisa hakuwa

anatumia gari lake.

“Kumbuka kuripoti kwangu kesho asubuhi. Nimechukua mradi wa jengo la kifahari katika eneo la Mbezi Beach.

Utaenda kuchukua vipimo kesho."

“Hakika.” Lisa alimpungia mkono wa kwaheri. Macho yake yaliikodolea gari hiyo aina ya Range Rover kwa mbali

kabla hajageuka kuelekea nyumbani.

Kwa bahati mbaya, alimgundua Alvin, akiwa amevaa nguo za kawaida za

mapumziko akimtazama chini kwa

hasira kutoka kwenye ngazi. Charlie

alikuwa ametulia mikononi mwake, akionekana kama alikuwa karibu kulala.

“Rafiki yako ni mwanaume?” Alvin

aliuliza kwa hasira, ndita zilizokuwa

zimekunjwa katikati ya macho yake

zingeweza kumfinya inzi hadi kufa.

Alipofikiria jinsi ambavyo alilazimika

kuvumilia chakula kilichotengenezwa

mgahawani vibaya wakati Lisa alifurahia

jioni hiyo kula na kucheka na mwanaume mwingine, hasira ilimpanda kama mawimbi ya bahari.

“Ndiyo, yeye ni mwandamizi wangu kutoka chuo kikuu…”

Alvin alimkatisha. “Lisa, ngoja nikukumbushe kuwa umeamua kuolewa na mimi. Afadhali uangalie matendo yako hata kama tuko kwenye ndoa ya mkataba. Sitaki kusalitiwa.”

Tabasamu usoni mwa Lisa likaganda.

“Unasemaje? Nilitoka tu kwenda kula

chakula cha jioni na rafiki. Je, unanifikiria miye ni mhuni sana?”

"Nani anajua? Nimekufahamu kwa muda mfupi tu.” Alvin aliongea kwa

tabasamu la kejeli. "Mbali na hilo, huwezi kwenda tu kwa chakula cha jioni na kusahau kuhusu jukumu lako kama

mhudumu wa Charlie. Unawajibika kwa

ajili yake kwani wewe ndiwe uliyemsababishia ugonjwa.”

“Charlie yuko sawa sasa. Nadhani hata

aliongezeka kilo chache,” Lisa alijibu kwa upole. Bila shaka angebishana naye ikiwa asingekuwa kaokoa maisha yake mara mbili.

Alvin alicheka. “Sawa, kwa nini

ameongezeka uzito? Unapaswa kujitafakari. Nataka umtunze paka, sio kumnenepesha.”

Lisa alishindwa cha kusema.

Kuongezeka kwa hamu ya kula kwa

Charlie lilikuwa kosa lake pia.

Alikaribia kushindwa kuzuia hasira

iliyokuwa ikifuruma kifuani mwake.

"Sawa, nitampa paka chakula kidogo

kuanzia sasa."

"Hilo halitasaidi pia." Alvin bado

alimkalia vibaya. “Je, ikiwa paka ndani yake atakuwa na utapiamlo?”

“Sawa, unataka nini basi? Samahani, lakini mimi si mfugaji wa paka kitaaluma.” hatimaye Lisa alisema kwa hasira.

“Hata mimi sijui.” Alvin naye akajibu kwa ukali. “ Ifanyie utafiti na umfikirie zaidi

Charlie. Mpeleke matembezini ukiwa huru. Usimpe chakula tu kisha umruhusu alale siku nzima.” Kisha

kusema hayo, Alvin alitembea kuelekea

kwenye bustani ya jirani na Charlie mikononi mwake.

Lisa aliishia kumshangaa tu mwanamume yule mwenye gubu.

Alitaka kushiriki naye furaha ya kupata

kazi mpya, lakini hakuweza kujisumbua

kuzungumza naye kwa sekunde

nyingine zaidi. Alipokuwa akiingia ndani

kuelekea chumbani kubadilisha nguo, sauti kali ilisikika nyuma ya mgongo wake. "Nina njaa."

Alitazama nje na kumwona mtu

aliyeketi kwenye bustani, akionekana kama mnyama mwenye njaa kali anayesubiri kulishwa.

Lisa alikataa, kwani bado alikuwa amekasirika kutokana na kejeli zake hapo awali. "Samahani, mimi ni mhudumu wa paka wako, sio mhudumu wako." Alisisitiza maneno matatu ya mwisho. Alvin alionekana kutopenda. Alichia tabasamu la kejeli na kuongea kwa sauti ya kutetema. "Huu ndio upendo unaotangaza kuwa wewe ni mke wangu?"

'Ninachotaka ni nafasi ya kuwa

shangazi wa Ethan! Umeipata hiyo!'

Lisa alijiwazia, lakini hakuthubutu

kuyasema maneno hayo kwa sauti.

Akiwa amekasirika kidogo, aliingia jikoni na kuanza kuandaa chakula.

Alvin alikuwa akisubiri chakula kwa hamu akiwa anazunguka bustanini na paka wake. Hakuna chochote zaidi ya chakula alichotayarisha Lisa kilichomtia hamu tena. Labda alikuwa amemtilia

dawa kwenye chakula alichokuwa anakula muda wote huo.

Baada ya kifungua kinywa asubuhi

iliyofuata Alvin alikuwa amevaa kiofisi

tayari kuelekea kazini alipogundua Lisa

naye alikuwa amebadilika na kuvaa

kimtoko-mtoko hivi. Lisa alikuwa

amevaa shati la waridi iliyokolea na

suruali ya jeans iliyombana kidogo.

Alionekana kama mfanyabiashara

hodari, lakini mavazi hayo pia

••••••

yaliangazia umbo lake mwanana.

Isitoshe, alikuwa amejipodoa kidogo na hereni za lulu zilining'inia chini ya masikio yake. Aliona ni vigumu kumvua macho mrembo huyo.

Alvin aligundua kuwa Lisa alikuwa akitoka. “Unatoka kwenye miadi yako tena?” Sauti yake ilikuwa ya chini

ikionyesha kutofurahishwa kwake.

“Hapana, naenda kazini. Nilipata kazi mpya jana. Nitakuwa nyumbani

kuandaa chakula cha jioni na pia kumtembeza Charlie baada ya hapo.”

Alvin hakupata maneno ya kubishana na hilo. Pamoja na hayo, hakuwa na wasiwasi kuhusu kazi yake.

Akamuuliza. "Unagawa vipeperushi tena?"

"Hapana. Mimi ndiye mbunifu mkuu

wakati huu." Alicheka kabla ya

kuchukua mkoba wake na kuondoka

mlangoni. Alvin alimfuata nyuma yake na kutoka naye pamoja. Koo lake lilihisi kukauka

huku akiibia jicho lingine la umbo lililopinda la yule mwanadada. “Unataka lifti?”

“Hapana, asante.” alikataa bila kusita. “Nitaendesha gari.” Alvin hakuwa na la kusema.

Saa mbili na nusu asubuhi Lisa aliingia

katika eneo lake jipya la kazi kwa wakati

ufaao. Ilikuwa ni mshangao kujua

kwamba wafanyakazi wengine wote

walikuwa vijana na wenye shauku.

Mbali na hilo, wote walikuwa wahitimu

tofauti ambao walikuwa wamesoma nje ya nchi.

Joseph alimtambulisha Lisa kwa

wafanyakazi wenzake kabla ya kuingia

naye ofisini. Kisha alitoa ramani. "Hii ni nyumba ya Bw. Kelvin Mushi yenye

ukubwa wa mita za mraba 3,000 katika

eneo maarufu la Mbezi Beach. Huyu mtu aliwahi kuwekeza ng'ambo biashara

zake na ndivyo nilivyokutana naye. Tumefahamiana kwa muda mrefu sasa.”

Joseph alitikisa kichwa kwa umakini. "Anapanga kutulia nyumbani hapa Dar

es Salaam kwa hiyo anataka

kutengeneza jumba hili kwa ajili ya

makazi. Fanya bidii kwenye mradi huu.

Hakuna kikomo cha gharama kwenye

ukarabati, lakini kila kitu lazima kiwe

kamili. Ana mradi mwingine unaosubiri kuzinduliwa mwishoni mwa mwaka.

Natumai kujenga naye ushirikiano wa muda mrefu.”

Tabasamu likatanda tena usoni mwa

Joseph. “Kwa kweli, rafiki wa kike wa

mpwa wa Bw. Mushi anatoka katika

historia ya ubunifu majengo na mambo

ya ndani, lakini Bw. Mushi hakutaka

kutumia kampuni hiyo kwa sababu

hapendi sana ubunifu wao hivyo

anakarabati jumba lake kwa siri bila

kumwambia mtu mwingine yeyote wa familia yao, kwa hivyo na wewe huna

budi kuficha hili. Usifanye mambo kuwa magumu kwa Bw. Mushi.”

Bila kukawia, Lisa alitoka ofisini na

kuendesha gari hadi Mbezi Beach. Hiki ni miongoni mwa viitongoji vya kifahari

zaidi hapa Dar es Salaam. Ni matajiri tu ndio wanaweza kumudu kujenga mali

hapo.

Gari lake lilisimamishwa na mlinzi

kwenye mlango wa geti, hivyo ikabidi

atembee hadi ndani. Mwanamume

aliyeonekana kuwa na umri wa miaka

30 hivi alikuwa amesimama kando ya kidimbwi cha kuogelea. Mtu huyo mrefu

alionekana kuwa na sura ya upole. Suti

nyeusi ya biashara iliyotengenezwa kwa

ufundi ilimpendeza sana.

Kwa mshangao, Lisa aliuliza kwa utulivu, “Bw. Mushi?”

“Ndiyo. Je, wewe ni mbunifu kutoka

kampuni ya Joseph? Wewe ni mdogo kuliko nilivyotarajia." Mshangao wa kweli uliangaza machoni pa Kelvin Mushi.

“Joseph alinitangulia mwaka mmoja

katika chuo kikuu. Bw. Mushi, unakaribishwa kunibadilisha ikiwa

haujaridhika baada ya kuona kazi yangu.” Maelezo ya Lisa yalikuwa

shwari na ya kujiamini. "Mbali na hilo, sidhani umri una uhusiano wowote na uwezo. Wewe mwenyewe ni kijana sana, Bw. Mushi.”

Kelvin alitabasamu. "Siwezi kubishana na hilo."

Lisa alimpatia Kelvin business card

yake. Kelvin akaitazama. "Lisa Jones Masawe. Jina maarufu sana hili."

“Ni jina la kawaida kabisa.” Lisa alihisi

moyo wake ukirukaruka. Kwa kuhofia kwamba huenda amesikia kuhusu

uvumi mbaya unaoenezwa na familia ya Masawe. “Ikiwa haujali, Bw. Mushi, unaweza kuniambia mawazo yako tunapozunguka jumba hili la kifahari.”

Kelvin aliongoza njia na kumuonyesha

kila sehemu ya jumba hilo. Mbali na hilo, alitaja matakwa yake ya kuwa na ukumbi wa mazoezi, ukumbi wa michezo, uwanja wa mpira wa kikapu, na bwawa la kuogelea la ndani.

Lisa alikuwa na wazo la jumla la liliendana na matamanio yake. Katika

chini ya nusu saa, alimpatia mchoro

mzuri mikononi mwake.

Kelvin aliutazama mchoro ule, hakuweza kupata kitu cha kubaini makosa. Mpango huo wa kubuni ndio hasa alikuwa ameufikiria. "Bi jones, wewe ni mzuri kama wabunifu wakubwa ambao nimewaona kutoka nje ya nchi. Sio mbaya. Wazo la bwawa hili la kuogelea la ndani ni la kibunifu kweli.”

"Itaonekana bora zaidi baada ya kuisanifu." Lisa aliongezea.

“Hakika, una muda wa wiki moja.

Ningependa kuanza ukarabati haraka iwezekanavyo.” Kelvi akampa Lisa business card yake. “Unakaribishwa kunitafuta ofisini kwangu michoro itakapokamilika. Hii ni kadi ya jina langu."

Kadi ile ilionyesha Kelvin Mushi alikuwa ni mkurugenzi wa kampuni ya

Usafirishaji, Golden Corporation.

Baada ya kuondoka kwenye jumba lile, Lisa alipanga kuangalia miundo ya majengo mengine ya kifahari katika

kitongoji hicho. Alipotoka tu nje ya geti, aliona Harrier nyeusi ikiingia kwenye

moja ya majengo makubwa ya kifahari. Hilo lilikuwa gari la Alvin.

‘Ina maana amenunua nyumba huku

pia?’ Lisa alijiuliza bila majibu kabla ya kushtuliwa na sauti ya kiume. “Kwa nini uko hapa?” sauti aliyoifahamu vizuri ilisikika nyuma yake ghafla. Ethan

alikuwa kasimamisha gari pembeni kidogo mwa barabara akitazamana naye. Lisa alitazama na kumwona

Ethan akitoka kwenye Lamborghini yake. Wakati huo alikuwa akigeuka ili

kuondoka, lakini alishtuka kidogo

kugongana naye hapo.

“Mimi ndiye ninayepaswa kuuliza. Wewe na Lina mnapanga kununua

jumba la kifahari hapa, au unatafuta nini huku?" Lisa alirudisha swali.

“Hapana. Niko hapa kuangalia nyumba ya mjomba wangu. Jumba lake linahitaji kukarabatiwa na ninapanga kumshawishi kukabidhi mradi huo kwa

Lina.” Ethan alimwambia Lisa huku akimkazia macho usoni. “Unaona Lisa, ningeweza kumshawishi mjomba akupatie huo mradi wa kukarabati jengo lake la kifahari kama mimi na wewe tungekuwa bado tunaelewana vizuri.”

Ethan alimwambia kwa kujidai.

Hapo awali Lisa aliliona gari la Alvin na punde akamwona Ethan mitaa hiyohiyo, je hii ilikuwa ni bahati tu? Kwa kuwa

wawili hao walikuwa wamefuatana na aliamini walikuwa na uhusiano wa mjomba na mpwa, Lisa alihisi kuwa

Alvin alikuwa amenunua jumba la kifahari huko Mbezi Beach na Ethan

alitaka amshawishi ili ampatie Lina kwa

ajili ya kulikarabati. Hilo lilimuuma sana

Lisa. Ethan alitabasamu kwa dharau alipoona hali ya mawazo imeifunika sura ya Lisa.

" Unajutia maamuzi yako sasa? Na bado, utajuta sana!”

Lisa alikasirishwa na maneno ya Ethan nusu ya kutema damu. Lisa alimshangaa Ethan kwa kufikiri alikuwa

akimuwazia yeye. Ni mawazo ya Alvin ambayo yalimfanya akose raha muda

huo. Alijiuliza kwanini Alvin anunue jumba huko kisirisiri kisha amkabidhi

Lina mradi wa kukarabati jumba hilo?

Hicho ndicho hasa kilikuwa kikimuuma

Lisa. hata kama hakuridhika na ubunifu

wa Lisa, ulikuwa ni uamuzi wake

kuchagua kampuni nyingine yoyote ya kubuni muundo wa ukarabati wa jumba

lake, lakini siyo kukabidhi mradi wa ukarabati kwa Lina!

"Sawa, mjomba wako ndiye mwenye

uamuzi wa mwisho juu ya nani atampa kazi ya ukarabati, sio wewe. Labda

atashawishiwa kwa urahisi na mke wake. Maneno yako ni kama kinyesi tu kwangu." Lisa alimjibu Ethan kwa hasira. Ethan alikunja uso baada ya kusikia hivyo. “ Mjomba wangu bado hajaoa. Isitoshe mimi na yeye zinaiva sana, na kwa kawaida huwa anakubali chochote ninachomwambia.”

Lisa alitabasamu kwa dharau. “Hakika

muombe akufanye mrithi wa mali zake na uone kama atakubali.”

“Umerukwa na akili.” Uso Ethan ulibadilika kwa hasira. “Si ajabu

kwamba Mjomba Jones na Shangazi

masawe walikufungia kwenye jumba lao

huko Moshi. Hakika unastahili.”

Maneno yake yalichochea chuki

iliyozikwa ndani ya moyo wa Lina. "Ethan, unafahamu lakini unachokiongea?"

“Kwani nimekosea? Uliwaambia waandishi wa habari kwamba familia ya Masawe ilikufungia na kukutesa. Lakini unaonekana mwenye nguvu na mwenye

afya kwangu, kana kwamba umekuwa ukiishi vizuri. Uwepo wako ni bahati

mbaya sana kwa familia ya Masawe. Unajua kwamba kwa sababu ya

shutuma zako, sifa ya Kibo Group

zimeharibiwa na bei yao ya hisa

imeshuka sana? Thamani ya soko ya kampuni ilipoteza dola milioni mbili kwa usiku mmoja.”

Lisa alihisi hamu kubwa ya kummeza

Ethan mzima mzima. "Kitu pekee

kinachonifanya nisikitike ni kwamba, mwanzoni nilipoteza muda wangu

kukupenda sana bila kujua kuwa huna

akili hata kidogo. Akili ulizonazo

zinakutosha kujua chakula tu na njia ya kwenda chooni, basi!"

Ili kuepuka asije akapandisha hasira

mbaya nakufanya mambo

yasiyotarajiwa, Lisa aliwasha gari, akakanyaga mwendo na kuanza kuondoka.

SURA YA34

"Subiri." Ethan

alimzuia na kumwambia. “Sherehe

yetu ya uchumba na Lina imepangwa

mwishoni mwa mwezi huu. Lazima

uhudhurie sherehe hiyo. Ni wewe

uliyeharibu sifa ya Kibo Group hivyo

unawajibika kuiokoa.”

“Bullsh*t! Niondokee hapa ,wenda

wazimu wewe. Siwezi kusubiri kuona

Kibo Group ikifilisika kabisa. Ulisaliti

uhusiano wetu na bado una jeuri ya

kunidai nijitokeze kwenye sherehe yako

ya uchumba. Una wazimu nini! Huna hata aibu?!" Lisa alilaani.

Ethan hakuonesha hata wasiwasi.

Alizidi kumzuia Lina na kumwambia tena.“Sherehe yetu itaambatana na kumbukumbu ya kuadhimisha miaka 80 ya kuzaliwa kwa bibi yako. Alikupenda

sana tangu ukiwa mdogo, unajua! Na afya yake inazidi kuzorota kila siku, na nani anajua amebakisha muda gani?

Bado hutaki kuhudhuria?”

Mwili wote wa Lisa ulimsisimka huku

akimtazama Ethan kwa hasira kali.

“Yaani sherehe ya kuzaliwa bibi yangu

mnaijumuisha na mambo yenu ya kijinga?”

"Na ukiacha kuja bibi yako atasema

unamdharau, kumbuka bibi yako ndiye

mtu pekee aliyebaki anakupenda!"

Maneno ya Ethan yalijaa dharau.

“Usijali. Nitakuja." Lisa alikubali kwa hasira na kuondoka. 'Nitakuwepo na mjomba wako Alvin. Nataka kukuangamiza wewe na mchumba

wako asiye na maana kabisa!’ Lisa alijisemea kimoyomoyo wakati anaondoka. 'Nataka kumfanya mjomba wako kuwa mtiifu kwangu 100%. Lina

hataweza kujiunga na familia yenu mradi tu sitakubali!' Lisa alijiwazia kwa hasira.

Ethan alitikisa kichwa kwa dharau

wakati akimwangalia Lisa akitokomea

kwa mbali. Baada ya Lisa kupotea machoni mwake, Ethan alitembea

kuelekea kwenye jumba la kifahari la mjomba wake, Kelvin Mushi.

Kelvin alikuwa akikagua mchoro

alioachiwa na Lisa kwenye kiti cha

mapumziko chini ya mti. Alikunja uso na

kuuficha mchoro ule kwa siri baada ya kugundua kuwasili kwa mpwa wake.

"Mjomba, lini utaanza kukarabati jumba lako?" Ethan alikuwa ameona mchoro

kabla haujafichwa.

"Ulisikia kutoka kwa bibi yako sivyo?"

“Ndiyo,” Ethan alijibu huku akitabasamu.

“Umelidhamiria kweli jambo hili? Acha

Kibo Group ishughulikie suala hilo. Lina mwenyewe ni mbunifu mzuri. Mpe

nafasi.”

Kelvin alizuia hamaki yake alipoinuka

na kusimama. "Ethan, najua mambo

kadhaa kuhusu wabunifu katika

kampuni ya Kibo Group. Mtindo wao wa ubunifu ni wa kifahari lakini ni wa

kizamani sana na unatofautiana sana

na malengo yangu. Nimeishi nje ya nchi

kwa muda mrefu sana na ninapendelea mitindo fulani ya kigeni.”

"Sawa, unaweza kuwasilisha mawazo yako kwa Kibo Group. Sifa ya kampuni yao imeathiriwa sana hivi karibuni. Mjomba, tafadhali unaweza kuwasaidia?”

"Hapana." Kelvin alipunga mkono wake hewani bila kusita. "Naweza

kukubaliana na chochote mbali na hili.

Nina viwango vya juu vya makazi

yangu. Nimekutana na Lina hapo awali. Kusema kweli, hana uzoefu na hajui

chochote kuhusu vifaa vya kisasa vilivyo

kwenye fasheni. Ataharibu tu nyumba yangu.”

Ethan aliona aibu kidogo. Ni mchumba wake walikuwa wakijadiliana, hata hivyo, hivyo alizidi kumpigania. "Lakini

alifanya vyema katika mradi wa Kituo

cha Utamaduni na Teknolojia..."

"Usisahau kuwa alishinda zabuni kwa

sababu tu nilimpambania! Ukaribu wangu na Mzee Kamote ndiyo ulimpa

nafasi hiyo." Sura ya kutofurahishwa ilijiosha usoni mwa Kelvin alipokuwa

akiongea kuhusu hili. "Mbali na hilo, unapaswa kushukuru kwamba Mzee

Kamote hakutufichua au tungekuwa katika matatizo makubwa."

Ethan alihisi moyo wake kuzama.

"Sawa, sio jambo kubwa ikiwa hukubaliani. Kwa hiyo unaenda kwa

mbunifu gani? Nauliza kwa udadisi tu na si kingine.” Ethan aliuliza huku macho

yake yakiwa yamelenga kwenye mchoro.

"Joseph Ruta, ni rafiki yangu kutoka

Uganda. Alifungua tawi hapa Dar es

Salaam.” Kelvin alikabidhi mchoro huo

kwa mpwa wake. "Hii imeundwa na

mmoja wa wabunifu wake. Alitoa

mchoro wa jumba zima la mita za

mraba 3,000 kwa chini ya nusu saa, bila

kusahau kutoa maelezo ya undani kikamilifu kulingana na mapendekezo yangu. Nimeridhika sana.”

“Lisa?” Ethan aliganda kwa sekunde kadhaa alipoona saini ya Lisa chini

kulia mwa mchoro. Alikumbuka kugongana naye getini hapo awali.

Ilivyoonekana, alikuwa hapo kubuni muundo wa jumba la mjomba wake.

"Ndio, huyo ndiye." Kelvin alijibu kwa

dhati. "Mjomba, huwezi kumwajiri Lisa," Ethan alisema kwa uchungu, "Yeye ni binti mdogo wa familia ya Jones Masawe niliyekuambia hapo awali. Aliwahi kuwa

mpenzi wangu lakini amekuwa na sifa

mbaya sana. Sio tu kwamba aliiba kazi

ya mtu mwingine, lakini pia aliharibu sifa ya wazazi wake mwenyewe.”

Hili lilimshangaza Kelvin. Haishangazi

alidhani jina hilo halikuwa geni akilini mwake. Lakini alipokumbuka tabia ya fadhili na adabu ya Lisa, alikunja uso.

"Sidhani kama anahitaji kuiga wengine, kutokana na talanta zake. Nimepata uzoefu mzuri wa kushughulika na watu wa aina zote katika ulimwengu wa biashara. Yeye ni kipaji adimu, na sidhani kama yeye ni mtu asiyeheshimika. Kinyume chake kabisa, Ethan, nadhani una chuki dhidi yake!”

“Kweli humjui vizuri Lisa mjomba!”

“Mbona unanishangaza?

Tulipozungumza kwa simu siku za nyuma, hukuweza kuacha kumpongeza lakini sasa umechukizwa naye ghafla.

Je, alikukosea kwa namna fulani? Ni

wewe uliyemsaliti kwanza nikikumbuka vizuri.”

Ethan hakuwa na neno la kukanusha

jibu ambalo hakulitarajia. Kelvin akaendelea kumhutubia. "Vile vile,

unaendelea kujivunia vipaji vya Lina, lakini sioni uwezo wake. Kama si kweli

kwamba yeye ndiye mrithi wa familia ya Masawe, nisingemtazama kwa mara ya pili mwanamke kama yeye.”

Kelvin alichukua mchoro kutoka

kwenye mikono ya mpwa wake na moja

kwa moja akaelekea mlangoni.

Kelvin alikuwa tayari ameondoka muda

mrefu wakati Ethan alipotulia tena

kiakili. SURA YA35

Lisa alitumia karibu siku nzima akifikiria

kuhusu sherehe ya uchumba wa Ethan

na Lina.Hatimaye, ilikuwa wakati wa

kurudi nyumbani. Aliharakisha kurudi

nyumbani mara moja, lakini Alvin

hakurudi mapema hadi ilipokuwa usiku

sana.

"Nadhani nilikuona Mbezi Beach leo."

Lisa alimwambia Alvin kwa uso mkavu.

“Ulikuwepo huko leo?” Alvin alikodoa

macho kwa mshangao.

“Ndiyo, ulikuwa unafanya nini pale?”

Tabasamu likatanda usoni mwake.

"Labda umenunua nyumba katika eneo hilo?"

"Hapana." Alvin alikanusha huku

akichukua ‘chopsticks’ kutoka mezani.

“Sam alikuwa amenisumbua

kumsindikiza huko kutazama eneo lake. Siyo kwamba siwezi kununua

nyumba kubwa ila ninahofia woga wako.

Majumba ya kifahari huwa ni makubwa sana, yatakutisha na majinamizi yako.”

Lisa alimsikia maelezo yake lakini

angemwamini ikiwa Ethan asingesema

wazi kwamba mjomba wake alinunua

jumba la kifahari huko Mbezi Beach.

Kwa akili ya Lisa, Alvin ndiye alikuwa

mjomba wa Ethan, kwa hiyo hakuelewa

nia yake ya kuficha jambo hilo kwake.

Alikuwa hapendi afahamu kuhusu mali

zake, au alikuwa akipanga kumpatia Lina kukarabati jumba hilo ndiyo maana

aliamua kumficha? Lisa angeweza kukubali uwezekano wa wazo la kwanza

lakini wazo la pili lilimchefua nyongo.

Aliichukia sana familia ya Masawe kwa

kujaribu kuchukua maisha yake, pamoja na kinyongo chake kisicho na mwisho

dhidi ya Lina.

"Ni sawa ikiwa ulifanya hivyo. Sitakulazimisha kuniajiri kama mbunifu wako,” alisema kwa mzaha nusunusu.

"Tayari nimesema sijanunua, unanilizamisha ili iweje?" Jibu lake lilikuwa la moja kwa moja.

Lina aliizungusha vidole vyake kwenye

meza na kubadilisha mada ya mazungumzo. “Sawa, basi, labda pengine kuna hafla utakayohudhuria hivi karibuni? Labda utahitaji mwenzi wa kike wa kuambatana naye?”

“Hapana.” Alvin alijibu kifupi.

“Um… Sawa.” Lisa alishangaa. Alitaka kuuliza, ‘vipi kuhusu sherehe ya uchumba ya mpwa wako?’ lakini alisita. Alijishaua tu kwa kusema, “lakini mimi

ninahitaji mwenza.”

Alvin akaziweka chopsticks juu ya meza na kumtazama moja kwa moja machoni.

"Unajaribu kusema nini?"

“Bibi yangu atafikisha miaka 80 mwisho wa mwezi. Kumbukumbu ya kuzaliwa

kwake inaadhimishwa pamoja na sherehe ya uchumba ya Ethan na Lina.

Sina chaguo ila kujitokeza. Bibi yangu

amekuwa mkarimu sana kwangu tangu

nilipokuwa mdogo. Je, ungependa kwenda pamoja nami?” Lisa alijipa

ujasiri kusema hivyo. Alimtazama kwa macho ya kutarajia.

Ilimchukua Alvin sekunde kadhaa kutoa jibu lake. “Nakumbuka nilikuambia kabla hatujafunga ndoa kwamba sitakutana na watu wa familia yako.”

"Kwa hiyo hata kwenye sherehe ya uchumba hutaenda?" Lisa aliuliza kwa kufoka.

“Kwa nini niende, Ethan au Lina wanahusiana nini na mimi?” Alvin

aliuliza Haikuwa na maana yoyote kwake kwani hakuijua familia hiyo hata

kidogo.

'Kwa hiyo wewe si mjomba wa Ethan?'

Lisa alitaka kuuliza hivyo, akasita. Hata hivyo, ikiwa angeuliza hivyo, huenda

angekisia kwamba alimjia kwa nia

isiyofaa. Hivyo akasema, “kwa sababu watu wengine wengi mashuhuri jijini

watahudhuria sherehe hiyo pia, kwa hivyo nilifikiri…”

“Samahani, lakini sina mpango wa kuhudhuria hafla za viwango vya chini kama hivyo.” Alvin alizima mada kwa

kauli ya kejeli.

Lisa alikosa la kusema. Kiwango cha chini? Alikataa kuhudhuria sherehe ya

uchumba wa mpwa wake kwa sababu

hiyo? Alikuwa bora kiasi gani wakati

huo? Je, huu ulikuwa ni mtazamo wa kiburi wa kila mtu aliyerudi nyumbani baada ya kukaa miaka mingi nje ya nchi? Maswali magumu yalitawala uso wake.

“Mbali na hilo, nitakushauri usiende pia.

Siwezi kuhangaika kwenda kukuokoa

tena pindi familia ya Masawe

itakapokufanyia ushenzi.” Alvin

alimuonya kwa ukali huku akimkodolea macho. Lisa alipoteza hamu ya kula ghafla.

Alichukua simu yake na kuanza kuchati na Pamela kupitia WhatsApp.

Lisa: [ Na ulisema Alvin anaweza kuwa na hamu kidogo nami? Samahani, lakini sijisikii hata kidogo. Kila sekunde ninayotumia naye hufanya damu yangu ichemke.]

Pamela: [Hey, endelea kujaribu. Je, tunaweza kutoka kula chakula cha jioni? Imekuwa siku nyingi sana.]

Lisa : [Hapana. Alvin atachukia nikiondoka nyumbani.]

Pamela: [Haya, wewe si mlinzi wake wa nyumbani. Unamdekeza sana.]

Akiwa hana chaguo lingine, Lisa alipanga vyombo na kutokea tena baadaye akiwa kabadilisha mavazi. “Nitatoka kwa muda kidogo baadaye.”

"Wapi?" Macho ya Alvin yalijawa na kero. "Unaenda kunywa pombe tena au kwa familia ya Masawe? Au unaenda kwenye miadi na mwandamizi wako?

Usisahau bado unapaswa kumpeleka

Charlie matembezini baada ya kula."

Lisa alipoteza ujasiri wa kusema ukweli. "Ninaenda kufanya shopping na Pamela. Hali ya hewa inazidi kuwa joto na ninahitaji nguo mpya."

Alvin alimtazama juu na chini kabla ya kutoa maamuzi. "Sawa, nahitaji nguo mpya pia, kwa hivyo ninulie chache pia.

Tumia tu kadi ya benki niliyokupa mara ya mwisho,” Alvin alisema kwa uvivu.

Lisa alikosa la kusema. Kwa kweli

hakuwa na nia ya kwenda shopping ila alitaka tu kufurahia chakula cha jioni na Pamela. “Sawa, sawa, nitakwenda kukunulia. Unavaa saizi gani?"

"Hata hujui ninavaa saizi gani bado una

ndoto ya kunikaribia kitandani kwangu?"

Alvin aliongea akiwa seroius, ilibidi

kwanza Lisa acheke.

"Sawa, unatafuta nguo za bei gani?"

Lisa alimuuliza tena.

“Yoyote, mradi utaipenda.” Alvin pia

hakuwa na uhakika. Baada ya yote, siku zote alikuwa na wabunifu binafsi wa

kutengeneza nguo zake.

Dakika kumi baadaye, Pamela alifika

akiwa kwenye gari lake. Lisa aliingia

ndani ya gari huku akionekana kukata

tamaa. “Twende dukani. Alvin anataka

nikamnunulie nguo.”

“Lakini vipi kuhusu chakula? Bado sijapata chakula tangu mchana nilikuwa busy kweli.” Pamela alisema kwa kuchanganyikiwa. Lisa hakuwa na jinsi zaidi ya kumwambia ukweli. Pamela alimtazama tena kwa dharau. “Heshima yako imeenda wapi? Umekuwa mnyonge sana kwa Alvin tofauti na zamani. Mbona kwa Ethan hukuwa hivi?”

“Huelewi. Alvin hutumia kisingizio cha jinsi nilivyosababisha Charlie awe mgonjwa dhidi yangu,” alijibu Lisa.

"Mbali na hilo, aliokoa maisha yangu mara mbili na ninataka kulipa fadhila."

"Hakuna mtu mwingine anayemdhibiti mkewe namna hii," Pamela alidhihaki.

“Sawa, achana naye. Najua mimi ni mlinzi wake wa nyumbani.”

Lisa aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha

abiria alionekana kukata tamaa.

“Unadhani nisipojishusha naweza kusimama mbele ya kina Ethan kama

shangazi yao? Sherehe ya uchumba wao inakaribia.”

Pamela alitikisa kichwa kufikiria hili.

“Labda Alvin anakuchukulia wewe kama mfanyakazi wa nyumbani ambaye unapika vizuri. Lazima ubadili mawazo yake kidogo, na njia bora ya kufanya hivyo ni kumwonjesha mapenzi yako.”

Lisa alibaki kimya. "Jaribu kuwa mke mpaka kitandani kwake, usiishie jikoni tu." Pamela akamtupia jicho la kustaajabisha. “Unajua ninachomaanisha.”

Lisa alipigwa na butwaa. Uso wake ukajawa na aibu. "Anaweza kunitoa kitandani mara moja."

“Unaweza kumlewesha hoi. Wanaume

hupoteza kujizuia mara wanapokuwa walevi. Mambo yatakuwa mazuri zaidi

ikiwa utapata mimba ya mtoto wake. Nafasi yako kama malkia wa familia

itaimarishwa bila wewe kuendelea kupigana. Sawa, ni lazima upange hili vizuri. Tegeshea karibu na siku baada ya hedhi yako kwani utakuwa na uwezo wa kunasa mimba zaidi wakati huo.”

Akili ya Lisa ilikuwa imechanganyikiwa na mawazo mengi tofauti. Hakuwa na

mpango wa kubeba mimba ndani ya uhusiano wao usioeleweka? “Lakini hanipendi. Familia kama hiyo sio mazingira bora kwa mtoto…”

“Lazima uwe umejitayarisha kwa hili

ulipoamua kuoana naye bila kusita,”

Pamela alimkatalia, “Mbali na hilo, si

unataka kulipiza kisasi wewe? Hii ndiyo

njia bora ya kujumuika katika familia ya

Lowe na kuwaletea matatizo kwa

kutumia nafasi yako kama mke wa Alvin

Kimaro. Fikiria kuhusu hili! Na hawawezi

kukutukana kwa sababu utapewa nafasi ya juu kuliko wao katika uongozi wa familia.” "Wazo zuri." Lisa alionekana kuafiki.

"Lakini kwa nini wewe hujafanya hivyo na Patrick?” Pamela akakosa majibu.

SURA YA 36

Nusu saa baadaye, wote wawili walifika

katika moja ya maduka makubwa ya kifahari ya Oyster Bay. Lisa hakuacha

kunung'unika tangu dakika ile alipoingia

dukani. “Kwa nini umenileta hapa?

Nguo zao ni ghali. Alvin ni mtu wa

kawaida na mchumi sana kwenye hela.

Pamoja na pesa zote alizonazo yeye

anaendesha Harrier tu. Ndiyo, avavaa

vizuri na anapendeza lakini nguo zake

hutengenezewa na wabunifu wake

binafsi, hakika amenituma kwa hili kama mtego tu. Atanifokea sana kwa

kumnunulia nguo za gharama kama hizi” "Lakini mfanyabiashara aliyefanikiwa kama yeye anapaswa kuvaa kitu cha gharama zaidi. Wewe unatakiwa umbadilishe. Angalia, vipi kuhusu mtindo huu?" Pamela alimkokota hadi kwenye duka la kifahari la nguo za kiume na kumuelekezea suti moja kali.

Lisa aliitazama kwa haraka. "Suti ni nzuri, lakini umbo lake haliendani na la Alvin."

"Sawa, basi mchukulie ile pale, ni nyembamba kama yeye, itamfaa sana au vipi," Pamela alishauri lakini Lisa

alikuwa bado na wasiwasi. Hata hakuwa na uhakika alitaka kumnunulia nini Alvin.

"Twende zetu. Ni ghali sana hapa.” Kwa aibu, Lisa alianza kumkokota rafiki yake

kuelekea mlangoni. Muuzaji akawasogelea na ghafla wakasimama kumsikiliza. "Suti hii ni mtindo mpya kabisa, imetengenezwa na mbunifu maarufu Sheria Ngowi. Kuna suti mbili tu kama hizi katika nchi nzima.”

"Hah, unaweza kuokoa muda na nguvu yako. Watu hohehahe kama yeye hawataweza kumudu.” Maneno ya

dhihaka yalivuma hewani. Kisha, Janet Kileo na Cindy Tambwe wakaingia machoni mwao.

“Miss Kileo, Bibi Tambwe…” Macho ya muuzaji yaling’aa huku mara moja

akikimbia kwenda kuwasalimia.

Janet alimtupia jicho la pembeni Lisa

huku akijigamba. “Kwa hiyo umejipatia bwana mpya? Lakini yeye ni mtu mdogo

tu hana lolote. Mtu wako ni mwanasheria uchwara tu. Hata

angekuwa na mafanikio kiasi gani katika kazi yake, bado anategemea matajiri tu kama sisi ili kupata pesa.”

Pamela alicheka kwa hasira. “Mwanasheria? Je! unajua kuwa mpenzi wake…”

Kabla Pamela hajamaliza usemi wake, Lisa alimshika mkono wake na kutikisa

kichwa. Ndoa yake na Alvin ilikuwa siri.

Alijiuliza ni mwanaume gani Janet

alikuwa amekosea na kudhani kuwa mi mpenzi wake.

Tabasamu la furaha likaangaza usoni

mwa Cindy. Alikumbuka jinsi alivyokuwa

akiambatana sana na Lisa hapo zamani

kwa sababu familia yao ilikuwa bora

zaidi. "Lisa, labda unapaswa kununua

mahali pengine. Nijuavyo mimi kuna

pesa chache tu kwenye kadi yako sasa.”

“Cindy, usivuke mipaka.” Pamela alikasirika. Kabla hawajakosana urafiki, Pamela alikuwa amemueleza Cindy juu ya hali ngumu ya Lisa, bila kutarajia Cindy angewageuka na kuwasaliti bila wasiwasi.

Kama ilivyotarajiwa, muuzaji alionyesha kutokuwa na subira aliposikia kwamba

kina Lisa walikuwa hawana pesa za kutosha. “Tafadhali muondoke ikiwa

hamna uwezo wa kumudu hili. Tuna upungufu wa wafanyakazi na hatuwezi kuhudumia kila mtu.”

"Nani kasema hatuwezi kumdu?"

Pamela akatoa kadi yake ya benki.

Janet alidhihaki, “Cindy, ni bora

ulivyoamua kuachana nao. Marafiki kama hawa watakuchoresha tu.”

Cindy naye akazidisha machungu ya

Lisa. "Kwa kweli, lazima apige vizinga kwa marafiki ili anunue nguo."

Lisa , ambaye kwa kawaida alikuwa mvumilivu sana, hakuweza tena kuvumilia dhihaka hizo.

“Hakuna shida hivi ni vitu vidogo sana kwangu nikitaka nanunua tu pesa ipo.”

Lisa aliwarusha roho. “Hili ni toleo la pekee, hakuna hata mmoja wenu anayeweza kugusa hapa.” Alichomoa kadi ya benki aliyopewa na Alvin na kumkabidhi muuzaji. “Si ulisema una seti mbili tu za hii suti? Nazitaka zote.

Sitaruhusu mtu mwingine yeyote kuvaa

nguo zinazofanana na za mpenzi wangu.”

Hii ilimshangaza muuzaji, lakini ni nani angekataa pesa? "Kwa seti zote mbili zitafikia jumla ya shilingi milioni tano."

Lisa alihisi miguu yake ikiishiwa nguvu.

Hakuwa na hakika kama Alvin angemvumilia kwa kumnunulia nguo za gharama ya shilingi milioni tano. Lakini, vipi ikiwa ingezidi kikomo cha kadi?

Alijiuliza huku akihisi angeibeba vipi aibu yake mbele ya wale wambea

waliokuwa wakimkodolea macho.

Alipoibia sura za Janet na Cindy

waliokuwa wakingoja kwa hamu aaibike ili wamcheke, alijilazimisha kutoa kadi.

'Naomba tu iwe na pesa za kutosha,' alijiwazia mara kwa mara.

"Lakini, ni lazima nikukumbushe kwamba hatukubali kurudishiwa bidhaa za toleo maalum, ukinunua umenunua,"

muuzaji alimpa angalizo mapema.

Lisa alihisi ubongo wake ukiganda, lakini akajisemea kimoyomoyo, ‘potelea mbali’.’ Cindy aliziba mdomo kwa mshangao wa madaha. "Lisa, natumai haukuwa umepanga kurudisha nguo baadaye."

Lisa alicheka kana kwamba alikuwa anasikia utani wa kuchekesha.

"Sitafanya kitu cha kimasikini kama hicho. Pia, acha kuniita Lisa . Kusikia ukisema unaita jina langu masikio yangu yanauma.” Aligeuka

kumwangalia muuzaji. “Fanya haraka uniandalie. Sitaki kuendelea kuwasikia mbwa vichaa wakinibwekea.”

“Wewe…” Donge la hasira lilitawala usoni mwa Cindy lakini hakuwa na cha

kufanya. Janet alimshika mgongo Cindy na

kumwambia kwa kujishaua. “Achana

naye. Ngoja tuangalie duka la gharama

zaidi. Kiukweli, nadhani nguo za hapa bado ni nafuu sana. Labda sweety

wangu hatazipenda.”

“Kweli.” Cindy alielewa maana yake

mara moja. Aliridhika hasa alipowazia sura ya Lisa yenye aibu baadaye

wakati kadi itapokataliwa.

Lisa akawakazia macho na kuwafanyia kiburi kana kwamba yeye ndiye tajiri

mkubwa duniani. Kadi ilikubaliwa bila shida yoyote. Muuzaji alimkabidhi begi

la shopping. "Hizi hapa ni nguo na risiti, Bibiye." Lisa alihisi kuguswa ghafla

wakati huu. Hakutarajia Alvin angempa kadi ya benki yenye zaidi ya shilingi

milioni moja.

“Inatosha. Twende!” Janet ambaye alisubiri pembeni kumuona

Lisa akidhalilishwa, aliunganisha

mikono yake na Cindy na kuondoka

huku akiwa amefadhaika moyoni.

Pamela alimpiga Lisa kwa kiwiko. "Sio mbaya. Alvin ni mkarimu sana, ila basi tu."

Lisa hakuweza kuachia tabasamu licha ya kujilazimisha. Alihisi mzigo mzito

ukimlemea kifuani. Miguu yake iligeuka kuwa mrenda alipokuwa akitoka nje ya duka na nguo za thamani ya shilingi milioni tano.

“Hapana, lazima atafikiri ninamfanyia ubadhirifu makusudi. Hivi unamjua Alvin wewe, hapa amefanya kunitega tena apate sababu ya kunisema baadaye.”

Lisa alihofia

“Acha kujiogopesha. Alvin ana thamani ya mamia ya mamilioni ya pesa. Kiasi

hiki kwake ni cha kununulia karanga tu.”

Pamela alimtuliza.

“Huelewi. Yeye ni mchumi. Akiwa na utajiri wote huo mfukoni mwake, anaishi katika nyumba ya vyumba vitatu tu, anaendesha gari la milioni 30, na anatumia tishu za bure tu zinazotolewa na kituo cha mafuta. Simu anatumia ya kichina, Saa kwenye mkono wake pia ni chapa ndogo isiyo na umaarufu. Hata sabuni anazoogea na losheni

anazopaka ni bei ya kawaida tu. Nyumbani kwake hataki kuajiri hata

mtumishi mmoja. Unafikiri ataacha

kunisema kwa kumnunulia nguo za milioni tano, tena kwa pesa yake?”

"Vema, yeye ... Yeye ni mzuri sana na pesa zake, basi." Pamela hakujua

matajiri wengine ambao waliishi

kichumi kama yeye. "Naweza

kukukopesha hiyo pesa, kama atakuzingua utamrudishia."

“Sawa. Nitaona jinsi atakavyojibu

kwanza. kama atanisema vibaya

nitamrudishia milioni tano yake. Wewe nitakulipa pole pole.” Lisa aliafiki.

Lisa alipoteza hamu ya kuendelea kununua baada ya hapo. Hakutaka

kukutana tena na wasichana wale wawili wasio na maana.

Lisa alikula chakula cha usiku na Pamela hadi saa nne usiku. Kisha, alielekea nyumbani huku akiwa na hofu.

Kwa kuogopa kwamba angemsumbua

Alvin aliyekuwa ndani ya nyumba, hakuthubutu kuwasha taa.

SURA YA37

"Umerudi

alitokea

ghafla kwenye mlango wa chumba cha

kulala, na kulikuwa na makali ya uhakika katika sauti yake.

Lisa alipata mshtuko na kujiona

mwenye hatia sana. Alijiuliza ikiwa

mapema sana!" Alvin

alitumia muda mrefu kumngojea arudi

nyumbani ili kuuliza ni pesa ngapi alizotumia. "Linapokuja suala la shopping, wanawake huwa wanasahau wakati."

Alvin akawasha taa pale sebuleni, kisha

akamtazama Lisa kwa sekunde mbili. Akamsogelea na kunyoosha mkono wake.

"Unataka nini?" Lisa hakusogea hata kidogo. Hata hivyo, baada ya kidole

chake cha shahada kugusa midomo yake, hali alianza kupata hisia ngeni

kwenye mwili wake. Lisa alitazama ncha ya kidole kile cha Alvin kwa butwaa.

Ukucha wake ulionekana nadhifu na mzuri, lakini alikuwa akijaribu kufanya nini? Akiwa amechanganyikiwa, alimng'ata kidole kwa upole kwa kutumia meno yake.

Mwili wa Alvin uliganda. Alihisi kana

kwamba mguso wa shoti ya umeme ulikuwa ukisafiri katika mwili wake mara

moja. Alimkazia macho kwa macho meusi ambayo yalionyesha kutokuamini. "Unafanya nini?"

'Hivi si ndivyo unavyotaka? Lisa aliachia kidole chake na kusema kwa sauti ya chini, "Uligusa midomo yangu na kuingiza kidole chako baada ya hapo, sasa mimi ningefanyaje ..?"

"Lisa, una akili chafu sana."

Alimpotezea kabisa. "Nilitaka tu kukuonyesha mabaki ya chakula kwa kidole changu kwa sababu haukufuta mdomo wako vizuri baada ya chakula."

Lisa aliaibika sana hivi kwamba

akainamisha chini uso wake. Alitamani

hata kuchimba shimo na kujifukia humo.

Hata hivyo, kilichofanyika kilifanyika.

Hakuwa na la kufanya ila kusema kwa

kusita, “Huwezi kunilaumu kwa hili. Una

kidole kizuri sana. Nilishindwa kuzuia hisia zangu nilipokiona.”

Alvin alitoa kidole chake kilichokuwa kinawaka kwa msisimko. Alicheka alipotamka maneno hayo yasiyo na aibu huku uso uso ukiwa mkavu kama kauzu. “Umeshika nini?”

Lisa alitetemeka, kisha akanong'ona, "Suti yako. Samahani, nilikununulia suti zenye thamani ya shilingi milioni tano

kwa bahati mbaya.”

Alvin alikunja uso kwani hakuwahi kuvaa suti ya bei nafuu namna hiyo.

Suti zake ziligharimu bei kama ya gari.

Moyo wa Lisa ulimshtuka alipomuoa

Alvin yupo kimya. "Ni nzuri na za

kipekee pia"

"Kwanini zote mbili zinafanana?" Alvin

alimkatisha maneno yake. “Huu?” Lisa alipigwa na butwaa. “Kwa sababu… Ni toleo maalumu. Kuna suti

mbili tu za aina hii katika nchi nzima. Sikutaka kuona mtu mwingine akivaa suti sawa na wewe maana itakuwa ni fedheha. Machoni mwangu, wewe ni mtu wa kipekee sana, mzuri, na mtanashati. Nadhani rangi hii inafaa zaidi kwako. Huwa nakuona umevaa

suti kama hizi na hata sijachoka nazo.

Tafadhali nisamehe kwa kuwa mbinafsi kidogo.”

Alipomaliza kuongea, alitazama sura yake kwa siri. Aligundua kuwa Alvin

alikuwa akimtazama na kukunja

midomo yake.

"Kazi nzuri. Nimependa ustadi wako wa kuchagua rangi” Alvin akanyoosha

mkono wake na kuyabana mashavu ya

Lisa. "Utakapostaafu kuwa mbunifu wa

majengo katika siku zijazo, unaweza kuwa katibu wangu. Utakuwa

ukinipangia nguo za kuvaa kila siku.”

“Umezipenda?” Lisa aliuliza huku akiyakodoa macho yake.

“Kwa nini nisizipende?”

“Nilikuwa na wasiwasi kwamba

utalalamika ni za gharama kubwa kwa sababu… niligundua kuwa nguo

unazovaa kwa kawaida hazionekani kuwa za gharama…” Lisa alilazimisha

tabasamu kwa aibu kwa kuogopa kuwa maneno yake yangeumiza jeuri ya

Alvin. “Hehee. Kwa kweli, hakuna ubaya

wowote. Ninaelewa kuwa wewe ni mtulivu na mtu usiyependa kujionyesha, na hilo ndilo linalonivutia sana kwako.”

Alvin alipigwa na butwaa. Hapo ndipo

akagundua kuwa nguo alizokuwa akivaa

kawaida zilionekana za bei rahisi kwa

Lisa. Alimshangaa sana Lisa kwa jinsi alivyomchukulia juu juu. hakujua kuwa

nguo zote alizokuwa anavaa Alvin Kimaro zilikuwa ni 'customized brand',

ama nguo zilizotengenezwa mahususi kwa wateja maalunu. Nguo zake zote

zilikuwa za kipekee za hazikufanana na wengine. Si zile za kuchagua chagua tu kwenye maduka.

“Ni sawa. Utaelewa baadaye.” Alvin akagusa kichwa chake kwa huruma, kisha akaingia chumbani.

Siku iliyofuata, Alvin alivaa suti ya kahawia aliyonunuliwa na Lisa.

Alipotoka nje ya chumba kile, Lisa alimtazama na kupigwa na butwaa

kwa muda. Ingawa alimuona akiwa

amevalia kila aina ya suti, hisia za ajabu

zilimjaa kichwani kwa sababu tu hiyo

ndiyo suti aliyomnunulia. Alihisi

mchanganyiko wa furaha na

kuchanganyikiwa. Ilionekana kana

kwamba alikuwa mume wake halisi wakati huo. Alvin akampiga jicho.

Alipogundua kuwa alikuwa akimtazama kwa butwaa, kwa namna fulani alikuwa katika hali ya uchangamfu.

Alipokuwa akitoka nje ya nyumba hiyo, kuna jambo lilimjia kichwani. “Sikuona

umenunua nguo yoyote jana usiku, kwanini” Alimuuliza

"Hapana, nilikuwa na kazi ya kukununulia wewe nguo." Alipokumbuka furaha ya kumnunulia mpenzi wake

nguo tabasamu lilisambaa usoni mwake.

"Nadhani ulikuwa na shida ya kwenda kula chakula cha jioni na si kununua nguo, ungesema ukweli tu." Alvin

alimdhihaki, akimuonyesha waziwazi.

"Ah, kwa nini unanifikiria hivi?" Ili

kuficha aibu yake, Lisa alisema kwa sauti nzito ya kutaniana, ”nilikosa tu nguo zinazonifaa, nitaenda siku nyingine.”

Alvin alihisi koo lake linamuuma.

Alifungua vifungo viwili kwenye shingo ya shati lake na kusema, “Kama una muda, nenda ukanunue nguo leo kwa kutumia kadi yangu. Nguo hizo zitakuwa malipo kwa kunipikia na kumhudumia Charlie kama mhudumu wangu.”

Alielekea ofisini kwake mara baada ya kumaliza kuongea.

Hans alipoingia tu kwenye kampuni ya mawakili, alipigwa na butwaa kuona suti ya Alvin. Kwa haraka akasema, “Bw.

Kimaro, sijawahi kukuona ukivaa suti za aina hii…”

“Lisa aliinunua madukani jana.” Alvin aliongea huku akifungua faili la kesi.

Sam, ambaye alikuwa amefika tu mlangoni, alisikia maneno hayo. "Wow, unavaa suti zinazouzwa madukani siku?” Sam aliuliza huku akitazama suti

ya Alvin kwa shauku na kuichunguza. "Ni toleo maalum la Sheria Ngowi…. Nimezoea kukuona ukivaa nguo zilizotengenezwa mahususi kwa ajili yako pekee, tena na wabunifu wa nje ya nchi, au ni kwa sababu Lisa alikununulia hii…?”

Kwa hali ya huzuni, Alvin alimtupia jicho la kijeuri. “Mwanamume mzima unakuja kuchunguza nimevaa nini leo, huna kazi za kufanya, eeh?”

“Sikuja kwa ajili hiyo.” Sam alisema.

Alvin alimtupia faili usoni mwake, na maneno “toka ofisini kwangu”

yakachomoka mdomoni mwake.

"Sawa sawa. Usiwe na wazimu. Niko

hapa kukuambia kitu.” Sam akamwambia. “Babu yangu

atasherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 80 kesho usiku. Amesikia

kwamba upo Dar hivyo ameniomba nikwambie kuhudhuria sherehe hiyo.”

Sam alichukua kadi ya mwaliko na kuiweka juu ya meza.

Alvin aliitazama kadi hiyo na kukumbuka kitu. Lisa pia alimwalika kwenye sherehe ya kuzaliwa ya miaka

80 ya bibi yake.

"Pia ni bora ukaja na mpenzi wako,"

Sam alikumbusha. “Kama unavyojua, dada yangu amekuwa akipendezwa nawe kwa miaka mingi. Pia, babu yangu

amekuwa akitaka sana kukuoza dada

yangu. Hataacha kukusumbua kwa hilo”

Alvin alijipapasa paji la uso huku

akiwaza ni nani aende naye kama mpenzi wake.

Lisa? SURA YA38

Siku mbili zile Lisa alikuwa busy sana na kazi huku pia akilifikiria ushauri

aliopewa na Pamela wa kuweka mambo sawa na Alvin. Siku hiyo jioni akiwa anawaza hayo, Alvin alimpigia simu.

“Uko wapi?”

"Ofisini." “Nitumie anwani yako. Nitakuchukua hapo chini ndani ya dakika 20. Nataka unisindikize kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa.”

Hapa ndipo Lisa alipoona fursa. Macho ya Lisa yaling'aa, lakini baadaye alijawa na kinyongo. “Tufanye dili, kama

utakubali kunipa kampani kwenye

sherehe ya kuzaliwa ya bibi yangu, na mimi nitakubali kukupa kampani leo.”

“Kama hutaki niitatafuta mtu mwingine.”

Alvin hakumbembeleza.

Alvin alipotaka kukata simu, Lisa alitupilia mbali kiburi chake na kukubali haraka. “Njoo unichukue. Katika uwanja wa mapenzi, yule anayependa sana ndiye anayepoteza. Nimejikuta nikipoteza kabisa moyo wangu kwako.

Alvin una nini?” Lisa alichombeza

kijanja. Alichukua chupa ya thermos na kuendelea kunywa kahawa yake. Hata

yeye alivutiwa na ustadi wake wa kumtania Alvin kimapenzi.

Sekunde chache baadaye, sauti ya

Alvin ilisikika upande wa pili. "Simu

yangu imeunganishwa kwenye gari

kupitia Bluetooth, na Sam ameketi

kando yangu anakusikia ukiongea upuuzi wako.”

Lisa alitema kahawa mdomoni mwake

ikamwagikia kwenye skrini ya kompyuta

bila kujijua. Sauti ya Sam baadaye ilisikika, “Si vibaya shemeji. Sikuwahi

kufikiri kama na wewe unajua maneno matamu ya mapenzi kiasi hiki.

Haishangazi Alvin--"

"Nakuja kukuchukua." Alvin alimwambia

Lisa na simu ilikatwa moja kwa moja

kabla Sam hajamalizia usemi wake.

Lisa alilala juu ya meza, akiona aibu hadi kufa. Alinyanyuka baadaye kidogo na kupakia vitu vyake na kushuka chini.

Wakati huo alipokea simu kutoka kwa

Pamela. “Mambo yalikuwaje? Ulifanikiwa

kufanya chochote na mume wako jana usiku?”

“Hapana,” Lisa alimjibu haraka, “lakini aliniomba nimsindikize kwenye hafla ya siku ya kuzaliwa usiku wa leo. Nadhani hii ndiyo nafasi. Lakini nina wasiwasi kama atakunywa pombe. Anapotoka kwa shughuli za kijamii usiku, sijawahi

kumuona akinywa pombe!”

Lisa alihema huku akijua kuwa Alvin

alikuwa ni mtu mwenye kujitambua.

"Hafla ya kuzaliwa?" Pamela alipigwa na butwaa kwa muda. “Ni siku ya

kuzaliwa ya babu ya Sam ya miaka 80?

Mimi pia nitakuwepo.”

“Nafikiri hivyo. Alvin hana rafiki

mwingine zaidi ya Sam.” Lisa alisema.

“Hiyo itakuwa poa sana, tutakutana.

Nitawapanga watu kunywa na Alvin na

kujaribu kumlewesha. Hilo

lisipofanikiwa, nitaleta dawa…” Pamela

alimhakikishia. “Hakika Alvin atakutaka

mwenyewe bila kupenda.”

Lisa akashusha pumzi ndefu. Hakuwa na uhakika kama alikuwa amejipanga

kiakili kwa hilo licha ya Pamela kuwa

ameanza kumsaidia kuandaa kila kitu

kwa haraka. Alisubiri kwa hamu kando ya barabara. Lakini Alvin alipofika Lisa

alionekana kuzama kwenye mawazo

mazito kiasi kwamba hakusikia mlio wa

honi.

Beep! Beep!

Alvin alimkazia macho Lisa aliyekuwa

kazama kwenye mawazo fulani

yaliyomfanya atabasamu kwa aibu.

Alikuwa amejifunika uso huku

kasimama kando ya barabara.

Alishindwa kabisa kumwelewa. Hakuwa

na uhakika ni nini kilikuwa akilini mwake

pia. Je, alikuwa kiziwi?

Sam alikodoa macho na kutabasamu.

"Alvin, kwa njia fulani ninahisi kuwa mke wako anafikiria juu ya kitu kichafu, na labda uko kwenye mawazo yake ..."

"Yeye si wewe, sawa?" Alvin alimtazama kwa ukali, ingawa alikuwa na mashaka pia juu ya hilo.

“Kusema kweli, kadiri ninavyomwangalia Shemeji, ndivyo namuona kuwa mzuri. Kwa kweli, nashangaa uliwezaje kumpata kabla yangu hali wewe ni mgeni na mimi

ninaishi naye kitongoji kimoja.. "

Kabla Sam hajamalizia sentensi yake, sauti kali ikamkatisha. Alvin alimwonya bila huruma, “usijaribu kuwa na mawazo machafu juu yake. Yeye si mtu ambaye

unaweza kumpata kirahisirahisi tu.”

Baada ya hapo, alifungua mlango na kutoka nje ya gari. Alitembea moja kwa

moja kuelekea kwa Lisa.

Lisa alipomwona Alvin ghafla alishtuka

kutoka kwenye mawazo kiasi kwamba

alipiga hatua mbili nyuma na kutaka

kudondoka kutokana na viatu vyake

virefu. Alvin alipomuona Lisa anakaribia kuanguka, alinyoosha mkono wake

kumshika kiuno na kumweka kwenye mikono yake ili aweze kujiweka sawa.

Ikiwa hii ingetokea siku nyingine yoyote, Lisa angekuwa na wasiwasi kidogo.

Hata hivyo, alikuwa akimuwaza Alvin

ambaye hana nguo muda mfupi uliopita.

Sasa kwa vile ncha ya pua yake ilikuwa

karibu na kifua chake, mwili wake

ulibadilika ghafla na kutetemeka kama

amepigwa shoti ya umeme.

“Ninatisha kiasi hicho, hata unataka

kuanguka baada ya kuniona?” Alvin

alinua kichwa chake na kumuuliza.

"Hapana, umenishtua tu." Haraka alirudi

nyuma na kujiweka sawa.

"Ingia kwenye gari." Alvin alifungua mlango na kukaa kwenye kiti cha dereva. Lisa aligundua kuwa kuna mtu alikuwa kwenye siti ya mbele, kwa hivyo bila

kupenda akaenda kwenye siti ya nyuma. Kwa aibu, hakuweza kukabiliana na Sam.

“Habari, Shemeji. Ulikuwa unafikiria nini sasa hivi, mbona hukusikia honi?” Sam

alionyesha tabasamu baya. "Kutokana na mwonekano wako, naweza kukisia kuwa ulikuwa ukimfikiria Alvin."

"Ndio, nilikuwa nikimfikiria," Lisa alisema bila kujali kwa sauti ya upole. Kisha, akatazama chini haraka.

Baada ya kuachia 'wow', Sam alijifunika

kifua chake na kusema kwa huzuni, “Sikupaswa kuuliza swali hilo. Kuona

haw lovey- dovey nyote wawili mlivyo, ninahisi kushikwa na wivu. Hata hivyo, Alvin hana utu wa kupendeza, na ana hasira mbaya. Pia ana tabia nyingi

chafu. Unapenda nini hasa kutoka

kwake?” Sam aliuliza kwa utani.

Moyoni mwake, Lisa alimpa Sam mia

kwa mia kwani alikuwa sahihi kabisa.

Hata hivyo, alimsifia tu Alvin ili kumlinda

kihisia, “Kwa kuwa sasa ninampenda, naona udhaifu wake wote kuwa ni sifa

zake nzuri. Kinyume chake, wanaume

wapole na waelewa hunifanya nihisi

kutokuwa salama. Napenda sifa zake

tu. Akinizingua na mimi namzingua basi, yanaisha!” Maneno ya Lisa

yalimvimbisha kichwa haswaa Alvin,

Akamgeuzia macho Sam na

kumwangalia kwa kejeli.

Sam alihisi kana kwamba alikuwa

amedhihakiwa na Lisa. "Sikupaswa kusema chochote kumbe?" Alvin

alimpuuza tu.

Lisa akasema, “Hapana, hapana. Wewe ni mcheshi, Sam Harrison. Uwepo wako unanifanya nihisi nimetulia zaidi.”

“Unamaanisha kwamba huna utulivu unapokuwa pamoja nami?” Alvin

aligeuka ghafla.

Lisa alisafisha haraka hali ya hewa.

“Hivi mtu aliyependa huwa ana utulivu kweli? Unapokuwa na mtu

unayempenda, unahisi kana kwamba

moyo wako unadunda kwa nguvu kila wakati na unashindwa kabisa kuutuliza."

Alvin aligonga usukani kwa kidole bila

kusema chochote. Pamoja na taaluma

yake ya uanasheria, alikuwa amekutana na mjuzi wa kubumba na kuchezea

maneno kama yeye.

Akiwa ameketi kando ya Alvin, Sam alishikwa na wivu. Hakuwahi kukutana na msichana yeyote ambaye aliendelea kukiri mapenzi yake kupitia hotuba

yake. Lisa akabaki kimya akicheza na simu yake katika siti ya nyuma. Ghafla, Pamela alimtumia video mbili. Pamela alikuwa na kawaida ya kumtumia video za vichekesho. Lisa alifikiria vivyo hivyo wakati huo, kwa hivyo alibofya video

hizo mara moja. Kabla hajajua niki

kitajiri, sauti kali ilijaza sehemu sehemu yote ya ndani ya gari. Tukio la ajabu

likaonekana kwenye kioo cha simu yake baadaye. Lisa aliingiwa na kiwewe cha ajabu na kuizima simu mara moja.

Hata hivyo, gari lilikuwa tayari

limesimama. Wanaume hao wawili

walimtazama kwa namna ya ajabu.

Mara moja, alitamani kukimbia kwa

kuruka nje ya dirisha.

“Aha… Acha nieleze. Nilikuwa nikisoma kitabu na mara kirusi kikaingia...” Lisa alibabaika.

Sam aligusa pua yake kwa sura ya aibu.

“Sawa shemeji. Ni kawaida tu, hata

mimi hutazama hizo vdeo kwa siri nyumbani. Sikujua kwamba na wewe

huwa utazama mpaka kwenye gari.”

Lisa alikosa la kusema.

Uso wa Alvin ulijawa na hali ya huzuni.

"Ninakuonya, usitazame tena mambo

machafu kama hayo hata kama ni kwa siri"

SURA YA39

Alvin alipandwa na hasira kila alipofikiria

kuwa Lisa alikuwa akimwangalia

mwanamume mwingine akiwa uchi

kwenye video. Hakuwa na haya kama nini! Sam alimtetea Lisa, "ili kuiweka kwa njia

nyingine, inaweza kuchukuliwa kama nyenzo ya kujifunza wakati mwingine.

Labda shemeji anajifunza kwa ajili yako."

Lisa aliitikia kwa kichwa chinichini,

akikubaliana na kauli ya Sam. Lakini

Alvin alizungumza kwa sauti ya huzuni,

“hakuna haja ya hilo. Hatahitajika

kufanya hivyo na mimi. Hata kama hilo

likitokea, mimii ndiye nitapanga tufanyeje, si yeye.”

Kauli ya Alvin ilikuwa tofauti kabisa na vile alivyoamini Lisa. Sasa alifahamu

kwamba Alvin hakuvutiwa naye hata

kidogo, aliinamisha kichwa chini kwa

kukata tamaa. Sam akamtazama kwa

huruma. Kisha akahema kwa masikitiko

baada ya kuona jinsi Alvin alivyokuwa

mkatili wa hisia zake na hana mapenzi naye. Baada ya nusu saa, gari lilisimama.

Lisa aliinua kichwa chake na kugundua kuwa walikuwa wamefika ‘Miracle studio’, saluni ambayo ilitoa huduma ya urembo na mitindo mbalimbali. Ingawa

hakuwahi kufika hapo awali, alisikia

kwamba ‘Miracle Studio’ ilikuwa saluni

ya kike inayojulikana zaidi kwenye huduma ya urembo na mitindo huko

Masaki.

Alvin akageuka na kusema, “Nenda wakakuhudumie kwanza, mimi kuna

jambo naenda kufanya. Nitakuchukua baada ya muda mfupi.”

Lisa alipigwa na butwaa. "Alvlisa, labda

hujui utaratibu wa saluni hii kuwa

haikubali mtu yeyote hata kama wewe

ni tajiri kiasi gani hadi uwe umeweka

appointment mwezi mmoja kabla.”

“Alvinani?” Sam akaangua kicheko. Muda mfupi baada ya kuanza kucheka, macho makali yakaelekezwa kwake. Uso wa Sam uliganda kidogo, kisha

akasema haraka, “Hatuhitaji kuweka nafasi. Nenda tu juu. Nimemjulisha mhusika mkuu kuhusu hilo.”

“Oh.” Lisa alipumua kwa siri kwa kuridhika. Kwa hakika, familia ya Harrison ilikuwa familia yenye nguvu sana, hawakuweza kupingwa kwa lolote. Mara tu alipopanda ghorofani, meneja wa saluni alimkaribisha na kumfanyia huduma binafsi ya urembo na mavazi yeye binafsi.

Saa moja baadaye, Alvin alikuwa

amerudi, lakini Lisa hakuwa amemaliza

kuhudumiwa. Alvin alikaa kwenye kochi

na kumsubiri kwa muda. Upesi mlango wa chumba cha watu mashuhuri

ulifunguliwa na Lisa akatoka nje akiwa

tofauti na alivyoingia. Alivalia vazi refu

lililopambwa kwa almasi mwili mzima. Sio tu kwamba vazi hilo lilikuwa la kung'aa, lakini pia lilifafanua sura ya umbo lake la kuvutia na kupendeza

kikamilifu. Nywele zake, ambazo zilionekana kuwa nyeusi kama mwani, zilijipinda kwa mawimbi na kuanguka juu ya mabega yake. Alionekana

mrembo na mwenye kuvutia kuliko siku zote.

Macho ya Alvin yalimtoka kwa hisia

inayowaka. Kwa muda mrefu alikuwa amejua uzuri wake. Tofauti na wanawake wengine wengi siku hizi, hakuwa amepitia upasuaji wa plastiki ama kuongeza makabrasha mengine

mwilini ili kuwa na uzuri kama huo.

Hakutarajia kuwa angeonekana kuvutia

sana hata akiwa amejipodoa kidogo tu.

"Alvlisa,

Mara tu Lisa alipoona macho yake, midomo

ninaonekana mzuri?"

yake iliangaza tabasamu la furaha.

Alitembea kuelekea kwake, akitumaini kwamba angeelekeza macho yake kwake.

Alvin alikaa kimya huku akikazia macho

yake kifuani mwake. Lisa aliona haya baada ya kuona hivyo. Alihisi macho ya

Alvin kama yanamchoma kifua. "Hey, unatazama nini?"

Alvin aliongea kwa mkazo, kinyume na matarajio ya Lisa. "Nenda ukabadilishe."

“Kwanini, kwani kuna shida gani?”

Lisa alichanganyikiwa.

"Nguo hii inakufichua sana, siipendi.”

Aligeuka na kushuka chini mara baada ya hapo.

Kwa hasira, Lisa alihisi bomu la atomiki

likilipuka kichwani mwake. Kutokana na

mtazamo wake mapema, ilikuwa

imempa hisia kwamba alikuwa

amevutiwa naye, lakini alivyobadilika

kwa kauli yake akashindwa kumwelewa kabisa. Msimamizi wa duka kando yake alisema

kwa tabasamu, "Bi Jones, Bw. Kimaro anakujali sana." Lisa alitoa macho na

kumtazama meneja wa duka. Macho yake yalionyesha hali ya kutokuamini.

“Kwa kawaida, mwanamume anapomjali sana mwanamke, anakuwa na wivu

naye. Asingetaka mwanamke wake avae mavazi ya kuvutia wanaume

wengine, na ni yeye pekee anayeruhusiwa kukuona hivyo.”

Kwa tabasamu meneja wa saluni

aliongeza, “Baada ya kufanya kazi hapa

kwa miaka mingi, nimekutana na

wanaume wengi lakini wachache wa aina ya Kimaro. Mimi ni mjuzi mzuri wa tabia za wanaume.”

Aliposikia maneno yake, Lisa alijawa na moto wa matumaini. Je, Alvin hakutaka watu wengine wamwone akiwa amevaa

nguo za kufichua umbo lake? Hiyo liliwezekana. Lisa alibadilisha na kuvaa nguo ndefu nyeupe ambayo haimkumbana sana. Ilimpendeza lakini haikuyafichua

maumbile yake. Baada ya hapo akashuka chini na bila kutarajia, alimuona Alvin akivuta sigara. Alvin alivuta sigara mara chache sana. Siku

hiyo labda ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona akifanya hivyo hadharani.

Hata hivyo, alionekana kuvutia tu alipovuta sigara. Kwa kuwa alikuwa akimpenda Alvin, chochote

atakachofanya hakika kingeonekana

kuwa kizuri tu kwake.

Lisa alimwendea na kumvuta mkono.

"Alvlisa, nguo hii ni sawa?"

Alvin alimtupia jicho la kuridhika. Wakati

huu, alikuwa amevaa kizamani, kistara na kujisikia kifahari. Lakini bado Alvin

alikuwa na uhakika kuwa Lisa angevutia macho ya watu usiku huo. Ghafla, alijuta kuchagua kumtoa nje. Alipaswa kumficha.

“Twende zetu.” Alvin aliiweka sigara kwenye sinia ya majivu na kuongoza kutoka nje.

Akiwa ameshika gauni lake, Lisa alitembea taratibu kiasi. Wakati

Alvin alipogeuza kichwa chake, uso wake ulikuwa umekunjamana.

Akamsogelea na kumuinua kiunoni moja kwa moja. Kwa ushirikiano, Lisa

aliweka mikono yake shingoni mwake, kisha akatazama kidevu chake kizuri.

Alichukuliwa na mshangao wa sura yake ya kuvutia.

Lisa akamuuliza kwa upole, “Hukuniruhusu nivae lile gauni kwa sababu ulihisi linaufichua sana mwili

wangu? Je, ni kwa sababu unanipenda au?” Pamoja na hayo, kulikuwa na hali ya ukimya. Baada ya kushuka chini, Alvin alimweka Lisa moja kwa moja

kwenye siti ya nyuma ya gari lake. Kwa sauti ya kejeli, alisema, "Kitaalam, wewe ni mke wangu, hata hivyo. Sitaki uvae kwa njia isiyofaa na kujidhalilisha.” Uso wa Lisa ulimtoka. Hakujisikia

kuzungumza naye katika safari yao yote. Gari liliingia ndani ya nyumba ya familia ya Harrison iliyojaa wageni. Msururu wa magari ya kifahari ulionekana kwenye

eneo la maegesho nje ya jumba hilo la kifahari. Lisa alikasirika kidogo kwani

hakuyaona magari ya akina Masawe na Mushi. Ethan angetokea pale, bila

shaka angeshangaa kumuona akiwa

amemshika mkono mjomba wake.

Waliingia ndani huku mikono ya Lisa ikiwa imeizunguka mikono ya Alvin.

Alvin aligeuza kichwa chake na kumpa ukumbusho, “Usiku wa leo, unaweza kujidai hadharani kwamba wewe ni mpenzi wangu.”

Macho ya Lisa yalimtoka. Dakika

iliyofuata, hata hivyo, Alvin akabadilika tena. “Usiwe na furaha kupita kiasi. Hii ni kwa sababu sitaki tu Mzee Harrison anitambulishe kwa msichana mwingine.”

Katika usemi huo, Lisa alijihisi kutumiwa kama ngao tu, na uwepo wake ukakosa maana ghafla! Lisa alikosa la kusema.

“Sawa. Niko tayari kukulinda kutokana na kila aina ya majanga na kukusaidia bila kujali!”

Kabla hajamaliza maneno yake, msichana mmoja aliyevalia gauni la rangi ya shampeni alitembea kuelekea kwa Alvin kwa umaridadi. "Alvin, ni muda mrefu umepita tangu tulipokutana mara ya mwisho."

Lisa alishindwa kuendelea na kitendo chake. Msichana huyo alikuwa binti mdogo wa familia ya Harrison, Angela Harrison, ambaye pia alikuwa dada mdogo wa Sam. Lisa alikuwa amemwona mara moja kwa mbali alipohudhuria hafla furani ya chakula cha jioni kipindi cha nyuma. Kutokana na usemi wake uliojaa sauti nyororo, Lisa alifikiri kwamba Angela angeweza kuwa mshindani wake.

“Alvin, vipi mbona mkeo hujaja naye

leo? Ni muda mrefu umepita tangu

nilipomwona mara ya mwisho. Nimem’miss sana.”

"Hajambo," Alvin alijibu kwa unyonge.

Angela kisha akapiga kelele. “Alvin, mbona umekuwa Dar kwa muda mrefu, lakini hukuja kuniona. Bado

unakumbuka kuwa uliahidi kutazama jinsi ninavyoimba na kucheza violin?

Hujatimiza ahadi.” Kwa hayo alimkazia macho Alvin kwa husuda.

Lisa alishikwa na wivu. Alikuwa

amesimama pale pale, lakini Angela alionekana kumchukulia kama hamuoni

vile. Lisa akajikoholesha na kusema.

“Alvlisa, unaweza kumtambulisha

kwangu? Yeye ni…?” Lisa alimshika mkono Alvin huku akionyesha sura ya kimahaba. SURA YA 40

Alvin alitabasamu alipoona jinsi

Lisa alivyopata wivu haraka. “Dada yake Sam.”

“Yeye ni nani? Kwa nini yupo karibu yako” Sura ya uchungu ikapita usoni

mwa Angela.

Akikunja midomo yake myekundu, Lisa alisema, “Halo, Bi. Harrison. Mimi ni mpenzi wake. Huenda hujaniona

hapo awali, lakini ulipaswa kusikia

kuhusu jina langu. Mimi ni Lisa Jones, msichana mrembo zaidi niliyetokea

kuuteka moyo wa Alvin.” Mdomo wa Alvin ulimsisimka kwa maneno yake ya aibu. Angela alitoa macho huku akiwa

haamini jinsi msichana huyo alivyokosa

aibu. Kisha akadhihaki, “Hehe.

Samahani, sijasikia kuhusu wewe kuwa

msichana mrembo zaidi. Hata hivyo, nimesikia kuhusu tabia ya kipumbavu ya

Lisa kutoka kwa familia ya Jones

Masawe hivi majuzi. Ulipoteza urithi

wako kwa dada yako, ambaye alitoka

mashambani, akapewa haki ya urithi wa familia ya Masawe, na baadaye ukafukuzwa kutoka kwa familia hiyo. Siamini kuwa Alvin angetaka kuwa na mtu kama wewe usiye na future yoyote...”

Lisa alihisi kana kwamba kuna kitu kimepenya moyoni mwake. Alikosa la kusema.

“Angie.” Macho ya Alvin yalimwelekea Angela. “Jiangalie. Lisa ni mpenzi wangu kweli.”

“Inawezekanaje?” Angela aligeuka rangi. "Hata halingani na hadhi yako nzuri."

Lisa hakuridhika, akajibu mapigo ya Angela, “kwanini nisiendane naye? Mimi ni beatuful na yeye ni handsome. Tunaposimama pamoja, tunaendana

vizuri kwa sura. Mtoto wetu wa baadaye

bila shaka ataonekana kuvutia.”

Mdomo wa Angela ukasisimka kwa hasira. Alisema kwa kejeli, “Unajidanganya. Utapunguza IQ ya kizazi cha Alvin."

Kuwatazama wanawake hao wawili

wakirumbana kulimfanya Alvin apate maumivu ya kichwa. Kisha akapiga paji

la uso wake na kusema. “Sawa, Angie.

Nitapeleka salamu zangu kwa babu

yako sasa. Tutaonana baadaye.”

Alipomaliza kuongea, alipiga hatua

kuelekea kwenye jengo kuu akiwa na

Lisa bila kumsubiri Angela ajibu.

Lisa akafunga mdomo wake, hakusema

neno lolote katika safari hiyo. Kwa vile

alikuwa akila vizuri na kulala vizuri kwa

siku za karibuni, mashavu yake

yalikuwa yamenenepa tena. Alionekana

mrembo sana.

Alvin alinyoosha mikono yake ili kuyabana mashavu ya Lisa huku

akimwambia. “Angie bado ni mtoto, na amekuwa akidekezwa tangu akiwa

mdogo. Usijishushe kwa madhaifu yake.”

Lisa akacheka. "Usijali, sitajishusha kufikia kiwango cha Angie. Kwa kuwa upo naye karibu sana, kwanini hukufikiria kumfanya ajifanye mpenzi wako? Baada ya yote, unalibebisha hadi jina lake, unamwita Angie. Mimi ni mtu wa kukaa tu kama picha, mtu ambaye hata jina langu linakukera.”

Alvin akajibu, “…Kwa hiyo ni kwa sababu nilimuita Angie na sikuiti Lisa?”

"Bila shaka hapana. Je, mimi ni mtoto mdogo kuweza kuona hisia za mtu?"

Lisa alidlazimisha tabasamu.

Alvin alijihisi mnyonge ghafla. "Angela

alikuwa akicheza na Sam na mimi nyuma ya nyumba tulipokuwa wadogo.

Ninamchukulia kama dada mdogo."

Hapo hapo wakafika kwenye jengo kuu. Akiwa amevalia suti yake safi, Mzee

Harrison alimpungia mkono Alvin kwa nguvu. “Alvin, yaani leo ndo unakuja

kuniona ingawa umekuwa Dar es

Salaam kwa muda mrefu sasa. Kwanini

kunisusa hivi? Unanidharau kwa sababu mimi ni mzee?” Aliongea huku akikenua

tabasamu la kizee, Mzee Harrison.

“Hapana kabisa. Unaonekana mdogo kuliko hapo awali, Mzee Harrison.” Alvin alimkabidhi mzee yule zawadi yake ya siku ya kuzaliwa.

Mzee Harrison alielekeza macho yake

kwa Lisa na Alvin akamtambulisha.

“Huyu ni mpenzi wangu.”

“Ah, hatimaye umepata mwenzi. Hiyo inasikitisha. Hapo awali nilipanga kukupatia mtu. Kuna wanawake wengi wa ajabu hapa." Mzee Harrison alimkabidhi zawadi Lisa . “Hii hapa ni zawadi kwa ajili yako tunapokutana kwa mara ya kwanza, mke wa mjukuu wangu. Alvin ameteseka sana katika maisha yake. Tafadhali mtunze.”

Lisa alifurahishwa. Hakuwa na uhakika

kama aikubali au laa. Isingeonekana vizuri kama angeikataa.

"Ikubali tu kwani ni ishara ya upendo ya Mzee Harrison kwako." Alvin alitikisa kichwa.

Lisa alipopokea zawadi hiyo, Alvin akampigapiga mgongoni. "Nisubiri

kwenye ukumbi wa wageni." Pengine

alikuwa amekwisha maliza kucheza

kipande chake, hivyo akamwona hana

umuhimu tena kuwa karibu yake. Lisa

akajiondokea zake.

Aliposhuka tu aligongana tena na Angela. "Ulikuwa unanisubiri hapa kwa makusudi, Bi.Harrison?"

Bila kustaajabisha, tabasamu lilitanda usoni mwa Angela. Angela alinyanyua kidevu chake kwa maneno ya jeuri.

“Afadhali ukae mbali na Alvin. Yeye si mtu unayeweza kumudu kuwa naye.”

“Itakuwaje kama sitakaa naye mbali, eeh?” Lisa aliuliza kwa shauku ya

kutaka kujua. “Unampenda sawa, lakini yeye anakuchukulia tu kama dada mdogo.”

Angela alibaki akihema. "Kwa hiyo?

Kwa familia ya kifahari kama Kimaro, wanajali kuhusu ndoa iliyolingana vizuri

katika suala la hadhi ya kijamii. Kusema

ukweli hata humjui vizuri Alvin.

Wanafamilia yake hawatakukubali kwa

sababu hulingani naye. Kwa sasa, anaburudika tu na wewe. Familia yake

itakutimulia mbali na hautakanyaga hata msingi tu wa geti.” Alidhihaki kwa kejeli na baadaye akaondoka kwa njia ya kiburi.Lisa alikasirishwa kwa namna

fulani na maneno yake lakini hakufikiria kabisa. Hata hivyo cheti cha ndoa

kingekuwa tegemeo lake kubwa kwa wakati wote.

Baada ya Lisa kuondoka kwenye jengo

kuu, punde alikutana na Pamela.

“Angalia, hii ndiyo pombe

niliyotayarisha. Nitatafuta mtu wa kumlewesha Alvin baadaye. Ikiwa

hajalewa, lazima uchukue mbinu

yoyote kwa kumfanya ale hii kitu.

Kumbuka, hii itaanza kutumika saa mbili

baada ya kuila." Pamela aliweka vitu

vile mikononi mwa Lisa.

Lisa alijisikia vibaya sana. "Je, hii

itasababisha madhara yoyote?"

“Mbona bado una wasiwasi nami kwa jinsi ninavyokupambania? Haina shida na haitaathiri afya yake.”

"Ikiwa atashtukia, hakika ataniua."

Lisa aliogopa.

“Labda awe hanithi lakini kama ni rijali hatatoboa! Ikiwa ningekuwa mwanamume nikaamka na kumwona

mwanamke mrembo kama wewe akiwa amelala kando yangu asubuhi na mapema, bila shaka ningehisi raha.

Alvin pia ni mtu wa kawaida.” Pamela alimtoa wasiwasi.

Lisa alivutiwa na maneno yake. Muda mfupi baadaye, Alvin alirudi.

Alvin alipofika tu mlangoni, kuna mtu wa ajabu alienda kumsumbua. "Bw.

Kimaro, sifa yako inakutangulia. Kwa

kweli, kwa muda mrefu nilitaka

kukufahamu. Ngoja nikupe toast.”

“Kunywa tu mwenyewe. Sihitaji kinywaji.” Baada ya kukutana na watu

kama yeye mara nyingi sana tangu ujana, Alvin hakutaka kuwa karibu nao.

Kisha Alvin aligongana na watu

wachache kama hao ambao alibaki

kuwa jeuri kwao. Pamela alipumua, akitazama tukio hilo kwa siri. “Jamani, mumeo ni mtu wa kipekee ambaye

haonyeshi heshima kwa wengine hata

kidogo. Bado hajanywa hata glasi moja

hadi sasa, ana kiburi. Watu wasiomjua wangedhani kwamba anatoka katika

familia yenye nguvu zaidi nchini.”

“Ngoja nimfuate.” Lisa alimwambia

Pamela huku akijongea kwa Alvin.

Muda si muda Alvin akamtazama

Lisa ambaye alimsogelea kimya kimya.

Lisa alifikiri kwamba Alvin angekuwa

busy kujichanganya na wengine na kuzungumza mambo ya biashara kama

watu wengine walivyofanya. Hata hivyo, walikuwa wakihudhuria sherehe ya kuzaliwa iliyojaa watu wa tabaka la juu ambapo ilikuwa ni kawaida kwa watu kupanua mitandao yao. Lakini Alvin alijitenga nao na kumpeleka Lisa nyuma ya ukumbi ambapo waliketi na kunywa.

“Si unatoka kwenda kujumuika?

Ninaona matajiri wachache kutoka sekta ya fedha.” Alijaribu kumshawishi atoke nje. Aliingiwa na hofu kwani asingeweza kufanya lolote ikiwa angeendelea kubaki naye.

"Sipendezwi." Alvin alipiga kinywaji

chake kama hataki hivi.

Lisa akapepesa macho. “Unataka nikumiminie mvinyo kidogo? Kuna

mvinyo hapa wa kiitaliano unaonekana

kuwa na ladha nzuri."

"Ikiwa unataka kuinywa, endelea. Lakini utafute kabisa pa kwenda endapo

utailewa na kufanya vituko.” Alvin alijibu na kumpa tahadhari.

Baada ya kukaa kimya, mara Lisa alisimama tena. “Ngoja nikuletee chakula, sawa? Hujapata chochote usiku wa leo.”

"Hakuna haja." Hakupendezwa na chakula kingine chochote zaidi ya chakula alichopika Lisa.

"Hapana. Chakula ni nishati kwa

wanadamu. Lazima ule kitu hata kama

hujisikii, jilazimishe kiasi.” Kwa hayo, Lisa alitoka kwenda kuchukua matunda na vyakula vingine.

Kwa siri, Lisa alitia kile kitu alichopewa na Pamela kwenye chakula. Aliporudi, aliweka chakula mbele ya Alvin. Kisha, akaweka kipande cha nyama ya mbuzi iliyochomwa karibu na mdomo wake.

Kwa kuwa ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya kitendo hicho kiovu, alihisi

kukosa amani. Mikono yake ilitetemeka hasa pale macho makavu ya Alvin

yalipomkazia usoni. Aliapa kwamba angekata tamaa ikiwa Alvin angekataa kula. SURA YA 41

Muda mfupi baadaye, Alvin aliinamisha kichwa chake na kula kipande cha nyama alichokuwa ameshika Lisa.

"Endelea kunilisha." Alvin alinogewa. Lisa alikosa la kusema. Hata hivyo,

aliendelea kumlisha chakula chote

kwenye sahani huku akihisi woga na

hatia. Alvin aliinuka mara baada ya kumaliza kula. “Twende nyumbani.”

Lisa alishtuka. "Tunaenda nyumbani saa hii?" Haikuwa imefika hata saa mbili bado. Ikiwa wangeondoka mara tu baada ya kula, bila shaka Lisa angekuwa mtu wa kwanza kushukiwa baadaye.

“Wewe usiondoke. Unaweza kukaa

hapa usiku kucha.” Alvin aliweka msimamo. Alvin aliona ni kupoteza muda kujichanganya na watu wengine, hakuwa pale kwa ajili ya kujionyesha.

Alijitokeza tu pale kwa ajili ya heshima yake kwa Mzee Harrison. Kwa

kuzingatia kwamba alikuwa akisisitiza

kuondoka, Lisa hakuwa na jinsi zaidi ya kuondoka pamoja naye.

Baada ya kuingia kwenye gari, alimkabidhi zawadi ambayo alipokea

kutoka kwa Mzee Harrison.

"Ishike," Alvin alisema kwa upole.

“Lakini ni ghali. Sidhani kama ni lazima nichukue…”

“Hii ni ghali kwako tu." Alvin alitabasamu

kwa dharau hafifu. Inavyoonekana, alikuwa akidhihakiwa kama maskini.

Lisa alitazama chini akaingiwa na hofu akijua kwamba kuna dhoruba ingetokea muda si mrefu.

Walipofika nyumbani, alimtazama kwa

siri Alvin kwa nyuma huku akiwa na

woga na wasiwasi, akijisemea

kimoyomoyo. 'Samahani, Alvin. Hakika

nitakutendea vyema siku zijazo. Nitii tu usiku wa leo.’

Baada ya kuingia ndani, Alvin alienda

kuoga. Kisha akaelekea kwenye

chumba chake cha maktaba ili ili

kufanya mkutano kwa njia ya video.

Katikati ya mkutano huo, ghafla alihisi

mwili wake unawaka moto. Hakujisikia vizuri hata baada ya kuvua koti lake.

“Uko sawa, bosi? Uso wako

umekunjamana.” Msaidizi wake upande wa pili wa video aliuliza kwa mshangao.

“Sijisikii vizuri. Tuendelee kesho.

Mfuatilie kwa uangalifu Jack Kimaro

huko.” Alvin alizima kompyuta yake na kurudi moja kwa moja bafuni kwa ajili ya kujimwagia maji baridi. Haijalishi

alijimwagia maji kiasi gani, bado alihisi joto likpanda kwa kasi. Alijua kwamba

kuna jambo lilikuwa baya kwake. Hakula wala kunywa sana usiku ule, lakini

kwanini… Subiri! Alikuwa amekula

chakula alichochukua Lisa. Kwa wazo

hili, uso wake ulionyesha hasira kali.

Alithubutuje!

Mlango wa bafuni ulipigwa teke kwa

kishindo. Jambo hilo lilimshtua sana

Lisa aliyekuwa akitandika kitanda

chake. Alimwona Alvin akimfuata, matone ya maji yamefunika mwili wake.

Uso wake ulijaa ukali. “Dawa yake

ilianza kumchukua ama?” Lisa alijiwazia. “Kuna nini… Una shida gani?”

Lisa alikurupuka huku akirudi nyuma kwa hofu. Ghafla, aliogopa.

"Uliweka nini kwenye chakula ulichonilisha kwenye sherehe?"

Alvin alimshika mkono na kumburuta kutoka sakafuni. Macho ya

Lisa yalimtoka. Hakutarajia kwamba angefahamu mapema namna ile.

“Mimi… sijui unasema nini.”

"Bado unakataa, huh?" Alvin akaibana shingo yake, macho yake yakidhihirisha chuki. "Nani mwingine angepata nafasi ya kufanya huu ujinga kama si wewe?"

Lisa alikuwa karibu kukosa hewa. Hakuwahi kufikiria kwamba majibu ya

Alvin yangegeuka kuwa ya kutisha sana. Aliogopa sana. “Ilikuwa… mimi

ndiye niliyefanya… Samahani!” hatimaye Lisa alikiri.

Shingo ya Lisa iliuma sana hivi

kwamba machozi yalitiririka usoni mwake. Alihisi kwamba alikuwa

amekutana ana kwa ana na Ziraili!

Alijuta sana!

“Mwovu kiasi gani wewe! Nilikuamini sana!” Hasira zikamlipuka Alvin kifuani.

Kwa nini afanye jambo kama hilo?

Alichochukia zaidi maishani mwake ni kudanganywa! Alimchukia, lakini

taratibu alianza kuhisi anapoteza

fahamu. Baada ya kutoka nje ya

udhibiti, akamtupa Lisa kitandani. Nguo

za Lisa zilichanika kwa sababu ya

vurumai hiyo. Aliamka na kukimbilia

bafuni kuoga tena.

Kelele ya mshindo wa mlango ikasikika.

Mshindo huo ulimfanya Lisa ahisi kama

umepiga moyoni mwake.

Lisa alitetemeka kwa woga huku

akijizuia kulia. Alipojiuliza ni nini kingeendelea baada ya hapo alikosa

nguvu kabisa. Alikuwa amekosea!

Alikuwa amekosea sana. Hakupaswa

kushawishiwa kutumia mbinu ya aina

hiyo! Lisa aliacha macho yake yatoe

machozi, akijihisi mwenye hatia sana.

Maji katika bafu yalimwagika kwa dakika

45. Akiwa na wasiwasi kuwa kuna

jambo limemtokea Alvin, Lisa alijipa

moyo na kuusogelea mlango wa bafu

na kuugonga. "Uko salama? Samahani.

Je! unanihitaji—”

mwanamke kama wewe.” Mlango wa

"Nyamaza. Afadhali nife kuliko kumgusa

bafuni ulifunguliwa kwa nguvu. Akiwa

amelowa kichwani hadi miguuni, Alvin alimtazama Lisa kwa macho mekundu yaliyoiva hasira. Lisa aliduwaa kwa mshangao. "Uliweka kiasi gani kwenye chakula?"

Alvin alikuwa katika hali mbaya lakini alijikaza tu na kujifanya mgumu.

Hakutaka kabisa kujishusha na kukubali msaada wa Lisa. Kwa hasira, alimvuta

bafuni na kumlowesha kwa maji ya baridi. Kabla hata maji ya baridi

hayajamwagika kichwani mwake, Lisa alianza kutetemeka. Ni pale tu Alvin alipogundua kuwa anashindwa kupumua ndani ya maji ndipo alipomwachia. Alilaani kwa sauti nzito na kuupiga mlango kwa nguvu. Kisha, akavaa nguo zake na kukimbia nje

haraka. Lisa alitoka bafuni kwa aibu.

Alitaka kumfuata, lakini alikuwa amechelewa.

Saa sita usiku Sam alikimbia hospitali na kumkuta Alvin akipokea dawa kwa

njia ya dripu kitandani. Wakati huo, alipigwa na butwaa, asijue amcheke au amhurumie Alvin kwa jinsi alivyokuwa akihangaika kumtuliza askari wake

aliyeng’ang’ana kusimama wima muda wote. Sam alijikuta akimuonea wivu

Alvin, alitamani tukio hilo lingemkuta yeye, asingelaza damu. Uso wa alvin

ulikuwa bado haujatulia kwa wakati huo.

“Kwa nini umekuja kutesekea hospitalini? Ulipaswa kumtii Lisa mara moja na kumaliza matatizo yako

nyumbani. Suala hilo lingetatuliwa

chumbani kwako.” Sam alimwambia

Alvin huku akizuia kicheko chake.

nitakachokufanyia.” Alvin aliyakodoa

“Sema hivyo tena uone

macho yake yenye uchungu. Alikasirika

sana hata akakaribia kumpiga chupa ya dawa kichwani. Hans alikunja uso. “Zingatia maneno

yako, Bwana Harrison. Bwana Kimaro

hapendi kabisa wanawake wanaotumia

mbinu za aina hii.”

Sam alipigwa na butwaa. Ilimjia

kumbukumbu kwamba Alvin alishawahi

kumsimulia kisa cha mama yake

kutumia dawa za nguvu za kiume

kumlazimisha baba yake kulala naye

kimapenzi na mimba iliyotokana na kitendo hicho ndiyo iliyomzaa Alvin.

Alvin alikua hana mapenzi ya baba yake. Alvin aliamini kuwa alikuja

duniani kwa kupitia mbinu hizo chafu za

mama yake. Kwa hiyo, alichukizwa na

matumizi ya mbinu hiyo, ambayo

ilitosha kuelezea kwa nini alichukizwa

sana na kitendo cha Lisa.

"Ikiwa hutaki kumuona tena, mwambiee aondoke," Sam alipendekeza baada ya kushusha pumzi.

Alvin alicheka. “Hata nikimfukuza anaweza asiondoke. Kwanza hana hata pa kwendai."

“Kwa nini usihamie kwingine? Nitakusaidia kutafuta sehemu nzuri huko Mbezi Beach.” Sam alipendekeza.

“Hapo ndipo mahali pangu. Kwanini niondoke?” Aliuliza kwa dharau Alvin.

Ghafla Sam aliinua macho yake na kuuliza kwa shauku, "umekaa naye kwa muda mrefu sasa, lakini kwanini huna hisia zozote kwake?"

"Hisia?" Alvin alidhihaki. “Vipi kuhusu hisia zako kwa mfanyakazi wa

nyumbani anayepika chakula cha

familia yako? Labda ningevumilia

uwepo wake kama asingenifanyia hivi, lakini sasa… sitamsamehe.”

Sam akatoa macho. “Vipi kuhusu kumlipizia kisasi? Mfungie chumbani

umlishe na yeye hivyo vitu halafu

mwache apate maumivu kama

unayopitia wewe.”

Alvin alijibu kwa ukali, "sitaki tena kusikia mawazo yako yakijinga, Sam.”

SURA YA 42

Saa kumi alfajiri, Alvin alimaliza dozi

yake ya dawa za dripu. Alirudi nyumbani tu baada ya ‘joto’ mwilini mwake

kupungua. Mara baada ya kuingia ndani ya nyumba yake, alimuona Lisa akiwa

amelala fofofo kwenye kochi lililokuwa

pale sebuleni. Hapo awali, alidai

kwamba aliogopa kutokana na ndoto

mbaya ikiwa alikuwa peke yake

chumbani. Hata hivyo, alionekana kulala vizuri wakati huo. Alvin alihisi yote

yalikuwa ni sehemu ya mbinu zake

chafu. Ni nini kilimpa haki ya kumfanya apate

maumivu makali na kupokea sindano ya dripu hospitalini na yeye akiwa amelala

kwa raha ndani ya nyumba? Kwa hasira kali, alichukua maji kutoka kwenye

meza na kummwagia moja kwa moja usoni. "Amka."

Lisa alishituka kwa mshtuko, akamkuta

Alvin akiwa amekaa upande wa pili wa kochi. Alihisi kama amekutana na shetani. Huku akitetemeka, Lisa aliuliza, “Ulirudi saa ngapi? Kwahiyo… Mambo

vipi sasa?”

"Kwa sababu yako, nilikuwa na dripu ya sodium chloride IV usiku kucha hospitalini." Alvin alipomtazama

Lisa, tukio la yeye kuteseka hospitalini

usiku mzima lilimpitia tena mawazoni. Ilimfanya ahisi kudhalilishwa sana.

“Lisa, ninachojutia zaidi maishani mwangu ni kukuoa. Sikupaswa

kukuokoa ulipokuwa umefungwa kwenye jumba la kizamani hapo awali.”

Lisa alipandwa na hasira, lakini hakuwa

na haki ya kukasirika. Kama ni yeye

ndiye angekuwa amentendewa kama

Alvin, bila shaka asingefurahi pia, hivyo

akaona jambo la maana ni

kumwangukia kwa msamaha.

“Samahani… samahani sana…

sitafanya tena wakati mwingine.”

"Wakati mwingine?" Alvin alibana

kidevu chake kwa nguvu. “Unafikiri bado

kuna wakati mwingine? Ninachukia

kukutazama tu. Ulitaka kunilazimisha

nilale na wewe kwa kutumia hila chafu.

Huna aibu? Wewe ni mchafu kama

makahaba wa barabarani!” Alvin

aliongea kwa hasira kana kwamba

ametiwa sumu.

Macho ya Lisa yalififia mara moja kwa kujawa na machozi, hakuweza kujizuia

tena kulia. Lisa alifikiri kwamba alikuwa mjinga sana. Alikuwa amefanya nini?

“Kulia ndo nini? Sitakuhurumia eti kwa sababu tu unalia.” Alvin alikerwa na kilio chake. “Sikiliza nikwambie, sitaki

kula chochote utakachotengeneza tena. Usionekane mbele yangu. Pia, usiingie

kwenye chumba changu cha kulala.

Uwepo wako hapa ni kero tu kwangu."

Alvin alielekea chumbani kwake mara baada ya kumaliza kuongea kwa hasira kali. Akiwa amelala chini, Lisa alikuwa

ameshuka moyo na amechoka kabisa.

Kwake, Alvin alikuwa ukuta usioweza

kuvunjika. Sio tu kwamba alishindwa

kudhoofisha ukuta huo, lakini pia Alvin

alimchukia kabisa sasa. Hah. Sawa.

Liwe liwalo. Asilazimishe kitu chochote ambacho si chake. Hakika ilikuwa ni kosa lake. Hakupaswa kumfanyia jambo la aina hiyo.

Yote aliyokuwa amefanya mpaka wakati

huo ilikuwa ni kumkosea tu Alvin, jambo ambalo lilimfanya ajione kuwa hana

maana kabisa kwake. Aliburuta blanketi lake na kurudi chumbani huku miguu

ikitetemeka. Wakati huo, alikuwa na kizunguzungu, mwili na roho vyote

vilikuwa vimekosa raha. Alijilaza

kitandani kupumzika. Muda si muda

alipitiwa na usingizi na kulala.

Kisha, aliamshwa na simu kutoka kwa

Pamela. “Kwa hiyo mambo yalikuwaje?

Uliifanikiwa?"

"Nini kimetokea?" Kwa tabasamu la uchungu, Lisa alimweleza tukio hilo

Pamela ambaye alizidiwa na hisia ya hatia. “Samahani Lisa, nimekuponza. Labda sikufikiria mambo vizuri…”

Lisa alimpoza rafiki yake aliyekuwa

akijihisi hatia. “Kwa vile hanipendi, sikupaswa kumlazimisha. Zaidi ya hayo, nilikutana naye kwa sababu za zangu binafsi. Pamela, unadhani sikupaswa

kuolewa na Alvin kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa Ethan?”

Pamela alipumua. “Tayari

yameshatokea. Nini kingine unaweza kufanya wakati tayari umefunga naye ndoa? Utakata tamaa na kudai talaka?"

Lisa alibaki kimya kwa muda. “Haki.

Ninapaswa kuomba talaka. Nahisi kama

sina amani kuendelea kuishi naye.” Lisa aliongea kwa uchungu na kukata simu.

Mlango wa chumba cha kulala ukiwa

umebaki wazi, aliona tayari

Alvin ameshatoka. Akashusha pumzi.

Baada ya tukio hilo, alionekana

kubadilika na kuwa mtu tofauti kabisa, jambo ambalo lilimfanya awe na wasiwasi mwingi.

Alipika chakula cha kawaida. Baada ya

kumaliza kula alipokea simu kutoka kwa

Joseph Ruta, bosi wake. "Lisa ,

umemaliza kutoa mchoro wa nyumba ya Bw. Mushi?"

“Nimemaliza."

“Sawa. Peleka mchoro kenye ofisi za

Golden Corporation utakutana na Kelvin

Mushi anakusubiria. Amekuwa

akihimiza kwa hilo.”

“Sawa.” Lisa hakuthubutu kuchelewa.

Alijiandaa haraka na kuelekea Golden Corporation.

Ofisi hiyo ilikuwa katika ukanda wa kibiashara katikati ya jiji, eneo

lililozungukwa na majengo marefu. Lisa

alijitambulisha vizuri kwa dada wa

mapokezi aliyemkuta kwenye ofisi za Golden Corporation. Dada huyo wa

mapokezi alimruhusu kupanda juu mara moja. Alipokuwa akingojea lifti, mtu

mmoja alitoka kwenye lifti nyingine. Kwa

kumbukumbu zake, alionekana kama

mama yake Ethan, Sonya Mushi. Sonya alishindwa kumtambua Lisa. Alielekea

tu kwa haraka kwenye mlango mkuu

akiwa na mkoba wake.

Wakati huo huo, lifti ilifika na mlio wa

‘ding!’ Lisa aliingia kwenye lifti huku

mashaka yakizidi kuibuka kichwani

mwake. Alikuwa amegongana na Ethan

maeneo ya Mbezi Beach alipokuwa

akitoka kuonana na Kelvin Mushi

kwenye jumba lake, na pale tena

alikutana na Sonya akiwa anaenda

kuonana na Kelvin pia. Ni bahati tu au kuna kitu ndani yake, je wawili wale walikuwa na uhusiano na Kelvin?

Lisa alianza kuunganisha nukta. Jina la ukoo la Kelvin lilikuwa ni Mushi. Je, anaweza kuwa jamaa wa Sonya?” Lisa

alijiuliza. Lakini, Lisa alikuwa hajawahi

kusikia kutoka kwa Ethan kabla ya hii

kwamba alikuwa na uhusiano na mtu mwenye nguvu kama Kelvin. Ghafla, kichwa kilimuuma kwa kuwaza mambo magumu aliyoshindwa kuyajua.

Lifti ilifika ghorofa namba ishirini na nane, Lisa alitoka kwenye lifti na baadaye akaingia katika ofisi ya bosi.

Ilitokea kwamba Kelvin Mushi alikuwa

akimsikiliza mgeni, kwa hivyo Lisa

alingoja kando kwa muda. Ni baada tu ya mgeni kuondoka ndipo aliwasilisha

mchoro na ufafanuzi wake kwa Kelvin.

“Kwa kweli, nilimpigia simu Joseph

kukuulizia bila nia yoyote ya kukuhimiza. Sikutarajia kuwa tayari ulikuwa umemaliza. Kwa kweli, wewe ni mzuri sana." Kelvin alichukua mchoro kutoka kwake. Alipopeleka macho yake kwa Lisa alipigwa na butwaa kwa muda. “Bi Jones, huonekani kuwa mchangamfu sana. Je, umekosa usingizi kwa kukesha ukiandaa mchoro huu?”

Lisa alipigwa na butwaa. Katika siku

mbili zilizopita, alikuwa amechoka kimwili na kiakili. Hakika, alionekana mnyonge. Kabla hajaondoka nyumbani alikuwa amejipodoa kidogo usoni.

Hakutarajia kwamba Kelvin angeona sura yake ya uchovu. "Ndiyo. Nilikosa usingizi hivi karibuni.” Alijibu tu ili

kumridhisha.

Kelvin alifikiri kwamba alikuwa

akisumbuliwa na kukosa usingizi

pengine kwa sababu Ethan na Lina

walikuwa wakienda kuchumbiana.

Hakuweza kujizuia kumuonea huruma

sana. Muda mfupi baadaye, jambo lingine likapita akilini mwake. Alikuwa

amesahau kushika kadi ya mwaliko

ambayo dada yake alimletea muda si mrefu!

Hata hivyo, alikuwa ameshachelewa.

Lisa aliishaiona kadi hiyo yenye

maneno 'Sherehe ya uchumba ya Ethan

Lowe na Lina Jones'. Alikazia macho na kutoa tabasamu hafifu. "Bw. Mushi, unajuana na familia ya Mushi na Masawe?"

Kelvin aliweka kadi ya mwaliko

pembeni, kisha akatoa kikohozi kidogo.

"Hao ni jamaa zangu wa mbali tu."

Alikuwa na wasiwasi kwamba huenda

Lisa angegundua kuwa yeye ndiye

mjomba wa Ethan, jambo ambalo

lisingemfurahisha kabisa. Zaidi ya yote, Lisa alikuwa binti kijana. Angeweza kukata tamaa katika kubuni

jumba lake kwa sababu hiyo. Kwa kumhurumia, Kelvin alitaka sana kumsaidia.

“Oh.” Jibu lake lilikuwa sawa na vile Lisa alitarajia. "Naomba nikueleze mchoro kwa undani, Bw. Mushi."

Kelvin aliitikia kwa kichwa. Kwa kuzingatia kwamba hakuwa mtaalamu wa mambo ya ubunifu wa majengo, alikuwa na uelewa mdogo kabisa wa mchoro wa kina. Hapo awali, Lisa alisimama mbele ya meza ya ofisi huku akielezea mchoro huo. Lakini, haikuwa rahisi kwani mchoro ulikuwa

umepinduliwa kutoka kwa pembe yake.

Kelvin alielekeza upande wake wa kulia. “Njoo usimame hapa.”

Baada ya kupata ruhusa yake, Lisa alipita kwenye dawati na kufika

upande wake wa kulia. Aliinama, kisha akanyoosha kidole kuelekeza eneo

fulani. "Niliogopa kuwa hakutakuwa na nafasi ya kutosha kuweka rafu za

vitabu, kwa hivyo nilipanga safu moja zaidi hapa ..."

Kelvin alitazama vidole vyake virefu na vyembamba vilivyofanana na ncha za machipukizi ya mianzi. Alikuwa

amesimama karibu naye. Ingawa bega lake lilikuwa umbali fulani kutoka kwake, aliweza kunusa harufu ya kiuvutia ya kiasili iliyotoka kwenye nywele zake.

Baada ya kufanya kazi na watu

mbalimbali kwa miaka mingi, Kelvin

alikuwa na uzoefu na harufu ya

manukato kutoka kwa wanawake

mbalimbali. Ilikuwa nadra kupata

wanawake kama Lisa ambao

walidumisha harufu ya asili, na aina hii ya harufu ilimfanya asisimke.

Kelvin alimtazama kwa kuibia binti huyo ambaye alikuwa na nywele nadhifu

nyeusi. Licha ya kuwa alivaa nguo za kawaida, suruali isiyobana na tisheti pana, alionekana mrembo na mwenye kuvutia.

"Bw. Mushi, umeridhika na mpango

kama huo?" Sauti ya Lisa ilimrudisha akilini ghafla.

"Ndio, inaonekana nzuri." Kelvin aliona

aibu kidogo kwani alishindwa kabisa

kukumbuka alichokisema muda huo.

Kisha, Lisa alitumia dakika 20 zilizofuata

kuelezea mchoro kwa undani, akidhani

kwamba Kelvin angeomba mchoro huo

urekebishwe kwa njia fulani. Baada ya yote, mbunifu yoyote hawezi kutimiza

mahitaji ya mteja kwa 100%.

Kelvin alisema kwa uthabiti,

“Nimeridhika sana. Hakuna kitu kinachohitaji kurekebishwa. Anza kazi kesho kulingana na mpango huu."

“Haraka hivi?” Lisa alishangaa.

"Naamini katika uwezo wako. Natamani ukarabati ufanyike haraka ili niweze kuingia ndani haraka iwezekanavyo. Hivi sasa, ninaishi na kundi la watu ambao kila wakati wananihimiza kuoa. Sipendi,” Kelvin aliongea kwa sauti ya utani.

“Bado hujaoa, Bw. Mushi?”

Lisa alishangaa.

Kelvin aliinua uso wake. “Kwanini?

Ninaonekana kama nimeoa?”

"Kwa kuzingatia umri wako na mafanikio

katika kazi yako, nilifikiri utakuwa umeoa."

“Sivyo.” Alisisitiza maneno hayo waziwazi. Lisa hakutaka kuendelea kujadili zaidi

suala hilo, akarudi kwenye kazi

iliyompeleka pale. "Nikirudi, nitajadili suala hili na timu ya ukarabati na kuwaomba waanze kazi ya ukarabati kesho." Lisa alimpa mkono kabla hajageuka na kuondoka.

Muda mfupi baada ya Lisa kuondoka,

Ethan akampigia Kelvin simu.

“Mjomba Kelvin, ulikubali kweli

kupendekeza jumba la rafiki yako lililoko

Kigamboni likarabatiwe na Kibo Group?

“Yote ni kwa sababu ya mama yako

ambaye alikuja ofisi kwangu

kunisumbua asubuhi na mapema.

Ulisema hutanisumbua, mjinga wewe.

Kwa hivyo ukamtuma mama yako

afanye hivyo, huh?" Kelvin alisema kwa

mzaha, “Hii itakuwa mara ya mwisho. Usiniombe nikusaidie tena masuala ya familia ya akina Masawe.”

“Mjomba Kelvin, kwani una matatizo na familia ya akina Masawe? Kwa kweli—”

“Naliweka hili wazi. Ndoa yako na familia ya Masawe inahusiana na familia ya Lowe, sio mimi.” Kelvin alikata simu mara baada ya kumaliza kuongea. Kila alipomuona Lisa alizidi kuchukizwa na familia ya akina Masawe ambayo ilikuwa ikimtendea bila huruma.

SURA YA 43

Saa kumi jioni baada ya kutoka kazini, Lisa alienda pharmacy kuchukua dawa ya homa kisha akaelekea nyumbani.

Ulipofika wakati wa chakula cha jioni, Alvin alikuwa bado hajarudi.

Alimtembeza Charlie kuzunguka uani

mara tu baada ya kumaliza kula chakula

chake cha jioni. Charlie alikuwa amechoka kutembea, hivyo alilala kwenye uzio akitazama

kundi la vijana wakicheza mpira wa kikapu jirani. Mwanamke ambaye pia

alikuwa akitembea na paka wake alikuja kumtazama Charlie. Alitabasamu na kusema, "Pengine paka wako atazaa baada ya mwezi mmoja."

Lisa alipigwa na butwaa kwa muda.

Kwa tabasamu, alisema, “Bibi, nadhani umekosea. Paka wangu ni mnene tu.”

“Sidhani hivyo. Niligongana na mumeo mapema na hata kumuuliza juu yake.

Mumeo alikiri kwamba paka ni mjamzito.”

"Mume wangu?" Lisa akashangaa. Je, bibi huyo alikuwa anamaanisha Alvin?

Hakika, Alvin alikuwa akitembea na

paka mara moja moja. Hata hivyo, Charlie hakuwa na mimba.

"Bibi, nina hakika umemchanganya mtu mwingine na Alvin." Lisa alimkosoa.

“Hilo haliwezekani. Naweza kuwa sioni

mbali, lakini mwonekano wa mumeo ni wa aina yake. Hakuna mtu mwingine

jirani anayefanana naye. Zaidi ya hayo, paka wangu anamfahamu paka wako

kwani wamecheza pamoja mara kadhaa.”

Mwanamke huyo alipokuwa akiongea,

paka wake alimsogelea Charlie. Charlie

mara moja akainama kumsalimia paka

huyo. Walionekana kuwa karibu kana

kwamba walikuwa marafiki wa zamani.

Lisa alikata tamaa kabisa. Je, Charlie

alikuwa na mimba? Subiri, Charlie

alikuwa paka wa kike au wa kiume?

Daima alikuwa akidhani kwamba

Charlie alikuwa paka wa kiume. Ilikuwa

ni kwa sababu Charlie kila mara alikuwa

akimsumbua Lisa, na zaidi ya hayo, jina lake lilisikika kuwa la kiume.

"Inaonekana, unaona vibaya, binti. Kutokana kwa tumbo lake kubwa, unaweza kuona wazi kuwa ni mjamzito. Je, mumeo hakukupa taarifa kuhusu hilo?”

“Asante kwa kunikumbusha. Ni mara yangu ya kwanza kufuga paka.”

Baada ya Lisa kumuaga bibi huyo kwa aibu, alichukua teksi haraka hadi hospitali ya mifugo. Baada ya daktari wa mifugo kumfanyia paka uchunguzi wa ultrasound, alishikilia miwani yake na kusema, “Paka wako atazaa hivi karibuni."

Msururu wa maswali uliangaza akilini

mwa Lisa. Kutoka kuwa mjamzito, hadi kujifungua hivi karibuni, na yeye hakuwa

na habari yoyote! Kwanini Alvin

alimficha jambo hilo? Lisa alijiona ni mjinga kwa kiasi fulani.

“Bado kuna siku kumi zaidi kabla ya tarehe zake kukamilika.” Daktari akaongeza, "Mwangalie kwa uangalifu kwa siku hizi. Hata hivyo, manyoya yake yanaonekana laini na ya kung'aa, kwa hivyo nadhani kwa kawaida ana lishe bora na inayofaa kabisa. Anapaswa kujifungua kwa njia ya kawaida.”

"Naweza kujua kama paka hutapika wakati wa ujauzito?" Lisa aliuliza.

"Paka wengine hufanya hivyo.

Wanaweza kupoteza hamu ya kula

katika tarehe za mwanzo za ujauzito."

Baada ya maelezo ya mtaalamu, Lisa alitoka nje ya hospitali kama hana akili. Wakati huo, alikuwa na mawazo ya kudanganywa na Alvin. Kulingana na

ratiba, Alvin alipaswa kujua kuhusu

ujauzito wa Charlie wakati wa kuchunguzwa hospitalini alipotapika ile

siku. Pia, Charlie alitapika si kwa

sababu Lisa alimlisha chakula

kisichofaa bali kwa sababu tu alikuwa mjamzito. Kwa hivyo, kwanini hata

amekuwa akimlaumu kuhusu jambo hilo

wakati wote huu? Kulikuwa na maana

gani kwa yeye kumdanganya Lisa kuwa

alimlisha chakula kibaya ili tu

amhudumie Charlie?

Hata hakuwa amefanya kosa lolote.

Hata hivyo, Alvin alikuwa

amembebesha lawama za

bure ambazo zilimfanya ajisikie

mwenye hatia sana kila alipomwona

Charlie. Alikuwa amedanganywa. Hilo

ndilo wazo pekee lililompata. Laiti

isingekuwa Alvin ambaye alimuokoa

mara mbili kabla ya hapo,

angemkimbilia kumpiga makofi mawili.

Lisa alipofika nyumbani, Alvin alikuwa bado hajarudi. Baada ya kunywa dawa, Lisa alijilaza kidogo akapitiwa na usingizi. Asubuhi, alisikia mlango wa chumba cha Alvin ukifunguliwa huku akipiga mswaki bafuni. Kuona hivyo, alijifuta mdomo na kutoka nje mara moja.

"Unafanya nini?" Alvin akauliza kwa hasira. Ikiwa Lisa alikuwa akipanga kumuomba msamaha, ni bora angeacha tu. "Ulikuwa unajua suala la ujauzito wa Charlie, sivyo?" Lisa alimkazia macho baada ya kumuuliza.

“Ana mimba?” Alvin akatazama pembeni kwa jeuri akijifanya hajui lolote.

“Acha kujifanya! Ulimwambia jirani yako

kuwa Charlie ana mimba. Nilipoenda

kwa daktari wa mifugo kuuliza kuhusu

hilo, niliambiwa kwamba atajifungua hivi

karibuni. Alitapika kwa sababu tu ni mjamzito na si kwa sababu ya chakula

nilichompa.” Lisa alizidi kukereka wakati akiongea. Kisha akapandisha sauti kwa hasira. “Alvin, unafikiri ni jambo la kufurahisha kunidanganya kwa

kunichukulia kama mpumbavu?”

Alvin alionesha hali ya kusikitika kidogo na kuongea kwa aibu kidogo. “Lisa , afadhali uelewe jambo hili wazi. Wewe ndiye uliyetaka kuhamia kwangu, na nilitimiza tu matakwa yako kwa kukupa nafasi ya kunifurahisha.”

“Kwa hiyo napaswa kukushukuru kwa

kunidanganya?” Lisa alizidi kuchemka kwa hasira.

“Ulikuwa hauna pa kuishi, nikakuhifadhi.

Zaidi ya hayo, nilikuokoa mara mbili

baadaye. Kama nisingekuwa mimi, unafikiri bado ungeweza kuwa hapa na

kuzungumza nami kijeuri?” Alvin

alikunja uso kwani Lisa alionekana kusahau hali yake. Wakati hakuwa na

pesa na mahali pa kukaa wakati huo, alikuwa amemkaribisha kwa fadhili.

Lakini Lisa, kwa kweli hakumuheshimu! Alithubutu vipi kumkosoa wakati huo?

Nani alimpa haki ya kufanya hivyo?

Lisa alikasirika na alishindwa cha kusema. Kwa kweli, Alvin alikuwa

mkombozi wake, lakini je, ilimaanisha kwamba angeweza kumtendea

anavyotaka? Sawa. Lisa ndiye

aliyekuwa amemwendea kwa nia mbaya

kwanza. Alistahili kudanganywa. Kwa

sura iliyofifia, hakusema neno lingine.

Alipogundua hilo, Alvin alijiamini zaidi.

"Lisa , unapaswa kutafakari juu ya

mtazamo wako. Ikiwa si Charlie ambaye

ni mjamzito na anahitaji matunzo ya mtu

wa kumhudumia nisingemvumilia mtu

kama wewe kukaa hapa.”

Lisa aliondoka kwa hasira. Alihisi kizunguzungu na wazimu sana hivi

kwamba alitaka kupigana naye. Laiti angejua mapema kama safari ya kuwa

Aunty wa Ethan ingekuwa ngumu vile, hakika asingemkaribia Alvin!

SURA YA 44

Saa mbili na nusu asubuhi,

Lisa aliendesha gari hadi Mbezi beach. Alielekea kwenye jumba la kifahari la Kelvin ili kusimamia maendeleo ya ukarabati. Alikaa kwenye

saiti siku nzima. Kelvin alifika alasiri ili

kutoa zawadi kama ishara ya kushukuru kwa juhudi za wafanyakazi.

Lisa alizidiwa na bahasha nene

iliyowekwa mikononi mwake. "Bw.

Mushi, zawadi hii labda ni zaidi ya ninavyostahili."

alimsihi Lisa huku akimkazia macho usoni kwa udadisi. “Unaonekana vibaya. Unaumwa?" "Labda ni homa ya kawaida tu." Lisa alijibu kinyonge.

"Pumzika kwa siku kadhaa uisikilizie hali yako. Naamini ukarabati utaendelea

kwa muda uliopangwa. Mimi si bosi

mbaya.” Sauti yake ilikuwa tulivu na ya kubembeleza.

Lisa aliitikia kwa kichwa. Mtu wa nje

alikuwa na huruma naye zaidi ya Alvin

ambaye aliishi naye pamoja. Alvin

hakuwa amemuuliza anajisikiaje hata

kidogo. Pengine alimchukia sana sasa, kwa nini ajisumbue? Mwanamke hawezi

kuishi kwa furaha na mtu asiyemjali.

"Asante, Bw.

Aliitikia tena na kuanza kuondoka zake.

“Ni ishara ndogo tu ya shukrani." Kelvin
Mushi."

Lisa likuwa amepiga hatua kadhaa tu kabla ya kuhisi kizunguzungu kichwani.

Kwa bahati nzuri, Kelvin alimwona haraka na kusogea

mbele kumshika asianguke. Joto

lililotoka kwenye mwili wake

lilimshangaza. “Una homa kali. Ngoja nikupeleke hospitali.”

“Niko sawa nitaenda tu mwenyewe…”

Lisa aliona haya.

"Bi mdogo, acha kujaribu kuwa mgumu. Unanifanyia kazi sasa na nitahitaji

kuwajibika endapo lolote baya

litatokea,” Kelvin alimwambia huku

akimbeba hadi kwenye gari.

Lisa alishindwa kupambana na udhaifu

ulioenea mwilini mwake na kujikuta

akipoteza fahamu muda si mrefu baada ya kuingia ndani ya gari. Kufikia wakati

alirejewa na fahamu, aligundua kuwa

alikuwa amelazwa katika kitanda cha

hospitali na bomba la dripu limewekwa mkononi mwake. Kelvin alikuwa

akimenya tunda kwenye kiti karibu na kitanda. "Ulikuwa na homa yenye joto

kali ya 102 ° F. Nilikaribia kukulipa fidia ya majeruhi kazini.”

“Samahani kwa kukusumbua.” Lisa

alijiinua na kuomba msamaha kwa

dhati. “Kuumwa kwangu hakuhusiani na kazi. Nilishikwa na homa jana na nikafikiri ningejisikia vizuri baada ya kumeza vidonge. Sikutarajia hali

ingekuwa mbaya zaidi. Hakika ilikuwa ni uzembe wangu. Sikupaswa kufanya kazi leo.”

“Ni sawa, ugonjwa huwa unatokea tu.”

Kelvin alibaki mpole tangu mwanzo bila

kuonekana kukasirika.

Lisa akazidi kujihis hatia. "Samahani

kwa kuanza ukarabati wa jumba lako kwa mkosi."

Tabasamu lilitanda usoni mwa Kelvin

baada ya kusikia Lisa akiomba

msamaha bila kukoma. "Acha kusema

hivyo. Mtu yeyote anaweza kupata homa wakati wowote.”

Lisa alikengeushwa kwa muda mfupi.

Hakuweza kujizuia kuwaza jinsi uhusiano wake na Alvin ungekua ikiwa

Alvin angekuwa na utu kama Kelvin. “Bw. Mushi asante kwa siku ya leo. Sio

lazima ubaki hapa. Naweza kumpigia rafiki yangu simu.”

"Nichukulie kama rafiki yako na utaacha kuhisi kama unanisumbua." Kelvin

alimtoa wasiwasi huku anampa tunda

lililokatwa.

“Bw. Mushi, kweli ukarimu wako

umepitiliza. Siwezi…” Lisa alishtuka chini ya macho yake.

Lisingekuwa jambo la kawaida kwake

kufanya urafiki na Kelvin iikiwa bado alikuwa yule mwanadada tajiri kama

hapo awali. Lakini, alikuwa tu mbunifu asiyejulikana sasa. Je, inawezekana

kwamba alipendezwa naye?

“Kila mtu anapaswa kutendewa sawa. Mimi ni kama binadamu mwingine yeyote anayehitaji marafiki.”

Kelvin alimuonea huruma sana yule

binti.

Akiwa nyumbani kwake mtaa wa

Buzwagi, Alvin alikuwa akipitia

chaneli za TV akiwa amechukuliwa na mawazo ya mbali sana. Hakuna hata

chaneli moja kati ya hizo 200+

iliyomvutia macho. Akaitupa rimoti

kando huku akihisi kuchanganyikiwa.

•••

Ilikuwa yapata saa

moja usiku muda

huo na Lisa bado hajarejea nyumbani.

Ilikuwa imepita saa moja tangu Alvin arudi nyumbani kutoka kazini na hapakuwa na dalili zozote za kuwepo Lisa. Hakumjali hata Charlie tena.

Ilionekana kweli alikuwa amefikia kikomo cha uvumilivu.

Charlie.

matunda.” Alvin akambeba paka mikononi mwake. Charlie alicharuka

mara kadhaa akigoma kubebwa. Paka yule mjamzito alikataa kutoka, lakini

Alvin alilazimisha kutoka pamoja naye.

Kulikuwa na maduka kadhaa yaliyokuwa kando ya barabara kuu ya mtaa huo. Alvin aliingia kwenye duka la matunda. Alitazama na kukagua

matunda kwa muda lakini hakuwa na uhakika wa kununua. Mawazo makuu

"Njoo,
Twende tukanunue

kichwani mwake yalikuwa juu ya Lisa!

Kwa nini Lisa hakuwa nyumbani bado?

Muuza duka la matunda akiwa

amesimama kando ya mlango alikuwa

akimtazama kwa siri kijana huyo mzuri wa kipekee. Nini kilikuwa kikiendelea

juu yake? Alikuwa akizunguka duka

mara nyingi zaidi kuliko alivyoweza

kuhesabu lakini hakuwa amenunua chochote. Pia alimuona akiendelea

kutupa macho kuelekea barabarani. Je, inawezekana kwamba alipendezwa

naye lakini alikuwa na haya kumuanza?

Sura ya aibu ilitanda usoni mwake.

Hatimaye, akapata ujasiri wa kumkaribia.

Bila kutarajia, Alvin akamkwepa muuza

duka yule huku akipiga hatua kubwa

kuelekea mlangoni. Akatoka nje akiwa

na ameghairi kununua chochote. Akiwa

amefika kwenye barabara inayoelekea

nyumbani kwake, hapo ndipo

alipogundua gari la BMW likiwa

limeegeshwa kando ya barabara ile upande wa pili. Mwanadada mrembo

alitoka kwenye gari.

Wow, Alvin alishuhudia mwanamume

mwingine alishuka kwenye gari

na kuajribu kumshika mpenzi wake.

Alikuwa amesalitiwa licha ya kubarikiwa na sura nzuri kuliko yeye. Iliuma sana

sana!

Upande wa pili wa barabara.

Lisa alimshukuru Kelvin kwa dhati

tena. Alipogeuka tu, alimuona Alvin

akimsogelea kwa hatua kubwa huku

akiwa amemkumbatia Charlie.

Mwangaza hafifu wa mbalamwezi

kutoka juu ulimulika uso wake wenye

huzuni. Alikosa la kusema!

Ilikuwa ni mara ya pili tu kwake kurudi

nyumbani usiku namna ile akiwa

amesindikizwa na wanaume tofauti.

Kwanini siku zote alikutana na Alvin?

Na mara zote mbili alikuwa na mwanaume mwingine aliyempa lifti

kumleta nyumbani? Alijua kwa vyovyote vile Alvin angemdhalilisha milele kwa

tukio hilo. Kwa hiyo, alijitetea kabla Alvin hajapata nafasi, “Sijisikii vizuri sana leo.

Kama kuna chochote unataka kuniuliza, tafadhali subiri kesho ili uniulize chochote.”

“Sidhani hivyo. Nahisi lazima utakuwa umechoka kwa kutumia siku nzima na jamaa yako. Vizuri? Ulipewa lifti ya kurudi nyumbani kwa Range Rover

mara ya mwisho na sasa imebadilika kuwa BMW, huh? Si mbaya, Lisa.

Unapanda matawi siku hizi. Jambo la muhimu ni kwamba, wanajua wewe ni aina ya mwanamke wa hali ya chini

ambaye unaweza kufanya lolote ili tu

kuingia kwenye kitanda cha mwanamume!”

Alikuwa ametoka tu hospitalini na hajaingia hata ndani. Kichwa chake kilikuwa kimeanza kujisikia vizuri lakini

homa yake ilianza kumpanda tena baada ya kusikia matusi ya Alvin. Hili lilimchosha sana kiakili. Alvin aliongea mara chache sana siku za nyuma lakini mbona amekuwa muongeaji ghafla?

"Sitaki kubishana na wewe." Ilikuwa

inachosha kurumbana kila walipokutana. Lisa aliinamisha kichwa chake na kuanza kuondoka.

Tabia yake ya kumpotezea ilimkasirisha zaidi Alvin. Akamshika mkono kwa nguvu. "Unamaanisha nini? Kwa hiyo huniongeleshi sasa kwa kuwa umepata mtu tajiri zaidi? Umetoka siku nzima na haujarudi nyumbani hadi usiku wa

manane. Je, ni makosa kwangu

kukuuliza kuhusu hilo?”

SURA YA 45

Kwa namna alivyomshika alikua

akimuumiza, lakini hakuwa na nguvu ya kuutoa mkono wake. Alichohisi ni kukata tamaa na uchovu. Aliinua macho yake kukutana na macho makali ya

Alvin. “Inakuathirije nikichelewa kurudi nyumbani? Ninakaa kwako, lakini

nimekuwa nikikupikia na kukusafishia. Isitoshe, ulinidanganya kuhusu mimi

kumpa Charlie chakula kilichomdhuru tumbo wakati kumbe paka wako ana

mimba. Paka anaendelea vizuri zaidi

kuliko hapo awali. Si lazima niwajibike

kwa ujauzito wake. Mimi si niliyempa mimba.”

“Unathubutu vipi kunijibu hivi?” Alvin

akamtupia macho ya jeuri na magumu. Uso wake ulikuwa umetanda hasira.

Mwanamke huyo alikuwa amefanya

jambo baya lakini alikuwa akibishana

kana kwamba alikuwa katika haki.

“Usisahau kuwa wewe ni…”

“Ninajua kuwa mimi ni mke wako kisheria, lakini je, umewahi kunitendea kama mke?” Lisa alicheka. "Kwa maoni yako, mimi si kitu zaidi ya mwanamke asiye na aibu, duni kuliko mtu yeyote unayemjua."

“Ikiwa ndivyo ilivyo, kwa nini ulitaka kuolewa na mimi? Alvin alikasirishwa na tabia yake ya kupindukia. “Ni vyema ukajua hilo…”

"Hiyo ni sawa. Sikujua hili hapo awali na niliendelea kufikiria ningeweza kupata nafasi. Niache tu kuanzia sasa! Tuko

kwenye ndoa ya mkataba tu hata hivyo, na ni mimi ndiye niliyekulazimisha.”

"Angalau unakumbuka kuwa ulilazimisha kuingia kwenye hii ndoa."

Sauti ya Alvin ilikuwa kali. “Sitaki kuwa

na uhusiano wowote na wewe.

Sitaki kuchafuliwa na ugonjwa mchafu utakaoleta nyumbani baada ya kuupata kutoka mahali pengine.”

Lisa alihisi damu ikikimbilia juu ya kichwa chake. Mwili wake ulikuwa ukitetemeka kwa hasira.

Alikuwa amepanga kukaa hadi Charlie ajifungue kwa kuwa paka huyo alikuwa amempenda kwa dhati. Lakini, aligundua kuwa asingeweza kukaa pale kwa dakika nyingine tena.

Lisa akafungulia tabasamu la kejeli.

"Hakika, ili nisichafue nyumba ya Bw.

Kimaro kwa uwepo wangu mchafu, nitahama wakati huu."

"Je, hii ni moja ya hila zako?"

Tabasamu la kujilazimisha lilienea usoni

mwa Alvin. Hakuamini angefanya hivyo.

Alikuwa ametumia bidii nyingi kujaribu

kulala naye, hata hivyo.

Bila kumjali, aliondoa mkono wake kutoka kwake na kukimbilia chumbani.

Alichukua begi lake na kuanza kufungasha vitu vyake kwa kasi ya radi.

Hakuwa na vitu vingi kwa hiyo haikuchukua muda.

Alvin alimtazama kando ya mlango.

Akiwa amechanganyikiwa, alifungua vifungo vya juu vya shati lake.

Mwanamke huyu alikuwa mzuri sana katika uigizaji. Hakutafakari makosa

yake mwenyewe hadi sasa. Je, asingemkaripia hata kama angekuja

nyumbani kwa gari la mwanamume mwingine?

Lisa alimaliza kupakia mizigo yake na kuiweka mezani ile kadi ya benki

aliyompa hapo awali. "Sikutumia senti ya ziada mbali na gharama za kila siku."

Hakufurahishwa na sauti ya hiyo.

“Nimefurahi kusema hivyo. Si mimi niliyekulipia gharama za chakula cha kila siku na ziara zile za hospitali?” Alisema kwa tabasamu la kejeli.

"Hakika, nitapata malipo ya kamisheni kutoka kazini kesho na nitakulipa."

Baada ya kumjibu hayo, Lisa hakuweza

kujizuia kukaa hapo kwa sekunde nyingine tena. Alichukua begi lake na kuelekea mlangoni. Kabla ya kuondoka, alimuona Charlie akimtazama kwa

huzuni. Machozi yalimtoka. Alishuka chini ili kumpigapiga paka kichwani.

'Samahani, siwezi kukutunza tena. Jitunze.'

kukasirishwa na tukio lililokuwa mbele yake. Uso wake ulikuwa umeharibika

kwa mikunjo ya hasira. Alifikiri

mwanamke huyo alikuwa anajifanya tu.

“Lisa usijutie uamuzi wako. Ukitoka

"Charlie, rudi hapa!" Alvin alihisi

kwenye mlango huu, sitakuruhusu

urudi hata ukipiga magoti kuomba.”

“Usijali kwa sababu sitafanya hivyo!”

Lisa aliinuka na kupiga hatua bila

kuangalia nyuma.

Kelele za kitu kikivunjika vipande vipande zilisikika nyuma yake wakati

akifunga mlango. Hata hivyo, haikujalisha tena.

Hatimaye Lisa aliondoka. Dakika 40

baadaye, alionekana nyumbani kwa

Pamela. Akiwa kazidiwa na usingizi wa kufa mtu, Pamela alipiga miayo ya

usingizi kwa mgeni ambaye

hakumtarajia. “Mmegombana tena?

Unapanga kukaa hapa kwa siku ngapi

wakati huu?" Pamela alimpokea kwa maswali.

“Ni mbaya zaidi wakati huu, sitarudi

huko tena.” Lisa alibadilisha slippers za nyumbani kabla ya kuingia.

"Unatania. Ulimtaka mwenyewe akuoe na sasa umebadilisha mawazo yako?"

Lisa alilazimisha tabasamu la uchungu. "Sio kila mpango utakupatia faida.

Nitaufikiria kama uwekezaji ulioshindwa."

"Una uhakika?"

"Ndio." Lisa alijilaza kwenye kochi.

Bado alionekana kutokuwa sawa.

"Nimechoka. Kweli, nimechoka sana."

Pamela alikunja uso. "Una homa?"

"Ndio." Lisa alipambana na machozi

yaliyokuwa yakimtoka. “Kila mtu aliliona

hilo isipokuwa Alvin. Natamani pia

kujaliwa na kutunzwa. Hata kama yeye

ni mjomba wa Ethan, siwezi kupata

heshima ya Lina ikiwa Alvin hatanipenda na kuniheshimu.”

Pamela alimtazama kwa makini na akagundua kuwa kweli amekata tamaa. Walikuwa marafiki bora kwa miaka mingi. “Hamna shida. Ninaheshimu uamuzi wako. Kwanini usikae hapa na mimi? Hata hivyo ninaishi peke yangu.”

”Sio wazo bora. Wewe na Patrick je…?”

Kwa aibu, Pamela alimkodolea macho rafiki yake. “Achana naye, anaishi kwao na huwa tunaonana kwa miadi.

"Lakini mmekuwa pamoja kwa mwaka mmojana bado hamtaki kuoana."

Lisa alipepesa macho na kujibu baada ya muda. "Amekuwa na shughuli nyingi

hivi karibuni tangu achukue uongozi wa kampuni ya familia yao. Tunaonana

mara moja au mbili tu kwa wiki, kwa

hivyo unaweza kuwa na uhakika. Nilipendekeza utafute mahali hapo awali kwa sababu Ethan alikuwa anakuja

kukutafuta hapa. Lakini sasa ameacha.”

Tabasamu usoni mwa Lisa likabadilika na kuwa dhihaka kwa kutajwa kwa mtu huyo. "Nadhani anachoweza kufikiria kwa sasa ni Lina."

“Basi, ni mtu mjinga sana. Sherehe ya uchumba wake inafanyika katika siku chache. Una uhakika unataka kuhudhuria hafla hiyo?" Pamela alimtazama kwa wasiwasi.

"Ndio, lakini nitaenda kwa sababu ya sherehe ya bibi yangu kwenye siku yake ya kuzaliwa."

"Naogopa akina Masawe watajaribu

kukuhadaa tena. Nasikitka sitaweza

kukusindikiza kwa sababu nina mtihani

chuoni siku hiyo. Lakini Patrick

anahudhuria tukio hilo pia. Nitahakikisha

yupo kukusaidia.”

Lisa alihisi utulivu usio wa kawaida. Hata ingekuweje, mpango wa kumtumia

Alvin kama njia ya kulipiza kisasi

ulikuwa umekwama! Alikuwa amepata

amani na hilo hatimaye. Alikuwa karibu

kupoteza maisha hapo awali na

heshima yake ilikuwa imekanyagwa. Hakuna kitu ambacho kingeweza

kumtisha tena.

Pamoja na hayo, ilimbidi atafute njia ya

kumlipa Alvin haraka.

SURA YA 46

Siku iliyofuata, bosi wake, Joseph Ruta, alirudi kutoka katika safari yake ya

kikazi nje ya nchi. Lisa alimfuata ofisini

akiwa na ombi maalum. “Je,

inawezekana kuomba malipo ya awali ya mshahara wa mwezi huu? Ninadaiwa

pesa na watu…” alisema kwa sauti ya chini, kwa aibu.

“Hakuna jambo kubwa. Unadaiwa kiasi gani? Niambie kiasi hicho na nitakutumia pesa mara moja.” Joseph alimwambia Lisa. “ Bw. Mushi

anaendelea kupongeza uwezo wako. Ninaweza pia kukulipa mapema juu ya mradi wa Mbezi Beach." Akatoa simu yake. "Je, Shilingi milioni ishirini zinatosha?"

Hilo lilimshangaza sana Lisa. "Hapana, hapana, milioni tano zinatosha."

Bado alikuwa na bahasha nzito

aliyopokea kutoka kwa mzee Harrison, pamoja na ile aliyopewa na Kelvin jana yake mchana. Alipanga kumlipa Alvin

ziada kidogo endapo angetaka kupiga

hesabu. “Usionekane umezidiwa sana. Mradi wa

Mbezi Beach wa Bw. Mushi unagharimu

zaidi ya shilingi milioni mia tano.

Kamisheni yako juu ya hili ni zaidi ya milioni hamsini kwa haraka haraka."

Joseph alihamisha milioni ishirini

kwenye akaunti ya Lisa mara moja.

“Endelea kufanya kazi hiyo nzuri,”

Joseph alisema ili kumtia moyo.

Lisa aliguswa sana. Aliamua kwamba

aangeendelea kuzingatia kazi yake kwa

moyo wake wote na kuachana na mawazo ya Alvin.

Tangu Lisa aondoke nyumbani kwa

Alvin, Alvin alikuwa amebadilika sana.

Hakuwa na raha na alikuwa mkali muda

wote. Sam alikuwa akimwonea huruma

na wasiwasi sana kwani hata kula

hakula vizuri.

"Lisa bado hajarudi?" Sam alimuuliza.

•••

"Sitaki kusikia jina la huyo mwanamke likitajwa masikioni mwangu." Alvin alijibu kwa dharau. Ilikuwa ni mida ya chakula

na mara tu aliposikia jina la Lisa likitajwa tumbo lake lilianza kunung'unika ghafla.

Sam alikuna ncha ya pua yake. "Najua umezoea chakula chake, lakini huwezi

kujiua kwa njaa kwa kuwa ameondoka."

"Sivyo," Alvin alijibu, akionekana kukasirika. "Hatimaye naweza kujiweka

sawa sasa kwa kuwa ameondoka."

Jasho lilitokeza kwenye paji la uso la Sam. Hakuwa amegundua upande huu wa rafiki yake hapo awali. Ghafla

alimshangaa Lisa kwa kuweza kuishi

na mwanaume huyo kwa muda mrefu.

Angekuwa ni yeye

angepandwa wazimu baada ya siku chache.

“Kesho ni sherehe ya uchumba ya Lina na Ethan. Lisa labda atakuwa huko pia. Familia ya Masawe ilinitumia mwaliko pia. Je! niende na… nimshawishi?”

Alvin alimgeuzia macho Sam na kumuuliza. "Nilidhani ni sherehe ya kuzaliwa kwa Bibi Masawe wa miaka 80?"

"Sijawahi kusikia hivyo." Sam akatikisa kichwa.

Uso wa Alvin ulionekana mzito.

Ilionekana kuwa familia ya Masawe

haikupanga kusherehekea siku ya kuzaliwa ya bibi kizee huyo hata kidogo,

sasa Lisa alipanga kwenda huko

kufanya nini? Mwanamke mjinga huyo.

Je, hakuogopa kuonewa tena na watu

hao? Alvin alijiwazia hayo na punde

akaona bora aachane nayo.

"Hakuna maana kufanya hivyo. Huu ni ujanja wake mwingine tu. Ngoja uone. Nina hakika atakuja na kuniomba

msamaha kabla ya uchumba.” Alvin alimhakikishia Sam.

Baada ya sekunde chache, alipokea ujumbe mfupi kwenye WhatsApp kutoka kwa Lisa .

"Angalia, inakuja." Akabonyeza ujumbe huo kuona Lisa amefanya uhamisho

mara tatu na kuweka shilingi milioni sita kwenye akaunti yake. Uso wa Alvin uliganda. Sam alisogea mbele kidogo ili kuibia.

Akiwa amechanganyikiwa, alisema, “Anatumia pesa nyingi kukuvuta tena.”

"Ndio." Uchangamfu wa Alvin ulirejea kidogo. “Ni lazima itakuwa moja ya mbinu zake nyingine.”

Status ilionyesha bado Lisa anaandika.

Alisubiri kuona angesema nini. Sekunde 20 baadaye, Alvin alipokea ujumbe mwingine wa maandishi. [Milioni sita zinajumuisha gharama za hospitali hapo awali. Nina hakika ni zaidi ya inavyotakiwa lakini ninahisi fadhili leo.]

Tabasamu la fumbo lilienea kwenye uso wa Alvin. “Naam, vizuri. Mwanamke huyu ana ujasiri wa simba.” Alijiwazia

Alvin.

Sam, ambaye alikuwa ameibia mtazamo wa ujumbe huo, alisema. “Hii lazima iwe mbinu ya kuvutia umakini wako. Sio tu kwamba anajaribu

kukuhonga pesa bali angalia jina lake la mtumiaji-Alvlisa,."

Alvin alijisikia vizuri zaidi aliposikia hivyo na akafunua tabasamu la kejeli. "Kwa hiyo? Haijalishi tena. Hata kama atapiga magoti mbele yangu na kuomba kwa

usiku tatu…” Hata hivyo, kabla

hajamaliza sentensi hiyo, Lisa alibadilisha jina lake la mtumiaji la WhatsApp na kuwa 'Mwanzo Mpya'.

Alibadilisha hata status yake kuwa: [Nataka tu kujali mambo yangu kuanzia sasa na kuendelea.]

Macho mazito na meusi ya Alvin

yalichuruzika kwa jazba. Aliiweka simu yake pembeni, na punde si punde, uso wake ukabadirika. "Usimtaje mtu huyu mbele yangu tena." Kisha, akaondoka kwa hasira. Sam alishindwa kabisa

kusema chochote. •••

Lisa aliingiwa na wasiwasi baada ya kutuma ujumbe huo wa kejeli. Hata

hivyo, pamoja na kumsaidia, Alvin

alikuwa amemdhalilisha sana kwa siku

za karibuni na alihisi anahitaji

kujisimamia yeye mwenyewe.

Hata hivyo, baada ya kutopata jibu

lolote kutoka kwa Alvin, alihisi kana

kwamba mzigo huo mzito umeondolewa

kifuani mwake. Hatimaye, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa na deni kwa

mwenzake tena.

Simu yake ilitetemeka ghafla. Kulikuwa na maandishi mapya ya WhatsApp.

Alinyanyua simu akidhani ni Alvin, kumbe ujumbe ulitoka kwa Kelvin. [Ni vizuri kuwa na mwanzo mpya.

Mwanamke anahitaji kujitendea vizuri zaidi. Ikiwa huna furaha na maisha, sio kwa sababu hautoshi. Baadhi ya watu au mambo fulani hayafai kuthaminiwa.]

Lisa alihisi kizunguzungu moyoni mwake. Alihisi matumaini zaidi kuhusu wakati ujao aliposoma ujumbe huo

wenye kutia moyo. Hata hivyo, aliona ni ajabu sana kwani ilionekana kana

kwamba Kelvin alijua alikuwa ameachwa.

Mbali na hilo, alikuwa amebadilisha

status yake sekunde chache tu zilizopita. Je, Kelvin alikuwa akimfuatilia

zaidi kwenye mitandao yake ya kijamii?

Baada ya kufikiria hili kwa ufupi, alijibu:

[Asante kwa kitia-moyo]

Hata kama Kelvin alikuwa

amependezwa naye kweli, Lisa hakuwa

na mpango tena wa kuwa na mpenzi.

Mahusiano yake yote ya awali yalikuwa

yamemuumiza sana. Isitoshe, hakuwa hata na talaka bado.

SURA YA 47

Zilkuwa zimebaki siku chache tu kufikia

siku ya kuzaliwa kwa bibi yake Lisa, Bibi

Masawe. Siku hiyo pia ndiyo ingekuwa

sherehe ya uchumba kati ya Lina Jones

na Ethan Lowe. Sherehe zote mbili

zilifanyika kwa pamoja katika hoteli ya

nyota saba ya ‘Heavens On Earth

Resort.’ Ni matajiri tu ndiyo wangeweza

kufanya sherehe katika hoteli hiyo.

Siku ya sherehe hiyo, familia ya Masawe na familia ya Lowe walikuwa

wametumia kiasi kikubwa sana cha pesa kukodisha ‘The Paradise Hall’, ukumbi wa kifahari zaidi wa sherehe unaopatikana katika hoteli hiyo.

Lisa alikuwa amesimama kwenye

mlango wa ukumbi huo akiwa na kadi ya mwaliko mikononi mwake. Hakuweza

kujizuia kuachia machozi ya huzuni machoni mwake. Wakati fulani huko

nyuma kabla Lina hajarudi, Jones

Masawe aliahidi kupanga harusi yake na Ethan katika hoteli hiyo hiyo na kwenye ukumbi huo huo. Kweli, sherehe ya uchumba ilikuwa ikifanyika na Ethan bado alikuwa bwana harusi. Lakini, aliyebadilika ni chumba wa kike, baala ya Lisa, alikuwa ni dada yake, Lina!

Lisa aliingia kwenye ukumbi wa

sherehe, akiwa amevalia nguo ile nyeupe aliyovaa kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Mzee Harrison mara ya mwisho. Kundi la waandishi wa

habari lilikuwa likingoja mlangoni kwa ajili ya kuripoti matukio ya sherehe hiyo ya familia hizo mbili maarufu. Waandishi walimvizia Lisa na kumrushia maswali mfululizo.

“Bi Lisa, si ulidai familia ya akina Masawe ilikufungia na kukutesa? Kwa

nini bado uko hapa kuhudhuria sherehe ya uchumba ya Lina na Ethan?”

'Je, ni kwa sababu akina Masawe

hawakukutendea vibaya hata kidogo?

Je! kila kitu kilikuwa ni uzushi wa mawazo yako mwenyewe?"

Lisa hakuwa mjinga. Alijua mara moja

kwamba waandishi walikuwa

wamepangwa na familia ya Masawe.

Bila shaka walikuwa wamehongwa na kuelekezwa cha kusema. Alitarajia jambo hili litokee, hivyo akaitikia kwa

utulivu. "Leo ni siku ya kuzaliwa ya bibi yangu, anatimiza miaka 80. Nipo hapa kusherehekea pamoja naye.”

“Kweli? Hatukusikia chochote kuhusu hilo. Tunajua tu kuwa sherehe ya leo ni ya uchumba kati ya familia ya Masawe na familia ya Lowe.”

“Lisa, mavazi uliyovaa ni ya kuvutia.

Ikiwa sijakosea, ni mavazi ya toleo la kipekee kutoka kwa mkusanyiko wa msimu wa joto wa brand ya kifahari. Si ulisema akina Masawe walikutendea vibaya sana, sasa umewezaje kumudu vazi la gharama kiasi hiki?”

Tabasamu la kejeli lilienea usoni mwa

Lina kabla hajauliza. "Sawa, familia ya Masawe imekulipa kiasi gani ili

kuniaibisha leo?"

“Haya siyo majibu mazuri. Wewe ni tofauti sana na Lina ingawa nyote wawili

mnatoka katika familia moja.”

“Hakika! Lina hata alituletea juisi na soda mapema. Umelelewa na wanandoa wa Masawe tangu kuzaliwa lakini adabu yako haiendani na familia

hiyo.” Waandishi walizidi kumshambulia

Lisa.

Lisa alikodoa macho. Kijana mtanashati

aliyevalia suti ya kijivu alikuja

kumuokoa. Vitisho vikali vilionekana

katika sauti yake. "Leo ni siku muhimu

kwa familia ya Masawe na Lowe.

Wageni wengi wa heshima watajitokeza

kwenye tukio hili, akiwemo Cindy

Tambwe. Hata hivyo kundi hili la

mapaparazi limemvizia msichana dhaifu

ili kumwaibisha. Je, yeye ni msanii au mtu maarufu mtandaoni? Kwa kuwa

mnapenda sana kumhoji, kwa nini

msimhoji kwa mazuri?”

Waandishi wa habari walitawanyika polepole, na kicheko cha kicheko

kikatoka kwenye midomo ya Lisa .

"Asante sana, Bw. Patrick Jackson. Umekuwa tofauti baada ya kuchukua

nafasi ya ukurugenzi katika kampuni yenu. Si ajabu rafiki yangu Pamela

anaanguka kichwa chini kwa ajili yako.”

Lisa alimpa sifa za shukrani mtu huyo, mpenzi wa Pamela, Patrick Jackson aliyemwokoa kutoka kwa mapaparazi.

"Acha wewe. Pamela amekuwa

akinipigia simu tangu jana usiku ili

kuhakikisha nakulinda kwa lolote.

Twende,” alisema huku akitabasamu.

Lisa alikuwa karibu kuitikia kwa kichwa

wakati mwanamke mrembo aliyevalia

mavazi ya manjano angavu alisonga

mbele ya mwanamume huyo kwa miguu

yenye viatu vya visigino virefu ili

kumshika mkono. “Patrick unatembea

haraka sana na siwezi kukupata. Karibu nianguke sasa hivi.”

Lisa alimtazama mwanamke

huyo. "Huyu ni Linda Sheba kutoka kwa familia ya Sheba. Pia amealikwa

kwenye sherehe ya uchumba usiku

huu,” Patrick alimtambulisha Linda kwa

Lisa.

"Loo," Lisa akadakia, akielekeza macho yake kwa mwanamke huyo na kumpa

mkono wa salamu. Alicheka na kuongea ki-nusu-utani. “Nilishtuka sana kumuona

akijibebisha kwako. Nilidhani ndiye

mpinzani wa Pamela."

Patrick akashtuka akamtazama Linda

aliyekuwa kamuegemea kichwa chake

kwenye bega lake, akamtoa taratibu na

kumwambia Linda kwa uchungu, “Linny,

nilikuambia hivyo mara nyingi hatuwezi

kuishi kama tulipokuwa wadogo tena. Watu wengine wanaweza kutufikiria vingine.”

“Nimezoea. Isitoshe, baada ya kuja hapa, kwa kawaida ninakuona kama

mwenza wangu kwa usiku huu.” Linda

alitoa ulimi kwa kucheza kabla ya

kumwambia Lisa , “Haya, mimi ni rafiki wa Pamela pia na huwa tunabarizi kila

wakati. Nitasikitika ikiwa utaathiri

uhusiano wao kwa kumpelekea maneno yasiyo sahihi.”

"Ni sawa, Lisa hajasema chochote kibaya." Patrick akampigapiga Linda

kichwani. “Twendeni tukaketi.”

Wote watatu walianza kutembea

kuelekea kwenye ukumbi wa sherehe

kwa pamoja. Lisa alimtazama kwa

haraka Linda kwa pembe ya macho

yake. Kwa sababu fulani, alimtilia

mashaka yule binti. Msichana huyo

hakika alikuwa na nia ya siri.

Tangu Lina alipomwibia Ethan, Lisa alihisi kana kwamba alikuwa

amesitawisha uwezo wa pekee ambao

ungeweza kuchanganua kwa usahihi

utu wa mwanamke. Isitoshe, mwanaume anawezaje kuwa na urafiki wa karibu hivyo na mwanamke

mwingine mbali na mpenzi wake? Hii

bila shaka haikuwa ishara nzuri.

Wakati huohuo, Jones Masawe na mkewe walimwona Lisa kwa mbali na

kumpa ishara kwa tabasamu. Lisa

hakutaka kuona sura zao bali alitembea

kuelekea kwao hata hivyo kwa sababu ya bibi yake.

Bila kutarajia, ghafla Mama Masawe

alimkumbatia karibu na kuzungumza kwa upendo. “Bw. Chande, huyu ni binti

yangu mwingine kipenzi, Lisa. Yeye sio

jasiri tu, bali pia mkarimu na mwadilifu.

Si muda mrefu uliopita, hata alishirikiana na polisi kama wakala wa siri ili kuangusha kikundi kinachotengeneza video haramu. Dada yake ataolewa hivi karibuni lakini yeye bado hajapata mchumba. Je, huna mtoto wa kiume mdogo…”

Msururu wa hisia ulipita usoni mwa huyo mzee Chande. Kwa kiasi fulani

video iliyomwonyesha Lisa akiwa karibu

kubakwa na Zakayo kabla hajaokolewa na Alvin ilikuwa imesambaa kwa watu wengi na kuathiri sana sifa yake.

Hakuna familia ambayo ingethubutu kumchukua tena.

"Oh, sawa, anaonekana kama msichana

mzuri. Nasikitika mwanangu mdogo

tayari yuko kwenye uhusiano. Huyo, si

Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari?

Imekuwa muda mrefu…ngoja nionane

naye mara moja.” Mzee Chande alitoa

udhuru na kuondoka haraka.

Jones Masawe alisema kwa kukata

tamaa, “Usijali, Lisa . Nitakutafutia

mume mwema leo.” Lisa alichukia sana kwa maigizo aliyoyaona yakifanywa na wazazi wake. Tayari alikuwa amekata tamaa kwa wanandoa hawa.

“Mnaweza kuacha kujifanya sasa. Ninyi ndio mliopanga waandishi wa habari mlango kwa ajili yangu, na sasa,

maneno yanawatoka kana kwamba sisi ni familia yenye furaha. Hakuna haja ya kuendelea kuigiza. Niko hapa tu leo kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Bibi. Sipendezwi na kitu kingine chochote.”

Mama Masawe alipunguza hasira yake na kusema taratibuo, “Lisa mwanangu, ni nini kilikupata hata ukakosa moyo

kiasi hicho? Haijalishi ni nini, tumekulea

tangu kuzaliwa kwako na tulitumia muda

mwingi na bidii kukuelimisha. Ni jambo

moja kwamba hutambui makosa yako

lakini hata unatudharirisha hadharani?

Je, dhamiri yako imekuacha? Mbali na matatizo yako na Lina, je kuna kitu

kingine tulichokukosea? Tulikupeleka katika nyumba ya zamani pia kwa faida yako mwenyewe!”

“Umesema kweli, sina sababu ya kuwachukia. Nyinyi wawili mlinileta

katika ulimwengu huu, lakini hiyo

haimaanishi kuwa nanyi mnaweza

kuchukua uhai wangu pia!”

Lisa alicheka kwa hasira.

Jones alipiga kelele, “Tangu lini

tukataka kuchukua uhai wako?

Kulikuwa na kila kitu kwenye ile nyumba

ya Moshi, kila kitu cha msingi

kilikuwepo. Na ile nyumba haijawahi

kukatika maji wala umeme, sasa

nilishangaa kusikia kuwa nilikuwa

nimekukataza kula au kupata maji.”

Jambo hilo lilimshangaza sana Lisa. Ina maana bibi kizee alikuwa ni mpango wa nani? "Lakini yule bibi mzee… " Kabla hata hajauliza swali lake, sauti kali

ilimkatisha ghafla.

SURA YA 48

“Lisa , umeikuja kweli!" Sauti ya Lina ya mshangao ikajaa chumbani.

Kabla Lisa hajajibu, Lina alimshika kwa mkono wake wa kushoto na kuunganisha na mkono wake wa kulia na wa mama yao. “Vipi mkuu! Hatimaye familia yetu imekamilika.”

Lisa aliinua mkono wake aliokuwa

ameushika Lisa na kusema kwa ukali, “Tafadhali sogeza mkono wako mbali. Sitaki mazoea na wewe!”

“Lisa , unamaanisha nini?” Sura ya aibu

ilisambaa kwenye uso mzuri wa Lina.

Haraka haraka akamshika Ethan mkono na kumsihi kwa upole. “Ethan, zungumza na Lisa . Tumealika wageni wengi leo na ni muhimu familia yetu iwe na amani kati yetu.”

Ethan alifikiri Lisa alimaanisha kuzua

matatizo tena hivyo akamwangalia kwa makini. Lakini, katika sekunde iliyofuata

alishtushwa kabisa na mvuto wa Lisa.

Lisa alikuwa amevaa nguo ndefu

nyeupe. Nywele zake nzuri zilikuwa katika hali ya kawaida lakini maridadi.

Alionekana kuvutia sana.

Lina alionekana mrembo pia, lakini ilikuwa hasa kwa sababu ya mapambo na mapodozi yake. Hakuweza

kulinganishwa na uzuri wa asili wa

Lisa hata kwa tabaka nene za

mapambo. Ikiwa sio kwa kila kitu

kilichotokea huko nyuma,

Lisa angekuwa mtu ambaye alikuwa

akimchumbia siku hiyo.

Uchungu mwingi ulimkumba Lina baada ya kumuona Ethan akimtazama

Lisa kwa butwaa. Alisema tu kwa lengo la kumshtua Ethan. "Lisa unaonekana mrembo leo. Natumai ulitumia masaa mengi kujiandaa kwa usiku wa leo.

Tazama, kila mtu hawezi kuacha kukutazama.” Aibu ilitanda kwenye uso mzuri wa Ethan huku akirudisha macho yake mara moja.

Mama Masawe alichukizwa na hali hiyo.

"Lisa , nimekualika hapa leo ili kutoa baraka zako, sio kuwa kivutio cha

sherehe. Leo ni siku kuu kwa dada yako.”

Bila kukawia, Lisa alijibu kwa huzuni, “Samahani kwa hilo lakini halikuwa kosa

langu kupendeza, ilinichukua dakika

kumi tu kujiandaa. Yote inakuja kwa

sababu ya uzuri wangu wa asili. Sipaswi

kulaumiwa kwa kuzaliwa mrembo kuliko

yeye. Hata hivyo si mimi niliyemzaa.”

“Wewe…” Mama Masawe hakupata neno la kumfaa Lisa kutokana na maneno yake ya kejeli.

Lisa aligeuka kumwangalia Lina kabla ya kucheka tena. “Una wivu wa siri

kwamba mimi ni mrembo kuliko wewe, sivyo? Sema moja kwa moja badala ya kujaribu kutupa vidokezo vya hila kushoto na kulia wakati wote.”

“Lisa sivyo namaanisha.

Ninakupongeza kwa dhati." Machozi ya huzuni yalikuwa yakibubujika taratibu machoni mwa Lina.

Ethan hakuweza tena kuvumilia. “Lisa umetosha? Wewe pekee ndiye

uliyekuwa mkali kwa Lina tangu mwanzo.”

"Hapo sasa, kuna mtu anajitokeza kukulinda, raha iliyoje?" Lisa aliongea kwa tabasamu la kejeli. Ethan alitoa macho kwa hasira.

Hatimaye Johes Masawe alizungumza, “Sawa, bado tuna wageni wanaingia.

Lisa nenda kwenye chumba cha faragha ukamwangalie bibi yako.

Utarudi tena sherehe itakapoanza."

“Nitaondoka baada ya kumuona bibi, sina shida na sherehe hii.” Lisa alijibu kwa jeuri kama kawaida.

“Itabidi umlishe chakula baadaye.”

Jones akamkatisha kwa kukosa subira, “Bibi yako alipooza baada ya kuanguka muda mfupi uliopita. Hawezi hata

kujilisha mwenyewe sasa hivi.”

Habari hizi ziliulipua moyo wa Lisa kama bomu. Hakuamini

alichokisikia. Ilikuwa imepita mwezi

mmoja tu tangu amtembelee bibi yake

mara ya mwisho na alikuwa mzima. Hili lingewezaje kutokea? “Mbona

unaniambia vitu vya ajabu?!” Lisa aliuliza kwa mshangao.

“Nenda, hutufai hapa. Hakuna kingine

unaweza kufanya mbali na kutukasirisha tu”

Lisa aliondoka kwa haraka kuelekea

chumba cha faragha. Bibi kizee

mwenye mvi alikuwa ameketi kwenye

kiti cha magurudumu, akitazama dirishani bila mwelekeo. Mwanamke

mwingine karibu naye alikuwa akimnywesha maji.

Machozi yalitiririka mashavuni mwake.

"Samahani bibi, nimekuja kukuona sasa hivi." Hakuwa amemtembelea kwa siku

chache zilizopita ili kuepusha kumfanya

bibi yake kuwa na wasiwasi.

Mbali na babu yake ambaye alikuwa

ameaga dunia, bibi yake ndiye pekee

aliyesalia katika familia ya akina

Masawe ambaye alimtendea mema

tangu akiwa mdogo. Tangu alipokuwa

msichana mdogo, Jones Masawe na mkewe walikuwa wakimkalipia bila hata

sababu. Bibi yake ndiye pekee aliyempenda kwa dhati bila masharti.

Hata hivyo, alipoondoka kutafuta elimu zaidi nje ya nchi, bibi yake huyo alirudi

Moshi.

"Bibi Masawe kwa kiasi fulani ni kiziwi sasa, kwa hivyo hasikii vizuri,"

mwanamke aliyekuwa akimhudumia alisema.

“Na wewe ni…” Lisa hakumtambua

mwanamke huyu. Shangazi Manka

ndiye alikuwa daima mlezi wa bibi yake.

"Familia ya Masawe waliniajiri kumtunza

Bibi Masawe. Unaweza kuniita

Shangazi Helen.” Alijitambulisha yule

mwanamke.

“Lakini vipi kuhusu Shangazi Manka?”

"Inavyoonekana, aliona shida kumtunza Bibi Masawe baada ya kupooza na akajiuzulu." Alijibu Helen

Jambo hilo lilimshangaza Lisa. Manka

alikuwa amemtunza bibi yake kwa zaidi ya miaka 30 na wote wawili walikuwa wamejenga uhusiano mzuri. Bibi

Masawe alimhitaji zaidi kwa kipindi hicho, kwa hiyo ilionekana kuwa

haiwezekani kwamba angeondoka wakati huo. Labda Manka alikuwa

akizeeka naye na kazi hiyo ilikuwa imemchosha. Alisikitika sana kufikiria

hali ya bibi yake. Alipiga magoti mbele

ya yule mzee na kuushika mkono wake.

“Bibi, mimi ni Lisa, niko hapa kukuona.”

Bibi Masawe alimtazama kwa

mshangao kabla ya kufunua tabasamu alilolifahamu. “Ni wewe, Sheryl.

Umekuwa nje siku nzima tena? Haraka ubadilishwe nguo safi. Baba yako

anatupeleka out kwa chakula cha jioni.”

Lisa alipigwa na butwaa kwa muda mfupi baada ya kusikia hivyo. Sheryl

alikuwa shangazi yake, lakini alikuwa ameaga dunia zaidi ya miaka 20

iliyopita.

“Bibi, umem’miss tena Shangazi Sheryl?” Bibi Masawe hakuonekana

kumuelewa na kuanza kunung'unika bila mpangilio. Lisa aliketi karibu na bibi

kizee huyo akihisi kukata tamaa.

Karibu saa 12 jioni, Jones alitokea tena

chumbani. "Mlete bibi yako nje kwa chakula."

"Naweza tu kumlisha humuhumu ndani kutokana na hali yake." Alihisi kuudhika kumtazama baba yake usoni.

"Sijakupa chaguo. Lazima utoke naye huko nje sasa hivi ili kula chakula cha amani na familia yetu. Vinginevyo, sitakuruhusu kuonana na bibi yako tena,” Jones aliagiza.

Lisa hakujua Jones alikuwa na maana gani. Alikuwa amesema maneno 'familia yetu'. Ilionekana kwamba alikuwa ameamua kumtenga kabisa na familia.

“Sawa, nitamleta.”

SURA YA 49

Lisa alimsukuma Bibi Masawe, aliyekuwa kwenye kiti cha magurudumu kutoka nje ya chumba hicho na kuelekea kwenye ukumbi wa sherehe.

Waliekezwa kuketi kwenye meza moja

na wanandoa waliokuwa

wakichumbiana, Lina na Ethan.

Baada ya kuketi, alimuona

Kelvin Mushi akiwa ameketi kwenye

meza kuu nyingine iliyotengwa kwa ajili ya jamaa wa karibu. Sura ya kuchanganyikiwa ilienea usoni mwa

Lisa. Hapo mwanzo Kelvin alimwambia

kuwa ni ndugu wa mbali kwa familia hizi

zote mbili lakini kwanini alikuwa amekaa

pamoja na Jones Masawe na Bibi

Masawe?

Kingine kilichomshangaza Lisa ni kuhusu Alvin. Kwanini hakuhudhuria

sherehe hiyo ingawa alikuwa mjomba

wa Ethan? Kinyume chake, Janet Kileo

na Cindy Tambwe, ambao walikuwa ni marafiki wa kudandia tu wa Lina, walijitokeza. Lisa alicheka kwa ndani.

Hakika Lina alikuwa amejitolea kujenga

uhusiano wa kinafiki na watu ambao

hakuwapenda.

Sherehe ya uchumba ilianza saa kumi na mbili na nusu jioni. Emcee wa shughuli alipanda jukwaani kumshukuru kila mtu kwa uwepo wake. Hatimaye, Ethan na Lina walialikwa kwenye jukwaa. Lina aliyekuwa amevalia nguo nyekundu alisimama karibu na Ethan aliyekuwa amevalia suti nyeusi. Wawili hao walionekana wakamilifu pamoja.

Wageni walianza kutoa maoni juu ya wanandoa. "Nilisikia kwamba binti wa

kwanza wa Masawe, Lina amekulia kijijini ilhali yeye ni mrembo na mwenye utulivu. Si ajabu kwamba Ethan amemwangukia.”

“Kulikuwa na uvumi mwaka jana

kwamba Ethan angechumbiana na Lisa.

Hakika ningemchagua Lina pia kama

ningekuwa katika viatu vyake. Utu mzuri

hushinda zaidi ya yote."

Kelele hizo zilipita masikioni mwa

Lisa kama dhoruba za upepo, lakini aliamua kuzipuuza na badala yake

akazingatia kumlisha bibi yake. Kilichomuumiza zaidi Lisa ni baada ya

Cindy, ambaye alikuwa ni rafiki yake wa zamani, kupanda jukwaani kukabidhi

pete za uchumba.

Cindy alisema kwa mzaha kwenye kipaza sauti, “Kwa kweli, nimemjua

Ethan kwa takriban miaka saba au minane sasa na ni kama kaka mkubwa

kwangu. Wasichana wengi walikuwa wakimfuata nyuma katika shule ya sekondari lakini hakuna hata mmoja wao aliyemvutia macho. Nilifikiri hakuna

mtu angewahi, hadi alipokutana na Lina na kumkubali mara ya kwanza.”

Akamtupia macho Lisa . “Lisa , utaungana nami na kuwapa salamu zako, sivyo?”

“Uko sawa.”

Lisa aliweza kuhisi kejeli katika kila neno lake. Cindy asingeweza kujuana

na Ethan kama Lisa asingalikuwa rafiki yake. Rafiki yake wa zamani sasa

alikuwa akimpongeza mpenzi wake wa zamani kwa ndoa yenye furaha. Je, hii

inaweza kuwa kejeli kiasi gani?

“Oh, hakika.” Lisa aliinua glasi yake

taratibu huku tabasamu la ajabu likienea usoni mwake. "Nimegundua hakuna mtu anayeweza kukosa aibu kuliko ninyi

watatu." Lisa alikohoa kidogo kama

anayejiweka sawa kwa jambo furani

kisha akasema. “Naomba kwanza

tushuhudie hadithi ya mapenzi ya hawa wachumba. Tafadhali elekezeni macho

yenu kwenye skrini, " Lisa alisema.

DJ aliweka wimbo mzuri wa kimahaba.

Lakini, onyesho la picha kwenye screen

lilikuwa linaonyesha picha za Lisa na

Ethan. Baadhi ya picha zilichukuliwa

walipokuwa watoto wadogo. Chache

kati ya picha hizo zilimwonyesha Ethan alipokuwa amesafiri maili nyingi kuvuka

anga na bahari ili kumtembelea Lisa alipokuwa akisoma nje ya nchi.

Walionekana wenye furaha sana kwenye picha.

Ni wazi kwamba wageni waalikwa katika

ukumbi wa sherehe walishtuka.

Familia za Lowe na Masawe hazikufurahishwa. Jones alipiga meza na kuinuka haraka. “Upuuzi gani huu?

Zima mara moja.”

Mara moja skrini ilifungwa, lakini sekunde chache za kuonekana picha zile zilitosha kusababisha ghasia kati ya wageni. “Nini kinaendelea? Je, Lisa na Ethan

walikuwa pamoja hapo awali?”

“Nani alifanya hivi? Inaweza kuwa

Lisa?" "Pengine. Nilifikiri alikuwa anafanya mambo ya ajabu tangu alipoingia ndani.”

Lisa alikunja uso kidogo kama alikuwa na machale kwamba kitu mbaya ilikuwa

karibu kutokea. Lisa hakuhusika na chochote juu ya jambo hilo lakini ni wazi, mtu fulani alikuwa akijaribu

kumseti. Mtu pekee ambaye angeweza

kufanya haya yote labda alikuwa Lina!

Mwanamke huyo kweli alitoa sadaka

sherehe yake ya uchumba kwa sababu ya kumdhalilisha Lisa? Ukatili ulioje!

"Ni nani aliyefanya hivi?!" Mama

Masawe alipiga kelele kwa hasira.

Fundi mitambo akasonga mbele haraka.

“Mama Masawe, samahani sana.

Tuligundua kuwa memory card

imebadilishwa.

"Nani amefanya kitu kibaya kama hiki?!"

Sonya, mama yake Ethan naye alipiga kelele.

Cindy alijibu mara moja, "Shangazi

Sonya, ni dhahiri kwamba kuna mtu

anajaribu kuharibu sherehe."

"Hiyo ni sawa. Lazima tujue ni nani yuko nyuma ya hili!” Sonya alisisitiza.

Wakati huo huo, Aunty Helen, ambaye

alikuwa akimtunza Bibi Masawe, alisimama kwa woga na kugugumia, “Nilimwona Lisa akiingia kwa siri

mapema kwenye chumba cha mitambo.”

Lisa alishtuka ghafla akaelewa kitu.

Alikaa kimya, lakini Jones tayari alikuwa

akimtazama kwa hasira. “Hivi ulikuwa

unafanya nini?”

Lina alionekana akiwa amepauka kama karatasi. "Lisa , sikuzuii kunidharirisha

nyumbani lakini unawezaje kunidharirisha hivi hadharani?"

Mama Masawe alikubaliana na Lina, "Umevuka mipaka wakati huu. Huwezi

kudhibiti hisia za mtu. Ethan amekuwa

akikuchukulia kama dada yake mdogo tangu utoto.”

Mara moja, Sonya akasogea mbele

kueleza hali hiyo. "Tafadhali

msiichukulie hii vibaya wageni

waalikwa. Ethan na Lisa walikua

pamoja tangu wadogo na amekuwa

akimpenda kama dada mdogo.

Lakini, mapenzi ni makubaliano ya

wawili, huwezi kubadili hisia za

mwenzako kama hakutaki. Si hivyo, Ethan?”

Ethan bila fahamu alimgeukia Lisa. “Samahani Lisa, nilikosea kukukosesha nia yangu. Kweli nilikuwaga nakuona wewe kama dada mdogo. Tulichonacho si mapenzi ya kimahaba.”

Baada ya kusema hivyo, aliona

Lisa akichezea pembe za midomo yake na kutabasamu. Kulikuwa na utulivu na kejeli machoni pake. Alihisi moyo wake ukirukaruka. Hakuwahi kuwa na aibu hivi hapo awali.

Kwa hasira, Jones Masawe

alimnyooshea kidole Lisa na kusema

kwa sauti kubwa, “Muombe radhi dada yako mara moja la sivyo sitakutambua kuwa wewe ni binti yangu!”

Lisa alitabasamu na kupiga makofi

taratibu huku akinyanyuka kuelekea

jukwaani. Alinyakua kipaza sauti kutoka

kwenye mikono ya MC na kusema. “Ni

onyesho la ajabu kama nini! Kwa kweli

siwezi kujua ni nani aliyepanga hii.

Alikuwa Mzee Masawe? Mama

Masawe? Au labda binti kipenzi wa familia ya Masawe, Lina…”

"Unaongea ujinga gani?" Jones

alikimbilia mbele kunyakua kipaza sauti

lakini Lisa akaruka haraka hadi kwenye

meza ambayo Kelvin alikuwa ameketi.

Lisa alisema kwa sauti kwenye maiki.

“Mzee Masawe, mbona unaogopa

ninachotaka kusema? Ulinilazimisha

kuhudhuria sherehe hii kwa kutumia

kisingizio kwamba ni siku ya kuzaliwa

Bibi yangu ya miaka 80, ili tu kudhibitisha kwa jamii kwamba familia ya Masawe inanijali! Ili tu uweze

kukomboa sifa ya kampuni ya Kibo

Group!”

Watu wote walikuwa kimya

wakimsikiliza. Lisa akaendelea. Niliitika

wito kwa heshima ya bibi na kujitokeza, lakini inaonekana kama umesahau kuwa kuna kumbukumbu ya kuzaliwa mama yako. Mama yako amerukwa na akili na kupooza, hata hivyo hukumtaja hata sekunde moja katika sherehe nzima. Wewe ni mtoto wake wa aina gani?”

Uso wa Jones Masawe ulikuwa umetapakaa kwa hasira na aibu.

“Ninazungumzia suala la wewe kuharibu sherehe ya uchumba, kwa hivyo acha kujaribu kugeuza mawazo. Nitataja siku ya kuzaliwa ya bibi yako baada ya hili."

“Hakika, turudi kwenye sherehe ya uchumba basi. Kulingana na maneno ya mlezi wa bibi aliyeajiriwa hivi karibuni, unamtuhumu binti yako mwenyewe bila

kusita! Je, umeangalia picha za usalama? Nimekaa chumba cha

faragha na Bibi tangu nilipokanyaga

mahali hapa na sikutoka hadi mapokezi yalipoanza. Ninaamini hoteli ya kifahari ya nyota saba kama hii itakuwa na kamera nyingi za usalama zilizowekwa." Lisa alisema kwa kujiamini. "Ikiwa picha za usalama zitaonyesha kuwa nimekuwa ndani ya chumba cha mitambo, licha ya kuomba msamaha, nitaomba radi ishuke na kunipasua vipandevipande"

"Labda ulimwagiza mtu mwingine kuifanya." Cindy aliropoka.

“Lakini Shangazi Helen alidai kuniona

mimi mwenyewe nikiingia kwenye chumba cha mitambo. Je, hilo si jambo linalopingana?” Lisa alimsuta.

Wageni walikuwa wakipata ufahamu

bora na picha kamili sasa.

Kelvin alikunja midomo yake kwa

tabasamu hafifu kabla ya kupendekeza

kwa upole, “Ikiwa ni hivyo, hebu

tukague picha za usalama. Hata hivyo

haitachukua muda mrefu.”

Sura ya hofu ilitanda usoni mwa Helen.

SURA YA50 Akiachwa bila njia mbadala, Lina alisema, “Pengine hii yote ni kutokuelewana. Angalau tuendelee na chakula kabla ya kuangalia picha. Nina

hakika kila mtu ana njaa sasa. Zaidi ya hayo, hatupaswi kukosa wakati huo mzuri—”

“Hatuwezi kuacha mambo hewani,”

Lisa alijibu kwa dhihaka, “Je, kuna

yeyote kati yenu aliyezingatia hisia zangu uliponituhumu kwa hilo?”

"Inatosha! Tumependekeza tukague picha baadaye. Unataka nini tena?”

Ethan alifoka kwa sauti ya chini huku

akimtazama Lisa aliyesimama juu ya

meza. “Unataka wazee wakuombe

msamaha mmoja baada ya mwingine?”

"Nyamaza!" Lisa alifoka kwa sauti.

"Majuto yangu makubwa ni kuangukia

kwenye ulaghai wako! Ulisema unanichukulia kama dada mdogo.

Ukweli ni kwamba, sisi wawili tumekuwa kwenye uhusiano tangu shule ya

sekondari hadi miezi miwili iliyopita.

Unafikiri sina uthibitisho kwa sababu

nimekaa kimya? Mungu anajua ni rekodi ngapi za sauti ambazo umenitumia

kwenye WhatsApp kwa miaka mingi.”

Kisha, alicheza rekodi za sauti kwenye maikrofoni. Sauti nyororo ya kubembeleza Ethan ilijaza chumba mara moja.

“Sawa, mpenzi Lisa usiwe na wazimu tena. Nitakununulia keki nikirudi

nyumbani usiku wa leo sawa?

Aliendelea kucheza rekodi kadhaa za sauti baada ya hapo. Wageni wote

walipigwa na butwaa. Wote walikuwa wamezungumza na mtu huyo hapo

awali, kwa hiyo waliitambua sauti yake.

Tabaka nene za vipodozi juu ya Lina hazikuweza kufunika weupe wa uso wake wakati huo. Ethan naye sasa aliona aibu kabisa. Hakuwahi kuwa na hasira kama hiyo hapo awali katika maisha yake. Akasonga mbele kwa nia ya kumshika Lisa aliyekuwa amesimama juu ya meza. Wakati huo

huo, mkono uliruka kutoka nje hewani ili kumzuia.

Alikuwa ni Kelvin Mushi, mjomba wake, akamtazama Ethan kwa ukali. “Tayari

umewakatisha tamaa wengine.

Usipoteze neema ya mwisho uliyo nayo

“Lisa , nimekumiss. Je, wewe hujanimiss?”

kama mwanaume.” Lisa alitabasamu.

Hakufikiri Kelvin angeangukia upande wake.

“Ethan Lowe, mwanzoni sikutaka

kukuweka wazi. Tulikuwa marafiki wa kucheza utotoni, hata hivyo. Na

unaweza kuwa kaka yangu mkubwa hata tusipokuwa pamoja. Hata hivyo, unatia aibu sana! Ni jambo moja

kwamba ulinitupa lakini kwa nini unitupe

kisha uanzishe uhusiano wako mpya na dada yangu? Wewe ni mwanaume wa aina gani?”

Lisa aliachiwa jukwaa sasa na yeye

akaendlea kulitumia vyema.

“Isitoshe, ni kweli mlikutana na Lina kwa

sababu ya mapenzi? Ni kwa sababu

yeye ndiye mrithi wa familia ya Masawe.

Uliniacha mimi uliposikia kuwa Lina

ndiye mrithi wa familia ya Masawe.”

Kisha akageuka na kumtazama Cindy.

"Mwimbaji mkubwa Cindy Tambwe!

Wakati mmoja tulikuwa marafiki bora. Je, ungemjua Ethan kama si mimi?”

“Wewe…” Cindy alikuwa akitetemeka

kwa sauti sasa.

"Acha wewe. Tulikuwa marafiki wa karibu kwa miaka sita yote ya sekondari

na tumepiga picha nyingi pamoja.

Usinilazimishe kuthibitisha.”

Lisa alipeperusha macho yake kwa

utulivu mbele ya wageni kabla ya kuwaangazia wanandoa wa Masawe.

"Hakuna haja ya kuangalia picha za

usalama kwa sababu familia ya Masawe

haitaruhusu ifanyike hata hivyo. Sitaki

kukaa kwenye sherehe hii kwa dakika

moja zaidi. Kusema kweli, ninachukizwa na nyinyi wanafiki wote.” Kisha, akatupa

kipaza sauti kando, akaruka kutoka

kwenye meza, na kuanza kutoka nje ya

ukumbi wa sherehe huku akitazamwa

na kila mtu. Familia za Masawe na

Lowe zilionekana kuwa na aibu sana.

Ethan alikuwa na aibu zaidi kuliko wote. Mwishowe, Zakaria Lowe, baba yake

Ethan, alijitokeza na kuwatangazia wageni, “Na tuanze sherehe wakati

wale vijana wanabadilisha na kupumzika ghorofani. Nadhani

wamechoka pia.” Alimtupia jicho la onyo

Ethan baada ya kusema hivyo kisha

akatoka jukwaani na kuelekea nyuma ya jukwaa.

•••

Wasiwasi ulimtawala Lisa huku

akisubiri lifti ifike. Ilibidi aondoke haraka

iwezekanavyo. Alikuwa amefanya hayo

yote kwa ujasiri tu kwa sababu walikuwa chini ya macho ya umma. Alikuwa

mbwa mwitu pekee sasa kwenye pori la simba. Wangeweza kuja kushughulika

naye bila msaada. Hata hivyo, lifti hiyo

ilichukua muda mrefu kwani ilipitia zaidi ya ghorofa 30 tofauti.

"Lisa, simama hapo hapo!" Sauti ya hasira ya Ethan ilisikika nyuma yake.

Alimtazama na kuona uso wake mzuri umepambwa kwa hasira kali. Hakuwahi

kuona hasira hii kwake hapo awali. Hakukuwa na shaka kwamba angeweza kumshambulia.

Wakati akifikira kujinasua na hatari hiyo katika akili yake, umbo refu lilipita mbele yake kama ngao. Alikuwa ni Kelvin.

“Ethan, unafanya nini?”

“Mjomba, mimi ndiye ninapaswa

nikuulize swali. Hili ni suala la faragha kati yangu na Lisa, wewe haalikuhusu."

“Mjomba?” Lisa alihisi kana kwamba

amepigwa na radi. Alisema nini? Je, Ethan alimuita Kelvin mjomba wake?

Akili yake sasa ilikuwa

imechanganyikiwa. Ikiwa Kelvin alikuwa

mjomba wa Ethan, basi Alvin alikuwa

nani? Oh hapana!

Kelvin alikunja uso huku akimuonya, “Simama hapohapo na ugeuke. Ni

sherehe ya uchumba wako usiku wa leo. Rudi juu haraka.”

"Yeye ndiye kaharibu sherehe ya uchumba wangu." Macho ya Ethan yalijaa miale ya moto. "Sifa niliyotumia

miaka mingi kuijenga iliharibiwa leo.

Hukuona jinsi baba alivyonitazama kwa hasira mapema?”

“Ni yeye ndiye aliyeharibu uchumba?

Unategemea Lisa angekaa kimya

pamoja na nyinyi nyote kuungana

kumshambulia?” Mwonekano wa

kukatishwa tamaa ulitawadha usoni

mwa Kelvin. “Ethan, uko sahihi kufanya

kazi kwa bidii kuelekea kurithi kampuni ya Lowe Enterprises, lakini huwezi

kuvuka mipaka. Yote yaliyokupata leo ni

kwa sababu tu ulivuka mstari dhidi ya

Lisa!” Maneno yake yalimgusa Lisa. Hakutarajia mwanaume huyu

kumuelewa vizuri hivi.

Akiwa ameshtuka, Ethan alisema kwa kusitasita, “Mjomba, umemsaidia

Lisa mara kadhaa leo. Kwanini? Je! ni kwa sababu wewe ni…”

Kelvin akamkatisha haraka Ethan

utadhani alijua alichotaka kusema.

“Nimepata fursa za kumfahamu, na kutokana na kile nilichokiona, yeye ni msichana wa tofauti sana. Ikiwa yuko

tayari kunipa nafasi, anaweza hata kuwa shangazi yako mdogo siku moja.”

Lisa alikuwa karibu kupoteza akili!

Ethan aliposikia hivyo alishtuka. Nani

angeweza kukubali mpenzi wake wa

zamani kuwa shangazi yake? Isitoshe, Ethan hakuweza kuyavumilia maumivu

ya moyo kwa kumfikiria Lisa akiwa na mwanamume mwingine.

“Mjomba, nadhani umepatwa na wazimu. Baadhi ya watu si kama wanavyoonekana juu-juu—”

“Nimekuwa na uzoefu wa kitaaluma kuliko wewe na pia nina umri mkubwa zaidi yako kwa miaka michache, kwa hivyo unaweza kuacha kuniambia la kufanya," Kelvin alimkatisha Ethan kwa upole. "Zaidi ya hayo, wewe ni mwanamume wa aina gani hata ukamkashifu mpenzi wako wa zamani ambaye kimsingi ulipaswa kuwa unamvika pete ya uchumba leo?"

Uso wa Ethan ulikuwa haufai kwa aibu, akajitahidi na kumwambia mjomba

wake. “Nasema hivyo kwa manufaa yako. Babu na Bibi hawatamkubali kamwe katika familia.”

“Ni kwa manufaa yangu au yako? Nina

hakika unajua jibu kuliko mtu mwingine yeyote.” Kelvin alimwambia.

“Ding.” Wakati huu, mlango wa lifti ulifunguka. Kelvin alimuongoza Lisa ndani ya lifti, akaufunga uso wa hasira wa Ethan upande wa pili wa milango ya lifti. Akiwa ndani ya lifti, Lisa alitawaliwa na hisia zilizomzidi uwezo. Kelvin akamtazama. Akifikiri kwamba

lazima angekuwa na hofu, alimpigapiga begani huku akitabasamu.

“Lisa umetisha! Ulithubutu vipi kuruka juu ya meza na kuongea maneno yale mbele ya kila mtu?” Kusema kweli, Kelvin alishindwa kuuzuia mshangao

wake. Pengine hiyo ilikuwa ni sherehe ya kukumbukwa zaidi aliyowahi

kuhudhuria. Hata hivyo, alionekana kuvutia zaidi aliposimama juu ya meza.

Ethan?” Lisa aliuliza jambo lililokuwa likimchanganya sana!

CHA 3

“Bw. Mushi… wewe ni mjomba wa

Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.