KURASA.....126-150
Sura ya 126 “Usifanye, usifanye.” Kwa kufikiria onyo
la Alvin jana yake, Willie alimzuia Lisa mara moja. “Alikataa kuniruhusu
nikuambie kuhusu hilo. Kwa kuzingatia
kwamba nimeshiriki video zangu za
faragha na wewe, tafadhali unaweza
kujifanya kuwa hujui lolote, Bi Jones?”
Lisa alishangaa kusikia hivyo kutoka
kwa Willie. Alvin alikuwa kweli mtoto wa
familia tajiri ya Kimaro? Kwa kuwa Willie
alikuwa akimheshimu na kumuogopa
sana Alvin, inawezekana kwamba Alvin
alikuwa na nguvu kubwa kuliko Willie?
Inawezekana kuwa yeye ndiye mrithi wa familia ya Kmaro? Asingeweza kamwe
kufikiria kuichokoza familia ya Kimaro.
Familia ilikuwa ngumu sana kwa mtu wa kawaida kama yeye kufikiria.
“Sawa, nakuahidi, lakini naweza kujua Lina alikufahamu vipi?” Lisa aliuliza huku akijilazimisha kutulia.
"Ni Stephen ambaye alimtambulisha kwangu," Willie alidhihaki, "Msaidizi wangu anafahamiana na familia ya Kileo. Stephen alitaka kuanzisha
uhusiano nami, kwa hiyo akamtuma mpenzi wake kwangu.”
Lisa alishangaa “Unafurahia kulala na rafiki wa kike wa rafiki yako?”
Willie alitoa kikohozi kidogo. “Kweli, mke si mtamu kama mchepuko. Inavutia zaidi kulala na mpenzi wa mtu mwingine.”
Lisa alikosa la kusema. Alikuwa na shauku kubwa ya kumuuliza ikiwa yeye
ndiye pekee mwenye tabia mbovu
katika familia nzima ya Kimaro au ikiwa kuna wengine wote walikuwa hivyo, ikiwemo Alvin, lakini hakufanya hivyo.
Baada ya kurudi ofisini, Lisa alikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa. Hapo awali aliolewa na Alvin kwa kudhani kuwa alikuwa mjomba wa Ethan.
Baadaye, aligundua kwamba alikosea na akafikiri kwamba Alvin alikuwa wakili tu. Nani alijua kuwa yeye alikuwa mtoto wa familia tajiri na maarufu zaidi nchini?
Naam, haikumshangaza. Badala yake, aliona kuwa ilikuwa na mantiki. Huenda
Alvin alikuwa akimpima. Ikiwa
angekutana na Alvin akajiweka wazi
utambulisho wake, angehisi kwamba
amempenda kwa ajili ya mali zake.
Vilevile Alvin angempeleka
kumtambulisha nyumbani kwao, familia yake labda isingemkubali.
Ghafla, alihisi kuchoka. Ili kujizuia
kuwaza kupita kiasi, alibofya kipande
kimojawapo cha video ambazo Willie
alimtumia. Mwanzoni, alikuwa akijaribu tu kuangalia juujuu. Kinyume na matarajio yake, video hiyo iligeuka kuwa ya kufurahisha sana hivi kwamba Lisa
ambaye alikuwa hajakomaa kama Lina aliguna.
Alipotambua kwamba alikuwa amezama
katika video hiyo, Shani alimkumbusha hivi kwa uchungu, “Bi Jones, ulisema
hutaitazama, sivyo? Zaidi ya hayo, Bwana Kimaro hatakuruhusu kutazama aina hii ya mambo.”
"Lo... Hatajua kama utatunza siri." Lisa
alitoa tabasamu la aibu. Kwa kuwa Alvin
asingemruhusu hata kutazama picha
zisizofaa za Willie, bila shaka
angemchuna akiwa hai iwapo angejua
kuhusu jambo hili. Shani alishindwa cha
kusema. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kulifumbia macho.
Lisa alipokuwa akiitazama video hiyo, wazo zuri lilimjia. Alimwita msaidizi
wake haraka. “Nakumbuka mjukuu wa Amiri alisema kwamba kuna mnada unakuja?”
“Ndiyo, ni usiku wa leo. Mratibu wa manada amekualika pia kwenye tukio.
Watu wengi matajiri wa hapa Dar na mikoa mingine watahudhuria.”
“Sawa. Hata mimi nitaenda.” Lisa alicheka. Leo itakuwa siku ya giza zaidi katika maisha ya Lina.
Hotelini Baada ya kutoka kwenye ofisi
za Mawenzi Investments, Willie alikuwa
tayari kufungasha vitu vyake na
kuondoka Dar. Kukaa katika jiji moja na
Alvin kulitisha maisha yake.
Alipousukuma tu mlango wa chumba,
alimuona mtu mrefu akiwa ameketi
kwenye kochi la ngozi, akifanana na mfalme. Miguu yake iligeuka kuwa
milegevu kama mlenda, na midomo yake iliendelea kutetemeka. “Kaka
Alvin, umekuja kwa wakati ufaao. Nilikuwa karibu kukuambia kuwa
nilienda Mawenzi Investments na kusuluhisha suala hilo. Hakuna mtu
atakayethubutu kumsababishia Lisa matatizo tena.”
“Najua. Umefanya vizuri sana.” Alvin
alikaa pale bila wasiwasi huku hisia za heshima kubwa zikitoka kwenye uso wake mzuri. Willie alijawa na furaha moyoni kusikia hivyo. Kabla hajaongea, midomo myembamba ya Alvin ilianza
kusonga. "Lakini ... hakushuku chochote?"
Mara tu Alvin alipomaliza kuongea, hali ya wasiwasi na hofu ilitawala mazingira.
Moyo wa Willie ulionekana kuganda.
“Usinidanganye, Willie,” Alvin alionya kwa upole, “unakumbuka kilichotokea ulipokuwa na umri wa miaka 18 baada ya kunidanganya, sivyo?”
Willie akatetemeka. Mwaka aliofikisha
miaka 18 ulikuwa mwaka wake wa giza kuwahi kutokea.
kama jani linalopigwa na upepo, Willie aliogopa sana kumficha. "Sasa anajua
kwamba unatoka katika familia ya Kimaro, lakini sikumwambia makusudi
kuhusu hilo. Yeye ndiye aliyenitega, na nilifanya makosa. Zaidi ya hayo, majina yetu ya mwisho ... "
Alvin akasugua macho yake. Alijua
mapema kwamba Willie, mpuuzi yule
kijana, angeshindwa kufanya kulingana na maagizo yake na kuishia
kumuumbua zaidi.
"Yeye ... alishuku." Huku akitetemeka
Willie alisema kwa kigugumizi, “Kaka
Alvin, una wasiwasi kwamba
atajikombakomba kwako na kukusumbua baada ya kukujua wewe ni nani? Kwa kweli, hii ni kawaida sana kwetu. Haijalishi tunaenda wapi, wanawake wengi humiminika kwetu. Hata hivyo, hadhi yake ni ya chini sana
kuwa mpenzi wako.
"Nyamaza." Macho makali ya Alvin yalimkumba. "Ondoka Dar mara moja."
“Sawa, sawa. naondoka sasa hivi kaka.”
Willie pia hakujisikia kubaki mahali hapo
pabaya palipomchachia. Mara moja
akafungasha vitu vyake na kuondoka
kama anayefukuzwa.
Alvin aliinuka na kuelekea kwenye
dirisha lililokuwa ndani ya chumba
hicho. Akili yake sasa ilikuwa
imevurugika kabisa Alikuwa mtu
mwenye shaka. Alipokuwa akiishi katika
neema ya utajiri wa familia ya Kimaro
tangu alipokuwa mdogo, wanawake
wengi walikuwa wamemtumia kwa
kisingizio cha kumpenda kwa sababu ya utambulisho wake, jambo ambalo lilimjaza chuki. Kwa hiyo, hakuwahi
kumwambia Lisa kuhusu utambulisho wake halisi, akitumaini kwamba
angempenda yeye kama yeye na si kwa utajiri wake. Hata hivyo hakuna marefu
yasiyo na ncha. Hatimaye Lisa alikuwa
amejua kuhusu utambulisho wake.
Angemwonaje?
Hans alimwambia kwa upole, “Usijali, Bwana Kimaro. Lisa alikupenda tangu
alipokutana nawe kwa mara ya kwanza
kwenye baa. Wewe ndiye anakupenda, na haihusiani na utambulisho wako.”
"Hiyo ni
Alvin alijisikia raha.
Kweli, kwa nini alikuwa anafikiria kupita
kiasi? Alikuwa ameanguka kwa ajili
sawa."
yake bila matumaini, kama yeye
mwenye alivyosema.
•••
Saa kumi na moja jioni, gari jeusi
lililoonekana kuwa la gharama kwa
mwonekano wake lilikuwa limeegeshwa nje ya mlango wa jengo la Mawenzi
Investments. Muda mfupi baadaye, Lisa alishuka kwenye gari huku yule
aliyekuwa kwenye kiti cha dereva akivua koti lake. Alionekana akiwa
amevalia shati jeupe chini ya fulana, ambayo ilisisitiza umbo lake refu. Akiwa na sura nzuri ya kuvutia, alitoka kama
mhusika kutoka kwenye kitabu cha hadithi za kubuni.
Ingawa alimuona kila siku, sura yake ya kuvutia haikukosa kumshangaza.
Hakika asngechoshwa na sura ya mwanaume huyo.
Alipojua kuhusu utambulisho wake siku
hiyo, alikuwa akipingana na mawazo
yake kila mara. Hata hivyo, wakati huo,
alikuwa na hakika kwamba asingeweza
kuvumilia kumwacha mwanamume huyo.
Siku zote alikuwa mtu ambaye alikaa karibu naye katika nyakati ngumu zaidi.
Siku hiyo, alimsaidia kukabiliana na dhoruba tena. Haijalishi jinsi gani safari yao ya mbele ingekuwa ngumu, alisisitiza kuwa pamoja naye.
“Mbona unanitazama?” Alvin alibana
ncha ya pua yake, alikuwaakijshtukia.
Lisa aliitazama saa iliyokuwa kwenye
mkono wake, jambo ambalo
lilimkumbusha jinsi alivyokuwa akimshangaa kwa aina ya nguo zake.
Ikamjia akilini kwamba huenda nguo
hizo zilikuwa zikificha utambulisho wa
Alvin kwa makusudi.
“Ninautazama uso wako mzuri. Pia, niko
katika hali nzuri leo. Uliona jinsi Jones
na Lina walivyofedheheka? Lina siku
zote alijifanya kuwa safi na aliishi kwa
unafiki wakati huo. Sasa, kila mtu anamdharau.”
“Ndiyo.” Baada ya kumsikia akipiga
kelele, Alvin aliinua macho yake na kuuliza, "Kuna chochote unachotaka kuniuliza?"
Sura ya 127
Lisa alipigwa na butwaa. Alikuwa amepanga kumuuliza Alvin kuhusu
utambulisho wake halisi. Hata hivyo, uhakika wa kwamba alimwomba Willie
afiche utambulisho wake ulionyesha
kwamba hakutaka kumfunulia. Katika
hali hiyo, hakujisumbua kumuuliza.
"Hapana." Alvin taratibu akadondosha macho yake. Lisa alimtazama wakati
huo na kusema, “Nitahudhuria mnada
usiku wa leo, kwa hivyo sitakuwa
nyumbani kwa chakula cha jioni.
Unataka… kwenda pamoja nami?”
Aliuliza kwa tahadhari ingawa alihisi kwamba Alvin asingekubali kwenda pamoja naye. Kwa kuzingatia tabia yake ya kiburi na dharau, asingependezwa na tukio la aina hiyo.
“Sawa.” Alvin akakubali.
“Huu?” Lisa aliduwaa, akifikiri kwamba alimsikia vibaya.
“Nimesema sawa. Mbona unashangaa?” Alvin alitazama sura yake iliyopigwa na tabasamu.
"Lakini hupendi kushiriki katika hafla
zinazofanyika Dar se salaam, leo imekueje?"
"Ninakuja ili kuzuia wanaume wowote wasikucheze." Alvin alijibaraguza.
Aliendesha gari kwa umakini huku
macho yake yakiwa yametazama
barabara iliyo mbele. Lisa aligeuza
kichwa chake na kutazama wasifu wake
kamili kwa muda. Hakuweza kujizuia
kumpa busu la shavuni. Usukani
uliokuwa mikononi mwake ulitetemeka, kisha akamwambia kwa utani, “Usinichezee kimapenzi ninapoendesha gari.”
Sentensi hiyo ilionekana kuwa ya kawaida. Lisa alicheka na kujibu, “Najua. Itasababisha ajali mbaya sana, si ndiyo?" "Hapana." Akamtazama. "Itasababisha moyo wangu kuruka."
Mapigo ya moyo wa Lisa yakagongana na kifua. Hali isiyoeleweka ilionekana
kujaa kwenye mishipa ya mwili wake
mzima. Moyo ulimwenda mbio zaidi
baada ya kumbusu. Wakati huo, alikuwa na hamu kubwa ya kumbusu kwa
mapenzi. Hata hivyo, alitilia maanani
zaidi usalama barabarani.
Saa moja na nusu usiku, Mnada ulikuwa
karibu kuanza katika jumba la mikutano
la Karimjee. Watu mashuhuri kutoka
Dar es Salaam na mikoa jirani waliingia
ukumbini mmoja baada ya mwingine.
Kama mwenyekiti wa Mawenzi
Investments, Lisa alionekana kuwa
kivutio cha tukio hilo. Umati ulimsonga
mara tu alipoingia ndani.
Ethan naye alikuwepo. Alivyoona jinsi
Lisa anafuatwa sana na watu kwa
mbali, Ethan alijawa na uchungu.
Kamwe katika ndoto zake hakutarajia
kuwa mpenzi wake ambaye awali
alimwacha kwa ajili ya Lina angekuwa
mwenyekiti mpya wa Mawenzi
Investments ndani ya muda mfupi.
Wakati huo watu wengi walimwona
mpumbavu. Kwa kweli, Ethan alikuwa
mpumbavu. Alimkosea kipumbavu sana
Lisa na kwa hivyo akakosa nafasi ya kuwa naye. Akiwa na mwanamume bora kando yake sasa, aliona kwamba asingekuwa na nafasi yoyote kwake.
Mchumba wake mpya, Tracy Laizer, alikuwa ameketi kando yake na kuubana mkono wake. "Nilisikia kwamba yeye ni mpenzi wako wa zamani, ni kweli?"
'Yote ni ya zamani." Ethan alilazimisha tabasamu. Alijua kwamba angeweza tu kufanya kazi kwa bidii ili kuifurahisha familia ya Laizer kwa sasa.
“Ni vizuri kwamba unajua. Maadamu unanipenda sana, familia yangu itakutegemeza,” Tracy alisema kwa upole.
Upande mwingine, Lisa naye alimwona
Ethan pia kwa sababu ya suti yake
nyeupe iliyovutia. Mwanamke wa ajabu
kutoka familia mashuhuri alisimama
kando yake. Moyoni mwake, Lisa alihema huku akimfikiria mwanaume
ambaye aliyemuona kuwa mkamilifu wakati ule. Kinyume na matarajio yake yote, mwanamume huyo aligeuka kuwa mtu ambaye angemsaliti kwa ajili ya mamlaka na umaarufu.
“Unamtazama Ethan?” Ghafla sauti ya Alvin ya kuonya ilisikika.
"Nilikuwa nikifikiria juu ya jambo fulani."
“Ulikuwa unafikiria nini?” Alvin alikasirika.
"Yajayo yanafurahisha. Onyesho nzuri inakuja. Utajua baada ya muda mfupi.”
Lisa aliinua uso wake, macho yake angavu yaking'aa kwa ucheshi. Uso wa
Alvin ukalegea taratibu.
Wanawake kadhaa ambao waliolewa na wafanyabiashara matajiri walimzunguka Lisa na kumpongeza.
“Mwenyekiti Jones, hili gauni umenunua wapi? Ni nzuri!"
"Mkufu uliovaa umetoka kwa Tiffany na ndio muundo mpya zaidi, sivyo?"
"Habari za jioni, the bosy lady?"
Ghafla Janet alishika glasi ya mvinyo
mwekundu na kumsogelea Lisa kwa nia mbaya. “Ah, Mwenyekiti Jones, sikutarajia kwamba ungekuwa na jeuri ya kushiriki katika mnada. Subiri kidogo, sina uhakika kama bado nitakuita
Mwenyekiti Jones sasa hivi.”
"Unamaanisha nini, Bi Kileo?" mmoja
wa wanawake hao, Madam Clark, aliuliza huku akihema.
Janet akahema. “Pengine ninyi nyote
hamfahamu kilichotokea. Nilisikia
kwamba Mwenyekiti Jones alimpiga
Willie Kimaro aliyetoka Nairobi wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya
Mawenzi Investments jana usiku.”
"Nini? Unamaanisha huyo Willie kutoka familia ya Kimaro?"
"Ndio, ni yeye." Janet akaitikia kwa
kichwa. “Rafiki yangu aliniambia
kwamba Mwenyekiti Jones alisababisha
uso wa Bwana Kimaro kuvimba, na
Bwana Kimaro alikasirika sana. Sijui
hata atafanya nini! Hiyo ilikuwa ni sawa na kujitakia matatizo makubwa sana
kwako, Mwenyekiti Jones. Hivi mtu
kama wewe unawezaje kuichokoza
familia ya Kimaro? Natumai utakuwa
uko salama na unaendelea vizuri
nitakapokuona tena.”
Wanawake wote walishtuka na kurudi
nyuma mmoja baada ya mwingine.
"Imekuwa muda tangu tulipokutana mara ya mwisho, Madam Ngololo."
Muda mfupi baadaye, kundi la wanawake lilitoa visingizio na kuondoka mahali hapo mara moja. Hawakuwa
tayari kukaribiana na mtu aliyeiudhi familia ya Kimaro. Tukio hilo halikuwa la mzaha. Walijua kuwa kwa kuwa Lisa
alikuwa ameichokoza familia ya Kimaro, alikuwa amejihukumu kifo. Ingekuwa haina maana kumsogelea.
Bila kujisumbua kuliweka wazi jambo
hilo, Lisa alimkazia macho Janet kana
kwamba ni mlemavu wa akili.
Ikizingatiwa kuwa alikuwa na uhusiano wa kirafiki na Lina, kwa nini Lina
hakumwambia ukweli?
"Halo, mume wangu ananiita."
"Lazima uwe na hofu, sawa? Pengine hukutarajia kwamba utapoteza nafasi ya mwenyekiti wakati ndio kwanza umeanza kuifurahia.” Janet alitabasamu kwa kuridhika kisha akageuka kumtazama Alvin. "Bwana. Kimaro, nakushauri ujiepushe naye ili usije ukaingizwa kwenye matatizo haya.”
Alvin alimwangalia tu bila kujali
alichosema. Janet alifikiri kwamba
maneno yake yalikuwa yameamsha
kupendezwa kwake, hivyo mara moja akasema, “Msaidizi mkuu wa Willie ni jamaa yangu. Ukija na kuniomba msaada, hakika nitakuunganisha naye.”
Kwa namna fulani, Lisa alihisi kucheka.
Hata Willie alimuogopa sana Alvin. Kwa
wazi, msaidizi maskini asingekuwa na maana yoyote kwake.
mbele huku akimshika mkono Alvin. Hakuwa
hata na muda wa kupoteza kumwambia Janet ukweli.
Akiwatazama wanaondoka, Janet alicheka nyuma yao. Aliweza kuwa ameridhika kwa muda huo, lakini kile
ambacho kingefuata kingemwacha akilia baadaye.
Mara baada ya kuketi, Alvin alimtazama
mwanamke aliyekuwa kando yake kwa namna ya kinyonge. “Kwanini
usingelifafanua sasa hivi hilo jambo lako? Au lina uhusiano wowote na madai yako kwamba yajayo yanafurahisha?”
"Unanielewa vizuri, Alvilisa." Lisa alitabasamu.
“Alvlisa, mpuuze tu huyu kichaa. Hebu tutafute nafasi tukae.” Alisonga
Alvin aligundua kuwa tangu Lisa awe
mwenyekiti, alikuwa na ujuzi zaidi wa kucheza na wengine. Baada ya kusema
hivyo, halikuwa jambo baya hata
kidogo. Ilibidi awe mwovu na mkatili
zaidi ili ahitimu kuwa mke wake katika siku za mbeleni.
Mnada ulianza muda mfupi baadaye.
Kwa kweli, mnada wa usiku huo ulikuwa tukio la kuchangisha harambee fulani.
Lisa aliinua kadi yake ya zabuni kwa picha mbili za uchoraji zenye thamani
ya shilingi milioni kadhaa. Bidhaa ya mwisho ilikuwa 'Mkufu wa Malkia'.
Ulikuwa ni mkufu unaometa na kishaufu
cha almasi ya rubi inayong'aa ukiwa
umeketi juu ya satin nyeusi. Mkufu huo
uliundwa kwa ustadi. Hata mnyororo
huo ulipambwa kwa almasi ndogo, ambayo ilifanana na safu ya nyota.
Wanawake wote walishangaa kuuona ule mkufu, na pia ulikuwa umemvutia Lisa. Alvin alimtazama Lisa kwa macho ya kina. Kwa wakati huo, mwendesha mnada alianzisha kwa shauku, "Sasa ni wakati wa kuvutia zaidi. Hapo awali, mfalme wa zamani wa nchi fulani alipata
mbunifu mzuri zaidi wa kuunda mkufu, na ilimchukua miaka miwili
kuukamilisha. Kito hiki kina karati 383.4 za almasi. Kuna uvumi kwamba ikiwa
mtu atampa mwanamke wake mpendwa Mkufu huu wa Malkia, watakuwa
pamoja milele. Huu ndio mkufu ambao kila mwanamke anauota. Zabuni ya
kuanzia kwa bidhaa hii usiku wa leo ni shilingi bilioni 1.6.”
Bei hiyo ya ajabu ilizua taharuki
ukumbini. Hata hivyo, upesi mtu fulani
akapaza sauti na kusema, “bilioni 1.7.”
Kwa udadisi, Lisa alitazama upande ule, na kugundua kuwa alikuwa ni Ethan.
Sura ya 128
Kila mtu alianza kumzungumzia Ethan.
“Ni Ethan kutoka Lowe Corporation. Ni mkarimu kiasi gani kwake.”
"Nilisikia kwamba yuko kwenye uhusiano na yule mwanadada kutoka katika familia tajiri ya Laizer, yule tajiri wa Tanzanite."
“Naona. Familia ya Laizer ni maarufu sana huko Mererani. Bwana Laizer ameopoa mawe ya thamani ya bilioni sana juzijuzi tu, atakuwa na pesa sana.”
“Hasa. Lakini mwenyekiti wa sasa wa Mawenzi Investments, Lisa Jones, alikuwa ni mpenzi wake wa zamani.”
“Mpenzi wa Lisa wa sasa hana kitu, yeye ni wakili tu. Nadhani hawezi kumudu kumnunulia mpenzi wake mkufu huu wa gharama.”
Wakiwa wameingia kwenye tmajibizano ya kidaku, ghafla umati wa watu
ukahamishia macho yao kwa Lisa. Lisa hakutarajia kwamba angehusika katika
mazungumzo hayo. Haraka alimshika
Alvin na kusema kwa sauti ya chini, “Usijisumbue kuhusu yale ambayo wengine wanasema. Maoni ni kama mapambo tu. Kimsingi, hayana faida yoyote isipokuwa kwa kuvutia pongezi kutoka kwa wengine. Ni kama vitu vya mitumba ambavyo havifai kuvitumia."
Alvin alimtazama Lisa kwa umakini.
Kwa kweli aliona kuvutiwa kwake na
Mkufu wa Malkia kupitia macho yake.
Alifikiri kwamba angemwomba
amnunulie, akizingatia kwamba alikuwa
amejua kuhusu utambulisho wake
kwamba alikuwa tajiri mkubwa kutoka
familia maarufu ya Kimaro. Kinyume na matarajio yake yote, itikio lake lilikuja
kama mshangao. Haishangazi kwamba
walisema mwanamke atasaidia kuokoa
pesa za mwanamume ikiwa kweli
alikuwa akimpenda. Alikunja mdomo
wake kuwa tabasamu la kupendeza, akainua kasia yake ya zabuni na kusema kwa sauti ya kiume na ya kiburi, "bilioni 2.5."
Akiwa ameduwaa, Lisa alihisi kana
kwamba kichwa chake kilikuwa
kinamlipuka. “Umerukwa na akili?
Nilikuambia usiweke dau lolote.”
"Bilioni 2.6." Janet, ambaye alikuwa
karibu, ghafla aliinua kasia yake ya zabuni.
Lisa alimshika mkono Alvin. “Acha
kuinua kasia yako. Hakika hawezi
kumudu. Anapandisha bei kwa
makusudi kujionyesha tu ili akuvute na wewe umpandie kwa juu.”
Alvin hakuweza kuwa na wasiwasi juu yake. Alitumia mkono mwingine kuinua kasia yake. "Bilioni tatu." Ukumbi mzima ulikumbwa na ghasia baada ya Alvin
kutaja bei hiyo iliyoonekana kufunga mnada.
Akiwa na shilingi bilioni 2.3 kuwa
kikomo chake, Ethan alimkodolea macho Alvin kwa uchungu. Alvin
alikuwa mkatili kiasi gani! Ethan alikunja ngumi kwa kutoridhishwa kwani si tu
kwamba alishindwa kumpiku Alvin
kumnyakua Lisa, bali pia alishindwa kumpiku kuunyakua ule mkufu.
Tracy aliyekuwa kando ya Ethan alipumua kwa husuda. “Sawa, inatosha.
Mkufu wa thamani ya bilioni tatu si wa mchezo hata kidogo."
“Ndiyo.” Ethan alitazama chini, akivumilia maumivu yake ndani kabisa.
Tena, Janet aliinua mkono wake ili kupandilia dau. Alvin alitoa macho yake ya ajabu ghafla. “Unaweza kuinua mkono wako na kuropoka bei unayotaka, lakini sitakupandilia tena.
Fikiri kwa makini ikiwa kuna pesa za kutosha mfukoni mwako kabla hujafanya hivyo.”
Mkono wa Janet ukaganda, akasita mara moja. Kwa kweli, alikuwa akijaribu tu kuongeza bei ili kumkomoa Alvin.
Stephen kwa haraka akaondoa kasia
yake na kumwonya kwa hasira, “Usiwe mpuuzi. Ikiwa kweli utatumia mabilioni ya pesa za familia yetu kwenye mkufu tu, niamini, nitakupiga kofi hadi kufa."
Akiwa amekasirika, Janet alinyamaza kimyaa! Lakini, kwa kweli alikuwa na
wivu wa ndani kwa ndani kwa wazo la utayari wa Alvin kutumia shilingi bilioni tatu kwenye mkufu kwa ajili ya Lisa.
“Kaka, mbona Alvin ni tajiri kiasi kwamba anaweza kutumia mabilioni ya shilingi kirahisi rahisi tu? Inawezekana kwamba anatoka kwa familia ya
Kimaro? Inawezekana kuwa ni ndugu yake na Willie Kimaro?”
"Nyamaza. Hiyo haiwezekani." Stephen hakukubaliana naye kabisa. “Sijawahi
kusikia hivyo. Tofauti na yeye, tunahitaji
kiasi kikubwa cha pesa kwa mtiririko wa biashara wa kampuni. Nadhani
anatumia mapato yake ya uanasheria kununua mkufu. Labda anafikiria kuwa
nafasi ya Lisa kama mwenyekiti wa
Mawenzi Investments ni ya kudumu na
kwamba thamani yake itakuwa ya
mamia ya mabilioni ya shilingi. Kwa
hivyo, anajaribu kugusa na kukamata
moyo wake kwa kutumia bilioni hizi tatu.
Kwa bahati mbaya, anashindwa
kutambua kwamba Lisa atapoteza
nafasi hiyo kwa muda mfupi tu.”
Hatimaye kulikucha kwa Janet, lakini alibaki na hasira. “Kaka, si alimkosea
Willie jana? Kwa nini hajamfundisha somo?” Stephen alipigwa na butwaa.
Alipokumbuka kutoweza kumpata msaidizi wa Willie siku hiyo, ghafla
alihisi kuzama. Punde si punde, alihisi kwamba alikuwa akiwaza kupita kiasi.
"Nilisikia Bwana Kimaro aliumia sana jana usiku, kwa hivyo huenda labda
hajapata nafuu."
“Kwa yote ambayo Lisa alimfanyia, hakika hatamwacha salama hadi ahakikishe kuwa amekufa." Janet alitoa tabasamu.
Sura ya 129
Hatimaye, Alvin alipata zabuni ya juu
zaidi ya mkufu huo kwa bei ya shilingi bilioni tatu. Msimamizi wa mnada kwa
tahadhari alimkabidhi Mkufu wa Malkia mbele ya macho ya kila mtu. Alvin
akautoa ule mkufu mwekundu uliokuwa unameremeta kwa umaridadi. Alipoutoa nje, alimwambia Lisa ambaye alikuwa ameduwaa kwa sauti nzito, “Simama.”
Lisa alisimama huku akionekana kuchanganyikiwa. Umbo lake la kuvutia lilionekana katika macho yake angavu na safi.
Midomo maridadi na myembamba ya Alvin ilijikunja na kuachia tabasamu la kupendeza. Akainama kidogo na kuuweka ule mkufu shingoni mwake.
Sauti yake ya kiume, tulivu ilisikika kwa mtetemo wa kupendeza. "Kuanzia leo na kuendelea, utakuwa malkia wangu."
“Wow!” Mwanamke mmoja kando yake alishtuka kwa mshangao.
Moyo wa Lisa ulikuwa unadunda.
Ijapokuwa bei ya mkufu huo iliufanya
moyo wake kumuuma sana kiasi cha
kuvuja damu, tukio hilo lilikuwa limegeuza mnada kuwa harusi yao.
Mwanaume huyo alikuwa ametimiza matakwa yake yote.
Kilichomshangaza zaidi Lisa ni tabia ya kimapenzi ya Alvin. Ule mkufu
mwekundu wa almasi uliokuwa umeketi
kwenye ngozi yake ya chokoleti ulikuwa unameremeta. Ulimfanya aonekane
kama malkia wa heshima. “Asante.
Nakupenda sana Alvilisa." Lisa
alisimama kwa vidole vyake na kumbusu mdomoni hadharani. Ilikuwa ni denda zito haswa la karibia dakika
nzima.
Baada ya busu, uso wake mzuri na wa
kuvutia ulianza kuona haya kwa sababu
aligundua kuwa watu wengi walikuwa
wakimtazama. Macho ya Alvin
yalimtoka kwa huzuni licha ya kuwa na
furaha kubwa moyoni. Hakika, mwanamke wake alikuwa akivutia zaidi
na zaidi. Alihisi hamu ya kuendelea kumbusu hadharani.
Ethan alitazama pembeni huku
akionyesha huzuni. Ilionekana kana
kwamba moyo wake ulikuwa
umepasuliwa kwa uchungu. Hapo awali
Lisa alipomwambia kuwa
amemwangukia Alvin, hakuamini
kabisa. Lakini hatimaye aliamini sasa.
Hakika, mwanamke aliyekuwa
akimchukulia kama mpenzi wake wa
pekee sasa alikuwa amempenda mtu
mwingine. Mtu huyo alikuwa bora zaidi
na mzuri kuliko yeye. Akiwa amejawa
na majuto, Ethan hakutaka kuendelea
kubaki mahali hapo hata kwa muda.
Aligeuka na kuwa karibu kuondoka.
Lakini kabla hajaondoka, skrini kubwa
ya video iliyokuwa jukwaani iliangaza
ghafla. Kila mtu alifikiri kwamba ilikuwa ni shughuli ambayo mratibu wa mnada alikuwa ametayarisha. Hata hivyo, wote walishangazwa na tukio hilo la ajabu kabisa. Sauti tofauti kabisa zilisikika upesi kutoka kwenye spika.
“Huogopi kwamba Stephen atajua kuhusu hili? Eeh?.”
"Tayari anajua, na hatajali. Yeye ndiye aliyenitaka nilale na wewe leo.”
“Haah! Unasema kweli?. Kama ni kweli basi nashukuru kwa heshima yake ya kunipatia mwanamke wake."
Mazungumzo ya kushtua yalisikika
katika ukumbi huo. Uso wa mwanamume ulikuwa umefichika, ilhali
uso wa mwanamke ulionekana wazi
kwa umma. Kwa kushangaza, alikuwa
Lina, msichana kutoka kwa familia ya
Jones Masawe, tajiri ambaye amekuwa
akinyemelea kiti cha Lisa kwa gharama
yoyote. Stephen hata alikuwa ameambatana naye na kujionyesha hadharani wakati
wa kuhudhuria hafla fulani na shughuli za kijamii siku za karibuni. Kwa hivyo, kila mtu tayari alijua kuwa Lina alikuwa mpenzi wa Stephen. Kilichoshtua kila
mtu zaidi ni kwamba Stephen
hakusalitiwa kuhusu jambo hili. Kweli
alipanga mpenzi wake alale na mwanaume mwingine.
Ilitisha sana! Mnada wa usiku huo
ulihudhuriwa na wanawake wengi
matajiri. Walimtazama Stephen kwa
dharau na karaha. Hali hiyo ilimfanya
Stephen aingiwe na hofu ya upofu.
Kamwe katika ndoto zake mbaya zaidi
hakufikiria kwamba kuna mtu
angethubutu kucheza video ya Willie na
Lina wakiwa wamelala pamoja. Nani
alifanya hivyo?! "Zima skrini! Zima
sasa!” Alinguruma kwa hasira. Lakini, hakuna mtu aliyemsikiliza. Kila mtu alikuwa akipiga porojo tu huku
wakitazama tamthilia hiyo ikiendelea.
“Mtu wa aina hii anatisha kweli. Kwa kweli alimtuma mpenzi wake kwa mwanamume mwingine kwa ajili ya kutimiza lengo lake.”
"Kwa bahati nzuri, sikukubali wakati familia ya Kileo ilipotaka kuwa na uchumba na binti yangu."
“Ndiyo. Haendani kabisa na mambo anayoyafanya. Ni bora nikae mbali na familia ya Kileo siku zijazo.”
"Huenda pia anamtumaga Janet kulala na wanaume, si ndiyo tabia yake?"
“Hilo linawezekana. Hapo awali nilikuwa
na hisia kwa Janet, lakini nitasahau tu juu yake. Sitaki kusalitiwa bure.”
Mbele ya shutuma za umma, Janet
alikasirika sana hivi kwamba alipiga kelele, “Nani alifanya hivi? Haina
uhusiano wowote na mimi!” Janet na Stephen, ambao mwanzoni walijisikia
fahari, walikuwa na aibu sana wakati huo.
Ethan alipokuwa anajiandaa kuondoka, uso wake mzuri ulibadilika rangi. Alifikiri
kwamba tayari alikuwa anajua rangi
halisi za Lina. Hakujua kuwa alikuwa anachukiza zaidi kuliko vile alivyofikiria kuwa. Hakujua hata Lina kweli alikuwa na wanaume wangapi. Mara tu
alipokumbuka kuwa alikuwa kwenye
uhusiano naye hapo awali, alihisi hamu
ya kutapika. Ethan alikuwa
amezungukwa na wageni waliokuwa
pembeni yake waliokuwa wakitazama
tamthilia hiyo. Wakaanza kumsema
waziwazi. "Nilisikia kwamba Ethan alimtosa Lisa kwa ajili ya Lina wakati huo."
"Pengine alivutwa na matumizi ya Lina ya mbinu za hila. Sikutarajia Bwana
Lowe kupendezwa na aina hii ya mwanamke.”
“Hasa. Lina ni mshenzi sana.
Ninashangaa kama Bwana Lowe pia
alikuwa akifanya uchafu wa aina hii na Lina wakati huo."
Akiwa mpenzi wake, Tracy hakuweza
kustahimili maoni hayo, kwa hiyo
aligeuka na kuondoka. Hakuweza
kueleza maumivu yake kwa kutumia
maneno, Ethan alimfuata haraka. Kabla
hajaondoka, alimuona Lisa akimtazama
kwa huruma na kejeli. Kwa wakati huo,
alionekana kuelewa kila kitu. Pengine hii
ndiyo ilikuwa adhabu na masaibu ya
mwisho ambayo alimletea. Alikuwa amefaulu. Kuanzia wakati huu na
kuendelea, angehisi kutapika kila alipomfikiria Lina.
Ni njia nzuri kabisa aliyotumia kuua ndege watatu kwa jiwe moja.
Lisa aliridhika kabisa na matokeo.
Tabia ya Lina isiyo na aibu iliwekwa wazi kwa watu wote wenye nguvu huko
Masaki. Ilikuwa nzuri kwake kwa vile
alifurahia ujasiri wa kutongoza
wanaume. Hakuna mwanamume mmoja ambaye angekuwa na ujasiri wa kutosha kumuoa katika siku zijazo.
“Umemaliza kuitazama?” Akiwa
amekunja sura yake sawasawa, Alvin
alizungumza kwenye sikio la Lisa.
Alifunika macho yake na kusema kwa
sauti ya hasira nzito, "Hivi ndivyo
ulivyomaanisha ulivyosema kuwa
yajayo yanafurahisha? Nilikuonya jana
usiku usiangalie miili ya wanaume
wengine isipokuwa wangu tu.”
Hali ya huzuni ilimfunika Lisa na kumfanya ashtuke. Kisha akapigwa na wazo. “Sikuikagua. Shani ndiye aliyefanya hivyo."
“Unadhani nitakubali uongo wako?
Unapima IQ yangu?" Alvin alicheka. Lisa alishindwa cha kusema.
"Nitashughulika na wewe tukirudi nyumbani," Alvin alimuonya vikali.
Muda mfupi baadaye, mratibu wa mnada alizima skrini mara tu alipopata fahamu zake. Hata hivyo, karibu video nzima ilikuwa imechezwa. Ilikuwa
imeharibu sifa za Lina na Stephen kabisa. Lisa akiwa ameridhika, akatembea hadi kwenye maegesho ya magari akiwa na Alvin.
nyuma yao
Sura ya 130
Stephen na Janet Kileo waliwakimbilia wakiwa wamefura. Uso wa Stephen
ulijawa na hasira kali. Hakutaka kitu zaidi ya kumnyonga Lisa akiwa hai.
Alvin alimvuta Lisa nyuma yake, umbo lake refu na kubwa likitoa ulinzi wa
nguvu kwa Lisa.
"Lisa Jones, wewe ndiye ulicheza ile video?" Stephen alifoka kwa hasira.
“Sawa, umenikera mno. Ikiwa sitakuua, basi jina langu si Stephen Kileo.”
Janet naye alisema kwa msisimko, “Unajua umemkosea nani? Huyo ndiye
Willie Kimaro! Hata kama umemficha uso, hatakuacha kwa kuwa
umesambaza video zake kama hizi.”
“Simama hapo!” Sauti ya ukali ikasikika
Lisa aliinua macho yake na kutabasamu
kwa dharau. “Umewahi kujiuliza hii video imetoka wapi na ni nani aliyenipa?
Au ulifikiri ningethubutu kurekodi kitu kwenye chumba cha Willie Kimaro?”
Stephen na Janet wote walikua hoi kwa wakati mmoja. Muda mfupi baadaye, Stephen akatikisa kichwa. "Hiyo haiwezekani. Video hii huwezi kuwa ulipewa na Wiliie Kimaro. Ulimkosea jana usiku, kwa hiyo tayari anakuchukia. Umepata mtu wa kudukua simu ya
Bwana Kimaro? Sawa, wewe ndiye uliyeanzisha hii. Nitampigia msaidizi wa Willie sasa hivi. Msaidizi wake ni rafiki yangu wa karibu sana.”
"Endelea kuota. Huenda hujui kuwa
Willie Kimaro aliondoka Dar asubuhi ya leo.” Lisa alitabasamu kwa uso
uliolegea. “Hivi mpenzi wako mzuri
hakukuambia? Asubuhi ya leo, Willie
alikuja Mawenzi Investments na kusema
kwamba hatafuatilia suala la jana usiku
tena. Willie pia alimdhalilisha sana Jones na binti yake. Sasa, kila mtu
katika kampuni anajua Lina Jones alipanda kitanda cha mwanamume mwingine kutafuta kufadhiliwa. Wale wawili baba na binti yake hawana hadhi tena ya kuja kwenye kampuni."
“Usijaribu kunidanganya. Hakuna kitu kama hicho." Stephen hakumwamini hata kidogo. Alipiga moja kwa moja nambari ya msaidizi wa Willie Kimaro.
Baada ya muda mrefu, simu
iliunganishwa na sauti iliyolaaniwa kutoka upande wa pili, “Stephen Kileo, unawezaje kuthubutu kuwasiliana nami?! Umeniharibia! Hata nilipoteza
kazi yangu.”
"Nini kimetokea?" Stephen aliuliza kwa sauti ya kuchanganyikiwa.
"Sijui. Vyovyote iwavyo, Lina Jones na wewe, nyinyi wawili ni mashetwain kabisa, mmemkasirisha sana Bwana
Kimaro. Tayari amerejea Nairobi bila kupenda.” Simu ilikatwa kwa haraka. Stephen aliganda kama sanamu ya mbao. Alimtazama Lisa ambaye alikuwa akitabasamu na ghafla akahisi damu
yake ikishindwa kutembea kwenye mishipa. "Ulifanya nini kwa Bwana
Kimaro?"
“Sina haja ya kujieleza kwa mtu kama wewe. Stephen Kileo, sikutaka
kushughulika nawe, lakini ni kosa lako
kumtambulisha Lina kwa Willie. Sasa, sifa yako imeharibika, na nadhani sio
watu wengi watathubutu kuwasiliana na
familia ya Kileo kwa ushirikiano katika
siku zijazo. Unaweza kuendelea na
ndoto ikiwa bado unataka kuoa mke
kutoka katika familia yenye hadhi sawa na yako.” Lisa akamaliza hotuba yake
na kuondoka zake kwa furaha huku
akimshika mkono Alvin aliyekuwa
kakasirika sana hadi kushindwa
kuongea. Janet aliyebaki nyuma alishika kichwa na kupiga kelele. "Stephen, haya
mambo yametokeaje?" 'Yote ni kwa sababu ya ujinga wa Lina. Yule mjinga hata hajitambui kabisa.”
Stephen aliitoa hasira yake. "Sitamsamehe Lina kamwe. Naelekea nyumbani.”
Gari lilikuwa kimya, hewa ya wasiwasi ilitanda kila kona. Alvin akaminya
midomo yake myembamba, umbo lake
maridadi lkionekana kutulia kama
sanamu. Lisa alimtazama kwa siri huku
akijaribu kumwongelesha bila mafanikio.
“Bado una hasira? Kwa kweli
nililazimika kukabiliana na Lina wakati
huu. Nilitamani kutapika kila
nilipoutazama mwili wa Willie Kimaro. Sasa, ninachotaka ni kwenda nyumbani na kuutazama mwili wako mzuri ili niweze kuosha macho yangu…”
“Sasa ndiyo unataka kunitazama?” Alvin ghafla alimkazia macho. Lisa akaguna na kukubali kwa kichwa.
"Sawa, nitakuruhusu uangalie usiku kucha." Alvin alikubali ghafla. Lisa alipigwa na butwaa na kukosa la kusema. Alvin alikunja uso na kumuonya tena. "Ikiwa hii itatokea tena ..." “Haitatokea tena,” Lisa aliapa, "Ikiwa itatokea, Mungu na aniadhibu nisiuone tena mwili mkamilifu wa Alvilisa
maishani mwangu."
"Nyamaza." Alvin alicheka. “Hiyo video bado ipo kwenye simu yako? Nitafuta
kila kitu kwenye simu yako tukifika
nyumbani. Willie Kimaro ni mchafu sana kijana yule, sijui tabia hiyo kaitoa wapi!"
"Nakubali. Ingawa nimeona kidogo tu, sijisikii vizuri hata kidogo.” Lisa alijifanya kuchukizwa. "Alvilisa, najua huna tabia mbovu kama hii, si ndiyo?"
“Utaijua tu tabia yangu, ikiwa ni nzuri ama mabaya.” Alvin alijibu akicheka.
Baada ya kurudi nyumbani, Lisa alivua
Mkufu wa Malkia wa almasi kwa
uangalifu baada ya kukaa chini ya taa ya mezani na kuuangalia kwa upendo.
“Ni mzuri sana. Hakuna dosari hata kidogo.”
"Nakumbuka ulisema haupendi vito vya mapambo." Alvin alitembea nyuma yake na kumtania, "Hata ulisema ni mtumba tu."
Lisa aliona haya na kusema kwa
kigugumizi, “Mimi… nadhani ni ghali sana. Ni shilingi bilioni tatu. Itachukua muda gani kupata kiasi hicho cha pesa?" "Ethan Lowe alikuwa tayari kutoa bilioni mbili kwa ajili ya mwanamke wake, kwa nini nijali kuhusu kiasi hiki?" Alvin alicheka kwa unyenyekevu. "Kwangu mimi, pesa haijalishi. Muhimu ni kwamba unaupenda."
Lisa akapepesa macho, mara akaelewa kuwa alikuwa akijaribu kushindana na Ethan. Hata hivyo, hiyo haikujalisha. Kadiri alivyokuwa akipambana na Ethan ndivyo ilivyokuwa ikionyesha kuwa anamjali.
“Alvilisa, Ethan kwa kweli hana
uhusiano wowote nami. Mimi pia
simpendi tena. Ninayempenda ni
wewe." Aligeuka na kumkumbatia shingo na kumbusu usoni.
Moyo wake uliuma. Hapo awali, ingawa alipata pesa nyingi, hata hivyo
ilionekana kama hazina faida yoyote. Sasa, ilionekana kana kwamba alikuwa
amepata maana ya kupata pesa.
Midomo yake myembamba ilijikunja
huku akimpa sura isiyoeleweka. "Ni hayo tu?"
Lisa alionekana kujua alichokuwa akiongea na kuinamisha kichwa chini.
Alvin alicheka na kumnyanyua. "Si ulisema unataka kunitazama?"
“Hapana…” Uso wa Lisa ukageuka kwa woga. Alikuwa ni hodari wa kusema
maneno makubwa, lakini ndani alikuwa ni mwoga kuyatekeleza.
"Kwa hiyo ulikuwa unanidanganya si ndiyo?" Alvin akakisugua kidevu chake
taratibu. Sauti yake ilisikika kana
kwamba ni sauti ya simba.
Mapigo ya moyo ya Lisa yalimuenda kasi, akazidi kuogopa. Alimsukuma kwa
haraka. “Si ulisema hukula chakula cha kutosha wakati wa chakula cha jioni?
Nitakwenda kukupikia.” Harakaharaka akamtoroka na kutoa tabasamu la hovyo chini ya macho ya Alvin.
Alvin alipotoka kuoga, Lisa alikuwa
amepika chakula chenye harufu nzuri na kumtengea. Hakuwa amekula
chakula cha jioni kilichopikwa na Lisa kwa muda mrefu na mara moja
akakichukua ili kukionja. Kilikuwa ni chakula cha kawaida tu, lakini hakujua
jinsi Lisa alivyokipika maana ladha
ilikuwa ya kipekee sana kila wakati. Lisa
alimsaidia kukausha nywele zake
zilizolowa maji huku akimwangalia akila
chakula kile kitamu.
“Upishi wangu bila shaka ni mtamu sana, lakini ulisema hukuupenda nilipokutengenezea mara ya kwanza. Wewe ni mnafiki sana, lakini wewe pia unajua kunipenda sana.”
Alvin aliona aibu. Ilikuwa ni kidogo sana
kwa mwanamume kuelezewa kama mnafiki. Alimvuta kwenye mapaja yake
na kuonyesha kutofurahishwa.
“Unamwita nani mnafiki mkubwa? Hebu
thubutu kusema tena?”
“Nakuzungumzia wewe. Bado unakataa kukiri… Mmh…”
Kabla Lisa hajamalizia, busu la kutawala la Alvin likaanguka kwenye midomo yake. Alimbusu bila kupumua, na hatimaye alipomwacha, alimwambia
akiwa amemshika mabegani
"Ukithubutu kusema tena nakuongeza zaidi ya hili..."
alirudia tena huku akicheka. Inaonekana
alikuwa amefanya kamchezo fulani ka makusudi.
Alvin akamkamata tena na kumpa busu. Wakati huu, alipigwa busu kali zaidi.
Mikono yake mikubwa ilimkumbatia kwa nguvu kumzuia asikwepe. Lisa alikuwa
na hasira na furaha kwa wakati mmoja.
Alvin alikuwa jabari kupita kiasi na
hakuruhusu mtu yeyote kuzungumza kwa utani juu yake.
Punde, Lisa alianza kulegea na
kuzidiwa na hisia, Alvin alimbeba hadi kitandani. Alvin alikuwa amevaa bukta
nyepesi tu alipotoka kuoga. Aliivua na
kumtazama Lisa na kusema kwa sauti
ya unyonge, “si ulisema unataka
kunikodolea macho ili kuosha macho yako? Unaweza kuanza sasa.”
“Wewe ni mnafiki, kwani uongo…” Lisa
Uso wa Lisa uliwaka moto. Hakuwahi
kufikiria kwamba Alvin angekumbuka jambo lile tena.
Umbo lake lilikuwa zuri sana. Hakuwa
na misuli kupita kiasi bali mtanashati na mwenye nguvu. Zaidi ya hayo, alikuwa
ametoka tu kuoga, hivyo harufu yake ya kiume na harufu ya gel ya kuogea
ilimfanya apate hisia nzuri za utamu.
Sur ya 131
Nywele za Alvin zilikuwa zimekaushwa tu na kuachwa zikiwa zimevurugika kwa fujo. Kwenye uso wake mzuri, kulikuwa na hisia zisizo na kikomo za kimapenzi zikitoka kwenye mwili wake wote.
Lisa alimtazama kwa shauku. Wakati
huo, alitaka sana kumshukuru Pamela.
Ni kosa alilofanya Pamela la
kumchanganya Alvin na Kelvin, mjomba
wake Ethan, ndilo lililompeleka Lisa
kwake. Alikuwa amemsaidia mara kwa
mara. Ni yeye pia aliyemfanya awe na ujasiri wa kuishi licha masaibu yote
aliyokutana nayo.
Usiku huo, alimpatia Mkufu wa Malkia, kwa gharama ambayo ilimfanya kuwa
mwanamke tajiri na aliyevutia kuliko wote Masaki nzima.
“Alvilisa…” Lisa alinyanyuka na kushika
shingo yake. Uso wake wa ajabu uliangaza kwa aibu. "Tunaweza ... tujaribu?"
Alikuwa ameamua. Bila kujali kama
familia ya Kimaro ingemkubali au la katika siku zijazo, alitaka kumpa Alvin
kitu cha thamani zaidi alichostahili.
Alvin aliganda! Yeye alikuwa sugu kwa
mambo hayo siku nyingi, na alikuwa
hajaenda mbali zaidi pia. Mbona Lisa
alikuwa ameamua ghafla…?! Au ni kwa
sababu alijua utambulisho wake halisi?
“Kwa nini?” Macho yake mazito yalimtazama kana kwamba alitaka kuona kupitia kwake.
Lisa alikuwa amefunikwa na aibu na hakuona sura yake ya kushangaza.
Alikuwa ameuzika uso wake mdogo katika kifua chake. “Kwa sababu
nakupenda. Sijawahi kuwa na uhakika wa hisia zangu kama nilivyo sasa.” Lisa
alijibu kwa aibu.
Alvin alisugua nywele zake laini na ndefu juu ya kichwa chake kwa udadisi.
Hakuridhika na jibu lile. Kulikuwa na wanawake wengi sana waliomzunguka ambao walitaka sana kumrukia kwa
sababu tu walijua utambulisho wake halisi, kwamba yeye ni mwanamume tajiri.
haongei wala hafanyi chochote na akaona aibu. “Usinielewe vibaya, ni moyo tu ndiyo umenituma, sina nia ya kukujaribu na wala sikulazimishi. Kama hutaki basi tuache…” Alimsukuma na kukaribia kuinuka, lakini mwili wa Alvin haukumruhusu kunyanyuka.
"Ikiwa utanishinikiza kwa njia hiyo, basi nitakubali kwa kusita," Alvin alisema kwa sauti.
Lisa alimtazama kwa hasira. “Si lazima ufanye kwa kusitasita. Sikulazimishi na sijali hata hivyo…” Kabla hajamaliza, Alvin akambusu. Wakati huo, alielewa.
Haijalishi alikuwa akifikiria nini, ni kweli alimtaka! Zaidi ya hayo, alikuwa amekiri
kwake muda mrefu uliopita. Hakukuwa na haja ya kutilia shaka kwamba alimpenda.
“Kwa nini? Je!… hutaki?” Lisa aliona
Dakika chache baadaye, aliufunga
mlango kwa nguvu na kwenda bafuni kuoga tena. Lisa alifoka kwa hasira ya kuachwa akiwa ‘ameiva’.
Dakika 20 baadaye, Alvin alitoka kuoga akiwa na sura tofauti. Hakumgusa tena Lisa wala kuwambia kitu chochote.
Moyo wa Lisa uliumia alipofikiria juu yake.
‘Sitathubutu kumwambia katika siku zijazo.’ Alijiapiza kimoyomoyo kwa unyonge. Alikumbatia shingo yake na kuuzika uso wake kifuani mwake.
Alikuwa na haya sana hivi kwamba hakuweza kuongea tenakwa muda mrefu. "Potezea tu kwa leo. Utakuwa
mwanamke wangu mapema au baadaye." Sauti ya Alvin
alipomkumbatia ilikuwa ya kutetemesha sana.
Wawili hao walipolala, hawakujua kwamba habari kuhusu tukio la hisani
usiku huo zilikuwa zimeenea mitandaoni. Kila mtu alijua kuhusu hilo.
Wakati huo, katika makazi ya Jones
Masawe, Jones kwa mara nyingine tena
alipokea simu kutoka kwa wadaku.
“Bwana Jones, umeona sura duni ya binti yako? Hehe, nipe basi binti yako
alale nami kwa usiku mmoja na nitafanya kazi nawe kwenye mradi."
"Nyamaza!" Mwili wa Jones ulitetemeka
kwa hasira huku akilaani, “Weka kinywa chako ksafi unapoongea na mimi!”
“Hehe, ningewezaje kuwa msafi kuliko
binti yako? Nani angethubutu kutaka
takataka kama hiyo?"
"F*ck off! Usinipigie tena.” Jones
aliivunja simu yake.
Alikuwa ameishi kwa miaka mingi na tayari alitumia nusu ya maisha yake, lakini hakuwahi kufedheheshwa kama ilivyokuwa siku hiyo. Hapo awali, alifikiria kwamba angeipata Mawenzi Investments kwa urahisi, lakini ilienda mbali zaidi na mikono yake. Si hivyo tu, hata alipoteza sifa na heshima yake ya mwisho. Alikasirika sana hivi kwamba alipoteza busara yake. Alichukua ufagio na kwenda juu ili kumpiga Lina.
“Wewe b*tch, yote ni makosa yako! Tangu uliporudi, tulipoteza Kibo Group na sifa yetu. Hata mimi pia nimefedheheshwa katika umri huu.
Mjinga sana wewe!”
"Hapana!" Lina alipiga kelele mara kwa mara na kuendelea kujificha. "Baba, nilifanya hivyo kwa ajili ya familia ya Jones. Ni wewe ulinishauri nimfurahishe Bwana Kimaro.”
"Nilitaka umfurahishe kwa zawadi, sio kulala naye, paka wewe!" Jones alipiga
kelele. Kadiri alivyokuwa akisema
ndivyo hasira zilivyozidi kuongezeka na ndivyo mikono yake ilivyozidi kuwa matata.
“Una kichaa? Ni binti yetu!” Mama
Masawe aliingia ndani na kumsukuma.
Alipoona sura ya Lina iliyochubuka na kupigwa, alilia kwa huzuni.
“Afadhali nisiwe na binti kama yeye!”
Jones alimnyooshea kidole na kumkaripia, “Ningejua kwamba haya yangetokea knisingekurudisha kabisa.
Ikiwa sio wewe kurudi, ningekuwa na ugomvi na Lisa? Ikiwa hukunitia moyo, ningemuua mama yangu kwa mikono
yangu mwenyewe? Isingekuwa wewe
hata Lisa angeingia Mawenzi
Investments angenisikiliza na kuniacha niwe mwenyekiti.”
Lina aligeuka rangi, na mwili wake ukatetemeka huku akijilaumu
mwenyewe.
Mama Masawe hakuweza kumsikiliza
tena. Alimkumbatia Lina kwa nguvu na kupiga kelele, “Inatosha! Ni wazi Lisa
ndiye aliyetulazimisha kufikia hatua hii, lakini bado unamlaumu na kumpiga
Lina. Unataka tu kumalizia hasira yako
kwa kumuonea mtu mwingine."
“Bado una ujasiri wa kusema hivyo?
Binti mzuri uliyemlea mwenyewe hana
haya wala aibu. Ninachojutia zaidi ni kwamba nilikuoa na kumzaa!”
"Sawa, kwa kuwa unajuta, tutaondoka!"
Mama Masawe alilia na kuushika
mkono wa Lina kabla ya kutoka nje.
Muda si muda, nyumba nzima ikawa
tupu na ya kutisha.
Sura ya 132
Jones alitetemeka upepo wa baridi
ulipovuma. Kwa mara ya kwanza, hisia ya majuto ilipanda moyoni mwake.
Ilikuwa wazi kuwa alikuwa na familia
nzuri. Ilivunjikaje kwa muda wa miezi mitatu tu?
Siku iliyofuata, Jones alipokea simu kwamba alikuwa amefukuzwa kutoka
kwenye bodi ya wakurugenzi wa Mawenzi Investments. Alikimbilia
kwenye kampuni hiyo kwa hasira, lakini mlinzi wa mlangoni hakumruhusu kabisa kuingia na kumfukuzia nje. Kwa
kuwa hakuwa na mahali pengine pa kwenda, Jones aliishia kulewa kwenye baa na alirudi tu nyumbani usiku wa
manane.
Usiku huo, kwa ulevi alisukuma mlango
wa nyumba yake kwa unyonge na
hakukuwa na taa ndani, na mwanga wa
mbalamwezi wa baridi ulipenya kupitia
madirishani. Kulikuwa na kiti cha magurudumu katikati ya sebule, na juu
yake aliketi mwanamke mzee mwenye
mgongo ulioinama na nywele
zilizotawanyika. Sura hiyo ilionekana ya kutisha haswa. Jones aliogopa sana hivi
kwamba miguu yake ilidhoofika.
Aligeuka na kujaribu kukimbia. Hata
hivyo, mlango ulifungwa nyuma yake, na sebule ikawa giza.
“Mama…” Jones alipiga magoti chini
kwa woga, akitetemeka kama jani
lililosukumwa na upepo.
“Mwanangu, mbona unaniogopa sana?”
Kiti cha magurudumu kiliteleza mbele
polepole, na sauti ya mwanamke mzee
ikasikika.
Jones alirudi nyuma kwa hofu. “Mama, mama, usije. Tafadhali, si mimi niliyekudhuru. Kuna mtu mbaya."
“Si wewe uliyenidhuru?” Kicheko cha kutisha cha yule kikongwe kilisikika pale
sebuleni. "Ulifanya hivyo kwa ajili ya hisa na pesa. Lakini kwa nini
umenidhuru? Si nilikutunza tangu ujana? Ulimwengu wa kuzimu hautaki
kunikubali kwa sababu mliniondoa kabla ya siku zangu, kwa hivyo imenibidi tu kurudi kukutafuta. Mwana…”
Kiti cha magurudumu kilikuwa kikikaribia zaidi na zaidi. Jones alipiga magoti chini
na kuinama kwa nguvu, machozi na vilio vikimtoka. “Mama, nilikosea. Nilikosea.
Nilianza kuhangaika, lakini sikutaka kukuumiza. Ilikuwa Mama Masawe.
Mama Masawe ndiye alikusogezea mto.
Nenda kwake badala yake.
“Kama hukukubali, angeniua?”
Mwanamke mzee alicheka na kulia
wakati huo huo.
“Mama, samahani.” Jones alibubujikwa na machozi, akijihisi mnyonge. “Nilitiwa moyo na wawili hao, mama na bintiye.
Sikutaka kukukuua, samahani. Tafadhali niache uende…”
"Kwa kuwa unajua kuwa ulikosea, nitakuondoa sasa." Mkono wa mwanamke mzee ulimshika, lakini
Jones aliogopa sana kusogea. Doa lenye unyevunyevu lilimtoka kwenye
‘gongo’ lake huku akijikojolea. Taa ziliwaka ghafla!
Maafisa kadhaa wa polisi walitoka jikoni, na mwanamke mzee kwenye kiti cha magurudumu akavua wigi lake kabla ya kusimama.
Jones alipigwa na butwaa na kutetemeka. “Shangazi Manka…”
"Bwana. Jones, kuna mtu aliripoti
kwamba unashukiwa kumuua Madam
Bibi Masawe. Na wewe mwenyewe
umekiri hapa. Polisi sasa
wanakukamata rasmi.” Afisa huyo akatoa pingu na kumfunga mikono.
“Hapana, hapana…” Jones alijitahidi sana kujificha. “Nilikunywa pombe kupita kiasi. Nilikuwa naongea ujinga tu.”
"Mjomba, nimerekodi kila neno ulilosema." Lisa alitoka na simu. Uso wake ulikuwa umejaa huzuni. “Ulikuwa mwana pekee wa kiume wa bibi. Alikuwa mzuri kwako na alikulea kwa uchungu, lakini mwishowe, ulipanga njama na wengine kumuua. Bado unakumbuka jinsi alivyokufa? Je, huoti ndoto mbaya? Je! dhamiri yako haikuumi?”
“Usiseme tena…” Jones alikuwa tayari
amekunywa pombe nyingi. Sambamba na jinsi alivyokuwa amepatwa na woga, akili yake ilikuwa karibu kuzimia.
Lisa alisema kwa ujeuri, “Tayari nimekusanya ushahidi mwingi. Ikiwa
hutaki kufa gerezani, bora utoe ukweli wako kwa uaminifu.
Vinginevyo, Mama Masawe bila shaka atajaribu kukwepa mashtaka
mahakamani baadaye.”
Jones hakumwamini. “Umekusanya ushahidi gani?”
"Bibi alitibiwa hospitalini, na hospitali ina rekodi zake za matibabu. Daktari
alisema kwamba ingawa bibi alikuwa
amepooza wakati huo, haikuwezekana afe ghafla hivyo. Pia kuna Aunty Helen
ambaye ulimwajiri badala ya Aunty
Manka kumtunza Bibi. Yuko tayari
kufika mahakamani sasa…”
Jones aligeuka rangi. Alijua kwamba
alikuwa katika matatizo.
Kama asingetoa ushahidi muda huo,
basi angeweza kuishia jela wakati
Mama Masawe angesukuma shutuma
hizo kwake. “Sawa, nitakiri. Ilikuwa
Mama Masawe. Alichukua fursa wakati
bibi yako alikuwa amelala na…” Labda
ilikuwa dhamiri yake ya mwisho, lakini
hatimaye Jones alianguka chini na kulia.
Lisa na Aunty Manka nao walilia. Hawakutarajia mwisho wa Madam Bibi
Masawe kuwa mbaya kiasi hicho.
Aunty Manka aliuliza, “Swali la mwisho.
Siku hiyo bibi madam Masawe
alipoanguka kutoka kwenye ngazi, ni Lina ndiye aliyemsukuma?"
Masawe alitikisa kichwa, lakini akifikiria
juu ya utu wa Lina, alihisi kwamba labda
alifanya hivyo. Hata hivyo, alikuwa na
binti mmoja tu na hakutaka aende jela.
"Kwa kweli sijui kuhusu hilo." Jones
Mwishowe, Jones alichukuliwa na polisi
kwa mahojiano. Lisa alitazama jumba la giza nyuma yake. Hapo awali palikuwa
nyumbani kwake, lakini sasa palikuwa mahali ambapo hakutaka tena kukanyaga. Alichukua funguo na kuzitupa kwenye nyasi kabla ya kugeuka na kutoka nje ya mlango.
Gari lao la kifahari lilikuwa limeegeshwa mlangoni. Alvin alikuwa amesimama
huku kaegemea gari. Kulikuwa na mvua kidogo usiku huo, na matone ya mvua
yalitua kwenye kichwa na mabega yake. Lisa alimtazama kwa mahaba, macho yake mazito na safi yalipendeza kama mwanga wa nyota pekee angani.
Wakati huo, Lisa, ambaye hakuwa na
nyumba, alionekana kuwa amepata
nyumba. Aliruka mikononi mwake, na
Alvin akafunua koti lake ili kumfunika
ndani yake.
"Alvlisa, hatimaye nimelipiza kisasi."
Lisa akasonga mikononi mwake. “Lakini sina furaha hata kidogo. Ninajuta
kwamba sikukaa zaidi na Bibi hapo awali. La sivyo, asingekufa vibaya hivyo.”
Machozi ya Lisa yalilowanisha shati kifuani mwa Alvin. Alvin hakujua jinsi ya
kuwafariji wengine. Alimsubiri amalize kulia na huku akimpigapiga tu kichwani.
“Umefanya vizuri usiku wa leo. Hakukuwa na ushahidi wowote bado
uliweza kumfanya Jones Masawe akiri yeye mwenyewe!"
“Nilicheza kamari, kupata ama kukosa.
Nilicheza kamari juu ya ubinadamu
wake. Nilicheza kamari kwenye kile
kilichosalia kwenye hatia na dhamiri ya
Jones. Nilicheza kamari kwamba
angekuwa mbinafsi kiasi cha
kumsingizia Mama Masawe.” Sauti ya
Lisa iliendelea kusikika. "Nilikuwa tayari
nadhani kwamba Jones asingefanya
hivyo mwenyewe. Ili kupunguza adhabu yake, bila shaka angesema kwamba ni Lina au Mama Masawe waliofanya hivyo. Kwa kweli sikutarajia Mama Masawe angekuwa mkatili kiasi hicho.”
“Mama Masawe ana uhakika wa kwenda jela. Twende, usiku umeenda sana.” Alvin alifungua mlango wa gari.
Lisa ghafla akashika mkono wake. Macho yake makubwa meusi
yalitazama ndani yake aliposema, “Alvlisa, nina wewe tu sasa. Utaniacha pia?”
“Sitafanya hivyo.” Alvin akainama na kumbusu kwenye paji la uso huku akiongea kwa upole.
Lisa alifumba macho. Kwa wakati huo, alifikiria kwamba asingemuacha kamwe
maishani mwake. Ni baadaye tu ndipo
alipogundua kwamba walikuwa bado
wachanga sana kwenye mapenzi, na kulikuwa na mambo ambayo
yangebadilika.
•••
Saa tisa usiku, Lina na Mama yake
walikuwa wamelala fofofo kwenye
chumba cha hoteli. Kengele ya mlango ililia ghafla.
"Ni nani huyo?" Mama Masawe
alifungua mlango kwa hasira. Alifikiri
kwamba ni Jones ndiye aliyewafuata kuwafanyia fujo.
Hata hivyo, mara mlango
ulipofunguliwa, kundi la polisi liliingia na kumfunga pingu. “Mama Masawe, unashukiwa kumuua Mzee Madam
Masawe. Upo chini ya ulinzi!”
"Nini?" Mama Masawe alipigwa na
butwaa na kuruka kwa haraka.
"Sikumuua mimi."
“Mumeo tayari ameshatoa maelezo
kamili kituoni. Ni wewe uliyemkaba mama mkwe wako kwa mikono yako
mwenyewe.” Macho ya polisi yalijaa dharau. Mwanamke huyo hata alimuua
mama mkwe wake mwenyewe! Mtu wa aina hii hakuwa na maadili kabisa. Polisi
hawakumpa nafasi ya kujitetea, wakamtoa nje.
“Mama, nini kinaendelea?” Lina
alikurupuka kutoka kitandani na kukimbilia kumshika, lakini polisi
hawakumruhusu kumgusa.
Sura ya 133
Mama Masawe akapaza sauti na kusema, “Baba yako ni mnyama!
Kaenda kunichongea polisi kuwa
nilimuua bibi yako. Lina, lazima ujilinde.”
Mama Masawe alichukuliwa upesi, na
Lina akaanguka chini. Alikuwa
ameteseka kijijini kwa zaidi ya miaka 20, na haikuwa rahisi kwake kuja mjini. Lakini, kabla hata mwaka haujaisha, familia yake ilisambaratika kabisa! Ikiwa kitu kingetokea kwa Jones Masawe na Mama Masawe, angekuwa na sifa gani za kuwa binti mkubwa wa familia ya Jones? Hapana, hapana. Hakutaka kurudi enzi hizo!
Alimpigia simu Stephen Kileo kwa
haraka. “Stephen, nakuomba. Tafadhali nisaidie. Mama na baba yangu
wamekamatwa na polisi. Maadamu utanisaidia, nakuahidi kuwa nitakuwa mkeo. Nitakupa nusu ya hisa za
Mawenzi Investments.”
“Lina Jones, nimeelewa sasa. Bahati
mbaya humwandama yule aliye pamoja
nawe. Kwanza, ilikuwa Ethan Lowe, na
sasa mama na baba yako wanaenda
jela. Sifa yangu pia iliharibiwa kabisa na
wewe. Potea na ukae mbali nami siku
zijazo. Kukuona tu kunanifanya nitamani
kutapika!” Stephen alikata simu moja
kwa moja. Lina alipigwa na butwaa kabisa.
Hakuweza kuelewa. Haikuwa kitambo
kirefu matajiri wote huko Masaki
walikuwa wamemshikilia. Ilikuwa
imechukua muda mfupi tu, na sasa, kila
kitu kilikuwa kimebadilika. Kila kitu
kilikuwa kosa la Lisa Jones! Aliamini ni Lisa aliyemharibia maisha na
kumdumbukiza katika hali hiyo mbaya.
Kwa nini Lisa alikuwa bado yupo hai?!
Moyo wa Lina ulikuwa umejaa wazimu.
Wakati huo alikumbuka kitu kama mtu
aliyeshukiwa na roho mtakatifu na
kufunuliwa jambo. Alikumbuka alikuwa
na picha za Lisa alizopigwa hotelini siku
ambayo Lina alimtengenezea njama za
kubakwa. Ni siku ile ambayo alilaghaiwa
kwenda kuwasilisha michoro yake
hotelini kwa ajili ya mradi wa Mawenzi
aliokuwa akiupigania kuupata, ambapo
kwa bahati nzuri aliokolewa na Kelvin.
Alikumbuka picha hizo zilikuwa kwenye
simu yake. Alipoziona, alishtuka kwanza kabla ya kusisimka mara moja.
Picha hizo zilikuwa za Lisa akiwa karibu
sana na Kelvin Mushi utasema ni wapenzi. Alijua kutoka eneo ambalo
picha zilipigwa kuwa ni wakati wa kumtia Lisa dawa ndani ya chumba cha
hoteli.
Hapo awali, Lina alitaka wanaume fulani
wambake Lisa, lakini Kelvin Mushi
alikuwa amefika kwa wakati. Lakini Lina
alifanikiwa kupata picha za video
zilizomwonyesha Kelvin akiwa kamnyanyua Lisa mikononi mwake.
Hakutarajia kamwe kwamba zingekuwa bado zimo kwenye simu yake.
kukaa na Alvin?” Lina aliwaza kwa
“Haha, kwa picha hizi, Lisa atawezaje
furaha. Sifa yake kama mwenyekiti wa Mawenzi Investments pia ingeathiriwa. Lina alitafuta haraka nambari ya mwandishi wa udaku!
•••
Saa tatu asubuhi Lisa alipoamka, alikuwa peke yake kitandani. Mvua
ilikuwa imenyesha usiku kucha na alilala usingizi mnono sana. Sasa kwa kuwa
alikwisha lipiza kisasi kwa kifo cha bibi yake na Bibi na Bwana Masawe wote
walikuwa jela, alihisi utulivu na raha kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu.
Pia ilikuwa ni nadra kwake kuamka akiwa amechelewa sana.
Alikaa na kuangalia muda lakini
akagundua kuwa kuna missed call nyingi kwenye simu yake. Nyingine
zilikuwa kutoka ofisini, nyingine kutoka
kwa Kelvin, na hata kulikuwa na missed calls nyingi zaidi kutoka Pamela.
Pamela alikuwa amempigia simu mara
saba au nane.
Haraka alimpigia tena huku akicheka.
“Mbona umenipigia simu mara nyingi sana asubuhi? Kuna kitu kilitokea?"
“Kuna kitu kilikutokea? Inamaana bado hujui?” Sauti ya wasiwasi ya Pamela ilisikika. "Nenda uangalie habari zinazovuma sasa."
Lisa alipigwa na butwaa alipoingia
mtandaoni. Aliona video iliyokuwa inatrend ikiwa na jina lake na Kelvin na kubofya habari ile. Matokeo ya utafutaji yakasomeka, 'Mwenyekiti mrembo wa
Mawenzi Investments afumwa kwenye pozi tata na mpenzi wake' ghafla yalitokea.
Lisa alihisi kuogopa. Alipobofya kwenye
makala hiyo, alipigwa na butwaa kuona
video ya Kelvin Mushi akiwa kambeba
juujuu huku akiwa kamwinamia kama
anambusu shingoni. Chumba kilikuwa na baridi, lakini ghafla alihisi joto sana!
“Unafanyiwa njama?”
Pamela alisema
kwa wasiwasi, "Kwa utu wako, haiwezekani kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu mwingine zaidi ya Alvin. Ninakuamini, lakini wengine wanaweza wasikuamini.”
Pamela alikuwa hajamaliza kuongea wakati mlango wa chumba cha kulala
ulifunguliwa kwa nguvu. Alvin aliingia kwa nguvu huku uso wake mzuri ukiwa
umefunikwa na hasira kali. Machoni mwake kulikuwa na sura iliyoonyesha
hakutaka kitu zaidi ya kumrarua vipande vipande. Lisa alikuwa hajamwona akiwa na hasira hivi kwa muda mrefu. Haraka
akakata simu na kumueleza. “Umeona hizo picha? Usielewe vibaya—”
“Kwa hiyo unataka nikupongeze, sivyo?"
Alvin aliikamata simu iliyokuwa
mikononi mwake na kumrushia. Macho
yake ya giza yalifunikwa na tamaa, karaha, na chuki. “Angalia wewe
mwenyewe hizo picha za kuchukiza.
Unadai kuwa humpendi Kelvin Mushi, lakini ulimkumbatia kwa nguvu na hata
kumvua nguo. Lisa Jones, mbona huna haya?” Simu yake iligonga kifua chake kwa
nguvu. Ilimuuma, lakini sio kama moyo wake ulivyouma. Ni wanaume wangapi
wangeweza kutulia ikiwa wangeona picha kama zile? Alikuwa kavurugwa kabisa na hizo picha zake.
“Hapana, nilifanyiwa njama, sema tu sikukuambia ukweli! Usiku huo, Lina Jones alinilazimisha kunywa dawa, na Kelvin Mushi alitokea kwa bahati nzuri
akaniokoa. Hakuna kilichotokea kati yetu." Lisa alitikisa kichwa kwa
masikitiko huku akieleza, “Nilijiloweka kwenye maji baridi usiku kucha.”
"Unanichukulia kama mjinga?" Kicheko
cha kutisha cha kijeuri kilisikika kutoka
kwenye koo la Alvin. “Uliponilisha kwa
hila madawa kama hayo, hata
mwanamume kama mimi nilishindwa
kuvumilia. Ilinibidi niende hospitalini
kuwekewa dripu ili nipate nafuu, lakini
wewe unasema ulishinda kwa
kujiloweka kwenye maji baridi tu?”
“Ninasema ukweli.” Lisa alilazimisha
kujibu malalamiko yake na kujaribu kueleza, “Naweza kuapa—”
"Nyamaza! Lisa Jones, kwa kweli
sitakuelewa!” Alvin ghafla akashika
kidevu chake kwa nguvu. “Unajifanya
kuwa msafi na mtulivu mbele yangu, ukisema kwamba unaogopa… Kumbe ni janja janja yako tu kuendelea
kunifanya mjinga?! Ngoja nikuulize.
Picha hizi zilipigwa lini? Nakumbuka…
nilienda Nairobi kwa siku chache na
Shangazi Linda akasema hukurudi
usiku kucha…”
“Sikufanya hivyo! Hakuna kilichotokea kati yangu na Kelvin, simpendi…” Lisa akatikisa kichwa kwa nguvu.
"Kwa hivyo mawazo yangu yalikuwa
sawa." Alvin hakumsikiliza hata kidogo. Macho yake yalijaa dhihaka na kejeli.
“Nilikupigia simu usiku ule. Simu yako ilikuwa imezimwa usiku kucha. Hah, kumbe ulikuwa na Kelvin Mushi, sivyo?"
Kadri alivyozidi kuongea ndivyo hasira zilivyozidi kumpanda. Ilikuwa ni kama
kuna jeraha kwenye moyo wake, na chumvi iliendelea kupakwa juu yake.
Ilimuuma sana hata akashindwa kupumua. Pamoja na mashaka na shutuma zake, moyo wa Lisa ukazidi kuwa mzito na mzito. Kulikuwa na uaminifu mdogo
sana kati yao. Kwa kweli hakujua jinsi ya kumshawishi. “Kama… Kama
huniamini, unaweza kuangalia
mwenyewe,” Lisa alikunja ngumi na
kusema bila kujielewa.
Alvin alicheka kana kwamba amesikia mzaha. Sauti yake ilijaa dharau
alipozungumza, “Baada ya kutazama hizo picha, kukutazama tu kunanifanya nijisikie mchafu. Sitathubutu kushika mwili wako mchafu. Kumbe ndiyo
maana jana machale yalishika nikaacha.”
Lisa alijeruhiwa sana moyoni mwake.
Jana yake usiku, alijisikia kana kwamba
alikuwa mwanamke mwenye furaha
zaidi duniani, lakini mara tu kulipopambazuka, ilionekana kana
kwamba dunia nzima ilikuwa
imeporomoka. Picha hizo zilitoka wapi?
Alikumbuka kwamba wakati
wanaondoka, Kelvin alisema kwamba
aliivunja kamera. Haraka akapiga
namba ya Kelvin.
Simu ilipounganishwa, sauti ya Kelvin ya wasiwasi ilisikika. “Lisa, tayari nimeshaona kila kitu. Mimi sina neno ila nina wasiwasi na wewe. Alvin atakuelewa kweli? Naweza kumpigia simu ili nimweleweshe?”
Sura ya 134
Hapo awali, Lisa alihisi mashaka kidogo, lakini baada ya kusikia sauti ya
Kelvin, alihisi kwamba alikuwa na mawazo potofu. Kelvin alikuwa muungwana sana. Asingeweza kamwe kueneza picha kama hizo.
“Amekasirika sasa. Ukimpigia simu
utazidi kumkasirisha zaidi.” Lisa alitabasamu kwa uchungu. “Si ulisema siku ile uliharibu kamera? Kwa nini…”
"Niliiharibu. Hata niliiangalia wakati huo hakukuwana picha zozote." Sauti ya
Kelvin ilionyesha jinsi alivyokuwa na
huzuni. "Nadhani kamere zilikuwa
zinahamisha picha wakati zikirekodi. Nilikuwa mzembe. Niligundua kuwa
picha hizo mtandaoni zilisambazwa na ripota baada ya kupewa na Lina.”
Lisa alitabasamu kwa hasira. Alikuwa amemdharau Lina. Picha hizi zilikuwa za uchochezi sana.
“Samahani.” Kelvin aliomba msamaha
tena. “Sijali kwa vile mimi ni mwanaume, lakini itaathiri sana sifa
yako. Ikiwa kuna chochote ninachoweza kukufanyia, nijulishe tu na nitajaribu niwezavyo kukusaidia.”
"Asante. Nina simu kutoka ofisini ninayohitaji kuipokea. Tuongee baadaye.” Lisa haraka akakata simu kwa Kelvin na kupokea simu kutoka kwa msaidizi wake, Tunu.
“Mwenyekiti Jones, njoo ofisini haraka.
Uvumi kuhusu kashfa yako unavuma na laini ya simu ya kampuni inashikiliwa na
waandishi wa habari. Inabidi
ushughulikie jambo hili haraka
iwezekanavyo.”
“Sawa, nitakuja mara moja.” Lisa
hakujali tena na kubadilisha nguo zake haraka kabla ya kushuka.
Alipotoka nje, aligundua kwamba Shani
hakuwepo na hakumfuata tena ili kumlinda. Moyo wake ukaingia giza.
Alvin ndiye alikuwa amepanga Shani
amlinde. Sasa kwa kuwa alitaka
kumuacha, alimfukuza Shani pia.
Baada ya kufikia kwenye kampuni hiyo, waandishi wengi walikuwa
wamesimama mlangoni. Aliingia kutoka
kwenye viwanja vya maegesho.
Alipopanda ghorofani, watendaji kadhaa
walikuwa tayari wakimsubiri ofisini.
"Mwenyekiti Jones, kuna wanamtandao wengi kwenye mtandao wanaokukaripia kwa kuwa... 'wazi' sana…” Paji la uso la
Freddie Ngololo lilijawa na jasho baridi. Tayari alikuwa ametumia neno lenye
ukakasi sana. “Kwa kifupi, hali si nzuri sana na sifa yako kama mwenyekiti wa kampuni naogopa kusema kwamba inaathiri sana.
Uso wa Lisa ambao tayari ulikuwa
umekunjamana ulizidi kuwa mbaya.
Mara nyingi alisoma magazeti ya udaku
mtandaoni na alijua vyema uovu wa watumiaji wa mtandao dhidi ya wanawake katika kashfa kama hizi.
"Je, idara ya PR ina mawazo yoyote?"
Lisa aliuliza huku akikuna kichwa.
Meneja Mkuu Ngololo alisema, “Idara
ilifanya mkutano mapema asubuhi.
Tunafikiri njia bora ni kutangaza rasmi
kuwa wewe na Kelvin Mushi ni wapenzi
ili kushusha joto. Kwa kweli, hata
wafuatiliaji wa habari hii wanasema
Kelvin Mushi na wewe mnaendana sana
na mnalingana vyema katika hali ya kijamii. Hakika utapokea mwitikio
chanya kutoka kwa watu mitandaoni na kashfa hii itageuka kuwa baraka
kwako.”
"Ndiyo…Ndiyo!" Meneja wa idara ya PR alitabasamu haraka na kusema, “Wakati
huo, tunaweza pia kuipandisha hadhi
Mawenzi Investments, Kwa taswira
yako kama mwenyekiti wa bodi, na taswira ya Kelvin Mushi kama
mwenyekiti wa Golden Corporation, mnaweza kuwa mabalozi wazuri wa kampuni.” Watendaji walikubaliana na wazo hili.
Kadiri Lisa alivyozidi kusikiliza ndivyo
alivyozidi kukosa la kusema. "Hapana, tayari nina mpenzi."
Meneja Mkuu Ngololo alianguka kwa aibu. “Sawa… Lakini ulipigwa picha ukiwa na Bwana Mushi. Ukikataa, itakuwa mbaya kwa picha yako, na kila mtu atakudharau kwa kuwa na maisha ya faragha yasiyo na uaminifu. Ikiwa suala hili halitashughulikiwa vyema, sura ya Mawenzi Investments itaathirika pakubwa.”
"Niliwekewa madawa ya kulevya wakati huo. Unaweza kueleza moja kwa moja kwenye tovuti rasmi.” Lisa alisimama na kuwatazama watendaji hao kwa macho makavu. "Hii ni kampuni ya mali isiyohamishika. Maadamu mali zetu zimejengwa kwa ubora mzuri, bado tunaweza kupata nyota zilizo na picha nzuri za kututangaza. Ikiwa kweli
tumeathiriwa, basi haiwezi kusaidia.
Siwezi kumuumiza mpenzi wangu kwa
sababu ya kampuni, kama vile baadhi yenu hamtawaacha wake zenu kwa ajili ya faida. Kila mtu ana msingi wake."
Umati ukanyamaza. Baada ya nusu dakika ya kimya, Meneja Mkuu Ngololo
alitikisa kichwa. "Tutafanya kama Mwenyekiti Jones anavyosema."
Baadaye, ukurasa wa Facebook wa
Mawezni ulichapisha taarifa kwa umma.
[Picha zilipigwa zaidi ya mwezi mmoja
uliopita. Mwenyekiti Jones alifanyiwa njama na kulishwa madawa ya kulevya.
Kwa bahati nzuri, Kelvin Mushi
alionekana kwa wakati na kumuokoa
Mwenyekiti Jones, lakini hakuna
kilichotokea kati ya pande hizo mbili.
Wawili hao bado ni marafiki wa karibu
sasa. Tunatumai kila mtu ataelewa na ataacha kujadili suala hilo.]
Kisha, Kelvin binafsi ali’share chapisho hilo. [Wakati huo, Mwenyekiti Jones alikuwa
ameleweshwa dawa za kulevya, lakini
aliokolewa haraka na kulowekwa
kwenye bafu baridi. Ni mwanamke
mwenye heshima sana. Natumai kuwa
watu hawatamwelewa vibaya na kumtusi kwa sababu ya picha chache.]
Baada ya chapisho kupakiwa, athari
ilikuwa nzuri ya kushangaza.
Watu wengi walimsifu Kelvin kwa kuwa
mungwana na msikivu, na Lisa kwa
kuwa hodari na jasiri. Baadhi ya watu
hata waliwashauri na kuwaambia wawe
wapenzi badala ya marafiki. Walisema
walikuwa ni kapo zinazofaa zaidi katika ulimwengu wa biashara.
Katika kampuni ya sheria, Jennings
Sollicitors, Ofisi ilionekana kuwa na giza la ukiwa. Alvin alikuwa amekaa siku
nzima kwenye simu yake. Asubuhi, kila
mtu alimkemea Lisa, lakini upepo
ulibadilika ghafla mchana. Kila mtu
alipiga kelele kwa Lisa kuungana na Kelvin.
Aliibomoa simu yake pale pale kwa hasira. "Hivi watu kwenye mtandao siku
hizi hawana kitu cha maana cha kufanya? Eti hawa wawili wanaendana vizuri? Hivi ni vipofu?”
Hans aliyekuwa amesimama pembeni aliitazama ile simu iliyosambaratika akiwa hoi. Angelazimika kununua simu mpya tena. Hakujua hata idadi ya simu
ambazo Alvin alikuwa amevunja tangu awe na Lisa.
“Bwana Kimaro, watu kwenye mtandao wote ni wavivu sana. Usiwajali.” Hans alimpoza kimawazo.
Alvin alikodoa macho. Hakutaka, lakini
alikuwa amesoma yale ambayo watu
walisema kuhusu Kelvin Mushi kuwa na mapenzi makubwa kwa Lisa, na Lisa
kuwa na hisia nzuri kwa Kelvin.
Kulikuwa na watu wanaotunga hadithi
ya mapenzi ya kipuuzi kuhusu
kupendana kwao kwa siri.
Tumbo la Alvin liliwaka kwa hasira.
Akaketi na kufungua laptop yake, vidole
vyake vikiruka kwenye keyboard.
Dakika chache baadaye, Hans
aligundua kuwa habari ya Kelvin na Lisa
ilikuwa imetoka kwenye habari
zanazovuma mtandaoni! Ilishangaza!
Bwana Kimaro kweli alikuwa amedukua
akaunti ya facebook ya Mawenzi moja kwa moja.
“Alvin...” Mlango wa ofisi ulifunguliwa
ghafla na Sam Harrison akaingia.
Alipomwona Alvin ambaye alionekana
kama mfalme wa pepo, alitetemeka.
“Nilifanya uchunguzi. Usiku huo, Lina
Jones aliingia na watu wachache na
alionekana kwenye jumba hilo la hoteli.
Wakati huo, pia alimwagiza meneja wa
hoteli hiyo kwamba hakuna mtu
anayeruhusiwa kuingia katika chumba alichopanga.”
Alvin alikodoa macho. Ilionekana kana kwamba tukio hilo la Lisa lilikuwa ni njama. Hata hivyo, jinsi alivyokuwa amembusu Kelvin kimahaba bado
ilimkasirisha. "Umegundua ni wakati gani Lisa na Kelvin waliondoka?" Aliuliza kwa huzuni.
"Asubuhi," Sam alikohoa kwa upole na kusema kwa sauti ya chini, "Walitoka asubuhi baada ya kubadilisha nguo."
Maneno hayo yaliposikika, Alvin aliivunja kompyuta moja kwa moja.
Mwanamume na mwanamke katika
chumba pamoja, na mwanamke hata
kulishwa madawa ya kulevya.
Inawezekanaje kuamini kwamba
hakuna kilichotokea kati yake na
Kelvin?
Sam alimtazama kwa huruma. Kusema kweli, pia hakuamini kabisa kwamba
Lisa hakuwa na hatia. “Sawa… Lisa pia ni mwathirika katika hili… Nilisikia
kwamba Lina Jones aliingia na walinzi wawili wakati huo. Kama Kelvin Mushi
asingetokea, matokeo yangekuwa mabaya zaidi.”
"Unamaanisha nini? Unasema
ninapaswa kumshukuru Kelvin Mushi?”
Macho jeuri ya Alvin yalimtoka.
"Mwishowe, yeye ndiye mjinga.
Anaendelea kuanguka kwa hila za
familia ya Jones mara kwa mara.
Baadaye, alijaribu hata kunihadaa na
kuwa marafiki na Kelvin. Ananichukulia
kama mjinga”
Sam alikuna ncha ya pua yake na
kusema. “Hata hivyo, tayari
nimekuchunguzia. Ni juu yako ikiwa
unataka kuachana naye au kuendelea naye.”
Alvin hakuwa na mahali pa kutoa
uchungu wake. Aliwasha sigara na kumwambia Sam. "Twende tukanywe
vinywaji vichache na mimi leo usiku."
Sura ya 135 Usiku huo, Alvin alikunywa glasi baada ya glasi ya pombe. Sam hakuweza
kumzuia. Uvumilivu wa pombe wa Alvin
ulikuwa mkubwa, lakini alikunywa sana
usiku huo na cha kushangaza alilewa kidogo. "Nimemkumbuka Sarah ghafla."
Alitazama usiku nje ya dirisha na
kunong’ona, “Kati ya wanawake wote
waliobahatika kuingia kwenye maisha
yangu, ndiye pekee aliyekuwa na moyo
wake wote kwangu. Hakukuwa na
udanganyifu na hakukuwa na usaliti.
Kwa nini alikufa?”
Sam alishika glasi yake, maumivu makali yakimtoka moyoni.
Kile ambacho wengine walikiona kwa
Alvin kilikuwa ni Kilima cha juujuu
kilichoonyesha ufahari wake, lakini Sam alijua kwamba Alvin alikua bila mapenzi ya wazazi wake. Ndani ya moyo wake
alikuwa ni mtu asiyejiamini sana katka
suala zima la mahusiano. Hata
alipokuwa akisoma shule, waliomwendea walikuwa na ajenda za siri na kumfanya aingiwe na mashaka makubwa. Wakati huo, Alvin aliumia
sana. Kama rafiki yake, Sam ghafla alijuta
kumwita Dar es Salaam. Hakutarajia
kwamba moyo wa Alvin, ambao siku
zote ulikuwa umeganda, ungehamaki
ghafla. Sam aliongozana naye kunywa
hadi Alvin akalewa sana. Ilikuwa ni mara ya pili Sam kumuona Alvin akiwa
amelewa kiasi hicho.
Kwenye meza ya vinywaji, simu mpya ilitetemeka kila mara. Lisa alikuwa
akimpigia simu Alvin mara kwa mara. Sam alichukua simu na kuitikia. Sauti ya Lisa ilisikika kutoka upande wa pili. “Uko wapi? Mbona umechelewa sana? Njoo nyumbani, tutayaongea tu yataisha sawa…"
"Alvin amelewa." Sam akamkatisha.
"Nakuja kumchukua mara moja," Lisa alisema kwa hofu.
"Hakuna haja. Hutaweza kumbeba hata hivyo. Nitamrudisha mimi mwenyewe.”
Baada ya simu kukatika, Lisa alisubiri mlangoni. Kulikuwa na mvua usiku huo
tena, na matone ya mvua yalidondoka
nje na kulowanisha kila kitu. Nusu saa
baadaye, Sam aliegesha gari lake.
Alipumua kwa huruma na upole baada
ya kumuona Lisa akiwa amesimama
kwenye upepo wa baridi.
Baada ya gari kuegeshwa, Lisa alifungua mlango wa siti ya nyuma.
Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumuona Alvin akiwa amelewa sana.
Uso wake mzuri ulionyesha wazi kuwa alikuwa amelewa, na alionekana
kupoteza fahamu pale kwenye siti ya nyuma. Yeye na Sam walimsaidiana
kumwingiza Alvin hadi chumbani pamoja. Lisa alimtazama Sam huku
akihisi mnyonge. “Bwana Harrison, asante. Mimi…”
“Ni sawa, Alvin aliniambia niachunguze jambo hili. Najua hukukusudia.” Sam
alikuwa na maumivu ya kichwa. Pia
hakujua la kusema. “Nitaondoka sasa hivi.”
Lisa aliona kuwa Sam alikuwa
akimchukulia tofauti na hapo awali.
Hakucheka na kutabasamu kama
alivyomfanyia siku za nyuma. Alikua na huzuni kidogo kwa sababu yake. Alijua
kwamba hakutaka kuzungumza naye sana, lakini hakuweza kujizuia kuuliza, “Bwana Harrison, unajua Alvin anachofikiria kuhusu hili?”
"Lisa, mwanaume yeyote angechukizwa na hilo," Sam alisema bila kuficha, "Ungemwambia Alvin juu ya hili mapema. Sasa kwa kuwa imejulikana bila wewe kusema, kusema kweli inatia uchungu sana.”
Uso wa Lisa ulipauka. “Hakuna kilichotokea kati yangu na Kelvin. Ni kweli."
“Ni bure kuniambia hivyo. Unahitaji Alvin
akuamini.” Sam akatikisa kichwa na kuondoka.
Lisa alibaki ameduwaa kwa muda.
Alielewa nini Sam alimaanisha. Alvin hakumuamini. Afanye nini? Alikuwa
anampenda kweli sasa. Hakutaka kumuacha. Alimtazama sana yule mtu pale kitandani. Huenda ikawa ni kwa sababu alikuwa amekunywa pombe
kupita kiasi na hakujisikia vizuri, hivyo tumbo lake pia likawa na usumbufu.
Aliendelea kupapasa tumbo lake. Kiyoyozi cha kuongeza joto kiliwashwa mle chumbani na hakuwa amevua koti lake, kwa hiyo jasho likatoka upesi
kwenye paji la uso wake. Lisa alichota beseni la maji ya baridi. Alivua koti lake, akafungua kola ya shati lake, na kuufuta uso wake mzuri kwa taulo.
“Sarah…” Mwanaume huyo alimshika
mkono ghafla, na manung’uniko ya chinichini yakatoka kwenye midomo
yake myembamba. Lisa aliganda kana
kwamba ndoo ya maji baridi
imemwagwa juu yake.
Sarah? Huyo alikuwa nani? Je, alikuwa mpenzi wake wa zamani?
Lisa aliuvuta mkono wake kutoka kwenye mshiko wake kwa nguvu.
Mkono wa mtu huyo ulishika hewa, na akamwita tena, “Sara”.
Aligeuka na kukaa pembeni ya kitanda.
Macho yake yalikuwa mekundu, na moyo wake ulikuwa umechomwa kana
kwamba alikuwa akichomwa kisu.
Inauma! Asubuhi iliyofuata, Alvin aliamka na hangover. Kichwa chake kilimuuma, na tumbo lake lilihisi kukosa raha pia.
Alitazama mazingira na kugundua kuwa alikuwa katika chumba chake cha kulala
katika nyumba yake. Kwanini Sam
alimrudisha pale? Kwa kweli hakutaka
kukutana na Lisa kabisa. Hata hivyo, alikuwa amekunywa pombe kupita kiasi
jana yake usiku na alikuwa akijisikia
vibaya sana muda huo.
Alipotazama huku na kule, ghafla aliona kikombe cha maji ya uvuguvugu na
vidonge viwili vya tumbo vimekaa kando ya kitanda cha kulalia. Macho yake
meusi yalimtoka. Alihisi ni Aunty Linda ndiye aliyemwkea dawa hiyo. Alichukua
dawa huku moyo wake ukiwa umechanganyikiwa. Alishuka tu baada ya kunawa na wakati tumbo lake lilihisi vizuri kidogo.
Shangazi Linda alipokuwa akifanya
usafi alimuona Alvin akishuka.
Alitabasamu. "Bi Kimaro anakuandalia kifungua kinywa sasa hivi."
Alvin akaenda kwenye meza ya chakula. Kulikuwa na nyama na
nguruwe iliyochomwa, supu ya kuku wa kienyeji, maziwa fresh, maziwa, juisi ya limao...
Mlango wa kuteleza wa jikoni ukafunguliwa, na Lisa akatoka na chungu cha mtori. Alivaa gauni la rangi ya waridi na aproni iliyofungwa kiunoni
mwake. Nywele zake zilikuwa zimefungwa kama mkia wa farasi, na kufunua uso wake mdogo na safi. Ilimfanya aonekane mpole na mtulivu.
"Ulikunywa sana jana usiku, kwa hivyo ni bora ukaanza kwa kula kitu chepesi asubuhi. Mtori ni rahisi kusagwa na hautakuwa mzigo kwenye tumbo lako.”
Lisa alisema huku akivuta bakuli la mtori na kuliweka mbele yake.
Alvin aliutazama ule mtori kisha
akamtazama Lisa. Taswira ya yeye
kushika shingo ya Kelvin na kumbusu
kwa nguvu ghafla ilionekana akilini
mwake. Kamba ya uvumilivu moyoni
mwake ilionekana kukatika kwa nguvu.
Alinyanyuka na kuumwaga mtori moja
kwa moja kwenye pipa la takataka.
Kisha akamtazama kwa macho ya jeuri. "Vitu unavyopika ni vichafu."
Uso wa Lisa ulibadilika ghafla. Baada ya muda mrefu, alipepesa macho yake ambayo yalikuwa yakitoka kwa machozi. “Kwa kuwa unafikiri mimi ni mchafu, kwa nini nisiondoke?” Kwanza
likuwa ameita jina la mwanamke mwingine alipolala, hata hivyo. Kwa
kweli, labda hakumpenda sana.
Alvin aliganda alipomsikia hivyo. Macho yake yaliyokuwa na damu kwa mbali
yalimtazama ghafla. “Unataka kuondoka? Unataka kwenda kwa Kelvin
kukaa naye sasa? Kila mtu kwenye
mtandao anawaambia nyinyi wawili
mnafaa kuwa pamoja. Nyinyi ndio
wanandoa wanaofaa zaidi katika
ulimwengu wa biashara.”
"Hapana." Lisa hakuweza kulala usiku
kucha kwani alijiona hana nguvu. “Naondoka kwa sababu hutaki kuniona.”
"Hata kama unanichukiza, unatakiwa kukaa katika nyumba hii," Alvin alifoka kwa hasira, "Maadamu nipo karibu, unaweza tu kuota kuwa na Kelvin. Acha nikuambie, Lisa Jones, kwa kuwa umenichokoza, usifikirie hata kuniacha nikiwa mzima!”
Kisha, akaondoka.
Lisa alitabasamu kwa uchungu. Hivi, alikuwa bado mzima? Tayari alikuwa amepoteza moyo wake kabisa.
Sura ya 136
Alvin alikaa kwenye siti ya nyuma ya gari lake. Alikuwa ametawaliwa na maamuzi ya hasira mapema asubuhi, lakini sasa ghafla alihisi njaa sana.
Tumbo lilianza kumuuma tena. Aliwasha
sigara kwa hasira. Ikiwa angejua
kwamba hilo lingetokea, angemaliza kula kifungua kinywa chake kwanza
kabla ya kupandisha hasira zake za kijinga. "Bwana Kimaro, ngoja nikununulie chakula." Hans alimtazama kwa wasiwasi.
“Sina njaa. Nenda uniletee Lina Jones
hapa,” Alvin alisema kwa upole, “Sikuzote nilitaka Lisa ashughulike naye, lakini haina maana sana. Nitamalizana naye mwenyewe.”
Hans aliitikia kwa kichwa. Ilionekana
kana kwamba ingemlazimu kumuombea
Lina kwa kile ambacho alihisi kilikuwa
kinaenda kumkuta. •••
Katika kampuni ya Mawenzi
Investments. Lina alifukuzwa moja kwa
moja na walinzi. Hakutaka kuondoka na
kuishia kupiga kelele mlangoni, “Hata
kama baba yangu alikamatwa, bado ana hisa kwenye kampuni na mimi bado ni mtoto wake. Nina haki ya kurithi hisa zake na kufurahia gawio langu.”
“Potelea mbali!” Yule mlinzi alimtemea mate isivyostahili. “Kila mtu anajua
kuwa wazazi wako walimuua bibi mzee
ili wapate hisa za Mawenzi Investments. Walimuua Mzee Madam Masawe.
Hawana utu kabisa. Mwenyekiti Jones
tayari ameomba mawakili wengi
kurejesha hisa za Jones Masawe. Utarithi nini? Endelea kuota!"
"Subiri. Nitakaporudi Mawenzi, nitafanya maisha yako kuwa mabaya zaidi kuliko
kifo. Lina alitetemeka kwa hasira.
Hata mlinzi alithubutu kumdhalilisha
sasa. Kweli dunia haikuwa ya haki. Ni
wazi alikuwa ametuma picha zote za
uchafu za Lisa na Kelvin kwa waandishi
wa habari jana yake, lakini sio tu kwamba ilishindwa kuharibu sifa ya Lisa, bali watu walianza hata
kumuoanisha na Kelvin sasa. Ilikuwa inakasirisha sana na kukatisha tamaa.
Alitembea kando ya barabara wakati gari lisilo na nambari ya leseni lilisimama ghafla mbele yake. Kisha, watu wawili wakamsukuma moja kwa moja kwenye gari.
"Unafanya nini?" Kabla Lina hajajibu, alifunikwa kwenye gunia na kupoteza fahamu. Muda si muda, ndoo ya maji
baridi ilimwagiwa juu yake na akapiga kelele kutokana na baridi. Gunia lilipasuliwa.
"Baridi ilikuwa nzuri?" Hans alimtazama kutoka juu.
Lina alitazama juu na kufikiria kuwa
anaonekana kuwa mzoefu kidogo.
Baada ya muda, alimkumbuka. "Ni wewe. Wewe ni msaidizi wa Alvin Kimaro…”
"Ni vizuri kukumbuka." Hans aliachia
tabasamu hafifu. Akageuka pembeni, akamfunua mtu aliyekaa kwenye sofa
ambalo halikuwa mbali. Mwanaume huyo alivalia suti nyeusi na kushika sigara mkononi, moshi ukitanda hewani. Macho yake ya wino yaliangaza na mwanga mweusi uliokuwa mkali kama kisu. Mwanamume huyo alitoa sauti ya kutisha. Lina alimtambua. Hofu isiyoelezeka ikapanda kutoka ndani ya moyo wake.
"Bwana. Kimaro, unajishughulisha na kazi ya kisheria. Unataka
kunyang'anywa leseni yako kwa kuvunja
sheria? Ninakuonya, afadhali uniache mara moja, la sivyo sitakuacha kamwe.”
Hans alicheka kana kwamba amesikia
mzaha. “Unacheka nini? Huwezi kuelewa nilichosema?” Lina alicheka. “Hebu
niambie, haufahamu kuwa mimi ni mwanamke wa Willie Kimaro? Unajua
Bwana Kimaro ni nani? Unajua kuwa ananipenda sana? Ikiwa huniamini, unaweza kuchukua simu yangu na kuangalia picha zetu pamoja.”
Alvin alimaliza kuvuta sigara na kuitupa
kwenye sinia ya majivu kabla ya kuinuka. Mwili wake mrefu ulitembea
polepole kuelekea kwake. Lina alifikiri anaogopa na akacheka. “Alvin Kimaro, wewe ni mwanasheria tu. Willie Kimaro
si mtu ambaye mtu kama wewe
unaweza kudiriki kumuudhi—”
Kabla hajamaliza, Hans alimpiga kofi
kwenye shavu na kumng'oa jino
mdomoni. Lina alipiga mayowe, “Willie hatakusamehe—”
Smack! Kofi jingine likasikika. Baada ya makofi kadhaa, Lina alipoteza meno
machache na hakuthubutu kuongea tena. "Nyamaza." Hans alitabasamu.
“Unafikiri Willie Kimaro ni nani?
Hujaelewa kwa nini Willie alibadili
mtazamo wake kwako haraka hivyo?”
Lina aliganda. Alimtazama Alvin na ghafla akakumbuka kuwa jina lake la mwisho lilikuwa Kimaro pia. “Hilo
haliwezi kuwa. Sijawahi kusikia mtu
anaitwa Alvin katika familia ya Kimaro."
“Unawajua watu wangapi katika familia ya Kimaro?" Hans alidhihaki. “Acha
nikwambie, Alvin Kimaro ndiye kaka
mkubwa katika familia ya Kimaro.
Amekuwa akisimamia familia tangu
akiwa na umri wa miaka 20.”
Ubongo wa Lina ulivuma kana kwamba anaota. Kila mtu alijua kwamba kaka
mkubwa, wa ajabu wa familia ya Kimaro alikuwa mtoto wa Leah Kimaro. Mtu
huyo alikuwa mtu wa chinichini sana, lakini mbinu zake za ukatili zilijulikana
sana. Aliingia katika kampuni hiyo akiwa na umri wa miaka 20. Mjomba wake wa pili alipokaidi, alimvunja mguu wake mbele ya umati.
Baada ya kuchukua jukumu la
kuongoza KIM International, alipanua biashara yake hadi ng'ambo kwa kasi ya radi na hata akaingia katika nyanja za
mawasiliano, fedha, na teknolojia
kwenye masoko ya nje ya nchi kwa
haraka haraka. Kwa wakati huo, alikuwa
ameingia kwenye orodha ya watu
miamoja tajiri zaidi Afrika, akiachwa kwa
karibu sana na kina Dangote, Mo Dewji,
Bhakresa na wengineo. Kulingana na uvumi, alikuwa mtu wa tatu tajiri zaidi
nchini Tanzania na pia wa kushangaza
zaidi. "Hiyo haiwezekani. Unasema uwongo!”
Lina alikuwa akiingiwa na wivu. Lisa
alimkamataje mtu kama huyo?
“Kwa nini nikudanganye? Huyo mjinga
Willie Kimaro aliogopa sana hivi
kwamba alikojoa kwenye suruali yake
alipomwona Bwana Kimaro. Hans alifoka. “Lina Jones, Bwana Kimaro
hakutaka kushughulika na wewe mara ya kwanza, lakini hukupaswa kumpa
Lisa Jones dawa ya kulevya. Na kwa
kweli hukupaswa kutoa picha hizo
kwenye vyombo vya habari.”
Lina alishtuka. Alipiga magoti mbele ya
Alvin na kutetemeka. “Bwana Kimaro, mimi ni mjinga. Nilikuwa mjinga.
Tafadhali nisamehe sana.”
Alvin akampiga teke kwa kuchukia. Ujeuri wa macho yake ulidhihirisha
kwamba hakutaka chochote zaidi ya kumwangamiza kabisa. “Unadhani
nitakuacha ukipumua?”
"Hapana, hapana, hapana. Haikuwa mimi. Sikupiga picha.” Lina akatikisa kichwa kwa hofu. “Nilitumiwa na mtu nisiyemjua. Ni kweli nilimpa Lisa dawa
usiku huo, lakini Kelvin Mushi alipokuja, kamera ya video iliyokuwa chumbani iliharibiwa.”
“Hukuwa wewe?” Uso wa Alvin ulikaza
zaidi huku alama ya mshangao ikimulika
machoni mwake, akiamini hadaa ya
Lina. "Naapa." Lina alikuwa amepoteza meno
kadhaa na mdomo wake ulikuwa
umejaa damu. “Kama ningekuwa na
hizo picha ningezitumia kumtishia Lisa
zamani. Ningewezaje kumruhusu kukaa
katika nafasi ya mwenyekiti kwa muda
mrefu hivyo na kuwaweka wazazi
wangu jela?”
“Kiapo chako hakina thamani.” Uso wa Alvin ulizidi kutisha, lakini aliamini
maneno ya Lina. Ikiwa hakuwa yeye, basi ni nani?
Alikuwa na wazo, na midomo yake
ikachanua katika tabasamu. Usiku huo, mbali na Lisa, ilionekana kana kwamba
kulikuwa na Kelvin pekee. Kwa Kelvin
Mushi haikuwa rahisi hata kidogo kwa
Lisa kumshuku. Lisa alijua kwamba
anampenda, lakini bado alikuwa tayari
kuendelea kuwa na urafiki naye. Kelvin
alikuwa ameenda ng’ambo kufungua
ofisi ya tawi alipokuwa kijana, kama
yeye tu. Anawajua watu wenye uthubutu
wa kuvuka mipaka na kwenda
kufanikiwa nje ya nchi huwa wajanja
wajanja sana. Alvin hakumwamini
Kelvin hata kidogo. Lina alijua kwamba alimwamini na akasema kwa haraka, “Bwana Kimaro, tafadhali niruhusu niende. Ninaahidi sitomsumbua Lisa tena. Nitaondoka Dar es Salaam.”
“Unadhani nitakuacha uondoke kwa amani?” Alvin alitabasamu kwa giza.
“Nimechunguza mambo yako. Ulikulia kijijini baada ya kuibiwa ukiwa mtoto mdogo, ukatolewa usichana wako na mwanakijiji ukiwa na umri wa miaka 15.
Baadaye katika shule ya sekondari, ulifumaniwa zaidi ya mara kumi na waume za watu. Uliwekwa kinyumba na tajiri mmoja na hata kutoa mimba zisizo na idadi. Ni aibu iliyoje. Hukuwa na maisha mazuri hata baada ya kurudi
kwenye familia ya akina Masawe.”
Uso wa Lina ulikuwa umepauka kwa
aibu. Hii ilikuwa historia yake ya giza. Alikuwa ameifunika kwa makini sana, lakini mtu huyu kwa kushangaza aliweza kujua juu yake. Alikuwa anatisha sana.
"Kwa kuwa unapenda wanaume sana, nitakuozesha mume wa kuishi naye."
Alvin alisema na kuondoka bila kuangalia nyuma.
Punde, mzee mfupi na mbaya mwenye umri wa miaka 50 aliingia. Alipomwona Lina, alimeza mate ya uchu. "Bwana
Kimaro, unaniruhusu nimuoe?"
Lina alimtazama Hans kwa uso wa kutisha. “Usimruhusu anioe. Nitakwenda na wewe. Unaweza kufanya chochote unachotaka. Unaweza kunifanya vile
Willie alinifanya pia!”
Hans alikwepa nyuma kwa kuchukizwa.
“Usinishike, nachukia mambo machafu.
Usimwogope sana. Anaonekana kuwa
mzee, lakini ana umri wa miaka 40 tu na amekuwa peke yake kwa miaka kadhaa
kwa sababu hakuweza kupata mke. Utamfuata kijijini na kumpatia mtoto.”
Kisha, Hans akaondoka, akimuacha
Lina nyuma. Alilia kwa kukata tamaa, lakini hakuna mtu aliyemjali. Wakati
huo, alijuta sana. Hakupaswa
kumlazimisha Lisa Jones kuondoka
nyumbani wakati huo. Hakupaswa
kumsukuma Bibi Madam Masawe chini
ya ngazi.
Lakini, hakuna na dawa ya majuto
katika ulimwengu huu.
Sura ya 137
Katika mlango wa kituo cha polisi, Lisa
alikuwa amemaliza tu kurekodi ushahidi
wake mara ghafla akasikia mtu akiliita
jina lake.
“Lisa.” Aligeuka nyuma na kumuona
Kelvin akija kwake huku akiwa na tabasamu usoni mwake. Hali ya hewa ilikuwa ya baridi, na alikuwa amejifunika kitambaa shingoni.
"Ni bahati tu nimekuona. Kwa nini upo hapa?” Lisa alilazimisha tabasamu kumsalimia. Kila alipokuwa akimuona, alizikumbuka picha zile na mgogoro kati ya Alvin na yeye.
"Kuna jamaa wa nyumbani alifanya
tukio la ajabu, kwa hivyo nilikuja kumdhamini." Kelvin alionekana hoi.
"Nilisikia kwamba Jones Masawe na Mama Masawe walikamatwa hivi majuzi. Je wewe…”
“Ndio, polisi waliniita hapa kuchukua maelezo yangu. Kesi hiyo itafikishwa
mahakama wiki ijayo kisha watasomewa hukumu.”
"Hongera, hatimaye umelipiza kisasi kwa bibi yako." Kelvin alifurahi kusikia hivyo.
“Asante.” Tabasamu la Lisa halikumfikia machoni. Alionekana kuchoka kabisa.
Kelvin alitembea pamoja naye kuelekea sehemu ya maegesho, huku akimtazama njiani. “Unaonekana umechoka. Umekuwa ukipumzika vizuri kweli? Na Alvin bado hajakuelewa tu…?!”
"Hatuwezi kuzungumza juu ya hili?" Lisa alimkatisha.
"Ni kosa langu." Kelvin alionekana kuwa na hatia. “Kosa lako kivipi? Ulinisaidia usiku ule.
Kama si wewe, ningefanyiwa ukatili
mbaya na pengine ningeweza kujiua
muda mrefu uliopita. Jana, hata
ulishirikiana nami kufafanua hali
ilivyokuwa na kuokoa sifa yangu.
Ninapaswa kukushukuru,” Lisa alitikisa
kichwa na kusema kweli.
Wawili hao walizungumza huku
wakitembea. Lakini kijana mmoja
aliibuka kando yao ghafla na
hawakumjali, wakidhani ni mpita njia tu.
Hata hivyo, ghafla mwanamume huyo
alitoa kisu cha matunda kutoka kwenye
mfuko wake wa suruali na kukichoma
kuelekea kifuani kwa Lisa.
“Lisaaa!” Kelvin aliona Lisa amechelewa
sana. Alipoona kile kisu kinataka
kumchoma, alinyoosha mkono haraka
kukizuia, na kisu hicho kikapenya
kwenye mkono wake.
Wakati Lisa anajibu, mtu huyo alikuwa
amechomoa kisu haraka ili kumchoma
Lisa tena. Kelvin angeweza tu kutumia
mwili wake kumkinga, na kisu kikapenya
sehemu ndogo ya mgongo wake.
“Msaada!” Lisa alilia. Kwa msukumo aliushika mkono wa mwanaume huyo.
"Wewe ni nani?!”
“Hutakiwi kunifahamu. Ni kosa lako kuwa mwanamke wa Alvin Kimaro.
Nimekuwa nikikufuatilia kwa muda
mrefu sasa.” Mwanaume huyo alifichua uso wake wa kutisha huku akiendelea
kudunga kisu kwenye mwili wa Kelvin
kana kwamba alikuwa na wazimu.
Kwa bahati nzuri, walikuwa karibu na kituo cha polisi. Polisi mmoja alisikia
kilio cha kuomba msaada na haraka
akakimbia ili kumshika mhalifu.
Punde, ambulensi ilifika na upesi
ikampeleka Kelvin hospitalini. Hata
hivyo, tayari alikuwa amepoteza damu
nyingi njiani na kupoteza fahamu. Lisa
alipiga simu kwa haraka kwa Ethan, ambaye alikimbia mara baada ya Ambulance kufika hospitali.
Mlango wa Emeregence Room
ulisukumwa, na daktari akatoka na fomu mkononi. “Kisu kilichomwa kwenye figo ya kushoto ya mgonjwa na inabidi itolewe mara moja ili kuokoa maisha yake. Familia ya mgonjwa iko wapi? Tafadhali saini mara moja.”
Lisa alipigwa na butwaa. Ethan pia aliona ni vigumu kukubali. "Daktari, lazima ni lazima figo iondolewe? Kwani hakuna namna nyingine?"
"Necrosis tayari imeingia kwenye figo ya kushoto, kwa hivyo haina maana sasa," daktari alisema bila msaada, "Kama
tungeweza kuiokoa, bila shaka tungeiokoa."
Ethan hakuwa na la kufanya zaidi ya
kuvumilia maumivu na kusaini zile karatasi. Lisa alitoa machozi ya uchungu. “Yote ni makosa yangu. Mtu huyo alitaka kuniua. Mjomba wako
ndiye aliyetumia mwili wake kunisaidia kuzuia kisu."
Ethan alikuwa na hisia tofauti.
Hakutarajia Kelvin angekuwa na hisia za kina namna hiyo kwake. Sasa, pia alikuwa na wasiwasi sana kuhusu usalama wa Kelvin. Angeweza tu kusema, “Usifikirie juu yake. Daktari alisema kuwa kuondoa figo yake
kutaokoa maisha yake. Mwili wa mwanadamu bado unaweza kufanya
kazi na figo moja tu. Anapaswa kuwa
mwangalifu zaidi katika siku zijazo."
Lisa alitabasamu kwa uchungu. Kelvin
alikuwa anaenda kupoteza figo.
Angewezaje kuwa mzima kama hapo
awali? "Umewajulisha babu yako?"
“Hapana, babu na bibi wamezeeka na sitaki kuwapandisha presha. Tusubiri hadi upasuaji wa Mjomba umalizike.”
Ethan alimtazama na kuhema moyoni
mwake. Aliogopa hasa kwamba babu na bibi yake wangezimia ikiwa wangejua ukweli.
Kwa bahati nzuri, saa tatu baadaye, Kelvin aliokolewa. Operesheni ilikuwa
imekwisha, lakini bado hakuweza kufumbua macho.
Muda si muda, polisi walifika hospitalini.
Walipomwona Lisa walimwambia. “Bi.
Jones, tumemhoji mhalifu. Mtu aliyetaka kukuua anaitwa Zigi Kabwe. Yeye si mwenyeji wa hapa Dar.”
Lisa alikasirika. “Hata simfahamu mtu huyu.”
Afisa huyo alitikisa kichwa. “Kulingana na maelezo yake, alikuwa na dada yake pacha anayeitwa Lily Kabwe. Miaka
mitano iliyopita, Lily Kabwe alikuwa na umri wa miaka 17 tu, lakini alivutia
macho ya Thomas Njau kutoka kwa familia ya Njau huko Nairobi. Thomas
alimbaka Lily kwa nguvu baada ya kukataa kulala naye na akaamua
kujirusha hadi kufa kutoka kwenye
jengo kutokana na fedheha. Familia ya
Kabwe ilimshtaki Thomas. Wakati huo, kulikuwa na karibu ushahidi kamili, lakini
familia ya Njau ilimwajiri Alvin Kimaro
kutetea kesi yao. Alvin Kimaro alidai
kuwa Lily alimtongoza Thomas lakini
Thomas alimdharau, hivyo akaamua
kujiua kwa sababu ya unyonge wake.
Mahakama haikushindwa tu
kumwadhibu Thomas, lakini hata
ilimfanya Lily aonekane kama mtu duni
asiye na maana. Mama yake hakuweza
kuvumilia na na akapata presha.
Amefariki hivi karibuni…”
Lisa alishtuka. Alijua tu kwamba Alvin hawezi kushindwa mahakamani, lakini hakujua kwamba alikuwa amechukua kesi nyingi zisizo na moyo wa utu. "Kwa hivyo, alitaka kuniua ili kulipiza kisasi kwa Alvin Kimaro?"
“Ndiyo. Alitoweka miaka mitano iliyopita baada ya kesi hiyo, na tuligundua tu kwamba alirudi Dar es salaam mwaka huu. Alitaka Alvin Kimaro ajue uchungu wa kufiwa na mpendwa wake, lakini…
Alvin Kimaro amezungukwa na walinzi na ni mwangalifu sana, kwa hivyo Zigi
Kabwe ameshindwa kutimiza lengo lake licha ya kujaribu kwa miaka kadhaa.”
Afisa huyo alimwambia, “Amekuwa akikufuata kwa muda, lakini umekuwa ukilindwa na mlinzi siku hizi za karibuni.
Ni leo tu ndipo alipata nafasi hiyo kwa sababu hukuwa na mlinzi.”
Ghafla, Lisa alionekana kugundua kitu.
Siku chache zilizopita, Alvin alikuwa
amepanga ghafla Shani afuatane naye
kama mlinzi wake. Haikuwa kumlinda
dhidi ya Jones na binti yake bali
kumtazama Zigi Kabwe. Hata hivyo, hakumwambia chochote.
Haukuwa ulinzi wake hata kidogo.
Kama Kelvin asingetokea siku hiyo, angekufa. Hofu isiyo na kipimo
ikaufunika moyo wake. Lisa ghafla
alifikiri kwamba hakumfahamu kabisa
Alvin kama alivyodhani.
"Kwa nini kulipiza kisasi kwako kwa kile
Alvin Kimaro alichofanya kwa mtu
mwingine?" Ethan alikasirika. “Lisa, nakushauri ukae mbali na Alvin Kimaro.
Nani anajua ni maadui wangapi
amewachokoza kwa miaka mingi?
Nilisikia huwa anaenda mahakamani
kuwatetea matajiri tu, madhalimu na
mafisadi, je ni haki za wangapi
amedhulumu? Lazima atakuwa
amepata pesa nyingi kwa njia isiyo halali."
Lisa alinyamaza, akiinamisha kichwa
chini na uso wa huzuni. Moyo wa Ethan uliumia. Ikiwa asingefanya chaguo baya
hapo kwanza, Lisa asingeangukia kwa
Alvin Sura ya 138
Saa nne usiku, Alvin aliingia kutoka nje
akiwa na uso jeuri na mkali. Alipanda
juu ndani ya dakika mbili kabla ya kushuka tena kwa haraka. "Lisa bado hajarudi?" "Hapana." Shangazi Linda aliogopa
kidogo sura yake.
“Mbona bado hajarudi?”
"Sijui. Yeye hapokei simu pia.” Aunty
Linda alipomaliza kuongea, hali ya joto ndani ya jumba hilo ilionekana kushuka na kumfanya ashtuke.
Alvin akatabasamu kwa ujeuri. Vizuri. Hata baada ya kumsaliti na Kelvin, bado hakujua jinsi ya kuishi. Ilikuwa tayari saa nne usiku lakini hakuwa amefika
nyumbani bado. Hata hakupiga simu nyumbani. Mwanamke huyo hakubadilika kamwe.
“Bwana Kimaro,” wakati huo, Hans alikimbia kutoka nje. “Nimepata habari.
Zigi Kabwe alimvamia Miss Jones nje ya kituo cha polisi leo, lakini Kelvin
Mushi alimzuia na kuchomwa visu vingi mwilini. Lisa yuko salama, lakini Kelvin amejeruhiwa vibaya na sasa anatibiwa hospitalini.”
Mwili wa Alvin uliganda pale pale huku
macho yake meusi yakiwa yamemtoka
ghafla. “Shani yuko wapi? Amechoka
kazi? Si nilimwambia amlinde Lisa?”
Hans alipumua na kukumbusha kwa upole, “Bwana Kimaro, ulisahau?
Ulipoona picha za Lisa na Kelvin kwenye vyombo vya habari siku moja
kabla ya jana, ulishindwa na kumwambia Shani aache kumlinda Miss
Jones. Ulimwambia Shani amwache Bibi Jones kwa hiari yake mwenyewe.”
'Nilimwambia asimlinde Lisa na kweli
aliacha kumlinda Lisa? Ana akili timamu?" Alvin alishindwa kujizuia tena.
Hans alikuwa kimya. Shani alifuata tu maneno ya Alvin kwa utii.
“Twende hospitali.” Alvin akatoka nje.
Baada ya kufika hospitalini, alivamia
moja kwa moja hadi kwenye wodi ya watu mashuhuri. Kelvin bado alikuwa
katika hali ya kukosa fahamu. Mrija wa
oksijeni ulikuwa umefungwa kwenye
pua yake, na Lisa alikuwa akifuta uso wake kwa kitambaa.
Tukio hilo lilimchoma macho Alvin bila
huruma. Hapo zamani alipokuwa
amelazwa hospitali, alikuwa amemtunza
vile vile. Sasa, alikuwa akimtunza mwanamume mwingine.
"Njoo hapa," alimtazama na kusema
polepole, "Tuondoke haraka."
Lisa aliacha harakati zake na kutikisa
kichwa. “Bado hajaamka. siwezi kuondoka.”
"Lisa Jones, huelewi nilichosema?"
Mwali wa hasira kweny moyo wa Alvin
ukawashwa papo hapo. Sauti yake
ilikuwa ya kikatili sana. "Ninakupa nafasi ya mwisho."
Sauti yake iliufanya moyo wa Lisa
kusinzia. Alikaribia kuchomwa kisu hadi
afe siku hiyo. Hakuona kuwa alikuwa
ametapakaa damu? Je, aliwahi kumjali?
"Alvin Kimaro, kuwa mwenye busara.
Kama si Kelvin, ningekuwa maiti kufikia sasa. Alimlinda mpenzi wako. Ni sawa
ikiwa huna shukrani yoyote, lakini mtazamo wako unawafanya watu wahisi
kwamba wewe ni mnyama mwenye damu baridi.”
“Mimi ni mnyama mwenye damu
baridi?” Alvin akapiga hatua kuelekea kwake. Alikuwa amemfanyia mengi,
akimlinda mara kwa mara, hata kumpenda. Hata hivyo, alikuwa
akimshutumu kwa kuwa na damu baridi? Maneno hayo mawili yaliupiga moyo wake kama kisu, na kusababisha maumivu yasiyovumilika.
"Unapaswa kuwa tayari umejua kwa nini
Zigi Kabwe alitaka kuniua," Lisa
alidhihaki, "Hivi kweli familia maarufu ya
Kimaro ina ukata wa pesa kiasi kwamba
unalazimika kupigania kesi isiyo ya haki
kwa pesa hizo kidogo? Au ilikuwa kwa ajili ya umaarufu? Ulifika kileleni na kupata sifa uliyonayo sasa katika ulimwengu wa wanasheria kwa
kuwakanyaga watu wengine?”
Alvin alikunja ngumi. Mishipa ya nyuma ya mkono wake ilitoka nje. "Lisa Jones, elewa hili. Mimi ni mwanasheria.
Wanasheria hushinda au kushindwa tu.
Mimi si mjumbe fulani wa haki.”
"Lakini mtu hawezi kuishi bila dhamiri."
Lisa akatikisa kichwa. Ghafla aligundua
kuwa yeye na Alvin walionekana kutoka dunia mbili tofauti kabisa.
“Nimekufanyia mambo mengi, lakini leo hii unasema sina dhamiri?”
Alvin alimtazama kwa hasira. Hajawahi
kumtendea mwanamke kinyume sana
hapo awali, lakini alipinga kila kitu katika
sentensi moja. “Kwa sababu Kelvin
alitoa maisha yake ili kukuokoa, kwa
hiyo unataka kuwa pamoja naye? Ni kweli, siku zote amekuwa akikufuata.”
"Acha kuongea ujinga." Lisa alikasirika.
"Amepoteza figo kwa sababu yangu. Siwezi hata kukaa na kumtunza? Hiki
ndicho kitu kidogo zaidi ninachoweza kumfanyia baada ya kuokoa maisha yangu.”
“Sijali. Njoo tuondoke mara moja. Kelvin Mushi sio mtu mzuri kama unavyofikiria
wewe. Kelvin ndiye aliyetuma picha hizo kwa siri kwa Lina. Alijifanya kama mtu
mzuri juu ya uso lakini alicheza hila za siri gizani. Alikuwa ni mnafiki tu.” Alvin
hakujali hata kidogo kuhusu hali ya Kelvin. "Nadhani wewe ndiye ambaye sio mzuri." Lisa alikasirika.
Muda huo Ethan aliingia kutoka nje
akiwa na nguo. “Lisa, nimekuletea nguo. Unapaswa kubadilisha haraka…” Kabla
hajamaliza, akamuona Alvin na uso wake ukiwa mweusi mara moja. “Nani
alikuruhusu kuingia humu? Ondoka haraka..."
Alvin alimtazama kisha akamtazama
Lisa kabla ya kucheka ghafla. “Si ajabu hutaki kuondoka. Mpenzi wako wa
zamani yuko pamoja nawe, na mpenzi wako mpya amelala kitandani. Una jozi
hii ya mjomba na mpwa wake
iliyozunguka moyoni mwako. Lazima uwe na furaha tele.”
"Nimekuozea, siku zote nimekuwa mtu kama huyo moyoni mwako." Macho ya
Lisa yalikuwa mekundu huku mwili
ukimtetemeka bila kuvumilika.
“Alvin Kimaro, umeenda mbali sana. Je, hilo ni jambo ambalo mwanadamu
anaweza kusema?” Ethan hakuweza kuvumilia. Akatupa zile nguo pembeni na kumpiga ngumi Alvin. Alvin aliinua mkono wake kwa urahisi ili kuizuia, na Ethan akanguruma kwa hasira.
“Hapana, wewe si binadamu hata kidogo. Lisa na mjomba wangu wamebeba tu matokeo ya matendo yako maovu. Walikaribia kupoteza maisha kwa sababu yako, lakini huna ubinadamu. Ondoka mbele yangu!”
"Nitaondoka, lakini sitaondoka peke yangu, lazima nimchukue mwanamke wangu." Alvin alinyoosha mkono kumnyanyua Lisa begani. Ethan alikimbia kumzuia, lakini Hans alimzuia haraka.
“Alvin Kimaro, niache! Usifanye hivi! nitakuchukia.” Lisa alianza kumpiga mgongoni, lakini Alvin alipuuza.
“Huchukii kuwa mimi ni mchafu? Je, huogopi kwamba nitakuchafua?” Lisa alipiga kelele.
Alvin akamshusha na kumtupa kwenye
gari. Hans akawasha gari na kufunga milango. Lisa alijua kwamba
asingeweza kushinda dhidi yake na akachagua kukaa mbali naye
iwezekanavyo, bila kumwangalia hata kidogo.
Moyo wa Alvin uliudhika sana, akawasha sigara ili avute katika safari nzima. Lisa alikohoa mfululizo. Alijua
kuwa hapendi kuvuta sigara hata kidogo
kabla ya hii, lakini sasa, alikuwa akivuta sigara mara kwa mara. Hakupenda
wanaume wanaovuta sigara, na hakupenda wanaume wasio na akili
kama yeye hata kidogo.
Baada ya kufika nyumbani, Alvin alimbeba tena na kumtupa kitandani.
Lisa alipanda na kusema kwa ujeuri,
“Utanifunga tena? Alvin Kimaro, mimi ni mwenyekiti wa kampuni sasa. Kuna
watu wengi nyuma yangu
wananitegemea. Siamini kwamba
utaweza kunifunga maisha yangu yote.”
“Kila saa ni ampuni, kampunii! kampuni, ni upuuzi tu kwangu.” Alvin alimuigiza kwa kubana pua. “Je, utaniamini
nikisema nitaifunga kesho?” Alvin alifoka na kumpa jicho la pembeni. "Si
tayari kabisa unajua utambulisho wa jina langu?"
Macho meusi ya Lisa yalitetemeka.
Ilibadilika kuwa tayari alijua. Je, Willie Kimaro alimwambia? Yule mwongo
aliyelaaniwa. Yeye ndiye alisema
atamficha Alvin. Ingawa hakuwa wazi
kuhusu utambulisho halisi wa Alvin
katika familia ya Kimaro, pamoja na
ujuzi wake, angeweza kweli kufanya
hivyo. Familia ya Kimaro ilimiliki 25% ya
hisa za kampuni hiyo, ukichanganya na
ujuzi wake wa sheria, kufumba na kufumbua tu alikuwa anaukosa uenyekiti wake!
"Alvin Kimaro, ungekuwa na furaha zaidi
ikiwa ningeuawa na Zigi Kabwe leo?"
Macho ya Lisa yalikuwa mekundu huku
machozi yakimtoka. "Ninamtunza Kelvin si kwa sababu ninampenda, lakini kwa sababu ninamshukuru."
“Sitakuruhusu umkaribie tena.” Macho ya Alvin yalikuwa yamepoa sana.
Alikuwa na hisia kwamba ikiwa
angemruhusu Lisa abaki na Kelvin kwa
muda mrefu, angempoteza milele. Japo
alikuwa amepoa kwake, bado hakutaka
kutengana naye baada ya kujua kuwa
alikuwa amenyweshwa dawa na Lina.
Hata hivyo, hakuweza kuondoa fundo
lililokuwa moyoni mwake. Bado alihitaji
muda. Sura ya 139
“Lisa Jones, kama kweli unanipenda, usiende kwa Kelvin Mushi tena. Hii ni nafasi ya mwisho ninayokupa.” Alvin alimtazama kwa kina, sauti yake
ikisikika kwa ukali na kishindo.
Lisa alipigwa na butwaa. Ingawa alimchukia na kumkasirikia, bado moyo wake ulimpenda. "Na wewe je? Unanipenda?" Ikiwa alimpenda, kwa nini
aliita jina la mwanamke mwingine wakati alikuwa amelewa?
"Naweza kukupenda, na ninaweza kuacha kukupenda wakati wowote."
Alvin alisema bila kujali kabla ya kugeuka kuondoka.
Lisa alikaa kitandani huku akishangaa
kidogo. Alvinaliweka wazi kuwa upendo
wake unaweza kubadilika wakati
wowote. Je, ni kwa sababu
hakumpenda vya kutosha?
Katika chumba chake cha maktaba, Alvin alisimama mbele ya dirisha akiwa
na glasi ya divai nyekundu, akitazama nje ya dirisha matone ya mvua
yakishuka chini taratibu. Alitumaini kwamba Lisa alimuelewa. Ndio, ingawa
alimpenda, ikiwa angetaka kuendelea kujihusisha na Kelvin Mushi, basi
angeweza tu kuachana na upendo huo. Ingawa Kelvin alikuwa ameokoa maisha
yake, Alvin alikuwa ameokoa maisha yake mara nyingi zaidi. Asingeweza
kuvumilia kumuona mwanamke wake
akimlipa fadhila kwa kumhudumia
hospitali. Alvin alikunywa divai nyekundu kwa machungu.
Hans alisimama nyuma yake kimya.
“Bwana Kimaro, kwa nini hukumwambia
Bi Jones kuhusu picha hizo?”
“Kuna faida gani kumwambia? Je, angeniamini? Kelvin Mushi ndiye
mwokozi wake sasa. Atafikiri kwamba
ninamsingizia kwa makusudi kwa sababu simpendi,” Alvin alidhihaki. Hans alikuwa kimya. Ilibidi akubali
kwamba Kelvin Mushi alikuwa amedhamiria sana. Ili kumlinda Lisa, hata alitoa sadaka maisha yake. Ikiwa hata yeye angelikuwa mwanamke, angeliguswa pia.
Usiku sana, Lisa alioga na kukaa kitandani huku akiwa ameduwaa.
Mwishowe, alichukua simu yake na kutuma ujumbe kwa Pamela, akimwomba aende hospitali kumuona Kelvin kwa niaba yake.
Pamela : [ Usiniambie! Kelvin Mushi

alipoteza figo kwa ajili yako?
Nini unadhani; unafikiria nini?
Usichanganyikiwe tu, sawa?]

Lisa: [ Sikuwahi kufikiria kwamba angefanya hivyo. Nina deni kubwa kwake. Sitaweza kumlipa maisha yangu yote.]
Pamela : [ Hapana, usifikirie sana juu yake. Chukulia tu ni ajali ya kawaida. Ninapanga kumleta Patrick nyumbani kwa Krismasi. Kisha nitaandamana naye hadi kwa familia ya Jackson katika Mkesha wa Mwaka Mpya.]
Lisa: [ Nyinyi watu mmesuluhisha matatizo yenu?]



Pamela : [Nilimchunia kwa nusu mwezi, na aliniahidi kukutana na Linda haraka
iwezekanavyo katika siku zijazo. Nitamtambulisha mpenzi kwa Linda pia.
Nataka kumpa Patrick nafasi moja zaidi.
Ninampenda kupita kiasi. ]
Lisa: [ Hongera kwa kumpata tena Bwana wako.]


Alipotuma tu ujumbe huo, mlango wa chumba cha kulala ulifunguliwa. Mkono wake ulitetemeka, na akazima skrini bila fahamu kabla ya kuweka simu chini.
“Unachat na nani?” Alvin alitoa harufu ya mvinyo mwekundu, na uso wake wote uliwaka kwa hasira. “Nionyeshe simu yako.”
Lisa hakuamini. Alvin hakuwahi kuangalia simu yake hapo awali, lakini alikataa kumpa kabisa. "Alvin, usiende mbali sana."
unawasiliana na Ethan Lowe au Kelvin Mushi nyuma yangu?” Alvin hakuwahi
kuwapenda wanaume ambao
walisisitiza kuangalia simu za wanamke
wao, lakini alipoona tabasamu kwenye midomo ya Lisa mapema, moyo wake
ulikosa raha ghafla. Alipaswa kuwa na uhakika Lisa alikuwa anachat na nani!
Lisa hakuwahi kufikiria kwamba
uaminifu kati yao ulikuwa umeshuka sana. Hata hivyo, huenda
asingemuelewa tena ikiwa angeona
yaliyomo kwenye simu yake, kwa hiyo
alisema tu waziwazi, “Nilikuwa niachat na Pamela . Alikuwa akizungumza
kuhusu mpenzi wake. Pia… ataenda
hospitali kumwona Kelvin. Siwezi
kwenda mwenyewe, lakini marafiki
zangu wanaweza kwenda kwa niaba
yangu.” Alitazama kinyonge jinsi sura
nzuri ya Alvin ikibadilika na kuwa mbaya
kwa hasira iliyoonekana waziwazi kwa
"Mbali sana? Nitajuaje kama
macho. Moyo wake ulihisi kuchoka ghafla. “Lisa Jones, wewe ndiye uliyekuwa unachat na Kelvin Mushi? Ni kitanda changu unacholala sasa ujue.” Alvin alichukua simu yake na kuivunjavunja ukutani. Kelele kubwa ilimfanya Lisa kuziba masikio yake kwa hofu.
Alvin aliinua mikono yake na kumkandamiza kitandani, akimbusu kwa nguvu kwenye mdomo. "Niambie, busu langu linakupendeza zaidi, au busu la Kelvin Mushi ndilo tamu zaidi?"
Akambusu kana kwamba ana wazimu.
Lisa alikuwa akiumia tu kutokana na busu hilo na kumsukumia mbali, lakini hakuweza kumzuia hata kidogo.
Alvin alikuwa amekunywa nusu chupa ya divai nyekundu katika chumba chake
cha maktaba. Ubabe wake ulionekana
kuongezeka mara moja. Alipokumbuka
busu lake na Kelvin, macho yake
yakawa mekundu huku akimbusu zaidi.
"Alvin unaniumiza bwana." Lisa alikwepa kwa maumivu.
“Kwanini unakwepa busu langu?
Unatamani ningekuwa Kelvin badala yake?” Alvin alikuwa tayari amezidiwa na moto wa wivu. Akararua nguo yake ya kulalia kwa nguvu. "Au aliufanya
usiku huo kuwa usiosahaulika sana, ndio maana umeenda naye kituo cha polisi leo? Huwezi kumwacha kabisa?”
Lisa aliogopa sana. Haraka haraka
akamshika mkono na kutikisa kichwa bila msaada. “Hapana, nimechoka.
Ninaogopa leo sitaki…”
“Hutaki kwa sababu ni mimi, sivyo?”
Alvin alicheka ghafla. “Akili yako imejaa
Kelvin Mushi sasa. Ungekuwa tayari
kama angekuwa yeye, si ndiyo?"
“Mbona unaendelea mbali sana Alvin, hutaki kunielewa kwanini?” Lisa alijisikia
kuchoka sana na kukata tamaa.
Alikaribia kufa siku hiyo, lakini hakumjali hata kidogo. Alijua tu jinsi ya kumtilia shaka.
Alitabasamu kwa huzuni na hakuhangaika tena, akamwacha afanye anavyotaka. “Sawa, fanya tu kama unataka. Fanya chochote unachotaka.”
Machozi yake yalimtoka kwenye pembe za macho yake na kutiririka kwenye nywele zake. Macho yake yalikuwa hafifu.
Siku zote alikuwa akitiliwa shaka, kukanyagwa, na kudhalilishwa naye, lakini bado alikuwa binadamu.
Mwili wa Alvin ukakakamaa kana
kwamba alipigwa ghafla kichwani.
Kwanini amekuwa hivi? Ilikuwa ni kama
amekuwa pepo. Hakuweza kujizuia kwa
mwanamke? Kweli alipoteza busara
kwa sababu ya mwanamke? Aligeuka na kukimbilia bafuni. Maji baridi
yakamwagika juu ya mwili wake, na ghafla akajichukia. Alipotoka kuoga, Lisa alikuwa amelala chali pembeni ya kitanda, mtupu kabisa hana chochote baada ya nguo zake kularuliwa na Alvin. Kama kware mdogo, alijikunyata, hana
msaada wowote, tayari kukwakupaliwa na mwenye mwenye njaa kali!
Alvin hakufanya chochote tena, alilala
upande wa pili wa kitanda kimya! Wawili
hao walitenganishwa kwa umbali, lakini
hakuna aliyemkaribia mwenzake.
Hakujua kuwa Lisa ambaye alikuwa
amemrudisha nyuma kimawazo
machozi yalikuwa yakimtoka. Hakupata
usingizi mpaka ilipofika usiku sana.
Kulipopambazuka, Alvin aliamka, lakini
Lisa hakuwapo tena kitandani. Haraka
akainuka na kushuka chini. Lisa alikuwa
amekaa kwenye meza ya chakula
akinywa uji wake wa ulezi. Macho ya Alvin yalilegea kidogo, na akashuka
haraka. Aliketi kando yake na kuuliza
kwa ukali, "Kiamsha kinywa changu kiko wapi?"
Sura ya 140
“Bwana Kimaro, kifungua kinywa chako kimefika.” Shangazi Linda alitoka na kifungua kinywa alichotengeneza.
Alvin akakitazama, na uso wake ukachukizwa mara moja. "Lisa Jones, kwanini hukuniandalia kiamsha kinywa?"
"Wewe ndio ulisema chakula changu ni kichafu kama mimi." Lisa alimtazama
kwa utulivu. Siku zote alikuwa hivi.
Alipomuelewa vibaya, alimdhalilisha
kwa kumwambia chakula chake ni
kichafu na asimpikie tena, lakini sasa
alitaka apike tena. Je, hakuchoka kumnyanyasa? "Nitengenezee sasa hivi." Uso wa Alvin ulikuwa mbaya kwa hasira.
"Hapana. Mimi siyo yaya wako.” Lisa alisimama baada ya kumaliza uji wake. "Naenda kazini."
Alvin aligeuka na kuongea na Shani aliyekuwa amesimama mlangoni.
“Mfuate kwa karibu. Akithubutu kwenda hospitali, mpige na umrudishe hapa.”
"Mimi sio mtumwa wako." Macho ya Lisa yalikua mekundu kwa hasira.
Tayari alikuwa ameamua kutokwenda hospitali, lakini bado alisisitiza kumlazimisha kumwekea mlinzi wa kumchunga. "Alvin Kimaro, usiende mbali sana."
“Kwa kuwa ulinichanganya, unapaswa
kuwa tayari kuwa mtumwa wangu.
Hakuna anayeweza kwenda kinyume na mimi.” Alvin hakujieleza sana, lakini maneno yake yalitosha kudhihirisha
hasira zake.
Lisa alichukua mkoba wake na kuondoka huku Shani akimfuata.
Njiani kuelekea ofisini kwake, haijalishi
Lisa aliendesha gari kwa haraka vipi, Shani alikuwa makini naye muda wote.
Kwenye maegesho, Lisa alishuka
kwenye gari na Shani akamfuata kwa
nyuma kwa kasi.
“Shani, unaweza kuacha kunifuata?
Sitaenda hospitalini.” Lisa alitmwambia
Shani kwa upole. Kwa kweli, hakuwa na
shida yoyote na mlinzi yule.
"Samahani, hili ni agizo la Bwana
Kimaro, bosi wangu."
“Agizo ni la Alvin, lakini usalama ni wa
kwangu. Najua namna ya kujilinda mwenyewe!” Lisa mwishowe alikasirika.
“ Sawa, Alvin alikuajiri? Anakulipa kiasi gani? Mimi nitakupa mara mbili." Lisa
akatoa kadi kwenye begi lake.
Shani hakujali. “Bi Jones, haijalishi
unanipa kiasi gani. Nilifunzwa na familia
ya Kimaro. Ninafanya kazi kwa ajili yao
tu.” Lisa alipigwa na butwaa. Je, familia
ya Kimaro ilikuwa na watu wengi kama
Shani? Familia ya Kimaro ilionekana
kuwa na mambo mengi zaidi kuliko vile alivyofikiria. “Kwa hiyo lazima umekuwa na Alvin kwa muda mrefu. Kwa maana
hiyo unamjua mtu anayeitwa Sarah?”
Hali ya wasiwasi ikaangaza kwenye
macho tulivu ya Shani. Ingawa lilitoweka
hapo hapo, Lisa bado aliliona vizuri.
“Nilimsikia Alvin akimzungumzia siku
moja akiwa amelewa. Lazima awe
mpenzi wake wa zamani. Walikuwa wanapendana sana?"
“Bi Jones, hayo yote ni ya zamani. Bwana Kimaro ana wewe tu moyoni mwake sasa,” Shani alisema haraka.
"Ndio hivyo?" Lisa alitabasamu kwa kujidharau. Alikuwa akimpima tu Shani, lakini jibu la Shani lilimhakikishia kwamba kweli Alvin alikuwa na mpenzi wa zamani anayeitwa Sarah. Alimwita jina lake wakati alikuwa amelewa. Je, iliwezekanaje kuwa Lisa ndiye pekee moyoni mwake sasa?
“Shani, asante kwa kuniambia hivi.”
Aligeuka na kwenda juu ofisini.
Shani alimfuata kinyonge. •••
Siku iliyofuata, saa kumi na nusu jioni, Pamela alitoka hospitali baada ya
kumtembelea Kelvin, akihisi huruma
moyoni mwake.
Kama asingekuwa amekosea na
kumchanganya Alvin na Kelvin hapo
mwanzo, huenda Lisa na Kelvin
wangekuwa tayari wameoana. Hapo
Kelvin asingepoteza figo pia. Hata
hivyo, haikufaa kujutia juu ya maziwa yaliyokwishamwagika sasa.
Akatoa simu yake na kumpigia Patrick.
“Patrick, unakwenda kuwachukua
wazazi wangu, au unaenda moja kwa
moja kwenye Mgahawa tuliokubaliana kukutana?”
“Niko na mkutano ofisini ambao
unaweza kuendelea hadi saa kumi na moja na nusu. Nitaenda huko moja kwa
moja baadaye. Nisaidie kuomba radhi
kwa wazazi wako kwa ajili yangu,”
Patrick alisema kwa sauti ya upole.
“Ni sawa, lakini usichelewe. Baba yangu
anachukia watu ambao hawatimizi
ahadi zao.” Pamela alimuonya kwa
upole. “Usijali, ni suala la maisha yangu. Hakika sitachelewa. Tayari
nimekuandalia zawadi ambayo wazazi
wako watapenda. Tutafunga ndoa
mapema, nami nitakuwa mumeo.”
Patrick akatabasamu kwa dhati. Moyo
wa Pamela ulikuwa mtamu alipokuwa akimsikiliza.
Baada ya kukata simu, Pamela
aliendesha gari kuwachukua wazazi
wake kisha akaenda Mambo Garden
Restaurant. Ilikuwa saakumi na moja
kamili jioni alipofika. Baada ya kuagiza
chakula, kaka yake Forrest alifika. Saa
kumi na mbili jioni bado Patrick alikuwa
hajafika. Babake Pamela alikosa subira, akasema, “Kwa nini bado hajafika? Si
sawa kutufanya wazee tungojee.”
Pamela alisema, “Baba, ni saa za jioni sasa. Pengine kuna msongamano mkubwa wa magari barabarani.”
Mama yake aliitikia kwa kichwa na kukubali. “Wafanyabiashara wana mambo mengi ya kushughulikiwa mwishoni mwa mwaka, hiyo inaeleweka. Kuwa na subira zaidi.”
Pamela alimpigia simu Patrick, lakini hakupokea, akajifariji. "Lazima asipokee kwa sababu yuko barabarani, atakuwa karibu tu hapa."
Baada ya nusu saa nyingine, Patrick hakutokea tu. Baba yake alikasirika. “Ni mara yake ya kwanza kukutana nasi lakini anatuletea dharau namna hii. Hata ukimpigia simu ni bure. Sidhani kama yeye ni mkweli hata kidogo. Sitakubali kukuruhusu uolewe naye.”
Wakati huu, mama yake hakusema
chochote, na Forrest pia alikuwa na uso wa kukata tamaa. “Achana naye. Sio
kama hakuna wanaume wengine ulimwenguni."
Pamela alihudhunika. Mbele ya
shutuma za familia yake, alijilazimisha kutotoa machozi. Yeye tu alijisikia
kukata tamaa sana kwa aibu. Zamani, alimuahidi mara nyingi, lakini sasa, hata
alikosa mkutano wa kwanza pamoja na wazazi wake. Je, alimpenda kweli?
Mama yake akasema. “Pamela, jambo
la muhimu zaidi katika maisha ya mwanamke ni kupata mwanaume
ambaye ni mzuri kwako kwa moyo wote.
Bado wewe ni mdogo, kwa hivyo
usikimbilie kuolewa. Sasa, tule. Chakula
kinakuwa baridi.” Wakati wote wa
chakula, ilikuwa kama anatafuna nta.
Mpaka mwisho, Patrick hakutokea, wala
hakupiga simu hata mara moja
kuelezea shida ni nini.
Baada ya kuachana na familia yake, Pamela aliendesha gari hadi ofisini kwa
Patrick. Ofisi yake ilikuwa tayari
imefungwa. Alianza kuhisi wasiwasi
kidogo. Alikuwa na wasiwasi kwamba
huenda Patrick alikuwa amepata ajali ya
gari au kitu kibaya. Hata hivyo, hakujua
namba za wazazi wa Patrick. Baada ya
kusita kwa muda, alimpigia simu Linda.
Hakutarajia kuwa mtu aliyemjibu
angekuwa ni mwanamume ambaye
sauti yake aliifahamu vizuri. “Habari, Pamela…”
Pamela alitazama sura yake iliyokuwa na ukungu kwenye dirisha la kioo mbele
yake na ghafla akacheka peke yake. Je,
alionekana kama mjinga? “Kwa nini
hukupokea nilipokupigia simu? Na
mbona unapokea simu ya Linda?”
“Pamela, samahani. Linda alipata ajali
ya gari jioni. Niko hospitalini sasa. Nilisahau kabisa hata kuchukua simu yangu ofisini,” Patrick alisema kwa hatia, “Oh, nimechelewa sana?
Mmemaliza kula? Tafadhali mwambie baba na mama smahani kwa kushindwa kuja.
Nitawaalika kwenye chakula cha jioni wakati mwingine.”
"Hakuna haja tena," Pamela alisema kwa sauti isiyo na maana.
"Pamela, ilikuwa ni dharura wakati huu ..." “Ndiyo, kila kitu kuhusu Linda ni dharura. Kwani amekufa? Kilema?
Kwani hana wazazi tena, ana wewe tu?"
Moyo wa Patrick ukasisimka. "Pamela, unawezaje kusema maneno kama haya? Kwani Linda alitaka kupata ajali?
Hata kama humpendi, unapaswa angalau umuonee huruma.”
Pamela alidhihaki. “Sawa, nimekuuliza swali. Kwani amekufa? Amepooza?
Mlemavu?”
Sura ya 141
“Umemaliza?” Patrick alikasirika.
"Yuko sawa kabisa, sivyo?" Pamela alielewa kila kitu sasa. “Patrick, niko serious. Usirudi kwangu tena baadaye. Tunaachana.”
"Inatosha. Unapaswa kujua ni mistari gani hupaswi kupita.”
“Imekwisha. Utakuwa na Linda tu machoni pako. Ndio, unaweza kwenda upande wa Linda ikiwa amepata ajali, lakini huwezi kuonana kabisa na familia yangu. Hukunipigia hata simu. Leo
ilikuwa siku muhimu kwetu, lakini haujali
hata kidogo. Katika siku zijazo, sitakuwa na matarajio zaidi kwako, na sitatumaini
chochote pia. Natumai hatutakutana tena.” Pamela akakata simu na kuuzika
uso wake mikononi huku akilia kwa uchungu.
Baada ya kulia alifuta kabisa
mawasiliano ya Patrick na Linda.
Alikuwa amechoka sana kuteswa na
watu hao wawili. Ilikuwa ni bora
asingekuwa na matarajio, matumaini, na
asingekuwa na maumivu. Wakati huo, alitaka kutafuta mtu wa kunywa na kuzungumza naye. Alitaka kumpigia simu Lisa, lakini akakumbuka kuwa Lisa
hakuwa huru sasa. Kwa hivyo, aliendesha gari hadi baa mwenyewe.
Baa zote za Masaki zilikuwa katika
barabara moja. Kulikuwa na baa chache tu ambazo watoto matajiri wangetembelea.
Saa
tano usiku, Sam na Alvin walishuka
kutoka kwenye chumba cha juu cha
jumba lake. Baada ya kula chakula cha
jioni usiku huo, Alvin hakutaka kurudi
nyumbani kwake, kwa hivyo Sam
aliongozana naye kwenye baa tena.
Lakini, Alvin hakunywa sana siku hiyo, labda kwa sababu alikuwa amechoka kwa kulewa jana yake.
"Alvin, unarudi Nairobi kwa ajili ya mwaka mpya? Kama utakuwepo, babu yangu alikuomba uje kwetu,” Sam
alisema huku akitembea. Alipotazama pembeni, mara akamuona mwanamke
ameketi kando ya baa hiyo. Alivaa koti la pamba la rangi ya manjano lililofifia
lililosaidiana na ngozi yake nzuri, na
nywele zake ndefu za mawimbi
zilining'inia kwenye mabega yake. Hata hivyo, alionekana kulewa kabisa.
Wanaume wawili waliokuwa kando yake
waliendelea kumvutavuta na kumsumbua.
“Siyo Pamela Masanja yule? Mbona anakunywa peke yake hapa?” Sam na
Pamela walikuwa wamekutana mara
kadhaa hapo awali, na alikuwa na
mtazamo mzuri juu yake. Alikuwa msichana mchangamfu na
anayejitambua na hakuharibiwa na mambo ya kupita. Alvin alimtazama na
kumtambua kuwa ni rafiki mkubwa wa
Lisa. Akasugua macho yake. Ikiwa kitu
kingetokea kwa rafiki yake, bila shaka
Lisa angekuwa na wasiwasi. "Nenda
ukawaondoe hao watu wawili."
Sam mara moja akasogea na kuwashika wale watu waliokuwa
wakipepea mgongoni mwa Pamela.
“Wewe sh*t... Bwana Harrison…”
Mwanaume huyo aliuona uso wa Sam
waziwazi na kumkoromea.
“Ondoka machoni mwangu mara moja.
Huyu ni rafiki yangu. Nitamuua yeyote
atakayethubutu kumgusa siku yoyote,” Sam alionya na kumpiga teke.
Wanaume hao wawili wakakimbia mara moja. Kila mtu alijua kuwa neno la Sam Harrison lilikuwa sheria kwenye baa za eneo hilo. Kumkasirisha ilikuwa ni sawa na kujitakia kifo.
“Pamela, njoo, twende. nitakupeleka nyumbani.” Sam alimsaidia Pamela kuinuka. Pamela alimuegemea huku akiyumbayumba kwani alikuwa
amelewa sana asiweze kutembea kwa usawa. Mdomo wake bado ulikuwa ukipiga kelele, “Siendi nyumbani! Bado nataka kunywa! Siku njema ya kutengana! Ni kwa kuagana na wabaya tu ndipo utakutana na walio sahihi…”
Sam alimsaidia kumkokota hadi kwenye gari, akionekana kuwa na huzuni.
“Mwanamke huyu ameachwa na mpenzi wake, sijui amekunywa kiasi gani?'
"Unakaa nyuma." Alvin alikwenda kwenye kiti cha mbele cha abiria, hivyo
Sam aliweza kukaa tu nyuma na Pamela. Hans akaendesha.
Mara baada ya Sam kuingia kwenye gari, Pamela alimshika kola na kumkaripia.
“Patrick Jackson, wewe b*stard, wewe *sshole! Nilikupenda kwa miaka minane, lakini una Linda tu machoni pako. Wewe ni kipofu?”
Mara Pamela akacheua kwa nguvu
kama anataka kutapika, lakini hakutapika. Akaendelea tu kuongea kilevi. "Nakulaani kuwa utasalitiwa na kila mwanamke katika maisha yako yote."
Sam alipigwa butwaa. "Pamela
Masanja, angalia kwa karibu. Mimi ni Sam Harrison.”
"Nani Sam Harrison?" Pamela aliinamisha kichwa chake. “Sijawahi kusikia habari zako. Unajaribu kuniteka nyara kwa sababu mimi ni mrembo sana?”
Sam alikosa la kusema na akamwelekeza mbele. “Unamfahamu
Alvin Kimaro? Ni mpenzi wa rafiki yako mkubwa, Lisa Jones.”
Pamela alimtazama kwa butwaa, na macho yake yakaangaza ghafla. “Oh, ni mjomba. Habari, Mjomba.”
Alvin akasugua macho yake. Pamela alikuwa akimuita kwa jina hilo la kipuuzi kila alipokuwa amelewa .
Lakini, Sam alicheka. “Umekosea. Yeye si mjomba wako.”
“Sijakosea. Yeye ni Mjomba.” Pamela
alitikisa mkono wake. “Sijakosea
kamwe. Ni yule mpuuzi mjomba wa Ethan Lowe. Mimi na Lisa tulikuona mara ya kwanza tukiwa kwenye baa.”
Alvin alikunja uso na kuuliza kwa sauti ya chini, "Mbona umenikazia macho?"
"Lisa alitaka kuolewa na wewe kulipiza
kisasi bila shaka. Ikiwa Lisa angeweza kuwa shangazi ya Ethan, hakika hilo
lingemkasirisha hadi kufa. Inaweza pia kusababisha ghasia katika familia ya Lowe, haha.” Pamela alikuwa amelewa kabisa akiropoka hovyo. “Oh, ngoja, wewe si mjomba wa Ethan. Sorry!
Nilikosea. Nimekuchanganya tena kama
nilivyochanganya kumwelekeza Lisa.
Yaani nikinywa pombe tu nakuonaga
kama mjomba wake Ethan sijui kwanini, hahahaaa…nisamehe sana mjomba!”
Macho ya Alvin yalizidi kuwa meusi
huku akisikiliza, Sam akameza mate
akihisi amepata siri kubwa.
“Vipi uliishia kunifananisha?” Alvin
alijaribu kulainisha sauti yake.
“Ninafanana na mjomba wako?”
"Sina mjomba." Pamela alionekana
mjinga. Baada ya muda, alijichanganya tena, "Mjomba, unapaswa kuwa mzuri
kwa Lisa. Usiwe na hasira naye. Ni mimi
niliyemtia moyo kukutumia dawa za
kulevya. Kwa kweli haikuwa na uhusiano wowote na Lisa… ” Kisha,
aliegemea mlango kwa butwaa na kulala. Ndani ya gari, iwe Hans aliyekuwa
akiendesha gari au Sam aliyekuwa
amekaa nyuma, wote wawili walihisi joto
la mle ndani lilikuwa limeshuka hadi
kufikia kiwango cha baridi. Baada ya
kuendesha gari kwa dakika tano, Alvin
ghafla alisema, "Simamisha gari."
“Alvin.” Sam alikuwa na wasiwasi kidogo. “Umechelewa sana, twende nyumbani kaka.”
"Ninahitaji kufikiria juu ya kitu pekee
yangu. Nyie mrudisheni kwanza.” Sauti ya Alvin ilikuwa ya nguvu.
Hans aliweza tu kusimamisha gari. Alvin
akatoka nje, akafunga mlango na kutembea peke yake kando ya barabara. Sam akahema. Ingawa kile
Pamela alisema hapo awali hakikuwa
wazi, alikuwa na dhana isiyo wazi juu ya kile kilichotokea.
Aliweza tu kupata picha kwamba
kutokuelewana kati ya Alvin na Lisa
kulisababishwa na mkanyiko huo wa awali. Maskini Alvin!
Sura ya 142
Katika jumba la kifaharila Alvin, Lisa
alitazama tena wakati. Ilikuwa saa sita
na nusu usiku, lakini Alvin alikuwa bado
hajarudi. Je, alienda kunywa nje tena?
Kwa kweli hakutaka kumjali na alitaka
kumpuuza tu, lakin alishindwa kuudhibiti moyo wake. Bila yeye, hakuweza kulala
hata kidogo.
Ghafla, sauti ya mlango kufunguliwa ikasikika kutoka chini. Haraka akajilaza
na kujifanya amesinzia. Dakika chache baadaye, mlango ulifunguliwa, na hatua za miguu zikakaribia kitanda. Aligundua kuwa Alvin alisimama kando yake.
Moyo wake ukasisimka.
Ghafla, taa ikawaka. Kisha, blanketi juu ya mwili wake lilitolewa. Sauti ya mwanaume huyo ilisikika kutoka juu yake. "Simama."
"Alvin, unafanya nini sasa?" Lisa aliketi
kwa uchovu na kumtazama. Macho ya
mwanamume huyo yalikuwa mekundu
kama damu na kumfanya aonekane
mwenye sura ya kutisha.
Alvin alimtazama usoni Lisa
aliyeonekana kutokuwa na hatia. Bado alikumbuka waziwazi mara ya kwanza
alipokutana naye, pamoja na kila neno na kila usemi wa hila aliosema. “Ngoja nikuulize. Kwanini ulinitongoza kule kwenye baa?”
“Mbona unauliza hivyo ghafla?” Lisa
alikwepa macho yake, hakutaka kujibu swali hilo.
Hata hivyo, Alvin hakumruhusu kujificha na kumshika kidevu chake. Macho yake malegevu yalifungwa kabisa na macho makali ya Alvin. "Ilikuwa ni kwa sababu ulinidhania kuwa mimi ni mjomba wa Ethan Lowe?"
Sauti ya Alvin ilionekana kusikika katika
ubongo wa Lisa kana kwamba alikuwa
amepigwa na radi. Akili ya Lisa ilikuwa
imepotea. Alvin alijuaje kuhusu hilo?
Alvin alimtazama na kuona wazi
mabadiliko yote katika sura yake. Uso wake ulibadilika rangi. Kulikuwa na hofu, mshtuko, na wasiwasi mkubwa machoni pake. Moyo wake pia uliongezeka mapigo inchi kwa inchi.
Alvin alijihisi kana kwamba alikuwa mpumbavu tu. Aliamini kwamba Lisa alimpenda mara ya kwanza tu alipomuona. Alifikiri kwamba alikuwa na uwezo mkubwa katika uhusiano huo, lakini alikuwa akichezewa naye tangu mwanzo. Mapenzi yake yote yalikuwa ya uwongo. Utamu wake wote ulikuwa bandia. Kila kitu kizuri kilikuwa bandia.
Hata hivyo, moyo wake uliguswa sana na mwanamke huyo mnafiki.
“Hapana… Hiyo si…” Lisa alishikwa na butwaa na hakujua la kusema.
"Mipango yako inanifanya niwe
mgonjwa sana." Alvin akamtikisa na kuufuta mkono wake kwa kitambaa
kana kwamba amegusa kitu kichafu.
Lisa alichomwa sana na matendo yake. “Sawa, nakubali. Ilikuwa kweli
mwanzoni, lakini baadaye"
"Kisha ulikutana na Kelvin Mushi
kwenye sherehe ya uchumba ya Ethan
Lowe na ukagundua kuwa mtu huyo
ndiye mjomba halisi wa Ethan, kwa
hivyo ndiyo maana mara moja ukaanza
kudai talaka, sivyo?"
Alvin alikuwa tayari ameshafahamu kila
kitu. Hakutambua hapo awali, lakini
sasa aligundua kwamba kulikuwa na kila aina ya mambo ambayo yalikuwa ya
kutiliwa shaka. "Kwa bahati mbaya,
baadaye ulifanyiwa njama na familia ya
Jones Masawe na ulikuwa karibu
kwenda jela. Hakuna mtu ambaye
angeweza kukuokoa, hivyo rafiki yako wa karibu angeweza tu kuja kuniomba na kuendelea kunidanganya, akiniacha nifikiri kwamba ulinipenda kweli.”
Midomo ya Lisa ilikuwa imepauka. Kwa kweli alikuwa na akili sana. Kila kitu kilikuwa kama alivyokisia. “Ndiyo, lakini uliponiokoa kwenye eneo la ujenzi, niliguswa moyo sana nawe.”
"Funga mdomo wako. Hakuna ukweli katika chochote kinachotoka kinywani mwako wala rafiki yako wa karibu."
Alvin alizidi kupandwa na hasira huku akiongea. Alishindwa kujizuia na kumkandamiza kitandani huku akiikaba shingo yake kwa nguvu.
“Hata kama hukuleweshwa na Lina
Jones kwenye hoteli usiku ule, ungetaka
kulala na Kelvin Mushi hata hivyo, kwa hiari yako mwenyewe. Yaani mimi
unanipetipeti tu kisha unaenda kulala na Kelvin, si ndiyo?”
"Kweli mimi ni mtu wa namna hiyo moyoni mwako?" Alipokuwa akibanwa, hakuweza kupumua. Upande huu wa Alvin ulimtisha sana.
“Si wewe? Nilitaka kulala nawe hapo awali, lakini uliendelea kunikatalia.
Baadaye, ulipogundua kuhusu utambulisho wangu wa kweli, mara
moja ulitaka kulala na mimi. Inasikitisha kwamba picha hizo zilinifanya nitambue
kabisa sura yako halisi. Unajua kwamba mtu wa mwisho aliyeniudhi tayari
amekwisha kwenda kuzimu?”
Alvin alikuwa kama mnyama mwenye hasira. Nguvu za mikono yake
ziliongezeka.
Uso wa Lisa ulikuwa mwekundu, machozi yaliendelea kumtoka. Nuru ya macho yake ikawa nyeusi, naye akafikiri
ya kwamba alikuwa karibu kukosa hewa na kufa. Alvin akamsukuma na kuupiga mto uliokuwa kando yake kwa nguvu.
Macho yake yaliyokuwa na damudamu yalimtazama. "Sitakuua kwa sababu sitaki kuchafua mikono yangu." Kisha, akafunga mlango kwa nguvu na kutoka chumbani.
Lisa alikumbatia magoti yake na kuzika
kichwa chake ndani yake. Moyo wake ulijihisi mtupu. Pengine, yote yalikuwa ni bahati mbaya tangu mwanzo. Lisa
alikuwa amemwendea Alvin kwa nia
chafu. Baada ya hapo, alimdanganya tena na tena ili atoke jela. Sasa kwa
kuwa uwongo wake ulikuwa wazi, uhusiano wao ulikuwa kama povu
ambalo lingepasuka kwa kuguswa
kwake. Lisa hakupata usingizi usiku mzima.
Aliamka mapema na kumuandalia Alvin
kifungua kinywa. Pengine kingekuwa kifungua kinywa cha mwisho alichomtengenezea Alvin.
“Mbona umeamka mapema sana? Ni saa kumi na mbili na nusu tu” Aunty Linda aliingia jikoni huku akipiga miayo.
Alipouona uso wa Lisa uliopauka, alipigwa na butwaa. “Jana usiku hukulala? Huonekani vizuri sana.”
"Anti Linda, haya ndio mapishi niliyoandika jana usiku." Lisa hakujali
kile Aunty Linda aliuliza bali alimwambia yake na kumkabidhi kijitabu. "Haya
ndiyo baadhi ya mapishi anayopenda sana Alvin. Yeye ni mbaguzi sana, kwa hivyo ninaweza kuhitaji kukusumbua ili
kumpikia katika siku zijazo.”
"Unamaanisha nini?" Shangazi Linda
alishtuka. Alijua kuwa wote wawili
walikuwa kwenye mzozo mkali muda
huo lakini migogoro ilikuwa ya kawaida
kati ya wanandoa. “Haraka weka mbali
hayo mawazo. Bwana Kimaro anapenda upishi wako. Hata nikipika
vizuri hataki kula chakula changu.”
"Hakuna jinsi… sioni namna nnyingine tena." Lisa alitoa kicheko cha
kujidharau. Kwa mtazamo wa mambo wakati huu, hakuthubutu kutarajia
kwamba angeweza kuendelea kukaa ndani ya nyumba hiyo.
Hata kama yeye mwenyewe alimwambia Alvin kwamba alikuwa
akimpenda, asingeamini pia. Angefikiri tu kwamba anapendezwa naye yote
kwa sababu tu ya utajiri wake alioufahamu. Isitoshe, walikuwa
wamepoteza imani katika kila mmoja
wao. Ikiwa wangebaki pamoja, huenda wasingeweza kuishi kwa furaha.
alikataa kupokea kijitabu hicho. Kwa
hayo, aligeuka na kuondoka. Lisa
“Usiongee ujinga.”
Shangazi Linda
hakuwa na la kufanya zaidi ya kukiweka
kwenye kabati la jikoni huku akiamini
kuwa Aunty Linda angekiona.
Asubuhi hiyo, aliweka juhudi nyingi
katika kuandaa kifungua
kinywa. Kifungua kinywa cha siku hiyo
kilikuwa sawa na kifungua kinywa cha
kwanza walichopata walipoanza kuishi
pamoja.
Saa mbili kamili asubuhi, Alvin alishuka
akiwa amevalia sweta jeusi na suruali
nyeusi. Kwa umbo lake refu, hakuwahi
kushindwa kufanana na mtu mashuhuri
aliyependeza na kung’ara bila kujali
alivaa nini. Lakini, uso wake tu ndiyo
ulitisha zaidi. Macho yake meusi
yalikuwa makali kama ncha ya mkuki, na kumfanya Lisa kutetemeka.
Shangazi Linda alitaka wapatane, hivyo
akatabasamu na kusema, “Bwana
Kimaro, Bi Kimaro aliamka mapema
sana saa kumi na mbili asubuhi ili
kukuandalia kifungua kinywa. Hata hakuniruhusu nimsaidie. Angalia kupikia
kwake"
“Anti Linda, endelea na unachohitaji kufanya kwanza,” Alvin akakatisha sentensi yake.
Aunty Linda akahema. Hakuwa na budi ila kuondoka. Sebule ya nyumba ilibaki na wao wawili tu. Charlie na wanae watatu walikuwa wakicheza kwenye
kochi. Alipowaona wakicheza kwa
furaha, Lisa alijawa na wivu wenye
huzuni. Alitamani bora kuwa paka
mwenye furaha muda wote kuliko
mwanadamu aliyeandamwa na matatizo tu, kwa kuzingatia maisha yasiyo na presha ya paka wale.
"Tia saini hii." Alvin akatupa hati kwenye meza ya chakula. Maneno
yaliyoandikwa ‘Divorce Agreement’
(Makubaliano ya Talaka) yalimtoboa macho Lisa. Alivuta pumzi kwa upole, lakini bado aliweza kuhisi maumivu.
Kwa kweli, bado alikuwa akimpenda. Wakati picha za Kelvin na yeye zilipofichuliwa kabla ya hilo jingine kuzuka, hakuwa ametaja nia yake ya kutengana naye au kumtaliki.
“Isaini. Nitamwomba mtu ashughulikie suala la talaka yetu.” Alvin akatazama pembeni. Kadiri alivyokuwa akiutazama uso wake wa kinafiki, ndivyo ilivyozidi
kumkumbusha jinsi alivyomdanganya kama mjinga.
Jana yake usiku, alikuwa ametumia usiku kucha akifikiria mbinu nyingi, kulingana na uzoefu wake, kulipiza kisasi kwake.
Ghafla, aliona haina maana tena baada ya mbinu hizo za kikatili kumpita
kichwani moja baada ya nyingine.
Hakujisikia tena kuishi maisha ya
namna hiyo. Kwa kuwa lilikuwa ni kosa tu, alitaka kurudisha kila kitu jinsi ilivyokuwa kabla ya hilo. Baada ya yote, alikuwa mpita njia tu ambaye hakuona kuwa wa kuthaminiwa. Lisa aliinyanyua ile hati taratibu na kuipitia. Alvin alipomsikia akiipekua ile hati, alikunja uso kwa kejeli.
“Tulipooana, nilikuahidi kuwa nitakulipa baada ya kuachana, na nilikusudia.
Lakini sasa sijisikii kukulipa hata senti moja. Unapaswa kujisikia bahati
kwamba ninakuacha oundoke na roho yako, vinginevyo... Ni bora nisiende mbali sana.”
“Sijawahi kuwaza pesa zako…” Lisa
alicheka kwa uchungu. Alibaini kuwa
mawazo ya Alvin yalikuwa kwenye pesa
zake, kwamba Lisa alikuwa akiziwinda.
Sura ya 143
Alvin hakujisumbua kumtazama Lisa machoni. Lisa aliinamisha macho yake kimya
kimya. Kwa mtazamo wa mambo, ilionekana kuwa hakuna kitu ambacho
angeweza kuelezea zaidi akaeleweka. Alichukua kalamu na kusaini karatasi.
Moyo wake haujawahi kuwa mzito hivi alipokuwa akisaini 'Lisa Jones'.
"Nimemaliza. Naenda ghorofani kufunga vitu vyangu, nitaondoka mara baada ya hapo.” Aligeuka na kuelekea juu. Alvin
hakuwa na mpango wa kugeuza kichwa chake. Lakini, mwishowe alitazama
nyuma na kujikuta anamtazama licha ya yeye mwenyewe kutaka.
Alikuwa amevaa nguo za kulalia za
waridi, na nywele zake zilianguka juu ya
mabega yake kama maporomoko ya
maji. Harufu kama ya mwerezi ilitanda
mahali alipotoka.
“Unafikiri bado nitaamini maneno yako?”
Alvin alikunja ngumi. Kadri alivyozidi
kukunja ngumi ndivyo alivyokuwa
akikosa hewa kifuani. Hapo awali
alifikiria alikuwa anamtisha tu na
asingesaini karatasi. Bila kutarajia, alisaini bila kusita zaidi. Pengine
hakungoja kukutana na Kelvin tena.
Hah…
Alidhihaki kwa kejeli. Kwa kuwa alikuwa
amepitia vikwazo vingi, hakika
asingekufa kwa sababu tu ya kuondoka
kwake. Nusu saa baadaye, Lisa aliburuta
masanduku yake chini. Kwa wakati huo, hakuna mtu aliyekuwa sebuleni, na
kifungua kinywa kizuri alichotayarisha
hapo awali kilikuwa kimeishia kwenye
pipa la takataka. Alikunja midomo yake
kwa huzuni, akajifuta machozi kwenye
kona za macho yake, akaondoka.
Alipotazama jumba hilo likiwa mbali
zaidi kupitia kioo cha nyuma cha gari, alinung'unika ndani kwa ndani, 'kwaheri, Alvin.' Alikuwa akipaona mahali hapo
kama nyumba yake pekee na Alvin
kama mwanafamilia wake pekee. Lakini
sasa, hatimaye alikuwa peke yake tena.
Kwa kuwa hakuwa na pa kwenda kwa
wakati huo, Lisa alielekea kwenye
nyumba ya Pamela. Baada ya Lisa
kubonyeza kengele ya mlango kwa
muda, Pamela alifungua mlango.
Nywele zake zilikuwa chafu na kulikuwa
na harufu kali ya pombe juu yake.
“Kwa nini umekuja na masanduku yako?” Akiwa amechanganyikiwa na kustaajabu, Pamela alitazama
masanduku mawili yaliyokuwa kando ya miguu ya Lisa.
“Nimepewa talaka, na nimefukuzwa
nyumbani kwa Alvin. Kwa vile sijanunua
nyumba, sina pa kukaa isipokuwa
mahali pako.” Lisa akaburuta
masanduku yake ndani ya nyumba. Alijilaza kwenye kochi kama kikaragosi
asiye na roho.
"Nini?" Pamela alipandwa na hasira. "Ni kwa sababu ya picha? Kama mpenzi
wako, asingewezaje kukuamini? Mimi naenda kumfanya alipe. Ameenda mbali sana…”
“Usiende kwake.” Lisa alimsimamisha
Pamela. “Tayari anafahamu kuwa
mwanzoni nilimwendea kwa sababu
nilimdhania kuwa ni mjomba wa Ethan.
Pia amegundua kuwa ulimdanganya kabla ya hili kwa ajili ya kunitoa jela.”
"Nini? Aliwezaje kujua?” Pamela alipigwa na butwaa.
"Sina uhakika. Ni mimi na wewe tu ndo tulikuwa tunajua kuhusu suala hili." Lisa alimtazama kwa sura ya kinyonge.
“Sikumwambia chochote. Kwa
kuzingatia harufu kali ya pombe juu yako, labda ulikunywa sana jana usiku.
Una tabia ya kuzungumza upuuzi baada ya kulewa.”
“Usinituhumu…” Pamela alishikwa na wazo alipokuwa akizungumza. Alishika nywele zake. “Sasa nakumbuka.
Nadhani Sam ndiye aliyenirudisha
nyumbani jana usiku, na nilikuwa
nimelewa sana wakati huo. Kulikuwa na mwanamume mwingine ndani ya gari, na alidai kuwa mpenzi wako."
Lisa alikosa la kusema. Alikuwa
kishajua tangu aliposikia akinuka
pombe. Bila shaka, Pamela alikuwa ameropoka bila kujijua. Pamela
aligonga kichwa chake kwa nguvu.
Alitamani angepasua kabisa ubongo
wake. “Samahani, Lisa.”
Akiwa amehuzunika,
Pamela alipiga magoti mara moja mbele
ya Lisa. “Nimekuingiza kwenye matatizo tena. Sijui jinsi ninavyoweza kukusaidia
wakati wa maisha yangu. Naona aibu sana kukukabili. Vipi kuhusu kukutolea ndugu yangu kama fidia ya kosa langu?
Ninaahidi kwamba atakupenda kikweli na atabaki mwaminifu kwako.”
"Acha kuongea ujinga." Lisa alipunga mkono wake akimaanisha kuwa alikuwa amechoka sana asiweze kumkaripia.
“Hata hivyo, bado ingekuwa vigumu
kwetu kuendelea na uhusiano wetu hata kama hukusababisha tatizo. Kuna suala
kuhusiana na Kelvin na... mpenzi wake wa zamani ambaye hawezi tu kumshau.
Kila mara hutaja jina lake anapokuwa amelewa.”
"Nini? Kwa nini wanaume huwa na macho ya kupepesuka?” Pamela alisaga meno kwa kufikiria kile
kilichomkuta yeye mwenyewe.
“Vipi, ulimpeleka Patrick pamoja na familia yako kula chakula cha jioni jana usiku, sivyo? Kwa nini uliishia kunywa pombe?” Lisa alianza kushangaa ghafla. “Inaweza kuwa hivyo… Patrick alikutosa tena?”
Pamela alisema kwa uchungu, “Linda alipata ajali, Patrick akaenda kumwangalia. Hakunipigia hata simu.
Nimeachana naye moja kwa moja safari hii.”
“Jamani. Ni balaa gani hili?” Lisa alitukana kwa hasira. Ghafla, akahema.
“Sawa. Ulinifanya niishie kuachwa, na wewe uko single sasa hivi pia. Ngoma droo. Nitakuchukulia tu kama kampani yangu. Hata Patrick akikuomba
urudiane naye wakati huu, usikubali kukutana naye tena.”
“Ndiyo, bila shaka. Mimi ndiye
niliyekuumiza. Maadamu haujaolewa, sitathubutu kuolewa. Ikiwa hutapata hata mwanamume mzuri wa kukuoa, tunaweza kushiriki katika uhusiano wa jinsia moja. Kwani wanawake wangapi wanasagana?”
“Potelea mbali. sina hamu na wewe.” Lisa, ambaye mwanzoni alikuwa
amekasirika, hakujua kulia au kucheka wakati huo.
Chini ya dakika 20 baada ya kuondoka, gari la Sam lilionekana kwenye jumba la Alvin. Alikimbia kwa kasi hadi ghorofani, akamkuta Alvin akiwa amesimama
kwenye kibaraza huku macho yake
yakiwa barabarani. Alikuwa ameshika
sigara, na sinia ya majivu iliyokuwa
kando yake ilikuwa imejaa virungu vya
sigara. "Alvin, kweli utarudi Nairobi?" Sam
alisema kwa hisia, "Nitaku’miss sana, na itakuwa tofauti kutokuwa na wewe karibu."
"Utani’miss kama rafiki au utakosa kuwa
nami kama chanzo cha mapato cha kampuni yako?" Alvin aliacha majivu ya sigara yadondoke bila kujali.
Kwa aibu, Sam alitoa kikohozi chepesi. "Angalia, ingawa umekuwa hapa kwa muda mfupi tu, umeipatia zaidi ya shilingi bilioni moja kampuni yangu ya sheria mwaka huu."
Alvin akaingiza mikono yake mfukoni. Macho yake meusi, mazito yalionyesha hali ya ujeuri.
Sam akahema. “Sawa. Kama ningelijua hili mapema, nisingekualika Dar es
Salaam. Kwa hiyo unaondoka lini?”
“Kesho. Tafuta mtu wa kuuza nyumba
hii." Baada ya kuongea kwa sauti ya kupuuza, Alvin aligeuka na kuingia ndani ya nyumba.
••• Asubuhi iliyofuata. Kitu cha kwanza alichofanya Lisa baada ya kuinuka
kitandani ni kumuandalia Alvin kifungua kinywa. Dakika akitoka chumbani, alipigwa na butwaa baada ya kuiona sebule hiyo asiyoifahamu. Alisahau
kuwa Alvin alikuwa ameachana naye. Hakuhitaji kuamka mapema ili kumpikia tena. Isitoshe, kusingekuwa tena na mlinzi wa kumuangalia. Kwa kweli, alikuwa ameachwa kama jongoo na mti wake.
Kama mwenyekiti wa kampuni yenye
thamani ya zaidi ya dola milioni 500, alipaswa kuishi maisha kwa uhuru
mkubwa zaidi. Alipaswa kufurahishwa na jambo hilo, lakini hakuweza kuhisi
furaha hiyo hata kidogo. Baada ya
kifungua kinywa, Lisa aliendesha gari
hadi hospitali kumtembelea Kelvin.
Hakuwa amemtembelea tangu siku
alipopoteza fahamu.
Sura ya 144
Lisa alikuwa akijisikia hatia kwa jinsi alivyomtendea Kelvin.
Alisimama mbele ya wodi akiwa na maua na matunda. Wakati anakaribia
kugonga mlango, mara akasikia
mwanamke akilia kwa sauti ya chini
ndani ya chumba hicho.
“Usilie mama.” Kelvin alimfariji mama yake. “Siwezi kulia vipi? Wewe ndiye mwana
pekee wa kiume katika familia ya Mushi.
Nilitarajia uendeleze ukoo wa familia ya Mushi, lakini angalia nini kimetokea.
Najiuliza ni nani aliyefichua suala hilo
kuhusu figo yako? Wanawake wote
ambao mwanzoni walitaka kuolewa na
wewe sasa watakukwepa. Hakuna atakayetaka kuolewa wewe.”
Kelvin alijibu, “Haijalishi, Mama. Hata hivyo, sijisikii kuoa bado.”
“Mimi ndiye niliyekuzaa. Unafikiri nitajisikiaje? Huwezi kuacha kumfikiria
Lisa? Hata ulihatarisha maisha yako kwa sababu yake.”
Akiwa ameshikilia kikapu cha matunda kwa nguvu, Lisa alisikiliza kile ambacho
Mama Mushi alisema mwishoni. “Hata hajali kuhusu wewe. Umelazwa hospitalini kwa siku nyingi, lakini hajakutembelea hata kidogo.”
“Inatosha mama. Ni chaguo langu.
Kumpenda mtu haimaanishi kuwa lazima uwe naye. Kumlinda na
kumwangalia akiishi kwa furaha ni zaidi ya kutosha.” Kelvin alieleza.
Lisa alihisi uvimbe kwenye koo lake.
Kuna kitu kilionekana kukwama kwenye
koo lake, jambo ambalo lilimfanya
akose raha. Kamwe hakutarajia
kwamba Kelvin angempenda sana.
“Mbona umesimama hapa?” Mzee
Mushi alikoroma kwa hasira nyuma ya
Lisa nje ya wodi.
Lisa alishtuka, na wale waliokuwa
chumbani wakamtazama.
Kwa hayo, aliingia chumbani kwa
kusitasita. Kelvin aliguswa kuwa huenda
Lisa alikuwa amesikia alichokisema.
Kwa hiyo, uso wake mzuri ulianza
kuona haya usoni. “Lisa, kwa nini
umenitembelea leo, Alvin hatachukia?”
“Nimefika hivi punde. Mimi na yeye
tayari tumeshaachana.” Lisa aliinua
kichwa na kumtazama. Alionekana
kuwa mwembamba sana ndani ya siku
chache tu. Gauni alilovaa lilionekana
kumlegea huku uso wake wa kifahari na mrembo ukionyesha kama mgonjwa anayesumbuliwa na utapiamlo.
"Mbona mmeachana ghafla?" Kelvin
alipigwa na butwaa. "Ilikuwa kwa sababu yangu?"
"Hapana. Kuna matatizo mengi sana kati yetu.” Lisa alibadilisha mada.
“Unaendeleaje sasa?”
"Anaendelea vizuri?" Mama Mushi
aliinuka akiwa na uso mchangamfu.
“Alipoteza figo, sasa figo moja si sehemu ya nyama yake tena. Hawezi
hata kurejesha kimetaboliki chake bado.
Kwa kuwa mikono yake inakabiliwa na uharibifu wa neva, anahitaji kupitia miezi michache zaidi ya matibabu. Mbaya
zaidi, maisha yake ya baadaye
yataathiriwa. Daktari alisema kuwa
hatakiwi kufanya kazi ama mazoezi
magumu, na anapaswa kuwa
mwangalifu katika lishe yake.
Vinginevyo, atapoteza maisha yake. Kwa kuzingatia kwamba kwa kawaida
anahitaji kusimamia kampuni kubwa kama hiyo, nadhani hawezi kuishi maisha marefu.”
Mzee Mushi alimkemea, “Unaongea upuuzi gani? Zingatia maneno yako."
“Nimekosea? Tayari tuko katika miaka ya mwisho ya uzee wetu, kwa sababu tulikuwa na mtoto wetu mmoja tu wa kiume, pengine tunapaswa kumtunza milele.” Mama Mushi alijifuta machozi usoni mwake. “Unafikiri kuna
mwanamke yeyote kutoka katika familia
yenye heshima ambaye yuko tayari
kuolewa naye? Maskini mwanangu, nina wasiwasi na maisha yako ya baadaye.”
Akiwa ameshikwa na hatia, Lisa
alihuzunika sana. Alikuwa mwishoni
kabisa mwa akili zake.
“Acha, Mama.” Kelvin alimsimamisha
katikati ya maumivu ya kichwa chake.
“Nimekosea? Ulijeruhiwa kwa sababu yake. Alikutunza hata siku moja?
Ingekuwa afadhali ungeokoa mtu
usiyemjua kuliko yeye,” Mama Mushi
aliongeza kwa uchungu, “Kwa maoni yangu, yeye ndiye anapaswa kuwa
mwangalizi wako milele ili akusaidie. Hata hivyo, huwezi kupata mke kwa
sasa, basi yeye awe fidia yake.”
“Mama…” Kelvin alishindwa kujizuia, na uso wake mzuri ukageuka kuwa wa kustaajabisha ghafla. Maumivu yalikuwa
makali sana hadi akatoka jasho la
baridi. Wakati huo huo, shinikizo lake la damu lilionekana kupanda juu ya
kiwango.
Kila mtu aliingiwa na hofu na kumpigia
simu daktari haraka.
Daktari alifika haraka na kuwakemea, “Mgonjwa amefanyiwa upasuaji
mkubwa, badala ya kumfariji, mnampandisha presha. Mnataka afe?”
Kila mtu alinyamaza mara moja. Hata
Mama Mushi alifunga mdomo kwa aibu. Kelvin alichoka sana hata akapitiwa na usingizi muda si mrefu.
Tena, Mama Mushi alimtazama Lisa kwa hasira. Lisa aliinamisha macho kwa
hofu. “Acha kulalamika mama. Nitalipa fadhila kwake. Kuanzia leo na
kuendelea, nitamtunza. Hata baada ya kupona, nitashughulikia lishe na maisha yake hadi apate mke.”
"Lakini vipi ikiwa hawezi kupata mke?"
"Hilo halitawezekana." Lisa alimtoa wasiwasi.
Mama Mushi alidhihaki. “Nani yuko
tayari kuolewa na mwanaume aliyekosa kiungo? Ikiwa kuna matatizo na figo
nyingine, labda atakufa kwanza. Isitoshe, sidhani kama kuna mtu
mwingine yeyote ulimwenguni angekuwa tayari kuhatarisha maisha
yake ili kukuokoa.”
Lisa alikaa kimya kwa muda wa nusu
dakika kisha akaongea taratibu kwa
sauti ya ukali, “Sawa. Ninaahidi atanioa.”
•••
Katika mgahawa, Pamela alipopata
habari hizo, karibu amwage kahawa.
“Umerukwa na akili? Unapanga
kurudisha fadhila kwa kutoa maisha
yako, huh?"
"Sina la kufanya tena." Lisa aliinywa
kahawa iliyokuwa na ladha chungu
sana. "Zaidi ya hayo, picha yetu
imesambazwa kila mahali. Kila mtu ana
hisia kwamba tuna uhusiano wa karibu. Hata hivyo ni sawa tu, alitoa figo yake
moja kwa sababu ya kuniokoa…”
Pamela alishtuka baada ya kusikia hivyo. “Kelvin anakupenda sana. Siku
zote amekuwa akikulinda kwa siri, lakini
wewe na
Alvin…”
"Hatutarudiana kamwe." Lisa alionyesha sura ya uchungu. Hakumwambia
Pamela kwamba Alvin alikuwa mtoto wa familia ya Kimaro. Lisa na Alvin
walitenganishwa na bahari, na wote
wawili walikuwa katika ulimwengu
tofauti. Kwa kuongezea, mawazo yao
yalikuwa tofauti kabisa.
“Sawa basi. Kwa kweli, wakati mwingine
ni bora kwa mwanamke kutafuta
mwanaume anayempenda zaidi kuliko
yeye. Kwa njia hii, mwanamke hatahisi
kuchoka.” Akikumbushwa kuhusu
uzoefu wake wa mapenzi, Pamela aliugua. "Kwa upande wangu ninapanga kufanya kazi huko Nairobi mara tu baada ya mwaka mpya."
Lisa aliinua kichwa chake kwa
mshangao. "Kwanini unaenda huko ghafla?"
“Si ghafla. Mwaka jana, kampuni ya Osher kutoka Kenya lilinipa nafasi ya mkemia mkuu wa vipodozi. Sikuweza
kuvumilia kuachana na Patrick, kwa hiyo nilikataa kazi hiyo. Kampuni hiyo
ilinipa kazi hiyo tena mwezi uliopita, na niliikubali jana.”
Pamela alitazama nje ya dirisha kwa
huzuni. "Nimekuwa nikifikiria juu ya
Patrick katika wakati wangu wote nikiwa
hapa Dar. Natamani kuona ulimwengu mpya, na ninaamini nitasahau kuhusu
uhusiano huo polepole baada ya muda."
"Inaonekana kama wazo zuri." Ghafla, hali hiyo iliacha pengo kwa Lisa kwani
rafiki yake wa pekee naye angemuacha.
"Ninaweza kuelekea Nairobi pia na
kukuza biashara ya Mawenzi
Investments huko mwaka ujao. Kuhusu
kifo cha mama yangu… nataka kuja kuchunguza pia.”
“Uko sahihi. Baba yako anatoka Nairobi pia. Nitakusubiri uje.”
Usiku, Lisa alipakua masanduku yake. Alipofungua moja, ghafla akakuta Mkufu
wa Malkia ndani yake. Wakati anahama
kwa Alvin alikuwa amepakia vitu vyake
haraka na kusahau kuviangalia kwa
uangalifu. Kwa kushangaza, alikuwa
amebeba na Mkufu pamoja. Kwa
kuzingatia kwamba kitu hicho kilikuwa
cha gharama kubwa, asingeweza
kubaki nacho.