MTAFITI
v
Hussein Issa Tuwa
vii
Hussein Issa Tuwa
Kwa Zaynab. My Khaleesi.
NCHI IMEINGIA MACHAFUKO. Watu wameuawa.
Wengine wamejeruhiwa na kutiwa vilema, ilhali wengi
wengine wakijikuta wamerundikwa mahabusu, wakisubiri
kufunguliwa mashtaka ya uchochezi na uvunjifu wa amani.
Kwa mara nyingine kati ya chache zilizowahi kutokea,
amani iliyokuwa ikisifika kutawala Tanzania ikajikuta majaribuni... nchi ikaingia doa jingine.
Taharuki ikazagaa, mashaka yakatawala, vurugu zikaenea.
Sio zile vurugu zilizowahi kutokea kule Mwembechai jijini
Dar, na kusababisha vifo vya baadhi ya waumini na kupelekwa gerezani kwa baadhi ya viongozi wa kidini, La!.
Sio zile zilizotokea kule visiwani Zanzibar zikihusiana na
uchaguzi wa vyama vingi… Hasha!
Na wala sio zile za kule mkoa wa Mbeya ambapo baadhi ya waumini wa madhehebu tofauti waliamua kugombea
haki ya kuchinja ng’ombe wa kuuzwa mabuchani kule
kwenye mikoa ya mpakani mwa Zambia hadi ikasababisha
mpaka wa Tanzania na Zambia kufungwa kwa muda, La
Hasha!.
Hizi zilikuwa ni vurugu za kipekee, kwani vurugu nyingine
zilizowahi kutokea zilikuwa zinahusisha aidha kundi moja
katika jamii dhidi ya jingine, na serikali ikaingilia kati na
7
Hussein Issa Tuwa
kuweka hali sawa; au kundi moja katika jamii dhidi ya serikali, hali makundi mengine yakiiunga mkono serikali… na serikali ikaingia na kutunisha msuli wake mnene
kurejesha utulivu. Sio hizi vurugu zilizoingia kipindi hiki. Hizi zilikuwa zina wananchi upande mmoja na serikali upande mwingine.
Naam ni vurugu kati ya wananchi wa Mtwara wakidai haki
ya kunufaika na gesi iliyovumbuliwa kwao, gesi yao… dhidi
ya serikali iliyokuwa ikisisitiza kuwa gesi hiyo lazima isafirishwe kwenda Dar es Salaam ili iweze kutumika vyema
kwa wananchi wote wa Tanzania.
Ni balaa!
Kwa nini gesi isibakie Mtwara na kuwanufaisha wanamtwara
waliokuwa wameachwa nyuma miaka nenda miaka rudi kabla ya hiyo gesi kugundulika? Ndipo upekee wa vurugu hizi
ulipojitokeza, pale wananchi wa Mtwara walipoungana na kuwa kitu kimoja, pasi kujali tofauti zao za kidini, kiitikadi za
vyama wala za timu zao za mpira. Wote wakawa kitu kimoja. Wao dhidi ya Serikali. “Gesi kwanza, Uhai baadaye”, ndio ikawa kauli mbiu yao.
Hatari!
Serikali ikatumia jeshi lake adhimu la polisi kuleta utulivu, likiwashinikiza wananchi waliovamia mitaa ya mji wa Mtwara warudi majumbani mwao, watulie. Wananchi
wakagoma. Wakatoka na silaha za kila aina. Wakarusha mawe. Biashara zikafungwa. Mioto ikawashwa
mabarabarani. Polisi wakajibu mapigo. Kwa nguvu... Nguvu kubwa.
Balaa juu ya Balaa!
8
Watu wakauawa. Wabunge wa upinzani wakakemea kwa
jazba. Na wao wakatiwa ndani kwa kauli zao
zilizonasibishwa na uchochezi. Vurugu zikapamba moto
maradufu. Utete wa hali ukaongezeka.
Vyombo vya habari vya ndani na vya nje vikapata la kupigia kelele. Serikali ikawa imeshikwa pabaya. Waziri mkuu akapoteza uvumilivu. Akatoa agizo kali kwa jeshi la polisi. Kama wananchi hawataki kutii amri nyie PIGENI
TU!
La Haula!
Wapinzani wakalivalia njuga agizo. Wakataka Waziri Mkuu ajiuzulu kwa kauli yake ile. Ile ‘PT’ inayotangulia kwenye
vibao vya namba za magari ya polisi kumaanisha ‘Police Tanzania’, ikabatizwa na kuitwa ‘Piga Tu’, kufuatia kauli ile tata ya waziri mkuu.
Wanaharakati wa Haki za Binadamu nao wakalifungia kibwebwe tamko. Waziri Mkuu sio tu ajiuzulu, bali pia ashitakiwe kwa kauli za kushinikiza uvunjwaji wa haki za binadamu.
Mwisho wa yote Waziri Mkuu akamwaga chozi bungeni kuomba radhi. Makubwa!
Hakika zilikuwa ni vurugu ambazo hazijawahi, na yumkini
hazitakuja, kutokea tena nchini Tanzania.
Vurugu za Gesi ya Mtwara.
Kifuatacho ni kisa cha yaliyotokea kabla ya vurugu zile…
9
Hussein Issa Tuwa
1ILIKUWA NI JUMATATU ya kawaida kwa
wafanyakazi wa ofisi mbali mbali zilizokuwa ndani ya jengo maarufu la ghorofa kumi lililokuwa katikati ya jiji la Dar. Muda ulikuwa ni saa mbili kasoro
robo za asubuhi na wafanyakazi wengi walikuwa wakiingia
ndani ya jengo lile kwa mwendo wa haraka, kila mmoja
akitaka kuwahidawatilakelakazi na kuanza wiki mpya.
Kila mmoja miongoni mwao, wake kwa waume, alikuwa
katika mavazi nadhifu ya kiofisi. Mavazi yaliyoonesha kuwa
alikuwa ni mtu mwenye kazi muhimu jijini na alikuwa
akijivunia hilo. Walikuwamo waliokuwa wamevaa suti, na
pia walikuwamo waliokuwa katika nguo za kawaida tu, lakini nadhifu na zenye heshima.
Tofauti pekee katika kundi lile la wafanyakazi waliokuwa
wakiingia ndani ya jengo lile asubuhi ile ilionekana kwa
mwanaume mmoja aliyepata umri wa kiasi cha miaka
arobaini na mitano hivi. Yeye hakuwa nadhifu kama wale
wenzake aliokuwa amejichanganya nao asubuhi ile.
Alikuwa amevaa suti iliyokunjamana kama kwamba
alikuwa amelala nayo usiku uliopita na kutoka nayo asubuhi
ile bila kujali. Shati lake jeupe lililokuwa chini ya koti la suti yake iliyokunjamana, lilikuwa na madoa bila shakayamchuzi
waainafulani, nalilikuwa limechomoka njeyasurualiyake ya suti, huku tai iliyokuwa shingoni kwake ikiwa imelegezwa
na imekaa upande, vifungo viwili vya juu vya shati lile
vikiwa vimefunguliwa na kuacha sehemu ya shingo na kifua chake vikiwa wazi. Hakuwa amechana nywele asubuhi ile, na macho yake yaliyomvimba yalikuwa mekundu, bila shaka kwa kukosa usingizi.
Jamaa alikuwa amekunja uso kwa namna ya kuwa na mawazo mazito kichwani, na alikuwa akitembea kwa hatua
za haraka huku akimung’unya midomo yake, ilhali akichezesha chezesha vidole vya mikono yake. Kama kuna
ambaye alikuwa akimtilia maanani yule mtu asubuhi ile, basi mara moja angemaizi kuwa jamaa hakuwa sawa sawa.
Lakini kwa muda ule kila mtu miongoni mwa wale
waliokuwa wakiingia ndani ya jengo lile alikuwa na harakati zake na hivyo hakuna aliyemtilia maanani.
Isipokuwa askari wa kampuni binafsi ya ulinzi iliyokuwa
ikisimamia usalama kwenye jengo lile. Yeye aliiona tofauti ya mtu yule na wengine waliokuwa wakiingia mle ndani na
akasimama kutoka kwenye kiti chake huku akimtazama kwa
makini yule mtu.
“Bwana Mochiwa… Bwana Mochiwa, uko sawa…?” Askari alimsemeshayule mtu, huku akimtazama kwa udadisi.
Bila ya kumjibu, yule mtu aliyetambulika na yule askari
kwa jina la Mochiwa, alimpita kama kwamba yule askari
hakuwepo kabisa eneo lile. Aliingia pamoja na wale
wafanyakazi wengine kwenye lifti iliyokuwa ikielekea
kwenye ghorofa za juu za jengo lile, na ni hapo ndipo
baadhi ya wale waliokuwa ndani ya ile lifti pamoja naye walipogundua kuwa bwana Mochiwa hakuwa sawa sawa.
Baadhi waliamua kutopanda ile lifti na kuiacha iende ili
waipande itakaporudi tena, ili tu wasisafiri pamoja na yule
bwana. Wale waliobaki ndani ya ile lifti pamoja na bwana
Mochiwa walianza kumtupia macho ya mashaka huku
waliokuwa karibu yake wakijisogeza mbali naye kwa kadiri
walivyoweza mle ndani.
Jamaa hakuwatilia maanani asilani. Alikuwa amekodoa
macho moja kwa moja mbele yake huku akiwa amekunja
uso, akimung’unya midomo yake taratibu na akiendelea kuchezesha chezesha vidole vyake.
Aliteremka ghorofa ya saba ya jengo lile, akiacha watu wachache wakiendelea na lifti ile kuelekea ghorofa za juu
ilhali baadhi ya watu wengine wakiwa wameteremka kwenye
ghorofa za chini. Alienda hadi kwenye mlango mkubwa wa
shaba na kioo kizito, juu yake ukiwa na maandishi
makubwa yaliyosomeka ‘Liquid Diamond Inc.’, yaliyokuwa
yakilinadi jina la kampuni iliyokuwa na ofisi zake kwenye
ghorofa ya saba na ya nane za jengo lile maarufu jijini.
Liquid Diamond Incorporated ilikuwa ni kampuni kubwa
yenye uwezo mkubwa sana wa kifedha, ikimiliki helikopta
zake binafsi na ikiwa ina matawi kwenye mikoa kadhaa
ambako shughuli zake za kitafiti zilikuwa zinafanyika, ilikuwa ni fahari ya kila aliyebahatika kuajiriwa nayo.
Lakini sio kwa yule mtu aliyetambulika kwa jina la Grayson Mochiwa asubuhi ile.
Aliusukuma ule mlango na kupita ndani.
Msichana aliyekuwa mapokezi alianza kutabasamu alipomuona, lakini ghafla sana tabasamu lake likanyauka na nafasi yake ikachukuliwa na mshangao mkubwa.
“Mista Mochiwa…sh’k…sh’kamoo! Mbona hivyo…?”
Yule binti aliuliza kwa mashaka, lakini yule bwana hakumjibu. Alimpita kuelekea ndani zaidi ya ofisi ile akimuacha binti akiwa ameduwaa.
Jamaa aliifuata korido ndefu iliyokuwa na milango kadhaa kila upande, milango ambayo ilizinadi idara mbali mbali za
kampuni ile, hadi mbele ya mlango ambao juu yake kulikuwa na maandishi yaliyosomeka ‘Chief of Research’, ambayo yalikuwa yakiunadi wadhifa wa mwenye ofisi ile, yaani mkuu wa tafiti katika kampuni ile.
Alisukuma ule mlango na kuingia ndani.
Binti mwingine aliyekuwa ameketi nyuma ya kompyuta mle ndani aliinuausowakekumtazamaaliyeingia,nayekama yule mwenzake wa kule mapokezi, mara moja akabaini kuwa bwana Mochiwa hakuwa katika hali ya kawaida.
“Sh’kamoo bosi…. vipi mbona uko hiv…”
Jamaa alimnyooshea mkono kumuashiria amuache, au asimuulize kitu. Au asiendelee kumsemesha. Lolote alilomaanisha, lilimfanya yule binti anyamaze na abaki akimtazama kwa mshangao.
Ile ofisi ya ‘Chief of Research’ ilikuwa imegawanywa katika sehemu mbili kwa ukuta mfupi wa kioo kizito
kilichoshikiliwa kwa vyuma laini au aluminiamu. Sehemu moja ndiyo alikuwa ameketi yule binti aliyekutwa mle ndani na bwana Mochiwa.
Jamaa aliingia kwenye ile sehemu ya pili ya ofisi ile na kusimama mbele ya meza moja kubwa iliyokuwa na kompyuta ya kisasa juu yake, simu mbili kwenye kona moja
na trei yenye mafaili kadhaa kwenye kona nyingine. Mbele ya meza ile kulikuwa kuna kibao kilichonakshiwa kwa
urembo wa kuvutia, na juu ya uso wa kibao kile kulikuwa kumeandikwajinalammiliki wa ofisi ile.
Grayson Mochiwa - Chief of Research.
Jamaa alilitazama jina lake likiwa kwenye kile kijibao
kwa muda, kisha akaketi nyuma ya meza yake, akaiwasha ile kompyuta, na kusubiri programu zilizokuwa ndani yake
zijiweke sawa huku uso wake ukionekana kuwa na wahka
mkubwa.
Programu zilipokuwa sawia alibofya sehemu
iliyomuwezesha kufungua baadhi ya mafaili aliyokuwa
akitaka kuyashughulikia, na hapo alipata mshtuko ambao
alikuwa akiuhofia tangu alipotoka nyumbani kwake asubuhi ile.
Kama jinsi ilivyokuwa kwenye kompyuta yake ya mpakato
(Laptop) aliyoiacha nyumbani kwake, mafaili aliyotaraji
kuyakuta kwenye ile kompyuta yake ya ofisini nayo
hayakuwepo kabisa.
“Oh No, No, No… NOOOOOH! Haiwezekani jamani,
haiwezekani, haiwezekani, haiwezekani!” Grayson Mochiwa alisema kwa fadhaa huku akipiga piga meza kwa upande wa ngumi yake.
Kwa namna fulani ile hali ilikuwa amemchanganya vibaya sana.
“Mista Mochiwa kwani vipi… mbona hivyo leo?” Yule binti aliyekuwa akifanya kazi kwenye upande wa pili wa ile ofisi ya mtafiti mkuu wa kampuni ile kubwa alimuuliza akiwa amesimama kwenye uwazi wa kuingilia sehemu ya ofisi ya yule mtu aliyeitwa Grayson Mochiwa.
Jamaa alibaki akiwa amejishika kichwa huku amejiinamia pale mezani, akitikisa kichwa chake taratibu kutoka upande
mmoja kwenda mwingine. “Mista Mochiwa! Ni nini lakini? Mbona unan’tisha…? Unaumwa…?”
Binti aliuliza kwa mashaka makubwa.
Grayson Mochiwa alibaki akiwa namna ile kwa muda
mrefu bila ya kumjibu. Binti alibaki akimkodolea macho yaliyojaa woga mkubwa. Alipoona Grayson haoneshi dalili za kumjibu wala kubadilisha hali iliyojidhihirisha mle ndani, aliamua kuiendea simu iliyokuwa mezani kwake ili awapigie wafanyakazi wenzao waje kumpa msaada. Alikuwa akianza
kugeuka kuiendea ile simu wakati Grayson alipoongea bila ya kuinua uso wake.
“Kila kitu kimeharibika! Hakuna ushahidi tena sasa… kila
kitu… bidii zote… juhudi zote… umakini wote… vyote ni bure kabisa! Just like that? Oh, My God!” Aliongea maneno
haya kwa sauti ya kukata tamaa kabisa.
Binti alipigwa
butwaa.
Alimgeukia tena.
“What… una maanisha nini Mista Mochiwa? Ni nini
kimetokea kwani…?”
Grayson Mochiwa aliinua uso wake taratibu na kumtazama kama kwamba ndio kwanza anagundua kuwa yule binti alikuwa pamoja naye mle ndani.
“Mista Mochiwa…?” Binti alimwita huku akizidi
kumtazama kwa mshangao, sasa akiamini kabisa kuwa yule bwana alikuwa amerukwa na akili.
“Wewe bado uko hapa ofisini? Muda wako wamafunzosiumeshakwisha?” Grayson Mochiwa alimuuliza
huku akiendelea kumtazama kwa namna ile ile ya kushangaza.
“Aam, actually No. Bado wiki mbili bosi na…” Binti alijibu huku akizidi kumshangaa.
Grayson Mochiwa aliguna kwa kebehi kabla ya kumwambia; “Fungasha virago vyako uondoke binti!
Hamna tena kitu cha kukufanya uendelee kubaki kwenye hii
kampuni… I mean, hii sio tena ile kampuni uliyoomba kuja
kufanya mafunzo kwa vitendo miezi minne iliyopita…”
“Ah, Mista Mochiwa… mbona sikuelewi? Hata hivyo
ndio namalizia ripoti yangu… na pia ninahitaji ripoti yako
kama msimamizi wangu wa mafunzo kwa vitendo ili
niiwasilishe chuoni. Vyote hivyo bado…”
“Ripoti yangu iko tayari!” Grayson Mochiwa alimkatisha
huku akivuta droo ya meza yake na kutoa rundo la makaratasi yaliyopigwa taipu vizuri kwa kompyuta na
kumsukumia.
“Utahitaji kuandika ripoti yako tu na kuiwasilisha huko chuoni kwako. Huna haja ya kuendelea kuwemo ndani ya ofisi hizi zilizojaa udhalimu, ufisadi na hujuma… chukua uondoke. Nimekuandikia ripoti nzuri tu, so you will be okay!”
Binti akazidi kushangaa.
“Lakini Mista, ni nini hicho ulichokuwa ukikisema hapo
mwanzo kuhusu kila kitu kimeharibika na kuwa hakuna
ushahidi tena…?” Binti alizidi kumdadisi.
“Kila kitu kimefutwa… sina jinsi wala
namna sasa…” “Ni nini hicho unachoongelea Mista Moch…”
“No… kuna njia moja tu iliyobaki! Moja tu na si vinginevyo...” Grayson alijisemea mwenyewe, akimsahau kabisa yule binti mawazoni mwake.
Sasa ule mshangao wa yule binti ukapanda daraja na kuwa taharuki. “Ni vitu gani hivyo vilivyofutwa… kwenye kompyuta yako, na vina umuhimu gani hata vikufanye uwe hivyo bosi?”
Grayson Mochiwa aliinuka ghafla na kuanza kutoka nje ya ile ofisi.
“Chukua ripoti hiyo na kusanya vitu vyako uondoke binti!
Haya mambo mengine hayakuhusu… achana nayo kabisa!”
Alimwambia kwa msisitizo huku akitoka nje ya ofisi ile.
Binti alibaki akiwa ameduwaa kwa muda, kisha akabetua
mabega yake na kutikisa kichwa kwa kuchanganyikiwa.
Alikusanya yale makaratasi aliyosukumiwa na Grayson na kurudi nayo mezani kwake. Akayaweka ndani ya mkoba
wake, na kurudia kufanya kazi zake akiwa ameketi nyuma ya kompyuta yake huku bado uso wake ukionekana kutatizwa sananahali iliyotokea mle ndani.
Grayson Mochiwa alisukuma mlango wa ofisi ya mkuu wa idara ya tehama na kumkuta msaidizi wa mkuu wa idara ile akiwa ameinamia kompyuta iliyokuwa mezani kwake, bila shaka akitengeneza kitu fulani ndani yake.
“Mafaili yangu yote yametoweka kwenye kompyuta zangu! What the fuck is going on? ” Alimuuliza kwa jazba bila ya hodi wala salamu.
Jamaa alimtazama kwa mashaka, akiona jinsi asivyo katika hali ya kawaida, macho yake yakiwa yamejaa shari isiyosemeka.
“Na… sijui ni vipi… unataka nikaicheki…?” Alimjibu kwa mashaka makubwa. Grayson alimtumbulia macho yenye ghadhabu.
“Uicheki mara ngapi? Si ni wewe ndiye uliyekuja kuniomba laptop yangu ili eti ukaiwekee programu mpya ya kuzuia virusi wewe?” Alimkoromea.
“Ndio… nilitumwa na bosi… na nilifanya hivyo kwa laptop za wafanyakazi wote mzee!” Kijana alijitetea.
“Na zaidi ya hiyo programu, kwenye laptop yangu ukaamua kufuta kumbukumbu zangu. Sio? Ndivyo ulivyoelekezwa?”
“Ha... hapana bosi Grayson… kwanza mi’ laptop yako
sikuishughulikia kabisa! Niliichukua tu kwako na nikampa bosi William… laptop zote za wakuu wa idara alizishughulikia yeye!” Kijana alijitetea.
“Alaa! Haya, yu wapi huyo mkuu wako wa kazi?”
“Ku… kwenye kikao cha wakuu wa idara huko juu…”
Jamaa alimjibu huku akioneshea kwa kidole chake juu ya dari.
Grayson Mochiwa aligeuka na kutoka kwa mwendo wa haraka nje ya ofisi ile. Alienda hadi mwisho wa ile korido ndefu ambako kulikuwa kuna ngazi fupi zilizomfikisha kwenye ghorofa ya nane ya jengo lile, ambako kulikuwa kuna ofisi ya mwenyekiti mtendaji wa kampuni na ukumbi wa mikutano.Alisukumamlangompanawakioowaukumbi ulewamikutano na kuingia ndani.
Watu watano waliokuwa wameketi kuizunguka meza kubwa ya mikutano iliyokuwa mle ndani walishituka na kumgeukia kwa hamaniko.
“Grayson…!?” Mwenyekiti mtendaji wa kampuni ile aliyekuwa ameketi mwanzo wa meza ile akitazama moja kwa moja kulemlangonihukuakiwa ameligeuzia mgongo dirisha pana la kioo lililokuwa nyuma yake, alitamka kwa mshituko, lakini hakuweza kupata neno zaidi. Alibaki akimkodolea macho ya mshangao yule mtu, kama jinsi wenzake wanne walivyokuwa.
Grayson Mochiwa aliwatazama wale watu mmoja baada ya mwingine, na kutuliza macho yake kwa mkuu wa idara ya teknolojia ya habari na mawasiliano ya kampuni ile.
“Mafaili yangu yote yamefutwa kutoka kwenye kompyuta
yangu ya hapa ofisini, na pia kwenye laptop yangu… what the fuck’s going on Bill?” Grayson alimuuliza kwa ukali, akichanganya kiingereza kilichomaanisha kuwa anataka kujua ni upuuzi gani uliokuwa ukiendelea.
William ‘Bill’ Maginga, mkuu wa idara inayohusika na masuala yote ya kompyuta na mawasiliano katika kampuni ile alimeza funda la mate na kupitisha ulimi kwenye
midomo yake huku akimtazama Grayson kwa mashaka.
“Hebu tulia kwanza Grayson…” Luis Kambesera, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ile alisema huku akisimama kutoka kwenye kiti chake.
“Shut the fuck up, Luis and sit-the-gaddem down, wewe!
Naongea na Bill kwanza, kisha n’tarejea kwako muda si mrefu kama hutojali!” Grayson alimkemea mwajiri wake huku akimnyooshea kidole chenye kutetema, akimaanisha kuwa afunge mdomo wake na akae kitini.
Bila kujali miguno ya mshangao iliyosikika mle ndani, Grayson alimgeukia tena yule mkuu wa idara ya tehama wakati Luis Kambesera akiketi kitini kwa kutoamini kile kilichokuwa kimetokea.
“Umefuta mafaili yangu yote kwenye kompyuta zangu… why?”
“Si… sijui unaongelea nini Grayson, na… na kama kuna some small computer glitch somewhere tunaweza kurekebisha mara moja tu, na…”
Grayson aliachia kicheko cha kebehi na kutikisa kichwa.
“Eti some small computer glitch somewhere…” Alisema kwa masikitiko, na kuendelea, “… yaani we’ unadhani kila mtu
ni mbumbumbu isipokuwa wewe tu na hivyo vijilugha vyako vya kikompyuta kompyuta, sio?”
Wote waliokuwa mle ndani walibaki wakimtazama kwa mshangao, woga na kutoamini.
“Unaita kufuta kumbukumbu zangu zote kutoka kwenye kompyuta zangu ni some small computer glitch? Kwamba ni kijitatizo kidogo tu cha kikompyuta? Are you serious? Haya, na email zangu pia siwezi kuzifungua… yaani password yangu
mwenyewe leo imekuwa ni batili! Najaribu kubadili password
ili nifungue email zangu, nalo pia linakuwa ni tatizo… eti jina langu halitambuliki! Can you believe that? Huo kama si mkono wako Bill, ni wa nani tena? Halafu unaniambia eti
(akabana pua kwa vidole vya mkono wake huku akimuigiza Bill namna anavyoongea) ni some small computer glitch… (akaacha
kuibana pua yake) wewe! Au unadhani na huu ubongo wangu wenye PhD nao una ‘some small brain glitch’, eenh?”
“Grayson!” Luis Kambesera alimfokea.
“Nimekwambia shut up Luis! Namalizana na huyu kibaraka wako kwanza, kisha n’tarudi kwako, usiniharakishe! Najua
hii ni njama yenu nyote humu ndani. Huyu mjinga hawezi
kufanya hayo aliyoyafanya kwenye kompyuta zangu bila
kupata maelekezo kutoka kwako!”
“Ni nini unachoongea lakini Grayson? Mbona
hatukuelewi…?” Suleiman Mwangi, mwanasheria wa kampunialiyekuwakimyamudawote alidakia.
“Eti jamani… kwani tatizo ni nini Grayson? Umekuja
hapa mchafu mchafu tu, halafu unatoa shutuma
zisizoeleweka… unamkosea adabu hata CEO wetu hapa…
ni nini yote hii?” Jamilla Mchebe, mkurugenzi wa fedha wa kampuni naye alidakia.
Macho mekundu ya Grayson yakamgeukia yule
mwanamama, na ghadhabu aliyoiona kwenye macho yale
ilimfanya yule mwanamama anywee wazi wazi pale kitini
alipokuwa amekaa.
Grayson akahamishia macho yake yenye ghadhabu kwa
mtuwamwisho mle ndani.
“Na wewe pia unataka kujitia huelewi kinachoendelea?”
Alimuulizakwa jazba.
Badala ya kumjibu, Mike Mwangati, meneja uzalishaji wa kampuni ile, alibetua mabega tu na kuendelea kumtazama
bila ya kumjibu. Grayson alimgeukia mkuu wa kitengo cha tehama.
“Okay... n’tarudi kwako baada ya muda mfupi sana Bill, kwanza nataka niwatoe ujinga baadhi ya watu humu ndani
ambao wanajifanya hawaelewi kwa nini leo niko hivi… yote
hiyo ni pamoja na shukrani za dhati kwa mafanikio yako
katika kunifutia kumbukumbu zote nilizokusanya kwenye
kompyuta zangu. Kumbukumbu ambazo zingeweza
kufumua hujuma kubwa ambayo hii kampuni yetu
inayopaswa iwe adhimu inayoifanya dhidi ya nchi yetu… na
nyinyi nyote mkiwa washiriki wakuu!”
“Khah!”
“What?”
“Eti nini…?”
Macho yaliwatembea wale wakuu wa vitengo muhimu
vya kampuni ile waliokuwa mle ndani, wakati mkurugenzi
mtendaji Luis Kambesera akibaki akimtazama Grayson kwa ghadhabu bila kutia neno.
“Mnajitia kushangaa? Poleni sana kwa kulazimika
kujidanganya wenyewe kwa sababu mimi hamnidanganyi.
Nyote mko pamoja katika hili, na mmefikia hapo kutokana na kazi nzuri ya kitengo changu. Lakini sasa ni wazi kwangu kuwa ingawa tulikuwa kwenye safari moja, nia yetu haikuwa moja…” Grayson aliwapasha.
“Grayson kuwa makini na maneno yako… yanaweza
kukutia hatiani bila kujijua…” SuleimanMwangi
alimwambiahukuakimnyooshea kidole. “Tena naomba uache kabisa kutushutumu kwa mambo yasiyokuwepo
Grayson, tafadhali sana!” Jamilla naye alimjia juu.
Grayson aliachia tabasamu la upande mmoja, kisha
akauliza huku akiwatembezea macho wote mle ndani.
“Kama hii sio hujuma, kwa nini mimi sikuwa na taarifa ya kikao hiki? Vikao vyote lazima wakuu wote wa vitengo
tushiriki, how come mimi sikupewa taarifa ya kikao hiki?”
Macho ya wote mle ndani yakamgeukia mkurugenzi
mtendaji Luis, ambaye bado alikuwa ameketi kitini kwake
akimtazama Grayson kwa hasira.
“Kwa nini sikuitwa?” Grayson aliuliza tena, na alipozidi
kukumbana na ukimya, akajitolea kutoa jawabu, “Kwa
sababu mlijua kuwa hayo mnayotaka kuyapitisha
nisingekubaliana nayo, si ndivyo?”
Kimya kiliendelea kumshambulia kutoka kwa wale
wenzake mle ndani.
Hilo halikumkatisha tamaa, akaendelea kutoa hoja zake.
“Okay, si tatizo. Basi sasa mi’ n’tajifanya kuwa naamini
kwamba hamjui kinachoendelea, na hivyo n’tawaeleza kila
kitu mnachotaka kukifanya nyuma ya mgongo wangu, na
jinsi ilivyowalazimu kumtuma huyu fala hapa ahakikishe
kuwa anafuta kumbukumbu zote nilizohifadhi kwenye
kompyuta zangu…” Aliwaambia huku akimwoneshea Bill
kwa kichwa chake, na akiingiza mkono wake wa kushoto
kwenye mfuko wa koti lake.
“Hatuna muda wa kusikiliza upuuzi wako! Kuanzia sasa
kazi huna! Hiki kikao kimeahirishwa mpaka muda
kitakapotangazwa tena!” Luis Kambesera alimkemea kwa
ukali huku akiinuka na kuanza kukusanya mafaili yake
kutoka pale mezani, wale wenzake nao haraka wakianza
kufanya hivyo hivyo.
Ghafla mkono wa kushoto wa Grayson ulichomoka kutoka kwenye
mfuko wa koti lake ukiwa umekamata bastola.
“Hatoki mtu humu ndani! Kikao ndio kwanza kinaanza
wananchi, na mimi ndiye nitakayekiongoza!”
Hah!
Taharuki ilitanda mle ndani. Jamilla Mchebe aliachia kilio
cha woga alipoiona ile bastola mkononi mwa Grayson, na
BillMaginga alipaliwa na mate ghafla.
“Grayson una wazimu? Au umelewa wewe?” Luis alimkemea kwa hasira, na Grayson akamcheka.
“Wote wanaosikia harufu ya pombe au bangi kutoka
kinywani mwangu mikono juu, tafadhali!” Grayson alisema
huku akiwaelekezea ile bastola wale wakurugenzi
aliowadhibiti mle ndani, na baadhi yao wakanywea kwa woga, wakiikodolea macho ile bastola.
“Hakuna? Good! ” Grayson alisema na kumgeukia mkurugenzi mtendaji wa kampuni ile. “Wananchi wamegundua kuwa sijalewa Luis… kwa hiyo hapa nina akili timamu, jambo linalokufanya wewe uwe mwongo uliyekubuhu pale ulipowaambia kuwa eti mi’ nimelewa!”
Mdomo ukamuanguka Luis, pua zikamtanuka na macho yakamuiva. “Unataka nini wewe lakini?” Mike Mwangati, meneja uzalishaji wa kampuni ile alisaili. Grayson akamtupia jicho kali, kisha bila ya kumjibu akamgeukia Luis Kambesera.
“Una lolote la kunieleza Luis juu ya hali hii?” “Juu ya nini wewe?” Luis alimbwatia kwa hasira.
“Juu yakwaninisijaitwakwenyekikaohikikamamkuuwa idaramuhimu kabisa kwenye kampuni hii… na zaidi ya hapo… unanieleza nini kuhusu hujuma mnayoiendesha dhidi ya taifa hili?” Grayson naye akambwatia, akiwa amemlenga bastola kifuani.
Akiwa ameketi upande wa pili wa meza ile akitazamana na Luis, huku wawili kati ya wale wakurugenzi wengine wa kampuni ile wakiwa kulia kwake pale mezani, na wawili
wengine wakiwa kushoto kwake pale mezani, Grayson
Mochiwa hakuweza kuuona mkono wa Luis ukienda chini
ya meza ile kwa uficho mkubwa wakati akimjibu.
“
Yah, Grayson… ninalo la kusema juu ya hayo…”
Alimjibu, na wote mle ndani wakaachia miguno ya
mshangao.
“Okay… nakusikiliza Luis…!” Grayson alimwambia huku
akimtazama kwa macho yaliyojaa ghadhabu.
Mkono wa Luis ukabonyeza kitufe maalum kilichowekwa usawa wa kiti chake chini ya meza ile, na kwenye chumba
kimoja kilichokuwa kwenye ghorofa za chini za jengo lile, kengele ya hatari ikaanza kugonga.
Mrindimo wa kengele iliyobonyezwa na Luis Kambesera ulivuma kwenye chumba cha ofisi ya usalama wa kampuni
ile. Mkuu wa usalama wa kampuni ile kubwa yenye ubia na kampuni nyingine kubwa kabisa ya nishati yenye makao
yake makuu Afrika ya Kusini alimakinika haraka sana na kengele ile. Alinyakua simu yake ya kiganjani na kubofya
kitufe kimoja tu na simu ile ikaanza kuita. Iliita miito miwili tu kabla sauti nzito haijamuitika.
“Yes,Boss?”
“Kuna tatizo ghorofa ya nane… nenda haraka!” Mkuu wa usalama wa kampuni alibwaka kwenye ile simu huku
akibofya bofya kwenye kompyuta iliyounganishwa kwenye
kioo kikubwa sana cha runinga ambayo ilikuwa
imegawanywa katika vichumba mbali mbali vilivyokuwa
vikionesha kila kilichokuwa kikitokea ndani ya ofisi
mbalimbali za kampuni ile, isipokuwa yale yaliyokuwa
yakitokea kule kwenye kile chumba cha mikutano kule ghorofa ya nane.
“Tatizo la aina gani?” Sauti nzito ilisaili, na mkuu wa usalama akasonya.
“Bado sijajua ila kengele imelia… nenda upesi
sana wewe!” Alibwaka tena kwenye simu na yule mtu mwenyesautinzitoaligunanakukatasimu.
Na hata pale alipokuwa akibofya bofya namna ile huku akiongea na yule mtu mwenye sauti nzito, kichumba kingine kilichokuwa kiza muda wote pale kwenye ile runinga kubwa kilicheza na picha ya kilichokuwa kikiendelea kule kwenye kile chumba cha mikutano ilionekana, nayeakaachia mguno wa hamaniko. Aliinua simu nyingine na kupiga kituo cha polisi, kisha akabonyeza kitufe cha kengele ya matatizo ambayo ilisikika kwa wafanyakazi wote waliokuwa kwenye ghorofa ya saba ambamo ndimo ofisi za ile kampuni zilikuwamo.
Akachukua kisemeo ambacho kiliwezesha sauti yake
kusikika na wafanyakazi wote waliokuwa kwenye ofisi zile
kupitia kwenye spika zilizokuwa zimetawanywa kwenye
kona mbali mbali za ofisi zile.
“Kuna hatari jengoni! Kuna hatari jengoni! Wafanyakazi
wote kusanyeni vitu vyenu na mtoke nje haraka sana lakini
bila papara… tokeni nje ya jengo haraka sana lakini bila papara… fanyeni hivyo sasa hivi… narudia tena…”
Alirudia tangazo hilo mara tatu huku macho yake yakiwa
yameganda kwenye kile kilichokuwa kikitokea kule kwenye
chumba cha mikutano, ghorofa ya nane.
Baada ya hapo aligeuka na kuuendea mlango kwa kasi.
Mlangoni aligeuka na kuitupia jicho jingine ile runinga,
kisha akachomoka mbio kutoka nje ya ile ofisi yake, akipeleka mkono wake kiunoni kujihakikishia kuwa alikuwa
amebeba bastola yake iliyokuwa kwenye mkoba maalum
uliopachikwa kiunoni kwake kwa nyuma na kufunikwa kwa
koti la suti yake nyeusi.
Bastola yake ilikuwepo.
Kule kwenye chumba cha mikutano hali ilizidi kuwa tete.
“Nasema kwamba unaweza kuwa hujalewa Grayson, lakini kwa hakika una wazimu wewe… hakuna ukweli
wowote katika hayo uyasemayo. Ni hiyo akili yako tu iliyofyatuka…” Luis alianza kumjibu kwa kiburi lakini hapo
ndipo alipoishia.
Mlipuko mkubwa wa bastola ulirindima mle ndani na wote wakaruka kwa woga huku wakipiga kelele, wakati
risasi kutoka kwenye ile bastola ikijikita ukutani, sentimeta
chache kutoka kwenye lile dirisha pana la kioo lililotoa
mandhari ya majengo yaliyokuwa nje ya chumba kile cha mikutano kutokea kule ghorofani.
“WACHA KUCHEZEA AKILI YANGU, WEWE!”
Grayson alibwata kwa hasira huku akiinuka kutoka kwenye
kiti na kumnyooshea Luis ile bastola kwa mkono uliokuwa
ukimtetemeka vibaya sana.
Taharuki ilizidi kutawala mle ndani.
Wale wakurugenzi waliowekwa kiti moto na Grayson sasa
walikuwa wamehamanika vibaya sana. Kila mmoja akijaribu
kumsemesha Grayson maneno ya kumrai atulize jazba na aweke bastola pembeni. Grayson sasa alikuwa
amehamishia akili yake kwa Luis Kambesera aliyetulia kitini
kwake huku akitweta kwa mchecheto usio semeka.
“Luis usinifanye mjinga! Mimi nimefanya utafiti wa kina
katika maeneo husika kule mikoa ya kusini kama jinsi ambavyo kampuni ilivyokubaliana na serikali… na nikawasilisha ripoti yangu kwako kama jinsi ambavyo matokeo ya utafiti wangu na wa timu yangu yalivyoonesha, na ilivyotakiwa! Sasa tena ilikuwaje ile ripoti yangu
ikageuzwa na kuwekwa ndivyo sivyo, eenh?” Alimfokea, na Luis alijaribu kufunua kinywa kumjibu lakini hakuna
kilichotoka kinywani mwake.
Muda wote yule mkurugenzi wa fedha Jamilla Mchebe
alikuwa akilia kwa maombolezo, na vilio vyake vilimkera Grayson.
“Hebu kelele na wewe malaya hapo, ebbo!” Alimgeukia na kumfokea huku akimnyooshea bastola, na yule mwanamke alilia kwa sauti zaidi huku akijiinamisha chini ya meza kwa woga.
Grayson akamgeukia tena Luis, na kumkuta akipeleka
mkono wake kwenye mfuko wa ndani wa koti lake.
“Tulia hivyo hivyo, Luis!” Grayson alimkemea, na Luis akabaki akimkodolea macho ya woga huku mkono wake wa kulia ukiwaumezama ndani koti lake.
“Unataka kufanya nini wewe, eenh?” Grayson Mochiwa
alimuuliza kwa hasira huku akimsogelea akiwa amemnyooshea bastola.
“Nothing, man!” Luis alimjibu huku akitetemeka, akimaanisha kuwa hakuwa akifanya lolote. Grayson
alimuwekea bastola kichwani na Luis akafumba macho kwa
woga. Huku bado akiwa amemuwekea ile bastola kichwani, Grayson alimzunguka na kusimama nyuma ya kiti
alichokalia ili aweze kuwaona na wale wakurugenzi wengine.
Akiwa amemsimamia Luis nyuma yake namna ile, alimwamuru autoe ule mkono kutoka ndani ya koti na auweke juu ya meza.
Na ni hapo, kwa kuwa sasa alikuwa amesimama mgongoni
kwa Luis na uso wake umeelekea kule mlangoni ambako awali alikuwa amepageuzia mgongo, ndipo kupitia kwenye
mlango wa kioo wa chumba kile cha mikutano, alipomuona mtu mwingine akitokeza mbio kwenye korido ya kuelekea
pale kwenye kile chumba cha mikutano.
Alikuwa ni mtu mrefu mwenye mwili mpana na kichwa
kidogo, na mara moja alimtambua kwani alikuwa ni mmoja
wawatendajiwaofisiyausalama ya kampuni ile, na Grayson alisita. Alijua kuwa hakuwa ameukomea kwa ndani ule
mlango. Alitaka kutimua mbio kuwahi kuukomea ili yule
mtu asiweze kuingia mle ndani lakini akaona kuwa umbali
ule ulikuwa mrefu sana, na hakujua Luis atachukua hatua
gani pindi akimgeuzia mgongo kuuwahi ule mlango…
*
KULE GHOROFA YA saba taharuki ilikuwa imetawala.
Wafanyakazi wote walikuwa wakitoka nje ya ofisi zile haraka haraka, wakiwa wamekusanya vitu vyao binafsi.
Binti aliyekuwa akifanya kazi chini ya usimamizi wa Grayson Mochiwa alichanganyikiwa kuona wale wafanyakazi wakitoka nje namna ile, ingawa hata yeye alilisikia lile tangazo la kuwataka watoke nje ya ofisi haraka bila papara.
Sasa huo ndio mwendo gani?
Yeye alikuwa ni mwanafunzi tu aliyepokelewa kwenye ile kampuni kufanya mafunzo kwa vitendo, yaani ‘field attachment’, na kuwekwa chini ya usimamizi wa Grayson Mochiwa. Hakuwa amewahi kufanya kazi popote kabla ya hapo, na hivyo yale mambo yalikuwa mageni sana kwake. Badala ya kutoka nje kama wale wafanyakazi, yeye alikuwa akihangaika kujaribu kumpigia simu Grayson kwa kutumia simu yake ya kiganjani ili ajue alipo na ikiwezekana amngojee watoke wote nje ya jengo lile.
“He! We binti! Twende nje haraka usizubae tena hapa, ala!” Yule binti wa mapokezi aliingia pale ofisini na kumwambia kwa wahka, na bila ya kusubiri iwapo yule msichana atafanya vile alivyomwambia au la, aligeuka na kutoka mbio nje ya ile ofisi.
Binti naye akakurupuka na kutoka mbio nje ya ofisi ile. Mlangoni
akaukumbuka mkoba wake, hivyo akarudi mbio mle ofisini na kuunyakua
kutoka juu ya meza alipouacha, lakini katika kiherehere chake, akauangusha
nao ukaangukia upande wa pili wa meza yake, chini ya kiti. Aliachia mguno wa hamaniko huku akizunguka upande wa pili wa ile meza, akasukuma kiti pembeni na kuinama chini ya meza yake ili auokote, na hapo akaona
kuwa kichupa chake cha losheni kilitoka nje ya mkoba ule na kusererekea
17 Hussein Issa Tuwa
2
mbali zaidi chini ya ile meza.
“
Oh, shit!” Alilaani na kujiingiza chini zaidi ya ile meza ili akichukue
kile kichupa, na hapo alishitushwa na kishindo kikubwa kutokea kwenye mlango wa kuingilia pale kwenye ile ofisi yake ndogo iliyokuwa mbele ya ile ofisi ya Grayson Mochiwa.
Alikuwa anataka kutoka kule chini ya meza kuangalia kulikoni wakati alipoona miguu ya mtu ikipita kwa mwendo wa mbio mbele ya meza yake, ikikimbilia kule ofisini kwa Grayson Mochiwa.
Alijibanza kule kule chini ya meza, na kupitia kwenye ule uwazi wa kioo ulioitenganisha ofisi yake na ile ya Grayson, alimuona yule mkuu wa usalama ambaye yeye hakumjua kama ni mkuu wa usalama wa kampuni ile, akiipekua kwa pupa ile meza ya Grayson. Alimuona na alimsikia akivuta na kuyabamiza madroo ya ile meza kwa namna ya kutafuta kitu kwa uharaka wa hali ya juu. Akamuona akipekua baadhi ya makabrasha yaliyokuwa pale mezani kwa vurugu na kiherehere kama anayetafuta kitu ambacho hajui kilipo.
Akh! Ni nini kinaendelea hapa?
Binti hakuelewa, na hata pale lile wazo lilipokuwa likipita kichwani mwake, alimuona yule mtu akiisukuma pembeni meza ya Grayson, naye akiinama chini yake labda kutafuta chochote alichokuwa akikitafuta chini ya meza ile.
Mnh! Hapa kuna kitu hakipo sawa hapa!
Binti aliwaza na kukurupuka kutoka kule chini ya meza, akijigonga kichwa chake kwenye ile meza na kujikuta akikisukuma pembeni na kukiangusha kiti kilichokuwa mbele ya meza ile. Hakujali.
Alichomoka kutoka kule chini ya meza na kuanza kuuendea mbio mlango wa kutokea, purukushani yake ile ikimshitua yule mkuu wa usalama aliyekuwa kule ofisini kwa Grayson.
“We!” Jamaa aliita huku akitoka mbio kule ofisini kwa Grayson, bila ya kujijua mkono wake ukichomoa bastola iliyokuwa kiunoni mwake. Binti alishtuka na kusimama huku akigeuka kumtazama yule jamaa na akaogopa vibaya sana alipoiona ile bastola iliyokuwa mkononi mwa yule jamaa.
“We’ ulikuwa unafanya nin…” Jamaa alianza kumuuliza, na binti akageuza na kutoka mbio nje ya ofisi ile, woga mkubwa ukimtawala.
Jamaa ana bastola, kudadadeki!
“Kuja hapa wewe!” Jamaa alimwita huku akimkimbilia, lakini binti
18 MTAFITI
alishatoka nje ya ile ofisi, ambako wafanyakazi wachache waliobakia
walikuwa wakielekea kwenye ngazi za kuteremka kwa miguu kutokea
kule ghorofani, wakifuata tararibu za kutotumia lifti wakati wa kujiokoa kwenye dharura kama zile.
Binti hakujali hayo.
Yeye aliitimkia mbio lifti iliyokuwa kwenye ghorofa ile na kubonyeza kitufe cha kuiita pale alipokuwa huku moyo ukimwenda mbio na machozi yakimchonyota.
Duh! Balaa gani hili sasa linaloniangukia Mwantumu miye, Ya Rabbi?
Kama vile lifti ilikuwa ikimngojea yeye, milango ilifunguka taratibu na kabla ya kuingia kwenye ile lifti, aligeuka kule alipotokea, na kumuona yule
jamaa akisukuma baadhi ya wafanyakazi waliozongana kwenye ile korido
huku akiwa ameinua shingo yake juu kutazama kule alipokuwa.
Macho yao yaligongana.
Binti akajitoma ndani ya lifti na kubonyeza kitufe cha kuiteremsha chini, na huku moyo wake ukicheza mdundiko ndani ya kifua chake, alibaki akiitazama milango ya ile lifti ikijifunga taratibu.
“Come on, Come on, come oooonnnn!” Aliisemesha milango ya ile lifti kuihimiza ifanye haraka kujifunga, huku yale machozi yaliyokuwa yakimchonyota hapo awali sasa yakimjaa machoni naye akijitahidi kuyarudisha huko yalipotokea.
Kabla ile milango haijajifunga vizuri, jamaa likaifikia ile lifti na kunyoosha mikono kuielekea ile milango na binti akaachia ukelele mkubwa wa woga, machozi yaliyokuwa yakimlenga sasa yakijipa uhuru kutoka machoni na kutiririkia mashavuni mwake.
Jamaa alichelewa kidogo sana na milango ikawahi kujibana, ikimuacha akajibamiza nje ya milango ya lifti ile. Lifti ikashuka kutoka kule juu, Mwantumu akijifuta machozi ndani yake, moyo ukimwenda mbio na woga usiosemeka ukimgubika.
Yule jamaa alikuwa na bastola!
Kwa nini…?
Kule ghorofa ya saba mkuu wa usalama hakupoteza muda. Aligeuka na kurudi mbio kuziendea zile ngazi za kushuka kwa miguu na kuanza kuzishuka kwa kasi, akitaka kuwahi chini kabla ya ile lifti. Aliwasukuma bila kujali wafanyakazi waliokuwa wakiziteremka ngazi zile, akilini akiwa na wazo hilo moja tu la msingi.
19 Hussein Issa Tuwa
Alipofika kule chini binti hakuwepo pale kwenye ukumbi wa mapokezi wa jengo lile. Jamaa akatoka nje ya jengo na kujaribu kumtafuta yule binti kwa kutazama huku na huko bila mafanikio. Hakushangaa, kwani alijua kuwa asingemkuta kwa kuwa yeye alishuka pale chini kwa ngazi kutokea ghorofa ya saba, wakati binti alitumia lifti.
Wafanyakazi wa ofisi yao walikuwa wamejirundika sehemu maalum ya kukusanyikia wakati wa dharura, na walikuwa wakiongea kwa sauti za chini miongoni mwao, wengine wakichekeshana kama kwamba hakukuwa na jambo la hatari lililokuwa likiendelea ndani ya jengo lile. Hakuna yeyote aliyejua kilichokuwa kikitokea kule juu, nao walidhani labda ilikuwa ni hitilafu ndogo tu ya umeme au labda kulikuwa kuna kitisho cha moto ambao hata hivyo hautakuwepo. Lakini vicheko vyao na fikra zao hizo zilibadilika pale walipoona kundi la askari wa jeshi la polisi wenye silaha likiingia ndani ya jengo lile kwa vishindo.
Mkuu wa usalama aliwaacha wale askari waende kule juu ambako tayari alishawaeleza kwenye simu kuwa kulikuwa kuna utekaji nyara unaoendelea kwenye ghorofa ya nane ya jengo lile. Alijihakikishia tena kuwa yule binti hakuwepo pale chini, kisha akaenda kufanya lile ambalo tangu pale alipomuona Grayson Mochiwa akiwa amewadhibiti kwa bastola wale viongozi wa juu wa kampuni ile, alijua kuwa alitakiwa alifanye.
Alivuka barabara kwa mwendo wa haraka na kuingia kwenye jengo jingine lililokuwa likitazamana na lile ambalo ofisi za kampuni yao zilikuwemo…
Lifti ilipofungua milango yake na kumshusha pale kwenye eneo la mapokezi la jengo lile, Mwantumu alitoka kwa mwendo wa haraka na kuongoza nje kabisa ya jengo lile la ghorofa kumi jijini. Alisimama kidogo nje ya lile jengo, akabandika miwani yake ya jua usoni na kuvaa kofia yake ya kepu, kisha akapotelea ubavuni mwa jengo lile. Aliibukia mtaa wa nyuma ya jengo lile na kuparamia moja ya bajaji zilizokuwa zikisubiri abiria pale barabarani, hali akiwa mwingi wa wahka.
“Wapi sista duu?” Mwenye bajaji alimuuliza huku akimchekea na akiiwasha bajaji yake.
Katika mazingira ya kawaida, kitendo cha yule jamaa kumwita “Sista
20
MTAFITI
duu” kingemzawadia jibu ambalo lingemfanya atahayari siku nzima, lakini ile haikuwa asubuhi ya kawaida na Mwantumu hakuwa katika ari ya kawaida kabisa.
“Mwananyamala!” Alimjibu bila kufikiri, hasa ikizingatiwa kuwa yeye alikuwa amepanga chumba maeneo ya Chang’ombe usalama.
Akili ilikuwa ikimzunguka kwa kasi sana. Alikumbuka kila alichokishuhudia kutoka kwa Grayson Mochiwa asubuhi ile, na hakuna hata kimoja katika yale aliyoyashuhudia kilichomletea amani moyoni mwake. Akakumbuka jinsi yule mtu alivyokuwa akipekuwa kwa pupa pale mezani kwa Grayson, na jinsi alivyomtoa kasi huku akiwa na bastola mkononi, na kwa mara nyingine akajithibitishia kuwa hakika mambo aliyoyashuhudia Liquid Diamond Incorporated asubuhi ile hayakuwa ya amani hata kidogo.
Sasa ni kwa nini?
Mwantumu hakuwa mtu wa kupenda rabsha rabsha hata kidogo, na labda ndio sababu hakuwa na marafiki wengi… kiukweli hakuwa na marafiki kabisa!
Isipokuwa mmoja tu.
Na ndiye huyo ambaye alijikuta akielekea kwake muda ule bila hata ya kufikiri.
Zay.
Rafiki yake na msiri wake mkubwa au labda ni sahihi zaidi angesema kuwa yeye ndiye aliyekuwa msiri mkubwa wa Zay. Lakini pia Zay alikuwa ndiye mtu pekee anayemuelewa na kumkubali kwa jinsi alivyo, na kwa
Mwantumu kukubalika na kueleweka vilikuwa ni vitu muhimu sana. Huwa hapendi kabisa watu kushindwa kumuelewa, na ilishamfunukia zamani
sana kuwa karibu kila mtu aliyewahi kukutana naye alikuwa hamuelewi...
Isipokuwa Zay.
Alitoa simu yake ya kiganjani kutoka mkobani mwake na kumpigia.
Simu yake ilikuwa ikiita tu bila majibu.
Shit!
Kule kwenye chumba cha mikutano Grayson akaamua kubaki pale pale
alipokuwa, akiwa amemuwekea Mkurugenzi Mtendaji Luis Kambesera
21
Issa Tuwa
Hussein
bastola kichwani na akitazama kule mlangoni kwa wahka.
Yule mtu mrefu mwenye mwili mpana na kichwa kidogo aliusukuma ule mlango wa chumba cha mikutano na kusimama hatua chache ndani ya chumba kile, akiuacha wazi makusudi mlango ule huku yeye akiwa makini sana. Alishaona kilichokuwa kikiendelea mle ndani tangu akiwa nje ya ule mlango wa kioo, na hivyo bila hata ya kuambiwa akainua mikono yake juu, viganja vyake vikiwa wazi mbele yake ili Grayson aone kuwa hakuwa na silaha yoyote.
“Okay Mista Mochiwa… hebu tulia kwanza tuyazungumze haya mambo…” Jamaa alisema taratibu huku akimtazama Grayson kwa macho yake madogo na makali yaliyojaa umakini.
“Nadhani wewe ndiye unayetakiwa utulie Bilanga!” Grayson alimfokea huku bado akiwa amemkwida Luis.
“Sijui mmekosana nini na wenzako hapo…” Yule mtu mrefu aliyetambulika kwa jina moja tu la Bilanga alianza kumwambia, lakini
Grayson akamkatisha.
“Hawa waliacha kuwa wenzangu pale walipoamua kunizunguka kwa matamanio yao ya kifisadi! Hawa ni wasaliti na mafisadi tu, sio wenzangu!
Nami n’tawaumbua kwa kuwaweka wazi mbele ya jamii pumbavu zao!”
Grayson alimaka.
“Mpumbavu mama’ako wewe, fala nini?” Mike Mwangati, meneja uzalishaji wa kampuni ile alimkemea kwa hasira.
“Shut up, Mwangati! N’takuwasha sasa hivi!” Grayson alimjia juu, na Mike Mwangati akabaki akimtumbulia macho yenye ghadhabu.
“Okay jamani sote tutulie na tulitazame hili suala kwa utulivu. Sawa?”
Bilanga alijaribu kuongea tena huku akiisogelea ile meza taratibu.
“Tulia hapo hapo!” Grayson alimkoromea, naye akasita.
“Okay… nimetulia.” Bilanga alisimama na kusema, kisha akaendelea, “Sasa unadhani ufanyalo ni sahihi, mista Mochiwa?”
“Nakujua sana wewe! Wewe ni mtu wa usalama wa kampuni, wewe na hawa wote lenu moja… toa bastola yako na uiweke sakafuni pole pole sana!” Grayson alimkoromea, lakini sasa sauti yake ilisikika ikitetema. Woga wa kile ambacho alikuwa akikifanya bila shaka ukianza kumuingia.
“Sina bastola yoyote mimi… ni wewe ndiye mwenye bastola hapo. Unaonaje ukiiweka chini halafu tukaongea?” Bilanga alimuuliza, macho yake yakienda kwa Luis kidogo, wakatazamana, akatikisa kichwa kidogo
22
MTAFITI
sana, halafu akayarudisha macho yale kwa Grayson.
“Wacha kucheza na akili yangu wewe! Najua kuwa una bastola na umekuja hapa kujaribu kunidhibiti ili uwaokoe hawa mabwana zako hapa…” Grayson alifoka, akamtupia jicho Jamilla, kisha akaongezea, “… na bibi yako hapa pia! Sasa huna namna, nimewadhibiti wao na wewe vile vile… toa bastola yako sasa hivi!”
Bilanga akauma meno na macho yake yakajifinya kwa hasira.
“Nimekwambia sina bastola!” Alimsisitizia, na Grayson akasonya.
“Unayo! Fanya nikwambiavyo wewe, ama sivyo …”
“Ama sivyo nini? Njoo uichukue basi hiyo bastola kama una hakika na ulisemalo!” Bilanga alimwambia kwa hasira, macho yake yakionesha kuwa alikuwa anamtamani sana… tena si kwa mema.
“Okay jamani, basi tuacheni sisi wengine twende zetu… tuna watoto majumbani!” Jamilla Mchebe aliropoka kwa wahka.
“Hebu nyamaza wewe! Ulipokuwa unashiriki kwenye huo ufisadi uliokufikisha hapo ulipo hukujua kuwa una watoto?” Grayson alimjia juu.
“Nani fisadi wewe lakini?” Luis alimkoromea kutoka pale kwenye kiti alipokwidwa, na Grayson akamdidimizia zaidi ile bastola kichwani.
“Nyote humu ni mafisadi, na wewe ndio kiongozi wao! Sasa nataka uanze kusema mwenyewe ni vipi ile ripoti yangu ikachakachuliwa namna ilivyochakachuliwa, wakati unajua kabisa kuwa nilikukabidhi ripoti ambayo…” Grayson alianza kumpasha.
“Polisi wataingia hapa muda si mrefu Grayson, na wakifika hutakuwa na namna ya kuiepuka jinai kaka. Bora uweke chini hiyo bastola ili wakifika wasikukute na kidhibiti mkononi!” Bilanga alimwambia Grayson.
Na hata pale alipokuwa akisema maneno yale, wote mle ndani walisikia vishindo vikubwa vikitokea nje ya chumba kile.
Kutokea pale alipokuwa, Bilanga alipiga magoti huku akiinua mikono yake na kujishika kichwa, akimtazama Grayson kwa macho ya kubeza.
“Manjagu nd’o wanakuja hao Grayson… tupa bastola now, au usubiri ukutwe ukiwa na kidhibiti mkononi!” Alimwambia kwa kitisho.
Macho yalimtembea kwa woga Grayson na hakujua achukue hatua gani. Na hata pale alipokuwa akihangaika na nafsi yake juu ya uamuzi gani achukue, kundi la askari wa jeshi la polisi sita wenye silaha lilifika kwa vishindo kwenye korido iliyokuwa nje ya kile chumba cha mikutano, na kwa kupitia kwenye ule mlango wa kioo ambao hata hivyo ulishaachwa
23 Hussein Issa Tuwa
wazi na Bilanga, wale askari waliweza kuona kilichokuwa kikitokea mle ndani na kumakinika vilivyo.
Walimnyooshea Grayson bunduki zao ilhali wakijipanga pale mlangoni kimakabiliano huku wakimpigia kelele za mfululizo kutoka kila upande kuwa ajisalimishe.
“Tupa silaha chini wewe!”
“Uko chini ya ulinzi!”
“Kaa chini!”
“Muache huyo raia mara moja, jambazi!” Grayson alihamanika.
Alizidi kumkwida na kumdidimizia bastola Luis.
“Sio jambazi! Sio jambazi mimi!” Alipiga kelele, lakini hakuna aliyemsikia.
“Msaada wana usalama… msaada! Anataka kuniua!!” Luis naye alipayuka kwa kelele, akitaka kuikoroga zaidi hali ile.
“Mwongo! Fisadi mkubwa huyu…” Grayson naye alipayuka.
Muda wote huo Bilanga alikuwa amepiga magoti akiwa amejishika kichwa na akimtazama Grayson kwa makini, jambo ambalo moja kwa moja liliwathibitishia wale polisi kuwa Grayson alikuwa amewateka watu wote mle ndani kwa mtutu wa bunduki.
“Simwachi huyu mpaka mnisikilize!” Grayson alibwata, sauti yake ikivunjikia njiani na kilio chepesi kikimchomoka.
“Hatujadiliani na watekaji sisi wewe, ebbo! Tupa silaha chini sasa hivi!” Kiongozi wa wale askari alimpigia kelele, na hapo hapo mwingine akamkemea.
“Halafu lala chini hapo hapo!”
Grayson Mochiwa alichanganyikiwa.
Mkuu wa usalama wa kampuni ya Liquid Diamond Inc. aliingia kwenye
jengo lililokuwa likitazamana na lile lililoihifadhi ile kampuni yao kwa mwendo wa kawaida na kuzama kwenye lifti pamoja na baadhi ya watu wengine, na kuteremkia ghorofa ya nane ya jengo lile.
Aliingia msalani pale ghorofa ya nane, na akiwa amejifungia kule msalani
alitoa glovu kutoka kwenye mfuko wa ndani wa koti lake na kuzivaa
mikononi mwake. Alitoka kule msalani na kwenda moja kwa moja hadi
24 MTAFITI
mbele ya mlango wa chumba kimoja miongoni mwa vyumba vya ofisi
kadhaa zilizokuwa kwenye ghorofa ile na kuufungua ule mlango kwa
kutumia kadi maalum ya kufungulia milango.
Alijifungia mle ndani kusimama hatua chache kutoka pale mlangoni na kutembeza macho yake mle ndani. Moja kwa moja mbele yake kulikuwa
kuna dirisha pana ambalo lilikuwa limefunikwa kwa pazia maalum za kiofisi. Katikati ya chumba kile kulikuwa kuna meza moja ikiwa na kiti cha kiofisi nyuma yake. Alienda hadi pale dirishani na kulisogeza pembeni lile pazia na kuchungulia nje. Kisha akageukia kule mlangoni alipotokea.
Kando ya ule mlango kulikuwa kuna picha moja kubwa sana ya mlima
Kilimanjaro iliyokuwa ikining’inia ukutani ikiwa kwenye fremu nzuri ya shaba nyekundu.
Alirudi haraka pale ukutani kando ya mlango na kuishusha ile picha kutoka ukutani na kuiweka sakafuni taratibu, akiisimamisha kwa
kuiegemeza ukutani. Alianza kuugongagonga ule ukuta kwenye ile sehemu ambayo awali ilikuwa imefunikwa na ile fremu, na mara sehemu ile ya ukuta ule wa mbao ikafunguka na kuacha uwazi. Aliingiza mkono wake
kwenye uwazi ule na kutoa bunduki kubwa yenye kiwambo cha kuzuia sauti iliyounganishwa na darubini kubwa.
Ilikuwa ni bunduki maalum kwa udunguaji kutokea mbali.
Aliikoki itakiwavyo ile bunduki na kurudi nayo hadi nyuma ya lile dirisha na kulifungua kidogo, akipenyeza mtutu wa ile bunduki kwenye ule uwazi na kuchungulia kule nje kwa kutumia ile darubini kali iliyomuwezesha kuona umbali mrefu kutoka pale alipokuwa.
Lile dirisha lilikuwa linatazamana moja kwa moja na lile dirisha pana la kile chumba cha mikutano kilichokuwa kwenye jengo lililokuwa upande wa pili wa barabara. Kupitia kwenye darubini ile, aliweza kumuona
Jamilla Mchebe akiwa amejiinamia pale mezani kule kwenye chumba cha mikutano. Aliizungusha ile darubini kwa kila aliyekuwemo mle ndani, na hatimaye kuituliza kisogoni kwa Grayson Mochiwa aliyekuwa amemkwida
Luis Kambesera…
Kule Liquid Diamond Grayson alikuwa kwenye wakati mgumu. Wale
askari walizidi kumzonga kwa mitutu ya bunduki zao kutokea kule
25 Hussein Issa Tuwa
mlangoni, ingawa sasa waliacha kumpigia kelele na badala yake walikuwa wakijaribu kumrai ili aweke ile bastola chini na ajisalimishe.
“Simuachi huyu! Laiti kama nyie mngejua hujuma alizolifanyia taifa hili huyu wala msingemtetea hapa!” Grayson alibwata, na hapo Luis akaingilia kati.
“Wewe mbaya wako si mimi, Grayson? Basi waache hawa wengine waende zao tubaki mimi, wewe na hawa wana usalama tu, eenh?”
Alimwambia kwa taabu akiwa bado amekwidwa pale kitini.
“Eti jamani!” Jamilla Mchebe alidakia, na hapo yule kiongozi wa wale askari naye akaongezea hoja.
“Ndio! Waache hawa raia wengine waende mzee…angalau itaonesha kuwa una nia nzuri…”
“Nia nzuri? Nia nzuri na mafisadi hawa?” Grayson alimtupia jicho lake lililoiva.
“Sasa unataka kuwafanyaje? Kuwaua wote?” Mmoja wa wale askari alimtupia swali, na Grayson akabaki akilitafakari swali lile kwa muda.
“Unajua hata hilo halitakuwa wazo baya, afande?” Hatimaye alisema kwa namna ya kupitisha maamuzi, na Jamilla akaachia mguno wa fadhaa.
“Acha ujinga mzee! Unajua kuwa hilo ufanyalo ni kosa kubwa sana la jinai…? Ni bora ujisalimishe!” Kiongozi wa wale askari alimwambia.
Grayson alimtazama kwa mashaka yule askari.
Alikuwa mrefu zaidi ya ule urefu wa wastani, mwili wake ulionekana kuwa umejengeka kikakamavu na hakuweza kuyaona macho yake kwani yalikuwa yamefichwa nyuma ya miwani myeusi iliyoonekana kuwa ni ghali na iliyomkaa vyema sana pale usoni kwake. Alikuwa amesimama kwa kujiamini hatua kama mbili kando ya Bilanga, miguu yake ikionekana kufanya matege kidogo ya kuingia ndani, kiasi akitembea ilileta picha ya magoti yake kutaka kugusana.
Grayson alimeza funda la mate.
“Ah! Sasa… yaani mimi ndio nijisalimishe, na hawa mafisadi waende nyumbani kwa watoto zao!” Grayson alimaka.
“Hilo la mafisadi sisi hatulijui! Tunalojua ni kwamba wewe umemuwekea huyo mtu hapo bastola kichwani…” Yule kiongozi wa wale askari alianza kumjibu.
“Fisadi! Huyu ni fisadi, sio mtu… nyie vipi?” Grayson alimkemea yule askari, na miguno ikazagaa mle ndani.
26 MTAFITI
“Okay, sawa! Sawa, fisadi… sisi tunaloona ni kuwa wewe umemuwekea huyo… fisadi… bastola kichwani, na kwetu hilo ni kosa! Weka bastola chini na ujisalimishe mzee. Labda baada ya hapo tutaweza kuwashughulikia hao mafisadi unaowasema!” Jamaa alimwambia kwa kubembeleza, na Grayson akamtolea macho.
“We’ unadhani mi’ ni mwehu sio?” Alimjia juu.
“Mi’ nadhani wewe ni mhalifu unayeendelea kutenda jinai hapo wewe! Tupa bastola chini au tunakuchabanga marisasi hapo hapo ulipo wewe, umesikia?” Yule kiongozi wa wale askari alimbadilikia, na hata alipokuwa akisema maneno yale, wale askari wenzake walitoa sauti za pamoja na kusonga mbele kwa hatua mbili huku bunduki zao zikiwa zimemwelekea Grayson, viatu vyao vizito vikitoa vishindo vikubwa kabisa mle ndani.
Jamilla Mchebe aliachia mguno mwingine wa fadhaa, wakati wale wenzake wote walibaki wakiwa wamejikunja kwa woga pale mezani, macho yakiwa yamewatumbuka, ilhali mioyo ikiwaenda mbio.
Na alipokuwa akiishuhudia ile hali ikielekea kumtupa mkono, Grayson alimsikia Bilanga akimtupia maneno ya chini chini kutokea pale alipokuwa amejipigisha magoti.
“Usiitupe hiyo bastola sasa, usiitupe! Umeshachelewa… ukiitupa jamaa wanakuua!” Bilanga alimtupia minong’ono ile akiwa amepiga magoti pale chini, na Grayson akamshangaa.
“Okay mzee… sisi tutaanza kuwatoa nje hawa raia wengine humu ndani sawa? Nataka utulie hivyo hivyo… ukileta tafrani kidogo tu askari wote humu ndani watakumiminia risasi!” Kiongozi wa wale askari alimwambia kwa utaratibu, na Grayson akakosa maamuzi.
“Tumeelewana?” Askari alimuuliza, na alipoona Grayson anazidi kukosa maamuzi akapitisha maamuzi.
Alimwita Jamilla huku akiwa amemwelekezea Grayson bastola yake. Jamilla alimsogelea yule askari kwa kusuasua huku akilia wazi wazi na wakati huo huo akimtazama Grayson kwa mashaka makubwa.
Grayson hakuwa na namna.
“Okay, toa nje huyo malaya! Haraka tena!” Alifoka, na Jamilla akalia kwa sauti huku akimkimbilia yule askari, ambaye alimsukumia kwa askari mwingine aliyemtoa Jamilla nje ya chumba kile.
“Muweke chini ya ulinzi huyo kwa sasa. Nitahitaji kuongea naye baadaye!” Inspekta alitoa maelekezo. Bilanga na Luis walitazamana kwa
27 Hussein Issa Tuwa
mashaka.
Kimya kilitanda kwa muda mle ndani.
“Malizia na hawa wengine basi, ubaki na huyo fisadi wako mmoja. Baada ya hapo tutaongea zaidi namna ya kulimaliza hili suala kwa amani…”
Yule askari alimwambia, na Grayson akaguna. Alitembeza macho kwa wale askari waliomzonga, na akajua kuwa akizidi kuleta ubishi wangeweza kumpiga risasi kweli.
Sasa afanyaje?
“Hapo ni kupambana tu wewe! Ukikubali watakuua, ukikataa watakuua vilevile! Pigana kiume sasa, si una bastola hapo?” Bilanga alizidi kumchochea, na Grayson akamtupia jicho la hasira. Akili yake ikafanya kazi haraka, na akajua kuwa Bilanga alimtaka afanye jambo la kijinga ili wale askari wamlipue… wamuue.
Kwa nini?
Akapitisha uamuzi.
“Okay… toa nje mipaka shume mikubwa hii… upesi tena!” Alifoka huku akimtazama Bilanga kwa hasira na akamuona yule jamaa akifura kwa hasira, akilini mwake akajithibitishia kitu.
Bila kusubiri maelekezo ya askari, wale wakurugenzi wengine wa kampuni ile kubwa walikurupuka kama mapaka kweli yaliyokurupushwa yakivizia
bakuli la nyama lililosahauliwa jikoni, wakipamiana mlangoni kabla ya kutoka nje ya chumba kile na kupotelea ghorofa za chini za jengo lile.
“Weka chini ya ulinzi wote hao!” Inspekta alibwata kuwaambia wale askari wake, na William ‘Bill’ Maginga, mkuu wa kitengo cha tehama alisikika akiachia mhemko wa fadhaa.
Sasa mle ndani walibaki yeye, wale askari, Bilanga na Luis.
Upande wa pili wa barabara, mkuu wa usalama aliendelea kufuatilia kila kilichokuwa kikiendelea mle ndani kupitia kwenye ile darubini ya bunduki yake. Muda wote, mtutu wa bunduki ile hatari ulikuwa umemwelekea
Grayson Mochiwa, kidole chake cha shahada kikiwa kinaelea juu ya
kifyatulio cha bunduki ile…
Kule kwenye chumba cha mikutano, Bilanga aliinuka taratibu kutoka pale alipokuwa amejipigisha magoti huku akimtazama Grayson kwa
28 MTAFITI
macho ya hasira, wakati huo huo wale askari walitoa tena sauti za pamoja na kusonga mbele kwa hatua mbili zaidi huku bunduki zao zikiwa zimemwelekea Grayson.
Grayson alizidi kumkwida Luis huku akimdidimizia ile bastola kichwani, macho yakimtembea kwa woga miongoni mwa wale askari.
Baada ya kuona kuwa ameshawaachia wale mateka wengine waliokuwa mle ndani, yule askari alimgeukia Bilanga, na kabla hajamwambia lolote Bilanga akawahi kujieleza.
“Naitwa Bilanga. Mimi ni afisa usalama wa kampuni… nitabaki nanyi humu ndani!” Alisema huku akimtazama Grayson kwa hasira kali.
“Wote mafisadi hawa…!” Grayson alibwata.
“Hebu muachie na huyo aliyebakia sasa, mzee! Weka hapo mezani hiyo bastola yako kwa upole zaidi…!” Askari alimkoromea, na Grayson aliikodolea macho ile mitutu ya bunduki iliyomwelekea, sasa akihisi mwili wote ukimtetema. Alimtazama Bilanga, na hapo aliona kuwa bado yule jamaa alitaka afanye jambo la kijinga ili wale askari wamchabange risasi.
Ili afe na siri mbaya ya wale mafisadi moyoni!
Sikupi faraja hiyo, mpumbavu we!
“Okay! Okay… najisalimisha kwenu wazee, najisalimisha!” Grayson alimaka na hapo hapo akaitupa chini bastola yake na akainua mikono yake juu.
Bilanga alifinya uso kwa hasira, wakati wale askari wakimzonga na kumdhibiti Grayson kwa kumsukasuka huku na huko. Luis Kambesera alikurupuka kutoka pale kwenye kiti na kubaki akiwa amepiga magoti sakafuni akitweta kwa hamaniko baada ya kuwekwa kwenye kitimoto kama alivyowekwa.
Wale askari walimnyanyua juu juu Grayson Mochiwa, naye akawa ametulia tu wakati akisukwasukwa namna ile katikati ya lile kundi la askari huku akimtazama Bilanga kwa macho ya ushindi.
Bilanga na Luis Kambesera walitazamana kwa macho ya viulizo kisha wakamtazama Grayson aliyebebwa juu juu kuelekea mlangoni, kichwa chake kikiwa juu kuliko vya wote wengine mle ndani.
Na hapo ilisikika sauti ya kioo kikipasuka na sanjari na mpasuko ule, Bilanga akashuhudia mboni za Grayson Mochiwa zikipindukia ndani ya macho yake na paji lake la uso likifumuka na kutawanya damu, mapande ya nyama, ubongo, na vipande vya fuvu kila upande mle ndani!
29 Hussein Issa Tuwa
E bwana we!
Grayson Mochiwa hata hakupata fursa ya kupiga yowe.
Wale askari walishtukia Grayson akitepweta na kuwawia uzito mikononi
mwao huku damu zikiwatapakaa ilhali hakuna sauti yoyote ya mlipuko wa bunduki au bastola uliosikika.
Si kimuhemuhe hicho kilichofuatia!
Askari walijitupa pembeni kila mmoja na upande wake, wakimuacha
Grayson akibwagika sakafuni bila kizuizi, bunduki zao zikiwa makini
mikononi mwao wakitaraji shambulizi jingine kutokea kusipojulikana, lakini hakukuwa na shambulizi lolote jingine.
“Nini kimetokea?” Bilanga alijitia kuuliza kwa wahka, na wale askari nao wakawa wanauliza hivyo hivyo. Upepo mkali uliingia mle ndani
kupitia kwenye lile dirisha lililobaki wazi baada ya kupasuliwa kwa risasi
iliyomuondoa Grayson Mochiwa duniani, baadhi ya makaratasi yaliyokuwa pale mezani kwa akina Luis yakitawanywa huku na huko na upepo ule.
Kelele za hamaniko zilisikika kutoka kwa wale askari mle ndani, zikichanganyika na sauti za mvumo wa upepo ule uliofurahia kupata nafasi ya kujivinjari ndani ya chumba kile baada ya kudhibitiwa kwa muda mrefu kufanya hivyo na kile kioo kipana kilichokuwa pale dirishani hapo awali.
Askari mmoja alitambalia tumbo hadi pale alipoagukia Grayson na kumtazama, kisha akamgeukia yule kiongozi wao kwa macho ya fadhaa.
“Jamaa amekufa afande!”
Kiongozi wao aliachia tusi zito sana la nguoni.
“Amekufa?” Aliuliza kwa hamaniko baada ya kuachia lile tusi la nguoni.
Bilanga na Luis walitazamana tena, na katika kutazamana kwao walipelekeana ujumbe wa pongezi.
“Er, afande…” Askari mwingine alimwita yule kiongozi wao, naye akamgeukia, wahka ukimpanda daraja kila dakika zilivyokuwa zikisogea mle ndani.
“Hii njugu imetokea huko nje na kupasua kioo cha hili dirisha afande!”
Yule askari aliyekuwa amejibanza kando ya dirisha pana la kile chumba cha mikutano alimwambia huku akionesha pale kwenye uwazi uliobakia
baada ya kile kioo kusambaratishwa kwa risasi, ambayo yeye aliita ‘njugu’, iliyomuua Grayson Mochiwa.
Yule kiongozi wao mwenye cheo cha Inspekta alitambaa na ukuta hadi pale dirishani na kujibanza upande wa pili wa dirisha lile. Alichungulia kwa
30
MTAFITI
makini kule ambapo alidhani kuwa ile risasi itakuwa imetokea, na mara moja akajua kuwa itakuwa imetokea kwenye lile jengo lililokuwa ng’ambo ya barabara, mkabala na lile walilokuwamo.
Aligeuka haraka na kumuoneshea kidole yule askari wake aliyemuonesha pale risasi ilipopitia.
“Wewe!”
Akawanyooshea kidole askari wengine wawili mle ndani.
“Wewe… na wewe! Twendeni!” Aliwaamuru huku akitoka kwa mwendo wa haraka kuelekea nje ya chumba kile, na alipofika mlangoni akawageukia Luis na Bilanga.
“Mko chini ya ulinzi nyie! Kaeni hapo hapo mpaka nirudi!” Aliwafokea, na alipoona Luis anataka kuongea maneno ya kupingana naye, akawageukia wale askari wawili waliobakia mle ndani.
“Wakitikisika tu hawa piga risasi, bloody swines! Kuna kitu hakipo sawa hapa!” Alifoka.
“Ndio afande!” Mmoja wa wale askari wawili aliitika kwa sauti, Inspekta akamgeukia yule askari mwingine na kumnyooshea kidole.
“Piga simu kituoni. Waje na askari zaidi na gari la kubebea maiti hapa. Lakini mwili usiondolewe mpaka nirudi!” Kisha bila kusubiri jibu akatoka mbio na wale askari wengine kujaribu kuwahi kule kwenye lile jengo lililokuwa mkabala na lile walilokuwemo, na labda kumuwahi muuaji kabla hajatoweka.
Huku nyuma, yule askari mwingine alikuwa akipiga simu kutekeleza yale maelekezo yake.
Dakika saba baadaye yule Inspekta na askari wake watatu waliingia kwenye lango kuu la lile jengo lililokuwa limepakana na lile ambamo mauaji yalikuwa yametokea. Waliingia kwenye lifti na kuiamuru iwapeleke ghorofa ya nane ya jengo lile…
31 Hussein Issa Tuwa
DAKIKA SABA KABLA yule Inspekta hajatoka na wale askari wake watatu kukimbilia kule kwenye jengo lililopakana na lile la Liquid Diamond Inc., Chabbi Cheka, mkuu wa usalama wa ile kampuni iliyokuwa imemwajiri Grayson Mochiwa, aliiweka chini ile bunduki yake hatari na kulifunga lile dirisha. Baada ya hapo aliirudisha pale kwenye maficho yake ya awali ile bunduki, na kuirudishia ile picha ya mlima Kilimanjaro pale ilipokuwa kabla hajaingia mle ndani. Alitembeza macho haraka mle ndani kuona iwapo kuna ushahidi wowote wa wazi aliouacha, na kuliona ganda la ile risasi moja aliyoitumia kutoka kwenye bunduki ile kumuondoa duniani mtafiti Grayson Mochiwa, likiwa limelala sakafuni chini ya lile dirisha lililokuwa likitazamana na lile la kile chumba cha mikutano kilichokuwa upande wa pili wa barabara. Aliliokota lile ganda na kuliweka mfukoni mwake, kisha akatoka nje ya chumba kile na kuubana ule mlango.
Akiwa ameshindilia mikono yake yenye glovu ndani ya mifuko ya suruali yake, alielekea maliwatoni ndani ya jengo lile, ambako alijifungia na kuzivua zile glovu na kuzishindilia ndani ya mfuko wa ndani wa koti lake la suti.
Alipotoka kule maliwatoni hakurudi kwenye lifti. Aliteremka kwa ngazi za miguu hadi ghorofa ya sita ambako hapo alipanda lifti hadi ghorofa ya pili. Kutokea ghorofa ya pili aliteremka kwa ngazi za miguu na kutokea mlango wa nyuma wa jengo lile.
Alijitokeza mtaani na kujichanganya na wapita njia wengine, akichukua uelekeo ambao ulimuwezesha kutokea nyuma ya lile jengo ambamo ofisi za ile kampuni yao zilikuwamo.
Aliingia tena ndani ya jengo lile kwa mlango wa nyuma na kupita moja
32 MTAFITI
3
kwa moja hadi ofisini kwake, ambako kwa kupitia kwenye ile runinga
kubwa, alianza kufuatilia kile kilichokuwa kikiendelea kule kwenye chumba cha mikutano.
Aliwaona Luis na Bilanga wakiwa wameketi kimya kwenye viti, na askari wawili wenye silaha wakiwalinda. Sakafuni, mwili wa Grayson ulikuwa umelala bila uhai.
Hilo halikumtisha, kwani alilitarajia. Luis na Bilanga watajua namna ya kujieleza kwa muda ule. Yeye alikuwa ana jukumu jingine la muhimu zaidi wakati ule. Alibofya kwenye kompyuta yake na kuanza kutafuta taarifa za yule msichana aliyemtoroka asubuhi ile kutoka kule ofisini kwa hayati Grayson Mochiwa.
Sura za wafanyakazi wa kampuni ile zilikuwa zikipita pale kwenye uso wa kompyuta ile moja baada ya nyingine hadi ilipofika ile ya yule binti. Alibofya sehemu kwenye ile kompyuta, na ile picha ikaganda pale kwenye uso wa kompyuta. Aliitazama kwa muda ile sura iliyokuwa ikimtazama kutoka pale kwenye uso kompyuta huku akimung’unya midomo.
“Wewe ni nani lakini mwanadada, eenh?” Aliiuliza ile sura na kubaki akiitazama namna ile kwa muda mrefu.
“Au, swali la msingi zaidi… uko wapi wewe muda huu, eenh?” Aliinong’oneza tena ile sura ya kwenye kompyuta, kisha akabofya bofya zaidi, na taarifa za ziada kuhusu yule msichana zikajianika pale kwenye kompyuta. Akiwa amekunja uso kwa umakini, Chabbi Cheka alizisoma taarifa za yule msichana aliyekuwa pale kwenye kampuni ile kwa miezi mitatu tu, akiwa ameenda kufanya mafunzo kwa vitendo.
Taarifa zilizokuwa kwenye ile kompyuta zilimtosha kufanya alilotaka kulifanya. Ni taarifa zilizobainisha jina kamili la yule binti, kabila lake, anapoishi, anuani yake ya posta na namba ya simu. Alibofya tena, na yale maelezo yakaondoka, sura ya Mwantumu ikarudi tena pale kwenye uso wa kompyuta.
“Halloo Mwantumu… uko tayari kukutana nami ana kwa ana kisura?”
Chabbi aliiuliza tena ile sura huku tabasamu baya likiwa limechafua uso wake.
Mwantumu alimlipa dereva wa bajaji na kuitazama nyumba ambayo
rafikiye Zay Kay, alikuwa anaishi. Alishampigia simu mara tatu zaidi akiwa
33
Hussein Issa Tuwa
ndani ya bajaji bila mafanikio yoyote. Hakushangaa sana kwani ni kawaida ya Zay kuwa hivyo mara kwa mara ampigiapo simu, lakini mara akiona
kuwa alikuwa amemtafuta basi naye humpigia. Lakini mpaka anafika pale nyumbani kwake hakuwa amempigia, na Mwantumu akaamini
kuwa hakika ile ilikuwa ni siku mbaya kwake, kwani kila kitu kilikuwa kikimwendea kombo.
Akijipa moyo kuwa huenda rafikiye huyo alikuwa amerudi asubuhi
ile kutoka kazini na hivyo alikuwa amelala, alisukuma geti la nyumba aliyokuwa akiishi rafikiye na kuzungukia upande wa mabanda ya uwani ambako ndiko Zay alikuwa amepanga chumba cha ‘self contained’.
Kwa muda ule wa asubuhi nyumba ilikuwa kimya naye akabisha hodi
mara kadhaa bila majibu. Alitoa ufunguo wake wa ziada na kufungua mlango na kuingia ndani. Ulikuwa ni utaratibu wao kuwa yeye huwa ana ufunguo wa ziada wa chumba cha Zay, na Zay huwa ana ufunguo wa ziada wa chumba chake kule Chang’ombe.
Chumba kilikuwa kimya, hakukuwa na mtu mle ndani. Alijibwaga kitandani na kujilaza chali akitafakari yale yaliyotokea kule kwenye ofisi za ile kampuni ya Liquid Diamond Incorporated.
“Ukweli wa wazi ni kwamba kule sirudi tena…!” Alijisemea.
Alijaribu kumpigia tena Zay bila mafanikio.
Akaingia kwenye sehemu ya kutuma ujumbe wa ‘WhatsApp’ ambao yeye na rafikiye hupenda kuutumia kwa kutumiana ujumbe wa sauti.
“Shosti uko wapi nakupigia simu hupokei? Mwenzio nimepatwa na mkasa mzito kule kazini! Nimefurushwa na jibaba lenye bastola, na yule bosi wangu kaingia anaropoka maneno ya ajabu ajabu eti kuna siri gani sijui wenzake wamezifuta kwenye kompyuta yake… yaani ni majanga!
Nipigie mara tu ukipata ujumbe huu Zay. Mi niko kwako hapa… leo nalala hapa hapa na kule ofisini tena mi’ basi!” Alisema kwenye ile simu na kuutuma ule ujumbe.
Alilala pale kitandani kwa muda, kisha akainuka.
“Hapana… lazima niende nyumbani kwangu nikachukue vitu vyangu… kesho napanda basi narudi chuo… sikai tena hapa jijini!” Alijisemea mwenyewe.
Alizunguka mle ndani kwa muda akilitafakari lile suala, na akaona ni uamuzi mzuri.
Ripoti ya bwana Mochiwa kama msimamizi wake wa mafunzo kwa
34
MTAFITI
vitendo kwenye ile kampuni tayari alishakuwa nayo… Yeye anaweza
kwenda kumalizia ripoti yake huko huko chuo na kuiwasilisha… mambo
ya kule Liquid Diamond hayamhusu… watajuana wenyewe!
Alichomeka simu yake kwenye mfuko wa suruali yake ya jeans na kutoka. Alikomea mlango wa chumba cha rafiki yake na kuondoka kuelekea
Chang’ombe ambako chumba chake ndio kilikuwapo.
Ni chumba alichokilipia kwa mwaka mzima, ingawa huwa anaishi humo mara chache sana anapokuja jijini wakati wa likizo kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, au UDOM kama kilivyofahamika na wengi, alipokuwa anasomea shahada ya uongozi wa biashara...
Huku katikati ya jiji, dakika ishirini za msako mkali kwenye lile jengo
lililopakana na lile la Liquid Diamond hazikuzaa matunda ya kumbaini
muuaji, ingawa zilimuwezesha yule Inspekta na wale askari wake kukibaini chumba ambacho walihisi kuwa mdunguaji alikuwa amejificha wakati akimdungua Grayson. Waliuvunja ule mlango na kuona kuwa zaidi ya meza moja na kiti, hakukuwa na kitu kingine chochote zaidi mle chumbani. Pia hawakuona dalili yoyote kuwa kuna mtu alikuwamo mle ndani muda mfupi uliopita. Chabbi Cheka hakuwa amefanya purukushani nyingi mle ndani.
Walitoka na kurudi tena kwenye jengo la maafa, na kukuta mwili wa Grayson Mochiwa ukiwa pale pale, na kukiwa kuna askari wa ziada waliokuja na gari la kubebea maiti.
Alisimamia zoezi la uchukuaji wa vipimo maalum vya kipelelezi kwenye eneo la tukio. Mwili wa Grayson ulipigwa picha ukiwa hauna uhai pale sakafuni. Dirisha ambalo risasi iliyomdungua marehemu ilipitia, lilipigwa pichwa. Umbali wa mwili upoangukia kutoka pale dirishani ulipimwa na kuwekwa kwenye kumbukumbu. Hatimaye, baada ya yote hayo, mwili wa mtafiti Grayson Mochiwa ukatolewa nje ya jengo lile, askari wakiwa wametanda pale nje, na wananchi wakikodoa macho.
Walirudi kule kwenye chumba cha mikutano na kukuta askari kadhaa wakiwa wameongezeka, na yule Inspekta akawaweka kiti moto Luis Kambesera na Bilanga.
“Mnaweza kuniambia ni kwa nini yule mtu ameuawa?”Inspekta alihoji
35 Hussein Issa Tuwa
huku akimtazama Luis.
“Khah, sa’ si’ tutajuaje?” Bilanga aliropoka, lakini Inspekta hakumtilia maanani. Alibaki akimtazama Luis kutokea nyuma ya miwani yake maalum yenye vioo vya ‘Polaroid’, ambavyo vilimuwezesha kuvaa miwani ile akiwa nje kwa ajili ya kuyakinga macho yake na jua, na pia vilimuwezesha kuvaa miwani ile akiwa ndani bila ya kuathiri uoni.
“Mi’ sijui wazee!” Luis alisema kwa wahka huku akijiona alivyohamanika kutoka kwenye vioo vya miwani ya yule Inspekta.
“Hujui vipi wakati tumemkuta jamaa kakutaiti kwa mtutu wa bastola hapa? Na wakati tumeshamdhibiti, anatokea muuaji anampiga risasi kutokea nje huko? Hii inaleta picha kuwa aliyemuua alikuwa upande wako mheshimiwa…” Inspekta alimkoromea, na Luis akameza funda la mate.
“Kwa hiyo mimi nd’o nimekuwa mtuhumiwa sasa?” Luis Kambesera aliuliza kwa hasira. Inspekta akatoa miwani yake na kuipachika kwenye kifungo cha pili kutoka juu kwenye shati lake la kiaskari, akiiacha ikining’inia kifuani kwake. Akamrudishia mtazamo wa hasira kwa macho yake madogo na makali sana.
“Mtu anapopigwa risasi na kuuawa, hayo ni mauaji! Na anapopigwa risasi na kuuawa mbele ya ulinzi wa polisi hayo ni mauaji na dharau… yaani muuaji amedharau jeshi la polisi. Amenidharau mimi! Nataka nimjue huyo muuaji, na mazingira yanaonesha kuwa kuuawa kwa huyu marehemu aliyetolewa humu ndani muda mfupi uliopita kunahusiana na hali tuliyoikuta humu ndani…”
“Basi mi’ sitaongea lolote bila ya wakili wangu kuwepo!” Luis alifoka.
Inspekta alimtazama kwa hasira.
“Nakuhitaji wewe na wakili wako kituoni leo hii!” Alitoa amri.
“Sawa!” Luis alimjibu kwa kiburi.
“Na nitahitaji kuwahoji wote wale waliokuwa kwenye hiki chumba pamoja nawe wakati sisi tunafika hapa!” Inspekta aliamuru tena.
“Sawa vilevile!”
Inspekta akamgeukia Bilanga.
“Ulijitambulisha kuwa we’ ni afisa usalama wa kampuni hii.”
“Ndio.”
“Una nini la kutueleza juu ya matukio tuliyokutana nayo hapa?
Usiniambie na wewe unahitaji wakili wako awepo!”
Bilanga alitikisa kichwa.
36
MTAFITI
“Hapana. Kilichotokea kwa jinsi nijuavyo ni kwamba kengele ya tahadhari ilisikika ofisini kwangu. Kwa kupitia kwenye runinga ya usalama nikaona kuwa Grayson alikuwa amewashikia bastola wakurugenzi wenzake humu ndani. Hivyo nikapiga simu polisi kisha nikaja huku… nami nikawekwa chini ya ulinzi kama mlivyonikuta.” Bilanga aliongopa.
“Kwa hiyo wewe ndiye uliyepiga simu kituoni?”
“Ndio.” Bilanga alimjibu kwa macho makavu, akijua kabisa kuwa ni uongo. Ulikuwa ni uongo wa muhimu kwa sababu hakutaka polisi waanze kuuliza ni wapi alipo huyo aliyepiga simu kama angesema kuwa si yeye aliyepiga ile simu. Alijua kuwa ni Chabbi ndiye aliyepiga simu, na ni Chabbi ndiye aliyemuondoa Grayson duniani.
Ilikuwa ni salama kwao kama Chabbi Cheka asingeonekana kabisa na wale askari kwa siku ile.
Inspekta alimtazama kwa muda mrefu.
“Kuna wafanyakazi wangapi kwenye hicho kitengo chenu cha usalama wa kampuni?”
“Aaah, come ooonn, haya maswali yote ya nini lakini?” Luis alidakia, na
Inspekta akamjia juu.
“Wakili wako amefika sasa mheshimiwa?”
Luis alimtazama kwa hasira, lakini hakuwa na jibu.
“Hata mi nilidhani hivyo hivyo… kwamba wakili wako hajafika. So keep quiet kwa sasa!” Inspekta alimkoromea, na kumgeukia Bilanga.
“Jibu swali, afisa usalama wa kampuni!” Alimwambia.
“Tuko wawili, na mwenzangu leo alikuwa na dharura, hakuja kazini…” Bilanga alimjibu.
Inspekta alimtazama kwa muda.
“Anaitwa nani?” Inspekta alimuuliza, na Bilanga akabaki akimkodolea kama kwamba hakuelewa ameulizwa swali kwa lugha gani.
Inspekta akambwakia tena na swali lile.
“Aamm, Chabbi, mzee. Anaitwa Chabbi Cheka!” Bilanga alimjibu. Inspekta alimtazama kwa muda.
“Okay… nadhani atakuwa anacheka na bahati yake tu kuwa amepatwa na dharura siku ya leo!” Alisema na kuwageukia wale askari wenzake.
“Twen’zetuni!”
Walianza kuondoka, na walipofika mlangoni Inspekta akamgeukia Luis.
“N’tahitaji maelezo yako kituoni bwana mkubwa!” Alimwambia, na
37 Hussein Issa Tuwa
MTAFITI
Luis akamkunjia uso. Wale askari wakatoka.
Luis na Bilanga wakatazamana.
“Sasa anataka kuwahoji nini wale wenzetu tena?” Luis alimuuliza Bilanga kwa mashaka.
“Anajua mwenyewe! Hiyo ni kazi yake, ningeshangaa kama asingetaka kuwahoji.”
“Unadhani atapata lolote akiwahoji?” Luis bado alionekana kuwa na mashaka.
“Mnh! Sina imani sana na Bill na Jamilla… wengine nadhani wako vizuri.” Bilanga alimjibu.
Luis aliuma meno na kukunja uso.
“Hakikisha hapati lolote kutoka kwa yeyote kati yao!” Hatimaye alisema.
“Sasa nalifanyaje hilo wakati tayari jamaa wako chini ya ulinzi?”
“Sio kazi yangu hiyo! Unadhani mi’ nawalipa hela nyingi kwa ajili gani? Hakikisha juu ya hilo Bilanga!” Luis alimkoromea kwa hasira. Bilanga aliguna, kisha akatoa simu yake na kuanza kuandika ujumbe.
“Mpigie Chabbi… nataka kuonana naye haraka sana!” Luis alimwambia, na baada ya kutuma ujumbe wake, Bilanga akatekeleza.
Simu ya Chabbi ilipoanza kuita, Bilanga akampa Luis simu ili aongee naye.
“Yes?”
“Luis hapa… nimeona umefanya lililo ndilo!” Luis alimwambia.
“Yah… nadhani tulishaongea kuwa hali ikifikia hatua mbaya basi hiyo ndio iwe plan B?” Chabbi Cheka alimjibu.
“Haswa! Na hali ilishafikia pabaya kwa kweli. Je kuna tatizo lolote upande wako ambalo tunatakiwa tuwe na mashaka nalo?” Luis alisaili.
“Yah. Kuna kuna kimeo kimoja tu… na ndio nakifanyia kazi hivi sasa …”
“Oh, ni kipi hicho?”
“Tutaongea tukionana Bosi…” Chabbi alimjibu bosi wake, na Luis akaelewa.
“Okay!”
Akamgeukia Bilanga huku akimrejeshea simu yake.
“Sasa unalifanyia vipi kazi hilo suala la kuhakikisha kuwa Inspekta hapati lolote kutoka kwa wale wenzetu? Muda hatuna kabisa ujue, na huyu
38
mjinga katukalia vibaya sana!” Alimwambia. Badala ya kumjibu, Bilanga
alibofya kwenye simu yake na kufika sehemu yenye ujumbe alioutuma.
“Kuanzia sasa sote maelezo yetu juu ya hili yatakuwa ni haya…”
Alimwambia huku akimpa tena ile simu ikiwa inaonesha ujumbe alioutuma dakika chache zilizopita akiwa mle mle ndani.
Luis aliusoma ujumbe ule huku akiwa amekunja uso, na baada ya muda uso wake ukachanua kwa tabasamu pana.
“Fabulous!” Alisema huku akimrejeshea Bilanga simu yake, akimaanisha kuwa kile alichokisoma kwenye ujumbe ule kilimfurahisha sana.
Mike Mwangati alikuwa anasoma ujumbe ulioingia kwenye simu yake muda mfupi baada ya kurudi ofisini kwake akiwa amesindikizwa na mmoja wa wale askari waliokuwa na yule Inspekta kule kwenye ukumbi wa mikutano.
MAELEZO YETU KWA INSPEKTA NI KWAMBA GRAYSON
ALIVAMIA UKUMBI WA MIKUTANO WAKATI KIKAO CHA
KAWAIDA CHA WAKURUGENZI KIKIENDELEA. AKADAI
APEWE HELA ILI AKALIPE MADENI YANAYOMZONGA HUKO
MITAANI KWA MAELEZO KUWA ASIPOLIPA HAYO MADENI
ANAWEZA KUUAWA NA HAO WANAOMDAI. MKURUGENZI
ALIPOMKATALIA AKAMTOLEA BASTOLA NA KUTISHIA
KUMUUA YEYE NA SOTE TULIOKUWA MLE NDANI. ZAIDI YA
HAPO HAUJUI LOLOTE. AKIZIDI KUKUBANA KWA MASWALI
MWAMBIE AMUULIZE LUIS. UJUMBE HUU UMETUMWA
KWAKO NA KWA WENZAKO WOTE. SOTE TUWE NA JIBU
MOJA. UKISHASOMA, FUTA KABISA KWENYE SIMU YAKO!
Ulikuwa ni ujumbe uliotoka kwenye simu ya Bilanga. Alibaki akitafakari juu ya ujumbe ule huku uso wake ukiwa na mawazo mazito. Na hapo
alimuona yule Inspekta akiingia mle ofisini kwake. Alibonyeza kitufe kilichomuwezesha kuufuta ujumbe ule kutoka kwenye simu yake, na
kuinua uso wake kumtazama yule Inspekta.
Moja kwa moja Inspekta alianza kumhoji juu ya tukio lililotokea
39
Hussein Issa Tuwa
kule kwenye ukumbi wa mikutano, naye akampa majibu kama jinsi alivyoelekezwa na ujumbe wa Bilanga.
Inspekta alimtazama kwa macho makali.
“Sasa kama na Grayson alikuwa ni mmoja wa wakurugenzi muhimu… kwa nini hakuwepo pale kwenye mkutano ule kabla, na badala yake akaja kuvamia baadae na kumshikia bastola bosi wenu?” Alimuuliza.
“Hilo mie sijui kwa kweli. Ni wajibu wa kila mkurugenzi akiitwa kwenye kikao kuhudhuria. Huwa inatokea wengine wanashindwa kuhudhuria kwa sababu moja au nyingine, lakini anayepewa taarifa hizo ni mkurugenzi mtendaji mwenyewe. Kamuulize Luis juu ya hilo.” Jamaa alimjibu bila kujali.
“Alisema ni watu gani hao wanaomdai, na ni kiasi gani alichokuwa anataka apewe?”
“Mnh! Unajua pale alikuwa anaongea zaidi na Luis na siye wengine tulikuwa tumepigwa na butwaa…” Mike alianza kujibu, lakini Inspekta alimkatisha.
“Sijakuuliza maoni ya hao wengine, nimekuuliza wewe! Aliwataja hao wanaomdai na ni kiasi gani alichokuwa anadaiwa?” Inspekta alimchachamalia, na Mike akamkunjia uso.
“Okay… mimi nilikuwa nimebutwaika tu na wala sikumbuki maneno mengi aliyokuwa akiyasema pale. Sikumbuki kumsikia akitaja mtu wala kiwango…” Alimjibu, na hapo hapo akapata wazo.
Kama Bilanga ametuelekeza tujibu hivi, ni wazi kuwa atakuwa ameshapangana na Luis juu ya hili. Kwa hiyo huu mzigo ni Luis ndiye atakayeubeba.
“Er… Unajua Inspekta… nikizidi kufikiria jinsi yale mambo yalivyokuwa yanaenda mle ndani, napata picha kama kwamba kulikuwa kuna maongezi ya awali kati yake Grayson na Luis, ambayo sisi… sorry… mimi, sikuwa nayajua. Kwa hiyo pale yule jamaa alikuwa amekwenda kumsisitizia Luis juu ya hilo jambo ambalo alishaongea naye kabla na bila shaka alishakataliwa kabla… ongea na Luis Inspekta. Mi’ sijui lolote zaidi kwa kweli. Nimepigwa na mshituko tu jinsi yule bwana alivyotubadilikia sote namna ile!” Mike aliongezea, na Inspekta akamkazia macho.
“Yule jamaa… Grayson ameuawa kule kwenye chumba cha mikutano unajua?” Alimwambia kwa mfumo wa swali, na Mike Mwangati akashituka kiukweli kabisa.
“Ame… kivipi?” Alihoji kwa mshituko wa ajabu, na Inspekta
40 MTAFITI
akajihakikishia kuwa ingawa kuna mambo alikuwa anahisi kuwa yule
jamaa alikuwa amemdanganya, hili la kuuawa kwa yule mtafiti wa kampuni
ile halikuwa kabisa mawazoni mwake. Alikuwa halijui.
“Kuna mtu kamdungua kwa risasi kutokea nje ya jengo hili…”
“AAAAH! Kawezaje na huku tuko ghorofani?” Mwangati alimaka.
Kwa hiyo kama kuna watu walihusika kupanga mauaji yale miongoni mwa watendaji wa kampuni ile, Mike Mwangati hakuwa miongoni mwao.
Inspekta aliwaza huku akimtazama kwa makini yule jamaa aliyekuwa mbele yake.
“Hilo ndilo nitakalohakikisha kuwa naligundua! Kwa nini ameuawa, na ni nani aliyeandaa mpango wa kumuua!” Inspekta alimjibu huku akiinuka
kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia na kuuendea mlango. Alipofika mlangoni alimgeukia.
“Nikiwa na maswali zaidi nitakuja tena bwana Mwangati!” Alimwambia.
“Karibu sana…” Jamaa lilimjibu huku likimtazama moja kwa moja machoni, bado uso wake ukionesha mshituko kwa taarifa ya kuuawa kwa Grayson.
Inspekta alitoka kuwafuata wale wakurugenzi wengine kwa mahojiano, na saa moja baadaye alikuwa ameshaongea na wote. Jamilla Mchebe, William Maginga na Suleiman Mwangi. Na kutoka kwa wote hao hakupata jambo lolote tofauti na yale aliyoyapata kutoka kwa Mike Mwangati. Ingawa Maginga na Jamilla walionekana kubabaika sana, bado maelezo yao hayakumpa nafasi ya kuwahusisha zaidi na tukio lile.
Kiufupi, Inspekta aliambulia patupu.
Na hilo ndilo lililompa taabu sana wakati akiondoka pale Liquid Diamond Incorporated.
Kwa nini wote wamekuwa na majibu yanayofanana takriban neno kwa neno kwenye maswali yake ya msingi kuhusu Grayson Mochiwa?
Inspekta hakuwa mbumbumbu. Alikuwa amefanya kazi chini ya wapelelezi mahiri sana huko nyuma, na alishapata kwenda kusomea zaidi fani za kipelelezi kwenye nchi mbalimbali, zikiwemo Uingereza na Israel. Alijua sana kuitathmini akili halifu, na kile alichokutana nacho pale Liquid Diamond hakikumridhisha kabisa kuwa kampuni ile haikuhusika na mauaji yale, hivyo hakuiamini kabisa ile hadithi ya Grayson kudai pesa kwa mtutu wa bastola namna ile.
Badala yake, akili yake ya kipelelezi ilimpa jibu moja tu la kuaminika...
41 Hussein Issa Tuwa
kwamba kulikuwa kuna hujuma kubwa sana ndani ya ile kampuni… na
kwamba kifo cha Grayson Mochiwa kiliandaliwa na ile ile kampuni ya Liquid Diamond Incorportaed.
Sasa swali linabakia… kwa nini?
Wakati Inspekta akikosa jibu kwa swali lile muhimu, sehemu nyingine ya jiji mwanadada Mwantumu aliteremka kutoka kwenye daladala pale kituo cha Usalama, Chang’ombe. Alivuka barabara na kuziendea bajaji zilizokuwa zimeegeshwa kando ya kituo kile kutega abiria. Aliongea na mmoja wa waendesha bajaji zile kuwa alikuwa anahitaji usafiri kwenda Mwananyamala, ila alitaka waende pale kwake, mtaa wa pili kuchukua begi lake la nguo kisha waelekee huko Mwananyamala.
Walikubaliana bei naye akaingia ndani ya bajaji ile hadi pale nyumbani kwake. Aliingia chumbani kwake na kurushia nguo zake haraka haraka kwenye begi lake la safari. Akachukukua mkoba wake mwingine wenye vitabu vyake vya chuo pamoja na kompyuta mpakato yake na kugeuka kutaka kutoka.
Na hapo ndipo alipoishia.
Mwili ulimfa ganzi Mwantumu na hakuamini macho yake. Yule mtu aliyekuwa akimkimbiza kule ofisini asubuhi ile, alikuwa pale chumbani kwake.
“Hello Mwantumu… wanikumbuka miye?” Chabbi Cheka alimuuliza huku akiwa amesimama mlangoni hali akiwa amemkunjia uso.
“Hah! Ume… unafanya nini hapa wewe?” Alimuuliza kwa woga huku akitazama namna ya kujinasua kutoka kwenye mtego ule hali akijilaumu kwa nini hakujikomea kwa ndani mara tu alipoingia mle ndani mwake. Jamaa alimtolea tabasamu baya.
“Nimekuja kuongea nawe kidogo tu…”
“Nd’o unifuate huku kwangu? Na umepajuaje hapa kwanza wewe?” Mwantumu alimjia juu.
Chabbi akamcheka.
“Taarifa zote za mahala unapoishi zilikuwepo pale ofisini, hivyo haikuwa taabu kwangu kuitambua nyumba namba kumi na nne mtaa wa Mkamba, Mwantumu. Kilichobakia kilikuwa ni kuja kukusubiria tu
42 MTAFITI
huku… na naona umeshafika!” Chabbi alimwambia huku akiingia ndani na akiufunga ule mlango.
Wakawa wamejifungia mle ndani.
“Naomba utoke humu ndani! Toka! Sina lolote la kuongea nawe!”Alimkemea huku akirudi nyuma.
“Si tatizo… labda mimi ninalo la kuongea nawe…” Chabbi alimjibu huku akiketi kwenye kiti kilichokuwa mle ndani na kukunja nne, na ndipo kwa mara ya kwanza Mwantumu alipoona kuwa alikuwa amevaa glovu mikononi.
Roho ikampasuka.
Akilini likampitia wazo kuwa yule bwana alivaa zile glovu kwa kuwa hakutaka kuacha alama za vidole vyake mle ndani mwake. Na hiyo ilimwambia kuwa yule mtu alikuwa amedhamiria kumfanya kitu kibaya. Akaikumbuka hali aliyomuona nayo Grayson Mochiwa asubuhi ile kule ofisini, na jinsi yule mtu alivyokuwa akimkimbiza na bastola mkononi kabla hajawahi kuingia kwenye lifti na kumtoroka...
“JAMANI NAKUFFF….!” Alianza kupiga kelele lakini kwa wepesi usiotarajiwa Chabbi Cheka aliruka kutoka pale kitini na kumzaba kofi kali la uso lililokatisha kabisa ukelele wake. Mwantumu alienda chali kitandani na Chabbi akamshukia juu yake pale kitandani.
“Kelele wewe… kelele!” Alimkoromea, na Mwantumu alitumbua macho kwa woga na kutoamini kile kilichomtokea. Ngozi yake ikawa nyekundu mara moja pale alipopigwa na alihisi mdomo ukimuumuka.
Akalia.
“Nimekufanya nini mimi lakini we’e baba… enh? Hebu niangalie hali yangu lakini!” Aliuliza kwa kuomboleza, machozi yakimtiririka.
“Ulipoondoka pale ofisini ulikuwa una mkoba… ulikuwa una nini na uko wapi sasa… mbona hukuja nao hapa?” Chabbi alimkoromea, na Mwantumu akachanganyikiwa.
“Mkoba? Ule ni… ni mkoba wangu, heeh!”
“Uko wapi?”
Ah! Nimeuacha kwa Zay…
Ni wazo lililompitia Mwantumu kichwani, na akajua kuwa hakutakiwa kabisa kulitamka wazo lile. Akapiga kimya, akilia kwa woga.
Chabbi akamchapa kofi jingine, kisha akambana mdomo ili asipige kelele.
43 Hussein Issa Tuwa
“Uko wapi ule mkoba nakuuliza we’malaya, eenh?”
“Umeibiwa!” Mwantumu aliropoka.
“Umeibiwa? Kivipi mwongo mkubwa wewe? Uko wapi ule mkoba nakuuliza!” Chabbi alimjia juu, na Mwantumu akalia zaidi.
“Naomba uniache baba’angu… kwani mnautakia nini mkoba wangu jamani?”
“Kuna makabrasha ulipewa na Grayson Mochiwa wewe… na ukayaweka kwenye ule mkoba wako… nayataka!” Chabbi alimwambia, na Mwantumu akazidi kushangaa.
Ameyajuaje yote haya huyu?
“Hah! Makabrasha? Ile si ilikuwa ripoti yangu ya field tu jamani? Hakukuwa na lolote zaidi mle! Hebu niachie huko!”
“Sasa basi ndio unipe ili nijiridhishe!”
“Nakwambia mkoba wangu umeibiwa kwenye daladala, we’ vipi?”
Jamaa alimtandika makofi matatu ya mfululizo, kisha akamuinua kutoka pale kitandani kama kimwanasesere na kumbwaga kwenye kochi. Mwantumu aliserereka hadi sakafuni kutoka pale kwenye kochi, na alianza kujiinua kutoka pale chini wakati alipokutana na mtutu wa bastola usoni.
Macho yakamtoka pima.
“Okay, huu mjadala tutaenda kuuendeleza mahala pengine Mwantumu… inuka!” Chabbi alimkoromea, pua zikiwa zimemtanuka, macho yakiwa yamemuiva.
“Unan… unan’peleka wapi…?” Mwantumu aliuliza huku akiwa amejiegemeza kwenye kile kiti. Na alipokuwa amejiegemeza namna ile, aliichomoa simu yake kutoka mfukoni mwake na kuisukumizia uvunguni mwa kochi lile.
“Utaongozana nami hadi kwenye gari hapo nje. Yule dereva wako wa bajaji nimeshamlipa na ameenda zake…”
“Hah!”
“Ndio! Nimemwambia kuwa nimekuja kukuchukua kwa hiyo ye’ aende zake… na ameenda!”
“Ah, jamani kwa nini hii lakini?”
“Na hutapiga kelele wala hutafanya rabsha huko nje. Nitakuwa nimekuwekea bastola ubavuni kwako muda wote…”
“Jamaani! Ni nini lakini…?” Mwantumu alilia kwa simanzi. Ukweli alikuwa haelewi lolote katika yale yaliyokuwa yanamtokea wakati ule.
44 MTAFITI
“Inuka!” Chabbi aliamuru.
Mwantumu akatii.
“Futa machozi… fasta!” Chabbi aliamuru, na huku akitetemeka vibaya, Mwantumu alitii.
“Okay… sasa tutatoka sote humu ndani mimi na wewe Mwantumu. Nitakuwa nimekushika mkono kirafiki tu lakini kwa mkono wangu mwingine utakaokuwa umefichwa na koti langu nitakuwa nimekuelekezea hii bastola ubavuni. Ukileta fyokofyoko tu kwa kuwa eti huko nje kuna macho ya watu mi’ nakuwasha halafu natoweka (akamtukania mama yake)… upo?”
Duh!
Nguvu zilimwisha kabisa Mwantumu.
“Na hakuna atakayesikia mlipuko wala nini… bastola imefungwa kiwambo cha kuzuia sauti hii. Watu wataona unaanguka tu, na mi’ nikitoweka!”
Mwantumu hakuwa na namna…
45
Hussein Issa Tuwa
ZAINAB KALINDO, wenzake wakipenda kumwita ‘Zay
Kay’ au ‘Zay’, mwenyewe akipenda kujiita ‘Zaynush’, alifumbua macho mazito na kujikuta akisonya pale yale macho yalipomkaidi na kujifumba tena. Alilazimisha kuyafumbua tena huku mwayo mrefu ukimtoka na akijinyoosha kivivu pale kitandani. Alitupa mkono wake kivivu kando yake pale kitandani kwa matarajio, na akajikuta akiachia mguno huku akiinua kichwa chake na kukigeuzia pale mkono wake ulipoangukia, yale macho yaliyokuwa mazito kufumbuka kutokana na usingizi na uchovu sasa yalikuwa maangavu na makini.
Mkono wake ulikuwa umeangukia kwenye mashuka tu ya pale kitandani, ingawa yeye aliutaraji uangukie kifuani au mgongoni kwa mpenziwe aliyekuwa amelala naye usiku uliopita.
Hayupo!
“Awww, shit, injinia… not again, bhana!” Alilalama huku akiinuka kutoka pale kitandani. Alitembea kivivu akiwa hana nguo hata moja mwilini kuiendea simu yake iliyokuwa juu ya meza iliyokuwa kwenye kona moja ya kile chumba cha ile hoteli ghali waliyokuwa wamepanga tangu siku tatu zilizopita. Alijibweteka kwenye stuli iliyokuwa mbele ya ile meza na kupeleka mkono wake kuichukua simu yake.
Mkono ukaganda juu ya simu ile bila kuichukua, macho yake yakiangukia kwenye karatasi iliyokuwa imegandamizwa na simu ile. Huku akitabasamu, aliisogeza ile simu pembeni na kuchukua ile karatasi. Kwa mwandiko wake mzuri, yule mpenziwe alikuwa amemuachia ujumbe.
Ulionekana mrembo mno usingizini miss nice buttocks, kiasi kwamba nikaona dhambi kubwa kukuamsha. See you end of the month! Ntakupigia. OX, OX,
46 MTAFITI
4
OX, OX.
Zay akaachia kicheko cha kivivu.
“Miss nice buttocks mwenyewe, injinia wangu!” Aliiambia ile karatasi huku akitabasamu, akilicheka lile jina la utani ambalo yule mpenziwe hupenda sana kumuita kwalo, akisifia jinsi makalio yake yalivyokuwa yanamvutia.
Zay hakuwa msichana mrembo wa kutisha ila alikuwa na mvuto ambao ni yeye tu alikuwa nao. Mpenzi wake huyo aliyekuwa akifanya kazi za
uinjinia wa barabara alikuwa akiishi Rwanda kwa muda ambako kampuni
aliyokuwa akiifanyia kazi ilikuwa imepata kandarasi ya ujenzi wa muda mrefu, hivyo huwa anakuja nchini kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi kujumuika naye. Ile ikiwa ni wikiendi ya mwisho wa mwezi, mpenziwe yule
aliingia jijini Ijumaa jioni na tangu siku hiyo amekuwa naye pale hotelini. Jioni ya Jumapili walienda sehemu mbalimbali za starehe na kurudi usiku sana. Kwa kuwa yule mpenziwe alitakiwa apande ndege alfajiri ya Jumatatu
kurudi Rwanda, mara waliporudi kutoka kwenye starehe zao za mitaani usiku uliopita walikubaliana kuzima simu zao ili wasisumbuliwe kabisa
wakati wakiwa kwenye starehe zao za chumbani.
Badala ya kuizima simu yake, yeye aliiziba sauti tu.
Ilikuwa ni kawaida ya mpenzi wake huyo, ambaye mwenyewe alishazoea
kumwita ‘injinia’ kutokana na kazi yake ile badala ya jina lake halisi la Mchebbe, kutomuamsha akiwa amelala kila anapoondoka alfajiri, na safari hii alimlazimisha mpenziwe aahidi kuwa wakati wa kuondoka ukifika atamuamsha ili waagane, naye alikubali kufanya hivyo.
Lakini hakufanya hivyo... akimuonea huruma kumkatisha usingizi wake baada ya mchoko wa usiku uliopita, na kwa namna fulani hili lilimfanya
Zay azidi kumpenda yule mpenziwe.
Alitikisa kichwa huku akitabasamu na kuchukua simu yake kwa lengo la kuangalia saa. Na ndipo alipoona kuwa kulikuwa kuna simu nane
alizopigiwa ambazo hakuzisikia.
Tano kati ya hizo zilikuwa ni kutoka kwa rafiki yake kipenzi, Mwantumu.
“Oooh, Mwantumu shosti wangu… nimekususa wikiendi yote hii
eenh… mnhu! Nilikuwa na mchuchu mwenzio!” Alijisemea peke yake
kama kwamba ndio anamwambia Mwantumu huku akimpigia simu
rafikiye yule.
47 Hussein Issa Tuwa
Simu ya Mwantumu ilikuwa ikiita tu bila majibu. Alijaribu mara tatu zaidi na matokeo yakawa ni yale yale.
“Oooh, rafiki yangu kipenzi amesusa kupokea simu yangu, eenh? Okay… nitamtoa out wiki hii kumpoza basi!” Alijisemea na kuingia bafuni kuoga.
Ambalo hakulijua ni kwamba iwapo angeipiga ile simu kiasi cha dakika tano tu kabla, basi ingeita kutokea chini ya kochi wakati Mwantumu akiwa na Chabbi Cheka mle chumbani kwake kule Chang’ombe. Na jingine ambalo hakulijua ni kuwa muda ule rafiki yake alikuwa kwenye madhila makubwa kabisa...
Kule Chang’ombe, Chabbi Cheka alimfikisha Mwantumu kwenye mlango wa abiria wa gari lake kubwa aina ya VX lenye vioo vilivyowekwa weusi bila tatizo lolote. Alimwamuru afungue mlango na aingie mle garini. Wakati yule mwanadada aliyehamanika akipanda kwenye gari lile, yeye alitazama kulia na kushoto na kuona kuwa mtaa ulikuwa kimya. Kwa tendo moja la haraka alimpiga kwa nguvu kisogoni kwa kitako cha bastola yake huku akimsukumia kwa nguvu ndani ya lile gari. Mwantumu aliangukia kwenye kiti cha abiria mle garini, fahamu zikimhama. Hapo hapo Chabbi akamsukumia ndani zaidi na kuufunga ule mlango wa upande wa abiria.
Akazungukia haraka upande wa dereva na kuingia nyuma ya usukani.
Akiwa mle garini, alikilaza kile kiti cha abiria haraka haraka, yule dada akiwa amelala bila fahamu juu yake, kisha akambana vizuri pale kitini kwa mkanda wa kile kiti, halafu akatoa plasta kubwa kutoka kwenye droo ya mle ndani ya gari na kumbandika mdomoni.
“Hizi kazi ilibidi zifanywe na Bilanga bwana, sio mimi…lah!” Alijisemea
mwenyewe huku akiliondoa taratibu lile gari kutoka pale mtaani huku
akiangaza kwa makini huku na huko nje ya gari lile. Hakuona yeyote aliyeonekana kufuatilia zile harakati zake.
Saa moja baadaye aliingiza gari lake kwenye gereji iliyojengwa kwenye
nyumba moja pweke iliyokuwa maeneo ya Mbagala. Aliteremka na kwenda
kulifunga geti la gereji ile iliyounganishwa na ile nyumba. Alimbeba
Mwantumu ambaye alishazinduka na alibaki akigumia tu kutokana na
48
MTAFITI
kuzibwa mdomo kwa ile plasta, na kuingia naye ndani zaidi ya nyumba ile
kupitia mlango ulioiunganisha ile sehemu ya gereji na nyumba kuu.
Alishuka naye ngazi kuelekea kweye chumba cha chini ya ardhi ndani ya nyumba ile, ambako huko alimbwaga sakafuni kama mzigo, Mwantumu akigumia kwa maumivu.
Chabbi alibaki akitweta huku akimtazama kwa msaada wa mwanga hafifu uliokuwa mle ndani.
“Hiki chumba kipo kiasi cha futi kumi na tano chini ya usawa wa bahari… hii nyumba iko pweke. Sasa ukijitia kupiga kelele elewa kwamba kwanza hakuna atakayekusikia, halafu kwa kuwa kipo chini ya ardhi kina hewa nzito kidogo… kitakachofuata ni kwamba utajikuta unashindwa kupumua
vizuri na hata kufa kwa kukosa hewa… okoa pumzi zako kwa kutopiga kelele wewe, sawa?” Alimsomea risala ndefu huku akimnyooshea kidole.
Mwantumu aliafiki kwa kichwa huku akiwa amekaa pale sakafuni, machozi yakimtiririka, mdomo ukiwa umebandikwa ile plasta.
“Good!” Chabbi alisema kisha akamuinamia na kumbandua kwa nguvu ile plasta, kitendo kilichoiumiza sana ngozi laini ya Mwantumu, naye alilia kwa maumivu aliyoyapata.
Alikurupuka haraka kutoka pale sakafuni na kujisotesha nyuma kwa woga hadi ukutani, na akabaki akiwa amejikunyata kwenye kona moja ya chumba kile.
“Please, we baba… ni… niache niende nyumbani mwenzio! Sina nijualo mimi kwa kweli!” Alilalama kwa kuombeleza.
Chabbi Cheka alivuta kiti cha mbao kilichokuwa mle ndani na kukikalia kwa namna ambayo ile sehemu ya kuegemea ikawa kwa mbele.
“Nilikwambia kuwa ule mjadala tuliouanza kule chumbani kwako tutauendelezea sehemu nyingine… sehemu yenyewe ndio hii. Hapa tuna faragha ya kutosha. Nikianza kukutesa kwa kuuchomachoma huo mwili wako mororo kwa sigara…”
“Mama yangu weee…”
“Nini? Unaogopa? Usiogope! Ukinijibu maswali yangu wala sitakufanyia hayo yote… lakini ukijitia ubabe, basi nitakufanyia hayo na zaidi ya hayo…!”
“Oooh, mama yangu jamanii!”
“Lia utakavyolia, piga kelele utakavyopiga… hakuna atakayekusikia
49 Hussein Issa Tuwa
Mwantumu… hapa ni mimi na wewe tu!”
“Nimekosa nini mimi lakini we’ baba jamani?” Mwantumu alizidi kusaili huku akilia.
“Nataka kujua juu ya yale makabrasha uliyopewa na Grayson… na usiniambie kuwa yameibiwa!” Chabbi alimkoromea.
“Ooh, mungu wangu, huyu baba ananitafutia balaa tu mimi jamani!”
Mwantumu alilalama huku akigeukia pembeni kwa kukata tamaa.
Chabbi akamkazia macho ya kuogofya.
“Ukweli babaangu… lile begi mi’ nimeibiwa kwenye daladala…”
Chabbi alikirusha pembeni kile kiti alichokuwa amekalia na kumrukia pale alipokuwa na kuushindilia teke ukuta jirani yake, na yowe la hamaniko na woga likamtoka Mwantumu.
“Wacha kucheza michezo na mimi wewe!” Chabbi alifoka, na kuongezea, “ We’ hunijui mimi wewe, eeenh?”
Mwantumu alikuwa akilia waziwazi.
“Watu kwenye daladala huwa hawaibiwi begi zima wewe, wanaibiwa vitu vya ndani ya begi! Sasa we’ unasema umeibiwa begi zima? Acha uongo!”
Alimkoromea, na Mwantumu akajua amenaswa.
Chabbi alibaki akimtazama huku akitweta.
“Limeibiwa begi… limeibiwa…”
“Okay, lete simu yako…upesi!”
“Simu pia imeibiwa… ilikuwa kwenye begi…”
Chabbi alimzaba kofi kali lililompigiza kisogo ukutani na hapo hapo akamdaka koo. Bila ya kujali vilio vya kuomboleza alivyokuwa akivitoa, alimsachi mifuko yote na kuona kweli hakuwa na simu. Alibaki akimtazama kwa muda mrefu.
“
Okay, Mwantumu… ni wazi kuwa hujui ni jambo gani ulilojitumbukiza ndani yake… lakini nakuahidi mwisho wake hautakuwa mzuri kwako.
Mi’najua umepewa yale makabrasha na kuna mahala umeyaficha… sasa kwa nini? Unataka kuishia kama Grayson, eenh?” Alimkoromea kwa kitisho.
“Mi’ sijui lolote! na sijajitumbukiza kwenye jambo lolote! Na ni nini unamaanisha kuwa nitaishia kama Grayson… amekuwaje kwani?”
Mwantumu aliuliza kwa wahka huku akilia kwa woga.
Chabbi Cheka alimtazama kwa muda mrefu bila ya kumjibu, kisha
50 MTAFITI
akashusha pumzi ndefu. Akamfunga kamba miguu na mikono mle ndani, halafu akasimama na kumtazama tena kwa macho yake ya kuogofya.
“Okay, nakupa muda ufikirie vizuri ni wapi ulipoficha hayo makabrasha wewe… nitarudi kuchukua jibu langu!”Alimwambia, na bila ya kujali vilio vya Mwantumu aliyekuwa akimuomba asimuache peke yake mle ndani, Chabbi Cheka alitoka nje ya chumba kile na kumfungia kwa nje.
Zay aliingia chumbani kwake pale Mwananyamala na alipouona mkoba wa rafikiye Mwantumu ukiwa kitandani kwake, alijua kuwa Mwantumu alifika pale ndani kwake, ingawa hakujua alifika pale lini. Yeye alikihama chumba chake tangu Ijumaa jioni, na ile ilikuwa ni Jumatatu mchana.
Hili halikumshangaza sana kwani alijua kuwa Mwantumu alikuwa ana ufunguo wa pale kwake kama jinsi yeye alivyokuwa na ule kule kwake.
“Sasa mbona ameacha mkoba wake wa ofisini hapa kwangu… ina maana hakwenda ofisini leo?” Alijiuliza huku akiuchukua ule mkoba na kuuweka kabatini kwake bila ya kuupekua.
Alitoa simu yake na kumpigia tena mwenzake huku akijibwaga kitandani. Simu iliita bila majibu kwa muda mrefu mpaka ikakata yenyewe. Alishangaa kidogo kwani haikuwa kawaida ya Mwantumu ambaye kwa kawaida hupoteza karibu theluthi nzima ya siku yake kucheza na simu, kutopokea simu baada ya kupigiwa mara nyingi namna ile.
Siku zote ugomvi wake na rafikiye yule huwa ni juu ya yeye alivyokuwa mvivu kupokea simu na hata kutotumia simu ipasavyo. Ni Mwantumu ndiye aliyemfundisha na hata kumzoesha kutumia baadhi ya vitendea kazi mbalimbali vipatikanavyo kwenye simu zao za kisasa, kama vile namna ya kutumia programu za ‘WhatsApp’ , ‘Viber’ na ‘Coco’…
Hapo alikumbuka kuwa angeweza kumtumia ujumbe wa sauti rafikiye, na alipokuwa anataka kuingia kwenye moja ya zile programu za kutuma
ujumbe kwa sauti ndipo alipoona kuwa kumbe Mwantumu alikuwa
amemtumia ujumbe wa sauti kwa programu ya ‘WhatsApp’
Alipousikiliza ule ujumbe alihisi kana kwamba kile chumba kiliyumba naye, na akajikuta akiserereka kutoka pale kitandani na kuketi sakafuni
bila kujitambua.
“What the…? ”
Aliusikiliza tena ule ujumbe.
51 Hussein Issa Tuwa
“Amekimbizwa na mtu mwenye bastola… ofisini?” Alijiuliza kwa kutoelewa.
Akausikiliza kwa mara ya tatu, na akainuka kutoka pale sakafuni na kuingia msalani, ingawa hakujua kule msalani alienda kufanya nini. Akatoka na kuketi upya kitandani, akili ikimzunguka.
Sasa Mwantumu yuko wapi saa hizi?
Kasema anakuja kukaa hapa kwangu, na kweli mkoba wake nauona… but… ye’ yuko wapi sasa?
Kwanini hapokei simu?
Mtungo wa maswali ulionekana kutaka kuendelea kujizonga kichwani mwake, naye akachanganyikiwa kweli kweli.
Alimpigia tena, na ile simu ikazidi kuita tu bila majibu… kama ilivyokuwa mara zote hapo kabla.
Shit!
Akainuka na kwenda hadi kwenye meza yake ya kujipodolea, ambayo juu yale alikuwa ameweka mkoba wake aliorudi nao kutoka kule hotelini mchana ule, na kutoa kijitabu kidogo cha kumbukumbu, yaani ‘diary’ ambacho alipewa zawadi na Mwantumu. Ile diary ilikuwa imetolewa na ile kampuni ya Liquid Diamond Inc., ambayo ilikuwa ikinadi uwepo wake nchini na duniani kwa kupitia kwenye ‘diary ’ ile. Kwenye ‘diary’ ile kulikuwa kuna maelezo ya anuani za posta na namba za simu za kampuni ile.
Alitazama namba za simu za kampuni ile zilizokuwa kwenye ile diary na akiwa amejawa wahka aliipiga moja ya namba zile kwa kutumia simu yake. Baada ya miito kadhaa ile simu ilipokelewa bila shaka na dada wa mapokezi.
“Liquid Diamond Incorporated… nikusaidie tafadhali?” Dada wa mapokezi alijinadi simuni.
“Er, Helloo… yah, ni… nilikuwa naomba kuongea na Mwantumu tafadhali!” Alisema simuni, na kutokea upande wa pili wa simu ile alimsikia yule dada aliyepokea ile simu akisita kidogo.
“Oh, na… nimwambie ni nani wewe?” Alimuuliza, na Zay akasita.
Kwa nini huyu dada wa mapokezi amesita?
“Yupo ofisini au hayupo dada’angu?” Zay aliuliza tena huku akianza kupata mashaka.
Dada wa mapokezi akasita tena kidogo kabla ya kumjibu.
“Okay, subiri kidogo kwenye laini tafadhali…” Alimwambia, na Zay akakata simu.
52
MTAFITI
“Stupid me! Stupid me! Veeerrry Stuuuppid Me!!” Alijikemea huku akiwa amekunja ngumi na akizizungusha hewani kwa hasira, kisha akatimba mguu wake sakafuni kwa hasira zaidi.
Akaanza kuranda randa huku na huko mle ndani mwake akiwaza.
Mtu Mwantumu kaniambia kabisa kuwa kuna njemba imemtoa kasi na bastola mle ofisini… na amesema kabisa kuwa kule ofisini yeye tena basi. Sasa atawezaje tena kuwa humo ofisini bwege mimi?
Alijisonya na kuingia tena msalani, na kwa mara nyingine tena hakujua alikuwa amekwenda kule msalani kufanya nini. Akatoka na kuchutama katikati ya kile chumba, akiwa amejishika kichwa.
Sasa Mwantumu atakuwa wapi lakini jamani?
Na kwa nini akimbizwe na mtu mwenye bastola kutoka kule ofisini kwao?
Aliinuka na kwenda kukaa kwenye kochi lililokuwa mle chumbani kwake, bado akili ikimchemka.
Sasa mimi bwege mkubwa nimeenda kupiga simu kule kule ofisini ambako tayari nimeshaambiwa… tena kwa sauti yake mwenyewe Mwantumu… kuwa kuna jibaba limemtoa kasi na bunduki! Sasa hii ni akili kweli hii?
Alijisonya tena na kutikisa kichwa kwa kuchanganyikiwa.
Alivuta taswira ya Mwantumu akikimbizwa na mtu mkubwa mwenye bastola mkononi, na machozi yakamchonyota na donge likamkaba.
Oh, Mwantumu rafiki yangu masikini!
Alihisi haja kubwa ikimnyemelea naye akaenda jikoni. Hakujua jikoni alikuwa ameenda kufanya nini wakati sasa alikuwa ana uhakika kabisa alihitaji kwenda msalani.
Akarudi pale chumbani na kuketi kitandani.
Sasa vipi kama wale watu wa kule kwenye ile kampuni wataikamata namba yangu na kuanza kunifuatilia na mimi?
Alitoka mbio hadi chooni, na safari hii alikitumia choo kwa kujisaidia haja kubwa lakini nyepesi, huku akilia kwa kusikitikia yale yaliyomkumba rafikiye.
Luis Kambesera aliwasili kituo cha polisi akiwa na wakili wake, na baada ya kuwasubirisha kwa kama dakika ishirini hivi, yule Inspekta alikwenda kumsaili. Ingawa kulikuwa kuna mwanasheria wa kampuni, Luis na Mike
walikubaliana kuwa Luis atumie mwanasheria tofauti na yule wa kampuni
katika kujibu maswali kuhusiana na kifo cha Grayson Mochiwa ili kuiweka
53 Hussein Issa Tuwa
mbali kampuni na tuhuma zozote ambazo askari wataamua kumuangushia
Luis kuhusiana na mauaji ya Grayson.
Lengo lao lilikuwa ni kuiepusha kampuni na tuhuma zozote za kuhusika na mauaji yale, na kama angekwenda mwanasheria wa kampuni kumuwakilisha Luis pale, basi moja kwa moja ingeweza kuchukuliwa kuwa kampuni ilikuwa inahusika na mauaji yale.
Hilo lingekuwa na matokeo mabaya sana kwa kampuni yao na hivyo ni jambo waliloazimia kuliepuka kwa kila hali.
“Okay mheshimiwa… nilikuwa naomba maelezo yako kuhusiana na tukio lote la pale ofisini kwako leo hii, kabla ya yale mauaji ya kukera tuliyoyashuhudia ndani ya jengo la kampuni yako.” Inspekta alianza kudai
maelezo, pamoja naye alikuwepo askari mwingine wa kike ambaye alikuwa pale kwa lengo la kunukuu maelezo yote yatakayotokana na mahojiano yale, kwa maandishi.
Luis alikuwa ameshajipanga.
Alimueleza kuwa Grayson Mochiwa alikuwa ni mmoja wa wakurugenzi wake pale kwenye ile kampuni anayoiongoza, akiwa ni mkuu wa tafiti, ikizingatiwa kuwa kampuni yao ilikuwa ikijishughulisha na uendeshaji wa tafiti za kitaalamu kuhusiana na vyanzo vya nishati nchini. Akazidi kumfahamisha kuwa katika miezi michache iliyopita Grayson amekuwa akikabiliwa na matatizo ya kifedha, matatizo ambayo yaliathiri sana utendaji wake wa kazi.
Akaendelea kumjuza kwamba alishafika ofisini kwake kutaka kampuni ile impatie mkopo mkubwa wa kama milioni nane hivi kwa ajili ya kulipa deni alilokuwa anadaiwa na watu ambao mwenyewe alidai kuwa ni hatari sana.
Hapa Inspekta aliinua nyusi zake kwa namna ya kustaajabia habari ile, lakini Luis hakutetereka. Akaendelea kumueleza ya kwamba kwa kuwa taratibu za kampuni haziruhusu jambo kama hilo, yeye alimkatalia ombi lake hilo na kumwambia atafute namna nyingine za halali za kulipa deni hilo.
“Nakumbuka jamaa alinitolea maneno makali sana siku hiyo… lakini sikubadili msimamo wangu. Akaondoka na hakuonekana kazini kwa siku tatu!” Luis alizidi kubainisha.
“Alikwambia ni watu gani hao waliomkopesha hizo hela, na ni kwa nini alikopa pesa zote hizo?” Inspekta aliuliza.
54 MTAFITI
“Hapana… hakuniambia alikopa hizo pesa kwa sababu gani, nami sikutaka kumuuliza. Mtu sikuwa na uwezo wa kumsaidia ya nini kumhoji maswali zaidi?” Luis alimjibu.
“Hao watu wanaomdai… alikwambia ni watu gani? Alikutajia majina yao labda…?”
“Hapana bwana… yeye alichoniambia wakati ule ni kwamba hao wanaomdai walikuwa ni watu hatari sana, na alikuwa anahitaji kuwalipa ili awe na amani…” Luis alisema, kisha akainama mbele pale mezani kwa namna ya kuteta na kuongeza, “… ila kuna tetesi nilizokuwa nikizisikia kuwa jamaa… marehemu… alikuwa ni mlevi sana wa kamari. Sasa huenda alikuwa anadaiwa huko kwenye hizo kamari alizokuwa akicheza. Ni tetesi tu lakini, mi sijui!”
Inspekta alimtazama kwa muda.
“Unaweza kutaja ni akina nani waliokupatia tetesi hizo?”
Luis alibetua mabega tu.
“Tetesi ni tetesi tu… mtu huwa unazisikia tu bila hata ya kujua ni nani hasa aliyesema kwa kweli. Leo unasikia hili kutoka hapa, kesho unasikia lile kutoka pale… mwisho wa siku tetesi inajijenga kichwani. Naweza kuwa siko sahihi bwana, lakini wewe ndiye mpelelezi… lifanyie kazi hilo!”
Alimjibu kwa kujiamini, na yule Inspekta akamchukia zaidi.
“Nitalifanyia kazi… usihofu. Niambie ilikuwaje hata marehemu akawa amekunyooshea bastola pale kwenye kile chumba chenu cha mikutano leo hii, ukiwa na wale wenzako.” Inspekta alisaili zaidi.
Luis alijitia kusikitika kwa muda.
Akauma midomo yake kama mtu anayejitahidi kuiziba kumbukumbu mbaya kutoka kwenye akili yake, na hata akafanikiwa kupata mlengolengo wa machozi machoni mwake.
“Ni hali ya kusikitisha kwa kweli…”
“Ndio tuelezee hiyo hali sasa!” Inspekta alimjia juu.
Luis alijikohoza kidogo, halafu akamtazama mwanasheria wake kama anayemtaka ushauri iwapo aeleze juu ya suala lile au la. Mwanasheria akamtikisia kichwa kuashiria kuwa aendelee tu kutoa maelezo aliyotakiwa.
Na ndipo Luis Kambesera alipomchafua vibaya sana hayati Grayson Mochiwa mbele ya yule Inspekta.
“Kama nilivyokwambia afande… Grayson alitoweka pale ofisini kwa siku tatu bila taarifa zozote baada ya mimi kumkatalia ombi lake la mkopo.
55
Issa Tuwa
Hussein
Kazi zikalala. Sheria za kazi zinasema wazi kuwa mfanyakazi asipoonekana
kazini kwa siku tatu mfululizo bila taarifa zozote kwa mwajiri basi huwa amejifukuzisha kazi mwenyewe…”
“Hata kama ni mkurugenzi?” Inspekta alidakia.
“Hata kama ni mkurugenzi… naye si mwajiriwa tu? Yeye angeweza
kunipigia simu tu na kunitaarifu kuwa ana tatizo au udhuru hiyo ingetosha… hakufanya hivyo!” Luis alizidi kumfitini marehemu.
“Kwa hiyo?”
“Kwa hiyo tulichukua jukumu la kumfukuza kazi… tukamwandikia barua iliyomtangazia nia yetu hiyo kwake na kumpa nafasi ya yeye kujieleza kwa nini hatua hiyo isichukuliwe dhidi yake. Nakala za barua hiyo zipo
kama mkizihitaji...”
“Kwa hiyo nd’o akakutolea bastola baada ya kupata barua hiyo? Mbona inaniwia vigumu kuamini, hasa ukizingatia kuwa uchunguzi wangu umeonesha kuwa jamaa alikuwa msomi mwenye PhD, jambo linaloniambia kuwa uwezo wake wa kufikiri na kuchanganua mambo ni mkubwa tu?” Inspekta alisaili.
Luis akasita kidogo.
“Afande, nadhani we’ umetaka maelezo. Mteja wangu anakupa maelezo. Kama una mashaka na maelezo yake unaweza kuchukua hatua zozote utakazoona zinafaa ndani ya misingi ya sheria, lakini sio kumbishia anayokueleza!” Mwanasheria wa Luis aliingilia kati, na Inspekta akamkata jicho kali.
“Haya ni mahojiano wewe… sio maelezo ya upande mmoja!” Alimkoromea, kisha akamgeukia Luis.
“Jibu swali hilo bwana!” Alimkoromea.
Ilikuwa zamu ya Luis kumkata jicho yule Inspekta.
“Okay… yeye hakutushikia ile bastola pale kwa ajili ya ile barua...” Luis alianza kujieleza, na Inspekta akamkatisha tena.
“Nilichoona mimi wakati naingia mle ndani ni kwamba alikuwa amekuwekea wewe bastola kichwani, na sio wewe na wale wengine mle ndani. La hasha… ni wewe peke yako nd’o ulikuwa umewekewa mtutu wa bastola kichwani!”
Luis alitetereka kidogo.
“Ah, ndio hivyo bastola ilikuwa kichwani kwangu, na wote wengine walizuiwa wasitoke mle ndani ama si hivyo angenilipua. Sa’ mi’ naona hiyo
56
MTAFITI
ilimaanisha kwamba sote tulikuwa tumetaitiwa pale!” Jamaa hakukosa jibu la kujitetea.
“Endelea!”
“Sawa.” Luis alisema na kumung’unya midomo kwa muda kabla ya kuendelea, “Kile kilikuwa ni kikao cha kumjadili yeye na hatima yake, na ndio maana hakuitwa kushiriki kikao kile. Matokeo yake akavamia kikao kile na kushurutisha apewe hela akalipe deni… akisema kuwa amekuwa akijificha kwa siku tatu mfululizo kuhofia maisha yake… na kudai kuwa watu wamekuwa wakimfuata nyuma kila aendapo na pale alikuwa amefanikiwa kuwatoroka ndio akaingia mle ofisini… Mi’ nikamwambia hatumuelewi, na kwamba kuanzia muda ule yeye hakuwa mfanyakazi wetu tena, ya kwamba kile kikao kilikuwa kinapitisha maamuzi kuhusu barua aliyoandikiwa ambayo hakuijibu. Hapo ndipo alipotoa bastola na kunitishia… tena akasema mbele ya kila mtu mle ndani kuwa amepewa muda mpaka saa nne asubuhi ile awe amelipa hizo hela ama si hivyo anauawa!”
“Mnh!” Inspekta akaguna.
“Ndiyo! Kwa hiyo akasema kama sisi tunaidhinisha kifo chake kwa kukataa kumpa hizo hela atakazo, basi bora yeye aanze kutuua sisi… akianzia na mimi!” Luis aliongopa akiwa macho makavu, na Inspekta akabaki mdomo wazi.
“Na… unataka kuniambia kuwa wote wale waliokuwemo mle ndani walisikia hayo maneno?”
“Si ulisema utahitaji kuwahoji na wao? So what happened? Hukuwahoji tena? Nenda kawahoji na wao usikie watakalokuambia, lakini hivyo ndivyo ilivyokuwa. Jamaa alinitolea bastola akisema kuwa hayuko tayari kufa wakati anajua thamani yake kwenye kampuni hii ni zaidi ya hizo milioni nane azitakazo…” Luis alimjibu, na kubetua mabega.
Inspekta alimtazama yule jamaa kwa hasira, akilini akikumbuka hali aliyokutana nayo alipokuwa akiwahoji wale watendaji wengine wa ile kampuni tata.
“Sio kazi yako kujua kama niliwahoji au la… nataka jibu lako. Walisikia yote haya unayonieleza kuwa yalijiri mle kwenye chumba cha mikutano?”
Alimuuliza kwa ukali.
“Sasa wataachaje kusikia wakati nao walikuwa mle ndani Inspekta? Of Course walisikia!” Luis alimjia juu.
Inspekta akaguna.
57 Hussein Issa Tuwa
“Basi kama walisikia yote haya hakika wote walikuwa wana ugonjwa wa kusahau maana hakuna yoyote kati yao aliyegusia juu ya hayo ya kufanya kikao cha kumjadili Grayson na azma ya kumuachisha kazi…” Alimjuza huku akimtazama kwa macho makavu.
Luis akameza mate na kumkodolea macho Inspekta akapata uhakika juu ya uongo wa yule jamaa, na kujithibitishia ile hisia yake ya awali kuwa ile kampuni ilikuwa inahusika na kifo cha Grayson.
“Walichofanya wakurugenzi wako ni kunipa majibu yanayofanana kama kwamba walikuwa ni wanafunzi waliokaririshwa majibu ya mtihani!”
Inspekta alisema kwa kebehi ya wazi.
“Hiyo ni shutuma dhidi ya mteja wangu afande?” Wakili wa Luis alidakia. Inspekta akamkata jicho kali.
“We’ unaonaje wakili… hudhani kuwa hiyo yaweza kuwa ni shutuma itakayomfaa mteja wako?”
Wakili alifinya sura mithili ya mtu anayejitahidi kubana ushuzi mkali, lakini hakutoa jibu.
Inspekta akamgeukia Luis.
“Kwa hiyo baada ya Grayson kukuambia kuwa atawaua wote mliokuwa mle ndani akianzia na wewe… nini kilifuata?” Akamuuliza, na Luis hakusita.
“Well… inaonekana jamaa waliokuwa wanamsaka walikuwa karibu naye kuliko alivyodhani… wakamuua!” Alimjibu kirahisi na kubaki akimtazama Inspekta kwa macho ya kusubiri swali jingine.
Inspekta alishusha pumzi ndefu na kumgeukia yule askari wa kike aliyekuwa anaandika yale maelezo.
“Umeyapata maelezo yote hayo mpaka hapo?” Alimuuliza, na yule askari akakiri kuwa ameyapata maelezo yote yale kwenye maandishi.
“Okay… kwa hiyo unataka kuniambia kuwa hao watu waliokuwa wanamdai Grayson milioni nane, ambao hata hawajulikani waliko, ndio waliomuua kwa kumdungua kwa risasi asubuhi hii?” Alimuuliza, na Luis akatoa sauti ya kukereka na swali lile.
“Akh! Mi’ nakueleza kile kilichojiri asubuhi hii kama jinsi ninavyojua… wewe ndiye Inspekta hapa, sio? Fanya upelelezi wako basi kujua iwapo hao waliomuua ndio hao waliokuwa wakimdai au vinginevyo!”
Inspekta alimtazama kwa muda mrefu bila ya kusema neno. Kisha bila kuondoa macho yake usoni kwa Luis alimwambia yule askari aliyekuwa akirekodi yale maelezo yake kwa maandishi.
58
MTAFITI
“Mpe bwana Luis Kambesera hayo maelezo ayasome kuona kama yako
sahihi kama alivyoyaeleza, Koplo!”
Koplo alimpa Luis yale maelezo aliyoyaandika.
Badala ya kuyapokea, Luis akamuashiria kuwa ampe mwanasheria wake, ambaye aliyapokea na kutumia muda mrefu kuyasoma. Muda wote
wakati mwanasheria anasoma maelezo yale, Inspekta na Luis walikuwa wanatazamana bila ya kuambiana lolote kwa midomo yao, ingawa macho yao yaliambiana mengi—yale ya Inspekta yakimwambia Luis kuwa alikuwa
hamuamini kwa asilimia mia moja, na yale ya Luis yakimwambia Inspekta
kuwa alikuwa hajali iwapo amemuamini au la, ila maelezo yake ndio hayo.
Fukuto lilikuwa linaelea baina ya watu wale wawili waliokuwa pande mbili tofauti za sheria.
“Maelezo yako sawa… unaweza kusaini!” Mwanasheria alisema, na ndipo Luis alipobandua macho yake kutoka kwa yule Inspekta na kusaini maelezo yake. Kisha yule mwanasheria naye akasaini sehemu inayomhusu kwenye ile karatasi maalumu ya kuchukulia maelezo na alipomaliza akamsukumia yule Inspekta yale maelezo pale mezani, naye akayapokea na kusaini sehemu inayomhusu.
“So, twaweza kwenda sasa Inspekta?” Luis alimuuliza.
Kwa kama nusu dakika zaidi, Inspekta alibaki akimtazama machoni bila ya kufanya bidii yoyote ya kuficha hisia alizokuwa nazo dhidi ya yule kiongozi wa ile kampuni kubwa ya tafiti za nishati nchini, kabla ya kumjibu.
“Muwe makini tu msijigonge mlangoni wakati mnatoka!”
Luis na mwanasheria wake walitoka nje ya kile chumba cha mahojiano huku wakitikisa vichwa.
Sehemu nyingine ya jiji, Zay alitoka msalani huku akijihisi kurudiwa na utulivu kiasi. Alijifuta machozi na kujaribu kufikiri kwa kituo juu ya hatua mwafaka ya kuchukua. Jambo la kwanza alilofikiri lilikuwa ni kwenda kutoa ripoti polisi.
Halafu akalifuta wazo hilo kwa muda.
Alijua kuwa polisi huwa hawachukui hatua ya kumsaka mtu aliyepotea mpaka baada ya saa ishirini na nne tangu asemekane kuwa amepotea.
Sasa Mwantumu hakupotea. Mwantumu alikuwa hapokei simu tu, na hilo sio la kuripoti polisi. Lakini pia ule ujumbe kuwa alikuwa amekimbizwa
59 Hussein Issa Tuwa
na jibaba lenye bastola kutoka kule ofisini ulitosha kumfanya akatoe ripoti polisi, akihofia usalama wa rafikiye.
Lakini polisi watamuelewa?
Watajua wenyewe. Mi’ n’tapeleka ripoti tu.
Lakini kwanza aliamua kujihakikishia kwa mara ya mwisho. Akaipiga tena namba ya rafikiye na hali ikawa ile ile. Alikuwa anataka kuiweka simu mfukoni ile aende polisi kutoa maelezo wakati wazo jipya lilipomuingia. Haraka alienda kwenye ile sehemu ya ujumbe wa sauti wa ‘WhatsApp’ aliotumiwa na Mwantumu na kutazama kama Mwantumu aliacha wazi ile programu iliyopo kwenye ‘WhatsApp’ ambayo iliwezesha kuonesha mahala alipo mwenye simu husika.
Ilikuwa wazi!
“E Mama we!” Alimaka kwa kiherehere huku akibofya kile kijimshale kilichowezesha kutafuta mahala mwenye simu iliyomtumia ujumbe alipo, na mara moja ramani ya mitaa ya Dar ikajitokeza na kimshale kikaonesha mahala simu ya Mwantumu ilipokuwa muda ule, na kinywa kikamuanguka Zay.
Kile kimshale kilionesha kuwa ile simu ipo Chang’ombe mtaa wa Mkamba, na kwa maana hiyo Mwantumu, yuko Chang’ombe mtaa wa Mkamba.
“Nyumbani kwake?” Alimaka kwa mshangao.
Bila kujishauri zaidi, alikwapua mkoba wake na kutoka mbio nje ya nyumba yake huku akipekua ndani ya mkoba ule kutoa ufunguo wa gari lake.
Huko nje, alijitosa ndani ya gari lake dogo aina ya Toyota Vitz na kuondoka kwa kasi kuelekea Chang’ombe, moyo ukimwenda mbio huku akijiuliza ni lipi litakuwa limemkuta Mwantumu kule nyumbani kwake hata akashindwa kupokea simu mara zote zile alizokuwa akimpigia.
Alizidisha kasi kuwahi kule nyumbani kwa rafiki yake kipenzi…
Dakika kumi na tano baada ya kutoka kusema uongo kule kituo cha polisi, Luis Kambesera aliingia ofisini kwa afisa usalama wa kampuni, na kumkuta Chabbi Cheka akiwa ameketi nyuma ya meza yake ilhali miguu ameipandisha juu ya meza ile.
“Okay, nimeshamalizana na yule askari mpuuzi… sasa niambie hali ikoje!” Alisema.
60
MTAFITI
“Funga mlango uketi bosi…” Chabbi alimwambia.
Luis alifanya alivyoshauriwa, na Chabbi akamuelezea kila kitu alichofanya tangu pale aliposikia ile kengele ya tahadhari iliyobonyezwa na Luis ikiunguruma mle ofisini kwake, hadi pale alipomuondoa Grayson duniani.
Kimya kilitanda kwa muda.
“Yah! Umefanya lililotakiwa Chabbi… hali ilikuwa tete.” Luis alisema, na Chabbi akaguna tu. Kuua mtu kwake halikuwa jambo kubwa sana.
“Unajua kama Grayson angeangukia mikononi mwa polisi, hatujui angeropoka maneno gani huko… lakini nakuhakikishia kuwa yasingekuwa ya kutupamba na kutusifia. Jamaa angetuharibia kila kitu!” Luis alisema.
“Yeah… hilo tulishalijadili mbona bosi? Ila kiutaratibu ingeleta mashaka sana kama pamoja na tafrani yote ile aliyoanzisha, bado tungeacha kupiga simu polisi …”
“Kweli!” Luis alikubaliana naye.
“Anyway, mi’ nilitaraji wale polisi wakimzonga angeweza kuhamanika na kuanzisha mashambulizi, na kuwalazimisha polisi wamuue. Hiyo ingekuwa poa sana kwetu… lakini nd’o haikuwa. So nilipoona ameamua kujisalimisha
nikajua hamna jinsi… nikamaliza mchezo!” Chabbi alimwambia.
“Ilikuwa ni hatua mwafaka sana! William alishafanikiwa kufuta kila kitu kwenye kompyuta zake. Grayson angeweza kutufanyia taabu kama
angeanza kuropoka hovyo juu ya hili suala, lakini kwa kuwa sasa kikwazo
pekee kilichobaki kimeshaondoka, shukrani za dhati zije kwako kwa kufanya litakiwalo kwa wakati utakiwao, tunaweza kusema kuwa tuko
salama kuendelea na mpango wetu kama tulivyopanga…” Luis alisema, na akaona Chabbi akitikisa kichwa.
“Siwezi kusema hivyo kwa asilimia mia moja Luis…”
“What… kuna nini? Au ndio hicho kimeo ulichoniambia kwenye simu?”
Luis aliuliza, sasa akiwa na mashaka kidogo.
“Yap… kuna kimeo kimoja, lakini nadhani mpaka sasa nitakuwa nimeshakidhibiti…”
“Kipi hicho? Na umekidhibiti kivipi?”
Chabbi alimtazama kwa muda.
“Unakumbuka tulikubaliana kuwa tumfuatilie Grayson kwa kila afanyalo hapa ofisini sio?” Alimuuliza, na kabla Luis hajajibu, akaendelea, “Basi nilikuwa nafanya hivyo kupitia kwenye hii kitu hapa…” Aliioneshea ile runinga kubwa mle ofisini kwake.
61
Issa Tuwa
Hussein
Luis alionekana kumakinika, akisikiliza maelezo yale.
“Na…?”
“Na nikamuona Grayson akimkabidhi yule binti wa field hapa… Mwantumu, makabrasha fulani kutoka kwenye droo ya meza yake huku akionekana wazi kuwa amehamanika. Na yule binti naye aliyasweka yale makabrasha kwenye mkoba wake…”
“Ah! Hiyo ni mbaya sana! Umefanikiwa kuyapata hayo makabrasha sasa? Yalikuwa yana taarifa gani?” Luis Kambesera aliuliza kwa wahka.
“Hilo bado nalifanyia kazi, bosi.”
“What do you mean bado unalifanyia kazi? Huyo binti yuko wapi sasa? Huwezi kuacha kimeo kama hicho Chabbi!” Luis alimaka.
“Relax boss. Binti yuko kwenye himaya yetu, ila makabrasha bado hatujayatia mkononi” Chabbi alimwambia.
“Sikuelewi, Cheka!”
Chabbi Cheka akamuelezea kila kilichojiri baina yake na Mwantumu. Jasho la wazi lilianza kumvuja Luis, ingawa mle ndani kulikuwa kuna kiyoyozi.
“Sasa mbona hukusachi humo chumbani kwake…? Haiwezekani kuwa ameyaficha humo ndani?”
“Haiwezekani… kwa kuwa mimi nimekwenda kumsubiri yeye pale kwake, na nikamuona akifika bila ya ule mkoba alioondoka nao hapa, ambao ulikuwa na yale makabrasha. Yule atakuwa ameyaficha mahala yale makabrasha…”
“Kwa maana hiyo hayo makabrasha yatakuwa na habari mbaya kwetu! Kama si hivyo kwa nini ayafiche? Mkamue mpaka aseme Chabbi!” Luis alisema.
“With pleasure!” Chabbi alimjibu, akimaanisha kuwa hilo atalifanya kwa furaha tele. Kimya kilitanda mle ndani kwa muda, kisha Luis akainuka.
“Hakikisha unapata hayo makabrasha Chabbi… na usiache kimeo chochote kikining’inia!” Alisema kwa msisitizo na kutoka nje ya ofisi ile akiwa amejawa wahka mkubwa.
Chabbi alibaki akiwa amekunja uso kwa mawazo mle ofisini. Kisha akampigia simu msaidizi wake.
“Njoo hapa ofisini Bilanga!” Alisema na kukata simu, na dakika tano baadaye Bilanga aliingia. Kwa dakika kama ishirini zilizofuatia, watendaji wale wa mambo yote mazito ndani ya kampuni ile walipeana habari ya
62
MTAFITI
yaliyotokea kwa kila mmoja wao.
“Sasa nataka urudi kule chumbani kwa yule binti ukakipekue kile chumba juu chini! Sidhani kama utakuta kile ambacho Grayson alimpa yule binti leo hii, lakini huenda kuna vingine vya kutuhusu ambavyo labda alivipata kabla ya leo!” Chabbi alimwambia, kisha akampa maelekezo ya namna ya kufika huko.
“Sio ishu bosi, hilo limefanyika. Je, nitawezaje kuingia humo ndani mwake? Una ufunguo…?”
“Mlango uko wazi ule… hatukuufunga wakati naondoka naye pale. Fanya fasta uende!” Chabbi Cheka alisisitiza.
“Poa. Niko njia moja hivyo… Sasa wewe utakuwa hapa muda wote?”
Bilanga alisema na kumuuliza huku akianza kutoka mle ofisini.
“Hapana. Mimi narudi kwa Mwantumu… naamini kufikia sasa atakuwa ameshakumbuka mahala alipouficha ule mkoba wenye makabrasha aliyopewa na Grayson!”
Zay aliteremka kutoka kwenye gari lake na kuiendea nyumba ambayo Mwantumu alikuwa amepanga huku akitazama kulia, kushoto, na nyuma yake kwa mashaka. Mchana ule mtaa ulikuwa kimya ilhali baadhi ya akina mama wachache wakiwa wameketi nje ya vibaraza vya nyumba zao.
Aliingia kwenye geti la nyumba ile na kuzungukia ubavuni mwake ambako chumba cha Mwantumu kilikuwa kimejichomeka upenuni kabisa mwa nyumba ile, kama kwamba kujengwa kwake kulikuwa ni matokeo ya maamuzi ya ghafla tu ya mwenye nyumba, baada ya kuwa ameshajenga ile nyumba kubwa.
Aliufikia mlango na kujaribu kuingiza ufunguo, na akashangaa kuona ule mlango ukijifungua taratibu baada ya kuugusa kidogo tu.
Kengele za hatari zikaanza kuvuma kichwani mwake.
Ama! Ina maana hakufunga mlango huyu?
“Mwammy!” Aliita huku akiusukuma ule mlango na kuingia ndani.
“Mwaam… eh!” Alianza kuita tena huku akiingia mle ndani, na hapo ndipo alipoishia, akasimama ghafla huku macho yakimtoka pima. Hali aliyoikuta mle ndani haikumpa amani hata kidogo kwani kwanza
Mwantumu hakuwemo kama alivyotarajia, na pili kile chumba kilimpa
63 Hussein Issa Tuwa
hisia kuwa kulikuwa kumetokea msukumano au mvurugano fulani. Kitanda kilikuwa kimevurugika, kochi lilikuwa limesukumwa pembeni kidogo, na begi la rafikiye lilikuwa limelalia ubavu sakafuni, wakati mkoba wa kompyuta yake mpakato ulikuwa umetupiwa nyuma ya lile kochi.
“Mmh!” Aliguna huku wasiwasi ukimvaa.
Kitu kimoja alichokijua kuhusu Mwantumu ni kwamba hata siku moja huwa haachi kitanda chake kikiwa hakijatandikwa. Hata kama alikuwa amejilaza kidogo tu, muda atakapoamka tu basi atahakikisha anatandika kitanda.
Sasa hii ya Mwantumu kutoka bila ya kutandika kitanda namna hii! Hapana, hakukuwa sawa kabisa pale.
Hiyo, akichanganya na namna lile kochi lilivyobaki likiwa limesukumwa pembeni namna ile na mabegi ya rafikiye yakiwa yametupwa shaghalabaghala mle ndani, vilimjuza kuwa kutokuwepo kwa rafikiye mle ndani hakukuwa kwa heri hata kidogo.
Lakini si niliona kupitia ile programu ya kutambua sehemu ambako simu yake ilikuwapo kuwa yuko hapa?
Ni wazi kuwa kama alikuwepo ila sasa hakuwepo tena. Atakuwa wapi sasa?
Aliitazama tena ile programu iliyokuwa kwenye simu yake, na akapata viulizo vikubwa akilini pale ilipozidi kumuonesha kuwa Mwantumu bado alikuwa pale pale Chang’ombe, mtaa wa Mkamba. Wahka ukampanda maradufu na kwa mara nyingine akatoa simu yake na kuipiga namba ya Mwantumu.
Ndipo alipoisikia ile simu ikiita kutokea chini ya kochi.
“Khah!” Alimaka huku akilisukuma pembeni lile kochi na kupeleka mkono wake kule uvunguni.
Alibaki akiwa amepiga magoti pale sakafuni huku akiitazama simu ya rafikiye ikiita mkononi mwake.
Mungu wangu!
Hawa watu wamemfanya nini Mwantumu lakini?
Na ni watu gani hao?
Aliinuka akihisi akili ikimzunguka, miguu ikimuwia uzito na mikono ikimtetema. Alibadili mkao na kuketi pale sakafuni badala ya kupiga magoti.
Nifanyaje sasa Mungu wangu… nini nifanye mimi?
64
MTAFITI
Alijua kuwa alitakiwa afanye kitu, kwani ilikuwa wazi kwake sasa kwamba Mwantumu alikuwa amefanyiwa kitu kibaya. Amefikwa na mabaya.
Roho ilimuuma.
Sasa ni nani kama si muovu aliyekubuhu tu atakayediriki hata kufikiria kumuumiza Mwantumu jamani?
Hasira zilianza kumfukuta na machozi yakaanza kumbubujika.
Aliipekua simu ya Mwantumu hadi akaipata namba ya mama mzazi wa yule rafiki yake, aliyekuwa akiishi Gezaulole ambako Mwantumu hakupenda kukaa kutokana na kuwa mbali na mjini. Alimuuliza yule mama iwapo Mwantumu alifika kule kwake, na akazidi kukata tamaa alipoambiwa kuwa huko pia hakuwepo.
“Kwani vipi mwanangu… kuna tatizo?” Mama Mwantumu alimuuliza kwa mashaka kidogo, na Zay akauma meno na kufumba macho kwa uchungu.
Nimwambie nini sasa?
“Tatizo lipo mama... kwani mpaka sasa sijui Mwantumu yuko wapi, na amenitumia ujumbe wa simu kuwa amepata matatizo kule ofisini alipokuwa akifanya mafunzo kwa vitendo…” Alimwambia huku roho ikimuuma.
Hakuweza kumdanganya yule mama kuwa hakukuwa na tatizo, wakati tatizo lilikuwepo. Tena kubwa sana. Hakuwa na maelezo mengine ya kumueleza yule mama wa watu.
Mama naye akazidi kumjaza wahka, akimuuliza maswali ambayo hakuwa na majibu kwayo, na akaanza kupayuka kwa vilio vya maombolezo simuni kama kwamba amefiwa.
Kwa namna fulani aliweza kumshawishi yule mama atulie wakati yeye anaendelea kufuatilia habari za mwanaye, kwa ahadi kuwa atamjulisha atakalofanikisha.
Alipokata simu alibakiwa na wazo moja tu kichwani mwake.
Lazima nikaripoti polisi… tena haraka sana!
Na kutokea nje ya chumba kile akasikia hatua za mtu zikielekea pale mlangoni kwa Mwantumu…
65
Issa Tuwa
Hussein
BILANGA, AKIWA NDANI ya mavazi ya mfanyakazi wa shirika la umeme Tanzania, alisukuma mlango wa chumba cha Mwantumu kwa mkono uliovikwa glovu na kuchungulia ndani. Chumba kilikuwa kitupu.
Akajitoma mle chumbani na hapo hapo akajifungia kwa komeo mle ndani. Alisimama katikati ya chumba na kuzungusha macho yake kwenye kila pembe ya chumba kile, kisha akaiendea meza ndogo iliyokuwa kwenye kona moja, juu yake kukiwa na madaftari, vitabu na makabrasha kadhaa. Alipekuwa vile vitabu kwa muda na kuona kuwa vilikuwa vinahusiana na masomo tu. Akahamia kwenye mkoba wa kompyuta mpakato ya Mwantumu na kuufungua, na kuona kuwa kulikuwa kuna ile kompyuta tu, na hakukuwa na makaratasi wala makabrasha yoyote mengine. Aliufunga ule mkoba na kuupachika begani.
Akaliendea lile begi la nguo lililokuwa limelalia ubavu kando ya kitanda pale sakafuni. Aliketi pale kitandani na kuanza kulipekua kwa pupa lile begi.
Kutokea chini ya uvungu wa kile kitanda, Zay alikuwa anakaribia kupoteza fahamu kwa woga. Alibaki akiikodolea macho miguu ya yule mtu ambaye hakumuona sura, akiwa amekaa pale kitandani, akitupatupa nguo za rafikiye huku na huko mle ndani kutoka kwenye lile begi.
Alikuwa anatetemeka vibaya sana kule uvunguni na woga aliokuwa nao ulimfanya ahisi kuwa yule jamaa angeweza kumsikia akipumua kule chini.
Akabana pumzi na kuanza kuomba dua kimya kimya, yale machozi ya hasira yaliyokuwa yakimbubujika hapo mwanzo, sasa yakashuka hadhi na kuwa machozi ya woga, huku yakitoka kwa wingi zaidi.
Na hata pale alipokuwa akibana pumzi na kujizuia kuangua kilio cha
66 MTAFITI
5
sauti kule chini, jamaa aliangusha kikopo kirefu cha uturi wa kujipulizia kutoka kwenye lile begi, na kile kikopo kikasererekea kule kule uvunguni. Ohooo…!
Alimsikia jamaa akisonya akiwa pale kitandani na hapo aliona akipeleka mkono wake uliovikwa glovu kule uvunguni ilhali bado akiwa ameketi pale kitandani kujaribu kukiokota kile kikopo.
Sasa hicho kikopo we’ cha nini tena?
Zay akapata hamu kubwa ya kwenda haja ndogo.
Mkono wa jamaa ukapapasa kulia ukakiacha kikopo kikiwa upande mwingine, ukapapasa kushoto, ukakikosa kikopo kikiwa milimita chache kutoka kwenye mkono ule.
Jamaa akasonya tena huku akijivuta chini zaidi, na Zay akaona kuwa sasa jamaa alikuwa anaelekea kuinama na kuchungulia kule uvunguni, na akajua kuwa hapo ndipo maisha yake yatakapohitimika.
Na hata lile wazo lilipokuwa likipita kichwani mwake aliuona mkono wa yule jamaa ukijisukuma ndani zaidi ya uvungu ule kiasi cha kukaribia kumgusa usoni!
Ubaridi ukamtambaa na akahisi moyo wake ukicheza chakacha ndani ya kifua chake. Taratibu sana alizishindilia mfukoni zile simu mbili zilizokuwa mikononi mwake, na ule mkono ukarudi tena kule kushoto kilipokuwa kile kikopo.
Ee Mungu hebu nisaidie basi japo kidogo jamani!
Alipeleka mkono wake taratibu na kukishika kile kikopo huku akihisi moyo ukiwa unataka kumchomoka kutokea kinywani mwake, na akawa anamsogezea yule jamaa kile kikopo ili akishike na aache kuuhangaisha ule mkono wake kule uvunguni. Na wakati anamsogezea kikopo kile, na huku mkono wake ukitetemeka vibaya sana, jamaa naye akasonya kule
kitandani huku bado amekaa na akaupeleka ule mkono wake kule kule
kilipokuwa kile kikopo kwa nguvu huku akiuzamisha ndani zaidi ya uvungu ule mkono naye akipiga goti.
Wakagusana mikono!
Ayyaaah!
Muda mkono wake ulipogusana tu na ule wa yule mtu Zay alijikuta
akiukamata kwa nguvu ule mkono bila hata ya kufikiri, na hapo hapo akimsikia yule jamaa akiachia mguno wa mshituko kule juu ya kitanda.
Kwa woga mkubwa na bila ya kujua alilokuwa analifanya, Zay aliuvuta
67
Issa Tuwa
Hussein
kwa nguvu ule mkono kule uvunguni huku akigumia, na bila kupenda
Bilanga alipiga mweleka, mkono wake ukivutiwa nyuma kupitia katikati ya miguu yake kutokea kule uvunguni na akapigiza paji lake la uso vibaya sana sakafuni. Ukelele ulimtoka, na akabaki akiwa amesambaratika pale sakafuni kama mtu anayesujudu ilhali mkono wake mmoja ukiwa umevutiwa uvunguni kupitia katikati ya miguu yake.
Moyo ukimdunda na mwili ukiwa unamchemka kwa mhemko wa woga wa kile kitakachomkuta pindi yule jamaa atakapokaa sawa na kumtia mikononi, Zay alijua kuwa pale alikuwa ameshalikoroga, na kilichobaki ni kulinywa tu. Alizidi kuung’ang’ania mkono wa yule mtu kwa mikono yake yote miwili kutokea kule uvunguni na akazidi kumvutia yule mtu kule uvunguni ili kumkosesha utulivu wa kupanga mashambulizi dhidi yake.
“Aaaarghh, weweeeee!” Bilanga alipiga kelele kwa hamaniko huku akijitupa huku na huko pale sakafuni ili kuunasua mkono wake kutoka kwenye ile himaya dhaifu lakini iliyomuweka katika mkao mbaya kiasi cha kumfanya ashindwe kutumia maguvu yake ipasavyo.
Ah! Huyu nikimwachia ataniua tu huyu…!
Zay aliwaza kwa woga hali akiwa amezidi kumng’ang’ania yule mvamizi huku akilia wazi wazi. Walikukurushana katika hali ile kwa sekunde kadhaa na Zay akaona kuwa jamaa lilikuwa linaelekea kumshinda nguvu.
Sasa woga wake ukamezwa na utashi wa asili wa kuokoa maisha yake.
Alipiga ukelele kwa hasira na akajikurupusha wima kutoka kule uvunguni
huku bado akiwa amemng’ang’ania yule jamaa mkono, akizivurumusha
chaga za kile kitanda pamoja godoro lake, ambalo lilimuangukia Bilanga
pale chini.
Haraka sana aliuachia ule mkono na kujirusha juu ya lile godoro
lililokuwa limemfunika Bilanga aliyekuwa anahangaika kujiinua kutoka
pale chini, na kumkandamiza tena kule kule. Kishindo kingine kilisikika pale Bilanga alipobamiza tena kichwa chake pale sakafuni, mguno wa hasira na maumivu ukimtoka, na Zay akazidi kujithibitishia kuwa jamaa akimtia
mikononi hakika atajuta kuzaliwa. Alijirusha tena juu na kujiangusha tena pale juu ya lile godoro, akimshindilia tena yule jamaa pale sakafuni, kisha akaruka pembeni, akaukwapua ule mkoba wa kompyuta mpakato ya rafikiye uliokuwa umeanguka pale sakafuni na kuuwahi mlango.
Haukufunguka na Zay akalia kwa fadhaa.
“N’takuua m’mi wewe (akamtukania mama yake)!” Bilanga alibwata huku
68
MTAFITI
akilitupa pembeni lile godoro na kusimama.
Mlango ulikuwa umekomewa kwa ndani!
Zay aligeuka huku akilia na kunyanyua chaga moja ya kitanda kile na kumsukumia yule mtu, kisha akafungua lile komeo kwa pupa na kujitupa nje ya chumba kile. Bilanga alilipangua lile chaga, lakini akapoteza mwelekeo na kuanguka tena sakafuni. Alijiinua haraka, tusi likimtoka hali akipepesuka na akiangaza huku na huko mle ndani, akili ikimuwanga.
Alimuona Zay akiishia nje ya kile chumba.
“WEWEEEEEE!” Alimpigia ukelele huku akimrukia mzima mzima pale mlangoni, lakini Zay aliwahi kuruka nje huku akilia na kuubamiza ule mlango kwa nje.
Kule ndani Bilanga alipiga mweleka chini ya ule mlango baada ya kumkosa adui yake, na akajiinua haraka kuwahi kuufungua ule mlango ili amfuate kule kule nje yule mtu aliyemkurupusha kijinga sana mle ndani, na kule nje Zay akawahi kuubana kwa komeo la nje ule mlango.
Kule ndani Bilanga akakwama, ukelele wa ghadhabu ukamtoka.
“MWIZIII… mwiziiii…! Jamani kuna mwizi ndani kwa Mwammyyyy…!”
Zay alikuwa akipiga kelele huku akikimbia kama vile yeye ndiye mwizi, rasta zikimpeperuka nyuma yake. Alitoka mbio nje ya geti na kuliparamia gari lake, na mlango ukagoma kufunguka.
“AAAAAHRGH!”
Akajaribu kuufungua tena, kwa mara nyingine mlango ukagoma. “Heeeeehhhh”
Akakumbuka ufunguo.
Akautoa kutoka kwenye mfuko wa suruali yake na kubonyeza kitufe cha kutoa loki za milango huku akitetemeka na machozi yakimmwagika, nyuma yake alisikia mayowe ya watu kadhaa, bila shaka ni kutokana na zile kelele alizopiga, lakini yeye hakujali tena.
Alijitupa ndani ya gari lake na kuchomoka kwa kasi kutoka eneo lile, huku akitupia macho kule nyuma kupitia kwenye kioo chake cha kuonea
nyuma, akitaraji kumuona mtu mkubwa akitoka mbio nje ya geti la ile
nyumba ya akina Mwantumu akilikimbiza gari lake.
Huko nyuma aliona kikundi cha watu wachache tu waliokuwa wamegeuzia
nyuso zao kule alipokuwa akitoweka na gari lake lakini hakuona mtu
mkubwa akitoka nje ya geti la nyumba aliyopanga Mwantumu. Alikunja
kona na kutoweka kutoka kwenye ule mtaa.
69 Hussein Issa Tuwa
Aliendelea kuendesha gari kwa kasi huku akilia bila ya kujua alikuwa anaelekea wapi. Yaliyomkuta yalikuwa ni makubwa sana na hakuwa na akili ya kujua alipokuwa akielekea. Baada ya kuendesha kwa muda bila ya kuwa na uelekeo maalum akaanza kuhisi kutetemeka mwili mzima kiasi akashindwa kabisa kuendesha gari.
Aliliegesha gari kando ya barabara na kujifungia milango yote kwa ndani, kisha akaulalia usukani wa gari lake na kuangua kilio kikubwa sana.
Muda mfupi baada ya Bilanga kutoka pale ofisini kwake kwenda kutekeleza yale aliyomuagiza kule nyumbani kwa Mwantumu, Chabbi
Cheka alitembelewa na mgeni mwingine pale ofisini kwake, wakati huo akiwa anajiandaa kurudi kule Mbagala kumbana zaidi yule mateka wake ili aseme ni wapi alipoficha yale makabrasha aliyokabidhiwa na mtafiti nguli, marehemu Grayson Mochiwa.
“Er, samahani mista Cheka…” Binti wa mapokezi aliyebisha hodi pale ofisini kwake alimwambia, na Chabbi akaguna tu huku akimtazama kwa macho yake ya kutisha.
“Ni nini?” Alimuuliza kwa kisirani.
“Ee, uliacha maagizo pale mapokezi kuwa mtu yeyote atakayekuja kumuulizia Mwantumu aletwe kwako…?” Binti alimwambia kwa swali.
“Yaa, sasa nashangaa unakuja wewe… huyo aliyekuja kumuulizia yu wapi?”
“Ah, hayupo…” Binti alijibu kwa woga na Chabbi akamtolea macho, akijiandaa kumkemea, lakini binti akamuwahi.
“Ila kuna mtu alipiga simu kumuulizia!”
Moyo wa Chabbi ukamlipuka, lakini akajikausha na kujifanya kama kwamba hakushitushwa na taarifa ile.
“Alaa… okay, huyo mtu alikuwa wa jinsia gani?” Chabbi aliuliza kwa utulivu, na binti akamtajia.
“Na alikwambia alikuwa anamtakia nini Mwantumu? Yaani mazungumzo yenu yalikuwaje?” Akauliza tena huku akijitia anauliza yale maswali kwa kutimiza wajibu tu, ingawa kichwani mwake maswali mengi juu ya huyo binti aliyepiga simu yalikuwa yanajitunga.
Binti wa mapokezi akamuelezea jinsi mahojiano yake na Zay yalivyokuwa
70
MTAFITI
asubuhi ile.
“Alikutajia jina lake”
“Hapana…”
“Kwa hiyo ulipomwambia asubiri ndio akakata simu?” Chabbi aliuliza, na binti akaafiki kwa kichwa.
“Nilitaka nimuunganishe na ofisi yako kwa simu, ndipo naye akawahi kukata simu.”
“Okay, taarifa nzuri lakini si ya muhimu. Huyo siye mtu niliyekuwa nikimtarajia… kwa hiyo akitokea mwingine, au yeye mwenyewe Mwantumu akitokea kuja hapa nijulishe mara moja… sawa?” Alimwambia, akitaka kuonesha kuwa na yeye hakuwa akijua mahala Mwantumu alipokuwa, na binti akabutwaika kidogo. Akabaki akiwa amesimama tu akimtazama.
“Unasubiri nini sasa?” Chabbi alimkoromea.
“In... ina maana huhitaji namba ya simu ya huyo binti aliyepiga simu kumuulizia?” Binti alimuuliza swali ambalo Chabbi alitaka aulizwe.
“Akh! Sasa nimekwambia huyo sio mtu wa muhimu… namba yake nd’o itakuwa muhimu?” Alimkemea, na binti akaanza kuondoka.
“Ah, anyway, hebu nipe tu hiyo namba basi!” Alijitia kubadili mawazo, akisema huku akijidai kupekua pekua mafaili yake pale mezani. Binti alirudi na kumpa kipande cha karatasi kikiwa kimeandikwa namba ya simu. Huku bado akiwa anajitia yuko bize na yale mafaili yake, Chabbi akamwambia, “Iweke tu hapo mezani…”
Binti alifanya vile na kutoka nje ya chumba kile, akijiona mjinga kwa kupeleka taarifa ambayo kumbe haikuwa na uzito wowote kwa Chabbi.
Huku nyuma Chabbi Cheka aliichukua ile namba na kuitazama kwa muda, uso wake ukiwa umesajili fikra nzito. Akakiweka mfukoni kile kijikaratasi, na kutoka kwenda Mbagala kuonana tena na Mwantumu.
Kilio kilimsaidia Zay kuondoa wahka, woga na hali ya kutojiweza iliyomgubika mara baada ya kutoka kwenye ule mtego wa kifo uliokuwa
umemzonga kule chumbani kwa rafiki yake. Kwa hakika hakuwahi kutaraji
hata kidogo kuwa ingefika siku akajikuta akipambana kutetea maisha yake
kama jinsi alivyofanya muda mfupi tu uliopita.
Sasa akiwa ameshamaliza kulia, na kitetemeshi kimemuisha, alijifuta
71 Hussein Issa Tuwa
machozi na kubaki akiitafakari ile hali aliyokumbana nayo kule chumbani kwa Mwantumu.
Yule mtu ni nani?
Hakuwa amemuona sura. Aliishia kumuona miguu tu, kumshika mkono wake mkubwa na kulisikia sauti lake baya. Hata pale alipomsukumia chaga ya kitanda kabla hajafanikiwa kutoka nje ya chumba kile, hakuwahi kumtazama kabisa usoni… lakini moja kwa moja alijua kuwa yule mtu aliyemkomea chumbani kwa Mwantumu, ndiye huyo huyo ambaye rafikiye alimwambia kuwa alikuwa akimkimbiza na bastola kutoka kule ofisini kwao.
Sasa kwa nini?
Mwantumu ameona nini huko… au amechukua nini huko, mpaka kufikia hatua ya kutolewa mbio ofisini kwa bastola, halafu hao watu wafikie hatua ya kwenda kukipekua chumba chake namna ile?
“Hapa ni kwenda polisi tu… sasa hivi!” Alipitisha azimio kwa sauti.
Aliliingiza tena gari barabarani, na ndio kwa mara ya kwanza alipobaini kuwa alikuwa amepaki kando ya uwanja wa taifa.
Heh, sasa huku nimekuja kutafuta nini tena?
Aligeuza kwa kasi, na kuchukua uelekeo wa kituo cha polisi cha Chang’ombe.
Huko aliingia kwa pupa pale kaunta ya mapokezi na kuanza kupayuka kwa wahka kwa yule askari aliyemkuta pale, akipuuzia mitazamo ya mshangao kutoka kwa baadhi ya raia na askari wengine wa jeshi la polisi waliokuwa pale.
“Msaada…! Haraka sana tena! Ku… kuna mwizi, no… jambazi… nyumbani kwa Mwantumu! Twendeni sasa! Na Mwantumu ametekwa! Ni hilo hilo jambazi linahusika… twendeni upesi lisije likatorok…”
“HEY!” Sauti kali ya kiaskari ilimkemea kutokea nyuma yake, naye akaruka kwa mshituko huku akigeukia kule ile sauti ilipotokea. Muda wote alipokuwa akipayuka kwa wahka namna ile, yule askari wa kike aliyekuwa pale kaunta alikuwa akimtazama kwa mshangao kama kwamba alikuwa mwehu.
“Tulia na ujieleze kwa utulivu mwanadada! Nini hii unakuja hapa na kuanza kupiga kelele kama mwehu?” Yule askari wa kiume aliyemkemea alimwambia huku akifika pale alipokuwa, akaingia ndani ya kile kituo na kuzunguka nyuma ya ile kaunta. Aliweka kofia yake ya kiaskari juu ya
72 MTAFITI
kaunta na kumtazama kwa macho makubwa. Zay alimkodolea macho kwa woga.
“Shk… sh’kamoo…!” Ndilo neno pekee lililomjia akilini wakati akimtazama yule askari.
Jamaa hakuijibu ile salamu yake. Alibaki akimtazama tu kwa macho ya kuuliza. Alikuwa ni mtu mzima, mwembamba na mrefu. Nywele zake zilikuwa nyeusi sana, ilhali ndevu zake zote za kidevuni zikiwa nyeupe sana kwa mvi.
“Hivi dada umejiona ulivyo lakini? Umetapakaa matandabui kwenye rasta zako, mavumbi kwenye nguo na usoni pia… umetokea wapi wewe?” Yule askari wa kike alimuuliza huku akimtazama kwa makini.
“Nimemuona akiingia na gari lake hapa kituoni kwa kasi kama anayekimbizwa, na nikajua hakukuwa na hali ya kawaida… ikanibidi nirudi ingawa nd’o n’likuwa naenda zangu nyumbani baada ya kumaliza zamu yangu…” Yule askari mtu mzima alisema, na Zay akajua alitakiwa ajieleze kwa utulivu ili aeleweke.
Alivuta pumzi nyingi mapafuni na kuzitoa, kisha akajilazimisha kuhesabu kimoyomoyo kuanzia moja mpaka kumi taratibu, kujipa muda wa kutuliza wahka aliokuwa nao.
“Ni nini hii unayopayuka kuhusu mwizi nyumbani kwa Mwantumu sijui, na kuhusu mtu kutekwa nyara?” Yule askari mtu mzima alimuuliza, lakini hapo Zay bado alikuwa anajilazimisha kuhesabu ili kupoza mtima, hivyo hakumjibu.
“Ongea basi dada! Kwanza umewakuta watu wengine hapa… ungepaswa usubiri zamu yako ya kusikilizwa!” Yule askari wa kike aliyemkuta pale kauta alimkemea.
Zay alijikohoza na kutaka kuanza kutoa maelezo yake kwa utulivu kadiri atakavyoweza, akilini akijua kuwa muda wa muhimu ulikuwa unapotea.
“Er, ni kwamba…”
“Pita ndani huku… njoo unipe maelezo yako huku ndani.” Yule askari mtu mzima alimwambia, na Zay akasita kidogo tu, kisha akapita haraka kule ndani na yule askari akamwongoza hadi kwenye chumba kimoja na kumwelekeza aketi kwenye kiti kilichokuwa nyuma ya meza moja mle ndani, wakati yeye akiketi juu ya meza ile.
“Okay bi mdogo… unaongea na detective Sajenti Pojo. Wewe ni nani, na hii habari uliyokuja nayo inahusu nini?” Yule askari mtu mzima
73 Hussein Issa Tuwa
alijitambulisha na kumuuliza.
“Sajenti tunapoteza muda... jamaa nimelifungia chumbani kule, hivyo nashauri tungewahi kwenda kulitia mbaroni kwanza kisha tutaelezana mambo yote! Muda ni wa msingi sana katika hili… inaweza ikawa ndio njia pekee ya kumpata Mwantumu!” Zay alimwambia kwa utulivu wa kulazimisha, lakini hata alipokuwa akisema maneno yale aliona kuwa alikuwa anakosea.
“Toa maelezo binti nataka kwenda nyumbani mie saa hizi! Unadhani unaweza kuja hapa ukapayuka tu ulilo nalo na sisi tukaacha kila kitu tukaenda utakapo? Hujanieleza cha kueleweka mpaka sasa!” Sajenti mpelelezi Pojo alimwambia.
“Okay, naitwa Zaynush… na nimekuja kutoa ripoti ya kupotea kwa rafiki yangu Mwantumu katika mazingira ya kutatanisha… na kwamba nilipoenda nyumbani kwake mchana huu kujaribu kumtafuta nikakutana na mtu nisiyemtambua akijaribu kukipekua chumba chake. Ndipo nikamfungia mle ndani na kukimbilia hapa kuja kutoa ripoti. Sasa si unaona? Kama tukimpata yule mtu pale ataweza kutujulisha mahala Mwantumu alipo!” Alisema kwa ufupi kadiri alivyoona itatosha kuokoa muda.
Sajenti Pojo aliinuka nakuweka kofia yake kichwani.
“Twende… maelezo kamili utakuja kunipa tukirudi!” Alimwambia huku akitoka mle chumbani na Zay akimfuata kwa mwendo wa haraka.
Dakika tano tu baadaye walifika nyumbani kwa Mwantumu wakiwa na askari mwingine wa kike ambaye Sajenti Pojo alimchukua pamoja nao kutoka kule kituoni.
Pale nje walikuta baadhi ya wananchi wachache wakiwa bado wamejirundika nje ya nyumba ile. Walipita moja kwa moja upenuni mwa ile
nyumba kubwa kuelekea kule kwenye chumba cha Mwantumu. Waliukuta ule mlango ukiwa umevunjwa vibaya na kubaki ukiwa wazi. Hakukuwa na mtu yeyote mle chumbani.
“Hah! Katoka…?” Zay alimaka kwa mshangao huku akimgeukia yule askari
“Si unaona? Jamaa kaondoka sasa! Hili ndilo nililokuwa nikilihofia!”
Alisema kwa hamaniko.
Sajenti Pojo hakumjibu waka kumuangalia. Aliingia mle ndani na kutazama jinsi chumba kilivyokuwa katika hali ya vurumai, moja kwa
74 MTAFITI
moja ikimfunukia wazi kwamba mle ndani palipita heka heka kubwa. Akamgeukia Zay.
“Hivi ndivyo ulivyokikuta hiki chumba kabla ya kuja kule kituoni?” Alimuuliza.
“No… sikukikuta hivi. Hii ni baada ya kupambana na hilo jamaa… kabla sijafanikiwa kuchomoka na kulifungia kwa ndani afande… ina maana jamaa limevunja mlango!” Zay alisema kwa mastaajabu, lakini Sajenti Pojo na yule askari mwenzake wa kike ndio walikuwa kwenye mastaajabu zaidi.
“Yaani hii sekeseke iliyopita humu ndani na wewe imekuhusu?” Pojo alimuuliza kwa mshangao huku macho yakimtoka.
“Heh, afadhali wana usalama wamefika… hili mbona balaa?” Sauti ya kike ilisikika kutokea kule nje na wote watatu mle ndani wakamakinika nayo.
Mama mwenye nyumba alifika, na alipomuona Zay uso wake ukaonesha kumtambua.
“Heh, Zay… kumbe ni wewe ndiye uliyekuwa ukipiga kelele huku ukikimbia hapa?” Aliuliza, na Zay akaafiki kwa kichwa.
“Heh, mbona balaa mwanangu? Lile jibaba limeufumua huu mlango kutokea humo ndani kana kwamba ulikuwa umeegeshwa tu!” Mama mwenye nyumba aliwajuza, na Zay na Sajenti Pojo wakatazamana.
“Vipi, uliweza kumuona sura yake…?” Pojo aliuliza.
“Mmh! Nimuone wapi? Huyu binti alivyotoka mbio huku akipiga kelele za mwizi watu waliuzingira huu mlango na mi’ nikiwemo… basi kabla hatujajua tufanyaje jibaba liliuparamia huu mlango kutokea humo ndani na kutoka nao nje mzima mzima!”
“Aaah?” Zay alimaka kwa mshangao.
“Hakuna aliyekaa tena hapa! Kila mtu alikimbilia upande wake!” Mama mwenye nyumba alimthibitishia.
“Mlikimbia?” Sajenti Pojo aliuliza.
“Sasa kumbe?” Mama mwenye nyumba alimjibu kwa swali, kisha akaendelea. “… jibaba limekwenda juu halafu limetanuka hilo! Usoni lilikuwa limejifunga kitambaa kuziba sura yake kuanzia juu kidogo ya pua kuja chini… utamjuaje? Lile kama jambazi basi ni jambazi lililokubuhu!”
Muda huu baadhi ya wanachi waliokuwa kule nje nao walikuwa wamekuja kuwazunguka pale nje ya chumba cha Mwantumu.
“Sasa… likaenda wapi baada ya hapo? Maana naona hii nyumba
75 Hussein Issa Tuwa
imezungushiwa ukuta kote… na njia pekee ya kutokea hapa ni kupitia huko upenuni na kutokea kule mbele getini!” Yule askari wa kike aliyekuwa na Sajenti Pojo akauliza.
“Oh! Yaani lilipochoropoka kutoka humo ndani jamaa lilitoka mbio moja kwa moja hadi kwenye ukuta ule…” Mama alijibu huku akiionesha sehemu ya nyuma ya ule ukuta ulioizunguka ile nyumba. Ulikuwa ni ukuta mrefu.
“Ah, halafu…?” Zay aliuliza kwa mshangao, akiwa hataki kuamini kuwa kuna mtu angeweza kuuruka ule ukuta mrefu.
“Ah, halafu?” Mama mwenye nyumba alimuuliza kama kwamba alikuwa ameuliza swali la kijinga kuliko yote, kisha akaendelea, “… mi’ nawaambia lile jamaa ninja! Yaani limeuruka huo ukuta kama vile lilikuwa linaruka kishimo cha mdako!”
“Hah!” Askari wa kike alimaka, na Zay akabaki kinywa wazi, akilini ikimthibitikia kabisa kuwa watu waliokuwa wakimsaka au wakimshikilia rafikiye hawakuwa wa kuchezea hata kidogo. Alimgeukia yule Sajenti mpelelezi, na akaona kuwa naye alikuwa akimtazama kwa macho yaliyomakinika, uso wake ukionesha mawazo mazito.
“Nadhani sasa mimi na wewe tunahitaji kurudi kituoni kwa maelezo ya kina!” Hatimaye Sajenti mpelelezi Pojo alimwambia.
Hilo ndilo Zay alilokuwa akilitaka sana wakati ule.
Walitumia dakika nyingine kumi kukichunguza kile chumba, lakini hawakuona kitu chochote cha kuwasaidia katika uchunguzi wao.
“Itabidi nije na watu wa kuchukua alama za vidole humu ndani baadaye… kwa sasa itabidi asiingie mtu yeyote kwenye chumba hiki. Wewe kaa hapa ulinde eneo la tukio…” Sajenti Pojo alimwambia yule askari wa kike.
“Wala msijisumbue ndugu zangu. Yule jamaa alikuwa amevaa glovu mikononi!” Zay alimwambia yule askari, ambaye kwa mara nyingine alisajili mastaajabu usoni.
“Una hakika?”
“Mia kwa mia afande! Lile jamaa lilikuwa jambazi kweli kweli nakwambia!
Hata sijui lilikuwa linamtakia nini Mwantumu jamani!” Zay alimthibitishia. Sajenti Pojo aliguna.
“Kwa hiyo angalau we’ ulipata kumuona sura yake?” Pojo aliuliza.
76
MTAFITI
“Sikumuona!”
“Heeeh! Hukumuona vipi wakati ulikumbana naye kwenye sekeseke yote iliyotokea humu ndani?” Sajenti Pojo alimtolea macho, na Zay akaishia kutikisa kichwa tu kwa masikitiko.
“Yaani we’ acha tu afande…mi’ nilimuona miguu yake tu!”
“Akh! Hii ni baab kubwa leo…” Sajenti Pojo alisema kwa mastaajabu.
“Sasa afande… mi’ n’takaa hapa mpaka saa ngapi?” Yule askari wa kike aliuliza.
“Mpaka huo mlango ubadilishwe na uweze kufungwa leo hii hii…” Pojo alimjibu, na kumgeukia mama mwenye nyumba, “si utaweza kuubadilisha leo hii hii huu mlango bibie?”
“Ah, hapa tatizo pesa tu… si unajua mi nilivyompangisha Mwantumu mlango ulikuwa mzima huo?” Mama mwenye nyumba alijibu kwa kujihami.
Zay alimuuliza atahitaji kiasi gani kuubadilisha ule mlango. Mama alipomtajia, alizama mfukoni na kutoa simu yake, kisha akamtumia pesa iliyohitajika pale pale kwa kupitia mtandao wa simu. Aliondoka na Sajenti Pojo kurudi kituoni kutoa maelezo yake kwa kina…
Bilanga aliingia nyumbani kwake na kupitiliza moja kwa moja hadi chumbani kwake na kuubamiza mlango wa chumba kile kwa hasira, tusi zito la nguoni likimtoka.
“Yaani nimekurupushwa na mwanamke namna ile mimi!” Alimaka peke yake mle ndani, kisha akasonya na kujibwaga kitandani, kisha hapo hapo akainuka na kwenda kuushindilia teke ukuta mle ndani na kuunguruma kwa ghadhabu.
“Nikimshika yule mwanamke atajuta kuzaliwa (akamtukania mama yake)!”
Alisema kwa hasira pevu, kisha akabaki akiranda huku na huko mle ndani.
“Na kwanza ni nani yule? Na alikuwa anafanya nini mle chumbani?”
Alizidi kujiuliza kwa sauti huku akienda kusimama mbele ya kioo kikubwa kilichokuwa kwenye mlango wa kabati lake kubwa la nguo na kujitazama.
Uso wake ulikuwa una nundu kubwa katikati ya paji la uso, na mdomo wake ulikuwa umechanika kidogo na damu ilikuwa imegandia pale
77 Hussein Issa Tuwa
alipojigonga wakati akitimbwatimbwa na yule mwanamke akiwa chini ya godoro kule chumbani.
Aliunguruma kwa ghadhabu kali na kupiga ngumi ndani ya kiganja chake.
“Yaani nikimshika yule mtoto!” Alijiapiza kwa hasira. Alirudi na kuketi kitandani huku akitoa simu yake, na kumpigia Chabbi Cheka.
“Okay, hebu anza kutoa maelezo yako kwa kituo sasa binti… tangu mwanzo hadi mwisho…” Sajenti Pojo aliwambia Zay mara waliporejea pale kituoni. Alikuwa amemwita askari mwingine wa kiume ambaye alikuwa ameshakaa tayari kuandika kile ambacho Zay atakuwa anakieleza.
“Sawa afande… kama nilivyosema mwanzo…” Alianza, lakini yule askari mwingine akamkatisha.
“Ngoja kwanza… jina lako….?” Alimwambia na kumuuliza huku akijiweka sawa kujaza sehemu maalum kwenye ile fomu ya kuchukulia maelezo.
“Oh, okay… Zay… aaamm, Zaynush!”
“Zaynush nani…?”
“Oh, samahani… jina langu halisi ni Zaynab… ila watu wamenizoea kama Zay Kay au Zaynush…”
Wale askari wakaachia miguno ya kukereka.
“Hebu acha ujinga wewe! Hayo majina yako ya kunasia wachumba huko usituletee hapa, umesikia? Hapa tunataka jina lako halisi… hebu lete leseni yako ya kuendeshea gari au kitambulisho chako cha kupigia kura!”
Yule askari mwingine alimjia juu.
“Samahani afande…” Zay aligwaya.
“Lete hivyo vitu nilivyokuomba wewe!” Askari alimwambia kwa kukereka, na Zay akampa leseni yake ya kuendeshea gari. Jamaa akasoma jina la pale kwenye leseni na kulihamishia pale kwenye ile fomu yake.
“Zaynab Kalindo… sasa mambo si hayo? Unataka kutuletea majina yako ya kifesibuku hapa! Haya tuendelee…” Yule askari mwenye nongwa
alimwambia huku akimrejeshea leseni yake, na kuendelea kumuuliza kabila lake, umri, mahala anapoishi na kazi yake. Baada ya hapo ndipo
Sajenti Pojo alipomtaka atoe maelezo yake.
78 MTAFITI
Akatoa ripoti ya kupotea kwa rafiki yake Mwantumu na akaomba jeshi la polisi lisaidie kumtafuta.
Wakamtaka maelezo ya mazingira ya kupotea kwa rafikiye, naye akajieleza kuwa hakuwa ameonana naye kwa siku tatu, ila asubuhi ya siku ile aliona simu nyingi alizopigiwa na rafikiye huyo ambazo hakuwa amezisikia wakati zikiita. Alipojaribu kumpigia rafikiye hakuwa akipokea bali simu yake ilikuwa ikiita tu.
Aliwaelezea alipofika nyumbani kwake kule Mwananyamala alikuta dalili kuwa rafiki yake alifika pale kwake kisha akaondoka, na hakuonekana tena mpaka muda ule. Kwa namna fulani alijikuta akificha kueleza juu ya ule mkoba wa rafikiye alioukuta kule ndani mwake. Halafu akawaeleza juu ya ule ujumbe wa sauti kutoka kwa Mwantumu ambao aliwasikilizisha wale askari.
Sajenti Pojo alimakinika sana na ujumbe ule kutoka kwa Mwantumu. Alitaka Zay amtumie ule ujumbe kwenye simu yake, lakini bahati mbaya simu yake haikuwa na uwezo wa kupokea ujumbe wa sauti kama ile ya kwake hivyo ikashindikana.
“Hamna taabu lakini afande… nitakuhamishia huu ujumbe kwenye flash disk nawe utaweza kuwa nao na kuusikiliza kwenye kompyuta au hata kwenye vifaa vingine vya kielektroniki…” Zay alimwambia,
“Yah! Fanya hivyo bi mdogo… fanya hivyo! Nataka niwe nao huo ujumbe!” Pojo alimwambia.
Akahoji ni wapi Mwantumu alikuwa anafanya kazi, na Zay akamtajia. Sajenti Pojo alikunja uso kwa tafakuri baada ya kusikia kuwa Mwantumu alikuwa akifanya mafunzo kwa vitendo kwenye ile kampuni kubwa ya tafiti nchini.
“Hmnh! Hiyo ni kampuni maarufu sana… una hakika hukukosea jina la hiyo kampuni?” Alimuuliza.
“Nina hakika na hilo kabisa. Miye mwenyewe nimeshawahi kumpeleka
Mwammy pale kazini kwake kwa gari langu mara kadhaa… ni hiyo hiyo
Liquid Diamond uijuayo afande!” Zay alimthibitishia.
“Okay. Tutalifuatilia hilo… endelea.” Pojo alimwambia, na Zay
akamalizia kwa kuwaeleza juu ya lile tukio zima lililomkuta kule chumbani
kwa Mwantumu ambako alijieleza kuwa alienda kumtafuta baada ya simu
yake kumpa habari kuwa alikuwa pale, na jinsi alivyoikuta simu ya rafikiye
ikiwa chini ya uvungu wa kochi mle ndani kabla ya kukurupushana na lile
79 Hussein Issa Tuwa
jibaba lililokwenda kupekua mle ndani.
“Mnh! Huyo mtu alikuwa anatafuta nini humo?” Pojo alijisemea peke yake kwa sauti.
“Sijui kwa kweli, ila afande hiyo inanipa picha kuwa Mwantumu atakuwa ametekwa na wale watu kutoka kwenye ile ile kampuni aliyokuwa akiifanyia mafunzo kwa vitendo…” Zay alisema, na Sajenti Pojo alitikisa kichwa kukubaliana naye.
“Ni kweli… itakuwa kuna kitu aidha amekichukua au wao wanadhani kuwa amekichukua kutoka kwao, na ndio maana lile jamaa lilikwenda kusachi kule chumbani kwake…” Pojo alisema, na kimya kilichukua nafasi kidogo.
Zay akaukumbuka ule mkoba wa Mwantumu alioukuta mle chumbani mwake asubuhi ile.
Oh, Mungu wangu! Au ndio kwenye ule mkoba…?
Alibaki kimya akili ikimtembea.
Hakuwa na maelezo zaidi, hivyo yule askari mwingine akampa yale maelezo yake ayasome kuona iwapo yalikuwa sahihi.
Alipothibitisha kuwa yalikuwa sahihi, aliambiwa aweke saini chini ya maelezo yale, naye akatekeleza.
“Okay... sasa tuachie tulifanyie kazi hili suala bi mdogo… hii ni kesi ya utekaji nyara hii, lakini hatuwezi kuithibitisha bila upelelezi…” Pojo alisema.
“Sawa… lakini muda ndio unakwenda hivyo afande. Sijui Mwantumu atakuwa kwenye hali gani huko aliko saa hizi afande!” Zay alisema huku akilengwa na machozi.
“Yah… mi’ n’taenda huko kwenye hiyo kampuni kuanza kuulizia, na ikifika asubuhi Mwantumu hajaonekana, basi tutatangaza kwenye vyombo vya habari kuwa amepotea na anatafutwa… kwa muda huu wewe nenda nyumbani tu ukapumzike. Jaribu kufikiria baadhi ya ndugu na jamaa ambao rafikiyo anaweza kuwa ameenda kwao na ufanye mawasiliano nao… ukipata lolote jipya nipigie simu mara moja… muda wowote!”
Sajenti Pojo alisema huku akimwandikia namba yake ya simu kwenye kijikaratasi na kumpa. Zay aliipokea na yeye akamwachia namba yake huku akipingana na lile wazo la yule askari.
“Mwantumu hawezi kwenda kwa mtu yeyote mwingine afande! Si umesikia kwenye ujumbe alionitumia kuwa alikuwa anakuja kulala
80 MTAFITI
kwangu? Na kwamba kule ofisini harudi tena? Sasa mbona kwangu
alikuja halafu akaondoka na hakurudi? Kuna kitu tu kimemkuta yule…
kwa nini simu yake ikawa chini ya kochi kule ndani kwake? Mwantumu ametekwa afande, na wahusika ni hao hao Liquid Diamond, nakwambia!”
Alimwambia kwa msisitizo.
“Unaweka pointi nzito sana hapo bi mdogo… acha tulifanyie kazi hili suala!” Pojo alimwambia.
Bila ya kuongeza neno, Zay alitoka na kurudi nyumbani kwake akiwa mchovu na aliyefadhaika sana.
Ilikuwa ni saa kumi na moja kasoro robo ya jioni wakati alipoingia nyumbani kwake pale Mwananyamala na kujifungia ndani kwa komeo. Bila ya kufikiri, kutokana na mazoea tu, aliwasha runinga yake kubwa pale sebuleni naye akapitiliza bafuni na kuoga kwa muda mrefu, muda wote akilia huku akijilaumu kwa yaliyomkuta rafikiye kipenzi.
“Ah, samahani sana Mwammy… yaani mi’ nilikuwa nakula starehe huko wakati wewe uko matatani? Umenitafuta rafiki yangu, nami nikashindwa kuja kukupa msaada kwa sababu ya starehe zangu za kimwili? Ooh, nisamehe Mwammy wangu... nisamehe, swahiba! Nitahakikisha hupatwi na lolote baya zaidi ya hilo linalokupata sasa hivi rafiki yangu… nitaenda juu chini, kusi na kaskazi, mbele na nyuma… mpaka nikukomboe! Nakuahidi hilo Mwammy… nakuahidi!” Alisema peke yake huku akilia kwa uchungu.
Alipomaliza kuoga alivaa suruali na fulana za mazoezi na kujibwaga kitandani akitafakari iwapo aende kazini usiku ule au asiende. Hakujiona kama alikuwa na uwezo wa kwenda kazini kabisa usiku ule.
Akiwa ni mchezesha kamari kwenye kasino kubwa jijini, kazi zake siku zote zilikuwa ni za usiku, na muda mwingi wa mchana alikuwa akiutumia kwa mambo yake binafsi. Mpenzi wake alimfungulia saluni ambayo ilimwongezea kipato na pia ndiye aliyemwongezea pesa za kununua lile gari alilokuwa nalo.
Alipiga simu kazini kwake na kujinadi ugonjwa.
Akabaki akiwa amelala pale kitandani, huku runinga ikiendelea kuongea peke yake. Na ndipo sikio lake liliponasa neno kutoka kule runingani ambalo lilimfanya akurupuke kutoka pale kitandani na kuidolea macho ya kutoamini ile runinga.
Habari ya kuuawa kwa mtafiti mkuu wa kampuni ya Liquid Diamond Incorporated asubuhi ile ilikuwa ikitangazwa kwenye runinga.
81 Hussein Issa Tuwa
MTAFITI
Na hata pale habari ile ilivyokuwa ikiendelea kuoneshwa, picha ya
Grayson Mochiwa ilioneshwa na baadaye akaonekana msemaji wa
kampuni ile akiongea kuwa lilikuwa ni tukio la kusikitisha sana na kwamba kampuni ilikuwa imepata pigo, kwani ilikuwa imepoteza mfanyakazi mmoja makini sana.
“Hah! Mochiwa!” Zay alimaka, akikumbuka kuwa Mwantumu alishawahi kumtajia jina la mtu huyo kuwa ndiye alikuwa msimamizi wake wa mafunzo kwa vitendo pale Liquid Diamond.
“
Oh, My God! Oh My God… ina maana… DUH!” Alichanganyikiwa kwa habari ile, na akazidi kujihakikishia kuwa Mwantumu alikuwa hatarini. Aliichukua simu ya Mwantumu, akikumbuka picha ambayo Mwantumu aliwahi kumuonesha kwenye ile simu yake. Alienda kwenye sehemu ya picha na kutafuta baadhi ya picha mpaka akaiona picha aliyokuwa akiitafuta.
Alibaki akiitazama ile picha huku akitetemeka vibaya sana.
Ilikuwani picha waliyopiga Mwantumu na hayati Grayson Mochiwa wakiwa kule ofisini kwao… walikuwa wameshikana mabega wakiichekea kamera, Mwantumu akiwa ameishikilia ile simu yake yenye kamera na kuigeuzia kwao ili ajipige picha ile akiwa na yule msimamizi wake wa mafunzo kwa vitendo.
Yule mtu aliyepiga picha na Mwantumu, ndio yule yule ambaye sura yake ilioneshwa pale kwenye runinga jioni ile, akitangazwa kuwa ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana pale ofisini kwao asubuhi ile.
“Watu wasiojulikana gani mmemuua nyie hao hao Liquid Diamond nyie?” Alisema kwa wahka, na hapo wazo likapita kichwani kwake.
Mwantumu alikuwa anafanya kazi na Grayson… na sasa Grayson ameuawa, na
Mwantumu ametoweka…
“Hivi vitu vinahusiana! Na Mwantumu watamuua!” Alisema kwa woga mkubwa huku akiinuka na kuanza kuranda huku na huko mle ndani.
“Kama bado hawajamuua tayari!” Aliongezea huku akichukua simu yake.
Lazima nimjulishe afande Pojo haraka sana! Liquid Diamond wanahusika!
Ile simu ikaanza kuita ikiwa mkononi mwake…
82
DAKIKA KADHAA KABLA simu ya Zay haijaanza kuita
ikiwa mkononi mwake kule Mwananyamala, sehemu nyingine ya jiji Chabbi Cheka alikuwa akipokea simu aliyopigiwa na Bilanga na kuipeleka sikioni huku akimtazama Mwantumu aliyejikunyata kwa woga kwenye kona ya kile chumba cha chini ya ardhi. Mwanadada alikuwa akilia kwa kuomboleza, akiwa ametutumkwa uso na ametapakaa damu kinywani na kifuani.
Chabbi wala hakumjali.
“Yah, unasemaje?” Aliuliza kwa kisirani kwenye ile simu.Yule mtoto wa kike alikuwa amegoma kusema chochote pamoja na mateso mazito aliyompa. Alikuwa akitweta kutokana na kutumia nguvu wakati akimpa Mwantumu mateso ili aseme mahala alipouficha mkoba wenye makabrasha ya mtafiti Grayson Mochiwa.
“Misheni imeshindikana bosi… mambo niliyokutana nayo kule sikuyatarajia kabisa!” Bilanga alimjuza simuni, roho ikimuuma kukiri kuwa alikuwa ameshindwa kwenye jukumu alilopewa na mkubwa wake, lakini ukweli ulikuwa ndio huo, hakuwa na namna.
“What do yo mean mambo uliyokutana nayo hukuyatarajia? Mi’ nilidhani nimekupa jukumu dogo tu?” Chabbi alimfokea simuni.
“Kulikuwa kuna mtu mle ndani… msichana… ametibua kila kitu, amepiga kelele za mwizi ikabidi nitimue…”
“Msichana…? Yukoje? I mean… ulimuona sura yake?” Chabbi aliuliza huku akimtupia Mwantumu jicho la pembeni, ambaye alimakinika pale aliposikia Chabbi anauliza kuhusu msichana kwenye maongezi yake.
“Sikuwahi kumuona sura yake bwana! Alikuwa amejificha uvunguni…. akanishtukiza na kabla sijamtia mkononi vizuri aka…”
“Unakurupushwa na mtoto wa kike wewe? Yaani… Dah! Okay, kwa
83 Hussein Issa Tuwa
6
hiyo umegundua nini mle ndani hata hivyo?”
“Nothing! Nakwambia nilikurupushwa kabla sijamaliza upekuzi, na mpaka muda wa purukushani sikuwa nimeona chochote cha kutusaidia!”
Bilanga alimaka kwa hasira kutokea upande wa pili wa ile simu.
“Awww… Shit, man… shit, shit, shiiit! Sasa hakuna waliokuona sura yako huko wewe?”
“Hakuna… nilihakikisha juu ya hilo!”
Kimya kilitawala kwa muda, kisha Bilanga akaongea.
“Nadhani yule msichana ni rafiki wa karibu sana na huyo binti uliyenaye huko Chabbi… na… nahisi yule atakuwa anajua kila kitu kuhusu huyo binti… inabidi naye tumtie mikononi Chabbi!”
Chabbi alimsikiliza kwa makini huku akimtazama Mwantumu, ugunduzi mpya ukimshukia.
“Okay… angalau hapo unaelezea jambo la msingi!” Chabbi alimwambia.
“Of Course nakwambia jambo la msingi! Ndio maana nataka unipe kazi ya kumsaka yule demu mwenye rasta mpaka nimpate Chabbi! Na nikimpata…”
“Unamleta kwangu! Tumeelewana? Unamleta kwangu huyo msichana na sio kumfanya utakavyo kwa sababu eti amekukurupusha huko, upo?” Chabbi alimkatisha, na upande wa pili wa simu Bilanga akaachia tabasamu baya.
“Nimekuelewa, bosi…!”
Chabbi alikata simu na kumkazia macho Mwantumu.
“Ni nani huyo aliyekutwa chumbani kwako kule wewe…?” Alimuuliza kwa hasira.
Oh, my God… Zay! Wameshamjua na Zay hawa! Yote kwa sababu yangu!
Mwantumu aliwaza, na wimbi jipya la machozi likambubujika. Alijua kuwa hata wamfanye nini, hangemsaliti rafiki yake… na alijua kuwa hakuwa na uwezo wa kuendelea kuvumilia mateso ya yule mtu mkatili asiye na chembe ya utu.
“Nakuuliza wewe!” Chabbi alimkemea huku akimfuata pale chini na kumbana taya kwa mkono wake mkubwa. Mwantumu alimtazama kwa macho yenye kuomboleza huku akimtikisia kichwa kukataa kuwa hajui lolote.
Chabbi alimtolea kile kijikaratasi chenye ile namba ya simu aliyopewa na yule binti wa kule mapokezi.
“Ndiye huyu mwenye hii namba ya simu?” Alimuuliza huku akimsogezea
84 MTAFITI
ile namba karibu na uso wake.
Mwantumu aliitazama ile namba, na moyo ukamnyong’onyea.
Owww namba ya Zay! Wameipata namba yake!
“Siijui hiyo namba!” Mwantumu alimwambia kwa woga mkubwa, na Chabbi akamtumbulia macho yake ya kutisha kwa muda mrefu, kisha akainuka na kurudi kwenye kiti chake.
“Okay… tutajua ukweli muda si mrefu mrembo wangu… na nikibaini kuwa umenidanganya…” Chabbi alimwambia kwa kitisho kilicho dhahiri, akiiacha ile kauli yake ielee hewani makusudi.
Mwantumu alijikunja pale chini na kulia kwa uchungu.
Oh, Mungu wangu… usiwaache wamuumize rafiki yangu Zay tafadhali! Hana makosa yoyote yeye… ni mimi ndiye niliyempelekea mashaka yangu kwake… basi yaache mashaka haya yaishie kwangu na usimwangushie na yeye tafadhali Mungu wangu… please!
Zay aliitazama ile simu yake ikiita mkononi mwake, na akashangaa kuona kuwa haikuonesha namba wala jina la mpigaji wa simu hiyo.
Ah! Inakuwaje hii sasa? Si nilisikia kuwa tume ya mawasiliano imefuta hizi habari za ‘private number’?
Pale kwenye simu yake kilichokuwa kikionekana ni maneno ‘identity hidden’, yaani utambulisho wa huyo aliyekuwa anampigia ile simu ulikuwa umefichwa.
Heh!
Simu iliendelea kuita naye akabaki akiitazama tu bila ya kuipokea, mawazo ya mashaka mashaka yakipita kichwani mwake.
Simu ikaacha kuita.
Alishusha pumzi za ahueni, akikumbuka uzembe alioufanya kwa kuwapigia simu wale watu wa ile kampuni ya Liquid Diamond, akijaribu kumuulizia Mwantumu…
Watakuwa ni wao?
Ile simu ikaanza kuita tena.
Akaipokea na kuiweka sikioni kwake, lakini hakuongea kitu. Upande wa pili alisikia mtu aliyempigia akihema tu lakini naye hakuongea kitu.
Wakabaki wakisikilizana tu… bila ya yeyote kati yao kusema neno. Alikuwa anataka kuikata ile simu, wakati mtu wa upande wa pili alipoongea.
85 Hussein Issa Tuwa
“Nani mwenzagu?” Ilikuwa ni sauti nzito ya kiume.
Zay alibana midomo kwa nguvu. Hakujibu. Alihisi yule mtu alikuwa anataka ajibu kitu ili bila shaka ajihakikishie kuwa yeye alikuwa mwanamke. Kwani alijua iwapo wahusika wa ile kampuni ya Liquid Diamond waliambiwa kuwa kuna binti aliyepiga simu pale kumuulizia Mwantumu, basi watakuwa wamejaribu kuipiga tu ile namba yake ili akiongea wajihakikishie kuwa hakika yeye ndiye aliyepiga ile simu na kumuulizia Mwantumu.
Sasa nijibu au…
“Oh, huongei? Okay sio ishu… nilidhani kuwa we’ ni Mwantumu…”
Ile sauti ilimwambia kwa upole na Zay akakurupuka.
“Mwantumu?” Aliropoka kwa hamaniko, kisha hapo hapo akaendelea bila kufikiri, “Yu wapi Mwantumu wewe, eenh? Yu wapi? Ukimgusa tu utapambana na mimi fala wewe! Tena nakwambia…”
“Tunaweza kubadilishana mali kwa mali bibie… lete cha kwetu nasi tukupe Mwantumu…”
“Whaaat?”
“HAKUNA CHOCHOTEEE! USIMSIKILIZEEEEEEE! NENDA POLISIIII!!” Sauti ya Mwantumu ilisikika waziwazi ikipiga kelele kutokea jirani na yule muongeaji.
“Hah! Mwantumu…? Mwantu…!”
Jamaa akakata simu.
“HAAAAAAH!” Zay alipiga ukelele kwa hasira na kubaki akiitazama ile simu kwa kutoamini.
Chabbi Cheka alirudisha simu yake mfukoni na kumtazama Mwantumu aliyekuwa amechutama kwenye kona ya kile chumba huku akimtazama kwa hasira, akiwa amevimbisha midomo kwa kiburi kikubwa.
Siwaruhusu wamguse Zay washenzi hawa! Siwaruhusu!
“Ulisema huijui ile namba Mwantumu… ulinidanganya! Na nilikuahidi kuwa nikigundua kuwa unanidanganya utajuta kuzaliwa…!” Chabbi alimwambia kwa hasira isiyosemekana.
“Una wazimu wewe! Mimi sina lolote mnalodhani kuwa ninalo… na huyo uliyempigia pia hajui lolote!” Mwantumu alimjibu kwa hasira, sauti yake ikitetemeka sio kwa woga tena bali kwa hasira.
86
MTAFITI
“Na unajuaje kuwa hajui lolote? Ni nani yule rafikiyo? Anaitwa nani?” Chabbi alimfokea.
“Nimekwambia sijui lolote! Unanionea bure tu! Ni bora uniachie na sitaenda kushitaki polisi!” Mwantumu alimfokea pia.
Chabbi akatikisa kichwa kwa masikitiko.
“Sasa nina hakika kuwa ule mkoba wenye zile nyaraka ulizopewa na Grayson uko kwa huyo rafikiyo…!”
“Sijapewa nyaraka zozote! Ni ripoti yangu tu ya field attachment, nayo imeibiwa kwenye daladala pamoja na mkoba wangu…!”
“Unapoteza muda bure tu we’ mtoto! Tupe huo mkoba wenye nyaraka za Grayson na kila kitu kitasahaulika… usiwe mjinga!”
“Hata kama nikiwa nao huo mkoba na kukupa… najua mtaniua tu.
Nyinyi ni watu wabaya sana. Ndio maana mista Mochiwa alikuwa katika hali isiyoeleweka leo! Kuna vitu vyake… taarifa zake mmemuibia nyie! Na sasa mnataka kumuingiza na huyo mdada kwenye hayo mashaka yenu bure…!” Mwantumu alifoka, na Chabbi akamtolea tabasamu baya.
“Mdada? Sasa kama humjui mwenye hii namba niliyokuonesha nashangaa umejuaje kuwa ni mdada?” Chabbi alimuuliza kwa sauti nzito ya kuogofya. Mwantumu alitaka kufungua kinywa kumjibu lakini jamaa alimrukia pale chini na kumbana koo kwa nguvu.
“Achana na habari za Grayson wewe! Ni nani yule niliyeongea naye kwenye simu sasa hivi, eeenh? Anakaa wapi? Utanipeleka mpaka nyumbani kwake…” Chabbi alimkemea lakini hakumalizia kitisho chake, kwani Mwantumu alishaamua la kufanya. Akiwa amebanwa koo namna ile pale chini alimpitishia haraka mikono yake iliyofungwa kamba pamoja shingoni kwa yule mtu mbaya kama jinsi mpenzi amuwekeavyo muhibu wake mikono mabegani wakati wa kucheza dansi ya taratibu, na wakati Chabbi akihamanika kwa kitendo kile kisichotarajiwa na akitaka
kujichomoa kwenye kumbatio lile la kifo, Mwantumu aliachia ukelele wa ghadhabu na kumng’ata kwa nguvu sana kwenye upande wa shingo yake
kama simba aliyekamata windo la pundamilia.
“Waaaarghh… wewwweeeeeekhhh!” Chabbi Cheka alipiga kelele huku
akijiinua kutoka pale chini alipokuwa amemchutamia yule binti ilhali
akirudi nyuma, lakini Mwantumu alizidi kumng’ang’ania na wote wawili wakapiga mweleka mzito, Chabbi chini, Mwantumu juu.
Chabbi alijaribu kuitoa mikono ya yule binti kutoka shingoni kwake
lakini haikuwezekana, na Mwantumu alizidi kudidimiza meno yake
87 Hussein Issa Tuwa
shingoni kwa yule adui, damu kutoka kwenye jeraha lile ikiwalowesha
wote wawili pale chini. Chabbi alikuwa akipiga kelele huku akijaribu
kumpukuta Mwantumu kutoka mwilini mwake bila mafanikio, kwani ile mikono iliyokuwa imefungwa kamba ilikuwa imembana shingoni.
Maumivu makali yalimtambaa kutokea pale ambapo meno ya yule binti aliyekuwa akiunguruma kama simba aliyetishiwa usalama wa watoto wake yalikuwa yamezama.
Alijiinua wima lakini akaanguka tena, na bado Mwantumu alikuwa amemng’ang’ania. Alijitahidi kumshindilia ngumi za mbavu kwa nguvu ili yule binti amuachie. Mwantumu alihisi maumivu makali, lakini hakuweza kujinasua kwa kuwa kwa namna fulani na yeye alikuwa amejizonga
shingoni kwa yule bazazi, na akazidi kumtafuna ile shingo kwa nguvu, akijua kuwa kwa vyovyote vile, akimuachia tu yule mtu atamuua.
Maumivu yalimzidia Chabbi na akiwa pale chini alimkamata mbavu yule msichana kwa mikono yake miwili yenye nguvu na kumtupa juu kwa nguvu. Mwantumu alitupwa juu, miguu yake iliyokuwa imefungwa kamba
ikielea hewani naye akibinukia kichwani kwa Chabbi ilhali uso wake bado ukiwa umezama shingoni kwa yule mtu mbaya, na hapo Chabbi Cheka alisikia sauti mbaya ya mvunjiko wa maungo, ikifuatiwa na kishindo kikubwa pale yule binti alipoangukia nyuma yake huku bado mikono yake ikiwa imemnasa shingoni.
Meno yaliyokuwa yamembana shingoni yakaachia, na mikono iliyokuwa imemzonga shingoni ikalegea.
Chabbi aliunguruma kwa hasira huku akijikurupusha na kujichomoa
kutoka kwenye ile mikono iliyolegea ya yule binti na kuinuka huku akipepesuka na akikohoa hovyo na kwenda kujiegemeza ukutani huku akiwa amejishika shingoni. Damu nyingi ilikuwa ikimchuruzika kutoka kwenye lile jeraha baya, na alihisi kuwa yule binti alikuwa amemnyofoa nyama ya pale shingoni au hata amemkata mshipa wa damu.
Oh, shit! Kuvujwa damu nyingi namna hii ni hatari sana!
“Ahh! Mpumbavu sana wewe! Hunijui mimi, eenh? Hunijui kabisa mimi wewe… sasa utajuta nakwambia! Utajutaa!” Alibwata huku akiwa amejishikilia ukutani na akimtazama yule binti aliyelala pale chini, shingo yake ikiwa imejikunja katika pembe isiyowezekana.
Alibaki akiwa amebutwaika akimtazama kwa mshangao yule binti aliyelala pale chini.
“Pumbaaavu!” Alifoka huku damu ikizidi kumbubujika.
88 MTAFITI
Huku akipepesuka na akiwa amejishika pale shingoni alipong’atwa ambako bado palikuwa panavuja damu kwa wingi, alitoka nje ya chumba kile cha chini ya ardhi na kumuacha Mwantumu akiwa amelala sakafuni mle ndani…
Baada ya yule mtu asiyejulikana kumkatia simu, Zay alibaki akiwa amebutwaika kwa sekunde kadhaa kama kwamba akili yake ilikuwa imekufa ganzi kwa muda.
Kisha akazinduka.
Jamaa wanaye Mwantumu!
Wanaye!
Alikurupuka kutoka ndani mwake na kujitupa ndani ya gari lake. Alitia moto na kuliondoa kwa kasi, akiisikiliza simu ya Sajenti Pojo ikiita kupitia kwenye visikilizio alivyopachika masikioni mwake kutokea kwenye simu yake iliyokuwa kwenye kiti cha pembeni yake mle garini.
“Haloo…vipi Zay…?” Sajenti Pojo alivuma masikioni mwake.
“Wanaye afande! Wanaye nakwambia! Wamenipigia simu sasa hivi, oh my God, wanaye Mwantumu nakwambia…! Nakuja huko huko!” Zay alipayuka simuni.
“Tulia Zay… tulia! Wanaye Mwantumu… kina nani? Na wamekupigia simu… kina nani? Na unakuja huku huku… wapi?” Pojo alimhoji, na Zay akafuta machozi yaliyokuwa yakimbubujika.
“Kwanza umeona TV jioni hii afande?” Alidakia mada nyingine.
Zay alikuwa amehamanika vibaya sana. Mambo mengi yalikuwa yanamtokea kwa mfululizo, na yote hayo yalikuwa ni mapya kabisa kwake.
“Mi’ sikuelewi bi mdogo. Nahisi kama unaendesha gari wewe... na pia una wahka mkubwa. Mi naomba uegeshe gari pembeni kwanza ndio tuongee kwa kituo…!” Pojo alimwambia.
Zay akatikisa kichwa kwa kukata tamaa.
Aliegesha gari kando ya barabara na kuhakikisha kuwa milango yake yote imefungwa, kisha akaanza kumuelezea yaliyotokea lakini Pojo akamkatisha.
“Sio kwenye simu Zay… uko wapi wewe sasa hivi?”
“Ah, sawa... mi’ nina gari. Niambie wewe ulipo ili nikufuate. Mi’ nilikuwa nakuja huko kituoni!”
89
Issa Tuwa
Hussein
“Ah, sasa mi’ siko ofisini saa hizi. Niko kwenye basi natokea mjini… naenda nyumbani… Tabata!”
Walikubaliana Pojo ateremke kwenye kituo cha basi kinachofuata na Zay amkute kituoni hapo. Kama dakika arobaini na tano baadaye Zay alifika kwenye kile kituo na Pojo akaingia garini.
Yule Sajenti wa polisi alimwambia aondoe gari kutoka pale kituoni na kumshauri wapaki hatua chache kutoka kwenye kituo cha basi kinachofuata baada ya kile alichomkuta. Ndipo Zay alipomueleza Pojo taarifa ya kuuawa kwa mtu aitwaye Grayson Mochiwa kama jinsi alivyoona na kusikia kwenye runinga jioni ile.
“Sasa na huyu naye ni nani? Anahusika vipi na kadhia hii?” Pojo alimuuliza, na Zay akamweleza.
“Ah! Yaani mtu aliyekuwa anafanya kazi na Mwantumu kwenye ile kampuni ameuawa leo hii, na Mwantumu naye ametoweka leo hii hii?”
Aliuliza kwa namna ya kujihakikishia kuwa amemuelewa vizuri yule binti.
“Ndio hivyo afande!”
“Kuna namna hapo…” Pojo alisema, na kuongezea “…kuna namna kweli kweli tena hapo!”
“Na sasa kama hiyo haitoshi afande… nimepigiwa simu jioni hii hii na mtu asiyejulikana na akitumia simu iliyoficha utambulisho wake…”
“Enhe?”
Akamuelezea juu ya namna ile simu ilivyoingia na sehemu ya mazungumzo yake na yule mtu mwenye sauti nzito yalivyokuwa.
“Na nilivyokuwa naongea naye afande, nilimsikia kabisa Mwantumu akinipigia kelele kuwa nisimsikilize yule mtu na niende polisi…!”
“What?”
“Ndiyo afande! Mwantumu alikuwa na yule mtu wakati ule… jamaa liliposikia Mwantumu ananipigia kelele namna ile likakata simu!” Zay alimalizia na akashindwa kuyazuia machozi.
“Watakuwa wanamtesa tu rafiki yangu wale…!”
Sajenti Pojo alikunja uso kwa tafakuri nzito.
“Kuna kitu hakipo sawa hapo bi mdogo… huyo jamaa alipokupigia hiyo simu… alikwambia anataka nini hasa?” Pojo alimuuliza.
Tunaweza kubadilishana mali kwa mali bibie… lete cha kwetu nasi tukupe Mwantumu…
“Er… alitaka niende alipo Mwantumu…” Zay aliongopa. Hakutaka kusema lolote kuhusu ule mkoba wa Mwantumu aliouacha nyumbani
90 MTAFITI
kwake. Hakujua una nini ndani, na kabla hajajua kilichomo ndani ya ule mkoba, hatomwambia yoyote juu ya uwepo wa mkoba ule.
“Ili iweje? Kwa nini walitaka uende huko?” Pojo alisaili zaidi.
“Sasa hapo ndipo Mwantumu aliponipigia ukulele kuwa niende polisi, na jamaa akakata simu… so sikuweza kujua ni kwa nini afande!” Zay alimjibu.
Pojo alikunja uso kwa mawazo zaidi.
“Haiingii akilini hiyo bi mdogo…” Alisema, na Zay hakuwa na la kusema.
“Yaani katika mazingira kama hayo, jamaa lazima angekutaka umpe kitu… pesa… au kitu kingine chochote ili ubadilishane naye na huyo Mwantumu.” Pojo alizidi kuongea, na kumgeukia moja kwa moja usoni, “Una hakika hajakutaka kitu kama hicho bi mdogo?”
Zay alimeza funda la mate.
“Ha… hapana, I mean, ndiyo, nina hakika afande!”
Kimya kilitanda kwa muda garini.
“Mi’ nilienda kule kwenye ile ofisi ya Liquid Diamond… na ndiko nitokeako.” Alisema kwa upole, na Zay akawa makini.
“Enhe…?”
“Ukweli sikufanikiwa lolote. Nilifika kwenye muda wa saa kumi na moja hivi. Watendaji wote walikuwa wameshaondoka. Ila nitakwenda tena huko kesho asubuhi tu kufuatilia juu ya suala hili…” Pojo alimjibu, na Zay akanyong’onyea.
“Sasa tunafanyaje?”
“Tunasubiri kesho tena kufuatilia suala hili Zay… hamna jinsi…” Sajenti Pojo alimwambia.
“Ile kampuni ina mambo ya kiza kiza afande, si bure! Kwa nini tusiianike tu? Haiwezekani watu wawili wote kutoka kwenye kampuni hiyo hiyo, tena kutoka kwenye kitengo kimoja, wakutwe na madhila mazito ndani ya siku moja!” Zay alitoa rai.
“Ni kampuni kubwa ile Zay. Ina hadhi sana hapa nchini.”
“Kwa hiyo?”
“Kwa hiyo lazima itakuwa na mbinu za kujilinda na kuficha machafu yoyote ambayo itakuwa inahusika nayo…”
“Sikuelewi afande…”
“Ninachomaanisha ni kwamba tukiiendea kichwa kichwa tu kwa jazba lazima tutafeli… inabidi kuwaendea kwa umakini mkubwa sana. Umakini huo wewe huna Zay. Kwa sababu mara nyingi umakini unaendana na
91 Hussein Issa Tuwa
subira… wewe huna uwezo wa kufanya subira hivi sasa. Ndio maana unatakiwa utuachie sisi tulifanyie kazi suala hili!” Pojo alimwambia.
Zay alimtazama kwa muda mrefu, kisha akashusha pumzi ndefu.
“Okay, afande. Nimekuelewa.”
“Vizuri. Sasa wewe nakushauri ukae mbali sana na ile kampuni… usijioneshe sura yako pale hata kidogo. Ningependa ujifiche sehemu ili hawa jamaa wasikujue kabisa. Maana sitaki tena nipate kazi ya kuanza kukusaka na wewe kabla hata huyo Mwantumu hatujampata…”
“Heh, ‘asa mbona unan’tisha afande?”
“Sikutishi… ndio hali halisi hiyo! Kama haya niliyoyasikia leo hii kuhusu kampuni ile ndio yako hivyo, inamaanisha kuwa hao wenye hiyo kampuni hawaoni tabu kumpoteza mtu yeyote, wakati wowote. Sio watu wa kuwachezea hata kidogo.”
Zay aliitafakari kauli ile kwa muda, na akaona inaleta maana.
Lakini sasa ndio nikae kiwetewete tu hivi hivi wakati sijui Mwantumu yu hali gani huko?
“Sawa afande…”
“Okay… tutawasiliana!” Pojo alimjibu na kuteremka kutoka kwenye gari.
“Ah, si nikupeleke nyumbani afande?” Zay alimuuliza, na Pojo akamcheka.
“Na kesho pia utanifuata nyumbani asubuhi kunipeleka kazini? Mi’ n’takwea daladala tu…” Alimjibu na kuondoka.
Zay alibaki kinywa wazi.
“Sasa si ungeniachia nikuongeze japo nauli afande?” Alijisemea peke yake, akimtazama yule afande akitembea kwa miguu kuelekea kwenye kituo cha basi.
Alipotoka hapo alitia gari moto na kuongoza moja kwa moja hadi kituo cha televisheni cha ITV. Huko alitoa ripoti ya kupotea kwa rafiki yake Mwantumu na akawapatia picha ya rafikiye huyo iliyokuwa kwenye simu yake.
Aliripoti kuwa Mwantumu alikuwa akifanya mafunzo kwa vitendo kwenye Kampuni ya Liquid Diamond Incorporated ya jijini, na kwamba mara ya mwisho aliondoka nyumbani kwake kwenda kwenye kampuni ile asubuhi ya siku ile kama kawaida, na hakurudi wala kuonekana tena.
Ikatolewa na namba ya simu maalum kwa yeyote atakayekuwa na habari za mahala Mwantumu alipo au alipoonekana au atakayemuona aripoti
92 MTAFITI
kupitia namba hiyo.
Ilikuwa ni namba ya pale pale ITV.
Zay alilitazama tangazo lile likienda hewani kwenye runinga baada ya taarifa ya habari ya saa mbili usiku ule akiwa nyumbani kwake.
Lile tangazo lilileta kizaazaa kikubwa.
Wakati akilitazama lile tangazo likimnadi rafiki yake kuwa amepotea, Zay alimkumbuka mama wa yule rafikiye. Hapo hapo akampigia simu na kumfahamisha kuwa bado Mwantumu alikuwa hajaonekana na kwamba
tayari ameshatoa taarifa za kupotea kwake polisi na pia ameshatoa tangazo kwenye chombo cha habari.
“Ah! Balaa gani tena hili? Na ile hali aliyo nayo jamani… hivi nitamuona tena mwanangu akiwa hai kweli miye jamani?” Mama alisema kwa kuomboleza, na Zay akameza donge lililomkaba kooni kwa uchungu wa hali ile na kwa kushindwa kumwambia ukweli wa kila kilichotokea kwa
Mwantumu kwa kuhofia kumtia mashaka zaidi yule mama.
“Tuombe Mungu tu mama… ataonekana tu…” Ndilo jibu pekee lililomjia kinywani mwake.
“Mimi kesho nakuja huko mjini Zay!” Mama alisema kwa msisitizo na Zay hakuwa na namna ya kumzuia mama asije kumsaka mwanaye. Wakati anaendelea kuongea na yule mama, alisikia simu yake ikimpigia mbinja za kumjulisha kuwa kulikuwa kuna simu nyingine ilikuwa inataka kuingia. Akaagana na yule mama na simu yake ikaita. Alikuwa Sajenti Pojo.
“Yes, afande?” Alipokea.
“Zay… nimeona tangazo kwenye televisheni usiku huu!” Pojo alisema kwa utulivu.
“Na mimi pia nimeliona afande.” Zay alimjibu.
“Unataka kuniambia kuwa wewe siye uliyelipeleka lile tangazo huko ITV?” Pojo alihoji, na Zay akajikuta akitabasamu pamoja na madhila aliyokuwa nayo.
“Ni mimi ndiye niliyepeleka lile tangazo afande. Sikuona sababu ya kuendelea kupoteza siku nzima bila kufanya bidii yoyote ya kumsaka
Mwantumu!”
93 Hussein Issa Tuwa
“Safi! Ulifikiria jambo zuri sana… nimeipenda hiyo!”
“Nhaaa?” Zay alishangaa.
Alitarajia yule askari angemjia juu kwa kitendo kile. Labda angemlaumu kwa kuingilia upelelezi ambao bado ulikuwa unaendelea.
“Ndiyo! Yatupasa tutumie kila njia ya kumpata rafikiyo. Baada ya hili tangazo sasa mimi kesho nitaenda na kidhibiti cha ziada kule Liquid Diamond…!” Pojo alisema, na Zay akalifurahia hilo.
“Okay… safi sana basi afande!”
“Ni safi, ila sio safi sana…”
“Ah, kivipi tena?”
“Nataka nikuase Zay… usipende kukurupuka kurupuka hovyo kwenye hili suala. Leo umekurupuka kwa jambo zuri kidogo, kesho unaweza kukurupuka kwa jambo litakalokuponza! Kuwa makini na mwenye subira katika hili jambo. Next time nitafurahi zaidi kama utanishirikisha
kama mpelelezi wako katika hatua unazotaka kuchukua… sawa?” Pojo alimwambia, na Zay akafinya uso kwa aibu.
“Okay afande… sawa!” Alimjibu, wakaagana na kukata simu.
Inspekta aliyekuwa akimhoji Luis K ambesera asubuhi ya siku ile naye aliliona lile tangazo, na akawa analitazama kama kwamba ni tangazo tu miongoni mwa matangazo mengi ya aina ile akiwa sebuleni kwake… mpaka pale aliposikia ikitamkwa na mtangazaji kuwa binti aliyepotea asubuhi ile alikuwa akifanya mafunzo kwa vitendo kwenye kampuni ya Liquid Diamond Incorporated ya jijini.
“AFANALEIYK!” Jamaa alikurupuka kutoka kwenye kochi alilokuwa amekalia pale sebuleni kwake huku akiwa ameitumbulia macho runinga yake pale nyumbani, akimshitua vibaya sana binti yake aliyekuwa akifanya kazi zake za shule pale sebuleni.
Jamaa wala hakuwa na habari kuwa alimshitua bintiye. Alibaki akiitazama ile habari ikimalizikia, na kwa mara ya kwanza tangu anunue ile runinga alitamani angekuwa na uwezo wa kurejesha nyuma taarifa ya habari ili aisikilize vizuri zaidi ile habari.
“Mnh! Hii si bure hii! Matukio mawili yanatokea ndani ya siku moja
94
MTAFITI
katika kampuni moja?” Alijisemea peke yake, akiwa hana habari kabisa na jicho kali alilokuwa anaendelea kutupiwa na yule binti yake pale sebuleni.
Inspekta aliona asubuhi haifiki upesi…
Akiwa ndani ya chumba cha hoteli moja ghali jijini chenye hadhi ya ‘Suite’ Luis Kambesera, mkurugenzi mtendaji wa ile kampuni kubwa ya tafiti za nishati nchini naye aliliona lile tangazo usiku ule. Alikuwa amejilaza chali kitandani huku mwanadada mrembo ambaye si mkewe akiwa amejilaza kifuani kwake, akikoroma taratibu. Alikunja uso na kumsogeza pembeni yule mrembo kutoka kifuani kwake, mapigo ya moyo yakimwenda mbio na mishipa ya kichwa ikimsimama.
“Oh, damn shit! Hii ni nini sasa?” Alijisemea kwa sauti ya chini huku akiinuka kutoka pale kitandani na kutoka nje ya chumba kile na kwenda kuketi kwenye sehemu ya sebule ya kile chumba alichokodi pale hotelini. Alitoa simu yake na kumpigia Chabbi Cheka.
Jamaa alikuwa hapatikani hewani.
Alisonya na kujaribu kumpigia tena, akiamini ni fitna za mitandao tu, lakini bado simu ya Chabbi ilikuwa haipatikani. Akajaribu kumpigia kwa namba nyingine ambayo pia ilikuwa ni ya Chabbi, na mambo yakawa ni yale yale.
“Akh! Kwa nini amezima simu huyu?” Alilaani, huku akiipekua ile simu yake na kuipata namba ya Bilanga na kumpigia.
Naye akawa hapatikani.
“Whaat?”
Aliijaribu mara tatu zaidi namba ya Bilanga, na bado matokeo yakawa bila bila.
Luis Kambesera alisonya na kurudi kule chumbani na kukuta yule mrembo bado akiwa amelala. Alivaa nguo zake haraka haraka, akatoa pesa kiasi cha shilingi elfu hamsini na kuziweka chini ya simu ya yule mrembo iliyokuwa juu ya meza mle chumbani. Akachukua funguo zake za gari na kutoka.
Akiwa njiani kuelekea ofisini kwake usiku ule ule, alipokea simu kadhaa kutoka kwa wale wakurugenzi wake wakuu, wote wakitaka kujua iwapo aliiona ile habari iliyorushwa kwenye runinga usiku ule.
“Nimeona! Tutaliongelea kesho ofisini suala hilo!” Ndilo jibu alilowajibu wote hao.
95 Hussein Issa Tuwa
MTAFITI
Akili yake ilikuwa ikimzunguka.
Je Chabbi amefanikiwa kuzipata hizo taarifa alizopewa Mwantumu na hayati Grayson?
“Ni bora awe amezipata kufikia sasa… maana waandishi wa habari wakishaanza kulivalia njuga suala la yule mtoto kupotea italeta tabu sana
kwetu bila ya kuwa na hizo taarifa mikononi mwetu!” Alijisemea peke yake.
Sasa Chabbi na Bilanga wako wapi lakini hawa, pumbavu zao?
Wakati Zay alipokuwa akiendesha gari kwenda kukutana na Sajenti Pojo
kule kwenye kituo cha basi jioni ile, Chabbi Cheka alikuwa akilivurumusha
VX lake kwa kasi kutoka kule mbagala kulikokuwa na ile nyumba ya uficho alipokuwa amemficha Mwantumu.
Alikuwa akiendesha gari kwa mkono mmoja tu wa kulia hali ule wa
kushoto ukiwa umebweteka kando yake ukivujiwa damu kutoka kwenye lile jeraha baya aliloachiwa na Mwantumu kwenye upande wa kushoto wa shingo yake, ukiwa umemvimba vibaya sana.
Maumivu makali aliyokuwa akiyahisi pale alipong’atwa na yule binti mpumbavu hayakuwa yakimpa taabu sana, kwani alishakutwa na maumivu makali zaidi ya yale katika sekeseke zake hapa duniani, ila alichokijua ni kwamba kasi ya ile damu iliyokuwa ikimvuja ilikuwa ni ya hatari.
“Ah! Yule mtoto atakuwa amenitafuna hadi mishipa pumbavu zake… sasa hii ni mbaya sana! Mbaya sana hii!” Alilaani huku akiendesha kwa kasi kuwahi sehemu ambayo alijua kuwa alitakiwa aende kwa ajili ya matibabu ya haraka.
Alitakiwa aende Kibamba kutokea kule Mbagala, na umbali uliokuwa baina ya zile sehemu mbili ulimkatisha tamaa, hasa akiizingatia foleni iliyokuwapo humo njiani.
Akili yake ilikuwa inamrudisha kule kwenye chumba alipomuacha yule binti akiwa pale sakafuni, na kila ilipomrudisha huko aliilazimisha ihame kutoka huko kwa kuwa hakutaka kumfikiria yule binti wakati ule. Alitaka kufikiria jambo moja tu, nalo ni kufika kwenye sehemu ya tiba ambako hataulizwa maswali wala kudaiwa PF 3.
Alijitahidi kupita njia za mkato, na alipofika maeneo ya matumbi kwa kutumia hizo njia za mkato akaanza kuhisi kizunguzungu.
“Shit, nini sasa hii?” Alilaani huku akijilazimisha kuendesha, lakini baada ya mwendo mfupi zaidi akaanza kuhisi macho yakiingia kiza.
96
“Ah! Damu nyingi imen’toka pumbavu zangu! Siwezi tena!” Alisema na kuliingiza gari kwenye kijinjia chembamba kando ya ile barabara kubwa. Alienda kwa mwendo mdogo hadi kwenye baa moja iliyokuwa kando ya barabara. Alilielekeza gari kwenye maegesho ya pale baa na kulizima. Alibaki akiwa amejifungia mle garini.
Alijitazama mkono wake na kuona kuwa ulikuwa umelowa damu nyingi, damu iliyotapakaa hadi kwenye kiti alichokuwa amekalia na kumlowesha suruali yake.
Akatukana.
Alitoa simu na kumpigia Bilanga.
“Njoo unichukue fasta Bilanga! Nahitaji tiba… unipeleke… Kibamba!” Alimwambia mwenzake kibabe.
“Hah! Tiba? Umekuwaje bosi…? Uko wapi?” Bilanga alisaili kwa mashaka. Kwa uelewa wake ni kwamba Chabbi alikuwa na yule binti dhaifu aliyemdhibiti… sasa tena atapataje madhila ya kuhitaji tiba? Tena tiba yenyewe ikapatikane Kibamba?
Bilanga alijua kuwa iwapo Chabbi alihitaji kupelekwa Kibamba kwa ajili ya tiba, basi tiba hiyo haikuwa ya tumbo la kuhara wala malaria. Alikuwa akihitaji tiba ya majeraha makubwa ambayo asingeweza kutibiwa kwenye hospitali yoyote nyingine bila ya kuibua maswali lukuki. Sasa ni nini kilichomkuta?
“Uko wapi Chabbi?”
Chabbi alifanikiwa kumweleza mahala alipokuwa.
“Okay subiri hapo hapo boss… nakuja… fasta!” Alimjibu.
Akachukua boda boda na kumwagiza dereva wa ile boda boda ampeleke kule alipokuwa bosi wake kwa mwendo wa kasi sana. Yeye muda huo alikuwa maeneo ya Ilala.
Jambo la kwanza Chabbi alilomwambia Bilanga baada ya kumkuta akiwa amejifungia mle kwenye gari lake kule kwenye maegesho ya ile baa ni kwamba azime simu zake zote, na amzimie na zile za kwake.
“Hatuhitaji kutafutwa na mtu yeyote hivi sasa!” Chabbi alifafanua kwa taabu.
Bilanga akatii.
Saa moja na dakika ishirini baadaye Bilanga aliingiza VX ya Chabbi kwenye nyumba moja iliyokuwa ndani kidogo kutoka barabarani huko
97 Hussein Issa Tuwa
Kibamba, mbele ya nyumba ile kukiwa kuna bango kubwa lililoinadi
nyumba ile kuwa ni hospitali ya mifugo.
Ingawa ni kweli pale palikuwa ni sehemu ya kutibu wanyama wa kila aina, ukweli wa ziada ulikuwa ni kwamba daktari yule alikuwa ndiye anayewatibu
wahalifu na majambazi wote wakubwa nchini, ambao huhitaji matibabu
bila ya kuulizwa maswali ya aina yoyote, kwa bei ya juu.
Wakati anaiingiza ile XV ndani ya wigo wa ile hospitali ya mifugo, Chabbi Cheka alikuwa ameshapoteza fahamu kitambo tu.
Nusu saa baadaye, baada ya yule daktari wa majambazi kumaliza kumtibu
Chabbi lile jeraha kwa kumshona na kumuongezea damu kiasi, alimuacha akiwa amelala usingizi wa madawa.
“Huyu hatoamka mpaka kesho. Itabidi alale tu hapa. Wewe unaweza kwenda urudi kesho mwende zenu!” Yule daktari mtu mzima alimwambia Bilanga, kisha akaongezea, “… na ukija uje na pesa yangu. Hii kazi ilikuwa ngumu sana… milioni na laki mbili!”
“Pesa sio ishu dokta… lakini mi’ simuachi mwenzangu hapa. N’takaa hapa hapa!” Bilanga alimwambia.
“Sio utaratibu! Hapa yuko salama… lakini sitaki wateja wangu wa kawaida wakija hapa kesho asubuhi wakute sura za ajabu ajabu…”
“Sasa ipi sura ya ajabu ajabu hapa?” Bilanga akamkoromea.
“Acha ubishi Bilanga! Ondoka hapa ukalale gesti huko mitaani, uje kesho asubuhi saa tatu umchukue jamaa yako… sijui kaenda kutafunwa na nani huko safari hii!” Yule daktari alimwambia bila kumwogopa, na Bilanga akamkazia jicho kali…
“Halafu we’ ujue kuna siku n’takuja kukubana kwenye kichochoro chenye kiza wewe!” Alimtolea kitisho kwa hasira, na yule daktari akaguna.
“Hebu fanya uende Bilanga! Uje na hela yangu kesho hapa!” Daktari alimjibu bila kujali kile kitisho chake, kisha akageuka na kurudi ndani mwake, akimuacha Bilanga pale nje.
Zay hakupata usingizi usiku ule. Alijaribu kulala kwa kuwa alijua kwamba siku itakayofuata ingekuwa na majukumu mengi sana kwake, hivyo ilikuwa ni muhimu sana apumzike. Alikuwa akijigeuza huku na huko pale kitandani, akili ikimzunguka, mawazo yakimrudisha kwenye hekaheka alizokumbana nazo siku ile. Alikumbuka yote, tangu alipokurupushana na lile jibaba lililokuwa limeenda kupekua chumbani kwa Mwantumu,
98 MTAFITI
hadi pale alipoenda kutoa ripoti polisi na ile simu aliyopigiwa na yule mtu asiyejulikana aliyemtaka awape chao ili wao wamrudishie Mwantumu wake…
Alikurupuka na kuketi wima pale kitandani, moyo ukimwenda mbio na macho yakiwa yamemkauka.
Alikuwa anamaanisha nini yule mtu kwa kauli ile?
Ni nini hicho ambacho waliamini kuwa yeye anacho kiasi kwamba wakachukua jukumu la kumteka Mwantumu ili awe kama kiokozi cha kumlazimisha yeye awarejeshee chochote hicho wanachoamini kuwa anacho?
Alisimama na kuwasha taa.
Akabaki akiwa amesimama huku bado mkono wake uko kwenye soketi ya kuwashia taa.
Hapana! Nalielewa vibaya hili suala… sio wamemteka Mwammy ili mimi niwape hicho kitu chao wanachoamini kuwa ninacho… ni kwamba wao wanaamini kuwa Mwantumu ana kitu chao… bila shaka ndio maana wakawa wanamkimbiza na bastola kule ofisini. Na baada ya kumtia mbaroni na kuona kuwa hana hicho
walichodhani kuwa anacho, na mimi kujipendekeza kwangu kupiga simu pale ofisini kwao, wakaamini kuwa labda Mwantumu amenipa mimi hicho kitu...
Yes! Hii inaingia akilini kidogo!
“Mnh! Au…?” Aliguna na kuanza kujiuliza huku akimakinika na wazo jipya lililopita kichwani mwake wakati ule. Haraka aliliendea kabati lake la nguo na kuutoa ule mkoba wa Mwantumu alioukuta mle ndani mwake mchana ule.
Aliuweka kitandani ule mkoba na kubaki akiutazama kwa wasiwasi. Je, sababu ya Mwantumu kutekwa itakuwa kwenye huu mkoba?
Na kama ndivyo… nikiwarejeshea hicho kitu wanachodhani kuwa
Mwantumu amewachukulia, watamuachia Mwantumu wangu?
Kwa namna fulani alijizuia sana kumtamkia Sajenti Pojo juu ya uwepo wa ule mkoba pale nyumbani kwake… kwanza ilikuwa ni kutokana na kutoutilia maanani tu, lakini pia hata alipomwambia juu ya ile simu aliyopigiwa na yule mtu anayetumia namba iliyojificha, na hata baada ya kuhojiwa vikali na yule askari, hakumwambia kuwa jamaa alitaka wabadilishane hicho kitu chao na Mwantumu.
Sababu ya kufanya hivyo hata hakuijua kwa kweli.
Sasa ilimfunukia wazi kuwa huenda majibu ya madhila yaliyomkuta rafikiye yakawa mle mkobani.
99 Hussein Issa Tuwa
Aliketi kitandani na kuufungua ule mkoba. Akatoa makaratasi yaliyopigwa taipu vizuri kwa kompyuta na kubanwa kwa vibanio maalum vya kubania makaratasi vitumikavyo sana ofisini.
Aliyatazama yale makaratasi na hakuyaelewa.
Akayaweka pembeni na kupekuwa zaidi mle mkobani.
Zaidi ya yale makaratasi aliyoyatoa mle mkobani, kulikuwa kuna baadhi ya vitu ambavyo moja kwa moja alivijua kuwa ni vya Mwantumu, vikiwemo vitabu vya masomo yake ya chuo.
Hakukuwa na kitu kingine chochote kisicho cha kawaida ambacho kingeweza kuwalazimisha wale watu kumteka rafiki yake.
Sasa mbona haileti maana?
Alirudia tena kuyatazama yale makaratasi kwa umakini zaidi.
Kulikuwa kuna makabrasha matatu ya makaratasi yaliyobanwa kwa namna tofauti. Kabrasha moja lililokuwa kubwa kuliko mengine, lilikuwa limeandikwa kwa lugha ya kiingereza, juu likiwa na nembo ya ile kampuni ya Liquid Diamond Incorporated.
Kwenye ule ukurasa wa mbele wa yale makarasi, kulikuwa kumebandikwa kijikaratasi maalum chenye gundi cha rangi ya njano, ambacho hata hivyo
kilikuwa kimebanwa kwa pini kwenye ile karatasi ya kwanza.
Juu ya kile kijikaratasi cha njano, kulikuwa kumeandiwa kwa mkono kwa kalamu yenye wino wa buluu. Yalikuwa ni maandishi ya kiingereza pia.
Kiingereza hakikumpa tabu kabisa Zay.
Alisoma yale maneno yaliyoandikwa pale kwenye kile kijikaratasi cha njano na ujumla wa tafsiri yake ukawa ni:
Ripoti kamili ya utafiti mkubwa kabisa niliowahi kuufanya katika taaluma yangu. Ni ripoti itakayobadilisha kabisa taifa la Tanzania, na najivunia kuitekeleza na kuikamilisha. Ripoti halisi nimeshaikabidhi kwa CEO leo hii. Yeeeyyy. G.
Alikunja uso. Ule mwandiko haukuwa wa Mwantumu. Yeyote aliyeandika kwenye kile kijikaratasi alikuwa anajiita ‘G’ au jina lake lilianzia na herufi hiyo.
Alidhani alimjua mtu huyo ni nani.
Aliitazama ile ripoti yenyewe, akiigeuza huku na huko, kisha akaanza kuisoma. Akabaini kuwa ilikuwa ni ripoti ya kitafiti tu iliyosheheni lugha nyingi za kitaalamu na ramani nyingi za maeneo ya Tanzania. Hakuweza
kuisoma yote ukurasa kwa ukurasa, bali alikuwa akiipitia sehemu kadhaa
100 MTAFITI
wa kadhaa za ripoti ile. Ilikuwa ni ripoti ya kurasa zipatazo sitini na saba hivi, na mwisho kabisa wa ripoti ile kulikuwa kuna jina la mwandaaji wa ripoti ile, pamoja na saini yake.
Alilitazama jina la mtu aliyesaini ripoti ile.
Grayson Mochiwa.
Alifinya uso na kumung’unya midomo kwa tafakuri.
Hii haikumletea maana hata kidogo.
Kwa nini Mwantumu awe na ripoti ya ile kampuni kwenye mkoba wake?
Ni kwamba inahusika na mafunzo yake kwa vitendo aliyokuwa akifanya pale kwenye ile kampuni? Hii pia iliwezekana, kwani kuna mara kadhaa Mwammy amewahi kwenda pale kwake akiwa na baadhi ya kazi alizopewa kule ofisini ambazo alizifanya akiwa pale nyumbani na kuzipeleka ofisini siku inayofuata. Je na hii ripoti inaweza kuwa ni sehemu ya hizo?
Au ndio hii ripoti wanayoitafuta wale watu?
Pia haikuleta maana.
Ni wazi kuwa ile ilikuwa ni ripoti ya ile kampuni, kwa hiyo lazima kutakuwa kuna nakala ya ripoti ile kule kwenye ile kampuni, au hata taarifa ile ikawa kwenye kompyuta za ile kampuni.
“Hii haiwezi kuwa ndio sababu ya kumtafuta Mwantumu namna ile, bwana!” Alijisemea mwenyewe.
Alitazama kabrasha lingine, na moja kwa moja akaona kuwa lilikuwa na ripoti ya mafunzo kwa vitendo ya Mwantumu, ambayo msimamizi wake Grayson Mochiwa alikuwa amemwandikia na kuisaini. Alilinganisha zile saini za kwenye zile ripoti mbili tofauti, na kuona zilifanana.
Rundo la tatu lilikuwa ni mjumuiko wa makarasi mbalimbali yaliyobanwa pamoja kwa pini za kubania makaratasi. Yalikuwa ni makaratasi yaliyoonekana kuwa ni ya zamani na hayakuwa yakihusiana na yale makaratasi mengine aliyotoa kwenye mkoba ule. Kulikuwa kuna risiti za manunuzi, vyeti va hospitali, na vipande vya magazeti. Ilikuwa kama kwamba mtu aliyeweka yale makabrasha mawili ya mwanzo aliyakumba na yale makaratasi bila ya kukusudia.
Zay alibaki akiwa amekunja uso pale chumbani.
Bado hakuwa na jibu juu ya kipi hasa wale watu waliomteka Mwantumu walikuwa wanataka kutoka kwake.
Alibaki akiwa amepumbaa bila ya ufumbuzi kwa muda mrefu sana, mpaka pale aliposhtushwa na vishindo vya mlango wake ukigongwa kwa
101 Hussein Issa Tuwa
nguvu. Alikurupuka kutoka kitandani alipokuwa amelala na kubaki akiwa ameketi huku akili ikimzunguka.
Ni nini hicho…?
Akasikia tena mlango wake ukigongwa kwa nguvu. Aliruka haraka na kuyakusanya yale makabrasha yote aliyoyatoa kwenye mkoba wa Mwantumu usiku uliopita, ambayo alikuwa amelala nayo pale kitandani.
Aliyasweka haraka ndani ya ule mkoba na kuranda nao huku na huko akitafuta mahala pa kuuficha, akili ikimhaha na mgongaji akizidi kugonga mlango wake kwa nguvu.
Mnh! Ni nani huyo?
Aliruka hadi jikoni na kuuweka ule mkoba ndani ya friji na kunyakua kisukumio cha chapati, kisha akaenda nacho mbio pale mlangoni huku akiwa amejiandaa kumshambulia huyo mgongaji kwa kisukumio kile, kama angekuwa ni mshari.
“Nani wewe?” Alihoji kwa ukali kutokea nyuma ya ule mlango.
“Zay! Fungua bwana… ni mimi!” Sauti ilimjibu kutokea nje ya ule mlango.
Mama Mwantumu!
Aliufungua haraka ule mlango na kumkaribisha ndani yule mama aliyesawajika uso kwa wasiwasi wa lolote ambalo lingekuwa limemkuta mwanaye.
Walikumbatiana kwa nguvu.
“Ni nini kimemkuta mwenzako Zay mwanangu lakini, eenh?” Mama alihoji kwa hamaniko.
“Ah, mama we acha tu…”
Walijifungia mle ndani, na Zay akamueleza yule mama kila kitu akijuacho, kinagaubaga.
Mama alichanganyikiwa vibaya sana…
102 MTAFITI
LUIS KAMBESERA ALIPITA kwa gari lake nje ya jengo
lililokuwa limehifadhi ofisi za kampuni yake ya Liquid Diamond Incorporated, na kushangaa kuona kundi la watu nje ya lango kuu la kuingilia ndani ya jengo lile. Alizungukia nyuma ya jengo lile ambako ndiko kulikuwa kuna maegesho maalum kwa wafanyakazi wenye magari wanaofanyakazi kwenye jengo lile. Ilikuwa ni saa moja na robo asubuhi, na bado akili yake haikuwa imetulia. Baada ya kurudi pale ofisini kwake usiku wa siku iliyopita akitokea kule kwenye ile hoteli ambako alimuacha kimada wake akiwa amelala, alikaa akiwa amezongwa na mawazo mazito juu ya yale mambo yaliyokuwa yakitokea kwenye ofisi yake. Saa sita usiku alitoka na kurudi nyumbani kwake kulala.
Na sasa, ikiwa ni asubuhi ya siku ya pili baada ya ile misukosuko mikubwa ya siku iliyopita, alikuwa amejiandaa kurekebisha kila dosari iliyoingia kwenye sura na jina la kampuni yake iliyopewa zabuni kubwa kabisa ya utafiti wa nishati nchini, ili kuendelea kulinda hadhi na zabuni ile muhimu sana kwa kampuni yake. Huku bado akiwa amezongwa na mawazo, aliegesha gari lake vizuri kwenye maegesho ya ndani ya jengo lile na kuelekea kwenye mlango wa nyuma ambao ungemuwezesha kuingia ofisini kwake bila kulazimika kuzunguka kule kwenye lango kuu la jengo lile.
“Bwana Kambesera!”
Alishtuka kusikia mtu akiita jina lake, na bila kufikiri mkono wake ukaenda kwenye mkoba maalum wa kubebea bastola aliokuwa ameuvaa kwa ndani ya koti lake huku akigeukia kule ile sauti ilipotokea.
Alishangaa kuona mwandishi wa habari akimfuata huku akiwa amemnyooshea kisemeo na mpiga picha wa televisheni akimfuata nyuma yake huku ile kamera ikiwa imemwelekea yeye moja kwa moja.
Awww, shit!
103 Hussein Issa Tuwa
7
“Je una kauli gani bwana Kambesera, kutokana na habari ya kuuawa katika mazingira ya kutatanisha kwa mmoja wa wakurugenzi wako Grayson Mochiwa hapo jana?” Mwandishi alimuuliza na Luis akapigwa butwaa.
“Yaani mmekuja kunivizia kwenye maegesho huku ili mniulize kuhusu hilo?” Aliuliza kwa kutoamini.
“Na pia una kauli gani juu ya kupotea kwa mfanyakazi wako mwingine katika mazingira hayo hayo ya kutatanisha jana hiyo hiyo?” Mwandishi akamtupia swali jingine kabla hata hajapata jibu la swali lake la kwanza.
“Sijui unapata wapi hizo habari kuwa eti ni mazingira ya kutatanisha. Nijuavyo ni kwamba hilo suala liko mikononi mwa polisi, kwa hiyo mimi siwezi kuliongelea!”
“Na vipi kuhusu huyo mfanyakazi aliyetoweka masaa tu baada ya kuuawa kwa mkurugenzi wako huyo hapo jana?” Mwandishi alizidi kumpiga maswali, na Luis akakunja uso.
“Yule hakuwa mfanyakazi wangu…”
“Lakini alipotea akiwa katika ofisi yako?” Mwandishi alihoji, na Luis akaamua kupiga kimya na kuingia ndani ya jengo kwa mwendo wa haraka huku akiwa amefura kwa hasira.
Hivi hawa akina Chabbi wako wapi wanaharamu hawa? Wangekuwepo wangewadhibiti mapema wale waandishi, pumbavu zao!
Alipitiliza moja kwa moja hadi ofisini kwake, na alipofungua mlango wa ile ofisi ya mbele ambako katibu muhtasi wake huwa anakaa, katibu muhtasi akajua kuwa hali haikuwa sawa.
Yule katibu muhtasi alisimama na kumtazama kwa uso uliojaa woga mkubwa.
“Mista Kambesera… nilitaka kukupigia kukutaarifu lakini hakuniruhusu kufanya hivyo!” Mwanamama alimwambia, na Luis akamshangaa.
“Unaongea vitu gani wewe asubuhi hii…?” Alimuuliza, na hapo hapo akaona macho ya yule katibu wake muhtasi yakitazama sehemu kando ya ule mlango alioushikilia wakati akiingia mle ndani.
Aligeuka na kutazama pale ambako macho ya katibu muhtasi wake yalikuwa yameelekea.
“Hello Luis…! Habari za asubuhi.”
“Wewe!” Luis aliuliza kwa mhemko.
“Si mwingine! Nilikuwa nina maswali ambayo ningehitaji majibu kutoka kwako…” Yule Inspekta aliyekuwa akimhoji jana alimwambia huku
104 MTAFITI
akiinuka kutoka kwenye kiti kilichokuwa kando ya ule mlango. Luis aliuma meno kwa hasira.
Hakika siku yake ilikuwa imeanza vibaya sana.
Alimkata jicho kali yule Inspekta kisha akaguna.
“Nadhani nilikwambia kuwa sitaongea nawe bila ya mwanasheria wangu kuwepo?” Alimuuliza kwa sauti baridi.
Inspekta alimtazama kwa macho makavu.
“Sihitaji maongezi. Nimesema nina maswali… sikia maswali yangu na ukijiona bado unamhitaji mwanasheria wako aje akujibie, basi tutaongozana hadi kituoni na utamsubiria mwanasheria wako ukiwa selo!”
Inspekta alimjia juu, na Luis akamtupia jicho la haraka yule katibu muhtasi wake, ambaye muda wote alikuwa akifuatilia ule mjadala kwa udadisi, na alipoona bosi wake amemtupia jicho akajitia kujishughulisha na kupanga mafaili mezani kwake.
“Tuongee ofisini kwangu!” Luis alisema kwa hasira huku akimuashiria Inspekta apitilize kuingia kule ofisini kwake.
“Niko nyuma yako.” Inspekta alimwambia huku akimuashiria kuwa atangulie yeye kule ofisini.
Wakajifungia ofisini kwa Luis ambako mwenyeji alimwelekeza mgeni waketi kwenye makochi ghali sana yaliyokuwa kwenye kona moja ya ofisi ile kubwa iliyonakshiwa vilivyo, ilhali meza kubwa ya kiofisi ikiwa hatua chache kutoka pale kwenye yale makochi.
Muda huo katibu muhtasi akaingia na kumuuliza Inspekta iwapo alihitaji kinywaji chochote kati ya chai, juisi au soda.
“Hapana… huwa sinywi wala sili nikiwa kazini… hapa nipo kazini. Labda umhudumie bosi wako hapa!” Inspekta alijibu, na binti akamgeukia Luis, ambaye alimuashiria atoke nje ya ile ofisi kwa mkono.
Katibu muhtasi akatoka, na wale mahasimu wawili wakatazamana.
“Okay, ni kipi ninachoweza kukusaidia Inspekta?” Luis aliuliza.
“Mwanadada aitwaye Mwantumu. Anasemekana kuwa ametoweka jana na hajaonekana mpaka leo… mara ya mwisho alionekana ndani ya ofisi hii hiyo jana. Unaweza kunieleza nini juu ya hilo?” Inspekta alienda moja kwa moja kwenye swali lake la msingi.
Luis alimtazama kwa mshangao. Hakutarajia swali lile kutoka kwa yule Inspekta aliyehasimiana naye. Alitaraji maswali zaidi kuhusu Grayson. Hii haikumpa faraja.
“Sijui lolote. Huwa sina kawaida ya kufuatilia mienendo ya kila anayeingia
105 Hussein Issa Tuwa
kwenye ofisi hii… silipwi kwa hilo!”
Inspekta akaguna.
“Nimeambiwa kuwa huyo binti alikuwa akifanya kazi na Grayson Mochiwa, aliyeuawa mbele ya macho yangu hapa ofisini kwako jana… utakubaliana nami kuwa hiyo inaleta haja ya kutaka kujua zaidi juu uhusiano wa matukio haya mawili kutokea siku moja, katika ofisi moja, na kwa watu waliokuwa wakifanya kazi pamoja… mimi nataka kuujua uhusiano huo bwana Kambesera. Utanisaidiaje katika hilo?”
Luis akatoa sauti ya kukereka kabla ya kumjibu.
“Hakuna uhusiano hapo… ni mkutaniko tu wa matukio mawili tofauti katika wakati mmoja bila ya kutarajiwa au kupangwa…” Alimwambia.
“Sasa hilo ndilo ninalopata tabu sana kuliamini kaka… mi’ nadhani kuna uhusiano katika matukio haya mawili.”
Luis akambetulia mabega.
“Fine! Uko huru kudhani utakavyo. Mimi halinihusu hilo… na kama huna la ziada naomba unipishe nifanye kazi nilizoajiriwa na bodi ya kampuni kuzifanya hapa!” Kambesera alimwambia kwa kiburi.
Inspekta alimtazama kwa macho makavu huku akiwa ameachia tabasamu dogo.
“Bado nina maswali kuhusu huyu binti aliyepotea… Mwantumu. Yeye aliajiriwa hapa kama nani?”
“Hakuajiriwa. Alikuwa ameomba na akapewa nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo kama sehemu ya kutimiza vigezo vya shahada yake aliyokuwa anasomea…”
“Na kwa nini aliwekwa chini ya hayati Grayson Mochiwa?”
“Nitakuachia ukaongee na afisa utawala huko… mimi ni mtu mkubwa sana kujibu maswali kama hayo!”
Inspekta alimtazama kwa jicho kali. Kisha akaweka kofia yake kichwani na kuinuka.
“Unajua kuna msemo nilipewa na babu yangu kitambo tu… kwamba akili nyingi hupoteza maarifa…” Alimwambia, na Luis akafyatua kicheko kifupi cha kebehi.
“Kwa hiyo ili tuwe na maarifa inabidi tuwe mambumbumbu? Come on Inspekta, unaongelea nini wewe?”
Ilikuwa zamu ya Inspekta kufyatua kicheko cha kebehi.
“That’s the problem Luis… una akili nyingi sana wewe!” Alimjibu na kuelekea mlangoni.
106 MTAFITI
Luis akabaki akiwa ameduwaa.
“Kwa hiyo hilo kwako ni tatizo?” Alimuuliza kwa hasira. Inspekta alisimama mlangoni na kumgeukia.
“Ndio maana unakosa maarifa ya kuelewa kuwa kwenye kifo cha Grayson na kutoweka kwa Mwantumu, kuna ujumbe wa wazi kwamba
kuna mchezo mchafu sana unaendelea kwenye hii kampuni yako!”
Alimjibu huku akimtazama kwa macho makavu.
Luis alimeza mate na macho yakamtembea. Inspekta aliliona hilo, na likamwambia kuwa alikuwa amegusa kwenye ukweli.
“Sasa ulidhani ningeweza kuwa na wadhifa kama huu iwapo ningekuwa mbumbumbu?” Luis alimtupia swali kwa hasira.
“See? Akili zako hizo! Bado hujawa na maarifa ya kuelewa kwamba
ninajua kuwa kuna mchezo mchafu mlioucheza hapa, na kwamba nitakutia hatiani tu Luis. Wewe huna maarifa ya kunidanganya hata kidogo. Hii kesi bado haijaisha… na wewe na kampuni yako mnahusika sana tu. Tarajia kuniona tena na tena mpaka kieleweke!” Inspekta alimwambia kwa kirefu.
“Toka ofisini kwangu!” Luis alimjia juu.
Inspekta akambetulia mabega.
“Na jiandae kukabiliana na waandishi wa habari… hivi niongeavyo tayari wameshajaa tele hapo nje wanataka majibu… hata sijui uliwezaje kuwapita huko, lakini nina hakika wataendelea kuwepo tu muda utakapotoka!”
Alimwambia na kutoka nje ya ofisi ile taratibu.
Luis alibaki akiwa amefura kwa hasira.
Yuko wapi Chabbi Cheka lakini?
Baada ya kutoka ofisini kwa Luis, Inspekta alimuomba katibu muhtasi wa Luis amwelekeze mahala ilipokuwa ofisi ya afisa utawala wa kampuni ile. Yule dada alimuita mfagiaji wa pale ofisini na kumuomba ampeleke
Inspekta kwenye ofisi aliyoitaka.
Mfagiaji alimuacha nje ya mlango wa afisa utawala wa kampuni ile na kuondoka zake. Inspekta alibisha hodi mara moja kisha akausukuma ule
mlango na kuingia ndani bila hata ya kusubiri ajibiwe na aliyekuwa humo ndani iwapo aingie au la.
Alisimama hatua chache ndani ya ofisi ile akiwatazama wale aliowakuta mle ndani kwa mshangao.
107
Issa Tuwa
Hussein
Sajenti Pojo aliinuka kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia mbele ya meza ya afisa utawala wa kampuni ile, mwanadada mmoja mtanashati aliyekuwa amevalia suti kali na usoni akiwa amevaa miwani ghali ya kusomea.
“Afande!” Pojo alisaluti kwa yule afisa aliyemzidi cheo na kubaki akiwa amesimama. Inspekta aliipokea saluti bila kujali.
“Er, afande… sijui wewe ni nani, lakini nilikuwa na mteja mwingine hapa. Au mko pamoja…?” Afisa utawala alisema, lafudhi yake ikimwambia yule Inspekta kuwa yule mwanadada angekuwa na utulivu zaidi iwapo angekuwa anamuongelesha maneno yale kwa lugha ya kiingereza badala ya kiswahili, na Inspekta akajikuta akitabasamu kidogo.
“Vipi… nimesema kitu cha kuchekesha afande, au?” Afisa Utawala alimuuliza kwa hasira kidogo, akihisi kuwa amedharauliwa. Bado ile ongea yake ilimpa picha ile ile yule Inspekta, na safari hii akajitahidi kuminya kicheko kilichokuwa kikimjia.
Yaani huyu binti amejilazimisha kuongea kiswahili kwa kuwa ameona anaongea na polisi! Laiti angejua!
“Inspekta Haroub Kwakwa, kutoka polisi kituo kikuu cha polisi… nilikuwa nahitaji kuongea nawe kidogo kuhusiana na binti aitwaye Mwantumu…” Yule inspekta alijitambulisha na kuongea.
Mihemo ya mshituko ikasikika kutoka kwa yule afisa tawala aliyemkuta mle ndani na kwa yule Sajenti pia.
“Hah… sasa nyinyi hamna mawasiliano? Huyu mwenzako naye amekuja kuniuliza suala hilo hilo!” Mwanadada mtanashati alimjibu, huku akitembeza macho baina ya wale askari wawili.
“Oh?” Inspekta Haroub Kwakwa alisema na kumgeukia Pojo, mboni nyeusi sana za macho yake zikimpelekea maswali yule Sajenti, kisha akamgeukia yule afisa utawala.
Inspekta Haroub Kwakwa alipata shambulizi baya machoni siku za nyuma, kiasi alikaribia kupoteza kabisa uwezo wake wa kuona. Lakini jeshi lilimtibia na kumponya, ila baada ya hapo mboni zake zilizobabuliwa kwa kulipukiwa na kijibomu kilichotegeshwa kwenye kompyuta mpakato aliyokuwa akiifanyia kazi wakati huo, zilibadilika rangi na kuwa nyekundu.
Hivyo siku zote yeye huwa anaweka mboni za bandia machoni, yaani contact lense, nyeusi. Na mara zote hulazimika kuvaa ile miwani yake ya jua yenye vioo maalum kwa ajili ya kuyahifadhi macho yake yale.
Kama angekuwa anawatazama wale watu aliokuwa nao mle ndani kwa
108 MTAFITI
zile mboni zake halisi bila ya zile za bandia alizokuwa nazo muda ule, bila shaka wale jamaa wangemkimbia tu kwa kumwogopa.
“
Interesting!” Alisema huku akiketi kwenye kiti kingine kilichokuwa mbele ya ile meza ya yule mwanadada, huku akimuashiria Pojo aketi kwenye kile kiti kingine. Alikuwa akimaanisha kuwa ile hali ya yeye kukutana na askari mwenzake mle ofisini wote wakiwa wameenda kuulizia habari za Mwantumu ilikuwa inashangaza.
“
Interesting indeed!” Dada alidakia mara moja, akiafikiana naye juu ya kushangaza kwa hali ile na Kwakwa akajikuta akitabasamu tena alipobaini jinsi yule binti alivyoshabikia kujibu kwa kizungu, akinasa kwenye ule mtego aliomtega ili kujithibitishia ile hisia yake ya kwanza, na pia kutaka kumwonesha kuwa hata polisi pia kizungu kinapanda.
“Er, afande… nilikuwa nimekuja hapa kwa kuwa…” Pojo alianza kujieleza lakini Inspekta Kwakwa alimuashiria anyamaze.
“Okay, kama Sajenti hapa ameshakuuliza kuhusu huyo binti aliyetoweka na umeshamjibu, basi mimi nitapata mrejesho kutoka kwake. Ila nataka ujue kuwa tunatoka vituo viwili tofauti…” Inspekta Kwakwa alimwambia yule afisa tawala wa kampuni ile tata.
“
Okay, afande Pojo hapa keshaniambia kuwa anatokea kituo cha polisi Chang’ombe, na nadhani nilikuwa nimeshamjibu maswali yake yote…”
Afisa Utawala alimwambia na Pojo akatikisa kichwa kuafiki.
“Mimi natokea kituo kikuu cha polisi… central, na ndiye mpelelezi ninayefuatulia kesi ya kifo cha Grayson Mochiwa…”
“Masikini Grayson…” Binti alisema kwa huzuni, kisha akajimakinisha na yaliyokuwa yanaendelea mle ofisini.
“Okay, nimeshajua kuwa mnatokea vituo tofauti. Kwa hiyo wewe nikusaidie nini afande Kwakwa? Maana umesema unafuatilia kesi ya kifo cha Gra… marehemu Grayson… lakini ulipoingia hapa umeanza kuulizia kuhusu Mwantumu. Vipi hapo?” Afisa Utawala alimhoji Inspekta, na Sajenti Pojo alionekana kutamani sana kusikia jibu la yule Inspekta kwa swali lile.
Inspekta alikaa kimya kidogo.
“Grayson alikuwa ni mkuu wa tafiti hapa Liquid Diamond… na huyo binti inasemekana kuwa alikuwa akifanya kazi katika kitengo cha tafiti… na ametoweka siku hiyo hiyo ambayo Grayson aliuawa ndani ya jengo la hii kampuni yenu. Hiyo inatosha kwa mimi kutaka kujua zaidi juu ya huyu binti!” Alimjibu kwa kirefu huku akikunja nne pale kitini.
109 Hussein Issa Tuwa
Binti alitikisa kichwa kuonesha kuridhishwa na maelezo yake, na uso wa Sajenti Pojo pia ukaonesha kuridhishwa na maelezo ya Kwakwa.
“Haya. Sasa ulitaka kujua nini kuhusu Mwantumu?”
“Nilitaka kujua huyu Mwantumu alikuwa hapa kwa muda gani kabla hajatoweka…”
“Nimeshamjibu afande Pojo hilo!”
“Na kwa nini aliwekwa chini ya usimamizi wa Grayson Mochiwa…”
“Oh, mimi ndiye ninayepanga ni wapi wanafunzi wanaokuja field waende kutokana na fani zao wanazosomea. Mwantumu alikuwa anasomea Shahada ya pili ya MBA… lakini shahada yake ya kwanza alisomea viwango vya kitafiti, yaani Statistical Research. Sasa hii ilikuwa inaendana kabisa na kitengo ambacho Grayson alikuwa anakiongoza… so nikamuweka awe chini ya Grayson.” Afisa alijibu.
“Ni kwamba mlitangaza kuwa mnahitaji mwanafunzi wa field katika taaluma hiyo au…?”
“Hapana. Huwa hatutangazi. Ni wanafunzi wenyewe kupitia vyuo vyao ndio huwa wanaomba. Kama hatuna nafasi huwa tunawakataa, lakini kama tunayo basi tunawasaidia…”
“Huwa mnaweka taarifa za makazi ya hao vijana mnaowapokea kwa ajili ya hizo field attachment?”
“Like… wanakaa wapi na vitu kama hivyo?” Afisa Utawala aliuliza, na Kwakwa akatabasamu. Bado binti alikuwa anapata tabu kuongea kiswahli moja kwa moja.
“Haswa!”
“Aammm… ndiyo. Lazima wajaze taarifa za wanakoishi, namba zao za simu, wazazi wao na vitu kama hivyo. Ni muhimu kwa ajili ya masuala kama vile akiumwa ghafla akiwa hapa ofisini au akipatwa na ajali yoyote wakati yuko kazini… inaturahisishia kuwasiliana na jamaa zake.”
“Safi. Na… ni nani anayetunza taarifa hizo?”
“Of course zinakuwa kwenye faili lake la ajira hapa ofisini, na…”
“Naambiwa Mwantumu hakuwa mwajiriwa wenu…”
“… na kwenye ofisi ya usalama pia. Kwa hiyo hata kama si mwajiriwa lazima taarifa hizo ziwepo kwenye ofisi ya usalama.”
“Ofisi ya Bilanga na nani vile…” Kwakwa alimchomekea.
“Chabbi… Bilanga na Chabbi Cheka!” Afisa utawala akatoa taarifa
bila kusita, kidogo akishangaa kusikia kuwa Inspekta Kwakwa alikuwa
anawafahamu wale watendaji wa kitengo cha usalama cha ile kampuni.
110 MTAFITI
Kimya kilijinafasi kidogo, kisha Inspekta Kwakwa akamtupia swali jingine.
“Kwa hiyo tangu atoweke hiyo jana… ninyi kama ofisi mmechukua hatua yoyote ya kuwasiliana na jamaa zake?”
“Amm… kwa mimi na kitengo changu hatukufanya lolote…”
“Kwa nini?”
“… kwa kuwa nami nimezisikia habari za kutoweka kwa huyo binti kupitia kwenye vyombo vya habari kama watu wengine…”
“Jana usiku?”
“
Yah, kwenye ITV…”
“Na ulipofika hapa ofisini leo asubuhi? Hukuona umuhimu wa kufuatilia?” Kwakwa alizidi kumbana.
“Ah, sasa hapo tena hilo suala linakuwa mikononi mwa ofisi ya usalama. Yaani jambo likishahusisha polisi na vyombo vya habari, basi moja kwa moja huwa linashughulikiwa na ofisi ya usalama na… au ofisi ya mwanasheria wa kampuni… ambaye pia ni msemaji mkuu wa kampuni. Mimi sihusiki tena hapo!” Binti alifafanua kiundani.
Kimya kikachukua tena nafasi mle ndani.
“Well? Kuna la ziada?” Binti aliuliza alipoona kimya kimezidi.
“Okay. Nadhani ni hayo tu…”
“Okay…”
“Ah, nilitaka kusahau… hiki kitengo cha usalama kinaripoti kwa nani kwenye hii kampuni?” Kwakwa alichomekea swali lililokuwa limemnanga tangu siku iliyopita alipokutana na Bilanga kule kwenye chumba cha mikutano kulipotokea mauaji. Afisa alisita kidogo.
“Wao wanaripoti moja kwa moja kwa CEO…”
“Kambesera?” Kwakwa aliuliza na binti akaafiki kwa kichwa, kisha akadakia haraka, “Look… ninahitajika kuendesha usaili wa ajira dakika tano zijazo… naomba mniache sasa…”
“Okay si tatizo.Mi’ nimeshamaliza hapa…” Kwakwa alimjibu huku akiinuka. Na Sajenti Pojo naye akainuka.
“Na mimi pia!” Pojo, aliyekuwa kimya muda wote akifuatilia mahojiano yale naye akathibitisha.
Wakaanza kutoka, lakini walipofika mlangoni, Kwakwa akamgeukia yule afisa utawala.
“Je, utakuwa unaweka mafaili ya ajira ya hao watu wa kitengo cha usalama…?”
111 Hussein Issa Tuwa
Mwanadada akamkazia macho.
“Inspekta! Unataka kunifungulia mashtaka au kitu gani? Mbona maswali mengi hivyo?” Binti hakujisumbua kuficha jinsi alivyokereka.
“Natakiwa niendeshe upelelezi wa kifo cha Grayson bibie… na kufanya hivyo yanipasa niulize maswali. Unaweka mafaili ya Bilanga na Chabbi, kama jinsi unavyoweka mafaili ya wafanyakazi wengine wote au huweki?”
“Siweki!”
“Good!” Kwakwa alimjibu na kumuongoza Pojo kutoka nje ya ofisi ile.
“Sasa mimi na wewe twende tukabadilishane taarifa kuhusu haya mambo Sajenti…” Kwakwa alisema huku wakitoka nje ya jengo lile.
“Sawa kabisa afande!” Pojo alikubali.
Ubavuni mwa lile jengo lililohifadhi ofisi za ile kampuni iliyoonekana kugubikwa na mambo ya kiza kulikuwa kuna mgahawa mmoja maridhawa. Kwakwa alimwelekeza Pojo waingie kwenye mgahawa ule ili kupeana habari wazijuazo kuhusu kesi zile mbili zilizoanza kama kwamba kila moja inajitegemea, na ambazo sasa zilielekea kuwa zinahusiana.
Moja ikiwa ni kesi ya mauaji, nyingine ikiwa ni kesi ya mtu aliyepotea kitatanishi.
Pojo alisita kidogo.
“Ah, afande… huu mgahawa… wa kinaizi sana bwana. Sasa mimi…”
“Usijali Sajenti… mi’ n’talipa kila kitu. Njoo tutete hapa bwana!”
Kwakwa alimtoa mashaka, na Pojo akabaki akitabasamu kwa aibu nyepesi. Waliingia mgahawani na kuchagua meza iliyokuwa kwenye kona na kuagiza staftahi.
“Okay Sajenti… niambie kuhusu suala la Mwantumu kwanza na kisha mimi nitakueleza kuhusu Grayson… halafu tuone kama hatufuatilii kesi mbili zinazohusiana.” Kwakwa alimwambia.
Ndipo Sajenti Pojo alipomueleza kila kitu kuhusu Zay, Mwantumu na kituko cha kule chumbani kwa Mwantumu. Inspekta Kwakwa alivutiwa sana na maelezo yale.
“Yaani huyu Mwantumu amemtamkia kabisa mwenzake… huyo Zay, kuwa kuna mtu kamtoa kasi kutoka humo ndani…” Akaoneshea kwa
kidole chake cha gumba ule upande ambao lile jengo lenye ofisi za Liquid Diamond Inc. lilikuwepo, “… na huyo mtu alikuwa na bastola?” Aliuliza.
“Haswa!”
“Na hayo maneno yamerekodiwa kwenye simu ya huyo rafikiye?”
Kwakwa akazidi kuuliza kwa nia ya kutaka kujihakikishia kile alichokisikia.
112 MTAFITI
“Hivyo hivyo!”
Tabasamu pana likachanua usoni kwa Kwakwa.
“Nilijua tu! Hawa jamaa wanahusika aisee… wanahusika kabisa na kupotea kwa Mwantumu na kuuawa kwa Grayson Mochiwa! Yule Luis Kambesera atakuwa anaficha siri kubwa sana katika hili!” Kwakwa alisema kwa msisitizo.
“Nakubaliana na wewe kuhusu kuhusika kwa hii kampuni katika matukio haya mawili, ila huyo Luis Kambesera umsemaye mimi simfahamu afande…”
“Ah, huyo ni Mkurugenzi Mtendaji wa hii kampuni. Nilikuwa na mahojiano naye jana, na nilikuwa na maongezi naye leo hii kabla sijafika pale kwa yule afisa tawala. Jamaa ni mbaya sana aisee!” Kwakwa alimjibu.
“Dah! Sasa tunafanyaje hapo afande?”
“Niite Kwakwa tu bwana, au Haroub. Vyovyote vile, lakini achana na hii mambo ya afande afande sasa!” Kwakwa alimkatisha.
“Unajua siwezi kufanya hivyo afande… sio taratibu zetu!” Pojo akamjibu, kisha akaendelea, “Ila mimi sina uelewa wa kifo cha huyo asemekaye kuwa ni Grayson… nilisikia kwenye taarifa ya habari tu lakini sijui undani wake…”
“Of course! We’ hujui kwa sababu sio kesi yako. Ya kwako ni ya Mwantumu aliyepotea kitatanishi, ya kwangu ni ya Grayson iliyoanza kuwa ya utekaji na baadaye ikawa mauaji… lakini ninaamini hizi kesi mbili zinahusiana, na anayeziunganisha ni Mwantumu.” Kwakwa alisema.
“Okay… kivipi?” Pojo alimhoji yule askari mkubwa kwake kicheo, na mdogo kwake kiumri.
Ndipo Inspekta Haroub Kwakwa alipomuelezea mkasa wote wa Grayson Mochiwa.
Alipomaliza Pojo alibaki akiwa ametumbua macho kwa kutoamini.
“Hah! Yaani ndio hivyo Inspekta? Basi hakika haya matukio yanahusiana na wahusika wakuu hapa ni hawa hawa watendaji wa hii kampuni!”
“Hakika! Sasa nataka tufanye kitu kimoja… wewe endelea na kesi yako ya kumtafuta Mwantumu, na mimi nitaendelea kuwachimba hawa jamaa wa hii kampuni… tutakuwa tunaendelea kufanya kazi pamoja na kupeana habari kwa karibu sana. Kwani bado naamini kuwa Mwantumu ndio kiunganishi chetu. Tukimpata tu tumemaliza mchezo!” Kwakwa alisema.
“Nakubaliana na wewe. Lakini pia kama sisi tumeweza kulijua hilo, basi na hawa jamaa pia watakuwa wamelijua hilo…” Pojo akatoa hoja.
113 Hussein Issa Tuwa
“Sawa. Kwa hiyo…?”
“Kwa hiyo nao watafanya kila waliwezalo kuhakikisha kuwa hatumuoni Mwantumu. Kwani nina imani kuwa yuko mikononi mwao!” Pojo alifafanua hoja yake.
“Yaa, kwa mujibu wa hayo maelezo ya huyo Zay… ni kwamba wanaye. Kwani si alimsikia kabisa sauti yake kwenye simu akimpigia kelele kuwa aende polisi?”
“Yah! Sasa hapa ni kujua tu wamemficha wapi na tumkomboe… hapo tutajua kila kitu!” Pojo alisema.
“Sawa kabisa. Sasa tunapajuaje hapo walipomficha, huo ndio mtihani tulio nao.”
“Sasa hilo linaelekea halitakuwa jepesi, maana pale ofisini sikupata lolote la maana zaidi ya mtaa na namba ya nyumba aishiyo, ambako nilishafika, na namba ya simu ya mama yake…” Pojo alimwambia.
“Sawa. Mimi nadhani sasa cha kufanya baada ya hapo ni kujaribu kuzifuatilia nyayo za Mwantumu kuanzia alipoondoka pale ofisini ile jana, hadi sehemu ambapo nyayo hizo zilipoishia. Naamini hapo katikati utagundua kitu kipya kitakachotupa mwanga zaidi. Sijui umenielewa?”
Kwakwa alimshauri mwenzake na kumwachia swali.
“Vizuri sana.”
“Good, sasa kitu kingine… nataka unikutanishe na Zay…” Kwakwa alimwambia, na Pojo akamwambia kuwa hilo halikuwa tatizo.
Kwakwa alilipia staftahi yao na kwa pamoja wakatoka nje ya mgahawa ule, akizipotezea shukrani za Pojo kwa kumnunulia staftahi asubuhi ile.
Zay alitoka nyumbani kwake asubuhi ile akiwa na ule mkoba wa Mwantumu ukiwa na yale makabrasha ndani yake, pamoja na ule uliokuwa na ile kompyuta mpakato ya yule rafiki yake.
Alikuwa amefanikiwa kumpoza mama Mwantumu aliyejawa wahka, na kumuacha pale nyumbani kwake akimwambia kuwa alikuwa anaenda kufuatilia vitu muhimu vya saluni yake kabla ya kwenda kazini jioni ile.
Alienda moja kwa moja hadi ofisini kwake kwenye ile kasino kubwa jijini ambayo muda ule wa asubuhi ilikuwa kimya. Aliingia mle ofisini na
kwenda kupitiliza hadi kwenye chumba cha kubadilishia nguo, ambamo
114 MTAFITI
humo, kila mfanyakazi alikuwa na kabati lake la kuhifadhia sare zao za kazi. Makabati yale huwa yanafungwa kwa namba za siri ambazo kila mfanyakazi alikuwa anazijua mwenyewe. Alifungua kabati lake na kuuweka ule mkoba wa Mwantumu mle ndani.
Alipotoka hapo alienda hadi kwenye mgahawa mmoja tulivu katikati ya jiji na kuangiza kinywaji, kisha akaitoa ile kompyuta mpakato ya Mwantumu na kuanza kuipekua kutafuta taarifa zozote ambazo labda zingeweza kumpatia mwanga juu ya kile kilichomkuta rafikiye.
Alidhani kuwa kufanya upekuzi ule akiwa nyumbani kwake isingekuwa rahisi kutokana na mama Mwantumu kuwepo, ambaye angeweza kuwa akimuuliza hili na lile kila mara na hivyo kumpotezea umakini.
Aliipekua ile kompyuta kwa saa mbili nzima, na hakuna chochote kisicho cha kawaida alichokibaini. Akiwa amekata tamaa, alibaki akiwa ameduwaa pale mgahawani wakati simu yake ilipoita.
“Ya!” Alisema simuni.
“Yatupasa tuonane bi mdogo… kuna mwenzangu inabidi nikukutanishe naye… unaweza kuonana nasi?” Sajenti Pojo alimuuliza.
“Oh? Mwenzako gani huyo afande… ni kuhusu hili suala letu?” Zay aliuliza.
“Yeah… ni Inspekta kutoka kituo kikuu cha polisi…” Pojo alimjuza.
“Kituo kikuu?”
“Ndio, polisi central…”
“Ahaa, okay” Zay alielewa na akamtajia mahala alipo.
“Okay tusubiri hapo hapo basi!” Pojo alimwambia na dakika ishirini baadaye, Inspekta Kwakwa na Sajenti Pojo walifika pale mgahawani alipokuwa. Walisalimiana na Pojo akawatambulisha.
“Mimi ni mpelelezi ninayefuatilia kifo cha Grayson Mochiwa. Pojo amenipa mrejesho wa mambo yaliyojiri baina yenu, sasa nilikuwa nahitaji kuisikia ile sauti ya Mwantumu uliyorekodi kwenye simu yako…” Kwakwa alimwambia.
“Sikuirekodi. Ni ujumbe wa sauti ambao Mwantumu alinitumia siku aliyopotea…” Zay alimsahihisha.
“Okay, sawa. Naweza kuusikia?”
Zay akamsikilizisha.
Baada ya kuusikiliza ule ujumbe Kwakwa alitikisa kichwa kwa mastaajabu.
115 Hussein Issa Tuwa
“Yaani hii ni evidence ya moja kwa moja kuwa ile kampuni inahusika na kutoweka kwa Mwantumu!” Alisema kwa hamasa, akimaanisha kuwa ule ujumbe wa Mwantumu aliotumiwa Zay ulikuwa ni ushahidi wa moja kwa moja dhidi ya ile kampuni ya Liquid Diamond Incorporated.
“Na ndivyo afande Pojo hapa alivyosema hapo awali Inspekta… tatizo ni kwamba sioni namna huu ushahidi ukitusaidia kumpata Mwantumu wazee!” Zay alisema kwa kukata tamaa.
“Kwa sasa bado tunakusanya ushahidi tu bibie, wakati ukifika utatusaidia sana kuwatia nguvuni wahusika!” Kwakwa alimwambia.
“Sieleweki. Sina haja ya kuwatia nguvuni hao wahusika mimi.
Ninachotaka ni rafiki yangu apatikane! Najisikia vibaya sana, hamjui tu!”
Zay alilalama kwa hamaniko.
Kwakwa akamakinika naye.
“Unajisikia vibaya? Kivipi? Unadhani ulisababisha Mwantumu kukutwa na hayo yaliyomkuta?”
“Hapana! Ila Mwantumu amenipigia simu mara tano nami sijaweza kuzipokea kwa kuwa niliziba sauti ya simu yangu kwa sababu nilikuwa nikijivinjari na mpenzi!, Sa’ unadhani mi’ n’najisikiaje hapo baada ya kujua kuwa alipokuwa kwenye matatizo rafiki yangu alikuwa akinipigia ili nimsaidie?” Zay alisema kwa hasira, na wale maafande wakatazamana.
“Oh, pole sana… ila usijilaumu kwa hilo. Si kosa lako…” Kwakwa alisema, na Zay akatazama pembeni akijifuta chozi.
“Sasa mnasema kuwa huu ujumbe wa Mwantumu ni ushahidi muhimu… na utusaidie basi kumleta rafiki yangu hapa!” Zay alisema kwa uchungu. Kimya kilichukua nafasi kwa muda.
“Er… Naomba unitumie huo ujumbe kwenye simu yangu basi, sista.”
Hatimaye Kwakwa alimwambia huku akitoa simu yake ya Android kama ile ya Zay, ila yake ilikuwa ni toleo jipya zaidi ya lile la Zay. Zay aliikodolea macho ile simu kwa matamanio, lakini hakusema kitu. Kwakwa akatabasamu kidogo alipoona jinsi yule binti alivyoistaajabia ile simu yake, lakini naye hakusema kitu.
Walipeana namba za simu na hapo hapo Zay akamrushia ule ujumbe wa Mwantumu, nao ukapokelewa kwenye simu ya Kwakwa.
“Safi! Nadhani hii itanisaidia sana kwenye upelelezi na ushahidi wangu dhidi ya wamiliki wa ile kampuni.” Alisema.
116
MTAFITI
“Okay, sasa nini kinafuata?” Zay aliuliza.
“Sisi tutaendelea na kazi. Pojo ataendelea kufuatilia nyenendo za Mwantumu saa kadhaa kabla ya kutoweka kwake… na labda hiyo itatupa mwanga fulani….” Kwakwa alimwambia, na Zay akaguna tu.
“Na wewe unatakiwa ukae mbali na ile kampuni Zay… baada ya kuwa wameshajua kuwa wewe ni rafiki wa karibu wa Mwantumu, huenda wakakufuatilia na wewe…nashawishika sana kukuweka chini ya ulinzi kwa usalama wako…” Pojo alisema, na Zay akamjia juu.
“Ah, uniweke chini ya ulinzi tena? Mi’ lazima nifuatilie rafiki yangu alipo bwana… siwezi kujificha tu wakati najua mwenzangu yuko mikononi mwa madhalimu huko!”
“Sawa. Lakini mazingira uliyomo yanaruhusu sana afisa wa polisi kukuweka chini ya ulinzi kwa usalama wako, ingawa nadhani kwa sasa ni mapema sana kufanya hivyo. Ila tukipata matukio ya kuashiria hatari kwenye maisha yako, hiyo ndio itakuwa njia pekee ya kukusalimisha!”
Kwakwa alimwambia, na Zay akatikisa kichwa kwa masikitiko.
“Mnh! Hilo mi’ haliniingii akilini bwana!” Alisema.
“Sio ishu kwa sasa…” Pojo alimwambia, kisha akaendelea, “… unaweza kuwa na picha ya Mwantumu ambayo naweza kuitumia kwa kuendeshea upelelezi wangu?”
“Picha ya aina gani… mi n’na picha zake nyingi tu, lakini karibu zote ziko kwenye mfumo wa dijitali…” Zay alimwambia.
“Ah, mi nilikuwa nahitaji picha ya kawaida ninayoweza kuishika mkononi na kuwaonesha watu!” Pojo alisema.
Zay alikunja uso.
Akatoa pochi yake ya kubebea pesa na kuifungua.
“Kama hii itafaa?” Alimuuliza huku akimfunulia ile pochi na kumuonesha picha mbili zilizokuwa zimepachikwa ndani yake, zikiwa na ukubwa wa pasipoti. Moja ilikuwa ikimuonesha yeye mwenyewe, na nyingine ikimuonesha Mwantumu.
Pojo na Kwakwa wote walipiga mshituko walipoiona picha ya Mwantumu.
“Ah! Ndi… ndio Mwantumu huyu?” Pojo aliuliza.
“Ndio yuko hivyo?” Kwakwa naye aliuliza.
“Yaaa, ndio Mwantumu huyu jamani… kwani vipi, kuna tatizo?” Zay
117 Hussein Issa Tuwa
aliwajibu na kuwauliza. Wale askari waligwaya kidogo.
“No, no problem… hatuku… sikutegemea kuwa angekuwa hivi… si tatizo lakini!” Kwakwa alimjibu.
Zay alitembeza macho kutoka kwa mmoja wa wale askari kwenda kwa mwingine. Pojo hakusema kitu.
“Hamna tatizo bibie…” Kwakwa alimsisitizia.
“Okay, fine. Sasa hii picha itafaa au haitafaa?” Hatimaye Zay alisema na kuuliza.
“Yah. Hiyo itafaa tu, sio mbaya!” Pojo alijibu haraka, na Zay akaichomoa na kumpa.
“One more thing… Mwantumu… hana marafiki wengine ambao unawafahamu anaoweza kuwa ameenda kwao?” Kwakwa alimuuliza swali la ziada.
“Huenda huko chuoni kwake UDOM… lakini kwa hapa Dar rafiki yake ni mimi tu. Na pia, Mwammy alikuwa nyumbani kwangu kabla ya kutoweka, hivyo kama si kutoweka bado angekuwa pale kwangu muda huu… na isitoshe, simu yake ninayo mimi hivyo kama si kutoweka na angekuwa kwa rafiki mwingine yeyote mbali na mimi, angenipigia na kunijulisha. Usipoteze muda kufikiria marafiki wengine ambao hawapo afande… Mwammy ametoweka. Mtafuteni!” Zay alimjia juu.
“Okay, umesomeka. Wacha sisi twende sasa bi Zay… in case of anything, tutawasiliana…” Kwakwa alimwambia, na Zay akasita kidogo.
Akaweka pesa alizozikunja pamoja pale mezani kwa mashaka.
“Iwasaidie kwenye mienendo ya hapa na pale jamani…” Alisema huku akiwatazama kwa wasiwasi wale askari.
Kwakwa na Pojo walizitazama zile hela na haraka Kwakwa akachukua kadi la orodha ya vyakula na bei zake lililokuwa pale mezani na kuzifunika zile hela. Zilipata kiasi cha elfu thelathini hivi, kisha wale askari wakatazamana na kumgeukia yule binti.
“Tumekuomba hela sisi?” Kwakwa alimuuliza akiwa makini.
“No! Ni mimi tu nimeamua kutoa mchango wangu jamani. Msinielewe vibaya!” Zay alijitetea.
Kwakwa akamgeukia Pojo.
“Sajenti, umemsikia mwenyewe kuwa kaamua kujitolea…”
“Yes, afande, lakini…”
118 MTAFITI
“Okay basi. Chukua hizo hela zikusaidie kwenye mienendo… no problem.” Kwakwa alimwambia. Pojo akazichukua na kuinuka. Kwakwa
naye akainuka.
“Basi hili naomba liwe ndio la mwisho bibie. Sisi tunafanya kazi kutimiza wajibu, hatuhitaji kupewa hela kila tunapokutana. Najua hii ni tabia mliyozoeshwa raia na baadhi ya wenzetu!” Kwakwa alimwambia, na Zay akaafiki kwa woga.
Wakaagana.
Chabbi Cheka alifumbua macho na kuyafumba haraka. Akauma meno kuzuia maumivu mepesi ya kichwa kisha akapitisha ulimi wake kwenye midomo yake, na akajihisi kama aliyekuwa akipitisha msasa kwenye midomo ile.
Koo lilikuwa limemkauka sana, kinywa kikiwa kikavu kuliko ilivyowahi kumtokea maishani. Akafumbua macho, na kukutana na uso wenye tabasamu wa yule daktari wake wa kificho.
“Naona umerudi kwenye ulimwengu wa walio macho sasa. Safi sana!”
Yule daktari alimwambia, akiwa amesimama kando ya kitanda alichokuwa amelalia.
“Maji… nataka maji!” Chabbi alimwambia, na kama aliyekuwa ameitarajia hali hiyo kutokea mara Chabbi atakapoamka, dokta alichukua chupa ya maji iliyokuwa kwenye kijimeza kando ya kile kitanda na kumpa.
Chabbi akayagugumia yale maji kwa pupa. Alipomaliza aliitupa sakafuni chupa tupu iliyokuwa na yale maji na akabaki akimtazama yule tabibu huku akilini akijilazimisha kukumbuka kila kilichotokea kabla.
“Uuuh… Bilanga yuko wapi?” Jamaa liliuliza huku likijiinua kutoka pale kitandani, likifinyanga uso wake bila shaka kwa maumivu liliyokuwa likiyahisi na kujaribu kugeuza kichwa chake ili kutazama pale alipojeruhiwa. Hakufanikiwa.
Maumivu bado yalikuwepo lakini sio kama ilivyokuwa jana.
“Ahsante kwa kushukuru Chabbi, lakini hii ni kazi yangu hivyo siku nyingine haina haja ya kunipa ahsante. Ukinilipa pesa yangu tu itatosha!”
Daktari alimwambia kwa fumbo, akimaanisha kuwa alitakiwa aanze japo kwa kushukuru kwa kupatiwa tiba na maji ndipo aanze kumuulizia huyo
119 Hussein Issa Tuwa
Bilanga wake.
Chabbi alimtazama kwa jicho baya.
“Hebu acha hizo! Yupo wapi Bilanga wewe?” Alimuuliza na kuteremka kutoka pale kitandani, kisha akiwa kidari wazi, alitembea kwa kuburuza miguu hadi kwenye bafu lililokuwa limeungana na kile chumba kidogo
alichokuwa amelazwa, na kujitazama kwenye kioo kikubwa kilichokuwa juu ya beseni la kunawia.
Plasta kubwa nyeupe ilikuwa imebandikwa sehemu ambapo shingo yake
ilikuwa inaungana na bega, na akauma meno kwa hali ile. Mkono wake bado ulikuwa umevimba kidogo na hakuweza kuuning’iniza moja kwa moja ubavuni kwake. Aliukunja na kuulaza kifuani kwake.
Alirudi pale chumbani na kumkata jicho kali yule daktari.
“Nahitaji kuanza pilika zangu miye… wapi nguo zangu?”
“Shati lako na koti vilikuwa havitamaniki kwa damu. Shati ilibidi nilichane ili nilitoe mwilini mwako, ila koti lako lipo. Ilibidi nikufulie usiku ule ule kwa kutumia mashine yangu ya kufulia hapa, na nikalikausha kwa hiyo hiyo mashine…” Jamaa alimjibu na hata wakati anamjibu vile, Chabbi aliliona koti lake likining’inia nyuma ya mlango wa ile wodi ndogo aliyokuwa amelazwa kwa masaa mengi.
Aliguna na kwenda kulichomoa lile koti kutoka pale mlangoni na kuanza kulivaa lakini daktari akamzuia. Akamvisha bandeji maalum ambayo ilipita shingoni kwake na kuushikilia ule mkono uliojeruhiwa kifuani kwake ukiwa umejikunja kutokea kwenye kiwiko.
“Okay… bei gani kwa huduma zako?” Chabbi alimuuliza huku akiwa amevaa koti mkono mmoja ilhali kwenye ule upande aliong’atwa aliliwekeza tu lile koti juu ya bega lake, mkono wa lile koti ukining’inia peke yake ubavuni kwake.
“Nilishamwambia Bilanga kuwa…”
“Bilanga simuoni hapa, na mimi ndiye mlipaji. How gaddem much?” Chabbi alimjia juu kwa kisirani.
“Milioni na laki mbili!”
Chabbi wala hakushituka.
“Gari langu liko hapo nje?”
“Yeah… lipo!”
Chabbi alitoka hadi kwenye gari lake, akafungua droo ya mle garini, na kutoa kijitabu cha hawala za fedha. Muda huo alimuona Bilanga
120
MTAFITI
akishuka kutoka kwenye bodaboda nje ya geti la ile dispensary ya wanyama kwa maana halisi ya wanyama, na pia kwa maana ya watu wenye tabia za kinyama kama yeye.
“Nenda kaniletee silaha nilizokuwa nazo wakati nafika hapa dokta… mi’ nakuandikia cheki yako hapa!” Chabbi alisema, na dokta akarudi ndani.
Dakika kumi baadaye, Bilanga alikuwa nyuma ya usukani wa ile VX, na Chabbi alikuwa amekunja uso kwa mawazo kwenye kiti cha abiria kando yake. Bilanga alikuwa amekifunika kile kiti cha dereva kwa nailoni kubwa alilolipata pale kwa yule daktari kuziba ile damu iliyokilowanisha kiti kile, ingawa kufikia muda ule ilikuwa imeshakauka.
“Ni nini kilichotokea kule bosi? Mbona imekuwa hivi?” Bilanga alimuuliza mwenzake huku akiendesha gari. Chabbi aliguna na kusonya. Akamweleza kilichojiri mpaka pale alipong’atwa na Mwantumu.
“Ah! Yule mtoto kumbe naye kiburi eeenh? Sasa umemfanyaje..?”
“Nimemwacha huko huko, nifanyaje? Ilinibidi nije kupata tiba haraka… si umeona ilivyokuwa? Ningechelewa ingekuwaje unadhani?” Chabbi alisema.
“Dah! Kweli. Kwa hiyo mpaka mkasa huo unakutokea alikuwa hajasema? Hebu niachie mimi nikaongee naye Chabbi!” Bilanga alisema kwa hamasa, na Chabbi akageukia nje.
“Haina haja tena Bilanga… yule binti hatakuwa na msaada wowote kwetu sasa!” Chabbi alimjibu kwa mkato, na Bilanga hakumuelewa.
“Ama! Hana msaada vipi wakati hajasema wapi kaficha makabrasha? Lazima aseme bwana! Kwani…”
“Hana msaada tena nakwambia… we vipi? Sasa hivi nguvu zote tuzihamishie kwa yule rafiki yake. Nadhani yeye atakuwa nayo hayo makabrasha… mtafute yule binti Bilanga. Mtafute na umpate leo hii!” Chabbi alifoka.
Bilanga akamtupia jicho la pembeni.
“Sikuelewi bosi!”
Badala ya kumjibu, Chabbi alimkata jicho kali. Bilanga akapiga kimya, mawazo mazito yakimchonyota kichwani, kama jinsi ambavyo ilivyokuwa kwa Chabbi.
Walienda kwa muda mrefu bila ya yeyote kati yao kuongea lolote, kisha Chabbi akaachia tusi zito la nguoni na kupigiza ubavu wa ngumi yake kwenye paja lake.
121 Hussein Issa Tuwa
Bilanga akamgeukia kwa macho ya kuuliza, na alipoona jinsi Chabbi alivyoiva kwa hasira, akapiga kimya. Maswali mengi zaidi yakijizonga kichwani mwake.
“Nataka yule rafiki yake apatikane leo hii, Bilanga!” Chabbi aliunguruma kwa hasira garini.
“Hilo ulishaniambia bosi.”
“Na sasa nimekwambia tena!” Chabbi alimkoromea kwa hasira kubwa. Bilanga hakumjibu.
Waliendelea na safari yao wakiwa kimya, na walipoanza kuingia mjini, Chabbi alimuamuru Bilanga ampeleke nyumbani kwake, Sinza Madukani.
“Sasa tunamueleza nini bosi Luis huko, Chabbi? Maana bila shaka atakuwa ameshatutafuta sana tangu jana… na nikifika kule ofisini lazima ataniuliza tu…” Bilanga alisema.
“Luis niachie mimi… nitampigia simu na kumuweka sawa juu ya kilichotokea…”
“Ambacho ni kipi Chabbi? Mi’ sikuelewi ujue!”
“Wacha nikajiweke safi kwanza Bilanga. Wewe fanya kila kiwezekanacho huyu rafikiye Mwantumu apatikane… kuna mambo makubwa sana ya muhimu kwenye kampuni ambayo yanaweza kuharibika kwa kiwango kibaya sana kama huyu mtoto hatopatikana!” Chabbi alizidi kusisitiza.
Bilanga akaguna.
“Chabbi mimi na wewe tunapaswa tufanye kazi pamoja bwana. Nataka uniweke wazi kwa kila kinachoendelea ili tupate kwenda sawa… kama Mwantumu amekutoroka nijulishe bwana tupange mkakati mbadala…”
“Hajanitoroka na hatotoroka. Utajua kila kitu kwa wakati mwafaka. Kwa sasa kumpata huyu rafikiye Mwantumu ndiyo first priority! Nitaongea na Luis na tutakutana tena wote kupanga mikakati. Sawa bwana?”
Bilanga hakumjibu.
Alimfikisha nyumbani kwake na kuingiza lile gari hadi ndani ya wigo wa nyumba ile.
Waliteremka.
“Itabidi hili gari likaoshwe vizuri sana Chabbi… hicho kiti chote kimeharibika kwa baka la damu… haileti picha nzuri.”
“Nitabadilisha viti kabisa… na hivi vya humu n’tavitia moto!” Chabbi alisema huku akielekea ndani kwake.
Bilanga alimuachia gari lake naye akaanza kulielekea geti la kutokea nje
122
MTAFITI
ya nyumba ile.
“Fuatilia hilo jukumu Bilanga!” Chabbi alimwambia huku akielekea
mlangoni kwake.
Bilanga alimuinulia mkono wake juu huku akiwa amemfanyia alama ya dole gumba, na akiendelea kutoka nje ya geti lile bila ya kugeuka. Ingawa
alikuwa ana uwezo wa kumiliki gari, yeye alipendelea zaidi pikipiki. Pikipiki yake kubwa na yenye nguvu aina ya BMW ilikuwa nyumbani kwake maeneo ya Ilala. Alikamata bodaboda pale Sinza na kumwambia dereva ampeleke nyumbani kwake.
Huko alioga na kubadili nguo, kisha akatoka akiwa amevaa suti nyeusi ya jeans. Akavaa kofia ngumu ya kuendeshea pikipiki, nayo ikiwa nyeusi na kutoka kwa mwendo wa kasi na lile pikipiki lake kubwa lenye nguvu.
Kabla ya kuanza mkakati wake wa kumsaka rafiki wa Mwantumu kama alivyoagizwa na Chabbi, aliamua kuelekea Mbagala…
123
Hussein Issa Tuwa
KULE LIQUID DIAMOND Incorporated, mkutano mzito ulikuwa ukifanyika kule ghorofa ya nane kwenye chumba cha mikutano. Wahusika wa mkutano ule walikuwa ni wale wale waliokurupushwa na hayati Grayson Mochiwa siku moja tu iliyopita.
“Jamani, kutokana na matukio haya mawili yaliyoimulika kampuni yetu hivi sasa, nimeona kuwa thamani ya hisa zetu kwenye soko la hisa la Dar es Salaam imeshuka sana. Hii imesababisha washirika wetu kule afrika ya kusini waje juu sana…” Luis Kambesera alikuwa akiwaeleza wenzake.
“Ah, sasa kwani ni kosa letu Grayson kuuawa? Wao lazima waelewe hilo!” William Maginga, mkuu wa idara ya tehama alisema kwa kukereka.
“Hizo ndio siasa za kibiashara kwenye makampuni makubwa kama hili letu wazee. Cha kufanya hapa ni kutafuta namna ya kurejesha imani ya wananchi na wanahisa kwenye kampuni!” Suleiman Mwangi, mwanasheria wa kampuni alichangia hoja.
“Yeah right… na sijui nd’o tunalifanyaje hilo! Maana jinsi vyombo vya habari vilivyolivalia njuga hili suala… na lile la kupotea kwa yule binti wa field attachment hapa, utadhani wametumwa!” Jamilla Mchebe naye alitia hoja yake, na Luis Kambesera akawa makini.
“Inawezekana ikawa wametumwa aisee… si unajua tuna makampuni pinzani kibao tu? Hasa miongoni mwa wale waliokuwa wakiitaka hii tenda tuliyopewa sisi na serikali?” Alisema huku akitembeza macho miongoni mwa wale wenzake, lakini Mike Mwangati, meneja uzalishaji hakukubaliana na hoja yake.
“Hoja haibebi maji hiyo Luis! Hao wapinzani sio waliosababisha Grayson afanye hayo aliyoyafanya na hata akakutwa na umauti kwa namna ya kutisha namna ile… na pia sio waliosababisha huyo binti apotee. Mi’ nasema haya mambo yametukuta na hao wapinzani kama wametia mkono
124 MTAFITI
8
katika hizi nongwa za waandishi wa habari ni kwamba wameona kuwa
kwenye matukio haya kuna nafasi ya kutupaka choo, nao wakaidakia …”
“Unamaanisha nini sasa, Mike?” Luis alisaili.
“Namaanisha tusihamishe maamuzi ya msingi kwenye suala hili kutoka pale ambako panatakiwa pachukuliwe maamuzi. Kujishughulisha na wanaoshabikia kuaibika kwetu badala ya kujishughulisha na kuiondoa aibu iliyotukumba ni kujidanganya!” Alisema, na mbinu ya Luis kupoteza malengo ikashindwa.
“Okay, sasa tunafanyaje?” Jamilla alihoji.
“Inabidi hapo ifanyike damage control waungwana! Hamna kingine!”
Suleiman Mwangi, mwanasheria wa kampuni alisema, akimaanisha kuwa kilichohitajika pale ni kuchukua hatua za kukata makali ya athari ambazo
tayari zimeshatokea kwenye kampuni yao kutokana na matukio yale mawili.
Kabla ya yeyote kati yao hajaongea, Luis alionekana akikunja uso kwa hasira, akipeleka macho yake kule mlangoni, na wenzake wakafuata uelekeo wa macho yake.
Inspekta Haroub Kwakwa alionekana kupitia kwenye kioo cha ule mlango mpana wa kile chumba cha mikutano akielekea kule walipokuwa.
“Huyu jamaa sasa anataka kunipotezea uvumilivu wangu… anataka nini tena?” Luis alisema kwa hasira, wakati Inspekta Kwakwa akisukuma mlango wa kile chumba na kuingia mle ndani.
“Unataka nini tena Inspekta? Si nimeshakujibu maswali yako yote? Sisi tuko kwenye mkutano wa kikazi hapa! Usifikiri kuwa tuko hapa kujibu maswali ya vijinjagu vyenye njaa bwana, unasikia wewe?” Luis Kambesera alimkoromea kwa hasira huku akiinuka kutoka kwenye kiti.
Inspekta Haroub Kwakwa alimtazama kutokea nyuma ya miwani yake maalum, kisha akawatembezea vioo vya miwani yake ile wote waliokuwa mle ndani. Akaona jamaa walikuwa wakigwaya na baadhi wakimtazama kwa macho ya ghadhabu.
“Nilidhani mlihitaji jeshi la polisi lifanyie uchunguzi kifo cha mfanyakazi mwenzenu… mkurugenzi mwenzenu… Grayson Mochiwa, na liwafikishe mbele ya sheria wahusika wa kifo chake?” Inspekta Kwakwa alisema huku akiwatazama wale watu wengine waliokuwa mle ndani, akimpuuzia kabisa Luis.
Jamaa wote wakapiga kimya.
“Okay. Inaelekea nilielewa vibaya kumbe… hamna yeyote mwenye haja
125
Issa Tuwa
Hussein
ya kumjua muuaji wa Grayson hapa…” Aliendelea huku akitoa ile miwani yake kutoka usoni kwake na kuipachika kwenye mfuko wa chati lake.
“Hapana, hakuna aliyesema hivyo…” Suleiman Mwangi, mwanasheria wa kampuni alidakia, lakini Kwakwa akampuuza.
“… bila shaka hiyo ni kwa kuwa Grayson alikuwa ni kikwazo kwenu nyote! Jambo ambalo…” Kwakwa alikuwa akiendelea, lakini Luis akamkatisha.
“Unaongea vitu gani wewe lakini? Ni wapi unapata hiyo habari kuwa eti Grayson alikuwa kikwazo…?”
“… jambo ambalo linawafanya ninyi nyote humu ndani kuwa ni watuhumiwa wakuu katika kifo chake!” Kwakwa alimalizia huku akiwa amemkazia macho yake yenye mboni za bandia zilizokoza weusi Jamilla Mchebe, mkurugenzi wa fedha wa kampuni ile.
“Hah!” Jamilla aligwaya vibaya sana, sambamba na miguno mingine kutoka kwa wenzake wote waliokuwa mle ndani, isipokuwa Luis.
“Unajua kuwa tunaweza kukuchukulia hatua za kisheria wewe? Unakuja kutushutumu bila ushahidi wowote hapa!” Yule mwanasheria wa kampuni alimjia juu, na Kwakwa akamtupia jicho kali.
“Jamani hebu tutulie basi, eenh?” Mike Mwangati, meneja uzalishaji alisema, kisha akaendelea, “Huyu askari amekuja hapa kwa namna alivyokuja kwa kuwa analo la kutuambia. Sasa badala ya kumsikiliza tumeanza kumjia juu…”
“Sio wote tuliomjia juu Mike… ajabu yeye anatujumuisha sote kwenye shutuma za kijinga!” William Maginga alimkatisha, na Mike Mwangati akatikisa kichwa kwa masikitiko baada ya kuona kuwa bado wenzake walikuwa hawamuelewi.
Haroub Kwakwa alikuwa akifuatilia mabishano yale kwa makini. Mike Mwangati akamgeukia Luis Kambesera.
“Mkurugenzi, hebu liweke sawa hili… Inspekta lazima analo lililomleta hapa, na wewe umeanza kumjia juu kabla hujamsikiliza…”
“Inatia moyo kuona kuwa angalau kwenye kampuni kuna baadhi ya watu wenye busara kidogo!” Kwakwa alisema, na akasikia misonyo kutoka kwa baadhi ya wale wakurugenzi mle ndani. Luis akameza mate na kumtupia Kwakwa miale ya kifo kwa macho yake.
“Huyu bwana alishakuja hapa na akanikorofisha sana. Sasa alipokuja tena namna hii, tena bila hata ya kuweka taarifa ya awali, mi’ nikajua kuwa amekuja kuendelea kunikorofisha tu!” Aliwaambia wenzake, kisha
126 MTAFITI
akamgeukia Kwakwa, “Okay Inspekta… ni nini kilichokuleta hapa sasa?”
Inspekta Kwakwa alimtazama kwa muda, kisha akavuta kiti cha ziada kilichokuwa mle ndani na kuketi mbali kidogo na ile meza kiasi cha kumuwezesha kuwaona wote mle ndani.
“Siku nilipokuhoji kuhusiana na mazingira ya kifo cha Grayson, uliniambia kuwa jamaa alikuwa amewataiti kwa bastola humu ndani kwa kuwa alikuwa analazimisha apewe hela kutokana na madeni yaliyomzonga baada ya kushiriki kwenye kamari…” Kwakwa alisema huku akitembeza macho kwa wote mle ndani.
Akaona macho yakiwatembea baadhi yao, na wengine wakitupiana macho ya haraka kisha wakajitia kutazama pembeni.
Hili lilimpa jibu alilokuwa analihitaji.
“Hivyo ndivyo ilivyokuwa! Kwani si umewahoji wakurugenzi wote hapa na wamekupa habari hiyo hiyo?” Luis alimjia juu.
Kwakwa alicheka.
“Na ndio maana nikakwambia kuwa hizo akili zako bwana Kambesera zinakukosesha maarifa kweli kweli. Yaani jamaa wamejibu maswali yangu kila moja kama alivyojibu mwenzake!”
“Sasa hilo ni tatizo kwako? Kama kitu kimetokea hivyo ulitarajia tukujibu tofauti na kilivyotokea?” William ‘Bill’ Maginga alimjia juu.
Kwakwa akafyatua cheko ya kebehi.
“Maarifa uliyokosa bwana Kambesera…” Alimwambia Luis, na kuendelea, “… na waliyokosa hawa jamaa zako, ni kwamba mnapokaririshana namna ya kujibu maswali… nyote mtajibu vile vile takriban neno kwa neno. Sasa kwa mtu makini kama mimi hilo linanipa picha kuwa katika majibu na maelezo yenu kuhusu tukio nililolikuta humu ndani jana, kuna mengi mnanificha. Sasa swali linakuja…” Kwakwa aliwapasha kwa kirefu na kuweka kituo huku akiona jinsi nyuso za wale wote mle ndani zilivyokuwa zikisawajika.
“Kwa nini?” Alihitimisha kauli yake kwa swali.
Kimya kilicholijibu swali lile kilikuwa kizito sana.
“We’ amini utakavyo, lakini hivyo tulivyokueleza ndivyo ilivyokuwa!”
Luis Kambesera aliuvunja ule ukimya kwa jazba.
Kwakwa alimtazama kwa kituo, kisha akamgeuzia macho yake mwanasheria wa kampuni.
“Kwa hiyo bado mnaitakidi kuwa Grayson alikuwa akidai apewe hela kutokana na madeni yaliyomzonga baada ya kushiriki kwenye kamari?”
127
Hussein Issa Tuwa
“Ndivyo, afande!” Suleiman alijibu.
Kwakwa akamhamishia macho ya viulizo Jamilla Mchebe.
“Ndiyo hivyo Inspekta…” Jamilla naye akaunga mkono hoja. Kwakwa akahamishia macho yake kwa Mike Mwangati.
“Nini?” Mike akamuuliza.
“Je, na wewe pia unathibitisha hilo, kuwa hayati Grayson alikuwa analazimisha apewe hela ili akalipe madeni huko?”
“Nasikitika kuwa hivyo ndivyo ilivyokuwa afande!” Mike Mwangati akamjibu, na Kwakwa akashusha pumzi ndefu na kubaki kimya kwa muda.
“Kuna kingine Inspekta? Tunahitaji kuendelea na kikao chetu hapa!”
Luis alimwambia.
Kwakwa aliinuka na kutoa karatasi mbili zilizokunjwa pamoja vizuri kutoka kwenye mfuko wa shati lake la kiaskari.
“Hapa nina karatasi mbili za kisheria…” Kwakwa alisema taratibu, na wote mle ndani wakawa makini maradufu.
“Moja ni kibali cha kuwaweka chini ya ulinzi ninyi nyote kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha Grayson Mochiwa, na kutoa ushuhuda wa uongo!”
Aliendelea kufafanua taratibu.
“Heeh!”
“Khaaaah?”
“Bull shit!”
“Toba Yarabi!”
Kila mmoja alihamanika kivyake kwa kauli ile ya Kwakwa.
“Ndio! Maelezo ya Luis yalikuwa ni uongo mtupu! Na maelezo ya kila mmoja wenu nilipowahoji pale jana yalikuwa ni uongo vile vile. Na sasa hivi mlipokiri wenyewe mbele yangu kuwa hayo ndio maelezo yenu, imenithibitishia kuwa nyote bado mna nia ya kuficha ukweli juu ya mazingira ya kifo cha Grayson, kwa hiyo nyote ni watuhumiwa wakuu katika kifo chake!” Kwakwa aliwaambia.
“Huo ni ujinga wa daraja la kwanza kabisa Inspekta!” Luis alimjia juu, na bila kumtilia maanani, Kwakwa akamkabidhi yule mwanasheria wa kampuni moja kati ya zile karatasi mbili alizokuwa nazo.
Jamaa aliitazama ile karatasi, na wenzake wakamuona akilegeza tai yake na akijikohoza kulegeza koo.
“Eeem… hii… hii karatasi ni ya halali wazee… ni kibali cha kutuweka chini ya ulinzi sote hapa… ni arrest warrant hii…!” Suleiman Mwangi alisema kwa hamaniko, ile karatasi ikitetemeka mikononi mwake.
128
MTAFITI
“Hah! Kivipi? Inawezekana hiyo?” Luis alifoka, na Kwakwa akacheka. Minong’ono ikaanza kutembea mle ndani baina ya wale wakurugenzi wengine.
“Hii ni karatasi halali Luis... of course tunaweza kushughulikia suala la dhamana tukatoka ndani ya muda mfupi tu lakini…” Mwanasheria alianza kufafanua.
“Tayari mtakuwa watuhumiwa mpaka hapo itakapothibitika kuwa ni wahusika kweli, au vinginevyo!” Kwakwa alimkatisha, na miguno mizito ikazagaa mle ndani.
“Sasa mimi najaribu kuvuta picha itakuwaje kwenye taswira ya kampuni yenu iwapo ikitangazwa na ikabainika kuwa wakurugenzi wake wakuu wote wako chini ya ulinzi kwa tuhuma za mauaji ya mkurugezi mwenzao. Oh La la! Sidhani hata kama hizo shea za kampuni yenu zitathaminika tena kwenye soko la hisa… si mmo kwenye soko la hisa nyie?” Kwakwa alisema, bila ya kujua kuwa alikuwa amegusa pale pale ambako tayari akina Luis walikuwa wakipajadili.
Duh!
Macho yaliwatembea wale wakurugenzi.
“Hapana… hatuhitaji kitu kama hicho wakati huu jamani!” Jamilla Mchebe aliropoka, na vikohozi vikasikika mle ndani.
Kwakwa aliwatazama wote kwa utulivu.
Wakurugenzi walitazamana.
“Er, kwa hiyo ndio tayari tuko chini ya ulinzi afande?” Suleiman Mwangi alimuuliza.
“Hiyo sasa itategemea na ninyi wenyewe!” Kwakwa alimjibu, na mitazamo ikatembea baina ya wale wakurugenzi, na ishara moja ikapita baina ya Luis na Mike Mwangati.
Luis akajikohoza kidogo.
“Okay Inspekta… ujumbe umeeleweka. Ni kiasi gani unahitaji ili hili jambo litoweke?” Alimuuliza, na Inspekta Kwakwa akatabasamu.
“Sasa hapo ndio umesema nilitakalo…” Akamjibu huku bado akitabasamu.
Wote mle ndani wakamakinika, wakitupiana macho na baadhi wakitabasamu kidogo.
Kumbe lilikuwa ni suala dogo tu!
Haroub Kwakwa alimuashiria yule mwanasheria wa kampuni amrejeshee kile kibali chake cha kuwatia ndani wale wakurugenzi, na jamaa akampa
129 Hussein Issa Tuwa
kwa ahueni kubwa kabisa.
“Okay, nitaahirisha kuwatia ndani muda huu, lakini kama nilivyosema…
hiyo itategemea na nyie wenyewe.” Aliwaambia.
“Tunakusikiliza afande!” Mwanasheria alisema, na Luis akabaki akimtazama Kwakwa kwa makini.
“Ninachohitaji ni hiki bwana Luis… nipe hicho, na nitaahirisha kuwaweka chini ya ulinzi nyote humu. Nadhani utakubaliana nami kuwa
ninachokihitaji hapo sio kikubwa cha kukushinda… au kuwashinda. Kazi kwenu!” Kwakwa alisema huku akimkabidhi Luis Kambesera ile karatasi nyingine aliyokuwa nayo, na akiiweka mfukoni ile ya kwanza.
Luis aliikunjua kwa pupa ile karatasi na kuisoma, huku wenzake
wakimtazama kwa udadisi mkubwa. Inspekta Haroub Kwakwa alitulia
kitini na kumtazama kwa makini, akisubiri jibu lake.
Wakati Inspekta Kwakwa akiendelea kuwaweka kiti moto wale wakurugenzi wa ile kampuni ndani ya lile jengo lililohifadhi ofisi za kampuni ile tata, nje jengo lile Sajenti Pojo naye alikuwa ana yake.
Alishaongea na askari wa kampuni binafsi ya ulinzi kwenye jengo lile, ambaye alimthibitishia kuwa siku ya tukio wafanyakazi wa ile kampuni iliyokumbwa na mkasa walitolewa nje ya ofisi zile baada ya kutokea kile kifo cha Grayson mle ofisini kwao. Hivyo ndivyo yeye na wengine wengi walivyoelewa, na Pojo hakutaka kubishana naye. Cha msingi ni kwamba yule mlinzi alithibitisha kabisa kuwa alimuona Mwantumu akitoka nje ya jengo kama jinsi wafanyakazi wengine wote, na baada ya hapo hakumuona tena.
Hakufuatilia tena ni nani alirudi ndani ya jengo na nani hakurudi kwa kuwa muda huo walikuwa kwenye hekaheka za polisi na baada ya hapo
zikaja hekaheka za kuutoa mwili wa marehemu nje ya jengo lile huku wakisukumana na wananchi na waandishi wa habari.
Pojo akaachana naye.
Ile taarifa ilimthibitishia kuwa siku ya tukio, Mwantumu alitoka mwenyewe ndani ya jengo lile.
Moja kwa moja mbele ya jengo lile kulikuwa kuna teksi kadhaa, na akataka kwenda kuwauliza madereva wa teksi iwapo yeyote kati yao alikuwa amembeba yule binti siku ile, lakini akajizuia.
130
MTAFITI
Kama ningekuwa nakimbizwa na mtu kutoka ndani ya hilo jengo, nisingekimbilia teksi zilizokuwa moja kwa moja mbele ya jengo...
Alizunguka nyuma ya jengo, na huko akazikuta bajaji nyingi zikiwa zimeegeshwa kusuburi abiria.
Yes, bajaji zilizoko nyuma ya jengo… inawezekana.
Baada ya kuuliza maderava wawili tu wa bajaji akapata jibu. Yupo dereva aliyembeba yule binti aliyeonekana kwenye runinga kuwa amepotea siku mbili zilizopita. Jamaa alikuwa ametoka na abiria. Pojo alimsubiri, na aliporudi akamuuliza alimpeleka wapi yule binti siku ile.
Jamaa akamwambia kuwa alimpeleka Mwananyamala, na mara moja Pojo akajua itakuwa alimpeleka kwa Zay.
“Je, hukutoka naye tena baada ya hapo?” Alimuuliza.
“Hapana afande… mi nilimuacha tu mbele ya ile nyumba aliyonielekeza kisha nikaondoka zangu.” Jamaa alimjibu, na Pojo akauma midomo.
Mwantumu alipofika kwa Zay nd’o akaondoka, bila shaka kwenda kule nyumbani kwake Chang’ombe ambako bila shaka baada ya hapo ndio akatoweka.
Akaingia ndani ya ile bajaji.
“Vipi, nd’o nikupeleke huko Mwananyamala? Si unajua kuwa hizi bajaji zinatumia mafuta lakini afande? Halafu ujue tajiri haelewi kama nilibeba polisi au la…”
“Twende Chang’ombe wewe… na hela yako utapata! Unaona polisi ndio watu wa dezo dezo tu, eeenh?” Pojo alimkoromea.
“Ah, sio hivyo afande… ila…”
“Endesha huko!”
Safari ya kuelekea Chang’ombe ikaanza…
Wakati haya yote yakiendelea, kule Mbagala Bilanga alitoka nje ya ile nyumba ambayo Chabbi Cheka alikuwa amemficha Mwantumu, ambayo naye alikuwa ana funguo zake, na kubaki akiwa amesimama kando ya pikipiki yake huku akiwa amekunja uso kwa mawazo, moyo ukimdunda kwa nguvu.
Alitoa simu yake kutaka kumpigia Chabbi, ndipo alipogundua kuwa hakuwa ameiwasha simu ile tangu siku iliyopita alipoizima wakati yuko na
131 Hussein Issa Tuwa
Chabbi kwenye hekaheka za kwenda kumpatia tiba kule Kibamba.
Aliiwasha haraka, na ilipokuwa sawia, akampigia Chabbi.
Simu yake ilikuwa haipatikani.
“Shit!” Alilaani. Akajaribu kumpigia kwa namba yake nyingine, nayo, kama hali aliyokuwa akikutana nayo Luis siku iliyopita, ilikuwa haipatikani pia.
“Ahhh, pumbavu zako Chabbi Cheka! Pumbavu zakooo Oh! Kwa nini hujawasha simu mpaka sasa wewe?” Alilaani kwa sauti.
Akaitazama tena ile nyumba aliyoifunga kama alivyoikuta, kisha akaparamia pikipiki lake na kuliondoa kwa kasi kutoka eneo lile.
“Sasa kilichobaki ni kwenda kumtafuta yule rafiki wa huyu mtoto tu, malaya mkubwa… hata sijui anafananaje, shenzz taipp!”
Alijisemea huku akikoleza kasi ya pikipiki lake kurudi mjini…
Lakini wakati yeye alipokuwa anamlaani Chabbi kwa kutopatikana
hewani, kule nyumbani kwake Chabbi Cheka alikuwa anachanua tabasamu la ushindi huku akiukodolea macho uso wa kompyuta yake ya mapajani.
“Nimekupata mwanaharamu!” Alisema peke yake huku akiitazama sura ya Zay iliyokuwa ikimchekea pale kwenye kioo cha kompyuta ile.
Alikuwa ameshaoga na amebadili nguo, akiwa amevaa suti kama
kawaida yake ila safari hii hakuwa wamevaa tai, na alikuwa amelazimisha
kuitoa ile bandeji iliyopita shingoni kwake na kuushikilia ule mkono wake
uliojeruhiwa, akiulazimisha ule mkono kufanya kazi kama kawaida.
Alikuwa ameingia kwenye mtandao wa facebook, na kumtafuta
Mwantumu kwa majina yake, na kwa bahati yule binti alikuwa amejisajili kwenye mtandao ule wa kijamii.
Akafuatilia baadhi ya mawasiliano yake aliyoyaweka kwenye ule ukurasa wake wa facebook, na akagundua kuwa Mwantumu amekuwa akimnadi mwanadada mmoja tu kuwa ni rafiki yake mkubwa, aliyeenda kwa jina la Zay… mara nyingine akimtaja kuwa ni ‘Zaynush’ au ‘Zay K’.
Picha moja iliwaonesha yeye na huyo Zay wakiwa wamekumbatiana huku wakiichekea kamera, ikiwa ni kuinadi siku ya kuzaliwa kwa huyo rafiki yake.
Chabbi akagonga sehemu yenye jina la huyo Zay ambapo alikuwa amemtakia heri ya siku ya kuzaliwa rafikiye, na alipofanya hivyo, moja kwa moja facebook ikamhamishia kwenye ukurasa wa huyo Zay. Akaenda kuzikagua taarifa za msingi za huyo Zay. Moja ya taarifa aliyoweka pale
132 MTAFITI
kwenye facebook ni namba yake ya simu.
Ilikuwa ni ile ile aliyopewa na yule dada wa mapokezi pale ofisini kwao
kuwa ndiye aliyepiga simu kumuulizia Mwantumu.
Ha ha ha ha haaa!
Na ndiye aliyeongea naye kwa simu siku alipokuwa na Mwantumu kule Mbagala…
Aliingia kwenye sehemu ya picha za Zay pale kwenye ukurasa wake wa facebook, na kuipata picha iliyomuonesha vizuri sana yule mwanadada.
Ha ha ha haaa!
“Tutaonana muda si mrefu Zay wangu… wala usikonde bibie!” Chabbi aliisemesha sura ya Zay ikiwa pale kwenye uso wa kompyuta yake.
Akiwa njiani kuelekea Chang’ombe Sajenti Pojo alijikuta akiketi wima ghafla mle ndani ya bajaji baada ya wazo jipya kumpitia kichwani. na akili ikimtembea.
Kama mimi nimeweza kujua mara moja mahala Mwantumu alipoelekea baada ya kutoka pale Liquid Diamond, basi hata na wale watu wanaomshikilia hivi sasa nao si wataweza kulijua hilo kwa kutumia mbinu ile ile niliyoitumia mimi?
Alitikisa kichwa kujilaumu kwa nini hakuliona hilo mapema.
Sasa kama wakifanya hivyo, huyu dereva wa bajaji atawapeleka moja kwa moja hadi kwa Zay, shenz’ taip!
Alizidi kujiwazia na akajikuta akiachia msonyo.
“Er, eti dogo… kuna mtu mwingine yeyote aliyewahi kuja kukuuliza mahala ulipompeleka yule binti kama jinsi nilivyokuuliza mimi leo hii?”
Alimuuliza dereva wake, na jamaa akatikisa kichwa bila kusita, kukana jambo hilo.
“Hakuna afande… wewe ndio wa kwanza!”
“Okay, safi… sasa kama akitokea mtu mwingine yeyote… yeyote yule, kukuuliza mahala ulipompeleka yule binti… unijulishe. Nitakuachia namba yangu ya simu… sawa sawa?” Pojo alimwambia, na dogo akatikisa kichwa kukubaliana naye.
“Poa tu haina noma kamanda… ila si unajua kupiga simu kunahitaji vocha afande?” Jamaa alimwambia huku akiizungusha bajaji yale kwenye mzunguko wa pale polisi Chang’ombe, kituo cha kazi cha Pojo.
“Halafu jaribu kuwa na uzalendo kidogo wewe! Yaani hata kunipigia
133 Hussein Issa Tuwa
simu tu kunipa taarifa za kipolisi unataka upewe na hela ya vocha? Kumbe mjinga sana wewe, eenh?” Pojo alimjia juu.
“Basi afande isiwe ishu… we utaniachia namba yako na mi’ n’takupigia tu kama ikitokezea hivyo, au vipi?” Jamaa alijirudi, na Pojo akamsonya. Alimwelekeza amteremshe mwanzoni mwa ule mtaa wa Mkamba ambao ndio Mwantumu alikuwa akiishi. Alimlipa hela aliyotaka, na akamuongezea elfu moja.
“Haya buku ya vocha hiyo, bwege wewe… akitokea mtu yeyote kukuulizia juu ya mahala ulipompeleka yule dada siku ile, unanipigia, sawa?”
“Mbona poa tu afande? Mi’ n’takupigia wangu… bora atokee tu huyo mtu!”
Wakapeana namba za simu.
Dereva wa bajaji alipoondoka tu Pojo akampigia Zay.
“Ya!” Zay alimwitika kwenye simu.
“Uko wapi bi mdogo?” Pojo alisaili.
Zay bado alikuwa ameketi pale kwenye ule mgahawa waliokutana nae akiwa na Kwakwa.
Akamwambia hilo.
“Okay… nadhani usirudi nyumbani kwako leo… kama unaenda nenda haraka sasa hivi, chukua vilivyo vyako uhame pale. Uko hatarini pale!” Pojo alimwambia kwa msisitizo.
“Akh! Sasa hizo ndio habari gani afande? Mi’ nihame pale niende wapi? Kwani kumetokea jambo jipya?” Zay alisaili.
Pojo akamwambia wazo lililompitia kichwani mwake, na kwamba huenda wale jamaa wakapajua kwake kupitia kwa yule dereva wa bajaji.
Zay alihamanika.
“Dah, sasa… sasa n’tahamaje wakati mama Mwantumu naye yuko pale kwangu sasa hivi? Amekuja kutoka Gezaulole huko kufuatilia masuala ya Mwantumu…”
“Basi nenda Gezaulole! Hapo kwa sasa ni hatari sana kwako. Hawa jamaa waliomteka Mwantumu wanaweza kukuibukia anytime, hasa ukizingatia kuwa ulimkurupusha mmoja wao kule nyumbani kwa rafikiyo…!” Pojo alimwambia.
Zay akabaki kimya, akili ikimranda.
“Upo wewe?” Pojo alimshitua.
“Yah… nipo. Nitalifanyia kazi afande…!”
“Usilifanyie kazi muda mrefu basi. Hama leo hii hii! Ama si hivyo nakuweka chini ya ulinzi kwa usalama wako!” Pojo alimwambia na kukata
134 MTAFITI
simu. Alienda moja kwa moja hadi kwenye nyumba iliyokuwa ikitazamana na ile ambayo Mwantumu alikuwa amepanga pale mtaani na kubisha hodi.
Alifunguliwa mlango na mama mtu mzima na akajitambulisha, ingawa mavazi yake tu yalikuwa yakijinadi.
“Nikusaidie nini afande?” Mama alihoji baada ya salamu na kutambulishana.
“Kuna binti alikuwa akiishi mtaa huu ambaye amepotea na habari zake zilitangazwa kwenye vyombo vya habari…” Pojo alianza, na mama akamkatisha.
“Ndio, Mwantumu… akiishi nyumba hiyo hapo…” Mama alimwambia huku akiioneshea nyumba aliyopanga Mwantumu.
“Ni kweli. Nilitaka kujua… ni lini ulimuona kwa mara ya mwisho?”
Mama alijikuna kichwa.
“Mnh, sikumbuki kwa kweli… ila jirani yangu hapo alisema kuwa alimuona ile siku ambayo nd’o wanasema kuwa alitoweka… aliondoka na gari kubwa tu la kifahari… anavyosema yeye lakini, mimi sikumuona!” Mama alijieleza na Pojo akawa makini zaidi.
“Nyumba gani hiyo, na huyo aliyekuambia kuwa alimuona Mwantumu ni nani?”
“Mama Boni wa nyumba ya pili hapo…” Mama alisema huku akiioneshea nyumba iliyofuata kutoka ile ya kwake.
Pojo alimshukuru na kwenda kumuulizia mama Boni wa nyumba ya pili.
Na huko akagundua kuwa siku ya mwisho Mwantumu kuonekana pale mtaani, yule mama wa hiyo nyumba ya pili alikuwa akinywa chai mezani kwake pale sebuleni kwake. Meza yake ya kulia chakula ilikuwa iko chini ya dirisha lake la mbele, na kupitia hapo dirishani aliona kila kitu kilichotokea pale nje ya nyumba ya akina Mwantumu siku ile.
Kupitia kwa Mama Boni, Pojo akajua kuwa siku ya tukio, Mwantumu alifika na bajaji pale kwake. Aliiacha bajaji ikimsubiri pale nje naye akaingia ndani ya ile nyumba aliyopanga. Kisha akatokea baba mmoja mrefu aliyevaa suti nyeusi na miwani myeusi ya jua. Aliongea na yule dereva wa bajaji, na bajaji ikaondoka. Yule baba aliingia ndani kwa akina Mwantumu na baada ya muda, alimuona akitoka akiwa ameshikana mikono na Mwantumu na kuingia naye kwenye VX lenye rangi nyekundu.
Pojo hakuamini!
“Okay… sasa, Dah! Ulipata kuziona namba za usajili za hilo gari… VX jekundu?”
“Aka! ’asa mi’ nihangaike na namba za gari kwa nini? Sikuiona namba
135
Issa Tuwa
Hussein
miye!”
“Okay, unadhani ukimuona tena yule mtu aliyetoka na Mwantumu siku ile, utaweza kumtambua?”
“Mnh! Sina hakika kwa kweli… labda avae nguo zile zile na miwani ile ile…”
“Vipi huyo dereva wa bajaji aliyekuja na Mwantumu halafu akaondoka…?” Pojo aliuliza zaidi.
“Ah, yule mbona ni mmoja wa madereva wa bajaji wa pale kituoni usalama?”
“Eeenh?”
“Kumbe? Yule alikuwa kijana wa hapo hapo kituo cha bajaji cha usalama. Hata mimi keshanibeba mara kibao na bajaji yake!”
“Unamjua jina lake?”
“Jina nd’o simjui, lakini kwa sura… namjua kabisa!”
“Safi sana. Mama nakushukuru sana. Umekuwa na msaada mkubwa!”
“Hamna shida… naombea mumpate tu mdada wa watu jamani. Maana ile hali aliyo nayo na haya mambo yanayowakuta watu kama yeye siku hizi!” Mama Boni alisema na kuishia kuguna.
Ile kauli ya mama Boni ilimfanya Pojo aitazame tena ile picha ya Mwantumu aliyopewa na Zay, na akahisi donge likimkaba kooni.
“Dah! Yaani we’ acha tu bi mkubwa…” Ndilo jibu pekee lililomjia kinywani muda ule, na kimya kikapita kidogo baina yao.
“Sawa basi bi mkubwa. Kama nikihitaji msaada wako kumtambua yule dereva wa bajaji nitarudi, sawa?” Hatimaye Pojo aliaga.
“Hamna shida baba’angu…”
Pojo akaondoka kuelekea kwenye kituo cha bajaji pale Chang’ombe usalama.
Zay aliendelea kubaki pale pale mgahawani akijifikiria baada ya kumaliza kuongea na Pojo. Akili ilikuwa ikimzunguka na bado alikuwa akihisi kuwa kuna kitu anakikosa katika kitendawili chote kile cha kifo cha Grayson Mochiwa, kutoweka kwa Mwantumu na yeye kupigiwa simu na mtu asiyefahamika akimdai kitu ambacho hakuwa nacho, na ambacho ni wazi kuwa Mwantumu pia hakuwa nacho huko walipomficha.
Ni kitu gani hicho?
Ni wazi kuwa kilikuwa kwenye ule mkoba wa Mwantumu… lakini ndo
136 MTAFITI
yale makabrasha tu? Kweli?
Na sasa Pojo anamwambia kuwa maisha yake yako hatarini, na kwamba
yule jamaa aliyemkurupusha kule kwa Mwantumu anaweza kumuibukia kule nyumbani kwake Mwananyamala…
Kwa hiyo akimbilie Gezaulole akajifiche?
Halafu Mwantumu aendelee kufichwa na bila shaka kuteswa na wale watu huko?
Hapana, hapana… hapana!
Alipitisha maamuzi.
“Sikimbii popote mimi! Kama kuja na kunikuta pale home waje tu. Tena ndio itakuwa vyema nipate kuongea nao… nijue ni nini wanachomtakia
Mwantumu. Kama ni yale makaratasi basi na wayachukue tu waniachie
Mwantumu wangu… siwezi kuvumilia kumpoteza eti kwa sababu ya makaratasi fulani tu yasiyo na maana yoyote kwangu!” Alijihamasisha.
Na hilo ndilo siku zote lililokuwa likimzuia kusema lolote kuhusu ule mkoba wa Mwantumu kwa askari. Alijua tu kuwa polisi wakiupata ule mkoba hawataweza kuwapa wale watu wabaya ili wamrudishe Mwantumu.
Kwanza wale jamaa ndio watapotea kabisa na bila shaka kum... oh, Mungu wangu! Wakijua kuwa polisi wanayo yale makaratasi si ndio watamuua kabisa Mwantumu kupoteza ushahidi na wao kupotea moja kwa moja?
Moyo ulimtetema.
Lakini kama anazo yeye, anaweza kuelewana nao na kubadilishana nao Mwantumu kwa yale makaratasi.
Lakini hata nikiwapatia hayo makaratasi… kama ndiyo wayatakayo… ni kweli watatuacha mimi na Mwantumu tuishi?
Mnh!
Si tutakuwa tumeshawajua sura zao?
Aliutafakari upya ushauri wa Pojo, na wazo jipya likamjia.
Vipi wale jamaa wakienda kweli nyumbani kwake muda huu na kumkuta mama Mwantumu huko?
“Oh, My God…!” Haraka alichukua simu yake na kumpigia yule mama, lengo likiwa ni kumwambia kuwa asimfungulie mtu yeyote pale nyumbani mpaka atakapofika.
“Hallo Zay…!” Mama Mwantumu alipokea simu, na Zay akashangaa kusikia mvumo wa gari pamoja na ile sauti ya yule mama.
“Er, Hello mama… vipi… uko barabarani?” Alijikuta akiuliza kabla
137 Hussein Issa Tuwa
hajamweleza kile alichotaka kumueleza, na yule mama akampa mlipuko wa moyo.
“Ndiyo mwanangu! Niko kwenye bajaji naenda huko kwenye ile kampuni iliyomchukua mwanangu! Siondoki huko mpaka nimpate mwanangu leo!”
“WHAAAAT…?” Zay alimaka huku akiinuka kitini na kuanza kuiweka kwenye mkoba wake ile kompyuta ya Mwantumu.
“Mama usifanye hivyo, please! Usiende huko! Hao ni watu wabaya sana na utajiletea mashaka makubwa! Mbona polisi wanalifanyia kazi hilo suala?” Alimwambia huku akiondoka kwa mwendo wa haraka, akisahau kulipia kinywaji alichokuwa ameagiza mara tu alipofika pale mgahawani.
Mhudumu akamkimbilia kumdai hela. Alimpa hela na kutoka haraka nje ya mgahawa ule bila hata ya kusubiri chenji.
“Hakuna kitu kama hicho!” Mama alimjibu kwa jazba.
“Akh! Mama!”
“Wao hawawezi kumchukua mwanangu hivi hivi tu na mi’ niwaangalie tu! Kama kufa basi n’takufa na mwanangu. Leo mimi na wao tu leo!”
Mama alikuja juu simuni, sauti yake ikivunjika kwa kilio kilichokuwa
kikimnyemelea, na Zay akaona kuwa mama alikuwa amedhamiria.
Hili hakulitegemea kabisa.
“Oh, Mungu wangu… sasa mbona mambo yanazidi kuwa magumu jamani?” Alijisemesha huku akiangaza huku na huko pale nje ya mgahawa.
Afanyaje sasa?
Akafanya lile ambalo alijua kabisa kuwa hakutakiwa kulifanya.
Alitoka nje ya ule mgahawa na kujitupa ndani ya gari lake kabla ya kuliingiza barabarani na kuchukua uelekeo wa kule zilipokuwa ofisi za Liquid Diamond Incorporated, wahka ukiwa umemjaa.
Sasa huyu mama akienda kuzusha vurumai pale atatoka salama kweli?
Alijiuliza huku akiwa amekunja uso.
Alikuwa amekata simu, akampigia tena yule mama.
“Uko wapi mama’angu sasa?”Alimuuliza.
“Mi nakaribia kufika huko. We’ jiandae kwenda kunitolea dhamana tu polisi maana vurugu n’takalowaangushia huko hawatakaa wasahau maishani mwao nakwambia!” Mama Mwantumu alisema kwa jazba, na Zay akaona dunia inazidi kumsaliti.
“Sasa hatuendi hivyo mama! Hebu nisubiri basi nije hapo mama, eenh?”
Alimbembeleza huku akizidi kukata mitaa ya jiji kuwahi kule kweye zile
138 MTAFITI
ofisi ambako alikuwa amedhamiria kutoonesha sura yake asilani mpaka
mkasa wa Mwantumu utakapokwisha.
Mama akamkatia simu.
Zay akamtukana kwa hasira yule mama.
Akampigia simu Sajenti Pojo.
Simu yake ilikuwa bize.
Akatukana tena, na dereva mwenzake akamchomekea gari mbele yake, naye akakanyaga breki ghafla na kubamiza honi kwa nguvu huku akitupia
tusi kubwa la nguoni yule dereva mwenzake. Jamaa akamnyooshea kidole
cha kati huku akitimua mbio na gari lake. Zay alitamani ashuke amkimbize kwa miguu halafu amtafune kwa hasira. Mwendo ukawa wa taabu katikati ya jiji. Magari yakazidi kuzongana, naye akajikuta akienda pole pole sana. Akasonya.
Akaegesha gari kando ya barabara, akalikomea vizuri milango na kuelekea Liquid Diamond kwa mwendo wa haraka.
Njiani akampigia simu Inspekta Kwakwa.
Simu ya Kwakwa ilikuwa inaita tu bila majibu.
Akatamani kulia huku akiongeza mwendo kuwahi kule kwenye ile kampuni iliyogubikwa mambo mengi ya nyuma ya pazia.
Kule kwenye chumba cha mikutano ndani ya ofisi za Liquid Diamond Incorporated, Luis Kambesera aliinua uso wake na kumtazama Inspekta Haroub Kwakwa kwa uso uliohamanika vibaya sana.
“What the hell is this?” Alimuuliza kwa wahka, na Kwakwa akamuinulia nyusi kama kwamba anayemuuliza “kwani huelewi?”
“Ni nini Luis…?” Jamilla Mchebe aliuliza kwa wasiwasi. Yeye ndiye mkurugenzi wa fedha wa kampuni, kwa hiyo alidhani alitakiwa ajue ni kiasi gani yule afande mwenye njaa alikuwa amemwandikia Luis kama rushwa yake ili alipotezee lile suala lenye madhara makubwa kabisa kwenye kampuni yao.
Sasa ilikuwa ni zamu ya Luis kulegeza tai yake, na Inspekta Kwakwa hakuweza kujinyima nafasi ya kuliacha tabasamu lililowasili usoni kwake lichanue.
“Luis…” Mike Mwangati alianza kuuliza lakini hapo Luis akaongea tena.
139
Issa Tuwa
Hussein
“Wewe una wazimu Inspekta! Tena una wazimu sana wewe!” Alifoka kwa hasira huku akimtikisia Kwakwa ile karatasi iliyokuwa mkononi kwake.
“Na pamoja na wazimu huo bado jeshi la polisi likaona ninastahili kuubeba huu uinspekta, na kunituma kuja kusimamia kesi hii… ajabu sana, eenh?” Kwakwa alimwambia na kumuachia swali la kejeli huku bado tabasamu likirandaranda mdomoni kwake.
“Kwani amedai kiasi gani, Luis?” Jamilla Mchebe aliuliza tena, na hapo Luis alimjia juu.
“Huyu khanithi anadai eti nimpatie Chabbi Cheka!” Luis alimaka kwa hamaniko, na kama umeme Inspekta Kwakwa aliruka kutoka pale kwenye kiti alichokuwa amekalia na kumdaka koo.
Hapo hapo mkono wa Luis ukachomoka kuelekea ndani ya koti lake, na Kwakwa akaupiga kwa nguvu ule mkono kwa kifimbo chake cha kiaskari kilichokuwa kwenye mkono wake mwingine. Luis aligumia kwa maumivu na Kwakwa akaukandamiza ule mkono wake uliokuwa unataka kuiwahi bastola iliyokuwa ndani ya koti lake pale kifuani kwake kwa kutumia kile kifimbo.
Duh!
“Wewe unamwita afisa wa polisi aliye kazini hanithi, bloody shwaini wewe? Yaani unaiita serikali hanithi mother fucker wewe?” Kwakwa alimkoromea kwa hasira huku akiwa amemkazia macho yake yenye mboni zilizokoza weusi huku akiendelea kumbana koo kwa nguvu. Luis alibaki akiwa ametumbua macho huku akikoroma kwa kubanwa koo namna ile.
“Hey! Acheni hizo nyinyi, alla!” Mwanasheria wa kampuni alifoka, na Mike Mwangati naye akaropoka kitu kuipinga hali ile, ilhali Jamilla Mchebe akipiga ukunga wa kike kwa woga.
Kwakwa akasikia viti vikisukumwa kutokea kule nyuma yake na akajua kuwa wale wafuasi wa Luis walikuwa wanataka kwenda kuwaamua pale walipokuwa.
“Wote tulieni hapo hapo mlipo nyinyi!” Aliwakoromea bila kugeuka huku bado akiwa amemkwida Luis pale kitini, na ukumbi wote ukawa kimya ghafla nyuma yake.
“Af… fande... acha hi… hizo kaka!” William Maginga, mkurugenzi wa tehama alibahatisha kumtamkia kutokea kule nyuma yake.
Kwakwa alimtazama Luis kwa muda zaidi, kisha akamsonya na kumsukuma nyuma kwa nguvu na kiti chake, na hapo hapo akainyakua
140 MTAFITI
ile karatasi kutoka mkononi mwake na akimwacha Luis akisambaratika vibaya sakafuni, yeye na kiti chake.
Kwakwa akawageukia wale wakurugenzi wengine mle ndani na kuwatazama kwa macho yaliyoahidi madhila matupu tu kwao.
Jamaa wakagwaya.
Luis Kambesera alijiinua kutoka pale sakafuni na kujiweka sawa kwenye kiti chake huku akijivutavuta vizuri tai na koti lake.
“Nakutaka utoke nje ya ofisi hii mara moja wewe!” Alimfoka huku akimwoneshea Kwakwa kidole kwa ghadhabu. Kwakwa alimtazama kwa jicho kali, kisha akampa mwanasheria wa ile kampuni ile karatasi ya pili aliyompokonya Luis.
“Waambie wenzako hii ni nini wewe!” Alimwambia.
Suleiman Mwangi alimtazama kwa hasira huku akiipokea ile karatasi.
“Hivi wewe unadhani huo uinspekta wako ndio unakupa mamlaka ya kuja kutushurutisha sisi namna hii humu ndani?” Alimuuliza kwa hasira.
“Waeleweshe wenzako hiyo karatasi inasemaje wewe!” Kwakwa alimkoromea. Jamaa alizidi kumtazama kwa macho yenye ghadhabu, na macho yake yakakutana na macho yenye ghadhabu zaidi ya zile za kwake. Akainama na kuisoma ile karatasi.
“Ah, wazee hiki ni kibali cha kumuweka Chabbi Cheka chini ya ulinzi kwa tuhuma za kuhusika na kupotea kwa yule binti Mwantumu katika mazingira ya kutatanisha…” Suleiman Mwangi alisema huku akiitazama ile karatasi.
“Khah! Sasa hiyo sisi inatuhusu nini? Yaani hilo ndilo lililomfanya Luis aje juu namna ile?” Mike Mwangati aliuliza huku akimtupia jicho Luis Kambesera.
“Good question!” Kwakwa alisema, akimaanisha kuwa jamaa alikuwa ameuliza swali zuri.
“Kuna zaidi hapa jamani…” Yule mwanasheria alisema, na wale wenzake wote wakanyong’onyea, wakijua kuwa hilo la zaidi ndilo lililomfanya Luis aje juu. Na hapo yule mwanasheria wa kampuni akawasomea maneno yaliyoandikwa kwa mkono kwenye kijikatarasi maalum na kubandikwa juu ya ile hati ya kumkamata Chabbi.
“Luis Kambesera, nakutaka umuwasilishe mkuu wa kitengo chako cha usalama wa kampuni ofisini kwangu kwenye kituo kikuu cha polisi jijini ndani ya saa ishirini na nne baada ya kupata waraka huu na kibali hiki cha kumuweka chini ya ulinzi mtu huyo. Iwapo hili halitatokea ndani ya muda
141 Hussein Issa Tuwa
huo, basi nitaitumia ile hati yangu nyingine na kukuweka chini ya ulinzi wewe pamoja na wakurugenzi wako wote katika kampuni yako. Mwisho wa kusoma.” Mwanasheria alimalizia na kuinua uso wake kuwatazama wale wenzake.
Duh!
Wakurugenzi wote mle ndani walinywea. Hakuna aliyeongea. Kimya kilikigubika kile chumba.
Kwakwa alikichukua kile kibali cha kumtia mbaroni Chabbi kutoka mikononi mwa yule mwanasheria, na kukibandua kile kijikaratasi kilichokuwa na ujumbe binafsi kwa Luis na kukiweka mfukoni. Kisha akakitupia pale mezani kile kibali cha kumuweka Chabbi Cheka chini ya ulinzi.
“Nimejifunza mengi sana kutoka kwenu humu ndani leo hii waheshimiwa. Mna saa ishirini na nne za kuamua ni nani kati yenu na
Chabbi Cheka aanze kuingia selo. Good day!” Kwakwa aliwaambia na kutoka nje ya chumba kile.
Jamaa wakabaki wanatazamana tu mle ndani.
“Sasa tunafanyaje jamani? Maana naona hili suala sasa linazidi kuwa baya tu…!” Hatimaye Maginga alivunja ukimya kwa hamaniko.
“Hamna mjadala… Chabbi aende tu polisi akajieleze. Unadhani kati ya uongozi mzima wa kampuni kuwekwa ndani hata kwa saa moja tu, na Chabbi asiyejulikana kabisa kwenye ngazi za utawala wa kampuni kuwekwa ndani, kipi kitakuwa na madhara zaidi kwa taswira ya kampuni?” Jamilla alitoa hoja kwa swali, na kabla yeyote kati ya wale wenzake hajajibu, alitoa jibu, “Ni sisi ndio tutaiathiri zaidi kampuni kama tukiswekwa ndani!”
Kimya kikazidi kutanda. Macho yakazidi kuwatembea mle ndani.
Jamilla alikuwa amelitamka wazo lililokuwa vichwani mwa karibu wote mle ndani, ingawa hakukuwa na aliyekuwa tayari kuliweka wazi wazo lile mbele ya wenzake.
“Sasa unadhani akiwekwa ndani Chabbi sisi ndio tutaokoka… jamaa kasema kuwa tuamue ni nani aanze kuingia selo kati yetu na Chabbi… kwa hiyo na siye selo inatuhusu wandugu. Ni suala la muda tu!” William ‘Bill’ Maginga aliitia doa hoja ya Jamilla.
“Yeah… Ni kweli. Maana jamaa kasema kuwa ataahirisha kutuweka chini ya ulinzi… sio ataacha kutuweka chini ya ulinzi!” Mwangati alisema kwa hasira.
“Na tayari tumeshajianika kwa kumtangazia mlungula ambao kumbe hata hakuwa na haja nao pumbavu zake… huyu ni askari gani huyu lakini?
142
MTAFITI
Ina maana ye’ ndio mzalendo sana, au…?” Mwanasheria wa kampuni
Suleiman Mwangi alisema kwa kuchanganyikiwa.
Muda wote Luis alikuwa kimya akiwasikiliza wenzake huku akiwa amefura kwa hasira.
Mambo aliyofanyiwa na Kwakwa mle ndani, mbele ya watendaji wake wakuu, yalikuwa ni ya kudhalilisha sana. Na hilo, pamoja na mengine mengi yaliyokuwa yakianishwa na wale wenzake mle ndani, lilimuudhi sana.
Yu wapi Chabbi Cheka lakini leo?
“
Okay, guys. Hebu tuliache hili kama lilivyo kwa sasa… nipeni saa mbili za kulifanyia kazi kisha tukutane tena hapa baada ya muda huo, sawa?”
Hatimaye alisema kwa utulivu wa kujilazimisha.
“Unataka kufanya nini sasa Luis? Hili suala linahusu sote hapa kuswekwa ndani na kijiinspekta kimoja kinachojitia ugangwe wa kwenye sinema za kimarekani, kwa hiyo sote tunatakiwa tuwe na kauli katika maamuzi unayotaka kuchukua. Mimi silali ndani ujue!” Mike Mwangati, mtendaji pekee asiyemwogopa Luis alisema.
Luis akakunja uso.
“Sasa ni sehemu gani ya sentesi kuwa tukutane tena humu ndani baada ya saa mbili ambayo hujaielewa Mike, eeenh? Baada ya saa mbili tutakuja kupitisha maamuzi sote humu humu ndani… kama tulivyofanya kwenye maamuzi mengine makubwa kuliko hata hili, huko nyuma. Sawa?” Luis alisema kwa ukali.
“Sawa.” Mmoja wa wale wenzake aliafiki, wakati wengine wakiinuka na kutoka bila hata ya kuongeza neno. William Maginga, mkuu wa kitengo cha tehama alihisi presha ikianza kumpanda…
Wakati Kwakwa akiwakabili wale wakurugenzi wa ile kampuni yenye maafa, na kabla Sajenti Pojo hajafika nyumbani kwa mama Boni kule
Chang’ombe, kule Sinza Chabbi Cheka ndio alikuwa ameshajiridhisha kuwa angalau alikuwa amepata mwanga wa kumwezesha kumtia mbaroni yule binti aliyeitwa Zay. Na kwa kulitimiza hilo alijiona kuwa alikuwa tayari kukabiliana na Luis Kambesera.
“Ukishamjua sura adui yako, tayari umeshajihakikishia robo ya ushindi!”
Chabbi alisema huku akizima kompyuta mpakato yake pale ndani. Baada
143 Hussein Issa Tuwa
ya tukio la kule Mbagala kati yake na Mwantumu, alikuwa amepata muda
mwingi wa kutafakari mustakabali wake, na sasa alikuwa ameshapitisha maamuzi muhimu.
Aliiwasha simu yake na kuiweka mfukoni mwake.
Hakuna ujumbe wowote mfupi ulioingia kumaanisha kwamba
wakati alipokuwa hapatikani hewani kuna mtu alimtumia ujumbe. Hilo halikumshangaza, kwani walikuwa na makubaliano ya msingi kabisa na Luis pamoja na Bilanga kuwa katu hawatatumiana meseji za simu katika mawasiliano yao. Wao wakihitajiana ni kupigiana simu tu. Ujumbe wa simu ulikuwa na tabia ya kuacha kumbukumbu zinazoweza kutumika kirahisi dhidi yao.
Aliingia chumbani kwake na kuchukua zana muhimu kwa kazi aliyokuwa amepanga kuifanya siku ile. Akiliacha gari lake, alitoka na kutembea kwa miguu hadi barabarani ambako alikamata teksi.
“Nipekele Chang’ombe usalama!” Alimuamrisha yule dereva wa teksi, na akiwa njiani kuelekea huko, simu yake iliita.
“Yes Bilanga, whats up?” Alipokea simu huku akifinya sura kidogo kutokana na maumivu aliyoyahisi mkononi kwake.
“Chabbi! Vipi bwana? Umekuwa hupatikani hewani kwa muda mrefu sana wewe… imekuwaje tena?” Bilanga alilalama simuni.
“Niko hewani sasa, na unaongea nami, kwa hiyo acha kulalama. Nilikuwa nahitaji utulivu kufanya uchimbaji wa habari kuhusu yule binti kwanza. Hebu ongea la kuongea sasa… kazi niliyokupa vipi?”Chabbi alimjibu msaidizi wake.
“Mambo mabaya sana aisee. Yatupasa tuonane mara moja bosi wangu!” Bilanga alimwambia.
“Kuonana sio ishu. Umepiga hatua gani katika kumtafuta yule binti? Mi’ kuna kimeo inabidi nikakimalize kwanza, kisha tutakutana ofisini kujadili jambo jingine zito zaidi. Baada ya hapo tutamjadili huyo binti…” Chabbi alitoa maelekezo.
“Kimeo gani hicho?”
“Sio suala lako hilo wewe, mbona maswali mengi… vipi?”
“Nimekwenda kule mbagala Chabbi… nimemkuta yule binti!” Bilanga alimwambia.
Ganzi ilimtembea Chabbi na akapiga kimya kwa sekunde kadhaa.
“Oyaa, unanisikia?” Bilanga alimuuliza.
144
MTAFITI
“Sikukutuma Mbagala Bilanga… nilikutuma kumtafuta …”
“Ilinibidi nifanye hivyo bosi. Hukuwa muwazi sana kwangu, na…”
“Okay. Acha kila kitu. Tukutane ofisini baada ya nusu saa… nakuja huko!” Chabbi alisema na kukata simu. Alijiegemeza kitini na kukunja uso kwa tafakuri kali.
Haikupita muda simu yake ikaita tena. Alikuwa ni Luis Kambesera.
“Yes?” Aliifokea ile simu iliyokuwa sikioni kwake.
“Ofisini kwangu! Sasa hivi, Chabbi!”Luis alifoka simuni.
“Nitakuwa hapo ndani ya nusu saa!” Chabbi alimjibu, na Luis akakata simu. Ni wazi kuwa alikuwa amekasirika vibaya sana. Chabbi alifinya tena uso kwa maumivu ya mkono.
Muda mchache baada ya mwendo wa kasi aliomshurutisha dereva wa teksi autumie, alikuwa amesimama hatua chache kutoka kwenye kituo cha bajaji pale Chang’ombe usalama. Macho yake makali yaliyokuwa
nyuma ya miwani yake ya jua yalikuwa yakiwakagua wale madereva wa bajaji waliozagaa eneo lile, akimtafuta yule ambaye alimkuta akimsubiri
Mwantumu pale nje ya nyumba yake siku alipomteka nyara.
Hakumuona.
Hilo halikumtia shaka, kwani alijua kwamba madereva wa bajaji hutoka kupeleka abiria na kisha hurudi tena vituoni mwao. Hivyo kama jamaa alikuwa ametoka na abiria, basi angerudi tu.
Tatizo ni kwamba atarudi baada ya muda gani? Hili kidogo lilimtia shaka, maana muda haukuwa upande wake kabisa.
Alitembeza macho kuitafuta bajaji ya yule kijana ambayo aliikamata sio tu namba zake za usajili bali pia maneno yaliyokuwa yameandikwa nyuma ya bajaji ile.
Baddi Gobbos p.a.k. Vampire.
Ndivyo ilivyokuwa imeandikwa kule nyuma ile bajaji, na Chabbi alikumbuka kuwa alitabasamu kidogo alipoona maneno yale siku ile alipokwenda kumteka Mwantumu kule nyumbani kwake. Alitembea taratibu akizitazama zile bajaji, na kweli, ile bajaji ya yule kijana ilikuwa ni miongoni mwa zile zilizopaki pale.
Kutokea upande mwingine wa barabara, Sajenti Pojo naye alitokeza eneo lile kutokea kule mtaa wa Mkamba na kuanza kuuendea ule msururu wa bajaji zilizoegeshwa pale.
Chabbi aliangaza tena eneo lile na bado hakumuona yule dereva wa ile
145 Hussein Issa Tuwa
bajaji aliyoikusudia. Muda huo bajaji iliyokuwa jirani na ile iliyoandikwa yale maneno ‘Baddi Gobbos p.a.k. Vampire’ ilipata abiria na kuondoka eneo lile.
Chabbi alienda moja kwa moja na kuingia ndani ya ile bajaji aliyokwenda kuifuata pale na kuketi ndani yake.
“Oyaaa! Nakuja bosi wanguuuu!” Alisikia sauti ikipiga kelele, na hapo alimuona yule dereva aliyekuwa akimsubiri Mwantumu siku ile, akikimbilia pale kwenye ile bajaji, akitokea kwenye kikundi cha jamaa waliokuwa wakifuatilia mchezo wa drafti hatua chache kutoka pale kwenye ule msururu wa bajaji.
Kijana aliingia nyuma ya usukani na kumgeukia.
“Ohooo, mkubwa ni wewe? Mambo vipi?” Alimuuliza kwa uchangamfu, wazi kabisa kuwa alikuwa amemkumbuka, na Chabbi aliuma meno kwa hasira. Alitaka kujihakikishia iwapo yule kijana atamkumbuka iwapo atamuona tena, na jibu alishalipata.
“Sema kaka... za tangu juzi? Wapi leo?” Dereva wa bajaji alimuuliza. Chabbi hakuwa na shaka tena kuwa kijana kamkumbuka.
“Chanika!” Alimjibu.
“Duh… huko tunaenda kwa elfu ishirini ka’ mkubwa!”
“Sio ishu… twen’zetu… n’na haraka kidogo!” Chabbi alisema huku macho yake yakitazama mbele na utulivu wa kutisha ukimuingia mwilini.
“Dah, halafu naoma anti yetu amepatwa na masahibu… nimeona ametangazwa kwenye TV kuwa amepotea… hajapatikana tu?” Dereva wa bajaji alimuuliza huku akiingia barabarani kutoka pale kwenye maegesho. Wakati huo Pojo akiifikia bajaji ya mwisho kabisa kwenye ule msururu wa bajaji, na kuanza kuwauliza madereva wa zile bajaji kuhusu dereva aliyembeba Mwantumu siku mbili nyuma, akiwaonesha ile picha ya yule binti aliyopewa na Zay.
“Eh… Yah… bado hajapatikana bwana…” Chabbi alimjibu yule bajaji wakiwa safarini.
“Dah! Noma sana aisee… hizo zitakuwa imani za kishirikina tu nakwambia mzee!” Dereva wa bajaji alisema huku akiendelea kuendesha, na Chabbi alikikazia macho ya ghadhabu kisogo chake kutokea kule nyuma alipokuwa ameketi.
Hakumjibu. Aliguna tu.
Huku nyuma, Pojo aliuliza madereva kama watatu hivi kabla hajatokea
146
MTAFITI
ambaye alikuwa akimfahamu Mwantumu miongoni mwa wale madereva wa bajaji pale kituoni.
Jamaa alimwambia kuwa alikuwa anamfahamu yule binti kwa kuwa mara nyingi huwa anachukua bajaji pale kituoni kuelekea mjini. Na akazidisha kueleza kwamba aliona akitangazwa kwenye runinga kuwa amepotea.
“Ni kweli, nami najua kuna mmoja wenu aliyembeba kwenye bajaji yake kutoka hapa kituoni ile siku aliyopotea… je mnamfahamu ni nani huyo miongoni mwenu?” Pojo aliuliza, na hilo jamaa na wale wenzake pale hawakuwa wakilijua.
Madereva wa bajaji wakaitana na kumzunguka Pojo pale alipokuwa, miongoni mwao wakielezana kile ambacho yule askari alikuwa anakiulizia.
“Er, sio kama ninamtafuta huyo dereva kwa ajili ya kumhusisha na kupotea kwa huyu binti jamani… la hasha. Natafuta habari tu kujua binti alitaka ampeleke wapi siku ile…” Pojo aliwatoa mashaka wale madereva wa bajaji, na minong’ono zaidi ikasikika. Muda huo mwenzao mmoja akafika pale na bajaji yale bila shaka akitoka kupeleka abiria sehemu. Akaenda kuwauliza kulikoni, na wenzake wakamueleza.
“Ah, huyo atakuwa Dimoso bwana! Si jana alikuwa anasimulia hapa kuwa yule msichana aliyepotea alimchukua hapa kwenda naye kwake ili akachukue mizigo yake ampeleke sehemu?” Aliwaambia, na Pojo akawa makini.
“Aaaa bwana!” Mmoja wa wale wenzake akauliza.
“Tena!” Yule mwenzao akasema huku akimtazama yule askari, kisha akaendelea, “Sasa walipofika huko tena nasikia yule dada akabadili mawazo sijui… jamaa akarudi hapa. Usiku wake ndio akaona kwenye TV ikitangazwa kuwa eti demu kapotea!”
Pojo akamsogelea yule jamaa.
“Okay… kwa hiyo huyo Dimoso yuko hapa sasa hivi? Naomba mniitie basi.” Alisema huku akiangaza huku na huko, na ndipo alipoambiwa kuwa Dimoso alikuwa ametoka muda ule ule na abiria.
Pojo akakunja uso.
“Tena muda huu huu afande. Yaani labda wakati we’ nd’o unafika hapa, na ye’ nd’o anachomoka na bajaji kule…” Mmoja wa wale madereva alimwambia huku akioneshea kwa kidole chake kule mwanzo wa ule msururu wa zile bajaji, na Pojo akakenua meno kwa uchungu wa namna alivyomkosa yule shahidi muhimu katika kumfuatilia mtu aliyemteka
147 Hussein Issa Tuwa
nyara Mwantumu.
Alifikiri haraka nini cha kufanya.
“
Okay, basi. Akirudi tu mwambieni aje anione hapo kituoni… nitakuwa namsubiri. Aulizie Sajenti Pojo, sawa jamani?” Aliwaambia na jamaa wakakubali.
Akageuka na kuanza kuelekea pale kwenye kituo cha polisi cha Chang’ombe, kilichokuwa jirani na pale kwenye kile kituo cha bajaji.
Ah, nimemkosa kidogo sana huyu jamaa… Dah!
Akili ilizidi kumzunguka.
Akasimama.
Akageuka.
Akarudi haraka pale kwa wale waendesha bajaji.
“Oyaa, kuna mwenye namba ya simu ya huyo Dimoso hapa?” Aliwauliza, na jamaa wengi tu pale walikuwa na namba ya simu ya yule mwenzao.
“Naomba nimpigie… huenda akawa hajaenda mbali, nami naweza kumsubiri hapa hapa, maana nyie hamkawii kusahau kumpa ujumbe akija hapa!” Pojo alisema, na jamaa wakacheka huku mmoja wao akitoa simu yake na kumsomea namba za simu za Dimoso.
Pojo aliipiga namba ya yule dereva, akilini akijua kuwa ni makosa makubwa kwa dereva, hasa wa bajaji, kuongea na simu wakati akiwa barabarani lakini
siku zote huwa anawaona wakifanya hivyo, na yeye alikuwa ameshapata mchemko wa hamasa ya kumfuatilia yule jamaa aliyeonekana na mama Boni akitoka na Mwantumu huku akiwa ameshikana naye mikono.
Hakuamini kuwa walikuwa wameshikana mikono kwa upendo.
Aliisikia simu ya Dimoso ikiita… na Dimoso naye aliisikia simu yake
ikiita wakati akiwa anakatisha njia za panya kutokea kule Chang’ombe kuelekea Chanika, abiria wake akiwa kwenye kiti cha nyuma mle bajajini.
Kwa kuwa alikuwa amepachika visikilizio masikioni ili simu ikiita wakati yuko barabarani asilazimike kuishikilia sikioni na badala yake aongee nayo tu huku bado mikono yake ikiwa imeshikilia usukani wa chombo chake cha usafiri, alibonyeza sehemu kwenye ule waya wake wa visikilizio iliyowezesha mawasiliano kufanyika kisha akaendelea kushikilia usukani wake huku akikata mitaa.
“Hallo! We’ nani mwenzangu?” Aliongea kwenye ile simu na kule nyuma, Chabbi Cheka akawa makini kusikiliza mazungumzo yale ya upande mmoja.
148 MTAFITI
“Nani?” Dimoso aliuliza tena, kisha akaendelea, wakati huu walikuwa wakipita njia ya vumbi iliyokuwa inaelekea kukutana na ile barabara kubwa ya Nyerere, ambako huko angekunja kushoto na kuchukua uelekeo wa uwanja wa ndege, Pugu na hatimaye Chanika.
“Polisi? Polisi wa wapi…?” Dimoso aliendelea kuhoji kwa sauti na kule nyuma umakini wa Chabbi kwenye mazungumzo yake ukazidi maradufu.
“Aha, ndio… mimi ndio Dimoso… naelekea Chanika na mteja muda huu…” Dimoso aliendelea kuongea simuni.
“Yaa, ni kweli afande… nilimbeba huyo dada bwana siku ile…” Dimoso alikuwa anasema huku bado akiwa kwenye mwendo wa kasi, na hapo ndipo apoishia.
Kutokea kule nyuma Chabbi Cheka alimkamata kichwa chake na kukizungusha kwa nguvu na kwa ghafla, shingo ya yule dereva ikivunjika huku ikitoa mlio mbaya na Dimoso akitoa sauti ndogo kama ya kohozi
lililomkwama kooni, kisha akajibweteka upande. Bajaji iliyumba na Chabbi
Cheka akajitupa mzima mzima nje ya bajaji ile na kuiacha ikizidi kusota vibaya bila uelekeo, dereva asiye uhai akiwa ndani yake.
Aliviringwa na kugaragazwa vibaya vumbini, maumivu makali yakimtambaa kwenye ule mkono wake uliojeruhiwa hapo awali, mayowe ya watu wachache waliokuwa pale njiani yakimfikia, kisha akajikita kwenye tuta la viazi kando ya barabara. Alijiinua haraka na kujitupa upande wa pili wa lile tuta ili kujificha kutokana na macho ya wapita njia aliojua kuwa wangerundikana eneo lile muda si mrefu.
Akiwa nyuma ya lile tuta alichungulia kule ilipokuwa ikisererekea ile bajaji, na akawahi kuiona ikiparamia tuta lililokuwa upande mwingine wa ile njia ya vumbi na kupinduka mara kadhaa kabla ya kulalia ubavu kule kando ya ile njia ya vumbi.
Bila kujali maumivu makali yaliyozidi kumtambaa pale alipoupigiza chini ule mkono wake uliojeruhiwa, alijisotesha kwenye majani nyuma ya lile tuta na kutazama kule ilipoangukia ile bajaji, ambako sasa kundi la watu lilikuwa likikimbilia pale ile bajaji ilipoangukia, kelele na mayowe vikirindima kutokea kila upande. Kundi la watu liliizunguka ile bajaji.
Alizidi kujibanza nyuma ya lile tuta kwa dakika kama tatu zaidi kuhakikisha kuwa hakuna aliyemuona, na alipojiridhisha, aliinuka haraka na kurukia pale kwenye ile njia. Akaangaza huku na huko, na kuona kuwa watu wote walikuwa wamezama kwenye kuifuatilia ile bajaji na dereva
149 Hussein Issa Tuwa
wake. Aliambaa kando ya ile barabara ya vumbi na kuelekea kule kwenye ile barabara kubwa kwa mwendo wa wastani, akihisi maumivu makali mkononi.
Hakuhitaji kwenda kuona kwa macho yake ili kujihakikishia kuwa yule dereva wa bajaji alikuwa amekufa. Kwa jinsi alivyoisikia ile shingo ikivunjika, jamaa atakuwa ameaga dunia tu.
Duh! Polisi walishaanza kumfuatilia yule dereva wa bajaji, pumbavu zao!
Aliwaza huku akiikaribia ile barabara kubwa ya Nyerere, ambayo kwa upande wake wa pili aliweza kuona teksi nyingi zikiwa zimejipanga.
Alivuka ile barabara na kuziendea zile teksi…
Kule Chang’ombe Sajenti Pojo alikuwa akiendelea kuongea na yule dereva wa bajaji wakati ghafla alipomsikia yule dereva akitoa sauti kama ya kuvuta kohozi, kisha akasikia mserereko na kishindo kikubwa, baada ya hapo kilichofuatia ni mayowe ya watu naye akabahatika kusikia baadhi ya maneno ya watu hao, kabla ile simu haijakatika, na alipojaribu kuipiga tena ikawa haipatikani. Imezimwa.
Mwili ukamwingia baridi. Alijua ambacho kitakuwa kimetokea na yale maneno aliyoyasikia kutoka kwa watu waliosikika ghafla tu baada ya kile kishindo yalimtia wasiwasi mkubwa.
“Ah! Amepindukaje sasa huyu?”
“Mzima kweli huyu jamani…?”
“Ah! Kafa huyu jamani…!”
“Sasa ilikuwaje lakini…?”
“Hebu pisha wewe…!”
Kisha simu ikakatwa, ikazimwa. Imeibwa.
Jasho likamtoka Pojo.
Wale madereva wa bajaji waliokuwa wakifuatilia mazungumzo yake na mwenzao wakapigwa butwaa.
“Vipi afande…?” Walimuuliza.
“Nyinyi! Kuna yeyote aliyeona Dimoso alikuwa amembeba abiria gani kueleka huko Chanika?” Badala ya kuwajibu, yeye aliwauliza, akiwa
150 MTAFITI
amebadilika ghafla.
Wale jamaa wakashangaa.
“Kumbe alikuwa anaenda Chanika?” Mmoja wao aliuliza.
Pojo akawatazama kwa ghadhabu. Walionekana kuwa hawajui lolote.
“Ni nani aliyemuona mtu aliyepanda bajaji ya Dimoso nauliza?”
Hakuna aliyemuona huyo abiria wake. Hakuna hata aliyejua kuwa alipotoka, Dimoso alikuwa anaelekea Chanika.
Na yeye mwenyewe hakujua kuwa alikuwa anaelekea kuzimu.
Pojo alitikisa kichwa, kisha akaondoka bila ya kuongea lolote zaidi, akiwaacha wale jamaa wakimkodolea macho kwa mshangao.
Yaani dereva wa bajaji apate ajali kirahisi namna hii?
Akaguna.
Siku ambayo mimi ndio nataka kuongea naye kuhusu mtu aliyeongea naye siku ile Mwantumu anatoweka pale nyumbani kwake?
Mnh!
Alitaka sana kujua ni nani huyo mtu na aliongea naye nini siku ile mpaka akaondoka na kumwacha Mwantumu mikononi mwake…
Sasa amepata ajali na kufa?
Si bure… lakini kama si bure ni vipi?
Alitoa redio maalum ya kipolisi na kuwasiliana na wenzake waliokuwa barabarani.
“Naamini kuna ajali ya bajaji njia ya Chanika au maeneo hayo… nahitaji kupewa taarifa za uthibitisho juu ya hilo tafadhali, over!” Aliongea kwenye ile simu.
Wenzake walimjibu kuwa watamjuza pindi taarifa hiyo ikithibitika. Bado Pojo hakutaka kuamini kile kilichotokea.
151 Hussein Issa Tuwa
ZAY ALITOKEZA KWENYE barabara ambayo kando yake ndio lile jengo lenye ofisi za Liquid Diamond zilikuwapo, na hata pale alipokuwa anaingia kwenye ile barabara, alimuona mama Mwantumu akishuka kutoka kwenye bajaji na kueleka ndani ya lile jengo kwa mwendo wa ushari.
“Ma’ Mwantumuuuu! Ma’ Mwantum!” Zay aliita huku akianza kutimua mbio kumuwahi, na hapo akashitushwa na honi kali ya gari huku akisikia msuguano wa tairi kwenye lami.
Yowe lilimtoka huku akigeukia kule msuguano ule ulipotokea, na hapo akashitukia akigongwa na kusukumwa kando ya barabara na gari lile, simu yake ikimtoka mkononi na kusambaratika barabarani.
Mayowe ya wapita njia wengine yalisikika naye akahamanika, macho yake yakiwa kwenye ile simu yake.
Ah! Nimegongwa na gari!
Alijitahidi kuinuka na kabla hajainuka vizuri mikono ikamshika huku na huko na kumuinua. Yeye akawa ameung’ang’ania ule mkoba wake huku bado ameikazia macho simu yake iliyosambaratika pale chini.
“Simu yangu! Simu yang…”
“Tulia binti… simu si lolote mbele ya uhai wewee…!” Sauti ilimwambia, na akaona mtu mwingine akiiokota ile simu.
Ah! Ushahidi wa ujumbe wa Mwantumu uko kwenye simu yangu!
“Simu yangu bhanaaa, ah!” Alimaka kwa jazba huku akijikung’uta kutoka mikononi mwa wale jamaa waliomshika.
“Hii dada… nilikuwa nakuokotea tu. Uko okay?” Mwanadada aliyemuokotea simu yake alimpa huku akimuuliza. Simu ilikuwa imesambaratika lakini alikuwa amemuokotea vipengele vyote vya simu ile.
152 MTAFITI
9
“Yah… niko sawa. Ahsante!” Alimjibu huku akiitumbukiza ile simu iliyosambaratika mkobani mwake.
“We fala nini? Unaingia tu barabarani ka’a unaingia ngomani?” Dereva wa lile gari lililomsukuma alifika na kumfokea. Hakuwa ameumia kwa kuwa jamaa aliwahi kufunga breki, na hivyo lile gari likamsukuma tu na kumtupa chini.
Zay alimtazama yule dereva na alitaka kumjia juu lakini hapo raia wengine nao wakamjia juu yule dereva kwa niaba yake.
Mama Mwantumu!
Zay aliwashukuru wale jamaa waliomsaidia na kujichomoa haraka kutoka kwenye lile kundi dogo la watu na kuanza kuelekea kule kwenye lile jengo aliloingia yule mama aliyeishiwa subira, akihisi maumivu hafifu mguuni.
Alisimama nje ya lile jengo na kutazama watu wote waliokuwa pale nje kwa matarajio ya kumuona yule mama bado akizubaazubaa pale nje. Hakumuona.
Alijisogeza na kuingia ndani ya ukumbi mpana ndani ya jengo lile, na ndipo alipomuona yule mama akiwa miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya lifti ambayo milango yake ndio ilikuwa inaishia kujifunga, bila shaka ikielekea kwenye ghorofa za juu za jengo lile.
“Ah! Ma’ Mwantum…!” Alianza kuita lakini ile milango ikawa imeshajifunga.
“Shit huyu maza! Shit, shit, shiiiitt!” Alijinong’oneza kwa hasira na kubaki akiwa amesimama pale kwenye ule ukumbi, asijue la kufanya.
Dakika chache kabla Zay hajafika pale kwenye ule ukumbi wa ndani ya lile jengo lililokuwa na ofisi za akina Luis Kambesera, Inspekta
Haroub Kwakwa naye alikuwa kwenye wakati mgumu, ingawa si kama ule
aliokuwa nao Zay muda ule. Mara baada ya kuachana na Luis Kambesera na timu ya watendaji wake wanafiki, alienda moja kwa moja hadi ofisini
kwake kusubiri matokeo ya maagizo yake kwa Luis na kupanga mikakati mingine ya kuikabili kesi ile iliyomletea hisia kuwa ilikuwa ni kubwa kuliko ilivyoonekana.
Simu yake ya kiganjani ikaita na alipoipokea katibu muhtasi wa mkuu
153 Hussein Issa Tuwa
wake wa kazi, mrakibu mwandamizi wa kanda maalum ya kipolisi akamtaarifu kuwa alikuwa anahitajika ofisini kwa bosi wake.
Aliingia ofisini kwa bosi wake na kusaluti kama ada, na mrakibu mwandamizi akamtazama kwa jicho kali.
“Nimepokea malalamiko kuwa umeenda kumkaba raia ofisini kwake Kwakwa… inahusu nini hii?” Mrakibu Mwandamizi alimkoromea, na Kwakwa akaachia kinywa wazi.
“Umepata malalamiko kutoka wapi afande?”
“Ina maana we’ hujui uliyemkaba ni nani huko leo hii?”
“Kwa hiyo Luis Kambesera, mkurugenzi wa ile kampuni ya tafiti za nishati nd’o amekupigia simu kulalamika juu ya hilo?” Kwakwa aliuliza zaidi, na mkuu wake akamjia juu.
“Unanihoji mimi sasa?” Alimuuliza, na Kwakwa akavuta pumzi na kuzishusha.
“Hapana. Ila…”
“Ila ulimkaba tu sio? Hivi hujui taratibu za kuwadhibiti watuhumiwa Kwakwa?”
“Jamaa katukana serikali na jamhuri kwa ujumla afande… no way ningemuachia hivi hivi tu!” Kwakwa akajitetea.
“Katukana serikali kivipi?”
“Kaiita serikali hanithi! Kwa hiyo ina maana mimi, wewe, IGP, Waziri wa mambo ya ndani na mkuu wa nchi na jopo lake zima la mawaziri pia kawajumuisha katika hilo… mi’ nikamtia mkononi!” Kwakwa alisema kwa hasira na mkuu wake akamtolea macho.
“Una uhakika ndivyo alivyosema hivyo au wewe tu ndio unataka kulifafanua kwa mtazamo wako?”
Kwakwa alimtazama bosi wake.
“Mkuu, yule jamaa anahusika na kifo cha yule mtafiti wa kampuni yake. Ni mtu mweusi sana rohoni yule! Na ninaamini kuna watu wengine weusi zaidi wa nyoyo anaowatumia kumfanyia machafu yake, na mi’ n’na hasira naye sana. Kama anadhani kuwa jeshi la polisi limemtendea vibaya kwa kumkaba basi awasilishe malalamiko yake rasmi… alishitaki jeshi la polisi kama kweli yeye ni mtakatifu!”
“Hajasema jeshi la polisi kuwa limemkaba… kasema Inspekta Kwakwa amemkaba! Na mara ya mwisho nilipoangalia rekodi zangu, huyo Inspekta Kwakwa ni wewe!” Mrakibu mwandamizi alimjia juu.
154
MTAFITI
Kwakwa akapiga kimya, moyo ukimtokota kwa hasira.
“Mi’ najua kuwa jamaa anaweza kuwa vyote hivyo unavyomsema, Kwakwa… lakini hukutakiwa kumkaba namna ulivyomkaba! Sio namna ya kuwatenda watuhumiwa hiyo!” Bosi alimjia juu, na Kwakwa akazidi kuchukia.
“Afande, mhalifu ni mhalifu tu. Vibaka wangapi huko mitaani wanachezea makofi ya polisi mpaka wanarukwa na akili wakati wakikamatwa na hawapigi simu kwako kulalamika? Sasa huyu muuaji kwa kuwa anakaa kwenye ofisi ya ghorofani ndio…”
“Sio hivyo! Hata kibaka akileta malalamiko yake yatasikilizwa! Angalia namna unavyoiendesha hii kesi Kwakwa… la si hivyo nakuhamisha kwenye
kesi na kuikabidhi kwa afisa mwingine! Sitaki kashfa kwenye jeshi letu mimi! Dismissed!” Mrakibu Mwandamizi alimkemea na kumfukuza kutoka mle ofisini kwake. Kwakwa akasaluti huku amenuna, kisha akatoka nje.
Na wakati alipokuwa akiongea na yule mkuu wake wa kazi, simu yake ilikuwa ikiita, naye hakuweza kuipokea.
Alirudi tena ofisini kwake na kutazama ni nani aliyekuwa akimpigia muda alipokuwa kwa mkuu wake wa kazi.
Zay.
Alimpigia ili kujua ni nini alikuwa anataka kumwambia.
Sasa simu ya Zay ndio ilikuwa haipatikani.
Alisonya na kuanza kuirudisha simu yake mfukoni, wakati ile simu ilipoita tena. Aliipokea na kuiweka sikioni.
“Afande! Sajenti Pojo hapa!” Pojo alisikika sikioni kwake, na kwa namna sauti yake ilivyojaa wahka, Kwakwa akajua kuwa mambo hayakuwa sawa.
“Yes, Pojo. Whats up?” Alihoji, na Pojo akampasha habari za yale aliyokutana nayo kule Chang’ombe. Kwakwa, kama ilivyokuwa kwa Pojo, alibaki hoi.
Bilanga alikuwa ameketi ofisini kwake akimsubiri Chabbi Cheka, huku akili ikimzunguka, uso akiwa ameukunja. Alikuwa ameingia ndani ya lile jengo kwa mlango wa nyuma na kupitiliza moja kwa moja hadi kule ofisini kwake. Hakutaka kabisa kuonana na Luis kabla hajaongea na Chabbi.
155 Hussein Issa Tuwa
Sasa nini kinachomchelewesha huyu jamaa lakini?
Wakati akiendelea kulitafakari hilo simu ya pale mezani kwake ikaita.
“
What?” Alimaka simuni, kisirani chake dhidi ya Chabbi akikihamishia kwenye simu.
“Er, bosi Chabbi hayupo, na…”
“Najua kwamba hayupo, sema shida yako!” Bilanga alimkoromea yule dada wa mapokezi aliyepiga ile simu.
“… yah ndio. Sasa aliagiza kuwa…” Binti alisita, halafu akaongea kwa sauti ya chini kama kwamba hakutaka mtu mwingine amsikie, “… mgeni yeyote wa Mwantumu apelekwe kwake. Sasa kwa kuwa ye’ hayupo…”
“Ni nani huyo aliyekuja kumuulizia Mwantumu?” Bilanga alimakinika ghafla.
“Anadai ni mama’ake… na hakuja kwa amani kabisa huyu bosi!” Dada alimhabarisha, na Bilanga alikuwa ameshainuka kutoka kitini kwake, akili ikimzunguka.
“Okay, tafuta mtu amlete hapa ofisini kwangu!” Alitoa maelekezo na kukata simu. Akatoa simu yake ya kiganjani na kumpigia Chabbi.
“Ebwana vipi? Mbona hiyo nusu saa imeshapita tena? Kila kitu kiko sawa?” Alimuuliza kwa wahka.
“Kila kitu kiko sawa sasa… kabla ya sasa hakikuwa sawa. Nd’o niko njiani nakuja… ilinibidi nirudi tena nyumbani kwanza!” Chabbi alimjibu, na Bilanga akauma meno kwa hasira.
“Sasa huku mambo yanazidi kuongezeka… mama Mwantumu kaja kuzusha vurumai hapa, na nimeagiza aletwe huku ofisini kwangu!”
Kimya kikapita upande wa pili.
“Oi! Upo…?” Bilanga akahoji.
“Yah… huyo mama naye anataka kuwa kimeo pumbavu zake, na kama ameshaanza kuja kuja hapo ofisini hakawii kutukusanyia kundi la waandishi wa habari hapo na kutujazia watu!” Chabbi alisema kwa hasira.
“Yote hayo nayajua… sasa tunafanyaje? Maana we’ mkuu wa kitengo ndio uko huko na mambo yako tu!” Bilanga alimlalamikia mwenzake.
“Kila nikifanyacho ni kwa maslahi ya kampuni Bilanga! Mdhibiti huyo mama hapo na hakikisha hakuna yeyote anayejua kuwa yuko
156 MTAFITI
hapo mpaka nifike!” Chabbi alimkoromea simuni, lakini sasa Bilanga
alikuwa amemakinika na mmoja wa wahudumu wa pale ofisini aliyekuwa
akimuingiza mle ofisini mwake mama mmoja mtu mzima aliyejitanda kanga na kichwani akiwa amejifunga kilemba chekundu.
Akakata simu…
Zay alifika eneo la mapokezi pale ghorofa ya saba ya jengo lile na kutembeza macho huku na huko kwenye eneo la mapokezi la pale Liquid Diamond Incorporated bila mafanikio, kwani hakumuona mama
Mwantumu kama alivyotarajia.
Alimfuata yule dada wa pale mapokezi.
“Er, dada… kuna mama’angu amefika hapa muda si mrefu, sijui ameelekezwa ofisi gani humu ndani?” Alimuuliza kwa mashaka, na yule dada akamshangaa.
“Mama’ako? Hapa ofisini?”
“Yaani alichukua lifti huko chini akiwa anakuja hapa. Alikuwa amejitanda kanga mwilini na kichwani amejifunga kilemba chekundu!” Zay alimjibu
kwa kuelezea jinsi mama Mwantumu alivyovaa, kama alivyomuona akiwa ndani ya lifti kabla ile milango ya lifti haijajifunga kule chini.
Dada alimtazama halafu akakwepesha macho na kuanza kujishughulisha na kusogeza vitu pale mezani kwake.
“Hakuna mtu kama huyo aliyefika hapa…!” Alimjibu kwa mkato.
“WHAT?” Zay alimaka huku akimtumbulia macho, na akaona lile swali halikutosha, “unadhani mi’ mpumbavu nini? Mtu nimemuona akipanda lifti kule chini kuja huku juu halafu nafika hapa unaniambia kuwa hayu…”
“Kuna ofisi zaidi ya kumi na tano kwenye hili jengo anti, unasikia?
Unajuaje kuwa alipokuwa kwenye hiyo lifti aliteremkia hapa au ghorofa za chini au huko juu?” Yule dada alimchachamalia, na Zay akamkodolea macho kwa kutoamini.
“Mi’ n’najua kuwa alikuwa anakuja hapa wewe! Usiniambie na yeye mmempoteza tayari kama mlivyompoteza Mwantumu!” Alimjia juu, na yule dada akaachia mguno wa mshangao.
157
Issa Tuwa
Hussein
“Unasema vitu gani wewe? Tumempoteza Mwantumu kivipi, sisi?”
“Niambie ni wapi mlipompeleka huyo mama wewe!” Zay naye akamjia juu, na hapo watu wengine watatu wakafika pale mapokezi kutaka huduma za yule dada.
“Anti n’takuitia askari sasa hivi hapa! Kama huna unalohitaji naomba uondoke! Mi’ sijamuona huyo mama’ako hapa, na niko hapa tangu saa moja asubuhi. N’na wateja wengine wa kuwahudumia!” Dada wa mapokezi alimtemea cheche.
“Nini kinaendelea hapa?” Sauti nzito ilihoji, na wote waliokuwa pale, akiwemo Zay, waligeuka kule ile sauti ilipotokea.
Mtu mrefu, mwenye mwili mpana na kichwa kidogo alikuwa amesimama kwenye mdomo wa korido iliyokuwa ikielekea ndani zaidi ya ofisi zile, akiwa amevaa suruali ya jeans na koti lake, vyote vikiwa vyeusi.
Kwa namna fulani Zay akauhisi moyo ukimlipuka wa woga mkubwa kabisa.
Lile jibaba lilikuwa likimtazama yeye moja kwa moja, na Zay hakuhitaji kusimuliwa kujua kuwa ule mtazamo ulikuwa ni wa chuki kali sana dhidi yake.
Ni yeye! Huyu ndiye yule yule niliyemkurupusha kule chumbani kwa Mwantumu huyu… ni yeye!
Alijikuta akinywea pale alipokuwa.
“Ah! Si huyu anti hapa ananiletea habari nisizozielewa mimi?” Dada wa mapokezi alimjibu yule jamaa huku akiwaelekeza wale wageni waliomkuta Zay pale mapokezi kuingia ndani zaidi ya ofisi zile.
“Habari zipi anazokuletea?” Jamaa liliuliza huku likiwasogelea taratibu pale walipokuwa, na Zay akajikuta akirudi nyuma huku akimaizi kuwa sasa alikuwa amebaki peke yake na wale watendaji wawili wa ile kampuni
iliyokuwa ikizidi kumjaza hofu kila dakika zilivyozidi kusonga.
“Anamuulizia mama’ake gani sijui, nami namwambia hapa hajafika… anabisha!” Mwanadada alimjibu yule jamaa mkubwa, na Zay akamgeukia yule mtu. Akakutana ma macho yenye kuogofya.
“Sasa ndio unamjibu mteja namna hiyo? Hujui namna ya kupokea
wageni hapa wewe?” Jamaa likambadilikia yule dada wa mapokezi ghafla.
158
MTAFITI
Zay na yule dada wakapigwa butwaa, yule dada wa mapokezi akiwa ndiyo aliyebutwaika zaidi.
Muda mfupi tu uliopita aliambiwa kuwa mtu yeyote akitaka kujua kuhusu mama Mwantumu aambiwe kuwa huyo mama hakufika pale. Sasa tena huyo huyo aliyempa maagizo yale anamgeuka baada ya kumwambia kuwa
yule dada alikuwa ameenda kumuulizia huyo mama Mwantumu. Alipepesa macho kwa kutoelewa, na alitaka kufunua kinywa kujitetea wakati Bilanga alipoachana naye na kumgeukia Zay, sasa akiwa na tabasamu pana usoni.
“Oh! samahani sana bibie… nadhani ni kutoelewana kudogo tu! Aaam, karibu ofisini tafadhali… karibu tuongee vizuri!” Alimwambia huku
akimtazama kwa uso wa tabasamu huku akimuashiria kwa mkono wake kuwa aelekee kwenye ile korido aliyotokea yeye muda mfupi uliopita. Zay alibaki akitembeza macho, moyo ukimwenda mbio na akili ikimzunguka.
Alitupa macho kulia na kushoto. Kulia kulikuwa kuna ile lifti iliyomfikisha pale mapokezi, kando ya ile lifti kukiwa kuna ngazi za kuteremka kwa miguu kutokea pale walipokuwa. Kwenye ukuta uliokuwa baina ya ile lifti na zile ngazi, kulikuwa kuna mtungi mdogo wa kuzimia moto, na kando yake kukiwa na kengele ya tahadhari wakati wa dharura ya moto, ikiwa imehifadhiwa kwenye kishimo maalum kilichochimbwa pale ukutani na kuzibwa kwa kioo kigumu.
Kushoto kwake ndio kulikuwa kuna ile kaunta ya pale mapokezi, yule dada akiwa nyuma ya kaunta ile. Moja kwa moja mbele yake ndio alikuwa amesimama yule jamaa mwenye mwili mpana na kichwa kidogo.
Yote haya aliyaona kwa mkupuo na yaliingia akilini mwake haraka sana.
Hakugeuka nyuma, lakini alikwishaona wakati anaingia eneo lile kuwa nyuma yake kulikuwa kuna ukuta tu ambao ulikuwa umebandikwa vibao
vilivyokuwa vikionesha uelekeo wa sehemu za kujisaidia. Kulia wanaume, kushoto wanawake. Au kinyume chake, hakukumbuka vizuri. Hilo halikuwa la msingi sana kwake kwa wakati ule.
Akamtazama Bilanga, ambaye haswa ndiye alikuwa tatizo kwake kwa wakati ule, na kuona kuwa jamaa bado alikuwa akimtolea tabasamu, na
kwa namna fulani, alijikuta akilifananisha tabasamu lile na jinsi ambavyo
159 Hussein Issa Tuwa
Ibilisi aliyelaaniwa anavyotabasamu mara akishafanikiwa kumuingiza mwanadamu kwenye dhambi.
Moyo ukamsinyaa kwa hofu.
Yaani mtu huyu huyu alikuwa akinitazama kwa chuki ya wazi kabisa muda ule alipofika hapa na kuuliza kilichokuwa kikiendelea, halafu tena huyu huyu sasa ananitolea tabasamu la ukarimu namna hii?
Mnafiki first class! Mamluki wa Ibilisi!
“Er, unajua nini…? Mi’ nadhani ningejiendea zangu tu…!” Alisema, sauti yake ikimsaliti katikati ya sentensi na kwa kutoa mtetemo uliodhihirisha kuwa alikuwa ameogopa vibaya sana.
Kwa namna fulani hili lilionekana kumfurahisha sana Bilanga.
“No, bibie… no! Its okay… karibu tu ofisini tuongee. Nadhani tunawajibika kukutaka radhi kwa namna huyu dada hapa alivyokukaripia.
Wewe ni mteja bwana, na hakutakiwa…” Bilanga alikuwa akimwambia huku akizidi kumsogelea lakini Zay akamkatisha.
“Sihitaji kuombwa radhi... nahitaji kuondoka zangu… nadhani nilifanya
makosa kuja hapa!” Zay alisema huku akianza kuiendea ile ngazi.
Bilanga akatafuna midomo kwa hasira.
Huyu binti ni nani? Ni wazi atakuwa anahusiana na Mwantumu huyu… au ndiye yule aliyenikurupusha kule kwa Mwantumu siku ile? Kama ndiye…!
Bilanga aliwaza haraka, lakini alichokitamka kilikuwa ni kingine kabisa.
“Okay, kama unadhani ni lazima uende sitakulazimisha… ila nilidhani nilisikia kuwa ulikuwa unamuulizia mama…?” Bilanga alisema na kuiacha kauli yake ikining’inia hewani kusudi kama swali, akimtaka Zay amalizie ile
kauli kwa kujibu ni mama nani aliyekwenda kumuulizia pale.
Mama Mwantumu! Nilikuwa namuulizia mama Mwantumu!
Fahamu zote zilimtuma Zay atoe jibu hilo, lakini kama ilivyokuwa kwa
Bilanga, akatamka jambo tofauti kabisa lile lililokuwa likivuma akilini mwake muda ule.
“Nadhani nimesema kuwa nataka kuondoka eneo hili!” Alifoka huku
akipiga hatua kubwa kuiendea lifti, akitaraji upinzani zaidi kutoka kwa yule jamaa.
Bilanga hakumzuia.
160
MTAFITI
Wala hakutikisika kutoka pale alipokuwa amesimama. Alibaki akimtazama tu, sasa lile tabasamu lake la kinafiki likiwa limeyeyuka usoni kwake, na badala yake ule uso wake mdogo ukaingia ubaridi wa dhamira iliyofichika.
Hapa hapafai…
Zay aliifikia ile lifti, na alikuwa anataka kubonyeza kitufe cha kuiita lifti pale alipokuwa wakati kengele ya lifti iliposikika, milango yake ikafunguka na Chabbi Cheka akatoka nje ya lifti ile…
La Haula!
Dakika chache kabla Mama Mwantumu hajafikishwa mbele ya Bilanga, wakurugenzi wa Liquid Diamond Incorporated walikutana tena kwenye kile chumba cha mikutano, ghorofa ya nane ya jengo lile, kama walivyokubaliana.
Luis Kambesera alikuwa ametoka kuongea tena na Chabbi Cheka kwa simu kabla ya kuingia kwenye kile chumba cha mikutano, na Chabbi alikuwa amemhakikishia kwamba alikuwa njiani kuelekea pale ofisini.
“Fanya fasta… mambo yamekuwa mazito kidogo huku….” Luis alimwambia.
“Nitafika hapo chini ya dakika ishirini bosi, usihofu.Tutayawekea mikakati yote hayo!” Chabbi alimhakikishia, naye akawa na nguvu ya kuwakabili wake wenzake.
Wakati huo alikuwa ameshamuagiza Suleiman Mwangi, mwanasheria wa kampuni apige simu kwa mrakibu mwandamizi wa polisi wa kanda maalum, ambaye ndiye alikuwa mkuu wa kazi wa Kwakwa, kulalamikia
‘usumbufu na manyanyaso’ waliyokuwa wanapata kutoka kwa yule Inspekta. Suleiman Mwangi aliweka bayana kwa mkuu wa kazi wa Kwakwa kuwa kampuni yake iko tayari kutoa ushirikiano wa kila hali kwa jeshi la polisi katika upelelezi wa mauaji ya Grayson, lakini haitakuwa tayari kabisa kufanya hivyo chini ya askari mwenye kiburi na manyanyaso kwa uongozi wa kampuni yao kama Kwakwa.
Sasa Luis alikuwa akiwatazama wenzake mle ndani.
“Haya jamani sasa tunaweza kuendelea na kikao chetu…” Aliwaambia.
“Okay, maamuzi yanakuwaje… Chabbi anaenda polisi au haendi?”
161
Hussein Issa Tuwa
Maginga aliuliza.
“Halafu akienda huko anaenda kusema nini?” Luis aliuliza, na wenzake wakamtolea macho.
“Unataka kusema kuwa haendi?” Jamilla aliuliza kwa jazba.“Sijataka kusema lolote… nimeuliza swali. Akienda huko anaenda kujieleza nini?”
Luis alikazia swali lake.
“Of Course anaenda kukana kuhusika na kifo cha Grayson! Kama askari watambishia basi na waoneshe ushahidi wao!” Mike Mwangati alitoa hoja.
Kimya kikapita.
“Sikilizeni jama… suala la Chabbi naomba kwa sasa tuliache kama lilivyo, mpaka Chabbi mwenyewe atakapofika. Mimi na yeye tutapanga mkakati juu ya hilo…” Luis alisema, na hapo Mike Mwangati akainua mkono, wazi akitaka kupinga hoja ile, lakini Luis akamuashiria atulie, na kuendelea, “Kisha tukishapitisha mkakati juu ya namna ya kulishughulikia hili suala nyote mtajulishwa kabla halijafanyika… hapo vipi?”
“Fair enough!”
“Hapo sawa…”
“
Good. Sasa nimeshaaza mkakati wa kumuondoa kabisa yule Inspekta kwenye kesi hii. Suleiman Mwangi alihakikisha juu ya hilo. Nadhani akiendelea na ukorofi wake kwetu hataendelea tena kuweko kwenye kesi hii. Lakini pia akija Chabbi, naamini kutakuwa kuna ushauri zaidi juu ya namna ya kumdhibiti!” Luis alisema na vichwa vikatikiswa mle ndani.
“Suala la msingi nadhani lilikuwa ni kujaribu kurejesha imani ya wananchi na wanahisa wa kampuni na washirika wetu kule sauzi kwenye hii kampuni. Hilo nadhani nd’o la muhimu sana kwa sasa. Inspekta Kwakwa na kifo cha Grayson vyote vinachukua nafasi za chini mbele ya hilo… sasa na tulijadili hilo basi. Tunafanyaje?” Luis alisema.
Mjadala uliendelea kwa muda, na hatimaye azimio likapatikana. Nalo lilikuwa ni kwa kampuni kutoa tamko litakalorejesha imani ya wananchi na wadau wake wote kwenye kampuni ile, na kusahau juu ya habari ya kifo cha Grayson Mochiwa.
“Okay Suleiman, andaa mkutano na waandishi wa habari. Tutaenda kuongea nao tukiwa na mkakati wetu huu akilini!” Luis alimwambia mwanasheria wa kampuni, ambaye pia huwa anabeba majukumu ya usemaji wa kampuni.
Ulionekana kuwa ni mkakati mzuri sana kwa wakati ule.
162 MTAFITI
Ghafla, kengele za hatari ya moto zikarindima jengo zima, na wakurugenzi wakataharuki huku wakianza kutimua mbio kutoka nje ya ule ukumbi wa mikutano…
Mara moja Chabbi Cheka alimtambua yule binti, na akabaki akimkodolea macho huku akili ikibofya maswali kibao kichwani mwake. Na hapo hapo
Zay akajua kuwa yule jamaa aliyetoka kwenye ile lifti hakuwa mtu mzuri na kwa namna fulani alikuwa amemtambua, ingawa yeye hakuwa akimjua na hakujua jamaa atakuwa amemtambua kutokea wapi. Alijaribu kumpisha ili yule jamaa atoke mbele ya ile lifti naye aingie na kutoweka kutoka eneo lile.
Chabbi Cheka alisimama pale pale alipokuwa, akimzibia njia ya kuifikia ile lifti huku akimtazama, na Zay akajua kuwa alikuwa amenaswa.
“Haraka ya wapi Zay…?” Hatimaye Chabbi alimuuliza kwa sauti ya chini huku akimtazama moja kwa moja machoni, na Zay akahisi mwili
ukimwingia baridi. Kutokea nyuma yake akasikia hatua za lile jibaba lenye
kichwa kidogo zikimsogelea pale alipokuwa na ndipo ilipomdhihirikia
kuwa hakika alikuwa amejiingiza kwenye mdomo wa mamba mwenye uchu.
Chabbi alipiga hatua kumfuata.
“Nadhani tunahitaji kuongea kwa kituo mimi na wewe Zay, kwa kuwa…” Alianza kumwambia, lakini hapo ndipo alipoishia kwani ghafla Zay aliruka pembeni na kulinyofoa ule mtungi wa kuzimia moto uliokuwa umepachikwa pale ukutani kando ya ile lifti.
“HEEEY!” Bilanga alimpigia kelele huku akijaribu kumuwahi, wakati
Chabbi akimrukia kujaribu kumzuia, lakini Zay aliwahi kukishusha kwa nguvu kitako cha lile tungi kwenye kile kioo kilichokuwa kimeihifadhi ile kengele ya hatari ya moto.
“WEWEEEEEE!” Chabbi aliropoka, na hapo hapo kelele kali za ile kengele zilirindima ofisini kote, maji yakirushwa kwa wingi kutokea
kwenye vitego maalum vilivyowekwa kwenye dari la ile ofisi, ambavyo vilikuwa vimetegeshwa maalum kufanya hivyo pindi ile kengele ya moto ikigonga, kwa lengo la kuuzima huo moto utakaokuwa unawaka.
Bilanga na Chabbi walimkimbilia kwa kasi, nyuso zikiwa zimekunjamana
163 Hussein Issa Tuwa
MTAFITI
kwa hasira.
Zay aliwatupia kwa nguvu lile tungi, na bila kutazama iwapo lile tungi lilimpata yeyote kati yao au la, alitimua mbio kuzishuka zile ngazi huku akipiga kelele kama mwehu, alilokuwa akilisema wala hakulijua. Alichojua ni kwamba alikuwa anapiga kelele na alitakiwa aendelee kupiga kelele mpaka msaada ufike.
Huku nyuma Bilanga aliruka pembeni kulikwepa lile tungi, yowe la hamaniko likisikika kutoka kwa yule dada wa pale mapokezi, naye akinusurika kupamiana na Chabbi Cheka, ambaye aliwahi kuruka pembeni kumpisha na kujaribu kuziwahi zile ngazi kumfuata yule binti. Walichelewa.
Kizaazaa cha mwaka kilitokea wakati kundi la wafanyakazi wa ile kampuni lilipotoka mbio kutoka kila upande wa ofisi zile na kuanza kuziwahi zile ngazi, wakipiga kelele za moto, ambao hata hivyo ulikuwa hauonekani, yale maji yaliyokuwa yakitoka kwenye vile vitego vya kuzimia moto yakiwalowesha na wengine wakiteleza na kupiga mieleka ovyo mle ndani.
Na kule kwenye chumba cha mikutano, wakurugenzi wa kampuni ile nao wakajazwa taharuki na kengele zile. Bila kujadiliana zaidi, nao walianza kukikimbia kile chumba cha mikutano.
Kule chini Zay aliendelea kuzishuka zile ngazi kwa kasi huku akipiga mayowe, sasa akiwa anasaidiwa na wale wafanyakazi waliokuwa wakizishuka zile ngazi kwa kasi na pupa.
Tatizo yeye alidhani wote wale walikuwa wanamkimbiza yeye, hivyo akazidi kupiga mayowe huku akiongeza kasi, akizishuka ngazi mbili mbili. Akajigonga magoti, akayumba vibaya, akapiga mweleka kwenye zile ngazi. Mikono yenye nguvu ikamnyanyua na kumvuta mbele kwa nguvu.
“Taratibu dada! Kimbia haraka lakini bila papara… kila siku tunaambiwa humu ndani... vipi wewe?” Jamaa aliyemuinua, bila shaka ni mmoja wa wafanyakazi wa ile kampuni, alimwambia huku akiendelea kukimbia na akimwacha akiwa anatweta kando ya zile ngazi, wafanyakazi wengine wakimpita mbio.
Kumbe nao wanakimbia moto! Pumbavu!
Alijiunga na lile kundi la wafanyakazi na kuanza kushuka nao zile ngazi haraka haraka huku akigeuka nyuma mara kwa mara kutazama iwapo wale jamaa walikuwa wanamfuata.
164
Hakuwaona.
Yule jamaa anajua jina langu, na ananijua!
Oh! My God, ni watu gani hawa?
Mwantumu kaingia kwenye balaa gani lakini?
Na mama’ake naye?
Alikuwa amechanganyikiwa vibaya sana wakati akitoka nje ya jengo lile na kukatisha barabara. Alianza kukata mitaa bila ya kujua ni wapi hasa alikuwa anaelekea…
Mara walipoona kuwa Zay amefanikiwa kuzusha tafrani pale ofisini na amewatoka, Bilanga na Chabbi waligeuza haraka, kila mmoja akichukua uelekeo tofauti bila hata ya kuambizana. Bilanga alijitoma ndani ya ile lifti na kushuka nayo chini, wakati Chabbi akirudi mbio kwenda kule ofisini kwake.
“Pumbavu! Hakuna moto bwanaaaa!” Alimaka huku akihangaika kupitisha ufunguo kwenye mlango wa ofisi yao, ambamo Bilanga alikuwa amemfungia mama Mwantumu muda wote, akiwa amemtuliza kuwa alikuwa anaenda kumuitia mtu ambaye angemueleza kwa kituo juu ya habari za mwanaye Mwantumu, baada ya kuona mabishano kati ya Zay na yule dada wa mapokezi kupitia kwenye runinga iliyokuwa mle ofisini kwake, kama jinsi ilivyokuwa ofisini kwa Chabbi.
Muda Chabbi alipoufungua tu ule mlango wa ofisi yao, ambapo alitakiwa aipite ofisi ya Bilanga kwanza ndio aifikie ile ya kwake, alikumbana na mwanamke aliyetoka mbio mle ofisini huku akiwa amehamanika vibaya sana na akipiga mayowe.
“HEEEEEY, NANI WEW…?” Chabbi alipayuka kwa hamaniko huku akisukumwa pembeni bila hadhari, kwani hakujua kabisa kama mle ndani kulikuwa kuna mtu na hakuwa amepata nafasi ya kuongea na Bilanga juu ya hilo mara alipofika pale mapokezi kutokana na ile tafrani ya Zay.
Mama Mwantumu alimpita ubavuni kwa kasi na kutoka nje ya ofisi ile.
Aliwahi kule kwenye ngazi, ambako bado kulikuwa kuna wafanyakazi wachache wakimalizikia kukimbia hatari ile ya moto usiokuwepo.
“SHIIIIT! AKH!!” Chabbi alilaani kwa hasira, lakini hakumfuata.
Alipitiliza moja kwa moja hadi ofisini kwake na kunyakua kipaza sauti
165 Hussein Issa Tuwa
cha kurushia matangazo mle ofisini. Akaanza kunadi kuwa wafanyakazi watulie na warudi kuendelea na kazi, kwani hatari ya moto ilikuwa imeshadhibitiwa.
Alilirudia lile tangazo kama mara tatu, kisha akazima kile kisemeo na kuketi kitini kwake pale ofisini, akitafakari jinsi mambo yalivyokwenda mrama kwa kasi ya ajabu ndani ya muda mfupi sana.
Yule Zay keshafika hadi hapa?
Alikuwa anataka nini?
Na yule mama aliyekuwa amefungiwa na Bilanga humu ofisini… ni nani?
Mwili ulimsisimka Chabbi Cheka, kama jinsi ambavyo huwa unamsisimka akabiliwapo na changamoto kama zile. Yeye siku zote huwa anajihesabu kuwa ni mtu wa sekeseke, na sekeseke zikiwa zinamtokea kama hivi ndio hujiona kuwa hakika yuko duniani.
Luis Kambesera alifika pale mlangoni kwake kama mzimu na kumtumbulia macho.
“Kumbe uko jengoni muda wote na hukuja kuniona? Si nilikwambia…”
Luis alianza kumlaumu kwa jazba, na Chabbi akamkatisha.
“Mi’ ndo nimeingia hapa muda huu huu… na kukutana na zahma hii!”
“Ni nini kinatokea lakini Chabbi? Mambo yanazidi kutuandama tu namna hii? Hii kengele ya moto imetokana na nini tena?” Luis alimaka.
“Sit down Luis… we need to talk!” Chabbi alimwambia huku akionekana kuwa mchovu sana, akimaanisha kuwa Luis akae wafanye maongezi.
“Tutaongelea ofisini kwangu!” Luis alijibu kwa kiburi na kugeuka kurudi ofisini kwake.
Chabbi alibenyua midomo kwa aidha kukereka au kudharau kitendo kile au kwa kuwa hakuwa na kingine cha kufanya wakati ule, mwenyewe ndio alikuwa anajua. Akapandisha miguu juu ya meza yake
Alitoa simu yake na kumpigia Bilanga, lakini ile simu ilikuwa ikiita tu bila majibu.
Maumivu makali yalimchoma kwenye lile jeraha aliloachiwa na Mwantumu shingoni kwake, naye akafinya uso na kuuma midomo kwa maumivu yale.
“Pumbavu sana Mwantumu! Pumbavu sana, sana, sana!” Alinong’ona kwa hasira, na kubaki akiwa ameketi pale ofisini namna ile kwa muda mrefu.
Kisha alisonya na kuinuka.
166
MTAFITI
Akaliendea jokofu dogo lililokuwa mle ofisini kwake na kutoa chupa ndogo ya pombe kali. Akaifungua, na akiwa amesimama pale pale mbele ya lile jokofu akapiga funda moja kubwa, kisha akaunguruma kwa faraja ya mshuko wa kinywaji kile kooni kwake. Akamung’unya midomo huku akilifunga lile jokofu, halafu akatoka na kinywaji chake mkononi hadi ofisini kwa Luis.
Wakati yale ya kule Liquid Diamond Incorporated yakiendelea, Inspekta Kwakwa na Sajenti Pojo walikuwa kwenye mtanziko mzito. Walikuwa ofisini kwa Inspekta Kwakwa pale kituo kikuu cha polisi au central kama kilivyozoeleka kwa wengi jijini Dar.
“Kwa hiyo unadhani kifo cha yule dereva wa bajaji si cha bahati mbaya?”
Kwakwa aliuliza tena, na Pojo akaafiki kwa kichwa.
“Kabisa afande… yaani kwanza jamaa aliyemkodi yule kijana amemchukua muda ule ule ambao mimi ndio nilikuwa nimefika pale… halafu wakati alipokuwa anataka kuniambia jambo muhimu kuhusu mtu aliyekuwa na Mwantumu siku ile hapo hapo ajali ikamkuta!”
“Ah! Sasa hiyo we’ inakwambia nini?”
“Inaniambia kuwa bila shaka huyo jamaa alikuwa naye kwenye bajaji muda huo!”
“Huoni kuwa kama hivyo ndivyo, na yeye pia basi atakuwa ameumia ajalini?” Kwakwa alisaili, na Pojo akatikisa tena kichwa kuafikiana na hoja ile.
“Inawezekana…”
“Lakini umeniambia kuwa askari waliofika pale eneo la tukio hawakuona maiti nyingine au majeruhi atokanaye na ajali ile zaidi ya huyo kijana…”
Kwakwa alizidi kumtahini yule Sajenti mtu mzima.
“Na ndio la kutia mashaka zaidi hilo afande…! Kwa nini mtu apate ajali kama ile akiwa na abiria, halafu abiria asionekane? Ina maana hata kama kaumia, mhusika aliona ni muhimu sana yeye kutoonekana eneo lile kuliko kusubiri kupatiwa msaada na wasamaria! Hiyo inakwambia nini wewe afande?” Pojo alisisitiza, na kumrudishia Kwakwa swali lake la awali.
Kwakwa alimtazama kwa muda akiwa amekunja uso.
“Hoja yako inaleta maana sana Sajenti…”
“Of course inaleta maana afande! Sasa suala linabaki kuwa huyo jamaa ni nani… na tutampata vipi?”
167
Issa Tuwa
Hussein
“Nadhani haitatuchukua muda mrefu tutamjua tu… na tukishamjua, kumpata si tatizo.” Kwakwa alisema.
Kimya kilitanda kidogo.
“Dah! Ila huyu jamaa ni mjanja sana aisee. Hapa tunapambana na mtu mjanja na makini sana afande. Yaani ameweza kujua kuwa kwa vyovyote vile tutamsaka tu yule mwendesha bajaji… sasa yeye akatuwahi, na kumpoteza!” Sajenti Pojo alisema kwa namna ya kulaani lakini pia kwa kustaajabia umakini wa mhalifu wao.
Kwakwa alimtazama kwa jicho kali, kisha akaguna.
“Unajua yeye anaweza kuwa mjanja au makini kama usemavyo, lakini sisi tuna busara.” Alimwambia. Pojo hakumuelewa, na akamwambia hivyo.
Kwakwa akapiga kimya kifupi.
“Unajua kuna mwandishi mmoja… anaitwa Poe… Edgar Allan Poe…” Hatimaye alimwambia, na Pojo akazidi kumtumbulia macho ya kuuliza.
“Yeye aliwahi kuandika kuwa ‘Nothing is more hateful to wisdom than excessive cleverness’. Unanipata hapo?” Kwakwa alimwambia, na kumalizia na swali. Pojo akafinya uso kuyatafakari maneno yale.
“Oho! Kwamba hakuna kinachoichukiza zaidi busara…” Hatimaye alisema huku uso wake ukionesha uelewa kwa maneno yale, na Kwakwa akamalizia tafsiri ya maneno yale pamoja naye.
“… kuliko ujanja uliopitiliza!”
Kisha wote wakaangua kicheko.
“Au hakuna kinachowachukiza zaidi watu wenye busara kama ujanja uliopitiliza! Mi nakubaliana sana na msemo huo kaka.” Kwakwa alisema.
“Yaani sikuwa nikiujua huo msemo kabla ya leo afande, lakini baada ya kuusikia leo hii, nakubaliana nao mia kwa mia!” Pojo aliafikiana naye.
“Kwa hiyo kaka, huyu jamaa anaweza kujifanya mjanja… ila kwa hili alilolifanya leo, ujanja wake umepitiliza… kwani hapo ametaka kutufanya sisi wenye busara zetu kuwa ni wajinga sana. Na hilo linatufanya tuwe na ghadhabu sana dhidi yake. Tutamtia mbaroni muda si mrefu pumbavu zake!” Kwakwa alimwambia mwenzake, na hapo simu yake ikaita…
Kule Liquid Diamond, Bilanga aliwahi kufika chini kabla ya wote waliokuwa wakishuka kutoka kule ghorofani kwa kutumia ngazi za miguu kwa kufuata ule utaratibu wa kutotumia lifti wakati wa hatari ya moto jengoni. Kwa kuwa yeye alijua kuwa hakukuwa na moto, alitumia
168 MTAFITI
lifti kushuka kule chini bila ya shaka yoyote. Akiwa upande wa pili wa barabara nje ya jengo lile, alimuona Zay aliyejaa wahka akitoka nje ya lile
jengo, naye akaanza kumfuatilia kwa mbali, akiwa makini kulivua lile koti lake la jeans na kulishika mkononi, akibaki na fulana nyekundu aliyokuwa ameivaa chini ya koti lile.
Alimfuata Zay wakati akikata mitaa kadhaa mjini na akaona moja kwa moja kuwa yule binti alikuwa amechanganyikiwa na hakuwa na uelekeo maalum. Simu yake ikaanza kuita, lakini hakuipokea, kwani hakutaka kupoteza umakini. Yeyote awaye, atampigia baadaye.
Baada ya mizunguko kadhaa mjini hatimaye yule binti akaingia kwenye mgahawa fulani, naye akabaki akiwa amesimama nje, ubavuni mwa mgahawa ule huku akili ikimzunguka. Hakujua iwapo ule mgahawa ulikuwa na mlango wa nyuma au la, na wakati huo huo alihofia kuzunguka huko nyuma kuthibitisha hilo kwa mashaka kuwa wakati akiwa huko nyuma yule binti atatoka huku mbele na kumpotea.
Afanyaje sasa?
Hakusubiri sana kupata jibu.
Yule binti alitoka nje ya ule mgahawa na kuendelea na safari yake, wazi kuwa hata alipoingia mle mgahawani hakujua alienda kufanya nini, hivyo akaamua kutoka. Ila sasa mwendo wake ulimwambia kuwa yule binti alikuwa ameshapitisha uamuzi juu ya mahala alipokuwa anataka kwenda, kwani alionekana akitembea kwa lengo na uelekeo maalum.
Zay alirudi hadi pale alipoegesha gari lake na kujifungia ndani yake.
Alikuwa akitetemeka mwili mzima. Hakuamini kuwa alifanikiwa
kuwachoropoka wale watu kule kwenye ile ofisi ya kifo. Sasa alikuwa na uhakika kabisa kuwa wale ndio jamaa waliomteka Mwantumu, kwani
aliikumbuka vizuri sana sauti ya yule jamaa aliyetoka kwenye lifti na kumwita kwa jina lake.
Ilikuwa ni ile ile sauti aliyoisikia kwenye simu siku ile alipopigiwa na kudaiwa awape chao ile wamrejeshee Mwantumu, na akamsikia Mwantumu
akimpigia kelele simuni.
Baridi ilimtambaa mwilini, na akakumbuka jinsi Sajenti Pojo alivyomuasa
kuhusu kuionesha sura yake kwenye ile ofisi, na jinsi alivyomtahadharisha
kuhusu uhatari wa wale watu.
Naam, sasa alijihakikishia kuwa wale jamaa walikuwa ni hatari kweli kweli.
“Lakini sasa ningefanyaje? Mama Mwantumu alikuwa ameshaingia mle
169
Issa Tuwa
Hussein
ndani… ningemuacha?” Alijisaili mwenyewe garini. Mama Mwantumu!
Oh, My God… mama Mwantumu!
Si watamuua wale watu jamani!
Alikurupuka na kuikusanya simu yake iliyosambaratika kutoka kwenye begi lake na kuiweka sawa, kisha hapo hapo akaiwasha. Na meseji ikaingia kabla hata hamjapigia mtu aliyetaka kumpigia.
UKO WAPI WEWE? NIPIGIE HARAKA SANA!
Ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Inspekta Kwakwa.
“Oh, laiti ungejua na mi’ nd’o n’likuwa nataka kukupigia!” Alisema peke yake na kumpigia yule askari makini.
“Ah, Zay…! Vipi wewe, mbona…?” Inspekta Kwakwa aliongea simuni na Zay akamkatisha.
“Mama Mwantumu yuko hatarini afande! Please nenda kamuokoe… watamuua!” Alipayuka, na upande wa pili Kwakwa akamakinika, akimtupia Pojo jicho la pembeni.
“Yuko matatani kivipi? Yuko wapi?” Alihoji.
“Kule kwenye ile kampuni! Kaenda na nadhani jamaa wamemteka…!”
“Sasa kaenda au katekwa…?”
“… mi’ nimechomoka kimajaaliwa tu afande!” Zay alizidi kupanda wahka simuni, na Kwakwa akazidi kujazbika.
“What do you mean umechomoka kimajaaliwa? Ulienda liquid Diamond wewe?”
“Ah! Huyu demu anataka kutuchanganyia habari sasa! Kaenda kutafuta nini huko tena?” Pojo alilalamika peke yake huku akimtazama Kwakwa.
“Like… Sikuwa na namna afande! Mama wa watu atakufa huko jamani! Nenda kamsaidie bhanaa!” Zay alipayuka, huku akisikia simu nyingine inataka kuingia.
“Mahabusu inakuhusu Zay! Tena nakutia ndani mimi mwenyewe mrembo mpumbavu… mimi mwenyewe! Ushakuwa hatari kwa maisha yako sasa, bloody shit!” Kwakwa alimfokea simuni na kukata simu.
“Twen’zetu!” Alimwambia Pojo huku akiongoza kutoka nje ya ofisi yake. Bila kubisha Pojo aliinuka na kumfuata, naye akiwa ameghadhibika vibaya sana.
Kule garini Zay alikata simu na hapo simu nyingine ikaingia.
“Zay mwanangu!”
170 MTAFITI
Alikuwa mama Mwantumu.
Heh!
“Mama! Uko wapi? Um… umetokaje kule…?”
“Oh, Zay mwanangu ni balaa kubwa! Wale si watu wazuri wale… mwanangu wanaye wale… wanaye, wanaye tena wanaye! Kwa nini lakini?”
Mama Mwantumu alilalama simuni huku akilia wazi wazi.
“Hebu ngoja kwanza mama. Yaani… umetoka kwenye ile ofisi?” Zay aliuliza, akili ikimuwanga.
“Nimechomoka kama ulivyochomoka wewe mwanangu!”
Khah!
“Unamaanisha nin… anyway, hapo ulipo chukua bajaji upesi elekea polisi central mama… tukutane central polisi. Mi’ naelekea huko!” Zay alisema kwa wahka, na kukata simu.
Akampigia Kwakwa.
“Mama Mwantumu katoroka kule! Nimemwambia aje central polisi!”
Alimwambia.
“Ama!” Kwakwa alistaajabu.
“Na mi’ nakuja huko, so nadhani na we’unisubiri hapo hapo tu afande, na usiniletee habari ya kuniweka ndani mimi!” Zay alimkoromea kisha akakata simu. Alitia gari lake moto na kuliondoa kwa kasi kutoka eneo lile.
Bila ya yeye kujua, harakati zake zote zilikuwa zimeshuhudiwa na Bilanga aliyekuwa amesimama mbele ya meza ya muuza magazeti akijitia kuperuzi vichwa vya habari magazetini. Aliitazama ile Vitz ya Zay ikiondoka eneo lile akiwa tayari ameshaikariri namba zake za usajili.
“Nimeshakujua sasa we’ malaya… kukupata haitakuwa taabu tena kwangu!” Alijisemea huku akirudi taratibu kule ofisini kwao…
“WHAAT?” Luis Kambesera alibwata kwa hamaniko baada ya kusikia maelezo ya Chabbi Cheka. Alimkazia macho yule mtu wake muhimu sana katika masuala yake yote ya haramu, ambayo yalikuwa mengi.
Chabbi Cheka alibaki akimtazama huku amejibweteka pale kwenye kochi mororo.
“Yaani pamoja na yote hayo bado makabrasha ya Grayson hujayapata Chabbi?” Luis aliuliza tena baada ya kuona kuwa Chabbi amepiga kimya.
171 Hussein Issa Tuwa
“Ndio bosi… hali ndio iko hivyo mpaka sasa. Lakini sio mbaya kihivyo, hali inadhibitika!” Chabbi alisema na kupiga funda jingine kutoka kwenye ile chupa ndogo ya pombe kali.
“Sio mbaya kihivyo? Hali hii ni mbaya sana Chabbi! Tena sasa ndio imekuwa muhimu zaidi kuyapata hayo makabrasha ya Grayson kuliko wakati mwingine wowote! Una hakika nyumbani kwa Grayson mlipekua vizuri kweli?” Luis alisema na kuuliza.
“Huko tulishamaliza kupekua tangu Grayson hajawa marehemu na sote tukajiridhisha kuwa hakuna kilichobakia kule…” Chabbi alimjibu
“Still… panahitaji kutazamwa tena…!”
“Hayo makabrasha najua aliye nayo Luis. Yaani we’ amini kuwa nitayapata tu!” Chabbi alimwambia, na Luis alipomtolea macho ya kuuliza, akamweleza kuhusu Zay, na kituko chote kilichosababisha zile kengele za moto kulia mle mjengoni mchana ule.
Luis akamjia juu vibaya sana.
“Unaona? Yaani sasa hata hao watoto wanadiriki kuja hapa ofisini kwetu?”
“Yule mpumbavu alikuwa anakuja kuulizia habari za rafikiye tu… kila kitu kitakuwa sawa Luis. Zay anayo makabrasha yale, na mi’ n’tayapata tu!” Chabbi alimwambia.
“Hujui usemalo Chabbi. Hebu sikia hii…” Luis alimwambia, na hapo akamweleza kinaga ubaga kile kilichotokea pale ofisini baina yao na Inspekta Kwakwa.
“Sasa unahitajika kuripoti kituoni na kujisalimisha kwa Inspekta Kwakwa, Chabbi. Ndani ya saa ishirini na nne!” Luis alimalizia, na Chabbi akamkazia macho.
“Nadhani ulisema tunatakiwa tuamue ni nani aende selo kati yangu na nyinyi wakurugenzi… sasa vipi we’ unaamua moja kwa moja kuwa mimi ndiye niende?” Chabbi alimuuliza, na Luis akagwaya.
“Ah, Chabbi… si unajua madhara kwa kampuni yatakavyokuwa ikiwa…”
“Achana na hilo. Naelewa… mimi natakiwa niende kujisalimisha kutokana na tuhuma za kutoweka kwa Mwantumu…” Chabbi alisema, na kubaki akiwa ameuma midomo kwa tafakuri.
“Of Course wakili wetu atakuja kukutolea dhamana fasta tu nawe utatoka, lakini cha msingi ni kwamba hakutakiwi kuwe na lolote la kukuoanisha na huyo binti. Na kwa maelezo yako ni kwamba hakuna…”
172 MTAFITI
“Hakuna ndio!”
“Alright. Vyovyote iwavyo, kusiwe na chochote cha kukuhusisha naye!” Luis alisema.
“Si nimekwambia kuwa hilo nimelimaliza mchana huu Luis? Hakuna lolote la kuniunganisha na kupotea kwa yule binti sasa!”
“Yah… safi sana! Limebakia hilo la wewe kwenda kwa Inspekta Kwakwa tu…” Luis alisema.
Chabbi alipiga kimya kwa muda mrefu. Kisha akashusha pumzi ndefu, akapiga funda jingine la ile pombe yake, na kuinuka.
“Sio taabu. Najua cha kufanya. Kisha nitaenda mwenyewe kwa huyo Inspekta!” Alisema huku akitoka nje ya ofisi ile, akimwacha Luis akimtazama kwa mashaka.
Nje ya ofisi ya Luis, Chabbi Cheka alimpigia tena Bilanga.
“Yes Chabbi… nilikuwa nataka kukupigia sasa hivi. Kuna mengi ya kuongea…” Bilanga alimwambia.
“Hakuna muda. Tunaelekea Mbagala sasa hivi!” Chabbi alimwambia, na Bilanga akapiga kimya kidogo.
“Oh!” Hatimaye alisema.
“Ndio. Tuna kazi ya kufanya kule!” Chabbi alithibitisha, na kukata simu. Walikutana pale ofisini kwao dakika chache baadaye.
“Huyu Inspekta Kwakwa… yukoje huyu?” Chabbi alimuuliza Bilanga, huku akirejesha nyuma mkanda uliokuwa umerekodi matukio yaliyokuwa yakitokea ndani ya zile ofisi, hususan ule uliokuwa umerekodi matukio ya kule kwenye chumba cha mikutano.
“Utamuona tu hapo kwenye mkanda…” Bilanga alimjibu.
“Of course najua kuwa nitamuona hapa… nataka kujua alivyo kiutendaji, sio kwa mwonekano…!” Chabbi alimjibu kwa kukereka.
“Utendaji wake pia utauona kwenye huo huo mkanda… jamaa sio mjinga kama askari wengine tuliowazoea Chabbi, na kwa hilo nimetokea kumchukia sana!” Bilanga alimwambia kwa kukereka pia.
Chabbi akaguna.
Akafikia ile sehemu ambayo Kwakwa alivamia kwenye ule mkutano wa akina Luis na kuanza kutazama kwa makini kila kilichojiri mle ndani hadi ile sehemu ambapo Kwakwa alimkaba koo Luis. Aliugandisha ule mkanda sehemu ile na kumtazama Kwakwa kwa muda mrefu.
“Okay… Kwakwa. Huenda ukawa ni mbabe kuliko askari wenzako,
173 Hussein Issa Tuwa
lakini safari hii umeingia choo cha kike fala wewe. Unaniita kituoni mimi?”
Chabbi aliiambia sura ya Kwakwa iliyoganda pale kwenye ile runinga yake
kubwa kwa hasira, na Bilanga akaguna. Chabbi aliitazama ile sura kwa muda mrefu zaidi kisha akainuka.
“Twen’zetu… huyu jamaa nitamfanyia kazi baadaye!” Alisema huku akiizima ile runinga.
“Okay, tunatumia usafiri gani sasa?” Bilanga aliuliza.
“Kila mtu kivyake… tukutane eneo la tukio!” Chabbi alimwambia.
“Poa!”
Wakatoka.
Saa moja baadaye, walikutana pale kwenye ile nyumba ambamo Chabbi alikuwa amemficha Mwantumu siku mbili zilizopita. Ilikuwa ni saa kumi na moja kasoro robo za alasiri…
174
MTAFITI
OFISINI KWA INSPEKTA Kwakwa pale polisi central hali ilikuwa imejaa fukuto. Inspekta Kwakwa na Sajenti Pojo walikuwa wamesikiliza kisa cha Zay kwa makini, wakiuliza maswali mara kwa mara kila walipoona kuna haja ya kufanya hivyo.
“Kwa hiyo mnaona wazee, sikuenda pale Liquid Diamond kwa kiburi au kwa kupenda… ma’ Mwantumu alishaingia mle ndani, na nikakupigia simu afande Kwakwa hukupokea. Sa’ mi ningefanyaje? Haitakuwa sawa kunitia ndani kwa sababu hiyo!” Zay alisema baada ya kumaliza maelezo yake.
“Hatukusema utawekwa ndani kwa kuadhibiwa Zay… ni kwa usalama wako wewe mwenyewe!” Kwakwa alimwambia.
“Hata hivyo, Inspekta… selo ni selo tu!”
“So ungependelea kuwekwa kaburini instead?” Pojo alidakia kwa hasira, na Zay akamkodolea macho kwa mshangao.
“Ndio maana yake! Wale jamaa ni wauaji na hawatasita kukuua kama utakuwa ni kikwazo kwao!” Pojo alimjia juu, na hapo mama Mwantumu akaachia kwikwi ya kilio.
“Ah, kwa hiyo na mwanangu nd’o wameshamuua hivyo!” Alisema, na wale askari pamoja na Zay wakatazamana.
“No, no, noo madam, sio hivyo! Hatujui hilo kwa sasa. Tunaamini kuwa
Mwantumu yuko hai, kwani chochote wanachokitaka kutoka kwake hawajakipata bado. Sisi tutajitahidi tumpate kabla hawajapata hicho wakitakacho kutoka kwake!” Kwakwa alimfahamisha yule mama, ambaye alibaki akilia tu huku akitikisa kichwa kwa kukata tamaa.
“Kwa hiyo unadhani utaweza kuwatambua tena hao jamaa wawili ukiwaona tena Zay?” Kwakwa aliuliza.
175 Hussein Issa Tuwa
10
MTAFITI
“Bila shaka!”
“Basi maisha yako yamo hatarini zaidi… mahabusu bado inakuhusu Zay… samahani sana, itabidi iwe hivyo.” Kwakwa alimwambia. Zay alipinga vikali, lakini na Pojo naye akamjia juu.
“Sikiliza bi mdogo. Hawa jamaa wamemuua shahidi pekee ambaye angeweza kumtaja na kumtambua mtu aliyeonekana akiwa na Mwantumu mara ya mwisho pale nyumbani kwake ile siku aliyotoweka. Yaani tukiwa tumebakiza dakika moja tu tumtie mkononi huyo mtu, wao wakawahi kumchukua kwa namna walivyomchukua…!” Alimwambia, na Zay akamakinika.
“Seriously?” Aliuliza.
“Kama hiyo haitoshi, wakati jamaa alipotaka kunitajia kwa simu huyo mtu aliyeonekana akiondoka na Mwantumu siku ile, akauawa hapo hapo na mimi nikisikia kupitia kwenye hiyo hiyo simu! Sasa tena hapo nakuachia mwenyewe uamue kama ni seriously au sivyo, lakini ukiniuliza mimi… ni very serious hii! Usiwe mjinga, Zay. Hawa jamaa watakuua ujue!” Pojo alimkoromea, na Zay akahamanika.
“Ah! Sasa jamani…” Alianza kulalama, lakini Kwakwa akaingilia kati.
“Tuna mambo mengi ya kufanya katika kumtafuta Mwantumu na kuwatia mbaroni hawa jamaa. Kuendelea kulijadili hili suala ni kupoteza muda wa muhimu. Zay na mama’ako hapa leo hamrudi makwenu. Mama hebu tuelezee na wewe mambo yaliyokukuta kule Liquid Diamond!”
Zay alishusha pumzi za kukata tamaa.
“Mimi nilienda hadi mapokezi na kumuuliza yule binti mahala walipompeleka mwanangu… binti akawa haelewi. Nikamjia juu. Nilikuwa na jazba kwa kweli. Ndio likatokea lile pande la baba lenye kichwa kidogo ka’a thumni…!” Mama Mwantumu alianza kujieleza, na pamoja na hali aliyokuwa nayo, Zay alijikuta akiachia kicheko kwa kauli ile, ingawa wale askari hawakuona cha kuwachekesha. Wao walikuwa makini kufuatilia maelezo ya yule mama.
“Huyo jamaa anaitwa Bilanga!” Kwakwa alisema, na Zay na Mama Mwantumu wakashangaa.
“Unamfahamu?”
“Nilikutana naye pale ofisini kwao siku Grayson alipouawa… anaonekana mnafiki sana yule…” Kwakwa alisema.
“Haswaa! Jamaa mnafiki kweli kweli yule!” Zay alithibitisha.
176
Mama Mwantumu akazidi kuwajuza kuwa Bilanga alikuja pale na kumuongelesha kwa ukarimu sana, naye akatulia. Jamaa akamkaribisha
ofisini kwake ambako baada ya mama Mwantumu kumwambia kuwa alikuwa ameenda kuuliza mahala mwanaye alipo, jamaa lilimwambia kuwa
Mwantumu alishaondoka pale ofisini tangu siku mbili nyuma baada ya kumaliza mafunzo yake kwa vitendo. Mama Mwantumu alipomwambia kuwa mwanaye hakurudi nyumbani tangu siku alipoonekana akiingia pale ofisini, jamaa akajitia kushangaa sana. Akamuonesha hadi barua ambayo alidai kuwa Mwantumu aliuandikia uongozi wa kampuni ile kuwashukuru kwa kumpokea na kumpa nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo kwenye ofisi zao. Na kuwaaga rasmi.
“Seriously?” Kwa mara nyingine Zay alimaka kwa kutoamini, na kabla yeyote hajajibu, akamgeukia Kwakwa.
“Uongo! Hiyo barua sio ya ukweli…!” Alisema.
“Of course itakuwa ya kughushi!” Pojo alidakia.
“Lakini ilikuwa ni saini ya Mwantumu kabisa kwenye ile barua!” Mama
Mwantumu alisema, kisha akaendelea, “ile habari ilinichanganya kidogo… lakini hapo tena nikaona yule jamaa amekuwa makini kwenye kuangalia kwenye runinga iliyokuwa upande wake mle ofisini, huku sura ikiwa imembadilika kabisa.
“Mara akanigeukia na kuniambia kuwa kama siamini yale aniambiayo, basi nimsubiri pale ofisini mara moja aende kuniitia mtu ambaye angekuja
kunihakikishia kila kitu na ambaye angeweza kuniambia mahala ambako Mwantumu anaweza kuwako.”
“Alikwambia hivyo?” Zay aliuliza kwa kutoamini.
“Ndio! Na akatoka kwenda kumfuata huyo mtu… lakini sasa nikashangaa
kuwa alinifungia kwa nje! Nikapatwa na wasiwasi... na nilipoenda kuchungulia kwenye ile runinga yake pale ofisini ndio nikakuona ukiwa pale mapokezi na yule dada pamoja na huyo jamaa. Sikuweza kusikia
mlichokuwa mkiongea lakini kila kitu kilichoendelea baina yenu nilikiona na nikajua mara moja kuwa nilitakiwa niondoke pale haraka sana. Na
nilipokuona ukitimua mabio na watu wengine walipoanza kukimbia hovyo kule nje huku vikengele vikirindima kutokea kila upande, nilijua hatari
imedhihiri. Nilijaribu kuuvunja ule mlango bila mafanikio. Niliogopa sana!
177
Tuwa
Hussein Issa
Ndipo mwenzake alipokuja kuufungua ule mlango kutokea nje nikampiga kumbo na kukimbia nje…!” Mama alimalizia maelezo yake na wale askari wakatazamana.
Kimya kikachukua nafasi kidogo.
“Hiyo barua iliyosemekana imeandikwa na Mwantumu… unayo?”
Kwakwa alimuuliza yule mama.
“Baba yangu wee, si niliiacha mle mle tena! Hali ilikuwa inatisha sana kwa kweli… nina wasiwasi sana na usalama wa mwanangu jamani!” Mama alimjibu.
“
Okay. Sasa sisi inabidi tuingie mtaani kuyafanyia kazi haya mambo. Ninyi mtabaki hapa mpaka hali itakapokuwa shwari. Twendeni niwapeleke mahala mtakapokuwa siku ya leo.” Kwakwa alisema huku akiwaongoza nje ya ofisi ile.
“Lakini mi’ nitahitajika kwenda kazini usiku huu afande… unadhani nikifukuzwa kazi itakuwaje?” Zay alihoji.
“Utapata nyingine Zay…we’ hutoki humu ndani leo!” Kwakwa alimwambia.
Walikabidhiwa kwa askari wa kike ambaye pamoja na akina Kwakwa aliwaongoza kuelekea sehemu iliyokuwa chini kabisa ya ardhi pale kituoni, na kuingizwa kwenye chumba kilichosheheni kila kitu, kikiwa na kiyoyozi kizuri sana.
“Mtakuwa hapa mpaka hapo tutakapoona kuwa mko salama kurudi uraiani!” Kwakwa alisema na Zay hakuamini.
“Ah, kumbe ni kuzuri hivi? Nilidhani mnatuweka jela kabisa!” Alisema, na Kwakwa akamcheka.
“Jela wanakaa kina Bilanga na watu wa jamii yao… ninyi ni mashahidi muhimu mnaohitaji ulinzi wa polisi kwa sasa… hapa kuna mahitaji yote muhimu, na Koplo hapa atawasaidia kwa lolote mtakalohitaji, ikiwemo chakula…” Kwakwa alimwambia.
Dakika tano baadaye yeye na Pojo wakaondoka.
“Hebu nenda ukafuatilie rekodi zetu kuona kama tuna kumbukumbu zozote za jinai zinazowahusisha huyu Bilanga na mwenzake Chabbi Cheka…” Kwakwa alimwambia Pojo, ambaye aliguna.
“Afande, mi kituo changu ni Chang’ombe bwana… na kule siwezi kuwa
178 MTAFITI
na kumbukumbu kama hizo!”
“Nitakukabidhi kwa afisa wa kitengo cha rekodi za jinai hapa central ili akupe msaada…”
“Oh? Okay. Na wewe…?” Pojo aliuliza.
“Narudi Liquid Diamond…”
Saa tatu baadaye Zay alikuwa amezongwa na mawazo mazito kuhusiana na kisa chote kile tangu kutoweka kwa rafiki yake Mwantumu hadi kule kukurupushana kwake na lile jibaba ambalo bado alikuwa anaamini kuwa ni yule mtu mpana ambaye Kwakwa aliwaambia kuwa anaitwa Bilanga, na kwenye kile kisanga cha kukata na shoka kilichowatokea yeye na mama Mwantumu ndani ya ofisi za Liquid Diamond Incorporated.
Muda wote aliokuwa akikabiliana na matatizo haya hakukumbuka hata kidogo kumfahamisha mpenziwe juu ya madhila yale na hili lilimtia simanzi sana, kwa kuwa Mchebbe alikuwa anapatana sana na Mwantumu.
Alimpigia simu na kumjuza juu ya yote yaliyotokea, kwa kadiri alivyoweza kuyakumbuka kwa wakati ule.
Mchebbe alihamanika vibaya sana.
Alimpiga maswali mengi sana juu ya hatua alizochukua na hali yake, akitilia mashaka sana usalama wake baada ya kusikia yale yaliyomkuta.
Pamoja na Zay kumhakikishia kuwa alikuwa salama mpaka wakati ule, bado jamaa hakuwa na amani kabisa.
“Nice Buttocks, kesho nachukua likizo ya dharura nakuja huko!” Mchebbe alisema kwa hitimisho.
“No Injinia wangu… usije bwana. Fanya kazi tu mpenzi uje kama itatokea dharura zaidi ya hii, kwa sasa hakuna lolote utakaloweza kufanya kubadilisha hali iliyopo!” Zay alimjibu, moyoni akifarijika sana kwa mpenziwe kutaka kuacha kila kitu ili aje kuwa naye katika kipindi kile kigumu.
“Hapana Zay, lazima niwe nawe huko kwenye masahibu kama hayo… kazi naifanya ili iweje? Ili niwe na maisha mazuri nawe! Sasa we’ ukiwa kwenye madhila kama hayo kazi itakuwa na faida gani?”
“Nakubali Mchebbe, lakini sio sasa! Sasa ukija na wewe utakuja kukaa humu ndani chini ya ulinzi pamoja nami? Sidhani kama Inspekta Kwakwa
179 Hussein Issa Tuwa
ataruhusu nitoke humu eti kwa kuwa wewe umekuja! Mi’ niliona kuwa natakiwa nikujulishe yaliyotokea huku, ila sitaki uje sasa hivi. Unaweza kuingia kwenye matatizo na wewe bure!”
Kimya kilichukua nafasi, na hatimaye Mchebbe akapoa.
“Dah, haya dear… inaleta maana. Ila elewa kuwa nitaacha kuja sasa hivi kutokana na hiyo hoja ya kuwa hata nikija sitaweza kuwa nawe kwa kuwa uko chini ya ulinzi, sio eti kwa kuwa nahofia kuingia kwenye hayo matatizo na mimi, sawa…? Kwa ajili yako nitaingia kwenye tatizo lolote bila hata ya kujishauri mara mbili, elewa hilo!” Alimjibu kwa upole lakini kwa msisitizo.
Zay akahisi kichwa chake kikielea hewani kama puto na moyo wake ukiyeyuka kwa faraja isiyo kifani. Chozi la mchanganyiko wa furaha na uchungu likamuanguka.
“That is so sweet honey… hujui nimefarijika kiasi gani tu kus’kia hivyo!”
“Huo ndio ukweli wa moyoni mwangu nice buttocks…” Alimjibu na kimya kikatawala kidogo, kisha akaguna, na kuuliza kwa hasira kidogo, “Hivi hao Liquid Diamond ni watu gani hasa, eenh? Ni kampuni gani hiyo yenye mambo kama hayo?”
“Hata sijui kwa kweli…” Zay alimjibu, na kuendelea, “… ni ajabu sana. Yaani kampuni kubwa kama ile, matangazo mengi tu magazetini na kwenye maruninga ikijigamba kusogeza maendeleo ya Tanzania pale yanapotakiwa yafikie… kumbe mambo yenyewe ndio haya?” Zay alijibu kwa fadhaa.
Na alibaki akiliwaza lile swali la Mchebbe kwa muda mrefu baada ya kuagana na mapenziwe.
Hivi hao Liquid Diamond ni watu gani haswa…?
Swali lile lilikuwa likijirudia tena na tena akilini mwake.
Usiku ule ule wakati Zay akilitafakari swali la mpenziwe Mchebbe kuhusu ile kampuni ya Liquid Diamond, Inspekta Kwakwa alikuwa akipata kinywaji chake akipendacho sana, Grand Malt, huku akitazama mechi ya mpira wa ligi ya Uingereza kwenye baa moja ya jirani na nyumbani kwake huku akiwa kwenye ari mbaya sana.
Ari mbaya aliyokuwa nayo ilitokana na kwamba siku ile ilikuwa imekwisha
180 MTAFITI
bila wao kupiga hatua yoyote kubwa kwenye kesi ya Mwantumu na ile ya Grayson Mochiwa. Aliporudi pale Liquid Diamond jioni ile alienda moja
kwa moja hadi ofisini kwa afisa utawala wa kampuni ile.
“Inspekta… una tabia ya kuibuka katika nyakati mbaya kabisa wewe. I am about to go home now. Unahitaji nini tena?” Afisa utawala wa kampuni ile, yule mwanadada apendaye kuongea kizungu kuliko Kiswahili, alimwambia mara alipoingia mle ofisini kwake, akimaanisha kuwa alikuwa anajiandaa kuondoka muda ule.
“Pole sana bibie… sitachukua muda wako mwingi…” Kwakwa alimwambia huku akiketi kwenye kiti kilichokuwa mbele ya meza ya yule afisa utawala kijana. Mwanadada alimuuliza atakacho kwa macho yake tu bila ya kutumia mdomo wake, na Kwakwa alimuelewa.
“Vitu viwili… barua ya aliyoandika Mwantumu ya kuacha kazi, na…”
“Kuacha kazi? Si nilikwambia kuwa hakuwa mwajiriwa bali ni mwanafunzi aliyekuwa anafanya mafunzo kwa vitendo hapa?”
“Okay, barua yake ya kumaliza mafunzo hapa…”
“Mwantumu hakumaliza mafunzo yake hapa… alikuwa amebakisha wiki mbili kabla hajatoweka!” Afisa tawala alimjibu, na Kwakwa akajitilia tiki jibu alilokuwa nalo kichwani. Ile barua aliyooneshwa Mama Mwantumu na Bilanga ilikuwa ni ya kughushi.
“Kwa hiyo hakukuwa na barua yoyote ya kuwaaga labda…?”
“Nope! Kingine afande…?”
“Okay. Kingine nilikuwa nahitaji kujua anuani ya nyumbani kwa hayati Grayson Mochiwa…”
Afisa utawala akamwelekeza mahala ambako hayati Grayson alikuwa amepangiwa nyumba na kampuni.
Kwakwa akainuka na kuaga, ila alipofika mlangoni akageuka.
“Unaonekana kuwa ni mwanadada mwerevu na makini sana wewe… hivi hukuona kampuni nyingine ya kufanyia kazi zaidi ya hii?” Alimuuliza, na yule dada akamtumbulia macho kwa mshangao.
Kwakwa akatoka bila ya kusubiri jibu.
Alipofika kule nyumbani kwa Mochiwa akakuta kundi la wanandugu waliokuwa wakijiandaa na harakati za maziko. Hakupata yeyote wa kumhoji kuhusu maisha ya Mochiwa kama alivyotaka. Hasa akizingatia ukweli aliougundua pale kuwa jamaa alikuwa akiishi peke yake baada ya kutengana na mkewe, ambaye hakuwa amebahatika kupata naye mtoto.
181 Hussein Issa Tuwa
Aliambiwa kuwa mkewe huyo aliyetengana naye alikuwa anatarajiwa
kuingia nchini usiku ule kutokea nje ya nchi.
Alipokuwa njiani kutoka huko aliwasiliana na Pojo kwa simu, ambaye alimfahamisha kwamba hakupata rekodi yoyote ya jinai kumhusu mtu aitwaye Bilanga, ila kuhusu Chabbi Cheka, kulikuwa kuna rekodi ya zamani sana ya kukamatwa kwa kosa la kuvuta bangi. Kosa hilo lilifanyika wakati Chabbi akiwa na umri wa miaka kumi na mitano.
Kwakwa alizidi kuharibikiwa ari.
Kibaya zaidi, mpaka muda ule aliokuwa pale baa, timu yake aliyokuwa akiishabikia sana kwenye ile ligi ya Uingereza ilikuwa imeshalambwa tatu bila. Na hata pale alipokuwa anapitisha wazo lile, timu yake ikakoswa koswa bao la nne.
Alisonya na kuinuka kuanza kurudi nyumbani kwake, na simu yake ikaita.
“Afande… kuna mtuhumiwa wako hapa kituoni!” Afisa wa zamu pale kituoni alimwambia na Kwakwa akastaajabu.
“Mtuhumiwa wangu?” Aliuliza huku akingalia saa yake. Saa nne na nusu usiku.
“Yeah… Chabbi Cheka!”
Mwanaharamu!
Akili ilimtembea haraka Kwakwa. Huyu fala kajisalimisha saa hizi?
“Muweke ndani mpaka kesho. Alale selo kwanza leo, mother fucker!”
Alisema na kukata simu. Aliendelea na safari ya kurudi nyumbani kwake akiwa amefura kwa hasira. Alikatisha kichochoro ambacho kingeweza kumfikisha kwake na kukutana na jamaa watatu waliokuwa wakija kutokea mbele yake huku wakiongea kwa kelele kuhusiana na ile mechi iliyokuwa ikiendelea runingani muda ule. Akapishana nao huku akiendelea na safari yake.
“Inspekta Kwakwa!” Ghafla mmoja wale watu aliita, na Kwakwa
akajitupa chini haraka huku akisikia sauti ya nondo ikipiga ukuta baada ya kumkosa.
Heh!
Alijipindua haraka pale chini na kuona mmoja wa wale watu watatu akimrukia pale chini huku akiwa ameinua mguu ili amkanyage. Aliudaka ule mguu na kuuvuta kwa nguvu, jamaa alijikuta akienda msamba huku
akipiga yowe. Hapo hapo yule mvamizi wa tatu alimuwahi pale chini
182 MTAFITI
na kumpiga teke la shingo, naye akatupwa pembeni huku mguno wa maumivu ukimtoka, na akatumia msukumo wa tele lile kujibiringisha pale chini na kusimama wima.
Yule jamaa aliyemkosa kwa nondo pale mwanzo alimgeukia na pigo jingine la ile nondo, na Kwakwa akaupiga teke ule mkono ulioshika nondo. Nondo ikamtoka jamaa. Hapo hapo jamaa akamtupia ngumi kwa mkono wake mwingine, na Kwakwa akaipangua ile ngumi kwa mkono wake kulia na kumshindilia bichwa la mdomo.
Jamaa akabweka kama mbwa koko huku akienda chini.
Kwakwa akamgeukia yule mvamizi wa tatu, na akakutana na ngumi nzito iliyompata chini kidogo ya jicho, naye akamaka kwa hasira. Jamaa akamtupia ngumi ya pili, lakini Kwakwa alijigeuza kistadi huku akiudaka ule mkono uliomtupia ngumi naye akibonyea chini kwa nguvu huku akipiga goti moja. Ilikuwa ni staili moja kali sana ya judo, na ile njemba ikatupwa hewani kama gunia na kujibabatiza ukutani huku ikipiga ukelele wa woga na maumivu.
Kwakwa alijiinua huku akimgeukia yule mjinga aliyemdaka mguu hapo mwanzo akiwa tayari amepandwa mori wa makabiliano na jamaa akatimua mbio.
Aliachia tusi zito huku akiwageukia wale wengine, na kuona nao walikuwa wameshaanza kutimua mbio zamani.
Aliachia tusi jingine zito kwa hasira.
Alijikung’uta vumbi huku akirudi nyumbani kwake, akiiona asubuhi haifiki upesi, kwani alijua kuwa Chabbi Cheka alikuwa anahusika na shambulizi lile.
Ambalo hakulijua ni kwamba ile asubuhi aliyoiwekea hamu sana, ingekuja na habari ambayo ingeibadili kabisa kesi ile…
Inspekta Kwakwa aliingia kwenye chumba cha mahojiano ambamo Chabbi Cheka alikuwa amepelekwa, akitokea mahabusu alipokuwa amewekwa usiku uliopita.
Alimkuta akiwa ameketishwa kwenye kiti cha mbao kwenye chumba kile hali amefungwa pingu mikononi, askari wawili wakiwa pamoja naye mle ndani.
Walitazamana.
183
Issa Tuwa
Hussein
Wakati anamtazama yule jamaa, Kwakwa alikuwa ameficha hisia zote kutoka usoni kwake. Si hasira, si furaha na wala si simanzi. Ilikuwa ni kama mtu anayetazama jiwe, na hili kidogo lilimvunja moyo Chabbi kwani alitaraji kuwa iwapo Kwakwa angekuwa hai asubuhi ile, basi angeingia mle ndani akiwa amefura kwa hasira.
Alimtazama yule afisa wa polisi na kuona kuwa alikuwa ana kinundu kidogo chini ya jicho lake na akajua kuwa jamaa zake walifanya kile alichowatuma usiku uliopita, ingawa sio kwa kiwango alichokitaka, kwani kama wangefanya kwa kiwango alichokitaka, Kwakwa asingekuwa pale mbele yake asubuhi ile. Badala yake angekuwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi au mochwari kabisa. Nondo ya kichwa ilitakiwa ihakikishe hilo.
“Vipi Inspekta… naona una kinundu chini ya jicho hapo… jana mkeo alikufumania nini?” Chabbi alimuuliza kwa kebehi huku akiwa amefanya tabasamu la upande mmoja, na hapo hapo mmoja wa wale askari waliokuwa naye mle ndani akampiga kofi kali la kisogo.
“Hebu kuwa na adabu wewe!” Alimkemea.
“Hapana Chabbi, niliteleza bafuni tu…” Kwakwa alimjibu na kuketi kwenye kiti kilichokuwa nyuma ya meza iliyokuwa katikati yao mle ndani.
“Oooh, pole sana afande.” Chabbi alijitia kumsikitikia, kisha akaendelea, “Haya nimekuja kuitikia wito… jana niliambiwa kuwa nahitajika hapa. Nashitakiwa kwa kosa gani?”
Kwakwa alibaki akimtazama kwa muda mrefu kwa yale macho yake yaliyokoza weusi huku akiuma uma magego yake, hasira iliyokuwa ikimfukuta ikijificha kabisa usoni kwake.
“Hujashitakiwa bado Chabbi… uko hapa kwa ajili ya mahojiano tu, kwa hiyo ningependa uwe na nidhamu ili tumalizane kwa amani.” Alimwambia na Chabbi akambetulia mabega tu.
Kwakwa akaamuru wale askari wamfungue zile pingu. Chabbi alifunguliwa na akabaki akiichuachua mikono yake kwenye yale maeneo ambayo pingu zilimbana.
Kwakwa akaanza kumhoji maswali ya kawaida yaliyohusu jina lake, kazi yake, kabila, anapoishi na umri wake. Baada ya hapo ndipo maswali muhimu yalipoanza.
“Unamfahamu Mwantumu, aliyekuwa akifanya mafunzo kwa vitendo kwenye kampuni unayofanyia kazi, ya Liquid Diamond Incorporated?”
“Nilikuwa nikimuona tu mle ofisini, lakini sikuwa nikimfahamu kiundani…”
“Sijauliza iwapo unamfahamu kiundani… nimeuliza iwapo
184
MTAFITI
unamfahamu!” Kwakwa alimkemea, na Chabbi akambetulia mabega tu.
“Unamfahamu… humfahamu?”
“Okay. Namfahamu!”
“Vipi kuhusu Grayson Mochiwa?” Kwakwa alimchomekea.
“Vipi kuhusu yeye?” Chabbi naye akamuuliza swali, na Kwakwa alichomoka kutoka nyuma ya ile meza na kumzaba makofi mawili makali sana kabla hata hajainua mikono yake kujikinga, na Chabbi akajikurupusha kutaka kuinuka, lakini wale askari wawili waliokuwa mle ndani wakamkamata mabega na kumketisha tena kitini kimabavu.
“Jibu maswali nikuulizayo wewe! Sio unajitia kuuliza maswali yako hapa. Unadhani tunacheza sisi?” Kwakwa alimkoromea akiwa amesharudi kitini kwake na kujiegemeza kwenye ile meza.
Chabbi alimkaziaa macho kwa hasira huku akijipapasa mashavu yake.
“Nakuuliza tena, vipi kuhusu Grayson Mochiwa… unamfahamu?”
“Ndiyo…”
“Kivipi?”
“Ah, ninalofahamu ni kwamba huyo jamaa amekufa. Na kabla ya kufa alikuwa ni mmoja wa wakurugenzi wa pale ofisini ninapofanyia kazi. Afande kwani nimekuja kuhojiwa kuhusiana na Grayson au Mwantumu hapa?”
“Utahojiwa yale ambayo tunaona unahitaji kutupa majibu kwayo!”
Kwakwa alimkoromea, na kubaki akimtazama kwa hasira.
“Okay!” Chabbi alikubali.
“Okay. Mara ya mwisho ulionana lini na Mwantumu?”
“Akh! Sasa tumesharudi kwa Mwantumu tena?” Chabbi alikuja juu kwa kukereka, na Kwakwa akamtumbulia macho ya hasira.
“Okay, Okay. Aaam… Sikumbuki kwa kweli, lakini nadhani ni siku moja au mbili kabla sijaugua, na baada ya hapo nikaona kwenye vyombo vya habari kuwa amepotea na anatafutwa. Ndipo nilipopiga simu ofisini kuuliza juu ya hilo, na kuthibitishiwa kuwa ni kweli huyo binti alipoondoka ofisini siku ya tukio hakurudi tena…!” Chabbi alijibu kirefu, na Kwakwa akamkazia macho ya kutoamini.
“Na wewe hujui alipo?” Alimuuliza.
“Khah! Sa’ mi’ n’tajuaje afande? Nakwambia siku hiyo mi’ sikuwa kazini nilikuwa mgonjwa!”
“Okay, ni lini mara ya mwisho kuonana na Grayson Mochiwa?”
Chabbi wala hakusita.
“Siku moja au mbili kabla ya kifo chake!”
185
Tuwa
Hussein Issa
Kwakwa alimtazama.
“Nipe mazingira ya kuonana naye siku hiyo moja au mbili kabla ya kifo chake…”
“Hakuna mazingira yoyote ya ajabu. Mi’ nilimuona tu akiingia ofisini, basi.”
“Unaweza kunielezea mazingira ya kifo cha Grayson?”
Chabbi akaeleza kwa kifupi tu jinsi alivyoelewa. Kuwa Grayson alivamia ukumbi wa mikutano akiwa na bastola, na kuanza kudai apewe hela kutokana na madeni yaliyomzonga, kisha watu wasiojulikana wakampiga risasi kutokea nje ya jengo alilokuwamo.
Mnhu! Eti watu wasiojulikana! Jamaa anajua kuongopa kweli kweli!
Kwakwa aliwaza.
“Naambiwa wewe ndiye mkuu wa usalama pale Liquid Diamond… ulichukua hatua gani baada ya kupata taarifa za kifo cha Grayson, na kutoweka kwa Mwantumu?”
“Ah, Inspekta…mi’ nilikuwa naumwa siku ya tukio, na nilipopata habari ya kifo cha Grayson, na kuambiwa kuwa tayari polisi wanalifanyia kazi, nikaushauri uongozi ushirikiane na chombo hiki cha dola kwa kila hali… sasa nashangaa tena nakuta naletewa hati ya kukamatwa kwa mahojiano!”
“Ni kwa kuwa tunaamini kuwa wewe unahusika na matukio haya mawili Chabbi! Unahusika na kifo cha Grayson na pia unahusika na kutoweka kwa Mwantumu. Una nini la kusema juu ya hilo?”
“Mna wazimu!” Chabbi alifoka, na Kwakwa akamrukia huku akiwa ameinua mkono juu kama anayetaka kumpiga. Chabbi aliruka wima akiwa ameinua mikono tayari kwa makabiliano.
Wale askari wawili waliwahi kumdaka na kumshika kutokea kila upande na kumdhibiti, wakamketisha pale kitini.
“Ala? Unataka kupigana na askari, Chabbi Cheka?” Kwakwa alimuuliza huku akitabasamu, kisha akaendelea, “Usikonde. Natumai nafasi hiyo itajitokeza tu kadiri tuendeleavyo… hapa sio mahala mwafaka!”
Chabbi alibaki akimtazama huku akitweta kwa hasira.
“Sihusiki na lolote katika hayo mimi!” Chabbi alimaka.
“Tutadhihirisha muda si mrefu juu ya hilo Chabbi Cheka. Na tutakapothibitisha hilo ndipo tutakapojua kwa yakini ni nani hasa mwenye wazimu kati yetu…!” Kwakwa alimwambia, na kuendelea, “… umesema ulikuwa unaumwa siku ya matukio ya kifo cha Grayson na kutoweka kwa Mwantumu… ulikuwa unaumwa nini?”
“Jipu!”
186 MTAFITI
“Unaweza kutuonesha cheti cha hospitali?”
“Sikwenda hospitali… nililikamua nyumbani!”
“Oh? Unajikamua jipu mwenyewe Chabbi?”
“Nilikamuliwa na mtu… Bilanga!”
“Oh! Of course… Bilanga! Nani mwingine, eenh?” Kwakwa alimwambia na Chabbi akamtupia jicho la hasira.
“Unaweza kunionesha mahala hilo jipu lilipo?” Alimuuliza.
“Hata kama liko sehemu nyeti, afande?” Chabbi alimuuliza.
“Tena ndio nataka haswa liwe sehemu nyeti… onesha jipu lilipo!”
Kwakwa alimjia juu.
Chabbi alitikisa kichwa kwa masikitiko.
“Liko hapa!”Alimjibu huku akijioneshea shingoni kwake, mahala karibu kabisa beg lake.
Kwakwa alimsogelea na kumshusha shati lake. Akaona ni kweli ile sehemu ilikuwa imebandikwa plasta iliyokuwa imelowa damu kidogo. Kwa kitendo cha ghafla aliikwanyua ile plasta kutoka pale begani na Chabbi alilia kwa uchungu kama mtoto.
“Aaaarggghh! Mshenzi weweeee!” Alibwata huku akijitutumua pale kitini lakini wale askari wengine wawili wakawa wamemshika.
Kwakwa alilitazama lile jeraha kwa muda huku uso wake ukiwa makini sana.
“Umesema hili ni jipu?” Alimuuliza, na Chabbi alizidi kulalama kwa maumivu, damu ikimvuja kutoka kwenye lile jeraha.
“Sasa unadhani ni nini hilo weweeee?” Aliuliza huku akigumia kwa uchungu.
“Na unasema Bilanga ndio kakukamua jipu hili?” Kwakwa aliuliza tena. Kabla Chabbi hajajibu, askari mwingine wa kike alikuja na kubisha hodi mle ndani.
“Tuko bize hapa, Koplo, alla!” Kwakwa alimkemea huku akimtazaa Chabbi kwa hasira.
“Ni muhimu afande… nakuomba tafadhali!” Yule Koplo alimwambia huku macho yakiwa yamemtoka pima, na Kwakwa akajua kulikuwa kuna jambo… tena zito.
“Tulia hapo hapo wewe!” Alimkemea Chabbi kwa hasira huku akimuoneshea kidole, kisha akatoka kumfuata yule Koplo.
“Ni nini Koplo…?” Alimuuliza yule askari wa kike wakiwa nje ya kile chumba cha mahojiano.
“Kumeingia taarifa hapa afande. Yule binti aliyepotea, Mwantumu…?”
187 Hussein Issa Tuwa
“Enhee?”
“Ameonekana!” Koplo alimwambia.
“Whaat? That’s good…! Ameonekana wap…”
“Amekutwa amekufa afande!”
“WHAT??” Kwakwa alibwata kwa mshangao zaidi, na kabla Koplo hajajibu akamtandika swali jingine.
“Ni wapi huko alipokutwa… na mmepataje habari hizi?” Alihoji, akili ikimzunguka.
“Mwili umekutwa maeneo ya Kongowe huko… askari wa kituo kidogo cha polisi cha kule ndio waliotupigia afande. Wanasema mwili umekutwa na mzee mmoja na kijana wake waliokuwa wanakata majani ya kupelekea ng’ombe wao!”
“Bloody shit! Sasa kuna askari wetu yeyote aliyeenda huko?”
“Hapana afande… ila nimeambiwa na hao askari wa Kongowe kuwa mpelelezi aliyekuwa anasimamia kesi hiyo, Sajenti Pojo wa kituo cha Chang’ombe yuko njiani kuelekea huko hivi tuongeavyo…”
“Holy Shit!” Kwakwa alisema na kujiegemeza ukutani huku akijisugua paji la uso kwa hamaniko kutokana na taarifa ile.
Ni taarifa iliyoigeuza kabisa ile kesi…
Inspekta Kwakwa alirudi kwenye kile chumba cha mahojiano na kusimama mbele ya kiti alichokalia Chabbi huku akimtazama kwa hasira isiyosemeka. Alitaka amrukie na ampe kichapo cha haja na kirefu, lakini alijua kuwa hilo lingemletea matatizo kisheria.
“Mrudishe mahabusu huyu!” Aliwaambia wale askari wawili waliokuwa wakimlinda Chabbi.
“Hey, sasa ndio unanifungulia mashtaka au vipi afande? Kama hunifungulii mashtaka basi huwezi kuendelea kuniweka zaidi hapa!” Chabbi alifoka, na Kwakwa alichukua stahamala yake yote kutomrukia na kumshindilia ngumi kadhaa.
“Nina saa arobaini na nane za kukuweka ndani kabla sijakufungulia mashtaka yoyote fala wewe! Hizo saa bado hazijaisha, kwa hiyo funga bakuli lako na kwenda ndani kule!” Kwakwa alimfokea kwa hasira, kisha akatoka haraka nje ya chumba kile wakati wale askari wawili wakimfunga pingu Chabbi na kumrudisha mahabusu.
Saa moja baadaye alifika eneo la tukio, na aliyoyakuta huko yalikuwa ni
188 MTAFITI
magumu sana kutazamika, hata kwa askari mzoefu kama yeye.
Wale askari wa kituo kidogo cha Kongowe walikuwa wamelizungushia utepe eneo husika, ambalo lilikuwa kwenye pori kubwa. Askari wa jeshi la polisi walikuwa wamelizingira eneo lote lile ilhali wananchi walikuwa wakitazama kwa udadisi mkubwa kutokea mbali. Sajenti Pojo alimfuata pale alipokuwa, wakiwa tayari wameshawasiliana kwa simu kabla hata Kwakwa hajafika pale.
“Pojo… najua ulishaniambia kwenye simu… lakini nahitaji kukusikia tena… umehakikisha kuwa ni Mwantumu kweli?” Kwakwa alimuuliza.
“Yes Sir. Ni yeye bwana… hamna shaka kabisa juu ya hilo!” Pojo alimthibitishia kwa mara nyingine, na Kwakwa akauma meno.
“This is very bad!” Alisema, akimaanisha kuwa ile hali ilikuwa ni mbaya sana.
“Ni hali mbaya kweli kweli afande…! Na inabadili kabisa mafikirio yetu ya mwanzo kuhusu kesi hii… tena vibaya sana!” Pojo alimwambia, na Kwakwa akakunja uso.
“What do you mean inabadili mafikirio yetu ya mwanzo?” Kwakwa aliuliza huku akitembeza macho eneo lile, kijua chepesi cha asubuhi kikidhibitiwa na Ray Bans alizobandika usoni ambazo zilimfanya avutie sana akiwa mwenye yale mavazi yake ya kiaskari.
Askari wa kitengo maalum cha kuchunguza maeneo ya maafa walikuwa wameshafika eneo lile, wakiwa na mbwa maalum waliopewa mafunzo ya kuchunguza maeneo ya maafa ya kijinai.
“Ni bora ujionee mwenyewe afande… labda mimi nimekuwa na uelewa tofauti…” Pojo alimwambia, na Kwakwa akaguna. Alilisogelea lile eneo lililozungushiwa ule utepe wa polisi uliozuia raia kutoenda zaidi ya pale ule uzio ulipowekwa. Katikati ya ule mraba wa utepe kulikuwa kuna mwili uliolala chini, kwenye majani, ukiwa umefunikwa kwa shuka kubwa jeupe. Aliuinua ule utepe na kupita chini yake. Aliuendea ule mwili uliolala pale chini na kupiga goti kando yake. Mara moja akajua kuwa yule marehemu aliyelala pale chini hakuwa amekufa siku ile, kwani ule mwili ulikuwa umeanza kutoa harufu.
Alibaki akiwa amepiga goti pale chini huku ameegemeza kidevu chake juu ya mkono wake aliokuwa ameulaza juu ya paja lake pale chini. Alitembeza macho kulizunguka eneo lile akiwa amepiga goti namna ile pale chini na kuona kuwa eneo lote lile lilikuwa ni mbuga tu isipokuwa sehemu moja umbali wa kama mita mia mbili hivi kutoka pale, ambako kulikuwa kuna kama kijimwinuko hivi, na juu ya kijimwinuko kile kulikuwa kuna kibanda
189 Hussein Issa Tuwa
cha makuti.
Alikitazama kwa muda kile kibanda, kisha akahamishia macho yake kwenye ule mwili uliofunikwa pale chini. Aliifunua ile shuka kumtazama yule albino aliyekuwa amelala chali pale chini. Alikumbuka jinsi alivyoshituka pale alipogundua kwa mara ya kwanza kuwa Mwantumu alikuwa albino, siku ile Zay alipowaonesha picha ya yule rafiki yake pale mgahawani.
Uso ukamkauka kwa simanzi iliyochanganyika na ghadhabu.
Naam, alikuwa ni Mwantumu kweli kama jinsi ambavyo alivyoziona picha zake hapo kabla, na alikuwa kama aliyelala usingizi wa kawaida tu pale chini.
Kitu pekee kilichomjulisha Inspekta Kwakwa kuwa ule usingizi wa Mwantumu haukuwa wa kawaida bali ni wa milele ni jinsi ule mwili ulivyokauka na kubaki ukiwa umelala kama gogo.
Mwantumu alikuwa hapumui.
Aliutazama ule mwili uliogandiwa damu sehemu mbali mbali, macho yake yakaangukia kwenye mkono wa kulia wa marehemu yule, na hapo moyo ukampiga mshindo. Alihisi damu ikimpanda kichwani pale unyama wa alichofanyiwa yule binti ulipodhihiri katika fahamu zake. Alifinya macho kwa kutoamini kabisa kile alichokuwa akikiona.
Lah! Ama kweli Pojo alikuwa sahihi…! Hii inabadili kabisa mafikirio yetu ya awali kuhusu kesi hii.
Alibaki akiwa anautazama ule mwili wa yule mwanadada mwenye athari ya ngozi huku akili ikimzunguka. Macho yake yakarudi tena kwenye mkono wa kulia wa marehemu yule.
Naam, hakika Mwantumu alikuwa albino, na kiganja cha mkono wake wa kulia kilikuwa kimekatwa.
190
MTAFITI
SAA MOJA BAADAYE asubuhi ile ile, uongozi wa kampuni ya Liquid Diamond Incorporated, pasina kujua kilichokuwa kimetokea kule Kongowe, ulitoa tamko kwa waandishi wa habari juu ya matukio yaliyoitokea kampuni yao, hususan kifo cha mkuu wake wa tafiti, hayati Grayson Mochiwa.
Ingawa Suleiman Mwangi ndiye angetakiwa aongee na waandishi wa habari kama afisa uhusiano na mwanasheria wa kampuni, ni Luis Kambesera ndiye aliongea mbele ya waandishi wa habari kutokana na uzito wa suala lile. Luis alianza kwa kueleza ni jinsi gani kampuni yao ilivyoshitushwa na kuguswa na kifo kibaya cha Grayson Mochiwa, na kuwa pamoja na kwamba wote walielewa kuwa kazi lazima ziendelee, na lazima kampuni ipate mtu mwingine wa kushika nafasi iliyoachwa wazi na hayati Grayson, ni ukweli usiopingika na yeyote ndani ya kampuni ile kuwa pengo la Grayson halitazibika asilani.
Alibainisha kuwa kama si kwa utaalamu na ufanisi wa hayati Grayson katika kuendesha utafiti mkubwa kabisa ambao serikali ya Tanzania iliituma kampuni yao iuendeshe, kampuni ile isingeweza kuwasilisha ripoti ya awali ya utafiti ule serikalini kwa wakati na kwa kiwango cha ubora wa juu kabisa.
Hakuishia hapo, aliendelea kwa kuyalaumu makampuni pinzani kwa kutumia tukio la kifo cha Grayson, na kupotea kwa mwanafunzi aliyejulikana kwa jina la Mwantumu, kuipaka matope kampuni yake.
“Liquid Diamond inawahakikishia watanzania na ulimwengu kwa ujumla kuwa haihusiki kwa namna yoyote ile na matukio haya mawili!” Luis alisema mbele ya waandishi wa habari, na kuendelea kulishambulia jeshi la polisi kwa kutolipa uzito unaostahili suala la uchunguzi wa kifo cha Grayson.
“Tumesikitishwa sana kuona kuwa badala ya kutuma wapelelezi
191 Hussein Issa Tuwa
11
waliobobea kwenye kazi, jeshi letu la polisi limekuwa likileta askari wasiokuwa na uzoefu hata kidogo na ambao hata sisi raia wa kawaida
tunaona kabisa kuwa hawajui wafanyalo!” Luis alisema kwa hamasa, na kuendelea, “Sasa sisi tunasema huo ni ushahidi wa polisi kuzembea na kutojali kabisa maisha ya raia wema kama Grayson Mochiwa. Tunatoa ombi kwa jeshi la polisi kuweka wapelelezi wazoefu katika kuchunguza kifo cha Grayson ili wahusika watiwe nguvuni mara moja! Hii italeta imani kwa jeshi letu la polisi na pia kuipatia familia ya hayati Grayson hitimisho na lipizo halali kwa kifo cha mpendwa wao!”
Kwa kumalizia maelezo yake, Luis alitangaza kuwa kampuni yao iko tayari kuisadia familia ya hayati Grayson kwa kila hali itakayoonekana inahitajika.
Baada ya hapo alijibu maswali machache kutoka kwa waandishi wa habari, kabla ya kuondoka na jopo lake la wakurugenzi aliokuwa nao pale Idara ya habari, Maelezo.
“Safi sana Luis… Safi sana!” Suleiman Mwangi alimpongeza baada ya mkutano ule, kama jinsi ambavyo wale wakurugenzi wengine wa kampuni ile walivyompongeza.
“Mnadhani hii itaturudisha kwenye muonekano mzuri mbele ya jamii sasa?” Luis aliwauliza wenzake.
“Yaani kwa sana tu. Unajua hapo sasa tumehamisha fikra za watu wote kutoka kwetu na kuzipeleka kwenye jeshi la polisi! Jeshi hili kila siku linaonekana halifanyi kazi zake kwa ufanisi, sasa na wewe leo kwenda kulisema wazi wazi tatizo hili hadharani kutazidi kuonesha ni jinsi gani linavyostahili kulaumiwa, na sio sisi…” Mike Mwangati alisema, na wale wenzake wakaafiki.
“Okay. Basi natumai sasa baada ya hii kauli yetu, yule Inspekta mwenye kiherehere atabadilishwa kutoka kwenye upelelezi wa kifo cha Grayson, shenz taipp!” Luis alisema kwa matumaini. Hakujua kuwa wakati ule tayari akina Kwakwa walikuwa wameshaugundua mwili wa hayati Mwantumu, albino.
Kule Kongowe, Inspekta Kwakwa aliufunika tena ule mwili na kuinuka kutoka pale alipokuwa amepiga goti. Akakutana na macho ya Sajenti Pojo yakimtazama kutokea nje ya ule utepe wa polisi uliolizingira lile eneo ambalo ule mwili ulikuwapo, akihisi unyevu gotini kwake. Alitazama
192 MTAFITI
sehemu ile na kugundua kuwa udongo wa lile eneo ulikuwa mnyevunyevu kiasi. Akarudi hadi pale alipokuwa amesimama Pojo.
“Hii inabadili kila kitu Pojo… nadhani muda si muda hutaendelea kuiongoza hii kesi.” Alimwambia na Pojo akaafiki kwa kichwa.
“Kuna yeyote aliyefuatilia kujua ni nani anaishi kwenye kile kibanda kule juu? Huenda akawa ameona kitu kuhusiana na tukio hili.” Kwakwa aliuliza na kusema huku akioneshea kwa kidole chake kule kwenye kile kibanda cha makuti kilichokuwa kwenye ule mwinuko.
“Yah, hilo ndio lilikuwa linafuata baada ya kuchunguza eneo hili.” Pojo alijibu, na Kwakwa akawageukia wale wataalamu wa kuchunguza maeneo ya maafa ya kijinai, au ‘Crime Scene Investigators’ kama wenyewe walivyopenda kujinadi.
“Oi, nataka nipate picha za alama zote za miguu na za matairi yoyote ya gari zitakazokuwa zimeachwa eneo hili… naona hii ardhi ni nyevunyevu kiasi… kwa hiyo kuna uwezekano kukawa kuna alama za viatu vya wahusika hapa!” Aliwaambia.
“Yes, sir… lakini, kwani wewe ndiye kiongozi wa upelelezi huu afande?” Yule kiongozi wao, ambaye alikuwa na cheo kidogo kuliko cha Kwakwa akamjibu na kumuuliza kwa heshima.
“Hapana, ila kesi yangu inahusiana sana na hii…” Alimjibu na jamaa akaafiki.
“Sasa nadhani baadhi ya vijana wako wangeongozana na hawa askari wa hapa kwenda kule kwenye kibanda kile pale na kufanya uchunguzi zaidi…” Pojo alimfuata kiongozi wa kile kikosi cha uchunguzi wa eneo la maafa na kumwambia.
“Ah, kwani nako ni eneo la maafa? Sisi tunachunguza eneo hili tu, wao wanaweza kuendelea na upelelezi wao huko.” Jamaa alitoa rai.
“Sawa. Ila nilikuwa namaanisha kuwa waende na mmoja wa hao mbwa wenu… si inabidi muwe nao wenyewe hao mbwa? Nadhani mbwa atasaidia… si umeona marehemu alivyo? Mkono wake…?” Pojo alifafanua.
Jamaa akamuelewa, na askari watatu wakaondoka kwenda kule kwenye
kile kibanda, mmoja akiwa anamwongoza mbwa ambaye alishanusanusa eneo lote lile lililouzunguka ule mwili pale chini. Wakati Pojo anawaelekeza
wale askari wengine kule kwenye kibanda, Kwakwa alitoa simu yake ya kiganjani, akaufunua upya ule mwili na kuupiga picha kadhaa kwa kutumia simu ile, kisha akaufunika tena.
“Tunahitaji picha zetu wenyewe pia. Hatujui ni lini tutaweza kuzipata
193 Hussein Issa Tuwa
picha walizopiga wale jamaa.” Kwakwa alimwambia Pojo huku wakiongozana kurudi kwenye gari alilofika nalo Kwakwa pale kwenye eneo la tukio.
“Au iwapo tutazipata kabisa!” Pojo alimjibu huku uso wake ukiwa umejaa tafakuri.
“Yah, hilo nalo pia…” Kwakwa aliafikiana naye. Pojo akaguna tu. Baada ya ukimya mfupi, Kwakwa akamuuliza, “Aaam, unaweza kusema nini kuhusu marehemu na eneo la tukio Sajenti?”
“Marehemu ameuawa sehemu nyingine afande, halafu akaja kutupwa hapa ili kupoteza ushahidi…” Pojo alijibu bila kusita.
“Swadakta!” Kwakwa alikubaliana naye, na kuendelea, “Nini kingine unachoweza kusema juu ya hili…?”
“Mnh, afande! Kwa hali tuliyomkuta nayo marehemu ni kwamba tuhuma zinawaondoka akina Chabbi afande… ndio kisa nikasema kuwa mafikirio yetu ya awali yote yanabadilikaa marehemu ni mlemavu wa ngozi… hii sasa inakuwa kesi ya mauaji yatokanayo na imani za kishirikina hii afande… mauaji ya maalbino.” Pojo alisema, na Kwakwa akatatizika sana na hili.
“Na hilo ndilo linaloniudhi Sajenti! Hawa jamaa wanajifanya wajanja sana hawa…” Alilalamika.
“Na ni wajanja kweli afande, sio wanajifanya… ni kweli wajanja! We’ unadhani hapa kuna cha kutafuta sababu ya mauaji tena wakati anaonekana kuwa ni albino ndiye aliyeuawa na amakatwa kiganja? Si kila mtu atajua ni moja kati ya wimbi lililoibuka nchini la kukata viungo vya maalbino?”
Pojo alimwambia kwa uchungu, na Kwakwa akaachia msonyo wa hasira.
“Na huwezi kusema kuwa Liquid Diamond inahitaji msaada wa kisangoma hata wafikie kumkata kiganja huyu marehemu. Hapa lawama inahamishiwa sehemu nyingine kabisa afande, bloody shit!” Pojo alizidi kunung’unika kwa hasira.
“Na hilo ndilo linalonikera Pojo… si unakumbuka maneno ya mwandishi Edgar Allan Poe?” Kwakwa alimwambia kwa hisia kali.
“
Yah… kwamba hakuna kinachoichukiza zaidi busara kuliko ujanja uliopitiliza?”
“Yah! Na wanazidi kunichukiza. Yaani ni lazima niwaumbue tu hawa…!”
Kwakwa aliazimia.
Pojo akaguna.
“Sawa kama unaamini hivyo afande. Ila kwa hali ilivyo mpaka sasa ni kwamba hii kesi sasa inahamishiwa kwenye kitengo cha mauaji na ukatili
194 MTAFITI
dhidi ya maalbino!” Alimwambia.
Ikawa zamu ya Kwakwa kuguna.
“Ni kweli usemayo Sajenti… ila nitarudi tena baadaye kwenye hoja hiyo. Kwa sasa kitu kikubwa kinachonijia akilini ni kwamba kuanzia muda mfupi tu ujao wewe utaondolewa kwenye hii kesi Sajenti.” Alimwambia, na Pojo akafyatua ulimi huku akitisa kichwa kwa masikitiko.
“Huo ukweli umeshanishukia akilini afande… najua kutokea sasa kesi hii itaendeshwa na kitengo maalum kilichoundwa kusimamia kesi za mauaji na ukatili dhidi ya maalbino… mbaya sana hii!” Alisema.
“Ambao ndio hao wanaingia…” Kwakwa alisema huku akilitazama gari jingine la polisi lililokuwa likielekea pale walipokuwa. Waliwatazama askari wengine wawili wakiteremka kutoka kwenye gari lile, mwanaume na mwanamke.
“Oh, Shit, afande… hivi hatuwezi kujenga hoja na mi’ nikaendelea kubaki kwenye hii kesi?” Pojo alihoji kwa hamaniko.
“Dah! Hilo litawezekana pale tu tutakapoweza kushawishi kuwa hii si kesi ya mauaji ya albino, Pojo…!”
“Na kutokea hapa nilipo afande Kwakwa... sioni ni jinsi gani tutaliwezaje hilo!”
Kwakwa akaguna na kupiga kimya kwa muda.
“Unajua Sajenti, hii hoja inayopikwa hapa na hawa jamaa kuwa huyu binti ameuawa kwa imani za kishirikina kwa kuwa ni albino haileti maana hata kidogo. Na ukishaondoa hoja zote zisizoleta maana au zisizoingia akilini, chochote kinachobakia, hata kiwe hakielekei kwa kiasi gani, ndicho ukweli.” Hatimaye Kwakwa alimwambia.
“Na hayo pia ni maneno ya mwandishi Edgar Allan Poe?” Pojo alimuuliza kwa kebehi kiasi. Kwakwa akafyatua cheko fupi ya simanzi.
“Hapana. Hayo yanatoka kwa mwandishi mwingine… Sir Arthur Conan Doyle.” Kwakwa alimjibu kwa utulivu. Pojo alisonya huku akiwatazama kwa hasira wale askari wawili waliokuwa wakielekea pale walipokuwa…
Kule polisi kituo cha central Zay alikuwa amezongwa na mawazo sana
kuhusu ile kampuni ya Liquid Diamond ambayo alikuwa ana uhakika kwa
asilimia mia moja kuwa ilikuwa inahusika na kupotea kwa rafikiye. Lile
swali alilouliza mpenzi wake Mchebbe kuhusu ile kampuni lilimtia chachu
kubwa ya kutaka kufahamu zaidi kuhusu kampuni ile.
195 Hussein Issa Tuwa
Asubuhi ile alipoamka, bila ya kujua kilichokuwa kikiendelea kule kwa
akina Kwakwa, aliichukua ile kompyuta mpakato ya Mwantumu na kwa
kutumia simu yake ya android kama modem, akajiunga kwenye mtandao wa intaneti, akaingia kwenye wavuti wa kampuni ile na kuanza kuperuzi kila kitu kuihusu.
Ndipo alipogundua kuwa Liquid Diamond Incorporated ilikuwa ni moja kati ya makampuni saba yaliyoshiriki zabuni ya serikali ya kufanya utafiti wa nishati mbadala nchini, nayo ikashinda zabuni ile.
Hiyo ilikuwa ni kama mwaka mmoja na nusu uliopita, na katika picha zilizokuwa kwenye wavuti wa kampuni ile, wakurugenzi kadhaa wa kampuni ile walioneshwa, pamoja na matukio mbalimbali muhimu katika
kampuni ile, likiwemo lile la kusainiwa mkataba mkubwa kabisa wa kufanya utafiti ule uliosemwa kuwa ni muhimu na wa kimapinduzi huko mkoani Mtwara.
Akajaribu kutafuta iwapo nakala ya ule mkataba itakuwa pale kwenye wavuti, lakini haukuwepo.
Alipitia picha kadhaa za watendaji na matukio kadhaa yaliyoihusisha kampuni ile, akiwatafuta akina Chabbi Cheka na Bilanga, lakini picha za wale watu aliokuwa akiwatafuta hazikuwepo, ingawa picha ya Grayson Mochiwa ilikuwepo.
Tukio lililoonekana kunadiwa sana na kampuni ile kwenye wavuti wao ule ni lile la kuwasilisha ripoti yao ya kwanza ya utafiti ule iliyopewa kandarasi ya kuufanya.
Ilinadiwa kuwa kampuni imewasilisha kwa wakati ripoti ya kwanza serikalini juu ya utafiti iliyotumwa kuufanya, na serikali iliwapongeza sana kwa hilo.
Picha ya mkurugenzi mtendaji wa kampuni ile aliyeitwa Luis Kambesera ilionekana mtandaoni pale akimkabidhi waziri wa madini na nishati ripoti ile huku wote wawili wakiichekea kamera, iliupamba ukurasa wa wavuti ile.
Zay akaguna, akimakinika na tarehe ya tukio lile.
“Mnh! Hii mbona inakuwa kama…?” Alijiuliza kwa mashaka huku akisogeza uso wake karibu zaidi na kioo cha ile kompyuta mpakato ya rafiki yake.
Ile tarehe ya siku tukio lile lilipotokea ilimgusa, kwani pale kwenye wavuti ilioneshwa kuwa tukio lile lilitokea wiki moja kabla ya kupotea kwa Mwantumu.
196
MTAFITI
Alikumbuka Mwantumu akimwambia kuwa kulikuwa kuna ripoti
muhimu sana kule ofisini ambayo yule msimamizi wake wa mafunzo kwa
vitendo, Grayson Mochiwa, alikuwa akiikamilisha na kwamba amekuwa akimpa kazi nyingi sana amsaidie, na kuwa siku nyingine wamekuwa
wakitoka mle ofisini usiku sana. Alikumbuka kabisa kuwa hiyo ilikuwa ni kama wiki tu kabla ya tukio la Mwantumu kutoweka. Na pia ilikuwa ni kama wiki tu kabla ya yule msimamizi wake wa field, Grayson Mochiwa kuuawa, ndani ya jengo la kampuni ile.
Na Grayson ndiye aliyekuwa mkuu wa utafiti kwenye kampuni ile...
Zay aliguna.
Kuna uhusiano wowote hapa?
Alisoma kwenye ule mtandao kuwa kutokana na kuwasilisha ripoti ile, kampuni ile ilipewa mkataba mwingine wa mwaka mmoja zaidi ili kuendeleza kazi ile kubwa na ya muhimu kwa maslahi ya taifa.
“Ni ripoti gani sasa hiyo? Ni ile niliyoiona kwenye makabrasha ya Mwammy, nini?” Alijiuliza.
Hakuwa na jibu.
“Dah! Sasa kama ni hivyo… si ni kwamba tayari hiyo ripoti ishajulikana na kila mtu sasa? Kwa nini iwe kama kwamba ni siri kubwa ambayo Mwammy hakutakiwa kuwa nayo?” Alijiuliza tena, na kwa mara nyingine hakukuwa na jibu.
Alizidi kupekua pale mtandoni kwa muda mrefu kutafuta hiyo ripoti, lakini si ile ripoti wala maelezo zaidi kuhusu yaliyomo kwenye ripoti ile, vilivyokuwepo pale mtandaoni.
Hili lilimchanganya.
“Lazima niipate hiyo ripoti iliyowafanya wapate mkataba mpya serikalini hawa… lazima niipate!” Aliazimia huku akichomoa simu yake kutoka kwenye ile kompyuta na kuanza kumpigia Inspekta Kwakwa. Kama kawaida, simu ya Kwakwa ilikuwa inaongea. Alizima kompyuta na kwenda kujisafi.
Kule Kongowe, wale askari wawili waliwafikia akina Kwakwa, na salamu za kiaskari zikatembea baina ya wale askari wawili wapya na Inspekta
Kwakwa, Pojo akiwa kimya kando yake.
197
Issa Tuwa
Hussein
“Inspekta Kelvin Waswa na Koplo mpelelezi Twilumba Ngasongwa, kutoka Anti-Albinism Unit… tunaamini hapa kuna mauaji yanayotuhusu?”
Yule Inspekta wa kile kitengo kipya katika jeshi la polisi cha kupeleleza kesi za mauaji na ukatili dhidi ya maalbino, au kama mwenyewe alivyokitambulisha, ‘Anti-Albinism Unit’, alijitambulisha yeye na yule mwenzake wa kike.
Walipeana mikono.
“Inspekta Kwakwa kutoka kituo kikuu cha polisi…” Kwakwa naye alijitambulisha, na kumuashiria Pojo kwa kichwa chake huku akimtambulisha, “Sajenti mpelelezi Pojo kutoka kituo cha polisi Chang’ombe!”
Ndani ya muda mfupi wale askari walitambulishana kila mmoja alikuwa pale kwa sababu gani, kisha Inspekta Kelvin akamgeukia Pojo.
“Tunaweza kwenda kuuona huo mwili…?” Alimuuliza, na Pojo akamuashiria kwa mkono wake kuwa waelekee tu kule kwenye mwili.
Wote wanne waliusogelea ule utepe uliuzunguka ule mwili, na wale askari wawili wa kitengo cha kuchunguza vifo vya maalbino wakaingia ndani ya uzio ule na kwenda kuutazama ule mwili. Pojo na Kwakwa waliwasubiri nje ya ule uzio, kwa lengo la kujaribu kupunguza kwa kadiri ilivyowezekana, idadi ya alama za viatu ndani ya lile eneo lililozungushiwa utepe.
Inspekta Kelvin na Koplo Twilumba waliutazama kwa makini sana ule mwili, huku Koplo Twilumba akiupiga picha ule mwili kutokea kwenye pembe tofauti, na akipiga picha maeneo kadhaa yaliyouzunguka mwili ule pale chini, ingawa tayari wale askari wa ukaguzi wa maeneo ya maafa walikwisha piga picha zao kabla ya wao kufika.
“Hawa jamaa hawawezi kuniachia niendelee na hii kesi, afande…!” Pojo alisema kwa simanzi wakati akiwatazama walivyokuwa wakijishughulisha kulikagua lile eneo na yule mhusika asiye hai wa eneo lile.
Kwakwa aliguna tu huku akiwatazama wale askari wa kile kitengo kipya kabisa kilichoanzishwa ndani ya jeshi la polisi kutokana na mfumuko wa mauaji ya maalbino nchini.
“Unajua, pamoja na kuwa Mwantumu alikuwa mlemavu wa ngozi, haikuniingia na bado hainiingii akilini kwamba kutoweka na hatimaye kuuawa kwake kunaweza kuhusiana na imani za kishirikina hususan kutokana na mazingira ya kutoweka kwake…mi’ siamini kabisa hili suala
198
MTAFITI
la mauaji ya albino kwenye suala la Mwantumu…!” Kwakwa alisema.
“Of course! Hasa ukizingatia ule ujumbe wa sauti aliomtumia Zay ile siku aliyotoweka! Kuna zaidi ya mauaji ya maalbino hapa afande! Waambie hawa jamaa watuachie tumalize hii kesi!” Pojo alimwambia kwa hamasa, na Kwakwa akaguna tena.
“Nawajua hawa Pojo… hawatakubali. Unajua jambo lolote lililojengwa katika misingi ya kisiasa kaka ni taabu sana kulibadili, hata ulielezee kwa mantiki gani! Hiki kitengo kimeundwa si kutokana na utashi wa jeshi letu kupambana na mauaji haya ya maalbino, bali ni kutokana na mashinikizo ya kisiasa na wanasiasa huko bungeni… matokeo yake hata hawa askari wa hicho kitengo nao wamekuwa na akili za kihivyo hivyo tu, pumbavu zao… watatukoroga tu hawa!” Kwakwa alisema kwa hasira.
Inspekta Kelvin na Koplo Twilumba walirudi pale walipokuwa.
“
Okay Inspekta… tumeona tukio. Ni albino yule…” Inspekta Kelvin alisema, na Pojo akatikisa kichwa kwa masikitiko bila ya kutia neno.
“
Yah, tulishaliona hilo kitambo tu… una rai gani sasa?” Kwakwa alimuuliza Inspekta mwenzake.
“Ah, hakuna mjadala… hii kesi sasa inahamia kwetu moja kwa moja. Itakuwa chini ya kitengo changu as of this moment. Kama kawaida, tutahitaji taarifa zote mlizonazo juu ya upelelezi wenu wa tukio hili nasi tutaendelea kutokea hapo mlipoishia.”
“Sajenti Pojo hapa ndio alikuwa anasimamia kesi ya kupotea kwa Mwantumu, ila ni kesi ambayo tumegundua kuwa ina uhusiano wa karibu sana na kesi ambayo mimi ninaisimamia. Ndio maana tuko pamoja hapa…” Kwakwa alimjibu.
Badala ya kufuatilia kile alichoambiwa na mwenzake, Kelvin akamgeukia Pojo.
“Okay Sajenti… naheshimu sana mchango wako mpaka sasa na najua kuwa ungependa kuendelea na kesi hii, lakini kama ujuavyo, suala likishahusisha kifo cha albino linakuwa chini ya kitengo chetu. Nitataraji ripoti kamili kutoka kwako mara moja, ili tulifanyie kazi haraka sana hili suala… si unajua jinsi masuala haya yanavyogusa hisia za wananchi, serikali na utawala kwa ujumla?” Kelvin alisema, na Kwakwa akazungusha macho kwa kukerwa na maelezo yale.
“Sawa tu afande… lakini tuna kila sababu za kuamini kuwa haya mauaji sio ya albino… yaani ni zaidi ya hicho mnachokiona hapo!” Pojo
199 Hussein Issa Tuwa
alimwambia kwa hamasa.
“Khah, sio mauaji ya albino wakati albino yuko pale chini amelala?”
Inspekta Kelvin alimjia juu, na Pojo akataka kumjibu, ila Kwakwa akamkatisha.
“Okay Inspekta. No problem. Ila tu nataka uelewe kuwa mimi nitakuwa naendelea na upelelezi wangu kuhusana na kesi nyingine ya mauaji ambayo ina uhusiano mkubwa na huyu marehemu. Nitataraji ushirikiano wako pindi nikihitaji habari zaidi juu ya marehemu huyu…” Alimwambia.
“Nami… na sisi… tutahitaji ushirikiano kama huo huo kutoka kwako Inspekta!” Inspekta Kelvin alimjibu, na Kwakwa akamgeukia Pojo.
“Let’s go!” Alimwambia na hapo redio ya Pojo maalum kwa mawasiliano ya kipolisi ikakoroma. Akabonyeza kisikilizio na kuuliza kulikoni.
“Afande! Kuna maendeleo mapya huku…!” Mmoja wa wale askari wa pale Kongowe aliyeenda kule kwenye kile kibanda kidogo kilichokuwa juu ya kilima alisema kwa wahka mkubwa.
“Ni nini tena kimejiri?” Pojo aliuliza huku akimtazama Kwakwa.
“Tumemkamata mtuhumiwa wa mauaji hayo afande! Tunaye hapa!”
Yule askari alivuma kwenye kile kifaa, na Pojo pamoja na wale wenzake waliokuwa wakisikia maongezi yale walimaka kwa mshangao mkubwa.
“WHAT?”
“Atiii?”
“Ndio afande!” Jamaa alimjibu kutokea kule alipokuwa, na bila kushauriana wale askari wanne walijitupa kwenye magari yao na kuyaondoa kwa kasi kuelekea kule kwenye kile kibanda.
Muuaji kapatikana mara hii?
Kwakwa alijiuliza huku akiendesha gari kwa kasi, akifuatiwa na gari la akina Inspekta Kelvin.
Simu ya Kwakwa ikaita muda huo, naye akaipokea huku akiendelea kuendesha gari.
“Inspekta Kwakwa hapa!” Alijinadi simuni.
“Nakuhitaji ofisini kwangu sasa hivi!” Mkuu wake wa kazi alimwambia, sauti yake ikionesha kuwa hakuwa mtu mwenye furaha.
“Aaaam, ndiyo afande… ila kwa sasa niko katikati ya kesi na niko mbali na ofisi… naomba nije mara tu nikimaliza…” Alimjibu.
“Nimesema nakuhitaji sasa hivi Kwakwa! Acha kila kitu uje hapa…
NOW!” Mkuu wake alifoka na kumkatia simu. Kwakwa aliitukana tusi
200 MTAFITI
la nguoni ile simu na kuitupia pembeni, Pojo akimtumbulia macho ya kuuliza, naye hakumpa maelezo yoyote. Alizidisha kasi kuelekea kule walipokuwa wameambiwa kuwa mtuhumiwa wa mauaji yale tata alikuwa amekamatwa, akili ikimzunguka…
Yale magari mawili yalisimama nje ya kile kibanda kwa misele mikali, wale askari wanne wakateremka na kubamiza milango bila kujali. Waliwasogelea wale askari watatu waliokuwa nje ya kile kibanda, ambao walikuwa wamemzingira mtu mmoja aliyekuwa amekaa chini, mbwa waliyekuwa naye akiunguruma vikali.
“Nini kinaendelea hapa askari?” Inspekta Kelvin alihoji, Kwakwa, Pojo na Twilumba wakiwa pamoja naye.
“Mtuhumiwa wetu huyu hapa afande!” Mmoja wa wale askari alimjibu na hapo hapo akamtandika teke yule mtu waliyekuwa wamemuweka chini ya ulinzi pale chini, na yule mtu ambaye kwa hakika alikuwa ni mzee, alilia kwa maumivu na woga mkubwa.
“Sielewi lolote juu ya hilo wanangu! Mnanikosea adabu bure tu mimi!” Yule mzee alilalama.
“Hebu kelele wewe! Nyie ndio mnaowakosesha amani bure tu ndugu zetu maalbino hapa!” Askari mwingine akamkaripia kwa hasira.
Akina Kwakwa walimkodolea macho kwa kutoamini yule mzee aliyekuwa akijizoazoa pale chini. Alikuwa amevaa kaptura kubwa ilhali akiwa kidari wazi. Shingoni alikuwa amevaa shanga nyingi pamoja na simbi zilizotungwa pamoja na kuwa kama mkufu wa aina fulani. Mikononi, sehemu baina ya mabega yake na viwiko, alikuwa amejifunga manyoya ya ndege wa aina fulani, ilhali usoni alikuwa amejipaka mchanganyiko wa rangi nyekundu na nyeupe.
“Mganga wa kienyeji?” Koplo Twilumba aliuliza kwa mshangao.
“Jamani mimi ni mganga kweli, lakini sijui lolote juu ya hilo mnalosema wajukuu zangu!” Babu alizidi kujitetea huku akibubujikwa machozi na akitetemeka kwa woga, damu ikimvuja mdomoni bila shaka kutokana na kichapo alichoambulia kutoka kwa wale askari kabla ya akina Kwakwa kuwasili.
“Mganga gani muuaji mkubwa wewe?” Mwingine katika wale askari
201 Hussein Issa Tuwa
alimkemea, na kama naye anayetaka kutilia mkazo hoja ile, yule mbwa wa polisi alimbwekea kwa kitisho yule mganga pale chini, ambaye alizidi kulia kwa woga, na wale askari nao wakaongeza kumpigia makelele kuwa anyamaze.
Ilikuwa ni tafrani mtindo mmoja.
“Hebu tuelewane basi kwanza jamani, ala!” Kwakwa aliwajia juu wale askari, na hapo hapo Kelvin akamgeukia yule askari aliyeonekana kuwa ndiye aliyempigia simu Sajenti Pojo.
“Er, ni nini kinachowafanya muamini kuwa huyu mzee anahusika na yule marehemu kule chini?” Alimuuliza.
“Kuna ushahidi wa wazi hapa afande… njooni mshuhudie!” Yule askari aliwaambia na kuwaongoza hadi nyuma ya kibanda kile, akiwaacha wale wenzake wawili wakimlinda yule mzee kule mbele ya kibanda. Kule nyuma, yule askari aliwapeleka hadi sehemu ambako kulikuwa kuna kiunga cha migomba na askari mwingine mwenye silaha akiwa amesimama kando ya kiunga kile.
“Tulipofika hapa na kujaribu kuulizia iwapo yule mzee aliona lolote kuhusiana na tukio la kule chini, mbwa wetu alianza kubweka kwa fujo huku akifukua fukua hapa…” Yule askari aliwaeleza, na akina Pojo wakaona kulikuwa kuna sehemu iliyokuwa imefukuliwa pale kwenye kile
kiunga cha migomba ilhali kopo chakavu likiwa kando ya shimo lile, “… na hili ndilo tulilokutana nalo!” Yule askari alimalizia huku akiwaoneshea ndani ya lile shimo.
Miguno ya mshangao iliwatoka Kwakwa na wenzake.
Ndani ya lile shimo dogo kulikuwa kuna kiganja cha mkono wa kulia wa yule albino aliyekutwa akiwa amekufa kiasi cha kama mita mia mbili kutoka pale kwenye kile kibanda.
Baada ya ule mkutano wao na waandishi wa habari, mwanasheria wa kampuni ya Liquid Diamond Incorporated, Suleiman Mwangi, aliingia kituo kikuu cha polisi jijini, na kupita moja kwa moja hadi kwa afisa wa zamu pale kituoni.
“Nimekuja kumtoa mfanyakazi wetu ambaye tunaamini kuwa yuko hapa kituoni, Chabbi Cheka.” Alimwambia yule afisa wa zamu baada ya
202 MTAFITI
kusalimiana. Yule afisa alimtazama kwa muda, kisha akachukua daftari kubwa na kulipekua kwa muda kabla ya kuona kile alichokuwa anakitafuta.
“Huyu bwana bado anahitajika kwa mahojiano. Mpelelezi wa kesi yake ni Inspekta Kwakwa, ambaye kwa sasa hayupo hapa kituoni.” Alimjibu, na Suleiman hakuridhishwa na jibu lile.
“Sasa mmemfungulia mashtaka yoyote ili twende mahakamani? Au mnamuweka tu ndani bila ya kumfungulia mashtaka? Unajua kuwa hilo ni kosa kisheria?” Suleiman alimjia juu, na yule afisa akamtazama kwa muda, kisha akarejea tena kutazama maelezo kwenye lile daftari lake, halafu akamtazama tena.
“Imeandikwa hapa kuwa huyu jamaa aliwekwa ndani jana saa nne usiku. Nikihesabu haraka haraka tu, naona kuwa tayari ameshakaa ndani kwa saa kumi na tatu… bado tuna muda mwingi tu wa kupumzika naye hapa kabla ya saa zetu arobaini na nane za kisheria hazijaisha mheshimiwa… hivyo jibu ni ndio, tutamfungulia mashtaka tu, ila hilo litaamuliwa na Inspekta Kwakwa…” Jamaa alimjibu kwa kirefu na Suleiman akafura.
“Okay, naweza kuonana naye?” Alimuuliza huku akimtazama kwa macho makavu.
“Dakika mbili tu!” Jamaa alimwambia.
“Nahitaji zaidi ya dakika mbili! Mimi ni mwanasheria bwana na ninajua haki za kuongea na mteja wangu!” Alimjia juu.
“Two minutes, mzee… na sekunde zimeshaanza kusogea hivyo!” Yule askari alimkoromea. Alikuwa ana hasira sana na ile kampuni yao kwa kuwapaka matope mbele ya waandishi wa habari asubuhi ile, kwani tayari habari zilishaenea miongoni mwa askari wote jijini.
“Vipi Chabbi… tunajitahidi kukutoa as soon as possible bwana, ila kuna mambo ya kisheria ambayo…” Suleiman alianza kumueleza Chabbi mara alipopewa fursa ya kuonana naye, lakini Chabbi akamkatisha.
“Fanya mnitoe humu bwana! Kuna mambo mengi ya kufanya huko nje ambayo ninyi hamuyawezi. Muda unakwenda!” Alimkoromea, na kuendelea, “Si unajua kuwa kama si mimi kujitolea kuwa hapa muda huu ni wewe na vibosile wenzako ndio mngekuwa mnasota humu ndani saa hizi?”
Suleiman alimeza mate na macho yakamtembea.
“Er, ndio nilikuwa nakueleza ya kuwa…”
“Sihitaji maelezo kaka! Nahitaji kutoka baada ya hizo saa arobaini na
203 Hussein Issa Tuwa
nane. Kwa sasa hapa ndipo haswa ninapohitaji kuwepo… ni sehemu ya mkakati wangu. Nileteeni msosi tu…” Chabbi alimwambia, na Suleiman akameza funda jingine kubwa la mate.
“Msosi uko nje kwenye gari… ngoja niwaambie wakuletee…” Alisema na kurudi pale kaunta.
“Afande, nahitaji kupiga simu kuagiza chakula cha mteja wangu…” Alisema, na yule afisa hakumjibu. Alipiga simu na kuagiza chakula kiletwe, na muda huo binti mmoja aliingia akiwa na viboksi maalum vya kubebea chakula vikiwa na lebo ya kampuni maarufu ya vyakula jijini.
Afisa aliwalazimisha waonje kile chakula pale pale, kisha akakichukua na kumpelekea Chabbi. Huku nyuma, akina Mwangi wakaondoka.
Kule Kongowe, akina Kwakwa walikuwa wameshazinduka kutoka kwenye ule mshituko walioupata baada ya kuoneshwa kiganja cha Mwantumu, na kumgeukia yule askari.
“Yaani hiki kiungo… kilikuwa kimefukiwa hapa, na mbwa ndio amenusa harufu yake na kukifukua?” Koplo Twilumba aliuliza.
“Kabisa! Tulipofukua zaidi ndio tukakikuta kikiwa kimefunikwa kwa hili kopo kwenye hilo shimo!” Yule askari aliwaambia.
Wote pale walichoka.
Koplo Twilumba alikipiga picha kile kiganja kikiwa mle mle ndani ya shimo, akalipiga picha na lile kopo lililokuwa limekifunika mle ndani ya shimo. Hata hivyo wale askari wa kile kitengo cha kuchunguza maeneo ya maafa ya kijinai nao walikuwa wameshapiga picha zao kabla wale askari wa kitengo cha Anti-Albinism hawajafika.
Yule mganga alipigwa pingu na kutupiwa ndani ya gari la akina Kelvin, kile kiganja kilichukuliwa na wale askari wa uchunguzi wa maeneo ya maafa ya kijinai na kuwekwa kwenye kifuko maalum cha kuhifadhia ushahidi. Lile kundi la askari likaondoka likiwa na yule mtuhumiwa mkuu wa mauaji yale, ambaye bado alikuwa akilalama kutofahamu lolote juu ya kiungo kile kilichokutwa nyuma ya kibanda chake, wala ule mwili uliokutwa bila uhai kule mbugani.
“This is too good to be true, Sajenti… hii ni kanjanja hii!” Kwakwa alimwambia
Pojo huku wakiingia garini na kuondoka eneo lile, akimaanisha kuwa kule
204 MTAFITI
kupatikana kwa kile kiganja pale kirahisi namna ile kulikuwa ni mbinu tu ya kuhamisha tuhuma kutoka upande moja na kuipeleka kwa yule mganga wa kienyeji.
Pojo alikuwa amepigwa na butwaa kiasi kwamba alikosa kabisa la kusema kwa muda ule. Kimya kifupi kilipita baina yao.
“Ina maana hawa jamaa wamemuua yule mtoto halafu wakamkata mkono makusudi ili ionekane kuwa ameuawa kutokana na imani za kichawi!” Hatimaye Pojo alisema kwa kutoamini. Kwakwa alibaki akiwa amekunja uso na ameuma meno kwa hasira.
“Halafu wakaenda kumtupa pale karibu na kibanda cha mganga wa kienyeji na kubambikizia kile kiungo pale kwake ili mganga ahukumiwe kwa matendo yao!” Pojo alizidi kusema kwa kutoamini. Bado Kwakwa alipiga kimya, akizidi kufurumia kwa hasira.
“Watu gani hawa lakini afande… eenh? Watu gani hawa?” Pojo alisema tena, na bado Kwakwa alikuwa amepiga kimya, ghadhabu zikimzuia hata kuongea.
Simu yake ikaanza kuita tena.
“Ni nani huyo anayepiga?” Kwakwa alimuuliza Pojo huku akiendelea kuendesha gari. Pojo aliichukua ile simu na kutazama.
“Mrakibu mwandamizi huyu afande!” Pojo alimjibu.
“Zima hiyo simu!” Kwakwa alimwambia, na Pojo akasita kidogo, kisha akatekeleza.
Kule chini walikuta mtu mwingine akiwa ameongezeka pale kwenye eneo la tukio. Alikuwa ni mchunguzi wa kitabibu wa polisi, na ule mwili wa marehemu Mwantumu ulikuwa anachukuliwa na kuingizwa kwenye gari maalumu la kubebea maiti, ukiwa chini ya uangalizi wa wale askari wa kitengo cha uchunguzi wa maeneo ya jinai, pamoja na yule mchunguzi wa kitabibu wa polisi. Kwakwa alimfahamu yule mchunguzi wa kitabibu, na mara moja akajua kuwa ndiye atakayeufanyia uchunguzi ule mwili.
Aliteremka garini na kumfuata.
Walisalimiana kidogo kisha akamwambia, “Nitahitaji kupata ripoti ya uchunguzi wako dokta Martha… ni muhimu sana kwa upelelezi wangu!”
Yule mchunguzi wa kitabibu wa polisi au ‘Police Medical Examiner’, alimtazama kwa muda kabla hajamjibu.
“Unajua ripoti yangu huwa inawasilishwa kwa kitengo cha uchunguzi wa eneo la jinai na kwa mpelelezi wa kesi husika, Kwakwa. Hiki ni kifo cha
205 Hussein Issa Tuwa
albino, kwa hiyo itabidi ripoti yangu iende kwenye kitengo cha uchunguzi wa mauaji ya albino Kwakwa… sasa wewe unahusikaje?” Dokta Martha, ambaye kiwadhifa wa kiaskari naye alikuwa ni Inspekta, alimjibu.
“Kesi yangu inahusika sana na huyu marehemu Martha, na nina hisia fulani ambayo nadhani itasaidia kwenye upelelezi wangu…” Kwakwa alimjibu.
“Hisia gani hiyo?” Martha alimuuliza, lakini hapo Inspekta Kelvin naye aliteremka kutoka kwenye gari lake na kuwafuata pale walipokuwa.
“Anyway… nitakutumia meseji basi Martha… okay?” Kwakwa alimwambia na kumkonyeza, kisha akarudi kwenye gari lake na kuondoka kwa kasi.
“Kwa hiyo mi’ tena ndio n’shapigwa kibuti afande?” Pojo alimuuliza kwa simanzi.
“Sio lazima iwe hivyo… wewe rudi kituoni kwako kwanza, ukawaandalie kina Kelvin hiyo ripoti… mambo mengine niachie mimi…” Kwakwa alimjibu kwa utulivu, akionekana mwenye mawazo sana.
Saa moja baadaye, akiwa amemteremsha Pojo kule polisi Chang’ombe, aliingia pale kituoni kwake. Badala ya kwenda kuonana na mkuu wake wa kazi, alipitiliza moja kwa moja hadi mahabusu ambako Chabbi alikuwa ameswekwa. Nje ya mahabusu ile, askari mmoja mwenye silaha alikuwa amepiga kambi akimlinda.
Chabbi alimtazama Kwakwa kutokea kule ndani kupitia kwenye nondo za mlango mzito wa chuma wa mahabusu ile, na Kwakwa akabaki akiwa amesimama pale nje huku akimtazama kwa hasira isiyosemeka.
Kwakwa akavua shati lake la polisi na kubaki na fulana mchinjo tu. Akavua mkanda wake uliokuwa na mkoba maalum wenye bastola nao akauweka chini nje ya mahabusu ile. Akavua na kofia yake na kuiweka juu ya ule mkanda wake, ikiifunika ile bastola yake pale chini.
Chabbi na yule Konstebo walibaki wakimtazama kwa butwaa.
“Konstebo… fungua selo, mtie pingu mikononi na umtoe kule nyuma ya jengo huyu fisi!” Kwakwa aliamuru huku akiendelea kumtazama Chabbi aliyekuwa akimtazama kutokea ndani ya ile mahabusu huku akijichokoa meno kwa kimbaka.
“Ennh? Unasema…?”
“Fungua selo umtoe kule nje huyu wewe!” Kwakwa alifoka, na haraka Konstebo akatii. Alimwongoza Chabbi aliyejawa udadisi hadi kwenye
206 MTAFITI
mlango mdogo nyuma kabisa ya jengo lile, Inspekta Kwakwa akifuata nyuma yao.
Ule mlango ulifungukia kwenye eneo jembamba la wazi, ambalo hatua kama hamsini mbele kulikuwa kuna ukuta wa wastani. Nyuma ya ukuta ule kulikuwa kuna mteremko mkali ulioishia kwenye kichaka cha minyaa, ambacho kilikuwa kinaishia kwenye eneo lenye harakati za eneo la bandarini.
Kwakwa alichukua furushi la funguo kutoka mkononi kwa yule Konstebo, na kuchagua mmoja ambao uliufungua ule mlango mdogo wa chuma. Alitoka nje ya jengo lile na kusimama pale kwenye ule uwazi mwembamba, Chabbi na yule Konstebo wakimtazama kwa viulizo vingi kutokea ndani ya jengo lile.
“Mfungue hizo pingu halafu aje huku nje!” Kwakwa aliamuru tena, safari hii Konstebo akagoma.
“Afande… unataka mahabusu atoroke? Akiuruka huo ukuta anaweza…
”Alianza kumbishia akiwa ametumbua macho, Chabbi Cheka sasa akionesha mshangao wa wazi kabisa.
“Fungua pingu hizo na aje huku nje huyo, alla!” Kwakwa aligomba. Konstebo alimeza funda la mate, kisha akatekeleza, akimsukumia Chabbi kule nje ambako Kwakwa alikuwapo.
“Funga mlango kwa huko ndani, halafu angushia huo ufunguo huku nje kupitia kwenye hizo nondo za huo mlango… kisha utoweke eneo hili!”
Kwakwa alizidi kutoa amri tata huku akimtazama Chabbi kwa makini.
“Unafanya nini wewe?” Chabbi aliuliza kwa mashaka, Kwakwa akampuuzia. Akamuona yule Konstebo akitekeleza lile agizo lake la kuwafungia kule nje na kuurushia ufunguo kule walipokuwa.
“Ondoka hapa Konstebo!” Alimwambia baada ya kuona pale ule ufunguo ulipoangukia.
Konstebo alimtazama kwa mashaka, na Kwakwa akamtutumulia jicho. Konstebo akaondoka haraka. Kwakwa akamgeukia Chabbi.
“Nimevua mamlaka yangu yote ya kiaskari kwa sasa Chabbi!”
Alimkoromea huku akiuokota ule ufunguo na kuuweka mfukoni mwake.
“Tuko wawili tu hapa nje fala wewe… na ule ukuta ni kitu pekee
kinachokuzuia kurudi uraiani kuendeleza mauaji yako.” Alimwambia huku akimsogelea taratibu.
“Unafanya nini Inspekta? Sikuelewi!” Chabbi alimuuliza.
207 Hussein Issa Tuwa
“Kwa sasa sio Inspekta… ni Haroub Kwakwa na Chabbi Cheka tu hapa, fala we… unajua natokea wapi sasa hivi mimi?” Kwakwa alimkoromea.
“We’ una wazimu? Unafanya nini lakini?” Chabbi alimuuliza.
“Natokea Kongowe…” Kwakwa alimwambia, na akaona kuwa Chabbi alitembeza macho kidogo na haraka akawahi kujikausha.
“Inahusu nini…?” Alijitia kuuliza kwa kiburi.
“Inahusu kukutia adabu mpuuzi mkubwa wewe. Na kama kweli we’ unajiweza basi hii ndio fursa yako ya kupambana nami… hutapata shutuma ya kumshambulia askari, wala mimi sitashutumiwa kuwa nimepiga mahabusu… ni mimi na wewe tu hapa muuaji mkubwa we! Ukinishinda nguvu na kutoroka, lawama inarudi kwangu.” Alimwambia.
Chabbi Cheka alikunja ngumi na akajiweka sawa kumkabili, uso wake ukionesha ghadhabu kubwa.
“Kwa nini unafanya hivi wewe? Ujue n’takubomoa kweli mimi!” Alimwambia huku akimlengeshea ngumi.
“Umemuua Mwantumu wewe! Kisha ukamkata mkono ili iaminike kuwa ni mauaji yanayotokana na imani za kishirikina!” Kwakwa alimtemea shutuma.
“Ah! Kumbe tayari mmeshajua kuwa ni mauaji ya maalbino yaliyozagaa nchi nzima? Sasa kwa nini bado mnaendelea kunishikilia mimi?” Chabbi alimjibu kwa kebehi.
“Wewe ubongo wako mtepweto? Mtu nimeshakwambia kuwa hapa uko huru kwenda kuendelea na mauaji yako huko uraiani, halafu unauliza nakushikilia kwa nini? Unatakiwa unidhibiti mimi ili uufikie ule ukuta tu, basi!” Kwakwa alimjibu akiwa amesimama vilevile alivyokuwa, mikono yake akiwa ameiachia kizembe kila upande wa mwili wake, akimtazama kwa hasira.
Chabbi alimfuata mbio huku akiunguruma kwa ghadhabu na kumtupia konde zito. Kwakwa hakukwepa wala kujikinga, na lile konde likatua sawia kwenye upande wa mdomo wake, likimchana mdomo na damu ikimchuruzika.
Hah!
Chabbi akaruka nyuma tayari kutupa shambulio jingine lakini akashangaa
alipoona kuwa Kwakwa hakuwa amechukua bidii yoyote kujikinga, na akashangaa zaidi pale alipoona yule afisa wa polisi mtata akiachia tabasamu baya usoni mwake.
208
MTAFITI
“Unampiga afisa wa polisi ukiwa chini ya ulinzi Chabbi?” Kwakwa alimuuliza huku akiwa amesimama palepale alipokuwa, na Chabbi akakunja uso kwa kutoelewa.
“Khah! Mtu umeniambia…” Alianza kumaka, lakini Kwakwa akamkatisha.
“Unaijua adhabu ya kosa hilo…?” Alizidi kumuuliza.
Chabbi alifunua kinywa kwa mshangao kutaka kumjia juu, na Kwakwa akamalizia.
“Kunyimwa dhamana aisee! Sasa sijui utatokaje kule mahabusu ulipojinadi kuwa utatoka!” Kwakwa alimtishia, na hapo Chabbi alimjia juu.
“Hah. We si ulisema…?” Alianza, na Kwakwa akamkatisha.
“Kwamba tukishambuliana nikiwa hivi nakuwa nimevua mamlaka yangu yote ya kiaskari?” Akamcheka kidogo, na kuendelea, “… hilo ni kweli, lakini nikirudi humo ndani na nikavaa tena mamlaka yangu nakuwa askari, na hili jeraha bado litakuwepo… nani atajua kuwa ulinishambulia kabla au baada ya kuwa kwenye mamlaka yangu, au nikiwa nje au ndani ya mahabusu?”
“Hujui usemalo wewe. Na mi’ hutaniona nikirudi humo ndani mbwa wewe!” Chabbi alimkemea, na Kwakwa akamcheka kwa kebehi iliyokera. Chabbi alikurupuka kwa hasira huku akiachia tusi zito na kumtupia konde jingine kali, na Kwakwa akayumba huku akiruka pembeni. Ngumi yake ikapiga hewa naye akapitiliza kama mkokoteni ulioachiwa userereke kutoka kilimani bila mwongozaji. Hapo hapo Kwakwa, ambaye sasa alikuwa nyuma yake baada ya kumkwepa namna ile, akamshindilia ngumi mbili nzito sana za mbavu, moja kila ubavu.
Chabbi akagumia kwa maumivu huku akitupa kiwiko kwa nyuma huku akigeuka. Pigo lake hilo pia likapiga hewa, na alipogeuka akakutana na pigo zito la ‘vibrating palm’, yaani kiganja chenye kutetema, litokanalo na mtindo wa makabiliano wa Tai Chi, ambalo Kwakwa alimpiga kwenye chembe kwa kitako cha kiganja chake. Chabbi alisukumwa nyuma kwa pigo lile na kusambaratika chini vibaya, akihisi maungo yake ya ndani
yakitetemeka na kichefuchefu kikimpanda.
Iilikuwa ni pigo hatari sana ambalo likipigwa kisawasawa lina uwezo wa kutikisa mapafu ndani ya mwili wa mshambuliwa na linaweza kusababisha
kifo hapo hapo. Kwakwa hakuweka nguvu zake zote kwenye pigo lile na
209
Issa Tuwa
Hussein
bado Chabbi alihisi kufa kufa.
Alijisukuma wima kwa shida na kujaribu kumtupia Kwakwa teke la mbavu, lakini Kwakwa akalipangua kirahisi lile teke na kumtandika mateke manne ya haraka haraka, mawili kila ubavu na Chabbi akajikuta anaishiwa pumzi na nguvu zikimyeyuka.
Kwakwa aliruka nyuma na kumtazama kwa dharau. Alikuwa anampiga makusudi maeneo ya mwili na sio usoni, kwani hakutaka kuacha ushahidi kuwa na yeye alimshambilia yule bazazi.
“Najua unahusika na kila lililomkuta Mwantumu wewe, na pia unahusika na kila lililomkuta Grayson Mochiwa…” Alimtemea maneno kwa hasira.
Chabbi alikuwa akitweta kwa taabu na hakuelewa kwa nini alikuwa anashindwa kuhimili mapigo yale. Hakujua kuwa Kwakwa alikuwa anampiga maeneo muhimu tu kwa lengo la kummaliza nguvu.
“Na siku nyingine ukitaka kutuma mabasha zako kuja kunifanyizia tafuta waliobobea kwenye fani, sio unanitumia vibaka wenye nondo miye, umesikia we’ fala?” Kwakwa alimwambia huku akimzunguka.
Chabbi alikurupuka na kumrukia kwa teke zito lililokuwa linamwelekea mgongoni, lakini Kwakwa alilitaraji hilo. Aliruka pembeni kwa wepesi wa ajabu, Chabbi akapitiliza na kujipamia mlangoni, na kutokea nyuma yake, Kwakwa akampitishia teke zito lililopita katikati ya miguu yake na kujikita kwenye korodani zake.
“Awwwwwwwrrggghhhh!” Chabbi alipiga yowe maumivu huku akijikunja kwa mbele, akijishika sehemu zake nyeti na kwenda chini bila kupenda. Kwakwa alimuacha akigaragara pale chini na kuufungua tena ule mlango mdogo. Akamshika ukosi wa shati lake na kumvutia kwa nguvu ndani ya lile jengo la polisi kutoka kule nje. Akaufunga ule mlango na kumuacha akitweta pale sakafuni.
“Hilo ni dokezo tu kutoka kwangu hanithi wewe!” Alimwambia huku akirudi kule mapokezi, yule Konstebo alifika pale akiwa ametumbua macho kwa kutoamini.
“Rudisha selo muuaji mkubwa huyo!” Kwakwa alimwamuru yule Konstebo huku akijifuta damu kwa shati lake la kiaskari.
“Ahhh! Nitakuua wewe! Nitakuua tu wewe nakwambia!” Chabbi alipayuka kwa ghadhabu huku akiwa amejikunja pale chini, mikono yake ikiwa imejishika sehemu yake nyeti.
“Oh yeah? Kama ulivyowaua Grayson, Mwantumu na Dimoso?”
210
MTAFITI
Kwakwa alimuuliza huku akivaa shati lake, na akimtazama kwa makini. Chabbi alibaki akimtumbulia macho kwa hasira.
“Hunijui mimi wewe… hunijui nakwambia! N’takufanya kitu mbaya sana mimi wewe!”Alimkoromea wakati yule Konstebo akimpiga pingu na kumburura kurudi kule mahabusu.
“Naona mibweko mingi, ming’ato haba mbwa wangu… fuck you!” Kwakwa alimwambia na akampa ishara ya kidole cha kati, kisha akaondoka huku akijifunga mkanda wake kiunoni.
Ukelele wa ghadhabu kutoka kwa Chabbi ulimfuata nyuma yake, naye akaachia tabasamu dogo la faraja.
“Hebu mpeleke upesi huko mahabusu huyo mwali wako Konstebo!”
Kwakwa alimkoromea yule Konstebo aliyekuwa akimlinda Chabbi pale nje ya selo hapo awali.
“Sasa nikamsikilize mrakibu anasemaje…” Alijiwazia, akiwa tayari ameshasikia habari za shutuma za Luis Kambesera akiwa garini kuelekea pale kituoni akitokea kule Kongowe, na kwa namna fulani alihisi alijua ni nini alikuwa anaitiwa. Akaona aanze na Chabbi kabisa, ili hata likitokea la kutokea huko kwa mrakibu yeye awe ameshakidhi haja zake kwa Chabbi.
Hakika alimchukia sana yule jamaa.
Alipofika kwa mrakibu mwandamizi, katibu muhtasi wa bosi wake yule alimkabidhi barua huku akimtazama kwa mshangao.
“Vipi unakuja na damu mwili mzima ofisini…?” Yule dada alimuuliza, na Kwakwa akampuuza.
“Inahusu nini hii barua?” Aliuliza, na yule katibu muhtasi alimtazama tu bila kumjibu.
Kwakwa aliketi kitini na kuisoma.
Ilikuwa inamfahamisha kuwa kuanzia wakati anaposoma barua ile, alikuwa ameondolewa kwenye upelelezi wa kesi ya mauaji yaliyotokea kule
Liquid Diamond Incorporated, na kwamba asubiri maelekezo mengine kutoka kwa mkuu wake wa kazi.
Barua ile ilikuwa imesainiwa na Mrakibu Mwandamizi.
“Naweza kuonana na mkuu?” Kwakwa aliuliza huku akili ikimzunguka na kichwa kikimuwanga.
“Alikuwa anakutafuta kwa muda mrefu… na ulipoona anakukera
211 Hussein Issa Tuwa
ukaamua kumzimia simu. Sasa na ye’ kafanya yake!” Yule dada alimjibu kwa msuto, na Kwakwa akamkunjia uso.
“Naweza kumuona au siwezi?” Alimuuliza, na yule dada akamjibu kuwa hakuachiwa maelekezo yoyote juu ya hilo, ila kama anahitaji kuonana na bosi wake aende tu.
Kwakwa alisonya na kuingia ofisini kwa mrakibu mwandamizi, aliyemkuta akiwa amejikunja mezani akisoma ripoti fulani iliyokuwa juu ya meza yake.
“Ulikuwa wapi wewe… na huo mdomo umekuwaje?” Alimuuliza huku akimtazama kwa makini. Kwakwa alisaluti kwa heshima, kisha akaketi kitini mbele ya meza ya mkuu wake wa kazi na kumuwekea ile barua juu ya meza.
“Mkuu sielewi sababu ya hii barua!”Alimwambia.
“Nimekuuliza swali… huo mdomo vipi?”
“Ah, nimepigwa afande… na yule mahabusu niliyemkamata kuhusiana na hii kesi ya Liquid Diamond…”
“
What? Kakupigaje na mtu yuko mahabusu? Au wewe ndio umeenda kumpiga huko naye akawa anajitetea?”
“Aw come on boss… mimi ni askari nijuaye taratibu za kazi afande! Kwa nini nimpige mahabusu? Yule jamaa ni hatari sana. Nilienda kujaribu kumhoji jambo dogo tu kabla sijaja kuonana nawe hapa, lakini alinishambulia kwa ngumi nzito sana. Ikabidi niahirishe mahojiano na nimrudishe mahabusu…” Kwakwa aliongopa.
Mrakibu akamtazama kwa mashaka.
“Hukumpiga?”
“Nenda kamtazame afande… huwezi kumkuta na kovu wala mchubuko! Ila kiukweli ilibidi nijizuie sana kumrudi afande…!” Kwakwa alizidi kumfitini Chabbi.
“Nakumbuka ulimkaba mkurugenzi mtendaji wa ile kampuni Kwakwa, sasa unaponiambia kuwa eti yule mahabusu kakupiga…”
“Mkuu, nilifuata maelekezo yako ndio maana sikumpiga. Nilijizuia sana kumrudi yule fala… sorry, yule mahabusu… kwa kuzingatia yale uliyoniasa mara ya mwisho. Lakini ukweli ni kwamba Liquid Diamond ni kampuni yenye mambo mengi sana ya nyuma ya pazia, na hawa ndio watu inaowaajiri!” Kwakwa alisema huku akijioneshea pale alipoumia mdomo, palipogandia damu.
Mrakibu alimtazama kwa muda mrefu kidogo, kisha akashusha pumzi ndefu
212 MTAFITI
“Okay, kuhusu hiyo barua… you are off the case, Kwakwa!” Alimwambia, akimaanisha kuwa ameondolewa kwenye ile kesi.
“Kwa nini imekuwa hivi afande?”Kwakwa alihoji.
“Bila shaka hujasikia jinsi tulivyopakwa matope na uongozi wa hiyo kampuni ya Liquid Diamond Kwakwa… lakini habari ni kwamba…”
“Nimesikia afande. Na ninaona kuwa hiyo ni mbinu yao tu ya kutaka kutupoteza malengo. Wao nia yao mimi nitolewe kwenye hii kesi kwa kuwa nimekuwa mwiba kwao, afande… naelekea kuufichua udhalimu wao!” Kwakwa alisema.
“Pamoja na yote hayo usemayo… waliyoyasema yamekuwa na madhara makubwa sana. Nimeitwa kwenda kutoa maelezo kwa IGP huko… nakupigia hupokei na hatimaye unanizimia simu…!”
“Ah! Kwa hiyo nd’o ukanitoa kwenye kesi afande… kwa kuwa sijapokea simu yako?”
“Sio kwa sababu hiyo wewe! IGP ameagiza uchunguzi ufanywe juu ya shutuma za Liquid Diamond… na sote twajua kuwa wewe ndiye afisa uliyekabidhiwa ile kesi, kwa hiyo madhara yote haya chanzo ni wewe. Lazima ukae benchi wakati uchunguzi unaendelea!” Mrakibu alimkoromea na Kwakwa akatikisa kichwa kwa masikitiko.
“Nini?” Mkuu wake wa kazi alihoji sababu ya kutikisa kwake kichwa namna ile.
“Yaani afande hiyo ni non-decision situation kabisa afande, na nasikitika kuwa wewe… jeshi letu la polisi kwa ujumla… limenasa kuanzia ndoano, chambo hadi mshipi kwenye mtego huo wa Liquid Diamond…!” Alisema kwa dharau kidogo, na Mrakibu akamshangaa.
“Non-Decision…?”
“Of course chief… si tunasoma kwenye saikolojia ya polisi siku zote bwana…? Mtu anahamisha mjadala kutoka kwenye suala la msingi na lenye madhara kwake, na kuupeleka kwenye suala lisilokuwa la msingi ambalo halina madhara kwake… si ndio Non-Decision situation hiyo iliyoelezwa na wataalam maarufu Baratz na Bachrach afande? Ni aibu kunasa kwenye mtego wa kijinga kama huo afande! Niache mie niimalize hii kesi…
nimeshapiga hatua kubwa mpaka sasa!” Kwakwa alimpasha bosi wake, na Mrakibu mwandamizi akabaki akimkodolea macho.
Walitazamana.
“Hebu nipe mustakabali mzima wa kesi mpaka hapo ulipofikia Kwakwa, ili nione iwapo kweli hiyo hoja yako ina msingi…” Alisema.
213 Hussein Issa Tuwa
Kwakwa akamueleza kila kitu.
Tangu pale alipoingia ndani ya zile ofisi za Liquid Diamond, hadi alipokutana na Pojo na namna walivyoanza kushirikiana, na jinsi hatimaye walipoenda kuukuta mwili wa Mwantumu katika hali waliyoukuta nao. Akahitimisha na namna wale askari wa kitengo cha Anti-Albinism walivyokwenda kuiteka ile kesi ya Mwantumu kutoka kwa Pojo.
Mkuu wake wa kazi alivua kofia na kujikuna kichwa huku akimtazama bila ya kumuona, akili yake ikiyanyambua yote aliyoelezwa na Kwakwa. Dakika zilisonga wakiwa kimya mle ndani. Kwakwa aliona bado yule mkuu wake alihitaji kushawishiwa zaidi.
“Na sasa mhusika wa kweli wa mauaji hayo afande yuko mle mahabusu hivi tuongeavyo! Ukimpa mtu mwingine hii kesi atapoteza muda tu mpaka aje ajiweke sawa, na hujui akina nani wengine watauwa katika muda huo… ile kampuni ni mbaya sana afande… kuna siri kubwa ndani yake. Mimi nitaifichua hiyo siri nikiendelea na hii kesi… na kulisafisha jeshi letu kutokana na zile shutuma zao uchwara!”Alishadidia.
Mrakibu Mwandamizi alimtazama kwa muda mrefu.
“Itabidi nikaongee tena na IGP…” Hatimaye alisema na Kwakwa akashuha pumzi za ahueni.
“Nashauri usiishie kuongea naye tu afande… nashauri umshawishi akubaliane nasi!” Kwakwa alisema, kiujanja akimjumuisha na yule mkuu wake wa kazi kwenye ule mpango wake.
“Okay. Nenda nyumbani sasa Kwakwa, na ukajitazame hapo ulipoumia. Mpaka nitakapokuja na majibu kutoka kwa IGP, bado uko nje ya kesi hii wewe!” Aliambiwa.
“Sawa afande… lakini nadhani nina wajibu wa kwenda kumuarifu mama wa marehemu na swahiba wake juu ya yale yaliyomkuta mpendwa wao kabla hawajayasikia kwenye vyombo vya habari… at least niachie nilifanye hilo kabla sijaenda nyumbani.” Alimwambia mkuu wake.
“No problem… fanya hivyo halafu nenda nyumbani mpaka nitakapokupa maelekezo mengine!”
“Yes Sir!”
Inspekta Kwakwa alitoka na kuelekea kule kwa akina Zay, huku akitamani asiwe yeye ndiye aliyepaswa kwenda kupasua habari ile mbaya kwa Zay na mama Mwantumu…
214 MTAFITI
“NOOOOOO!”
Pwaaa!
Zay alimzaba kofi kali sana yule Inspekta, kisha akabaki akimkodolea macho ya kutoamini, woga na mshangao pia, midomo ikimtetema na machozi yakijijenga machoni mwake huku sauti za nusu muungurumo, nusu kilio zikimtoka, akipeleka mikono yake iliyokuwa ikitetemeka mdomoni mwake, labda akijaribu bila mafanikio kuuziba mdomo ule usitoe zile sauti.
“Pole sana Zay…” Inspekta Kwakwa alisema kwa huzuni huku akiuhisi mchonyoto wa kofi alilozabwa na yule binti, bila ya kunyanyua mkono wake kujishika pale alipopigwa kofi lile, akili ikimzunguka.
“No, afande no! Hai… haiwezekani! Mwammy? Mwammy afe? Nooo Inspekta, noooo… ho ho ho ho hoooooooo Mwammy wangu miye jamaniiiiii… uuuuuuh….!” Zay alibwata kwa hamaniko na kuishia kuangua kilio kikubwa mle ndani huku miguu ikimwisha nguvu na akijibweteka chini bila angalizo. Inspekta Kwakwa akawahi kumdaka na kumketisha kitini taratibu, kisha akamwendea mama Mwantumu ambaye mara aliposikia tu ile habari ya kunyong’onyeza moyo aliachia sauti hafifu ya fadhaa iliyotoka sanjari na ule ukunga mkubwa kutoka kwa Zay, kisha mama yule akabweteka pale pale kwenye kochi alilokuwa amekalia, akapoteza fahamu.
Kwakwa alijikaza na kujaribu kumzindua yule mama bila mafanikio. Zay alibaki akilia kwa uchungu, akimrundikia Kwakwa kila aina ya lawama… na akijilaumu yeye mwenyewe kwa jinsi alivyokuwa akila raha na mpenzi wakati mwenzake alipokuwa akimtafuta akiwa kwenye matatizo.
“Usijilaumu namna hiyo Zay… hii ni ahadi ya Mungu tu imetimia… ila
215 Hussein Issa Tuwa
12
mwenzetu ahadi yake ndio iliandikwa iwe hivi…!” Kwakwa alimwambia huku akielekea mlangoni.
“Ahadi? Ahadi gani dhuluma hii? Mwammy kauawa na wale watu afande! Tena kusudi… kusudi Inspekta…! Halafu unamsingizia Mungu? Nooo… Mwammy wangu miye jamaaaa…” Zay alimpayukia kwa simanzi
huku akimnyooshea kidole kilichokuwa kikitetemeka na kumalizia kwa kilio kikubwa zaidi huku akijishika kichwa.
“Unakufuru bibie… don’t say that!” Kwakwa alimwambia kwa upole, donge kubwa likimkaba. Chuki isiyosemekana ikisheheni moyoni mwake dhidi ya Chabbi Cheka na wenzake.
Zay hakumsikiliza. Aliendelea kulia kwa uchungu na kwikwi.
Kwakwa alitoka nje na kwenda kutafuta msaada wa watu wa kumhudumia mama Mwantumu.
Alirudi dakika chache baadaye akiwa na askari wawili wa kike pamoja na daktari wa polisi wa kike pia, ambao kwa pamoja walimuinua yule mama na kumlaza kitandani, kisha wakaanza kumhudumia ili arejeshe fahamu.
Zay alikuwa akiendelea kulia kwa uchungu huku akijitupatupa huku na huko pale sakafuni, na Inspekta Kwakwa alibaki akimtazama kwa huzuni kubwa kabisa. Kwa namna fulani, kifo cha Mwantumu kilimfanya ajione kama aliyeshindwa kutimiza wajibu wake ipaswavyo, ingawa ndani kabisa ya fahamu zake alijua kuwa hakutakiwa kujilaumu namna ile.
Alibaki akiwa amesimama namna ile kwa muda mrefu, vile vilio vya Zay vikimsononesha vibaya sana, kisha alimwita mmoja wa wale askari wawili wa kike na kutoka naye taratibu nje ya kile chumba.
“Mimi naondoka… hakikisha hawa akina mama hawatoki humu ndani kabisa!” Alimwambia.
“Unaenda wapi sasa Inspekta? Si unajua hii ni kesi yako na hawa ni wateja wako? Wakishatulia watataka kuonana nawe… wasikie lolote kutoka kwako…” Yule askari alimwambia, na Kwakwa akauma meno.
“Najua… ila kuna mambo fulani yamejitokeza itabidi niyaweke sawa kwanza, na wakati sipo hapa sitaki utokee uzembe hawa watu wakaachiwa kuondoka hapa… wanaweza kwenda kufanya mambo ya kijinga na kujiweka kwenye hatari kubwa zaidi!” Kwakwa alimwambia.
Yule askari alielewa. Kwakwa akaenda kwa askari wa mapokezi.
“Nahitaji kutazama viatu vya mtuhumiwa wangu mle ndani… Chabbi Cheka. Si vipo hapa?” Alimuuliza.
216 MTAFITI
Jamaa akaafiki, na kuingia kwenye chumba ambamo viatu vya mahabusu wote huwa vinahifadhiwa, kwani wahalifu wakiingizwa mahabusu huwa wanavuliwa viatu na mikanda yao ya suruali.
Kwakwa alitazama soli za vile viatu kwa muda. Zilikuwa safi tu. Hazikuwa na matope ya aina yoyote, na wala hazikuwa ni soli zenye urembo wa aina yoyote kule chini, ambao ungeweza kubaki kwenye udongo na kuacha alama za moja kwa moja. Alimrudishia yule askari vile viatu na kutoka nje ya jengo lile kwa unyonge mkubwa.
Akiwa nje ya lile jengo la kile kituo kikuu cha polisi, alitoa simu yake na kumpigia dokta Martha, mchunguzi wa kitabibu wa polisi aliyekutana naye kule Kongowe asubuhi ile.
Dokta/Inspekta Martha Ndimbo, mchunguzi wa kitabibu wa polisi, alikuwa ameshaufikisha mwili wa marehemu Mwantumu kwenye maabara ya ofisi ya mchunguzi mkuu wa kitabibu wa polisi, ambayo ilikuwa
imehifadhiwa kwenye jengo la hospitali ya taifa ya Muhimbili. Alikuwa akijiandaa kuufanyia uchunguzi ule mwili ili kujua sababu ya kifo, muda wa kifo, mazingira ya kifo na vitu kama hivyo. Baadhi ya majibu ya uchunguzi ule aliotarajia kuufanya yangepatikana ndani ya muda mfupi tu siku ile ile, na baadhi ya vipimo vingehitaji angalau siku moja zaidi kabla majibu yake hayajawa dhahiri. Aliingia kwenye chumba chake cha kubadilishia nguo na kuvaa joho maalum la kitabibu linalohusiana na uchunguzi wa aina ile, ambalo lilikuwa la kitambaa cheupe cha nailoni gumu.
Akiwa kwenye harakati zile, ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yake, na alipoutazama akaona kuwa ulikuwa umetoka wa Inspekta Kwakwa.
Hapo hapo akampigia simu.
“Kwakwa… una sababu zozote za msingi za kunitaka niufanyie huu mwili uchunguzi huo?” Alimuuliza.
“Si nilikwambia kuwa ninahisi kuna ushahidi muhimu hapo? Basi hebu nichunguzie hilo dokta, kisha mwenyewe utajua kuwa ombi angu lina msingi au la…” Kwakwa alimjibu.
“Okay… lakini ujue kuwa ripoti yangu haitakuja kwako Kwakwa…”
Martha alimkumbusha.
217
Issa Tuwa
Hussein
“No worries. Naelewa hilo. Ila hilo utakalogundua, kama lipo… si utaniambia japo kwa mdomo?” Kwakwa alihoji, na Martha akasita kidogo.
“Oh come on Martha… askari mwenzako anakuomba msaada hapa, eenh?” Kwakwa alimhimiza.
“Okay… kwa mdomo tu, si vinginevyo!” Hatimaye Martha alikubali.
“That’s all I asked for Martha. Ni baada ya muda gani unadhani utakuwa umejua juu ya hilo?” Kwakwa alizidi kusaili.
“Hiyo inaweza kujulikana kesho…” Martha alimjibu.
“Okay, sio mbali…” Kwakwa alihitimisha, wakakata simu.
Kiasi cha kama saa moja tu baadaye, habari za kuokotwa kwa mwili wa Mwantumu ukiwa umeuawa, na kifo kile kuhusishwa moja kwa moja na imani za kishirikina zikawa zimezagaa kwenye takriban vyombo vyote vya habari nchini.
Kule Liquid Diamond Incorporated, Bilanga aliingia ofisini kwa Suleiman Mwangi na kuketi kitini mbele ya meza ya yule mwanasheria wa kampuni.
“Unasemaje Bilanga?” Mwangi alimuuliza kwa mashaka. Hakuwa akimpenda yule jamaa hata kidogo, kwa kuwa alikuwa anamwogopesha sana… kuliko hata Chabbi Cheka.
“Umesikia habari redioni na kwenye runinga muda huu?” Bilanga alimuuliza, na Mwangi akamtolea macho.
“Yaani umekuja hapa kuniuliza hilo Bilanga? Look, mi n’na kazi hapa na…”
“Yule demu Mwantumu… amekutwa ameuawa na mganga wa kienyeji huko… inaelekea alikuwa ametekwa kwa imani za kishirikina. Si unajua kuna watu wana imani kuwa maalbino ni bidhaa muhimu kwenye haya mambo ya kichawi chawi bwana?” Bilanga alimweleza na kumuuliza, huku akimtazama moja kwa moja machoni. Mwangi akatumbua macho.
“Anh?”
“Of course… fungua redio yoyote usikilize… au runiga. Na huyo mganga keshatiwa nguvuni!” Bilanga alizidi kumpasha habari.
“Wacha bwana!” Mwangi alisema kwa kutoamini, na Bilanga akainuka. Akaanza kutoka nje ya ofisi ile bila kumjibu lolote.
“Ah, basi ina maana polisi hawana tena sababu ya kuendelea kumshikilia
218
MTAFITI
Chabbi!” Mwangi aliropoka huku akiinuka kutoka kwenye kiti chake.
“Nd’o maana’ake!” Bilanga alimjibu bila ya kugeuka, akapotelea nje ya ofisi ile.
Huku nyuma, Suleiman Mwangi alikuwa anajishughulisha kuvaa koti lake, na alipomaliza, alinyakua mkoba wake wa kazi na kutoka haraka nje ya ofisi ile…
Kule Chang’ombe, Sajenti Pojo alimaliza kuandika ripoti yake kuhusu ile kesi ya kupotea kwa Mwantumu na kubaki akiwa amenuna kitini pale ofisini kwake. Alichukua simu yake na kuitafuta, na kuipata, namba ya simu ya Inspekta Kelvin wa kitengo cha maalbino. Akabaki akiitazama tu ile namba huku kidole chake cha gumba kikielea juu ya kibonyezeo cha kumuwezesha kuipiga ile namba. Alibaki namna ile kwa muda mrefu, akiona kuwa kumpigia yule Inspekta na kumfahamisha kuwa ripoti yake iko tayari ndio kujigongea muhuri wa kupokonywa ile kesi.
Simu yake ikaita mkononi mwake, naye akashituka huku akitazama kujua ni nani aliyekuwa akimpigia. Alikuwa Inspekta Kwakwa.
“Yes afande!” Alipokea, na Kwakwa akampa habari mbaya zaidi.
“AAAGH… Sasa watakutoaje kwenye kesi na wewe afande? Sa’ si nd’o hawa jamaa wanakuwa huru kufanya watakalo bila mtu yoyote kuwadhibiti afande?” Alimaka kwa hamaniko.
“Yea… mpaka sasa hali nd’o iko hivyo Sajenti. Sijui itaendelea kuwa hivi kwa muda gani zaidi, lakini hapo ndipo jeshi letu lilipotufikisha kaka… too bad!” Kwakwa alimwambia, na Pojo akaguna kwa fadhaa.
“Kwa hiyo nd’o tushakatwa miguu na mikono pia?”
“Kwa muda. Natumai Mrakibu alinielewa… bila shaka na IGP pia ataelewa na nitarudishwa kwenye kesi!” Kwakwa alimwambia, na upande wa pili Pojo aliachia pumzi ndefu za kukata tamaa.
“Kwa hiyo sasa uko home?” Pojo aliuliza.
“Yap… lakini sitakuwa hapa kwa muda mrefu sana…” Kwakwa alimjibu na kukata simu. Alimalizia kuvaa viatu vyake vya raba na kutoka nje ya nyumba yake, akiwa amevaa nguo za kiraia. Suruali ya jeans, na shati la mikono mifupi ambalo hakulichomekea. Aliingia kwenye gari lake aina ya
Suzuki Escudo yenye rangi nyekundu metallic, alilonunua kwa mkopo wa
219 Hussein Issa Tuwa
dhamana ya ajira yake, na kuingia barabarani, uelekeo ukiwa ni maeneo ya Sinza.
Akiwa ni mtaalamu wa masuala ya kompyuta ndani ya jeshi la polisi kwa muda mrefu kabla hajaingia kwenye kazi za upelelezi wa kesi, hakupata tabu kujiingiza kwenye mtandao wa rekodi za tume ya uchaguzi na kupekuwa habari za mpiga kura Chabbi Cheka zilizokuwa kwenye mfumo wa kumbukumbu za tume ile. Yote hayo aliyafanya akiwa pale pale nyumbani kwake kwa kutumia kompyuta yake yenye uwezo wa hali ya juu.
Haroub Kwakwa alikuwa ni mjuzi sana wa kupekua na kuvunja vikwazo vya kumbukumbu za kimtandao, au kwa lugha iliyozoeleka, alikuwa ni mdukuzi, au ‘hacker’, aliyebobea.
Kwa kuingia kwenye kazidata ile ya tume ya uchaguzi, aliweza kujua habari zote za Chabbi, hususan anuani ya mahala anapoishi.
Na ndiko alipokuwa anaelekea akiwa kwenye gari lake.
“Naombea tu asiwe amehama kwenye ile anuani aliyoiainisha kwenye rekodi za tume ya uchaguzi… muuaji mkubwa!” Alijisemea.
Aliupita mtaa ambao nyumba ya Chabbi ilitakiwa iwepo na kwenda kuegesha gari lake mwisho kabisa wa mtaa ule. Kisha alirudi kwa miguu, akitembea taratibu pale mtaani huku akitazama namba za nyumba, baadhi zikiwa na namba, baadhi zikiwa hazina namba.
Aliifikia nyumba aliyohisi kuwa ndiyo ya Chabbi.
Aligonga geti mara kadhaa bila kupata majibu, muda wote akiitazama loki ya geti lile, na akajua ni ufunguo gani hasa katika rundo la funguo zake malaya ambao ungelifungua geti lile. Alitoa funguo zake, akachagua mmoja na kulifungua.
Akajitoma ndani.
Ile nyumba ilikuwa kimya sana. Alitazama huku na huko ndani ya eneo la nyumba ile huku akivaa glovu za mpira alizotoa mfukoni mwake na kuizunguka kwa tahadhari kubwa ile nyumba.
Hakukuwa na dalili ya uhai hata kidogo.
Akaliendea gari aina ya VX jekundu lililokuwa limeegeshwa ndani ya wigo ule, akikumbuka kuwa Pojo aliambiwa na jirani wa Mwantumu kuwa siku ya tukio Mwantumu aliondoka na mtu wakiwa kwenye VX jekundu.
Hapa ndipo. Na Chabbi ndiye haswa mtuhumiwa wetu.
Alichungulia ndani ya lile gari, na alishangaa kuona kiti cha dereva kikiwa kimetapakaa damu.
220 MTAFITI
Mnh!
Alizidi kumakinika, akilikumbuka lile jeraha aliloliona baina ya shingo na bega la Chabbi, ambalo mwenyewe alidai kuwa lilikuwa jipu.
Jipu gani linaacha donda kama lile, shenz’ taip wewe?
Akapiga picha lile eneo lililotapakaa damu kwenye lile gari kwa kutumia kamera ya simu yake, kisha akaiendea ile nyumba.
Aliujaribu mlango wa mbele akakuta umefungwa. Alitumia moja ya funguo zake na kuufungua, kisha akazama ndani.
Kimya kila upande. Hakuna dalili ya uhai.
Sebuleni akaona picha kubwa ya ukutani ikimuonesha Chabbi akiwa kwenye suti na akicheka kwa furaha.
Akaioneshea kidole cha kati ile picha.
Akaanza kukagua vyumba vyote mle ndani hadi akakifikia chumba cha Chabbi. Aliliendea moja kwa moja kabati la nguo na kulifungua. Sehemu ya chini ya lile kabati ilikuwa imepangwa viatu vingi. Akainama na kuanza kuzikagua soli za vile viatu pea moja baada ya nyingine.
Akasikia kishindo hafifu nyuma yake.
Akainuka haraka huku akigeuka, mkono wake ukiiendea bastola aliyokuwa ameichomeka kiunoni kwake, kwa nyuma.
Alichelewa.
Alipigwa na kitu kizito kichwani, akapepesuka vibaya, akapigwa tena kisogoni kwa nguvu zaidi.
Akaenda chini kama mzigo, fahamu zikimhama…
Suleiman Mwangi alimtazama yule afisa wa zamu pale kituo cha polisi kwa jicho kali.
“Nimesema nahitaji mteja wangu aachiliwe mara moja! Amekamatwa akihusishwa na mtu aliyepotea, sasa huyo mtu kaonekana na mtuhumiwa anayehusika na kupotea na hatimaye kifo chake amepatikana… kuna sababu gani tena ya kuendelea kumshikilia mteja wangu? Nasema aachiwe mara moja!” Alisema kwa msisitizo.
Afisa wa zamu naye alimtazama kwa jicho kali.
“Na mimi nimekwambia kuwa hatujamaliza mahojiano naye huyo mteja wako! Tukimalizana naye, na tukajitosheleza kwa hahusiki kwa namna
221 Hussein Issa Tuwa
yoyote ile, basi anaachiwa…”
Mwangi alimtazama kwa jicho kali zaidi, kisha akatikisa kichwa kwa kuchanganyikiwa.
“Unajua kuwa mimi ni mwanasheria na ninazijua haki za kumuweka mtu mahabusu bila kumfungulia mashtaka?”
“Sasa kwa nini unatupotezea muda bure kama sheria unazijua?”
Sauti nyingine ikadakia kutokea nyuma yake, na Mwangi akageuka kwa mshituko. Sajenti Pojo alikuwa amesimama nyuma yake pale mapokezi, akiwa kwenye sare zake za kazi.
“Na… na we’ ndio nani?” Mwangi alimuuliza.
“Mwanasheria si unazijua sheria wewe? Saa za halali ambazo polisi tunaweza kukaa na mtuhumiwa mahabusu bila kumfungulia mashtaka si bado hazijaisha?” Pojo alimuuliza huku akimtazama kwa hasira.
“Excuse me… wewe ni nani tena?” Mwangi alimuuza tena huku akimtazama kwa makini.
“Umeshapata jibu mheshimiwa, naomba utuache tufanye kazi yetu… zikipita hizo saa arobaini na nane na mteja wako hajaachiwa ndio…” Yule askari wa zamu alianza kumjibu, lakini kabla hajamalizia jibu lake, Pojo akadakia na kulimazia alivyotaka yeye.
“Ujue kuwa tumeshamfungulia mashtaka… na ataendelea kuwa mahabusu mpaka hizo taratibu zenu za kisheria zitakapofuatwa!”
Mwangi alimtazama kwa hasira.
“Sasa mtamfungulia mashtaka gani wakati tayari mtuhumiwa keshakamatwa huko ninyi? Kuna mganga wa kienyeji ndio amehusika, vyombo vyote vya habari vimetangaza, sasa nashangaa…” Mwangi alikuja juu, na Pojo akamkatisha.
“Sasa huyo mganga alimfanyia hayo aliyomfanyia yule marehemu kwa shida zake yeye binafsi au za huyo mteja wake aliyekuwa akimfanyia hizo dawa za kienyeji?” Pojo alimuuliza, na Mwangi akatumbua macho.
“Yaani…?”
“Yaani ukienda kwa mganga akakwambia kalete jogoo mwekundu, anayeenda kumkamata huyo jogoo na kumpeleka kwa mganga ni mganga mwenyewe au wewe mteja unayetaka kutibiwa?” Pojo alimuuliza kwa ukali.
Mwangi alizidi kutumbua macho.
222 MTAFITI
“Kwa hiyo sasa ndio mnataka kusema mteja wangu ndiye aliyempeleka huyo marehemu kwa mgan… (akasonya), mna wazimu nyie! Mnataka kumbambikizia kesi mteja wangu, eeenh?” Alisema kwa jazba, na Pojo akashindwa kujizuia kucheka.
“Hebu sikia ni nani anayelalamika kubambikiziwa kesi sasa! Hebu nenda zako mwanasheria… njoo baada ya saa arobaini na nane kutimia usikie hatima!” Alimwambia.
“Huu ni unyanyasaji! Nahitaji kuonana na mkuu wa kituo… sasa hivi tena!” Alifoka.
“Hapana. Unahitaji kuonana na afisa anayesimamia kesi ya mteja wako… unahitaji kuonana na Inspekta Kwakwa, ambaye kwa sasa hayupo hapa na hatujui atarudi baada ya muda gani!” Yule afisa wa mapokezi alimjibu, na Pojo akajua kuwa hakuwa akifahamu yaliyomkuta Kwakwa kwenye kesi ile.
“Hamna mamlaka ya kunizuia kuonana na mkuu wa kituo… ni haki yangu. Nahitaji kuonana naye!” Suleiman Mwangi alimaka.
Afisa wa zamu akamwelekeza kule kwenye ofisi ya mkuu wa kituo, na wakati akienda huko, yule afisa wa zamu akamgeukia Pojo.
“Vipi kamanda… imekuwaje uko hapa saa hizi?” Alimuuliza, wote wakiwa na vyeo vinavyofanana.
“Ah, nimekuja kuonana na wale akina mama wawili, Bi. Zay na mama Mwantumu… nahitaji kuwapa pole kwa msiba wa mpendwa wao. Natumai unafahamu juu ya hilo?” Pojo alimwambia.
“Yaa, nafahamu. Ni hali ya kusikitisha sana…” Afisa wa zamu alisema, na Pojo akaishia kubana midomo yake tu kwa uzito wa jambo lile. Yule askari akamwelekeza sehemu husika, naye akaenda huko kwa moyo mzito kabisa. Dakika tano baadaye Suleiman Mwangi alirudi pale mapokezi na kupitiliza moja kwa moja nje ya kituo kile bila kuaga.
“Vipi mheshimiwa… umefanikiwa?” Yule afisa wa zamu alimuuliza, lakini Mwangi hakumjibu.
Afisa aliinua simu na kumpigia katibu muhtasi wa mkuu wa kituo.
“Imekuwaje na huyo mwanasheria wa ile kampuni ya Liquid Diamond… ameonana na mkuu?” Alimuuliza.
“Ah, hapana… mkuu hayupo ofisini kwa sasa. Ameenda kwenye kikao
223
Issa Tuwa
Hussein
na IGP kujadili juu ya tuhuma za hiyo hiyo kampuni yao dhidi ya jeshi la polisi!” Katibu alimjibu.
“Na hivyo ndivyo ulivyomwambia?”
“Sasa nimwambie nini kingine? Hiyo ndiyo hali halisi!” Katibu muhtasi alimjibu, na afisa wa zamu akaachia kicheko cha faraja.
Bilanga alikuwa kwenye wakati mgumu. Alikuwa akitafuta funguo za gari la Chabbi Cheka bila ya mafanikio. Yeye alikuwa ametumia usafiri wake wa pikipiki kufika pale kwa Chabbi, nao haukuwa mwafaka kwa lile alilokuwa anataka kulifanya.
Alirudi kule ndani na kumtazama Inspekta Kwakwa aliyejibweteka bila fahamu pale sakafuni, miguu yake akiwa ameitawanya huku na huko ilhali kichwa chake kikiwa kimelalia mbele, kidevu chake kikijiegesha kifuani kwake. Alikuwa amemuegemeza ukutani na amemfunga mikono kwa nyuma ya mgongo wake kwa kutumia kamba aliyoipata jikoni kwa Chabbi.
“Mshenzi ana bahati sana huyu (akamtukania mama yake)…!” Alijisemea peke yake.
Alienda tena jikoni halafu akarudi na bakuli la maji. Akammwagia kwa fujo yale maji, na Kwakwa akashituka huku akiachia sauti ya mhemko, akatikisa kichwa na kumtumbulia macho kwa mshangao kidogo.
“Amka fala wewe… ulikuwa unatafuta nini humu, eenh?” Bilanga alimkoromea.
Kwakwa akataka kujitutumua kutoka pale chini lakini akashindwa kufanya hivyo kutokana na vile alivyofungwa.
“Bilanga…?” Aliuliza, mara moja akili yake ikianza kumtembea, akitafuta namna ya kujinasua.
“Ulikuwa unafanya nini humu wewe nakuuliza?” Bilanga alimtupia tena lile swali huku akimtazama kwa hasira.
“Nifungue wewe… umemfunga afisa wa polisi kinyume na halali unajua…? Utaingia taabuni bila kupenda!” Kwakwa alimwambia, akijaribu kupoteza muda ili apate namna ya kujitanzua.
Bilanga akamtandika tele kali la uso naye akaenda chini bila hadhari, damu ikimtoka kinywani.
“Jibu swali wewe nakwambia!” Alimkemea kwa hasira.
224 MTAFITI
Kwakwa alibaki akiwa amelalia ubavu pale sakafuni, akisubiri kitakachofuata.
“Na kama ningekuwa na ufunguo wa hilo gari hapo nje ningeshakubeba na kukupeleka sehemu mwafaka kukushughulikia, sukununu we!” Bilanga alimkemea huku akimnyanyua kibabe kutoka pale chini na kujaribu kumketisha tena.
Kosa.
Ile anamvuta tu kutoka pale chini Kwakwa alirudi na bichwa la nguvu sana lililojikita usoni kwa Bilanga, paji lake la uso likikutana sawia na mwamba wa pua wa yule mtu mpana. Bilanga alibweka kwa mshituko na maumivu, na hapo hapo Kwakwa akajitupa mzima mzima kutoka pale chini na kubaki akiwa amepiga magoti pale sakafuni huku mikono yake bado ikiwa imefungiwa mgongoni.
Bilanga aliyezinduka kwa pigo lile alijiweka sawa na kumwendea mbio huku akiunguruma kwa ghadhabu.
Kwakwa akajisukuma wima kutoka pale alipokuwa amepiga magoti na hapo hapo akamrushia teke zito. Bilanga akawahi kulipangua lile teke na hapo hapo akamtupia ngumi kali huku akimtukana.
Kwakwa alibonyea na kujigeuza kiufundi, Bilanga akapiga hewa na kupitiliza mbele akiwa amepoteza uelekeo.
Kwakwa akageuka haraka na kumpiga teke kwa nguvu nyuma ya goti lake, na bila kupenda Bilanga akapiga goti, Kwakwa akiwa nyuma yake.
Hapo hapo Kwakwa akamtandika teke jingine zito la kisogo na Bilanga
akaenda chini kama gogo, yowe la ghadhabu likimtoka.
Huku nyuma Kwakwa akajibwaga chini haraka, akapitisha mikono yake
iliyofungwa kamba mgongoni kwake chini ya miguu yake kwa nyuma
huku mwenyewe akijikunja sana, na kuitolea kwa mbele ile mikono yake
ikiwa bado imefungwa vile vile. Wakati huo Bilanga naye akajibiringisha pale chini na kumgeukia kwa ghadhabu.
Akamkuta Kwakwa akiwa ameshasimama wima, miguu ameitanua
kimakabiliano, mikono yake iliyokuwa imefungwa mgongoni kwake sasa
ikiwa imefungwa pamoja kwa mbele na ameiinua pamoja mbele yake
kama kwamba mikono ile ilikuwa ni rungu la kupigania.
Bilanga akasita.
“Mmemuua yule mtoto nyie!” Kwakwa alimkemea, na Bilanga akaachia
ukelele wa ghadhabu huku akimrukia kwa teke zito. Kwakwa alijiyumbisha
225
Hussein Issa Tuwa
pembeni, lakini kidogo ile mikono iliyofungwa pamoja ikampoteza
mahesabu na soli ya Bilanga ikajikita sawia kifuani kwake na kumtupa
nyuma hadi ukutani, upepo ukimtoka.
Hapo hapo Bilanga akamfuatilizia na ngumi nzito, lakini Kwakwa akajipindua pembeni, na ile ngumi ikajikita ukutani kwa kishindo, Bilanga
akiachia yowe la uchungu. Hapo hapo Kwakwa akamshindilia goti la kwenye korodani, na Bilanga akalia kwa uchungu zaidi huku akijipinda, akimuachia Kwakwa nafasi aliyokuwa anaitamani muda wote pale kichwa cha yule mtu mrefu kilipomuinamia usawa mwafaka.
Akamshushia pigo zito kwa mikono yake yote miwili kisogoni na Bilanga akaenda chini, akiangukia goti moja. Kwakwa akarudi nyuma hatua moja na kumfyatua teke kali sana la uso. Bilanga akaenda chali mzima mzima, akigaragara kama joka lililokatwa kichwa, damu ikimtoka mdomoni na puani.
Kwakwa alianza kuzitafuna zile kamba haraka haraka ili aikomboe mikono yake, lakini hapo Bilanga alikurupuka kutoka pale chini huku akiinyakua stuli ndogo iliyokuwa mle chumbani na kumtupia. Kwakwa
akajirusha pembeni kuikwepa ile stuli huku akimuona yule jamaa akitoka mbio kuuwahi mlango wa kutokea nje ya chumba kile, naye akamfuata mbio nje ya chumba kile, bado akiwa amefungwa ile mikono. Aliusikia mlango wa mbele wa ile nyumba ukibamizwa. Akawahi pale mlangoni, lakini akasikia na geti nalo likibamizwa huko nje. Akatoka kasi nje ya nyumba ile, na akasikia mvumo wa pikipiki kutokea nje ya geti lile, na akatoka nje kwa pupa.
Akafanikiwa kumuona Bilanga akitokomea kwa kasi akiwa kwenye pikipiki kubwa, vumbi likielea hewani nyuma yake.
Lah!
Alimtazama yule jamaa akitokomea huku akitweta kwa hasira na pia kwa mchemko wa makabiliano.
“Tutakutana tena tu, Bilanga… hilo nakuahidi, mwanaharamu mkubwa!”
Alisema kwa hasira, na kurudi tena ndani ya ile nyumba. Alijifungua zile kamba na kujishika kisogoni ambapo Bilanga alimpiga kwa kitu kizito.
Palikuwa pana nundu kubwa.
“Shit!”
Alirudia kutazama vile viatu vya Chabbi Cheka pale kabatini, na akaibuka na pea moja ya viatu vya buti ambavyo alivitilia mashaka. Akaenda jikoni
226
MTAFITI
na kupata mfuko wa plastiki na kuviweka humo ndani, kisha akauweka ule mfuko wenye vile viatu mle mle kabatini.
Alitoa simu yake na kumpigia Pojo.
“Sajenti… nataka uchukue kibali cha kusachi nyumba na uje na askari hapa Sinza… kuna nyumba nataka uipekue hususan kwenye kabati la nguo ambapo utakuta viatu vikiwa ndani ya mfuko wa nailoni… na pia ndani ya wigo wa nyumba hii kuna gari ambalo nataka mliweke chini ya ulinzi kwa uchunguzi zaidi!” Alimwambia simuni.
“Sinza sehemu gani afande?” Pojo alimuuliza huku akiwatazama Zay na Mama Mwantumu aliokuwa nao kule mafichoni muda ule. Kwakwa akamwelekeza.
“Okay, kwa hiyo tutakutana hapo?” Pojo alimuuliza baada ya kupokea maelekezo.
“Ah, hapana… si unajua mimi sasa hivi sitakiwi kujihusisha na hii kesi? Ndio maana nataka wewe ndio uje uvichukue hivi viatu kama ushahidi, lakini uwe una kibali halali vinginevyo mawakili wa Liquid Diamond wataupinga ushahidi wote tutakaoupata humu ndani.” Kwakwa alimfahamisha.
“Okay… nimekusoma…” Pojo alimjibu, kisha akawageukia wale wanawake wawili waliojaa simanzi isiyosemeka.
“Samahani jamani… sisi bado tunalifanyia kazi hili suala… kuna jambo nimetakiwa kwenda kulifanya hivi sasa. Naomba niwaage!” Aliwaambia.
Ni Zay tu ndiye aliyemjibu kwa kumtikisia kichwa. Mama Mwantumu hakuwa katika hali ya kuongea kabisa. Alikuwa akibubujikwa na machozi mfululizo.
Ilimchukua Pojo kiasi cha saa nzima kabla hajapata kibali cha kuipekua
nyumba ya Chabbi Cheka. Hii ilitokana na kwamba yeye kama yeye
hakuwa na kesi yoyote ambayo ingehalalisha kwenda kuipekua nyumba
ile, na hata ile kesi yake iliyohamishiwa kwa Inspekta Kelvin na Koplo
Twilumba wa kitengo cha ‘Anti-Albinism’, haikuwa ikihusiana kwa namna
yoyote iliyokuwa wazi na nyumba ya Chabbi Cheka, ikizingatiwa kuwa
mtuhumiwa wa mauaji ya Mwantumu tayari alikwisha patikana. Na pia
hakuweza kusema kuwa alitumwa na Inspekta Kwakwa kwenda kufanya
upekuzi ule, kwani muda ule Kwakwa alikuwa ameshatolewa kwenye
upelelezi wa kesi ile na hivyo kama angejulikana kuwa alimtuma Pojo
kumfanyia kazi ile basi ingekuwa ameenda kinyume na amri halali ya
227 Hussein Issa Tuwa
wakuu wake wa kazi.
Hatimaye Pojo alipewa kibali kile kwa kigezo kuwa alikuwa anamhisi
mhusika kutokana na kifo cha dereva wa bajaji kule njia ya Chanika, kwani mashahidi kadhaa walikuwa wameelezea kuwa mtu aliyeonekana na marehemu mara ya mwisho alishabihiana na Chabbi.
Huo ulikuwa ni uongo, lakini hakuona namna nyingine ya kufanikisha lile alilotakiwa kulifanya.
Ni baada ya kupata kile kibali au ‘search warrant’, ndipo alipochukua askari wengine watatu na kuelekea kule alipoelekezwa na Kwakwa, nyumbani kwa Chabbi Cheka.
Hakuwa amejiandaa kabisa kwa lile aliloenda kukutana nalo huko…
Baada ya kumpa Pojo maelekezo ya namna ya kufika pale kwa Chabbi, Kwakwa aliisikia simu yake ikiita, wakati huo akiwa anatoka nje ya geti la nyumba ya Chabbi Cheka baada ya kuukomea kwa nje mlango wa mbele wa nyumba ile.
Alikuwa ni dokta Martha.
“Niambie dokta…”Alimwambia.
“Naomba tuonane Inspekta Kwakwa…!” Yule tabibu alimwambia.
“Taja muda na mahala… nitakuja fasta!” Kwakwa alimjibu.
Dokta Martha akamtajia.
“Naja!” Kwakwa alisema huku akiliendea gari lake.
Nusu saa ya mwendo wa kasi na kuchomekeana na daladala baadaye, aliingia kwenye mgahawa uliokuwa jirani na kitengo cha tiba ya mifupa (MOI) pale hospitali ya Muhimbili na kuangaza huku na huko kumtafuta dokta Martha, lakini hakumuona. Alichagua kiti kilichokuwa mahali mwafaka kuweza kuona kila anayeingia mle mgahawani na pia kumuwezesha kutoka mle mgahawani kwa urahisi pindi ikitokea haja ya kufanya hivyo.
Akatoa simu yake na kumpigia.
“Ushafika?” Martha alimuuliza simuni kwa sauti yake ya kuliwaza.
“Yap!” Kwakwa alijibu huku akikunja uso kwa maumivu aliyokuwa akiyahisi kutokea pale kwenye lile nundu alilobakishiwa na Bilanga.
Dakika tano baadaye dokta Martha aliingia na kuketi pale kwenye meza aliyokuwako, wakitazamana.
“Okay, dokta… una nini la kuniambia? Uliniambia kuwa majibu ya kile
228
MTAFITI
nilichoomba unitazamie kwenye uchunguzi wako wa ule mwili yatapatikana
kesho… vipi wanipigia leo hii hii? Au kuna jingine?” Kwakwa alimuuliza.
“Hapana Kwakwa … hakuna jingine, ni hilo hilo…”
“Okay… nakusikiliza…” Kwakwa alimwambia, na dokta Martha akajiramba midomo na kukaa kimya kwa muda kabla ya kuongea.
“Ulinitumia ujumbe wa simu ukinitaka nimchunguze mdomoni yule marehemu, Kwakwa…” Dokta Martha alimwambia, na kuendelea, “… na pia ulinitaka nifanye vipimo vya ile damu iliyomgandia marehemu mwilini kama yote ni yake…”
“Ndivyo! Na ukaniambia majibu ya yote hayo yanaweza kupatikana kesho…” Kwakwa alimjibu, moyo ukimwenda mbio.
“Ni kweli Kwakwa, ila nimeona kuwa hisia zako zilikuwa sahihi… nimekuta vipande vya nyama na binadamu kinywani mwa marehemu… vimegandia kwenye meno yake!” Dokta Martha alisema, na Kwakwa akamung’unya neno ‘yes’ bila ya kulitamka kwa sauti huku akikunja ngumi ya ushindi pale mezani.
“Nilijua tu!” Alisema kwa hamasa, na kuendelea, “huo ni ushahidi muhimu sana kwa kesi yangu dokta… ushahidi huo unamtia hatiani moja kwa moja mtuhumiwa wangu!”
“Yaa, too bad ripoti yangu haiji kwako Kwakwa… sasa sijui utawezaje kutumia ripoti ya uchunguzi wangu kwenye mwili wa Mwantumu kukusaidia kwenye kesi yako.” Dokta Martha alimwambia.
“Hilo niachie mimi… nitaipata tu hiyo ripoti na nitaitumia kumtia hatiani mtuhumiwa wangu!” Kwakwa alisema kwa kujiamini.
“Inatisha sana Kwakwa… inakuwaje mtu anakutwa na vinofu vya nyama ya binadamu kinywani?” Dokta Martha aliuliza kwa mastaajabu.
“Nina dhana ambayo inaweza kujibu swali hilo… nadhani yule binti… alipambana na mbaya wake, na akamng’ata…” Kwakwa alimwambia, na Dokta Martha akatumbua macho, pia akiacha kinywa wazi.
“Inawezekana aisee…!” Hatimaye alisema kwa mastaajabu.
“Nina asilimia nyingi sana kuwa hivyo ndivyo ilivyotokea…” Kwakwa alimwambia.
“Sasa utathibitishaje hilo?” Martha alimuuliza, na Kwakwa akaachia tabasamu baya.
“Nitakuletea mtuhumiwa umchunguze… na uthibitishe iwapo hicho kipande cha nyama ulichokitoa kinywani kwa marehemu, kinaoana na vinasaba vya mtuhumiwa wangu!” Kwakwa alimjibu, na Martha akatikisa kichwa.
229
Issa Tuwa
Hussein
“Ah, ama kweli Kwakwa una mbinu! Anyway, yangu yalikuwa hayo tu… yanipasa nirudi kazini sasa.” Alimwambia.
“Hamna taabu dokta. Hakika leo umenipa habari nzuri sana tangu kesi hii ianze. Ahsante sana!” Kwakwa alimwambia.
“Usijali… tuko kwenye kazi moja… vitengo tu ndio tofauti!” Dokta
Martha alimjibu.
“Okay… let me go sasa…” Kwakwa alimwambia huku akiinuka.
“Amm… ningekuwa wewe ningeenda kubadili shati kwanza Kwakwa, kisha nd’o nikaendelea na mambo mengine…” Dokta Martha alimwambia
huku akimuoneshea kwa kidole chake sehemu ya kifuani.
Kwakwa aliinamisha uso na kujitazama pale kifuani.
“Usiniambie umetoka kutiana mateke na watu huko saa hizi!” Dokta
Martha alimwambia huku akimtazama kwa macho ya kushutumu.
Kwakwa wala hakuzingatia yale aliyokuwa anaambiwa japo aliyasikia. Akili yake ilikuwa imekamatwa na kile alichokuwa akikiona pale kifuani kwake.
Alama ya soli ya kiatu cha Bilanga ilikuwa imebaki kwenye lile shati lake jeupe, ambalo muda anapambana na Bilanga lilikuwa limetota maji aliyomwagiwa na yule bazazi ili kumzindua kutoka kwenye ile hali ya kupotewa na fahamu.
Aliinua uso wake na kumtazama dokta Martha.
“Kama ulivyosema dokta… kazi moja vitengo tofauti…” Alimwambia huku akitabasamu, na dokta Martha akatikisa kichwa kwa mastaajabu.
“Sasa hilo ndio la kukufanya utabasamu kwa raha namna hiyo Kwakwa? Ama kweli wewe…”
“Hapana dokta… unapoona ushahidi mwingine unakufuata hadi nguoni, yakupasa ufurahi tu! Hawa jamaa hawapindui nakwambia… mi’ n’nao tu!” Alimjibu huku akitoka nje ya mgahawa ule. Dokta Martha alisimama na kubaki akimtazama kwa mastaajabu. Kisha naye akageuka na kurudi ofisini kwake.
Bilanga alisukuma mlango wa ofisi ya Luis Kambesera na kupitiliza moja kwa moja hadi kwenye lile kochi la kifahari lililokuwa mle ndani na kujibwaga juu yake. Luis aliinua uso na kumtazama kwa macho ya kuuliza.
Aliona kuwa jamaa alikuwa ametutumkwa mdomo na uso ulikuwa umemchubuka. Ule mtazamo wake wa kuuliza ukasaidiwa na kauli kutoka
kinywani mwake.
230
MTAFITI
“What is it, Bilanga… mbo’ unaingia bila hodi… na huo uso umekuwaje?”
“Tunafanya nini kuhusu Chabbi, Luis…?” Badala ya kumjibu Bilanga alimuuliza lile lililompeleka pale ofisini kwake muda ule.
“Tunalifanyia kazi…” Luis alimjibu, lakini Bilanga alikuwa anaendelea kuongea.
“Ataendelea kubaki mahabusu mpaka lini? Unajua kuwa Chabbi hakukamatwa na polisi bali alijipeleka mwenyewe? Na unajua kwa nini alijipeleka mwenyewe? Kwa kuwa ilikuwa ni aidha yeye au ninyi nyote! Sasa naona mnajibweteka tu kama kwamba hakuna linalotokea! What are you doing kumtoa?” Bilanga alimkoromea kwa kirefu. Luis alijiramba midomo na kushusha pumzi ndefu.
“Tunafanya kila linalowezekana kisheria Bilanga… Mwangi ameshaenda huko na amekutana na kikwazo kidogo…” Alimjibu.
“Na mnakifanyia nini hicho kikwazo kidogo?”
“Si kikwazo cha kufanyiwa lolote kwa sasa… ni kikwazo cha muda. Naona kila kitu kiko sawa, polisi hawana la kuwawezesha kuendelea kumshikilia
Chabbi sasa… kwani mhusika wa kifo cha Mwantumu si keshapatikana?
Tunasubiri hayo masaa arobaini na nane yaishe tu nasi tukamtoe. Chabbi ni big boy bwana, atahimili hayo masaa machache yaliyobakia… amekuwa kwenye mangapi mazito zaidi ya hili?” Luis alimwambia kwa kirefu.
Bilanga akatikisa kichwa.
“Huelewi ugumu wa mambo Luis… Chances are, Chabbi hatotoka mle ndani. Huyu Inspekta Kwakwa huyu… ni balaa. Naamini atatafuta njia tu ya kuhakikisha kuwa Chabbi anaendelea kubaki mle ndani…”
“Kwakwa hana jipya tena yule… tumeshamfitinisha na mabosi wake. Kwa jinsi tulivyomchafua mbele ya waandishi wa habari lazima atatolewa tu kwenye ile kesi. Fanya kazi acha visingizio Bilanga!”
“We’ humjui Kwakwa inaelekea… Yule si mtu wa kufuata sana taratibu ujue! Anaweza kutolewa kwenye kesi na bado akatuhenyesha tu. Usijiaminishe sana Luis!” Bilanga alimjia juu.
“Kwa nini wasema hivyo?”
Bilanga akaguna.
“Unaona hii?” Alimjibu huku akimuoneshea ule mdomo wake ulioumuka, na Luis akamtumbulia macho ya kuuliza.
“Ni yeye huyu!” Bilanga alimwambia.
“Wacha bwana!”
231 Hussein Issa Tuwa
“Ooo! Nimemkurupusha chumbani kwa Chabbi akipekuwa sijui vitu gani tu mle… tumetiana mikononi ikanibidi niahirishe pambano… jamaa mjinga kweli kweli yule nakwambia!”
“Ah! Sasa alikuwa anatafuta nini huko?”
“Ushahidi wa kuzidi kumshikilia Chabbi, nini kingine?” Bilanga alimwambia, na Luis alichanganyikiwa.
“Sasa na we’ umefanya nini juu ya hilo? Umeahirisha pambano kivipi… uliumwaga?” Alimuuliza kwa kushutumu. Bilanga alimtazama kwa hasira.
“Ungekuwa wewe ungefanyaje?”
Luis hakuwa na jibu.
“Wewe kazi yako ni hapa ofisini, na kule kwenye mambo yako ya haramu ndio umetuajiri sisi tukufanyie… elewa kuwa kuumwaga kama mwenyewe ulivyosema ni sehemu ya mbinu za medani!” Bilanga alimsimanga kwa hasira, na kuendelea, “… naweza kuwa nimelifanyia kazi na kulidhibiti hili la leo, lakini elewa kuwa Inspekta Kwakwa hataacha kutufuatilia. Na Chabbi akiendelea kubaki kule mahabusu, kinachofuata ni nyie nyote kuswekwa ndani… ukizingatia kuwa makabrasha ya Grayson bado hayajapatikana!” Bilanga alimwambia na Luis akauma meno wazi wazi.
“Hivi kwa nini hatokei mtu akamuua huyu Kwakwa, lakini? Kwa nini anakuwa kimbelembele kwenye mambo namna hii?” Luis alisema kwa hasira.
Bilanga alimtazama kwa muda mrefu bila kusema neno, kisha akainuka na kuelekea mlangoni.
“Fanya hima Chabbi atoke tufuatilie yale makabrasha Luis… ama sivyo sote tunazama hapa kwa kimbelembele cha Inspekta Kwakwa, bloody fools!”
Luis alibaki akiwa amekodoa macho mle ofisini kwake.
Huku akiamini kuwa Pojo atakamilisha lile jukumu la kuchukua ule
ushahidi wa viatu vya Chabbi kule nyumbani kwake, Inspekta Kwakwa aliamua kuelekea sehemu ambayo aliahirisha kwenda muda mrefu, tangu
ile siku ambayo kifo cha Grayson Mochiwa kilitokea. Hakuwa na sababu ya kwenda huko hapo kabla kwani hakujua alitakiwa akamtafute nani.
Lakini sasa alikuwa anajua ni nani haswa aliyekuwa anaenda kumtafuta na alikuwa ana imani kuwa akifanikiwa kumuona atakuwa amepata ushahidi
232
MTAFITI
mwingine muhimu dhidi ya Chabbi na wenzake.
Simu yake ikaita, na alipoona kuwa ni Pojo, akaiweka sikioni kwa hamu ya kusikia kuwa yule Sajenti amefanikisha lile jukumu alilomtuma, lakini wahka mkubwa ulioambatana na sauti ya Pojo simuni ukamkata maini.
“Inspekta najua kuwa ulitaka nije nichukue ushahidi muhimu hapa nyumbani kwa Chabbi, lakini hili nililokutana nalo hapa na kinyume kabisa na hilo!” Pojo alimwambia simuni na Kwakwa akaegesha gari pembeni.
“Ni nini Pojo?”
“Hii nyumba inawaka moto hapa, na nimekuta raia kijiji!” Pojo alisema, akimaanisha amekuta raia wengi eneo lile, na Kwakwa akaachia mguno wa mshangao.
“Seriously?”
“Yes, afande… seriously!”
Kwakwa akamtukania Bilanga bibi yake.
“Kwa hiyo, dah… na hilo gari hapo nje?” Alimuuliza.
“Gari lipo afande… lakini halina viti viwili vya mbele…”
Kule alipokuwa Kwakwa akamlaani tena Bilanga.
“Nakuja huko…!” Alisema, na kugeuza gari kwa kasi, kwa mara nyingine akiahirisha kwenda kule alipokuwa amekusudia kwenda kabla ya kupokea ile simu ya Pojo.
Simu yake ikaita tena.
“Nimesema nakuja!” Alimaka simuni, tayari akili ikiwa imemuwamba.
“Babu taratibu, eenh?” Katibu muhtasi wa mkuu wake wa kazi alimwambia kimipasho.
“Oh, ni wewe, sorry… nilidhani ni mtu mwingine!” Alimtaka radhi.
“Unahitajika na mkuu hapa ofisini… sasa hivi!” Katibu muhtasi alimwambia, na Kwakwa akauma meno.
“On my way!” Alimwambia, akimaanisha kuwa alikuwa anaenda huko alikoitwa, na kukata simu. Akapeleka gari pembeni ya barabara na kugeuza tena, akichukua uelekeo wa kule ofisini kwake.
Sasa ndio kwenda kujua mbivu na mbichi huko…
Alijiwazia huku akielekea kule ofisini kwake.
Wakati huo huo, kule Sinza Sajenti Pojo alibaki akiwa ameduwaa.
Alikuwa amesimama na wale askari wenzake watatu alioenda nao
kuifanyia upekuzi nyumba ya Chabbi huku akitazama kwa fadhaa wakati
ile nyumba ikiendelea kuteketea kwa moto mkubwa. Muda ule askari
233 Hussein Issa Tuwa
wa kikosi cha zimamoto walikuwa wakiendelea kuuzima ule moto, na walikuwa wanaelekea kufanikiwa. Alikuwa amepashwa habari na wale
wazimaji moto kuwa ule moto ulionekana kuwa ulianzia kwenye chumba cha kulala cha mwenye nyumba.
Alitikisa kichwa na kujisogeza pembeni, mbali na wale wenzake, akili ikimuwanga.
Ama hakika hawa shwaini wana siri nzito na mikakati minene! Yaani nilikuwa
nataka kupata ushahidi wa kumuunganisha Chabbi na Mwantumu kutoka kwa yule dereva wa bajaji… jamaa akakutwa na umauti kwa namna ya ajabu kabisa!
Alijiwazia kwa fadhaa kubwa.
Na sasa leo tena nakuja kufuata ushahidi mwingine wa kumtia huyo huyo
Chabbi hatiani hapa nyumbani kwake, eti nako nyumba inaungua moto! Tena moto unaanzia kule kule chumbani kwake ambako ndiko Kwakwa aliniambia kuwa ushahidi ulikuwepo!
Alizidi kujiwazia kwa masikitiko.
“Dah!” Aliguna kwa sauti na kutikisa kichwa.
Walisubiri hadi ule moto ulipozimwa kabisa, ndipo walipoingia mle ndani
kujaribu kuona watakachojaaliwa kukiona, ambacho labda kingewasaidia kwenye upelelezi wao.
Hakuna walichokuta zaidi ya rundo la majivu kule chumbani kwa
Chabbi Cheka...
Kama ilivyokuwa kwa Inspekta Kwakwa, Pojo naye akamlaani Bilanga.
234
MTAFITI
MUDA MFUPI BAADA ya Bilanga kutoka ofisini kwa Luis, vigogo wa ile kampuni ya Liquid Diamond Incorporated walikutana tena kwenye chumba chao cha mikutano, chumba ambamo ndani yake ndio maafa yote yaliyokuwa yakiendelea jijini muda ule yalipoanzia.
Luis Kambesera aliwatazama wenzake huku akimungu’unya midomo.
“Wandugu nadhani mna haki ya kujua hali halisi tuliyo nayo hivi sasa…” Alianza kuwaeleza.
“Ambayo ni hali gani hiyo Luis?” Mike Mwangati, meneja uzalishaji aliuliza huku wale wenzake wakikaa vizuri kusikiliza.
“Hali bado ni nzuri upande wetu, ila kwa namna ilivyo inaweza kugeuka wakati wowote. Chabbi bado yuko mahabusu na tunataraji baada ya saa nne usiku kesho atakuwa huru, na kila kitu kitakuwa sawa!” Luis alimjibu huku akitembeza macho yake kwa wote mle ndani.
“Sasa ni kipi ambacho kinaweza kuigeuza hali hiyo? Ni wazi kuwa hilo linakutia mashaka ndio kisa ukatuita hapa…” William Maginga, mkuu wa kitengo cha tehama kwenye ile kampuni alihoji.
“Nakubaliana na Bill… kuna nini kilichojificha hapo?” Jamilla Mchebe akadakia.
“Kuna habari kuwa pamoja na kwamba polisi hawana lolote la kuendelea kumshikilia Chabbi mpaka sasa, wanaenda juu chini kutafuta makosa ya kumbambikizia ili waendelee kumshikilia zaidi baada ya hizo saa arobaini na nane za kisheria zinazoisha kesho saa nne usiku!” Luis aliwaambia, na mashaka yakatembea mle ndani.
“Sasa… wanaelekea kufanikiwa katika hilo unadhani?” Maginga aliuliza.
“Na kama wakifanikiwa, na Chabbi akaendelea kuwa chini ya ulinzi…
235 Hussein Issa Tuwa
13
unadhani atasema kuhusu haya tuliyoyafanya? Maana akisema mjue nd’o tumekwenda na maji hivyo!” Jamilla alisema.
“No… Chabbi ni mgumu… na anajua nini inamaanisha kuwa mwaminifu kwa wenzake… hatosema!” Luis alijibu.
“Na vipi kuhusu ile hati ya sisi sote kuwekwa ndani? Mi’ naona kama Chabbi ataachiwa katika hili, Kwakwa atatujia sisi… sasa je, sisi tunaweza kukaa kimya na kutosema juu ya hili tulilolifanya?” Mike Mwangati aliingiza hoja.
“Na hilo ndilo nililokuwa nataka kuliongelea wazee. Chabbi hatosema hata afanywaje! Lakini kama hali ikigeuka tukaja kuwekwa sisi chini ya ulinzi… tutaweza kuziba midomo yetu pamoja na vitisho na mikwara tutakayotemewa na wana usalama? Hilo ni la msingi sana. Ndio maana nimeitisha mkutano huu!” Luis alisema, macho yake yakitembea baina ya William ‘Bill’ Maginga na Jamilla Mchebe.
Macho yaliwatembea wale watendaji wake.
“Ah, mi’ niko vizuri… hawezi kunitisha mtu nikasema lolote ambalo sitaki kulisema!” Mike Mwangati alisema kwa kujiamini.
“Sina shaka juu ya hilo kutoka kwako, Mike…” Luis alisema.
“Mimi ndio kabisa! Nina kila mbinu za kiuanasheria za kuwageuzia maswali yao yote wao wenyewe!” Suleiman Mwangi alijinadi.
Macho yakabaki kwa Jamilla na Maginga.
“Ah, kwani watakuwa wanatutesa? Polisi hawaruhusiwi kufanya hivyo, right?” Maginga alisema kwa mashaka.
“Wanaweza kutumia mbinu zozote kupata walitakalo kutoka kwetu Bill, kwa hiyo lolote liwalo, midomo inabidi ifungwe na jibu letu liwe…” Luis alianza kueleza na Mwangi akadakia.
“Moja? Sote tuwe na jibu moja?”
“Not necessary… sio lazima liwe moja neno kwa neno… tulishafanya kosa hilo hapo awali, si mnakumbuka? La msingi ni kwamba kusiwe na yeyote kati yetu atakayesema kuhusu tulilolifanya… that is very important!”
Luis alisisitiza.
Kimya kilitanda kwa muda.
“Mnh, kwa kweli mi’ kulala selo siwezi jamani…” Jamilla aligwaya vibaya.
“Sasa inabidi ufikirie na yale mamilioni yaliyotupiwa kwenye akaunti yako kwa kukubali kwako kushiriki katika hili Jamilla… na sote hapa!
Tusifikiri yale mamilioni tuliyokomba yalikuwa hayana kazi… hapa ndio
236 MTAFITI
tunayafanyia kazi hivyo! Sote tulijiona kuwa tutaweza kuucheza huu
mchezo na matunda tumeyaona… tulioona kuwa hawawezi kuucheza
huu mchezo hatukuwashirikisha kabisa… na sote tumeona mwisho wao ulikuwaje. Hapa hakuna kurudi nyuma wandugu! No way back! Tupo?”
Luis alikuja juu, na kila mmoja mle ndani akagwaya.
“Ah, basi fanyeni kila liwezekanalo tusifikishwe huko polisi jamani… yaani huyu Kwakwa ndio anatufikisha katika hali hii kweli?” Jamilla Mchebe alisema kwa wahka na mashaka mazito.
Wenzake walimtazama, na kutazamana.
“Er, naamini hatutafika huko kwa kweli jamani… yaani hata kama
Kwakwa alikuwa ana nia ya kutusweka ndani na sisi…” Mwangi alianza
kutoa maelezo, lakini Maginga akadakia, akimkatisha.
“Siyo kama alikuwa ana nia… ni kwamba jamaa bado anayo nia hiyo yule!”
Mwangi na wenzake walimtazama, kisha Mwangi akaendelea, “Iwe iwavyo bwana… lakini hilo la Kwakwa kutukamata kwa sasa halitakuwepo kwa kuwa tumeshalizima kwa ile kauli yetu kwa waandishi wa habari asubuhi ya leo!” Suleiman Mwangi aliongea.
“Kivipi Mwangi, pray tell?” Jamilla alidakia kwa bashasha.
“Ah, jambo liko wazi! Wakitukamata sasa hivi itaonekana wazi kuwa tunakamatwa kwa kuwa tumediriki kuuweka hadharani udhaifu wa jeshi la polisi, kwa hiyo tunaadhibiwa… watawekwa kwenye wakati mgumu sana na waandishi wa habari… yaani hao hata kama wanatutamani kutuweka ndani…itabidi wasubiri tu kwa sasa!” Mwangi alimalizia, na wenzake wote pale ndani wakalifurahia hilo, wakipiga makofi kujipongeza juu ya hatua yao ile.
“Okay guys, tuwe katika tahadhari kwa lolote kutokea sasa… yeyote atakayewekwa kona na wana usalama, msimamo uwe ni mmoja tu!” Luis alisema. Kikao kikafungwa, wakatawanyika.
Wakati hayo yanaendelea kule Sinza na pale Liquid Diamond, kule kituo kikuu cha polisi askari wa kike aliingia kwenye chumba ambamo Zay na mama Mwantumu walikuwa wamefichwa.
“Er, poleni tena jamani…” Yule askari alianza kwa kuwaambia, na Zay
237 Hussein Issa Tuwa
na mama Mwantumu walimtazama tu kwa macho yaliyovimba na kuiva kwa kulia.
“Ennh, inabidi sisi tuendelee na kazi zetu kama kawaida, na sehemu ya kazi hiyo ni kwa nyinyi wanandugu kwenda kuutambua na kuuthibitisha rasmi mwili wa marehemu…” Alisema yule askari, na hapo mama Mwantumu aliangua kilio kipya, akilalama kwa mwanaye mpenzi kuitwa marehemu.
Ilikuwa ni kazi kubwa kwa yule askari kumuelewesha, na kazi kubwa zaidi kwa Zay kumnyamazisha yule mama.
“Uko… yuko wapi Mwantumu muda huu?” Zay aliuliza.
“Muhimbili… mochwari!” Yule askari alimjibu.
“Okay, tunaendaje huko?”
“Kuna usafiri wa polisi hapa utatuchukua mpaka huko na baada ya hapo utaturudisha…”
“Kwa hiyo tunaenda na wewe?” Zay alizidi kuuliza.
“Yeah… pamoja na askari wengine wawili …” Askari alimjibu.
“Afande Kwakwa atakuwepo kwenye msafara?”
“Am, no… yeye hatokuwepo kwenye huu msafara. Kwani vipi anti?” Askari aliuliza.
“Bila Kwakwa au Pojo hatuendi!” Zay alijibu kwa kiburi, na yule askari akashangaa.
“Pojo ndio nani? Simfahamu huyo miye…”
“Basi aje Kwakwa!” Zay alimjibu na yule askari akamjia juu.
“Halafu we us’take kun’changanya m’mi saa hizi, unas’kia? Mi’ nafanya kazi yangu tu hapa. Najua kuwa una simanzi ya kufiwa na rafikiyo… hata mimi nimefiwa sana tu maishani mpaka usawa huu… kwa hiyo…”
“Nimesema bila Kwakwa hatuendi popote!” Zay alimkaripia, na yule askari alimtazama kwa muda, kisha akamgeukia mama Mwantumu.
“Ndio hivyo hivyo, mama!” Mama Mwantumu naye alimjibu kwa ubishi.
Yule askari aliwatazama kwa muda zaidi, kisha akageuka na kutoka nje bila ya kutia neno zaidi.
Muda huo, sehemu nyingine ya jengo lile lile, Inspekta Kwakwa alikuwa akimtazama Mrakibu Mwandamizi kwa mshangao usiosemeka.
“Yaani imeamuliwa niendelee kukaa nje ya kesi hii afande?” Aliuliza kwa mastaajabu yaliyouzidi ule mshangao uliojinadi usoni kwake.
“Nasikitika hivyo ndivyo ilivyoamuliwa Kwakwa…” Mrakibu alimjibu,
238 MTAFITI
na bado Kwakwa hakumuelewa.
“Pamoja na ushawishi wote ule niliokupa afande?” Alimuuliza kwa hamaniko dhahiri.
“Pamoja na yote yale uliyonieleza na yangu niliyoongezea…”
“Aka!”
“Ndio hivyo Kwakwa…”
“Siamini kuwa IGP amekubali kunasa kwenye ghilba ya Liquid Diamond kirahisi namna hii aisee…!” Kwakwa alisema kwa hamaniko.
“Sijasema kuwa tumeangukia kwenye mtego wa Liquid Diamond Kwakwa… upelelezi wa tuhuma za Liquid Diamond dhidi ya jeshi utaendelea, na kwa kuwa wewe ndiye afisa uliyekuwa unasimamia upelelezi ule ni lazima ukae pembeni kupisha uchunguzi…”
“Ah, mkuu! Sa’ si nd’o hilo ninalosema la Non-Decision situation hilo? Sasa badala ya kuwachunguza wao kuhusiana na kifo cha Grayson na sasa cha Mwantumu pia, tunaanza kujichunguza sisi wenyewe kuhusu namna tulivyoendesha uchunguzi ule? Mkuu jeshi tunalipeleka wapi lakini?” Kwakwa alijazbika.
“Uchunguzi huo utafanyika, kwa kuwa ni lazima jeshi lizingatie malalamiko ya wananchi… lakini pia upelelezi wa vifo vya watendaji wawili wa kampuni ile utaendelea kama kawaida… isipokuwa sio wewe utakayeuendesha upelelezi huo!”
“Hah?”
“Hayo ni maamuzi ya IGP, na hayana mjadala!” Mrakibu alimwambia, na Kwakwa akajiona akizamishwa kwenye bwawa la usaliti wa hali ya juu.
“Hapana mkuu… rudi kwa IGP. Mwambie arekebishe maamuzi yake… niachiwe niimalizie hii kesi!”
“Hilo suala limekwisha Kwakwa… siwezi kurudi huko. Kuna askari wengi tu wengine wanaoweza kuukamilisha upelelezi huu…”
“Lakini sio kwa uharaka wala umakini kama wangu!”
“Mjadala umeisha Kwakwa…!”
“No haujaisha afande! Nina ushahidi kuwa wale jamaa sio watu wazuri… nipe ruhusa nionane na IGP basi afande, eenh?”
“Atakapopangwa afisa mwingine wa kusimamia upelelezi huo utahitajika umpe mustakabali wote wa kesi ili aendelee nao, pamoja na huo ushahidi unaosema kuwa unao… nawe usubiri kupangiwa kazi nyingine. Hiyo sasa ni amri!” Mrakibu alimkaripia.
239
Issa Tuwa
Hussein
Kwakwa alifunua kinywa na kukifunga. Alijaribu kuongea tena lakini neno pekee lililokuwa likimjia akilini mwake wakati ule lilikuwa ni tusi zito sana dhidi ya mkuu wake yule wa kazi.
Akaamua kusaluti na kutoka nje kwa ghadhabu.
“Ah! Afadhali nimekuona Inspekta…. hawa wachumba zako bwana mi’ siwawezi… kamalizane nao mwenyewe!” Yule askari wa kike aliyekuwa akibishana na akina Zay alimwambia huku akimfuata kwa mwendo wa haraka pale alipokuwa akielekea nje ya kituo kile.
“Una maana gani?”
“Eti hawataki kwenda na askari yeyote kuutambua mwili wa marehemu wao bila ya wewe au somebody Polo sijui…” Yule askari alimwambia.
“Pojo! Sio Polo wewe, vipi? Kama wamekataa ni sawa… wanahitaji kuwa na watu waliowazoea kwenye zoezi kama hilo… wacha nitaenda kuongea nao.” Kwakwa alisema.
“Okay… lakini, kwani umesharudishwa kwenye kesi? Hamna siri ujue humu… tunajua kuwa umesimamishwa kuendelea na kesi hii…!” Yule askari wa kike alimwambia.
Kwakwa alimtazama kwa hasira.
“Ndio maana nasema nitaenda kuongea nao ili waende nanyi tu… ila nitataka umchukue Sajenti Pojo wa kituo cha Chang’ombe kwenye msafara huo… linawezekana hilo?” Kwakwa alimjibu.
“Yah, kama huyo Pojo unamfahamu na ni askari mwenzetu…”
“Okay, naenda kuongea nao na nitampigia Pojo aje hapa…”
Kwakwa alisema na kuelekea kule chumbani kwa akina Zay. Nusu saa baadaye, Pojo alikuwa ameambatana na yule askari wa kike pamoja na askari mwingine mmoja, kuwapeleka akina Zay Muhimbili kuutambua rasmi mwili wa Mwantumu.
Inspekta Kwakwa alikuwa amekunja uso kwa ghadhabu zisizosemeka pale ofisini kwake, miguu akiwa ameipandisha juu ya meza, akizungusha zungusha kalamu mkononi mwake, akili ikimzunguka.
Yaani ndio nimeondolewa kwenye hii kesi kirahisi namna hii?
Alikuwa akijiuliza kwa mara ya tatu swali lile.
Ina maana hata IGP pia ameshindwa kuzingatia hoja zangu?
240 MTAFITI
Aliguna na kutikisa kichwa.
Sasa si ndio hawa Liquid Diamond watapata fursa ya kuzidi kupoteza ushahidi
muhimu…au hata Chabbi akaachiwa na kupotea kabisa jijini?
Alisonya na kubaki akiwa amekaa namna ile kwa muda mrefu, kisha akapiga kofi pajani kwake kwa hasira na kuinuka.
Hapa kuna mtu mmoja tu wa kuliweka sawa hili…
Aliwaza na kubaki akiwa amesimama katikati ya ofisi yake huku akiwa ameshika simu yake, bado akionekana mwenye mawazo.
“Yah, sina jinsi kwa kweli… ni yeye tu ndiye atakayeweza kulipatia ufumbuzi hili suala…!” Alijisemea, kisha akapiga namba iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ile simu yake. Alibaki akiwa amesimama pale katikati ya ofisi, akiisikiliza ile simu ikiita.
Simu ilipokewa upande wa pili na sauti nyororo aliyoijua sana.
“Sema Dracula… mzima wewe?” Ile sauti nyororo ilimuuliza huku mwenye sauti ile akicheka kwa uchangamfu, na Kwakwa akajikuta akiachia kicheko chepesi pamoja na ghadhabu alizokuwa nazo.
“Aww, come on shem… mi n’shakwambia huo utani wako huo! Mi’ nimeathirika macho… hiki ni kilema hiki! Sasa we’ unan’fanyia matani!”
Kwakwa alimwambia yule mtu aliyepokea simu yake huku akicheka, na upande wa pili wa ile simu yule mwanadada aliyependa kumtania kwa
kumwita ‘Dracula’ kutokana na yale macho yake halisi yenye mboni nyekundu, alizidi kumcheka.
“Vipi… unamtaka huyu bwana bila shaka…?” Hatimaye yule dada alimuuliza.
“Ndio maana nikapiga namba yake na sio yako… how come yuko home saa hizi… hakwenda job leo?” Kwakwa aliuliza, na hapo sauti nyororo ya yule mwanadada wa upande wa pili, ikabadilika na kuwa nzito na yenye kuvuma simuni.
“Nini wewe unachombeza wake za watu simuni saa hizi, eenh?”
Kwakwa akagutuka.
“Ala! Mkuu? Jambo afande!” Alisema na kusalimu kwa heshima, na jamaa wa upande wa pili akamcheka.
“Whatsup, Kwakwa?” Jamaa aliuliza.
“Ah, mkuu I am in trouble! Nahitaji kuonana nawe mkuu…” Kwakwa alisema kwa mashaka, akimaanisha kuwa alikuwa mwenye matatizo.
“Okay… njoo nyumbani tuongee basi…” Jamaa alimwambia.
241 Hussein Issa Tuwa
“Like, now…?” Kwakwa aliuliza, akiuliza iwapo aende muda ule ule.
“Unless kama hiyo shida yako iko kesho au wiki ijayo…” Jamaa alimjibu, na Kwakwa akafyatua kicheko.
“Ah no, ni leo hii… na… saa hivi. Nakuja basi, chief!” Kwakwa alijibu kwa wahka kidogo, na jamaa wa upande wa pili akamcheka na kukata simu. Kwakwa alitoka na kuingia garini kwake, na huku moyo ukimwenda mbio, alichukua uelekeo wa mikocheni…
Zay na mama Mwantumu walisimama hatua chache kutoka kwenye meza ndefu ya chuma, mwili wa binadamu ukiwa umelazwa chali juu ya meza ile ukiwa umefunikwa kwa shuka jeupe kutokea kichwani hadi miguuni.
Dokta Martha aliwasogelea na akijitambulisha kwao. Kisha naye akataka kuwatambua.
“Eh, Bi mkubwa hapa ndiye mama wa mtu ambaye mpaka sasa tunaamini kuwa ni Mwantumu, na huyu hapa ni rafiki wa Mwantumu… wote wanamfahamu vizuri Mwantumu hivyo ndio wamekuja kuutambua huu mwili iwapo ni yeye au vinginevyo.” Sajenti Pojo alimwambia baada ya kuona kuwa si Zay wala mama Mwantumu aliyeonekana kuwa tayari kumjibu yule daktari wa polisi.
“Okay… aam, sitahitaji muda mwingi kutoka kwenu eenh… nitaomba tu mumtazame huyu marehemu hapa na mniambie iwapo ndiye huyo ndugu yenu au siye, okay?” Dokta Martha alisema na Zay na mama Mwantumu walimkubalia kwa vichwa, Zay akihisi miguu ikimuisha nguvu na utumbo ukimcheza.
Dokta Martha aliuendea ule mwili na kusimama upande mmoja wa ile meza na kuwaacha wao upande mwingine. Sajenti Pojo alibaki akiwa amesimama hatua kama tano nyuma yao, pamoja na wale askari wenzake aliokwenda nao pale.
“Mkiwa tayari mniambie nami nitaifunua hii shuka, okay?” Dokta Martha aliwaambia huku akiwatazama wale wana ndugu wa marehemu.
Zay na Mama Mwantumu walishikana mikono kwa nguvu huku wakiwa wamesimama bega kwa bega ubavuni mwa ile meza, mama Mwantumu akilia kwa sauti ya chini.
242
MTAFITI
Eh Mungu jaalia huyu asiwe yeye… tuendelee kumtafuta tu Mwantumu wetu
lakini asiwe yeye huyu, eee Mungu wangu… please! Please… please…
Zay aliwaza huku moyo ukimwenda mbio, na akihisi kukabwa na donge kubwa kooni.
“Mko tayari? Nifunue…?” Dokta Martha aliuliza tena na akaona mama
Mwantumu akitikisa kichwa kukataa hali ile, machozi yakimbubujika. Zay alimgeukia yule mama huku akimbinya mkono wake kama kwamba anataka kumkumbusha kuwa wako pamoja kwenye suala lile.
“Inabidi tujue mama… inabidi tu!”Alimnong’oneza, na yule mama alizidi kulia huku akitikisa kichwa kwa nguvu zaidi. Zay aliuma midomo na kumtazama dokta Martha.
Akampa ishara kwa kichwa kuwa aifunue ile shuka.
Dokta Martha akaifunua.
La Haula!…
“Mwantumuuuu!”
Wote wawili walilipuka kwa vilio vikubwa, mama Mwantumu akijiangusha kifuani kwa yule marehemu aliyelala chali pale mezani na kumkumbatia huku akilia kwa uchungu usio kifani, miguu ya Zay ilishindwa kuendelea kumbeba naye akaenda chini kama mzigo, akiita jina la Mwantumu tena na tena.
Sajenti Pojo na wale askari wenzake walibaki wakiwa wamesimama vile vile, wakiwatazama wawili wale wakimlilia mpendwa wao kwa uchungu namna ile. Dokta Martha alijitahidi kupambana na machozi yaliyokuwa yakimlenga. Hakukuwa na haja ya kusikia kauli rasmi kutoka kwa wale wanandugu, kwani ilikuwa wazi kwake na kwa wale askari waliokuwa na Pojo mle ndani, kuwa yule marehemu wao pale juu ya meza alikuwa kwa hakika, ni Mwantumu…
Inspekta Kwakwa aliingiza gari lake ndani ya geti alilofunguliwa na askari wa ngazi ya chini kabisa katika jeshi la polisi na kuliegesha sehemu mwafaka ndani ya wigo wa ile nyumba nzuri iliyokuwa eneo la nyumba za serikali zilizokuwa kule mikocheni, jirani na tawi la benki ya CRDB jijini Dar.
Na hata pale alipokuwa akiubamiza mlango wa gari lake na kugeuka
243 Hussein Issa Tuwa
kuelekea kule kwenye ile nyumba, mlango wa mbele wa ile nyumba ulifunguliwa na mwanadada mmoja mrefu mwenye weusi wa kahawia wenye mvuto wa aina yake alitoka na kusimama kwenye ngazi ya juu pale kibarazani akiwa amejishika kiuno, huku tumbo lake kubwa likiwa limechomoza mbele.
“Aaah, mara hii umefika? Ama kweli we’ Dracula… umepaa nini?” Yule mwanadada alimtania tena huku akicheka, na Kwakwa akamtikisia kidole cha shahada kwa namna ya kumkanya.
“Halafu we’ usingekuwa mke wa mkuu wangu wa kazi wewe!” Alimwambia huku akipanda zile ngazi fupi na kumfikia pale kibarazani alipokuwa amesimama.
“Nhaa! Halooo… ungenifanya nini kwani?” Yule mwanadada aliyesuka
‘dreads’ nene za kuvutia alimcheka tena huku akimkumbatia na kumbusu shavuni. Kwakwa alicheka na kumbusu shavuni pia, kisha akamshika mabega na kumsukuma nyuma kidogo ili amtazame vizuri.
“Ah, look at you! Pendeza sana wewe, eenh? Lini unan’letea huyu anko wangu sasa? Sio kukaa kunitania tania tu hapa… mlete mtetezi wangu fasta tupate kukuweka mtu kati hapa, alla!” Alimwambia kwa masihara, na yule mwanadada mwenye mvuto wa haja akacheka kwa furaha.
“Bado miezi kama miwili tu sasa… anyway, karibu Kwakwa… jamaa yako alikuwa anaoga na sasa anavaa nadhani…” Mwanadada alisema, na Kwakwa akasaili kulikoni awe anaoga muda ule huku wakiingia ndani. “Ah, nilimpa kazi ya kupalilia bustani yangu ya maua hapo… basi si kujichafua huko!” Mwanadada alisema na Kwakwa akacheka kwa furaha, akivuta picha ya huyo mkuu wake akipinda mgongo kupalilia maua.
“So kinachokuchekesha ni kwamba nimekuwa bushoke kwa kupewa kazi ya bustani au ni kwa vile tu ukimuona mke wangu we hujisikia kucheka tu?” Ile sauti nzito aliyoongea nayo simuni muda mfupi uliopita ilimuuliza kutokea ubavuni kwake, na Kwakwa akashtuka huku akisimama kutoka kitini na kukauka kwa saluti kali.
“Jambo afande!” Alisalimu kwa mujibu wa sheria, na yule mwanadada akamcheka zaidi.
Mtu mrefu aliyejazia vilivyo kimazoezi, akiwa amevaa suruali ya michezo na fulana mchinjo aliipangusa ile saluti bila kujali.
“Aw, come on Kwakwa! Achana na jambo afande zako hapa, vipi wewe?”
Alimwambia na kumuuliza huku akimpa mkono, na Kwakwa akaupokea
244 MTAFITI
ule mkono huku akitahayari kidogo.
“Mambo vipi wewe, eenh? Long time sio… all okay? Nahisi kama kwamba mambo si shwari upande wako… what is it?” Kamishna John Vata alimuuliza huku akimtazama moja kwa moja usoni.
E bwana we!
“Ah, you can say that again Kamishna…!” Kwakwa alimjibu mkuu wake ambaye pia alikuwa ni rafiki yake mkubwa, akimaanisha kuwa lile alilolisema lilikuwa ni kweli kabisa kiasi kwamba anaweza kulisema tena bila wasiwasi wowote.
“
Okay…” Vata akamgeukia mkewe.
“Tigga… siye tunaenda kuongelea ofisini kwangu kule basi. Naomba umletee Kwakwa Grand Malt, okay?” Alimwambia,
“Yes Sir!” Tigga Mumba, mke wa Kamishna John Vata, alimjibu kwa uchangamfu huku akisaluti kimasihara, na kuelekea jikoni, wakati Vata akimwongoza Kwakwa kwenye chumba ambacho hukitumia kama ofisi yake ya nyumbani.
Ikiwa imethibitika kuwa yule marehemu alikuwa ndiye hasa Mwantumu, Zay na yule mama walirudishwa kule mafichoni wakiwa hawajiwezi kabisa kutokana na kumuona mpendwa wao akiwa hana uhai tena.
Ilibidi Zay achukue jukumu la kuwapigia simu ndugu wachache wa mama Mwantumu kuhusu kuthibitika kwa habari ile, ambao siku zote walikuwa wanajua kuwa Mwantumu alikuwa amepotea na anaendelea kutafutwa. Kwa mujibu wa maelezo ya dokta Martha, polisi walikuwa wameshamaliza uchunguzi wao kwenye ule mwili na wanandugu walikuwa huru kuuchukua ule mwili wa mpendwa wao na kwenda kumlaza kwenye malalo ya kudumu.
Taratibu za mazishi zikaanza kufanywa mara moja, na ndugu wa mama Mwantumu wakaja pale kituo cha polisi kumchukua.
“Ah, sasa hili litakuwa gumu… mama yuko chini ya ulinzi kwa usalama wake…” Yule askari wa kike aliyebishana na Zay hapo awali alisema, na Pojo akaingilia kati.
“Kwani wewe ndiye unayesimamia hii kesi sasa hivi? Maana kwa hali inavyoonekana, mama si tishio tena kwa wale watu wabaya… ila Zay bado tishio. Mama hana ajualo ati!”
245 Hussein Issa Tuwa
Yule askari alienda kwa Mrakibu kupata maelekezo, maana bado kesi ilikuwa haijapangiwa mpelelezi mpya. Dakika kumi na tano baadaye alirudi.
“Okay… mama anaweza kwenda, lakini Zay atabaki hapa hapa…” Alisema, bila shaka hayo yakiwa ni maelekezo ya mrakibu.
Zay na mama Mwantumu waliagana kwa vilio vya uchungu.
“Nitakuja mazikoni mama… nitakuja tu. Naomba mniletee taarifa kuhusu siku na sehemu ya maziko nami n’takuja…!” Zay alimwambia huku akibubujikwa machozi.
“Wajomba zake wamesema tutazika kesho… kule kule kwangu… Gezaulole… shambani kwetu!” Mama Mwantumu alimjibu kwa simanzi iliyokithiri.
“Ntakuja…” Zay alimjibu, kisha akaachana naye na kurudi kujifungia mle chumbani alimokuwa amefichwa tangu siku ile alipofikishwa pale kituoni na Inspekta Kwakwa. Akiwa mle chumbani, alimpigia simu yule mpenzi wake aliyekuwa Rwanda na kumpasha habari.
Huku nyuma Pojo alimtazama yule askari wa kike aliyekabidhiwa usalama wa Zay akiwa pale kituoni.
“Sasa naona mimi wajibu wangu hapa nimemaliza… naenda zangu.” Alimwambia.
“Poa tu…”
“Kwa hiyo bado hajapatikana mtu mwingine wa kuendelea na hii kesi, sio?” Alimdodosa yule askari mwenzake wa jinsia tofauti.
“Yap! Mpaka sasa bila bila!” Yule askari alimjibu.
Pojo akatoka nje ya jengo la kituo kile huku akitikisa kichwa kwa masikitiko. Alitoa simu yake na kumpigia Inspekta Kwakwa.
“Naomba nikupigie baadae kidogo Pojo… niko katikati ya mjadala mzito hapa… unless kama kuna dharura!” Kwakwa alimjibu simuni, na hapo hapo Pojo akakata simu. Aliamua kurejea nyumbani kwake akiwa amechanganyikiwa vibaya sana.
Inspekta Kwakwa aliizima simu yake na kuiweka pembeni huku akimtazama Kamishna John Vata.
“Sasa hiyo ndio hali halisi Kamishna Vata… na matokeo yake mimi sasa niko nje ya kesi na sijui nini hatima yangu itakuwa!” Kwakwa alikuwa
ameshamuelezea Vata mkasa wote wa ile kesi wakati simu ya Pojo
246
MTAFITI
ilipoingia, na hapo alimalizia maelezo yake.
“Kwa hiyo unataka nini kutoka kwangu sasa?” Vata alimuuliza kwa utulivu.
“Akh, Kamishna! Hilo ni la kuuliza tena? Mi’ nataka nipewe nafasi niimalizie hii kesi. Na ni wewe tu ndiye utakayeweza kunirejesha kwenye hii kesi bwana!”
Vata alicheka kidogo.
“Na kwa nini unakuwa na imani hiyo, Kwakwa?” Alimuuliza.
“Ah, Kamishna! Mi’ najua kuwa wewe unaongea na IGP vizuri sana, na pia najua kuwa yeye anakuheshimu sana kwa kuwa ulitakiwa upewe wewe hiyo nafasi ya IGP, ila umri ndio kidogo ukakutupa mkono… mi’ najua hayo kwa sababu wewe mwenyewe umeniambia! Yule IGP anajua kuwa amekalia kile kiti akiwa ni chaguo la pili kutoka kwako na anakuheshimu sana kwa hilo… ongea naye kiutu uzima aisee. Mi’ nawasambaratisha wale Liquid Diamond kama wamesimama tu Kamishna, na we’ unajua hilo… nilikuwa nimebakiza hatua chache sana! Kwa nini IGP anafanya hivi?”
Kwakwa alisema kwa hamasa, na Vata akamtazama kwa muda mrefu, kisha akashusha pumzi ndefu kabla ya kuongea.
“Unajua sasa hivi Tigga anakaribia kujifungua…” Alisema na Kwakwa hakumuelewa.
“…naye alikuwa ameazimia kuwa anataka akajifungulie Marekani. Ndio maana nilikuwa nimechukua likizo ili nimpeleke huko. Tunapaa kesho usiku…”
“Ama! Sasa mbona hata hukunijulisha Kamishna? Yaani ungeondoka bila kuniaga?” Kwakwa alisaili kwa fadhaa.
“Kesho haijafika… definitely ningekupigia simu tu kukuaga…” Kamishna
John Vata alimwambia, na bado Kwakwa hakuelewa kwa nini anamueleza jambo lile.
Akauliza.
“Aam, sasa kwa nini unaniambia hilo sasa hivi Kamishna? Ina maana huwezi kunisaidia katika hili kwa kuwa unasafiri na mkeo…?” Alimuuliza kwa kutoamini.
John Vata alimtazama kwa nukta ndefu kidogo kabla ya kutoa jibu lililomuacha hoi Inspekta Kwakwa.
“Ni mimi ndiye niliyezuia wewe kuendelea na upelelezi wa kesi hii
Kwakwa!” Vata alimjibu, na bila kujitambua Kwakwa aliinuka kutoka
247 Hussein Issa Tuwa
kitini alipokuwa amekaa na kubaki akimkodolea macho kwa kutoamini.
“Say WHAT?” Alidhihirisha kutoamini kwake kwa kumtupia swali rafiki na mkuu wake wa kazi wa zamani. John Vata alibaki akimtazama kwa utulivu, akichezea ndevu zake zilizokuwa zimekatwa kwa mtindo aupendao sana, mtindo wa timberland.
Walibaki wakitazamana namna ile kwa muda wa kama dakika moja hivi, kisha taratibu Kwakwa akaketi tena kitini.
“Nahitaji ufafanuzi Kamanda….”
“Of course…” Vata alimjibu, huku akijiweka sawa pale kitini kwake...
Zay alijibwaga kitandani mle ndani na kulia kwa uchungu mkubwa sana. Alilia kwa muda mrefu, na kadiri alivyokuwa akiendelea kumlilia rafikiye namna ile, ndivyo uchungu wa kufiwa ulivyokuwa ukiyeyuka na nafasi yake kuchukuliwa na ghadhabu zisizosemeka dhidi ya ile kampuni mbaya ya kuendesha tafiti za nishati nchini.
Hivi ni tafiti gani hasa hizo wanazoendesha, eenh? Tafiti za siri kiasi cha kuhalalisha vifo vya watu wanaoonekana kugundua kitu kuhusu tafiti hizo?
Je, kifo cha Mwantumu ni kwa kuwa aligundua kitu katika hizo tafiti zao?
Na yule mtafiti wao mkuu… Grayson… naye aliuliwa kwa hizo hizo tafiti au…?
Alijiuliza kwa hasira, na hapo ikamuingia azma ya kuhakikisha kuwa ile kampuni inaangamia na wale watendaji wake wanatupwa jela kwa maisha yao yote yaliyobaki kutokana na kuhusika na kifo cha rafiki yake.
Yeye, kama mama Mwantumu na akina Sajenti Pojo hakuamini kabisa suala la mganga wa kienyeji kumtorosha rafikiye na kumuua kwa ajili ya imani za kichawi. Kwa namna fulani alijua kuwa akina Chabbi walikuwa wanahusika. Na akihusika Chabbi basi ni kwamba na Liquid Diamond nayo ilikuwa inahusika kwa asilimia mia moja. Alisonya na kujipangusa machozi huku akiinuka kutoka kitandani alipokuwa amejilaza.
Alichukua simu yake na kumpigia Inspekta Kwakwa.
Simu ya Kwakwa iliita kidogo kisha ikazimwa.
“Ah pokea simu Kwakwa! Ah!” Alimaka kwa hasira, na kumpigia Pojo.
248
MTAFITI
“Yes bibie…unasemaje?” Pojo alimuuliza simuni.
“Afande Pojo, nimempigia Kwakwa naona hataki kuongea nami, na…”
“No, yuko kwenye kikao kizito kwa sasa inaelekea, maana hata mimi hakuweza kuongea nami simuni… whats up?” Pojo alimjibu na kumuuliza.
“Kuna kitu nimekigundua kuhusu hii Liquid Diamond ambacho hakijanikalia sawa…” Zay alimjibu, na kuendelea kumjuza juu ya utafiti wake kwenye ule wavuti wa ile kampuni na kugundua kwake juu ya ripoti waliyoiwasilisha serikalini, ripoti ambayo iliwawezesha kupata mkataba mwingine wa mwaka mmoja kutoka serikalini kuendelea kufanya utafiti wa nishati nchini.
“Ah, okay… sasa ni kipi ulichoona kuwa hakipo sawa hapo?” Pojo alimuuliza baada ya kuwa ameshaelezwa juu ya ule ugunduzi wake wa ile ripoti ya Liquid Diamond kwa serikali.
“Nataka kuiona hiyo ripoti… unadhani nitaipata wapi?” Zay alimwambia na kumuuliza.
“Si hapo hapo kwenye tovuti yao! Umeangalia humo?” Pojo alimuuliza.
“Nimepekuwa mpaka macho yametaka kuniingia ndani afande, hiyo ripoti haipo kwenye tovuti yao nakwambia! Na hilo nd’o mi’ silielewi… kama hiyo ripoti ni ya wazi kiasi cha kuinadi mtandaoni, kwa nini isiwekwe hapo?” Zay alihoji, na Pojo akakiri kuwa hata yeye haoni kwa nini isiwe kwenye mtandao.
“Sasa swali linakuja afande… kama hapa mtandaoni haipo, ni wapi naweza kuipata hiyo ripoti, ukiachilia mbali pale Liquid Diamond kwenyewe?” Zay aliuliza.
“Hmmm… sijui… ila… okay. Sehemu nyingi… wizara ya madini na nishati kwa kuanzia, ofisi za Ewura vilevile… na hata maktaba ya taifa pia, kama wakitaka kufuata taratibu, ingawa nisipoikuta maktaba sitashangaa…” Pojo alimjibu.
“Ila ukiikosa huko wizarani na… na Ewura labda…?” Zay aliuliza kwa hamasa.
“Nitashangaa sana!”
“Then naomba unipatie hiyo ripoti kutoka wizarani au Ewura afande… nataka kuiona!” Zay alimwambia.
“Kwa nini… kuna kitu umegundua?”
“Sijui… ila nadhani nikiiona hiyo ripoti ndio nitajua kama nimegundua kitu au la…”
249 Hussein Issa Tuwa
MTAFITI
Kimya kilichukua nafasi kwa muda, kisha Pojo akaongea.
“Okay, wacha nijaribu… ila naona muda umesonga sana, na huko wizarani mida hii ni muhali sana kukuta mtu ofisini…”
“Jaribu afande. Kama mi’ nisingekuwa chini ya ulinzi hapa ningeenda mwenyewe…”
“No. We’ tulia tu huko… mi’ n’taenda!” Pojo alimjibu.
“Niliitwa kwenye kikao cha dharura mara baada ya wale jamaa wa Liquid
Diamond kutoa shutuma nzito dhidi ya jeshi letu la polisi, Kwakwa…”
Vata alianza kumpa maelezo.
Kwakwa alibaki akimtazama kwa makini.
“Kilikuwa ni kikao cha maamuzi, na kilichoamuliwa pale kilikuwa ni kwamba shutuma zile, pamoja na kwamba zilikuwa zinatolewa na watu ambao tayari tuna mashaka nao, ni lazima zifanyiwe kazi… na kitengo changu cha Majukumu Maalumu ndio kikakabidhiwa kazi hiyo ya kuchunguza namna wewe ulivyoendesha upelelezi wako pale Liquid
Diamond hata wale jamaa wakaja na shutuma nzito namna ile…”
“Ah, ile geresha yao tu Kamishna! Mi’ nilimwambia mrakibu wangu pale kuwa ile ilikuwa ni…”
“Non - Decision?” Vata alidakia, na Kwakwa akaachia kinywa wazi.
“Kakwambia juu ya hilo?”
“Nilikuwepo wakati mrakibu wa kituo chenu akitoa maelezo yako kwa
IGP… na sote tulikubaliana nayo, lakini bado shutuma ilibidi zifanyiwe kazi!” Vata alijibu, na Kwakwa akashangaa.
“Kumbe muda wote huo tangu mi’ nakupigia simu hadi nakuja hapa kujieleza ulikuwa unajua kila kitu kamanda?”
“Yah, na ningeshangaa sana kama usingenipigia… nilitaraji simu yako!”
Duh!
“Sasa… ina maana ikawaje tena baada ya kusikia hoja zote hizo bado
IGP akaamua vile?” Kwakwa alisaili.
“Ameamua kwa kushauriwa nasi, si yeye tu. Ila hili la wewe kutorejeshwa kwenye kesi ni mimi ndiye niliyelisisitiza…”
“Why?”
“Nilisisitiza kuwa kwa sasa asipewe askari yeyote hii kesi mpaka kikosi changu cha majukumu maalumu kitakapojiridhisha juu ya ukweli au uongo wa zile shutuma za Liquid Diamond, na nilikuwa nimetoa muda
250
mpaka leo mchana saa tisa kuwe kumeshafanyika maamuzi. Yaani ukweli uwe umejulikana!”
Ebwana we!
Kwakwa akatazama saa yake.
“Saa sita sasa mkuu… kuna hatua zozote ambazo watu wa kitengo chako wameshazianzisha? Maana inabidi wanisikilize na mimi!” Kwakwa alisaili.
“Hatua si ndio hizi zinaendelea Kwakwa? Naongea nawe hapa!” Vata alimjibu, na Kwakwa akashangaa tena.
“Yaani…?”
“Ulidhani ningekutumia askari wangu waje wakuhoji? No way. Mimi nataka nisikie maelezo yako tu yananitosha kufanya maamuzi. Kama mpaka muda huu ungekuwa hujapiga mimi mwenyewe ningekuita hapa!”
“EH!” Kwakwa aliguna.
“Ndiyo! Mi’ nakujua Kwakwa…nimeku-groom mwenyewe bwana!” Vata alimwambia, akimaanisha kuwa ni yeye mwenyewe ndiye aliyemfundisha kazi, na Kwakwa akajiona kama anayeelea angani.
“Unaona? Nilizuia mtu yeyote, na wewe ukiwemo, kupewa ile kesi kwa muda tu mpaka nitakapoongea nawe, na sasa nimeshaongea nawe.
Nataka uniambie jambo moja tu… una ushahidi wowote kuwa wale jamaa walitaka kukuhonga pale ulipowapelekea zile arrest warrant mbili kama ulivyonisimulia hapa?” Vata alimuuliza.
Kwakwa alibaki akimkodolea macho.
“Kama sina?” Alimuuliza.
“Then nitakuwa na kazi ngumu kidogo kulishughulikia suala hili… na muda ndio sina, kesho usiku napaa. Itabidi msaidizi wangu ashughulikie hili suala…”
Kwakwa alivimbisha mashavu na kupuliza upepo nje ya kinywa chake kama anayejaribu kuzima moto.
Luis Kambesera alikuwa amejikunja ofisini kwake akifuatilia ripoti muhimu za kikazi kwenye kompyuta yake pale mezani, wakati katibu wake muhtasi alipompigia simu.
“Bosi kuna afisa wa polisi hapa anataka kuonana nawe…” Katibu alisema, na Luis akamakinika.
“Ni yupi huyo? Yule yule au…?”
251
Issa Tuwa
Hussein
“Hapana… mwingine…”
Luis akaachia tabasamu pana usoni.
Polisi wameingia geji… Kwakwa keshatupwa nje ya kesi pumbavu zake!
“Okay, mwambie apite!” Alimwagiza katibu wake naye akajiweka sawa kitini, akisubiri ujio wa huyo afisa mpya aliyekabidhiwa kesi yao. Jamaa aliingia, naye akainuka kutoka nyuma ya meza yake na kwenda kumpokea huku akijitambulisha na kumpa mkono.
“Luis Kambesera… mkurugenzi mtendaji hapa…”
“Kamishna Mnde Mwasandende… kitengo cha majukumu maalumu ndani ya jeshi la polisi!” Kamishna Mnde Mwasandende alijitambulisha huku naye akiunadi wadhifa wake ambao hata hivyo ulikuwa umeanikwa kwenye yale mavazi yake ya kiaskari aliyoyavaa.
“Oh! Kamishna? Interesting!” Luis alisema huku akimkaribisha kwenye moja ya yale makochi yake ya kifahari pale ofisini. Yule afisa aliketi kwenye kochi kama alivyoelekezwa.
“Ndio Kamishna. Nikusaidie nini tafadhali?” Luis aliuliza, kisha akaendelea, “Naamini uko hapa kuhusiana na matatizo yaliyotukuta hapa ofisini kwetu, bila shaka…”
“Ofisi yenu ina matatizo mengi bwana Kambesera… sasa ni yepi hayo unayodhani kuwa yamenileta hapa?” Kamishna Mnde alimuuliza, na Luis akajichekesha kibwege.
“Ah, nilikuwa namaanisha lile la kuuawa kwa mtafiti wetu hapa… ambalo awali lilikuwa linasimamiwa na Inspekta mmoja anayeenda kwa jina la Kwakwa? Kijana mmoja mkorofi sana yule!” Luis alimwambia, na yule Kamishna alimung’unya midomo kidogo.
“Aaam, niko hapa kutokana na shutuma ulizolitupia jeshi la polisi leo asubuhi bwana Kambesera, hivyo nadhani ni sahihi kuwa hilo linamhusisha huyo Inspekta Kwakwa… kazi yangu ni kutafuta kujua ni jinsi gani aliiendesha hii kesi hata ikafikia hatua ya kampuni yako, kupitia wewe mwenyewe, kutoa shutuma nzito kama zile…” Mnde aliuliza. Luis akapepesa macho kidogo.
“Oh, hilo? Basi itabidi niwaite watendaji wangu wote hapa kwa kuwa…”
“Haitakuwa lazima bwana Kambesera. Nahitaji maelezo yako tu… ni jinsi gani Kwakwa alionekana kuwa hajui kazi yake na kwamba alikuwa anachelewesha uchunguzi wa kifo cha bwana Mochiwa?” Mnde alimbana
252 MTAFITI
kwa swali.
“AH, jamaa si alinikaba hapa mbele ya kila mtu! Hana maadili kabisa yule…”
“Kwa nini alikukaba?”
“Ah, of course nilipandwa na jazba kidogo kutokana na maswali yake, kwa hiyo nikatukana kidogo, basi ye’ akanirukia na kunikaba vibaya sana!”
“Ulitukana kidogo, au ulimtukana, bwana Kambesera?” Jamaa liliendelea kumsaili kwa utulivu.
Luis akagwaya.
“Ah sikumbuki vizuri tena, lakini najua kuwa sikumtukana…”
“Ah sasa hukumbuki vizuri? Ukitakiwa ukatoe ushahidi mahakamani utasema hukumbuki vizuri?”
Luis alimtazama kwa mashaka.
Hakuelekea kutoa jibu muda wowote wa karibuni.
“Okay, tuache hilo… kuna kipi kingine ambacho kimekufanya uone kuwa jeshi la polisi halijatilia maanani kupatikana kwa wauaji wa Grayson kwa kuleta wapelelezi ambao hawajui kazi yao?”
Kimya.
“Mista Kambesera… naomba jibu tafadhali maana natakiwa nirudishe ripoti ofisini ili ikibidi Kwakwa achukuliwe hatua…”
“Yaani siye tunalotaka ni kuletewa mpelelezi mwingine tu basi! Hatuhitaji kufungua kesi wala nini, ila Kwakwa kwa kweli tunaomba aendelee kuwa nje ya hii kesi!” Luis alijifaragua.
“Hujajibu swali langu Luis!” Mnde alimwambia kwa upole zaidi, huku akimtazama moja kwa moja machoni.
Luis akapepesa tena. Kimya kikatanda mle ndani kwa muda. Kamishna Mnde alitoa simu ya kisasa kutoka mfukoni mwake na kuanza kuibofya bofya, na mara Luis alishituka kusikia sauti yake kutokea kwenye simu ile.
“Er, kwa hiyo ndio tayari tuko chini ya ulinzi afande?” (Suleiman Mwangi)
“Hiyo sasa itategema na ninyi wenyewe!” (Kwakwa )
“Hah… hiyo nin…” Luis alianza kupayuka, na Kamishna Mnde ambaye hakuwa Mnde akamnyooshea mkono kumnyamazisha. Ile simu iliendelea kutema ilichorekodi.
“Okay Inspekta… ujumbe umeeleweka. Ni kiasi gani unahitaji ili hili jambo litoweke?” (Luis)
253 Hussein Issa Tuwa
“Ohh Noo!” Luis alimaka, na Kamishna John Vata aliyejitambulisha kwake kwa jina bandia aliizima ile simu ya Kwakwa na kumtazama.
“Huu ushahidi unakutia ndani wewe na wenzako wote mliokuwa nao wakati mjadala huu ukiendelea Luis!” Alimkoromea.
Midomo ilikuwa ikimcheza Luis na macho yalikuwa yakimtembea.
“Umeenda kulipaka matope jeshi la polisi kwa ujinga ujinga tu? Uliona ukifanya hivyo ndio Kwakwa ataondolewa kwenye kesi sio?” Vata alizidi kumkoromea.
Luis alianza kulegeza tai yake, na vipele vya jasho vikaanza kumuota kwenye paji la uso.
“Dah, naona kulikuwa kuna kutokuelewana kidogo tu hapo Kamish…”
“SHUT UP!” Vata alimfokea vikali, na Luis akaruka kutoka kwenye lile kochi kwa mshituko.
“Sasa this is what you do, fala wewe…” Alimwambia huku akimtazama moja kwa moja usoni, na kuendelea, “…utanyanyua simu na utampigia IGP sasa hivi… kisha utamtaka radhi kwa kauli zako za leo asubuhi, na utamwambia kuwa ulikuwa umepandwa na jazba tu, na kwamba unataka kufuta kauli yako, na pia uko tayari kushirikiana na Inspekta Kwakwa kwenye upelelezi wake wa kifo cha Grayson Mochiwa!”:
“AAAH!” Luis alimaka.
“Oh, yes! Ukifanya hivyo huu ushahidi hautatumika dhidi yako hivi sasa… ukishindwa, unatumika sasa hivi na n’takutia pingu hapa hapa na kukuburura lupango kwa kujaribu kumpa rushwa afisa wa polisi. Chaguo ni lako.” Vata alimwambia huku akimtazama kwa hasira. Luis alimtazama kwa mashaka.
“Nitakuwa na uhakika gani kama hata nikimpigia IGP na kumwambia hivyo ulivyotaka hautaendelea na kuutumia huo ushahidi dhidi yangu?” Alimuuliza.
“Hutakuwa na uhakika wowote! Unapiga simu au hupigi?” Vata alimkoromea.
Kwa ajizi kubwa Luis aliinuka na kwenda mezani kwake. Akampigia katibu wake muhtasi na kumuomba amuunganishe na ofisi ya IGP.
John Vata alimtazama wakati akimueleza IGP yale maneno aliyomwelekeza, na Luis alipoweka simu chini, Vata aliinuka.
“Usitembee tembee mbali na jiji Luis… Inspekta Kwakwa atakuja
254
MTAFITI
kukuweka chini ya ulinzi ndani ya siku hizi hizi za hapa karibuni!”
Alimwambia huku akiuendea mlango wa kutokea nje ya ofisi ile.
Luis alijibweteka kitini kama kiwete.
Nje ya jengo la Liquid Diamond Incorporated, Kamishna Vata alifungua mlango wa gari la Kwakwa na kujitupa kwenye kiti cha abiria, huku akimrudishia Kwakwa ile simu yake iliyorekodi ule ushahidi muhimu.
“Biashara imekwisha hapa… rudi kwenye kesi uendelee na kazi!” Alimwambia huku akifunga mlango wa lile gari, na Kwakwa akamkodolea macho ya kuuliza.
“Umemwambia nini Luis huko? Na unamaanisha nini kuwa nirudi kazini? Si inabidi IGP…” Kwakwa alimwambia lakini hapo simu ya Vata ikaita, na Vata akamuashiria akae kimya.
“Hello Sir!” Alipokea ile simu, na mara moja Kwakwa akajua kuwa Vata alikuwa anaongea na IGP. Akawa makini kufuatilia mazungumzo yake.
“Huyu jamaa wa Liquid Diamond anataka kucheza na sisi!” IGP alisema simuni, na Vata akamuuliza kivipi.
“Ah! Amepiga simu hapa ananiambia kuwa yote yale aliyosema asubuhi kwa waandishi wa habari yalikuwa ni jazba tu na kwamba anaomba msamaha… na yuko tayari kushirikiana na Inspekta Kwakwa katika upelelezi wake wa kifo cha Grayson! Can you believe this?” IGP alibwata simuni.
“Doh! This is major aisee…” Vata alijitia kushangaa, akimaanisha kuwa ile habari ilikuwa ni babu kubwa, kisha akaendelea kwa kusaili, “… sasa we’ umemjibu nini mkuu?”
“Nimemwambia sitapokea hiyo samahani yake simuni wakati ye’ kalitusi jeshi hadharani… akaite tena waandishi wa habari awaeleze kuwa alikurupuka na akaombee radhi yake huko huko, bloody bastard!” IGP alitanabahisha kwa jazba.
“Safi sana!” Vata alimpongeza bosi wake, Kwakwa akimtupia jicho la kuuliza, naye akimuashiria kwa mkono wake kuwa atulie tu.
“Sawa. Sasa hao vijana wako walifikia wapi katika upelelezi wao dhidi ya Kwakwa?” IGP alimuuliza, na Vata akaachia tabasamu la upande mmoja.
“Er, tumeshapata maelezo ya Kwakwa, na sasa ndio nimewatuma
255 Hussein Issa Tuwa
waende huko huko Liquid Diamond kufuatilia zaidi, afande…!”
“Ah! basi waite warudi Vata! Haina haja ya kupoteza nguvu kazi bure…”
IGP alisema.
“Oh!” Vata akajitia kushangaa.
“Yes! Na sasa kesi inabidi iendelee tu… ila sijui tumpe nani tena maana…”
“Ah, mi nashauri umwachie Kwakwa aendelee na kesi yake tu mkuu… amalizie tu sehemu iliyobakia!” Vata alisema na kando yake Kwakwa akapiga ngumi ya ushindi hewani.
“Unadhani hiyo ni move nzuri Vata?” IGP alihoji.
“Of Course ni move nzuri… kwa mujibu wa maelezo ya Kwakwa, kijana hakuwa na kosa lolote… ni wale jamaa tu walitaka kumpikia fitna ili atolewe kwenye kesi. Na hiyo inanipa picha kuwa Kwakwa alikuwa anafanya vilivyo ndivyo kiasi akawa mwiba kwao!” Vata alisema kwa ushawishi mkubwa, na Kwakwa akajihisi kichwa kikimjaa kama puto.
“Mnh! Hudhani kuwa Kwakwa anaweza kurudi kwenye kesi akiwa na kinyongo dhidi ya wale watu, na matokeo yake akafanya mambo hayo hayo aliyosingiziwa na wale jamaa…? Au akapoteza umakini kwenye kazi na kujikita kwenye kisasi zaidi?” IGP alitoa mashaka yake.
“Sio Kwakwa mkuu! Kwakwa ni askari makini sana… nashauri umrudishe kwenye kesi aimalize mkuu… afterall, alishapiga hatua kubwa tu… ila mpe muda maalum. Kama hataimaliza ndani ya muda huo basi nd’o apewe mtu mwingine!” Vata alisema, na Kwakwa akakunja uso.
“Sawa afande… ahsante afande…!” Kwakwa alimsikia Vata akiagana na IGP huku akili ikimzunguka.
“Dah! Ahsante sana Kamishna! Yaani umenipigia debe la nguvu!
Natumai IGP kakubali?” Alimuuliza.
“Yeah… nadhani utapigiwa simu muda si mrefu… nipeleke kwa mke wangu sasa Kwakwa.” Vata alimjibu.
“Okay, haina taabu. Ahsante sana kwa mara nyingine… ila sasa hii ya kunipangia muda maalum wa kuimaliza hii kesi inahusu nini, Kamanda?” Kwakwa alimuuliza, na Vata akatabasamu tena.
“Unataka IGP aone kuwa nakupendelea sana? Ile ni kumfanya aone kuwa hapa hapendwi mtu… ni kazi tu. Na kwamba hata wewe ukishindwa kutimiza malengo unawekwa benchi!” Vata alimjibu na wote wakacheka kwa pamoja. Muda huo simu ya Kwakwa ikaita. Alikuwa ni mrakibu
256 MTAFITI
mwandamizi. Kwakwa akamtazama Vata huku akitabasamu, na Vata akacheka zaidi.
“Si nilikwambia?” Alimuuliza.
Kwakwa alipopokea ile simu, mrakibu alimfahamisha kuwa amerudishwa kumalizia ile kesi… na akamwambia kuwa amepewa saa arobaini na nane awe ameimaliza.
Siku mbili!
“Ah, hizo si siku mbili tu? Basi kwa hali hiyo itabidi nipate msaada afande!” Kwakwa alisema.
“Kama upi?” Mrakibu aliuliza.
“N’tahitaji msaada wa Sajenti Pojo wa kituo cha Chang’ome kwenye kesi hii afande… jamaa ana historia ya nyuma inayohusiana na kesi hii kwa hiyo nilikuwa nadhani…”
“Sawa limepita hilo! Nitaagiza aripoti haraka hapa kituoni ili ukutane naye hapa!” Mrakibu alimkatisha na Kwakwa akatupa ngumi hewani, akiachia usukani kidogo, na kuukamata tena.
“Saa arobaini na nane Kwakwa! Ikishindikana hapo, kesi hiyo naihamisha kwa mtu mwingine!” Mrakibu alimwambia.
“Usipoteze muda mkuu… huyo mtu mwingine mtafutie kazi nyingine tu ya kufanya… huu mziki mi’ naumaliza!” Kwakwa alimjibu.
“Mziki?” Mrakibu alisaili kwa mshangao, na Kwakwa akaaga haraka haraka na kukata simu, kisha akaangua kicheko kikubwa, na alipomwambia Vata alichokuwa anacheka, naye akaungana naye kucheka.
Vata akamuelezea Kwakwa kila kitu kilichotokea baina yake na Luis Kambesera wakati alipokuwa ndani ya Liquid Diamond.
“Mnh! Kwa hali hii afande nadhani Luis asiwe mbali na macho yetu kuanzia sasa! Anaweza kuingia mitini huyu!” Kwakwa alisema.
“Kweli kabisa!”
“Basi naomba msaada mmoja… nipatie askari wa kumfuatilia kila aendapo kuanzia muda huu. Inawezekana sasa hivi akatoka hapa na ndo akatoweka kimoja!” Kwakwa alisema.
“Good point!” Vata alisema, kisha akatoa simu na kuwapigia askari walio chini ya kitengo chake cha majukumu maalumu. Akaagiza askari wawili wenye nguo za kiraia wafike pale walipokuwa haraka sana, na dakika kumi baadaye askari wawili, mwanaume na mwanamke walifika eneo lile ingawa hawakuenda moja kwa moja pale kwenye gari lao.
257
Issa Tuwa
Hussein
“Tunakuona afande!” Mmoja alimwambia kwa kutumia simu akiwa hatua kadhaa kutoka pale gari la Kwakwa lilipokuwa.
Vata akatoa maekelezo kuwa wajiweke sehemu mwafaka kuthibitisha kuwa Luis Kambesera hatoki nje ya upeo wa macho yao. Wote wawili walikuwa wanamfahamu Kambesera kutokana sio tu na umaarufu wake nchini tangu awali, bali pia kutokana na ule mkutano wake wa kulidhalilisha jeshi la polisi.
“Je tuna hakika kuwa hivi sasa bado yumo humo ndani?” Yule askari aliuliza.
“Tangu tumekaa hapa nje hajatoka, lakini najua kuna mlango wa nyuma huko pia… mmoja wenu aingie ndani akahakikishe hilo, na baada ya hapo afuatiliwe. Kila kitakachoendelea kutoka kwake kiripotiwe kwa Inspekta Kwakwa… nitampa namba zenu awapigie kujitambulisha kisha mtaendelea kuwasiliana. Tuko pamoja?” Vata alizidi kupanga mashambulizi.
“Kwa sana afande!”
“Good!” Vata akakata simu na kumgeukia Kwakwa.
“Okay Inspekta… nipeleke kwa mke wangu sasa, alla! Kazi yangu imeisha hapa… Washington D.C. inanihusu sasa!” Vata alisema huku akitabasamu.
“Okey dokey!” Kwakwa alimjibu huku akiliondoa lile gari kutoka pale lilipokuwa limeegeshwa.
258
MTAFITI
WAKATI VATA ALIPOKUWA akimpa Kwakwa habari za aliyokutana nayo kule ofisini kwa Luis pale nje ya jengo la Liquid Diamond, na kabla ya ujio wa wale askari wa kikosi cha majukumu maalumu kuweka doria dhidi ya Luis pale nje, ndani ya lile jengo Luis Kambesera alikuwa kwenye hali mbaya sana. John Vata alimuachia kizunguzungu cha akili na hakujua afanyaje.
Dah! Kumbe yule Kwakwa aliturekodi pale tulipokuwa tukiongea naye kule
kwenye chumba cha mikutano siku ile!
Aliwaza kwa hasira na kusonya, kabla ya kuanza kurandaranda huku na huko mle ofisini mwake.
Sasa niwaambie wenzangu kweli juu ya hili kweli?
Alizidi kujiuliza. Hapana aisee, hii itasababisha mtafaruku mkubwa na bila shaka kila kitu kitaharibika… shit! Kila kitu tayari kimeshaharibika sasa!
Alizidi kujiwazia mwenyewe.
Sasa na huyu IGP naye ananiambia eti niite waandishi wa habari nimtake radhi na nibadili kauli yangu hadharani, pumbavu! Si ndio thamani ya hisa zetu zilizoanza kupanda itaporomoka zaidi kuliko hata ile mwanzo?
Alijiambia.
Oh, pamoja na ujinga wake, Kwakwa alisema kweli… akili nyingi, hakika hupoteza maarifa! Natokaje sasa kwenye balaa hili?
Alibaki akiwa amekodoa macho kwa kutojua cha kufanya.
Muda mchache kabla Inspekta Kwakwa hajapokea simu iliyomrudisha rasmi kwenye kesi yake, sehemu nyingine ya jiji simu ya Zay iliita, na
259 Hussein Issa Tuwa
14
mpigaji alikuwa ni Sajenti Pojo.
“Ndio afande… nipe habari. Umefanikiwa?” Zay aliuliza kwa wahka.
“Yes and No, bibie…”
“Khah! Sa’ ndo jibu gani hilo afande?” Zay alihoji kwa kukereka. Alikuwa amepandwa na wahka sana wa kuipata ile ripoti iliyoipa sifa kubwa ile kampuni ya mauaji kwani alihisi kuwa sababu ya vifo vya Mwantumu na Grayson ilikuwa kwenye ripoti ile.
“Okay. Hapa wizarani nimekuta wahusika wote wametoka… kwa hiyo sikuweza kuipata hiyo ripoti…” Pojo alimjibu.
“Lakini wamesema hiyo ripoti ipo?” Zay alizidi kusaili.
“Look, jamaa niliyemkuta ni karani tu, hajui vitu vingi… ila kuna jambo moja kaniambia ambalo nadhani linaweza kutusaidia katika hili…”
“Nalo…?”
“Tovuti ya wizara…”
“Exactly!!!” Zay alidakia, na Pojo alikuwa anaendelea kuongea, “… jamaa aliniambia kuwa siku hizi nyaraka zote muhimu kwa umma huwekwa kwenye tovuti ya wizara... hivyo nilikuwa nadhani ujaribu kutafuta huko…”
“Yaani hapa nimeshaingia kwenye mtandao naisaka tovuti ya wizara afande…!” Zay alimjibu na kukata simu hapo hapo. Kule alipokuwa, Pojo alibaki akiitazama ile simu iliyomkatikia ghafla sikioni bila hata kuagwa.
“Ahsante kwa kushukuru bi. Zaynush…!” Alijisemea, na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwake, hamu ya kurudi kazini ikiwa imemtoka kitambo. Simu yake ikaita.
Alikuwa katibu muhtasi wa mrakibu msaidizi wa polisi makao makuu.
“Sajenti Pojo?” Katibu muhtasi alimuuliza.
“Ndiye mimi!”
“Unahitajika hapa polisi central haraka sana… unatakiwa uonane na mkuu wa kituo… mkuu wako wa kituo cha Chang’ombe anayo taarifa ya kuitwa kwako huku!” Katibu muhtasi alimwambia na Pojo akamakinika.
“Eh, ni… ni kuhusu nini, sijui?” Alimuuliza.
“Utajua ukifika!” Mwanadada alimjibu na kukata simu.
Heh, kwa mrakibu wa central tena…?
Pojo alijiuliza huku akibadili uelekeo na kuelekea kituo kikuu cha polisi.
260 MTAFITI
Simu yake ikaita tena.
“Tumerudi rasmi kwenye kesi Pojo! Na tuna saa arobaini na saba na nusu tu kuimaliza kesi hii, kwa hiyo…” Kwakwa alimwambia simuni na Pojo akamkatisha.
“Wow, wow, wow Inspekta! Unamaanisha umerudishwa kwenye kesi bwana, sio tumerudishwa, okay? Na…” Kwakwa alimkatisha.
“Umehamishiwa kituoni kwetu kwa muda na utafanya kazi nami kwenye hii kesi… mrakibu amepitisha hilo, Pojo!” Kwakwa alimwambia na mara moja Pojo akaunganisha ile habari na simu aliyopigiwa na katibu muhtasi wa mkuu wa kituo chao kikuu na ukweli ukamfunukia.
“Yes!” Alisema kwa ushindi.
Kwakwa akataka wakutane sehemu ili wapange mikakati lakini Pojo akamwambia kuwa alikuwa ameitwa kwa mrakibu ambaye pia ndiye mkuu wa kituo cha polisi cha ‘central’.
“Okay… huko unaenda kuambiwa haya haya nikuambiayo, lakini kwa kuwa umeitwa na mkubwa nenda tu… baada ya hapo nipigie ujue nilipo tupige kazi… looks like suala la kulala leo halitakuwepo!” Kwakwa alimwambia.
“No problem… kwa hiyo kwa sasa we’ unafuatilia suala gani afande?”
Pojo aliuliza.
“Sasa namrudia rafiki yangu Bilanga! Kuna mambo sijamalizana naye!”
Kwakwa alimjibu.
“Duh!” Pojo aliguna, na Kwakwa akakata simu…
“Bingo!” Zay alisema kwa ushindi pale alipofanikiwa kuipata ile ripoti aliyokuwa akiisaka kwa udi na uvumba, ikiwa imewekwa kwenye ile tovuti ya wizara ya madini na nishati.
“Nimeipata sasa… let’s see inasemaje…!” Alijisemea na kuanza kuisoma kwa makini.
Ilikuwa ni ripoti ndefu na iliyoandikwa kitaalamu sana, lakini kila
alipokuwa akiendelea kuisoma alikuwa anaona vitu vipya kabisa. Na alipomaliza alibaki akiwa mdomo wazi, kichwa kikimzunguka na moyo ukimwenda mbio.
261 Hussein Issa Tuwa
Ile ripoti ilikuwa tofauti kabisa na ile aliyoikuta kwenye mkoba wa Mwantumu.
“Oh, my God…!” Alijisemea huku uelewa mzito ukizama akilini mwake, na moyo ukamuingia ubaridi.
“Liquid Diamond wameichakachua ripoti ya Grayson Mochiwa (akaitukana tusi la nguoni ile kampuni)… na wameidanganya serikali big time!” Alisema tena peke yake, sasa woga mkubwa ukimkumba pale ule ukweli wa kilichotokea ulipozidi kumshukia…
“Mungu wangu…! Mungu wangu…! Ina maana Mwantumu alilibaini hili nd’o ikalazimika auawe ili kuzibwa mdomo?” Alisema huku akijiziba mdomo kwa woga.
Alilia kwa uchungu mkubwa sana.
Alimlilia upya rafiki yake kipenzi, akiwa amepata sababu ya kilichomuua… na akiwa anajua kuwa aliyemuua si mganga wa kienyeji bali ni Liquid Diamond Incorporated. Alilia kwa kuwa alikuwa ameshakutana na watu waliomuua rafiki yake uso kwa uso, na alijua kuwa na yeye pia alikuwa kwenye orodha yao kwa kuwa waliamini kuwa naye anayajua yale ambayo
Mwantumu na Grayson waliyajua kabla ya vifo vyao…
Na kweli, sasa naye alikuwa anayajua hayo. Na kwake, hiyo ilikuwa ni hukumu tosha ya kifo kutoka kwa mafisadi wa Liquid Diamond Incorporated…
Alilia kwa kujutia mawazo yake finyu ya hapo nyuma kwa kutaka kukubali
kuonana na wale mafisadi ili awape yale makabrasha nao wamrudishie
Mwantumu wake kama walivyoahidi… sasa alijua kuwa kama hilo lingetokea, basi na yeye angekuwa marehemu kama Mwantumu muda ule.
Alilia kwa hasira…
Akiwa ameghadhibika kupita maelezo, alitamani pale pale alipo awakamate wale watendaji wabaya wa ile kampuni dhalimu na awafinyange
kwa mikono yake midogo kisha awatumbukize kwenye kitu kama ndoo
hivi na aifunike ile ndoo kwa mfuniko usiofunguka… kisha achukue
gongo kubwa aanze kuipigapiga ile ndoo kwa nguvu nao wakiwa humo
ndani… na awe anasikia mayowe yao ya uchungu na woga kutokea humo ndani ya ndoo.
Aaah, hakika mayowe yao yangekuwa ni muziki mzuri sana masikioni mwangu,
262
MTAFITI
pumbavu zao!
Ndio alikuwa amekasirika kiasi hicho.
Huku akijifuta machozi na kwa hasira, alichukua simu yake na kuanza kupiga…
Sehemu nyingine ya jiji Inspekta Kelvin wa kitengo maalum cha kushughulikia kesi za mauaji na ukatili dhidi ya maalbino alikuwa kwenye wakati mgumu sana, na hasira iliyochanganyika na kuishiwa subira vilikuwa vimemtawala.
Alichukua chupa ya maji ya kunywa na kuyagugumia kwa pupa, kisha akaiweka ile chupa juu ya meza iliyokuwa ndani ya chumba cha mahojiano alichokuwamo muda ule, na kumtazama kwa mara nyingine yule mganga wa kienyeji aliyekuwa pamoja naye mle ndani.
Yule mzee alikuwa akitetemeka vibaya sana kwa woga huku akibubujikwa machozi kama mtoto.
“Sijui kitu mimi! Sijui lolote jamani…” Mzee alizidi kurudia maneno yake ambayo amekuwa akiyasema mfululizo tangu akamatwe kule nyumbani kwake maeneo ya Kongowe kuhusiana na kifo kibaya cha albino Mwantumu.
Kelvin alirudi hadi pale alipokuwa ameketi yule mzee na kumchapa kofi kali la uso.
“Hebu acha ubishi usio na msingi we’ mzee! Sema ni nani uliyemtuma akuletee kile kiungo cha albino ili upate kumfanyia chochote hicho ambacho ulidhani ulikuwa unatakiwa ukifanye ili umuondolee matatizo yake, mchawi mkubwa wewe?” Alimkemea tena kwa hasira, jasho likimtoka kwa kumshinikiza bila mafanikio yule mzee kukiri kuhusika na ule mwili uliokutwa hatua chache kutoka kibandani kwake, hususan kile kiungo cha mwili ule kilichokutwa uwani kwake.
Mzee alilia kwa uchungu na kuinua uso wake kumtazama kwa hasira pia.
“Sasa nakwambia mimi sihusiki na hilo wewe kijana, kwa nini hunielewi?”
“Mwongo!”
“Ni ukweli mtupu huo wewe! Badala ya kutafuta wauaji wa kweli unaning’ang’ania mimi kwa kuwa ni mganga wa kienyeji?”
“Kelele wewe! Sitaki kusikia hayo… nataka kisikia ukikubali kuhusika na ule mwili!” Kelvin alimbwatia huku akimsukasuka kwa nguvu.
Mzee alilia tena kwa woga.
263 Hussein Issa Tuwa
Inspekta Kelvin alimwachia na kurudi kujiegemeza kwenye meza iliyokuwa mle chumbani huku akimtazama kwa hasira, akitweta. Mzee alibaki akiwa amejiinamia huku akilia kwa uchungu, kisha akainua uso na kumtazama kwa hasira iliyoiva.
“Ah! Unanifanya hivi mimi we’e kijana kweli? Mimi…? Majambo mwana wa Mtambuka Karogo, kiboko ya wachawi na mtawala wa mashimo saba ya mfalme wa majini? Kweli?” Mzee alimuuliza kwa hasira ya kuapiza.
“Hebu kelele huko wewe us’ta’a kun’tisha m’mi hapa, ebbo!” Kelvin alimkemea, na mzee akaachia cheko ya kukata tamaa.
“Ah! Basi elewa kuwa nikitoka hapa kijana nguvu za kiume huna… nakuvunja vunja nguvu zote wewe!” Mganga alimjia juu, na Kelvin alimtokea mbio kwa lengo la kumpa kichapo kingine, lakini hapo Koplo
Twilumba aliwahi kumdaka na kumzuia.
“Afande!” Yule dada alimwita huku akimzuia kwa kumuwekea mikono yake kifuani. Kelvin alibaki akimtazama huku akitweta kwa hasira. Koplo
Twilumba alimtazama mkuu wake wa kazi na kumuashiria kwa kichwa kuwa waende chemba kidogo.
“Afande… mi’ nadhani huyu mzee hajui kitu aisee… yumkini huu mchezo umechezwa ili jumba bovu limuangukie yeye…” Twilumba alimwambia mwenzake wakiwa pale chemba, na Kelvin alimtolea macho.
“Khah! Yaani unataka kuniambia unaamini kuwa yule mzee hahusiki?”
“Kwa jinsi tulivyomhoji afande kama angekuwa anahusika angeshasema yule! Hebu twende tukaongee tena na wale askari waliokuwa wakiendesha ile kesi ya yule binti aliyeuawa… yumkini walikuwa sahihi kuwa huyu mzee kabambikiwa tu…” Koplo Twilumba alisema, na Inspekta Kelvin aliishiwa nguvu. Alikuwa akiamini kabisa kuwa kukabidhiwa kile kitengo cha ‘Anti-Albinism’ ilikuwa ni nafasi nzuri ya kujipatia umaarufu na kupandishwa cheo haraka, sasa kukubali kuwa yule mzee alikuwa hahusiki wakati tayari imeshanadiwa kuwa kitengo chake kimeweza kumnasa muuaji wa albino ndani ya muda mfupi sana, kungekuwa na athari kubwa sana kwenye malengo yake.
Alisonya kwa hasira…
Inspekta Kwakwa alisukuma mlango na kuingia ndani ya chumba cha kutathmini ushahidi kilichokuwa kwenye kitengo cha kuchunguza maeneo ya maafa ya kijinai, au ‘Crime Scene Investigation Unit’, na kukutana na mmoja
264 MTAFITI
wa watendaji wa kitengo kile akiwa anamsubiri. Ilihitaji ruhusa maalum
kuingia kwenye chumba cha kitengo kile, na Kwakwa alikuwa ameshapata
ruhusa hiyo kupitia kwa mkuu wa kitengo kile aliyewasiliana naye awali.
“Okay Inspekta… ulisema unahitaji msaada wetu kuhusiana na kesi unayosimamia? Ya yule albino aliyeuawa Kongowe?” Jamaa alimuuliza.
“Yes… unakumbuka kule kwenye eneo la tukio nilikwambia kuwa ningehitaji kuona picha za alama za viatu au miguu zilizokutwa eneo la tukio?” Kwakwa alimwambia na jamaa akaafiki kwa kichwa.
“Je ulipata alama zozote zilizoweza kuonekana kwa ufasaha?” Alimuuliza. Jamaa akamwambia kuwa walipata alama kadhaa ambazo waliweza kuzibaini moja kwa moja kuwa ni za viatu.
“Ila hatuwezi kuwa na uhakika sasa iwapo ni za wauaji wa tukio lile au ni za mmoja kati ya askari wenzetu… maana hata sisi wenyewe hatukuweza kuepuka kulikanyaga eneo…”
“Alama za soli za askari zinajulikana aisee… hebu naomba nione hizo ulizonazo.” Kwakwa alimwambia.
Akaingizwa sehemu nyingine ndani ya ofisi za kitengo kile, ambamo humo yule jamaa aliiendea kompyuta mpakato iliyokuwa juu ya meza, ambayo ilikuwa imeunganishwa na kifaa kilichowezesha yale yaliyokuwa kwenye kompyuta ile yaonekane kwenye ubao mkubwa sana mweupe uliokuwa kwenye ukuta wa chumba kile. Jamaa alibofya kwenye ile kompyuta na mara picha moja ya alama ya kiatu ikaonekana ukutani, ikiwa jirani na alama nyingine ya kiatu.
Kwakwa akawa makini kutazama ile picha ya soli ya kiatu pale ukutani, na jamaa akabofya tena na zile picha zikawa zinabadilika badilika zenyewe pale ukutani.
Kulikuwa kuna picha za alama nne tu za soli za viatu, nazo zilikuwa zikijirudia tena na tena, lakini ilipofika ile alama ya tatu moyo wa Kwakwa ukafanya mlipuko.
“Hebu hiyo!” Alisema na jamaa akabofya, ile picha ikaganda pale ukutani. Walibaki wakiitazama ile picha.
Ilikuwa ni soli ya kiatu kizito, na hata kutokea pale walipokuwa waliweza kuona maadishi yaliyokuwa kwenye soli ya kiatu kile yakiwa yamejipiga muhuri kwenye ardhi nyevu nyevu ya lile eneo ambalo mwili wa Mwantumu ulikutwa.
Neno ‘CAT’ lilionekana wazi wazi pale ukutani.
265 Hussein Issa Tuwa
Kwakwa alilitoa lile shati lake jeupe alilokuwa amelivaa awali kutoka kwenye mfuko wa nailoni aliokuwa nao na kulitandaza vizuri juu ya ile meza mle ndani.
“Hebu angalia hii alama kwenye hili shati kamanda…” Alimwambia yule askari.
Jamaa aliitazama kwa makini ile alama ya soli pale kwenye shati, akakunja uso huku akiguna, na kuigeukia ile alama ya soli iliyokuwa pale ukutani, kisha akaigeukia tena ile ya pale kwenye shati.
“Inspekta hii ni soli ya kiatu hichi hichi!” Jamaa alisema, akiitazama ile soli iliyobaki pale kwenye shati la Kwakwa, lile neno ‘CAT’ likionekana waziwazi pale shatini.
“Are you sure…?” Kwakwa aliuliza huku moyo ukimwenda mbio.
“Mia kwa mia Inspekta. Hizi alama zote mbili zimetokana na kiatu cha aina moja…!” Jamaa alimthibitishia, na tabasamu baya likatanda usoni kwa Inspekta Kwakwa pale hisia yake ya tangu awali ilipothibitishwa na mtaalamu.
“Gotcha, Bilanga!” Alisema kwa ushindi.
“Duh! Hongera sana Inspekta… yaani kama unamfahamu huyo mwenye hicho kiatu, basi kwa ushahidi huu ni wazi kabisa kuwa huyo ndiye mtu wako!” Jamaa alimwambia.
“Nitaihitaji hiyo picha ili kuiunganisha na huu ushahidi wangu…” Kwakwa alisema.
“No problem… fuata taratibu tu kamanda!” Jamaa alimjibu.
“Si tatizo, ila kwa sasa nahitaji angalau kopi tu…”
Jamaa akamtolea kopi ya rangi ya ile alama ya soli ya kiatu cha Bilanga iliyokuwa kando ya mwili wa marehemu Mwantumu. Dakika tano baadaye, Kwakwa alitoka nje ya ofisi zile akiwa na ushahidi aliokuwa anauhitaji ili kumuunganisha Bilanga na mauaji ya Mwantumu.
Simu yake ikaita. Alikuwa ni Sajenti Pojo.
“Okay, sasa niko rasmi kwenye kesi ya Liquid Diamond afande, na wewe ndiye bosi wangu kwenye kesi hii!” Pojo alimwambia, na kuendelea, “Nikukute wapi boss?”
“Anzia kazi hapo hapo ofisini Pojo…” Kwakwa alimwambia, kisha akamuagiza achukue kibali cha kumtia mbaroni mtu aitwaye Bilanga anayefanya kazi kwenye kampuni ya Liquid Diamond Incorporated.
“Okay boss… kwa hiyo tunamtia mbaroni kwa tuhuma zipi?”
266 MTAFITI
“Mauaji ya Mwantumu!” Kwakwa alimwambia.
“E bwana we! Kwa hiyo ushahidi…?” Pojo aliuliza.
“Upo… tena wa kutosha!”
“Mnh! Sasa kimewanukia!” Pojo alisema na kukata simu. Kule Liquid Diamond, Luis Kambesera alikatishwa kutoka kwenye mashaka yake na simu iliyoita kutoka pale mezani kwake.
“What?” Alihoji kwa kisirani.
“Simu yako kutoka wizara ya madini na nishati bosi…” Katibu muhtasi wake alimjuza, naye akawa makini ghafla.
“Oh, okay…” Alimjibu, kisha aliongea na huyo mtu aliyepiga kutoka wizara ya madini na nishati.
“Er, hello… Luis Kembesera hapa, nani mwenzangu?”
“Najua mlilofanya Luis!” Zay alimkoromea kwa hasira kwenye simu, na Luis akachanganyikiwa.
“Who is this? Na… unamaanisha nini…?”
“Mmechakachua ripoti ya Grayson Mochiwa na kulisaliti taifa nyie!” Zay alimtemea maneno yaliyotembeza ubaridi mwilini kwa Luis.
“Un... nasemaje wewe? Who are you?” Alibwabwaja.
“Halafu mkamuua Grayson!” Zay alizidi kumsimangia makosa yake.
“Ni nani wewe nakuuliza?” Luis alimaka, mtetemo hafifu ukisikika kwenye sauti yake.
“Ila mlipomuua na rafiki yangu Mwantumu…”
“Ah! Ni wewe!”
“… ndipo mlipokosea Luis. Nitawamaliza! Nitawaanika wazi wazi hadharani mafisadi na wauaji wakubwa nyie… mmelipwa kiasi gani kwa kulisaliti taifa namna hii, eenh?”
“Hujui usemalo wewe, na kama unayajali maisha yako…”
“Mtalipa kwa gharama ya juu sana kwa hilo Luis, take it from me… kwa kifo cha Mwantumu, mtalipa! Tena kwa riba kubwa kabisa!” Zay alizidi kumkoromea kwa chuki ya wazi.
“We mtoto hebu sikiliza wewe! Kama unayajali maisha yako machafu…”
Zay akamkatia simu.
“AAAAARGGHHH!” Luis alipiga ukelele wa ghadhabu na kuibamiza
267 Hussein Issa Tuwa
mezani ile simu. Katibu muhtasi aliingia mbio mle ofisini macho yakiwa yamemtoka pima.
“Kuna nini tena bosi??” Alihoji kwa mshangao.
“GET OUUUUUUUUTT!” Luis alimfokea huku macho yamemtumbuka kwa hasira.
Katibu Muhtasi alitoka mbio nje ya ofisi ile.
Luis alihisi mwili ukimtetemeka na akili ikiwa imeganda kwa muda. Alikuwa akihema kwa nguvu huku macho yakimtembea kama mjusi.
Aliinuka kutoka pale alipokuwa amekaa, akanyakua mkoba wake wa kazi na kuelekea mlangoni, kisha akasimama kabla hajaufikia ule mlango.
Naenda wapi sasa?
Alirudi na kuketi kwenye kochi lake pale ofisini. Alijiinamia na kuisubiri akili yake iganduke. Akili iligoma. Alichukua simu yake kutaka kupiga, lakini alihamanika pale alipoona kuwa mikono yake ilikuwa ikitetemeka vibaya sana kiasi hata kubofya namba za mtu aliyetaka kumpigia ikawa vigumu.
Oh, hell!
“MAIMUNAAAA!” Alimwita katibu muhtasi wake kwa kelele, anaye akaja mbio mle ndani, macho yakiwa yamemtumbuka kwa woga.
“Niitie Bilanga hapa… NOW!” Luis aliagiza, na katibu muhtasi akatoka mbio nje ya ofisi ile.
Baada ya kuongea na Pojo, Kwakwa akampigia simu Dokta Martha.
“Ulisema ripoti ya uchunguzi wako itakuwa tayari kesho sio…?” Alimuuliza.
“Yah, yaani kesho itakuwa tayari kukabidhiwa kwa askari wa kitengo cha ‘Anti-Albinism’, vipi kwani?”
“Na imeeleza kuhusu kilichokutwa kinywani mwa marehemu kama ulivyonieleza?”
“Of course… kwa nini isieleze hilo?”
“Good. Nafanyia kazi namna ya kukuletea mtu wa kumpima ili kutambua iwapo mabaki ya nyama ya binadamu yaliyokutwa kinywani kwa marehemu yametokana naye, sawa? Nataka niwe na uhakika iwapo hiyo ripoti yako
imeeleza hivyo… maana nitaomba kuitumia kwenye kesi yangu!” Kwakwa
268 MTAFITI
alimwambia.
“Mnh, na wewe! Sawa, hilo limo kwenye ripoti yangu!” Dokta Martha alimwambia.
“Good girl!” Kwakwa alimjibu na kukata simu.
Pojo akampigia kwamba tayari ameshapata kibali cha kumkamata Bilanga.
“Okay Sajenti. Tukutane kwenye ule mgahawa uliokuwa nje ya Liquid Diamond… tupate msosi kwanza pale halafu tuingie mzigoni. Kwamba leo hatulali halina ubishi, ila la kutokula halipo aisee... hii itakuwa ndio nafasi pekee ya kula. Chukua bodaboda uje fasta!” Alimwambia. Walipokuwa wanakula dakika kumi baadaye, simu ya Kwakwa ikaita.
“Inspekta! Nimegundua jambo kuhusu Liquid Diamond…! Njoo unitoe humu mahabusu haraka sana, muda wa kujifichaficha umeisha sasa… nataka kulipiza kifo cha rafiki yangu!” Zay alimwambia kwa wahka simuni.
“Wo, wo, woooo bibie, wo! Pole pole basi. Unamaanisha nini kuwa umegundua jambo kuhusu Liquid Diamond?” Kwakwa alihoji huku akimtazama Pojo aliyekuwa akimtazama kwa viulizo vingi. Kwa haraka haraka Zay akamwambia juu ya ule ugunduzi wake, na Kwakwa akabaki mdomo wazi.
“Un… una ushahidi juu ya hilo?” Alimuuliza kwa upole, na Pojo akazidi kumakinika na mjadala ule, na ilionekana kuwa Zay alimjibu kuwa anao ushahidi wa hicho akisemacho.
“Na umekuwa na ushahidi huo tangu lini kama naruhusiwa kuuliza?”
Kwakwa aliuliza kwa hasira baridi.
“Ah, mi sikujua kama ni ushahidi au ni kitu cha maana… mpaka niliposoma hii ripoti iliyowasilishwa na hiyo kampuni serikalini… ndipo nilipounganisha mbili na mbili nikapata jibu!” Zay alijitetea na Kwakwa akajizuia sana kumvurumishia matusi.
“Okay… subiri, tunakuja!” Alimjibu.
“What is it?” Pojo aliuliza, na Kwakwa akamweleza yale aliyoambiwa na Zay. Pojo alibakia kutikisa kichwa.
“Mtoto mjinga sana yule! Yaani kumbe alikuwa ana mambo yote haya halafu anatuacha siye tunahaha ovyo mitaani!” Alisema.
Kwakwa alikuwa amekunja uso kwa tafakuri nzito.
“Okay, kwa hiyo tunaenda naye huko alipoficha huo ushahidi sasa?”
269 Hussein Issa Tuwa
Pojo alimuuliza.
“Hapana. Tunamalizia msosi wetu kwanza, kisha tutaenda kumsikiliza. Huku kwenye hilo jengo hapo linalotazamana na Liquid Diamond… kuna mahala nilitaka kwenda awali halafu nikaahirisha. Tunaenda hapo kwanza kisha tunaenda kwa Zay…” Kwakwa alimjibu.
Ilikuwa ni saa nane na nusu mchana.
“Kwa nini tunakuja hapa kipindi hiki Inspekta, wakati naamini kuwa siku ya tukio tu la kuuawa kwa Grayson ndio ulitakiwa uje hapa kufanya upekuzi?” Pojo alimuuliza Kwakwa wakati wakiingia ndani ya lile jengo la ghorofa lililokuwa limepakana na lile la Liquid Diamond Inc.
“Nilikuja siku ile… Ila kwa siku ile sikujua nakwenda kumtafuta nani… leo ninajua nakuja kumtafuta nani hapa… lets go!” Kwakwa alimjibu. Pojo hakumuelewa, lakini akaamua kunyamaza tu, alijua angejua yote wakifika huko waendako.
Waliingia ndani ya jengo lile na kwenda moja kwa moja hadi ofisi ya utawala wa jengo na kujitambulisha kwa afisa tawala wa jengo, ambaye alikuwa ndiye msimamizi wa taratibu zote za ofisi kadhaa zilizopanga kwenye jengo lile.
“Ah, nakukumbuka wewe… si ndiye uliyekuja kuvunja mlango kule ghorofa ya nane siku ile yalipotokea mauaji jengo la pili?” Afisa tawala alisema, na Kwakwa akatabasamu.
“Yap, ndio mimi…”
“Haya, leo unataka kuvunja nini afande?” Afisa tawala aliuliza.
“Tunahitaji kuonana na wahusika wa usalama wa jengo tafadhali, kuna kesi ya jinai tunaifuatilia” Kwakwa alimwambia, na yule afisa tawala wa jengo akashangaa kidogo.
“Una maana kuna jinai nyingine tena… au ni mwendelezo wa yale yale ya siku ile?” Jamaa aliuliza.
“Ni upelelezi wetu wa tukio lile lile. Bado unaendelea… unaweza kutupeleka kwenye ofisi ya usalama wa jengo? Najua mnacho kitengo hicho kwa kuwa nimeona kamera kadhaa kwenye jengo hili…”
“Of couse… of course…!” Jamaa alisema huku akiwaongoza kwenye ofisi ya usalama wa jengo. Huko walikuta askari wawili wa kampuni binafsi ya ulinzi wakiwa wamekaa wakifuatilia runinga kadhaa zilizokuwa zikionesha maeneo mbali mbali ya jengo lile. Afisa tawala aliwatambulisha wale askari
270 MTAFITI
wawili na kuwataka wale askari wa kampuni ya ulinzi binafsi wawape ushirikiano.
Kutokea kwenye moja ya zile runinga mle ndani, Kwakwa aliweza kuona eneo la lango kuu la kuingilia ndani ya jengo lile, ambayo ilionesha watu wengi wakiingia na kutoka mle ndani, ilhali wengine wakiwa wameketi kwenye viti vya kusubiria pale kwenye eneo la mapokezi, na wengine wakiwa wamesimama mbele ya kaunta, wakiongea na wanadada wa pale mapokezi. Kwakwa aliioneshea kidole ile runinga iliyokuwa ikionesha eneo la lango kuu na mapokezi.
“Nahitaji kuona mikanda iliyorekodi matuko ya eneo hili… kwa siku tatu zilizopita…” Alisema.
Mmoja wa wale askari wa ile kampuni binafsi ya ulinzi alitaka kuleta ubishi, lakini alipokutana na jicho kali kutoka kwa Kwakwa, akagwaya. Walipewa furushi la mikanda maalum ya kurekodi matukio ambayo ilikuwa ni midogo kuliko ile iliyozoeleka kikawaida, na kuelekezwa kwenye chumba kingine ndani ya ile ofisi ya usalama, ambamo kulikuwa kuna runinga nyingine kubwa na deki maalum ya kuchezeshea ile mikanda.
Walikaa na kuanza kuangalia ile mikanda, mmoja baada ya mwingine. Muda ulizidi kwenda na kile alichokuwa akikitafuta Kwakwa hakikuonekana. Zay aliwapigia simu mara mbili, nao wakamwambia aendelee kuwasubiri.
Wakiwa wamebakisha mikanda miwili tu katika lile rundo la mikanda, ghafla Kwakwa alikurupuka kutoka kwenye kiti chake na kuiwahi ile runinga.
“Hapo, hapo, hapo!” Alimaka huku akioneshea kwa kidole chake ile picha iliyopita mbele ya macho yao pale kwenye runinga. Haraka Pojo aliurudisha nyuma ule mkanda na kwa pamoja wakaanza kuiangalia tena ile sehemu ambayo Kwakwa aliiona.
Ilikuwa ikionesha harakati za watu wakiingia na kutoka kwenye ule ukumbi wa mapokezi wa jengo lile, kupitia kwenye lango kuu. Katika harakati za watu wale, macho ya Kwakwa yalikuwa yamevutiwa na mtu mmoja mrefu aliyekuwa amevaa suti nyeusi, aliyeingia jengoni haraka sana akiwa katikati ya kundi la watu.
“Pozi hapo!”
Pojo akabonyeza sehemu kwenye rimoti ya runinga ile na ile picha ikaganda.
“Son of a bitch!” Pojo alisema kwa kutoamini pale alipojikuta akiitazama sura ya Chabbi Cheka akiwa amejitahidi kuinamisha uso wake bila
271 Hussein Issa Tuwa
mafanikio, akiwa katikati ya kundi la watu waliokuwa wakiingia ndani ya jengo lile.
“Tembeza kidogo mkanda halafu pozi tena…” Kwakwa alisema huku moyo ukimwenda mbio.
Pojo alifanya alivyoambiwa, na hapo Kwakwa akaziona vizuri tarehe na muda ambao lile tukio lilikuwa linatokea.
Ilikuwa ni tarehe ya siku ile ile ambayo Grayson Mochiwa aliuawa.
Na muda ulikuwa ni dakika kumi na tano kabla ya kuuawa kwa Grayson Mochiwa.
E bwana we!
“Kwisha habari yako Chabbi Cheka!” Hatimaye Kwakwa alisema kwa ushindi.
“Dah! jamaa kumbe nd’o aliyemuua Grayson aisee!” Pojo alisema.
“Yes! Ni yeye tu! Huu mkanda unamuweka mahala pa tukio, katika muda wa tukio, na kwenye siku ya tukio… lakini bila kitendea kazi cha tukio! Jamaa hana bunduki hapa! Inakwambia nini hiyo?” Kwakwa alisema na kuuliza.
“Ah, inaweza kuwa kaificha nguoni... si watu hawakaguliwi wakiingia humu bwana? Inawezekan—Mnh, hapana aisee…!”. Pojo alianza kujibu, lakini akawahi kujirekebisha na kupiga kimya.
Kwakwa alimtazama kwa makini.
“Hapana nini Sajenti?”
“Haiwezekani bwana! Kumuua mtu aliyeko jengo la pili kutokea dirishani kule juu mtu anahitaji bunduki kubwa zaidi ya bastola. Na kama huyu fala alipita na silaha yoyote pale langoni siku ile, basi ilikuwa ni bastola na sio bunduki kubwa ya wadunguaji…!” Pojo alisema.
“Haswaa! Jamaa atakuwa aliificha bunduki ndani ya hili hili jengo tangu awali… nadhani alikuwa ameiandaa makusudi kwa mazingira kama yale ya kifo cha Grayson… hawa jamaa hatari sana aisee!” Kwakwa alisema.
Wakiwa na ule mkanda uliomuonesha Chabbi akiingia ndani ya lile jengo, walirudi kwa afisa tawala.
“Tunauchukua huu mkanda kama ushahidi, kesi yetu ikiisha tutaurudisha. Wale askari wenu kule tumeshawaambia hivyo, na wamerekodi mwenye kumbukumbu zao nami nimesaini kuuchukua. Ila tunataka kwenda tena kwenye ile ofisi kule juu… je tukavunje tena mlango?” Kwakwa alisema na kuuliza. Jamaa akampa kadi maalum ya kuufungulia ule mlango haraka haraka.
“Hivi ile ofisi inamilikiwa na kampuni gani?” Kwakwa alimuuliza huku
272 MTAFITI
akiipokea ile kadi.
Jamaa alibofya kwenye kompyuta yake kidogo, kisha akampa jibu.
Kampuni ijulikanayo kama Al-Habibi Holdings ndiyo ilikuwa
imekodisha ofisi ile kwa muda wa mwaka mmoja. Mara moja Kwakwa na Pojo walijua kuwa ile ilikuwa ni kampuni hewa, na kwamba mmiliki
halali wa chumba kile ni wale wale Liquid Diamond Incorporated, kupitia mkono wa Chabbi Cheka.
Walielekea kwenye lifti ambayo ingewafikisha kwenye ghorofa ya nane, na kwenye kile chumba ambacho waliamini kuwa ndicho alichotumia
Chabbi kumdungua Grayson Mochiwa…
Ndani ya muda ule ule, Luis Kambesera alikuwa akimtazama Bilanga
kwa matarajio, wakiwa mle ofisini kwake, kwenye lile jengo lililokuwa
limepakana na lile walilokuwamo akina Kwakwa.
“Una hakika kakutamkia kuwa anao ule ushahidi, Luis?” Bilanga aliuliza.
“Sasa si ndo nakwambia mimi hapa Bilanga? Kasema anajua tuliyofanya kulisaliti taifa… na kwamba atatuweka wazi mbele ya hadhara… hilo halikwambii kuwa anajua analosema yule mtoto? Halikwambii kuwa ana ushahidi juu ya hilo?” Luis alimjia juu.
“Sasa kama anao anasubiri nini kuuanika?” Bilanga alihoji.
“Hata sijui! Na sitaki kusubiri kujua… hatua lazima zichukuliwe tena haraka sana… tumeshafikia mahala ambapo hatuwezi kurudi nyuma tena!” Luis alisema kwa wahka, kisha akaendelea, “… sipati picha akina Maginga na Jamilla wakisikia juu ya hili itakuwaje!”
“Wote wengine hawahitaji kujua lolote kwa sasa… wacha mi’ nilifanyie kazi hili…!” Bilanga alisema.
“Kivipi Bilanga, kivipi? Unajua huyo mtoto alipo?”
“Hapana… yaani binti kapotea ghafla tu jijini… nahisi wale askari watakuwa wamemficha, wajinga wakubwa!” Bilanga alisema, na Luis akatupa mikono hewani.
“Ah, sasa hiyo mbona ndio mbaya zaidi? Yaani awe na ushahidi wa jambo hili, halafu awe mikononi mwa askari na bado awe hajawaambia lolote kweli?”
“Si ndo nakwambia mtoto mwongo tu, malaya yule? N’na hasira naye sana yule mimi, shenzi zake… nitamtaiti tu!”
273
Tuwa
Hussein Issa
“Sasa how, Bilanga, na we’ hujui alipo? Mi’ naona ni kweli kuwa yuko na askari!” Luis alimhoji.
“Sasa mi’ n’tawafuatilia hao askari… nao ndio watakaonipeleka kwa huyo mtoto wa kike… na nikishamuona tu namaliza mchezo. Sasa awe ametoa hiyo siri au hajatoa mi’ sitajali… naua tu!” Bilanga alisema na Luis akamjia juu.
“Unamuua kivipi wewe? Hujui kuwa hapo cha msingi ni huo ushahidi anao dai anao? Unatakiwa uupore ule ushahidi kutoka himayani kwake kwanza, ndio mambo ya kumuua yafuate!”
“Poa tu!” Bilanga alimjibu kwa kisirani na kuinuka kuuendea mlango wa kumtoa nje ya ofisi ile. Alipofika mlangoni akamgeukia, na kumwambia, “Na sasa ni muhimu zaidi Chabbi akatolewa kule mahabusu, Luis… hakikisha hilo!”
“Yeah… ntalifuatilia!” Luis alimjibu, na kubaki akiwa ameduwaa mle ndani. Maneno ya Zay yalivuma tena kichwani mwake.
… Nitawamaliza! Nitawaanika wazi hadharani mafisadi wakubwa nyie… mmelipwa kiasi gani kwa kulisaliti taifa namna hii, eenh?
“Oooh!” Aligumia na kubaki akiwa amejishika kichwa pale ofisini kwake, moyo ukimwenda mbio huku ukimpiga kwa nguvu…
Kwenye lile jengo la jirani, Kwakwa na Pojo waliranda ndani ya ile ofisi yenye samani haba bila ya kuwa na uelewa wowote. Walikuwa wamesaka kila kona, wakijaribu kutafuta sehemu za siri mle ndani ambamo bunduki kubwa ingeweza kufichwa, lakini hawakuona lolote. Ilikuwa kama siku ile ambapo Kwakwa alikwenda kuchunguza chumba kile baada ya kifo cha Mochiwa.
“Ile bunduki ilikuwa humu ndani kabla ya kifo cha Grayson, Pojo! Na nina imani kuwa bado iko humu humu, kwani jamaa asingeweza kabisa kutoka na silaha ya aina yoyote ambayo ingemlazimu aibebe wazi wazi mkononi… na silaha iliyofanya mauaji yale, hasa ukizingatia risasi iliyokutwa kichwani kwa marehemu, ilikuwa ni kubwa!” Kwakwa alisema, na Pojo akawa amesimama huku amebutwaika.
“Nini wewe?” Kwakwa alimuuliza baada ya kumuona akiwa ameganda kama aliyebaini jambo.
Pojo aliioneshea kidole ile picha kubwa ya mlima Kilimanjaro iliyokuwa
274 MTAFITI
kwenye moja ya kuta za chumba kile.
“Mh, inspekta! Hivi kweli mtu ashindwe kuiwekea samani za maana ofisi yake kama hivi…” Alisema, na kuendelea, “... halafu apoteze muda kuweka fremu ya picha ya mlima Kilimanjaro kubwa namna ile? Hainiingii akilini aise!” Pojo alisema, kisha akaenda kuishusha ile picha kutoka pale ukutani. Wakabaki wakiutazama ule ukuta pale ambapo ile fremu kubwa ilikuwa imeuziba.
Pojo aliipapasa papasa ile sehemu ya ukuta iliyokuwa imefunikwa na ile fremu kwa muda lakini hakuweza kugungua chochote. Kwakwa aliketi kwenye kiti kilichokuwa mle ndani na kubaki akimtazama huku akili ikimwenda mbio.
“Awww, shiiiit!” Akiwa amekasirika na kuchanganywa na hali ile, Pojo aliupiga ule ukuta kwa ubapa wa ngumi yake na kugeuka kutaka kuondoka
Kwacha!
Ilisikika sauti kutokea nyuma yake na kutokea pale alimuona Kwakwa akiachia mdomo wazi. Aligeuka haraka kule ukutani ilipotokea ile sauti, naye kinywa kikamuanguka. Ile sehemu ya ukuta iliyokuwa imefunikwa na ile fremu, ilikuwa imejifungua na kuacha uwazi fulani pale ukutani.
Na ndipo walipoikuta ile bunduki kubwa itumiwayo na wadunguaji kwenye medani za vita, iliyotumiwa na Chabbi Cheka kumuondoa duniani mtafiti Grayson Mochiwa.
“Shenzi kabisa Chabbi Cheka!” Kwakwa alisema kwa mastaajabu.
“Ah, ama kwa hakika sasa habari yake imekwisha…!” Pojo naye aliafiki.
“Yap! Ushahidi unazidi kumkolea tu, Chabbi Cheka. Muda si mrefu atakuwa amenona tuhuma, Shenz Taip. Twende kwa Zay sasa!” Kwakwa alisema.
Walitoka wakiwa na ile bunduki ya Chabbi Cheka ikiwa imefunikwa kwa upande wa pazia waliloling’oa kutoka kwenye dirisha la chumba kile.
Ilikuwa ni saa tisa kasoro dakika kumi alasiri.
“Jamani hili gari halina kiyoyozi?” Zay aliuliza akiwa kiti cha nyuma cha gari aina ya Landrover Discovery mali ya jeshi la polisi, Kwakwa akiwa nyuma ya usukani na Pojo akiwa kando yake kule mbele.
“Hili ni gari polisi mwanadada, sio la kuendea pikiniki… AC ilikufa
275 Hussein Issa Tuwa
zamani na hakuna aliyejishughulisha nayo…” Kwakwa alimjibu kutokea kule mbele.
“Joto!” Zay alisema, huku akijipepea kwa mkono wake ambao hata hivyo haukusaidia kumletea huo upepo aliokuwa akiuhitaji, na ile hewa iliyokuwa ikiingia mle garini kupitia madirishani haikuwa na msaada wowote kwake.
Walikuwa wanaelekea kule kazini kwake alipoficha yale makabrasha ya Mwantumu yenye ushahidi kuwa Liquid Diamond walichakachua taarifa waliyoiwasilisha serikalini. Wale askari walikuwa wamemsema vibaya sana kwa kukaa na taarifa ile siku zote hizo bila kusema, naye utetezi wake ukawa ni ule ule. Kuwa hakuyaona yale makabrasha kuwa yana umuhimu mpaka pale alipopata wazo la kuitafuta ripoti iliyowasilishwa serikalini na kampuni ile dhalimu… na kuilinganisha na ile iliyokuwa kwenye mkoba wa Mwantumu.
Waliingia ndani ya ile kasino aliyokuwa akifanyia kazi, ambayo kwa muda ule wa ngwe ya pili ya mchana, bado ilikuwa haijachangamka. Wale askari walikuwa naye sambamba mpaka ndani, baadhi ya wafanyakazi wenzake
waliomuona wakimsalimia kwa macho ya kuuliza, naye hakuwapa muda wa kumuongelesha zaidi.
Walipofika pale kwenye eneo la kubadilishia nguo aliwaomba wale askari wamsubiri nje ya mlango kwani haingekuwa mwafaka kwao kama wanaume kuingia sehemu ya kubadilishia nguo ya akina mama.
“Okay… fanya fasta basi tuondoke hapa!” Kwakwa alimwambia.
Alipitiliza hadi kwenye lile kabati lake na kulifungua.
“Khah! What the…?”
Akabaki amepigwa butwaa, kwani vitu vyake vyote havikuwemo. Si nguo, wala si ule mkoba wa Mwantumu uliokuwa na yale makabrasha. Miguu ikamlegea na moyo ukamuingia ubaridi.
Alichanganyikiwa huku akizikodolea macho zile nguo alizozikuta mle kabatini. Hazikuwa za kwake kabisa.
Eh, Mungu wangu!
Akakaa sakafuni.
Mungu wangu! Ni nini kimetokea hapa, eenh?
Alijiuliza na akili ikamuwanga.
Hivi inawezekana kweli ikawa hawa shwaini wamekuja kuchukua hivi vitu vyangu na ule ushahidi muhimu?
276 MTAFITI
No Way!
“There you are! Nilisikia umeonekana mjengoni Zay… vipi wewe?” Sauti ya kiume ilimshitua na akaachia kiyowe cha mshituko huku akiigeukia ile sauti.
“Oh, bosi! Sh’k… sh’kamoo!”
Alikuwa ni bosi wao, raia wa Italia lakini anayeongea kiswahili kizuri sana.
“Ngu... nguo zangu wapi bosi, eenh? Nazitaka!” Zay alimwambia huku akimtazama moja kwa moja machoni.
“Jibu swali Zay! Vipi wewe? Hutaki kazi? Unatoweka tu bila taarifa za kueleweka? Sasa nyumba siku hizi inapunwa tu kule kwenye blackjack…!” Mtaliano alimkomalia, akimaanisha kwa kuwa Zay alikuwa ndiye mchezeshaji mzuri wa kamari ya ‘blackjack’ pale kwenye kasino, kutokuwepo kwake kulisababisha kasino yao ipunwe na wacheza kamari.
Zay alikuwa na mawazo mengine kabisa muda ule.
“Mbona hili kabati nimekuta limewekwa nguo zisizo sio zangu?”
“Kwa hiyo umekuja kuchukua nguo zako uondoke? Ndio umeacha kazi? Sisi bado tunakuhitaji hapa Zay… kama una matatizo maliza tu halafu uje uendelee, sawa?”
“Bosi! Nataka nguo zangu… unazo wewe?” Zay alikuja juu.
“Of course! Ilibidi niweke mchezeshaji mwingine kwa muda bwana, na ilibidi nimpe kabati lako… kila kitu chako kiko kwenye safe yangu ofisini… come!” Mtaliano alimjibu huku akiondoka kuelekea ofisini kwake, na Zay akashusha pumzi za ahueni huku akimfuata.
Duh!
Kule ofisini Mtaliano alifungua kabati lake la chuma na kumtolea nguo zake alizoacha kule kabatini kwake na ule mkoba wa Mwantumu uliokuwa na yale makabrasha. Aliukwapua ule mkoba kwa pupa na kupekua ndani yake.
Makabrasha yake yote yalikuwa vilevile alivyoyaweka.
Pumzi za ahueni zikamshuka.
“Sasa utarudi kazini lini Zay? Nafasi yako bado iko hapa…”
“I have to go boss. Ni kweli… nina matatizo kwa sasa lakini kama kazi yangu bado ipo basi nashukuru…!” Alimwambia huku akitoka nje ya ofisi ile. Alipofika mlangoni akasita. Akageuka. Ofisi ya bosi wake yule ilikuwa
277 Hussein Issa Tuwa
imesheheni zana zote muhimu za mawasiliano. Kompyuta, mashine za fotokopi, skana…
“Er, bosi naomba nitumie kompyuta yako mara moja basi… hivi niko safarini kwenda kwenye maziko ya rafiki yangu na sitakuwa na muda wa kutumia kompyuta… dakika tano tu!” Alimuomba, na yule bosi wake akamtazama kwa viulizo.
“Please bosi! Sina muda… kuna watu wananisubiri hapo nje!”
“Okay… fanya upesi. Na hakikisha ukimaliza matatizo yako unarudi kazini Zay, sawa?” Mtaliano alimwambia.
“Ndiyo bosi… ndiyo!” Zay alimjibu huku akiketi nyuma ya kompyuta ya bosi wake pale ofisini.
“Ukimaliza ufunge mlango wakati unatoka!” Bosi alimwambia huku akitoka. Zay wala hakumsikia, alikuwa amezama kwenye ile kompyuta akifanya alilodhani kuwa alitakiwa alifanye bila kusubiri.
Kule nje akina Kwakwa wakaanza kupata wasiwasi…
Pojo akampigia simu, akataka kujua kulikoni.
“Kila kitu kiko sawa afande… nipeni dakika nyingine kama kumi tu, kuna mambo ya kiofisi natakiwa niyaweke sawa kidog o!” Zay alidanganya.
Dakika kumi na tano baadaye alitoka nje ya ofisi ya yule bosi wake na kwenda kuungana na akina Kwakwa.
“Umepata?” Kwakwa alimhoji.
“
Yah… hii hapa…” Zay alimkabidhi ule mkoba wa Mwantumu, yale makabrasha yakiwa ndani yake. Mfuko mwingine wa plastiki uliokuwa na zile nguo zake nyingine alibaki nao mwenyewe.
Kwakwa akamkabidhi Pojo ule mkoba.
“Shikilia huu mkoba kwa moyo wako wote Pojo. Liwe liwalo, ima fa ima, usikutoke mikononi mwako. Kwa sasa huu mkoba ndio la msingi kwako, mengine yote yanafuatia. Tutaenda kutathmini kilichomo tukifika ofisini. Lets go!” Kwakwa alisema huku wakitoka.
Ile kasino aliyokuwa akifanyia kazi Zay ilikuwa maeneo yaliyojificha sana kule Msasani peninsula, na wakati wakirudi iliwalazimu wapite kwenye
mitaa pweke ya Oysterbay kabla ya kuja kutokea Toure Drive na hatimaye
278 MTAFITI
Ocean road, bandarini hadi kule kituo kikuu cha polisi au central.
Huko kote hawakufika.
Wakiwa katika moja ya ile mitaa pweke ya Oysterbay, Kwakwa alishtukia pikipiki moja kubwa ikichomoza kwa kasi kutokea kijimtaa cha pembeni na kuelekea kuwapita, lakini alitaharuki pale yule mwendesha pikipiki alipokuwa usawa wa dirisha lake, alipowatupia kitu kama kichupa cha pafyumu hivi ndani ya gari lao kupitia kwenye dirisha la ule upande wake.
“BOMUUU!” Kwakwa alipiga kelele huku akilipeleka gari pembeni, likiyumba vibaya. Hapo hapo mlipuko hafifu ulisikika mle garini na moshi mkali na mzito ukatanda gari zima, ukiwapalia na wafanya wakohoe ovyo. Zay alipiga kelele wakati lile gari likajibabatiza kiubavu kwenye mti kando ya barabara. Kwakwa akatupa macho kule mbele bila kujali ule moshi uliompalia huku ukimchonyota machoni. Alimuona yule mwendesha pikipiki akiruka kutoka kwenye pikipiki yake na kuwarudia mbio pale walipokuwa, bastola ndefu ikiwa mkononi mwake.
“Tumevamiwa, pumbavu zetuuuu!” Pojo alimaka huku akiuvaa begani ule mkoba, akipitisha mkanda wa mkoba ule kukikata kifua chake na hapo hapo akajitupa nje ya gari. Kwa pembe ya jicho lake alimuona mtu aliyevaa nguo nyeusi tupu huku kichwani akiwa amevaa kofia ya kuendeshea pikipiki iliyoziba sura yake, akiufungua kwa nguvu mlango wa dereva.
Kwakwa alikuwa ameshatoa bastola yake lakini ule moshi ulikuwa umemwingia machoni, akawa haoni kabisa. Alisikia vilio vya Zay kutokea kule nyuma, ndani ya gari.
“Toka nje mrembo!” Alibwata huku akijitahidi kutazama hivyo hivyo na moshi ukimchonyota.
Na hata pale alipokuwa akiufungua kwa nguvu ule mlango, yule mvamizi alimuona Pojo akiangukia nje ya gari kutokea mlango wa upande wa pili akiwa na mkoba begani. Akaubamiza tena ule mlango ambao ulimsukuma
Kwakwa na kumuangushia tena ndani ya gari, bastola yake ikimtoka na kuangukia nje ya gari lile.
Kule nje jamaa akainua bastola na kumwelekezea Pojo, ambaye aliwahi
kujitupa nyuma ya mti huku naye akichomoa bastola yake, lakini hapo
Kwakwa akazinduka na kuusukuma tena kwa nguvu ule mlango naye
akajitupa nje huku akikohoa na kujibiringisha hadi miguuni kwa yule mvamizi na kumgonga. Risasi ya mvamizi ikaenda hewani badala ya
kule kwa Pojo, sauti mithili ya chafya na mtoto mchanga ikisikika kutoka
279 Hussein Issa Tuwa
kwenye ile bastola iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti, au ‘perforated cylinder.’
Hapo hapo jamaa akamuinamishia Kwakwa ile bastola yake ili amlipue, lakini Kwakwa aliwahi kujigeuza pale chini na kumzungushia dochi kali lililompata jamaa sehemu ambapo kifua chake kilikuwa kinaishia na tumbo lake linaanzia, na jamaa akajikunja bila kupenda. Na hapo bastola ya Pojo ikakohoa, risasi ikamkosa yule jamaa kidogo sana. Jamaa akajitupa pembeni huku ameinama, akimuacha Kwakwa pale chini na kumkimbilia
Pojo huku akimtupia risasi za mfululizo na akipiga kelele kama kwamba
alikuwa hajali iwapo na Pojo naye atamtupia risasi na kumdhuru.
Pojo hakulitarajia hili na alihamanika huku naye akimtupia risasi yule
jamaa ilhali akirudi kinyuma nyuma, risasi za kila mmoja zikimkosa mwingine kwa bahati tu.
Huku nyuma Kwakwa alijiinua na kuiona ile hali. Aliangaza huku na huko kutafuta bastola yake na kuona kuwa ilikuwa imeangukia mbali na alipokuwa.
Shenz Taipp!
Alimkimbilia yule mvamizi kutokea nyuma.
“POJO KIMBIA NA USHAHIDIII!” Alibwata huku akimrukia yule mvamizi, akimkumba vibaya na wote wawili wakaenda chini kwa kishindo, bastola ikimtoka yule mvamizi. Kule alipokuwa, Pojo aligeuka na kujitupa nyuma ya mti, akajiweka sawa na bastola yake tayari kushambulia, akijua kuwa alikuwa amebakiwa na risasi mbili tu.
Kule kwa akina Kwakwa, mvamizi alijiinua haraka sana na kugeuka kwa pupa akimtafuta Kwakwa pasina kumuona.
“Hey!”
Jamaa akageuka nyuma haraka, kufuata kule sauti ya Kwakwa ilipotokea na akapokea teke kali la shingo lililomsukumiza pembeni, kisha akajirusha mzima mzima kumrukia adui yake. Kwakwa akampisha kiulaini naye
akapitiliza kama boya, na hapo hapo akamtandika teke jingine la kisogo na jamaa akaparamia vumbi huku akiserereka vibaya ardhini.
Muda huo gari lilitokea eneo lile, na dereva alipoona ule mpambano
akakoleza kasi na kutokomea vibaya sana. Lile gari liliwapoteza malengo kidogo, na Bilanga aliyekuwa kwenye mavazi ya kuendeshea pikipiki akatumia nafasi hiyo kurukia pikipiki yake na kuitia moto.
“Pummbaavv!” Kwakwa alipiga ukelele na kuirukia bastola yake
280 MTAFITI
iliyokuwa pale chini, akaikwapua huku akijibiringisha pale chini na kumtupia risasi mbili za haraka haraka. Moja ikamkosa, na moja ikaupiga usukani wa ile pikipiki, na Bilanga akayumba vibaya na ile pikipiki nusura aanguke.
Kwakwa alijiinua na kumtokea mbio huku akimtupia risasi nyingine mbili na Pojo naye alijichomoza kutoka nyuma ya ule mti na kumtupia risasi yule mvamizi, ambaye alinusurika na zile risasi zote kwa vile tu ile pikipiki ilikuwa ikiyumba vibaya wakati ule, kisha akakunja kona na kutokomea kwa kasi kutoka eneo lile. Mpango wake wa kwanza wa kuupora ule ushahidi wenye madhara makubwa kwao ulikuwa umeshindikana.
Kwakwa na Pojo walirudi mbio pale kwenye gari. Walimkuta Zay akiwa amejikunyata ubavuni mwa tairi la nyuma ya lile gari akilia huku akitetemeka vibaya sana.
“Okay, tuko salama… let’s get out of here!” Kwakwa alimwambia huku akimuinua kutoka pale chini na kumsukumia ndani ya gari kwa pupa.
281
Hussein Issa Tuwa
“
Wal… walitaka ku… ku… kutuua!” Zay alipayuka kwa wahka na woga, kama kwamba wenzake hawakuwa wakilijua hilo.
“Ni Bilanga yule… alitaka kuupora ule ushahidi, mwoga mkubwa! Twen’zetuni kabla raia hawajaleta kiwingu hapa!” Kwakwa alisema huku akitweta.
Waliingia kwenye gari lao na haraka Kwakwa akajaribu kuliwasha. Likakubali.
Akalitoa kwa pupa kutoka pale chini ya mti na kuliingiza kwa fujo kwenye ile barabara ya msasani, maarufu “Msasani Road”, akishika usawa wa kule kule ambako mvamizi Bilanga alitowekea na pikipiki lake kubwa. Ile barabara ilimfikisha kwenye makutano na barabara nyingine, barabara ya Ghuba. Alikunja kushoto kwa kasi na kuingia barabara ya Ghuba kwa lengo la kuifuata ili imfikishe Toure Drive.
“SAL-LAALA!” Alijikuta akibwata kwa hamaniko mara tu baada ya kuingia kwenye ile barabara, kwani kutokea kule alipokuwa akielekea, alimuona Bilanga akiingiza barabarani kwa kasi ile pikipiki yake, wazi kuwa alikuwa ameiegesha kando ya barabara kuelekea kule ambako alitaraji wao wangetokea. Honi kali ilivuma pale gari lililokuwa likitokea kule kwenye ile barabara ya Toure kuelekea kule wao walipokuwa wakitokea, liliposhtukizwa na namna Bilanga alivyoiingiza pikipiki yake barabarani kwa pupa bila kujali.
Na hata pale alipokuwa akikiona kitendo kile, Kwakwa alimuona Bilanga akihama kutoka upande wake wa barabara ile pweke na kuingia upande ule waliokuwapo kwa kasi ile ile ya ajabu, akiwa ameielekeza ile pikipiki moja kwa moja usawa wa gari lao huku akiwa amenyoosha mbele mkono wenye bastola hali kwa mkono mwingine akiwa amekamata usukani wa pikipiki yake.
Bila kujali kelele za hamaniko kutoka kwa wenzake mle garini,
282 MTAFITI
15
alijilazimisha kutokanyaga breki, na wakati huo huo alinyonga usukani na kulielekeza gari nje ya barabara, sio kwa kuikwepa ile pikipiki bali risasi alizozitarajia kutoka kwenye bastola ya yule hasimu wao.
“LALA CHINII!” Alibwata huku akilipeleka gari nje ya barabara.
Muda huo huo kioo cha mbele cha gari lao kikatawanywa vibaya kwa risasi, mvua ya chenga za vioo ikawanyeshea ovyo mle ndani, na wale wenzake wakaachia mayowe zaidi.
Kutokea nyuma yake ulisikika msuguano mkali wa matairi kwenye lami. Gari lao likaserereka vibaya. Mshindo mkubwa ukasikika pale gari lao lilipogongwa vibaya na gari lililokuwa nyuma yao na kusukumwa mbele huku likizungushwa nyuzi mia na themanini, mlango wake wa nyuma ukifunguka na Pojo akitupwa nje kama kimwanasesere.
Gari likasimama kando ya barabara huku likitikisika vibaya, likiwa limegeukia kule kule lilipotokea.
Bilanga aliiyumbisha pikipiki yake, akalikwepa lile gari lililoligonga gari la akina Kwakwa na kuruka haraka kutoka kwenye pikipiki yake. Akaliendea mbio gari la akina Kwakwa huku bastola yake ikiwa wazi mkononi.
Kwakwa alijitupa nje ya lile gari. Akapiga mweleka mzito. Aliinuka kwa kuyumba yumba huku akijaribu kuliweka sawa akilini mwake lile tukio, lakini Bilanga akaenda hewani na kumbabatiza kifuani kwa soli ya kiatu chake na kumpeleka tena chini kwa kishindo.
Hapo hapo Bilanga akaligeukia lile gari lao, akili yake ikiwa kwa Pojo aliyemuona akikimbia na ule mkoba hapo awali pale alipowashambulia mara ya kwanza wale askari mtaa wa pili tu kutoka pale waipokuwa wakati ule.
Aliufungua kwa pupa mlango wa nyuma wa lile gari na kukutana uso kwa uso na Zay aliyeachia yowe la woga, lakini Pojo hakuwemo. Aka!
Alitupa macho upande wa wa pili wa lile gari, na huko akamuona Pojo akijizoazoa kutoka kule alipoangukia huku bado akiwa na ule mkoba begani. Akamlenga kwa bastola yake.
Zay akaona kile kitendo, na hapo hapo akausukuma kwa nguvu ule mlango kwa miguu yake kutokea ndani ya lile gari na ule mlango ukambabatiza Bilanga tumboni na kifuani, naye akasukumwa nyuma, akapepesuka.
Alijiweka sawa na kutaka kumrudia Zay, kisha akaghairi na kuanza kulizunguka lile gari ili amfuate Pojo kule alipokuwa, lakini sasa Kwakwa alikuwa ameshajiweka sawa. Alimrukia mzima mzima na kumkumba
283 Hussein Issa Tuwa
kama mcheza raga, na wote wawili wakaenda chini kwa kishindo na kabla ya kila mmoja kubingirikia upande wake.
Kule alipokuwa, dereva wa lile gari lililowagonga akina Kwakwa akaona uhai ni bora kuliko kushuhudia mpambano au kusubiri askari wa usalama barabarani. Akatia gari lake moto na kuchomoka kwa kasi kutoka eneo lile, lakini hapo hapo alikanyaga breki kali huku yowe kubwa likimtoka pale alipoona askari mwingine wa jeshi la polisi akirukia barabarani mbele yake huku akiwa amemnyooshea bastola.
Gari likasota barabarani na kabla halijasimama vizuri yule askari alijirusha tena kando ya barabara na kukimbilia ubavuni mwa lile gari, akafungua mlango wa abiria kwa mabavu na kujitupa ndani.
“ENDESHA GARI WEWEE!” Pojo alimfokea yule dereva huku akimuoneshea bastola, na kama punda aliyetekenywa, dereva wa lile gari alizinduka na kulichomoa kwa kasi lile gari lake kutoka eneo lile.
Huku nyuma, Bilanga alibiringika wima na kugeuka kwa hasira kule alipohisi kuwa Kwakwa alikuwepo, akiwa ametanguliza bastola yake, lakini Kwakwa alikuwa ameshajitupa wima na akaipiga teke kali ile bastola kutoka mkononi mwake.
Bilanga akamsukuma kwa nguvu na kugeukia kule alipotaraji kumuona Pojo, na ndipo alipomuona yule askari akijitupa ndani ya lile gari jingine.
Ukelele wa ghadhabu ukamtoka na kutimua mbio kuiwahi pikipiki yake ili alikimbize lile gari. Kwakwa akamrukia na kumbabatiza ubavuni kwa soli ya kiatu chake, naye akajibamiza vibaya kwenye gari la akina Kwakwa na kuangukia goti moja pale chini.
Hapo hapa Kwakwa alimrukia tena, lakini Bilanga akajisukuma pembeni na soli ya kiatu cha Kwakwa ikaishia kujikita kwa nguvu kwenye ubavu wa gari lao. Bilanga akajiinua haraka na kumgeukia kwa ghadhabu. Akakuta Kwakwa akiwa amejipanga kwa mtindo wa karate kukabiliana naye.
“Ushahidi wa ufidhuli wenu uko mikononi mwetu sasa, shenzz taipu wewe! Jisalimishe!” Alikoromewa.
Watu wachache walianza kukimbilia eneo lile kuona kilichokuwa kinaendelea.
“Kamsalimishe mama’ako!” Bilanga alimaka huku akimrukia kwa ghadhabu. Kwakwa akajizungusha ili amkwepe lakini mwenzake hakuwa na nia ya kumshambulia bali kumtia mikononi. Akajikuta amekwidwa shati sehemu ya kifuani. Akaishika ile mikono iliyomkamata shati na kujaribu kumtupa yule jamaa kwa judo kali, lakini hapo kofia gumu la kuendeshea pikipiki lililokuwa kichwani kwa Bilanga likamshukia kwa
284 MTAFITI
nguvu sana utosini.
Maumivu makali yakamtambaa huku akihisi vimulimuli vingi vikielea mbele ya macho yake.
Kabla hajajiweka sawa, Bilanga akamshindilia bichwa jingine huku bado lile kofia lake gumu likiwa kichwani kwake, na kwa mara ya pili Kwakwa akahisi mlipuko wa maumivu makali sana pale utosini alipopigwa mara ya kwanza, huku vile vimulimuli vilivyokuwa vikielea mbele ya macho yake vikififia na maungo yakimlegea.
Kutokea kule kwenye gari, Zay aliiona ile hali, na akajua kuwa Kwakwa alikuwa amezidiwa. Akatoka nje ya lile gari na kuanza kutimua mbio huku akipiga kelele za kuomba msaada.
Bilanga alimwachia Kwakwa na kurudi nyuma tayari kumshindilia teke lakini alimuona yule askari mbabe akienda chini kama mlevi.
“Kih… mbia… Zz… zaiiih!” Kwakwa alijitahidi kumpigia Zay kelele akiwa pale chini. Bilanga aligeukia kule kwa Zay, na hapo hapo akatimua mbio kumkimbiza, akimwacha Kwakwa akisambaratika chini bila kizuizi.
Kwakwa alijitahidi kuinuka lakini kichwa kilimuwia kizito, kizunguzungu kilimwelemea, na kiza kikamtanda machoni. Akaanguka tena chini. Alijua kuwafahamu zilikuwa zinamhama na hakuwa na la kufanya.
Sasa wale wapita njia wachache nao walianza kumpigia Bilanga kelele, lakini yule mtu mkubwa alipiga hatua nne kubwa na kumdaka shingo Zay kutokea nyuma na kumvuta kwa nguvu.
“Bilan… ngaa!” Kwakwa aliita kwa taabu huku akimuona kwa shida jinsi yule jamaa akimtia Zay mikononi.
“Noo! Niachh…” Zay alianza kubwata, lakini hapo hapo Bilanga akamshindilia bichwa la nguvu kisogoni kwa lile kofia alilokuwa amevaa, na Zay akatepweta mikononi mwake.
Hapo hapo Bilanga akamkwapua na kukimbia naye akiwa amembana kwapani mithili ya jamvi lililosokotwa, kuelekea kwenye lile pikipiki lake kubwa.
“Zah… Zaiii…!” Kwakwa aliita kwa fadhaa, kisha kiza kikamgubika na fahamu zikamtaliki.
Alipozinduka alijikuta akiwa amezingirwa na raia wachache waliokuwa wakijibidiisha kumsaidia, wakiwa wamemmwagia maji usoni. Alikurupuka wima na kupepesuka.
285 Hussein Issa Tuwa
“Tulia kwanza afande... tulia!” Mmoja wa wale raia alimwambia huku akimshika bega kumsaidia. Akaupangusa mkono wa yule raia kutoka begani kwake, huku akijiegemeza kwenye gari lao lililobondeka.
Alisikia raia mwingine akimpa pole, lakini hakumjali.
“Zay...? Zah... kuna binti nilikuwa naye! Aliokoka?” Aliuliza kwa wahka huku akitembeza macho kwa pupa huku na huko eneo lile, akihisi kizunguzungu chepesi.
“Ah! Lile jambazi limemchukua...!” Yule raia alimjibu, na Kwakwa akahisi ukakasi kinywani. Taswira ya Bilanga akiiendea mbio pikipiki yake huku akiwa amembana Zay kwapani kwake kama kijimzigo kisicho maana ikamrudia.
“Oh, Shit!” Alinong’ona kwa hasira.
Mkono wake ukapapasa pale kichwani alipopigwa na Bilanga. Alihisi maumivu makali kutoka kwenye uvimbe uliochipua eneo lile. Kinyongo kikali kikachipua moyoni mwake dhidi ya lile jitu kubwa lenye kichwa kidogo.
Muda huo ving’ora vya magari ya polisi vilisikika vikielekea eneo lile, na kama siafu waliodondoshewa kaa la moto wale raia wakaanza kutawanyika, kila mmoja na kwake. Alitaka kuwaita ili wampe maelezo zaidi, lakini alijua hawangerudi. Hakuna aliyetaka kujitia ushahidi mbele ya polisi, naye hakuwalaumu.
“Dah! Huyu Bilanga huyu!” Kwakwa alimlaani yule hasimu wake huku akijikung’uta vumbi, kile kinyongo kikali kilichomchipua moyoni dhidi yake kikinawiri kwa kasi.
Kichwa kilikuwa kinamgonga vibaya sana na akajiwekea ahadi ya kumlipizia kisasi kizito yule adui yake pindi watakapokutana tena.
Alibaki akiwa ameegemea lile gari lao huku akiyatazama magari mawili ya polisi yakielekea kwa kasi pale alipokuwa, bila shaka baada ya kuliona lile gari lake la polisi likiwa kando ya barabara katika hali isiyo ya kawaida.
Dakika mbili baadaye askari wa jeshi la polisi walifika pale alipokuwa, na baada ya salamu mwafaka na kutambulishana, kiongozi wa ule msafara alimfahamisha kuwa walikuwa wanatokea kituo cha polisi cha Oysterbay na kwamba walipewa taarifa kwa njia ya simu na Sajenti Pojo kuwa kulikuwa kuna afisa wa polisi aliyekuwa matatani dhidi ya jambazi hatari sana eneo lile na kwamba msaada ulikuwa unahitajika.
“Ni kweli... ila bahati mbaya jambazi limewahi kutoroka...” Kwakwa
286
MTAFITI
alisema kwa hasira.
“Ina maana limekushinda nguvu?” Kiongozi wa ule msafara alimuuliza kwa kushutumu, na Kwakwa akamkata jicho kali.
“Labda tuseme limeniotea tu!” Hatimaye alimjibu huku akigeuka na kuingia kwenye gari lake.
“Ah, sasa unaenda wapi?” Yule askari alimuuliza.
“Harusini.” Kwakwa alimjibu kwa jeuri, na wale askari wakaachia miguno ya mshangao.
“Inspekta... si’ tumekuja kutoa msaada hapa, halafu wewe...” Yule kiongozi wa msafara alimjia juu, akishindwa kumalizia kauli yake kwa hasira.
Kwakwa alibamiza mlango wa gari lake na kuombea gari lile lisimgomee kuwaka.
Akapiga stata na gari likavuma kwa nguvu huku likitoa muungurumo usio wa kawaida. Akaondoka kwa kasi kutoka eneo lile bila hata ya kuwatazama wale wenzake aliowaacha vinywa wazi.
Kabla hajafika kituoni kwao simu yake iliyokuwa sehemu fulani mle garini ikaanza kuita. Akaegesha gari pembeni na kuichomoa kutoka pembeni ya kiti cha dereva ilipokuwa imeangukia bila shaka wakati wa hekaheka walizokumbana nazo.
Ilikuwa ni namba ya Zay ikiita.
Alikunja uso kwa muda huku akiitazama ile simu ikiendelea kuita, kisha akaikata na kuitupia kwenye kiti cha abiria. Akarudisha gari barabarani na kuendelea na safari yake.
Ile simu iliita mara mbili zaidi kabla hajafika pale kituoni kwake, na mara zote hizo hakuipokea.
Alimkuta Pojo akimsubiri kwa wahka pale kwenye eneo la mapokezi pale kituoni kwao.
“Vipi afande? Umewafanya nini wale askari wa Oysterbay?” Pojo
alimlaki kwa swali, wahka mzito ukijidhihirisha usoni kwake, na kabla
Kwakwa hajamjibu akaendelea, “Wamenilalamikia sana!”
“Achana nao!” Kwakwa alimjibu huku akipitiliza kuelekea ofisini kwake kwa mwendo wa haraka.
287 Hussein Issa Tuwa
Pojo akamfuata huku uso ukiwa umemjaa viulizo.
“Na wewe...? Uko poa? Na Zay…? Yuko wapi?” Maswali yalizidi kumtiririka Pojo.
“Ule ushahidi... uko salama?” Badala ya kumjibu, Kwakwa alimtupia swali lililokuwa la msingi zaidi kwake kwa wakati ule.
“Oh, Yes. Uko salama kabisa afande... si uliniambia kuwa lolote liwalo miye wajibu wangu ulikuwa ni kuunusuru ule ushahidi?” Pojo alimjibu kwa mashaka huku akiendelea kumfuata kwa mwendo wa haraka.
“Safi! Umefanya vyema sana... vile ndivyo haswa nilivyotaka ufanye kwenye mazingira yale!”
Waliingia ofisini kwa Kwakwa na kujifungia.
“Zay yuwapi sasa?” Pojo alihoji tena.
“Bilanga kamteka.” Kwakwa alimjibu huku akijipapasa pale alipotolewa nundu na Bilanga.
“Kamteka!!?” Pojo alimaka.
“Ndiyo… na mashahidi wachache waliokuwa eneo la tukio wamelithibitisha hilo.”
“Ina maana... we’ mwenyewe hukumwona wakati akitekwa?” Pojo alimtumbulia macho.
“Nilimwona kwa shida kabla sijapoteza fahamu, na nilipozinduka mashuhuda wakanithibitishia hilo.”
“Ulipoteza fahamu?” Pojo akamaka tena.
Kwakwa akasonya na kutikisa kichwa kwa kukereka. Kile kidonge cha Bilanga kumpiga mpaka akazimia kilikuwa kichungu sana kukimeza. Ukimya wake ulikuwa jibu tosha kwa Pojo.
“Sasa umechukua hatua gani kumfuatilia Zay?”
“Sijachukua hatua yoyote mpaka sasa… ila nilipigiwa simu kwa namba yake wakati nakuja huku…” Kwakwa alimwambia.
“Aha! Akasemaje? Kwa hiyo yuko salama?” Pojo alisaili kwa bashasha.
“Sijui…” Kwakwa alimjibu na Pojo akatoa sauti ya kustaajabu, “… kwa sababu sikuipokea.” Kwakwa alifafanua.
Pojo akamtumbulia macho na kumshikia kiuno.
“Yaani Zay anatekwa na Bilanga, halafu muda mfupi baadaye anakupigia simu na wewe huipokei… makusudi? Afande niwie radhi… hivi uko vizuri kichwani kweli leo wewe?” Alimuuliza.
Kwakwa alimkata jicho.
288
MTAFITI
“Nitajifanya sijaisikia hiyo kauli yako ya utovu wa adabu Pojo…”
“Ndio maana nilikutaka radhi mapema afande, lakini hiyo ni kwa kuwa unayoniambia hayaniingii akilini kabisa!” Pojo alisema huku akiketi kitini.
“Hebu lete huo ushahidi tuuone kwanza, kisha ndio tuelezane kwa kituo kuhusu Bilanga na Zay. Hiyo simu itapigwa tena tu.” Kwakwa alimwambia.
Muda huo simu ya Kwakwa ikaita tena.
“Si n’likwambia?” Kwakwa alisema huku akimuoneshea Pojo ile simu, jina la Zay likionekana wazi wazi pale kwenye kioo cha ile simu.
“Oh, afadhali… sasa si unaipoke— Khah!?” Pojo alianza kuuliza lakini akaishia kumaka pale alipoona Kwakwa akiikata ile simu na kuiweka ndani ya droo ya meza yake kisha akaifunga ile droo kwa kuibamiza.
“Afande!!” Alibwata huku akimtazama kwa mshangao mkubwa.
“Hebu kwanza tuuone huo ushahidi uliotaka kutupotezea maisha, Pojo! Baada ya hapo nd’o tuongelee kilichojiri baada ya we’ kukimbia nao… kisha nd’o turudi kwenye hii simu ya Zay, sawa?” Kwakwa alimwambia.
Pojo alitaka kupinga, lakini jicho kali la Kwakwa likamwambia asiendelee kuhoji suala lile.
“Sasa tunatia ndani watendaji wote wa Liquid Diamond, bloody suckers!
Yaani hawa jamaa ndio wamelisaliti taifa namna hii?” Kwakwa alisema kwa hasira baada ya kuzisoma zile ripoti mbili zinazoongelea suala moja
lakini kwa maudhui mawili tofauti kabisa.
“Ni kweli kabisa afande, hii inadhihirisha kabisa kuwa hawa jamaa waliipa serikali ripoti potofu kwa makusudi... kwa maslahi yao binafsi!”
Pojo alidakia.
“Achilia mbali hilo la kuipotosha serikali, ambalo moja kwa moja linawatia kwenye kosa la kuhujumu uchumi… ambalo ni sawa na uhaini…”
Kwakwa alisema, na kuendelea, “… zito zaidi hapa ni kwamba hizi ripoti
mbili zinathibitisha kabisa kuwa Liquid Diamond inahusika moja kwa moja na vifo vya Grayson Mochiwa, na Mwantumu!”
“Nakubaliana nawe, afande.”
“Of Course inabidi ukubaliane nami! Sababu za Liquid Diamond kuwauwa wale watu ziko wazi kabisa hapa Pojo!” Kwakwa alisema huku
akizioneshea zile ripoti mbili, kisha akatikisa kichwa kustaajabia namna
289 Hussein Issa Tuwa
ule ushahidi ulivyopatikana na jinsi ulivyoigeuza ile kesi.
“Yaani hapa ni kwamba Zay kaimaliza hii kesi, Pojo… imekwisha. Kilichobakia ni kuua ndege wawili kwa jiwe moja tu sasa.” Kwakwa alisema.
“Sijakuelewa… ndege wawili kwa jiwe moja?” Pojo aliuliza.
“Kumkomboa Zay…” Kwakwa alimjibu huku akimuinulia dole gumba la mkono wake, kisha akamuinulia kidole chake cha shahada baada ya kile cha gumba, “… na kuwatia mbaroni akina Luis K!” Alimalizia.
“Oh, okay… nimekusoma. Sasa si ungenieleza kwanza kile kilichojiri kule barabarani hata Bilanga akamteka Zay?” Pojo alimwambia.
“Haina shida Pojo…” Kwakwa alimjibu, kisha akamuelezea kile kilichojiri.
Alipomaliza, Pojo alibaki akiwa amekunja uso kwa tafakuri.
“Sasa… Bilanga kamchukua Zay ili iweje bosi, maana ushahidi tayari siye tunao. Hainiingii akilini hii!” Alisema huku bado uso wake ukiwa umekunjamana kwa tafakuri.
“Kwa nini haikuingii akilini? Huoni kwamba kamchukua Zay ili iwe kama kiokozi cha huo ushahidi? Kwamba tumpatie huu ushahidi ili naye aturudishie Zay?” Kwakwa alimwambia huku akimtazama kwa makini.
Pojo akafyatua sauti ya kukereka.
“Ah, tatizo huu ushahidi ni wa maandishi, Afande. Siye si tunaweza kuutoa fotokopi tu na kubaki na nakala? Unataka kuniambia Bilanga na mabosi wake wameshindwa kulijua hilo?” Alisema na kuhoji.
“Uko sahihi. Na iwapo tungekuwa tunapambana na Bilanga peke yake ningesema inaweza kuwa halielewi hilo… lakini kwa kuwa yuko na watu kama akina Luis K na yule mwanasheria wao…”
“Suleiman Mwangi…”
“Yes, yule! Hatuwezi kukubali kuwa hawalijui hili… wanalijua sana, ila wana jambo wanalojiaminisha kwalo tu ndio maana wanaudai huu ushahidi pamoja na kujua kuwa tunaweza kuutoa kopi.”
“Nakubali. Kwa sababu kimsingi walitakiwa waupate huu ushahidi kabla haujaingia mikononi mwetu. Sasa madhali tayari uko mikononi mwetu, suala linalobakia ni kukijua hicho wanachojiaminisha nacho kiasi wanalazimisha tuwapatie huu ushahidi ilhali wanajua wazi kuwa tunaweza kuutoa kopi.” Pojo alimwambia kwa kirefu, na Kwakwa akatabasamu.
“Uko vizuri Sajenti. Hivyo ndivyo akili ya mpelelezi inapaswa iwe.”
290 MTAFITI
“Ahsante… lakini bado sijapata jibu la swali letu la msingi… kwa nini
Bilanga kamteka Zay katika mazingira kama haya?”
“Kuna njia moja tu ya kulijua hilo.” Kwakwa alimwambia.
“Ambayo ni ipi hiyo, afande?” Pojo alimuuliza, lakini hapo mzizimo ukasikika kutokea kwenye droo pale mezani ya Kwakwa. Badala ya kujibu swali aliloulizwa, Kwakwa aliifungua ile droo na kutoa simu yake iliyokuwa inaita kwa mtindo wa kuzizima, bila kutoa mlio. Alimuashiria Pojo asubiri huku akiipokea ile simu na kuiweka kwenye spika, ili wote wasikie.
“Afande Kwakwa! Mpe anachotaka huyu mtu please! Atani-YALAAAH!”
Sauti ya Zay ilivuma kwa wahaka kutoka kwenye ile simu, kabla haijakatishwa na kichapo kikali cha kofi kilichomfanya amalizie kauli yake kwa ukelele wa uchungu.
Pojo aliuma meno kwa hasira na akafinya macho kwa uchungu, Kwakwa akamung’unya midomo.
“Kwakwa upo hapo?” Bilanga alidakia.
“Unataka nini, Bilanga?” Kwakwa aliuliza kwa utulivu mkubwa.
“Kwa nini ulikuwa hupokei simu muda wote, fala wewe?” Bilanga alimfokea simuni, na Kwakwa akamcheka.
“Kwa kuwa nilijua kuwa ni wewe ndiye uliyekuwa unapiga tangu mwanzo, ukitumia simu ya Zay. Nilikuacha utapetape kwanza.” Alimjibu, na Bilanga akasonya.
“Ujinga wako umemponza huyu binti sasa! Nimemtesa sana mimi kwa kiburi chako!”
“Poa tu.”
Kimya kikapita, bila shaka silo jibu ambalo Bilanga alilitaraji.
“Vipi umeishiwa vitisho?” Kwakwa alimhoji.
“Sa’ s’kia we’ zoba. Ukitaka kumuona tena huyu Malaya——”
“Malaya mama’ako!” Sauti ya Zay ilisikika. Ikafuatiwa na kichapo kikali cha kofi, na kwa mara nyingine wale askari walimsikia Zay akitoa kilio cha maumivu.
“Wallahi nikikutia mikononi utajuta kuzaliwa Bilanga.” Kwakwa alimwambia kwa utulivu usio shaka.
“Kama ulivyonijutisha kule barabarani leo hii, sio?” Bilanga alimjibu kwa kejeli, na Kwakwa akauma meno kwa hasira.
“Muda mfupi tu ujao, Bilanga. Utajuta. Sana tena!” Kwakwa alimtabiria majuto makubwa hasimu wake, ambaye alimfyatulia cheko ya bezo.
291 Hussein Issa Tuwa
“Mi’ huniwezi zoba wewe! Usijitie ushababi usio kuwa nao hapa. Sasa kama n’livyokuwa nasema… ukihitaji kumuona tena huyu Malaya koko hapa hakikisha unaniwasilishia huo mkoba aliokimbia nao yule kijakazi wako, na kila kilichomo ndani yake. Umes’kia wewe?” Bilanga alimkoromea kwa tambo.
“Vizuri sana. Taja muda na mahala Bilanga, nami nitakuwasilishia ukitakacho.” Kwakwa alimwambia kwa utulivu ule ule.
“Utapokea ujumbe mfupi ukiwa na maelekezo.” Bilanga alimjibu na kukata simu.
Wao wakatazamana.
“Inakuingia akilini hii, Afande?” Pojo aliuliza.
Kwakwa alikuwa amekunja uso kwa tafakuri.
“Kuna kitu hakipo sawa aisee…” Alisema kwa namna ya mtu anayejiwazia kwa sauti.
“Hakipo sawa kweli kweli afande! Mi’ siamini kuwa hawajui kwamba tunaweza kutoa nakala ushahidi wote huu na tukabaki na nakala zote.”
Pojo alisema.
“Kwa nini Zay kaniambia nimpe Bilanga anachotaka?” Bado Kwakwa alikuwa anaongea kama anayejiwazia kwa sauti.
Pojo akamshangaa.
“Zay si ameteswa afande? Lazima akwambie vile ili asiendelee kuteswa! Hilo nalo la kuuliza?” Alimjibu kwa maswali.
Kwakwa akamkata jicho huku bado akiwa amezama kwenye tafakuri. Pojo akabetua mabega na kubaki akimtazama.
“Hivi we’ unaona Zay ni mtu wa kukubali kushindwa kirahisi rahisi tu yule, hata kama ameteswa?”Alimuuliza.
“Ah afande, yule mtoto wa kike bwana! Akiteswa kidogo tu atafanya chochote atakachoamriwa…”
“Na bado Bilanga alipomwita malaya akadiriki kumwambia kuwa mama yake ndiye malaya pale pale kwenye mateso? Wakati muda mfupi tu uliopita katoka kutulilia kuwa tumpe tu Bilanga huu ushahidi kwa hofu kuwa tusipofanya hivyo yeye atauawa? Hapana aisee… kuna kitu hakipo sawa hapa, Pojo.” Kwakwa alisema.
“Kwa hapo mi’ sikuelewi afande.”
“Fikiri zaidi Pojo! Zay kweli akubali ushahidi urudi kwa Bilanga na kifo cha rafiki yake kikose kulipizwa? Kirahisi namna hii?” Kwakwa alizidi
292
MTAFITI
kumchagiza.
“Afande, kwani we’ unaonaje? Maana mi’ sielewi unaelekea wapi na haya maswali yako…” Pojo alimwambia kwa kutatizika.
Kwakwa aliguna na kupitisha kimya kwa muda.
“Sawa. Hebu tusubiri hayo maelekezo yao basi…” Hatimaye alisema baada ya kushusha pumzi ndefu.
“Sawa afande, lakini kabla simu ya Bilanga kuingia… ulikuwa unasema kwamba kulikuwa kuna njia moja tu ya kujua ni kwa nini Bilanga na wenzake wamemteka Zay huku wakijua kuwa tunaweza kuutoa kopi huu ushahidi?”
Kwakwa alimtazama kama kwamba hakuwa akielewa anachoongelea.
“Oh, wakati ule? Nilikuwa nasema kuwa njia pekee ni kusubiri madai watakayokuja nayo kwa kuwa nilijua wangeendelea kutupigia simu tu, kwa kuwa wakitakacho tunacho.”
“Na sasa ndio wameshapiga… lakini jibu bado hatujalipata.”
“Si atatuma ujumbe wa simu …? Tutajua tu, Sajenti wangu.” Kwakwa alimjibu kwa kujiamini.
Walibaki kimya mle ndani kwa muda mfupi tu, kisha mlio wa ujumbe mfupi ukarindima kutoka kwenye simu ya Kwakwa.
“Kipyenga hicho!” Kwakwa alisema huku akiichukua simu yake na kutazama ujumbe aliotumiwa.
Fika kwenye machimbo ya mawe yaliyofungwa eneo la kunduchi ndani ya saa moja kutoka sasa. Ukitokea Mwenge machimbo yatakuwa kushoto kwako. Alama kubwa ni Mbuyu mkubwa katikati ya machimbo yale. Utaona kitambaa kikubwa cheupe kinapepea kwenye moja ya matawi ya mti huo. Uje peke yako. Usije na gari, NA ULETE NYARAKA
HALISI!
Alipomaliza kuusoma ujumbe ule uliotumwa kutokea kwenye namba ya Zay, akampa Pojo ile simu ili naye ausome. Pojo aliipokea ile simu na kuusoma.
Akamtukania Bilanga mama yake huku akimrejeshea Kwakwa ile simu.
“Mshenzi anajua kuwa tutautoa kopi huu ushahidi, ndio maana anasisitiza kuwa tupeleke nyaraka halisi!” Alisema.
“Nipeleke, sio tupeleke!” Kwakwa alimrekebisha, huku akiinua mkono wake nakutazama saa yake.
293 Hussein Issa Tuwa
Muda ulikuwa ni saa kumi na moja kasorobo jioni.
“Ah, sasa unataka kuniambia na wewe utafuata maelekezo yake hayo?”
Pojo alimhoji.
“Kama alivyotaka!” Kwakwa alimhakikishia, na Pojo akatupa mikono hewani kwa kukata tamaa.
“Kwa nini lakini, Afande? Huyu ni mhalifu, na sisi ni serikali! Kwa nini atuwekee masharti namna hii?”
“Kwa kuwa anaye mtu wetu, ambaye anajua kuwa hatutaki adhurike.”
“Mi’n’litaraji tutatumia nafasi hii kumzidi kete na kumuweka chini ya ulinzi! Nilitaraji tungeenda pamoja.” Pojo alizidi kulalama.
“Ni kweli, lakini hata kama ningejitia kukubali sharti lake halafu nikaenda nawe kwa uficho, unadhani tungeendaje huko kama si kwa kukuficha kwenye buti la gari nitakaloenda nalo? Sasa ye’ keshasema kuwa nisiende na gari. Unadhani ni kwa nini? Ni kwa kuwa tayari amelitarajia hilo. Kwa hapa huyu bwege katubana kila kona!” Kwakwa alisema.
“Dah!(akamtukania tena Bilanga mama yake) ina maana na siye nd’o tunamtii tu mshenzi yule kama mabwege, afande?” Pojo alilalama.
“Una wazo tofauti lenye tija, Sajenti?” Kwakwa alimhoji huku akimtazama kwa kutahini.
Pojo akafyatua ulimi na kutikisa kichwa kwa kutoridhika.
“Kuna msemo usemao ‘ukitaka kuruka mbele na ufike mbali, sharti kwanza ukubali kurudi nyuma’, Pojo… hapa lazima tukubali kurudi nyuma tu.” Kwakwa alimwambia, na Pojo akafyatua kicheko cha simanzi.
“Na huyo ni nani sasa, Shaaban Robert?” Alimuuliza kwa kukereka.
“Hapana. Ni methali ya kihindi hiyo… na naona inaleta mantiki sana kwenye hali tuliyo nayo hivi sasa.” Kwakwa alimjibu.
“Kwa hiyo mi’ nibaki nakusubiri tu hapa?” Pojo alimuuliza.
“Akili kichwani mwako, Pojo. Niletee yale makabrasha niende zangu miye!” Kwakwa alimjibu.
Pojo alitekeleza bila kutia neno.
Kwakwa aliichukua ile ripoti halisi ya mtafiti Greyson Machibya, akainuka nayo hadi kwenye kabati la bati lililokuwa kwenye kona ya ofisi yake na kufungua droo mojawapo kwa ufunguo maalum alioutoa kwenye droo ya meza yake. Akatoa kifaa cha kubania makarasi na kuongezea kuibana ile ripoti kwa pini mbili zaidi, kisha akakirudisha kile kifaa kwenye ile droo.
“Nipe hiyo nakala ya huu ushahidi.” Alimwambia Pojo, ambaye alimpa
294 MTAFITI
bila ya kutia neno. Kwakwa akaiweka ile nakala ya ushahidi ndani ile droo ya lile kabati la bati na kuikomea ile droo.
Akaiweka ile ripoti halisi kwenye ule ule mkoba waliotoka nao kule kazini kwa Zay kabla hawajavamiwa na Bilanga kule barabarani.
“Narudi sasa hivi!” Alimwambia Pojo huku akitoka nje ya ile ofisi, ule mkoba akiwa ameuacha pale mezani kwake.
Alirudi dakika kama kumi baadaye akiwa amefumbata kofia jeupe la kuendeshea pikipiki kwapani huku akiwa ameshikilia ufunguo wa pikipiki ya jeshi la polisi mkononi.
Aliufungua tena ule mkoba na kuhakikisha kuwa ule ushahidi ulikuwa kama alivyouacha. Akaupachika begani ule mkoba, mkanda wa mkoba ule
ukikikata kifua chake kutoka bega lake la kushoto na kuuacha ule mkoba ukining’nia kwenye ubavu wa paja lake la kulia.
Aliangalia saa yake.
“Sasa ni saa kumi na moja kasoro… ina maana ndani ya dakika arobaini na tano hivi natakiwa niwe Kunduchi... vyema niwahi kabla jua halijazama. La sivyo hata hicho kitambaa cheupe sitaweza kukiona.” Alisema, na hakujibiwa.
“Tutakuwa kwenye mawasiliano kwa njia ya simu muda wote…”
Aliendelea kumwambia Pojo aliyenuna huku akitoka, “… kwa hiyo kaa tayari kuchukua hatua yoyote mwafaka kwa mujibu wa namna mambo yatakavyojidhihirisha.”
Hakupokea jibu lolote kutoka kwa yule msaidizi wake.
Kitambaa cheupe kilionekana waziwazi kikipepea kutoka kwenye tawi la juu kabisa la Mbuyu mkubwa uliokuwa kiasi cha kama mita mia na hamsini kutoka pale alipokuwa ameegesha pikipiki yake kubwa ya polisi.
Alitembeza macho huku na huko kwenye eneo lile kame na pweke. Jua la
mwisho mwisho lilijitahidi kuathiri uoni wake, lakini halikufua dafu kwa miwani yake ghali ya lebo ya Oakley aliyokuwa ameibandika usoni kwake.
Eneo lile lilikuwa limechimbwa mashimo makubwa makubwa kutokana na shughuli za kuchimba kokoto zilizokuwa zikifanyika bila kujali utunzaji wa mazingira, kabla ya serikali kupiga marufuku shughuli hizo na eneo lile kufungwa.
295 Hussein Issa Tuwa
Sasa lilikuwa kama mji wa magofu, ulioachwa na wakaazi wake na kubaki
kuwa makazi ya wadudu na bila shaka maficho ya majambazi na wakorofi
kama akina Bilanga.
Alimpigia Pojo kwa simu maalumu ya polisi na kumfahamisha kuwa alikuwa ameshafika eneo la tukio, na kumjuza kuwa kuanzia muda ule
simu ile itakuwa wazi hewani naye atakuwa anasikia kila kitakachokuwa kinajiri kati yake na Bilanga.
“Sasa unadhani hata nikisikia nitakuwa na msaada gani kwako kutokea huku niliko afande?” Pojo aliuliza.
“Ndio maana nikakwambia akili kichwani mwako! Hawa watu vichaa sana aisee. Hatuwezi kuyaweka maisha ya binti mwingine asiye na hatia hatarini kwa kukiuka matakwa yao waziwazi… tumia akili yako Sajenti!”
Kwakwa alimkoromea, kisha akaiweka simu yake kweye mfuko wa kifuani wa shati lake bila kuikata.
Aliikwea tena pikipiki yake na kuendesha kuelekea kule ambako ule mbuyu mkubwa ulikuwepo, akiendesha kwa umakini kutokana na mawe makubwa yaliyozagaa eneo lile na mashimo yaliyotapakaa bila mpangilio.
Aliiegesha pikipiki yake kando ya ule mti na kutembeza macho eneo lililomzunguka. Kiasi cha kama mita arobaini kutoka pale alipokuwa aliona tingatinga la mfumo wa kijiko cha kuchimbia mashimo makubwa ardhini, likiwa limelalia upande kwa namna ya kutelekezwa, ilhali kile kijiko chake kinachotumika kuchimbia ardhi kikiwa kimeinuliwa juu. Hatua kama kumi na tano mbele zaidi ya lile tingatinga kulikuwa kuna kichuguu kirefu, na akahisi mtu angeweza kujificha pale na kuweza kumuona kwa urahisi pale alipokuwa.
Alichutama kando ya pikipiki yake huku akitoa ile miwani yake usoni na kuipachika kwenye kifungo cha juu kwenye shati lake. Alitembeza macho kwa makini eneo lile lililogubikwa ukimya wa kuogofya.
Hatua kadhaa nyuma yake kulikuwa kuna rundo la mawe makubwa yaliyofanya mlima mkubwa kiasi, nako akahisi anaweza akajificha mtu na kumuona kwa urahisi kutokea pale alipokuwa.
Alitupa macho juu ya ule mti na hakuona dalili yoyote ya kuwepo mtu juu ya mti ule. Akajisogeza kwenye shina la ule mti na kuketi akiwa makini, mkono wake ukiwa tayari kuchomoa bastola yake kujihami pindi ikitokea haja ya kufanya hivyo. Akatupa tena macho yake kule kwenye lile tingatinga, akijaribu kuona iwapo kulikuwa kuna mtu ndani ya chombo kile.
296 MTAFITI
Muda wote huo alikuwa akiongea kwa sauti kuelezea mazingira yale kwa faida ya Pojo ambaye alijua alikuwa anamsikia kutokea upande wa pili wa ile simu yake ya polisi.
Simu yake ya kiganjani ikaita. Akaipokea na kuiweka sikioni.
“Simama kutoka hapo chini ya mti na uioneshe hewani bastola yako Kwakwa!” Bilanga alimkoromea kutoka kwenye simu, na akajua kuwa muda wote yule bazazi alikuwa akimuona kutokea kwenye moja ya sehemu ya uficho kwenye eneo lile.
“Sasa nikinyoosha mikono yote juu nitawezaje kuongea nawe kwa hii simu wewe?” Kwakwa alimkoromea huku akitembeza macho huku na huko.
Yuko wapi huyu?
“Sio kazi yangu hiyo! Nataka nione mikono juu na unisikie nikikupa maelekezo, bozo we!”
“Sawa bwana.” Alimjibu huku akiinuka na kunyoosha mkono wake wa kulia juu, ukiwa na bastola. Huku wa kushoto ukibaki sikioni ukiwa umeshika simu.
“Tupa hiyo bastola hapo chini ya mti kisha piga hatua kumi mbele!” Bilanga aliamuru, na Kwakwa akatii.
“Sasa nataka niuone huo mkoba wenye ushahidi hewani!” Bilanga akaamuru zaidi.
Kwakwa akatekeleza kwa kutumia mkono wake wa kulia huku ule wa kushoto bado ukiwa umeshikilia simu sikioni.
“Chutama na utoe makabrasha yaliyomo humo mkobani kisha usimame tena wima uyaoneshe hewani hayo makabrasha!” Amri zilizidi kumiminika.
Kwakwa akafanya kama alivyoamrishwa.
“Okay, una hakika kuwa hizo ni nyaraka halisi? Sio fotokopi?” Aliulizwa.
“Kwa nini usijitokeze ukaja kujionea mwenyewe, Bilanga? Kwa nini uandikie mate na wino bwelele tu hapa?” Kwakwa alimkoromea kwa hasira.
“Huko kwenye nafasi ya kutoa majibu ya kifidhuli fala wewe! Kumbuka Zay yuko himayani mwangu bado!” Bilanga alimkoromea.
Kwakwa akapiga kimya.
“Jibu swali langu Kwakwa! Ni nyaraka halisi hizo?”
“Zingekuwa vinginevyo ningekwambia uje uhakikishe hapa? Kila kitu kipo kama ulivyoelekeza Bilanga… Zay yuwapi?” Kwakwa alimjibu.
297 Hussein Issa Tuwa
“Zay bado yu hai... na utampata nitakapojiridhisha kuwa bidhaa niliyoitaka ndiyo niliyoipata. Rudisha mkobani hizo karatasi kisha uuweke hapo chini huo mkoba!” Bilanga alimfokea simuni.
Kwakwa hakutaka kupoteza muda zaidi maana hakutaka kukutwa na kiza eneo lile. Alifanya alivyoamriwa.
“Sasa nataka upige hatua kumi na tano za ubavu-ubavu kuelekea kushoto kwako!” Bilanga alimwamuru tena. Kwakwa alielewa kuwa amri ile ilikuwa imekusudia kumuweka mbali na ule mkoba na ile bastola yake.
Akajua Bilanga alikuwa anataka kujitokeza, kuja kuufuata ule mkoba.
Akafanya kama alivyoamriwa na ndipo alipomuona Bilanga akijitokeza kutokea nyuma ya ubavu uliofichika wa lile tingatinga.
Alitembea kwa mwendo wa haraka huku akiwa amemwelekezea bastola kubwa, na shingoni akiwa amening’iniza darubini ambayo bila shaka ndiyo aliyokuwa akiitumia kumtazama muda wote ule kutokea kule ubavuni mwa lile tingatinga.
Kwakwa alibaki akiwa ameinua mikono yake usawa wa mabega huku akimtazama kwa makini.
“Serikali imetimiza sehemu yake ya makubaliano Bilanga... na wewe timiza sehemu yako. Zay yuwapi?” Alimuuliza.
Bilanga hakumjibu.
Aliuchukua ule mkoba na kutoa yale makabrasha yaliyobanwa pamoja vizuri. Aliyatazama kwa muda huku akimtupia Kwakwa macho ya mara kwa mara, bastola yake ikiwa makini kwenye mkono wake mmoja.
Alitikisa kichwa kuashiria kuridhika, kisha akautupa chini ule mkoba akibaki na yale makaratasi mkononi. Akamnyooshea tena bastola kwa mkono mmoja huku kwa mkono mwingine akizizamisha zile karatasi ndani ya fulana yake iliyokuwa chini ya jaketi lake la jeans.
“Safi sana. Kweli umetimiza wajibu wako... nitawafahamisha wenzako ni wapi watampata Zay nikishafika salama huko niendako!” Alimwambia, na Kwakwa akakunja uso.
“Unamaanisha nini sasa? Kwa nini uwafahamishe wenzangu wakati mi’ nd’o nipo hapa kwa ajili ya Zay?” Alimuuliza huku akishusha mikono yake taratibu.
“We!” Bilanga alimkemea huku akiikoki bastola yake, na Kwakwa akainua tena mikono yake juu.
“Unadhani hatujui kuwa umetoa kopi hizi nyaraka?” Aliulizwa, naye
298
MTAFITI
akaachia mguno.
“Sasa hiyo inahusiana na nini? Maelekezo yako hayakunikataza kutoa kopi! Yalinidai nakala halisi… ndio hizo hapo!” Alimcharukia.
“Ni sawa. Na sisi tulijua kuwa utafanya hivyo… usilolijua ni kwamba ushahidi wa fotokopi bila nyaraka halisi hauna mashiko mahakamani wala popote pale!” Alijibiwa, na hapo Kwakwa akapata jibu la kwa nini wale watu walidai nyaraka zile pamoja na kujua kuwa watazitoa kopi.
“Sawa tu… nirejeshee Zay wetu basi na we’ uondoke na hizo nyaraka zako basi!” Alimwambia kwa kukereka.
“Sio kirahisi namna hiyo Kwakwa!” Bilanga alimkemea, na Kwakwa akamtumbulia macho. “Umetusumbua sana wewe!” Bilanga alimwambia, na kabla Kwakwa hajatia neno akaendelea kwa hasira, “Umetukosesha sana raha na kutunyima sana usingizi, mshenzi mkubwa we!”
“Sa’ nd’o unataka kufanya nini, Bilanga? Ushahidi ushaupata huo, hizo blaa blaa nyingine zote za nini... ? Zay yuwap—”
K-PAA! K-PAA!
Risasi mbili zilijikita kifuani kwake, na Kwakwa alihisi maumivu makali kifuani huku akitupwa nyuma kwa msukumo wa risasi zile kutoka kwenye bastola ya Bilanga.
“Hizo ni salamu kutoka kwa Luis!” Bilanga alimpigia kelele huku akiwa amesimama pale pale.
Kwakwa alibwagika chini kwa kishindo huku ukelele wa uchungu ukimtoka. Vumbi kubwa lilitimka kutokea pale alipoangukia naye akaurudisha nyuma mguu wake wa kulia huku akipeleka mkono wake kwenye sehemu ya chini ya mguu ule.
Bilanga akamnyooshea tena bastola akiwa pale chini.
“Na hii ni kwa ajili ya Chabbi Chek—”
K-PAA!
Risasi ya Kwakwa ilimkosa na kumgutua. Aliruka nyuma na kumnyooshea tena bastola kwa lengo la kummalizia, lakini hapo hapo milipuko mingine miwili ya risasi ilisikika kutokea nyuma yake, pale kwenye kile kichuguu cha mawe makubwa. Vumbi lilimtimkia kiasi cha milimita chache tu kutoka miguuni kwake.
Bilanga akageuka na kutimua mbio kwa mtindo wa zigizaga kuelekea kule kwenye lile tingatinga.
Kutokea kule kwenye kichuguu cha mawe, Sajenti Pojo alichomoka
299 Hussein Issa Tuwa
mbio bastola ikiwa makini mkononi mwake.
“Uko chini ya ulinzi Bilangaa!” Alimpigia kelele huku akimkimbiza na hapo hapo akamtupia risasi nyingine, ambayo ilimkosa na kujikita kwenye lile tingatinga.
Bilanga alijirusha mbele na kujiserereshea ubavuni mwa lile tingatinga, akajigeuza na kumtupia Pojo risasi mbili za haraka haraka. Pojo akajitupa chini, vumbi lililotimuliwa na risasi za Bilanga likamgubika naye akashindwa kuona wala kulenga shabaha vizuri.
Mvumo wa pikipiki kubwa ukasikika kutokea kule ubavuni mwa lile tingatinga na Pojo akajua Bilanga alikuwa anatoroka na ushahidi bila ya kuwarejeshea Zay.
“Pumm-baaav!” Alibwata huku akijiinua na kukimbia kule kwenye lile tingatinga huku akiwa amenyoosha bastola yake.
Bilanga alichomoka kwa kasi na lile pikipiki lake na kulielekeza moja kwa moja kule kwa Pojo huku akimrushia risasi.
Pojo akaruka pembeni na kujibanza kwenye ule mbuyu. Bilanga akampita kwa kasi. Yeye akajigeuza na kumtupia risasi nne za mfululizo huku akimtukana kwa sauti.
Mvumo wa pikipiki ya Bilanga ulizidi kutokomea nyuma ya vumbi kubwa ililoliacha nyuma yake.
Akatupa macho kule ambako Kwakwa alikuwepo, na ganzi ikamtambaa mwilini alipomuona yule mwenzake akiwa amelala chali hali mikono akiwa ameitawanya kila upande.
“Kwakwaa!” Aliita kwa kihoro, akihisi miguu ikimwisha nguvu.
Inspekta Kwakwa alikuwa amelala tuli, hakuitika wala kutikisika.
“Oh, no…!”
Bilanga aliingia ofisini kwake pale Liquid Diamond akifuatiwa na nesi
wa kiume kutoka kwenye kitengo cha huduma ya kwanza cha ile kampuni, aliyekuwa na mkoba wake wa kutolea tiba mkononi. Kwa mshangao
wa yule nesi, yeye alipitiliza moja kwa moja hadi kwenye meza yake na kuitandika teke kali kwa kiatu chake kizito.
“Pumbaaf Pojo, Pummm-Baaaf!” Alimlaani Pojo kwa kumkurupusha
namna ile na pia kwa kumjeruhi kwa risasi wakati alipokuwa akitoroka
300 MTAFITI
kwa lile pikipiki lake kubwa kule Kunduchi.
Kiganja chake kilikuwa kimetapakaa damu iliyokuwa ikichuruzika
kutoka sehemu kwenye mkono wake na kuishia kiganjani kwake kutokea chini ya mkono wa jaketi lake la jeans alilokuwa amevaa. Hakuhitaji
kabisa kulazwa na majeraha yoyote yale katika muda ule ambao Chabbi
hakuwepo, kwani sasa jukumu la kuhakikisha kwamba masuala yote ya kiusalama ya kampuni ile yanakuwa ndani ya mstari lilikuwa chini yake.
Bila kuuliza maswali, yule nesi alimsaidia kuvua lile jaketi lake na kumtazama begani ambako risasi ya Pojo ilimchuna. Akamfahamisha
kuwa halikuwa jeraha kubwa kiasi cha kumfanya ashindwe kuendelea na majukumu yake, lakini damu iliyokuwa ikimchuruzika ilihitaji kudhibitiwa.
“Okay, dhibiti hiyo damu, halafu niache niendelee na majukumu yangu!” Bilanga alimkoromea kwa kisirani.
Nesi alimhudumia kwa utulivu, na dakika kumi baadaye lile jeraha lilikuwa limeshadhibitiwa na nesi akaaga. Bilanga alibaki akitafakari matukio ya siku ile kwa muda mle ofisini kwake.
“Shit! Chabbi naye hatoki tu huko mahabusu bloody kenges?” Hatimaye alijiropokea mwenyewe. Akaangalia saa yake. Saa moja na robo usiku. Muda ulikuwa umesogea sana.
Akampigia Suleiman Mwangi, mwanasheria wa kampuni.
“Oya! Vipi kuhusu Chabbi? Namhitaji sana hivi sasa… muda wa kutoka si ndio umekaribia huu? Umesikia kuwa kuna mashtaka yoyote yaliyofunguliwa dhidi yake?” Alimuuliza, na Mwangi akamjibu kuwa hakukuwa na mashtaka yoyote yaliyofunguliwa dhidi ya Chabbi mpaka muda ule.
“Nenda kamtoe bwana! Yule Kwakwa sio tatizo tena kwetu hivi sasa, lakini mambo si mambo. Chabbi lazima atoke aisee!” Alimwambia kwa shinikizo.
“Muda wa kumtoa ni saa nne usiku! Japo ni vigumu mtu kuachiwa muda kama huo, tutashinikiza na atatoka. Lakini… unamaanisha nini kuwa Kwakwa sio tatizo tena kwetu?” Mwanasheria alihoji.
“Namaanisha hivyo hivyo ambavyo wote humu ndani tulivyokuwa
tunatamani iwe! Lakini we’ hilo lisikushughulishe sana kwa sasa, my learned brother. Cha msingi… hakikisha Chabbi anatoka leo!” Alimjibu.
“Ah, Bilanga bwana! Na vipi kuhusu ule ushahidi waliotoroka nao…?”
“Tunao tayari!” Bilanga alimjibu kwa mkato na kukata simu.
301 Hussein Issa Tuwa
Aliinuka na kwenda ofisini kwa Luis Kambesera akiwa amebakiwa na fulana mchinjo tu baada ya kuvua fulana na jaketi lake vilivyoraruliwa kwa risasi ya Pojo na kulowa damu. Ile bandeji aliyofungwa na yule nesi ilionekana waziwazi begani kwake, naye wala hakujali.
Alimkuta Luis akiwa amejibweteka kihasara hasara ofisini kwake. Hakuwa ametoka kwenda popote siku ile na hata chakula kilimshinda.
Alimrushia lile kabrasha alilopewa na Kwakwa pale mezani kwake.
“Huu ndio ushahidi waliokuwa nao wale shwaini!” Alimwambia.
“Umeupata? Oh, safi sana!” Luis alijikurupusha kitini na kuunyakua ule ushahidi. Akaanza kuyapekuwa haraka haraka yale makaratasi.
“Mwanaharamu alibaki na nakala halisi (akamtukania Grayson mama yake)!” Alisema na kumalizia kwa kusonya.
“Yah, na kama tulivyojadili na Suleiman, wale askari watakuwa wamebaki na kopi ya hiyo kitu, na yeye alisema hilo halitakuwa tatizo iwapo tutaipata nakala halisi… hiyo hapo sasa!” Bilanga alimwambia.
“Kweli. Ngoja nimwite hapa ili…” Luis alianza kuongea huku akiinua uso wake kutoka kwenye ule ushahidi, na ndipo kwa mara ya kwanza akili yake iliposajili kuwa Bilanga hakuwa katika vazi la kawaida.
“Umekuwaje wewe? Hiyo bandeji…?”
“Ah, Pojo huyu. Kanipunyua kwa risasi, mviziaji mkubwa! N’tamkomesha tu shenzi zake!”
“Dah, hii hali inazidi kuwa ngumu kwa kweli…” Luis alisema huku akitoa simu yake ya kiganjani, bila shaka akitaka kumpigia Mwanasheria wao, Suleima Mwangi.
“Achana na Suleiman kwa sasa. Nimemshauri afuatilie kutolewa kwa Chabbi haraka sana, maana mambo ni magumu kuliko unavyodhania, kwa kweli.” Bilanga alimwambia, na Luis akamakinika.
“Kivipi?” Aliuliza.
“Nimembatiza Inspekta Kwakwa… sasa anaitwa marehemu.”
“Whaaaat??” Luis alikurupuka kutoka kitini, macho yakiwa yamemkodoka vibaya sana.
Bilanga akakunja nne pale kitini na kufumbata mikono yake kifuani.
“Naam. Mshenzi hayuko tena duniani, kama ambavyo najua wewe ulitaka na wote miongoni mwetu tulitamani.”
“Ohhh!” Luis alilalama kwa kukata tamaa, na kujibweteka tena kitini kama mzigo.
302 MTAFITI
“Ooo nini sasa bosi? Hali ndio hiyo... niliiona nafasi na sikuweza kujizuia. Najua hili ndilo sote tulikuwa tunalitaka… na nakumbuka kukusikia ukitamka dhahiri shahiri kuwa unataka sana jamaa afe. Sasa nini tena?”
“Akh, Bilanga! Hiyo ni kweli lakini huu haukuwa wakati mwafaka kabisa bwana!”
“Mi’ ndo n’shafanya na wala sijutii. Najua mnazo namna za kulidhibiti hili.”
“Oooh!” Luis alibwabwaja tena, na Bilanga akatupa mikono hewani kwa kukereka.
“Bosi. Tunahitaji kufanya kitu zaidi ya hizo ooooo, oooo zako sasa! Muda ni wa msingi sana hapa. Kama ujuavyo, Chabbi bado yuko kwenye himaya yao kule. Hii ndio nafasi ya kumtoa maana Kwakwa nd’o alikuwa kizibo na polisi hawana namna yoyote ya kumhusisha Chabbi na kifo chake.”
“Sasa huoni kuwa sasa nd’o wataanza kukusaka wewe?”
“Wanisake tu! Si mpaka wanikamate? Na hata wakinipata hawatakuwa na ushahidi wowote wa kunihusisha na kifo cha Kwakwa zaidi ya kile watakachoambiwa na Pojo au kile kimalaya chao…”
“Sasa dogo hilo Bilanga? Huoni kuwa ndio umetuingiza kwenye matatizo zaidi? Utauepuka vipi ushuhuda wa Zay na Pojo kuhusu kuhusika kwako na kifo cha Kwakwa wewe?” Luis alishutumu, na Bilanga akaachia tabasamu la kuogofya.
“Unadhani hilo ni zito kuliko hili lililopo hapa mezani kwako hivi sasa?” Alimuuliza huku akiuoneshea kidole ule ushahidi alioupora kutoka kwa Kwakwa muda mfupi uliopita. Luis akautazama ule ushahidi kwa kugwaya.
“Ah, hii hali mbaya sana!” Alilalama, kisha akaendelea, “Yote ni mazito haya, na hayatuweki mahala salama hata kidogo. Kuupata huu ushahidi kumetuwekea mazingira ya kujivua kwenye tuhuma za kuhusika na kifo cha Grayson, lakini hakutuvui na kuhusika kwako na kifo cha Kwakwa. Pojo na Zay ni mashuhuda kuwa wewe umehusika. Huoni kuwa kuhusishwa kwako na kifo kile kunatuhusisha na sisi moja kwa moja?”
“Zay na Pojo niachie mimi. Kuwaangamiza hao ni kazi ndogo sana kwangu. Cha msingi ni wewe kudhibiti mazingira kiasi kwamba fotokopi ya ushahidi huu isikubalike kutumika mahakamani, kama tukifikia huko.” Bilanga alimkoromea kwa kujiamini kulikotisha.
303
Issa Tuwa
Hussein
“Na we’ umekuwa mwanasheria sasa, Bilanga?”
“Ndivyo nilivyoambiwa na Suleiman, na sina sababu ya kutokubaliana naye! Fanya udhibiti hii hali ya huu ushahidi, Luis!”
“Doooh!”
“Ndiyo hivyo. Itakubidi umpigie simu mkuu!”
“Oooooohhoo!” Luis akazidi kuchanganyikiwa, ujasiri ukamtaliki. Bilanga akasonya na kuelekea mlango wa kutokea nje ya ofisi ile, na alipofika pale mlangoni alimgeukia na kumtazama.
“Piga simu hiyo bosi sasa! Haya mambo hayazibiki kwa kuzidi kukaa kimya tena! Tutajitahidi kuyadhibiti kutokea hapa yalipofika, yakishindikana basi plan B nd’o kitakachofuatia. … piga hiyo simu sasa hivi!” Alimwambia kwa hasira na kutoka nje ya ofisi ile. Huku nyuma Luis Kambesera alibaki akiwa amejiinamia huku akiwa amejishika kichwa kwa kukata tamaa. Alibaki katika hali ile kwa muda mrefu sana. Kisha akaguna na kutoa simu yake ya kiganjani.
Akapiga simu ambayo Bilanga alimsisitiza sana aipige, na ambayo yeye alikuwa akichelea kuipiga kwa muda mrefu sana. Ni namba ya simu ambayo alijua kuwa kwa pale walipofikia, hakukuwa na namna ya kujaribu kujiokoa kutoka kwenye zahma ile isipokuwa kwa kuipiga namba ile… na kuongea na mtu pekee ambaye angeweza kuwavusha kutoka kwenye ile zahma ambayo yeye na wale watendaji wenzake wa Liquid Diamond Incorporated walijitumbukiza kwayo.
Aliisikiliza ile simu ya yule mtu aliyempigia ikiita huku moyo ukimwenda mbio, na akili ikimzunguka…
Kule Kunduchi, mara tu baada ya kutorokwa na Bilanga, Pojo alimkimbilia Kwakwa kwa pupa na hamaniko pale alipolala chali kama gogo. Alijibwaga kando yake pale chini na kumtikisa kwa wahka.
“Afande! Afande Kwakwa... !” Alimwita kwa kiherehere, akimtazama kwa pupa mwilini kutafuta mahala ambapo risasi ya Bilanga iliuingia mwili wake, lakini hakuiona.
“Uunh! Ah! Nilijua tu kuwa huyu shwaini angetugeuka, bloody fool!” Kwakwa alisema kwa maumivu huku akiinuka na kuketi pale chini.
Pojo akamtumbulia macho.
304
MTAFITI
“Ha-hajakupiga risasi? Mbona nilikuona kabisa uki—” Alikatisha kauli yake alipomuona Kwakwa akiitupa pembeni bastola ndogo ambayo awali aliichomoa kutoka kwenye mkoba maalum alioufunga juu kidogo ya kifundo cha mguu wake wa kulia, na kulivuta kwa pupa shati lake la polisi.
Vifungo vya shati lile vilikatika na kudhihirisha fulana ya deraya maalum kwa kuzuia risasi aliyovaa chini ya shati lile. Sehemu ambapo risasi za Bilanga ziligota kwenye fulana ile zilionekana wazi wazi, usawa wa upande wa kushoto wa kifua chake.
“Dah!” Pojo aliachia mguno wa ahueni alipoona hali ile.
“Mjinga alidhamiria kuniua yule, shenzz taip! Sasa hakika kinyongo changu dhidi yake kimepevuka, habithi mkubwa!” Kwakwa alisema kwa kutweta.
“Sa’ si unaona umuhimu wa kuja pamoja afande? Unadhani nisingetokea muda ule...” Pojo alimwambia kiongozi wake kwa kushutumu.
“Mi’ n’lijua kuwa ungekuja tu Pojo! Hata hivyo nilikuwa nimejiandaa na hili... si unaona?” Kwakwa alimjibu huku akimuashiria amsaidie kuinuka.
Pojo alimshika mkono na kumuinua, naye akainuka huku akiikwapua ile bastola yake kutoka pale chini.
“Ina maana ulivyonizuia kuja nawe huku… ulijua kuwa sitotii?” Pojo alisaili.
“Askari makini lazima ufike wakati utumie maamuzi yako binafsi na ufuate hisia zako. Sio kila wakati ufuate maelekezo tu!” Kwakwa alimwambia huku akichechemea kuelekea kule kwenye lile tingatinga.
Pojo akaguna.
“Kwa hiyo unanifundisha nini Afande?” Alimuuliza.
“Kuwa uwe tayari kusimamia maamuzi yako na kuwajibika kwayo hata kama yataenda kombo! Hebu kaniokotee bastola yangu nyingine pale chini ya mti... ” Alimjibu bila kujali lakini kwa kugumia, bado maumivu ya mikito ya zile risasi kifuani kwake yalikuwa yakimtawala.
Pojo alimletea ile bastola yake naye akaifutika mfukoni, akabaki na ile ndogo mkononi.
Wote wawili walikuwa wametapakaa vumbi vibaya sana, lakini hilo halikuwashughulisha hata kidogo.
“Sasa itakuwaje... ushahidi tumepoteza na Zay hatunaye!” Pojo aliuliza kwa kuchanganyikiwa.
“Huo ushahidi sio tatizo. Tumpate Zay kwanza... nahisi yupo hapa...
305
Issa Tuwa
Hussein
kwenye tingatinga lile...” Kwakwa alimjibu, na ingawa bado alionekana kutoridhika na jibu lile, Pojo alikimbia hadi kwenye lile tingatinga.
Akasikia sauti ya lile bati gumu la kile kijiko kilichokuwa kimeinuliwa juu likigongwa gongwa kutokea kwa ndani. Alimgeukia Kwakwa na kumuona akielekea pale alipokuwa, kwa kuchechemea.
“Zay!” Pojo aliita, na ile sauti ya kile chuma kizito cha kile kijiko kugongwa gongwa ikazidi, ikifuatiwa na migumio ya shida kutokea ndani ya kile ‘kijiko’.
“Zay huyo!” Kwakwa, aliyefika pale alipokuwa, alimwambia huku akikioneshea kile kijiko.
“Lah! Kampandishaje huku juu mshenzi yule!” Pojo alisema kwa mastaajabu huku akienda kule kwenye sehemu ya kuendeshea lile tingatinga, akitaraji kukuta ufunguo ili ajaribu kukishusha chini kile kijiko.
“Huwezi kukuta ufunguo huko. Mawe hayo...! Hapo chini...” Kwakwa alimwambia huku akioneshea mapande ya matofali yaliyozagaa sehemu chini ya kile kijiko cha tingatinga.
Wakaelewa kuwa Bilanga aliyapanga yale mawe kama jukwaa la kumuwezesha kumtumbukiza Zay ndani ya kile kijiko, kisha akayasambaza pale chini ili isiwe rahisi kwao kung’amua mahala Zay alipo au iwawie vigumu kumtoa Zay kwenye kile kijiko.
Walishughulika haraka haraka kuyapanga upya yale mawe, kisha Pojo akaparamia kule kwenye kijiko.
Akamkuta Zay akiwa amefungwa mikono na miguu kwa nyuma ndani ya kile kijiko, huku akiwa amezibwa mdomo kwa plasta kubwa.
Walishirikiana kwa shida kumtoa na kumlaza chini kando ya lile tingatinga. Pojo alitumia kisu kidogo kilichokuwa kwenye kishikizio cha funguo zake kuzikata zile kamba alizofungwa nazo.
Kwakwa akaibandua ile plasta kubwa aliyobandikwa mdomoni, na Zay akalia kwa maumivu.
“Mshenzi sana... mshenzi sana yule!” Alilaani kwa uchungu huku akijaribu kuinuka, lakini Pojo alimrudisha pale chini.
“Tulia kwanza, Zay... tulia. U hali gani?” Pojo alimuuza.
“Hilo si la kuuliza afande...” Zay alimjibu kwa hasira.
“Kweli. Pole sana... lakini uko salama sasa.” Kwakwa alimwambia huku akimtazama kwa huruma iliyodhihiri.
Zay alikuwa amechakazwa vibaya. Uso ulikuwa umemvimba. Mdomo
306 MTAFITI
wake wa chini ulikuwa umechanika na damu ilikuwa imegandia mdomoni pale. Shavu lake moja lilikuwa limetutumka na alama za vidole zilionekana wazi wazi shavuni pale. Sehemu juu ya jicho lake moja ilikuwa imevimba. Nywele zake zilikuwa zimemtimka na zimejaa vumbi, michanga na majani.
Alikuwa kama bondia aliyetoka kwenye pambano gumu kabisa ulingoni.
“Dah huyu Bilanga huyu!” Kwakwa alisema kwa hasira.
“Na... naomba tuondoke hapa afande... sijisikii vizuri kabisa. Kanitesa sana yule mshenzi!” Zay alisema.
“Na atajuta sana kwa hilo Zay... niamini mimi!” Kwakwa alimwambia huku akimsaidia kuinuka.
Yowe likamtoka Zay na akarudi tena chini.
“Siwezi kusimama!” Alilalama.
Miguu ilikuwa imemuisha nguvu kutokana na kukunjwa nyuma kwa muda mrefu, ikiwa imefungwa kwa kamba kama jinsi alivyokutwa na Pojo ndani ya kile kijiko.
Sajenti Pojo alimbeba kwa kumpakata mikononi mwake, na kuongoza njia kuelekea kule barabarani huku Zay akiwa amejishikilia kifuani kwake kwa kumzungushia mikono yake mabegani. Inspekta Kwakwa alifuatia nyuma yao.
“Umekuja kwa usafiri gani Pojo... pikipiki?” Kwakwa aliuliza.
“Hapana... nimekuja kwa gari... nilijua kuwa tutarudi na Zay, hivyo pikipiki isingekuwa mwafaka!” Pojo alijibu huku akiongoza njia pasina kuonekana kutatizwa na uzito wa Zay mikononi mwake.
Walipoifikia Land Rover iliyomfikisha Pojo eneo lile, kiza kilikuwa kimeshaingia. Pojo alimuweka Zay kwenye kiti cha nyuma, kisha yeye akaenda kuketi nyuma ya usukani. Kule nyuma, Zay alijilaza pale kitini huku akigumia kwa maumivu.
“Turudini kituoni kwanza... mi’ n’tawafuata kwa nyuma.” Kwakwa alimwambia Pojo kwa dirishani.
Pojo akageuza gari kwa kasi na kukamata uelekeo wa katikati ya jiji.
Kwakwa alibakia kitazama ile Land Rover ikiondoka eneo lile huku akitoa simu yake ya kiganjani. Akampigia dokta Martha Ndimbo na kuisikiliza simu ikiita upande wa pili huku akiiendea pikipiki yake.
“Whats up, Kwakwa?” Sauti ya dokta/inspekta Martha ikayaburudisha masikio yake.
“Eh, mambo vipi Martha?” Alimsalimu na baada ya kujibiwa salamu
307 Hussein Issa Tuwa
yake, akaenda moja kwa moja kwenye nia ya yake, “Kuna dharura Martha, nakuomba ofisini kwetu kama ndani ya nusu saa hivi!”
“Inahusu nini?”
“Kuna shahidi muhimu anahitaji matibabu.” Alimjibu na kukata simu, kisha akatoa kifaa kingine mithili ya simu ya kiganjani na kukiwasha.
Zilisikika mbinja kadhaa kisha kioo cha kifaa kile kikaonesha ramani ya maeneo kadhaa ya jiji la Dar kwa kutumia mfumo wa google maps.
Kwenye sehemu moja kwenye ramani ile kidoa chekundu kilionekana
kikikonyeza konyeza. Akabofya kwenye kile kifaa na mahala ndani ya jiji la Dar lililokuwa likioneshwa na kile kijitaa chekundu likabainishwa kwenye uso wa kile kifaa chake maalum.
Liquid Diamond Incorporated.
Tabasamu la hasira likajijenga usoni kwake. Alitaka kujua ni wapi Bilanga angeupeleka ule ushahidi aliowashinikiza wampatie kwa kubadilishana na Zay, na sasa ile pini maalum aliyotumia kubania yale makaratasi aliyomkabidhi Bilanga, ambayo ilikuwa ikiwasiliana moja kwa moja na kile kifaa kilichokuwa mkononi mwake, ilimthibitishia kuwa Bilanga
aliyapeleka yale makaratasi kwenye jengo la Liquid Diamond, na hivyo, Luis Kamberesa alikuwa anahusika moja kwa moja na matendo ya Bilanga.
Alibofya sehemu kwenye kile kifaa, ambayo iliwezesha ile kumbukumbu ya mahala ile pini iliyobana yale makabrasha ilipokuwa na muda husika, kuhifadhiwa moja kwa moja ndani ya kifaa kile. Kisha akaituma kumbukumbu ile kwenye anuani yake ya barua pepe ya kazini, moja kwa moja kutoka kwenye kifaa kile.
Alijua fika jinsi watendaji wakuu wa Liquid Diamond walivyokuwa wepesi kukana kuhusika na matendo ya wale mbwa wao wa mauaji, na ushahidi ule uliwahusisha moja kwa moja na yote yaliyofanywa na Bilanga tangu alipomteka Zay hadi alipomtwanga yeye risasi kwa azma ya kuua.
Akiwa ameshajiongezea ushahidi zaidi dhidi ya kampuni ile dhalimu, alikwea pikipiki yake na kuondoka kwa kasi kuwafuata akina Pojo.
Saa moja baadaye alikuwa ameketi na akina Pojo kwenye sebule ya ile nyumba cha chini ya ardhi pale kituo kikuu cha polisi.
“Huyu shahidi wako anahitaji mapumziko ya kisaikolojia zaidi kuliko
308 MTAFITI
vinginevyo, Kwakwa...” Dokta Martha alimwambia huku akimuoneshea
Zay aliyelala chali kwenye kochi refu la pale sebuleni huku akiwa amefumba macho na amefumbata mikono yake kifuani.
Zay alikuwa anasikia kila kitu kilichokuwa kinazungumzwa pale sebuleni na aliendelea kubaki kimya.
Baada ya Pojo kumfikisha pale kwenye ile nyumba ya siri iliyopo chini ya sakafu ya kile kituo kikuu cha polisi kiasi cha saa moja iliyopita, alijikongoja hadi bafuni na kuoga kwa muda mrefu.
Alijisugua mwili wake kwa nguvu huku akilia kwa hasira. Wala hakujali maumivu aliyokuwa akiyapata kwa kujitonesha majeraha aliyoachiwa mwilini na mtekaji yule katili, Bilanga; kama kwamba kule kujisugua
namna ile kungelifuta kabisa maishani mwake lile tukio baya la kutekwa, kuteswa na kushikwashikwa mwili wake kikatili, na mtu yule mshenzi. Madhila aliyopitia mikononi mwa Bilanga yalimfanya ajihisi kudhalilika kusiko kifani. Hasira yake juu ya hali ile ilizidi kuchochea ari ya kisasi kwa yale aliyofanyiwa yeye binafsi, na kiu ya lipizo kwa kifo cha rafiki yake.
“Unamaanisha nini, Martha... kwamba hajaumia sana mwilini?” Kwakwa alihoji huku akitembeza macho kwa Pojo, Zay na kuyarudisha tena kwa Martha.
“Majeraha aliyopata mwilini ni ya kuteswa... kupigwa, kufinywa na kufungwa kamba kwa nguvu. Ni majeraha ya kawaidia na yatapona tu baada ya muda...
“Ila majehara ya kisaikolojia ndiyo ambayo yanamsumbua zaidi huyu binti. Kateseka sana kisaikolojia wakati yuko mikononi mwa hao watu waliomteka...”
“Mtu!” Zay alimrekebisha kwa hasira, akiwa bado amefumba macho pale kochini.
Dokta Martha akasita. Yeye na Kwakwa wakatazamana kisha wote wakamgeukia Zay.
“Ni mtu mmoja tu aliyeniteka na kunifanya hivi... mmoja tu!” Zay alifafanua kwa fadhaa huku bado akiwa amefumba macho.
“Oh, okay…” Dokta Martha alisema, kisha akaendelea, “… huyo mtu aliyemteka amemuumiza sana kisaokolojia huyu binti kwa namna alivyomtesa. Binti anahisi kuwa amedhalilishwa sana...”
“Sihisi, dokta. Nimedhalilishwa kweli!” Zay alidakia tena kwa kisirani.
“Ni kweli, na sikuwa namaanisha kuwa hukudhalilishwa, bali nilikuwa
309 Hussein Issa Tuwa
najaribu kuzielezea hisia zako baada ya tukio lile…” Dokta Martha alimwambia haraka, wakati akina Kwakwa wakitazamana.
Pojo aliiona wazi ghadhabu iliyotawala usoni kwa Kwakwa, naye aliiona bayana shaka iliyotanda usoni kwa Pojo.
“Ah, hebu ngoja kwanza dokta, kwa hiyo... ina maana alim... alim....”
Pojo alishindwa kujilazimisha kulitamka neno lililojengeka kichwani mwake.
“Hajanibaka bwana!” Zay aling’aka kwa kukereka.
“Oh! No, no, no.... hajabakwa aisee...! Ni kwamba mkasa mzima ule umemuacha akiwa ameathirika kisaikolojia tu!” Dokta Martha naye alidakia kwa pupa.
“Huyu Bilanga atapata taabu sana nikimtia mkononi aisee, Dah!”
Kwakwa alisema taratibu huku akitikisa kichwa, tabasamu la hasira likielea kinywani mwake.
“Okay, kwa hiyo unashauri nini sasa?” Pojo alimhoji dokta Martha.
“Apumzike na awe na watu wake wa karibu tu kwa kumfariji. Hayo majeraha yake nimeyatibu na kuna dawa nimempa. Aendelee kuzitumia.”
Martha alimjibu huku akimtupia jicho Kwakwa.
“Okay Dokta shukrani sana.” Kwakwa alimwambia huku akiinuka na kumpa mkono, kumaanisha kuwa kazi yake pale ilikuwa imekwisha.
Martha aliupokea mkono na kuagana naye.
“Kuwa makini kwenye mambo haya Kwakwa. Inaelekea hawa watu unaokabiliana nao safari hii, sio wa mchezo hata kidogo.” Alimwambia.
Kwakwa aliguna tu.
“Haya binti, ugua pole. Fuata ushauri wangu. Usiache kutumia dawa nilizokupa na usiendelee kuliwazia sana tukio lile, okay?” Martha akamuaga na kumuusia Zay, ambaye bila ya kufumbua macho wala kumgeukia, alimuinulia mkono kwa ishara ya kumuaga.
Martha alichukua mkoba wake wa kitabibu na kutoka nje ya sebule ile huku akitikisa kichwa.
Wakabaki watatu tu mle ndani.
Zay aliinuka na kuketi kitini.
“Dah! Hii ni ngumu sana kwetu Zay. Dokta kasema usiyawazie sana haya uliyokutana nayo kule kwa akina Bilanga, lakini sisi ni muhimu sana tuyajue kutoka kwako!”
“Mnataka kujua nini, kwa mfano, Inspekta?”
310 MTAFITI
“Ah, kila kitu. Ni nini kilikutokea huko kwa Bilanga? Je, unaweza kujua ni wapi alikupeleka? Na je, kuna watu wengine ambao Bilanga alikuwa anashirikiana nao? Na… ni nini hasa alichokuwa anakitaka kutoka kwako hata akakutesa namna hii?” Kwakwa alimjibu na kumhoji kwa wakati mmoja.
Zay aliguna kabla ya kumjibu.
“Mi’ n’tawaeleza tu, Inspekta. N’tawaeleza kwa kuwa baada ya haya yote, sioni tena sababu ya kuendelea kuwachekea hawa watu. Ni kuwalipua tu!” Zay alisema kwa kisirani. Akina Kwakwa wakatazamana.
Ni baada ya kusikia maelezo ya Zay ndipo wale askari walipoelewa kuwa baada ya kumnyakua Zay na kukimbia naye kule Oysterbay, Bilanga alipiga kwa nguvu kisogoni yule binti kwa kitu kizito, bila shaka kitako cha bastola, na Zay akapoteza fahamu. Hivyo alisafiri naye hadi mahala alipopakusudia ingawa Zay hakuwa na uhakika iwapo alimfikisha huko kwa kutumia usafiri ule ule wa pikipiki au alibadili usafiri njiani na kutumia gari.
Fahamu zilipomrudia alijikuta akiwa amefungwa kamba miguu na mikono kwenye chumba kichafu kilichotoa harufu mbaya na kikiwa na alama za michirizi ya damu iliyogandia sakafuni na ukutani.
“Ni wazi kuwa kile kilikuwa ni chumba cha mateso, Inspekta, na kwa kweli niliogopa sana…” Zay alikiri katika maelezo yake, lakini kilichonasa zaidi udadisi wa wale askari ni kauli yake iliyofuatia.
“… na nina hakika kile ndicho chumba ambamo rafiki yangu Mwantumu aliteswa na hatimaye kuuawa!”
“Eeenh?”
“Kabisa Inspekta!” Zay alisema huku machozi yakimtanda machoni, kisha akaendelea, “Na ile damu niliyokuta imegandia kwenye kuta na sakafu za mle ndani? Ni damu ya Mwantumu ile!”
Akaangua kilio upya.
Kwakwa na Pojo wakatazamana.
Kilikuwa ni kilio kifupi lakini cha uchungu dhahiri. Wale askari walitazamana, kisha kwa namna fulani Kwakwa alifanikiwa kupata maneno ya kumtuliza kutokana na kilio kile.
Zay alijifuta machozi na kubaki amejiinia huku alivuta kamasi jepesi lililozaliwa na kilio kile.
“Kwa nini unasema hivyo Zay...” Kwakwa alimuuliza, “... kuna ushahidi
311
Issa Tuwa
Hussein
wowote ulioukuta kwenye hiyo sehemu uliyopelekwa unaomhusisha
Mwantumu moja kwa moja na sehemu hiyo?”
Zay aliinua uso na kumtazama kwa muda kwa macho yaliyowiva, kisha
akaafiki kwa kichwa huku akiwa amebana midomo yake kama anayehofia
kuangua kilio kingine iwapo angejaribu kuongea.
Askari walitazamana.
Wakamgeukia tena yule binti kwa nyuso zenye hamu ya kutaka kujua
zaidi, na kabla hawajaweza kuitamka hamu iliyowajaa, walimuona Zay
akiingiza na kuutoa mkono wake wa kulia kwenye mfuko wa suruali yake ya jeans. Aliitazama ngumi aliyofumbata kwa vidole vya ule mkono wake, kisha akamnyooshea Kwakwa ule mkono huku ukiwa umefumbata kitu ndani yake.
Kwakwa alipokea kwa mashaka kile alichopewa. Pojo akajisogeza karibu naye na kwa pamoja wakajikuta wanakikodolea macho kifungo kikubwa cha aidha koti au blauzi, chenye mchanganyiko wa rangi nyeusi na manjano, kilicholala kwenye tumbo la kiganja cha Kwakwa. “Hii nini, Zay? I mean, najua kuwa ni kifungo lakini… kinahusikaje na hilo ulilolisema kuhusu
Mwantumu?” Kwakwa aliuliza kwa hamasa.
“Naam, bibie… tueleze, kinahusikaje hichi kifungo?” Pojo naye alidakia. Zay aliwatazama huku akimung’unya midomo kwa muda.
“Kimetoka kwenye blauzi ya Mwantumu, hicho…” Aliwajibu huku akiwatazama usoni, mmoja baada ya mwingine. Wale askari walibaki wakimtazama kwa macho yaliyomsukumia swali la “kwa hiyo?”, pasina kulitamka.
“… na nimekikuta kule kwenye chumba ambacho Bilanga alikuwa amenifungia na kunitesa.”
“Eeenh?”
“Aaanh?”
“Ndiyo, wazee.” Zay aliwajibu kwa uhakika usio na chembe ya shaka.
Askari walitazamana, kisha wakamgeukia. Halafu kama aliyekumbuka jambo, Kwakwa akatoa simu yake na kuingia sehemu inayohifadhi picha simuni. Akaifungua ile picha aliyopiga kule Kongowe siku mwili wa Mwantumu ulipogunduliwa.
Picha ilimuonesha marehemu akiwa amevaa koti jeusi juu ya blauzi iliyoonekana kuwa ni ya njano. Akaigusa ile picha na kuikuza pale kwenye kioo cha simu yake, Pojo akifuatilia kila hatua kwa kuchungulia kutokea
312 MTAFITI
juu ya bega lake.
Naam. Eneo la kifuani alilolikuza kwenye picha ile lilibainisha wazi wazi
kuwa ile blauzi aliyovaa marehemu chini ya lile koti ambalo lilikuwa wazi sehemu ya mbele, ilikuwa na kifungo kimoja tu.
Kilikuwa ni pacha wa kile kifungo kilichokuwa mkononi mwa Kwakwa muda ule.
Askari wakamgeukia Zay, wakamtaka awajuze zaidi. Ndipo Zay alipowajuza kuwa alipozinduka alijikuta peke yake, akiwa amefungwa kamba miguu na mikono, ndani ya kile chumba chenye hewa nzito.
Pamoja na kupiga kelele za kuomba msaada, sio tu hakuna aliyemjibu bali pia alipata hisia kuwa sauti yake ilikuwa haitoki kwenda kokote zaidi ya kurindima mle mle chumbani. Alijaribu kujipapasa kwa taabu mifukoni ili atoe simu kwa nia ya kuwapigia wale askari, lakini ile simu haikuwa tena mfukoni mwake. Hakujua iwapo ilianguka katika zile hekaheka za kutekwa au Bilanga aliichukua kutoka mfukoni mwake wakati alipokuwa amepoteza fahamu.
Ulipita muda wa kama nusu saa hivi kabla Bilanga hajaingia mle ndani, akiwa ameishika ile simu yake aliyokuwa akiitafuta. Bila ya kumsemesha, Bilanga alimkamata mkono wake kwa mabavu na kudidimiza kidole chake cha shahada kweye sehemu ya kufungulia loki ya ile simu, ambayo ilikuwa inafunguliwa kwa kutumia alama za vidole vyake tu.
Baada ya hapo yule bazazi aliketi sakafuni na kuanza kuitumia ile simu kufanya mawasiliano, bila ya kujali jinsi Zay alivyokuwa akimtupia jicho la ghadhabu na kumshinikiza amuachie.
Ni katika muda ule ambao alikuwa peke yake mle ndani kabla Bilanga hajaingia na ile simu yake, ndipo yeye alipopata fursa ya kuyakagua kwa macho yale mazingira aliyokuwamo kwa msaada wa mwanga hafifu wa taa ya balbu iliyokuwa inawaka mle ndani.
Na ndivyo alivyoweza kuiona ile hali ya chumba kutapakaa damu na mabaki ya kiti cha mbao kilichovunjika, kabla macho yake hayajavutwa na mng’ao uliotokana na ule mwanga wa taa kupiga kwenye kile kifungo, kikiwa hatua chache kutoka pale alipokuwa amelazwa.
Akitaraji labda kingekuwa ni kipande cha chupa ambacho angeweza
kukitumia kujaribu kuzikata zile kamba atoroke, alijisotesha hadi pale kilipokuwa. Alipokiona tu alikitambua, na ndipo maizi ya kile
alichowaambia awali kuwa alikuwa ameshikiliwa kwenye chumba ambamo
313 Hussein Issa Tuwa
rafikiye aliuawa, ilipomshukia.
“Woga ulionishika ulikuwa mkubwa sana kwa kweli...” Zay alisema
baada ya maelezo yale. “Mwili ulinitetema na moyo ulinitukuta. Kuwa kwenye chumba ambamo rafiki yangu aliuawa kulinithibitishia hukumu ya kifo kutoka kwa Bilanga...”
“Aise!”
“Yaah... lakini baadaye nikajipa moyo kuwa bado kuna kitu ambacho Bilanga na wakuu wake wanakitaka kutoka kwenu... nikajiaminisha kuwa mtatumia hilo kuwa ndio njia ya kuniokoa”
“Pole sana Zay. Uliyokabiliana nayo ni mazito sana... sasa ilikuwaje ukakichukua hicho kifungo katika mazingira yale... ulikuwa umefungwa kamba mikono na miguu, sivyo?” Kwakwa alimwambia na kumhoji.
“Nilikiramba kwa ulimi.”
“Eenh?”
“Yah. Kikaniganda ulimini, nikakibana mdomoni. Kisha nikakitemea ndani ya fulana yangu nyepesi niliyokuwa nimeivaa chini ya blauzi yangu na kuichomekea kwenye ile suruali niliyokuwa nimevaa...” Aliwaambia, na kuwaacha midomo wazi.
“Dah lazima nikupongeze kwa ujasiri huu Zay... hiki kifungo ni ushahidi mwingine unaowahusisha moja kwa moja Liquid Diamond na kifo cha Mwantumu... je utaweza kutupeleka huko kwenye hiyo nyumba uliyokuwa umeshikiliwa?” Pojo alimpongeza na kumuuliza.
Uso wa Zay ukaingia fadhaa.
“Nasikitika kuwa hilo sitaweza...” Alimjibu, na kufafanua kuwa baada ya yote aliyokutana nayo ndani ya kile chumba cha mateso, siku aliyokuwa anarudishwa kwao kwa ajili ya kubadilishwa na ule ushahidi aliowaachia, Bilanga alimdunga sindano iliyomlaza usingizi. Hakujua kilichotokea mpaka alipozinduka na kujikuta ndani ya kile kijiko cha tingatinga kule kunduchi.
Kwakwa na mwenzake walichoka.
“Dah! Laiti tungeweza kuifikia hiyo sehemu tungeuongezea nguvu ushahidi wetu...” Pojo alisema.
“Yah, lakini hata hivyo, ushahidi ungekuwa una nguvu zaidi iwapo tungekikuta hicho kifungo kule kule kwenye eneo la tukio... sio kwa hivi tulivyokuwa nacho huku hivi sasa...” Kwakwa alisema.
“Vifungo vilikuwa viwili.” Zay aliwaambia, na kwa mara nyingine askari
314
MTAFITI
wakamtolea macho.
“Seriously?” Kwakwa alijikuta akibadili lugha pasi kupanga.
“Ndiyo, afande!” Zay alimthibishia, na kuendelea, “… nami nilikiacha kile kingine kwa lengo hilo hilo... kwamba mkifika kwenye ile nyumba muukute ushahidi huo. Sikujua kuwa Bilanga alikuwa amejiandaa kunifanya nisiweze kupajua tena mahala pale.”
Kwakwa akamtukania Bilanga mzazi wake na kusonya kwa hasira.
“Pamoja na uzoba wake, lazima nikiri kuwa Bilanga ana mikakati mzito sana, aisee!” Pojo alisema, na Kwakwa akasonya kwa hasira zaidi.
“Sasa ilikuwaje hata akakupiga namna hiyo... ulijaribu kupambana naye au kumsemesha kijeuri?” Pojo akahoji tena swali ambalo Kwakwa alianza
kuliuliza awali na kwa namna fulani halikujibiwa.
Zay aliinama kidogo na kutikisa kichwa.
“Bilanga alikuwa amedhamiria tu kunipiga... ndiye niliyemkurupusha kule chumbani kwa Mwantumu kipindi kile... hilo lilimkera sana.
“Ulipokuwa hupokei simu akanigeukia na kunipa kipondo kizito, akisema kuwa aliniwekea hamu ya kunipiga kwa muda mrefu kwa kuwa nilimdhalilisha sana nilipomkurupusha kule kwa Mwantumu!”
“Dah! Huyu jamaa huyu! Yaani nikimpata!”
“Yaani ni kwa hilo tu nd’o akakupiga namna hiyo?” Pojo aliuliza kwa kutoamini.
“Hapana. Na mi’ si nilimtukana? Nilimwambia kuwa najua kwamba pale ndipo walipomuulia rafiki yangu... nikamwambia kuwa Kwakwa akimtia mikononi atajuta... nikazidi kumuudhi, naye akazidi kunipiga!” Zay alisema. Pamoja na kwamba ile taarifa haikuwa nzuri, Kwakwa alijikuta akitabasamu.
“Na hujakosea Zay. Nikimtia tena mkononi atajuta sana, yule bwege. Kwa hayo alokufanyia na kwa yale alonifanyia mimi binafsi!” Alisema.
Kimya kidogo kikatanda.
“Sasa labda na mi’ ningejua ni nini kilichotokea upande wenu. Mmegundua nini kwenye yale makaratasi? Najua kuwa mtakuwa mmebaki na kopi, right?” Zay alihoji.
Kwakwa alishusha pumzi ndefu, kisha akaafikiana naye kwa kichwa.
“Sawa. Nilitaraji ingekuwa hivyo...”
“Na ndio sababu ukawa unasisitiza kuwa tumpe tu Bilanga zile karatasi?”
Pojo alimuuliza.
315 Hussein Issa Tuwa
“Of course! Hilo na pia ukizingatia nilikuwa nateswa... sikuwa na jinsi!”
Zay aliwajibu bila kusita.
“Una hakika kuwa ni hilo tu, Zay? Sikuoni kama u-mtu wa kukubali kushindwa kirahisi rahisi namna ile...” Kwakwa alimuuliza.
Zay alimkata jicho kali.
“Sikuelewi afande. Ulitaka nisemeje? Kuwa msimpelekee zile karatasi, acheni anitese tu?” Alimuuliza.
Kwakwa alibaki akimtazama usoni kwa muda, kisha akaamua kutouendeleza mjadala ule.
“Okay. Haina shida. Tuachane na hilo.”
“Bora!” Zay alisema, na kuingiza hoja, “Kwa hiyo... tunaweza kuzipitia pamoja hizo katatasi?”
Kwakwa alitaka kusita lakini akabadili mawazo.
“Haina shida.”
Na ndipo Zay alipopata fursa ya kuyapitia kwa kituo yale makabrasha. Akazitazama kwa muda zile ripoti mbili zilizokuwa zimewekwa ubavu kwa ubavu juu ya meza iliyokuwa mbele yake.
Ile ya Grayson Mochiwa ikieleza kuwa utafiti wa kutafuta nishati nchini ambao kampuni ile iliufanya, umebaini kuwa kuna kiasi kikubwa sana, sana, tena sana cha gesi asilia kwenye mikoa ya kusini mwa Tanzania, hususan kule Mtwara. Ripoti ilionesha hadi takwimu za matarajio ya kitaalamu zilizoonesha kuwa gesi ile ilikuwa na uwezo wa kulitosheleza taifa kinishati kwa miaka na miaka itakayokuja, na kwamba itakuwa na uwezo wa hata kuuzwa nje ya nchi bila ya kuathiri mahitaji ya nishati hiyo kwa taifa.
Ulikuwa ni uvumbuzi wa kimapinduzi kwenye uchumi wa taifa.
Grayson Mochiwa alisaini upande mmoja wa ripoti ile na upande mwingine ulitakiwa usainiwe na mkurugenzi mtendaji wa kampuni, Luis Kambesera.
Upande wa Luis haukuwa umesainiwa.
Ile ripoti nyingine ilieleza kuwa utafiti wa kutafuta nishati nchini ulibaini kuwa hakukuwa na kiasi cha kutosha cha nishati ya gesi nchini kiasi cha kuwezesha uwekezaji wa maana kwenye nishati hiyo. Ilieleza kuwa kuna maeneo machache yenye nishati hiyo, na kwamba iwapo serikali itataka kuivuna nishati hiyo, basi gharama za kuichimba nishati hiyo zitakuwa ni kubwa kuliko thamani ya ile nishati yenyewe. Ripoti ile ikahitimisha kuwa
316
MTAFITI
utafiti wa kampuni ile iliyobobea kwenye mambo ya tafiti za nishati, uliona uwezekano wa kugundua maeneo yenye gesi nyingi zaidi nchini, iwapo itaongezewa muda zaidi wa kulitafiti hilo, hususan iwapo itaongezewa mwaka mmoja zaidi. Ripoti iliishia na kutoa tathmini ya fedha ambazo serikali ilitakiwa iilipe kampuni ile ili kuendesha utafiti ule wa ziada kwa mwaka mmoja zaidi.
Mwisho wa ile ripoti kulikuwa kuna saini ya Grayson Mochiwa kama mtafiti mkuu kwa upande mmoja, na upande mwingine kulikuwa kuna sehemu ya kusainiwa na Luis Kambesera kama mwenyekiti mtendaji wa kampuni ile.
Sehemu zote mbili kwenye ile ripoti iliyowasilishwa serikalini, zilikuwa zimesainiwa. Ingawa kwanza hakuona utofauti, lakini wale askari walimuonesha naye akakubaliana nao, kuwa kulikuwa kuna utofauti kati ya zile saini mbili za Grayson Mochiwa kwenye zile ripoti mbili.
Saini ya kwenye ripoti moja ilikuwa imeghushiwa...
Zay aliinua kichwa kutoka kwenye zile ripoti mbili na kuwatazama wale askari kwa uso uliojaa hamaniko.
“Hii ni kesi ya wazi kabisa kwa Liquid Diamond na watendaji wake jamani. Kilichobaki hapa ni kuwalipua tu!” Alisema kwa jazba baada ya kumaliza kupitia yale makabrasha. Akina Kwakwa wakatazamana.
Naye akawatazama kwa macho ya kuhoji.
“Nini?” Aliwauliza kwa mashaka.
“Tuwalipue kivipi Zay?” Kwakwa alimuuliza kwa utulivu.
“Kwa kuliweka wazi hadharani hili jambo tu! Waandishi wa habari wakiipata hii kadhia, Liquid Diamond hawatakuwa na pa kukimbilia!
Turufu yao ya kutumia vigogo wa ngazi za juu kulizima hili jambo itakuwa ishageuka garasa!” Mwanadada alimjibu kama kwamba lile lilikuwa ni jibu la wazi kabisa kwa swali lake.
Kwakwa alishaanza kumtikisia kichwa kumpinga kabla hata hajamaliza kuongea.
“Unajua huo sio utaratibu wa vyombo vya dola Zay. Hili suala tutalipeleka kwa taratibu zote ili Liquid Diamond wasipate pa kutokea...” Alimwambia.
317 Hussein Issa Tuwa
“Na mi’ sijasema eti nyie nd’o muende nalo kwenye vyombo vya habari hili suala!”
“Hata kama...” Kwakwa alianza kutetea hoja yake, lakini Zay alimkatisha.
“Hivi hamjui kuwa hizo taratibu ambazo mnataka kuzichukua... na wao wanazijua na wameshajiandaa kuwadhibiti? Tunaongelea kadhia ya mamilioni ya fedha na kashfa kubwa kwa vigogo hapa... unadhani wao watakaa kimya tu? Hivi kweli bado unaamini kuwa utaweza kuimaliza hii kesi kwa kuwa tu umevaa hizo sare zako, afande?”
“Acha kulitilia mashaka jeshi la polisi Zay! Tunajua sana kuwa tunawekewa mikakati ya kutudhibiti! Hii mikakati ilianza zamani sana, lakini bado tupo kwenye kesi. Hapa lazima tufuate taratibu za kiaskari na kisheria, na wewe huna mamlaka ya kutuelekeza nini tufanye kwenye hii kesi!” Kwakwa alimchachamalia.
Zay alitikisa kichwa kuashiria kutokubaliana na mtiririko wa mawazo yake.
“Sijawaelekeza cha kufanya mimi! Nimetoa tu mawazo yangu ya namna ambayo mimi ambaye sio askari kama nyie, ninavyoiona namna ya kuliangusha hili likampuni linaloonekana kutoshindwa na jambo kwa sababu lina vigogo wakubwa nyuma yake!”
“Naomba utuachie tulifanyie kazi hili kwa namna ambayo tunajua inapaswa iwe! Kwa sasa wewe tulia tu hapa... pumzika. Uko salama. Ni shahidi muhimu sana kwenye hii kadhia wewe, hivyo tunaomba ubaki kuwa hivyo mpaka muda wa wewe kuja kutoa ushahidi utakapofika. Usitafute njia ya mkato itakayotukosesha ushindi dhidi ya hii kampuni, Zay!” Pojo alidakia. Zay akamkata jicho baya.
“Sasa tuna ushahidi wa kutosha kupata kibali kutoka kwa wakubwa wetu
kuweza kuwaweka chini ya ulinzi watendaji wote wa Liquid Diamond...”
Kwakwa aliongezea, lakini tayari Zay alikuwa akimtikisia kichwa kuashiria kutokubaliana naye.
“Kwakwa! Mimi nd’o n’louleta kwenu huu ushahidi, na Mwantumu ndiye aliyehakikisha kuwa hauangukii mikononi mwa hao akina Luis na akapoteza maisha kwa hilo... na sasa nd’o hivyo tumebakiwa na fotokopi tu! Ina maana tumepoteza karatasi halisi! Tayari hapo Liquid Diamond wameshajiongezea turufu dhidi yetu! Bado tu mnataka kuzidi kupoteza muda?”
“Mara nyingi kufuata taratibu huonekana kuwa ni kupoteza muda
318 MTAFITI
machoni mwa raia, lakini tuamini sisi... hii ndio njia sahihi zaidi ya kuwabana hawa adui zetu, Zay” Pojo alimwambia.
Zay akatikisa kichwa tu kwa kusikitishwa na jibu lile.
“Kwa hili la leo tayari wameshaona kuwa wako kwenye hali mbaya.
Hivi mnavyozidi kupoteza muda kutaka kwenda kuomba vibali vya kuwakamata huko kwa wakuu wenu, wenzenu wanazidi kujipanga huko...
hukawii kusikia huyo mkuu wenu wa kazi kahamishwa kitengo muda huu huu na likawekwa jitu lao. Mnadhani mtafanyaje hapo?” Zay alimjia juu.
“Unajua wao wanaamini kuwa mi’ n’shakufa hivi sasa... Bilanga na wakuu wake hawatakuwa makini kama ambavyo wangekuwa iwapo wangejua kuwa niko nyuma ya kila hatua zao... wakiwa na imani kuwa Bilanga amefanikiwa kuniua kule Kunduchi, hawatakuwa na umakini huo...”
“That’s the problem, Kwakwa.” Zay alimjibu kwa jazba, akitumia kizungu kumaanisha kuwa hilo ndilo lilikuwa tatizo kwenye lile walilokuwa wakilijadili muda ule.
“Kivipi?” Kwakwa alihoji.
“Wewe unafikiria kumkamata Bilanga na wenzake... mimi nafikiria kuisambaratisha kampuni nzima ya Liquid Diamond! Unaona tatizo hilo? Hatufikirii kitu kimoja, nd’o maana hatuelewani afande Kwakwa! Mi’ nataka tung’oe shina, we’ unakazana na matawi… seriously? Angusha
kampuni, unawaangusha Luis, Bilanga, Chabbi... hadi bodi nzima ya kampuni ile!” Zay alimwambia kwa msisitizo.
Kimya kikatanda.
“Linaingia akilini sana ulisemalo Zay, na nakupa saluti ya heshima kwa mtazamo wako huo. Lakini mi sioni kuwa tuko tofauti sana. Kwa huu ushahidi tulio nao…” Kwakwa alimwambia huku akizioneshea zile ripoti mbili za mtafiti Grayson Mochiwa, na kuendelea, “… na huu tuliokusanya wa vifo vya Grayson na Mwantumu, na kutekwa kwako na Bilanga, ni kupitia kwa hawa watendaji wa hii Kampuni ndivyo tunavyoweza hatimaye
kuifikia kampuni yenyewe na kuisambaratisha …”
“Lakini mi’ sioni ni jinsi gani hizo ripoti zitasaidia kuihusisha pasina chembe ya mashaka, Liquid Diamond na vifo hivi jamani… huoni kuwa huo ni mzunguko mrefu? Ile kampuni ni kubwa mjue, bila ushahidi wa kutosha tunaweza kushangaa tunaambulia kumpata huyo Bilanga labda hata na huyo Luis, lakini Kampuni ikaendelea kuwepo na wala isionekane
kuhusika na vifo. Tukiwapiga kwa hilo la kashfa ya kughushi ripoti
319 Hussein Issa Tuwa
muhimu kama hii? Tunawamaliza wote kwa pigo moja tu!” Bado Zay alikuwa ameshikilia mtazamo wake.
Kwakwa alitikisa kichwa kupingana naye.
“Kuna kitu katika sheria kinaitwa ‘probable cause’ Zay… yaani hapo tunatazama ni nani mwenye sababu ya kutaka Grayson na Mwantumu wafe. Au kwa ufasaha zaidi, ni nani ambaye angenufaika, kwa vifo vya Grayson na Mwantumu. Hizi ripoti mbili zinatupa ‘probable cause’ ya Liquid Diamond kutaka Grayson, na yeyote aliyejua kuhusu uwepo wa hii ripoti halisi ya Grayson, afe.
“Nakuhakikishia alipoenda kuwashikia bastola wale wenzake siku ile hadi akalipuliwa kichwa na Chabbi Cheka, mtafiti Grayson Mochiwa alikuwa anawashutumu kuhusu hili hili la kuchakachua ripoti yake. Yeye ndiye kafanya utafiti, yeye ndiye aliyeandaa ripoti nzuri tu na kuiwasilisha kwa mkurugenzi mtendaji Luis… halafu anashangaa kinachokwenda kukabidhiwa serikalini na kunadiwa kwa umma ni kitu tofauti kabisa!”
Kwakwa aliongea kwa kirefu.
“Sasa hii hali ni lazima iwekwe wazi mbele ya umma afande Kwakwa.
Hawa jamaa lazima tuwaanike ili walichokifanya kijulikane, kabla hawajakimbilia kwa vigogo wao na kujiwekea kinga fulani ya kutoingilika tena!” Zay alisema, na Kwakwa akaguna.
“Hapana Zay. Kama nilivyokwambia hapo mwanzo, mambo hayaendi hivyo. Si tumeshaliongelea hili? Hii ni kesi kubwa sana iliyochukua uzito mwingine kabisa sasa. Hii sasa imekuwa kesi ya uhujumu wa uchumi. Ni suala la Mkurugenzi wa makosa ya jinai mwenyewe sasa!” Kwakwa alimwambia, na Zay akamakinika.
“Meaning what?” Alimuuliza, akimaanisha kwamba alitaka kujua ile kauli ya Kwakwa ilikuwa inamaanisha nini.
“Okay… kiutaratibu, hatutakiwi kuiweka hadharani hii habari bali tuiwasilishe kwa wakuu kama ushahidi wa kuwatia nguvuni akina Luis…”
Alimwambia, na Zay akatikisa kichwa kwa kukata tamaa.
“Ushahidi wa fotokopi? Ambao hata mbumbumbu Bilanga keshakwambia kuwa hauna nguvu mahakamani? Acha hizo Inspekta!
Yaani mi’ nilijua tu kuwa itafikia huko… nilijua tu!”
“Hilo la mahakamani sio kazi yetu! Kazi yetu ni kuwatia nguvuni
wahalifu, na ili kuliweza hilo, lazima taratibu zote zifuatwe! Wahalifu kibao
wanaachiwa huko mahakamani kwa vile tu taratibu za kuwatia nguvuni
320 MTAFITI
hazikufuatwa. Hatutaki kuwapa akina Luis nafasi ya kuchomoka hapa!”
Kwakwa alimwambia kwa msisitizo.
“Mnisamehe kama naonekana mbishi, lakini kiukweli hizi siasa mnazoniletea za kuuweka tu huu ushahidi kabatini kwa mkurugenzi wa makosa ya jinai ka’a mapambo mi’ sizielewi na siziafiki hata kidogo!” Zay
alimjia juu.
“Zay, we unajua ni jinsi gani mimi… sisi… tulivyo makini kwenye kazi. Na mpaka sasa unajua ni upande gani tuliopo katika hili. Lakini kama ulivyosema, Liquid Diamond ni kampuni kubwa. Tukikurupuka bila kufuata taratibu kwenye hili la uhujumu wa uchumi, wanaweza kuachiwa hivi hivi! Hapa ni kufuata taratibu tu Zay. Mchango wako na wa Mwantumu
mbona uko wazi tu? Tuamini sisi… tutahakikisha kuwa kupitia kwa akina Bilanga, Chabbi, Luis na wenzao, Liquid Diamond inaanguka, na kwa kufanya hivyo, na wao binafsi wanapata kinachowastahili!” Kwakwa alimwambia, na bado Zay hakuonekana kuridhika.
“Kwa hiyo kumbe hata hao akina Chabbi na Bilanga walikuwa wanasubiri DCI apitishe taratibu zake?” Alihoji, akitamka DCI kumaanisha Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai.
“Wao kesi yao iko wazi… mauaji! Hao wako katika eneo letu la kujidai. Ndo maana tukasema kuwa tunawatia nguvuni tu, na wao ndio watawataja wakuu wao! Chabbi hakumuua Grayson kwa utashi wake tu… na wala hakushirikiana na Bilanga kumuua Mwantumu kwa kufurahisha nafsi yake tu. Alitumwa kufanya hivyo! Kama jinsi ambavyo Bilanga hajakuteka wewe kwa kujifurahisha tu… alikuwa anatekeleza matakwa ya wakuu wake.”
“Ambao ni Liquid Diamond chini ya Luis Kambesera!” Pojo alikazia hoja.
“Haswa!” Kwakwa alitilia mkazo, na kuendelea, “Kwa hiyo Liquid Diamond na Luis K hawachomoki, Zay. Si kwenye uhujumu wa uchumi, si kwenye mauaji. Suala hapa ni lipi kati ya haya mawili litawaganda mwanzo! Na kwa hali ilivyo, hili la mauaji ndilo litakalowanasa mwanzo. Na wakigandwa na hili, lile la uhujumu uchumi litawakuta tu… DCI atajua jinsi ya kukabiliana na suala la fotokopi. We’ tuache tuhakikishe taratibu zinafuatwa tu kwenye hili la kuchakachua ripoti ya Mtafiti na kuihadaa serikali!” Kwakwa alimwambia.
Zay akatikisa kichwa kwa masikitiko na kutoridhika.
“Kwa nini unakuwa mgumu kutuamini ghafla namna hii Zay?” Pojo
321
Issa Tuwa
Hussein
alimuuliza. Zay alimtazama kwa muda.
“Si kwamba siwaamini afande Pojo… sina mashaka nanyi hata kidogo. Ni huo utaratibu wenu ndio unaonitia mashaka…” Alimjibu. “Kivipi?”
Zay akaguna.
“Hivi kwa nini mnakuwa wagumu kukubali kuwa hawa Liquid Diamond wana mtu… au watu… wakubwa tu serikalini wanaowabeba? Watu humo humo serikalini ambao wameridhia Liquid Diamond iwasilishe ripoti feki kwa maslahi yao binafsi na ya hao Liquid Diamond vile vile? Au mnadhani kila mtu ana mioyo kama yenu ya kupenda kazi yake na uaminifu kwa taifa letu? Get real, guys!” Zay aliwajia juu, na wale askari wakabaki vinywa wazi.
“Okay, tunajua kuna uwezekano wa hilo, lakini taratibu zinatutaka tulishughulikie hili suala kwa mfumo huo, Zay! Kama kuna mchezo mchafu ulioihusisha serikali kwa namna fulani katika hili, vitajulikana tu huko mbele, sio?” Kwakwa alimwambia, na simu ya Zay ikaita.
Alipoipokea alibaini kuwa alikuwa ni mama Mwantumu akimpigia kwa kutumia simu ya mmoja kati ya jamaa zake. Mama yule alimjuza kuwa
Mwantumu atazikwa kesho yake saa saba mchana kule shambani kwa mama yake, Gezaulole.
“Itanibidi niende mazikoni kesho… Gezaulole!” Zay alisema baada ya kuongea na simu ile.
“No!” Kwakwa alipinga.
“Huwezi kwenda!” Pojo naye alipinga, na Zay akawajia juu.
“Naenda! Rafiki yangu afe kwa kuwa nilishindwa kuwa naye wakati aliponihitaji, basi hata kwenye maziko yake nisiende? No way! Mi’ naenda!
Kwanza walichokitaka kutoka kwangu si wameshakipata?”
“Bado uko hatarini sana tu, Zay! Si umeona jinsi Bilanga alivyokufanya?
Sasa hivi wewe ni sumu kwa Liquid Diamond, wataendelea kukuwinda tu! Utabaki chini ya ulinzi mpaka tuwadhibiti, kisha utaenda kuhani!”
Kwakwa alimwambia.
“Basi wawekeni wao chini ya ulinzi aisee, sio mimi, khah! Mi’ lazima nikamzike rafiki yangu!” Zay alimjia juu.
Akina Kwakwa wakatazamana.
“Look Zay. Tungeweza kwenda nawe na kukuwekea ulinzi muda wote ukiwa huko. Lakini baada ya hili la leo, hakika sisi tutakuwa na kazi kubwa
sana ndani ya siku mbili hizi ya kuwadhibiti akina Bilanga, na bila shaka
322 MTAFITI
tukahitajika sana kwa DCI… hatutaweza kwenda nawe huko…” Kwakwa alimwambia.
“Sijataka mje nami miye! Nitaenda mwenyewe!”
“Hauwi mwenye busara hapo Zay!” Pojo alimwambia.
“Poa tu!” Alimjibu na kuondoka kwa kisirani kutoka pale sebuleni, na sekunde chache baadaye mlango wa chumba alichopewa ukasikika ukibamizwa, mbamizo ule ukifuatiwa na sauti ya ufunguo ukikomewa mlangoni.
Kwakwa na Pojo walibaki wakitazamana.
Dakika ishirini baadaye usiku ule ule, walikuwa wakiongea na IGP pamoja na Mrakibu Mwandamizi juu ya ule ushahidi mpya wa fotokopi uliopatikana, ile ripoti halali ya hayati Grayson Mochiwa mtafiti ikiwa mezani kwa IGP, kando ya ile ya kughushi iliyotangazwa kwa umma.
“Lah! Lazima niseme kuwa kwa kuupoteza ule ushahidi wa nakala halisi haliifanyi hii kesi kuwa nyepesi hata kidogo! Sisemi kuwa mlilofanya sio sahihi, hapana. Mmefanya kazi nzuri. Mmeokoa maisha ya shahidi muhimu lakini ndio mmepoteza ushahidi mkuu kwenye hii kadhia. Mpaka hapa naona tuna kazi kubwa ya kujenga hoja mahakamani ili ushahidi wa fotokopi ukubalike. Sio jambo dogo hata kidogo hili kwa maoni yangu, lakini huenda DCI akawa na namna ya kulipatia ufumbuzi. Nimemwita… atafika muda wowote sasa.” IGP alisema, na Mrakibu Mwandamizi akakohoa kidogo.
“Er, ni sawa kabisa mkuu… lakini inabidi tuwaweke nguvuni haraka sana ama si hivyo watatuteleza hawa, DCI asije akatukawiza…”
“Hiyo ndiyo kazi yake. Kutuhakikishia kuwa tuna kesi ya kuwabana nayo kwa huu ushahidi wa fotokopi, au la … ili baadaye wasije wakaachiwa
mahakamani kwa aidha ushahidi huu wa fotokopi kutokubalika au kwa kutofuata taratibu katika kuwaweka nguvuni watuhumiwa. Nimemwita
DCI ili angalau aweze kutoa maoni yake iwapo tunaweza kuwakamata watuhumiwa wote na kuwaweka chini ya ulinzi tu kwanza. Kisha taratibu
nyingine za kuwafungulia mashtaka ndio zitafuate…” IGP alisema. Kwakwa na Pojo wakatazamana.
Muda huo katibu muhtasi wa IGP alifika na kuarifu kuwa Mkurugenzi
323 Hussein Issa Tuwa
wa Makosa ya Jinai alikuwa amefika.
“Fabulous! Mwambie aje tu!” IGP alijibu na sekunde chache baadaye Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai akaingia.
IGP akampa muhtasari wa kile kilichokuwa pale mbele yao, naye akawauliza akina Kwakwa maswali kadhaa kuhusiana na ule ushahidi waliokuwa nao.
“Er, okay… kwa haya maelezo niliyopata mpaka hapa naona tukiachilia mbali suala la kuwa ushahidi uliopo ni wa fotokopi, bado kuna mazingira kadhaa ya kutuwezesha kuwatia nguvuni hawa jamaa…” Hatimaye DCI alisema na kutulia kidogo, kisha akaendelea, “… hata hivyo itanibidi nipate muda wa kuzisoma kwa undani hizi ripoti mbili na kuzioanisha na maelezo yote haya kabla sijajisikia salama kushauri wakamatwe…”
Mrakibu akazungusha macho kwa kukata tamaa, lakini hakusema neno.
“Utahitaji muda gani kabla hujatoa ushauri wako juu ya hili?” IGP alimuuliza.
“Ni vigumu kusema… nipe japo saa mbili kutoka sasa…” DCI alisema.
“Ambazo zinatosha sana kwa hawa jamaa kutoweka na tusiwapate tena! Hatuwezi kuwawekea japo vizuizi vya kusafiri nje ya nchi?” Kwakwa alidakia.
“Kwa kigezo gani? Hata hilo linahitaji tuwe tumejiridhisha kuwa ushahidi wetu unaweza kusimama mahakamani na kuwatia hatiani!” DCI alizidi kufanya kazi yake.
“Okay, lakini hilo si kuhusiana na hii tuhuma ya kuhujumu uchumi? Vipi kuhusu mauaji?” IGP alisaili.
“Okay, kwa hili la mauaji ya Grayson na Mwantumu, hususan kutokana na ushahidi wa Kwakwa dhidi ya huyo Bilanga na mwenzake sioni tatizo… ushahidi unaonekana ni mzito wa kutosha, hao wakamatwe tu…” DCI alijibu, na bashasha ikatambaa usoni kwa Kwakwa.
“Ahsante!” Kwakwa alisema huku akimtupia jicho la pembeni Pojo.
“Na sasa hawa wakurugenzi wa hii kampuni, ambao nina hakika ndio vinara wa yote yalofanywa na akina Chabbi… ndio tusubiri tu kwa hizo saa mbili?” Mrakibu alizidi kusaili, lakini kabla DCI hajajibu, IGP alipenyeza hoja.
“Look, vipi tukiwakamata kwa mahojiano zaidi kuhusiana na hili hili la vifo vya Grayson na Mwantumu, wakati wewe unapitia hayo makabrasha na kujiridhisha? Haileti maana watendaji wao wawili wahusishwe na vifo
324
MTAFITI
vya watu wengine wawili kutoka kwenye hiyo hiyo kampuni yao halafu wao wasikamatwe hata kwa mahojiano tu!”
“Kweli afande! Mi’ nadhani hilo inabidi liwezekane tu… na muda wakiwa chini ya ulinzi kwa mahojiano kuhusiana na hili, kama DCI atakuwa ameshajiridhisha kwenye hilo la uhujumu uchumi, mashtaka yanawabadilikia wakati tayari tunao…!” Kwakwa alidakia kwa hamasa.
“Sio yanawabadilikia… yanawaongezekea… hili la mauaji pia litaendelea kuwahusu!” Mrakibu alimsahihisha.
“Kweli kabisa!” IGP aliunga mkono.
Macho yote mle ndani yakamgeukia DCI.
“Hmm, ni hoja nzito hiyo. Nadhani… yes, tunaweza kuwashikilia hao wakurugenzi kwa mahojiano juu ya vifo vya Mwantumu na Grayson tu kwa sasa… lisiongelewe lolote kuhusu hizi ripoti mbili mpaka hapo tutakapojiridhisha. Hilo naona limepita mkuu…” DCI alimwambia IGP.
“Okay, good! Basi litokee bila kuchelewa. Jamaa watiwe ndani fasta!” IGP alisema.
“Yes sir!” Mrakibu aliafikiana naye, na kuendelea, “Sasa kwenye kuwakamata hawa watu, itabidi tupate nguvu ya ziada… wanatakiwa wakamatwe kwa wakati mmoja, hivyo nitaongeza askari wengine kwenye hii kesi sasa, mkuu!”
“Nakubaliana nawe!” IGP alimjibu, na Kwakwa akajikohoza kidogo. Wakamgeukia kwa macho ya viulizo.
“Er, mi’ nilikuwa naomba Bilanga na Chabbi Cheka niachiwe mwenyewe wazee…” Alisema.
“Sioni tatizo kwenye hilo… isipokuwa tu kwamba Chabbi tayari tunaye!” Mrakibu alisema.
“Sio kwa mauaji afande… tunaye kwa tuhuma za kuhusika na kupotea kwa Mwantumu, ambaye sasa ni marehemu! Na pia tayari tumeshakaa naye kwa saa takriban arobaini na nane…” Kwakwa alisema.
“Good point!” IGP aliunga mkono, na kuendelea, “Sasa ndio aidha afunguliwe mashtaka ya mauaji, au akamatwe tena kwa saa arobaini na nane nyingine kwa tuhuma za mauaji moja kwa moja, lolote litakalotangulia”.
Muda huo Kwakwa alisikia ujumbe mfupi wa simu ukiingia kwenye simu yake, ila hakuusoma, kwani isingekuwa nidhamu kwa wale wakubwa zake. IGP akamgeukia DCI.
“Sasa kalifanyie kazi hilo la uhujumu uchumi kutokana na hizo ripoti
325 Hussein Issa Tuwa
mbili za fotokopi za Liquid Diamond, DCI… fanya uchunguzi wako, wahoji unaodhani utahitaji kuwahoji, fanya mawasiliano unayoona
yanastahili ili kujiridhisha, kisha tupe mustakabali wa iwapo tuna kesi au hatuna. Uzuri ni kwamba bila shaka muda huo ukifika, watuhumiwa wote tutakuwa nao kwa tuhuma za mauaji ya Grayson na Mwantumu! Ikiwa ushahidi wa fotokopi utaweza kutumika, basi hii itakuwa ni open and close case jamani, shukrani nyingi kwenu Kwakwa na Pojo!” IGP alisema.
Pojo alihisi moyo ukimpoteza mapigo alipomsikia IGP akimtamja kwa jina namna ile.
Dakika tano baadaye walitoka nje ya ofisi ya IGP wakiwa na kibali cha kuwatia mbaroni watendaji wote wa Liquid Diamond sio kwa tuhuma za uhujumu wa uchumi na ufisadi kwa kuipa serikali ripoti iliyochakachuliwa kwa maslahi yao binafsi, bali kwa mahojiano kuhusiana na vifo vya albino Mwantumu Uledi na mtafiti Grayson Mochiwa.
Kama alivyosema IGP, kulikuwa kuna matumaini kuwa ile ingekuwa ni open and close case… kesi ya kufungua na kuifunga hapo hapo.
Sivyo ilivyokuwa...
326
MTAFITI
NDANI YA MUDA ambao Zay alikuwa akipatiwa matibabu na Dokta Martha kule kwenye chumba cha chini ya sakafu ndani ya kituo kikuu cha polisi, sehemu nyingine ya jiji, simu iliyokuwa ikiita sikioni kwa Luis Kambesera, ilipokelewa.
“Umenipigia… ina maana kuna tatizo kubwa!” Sauti iliyopokea ile simu ya Luis ilisema, na Luis akahisi kitetemeshi.
“Er, ndio mheshimiwa. Hali imekwenda vibaya upande wetu… kopi ya ripoti ya mwanzo ya…” Luis alianza kuongea.
“Inatosha!” Sauti kutoka upande wa pili alimkatisha, na Luis akabaki ameduwaa na simu sikioni.
“Utaingia kwenye gari nitakalokutumia hapo ofisini kwako baada ya muda mfupi. Dereva atakuleta mahala ambapo tutaongea vizuri juu ya hili, okay?” Sauti iliyomkatisha ikampa maelezo.
“Okay mheshi…” Luis alianza kujibu lakini ile simu ilikuwa imeshakatwa. Aliitoa sikioni ile simu na kuikodolea macho kama kwamba ndio kwanza alikuwa anaiona ikiwa mkononi mwake.
Dakika ishirini baadaye, baada ya kuelekezwa kufanya hivyo kwa njia ya simu, alitoka nje ya jengo la ile ofisi yake na kuingia kwenye sehemu ya nyuma ya gari jeusi aina ya Toyota Brevis yenye vioo vilivyotiwa weusi.
Alishituka kumkuta Waziri wa Madini na Nishati akiwa ameketi kule
nyuma alimoingia.
“Ah, mheshimiwa… si ulisema kuwa…?”
“Dereva atakuleta mahala ambapo tutaongea? Change of plans… tutaongea humu humu garini…” Yule mtu miongoni mwa wazito kabisa serikalini, ambaye pia alikuwa mbunge alimwambia.
E bwana we!
327 Hussein Issa Tuwa
16
MTAFITI
“Oh, okay…” Luis alisema huku lile gari likianza kuondoka taratibu
kutoka eneo lile. Mmoja wa wale askari wawili waliowekwa na Kamishna
John Vata kumfuatilia Luis kila atakapoenda, alipanda pikipiki yake na kuanza kulifuata lile gari kwa umakini. Yule askari mwingine wa kike
alituma ujumbe mfupi wa simu kwenda kwa Inspekta Kwakwa.
Kenge katoka bwawani, tuko makini nyuma yake. Fuatilia mmiliki wa Brevis
Tango 636 Alpha Alpha Bravo. Kwenye msafara wa kenge naye yumo. O&O.
Yeye alibaki pale pale nje ya jengo lenye ofisi za Liquid Diamond, kusubiri iwapo Luis atafanikiwa kwa namna moja au nyingine, kumchenga
mwenzake huko walipoelekea, na kurudi pale ofisini.
Ndani ya Brevis, Luis Kambesera alimuelezea yule mzito juu ya hali
waliyokuwa nayo, na yule mzito akabaki akiwa amekunja uso kwa tafakuri.
“Mimi na wenzangu tumekuwa tukifuatilia kwa mbali matukio yaliyokuwa yakinadiwa hivi karibuni kwenye vyombo vya habari kuhusiana na kampuni yako. Na kwa kuwa tulikubaliana tangu awali kwamba likitokea tatizo wewe na wenzako mtalishughulikia kwa namna muwezayo bila kutuhusisha, sisi tulikaa kimya…” Mzito alisema.
“Ni kweli. Lakini pia tulikubalia kuwa pale tutakapoona kuwa jambo ni zito kwetu tuje kwenu!” Luis alijitetea.
“Na ndio maana nilipopokea simu yako tu nikakwambia kuwa kuna tatizo ndio maana umenipigia… nalijua hilo. Ni nani mwingine anayejua kuhusu mkutano wetu huu miongoni mwa watu wako?”
“Kuna mmoja tu ambaye anajua kuwa kuna mzito nawasiliana naye juu ya hili kwa sasa, lakini kama ilivyo kwa wote wengine, hajui ni nani wala ana wadhifa gani na anatokea wapi.”
“Una hakika wenzako hawajui lolote juu ya uhusika wangu na wa wenzangu?”
“Hawajui. Wao walilikubali lile ambalo mimi nilikubaliana na nyinyi… kuwa ugunduzi wa hii gesi kule mtwara utakuwa na faida kwa taifa, lakini sio kwetu sisi binafsi. Ili utunufaishe sisi binafsi, ilibidi tukubaliane
kuibadilisha ile ripoti ya Grayson… na faida ya kufanya hivyo wameiona kwa yale mamilioni yaliyotupiwa kwenye akaunti zetu! Nanyi bila shaka mmeiona faida hiyo kupitia kwenye akaunti zenu.”
“Okay. Nieleze kilichokufanya unipigie simu.” Mzito alimwambia, na Luis Kambesera akamueleza hali halisi.
Alipomaliza aliulizwa swali.
328
“Tunajuaje kama wewe mwenyewe ukiwekwa kikaangoni na vyombo kama Takukuru… hutatugeuka?” Waziri wa Madini na Nishati alizidi kuhoji.
“Ah, ili iweje, mkuu? Kampuni yangu bado inahitaji kupata malipo kutoka serikalini kwa kuendesha huu utafiti, tatizo Grayson akaufanya na kuukamilisha ndani ya muda mfupi sana! Haikuwa na maslahi kwetu kuinadi sasa hivi hii gesi! Ni kwamba mapato yetu yangekatika.
“Lakini la pili ni kwamba kampuni yetu kuu kule Afrika Kusini inanufaika kwa kuiuzia gesi Tanzania, sasa nikisema juu ya hili kwa kubanwa mbavu kidogo tu na wana usalama si itakuwa ni sawa na kuinadi tu hii gesi kule Mtwara? Haitakuwa na maslahi tena kwa kampuni yetu kwani tutapoteza soko letu la Tanzania… kwa hali hii mimi na nyinyi bado tunahitajiana sana. Siwezi kusema mkuu.”
Kimya kilipita kwa muda garini, kisha mkuu akashusha pumzi ndefu.
“Sasa kuhusu hili tatizo lako… Si umesema kuwa tayari ile ripoti tata mmeshaitia mikononi mwenu? Unahitaji msaada gani kutoka kwetu?”
Hatimaye Waziri wa Madini na Nishati aliuliza.
“Ni kweli, lakini tuna hakika wale askari watakuwa wamebaki na kopi, kwani tayari ilishakuwa mikononi mwao kabla hatujaikomboa.”
“Kwa hiyo kumbe tatizo hamjalitatua kikamilifu?”
“Ndio maana twahitaji mkono wenu sasa hapa mkuu!” Luis alisisitiza.
“Kivipi?”
Luis akashusha pumzi ndefu na kutulia kidogo.
“Tunataka mtulinde iwapo ule ushahidi wa fotokopi utatumika dhidi yetu.
Tunaloomba kutoka kwenu ni uhakika kuwa ushahidi ule hautakubaliwa na mahakama kwa namna yoyote ile! Naamini mnao majaji mnaowamudu mkuu… tusaidieni kwenye hili tu!”
“Kuna jingine?”
“Ndio mkuu…”
“Nalo… ?”
“Tunahisi tumemuua Inspekta Kwakwa.”
“Whaat?”
“Ndio mkuu... ilibidi iwe hivyo ili tuitie tena mikononi mwetu ile nakala halisi ya ripoti ya Mtafiti.”
“Doh! Hii ni mbaya sana aisee!” Mkuu alinung’unika.
“Najua. Lakini hii ripoti ya Grayson ni mbaya zaidi mkuu! Kopi yake
329 Hussein Issa Tuwa
ikiruhusiwa kutumika mahakamani sote tunazama… sisi na nyinyi!” Luis alisisitiza, na fisadi mwenzake akamkata jicho.
“Please, mkuu!” Luis alibembeleza.
“Hili la Kwakwa mtakabiliana nalo vipi?”
“Yule fala ilibidi afe tu mkuu. Kama si sasa basi hata baadaye. Sishauri upoteze muda wako kufikiria juu ya hilo.”
“Kwa hiyo unatuambia kuwa hilo la kumuua askari wa jeshi la polisi ni lenu, sisi halituhusu… ndivyo?”
“Ndivyo kabisa Mkuu. Mi’ niwekeeni mazingira ya kuidhibiti kopi ya ripoti ya Mtafiti isikubalike mahakamani tu, basi!”
“Okay… nitalifanyia kazi...” Hatimaye waziri aliyekabidhiwa wizara nyeti kabisa kwa taifa alisema, kisha akahitimisha kikao, “… wewe nenda kadhibiti hali upande wako, na mimi nitadhibiti hali kwa upande wangu. Dereva, mteremshe hapa. Atachukua teksi kurudi ofisini kwake!”
Brevis ikaegeshwa pembeni. Luis akateremka. Brevis ikaondoka.
Yule askari aliyekuwa akiifuata ile Brevis wala hakutetereka. Kazi yake ilikuwa ni kumfuatilia Luis na sio Brevis. Alipitiliza kidogo na kuegesha pikipiki yake kando ya barabara na kujitia kuwasha sigara. Luis alikamata teksi. Kijana wa Kamishna Vata akaingiza pikipiki yake barabarani na kumfuata tena hadi pale Liquid Diamond.
Saa nne usiku ule Chabbi Cheka na Suleiman Mwangi waliteremka ngazi za kituo kikuu cha polisi jijini Dar na kuliendea gari la Suleiman lililokuwa limeegeshwa nje ya kituo kile, miongoni mwa magari mengine pale nje.
Kukiwa hakuna mashtaka mengine yaliyofunguliwa dhidi yake, polisi hawakuwa na sababu tena ya kuendelea kumshikilia pale kituoni.
“Duh, Bilanga anakusubiri kwa hamu kubwa sana Chabbi… mzigo
ulikuwa unamuelemea kweli kweli! Lakini kikubwa… Kwakwa hatunaye tena duniani. Bilanga kahakikisha hilo!” Suleiman alikuwa akimwambia.
Chabbi alisita kutoa jibu alilokuwa ameliandaa pale alipomuona Inspekta
Kwakwa akiwafuata kutokea mbele yao, akifuatana na Sajenti Pojo.
“Naona uko huru sasa Chabbi Cheka!” Inspekta Kwakwa alimwambia huku akisimama mbele yake. Chabbi na Suleiman walimtumbulia macho kama walioona mzuka.
330 MTAFITI
“What? Wenzako walikwambia kuwa Inspekta Kwakwa mnaa… amekufa?” Kwakwa alimuuliza kwa kebehi huku akimsimamia moja kwa moja mbele yake.
Suleiman Mwangi hakuwa hata na hali ya kuongea. Alichokuwa anakiona kilikuwa kinyume kabisa na kile alichohakikishiwa na Bilanga kabla hajafunga safari ya kwenda kumtoa Chabbi pale kituo kikuu cha polisi.
Chabbi alimkata Kwakwa jicho la hasira kali, kisha akamzunguka na kutaka kuendelea na safari yake bila kumjibu, lakini Inspekta Kwakwa alimkatama mkono kwa nguvu.
“Hey!” Chabbi alimaka huku akiuvuta mkono wake kwa nguvu lakini hapo hapo Sajenti Pojo akamdaka mkono wake wa pili.
“Saa arobaini na nane za kwanza zimeisha Chabbi. Sasa nakuweka tena chini ya ulinzi. Safari hii ni kwa tuhuma za mauaji ya Grayson bin Mochiwa na Mwantumu binti Uledi!” Kwakwa alimwambia.
“Whaat? You must be kidding!” Suleiman Mwangi alimaka kwa hasira, akimaanisha kuwa lazima Kwakwa atakuwa anafanya masihara au anatania.
“Una wazimu! Sihusiki na mauaji yoyote mimi!” Chabbi alifoka huku macho yakimtembea.
“Basi huna haja ya kuwa na wasiwasi kwa sababu utatuthibitishia kuwa hukuhusika baada ya mahojiano, sio?” Kwakwa alimwambia huku akitoa pingu.
Ghafla Chabbi alijirusha juu na kujiachia, akijilegeza mwili na akina Kwakwa wakalazimika kumuachia akienda chini. Hapo hapo jamaa akajizungusha pale chini na kumchota ngwara kali Sajenti Pojo, ambaye alienda chini bila kupenda, Suleiman Mwangi na Kwakwa wakiachia mayowe ya hamaniko.
Chabbi akajitupa wima haraka na Kwakwa akaruka nyuma huku akipeleka mkono wake kwenye bastola yake, lakini hapo pikipiki ilichomoza kwa kasi sana kutokea ule upande wa stesheni ya treni, huku mwenye ile pikipiki akitupa risasi za mfululizo eneo lile na jiji likarindima kwa milipuko ya risasi.
“Mwanaharrrraaaaamm!” Kwakwa alijitupa chini huku akichomoa bastola yake, na Pojo akamvuta Mwangi mguu na kumbana pale chini alipokuwa ameangukia baada ya kuchotwa ngwara na Chabbi.
Kelele za askari wenzao wakitoka mbio nje ya kituo kile huku wakiwa
331 Hussein Issa Tuwa
na silaha zilisikika.
“CHABBI
Bilanga alipiga kelele huku akiizungusha pikipiki yake eneo lile na hapo hapo Chabbi akairukia, akimshikilia mabegani, na Bilanga akaichomoa kasi ile pikipiki, akichukua uelekeo wa daraja la railway.
Kwakwa alipiga goti pale chini na kutupa risasi moja, mbili, tatu… na akamuona Chabbi akisukumwa mbele kwa nguvu, yowe likimtoka na damu ikiruka kutoka sehemu fulani ya mwili wake.
“Lete gariiiiih!” Alipiga kelele huku akiinuka na kuitokea mbio ile pikipiki iliyokuwa ikizidi kutokomea, akizidi kuitupia risasi za mfululizo, sasa akisikia na milipuko ya risasi nyingine kutoka kwa wale askari wenzake, sanjari na miunguromo ya magari.
Kule mbele alimuona Bilanga akikunja kona kwa kasi kuingia mtaa mfupi wa Lugoda, maarufu pia kama mtaa wa majani ya chai, ambao ungemfikisha kwenye barabara ya Nyerere, lakini ile kasi ya kukata kona na nguvu ya mvutano vilimtupa pembeni vibaya sana Chabbi Cheka kutoka kwenye ile pikipiki na kumgaragaza kando ya ile barabara.
Bilanga alikamata breki na kuizungusha kwa ustadi ile pikipiki kumtazama mwenzake, lakini mayowe ya askari waliokuwa wakiwakimbiza kwa miguu ilhali wengine wakiwa kwenye magari nyuma yao yaliwafikia pale walipokuwa, na Bilanga akaizungusha tena pikipiki yake na kuielekeza kule alipokuwa akikimbilia hapo awali, akimrushia mwenzake bastola kwa nyuma naye akatokomea.
Chabbi alimtazama Bilanga akitokomea akiwa amelala pale chini na akajua kuwa aikuwa amebaki peke yake. Aliunguruma kwa hasira na maumivu. Risasi ilikuwa imempata nyuma ya bega lake la kushoto, na akauhisi mkono ule ukiwa hauna nguvu kabisa. Aliinuka kwa taabu, na akakoswa koswa kugongwa na gari lililokuwa likiingia kwenye ule mtaa. Aliinyakua ile bastola aliyotupiwa na Bilanga na kujaribu kukimbia lakini mguu wake nao ulikuwa umeumia, na hakuweza kukimbia kama alivyotaka.
Alikimbia kwa kuchechemea kufuata ule uelekeo aliochukua Bilanga, lakini hapo magari ya polisi yakawa yamemfikia huku wale askari waliokuwa wakimkimbiza kwa miguu, Kwakwa miongoni mwao, wakifuata nyuma.
“Simamaa wewe!” Mmoja wa wale askari waliokuwa kwenye gari alimpigia kelele.
Chabbi Cheka aligeuka huku akichechemea, na kujiona akiwa
332
MTAFITI
TWEN’ZETUUUU!”
amemulikwa na taa za magari ya polisi. Alibaki akiwa amesimama akiyumbayumba katikali ya ile barabara pweke, bastola ikiwa inaning’inia mkononi kwake, jasho likimtoka, na damu nyingi ikimvuja kutoka begani alipopigwa risasi na Kwakwa, michubuko mingi ikimchonyota mwilini.
“TUPA SILAHA CHINI NA UJISALIMISHE WEWE!” Mmoja wa askari waliokuwa kwenye ile landrover ya polisi alibwata tena.
“JISALIMISHE CHABBI… HUNA KIMBILIO TENA!” Kwakwa alimpigia kelele.
Chabbi Cheka alipandwa na ghadhabu. Alijua kuwa pale alikuwa amenaswa, hakuwa ujanja tena. Aliachia tusi zito huku akiuinua ule mkono wake wenye bastola kuwaelekezea wale askari huku akiwafuata kule kule walipokuwa.
“CHABBI NNOOO…!” Kwakwa alipiga kelele, sauti yake ikimezwa na milipuko mfululizo ya bunduki wakati wale askari walipommiminia Chabbi risasi za mfululizo, na kupitia kwenye mianga ya taa za yale magari, Kwakwa alimuona jamaa akitekenyeka mwili mzima wakati risasi zilipomchakaza vibaya sana miguu yake.
Alienda chini kwa kishindo huku akipiga kelele za maumivu.
Wale askari walimkimbilia huku wakiwa wamemnyooshea bunduki tayari kummaliza iwapo atajaribu kutaka kupambana zaidi. Lakini ile bastola ilikuwa imeshamtoka na Chabbi alibaki akipiga kwikwi za kutisha pale chini, damu ikiwa imetapakaa eneo lote lile, miguu yake ikiwa haitamaniki kwa kuchabangwa risasi nyingi.
“Beba huyu hadi hospitali, Bloody swine! Anataka kushindana na nguvu ya dola hapa?” Kwakwa aliamuru kwa hasira, na kusonya.
Chabbi Cheka alibebwa kama mzoga na kutupiwa nyuma ya ile landrover iliyokuwa katika muundo wa pick-up, na kuondolewa kwa kasi kutoka eneo lile. Raia wachache waliotokea kuwa eneo lile usiku ule walibakiwa na taharuki kubwa…
Muda huo huo, sehemu nyingine ya jiji simu ya Luis Kambesera iliita, naye akaipokea kwa pupa.
“Chabbi hatunaye tena Luis…!” Bilanga alimwambia simuni.
“What do you mean hatunaye tena?” Yeye alifoka kwa swali huku nyuma
333
Hussein Issa Tuwa
kabisa ya ubongo wake akielewa ni nini Bilanga alichokuwa anamaanisha.
“Nilijaribu kumtorosha wakati polisi walipotaka kumkamata tena. Akapigwa risasi na kuanguka kutoka kwenye pikipiki. Sikuweza kumsubiri. Na nilipokuwa nakimbia nilisikia milipuko mingi sana ya risasi. Naamini atakuwa ameuawa, Luis. Sasa ni mimi na wewe tu…!” Bilanga alisema.
“Akh! Sasa Kwakwa si amekufa? Kuna askari gani tena mwingine anayeweza kujaribu kumshikilia Chabbi baada ya kuachiw—
“Kwakwa yu-hai, Luis.”
“Whaaa— si ulisema…?”
“Sahau nilichosema, Kwakwa hajafa Luis… jamaa atakuwa alivaa bullet proof (akamtukania mama yake)!” Bilanga alimjibu kwa kisirani.
“Ohh, mungu wangu! Naomba uje hapa upesi Bilanga… we need to go!” Luis alisema, akisahau kila alichoongea na yule Waziri wa Madini na Nishati.
Usiku ule ule, Jamilla Mchebe alijikuta akikabiliwa na askari wa kike wawili, akiwa na mumewe na mwanaye wakitoka kutazama filamu pale Mlimani City.
“Bi Jamilla Mchebe?” Askari walimuuliza, na mwili ukamuingia baridi
Jamilla.
“Ni nini?” Aliuliza kwa mashaka.
“Sisi ni askari kutoka kituo kikuu cha polisi jijini. Tunakuomba uongozane nasi kituoni kwa ajili ya mahojiano fulani…”
“
WHAT? Hebu acheni utapeli nyinyi!” Mumewe alikuja juu, na mwanaye akaanza kulia.
“Mzee, chukua mwanao umpeleke nyumbani. Mkeo anahitajika kituoni kwa mahojiano kuhusiana na mauaji… hapa tayari yuko chini ya ulinzi!”
Mmoja wa wale askari alisema huku akitoa pingu.
“No! No please, no! Msinitie pingu jamani… sio mbele ya mwanangu!
N’takwenda!” Jamilla alisema huku akilia, na mumewe akabaki akiwa amepigwa butwaa, mwanaye akizidi kulia.
Walimtazama Jamilla akiingizwa kwenye gari la polisi na kuondolewa kwa kasi kutoka eneo lile, watu wakiwa wamefanya kikundi kutazama tukio lile.
Usiku ule ule, William Maginga na Mike Mwangati nao walitiwa nguvuni.
334 MTAFITI
Suleiman Mwangi yeye alibakishwa kule kule kituoni baada ya lile tafrani la kukamatwa kwa Chabbi na Bilanga kujaribu kumtorosha.
Mtandao wa Liquid Diamond ulikuwa unadhibitiwa kwa mkupuo…
Muda huo huo, sehemu nyingine ya jiji, simu ya Luis Kambesera iliita. Aliitazama na kushangaa kuona ni namba ya mke wa William Maginga.
“Oh shemeij ni nini kinatokea lakini, eenh?” Mwanamama alikuwa akilia simuni, na Luis akajua kimeshanuka.
“Ni… Ni nini kivipi? Sikuelewi shem…” Alijifaragua kuuliza huku akili ikimchemka.
“Polisi wamekuja kumkamata mume wangu hapa shemeji…”
“Atii?”
“Eti wanasema ni kuhusiana na mambo ya kazini kwenu huko… shemeji ni kitu gani lakini hiki kinachotokea?” Mke wa Maginga alizidi kulia, na Luis akakata simu.
Bilanga yuko wapi lakini?
Simu ya Inspekta Kwakwa nayo iliita.
“Yes!” Aliongea na aliyempigia.
“Lile gari uliloagiza tulifatilie usajili wake afande!” Askari wa kitengo cha intelijensia ndani ya jeshi la polisi alisema simuni.
“Yah, lile T636 AAB Brevis? Umegundua nini juu yake?” Kwakwa alihoji, akikumbuka ule ujumbe ulioingia kwenye simu yake kutoka kwa mmoja wa vijana wa Kamishna John Vata, ambao baada ya kupata fursa ya kuusoma, aliagiza askari wa kitengo cha intelijensia wafuatilie usajili wake.
“Linamilikiwa na mheshimiwa Kalugila Mashozi afande!”
“Whaat? Huyu waziri wa madini na nishati… mbunge?”
“Ndiye huyo…”
“Son of a bitch!” Kwakwa alisema na kukata simu, kisha hapo hapo akampigia mrakibu na kumpasha habari.
“Seriously?” Mrakibu aliuliza, na hapohapo akaongezea, “Namtaka Luis Kambesera sasa hivi! Nitamhoji mimi mwenyewe bloody shenzi! Atasema ni nini kinaendelea kati yake na huyu waziri Shenzz Taipp! Namtaka!”
Mrakibu alifoka.
335 Hussein Issa Tuwa
“With pleasure sir! Hivi niko njiani kwenda kumtia nguvuni… wenzake wote wako mikononi mwetu tayari. Bado yeye na Bilanga tu …” Kwakwa alisema “… na hivi niongeavyo ni kwamba tunafuatilia nyenendo zao kwa karibu sana”
Muda huo alikuwa akiendesha gari la polisi kuelekea Liquid Diamond, Sajenti Pojo akiwa kando yake mle garini.
Luis Kambesera alitokeza kwenye eneo pana la wazi lililokuwa juu kabisa ya jengo tofauti kabisa na lile ambalo ofisi za Liquid Diamond zilikuwemo, na kutembea kwa mwendo wa haraka kuiendea helikopta iliyokuwa imeegeshwa sehemu maalum katikati ya eneo lile, Bilanga akimfuatia nyuma yake.
Kitu pekee ambacho kingeweza kuihusisha kampuni yake na sakata zima la ile ripoti halisi ya mtafiti Grayson Mochiwa alikuwa ameshakiteketeza, kwani makapi ya ile ripoti muda ule yalikuwa kwenye moja ya mapipa ya kutupia makapi ya karatasi zilizotafunwa kwa mashine maalumu kwa kazi hiyo, iliyokuwa kwenye moja ya ofisi zilizokuwa kwenye jengo lile.
Ni yeye, Bilanga na Chabbi tu ndio waliojua kuwa lile jengo nalo lilikuwa ni miongoni mwa majengo yanayomilikiwa na Liquid Diamond.
Ilikuwa ni helikopta inayomilikiwa na Kampuni yake, ambayo aliagiza ije eneo lile na kuwatorosha nchini usiku ule ule.
Kutokana na namna mambo yalivyobadilika ghafla, alikubaliana na Bilanga kuwa hawakuwa na namna yoyote zaidi ya kuingia kwenye kile ambacho awali alikiita plan B, ambayo ilihusisha uwepo wao na wa ile helikopta mahala pale muda ule.
Na ni kwa sababu hiyo hiyo ndio maana hawakuwa kwenye jengo lenye ofisi zao za siku zote kwa muda ule, kwani huko ndiko ambako askari wa polisi wakiongozwa na Inspekta Kwakwa asiyehongeka, wangeanzia. Na wao hawakuwa tayari kukutwa nao.
Ingawa walishangaa kidogo kuona lile eneo la kule juu likiwa kiza kinyume na kawaida, mapangaboi ya ile helikopta yaliyokuwa yakizunguka yaliwatia moyo kuwa rubani wao alikuwa tayari kuwatorosha nchini kama
Luis alivyoagiza muda mfupi tu uliopita.
Luis alianza kukimbia kwa hatua ndogo ndogo kuiwahi ile helikopta, mkononi akiwa ameshika mkoba wa safari ambao ndani yake kulikuwa
336 MTAFITI
kuna rundo la hela, cheki za kusafiria na kompyuta mpakato yake ambayo ilikuwa ina siri zote za kampuni yake.
Nyuma yake, Bilanga naye alianza kukimbia, akiwa na begi jingine lenye hela begani na bastola mkononi.
Luis aliingia kwenye ile helikopta kwa pupa.
“Haya twen’zetu rubani… twende!” Aliamuru kwa wahka na rubani aliyekuwa kwenye kiti chake ndani ya ndege ile alimgeukia.
Mdomo ukamuanguka. Macho yakamtumbuka.
“Wapi, Luis K…? Ukonga, Isanga au Butimba?” Sajenti Pojo alimuuliza huku akiwa amemwelekezea bastola kutokea kwenye kile kiti cha rubani. Muda huo huo Luis akamuona yule rubani wake aliyemkusudia akiwa amejikunja kwenye kona ndani ya ile helikopta akiwa hana fahamu na amefungwa pingu.
Mwili ulimfa ganzi. Akili ikamkwama.
“Aaaah! Vipi tena Luis...? Mbona…?” Bilanga alianza kuuliza kutokea nyuma yake, nje ya ile helikopta, lakini hapo alimuona Luis akiinua mikono juu na akianza kuteremka kutoka kwenye ile helikopta kwa kurudi kinyuma nyuma.
Akajua hali si shwari.
Aligeuka haraka na kuanza kukimbia kurudi kule ndani ya jengo.
“Siku zote mwenda tezi na omo marejeo huwa ni ngamani tu, Bilanga!”
Sauti ya Inspekta Kwakwa iliwafikia wote wawili kutokea sehemu fulani kule kule kwenye mlango waliotumia kuingilia kwenye eneo lile.
Bilanga alisimama ghafla, akabonyea huku akiilengesha bastola yake huku na huko kwenye eneo lile pasina kumuona msemaji. Nyuma yake alimsikia Luis akiachia sauti ya hamaniko na kukata tamaa.
Aligeuka, na kumuona Sajenti Pojo akiwa amesimama nje ya ile helikopta akiwa amemwelekezea Luis bastola. Aligeuka kule sauti ya Kwakwa ilipotokea hapo awali, lakini kiza kikazidi kuwa kikwazo kwake.
“Kwakwa! Jitokeze!” Alibwata kwa hasira.
Kimya.
“Jitokeze wewe, nakwambia!” Alifoka tena huku akijitahidi kutafuta mahala hasimu wake alipokuwa, na alipozidi kujibiwa na ukimya, alianza kurudi nyuma taratibu huku akiendelea kuilengesha bastola yake huku na huko, tayari kumshambulia yeyote atakayejitokeza mbele yake.
Ghafla mwanga mkali wa kurunzi kubwa ukammulika usoni kutokea mbele yake.
“YAAAAARGHH!” Aliachia ukelele na hapo hapo akafyatua risasi,
337 Hussein Issa Tuwa
mlipuko mkubwa ukarindima eneo lile naye akashtukia akipigwa teke kali mkononi.
Bastola yake ikatupwa pembeni na sauti ya silaha ile kusambaratika ikasikika.
“AH!”
Akatupa ngumi kali kuelekea kule alipohisi kuwa teke lilitokea, akapiga hewa.
Hapo hapo taa zote za eneo lile zikawaka. Macho yao yalipoweza kutazama sawa sawa, walijikuta wakiwatumbulia macho askari watatu wenye silaha, wawili wakiwa wamemwelekezea Luis zile silaha zao, na mmoja akiwa amemwelekezea yeye hali Inspekta Kwakwa akiwa amesimama hatua mbili tu mbele yake, huku amefumbata mikono kifuani.
“Wha…? Mmefikaje huku nyinyi? Yaani, mmejuaje…?” Luis alimaka kwa woga.
“Hujapata kusikia msemo kuwa mkono wa sheria ni mrefu, Luis?” Pojo alimuuliza kwa ukali, na Luis akagwaya.
Bilanga alibaki akitweta huku akimtazama Kwakwa kwa ghadhabu kuu, akiwa amejishika mkono pale alipopigwa teke. Kwakwa alimtazama kwa jicho la kukamia bila kumwambia lolote, na wakabaki wakitazamana namna ile kwa muda, kisha bila kuhamisha macho yake kwa Bilanga, Kwakwa alipaaza sauti.
“Pojo!”
“Afande!” Pojo aliitika huku bado yeye na askari mwingine wa kike wakiwa wamemwelekezea Luis silaha zao.
“Huyu fala aliyesimama mbele yangu hapa…” Kwakwa alipaza tena sauti huku bado akiwa amemkazia macho Bilanga, na kuendelea, “… akijaribu japo kukwepua tu, piga risasi ya goti. Sawa?”
“Yes Sir!” Pojo alijibu huku akiikoki bastola yake na kuigeuzia kwa Bilanga, akimuacha Luis chini ya ulinzi wa yule askari wa kike.
Kwakwa akamwendea Luis, na kumtazama kwa macho yaliyojaa dharau.
“Unakumbuka niliwahi kukwambia kuwa akili nyingi hupoteza maarifa, Luis?”Alimuuliza.
Luis alibaki akimkodolea macho mithili ya mtu aliyeona jini, wazi kabisa maneno ya Kwakwa hayamuingii akilini.
“Ulipomtuma yule kibaraka wako aje kuupora ule ushahidi dhidi yenu kutoka mikononi mwetu, ulijiona mjanja sana, sivyo?”
Bado Luis hakuwa na uwezo wa kujibu lolote, akabaki akimkodolea macho kwa kuchanganyikiwa tu.
338 MTAFITI
“Basi nafarijika sana muda huu kukujuza kuwa ni ue ule ushahidi ndio tumeweza kuufuatilia hadi tukajua kuwa mko nao kwenye jengo hili.”
Kwakwa alimwambia, na hili likamzindua Luis.
“Haiwezekani!” Alipayuka, “Nimeteketeza kila kitu, na—”
“Of couse, umeteketeza karatasi zote, lakini sio pini iliyokuwa imeyabana yale makaratasi, sivyo? Ile pini itakuwa inazagaa sehemu fulani ndani ya jengo hili muda huu… siye tumeifuata hiyo pini. Ujanja mwingi…?”
Kwakwa alimwambia na kumuacha na methali ile ili amalizie mwenyewe, lakini Luis hakuwa na hali ya kuweza kuimalizia. Hakuelewa alipokosea.
“Sasa kwa huo huo ujanja wako uliopitiliza, umeshakiri mwenye hapa kuwa ni kweli ile ripoti halisi ya Mtafiti Grayson ulikuwa nayo na sasa umeiteketeza… kwa hiyo ni kweli kuwa kila alilofanya Bilanga hadi akazipata zile karatasi kutoka kwetu, alilifanya kwa kufuata maelekezo yako. Umenasa Luis Kambesera!”
“Oooh!” Luis aligwaya.
“Usimjibu lolote zaidi huyo fala, Lu—”
Paaaa!
“EEEEYYH!”
Bilanga alibaki akimtumbulia macho Pojo aliyetoka kuchimbua sakafu ngumu ya pale aliposima kwa risasi.
“Ukiropoka tena nakukongoroa goti hilo, Bilanga. Just shut up, wakati bosi wako anasimangwa kule, ebbo! Kimya!” Pojo alimkoromea, akitilia msisitizo agizo lake kuwa Bilanga akae kimya kwa yale maneno ya kizungu. Bilanga alimkata jicho baya, naye akambetulia mdomo kwa dharau.
“Nadhani sasa unaielewa maana ya ile kauli niliyokwambia kule ofisini kwako kwenye hilo jengo la jirani hapo…” Kwakwa alikuwa anaendelea kumwambia Luis, huku akioneshea upande ambao jengo halisi la Liquid Diamond lilikuwepo, kwa kidole chake cha gumba, “… kwamba ujanja mwingi, mbele kiza?” Alimalizia.
“Toka hapa! Huna lolote la kunikamatia mimi! Huna ushahidi!” Luis alimaka, na Kwakwa akamcheka.
“Ushahidi wa kwanza tuko nao hapa hapa Luis… si unajua kuwa Chabbi Cheka alimdungua mtafiti makini Grayson Mochiwa kutokea kwenye chumba kilichomo kwenye jengo hili?” Alimwambia, na akafarijika sana alipoona mdomo wa chini ukimuelemea Luis.
“Sasa we’ uliona ujanja kutukimbia kutoka kwenye lile jengo lenu la kila siku na uje utorokee huku… matokeo yake sasa ndio umetuthibitishia moja kwa moja kuwa jengo ambalo muuaji alilitumia kujificha wakati
339 Hussein Issa Tuwa
anamdungua Grayson, linahusika nawe.” Alimwambia.
“Aaah!” Luis alizidi kugwaya.
“Sisi tuko makini sana, Luis. Na unajua ni nini kinachowachukiza zaidi watu makini?” Alimuuliza, na bila kusubiri jibu lake, akamjibia, “ Ujanja uliopitiliza.”
“Ah, jamani… nina hela hapa. Nyingi tu za kuwatosha nyote ninyi…” Luis aliropoka.
“Usijiogezee makosa Luis!” Kwakwa alimwambia bila kutetereka.
“Huo ushahidi wote ni wa kimazingira tu, jamani! Sio wa moja kwa moja… maana hata huo wa hiyo ripoti halisi ya utafiti… haupo tena! Chukueni hela mtuachie!” Luis alizidi kujaribu kuondoa udhia kwa harufu ya rupia.
“Funga bakuli hilo Luis! Siye tumekuja kukuweka chini ya ulinzi ili ukajibu tuhuma zinazokukabili. Nakala ya ripoti halisi ya utafiti wa Grayson
Mochiwa? Ile ambayo wewe uliificha na ukatoa ya kwako uliyoichakachua
ukishirikiana na waziri wako Kalugila? Tunayo!” Kwakwa alimfokea kwa hasira, na Luis akatumbua macho kwa kutoamini.
“Mnhu! Tangu lini ushahidi wa fotokopi ukazingatiwa mahakamani Kwakwa? Hapo hamna lolote dhidi yangu! Chukueni hela hii, mtuachie nyinyi!” Luis alimbishia, lakini kitetemeshi kilichoambatana na kauli yake kiliusaliti woga mkubwa aliokuwa anajaribu kuuficha.
Kwakwa akamcheka tena.
“Si unajua kesi za uhujumu wa uchumi huwa hazina dhamana? Tunakusweka ndani tu wakati vyombo vya sheria vinalifanyia kazi hilo suala la ushahidi wa fotokopi, kaka.” Alimwambia.
“Aa—Na-Nahitaji wakili wangu!” Luis alibwata, na Kwakwa akamcheka zaidi.
“Uko chini ya ulinzi Luis Kambesera… wakili wako atakukuta huko huko mahabusu, shwaini tasa wewe!” Kwakwa alimkemea kwa hasira, kisha akamgeukia yule askari wa kike aliyetoka kwenye kitengo cha
Kamishna John Vata.
“Hebu livishe bangili hili bwabwa, hapo!”Alibwata, akimaanisha kuwa amfunge pingu.
Luis alitaka kujitutumua huku akipiga kelele, lakini Kwakwa aliruka na kumzaba kofi kali la uso. Yowe baya likamtoka. Hapo hapo akamfyeka ngwala kali, na Luis akaenda chini kwa kishindo. Yule askari wa kike akamrukia pale chini na kumbana pingu, ambazo awali Kwakwa aliziita bangili, mikononi.
340 MTAFITI
“Ah! Huu ni ukatili wa kipolisi, huu! Mtaonana na wakili wa—”
Pwaa!
Alichapwa kofi kali na mmoja wa wale askari wengine, naye akabweka kama mbwa aliyeshitukizwa. Askari wengine wawili walimburura kimabavu na kwenda kumfunga mikono yake kwenye chuma la ile helikopta kwa kutumia pingu nyingine.
Mjivuni Luis Kambesera akaangua kilio cha kukata tamaa.
Kwakwa akamrudia Bilanga huku akitoa pingu yake.
“Sasa wewe mwenye kichwa ka’ kokwa ya mbirimbi wewe” Alimwambia huku akimtazama kwa dharau, “Nakutia pingu mwenyewe, shenz taipu!”Alimalizia huku akimning’inizia pingu usoni.
“Kwa kosa gani?” Bilanga alimkoromea.
“Mengi sana Bilanga! Mengi!”
“Hamna lolote! Blaa Blaa tu!”
“Okay… tuanze na blaa blaa ya kosa la mauaji ya Mwantumu Uledi!”
“Sio mimi na hamna ushahidi wa hilo!”
“Ni nani kumbe… Chabbi? Maana usitake kun’tajia mganga wa kienyeji hapa!”
“Mi’ nd’o n’navyojua hivyo!”
“Alaa? Sasa vipi alama ya soli ya kiatu chako ikakutwa kando ya mwili wa marehemu kule Kongowe?” Kwakwa alimuuliza na macho yakamtembea Bilanga. Hili halikuwa kabisa kwenye matarajio yake.
“Uongo! Na hata kama ni hivyo, utathibitishaje kuwa ni soli ya kiatu changu? Nd’o mnavyobambikia watu kesi hivyo, eenh?” Bilanga alimaka.
“Ushahidi uko sana Bilanga, tena usiopingika!”
“Bull Shit!”
“Okay. Kama alama ya soli ile ile tuliyoikuta kando ya mwili wa marehemu ndio ile ile ambayo uliiacha kwenye shati langu lililowa maji baada ya kunishindilia soli yako yenye tope kifuani kule nyumbani kwa Chabbi Chela ni Bull Shit, basi kwa hakika uko kwenye deep shit, Bilanga.” Kwakwa alimwambia, akimaanisha iwapo yeye aliufananisha ushahidi dhidi yake na kinyesi cha ng’ombe, basi hakika yeye ndiyo alikuwa amezama kabisa kwenye hicho kinyesi cha ng’ombe.
“Sikubali ubambikiwaji huo!” Bilanga alifoka, akiwa makini na mdomo wa bastola ya Pojo uliokuwa umemwelekea.
“Utaenda kuukatalia mahakamani ubambikiwaji huo, Bilanga. Kwa sasa nakuweka chini ya ulinzi kiulaini kabisa.” Kwakwa alimwambia.
“Sina kosa lolote katika yote hayo iliyoyataja Kwakwa. Unajisumbua tu!”
341 Hussein Issa Tuwa
“ Hivyo eenh? Haya, na vipi kuhusu kosa la kushiriki kwenye njama za kumuua Grayson Mochiwa?”
“Mnhu! Kivipi?”
“Utajua tu muda ukifika, fala wewe!”
“Hayo yote ni maneno tu! Sihusiki na lolote mimi kwenye hayo!” Bilanga alimjia juu.
“Na vipi kwenye kosa la utekaji nyara na utesaji? Tuna shahidi aliye hai anayesubiri muda tu wa kwenda kutoa ushuhuda mahakamani juu ya yale uliyomfanyia wakati ulipomteka, na juu ya kule ulipompeleka baada ya kumteka, na kile alichokiona kule ulipompeleka. Vipi hapo?”
Kimya.
“Na vipi kuhusu kosa la kumpiga risasi afisa wa jeshi la polisi akiwa kwenye harakati za kutimiza majukumu yake?” Kwakwa alizidi kumuuliza, huku akimtazama kwa macho yenye ghadhabu kubwa.
Bilanga alimrejeshea jicho la hasira iliyokosa pa kutokea, midomo ikitetema.
“Niendelee Bilanga? Maana orodha bado ni ndefu…”
Bilanga alibaki akimshindilia mangumi kimoyomoyo.
“Huna tena majibu ya kifidhuli? Unadhani hayo makosa yamekutosha?”
Kwakwa alimuuliza kwa kebehi, kisha akaendelea, “Na hapo bado kuna kosa la kushirikiana na wakuu wako wa kazi mabaradhuli wakubwa, kwenye njama za kulihujumu taifa… na kwa kuichoma moto nyumba ya Chabbi Cheka ili kupoteza ushahidi … oh, Bilanga mlolongo ni mrefu sana! Leta kono hilo nilitie pingu hapa!” Kwakwa alimwambia kibabe.
“Unapata jeuri kwa kuwa uko na wafuasi wako wenye silaha hapa, sio?”
Bilanga alimtemea maneno ya hasira.
“Afande tunamchelewesha huyu bwana!” Mmoja wa wale askari waliokuwepo pale alifoka.
“Tulia askari! Hana muda mrefu wa kubaki wima hapa huyu!” Kwakwa alimpigia kelele yule askari bila ya kugeuka, macho yake akiwa ameendelea kuyakaza kwa Bilanga.
“Sa’ s’kia Bilanga… ” Alimwambia, “… hata kama ningekuwa peke yangu na sila silaha… ningekutia nguvuni tu wewe!” Alimalizia huku akimshika mkono ili amfunge pingu, lakini Bilanga akachomoa mkono wake kwa hasira.
“Hebu niache wewe! Mimi sio ligi yako Kwakwa… mara ngapi n’shakutoa knock-out bwana? Unaona macho ya watu hapa eenh?” Bilanga alimjibu kwa hasira.
342 MTAFITI
Kwakwa alimtazama kwa uso ulioficha hisia huku akimung’unya midomo.
“Kwani uongo? Kama ungekuwa peke yako we’ usingetoka mzima leo hii, pusi mkubwa!” Bilanga akamwambia.
Tabasamu baya likamchanuka Kwakwa.
“Sasa umekuja nilipokuwa napataka Bilanga... unaitishia serikali?” Alimwambia, na kumuuliza.
“Mi’ naongea na wewe, sio serikali. Na sikutishi Kwakwa, nakwambia!”
“Okay, si unakumbuka nilikwambia kuwa nikikutia mikononi utajuta, Bilanga?”
“Nakumbuka sana! So what?” Bilanga alimuuliza, akinaamisha kwa hiyo ndio iweje kama anakumbuka juu ya jambo lile.
“Na ambalo huenda hulijui, ni kwamba nilimuahidi Zay kuwa pindi nikikutia mikononi, utapata tabu sana Bilanga… mi’ huwa sikiuki ahadi zangu aisee!” Kwakwa alizidi kumwambia.
“Oh, yeah? Nina imani kuwa ulisema vile kwa kuwa ulijua tutakapokutana tena utakuwa umezingirwa na askari wenzako wenye silaha!” Bilanga alimwambia.
“Nafurahi kuwa unakumbuka majuto niliyokuahidi. Ambalo nataka nikuhakikishie hivi sasa ni kwamba nilipokuwa nakuahidi hivyo, sikuwa nikiwafikiria kabisa askari wenzangu wala silaha zao… nilikuwa nafikiria mkabala baina yangu mimi…” Kwakwa alisema na kijitomasa kifuani kwa kidole chake cha shahada, kisha anamgeuzia Bilanga kile kidole, “… na wewe!”
Bilanga akafyatulia cheko ya bezo.
“Sasa nashangaa kuona umekuja na mamluki kibao!” Alimwambia huku akitawanya mikono yake kuwaoneshea wale askari.
“Okay… Pojo na wote wengine!” Kwakwa aliita kwa sauti, bila kuhamisha macho yake kutoka usoni kwa Bilanga.
“Afande!”
“Shusheni silaha zenu chini… na asiingilie yeyote hapa. Nataka nimpe kichwa thumni hapa, nafasi ya kunionyesha ubabe wake!” Kwakwa aliamuru huku akitandaza mikono yake tayari kupambana.
“Hah! Afande! Una hakika…?” Mmoja wa wale askari wa Vata alimaka.
“Si m’memsikia alivyosema?” Pojo aliingilia kati, kisha akaendelea huku akishusha bastola yake na akirudi nyuma, “Wote shusha silaha, kaeni pembeni!”
Bilanga hakuuweka.
343 Hussein Issa Tuwa
MTAFITI
Aliunguruma kwa hasira na kumrukia Kwakwa kwa bichwa la nguvu
lililojikita katikati ya kifua na tumbo lake, na kumkumba hadi chini.
Kwakwa aliachia ukelele wa mshituko na pumzi ikamtoka wakati akienda chini kwa kishindo na kubaki chali, Bilanga akiwa juu yake.
Bilanga akamdidimiza makonde mawili mazito sana ya uso akiwa pale chini, na Kwakwa akahisi ladha ya chumvi kinywani. Bilanga akamshika ukosi akiwa pale chini na kumvuta huku mwenyewe akijivuta kumshindilia kwa kichwa cha uso, na Kwakwa akachukia.
Hapo hapo alitumia mtindo wa judo na kumtupa hewani yule jamaa
kwa miguu yake. Bilanga akatupwa hewani. Yeye akajibiringisha pembeni wakati Bilanga akiangukia mgongo kwa kishindo pale sakafuni.
Bilanga aliuguruma tena huku akijiinua haraka na kugeukia kule alipojua kuwa Kwakwa alikuwako, lakini akakutana na teke zito la upande wa kulia wa uso wake naye akayumba kushoto.
Akageuka kwa hasira kule lilipotokea lile teke. Kumbe Kwakwa hakuwa ameushusha ule mguu uliorusha lile teke la kwanza, hivyo akamtandika tele la pili kwa mguu ule ule, lililotua upande wa kushoto wa uso wake na Bilanga akapepesukia kulia.
Kwakwa akaushusha mguu wake haraka, akaudundisha chini kisha akaenda hewani huku akiukunjua mguu wake mwingine na kumfyatua teke jingine kali la kidevu.
Bilanga akatupwa nyuma kama gogo na kusambaratika vibaya sakafuni, wale askari wakiachia miguno ya mshangao. Bilanga alijaribu kujiinua kwa pupa huku akitema damu, lakini akaenda tena chini bila kupenda.
Kwakwa alibaki akiruka ruka kimakabiliano, akimtazama kwa makini. Bilanga alimtazama kwa hasira kutokea pale chini, na kutema rundo la mate mekundu sakafuni.
“Inuka Bilanga. Ile taabu niliyomuahidi Zay kuwa utaipata nikikushika ndio hii sasa!” Aliambiwa na mpinzani wake, naye akachukia.
Alikurupuka na kumwendea mbio kwa hasira, akiwa amekunja ngumi, lakini kwa hatua isiyotarajiwa Kwakwa aliruka hatua moja mbele kumfuata, akaenda hewani na kumshindilia miguu yake yote miwili kifuani.
Bilanga akatupwa tena nyuma huku akiachia mguno wa maumivu na kujipigiza kwenye ukingo wa lile eneo walilokuwepo kwa kishindo, kabla ya kusambaratika sakafuni kama gunia tupu.
Akabaki akitweta pale chini.
Kwakwa naye alijibwaga chini kwa kishindo baada ya kumrukia yule adui yake namna ile, lakini hapo hapo alijirusha wima na kusimama tayari
344
kimakabiliano. Aliona bado Bilanga hajaweza kujiinua. Akamfuata na kumzunguka pale alipokuwa.
“Ulikuja kutushambulia kwa bomu la machozi sisi, paka wewe, eenh?”
Alimuuliza kwa hasira kisha akamtandika teke kali la kichwa, na Bilanga akagaragazwa tena sakafuni kwa msukumo wa teke lile, akigumia kwa uchungu. Akajitahidi kuinuka, na kufanikiwa kupiga goti moja pale chini, na kubaki akitikisa kichwa kuweka akili sawa.
“Halafu ukamteka na kumtesa shahidi muhimu kwenye upelelezi wetu, eenh?” Kwakwa alimuuliza tena, na hapo hapo akamtandika teke jingine la uso, na Bilanga akatupwa nyuma kwa nguvu, damu na meno vikiruka kutoka kinywani mwake.
Askari wenzake waliachia kelele za kuchagiza.
Bilanga aliinuka kwa shida na kusimama wima, akiwa amekinga ngumi kibondia. Damu ilikuwa imemtapakaa kifuani kutokea kinywani kwake na alikuwa akiyumba kama mlevi aliyeelemewa na kinywaji.
Kwakwa alikuwa akimtazama kwa utovu wa huruma.
“Halafu ukadiriki kunipiga risasi mimi, eenh? Ulitaka kuniua!” Alimuuliza kwa hasira, na kabla Bilanga hajajibu alimrukia tena na kumbabatiza kifuani kwa soli ya kiatu chake.
Bilanga alisukumwa nyuma kwa teke lile na kutaka kuwaangukia wale askari ambao walimkwepa naye akajibwaga chini kwa kishindo. Alijaribu kuinuka lakini hakuweza. Akaanguka tena sakafuni.
Akabaki chali pale chini, akiwa ametawanya mikono na miguu yake huku na huko, damu ikimvuja kinywani na akitweta kwa taabu.
Luis hakuamini macho yake.
“Piga pingu huo mzoga tuondoke nao sasa, bloody shwaini!” Kwakwa alisema kwa hasira huku akijikung’uta mikono yake.
“Duh! Si mchezo aisee!” Mmoja wa wale askari waliokuwa nao alisema, wakati Pojo akimgeuza Bilanga kifudifudi na kumfunga pingu kwa nyuma.
Luis na kibaraka wake walitolewa nje ya jengo lile wakiwa chini ya ulinzi, mbio zao za sakafuni zikiwa zimeishia ukingoni.
Kwakwa alimpigia simu mkuu wake wa kazi kumpa ripoti, wakati wakiwa njiani kuelekea kituoni na wahalifu wao.
“Msweke ndani mpaka kesho asubuhi, aonje raha ya lupango kwanza.
Nitakuja kumhoji mwenyewe!” Mrakibu alisema alipopewa habari kuwa tayari Luis yuko mbaroni.
Usiku ule ule Kwakwa na Pojo waliandaa ushahidi wao dhidi ya wale watuhumiwa waliowakamata, wakiandika ripoti kamili ya kila kilichojiri,
345
Issa Tuwa
Hussein
ikibainisha kila ushahidi waliokusanya dhidi ya ile kampuni na wale watendaji wake Walipomaliza, Kwakwa akampigia simu Inspekta Kelvin wa kitengo cha Anti-Albinism.
“Inspekta, samahani kwa kukupigia simu usiku mkubwa. Naona umuachie tu huyo mganga wa kienyeji… wauaji halisi tunao mbaroni na kuna kila ushahidi kuwa walimbambikia ushahidi huyo mzee ili kukwepa tuhuma za mauaji ya huyo binti… lakini sasa tuhuma zimewaganda. Niko tayari kuongea nawe juu ya ushahidi tulio nao dhidi yao…” Kwakwa alimwambia yule Inspekta mwenzake.
“Ah, Inspekta nadhani uko sahihi bwana... tuonane kesho tupeane dondoo ili nijiridhishe na huo ushahidi wenu kabla sijamwachia huyu mzee…”
“Poa.”
Zay alifurahi pasina kifani alipopewa habari za kukamatwa kwa wale wahalifu wa Liquid Diamond, hususan Bilanga aliyemtesa.
“Ila nigekuwa na furaha zaidi iwapo wangekufilia mbali, wauaji wakubwa!” Alisema.
“Ah, hili lililowakuta ni bora zaidi... wanaelekea kwenye hukumu ya kifo au kifungo cha maisha… na Chabbi ndio hatoweza tena kutembea, kutokana na tathmini ya awali ya madaktari… miguu imevunjwavunjwa vibaya sana kwa risasi... mwenyewe anadai bora angeuawa tu!” Kwakwa alimwambia.
“Sa’ si mngemuua tu? Mwenyewe kataka afe nyie mnabakisha bwana!”
Zay alisema kwa hisia kali, na Pojo na Kwakwa wakatazamana.
“Sheria haifanyi kazi hivyo bibie…” Kwakwa alimwambia.
Asubuhi ya siku iliyofuata ilikuja na mshituko mkubwa kwa Zay, pale alipogongewa hodi na kuambiwa kuwa alikuwa ana mgeni. Alishangaa, kwani hakuwa akitaraji mgeni yeyote, lakini mshangao wake ukawa shangwe pale alipoona kuwa mgeni mwenyewe alikuwa ni mpenzi wake Mchebbe. Aliruka kwa furaha huku ukelele wa furaha ukimtoka na kumkumbatia kwa nguvu, furaha yake ikihamia kwenye kilio cha uchungu.
346 MTAFITI
“Okay, nice buttocks, Okay. The handsome guy is here to scare the ugly guys away, okay…? Relax babes!” Mchebbe alimwambia kwa kuchombeza huku
akiwa amemkumbatia kwa upendo, akimaanisha kuwa kijana mwenye mvuto, yaani yeye, ameshafika kuyafukuza majamaa yenye sura mbaya, na kwamba atulie tu.
Hili liliamsha kicheko kilichochanganyika na kilio kutoka kwa Zay, na wote wawili wakabaki wakiwa wamekumbatiana namna ile kwa muda mrefu pale chumbani kwake kwenye kile kituo cha polisi.
“Inspekta Kwakwa amekuwa na msaada mkubwa sana kwangu, na ameniambia kuwa sasa naweza kurudi nyumbani kwangu… maana wale watu wabaya tayari wameshakamatwa!” Zay alimwambia mpenziwe, na Mchebbe akamuachia na kumkalisha kitandani.
“Er, Zay… nilikuwa nimechukua jukumu bila kukushirikisha mpenzi, naomba usichukie…” Alisema, na Zay akawa makini.
“Ni nini tena mpenzi, mbona unanitisha?”
“Si jambo baya sana… kama utalichukulia poa…” Mchebbe alimjibu, na alipoona anazidi kumchanganya, akaendelea, “… nilikuwa nimechukua tiketi mbili za kurudi Rwanda babes... niliona baada ya maziko tungeenda wote kule, ubadili upepo kidogo.” Mchebbe alimwambia huku akimtazama kwa mashaka.
Zay alimtazama kwa muda kama kwamba alikuwa anamshangaa, kisha uso wake ukaachia tabasamu pana la furaha.
“Aaa Dear, mbona ningependa sana iwe hivyooo!”
“Ungependa?” Mchebbe aliuliza huka akiwa amefarijika sana.
“Of course dear, of course!” Zay alisema kwa furaha huku akijirusha tena kifuani kwa mpenziwe. Walikumbatiana kwa furaha.
Maziko ya Mwantumu yalifanyika saa saba mchana ule kule Gezaulole. Zay, Mchebbe na wale askari wawili walihudhuria kule msibani, wale wanaume wakienda hadi kule makaburini kuzika. Ilikuwa ni simanzi
kubwa sana kwa Zay kujua kuwa rafiki yake ndio anaenda kwenye malalo ya milele.
Muda wote alikuwa akifuatilia sana simu yake hasa kwenye mtandao wa facebook, na ilipotimu ile saa saba, muda ambao rafiki yake ndio alipangwa
347 Hussein Issa Tuwa
kulala kwenye malazi ya milele, kila kitu kikalipuka, na njozi za yule waziri wa Madini na masuala ya nishati kulizima sakata la kampuni ya Liquid Diamond zikayeyuka vibaya sana, tena kwa kishindo…
Wakiwa kule makaburini, Inspekta Kwakwa alipigiwa simu na Mrakibu mwandamizi.
“Kwakwa! Uko wapi wewe?” Aliulizwa.
“Ah, si n’likwambia kuwa nitakuwa mazikoni kumzika Mwantumu afande... kwani vipi?”
“Vipi? Kila kitu kimeharibika huku! Hakuna siri tena! Hivi niongeavyo mimi na DCI sote tumeitwa kwa IGP huko... NI BALAA!” Mrakibu alimbwatia kwenye simu.
“Akh! Balaa la nini tena bosi? Bilanga katoroka?”
“AKH! Ile ripoti ya Grayson…”
“Imefanyaje?”
“Iko wazi mtandaoni! Watu… wananchi wamekuja juu vibaya sana mitandaoni humu… facebook inarindima Liquid Diamond tu. We’ uliitoa kopi ile ripoti kabla hujaiwasilisha kwangu, eenh?” Mrakibu alieleza na kuuliza.
“Mimi? No! Sikuitoa kop... OH! Oh…!” Kwakwa alisema huku akili ikimjia juu ya kilichotokea.
“Ni nini?” Mrakibu alimuuliza.
Kwakwa alipiga kimya.
“Nadhani namjua aliyefanya hivyo afande!” Hatimaye alisema.
“Ni nani huyo Kwakwa... ni nani?”
“Ah! Nadhani ni Zay afande!”
“Oh Shit!” Mrakibu alimaka na kukata simu.
Kwakwa alirudi nyumbani kwa akina Mwantumu na kumkabili Zay.
“Umefanya nini Zay…?”
“Nimeizika Liquid Diamond Inspekta… muda ule ule ambao rafiki yangu anazikwa, na yenyewe inazikwa bloody fools. Nifanyeni lolote mtakalo!” Zay alimjibu na Kwakwa akabaki akimtazama kwa kutoamini.
“Ni siku ile ulipoenda kuifuata hii ripoti kule kazini kwenu na ukatusubirisha nje kwa muda mrefu, sio? Ndio siku ulipohamishia ile ripoti kwenye mtandao wako?” Alimuuliza.
“Nilijua ile ripoti ikifika kwa wakubwa zenu sitakuwa na mamlaka nayo tena. Na kweli! Nilijaribu sana kukuelewesha kuwa nilitaka sana kuwalipua
348 MTAFITI
Liquid Diamond… hukutaka kunielewa. Sikulaumu. Naamini na wewe hutonilaumu kwa hili!” Zay alimwambia.
Kwakwa akafyatua cheko hafifu ya kutokujali.
“Na ndio maana siku ile uliposhikiliwa na Bilanga, ulikuwa unatushinikiza kuwa tumpe tu ule ushahidi, siyo? Ulijua kuwa tayari ulikuwa umeshapanga hili litokee.” Kwakwa alimwambia.
“Ni kweli Kwakwa. Kwangu hili lilikuwa ni muhimu kuliko yote. Nashukuru limetimia!” Zay alimjibu huku akimuonesha mtandao ule kupitia kwenye simu yake.
Ukurasa wa facebook alioutengeneza na kuuita UFISADI WA LIQUID
DIAMOND INCORPORATED ulikuwa umeanika wazi kila kilichotokea kwenye zile tafiti za nishati nchini, na jinsi mtafiti Grayson Mochiwa na rafiki yake Mwantumu walivyouawa na watendaji wa ile kampuni iliyoaminiwa na serikali.
Na mwisho ule ukurasa ukaianika wazi ile ripoti ya Grayson iliyofichwa, ikionesha jinsi utajiri wa gesi ulivyotanda kule Mtwara wakati wananchi wa huko wakiteseka kwa dhiki na umasikini.
“Oh my God! Zay…! Umelipua bomu nchini…” Kwakwa alisema kwa mashaka.
“Watu wanastahili kujua. Niliipanga hii habari itoke hewani ikifika saa saba kamili mchana leo hii... na naona nimefanikiwa!” Zay alisema kwa ushindi.
Kwakwa alibaki akimtazama kwa mastaajabu huku akitikisa kichwa, tabasamu jembamba likiranda mdomoni mwake.
Asubuhi iliyofuata Zay na Mchebbe walipaa kuelekea Rwanda.
349 Hussein Issa Tuwa
YALIYOTOKEA BAADA YA zile vurugu za gesi ya Mtwara ni kisa kingine kabisa kilichowahusisha sio tu wote walioshiriki
kwenye kuutekeleza na kuupinga ufisadi ule wa Liquid
Diamond, bali pia wengi wengine waliolazimika kuingia kwenye kadhia
ile kutokana kuhusika kwao na moja ya pande mbili zilizokuwa zikisigana
kwenye kadhia ile— upande wa haki na ule wa batili.
Itoshe tu kwa hapa kusema kuwa, kutokana na habari ya gesi ya Mtwara
kuwekwa wazi na Zay kupitia mtandao wa intaneti na kupambishwa
vilivyo na vyombo vya habari, baada ya muda wananchi wa Mtwara nao
wakaja juu, wakiidai gesi yao kwa nguvu moja. Kwa miezi kadhaa, nchi
iliingia kwenye mtafaruku wa gesi ya Mtwara, na kwa namna fulani suala
la Zay kurusha ile habari hewani likapotea tu, na ule ukurasa wake wa facebook ulioianika Liquid Diamond ukafutwa.
Katikati ya vurugu zile zilizomfikisha hadi waziri mkuu kumwaga
chozi bungeni, Waziri wa madini na nishati alitangaza kujiuzulu, na kwa kuwa watuhumiwa wote muhimu walikuwa mbaroni haikuchukua muda
kabla mwenyekiti wa ile kamati ya bunge hajang’amuliwa na kamati yake kuvunjwa. Hatua nyingine za kisheria ziliendelea kuendeshwa dhidi ya wote waliohusishwa akiwemo yule waziri aliyejitia kujiuzulu.
Ilikuwa ni kesi iliyounguruma kwa muda mrefu, huku mbinu chafu za Liquid Diamond zikizidi kutumika kujaribu bila mafanikio kujiengua kwenye tuhuma.
Mwishowe, Luis Kambesera, Bilanga na Chabbi Cheka walifungwa vifungo vya maisha kwa makosa ya kuhujumu uchumi wa nchi na pia kupanga njama na kutekeleza mauaji ya Grayson Mochiwa na Mwantumu Uledi. Wale watendaji wengine wa ile kampuni yenye mambo ya nyuma ya pazia walihukumiwa kwenda jela miaka saba kila mmoja.
Wakati hayo yote yakiendelea, siku chache tu baada ya kurejea Rwanda akiwa ameambatana na mpenzi wake, Mchebbe alisaini mkataba mrefu
zaidi kule Rwanda, na akafanikiwa kumpatia Zay kazi kwenye kasino kubwa sana jijini Kigali, ili tu awe naye kule kwenye nchi ngeni.
Mijadala yao kule Rwanda ikawa inaelemea zaidi kwenye suala la ndoa.
Inspekta Kwakwa na Sajenti Pojo wote walipandishwa madaraja kutokana
350 MTAFITI
HITIMISHO
na utendaji wao uliotukuka kwenye kesi ile, huku Pojo akihamishiwa
kwenye kile kituo kikuu cha polisi, maarufu kama central, na kujumuika na mkuu wake mpya wa kazi, Haroub Kwakwa.
351
Hussein Issa Tuwa
*