SIMULIZI: SAIDA
MTUNZI: SIMULIZI ZA SUMMY
WHATSAPP: 0624853116
SEHEMU YA: 151 HADI 175
Sehemu ya 151
Dr khairat alilia kwa huruma aliamini
amefanya makosa makubwa Sana. Hivi
kwa Nini alienda kupigana na Saida asubuhi ya siku hiyo?.
" Mustafa naamini hautafata
wanachotaka ndugu zako' sio?" Dr
khairat aliweka macho ya huruma mbele ya Mustafa akitamani Mustafa
abadilishe mawazo Yake..
Mustafa alimwangalia Kisha akamjibu
bila kujari. " Hapana, lazima niisikilize
familia yangu, hata hivyo sikuwahi
kukupenda, nilikuoa wewe kwa sababu
tu ya kujisaidia, lakini wewe umefanya
Nini? Umenigeuka ghafla na Kisha
kutafuta Vita ya nguvu na familia yangu". Mustafa alimkazia macho
khairat aliemuogopa ghafla.
" Mustafa naomba unisamehe, sikutaka
Vita nao, nilitaka uwe upande wangu"
Dr khairat alikua bado kapiga magoti
akimbembeleza Mustafa.
" Ooh! Yawezekana, lakini nadhani kwa
Sasa Sina maana kwani sipo upande wako, nilionekana kutokua upande wako
kwa kua nilienda kulala kwa mke wangu, mwanamke ambae unatambua kabisa kua
yeye ndo safari ya mapenzi katika uhai
wangu" hapo Dr khairat alihisi kufa.
" Mustafa nilikupenda kabla Yake, nilikupenda kabla hata hujamuoa mama
Shayma, nilikupenda kabla hata
sijaolewa na kumpata Adil. Nawezaje
kukubali kushindwa upendo wako?" Dr khairat alifungua moja kwa moja
Mustafa akabaki amemshangaa.
" Ina maana ni kweli Saida alikua sawa, hukuwahi nichukulia kama rafiki yako, Bali ulihitaji kua mwanamke wangu? "
Mustafa aliinuka alipokua
amechuchumaa na kusimama Kisha
akaendelea. " Ukweli ni kwamba, siwezi
kua na mwanamke muongo na mnafiki
hata kwa sekunde moja, khairat we
umefanya Mambo mengi Sana kwa ajiri
ya kua na Mimi, hata siwezi kufikiri
Kutamka Ni jinsi gani uliamua kujifanya
kichaa'" Lo! Dr khairat alipigwa na
vumbi ya butwaa. Inamaana Mustafa alifahamu kua alijifanya?
" Mustafa hapana, najua wewe unaniamini ee! So ndio?" Aliinuka pia na kujaribu kuushika mkono wa Mustafa ili apate umakini wake lakini Mustafa alimsukuma mbali.
" Usithubutu kunisogelea kwa machozi ya kinafki wewe mwanamke" macho
makubwa ya Mustafa yaligeuka madogo
ghafla na kujifinya kwenye ngozi yake kana kwamba yalifichama humo.
" Hakuja ambacho sikua nafahamu wewe hapo Dr khairat, nilifahamu kila kitu
dhidi yako, nilijua Jambo Hilo mapema, niliamua kunyamaza nikiamini kabisa
unafanya hayo kwa ajiri ya mtoto
wako. Lakini bado ulitamani kumuua
Hizaan. Sidhani Kama unafaa kua
binadamu" Mustafa aliwaka kwa chuki
dhidi Yake Dr khairat akaogopa zaidi.
" Mustafa hapana ! Haikua akili yangu?
Naapa Mustafa nakupenda Sana, yote ni kwa ajiri yako wewe" Dr khairat
alisimama mbele na kujaribu
kumbembeleza kwa kumshika mabega
Yake. Mustafa hakuacha kumfukuza
kwa kumsukuma mbali kwa Mara
nyingine...
" Isingekua tatizo iwapo ungenipenda tu khairat, huenda ningekuona hata mke wa pili, lakini mwisho wa siku nafaa
kuona zaidi ya rundo la takataka. Kweli
ulithubutu kuchangia kifo Cha mama
Shayma?" Dr khairat aliganda Kama
sanamu badala ya kulia maneno hayo
kutoka kwa Mustafa yalimshtua. Ilikua
kana kwamba akiwa ndani ya katakana
la Moto na kuunguzwa. Inamaana
Mustafa anafahamu' Jambo Hilo pia?
Kwani Kuna mtu alifahamu juu ya Hilo zaidi yake na bwasha. Bila Shaka
hapana? Em subiri? Bwasha Ni mtu wa Azraj huenda alimwambia Azraj?. Ila
ndo Azraj amwambie Mustafa? Bila
Shaka Jambo Hilo haliwezekani.
" Mustafa hapana, inaonekana
umenichanganya na mtu mwingine?" Dr khairat licha ya kua wazi kwa kila
Jambo bado alizidi kumkana Mustafa.
Ni jinsi gani mwanamke huyu alikosa
haya? Alikua bado akikana makosa Yake
mwenyewe?.
" Yawezekana upo sahihi, nilikufananiaha na mtu ambae, sikufaa
kufananisha nae" Mustafa alijibu na kutaka kuondoka. ..
Dr khairat bila kujizuia aliuliza moja
kwa moja, ndani ya moyo wake Mustafa
alitabasamu kwa Ni swali ambalo alikua
akilingoja kwa muda mrefu Sana. Na
kwa akili ya khairat iliyopaniki bila
Shaka angempa ukweli kamili. " Aah'
nasikitika kukwambia ya kwamba, watu wa Badru Ni wamoja, hata Kama
tukigombana nje, kwa ndani Ni watu
ambao tutazidi kushikamana na kufanya
vitu pamoja, Kuna muda lazima
tumuaminishe adui kua sisi tunamsaida afikie lengo lake. Kisha
tumsambaratishe Mara moja" kwa kweli
Dr khairat alitafakari maneno hayo na
kumuelewa moja kwa moja Mustafa.
Alimaanisha wao wanaweza kugombana upande mmoja lakini upande wa pili
" Mustafa Nani kakwambia haya yote?"
wanashirikiana, hiyo inamaanisha mtu
kutoka kwa familia ya Badru
anaemsaidia ndo kamuuza yeye??.
" Hapana haiwezekani" hakutaka
kukubali kua Azraj Badru alimzunguka.
" Huwezi kusema ni...." Dr khairat
alipigwa na baridi usoni..
" Ni sahihi unachowaza, Mimi na Azraj
sio maadui Kama unavyodhani?*
Mustafa alifungua mlango wa gari Kama
atadondoka Ila moyoni hakumaanisha.
." Hapana Mustafa huo sio ukweli,
Azraj hawezi kua mzuri kwako kwani
kila kitu kikienda kwa amri Yake" Dr
khairat bila Shaka alichanganyikiwa na
kutaka kuweka kila kitu wazi. Hta hivyo
Azraj kamuuza. Na yeye alikua mjinga
kiasi gani? Alimuamini huyo mtu ?
" Kaa kimya!!" Mustafa alionekana
kukasirikia na kugeuka kumpiga Kofi bila
kusubiri Dr khairat akaficha uso wake huku akiongea.
" Hapana Mustafa nasema ukweli, Azraj sio mtu mzuri kwako, hata kifo
Cha mama Shayma alihusika yeye, ana
kambi kubwa ya magaidi ambayo
ananitumia kukuangamiza wewe, hata
mama Shayma alikua amelengwa kwako, na mwisho aliishia kufa baada ya
kwenda kinyume nae, sidhani Kama
unafaa kumuamini, hata hivyo
aliniaminisha kua hakupendi na anakuaibisha kua anakusaidia Hilo
haliwezekani, Sasa au baadae Azraj
anaweza kuudhibiti familia nzima ya
Badru na kuiweka chini yake." Mustafa
alipigwa na butwaa akamtegea sikio Dr khairat.
" Hivi karibuni atafanya nyie wote mumsujudie,. Kweli Ni ndugu yenu lakini
ana Mambo mengi huyo mtu usimuamini, amepiga hatua kubwa kukufikia"
Mustafa alionyesha sura ya
kuchanganyikiwa kana kwamba ahakua akijua. Aligeuka klna kumtetea sikio
vyema Dr khairat aliekua akijieleza kwa
kila kitu juu ya Azraj. Taarifa zote
haikuweza kumshtua Mustafa. Lakini
taarifa juu ya mke wake wa kwanza ndo
taarifa pekee ambayo ilikua mpya na
mgeni kwake. Alihisi kuchoka.
Alikumbuka Ni vipi alikutana na
mwanamke huyo. Alikua mwanamke
mpole na asie na hatia alimuamini na
kumpenda kwa wakati mmoja. Lakini
kumbe alikua na sifa chafu Kama hiyo na hakua aliitwa Saida pia?. Alimkaba Dr khairat Koo lake bila kufikiria " huo
ni uongo" Mustafa aliunguruma huku Dr khairat alidhani labda Mustafa amechanganyikiwa juu ya Azraj.
" Huo no ukweli Mustafa, yeye ndo kila kitu, na yeye ndo alitaka nimuue Hizaan
ili nisisumbuliwe na mtu nikiwa na wewe, huku yeye alimpata Saida ki urahisi, hata Ile video ya kipindi kile yeye ndo
aliitengeneza, Mustafa Azraj amefanya mengi kutuunganisha na wewe" Dr khairat alikili kila kitu mbele Yake.
Akiwa Hana matumaini ya kumpata
Mustafa Tena ? Kwa Nini amuache
Azraj aliemsaliti.
Mustafa hakuweza kusubiri kuondoka
hapo kimya. Dr khairat hakuweza
kumzuia kuondoka pia. Alimuacha aende tu, lakini ukweli inauma Sana, Azraj
pekee ndo alikua tumaini lake hapo
awali kumfikia Mustafa lakini mwisho
wa siku hata yeye hakua mtu mwema, aliweza kumuumbua kwa Mustafa. Dr
khairat alilia kwa sauti. Kwa bahati
nzuri mtoto pamoja na mfanyakazi wake
hawakuwapo? Bila Shaka alikua akienda
kukumbuka mbele ya mtoto wake.
Katika jumba la Badru Mustafa aliwasili
akiwa amechanganyikiwa kabisa. Kwa
taarifa alizopewa juu ya mama Shayma.
Hivi Ni kweli alichosikia au alisikia
vibaya. Hakuweza kuchelewa kumpigia
simu Dr Neema ambae alijibu Mara moja simu Ile.
" Nakuhitaji nyumbani Mara moja"
Mustafa alikua skate simu lakini Dr Neema alimsimamisha.
" Boss nafaa kufahamu iwapo, Ni
nyumbani wapi? Maana una sehemu tatu
za kuishi" Mustafa alihisi kupagawa . "
Inamaana makazi ya familia ya Badru
hujui yalipo" baada ya Mustafa kufoka
Dr. Neema alijibu Mara moja kua
atafika Mustafa alikata simu na
kuteremka kwenye gari akakutana naaumbile ya watoto wake wasio na hatia.
" Baba" walimuita na kumrukia.
" Bamdogo muksin kamleta mama" Kim
hakuchelewa kuongea.
" Mama ameumia baba, inabidi umpe
funzo Yule mwanamke mchawi" Shayma
hakuacha kumkumbusha Mustafa juu ya ushetani wa Dr khairat kumshambulia
mama Yake na kusababisha achukuliwe na polisi, Kisha arejee akiwa ameumia.
Mustafa alimwangalia binti Yake
shayma kwa maumivu makubwa. Ni kweli
alikua binti Yake ambae alimpata
kutoka kwa mwanamke asiefaa.
Alimzaa na mwanamke aliejitambulisha
kwake kwa mapenzi na taswira ya
uongo? Yaani aliagizwa na Azraj, alipata maumivu zaidi kila alipokumbuka
Hilo. Alikua amependa kwa Mara ya kwanza bila kusikia. Hakua alielewa
Wala kuambilika lakini ilimuuma zaidi
kila alipokumbuka maneno ya Dr khairat. " Alikua kahaba kwenye
makasino, aliokotwa huko na Bwasha"
Lo! Dr khairat alifikiria hata alivyokua
akimtamkia hayo maneno.
" Hakua akikupenda hapo mwanzo, Wala
hakua aliitwa Saida, aliitwa Raina.
Alikufa baada ya kwenda kinyume na
Azraj, usimuamini azraj, kosa
alilofanya mama Shayma Ni kukupenda
wewe" Mustafa alihisi kurukwa na akili
zake. Mbona Kama hawezi kuamini
alihisi kumpata Azraj mapema Sana.
Hawezi kumsuburi Dr Neema.
" Baba unaenda wapi?" Shayma na Kim
waliogopa inamaana baba Yao
alichanganyikiwa na Mimi mpaka
aondoke bila kumuona mama yao.?
Mustafa hakuweza kujibu swali la hao
watoto. Aliondoka zake hapo.
" Baba, mama anakusubiri" walimuita
lakini waliishia kuona gari uliishia getini"
" Ameondoka tayari, mnafaa kwenda ndani" Najma aliwashika mikono wale
watoto wawili waliopata huzuni.
Alichuchumaa kando Yao baada ya kuona Hali zao.
" Mnakosea Sana, hamfai kua hivi?"
Najma alijaribu kuwabembeleza. "
Mnafaa kuturahi kwani hivi Sasa mama
amekua na baba wataishi pamoja na
nyie milele, sio kwa aunt khairat
Tena?" Najma aliongea kuwakumbusha.
" Kweli aunt" Shayma alihisi kufurahi.
" Ndio huo ni ukweli, au unasemaje
Kim?" Kim aliinua kichwa chake na
kujibu. " Nakuamini" Kisha uso wake
ukasinyaa baada ya kumkumbuka
HudHud ambae bila Shaka angerejerea
neno Hilo Mara moja iwapo Angekua kando Yao.
" Twendeni kwa mama Sasa, baba atakuja mapema au baadae" Najma
aliingia nao ndani akakutana na Salma akizunguka huku na kule.
" Weee nae vipi?" Salma hakuweza
kujibu isipokua alikaa kimya akionekana kuchanganyikiwa. " Hapana najua siku
bado" Najma alitoa macho nje.
.Salma alimtazama najma ana kuweka sura ya huruma. Ni kweli, siku zilikua
bado, lakini aligombana na Azraj wakati wao hawakuwepo. Azraj hakujari juu ya
ujauzito wake mkubwa hata alimsukuma
ukutani. Bila Shaka hayupo salama
kabisa.
Najma alipata khofu na kupaza sauti
Mara moja. " Mama" watu waliokua na
Saida mapema Sana walikimbia upande
wa najma ambapo sauti ilitokea. Najma
alishtuka zaidi na kuwaomba watoto
waondoke hapo. Kwani sio tu alihisi
tofauti kwa Salma. Bali pia aliona damu zikimtoka.
" Salma Kuna Nini?, Nini kilikupata
jamani?" Najma alipata khofu alijiuliza
Ni kipi kimemkuta mwanamke huyo na
kwa Nini hawezi kuongea. Bi Shayma
aliongozana na na wanawake wengine
waliokua ndani ya nyumba Ile Kisha
wakamuacha Saida akiwa amelala
chumbani kwake. Kwani alikutana na
Hali isiyoeleweka huko sero pia Hadi
akawa mgonjwa ghafla
" Salma!!!" Kila mtu alishtuka. Ni kweli
alikua karibu kujifungua lakini hakua
amefika siku maalum. Ilibidi waingie
nae kwenye gari na Kuondoka wote kwa
pamoja. Dah! Wanafamilia wa Badru
walionekana kua na upendo wa Hali ya juu' kwa Salma na sio kwake tu.
Huenda watu wanaweza kua
wanawasema vibaya huko nje lakini
ukweli ni kwamba Hawa watu ni watu
wema Sana.
Salma alihisi hatia juu Yao.
Wanamthamini Sana Azraj lakini Azraj
ni nyoka asiestahili kukaa katikati ya kundi Hilo la watu wazuri. Binadamu
asieona thamani ya mtoto wake
mwenyewe anastahili kweli kuishi katika
hii dunia?. Yalikua maneno ambayo
yalikatiza katika akili ya Salma akiwa
na uchungu mkali. Hakuweza kutoa sauti
katika mdomo wake hata
kidogo. Na
Hali hiyo iliwashangaza watu wote.
Kama mwanamke alifaa awe amepiga
kelele nyingi kwa nguvu kwa sababu ya
uchungu lakini alionekana kuumia kimya kimya bila Kutamka neno, Wala kutoa sauti yoyote Ile.
Sehemu ya 152
Wakati watu wote wameondoka ndani ya jengo la Badru kuelekea hospitali ndani ya nyumba alibaki Saida watoto wake
zarina, Asia pamoja na Bibi. Saida alirejesha fahamu zake na kuamka moja kwa moja alikumbuka kilichomkuta huko sero ndani ya dakika chache. Hakika
alipangiwa njama. Yaani aliingia tu sero na kuambulia kichapo Cha wafungwa waliokuwepo mle ndani.
" Khairat huyu mshenzi, alithubutu vipi
kunifanyia hivi?" Saida alishika kichwa
chake akiwa amechanganyikiwa. "Mama umeamka? " Aliingia Shayma akiwa
kaongozana na mdogo wake. Walikua
Kama mapacha bila Shaka
wangeongozana kila sehemu.
" Ndio nimeamka kipenzi" Saida
alijikaza kuvumilia maumivu Yake. Moyo
wake ulimtuma amtafute Najma akampe
funzo Dr khairat haiwezekani ampeleke
sero kwa masaa kadhaa.
" Aunt najma Yuko wapi?" Watoto
Hawa wawili walipata wivu mama Yao
hata hakujari kuhusu wao alimuulizia
aunt najma moja kwa moja Bora
angeuliza kuhusu baba Yao.
" Kwa Nini aunt najma, inamaana hata
sisi hatupo" Saida alihisi kulia Hawa
watoto walikua Kama baba Yao tu, wangewaza kupendelewa na yeye zaidi
kabla hajatangulizwa mtu mwingine.
" Hapana nyie mpo mbele yangu
wapenzi, niliwamiss Sana, na nawapenda
Sana, lakini si mnamjua aunt najma, nataka tukampe SoMo la ziada yule
mchawi aliekuja kupigana na mimi
asububi nyumbani' Saida aliwaambia
watoto wake mipango aliyokua nayo
wakafurahi.
" Wao mama, lazima apate SoMo lake"
Shayma aliongea.
." Mama usisahau kuharibu pua Yake"
Kim alitoa mawazo mabaya zaidi, alifaa
kuharibu Hadi pua. Kweli huyu mtoto
alistahili kua mtoto wa Mustafa.
" Watoto wa hovyo nyie, mbona
mnanitisha Sasa"
" Sisi ni watoto wa Mustafa Badru, huwa hatuachi Jambo lipite bure"
Mustakim aliongea kauli ambayo baba
yake' huwa anapenda kumwambia.
" Hiyo ni kweli mama, damu ya Mustafa
Badru inatembea ndani yetu" Saida
alihisi kucheka. Baada ya kusikia
maneno hayo.
" Haya Sasa, huyo Mustafa Badru Yuko
wapi? Mbona simuoni?" Saida hakua
akifahamu iwapo Mustafa ameachana na Dr khairat tayari.
" Aah'" Shayma alikumbuka.
"Mama baba ametoka Mara moja na
atarejea, lakini akirejea kumbuka kua
mwema kwake hayupo vizuri kabisa ki
fikra" Shayma alimshauri Saida. Lo!
Huyu binti huyu. Anawezaje kugundua
iwapo mtu hayupo vyema ki fikra?.
" Sawa bila Shaka ntafanya hivyo, twendeni sebureni, nahitaji kuonana na wengine" Saida aliwasogeza mbele Kisha akainuka kitandani.
" Bila Shaka wengine ni kina dada zarina pamoja na dada Asia." Shayma alimhoji.
" Kwani hakuna wengine zaidi Yao"
" Labda wakina anko getini" Kim alimkumbusha.
" Hiyo inamaanisha nini? Wengine wako wapi Hadi Bibi?" Saida alihisi kuchanganyikiwa.
." Hawapo wamempeleka aunt salma
hospitalini nipo njiani kupeleka chakula
inasemekana tayari kaingizwa kwenye
chumba Cha upasuaji zarina aliingia
chumbani akitabasamu kwa majonzi.
Saida alishtuka hiyo ilimaanisha kwamba
Salma amefikia wakati wa kujifungua na ameshindwa kujifungua kawaida?.
' hiyo ilimaanisha nini? Alikua
akiendelea vizuri hapo awali,
angejifungua kawaida tu' Saida
alimwangalia zarina ambae alijibu swali
lake bila kuulizwa.
" Aah' ki ufupi waligombana na Kaka
Azraj sisi hatujui chanzo Ni nini lakini
walionekana kubishana Sana, na mwisho
Azraj aliondoka chumbani kwa hasira na kumuacha mwenyewe, wakati huo huo
watu wengine walirejea wakiwa na fikra
zote juu yako, baada ya hapo Najma
ndo alishtuka kuhusu Salma na Sasa
wapo hospitali" Saida hakuweza kusubiri
kuinuka ajiandae waelekee huko.
" Twende huko haraka" Saida aliingia
bafuni ajiweke sawa kwani hakua
ameoga wakati alipotoka sero alifika na kulala atibiwe.
Shayma na Kim walihisi upweke na huruma juu ya aunt Salma kwa wakati
mmoja. Kim hakua alipendezwa na aunt
Salma mwenye ulimi mchachu Kama
ndimu, ambae hakuweza kuvumilia
kumsema kila wakati.
" Mama aunt Salma atakua salama?"
Shayma alipata khofu.
" Bila Shaka mpenzi" Saida alikipaoasa
kichwa chake kidogo na kuelekea
bafuni.
" Haya twendeni" zarina aliwachukua
Wal watoto wawili na kuondoka nao
hapo chumbani.
Baadae Saida na zarina walikua njiani
kuelekea hospitalini. Wakiwa kwenye
gari Saida alionekana mchovu na
aliechoka. Moyo wake ukipata wasiwasi
ghafla bila kujua. Zarina aliuona uso
wake uliopoteza furaha.
" Bi mdogo!" Zarina alipata uwoga.
" Nipo sawa" Saida alimtoa khofu Ila
zarina bado alibakia na mashaka kwani
Nini kilimkumba Saida?. Ghafla gari ilipiga breki bila kutarajia.
" Huwezi kua Makini unapo endesha???"
Saida alifoka akimlenga dreva aliekua
kawabeba.
" Samahani madamu, Kuna mtoto mdogo
kasimama barabarani Analia
nimeshindwa kukatiza". Saida alishtuka.
" Mtoto? " Hii ukimaanisha Nini? Mi
saa Saba za mchana alafu mtoto
barabarani kasimama akiw mwenyewe?
Ilibidi achungulie kuhakikisha.
" La! Haula Ni mtoto wa miaka miwili tu na haelewi aende wapi? Mtoto alizidi
kulia na Saida akapata huruma na kuteremka ndani ya gari.
" Bi mdogo hapana" zarina alipata hofu na kuhusu hatari zaidi.
" Ni mtoto! Ni mdogo" Saida hakuweza
kujizuia moyo wake wenye huruma na kuelekea alipo mtoto Yule.
" Hapana Bi mdogo ungeacha nimuone
Mimi" Dereva aliongea na kumuelekea mtmto ambae alifikiwa na Saida kabla ya dereva.
" Mpenzi mama Yuko wapi?" Saida
alijaribu kumshika mtoto na kushangaa anashika hewa, sauti ya mtoto akilia
iliendelea lakini bado ilionekana Kama
Maruerue. Saida alishtuka na kuogopa
kwa wakati mmoja. Alikua kaona Nini?
Inamaana Ni mzimu au. Dereva pia
alishangaa kwa macho Yao pale
anaonekana kuwepo mtoto lakini mtoto asiegusika Ni binadamu kweli.
Khofu iliwatanda wawili hao na kubaki wametizama kwa mshtuko. Wakati
huohuo walitokea vijana wawili waliovalia suti myekundu mbele ya Saida na dereva.
" Nyie kina kina Nani?" Kwa khofu na uoga saida pamoja na dereva waoihoji.
Ndo wakati huo zarina pia aliona
kilichopo mbele Yake. 'Mungu wangu, walivamiwa' hakuweza kutulia ndani ya gari alishuka akiwa na khofu Sana
hawakua na mlinzi hata mmoja Mungu
wangu.
" Bi mdogo" zariza alitetemeka. Na
ghafla nyuma Yao wakatokea wanaume
wawili hivyo kwa ujumla wakawa wanne.
Wanaume hawa walishika visu mikononi
mwao, na Ile taswira ya mtoto
ikayeyuka baada ya kujitokeza mwanga
Kama radi alipokua kasimama mtoto
Yule. Na watu wawili kutoka kulia kwao
wakaja na spika ambayo ilicheza sauti ya kilio Cha mtoto. Inamaana
walichezewa mchezo wa mawazo ya akili. Walichezewa ki fikra. Walikua
kwenye ( Illusion)
Saida alihisi kuchanganyikiwa na kuogopa Sana. Yaani siku za hivi
karibuni Mambo yamekua ya kutisha
Sana kwenye Maisha Yake.
" Mnata taka Nini?" Saida aliuliza huku
akijaribu kujiepusha nao hao watu
" Oohh bi Mustafa" mwanaume mmoja
mwenye sura mbaya ambae Saida
hakuwahi kumuona katika Maisha Yake.
Alisimama mbele Yake. Saida
alimtazama kwa Makini hakuweza
kumtambua na kitu pekee alichopata
kukuona kwa mwanaume huyo ni chuki na hasira nyingi mno dhidi Yake.
" Msithubutu kumgusa yeyote Katika
sisi" zarina alifoka na kupigwa risasi ya tumbo ghafla. Saida alishtuka kiasi
kwamba uso wake ulipauka nithili ya jivu, hakufahamu kabisa Kama ilikua
rahisi kiasi hicho kwa mtu kufa. "
Zarinaaaaaa" aliita kwa sauti na uoga.
Zarina pia alishangaa na kubaki
ameshika tumbo lake kwa maumivu. "
Sipendi kuongeleshwa na mbwa nikiwa
naongea na mwenye mbwa" bwasaha
alisema bila kusita Hali hiyo
ilimkasirisha dereva na kujikuta
akipaniki. " Unaweza kumfanyia hivyo, yeye ni mwanamke tu" na hapo dereva
aliekua kavimba kifua kumfata Bwasha
lakini aliishia kukamatwa na kupiga
nyuma ya feel zake akawa mgumu
kwenda chini. Watu wale makatili
wakamchoma vizu vya miguu. .dereva
akashuka chini mwenyewe bila kupenda huku akipiga kelele
" Wanadamu wengine bhana hawana hata maana aliweza tu.kumpiga risasa mbili kwenye paji la uso wake" Saida
alichanganyikiwa kwa bado zarina hakua
amekufa Ila dereva hakuatahili hata
salaam take ya mwisho . Zarina
akabaki akiliankwa uwoga. Huku Saida
ameshikiliwa zarina alijikuta haelewi
anayoyashuhudia.
" Hapana jamani" Saida alipiga kelele
na kubaki haelewi.
." Bi mdogo usiogope, bila Shaka
hawatakudhuru" aliongea zarina ambae
ambae alipata maumivu makali kwa
risasi moja ya tumboni. Alikua kwenye maumivu makali zaidi.
" Zarina hapana" Saida alichanganyikiwa na kuanza kupiga kelele akiwa haelewi
Kama anamshuhudia hicho kitu. Bwasha
alianza kucheka kwa Nguvu Sana.
" Mleteni" neno lake moja lilimtosha
Saida. Watu wale hawakua na masihara
hata Saida alimkumbatia zarina kwa
kuogopa. Zarina akaanza kufoka.
" Nyie Ni wanawake wenzangu
mnawezaje kumuwinda mwanamke mmoja
kwa watu wengi" Bwasha hakuchelewa
kulenga shabaha Yake vyema na
kumpiga risasi zarina ya nyongeza
aache ujinga.
" Fanyeni haraka, hii Ni Barabara.
Pengine Isha funguliwa" Bwasha
aliamuru na kuondoka akiwaacha vijana
wake walimaliza kazi. Saida alihisi
kupagawa, hakuamini amekishuhudia kifo kikija na kuondoka na uhai wa mtu.
Saida alitekwa ki ulaini sana hakupiga
hata kelele.
Mustafa alikua na hasira na Azraj
hivyo aliamua kwenda kumtafuta kwa
kujua yeye chachu ya kifo Cha mama
Shayma na yeye ndo alimletea mama
Shayma ili kumuangamiza yeye. 'hakika
hawezi kusubiri Tena, hata hivyo tayari
ameachana na Dr khairat na pia anao
ushahidi mwingi Sana dhidi yake, hawezi kusubiri Tena! Kuhusu huyo mtu
alienyuma yake bila Shaka
watamfahamu kuppitia Azraj.
Lakini kabla hajafika aendako njiani
alitingwa na pikipiki ya kijanga aina
TVS akashindwa kuendelea na safari.
Aliteremka kijana mdogo mwenye Rasta
kichwani Mustafa akamtazama Mara
mbilimbili akimvutia picha aliwahi
kumuona wapi? Kwani taswira Yake
haikua ngeni kwenye macho Yake.
' ah' ni yeye kijana anaefanya kazi
karibu zaidi na Dr Neema , hamfahamu
jina lake lakini amemuona nae Mara
kadhaa, kijana huyu mwaminifu kwa Dr
Neema alikua akitaka Nini?'
" Mkuu naitwa Feisoo, Ni kijana wa kazi wa Dr Neema, nime nimekuja
nikihitajo msaada wako" alikua
akihemea juu juu na kuonyesha wasiwasi
wa Hali ya juu' Hadi Mustafa akashtuka.
" Unamaana gani? Mbona una khofu
Sana we kijana mdogo?"
" Bwana mkubwa, Dr Neema alitekwa, alirejea akiwa njiani kuonana na wewe"
" Mmh????" Mustafa alibaki haelewi
hivi ninkweli yeye ndo alimuita Dr Neema lakini alisahau kabisa! Sasa
iweje atekwe na alitekwa na Nani?.
Akiwa anajiuliza wakati huo simu Yake
iliita. Aliangalia mpigaji wa simu alikua
Nani hakupata kuielew simu Ile lakini
alipokea. Kwani alikua na wasiwasi
pamoja khofu kwa wakati huo.
" Habari yako Bwana Badru, ahahaha"
kicheko Cha dhihaka baada ya salamu
kutoka upande wa pili wa simu
kilimuacha hoi Mustafa, alipata hasira
kana kwamba alikaza mikono Yake akiwa haelewi Ni mtu gani huyo?
" Usimkasirikie bwana Badru, Ni kazi kwani Ni habari ndogo tu nahitaji kukupatia" sauti Ile ya mikwaruzo
Mustafa aliivutia picha kwa kweli hakuweza kukifahamu kabisa.
" Wewe ni Nani??" Mustafa alifoka
akihisi kabisa kwamba huyo atakua mtekaji wa Dr Neema.
" Ooh!! Mbona una haraka hivyo, utanifahamu kwa haraka Sana, fungua
simu yako bila Shaka utakutana na ujumbe mzuri na wa kuvutia" mwanaume
Yule alikata simu wakati simu inakatika
kuna video iliingia, Mustafa akashtuka
na kumwangalia kwanza feisoo aliekua pembeni Yake.
" Bwana mkubwa? Ni salama. Kwa sister Neema" kijana Yule alikua na
khofu Kwani alimchukulia Dr Neema
Kama sister na sio tu boss.
" Sijajua" Mustafa alimjibu taratibu
lakini taratibu Yake iliashiria khofu kidogo juu Yake. Feisoo alipata
wasiwasi. Ndo wakati huo Mustafa
akijiandaa kufungua video iliyomaliza ki download Ila kabla haja play simu Yake
iliita. Alikua kiongozi na mkufunzi wa Askari wa Badru. Ni mtu muhimu hivyo
alilazimika kupokea simu.
" Halo" Mustafa aliitikia simu.
" Bwana mkubwa, tuna tatizo"
mwanaume huyo ambae hakuwahi
kuongea kwa wasiwasi Wala khofu
yoyote Ile. Siku hiyo alikua akiogopa.
Mustafa alitambua khofu Yake kwa
wakati mmoja, kidogo kichwa chake kilipuke, alikua na matatizo juu ya
matatizo hakika dunia haikua tayari
kumpa nafasi ya kujitetea kwa sekunde moja, tayari ilimpa tatizo jingine.
" Bwana mkubwa, Dani amejulikana na wapinzani, na alikua na ushahidi dhidi
ya kiongozi wao, na Sasa tunavyoongea
sidhani Kama atakua hai?" Bwana huyo
alitia machungu sauti Yake mpaka
Mustafa akachanganyikiwa alikua kijana aliejitoa kwa ajiri ya Badru lakini
tayari ametambulika kirahisi. Bila
Shaka Mustafa ana kibarua kizito.
Mustafa hakuweza kumpa mrejesho
wowote ule Kama jibu alitamani kukata
simu kabla hajapewa bomu zaidi, yaani
bomu la nuclear. " Bwana mkubwa, mkeo pia Bi Mustafa Badru, ametekwa
nyara na kikundi Cha Azraj Badru"
mwanaume Yule alimaliza kuongea na
kumfanya Mustafa ahisi Kama ngome za masikio yake' zimesiziii
Mustafa alikuaaaa.. labda hakua
amesikia vyema. Yaani mke wake yeye
aliemuacha nyumbani kwao! Akiwa
amelala baada ya kutoka sero, ki rahisi tu ametekwa? Hapana bila Shaka sio
ukweli. Mustafa alimkatia simu huyo
mtu anaeongea upuuzi. Na kuishika simu
Yake. Alifungua video aliyotumiwa akiwa
natetemeka mwili mzima, mikono Yake
pia ulishindwa kutulia. Kwa kweli
hakuweza kuamini alichokua ameambiwa.
Ila Sasa dah! Ni kwamba ameshuhudia
mwenyewe.
' yaani Ni Saida. Alirejea kweli?'
lilibaki swali kwenye akili Yake. Ilikua
ngumu kwa Mustafa kukubaliana na Hilo
lakini video hiyo ilidhihirisha Hilo.
Sehemu ya 153
Mustafa alihisi kusizi kichwa. Akiwa
ameshika simu ambayo kioo chake
nilionyesha video ambayo ilikua ilicheza
alihisi kutetemeka mwili na akili. Feisoo
alikua nje bila kukatibishwa ndani ya gari hakuweza kusubiri kuingia ndani ya gari bila kuambiwa karibu. Aliingia moja
kwa moja na kutupia akili Yake kwenye
kioo Cha simu ya Mustafa.
" Bwana mkubwa" alimuita Mustafa
aliekua amepoteza akili Yake kwenye
kioo Cha simu. Kwa kweli lazima
apotee.
Ni ukweli kwamba mke wake alitekwa
kirahisi hivyo. Saida alionekana akiwa
amefungiwa kwenye chumba kidogo
chenye mwanga hafifu huku akipiga
kelele. Kelele na maneno Yake ya
kumpa faraja lilikua Ni jina la Mustafa.
" Mniache niende, Mustafa akifahamu
atawaua mbwa nyie, mliwezaje
kuniteka? Mustafa atanitoa hapa bila
shaka, hata iwe kwa kuchelewa. Na
sitawasamehee. Mustafa najua
utaniokoa!!!" Saida alikua akiupiga
mlango kwa nguvu lakini hakuna alieweza
kumjibu kabisa.
Mustafa alivurugwa kidogo, mwanamke
huyu alikua hatarini lakini aliamini mtu
pekee wa kumuokoa alikua yeye. Bila
Shaka alikua sahihi mtu pekee wa kumuokoa hakua mwingine zaidi yake.
Akili ya Mustafa ilovutugika akatamani
kumpigia mwanaume Yule lakini namba
haikuweza kupita. Ishara Ni kwamba
hakua na uwezo wa kupiga isipokua
mpaka apigiwe.
" Bwana mkubwa, Dr Neema je?"
Mustafa alitamani amfukuze huyo
kijana tayari alihamishia mawazo take
kwa Saida lakini bado alikua akiulizwa
kuhusu Dr Neema hakuona Kama
anamuongezea mawazo.
Mustafa alimpigia simu mkufunzi wa
Badru kambi. " Bwana mkubwa"
mwanaume Yule aliita.
" Hamkua mkifahamu iwapo mke wangu atatekwa??"
Mustafa alifoka mwanaume
Yule akatulia.
" Bwana mkubwa, ki ufupi tulifahamu
juu ya Hilo, Ila hutukufahamu Kama
itakua haraka kiasi hicho" mwanaume Yule alipata.maumivu.
" Kwa hiyo mnamaana gani? Kulikua na haja.gani ya kuwatoa sadaka vijana
wetu wa tatu kuhusika na kikosi Cha
wanaharamu iwapo hamuwezi kumlinda hata mke wangu tu" Mustafa alitamani
kua karibu Yake.
" Bwana mkubwa ipo namna, hata hivyo ni rahisi kupatikana kwa Bimdogo. Kwani
tunafahamu fika kwa nini amechukuliwa, Jana usiku Ni wakati ambao Jambo Hilo
lilipangwa, na limetekelezwa leo.
Tafadhari Bwana mkubwa Kama
unaweza kuja njoo tukueleweshe"
Mustafa alikua mwisho wa akili Yake.
" Hivi!! Una una akili timamu wewe?
Mke wangu ametekwa, sijui kuhusu
usalama wake, alafu bado unataka nine huko? Huna akili hata kidogo" alifoka
Mustafa na kukata simu. Feiso alihisi kusikitika kabisa. Alikua mwanaume gani asie jua kusikiliza mawazo ya wengine.
" Bwana mkubwa, Ni vyema ungemsikiliza huenda ana mpango, usichukue maamuzi mkononi bila fikra
kamili ukaharibj juhudi yako ya muda
mrefu'" Mustafa alimwangalia huyu
kijana mgeni kwenye macho Yake japo
alikua akimfahamu hata hiivyo alikua
Nani mpaka ampe ushauri. " Toka nje"
Mustafa alimsukuma nje kabisa ya gari
lake.
" Bwana mkubwa tafakari juu take tafadhari, sister Neema pia yupo
hatarini" feiso alipiga kelele akiwa
anajiweka sawa. Lakini wakati huo huo
Mustafa aliwasha gari Yake na kuanza kutumia mbio.
Feisoo hakuacha kumfata Mustafa
kwani aliogopa hasira alizoziona kwenye uso wake.
" Bwana mkubwa nitakufata " alimwambia huku akiifata gari kwa
Makini zaidi.
Katika hospitali ya Saifeee. Mlango wa chumba Cha operesheni ukisukumwa na kitanda Cha magurudumu kikasukumwa
nje na wauguzi, wanawake wa familia ya
Badru walikimbia haraka kwenda
kuonana na Dr baada ya mwili kuingizwa
katika chumba Cha Leba ambacho ni binafsi.
" Dr Fatma, Salma ana Hali gani?" Bi
Azat hakuweza kujizuia kuuliza, alikua
msimamizi hapo pia katika hospital hiyo hiyo lakini hakua na ujuzi wowote wa kidaktari. Alikua na usimamizi katika
Jambo lakini bado hakua daktari.
" Bi Badru, tafadhari naomba mnifate"
aliwaita wanawake watatu watu wazima ambae alikua Bi Shayma Bi Sonia, pamoja na Bi Azati. Wanawake hao
walimtii Dr Fatma na kumfata hapo
moja kwa moja.
Wakati huo wanawake wadowadogi wa familia ya Badru wao waliingia leba
kumuona Salma. Huku wakikabidhiwa
mtoto mikononi mwao. Wao alikua
mtoto wa kike, mzuri na mwenye Afya
lakini alionekana kuchoka Sana.
" Jamani ni mrembo" Mariam hakuweza
kujizuia kumbusu lakini Najma tayari
alipata.khofu.
" Kweli Ni mrembo. Najma alipoteza
tabasamu lake na kuamua kuongea tu khofu Yake nje "lakini vipi kuhusu Saida
na zarina mbona hawatokei mpaka hivi Sasa?" Muzda pia alishtuka. Ni kweli
walikua na mgonjwa lakini Saida alikua
afike hapo muda so mrefu.
" Hiyo Ni kweli wamechukua muda mrefu' Sana" Muzda aliongea na simu
Yake ikaita kwa wakati huo.
" Ni Saida ?" Watu wote walimgeukia
" Hapana sio yeye ni Lilian" Muzda
alijibu na kuwafanya wengine wazidishe
khofu. Mwanasheria Lilia alikua rafiki
yake' Muzda tangu mwanzo. Na hata
alishirikiana na Dr khairat kwa sababu
zake maalum hapo kabla, na alimsaidia
Mustafa kukusanya taarifa za kutosha
kwani aliaminiwa na Dr khairat. Mpaka hivi Sasa.
." Kampokee" Najma alimuondoa ndani ya wodi na Muzda hakusita kuondoka na kwenda kupokea simu.
" Lilian" muZda alijaribu zuia khofu
Yake ambayo iliutesa moyo wake kwa
wakati huo.
" Muzda una wakati sasa,? Namtafuta
bwana mkubwa hapatikani, nimepata
taarifa zaidi za kumpa" Lilian aliongea
Muzda akabaki kimya.
" Kwa kweli Hali yetu kwa Sasa sio
nzuri Lilian unaweza kuniacha, maana
hapa nilipo nimevurugwa" Muzda
alimwambia Lilian ambae alihisi kulia.
" Hivi taarifa ya kuuvuruga zaidi ya
taarigmfa niliyonayo Mimi, Muzda najua
huenda mnamatatizo na unatamani
nisikuoe taarifa mbaya lakini lazima niseme. " Mwanasheria Lilian aliongea na kumtaka Muzda amsikilize kwa namna yoyote Ile.
" Muzda nimemfahamu mtu anaefanya kazi nyuma ya Azraj. Ni muhimu Sana kweu kujua, najua nyie wanawake
hamfahamu lolote kuhusu hili ni Kati
yangu na Bwana Mustafa Badru lakini acha niongee" Muzda alishtuka na
akawa haelewi Lilian ana maana gani?
" Sikuelewi nyuma ya Azraj, Kaka
yangu Azraj kapatwa na nini kwani?"Muzda alishtuka. Inamaana
Azraj alikua anafanya kazi gani na mtu gani?
" Muzda Azraj anafanya kazi na mjomba wenu nyinyi, huyo mjomba
mwenyewe Ni A_ aaaaghhhhh" Lilian
alipiga ukunga ambao ilimfanya Muzda
ashtuke bila kutarajia.
." Lilian, Lilian kimekupata kitu gani?"
Muzda alipata khofu, hakuna hata
kimoja ambacho aliongea Lilian kusema
kwamba Muzda alielewa. Ni
kweli.hakuelewa kwa sababu yalikua
mambo yake na Mustafa.
" Muzda kuna Nini?" Najma alimuuliza
kwa khofu.
." Ni Lilian, nahisi Kama Kuna kitu
kibaya.kimemtokea?" Muzda alikua
akitetemeka mithili ya kukata roho.
Bila kuchelewesha muda aliinua simu
Yake ampigie Lilian Tena lakini wakati
huo huo simu ya Najma iliita. Ilikua simu iliyopigwa kutoka nyumbani
" Atakua Saida, labda hawakua wamekuja bado?" Najma alitamani.iwe
hivyo kwani moyo wake unaogopa mithili ya kupoteza uhai. " Hallo" Najma
aliitikia simu baada ya kupokea.
" Bi mdogo, Bi mdogo hapa nyumbani.
Mhhii Bi mdogo zarina na dereva wa
Saida wame... Wame... Wamekufa"
sauti ya Asia ilimfanya Najma ahisi
kupoteza uhai zaidi ya hapo awali miguu
Yake iliishiwa nguvu na akakosa sehemu ya kujishikiza.
Alikua amesema Nini huyu Asia asie na adabu, alikua akimchezea ki fikra. " Bi
mdogo wamekufa vibaya Sana kwa
risasi" asia alizidi kulia.
.
" Nyamaza !!!!" Najma alipiga kelele
akiwa haamini anachoambiwa, mwili.wake ulitetemeka kiasi kwamba moyo ungetengana na.kiwiliwili.
" Wifi!!!" Muzda alimsogelea akiwa haelewi kinachojiri .
"Nini?" Muzda alimnyakua simu. Na
kuweka sikioni. Sauti ya vilio vya watu wakiita majina aliyoyafahamu ilipenya
vyema kwenye masikio yake'. Alijikuta
aling'ata ulimi wake bila kufikiria.
Alisikia zarina. Na jina la dereva wa
Saida hiyo ukimaanisha hata Saida anaweza kua amee.... Hapana hawezi
kufikiria huo upuuzi'
" Asia Kuna Mimi hapo?" Muzda aliuliza
kwa kuogopa jamani Kuna mini kwani
kwa nini watu wanalia bila mpangilio.
" Binti Badru Ni zarina na dereva wa bi mdogo, wamekufa wamekufa vibaya
Sana jamani" Asia alijibu kwa kuamua.
Alikua na machungu lakini lazima ataoe
taarifa. Muzda alihisi kupeteza dira ya ulimwengu alikua Kama Najma tu.
Alishika chini kwa maumivu na hapo
Asia alikata simu baada ya kuona ukimya.
" Hapana! Hapana sio kweli, bila Shaka
huo haiwezi kua ukweli so ndio?" Muzda
alimgeukia Najma aliekua amepoteza
kabisa yaani ni Kama dunia ilisimama kwa klmuda ikimsubiri ashuke.
" Wifi natumai wifi Saida atakua mzima
kabisa Tena mwenye Afya" Muzda
aliongea akiwa na Imani kabisa na Hilo
lakini kwa ninj watumishi wa.nyumbani
kwao hao wawili wapoteze Maisha
ghafla na bila sababu?.
Sehemu ya 154
Bi Shayma na wenzake walirejea kutoka
katika ofisi ya Dr Fatma wakiwa
wamelegea mwili na akili. Kila mmoja
alikua na mawazo Yake kwenye kichwa
chake. Kila mtu alikumbuka maneno
ambayo waliambiwa
" Bi Badru, nimewaita hapa watatu kwa
kua nyie Ni watu wazima na
mnajitambua kuliko ningeongea hapo
mbele ya vijana wenu wadogo" Dr
Fatma aliongea bila kupoa.
" Tunakusikiliza " walimtolea macho na kumpa umakini wa masikio.
" Ki ufupi ni kwamba, haikua kazi rahisi
kumuokoa mwanamke huyu pamoja na
mtoto wake, inaonekana amepitia
misukosuko mingi Sana ya ki saikolojia
kwanzia siku apate ujauzito, licha ya hivyo alikua ajifungue salama kabisa.
Lakini kutokana na hitlafu zilizojitokeza
amelazimika kujifungua kwa kupasuliwa.
Kwa nini alikua akiteseka"
Watu wote walimtolea macho Dr fatma.
Na kukumbuka Ni vipi walimtunza vyema
Kama malkia akiwa na ujauzito hiyo
inamaana gani walimtesa?.
" Haiko hivyo Dr Fatma, itakua
umechanganya Majibu yasm Salma na
mtu mwingine alikua sawa tu, labda
hasira za mimba ndo zilimfanya
aonekane tofauti." Bi Sonia alijibu. ..
" Hapana , acha niwe mkweli mbele
yenu" Dr Fatma alilazimika kuongea
ukweli ambao hakupanga kuusema.
" Ukweli gani?" Watatu wale
walimuuliza.
Dr Fatma akihema kwanza na
kukumbuka kua yeye ndo alikua Dr wa
Saida alipokua mjamzito mpaka
anajifungua Mustakim, na hata kwa
Salma yeye ndo alikua Dr wake. Hivyo
Ni rahisi kuelewa Hali ya kila
mwanamke na kwa Salma alimuweka
karibu zaidi mpaka akamwambia ukweli wake.
" Ukweli Ni kwamba, bwana azrja
Badru alitaka kumuua Salma na mtoto
kwa wakati mmoja, shida Ni moja tu, hamtaki mtoto huyo tangu mwanzo.
Hata ujio wa Salma katika familia yenu
sio Kama alikua anapenda kutokea
mahali hapo, hapana Ni kwa sababu
alikua akitafuta ulinzi baada ya kuokolewa na Mustafa Badru asiuwawe
na watu wabaya ambao Ni vijana wa Azraj Badru" taarifa hiyo ilikua taarifa
isiyoelezeka Wala kuaminika katika
masikio Yao. Walihisi kana kwamba
labda Dr Fatma alikua akiomba mashairi ya majonzi.
" Unaongelea mini wewe? Acha kuongea
maneno yasiyoeleweka"
Dr Fatma alikua na ushahidi kadhaa
dhidi ya Azraj. Ukweli Ni kwamba yeye
pia Ni Dr anaeshirikiana na Mustafa.
Na anategemea Sana katika kambi ya
Badru Jambo ambalo watu wengi
hawafahamu kabisa. Alichomeka flash
ya matukio kadhaa yaliyomtokea
Mustafa na kutoa maelezo juu yake.
Tangu hapo awali kipindi Mustafa
alipokea mgonjwa mwenye dawa za
kulevya katika mwili wake. Ulikua ni mpango wa Azraj Badru alitaka
kumchafua. Sio tu hivyo alionyesha
picha za mama Shayma ambae
alishafatiki miaka minne nyuma.
Mwanamke huyo alikua akifanya huduma ya kuuza mwili wake katika majumba ya
kifahari na makasino mbalimbali. Bi
Shayma na Bi Azat walipauka baada ya
kuona Hilo. Na kubaki wameshika
midomo Yao. Kisha akawahi yesha picha ya Karibu ya Azraj na mama shayma
wakiwa nje ya nchi wakiionekana kukiss.
" Huu Ni upuuzi gani?" Bi Shayma
alifoka akiwa haamini inawezekanaje
Azraj kijana wake mwema kupita.wote awe Kama huyo mwanaume kwenye
picha? Hapana utakua umemkosea'
" Huo ndo ukweli Bi Shayma , Bi Azat na Bi Sonia, nyie Ni ma boss zangu, nitakua Sina akili iwapo nitamshtaki
Azraj kwenu kwa kusudi bila sababu ya
msingi. Hii ilikua Siri ambayo ningekufa
nayo siku moja lakini siwezi Tena kwa
sababu Nina khofu juu yenu." Dr Fatma
aliongea.
Kisha aliwaonyesha picha ya Dr khairat
akiwa na Azraj katika ofisi ya Azraj
iliyokua ikirusha taarifa. Na wakati huo
huo akaonekana Azraj akiwa karibu na Dr hizaan. Watu walishtuka. Dr Hizaan
alikua mume wa Dr khairat na Ni watu
ambao walitalikiana na hawakua
wakipatana lakini Azraj alionekana kua
karibu na watu hao kwa wakati mmoja.
Na katika siku hizo ndo uadui wa wawili
hao uliongezeka. Mtu mzima mwenye
akili zake timamu lazima ajiongeze
kabisa kwamba watu hao walikua
wakichokganishwa.
" Bwana Azraj Mimi na Dr Neema
tumemfatilia muda mrefu' Sana, kwa
sababu sisi ni Askari wa kike wa Badru.
Tupo kwa ajiri ya usalama na ulinzi wa
pembeni wa bwana Mustafa Badru"
Dr Fatma alisita kwanza. " Hivyo Ni
vitu vichache alivyofanya bwana Azraj.
Sio tu kumfanya Mustafa amuoe
mwanamke kahaba na kuzaa nae mtoto,
lakini pia aliishia kumuua baada ya
mwanamke huyo kwenda kinyume nae na
kumpenda Mustafa na Kisha akazaa
nae." Bi Shayma alihisi kudondoka
katika siku alijiona kua mpumbavu na mama asiejua na akili Ni siku hiyo. Hivi
aliwezaje kumtambua azraj Kama kijana
wake mwema kuliko Mustafa?
Bi Sonia pia jasho jembamba lilitoka.
" Bi Azat samahani, bwana mkubwa
hakuwahi kutamani utambue hili lakini
nalazimika kukupa taarifa hii, ukweli Ni kwamba miezi kadhaa nyuma Maulid
alitoweka na kusemekana alienda
akwenye ziara ya michezo Hilo Jambo
halikua la kweli" dr Fatma aliongea
huku akimtazama Bi Azat ambae tayari
usi wake ulishtuka.
" Ndio Bi Azat kijana wake alibaki
kidogo awe muathirika na mtumishi wa
madawa ya kulevya, pongezi kubwa na
shukrani kwa Kaka wa pili bwana Muksin
Badru" Bi Sonia alitoa macho kwani
muksin alifanya Nini kwa kusifiwa.
Bi Azat alikua ameshtuka kiasi kwamba
hakujua anafaa kuuliza Nini?
" Ukweli Ni kwamba, Kaka wa pili
muksin Badru alimtambua mapema na kumpeleka kambini kwa ajiri ya kumpa
SoMo, na huko tuliweza kumtibu
taratibu na kumuadhibu adhabu ambazo
hakuatahilk kuzipitia wakati huo kwa
sababu alikua mdogo lakini ili apate
SoMo lake ilitulamzimu." Bi Azat alibaki
hoi hakuweza kuongea kitu.
" Unataka kusema hiyo pia ilikua kazi
ya Azraj?" Bi Shayma alihisi kumuogopa
Azraj kila alipoambiwa matukio Yake.
Alikua kijana wake wa aina gani?
Aliwezaje kua katili kiasi hiki.
" Bila Shaka anaweza asiwe yeye, Ila kwa sababu watu wanao toa huduma
hiyo walikua watu wake bila Shaka ni yeye, alafu mbaya zaidi Ni kwamba
hayupo mwenyewe, Kuna mtu nyuma
Yake"
Watu wote walikaa kknya kwa uwoga.
" Huyo mtu nyuma Yake ndo
alisababisha mpaka Kaka mkubwa
akaingia kwenye. Ndoa na Dr khairat ili
afanikiwe kumfahamu, na alitamani
afanikiwe kumteketeza bomu
lililopangwa juu ya familia Yake mapema
kabla hajawa mrithi wa familia ya
Badru afrika mashariki. Ndo maana
bwana mkubwa alikua alivumilia kila
kinachoendelea. Akiwa na dhumuni moja
tu familia Yake iwe salama.
.bi Shayma alihisi kulia siku zote alikua
akimuona kijana mkaidi na asie faa, lakini kumbe alikua akipitia Mambo
mengi kwa sababu Yao.
" Najua mtakua mnajiuliza kwa nini
nawaambia Mambo yote haya kwa
wakati huu, lakini ukweli Ni kwamba
siwezi kukaa kimya kwani nahisi hatari
dhidi yenu, mpaka hivi Sasa navyoongea na nyie. Wenzangu wawili tayari Ni mateka wa Azraj."
" Dr Neema na kijana wetu mkoja
kutoka Badru kambi, ameshikiliwa na watu hao. Hivyo Nina khofu na uoga
dhidi yenu nyinyi Azraj Hana khofu
wala uwoga wa kupoteza chochote. Na
hata mtoto wake pamoja na Salma Ni
viumbe ambao hawana maana kwake
yeye"
" Kwa nini anafanya yote haya?" Bi
Shayma alihisi hasira na kuunguruma bila kusubiri.
" Nachojua Mimi anataka kua mrithi wa kwanza wa Badru na kuchukua kila kitu
Cha bwana mkubwa Mustafa, hata mke
pia ndo maana amewagombanisha Sana,
amemchafua Sana Bwana Badru, na
sababu muhimu ya Mimi kuwaambia
haya ni kuwaweka salama kwani mpo
kwenye siku za hatari zaidi. Ni
kuelekea mkutano wa mwisho wa kumpa
urithi na umiliki bwana mkubwa awe
mrithi wa familia lakini hawataruhusu
Hilo. Hivyo basi sitaki kazi na juhudi
tuliyipambania muda mrefu' iende bule.
Tumetumia jasho jingi.pamoja na nguvu
nyingi kwa ajiri ya Badru. Hivyo na nyinyi mnafaa kutupatia sapoti"
Bi Shayma na wenzake walirejea
kwenye fahamu zao huku walitazamana.
Hivi Ni kweli mtu Yule alikua Azraj.
Ambae alifanya Mambo mengi kwa
wema na unyenyekevu, lakini ameishia
akiwa na kisasi na familia ambayo
imempa jina impempa uwezo elimu na mapenzi ya familia. Lakini yeye alikua na Nia chafu kiasi hicho.
Wakiwa kwenye mawazo yaliyowakatisha
tamaa, walikutanishwa na msumari
mwingine ambao ilisafiri moja kwa moja
kwenye ngome na kwenye kina Cha moyo wao.
" Mama zarina na dereva wa Saida, wamefariki kwa kupigwa risasi. Mama
Saida hajulikani alipo mpaka Sasa"
alikua Mariam aliekua akilia baada ya
kumkumbatia Bi Sonia. Na kuwafanya
wanawake hao watatu waliokua na khofu
kuongeza khofu yao.kiasi Cha BP ya Bi
Shayma kupanda na kupoteza udhibiti wa mwili wake.
Alipoteza fahamu zake bila kusubiri.
" Wifi" Bi Azat aliita kwa uwoga. Huku
Bi Sonia alimdaka kwani yeye ndo
aliekua karibu.
' Mungu wangu Ni laana gani hii
umeipata familia Yao?' Bi Sonia
alichanganyikiwa na Mariam akaenda
kumuita daktari haraka kwani Najma na
Muzda tayari walitangulia nyumbani
huku Bu zaina alibaki kumuuguza Salma.
Kwa kweli hata yeye pia akili Yake
haikua hapo. Zarina alikua sawa na
binti Yake anawezaje kufa.
.hapana sio sawa alikua bado binti
mdogo tu mwenye umri mchanga.
Mustafa hakuweza kwenymda moja kwa
moja kumtafuta Azraj hapana. Isipokua
alifata ushauri wa feisooo licha ya
hivyo alifanya maamuzi Yake mwenyewe
hakua tayari kukurupuka na kuharibu
juhudi za watu za miaka mingi.
Alienda katika kambi ya Badru. Huko
alikutana na Askari mkuu wa kambi hiyo
akiwa amevurugwa na kuchanganyikiwa .
Vijana wote walijilanga na kujigawa
katika usawa wao wakisubiri kupatiwa
maagizo wakamilishe mission zao. Kwa
kweli hii kesi ya Azraj iliwachukulia
muda mpaka walihisi kuichoka. Japo
baadhi ya vitu walikua wakifanya na
kuhakikisha usalama lakini Jambo la Azraj lilikua la kuendelea tu.
" Bwana mkubwa, type amri yako na tutaisambaratisha kambi ya maharamia"
wakiongea kwa utiifu wakimuomba
Mustafa awape hiyo nafasi
wakammalize Azraj kwani wanashuhudia
kile kinachomkuta mwenzao. Na Askari
wa Badru Ni Askari wanao hurumiana
sana
" Bwana mkubwa Badru, nashukuru
umenisikiliza kwanza" Mustafa
alimtazama mwanaume huyo mtu mzima
kwa macho makavu.
' alimsikiliza kwa sababu hakua na jinsi, asingekua mjinga kupoteza kila kitu au
kuwaweka hatarinj zaidi wanafamilia
wengine kwa sababu ya mwanamke wake
tu, bila Shaka huo Ni ubinfasi
uliokithiri.
Alisogea kwenye chumba Cha
mawasiliano, ndipo alipifanikiwa kuona
video inaykruka live kutoka katika
vyumba vya nyumba yenye Giza, na mwanga wa jua ndo ulitumika Kama taa
kumulika ndani ya vyumba hivyo.
Alipata kumuona Dr Neema alipitia
matesk makali kutoka kwa Bwasha.
Mustafa aliitazama sura ya mwanaume
Yule akahisi hasira baada ya kuikumbuka. Bila Shaka alijitahidi
kabisa kutoka ndani ya nafsi yake,
yaani siku ikitokea kakutana na Bwasha ana kwa ana bila Shaka atammaliza kwa
mikono Yake mwenyewe. Hatampa
nafasi ya kutoroka.
." Sitasema Wala kuongea neno lolote
lile. Hata Kama nakata roho" Dr Neema
alipiga kelele ya.maumivu baada ya
kuongea maneno hayo kwani chuma Cha
Moto kilibandikwa mgongoni kwake.
" Hawa washenzi wanaweza kumuacha
Dr Neema" feiso alipiga kelele na
kupaniki kwa wakati huo. Kwa kweli
alimuonea huruma. Mwanamke huyu
alimchukulia Kama mdogo wake. Lakini
alikua akiteseka hivyo bila sababu.
Bwasha alichukua simu na kuanza
kumrekodi Dr Neema asijue ya kwamba
hata wao pia walikua wakirekodiwa.
Dah! Mwanaume huyu Hana akili.
Aliitika video hiyo huku Mustafa na
wanakambi wakimuona. Ujumbe huo
uliingia moja kwa moja kww ye simu ya
Mustafa. Kisha simu yake ikaita kabla hajafungua.
" Hallo Mustafa alifanya kana kwamba aliweka utulivu"
" Wewe nk Nani?" Mustafa alijifanya
kukasirikia kana kwamba hakua akimjua.
" Acha papara bwana Mustafa Badru, Ni rahisi tu kunifahamu Mimi ahahaha"
Bwasha aliongea huku akizunguka
zunguka ndani ya chumba hicho
ambacho kilikua sawa na kuzimu.
" Unataka Nini kwani? Mke wangu
namtaka mnaweza kuniambia mnataka
niwape Mimi mumuache huru!!!!!????"
Mustafa alifoka hapo Bwasha
alionyesha mshangao.
" Oh! Bwana Mustafa Badru unaonekana
kujawa na hamaki, Ila usikhofu
nitakwambia Ila sio kwa sasa" Bwasha alikohoa kidogo.
" Ila kwa sasa Kuna ujumbe ama zawadi nimekutumia, utazame" Bwasha alikata
simu Yake na kuondoka eneo Hilo moja
kwa moja. Mustafa alitamani kumuua
huyo mwanaume. Aliwahi kumtengenezea
tukio la ajabu yeye Dr khairat Kisha akamuacha tu.
" Bwana mkubwa, wengine wanaweza
kustahimili, Ila sidhani Kama Dani
ataweza" Gharib alihisi kukata tamaa.
Ndo wakati huo huo Mustafa aliona
katika chumba alichokua Dani.
Kijanadogo Kama yeye alipitia magumu ya Maisha alikua bado kijana lakini
alikua akipewa adhabu ya kubanwa
katika sehemu zake za Siri Kama adhabu ya kua msaliti.
Dani alikua akilia na kupiga kelele kwa maumivu mkali sana. Kibaya zaidi mtu
aliekua akimpa adhabu hiyo alikua Nevi. Mwenzake ambae ametoka nae katika
kambi moja ya Badru. Na alikua rafiki yake' kabisaaa wa kufa kuzikana.
Sehemu ya 155
Mustafa alihisi maumivu kila
alipokumbuka kua yeye ndo alikua
chachu ya kuwafanya vijana hao watatu kutokea huko. Lakini mwisho maisha ya
Dani yamegeuka mabaya zaidi ya kuzimu.
" Kitu gani kifanyike" gharib alihoji
akitamani kupewa nafasi ya kwenda kupambana na hao watu.
" Bila Shaka ipo njia" Mustafa aliongea
wakati huo feisoo alimsogelea Mustafa
haraka akiwa na Imani na yeye
atawekwa miongoni mwao wanaoenda
kumsaidia Dr Neema.
Majira ya jioni Mustafa aliendesha gari
kuelekea nyumbani kwako akiwa na feisoo. Feisoo alikua akilalamika kwa
nini amechukuliwa na Mustafa.
" Bwana mkubwa ungeniacha pia
niungane nao, nahitaji kumuokoa sister
Neema. Yule mwanamke ni zaidi ya
ndugu kwangu, amenitoa mbali Sana"
" Na hiyo ndo sababu sijakuruhusu
uungane na Askari wa Badru, kwani
wewe pekee ndo una Moto laini wenzako
wako tofauti utawahatibia mission Yao."
" Lakini angalau ningekua karibu Yake"
Mustafa alihisi kumpiga kwani aliongea
Sana, lakini hakuweza kwa sababu
alielewa maumivu Yake. Alikua na maumivu ya kumpoteza Saida Mara
kadhaa lakini afadhari alikua akimuona na anaona yupo salama. Ila hii ya Sasa ni too much. Hayupo nae kabisa na hawezi kwenda kumfanya chochote.
Ni Asubuhi nyingine Katika jengo la familia ya Badru majonzi yalitawala
nyumba, hakuna aliekua na amani kabisa
kwani nyumba hiyo ulikua na msiba
usioelezeka Asia alikua akitiririka
machozi Kama maji ya mvua. Hakuweza
kuamini Kama kweli amempoteza dada
mzuri Kama Zarina.
Aliweza tu kumkumbuka Zarina Ni mtu
wa Aina gani? Alitoka nae mbali Sana.
Walikutana hapa kwenye jengo la Badru
wakiwa Bado ma binti wadogo Sana
yaani waliokua na miaka 12 tu waliletwa na Bi zaina ambae aliwachukua kutoka
mitaani na kuwalea Katika mazingira ya utendaji wa kazi na wa kujitegemea
Katika Maisha Hali Yao ya Maisha
ilibadirika kutoka kwa watu wasio na maana na kua watu muhimu na wa maana Katika ulimwengu huu. Lakini
Sasa wameishia kutenganishwa na umauti.
"Zarina, nisamehe dada YANGU" Asia
alikua Sana akiwa kaukumbatia mwili wa zarina uliokua umehifadhiwa Katika
chumba chake alichokua akilala
walisubiri kuufanyia mazishi. Asia
alijishisi mwenye hatia kwani nu yeye
alitakiwa kwenda kumpeleka chakula
hospitali mwisho alikumbuka ilivyokua.
" Nataka kwenda hospital lakini najisikia vibaya" alihisi kutapika baada ya kuongea hivyo, zarina akamsogelea na kuanza kuhisi Hali ya hewa ikiwa
tofauti kwake.
" Wewe!" Zarina alishtuka
" Mmhh, usiwaze upuuzi kwenye akili yako Sina ujauzito" Asia alijitetea lakini ki ufupi ni kwamba alikua
hajiamini pia.
" Sijasema una ujauzito, mbona umejishtukia" Zena alitweta na kumsogelea akaanza kumkagua kwenye
shingo Yake. Asia hakua anaelewa
maana ya zarina hivyo akabaki anaainua
shingo Yake kumkwepa. Hakujua kua
wakati anafanya hivyo ndo alikua
akimpa nafasi ya kukaguliwa kwa
ukaribu zaidi.
." Unafanya Nini?" Asia alihoji kwa mashaka.
" Asia kua mkweli na Mimi, mwezi huu sikuona ukibadili pedi kabisa" zarina
aliongea kulingana na mazoea
waliowekeana hivyo wangeonana pindi
wakiingia kwenye siku zao lakini zamu
hii mwenzie hajaenda safari ya mwezini.
" Aah! Kwani si huwa inatokea tu napita
mwezi mmoja Ni kawaida" Asia
alijitetea.
" Acha ujinga Asia utaumbuka vibaya
Sana" zarina alishika kidole chake Cha
shahada na kumgusisha shingoni. Asia
alianza kubinya mashavu Yake akiwa
hamuelewi. Asia alijisikia Ni jinsi gani
mapigo ya moyo kwenye shingo Yake
yalivyo Kasi bila kutulizana.
" Nimekua hivi kwa siku kadhaa Sasa
hata sielewi shida Ni nini? Labda
mabadiriko ya Hali ya hewa. " Asia kwa akili zake finyu hakuelewa Kama tayari
amejishtaki kwa kweli zarina alihisi
kumcheka
" Pumbavu zako' wewe una nafsi mbili
katika mwili wako ndo maana mapigo ya moyo wake yanaenda Kasi" zarina alihisi
kulia kwa wakati huo aliwezaje kua na dada asie na akili. Asia aliziba midomo
Yake haraka
" Acha utani" aliuma meno Yake baada
kuongea na kuachia mikono Yake. Sure
Yake ijaa aibu na uwoga kwa wakati huo huo.
" Namaanisha nyau wewe, hee sijui
utawaambia Mimi Wana familia?"
Zarina alikosa la kusema. Asia alianza
kulia bila kujua alikua na mimba. Bila
Shaka Ni mimba ya Gharib.
" Haya Sasa haraka, nielekeze vyema Ni huko kigamboni ndo umeikamatia?"
Zarina alihisi hivyo kwani Asia alikua
mfanyakazi kipenzi wa Saida, hivyo
angeishia popote pale ambapo Saida
angehamishiwa na Mustafa iwe kwa
kutaka ama kutotaka.
" Ahaaaa!!! Zarina mi nahisi kua
marehemu jamani, nitamwambia nini Bi mdogo" Asia alikaa kitandani na kuzidisha kulia.
" Najua huna la kumwambia Ila kwa
Sasa acha niende hospitali hakikisha
unaniangalia Majibu kamili" zarina
alimwambia Asia akiwa na Imani kabisa
mtu huyu mwenye stress hawezi kwenda
popote Tena.
" Hapana zarina, haikua zamu yako', acha niende tu natia aibu Mimi" Asia
alizidisha kulia alikumbuka namna
alivyokua akizagamuana na Gharib kwa
kificho tangu hapo mwanzo. Saida na
Mustafa walikua wakiingia chumbani
kwao Basi na wao wangepeana wakati wa kutafutana, mwisho walikubaliana na hatimae Sasa wakavunja amri ya sita.
Dah! Mungu sio Asmani Yale yote
waliyoyaweka Siri leo hii yamewekwa hadharani.
" Aibu hoi Mimi nimemtia aunt zaina
hawezi nisamehe bila Shaka, amenilea
vyema Sana jamani"
" Hebu nyamaza mshenzi kabisa, kwamba saa hii ndo unakuta, kipindi
unafanya miguu yako hukua na
kumbukumbu kua Kuna mtu anaitwa aunt zaina. "
" Zarina naomba nitoroke" Asia alikua mwisho wa akili zake.
" Sio tu kutoroka, inabidi ukiri mbele ya familia kua wewe ni mjamzito na ujauzito huo Ni wa Nani? Naimani
kabisa makaka wa familia watamtafuta mtu huyo na atakuoa na mtalea mtoto
wenu. Ni wasichana wangapi
wameondoka hapa na Wana miji Yao
kwa mfumo wako" Asia alipata aibu na
yeye pia amekua miongoni mwao? Lakini
tatizo Ni hisia hakuna mwanadamu
Wala kiumbe mwenye uwezo wa kuuzuia moyo kupenda.
" Zarina!!!!!!
" Mi naenda, ngoja kwanza nimuone Bi
mdogo alafu naenda, usiwaze Sana
sawa, kwanza unafaa kumshukuru
Mungu Sana, kwa Sasa wewe ni mkubwa na tayari umeshika ujauzito hiyo
inamaanisha utamiliki Wana katika hii
dunia, hautaishia Kama aunt zaina ambae Hana mtoto. Ila anao sisi sawa
kipenzi changu" zarina aliweza kumbusu na kuondoka baada ya kumtoa moyo.
Asia bado hakua na Imani kabisa.
Baada ya hapo ndo taarifa zilirejea mili
miwili ikiwa kwenye machela baada ya kutolewa mochwari na Sasa zarina
anaenda kuishi katika nyumba Yake ya milele. " Da zarina" Asia hakuweza
kujizuia kulia.
Baada ya Asia kulia kwa sauti zaidi
alisikia mtu mwingine akilia kwa
maumivu zaidi nyuma Yake. Alikua
afsat. Kwa kweli hakuna binti alikua
karibu zaidi na zarina katika mabinti
wote was Badru Kama Afsat. Zarina
alimlea kwanzia akiwa mtoto mdogo. Bj
Azat aliamini Sana mikono ya zarina
alipokua alimuachia binti Yake alipokua
mtoto mdogo. Hivyo Afsat alimuona
zarina Ni zaidi ya dada hakuwa tu
akimuita dada Kama mtumishi wa ndani
Bali alikua mama Yake mdogo pia.
Alimpa cheo hicho kwa sababu alimlea
kwa moyo mkunjufu.
Asia alielewa Hali Yake na kumkumbatia
Mara moja.
Wanawake wote walijiandaa Sasa
kwenda kuuaga mwili wa zarina
chumbani kwao. Waliuaga kwa
kumbukumbu nzuri kila mmoja. Kila mtu
alilia kivyake na kumbukumbu take juu ya huyo binti.
Bi zaina alizidiwa kabisa kwani aliwalea mabinti hao wawili Kama mabinti zake
Sasa, mmoja wapo alikua amefariki
inaumiza kiasi gani? Inauma Sana
jamani.
" Aunt zaina" Asia alimkumbatia aunt
zaina kwa uchungu mno. Na hapo bi
Shayma alikuja kumpoza. Ni kweli dunia
hii imechanganyikiwa bila Shaka.
Baadae mwili wa zarina ulitolewa nje
kwa ajiri ya maandalizi ya swala
aswaliwe maiti Kisha akazikwe. Yalikua
maumivu makubwa Sana pale ambapo
mwili wake ulichukuliwa. Kila mmoja
alimkumbuka zarina kwa nafasi Yake
jamani. Kim na Shayma walikua na
misiba miwili kwa wakati huo Ni kweli
kabisa walifiwa na ndege wao mpendwa
HudHud lakini Sasa wameondokewa na dada Yao kipenzi zarina. Na mbaya zaidi mama Yao haonekani. Ilikua Hali
ya huzuni na majonzi kwa watoto hao wawili. Waliweza tu kutembea
wakimuelekea baba Yao aliekua akisali na wanaume wengine mahali ambapo maiti ilikua ikiswaliwa.
Huwezi amini hata Azraj alikua
akiswalia maiti da! Kikulacho ki nguonj mwako. Azraj Badru, hakuweza hata
kuinusurimu nafsi ya vijakazi wawili wasio na hatia kosa atimize lengo lake.
Japo sio yeye aliefanya lakini Ni kwa
amri Yake Saida atekwe.
Mustafa alikua akitamani kummeza huyo
mwanaume aliekua kwenye safu alishiriki
ibada ya maiti. Na yeye ndo anajua
mke wake Yuko wapi? Na yeye ndo
chanzo Cha kila Jambo hapo.
" Kim njoo" Muzda alimchukua Kim eneo
Hilo huku alimshika Shayma mkono na
kurejea nao sehemu walikua wamekaa
wao. " Baba mama Yuko wapi?" Shayma
hakuweza kunyamaza Tena walikua
watoto wadogo alafu wamempoteza mtu
kwa Mara ya kwanza katika Maisha
Yao, alafu mama Yao haonekani.
Mustafa alihisi kufa kwa hasira kila
alipokua akimwangalia Azraj na kusikia
sauti za watoto wake waliokua
walimuuliza juu ya mama Yao. Alitamani
kuruka kwa nguvu na kumtwanga Azraj
ngumi ya uso lakini hapana, acha
auheshimu mwili wa dada zarina. Alikua
sawa tu na mdogo wake Muzda.
' Azraj Badru, kwa kweli nafsi yangu
inashindwa kujizuia kila nikikuona bila
Shaka nitakuua, subiri tu tumalize
mazishi' Mustafa alituna kwa hasira na
wakati huo waliweza kumnyanyua
machera na kuondoka nayo kuelekea
makaburini. Ilikua huzuni Sana kwa
watu walipobaki nyumbani wakiusindikiza
kwaacho.
Saida akiwa katika kichumba kidogo
chenye joto Kali na mwanga hafifu
Sana wa jua ambao ulipenywa kutokea
kwenye tundu Bali halikua likifahamika
iwapo kimetokea juu au upande gani wa ukuta. Alikua na maumivu ndani Yake.
Alikua akimkumbuka Sana zarina.
Zarina binti mdogo unri wake Ni sawa
tu na Muzda na Mariam alikua dada wa
karibu Sana na Asia. Mtumishi wake
kipenzi. Na yeye pia alikua karibu nae
zaidi. " Bi mdogo Kaka mkubwa kakutumia hii, hakikisha unaisoma"
kumbukumbu hiyo ilimjia Saida kichwani na kujikuta akitokwa na machozi.
" Bi mdogo naenda kumchukua Shayma
shule kwa niaba yako haonekani kua sawa" zarina alimuaga hivyo siku moja
alipokua amevurugwa na Vita ya
mapenzi Kati Yake na Mustafa na Dr khairat.
" Ahaha, bi mdogo inachekesha ndo
ukaamua kuchoma nguo za Kaka mkubwa
kwa sababu hakulala kwako?" Asia ulimi
ulimponyoka siku hiyo na zarina
akamwangalia kwa jicho la kumkanya
Hadi Saida akacheka.
" Mbona ananiangalia hivyo?" Asia
alipata aibu na kuziba macho Yake.
" We mwanamke huna haya, nilidhani we ni mkubwa Ila akili huna, unawezaje
kuongea maneno hayo" zarina alikasirishwa nae siku hiyo.
" Msijari hata hivyo Kuna wakati huwa
napenda kutoa hasira zangu kwa kuweka baadhi ya Mambo wazi" zarina akatega
masikio vyema kusikiliza hayo Mambo
wazi anayotaka kuyasema Saida.
" Ehhe" Saida alicheka hoi, bila Shaka
huyu ndo alijikuta hataki kujua Mambo ya Bi mdogo wake.
'" ahahaha umbea huo" alimtulia mto uliokua karibu zarina akaona haya.
" Bi mdogo itabidi uuchome na mwili
wake Sasa vipi Kama anashikwa
shikwa?" Zarina alichochea Saida
akahisi aibu kwenye uso wake.
" Zarina mjinga wewe mkoswa aibu"
alijikuta anaanza kunikimbiza bila
kusubiri. Saida alitabasamu baada ya
kuimiss kumbukumbu hiyo nzuri baina
Yao. Lakini alikumbuka namna
wangebushana Sana pindi wakienda
sokoni. Kuna wakati alikua alilazimika ku
sarenda ili zarina asijione ameshindwa
huku Asia akijiima yatima wa mapishi.
Lakini Leo hii!! Leo zarina hawezi
kufanya yote hayo! Alikufa mbele ya
macho Yake bila Shaka. Alikufa
akimshuhudia. Hajui Ni kwa nini na
shida ilikua Nini Hadi wamuue zarina.
Iwapo walimuhitaji yeye badi
wangemchukua tu, hakuna haja kabisa
ya kumuua zarina wake. Saida alihisi
Kama tumbo linamkata alianza kulia kwa
hofu Sana.
Sehemu ya 156
Saida akiwa analia kwa kukata tamaa
wakati huo ndo mazishi yalikua
yakiendelea, mvua zilikua zikinyesha
kwani kipindi hicho ulikua msimu wa
mvua. Saida aliweza kuikumbuka ndoto
nzuri aliyoiota akiwa na Mustafa
kwenye Maisha ya kale mvua ilionyesha
Kama hivi na wao walikua na wakati
mzuri Sana. Hiyo inamaanisha nini?
Wakati wamateso umeanza ama
umekaribia kuisha.
" Mungu wangu ulie hai milele, nakuomba dua hii kwa ajiri ya zarina.
Hakika yeye ni binti mzuri na asie na hatia kwangu Mimi na kwa wengine.
Alikua dada mzuri kwa kila aliefaa
kumuita dada, na alikua mtoto mzuri
kwa kila aliekua akimuita mwanangu, alikua mamdogo mzuri kwa wale
aliewachukulia Kama watoto kwake. Na
alikua aunt mzuri kwa watoto wangu.
Sina haja ya kusema yote haya isipokua
wewe unanifahamu zaidi. Kwani Ni
kiumbe ulientengeneza kwa mikono yako mwenyewe ewe mola wangu. Dua yangu
sidhani Kama itafaa kwani nipo kwenye
mazingira ambayo Sina uhakika Kama Ni
matakatifu. Lakini naimani Ni takatifu
kwa sababu imetoka katika kina cha
moyo wangu. Naomba unisamehe Yule
binti makosa aliyotenda kutokana na mapungufu ya kibunadamu. Ya Allah
msamehe makosa Yake. Kilio changu
hakina ukubwa Wala maana bila maombi
yanayofaa kumsafishia njia na kumuondoshea madhira aliyotenda akiwa
Kama binti wa adamu... Ipokee salama roho take ewe mola wangu" Saida
aliomba dua hiyo akihisi kabisa Kuna
kipande Cha uhai kinachomolewa ndani ya moyo wake.
" Zarina" Saida alilia Sana siku hiyo na kubaki amejinkunja ndani ya chumba
hicho kisichojulikana kipo upande upi wa dunia. " Natumai Mustafa wangu kwa Sasa yupo anashughurikia mazishi yako.
Naomba umpe salamu za mwisho
aniletee kabla akuweke katika nyumba yako ya milele. Nakupenda Sana zarina.
Nitakuombea siku zote katika Maisha
yangu ya mwisho yaliyobaki.
Nitamuweka katika orodha ya watu
wataokumbukwa na Mimi pamoja na
wanangu. Najua maombi ya watoto Ni masafi na salama" Saida alikua akilia
Sana
" Na dereva wangu pia, sikua nimekufahamu kwa muda mrefu ni wiki
mbili tu umekua dereva wangu lakini
umeishia kupoteza uhai wako kwa
sababu yangu. Naomba unisamehe wewe baba, natambua una familia yako
naomba niwe msaada wao iwapo
nitabahatika kutoka hapa nikiwa hai,,
naomba unihukumu kwa kua mzembe,,, bila Shaka ulinizuia nisiteremke, Kama
ningekusikia bila Shaka huenda
ungeokoa Jambo,,,, nimeishia kukuacha
maiti wewe pamoja na zarina" Saida alihisi maumivu jamani. Upande wa pili watu walikua wakimalizia
mazishi ya maiti mbili. Zarina pamoja na dereva wa Saida. Masikini
mwanaume huyo alikua na mke' mwenye
mtoto mmoja pamoja na ujauzito.
Inauma Sana. Mtoto Yule alikua na umri wa miaka minne sawa kabisa na
Shayma huku mke wake akiwa na
ujauzito mkubwa tu Ni Kama miezi
Saba tu bila Shaka anaweza jifungua kwa presha. Iwapo hawezi jizuia.
Baada ya mazishi Mustafa alikua
akimalizia kuweka mchanga kwenye
kaburi la zarina. Alihisi maumivu makali
sana kwa wakati huo. Moyo wake
ulimwambia aangalie nyuma Yake.
Aliweza kugeuka na kupigwa na butwaa
alipigwa na butwaa baada ya kumuona
binti mwenye umbile sawa na la mdogo wake Muzda alikua amevaa vazi jeupe
huku kajitulia mtandio na nywele zake
zilibanwa vyema Sana katika vazi Hilo.
Alikua akiona vibaya au alikua kwenye
mawazo Yake.
Akiwa anashangaa alimuona mke wake
kipenzi akija katika vazi la kijani
kibichi, lakini alionekana kutoutambua
uwepo wa Mustafa. Mustafa alibaki
haelewi hayo ni maruerue gani alikua akiota.
" Kaka mkubwa shikamoo" ilikua sauti ya kijakazi wao ambae kwa Sasa
wametoka kumfanyia mazishi. Alikua
zarina. Aliitikia bila kwa ishara akiwa
bado haamini.
" Samahani Kaka mkubwa, usishtuke
Mimi ni nafsi hai iliyopumzika kwa
amani kwani nimeombwa nikupe salaam
hizi kabla sijasafiri milele" zarina
alitabasamu kwa tabasamu lake lilelile
Mustafa akawa haelewi. " Nadhani
unaweza kuelewa namna gani moyo wa
bi mdogo ulivyo msafi, aemniombea dua
nzito kabla sijasafiri nilikua najilaumu
kwa ninj naondoka bila kumuona, lakini
kwa maombi tu nashukuru nimemuona.
Mwambie bila Shaka zarina atapumzika
kwa amani. Na hatohangaisha nafsi
Yake kabisa" Mustafa alihisi kulia na
kutabasamu kwa wakati mmoja. Wakati
huohuo aliona Ile taswira ikiishilia
taratibu pamoja na Ile taswira ya
Saida ambayo haikuongea chochote
ilipotea kabisa
Mustafa alibaki bila kuelewa kwa nini
watu hao wamemtolea ghafla na
kuondoka bila kueleweka. Ila hapana
ameelewa bila shaka. Baada ya
kumkumbuka Saida kua hakua hapo na
zarina alikufa akiwa na Saida. Na
wakati huo Saida ndo alitekwa bila
Shaka ana sababu za kuagwa na nafsi
Safi Kama zarina asie na hatia.
" Kaka Mustafa" Maulid alimshtua
Mustafa aliekua amezama kwenye
mawazo.
" Nipo dogo" Mustafa aligeuka na kumwangalia Maulid. Kisha
akatabasamu.
" Kaka naomba niongozane na wewe,
Kaka muksin yupo anashughurika na
masuhara ya mirathi huko yemen. Alafu
wewe una wakati mgumu naomba tuwe
pamoja. Bila Shaka naweza kua mdogo
kwako lakini nikawa na njia ya
kukusaidia kwa chichote" Mustafa
alimuangalia alivyokua mdogo, bila
Shaka hawezi kuruhusu bwana mdogo
Kama huyo kuingia kwenye hii Vita ya
muda mrefu' hayupo tayari kumpoteza
mtu mwingine.
" Hapana dogo, kwa Sasa kila kitu kipo
sawa nitakujulisha bila Shaka iwapo
utahitajikq" Mustafa asingeweza
kumkarisha tamaa kijana mwenye akili
timamu Kama Maulid bila Shaka
anaweza kuchambua Mambo.
" Tuondoke Basi" Maulid alitabasamu na
kuongozana na Kaka Yake Mustafa
ambae alikua amebakia mwenyewe
makaburini.
" Kaka una uhakika Kama Kaka Azraj
anaweza kua anahusika kwa lolote na Jambo hili?" Maulid aliuliza na hapo Mustafa akamtazama.
" Unamaanisha nini?" Mustafa aliweza tu kushtuka kwani hawakujua watu wote.
" Kaka kwa Sasa nahisi hata wakina mama wanaofahamu Hilo. Kwani
nimewasikia wakizungumza kwa huzuni
kabla hatujauchukua mwili wa mamdogo zarina" Maulid alimwambia na Mustafa
akashtuka Sana.
" Una jisikia unacho ongea?" Mustafa
alikua kwenye butwaa.
" Sijui lakini Kaka hata Mimi, niliwasikia
wewe na Askari wa Badru kipindi hicho
nipo kambini kutumikia adhabu yangu
mkisema juu yake. Najua nilikosea
lakini sikua na njia, haikua rahisi kuziba
masikio " Mustafa alimsogelea zaidi na kuvuta sikio lake.
" Hufai kusikia kila kitu, twende
haraka" alimvuta na hapo Maulid aliweza tu kukunja kichwa chake. Kwa
kweli Kaka zake wanapenda kumuona
mdogo akiwa Hana makosa
watamdekeza zaidi Ila ikitokea kafanya
kosa Basi watamnyanyapaa kabisa.
Waliwasili katika jengo la Badru na
hapo Mustafa akawa anamwangalia
Azraj ambae alitabasamu na kumfata
kwa unafiki Kama ilivyo kawaida yake.
" Pole bro, najua Ni ngumu lakini Sasa
tutafanya nini nikuwaachoa tu police"
Azraj alimpa pole ya kinafki kwa kweli.
Mustafa alishindwa kumvumilia na
kumpiga teke la nguvu Azraj akaangukia
chini mbele ya kila mtu.
" Bro una matatizo!!!" Azraj alifoka kwa
nguvu akitafuta usaidizi wa Wana
familia lakini hakuna hata mmoja
aliejisogeza. Kibaya zaidi Bwana
Rashid, Bwana Yusuph , na Muksin
Badru wote hawakuwepo kwa muda.
Japo muksin aliondoka Jana Yake baada
ya kumtoa Saida sero. Hivyo kila kitu
kilikua chini ya amri ya Mustafa
" Gharib, Sajo, feisoo pelekeni huyu
jamaa sero" Mustafa aliongea bila
kusita. Azraj akainuka juu kumpinga.
" Kwa kosa gani? Una matatizo wewe?
Umekua ukininyanyasa siku zote
unadhani nakuvumilia tu bila sababu."
Azraj alifoka aliwaangalia wanawake
waliokua pembeni Yake lakini
hawakuweza hata kujitingisha
kumtetea. Hali Ile iliwachanganya
Muzda na Mariam pia. Haikua kawaida.
Bila Shaka bi Shayma angeumiza kichwa
chake akiwawaza hao wawili
wanaopigana.
Feiso alikua na hasira na Azraj kiasi
kwamba alimsogelea kwa papara ili
amkamate lakini tayari Azraj alishtuka
kwamba hapa sio salama. Aliweza
kuruka haraka na kumpiga teke la
kichwa feisoo akaanguka chini bila
kutarajia. Hapo napo Azraj
hakuchelewa kuchomoa bastora Yake
nje Kisha akafyatua risasi juu. Kila mtu
ndani ya jengo alipata mshtuko na
kulala chini ki vyake vyake. Hapo ndo
wakati ambao Azraj aliweza kumnyakua
Shayma kutoka kwenye mikono ya Muzda.
" Babaaa!!!" Sahyma alipiga kelele bila kuelewa jamani. Alikua akiwekewa
bastora kwenye kichwa chake.
" Mjomba muache da sima" Kim
alimfata Azraj ambae hakuweza
kumuonea huruma huyo mtoto aliweza tu kumpiga teke kubwa mtoto mdogo
akapepesuka Kama ndege.
" Kiiiiim!!!! Kila mmoja ndanj ya nyumba
aliogopa. Hadi wageni waliokuja
kushiriki msiba.
" Unadhani unafanya nini Azraj!!"
Mustafa alifoka kwa nguvu. Huyu Azraj
anakichaa anawezaje kuwatumia watoto
wake wadogo Kama ngao.
" Nafanya nachostahiri kufanya, kwani
nyie wanawake wa Badru Kuna kitu
mmetambua?" Azraj alitabasamu na bastora Yake mkononi. Mustafa alihisi
hasira kiasi kwamba aliwaza alishindwa kujizuia kutoa bastora Yake nje. Azraj
kwa ushenzi akalenga bastora Yake
uelekeo wa kichwa kidogo Cha Shayma
ambae alifumba macho akilia kwa sauti na kujikojolea juu.
" Baba niokoe mjomba Azraj anatisha.
Yeye ni zaidi ya shetani" Shayma alikua
akilia huku akihisi mwili wake unachomwa Moto kwa uwoga.
" Azraj unakichaa, unathubutu kufanya unyama wako hata kwa watoto wadogo"
Bi Shayma alimsogelea Kim na kumuweka sawa mtoto aliekua amepoteza fahamu zake.
" Sina jinsi mama yangu, nakuelpenda
Sana lakini kwa hili sitaweza kupata
huruma na nafsi yoyote Ile." Azraj
alijibu bila kujizuia. Wakati huo huo
walitokea watu wengi ambao walivaa
makanzu kwa ajiri ya msiba. Lakini
waliondoka kanzu zao nyeupe na kubakia
kwenye sare zao nyekundu.
Hapo ndo Mustafa akatambua kabisa.
Azraj alikua kajiandaa mapema. Ni
Kama alipata hisia kua amejulikana.
" Mustafa Badru, imekua kazi rahisi
kwako kunifatilia kwa muda mrefu si ndio. Lakini ulifaa kuniwekea ulinzi
tangu hapo kabla kwa ninj hukutumia akili?" Azraj alimwangalia Mustafa kwa
dharau na kumuona mtu asie na maana na asiejua Vita kwenye.
Sehemu ya 157
Mustafa alimtazama Azraj akabaki amemwangalia kwa Makini. " Azraj
mwanaharamu hufai hata kidogo kuitwa
Azraj Badru hata Kama ulizaliwa na
baba yangu, lakini bado utabaki kua
haramu ndo maana unaweza mtumia
mtoto Kama ngao ya kutoroka. Iwapo
unaniamini muache Shayma aende zake
tupambane kiume" Mustafa alimwambia
bila kua na uoga wowote ule. Azraja
alihisi kumcheka.
" Unadhani unaweza kupambana na Mimi
hata nimumacha binti yako" Azraj
alishindwa kujizuia kucheka kwa Mara
nyingine. Inabidi ujipime ugonjwa wa
akili Bwana Mustafa Badru, inamaana
huoni kabisa umebugi kwa ujuzi gani ulio
nao?" Mustafa alibaki kumwangalia.
" Bila Shaka unalinga kabisa kwa
sababu tu umepata mafunzo makubwa
kutoka kwa wanajeshi wa Badru, lakini
Ni ki kambi kidogo ambacho jlhakina
maana. Ila Hilo kuhusu Mimi hivi
unanifahamu vyema hata kidogo."
Alimuachia Shayma baada ya
kumsukuma Mustafa haraka Sana
aliwahi kumdaka binti Yake asiende chini.
'" baba naogopaaaa!!!!" Shayma
alizidisha kulia na kuhisi kichwa chake
kinamuuma. Mustafa alimsogeza kwa
mama Yake na bi Shayma akampokea.
Kwa kweli Bibi alikua amezeeka alafu
anaona maruerue Presha yake ilipanda
akashindwa kuvumilia. " Azraj mjukuu
wangu nini kilikukuta jamani mbona
familia ya Badru haikuwahi kukunagua na kujifanya wa kando japo hukua
mzaliwa halali wa ndoa ya Rashid na
Shayma" Bibi alihisi kulia na kulia zaidi.
Azraj alimsogelea huyo Bibi kizee huku
Askari wake wenye suti nyekundu
wakiwa wamelenga bastora zao
kuwaelekea wanafamilia.
" Upo sahihi bila Shaka, Ni kweli
kabisa upo sahihi, huoni Kama mlinijari na kunipa nafasi ya kua mtoto wa oiki
ilhali Mimi ndo mkubwa. Hata
mwonekano inaonyesha kabisa Kati
yangu na Mustafa Mimi ndo mkubwa"
Mustafa alitabasamu.
" Azraj Badru unaweza kukaa kimya
baada ya kukata mshipa wako wa aibu"
Bi Shayma alifoka bila kujari na
kuinuka haraka. Hata Kama alikua
mbaya bila Shaka asingemdhuru yeye
alikua mama Yake, japo hakua amemzaa bado alimlea kwa mapenzi na kwa wema
anawezaje kumdhuru?
" Bi Shayma Rashid, simama hapo hapo, usisogee kwangu" Azraj aliweka sura ya hasira na misukosuko kwa wakati huo
mpaka Bi Shayma akapata khofu
mwisho wa Maisha Yake ulikua mbele
Yake. " Hivi Ni kweli Waswahili
wanavyosema, " kua mtoto usiemzaa sio wako" Jambo Hilo lilimuuma Sana.
Mustafa alimuonea huruma Sana mama
Yake ambae alimlea Azraj na kumpa
kipaumbele zaidi yake akijua Azraj ni
kijana sahihi kumbe ndo hasara
iliyopindukia. Mustafa aliweza tu kusimama mbele ya mama Yake na kifua
chake kipana kikamuelekea Azraj. Kwa
kweli amepitia mengi Sana kiasi kwamba
amehisi kuyazoea matatizo. Amejikuta
amekua ndugu Yake na matatizo bila
kutarajia.
" Azraj Badru umenivunja moyo wangu
kwa hakika" Bi Shayma alishindwa
kuzuia kutoa machozi Yake.
" Sikua nimeamini baada ya kuambiwa na mtu lakini kumbe,,, kumbe bado
nilikua najidanganya juu yako" Bi
Shayma alihisi akidumbukiziwa kitu Cha
Moto kwenye moyo wake uliokomaa na kuishi kwa miaka kadhaa.
" Hapana mama sio kosa lako" Mustafa alimjibu.
" Kosa Ni la kwangu Mimi, nilifaa
kumuonyesha rangi yake mapema Sana"
Mustafa aliongea Azraj akawa
anashangaa hivi ymhuyu Mustafa
anajiamini ninj?. Au atakua kaita police, bila Shaka hakuna polisi
wanaoweza kuwasili hapo kwani tayari
mjomba amiri amedhibiti Hilo.
" Mustafa Badru, unaweza kukaa
kimya, nadhani unafahamu zaidi ya yote
kua azraj Badru anataka kitu gani?"
" Usiniite Azraj Badru, jiite jina la
mkuu wako bila Shaka itapendeza Sana"
Mustafa aliongea akiwa kakunja mikono
Yake kwenye kifua chake kipana bila
hata kutiskisika.
" Azraj!!! Bi Shayma bado alibaki
haamini kwa nini haya yatokee.
" Acha unafiki wako Bi Shayma Rashid"
Azraj alifoka kumuelekea yeye.
" Unasema ukinipenda na ku ichukulia
Kama kijana wako unataka niamini Hilo.
Unadhani nitaamini Jambo hilo?
Ulinipenda Mimi Kama kijana wako?
Ulijifanya unanipenda unanithamini kwa macho ya watu na kwa unafiki lakini
chini kabisa ya jioni Cha moyo wako
imuhifadhi Mustafa ambae ndo pekee
uliemzaa" Bi Shayma alihisi Kama
anatupiwa matope usoni mwake.
" Azraj niliwahi kuonyeshea Hilo kweli?
Hata Kama ndio nilikua mdahifu sikufaa
kumpenda Mustafa hata kidogo?" Bi
Shayma alihisi Kama atakufa kwa ukweli
uliojimwaga mbele Yake.
" Hapana bila Shaka, sio kidogo Ni
Sana, yaani ulimpenda Sana. Ukiniita
kijana mwema mtiiifu na mnyenyekevu.
Nawezaje kua jeuri kwa mwanamke
ambae sio mama yangu wa kunizaa bila
Shaka nigeishi Maisha ya kuzimu zaidi
ya jahanamu nikiwa hai." Bi Shayma
alihisi kulia hivi' kweli alikua na roho
mbaya kiasi hicho?.
" Kaa kimya wewe mwana asie na
shukrani " Bi Azat alisimama juu na
kumfata Azraj bila kusubiri kujizuia
hasira Yake. " Shayma amekuchukulia
mtoto zaidi ya alivyomchukulia Mustafa
lakini hayo ndo malipo unayompa,
akikupenda zaidi ya mama yako wa
kambo, alikua sawa na mama yako
mzazi wewe Azraj uliwezaje kubadilika
hivi. Kwa nini inaumiza hivi" Bi Azat
alitamani achimbe shimk akae humo kwa
sekunde kadhaa kwa kweli hawezi
kumvumilia huyu mwana
" Kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo
wangu siwezi kukuzaba Kofi wewe
mwanamke, ambae ni shangazi yangu
Mimi" Mustafa alishtuka inamaana
mama Yake ndio alionekana sio chochote
kwa Azraj Ila aunt Azat alikua wa maana Sana.
" Bora nife kuliko kua na sababu kwako
Azraj. Kwa Mambo uliyofanya nahisi
aibu kujiita mwanafamilia wa Badru."
." Hapana Sina haja ya kueleza Ni vipi bi Shayma Rashid Badru alionyesha
upendo wake kwangu, ningekua kijana wa muhimu kwake bila Shaka
angenipigania na kuniweka katika njia
sahihi kabisa. Upendo wa mama my
f**t' Ni upendeleo gani anganifanyia
iwapo angenitafutia mwanamke Kama
saida pia! Huoni Kama ningetunukiwa
zaidi. Familia ya Badru haikuwahi
kunipa nafasi yoyote Ile katika haya
Maisha"
Watu wote walishtuka Ni kitu gani
ambacho wao hawakumpatia azraj. Bila
Shaka alipata kila kitu kutoka kwao na
hawakuwahi kumshibuti hata katika
matumizi ya pesa bila Shaka angetumia anavyotaka. Lakini mwisho wa siku
umeonekana wameiishia kufuga nyoka wa midomo miwili.
Mustafa alimwangalia kwa hiyo mpaka
hapo bado aliweza kumtaja Saida
kuonyesha Ni jinsi gani alimtaka
mwanamke wake. Mustafa alikua na sababu kubwa ya kumchelewesha Hali
kwa kweli hakua na sababu ya kupigana na huyo kwenda wazimu. Kwa wakati
huo.
" Azraj kwani ulisema unahitaji kuoa
tukashindwa kukutafutia mwanamke,
bila Shaka tulitamani unuoe Salma
baada ya kujifungua"
" Salma Bullsh**t" na hapo mseme bado nilikua wa muhimu kwenu. Angalia
mwanamke mliemuozesha Muksin. Najma
Sabodo binti wa Sabodo" Najma
aliwatazama Mariam na Muzda pamoja na mama Yake mkwe. Hilo nalo lilikua
kosa kwake jamani bila Shaka yeye na
muksin walioana kwa sababu
walipendana.
Wakati huo simu ya Muzda iliingia
meseji, ulikua ujumbe kutoka kwa yasiri
lakini alikua na khofu kiasi kwamba
aliishia kuutazama kwa macho tu. '
Yasir nisamehe Sina namna nipo kwenye
mdomo wa mamba' nu maneno ambayo
aliyatamka ndani ya moyo wake pekee.
Saida, Ni binti ambae mlitufanya
wajinga sisi wengine hapk awali kwa
kumuoa kutoka kijijini, lakini ukweli Ni
kwamba alikua binti aliekulia Maisha ya kifahari na kukutana na watu
mbalimbali akapata ujuzi mbalimbali na
kua mwanamke mashuhuri katika suhara la mapishi na ubunifu wa mavazi
mapambo na mapishi. Ni mwanamke bae
hakua wa kitajiri Sana lakini ana utajiri wa akili, kibaya zaidi Ni mzuri kupita
kiasi. Ni jinsi gani Mustafa asingeweza mkataa hata Kama angetaka"
Lisala ya Azraj ilimfanya Mustafa
ampige ngumi ya mdomo. Azraj
aliushika mkono wake alipokua
akiupeleka Mara ya pili. Alimpiga pia.
" Ndio, nadhani inaeleweka ikija kwa
" Mustafa Badru !! Unadhani Leo hii
utaniweza bado hufahamu Mimi
nimepata mafunzo kutoka kwa watu gani?" Mustafa alitabasamu.
" Nafahamj Azraj Badru. Bila Shaka
umepata huu ujuzi kutoka kwa Husei.
Marzuku mkufunzi wa majeshi ya
alshabab na Boko Haram, lakini pia
mwalimu huyo Ni mkufunzi ambae
amefuliwa kutoka Madina na alikua
miongoni mwa watoto wa wanaume
mashuhuri waliopigana Vita ya Badri na mtume wetu Muhammad. Ila hiyo haina
maana kwamba utanizidi kwa ujuzi huo
wako mdogo"
Azraj alishangaa Sana, alifahamu fika
juu ya mwalimu wake wa mafunzo hiyo
ilikua na maana gani?.
" Ni kwa sababu moja tu, huyo mwalimu
wako wewe, aliwahi kua mwanafunzi wa mwalimu fulani pia, ndk maana
nakwambia usjiamini kupita kiasi"
Mustafa alimpiga ngumi ya mdomo
Azraj akatapika damu baada ya nyama na meno Yake kugusana. Hakua tayari
kukubari kushindwa hivyo yeye pia
aliarusha ngumi kumuelekea Mustafa
akakwepa ngumi kadhaa.
Azraj alijiamini Sana kwa kumuona
mustafa alikua slow kwenye ngumi zake na yeye alikua haraka, walipigana
mateke kadhaa mieleka kwa knock out
kadhaa kwa kweli walikua wameamua
kuminyana siku hiyo, Mustafa alikua na.
Usongo na Azraj tangu mwanzo na Wala
hakutaka kupoteza nafasi hiyo kwani si
amejileta mwenyewe. Azraj alianza
kuchoka na kuona huu Moto mbona
hatari Mustafa alikua hatari zaidi ya siku zote. Azraj Imani Yake ilianza
kufifia maana tayari alikua amempiga
Mustafa Ila hakua amemuumiza Kama
namna yeye alivyoumizwa.
Watu wa Azraj walipoona Hali ya Azraj
imeanza kua mbaya walishtuka na
kumsogelea Mustafa kwa wakati huo
wakimnyooshea bastora. Azraj aliwaka
ishara ya vidole viwili haraka walimteka
Bi Shayma aliekua amechanganyikiwa
kwa wakati huo. Na kumuwekea bastora
kichwani
Azraj alijiweka sawa na kumkuanza
kutoka nje ili akimbie. Lakini hakufika
mbali kwani pale mlangoni alikutana na
Askari waliokua wakifatilia kesi ya
mauaji yaliyotokea Jana Yake.
walimuangalia Azraj aliepata khofu na
kutoa amri ya ishara kua watende kile ambacho kitakua msaada kwao. Kuna
kijana mmoja alichomoa bomu la moshi na hapo wakalifungua,, Mustafa aliona
kabla hivyo akawahi kuziba macho Yake
pamoja na Gharib. Kwa sekunde moja tu tayari nyumba nzima ilijaa mfuke wa
Moshi. Na watu wakaanza kukohoa.
Baada ya dakika mbili Moshi ulianza
kupotea na watu wakabaki wakikuna
macho Yao. Watu pekee waliosalimika
miongoni mwao alikua Mustafa na
Gharib pamoja na feisoo.
Mustafa ambae alishtuka na
kumuangalia mama Yake aliekua
" Bwana mkubwa" vijana wake
" Bwana mkubwa" Gharib alimuita
akihangaika na macho Yake yaliyotoa machozi bila kutarajia.
" Bi Badru upo salama" Askari waliwasili hapo waliuliza kujari kwanza usalama wa raia kilikua kitu Cha kwanza. Mbele Yao hakukua na Azraj Wala mtu yeyote
mwenye suti nyekundu. Hilo halikua na maana kwa Mustafa kwani wanafamilia wengine walikua salama.
" Azraj Badru, Anza kuhesabu chini na kuzimu yako kuanzia hivi Sasa!"
Mustafa alikiri Hilo na Askari polisi wakabi wamemtaza.
" Bwana mkubwa Badru, tunafaa kufanya Jambo lolote kwa wakati huu?"
Askari alieshikka kesi hiyo alihoji.
." Huna haja na Hilo, kwani nadhani
mpaka hapo unaelewa muuaji Ni Nani?
Tukikamilisha ufatiliaji wetu Kama
Badru guard tutawaeleza
kilichopatikana na kuwapatia watu wenu"
Mustafa hakuweza kuongea zaidi ya
kumuelekea mama Yake.
" Mnafaa kujiandaa Sasa muondoke hapa wote, nahitaji kuanza vita yangu
Mimi pekee yangu" Mustafa alimwambia aunt Sonia ambae angalau alikua
kwenye fahamu zake.
" Lakini vipi kuhusu Saida" bi Sonia alipata khofu dhidi ya Saida. Kuhusu
Salma watamchukua hivyohivyo pamoja na mtoto lakini vipi kuhusu Saida?.
Mustafa alitabasamu baada ya kuikumbuka uhusiano mbaya uliokua Kati ya wawili hao bi Sonia hapo mwanzo
hakuwahi kabisa kjmoenda Saida.
" Hatuwezi kumuacha bila Shaka?" Bi
Sonia aliuliza Tena.
" Hilo haliwezekani mamdogo, inabidi
mjiandae tu. Kwani hii ndo nafasi pekee
iliyobaki kumaliza matatizo katika
familia hii" Mustafa alimkumbusha bi
Sonia ambae aliitikia kwa kichwa na
kutamani iwe hivyo kabisa kwani
amechoshwa na hizi karaha.
" Aunt hakikisha unajiandaa vyema
Sana na wanao" Mustafa alimkumbusha
bi Azat alieonekana kua kwenye
dilemma. Hao wengine wanaelewa Cha kufanya.
" Lakini Kaka Mustafa, nitabaki na
wewe, Mimi pia Ni mwanaume wa
familia hii" Maulid aliongea na
kuwafanya watu wachangnyikiwe hivi
walionekana kua kwenye wasaa wa utani.
" Hayupo kwenye utani Maulid." Bi Azat alimfokea.
" Namaanisha mama, ki ukweli
sijafurahishwa kabisa na Kaka Azraj
nahitaji kumpa SoMo kwani aliwahi
kunifanyia muhusika wa mihadarati.
Siwezi kuliacha lipite" Maulid alipata
maumivu na hapo bi Azat akaziba
midomo Yake hiyo unaweza kua kweli
eeh.
" Sawa iwapo unasisitiza. Lakini
uanaume wako katika familia hii
utakamilillka iwapo utaweza kuilinda
familia yetu dhidi ya wabaya nikiwa
mbali nanyi, fanya hivyo haraka Sana, walinde kwenye uwepo wako na
ninapokosekana Mimi" kwa Hilo Maulid aliona sawa iswe tabu.
" Mamdogo bila Shaka nitakua nyuma yenu nikiwa na Saida. Nyie tangulieni"
Mustafa aliamini Sana juu ya kike alichokisema.
Ni kwa nini Mustafa alimuamini Sana aliposema kuondoka kwake na Saida. Ni
kwa sababu alitambua zaidi kua
atamshinda Azraj.
Ni kweli baada ya Azraj kurejea katika
kambi take ya umafia. Alishtuka Sana baada ya kukuta eneo Hilo likiwaka
Moto. Yaani haijulikani ilikuaje kambi
hiyo ambayo ilikua ngumu kujulikana kwa
wakati mmoja iwake Moto ghafla.
" Nini kimetokea hapa?" Azraj alifoka
huku akimuona Bwasha anavyohangaika
kuzima Moto akiwa na watu wengine.
" Hakuna anaejua Bwana mkubwa?"
Bwasha alijibu na wakaendelea kuzima
Moto ambao haukujuliakana Ni. Wapi
ilitokea?" Azraj akapiga heaabu za
haraka na kumuona Bwasha Ni
mpumbavu Hana akili.
Alichomoa Mkanda wake Kama kawaida
na kumrushia I'll ampige. Bwasha
haraka Sana aliukwepa Ile Mkanda. "
Unawezaje kunipiga bila sababu"
alikasirika kwa kweli. Hata Kama
alipigwa ndo hasira Yake aihamishie
kwake.
" Unawezaje kua mjinga" mateka
umewatoa ndani? " Azraj alihisi hasira.
" Ndo unipige??? Bila Shaka nimewatoa
ndani wote" Bwasha alihisi atasifiwa
kwa Jambo hilo, Azraj alihisi
kuchanganyikiwa. Huyu Bwasha ana
ukubwa wa mwili lakini akili Hana.
" Kwa nini umewatoa wewe mbwa" Azraj
aliurusha Mkanda kwa Mara nyingine.
Huku Nevson aliwaangalia kwa Makini na kutabasamu Sana moyoni.
" Bwana mkubwa, bwana Bwasha
alihofia kua wataungua Moto hivyo
akaamua kuwatoa kwani bado wana
umuhimu kwetu" Nevi alimtetea Bwasha
" Kaa kimya sh**zi" Azraj alimrushia
Nevi pia Mkanda. " Huo Ni mtego na nyie mmeingia"
Azraj haraka Sana alishuka chini kabisa
wakati huo jengo Hilo lisiloeleweka
likiwaka Moto kabisa. Na hapo Nevi
pamoja na Bwasha walimfata nyuma
Azraj kumpa escort.
'Mungu Saida tumpate bi mdogo'
yalikua mawazo ya nevi ambae alikua
tayari amefanikisha kuwapata watu
wengine na wiondolewa tayari katika
jengo Hilo kwa hivyo wamechukuliwa
tayari Badru guard bila watu hawa
kufahamu. Isipokua Saida ndo hakua
amepatikana.
Na kwa kua azraj amekuja kwa
kuchanganyikiwa bila Shaka atampata
Saida. Ili amuokoe kwani anaonekana
kumpenda Sana. Na iwapo atampata
Saida Wana jeshj wa Badru gauard
watavamia eneo Hilo na kumvamia
wamnyakue haraka Sana.
Walitembea katika vymba vyote
ambavyo vilikua vikifuka Moshi na moto
ilizidi kutanda ndani ya nyumba hiyo. "
Bwana mkubwa kua Makini utapatwa na shida. " Nevi alionekana Sana kumjari
Azraj ambae hakua tayari kuijari afya
Yake.
Hatimae walifika katika chumba
alichokuwepo Dr Neema na kukuta
kutupu tayari. " Bwana mkubwa Ni
ukweli niliwatoa kasoro mmoja ambae
sikufahamu yupo sehemu gani?" Azraj
hakuweza kumjibu chochote zaidi
aliweza tu kung'oa kiti ambacho kilikua
Cha Moto kupita kiasi kwani kilikua kitu
Cha chuma. Kwa kweli nevi alishtuka
Sana.
Hivi Ni kweli kabisa Saida alikua
amewekwa sehemu mbaya Kama hiyo. "
Kwa nini Albert aliondoka bila
kumwambia Jambo Hilo?" Nevi alishtuka na kupiga tathmini juu ya huu Moto hivi
itakua rahisi kutoka nae nje.
"Haraka Sana vunja hapa!!" Azraj
aliamuru wakati huo Bwasha alikua
akifanya Mambo taratibu nevi hakuweza
kumvumilia, haraka Sana alianza
kuvunja. Baada ya kuvunja kwa muda
kidogo huku wakikwepa mabanzi na
vifusi vya ukuta ambavyo vilianza
kuporoka. Hatimae walizama ndani ya ya jengo Hilo. Hilo Ni jengo ambalo
lilikua na vyumba visivyoeleweka dah!
Baada ya kushuka ndani Yake
kilionekana kua na korido za kutosha.
Hapo Nevi akashtuka na kuhisi Kama
Kuna Siri nyingi Sana ndani ya vyumba
hivyo. " Saida" Azraj aliweza kumuita
Saida bila kusita. Na hapo Nevi
alitambua moja kwa moja kua Saida
alikua sehemu gani? Bwasha alishtuka
boss wake alichanganyikiwa na Saida
kiasi gani? Mbona hapo mwanzo hata
yeye hakumpa ruhusa ya kwenda
kumuona, aliweza tu kurekodi video na
kumletea kisa hakuweza kumuamini ila
saa hii kaingia Hadi na mlinzi mwingine mgeni.
" Bwa mkubwa" Bwasha aliita akiwa na lengo la kumsema Ila wakati huo tayari
Azraj ameingia kwenye chumba
ambacho amemuhifadhi Saida na kubaki
akiwa na butwaa kubwa isiyoelezeka. "
Saidaaaa" Azraj aliita kwani Saida
hakua ndani ya chumba hicho. Alikua
wapi??? Azraj hakutaka kuamini kabisa
Kama Saida atakua tayari amenyakuliwa na Mustafa.
Sehemu ya 158
Nevi pia alishangaa au Albert alitoa
ramani mapema kwa Badru guard kabla
hajaongozana na bwana Amiri Kama
mlinzi wake? Ila hadhanii??
" Kuna mtu aliingia huku??" Azraj
macho Yake yaliwaka Moto kwa hasira
wakati huo ubao wa singboard
uliporomoka baada ya kushuka Moto.
Nevi haraka Sana akakinga bila kujari
kuhusu mwili wake akamkinga Azraj.
" Nauliza Saida Yuko wapi? Hakuna mtu
aliekuja hapa, hawezi kua ametoroka
kwani mlango ulikua umefungwa atakua
wali mwanamke wangu?" Nevi alishtuka na kujikuta akitaka kumsukuma mbali.
Anamuita Bi mdogo wake mwanamke
wake. Hivi ana akili timamu?
" Bwana mkubwa tunafaa kuondoka Hali so nzuri" Nevi alimsiaitiza huku Bwasha
alifungua mlango maana tayari Hali
ilizidi kua Tata na milango ingejiloki
mwisho wakakosa pa kupita.
" Mmeshindwa vipi kuwalinda, hiyo inamaanisha kabisa na mliowatoa nje
tayari wamechukuliwa"
" Bwana mkubwa tuondoke hapa"
Bwasha pia alimsisitiza na kujitahidi
kukimbia eneo haraka Sana. Moto
ulikua ukiporomoka na kufanya jumba
like ligeuke kua Kama jahanamu ndogo.
Nevi aliona hiyo hatari akatamani
kujizolea baadhi ya pointi kwa Azraj na
kuwaounguzia kazi Badruguard kwa
kumuondoa Bwasha huyu kichefu chefu.
Hata alimuua zarina. Hakua na
mahusiano nae lakini taratibu alikua
ameanza kumuelewa. Kila alipokumbuka
Jambo Hilo kwa kweli asingeweza
kumvumilia huyu mshenzi.
" Bwana mkubwa haraka" Nevi
alijitangiza mbele na kukaa eneo ambalo
lingetumika watu kupanda na kutokea
njia ngazi tayari ilikua ikiwaka Moto
hivyo wasingetoboa kabisa kupita.
Azraj alimwangalia kwa jicho la uaminifu Nevi.
" Sawa" alikumbuka kutoa tamko Hilo na haraka Sana akaukanyaga mgongo
wake Kisha akapanda na kutokea nje.
Alipofika nje Azraj ilikua zamu ya nevi
kupita ndo afate Bwasha. Bahati mbaya
Sana ukuta wa juu uliporomoka na
kwenda eneo la chini na kuwafanya
wawili hao wakwame.
" Nyie huko chini wahini tuondoke"
Azraj aliona Hilo kwani eneo alilokua
yeye ndo lilikua likiporomoka.
" Bwana mkubwa tusaidie" Bwasha
alipiga kelele Nevi akatabasamu, huyu
alijikuta mwanaume katili huku alikua
akiogopa kukwama kwenye eneo rahisi
Kama Hilo. Bila Shaka Nevi alikua
mzoefu Sana wa kukwepa mitego ya
panya iwe na isiwe bila Shaka atapata
njia ya kutokea.
" Bwana mkubwa sisi tupo tayari kufa
kwa ajiri yako" Nevi alitoa sauti ya
uaminifu zaidj kwa Azraj ambae alihisi
tu kuwaonea huruma.
" Bwana mkubwa hapana, Mimi na wewe tumetoka mbali Sana" Bwasha
alimkumbusha Azraj ambae alihisi
kuchanganyikiwa" Nevi akaona anaweza
kupoteza lengo.
" Bwana mkubwa kumbuka umeanza
muda mrefu' mission hii, umepitesa
damu nyingi na watu wengi Sana
uliowaoenda na kuawaamini wamekufa, kumbuka una mtoto Sasa. Kumbuka upo
kwenye levo ya mwisho sisi Ni vijakazi
tu. Nenda ukaendelee na Vita" Nevi
alimchochea Azraj ambae alipata hisia
chanya juu ya maoni hayo na maraoja
akaondoka zake na kuwaomba kila la kheri wawili hao.
" Natumai hamtakubali kufa kizembe
Bwasha, nakuamini Sana" Azraj aliongea
huku sauti yake ikipotelea kabisa.
" Unakichaa wewe" Bwasha alimfokea
bevi huku akijaribu kuinua kufusi
ambacho kilikua juu Yao. Na muda wote
walikua wakiongea kwa shida Sana. Na
Moto ulikua umetanda zaidi.
" Ndio Bwasha, siku zote Askari
tunaotoboa na kuitwa Badruguard huwa
Ni vichaa kabisaaa!!! Alijibu nevi na
kuinua kifusi kile kwa kukisukuma na
mkono mmoja tu. Hakika Bwasha
alishtuka Nevi alionekana bwana mdogo
asie na nguvu kumshinda yeye. Alisikia
kuhusu Badruguard lakini hakumjari
kwani Ni neno ambalo alikua akiliongea
Dani wakati anaadhibiwa. Na wakati
huo Dani na Nevi walikua maadui
" Wao we ni super extra power"
Bwasha alikunja mkono wake na
kutunisha msi wake akimpa sofa nevi
Kisha akasogea eneo ambalo lilibaki na
uwazi akihaelewi Ni wapi alitie? Anyway
yeye ni mwanaume bila Shaka atapanda
ukuta Mara moja na kutokea nje.
" Upo sahihi, Mimi ni extra super power,super mind, super fighter. Na
Leo ntakuonyesha uwezo wangu Bwana
mdogo" na hapo Nevi aliweza kumpiga
Bwasha teke la nguvu Sana la mgongoni.
Nevi alijikuta akiangukia pia bila
kutajia. Haa!!! Nini? Inamaana?
Alipigwa na Nevi?
" Wewe?? Bwasha alifoka akitaka
kuinuka lakini mgongo wake ulicheza
ishara kabisa uti wake wa mgongo
uliivunjika. Eehh!!! Alipitia nini kwenye
mguu wa huyu Kaka mdogo nevi.
" Nevi wewe?? Unakichaa umenivunja
mgongo" Bwasha alilalamika na kutaka
kuchomoa bastora Yake haraka lakini
ajabu alishangaa hakua nayo. Bwasha
alimwangalia Nevi amabae aliinua mikono
Yake miwilijuu akimuonyesha bastora. "
Ajaab! Ninazo zote" Nevi alikwepa
kifusi ambacho kilikuja kwake ghafla na
kuruka kabla hakijafika chini Kisha
akakisukuma kwa mguu wake
kikimuelekea Bwasha, lilitua kwenye
kichwa Cha Bwasha ambae aliona nyota
nyota akiwa haamini hivi Ni kweli? Huyu
alikua nevi
Mpaka hapo Bwasha hakuweza kuamini
Kama waliishi na msaliti kwa kumpa
Imani kamili. Nevson. Alikua msaliti.
Bwasha alianza kupiga kelele za nguvu
iwapo Kuna mtu nje Basi afahamu
kabisa huku Ni hatari.
Sauti Ile Azraj alijisikia kwa mbali na
kuhisi tayari amewapoteza Askari wake
mahiri na mashuhuri. Lakini alikosea
kwani ilikua ishara kutoka kwa Bwasha
kua wanasalitiwa. " Bwana mkubwa ana
kuamini Sana nevson" Bwasha alishindwa
kuvumilia kutoa uvimbe uliokua umejaa
moyoni mwake wakati huo.
" Bila Shaka, hata yeye aliaminiwa
Sana na wanafamilia wa Badru" vifusi
vilianza kushuka kumuelekea Bwasha
ambae alikua akizidi kua na Hali mbaya
sio tu hivyo, hata vifusi ambavyo
vilimshukia yeye bila Shaka angevipiga
mateke na vimfate Bwasha.
" Mbwa wewe!!!" Bwasha alimtukana.
" Bila Shaka wewe ndo mbwa, shetani wa kirundi wewe. Umenifanya
nimuadhibu Dani kwa mikono yangu,
umemuua zarina, unajua alikua Nani
kwangu?" Nevi hakuweza kuvumilia
baada ya kuikumbuka sura nzuri yenye
tabasamu Kama sura ya zarina.
Alichomoa kisu chembamba kutoka
kwenye kiuno chake chembamba na kuchomeka kwenye mshipa wa shingo ya
Bwasha. " Roho inaniuma Sana kuona umeenda kufa kifo kirahisi namna hii, sikitegemea ufe kwa Raha hivi wakati una roho za watu wengi Sana kwenye mikono yako, lakini ntafanya nini?
Nafaa kubaki hai ili nijipongeze kwa kukuua wewe" Nevi. Alimkandamiza kisu
hicho kwenye macho Yake kwanza.
Bwana alipiga kelele kwa maumivu makali. Tayari alitia kisu kwenye shingo
Yake haikutosha bado amemtoboa macho Yake. " Wewe ni katili zaidi
yangu Nevi" Bwasha alipiga kelele.
" Natamani niwe zaidi ya hapa Bwasha
lakini sijui
Nevi aliongea na kupolitisha kisu kwenye
ngoma za masikio yake'. Huku
akitukata mshipa mwingine wa shingo.
Bila Shaka mpaka hapo kwa kweli
Bwasha hawezi kupona.
Kutokana na mafunzo waliyopewa
Badruguard lazima umuache adui
amekufa kweli kweli asije fufuka hata
kwa bahati mbaya. Na kweli nevi
alihakikisha Hilo. Kisha anatafuta njia ya kutoa katika jengo Hilo. Bila Shaka
asingetokea kwa Azraj akiwa na afya
kiasi hicho wakati aliwaachia kwenye
Hali mbaya. Hivyo atalazimika kupotea
mbele ya Azraj kwa wiki kadhaa Kisha
ndo amtokee kwa kisingizio Cha alikua
akifanyiwa matibabu"
Azraj alihisi kupagawa baada ya kupelekewa kwenye gari ambayo mateka walihifadhiwa. Alihisi kupagawa baada ya kuwakosa watu wawili pia ambao
alikua Dr Neema na Dani.
" What the heck" watu hawa wameenda
wapi? Azraj alihisi kua mwisho wa dunia yake. Yaani hata watu hao wawili
hawakuweza kuwapata.
" Mna maana gani Sasa iwapo hamuwezi
kuwalinda mateka kabisa" Azraj alihisi
hasira na kuanza kuwapiga vijana wake
ambao waliishi kumtii kwa sababu
waliogopa kukosa kidonge Cha uhai. "
Bwana mkubwa tusamehe sisi tulidhani
tunawaokoa mateka muhimu"
Azraj kichwa chake kilimuuma akaanza
kupiga mateke gari iliyokua tupu kabisa.
Wakiwa hapo ghafla Askari wa Badru
guard waliwasili na kuanza mashambulizi
wakiwa na Askari police wa kutosha.
Azraj alishtuka baada ya kuwaona hao
Askari alitamani kumuita Bwasha ambae
anamuamini Sana katika ulengaji
shabaha lakini Sasa hata yeye
hakuwepo eneo Hilo. Azraj haraka Sana
alitafuta njia na kukimbia akiwa
amepoteza muelekeo kabisa. Amekua
mtj wa kukimbia Sasa? Hivi kwa Nini
Mambo yamekua mabovu, kwani alifeli
wapi?
Baada ya Azraj kukimbia Askari wa
Badru guard pamoja na Askari wa
serikali walijitahidi kutafuta ushahidi
uliosalia pale baada ya kuja zimamoto
na kuzima Moto. Na kuwakamata
baadhi ya watu waliweza kuwakamata.
Na kuhakikisha wameiteketeza Ile ngome kabisa. Lakini katika upekuzi wao
waliupata pia mwili wa Bwasha.
Baada ya mkufunzi mkuu wa Badruguard
kuuona mwili wa Bwasha na technique
iliyotumika kumuua mwanaume huyo
moja kwa moja aliamini kabisa mtu huyo
kauwawa na mwanafunzi wake.
" Samahani iwapo nitaingilia kazi yenu,
Ila nakuomba huu mwili nichunguze kwa
dakika kadhaa" polisi hawakua na ujasiri wa kumpiga bila Shaka walimruhusu
auchunguze.
Katika kambi ya Badru Mustafa aliwasili baada ya kuwafikisha Dr Neema pamoja na Dani wakiwa hoi. Feiso alifurahi
haswa alipompata Dr Neema.
" Sister unetoboa? We ni kiboko!" Feiso
ionyesha shangwe katika uso wake lakini
mdomo wa Dr Neema ikitetemeka kwa
furaha hafifu kwani alikua hoi. " Ulihisi
nakufa" sauti hiyo ilitoka ndani kabisa ya tumbo lake feiso akaweza kumuonea tu huruma.
" Bila Shaka utapona sister " feiso
alimpoza maumivu Yake Dr Neema
alitabasamu na kufumba macho Yake
kwa uvivu ki ukweli alikua na maumivu makubwa Sana.
" Oi msela Hali haikua nzuri kwako eeh!!
Ila usijari wewe ni Badru guard" Dani
aliambiwa kitu ambacho hakuweza
kutulia baada ya kuwaona marafiki
zake. Alihisi kufurahi moyoni japo
alikua na maumivu makali kwenye
maeneo yake. " Niko mzima, nitafutieni
mwanamke" wenzake walicheka kwa
uchungu kwani wakiamini kabisa kwamba
kwa Sasa Dani haiwezi kua rahisi kwake kuweza.
" Mimi bado Nina kazi ya kufanya"
Mustafa aliongea kwa maumivu kwani
imekua kana kwamba hajakamilisha kazi
yake. Ki ufupi haikua rahisi kufanya
maangamizi dhidi ya Azraj lakini bado
hakuweza kumpata Saida.
Askari wote wa Badruguard walikaa
kimya na kuhuzunika kwani walielewa
hisia kamili za boss wao. " Mkuu
tutaandamani na wewe kila Kona, Ni
muhimu Sana kutambua uwepo wa Bi
mdogo" Gharib alikua na hasira kila
alipomuwazia Azraj kumchukua Saida
alikua mwanamke mzuri Sana na alieishi
vyema na kuvumilia madhaifu mengi ya Mustafa.
" Sihitaji kusaidiwa Sana linapokuja
suhara la mke wangu, kwa Sasa nawapa
jukumu la kuiangalia familia nzima ya Badru. Fanyeni maandalizi mapema
muiondoe hapa familia yangu sitaki
misukosuko mingine nikiwa nahangaika
kuweka Mambo sawa"
Sehemu ya 159
Majira ya usiku wa saa tatu Muzda
alikutana na Yasir Sabodo katika hotel ya kifahari jijini Dar. Muzda
alitabasamu baada ya kuonana nae.
" Nilidhani hautafika mpenzi" Yasir
alimpokea Muzda. Walikua wachumba
ambao uchumba wao ulianza Kama
masihara jamani.
Ni siku ambayo Yasir alijitokeza kwenye
ofisi ya Muzda kwa kutumia mualiko wa
Lilian Masele. Sasa baada ya Yasir
kujitambulisha hapo Najma alibaki
akicheka kwani alikua akimfahamu
vyema mtu huyu.
Kwa kweli Muzda hakuweza kumuelewa
hapo mwanzo Ila yasiri hakuacha
kumfatilia. Muda mwingine alimfata
akiwa kaandamana beach na rafiki
zake. Kuna wakati angemtumia Mariam
ili kumfikia lakini Sasa Muzda bado
alimuona Kama mtu wa ajabu. Bila
Shaka alikua wazimu alifanya yote hayo
eti Lisa alikua akimpenda.
Kamati kuu ya kichwa Cha Muzda alikua
Saida na Najma bila Shaka
angewatumia watu hao wawili kufanya
chaguo sahihi la Maisha.
" Kwa hiyo wewe unataka nikupe sifa
mbaya za Kaka yangu mwenyewe, bila
Shaka una wazimu lazima umkubali
kwani sitaki kuona akiwa singo milele"
Najma aliongea. Saida akacheka hoi.
" Ni kweli wifi, yaani hata sijui Kaka
yasiri tumuite shemeji sijui tumuite
Nani Ila ndo hivyo anaonekana
kumpenda Muzda anatusmbua Sana hata
tukitoa ku jivinjari na marafiki zetu
kikubwa Muzda akubali kuongea nae"
" Kwani we wifi unanifahamu Yasir, kwa
kweli sidhani Kama ananifaa namuona
Kama Kaka Mustafa" Muzda na wengine
kwa wakati huo walikua walimchukia
Mustafa.
" Hamna kitu Kama hicho, Yasir
nimemfahamu muda mrefu' Sana kijana
mstaarabu na mwema, sikua ndugu Yake
lakini aliniheshimu na kuniamini Kama
dada Yake mpaka Leo hii, kwa nini tusiunganishe udugu moja kwa moja.
Aoe nilipo olewa alafu ule ukaka udada
ukamilike" Saida alimchochea Muzda
baada ya kumuona akiwa amenogea
Sana kwenye Hilo Penzi.
Kwa kua Baraza limeamua kwani yeye ni Nani kukataa. Haikuchukua muda
alimkubali Yasir na Yasir hakua na lengo
la kumchezea moja kwa moja alienda
zake kumchumbia nyumbani kwao.
Familia ya Badru ilimpokea kwani tayari
walikua nk wanafamilia baada ya
kuwaunganisha muksin na Najma
hatimae Sasa Muzda nae anaenda kua wa Sabodo familia.
" Jamani da Muzda umeniibia mchumba wangu" hiyo siku Afsat alilalamika bila
kusubiri kwani alikua na hisia za mihemko juu ya Yasir.
" Ohoo itaendelea nae hata hivyo ni ruksa" Yasir alitabasamu baada ya kumuona huyo binti mdogo aliekua
akimzimia.
Kumbukumbu iishie Hali tuendelee na mkasa.
" Sitaki uniache" Yasir alilalamika Muzda akahisi haya.
" Nawezaje kubaki? Familia nzima
inaenda Yasir " Muzda alimwambia Yasir
bila kujari lakini moyoni alihisi kua
mpweke.
" Huwezi kubaki na Mimi hata kwa wiki moja ili twende wote wiki ijayo" Muzda
alipata khofu kidogo. Ni kweli kwamba
mwanaume huyu alikua akijua
kumdekeza na kumpatia kila ambacho
likipenda na hakuwahi kumtaka
wafanye.ngono Ila hii kubaki ya ghafla
mbona itamtiahia amani.
" Nakuomba, nimezoea kuiona sura yako
kila kukicha hivyo sitaki ukae mbali na
Mimi" Yasir alimwambia huku aliushika
mkono wake.
" Yasir, naanzaje Sasa kubaki. Na wewe wakati sisi hapa bado hatu_"
" Shh.. usiwe muoga unapoongea na
Mimi, Mimi na wewe tupo sawa kabisa"
Yasir hakua anapendezwa na Hali ya
Muzda kumchukulia mkubwa sana Kama
alivyo Kaka Yake
" Samahani" Muzda alimuomba samahani.
" Ki ukweli sitaki" Yasir alijidekeza
Muzda kapata aibu zaidi. Alifaa
kumbembeleza eti.
" Mi ki ukweli sio Kama nakua
nakuchukulia Kama mkubwa isipokua
napata aibu kuongea baadhi ya vitu
mbele yako wewe, ni tatizo niliwahi
kukuheshimu kupita kiasi" Muzda
aliongea kwa hasira na yasiri
akatabasamu.
" Usijari upo huru kuongea kila kitu
mbele yangu, maneno Kama , sipo
tayari ku sexz natamani romance
naomba uni hug, Ni maneno ya kawaida
kwa wapenzi. Hata ukiwa na khofu
labda mi sio rijari unaweza sema babe
twende nikutest nione Kama jogoo
anawika" Muzda hakuweza kuvumilia
kuziba uso wake kwa mikono huyu Yasir
haoni aibu kuongea maneno hayo mbele
Yake.
" Unanitia aibu" Muzda alilalamika
" Aibu ya nini? Mimi ni mume wako
mtarajiwa au Kuna mtu mwingine ambae
utaongea nae maneno hayo hapo
baadae."
" Yasir bhana mi sitaki" Muzda
alijiinamia kwenye meza na Yasir
akazunguka upande wake. Akakaa Kari u yake. Muzda alihisi Kama atapoteza
joto mwilini mwake.
" Yasir Mimi kwa kweli! Napata tabu
kukaa na wewe naomba unikalie mbali"
Muzda alitania Yasir akataka kumkalia
mapajani. Muzda alipiga kelele.
." Yasiri unafanya nini?" Muzda alihisi
kumla nyama mbismchi.
" Mimi hapa!! Aah' umesema nikukalie mbali"
" Ndo mapajani"
" Basi we nikalie Mimi" Yasir alimvuta
Najma na kumetisha kwenye mapaja
Yake. Kisha Muzda akiwa haelewi Yasir.
Aliweza kumpa romance tanmmu. Hapo
Muzda ubishi wote kwishaaaa.
" Yasir" Muzda aliita kwa sauti ya kudeka akiwa kamlegezea macho Yasir.
" Nakupenda Sana binti Badru, ki
ukweli sitaki ukae mbali na Mimi hata
kwa dakika mbili" Muzda alihisi Kama
amepewa dunia nzima yeye na yasiri
pekee Yao.
" Sina jinsi Yasir"
" Sema Sina jinsi honey" Muzda alipata aibu yasiri akamng'ata midomo Yake kidogo.
" Honey" alijikuta akivuta bila kutaka.
" Sasa je?" Yasir alitabasamu na hapo Muzda joto lake likapa da na mashavu yakawa mekundu Sana kwa hisia. Bila
Shaka alipoteza muda wake bure kwa Yule mshenzi Hamimu hata hakua
romantic Kama Yasir alikua tu muongeaji Sana.
" Njkurejeshe Sasa nyumbani, mmiliki wa moyo wangu" Muzda alitabasamu.
" Asante " alimwambia yasiri
akaonekana kununa. Muzda alimsogelea na kumbusu lakini ai u aliokua nayo
alitamani hata ajifiche sehemu Ila
haiwezekani
neno Hilo na kumbeba juu, miguu Yake
haikua na shida ila alilazimika kumbeba.
Katika jengo moja dogo lipatikanalo
katika kisiwa Cha ukerewe jijini
mwanza. Ni apartment ndogo lakini Ni ya kifahari Sana. Saida alionekana
kulala katika chumba kimoja akiwa
ametulia. Ni majira ya usiku Sana mida ya saa nane.
Bwana amiri alikaa pembeni akivuta
sigara huku akimwangalia mwanamke
huyo ambae alichukua muda mrefu'
akiwa amelala. Kwa nini alichukua muda
mrefu' kuamka alimpa tu dawa za
usingizi na sio za kuzimia.
Nje ya chumba Ni Kama Kuna mtu
alikua akigonga mlango na sauti ilisikika
" Always love you" Yasir alimtamkia
kwa mbali. Hakuweza kukaa ndani
Tena. Aliweza kutoka ndani ya chumba
hicho Kisha akaufungua mlango vyema zaidi. Aliteremka kutoka ngazi Hadi
ngazi kwa uangalifu. Na hatimae aliweza kuufikia mlango wa kuingilia
ndani ya nyumba hiyo.
Azraj aliingia ndani akiwa kaongozana na vijana wake kadhaa walikua wawili
tu. Alionekana kukasirikia Hadi mwisho.
" Upuuzi, siamini hiki" alikua na hasira
kiasi kwamba alitamani kujiua.
" Unataka kujiua, usitumie mwili wako kwa maumivu makali, fanya utumie bastora. " Bwana amiri aliweza
kukamata bastora na kumpatia.
" Fanya haraka Sana" Azraj
alimwangalia mjomba wake akapandwa
na hasira mwisho akamkaba shingo Yake bila kusubiri.
" Unajua hasara na Hali niliyopitia leo., Hivi unaweza niambia kila kitu
kiliaharabika vipi?" Azraj alibana meno yake akiongea alitamani kumuua yeyote atakae muudhi.
" Mi ntajuaje? Kikubwa bado tunayo ngao unaweza kujituliza Azraj Badru"
Azraj alibaki kamshangaa anamaana
gani huyu mwanaume mtu mzima .
" Subiri kwanza" Azraj alimzuia mjomba
wake asitamke neno kwanza akatoka nje na kwenda Hadi nje. Alifungua mlango wa pili wa gari na kumuangalia mtu
aliekua amelala kwenye siti ya gari.
Alikumbuka maneno ya mwisho ya nevi
kwani aliamini kabisa mwanaume Yule
kwa Sasa atakua maekufa bila Shaka.
" Bwana mkubwa, lazima ushjnde bwana
mkubwa, kumbuka unae mtoto hivi
Sasa" maneno Yale yalijirudia Sana katika ngome za masikio yake'. Nevi
alikua akijaribu kumpa morali ya kuipambania kiti alichokua aliamini Ni
Cha kwake teangu mwanzo sema.
Alidhurumiwa ama ipoje?
Alimuangalia mwanamke aliekua amelala
kwenye siti ya gari na kutamani kulia, hakuwahi kupendwa na binadamu yeyote
Yule katika huu ulimwengu Kama
alivyopendwa na mwanamke huyu. Salma
bila Shaka alimpenda Sana. Na hata
alimzalia binti.
" Samahani Sana" kwa Mara ya kwanza
Azraj alipata huruma juu Yake na
kujiona mkosefu, alimkosea Sana na
hata alitaka kumuua mtoto wake
mwenyewe. Kitu pekee alichofanya
akakumbuka kabla ya kutoroka na
kuondoka kabisa katika jiji la Dar
aliweza kwenda hospitalini ambapo
alitambua kabisa atamkuta Salma.
Alijua fika hawezi kuruhusiwa kuingia
kwanj chumba kile kilikua chumba
maalum na Cha watu mashuhuri.
Ingekua kabla Mambo hayajamuendea
vibaya bila Shaka angeingia kwa
kujiandaa na kujiamini Sana huku
akitamba Kama Azraj Badru.
Ah! Potelea mbali, hata hivyo familia ya Badru haikuwahi kumthamini. Hajutii
kuachana nayo. Aliweza tu kupata
mavazi na vyeti kadhaa ambavyo Ni
muhimu Kama daktari kuingia navyo
kwa.mzazi aliefanyiwa upasuaji. Aliweza
kuingia ndani yaile wodi akiwa na lengo
la kumchukua Salma na binti Yake.
Walibaki watu wawili muhimu zaidi
katika Maisha Yake. Na penyewe Ni baada ya maneo kutoka kwa nevi.
Hatimae alifanikiwa kuondoka nae pale na Sasa amefanikiwa kwenda nae
mafichoni. Alimbeba taratibu na kutembea nae kuelekea ndani ya
nyumba hiyo. Alipofika mlangoni
alipokelewa na mjomba wake aliebaki
kumshangaa
"Wewe ?? Huyo mwanamke ulimkataa
Mara kadhaa" bwana amiri alimwambia
Azraj aliemwangalia kwa jicho la hasira.
" Wewe mbona hukuachana na aunt
Azati hata Kama hukua ukimpenda??
Azraj hakutaka kufatiliwa Sana.
" Hujui Ni jinsi gani mwanamke huyu
nimekosea Bora ungeniacha tu" Azraj
alihisi hatia kidogo.
" Sawa nipe sikionlako kwanza" mjomba
wake alimwambia na hapo Azraj akahisi
kuushika kwani hawezi kuongea tu. Kwa
kweli siku hiyo hakua anataka shida na mtu.
" Azraj unafaa kumpeleka mwanke huyo
chumbani kwanza Kisha uingie chumba
Cha wageni ukamuone mgeni wako"
Azraj hakuweza kumuelewa. Ila
taratibu alimuinua Salma na kuingia
kwenye chumba chake ambapo aliweza
kumlaza kwa utulivu. Alihakikisha
hajamtonyesha kidonda chake. Kisha
akatembea kuelekea chumba Cha jirani.
Aliufungua mngo ambao uliofungwa
vyema Sana. Baada ya kuufungua
hatimae alizama ndani ya chumba
hicho. Azraj alitupa macho kitandani
kwa kua kitanda ndo picha kubwa ya chumba. Hakuamini alichokiona. Ki
ukweli ni habari ambayo ilimfurahusha
sanama baaada ya kuburuzika kwa muda
refu.
Sehemu ya 160
Alikua Saida jamani dahh.. hawezi
kujizuia kuamini Hilo. Hivi Ni kweli
alikua Saida. Ilibidi asogee mpaka pale
kitandani alisogea zaidi na kumuona
mwanamke Yule ambae kwa Mara ya
kwanza alipomuona tu aliufanya moyo
wake kuruka ruka kwa hisia Kali.
Aliufanya moyo wake utambue maana
halisi ya kumpenda mtu.
Hakika hakuna kitu kikubwa kizuri na Cha muhimu na Cha thamani, alichowahi
kufanyiwa na mjomba wake Kama
alivyofanyiwa leo. Ni habari nzuri
iliyoje? Kumletea Saida hapa? Hakika
inafurahisha, hakika ilikua dua kubwa ya kijana wake Nevi kabla ya kifo
chake alimpa maneno ya kumtia moyo
kua asikate tamaa asichoke kupambana, na kweli amejitahidi Sana kupambana.
Japo ataonekana looser lakini bado
hajawa looser kwani anayo karata ya ushindi. Hata ikitokea Mustafa
amempata bado hawezi kumuondoa
Saida upande wake. Azraj alimsogelea
Saida iekua kalala kitandani kwa utulivu
mwingi Sana bila kuamka. Aliweza
kufurahia kuziona lips za mwanamke
huyu kwa muda mrefu lakini hakuwahi
kuzinyonya hata siku moja. Kwa nini
asijaribu leo tu. Angalau itamtuliza
machungu na majonzi aliyopitia. Hata
hivyo amewatoa kafara vijana wake
wawili na wa muhimu amabao Ni Bwasha
pamoja na Nevi Lisa Saida kwa nini
asijifahidie tu hata kwa busu.
Alinisogeza uso wake kwa Saida. Na
kujaribu kuitafuta lips ya Saida angalau
kidogo. Kisha akagusanisha midomo
Yake na midomo ya Saida. Saida akiwa
amelala alihisi Kama midomo Yake
ilisongwa na msukumo kutoka upande
mwingine. Hakika alikua mwanaume
ambae uso wake ulikua sawa na uso wa
kipenzi chake Mustafa. Lakini bado
hakua na harufu Wala Radha tamu
Kama ya Mustafa. Alimsukuma mtu
huyo bila kufumbua macho Yake. Azraj
akashtuka. Na kusogea mbali kidogo.
." Uuu wewe? Wewe ni Nani?" Saida
alikua akiweweseka alikumbuka tukio
lililomtokea muda mfupi uliopita. Akiwa
katika like chumba Cha Giza alisikia
kelele watu wakipiga mayowe na kujaribu kuzima moto.
" Msaadaaa" alianza kupiga kelele akiwa
haamini Kama atapona. Moshi ulitawala
ndani ya chumba kile mikono Yake
ilivmfungwa. Miguu Yake ilikua wazi lakini bado isingemsaidia.
" Nakufa huku" singboard zilianza
kuyeyuka na kudondoka kidogo kidogo, kitu pekee alichoweza Saida Ni kupiga
kelele huku akijaribu kukwepa. Mtoto
wa kike alihisi Kama atakufa kila
alipokua akiwakumbuka watoto wake
wawili wasio na hatia na Mustafa alieoa
mwanamke ambae ni Dr khairat mwenye
roho mbaya. Bila Shaka Maisha Yake
Ni Kama ya kuzimu jamani. " Kwani
nilikukosea nini Mungu wangu Mimi? Kwa
ninj naishi Maisha haya ya Allah "
Saida alilia.
Ndio ghafla chumba kilipokua
kimetapakaa Moshi na yeye akiwa
amejikunyata sehemu, bahati nzuri
mlango ulisukumwa kwa utulivu baada ya
kufunguliwa aliingia mwanaume wa
makamo ambae kwa kweli hakuweza
kumuona vyema kwani yeye alikua
ameshauguta Moshi vya kutosha.
" Tafadhari Kaka mtekaji naomba
unitoe humu ndani, siogopi kufa lakini
nawaoneeni huruma iwapo mume wangu
atagundua mmeniua" Saida aliongea
kana kwamba hakuogopa kufa.
" Lakini mmeachq, ulimpa talaka wewe"
mwanaume huyo alikua na sauti isiyoeleweka.
" Sidhani Kama ni hivyo Kaka mtekajiz
nahisi Kama Yule mchawi dr khairat
amekutuma. lakini ukweli Ni kwamba
Mimi na mume wangu hatukuwahi
kuachana, na sikuwahi kumpa talaka
mume wangu" wakati wote huo Saida
alikua akiongea kwa taabu hivyo
hakuweza kustahimili na alipoteza
fahamu zake. Alihisi Kama Kuna mtu
alimnyanyua kwenye bega lake. Na
baadae alikua kwenye gari. Na mwisho
alijihisi Kama vile wapo angani
wanapata. Na hatimae hajui nini
kulifata. Saida alifungua macho Yake
haraka Sana.
" Mustafa" alihisi kabisa mtu
aliemuokoa alikua Mustafa. Ndipo
alipotupa macho Yake aliona umbile la
mwanaume aliekua na mwili sawa na
Mustafa wake lakini hakuonekana Kama
Mustafa japo alimgeuzia mgongo.
" Wewe sio Mustafa, lakini natumai
wewe ndo umeniokoa Mimi" Saida
aliongea na kuamua kupoteza tukio la kupigwa busu"
Azraj aliona Sasa huu ndo wakati wake
sahihi, anafaa kumfanya Saida aamini
kua amemuokoa! Alitaka kugeuka Ila
hapana? Subiri iwapo atasema
amemuokoa Saida atalazimisha
kuondoka na kurejea nyumbani. Na
hataweza kumuamini Tena ! Kwani
lazima Dr khairat aje hapa.
Kumhudumia Salma na yeye bado
hajampata binti Yake. Itabidi atumie tu uhalisia hawezi kujificha daima Ila
hatamwambia moja kwa moja.
" Ni wewe sio" saida alihoji akijaribu
kuangalia mazingira ya hapo ndani.
Aliamini yupo sehemu salama.
Alipowangalia mwanaume huyo kwa
Makini kabla hajageuka bila Shaka
alihisi kumfahamu kwa ukaribu Sana.
" U wewe nii!!! Azraj !!! Saida alibaki
kwenye mshangao, uso wake ulipauka
bila kutarajia. Na hapo Azraj aliweza
kugeuka na kujidhihirisha uso wake
mbele ya Saida.
" Ndio ni Mimi bila Shaka" Saida
alipigwa na bumbuwazi. Alikua Azraj ?
Azraj Badru.
" Hapa Ni wapi? Mbona tupo eneo
tofauti na nyumbani?" Saida hakuweza hata kumpa shukrani alienda moja kwa moja kwenye maswali.
" Kwa sababu nyumbani sik Salam Tena, Kuna maafa yakijiyokeza tangu
kutoweka kwako, zarina alikufa dereva wako alikufa, bila Shaka Kuna mtu
mkubwa ambae familia ya Badru
ilimchokoza vibaya Sana" Saida alihisi kushtuka.
" Vipi kuhusu?" Moyo wake ulizama
kwenye Moto baada ya kuwakumbuka
watoto wake wawili. " Watoto wangu
Azraj ? Wanangu pamoja na Mustafa"
Azraj alihisi kumpiga haina shida
kuwauliza watoto lakini huyo Mustafa ana maana gani kwake?.
" Saida pumzika, kwani watoto wako wapo salama bila Shaka" Saida
alimshusha pumI na Azraj hakua tayari
kuongea nae. Aliondoka ndani ya
chumba na kuelekea nje ambakk kwa
Saida Ni sawa na kusikojulikana.
Kesho yake Dr khairat alifikishwa
katika nyumba hiyo kuja kumuhudumia
Salma aliekua mahututi. Alipigwa
marufuku kusogea kwenye chumba
alichokua Saida. Kwani alifungiwa ndani
kabisa na kuzuiliwa kutoka nje. Aliweza
kumpa huduma kadhaa Azraj pia ambae
alikua na majeraha kutokana na kipigo
kutoka kwa Mustafa
" Bila Shaka bado haujalingana nae
katika kupigana" Dr khairat alikua bado
alivutiwa na Mustafa.
" Sio.kama simuwezi, isipokua nilihofia
usalama wangu zaidi" dr khairat alihisi
kumcheka kwani alionekana kushindwa kabisa.
" Mwanao hajambo?" Dr khairat alishangaa haikuwahi tokea Azraj
akamuuliza Adil.
" Upo sawa kweli?" Alimuuliza bila kusubiri.
" Ndio nipo sawa, inashangaza kuona namuulizia mtoto?" Azraj alikunja
midomo Yake na kumwambia. " Nimehisi
Kama natamani kua baba pia, Ni Raha
Sana kua mzazi?" Alimuuliza Dr khairat
aliebaki Hana neno juu yake.
" Ukiwa mzazi, jiandae kufanya kila
kitu, na kubeba jukumu la kumpatia kila
anachostahili mtoto wako" Dr khairat alimkumbusha. " Mimi nimeshindwa
kumpa kila ambacho alistahili kupata
mtoto wangu, lakini ntahakikisha
nawalipa wale wote walioingilia furaha
Yake." Azraj alitabasamu hakika huyu
mwanamke Ni wa kushikamana nae
mwanzo mwisho.
" Kwa hiyo umeamua kumuoa Salma
Sasa, hatimae umeutambha moyo wako?" Dr khairat alimuuliza Azraj
huku alimvisha Shati Yake na kumfungia
vishikizo.
" Naanzaje kufanya hivyo, unafahamu
kabisa simuhitaji, bila Shaka nitamuoa
Yule Yule niliempigania siku zote" Dr khairat alitabasamu inamaana mpaka
hivi Sasa hakuweza kumkatia tamaa
Saida.
" Siwezi kata tamaa Kama mwanamke"
Dr khairat alihisi kupigwa na baridi
Azraj alikua akimsemeamo na yeye.
Alimsukuma akimtomasa mbavu zake.
Azraj alikua kua Dr khairat amepata
chuki ya chombezo ghafla. Alimuona
mwanamke huyu wa ajabu waliweza
kumudu kukaa siku nyingi hivyo bila
kunaniliu. Alimvuta karibu Yake nmdr
khairat akaangukia kwenye mbavu zake.
Dr khairat alikua na muda mrefu' Sana hivyo alikua na hamu. Hata alitamani
Azraj afanye tu anavyotaka hata Kama
hawapendani.
Azraj hakua na uhakika iwapo Dr
khairat atamkubalia, lakini alipoanza
kumbusu Dr khairat aliweza kutulia.
Hiyo ulimaanisha kabisa yupo tayari.
Kwa nini na yeye asiendeleze hamu na hamasa.
Hatimae ni wiki mbili kupita baada ya
hekaheka na sakata kubwa kuikumba familia ya Badru. Ni ndani ya jiji la Johannesburg, South Africa.
Ni katika ghorofa kubwa Sana na refu kwenda juu. Ndani ya chumba Cha
mkutano watu wa asili ya kiarabu kwa
asilimia kubwa walipatikana katika meza
ndefu ambayo hutumika kwa ajiri ya vikao mahofisini.
Watu wanaofahamika Kama wanafamilia ya Badru walionekana hapo. Alipatikana
Bwana Rashid Badru, Yusuph Badru.
Mustafa Badru , Muksin Badru pamoja
na mwanaume ambae yeye sio wa
familia ya Badru Ila ameoa kutoka
katika familia ya Badru alikua bwana
Amiri. Watu wengine walikua Ni mababu wa familia ya Badru kutoka katichi nyingine au chi mbalimbali. Familia ya Badru tunayoitambua sisi Ni familia
inayo tawala ndani ya nchi za afrika
mashariki. Lakini bila Shaka Badru Ni
familia kubwa iliyotambaa duniani kote na wanaishi katika nchi zote. Wakiwa na utajiri tofauti tofauti.
Siku hiyo ilikua siku maalum ambayo, warithi wa familia, wangekabidhiwa mirathi na majukumu ya kuziongoza
familia zao za Badru. Na watu wote
walitegemea na kusubiria kuuona ushindi wa watoto wa wakubwa zao. Kama ilivyo
kwa upande wa Badru inayopatika
Africa mashariki Ni Mustafa ndo
anaetarajiwa bila Shaka.
Azraj alionekana mtu ambae alijiamini
kupita kiasi na aliamini kwamba siku
hiyo itakua siku yake maalum ya kuanza kutawala. Huku Mustafa akionekana
kunywea Sana na kupotea katika maono ya muelekeo wake. Kwa kweli Azraj
alikua amemshika pabaya.
Alikumbuka kua walipigiana simu na kuwekeana makubaliank kadhaa.
Alifanikiwa kupewa na kuvikwa taji la urithi wa familia ya Badru hiyo ni sawa na kua mtawala wa familia ya Badru
katika nchi za Africa mashariki.
Anakua kinara na mwenye kauli ya mwisho. Hivyo anafaa atamke
hadharani kua anakabidhi kila kitu kwa
Azraj Badru na yeye hatakua mrithi
Wala mmiliki Tena.
Hapo ataweza kupatiwa mke wake bila
Shaka. ' hivi nifanye hivyo kweli?,
Nikubali kupoteza madaraka yangu yote na kumkabidhi Azraj Lisa nimrejeshe
Saida upande wangu. Na iwapo
sitafanya hivyo bila Shaka ataninyakua mke wangu na kumfanya anavyo taka.
Tatizo sifahamu Ni wapi amemuweka mke wangu, kwani Hana kifaa chochote
Cha mawasiliano akiwa huko. Wala Hana
hata gari tutambue Ni wapi anatokea ?
Mustafa alihisi kupoteza muelekeo.
Kweli bhana kikao kiliendelea kulingana na mgawanyo na mlingano wa Mali za
Badru zinazotambulika. Warithi wengine
wote walipata kulingana na vile ambavyo
wao walitarajia. Na waliliridhika. Shida
ikaja Sasa kwa hawa.waarabh wa bongo
wananitumia kiswahili Kama lugha ya
taifa. Mustafa alipewa mirathi Kama
ivyotarajiwa pia.
Na hapo akainuka Kama ilivyo desturi
ayoe neno na kisha atamke Ni agizo
gani ambalo halikua sawa katika utawala
wa baba yake' na hivi Sasa yeye Kama
Badru mkubwa anatakiwa kurekebisha.
Mustafa alisimama kwa kujiamini na
kujiuma kwa wakati mmoja. Alikua
alijilazimisha ujasiri ambao ulimpungia
mkono mbali. Alijikaza Kama Mustafa
Badru Kama baba wa watoto wawili.
Kama mrithi wa Badru hivi Sasa
ameshika nafasi hiyo tayari na Kama mine was Saida. Anaemtaka mwanamke wake.
" Mimi Mustafa Badru, napokea kwa
dhati agizo na desturi iloyowekwa tangu
enzi za mababu zetu. Na sisi
tuakaendeleza. Nakubakiana kwa dhati na mirathi hii na ninatoa ahadi kua
nitasimama wima na vyema zaidi familia
pamoja na kampuni na biashara zote zinazohusiana na Badru. " Azraj
alimtazama kwanza akiwa hamuelewi
huyu jamaa mbona kama anaenda
kinyume na mipango.
Watu wakimpigia makofi ya kutosha
Mustafa na kuzidi kumsikiliza.
" Najua ni kazi ngumu Sana kusimama
nikiwa mwenyewe kileleni, mpaka kufikia
hapa ki ukweli nimepambana Sana na
nimepitia vikwazo vingi Sana. Lakini
sikua pekee yangu, nilikua na mdogo
wangu ambae alisimama kando yangu
siku zote Kama mtetezi wangu, naa ni mrithi wa pili ambae ataishikilia nafasi
yangu iwapo nikiwa katika Hali
mahututi, au ukikosekana uwepo wangu,
napenda kumtaja na kumuweka wazi
mbele yenu bila pingamizi nae Ni .
Bwana Azraj Badru ...."
Watu wote walimtolea macho Mustafa
ambae alionekana Kama alikua
akimaanisha kumchafua Azraj badala ya muksin. Hiyo ilimaanisha nini?
Sehemu ya 161
Azraj alitabasamu baada ya kuona
Mustafa kamtaja yeye, alikua na
uhakika' wa kusimama Kama kinara.
Nafasi hiyo ilikua kubwa Sana na
muhimu pia, kua nafasi hiyo ilimaanisha
anaweza kua namba moja badala ya
mbili wakati wowote kwani akiamua
kumuondoa Mustafa ili yeye awe mrithi mi kitendo cha dakika mbili tu.
Muksin alikua Kama anakabwa na shingo
huyo Kaka Mustafa alikua na matatizo gani? Alipoteza akili ama amesikia
vibaya. Na uchague wote was Azraj
Bado kamchagua Azraj. Sio shida iwapo
Angekua Azraj wa zamani lakini huyu
wa Sasa aliesababisha madhira
makubwa Sana kwa familia ya Badru.
Bwana Rashid Badru na bwana Yusuph
pia walihisi nikitu kipya kwenye ngome
za masikio Yao. Mustafa alikua
akimtaka Azraj Kama mrithi wa pili wa Badru, au hapana.... Bila Shaka alikua
Bado hajamaliza kuongea.
" Ndio kaka mkubwa" Azraj alijiweka
katika nafasi Yake vyema na kujikubali
Kama Kaka wa pili akainuka akionyesha
unyenyekevu wa Hali ya juu' kwa wazee
wote wa Badru baadhi ya wazee wa Badru walimfahamu vyema Azraj kwa
kweli hakuridhika nae, Tena isitoshe
alikua kijana wa nje ya ndoa ndo
kabisaa. Walimchukulia Kama kijana
aliepatikana kwa njia chafu.
" Aah unaweza kukaa kwanza" Mustafa
alikua Bado ameziweka sura za watu
fulani matatani, hakuna aliekua kwenye
fahamu zake.
" Usijari Kaka mkubwa, Azraj kwako Ni mtiifu daima" Mustafa alihisi kutapika
anajiita mtiifu daima wakati amemnolea panga shingoni. Azraj alikaa.
" Ni Kama vile nimetamka neno baya
wazee wangu wa Badru mbona macho
yenu yamenielekea?" Mustafa
alikumbuka kuwauliza.
" Kikubwa nacho hitaji na kutarajia
tupo kwenu bila Shaka sio macho tu, nahitaji masikio pamoja na moyo wa kila
mmoja wenu hapa" Mustafa aliongea na kuwarurisha watu kwenye kikao
ambacho kilikua kimeingia mchanga
muda si mrefu'. Azraj alihisi kusikitika, bila Shaka hii ndo familia Yake kubwa
ya Badru. Familia ambayo bila Shaka
angejivunia kupita maelezo kila wakati
kua yeye ni Badru hapo mwanzo. Hata
hakuna mmoja wao ambae aliwahi
kumkubali.
" Nahitaji kuendelea" watu wote
waliacha minong'ono na kuweka masikio
Yao sawa. Mustafa aliweza kuendelea.
" Ningependa kufanya maamuzi ya
kumchagua mtu ambae anafaa na
kustahili kua mkono wangu wa pili katika
biashara na kampuni zote za Badru,
lakini mtu mmoja hapa hastahili hata
kuwepo katika nafasi yoyote. Na
thamini Sana hadhi na heshima ya
wazee wa Badru," watu walimshangaa na kurejea kwenye ufahamu wao baada ya kunong'ona maneno kadhaa
" Azraj Badru.. kiukweli sidhani Kama
unafaa Wala kustahili kuwepo ndani ya
kikao hiki" Mustafa alifinya nyusi zake na kupandisha macho Yake juu. Kila
aliehudhuria hapo alitoa macho ya
mshangao. Huyu Azraj ndo mtu pekee
alietajwa hapo awali na kuweka
tahadhari kwenye vifua vya watu lakini
Sasa hivi tu. Anaweza kutajwa Kama
mtu asie faa.
Bwana Rashid alishusha pumzi zake na watu wengine. Azraj alihisi kana
kwamba alimwagiwa mchanga kwenye
mwili wake. Yaani magunia matatu
mfululizo yaliyojaa mchanga yalimwagika
juu Yake. Hapana kwa kweli huyu
Mustafa amejisahau. Aliinuka kwa
Jazba huku akimtolea mustafa macho ya hasira.
" Mustafa Badru unawezaje kuniita mtu
asie faa mbele ya wazee wa familia, bila Shaka Mimi ni mtu muungwana zaidi
yako" Bwana Rashid Badru hakuwepo
wakati Azraj akizua varangati
nyumbani. Lakini tayari alifahamu kila
kitu. Alihisi hasira kana
kwamba
hakutaka kuvumilia pale mbele ya wakuu
wa familia na kutamani kumpiga vitungu vya kichwa huyo mwana haramu.
" Azraj Badru you amri yangu na utoke nje ya kikao hiki" Mustafa alimuamuru
Azraj ambae hakua tayari kutoka hapo.
Alitamani kutoa hata bastora Yake
amtumie yeyote hapo Kama ngao
kumlazimisha Mustafa amtangaze Kama
mrithi namba mbili lakini haikua rahisi
kwake. Kwani hapo walikua watu wengi
na wote Wana nguvu na siraha za
makali zaidi Yake.
Alimwangalia bwana Amiri ambae alimpa
ishara kua ikiwezekana amteke yeye
lakini Azraj hakuweza kufanya hivyo.
Alielewa matokeo zaidi, hata hivyo
hawezi kuwasamehe watu Hawa
waliomfanya yeye kua wa kando zaidi.
Wanastahili kulipwa hakuna hata mmoja
aliewahi kumchukulia waaana. Walikua
matajiri kiasi kwamba walikua kileleni
Africa mashariki lakini hakujua Hilo, inamaana yeye alikua mdudu asiestahili
kabisa hapo.
Aliweza kutoka nje akiweka sura kavu
ya maumivu ambayo hakuweza
kuyaeleza, alimwangalia Bwana Rashid
Badru aliekua baba yake Ila hakuweza
kumtupia hata jicho. Kwa kweli hakua
na thamani kwa yeyote, hata yeye pia
hafai kumthamini yeyote. Moyo wa
Azraj ulitangaza Vita mpya kabisa'. Sio
kosa lake bila Shaka Ni kosa la bwana
Rashid Badru kumzaa yeye akiwa nje ya
ndoa. Kwa nini anyanyapaliwe na
kutengwa! Ni kosa la yeye kuzaliwa nje
ya ndoa? Ni kosa lake kuzaliwa katika
familia yenye miiko? Sio kosa lake bila
Shaka. Lakini kwa nini hawakumuona wa
maana tangu hapo awali? Wao ndo
wamefanya awe mbaya japo alikua na
Nia mbaya tangu mwanzo.
" Unachelewesha mkutano huu!!!
Mustafa alimtolea macho makavu Azraj
ambae hakuweza kuwapinga watu hao na
kutoka zake nje akiwa anapata maumivu ya moyo na kuuburuta uso wake kua
wenye kisasi pia.
" Bwana Rashid Badru, nitaanza na wewe!" Azraj alitoa kauli hiyo ambayo haikusikiwa na yeyote zaidi Yake.
Mustafa aliweza kuendelea na
mazungumzo Yake mbele ya wakuu, na
mwisho aliweza kumchafua muksin Kama
msaidizi wake. Kwa kweli muksin alikua
kijana mwerevu na mvhapakazi kupita
maelezo, alikua kijana aliejituma wakati
wote na kuhakikisha Badru inaenda
kwenye njia inayostahili. Muksin
alisimama kwa tabasamu na
kujitambulisha kwa shangwe na kuomba
akaribishwe katika uwanja wa watu
wazima kutoka ukok wa Badru.
Hatimae kikao kilihitimishwa na watu
wakajigawa, watu wote walimaliza
shughuri iliyowakutanisha hapo na kusambaa majumbani kwao. Bwana
Rashid aliwakaribisha baadhi Yao ambao
hawakua na shughuri kubwa kuhudhuria
mlo wa jioni pia alikua na lengo la
kuwaalika kwenye harusi ya binti Yake
inayokimbia hivi karibuni. Muzdarifa
Badru.
" Hakika Rashid umezeeka Sasa,
inasemekana kua mwanaume akiozesha
mabinti zake ujue uzee umemuendea
kwa Kasi, kwani binti ataenda kuleta wa
jukuu haraka zaidi ya kijana" ndugu
take mmoja alimtania bwana Rashid
akaachia cheko la ki boss.
" Ni bure ikiwa nitakufa bila kuifanya
harusi ya binti yangu mwenyewe, sitaki
kumpa.majukumu mengi mdogo wangu, au unasemaje Yusuph?" Bwana Rashid
alitania.
Bwana Yusuph alitabasamu mwanaume
huyu alikua mkubwa lakini alikua bado
Ni mtu mwenye tabasamu changa
aliemuacha mdomo wazi kila mmoja wa Koo za Badru.
" Yusuph anatamba na meno Yake
mazuri yaliyojaa ucheshi, hakika
alierithi sura nzuri ya mama, nahitaji
kumuona Bi saifu Badru" mwanaume
huyu wa makamu ya bwana Rashid
aliongea akiwa na maana ya
kumkumbuka Bibi Mustafa
Bwana Rashid alitikisa kichwa akiashiria
yupo sahihi anafaa kabisa kwenda
kuonana na Bibi Mustafa, kwani
watamfanya asahau makui waliyokutana
nayo. Safari ilianza baada ya watu
wote kuingia kwenye gari zao.
Ni katika jumba moja la kifahari zaidi
ndani ya jiji kubwa la Johannesburg
nchini Africa kusini. Ndani ya mtaa wa
kitajiri watu walikua wanaendelea na
shughuri zao ndani humo.
Alionekana Asia akipata tabu kupika
chakula ambacho kilimnyima Raha, alihisi kichefu chefu kila dakika na
kujificha ili atapike.
" Da Asia, kwa nini mama yangu harudi, anakuja lini nimemiss kula chakula
chake" Shayma alikua akilalamika Asia akahisi kulia bila Shaka Hana la kujibu.
" Mama tarudi leo au baadae usichoke kusubiri sawa kipenzi" Asia aliyashika
mashavu Yake na kumbembeleza
Shayma ambae kwa hakika akili Yake hukuweza kuamini Hilo.
" Baba pia anatuweka mbali nae, yupo karibu na sisi lakini yupo mbali Sana na sisi dada, au na yeye anamkumbuka mama?"
Asia alihisi uchungu kila akimuona
Mustafa anahangaika, bila Shaka na
Gharib ana hangaika akiwa pembeni ya
Mustafa, wote wanatamani kumpata
Saida lakini Ni vipi? Hata yeye
anatamani Saida apatikane kwani
angempa ushauri na suluhisho juu ya kilichomkuta hivi Sasa lakini atafanya
nini? Saida hayupo, zarina amekufa, Maisha yamemuo gezea majukumu. Na
khofu bado imetawala kichwani kwa nini
Maisha yapo hivi kwa familia ya Badru, bila Shaka Hawa Ni wanafamilia wema na wazuri.
" Da Asia, Nina hisi njaa Sana" Kim
alikuja akiwa na sira ya kusikitisha
Sana, watoto Hawa hapo awali hawakua
wakila chakula Cha mtu yeyote mwingine
isipokua mama Yao Saida. lakini mwisho wa siku leo hii wanalazimika kula
chakula alichopika Asia tu. Au Najma
kwani Najma alikua na upishi sawa na
mama Yao. Lakini kwa Sasa yupo bize
na Mambo Fulani Fulani ambayo haupo sawa.
" Nawaandalia chakula Sasa hivi" alijibu na kuwaangalia chakula haraka Sana.
Ndani ya jengo Hilo Hilo, Mustafa
alionekana akiwa kasima dirishani ndani ya chumba chake, chumba ambacho
aliwahi kutumia akiwa na Saida hapo
awali Saida alipokua amejifungua.
Kilichobadirika Ni mandhari tu lakini
chumba Ni kilele yaani kitanda na vitu
vinavyopatikana ndani Yake vyote Ni
vipya na vigeni Ila kuhusu kumbukumbu
za Saida bado Ni zile zile, aliishi nae
hapo wakiwa na watoto wao wawili na
wazuri. Walikua na furaha Sana kipindi
hicho, na wakati huo ndo waliweza
kumpata HudHud.
Hatimae akimkumbuka HudHud , ndege
mzuri wa Shayma ambae kwa Sasa
imeshabaki kua kumbuku tu, kua
waliwahi kuishi na kiumbe aitwaye
HudHud. " Mke wangu" Mustafa alivuta
Moshi wa sigara ndani Yake. Kisha
akautoa kupitia pua Yake.
" Nimekumiss Sana, kwa nini tusibaki
pamoja daima?" Mustafa alilalamika na kuzidi kuvuta sigara kwa machungu.
Alikumbuka namna ambavyo alikubaliana na Azraj wiki moja nyuma.
Mara baada ya familia kusafiri
kuondoka nchini Tanzania. Mustafa
hakuweza kuondoka hapo alibaki
akimtafuta Saida kwa Hali na Mali.
Lakini haikua rahisi kumpata Saida
Wala kupata wapi azraj anaweza
kupatikana.
Siku moja alipigiwa simu kupitia namba
ngeni, iliyokua na code ngeni pia, ilikua
watsap voice call. Alipokea na kusikiliza
mtu huyo atakua Nani? Kwani hivi Sasa
analazimika kupokea simu zote anazopigiwa maana hajui na hamfahamu
wapi mwanamke wake alipo?
" Mustafa Badru naongea" Mustafa alijitambulisha.
" Nafahamu Kaka mkubwa, Mustafa Badru" Azraj aliongea huku Mustafa
akishtushwa na sauti ya huyo mwendawazimu.
" Hakika Azraj wewe ni muoga, kwanza
umekimbilia wapi? Na wapi ulipomuweka
Saida mpaka Sasa? Au nibaki nikikuona
wewe Kama mwanaume alieshindwa"
Mustafa alimdhihaki.
" Mimi sio muoga Mustafa Badru, amini na tambua kua Nina weza kufanya
lolote lile kwako nikiamua, kwani
hakuona anaeutamvua uwezo wangu hata
katika Askari wako" Azraj alijitapa
Mustafa akatabasamu na kufikiria
kimoyo moyo, bila Shaka anajua na
anaitambua jeuri ya Azraj. Anajivunia
mtu alienate nyuma Yake kana kwamba
yeye Mustafa hakua akamtambua mtu
huyo. Basi hakukua na sababu ya yeye
kumuoa Dr khairat. Iwapo
asingetambua mtu huyo. Na Lilian
Masele asingekua na maana yoyote Ile.
" Umeogopa bwana Mustafa??" Azraj
alimcheka Sana kwa nguvu na kwa
dharau Mustafa akatulia.
" Usijari Nina njia bila Shaka ya
makubaliano, kwani mke wako Ni wa
muhimu zaidi na unampenda Sana, Ila
usisahau bwana Mustafa, mi pia Nina
hisia nae, nadhani Hilo hata wewe una
lihakiki kabisa kua Nina mpenda mke
wako kipenzi Saida.
Mustafa alihisi kumuua iwapo Angekua
karibu nae, anawezaje kukiri waziwazi
kua anampenda mke wake? Azraj Badru
Ni zaidi ya mnyama. " Uko wapi azraj, natambua haupo Rwanda, umetumia
mbinu chafu tu ili kunizuga lakini
hakuna Cha maana ulichofanya, mbinu
hizi ni za kitoto kabisa"
Sehemu ya 162
Azraj alikasirika kidogo na kumuona
Mustafa kua mtu mwenye jeuri bila
Shaka alikua Rwanda, angewezaje
kuishi Tanzania kwa Uhuru na kuongea
nae kwenye simu bila Shaka angempata.
" Acha ujinga Bwana mdogo, unaweza
pewa cheo Cha kua mkubwa Ila nikabaki
Kaka kwako" Azraj alimwambia.
Mustafa aliweza tu kuguna.
" Usiishie kuguna, iwapo unahitaji
usalama na kumtaka mke wako akiwa hai, ingefaa tuwekeane mikakati
mapema Bwana Mustafa, kwani hitaji
langu Mimi ni lile lile lisilobadirika.
Nahitaji unifatishe"
" Sahau bwana mdogo" Mustafa
aliongea akiwa anamaanisha, hakika
hawezi mfanya Azraj awe mrithi wa Badru.
" Ni sawa, hata uniite hivyo, nahitaji
nafasi ya mrithi wa pili wa Badru,
sihitaji mengi Wala sitakupokonya
nafasi yako, nipatie cheo hicho kila kitu
litaenda sawa, hakuna asiependa kuvuna
alichokipanda, nimewekeza juhudi nyingi
Sana juu ya Badru, sitaki kua yeyote
asie faaa" Azraj alishushia mvinyo
mwekundu huku Mustafa akizidi
kumtetea sikio.
" Vipi Kama sitafanya Bwana Azraj
mwanaharamu?" Kwa kweli Mustafa ana
kiburi hata katika Hali hiyo hakuwaza
kabisa kuhusu Saida.
" Usisahau ninae mwanamke wako"
Azraj alimkumbusha Mustafa aondoe
kiburi chake la sivyo asahau kuhusu
Saida"
" Unamaanisha, kabisa utamrejesha
kwangu Azraj Badru" Mustafa aliweka
umakini juu ya Hilo.
kinyume na maneno yetu" Azraj alimjibu
Mustafa. Kisha aliweza kukata simu
Yake na kumtumia ujumbe watsap.
Mustafa aliifungua ilikua video ambayo
ilimuonyesha Saida akiwa ndani ya
chumba kimoja kisafi na nadhifu, Kisha
Azraj alikaa karibu Yake na kuniamsha
kwa upole. Kisha akambusu kwenye
shavu lake akiwa amelala. Mustafa
alihisi uvimbe kwenye kifua chake.
Yaani alimbusu mke wake akiwa kalala.
" Saida amka unywe chai" wakati huo
Azraj alionekana akiwa kavaa bukta na
juu hakuvaa chochote. Saida aliinuka na
kumwangalia bila kuuweka uso wake
pembeni.
" Afadhari umeamka" Azraj
alitabasamu mbele ya Saida ambae
" Wanaume hatuna desturi ya kwenda
alipapasa macho Yake kuondoka uchovu aliokua nao baada ya usingizi.
" Ningeamka bila Shaka" Saida alijibu akizidi kujinyoosha, huyu mwanamke
alivaa nguo laini na nyepesi za kulalia, Mustafa alihisi kufa kwa wivu, moja
kwa moja alihisi Kama Kuna kitu hakipo
sawa kabisa hapo. Saida aliinuka
kitandani na kuanza kuteremsha mguu
wake mmoja mlaini kutoka kitandani
mguu huo wenye rangi mchanganyiko
mrefu' kiasi na mnene ulikua wazi
kabisa mpaka usawa wa mapaja Yake, inamaana alivaa nguo Kama Ile mbele ya Azraj?. Kwa kweli Mustafa angekufa.
Kisha akafatisha mguu wa pili na
kujaribu kuinuka, kulingana na uchovu
kiasi kadhaa alishindwa kuinuka
kitandani, hivyo Azraj akamshika mkono
kumsaidia. Uvimbe wa Mustafa ndani ya
kifua chake ilizidi aliwezaje kushuhudia
video mbaya Kama hiyo. Bila kufikiria
Wala kutarajia aliitupia mbali simu
Yake. Na kuanza kulalamika.
" Azraj ntakuua" alitamani kumpata
Azraj Mara moja amfanye awezavyo
walau amfinyange anawezaje kumfanyia
hivyo anawezaje kumuweka karibu hivyo
mke wake. Na kwa nini Saida
hajamchukia Azraj kwa nini? Mustafa
kwa wakati huo alishindwa kuyazuia
machozi kupenya kwenye mboni za
macho Yake.
Hatimae baada ya siku mbili akimtafuta
Azraj kwa namba Ile hakuweza
kumpata, mawazo yalimzonga na kuamua
kusubiri, aliamini kabisa bila Shaka
Azraj atamtafuta yeye. Hakika wakati
huu Hatampuuza Wala kumdharau.
Haikua rahisi kwake na Saida kua
vyema katika siku za hivi karibuni kwa
Sasa bila Shaka anamtaka Saida tu.
Kweli Azraj alimtafuta kesho Yake na
kuamua kuweka miadi nae.
Azraj alitokea Dar es salaam akiwa
mwenyewe kabisa, hakuongozana na
chawa yeyote Yule. Mustafa pia
alijitokeza kwake akiwa mwenyewe.
Yalikua majira ya usiku wa saa mbili
katika mgahawa wa hadhi ya kawaida
Sana. Wawili hao walikua ndugu kabisa
waliochangia baba isipokua walitoka
katika matumbo ya mama tofauti.
" Mustafa Badru, ahahaha, siamini
unewasili hapa" Azraj alimwambia akiwa
anasubiri kupewa kinywaji kizuri kutoka
kwa mtu maalum. Ambae ni mdogo wake.
" Bila Shaka wewe ndo imeandaa miadi hii kwa nini usinihudumie wewe"
Mustafa alimwambia Azraj ambae
alihisi Kama bado huyu dogo hawezi
kuacha dharau.
." Mustafa Badru chunga dharau zako'"
Azraj alimwambia na kummiminia
kinywaji moja kwa moja. Azraj alipata
kinywaji na Mustafa pia, walitumia
kinywaji Cha chupa mom hatua kwa
hatua mpaka wakamaliza.
" Nadhani Sasa tunaweza kuendelea"
Mustafa alitamani Sana kusikia huyu
Azraj anataka nini?
" Unaweza sema kilichokufanya utake
kuonana na Mimi wakati tungekamilisha
kila Jambo hata kwa mazungumzo tu?
Mustafa alimwambia Tena.
Azraj alitabasamu na kuongeza
kinywaji. " Bila Shaka dogo hukufunzwa
adabu, Mimi ni Kaka yako ulifaa
kuniheshimu kwanza kabla hujaenda
moja kwa moja kwenye hoja." Mustafa
aliufunga mdomo wake kimya
" Sawa nitasema" akimalizia glass kisha
akaongea. " Azraj Badru,. Mustafa
Badru, Muksin Badru, mkhi! Azraj
aliweza kufinya midomo Yake na
kumwangalia Mustafa aliekua na maneno makavu.
" Ni rahisi Sana Mustafa nifanye kitu
ambacho nilikuomba, bila Shaka
utampata mwanamke wako, akiwa hai na
bila kuguswa na Mimi, hakika mwanamke
Yule anajua kudeka, na Mimi pia najua
kudekeza sana, tofauti na wewe
uliemuumiza Mara kadhaa haimtachukua
mwaka mzima kukusahu, bila Shaka Ni
miezi kadhaa tu" Mustafa alijikuta
akiifinya glass ya mvinyo mpaka
akasababisha kuipasua bila kujua.
" Usikasirike bila Shaka ntamtunza
iwapo hautakubali kunipatia urithi wa familia Kama mrithi wa pili."
Mustafa aliinuka na kumkamata shingo
Yake kwa nguvu Sana, hapo Sasa Azraj
alikishika kifua Cha Mustafa na kumtuliza haraka Sana.
" Unaweza kutulia bwana Mustafa
Badru, mi mwenzio Ni wanted, ikitokea
nimekamatwa hapa that means hata
mwanamke wako atakufa njaa kwani Ni
Mimi pekee anaye muhudumia" Azraj
alivuta nyusi Yake. Mustafa akapoa kwa
nini alikua mzembe kumlinda Saida. Ni
kweli kabisa Saida alikua sahihi hawezi
kuitwa mume ikiwa Hana uwezo hata wa kumkinda HudHud mpaka alikufa vipi
kuhusu kumlinda yeye Sasa.
" Ok. Fanya Kama nilivyokwambia, Kisha utampata mwanamke mwanamke wako akiwa salama katika anwani hii"
Ila ukithubutu kwenda kinyume na
Mimi,,,, bila Shaka hiyo imekula kwako
bwana Mustafa Badru." Azraj aliinuka
baada ya kumkabidhi kadi mikononi
mwake Kisha akaondoka zake kimya.
Mustafa alibaki pale akiwa haamini, hivi
amekuaje mdogo hivi kwa Azraj? Bila
Shaka angempiga kila Mara pindi
alikutana nae, lakini. Sasa hamna
ambacho anaweza fanya kwa Azraj saa
hii. Kumbukumbu Yake uliishia hapo akaendelea kuvuta sigara.
Bila Shaka Kuna kitu hakikua sawa kwake. Kwa nini alimuachia mwanaume
Yule mke wake. Akiwa ahapo alikumbuka kua alipigiwa simu na mwalimu wa vijana kutoka Badruguard na kumpatia taarifa kua, ndani ya
nyumba ambayo walipewa maelekezo
bila Shaka Saida hakuwepo pale, na hakuweza kabisa kupatikana.
Akiwa hapo simu Yake iliita, aliangalia
mtu anaempigia alikua, Azraj Badru.
" We mwana haramu umeenda kinyume na maneno Yake, utajiitaje mwanaume?"
Azraj alianza kwa kumtukana moja kwa
moja. Mustafa alipata maumivu kuitwa
hivyo, Ni lini yeye alikua mwana
haramu? Bila Shaka yeye ndo mwana
haramu?
" Nilifanya kitu sahihi Kama bwana
mkubwa Badru, kumbuka kabisa hivi
Sasa, cheo changu kimebadirika kutoka
kuitwa Kaka mkubwa Badru na kuitwa
bwana mkubwa Badru, kua Makini
Azraj"
" Ni sawa lakini mpaka uwe bwana
mkubwa bila Shaka lazima wewe uwe
mwaminifu na uweze kwenda na maneno yako"
" Lakini so lazima kwenda na maneno ya mtu asiefaa, Azraj. Mimi sio mpumbavu
kufanya Mambo Kama mtoto, sipo Kama
wewe kuwatumia wengine Kama chambo
ili nipate kitu. Unadhani sikujifahamu
Nia yako. Iwapo labda ningekuoatia
nafasi ya pili kua mrithi wa Badru kwa
maandalizi uliyoyafanya tangu ukiwa
mtoto mdogo bila Shaka utawageuza
watu wote kutoka katika familia kua watumwa wako.
Hata baba aliekuzaa unaweza mfanya mjakazi wako, kwa sababu uanahisi
Kama ulidhurumiwa ilhali ulitengeneza
mazingira hayo mwenyewe"
" Mustafa usinifundishe, ninajua
nachokifanya, utajuta kwenda kinyume na Mimi"
" Bora nimpoteze mtu mmoja katika
haya Maisha kuliko nipoteze familia
nzima ya Badru, mama yangu, watoto
wangu ndugu zangu wote ni wa thamani,
huna Cha kufanya kwa mke wangu kwani
hata wewe pia unampenda, bila Shaka
nitamkumbu Sana iwapo atakufa"
Mustafa alitoa maneno ambayo
yalimuacha mdomo wazi Azraj hakuweza
kuamini maneno hayo.
" Mustafa usije ukajuta!!" Azraj alikata simu na kufagia kila kitu
kilichopatokana kwenye meza ya kioo
aliyokua akitumia ndani ya chumba
chake Cha hotel. Hivi huyu Mustafa
Badru, alijiamini nini haswaa?. Azraj
alibaki na hasira mpaka akahisi kifo
kinastahili juu Yake.
Alichukua simu Yake na kupiga sehemu.
Simu iliita Kisha ikajibiwa haraka. "
Nahitaji ticketi ya ndege Sasa hivi"
alikata simu baada ya kuwafokea watu
wasio na hatia.
Ni siku nyingine Tena alfajiri Azraj
alionekana kutokea katika viunga vya
uwanja wa ndege, JK nyerere.
Alichukua alikwea ndege nyingine
ambayo ilikua fast jet ambayo
ilimpelekea haraka mpaka jijini mwanza.
Aliteremshwa na ndege katika uwanja
binafsi uliopatikana katika katika visiwa
vya ukerewe jijini mwanza. Aliongoza
njia moja kwa moja na kuchukua gari
ndogo aliyoletewa na kijana wake
mmoja.
Gari iliendeshwa mpaka kwenye
apartment aliyokua akiishi tangu amuibe
Saida. Alifika na kufungua mlango kwa
hasira baada ya kuupiga teke kubwa.
Salma ambae alikua aliendelea vizuri
wakati huo alimtokea Azraj akiwa na hasira Sana baada ya kumuona. "
Utaniondosha hapa lini we mbwa,
nahitaji kupatana na mtoto wangu, haikua kazi rahisi kupata mtoto Azraj!!!
Namtaka binti yangu, kwa nini
umeniweka mbali na binti yangu"
Azraj alikua na hasira tayari alafu
bado mwanamke huyu anamzungusha
kichwa chake, aliweza tu kumsukuma
huko na kusababisha Salma kiloshika
tumbo lake kwa maumivu, alichukuliwa
hospital akiwa hajapona vizuri lakini
bado alilazimika kuishi kwa kuhangaika.
Yote ni kwa sababu alizaa na shetani
ambae ni Azraj Badru.
" Azraj Badru, umelaaniwa wewe ni mtoto mwenye laana, bila Shaka
umezaliwa kwa laana" Salma alilia kwa
maumivu na mwishowe alipoteza nguvu zake kwa kweli hakua mzuri wa kukubali
chakula kwanzia arjeshe fahamu zake.
" Madam twende ndani tafadhari"
mjakazi aliewekwa kwa ajiri Yake
alijaribu kumuomba Ila Salma hakua
tayari kabisa. " Nitokee hapa!! Salma
alilia na kujilaumu kwa nini aliishi katika hii dunia.
Azraj aliongoza njia kuelekea juu, huko
alifika na kufungua mlango wa chumba
Cha Saida. Baada ya kujifungua kwa
hasira, Saida aliekua amekaa kitandani
huku akiwa amepoteza matumaini, alikua
akiishi Maisha gani haya ya kufungua
chumbani, Bora hata mfungwa alikua
akiweza kutoka nje na kufanya kazi.
Ila yeye Sasa anahisi alipoteza Maisha
taratibu.
" We mwanamke " Saida alishtuka na kuamka kitandani akiwa hamuelewi huyu
mwanaume aliemfanya mateka.azraj
alikamata mkono wake na kumkumbatia
kwa nguvu.
" Azraj unakichaa, niachie haraka, mi ni mke wa Kaka yako niachie haraka
Sana Azraj" Saida alilalamika.
" Tulia" alimuamuru Saida ambae
hakuweza. Azraj alimshika kwa nguvu
kiuno chake na kuanza kumbusu baada ya kukibana kichwa chake kwa mikono
Yake mikubwa.
Sehemu ya 163
Azraj alikua kichaa' bila Shaka alikua
akifanya nini? Tayari alimfanya mateka
wake ndani ya hiyo nyumba, tayari
amemtii ameweza kutulia bila
kufurukuta ili asije kumbaka Kama
alivyo ahidi. Lakini Sasa mbona Kama
anaenda kumfanyia vitu visivyostahiri.
Azraj alimuachia kidogo huku akiachia
tabasamu la kikatili na la kuchukiza, Saida akazidi kulia na kuchanganyikiwa zaidi. " Azraj unadh_" Azraj hakuweza
kumuacha hata aongee alianza kumbusu
Tena kwa Mara nyingine . Alimbusu
Sana mpaka Saida akachanganyikiwa
huyu mwanaume alikua akimbusu kwa
lazima bila sababu maalum. Kisha Azraj
alichoka na kumsukuma Saida kitandani
huku yeye akibaki amesimama.
" Hii ni kidogo tu ya kile ambacho
ntakufanyia Saida, Sina jinsi zaidi ya hivi, nakupenda lakini huwezi kua wangu
hata nikiwa mwema kwako, Bora wakati
mwingine nitumie nguvu ili niweze
kujifariji"
" Azraj kwa nini umebadilika hivi, kwa
nini umekua katili hivi? Inamaana
umesahau kabisa Mimi ni shemeji yako?
Saida alilia kwa uchungu akiwa haamini
Kama atawahi kutoka hapo siku moja, hakika alichoka Sana kuishi hapo.
Aliwamiss watoto wake alimmis mume wake pia.
" Sio kosa lako, isipokua Yule unaemuita mume wako wakati tayari mmeachana "
Azraj alifoka. " Huwezi kua shemeji
YANGU Tena wewe, sitakuruhusu uende kwa Mustafa" Azraj alimfokea Saida
maneno makali akiwa na macho mekundu.
Saida hakua na la kufanya zaidi ya
kujivuta na kujikunja kitandani Kama
mtoto asie na mama. Alikua na wakati
mgumu Sana hapo. " Azraj siamini
Kama Ni wewe, Mustafa alikua sahihi
wewe ni mtoto usie faa, hukustahili
kuzaliwa katika familia ya Badru" Saida
akiwa amejikunja Azraj alimsogelea na kumvuta ili watazamane.
" Huyo Mustafa ana kipi Saida?
Unadhani anacho kile ambacho Sina?
Azraj alitoa macho Saida akafumba
macho Yake kwa kumuogopa. " Bila
Shaka Nina kile kinachokupa furaha
ukiwa nae!!" Saida alihisi kuyabana
masikio yake' anahisi anaweza
kumfurahisha Kama Mustafa, aha' ana wazimu huyu' Saida alitulia.
" Kwanza nashangaa mume wangu mume
wangu, huyo mwanaume wako sio Kama
mmeachana tayari" Azraj alimsukuma
hapo kitandani saida kwa kiasi fulani
akatulia. ' hapana Azraj Ile haikua
talaka ya kweli, haijulikani popote bila
Shaka mamkwe aliileta tu ili kumtisha
Mustafa, Ila Mimi na Mustafa
hatukuwahi kuachana' Saida asingeweza
kutoa maneno hayo nje wee!; Iwapo
Azraj angefahamu bila Shaka
angembaka hapo hapo kwa kumdanganya na kumfanya awe shahidi wa kuvunja
ndoa kwa talaka ya uongo.
" Mustafa Ni Kama Hana wazo la kukuokoa kutoka kwangu. Hiyo
inaashiria kwamba ameridhika uzidi
kubaki kwangu na Mimi" Saida alitoa
macho akiwa alhaelewi bila Shaka
Mustafa hawezi kufanya hivyo.
" Ndo amegoma kunipa madaraka hata
kua mrithi wa pili wa Badru, atajuta, Ila iwapo anatamani nikufanye mke
wangu nitafanya hivyo asiwaze"
Upande wa Dr khairat alikua
akimwagilia moyo taratiiibu akimsubiri mtoto wake atolewe shuleni ili aondoke nae, Ni majira ya saa tano. Alikua bize anaperuzi mtandaoni kabla akutane na
taarifa za kuahtua kutoka kwa wanamtandao.
[ Tamaa ya pesa yavunja ndoa,. Na kunusurika kifo.] Caption ilisomwa hivyo, Kisha akashuka chini kwenye maelezo.
[ Aliamua kumuua mume wake, ili
aolewe na mwanaume tajiri, lakini
mwisho wa siku amekosa vyote baada ya mume kunusurika na kifo hicho Cha
kukusudia_ Lo! Taarifa hiyo Ni Kama
ilimlenga yeye kabisa.
Mume anusurika na ajari, Kisha
mwanaume tajiri arejea
kwa familia
Yake, kwa Sasa amebaki mwenyewe na
tamaa zake pamoja na mtoto aliezaa na mume wake]
Dr khairat alichanganyikiwa na kuangalia picha iliyokuwepo pale. Ilikua
niii!! Bila Shaka picha Yake? Hee! Alitoa macho nje. Ilikua picha Yake kweli, yeye akiwa na mtoto wake Adil pamoja
na Mustafa, huku picha nyingine akiwa
yeye Dr Hizaan pamoja na mtoto wao.
Dr khairat alihisi uwoga moyoni Ni mtu
gani huyo mwenye uwezo wa kupost kitu
Kama hicho?. Akasoma account
iliyotumika.
" Haa! Ilikua akaunt ya Hizaan?"
Hizaan Yuko hospital mahututi sio wa
kupona leo Wala kesho kwani Nini
kimemkuta? Amewezaje kutoka
hospital?. Ilibidi achungilie komment za
watu, make hata Sasa hivi kazini aendi
duh! Kapoteza vitu vingi sana. Alafu
bado kamkosa Mustafa. Yote kwa
sababu ya saida. Achana na Saida mwenda wazimu! Ngoja kwanza aangalie
maonj ya wanamtandao juu ya picha yake. Alipofungua eneo la maoni
alijilaumu Sana khaa amewezaje sasa
kuyawaza maoni ya wanamtandao Bora angeacha tu?. Yalikua Kama ifuatavyo.
[ Waoo!! Ni Dr khairat mwanamke asie kua na haya!! Mwanamke ambae
amefanikiwa kua funzo katika jamii kwa
kutaka kumtoa roho mume wake ili aolewe na mume wa mtu mwingine]
[ Dr khairat! Kweli Mimi Nina roho
mbaya Sana lakini mwanamke huyu hapo
ilizidi, alifanya ukatili usiyoelezeka, hata kama alimchoka mwanaume wake
asingefikiria hatua ya kumuua]
[ Dr Hizaan alibugi step kubwa kufanya maamuzi ya kumuoa huyo mwanamke, au Waswahili walipatia kusema mapenzi upofu, hata sio mzuri kulinganisha na utanashati alio nao Dr Hizaan, na Dr hizaan Ni mwanaume aliempenda kujitunza]
[ Mwanamke Kama yeye ni kichefu chefu, kwani serikali haipo kushughulika nae] mtu mmoja alitamani hata angemuua Dr khairat.
[ Mmh! Alijifanya kichaa' ndo maana aliruhusiwa kutoka police Ila Hana lolote mbwa yule, kila siku tunamuona anapiga mat*k* mtaani, na anaishi vizuri tu ] mmoja wao alijibu.
[ What the heck, hivi mwanamke Kama
huyu anafaa kupumua kwenye dunia, Kama Kuna mtu alishuhudia video namna
gani aliendesha kabisa kwenda
kumfanyia unyama mume wake wa zamani, bila Shaka ungeelewa hakua
kichaa' mbona hakumgonga mtoto
wake?] Watu walikua mwisho wa hasira zao.
[ Kunayo video kwani?] Mtu mmoja
alilazimika kuhoji. [ Ndio ipo, ipo video Kama unahitaji,
fuata link hapo tukutane telegram] mtu
huyo alishusha link akisubiri watu wajoin
kwenye group lake. Dr khairat
alikasirika Ni mtu gani huyo aliethubutu kumrekodi. Bila Shaka ilikua njama Yao
watatu tu aweze kumpata mtoto wake
na Mustafa upande wake. Mbona Kama
Mambo yanamrudi.
Au atakua.... Lilian!! Hapana
haiwezekani, bila Shaka hawezi kua
Lilian, Lilian ni mtu aliemsaidia sana na wameambizana Mambo mengi Sana, kwa
hiyo atakua Nani Sasa? Azraj ? Dr khairat aliinuka kwani Azraj ndo mtu
pekee aliempa mpango huo hapo kabla.
Na kitu kingine mbona Kama Azraj
alionekana kua karibu na yeye pamoja
na Hizaan kwa wakati mmoja?
Au Azraj ndo anahusika kumfanyia hivi.
Dr khairat alipandwa na hasira Kisha
akachukua simu Yake na kupiga simu
sehemu ambayo aliijua mwenyewe. Kisha
haikuchukua muda kijana wake mdogo
Adil aliwasili na hapo Dr khairat
alimshika mkono.
" Mama baba anarudi lini?" Adil
alionyesha huruma kwenye macho Yake"
Dr khairat alihisi huruma baada ya
kuulizwa hivyo.
" Atarudi tu we usijari, tuendelee kusubiri so unajua huwa yeye anakazi
nyingi mno" Dr khairat alimuingiza
kijana wake kwenye gari Kisha
akaendesha mpaka nyumbani. Kitu
ambacho hakuweza kufahamu ni kwamba
Kuna mtu alikua akimfatilia nyuma
Yake.
Dr khairat aliwasili maeneo fulani ya
Barbara, ilikua njia panda, ghafla gari
Yake ikapata pancha bila kutarajia.
Wakashindwa kuendelea na safari yeye na kijana wake.
" Mama Kuna nini? Adil alihoji.
" Mwanangu sijafahamu pia, nafaa kuchunguza kwanza" ilibidi ateremke
kwenye gari Yake na kwenda kuangalia.
Alihisi kulia baada ya kuona gari Yake
Imepata pancha, hakua anafahamu'
namna ya kurekebisha ili aendelee na safari yake.
" Mama!!" Adil alimuita kwa huruma.
" Adil gari yangu Ina pancha" Dr
khairat alihuzunika Sana alikua
akimchelewesha mwanae kwenda
nyumbani.
Ilimlazimu kuomba msaada kutoka kwa
wanaopita barabarani lakini hakuna
aliesimama kabisa. Wakati anahisi
kukata tamaa bahati nzuri Kuna kijana
alipita akiwa na pikipiki Dr khairat
akamsimamisha pia. Kijana huyo
alisimama na hakushtuka kwenye pikipiki
Yake.
" Kuna sister" kijana huyo aliekua kavaa
helmet aliongea.
" Aah' samahani Kaka yangu, gari
yangu Imepata hitlafu hapa masaa
kadhaa yamesogea Ila nimeshindwa kusaidika" dr khairat alitoa huruma.
" Samahani bhana, nenda garage" kijana yule aliwasha pikipiki Yake na
kuondoka zake. Dr khairat alihisi kuchanganyikiwa. Hivi alikua na siku
mbaya kiasi gani?
Akiwa anawaza Sana ghafla kijana yule alirejea na kipaji mbele ya gari Yake. "
Mbona umerudi Sasa" Dr khairat alimuuliza.
" Nina sababu ya kurejea" kijana yule
aliteremka kwenye pikipiki Yake baada ya kuipak Kisha akatoa helmet na kupangusa nywele zake akijaribu kuzirekebusha.
" Asante kwa kurejea bila Shaka
utanisaidia" dr khairat alikua mpole kwa
huyo kijana kana kwamba labda aliwahi
kua mwanamke mwema. Kijana yule
akipandisha nyusi moja juu na kuachia tabasamu.
" Popote alipo nevi, hakuna
kisichowezekana, na Nevi huwa hatoi msaada bure" dr khairat alimwangalia
Sana huyo kijana akiwa haelewi kijana
huyo anamaanisha nini? Alionekana kua na sura ya kawaida mno.na kijana
mdogo tu.
" Bila Shaka sio msaada wa kuvunjiana heshima" dr khairat alipata hisia mbaya.
" Ahahaha, Nevi sio mtu wa kupenda
kit*mb* , Ni mtu mmoja ambae huwezi amini lakini Ni kweli, Nevi bado bikira wa kiume" Dr khairat alihisi kucheka.
" Sawa bwana nevi" alikaa kimya kwani
wakati huo nevi alikua akifanya
marekebisho kwenye Ile gari, aliweza
kuchomoa msumari ambao alimuweka
mwenyewe akiwa kamlenga Dr khairat na kweli aliingia kwenye mtego wake.
Kisha akafanya marekebisho pale. Gari
ikakaa sawa baada ya kuziba pancha na kujazwa upepo.
" Inashangaza, ulisema nipeleke gari garage wakati na wewe ni fundi gereji
mzuri tu" dr khairat alivutiwa nae.
" Aah' nevi yupo hivyo, nilikua nawahi
kwenye harakati zangu nimepigiwa simu.
Haya Sasa hutaki kufahamu nahitaji nini?" Dr khairat alihisi kulia. Alitamani
kabisa kijana huyu mdogo asiseme masuhara ya kulalana.
Nevi aliweza kuchomoa picha kwenye
mfuko wa koti lake Kisha akamkabidhi
Dr khairat. Ilikua picha ya Nevi, akiwa
na Bwasha pamoja na Azraj. Dr khairat alishtuka na kumwangalia Mara tatutatu
nevi. Nevi hakuwaza hata kidogo juu yake. Aliweza kutabasamu tu..
" Hii inamaanisha?" Dr khairat alikosea Ni jinsi gani amuulize anamfahamu vipi Azraj. Nevi akawahi kumwambia. "
Sitaki kuzunguka sister Ila ukweli ni kwamba, huyu ni boss wangu Mimi, tulipotezana kwenye ajari ktlutokana na matatizo. Na sijui nampata vipi, nimejaribu kumtafuta Sana tu nashindwa kumpata. Lakini hapo nyuma niliwahi kukuona nae Mara kadhaa ndo maana nikarejea kukupa msaada na wewe unisaidie pia"
Sehemu ya 164
Dr khairat alishindwa kumjibu. Kwani haikua rahisi kumfikisha mtu kwa z
Azraj bila kumfahamu kabisa. " Huna haha ya kujieleza unachotaka kuniambia
kwani Mimi pia namfahamu boss wangu, ok em fanya hivi, chuki hii namba yangu ya simu, utanipigia iwapo makuliano
yenu yakienda vyema. Ila ukimuonyesha tu hiyo picha ataelewa moja kwa moja.
Mwambie kua nevi nipo hai iwaoobado
ananihitaji, nipo tayari kumtumikia" nevi aliweza kuondoka zake. Na kudandia
pikipiki Yake Kisha huyoooo.
Dr khairat alibaki hewani asielewe
iwapo anastahili kufanya alivyoombwa au iweje? Alichezesha midomo Yake
Kisha akageuka na kuingia kwenye gari
akiwa anahisi kuchanganyikiwa, kwa
wakati huo tayari Adil kwenye gari
Yake aliainzia.
Upande wa nevi aliendesha pikipiki
mpaka Hilo mbele kidogo na kusimamisha. Alihisi kupumzika nafsi
kwa wakati huo maana angalau alipata
mwelekeo kwenye kazi Yake. Aligeuka
upande wa kushoto na kukunja ndota za
uso wake akitabasamu baada ya kuweka
mikono Yake mfukoni.
" Usiniangalie kwa ubaya" kijana mmoja
aliekua mfanyakazi mwenzako katika
kambi moja ya Badruguard aitwae
Albert aliweza kumfikia. Albert pia
alikua na Nevi katika mission moja ya
kumchunguza Azraj na boss wake.
Alikua Kama mlinzi wa bwana amiri, lakini mwanaume huyo alikua mpumbafu
alimtumia yeye Kama mlinzi wa uchochoroni na kuongozana nae kwenye
sehemu za kawaida tu. Ila kila
alipohitaji kwenda kewenye Mambo
Yake ya faragha bila Shaka angeenda mwenyewe tu.
" Ni vipi unaamini kwamba utafanikiwa?"
Albert alipata wasiwasi.
" Ninao uhakika bila Shaka,
nitafanikiwa mwenzio kwa sababu
nafamu, sio tu najua yaani Ni uhakika
kwamba naaminika kwa Azraj Badru"
Nevi alijitamba.
" Sawa Basi mi natambaaa" Albert
aliupiga mkono wa Nevi kwa kupeana
tano ya wanaume kisha akatokomea
barabarani kw aipi tofauti.
Ndani ya apartment iliyochangamka
Azraj alitembea kuelekea kwenye meza ya chakula majira ya mchana, wafanyakazi wa kike wawili waliokua na kazi ya kuandaa chakula walitokea
wakiwa na hotpot kubwa kwa ajiri ya chakula Kisha wakatenga mezani.
Azraj alimimina Maji kwenye glass
Kisha akanywa. Taratiibu akimwangalia
mwanamke aliekua amekaa kando yake.
Mwanamke huyu alionekana kushuka
sura kwa huzuni Sana. Alikua amechoka na mdhaifu kwa sababu alikua mgonjwa, anahisi kulia tu wakati wote na kutamani Bora angekufa jamani.
" Salma utakula". Azraj alimfokea
Salma hakuweza kujitingisha hata
kidogo.
" Sina hamu na chakula Chako Azraj"
Salma alijibu kwa hasira na kumfanya
Azraj achanganyikiwe, alishusha pumzi zake kwanza na kumwangalia Tena.
." Kwa usalama wako na binti yangu kula chakula" Salma alichukua imma
akachomoa kipande Cha samaki na kumtupia Azraj usoni.
" Nikiwa hai huwezi kua na binti Azraj, wewe ni mnayama sanaz itakua aibu kwa binti yangu kuzaliwa na mwanaume Kama
wewe" Salma alihisi kufa mwenyewe.
" Bila Shaka ni binti yangu wa pekee, ambae nahitaji awe salama na akikuona
usiwe na shida ushindwe kumlea ukiwa
mgonjwa" Azraj alimsogelea na kuanza
kumlisha. Salma hakua tayari kula hivyo
Azraj alikua akitumia ya lazima
kumlisha huku Salma akitaabika kwani
alikua akimuumiza, yeye ni mgonjwa
alietoka kujifungua muda si mrefu' na
alijifungua kwa kisu. Lakini bado Maisha
Yake yalikua mabaya zaidi ya kuzimu
hai. Hakua na namna zaidi ya kula kwa wakati huo.
Alijuta kumfahamu Azraj alijilaumu kwa
nini alimpenda mwanaume anaitwa Azraj
katika huu ulimwengu. Yeye alikua binti
mdogo asie na hatia, alimpenda mtu
huyu na kuamini kila kauli aliyokua
akimwambia, alijilaumu kwani Kuna
wakati alimuonea huruma Azraj kwa
kutengwa na familia Yake kwa vile
alikua kijana wa nje ya ndoa Ila mwisho wa siku ilikua Bora kwake kukaa upande
sahihi baada ya kushuka ujauzito.
' Azraj Badru , wewe ni mdudu usie
faa bila Shaka ntakua siku moja' Salma
alitamani kumuua wakati huo uwezo
Hana kabisa. Baada ya muda Azraj
hakua maeneo ya nyumbani pale Salma
alitamani kufahamu Kuna kitu gani ndani ya chumba Cha wageni ? Hivi kwa nini
anazuiliwa hata kukisogelea.
Aliangalia mlango na kuona mlinzi
aliekua akilinda eneo Hilo kasimama kwa
uangalifu na hatikisiki Kama kisiki.
Lakini kwa kweli yeye ni binadamu bila
Shaka Kuna muda atahitaji hata
kwenda haja ndogo, Kama mwanadamu
akienda haha ndogo Basi Salma
ataitumia nafasi hiyo kwenda kutambua Kuna kitu gani? Ndani ya chumba hicho.
Wakati yeye anawaza hayo, Saida
alikua amesimama dirishani akiangalia
nje kupitia kioo kilichofungiliwa tinted.
Alitamani kufa baada ya kuona anaishi
kuzimu hai. Lakini vipi kuhusu watoto
wake wawili, Ni wadogo Sana bado
Wana muhitaji. Moyo wake uliuma kila
alipokumbuka kuhusu tukio la alfajiri
kutaka kubakwa bila kutarajia aliziba
uso wake kwa maumivu na kujikuta
upya.
" Mustafa uko wapi?" Ni kipindi
ambacho alitamani kumuona Mustafa
moja kwa moja na kujitahidi ya kwamba
hatakaa akae mbali nae hata kwa
bahati mbaya.
" Nilikosea nini dunia? Kwa nini Maisha
yangu yamegeuka Giza baada ya kuoana
na Mustafa, siikatai furaha yangu
kubwa ipo kwake lakini bado walimwengu
wanaona tabu kuona furaha yetu
ikimea" Saida alizidisha kilio. Ama kweli
alimkumbuka Mustafa wake.
Alijikunyata kwenye kitanda na
kuzidisha kilio alikua Amelia Sana kiasi
kwamba Hadi macho Yake yalikua
yakitiriraha machozi bila yeye kujijua.
Kulingana na Hali ilivyo alitamani awe
amekufa zamani tu. Ila Sasa
atafanyaje ana watoto wanaomsubiri.
Tukirejea nchini Africa kusini, bwana
Rashid alikua ameketi kwenye bustani
na kijana wake Mustafa. Mustafa
alionekana mnyonge na mwenye mawazo
mengi Sana hivi kwamba alitia huruma
kwa kumtazama tu. Bwana Rashid
aliweza kuzungumza kila alichokua nacho
ndani ya nafsi Yake.
" Naomba unisamehe Sana kijana
wangu, makosa niliyoyatenda Mimi
katika ujana wangu, yamegeuka kua
hadithi isiyotamani kusimuliwa" Bwana
Rashid ki ufupi alihisi Kama yeye ndo
mkosefu namba moja kwa wakati huo.
Kwani bila yeye kusababisha kuzaliwa
kwa Azraj dunian mambo yasingeenda
hovyo Kama hivi. Mustafa alimtazama
baba yake' na kumsikitikia. Hakua na
Hali Kama yake lakini bila Shaka alikua na maumivu zaidi maana yeye alikua
katika majuto.
" Mh! Baba hapana, sio sahihi
unavyosema" Mustafa alihitaji
kumuondoa khofu. " Sio kosa lako
kuzaliwa kwa Azraj. Ni Mungu alipanga
azaliwe na kingine Azraj asingekua hivi
alivyo iwapo asingepata shinikizo kutoka
kwa mtu Fulani akiwa bado mtoto
mdogo" bwana Rashid alishtuka
shinikizo? Shinikizo gani?
Bwana Rashid aliuliza moja kwa moja
lakini Mustafa hakua tayari kumuingiza
baba yake' kwenye Mambo hayo kwani
umri umeenda ana Mambo mengi ya kushughurika nayo haswa ya kampuni, iwapo na yeye akijiingiza kwenye
Mambo ya kumdaka Azraj vitu vingi vitaenda mrama.
" Baba tuachane na yote, nilikua
naonekana Kama kijana anaechukiza
mbele ya macho Yake lakini ki ukweli
ulikua ukinipa kipaumbele zaidi katika
Maisha , ulikua ukionekana kumpendelea
Azraj tangu zamani, lakini mwisho wa siku ulismama na Mimi hata nipokosea
ungenionya kwa adhabu Kali za familia
lakini huwahi kuniacha nianguke, nimewakwaza Sana Wana familia lakini
" Shinikizo kutoka kwa mtu gani?"
hukuwahi kunitoa katika nafasi ya kua
mrithi na msimamizi wa familia ya
Badru hiyo ilikua na maana gani???
Mustafa alikua anajiuliza swali Hilo kwa
muda mrefu lakini mwisho wa siku alikua
alibaki nalo moyoni Ila leo ameamua kuuliza tu.
" Aah'! Mustafa, wewe ni kijana wangu
mkubwa katika familia, na huo ndo
ukweli unaofahamika kwa kila mmoja.
Ila huo sio ukweli" bwana Rashid
alicheza karata iliyokua mkononi
mwake.
Mustafa alimtazama kwa Makini na
kumjibu kwa kiulizo. " Hiyo inamaanisha
kwamba, Azraj anasema ukweli kila
akiongea na Mimi baba?"
Bwana Rashid hakuelewa Ila alihisi kana
kwamba Mustafa anafahamu' Jambo. "
Kwa maana hiyo unafahamu pia?"
" Baba sikua na uhakika na Hilo, kila
aliponambia, nilidhani anaongea tu kunikebehi?" Mustafa hakika alishangaa.
" Huo ndo ukweli, yeye ni mkubwa zaidi yako wewe! Sikumzaa nje ya ndoa, akikusaliti ndoa yangu Bali nimzaa kabla ya ndoa, anakuzidi wewe mwaka mzima na miezi kadhaa, lakini sikua na shida
hapo awali nilipokua na mama Yake, Ila hakua mwanamke mzuri, aliutumia mwili wake kwa ajiri ya maskahi yake. Kwa kua sikua na shida na pesa niliona haina
haja kumnyima kwani bado Nina nguvu
za kutafuta Kama kijana wa Badru, na pia alinipendeza, sio kwa akili na uzuri
Bali alikua akinitosheleza katika
nahitaji ya kimwili, Ila baada ya
kumuoa Shayma, akili yangu ilibadirika, kwani nilipata mwanamke ambae,
aliufanya moyo wangu uwaone wanawake
wengine waliumbwa kupoteza muda
katika hii dunia" bwana Badru alihisi
kucheka kila alipomkumbuka Shayma wa enzi zao.
" Mwanzo sikua nampenda kwani
nilimuona kwa shinikizo la familia, lakinia kadiri siku zilivyozidi kwenda
nilizidi kumuona mzuri na mtamu, nilimuona anastahili kua wa kwangu.
Niliona Kama nilikua mjinga kudanganya
huko nje. Ki ukweli Maisha yangu na
Shayma yalikua Kama Maisha yako na
mke wako Saida. Nahisi Kama historia
inajiludia kwa kiasi fulani. Tulipitia
changamoto nyingi Sana, na aliwahi
kutekwa Kama hivi pia nilihangaika Sana
wakati huo. Lakini sikuweza kukata
tamaa, Hata hivyo baadae nilimpata
baada ya kutumia akili nyingi Sana. Kitu
pekee kilichoweka utofauti Kati yangu
na wewe Mustafa. Mimi nilikua na
maadui ambao walikua wafanyabiashara
wenzangu na sio ndugu zangu. Ila kwako
wewe??
Daaah!! Bwana Rashid aulishika uso
wake kwa majuto. " Acha nijibu swali
lako kwanza" alicheza kadi na kumtoa
Mustafa mchezoni baada ya kumpiga
bao moja la ushindi. Mustafa hakuweza
kuumia Wala kufurahia kwani alikua
akicheza cheza tu bila kumaanisha. " Ki
ufupi ni kwamba, wewe na Azraj Ni
watoto wangu, niliwazaa mwenyewe,
nawafahamu fika tangu mkiwa wadogo, niliweza kutambua mapema Sana akili
ya Azraj, Kama nilivyoitambua ya kwako wewe, Azraj Ni mtu Safi mwema
mtaratibu na mstaarabu mbele ya kila
mtu, lakini hawezi kua msafi wa nafsi
kwa kujifanya, nilielewa Hilo kuanzia
siku ya kwanza nilipomleta hapa, na
alifanya kila Jambo kumpendeza
Shayma na wanafamilia wengine ili
kuvutia umakini wao, kitu ambacho
hakua nacho kabla ya kuja nyumbani
kwa familia hii! Hivyo nisingeweza
kuzama kwenye njama Yake.
" Ikiwa wewe ni kijana anae onekana
katili asie jari, na mkaidi na mwenye
kiburi, huo Ni uhalisia wako ambao
hukuwahi kuuficha Wala kuuweka
kando, utaonyesha hasira yako waziwazi
pindi utapokasirika, utaonyesha furaha
yako waziwazi pindi ukifurahiz na utaonyesha huzuni yako Mara tu unapohuzunika, na zaidi hutasubiri
kutoa lililopo moyoni mwako pindi
unapoamua Jambo. Huo ndo uanaume
halisi na hiyo ndo namna ambayo
mwanaume wa Badru na mrithi na kiongozi wa Badru anafaa kua. Macho
yako yamejaa uhalisia na macho ya Azraj yamejaa tamaa na ufedhuri" kwa
maneno hayo Mustafa alikosa neno, kwa
hiyo ndo sababu baba yake' alikua
mkali kwake kila alipokua akifanya
makosa. Ni kwa sababu hakutaka
kumuona akiharibikiwa . Maana
alimuandaa kua mrithi na msimamizi wa familia ya Badru mapema zaidi kabla ya muda.
Sehemu ya 165
" Kitu kikubwa ambacho Mimi nakuomba
Ni wewe kupambanaia furaha yako
kijana wangu, una safari ndefu bado
ambayo unakusubiri wewe kwenda na
kuitikia, usiwahi kukata tamaa Wala
kuyumbishwa na watu wasio kua na
maana bila sababu" Bwana Rashid
alikunja ndita ya uso wake na
kumtazama vyema Mustafa
Mustafa alitabasamu. Na kuzidi
kumsikiliza. " Katika haya Maisha
ambayo tumeishi Mimi na wewe,
nimekua mkali Mara nyingi zaidi kwako
wewe, kwa sababu ya Mambo ambayo
yalikua yakifanyika nyuma ya pazia na
ukiyavumilia, nilifahamu kabisa tangu
mwanzo ya kwamba Mustafa wangu
hawezi kufanya. Hili, Mustafa wangu
hawezi kutenda upuuzi huu! Ila nyuma
yake bila Shaka Kuna mtu anatenda
kwa kutumia taswira Yake kumchafua.
Ila nilipima uvumilivu wako, nilipima
subira yako he utaweza kuvumilia "
Mustafa alihisi kutabasamu kumbe baba
yake' alikua akimuamini kiasi hicho.
Mbona Saida hakua muelewa kwake?
Hapana Saida alikua akimuelewa tatizo
wivu na maumivu Kama mwanadamu
anaesalitiwa lazima Imani ishuke.
" Unatambua ya kwamba Mimi sitaishi
milele nikiwa na wewe, japo sifahamu
Ni Nani ataanza kutangulia Kati yangu
Mimi na wewe Ila kitu kikubwa
unachofaa kufanya ni kusimama imara
na kuiongoza Badru kwenye msitari
unaofaa, kwenye njia iliyonyoooka, kwa
Sasa utamuozesha Muzda, katika
familia nyingine lakini haina maana
kwamba umemgawa Kama mwanamke
alieolewa bado atabaki kua dada yako
ambae unafaa kumuangalia kwa ukaribu zaidi"
Mustafa alihisi Kama amekaa kwenye
meza ya wosia siku hiyo.
" Unae muksin kando yako, lakini kijana
huyu bado Ni mdogo Sana ki mawazo, na yeye ndo mtu pekee mwenye mitihani
mikubwa zaidi hapo mbele kwani ameoa
mwanamke ambae, Ni mwema mzuri
lakini atakae gombaniwa na wengi Sana, watu wengi watajaribu kuthubutu
kuiyumbisha ndoa Yake ili wampate
mwanamke wake kwa tamaa za Mali, na
Kuna wakati yatatokea mengi ya
kutokea, Kama Kaka unafaa kusimama
nae kidete na umueleze ya kwamba kitu
kikubwa anafaa kutanguliza katika
Maisha Yake ya ndoa, Ni Imani Kisha
upendo. Upendo bila Imani hakuna
ukamilifu wowote ndoani. Kwa hayo mke wake hawezi kuyumbishwa na kisiki
chochote Wala mwamba wowote kwani
atakua na Imani ya mume wake."
" Kitu kikubwa nakusihi Mustafa wangu
kwani wewe ndo kijana mkubwa na kiongozi wa familia hii hivi Sasa na hapo baadae, wazongatie Sana binamu zako', Afsat na Maulid, haswa Maulid
bado Ni kijana mdogo na bado anakua, katika makuzi Yake unafaa kumuweka
karibu na kumpa mafunzo mengi stahiki
aamini ya kwamba yeye ni Badru, kwani
mtihani mkubwa utakao upitia kwa
kijana huyo, Ni jina lake la ukoo, wafanyabiashara wengi na watu wengi
ulimwenguni, bila Shaka watamshawishi
Sana kwa vitu vizuri ili wamfanye
kwenda kinyume na wewe na familia pia, wataweza hata kumuaminisha yeye kua
sio Badru, Bali ni wa ukoo mwingine,
kikubwa unachofaa kufanya mwanangu
Ni kuufunga Mkanda ukaze"
" Baba unaongea maneno ya kuumiza na kuudhi kana kwamba Kuna mahali
unahitaji kwenda, sihitaji kusikia
maneno hayo toka kwako, Nina Mambo
mengi Sana ambayo yanauvuruga ubongo
wangu kwa Sasa" Mustafa alihisi kana
kwamba baba yake' aliongea kama mtu
anaetaka kufa. Bwana Rashid
alitabasamu baada ya kuiona hasira
Yake. Moja kwa moja alimuelewa
Mustafa aliogopa kuona baba yake'
akimpa wosia akidhania labda atakufa.
" Usiogope Mustafa, Rashid Ni kwamba usio yumbushwa" bwana Rashid aliamka na kukunja mikono Yake Kama mpiga
ngumi na kumfanya Mustafa apate
kutabasamu. Kuna wakati baba yake' alikua na vituko Kama vya mkijana wake mdogo Mustakim.
" Mimi Ni kijana wa saifu Badru, nawezaje kutikisika" Mustafa alipata
kucheka sana.
" Mimi kesho nataka niondoke niende
Tanzania" Mustafa alimuaga bwana
Rashid ambae hakuweza kumpinga.
" Utakwenda mwenyewe huko??"
" Bila Shaka, lakini itabidi niende
mwenyewe" Mustafa alimwambia baba
yake' akamkubalia, hakua na haja ya kumpinga moja kwa moja.
Mustafa alikua akirejea Tanzania kwa sababu ya mke wake tu na so kingine.
Baada ya kuongea na baba yake'
alitafuta eneo akajitenga pekee Yake
Kisha akapiga video call. Simu Yake
ilipokelewa na mwanaume wa makamu
kutoka Badru guard. " Bwana mkubwa"
mwanaume huyo aliita.
" Mmeshapata njia??" Mustafa aliuliza moja kwa moja.
" Bila Shaka itapatikana, nevi hawezi kuacha pengo"
" Vyema Sana" Mustafa aliitikia Hilo na kuona Bora iwe hivyo.
" Lakini bwana mkubwa?? Mwanaume huyo alikua na Shaka yake.
" Nakusikiliza"
" Inabidi familia ya Bwana Amiri irejee
Tanzania pamoja na mtoto wa Azraj arejee pia" Mustafa alipata maswali kwenye akili Yake.
" Unataka turejee kwenye misukosuko na wanafamilia?, Sitaki kumuumiza
yeyote Katika familia yangu" mustafa alipinga.
" Hapana bwana mkubwa, sio kwa ajiri ya hatari, inabidi nevi apate Imani
kamili kutoka kwa Azraj, hata hivyo
familia ya Bwana Amiri haiwezi
kudhurika kwani yeye ndo Mastermind wa Azraj, na anaonekana kunipenda familia yake Sana"
" Nyamaza wewe tumia akili, Kuna
jambazi mwenye uwezo wa kua na huruma na familia Yake, mtu huyu katili
aliweza kumtoa dada Yake sadaka kwa
ajiri ya maskahi Yake unadhani anaweza kua na huruma na shangazi yangu??
Mustafa alifoka Sana.
" Samahani bwana mkubwa lakini kwa
kweli itapendeza iwapo familia Yake
itamshuhudia wenyewe"
Mustafa alitafakari Sana Kisha akaona
Hilo Ni Jambo zuri na aliweza tu kumjibu Kama hakua na uhakika na wazo lake lakini ukweli, alikua tayari
amemkubalia kidogo kidogo. "
Nitafikiria" Kisha aliikata hiyo simu.
Siku nyingine tena nchini Tanzania jijini
mwanza, katika visiwa vya ukerewe.
Hatimae Salma alifanikiwa kupata
upenyo wa kuingia katika chumba
alichokua Saida. Hii Ni baada ya Azraj kwenda na chai ndani ya chumba hicho
Kisha akatoka kwa ghafla Sana.
Saida hakujua Kama Ni Salma alieingia
humo ndani hivyo bado aliinamisha uso wake chini akiwa hana matumaini.
Salma alipoingia mle ndani hakuweza
kuufunga mlango vyema akiwa na wazo
la kutoka haraka baada ya kutambua
Kuna nini ndani Yake? Alishtuka Sana
baada ya kumuona mwanamke
aliemfahamu kwa kusihi nae siku kadhaa
ndani ya nyumba hiyo.
' Ya Allah, alikua Saida? Moyo wa
Salma ulipiga kwa nguvu akiwa haamini
iwapo amemuona saida, inamaana Azraj
alitimiza adhma Yake ya kumteka huyo
mwanamke. Salama alihisi majuto
kwenye nafsi Yake.
.bila Shaka sababu kubwa iliyompelekea
yeye kuzimia siku hiyo, ilikua Ni baada
ya kusikia maelezo kadhaa kutoka kwa
Azraj akiongea na simu na mwanaume
ambae yeye hakuweza kumfahamu, alikua nyuma Yake na alisikia tu neno. "
Bila Shaka atekwe leo, muda umeisha"
Ni azraj aliongea maneno hayo kwa mtu
fulani.
Salma alishindwa kuelewa Nani
anazungumziwa. Mpaka pale ambapo
azraj alirejea kauli take akisema. "
Usifanye Kama humjui Saida mke wa
Mustafa wewe, sitaki nianze kutoa
maelezo nimesema umteke mapema
haijalishi ni katika Hali ipi? " Kisha
Azraj alikata simu Yake. Na kugeuka
nyuma akakutana na Salma ambae
alijikuta hawezi kuuzui mdomo wake
kupiga kelele kwa sauti.
" Azraj Badru unathubutu vipi kua katili
kiasi hiki?" Alitulia akitamani kummeza
sema tumbo lake lilimpa usumbufu
kidogo. " Unapanga kumteka Saida
unakichaa, yeye ni mke wa Kaka yako"
kwa neno Hilo Azraj hakuweza hata
kujari Hali Yake alimsukuma mbali.
Salma alipiga kelele kwa maumivu
alijuta kuongea na hapo akapata
madhara na hitlafu kwenye tumbo lake.
" Nitakufanya ufe iwapo hutaweza
kufunga mdomo wako, haya Mambo
hayamuhusu" aliubama mdomo wake bila
kujari kuhusu maumivu aliyokua nayo. "
Azraj Badru wewe ni mbwa!!" Salma
alimtukana Azraj akamzaba Kofi la
nguvu Salma akapiga kelele kwa maumivu.
Baada ya hapo Azraj aliondoka na yeye akawa hoi. Mpaka pale Najma
alipokutana nae, hakua na uwezo hata wa kutoa sauti kwani alikua na maumivu
makubwa hivyo alihisi akiongea anaongeza maumivu.
" Saida" alimuita akiwa ameziba mdomo
wake, alihisi kulia na kusikitika kwa
wakati huo, kwa nini waliangukia kwenye mikono ya huyu shetani. Saida alishtuka
baada ya kusikia sauti ya kike ikimuita, alitia macho Yake mbele ambayo yalikua madhaifu kwa wakati huo.
Saida alihisi Kama ndoto, aliweza
kumuona salma mbele Yake, Basi haraka
Sana alimkimbilia na kushika mikono
Yake ili kuhakiki iwapo hakua akiota. Ni
kweli kabisa alikua sahihi, alikua yeye
bila Shaka." Sss Salma!! Saida pia
alishangaa
" Umefika vipi hapa? Mwanao hajambo?
Ulijifungua mtoto gani?" Saida alikua na maswali mengi kwa Salma Alie kua na khofu kua azraj anaweza kumkuta.
" Saida, mwanangu hata sijui alipo, Saida Maisha yangu yapo juu chini,
nilipasuliwa na hapa ni nimetekwa na Azraj, na mtoto wangu sijamuona
kwanzia nimzae, kila siku ananitishia
kua nikiondoka atamuua. Na kibaya
zaidi sipajui hapa!! Saida kwa nini
hatimae ulikubali kutekwa??" Salma
alihisi kulia. Saida pia.
" Salma umewezaje kuingia humu? Kwani
mlango uliachwa wazi??" Kulingana na
Hali Yao ya kukutana katika mazingira
Tata walijikuta wakiongea mada ambazo
ziliwanyima kuelewana kabisaaa.
Mara Salma akashtuka kua hafai
kukutwa humo ndani, haraka Sana
alipata mawazo na kutaka kuondoka. "
Saida acha niondoke haifai kwa Azraj
kutambua Kama tumeonana. Bila Shaka
tutapata wasaa mzuri wa kuongea iwapo
ikiwezekana "
" Salma jamani?" Saida alihisi kulia
" Natamani kuondoka hapa" Saida
alinung'unika Salma alihisi Kama muda
wa kumjibu umeisha alikua na wasiwasi
Sana, hivyo alirejea moangani na
kuachia mikono ya Saida iliyokua
imemshika na kufungua mlango haraka
Sana akatoka. Kama bahati, wakati
anaondoka na kuingia katika chumba
Cha jirani Azraj pia alirejea kwenye
chumba alichokuwemo Saida.
" Lo! Kingeumana iwapo Azraj
angemkuta" Saida aliwaza Hilo na
kubaki amemtazama Azraj huyo
mnayama, kwa nini hakumuelewa
Mustafa hapo kabla? Bila Shaka majuto
Ni mjukuu na bahati mbaya hakuna
dawa ya majuto zaidi ya maumivu.
" Nataka kuondoka hapa Azraj, bila
Shaka nitamshawishi Mustafa amuoe
unachotaka Ila ungeniacha huru
kwanza" Saida alihisi kabisa anapiga
kelele kwenye Banda la kunguru maana
hawezi kumsikiliza. " Ni sawa" Azraj
alimjibu Saida akabaki akimshangaa.
Sehemu ya 166
Alisema sawa hiyo ilimaanisha nini?
Saida hakua amemuelewa hivyo
akatamani kuuliza Tena? " Upo tayari
kwa Hilo?" Azraj alimwangalia huyo
mwanamke mwenye sura nzuri na akili
nyingi, lakini kwa wakati huo alihisi
kabisa ubongo wa Salma umedumaa.
" Unawaza kupita kiasi wewe?" Azraj
alimwambia na kummiminia chai anywe, Saida hakua tayari kabisa kunywa chai.
Azraj hakuweza kumlazimisha.
" Ni sawa ikiwa hutaki kula, kwangu
Mimi sio tatizo Wala Sina hasara binti
Abdul" Azraj alijitupia pale kitandani na
Saida akainuka haraka na kusimama
kando. Azraj alimwangalia kwa jicho la kushangaza. Aliwaza nini?.kwamba
alitaka kumbaka?. Ahaha! Ni vizuri
lakini hata hivyo hakuwahi kumuamini.
" Huyo Mustafa unaesema atanipa nachotaka kikubwa uwe huru kaa ukijua ya kwamba anafahamu' kuhusu uwepo
wako hapa, na anafahamu' kua nimewahi kukubusu kwa lazima. Sema
ndo hivyo amekutelekeza, alitanguliza
pesa na utajiri mbele akapotezea
kuhusu wewe" Azraj alimwambia saida
ambae hakuweza kumwamini hata punje.
Baada ya kuona sura ya Saida ikiangalia
pembeni Azraj aliamini kabisa
mwanamke huyu hajamwamini.
Alimuangalia Saida alivyokua amekonda
Kama mfuko wa mifupa. Duh!
Mwanamke huyu aliwahi kua mwanamke
mzuri Sana na wa kuvutia kupita kiasi
Ila inashangaza amekua mwembamba
ghafla. Ameng'aa Sana kwa kua
aliwekwa ndani lakini Ni Kama
amepoteza nuru machoni.
" Saida, wewe ni mzuri Sana moja kwa moja yaani. Ila ulikosea maishani
mwako kuolewa na kiumbe ana itwa
Mustafa hakuwahi kua na mapenzi ya
dhati mwanaume yule, fikiria hata
hakuwaziii" Saida alichoka kumsikiliza.
" Ni sawa iwapo Mimi namuwaza, Ni mwanaume ambae nampenda kushinda ukweli wowote unaokuja mbele yangu"
Saida alimwambia bila kupepesa macho
akimaanisha, Azraj alihisi kumpiga lakini
atasema nini?
" Mmh!! Endelea kumpenda, lakini
hautarejea kwake kamwe" Azraj
alimwambia na kuinuka aondoke zake.
" Haijalishi, kikubwa ndani ya nafsi
yangu nitakufa na jina Mustafa, inatosha kabisa, iwe ananipenda au laa,
Mimi nikimpenda hiyo inatosha, sio
Kama sifahamu kua ulikua mpango wako
kumfanya mume wangu amue khairat
yule mchawi mwenzio, wewe ni muoga
Sana Azraj unapenda kutumia wanawake
Kama ngap na nyenzo za kufanyia
maovu, unazidiwa hata na walinzi wako, kwa hakika huna maana!!" Saida
alimsema awezavyo Tena kwa hasira.
" Uuwewe!!! Azraj aligeuka na kumfata
alipo, Saida Mara hii hakuweza
kushtuka kwani alimzoea kwa Tabia
hiyo. Alibaki kasimama wima akisikiliza maumivu mkononi mwake.
" Sikuwahi kua muoga Saida, Mambo yote haya kasababisha mwenyewe, alinidhurumu kila kilichostahiri kua
changu, baba pia alimpendelea yeye
mama yangu akiwa hai, kwa ajiri ya
mama Yake, mama yangu alikua Hana
maana kwa baba mwisho kifo
kikamkuta, na kwa sababu yake, Mimi
naonekana kua mdogo ilhali namzidi
mwaka mzima na nusu Ila bado
imenibusi kurejesha umri wangu chini ili
niishi Kama Badru, ni makosa yangu
kuzaliwa na bwana Rashid, ufuska na
uzinzi alioutanguliza mbele ndo vitu
vilivyomponza huyo bwana Rashid, na
kuyafanya Maisha yangu yawe zaidi ya
mbuzi" Saida alibaki akimwangalia bila
kumjari, wakati huohuo Azraj alijikuta alidondosha chozi. Na kuzidi kuongea ..
" Laiti Kama ningepata kile ambacho nastahili kutoka kwa watu wa Badru, nisingefikia huku Saida, Ni mtu gani
asiependa kuiona familia Yake ikifurahi na kuishi kwa amani, lakini Mimi
walinipa tabasamu la juu juu bila haki yoyote, sijawahi fanyiwa Cha maana
katika familia Ile, siku zote
wamenifanya kua wa kando tu. Ndo
maana sikua na namna zaidi ya kutafuta
haki yangu kwa nguvu, siku zote wao
wamemtanguliza Mustafa zaidi katika
haya Maisha. Baada ya Mustafa akawa
muksin, ahahahhah!! Saidaaaaa mpaka
hapo huelewi bado machungu yangu,
Mimi pia Ni kijana wao, lakini
walinibagua moja kwa moja hawakunipa
nafasi yoyote Ile" Saida alimuonea
huruma kidogo Azraj alipokua
alidondosha machozi na kuona kweli
hakutendewa haki. Alifaa kupewa
kipaumbele chochote pia Ni Kam vile
alitelekezwa! Saida aliguswa na hali yake.
Kisha akakumbuka Jambo. " Azraj Sina
uhakika sana, lakini nahisi ulianza
kufanya Mambo ya kiovu zamani,
huwezi kumiliki kundi la wauaji na watekaji katika haya Maisha muda
mfupi tu, nahisi walikua watu wako
tangu muda mrefu', na bwana Rashid
Ni mfanya biashara mkubwa alievuka
Mito, milima na mabonde, hivyo
anakuelewa zaidi ya mtu yeyote, huenda alikutambua kabla ndo maana
hakutaka kunipatia nafasi yoyote katika
urithi, Ila hakukunyima nafasi katika
kampuni, na mwisho we uliweza kumiliki
kampuni ya habari na matangazo kupitia
yeye, una pesa za kutosha kufanya
Maisha yako unayotaka, una nyumba
kadhaa ambazo unaweza kuishi bila
kuwaza, kwa sababu ukipata kutoka
katika familia ya Badru, ukisema
hukupewa chochote unakua sawa na
mwanaume asie ridhika na binadamu
asie na shukrani, bi Shayma
alikutanguliza mbele zaidi ya Mustafa, hakika inauma kiasi gani kuona
umewageuka." Saida alinyamaza na kupoteza huruma aliyokua kamuonea
Azraj asie na shukrani. Bila Shaka mtu
huyu Hana maana kabisa
" Wewe ni mwanamke wa Mustafa, bila
Shaka ulimezeshwa sumu nyingi dhidi
yangu, hivyo hata niseme nini? Siwezi
kueleweka kwako" Azraj alibana machungu yake na kuondoka zake
kimya. Hakuweza kubishana Wala kujibizana nae Tena.
Saida aliingalia chai pale mezani na kitafunwa kilicholetwa, aliweza tu kukaa na kuanza kutumia, Hana namna hata
hivyo lazima ale ili aishi, bado anao
watoto wawili wanamngoja, bila Shaka
Mustafa atamuokoa siku moja, iwe
Sasa au baadae.
Azraj baada ya kutoka chumbani
aligongana na mgeni sebureni. Alikua Dr
khairat ambae alijaribu kusalimiana na
Salma Salma akampuuza. " We
mwanamke sikuwahi kujua Kama
unadharau kiasi hicho" dr khairat
alimwambia Salma Azraj akamsikia.
" Ni haki Yake kua na dharau, hata
hivyo yeye ni mwanamke wangu Mimi"
Azraj aliufungua mdomo wa Dr khairat
ambae alikua akilala na huyo mwanaume
pia, Ila bado hakuona aibu kusema
Salma Ni mwanamke wake.
" Koma, ilikua bahati mbaya nikawa
mwanamke wako!!" Salma alitoa maneno
ya simu kumuelekea Azraj ambae alikaa
kimya. Kweli huyu mwanamke hapo
kabla alimpenda Sana Tena alimpenda
kwa dhati, na yeye alichezea nafasi
hiyo, na hata kusababisha chuki
kumjaa.
" Khairat karibu" Azraj alimkaribisha.
Dr khairat ambae aliweza kukaa kwenye
meza ya chakula na Azraj akakaa pia.
Salma alikua amekaa kwenye sofa yaani
mbali nao, Ila alipowaona karibu
aliinuka maksudi tu na kuwafata,
alitembea kuwapeleka Kisha akaenda
kulalia mapaja ya Azraj. Kitu hicho
kilimshangaza Azraj Sana.
" Wewe" Azraj alitamani kumfokea Ila
kwa Sasa hataki kuyafanya Mambo kua
makubwa aliweza tu kunyamaza. .
" Hata hivyo Mimi ni mwanamke wako, unafaa kunivumilia hata nikikukalia
nikiwa uchi" Salma aliongea
akimwangalia Dr khairat.
" Bila Shaka huwezi!! Dr khairat
alimwangalia hapo Salma akawahi
kuongea. " Ooh siku hizi mnafanya kazi
ya kukulana nyie wawili ndo maana
unahisi wivu kwenye koo lako, usijari
Sina hamu na mnyama Kama yeye" dah!
Salma alikua na maneno makali lakini
hakuna uongo aliosema hata hivyo.
Azraj aliweza kuinuka hapo Salma pia
alilazimika kuinuka. Azraj alihisi Kama
itakua tatizo kuongea na Dr khairat
huku wakiwa nae hapo, aliweza tu
kumbeba Salma na haraka Sana
akaongoza njia kwenda nae katika
chumba chake. Alimuweka huko na
kutaka kumfungia.
" Tulia hapa, dr khairat akiondoka ntakufungulia mlango" Azraj alimwambia.
" Nakuchukia Sana wewe ni mbwa, wewe ni ibilisi, inatosha zaidi ya
volkano nyoka wewe" Azraj majina yote
hayo hakuwahi kuyapenda lakini kwa
Sasa alishayazoea, bila Shaka Salma na
Saida wangemuita vile watakavyo. Hata
hivyo mtoto wake amekaribia
kupatikana atamfanya Salma atulize mdomo wake na ata deal na mtoto tu.
" Nimerejea" alikunywa Maji kwenye glass Kisha akamwangalia Dr khairat.
" Inaonekana huna bahati ya kupenda
mwanamke mwenye ulimi msafi Azraj??
Dr khairat alihisi kusikitika.
" Ahh kawaida" Azraj Hilo halikumuumiza kichwa.
" Aah', naenda kwenye point Azraj" dr
khairat aliushika mkoba wake na
kuchomoa picha aliyopewa na Nevi Jana
Yake. Azraj aliipokea na kuitazama
akabaki ameduwaa na kushtuka kwa
wakati huo." Uuwewe!! Hii picha ulii
uliiokota wapi?"
Dr khairat alitabasamu Kisha akichukua
kutoka kwa Azraj na kumueleza. "
Angalia kwa Makini, bila Shaka huyu ni kijana unaemfahamu" Azraj alitikisa
kichwa na kuanza kueleza bila kusubiri
huku akionyesha masononeko kwenye
Koo lake.
" Yeye ni Nevi, kijana wangu, alikua shupavu na mwaminifu kwangu, alinitendea vile ambavyo nafsi yangu
iliridhishwa nae, Ni kijana aliekua na nguvu na hakuwahi kua muoga, sikua
nimekaa nae kwa kipindi kirefu lakini
nilimuelewa Sana Nevi, inasikitisha ya
kwamba vitu vizuri huwa havidumu
kabisa" Dr khairat alishangaa hakuwahi
kumuona azraj akimsifia mtu namna
hiyo.
" Natamani Angekua hai, nilipoteza
mashujaa wawili kwa uzembe wangu
mwenyewe, bila Shaka Nevi au Bwasha
wangekua hapa, nisingekua nasota
namna hii, tayari ningemmiliki Mustafa
na familia Yake mikononi mwangu, na
hata binti yangu angeshapatikana, kwa
Hawa vijana ambao mpaka Leo hii
hawajampata, hii Ni sawa na kipande
Cha keki kwa nevi au Bwasha" Azraj
alijaribu kuyazuia maumivu ambayo
yalimpungia mkono na kumuacha
mwenyewe.
" Unaposema alikua, angekuepo, Ni
Kama unamzungumzia mtu aliekufa
Azraj, ilhali mtu huyu yupo hai??
Azraj alishtuka yupo hai? Nevi yupo
hai? Huyu Dr khairat ana masihara ya
nje nje, hawezi kua hai kabisa?
Walikufa kwa Moto baada ya kuangukiwa na ukuta wa Moto. Nevi
aliwezaje kuponea na kuishi kwa
pamoja? " Hiyo haiwezekani, walikufa
mbele yangu yeye pamoja na Bwasha"
Azraj alimwambia Dr khairat ambae
hakuweza kukubaliana nae.
" Hapana Azraj, niamini Mimi, huyu kijana yupo hai, na aliweza kunisaidia'
Mimi kuziba pancha ya gari langu, baada ya kunifananisha Kama
aliwahinkutuona Mimi na wewe tukiwa
pamoja, na akasema kua anakutafuta
Sana, mlite Hana baada ya ajari
mbaya, Ila anataka kua kando yako
Kama kijana wako muamifu siku zote"
dr khairat alimwambia azraj ambae
aliruka kwa tabasamu.
" Hivi unaweza kua kweli, nevi bado yupo hai? Nevi bado ana ishi? Hakika
hii ni habari njema, itabidi nimtafute, hakukuachi hata namba za simu na jinsi ya kumpata" aah' kwa kweli Azraj
anajitafutia matatizo. Maaana nevi Ni
sawa na mwisho wake mpya.
Sehemu ya 167
" Aliniachia kadi" dr khairat alimpatia
Azraj kadi aliyopewa na Nevi. Azraj
alifurahi alitamani kumbeba juu Dr
khairat kwa kazi kubwa aliyofanya.
" Nashukuru Sana khairat, nashukuru
Sana kwa hiki ulichokifanya." Azraj
alimshukuru
" Sio inshu kubwa, hata hivyo sikua
nimemuamini kabisa, sikuweza
kumuelezea iwapo nakufaham wewe"
" Sio kosa lako, we ni mwanamke Makini
Sana" alimaanisha sio rahisi kumuamini usie mjua.
Wakati huo huo Dr khairat akakumbuka
shida Yake pia . " Azraj ki ufupi na Mimi Nina tatizo" Dr khairat
alimwangalia Azraj aliekua na tabasamu la kumpata nevi.
" Tatizo lipi?" Bila hata kumtazama
usoni alimuuliza. Dr khairat alijihisi
kutengwa. " Aahh, Ni kuhusu hizaan, yeye yupo hospital amelazwa haijulikani atakua hai au la, lakini Kuna mtu
anatumia account Yake kunitishia
amani" dr khairat alizungumza kutokana na mashaka yake.
" Hiyo inawezaje kua? Bila Shaka sio
sahihi ukiachilia mbali familia Yake Dr
Hizaan alikua na mtu gani mwingine
ambae angetumika kukulipizia wewe
kisasi chake" Azraj alipata Shaka
kidogo.
" Sifahamu, lakini natumai utamfahamu
mapema tu. Kwani wewe na Mambo ya
mtandao Ni mtu na baba yake'" Dr
khairat alimwambia Azraj bila
kuchelewa.
Azraj alitafakari Sana kuhisi Dr hizaan
Wala hakuweza kupata jibu. Ok alimpa
matumaini Dr khairat kua lazima atajua
tatizo liko wapi?
" Sawa nakuamini" dr khairat aliweka
matumaini yake kwa Azraj hata hivyo
Hana mtu ambae amebaki nae Kama
tegemeo zaidi ya Azraj na mali alizopewa na Mustafa.
" Vipi kuhusu Yule rafiki yako'
mwanasheria, mbona siku hizi sipati
taarifa zake?" Azraj alipata khofu.
Dr khairat pia alikumbuka kua ana siku
kadhaa bila kuwasiliana nae na haelewi
kwa Nini alipotea ghafla baada ya yeye
kuachwa na Mustafa. " Mmh!
Mwenyewe sielewi hapa, Kuna siku
bwana Amiri akisema kua anamuhisi
vibaya" Dr khairat alidumkiza kipande
Cha tango mdomoni bila hata wasiwasi.
" Wewe!!, Unao wazimu, uliwezaje
kukaa na mtu ambae boss wako ana
Mshakia??" Azraj alihisi kuvurugwa.
" Usikhofu, Shaka yetu ilikua sahihi
japo tayari alituchoma lakini kwa Sasa
Hana muda kwani tayari
anashughurikiwa" dr khairat alizidi kula
tango. Khofu take ya mwanzo ilikua kumpa Azraj wasiwasi tu.
" Uppff" Azraj alipumua " hapo sawa, lakini nataka nimuone nimpe funzo la dunia" azraj alitamani amuue hata
akiwa maiti. Alikaa kwenye kiti na kumnyakua Dr khairat kipande Cha
tango alilokua kadumkiza mdomoni mwake.
" Wewe!!" Dr khairat alitoa macho.
Azraj akapenda pozi lake na kumbusu midomo Yake. Dr khairat alitabasamu.
" Nahisi Kama nakutaka" Azraj alimtania.
" Si ufanye kwa ustaarabu Sasa" dr khairat alilinga.
" Mmhh, ustaarabu gani we mwenyewe
unataka" Azraj hakusubiri Dr khairat
awe tayari kwani huyu hakua Salma
aliweza tu kuushika mkono wake na dr
khairat akajiinua kwenye kiti na kuongozana nae chumbani.
Siku nyingine Tena majira ya saa nne
za usiku familia ya bwana Amiri ilikua
mezani ikipata chakula. Bwana Amiri
hakuonekana kurejea kwa wakati huo
Hadi mke wake na watoto wake
wakapata khofu.
" Hamna haja ya kumuwazia baba, sio
Mara moja kwake kuchelewa kurejea
nyumbani'" Maulid alikaa zake mezani
na kupata chakula.
" Hukuwahi kua na moyo kabisa, bahati
mbaya iliyoje nikazaliwa tumbo moja na
hii mbuzi" Afsat alisononeka na kuinama
karibu na mtoto aliekua akichezesha
mikono Yake kwenye tenga dogo la kubebwa mtoto.
" Azmina! Mambo" aliweza kumbusu na kuendelea kula. Alishtuka baada ya kukutana na macho ya Maulid kwa
.mara nyingine. " Unakichaa, utaniangalia hivyo mpaka saa ngapi?"
Afsat alichoshwa na tabia ya Kaka
Yake.
" Hamuwezi kuishi kawaida kwani?
Mbona niliwazaa kwa masaa tofauti
Sana!" Bi Azat alihisi kulia kwa vihoja
vya watoto wake mwenyewe. Hata hivyo
ana wasiwasi Sana na mume wake
ambae hajarejea mpaka saa hii? Hata
hivyo mume wake ni mwanaume mtulivu
na anae yajua mahaba hafai kumhofia kabisa.
" Mama mbona hujari kuhusu Mimi
kabisa, Afsat kaweka pilipili kwenye
kachumbari!!" Maulid alihisi kulia huyu
mwanamke anafahamu' kabisa kua yeye
Hali pilipili lakini bado aliweka pilipili
kwenye kachumbari.
" Aahh!! Huyu ana wazimu, alitaka Nile
kachumbari isiyo na pilipili. Bila Shaka
ningekufa na kiwewe, Kama huwezi kula acha "
" Usinijibu vibaya mi Ni Kaka yako bado. Kwa nini nahisi kuichukia sura
yako ya kiume kila nikiitazama. Bora
ningezaliwa pekee yangu tu. Mwanamke
mwenyewe hujari kuhusu Mimi kabisa"
Afsat alichukizwa nae alikua na sura ya
kiume? Aliinuka haraka na kwenda
kufinya masikio yake' mabaya Kama
punda. Alivuta hayo masikio mpaka
Maulid akahisi kupiga kelele. Bi Azat aliweza tu kuchukua sahani lake la chakula na kuhamia sehemu nyingine. Amechoshwa na hao wazimu wawili.
" Unathubutu kusema Mimi Nina sura ya kiume. Ungepata wapi ujasiri wa kuniita dada, nyau wa kirusi wewe!"
Afsat alienda zake kukaa na kuendelea
kula taratibu. Maulid aliugua kila
alipotamani kachumbari yake na kuona
Ina pilipili, aliweza tu kuichukua na kuimimina kwenye pipa la takataka.
Bora wakose wote kuliko kumuacha
Afsat afurahie pekee Yake.
" Aaaaaaaaahhh... Mama mi ntaua mtu
siku moja" Afsat bila kutafakari
alijikuta akilia Sana na kusababisha
kilio kwa mtoto mdogo aliekua pembeni
Yake. Maulid alimnyanyua mtoto na kutokomea nae mbali kabisa na huyo
mwenda wazimu wa kike.
" Na akija baba namwambia ulichokifanya" Afsat alibaki akilia bila msaada.
Wakati hayo yakiendelea Nevi alikua
amesimama nje ya nyumba hiyo huku
akiwatazama watu wa familia hiyo
kupitia mwanga wa taa. Alijikaza
kuwaangalia watu hao akiufikiria mpango alionao juu Yao.
" Bado unasoma ramani nyumbani
kwangu" sauti ya mwanaume nyuma
Yake ilisikika. Alikua mwanaume wa makamu ambae alionekana kumfahamu
alikua tu ametoka kushuka kwenye gari
Yake nyeusi ya kifahari akiwa
ameshikiliwa fimbo ndogo nyeusi. Alikua
mkakamavu kwa kumtazama kutokana na mwanga hafifu wa taa uliomulika
kutokea kwenye Kona za fensi ya nyumba hiyo. Nevi alirekebisha kofia take Kisha akajibu.
" Samahani bwana mkubwa nitaondoka hivi Sasa" Nevi hakuweza kukaa hapo
Tena aliondoka zake kimya. Bwana
Amiri alitikisa kichwa na kuingia ndani ya nyumba Yake huku dereva wake
akiingiza gari Yake kimya kimya.
Kwa juu kabisa ya nyumba hiyo Maulid
alifanikiwa kuona tukio kilitokea hapo
muda mfupi. Yaani Ni kwamba Kuna mtu
alikua akiwachunguza wao na baba
yake' alimkuta Ila aliweza tu kumuacha
aende zake. Alipata hisia Hadi dhidi
Yake.
" Hakikisha unatenda mema kwa ajiri yako na Badru pia, unatambua thamani
kubwa ya kua mwana halali na mwana
familia wa Badru sio" sauti ya kike
ilipenya vyema kwenye masikio yake'
bila Shaka sauti hii Ni sauti bayo amezoea kuitii. Lazima atii.
" Wewe sio wa Badru, usiishie kujirahisi
kwa kila wanachokwambia ufanye siku
moja watakupiga teke Kama mvu asie
takiwa bila kutarajia, itabaki huna jina
la urithi na utakumbuka kua baba yako
hakua wa ukoo wa Badru" maneno hayo
yaliuvunja moyo wake kimya kimya
alipokua akirubuniwa na mtu huku
akimtaka atumie madawa ya kulevya.
Hakika hawezi msamehe mtu huyo hata
kwa bahati mbaya.
" Unafaa kuisimamia Sana na kusimama
imara Kama bwana mkubwa kutoka
familia ya Badru Mustafa, haswa
Maulid, Ni kijana ambae atakuja
kukupa mtihani hapo baadae kwa kua
atakutana na washawishi wengi Sana
watao mrubuni kupitia jina lake la ukoo
kwa kua yeye sio Badru ki
uhalisia......" Maulid alikumbuka kua
alidokoa mazungumzo Kati ya mjomba
wake na Mustafa. Kwa kweli walikua
wakiwatunza na kuwajari vyema yeye na
dada Yake tangu walipozaliwa na hata
walimuokoa kutoka kwenye uraibu wa
madawa ya kulevya, kwani Angekua
mgeni wa Nani leo? Mwisho wa siku
aisaliti familia ya Badru, hapana Hilo
Ni Jambo lisilo wezekana. Na kwa
hakika Kuna namna fulani hataki kuamini
lakini Ni ukweli kwamba baba yake' haonekani kua mwema kiasi Fulani. Na
ana Mambo kadhaa ambayo siku hizi amekua akiyatilia mashaka.
Akiwa hapo alisikia sauti za vicheko
vikendelea kwa watu ambao ni kama vile
walikua wakitembea. Bila Shaka alikua
Ni baba pamoja na mama yake. Hakua
na jinsi zaidi ya kuelekea chumbani kwake.
Asubuhi aliamka mapema Sana kuliko
alivyotarajiwa. Hiyo ilikua Ni kwa
sababu makelele ya mtoto aliekua
akibembelezwa ayakuweza kukata. Na
mbaya zaidi kelele hiyo aliisikia kwa
karibu zaidi kana kwamba mtu aliekua
akimbembeleza mtoto alikua karibu
Yake zaidi.
Alishindwa kukaa na kuamua kwenda
bafuni moja kwa moja. Baada ya kutoka
bafuni alisikia sauti ya mtoto ikizidi
akaamua kufungua mlango.
Lo! Alikua mdogo wake Afsat huyu
mjinga inamaana hakujua Kama hapo ni mlangoni kwake? Maulid alikata tamaa.
" Hivi wewe!! Ikitokea siku umeamka na akili timamu, Kuna kitu kitapungua
kwenye Maisha yako?" Swali Hilo
lilimuelekea Afsat moja kwa moja na Wala hakumjari alizidi kuzungukia eneo
Hilo hilo
" Afsat ondoka hapa, nahisi kukulamba
makofi mapema tu" Maulid alimwambia
afsat akaanza kupiga kelele.
" Baba kwa nini maulid ana makelele
hivyo. Anaongea kwa kugomba Hadi
mtoto anaogopa. Nyamaza Azmina.".
Afsat hatimae aliamua kuondoka eneo
Hilo akiwa anambembeleza mtoto wa Azraj. Maulid alichoka.
" Badala ya vitu vyote vizuri kunipenda
Mimi katika huu ulimwengu, naishia
kupata dada mjinga asie na akili Kama
huyu"
Akiwa analalamika juu ya ndugu Yake
alimuona baba yake' alitafuta Kona kwa
mbali ili aweze kuzungumza na simu.
Asingemtilia Shaka iwapo baba yake'
asingekua ana geuka huku na kule
kujificha ili aongee na simu. Ni
nyumbani kwake hapo lakini bado alikua
akii, alikua akijificha kuongea.
Hilo haliingii akilini. Maulid taratibu
alisogea kimya kimya alimfata baba
yake' ambae alijitenga zaidi kwenye balcony. Kwa wizi akawa anamsikiliza.
" mtoto wako makosa njia ya kukupatia, unadhani ni rahisi Sana kwangu Mimi
kumuondoa mtoto hapa, ikibidi uachsne na suhara la mtoto, kwani hapa si analelewa vyema tu" Maulid alishtuka
na kupata jawabu moja kwa moja. Hiyo
simu ya baba yake' lazima mtu wa upande wa pili atakua
' Kaka Azraj, hiyo Ni ngumu jamani, kwani baba anafahamu' wapi Kaka
Azraj alipo?, Hiyo inamaanisha hata
uwepo wa Shem Saida anafahamu' pia?
Anafahamu' Shem Saida atakua wapi?'
Maulid aliziba pumzi zake kwenye fikra.
Ni Kama vile moyo wake ukimuuma Sana
hivi aliekua akizungumza na Azraj alikua
baba yake'?? Yawezekana sio kweli
amechanganyikiwa.
" Huyo Nevi Jana alikua Aki spy
nyumbani kwangu kizembe Sana, Sasa
kwa mfano mtu yeyote kutoka familia
ya Badru angemkuta hapo ingekuaje?
Ana bahati kwamba Mimi ndo nilifika
pale mapema mwambie aache uzembe,
sitaki kua mashakani kabla sijafanikiwa
kumilik kitu Cha thamani kutoka katika
familia ya Badru"
Maulid alihisi kunyeshewa mvua.
Inamaana baba yake' Ni kweli hakua
mtu mwenye Nia nzuri na familia ya
Badru, inaumiza Ni familia iliyompa
thamani baada ya kumuoa mama Yao??.
Sehemu ya 168
Katika fahamu na fikra zake anaamini
kabisa kua baba Yao asingekua
chochote bila Badru. Lakini kwa
inavyoonekana Ni wazi kabisa anaisaliti
familia ya Badru yawezekana kabisa
hisia zake zilikua Sawa.
Aliona baba take amemaliza kuongea na
simu akaamua Kuondoka zake kimya
kimya asigundulike Kama kapata hisia
mbaya kwa baba Yake. Lakini ki ufupi
aliamua kua atamfatilia awezavyo
haijalishi itakua mgumu kiasi gani? Ila
hata yeye lazima atende Jambo kwa
ajiri ya familia Yake.
Huku kisiwani Saida aliugua msongo wa
mawazo na kujikuta anapoteza fahamu
kabisa. Ulikua mgumu kwake yeye Kama
binadamu wa kawaida kufungiwa ndani
muda mrefu vile. Kwa kweli hakua
anaelewa kwa nini Azraj hayupo tayari
kumuachia mbona anamuumiza hivi.
Azraj alishtuka baada ya kuingia
chumbani kumletea kufungua kinywa
akakuta saida amelala bila kujitingisha.
" Saida" akipata mshtukk na kuweka
kiamsha kinywa mezani haraka Sana
Kisha akasogea kumkagua akagundua
kwa kweli Saida amepoteza fahamu
zake kabisa.
" Saida amka" aliogopa na kufungua
mlango haraka akamuinua na kumtoa
ndani ya chumba akampeleka sebureni.
Wakati huo huo aliweza kumuita Dr
khairat aliekua kalala chumbani kwake
na nightdress
" Azraj Kuna nini asubuhi hii!! Hujui
Kama usiku ukinichosha" aliongea kivivu
akiwa na lengo la kumkomoa Salma
iwapo yupo karibu asikie. Salma alikua
na stress zake Wala hakua anajua
Kama Saida katolewa chumbani alipokua
kafungiwa na kumpelekea sebureni
maana yeye alikua katika upande
iliyojitenga na. Chumba alichokua Saida
alikua tu akimuwaza mtoto wake na
kuhisn labda atakufa siku moja bila
kuiona hata sura ya mtoto wake mzuri.
" Acha upumba** hujui Kama Saida
yupo mahututi!!" Azraj alifoka Dr
khairat akashtuka na kuhisi hasira kwa
wakati mmoja huyo mwanamke Saida.
Kwa nini kila mtu anajari kuhusu yeye
hata yeye hawamuoni wa thamani
kabisa.
" Acha kuchelewa twende
ukamwamgalie" Azraj alimkokota mkono wake hapo ndk Salma akaelewa ya
kwamba Saida alikua amepata na shida.
Alihisi kushtuka na bila kufikiria kua
anatakuwa azingatie hatua zake
akitembea kwa sababu ana mshono
AMBAO bado haujapona. akajikuta
anakimbia kuelekea huko chini
walipoenda WAWILI hao.
" Azraj mbona unafanya ionekani Kama
mtu huyo anakata roho!!" Dr khairat ki vivu na kinyonge alihisi huzuni.
" Yeye ni wa muhimu Sana khairat, hujui Mimi kitatokea kwetu sisi iwapo
mwanamke huyu atakufa, fanya haraka
Sana umtibu na ujue anatatizo gani? La
sivyo utanitambuw" Dr khairat aliwaza
kumuua Saida akiwa ana mtibu
haiwezekani Azraj amjari Saida kiasi
hicho! Lakini Sasa atamuua vipi? Dahh!!
Inakera kwa nini awe Saida kwa kila
mmoja.
" Harakisha " Azraj alimuharakisha Dr
khairat akawa Hana namna zaidi ya
kuchukua vifaa amba yo viliandaliwa na hapo akaanza kumkagua kwanza.
" Saida!!!" Salma alipiga kelele kwa
mshtuko na mshangao wa kinafki kana
kwamba hakua akiufahamu uwepo wa
Saida hapo.
" Azraj Saida kufika vipi hapa??"
Salma aliuliza kwa hasira Azraj
akamsogelea.
" Tulia ujue haya...." ki ufupi Azraj
ana hisia kidogo na Salma na haelewi
iwapo alikua akimpenda tangu zamani au
ni hivi Sasa. Kwa Sasa anajikuta
anamuonea huruma na kuogopa
kumuumiza.
" Usithubutu kunigusa Bastard!!" Salma
alitoa macho makali Dr khairat akahisi
kucheka huyu mwanamke anajitafutia
kifo kwa jinsi Azraj alivyomkatili alafu
kana mtukana.
Azraj alihisi kuumia baada ya kuiona
hasira Yake Ila hakuacha kumgusa,
alimshika kwa lazima na akapitisha
mikono Yake tumboni amkumbatie.
" Hivi unaweza kuniacha Mimi wewe!!"
Salma alinung'unika Azraj hakua tayari
kwa Hilo. Kwa wakati huo alihisi kabisa
moyo wake ukidunda kwa kumkumbatia
Salma nyuma kj ufupi alijishtukia maana
mwili wake kidogo ulisisimka Sana
tofauti na akiwa Dr khairat hii Ni
hisia?? Hakuweza kuelewa lakini kadri
Salma alivyozidi kufurukuta ndivyo
alivyokua akizidi kumpa tabu mwanaume huyo. Alijikuta hasikii hata kelele zake
hiyo inamaanisha nini jamani, mbona hakuwahi kuhisi hivyo akiwa nae hata siku moja.
" Azraj Ni lini na siku gani utaacha
unyama, mbona unatisha Sana?,
Unaweza kufanya kila unachoweza lakini
kwa nini umemteka Saida na kumleta
hapa? Binti wa watu aliwahinkukosea
nini? Tangu mwanzo unamuandama
Sana" Salma alilalamika bila kujua
Azraj hakua hata akimsikia.
" Aah' we mwanamke nyamaza nahitaji
kuongea nae" Dr khairat alimkanya
Salma ambae alipandwa na hasira, alitamani kumtema huyo mwanamke
kutoka kwenye kuraza zake za ubongo
iwe Kama hawakuwahi kukutana kabisa
lakini atafanya nini Sasa. Macho Yake
yalishaichukua hiyo taswira na ubongo
wake umeinakili.
" Azraj hajambk hivi Sasa" Dr khairat
alimwambia Azraj ambae alirejea
kwenye fahamu zake na kumuachia
Salma Kisha akamsikiliza Dr khairat.
" Hapo sawa, ataamka baada yamuda gani?" Alitamani kufahamu.
" Hauchukui muda Ila amejawa na stress, aliendelea kupata stress
anaweza kujiua baada ya kuathirika kisaikolojia"
Azraj alihisi kuchanganyikiwa, hivi kwa
nini Mustafa sio muelewa Kama
angemsikiliza mapema bila Shaka haya
yote yasingejitokeza, itabidi afanye
Jambo kabisa la kumkumbusha Mustafa
kua Saida yupo mikononi mwake. Hataki
Saida amfie bila fahida yeyote.
" Sawa nimekuelewa we nenda" Salma
alijaribu kusogea karibu na alipolala
Saida akiwa na macho ya huruma juu
Yake. Azraj alimtazama huyo
mwanamke na kugundua kua ana moyo
Safi na mnyenyekevu.
Majira ya usiku wa siku hiyo Mustafa
akiwa amelala chumbani kwake usingizi
haukuweza kupita aliwasiliana na Nevi
ambae alimwambia ndo anaelekea
kazini.
" Asante nevi, hakikisha unafanya kile
ambacho unastahili Kama mwanaume, hakika ukifanikiwa, nitakupa zawadi
kubwa maishani mwako" Mustafa alimpa
ahadi nevi kijana mdogo wa kambi ya
Badru.
" Sawa Bwana mkubwa, huo Ni wajibu
wangh sihitaji zawadi inakua Kama
rushwa kwa sababu hata wenzangu
hufanya kazi zaidi" Nevi aliweka
tabasamu na kuondoka zake kimya.
Mustafa aligeuka na kukitazama kitanda kilivyo kitupu na kimejaa ukiwa, Ni
kitanda ambacho walizoea kujirusha na
kujiachia kadri wawezavyo yeye na
Saida. Wakati mwingine na watoto wao.
Nyakati hizi zilikua nyakati Safi Sana
kwenye Maisha Yake na kamwe hawezi
kuzisahau. Lakini inashangaza Sana ya
kwamba kwa Sasa zimekua Kama
kumbukumbu tu.
" Mke wangu" aliweza kuuvuta mto
ambao Saida alikua akipenda kuuegemea
ili alale. Alikumbuka kua alikua
akimkera Saida Basi Saida Kama
hajisikii kuongea nae atachukua tu mto na kutegemea alale bila kumsemesha.
Hata angemsemesha vipi Saida
angemjibu mikato tu. Kama vile sawa' haya' sawa' Basi yeye angechukizwa na kufoka Sana ili Saida aongee. Hata
angeuvuta mto wake na Saida
angelaumu Sana.
Katika nyumba ya bwana Amiri majira
ya usiku huo huo alikua ametoka nje ya nyumba na akachelewa kurejea.
But Azat alionekana kuchanganyikiwa maana hakua akimuona mwanae wa kiume pia.
" Afsat Kaka yako ameenda wapi?"
" Mama acha nae, anajikuta mkubwa
siku za karibuni" afsat alijibu bila kujari.
." We ni mshenzi kilimkuta Jambo baya kwa mfano"
" Hakuna baya litamkuta anajikuta
mkubwa Sana yule, India Shaka mama
yangu njoo tu umchukue azmina umpe
chakula na umbadili.nepi nataka kwenda kulala" aliongea huku akipakia vipande
vya tango vilivyokatwa kwa mfumo wa matairi kwenye uso wake.
" Wewe kwa Sasa nj mwanamke, hata uliwahi kumtamanj Yasir Sabodo
mchumba wa Muzda jifundishe pia" Bi
Azat alimjibu bila kujari.
" Mama mi nawezaje kumshika neoi
zake" afsat alijionea huruma mikono
Yake
" Basi muite Maulid aje ambadili" afsat
alichanganyikiwa.
" Sawa tu, na hata.sielwi huyo mshenzi
Yuko wapi?" Wakati wao wanawaza
Sana juu.ya Maulid Maulid alionekana
kua amelala kwenye eneo ambalo
kilionekana kutembea kutoka eneo moja
kwenda eneo jingine. Ilikua Ni wapi
yupo maana alionekana amejibana Sana.
Aliweka sikio lake vyema na Makini
akisikiliza sauti za watu waliokua
wakiongea mle ndani.
" Huyu binti Ni mshenzi Sana hawezi
hata kunipa like nachotaka na Nina
uhakika kabisa anafahamu' Mambo
mengi" ilikua sauti ya baba yake' kabisa.
" Mkuu yeye ni mwanasheria mdogo tu, nadhani hamfahamu kweli Kama
anavyodai, Mustafa sio mjinga
kumuamini mtu mdogo Kama huyo"
" Acha ujinga Lilian Masele sii
mwanasheria mdogo tu, hujui historia
yake kwanza yeye sio mwanasheria wa kawaida, ndo maana Mustafa alimuamini
Sana.
Hapo Maulid akaelewa kabisa bila
Shaka Kuna mtu amechukuliwa mateka
huko. Lazima afate nyuma ili afahamu
Ni mtu gani huyo kwanza. Na akiweza
amtoroshe ili afelishe mipango ya baba yake'
Sehemu ya 169
Safari iliendelea mpaka akiwa kwenye
buti katulia kimya, maulid alihisi Kama
gari imesimama ghafla akajigonga kidogo na kutoa sauti. 'Ai'kisha
akashtuka na kujituliza
Bahati nzuri bwana Amiri na dereva
wake hawakupata mashaka yoyote Kama
Kuna mtu anawafatilia. Muda kidogo
gari iliendelea na safari na hiyo ika
hauweni kwa bwana mdogo maulid
Badru. Uhuu! Alipumua. Baada ya
masara kuchukua muda wake gari
ilisimama hatimae.
Kwa kua maulid alidhania baba yake
atakua na biashara mbaya na bila
Shaka Kuna mtu amechukua mateka.
Hivyo gari itakua imesimama sehemu ya
jumba chakavu na kutisha au kwenye
nyumba yenye ukimya. Lakini Cha
kushangaza baada ya yeye kufungua
buti na kutoka ndani ya gari ajabu
alishtuka kuwaona watu hao wawili
wakiingia kwenye baa. Iliyojaa watu
mchanganyiko.
Alishangaa lakini hakua na Budi zaidi ya kuwafata watu hao nyuma. Mara
wakaingia baa na kukaa kwanza
wakaagiza kinywaji. Na yeye akaagiza
bila kupenda na kuanza kutumia mdogo
mdogo kinywaji laini. Baadae aliemuona
baba Yake aliinuka na kuelekea maeneo ya washroom akaona akaushe asifatilie.
' Ila hapana hata wanajeshi was Badru
huwa wanasema ukifamfatilia mtu
usimpe mwanya was Imani'. Alieweza tu kuinuka eneo Hilo na taratibu akamfata
baba Yake nyuma.
Dereva aliekua kaambatana na bwana
amiri alihisi Kama Kuna mtu anamfata
nyuma baba Yake akataka afatilie Ila
akaona asite tu kwanza maana mtu
huyo Ni bwana mdogo tu anaeonekana
kua na haja zake mwenyewe.
Baada ya Bwana Amiri kwenda chooni
Katika baa hiyo, alikata Kona kuelekea
kwenye Bomba la kupitisha maji
machafu mtu ambae halifaham vyema
eneo Hilo hawezi kujua Wala kukisia
kabisa Kama eneo Hilo Lina mlango wa
kupitia. Aliangalia nyuma huko na kule
hakuweza kuona mtu wa kumshakia
kwani watu walikua wakitoka chooni na
kuingia hakuna ambae alikua na habari
nae.
Aliweza kupanda juu ya Bomba la
majiachafu Kisha akasererka kuelekea
eneo ambalo Bomba lilifata. Maulid
aliekua amebana kwenye Kona alibaki
hoi, kwani baba Yake alikua akielekea
wapi? Akasubiri kidogo ili asije akaenda
kwa papara na kukutana nae. Akiwa
anasubiri subiri akaona sio mbaya muda
umeendelea. Akafanya tu maamuzi ya
kuelekea huko huko. Alifanya Kama
ambavyo baba Yake alifanya na mwisho
Bomba lilimsereresha mpaka chini ya
mtaro uliokua ulitoka harufu mbaya
Sana. Bahati nzuri eneo lile lilikua
kavu. Aliangalia pembeni na kuona suti aliyokua amevaa baba Yake ikiwa
imetundikwa. Duh! Ni ajabu, kwa hiyo
alilazimika kuvua nguo ndo aende, labda
lilikua kuchafu? Hata hivyo yeye hawezi
kuvua nguo make hakua anapajua. Akiwa
anatafakari alihisi Kama nyayo za mtu
akizidi kusonga kuelekea aendako yeye.
Ilimlazimu awahi kupita kwenye hizo
njia za chinichini.
" Baba anampango gani na hii dunia?
Mbona anahangaika Sana" alijisemea taratibu na mwisho akazidi kumfata.
Ndani ya njia hizo za chini kwa chini
hatimae alifanikiwa kumuona baba Yake
akiingia kwenye kijilango kimoja na hapo
akaona acha asukume mlango aone
kutakua na kitu gani huko?. Asukuma
mlango taratibu na kufanikiwa kuingia
ndani ya mlango huo dogo.
La haula! Inashangaza. Mlango mdogo
uliopatikana chini ya njia za ndani kwa
ndani ya baa hiyo isiyojulikana hata
kwa watu wa daraja la juu, lilikua
chumba kikubwa mithiri ya ukumbi
AMBAO ungeweza kujaza watu
takeibani 500 kwa ajiri ya sherehe. Da!
Binadamu wanaweza kubuni Mambo, Kama hufahamj huwezi jua Kama
kwenye baa hiyo Kuna Mambo ya Siri.
Hilo halikumshangaza Sana Maulid
isipokua Kuna Jambo kubwa na
kushangaza zaidi ambalo lilimuacha hoi!!
Yaani alibaki ametoa macho akiwa
haamini Kama anaona kwa macho Yake
mwenyewe au Kuna mtu anammulika macho aone.
Nusu ya chumba like ilisheheni ma
dorali ya fedha za kimarekani unaweza
sema Bwana Amiri alikua akihujumu
uchumi. Pesa zote hizo!! Alikua
akizitumia kwa Jambo gani? Maulid
alishtuka mithiri ya moyo kuchomoka.
Aliushikilia moyo wake uliokua ukienda
Kasi.
Akiwa anatamalaki alihisi kusikia kelele ya kike ikitokea upande anaoelekea
yeye kwa nguvu.
" Utakufa siku moja we shetani??"
Maulid akipata khofu na kujidhibiti, kilikua na nini zaidi mbele Yake, ndipo akarejewa na fahamu zake ya kwamba
alikua akimfatilia baba Yake na hivi
Sasa haonekani. Wazo la kuendelea
kumfatilia likamjia akapiga hatua
kuelekea mbele kwani kilikua na upenyo
mwembamba katikakati ya zile pesa
nyingi Sana alipita na kupita hatimae
alifanikiwa kuona uwazi mkubwa zaidi
ndani ya ukumbi uleule kwa maana ya
kwamba pesa ziliacha nusu ya sehemu
mbele ikiwa wazi.
Alisimama kabla ya kusonga mbele.
Mungu wangu!! alikua baba Yake
akimtoboa mwanamke mwenye umri
mdogo Sana sawa na dada zake wawili
Muzda na Mariam kwenye upaja?
Maulid alishtuka mno. Na chini ya kiti
alichokua ameketishwa mwanamke huyo
kulisheheni matone ya damu. Maulid
alipigwa na butwaa, hivi kweli
mwanaume huyo alikua baba yake'
mzazi kabisa ambae yeye anamfahamu, Ni mwanaume ambae familia Yake nzima
unamuamini na kumpa heshima zote?
Bila Shaka hakua yeye amerananishwa.
" Utasema kwa ufasihi Ni wapi Mustafa
amehifadhi muhuri wa familia ya Badru
bila kusita sita" bwana Amiri alipitisha
Tena chuma kilichochemka kwenye mwili wa mwanamke. Huyo.
Mwanamke huyo alipiga kelele kwa
maumivu na kulegea kabisa hatimae
alikaribia kuzimia, bwana Amiri na vijana wawili waliokua wakimtunza huko
chini huyo mwanamke mateka, hawakuweza kumruhusu azimie
walimwagia Maji ya baridi Sana kana
kwamba alihisi kuganda baada ya kuzunduka. Kwa sura iliyochoka na
kukosa mwangaza usoni mwake yule
mwanamke aliinua uso wake huku
akitetemeka. Alikua ametobolewa
usonwake na ulijaa vidonda vingi mno.
Kwa kujitahidi Sana alitumbua macho
Yake yaliyotetemeka Kisha akaingia kwa taabu.
" Sitasema hata nikiwa maiti" Bwana
Amiri alichoshwa na msimamo
wa.mwanamke huyo, bila Shaka Hilo
lilibaki tumaini lake la mwisho kupata
muhuri wa familia ya Badru, hasingemuitaji mustafa Wala yeyote kuiteka familia ya Badru, na mtu pekee
anaefahamu huo muhuri Ni Nani? Ni
mwanasheria wake wa Siri, mwanasheria Lilian Masele hakuna
mwingine. Mustafa alimtumia mwanamke huyu mdogo na mwaminifu aende
kinyume nae Mara kadhaa ili kuondoka
mashakani kwa maadui zake wa kibiashara kua mtu huyu ni mtu wake.
Lakini kwa utafiti wa bwana Amiri
haraka Sana japo sio Sana
amemtambua mwanasheria Lilia kua
hakua mtu wa upande wao Bali alikua wa Mustafa.
" Kwani Mustafa alikulisha nini?
Alikoroga bendele iliyoandikwa jina
Mustafa aaminiwe Kisha akakunywesha!!!
Huna huruma na wewe mwenyewe
kabisaaa!!" Bwana Amiri aliminya macho Yake akiwa haamini.
" Yawezekana ukawa sahihi" akisema bi
Lilian Masele akiwa Hana shida na
kujikomboa kutoka kwa mtu huyo.
Bwana Amiri aliinua chuma na kuelekea
kwenye masikio yake' akiwa na lengo ya
kupitisha chuma kutoka upande mmoja
kwenda mwingine.
Maulid aliogopa alihisi kana kwamba
anamuona jini mbele Yake, hapana !
Hapana! Hapana! Haiwezekani! Bila
Shaka huyo hawezi kua baba yake'.
Anataka kumtoboa mtu masikio.
Maulid alitetemeka kiasi kwamba miguu
ilimsaliti na kujikuta anadondoka.
Kishindo Cha Maulid kudondoka
kilimshtua bwana Amiri na vijana
waliokua karibu yake. Kwa haraka Sana
waligeuka kuangalia atakua Nani?
Maulid hakuweza kujisaidia' kuyakwepa
macho Yao aliwatozama na wao
wakamwangalia. Kijana mmoja ambae
alitambua kabisa Maulid hakufaa kuona tukio lile na akatoka akiwa hai.
Alinyoosha bastora yake kumlenga
Maulid ambae alibaki akitoa macho tu.
Kabla mwanaume yule hajabonyeza
trigger Maulid alitoa sauti ya kushangaa. Na kumfanya asite.
" Baba!!! Ki ufupi hakuna kitu kinauma
Kama kuutambua ukweli mchungu wa
mtu wako wa karibu.kama ilivyotokea
kwa maulid. Yaani alihisi maumivu
ambayo hayaelezeki
Hivi Ni kweli kabisa? Baba yake' alikua
gaidi? Hapana hapana, Hilo Ni Jambo
lisilowezekana. Bwana Amiri baada ya kumtazama mwanae alipata maumivu
pia, sio kwa kua alikua mtoto wake
isipokua Ni kwa sababu alifahamu
ukweli wake kabla ya yeye kufanikiwa.
" Kwa Nini umesita?" Kauli hiyo bwana
Amiri aliitamka akimaanisha kwa nini
mwanaume huyo aliekua kaielekeza
bastora kumlenga Maulid amesita
kumuua.
" Bwana mkubwa!!!" Mwanaume huyo alishangaa Sana, Ni kwamba tayari
Maulid kamuita yeye baba alafu alifaa
kumuua pia?
" Baba wewe!! Ni gaidi??" Maulid hakua
akiamini anachosikia inamaana hata
alikua tayari kumuua? Huu haiwezi kua ukweli?
" Bonyeza trigger" bwana Amiri hakua tayari kuyajibu maswali ya Maulid
isipokua alimaanisha alichodhamiria, hivyo Kama Maulid kamfatilia saa hii, hiyo inamaana Ni mtoto asiefaa kwake.
" Mkuu?!" Mwanaume aliekua ameshika bastora alihisi kutetemeka. Bora yeye
alihisi kutetetma alishangaa iwapo mtu
anathubutu kumuua.mtoto wake wa
kumzaa, Maulid yeye alitetemeka akiwa
haamini Kama kweli huyo alikua baba aliemzaa yeye. Ki ufupi alipotea kidogo
kwenye mawasiliano hayo!
" Tress the trigger" bwana Amiri alihisi
Kama vile anacheleweshwa alimpokonya
bastora mwanaume yule na Mara moja
akanyoosha bastora kumuelekea Maulid
aliebaki hatambui kinachojiri maeneo hayo. "Bang! Bang! Bang!" Milio mitatu ya risasi ilisikika ndani ya ukumbi huo na kufanya ukimya wa sauti ya viumbe hai
waliokua eneo Hilo Zima kuchukua
nafasi Yake. Na mwisho Maulid
alionekana akienda chini.
Sehemu ya 170
Ndani ya chumba kulikua na ukimya
usiotarajiwa huku Maulid alionekana
kualala chini bila matumaini. Alikua
amejilaza chini na kufungua macho Yake
mawili bila tatizo. Ni kwa sababu hakua
amekufa alikua hai! Masikio yake'
yalicheza baada ya kusikia hatua za mtu akimsogelea. Mtu huyo alikua
akitokea nyuma Yake kulingana na hatua zilizokua zikimsogelea. Kisha hatua hizo
zikaelekea usawa wake mwenyewe. Mtu
huyo alifika mbele na kuinama kwenye
usawa wa.uso wake. Maulid kwa
kutetemeka aliinua uso wake na kumwangalia mtu huyo huku macho yake
yakibubujikwa na machozi.
" Bwana mdogo, upo sawa" sauti ya
mwanaume huyo ambayo aliisikia vyema
Sana ilikua sauti njema kwake na ya matumaini makubwa, lakini kutokana na mshtuko aliokua nao hakuweza kujibu
kitu. Mtu huyo hakua mwingine Bali
alikua shemeji yake mtarajiwa Bwana
Yasir Sabodo.
Maulid alitabasamu hakika mtu huyu
alifika kwa wakati ufaao. Na hakua
amekuja pekee Yake, alikuja na watu
wengine Kama sita hivi kwa ajiri ya msaada.
" Baba yangu kweli Ni gaidi??" Maulid
alimhoji Yasir ambae alimuonea huruma na mwisho akamuitika kwa kutikisa
kichwa kua yupo sahihi.
" Mmemkamata?" Maulid alihoji.
" Amefanikiwa kutoroka, nadhani atapenda mafichoni" baada ya Yasir
Kutamka hivyo Maulid akamkumbuka
huyo baba yake' mkatili bila Shaka
hawezi kua ameenda mafichoni bure
mtu huyo mbaya nii??? Ni baba yake'
yeye pamoja na dada Yake Afsat. Aah'
hapana haiwezekani na asubuhi
akizungumza suhara la mtoto ambae ni
azmina! Bila Shaka atakua ameelekea
nyumbani kwao.
" Hapana shemeji Yasir huyu baba
yangu hawezi kua ameenda mafichoni, bila Shaka atakua ameelekea nyumbani"
Maulid aliekua amepoteza nguvu ghafla
alihisi kujiwa na nguvu upya, anafaa
acheze nafasi Yake Kama kijana
mkubwa wa bi Azat Badru, baba yake'
anaefahamika kama mwema Sana, iwapo
yeye kamgundua na alibaki kidogo
amuue vipi kuhusu mama Yake na mdogo
wake? Hapana acha awahi Maulid
aliinuka haraka bila hata kutazama
nyuma. Alikimbia moja kwa moja
kuelekea nyumbani kwao na kuwaacha
Yasir na vijana wake wakifanya kazi
Yao.
Kazi waliokua nayo hapo Ni kumuokoa
Lilian na kuwakamata vyema vijana
wawili wa bwana Amiri, maana wao ndo
sababu Hadi Bwana Amiri amefanikiwa
kukimbia. Na wanafaa kuwasubiri police
wawasili sehemu hiyo kuja kuchukua
ushahidi wote.
Maulid akiwa amefanikiwa kutoka nje
kabisa ya Ile baa alikua hoi alikimbia
na kusahau iwapo anafaa hata achukue
taxi au pikipiki angalau awahi kuliko
kukimbia. Alikumbuka namna ilivyokua
mpaka Yasir akafika eneo Hilo kwa wakati.
Ni baada ya yeye kuwa na mashaka na baba yake' usiku wa Jana tu.
Alikumbuka siku ambazo walikua south
Africa dada Yake Muzda alilalamika kua
hampati rafiki yake' kwa muda Sasa, na hajui atakua wapi?
Kisha usiku mmoja kabla hawajarejea
Tanzania alimsikia baba yake' aliongea na simu. " Amefanikiwa kuongea??"
Hajui mtu wa upande wa pili alijibu nini? Lakini bila Shaka jibu lake halikua la kumfurahisha baba yake'. "
Hakikisha anaongea hafai kufa bila
kusema muhuri wa familia ya Badru uko wapi?, Nitawaua asiposema ukweli, maana tumezunguka sehemu zote lakini
hatujabahatika kufahamu" baba yake' alisita Kisha akaongea.
" Hakikisha anaongea, nitakufa
asipoongea, hii Ni kazi ilionichukua
Maisha ya watu wengi, amini Lilian ndo
mwanasheria wa Siri wa mustafa, jitahidi aseme ukweli, Jambo hili ni
muhimu, nilimtoa Hadi dada yangu kwa
ajiri hii" Maulid alishtuka Sana kwa
maneno hayo na kuamua kufatilia lakini
hakua na namna ya kumfatilia baba
yake' wakiwa afrika kusini. Mwisho wa siku walipata taarifa kua wanafaa
kurejea nchini.
Wakiwa kwenye maandalizi Muzda
alijikuta akimtolea bila kutarajia,
alimpa ombi ambalo hakuna hata mmoja
anaweza fikiria Kama yeye atafanya
kwa kweli. Maulid alichukuliwa mdogo
siku zote kwatika vijana wa familia
hivyo akili yake nzima alijiweka katika
kipaji chake, lakini hatimae dada Yake
Muzda alimuomba Jambo.
" Maulid naomba ukienda huko unisaidie
kumtafuta lilian, ushikamane na Yasir
mumtafute lilian" Jina lilian liliucheza
ubongo wake Kisha akakumbuka ndo jina
ambalo alimsikia baba yake' akilitamka.
Hivyo akafanya maamuzi ya kuchuja
Kati ya Maji na mafuta. Kwa nini abaki na mashaka kwa baba yake'.
Ndipo alipofika Tanzania alimtafuta
Yasir na kumwambia, yasiri akamjibu
kua mtu wa kwanza anaeshakiwa alikua
baba yake' na Maulid hakutaka kupinga
kwani hata yeye alikua na mashaka nae.
Kwa hiyo siku hiyo kabla hajaenda
kumfatilia baba yake' kwenye safari
zake. Alimpigia simu Yasir. " Ndo
wakati huu" alimwambia Yasir akamjibu.
alifanya hivyo akiwa anaamini kabisa
atakua salama mikononi mwao shemeji yake.
." Washa simu yako niifatilie" Maulid
Na kweli bhana Yasir alifanikiwa kufika hapo kwa wakati na aliweza hata.
¥Turudi nyuma kidogo ili mtambue ilikuaje risasi tatu kusikika na Maulid
akawa hai na kwa nini bwana Amiri alitoroka? ¥
Wakati ambao bwana Amiri akijiandaa
kufyatu risasi na aliweza kubonyeza trigger Kama alivyosema
" Tress the trigger" akafyatua risasi na kuruhusu kutoka kwenye mdomo wa bunduki. Lakini mwishowe risasi Ile
haikufaulu kwani Maulid alijirusha chini upande mwingine na risasi mbili
mfululizo zikasikika kutoka nyuma ya Maulid. Yasir alifyatua risasi hizo mbili
mfululizo kuelekea kwa bwana Amiri
aliebaki amesimama kwa kuduwaa.
Kwani risasi zilikatiza kwenye usawa
kidogo Sana na pua pamoja na macho
Yake. Kwa hakika mtu huyu hakua na
lengo la kumuua kwa shabaha aliyokua nayo.
Ina maana atakua polisi? Maana mtu
huyo hakua amejitokeza tayari. Akaona
kuliko abaki hapo kutafakari anaweza
Kamatwa na polisi wakati wanaushahidi
Tosha kwamba yeye alikua amehifadhi
kiasi kikubwa Cha pesa eneo Kama lile
ambalo aliruhush na pia ndani ya
chumba hicho kulikua na vitu vyake vingi
vya Siri Kama madawa ya kulevya, vipande vya dhahabu, pembe za ndovu, na kadharika vudivyokua halali, na kwa
kweli wakati huu uhai Ni muhimu Sana.
" Huyu mjinga asie na akili amenichoma"
alimaanisha Maulid huku alikimbia kwa
kupitia njia nyingine kabisa kwani
aliamini hapo hawezi kuponea Tena.
Wakati huo pia ndo Yasir aliwasili na vijana wake watano. Na hapo ndo Maulid alisalimia pamoja na Lilian.
Katika nyumba ya bwana Amiri kimya
kilitawala huku watu wakiwa hawaelewi
kwa nini watu wawili. Pamoja na mtoto mdogo.
" Mama mi naogopa Sana, Ni usiku wa saa sita sasa na Maulid hajarejea
nyumbani na marafiki zake wote Ni Kam
hawafahamu alipo" Afsat alilalamika kwa uwoga.
" Usifanye Kama vile Mimi tumbo la uchungu halinikumbushi kuhusu yeye"
hofu ilitanda baina yao na hapo bi Azat
alimbeba azmina aliekua amelala na kuamua kumpeleka kulala chumbani.
." Mama naogopa" afsat aliinuka na kumfata mama Yake.
" Unaogopa nini Sasa?" Bi azat hakua na budi zaidi ya kuongozana nae, hata
hivyo wote kwa pamoja walikua na khofu.
Huku nje bwana Amiri aliwasili katika
nyumba Yake akiwa na wasiwasi wa Hali ya juu' huku akiwafukuza walinzi kwa
kudanganya kua anawapa ofa hataki
kuwaona kwa usiku huo.
" Boss lakini Ni wajibu wetu kuilinda
familia ya Badru bila kuchoka" mlinzi mmoja.alijibu
" Kwa hiyo Sina haki ya kutoa neno juu ya familia nyangu mwenyewe" aliwaka
kwa hasira macho Yake yakajaa damu, na hapo ikabidi walinzi wafanye Kama
walivyoambiwa na hatimae waliondoka
kabisa katika jengo Hilo. Na haikua tu walinzi Hadi kwa wafanyakazi wa ndani
walipewa amri ya kuondoka hapo.
Haijulikani Ni kitu gani bwana Amiri
alipanga kwenye kichwa chake. Ila
alinyoosha njia moja kwa moja mpaka
kwenye chumba ambacho alihisi Kuna
watu walikua wakiongea. Alifika na kuwakuta Mke pamoja na binti Yake
wakiwa wanabembelezana kuitafuta
usingizi. Aliwasalimia na hapo afsat
aliinuka na kumkumbatia baba yake'.
" Baba Maulid haijulikani aliko! Mpaka saa hii saa sita" afsat alivuta kamasi.
" Naogopa baba" alimwambia.
" Huna haja ya kuogopa mpenzi"
aliongea kisha akainama alipo mtoto wa
Azraj. Ma'am bila Shaka Maulid alikua
sahihi, mwanaume huyo amekuja moja
kwa moja nyumbani kwao kumchukua mtoto.
" Mume wangu ndo amesinzia hivi Sasa baada ya muda mrefu', unafaa
umuache iwapo umemkumbuka
utamwangalia hata kesho" Bi Azat aliongea.
" Hili la leo halisubiri kesho!!" Bwana
Amiri alitoa macho makali ambayo bi
Azat kamwe katika Maisha Yake
hakuwahi kuyashuhudia kutoka kwa
mume wake huyo.
" Una tatizo kwani??" Bi Azat alihoji huku afsat akiwa kashangaa.
" Ndio nalo tatizo na nyinyi Wana
familia wa Badru" aliongea kwa sauti ya
tetemeko ambayo iliyakumba vibaya
Sana masikio ya Bi Azat na Afsat moja
kwa moja. Wakiwa akwenye butwaa
bwana amiri alimchukua mtoto na kuondoka nae.
Hapo afsat akili ikamcheza. " Baba azmina, hapana baba unampeleka wapi mtoto?" Bwana Amiri hakua anataka
kujua kitu aliweza tu kuwafungia mlango watu hao ndani ya chumba Kisha
akanyoosha njia kuelekea anakojua yeye mwenyewe.
" Baba huwezi kwenda na azmina, Ina maana kweli baba unashirikiana na Azraj. Ina maana ni kweli Maulid alivyosema. Maneno Yale yalikua
yakijirudia kwenye masikio ya Bi Azat na kubaki haelewi chochote.
Sehemu ya 171
" Kwani wewe unamana gani? Maulid
alisema nini?" Bi Azat alihoji akiwa
hataki kuamini maneno aliyotamka afsat
mwanzo.
" Mama mwenyewe siamini Ila Maulid
alisema eti baba ana Mambo mengi
Sana anaficha sirini na kingine
anashirikiana na Kaka Azraj kuiangusha
familia ya Badru" maneno hayo yalikua
Kama radi Kali kwenye ngome ya
masikio ya Bi Azat, Hawa watoto
hawana akili wakimzungumzia mume
wake bila Shaka. Huyo Ni baba Yao!!
" Nyamaza huo ujinga!!" Bi Azat
alifoka. Kisha akasikia sauti ya mtoto
akilia huko nje. Kwa kweli akili Yake
haikua woman hata kidogo, iwapo
angepatikana mtu wa kusoma ubongo
angeelewa Hali Yake.
" Azmina" Afsat alianza kupiga kelele.
Juu kabisa ghrofani bwana Amiri
alifanikiwa kupanda akimngoja Nevson ambae aliwasili kwa wakati mzuri.
"Bwana mkubwa " Nevson alimsogelea akiwa na lengo la kumchukua mtoto kweli.
" Humpeleki kokote'" sauti ya kufoka ilisikika nyuma ya Bwana Amiri na
kwenye masikio ya Nevson. Kwa upande wa Nevi alihisi Raha Sana kwa kua
tayari familia ya bwana Amiri
imegundua ukweli.
" Bwana mkubwa" Nevi alionyesha
unyenyekevu na subira ili apewe amri ya kutii.
" Ondoka na mtoto haraka" alimsogelea
nevi. Lakini Maulid alikimbia haraka
Sana kuelekea kwao. Nevi akasita
kusogea.
" Huwezi kwenda nae mahari yeye ni mtoto wa Kaka Azraj, ni.muhimu kwa
Kaka Mustafa" Maulid alimlalamikia baba yake'.
" We Bwana mdogo una shida gani na Mambo ya watu wazima" bwana Amiri alifoka. " Familia ya Badru imekugeuza
mtumwa wao" bwana Amiri alihisi
kupata hasara kutokana na kuzaa mtoto
Kama huyo.
" Ndio bila Shaka, nipo tayari kuishi
Kama mtunwa wao kuliko kuishi Kama
wewe. Huwezi mchukua mtoto baba. Ni wa muhimu" Maulid alikazia dhamiri
yake kwani yeye hakufahamu iwapo
Nevi Ni kijana wa musatafa, bila Shaka
angekuja Hilo haraka Sana angempa
nevi kwa mikono Yake mwenyewe.
" Nevson mchukue mtoto" bwana Amiri
aliamuru na kuchomoa bastora aliyokua
nayo. Hakusita kumuelekezea Maulid
kwa Mara nyingine kwa kweli alidhani
anastahili kumpoteza huyo mtoto ambae
kamuingiza matatizoni.
Nevson aliona acha asiweke vikwazo
Kati ya baba na mtoto bila Shaka
mwanaume huyu hata awe katili kiasi
gani hawezi muua mtoto wake
mwenyewe. Kitu ambacho nevi aliwazia
Ila ki uhalisia hakua akamuelewa bwana
Amiri. Aliweza kufanya haraka kwa
spidi yake ya ajabu akamchukua mtoto.
Maulid alijaribu kumsogelea Nevi na
kumvuta bega lake. Kwa nguvu za Nevi
aliweza tu kumsukuma kwa kikumbo
kimoja tu na hapo Maulid alidondoka
chini, Nevi hakusita kuruka kutoka juu ya ghorofa na kutangulia chini akiwa na
mtoto mdogo mikononi mwake.
Maulid alishuhudia tukio Hilo Kisha
akapiga kelele. " Hautafika nae mbali, bila Shaka utakamatwa" Maulid alifoka
kwenye ukweli ambao hajui Kama
hakustahili kumletea shida nevi. Kwani
nevi Ni wa Mustafa.
" Unadhani atakamatwa kizembe kwa
mipango yako finyu, hayupo Kama mbwa wa Badru" bwana Amiri alimwambia
huyo mwanae mpumbavu Kisha
akajiandaa kuondoka.
" Huendi popote baba" Maulid alimzuia.
" Wewe Nani Hadi nisiende pop0te"
bwana Amiri hakuweza kumjari
akajiandaa kuruka kutoka juu ya
ghorofa lakini hakuweza kufanikiwa
kwani tayari Maulid alimfunga kamba
mguuni mwake.
" Wewe!!" Bwana Amiri alishindwa
kujizuia kumuelekezea bastora huyo
mtoto mpuuzi.
." Siogopi kuuliwa na wewe hivi Sasa?
Hapo mwanzo sikujua Kama wewe ni
gaidi ndo maana nilibaki na bumbuwazi
baba, lakini hivi Sasa sitakuacha uende
ukaendelee kutenda maasi, lazima
nikushikilie ili ukakiri madhambi yako
yote baba, kwani ushahidi kamili juu ya
ugaidi wako upo mikononi mwao polisi na
wanajeshi wa Badru tayari
wamekabudhi, na kwa Sasa sidhani
Kama unazo hata hizo sekunde za
kutoroka" Maulid aliongea akiwa
anapata maumivu makubwa kwenye moyo wake.
Ki ufupi inauma kuzaliwa na mzazi
ambae wewe huyo huyo utatumika siku
moja kumkabidhi kwenye mikono ya usalama ili akaadhibiwe.
" Una wazimu wewe!! Unadhani hao
polisi sijui serikali watanifanya nini?
Hakuna wa kunifanyia chochote. Mimi
Ni mtu mkubwa zaidi ya Badru, nilibaki
kidogo nimiliki ulimwengu mzima wa
utajiri Kama sio wewe mwanaharamu"
bwana Amiri alihisi hasira akashindwa kuidhiti na mwisho alibonyeza trigger ili
akiweza amuue huyo mtoto.
." Nitachagua njia sahihi Maisha yangu
yote aijalishi nini kitatokea? Nitabaki
upande wa Badru tu" Maulid alipiga
kelele huku alifunga macho yako baada ya risasi kuchomoka kwenye bastora.
" Baba mauuuuuu!!!!!! Sauti ya bi Azat
ilisikika kwa ukaribu zaidi akionyesha Ni
kiasi gani alipigwa na butwaa kushuhudia tukio Hilo.
" Bang" kama kawaida Pam parika
mlango wa chuma ukiifungua hauna
huruma, risasi hiyo isiyo na huruma
ilisafiri moja kwa moja kuelekea kwenye
mwili wa binadamu ambae alikua
amejiandaa kuipata. Maulid aliekua
amefumba macho yake alifungua macho
akiwa haamini alikua amesubiri risasi
imuingie, lakini mwisho wa siku Ni Kama
vile hakupata tatizo lolote kwenye mwili
wake zaidi ya uwoga na mapigo ya moyo
wake kudunda. Na kingine mbele Yake
kulikua na umbile la mtu amesimama .
Alikua afsat ambae alisimama mbele
Yake huku akimpa tabasamu murua
linialochanua kwa maumivu. Machozi
yalimtoka afsat akiwa kamwangalia
Maulid. " Mm mau" alijikuta akienda
kumuangukia na hapo Maulid aliweza
kumdaka afsat aliekua akimdondokea na wawili hao wakakumbatiana. Maulid
akiwa amemkumbatia Afsat mkono wake
ulikua na majimaji baada ya kumgusa
mgongoni usawa wa bega lake la kushoto. Majimaji hayo yalikua na harufu Kali kana kwamba yalikua, yalikua! Hapana Ni damu!!
Nini?? Kichwa Cha Maulid kilicheza
Kama kitenesi, Ni Ni kweli kwamba?
Sio yeye aliepatwa risasi lakini dada
Yake kipenzi Afsat ndo ameishia
kusimama mbele Yake na kumkinga kwa mgongo. Wake. Na mwisho afsat
ameambulia kupigwa risasi na baba Yao katili.
" Kweli...yeye .... ni Ni baba yetu
sisi?? Afsat alijikuta akihoji swali Hilo
kwa Kaka Yake.
Bwana Amiri haikumshtua kwani alikua na hasira pia, Ni bahati mbaya iliyoje
kupata watoto ambao hawakua
wakimsikia na kua upande wake. Aliinua
Tena bastora take na kuilekeza kwa
wawili hao waliokumbatiana. Bi Azat
ufaham ulimrejea eneo alilokua, alishindwa kusita kukimbia na kuushika
mkono wa mwanaume huyo mpumba**
aliikua akiwaua watoto wake mwenyewe.
" Wewe ni kichaa', wewe ni shetani wa aina gani? Wao Ni watoto wetu
wadogo" Bi Azat alibubujikwa machozi
akijilaaani kuzaa na mbwa Kama hiyo
katika ulimwengu, aliwezaje kuolewa na mwanaume Kama huyo? Kwa nini
hakumfahamu kabla.
" Sio watoto wetu , Ni watoto wako na
Ni zao la Badru damu haramu maishani
mwangu" bwana Amiri alimuweka ukatili wake mbele. Bi Azat alijikuta akilia
Kama mtoto ili huyo mwanaume awaache watoto wake. Mwisho wa siku Ni
kwamba Bwana Amiri aliweza
kumsukuma Bi Azat msumbufu na kusababisha Bi Azat adondoke kutokea
hapo na kuangukia upande wa pili.
" Aaggghhh" sauti ya kukwaruza kwa
uwoga ya Bi Azat ilisikika.
" Mamaaaa!!!! Maulid alipiga kelele huku
Afsat alizidisha kilio. Familia Yao
iliyokua na furaha siku zote imegeukaje kua hivi??
Maulid aliweza kumuweka chini afsat na haraka akainuka amkimbilie mama Yake.
Kwa kweli baba yake' hakumruhusu
alikua na hasira nae kiasi kwamba
alidhamiria kumuua tu. Huyu mshenzi
ndo sababu ya kila kitu. Akimlenga
bunduki na kutaka kummaliza. Maulid
akili Yake ilimlenga mama Yake tu.
Risasi ilimfata Maulid ambae kidogo
impate lakini bahati nzuri Kuna risasi
ilitokea zaidi ya spidi yake na kukigonga risasi hiyo.
Maulid hakuweza kugeuka nyuma Wala
mbele isipokua bwana Amiri alishtuka
Sana baada ya kuwaona watu waliwasili
eneo Hilo. Walikua vijana watatu mbele
Yake. Mashuhuri na mashupavu. Alikua
Mustafa Badru, muksin Badru, pamoja na Yasir Sabodo. Nyuma ya kila mmoja
kulikua na mlinzi mmoja. Gharib.
Halisubiri kuamriwa na akakumbuka
kwenda kumpa tafu Maulid aliekua
akihangaika kumuokoa mama Yake
alieshikilia nguzo ya balcony ili
asidondoke chini akapiteza uhai wake.
Na wakati huo muksin aliweza tu
kumuinua Afsat akisaidiana na mlinzi
wake haraka Sana wakaelekea hospitali.
Bwana Amiri alihisi kuyaona mauti
Yake. Hakuweza kusubiri kuruka kutoka
ghorofani na kuishikilia kamba iliyokua
imeandaliwa kwa ajiri Yake kushuka.
Mustafa pia hakuchelewa kumfata, na
kwa bahati nzuri Yasir alikua mzuri
Sana kwenye kulenga shabaha. Aliilenga
Ile kamba vyema Sana na akafanikiwa
kuikata karibu kabisa na mikono ya bwana Amiri.
Kwa mshtuko wa kukoswa na risasi Tena
mwanaume huyo alijikuta akiachia
kamba na kudondoka kifudifudi. Sio tu kwamba alipata maumivu ya mat*k*
baada ya kudondoka lakini kwa kweli
bado alikutana na teke kubwa la uso
alilopewa na Mustafa Badru huyu mtoto
asie na aibu.
Baada ya Gharib kumuokoa Bi Azat
ambae hakuamini kwa kila tukio
lililojitokeza hapo, na kuhusu mume
wake kwa kweli akili Yake ilipararaizi
kwa muda na mwisho alipoteza fahamu
zake kwa mshtuko. Maulid pamoja na
Gharib walilazimika kuongozana ili
kumpeleka hospitali.
Yasir aliandamana na Mustafa
kumuadabisha huyo mbwa mwitu wa makamo bwana Amiri, isingekua rahisi
kwa wao kumuacha salama. Walianza
kumtembezea kichapo bila kusuburia.
Wakati huo wao walimpiga Sana, Maulid na gharib walikua ndo wanamuingiza Bi
Azat kwenye gari. Maulid alimkumbuka
Afsat dada Yake kipenzi ambae alijitoa
kumuokoa yeye. Alikua kwenye maumivu
makali kiasi gani?.
Roho ya unyama na maumivu kwa
pamoja ikamvaa Maulid ambae aliomba
Gharib asimamishe gari. Kisha
akachomoka na bastora kwenye siti ya gari kwani Ile ilikua gari ya Mustafa.
" Wewe!! Gharib alimtahadharisha. Kwa
kweli Maulid alifanya Kama vile hakua
amesikia huyo mwanaume ambae yupo
sawa na Kaka Yake muksin. Hawezi
kukubali na kuyavumilia maumivu ya
ghafla aliyoyapata kupitia baba Yao
huyo asiesatahili alikua tayari
kuwaangamiza?
Kwa nini amuache. Ki ufupi so sahihi
kumpa nafasi adui. Wakati ambao
Mustafa na Yasir walikazana
kumuadhibu bwana Amiri Kama kitenesi.
Alitokea Maulid na kumlenga bastora
ambayo ilikua na uwezo wa kumiliki
risasi 12 kwa wakati mmoja.
Mustafa na Yasir wakiwa hawana moja
Wala mbili, walishtuka kuona risasi
ikizama na kusababisha damu kuruka
kutoka kwa bwana Amiri. Nini? Alikua
Nani huyo aliefanya hivyo?
" Maulid acha kuchukua Sheria
mkononi?" Mustafa alimfokea lakini
Maulid hakuweza kumuacha baba yake' huyo asiesatahili uhai. Alifyatua risasi
Tena na Tena mpaka pale alipoona
zimeisha kwenye bastora. Hakuna
aliemsogelea. Kabisa.
Sehemu ya 172
Ni siku mbili zilipita tangu tukio Hilo la kutisha lijitokeze. Ndani ya kisiwa Cha
ukerewe jijini mwanza Salma alionekana
kua na furaha na kupata ahueni ya
Maisha baada ya kuletewa mtoto wake
kwenye mikono Yake.
Lakini bado hakua na Amani kabisa
katika eneo Hilo. Bado walilazimika
kuishi na Azraj. Saida akiwa amejikalia
chumbani mlango wake ghafla ulifunguliwa.
" Unataka nini Azraj, ndhakwambia chukua uhai wangu kwanza ndo ufanye
unachotaka kufanya" Saida alifoka.
" Hapana shem sio Azraj, Ni Mimi nevi"
Saida alishtuka alikua nevi, nevi ndo
Nani? Kijana wa Azraj Badru.
" Ondoka hapa, sihitaji kula, Leo ni siku ambayo nitaicha ipite tu. Saida aliongea bila kuogopa. Alikua
amechoshwa na Hawa watu ambao
walimfungia jumla kwenye hicho chumba na kumnyima haki.zote za kibinadamu, kwa kweli hapo mwanzo aliamini
ataokolewa na Mustafa Ila inaonekana
hata Mustafa pia Hana muda nae.
Hivyo hataki kula, Ni sawa hata akifa.
" Shem, Mimi naitwa Nevson Ni kijana
mtiifu wa Mustafa Badru, natokea
katika kambi ya Badruguard. Nimekuja
huku kwa ajiri yako" kwa utambulisho
huo Saida alijikuta akimkumbuka
Gharib. " Mimi naitwa Gharib, kijana
mtiifu wa Kaka mkubwa, Mustafa
Badru" alihisi kumuamini.
" Sio rahisi kwako kunifahamu kwa
sababu Mimi Ni Askari wa Siri Sana na
nafanya kazi na magaidi pamoja na
maadui Mara nyingi, hivyo kwa Sasa
natambulika Kama Askari wa Azraj
mvhapakazi na mwaminifu, lakini Mimi
ndo niliemuua Bwasha" aliongea nevi
Saida akabaki haelewi kabisa.
" Sasa Kama Ni kijana wa Mustafa, huyo Mustafa mwenyewe atakua wapi?
Tayari nimemaliza mwezi Sasa na siku
kadhaa bila kuwekana nae machoni, au sikua na umuhimu wowote ule kwake, kwa nini asimpe Azraj kitu anataka ili anichukue? Kwa kweli Mali Ni muhimu
na za maana Sana kwake kuliko Mimi?"
Saida alikata tamaa.
Nevi alipata hisia chungu na kwa Mara
ya kwanza akahisi kumkumbuka Zarina.
Alikua Ni mjakazi tu kutoka katika
familia ya Badru, Mara nyingi alikua
akimuona kwa kumtupia jicho bila hata
kumsogelea, na alihisi maumivu kila
alipomuona akiteseka na Mambo kadhaa
ambayo aliyafanya bila Shaka
angeongozana na Saida au Asia, na yeye angevizia masaa ya kwenda
sokoni, au kumchukua Shayma shule ili
amuone zarina. Lakini Sasa Ni
marehemu, na tangu afariki msichana
huyo ndo siku ambayo Saida alifungua
hapo katika eneo Hilo. Hata yeye alikua na upweke mwingi Sana baada ya kusikia kifo chake. Kwa maana hiyo.....
" Samahani shemeji, najua umekua
mpweke Sana hapa, lakini Bwana
mkubwa hakuwahi kusahau, hakuwahi
fikiria kukuacha mwenyewe, hata yeye ni mpweke pia Ni mpweke zaidi. Yaani
amekua akifanya Mambo mengi hivi
Sasa. Lakini hajakusahau" nevi aliweka
sura ya huruma kwa Saida ambae
alibaki kamtolea macho.
"Kwa Nini hakukutuma mwanzo mpaka
Sasa hivi ndo anakutuma, siwezi
msamehe Mustafa kwa hili, hivi anajua
nateseka kiasi gani Mimi?" Saida alilia
Sana na kushindwa kuzuia hisia zake.
" Shem tafadhari, usiku wa leo, usiku wa leo bwana mkubwa atakuja
kukuokoa, tayari nimechora ramani, na hivi Sasa nimekuja kukupa mpango
stahiki na kitu unachotakiwa kufanya"
Nevi alimwangalia Saida ambae
alionekana kukubaliana nae bila kusita.
" Hakikisha Shem unafata maelekezo
yangu, na zaidi Sana haifai kufahamika
Kama Mimi ni kijana wa Mustafa"
alimkumbusha Saida ambae aliweza tu kuitikia kwa kichwa. Hatimae Saida
alihisi kuridhika baada ya kuambiwa maneno hayo.
Majira ya mchana nyumbani kwa Dr
khairat alikua amemaliza kupata
chakula chake Cha mchana. Akiwa
anatamani kulala apumzishe akili kwani
siku hizi amekua akipata ndoto mbaya
Sana kuhusu Dr Hizaan. Alitamani
apigiwe simu siku moja hata aambiwe kua mtu huyo amekufa.
" Trriiii" eehh! Tayari simu ikawa imeita bila kujiuliza alihisi huenda maombi
Yake yamejibiwa ki urahisi hivyo
alipokea simu hiyo bila kuangalia mpigaji
Ni Nani?
" Kafa tayari" aliongea kimasihara tu alidhani atapewa taarifa ya swali kua
Nani kafa? Ila ajabu alipewa taarifa
ambayo hakuitarajia.
" Nawezaje kufa mpenzi wangu?
Nahofia kukuacha mjane" Dr khairat
alihisi kulipuka kwa mawazo. Alikua
akiongea na Nani? Hapo ndo akili
ikamtuma aangalie kwenye simu iwapo
anachokiwaza nu sahihi ama anataniwa.
Alipoiangalia kwenye kioo Cha simu
Yake!! Haa! Hakika haliingii akilini. Ni Dr Hizaan.
" We Nani?" Alihoji kwa pupa na kuhisi
uoga kwa wakati.huo huo.
" Mimi hila Shaka Ni mine wako, baba
wa.mtito wako khairat wangu, mume
wako nimekumiss mpaka naumwa, mke
wangu nimechoka kulala pekee yangu
hapa kitandani unaweza kuja kulala na Mimi!" Dr khairat alihisi
kuchanganyikiwa hapana jamani! Sio
sawa, mtu huyu hafai kwenye Maisha, na sio sawa akiongea na hiyo simu.
Haraka Sana alikata simu akiwa haamini kabisa.
'huyu mtu atakua Nani kwani?"
Alijiuliza na mwisho alipiga simu kwa
mtu mmoja hapo Aga Khan kuulizia
iwapo Dr Hizaan amezinduka ama bado.
Alipewa jibu la bado na hawana uhakika
Kama mtu huyo atazinduka hivi karibuni. Akili ya Dr khairat Ni
kama.ilitaka kuluzi. Hakua kwenye akili zake timamu.
" Khairat uliamua kuniua ili uolewe na mume wangu? We ni mwanamke kweli?"
Sauti hiyo Sasa ilimfanya kichwa Cha
Dr khairat kulipukwa kwa radi na mshtuko alisikia sauti Kama hiyo wapi?
Ni mama. Shayma? " Uuu wewe were Ni Nani?" Aliinuka kwenye meza ya chakula na haraka akaanza kukimbilia
chumbani kwake, kwa kweli hakuamini
anasikia marue rue katika umri wake
mdogo Sana. Ndo kwanza kijana wake
bado Ni mdogo na mwenye umri wa miaka mitano tu. Anaanzaje kuzeeka.
Majira ya usiku wa saa mbili Mustafa
aliwasili katika apartment ambayo aliitambua kabisa baada ya kufungua
geti kwa kishindo. Hee!! Walinzi
waliokua wakilinda walishtuka mno
baada ya kuwasili kwa mwanaume huyo.
Alikua alikua Nani? Mustafa Badru.
" Hurushusiwi kuingia" mlinzi mmoja
ambae alinyoosha gobore lake kana
kwamba alikua akiwinda swala msituni
alimtisha Mustafa ambae alimpiga teke
moja na kumsababishia maumivu ya kiuno huyo mwanaume.
Na wakati huo huo wanajeshi kadhaa
wa Badru waliingia ndani walifatana na
Mustafa. " Hii pants azraja Badru iko
wapi??? Mustafa alihoji kwa sauti.
Azraj alikua chumbani kwake amekaa
akiwa mwenye huzuni Sana na alikunywa
Sana pombe baada ya kufiwa na mjomba wake. Lakini Ni Kama alisikia
vibaya hivi? Au pombe ilimzidia? Alikua ameisikia sauti ya Mustafa akimuita.
" We panya mdogo hujui maana ya
kutoka pango ulilojificha ama?" Mustafa alipiga makelele. "Pffff" Azraj alijikuta
akitema pombe bila kutarajia kweli
alikua hajasikia vibaya eti ni Mustafa
Badru alimuingilia kwenye mjengo wake.
" Mshenzi huyu amepajuaje hapa??"
Azraj na ulevi wake aliinuka na kuchukua mashine Kisha akatoka nayo
nje akiwa na dhamira ya kufanya
mauaji ya nguvu.
" Mustafa, bwana mkubwa hatimae
umekuja kutuokoa kutoka kwenye
mikono mibaya" Salma alishangiria huku
akitembea kuelekea kwa mustafa.
Azraj alihisi kuchanganyikiwa huyu mwanamke anawazimu. Aliinua bunduki
take akiwa kule kule juu na kuilenga miguu ya Salma ambae alishtuka na kupiga kelele.
" Unathubutu kuelekea wapi na mtoto wangu? Rudisha makalio ndani!! Azraj
alimfokea huyo mwanamke ambae hakua msikivu.
" Siwezi kubaki hapa Tena, sitaweza shetani wewe" Salma alilalamika Azraj
akainuka bunduki kumtishia. Hata hivyo
Salma hakuweza kujari alizidi tu kutembea.
Sehemu ya 173
"Usithubutu kwenda popote Salma la sivyo wewe na huyo mtoto wako wote
kwa pamoja mtakua hatarini" Azraj alimtisha.
" Ni sawa!" Salma alijibu bila kufikiria
akiamini kabisa Hilo haliwezi kua. Kwa kweli Azraj Ni sahihi kwamba
anampenda yeye na mtoto Sana tu.
Salma alisogea kumuelekea Mustafa na wakati huo huo Azraj akainua bunduki
yake akimlenga Salma kumuelekea
mtoto Kama masihara hivi anamtishia
Salma. Salma hakuweza kuogopa khofu
Yake.
" Tambua huyu ndo binti yako wa pekee na huwezi pata mtoto popote pale"
Salma alimtishia Azraj ambae hakuweza
kujari hata kidogo vitisho vyake. Ayaa
Azraj akimlenga mtoto kweli akiwa na lengo la kuipalaza risasi kwenye uso wake.
" Utakua mtu wa kudharauliwa Sana
iwapo utamdhuru mtoto .dogo Azraj
Badru, mwana haramu" Mustafa
alitamka maneno ya kuumiza Sana kwa
Azraj na Azraj akataka amuonyeshe
kua hamdhuru mtoto isipokua anamfunza
adabh Salma. Salma alizidi jeuri.
" Bwana mkubwa, bila Shaka nitaenda na wewe" Salma alitabasamu na kuitua
Imani yake yote kwa Mustafa. Mustafa
alitabasamu kuonyesha kabisa ameridhika.
Mustafa akijiandaa kumpokea yeye
pamoja na mtoto, Azraj akaona huu
upuuzi gani? Kwa kweli siku za hivi
karibuni anahisi kumpenda Salma na hayupo tayari kutengana nae. Na isitoshe wanae binti Yao wa pekee.
Akiwaza hayo alijikuta tayari
amebonyeza trigger Ila hajaiachia. " Unafikiri unafanya nini Mustafa Badru??" Sauti ya nevi akiwa
amemshika Saida mateka kutoka katika
chumba alichokua ilisikika na kuidhuru
attention ya Azraj aliejikuta akiachia
trigger akiwa amesahau ya kwamba
akimlenga mtoto wake. Risasi ilinyooka
moja kwa moja na kukifikia kichwa
kidogo Sana Cha mtoto ambae alitoa
sauti moja tu na kukata sauti wakati huo huo. " Ng'aaa" hakutoa neno
jingine kabisaaa.
Ghafla Sana Salma aliekua amemshika
mtoto wake alihisi kupauka huenda
labda Kuna mtu alimmwagia jivu kutoka
utosnini mpaka usoni mwake. Nini hicho
aliona? Ni tundu! Tundu ! Tundu la risasi kwenye uso wa binti yake? "
Hapanaaaa!!! Salma alipiga kelele kiasi
kwamba sauti ilikata kwenye Koo lake.
Azraj pia alishtuka bila kutarajia alikua
amefanya nini?? Uso wake ulipigwa na mpasuko wa Karne. Ina maana kweli
kabisa alimuua binti Yake mwenyewe??
Azraj hakuweza kuamini alijikuta
akidondosha bunduki aliokua
ameishikilia. Na wakati huo huo alidondoka baada ya miguu Yake
kukoswa nguvu.
Mustafa pia ndo alibaki hoi kabisaaa,
yaani hakuweza kuamini hata kidogo nini
hiki aliona?? Hivi kweli Azraj kamuua
binti Yake mwenyewe. Huyu Ni
binadamu kweli???
Saida pia alibaki kwenye sintofahamu
hivi kweli kabisa Azraj alikua kamuua
binti Yake mchanga mwenye mwezi
mmoja tu? Haiaminiki hata kidogo.
Hakika alichanganyikiwa. Hakika
ninmaumivu yaliyoje kwa Salma jamani?
Amekubali kuishi kwa mateso na kupambana kwa juhudi zote ili kumuokoa
huyo mtoto Ila mwisho wa siku
amejikuta akimshuhudia binti Yake
akifa mwenyewe baba yake' mzazi ndo
kamuua. Kwa Nini alizaa na mwanaume
huyu? Inamaana hakua macho muda
akipewa mimba?
Mtu pekee ambae alikua na maumivu ya
mwisho na yasiyoeleweka alikua Salma
ki ufupi Salma alihisi Kama ubongo wake utakua wa Moto, hapana sio kweli?
Mawazo aliyo nayo sio kweli hata
kidogo? Huo sio ukweli?
' Haiwezekani? Haiwezekani? Hauwezi
kua ukweli huuu!! Jamani Kama Kuna
mtu aniamshe" Salma alichanganyikiwa.
Kwa Hali hiyo Mustafa alijikuta akiruka
kwa nguvu Sana kumuelekea Azraj huyo
mwana haramu aliesababisha kifo Cha
mtoto mdogo moyo wake uliuma alihisi
Kama vile mtoto Yule alikua sawa na
Shayma wake au Kim. Hivi mtu wa kawaida anawezaje kumdhuru mtoto
mchanga Kama azmina?
" Azraj Badru, unaweza kujiita
binadamu???" Mustafa alimfokea akiwa
hawezi kusubiri mbona Kama hamfikiii.
Moyo wake uliuma Sana kwa nini
jamani? Kwa nini Azraj amemuua huyo mtoto.
" Usithubutu kusogea" nevi
alimkumbusha Mustafa kua alikua na
Saida kama mateka mikononi mwake
hivyo ajitulize la sivyo ataimba haleluya.
Mustafa alisita wakati huo huo na nevi akasogea akiwa na Saida mikononi
mwake. " Bwana mkubwa Azraj naomba
unisamehe nitamtoa huyu kwa ajiri ya mustaqabali wetu" alizidi kumshika
Saida mateka huku Mustafa kailata
maumivu makali kila alipofikiria
kumuacha azraj aende. Kwa nini Nevi
ametaka wamuache mbona Kama
wamekamilisha wakimpa mwanya wa.
Kutoroka safari hii pia.
" Bwana mkubwa Azraj inuka
tuondoke"Nevi alimkumbusha.
" Usiendeshwe na hisia bwana mkubwa, yeye ni mwanao tu utapata mwingine"
nevi alimwambia Azraj ambae aliweza
kuinuka Tena. Alimwangalia Salma
aliekua akipiga kelele huko chini na
kulia kwa nguvu akiwa haamini iwapo Ni kweli binti Yake amekufa.
" Azmina wangu!! Mwanangu amka hapo, amka unyonye mpenzi, Sasa mama
atakupa nyonyo, binti yangu jamani
aamka" Salma alilia kiasi kwamba
alitamani achimbe shimo ajizike na binti
Yake iwapo amekufa kweli.
Moyo wake ulihisi maumivu makali mno
kila alipokumbuka siku ambayo
alijigundua yeye ni mjamzito. Bila
Shaka alifurahi Sana Sana yaani. Na
Tena sio tu hivyo Bali Tena alikumbuka
siku ameenda kwa mtoto wake na
kumueleza kua wapo mbioni kuitwa
wazazi. Mwisho aliambulia matusi na nusu kipigo kufokewa na alilazimishwa
kumtoa huyo mtoto. Tatizo alikua
mwanaume huyo huyo.
" Boss tuondoke" nevi alimkumbusha
huku akimtanguliza Saida nje na wakati
huo Azraj aliweza kutoka nje kabisa ya lango. Na hapo Nevi aliwasha gari
ambayo Azraj alikua kaingia tayari.
" Bwana mkubwa naondoa gari"
" Sawa" Azraj alimuitikia kwa
kutokuzingatia kabisa. Nevi alihisi
maumivu na tabasamu kwa kmwakati
mmoja. Na hapo Mustafa aliweza
kumvuta Saida upande wake.
Saida alikua na hasira na Mustafa kiasi
kwamba hakua tayari kuguswa nae.
Alimkimbilia Salma ambae alikua
akiombeleza kifo Cha binti yake. Saida
alijaribu kumgusa lakini Ni Kama Salma
alikua mfu anaeongea hakua alielewa
kitu zaidi ya kuchanganyikiwa. Mustafa
aliweza tu kumuinua na kumuingiza
kwenye gari aliyokua nayo Kisha Saida
akafata nyuma Yao akiwa amebeba
kiwiliwili kidogo Cha mtoto mchanga
ambae kwa Sasa anaitwa marehemeu"
Mustafa alishangaa kazi imekua rahisi
lakini ya majonzi matupu, hakuja kwa
lengo la kuondoka vizuri hivyo, alikuja
kwa lengo la Vita kabisa na Azraj na
hatimae Basi leo angemnasa huyo
mwana haramu. Lakini Mambo
yamekwenda ndivyo sivyo kwa ujinga na
uzembe wa Azraj kwa nini amemua binti
Yake mwenyewe.
aliweza kumwambia Gharib aondoke na
Salma huku yeye na Saida waliingia
katika gari nyingine. Kwa kweli Saida
alikua amechoka amekonda na amepoteza mvuto wake baada ya kukaa
mateka kwa muda wa mwezi na siku
kadhaa.
Hakuweza kustahimili furaha aliyokua
nayo kwamba atakua huru hivi Sasa.
Mwisho alitamani kumzaba makofi huyo
bwana Mustafa lakini hakuweza kwa
sababu alipoteza fahamu zake. Kwa
kweli ameteseka Sana.
Majira ya asubuhi Sana Saida alifungua
" Gharib, nadhani unaelewa kazi yako"
macho Yake akiwa na uchovu wa kutosha baada ya kulala usingizi wa
kuzimia tangu usiku. Aliweza kuamka na kujaribu kuuvuta mkono wake ili
ajioanguse uso baada ya kufungua
macho Yake. " Aiii" mkono wake
ulikwama.
Kwani alikua na nini mikononi mwake?
Alikua na kanyira alifungwa drilu
kwenye mkono wake.
" Aahh Nani Tena huyo??" Alijikuta
akikumbuka Maisha ya karaha na misukosuko aliyopitia hivi karibuni.
Lakini mwisho wa siku Jana Yake
alisaidiwa mwishowe na mume wake.
" Mustafa hatimae alinisaidia huyu
mwanaume mbaya" Saida alihisi kulia
alimuacha siku zote hizo kwa Azraj. "
Mustafa Badru we ni mchawi uliwezaje
kuniacha mateka masiku yote haya hivi
uliwahi kunipenda kweli??" Alipiga kelele
akihisi labda Mustafa alikua bafuni.
Lakini pia alikaa kimya baada ya kuhisi
harufu nzuri ya mapishi kwa ukaribu.
Sana.
" Haa!! Hapa Ni wapi?" Saida alianza
kupepesa macho eneo alilokuwepo? Ni kweli aliamka tu kudili na kumbukumbu
zake hata hakuweza kuwaza kuhusu
eneo Hilo. Kilikua Ni kijichumba kidogo
Sana. Mungu wangu, hakukua na choo
ndani humo. Chumba kulikua na kitanda tu. Mmhh kitanda? Mbona Kama vile
godoro lipo chini. Saida alitazama Tena na kupiga kelele kwa nguvu.
" Aaaaahhhhhhh" Mustafa haraka Sana
aliingia ndani baada ya kumsukuma mlango.
" Vipi Tena na wewe?" Ni usumbufu ulioje kua na mwanamke muoga Kama
Saida alipiga kelele kwa sababu tu aliona mende kwenye sakafu dah!!
" Mustafa Badru wewe ni mchawi, umenileta hapa kunipambanisha na mende, wewe na yule mtekaji
mnapishana nini Sasa?" Saida alilalamika na hapo Mustafa akabaki
amemuangalia.
" Saida" alishuka miguu Yake na kuangukia magoti take kwenye godoro
alilokua kalala Saida. Kwa kweli alikua
kammis Sana mwanamke huyo.
Alionekana mpotevu asie jua kwao kwa
jinsi alivyokua amekondeana Kama
karatasi.
" Mustafa usiongee, wewe ni mbaya
Sana Mustafa, kwa nini ilimuacha
mwenyewe??" Saida alijikuta kulia na kuanza kumlaumu. Mustafa pia alijihisi
hatia na maumivu kwa wakati mmoja, aliwezaje kumuacha siku zote hizo.
Macho yake yalishindwa jizuia na mwisho wa siku alidondosha machozi
Yake ya thamani.
Sehemu ya 174
" Ida Nili kukumbuka Sana mke wangu, nilikumiss Sana, nilikua nikihisi kifo kila
sekunde na dakika bila uwepo wako
maishani mwangu. Unajua inauma kiasi
gani kukaa bila wewe??" Mustafa alitoa
chozi na msisitizo kwa kila neno
akilitamka kwa kweli alikua akiumia
mno, Ni mwanamke pekee alieuteka
moyo wake? Lakini. Bado alilazimika
kukaa mbali nae' kwa ajiri ya kuokoa
familia nzima. Kwa ajiri ya Saida bila
Shaka yupo tayari kutoa kila kitu.
Lakini Saida pia asingemuona wa maana
iwapo angeitelekeza familia nzima kwa ajiri Yake.
" Mustafa kwa nini ulisita mpenzi wangu?" Saida alimuuliza baada ya
kuushika mkono wake mmoja" Mustafa
alimwangalia kwenye macho Yake mazuri
ambayo kwa Sasa jamani yamepoteza mvuto.
" Ningewezaje mke wangu? Hata wewe
ungeniona poyoyo iwapo ningemkabidhi
Azraj kila kitu kwenye Maisha yetu
tusingekua kitu. Licha ya kitu tungekua
chini yake tungekua watumwa wake.
Unadhani Mimi na wewe tungeipata furaha maishani mwetu??"
" Mustafa nisamehe, nilihisi Kama umenitenga" Saida alipata hatia kwa
kumshuku vibaya. Lakini pia akimuonea huruma alikua mwanaume mmoja tu na binadamu wa kawaida Ila alilazimika kubeba majukumu kibao kwenye mabega Yake.
" Ida natumai wewe ni mzima Sana si ndio" Mustafa alimhoji akikumbuka video ambazo Azraj alikua akimtumia
kila alipokua akimbusu Saida kwa nguvu na mwisho akimlalia juu Yake.
Saida alihisi majuto, bila Shaka yeye ni mzima lakini so msafi Tena kwa
Mustafa. Alimruhusu Azraj ambusu.
" Mustafa Mimi sikustahili Tena. Yule
Azraj mshenzi aliweza kunibusu"
Mustafa alitamani asisikie kauli hiyo
kutoka kwake angalau angepata nafuu
" Mimi kwa kweli, sidhani Kama naweza
Tena kwako! Mustafa tutawalea watoto tu, nimekuvunjia heshima" Saida alitoa machozi.
" Najua kila kitu mke wangu" Mustafa aliweza kumkumbatia. Hata hivyo
haikua Nia Yake na bado hata alikua
shujaa kujisimamia kwa mwanaharamu
yule Azraj. Aliweza Kama Angekua
mdhaifu bila Shaka angefanya nae
ngono Ila aliweza kujisimamia japo
alikua kwenye Hali mbaya.
" Alikua akinitumia video za kila
alichokua akifanya na wewe. Lakini
mwisho wa siku wewe bado Ni mke
wangu, uliweza kujilinda dhidi Yake na
hakufanikiwa kukuingilia kimwili, hiyo inamaanisha wewe bado Ni msafi"
Mustafa alimwambia Saida ambae bado alipata hatia.
" Mustafa mi sio mzuri Tena, nimekonda Kama nini jamani" Saida
alianza kulia upya na hapo Mustafa
akalazimika kumbembeleza.
" Unafaa ukale, inabidi utumie dawa
kwa muda wa wiki mbili na utumie
chakula kizuri na Cha asili vile
iwezekanavyo ili urejee katika Hali yako ya kawaida kabla haujakutana na watoto wetu wapenzi". Saida alitoa
tabasamu mwanana baada ya kuambiwa hivyo.
Ghafla moyo wake ulimuuma, bila Shaka
aliwakumbuka Sana watoto wake. " Ona
Sasa, ushaanza zako', una majukumu
huko ya kurekebisha, sio tu majukumu, una takiwa kudhuru kaburi la mpendwa
wako zarina pia, hivyo jitahidi ukae
katika Hali nzuri Sana mke wangu"
Mustafa alimkumbusha na kuinuka kutoka nje kwanza.
Saida aliweza tu kumsubiri arejee.
Mustafa aliweza kumtoa nje baada ya
kumtolea dripu Kisha akampeleka nje
kupiga mswaki. Saida alihisi Kama
alikua ndotoni. Ni eneo gani Hilo
ulimwenguni jamani? Mbona Kama wapo maporini kabisa?.
" Usishangae tupo kijijini huku, shinyanga kwenu" Mustafa alimwambia
Saida akabaki hoi. Walikua shinyanga.
Na hii Ni nyumba gani? Hapakua kwao
kabisa?.
huku, ili uwahi kutengamaa huku
ukizikumbuka kumbukumbu zako TAMU
za utotoni" Saida alitabasamu na
kumkumbatia mgongoni. Walikua kwenye
nyumba ndogo Sana ya vyumba viwiwli.
Yaani chumba na Sebure.
Nahisi nitapona haraka Sana mume
wangu" Mustafa alihisi Raha Sana
kukumbatiwa nae. Hakika hata yaye pia
alikua amemiss Hilo kumbatio. Saida
alihisi kana kwamba wamekuja kuishi
kwe
Dr khairat alikua bado amelala kwani
ndo kulikua Kuna chwea na anga
taratibu linaanza kupata mwangaza
mweupe. Alipata usingizi wa kutisha na
Kisha kuota ndoto mbaya usiku kucha
" Ndio mpenzi, nimeamua nije nikuuguze
Sasa ndo Kama hivyo Tena ameamka
akiwa amechoka mno.
" Aahhh" alipiga mwayo.
" Mama, niandae kwenda shule mbona
siku hizi unachelewa Sana?" Adil
alimuuliza mama Yake Kwani alikua
hamuelewi siku za hivi karibuni.
" Usijari nakuandaa." Alimjibu Adil
Mara akashtuka baada ya kutazama
dirishani. Dirisha likiwa wazi aliweza
kuona kivuli Cha mwanamke mrefu'
mwenye nywele ndefu pia. Ni Kama
alikua kavaa gauni jeupe. Na alionekana
kumpa mgongo. Bila kusita alijikuta
alihoji kwa khofu. " We ni Nani?"
Adil aligeuka na kutazama dirishani
mahali ambapo mama yake ametazama.
Hakika hakuweza kuona chochote,
aliyarejea macho ya mama Yake Kisha akanena.
" Mama! Hakuna mtu huko" Dr khairat alimgeukia mwanae kwa wakati huo. "
Ni huoni chochote?" Alipata mshangao.
" Hamna kitu mama" Adil alimsontea
kidole dirishani na yeye akaona kweli
hakukua na chochote. Dr khairat alihisi
kuvurugwa. Haamini kabisa kwenye
Mambo ya mizimu na majini japo aliwahi
kumuwekea Mustafa dawa Fulani ili awe
wake ki uchawi. Lakini ilishindikana
yaani Mustafa hakuweza kurogeka. Ila
hii Hali ya kua anaona Marue rue kwa
kweli inatisha.
" Mama nachelewa" Adil alilalamika na
hakua tayari kuandaliwa na mfanyakazi
kwani mfanyakazi aliepo kwa Sasa Ni
no na yeye hakua amemzoea.
Dr khairat haraka Sana alimuandaa
mtoto wake na kumpeleka shuleni.
Alipofika huko shuleni alimkabidhi kwa mwalimu wake wa darasa. Wakati huo
pia Muzda alikua amemfikisha Shayma
shule kumkabidhisha kwa kweli alifaa
kumkabidhisha kwani hawakuwepo nchini
kwa muda mrefu. Wanne hao walikutana
bila kutarajia.
" Aunt Muzda, nataka nihame hii shule"
Shayma aliongea kwa sauti mbelel ya waliku wake baada ya kuwaona Dr
khairat na kijana wake.
" Kwa nini mpenzi? Hii shule ninnzuri
mno" mwalimu alijaribu kumbembeleza, Kwan Ni donge Nene ambalo litawahama
iwapo Shayma akiichukia shule Yao. "
Kwani nini mbaya na shule"
" Shule sio tatizo mwalimu, tatizo Ni huyu mwanamke mchawi!!" Dr khairat
alihisi kufa kufa huku walimu waliona aibu na Muzda akitabasamu. ..
" Nalazimika kuonana nae kila siku nikija shule ntakufa kwa hizi nyayo zake tu" Shayma Ni mdogo lakini
anaulimi mkali kupita maelezo . Dr khairat alishindwa kujizuia kumuinulia
mkono wake ampige.
" Lo! Thubutu utue mkono wako kwa binti yangu" macho ya Muzda yalimtoka
mithili ya mjusi aliebanwa na mlango huku akiwa kaudaka mkono wa Dr khairat.
" Una timamu wewe, hivi umewahi
kumfunza adabu huyo binti yako?? Hiyo
Ni njia gani ya kuongea na watu wazima??" Dr khairat alitamani amuue
huyo mtoto kwa kumfedhehesha mbele ya walimu waliokuwepo.
" Shayma wewe unatabia mbaya Sana" Adil alilalamika.
" Angalau haikinganishwi na ya muuaji
Kama wewe na yako, nyie Ni mashetani
wawili" Shayma alizidi kutoa makali
yake Tena alipomkumbuka HudHud ndo kabisaa. Walimu hawakua na neno dhidi
ya huyo mtoto na Muzda hakujari
kuhusu tabia hiyo japo alikua mdogo
alistahili kumkanya lakini yeye pia
aliwachukia hao wawili kwa wakati huo.
" Umeniona huyo mtoto alivyokua Hana
adabu" dr khairat alijivuta kumsogelea
shayma. Wee Muzda hakusubiri
kumsukuma mpaka akadondoka chini.
Kwa kweli alitamani Sana kupata muda
wa kumuadabisha huyu mwanamke
mchawi. Kwa sababu Yake na huyo
mwendawazimu Azraj wao wamepitia
nyakati ngumu Sana.
" Aunt Muzda mpige Sana" Shayma
alichochea alikua na hasira nae kana
kwamba alifahamu huyo mwanamke
alimuulia mama Yake.
" Muache mama yangu!!" Adil alifoka na kwenda kujaribu kumzuia muzda
asipigane na mama Yake.
" Unathubutu vipi kuwazuia, usiiingilie ugomvi wa wakubwa mama yako hajakufunza" Shayma alimvuta Adil pembeni. Daa! Mtoto ana akili mbovu huyu.
" Usiseme mama yangu hajanifunza, unataka nikuache apigwe" Adil alilalamika.
" Kwani yeye so mkubwa, Tena yeye ni mzee kuliko aunt yangu, iwapo
anajiamini anaweza kumpiga pia, sio haki sisi kuingilia" Shayma alimchochea
Adil ambae aliwaza na kuamini kwa
wakati huo huo kua mama Yake bila
Shaka ananguvu za kumshinda Muzda.
" Mama moige huyo mwanamke bila
Shaka utamshinda" Shayma alihisi
kucheka kampumbaza kizembe kabisa.
" Huo ndo umwanaume usiiingilie ugomvi wa wanawake" Shayma alitabasamu
kimya kimya akiamini kabisa aunt Yake
Muzda atamshinda huyo mchawi.
Dr khairat alijaribu kumzuia huyo
mwanamke mdogo asimoige kwani
aliamini matokeo take iwapo atamdhuru, isitoshe yeye na Azraj kwa Sasa Wana
Hali mbaya. Na Muzda kachumbiwa na
Yasir Sabodo. Aha aa, sijui itakua vipi
kwake Kama akimuumiza. Kwa ajiri hiyo
Muzda alijikuta anauoiga uso wa Dr khairat unavimba na kua mwekundu
Kama nyanya.
Walimu waliokua pembeni walihisi
kumuhurumia Dr khairat lakini wakati
huo huo pia walifurahia tukio Hilo, kwani kwa Sasa taarifa zinazo sambaa
kuhusu yeye Ni jinsi alivyo mwanamke
muovu. 'acha akome' fikra za
wanawake wengi zilimaanisha Hilo.
Saida alikua amekaa kwenye godoro
ambalo halikuweza kumiliki hata kitanda
ndani ya chumba. Wakati ambao alifika
mustafa. Na kuanza kumnywesha supu
kwa mapenzi.
" Mustafa wewe, bila Shaka ulichoka
Sana kufanya kila kitu ukiwa
mwenyewe, nakuonea huruma" Saida
alimaanisha alichokisema. Mustafa
alimtazama sura Yake ambayo
alionekana kua na furaha lakini bado
hakua amerejea kwenye uzuri wake
awali klvaada ya kupitia kipindi kigumu
Cha Maisha akiwa kifungoni. Ila bado
alimuonea huruma yeye aliekua huru vioi
kuhusu yeye?
" Mpenzi wewe hapo, ndo unafaa
kuonewa huruma. Mumeo Ni mwamba
usioyumbishwa. Unafaa kushukuru
kwamba Ni akili tu na sio nguvu nyingi
nilizotumia kuweka Mambo sawa"
alimkumbatia kwanza na kumbusu.
Hakika alimiss midomo Yake.
Wakati anambusu ghafla Saida
alikumbuka namna ambavyo Azraj alikua
akimbusu Mara moja alihisi hatia
kuhusu usaliti huo na kumsukuma
Mustafa pembeni. Mustafa
hakupendezwa na Hilo Jambo, kwa nini
alimsukuma? Na uso wake ulionekana
kufadhaika kana kwamba busu lake
lilitisha.
Sehemu ya 175
" Ida" alimuita na kubaki kamtazama.
" Mustafa samahani" Saida alihisi kulia
" Samahani haisaidii, sitaki uwe na mawazo hayo machafu, kwangu Mimi
wewe ni kila mwanzo na mwisho wa hisia
zangu, sijari kuhusu Nani au nini
kimetokea still we ni wangu" Mustafa
alimkumbatia mke wake Saida
akashindwa kujizuia kulia.
' Ni kweli yeye ni mume wake, haijalishi alipitia wakati gani mgumu
hata yeye alipitia wakati mgumu pia
bila uwepo wake. Na hamna kitu
kinauma Kama kushuhudia mpenzi au
mke wako anafanyiwa matukio ya
kimahaba na mtu mwingine, Sasa kwa
nini Mustafa ajifanye Kama asie moyo?
Ina maana hakua akimuonea kichefu
chefu kabisa.
" Usiniwazie vibaya mke wangu, iwapo
nitaulizwa mwili ambao nakupenda
katika Maisha yangu, iwe kuubusu au
kukupenda kupita kuutomasa na
kuichezea nitakavyo bila Shaka Ni wa
kwako, hakuna mwili mwingine, siwezi
kuacha kuufikiria hata Kama
ungefanyiwa kitu gani?" Mustafa alisita
kuongea na kumvuta Saida mbele Yake
akitaka watizamane uso kwa uso.
" Mimi.... Na..mmh" hakuweza
kumaliza kuongea Mustafa alianza
kumbusu Tena. Hayupo tayari kuikosa
hii midomo mizuri na mitamu hata ikiwa
imechanika chanika kwa vidonda, bila
Shaka anampenda hivyo hivyo,
ananipenda hivyo hivyo midomo mitamu ya Saida.
Saida hakua na ujanja zaidi ya kutulia
akipewa Hilo busu lake la milele. Hakika
hafikirii Kama katika haya Maisha Kuna
mwanaume mwingine atawahi kumbusu
zaidi ya Mustafa wake.
Baada ya busu hiyo Saida angalau akili
Yake ilitengamaa na kuacha kujilaumu, Mustafa aliweza kumlisha supu
iliyokuwepo. Saida alikunywa na kula
alichoandaliwa na mume wake kwa
utiifu. Hatimae baada ya muda alitumia
dawa kwa wakati kwa kweli Mustafa
alikua muuguzi mzuri Sana.
Dr khairat alirejea nyumbani kwake
baada ya kutoka shuleni, hakika alikua na maumivu Sana, aliteremka kwenye
gari Yake na kuisogelea nyumba Yake.
Alikua na maumivu kiasi kwamba alikua
akihema kwa nguvu. Ghafla akahisi
Kama Kuna mtu anapiga nyuma Yake
akashtuka na kugeuka nyuma. Aliangalia
kwa uwoga na kushangaa hakukua na mtu yeyote. Alipotezea na kudhani Ni
Marie rue labda anaona. Akaendelea na
safari Yake, alipiga hatua kadhaa kabla
asikie sauti ya mtu akicheka kwa nguvu
nyuma Yake
" Ahahahaahaha ahahaha" sauti hiyo ya kicheko kikali ilimshtua Dr khairat
ambae aligeuka haraka na kutazama
nyuma kwa uwoga na hofu ya hali ya
juu. Asalala hakukua na mtu.
" Uuuu wewe Ni Nani??? Kwa nini kwa
nini unanitisha???" Dr khairat aliziba
masikio yake' maana Ile sauti
haikuweza kukoma alipiga kelele wakati
huo. " Achaaaaa achaaa tafadhari
unaniumiza masikik yangu, hii hhh"
akihema juu juu na kuziba masikio kwa
hofu. Sura Yake iliyokua imechakaa
kipigo ilimuuma Sana.
Dr khairat hatimae alikumbuka kua
alikua na miguu, aliweza tu kukimbia
kuelekea ndani, ghafla akaanza kuisikia
sauti ikitokea ndani, Sasa hii haikua
sauti ya kike ilikua sauti ya kiume
ambayo aliizoea. " Kipenzi, Adil
anaumwa !!!! Kipenzi, nataka kumbeba
mtoto wetu" hayo yalikua maneno ya Dr Hizaan kabla hawajatalikiana. Kwa nini
anaisikia hivi sasa? Hapana jamani? Hii
sio haki, na hii haiwezi kua kweli
kabisa. Kwani Dr Hizaan. Yupo hospital
amelazwa.
" Usinitishie wewe sio Hizaan, wewe sio
Hizaan najua, unathubutu vipi kunitishia
hakika huniwezi kwa lolote" dr khairat
alijaribu kuweka ujasiri wa kulazimisha
Mara ghafla akasikia sauti ikitokea
kusikia eleweki ikimhoji.
" Kweliii??? " Dr khairat alishtuka
mapigo ya moyo wake yalikua mwisho
kabisa wa speed Kali, kwa nini Mambo
mabaya yamekua upande wake siku hizi.
Alihisi Kama atakufa, lakini bado alifaa
kuwaonyesha watu hao kua Hana uoga kabisa.
" Ndio sikuogopi kabisa" alijibu na kujitahidi kuitafuta hiyo sauti isiyoonekana.
" Ooh noo, kipenzi umeyakoroga" sauti ya Dr Hizaan ilimjibu, sio Siri Dr
khairat alihisi kuchanganyikiwa, mbona
Sasa atakua chizi hivi karibuni. Mara
ghafla akaona kamba ikimrukia na
alieirusha hamuoni, bahati mbaya alihisi kusukumwa na mtu bila kutarajia.
Aliemsukuma alikua Nani ? Alijikuta
tayari amenasa kwenye mtego wa
kamba iliyokuja Kasi upande wake na
akaanza kuvutwa.
" Hapana jamani, hii sio sawa, nisamehe nisamehe, sirudii kukudhihaki"
Dr khairat alipiga kelele kwa nguvu na kuhisi Kama vile atakufa. Ndani
alikuwepo mfanyakazi wake tu na kwa nini alikua hamsikii jamani?.
" Saadaaaaaa" alipiga kelele kumuita na hatimae msichana wa kazi mwenye umri
mdogo mdogo alitokea ndani, huyu Ali
mpya tofauti na wa kwanza. Alipomuona
Dr khairat alihisi Kama atazimia, maana
ghafla akiwa pale chini alishangaa kuona
hamna kamba inayomvuta Tena Wala zile sauti za kutisha hazikuwepo Tena.
" Dada Kuna nini?, Mbona upo chini?"
Binti yule alikimbia na kwenda kumuinua
kutoka hapo chini akijaribu kumuweka
sawa. Dr khairat hakuamini kua hakuna
mwingine ambae anahisi hayo maruerue zaidi yake.
" Dada kwa nini una majeraha mwili mzima?" Dr khairat kwa kweli hakua na ujasiri wa kumjibu msichana huyu
kwamba alikua kapigwa na msichana
mdogo zaidi Yake, na mbali na Hilo
Hana uwezo wa kumuuliza iwapo Kuna
watu walikuja hapa kabla Yake.
" Hapana Ni ajari tu" alijikaza kukaa
sawa huku aliinuka na kujaribu
kutembea, daahh Maisha haya, miguu
Yake iliyokua na kamba tayari
ilifunguliwa na kuachwa huru lakini
tayari alikua na alama miguuni.
Alikishika shingo Yake na kujilaza
kutembea kuelekea ndani, " namtaka
binti yangu, ulifaa kuniua pamoja nae"
sauti hiyo ilimfanya Dr khairat apige
kelele Tena. msichana wake wa kazi
alishindwa kabisa kumuelewa alikua na shida gani?
Baada ya Azraj na nevi kufanikiwa
kumtoroka Mustafa pale kisiwani
mwanza, walitokomea katika Kijiji
kimoja kilichojitenga huko singida kwela
wanyaturu. Nevi hakua tayari kumdhuru
na kumuonyesha Azraj kua yeye sio mtu
wake Kama anavyodhani baada ya
kupokea taarifa kutoka kwa master wake.
Walifaa kupata nyaraka za ramani ya
viwanda vipya ambavyo vilikua
viliandaliwa na kampuni ya Badru, lakini
pia Bwana Badru alihitaji kumuadhibu
Azraj kwa fedheha aliyomsababishia,
hakutaka aishie mikononi kwa Mustafa
iwapo alimzaa mwenyewe anafaa
kumuadabisha ipasavyo na pia
amkabudhi katika mikono ya Sheria.
" Unawaza nini dogo?" Azraj aliekua na huzuni alihisi Kama vile nevi alikua
amepoteza ki fikra.
" Hapana boss, nipo nawaza kuhusu
Maisha haya, sisi Ni watu wa matukio
lakini vipi tumeishia hivi, tumeishia
kutumia fedha na Mali bila kuingoza
fedha sijazoea haya Maisha Mimi" Nevi
alikua mwema Sana na mzuri kwenye
kuigiza.
" Upo sahihi, haujazoea Maisha haya
lakini usijari, mwisho wa kuteseka
unakuja, kwani Nina kitu Cha thamani
Sana ambacho Badru wanategemea, bila
Shaka hawawezi kuniangamiza" alitoa
macho Yake ya tamaa na maovi kwa
upana.
" Kitu gani hicho boss, wakati kwa Sasa
hata mtoto wako u.empoteza, huna haja ya kusita sita Ni mwendo wa
kufanya matukio bila uwoga" Nevi
akilitamka neno uwoga alimtazama
Azraj alieonekana kukosa moyo jinsi
alivyoshukwa na sura.
Hakika Ni kweli alikua amepoteza mtoto
wake. Yote Ni kwa sababu Yake
mwenyewe, kwa nini alimpotezea mtoto
wake? Kwa nini alifanya mzaha kwenye
uhai wake? Ni kweli kwamba alikua
amemkataa hapo awali tangu akiwa na
mimba lakini alimpenda baada ya kuhisi
kua baba kwa Mara ya kwanza, Ila
mwisho wa siku aliishia kukaa nae kwa
siku kadhaa tu Kisha akamuua.
" Boss samahani, sikufaa Kutamka
kumhusu" Nevi aliomba samahani.
" Hapana sio kosa lako" Azraj alijaribu
kujituliza na kutamani kujua kuhusu
Salma pia, kwa kweli alikua amechelewa
Sana kumuelewa huyo mwanamke. Ila
sio sawa kufanya hivyo anafaa kusahau
juu yake pia kwani Salma hatoweza
kumsamehe hata aliishusha mbingu
Kama ushahidi wa kuombea msamaha.
" Dogo, Nina kazi ya muhimu usiku wa leo, jiandae mapema" Azraj alimwambia
Nevi ambae hakutambua Ni kazi gani?
Lakini moyoni Azraj aliapa kumpata
bwana Rashid Badru na kummaliza usiku
huo kwani yeye ndo chanzo Cha mateso
yake. Alikua baba yake' lakini hakuwahi
kumfikiria Kama mwanae alimtanguliza
Mustafa mbele.
" Sawa boss" alijibu Nevi na kusogea
jikoni ambapo Ni Kama chakula kiliiva
huko.
" Rashid Badru, kwa ajiri yako wewe
Mimi nilizalimu nikiwa mwana haramu, kwa ajiri yako wewe mama yangu
alifariki, na kwa ajiri yako wewe
Maisha yangu yamekua kituko
kisichoeleweka. Na kwa ajiri ya mwanao
mpendwa Mustafa na familia yako
mjomba wangu hivi Sasa anapumulia
kaburini, bila Shaka adhabu ya kifo inakustahili.
Iwapo ukifa wewe, nitakua nimeua
familia nzima ya Badru kwa maumivu
ambayo watayapata moyonj mwao, hakika watahitaji msaada wa kupozwa.
Haswa Mustafa nataka uonje Radha ya
kumpoteza mzazi unampenda Sana Kama
nilivyompoteza mama yangu Mimi."
Unahisi nini kinafuata?
Tukutane sehemu ya 176