"Hapana, utakuwa Bi Jones
daima."Aunty Manka aliongea kwa sauti dhaifu.
“Aunty Manka, ni sawa, tayari ninajua ukweli kwamba nilichukuliwa na familia ya akina Jones. Nina hakika unajua hilo pia baada ya kuwa mlezi wa bibi yangu kwa miaka mingi iliyopita.”
“Nani kasema hivyo?” Aunty Manka
alijibu huku akiwa amekasirika. "Bila shaka wewe ni sehemu ya familia ya Jones!"
Jambo hilo lilimshangaza Lisa. “Nilisikia
kutoka kwa Lina. Mbali na hilo, sidhani kama wanandoa wa Jones wangefanya
mambo hayo kwa binti yao wa kuzaa wenyewe.”
“Haya yote lazima yamekuwa magumu sana kwako. Familia ya Jones imekosa utu kabisa." Aunty Manka alikohoa mara
kadhaa kwa hasira. "Sio tu kwamba
walinifukuza nyumbani kwao, lakini hata
walikuambia kwamba wewe si mtoto
wao. Ina maana wamesahau ahadi
walizotoa kwa babu yako na bibi yako??" "Anti Manka, ulifukuzwa nyumbani?" Lisa alishtushwa na habari hii. "Lakini
nilichosikia kutoka kwao ni kwamba uliondoka kwa sababu haukuwa tayari kumtunza Bibi baada ya kupooza."
“Bibi Masawe amenisaidia sana na alinitunza maisha yangu yote. Nisingeweza kumtupa alipokuwa akinihitaji sana.” Aunty Manka alijibu. Macho yake yaling'aa kwa machozi.
“Bibi mdogo Lisa, kwa kweli wewe si binti wa Jones Masawe. Mama yako
mzazi ni Sheryl Masawe, yule
mwanamke unayeamini kuwa ni shangazi yako. Alikuwa na mimba yako
kabla ya ndoa. Babu na Bibi yako
waliogopa kupoteza heshima yao, bila
kusahau kwamba hii ingeweza kufanya
iwe vigumu kwa mama yako kuolewa
tena. Ndiyo maana walikukabidhi kwa
Jones Masawe ambaye ni mjomba
wako.”
Lisa alihisi ulimwengu wake ukipinduka chini-juu. Kamwe asingetarajia kuwa
Sheryl alikuwa mama yake. Ilikuwa na maana sasa kwamba babu na bibi yake
walimchukua kutembelea kaburi la Sheryl kila tarehe ya kumbukumbu ya kifo chake. Haishangazi pia alifanana
naye sana! Hata Alvin alishawahi
kumwambia hivyo siku walipokwenda kumtolea sadaka bibi yake kaburini.
"Baada ya kukuzaa, mama yako
alifunga safari ya kikazi kwenda Kigoma
na kwa bahati mbaya akatoweka
kwenye ajali ya kimbunga," Aunty
Manka alisema katikati ya kwikwi.
“Kilikuwa kimbunga cha ajabu na cha
kutisha na zaidi ya watu kumi walikufa.
Kufikia wakati walipoupata mwili wake, ulikuwa umeharibika sana, hata
hawakuweza kumtambua.”
Lisa alihisi kukosa hewa kana kwamba
hewa yote ilikuwa ikitolewa kwenye
mapafu yake. Kelvin, ambaye alikuwa
akisikiliza kando, alimpigapiga begani kwa upole.
Aunty Manka aliendelea, “Mama yako
alikuwa mwanamke aliyefanikiwa ingawa alikuwa mdogo. Mawenzi
Investiments, ambayo ni kati ya biashara 100 zilizofanikiwa zaidi
Tanzania, ilianzishwa na yeye peke yake.
"Mama yangu ndiye mwanzilishi wa Mawenzi Investiments?" Sura ya mshangao iliwaka usoni mwa Lisa. Mwanga wa upeo ulipita akilini mwake."
Sasa aliweza kutambua ni kwanini
Jones alifanikiwa kuwa mwenyehisa
mkuu wa Mawenzi Investiments."
"Nini? Jones ndiye mmiliki mkuu wa hisa?" Aunty Manka alicheka.
“Inawezekana bibi yako ana…”
"Bibi alifariki siku chache zilizopita." Lisa
alimkatisha ghafla. Aunty Manka alitoa
macho kwa mshtuko. Dakika chache
baadaye, hatimaye machozi mengi
yalimtoka kwenye kona za macho yake.
Aunty Manka alijikaza na kusema kwa
unyonge, “Bibi yako asingekufa ghafla.
Hakika kuna mengi nyuma ya kifo
chake! Lisa, kuna kitu unahitaji kujua. Baada ya mama yako kufariki, babu na bibi yako walikuwa wakisimamia
Mawenzi Investiments kwa siri. Ili
kuhakikisha Jones atakutunza, aliweka wosia. Wewe na Jones kila mmoja
angepewa 30% ya hisa za kampuni hiyo mara tu utakapokuwa mkubwa na baada ya bibi kufa.”
Lisa alianguka kwenye kiti alipopokea
habari hiyo ya kutisha kama bomu.
“Baada ya Kibo Group kushuka, kuna
uwezekano kwamba Jones Masawe alipanga njama ya kumuua bibi yangu ili
kurithi hisa zote za Mawenzi
Investiments? Hapana, hilo
haliwezekani. Yeye ni mama yake, baada ya yote.” Lisa alishindwa kuamini.
Kelvin alishusha pumzi na kusema.
“Jones amezoea kuwa katika nafasi ya
madaraka maisha yake yote. Huenda
hujui hili lakini watu wanaweza kufanya
lolote ili kudumisha maisha yaliyojaa
utajiri na ushawishi. Tangu mwanzo wa wakati, kumekuwa na rekodi za ndugu
wa damu kushambuliana, kurogana na kuuana wakipigania kuwa warithi wa
familia tajiri. Isitoshe, bibi yako alikuwa amepooza kabla ya hii. Pengine
alimwona kuwa mzigo.
Sura ya 102
Aunty Manka aliitikia kwa kichwa. “Pia, sikuwahi hata siku moja kuamini kuwa
kupooza kwa bibi yako ilikuwa ajali. Siku
moja Lina alikuja nyumbani na mara bibi
yako akaanguka kutoka ghorofa ya pili
muda mfupi baada ya kupanda. Tangu
siku hiyo nikafukuzwa na baadaye
nikasikia kuwa bibi yako amepooza."
Lisa aliinua macho yake kutoka chini
huku mshtuko ukipita ndani yake. Mtu
kama Lina angewezaje kuwa mshenzi
kiasi hicho kumdhuru bibi yake
mwenyewe?
"Nina hakika kwamba lazima
amegundua kuhusu uhusiano wako na Mawenzi Investiments na kwamba
wewe si binti wa kuzaliwa wa Jones"
Aunty Manka alikisia.
"Shangazi Manka, ulipaswa kuniambia kuhusu hili mapema." Lisa alijisikia hatia
sana.
“Nilitaka sana lakini nilishindwa kwa
sababu familia ya Jones ilikuwa
ikinitafuta ili kunidhuru. Sikutaka
kukuingiza katika matatizo makubwa.
Nadhani Jones hakuridhika bila kujua
asilimia 30 ya hisa zimeenda wapi, au labda alitaka kuniua ili nipeleke siri hii
kaburini. Ndiyo maana nimekuwa
nikiishi kwa kujitenga na kujificha, bila
kuthubutu kuonyesha uso wangu
hadharani. Na hata namba za simu
nilibadilisha.” Aunty Manka alimshika
Lisa mikononi na kumwambia, "mtafute
mmoja wa wanahisa huko Mawenzi
Investiments anayeitwa Chris Maganga.
Mama yako aliokoa maisha yake hapo awali. Anazo nyaraka zinazohitajika za kampuni ya Mawenzi."
“Sawa.” Lisa alikubali kwa huzuni, hatimaye akauliza kwa msisitizo, “Shangazi Manka, unajua baba yangu halisi ni nani?”
Mwanamke yule mzee akatikisa kichwa, akihema. "Sina hakika, lakini nadhani anaishi huko Nairobi."
Mwanga wa matumaini ukaangaza machoni mwa Lisa. Ilionekana kuwa
angeweza kupata nafasi ya kukutana na baba yake mzazi siku moja. Hata hivyo, kwa nini alimtelekeza yeye na mama yake? Labda alikuwa ameanzisha familia nyingine kwa muda mrefu.
Wanawake wote wawili katika wadi ya hospitali walinyamaza kimya. Bila kujali, Kelvin alipendekeza, “Kwa ajili ya
usalama wa Aunty Manka, ni bora
tukimhamishia hospitali nyingine ili
akina Jones wasimpate. Namfahamu
mkurugenzi mkuu wa hospitali binafsi
ambaye anaweza kutusaidia.”
“Uko sahihi. Aunty Manka hawezi
kubaki hapa,” Lisa alikubali.
Baada ya hapo, walitumia saa iliyofuata
kuwasilisha makaratasi yaliyohitajika kwa ajili ya uhamisho huo. Hata hivyo,
alipokuwa akiandaa taratibu pale
mapokezi, Lisa alishindwa kumuona
Angela Harrison, yule dada mdogo wa Sam Harrison aliyekuwa anampenda
sana Alvin, ambaye kwa bahati mbaya
alikuwepo kwa ajili ya kumfanyia
uchunguzi wa kawaida mama yake.
Alichukua picha ya Lisa akiingia kwenye lifti na Kelvin.
Angela alimtumia Alvin picha hiyo bila
kusita. [ Alvin, huyu si mpenzi wako?
Ina maana mmeachana? Nilimwona
akiwa na mwanaume mwingine.] Angela
alifurahi baada ya kutuma ujumbe huo.
Kwa muda mrefu alikuwa
amekasirishwa na Lisa na alikuwa
akitafuta nafasi ya kumgombanisha na
Alvin. Sasa, hatimaye alipata nafasi ya kumchongea.
Alvin ambaye alikuwa anatoka kazini
ghafla alisikia simu yake ikitetemeka. Uso wake ulianguka mara ya pili
alipobonyeza ujumbe huo. Picha hiyo ilidhihirisha wazi Lisa na Kelvin wakiwa pamoja hospitalini. Akampigia simu mara moja. “Uko wapi?”
“Um… Hospitalini,” alikiri baada ya kusitasita kwa muda mfupi.
Uso wa Alvin ulilegea kidogo. Angalau hakusema uwongo juu ya hili. “Upo pamoja na nani?”
Lisa alimtupia jicho la haraka Kelvin ambaye alikuwa akiongea na daktari aliyehusika kabla ya kwenda pembeni.
"Nipo na daktari. Mlezi ambaye alikuwa akimtunza bibi yangu ametoka tu kufanyiwa upasuaji. Yeye hana ndugu au jamaa wa karibu wa kumwangalia.
Labda nitachelewa kufika nyumbani
baadaye kidogo leo."
Alvin alijua Lisa alikuwa anadanganya.
Alijua alikuwa na Kelvin. Nia ya hatari
ikaangaza machoni pake. Alvin alijisikia vibaya kwa kuona Lisa akiwa na shida
angependelea kutafuta msaada kutoka kwa Kelvin badala yake. Uhusiano wake na mwanaume huyo ulikuwa wa karibu kiasi gani, kweli?
"Umekasirika?" Lisa aliuliza kwa tahadhari baada ya ukimya wa muda
mrefu kutoka kwa Alvin. "Muuguzi wa zamu anaweza kuja saa tatu usiku, kwa hivyo itabidi nisubiri hadi wakati huo."
"Sawa!" Alvin alijibu kinyonge kabla ya kukata simu ghafla. Kisha, alijaribu
kutuliza hasira yake iliyokuwa ikimpanda kwa kukisugua kichwa chake taratibu.
Alvin alijikumbusha kuwa asiwe na huzuni sana. Alihisi huenda labda Lisa hakuwa na mpango naye ndiyo maana
mara nyingi alikuwa akitaka kuwa karibu na Kelvin.
Simu ilikatika ghafla. Lisa alibaki
akiitazama simu ile kwa sekunde
kadhaa mpaka Kelvin alipomshtua. "Alikuwa Mheshimiwa
Kimaro? Anakuja kumuona Aunty
Manka? Basi labda niende ili kuzuia
ugomvi usio wa lazima.”
"Hapana, hakusema kama anakuja au la." Ghafla, hisia ya ajabu ikatokea moyoni mwake. Hiyo ilikuwa ni hisia
yake tu. Alvin alikuwa hajasema lolote kuhusu kwenda ama kutokwenda
kumuona Aunty Manka.
Kelvin alionekana kushtuka lakini punde
akaonyesha tabasamu. “Naam, ni kawaida. Yeye si familia hata hivyo.”
Alichana na mada hiyo na kumwambia, “nilizungumza na daktari mapema kwa
hiyo usiwe na wasiwasi sana.”
“Asante.” Lisa alikuwa na shukrani za
dhati kwa Kelvin. Asingefanikiwa sana
siku hiyo bila msaada wake. Kwa kweli, alifikiria kumwomba Alvin msaada hapo
awali lakini alipokumbuka tabia yake ya
dharau na kutojali, alikuwa na hakika
kwamba wasingeishia pazuri. Pia
alikumbuka kwenye makubaliano ya ndoa yao alishawahi kumwambia
kwamba hataonana na ndugu zake.
"Ni sawa. Naam, naweza kuondoka
sasa. Nina miadi ya chakula cha jioni kazini jioni hii." Kelvin alielewa umuhimu wa kutovuka mipaka.
“Sawa.” Lisa akamsogeza mpaka
mlangoni.
Alvin hakumpigia simu usiku mzima.
Hatimaye Lisa aliendesha gari hadi nyumbani baada ya muuguzi kujitokeza.
Ukiachana na Charlie na watoto wake
watatu waliokuwa wakicheza huku na kule, alikuwepo Aunty Linda pekee
aliyekuwa akitazama TV sebuleni.
"Mheshimiwa Kimaro yuko wapi?" Swali
hilo lilimshangaza sana Aunty Linda.
“Si alikuaga? Bw. Kimaro alinipigia simu
mapema jioni hii akisema anaenda kwa
safari ya kikazi hadi Nairobi. Hatarudi
kwa siku chache.”
Lisa alipigwa na butwaa na kukaa
kimya. Kwa kweli hakuwa na habari
kuhusu hilo. Lisa aliingiwa na simanzi
sana. Akiwa mpenzi wake, Alvin
hakuuliza kuhusu hali ya Aunty Manka
wala hakumjulisha kuhusu kwenda
safari zake za kikazi. Nini kilikuwa kikiendelea naye?
Baada ya kuelekea ghorofani, alimpigia simu Alvin. Kelele ya mandhari
iliyosikika nyuma ilikuwa kubwa kwenye simu. Aliweza kujua mara moja kwamba
alikuwa mahali fulani pa starehe kama
baa au klabu.
“Uko wapi? Si umeenda kwa safari ya kikazi?” Lisa alimuuliza kwa mshangao.
"Ndio." Sauti yake ilionyesha kutojali.
Lisa hakufurahishwa na jibu hilo.
“Mbona hukuniambia?”
“Kwani ni lazima nikuage kila ninaposafiri?” Sauti yake kujeuri na ya dharau ilimkatisha tamaa.
"Sawa, sitauliza tena siku nyingine."
Lisa alikata simu, akajilaza kitandani na kuanza kulia.
Hata hivyo, Lisa alifurahishwa sana na taarifa alizopata kutoka kwa Aunty
Manka siku hiyo, kwamba mtu alyeamini
kuwa ni shangazi yake kumbe ndiye alikuwa mama yake, na yeye ndiye
mrithi wa Mawenzi Investments. Alitamani kumwambia habari hizo Alvin lakini hakumpa hata nafasi hiyo.
Sura ya 103
Siku mbili zilizofuata, Lisa alitumia juhudi nyingi kupata anwani ya nyumbani ya Chris Maganga. Lakini, mtu huyo aliishi Mwanza muda mwingi.
Hakuwa na chaguo ila kuchukua ndege ya mapema kuelekea huko.
Baada ya kufika kwenye jumba lake, mlinzi alifungua mlango na kuuliza, “Shida?”
Lisa akajitambulisha moja kwa
moja.“Tafadhali mwambie Bw. Maganga
kwamba mimi ni binti ya rafiki yake wa zamani, Sheryl Masawe.”
Mlinzi alimpandisha juu na chini kwa
mashaka kabla ya kupiga simu.
Alipopata jibu, mlinzi huyo alimkaribisha
Lisa ndani kwa upole, “Bw. Maganga anakungoja ndani.” Akaingia mara moja.
Alitarajia kuona kuwa Chris Maganga angekuwa mzee katika miaka yake ya mapema ya 70, kwa hivyo alishangaa kumwona mwanamume wa makamo
ameketi kwenye kochi. Mtu huyu
alionekana mdogo kuliko miaka 40.
Ingawa kulikuwa na mikunjo kwenye
pembe za macho yake, alionekana kuwa bado kijana kabisa. Lazima alikuwa mzuri sana alipokuwa mdogo.
“Wewe ni… Mjomba Chris?” Lisa aliuliza kwa wasiwasi.
Alama ya mshangao ilimtoka Maganga machoni mwake alipokuwa
akimchunguza binti huyo. “Miaka 20
imepita kwa kufumba na kufumbua.
Mtoto mdogo wa kike kutoka wakati huo
umekua sana. Unafanana na mama yako kweli.”
Lisa alikuwa na hamu ya kutaka kujua.
"Nilisikia mama yangu aliokoa maisha yako hapo awali, kivipi?"
"Hiyo ni sawa. Usidanganywe na unachokiona sasa. Wakati fulani
nilikuwa kijana mdogo mwenye madeni makubwa. Kwa bahati nzuri, nilikutana na mama yako, akaniajiri na kuanza kumfanyia kazi. Ndivyo nilivyofika hapa
nilipo leo.” Chris Maganga aliachia tabasamu hafifu huku akikumbuka yaliyopita.
Lisa alipepesa macho taratibu. Machale yake yalimwambia kwamba huenda mwanamume huyo aliwahi kupendezwa na mama yake kimapenzi kwa namna alivyoongea kwa hisia kila alipomtaja mama yake.
"Kwa bahati mbaya ... alikufa angali bado mwanamke mdogo sana,"
Maganga alisema kwa majuto. “Ndiyo.
Sielewi kwanini mama yako aliamua
ghafla kuelekea Kigoma. Wengine walisema ni bahati mbaya lakini
sikuweza kamwe kuondoa hisia
kwamba kuna mtu alikuwa nyuma ya hili. Asingesombwa na kimbunga kama si kwa hili…” Huzuni ilikuwa imeandikwa usoni mwa Chris.
Lisa aliona habari hiyo kuwa ngumu kumeza. "Unamaanisha kuwa mama yangu aliuawa?"
"Ndio, babu na bibi yako hawakujua
lakini nilikuwa nikimfanyia kazi wakati huo." Maganga alifumba macho ghafla.
“Nilichunguza baadaye. Mtu
aliyesababisha kifo chake anaweza
kuwa yuko Nairobi.” Chris alisema na kunyanyuka mara moja kuelekea
chumbani. Lisa alitikisa kichwa kwa unyonge.
"Hizi ndizo hati ambazo babu yako
alinikabidhi ili nizihifadhi." Chris
alishusha pumzi huku akimkabidhi
Lisa faili alilorejea nalo kutoka
chumbani. “Kwa bahati nzuri, babu yako
alikuwa na mpango mbadala dhidi ya
Jones ingawa nina uhakika hakutaka
siku hii itokee. Lakini Jones hakuwa na uhusiano wowote na mafanikio ya Mawenzi Investiments leo. Alitengewa asilimia 30 tu ya hisa kwa sababu ya kukulea, na bado hajashukuru.”
'Hiyo ni sawa. Kama wasingenifukuza mimi, angeweza kupata hisa zote baada ya Bibi kufa, lakini hakutaka kusubiri. Badala yake alimuua bila huruma.” Alizungusha vidole vyake kwenye faili. "Kwa hati hizi, anaweza
kusahau kuhusu kuwa mwenyekiti wa Mawenzi Investiments mwezi ujao."
"Usijali, nitakusaidia kupata nafasi hiyo." Chris akatabasamu.
“Asante Mjomba Chris.” Lisa alihisi kuguswa. “Umekuwa ukifanya kazi kwa ajili ya mama yangu kwa muda mrefu.
Ulishawahi kumuona baba yangu?"
Aliuliza kwa kusitasita.
Uso wa Maganga ulianguka kabla ya
kujibu baada ya muda mrefu, “Nimewahi. Lakini usifadhaike sana.
Hajui uwepo wako."
Ghafla, Lisa alihisi faraja. “Sawa. Ili
mradi tu nimefahamu ukweli kuhusu wazazi wangu.”
“Kwa kweli mchango wake ndiyo uliofanya Mawenzi Investiments kufanikiwa leo. Lakini ... tayari ana familia." Chris alimtazama kwa huzuni.
Lisa alielewa. "Nilitarajia tu. Miaka 20 ni mingi sana. Hakuna mtu ambaye
angengojea milele."
Chris akamuonya. "Kuwa makini na Jones, amekuwa akijaribu kupata upendeleo kwa wanahisa na
wafanyikazi wa ngazi za juu wa kampuni. Lazima uchukue hatua kwa tahadhari."
"Ndio. Hakika nitarudisha kilicho changu.” Lisa alimhakikishia.
Alasiri hiyo, Lisa alikataa mwaliko wa
Maganga wa kukaa muda mrefu na
akapanda ndege ya kurudi Dar.
Aliwasha simu yake baada ya kushuka
kwenye ndege lakini bado hakukuwa na
habari yoyote kutoka kwa Alvin. Hisia ya uchungu ilionekana moyoni mwake.
Alijiuliza nini kilikuwa kimeharibika tena
kati yao.
Baada ya kuwaza mara mbili, aliamua kumtumia ujumbe. [Uko wapi?] Bado
hakusikia majibu kutoka kwake baada ya muda mrefu. Aliamua kuachana na
Alvin na kumtafuta shoga yake Pamela
ili kumpasha habari.
"Hongera, bosi wa baadaye wa
Mawenzi Investiments! Ah, utakuwa na thamani ya mamia ya mabilioni ya
shilingi hivi karibuni. Ninapaswa kukaa karibu nawe na kamwe usinisahau.”
Pamela alicheka vibaya. “Unafikiri Cindy atajisikiaje mara tu atakapojua?”
"Hakuna maana kufikiria juu ya watu wanaoyumbishwa na upepo." Lisa
akatikisa kichwa. “Angekuwa pamoja
nami ningemdhamini hata kwenda
kufanya shooting Afrika Kusini au Ulaya.”
"Lakini nilisikia kwamba ... amepata
bwana tajiri," Pamela alinong'ona, "mtu mashuhuri huko Nairobi. Umaarufu wake umekuwa ukiongezeka hivi karibuni."
Wakati huo huo, Sam alimtumia Lisa ujumbe kwenye WhatsApp. [Lisa, umepata chakula cha jioni? Kama bado
unaweza kuja Millionaires' Pub kwa muziki? Alvin yuko hapa pia. Unaweza
kuja na rafiki yako.]
Moyo wa Lisa uliruka kwa kumfikiria
Alvin. Alimuonyesha Pamela ujumbe huo. "Vipi, twende?"
“Twende.” Pamela alikonyeza macho.
“Ulikuwa unaniambia tu kwamba Alvin
hajazungumza na wewe kwa siku kadhaa. Nini tatizo?”
Lisa akakunja uso kabla ya kusema
tena kwa kufadhaika, “Lazima kuna
jambo linamsumbua. Alikuwa vizuri tu siku chache zilizopita lakini
sasa…Ananiona kama toy! Hajafika
nyumbani kwa siku chache sasa, sijui….”
"Ah, nasikia harufu ya wivu kutoka
kwako!" Pamela alitania.
“Mimi sina wivu. Sipendi tu anavyonichukulia, yaani anapenda niwe nambembeleza na kumyenyekea kila
dakika.” Lisa alikataa kukubali. “Haya, ni bora kwa kuwa mali zangu zitarudi, hatimaye nitapata uhuru wangu tena.”
Kabla hawajaondoka, Lisa
alimkumbusha kitu Pamela. "Sawa, uliendesha gari kuja hapa lakini nina
uhakika kuwa utakunywa pombe
baadaye huko Club, nakushauri
ungemwambia Patrick akuijie baadaye.”
‘Wazo zuri, ngoja nimpigie simu.”
Pamela aliafiki.
Patrick ambaye ni mpenzi wa Pamela
alipopigiwa simu alijibu kinyonge sana, “bado kuna vimeo vichache ninayohitaji
kuvikamilisha ofisini jioni hii, nitakutumia pesa ya usafiri utachukua taxi.”
Katika dakika chache, Pamela alipokea
shilingi laki mbili kwenye akaunti yake
ya m-pesa. Hakuweza kumlaumu au
kumkasirikia tena mpenzi wake, kwani
alionyesha kumjali hata hivyo.
Sura ya 104
Millionaires' Pub ni Club ya starehe
iliyopo Masaki ambayo hutoa huduma
kwa matajiri wenye hadhi ya umilionea pekee. Huwezi kuingia kama humo
kama weye ni hohehahe ama hadhi yako ni chini. Si ajabu kukuta bia
ambayo inauzwa elfu na mia tano
mitaani pale ikauzwa elfu hamsini au zaidi. Usishangae kuuziwa sahani ya chipsi kwa elfu hamsini, na vitu kama
hivyo.
Saa mbili usiku, Lisa na Pamela ndo
kwanza walikuwa wanaingia pale
Millionaires' Pub walipoona
mwanamume na mwanamke
wakitembea kuelekea kwao kutoka
upande wa pili. Mwanamke aliyevalia
vizuri alionekana mrembo wa kuvutia
sana. Mwanaume naye alikuwa
ametokelezea kiroho safi. Kwa kweli
walikuwa wamevunja kabati siku hiyo. Papo hapo, Pamela alihisi
kufadhaika kabisa. Mwanamume
aliyekuwa ametoka kumwambia muda si mrefu kwamba alikuwa amebanwa sana na kazi ofisini alikuwa
amesimama mbele yake akiwa na mwanamke mwingine.
Lisa alikunja uso. Alimvuta rafiki yake hadi kwa wawili hao na kusema kwa
tabasamu la kubandika, “Bw. Patrick, ni sadfa iliyoje! Nilidhani ulimwambia
Pamela unafanya kazi za ziada ofisini?
Ulisema ulikuwa na shughuli nyingi na usingeweza kuja kumchukua baadaye, mbona sasa upo hapa tena na mtu
mwingine?" Kauli yake ya moja kwa moja ilimfanya Patrick aone haya.
"Ilibidi nifanye kazi ya ziada lakini Linda
alniipiga simu kusema kuna mtu
alikuwa akimsumbua, kwa hivyo nilifika hapa mara moja kumsaidia."
Linda akaongeza haraka, “Hiyo ni kweli.
Pamela, nina hakika umewahi kusikia
kuhusu Master Cook. Yeye ni mkorofi kama nini."
Pamela alitingisha tu kichwa chake. Lisa alisema, akitabasamu. “We binti, nakuonea wivu sana kwa kuwa na kaka anayekujali. Sio tu kwamba
anahudhuria kila sherehe na wewe
kama mwenza wako wa kiume bali pia
anakimbia haraka mara moja kukuokoa unapokuwa na matatizo. Lakini huenda
usiweze kupata mchumba ikiwa utaendelea na tabia hii. Wanaume
wengine wanaweza wakafikri kuwa nyinyi wawili ni wapenzi.”
Bila kutarajia, sura iliyochanganyikiwa ilitanda kwenye uso wa Linda. “Lisa, unajaribu kusema nini? Kwa nini
huamini kwamba sisi hatuna uhusiano mbaya? Umefikiria jinsi maneno yako
yanavyoweza kumuathiri Pamela?"
Patrick pia alikunja uso baada ya
maneno hayo ya Lisa. Linda akageuka
kumtazama kwa hatia. “Patrick,
samahani. Unapaswa kwenda kwa
Pamela. Nitatoka mahali hapo haraka nikihisi hatari yoyote.”
Kwa hasira, Patrick akamtupia jicho
Lisa. "Bi Jones, kama kuna mambo
ambayo huelewi, nakushauri usiwe unachonga mdomo wako."
Lisa akafuatia na kusema. "Nilikuwa tu nampa ushauri wa kirafiki ..."
“Tunajua tunachofanya bila kuhitaji ushauri wako,” alikatishwa kwa maneno yaliyonyooka.
“Kweli? Nadhani hujui unachofanya.”
Pamela alihisi hasira ikizidi kumpitia rafiki yake alipotukanwa. "Unakimbia mara moja kila wakati Linda anapokuhitaji. Lakini vipi kuhusu mimi?
Nilienda hospitalini peke yangu
nilipougua na nilichukua teksi
kunipeleka nyumbani baada ya kurudi
kwa safari ya ndege usiku wa manane.
Siku hizi hata hutoki kula chakula
pamoja nami tena…”
“Tafadhali usimsikilize rafiki yako. Moyo
wa Patrick upo kwako tu.” Linda alisema
kwa haraka.
"Funga mdomo wako." Pamela
alimfokea mwanamke huyo, “Kama mnapendana kwanini msiweke wazi tu nikawaachia uhuru wenu?”
“Pamela, sikuwa…” Machozi yalitiririka mashavuni mwa Linda.
Patrick hakuweza kuvumilia zaidi na
mara moja akapiga hatua mbele ya Linda. “Pamela Masanja, una tatizo gani? Linda hajafanya lolote la kukukera. Kwanini ukubali
kushawishiwa kwa urahisi na rafiki yako? Jifunze kufikiri kwa kujitegemea,” alifoka.
"Uko sawa, mimi ni mjinga, na ndiyo sababu nilikukubali." Kisha kusema
hayo, Pamela akamshika Lisa kwa
mkono na kuondoka hadi ghorofa ya pili.
Nyuma yake, Linda alimhimiza
mwanaume huyo. “Patrick, mfuate
haraka ukambembeleze. Amekasirika.”
"Aah! Achana naye bana. Kwa nini
unamjali? Hukusikia alichosema sasa hivi?”
“Nilisikia kila kitu. Lakini….”
"Achana naye..."
Pamela alisikia sauti zao zikitokomea kwa mbali nyuma yake. Machozi ya hasira yalianza kuteremka kwenye mashavu ya Pamela alipokuwa
akipanda ngazi. Kwa bahati nzuri, Lisa alikuwepo kumshikilia.
"Samahani, sikupaswa kusema hivyo."
Lisa alimfariji.
“Siku zote nilitaka kusema hivyo, sema wewe umenisaidia tu." Pamela alifuta machozi kwa nyuma ya mikono yake.
"Uligundua kuwa kuna kitu kibaya
baada ya kuona mwingiliano wao mara
mbili. Lakini mara ambazo nimemwona
Linda akiwa na Patrick zinakaribia
kulingana na zile nilizotoka na Patrick.”
Jambo hilo lilimshtua Lisa. Alikuwa
akisoma nje ya nchi kwa miaka
michache iliyopita, kwa hivyo
hakufahamu sana juu ya maisha ya mapenzi ya rafiki yake. Tabasamu la uchungu lilienea kwenye uso wa Pamela.
“Mara saba kati ya mara kumi tulizotoka na Patrick, alikuwa na Linda, hata
kwenye ukumbi wa sinema. Mara nyingine tatu tulipokaa peke yetu, angeondoka baada ya muda mfupi kwa sababu alipigiwa simu na Linda.”
“Mbona hukuniambia?” Lisa alijisikia vibaya lakini pia alikasirika kwa wakati
mmoja. “Basi, sikupaswa kuwa mpole. Ningewapaka zaidi ya hapo.”
“Sikutaka kukuona wewe na Patrick mkipigana,” Pamela alisema kwa
huzuni, “Ninampenda sana na nilijaribu kwa muda mrefu kumfanya awe pamoja
nami. Pia niliiambia hadi familia yangu
kwamba nitampeleka nyumbani
Krismasi hii. Ndiye mtu ninayetaka kuolewa naye.”
Lisa alisema kwa hasira, “Ikiwa siku
zote anachukua upande wa Linda, inawezekana kwamba mtatalikiana hata mkifunga ndoa.” Hii ilimshangaza
Pamela. Alionekana kuchanganyikiwa kabla ya kutikisa kichwa polepole.
“Usifikirie sana kwa sasa. Zimisha hisia zako na pombe. Nitakupeleka nyumbani baadaye.” Lisa alimshika mikono na wakatembea kuelekea ukumbi binafsi
aliokodisha Sam kwa ajili ya ‘bata’ hilo usiku ule.
Mlango ulisukumwa na mbele yao
wakaonekana watu kumi au
zaidi waliokuwa wameketi ndani ya ukumbi huo wa kupendeza. Kati ya
umati mkubwa, alimjua tu Sam
Harrison, Clark Zongo, na mtu aliyeketi
kwenye kona ya mbali… Alvi Kimaro.
Kiyoyozi kilikuwa kimewashwa. Alvin
alikuwa amevaa shati jeupe na
ameshika glasi ya mvinyo katika mkono
wake wa kushoto. Ilikuwa ngumu
kutomtambua mtu huyo aliyeonekana
kama mfalme miongoni mwao.
Pia alikuwa katikati ya tahadhari, alikuwa makini zaidi hata katika chumba kilichojaa watu. Hata hivyo, Alvin
hakumtazama Lisa tangu alipotokea. Macho yake hayakutilia maanani kabisa
ujio wake. Jambo hili lilimtia aibu Lisa. Ghafla, alijutia uamuzi wake wa kwenda pale.
"Halo, warembo Lisa na Pamela!" Sam
aliwasalimia kwa shauku. "Nendeni mkakae na Alvin." Baada ya kusitasita
kidogo, alimnong’oneza Lisa sikioni, “Alvin hayupo hapa kimawazo. Nenda ukaongee naye.”
Lisa pia aliingiwa na kiburi, kwanini yeye awe wa kwanza kumfuata
Alvin? Kwa kweli alishindwa kutembea
kumfuata wakati Alvin alikuwa akijifanya
hamjui kabisa. Kwa hivyo, Lisa alibaki
kama kaota mizizi kwenye miguu.
Kwa bahati mbaya au nzuri, Clark
Zongo alimpa ishara na kusema, “Lisa, njoo uketi hapa.”
Watu wengi walimgeukia waliposikia
hivyo. Pamoja na hayo, bado Alvin
alikuwa busy tu akiongea na mtu aliyekaa karibu yake. Uso wake
uligeukia upande mwingine na kumpuuza kabisa Lisa kana kwamba
hakuwa na uhusiano wowote naye. Kwa hasira, Lisa alimkokota Pamela
kuelekea kwa Clark. "Bwana Zongo..."
"Lisa, njoo tafadhari nina deni kwako.
Nimekuwa nikikusudia kukuomba
msamaha siku nyingi lakini sikupata
nafasi ya kuonana na wewe,” Clark
Zongo alisema kwa dhati. "Sikuelewa
mara ya mwisho na karibu nikutupe gerezani. Ingawa ulishinda katika kesi
ya mahakama, angalau nilipata kujua ni nani hasa aliyekuwa akijaribu
kunichezea.”
"Bwana Clark, bila samahani, bila shaka
mahakama iliwawajibisha wale wote
waliohusika kwa kile kilichotokea."
"Sawa, acha yaliyopita yawe yamepita basi." Wawili hao walipeana toast kabla
ya kuanza kujadili mradi wa hoteli ya
Lublin.
Kwa pembeni kabisa, Alvin, ambaye
aliwaona wakipiga soga na kucheka
kwa furaha, alihisi hasira ikipanda ndani yake. Joto la hewa karibu naye
lilionekana kuwa limeshuka sana.
Sura ya 105
Wakili aliyekuwa akizungumza na Alvin
alihisi tofauti ya ghafla katika
mazungumzo ya Alvin na akanyamaza
haraka. Alichukua glasi yake ya mvinyo
na kwenda kujiunga na mchezo wa pool pembeni.
Sam alimfuata Alvin. Aliketi karibu na rafiki yake na kumwambia taratibu.
“Kaka nimeshamkaribisha Lisa hapa
kwa wema. Utaacha lini tabia yako ya kumkaushia?"
“Una uhakika hukumwalika hapa kwa
ajili ya Clark Zongo?” Alvin alidhihaki
kwa kejeli.
“Noo.” Sam hakuwa na uhakika wa
kusema. "Kweli, wewe ndiye ambaye
hukuonyesha kupendezwa alipojitokeza."
Tabasamu la kujilazimisha likaangaza usoni mwa Alvin. "Hah, achana naye.
We endelea na mishe zako tu.”
Wakati huo huo, watu wengine
wachache waliingia ukumbini. Alikuwa ni Stephen Kileo pamoja na dada yake, Janet Kileo wakiwa wameambatana na Lina Jones. Sam alishindwa cha
kusema. Hakuwa amewaalika watu
wale na hakujua walijuaje kwamba
ameandaa ‘bata’ kwa ajili ya marafiki
zake. Ilionekana kama vile alipanga
kualika maadui wakubwa katika chumba
kimoja. Alikuwa na utabiri kwamba kitu
kibaya kingetokea.
Stephen Kileo alikagua chumba kwa
macho makali kabla ya kuelekea kwa
Sam. “Bw. Harrison, nilikuwa tu
nikitembea na marafiki zangu kwenye
ukumbi mwingine. Master Cook
akaniambia kwamba wewe pia uko
hapa, kwa hiyo nilikuja kukusalimu. Na huyu… lazima awe wakili anayeheshimika, Bw. Kimaro. Nimesikia mengi juu yako na nimefurahi hatimaye kukuona ana kwa ana.”
Alvin hakutetereka, aliendelea kubaki na sura ya dharau na kutojali usoni mwake.
Lakini, Sam hakuweza kufanya vivyo hivyo. Ilibidi amjali Janet na kaka yake.
Stephen ndiye aliyekuwa kaka mkubwa na mrithi mpya wa biashara za familia ya Kileo, kwa hiyo ilimbidi aonyeshe heshima. Mbali na hilo, familia ya Kileo ilikuwa ikipata nguvu na ushawishi mkubwa wakati huo.
"Hongera, Bw. Kileo, kwa kuchukua biashara ya familia." Sam alimtupia jicho la haraka Lina huku akiweka tabasamu usoni mwake. "Lakini kwa nini uko na mwanamke wa familia ya kutisha ya
Jones? Kwani hakuna samaki tena
baharini mpaka unaamua kwenda kuvua kwenye vidimbwi?"
Stephen alicheka kwa sauti kubwa
kabla ya kumshika Lina karibu na
kumbatio lake na kupiga kelele, “Sikilizeni kila mtu, wacha
nimtambulishe mpenzi wangu, anayejulikana pia kama binti Jones
Masawe—mwenye hisa mkuu wa Mawenzi Investiments.”
Kila mtu aliingia kwenye mjadala mkali. Wote Sam na Alvin walishtushwa na
habari hiyo."Hapana, tangu lini Jones
Masawe akawa mwenye hisa mkuu wa
Mawenzi Investiments?"
“Unadiriki kutudanganya?” Alvin aliuliza.
“Stephen, tuachane nayo,” Lina alisema kwa haya.
“Kwanini? Sio uongo kusema wewe
ndiye mwanamke kijana tajiri kwa sasa, kutokana na hadhi yako mpya.” Stephen akambusu Lina shavuni. "Hata sijui
niliwezaje kupata hazina kubwa kama wewe!"
"Acha bwana." Lina alishusha macho
yake chini huku akionekana kuwa na aibu.
Janet alimtupia jicho Lisa aliyekuwa
kando kabla ya kusema kwa sauti, “Ndugu yangu hapa hapakufai. Ukijilinganisha na wengine wewe humu una nini? Humu tunaingia watoto wa matajiri tu kama vile warithi wa Mawenzi Investiments, pesa ni za kusaini tu muda wowote. Na wewe mpaka usubiri kuajiriwa au kupewa vijihela na bwana wako utaweza wapi mambo haya?”
Chumba kikawa na fujo. "Wow, kwa hiyo Lina ndiye atakuwa mrithi wa Mawenzi siku zijazo?"
"Halo, Bi Jones, nilikuwa na mpango wa kukutana na watendaji wa Mawenzi Investiments hapo awali. Tunaweza kupata nafasi ya kuonana na kuongea jambo?” Jamaa mmoja akaona fursa papo hapo.
Lina aligeuza uso wake wenye tabasamu na kusema. “Bila shaka.
Msipojali, nyote mnakaribishwa
kujumuika nasi katika ukumbi niliokodi upande wa pili.”
“Twendeni.” Stephen alisema kwa
bashasha. “Sam Harrison, mnakaribishwa pia.”
Baada ya dakika chache, ni Lisa, Pamela, Alvin, Clark, na Sam pekee
ndio walioachwa kwenye ukumbi wa faragha uliokuwa umechangamka sana
hapo awali.
“Nakufahamu wewe Stephen Kileo.
Unafanya hivi kwa malengo yako, siyo bure, sawa?” Sam alimuuliza Stephen
kwa sauti ya chini kabla hajaondoka.
"Nadhani unanijua vizuri. Watu wenye fedha hufuata pesa zilipo." Stephen
alimjibu kwa kejeli. "Labda hivi karibuni pia mtalazimika kuniabudu kama kijana
tajiri zaidi Masaki nzima, tehtehteheee…”
"Utakuwa unaota kama bado unafikiria
kupata mafanikio kwa njia za kijima
kama hizo." Sam alimnyooshea kidole
Lina na kucheka kwa kejeli. “Mwanamke
gani huyu unayejivunia? Alikuwa
mchumba wa mtu mwingine mwezi
uliopita tu, leo unatutambia kwa
mbwembwe utadhani umepata bikira?"
Hasira kali ilujaza uso wa Lina ndani ya sekunde chache. “Sam, chunga kauli
zako. La sivyo, mara baba yangu atakapokuwa mwenyekiti wa Mawenzi
mwezi ujao, ninaweza kuiangusha familia ya Harrison mapema kabisa.”
Lisa aliyekuwa akisikiliza pembeni alicheka kejeli. “Usijiaibishe sana.
Itakuwa aibu kubwa kama hilo halitatokea.”
"Hiyo ni sawa." Pamela alicheka kwa furaha. "Familia ya Jones ina sifa
mbaya. Ni bora kutolichafua jina zuri la Mawenzi Investiments pia.”
"Nimekubali," Sam aliingia pia, akicheka.
"Chekeni mnavyotaka, ongeeni yote
mnayotaka, ila nitawaona nyote
mkifyata mikia yenu baada ya mwezi
mmoja tu." Kwa uso ulionyooka, Lina
alimshika Stephen kwa kifundo cha
mkono na kuondoka kwenye ukumbi ule
wa matajiri.
Janet aliyeachwa nyuma, alijisogeza
karibu na Alvin huku akitabasamu kwa
upole. "Bwana Kimaro, kwanini usiende na sisi? nina machache ya kukuambia.”
Alvin alimtazama tu kwa kejeli. Janet
hakujali kuonekana mtovu wa akili.
Tangu alipomwona Alvin kwa mara ya
kwanza kule kwenye mgahawa wa Grapefruit, kwa kweli alivutiwa naye
sana. Hakuwahi kumwona mwanaume mwingine wa kifahari zaidi yake.
Pamoja na uzuri wake, Janet aliona
Alvin haendani naye kwa hadhi ya utajiri
wa familia yake. Hata hivyo, baada ya
kujua kwamba alikuwa wakili bora zaidi
wa kimataifa, alifikiri kwamba
wangeweza kulingana kikamilifu.
"Bwana Kimaro, labda hujui mengi
kuhusu familia ya Kileo.” Janet
aliendelea kujinadi huku akitabasamu.
"Familia ya Kileo ina utajiri wa zaidi ya
shilingi bilioni 50 za mali na kwa sasa
tunawekeza katika biashara ya mavazi, usafiri, fedha, teknolojia na sekta
nyinginezo. Hivi karibuni, tutashirikiana na Mawenzi Investiments, ambayo ni mojawapo ya makampuni 100
yaliyofanikiwa zaidi Tanzania. Siku
zijazo kwa kweli naamini tutazipita
familia zote tajiri hapa jijini.”
"Pfft." Kicheko kilimponyoka Sam
mdomoni bila kupenda. Alitamani sana
kumfokea yule binti asiye na haya
ambaye alikuwa akijitongozesha kwa
mtu tajiri zaidi kuliko familia yake.
Uso wa Alvin ulimsisimka huku
akitamani sana kumsukuma yule binti.
Harufu kali ya pombe iliyokuwa ikimtoka
mdomoni ilikuwa inashambulia pua
zake. Hata hivyo, baada ya kumwona
Lisa akiwatazama pembeni, aliizuia ile
jazba yake na kuibana midomo yake
kimya kimya.
Akifikiri alikuwa amepata nafasi, Janet
kwa ujasiri alilaza kichwa chake kwenye
bega la Alvin na kumwambia kwa
mahaba. "Ikiwa uko tayari kuwa mtu
wangu, utakuwa na pesa nyingi kuliko utakayopata maisha yako yote kwa
kufanya kazi kama wakili."
Macho ya Alvin yaliganda. Janet akajua hiyo ilikuwa ni ishara ya kueleweka, akazidi kumnong'oneza sikioni, "Lisa hakufai, yeye sio maskini tu bali pia mjinga. Mimi ni bora kuliko yeye.”
Mkono wake ukasogea taratibu kwenye kifua cha Alvin. Lisa hakuweza
kutazama tena kwani hisia kali za hasira
zilimpanda. Alichukua glasi ya mvinyo na kumkimbilia Janet kabla ya kumtupia usoni. Vipande kadhaa vya barafu hata vilitua kwenye kichwa chake.
"Ah, Lisa Jones! Umerukwa na akili!”
Janet alipiga kelele kwa hasira na akasimama kwa nguvu. Mara moja
akatoa leso ili kujifuta uso na mwili wake.
“Nadhani wewe ndiye uliyerukwa na akili. Ni dhahiri kwamba uko kwenye
joto, kwa hivyo ninakusaidia
kukupunguzia joto." Lisa akakaa
mapajani mwa Alvin kabla ya kusema kwa ujeuri, “Ninakuonya kuwa kaa naye
mbali, huyu ni mtu wangu. Nitakukata mkono ikiwa nitakuona ukimgusa tena.”
“Mtu wako?” Janet alicheka kana kwamba ameambiwa utani. “Ulikuwa
umekaa mbali naye sana hapo awali, una uhakika kuhusu hili? Mapenzi ya upande mmoja huishia katika fedheha wakati mwingi.”
Lisa alikosa kujiamini kwa sababu muda
wote Alvin alikuwa kimya. Hata hivyo, kejeli za Janet zilimfanya asiwe na chaguo zaidi ya kumlinda mtu wake.
Wakati huohuo, sauti kali ya Alvin
ilisikika nyuma yake. “Hebu tokeni nje.”
Sura ya 106 Rangi zote zilitoka kwenye uso wa Lisa
ndani ya sekunde chache, akidhani
kwamba kauli hiyo ilimlenga yeye pia.
“Ninamaanisha wewe.” Alvin aliinuka
taratibu, akaupanua mguu wake mrefu
na kumpiga teke Janeth kwenye kochi. Kila mtu alishtuka. Binti huyo alipiga
kelele, "Alvin Kimaro, unafikiri wewe ni nani?! Unathubutuje kunipiga teke!
Sitakucha kwa hili.”
“Oh, kweli? Ngoja nione basi.” Akiwa na sura ya kuchukizwa usoni mwake, alinyakua kitambaa kutoka mezani na
kujifuta bega kwa uangalifu ambapo
Janeth alikuwa ameegemeza kichwa
chake muda mfupi kabla.
Hasira ndani ya moyo wa Lisa ilitoweka
ghafla baada ya kuona vile. Angalau
Alvin alifanya jambo sahihi. Vinginevyo, angeweza tu kumchukia milele.
“Alvin, utajuta kwa hili. Ngoja uone. Siku
moja, utakuja kuniomba mwenyewe
nilale na wewe.” Janet aliuma meno na kuondoka baada ya kudhalilishwa.
Sam alimkaripia yule binti, “pumbavu!
Unadhani unastahili kulala na Alvin
wewe? Takataka! Rundo la kinyesi wewe!”
Pamela na Clark walishindwa kuzuia
vicheko vyao. Lisa na Alvin pekee ndio walibaki na nyuso zilizonyooka.
“Una hata jeuri ya kusema hivyo?
Tazama umati mchafu ulioalika leo.”
Alvin alimshushua rafikiye Sam kwa tabasamu la kejeli.
Sura ya aibu iliufunika uso wa Sam.
"Sijawaalika mimi wehu hawa
wamevamia tu. Bora wameenda, njooni tunywe na tuendelee na furaha. Ni wale
wa kweli tu ndio waliobaki humu.”
Aliongoza na kuchagua wimbo. Pamela alimfuata pia na kuchangua nyimbo
kadhaa na kuziweka kwenye playlist.
Ukumbi mkubwa ukawa mtupu ghafla.
Kwa bahati mbaya, Lisa alikuwa
ameketi kati ya Alvin na Clark. Uso
wake ulitiririka kwa aibu. Kweli, alikuwa
amedai hadharani tena kwa kiburi
kwamba Alvin alikuwa mtu wake muda si mrefu. Oh hapana…
iliyokuwa karibu naye huku akimtaka
Lisa asogee. Hakuwa na la kufanya
zaidi ya kujisogeza karibu zaidi na Alvin hata wakagusana kabisa.
Akamkumbatia mkono mmoja na kumshika kidevu kwa mwingine.
"Ulitangaza mapema kwamba mimi ni mtu wako?" Alisema, akiinua macho
yake kumtazama.
Lisa alihisi mashavu yake yakiwaka
moto. Alipotazama moja kwa moja ndani ya kina cha macho yake yenye
giza, hakuweza kujua ni nini kilikuwa akilini mwa Alvin, lakini alimtazama na kusema, “Hiyo ni kweli, wewe ni mtu wangu. Nirekebishe wakati wowote
ikiwa unaona kuwa hii si sawa. Naahidi
sitakusumbua tena.” Hisia ngumu
ikaangaza machoni pake. Hakujua
kama ahisi hasira au furaha.
Alvin alionyesha kuguswa na kufurahi
ghafla. “Sawa, nimefurahi bado
unakumbuka msimamo wako. Lakini
"Sogea karibu." Alvin akapapasa nafasi
kwa nini huwa unasahau niliyosema?
Kwanini unafurahia kuzungumza na wanaume wengine?"
Lisa alishtuka, akakumbuka alikuwa anazungumza tu na Clark mara baada ya kuingia ukumbini mle. “Clark alikuwa akinishukuru mara baada ya kuniona.
Nilitaka kuja kuketi karibu nawe lakini
wewe… Kwanza hujafika nyumbani kwa
siku chache zilizopita na bado uliendelea kunipuuza hata uliponiona nikiingia. Ulijifanya hunijui kabisa.” Sauti yake ilishuka kuelekea mwisho.
Ilionekana kuwa alikuwa na aibu na alihisi kama alikuwa amekosewa.
“Una jeuri ya kusema hivyo? Nachukia
sana wanawake wanaponidanganya,”
Alvin alisema huku akikoroma. “ Mimi
simaanishi Clark Zongo. Nilikuambia
usikae karibu na Kelvin lakini
hukunisikiliza. Unafikiri ninaweza
kukuvumilia na kukusamehe kila mara?”
Hatimaye ikawa wazi kwake.
"Unamaanisha tukio la hospitali siku
chache zilizopita, ulijuaje?" Aliendelea kuwa na uso ulionyooka ingawa macho
yake yalionyesha wazi kutofurahishwa.
"Nilikuwa Mbezi Beach wakati huo
nilipokea simu kuhusu Aunty Manka. kelvin alikuwepo kwa bahati kwenye
saiti kuangalia maendeleo ya kazi.
Alinisikia kwenye simu na kuniambia
kuwa anamfahamu mtu kutoka
hospitalini hivyo alitaka kunisaidia ndo
nikaongozana naye. Ni hayo
tu,”Lisa alieleza.
Alvin hakujisikia faraja aliposikia hivyo
lakini alikata tamaa zaidi. “Hukuja
kwangu mara moja ulipohitaji msaada.
Badala yake, ulimgeukia mtu ambaye
anavutiwa nawe. Lisa Jones, mimi ni nani kwako na Kelvin ni nani kwako?"
“Hapana, nilizungumza na Kelvin na anaelewa pia—”
“Usithubutu kuniambia kwamba
anakuona tu kuwa rafiki sasa hivi.”
Alitabasamu kwa kejeli. "Kwa hivyo
utakuwa sawa na mimi kuwa na urafiki na wanawake ambao walijaribu
kunishawishi hapo awali?"
Hilo lilimshangaza. Baada ya kujiweka
katika viatu vyake, hatimaye aligundua kosa alilofanya.
"Samahani." Muda mrefu baadaye, aliinamisha kichwa chake. “Nitakupigia simu mara moja nikihitaji usaidizi siku nyingine na sitakubali msaada kutoka
kwake tena. Hakika nakujali wewe tu.”
Alvin akamuachia na kuwasha sigara.
Alipovuta pumzi na kuzitoa, moshi ukafuka kimya kimya.
Kwa bahati mbaya, aligundua wimbo wa mapenzi ambao Pamela alikuwa
ameweka ulikuwa ukiisha. Wazo
likamjia akilini. Alikimbilia kwenye
mashine ya kucheza muziki na kuuweka
wimbo huo kwenye playlist. Baada ya
dakika chache, wimbo wa mapenzi
uliokuwa ukitamba ulijaza chumba. Kila
mtu alijua ni wimbo gani huu na mara
akageuka na kumtazama Lisa kwa
mshangao. Mashavu yake yalimtoka kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kujaribu kitu kama hiki hadharani. Hata hivyo, alipoona mwonekano mzuri wa Alvin, alivuta pumzi ndefu kabla ya kuogea hadharani kwa aibu. "Ningependa nitoe dedication ya wimbo 'Tupendane' kutoka kwa Wananjenje, kwa mtu ninayempenda."
Alimtazama Alvin haraka baada ya kusema hivyo. Alvin aliinua macho yake
kumtazama. Mwangaza mkali
ulioning'inia kutoka kwenye dari
ulimwangazia usoni mwake. Aliona mashavu hayo mekundu na macho yaliyokuwa yakimeta kama nyota
zinazometa angani usiku. Alihisi kuna
kitu kilikuwa kinaonekana moyoni
mwake. Sam alipiga mluzi na kuanza kupiga
makofi. “Oh, jamani Lisa! Alvin, umesikia hivyo? Anakiri kukupenda.”
Alvin aligeuza uso wake bila kutoa
maoni. Alisimama na kumtazama moja kwa moja Lisa.
Lisa alinyanyua kipaza sauti na kukisogeza kwenye midomo yake
taratibu.
"Mpenzi wangu, ninaombaa…nikueleze pendo, langu lililo moyoni, moyoni mwanguuu…,
"Mpenzi wangu, Mwenyezi Mungu, muumba ardhi na mbingu, ndiye shahidi wa pendo, mhh…moyoni mwanguuu…
"Mapenzi niiii…kuvumilianaaa…Nami mpenzi, nimekuvumiliaaaa…,
"Mapenzi niii ...Kuaminianaaa….Nami mpenzi nimekuaminiiii…."
Hakuwa amemsikia akiimba hapo awali.
Sauti yake tamu na nyororo ilituliza
moyo wake na kutoa burudani masikioni
mwake. Kusikiliza muziki haikuwa tabia
ya Alvin, sembuse muziki wa kiutu
uzima kama huu, lakini, alihisi wimbo
huo kuwa mzuri sana wakati huo.
Nyimbo iliisha. Ilikuwa huzuni sana
kwamba iliisha haraka. Watu wote
walianza kupiga makofi. Wote wawili
Sam na Pamela walianza kupiga kelele.
" Busu, busu, busu ..."
Akiwa na aibui, Lisa alimkodolea macho
rafiki yake wa karibu akitamani kwenda kujiunga naye.
"Njoo hapa." Alvin akampungia mkono.
Lisa alitembea kuelekea kwake kwa
aibu. Alvin alimweka kwenye mapaja yake, akamshika uso wake mdogo, na
kufunga midomo yake kwa midomo yake.
Lisa, akiwa na aibu kufanya hivyo
hadharani, alitamani apotee hewani
papo hapo. Hata hivyo, alipofikiri
kwamba hakuwa na hasira naye tena, alimbusu kwa upendo.
Bila kutarajia, Alvin alipoteza fahamu
zake kabisa katika busu hilo. Moyowake
uliachilia kabisa chuki za mvutano wote
uliokuwa ukijengeka ndani yake katika
siku chache zilizopita. Hata hivyo, wengine bado walikuwa wakiwatazama.
Lisa alijisikia kulia kwa aibu. Haraka
alitazama huku na huko baada ya busu kuisha, akagundua kwamba wengine
tayari walikuwa wameenda upande mmoja kucheza pool.
Sam alicheka na kumwambia. “Njoo ujiunge nasi kwa kuwa umemaliza kumbusu. Tayari tumemaliza mechi chache tangu wakati huo.” Alihisi
mashavu yake yakimtoka kwa mara nyingine.
“Hapana,” Alvin alijibu kwa uvivu na kuuzika uso wake kwenye nywele zake ndefu. “Tunaelekea nyumbani.”
"Bado." Lisa alimzuia. "Pamela amekuwa akinywa pombe. Nahitaji kumsindikiza kwenda nyumbani.”
"Atachukua teksi."
Lisa alisita kwa muda mfupi kabla ya kukataa. "Hapana, aligombana na mpenzi wake na niliahidi kumrudisha nyumbani. Siwezi kumpuuza kwa
sababu nimekuona wewe.”
Sura ya kukasirika ikaangaza tena usoni
mwake. "Unamaanisha nini, mimi si muhimu kuliko rafiki yako?”
"Bila shaka wewe ni muhimu sana, lakini marafiki ni muhimu pia." Lisa
aliweka wazo hilo moyoni na kujibu kwa sauti ya kupendeza, “Hey, acha kuwa
na haraka kupita kiasi. Hatujawahi
kutoka na kufurahi kama hivi, kaa
kwanza. Kuna mengi zaidi nataka kukuambia.”
Alvin alilegea na kukaa. Bila kujizuia, Lisa alimweleza yote aliyoyasikia kutoka
kwa Aunty Manka katika siku chache zilizopita.
Alvin alitabasamu kwa furaha huku
akielewa picha kubwa sasa.
"Inaonekana kujeruhiwa kwangu
kwenye saiti ya ujenzi mara ya mwisho
haikuwa ajali pia lakini mpango kutoka
kwa familia ya Jones. Kweli, vizuri, wanathubutuje kunidanganya?"
Mtu wa mwisho aliyemsababishia
madhara hakuwa tena katika ulimwengu
huu. Wawili hao, baba na binti Jones
walikuwa na hamu ya kuishia gerezani. Alvin akatoa simu yake kuitafuta namba ya Hans.
"Unafanya nini?" Lisa aliuliza.
"Nataka kumwambia Hans aandae hati ya mashtaka kwa ajili ya bwana na bibi
Jones, nawashtaki kwa mauaji." Kiburi kilionekana katika sauti yake.
“Usifanye kwa kukurupuka. Familia ya Jones Masawe imeanza kupata
ushawishi mkubwa kwa sasa na huwezi kumudu kuwashtaki, wanaweza
wakakusumbua sana. Mbali na hilo, wanapanga kuunganisha nguvu na familia ya Kileo kupitia ndoa. Wataipiku hata familia yenye nguvu zaidi hapa
Masaki kwa sasa, familia ya Harrison.”
Alvin akanyamaza. Eti hawezi kumudu
kuwashtaki? Alvin alihisi kucheka.
"Usijali,
Lisa alimfariji
kwa dhati. “Ninapanga kujiunga na
Mawenzi Investiments kupigania nafasi
ya Mwenyekiti wa bodi iliyo wazi.
nitalipiza kisasi."
Nitahakikisha kwamba familia ya Jones
inaangamizwa mwishowe na mimi
binafsi nimtupe gerezani muuaji wa bibi yangu.”
Alvin alimwangalia Lisa na
kumlinganisha na uzito wa maneno aliyotamka. Hakuweza kujua kama Lisa
aliongea kwa dhati ama kwa kujiridhisha tu. Hakuongea lolote bali uso wake
haukuonyesha imani kwa maneno ya Lisa.
Lisa alikohoa kidogo na kuendelea.
"Niamini kwamba nina ushahidi wa 100%. Mawenzi Investiments
ilianzishwa na mama yangu na lazima
niirudishe. Hilo likitokea… ninaweza
kukusaidia kifedha pia ikiwa unataka
kustaafu kutoka kwenye kazi ya uanasheria.”
“Umh, sawa. Nitasubiri siku hiyo.”
Tabasamu la fumbo lilimwangazia usoni mwake.
Hakika, ikiwa ndivyo alitaka, basi Alvin
asingeingilia kati. Hakuweza kusubiri
kuona ni kiasi gani alikuwa amekomaa
katika miezi michache iliyopita. Baada ya yote, ilibidi akabiliane na familia yake
siku moja kwa kuwa walikuwa wamefunga ndoa.
Lisa na Alvin walibarizi pamoja hadi saa tano usiku. Pamela hakuweza kuacha
kuangalia simu yake kila baada ya dakika tano. Alikata tamaa kabisa
kwamba Patrick alikuwa hajampigia simu tangu wakati huo. Alikunywa
pombe nyingi zaidi kuliko kawaida kwa
sababu ya hali yake mbaya kimawazo.
Lisa hakunywa sana pia kutokana na kelele za kina Lina waliovamia ghafla.
Alvin akawapa lifti ya kwenda nyumbani
wale wanawake wawili. Wakiwa njiani,
Pamela ghafla alilia kwa sauti kubwa na
kuanza kupiga kelele kuhusu mpenzi
wake mchafu. Lisa aliingilia kati
kumfariji.
Alvin alikuwa akipata maumivu ya
kichwa kutokana na kelele za hao
wanawake. Kwa hiyo, alikanyaga
mwendo na kuongeza kasi ili
kuharakisha safari ya kuelekea nyumbani kwa Pamela.
"Asante, ah, asante, mjomba." Pamela alifungua mlango na akatoka nje ya gari
kwa uangalifu na miguu yake iliyokuwa imelegea kama mlenda. Hakusahau
kumsujudia mwanaume huyo.
"Tafadhali mtunze vizuri mpenzi wangu
Lisa kila siku, usiwe kama huyu mbwa wa kiume Patrick..."
Sura ya 107
Wakati huo, Lisa alishtuka sana hadi
akakosa hata amani. Haraka akasema, “Hiyo ni… Unaweza hata kutembea
kweli? nitakupandisha juu.”
“Hapana, mimi si mlevi. Sitawahi
kulewa.” Pamela alipunga mkono bila
utulivu na kujikongoja hadi jirani.
“Mjomba?” Pamela alizidi kumuita Alvin, ambaye aliinua tu macho yake kwa kushangaa.
Lisa alimwambia kumtoa shaka, "ni kwa
sababu unafanana kidogo na mjomba wake, kwa hivyo anakuita 'Mjomba'
kujifariji."
“Mwambie asiniite hivyo. Sina uhusiano naye.” Alvin akawasha gari, na Lisa akapumua. Kwa bahati nzuri, hakushuku chochote. Pamela alikuwa
kimwita Alvin mjomba kwa maana ya mjomba wa Ethan.
Wakati wa kurudi nyumbani, pombe na usingizi vilimkamata Lisa kwa pamoja.
Akalala kama pono. Baada ya muda
usiojulikana, alihisi kuna mtu akimbeba kwa upole. Alifumbua macho kwa
kuduwaa na kuona wazi uso mzuri.
Akifikiri alikuwa anaota, aliinua midomo
yake minono na kuizungusha mikono
yake shingoni.
“Alvilisa, usikasirike, sawa?
Nimekukumbuka sana siku hizi chache.
Nimechoka. Mambo mengi yametokea
hivi karibuni na ninataka mtu wa
kuzungumza naye. Nina wewe tu sasa.
Utakuwa karibu nami kila wakati, sawa?"
Kisha, alilia ghafla huku akimkumbatia.
Machozi yake yalishuka shavuni mwake na kutiririka shingoni mwake. Alvin
alipigwa na butwaa. Pengine alichanganyikiwa baada ya kuzinduka na kudhani bado hajarudi. Moyo wake ulijawa na dalili za maumivu. Lazima
siku hizo chache alikuwa na msongo wa mawazo sana. Baada ya yote, bado
alikuwa mwanamke. Mambo mengi
sana yalimtokea lakini hakuwa karibu
naye. "Ndio, nitakaa karibu nawe kila wakati," alinong'ona sikioni mwake.
Sauti ya upole ya Alvin ilimtuliza taratibu
Lisa. Alifumba macho na kulala begani mwake. Alvin alimbeba juu juu na kumuweka kitandani taratibu. Kuangalia
mashavu yake laini, akahema. Alikuwa
amechoka kabisa wakati huo. Siku
chache alizokuwa hayupo hakulala
hata kidogo.
Wakati anakaribia kwenda kuoga, kuna
mtu aligonga mlango polepole nje.
Alifungua mlango na kumuona Hans akiwa amesimama nje, akamwambia kwa sauti ya chini, "Kuna kitu kimetokea."
Alvin alitoka nje ya mlango, na Hans akamkabidhi picha ya mtu fulani.
"Nilipata habari kwamba Zigi Kabwe amefika Dar es Salaam kukutafuta.
Naamini yuko hapa kulipiza kisasi cha dada yake tena.”
"Alijuaje kuwa niko Dar?" Mwanga wa tahadhari ulimulika machoni mwa Alvin.
"Ulikuja Dar na kushughulikia kesi
kadhaa kubwa, haswa kesi ya Kibo
Group ambayo ilivuma sana. Ingawa
nimejaribu kuficha sana jina lako,8 lakini
mitandao sasa imeenea mno…” Hans
alikunja uso na kutafakari kabla ya
kusema, “Mtu huyu amekuwa
akikusumbua tangu miaka mitano
iliyopita. Kwani huwezi ku…”
“Hakuna haja.” Alvin alikunja uso na kumkatisha.
Hans alikuwa na wasiwasi. "Ninajua
unaweza kufikiria moyoni mwako jinsi
anavykuchukia kwa sababu ya kesi ya
dada yake, lakini yeye ni- ... Yeye ni hatari sana na ameapa kulipiza kisasi
kwa mtu unayempenda. Lisa atakuwa hatarini.”
"Mletee mtu wa kumlinda." Alvin aliamuru.
Siku iliyofuata, Lisa aliamkaalibadilisha nguo zake za kulalia na kushuka chini.
Aliona kwamba kulikuwa na mwanamke
kijana mwenye nywele fupi na umbo
thabiti.
“Habari, Bi Jones. Mimi ni mlinzi wako, Shani. Nitawajibika kwa usalama wako kuanzia sasa.” Lisa alipepesa macho na kumtazama Alvin aliyekuwa amekaa
pembeni. “Umenitafutia mlinzi?”
“Mmh, familia ya akina Jones inapanda
tena. Huna bahati, kwa hivyo nitakuwa
na amani zaidi ikiwa kuna mtu kando yako." Alvin hakumwambia ukweli, asije
akakasirika siku nzima. kuna jambo
alikuwa akimficha Lisa.
"Alvlisa, wewe ni mzuri sana kwangu."
Lisa alikumbuka mara ya mwisho
alipoangukia kwenye mtego wa Lina. Baada ya kufikiria kidogo, hakukataa.
“Ni vizuri kwamba unajua. Macho ya Alvin yalikuwa ya upole, lakini yakawa
makali tena alipomgeukia Shani.
“Mlinde vyema. Ikiwa mtu yeyote
ataweka mkono juu yake, utawajibika kabisa. Pia, nijulishe ikiwa mtu wa jinsia
tofauti atamkaribia.”
Shani akaitikia kwa kichwa.
“Imeeleweka.”
Kwa pembeni, Lisa alikosa la kusema.
"Unanipeleleza tu kwa kisingizio cha ulinzi, sivyo?"
Alvin alibana mashavu yake. “Sitaki
upate shida, bado nasubiri kwa hamu
kustaafu kazi yangu baada ya wewe
kuipata Mawenzi Investiments.” Sauti ya
sumaku ilimfanya Lisa ashindwe kabisa
kusema lolote.
Baada ya Alvin kwenda kazini, alimuuliza Shani huku akitabasamu, “Unamfahamu Alvilisa?”
Aliposikia jina la 'Alvilisa', Shani alitabasamu na kujibu kwa heshima, "Ndiyo."
Lisa alitazama huku na huku na kuuliza, “Basi lazima ujue kama amewahi kuwa na mpenzi zamani. Amekuwa nao wangapi na…"
“Bi. Jones, unaweza kumuuliza Bw.
Kimaro kuhusu hili wewe mwenyewe.”
Shani aliifuta mada hiyo kwa maneno
machache. Lisa alikata tamaa ghafla.
Mlinzi huyu alionekana kuwa na msimamo sana.
Baadaye siku hiyo, Lisa alijiuzulu kazi
yake huko kwenye kampuni ya zamani
na kufanya maandalizi yake kwa ajili ya
kujiunga rasmi na Mawenzi
Investiments.
Nako katika makazi ya Jones, Jones
Masawe alikuwa katika hali nzuri baada
ya kupokea simu kutoka kwa
mwenyekiti wa bodi ya Mawezi Investments. "Mwenyekiti Amiri hatimaye alikubali kuniunga mkono.
Nafasi ya mwenyekiti itakuwa yangu kesho.” Jones alimwambia mkewe.
"Mpenzi, pongezi." Mama Masawe alitabasamu kwa kiburi. Habari za hadhi ya Jones kuwa mwenye hisa mkuu wa Mawenzi Investiments zilikuwa
zimeenea kila mahali, hivyo wanawake wale matajiri waliokuwa wakimdharau walikuwa wanakimbilia na kumtamani tena. "Unapochukua nafasi ya mwenyekiti na Lina na Stephen watakapooana, familia yetu ya Masawe itasimama kileleni mwa matajiri wa jiji hili."
"Hiyo ni sawa. Muda mrefu tulikuwa
tukiongozwa na familia za Harrison na Zongo, lakini hivi karibuni, tutazipita na
kuwa familia yenye nguvu zaidi hapa
Masaki.” Jones alizidi kuibuka mshindi
kadiri alivyozidi kuwaza juu yake na
hakuweza kujizuia kuangua kicheko.
Lina naye akacheka. “Baba
umeshampata Aunty Manka? Yeye ni bomu linalosubiri kulipuka. Atatuharibia
usipoangalia"
“Ndiyo, yule mwanamke mzee anajua
mambo mengi sana,” Mama Masawe alisema kwa haraka.
"Kwa hivyo hata kama anajua mambo?
Mimi ndiye niliye madarakani sasa. Lisa
ni msichana mdogo tu. Anaweza
kunifanya nini?” Jones alidhihaki bila
kuweka umuhimu wowote kwa watu hao hata kidogo. "Hata kama ana Alvin
Kimaro nyuma yake, ninashuku kuwa
Alvin hatabaki hai kwa muda mrefu."
"Baba, huyu Alvin hata asikutishe, habari zimeenea kuwa anatafutwa na
mtu hatari anayeitwa Zigi Kabwe." Lina
aliachia tabasamu la ajabu. “Tangu kifo
cha dadake, anamchukia sana Alvin
kiasi kwamba hatamuacha hadi amuue.
Kusudi lake lote la kuishi ni kumuua
Alvin Kimaro.”
"Hiyo ni habari nzuri sana." Jones
alimpa tano za kumsifu. "Endelea kupeleleza habari zake, kama atamuua atakuwa ametusaidia sana." Lina
hakuweza kuficha furaha yake. Baada ya kumiliki Mawenzi investiments, angekuwa sosholaiti nambari moja jijini Dar es Salaam. Hakutaka kuvumilia tena wengine kumdharau.
Sura ya 108
Siku iliyofuata saa tatu asubuhi, mkutano wa mwaka wa wanahisa wakuu ulifanyika. Jones Masawe alifuatana na Lina wakaingia ukimbini
kwa hatua kubwa. Alipokelewa na watu wote waliosalimiana naye kwa kupeana naye mikono.
“Mwenyekiti Jones, hongera! Ninaamini nafasi ya mwenyekiti itakuwa yako
mara mwenyekiti Amiri atakapoondoka madarakani.” Mwanahisa mmoja
alimpokea Mzee Jones Masawe kwa
bashasha.
"Unasema nini? Ndo kwanza nimejiunga na Mawenzi Investiments na bado sijaelewa kabisa mambo ya ndani
yanavyofanyika,” Jones alijibaraguza kwa unyenyekevu huku akizuia nia yake isijulikane.
“Una nini cha kukuzuia? Hivyo ndivyo
watendaji tunaowaajiri kwa mishahara mikubwa wanavyokufikiria” mtu
mwingine alisema kwa kujipendekeza, “Maendeleo ya baadaye ya kampuni yanakutegemea Mwenyekiti Jones sasa.”
“Ndiyo, ndiyo, Mwenyekiti Jones. Hata mimi na familia ya Levy tutakuwa tunakutegemea wewe na Mawenzi Investiments,” Bwana Levy pia aliunga mkono.
"Hakuna shida, kama ndivyo
mlivyoamua." Jones hakuweza tena
kuzuia sura ya furaha usoni mwake na kucheka.
Mwenyekiti aliyekuwa anaachia ngazi, Amiri Gumbo, alikunywa chai ili
kulainisha koo lake na kuuliza, "Kila mtu amefika?"
"Kila mtu amewasili, isipokuwa hakuna
mwakilishi wa KIM International inayomiliki asilimia 2`5[ ya hisa, labda na BwanaChris Maganga. " Bwana Issa Kawe, katibu wa bodi, alisema, "Lakini
kila mtu anajua kwamba KIM International kamwe haishiriki katika
masuala ya kampuni na inasubiriaga tu gawio la faida, na Chris Maganga huwa
hahudhurii mkutano wa wanahisa kwa
sababu anaishia mbali. Kwa hiyo hatuna
haja ya kusubiri"
"Kwa hali hiyo, acha kikao cha bodi
kianze." Mwenyekiti Amiri aliidhinisha. Mwenyekiti wa bodi na kiongozi wa mkutano, Mzee Amiri alisema, “Sasa
nina umri wa miaka 70 na afya yangu si nzuri kama ilivyokuwa zamani. Nataka
kuachia nafasi yangu nijali afya yangu, hivyo nafasi ya mwenyekiti lazima
ijazwe na mtu mwenye uwezo. Kwa
bahati ni kwamba mwaka huu, Bibi
Mkubwa Masawe alifariki na 60% ya
hisa zake zilipitishwa kwa mtoto wake, Jones Masawe. Katika siku zijazo,
atakuwa mwenye hisa mkuu wa
kampuni na atakuwa na mamlaka kamili
ndani ya bodi. Kwa hiyo tunaweza kufikira kumwachia kiti hiki cha
mwenyekiti kama hamtajali.”
Chumba cha wanahisa mara moja
kilimtazama Jones Masawe kwa wivu.
Uso wa Jones ukanyanyuka juu kwa sifa.
Bwana Levy, mmoja wa wanahisa,
akatabasamu na kusema. "Mwenyekiti Jones yuko katika umri wake wa
dhahabu na ni mkomavu na thabiti.
Naamini ni bora achukue nafasi ya mwenyekiti.”
"Ndio, tunakubali." Ukumbi mzima
ukaripuka kwa makofi.
“Acha awe Mwenyekiti Jones. Anafaa kwa nafasi hii." Maneno ya watu fulani
yakasikika. Chumba kikubwa cha
mikutano kilijaa kila aina za sauti za
kuunga mkono.
Mwenyekiti Amiri Gumbo aliitikia kwa kichwa na kusema, “Kwa kuwa huu ni uchaguzi, bado tunapaswa kufuata utaratibu wa kawaida. Kila mtu
anayemkubali Jones Masawe anyanyue mkono wake juu."
Wanahisa wa bodi waliinua mikono yao, na Mwenyekiti wa mkutano akahesabu.
“Kura kumi kati ya wanahisa 15.
Inaonekana kama nafasi yangu ni ya
Bwana Jones sasa. Hapana, nikuite
Mwenyekiti Masawe sasa hivi.”
Jones Masawe aliinuka na chemchemi ya majivuno katika hatua yake.
"Asanteni kwa ushirikiano wenu. Kwa
kuwa mmeniamini na kuniwezesha
kuchukua wadhifa wa mwenyekiti, bila
shaka nitaifikisha Mawenzi Investiments hadi kwenye orodha ya makampuni 10 bora Tanzania, au hata 100 bora Afrika.
Nitamwezesha kila mtu kupata faida
nzuri zaidi kila mwaka.”
"Tunaimani na wewe." Kila mtu aliinua
mikono yake na kupiga makofi.
Mwenyekiti Masawe hakuweza kuacha kutabasamu. Mwili wake wote
ulionekana kuelea kwenye ombwe la furaha. Alikuwa mwenyekiti wa Kibo
Group kwa nusu ya maisha yake, lakini
Kibo Group haikuwa chochote
ikilinganishwa na hadhi ya Mawenzi Investiments. Katika siku za usoni, Dar
yote ingekuwa chini ya miguu yake.
Na wale ambao hawakumpigia kura siku
hiyo …! Akamgeukia Lina na kusema, “Niandikieni majina ya wale ambao
hawakuniipiga kura.”
“Usijali, Baba. Nimeandika majina yote.”
Lina alijibu kwa jeuri kama ya baba yake. “Baba naweza kuwa na nafasi ya meneja mkuu wa kampuni? Sihitaji tena
kuwa meneja wa mradi wa ukuzaji mali, ni nafasi ndogo sana kwangu hiyo.”
“Kuwa na subira. Nitalizungumza
kwenye kikao baadaye.” Baba yake
hakumvunja moyo.
Lina alitetemeka kwa furaha. Katika siku
zijazo angekuwa binti mdogo mwenye utajiri wa thamani ya makumi ya mabilioni ya shilingi. Mtandao mzima wa watu mashuhuri nchini ungekuwa kituo chake, achilia mbali Dar es Salaam. Kwa Lisa, angekuwa mchwa tu.
“Mwenyekiti Jones, kaa kiti changu. Mahali hapa ni mali yako sasa."
Mwenyekiti mstaafu, mzee Amiri akainuka. "Mkutano unaofuata wa wanahisa utakuwa mikononi mwako."
"Mwenyekiti Amiri, wewe ni mwema sana." Mwenyekiti Jones alisema kwa furaha, na miguu yake mara moja
ikasogea kuketi.
Ghafla, mlango wa chumba cha
mkutano ulifunguliwa kwa kishindo, na mzee wa makamo aliyevalia suti nyeusi
akaingia ndani akionekana mwenye
nguvu na mamlaka. Nyuma yake, mwanamke kijana alimfuata. Suti yake ya kifalme ya bluu ilifunika ngozi yake
nzuri, na nywele zake ndefu ziliwekwa
juu ya mabega yake. Haiba yake
ilisisitiza sifa zake za kupendeza. Uso wake mdogo haukuwa na hisia, lakini
ulibeba tu hali ya tahadhari
kwa mwonekano wake. Wakati huo, nyuso za Jones na Lina zilibadilika papo hapo.
Lina akapiga kelele kwa nguvu, “Lisa, unafanya nini hapa? Toka nje! Hii ni mali ya Mawenzi Investiments. Nani alikuruhusu kuingia humu? Ondoka sasa hivi!”
Sauti yake ilikuwa ya kiburi, lakini Lisa
naye alikuwa ameshiba dharau huku
Chris Maganga akiuliza, "Kwani
nimepoteza haki yangu ya kuleta mtu
kwenye mkutano wa wanahisa kwa
sababu tu sijaja kwenye kampuni kwa
miaka michache?"
Jones Masawe alihisi tu kwamba mtu
huyo hakuwa mgeni machoni pake, lakini hakumtambua. Mwenyekiti
aliyetoka madarakani Amiri alisimama na kusema, “Bwana Maganga, si
unaishi Mwanza kwa sasa? Kwanini
umekuja ghafla kwenye mkutano wa kampuni leo?”
Uso wa Lina ukapoa. mara moja akawa
ametambua kwamba huyo ndiye
mwenyehisa ambaye alionekana mara chache sana kwenye kampuni, Chris
Maganga. Hata hivyo alikuwa na 10% tu ya hisa ukilinganisha na baba yake
aliyekuwa na 60%. zaidi ya hayo, Jones
Masawe alikuwa tayari ni mwenyekiti wa
Mawenzi Investiments, hivyo Lina
hakuwa hata na tone la wasiwasi
moyoni mwake. Hakuonyesha heshima
yoyote kwa Chris na alimdhihaki bila
kujali, akisema, "Ni kweli, unaweza
kuingia kwenye mkutano kama
mwanahisa, lakini huwezi kutumia
nafasi yako kuleta takataka."
Alimtazama Lisa baada ya kuongea.
Lisa aliinua ndita zake na kucheka.
“Unajizungumzia wewe mwenyeweee, au kuna takataka nyingine?”
"Lisa, bado unaota?" Lina alidhihaki,
“Baba yangu sasa ni mwenyekiti wa
Mawenzi Investiments. Ninaweza kuja hapa wakati wowote ninapotaka. Unafikiri wewe ni nani?”
“Hata sijapiga kura. Ilikuwaje akawa mwenyekiti mpya?" Chris akaburuta kiti na kuketi.
Sura ya 109
Mwenyekiti Jones alimdharau Chris.
“Inaonekana kwamba Bwana Maganga hajaridhika nami, lakini tayari kuna watu
kumi katika kampuni ambao walinipigia kura. Hata ukipiga kura haina maana.”
“Ndiyo.” Mwenyekiti mstaafu Amiri alijisikia vibaya. “Bwana Jones ndiye mwenyekiti mpya. Hakuna anayeweza kubadilisha hilo. Kura moja
haitabadilisha matokeo.”
“Pia ndiye mwanahisa mkubwa ambaye
anamiliki asilimia 60 ya hisa. Unawezaje kujilinganisha naye?” Baadhi ya watu
walianza kudhihaki.
Mwonekano wa Mwenyekiti Masawe ulikuwa wa kiburi. "Bwana Maganga, ikiwa uko hapa kuleta shida, usinilaumu
kwa kuagiza walinzi wakutoe nje."
"Nani alisema wewe ndiye mwenyehisa mkubwa?" Chris akatabasamu. "Una 30% ya tu ya hisa."
Jones alikunja uso. "Mama yangu alipofariki, nilipewa 60% ya hisa."
"Si zako." Chris akazitupa zile nyaraka zilizokuwa mkononi mwake mezani.
“Bibi Mkubwa Masawe alitoa wosia
kabla hajafa. Baada ya kufa, Lisa Jones
atakuwa na 30% kati ya 60% ya hisa.
Vipi, unapanga kuchukua kila kitu bila
kusema chochote?"
Wakati kauli hii inatolewa, chumba
kizima kilikuwa na ghasia. Nyuso za
Jones na Lina zilibadilika sana.
Mwenyekiti mstaafu Amiri alichukua
nyaraka na uso wake ukageuka ghafla.
'Ni kweli. Muhuri na saini ya Bibi
Masawe viko juu yake."
“Hilo haliwezekani…” Jones alipiga
meza na kusimama.
"Ni nini kisichowezekana juu yake?"
Lisa alienda kutazama umati wa watu.
"Ninaamini kuwa wanahisa wote
wanajua kuwa Mawenzi Investiments
ilianzishwa na Sheryl Masawe zaidi ya miaka 20 iliyopita. Mimi ni binti wa
Sheryl, na hii ni kampuni ya mama yangu. Babu na bibi yangu walimpa tu
30% ya hisa kwa sababu Jones
Masawe alinilea, lakini hajatosheka na anataka kumiliki yote.”
“Funga mdomo wako!” Jones alijaribu
kumpiga kofi, lakini kuna mtu alikuwa mwepesi kuliko yeye, Shani alimshika
mkono na kumminya kwa nguvu, na kumfanya apige kelele kwa maumivu
mara moja.
"Wewe ni nani? Niache mara moja, la sivyo!” Jones Masawe alijitetea
kinyonge.
"Ukithubutu kumpiga mwajiri wangu tena, nitakuvunja mkono." Shani alionya
kwa upole kabla ya kuachilia mkono
wake. Jones alipiga hatua chache
nyuma. Mkono wake ulikuwa umekufa ganzi kwa maumivu.
Lina alimuunga mkono baba yake na kusema kwa kutokuamini, “Lisa, unazungumzia nini? Kwa ajili ya utukufu na mali, ungeweza hata kumkana baba yako mzazi? Kila mtu anajua kwamba
Sheryl Jones hajawahi kuolewa.
Angewezaje kupata binti? Umekuwa wazimu?"
“Sivyo ulivyosema hapo awali?” Lisa alimuumbua “Uliniambia mwenyewe kuwa mimi si binti wa Jones Masawe bali ni mtoto wa kuokota kwenye vituo vya watoto yatima.”
Macho ya Lina yaliangaza kwa dhihaka.
“Nilikuwa naongea upuuzi tu wakati ule.
Wosia wa babu na Bibi unasema waziwazi.”
Mwenyekiti Amiri alitikisa kichwa tena
kinyonge. "Ndio, imeandikwa kweli
kwamba Lisa Jones ni binti wa Sheryl Masawe."
Jones Masawe alikunja ngumi kwa
nguvu na kusema. “Hata kama ni kweli, hisa zote zimehamishiwa kwenye jina langu. Ni upuuzi kuendelea kuongea. Kikao hiki cha bodi hakiwezi kubadilisha ukweli kwamba mimi ni mwanahisa mkuu.”
“Nani alisema kwamba hisa zote
zimehamishiwa kwa jina lako?” Lisa
alitabasamu kijeuri. “Hujatazama? 30% ya hisa zimehamishwa kwa jina langu
kwenye Idara ya Viwanda na Biashara.”
Uso wa Jones ukabadilika. Hakuweza
kuvumilia tena na akachukua simu na kupiga moja kwa moja kwenye idara ya viwanda na biashara. Chini ya dakika
moja tu baadaye alimgeukia Lisa kwa
macho makali, hakutaka kingine zaidi ya kumchuna ngozi akiwa hai.
Lisa akaugeukia umati. “Imekuwa bahati
sana. Bibi yangu alifariki ghafla baada ya kupooza ghafla pia. Taarifa za kifo
chake niliambiwa na mtu baki, na ni kitambo kifupi tu baadaye nikagundua
kuwa nina uhusiano na Mawenzi
Investiments. Vinginevyo hisa zangu zote zingekuwa mali ya mjomba.”
Umati wote ukalipuka kwa minong’ono.
“Mungu wangu, inaonekana kwamba
kuna kitu cha ajabu juu ya kifo cha Bibi Masawe.”
"Hiyo ni kweli. Yule bibi alikuwa mwenye afya nzuri tu nilipomuona siku si nyingi...”
“Tsk, kweli hafai. Alikuwa ni mama yake mzazi!”
“Lazima tumwepuke mtu huyu. Anatisha!”
Mtazamo wa kila mtu kwa Jones ukabadilika.
Jones aligonga meza kwa hasira. “Lisa
Jones, jaribu kuongea upuuzi tena uone!”
“Mjomba, sijakutusi. Kwanini unajihami
sana? Kweli hauna hatia kwenye hili?”
Lisa alipaza sauti kwa macho makali.
“Lakini sikuamini kabisa kama
ungemuua mama yako mzazi. Kama
ulimuua, bibi yangu hata kuacha uishi kwa amani.”
Jones alikurupuka na kutokwa na jasho baridi. Haraka alibadilisha mada katika
hali mbaya. “Unapanga kufanya nini hapa?”
"Bila shaka, ni kugombea dhidi yako kwa nafasi ya mwenyekiti." Lisa
alimtazama kila mtu. "Sasa nina 30% ya hisa, sawa na Jones Masawe, kwa
hivyo ninastahili kushiriki."
"Lazima una wazimu." Jones alionekana
kama amesikia utani mkubwa. "Una miaka mingapi? Wewe ni msichana
mdogo tu mjinga. Huna uzoefu na huna uwezo. Nani atakuwa na imani na wewe
kukukabidhi kwa hiari kampuni kubwa kama hii?”
"Hiyo ni sawa." Bwana Levy akaitikia
kwa kichwa. "Hatutaki kuingilia ugomvi
wako na familia ya Jones, lakini
kusimamia kampuni sio mzaha."
“Ndiyo, Mawenzi Investiments haikosi
watu. Hata iweje, huyu binti mdogo
hawezi kuwa mwenyekiti.” Baadhi ya wanahisa walikunja uso na kupinga.
Jones Masawe aliridhika sana na akaketi tena na kunywa chai yake.
Baada ya yote yaliyosemwa na kufanyika, ilionekana kuwa nafasi ya mwenyekiti bado ilikuwa ni yake.
"Kwanini siwezi kuwa mwenyekiti?" Lisa
aliuliza bila kuhangaika, “Kama sote
tunavyojua, Jones Masawe aliwahi
kuwa mwenyekiti wa Kibo Group
aliyorithi kutoka kwa babu, lakini chini ya uongozi wake, Kibo Group ilisusiwa na mtandao mzima wa wafanyabiashara na hata ikamlazimu kuiuza kwa hasara.
Mtandao bado unazungumza juu yake
sasa. Sifa yake imeharibika kabisa na hakuna anayemwamini. Aliongoza
kampuni hiyo kupokea hongo, huku
ufisadi na visasi vingine vikiwa
vimeshamiri. Ikiwa ataiongoza Mawenzi
Investiments, ulimwengu wa nje utatilia
shaka ubora wa bidhaa na mali za
Mawenzi Investiments.” Taarifa hii
iliposemwa, wanahisa kadhaa walikubali kwa kutikisa kichwa. Uso wa Jones
ulizidi kuwa mgumu huku akimkazia macho Lisa, hakutaka kitu zaidi ya kumla akiwa hai.
Lina alisema kwa hasira, “Bado una ujasiri wa kusema hivyo! Kwani sifa ya Kibo Group ingeharibika ikiwa si wewe?
Yote ni makosa yako."
Sura ya 110
Lisa alicheka kwa madaha. “Ndiyo, mimi ndiye niliyeibua ufisadi wa mpwa wa mtu fulani. Aliingiwa na pupa ya tamaa ya pesa kuanza kuharibu miradi ya
ujenzi kwa kutumia vifaa feki
akishirikiana na wewe Lina. Huwezi
hata kujenga nyumba lakini sasa
unataka kuwa mbunifu. Nani atathubutu
kukubali mradi uliobuniwa na wewe?"
"Ndio, hiyo haitafaa." Bwana Haruna, mmoja wa wanahisa alikuwa wa kwanza
kupinga hadharani dhidi yake.
“Nataka kutafakari upya pia. Hatuwezi
kuharibu sifa ya Mawenzi Investiments.”
Mwanahisa mwingine akadakia.
Wanahisa walipoanza kurudi nyuma, Lisa alisema kwa sauti ya upole kwa kila mtu, “Ni kweli kwamba mimi ni mdogo, lakini nina mawazo wazi na makini.
Ikiwa sijui chochote, naweza kuwauliza
wazee wangu waliopo hapa kwa
ushauri. Haikuwa rahisi kwa Mawenzi
Investiments kufikia kiwango ilichopo.
Haijalishi ni faida ngapi ambazo Jones
ameahidi kwa kila mtu, lengo letu kuu ni kukuza faida ya kampuni ili tupate gawio bora zaidi.
“Ndiyo hivyo,” hatimaye Chris
alizungumza. Sauti yake ilikuwa na mamlaka sana. "Wasifuwa bosi wa
kampuni kubwa kama hii ni muhimu
sana. Nitamuunga mkono kikamilifu Lisa
ikiwa atakuwa mwenyekiti. Kila mtu
anapaswa kujua kwamba niliwahi pia
kumsaidia Sheryl. Ni shukrani kwa
Sheryl kwamba Mawenzi Investiments
ndivyo ilivyo leo.”
"Bado tunaamini katika uwezo wa Bwana Maganga." Bwana Haruna alikubali kwa kutikisa kichwa.
“Kwa hali hiyo, tupige kura tena. Una maoni gani, Mwenyekiti Amiri?" Chris Maganga alimtazama Mkwenyekiti Amiri na kumkumbusha, “Mwenyekiti Amiri, kama ningetaka kushindana na wewe katika nafasi ya mwenyekiti hapo awali, usingekaa kwa furaha hapa leo.”
"Nakubali." Mwenyekiti Amiri alikwepa kumtazama Chris Maganga na kutikisa kichwa. "Wacha tuanze kupiga kura upya."
Kila mtu aliinua mkono wake mmoja
baada ya mwingine, na matokeo ya mwisho yalikuwa tisa kwa saba. Lisa ni tisa dhidi ya saba za Jones.
"Wacha tumpongeze Lisa Jones kama mwenyekiti mpya." Chris aliongoza kupiga makofi.
Jones Masawe alipiga meza, uso wake
ukiwa na hasira. “Uchaguzi huu si mchezo. Unawezaje kurudia mchakato wa kupiga kura? Ni mimi niliyechaguliwa hapo awali. Unafikiri wewe ni nani?”
"Bwana Jones anaonekana kutoshawishika." Kulikuwa na kitu kingine kilichojificha chini ya tabasamu la Lisa. "Lazima uelewe kwamba kama si ukarimu wa mama yangu, usingekuwa na uhusiano wowote na kampuni hii. Unapaswa kuridhika na ulichonacho.”
“Wewe…!” Jones alimkazia macho.
Hakuamini yule binti ambaye aliwahi kuwa adabu sana mbele yake sasa alithubutu kuwa mkaidi mbele yake.
“Ikiwa utaendelea kufanya fujo, ninaweza kuwaita walinzi wakutoe nje,”
Lisa alionya bila huruma.
Jones alipandwa na hasira. Kulikuwa na wanahisa wengi hapo, lakini hakuna
hata mmoja aliyemtetea.
"Bw. Jones, kaa chini." Mwenyekiti Amiri
alihema kwa nguvu. "Tayari
tumechelewesha hii kwa muda wa kutosha. Bado kuna mambo mengi tunapaswa kuyashughulikia katika mkutano huu."
"Ni sawa, lakini kabla ya hapo, ni wakati wa watu wa nje ambao hawana uhusiano wowote na mkutano kutoka
nje." Lisa alimtazama Lina.
Lina alikuwa akifedheheshwa
hadharani, na macho yake yakiwa mekundu, aliongea kana kwamba
amedhulumiwa, “Lisa, najua hunipendi, lakini—”
“Nimesema kitu kibaya? Kwani wewe una sifa za kukaa hapa?” Lisa alidhihaki. “Bi. Jones hajui hata sheria za nidhamu za kampuni."
"Inatosha, nenda nje," Mwenyekiti Amiri alisema bila subira.
Lina alijawa kiburi, akatuna kama puto
lililopulizwa, lakini hakuwa na ujanja
zaidi ya kutoka nje. Mlango wa chumba
cha mikutano ukafungwa tena, naye
alikasirika sana hivi kwamba machozi
yakamtoka.
Muda si muda, Stephen Kileo alimpigia
simu. "Lina, hongera! Baba yako lazima awe mwenyekiti mpya wa
Mawenzi sasa.” Sikio la Lina lilihisi uchungu kana kwamba alipigwa kofi
kali. Stephen hakujua na akaendelea kusema, “Baba yako anapochukua ofisi, mradi wa Nairobi ambao tulijadili mara ya mwisho unaweza kuanzishwa mara
moja. Kisha, familia za Kileo na Masawe zitashirikiana kuunda hotel ya nyota
tano huko Nairobi. Hivi karibuni, iwe ni Nairobi au Dar es Salaam, itakuwa ulimwengu wetu. Hahahaa, nataka sana kuona nyuso zilizoshindwa za familia za Harrison na Clark sasa…! Hee..Lina, mbona huongei chochote?” Stephen, ambaye alikuwa akizungumza kwa
muda, hatimaye alishtuka kwa kuona
kimya chake.
"Ni Lisa ndiye ameshinda nafasi ya uenyekiti." Hatimaye Lina akaongea
ukweli mchungu.
"Nini?" Stephen akapiga kelele. “Si ulisema una uhakika 90% baba yako
atakuwa mwenyekiti? Wewe na baba yako mnafanya nini? Hamwezi hata
kumshughulikia Lisa Jones?”
Uso wa Lina ulihisi joto aliposema bila
raha, “tungejuaje kwamba angeungana na Chris Maganga? Sisi pia tulishikwa na bumbuwazi.”
“Kweli mambo ndiyo yamegeuka kuwa hivi? Hata nilijitapa nikisema kuwa
mpenzi wangu ni binti wa mwenyekiti wa Mawenzi. Ni fedheha iliyoje sasa eeh....! sitaki kusikia hii tena." Stephen alilaani sana.
Sauti ya Lina ilikata. “Stephen, unamaanisha nini kusema hivyo? Sasa
unanichukia kwa sababu baba yangu
hakupata nafasi ya mwenyekiti?”
Stephen alirudi kwenye fahamu zake
ghafla. Hata kama baba yake Lina
hakuwa mwenyekiti wa Mawenzi
Investiments, mwaka wa gawio ulikuwa
unatosha kuwafanya wawe na pesa
nyingi mno. Alicheka kwa haraka na kusema, “Bila shaka, usinifikirie vibaya.
Nimekasirishwa tu na dhuluma uliyotendewa. Nakupenda wewe, sio utambulisho wako."
“Usijali. Hii ni ya muda tu. Lisa hatakaa katika nafasi ya mwenyekiti kwa muda mrefu,” Lina alisema kwa ukali.
“Uko sahihi. Si rahisi kufanikisha mambo makubwa ikiwa Lisa atakuwa mwenyekiti.” Stephen pia alitabasamu kwa huzuni. "Sitaacha juhudi yoyote kukusaidia."
"Asante." Lina akajibu na simu ikakatwa.
Mkutano uliisha saa sita mchana.
Mmoja baada ya mwingine, wanahisa
walipeana na mwenyekiti mpya mikono na kuondoka kwa heshima.
"Mwenyekiti Jones, nitakupeleka ofisini kwako." Msaidizi wa mwenyekiti, Tunu
Omari, alimjia Lisa kwa hatua kubwa.
Alikuwa na tabia njema na mwenye
bidii.
“Sawa, nipeleke huko.”
Alikuwa ameanza kuondoka tu wakati
Jones alipomzuia njia. Maneno yake yalikuwa ya huzuni na ya kutisha. "We
paka malaya, lazima utajuta mwenyewe. Umeweza kuketi kwenye
kiti hicho, lakini hiyo haimaanishi kuwa utaendelea kukaa muda mrefu—”
“Paah!” Lisa aliinua mkono wake na kumpiga kofi Jones Masawe bila
huruma wala aibu.
Jones hakuwahi kutarajia kitu kama
hicho. Alishikwa na machozi na hasira
sawasawa. Hatimaye alipojibu, alitoa
meno yake kwa hasira na kumkimbilia ili kumfundisha somo. Lakini, Shani
alisimama mbele ya Lisa na kumpiga
teke Jones, na kumfanya aruke mita
kadhaa chini. Hakuweza kuinuka kwa
muda mrefu kwa sababu ya maumivu.
“Wewe… Wewe msichana usiye na
shukrani! Unathubutu vipi kumpiga
mzee? Utapata laana ya Mungu.!"
Jones alinguruma kwa hasira.
"Uliniita malaya, kwa hivyo kama mkuu wako, ni kawaida tu kukufundisha somo." Lisa akapuliza kiganja chake kilichokuwa kikiwaka kwa maumivu.
“Zaidi ya hayo, kwani wewe na mkeo mmenipiga makofi mara ngapi? Sijafikia hata chembe ya makofi mliyokuwa mkinipiga bila hata kosa.”
“Kwa hiyo tulikuwa tunakuonea?
Tulikuwa tunakulea. Tunakudai deni
kubwa la shukrani kwa kukulea,” Jones
Masawe alisema kwa huzuni.
Sura ya 111
Macho maangavu ya Lisa yaligeuka na kuwa makali kidogo. “Umenileaje?
Ulinisaidia nilipokuwa nasoma?
Niliposhikwa na homa, babu na bibi ndio
waliniuguza. Kuhusu gharama za
maisha ulizolipa, babu na bibi yangu
walitumia hisa za mamia ya mamilioni
kukufidia, lakini hujaridhika!” Hasira ya
Jones ilisababisha koo lake kukwama.
Lisa akasogea mbele na kumtazama kwa juu. “Ni sawa, lakini hata mama
yako mzazi ulimuua, unaweza kujihesabu kuwa wewe ni binadamu?”
Jones Masawe aliruka juu kama paka ambaye mkia wake umekanyagwa. "Bibi
yako alikufa kwa ugonjwa."
“Ndiyo, inasikitisha kwamba Bibi alikufa
nikiwa sina msaada. La sivyo, kuchunguza maiti yake kungetosha
kwetu kugundua sababu ya kifo chake,”
Lisa alidhihaki, akisema, “Lakini
sitakuacha. Hakika nitakulipa pole pole
maumivu yote niliyopata, ikiwa ni pamoja na kumlipizia Bibi.” Kisha, alitoka kwenye chumba cha mikutano
bila kuangalia nyuma. Alipotoka nje, mwili wake ulikuwa ukitetemeka kwa
msisimko.
Muda wote huo, alikuwa
amenyanyaswa na kuonewa na familia ya akina Jones. Alikaribia kupoteza
maisha mara kadhaa. Kuanzia siku
hiyo, angekuwa na nguvu ya kujilinda
yeye na watu wanaomzunguka.
Baada ya kurudi ofisini kama
mwenyekiti, mara moja alimwomba
Tunu aende kuleta taarifa muhimu
kuhusu uongozi wa juu wa kampuni.
“Mwenyekiti Lisa, huhitaji kuwa na haraka hivyo. Kula chochote kwanza.
Nitakuagizia …”
"Agiza mtu alete kitu rahisi."
Baada ya Tunu kuondoka, Lisa
alimgeukia Shani na kusema, “Asante.
Kama usingekuwepo leo, Jones
angenipiga bila shaka.”
"Karibu. Ni wajibu wangu kukulinda.”
Shani aliachia tabasamu hafifu. "Ikiwa unashukuru, basi mshukuru Bw.
Kimaro."
Lisa naye alitaka kumweleza Alvin
habari hiyo njema na kumpigia simu.
"Alvlisa, unafanya nini?"
“Kula.” Jibu la mtu huyo lilikuwa fupi
sana.
Lisa alikosa furaha na akapiga kelele.
“Mbona hauulizi kama nimefaulu leo?
Hunijali hata kidogo, hmph.”
"Shani tayari amenitumia ujumbe saa moja iliyopita." Sauti ya chini ya Alvin
ilichanganyika na tabasamu.
"Mwenyekiti Lisa alijitokeza katika
mkutano wa wanahisa leo, akionekana kama mwanamke wa chuma.
Inaonekana kama ninaweza tu kuwa mwanamume anayesimama nyuma ya mwenyekiti katika siku zijazo.”
“Hadhi yangu si ya kawaida kwa sasa
na wanaume wengi wanataka kuwa wao wanaosimama nyuma yangu. Jihadhari, afadhali uwe mtiifu na unisikilize, ama sivyo watachukua nafasi yako.” Lisa
alifoka kwa utani huku akitabasamu.
Sikuzote Alvin ndiye aliyekuwa na mamlaka juu yake na kumsimamia, lakini hatimaye alihisi kwamba alikuwa
huru kutoka katika hadhi yake ya chini.
“Ndiyo, nitakuwa mtiifu. Nikirudi usiku
huu, nitakuhudumia hadi
utakaporidhika,” Alvin alisema kwa utata.
Simu iliyokuwa sikioni mwa Lisa ilifanya
ionekane kama alikuwa akipumulia sikioni, na ghafla aliona haya huku
akikemea, “Wewe mpuuzi, nitakata simu sasa hivi.”
"Nazungumza juu ya kukupa massage."
Alvin alicheka. “Au unawaza nini?
Inaweza kuwa…”
"Sahau…" Lisa akakata simu huku
akicheka. Alipogeuka pembeni, alimuona Shani akiwa na tabasamu
usoni mwake na kuhisi aibu zaidi.
Baada ya kula, Tunu alimletea orodha ya watendaji wakuu wa kampuni na kuiangalia. Lisa aliitazama na kuikazia macho post ya Lina. Meneja mkuu wa mradi wa maendeleo ya mali. Alidhihaki
papo hapo, akitambua ukweli wa jinsi
alivyokaribia kufa alipoenda kwenye
eneo la ujenzi mara ya mwisho.
"Ina maana hakuna mtu mwingine
katika kampuni yangu? Kwa nini huyu
kanjanja asiye na elimu wala uzoefu
anachukua nafasi hiyo muhimu?" Lisa alisema kwa kusikitisha, "Watendaji wa kampuni wanakuja lini? Nataka kuwa na mazungumzo mazuri nao.”
Tunu aliona mawazo yake na akasitasita kabla ya kusema, "Walitoka kwa chakula cha mchana na Jones Masawe."
Uso mzuri wa Lisa uliingia giza mara moja. Alikuwa ametoka tu kuchukua
nafasi ya mwenyekiti, lakini sio tu kwamba watendaji wakuu
hawakumtembelea, lakini hata walitoka kwa chakula cha mchana na Jones.
Ilikuwa wazi kwamba hawakumchukulia kwa uzito hata kidogo.
Tunu aliitikia kwa kichwa. "Meneja Mkuu
Changala ameshikilia wadhifa muhimu
katika kampuni kwa miaka kumi. Wakati
wa umiliki wake, aliongeza faida ya
kampuni kwa 10%, na wanahisa
wameridhika naye sana. Ikiwa… Ikiwa
Mwenyekiti unataka kumfukuza kazi, ninahofia itasababisha kutoridhika sana miongoni mwa wanahisa.”
“Sawa, nimeelewa. Unaweza kwenda nje kwanza.” Lisa akanyamaza kimya, kisha, alienda kukagua idara kuu za kampuni. Hata hadi jioni, hakuna hata
mmoja wa wasimamizi wakuu aliyefika kumuona.
Kulipoingia giza, Lisa alimwambia Shani, “Nifanyie msaada na uajiri mpelelezi binafsi. Nataka kujua kuhusu jambo fulani.”
Saa moja jioni, Lisa alirudi nyumbani akiwa na rundo la hati mikononi mwake.
Alvin alikaa sebuleni akiwa amevaa
nguo za kawaida huku mikono yake
ikiwa inatetemeka kidogo. Alionekana
mwenye hofu kwa mbali, akimsikiliza
Hans alipokuwa akiripoti kitu kwake kwa
heshima. Lisa alibadilisha viatu na
kuingia ndani. Alvin akageuka, na
midomo yake maridadi iliinama chini.
"Mwenyekiti Lisa, hatimaye yuko tayari
kurejea."
"Nimekuwa nikifanya kazi kwa muda wa ziada katika kampuni yangu. Vipi, umekula?" Lisa aliona kuhudhunishwa kwake na akaelezea kinyonge. Alvin alishika midomo yake lakini
hakuzungumza. Aunty Linda alijitokeza kueleza, “Bw. Kimaro hapendi chakula
ninachotengeneza. Anataka chakula unachopika wewe mwenyewe.”
Lisa alishusha pumzi. Alikaa kando yake kwa uchovu na kumuegemea
begani. “Nimechoka baada ya kufanya kazi siku nzima na siwezi kufanya
chochote. Upikaji wa Aunty Linda unafanana na wangu, kwa hiyo jaribu tu kula.”
"Kwanini, mambo hayakwenda sawa
kwenye kampuni?" Alvin akageuka
kumwangalia. Nywele zake zilisonga
kwenye sehemu ya juu ya pua yake, na
kumfanya anuse harufu hafifu.
“Mmh, hao watendaji wa ngazi za juu
hawanitilii maanani hata kidogo. Bado kuna vita ngumu kupigana." Kadri Lisa
alivyozidi kuongea ndivyo alivyozidi kuzama kwenye hisia za kumuegemea
Alvin. Alijihisi amani bila kufikiria chochote.
Alvin alikunja uso kabla ya kumwambia
Hans, “Nenda kwenye kampuni yake
kesho ukamsaidie kupanga mambo yake. Hakikisha wanakuwa watiifu ndani ya siku moja.”
"Nimeelewa," Hans alijibu mara moja.
Alikuwa msaidizi wa milionea mkubwa nchini. Kiasi hiki kilikuwa kipande cha keki.
Lakini, Lisa alisema haraka, "Hapana.
Ingawa Hans kwa kawaida ana uwezo
mkubwa, yeye ni msaidizi wako tu na
hajui chochote kuhusu kampuni ya
Mawenzi. Ataliwa na hilo genge la watu
mpaka hata mifupa yake haitabaki.
"Hans huyu, ambaye yeye ndiye
amezowea kula watu, leo hii aje aliwe
yeye?" Alvin akacheka. "Hiki kitakuwa
kichekesho cha mwaka."
'Ninathamini nia yako nzuri, lakini hili
nitapambana nalo mwenyewe" Lisa
alisema kwa unyoofu, "pia nilipata
sababu iliyonifanya ulijeruhiwa kwenye eneo la ujenzi mara ya mwisho. Hakika
nitalipiza kisasi kwa ajili yako.”
“Sawa. Mwanamke wangu wa nguvu
sasa ana uwezo kweli kweli." Alvin alisugua nywele zake na kumwambia
kwa mapenzi, "una njaa, kwa hivyo nenda ukale."
"Na wewe je?"
“Kama utanipikia nitakula.”
Sura ya 112
Lisa alimtazama kwa makini kwa muda.
Hakukuwa na cha kufanya kwa jinsi
alivyomuona mumewe, zaidi ya kwenda
jikoni na kupika chakula ili ale.
Hans alitazama umbo la Lisa likipotea
kabla ya kuendelea kuongea, “Baada ya
siku chache, Willie Kimaro ataingia Dar.
Watu hapa tayari yanajua kuhusu hilo. Nahofia itasababisha zogo.”
“Yeye ni kipande cha takataka tu. Mahali kama hapa tu ndio patamchukulia kama mtu mwenye nguvu,” Alvin alidhihaki.
"Unataka kupanga kukutana naye?" Hans aliuliza.
"Hapana. Bado hastahili.” Alvin akasimama. “Usiku umeenda sana.
Rudi nyuma." Hans na Shani wote waliondoka.
Lisa alikuwa amevaa vazi la jikoni akiwa amezama kwenye mapishi akimpikia mumewe. Taa ya jikoni yenye joto iliangaza juu ya kichwa chake, na kumpa mumewe hamu ya kumshika.
Akamsogelea na kumkumbatia kwa
upole kwa nyuma, akaegemeza kidevu chake kichwani. “Ongeza zaidi. Chapati
hizi hazitatosha kuniridhisha.”
"Ushukuru tu kwa kuwa ninakupikia."
Lisa alisema kwa kujigamba. "Ikiwa
unataka kula, basi katakata hiyo nyama ya nguruwe wewe mwenywe."
Alvin alionekana kusikia kitu kisichoaminika. “Unathubutu kuniagiza?”
Lisa alifikiria kabla ya kuchukua kadi kutoka mfukoni mwake na kumkabidhi.
"Hii ni nini?" Alvin aliuliza kwa mshangao.
"Kuna milioni 500 ndani yake. Ni ada ya kesi uliyonitetea hapo awali…” Lisa
alikuwa bado hajamaliza kuongea akahisi hali ya hewa iliyomzunguka
imebadilika ghafla. Macho ya Alvin yalionekana kufunikwa na unyonge, na kusababisha akose raha.
“Unamaanisha nini kwa hili?” Alvin
aliishika kadi kwa vidole viwili na
kudharau kwa macho yake. "Umekuwa mwenyekiti leoleo tayari umechota pesa
zote hizi kwenye kampuni, si utafilisi
kampuni wewe?"
"Wala," Lisa alijibu akitabasamu kwa
kuridhika, "sema tu ni deni lililokuwa likininyima amani."
"Una pesa sasa, kwa hivyo unataka kufuta uhusiano wetu, si ndiyo?" Alvin
aliuliza na kukaribia kuichana kadi hiyo vipande viwili. "Endelea kuota. Ulitia
saini wewe mwenyewe karatasi.
Haijalishi una nafasi gani, itabidi uendelee kukaa nami kwa utiifu.”
“Huwezi kunisubiri nimalizie…?” Lisa
aliitazama ile kadi na kuikandamiza miguu yake kwa hasira. "Nataka
kukulipa deni lako ili niishi na na wewe kwa usawa. Sitaki kuwa mtumishi wako.
Nataka kuwa mpenzi wako kwa kila maana ya neno hilo.”
“Hiyo ina maana gani?” Alvin alikunja uso, alikuwa haelewi.
Lisa akashusha pumzi ndefu. “Siku zote
nimekuwa nikijisikia kuwa duni kwa
sababu tulisaini mkataba na ulinisaidia
katika kesi hiyo. Mimi ni kama mpenzi
wako na mtumishi wako, na daima ni
lazima niwe mnyenyekevu mbele yako.
Siwezi kukukosoa pia. Hali hii inanifanya nijihisi kama mtumishi wako tu. Nachukia hilo. Ikiwa tutaondoa hayo mashariti, ninatumaini kwamba
tunaweza kuwa kama wanandoa wa kawaida.”
“Tangu lini nikakuchukulia kama mtumishi? Si ni wewe nduye umekuwa ukiniudhi mara nyingi zaidi?” Alvin alimkazia macho. Hakuweza kuelewa mawazo ya mwanamke huyo. “Unataka kunipa pesa ili usinipikie tena, sivyo?”
Lisa alikosa la kusema kabisa. “Hebu ngoja nuikueleweshe tena. Natumia hii milioni 500 kuvunja makubaliano ya awali ya mkataba wa ndoa. Nataka
kuwa mpenzi wako rasmi. Nikitaka
kupika, nitapika, na ikiwa sitaki kupika, sipiki. Nitakasirika ikiwa ninataka
kukasirika, na nitapigana na wewe ikiwa
ninataka kupigana. Nitafanya kila kitu kwa uhuru.”
Kifua cha Alvin kilitanuka kwa hasira.
Alitaka kuitupa ile kadi moja kwa moja kwenye moto ili iwake. Lisa aliruka
ghafla na kumbusu kwenye midomo. Akikumbatia shingo yake na kusema kwa umakini, “Alvilisa, sijui kama umewahi kuwa na mpenzi hapo awali, lakini hivi ndivyo wapenzi wa kawaida wanavyokuwa. Utakuwa pipa langu la takataka na sufuria yangu ya asali. Ninakupenda, kwa hiyo nataka kukupenda kwa usawa.”
Mdomo wa mwanamke ghafla ulikuwa
mtamu kama asali. Hasira za Alvin zilikatika ghafla. Akimtazama usoni, alisita kabla ya kusema, “Makubaliano yanaweza kusambaratika, lakini usinipe pesa. Wewe ni mwanamke wangu.
Ikiwa nitakushtaki kwa kesi hiyo, nawezaje kujiita mwanaume?"
“Lakini…”
"Nyamaza. Sema neno moja zaidi nami nitakufundisha somo.” Alvin akaendelea
kumnyonya mdomo. Uso wa Lisa ukawa
mwekundu mara moja huku akikanyakanyaga miguu yake.
“Mhhhhh…Wewe mpuudhiii.”
“Vipi mimi ni mpuuzi? Wewe ndiye
unayetaka tuwe kama wanandoa wa kawaida. Wanandoa wa kawaida wako hivi." Alvin alitabasamu vibaya. Lisa alipigwa na butwaa na kumkodolea macho ghafla. “Unaonekana una ujuzi sana. Lazima uwe mzoefu sana. Nina
hakika ulishawahi kuwa na wapenzi wengi sana kabla yangu.”
Uso mzuri wa Alvin ukakakamaa, na macho yake yakageukia pembeni.
"Usifikirie ujinga. Nimekuwa na mpenzi mmoja tu." Alvin hakutarajia angekuwa na wivu kiasi hicho na alikuwa hana la kusema.
“Bado una hisia naye? Uso wako unapomtaja unachangamka.” Lisa alizungumza. Hali yake ya furaha ilipotea mara moja.
“Amekufa.” Alvin alikunja uso kwa huzuni.
Lisa aliganda, ghafla asijue la kusema.
"Samahani."
“Acha kufukua makaburi. Hukuwa pia na Ethan Lowe hapo awali?” Alvin alikumbusha kwa huzuni.
Lisa hakuweza kusema chochote na akawasha jiko tena kwa utiifu. Alvin
akairudisha kadi mfukoni mwake na kutoka nje. Ni baada ya kutoweka tu ndipo Lisa alikumbuka kuwa alimwomba akate nyama lakini hakufanya. Mjinga!
Mlegevu!
Baada ya chakula cha jioni, Lisa
alimsumbua sana Alvin kuhusu kuvunja mkataba wao. Alvin hakuweza
kumshinda Lisa kwa king’ang’anizi ikabidi tu kuuondoa.
"Unaweza kuvunja mkataba, lakini bado
huwezi kuwasiliana na mtu yeyote
kutoka jinsia tofauti kama Kelvin Mushi
au Ethan Lowe. Lazima uje nyumbani
kwa wakati pia. Huruhusiwi kuchelewa
kutoka nje,” Alvin alikumbusha kwa
utulivu, “Pia, huruhusiwi kuniacha.”
"Ndio, ndio, ninajua tayari. Wewe ni mzuri sana, naanzaje kukuacha? Kuna msingi imara wa upendo kati yetu sasa.”
Maneno ya Lisa yalijaa mahaba. Lisa alichukua hatua ya kuketi kwenye
mapaja yake na kumbusu. Hali ya Alvin ilikuwa taabani, na akatoa mkataba bila shuruti.
Lisa alichoma makubaliano hayo, na lile
jiwe kubwa lililokuwa likimwelemea
moyoni likaonekana kumshuka. Usiku
mzima, alilala akiwa mwepesi sana.
Alvin pia alihisi kuwa sasa yuko
mchangamfu zaidi. Alipomwona hivyo, ghafla alihisi furaha hata yeye bila kujali
kuwa makubaliano yao yalikuwa yamechomwa.
Sura ya 113
Siku mbili zilizofuata ambazo Lisa
alienda ofisini kwake, hakuna kiongozi
yeyote aliyekuja kumuona. Hakuna
aliyeripoti chochote kuhusu kampuni hiyo kwake pia. Mambo mengi
aliyojifunza yalitoka kinywani mwa
Tunu. Hakuna mtu katika kampuni
aliyeonekana kumchukulia kwa uzito kama mwenyekiti.
Saa sita mchana, alienda kwenye
mgahawa kwa chakula cha mchana, lakini hata baada ya kungoja kwa dakika
20 kwenye chumba cha chakula, hakuna mtu aliyetoa chakula hicho.
Tunu alienda kuongea na mhudumu wa
mgahawa na kurudi akiwa mtupu baada ya dakika tano hivi huku akihema kwa hasira. “Wako pia hapa. Chakula
ulichoagiza kimeishia kwenye chumba
cha Jones na Meneja Mkuu Changala.
“Wapo chumba jirani?” Lisa alikodoa macho.
“Ndiyo,” Tunu alisema kwa hasira, “watu
katika mgahawa wote wanawahudumia wao tu.”
Hali ya Lisa ilikuwa ngumu. Hakutarajia
kwamba Jones alikuwa ameshinda hata
wafanyakazi wa mgahawa. “Achana
nao, sitakula hapa tena. Rudi ofisini na uagize usafiri.”
Lisa alisimama na kutoka nje. Kisha
akamuona Lina akiwa amesimama
kando ya mlango huku akionyesha
dhihaka. "Mwenyekiti Lisa, inaonekana
kwamba kuwa mwenyekiti sio jambo la kufurahisha. Ulikuja kwenye mgahawa
kula lakini hakuna hata mtu mmoja hapa
wa kukuhudumia, kwa hivyo lazima
uagize take-out. Maskini wewe."
Lisa alimwangalia Shani. Bila kusema
neno, Shani alinyanyuka na kumpiga
Lina usoni, na kusababisha shavu lake
kuvimba mara moja. Shani kisha
akampiga kofi lingine upande wa pili wa
uso wake, na kumfanya Lina ashindwe
kusema lolote kutokana na maumivu
hayo. Alimkazia macho Lisa lakini
hakuthubutu kupiga hatua tena.
Lisa alitabasamu. "Naweza hata
kumpiga baba yako Jones, sembuse wewe? Usipotazama maneno yako
wakati ujao, nitakupiga hadi ujifunze somo lako.” Kisha, akamsukuma Lina
pembeni na kuondoka huku akitabasamu. Lina alishika mashavu yake, chuki ikimchoma machoni. 'Lisa, ngoja tu uone. Nitakuua wewe mimi binafsi siku moja.' Lina aliishia kujiapiza mwenyewe kimoyomoyo.
Saa tisa alasiri Kwenye ghorofa ya 17 ya jengo hilo, mkutano ulikuwa ukiendelea bila uwepo wa Lisa. Meneja mkuu, Lazaro Changala, alikaa kwenye kichwa cha meza, akifuatiwa na wasimamizi wakuu wa Mawenzi Investiments.
Naibu Meneja Ngololo alisema, "Meneja
Mkuu Changala, Mwenyekiti Lisa
alichukua nafasi hiyo. Ni sawa kama
tusipomwita kwa ajili ya mkutano wa kwanza wa mwanzo wa juma?”
"Unafikiri yeye ni nani?" Lazaro
Changala alisema kwa dharau, “Yeye ni msichana mdogo tu asiyejua lolote.
Sawa, tuanze mkutano. Meneja Lina Jones, je, kampuni ya mapambo ya mradi wa ukuzaji mali imekamilika?”
Lina alivaa barakoa kufunika uso wake
huku akivumilia maumivu usoni mwake. "Bado. Bei zinazotolewa na kampuni za ujenzi ni kubwa mno. Ninafikiri kwamba tunaweza kuiomba timu yetu ya ujenzi ili
kushughulikia sisi wenyewe. Hivi majuzi niliandaa muundo na kila mtu aanaweza kuona sasa."
Kisha alitoa rundo nene la makaratasi yenye michoro ya miundo juu.
Watendaji wote walimjaza sifa. "Miundo hii ni ya kibunifu sana. Ni ya hali ya juu na imechorwa kisomi, lakini sio ya anasa kupita kiasi. Ina mchanganyiko wa ladha nzuri sana."
“Umezibuni wewe mwenyewe, Meneja Jones? Unashangaza.” Lazaro
Changala hakuamini. "Ni bora zaidi
kuliko jumba lililojengwa katika mradi wa maendeleo uliopita."
Lina alijifanya kuwa mwenye kujua na kusema, “Karatasi ya makadiro ya gharama pia iko ndani. Nilifanya makadirio na ni gharama nafuu zaidi kuliko tukiajiri kampuni ya ujenzi kutoka nje.”
Lazaro alijawa na sifa. “Meneja Jones, umefanya kazi nzuri. Miundo hii lazima iwe imechukua muda wako na juhudi nyingi."
"Sijalala kwa siku kadhaa, lakini nina furaha sana kuchangia kampuni." Lina alijisifia.
Kabla Lina hajamaliza, mlango wa chumba cha mkutano ulisukumwa. Lisa aliingia kutoka nje akiwa na watu wengine. "Kila mtu yuko kwenye mkutano? Mbona hakuna hata aliyenipa habari kuhusu tukio kubwa kama hili?”
Lisa alifoka mbele ya meneja mkuu
Lazaro Changala..
Lazaro hakubabaika. Uso wake ulikuwa
unatabasamu kama kawaida, lakini macho yake yalikuwa ya dharau.
“Mwenyekiti Jones, wewe ni mdogo sana kuliko mimi. Hata nikikwambia kuna vitu unaweza usivielewi kwa hiyo sikukupigia simu.” Baada ya kuongea, chumba cha mkutano kilikuwa kimya sana.
Kila mtu alingoja kutazama mchezo wa kuigiza ukiendelea wakati Lisa angekasirika, lakini uso wake mzuri ulionyesha tabasamu tulivu. “Meneja
Mkuu Changala, nimesimama hapa kwa muda mrefu sasa. Kwa hiyo utaendelea na tabia hii hadi lini? Umeshindwa kujua ni nani anayesimamia kampuni baada ya kukaa kwa muda mrefu sana?”
Alikuwa akicheka waziwazi, lakini hasira
machoni mwake iling'aa sana. Mara
moja Lazaro aliona aibu.
Lisa aliwageukia Shani na Tunu.
"Inaonekana kama Meneja Mkuu
Changala amejisahau kidogo. Tafadhali
mkumbusheni maana ya heshima ni nini.” Kabla Lazaro hajajibu, aliburutwa chini na Shani kwa mkono mmoja.
Alikasirika wakati akiburutwa akatoka akifoka kwa hasira.
“Hebu tuendelee na mkutano. Mlikuwa mnazungumza nini?” Lisa alimkatisha na kutazama umati wa wafanyakazi.
"Tulikuwa tunazungumza juu ya muundo wa mradi wa maendeleo. Meneja Jones alikuja na miundo fulani. Meneja Mkuu Changala na sisi wengine tunahisi kuwa muundo uko vizuri sana.”
Naibu Meneja Ngololo alikabidhi miundo kwa shida.
Moyo wa Lina ulidunda. Hakuwahi
kufikiria kuwa Lisa angetokea. Lisa bila shaka angetambua miundo hiyo. Hata
hivyo, haikujalisha. Hata kama Lisa
angelisema kwamba Lina aliiba michoro yake, hakuna mtu angemwamini.
Badala yake, ingechochea tu wafanyakazi kumdhihaki. Lisa alichukua
miundo na kisha akamnong'oneza
Shani maneno machache. Baada ya Shani kutikisa kichwa na kutoka nje, Lisa aliendelea, "Miundo ni nzuri. Inaonekana ilichapishwa saa moja asubuhi ya leo. Meneja Jones, lazima umekesha hadi usiku sana
ukitengeneza miundo hii.”
"Ndio, Meneja Jones alisema hakuwa amelala kwa siku kadhaa." Mtu mmoja alidakia.
"Meneja Jones anafanya kazi kwa bidii sana." Mwingine akaongezea sifa juu yake.
Chumba cha mkutano kilisikika kwa
pongezi. Lina alijivunia sana. Alikuwa amechelewa kuzichapisha kwa makusudi.
"Mwenyekiti Jones, una maoni gani kuhusu miundo yangu?" Lina alijibaraguza kuuliza.
"Miundo ni mizuri sana. Lakini unafahamu kwamba nilipoteza rasimu ya muundo sawa na hii nusu mwezi
uliopita.” Lisa aligeuza maneno yake ghafla.
Kila mtu alipigwa na butwaa, lakini Lina
hakuwa na wasiwasi. Badala yake, alijifanya kupepesuka na kuziba mdomo wake. “Hauna maana ya kumaanisha kwamba nilikunakili, sivyo?”
"Mwenyekiti Jones, una wivu na talanta ya Meneja Jones?" Lazaro Changala
alicheka kwa uchungu. “Kila mtu anajua kwamba nyinyi ndugu wawili
hamwelewani, lakini hakuna haja ya kuhusisha kampuni katika marumbano yenu.”
Kwa muda, kila mtu alimtazama Lisa
kwa dharau. Alikuwa mdogo sana kuwa mwenyekiti.
“Nilijua nyinyi hamtaniamini.” Lisa
akashusha pumzi. “Kwa bahati nzuri, tayari nilitoa taarifa polisi siku kumi
zilizopita. Data yangu ya asili ya
muundo wakati huo imekabidhiwa kwa
polisi pia. Wana rekodi ya kesi hiyo, kwa
hivyo itakuwa wazi tutakapoiangalia."
Lina aliingiwa na hofu na haraka
akajifanya analia. "Mimi ni meneja tu Mwenyekiti Jones, kwanini unifanyie hivi? Nilimaliza miundo muda mrefu
uliopita na niliichapisha kwa
kuchelewa.” Mwonekano wake mpole uliwafanya watendaji wengi wafikirie kuwa Lisa alikuwa akimlenga kimakusudi.
Lisa akatoa michoro na kuuliza, “Unasema kwamba ninakusingizia? Sawa. Kwa kuwa michoro hii iliundwa na wewe, unapaswa kujua aina na mwelekeo wa nyumba. Je, ina sakafu ngapi? Vitalu vingapi? Ni kubwa kiasi gani?" Lina alipigwa na butwaa na akajibu tu baada ya muda mrefu, "Kuna
vitalu sita, na vinakaa kusini huku
vinatazama kaskazini ..."
Sura ya 114
Mara tu baada ya kumaliza
kuzungumza, watendaji wachache
waliokuwa wakijadili muundo huo
walikunja uso.
Lisa kisha akauliza, “Kwa nini unahitaji
kabati kubwa katikati hapa?”
"Kwa ajili ya nafasi kubwa ya kuhifadhia." Lina alijibu bila kujiamini.
Lisa alifoka. “Ni kwa sababu kuna nguzo
kubwa katikati ambayo haiwezi kung’olewa, nikachagua kuweka kabati
kubwa hapo.” Lina akabaki ameduwaa, hana cha kumkosoa Lisa. “Na kwa
kuongezea, ni jumba lenye ghorofa mbili na ukubwa wa mita za mraba 128.7.
Iinakaa mashariki, likitazama magharibi.” Uso wa Lina ulipauka mara
moja kwa aibu.
Lisa alikodoa macho. "Unadai kuwa
ulitengeneza hizi, lakini hujui chochote
kuhusu maelezo yake ya kitaalamu, ungewezaje kuwashauri mafundi?
Wewe ndiwe msimamizi wa mradi, ilhali
hujui lolote kuhusu aina ya nyumba na ni majengo mangapi yanajengwa katika
mradi huo, unafaa kweli wewe?”
Lina hakuweza kukanusha neno lolote
kwa sababu hakuwa anaelewa chochote kuhusu michoro hiyo. Kundi la wafanyakazi waliokuwa kwenye
mkutano huo lilitingisha vichwa vyao
mmoja baada ya mwingine, wote wakiwa wamekata tamaa sana.
Wakati huo huo, Shani aliingia na maafisa wachache wa polisi. Mmoja
wao alimfunga pingu mikononi Lina. “Bi. Jones, tulipokea ripoti kwamba umeiba
kazi ya mtu mwingine. Tafadhali fuatana nasi hadi kituoni kwa ajili ya uchunguzi.”
“Hapana, sitaki! Sikufanya hivyo!” Lina alipiga kelele kwa hofu.
“Acha kupiga kerere weye, hiri ni jeshi ra porisi, tii sheria bira shuruti.” Polisi
mmoja mwenye sura mbaya zaidi
alimuadabisha Lina. Polisi hao wawili
walimnyanyua na kumtoa nje bila subira.
“Ninafanyiwa njama tu! Mimi sikuiba. sikufanya hivyo!” Lina alilalamika bila msaada.
Mayowe yake yalipofifia, Lisa alitazama
kwenye chumba cha mikutano kabla ya kumgeukia Lazaro Changala. “Meneja
Mkuu Changala, nilisikia kuwa wewe
ndiye uliyemteua Lina Jones kuwa
meneja wa mradi huu. Nina shaka na maono yako na uwezo wako wa kuongoza kampuni."
Lazaro Changala akaingiwa na hamaki
na kujibu kijeuri. “Kama Mwenyekiti
Jones unatilia shaka uwezo wangu basi niondoe kama unaweza.”
Alimwangalia moja kwa moja Lisa
alipomaliza kuongea. Hakuamini kama
Lisa alikuwa na ujasiri wa kumwondoa
kwenye nafasi yake. Bodi ya wakurugenzi wa Kampuni
wasingemwacha salama.
“Inawezaje kuwa hivyo? Meneja Mkuu
Changala ameongoza utendaji wa kampuni kwa mafanikio mengi. Kwa
kawaida, nakuamini.” Lisa alitabasamu
ghafla na kubadilisha mawazo yake.
"Mkutano huu nitakuachia ili uendelee
nao." Kisha akamaliza kuongea na kuondoka zake. Lazaro Changala alimtazama nyuma kwa dharau.
Alifamini kwamba asingemfanya lolote kwa sababu alikuwa na uzoefu zaidi
kuliko yeye.
Hata hivyo, baada tu ya Lisa kuondoka tu, kuna kituko kilitokea ghafla. Mke wa
Lazaro Changala aliingia ndani ghafla
na kumpiga kofi usoni. "Lazaro Changala, wewe mwanaharamu!
Unathubutuje kuwa na mchepuko nje?
“Kama nisingekuoa enzi hizo, leo hii
ungeweza kuingia Mawenzi Investiments ukiwa na jeuri hivi?”
Changala alichukia kupitiliza.
“Kwa hiyo unanifanyia makusudi siyo?
Umenitumia miaka yoote hiyo hadi
umenizeesha ndiyo unaamua kurudi
kwa mabinti? Nitapambana nawe.”
Mama yule wa makamo aliwaka kwa hasira.
Habari za ghasia kwenye chumba cha
mkutano zilienea haraka katika kampuni
nzima. Tunu alicheka wakati wa kuripoti
habari hiyo kwa Lisa. “Hukuona jinsi uso wa Meneja Mkuu Changala ulivyokuwa
karibu kupasuka alipopigwa kofi. Alifedheheka kabisa. Hata aliamua
kumpiga vibaya mke wake hadharani.”
'Huu ni mwanzo tu." Lisa alitabasamu
na kumpigia simu Sam. “Sam, huna namba yoyote ya mwandishi wa habari?
Kuna mambo ya kuruhashisha hapa nataka yaripotiwe kwa jamii.”
“Haha, hakuna shida, nitakutafutia.”
Sam alijibu kwa furaha. “Ni mara
chache sana shemeji yangu huwa anaomba msaada wangu…lakini ni jambo gani hilo?”
Lisa akaeleza kituko kilichomtokea
Meneja Lazaro Changala.
Kabla Sam hajaendelea kusema, ghafla
alihisi kushtuka. Akatazama upande
wake alipokuwa amekaa Alvin huku uso
wake ukiwa unapunguza furaha
taratibu. Alijiuliza kimykimya. “Lisa, kwa
nini haombi msaada wa Alvin? Kwani
Alvin hawezi kushughulikia mambo
kama haya? Au kwa sababu Meneja
Changala ni mkorofi na mtu hatari
anahofia atamsababishia Alvin matatizo?”
Lakini Alvin asingeshindwa
kushughulikia hilo. Familia ya Kimaro
ilimiliki kampuni yenye nguvu zaidi ya
vyombo vya habari nchini, lakini Lisa
hakuwa amepata nafasi ya kufahamu
hilo kwa hiyo ikabaki kuwa ni siri ya
Alvin hadi muda huo.
Sam alikosa la kusema. “Lisa, unaenda mbali sana. Huogopi kwamba Meneja
Mkuu Changala ataniletea shida?”
"Atakuletea shida gani? Wewe ni kijana wa familia tajiri ya Harrison, atathubutuje kukugusa?” Lisa alicheka.
“Ukinisaidia, Mawenzi Investiments
itashirikiana nawe katika siku zijazo.
Ninahakikisha kwamba familia ya
Harrison inashirikiana na Mawenzi
katika miradi ambayo familia yenu
inashughulikanayo. Familia ya Jones
haitakuwa na nafasi.”
“Oh jamani, shemeji hakika unajua
kunipanga.” Sam akakosa ujanja.
“Usiseme hivyo. Wewe ni rafiki wa Alvin, kwa hiyo sisi sote ni familia.”
Sam karibu aanguke kwa kicheko.
“Sawa, uko sawa.”
Baada ya kukata simu, Sam alifurahi sana. "Lisa ni mcheshi sana. Kila kitu anachosema ni sehemu ya mkakati.
Nilikuwa na wasiwasi asingeiweza nafasi yake kama mwenyekiti.
Inaonekana kwamba yuko thabiti kuliko nilivyokuwa namfikiria.”
“Unajua unazungumzia mwanamke wa nani?” Alvin alitabasamu kwa kiburi, lakini ghafla alifikiria kitu na kumtazama
Sam kwa uso kuchukia.
Sam alijibu akiwa na uso uliotulia. “Una
wivu kwa sababu Lisa amenipigia simu
kuniomba msaada? Lisa ni mjanja sana, anataka kukulinda. Ana wasiwasi
kwamba utaumizwa na Lazaro
Changala. Nakuonea wivu sana kwa
kuwa na mwanamke kama huyu."
Alvin akatabasamu. Alichokisema Sam kilionekana kumwingia akilini. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mwanamke
kujaribu kumlinda. Moyo wake ulijawa na hisia za furaha sana. “Uko sahihi.
Alisema atanitunza.”
Tabasamu tata lilichanua kwenye uso wake mzuri, na kusababisha uso wa Sam kuwa na matuta kila mahali. “Alvin, huna aibu sana. Tayari wewe ni tajiri
sana lakini una ujasiri wa kuruhusu
mwanamke akutunze?”
Macho ya Alvin yalimtoka kwa furaha.
Aliukumbuka usumbufu wote ambao
Lisa alimsababishia hapo awali, sasa
ulikuwa umefika muda wa kula
matunda.
Sura ya 115 Siku iliyofuata, habari za mambo ya
meneja mkuu wa Mawenzi Investiments
kupigwa na mkewe ofisini zilienea
mtandao mzima. Lazaro Changala alikasirika. Sifa yake iliharibiwa kabisa.
Picha zake akipigwa na mke wake
hadharani zilienea kila mahali, na hata
video yake iliyomwonyesha akiwa na mchepuko wake ilisambaa.
Katika ofisi ya mwenyekiti, Meneja
Mkuu Changala aliingia kwa hasira na kumwelekeza Lisa kidole cha usoni.
“Umefanya nini? Kwanini umesambaza picha zangu mtandaoni, zinakuhusu nini?”
“Sijui unazungumza nini Bwana Changala.” Lisa alikaa tuli kwenye kiti
chake huku akionyesha uso wa kujiamini. "Meneja Mkuu Changala, sikuwahi kutarajia ungekuwa mtu kama
huyo. Umetukatisha tamaa sana.
Umeharibu hata sifa ya kampuni.”
“Unawezaje kuthubutu kusema hivyo, wewe b*tch?! Usifikirie kuwa sijui
kwamba wewe ndiye upo nyuma ya hili.
Unafikiri unaweza kunichezea mimi?"
Lazaro Changala alimwendea Lisa na
alikuwa karibu kuinua mguu wake ili kumpiga teke, lakini Shani alimkimbilia na kumsukuma kwenye ukuta.
"Wewe b*tch, niachie!" Lazaro
Changala alipiga kelele bila kujizuia.
Lisa alipiga intercom kuita usalama.
“Fanya haraka umtoe. Nadhani hali ya
Meneja Mkuu Changala si nzuri kwa
sasa, kwa hivyo nitamkabidhi Naibu
Meneja Ngololo masuala ya kampuni.”
"Lisa Jones, we subiri tu! Unathubutuje
kunifanyia mambo kama haya?
Endelea, siku yako yaja!" Baada ya
Lazaro Changala kuvutwa nje, Naibu
Meneja Ngololo aliingia kwa haraka.
Akiwa amekabiliana na sura nzuri ya
Lisa tena, ghafla alihisi hofu moyoni
mwake. Watendaji wa kampuni hiyo
hawakumchukulia Lisa kwa uzito hapo
awali, lakini ilikuwa ni siku moja tu na
sifa ya Meneja Mkuu Changala
iliharibiwa kabisa. Kila mtu sasa alitia
adabu kwa Lisa. Hakuna aliyekuwa na
ushahidi wowote, lakini wote walikuwa
na uhakika kwamba Lisa alikuwa na mchango mkubwa katika hilo.
"Naibu Meneja Ngololo, wewe ni mtu mwenye uwezo na uzoefu, lakini daima
ulikuwa unakandamizwa na Meneja
Mkuu Changala kwa makusudi. Lazima
ulijisikia vibaya, sivyo?" Lisa mwenyewe aliinuka na kummiminia kikombe cha kahawa.
Naibu Meneja Ngololo alishtuka na
akapokea kahawa haraka, kisha akasema, “lakini Meneja Mkuu
Changala amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Watu wengi katika
kampuni wanatii maagizo yake, na wakurugenzi wengi wanampenda pia.”
Lisa akaenda moja kwa moja kwenye
maamuzi yake kwa uhakika. “Nitakupa muda wa wiki moja. Amua ikiwa
unataka kupaa angani au ubaki chini ya
Lazaro Changala kama nyumbu wake
maisha yako yote." Moyo wa Naibu
Meneja Ngololo ulitetemeka sana.
Wakati huo huo, Tunu alikimbia kutoka
nje. “Mwenyekiti, Meneja Mkuu
Changala alipigwa na kundi la wanawake wakati alipotoka nje ya geti la kampuni. Ni wanawake kutoka umoja wa wanawake wanoteswa na waume zao majumbani, wanaochukia watu
wote wanaosaliti wake zao. Walimpiga nusura kumvunja mguu na kichwa
kilikuwa kikivuja damu. Anapelekwa hospitali sasa hivi.”
Naibu Meneja Ngololo ghafla alitazama
juu na kuona uso wa Lisa usio na hisia.
Miguu yake ilitetemeka kwa hofu.
“Nitafanya hivyo. Namfahamu Lazaro
Changala vizuri sana. Ninaweza
kuchukua udhibiti wa kampuni katika
wiki moja. Nitakufanyia kazi Bibi
Mwenyekiti,” alisema kwa sauti.
“Vizuri sana, nakuamini. Fanya hivyo ili
Changala asiwe tena na nafasi katika
kampuni hii.” Lisa aliongea kwa umakini na mamlaka. Pembeni, Shani
alimtazama na kugundua kuwa tabia ya
Lisa ilizidi kufanana na Alvin wakati
anafanya kazi. Baada ya Naibu Meneja Ngololo
kuondoka, Lisa alijilaza kwenye sofa kwa uchovu na kusema kwa sauti yenye
hatia, “Mimi ndiye niliyemtengenezea njama hizi Lazaro Changala. Shani, unafikiri mimi ni mbaya?"
"Hapana," Shani alijibu kwa urahisi, "Kama hutakuwa mkatili, utawaongozaje mbwa-mwitu hao chini?"
"Ndio, nahitaji kuwa na udhibiti kamili
juu ya Mawenzi Investiments. Lazima
nilipize kisasi kwa bibi yangu." Lisa alikunja ngumi. Ilibidi alipize kisasi cha mama yake pia. Mzigo uliokuwa juu
yake ulikuwa mzito sana kwa yeye kuwa na huruma tena.
Katika wiki moja tu, Naibu Meneja
Ngololo alipanga upya kila kitu katika
kampuni ya Mawenzi Investiments
haraka. Aliwafukuza wafanyakazi wote
ambao walikuwa kinyume na Lisa
kutoka kwenye uongozi wa juu.
Kuhusu Lina naye alifukuzwa kazi bila
huruma. Lina hakujua juu ya suala
kubwa lililokuwa linaloendelea huko nje.
Alipokuwa kizuizini, wafungwa
walimpiga na kumwagilia maji baridi kila
siku. Kwa sababu ya hii, ngozi yake
iliharibiwa kabisa. Baada ya Lina
kuteseka kwa siku saba hadi nane, Jones alijitahidi kumwokoa kutoka
katika kituo hicho baada ya kutumia
kiasi kikubwa cha pesa. Alitoka akiwa
amebebwa.
Alipoona uso wake umevimba, Mama
Masawe alimkumbatia na kulia kwa uchungu.
“Mpenzi wangu, umepatwa na nini?
Nani alikupiga? Sitamwacha mtu huyo
abaki salama.”
“Baba, mama, lazima mlipize kisasi kwa
niaba yangu. Inauma sana… Ooohoohooo!” Lina alilia sana. Uso wa Lina
ulimuuma sana hata akashindwa kuinua macho.
Uso wa Lina uliokuwa umevimba
ulimjaa Stephen kwa karaha.
Mwanamke huyu alizidi kuwa mbali na mawazo yake. “Usijali, msichana mzuri.
Baba yako hakika atawarudia watu hao
kwa kukuumiza.” Stephen Kileo alisema
mdomoni lakini moyoni alikuwa
amekerekea sana.
Jones alipandwa na hasira. Alipogeuka, aliona kwamba Stephen alikuwa ametulia tuli. Alimwamia kwa hasira,
“Stephen, fanya haraka umchukue Lina. Anahitaji kupelekwa hospitali sasa hivi.”
“Sawa, sawa.” Stephen alitenda kulingana na maagizo ya Jones bila
kupenda. Tangu Lina aingizwe kwenye
kituo cha polisi, hakuwahi kuoga. Harufu
mbaya iliyotoka kwake ilikaribia
kumfanya ashindwe kuvumilia. Wakati
huo, alijuta sana. Ikiwa angejua
mapema kwamba hii ingetokea, wala
asingejihusisha na Lina kabisa.
Katika hospitali, akiwa na macho
mekundu, Lina alimwamuru daktari, “Nipe dawa bora zaidi. Nahitaji kupona
ndani ya siku tatu zijazo nirudi ofisini.”
"Samahani, hatuna dawa kama hiyo."
Daktari alimshangaa.
“Mnafanya nini hapa kama hamna
dawa? Kundi la watu wasio na maana.
Mama, nataka kuhamishwa hospitali
nyingine. Nataka kupona haraka iwezekanavyo na nirudi ofisini
kushughulika na Lisa.” Akiwa na uso uliovimba, Lina alionekana kuwa mbaya
zaidi alipokasirika.
Akivumilia chuki yake kwa Lina, Stephen alisema kwa unyonge, “Huwezi kurudi ofisini tena. Umefukuzwa kazi.”
"Nini?" Lina alitoa macho akiwa haamini
kabisa. “Lisa amerukwa na akili?
Anathubutuje kunifukuza kazi?! Meneja
Mkuu Changala alitoa idhini yake kwa hili?"
Jones Masawe alikunja uso na kujibu
kwa kuudhika, “Lazaro Changala ni
majeruhi na sasa yuko katika wodi
maalumu ndani ya hospitali hiihii.
Hawezi kuruhusiwa katika siku kumi
zijazo au hata nusu ya mwezi. Hivi sasa, Freddie Ngololo ndiye
anayesimamia kampuni nzima. Lisa alimpandisha cheo na kuwa meneja mkuu.”
Lina alipigwa na butwaa kujua jinsi
mambo yalikuwa yamebadilika sana
alipokuwa kizuizini kwa siku chache tu.
“Hili haliwezekani, ni yeye ndiye
aliyepanga njama za kumpiga Meneja
Mkuu Changala? Umepiga simu polisi?"
"Hapana." Akiwa amechoka kabisa
kimawazo, Jones aliongeza, “Iilikuwa ni kundi la wanawake wanaoteswa na
waume zao ndio ambao walimpiga
Lazaro Changala. Nilisikia kwamba ni
kwa sababu walikasirika kujua kwamba
Lazaro Changala alimsaliti mkewe.
Lazaro Changala sasa yuko kwenye
kina kirefu, na wafanyakazi wengine
walio kwenye usimamizi mkuu wa
kampuni tuliowahonga wote wanaogopa
sasa kumuudhi Lisa. ”
Lina alipatwa na wazimu. "Hujafanya lolote?"
"Lisa amebadilika kabisa. Tulitumia
miaka mingi kumlea na haya ndiyo anayotulipa sasa.” Mama Masawe
alisema kwa chuki, “Jones, lazima ulipize kisasi kwa niaba ya Lina na upate mamlaka tena kwenye kampuni ya Mawenzi Investiments.”
Katika siku chache ambapo Jones
Masawe alikuwa kama mwenyehisa
mkuu wa Mawenzi, Mama Masawe alifurahia kupendelewa na wanawake wengi matajiri. Hakutaka fahari hiyo ipotee na kurudi katika siku zile za dhiki baada ya kufirisika.
Sura ya 116
“Ni rahisi sana kupata tena mamlaka," Stephen Kileo alisema ghafla.
Wakishangazwa na maoni hayo, Jones
na familia yake walimtazama kwa makini. “Stephen, tuambie haraka wazo
lako. Sisi ni familia,” Lina akasema mara moja, “Mara tu Lisa atakapoanguka madarakani, tutaoana mara moja.”
Stephen alikodoa macho na kusema; "Willie Kimaro kutoka familia ya Kimaro
anakuja Dar kwa ukaguzi wa miradi
waliyowekeza hapa jijini. Kma tutaweza kumfurahisha, tunaweza kumtumia kuwamngusha Lisa.”
Macho yao yote yakang'aa. Willie
Kimaro alitoka familia tajiri ya Kimaro. Yeye na Alvin Kimaro walikuwa watoto wa kaka na dada, yaani mtu na binamu yake. KIM International, ni kampuni ya familia ya Kimaro na ilikuwa ikimiliki
asilimia 25 za hisa za Mawenzi
Investments. Kwa maana hiyo ilikuwa na nguvu kubwa kwenye bodi ya wakurugenzi. Kama kweli KIM
International ingeungana na Jones
Masawe kumwangusha Lisa, basi
angeondolewa kwenye nafasi yake ya
Mwenyekiti na mtendaji mkuu wa Kampuni ya Mawenzi.
Mgawanyo wa hisa katika Kampuni ya Mawenzi ulikuwa ni 30% kwa Lisa, 30% kwa Jones Masawe na 25% kwa KIM
International, 10% Chris Maganga na 5% zilizobaki zilimikiwa na wanahisa wengine wadogowadogo. Kwa hiyo
wanahisa wakubwa walikuwa wanne, Lisa, Jones Masawe, KIM Internatonal na Chris Maganga. kama wawili kati yao
wangeungana basi ilikuwa rahisi
kumwangusha mwingine, ndiyo njia
aliyotaka kutumia Jones Masawe, kutafuta njia ya kuungana na KIM
International kumwangusha Lisa. Jones alitetemeka kwa fadhaa. "Familia
ya Kimaro ndiyo inamiliki KIM
International. Ingawa Willie si mzao wa moja kwa moja wa familia ya Kimaro, tutaweza kumtumia kuunganisha nguvu
yetu mradi tu tufahamiane na familia ya
Kimaro. Ikitokea hivyo, hatutasumbuliwa na Lisa tena.”
"Ni wazo zuri sana." Stephen aliitikia
kwa kichwa. “Sifahamiani na Willie lakini najuana na msaidizi wake. Kwa kuwa
msaidizi wa Willie nipo naye vizuri, nitajitahidi anisaidie kuwa karibu naye
na kuwatambulisha nyinyi kwake. Ili kumteka kwa urahisi mnatakiwa
kuandaa zawadi ya kumfurahisha. Willie anavutiwa na vito vya thamani, na pia wanawake warembo!"
“Asante Stephen. Ninajuta kutokutana na wewe mapema. Wewe ndiye ninayeweza kukutegemea kwa sasa.”
Lina alimtazama kwa hisia za kuguswa.
"Ni jukumu langu kukusaidia. "Stephen alijaribu kuficha chukizo lake kwake.
••••
Ndani ya Mawenzi Investiments, saa
kumi na mbili za jioni, Lisa alipozima taa
na kutoka nje ya ofisi, mjukuu wa
mmoja wa kwakurugenzi wa bodi ya
Mawenzi, Amiri Gumbo alikuwa nje
akimsubiria na alipomuona alimsalimia
kwa shauku.
“Lisa, unatoka kazini. Ningependa
kukukaribisha kwa chakula cha jioni
kwenye hoteli maarufu ambayo hutoa
chakula kizuri…”
Lisa alikuwa mwisho wa akili yake.
Tangu alipoanza kupata tena mamlaka
katika kampuni, wakurugenzi wa bodi
wote walijaribu kujipendekeza kwake
kwa kuwatambulisha watoto wao na
wajukuu zao kama washirika wake watarajiwa.
"Nashukuru, lakini nilipanga kula
chakula cha jioni nyumbani ... " Lisa
alimtosa kwa upole.
“Ngoja basi nikupeleke nyumbani.”
Kijana yule aliongea kwa shauku.
“Mkoba wako unaonekana kuwa mzito.
Acha nikusaidie kuubeba.”
Kabla hajaugusa, Shani alishika mkono
wake. Macho ya mwanamke huyo
yalimtoka kwa ukali, jambo lililomfanya
kijana yule ashtuke. Alikuwa amesikia
kwamba mlinzi wa Lisa alikuwa mkatili
na hasa stadi wa kupiga watu makofi.
“Ikiwa utafanya hivyo kwa mara
nyingine, sitasita kukuvunja mkono,” Shani alimwonya kwa ukali.
Kijana yule alirudi nyuma kwa aibu.
"Unajua mimi ni nani? Sawa, hata hivyo
wewe ni mlinzi tu. Ulinzi ni kazi gani?
Hata mbwa anaweza kulinda, kwa hiyo
mimi siongei na mbwa, naongea na mwenye mbwa.” Kijana yule aliropoka tu kwa aibu ya kuadhibiwa na mwanamke.
Wakati huo lifti ilikuwa tayari imefika.
Kiijana huyo alipoona Lisa anaondoka akamfuata akiwa na maneno ya kuvutia.
“Lisa, umesikia kuhusu mkufu wa Malkia? Kuna stori kuwa miaka mingi
iliyopita, mfalme alimpa malkia wake
mpendwa mkufu. Mtu yeyote ambaye
atavaa mkufu huo atafikia furaha katika
uhusiano wake. Mkufu huo utauzwa
kwa mnada hivi karibuni kule Mlimani
City. Nitakununulia, sawa?"
kifupi. Kijana yule alionekana kumganda kama jojo iliyong’ang’ania kwenye nguo
ambayo ilikuwa vigumu kuiondoa. Mara tu Lisa alipotoka nje ya jengo hilo, aliona mtu aliyemfahamu vizuri akiwa amesimama kwenye mraba. Alijawa na mchanganyiko wa mshangao na furaha. Taa za rangi mbalimbali ziliwaka
polepole usiku. Alvin, ambaye alisimama kando ya geti kuu, alikuwa
amevalia suti nyeusi na koti la rangi ya parachichi kana kwamba alikuwa
ametoka kushiriki katika Wiki ya Mitindo ya Paris. Alionekana mtanashati sana, na sura yake ilikuwa ya kuvutia kweli.
Hata hivyo, macho yake meusi
yaliangaza kwa huzuni dakika moja
alipomwona mtu aliyemfuata Lisa kwa nyuma.
hakugundua mawazo ya Alvin.
Alimkimbilia na kuzungusha mikono
yake kwenye kiuno chake kwa furaha.
"Hapana Asante. Sihitaji.” Lisa alijibu
"Alvlisa, kwa nini uko hapa?" Lisa
Unyogovu ndani ya macho yake
ulipungua polepole. Alimwangalia yule kijana kwa macho mabaya. "Inaonekana nilikuja kwa wakati mbaya, ona sasa nimevuruga miadi yako."
"Yeye ni nani, Lisa?" Yule kijana naye alikasirishwa na Alvin. Huku wote wawili
wakiwa wamevalia kifahari, jinsi Alvin
alivyokuwa na umbo bora na maridadi
ilimfanya yule kijana aonekane mtu wa chini sana.
Alvin alikaa kimya. Aliinua uso wake
huku akimwangalia Lisa, akiwaza ni namna gani atamtambulisha kwa mwanaume huyo.
“Ni mpenzi wangu,” Lisa alijibu moja kwa moja. "Ninajua nia ya babu yako,
Mzee Amiri Gumbo, lakini tayari
ninampenda mtu mwingine. Tafadhali
pia mwambie babu yako kuwa nina
shughuli nyingi hivyo asitume tena
vijana wake kuja kunisumbua. Sina
wakati wa kukaa kuongea na vijana
wadogo kama nyinyi."
Hakutaka kukata tamaa, yule kijana
mjukuu wa Mzee Amiri alisema, “Wewe ni mjanja. Afadhali ufikirie kwa busara.
Ukiolewa na familia ya mkurugenzi katika kampuni, itatusaidia sote wawili.
Kwa maoni yangu, mpenzi wako hana kitu kingine isipokuwa sura ya mauzo tu.
Yeye si mpenzi mzuri kwako.”
Uso wa Alvin ukaingia giza huku mikono
ya Shani ikianza kumuwasha na kuchezacheza kwa nguvu, akisubiri tu
ruhusa ya bosi wake ili agawe kichapo.
Shani alimtazama kijana yule kana
kwamba ni mtu wa ajabu sana.
“Asante kwa ushauri wako, lakini ndiye
ninayempenda. Nimeanguka katika
kumpenda bila matumaini, na ndiye
anayestahili upendo wangu. Tafadhali ondoka sasa hivi.” Lisa alimfukuza kwa
namna ya kudharirisha sana.
"Kwa kweli hujui ni nini kinachokufaa."
Kijana yule alimkodolea macho Lisa
kabla hajaondoka kwa kukata tamaa.
Lisa akashusha pumzi. Aligeuza kichwa
chake na kukutana na macho ya Alvin yaliyochangamka. Alishtuka kwa
kufikiria maneno ambayo alikuwa ametoka kusema yangekuwa yamemuudhi. “Nilitaka tu asiendelee kunisumbua. Usielewe vibaya…”
“Kwani umekosea nini?” Alvin aligeuka ghafla. Akayakazia macho yake huku
akitoa tabasamu la busara. “Ina maana unanipenda bila matumaini?”
“Tatizo lenu wanasheria kila kitu lazima mtafsiri.” Lisa akacheka.
“Hili lipo wazi wala halihitaji tafsiri, kwamba unanipenda tu lakini huna matumaini yoyote na mimi, sivyo?” Alvin alidadavua na kumchosha kabisa Lisa.
Lisa akakosa la kusema.
Ukimya wake ukamfanya Alvin
atabasamu. "Ingia kwenye gari."
Lisa alimwambia Shani aondoke na gari
lake kisha yeye akaingia kwenye gari la
Alvin. Gari ilisafiri hadi barabara kuu na
ili kuondoa upweke, Lisa alijaribu
kuanzisha mazungumzo mengine. "Umekula?"
Tumbo la Alvin lilinguruma hata kabla
hajajibu. Baada ya kimya cha sekunde mbili, Lisa alicheka. "Ni saa kumi na mbili tu sasa hivi. Mbona tayari una njaa? Hukula chakula cha mchana?”
“Chakula cha ofisini hakikuwa na ladha nzuri,” Alvin alisema kwa hasira, “Ni muda mrefu umepita tangu unipikie. Unafikiri kwamba kuvunjika kwa
mkataba ndiyo mwisho wa makubaliano? Kumbuka bado sisi ni wanandoa.”
"Nina mengi kwenye kichwa changu sasa hivi." Lisa alihisi kuchoka kabisa.
“Nitatayarisha kifungua kinywa ili uende nacho ofisini kila asubuhi, sawa?”
"Unanichukulia kama mwanafunzi?"
Alvin alimkazia macho. Sekunde chache
baadaye, aliongeza, "Sawa basi, utakavyopenda mwenyewe." Lisa alikosa la kusema.
Ni mabadiliko ya haraka kama nini
katika maisha ya Lisa ndiyo yaliyomnyima raha Alvin. Tangu aanze
kufanya kazi huko Mawenzi
Investiments, hakuwahi kumwandalia
chakula kitamu kama zamani, Alvin ali’miss sana mapishi yake.
“Nisikilize. Tukifika nyumbani usiku huu, ninataka kula nyama ya choma ya
nguruwe, saladi ya…”
Lisa alimshika mkono na kupiga kelele
za furaha kabla hajamaliza sentensi yake. “Tulia…Acha! Wacha nikupeleke
tukale vyakula vya uswahilini usiku wa leo. Ghafla natamani miguu ya kuku, shingo, vichwa, firigisi na vipapatio vya kuku vilivyokaangwa, mihogo ya
kuangwa na kachumbari...”
“Una kichaa? Unawezaje kunilazimisha kula takataka za aina hii?" Alvin
alishtuka na kukasirika sana hata ndita
zake zilikuwa zimejikunja.
“Umekosea kusema hivyo. Watu wengi
wanaishi kwa kula aina hii ya chakula,
sawa? Weka vizuri kauli zako. Hata
kama hupendi lakini mimi nina hamu ya firigisi za kuku zilizokaangwa. Kama
mume wangu ni wajibu wako
kunisikiliza, haya ndiyo makubaliano yetu mapya!”
Lisa aliendelea kukuna mikono yake.
Wakati mkataba ulipovunjika na makubaliano mapya yalipoanza
kutumika, msimamo wao katika
uhusiano haukuwa kama zamani na
ilimbidi Alvin amsikilize. Sasa, angeweza kufanya chochote alichotaka
na kula chochote alichotamani na roho yake.
Alvin hakuwa na la kufanya zaidi ya kuendesha gari hadi Coco Beach na kuegesha kando ya barabara. Wawili
hao waliingia kwenye vibanda vya
wakaanga nyama za kuku pamoja.
Sura ya 117
Msongamano wa wateja wengi
waliokuwa wakiingia na kuondoka pale
Coco Beach pamoja na harufu ya
nyama vilimyima kabisa amani Alvin.
Alikosa raha hadi akakunja uso.
“Nenda ukachukue kiti. Chukua kiti hicho kiko wazi..." Lisa alimwambia
Alvin aliyekuwa amesimama tu akishangaashangaa. Lisa alionekana
kutokuwa mgeni sana kwenye mazingira kama hayo.
Lisa alinyoosha kidole kuwelekeza Alvin kwenye meza tupu ambayo ndo kwanza
mteja alikuwa ametoka. Takataka za mabaki zilizokuwa mezani hazikuwa
hata zimesafishwa.
"Sitakaa hapo mimi." Alvin alimpiga Lisa
jicho kali. Lisa akamfuata na kumsisitiza. Maneno ya Lisa ya
kubembeleza yalimfanya Alvin akose la kusema. Kwa hayo, akasogea pale na
kuketi kwa kusitasita.
Dakika kumi baadaye, Lisa aliandaa mlo
kamili wa familia, ambao ulijumuisha
firigisi na kila sehemu ya kiungo cha
kuku vikiwa vimekaangwa, mihogo ya kukaangwa, kachumbari na aiskrimu.
“Kula hii firigisi ya kuku, ni tamu.” Lisa alinyakua kipande na kumlisha kwa shauku. Alvin akakwepesha na kusukuma mkono wake pembeni.
"Ngoja nikuonyeshe kitu." Alvin akatoa simu yake na kusogeza hadi kwenye ukurasa unaoonyesha habari mbaya kuhusu nyama za kukaangwa hovyo mitaani. Kisha, akampitishia Lisa.
Baada ya kuangaza macho kwenye
picha mbaya ya sahani ambayo ilikuwa na vipande vichache vya vipapatio na zaidi ya miguu kumi ya kuku, Lisa alijawa na karaha. "Alvin, huwezi kupata
madhara kwa kula chakula hiki mara moja tu."
"Vitu vya aina hii vina kiasi kikubwa cha
viambato vya sumu. Baada ya leo,
huruhusiwi kula aina hii ya chakula tena. Wewe hata si mtoto.” Alvin alidhamiria.
Lisa hakuweza kuwa na wasiwasi juu
yake. Aliinamisha kichwa chini na kupiga msosi kisawasawa. Baada ya kula vipande kadhaa, aligundua kuwa vingine vilikuwa na ladha mbaya, na badala yake akaviingiza kinywani mwa Alvin.
Huku mdomo wake ukiwa umejaa chakula ghafla, Alvin alimtupia jicho la hasira. Lisa alijifanya kuwa mwadilifu.
“Si wapenzi wa kiume hutakiwa kula
chochote ambacho wasichana wao huwalisha? Angalia wanandoa kando yetu. Ndivyo wanavyofanya pia.”
Wapenzi vijana walioketi kando yao
walikuwa wanafunzi wa chuo kikuu.
Baada ya msichana kukerwa kidogo na kipande cha nyama alichokuwa
anatafuna mdomoni, alimpa mpenzi
wake. “Haina ladha nzuri. Unaweza kula?”
Mpenzi wake naye akajibu, "Unafikiri
naweza kusema hapana?"
Lisa naye alikoroma kwa wivu. “Kwanini
hutaki kula firigisi niliyoiuma, unanionea kinyaa, huh? Kumbe hunipendi?” Alvin
alishindwa cha kusema.
Lisa aliyekaa mkabala naye alikunja uso
huku akimwangalia. “Jinsi ninavyowatamani. Ninapenda kuwa
kwenye uhusiano kama huo."
"Nyamaza." Huku akifungua mdomo, Alvin alichukua kipande cha kuku
kilichobaki mkononi mwake na kukiuma.
Kwa wakati huo, Alvin bado hakuweza
kumwelewa Lisa hata kidogo. Alikuwa
akimtii, lakini kwa nini kulikuwa na
badiliko kubwa hivyo ndani yake sasa?
Baada ya hapo, walimaliza kula firigisi
zote za kukaanga, na hata ice cream
iliyobaki. Hawakutambua kuwa kuna
mtu alikuwa amewapiga picha kwa siri
na kuiweka kwenye group whatsapp la
kikundi cha wanasheria wenzake na
Alvin.
Sam alikuwa akipata nyama choma
katika mgahawa mmoja wa kisasa alipoona picha hiyo. Karibu apaliwe na minofu ya nyama. Haraka alisevu picha hiyo na kuisambaza kwenye makundi mengine aliyokuwa na marafiki zake.
Chester: [ Macho yangu yananidanganya? Alvin angewezaje kuingia Coco Beach?]
Rodney: [Damn! Sijawahi kuona
Alvin akila firigisi za kukaangwa uswazi.
Huyu ni Alvin kweli? ]
Sam: [Nooooo. Hii ni kweli.
Mwanasheria mwenzetu kutoka
kampuni yetu alimpeleka binti yake
huko Coco beach na kumwona Alvin
akila vipande vya nyama ya kuku wa kukaangwa kwa furaha pamoja na Lisa.]
Chester: [ Hiyo ni mbaya
sana, si hadhi ya Alvin. Utakaporudi,
nitakupokea kwa mlo wa hali ya juu wa Kijapani.]
Rodney: [Nakubali. Rudi haraka, Alvin.
Nitamwomba mmoja wa wapishi wakuu Kenya akuhudumie.]
Sam: [ Nathubutu kuweka dau la milioni tano kwamba Alvin hawezi
kuhangaika kuhusu nyinyi. Nina hakika hatajali kula hata Losholi la kimasai ama
kichuri cha kikurya mradi tu Lisa yuko karibu naye.]
Ni pale tu Alvin alipotoka kwenye eneo la ufukwe huo ndipo alipogundua fujo
zilizokuwa zikiendelea kwenye group
hilo la whatsapp. Alifadhaika sana na kujawa na hasira.
Baada ya kuingia kwenye gari, Lisa
alimsogelea na kumbusu mdomoni.
Macho yake meusi angavu yaliwasilisha
hisia za furaha na mahaba. “Asante, Alvilisa. Nimefurahia sana chakula cha
jioni ya leo."
Alvin hakuonekana kufurahia kabisa.
"Kwa hiyo unajaribu kunifanya nisahau
kuhusu jambo hili kwa njia hii, huh?
Unajua kuwa hii ni mara yangu ya kwanza kuingia Coco Beach usiku wa leo na kula chakula cha ajabu?”
Lisa alihisi kuwa Alvin alikuwa
anajifanya tu kuchukia. Wakati
mwingine, wanawake hutawala kwa
urahisi tu. Mara baada ya kugundua
kuwa Alvin alifurahia kitu alichomfanyia, alimwongezea dozi ili kumlainisha
kabisa. Aliuma mdomo wake wa waridi, kisha, akaweka mikono yake shingoni mwake na ulimi uliojaa mate na akambusu tena.
Safari hii, Alvin alimshika kichwa na kumpiga busu refu. Alipoanza kuvuta
pumzi za uchovu ndipo alipomwacha
apumue.
Sura ya 118
Katika hoteli moja ya kifahari, Stephen
Kileo na dada yake Janet walikuwa wakimfanyia mapokezi ya heshima mtu
mmoja maarufu aliyeketi katikati ya kochi. Mtu huyo alikuwa ni Willie Kimaro
ambaye alikuwa ametoka Nairobi. Willie na Alvin walikuwa mtu na binamu yake.
Familia ya Kimaro ilikuwa familia ya kifahari sana na utajiri wa kutupwa.
Ilimiliki makampuni mengi hapa
Tanzania na Kenya, yakiwemo ya mawasiliano, Vyombo vya habari, usafirishaji na hata vituo vya mafuta ya
magari. Pia walimiliki hisa kwenye
makampuni mengine makubwa nchini
ikiwemo Mawenzi Investiments. Ni vile tu Alvin hakuwa tayari kujionyesha kwa
watu kama alitokea kwenye familia hiyo
ndiyo maana watu wengi hawakumjua
kiundani. Hata hivyo Kimaro ni jina la
ukoo kwa familia nyingi za kichaga
hivyo ilikuwa rahisi sana kwa Alvin
kuficha uhusiano wake na familia yake.
“Bwana Kimaro, ngoja nikutambulishe kwa mpenzi wangu, Lina.” Stephen Kileo alikuwa ameambatana na Lina.
"Baba yake, ambaye ni mwanahisa mkubwa katika kampuni ya Mawenzi Investiments, amekuletea zawadi usiku wa leo."
Usiku huo, Lina alivaa nguo ndefu ya rangi isiyokolea iliyokazia mikunjo ya mwili wake maridadi. Ingawa hakuwa mrembo kama Lisa, alikuwa
amependeza sana. Familia ya Jones ilichukuliwa kuwa mojawapo ya familia
za juu zilizo na ‘mbegu’ nzuri. Alikuwa amejipodoa ipasavyo usiku huo.
Alipotabasamu kwa upole, hakika alionekana kama malaika aliyeshuka
duniani kwa bahati mbaya.
Macho ya Willie Kimaro yaliangaza kwa
hisia. Lina alikuwa na mawenge sana
na wanaume matajiri. Ikiwa angeweza
kumvutia kimapenzi mwanamume yule
kutoka familia maarufu ya Kimaro,
asingekuwa na muda na watu kama
Stephen Kileo tena. Lina alimfuata kwa tabasamu la kichokozi. “Willie, familia yangu ingependa kukupa zawadi hili. Mkufu wa dhahabu wenye kidani cha jiwe la thamani la Tanzanite kutoka Mererani, umenakshiwa na sonara maarufu hapa jijini, Enjipai Jewellery."
Alipomaliza tu kuongea, alifungua boksi. Macho ya Willie yakaangaza. “Woooh!
Kidani hiki kina thamani ya mamilioni ya pesa, sivyo?”
“Sio muhimu sana, ilimradi tu unaipenda," Lina alijibu huku akijaribu kumfurahisha.
“Hahaah! Kwa kweli sikutegemea.
Nakupenda sana wewe!” Willie alisugua
kidani kwenye sehemu ya juu ya pua yake. Haikujulikana kama alimaanisha kuwa anampenda Lina au kidani.
Ghafla, kimya kikatanda kwenye
chumba kile cha kifahari cha Hoteli maarufu. Macho ya kila mtu yalikuwa
kwa Willie. Stephen alitabasamu kwa
utulivu, na mara akanyanyuka yeye na Janet wakatoka nje. Kisha Lina alikaa na Willie kwa muda wote wa usiku.
Aliimba na kuzungumza naye. Kwa vile
alikuwa mzuri katika kukonga nyoyo za wanaume, mara alimfanya Willie acheke kimoyomoyo.
Baadaye Lina alielekea mapokezi mara moja. Dakika alipotoka nje ya kaunta, alimuona Stephen akisubiri nje.
“Asante kwa usiku wa leo, Stephen.
Natumai Willie anaweza kuisaidia
familia yangu kurejesha nafasi ya mwenyekiti wa Mawenzi Investiments.”
Lina alitabasamu huku akizungusha mkono wake kiunoni kwa Stephen.
"Natumai atasaidia." Stephen
alitabasamu bila huruma. “Kwa hiyo
Willie na wewe—”
Lina akamkatisha mara moja, “Usinielewe vibaya. Unajua kuwa wewe bado ndiye ninayekupenda. Sasa hivi, Kimaro bado nina maongezi naye—”
“Ninaelewa. Sina wazo lolote baya
kuhusu hilo.” Stephen alimpiga piga nyuma ya mkono wake. "Ni wakati tu familia yako itakaporejesha kiti chake cha uenyekiti wa kampuni ya Mawenzi ndipo familia zetu zote mbili zinaweza kufanya maendeleo zaidi na kufikia mambo bora zaidi."
"Ni vizuri umeelewa." Lina hakuwa
akimfikiria kabisa Stephen moyoni mwake tena baada ya kuona Willie amekaa mkao wa kueleweka.
"Kilicho muhimu zaidi kwa sasa ni kumfurahisha Willie Kimaro." Stephen alipitisha vidole vyake kwenye nywele zake. “Nitakusubiri.”
“Asante.” Lina alijibu kisha akarudi na keti kando ya Willie tena. Wakati huo, Willie aliweka mkono wake kiunoni mwake na kuanza kumpapasa kama alivyotaka.
Saa tano usiku, Willie alikuwa amelewa.
Stephen alimuomba Lina ampeleke
chumbani akapumzike.
Sura ya 119
Baada ya Lina na Willie kuondoka, Janet alimwambia Stephen kwa
mshtuko, “Umerukwa na akili, Lina si mpenzi wako? Kwa nini
hukunitambulisha mimi kwa Willie? Bila
shaka ningeifaidisha familia yetu ikiwa
ningekuwa binti-mkwe wa familia ya Kimaro.”
“Willie hakuvutiwa nawe,” Stephen alijibu kwa dharau huku akiwasha sigara.
Janet alipandwa na hasira.
"Unamaanisha nini? Machoni pako, mimi si mrembo kama Lina, huh?
Kwanza mimi sikukulia kijijini kama yeye—”
“Ninafanya hivi kwa faida yako.”
Stephen akamkatisha. “Willie ana tabia
chafu ya kulala na wanawake hovyo, hajali hata kama ni mpenzi au mke wa mtu.”
Janet alipigwa na butwaa. Stephen
aliongeza, “Wewe ni dada yangu wa damu. Ikiwa kuna njia rahisi ya
mafanikio makubwa, bila shaka
ningekupendelea wewe kwanza. Hata hivyo, Willie ni mhuni na malaya sana. Amewahi hata kuua mwanamke.”
"Una uhakika?" Janet akatetemeka.
“Ni kweli kabisa. Isingekuwa jamaa yetu
ambaye anafanya kazi kama msaidizi wake, nisingelijua hilo.” Stephen
alisimama taratibu na kusimama.
“Vinginevyo, kwa nini unadhani nilimpa
Lina nafasi kubwa namna hii? Yeye hana heshima pia.”
Stepehen alitulia kidogo kisha
akaongeza tena, “Lakini usijali. Willie
atashukuru kwamba nilimpa nafasi ya kuwa karibu na Lina. Katika hali hiyo, nitapata fursa ya kuwa rafiki wake wa karibu. Nitatumia nafasi hiyo kuinufaisha
familia yetu kibiashara.” Mara Janet akaridhika.
Asubuhi iliyofuata Lina aliporejewa na fahamu, alishtuka baada ya kumuona
mwanaume aliyekuwa pembeni yake
ambaye alikuwa akimtumbulia macho. Huku kila kitu kilichotokea jana yake
usiku kikimulika akilini mwake, alihisi kana kwamba alikuwa ameenda kuzimu
kwa mara nyingine tena. Mtu huyo
alikuwa anatisha, kwa kweli. Kifupi
alikuwa mnyanyasaji. Wakati huo, Lina
alikuwa ameumizwa vibaya sana
kutokana na kuingiliwa kinyama
kinyume na maumbile.
“Umeamka?” Willie alipogeuza kichwa chake na kumwangalia Lina, mtetemeko ulimtawala mwili mzima.
“Umenifanyaje hivi?” Lina aliuliza
kinyonge huku akishika sehemu zake
zilizokuwa zinawaka kwa maumivu.
“Kwanini? Hujaridhika na mimi?" Willie
aliwasha sigara, macho yake yakimeta
kwa chuki.
"Hapana." Lina alilazimisha tabasamu.
Kwa kuwa alikuwa ameyataka
mwenyewe kulala naye, alifikiri kwamba
haikuwa na maana tena kujutia yaliyomkuta. Aliuma meno na kujifanya
kuwa na haya. Aliongeza, "Ni furaha yangu kuweza kulala na wewe, Mpenzi
Kimaro."
'Ni vizuri kwamba umefurahia. Kwa
kweli wewe mtoto ni mtamu sana.”
Willie alivuta sigara, akimwangalia Lina
kwa udadisi. "Ilikuwa mara yako ya kwanza kufanya jana usiku?"
Lina alipigwa na butwaa. Alikumbuka
kwamba alikuwa amefanyiwa upasuaji
wa plastiki kurudisha bikra yake
kimakusudi ili kumfurahisha Stephen
endapo kama wangekutana kabla ya hapo. Hakutarajia kwamba angelala
ghafla na Willie jana yake usiku.
Inavyonekana, Willie hakuelewa jambo hilo.
“Ndiyo-Ndiyo.”
"Sikutarajia." Willie akamgusa kidevu
chake. "Huogopi kwamba Stephen atachukia?"
"Kama nilivyosema, ni heshima yangu kuweza kulala na wewe kwa usiku kucha nikizingatia hadhi yako nzuri,"
Lina alijibu kwa kujiamini. Aliposikia hivyo, Willie aliangua kicheko.
“Inavutia. Nakupenda sana. Nitakuwa Dar kwa muda, na utanisindikiza katika muda wangu wote hapa.”
“Sawa.” Lina alilazimisha tabasamu.
"Nashangaa ni mradi gani uliokuleta hapa Dar, bila shaka ni mkubwa sana!"
“Oh. Kando na kuhudhuria hafla ya Mawenzi, Kampuni ya teknolojia chini ya familia ya Kimaro ingependa kuwekeza katika sekta ya viwanda.
Nimekuja kutazama fursa.”
Lina aliuliza kwa tahadhari, “Utawekeza kiasi gani?”
"Pengine mamia ya mabilioni ya shilingi.
Hakuna kikomo kwa kiasi, ukomo
utategemeana na fursa
itakayopatikana.” Willie alijibu kwa kawaida.
Roho ya Lina ilimruka. Ikiwa Mawenzi
Investments ingeweza kufanya kazi
kwenye mradi huu, Jones na hadhi yake
ingeinuliwa.
"Mpenzi Kimaro, nadhani ungetaka
kufanya kazi na kampuni ya ndani kwenye mradi mkubwa kama huu..."
"Mawenzi Investments ana nia ya kushiriki katika hilo, huh?" Willie alitoa
tabasamu la nguvu.
“Mpenzi, ningependa kushirikiana nawe kwa ajili ya mradi huu, lakini
nimefukuzwa kutoka kwenye kazi yangu
huko Mawenzi Investments. Baba
yangu pia amenyang’anywa cheo cha uenyekiti wa Kampuni” Akiwa amekata
tamaa, Lina alitoa tabasamu la uchungu. "Baba yangu na mimi wote
tupo hatarini ..."
"Naweza kukutatulia chochote mradi tu ufanye wajibu wako vizuri katika
kuniweka sawa." Tabasamu likaangaza
usoni mwa Willie. "Wanawake wote
wanaonizunguka hawajawahi
kushindwa kupokea thawabu nzuri kutoka kwangu."
"Kwa hali hiyo, hakika nitakutendea vizuri." Kwa dhamira mbaya, alimbusu
kwa hiari yake mwenyewe.
Muda mfupi baadaye, kilio cha Lina
kilisikika kutoka chumbani kwa mara nyingine tena. Willie alimgeuza tena na kuanza kumshughulikia kinyama. Akiwa analia kwa uchungu, alijiwazia, 'Lisa, ninateseka sana sasa kwa ajili yako.
Hakika nitakulipa na riba katika siku zijazo!”
Mwaka ulikuwa unaelekea ukingoni.
Maadhimisho ya kumbukumbu ya
Mawenzi Investments yaliadhimishwa
katika hoteli ya nyota saba.
Sio tu kwamba
Mawenzi Investments
alialika watu mashuhuri wachache kwa
usiku huo, lakini idadi kubwa ya
wafanyabiashara wenye nguvu pia
walikuwa wamejitokeza.
•••
Ilikuwa ni saa moja kamili jioni ambapo
Lisa akiwa ni mwenyekiti aliyeteuliwa hivi karibuni, aliwasili katika hoteli hiyo.
Lisa aliendesha polepole hadi hotelini kwa gari aina ya Range Rover.
Mlango wa gari ulipofunguliwa, alionekana akiwa amevalia gauni refu
jeusi la mtindo wa zamani na akiwa
ameshikilia mkoba wa zamani
uliopambwa. Kwa kawaida si rahisi
kuwa kivutio cha watu kwa mtu aliyevaa
nguo nyeusi. Hata hivyo, Lisa alibaki
mrembo na mzuri akiwa na uso wake
mwanana na wa kuvutia na mdomo
uliokolea lipstick nyekundu iliyofanana na waridi linalochanua.
Waandishi wa habari walianza
kuchukua kamera zao ili kupiga picha
zake. Kwa wadhifa wake na
utambulisho wake, angeweza
kuchukuliwa kuwa C.E.O mwanamke
mwenye umri mdogo na mrembo zaidi
jijini Dar es Salaam. Lisa akapiga pozi
kwa ajili ya picha, lakini muda mfupi
baadaye, kelele za ghafla zikasikika
kando yake kutoka kwa waandishi wa habari.
“Fanya haraka utazame! Je, hili si toleo la pekee la Bugatti Veyron L'Or Blanc?"
“Nilisikia limetengenezwa kwa chuma cha titanium. Linagharimu zaidi ya Shilingi milioni mia saba!"
“Angalia namba ya usajili, ni private number. KIMARO! Inashangaza.”
“Kweli inashangaza. Ni nani huyo? Yuko
hapa kuhudhuria sherehe ya ukumbusho wa Mawenzi Investments?”
“Tazama! Mlango unafunguliwa.”
Akiwa amezungukwa na sauti za watazamaji, mwanaume mmoja aliyevalia suti ya bluu iliyokolea alitoka
kwenye kiti cha dereva. Sifa zake
zilitamkwa, na tabasamu la kishetani lilionekana usoni mwake.
Kulikuwa na vifijo kutoka kwa waandishi wa habari katika umati huo.
"Yeye ni mzuri sana!"
“Namfahamu yeye ni nani. Yeye ni Willie kutoka familia ya Kimaro."
"Familia ya Kimaro? Familia yenye
utajiri zaidi hapa Tanzania?”
“Ndiyo. Ni hiyo familia ya Kimaro!
Wanakaaga Nairobi.”
"Mungu wangu. Mawenzi Investments
wana uhusiano na familia ya Kimaro?”
Katikati ya majadiliano ya umma, mlango wa abiria ulifunguliwa. Akiwa amevalia gauni jekundu, Lina alitoka nje
ya gari kwa kuvutia huku akiushika mkono wa Willie. Sauti ikazidi kuvuma
tena kutoka kwa umati.
“Huyu ni nani?”
"Lina, binti ya Jones Masawe ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa bodi ya Mawenzi Investments."
“Kwa hiyo yuko kwenye uhusiano na Willie. Anajaribu kugeuka kutoka kuwa
mkulima hadi kuwa binti wa kifalme, huh?
"Kwa kuwa sasa ana uhusiano na
familia ya Kimaro, familia ya Harrison na
familia ya Zongo sasa watamheshimu Jones."
Maneno hayo yalimfanya Lina azidi
kuridhika. Ilifaa kujipendekeza na Willie kama mtumwa kwa siku chache ili apate
taji la utukufu na heshima siku za baadaye. Alipogeuza macho yake, alitokea kumwona Lisa aliyekuwa mbele yake akiwa anamshangaa bila ukomo.
Akiwa amekunja midomo ya waridi, Lina alimshika Willie mara moja na kuelekea kwa Lisa. "Halo, Lisa. Willie, huyu ni dada yangu, ambaye pia ni Mwenyekiti na CEO wa Mawenzi Investments.”
Sura ya 120
Baada ya kumwona Lisa mapema, Willie alimtazama kwa shauku. Hakujua
kamwe kuwa Lisa aliyekuwa amemsikia
mapema alikuwa mwanamke mwenye
sura nzuri kama hiyo. Uzuri wake
ulionekana kuwa wa aina yake miongoni
mwa mamia ya wanawake aliokuwa
amekutana nao.
"Halo, Bi Jones." Willie alinyoosha
mkono wake kwa kumpa salamu. Lisa
pia alishangaa kwamba Lina aliwezaje
kupata ushirikiano na mtu kutoka kwa
familia ya Kimaro. Lisa hakuwa na la
kufanya zaidi ya kunyoosha mkono
wake bila kupenda, akijua kuwa hawezi
kukataa salamu yake bila sababu.
Nani alijua baada ya Willie kumshika
mkono, alichora miduara kwenye
kiganja chake kwa utani kwa kutumia
kidole chake kidogo na kumchoma
kichokozi Lisa. Mabadiliko kidogo
yalionekana katika uso wa Lisa. Alijaribu
kujinasua kutoka kwa mguso wake,
lakini kwa makusudi Willie alimshika
kwa nguvu na kumzuia.
"Bi Jones, unataka kunishika mkono
wangu hadi lini?" Willie alitabasamu kwa
ujanja.
Lina mara moja akainua mdomo wake
na kusema, "Unafanya nini, Lisa?" Hapo
hapo Lina akamvaa Lisa na
kumwanzishia varangati, akidhani kwamba Lisa alijaribu kumchombeza Willie.
Waandishi wa habari waliosimama
kwenye ukingo wa zulia jekundu walichukua picha za watatu hao mara moja. Pamoja na dada wawili kutoka kwa familia ya Jones wakipigana juu ya mtu maarufu wa familia ya Kimaro, lilikuwa tukio ambao lingetengeneza kipande cha habari nzuri.
“Kwanini hukumuuliza alichonifanyia pia?" Akiwa na tabia ya utulivu, Lisa hakuwa na jeuri wala kujidharau. “Hivi nyie mnafikiri kwamba mimi kama mtu anayesimamia Mawenzi ningemtongoza mpenzi wa binamu yangu bila aibu?
Samahani, hata hivyo si mpenzi wako.
Ninavyokumbuka, Stephen ndiye mpenzi wako, sivyo?”
Waandishi wa habari walianza
kushangaa. “Kweli? Stephen ni mpenzi
wa Lina kweli, lakini kwa nini alikuja na Willie leo?”
“Sasa kwa kuwa alikutana na Willie, inawezekana kwamba anajaribu kumtosa Stephen?”
“Hilo linawezekana. Hapo awali alikuwa mchumba wa Ethan, lakini Ethan alipokabiliwa na wakati mgumu, mara moja alimbwaga kwa kushutuma za usaliti.”
“Ni fedheha iliyoje! Willie anavutiwaje na mwanamke wa aina hii?"
Uso wa Lina ulikuwa mweupe kama
karatasi wakati huo. Willie hakutambua
kwamba Lina alihusishwa na habari
nyingi mbaya. Aliishia kujiingiza kwenye matatizo.
Bila bughudha, Lisa alijiondoa kwa
nguvu kutoka kwa Willie na kugeuza
mkono wake kwa maumivu. "Ulinibana
mkono wangu kwa nguvu sana hadi
unauma, Bwana Kimaro."
Mkono wake, ambao hapo awali ulikuwa
wa kawaida, ulikuwa mwekundu wakati
huo. Waandishi wa habari waliposogea karibu, waliweza kuiona ngozi yake nyekundu vizuri. Macho ya Willie yakaangaza kwa dharau mara moja.
Hawakutarajia mtu kutoka kwa familia ya Kimaro angekosa haya. Siku zote Willie alikuwa mtu wa kupenda kunyenyekewa na wengine.
Ilikuwa ni mara yake ya kwanza
kudhalilishwa na mwanamke hadharani.
Macho yake yalionyesha uhasama, lakini alitabasamu kwa unyonge.
"Samahani kwa kukuumiza bahati mbaya." Akamsogelea Lisa hadi karibu na kumnong’oneza, “Utanijua mimi ni nani, Lisa.”
Alipomaliza tu kuongea, aliingia moja kwa moja ndani ya hoteli hiyo. Na Lina
alimfuata haraka. Lisa alipoutazama mgongo wa Willie, alihisi kana kwamba
alikuwa amelengwa na nyoka mwenye sumu kali. Alikuwa na hasira ya kuzama.
Willie alipanda lifti uso wake ulikuwa na hali ya huzuni. Akiwa ameingiwa na mawazo ya wasiwasi, Lina alisema kwa
utulivu, “mpenzi, natumai hautajali kuhusu hilo. Lisa anajidai na anajigamba kwa kuwa yeye ndiye mwenyekiti wa kampuni na kufanya mambo yasiyo ya kiungwana.”
“Yeye ni nani wa kufanya hivyo? Yeye ni mwenyekiti tu wa kampuni, kufumba na kufumbua anaweza kukuta kiti hicho
kina mtu mwingine.” Willie alikuwa akifuka kwa hasira.
"Kwa kweli, yeye si kitu ikilinganishwa na wewe. Labda ni kwa sababu ana
mpenzi mwenye nguvu, na yeye ni mwaminifu sana kwake.” Baada ya
kukaa siku chache na Willie, Lina alijua
kuwa Willie alipenda sana kusifiwa.
Kwa hakika, macho ya Willie
yalionyesha kupendezwa kwake dakika tu aliposikia hivyo. Alipenda sana
wanawake ambao muda wote walikuwa
wakimsifia, kumbembeleza na kumpetipeti. Zaidi ya hayo, ukizingatia jinsi Lisa alivyokuwa mkali muda si mrefu, alifanana na waridi lenye miiba na alionekana mrembo zaidi kuliko Lina.
Alipoona hali ya kuvutia machoni pake, Lina alitabasamu na kusema, “Ninaweza kumfanya alale nawe kama utapenda.” Lina alisema bila aibu. Kwa
kuwa amekuwa akidhalilishwa na Willie kama mbwa kwa muda waliokuwa
pamoja, alitaka Lisa pia aonje adha hiyo.
"Wewe ni mwanamke mbaya sana."
Willie alimpiga jicho la mshangao.
"Furaha yako ndiyo muhimu kwangu.
Hutaki kumfundisha somo?” Lina aliuliza
kwa kupendeza.
Willie aliinua macho yake. Aliwasha
sigara kisha akasema kwa uovu, “Wale
walionidhalilisha wote waliishia katika
hali mbaya sana. Lisa pia anastahili kujuta!”
•••
Sherehe kuu ya kumbukumbu ya
kampuni ya Mawenzi ilianza rasmi. Lisa
alipaswa kuwa kivutio cha tukio hilo,
hata hivyo, wageni wote walimzunguka
Willie, Jones, na Lina badala yake.
Kwa macho ya wengi, familia ya Kimaro
ilionekana kuwa ya hadhi ya kipekee.
Ingawa Willie hakuwa mzao wa moja
kwa moja wa Kimaro, uwepo wake jijini
Dar es Salaam ulikuwa na nguvu ya
kutosha kupata heshima kutoka familia
kubwa za kitajiri.
Chris Maganga akajongea kuelekea
kwa Lisa na kumuuliza. "Jones Masawe
aliwezaje kujenga uhusiano na Willie
Kimaro?"
"Nadhani Lina alilala naye." Lisa
alifanya dhana ya kuridhisha. Tayari
aliweza kuona tabia mbaya ya Willie
kupitia tukio fupi alilokutana nalo
mlangoni wakati wanaingia.
Sura ya dharau iliosha usoni mwa Chris.
“Babu na bibi zako walikuwa na sifa ya
uungwana na uadilifu, hii tabia chafu
yenye aibu ameitoa wapi dada yako?”
“Ni kwaida yake kujua ndani ya kila
suruali ya mwaname aliyefanikiwa kuna mdudu gani.” Lisa kichwa kilimuuma.
Hapo awali, alikuwa na uwezekano mkubwa wa kumvutia kila mtu, lakini
mwonekano wa Willie ulimfunika kabisa. Willie alikuwa amevutia umakini wa
wasanii, waalikwa, wakurugenzi wa kampuni na wasimamizi wakuu.
Kwa wakati huo, wakurugenzi wawili wa bodi ya kampuni ya Mawenzi, Amiri
Gumbo na Mzee Levy walimwendea na kumwambia. "Lisa, ulipaswa kuwa wa
kwanza kutoa hotuba kwenye jukwaa
usiku wa leo. Lakini baada ya
kujadiliana na wakurugenzi wengine, tuliamua kumwacha Bwana Kimaro
aanze kwanza, akifuatiwa na Jones
kisha—”
“Nyie watu ni wazima kweli?” Chris
alipandwa na hasira. “Bwana Kimaro
hata hajui kinachoendelea katika
kampuni yetu, wao huja kuchukua faida
tu. Unahitaji kujua kuwa usiku wa leo ni sherehe ya kumbukumbu ya Mawenzi
Investments. Pia, kwa nini Jones
anapanda jukwaani kabla ya mwenyekiti? Hii haina maana.”
Mkurugenzi Amiri alijibu kwa aibu,
“Angalia Bwana Kimaro ni nani. Ukweli
kwamba amejitokeza kwenye sherehe
ya ukumbusho wa Mawenzi
Investments unaonyesha kwamba
anatufikiria sana. Zaidi ya hayo, yuko
tayari kupanda jukwaani kutoa hotuba,
ambayo ni heshima yetu kubwa. Bei ya hisa za kampuni yetu itaongezeka
kesho. Kuhusu Jones, ni Bwana Kimaro
ambaye alimwomba azungumze. Ana
uhusiano wa karibu naye. Huwezi
kunilaumu kwa hili.”
Uso wa Lisa ulibadilika kidogo.
“Itakuwaje kama sikubaliani?”
"Hapana," Mkurugenzi Levy alijibu kwa
njia ya moja kwa moja, "Sote tulifikia
uamuzi huu kwa ajili ya kampuni.
Lazima ukubaliane nao.”
Lisa alicheka. "Ikiwa Willie ataamua
kumpendekeza Jones kuwa mwenyekiti, nyinyi pia mtakubaliana naye? Je! ni
Sheryl au Kimaro ambaye alianzisha
Mawenzi Investments?"
"Tunafanya hivi kwa ajili ya matarajio ya kampuni," Mkurugenzi Levy alisema
kwa kukerwa, "Kwa kuzingatia hali ya familia ya Kimaro, utajiri wa familia yao
una thamani ya mamia ya mabilioni ya shilingi.” Mkurugenzi Amiri alikubali kwa
kichwa pia.
Saa mbili na nusu usiku, Willie alipanda
jukwaani na kutoa hotuba, akifuatiwa na Jones Masawe…
Sura ya 121
Saa tatu usiku, Lisa alikuwa kwenye
chumba chake cha mapumziko baada ya kumaliza kutoa hotuba yake.
Alisimama kwenye kioo akipaka lipstick
yenye rangi ya hudhurungi kwenye
midomo yake maridadi, huku akitafakari hotuba aliyotoka kuitoa punde.
Lina akaingia ghafla. Akiwa na tabasamu la ufidhuli, alisema, “Pengine hukutarajia kwamba hivi karibuni ungeweza kupoteza nafasi yako ya uenyekiti ambayo ndiyo umeipata hivi punde, sivyo?”
"Wewe bado hujabadilika kabisa Lina."
Lisa aligeuza kichwa chake na kukutana na macho ya Lina. “Kwanza, ilikuwa
Ethan, ikifuatiwa na Stephen na sasa
Willie. Umelala na wanaume wangapi zaidi kabla ya hawa? Wewe ni zoazoa, cha wote, au chakula cha wageni?”
Kauli fupi kama hiyo iligusa ujasiri wa Lina ghafla na kusababisha damu yake
kuchemka. “unanionea wivu, huh? Sasa
ninakupa nafasi hii pia. Ni heshima
kubwa sana kuweza kulala na Willie
Kimaro sivyo? Nadhani utafurahia pia, yupo vizuri kwa bedi.”
Mara tu alipomaliza kuzungumza, Willie
aliingia ndani ya chumba akiwa
amevimba kama mbogo.
"Bwana Kimaro, nitakusaidia kulinda
nje." Lina alifunga mlango wa chumba mara baada ya kusema hayo.
“Unataka kufanya nini?” Lisa alijaribu kukimbia, lakini Willie alimshika mkono.
Kukiwa na mlango kati yao, alisikia sauti ya mlango ukiwa unafungwa.
Wimbi la wasiwasi lilimkumba Lisa.
Shani hakuwemo chumbani wakati huo.
Alimwambia abaki tu nje kwenye
gari kwani hakutarajia tukio kama hilo
kutokea wakati wa hafla ya ndani ya kampuni.
“Niache niende, Kimaro.” Lisa alimuuma
Willie kwa nguvu.
Willie aliachia mkono wake kwa
maumivu kisha akacheka. “Hakika
wewe ni mjanja. Hiyo inavutia. Napenda
wanawake wachangamfu kama wewe.”
“Una kichaa?” Lisa alishangaa, “familia ya Kimaro ni moja ya familia zenye
heshima kubwa. Sikutegemea kama
kuna mtu mwenye kuchukiza na mchafu
kama wewe katika familia yenu, au wewe si mtoto halisi wa familia ya Kimaro?” Lisa alikosoa.
“Endelea kunikosoa. Kadiri
unavyonikosoa, ndivyo nitakavyokuletea taabu zaidi.” Willie alidhihaki.
“Wakurugenzi wa kampuni yako wote wananichukulia kama mheshimiwa.
Jones Masawe ameniomba nimsaidie kupata nafasi ya mwenyekiti kesho.
Ninaweza kusema kitu kwa urahisi na kukufanya upoteze nafasi yako mara
moja. Unajua nina nguvu ya 25% ya hisa za kampuni. Kwa hivyo, nitafikiria upya ikiwa utanihudumia vizuri usiku wa leo.”
Akiwa na mawazo, Lisa alijifanya kuwa na hofu na kusema, “Hii ni kweli?”
“Bila shaka.” Willie alifoka, akijua kuwa
Lisa tayari alikuwa anaingia kwenye
anga zake.
"Lazima unisaidie, Bwana Kimaro," Lisa
alidakia na kusema kwa huruma,
“Vizuri sana kwa kuwa umeelewa. Unajua kilicho bora kwako. Njoo hapa
basi.” Willie alifungua mikono yake. Lisa akajitupa mikononi mwake. Harufu
ya kuburudisha ya mwili wake ilijaza pua yake. Kwake, umbo lake lilikuwa
bora zaidi kuliko la Lina. Moyo wa Willie
ulikuwa unawaka. Alipotaka
kumkumbatia kwa nguvu, alipigwa na nguvu kubwa.
Willie akainama kwa uchungu. Lisa
alikuwa amechukua kalamu ya
chuma kutoka kwenye mkoba wake na
kumchoma nayo Willie kwa nguvu
kwenye mbavu. Kalamu hiyo ilikuwa na
kichwa chembamba kilichopenya
kwenye nyama kama risasi. Willie
aliganda kwa maumivu na hakuweza
kusogea hata kidogo.
Lisa alivua viatu vyake virefu na
kumpiga usoni na mwilini kwa visigino
vikali vya viatu vyake. Alimpiga hadi
chini, na akaishia kuwa kama samaki
"naweza kukufanyia chochote."
aliyetolewa baharini na kuwekwa nchi
kavu, asiweze kusogea hata kidogo.
Baada ya kuona amefanikiwa kumdhibiti
Willie yeye mwenyewe, Lisa hakuwa na haja hata ya kumpigia Shani.
Baada ya kumpiga Willie, Lisa alishtuka
kuona uso wake umevimba. Alifikiria
kwa muda na kugundua kuwa alihitaji
kumfanyia zaidi ya hivyo, na akamvua
nguo zake pia.
“Unataka kufanya nini?” Willie alilalama
kwa uchungu. Siku zote ndiye aliyekuwa
akiwavua nguo wanawake. Yeye
kamwe hakuwahi kufikiri kuwa kuna siku
nguo zake zingekuja kuvuliwa na
mwanamke. Macho wake yalidhihirisha
ukali. Alitamani kumpasuapasua Lisa
lakini hata hivyo hakuwa na nguvu hata
kidogo ya kupinga kwani alipigwa
vibaya viatu vya mbavuni na usoni.
Baada ya kumvua nguo, Lisa alichukua
simu yake na kumpiga picha zaidi ya
kumi kutoka pembe tofauti. Alimtisha
kwa njia ya dharau, “Ikiwa utathubutu
kuniletea matatizo kuhusu kilichotokea leo, nitatupia picha zako hizi chafu
mtandaoni. Hebu tuone kama familia ya Kimaro inajali utu wao.”
“Wewe…” Willie alikasirika. Katika kipindi cha miaka 25 ya maisha yake, hakuna hata mwanamke mmoja aliyekuwa na ujasiri wa kumfanyia hivyo. “Nakuonya! Nitakushughulikia, Lisa."
“Na mimi nitakushughulikia pia.” Lisa alimjibu kwa dharau. “Ni mara yangu ya kwanza kuona mwili mbaya kama huu. Unakera na kuchukiza kama nini!"
Lisa akampa kidole cha kati na kuziitupa nguo na simu ya Willie dirishani. Baada ya hapo, alimburuta hadi chooni na kumfungia humo. Kisha Lisa alitoroka
kupitia dirishani ili kumfanya Lina asielewe chochote.
Willie alilala kwenye sakafu baridi ya choo kile akiwa uchi. Hata baada ya
kutumia muda mrefu kuomba msaada
kwa sauti dhaifu, hakuna mtu aliyekuja kumsaidia. Ni baada ya nusu saa kupita ndipo
alianza kupata nguvu. Alitetemeka huku akinyanyuka na kuufungua mlango kwa nguvu. Baada ya kusikia kelele, Lina alikimbia kwa uangalifu kuelekea kwenye chumba hicho na kufungua mlango.
Pindi alipouona tu uso wa Willie uliojeruhiwa, alipiga kelele kwa mshtuko. “Imekuwaje tena mpenzi…”
“Nyamaza, mpuuzi wewe!” Willie
alimpiga Lina kibao cha usoni na kumpiga mateke machache dhaifu kwa hasira. “Nilikuwa nakuita sasa hivi.
Ulikuwa kiziwi?”
“Usinipige, mimi sikusikia. Niliogopa kukusumbua, na nilikuwa nimesimama mbali sana… Ohoo-hoo!” Lina alipiga magoti na kumsihi. Mwanaume huyo
alitisha sana alipokuwa na Lina, utadhani si yeye aliyekuwa kama panzi
mbele ya Lisa muda mchache uliopita.
Willie alianza kutetemeka tena. Kwa hasira alifoka na kuapa, “Lisa, nikishindwa kukuua, nitakula mavi yangu!”
Sura ya 122
Alvin, ambaye alikuwa na mkutano wa video katika chumba chake cha maktaba, alisikia sauti ya gari kutoka chini. Wakati huo alikuwa anasikiliza mipango mbalimbali ya maendeleo ya miradi yake. "Mpango huu hauwezekani. Njoo na mwingine."
Alipomaliza tu kuongea, alikatisha mkutano na kuelekea chini.
Akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa, Lisa akaingia mlangoni. Alisahau hata
kubadili viatu vyake. Alvin alikodoa
macho na kutazama gauni lake refu
jeusi. Alionekana kuvurugwa tofauti na alivyoondoka.
"Potea, wewe huna maana kabisa!"
Akiwa amekunja uso, Alvin alimtupia macho ya mshangao na udadisi Lisa.
Alipoyaelekeza macho yake chini, ghafla aliona ufa kwenye pindo za gauni
lake. “Mbona nguo yako imetatuka?” Macho yake meusi yalikuwa yakimtazama kama mshale.
Alipojitazama tu chini ndipo alipogundua. Labda nguo hiyo ilikuwa
imeshikana na kitu chenye ncha kali
alipotambaa nje ya dirisha kutoka
kwenye chumba kile cha hoteli.
“Nilinasa sehemu kwa bahati mbaya.”
Lisa aligeuza macho yake, hakutaka
ajue kwamba alikuwa amemchokoza
Willie Kimaro. Hata hivyo hakujua
kabisa kama wana uhusiano wa aina
yoyote. Kwa mawazo yake, Alvin
alikuwa wakili tu, na asingekuwa na
uwezo wa kuwa na uhusiano wowote na
familia tajiri ya Kimaro. Alijua ni majina ya ukoo tu ndiyo yamefanana.
"Una tabia mbaya ya kunitazama kila wakati unaposema uwongo." Alvin
alishika kiuno chake chembamba kwa nguvu, macho yake meusi yakionyesha hisia kali ya ukali. “Ulihudhuria sherehe ya ukumbusho usiku wa leo, sivyo?
Nani alikuletea shida?”
“Hakuna aliyenifanya chochote. Haya, nani anaweza kunigusa wakati mimi ni mwenyekiti?” Lisa alimsukuma na kwenda juu. “Naenda kuoga."
"Usinifiche Lisa." Alvin akamvuta
kuelekea kwake tena. “Angalia jinsi ulivyokosa amani kwa sasa. Afadhali
unieleze ukweli kama unanichukulia
kama mume wako.”
Lisa alipiga kelele, na macho yake
yakawa mekundu licha ya yeye
mwenyewe kupenda. “Nimemkosea mtu
ambaye sikupaswa kumkosea katika
ulimwengu mzima wa kibiashara.
Alvlisa, kama… Ikiwa… mtu huyo ananilenga, usithubutu kufikiria
kunisaidia. Afadhali unikane kabisa
kuliko kunisaidia vinginevyo utapoteza
kila kitu. Yeye si sawa na Clark
Zongo…”
Alvin aliinua macho yake na kuuliza.
“Unaamaanisha nani huyo anaweza kunitisha mimi?”
"Willie Kimaro, kutoka familia ya
Kimaro." Lisa alisema huku akihema.
“Biashara zao kubwakubwa
zimetapakaa kwenye ukanda wa Afrika
Mashariki yote, pia wanamiliki asilimia
25 za hisa za Mawenzi.”
Alvin alishindwa cha kusema. Hilo
lilimshangaza sana. Tangu lini Willie, yule bwana mdogo mpuuzi tu, akawa
mtu ambaye kwa hakika anaogopwa
kiasi kile na matajiri wa Dar es Salaam? Ina maana Lisa hakumchukulia
yeye kama mtu mwenye nguvu?
Anyway, halikuwa kosa lake kwa
sababu alimficha utambulisho wake halisi.
“Umeshtuka sana?” Lisa alituliza baada ya kumuona Alvin akiwa kimya sana, hivyo mara moja akamfariji. “Lakini usijali. Kwa bahati nzuri, nilikuwa na kalamu ya chuma kwenye mkoba, alipojaribu kunivamia chumbani
nilimchoma na kalamu kwenye mbavu akaanguka, nikampiga sana na visigino vya viatu. Kisha, nilimvua nguo zake na kumpiga picha…”
“Ulimvua nguo?”
Macho ya Alvin
yalionyesha hasira na huzuni, na
kusababisha hali ya mazingira kuwa tata ghafla.
"Ah ... nilikuwa najaribu kumtisha tu akae mbali na mimi, nimemwambia akijaribu kunifuatilia wakati mwingine nitamdharirisha mtandaoni." Kwa kupoteza, Lisa alieleza, “Sikuwa na la kufanya. Unafikiri nitakuwa nimekosea sana?”
“Una akili?” Alvin alishusha pumzi ndefu huku akihofia kuwa angepatwa na wazimu. “Kwa hiyo umeona na nanihii yake?”
Akiwa chini ya macho ya hatari ya mwanaume huyo, Lisa alikuna kichwa na kukohoa kidogo. "
Eeh..Aah..Hapana. Inachukiza. Yeye ni ngozi na mifupa tu, na umbile lake si zuri kama lako pia. Kinyume chake, wewe ni mrefu na umejengwa vizuri.
Ninapokutazama, ninavutiwa na wewe.
Kukutazama kwa mara ya pili
kunanipaga wazimu kwe—”
“Nakupandisha
ya Alvin yalimtoka huku akivaa tabasamu la sifa.
Lisa alijisikia mkanganyiko wa kimawazo. Akijihisi hana cha kusema, alimwambia, “Sasa si wakati wa kuzungumzia jambo hili…”
“Nipe simu yako.” Alvin alinyoosha mkono wake kuelekea kwake.
Mara moja akampitishia simu yake.
Alvin alipozitazama zile picha alizidi kusononeka. Muda mfupi baadaye, alihamishia picha hizo kwake na kuziondoa zote kwenye simu ya Lisa.
“Haya, kwanini umezifuta…” Lisa alikosa raha.
"Kama mwanamke wangu, huoni aibu
kuweka picha za mwanamume
mwingine kwenye simu yako?" Akiwa
anamwangalia kwa ukali, alionya, "tena
wazimu?” Macho meusi
umepiga picha ukiwa umezingatia
kabisa sehemu zake za siri!" Lisa alikosa la kusema. Aliinamisha kichwa
chini bila kutamka neno lolote.
“Nenda ghorofani ukalale. Usifikirie mambo kupita kiasi kwani tayari
umempiga picha kama hizo. Familia ya Kimaro inajali sana hadhi yao,
hawawezi kukuacha salama pindi utakapozisambaza picha hizi.” Alvin
alisema kile ambacho hakumaanisha kumfariji.
“Kweli?” Lisa alikuwa na shaka juu
yake. "Lakini sidhani kama Willie ni mtu anayejali hadhi ya familia yake.
Anastahili kutendewa vibaya kama hivyo. Nilimpiga vibaya sana.”
“Hujui ni kiasi gani wanaume wanajali
utu wao ikilinganishwa na wanawake.
Wewe si mwanaume, kwa hivyo
hutaelewa. Naamini hatakuwa na ujasiri
wa kukutafuta. Umelishughulikia jambo
hili vizuri sana,” Alvin aling’oa risasi na kuendelea kueleza kimafumbo.
Ni mara chache alimpongeza Lisa. Kwa hivyo Lisa alishtuka kidogo aliposikia pongezi zake. Labda Alvin alikuwa sahihi. Huenda alikuwa haelewi kabisa wanaume.
"Baada ya kusema hivyo, usivue nguo za mwanaume tena." Baada ya kutulia, Alvin alimuonya kwa huzuni, "Bila shaka, isipokuwa mimi tu." Lisa
alishindwa cha kusema na kubaki anacheka tu.
“Nenda ukaoge. nitakusaidia kwa hilo.”
Alvin hakujali macho yake ya kusema, akauweka mkono wake kiunoni na kumbeba juu juu moja kwa moja.
“Sitaki." Lisa alipiga kelele kwa aibu.
Alikuwa ameweka wasiwasi na hofu
nyuma yake.
Usiku, ilimchukua Alvin muda kutafuta usingizi wake bila mafanikio. Mwishowe aliamua kushuka chini, akaingia kwenye gari na kuondoka kwenye nyumba yake ya kifahari.
•••
Usiku wa manane, Willie alirudi hotelini baada ya kufungwa majeraha yake hospitalini. Kwa hasira kali, akatoa simu yake ili apige.
"Kwa ndoano au kwa hila, nyinyi watu lazima mumtie Lisa kuzimu. Sitaki kusikia anaendelea kuishi mbwa yule.”
Alipomaliza tu kuongea, mlango ukasikika ukigonwa kwa nguvu. “Ni nani huyo mwenye kelele anayebisha saa za usiku hivi? Una hamu ya kifo, huh?"
Willie alikimbia kuelekea mlangoni ili
kuufungua, lakini akafunikwa na gunia.
Ghafla, mtu fulani alianza kumpiga.
Mtu huyo alikuwa mkatili na mkali.
Aliendelea kuupiga teke mwili wa Willie kwa nguvu. Wakati gunia liliipofunuliwa.
Mtu mrefu na mpana aliingia ndani. Mwanaume huyo alikuwa amevalia
sweta nyeusi. Vipengele vyake vya kuvutia vilipoainishwa chini ya taa zenye
giza kwenye chumba, Willie alihisi hofu na hali ya hatari iliyouzunguka mwili
wake.
“Alvin… Hapana, ninamaanisha kaka
Alvin. Kwa nini… Kwa nini uko hapa?”
Willie angeweza kumtambua mara ya kwanza. Kwake, mtu huyo
alifananishwa na shetani. Alikuwa
mwanaume pekee katika familia nzima ya Kimaro ambaye Willie alikuwa anamuogopa.
"Umekuwa ukifanya kazi na Jack
Kimaro hivi karibuni lakini hukujua
nilipo?" Huku mikono yake ikiwa
mfukoni, Alvin aliingia ndani kwa
majivuno na kumkanyaga Willie kifuani.
Willie alitetemeka kwa hofu. “Kaka
Alvin, sijui unasemaje. Ndiyo, ni Jack ambaye amekuwa akisimamia KIM
International hivi karibuni, lakini… Lakini sote tunafahamu kuwa uwepo wako
katika kampuni ni wa umuhimu mkubwa. Kwa kweli, wewe ndiye bosi wa KIM International.”
"Ujuzi wako wa kuongea maneno ya kuhadaa umeongezeka. Hivi ndivyo unavyofanya mbele ya Jack pia?" Alvin
alimpiga teke Willie kidevu kwa madaha kwa kutumia ncha ya kiatu chake. “Bado ninakumbuka mambo yote ambayo baba yako alifanya. Alimsaidia Jack kushusha cheo changu.”
“Hapana, kaka Alvin. Sote tunakungoja.”
Willie aliogopa sana kufanya kelele yoyote.
"Mnaningojea wapi wakati umekuja Dar es Salaama kimyakimya kukagua
biashara na kufanya mipango ya
kupanua uwekezaji?" Sura ya dharau
iliosha usoni mwa Alvin. "Mnajaribu
kubadilisha teknolojia za kimsingi za
kampuni wakati mimi sipo karibu, huh?"
Sura ya 123
Huku akiendelea kumkaripia kwa hasira, Alvin alikanyaga kifua cha Willie. "Leo, umeonekana kuwa wa kushangaza
sana huko kwenye sherehe za
Mawenzi, huh? Kwa tabia zako chafu, unawezaje kuthubutu kuanzisha fujo
huko hotelini? Huenda usijali kupoteza
sifa yako, lakini familia ya Kimaro inajali
sana hadhi yake. Unajichukulia kama
bosi wa KIM international na kisha
unatumia nafasi hiyo kufanya mambo ya hovyo ya kushusha hadhi ya kampuni?"
“Kaka Alvin, najua ni kosa langu.
Sitafanya tena,” Willie aliendelea
kumsihi kwa woga.
"Hapana. Nadhani wewe ni jasiri sana.
Unathubutu hata kujaribu kupata kipande cha mapenzi ya mwanamke wangu.” Alvin alicheka kwa huzuni.
Willie alipigwa na butwaa. "Lina ni mwanamke wako?"
"Sitavutiwa na mwanamke mchafu wa aina hiyo." Alvin akainama taratibu na kuchuchumaa. Macho yake ghafla
yakageuka kuwa makali sana.
Akiwa amepigwa na mawazo, Willie akauliza kwa mshangao, “Unamaanisha… Lisa…?”
“Ni vizuri kwamba unamkumbuka.
Sipendi kudhani kwamba nilimuonea mtu asiye na hatia baada ya kumalizana na wewe.” Alvin akajiweka sawa.
Willie alifahamu mbinu ambayo Alvin
angetumia. Akiwa amechoka, mara
akatambaa kwa shida. Alipiga magoti
sakafuni na kumsujudia Alvin. “Pole, kaka Alvin! Kwa kweli sikujua. Ni kosa langu. Nilikuwa kipofu. Tafadhali niruhusu niachane na…”
Alvin alimpiga teke kali hadi akajibamiza ukutani. Willie alitema damu iliyojaa mdomoni. "Kwa kuwa huwezi kudhibiti hiyo sehemu yako ndogo ya mwili, wacha tuiondoe kabisa..." Alvin akapiga hatua kuelekea kwake.
"Hapana." Willie alitetemeka kwenye buti zake. “Kaka Alvin, sitarudia tena. Ukiharibu, bibi yangu ataumia moyoni kwani ananipenda. Pia Babu atakasirika.”
"Sawa, niambie ninachoweza kufanya ili nifikirie kukusamehe." Alvin alimkanyaga kwa nguvu kwenye
‘jongoo’ lake.
Machozi yalitiririka usoni mwa Willie
kutokana na maumivu. Akiwa ameshikilia sehemu ya chini ya suruali ya Alvin, aliomba na kusihi, “Hapana, hapana. Naweza kufanya vile
unavyotaka. Nitapiga magoti na kuomba msamaha kwa Lisa kesho.”
“Sawa. Kumbuka ulichosema.” Alvin
aligeuza kichwa chake na kumwambia mtumishi wake wa chini, “Kwa vile
anafurahia kufanya wanawake vibaya, vua nguo zake na umpeleke kwenye
kibaraza. Wacha apigwe na upepo baridi wa baharini usiku kucha, labda
ataikumbuka siku ya leo kila atakapokuwa anafikiria kufanya ujinga.”
Mtetemeko ulishuka kwenye uti wa
mgongo wa Willie. Kabla ya hapo, Lisa
alikuwa amemvua nguo na kumwacha
amelala kwenye sakafu ya choo kwa
muda wa nusu saa, na kumfanya
ashikwe na baridi. Mbaya zaidi alikuwa
anaenda kupigwa na upepo wa baharini
kwa usiku mzima. Ilikuwa ni saa sita usiku na dakika kadhaa. Wawili hao
walikuwa wakatili kwelikweli.
“Kaka Alvin, nitaganda hadi kufa.” Willie alijitetea.
“Usijali. Kwa kuzingatia kuwa wewe ni binamu yangu, sitakuacha ufe.
Ambulance ya hoteli hii iko kwenye
standby hapo chini. Utaokolewa mara moja ukibaki na pumzi yako ya mwisho."
Alvin akampiga bega huku
akimkumbusha kwa sauti ya upole. Kwa
hayo, aligeuka na kuondoka.
Willie alikuwa kwenye hatihati ya kuanguka. Aliapa kwamba
hatamchokoza Lisa tena.
•••
Saa mbili kamili asubuhi, Lisa alipokuwa
akiandaa kifungua kinywa jikoni, alipokea simu kutoka kwa Chris
Maganga. "Lisa, wakurugenzi wanataka kufanya mkutano mkuu wa dharura leo asubuhi." Chris alieleza. “Wanadai kwamba ulimpiga Bwana Kimaro jana usiku, kwa hivyo wanaomba ufukuzwe kwenye nafasi yako ya mwenyekiti. Pia, ikiwa hautapiga magoti na kuomba msamaha kwa Bwana Kimaro, watakuondoa kwenye bodi ya wakurugenzi pia."
Lisa aliondoa apron yake mara moja. “Nakuja sasa hivi.” Alipokata simu, alielekea mlangoni kama upepo.
“Kifungua kinywa changu kiko wapi?”
Akiwa amevalia nguo za kulalia nyeusi, Alvin alitokea akishuka chini kivivu huku
akipiga miayo. Haijalishi alivaa nini, alikuwa akivutia tu kwa macho kutokana na umbile lake lenye nguvu.
"Kuna jambo la dharura limetokea ofisini. Shangazi Linda atakuja
kukuandalia.” Lisa alibadilisha viatu
vyake haraka na kukimbilia nje ya jumba hilo. Ndita za Alvin zilijikunja
sana. Ilikuwa ni muda mrefu sana tangu apate kifungua kinywa kilichoandaliwa naye.
Saa mbili na nusu asubuhi Katika
chumba cha mkutano, wakurugenzi
wote walikuwa na nyuso za huzuni na zenye hasira. Kwa kutajwa kwa Lisa, walitamani kumla.
"Chris ndiye wa kulaumiwa kwa jambo hili. Kama asingemtetea Lisa na kuwa
mwenyekiti, Mawenzi Investments isingeiudhi familia ya Kimaro."
“Amerukwa na akili? Alithubutu vipi
kumpiga Willie? Kimaro ni familia
mashuhuri, na kwa wazi hatuwezi
kumudu kuwachokoza.”
"Nilisikia mtu ambaye alimuudhi Willie
kabla ya huyu alikuwa bilionea kutoka
Kenya. Familia yake ilifilisika kwa
usikummoja tu.”
“Ndiyo. Willie anatisha."
Katikati ya majadiliano ya wakurugenzi, Jones Masawe alishusha pumzi ndefu.
“Yote ni makosa yangu. Sikupaswa kumruhusu Lina kumleta Willie jana.
Lakini nilisikia Willie alikuja hapa kwa
ajili ya ukaguzi, na nilikuwa na
matumaini kwamba Mawenzi
Investments ingeweza kufanya kazi na KIM International.”
“Kweli. Ikiwa tungeweza kushirikiana na KIM International, ingeinufaisha sana
Mawenzi Investments.
“Tulikosea. Tungemfanya Jones kuwa mwenyekiti.”
“Najutia uamuzi wangu pia. Sikupaswa
kumpigia kura Lisa wakati huo.”
Akihisi mnyonge, Mkurugenzi Amiri alisema, “Sasa kwa vile mambo
yamekuwa hivi, hatuna chaguo ila
kumwondoa katika nafasi yake ya
mwenyekiti kwa ajili ya matarajio ya Mawenzi Investments. Labda Jones
ndiye pekee anayeweza kutusaidia kukabiliana na dhoruba wakati huu.
Baada ya yote, binti yake ana uhusiano wa karibu na Willie.
Jones alipunga mkono kwa
unyenyekevu. “Sina hakika kama
naweza kusuluhisha hili. Baada ya
kusema hivyo, Bwana Kimaro
anampenda sana Lina. Ataenda naye
popote aendako. Una maoni gani, Lina?"
Akivumilia maumivu kutoka kwenye
majeraha yake ya sehemu za siri
yaliyosababishwa na Willie jana yake, Lina alilazimisha tabasamu tamu.
"Bwana
Hata aliniambia mambo mengi kuhusu mradi huo.”
Kila mtu alishangilia kwa furaha.
Mkurugenzi Amiri alisema, "Ni mpango wetu sasa. Jones atakuwa mwenyekiti wetu mpya.”
Lisa aliusukuma mlango na kujipenyeza ndani. Macho ya wazi na makali yaliwakumba wakurugenzi wote.
“Kwangu, ninyi nyote ni wakurugenzi wa
Mawenzi Investments, ambao pia mnachukuliwa kuwa wazee wangu.
Nilimpiga Willie jana usiku, ndiyo! Lakini kuna yeyote kati yenu aliyeniuliza kwa nini nilifanya hivyo?” Kila mtu alipigwa na butwaa.
Lisa aliongeza kwa hasira, “Jana usiku,
Willie alinifungia kwenye chumba changu cha hoteli na karibu kunibaka.
Lina alisimama nje ili kumsaidia
Kimaro ananipenda sana.
kufuatilia hali ya nje. Kwa sababu ya
njama yao chafu, mimi, kama
mwenyekiti wa Mawenzi Investments, nilikuwa karibu kuharibiwa. Kwa nini?
Kwa sababu Willie ni mjanja na hajali
kabisa. Hakuwa tu anajaribu
kunidhalilisha mimi bali pia Mawenzi
Investments nzima.”
'Hilo ni jambo lisilo na akili kwa Willie," mkurugenzi alinong'ona.
“Vipi Lina anathubutu vipi kufanya vile?!
Hiyo inatisha.”
“Sikufanya hivyo. Lina alisimama mara
moja. “Wewe ndiye uliyetaka
kumtongoza Bwana Kimaro, lakini
hakuwa na hamu na wewe. Anaweza
kupata mwanamke yeyote anayemtaka
kwa urahisi. Kwa nini atake
kujilazimisha kwako?”
Jones alisema kwa mzaha, “Hata
waandishi walikupiga picha ukiwa
umemshika Bwana Kimaro kwa mkono wake kwenye lango la hoteli jana usiku.
Hata hivyo, Bwana Kimaro alidai kuwa ulimvua nguo.
"Ni aibu kama nini!"
"Ni aibu kubwa kuwa na mkurugenzi kama huyu Mawenzi Investments." Kila mtu alimtazama Lisa kwa dharau.
Mkurugenzi Amiri alikunja uso na kusema. “Acha kujitetea. Umeingia kwenye matatizo makubwa wakati huu.
Tunataka tu kuilinda Mawenzi Investments. Kwa kuwa lilikuwa ni kosa
lako, unapaswa kubeba jukumu.
Kusema kweli, huwezi tena kukaa katika kampuni tena.”
Mdomo wa Lisa ulitetemeka kwa kejeli
huku macho yake yakionyesha sura ya jeuri. "Kwa hivyo mnapanga kunifukuza
kutoka kwenye bodi ya wakurugenzi?"
Jones alitabasamu kwa dharau. “Hilo
ndilo jambo pekee tunaloweza kufanya.
Afadhali ufungashe na kuondoka sasa
hivi.”
Lisa alidondosha macho yake. Alikuwa amechanganyikiwa kabisa na kampuni
hiyo. Wakati huo, mfanyakazi mmoja
alikimbia ndani na kupiga kelele, "Willie
yuko hapa! Sasa yuko chini, na anataka kukutana na Mwenyekiti Jones.”
Sura ya 124
"Nilijua Bwana Kimaro angefanya jambo
kuhusu hilo." Jones Masawe
alimwonyesha kidoleLisa na kumwambia, "Tazama, Bwana Kimaro
yuko hapa sasa. Afadhali umalizane
naye peke yako.”
"Usiende kinyume naye kamwe." Lina
alijaribu kumpiga teke alipokuwa chini.
"Ikiwa utamkosea tena Bwana Kimaro, hata mimi sitaweza kumtuliza kwa niaba yako."
"Hebu tumshike tu na kumpeleka chini."
Pendekezo la Jones lilikubaliwa mara moja na wengi.
Maofisa usalama wanne hadi watano
mara moja wakatembea kuelekea kwa
Lisa. Akiwa amekunja uso, Shani
akawazuia mbele ya Lisa. "Ikiwa nyinyi watu mtathubutu kumgusa, msinilaumu kwa kukosa adabu."
“Nyie mnangoja nini? Washikeni wawili hao sasa hivi." Jones Masawe bado
alimchukia Shani kwa kumpiga teke siku
nyingine. Sasa ikaja nafasi ya kulipiza
kisasi kwake.
Lisa alipogundua kwamba
wangepigana, alimzuia Shani. “Ni sawa.
Hakuna haja ya kunishika. Nitaenda
huko peke yangu." Mara tu alipomaliza
kusema, alikuwa wa kwanza kutoka
kwenye chumba cha mikutano.
Lina alipendekeza, “Twendeni
tukaangalie pia. Ni afadhali kujionea kuliko kusimuliwa.”
“Kweli. Hata hivyo, inabidi tumzuie asimkasirishe Bwana Kimaro zaidi.”
Kila mtu alishuka pia. Wakaelekea
kwenye chumba cha mapokezi pale chini. Akiwa amefungwa bandeji nene
chini, Bwana Kimaro alikuwa
amejikunyata huku akiwa ameshikilia
kikombe cha kahawa ya moto. Kutoka kwa sura ya uso wake mzuri, ilionekana
wazi kuwa alikuwa ameshikwa na homa na kuugua. Lisa alipofikiria juu ya tukio la Willie
akiwa amelala kwenye sakafu ya choo
akiwa amevua nguo zake jana yake
usiku, hakuwa na uhakika ni muda gani
alikuwa amepatwa na homa hiyo.
Pengine alishikwa na homa kwa sababu ya tukio hilo, ambalo lilimfanya akose
raha kabisa. Kwa kweli alihisi kwamba mtu asiye na haya kama Willie huenda
asisumbuliwe kuhusu picha hizo.
Lisa hakuwa na wasiwasi juu yake mwenyewe kwa vile hakuwa na ndugu
pia. Hakukuwa na kitu kingine chochote alichokuwa na wasiwasi nacho, isipokuwa kwamba Alvin angeweza kuvutwa kwenye matatizo tena.
"Samahani sana, Bwana Kimaro."
Jones Masawe alimsogelea na kisha
akainamisha kichwa kwa kumwomba
msamaha kwanza. “Natumai utakuwa
mkarimu wa kutusamehe. Usitazame
kiwango cha makosa yetu.”
“Hasa.” Mkurugenzi Amiri aliongeza
mara moja, "Tumemfukuza Lisa kutoka
kwenye nafasi ya mwenyekiti na
kumfukuza kutoka bodi ya wakurugenzi."
Willie Kimaro alikuwa ameganda tu, na moyo wake ulikuwa ukitetemeka kwa
nguvu. Aliinua kichwa chake huku macho yakiwa yametapakaa damu.
"Kwa hiyo yeye si mwenyekiti tena?"
“Ndiyo.” Jones alisema kwa uungwana, “Ni kwa sababu alikudhalilisha.
Hatukufikiri Lisa angekuwa na ujasiri wa kukufungia kwenye chumba na kukutongoza. Hiyo haikuwa aibu kwake.” Bila shaka, Jones alijua ukweli
vizuri. Hata hivyo, ili kumpa Willie njia ya kutoka, alimshtaki Lisa huku akiamini
kwamba Willie angemshukuru.
Alipokuwa akiwaza kabla hajaongea, Willie alimuangaza kwa hasira. Kabla
Jones hajapata fahamu zake, Willie aliinua mguu wake na kumpiga teke
kali. “Nani aliwaambia nyie kumfukuza
Lisa kwenye nafasi hiyo? Nani alisema
kuwa alinitongoza? Nyinyi mnajaribu
kuniletea matatizo!” Willie alimpiga teke
Jones Masawe kwenye mwili wake kwa
nguvu. Alikuja kuchelewa sana kuokoa
hali hiyo. Ikiwa Alvin angejua kuhusu
hilo, labda angepoteza maisha yake
kabisa.
Kila mtu alishtuka sana, na hata Lisa pia. Lina akapiga kelele. Alimkimbilia
Willie kwa haraka na kumshika mkono.
“Acha kumpiga teke, Bwana Kimaro.
Huyu ni baba yangu—”
“Nyamaza, btch!” Willie alimpiga kofi usoni, na baadaye akaanguka chini.
"Yote ni kazi yako. F*ck! Ninachojutia
zaidi ni kukufahamu wewe malaya mkubwa!”
Kama si Lina, Willie asingemkasirisha
Lisa, akifuatiwa na Alvin. Licha ya
kupigwa na kjeruhiwa, alikabiliwa na
upepo wa baridi wa usiku kucha kwenye
kibaraza cha hoteli kwa muda wote wa jana yake usiku. Akiwa ameganda kwa
baridi, karibu apate hamu ya kuruka
kutoka kwenye jengo ili kumaliza mateso yake. "Unafanya nini, Bwana Kimaro?" Lina alihisi kizunguzungu baada ya kupigwa kofi hadharani. Alipokuwa na Willie kwa
siku chache zile, Willie alijifurahisha
naye kila siku. Alimfanya na kumgeuza kwa jinsi alivyotaka. Akitaka kwa bibi, twende! Akitaka kwa mpalange twende!
Akitaka mdomoni, haya! Alifanya hayo
yote kwa nia moja tu ya kujisaidia yeye na Jones kubadilisha mambo katika kampuni.
Hata hivyo, kabla ya kumfanya Lisa
ajifunze somo lake, badala yake yeye
ndiye aliyepigwa.
Akiwa na huzuni, Lina alilia. “Bwana
Kimaro, alikuwa Lisa. Yeye ndiye
aliyekuumiza.”
“Najua. Sihitaji uniambie.” Macho ya Willie yakatulia kwa Lisa.
Moyo wa Lisa ulimshtua. Haraka akatoa simu yake na kuizungusha kama
ukumbusho kwake. “Bwana Kimaro, wewe—”
“Bi Jones, kuhusu tukio la jana usiku, lilikuwa kosa langu.” Willie alimsogelea na kumuomba msamaha wa dhati.
Umati ukakosa la kusema. Lisa naye alishindwa cha kusema. Alipigwa na butwaa kabisa. Kumbe kutumia picha
zake zisizo na heshima kumtishia
ilifanya kazi? Kweli Alvin alikuwa sahihi, familia ya Kimaro walikuwa wanajali
zaidi kuhusu utu wao. Hawakuweza
kumudu kuipoteza heshima yao.
Lina na Jones walipapasa macho yao
kwa nguvu. Walitilia shaka sana ikiwa
macho yao yalikuwa yanawadanganya.
"Bwana Kimaro, nadhani umekosea."
Lina akaongeza ujasiri wake tena na
kuvuta upindo wa shati la Willie.
"Umesahau jana usiku"
“Funga mdomo wako!” Akihisi kukosa subira, Willie alimpiga Lina teke.
“Nilikukera kwa bahati mbaya baada ya
kulewa jana usiku, Bi Jones. Samahani kwa tabia ya ghafla na ya kimbelembele. Mimi ni fisadi ambaye sistahili kuwa binadamu. Bahati nzuri
uliniamsha kwa kunipiga, au ningeharibu sifa ya familia ya Kimaro na kuwadhalilisha wazee wangu.”
Umati ulishangaa na kuhisi kuwa
ulimwengu umegeuka kuwa ndoto. Lisa
alipepesa macho na kumtazama Willie
kwa makini. Je, ilikuwa ni kalamu ya
chuma aliyomchoma mbavuni jana yake
usiku ambayo ilikuwa imeharibu ubongo
wake, au? Alikumbuka vizuri kwamba
hakuwa amelewa jana yake usiku.
Ingawa alikuwa na picha za kumtishia, hakuhitaji kuwa na tabia ya unyenyekevu hivyo.
Mkurugenzi Amiri alikuwa mwishoni mwa akili yake. “Lakini sisi…”
“Lakini nini? Nyinyi watu mnawezaje
kuthubutu kumfukuza Lisa kwenye
nafasi ya mwenyekiti na kumfukuza nje ya bodi ya wakurugenzi?!” Macho ya Willie yakawa magumu huku
akiwatazama wakurugenzi. “hivi nyinyi
wazee mnafikiri kwamba bado mna
nguvu sana na hamwezi kufikiria
kustaafu? Au mnafikiri kwamba bila
nyinyi Mawenzi Investments itafilisika?"
Wakurugenzi walitetemeka na
hawakuhisi kwamba walikuwa na umri
wa kutosha kustaafu bado. Bado
walipanga kufanya kazi kwa miaka kumi
hadi 20 kwenye kampuni.
"Bwana Kimaro, tulikuwa bado hatujalipisha hilo," Mkurugenzi Amiri
alisema mara moja kwa sauti ya kutetemeka, "Hakufukuzwa kazi yake.
Yeye bado ni mwenyekiti, na hii haitabadilika kamwe.”
Mwili wa Jones ulitetemeka. Akiwa
amezidiwa na hali ya kutokuamini, alinguruma kwa fadhaa. "Unasema nini, Amiri Gumbo? Nyinyi mlinichagua kama mwenyekiti asubuhi ya leo!”
Mkurugenzi Levy alimtazama kwa
hasira. "Wewe na binti yako ndio mlidai
kuwa Bibi Jones alimkosea Bwana
Kimaro. Kumbe haikuwa hivyo.
Hatuwezi kufanya lolote kwa sasa.”
“Hasa.” Wakurugenzi wakaanza
kumgeuka. "Kila mtu anajua kwamba una tamaa ya
kuwa mwenyekiti, lakini haukupaswa
kupeleka mambo mbali sana huku ukipuuza utu wako." mwingine
akamshushua.
"Hata hivyo, Lisa ni sehemu ya familia ya Jones. Hukupaswa kumtendea ukatili
hivyo.” Wanahisa walianza kumwambia Jones. Jones na Lina walionekana
wameanguka kutoka mbinguni hadi kuzimu. Kwa hasira, Jones alimfokea
Lina, "Ni nini kinaendelea duniani?!"
"Sijui." Lina alikuwa ameduwaa, akishangaa kwa nini kila kitu kilikuwa
kimebadilika kabisa usiku mmoja.
Lina ndiye aliyesema kwamba alikuwa
amemweka Willie kwenye kiganja cha
mkono wake. Yeye ndiye aliyesema
kwamba Willie angewasaidia. Yeye
ndiye aliyesema kwamba Willie
alimchukia sana Lisa hivi kwamba
asingeweza kungoja kumuua.
Kwa sura ya kusihi, macho yake yakatua kwa Willie. “Bwana Kimaro, Lisa alikuroga au? Si ulisema hivyo... unanipenda sana?”
Sura ya 125
"Ninakupenda?" Mwitikio wa Willie ulikuwa kana kwamba alisikia mzaha.
“Uliingia kitandani kwangu licha ya kuwa una mpenzi. Unafikiri ningekuacha bure? Huna tofauti na makahaba
wanaojiuza huko nje.” Kofi lilitua kwenye
shavu lake, lakini safari hii, lilionekana
kuwa limetua moyoni mwake pia. Lina
karibu aanguke chini kabisa.
Kulikuwa na idadi kubwa ya watu karibu
naye, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi
na wanahisa wa Mawenzi Investments.
Hali hiyo ilikuwa imezua tafrani
miongoni mwao, wakamtazama kwa
dharau. “Sikutarajia angekuwa mtu wa aina hii.
Kabla ya hili, alinipa hisia ya kuwa safi na mtukufu.” Mnong’ono ulisikika.
“Ndiyo. Wanaume wengi katika kampuni
walimwona kama mungu wa kike.”
Mwinginea naye akatoa yake.
“Bahati nzuri sikumtambulisha kwa
mwanangu. Hakika hana aibu.”
Katikati ya fedheha ya mara kwa mara, uso wa Lina ulibadilika rangi. Alikuwa
ameweka juhudi nyingi katika kujenga
sifa ya kuvutia kabla ya hii, lakini yote
iliharibiwa wakati huo.
Kama mwanaye, Jones Masawe
alitetemeka kwa aibu. “Umeenda mbali
sana, Bwana Kimaro. Lina anakupenda
kweli. Alianguka kwa ajili yako mara ya kwanza.”
Bila kutarajia, Willie aliangua kicheko kana kwamba maneno ya Jones
yalikuwa ya mzaha. “Anapenda nini kuhusu mimi? Kusema ukweli, baada ya
kuwa na wanawake wengi, ninatambua kwamba yeye ndiye mwanamke
mlegevu zaidi. Bwana Jones, ninafurahia jinsi unavyomchukulia binti
yako kama kitu kwa ajili ya mali na mamlaka.”
Matamshi hayo yalibadilisha mtazamo wa umma kuhusu Lina na Jones kwa
mara nyingine tena. Lisa, ambaye
alikuwa akitazama tu tukio hilo, naye alishangaa. Hakushangaa kwamba
Willie alikuwa mpotovu, kilichomshtua zaidi ni kwamba Lina aliweza kukubali.
Lisa alitoa kikohozi chepesi kisha
akatabasamu na kumtazama Lina.
“Dada siwezi kujizuia kukuona kwa
mtazamo tofauti sasa. Je, wakati huo
ulinipokonya Ethan kwa kutumia mbinu
kama hiyo?” Swali hilo liliukumbusha mara moja umma wa watu kuhusu
uhusiano wa awali wa Lina na Ethan.
Kila mtu alimtazama Lina kwa unyonge sana. Hata walijiweka mbali naye, wakiogopa kwamba angewachafua.
Kutetemeka kulitawala mwili mzima wa
Lina. Alitoa macho yake moja kwa moja, akijifanya kuzimia kwa hasira kali.
“Linal” Jones alimbeba upesi na kutoka
ukumbini kwa aibu.
Willie alikunja uso. Kisha akageuza
kichwa chake na kumtazama Lisa.
"Alikuwa na mpenzi hapo awali?"
“Ndiyo. Hata wakachumbiana kwa
sherehe kubwa. Hata hivyo, mara moja
alimlenga mtu mwingine kwa sababu
mpenzi wake wa zamani aliondolewa
kwenye madaraka ya kampuni.” Lisa
alimtupia jicho la ajabu. "Ulidhani kuwa
wewe ndiye mwanaume wa kwanza kulala naye?" Willie alishindwa cha kusema. Hakika hilo ndilo alilolidhania lakini hakuweza kujihakikishia.
Akifikiria kwamba alimsaidia
kushughulika na Jones na Lina, Lisa alimkumbusha hivi kwa fadhili, “Mambo fulani yanaweza kutengenezwa tu katika ulimwengu huu.”
Kwa kujieleza kwa aibu, Willie alitabasamu bila kupenda. "Sasa naweza kustahili mshamaha wako, Bi Jones?"
Kwa kweli, Lisa hakuelewa ni nini
kilikuwa kikiendelea kichwani mwake.
Kabla hajamjibu alimuuliza, “Naweza
kuwa na maneno machache nawe, Bwana Kimaro?”
“,..Bila shaka, najua hili, hehee! Asante kwa kunikumbusha.”
“Hakika. Hakuna shida." Lisa alitoka ofisini huku Willie akimfuata. Miguu
yake ilitetemeka baada ya kumtazama Shani aliyekuwa pembeni yake.
Shani alimtazama kwa tabasamu. “Uko sawa, Bwana Kimaro?”
“Mimi…Niko sawa. Kweli, wewe ni mtaalamu sana." Willie alihisi bomu la atomiki likilipuka kichwani mwake. Lisa alilindwa na Shani mahiri, ambaye alitoka ONA.
ONA lilikuwa kundi la siri zaidi la chini kwa chini chini ya familia ya Kimaro.
Ilijumuisha maveterani kutoka jeshini na washiriki kutoka kwenye tasnia za
sanaa ya mapigano ya kimwili. Kwa
muda huo, ilisimamiwa na Alvin pekee.
Lisa alimroga vipi Alvin hadi akawa
naye? Shani alikuwa anashangaa kila
siku, alimfahamu vizuri Alvin.
Jinsi Willie alivyomtazama Lisa sasa ilikuwa tofauti kabisa.
Lisa alisimama baada ya kufika umbali fulani. Shani kwa makusudi alienda mbali zaidi ili kuwapa nafasi wawili hao. Lisa alikaa kimya akimsubiri Willie amuulize kuhusu zile picha. Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda mrefu, hakusema neno. Alimtazama hata kwa mchanganyiko wa kupendeza, woga, na hofu. Lisa alikosa la kusema kabisa. “Vema…
Bwana Kimaro, unakumbana na madhara yoyote kutokana na kupigwa jana usiku?”
“Hapana kabisa. Badala yake nimekuwa mwenye busara.” Willie alitabasamu. “Bi
Jones, ni heshima yangu kubwa kuweza
kukutana nawe hapa Dar es Salaam.
Tunaweza kuwa marafiki?"
Willie alipunga mkono wake. "Unaweza kuhifadhi picha ukipenda."
Lisa alijikuta midomo yake ikitetemeka. Kwa nini ahifadhi picha zake zisizo na heshima? “Usinilaumu kwa kukuvua nguo na hata kukufedhehesha jana usiku…”
Willie aliganda na kusema kwa kusitasita, “Ulikuwa unasema ukweli tu.
Ningewezaje kukulaumu… Ah-choo!”
Alijifuta pua kwa aibu huku komeo lake likishuka. "Bi Jones, nijulishe ikiwa unahitaji msaada wowote. Nitajitahidi kukusaidia.”
Baada ya kuwa kimya kwa muda, Lisa aliuliza, "Labda ulipiga picha za Lina
akiwa amelala nawe, sivyo?"
Willie alipigwa na butwaa. Kwa jinsi
“Lakini picha…”
alivyokuwa akimtazama Lisa ni kana
kwamba ni rafiki yake wa karibu. "Sikutarajia ungenijua vizuri."
Lisa alijisikia vibaya. Kwa hakika
alikutana na baadhi ya vitabu vya
saikolojia na akajifunza kwamba
wapotovu kama yeye kwa kawaida wangepiga picha za aina hiyo. “Hapana, mimi—”
"Naelewa. Nina idadi kubwa ya video zake. Unapanga kushughulika na Lina, sivyo? Ninaweza kukutumia video hizo
sasa, lakini… Usiwahi kuzionyesha kwa mtu yeyote, hasa mpenzi wako.”
Ikiwa Alvin angegundua kuwa Lisa
alitazama video hizo, bila shaka
angemtoa utumbo Willie akiwa hai. Lisa
alipigwa na butwaa. Wazo la ajabu
likaangaza akilini mwake. “Sawa.”
Aliitikia kwa kichwa.
Willie alimtumia video hizo mara moja.
Alipopokea video hizo, Lisa alionekana
kutojali kwa nje, lakini msukosuko wa
mhemko ulikuwa tayari umeanza ndani yake. Kwa kweli, alikuwa ameomba tu video hizo kwa njia ya kawaida. Alidhani kwamba Willie asingeweza kuzituma
kwake kwa kuzingatia tabia yake ya kishenzi jana yake usiku. Hata hivyo, alionekana kuwa tofauti kabisa leo.
Alikuwa na hakika kwamba haikuwa tu
kwa sababu ya picha zisizofaa
alizotumia kumtishia, kulikuwa na sababu nyingine.
"Alvin, kwa nini uko hapa?" Ghafla, alitazama mahali fulani nyuma ya Willie wakati akiuliza.
Willie alitetemeka sana kwa hofu. Alivaa
tabasamu la kubembeleza na kugeuka
nyuma, na kugundua kwamba
hakukuwa na mtu nyuma yake. Alipigwa
na butwaa kwa muda. Hapo hapo
akahamishia macho yake kwa Lisa
ambaye alikuwa na sura ya ajabu machoni mwake.
“Bwana Kimaro, unamfahamu Alvin?
Kwa nini ulionekana kuwa na wasiwasi na hofu nilipoita jina lake?” Wazo
lisiloaminika likamwingia taratibu kichwani Lisa. "Majina yenu nyote wawili ni Kimaro. Je! inaweza kuwa hivyo…”
“Sijui unasema nini. Hata simfahamu Alvin.” Akiwa amechoshwa, Willie alitikisa mkono wake kwa haraka.
Lisa alicheka. "Kwa kuzingatia utu wako, wewe ndiye mtu ambaye
utafanya chochote ili kufikia malengo yako. Wewe ni mkatili na unapenda
kulipiza kisasi, kwa hivyo haishangazi
kwamba hata picha zako nilizonazo
hazikubabaishi. Kama huna mpango wa kuniambia, nitarudi na kumuuliza Alvin
kisha…”