MDUNGUAJI
Kitabu cha TuwaKadabra Productions
DAR ES SALAAM
UCHAPWAJI
Chapa ya kwanza imetolewa na TuwaKadabra Productions na kuchapwa na ABANA
Printers, Dar es Salaam, 2012. Chapa hii ya pili (nakala laini) imetolewa mwaka 2023 na TuwaKadabra Productions Limited,Dar es Salaam; na ni mahsusi kwa tovuti ya Hussein Tuwa tu.
KANUSHO
Hii ni kazi ya kubuni.
Majina, wahusika, mahala na matukio yaliyotajwa katika kitabu hiki ni ama yanatokana na ubunifu wa mtunzi au yametumika kibunifu tu. Pale ambapo jina la mtu halisi na maeneo halisi vimetajwa basi ni kwa ajili ya kuleta uhalisia kutokana na kisa cha riwaya. Vinginevyo, kufanana kwa aina yoyote na mtu yeyote wa kweli, aliye hai au aliyekufa, matukio, au maeneo yoyote ni kwa ama bahati tu au kwa lengo la kuleta uhalisia kutokana na kisa cha hadithi hii.
Haki zote zimehifadhiwa
Hakimiliki © 2022 Hussein Issa Tuwa
Hakimiliki ya usanifu wa jalada © 2008 Husssein Issa Tuwa
ISBN 978-9976-89-192-8
Kwa wapiganaji wote. Walio hai na waliopoteza maisha… kwa ama kupigania nchi yetu, au kuiwakilisha nchi yetu katika medani za vita.

SEHEMU YA KWANZA SIERRA LEONE, MWAKA
2000
Msitu wa Tumbudu, Mashariki mwa Sierra Leone
Mvua kubwa iliyoambatana na radi za kutisha ilikuwa ikinyesha kwa
nguvu. Msitu mnene ulikuwa umetanda na kuifanya ile mvua ionekane kubwa zaidi. Kwa ukimya wa hali ya juu, wapiganaji kumi wa kikosi maalum cha kulinda amani chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa katika mpango wake wa ReCAMP (Reinforcement of African PeaceKeeping Capacities) kilisonga mbele kwa uficho mkubwa kabisa, kuelekea eneo lililohisiwa kuwa ni la waasi wanaoipinga serikali iliyopo madarakani ya rais wa kidemokrasia wa Sierra Leone, Ahmed Tejan Kabbah.
Ulikuwa ni mwendo wa taabu kwa mtu wa kawaida, lakini hawa hawakuwa watu wa kawaida. Hawa walikuwa ni wapiganaji siyo tu waliobobea katika medani za vita, bali pia waliopata mafunzo maalum ya kupambana katika vita vya msituni na mijini dhidi ya waasi kwa lengo la kuleta amani katika nchi za Afrika, ndani ya mazingira ya Kiafrika.
Kiza kizito kilichotanda msituni kilikuwa kikizimika kwa muda pale radi ilipopiga na kufanya usiku ule uwe kama mchana kwa sekunde, na kisha kiza kile kiliendelea kuutawala msitu ule mnene wa ki-ikweta uliosheheni kila aina ya hatari. Ni msitu uliokuwa na idadi kubwa ya nyoka wa hatari na wenye sumu kali, na wanyama wa mwituni wasiokuwa na subira kwa kiumbe chochote kitakachokatiza mbele ya macho yao. Isitoshe, msitu ule ulikuwa umehifadhi wapiganaji wa kikundi cha waasi cha RUF(Revolutionary United Front) kilichokuwa kikimtii muasi Forday Sankoh, kilichokuwa kikisaidiwa na waasi wa kikundi kingine cha kivita, Armed Forces Revolutionary Council (AFRC).
Vikundi hivi viwili vimekuwa vikiishurutisha serikali ya Ahmed Tejan
Kabbah kuachia madaraka na kujumuisha baadhi ya viongozi wao katika serikali ile ya kidemokrasia, jambo ambalo serikali iliyokuwa madarakani haikuwa tayari kukubaliana nalo; hivyo vita vikawa vinaendelea kwa miaka
MDUNGUAJI na miaka. Hata uliposainiwa mkataba wa amani ambao kwa kiasi kikubwa ulibana vitendo vya uasi na kuunga mkono juhudi za kidemokrasia katika nchi hii yenye utajiri mkubwa wa almasi, waasi waliamua kuvunja mkataba ule na kurudi msituni kuiondoa serikali ile madarakani kwa nguvu.
Ndipo jeshi la Umoja wa Mataifa, likiwa na ridhaa ya umoja wa nchi za Afrika, lilipotuma kikundi chake cha kulinda amani katika huu mpango wake wa ReCAMP ndani ya Sierra Leone, ili kulisaidia jeshi la serikali dhidi ya waasi wale.
Wapiganaji walisonga mbele taratibu, wakiwa makini kutotoa sauti yoyote isiyo ya lazima,itakayowawezesha adui zao kuwabaini na kuwashambulia.
Adui walikuwa na nafuu mbili katika hili: sio tu ule msitu ulikuwa kwenye nchi yao wenyewe, bali pia ulikuwa katika eneo la mashariki ya Sierra Leone, lenye utajiri mkubwa wa almasi, ambalo wao walikuwa wakilishikilia.Hivyo kwa wapiganaji wa hiki kikundi cha kulinda amani, ilikuwa ni kama walioingia uwani kwa adui yao,kwani waasi walikuwa wakizijua zaidi kona za msitu ule kuliko wao.
Lilikuwa ni kundi lililojumuishaWatanzania watatu, Wa-Naijeria wawili, M-Senegali mmoja na wapiganaji wenyeji wanne kutoka kwenye jeshi la serikali ya Sierra Leone.Katika kampeni za usalama kama hizi, wapiganaji wa aina hii huwa wanatambuana kwa majina maalum ya uficho, yaani Code names.
Ndani ya mpango huu wa Umoja wa mataifa, askari wanaounda jeshi hili maalum huwa hawabanwi na utaifa wao wala eneo ambalo nchi zao zinatokea. Hivyo, ingawa Sierra Leone iko Afrika ya Magharibi, wapiganaji wa jeshi hili maalum hawakutoka katika lile jeshi la nchi za Afrika ya Magharibi(ECOWAS) pekee, bali pia lilijumuisha wapiganaji kutoka Afrika ya Mashariki na Kati.
Katika kambi ya jeshi hili kulikuwa pia kuna wapiganaji kutoka Kenya, Uganda na Zimbabwe.
Code name “Vampire” alifikicha macho na kukung’uta maji ya mvua yaliyokuwa yakimtiririka usoni na kutazama upande waliokuwa wakielekea huku akiwa ameinama na bunduki yake aina ya AK-47 ikiwa makini mikononi mwake. Mgongoni alikuwa amebeba begi maalum lililokuwa limehifadhi redio maalum ya mawasiliano katika medani ya vita ambayo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kuwasiliana na kambi yao iliyokuwa kiasi cha mwendo wa saa mbili nyuma yao. Huyu alikuwa mmoja wa wale wapiganaji watatu wa Kitanzania na kazi yake katika kampeni hii ilikuwa ni mawasiliano, kwani yeye alikuwa ni mtaalamu wa mawasiliano katika medani za vita. Hatua chache mbele yake alikuwako mpiganaji hatari aliyejulikana kwa jina la uficho “Alpha”. Naye
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
alikuwa Mtanzania, na alipata jina hili kutokana na kazi yake katika kikosi
hiki, ambapo kijeshi yeye alikuwa ni yule askari anayejulikana kama “runner”
yaani mkimbiaji. Kama “runner” yeye ndiye anayetangulia kuingia eneo lolote lile na kulichunguza, halafu anatoa ishara maalum kwa kikosi kinachokuwa
nyuma yake kuwa eneo ni salama, nao wanasonga mbele, na ikiwa si salama
wanabadili uelekeo.
Code name Vampire (Mzuka) - aliyepata jina hilo kutokana na uwezo wake wa kucheza na vifaa vya mawasiliano na hivyo kuweza kunasa mawasiliano
mbalimbali ya adui kama inavyoaminika kuwa mzuka unaweza kusikia na kuona mambo ya watu bila wao kujua juu kuwepo kwake eneo husika - alikuwa
makini akisubiri ishara kutoka kwa Alpha, nyuma yake wapiganaji wenzake wakiwa wamebana kimya nao wakisubiri.Alipopokea ishara kuwa mambo ni shwari, aliwaashiria wenzake nao wakasonga mbele kwa mwendo wa kunyata na tahadhari kubwa.
Ingawa jina la uficho Alpha alijulikana hivyo kwa wale wapiganaji wengine, jina la uficho Vampire alimtambua kuwa ni Kanali Nathan Mwombeki. Pamoja nao kulikuwapo mpiganaji mwingine aliyejulikana kama “Swordfish” yaani papa upanga. Huyu naye alikuwa ni mpiganaji wa Kitanzania ambaye jina lake halisi ni Abdul-hameed Babu, kutoka jeshi la Tanzania visiwani. Huyu alikuwa ni mtu hatari kabisa katika makabiliano ya uso kwa uso katika medani za vita,hivyo akapewa jina la aina ya samaki hatari sana, jamii ya papa upanga (Swordfish). Hawa ndiyo pekee katika kikosi kile ambao mpiganaji Vampire aliwatambua kwa majina yao halisi. Wengine waliobaki aliwajua kwa yale majina yao ya uficho tu. Katika wale wanaijeria wawili kulikuwa kuna “Stealth”, ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa kampeni ile, na “Glimmer”. Yule wa Senegali, ambaye alikuwa mwanamke, alijulikana kama “Honey-Bee”, ambaye alikuwa hodari sana wa kupiga shabaha.Kisha kuna wale wanne ambao ni wenyeji wa Sierra Leone. Baina yao kulikuwa kuna “Black Angel”(Malaika mweusi), “Cheetah”(Duma), “Eagle”(Tai), na “Black Mamba”(Nyoka mwenye sumu kali). Kutokana na mchanganyiko huu, maongezi yote baina ya wapiganaji wale yalikuwa ni kwa lugha ya Kiingereza.
Lengo la msafara huu wa kikosi hiki cha watu kumi lilikuwa ni kupeleleza tu, na baada ya kugundua uhakika wa walichokuwa wakikitaka, “Vampire”
alitakiwa kutoa taarifa kwenye kambi yao waliyoiacha nyuma yao kwa kutumia
ile redio aliyoibeba mgongoni, akitoa maelekezo maalum ya kijeshi jinsi ya kufika pale walipo ili wapange shambulizi dhidi ya kambi ya waasi iliyokuwa imejificha ndani kabisa ya msitu ule.
MDUNGUAJI
Vampire ndiye aliyefanikiwa kunasa mawasiliano ya redio baina ya kundi moja la waasi na jingine, na katika mawasiliano yale, aliweza kubaini uelekeo zilipokuwa zikitokea amri zao za mashambulizi. Kama wangeweza kuibaini sehemu hii, kulikuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuwaangamiza viongozi wakubwa wa waasi na hivyo kuwapunguza nguvu kwa kiasi kikubwa. Hili
liliifanya kampeni ile iwe muhimu sana.
Amri yao ilikuwa wazi. Wasishambulie. Kazi yao ni kuitafuta kambi ya waasi na wakiigundua, watume mawasiliano kambini na ndipo wapiganaji wengine watakapoungana nao kwa ajili ya kufanya shambulizi. Kijeshi kampeni kama hii huitwa “reconnaisance mission”, au “recon”.
Vampire aliwatazama Watanzania wenzake na alijivunia kuwa miongoni mwao, kwani wao walipewa nafasi kubwa katika jeshi hili kutokana na uwezo wao wa kuendesha vita vya nchi kavu na hasa vya msituni.Ghafla alisikia sauti kama ya ujiti ukikatika na hapohapo yowe dogo la mshituko lilimtoka mmoja wa wale wapiganaji wa ki-Sierra Leone aliyekuwa karibu sana na yeye. Alijitupa chini huku akimsikia mpiganaji wa ki-Naijeria akipiga kelele. “Tunashambuliwa!”
Wakati huohuo alihisi akipigwa na kitu kizito na akitupwa hadi kwenye dimbwi la maji. Alijipindua haraka akiwa tayari kujibu mashambulizi, lakini adui hakuonekana.
Kimya kilirudi upya.
Wapiganaji walikuwa wamelala chini kwenye tope na maji ya mvua, huku wameshikilia bunduki zao kwa umakini mikononi mwao, macho yakiwatembea huku na huko mle msituni.
Kimya.
Sasa wapiganaji walikuwa makini sana,na hakuna hata mmoja aliyefyatua risasi. Mafunzo yao yalikuwa thabiti.Usishambulie adui usiyemuona. Unaweza kufanya adui ajue kwa urahisi zaidi mahala ulipo.Sauti za vyura na wadudu mbalimbali wa msituni zilizosita kwa muda katika mvurugano ule wa dakika mbili zilianza upya.
Jina la ufichoCheetah wa SierraLeone alikuwa amelala chali kando ya dimbwi dogo la maji akiwa ametawanya miguu na mikono yake kila upande. Kichwa chake kilikuwa kimezama ndani ya lile dimbwi dogo la maji ilhali mwili wake ukiwa umetulia tuli. Hakukuwa na shaka kabisa miongoni mwa wapiganaji wale kuwa mwenzao mmoja alikuwa ameuawa kwa risasi.
Lakini mshambuliaji ni nani? Yuko wapi? Mbona haukusikika mlio wa bunduki?
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Vampire alisikia kitu kingine. Harufu ya kitu kama nyaya za umeme zilizopata shoti.
Ni nini kinatokea?Aliwatazama wenzake. Jasho lilikuwa likimvuja na moyo ulikuwa ukimpiga kuliko kawaida.
“Alpha! Alpha! Tupe hali halisi!” Stealth kutoka Naijeria alinong’ona. Wote wakawa wanasikiliza kutoka kwa Alpha.
“Kimya tu. Hakuna dalili ya adui! Tutulie, atajaribu kushambulia tena!”
Alpha kutoka Tanzania alijibu. Vampire alitoa kifaa chake cha mawasiliano na kujaribu kutoa taarifa kwenye kambi yao.Na hapo alielewa ni nini kilichompiga na kumtupa pembeni kwa nguvu wakati yule mwenzao aliposhambuliwa. Redio yake aliyokuwa ameibeba mgongoni ilikuwa imepigwa na risasi! Na ule msukumo wa ile risasi ndiyo uliomtupa pembeni kwa nguvu.Alijaribu kufanya mawasiliano na kambi yao lakini ile redio haikuitika hata kidogo.
“Redio yetu imekufa!”Aliwaambia wenzake waliokuwa wamejilaza kila mmoja upande wake.
“Oh, Shiit...! Kwa hiyo sasa hatuna kabisa mawasiliano na kambi yetu!”Honey-Bee kutoka Senegal alilaani.
“Mmoja aje kunikinga nijaribu kuitengeneza! Nadhani nitaimudu!” Vampire alisema kwa kihoro huku akitembeza macho huku na huko. Ukweli ni kwamba alikuwa akiwahisi tu wenzake lakini hakuwa akiwaona kutokana na kiza na vile wote walivyokuwa wamejilaza kwenye majani na matope kujikinga na shambulizi.
Glimmer wa Naijeria alijiinua na kumkimbilia huku akiwa amejikunja, bunduki yake ikiwa imekamatwa makini mikononi mwake, lakini kabla hajamfikia alipiga yowe kubwa huku akitupwa hewani na bunduki ikimtoka mikononi.Kelele za kuhamanika zilizagaa eneo lile wakati wapiganaji wakizidi kujishindilia kwenye majani na matope huku wakilalamika kwa kushambuliwa pasipo kumuona adui.
“Glimmer amepigwa risasi!” Jina la uficho Swordfish kutoka Tanzania Visiwani aliropoka kwa kihoro.
“Adui yuko karibu!” Stealth alibwata huku akigeuka huku na huko, bunduki yake ikiwa tayari kushambulia.
“Yuko wapi?!” Alpha kutoka Tanzania alipiga yowe.
“Honekani! Anavizia tu...!” Vampire alibwata kwa hasira, akimjibu Mtanzania mwenzake.
“Ni mdunguaji, Mungu wangu...a Sniper!” Honey-Bee kutoka Senegal alibainisha kwa kihoro kikubwa zaidi.
MDUNGUAJI
“Mdunguaji...? Oh, Shit!” Swordfish kutoka Tanzania visiwani alilaani huku akijiegemeza kwenye mti akielekeza bunduki yake huku na huko.Ulikuwa ni mtafaruku mkubwa.
“Jificheni!”Vampire alipiga kelele.
Kila mmoja alijizatiti kujificha pale alipokuwa huku akiwa ameweka bunduki yake makini. Macho yaliwatembea kujaribu, bila mafanikio, kumuona adui yao katika ule msitu mnene uliotanda kiza kizito.
Kimya kilitanda upya. Wawili tayari walikuwa wameuawa. Walikuwa ndani ya eneo la adui na hawakuwa na mawasiliano na kambi yao.
Na sehemu fulani ndani ya msitu ule, Mdunguaji alikuwa amejificha akisubiri yeyote kati yao atikisike tu, amuondoe duniani.Kwa hakika kilikuwa ni kipindi kigumu kwa wapiganaji wale, na Vampire aliuona mwisho wao ukiwasogelea kwa kasi sana.
Wapiganaji walibana kimya katika maficho yao kwa muda wa saa mbili bila yeyote kati yao kutikisika. Walikuwa makini sana kujaribu kuuchunguza msitu ule kwa macho yao na kwa kutumia darubini maalum za kuonea usiku (Night Vision Goggles) ili angalau kujua ni wapi adui yao, mdunguaji, alipokuwa amejificha akiwavizia.
Lakini hakuna aliyeona kitu chochote. Ingawa walikuwa na kurunzi kali za kuwawezesha kuona katika usiku ule wenye kiza na mvua, hawakuthubutu kuzitumia kabisa. Kwani kwa kufanya hivyo wangekuwa wanamualika kabisa mdunguaji pale walipo na hivyo kujithibitishia kifo.
Katika zile saa mbili, Honey-Bee kutoka Senegal alifanikiwa kuua nguruwe mwitu mmoja na kumdodosha sokwe mmoja kutoka juu ya mti. Yaani kitendo cha yule nguruwe mwitu kukurupuka kutoka kwenye kichaka alichokuwa amejificha tu kilimtosha yule mwanamke mwenye shabaha na hisia za ajabu kumtupia risasi na kumuua palepale, akidhania ni mdunguaji aliyewaangamiza wenzao wawili hapo awali. Mlio wa yule mnyama wakati akikata roho uliwajulisha wote kuwa ni nguruwe mwitu ndiye aliyeuawa na kwamba mdunguaji bado anaishi.
Wapiganaji wote walikuwa makini sana, lakini wote walijua kuwa ni HoneyBee ndiye atakayemmaliza adui yao kutokana na wepesi wake wa kutupa risasi popote pale mtikisiko au mlio wowote utakapotokea.
Muda mfupi baada ya risasi ya Honey-Bee kukatisha maisha mabovu ya
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
nguruwe mwitu, Sokwe aliyekuwa juu ya mti alijitikisa kidogo tu katika harakati za kurukia matawi na hapohapo Honey-Bee alitupa risasi eneo lile na wapiganaji walisikia mlio wa uchungu kutoka kwa mnyama yule ukifuatiwa na kishindo kikubwa. Inaelekea ile risasi haikuweza kumuua yule Sokwe palepale kwani alijiinua na kujaribu kukimbia lakini hapohapo aliruka juu huku akitoa mlio mwingine wa uchungu na kuanguka tena chini akiwa ameshakufa.
Sokwe mtu alipigwa risasi mara mbili, lakini Honey-Bee alifyatua risasi mara moja tu.
Wapiganaji wote walielewa kilichotokea. Walisikia mlio wa bunduki ya Honey-Bee ilipomdungua yule Sokwe kutoka juu ya mti, lakini hawakusikia mlio wa bunduki iliyotuma risasi ya pili na kummaliza yule Sokwe.
“Ni Mdunguaji! Mdunguaji bado yuko humu!” Honey-Bee alisema kwa hasira, kwani ni wazi kuwa ni Mdunguaji ndiye aliyemmalizia yule Sokwe, bila shaka akidhani alikuwa ni mmoja wa wale wapiganaji akijaribu kukimbia kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Umakini wa mdunguaji huyu ulieneza hofu miongoni mwa wale wapiganaji shupavu.
“Duh! Ebwanaee! Huyu jamaa kiboko!” Vampire alijisemea peke yake, huku akizidi kujichimbia kwenye majani yaliyonyeshewa mvua.Kila mmoja kati ya wapiganaji wale alitikisa kichwa kuafikiana na kauli yake, isipokuwa Honey-Bee kutoka Senegali.
“Oh, yeah? okay...Tutaona basi!” Alisema kwa hasira, na kimya kilitawala. Hakukuwa na mtikisiko wowote kutoka kwa mdunguaji wala kutoka kwa wanyama waliokuwepo mle msituni.
Na wapiganaji wanane waliobaki hai katika kile kikosi maalum walizidi kuingiwa na hofu, kwani walijiona kama bata waliokaa kusubiri kudunguliwa na risasi za mwindaji ambaye walikuwa na imani kuwa alikuwa akiwaona bila wao kumuona.
“Haya, haya we’ mdunguaji mmwaga damu! Jitikise...jitikise kidogo tu, ili nikumalize...!” Honey-Bee alinong’ona kwa hamasa huku akiangaza huku na huko, akiwa amekamata bunduki yake tayari kwa kushambulia, ile miwani maalum ya kuonea usiku ikiwa imeshikiliwa kichwani kwake kwa mikanda maalum na kumuwezesha kuona katika kiza cha msitu ule.
“Huyo ni mtaalamu...hatajitikisa mpaka sisi tujitikise...!” Stealth alinong’ona huku naye akiangaza mle msituni.
“Na atakapojitikisa basi mmoja wetu anakuwa mfu...!”Swordfish alimalizia ile kauli ya Stealth kwa ghadhabu.
“Yeah... lakini kufikia wakati huo na yeye...awe mwanaume au mwanamke...
MDUNGUAJI
atakuwa amekufa pia, nakuahidi hilo!”Honey-Bee alinong’ona kwa hasira na kujiamini.
Lakini mdunguaji hakushambulia tena na usiku ulipita ilhali wapiganaji wakiwa katika hali ngumu sana wakijaribu kumvizia mdunguaji bila mafanikio.
Walipitisha usiku ule kwa kutafuna bisikuti zao maalum na kushushia kwa maji
kila mmoja aliyobeba kwenye chupa maalum, huku wakioga mvua iliyokuwa
ikipiga kwa nguvu kiasi hata makoti yao ya mvua yalionekana kutosaidia. Kulipokucha, mvua ilikuwa imepungua na msitu ulianza kuchangamka kwa
sauti za ndege waliokuwa wakiimba kwa furaha bila kujua kuwa kulikuwa kuna
viumbe wengine wa Mwenyezi Mungu katika msitu ule waliokuwa hawana
raha hata kidogo kwa hofu. Baadhi ya wanyama walianza kujitokeza na kufanya purukushani nyingi pale msituni hasa pale kwenye ile mizoga ya yule nguruwe mwitu na sokwe waliouawa katika ile vita ya kuviziana baina ya wapiganaji na mdunguaji, ambayo kwa hakika ilikuwa ni vita kati ya mdunguaji na HoneyBee, mwanamama mkali wa shabaha kutoka jeshi la Senegal.
Na wakati wale wanyama wakifanya vurugu kugombea ile mizoga, wapiganaji walikuwa macho na makini wakitaraji kuwa zile purukushani za wanyama zingeweza kumlaghai mdunguaji kiasi cha kufanya kosa la kujitokeza au kujitikisa japo kidogo, akiamini kuwa ni wale wapiganaji ndiyo waliokuwa wakifanya zile vurugu ili nao wamshambulie, lakini haikuwa hivyo.
Ilikuwa ni kama kwamba mdunguaji aliamua kutokomea msituni na kuwaacha wakihamanika kwa hofu.
“Unadhani ameondoka...?” Swordfish kutoka Tanzania Visiwani aliuliza kutokea chini ya majani alipokuwa amejichimbia huku mtutu wa bunduki yake ukichomoza tayari kujibu shambulizi.
“Mnnhu! Hata kidogo! Huyu mwanaharamu bado yupo! Yaani ninamuhisi kabisa!”Honey-Bee alisema kwa hasira.
“Kwa hiyo sasa tunachukua hatua gani Stealth?” Black Mamba kutoka jeshi la serikali ya Sierra Leone alimuuliza kiongozi wao kutokea chini ya gogo kubwa la muembe lililokuwa limeangukia juu ya jiwe kubwa na hivyo kumpa maficho salama dhidi ya risasi ya mdunguaji. Badala ya kujibu Stealth alimgeukiaVampire.
“Redio yetu iko kwenye hali gani Vampire? Unaweza kuitengeneza?”
Vampire alikuwa amelalia tumbo nyuma ya mti mkubwa, bunduki yake ikiwa kando yake na ile redio ikiwa imelala mbele yake ikiwa imefunguliwa sehemu fulani naye akijaribu kuitengeneza.
“Ndiyo naishughulikia...sina uhakika kama itatengemaa!” Alimjibu huku
akiendelea kujishughulisha na ile redio iliyokuwa imelazwa juu ya lile koti lake la mvua.
“Hali ya usalama ikoje Alpha?”Stealth alimgeukia Alpha, “runner” wa kikosi kile. Alpha alimjibu kwa ishara maalum za kijeshi kuwa anataka atoke eneo alilokuwepo na kuchunguza hali ilivyo. Stealth, kiongozi wa kampeni alipitisha
maamuzi mara moja.
“Black Mamba na Swordfish! Mkingeni Alpha! Mimi na Honey-Bee tutakuwa tukisubiri mtikisiko wowote kutoka kwa huyu mdunguaji mmwagaji damu!”
Alitoa maelekezo na mara moja wale wapiganaji walijipanga na kijiweka sawa huku wameshikilia silaha zao kutekeleza maelekezo yale.
Stealth aliwaeleza wapiganaji wengine huku akiwa anatembeza macho msituni kutafuta mwenendo wowote ambao ungemjulisha sehemu aliyojificha mdunguaji.
“
Eagle na Black Angel mumkinge Vampire wakati anaishughulikia redio!”
Eagle na Black Angel walijiweka sawa kumkinga Vampire aliyekuwa akihangaika na na redio yake.
Alpha alijiinua taratibu kutoka pale alipokuwa amejibanza, baina ya miti miwili iliyoota karibu-karibu sana, na kukimbia kwa kasi akiwa amejikunja kutokea kiunoni, huku ameishikilia bunduki yake kistadi.Nyuma yake Black Mamba kutoka Sierra Leone na Swordfish kutoka Tanzania walikuwa tayari
kushambulia, macho yao yakiangaza juu ya miti kulia na kushoto kwa Alpha.
Wakati huohuo, Stealth kutoka Naijeria alikuwa amekaza macho yake kutafuta
mtikisiko wowote utakaotokea juu ya miti katika ule upande ambao Alpha alikuwa akikimbilia.Honey-Bee naye alikuwa katika hali ileile, akiangalia maeneo ya juu ya miti iliyokuwa nyuma ya Alpha.
Hapo wapiganaji wote walikuwa makini na tayari kwa makabiliano kutokea upande wowote ule ambapo ingelazimu. Na katika mazingira yale, Vampire alikuwa akiishughulikia ile redio yake kwa utulivu mkubwa.Akili yake ikiwa imezama katika kazi iliyokuwa mikononi mwake, usalama wa maisha yake akiwa ameukabidhi mikononi mwa wale wapiganaji wenzake waliokuwa wakimkinga na shambulio, Eagle na Black Angel wote kutoka Sierra Leone.
Alpha alipotelea msituni kwa muda mrefu. Wapiganaji wenzake walikuwa wakisubiri kwa umakini uleule. Walishaanza kupata hofu kuwa naye ameshambuliwa na mdunguaji hatari, wakati aliporejea kwa ukimya wa hali ya juu.
“Kote kweupe...hakuna hatari. Tunaweza kusonga mbele!” Aliripoti huku akihema kwa nguvu.
MDUNGUAJI
Wapiganaji walimgeukia Vampire. Alikuwa ameifunga kama ilivyotakiwa ile redio yake ya mawasiliano vitani na mkononi alikuwa ameshika risasi aliyoitoa kutoka kwenye ile redio.
“Itaweza kufanya kazi, lakini itachukua muda. Hebu angalia hii!”Vampire aliwajibu wenzake huku akimrushia Stealth ile risasi aliyoitoa kwenye redio. Stealth aliitazama ile risasi na kukunja uso. Aliipitisha kwa kila mmoja wao aione.
“Hii ni risasi kutoka kwenye bunduki aina ya Ghalil Sniping Rifle, ambayo hutengenezwa Israeli. Silaha moja hatari sana na ni maalum kwa wadunguaji!”
Honey-Bee alisema huku akiitazama ile risasi.
“Unataka kuniambia kuwa na wa-Israeli nao pia wamo kwenye hii vita?”
Vampire aliuliza kwa mastaajabu.
“Nooo! Ni hawa hawa waasi. Wao wanapata silaha kutoka karibia kila kona ya dunia.” Black Angel alijibu.
“Lakini wanawezaje kumudu kununua silaha hizi? Lazima kuna mtu anayewasaidia.Vita hutumia gharama kubwa!”Swordfish aliuliza na kuchangia hoja.
“Mnnhu!Si wanabadilishana almasi kwa hizo silaha? Baadhi ya nchi... wafanyabiashara wa Kizungu, ki-Asia na ki-Israeli...wanashiriki kwenye biashara hii. Si ajabu kabisa kwa waasi kuwa na silaha za kila aina.” Stealth aliongezea.
“Na Charles Taylor naye anawasaidia sana hawa waasi, bloody swine, mi’ ananiudhi kweli!” Black Angel alilaani zaidi.
“Na ndiyo maana basi almasi zinazotoka eneo hili zinaitwa ‘almasi za damu’...damu nyingi inamwagwa kwa ajili ya hizi almasi!” Vampire alimalizia.
“Sasa tunasonga mbele au vipi?” Alpha aliwauliza wenzake.
“Hatuna uwezo wa kuwasiliana na kambi yetu. Bila shaka waasi wanajua kuwa tupo hapa sasa. Kwa hiyo tunarudi kambini! Mpango wote umesitishwa.”
“Negative! Nashauri tuendelee kusonga mbele...kote kuko salama.Bila shaka mdunguaji ameingia woga na kukimbia. Kwa jinsi Honey-Bee alivyomkosakosa na kuishia kuwaua wale wanyama...” Alpha alipingana na Stealth. Vampire aliinua uso kumtazama Mtanzania mwenzake.
“Halafu tunafanyaje tukifanikiwa kuigundua hiyo kambi ya waasi, Alpha?” Alimuuliza. Alpha alimtazama kama kwamba alikuwa hana akili vizuri.
“Khah! Tunatoa taarifa kambini kuita wapiganaji wenzetu! Kwani huo si ndiyo mpango?”
“Lakini hatuna redio Alpha! Tutatoa vipi taarifa kambini...?” Black Mamba,
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Stealth na Swordfish wote walimjibu kwa pamoja; kila mmoja kwa maneno yake lakini ujumbe ukiwa ni huohuo. Alpha aliwatazama wapiganaji wenzake na kubabaika kidogo kabla hajajibu.
“Ah...! Kwani Vampire si alisema kwamba anaweza...”
“Itachukua muda Alpha! Hatuwezi kuhatarisha maisha yetu bila ya sababu!”
Vampire alimkatisha kwa ukali, akilini akimshangaa Mtanzania mwenzake kwa kung’ang’ania jambo la hatari kama lile. Hata kama ni ushujaa, wakati mwingine kurudi nyuma ni sehemu ya ushujaa vilevile.
“Na mimi ndiye kiongozi hapa, na ndiye ninayefanya maamuzi!” Stealth alikatiza mjadala ule.
Iliamuliwa kuwa kikosi kirudi nyuma na kuripoti kambini kwao.
“Na tunarudi vipi huko kambini! Kwa hakika Mdunguaji bado yuko! ” Honey-Bee aliuliza.
“Kwa yakini si kwa njia ileile tuliyojia. Tunabadili njia!” Stealth alielekeza.
Kwa dakika tano zilizofuata wapiganaji walitazama ramani yao na kukubaliana kubadili njia ambayo ingewarudisha kambini kwao. Kwa mara nyingine tena “runner” Alpha alipotea msituni kuifuata ile njia kwa ukimya wa hali ya juu, na muda mfupi baadaye alirudi na wapiganaji wanane waliobaki wakaanza safari ya kurejea kambini kwao, wakiwa wamewabeba maiti wao kwenye machela za dharura zilizotengenezwa kwa miti.
Black Mamba na Swordfish waliubeba mwili wa Cheetah ambaye risasi ya mdunguaji ilimpata katikati ya paji la uso. Black Angel na Eagle waliubeba mwili wa Glimmer ukiwa na risasi ya mdunguaji kichwani, ikiacha tundu dogo juu kidogo ya sikio lake la kushoto. Nyuma yao alifuata Vampire. HoneyBee alikuwa nyuma kabisa ya msafara ule akiangaza huku na huko, bunduki yake ikiwa makini mikononi. Alpha alikuwa mbele ya ule msafara akifuatiwa na Stealth. Wote walikuwa makini sana kwani ukimtoa Alpha, hawakutaka kuamini kwamba yule mdunguaji alikuwa ameamua kuwaachia tu. Vampire alikuwa na mawazo mengi kichwani mwake kuhusiana na tabia aliyoonesha Alpha, Kanali Nathan Mwombeki kutoka Tanzania.Msafara uliendelea kwa uficho na umakini wa hali ya juu kwa muda mrefu na wapiganaji walianza kuamini maneno ya Alpha kuwa huenda ni kweli mdunguaji aliogopeshwa na risasi za Honey-Bee na kuamua kukimbia.
Risasi ilipita milimita chache juu ya bega la Black Angel na kujikita kifuani kwa Eagle. Yowe kubwa lilimtoka yule mpiganaji huku akiachia machela aliyokuwa amebeba na mwenzake, naye akitupwa nyuma kwa msukumo wa risasi ya mdunguaji. Kizaazaa kiliamka upya msituni. Mdunguaji bado alikuwa
anaendeleza mashambulizi yake ya kuvizia.
Honey-Bee na Vampire walimimina risasi upande risasi ya mdunguaji ilipotokea huku wapiganaji wengine wote wakijitupa chini na kujificha huku nao wakitembeza bunduki zao huku na huko kutafuta adui alipo. Miili ya wale marehemu wawili ilitupwa chini wakati wapiganaji walipokuwa wakijaribu kujinusuru.
“Yuko kule!” Honey-Bee na Vampire walipiga kelele kuelekeza kule risasi zilipotokea huku wakimimina risasi za mfululizo. Stealth aliinuka na kutoka mbio kuelekea kule iliposemekana kuwa ndipo mdunguaji alikuwako huku naye akitupa risasi akiwa ameinama.
“Jificheni!” Swordfish alipiga kelele kutokea nyuma ya mti na hapohapo risasi ya mdunguaji ilipiga na kubanjua gome la ule mti milimita chache kutoka kichwani kwake naye akalaani bahati yake huku akijitupa chini na kujigeuza huku akimimina risasi kuelekea kule alipohisi risasi ilitokea.
Kwa dakika kadhaa msitu ulirindima milio ya risasi kutoka kwa wapiganaji, wote wakishambulia eneo lililoaminika kuwa mdunguaji alikuwako.
“Pumbavu! Tunapiga risasi ovyo!” Honey-Bee alipiga kelele huku akijitupa nyuma ya kichuguu cha mawe kilichokuwa karibu yake.
“Acha kushambulia!” Stealth aliwapigia kelele wapiganaji wake akiwa amejibanza nyuma ya mti.
Black Angel alimtupia macho Eagle aliyekuwa anagaagaa chini huku akilia kwa uchungu akiwa amejishika kifuani ambapo risai ilimpata, damu ikichuruzika kutoka kwenye vidole vyake na mdomoni, macho yakiwa yamemtoka kwa woga mkubwa kabisa. Alijaribu kujiinua lakini alishindwa.
“Kaa hapohapo Eagle.Tulia...!” Vampire alimpigia kelele akiwa amejibanza nyuma ya mti sambamba na mti ambao Stealth alikuwa amejibanza nyuma yake.
“Acha kushambulia! Acha kushambulia...!” Stealth alibwata kwa nguvu.
Wapiganaji waliacha kushambulia, na kimya kikatanda tena msituni isipokuwa kwa sauti za Eagle aliyekuwa akitapatapa kutokana na jeraha baya la risasi ya mdunguaji. Hakuna hata mmoja miongoni mwa wapiganaji aliyethubutu kwenda kumsaidia kwani kwa kufanya hivyo angekuwa anajianika peupe ili mdunguaji ammalize.
Black Angel alimtazama M-Sierra Leone mwenzake akikata roho peke yake bila msaada wowote na ghadhabu zilimpanda. Alichomoka kutoka alipokuwa amejibanza na kugeukia ule upande risasi za mdunguaji zilipotokea na kuanza kumimina risasi huku akipiga kelele kwa hasira.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Njoo basi ewe muoga! Jitokeze! Jitokeze basi!”
“Black Angel, Nooo!” Swordfish alimpigia kelele kumzuia lakini tayari alikuwa ameshajitokeza na akiendelea kumimina risasi. Honey-Bee alikuwa akiangalia kwa makini ule upande aliokuwa akiutupia risasi Black Angel. Wapiganaji wengine wote walikuwa wakimpigia kelele arudi kwenye maficho lakini Black Angel alikuwa amepandisha jazba. Aliendelea kumimina risasi huku akisogea kule ilipoaminika kuwa mdunguaji alikuwepo.
Wenzake walibaki wakimtazama kwa uchungu, wakitarajia kuwa muda wowote angeanguka akiwa maiti, kwani Black Angel alikuwa amejianika wazi mbele ya mdunguaji hatari kutokana na hasira zilizomnyima kabisa uwezo wa kufikiri sawasawa.Lakini hakuna kilichotokea.
Hatimaye Black Angel aliacha kushambulia ovyo na kubaki akiwa ameshangaa kuwa pamoja na kujianika namna ile mdunguaji hakumshambulia na kumuua.
“Lala chini, Black Ang...” Stealth na Vampire waliita kwa pamoja lakini walichelewa.
Muda huohuo Black Angel alitupwa hewani, bunduki yake ikimtoka na kubwagwa chini akiwa maiti. Risasi ya mdunguaji ilimpata sawia katikati ya paji la uso, naye alipatwa na mshituko hakuweza hata kupiga yowe. Na katika sekunde ileile bunduki ya Honey-Bee ilikohoa na mguno hafifu ulisikika kutokea juu ya mmoja kati ya miti ambapo risasi ya mdunguaji ilitokea.
“Mdunguaji amepigwa risasi!” Swordfish alibwata na wapiganaji walianza kumimina risasi kule mguno ulipotokea, na kwa dakika zipatazo tatu mfululizo risasi zilichakaza matawi ya miti iliyokuwa katika eneo lililohisiwa kuwa mdunguaji alikuwako.
Kisha kimya kikatwala.
Wapiganaji walitulia kuangalia matokeo ya shambulio lao na walivunjika moyo kwa kutoona mwili wa mdunguaji ukidondoka kutoka juu ya mmoja wa miti ile.
Mwili wa Black Angel ulilala ukiwa hauna uhai hatua kadhaa kutoka pale ulipolala mwili wa Eagle.Wapiganaji wanne wa kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa walikuwa wameuawa. Sita walibaki hai. Na bado hawakuwa na uhakika wa kuifikia kambi yao salama katika idadi ile, kwani iliwadhihirikia wazi kuwa mdunguaji alikuwa amejeruhiwa, lakini bado alikuwa hai.
Na wote walijua kuwa ni salama zaidi kumuua Mbogo kuliko kumjeruhi.
Msako mkali katika eneo lililohisiwa kuwa mdunguaji angeweza kupatikana haukuzaa matunda. Hakukuwa na dalili yoyote ya mdunguaji zaidi ya uwepo wake kudhihirishwa na ile miili ya wale wapiganaji wenzao waliouawa kwa risasi kutoka kwenye bunduki yake.Zaidi ya hapo, hakukuwa na mdunguaji wala alama za sehemu aliyopitia. Ilikuwa ni ajabu na kweli.
“Kwa hakika huyu mdunguaji ni hatari sana!” Swordfish alisema kwa kuhamanika akiwa amejishindilia kwenye kichaka.
Yaa! Hakika ni Mdunguaji hatari sana…Mdunguaji ambaye inaelekea anajua kila hatua tunayopanga kuchukua mapema mno! Vampire alijiwazia peke yake, lakini alibaki kimya akihisi donge likimkaba kooni na mwili ukimtetemeka. Hakujua iwapo alitetemeka kwa woga, hasira au kwa baridi ya maji ya mvua.
“Na muda mfupi tu ujao atakuwa ni marehemu hatari sana tu mzee! Nakuahidi hilo!”Honey-Bee kutoka Senegal alimjibu Swordfish kwa ghadhabu huku akiangaza msituni kwa makini, bunduki yake ikiwa tayari mikononi mwake.
“Na ni vipi hata huyu mdunguaji muuaji akajua kuwa tumepitia njia hii?”Stealth kutoka Naijeria alibwata kwa hamaki, akiwa amejificha nyuma ya mti mkubwa, jasho likimtoka, mishipa ya shingo ikiwa imemtutumka kwa hasira.
“Lakini msitu wote umetapakaa wadunguaji, jamani!” Alpha alipiga kelele akiwa amejificha nyuma ya kichaka, bunduki yake ikiwa imeelekea kule ilipodhaniwa kuwa mdunguaji alikuwako. Lakini Honey-Bee hakukubaliana kabisa na rai yake.
“No way Alpha! Hapa kuna mdunguaji mmoja tu, naye...awe mume au mke...hivi sasa amejeruhiwa!”
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Kweli n’na hakika kuwa Honey-Bee amemchapa risasi...sasa mbona hata damu haionekani?” Stealth alimaka.
“Mvua komredi...mvua inapoteza ushahidi,lucky bastard!” Swordfish alimjibu.
Nusu saa badaye mvua ilikuwa imeacha kunyesha kabisa, na bado Stealth alikuwa ana jambo linalomsumbua juu ya mdunguaji yule.
“Sasa ni jinsi gani ameweza kujua kuwa tumepitia njia hii, eenh? Hebu mtu na anieleze hilo!” Alifoka kwa hasira, huku akitamka maneno ya kulaani hali ile. Alikuwa amekasirika vibaya sana. Kwa hakika mdunguaji alikuwa amewachanganya akili wapiganaji kwa kiasi kikubwa kabisa.
“Hey! Tumo ndani ya eneo la adui wapiganaji! Ni nini mlichotarajia jamani? Sherehe ya makaribisho? Aaakh!” Alpha aliwajia juu wenzake.
“Huo ni utovu wa nidhamu mkubwa kabisa Alpha! Na bado hilo haliielezei hii hali ya mdunguaji kujua nyendo zetu, kwani nami naamini kuwa kuna mdunguaji mmoja tu na si zaidi ya hapo!” Stealth alimkemea Alpha.
Wakati yote haya yanaendelea, Vampire alikuwa akishughulikia kifaa chao cha mawasiliano kwa bidii. Jasho lilikuwa likimtoka na akili yake ilikuwa ikichemka kwa namna ya ajabu sana. Kwa mazingira yaliyokuwapo, kufanya mawasiliano na kambi yao ndilo lilikuwa jambo pekee la kuwaokoa. Hapo mwanzo hakuweza kufanya lolote juu ya ile redio kutokana na kukosa muda uliohitajika kuitengeneza. Lakini hali ilionesha kuwa mdunguaji alikuwa amewabana kwenye kona na hawakuwa na namna ya kujinasua bila ya mmoja wao kuuawa. Vampire alikuwa ni mtu wa mikakati, aliyependa kutumia muda wake vizuri; hivyo wakati wapiganaji wenzake wakiumiza vichwa na kubishana juu ya namna mdunguaji alivyoweza kuwaibukia na kuwaua wenzao kila walipokimbilia, yeye aliona ni bora atumie muda ule kutengeneza kile kifaa chao cha mawasiliano.
“Kwa heshima zote Afande!Sote tunajua kwamba tumo ndani ya eneo la waasi...si ajabu kwa adui kuzagaa msitu wote huu...” Alpha alimjibu mkuu wao kwa msisitizo.
“Kweli jamani! Nadhani nakubaliana na Alpha...” Black Mamba alidakia.
“Nasema kuna mdunguaji mmoja tu mabwana! Ndiyo maana anatuua mmoja baada ya mwingine, vinginevyo tungekuwa tunauawa kwa mpigo, au mnaonaje?” Honey-Bee alisisitizia hoja yake ya awali.
“Nakubaliana na Honey-Bee...” Swordfish alimuunga mkono yule mpiganaji wa kike.
“Kwa hiyo sasa tunafanyaje wapiganaji? Tunakaa tu hapa tukibishana
MDUNGUAJI
wakati mdunguaji akichagua nani mwingine miongoni mwetu wa kumuua?”
Black Mamba alimaka kwa hasira.Na wakati huu redio ya Vampire ilitoa mkoromo hafifu na sehemu iliyokuwa na taa ndogo nyekundu iliwaka. Hii ilikuwa dalili nzuri, na Vampire alizidi kupata moyo. Alivua gwanda lake la juu lililokuwa likimbughudhi wakati akiishughulikia ile redio kwa joto na kubaki na fulana yake ya kijeshi, akilitupia pembeni lile gwanda na kuzidi kuzama kwenye ufundi wake. Black Mamba aliyekuwa karibu yake naye alivua gwanda lake na kubaki na fulana iliyofanana na ile ya Vampire, naye akitupia gwanda lake karibu na lile la Vampire. Baada ya mvua ya usiku uliopita, jua lilikuwa limetokeza na hali ya hewa ilikuwa nzito iliyochanganyika na joto.
“Nasema tuendelee na safari ya kurudi kambini, lakini tuwaache wenzetu waliouawa huku huku!” Stealth alisema.
“Nasema kuna msaliti miongoni mwetu!” Vampire aliropoka huku bado akiendelea kutengeneza redio yake bila hata ya kuinua uso wake.
Kimya kizito kilitawala.
Wapiganaji wenzake walibaki wakimtazama kwa butwaa iliyokithiri. Lakini Vampire alikuwa ameshatoa hoja yake na sasa alikuwa amezama katika kutengeneza redio yake, ambayo sasa ilikuwa inatoa sauti hafifu za mbinja huku taa nyekundu na ya njano zikiwaka kwa pamoja. Sasa alichohitaji ni kwa ile taa nyekundu kuzimika na ile ya njano kuwaka peke yake, na hapo redio yao ingetengemaa.
Na sekunde hiyohiyo wapiganaji wenzake walilipuka kwa kauli za mishangao bila mpangilio, kila mmoja akitoa wazo lake dhidi ya ile hoja ya kuwepo msaliti miongoni mwao.
“Huo ni wazimu mtupu Vampire!” Alisema Black Mamba.
“Unafanya masikhara!” Swordfish alimaka.
“Hilo linawezekanaje, bwana?” Alpha alihoji.
“Msaliti...?Miongoni mwetu? Aaaw Vampire! Kwa lengo gani, sasa?” Black Mamba alibwata tena.
“Uko sahihi kabisa komredi! Kuna mtu anatuuza kwa mdunguaji hapa, lakini kwa nini? Na kwa namna gani?” M-Senegali Honey-Bee alisema, akiungana na Vampire.
Ulikuwa ni mgongano wa mawazo miongoni mwao. Wote walishangazwa na hoja ile, kila mmoja kwa namna yake;isipokuwa Vampire mwenyewe, ambaye alikuwa akiendelea kuishughulikia redio yake, na Stealth kutoka Naijeria ambaye alikuwa akiitazama hali ile kwa udadisi na umakini mkubwa.
Yeye alikuwa kiongozi wa kikosi kile, na alitakiwa awe makini ili aweze kufanya
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
maamuzi ipasavyo. Lakini tayari alishaona kuwa hali ilikuwa imefikia pabaya.
Kimya kilitanda upya miongoni mwa wapiganaji.Walianza kuangaliana
kwa mtazamo mpya, kila mmoja akijaribu kumpima mwenzake akilini mwake iwapo iliwezekana akawa ndiye msaliti kwa mujibu wa kauli ya Vampire, kama ilivyoungwa mkono na Honey-Bee.
Haikuwa hali nzuri hata kidogo.
Hawa ni watu wanaofanya mambo yao yote kama kitu kimoja; kila mmoja akikabidhi usalama wa maisha yake kule porini katika mikono ya mwenzake, na ikibidi, wote wakiweka usalama wa maisha yao kwa mmoja kati yao. Hiyo ndiyo kanuni yao kuu ya mapambano katika medani ya vita. Wote waliijua na kuiamini kanuni hii. Lakini baada ya kauli ya Vampire, wapiganaji wale walipoteza kabisa imani na kanuni ile na badala yake shaka na kutoaminiana vilitawala mioyoni mwao; kila mmoja dhidi ya wenzake.
Stealth, kiongozi wa kampeni ile ya kivita iliyovurugika, aliwatazama wapiganaji wenzake mmoja mmoja, kama kwamba kwa kufanya vile angeweza kutambua, kwa kuangalia tu, iwapo kulikuwa kuna ukweli katika kauli ya Vampire.Na kama ndivyo, basi labda kwa kuwaangalia namna ile angeweza kujua ni yupi miongoni mwa wapiganaji wale alikuwa akiwasaliti.Na kwa nini?
Alijikuta naye akikodolewa na macho manane ya wapiganaji wanne, yakitaka kuona ataamua nini na atachukua hatua gani. Ukimya mzito ulitanda baina yao, ukisindikizwa na sauti za ndege na wanyama wengine wa msituni. Upepo uliotikisa matawi ya miti iliyowazunguka ulikuwa ukija na hewa ya joto iliyoongezea mashaka yaliyotawala muda ule. Hatimaye Stealth alituliza macho yake kwa mpiganaji pekee ambaye hakuwa akimkodolea macho wakati ule, na macho ya wapiganaji wote wengine nayo yakamgeukia Vampire ambaye muda wote ule alikuwa ameinamisha kichwa chake akiendelea kutengeneza ile redio yao ya mawasiliano.
“Vampire!” Stealth aliita kwa sauti yake nzito iliyojaa mamlaka ya kijeshi, na Vampire kutoka Tanzania aliinua uso wake na kumtazama kiongozi wao. Alikutana na macho kumi ya wapiganaji wenzake watano waliobaki pamoja naye katika kizaa zaa kile, kila jozi ya macho ikiwa na hisia zake. Alimtulizia Stealth macho ya kuuliza bila ya kusema neno.
“Hiyo ni shutuma nzito na mbaya sana mpiganaji!” Stealth alimwambia huku akimtazama kwa macho makali. Vampire hakutetereka hata kidogo.
“Ni shutuma nzito na mbaya, lakini yenye kuleta maana sana Afande!” Alimjibu huku akimtazama machoni.
“Ni nini kilichokufanya useme hivyo, mpiganaji?” Stealth alimuuliza kwa
MDUNGUAJI ukali.
“Ndiyo Vampire. Tuambie...” Swordfish kutoka Tanzania alianza kudakia, lakini Stealth alimnyamazisha kwa ukali.
”Hebu kelele wewe!” Halafu hapohapo akamgeukia tena Vampire, akimwacha Swordfish akifunga mdomo wake kabla hajatoa dukuduku lake.
“Nilichofanya ni kutumia akili yangu ya kuzaliwa tu, Afande! Kama jinsi ambavyo sote tunatakiwa tufanye!” Vampire naye alimpayukia Stealth kwa ukali, na kubaki akimtazama kwa macho yaliyojaa ghadhabu.
“Aaaaw, Vampire! Akili ya kuzaliwa pekee haitoshi kukufanya utoe shutuma nzito kama hiyo bwana...” Black Mamba alimaka kwa kukereka na kigezo alichotumia Vampire kutoa shutuma kama ile.
“Akili ya kuzaliwa ndiyo kila kitu humu msituni Mamba, na wewe...kila mmoja wetu... unajua hilo! Vampire yuko sahihi kabisa wapiganaji! Yaani unahitaji kutumia hiyo mi-akili yako ya kuzaliwa tu kujua kuwa kuna mtu anayempa mdunguaji habari za mienendo yetu!” Honey-Bee alimchachamalia Black Mamba na kuwageukia wenzake waliobaki, akimtetea Vampire.
Wapiganaji wengine walianza kuchachamaa kuipinga ile hoja lakini Stealth hakutoa nafasi hiyo.
“Sasa basi, wapiganaji!” Alifoka na kurudisha nidhamu baina ya wapiganaji. Jahazi lake lilikuwa linazama katika dhoruba kubwa la kutoaminiana na kufarakana, na hiyo ni dhoruba mbaya kabisa katika medani ya vita kama ile.
Aliwatazama wapiganaji wenzake kwa hasira.
“Mna matatizo gani ninyi lakini, eenh?”
“Kwa heshima zote Afande! Hilo swali unatakiwa umuulize Vampire!
Kwa nini anataka kuzidi kuichanganya hali tuliyo nayo na hii laghai yake ya msaliti...?”
“Kimya mpiganaji!” Stealth alifoka na kubaki akihema kwa hasira huku
akiwatazama wale wapiganaji wenzake mmoja baada ya mwingine.
“Ni nini kanuni yetu ya makabiliano katika mpango huu, wapiganaji?”
Alibwata kuwauliza wapiganaji wake.
“All for one, and one for all, Sir!” Walijibu kwa pamoja, wakimaanisha
“Wote kwa ajili ya mmoja wetu, na mmoja wetu kwa ajili ya wote”, ingawa
Vampire hakuwa na hamasa kubwa ya kutoa jibu lile.
Hiyo haiwezi kuwa sahihi iwapo mmoja wetu anatusaliti bwana! Alijiwazia peke yake kwa hasira.
“Na ni ipi kanuni ya makabiliano dhidi ya wasaliti, wapiganaji?” Stealth aliuliza tena kwa sauti kubwa ipaswayo kutolewa wakati wa kuongoza gwaride
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI la kijeshi.
“Tunawauwa wasaliti mara tunapowabaini, afande!” Wapiganaji wote walijibu kwa pamoja.
Stealth alibaki akiwatazama mmoja baada ya mwingine huku akihema kwa hasira. Kisha akasema kwa sauti ya kunong’ona lakini iliyosikika na kila mmoja wa wapiganaji wale. Sauti iliyojaa hasira, kitisho na azma ya kutekeleza kitisho chake.
“Sasa wapiganaji...kama kuna msaliti miongoni mwetu, namtaka ajitokeze mbele sasa hivi!Hiyo ndiyo njia pekee itakayomnusuru na kifo!”
Kimya kilitawala na hakuna mpiganaji hata mmoja aliyejitokeza mbele.
“Kwa heshima zote Afande! Unamaanisha kuwa iwapo huyo msaliti ni mwanaume au mwanamke, ajitokeze mbele, au siyo?”Black Mamba alivunja ukimya ule.Honey-Bee, mwanamke pekee katika kundi lile alimtupia macho ya ghadhabu, lakini hakusema kitu.
“Hivyo ndivyo haswa ninavyomaanisha, wapiganaji!” Stealth alijibu kwa hasira, huku akitembeza macho miongoni mwa wapiganaji wake.Hakuna aliyejitokeza mbele. Stealth aliwaangalia kwa muda mrefu zaidi.
“Sawa! Sasa tutapiga kambi hapa kwa muda tukisubiri Vampire ajaribu tena kuiamsha redio yetu...Kama kwa namna yoyote ile tutakuja kugundua kuwa kweli kuna msaliti miongoni mwetu, basi Mungu na anisaidie wapiganaji, kwani nitamuua mimi mwenyewe! Awe mwanaume au mwanamke!”
Wapiganaji wote walibaki wakimtazama kwa hasira, bila ya kusema lolote. Hakuna aliyependa kuhisiwa usaliti wakati kwa hakika si msaliti.Kwa mara nyingine kila moja alijibanza mahali pake katika msitu ule wa kifo. Wote walikuwa makini kuangalia iwapo wataweza kumuona mdunguaji. Vampire alijiegemeza chini ya mti na kuendelea kucheza na kile kifaa chao cha mawasiliano. Honey-Bee alimsogelea pale alipokuwa na kuketi kando yake.
“Uko sahihi Vampire...tuna msaliti miongoni mwetu.” Alimwambia kwa sauti ya chini. Vampire aliacha kuishughulikia redio yake na kumtazama kwa muda.
“Hilo liko wazi kabisa...na...nashukuru kwa kuniunga mkono. Sijui kwa nini wengine wanakuwa wagumu kuliona!” Alimjibu yule mwanadada mwenye shabaha.
“Shauri lao! Ukweli ni kwamba msaliti tunaye humu humu...na hiyo ni mbaya sana...”
“Yeah...yaani ni kwamba tunatembea na wakala wa kifo!”
Honey-Bee alipiga kimya kwa muda, kisha akamwambia, “Unaonekana
MDUNGUAJI
kuwa u-mtu mzuri Vampire...na...nisingejali kabisa kukutana nawe kwenye
mazingira tofauti na haya...”
Vampire alitabasamu. “Nawe uko bomba Honey-Bee...nakutamania sana jinsi unavyoweza kupiga shabaha kwa namna yako...ukiwa mwanadada pekee miongoni mwetu.”
Honey-Bee alicheka kwa sauti ya chini, kisha uso wake ukawa makini. “Vampire...mi’ nisingependa kurudishwa nyumbani nikiwa maiti eti kwa kudunguliwa kama njiwa na mdunguaji...Nikifa katika mapambano ya wazi na adui sitajali, lakini hivi...? Hapana. Hiyo si namna yangu ya kufa kishujaa...”
“Of Course hakuna anayependa kufa namna hii...” Vampire aliafikiana naye, asijue ni wapi yule mpiganaji mrembo alikuwa anaelekea na mjadala ule.
“Sasa basi mi’ nakuomba kitu kimoja Vampire...” Honey-Bee alimwambia na kubaki kimya kwa muda, kisha akaendelea, “...iwapo nitauawa huku msituni nawe ukanusurika, nitaomba nikupe namba yangu ya simu, ambayo sasa anayo mama yangu huko Senegali...umpigie...umweleze jinsi gani nilivyopigana kishujaa huku msituni. Mpe hali halisi tafadhali.”
Vampire alipiga butwaa.
“Ah, Honey-Bee...sasa utajuaje iwapo mi’ n’tanusurika? Mi’ naweza kufa, we’ ukabaki!”
“I know...ila hapa ninaweka akiba ya maneno tu. Kwa sasa ni wewe ndiye ninayeweza kukuamini katika hili...na Stealth of course, lakini siwezi kumpa ombi hili yeye...nakuomba wewe Vampire...utanifanyia hivyo niombavyo?”
“Okay...sijui nitaihifadhi vipi namba yako, lakini nitafanya hivyo iwapo itabidi....”
“
Oh, thank you Vampire....namba yangu ni rahisi sana. Ni triple 7, double 7, MTN...huwezi kuisahau hiyo...”
“Ah, yaani unatumia mtandao wa MTN wa Senegali...na tarakimu saba ziwe tano...saba-saba-saba-saba-saba?” Vampire aliuliza kutaka kuhakikisha alichokisikia. Honey-Bee aliafikiana naye, na kumtajia zile namba za mwanzo za ile kampuni ya simu ya MTN. “Na kama ukizisahau hizo namba za mwanzo, basi we shika hizo saba-saba tu, halafu ulizia code namba za MTN kwa Senegali...utampata tu mama yangu...” Honey-Bee alimwambia.
“Okay, hilo limepita...lakini najua kuwa sitalazimika kuitumia hiyo namba...kwani naamini kuwa sote tutatoka salama tu humu msituni...”
“Basi na iwe kutoka kinywani mwako moja kwa moja hadi kwenye sikio la Mungu, Vampire.” Honey-Bee alimwambia huku akimpigapiga begani. Vampire alitabasamu, kisha naye akampa namba ya simu ya mkewe kule
Tanzania. Honey-Bee alitoa kalamu kwenye kombati lake na kuiandika ile namba kwenye mkono wa kombati lake kwa ndani.
“Okay...endelea kutengeneza redio yako sasa...tujaribu kutimiza ahadi zetu Vampire.” Alimwambia huku akisota kurudi mahala alipokuwa amejibanza awali. Vampire alimfanyia ishara ya saluti na kurudia kwenye kazi yake.
Dakika kumi baadaye ile taa nyekundu kwenye kile kifaa chao cha mawasiliano ilizimika na Vampire alimfahamisha Stealth kuwa hatoweza kuendelea kuishughulikia zaidi ile redio, na badala yake waendelee na safari
wakati akiendelea kuijaribu huku wakisonga mbele. Stealth alikubaliana naye, na Alpha alitumwa tena kuchunguza njia. Vampire alikuwa akimalizia kuifunga upya redio yake, wakati ghafla taa nyingine kwenye redio ile, taa ya kijani, ilipowaka.Moyo ulimlipuka na kuanza kumwenda mbio, kwani kuwaka kwa ile taa kulimaanisha kitu kikubwa sana kwake.
Huku umakini wake ukiongezeka maradufu, alichomoa kifaa kilichokuwa
kama mkono wa simu kutoka kwenye ile redio yao ya mawasiliano na
kumwambia Black Mamba aliyekuwa karibu naye aibebe ile redio mgongoni na kupachika visikilizio masikioni mwake, kisha akamwambia aelekee kwenye
kichaka kilichokuwa karibu yao, huku yeye akinyata kwenda mbali na pale walipokuwa na kujaribu kuwasiliana naye kutokea kule alikoelekea.
Black Mamba alitekeleza maelekezo ya Vampire haraka wakati Stealth na
Swordfish wakiificha chini ya shina la mti mkubwa ile miili ya wenzao waliouawa kwa kuifunika kwa matawi ya miti na majani, Honey-Bee akiwalinda kwa umakini dhidi ya shambulizi kutoka kwa mdunguaji. Hawakuwa na habari juu ya kile kilichokuwa kikiendelea baina ya Black Mamba na Vampire.
Black Mamba alianza kupata matumaini ya mawasiliano na kambi yao. Lakini Vampire alikuwa na mawazo mengine kabisa. Kwani kuwaka kwa ile taa ya kijani kulimaanisha kitu tofauti kabisa na hicho.
“Hello, hello, Black Mamba do you read me?” Alisema kwenye kile kifaa, akiuliza iwapo Black Mamba alikuwa “akimsoma”, akimaanisha iwapo alikuwa akimsikia. Lakini hakusikia jibu lolote kutoka kwake.
Alizidi kujichimbia msituni, mbali na alipomuacha Black Mamba, huku akijaribu kutafuta eneo ambalo lingempatia wepesi wa mawasiliano.
“Black Mamba!Black Mamba. Vampire to Black Mamba! Do you copy?”
Alizidi kuongea kwenye kile kifaa akimuuliza Black Mamba iwapo alikuwa
MDUNGUAJI
“akimnakili”. Zote hizi zilikuwa ni lugha zao za mawasiliano zilizomaanisha
iwapo walikuwa wanasikilizana. Sasa alisikia mikoromo hafifu, naye alizidi kujiingiza msituni akijaribu kupata sehemu ambayo ingemletea mawasiliano kwa wepesi zaidi. Aliining’iniza vizuri bunduki yake mgongoni, na kutoa bastola iliyokuwa ikining’inia kwenye mkoba maalum kiunoni mwake, ambapo kama kwa wenzake wote, pia alikuwa amening’iniza chupa maalum ya maji ya kunywa, kisu maalum cha makabiliano ya ana kwa ana na mabomu matatu ya mkononi. Zaidi ya hapo, shingoni alikuwa amening’iniza darubini ya kumwezesha kuona mbali na ile miwani maalum ya kuonea wakati wa usiku.
Bastola ikiwa tayari katika mkono wake wa kushoto na kile kifaa chake cha mawasiliano alichokichomoa kutoka kwenye redio yao kikiwa katika mkono wake wa kulia, alitazama huku na huko kutafuta sehemu iliyokuwa na mwinuko ambako alijua kuwa angeweza kupata mawasiliano ya majaribio na Black Mamba kwa urahisi zaidi.
Moyo ulikuwa ukimpiga kwa nguvu, jasho likimtiririka na woga ukiitekenya nafsi yake, kwani pale alikuwa peke yake na alijihisi kuwa amejianika waziwazi mbele ya mdunguaji hatari.Bila ya kuwa na kinga ya wenzake hakuwa na amani kabisa,lakini pia alijua kuwa mawasiliano na kambi yao lilikuwa ni jukumu lake. Na kama kulikuwa kuna dalili za ile redio yao kutengemaa, ni yeye ndiye aliyetakiwa kuzifuatilia dalili hizo mpaka mwisho.
Kiasi cha kama mita hamsini hivi kulia kwake, aliona mwinuko uliokuwa umezungukwa na miti mirefu iliyoshonana vilivyo. Bila ya kusita alijikunja kutokea kiunoni na kukimbia kwa mtindo wa zigi-zaga kuuendea, bastola yake ikiwa imetangulizwa mbele huku akitembeza macho eneo lote lile. Hisia ya ajabu iliutawala mwili wake wakati akiukimbilia ule mwinuko, kwani alikuwa akitarajia risasi ya mdunguaji kuuiingia mwili wake wakati wowote na kumuondoa duniani. Hiyo ilikuwa ni hisia mbaya sana na alizidisha kasi. Hatimaye alijibwaga chini ya ule mwinuko akiwa salama. Alitazama kule alipotokea na maeneo yaliyomzunguka huku akitweta kwa wasiwasi mkubwa, bastola yake ikiwa tayari kutema risasi iwapo itatokea hali ya kutishia uhai wake.
Kimya.
Aliinua darubini yake na kutazama tena eneo lile, lakini bado hakukuwa na kitu chochote kilichoonekana kuwa nje ya utaratibu.
“
Vampire to Black Mamba! Vampire to Black Mamba! Come in Black Mamba! Talk to me Black Mamba!” Aliongea kwenye kile kifaa cha mawasiliano
alichokuwa nacho, akijaribu kumpata Black Mamba aliyebaki na redio yao
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
kule nyuma, lakini hapa ndiyo kimya kilikuwa kizito zaidi kwani hata ile sauti ya mikoromo haikusikika. Hii ilizidi kumtia wasiwasi.
Alianza kuuparamia ule mwinuko kwa tahadhari kubwa, na alipofika juu ya ule mwinuko tu kile kifaa chake cha mawasiliano kilianza kutoa kelele za mbinja za mfululizo huku ile taa ya kijani ikiwaka na kuzimika haraka haraka. Mara moja Vampire alijitupa chini na kujibanza nyuma ya mti uliokuwa karibu naye, moyo ukimwenda mbio maradufu na macho yakimtembea huku na huko.
“Hallo, Hallo, Black Mam...,” alianza kuongea tena kwenye kile kifaa chake lakini hapo hapo akakiweka mbali na sikio lake, kwani muda huo kilitoa mlio mkali sana wa mbinja za mfululizo. Haraka sana akakizima na kubaki amelalia tumbo pale juu ya ule mwinuko, hisia zake zote zilikuwa makini sana. Sasa alikuwa akisubiri mtikisiko wowote tu usio wa kawaida ashambulie.
Kimya!
Akili ilikuwa ikimtembea kujaribu kusoma tafsiri ya kila hisia iliyomjia, na moyo ulikuwa ukimdumda mithili ya mpira wa ‘cha ndimu’ unavyodunda sakafuni. Hii ilitokana na maelezo aliyoyapata kutoka katika kile kifaa chake cha mawasiliano, kwani pamoja na kuwa hakikuweza kumpa mawasiliano ya maongezi baina yake na Black Mamba, kilimueleza jambo ambalo yeye, kama mtaalamu wa mawasiliano wa kiwango cha juu kabisa, alilielewa vizuri sana.
Kwa namna kile kifaa kilivyofanya, ilimaanisha kitu kimoja tu. Kitu ambacho alikihisi tangu pale ile taa ya kijani ilipowaka kwa mara ya kwanza akiwa na Black Mamba. Sasa alijithibitishia kuwa zile hisia zake za awali zilikuwa sahihi.
Ingawa jasho lilianza kumtoka muda mrefu uliopita, sasa alilihisi upya, kwani lilibadilika na kuwa la baridi kuliko kawaida.Alitazama tena eneo lile kwa darubini yake kwa umakini zaidi, lakini msitu ulionekana kuwa tulivu tu.
Lakini hii si kweli! Kuna kitu hapa...lakini wapi...?
Alikiwasha tena kile kifaa chake cha mawasiliano, na ile sauti kali ya mbinja za mfululizo ilisikika, safari hii ikiwa kali zaidi. Vampire alichanganyikiwa vibaya sana. Alikizima na kubaki akikitazama kile kifaa kama kwamba kilikuwa kina wazimu.
Lakini alijua kuwa kile kifaa hakikuwa na wazimu. Badala yake, kwa kufanya vile kilivyokuwa kikifanya, kilikuwa kikiendelea kumueleza jambo lenye ukweli usiopingika, naye akiwa mtaalamu wa mawasiliano na vifaa vyake, anayeaminiwa na jeshi la Tanzania na hata lile la Umoja wa Mataifa alilokuwa akilitumikia wakati ule, alielewa maana ya kile kifaa kufanya vile.
MDUNGUAJI
Kwa kutoa ile sauti kali namna ile na ile taa ya kijani kuwaka na
kuzimika harakaharaka namna ile, ilimaanisha kulikuwa kuna kifaa kingine
cha mawasiliano katika mzunguko wa mita zipatazo mia moja kutoka pale alipokuwa!
Lakini hilo halikutakiwa kumtoa jasho namna ile, kwani ingewezekana
ikawa ni ile redio yao iliyobaki kwa Black Mamba ambayo ndiyo iliyokuwa
ikiingilia mawimbi ya sauti aliyokuwa akijaribu kuyatuma kwa kutumia kile
kifaa cha mawasiliano alichokuwa nacho.
Kilichomtoa jasho na kumfanya awe makini kuliko kawaida ni uelewa
kwamba kama ingekuwa ni ile redio yao aliyobaki nayo Black Mamba, basi taa ambayo ingekuwa ikiwaka na kuzimika kwenye kile kifaa chake ni ya njano na siyo ya kijani! Kwani kwa wakati ule kifaa alichokuwa nacho mkononi
kilikuwa kinatuma mawasiliano, na ile redio aliyobaki nayo Black Mamba
ilikuwa ikipokea mawasiliano. Kuwaka kwa taa ya kijani kulimaanisha kuwa
kulikuwa kuna kifaa kingine cha mawasiliano ndani ya wigo wa mita mia moja
kutoka pale alipokuwa, ambacho nacho pia kilikuwa kikituma mawasiliano
kama yeye alivyokuwa akijaribu kufanya, na siyo kupokea mawasiliano kama
jinsi ambavyo kifaa alichobaki nacho Black Mamba kilivyotakiwa kifanye.
Hali hii ilisababisha mawimbi ya kutuma mawasiliano kutoka kwenye kifaa
chake yaingiliane na yale ya kifaa kingine kilichokuwa kikitumika kutuma
mawasiliano katika eneo lile.Kwa hiyo kulikuwa kuna mtu...au watu...wengine
waliokuwa wakitumia kifaa cha kurushia mawasiliano katika eneo lile!
Ni nani? Na anatuma...au wanatuma... mawasiliano kutokea sehemu gani?
Hisia zake zikiwa katika kiwango cha juu kabisa cha umakini, Vampire alitambaa kijeshi kwa kutumia tumbo juu ya kile kichuguu na kuchungulia upande wa pili wa ule mwinuko huku akihakikisha kuwa hakuweza kuonekana kirahisi kutokea upande wa pili wa ule mwinuko. Aliona mteremko mkali uliokuwa umetapakaa mawe makubwa makubwa na miti mingi mirefu kama ile iliyokuwa juu ya kile kichuguu.Miti hii ilishonana sana kiasi cha kuifanya sehemu ile ya msitu ule mnene izidi kuogopesha.
Alitazama huku na huko kwenye ule mteremko kwa kutumia darubini yake bila ya kuona kitu chochote cha kuweza kuvuta udadisi wake. Alipowasha tena kile kifaa chake cha mawasiliano, zile mbinja ziliongezeka maradufu, ile taa ya kijani ikiwaka mfululizo, na kwa mbali akisikia muingiliano wa mawimbi ya sauti waziwazi, jambo lililomhakikishia kuwa ni kweli kulikuwa kuna mtu au watu waliokuwa wakitumia kifaa au vifaa vya mawasiliano katika eneo lile.
Na walikuwa karibu sana na pale alipokuwa.
Je, anaweza kuwa ni mdunguaji akijaribu kuwasiliana na wenzake baada ya kujeruhiwa na risasi ya Honey-Bee?Au ni kwamba ndiyo amefika karibu na ile kambi ya waasi waliyokuwa wakiisaka?
Yote hayo yaliwezekana, kwani tangu awali ni yeye ndiye aliyeweza kunasa
mazungumzo ya waasi kwa kutumia ile redio walipokuwa kule kambini kwao. Ni ugunduzi huo ndiyo uliosababisha wao kutumwa kwenye operesheni ile ya hatari ambayo hadi wakati ule ilikuwa imeshagharimu maisha ya wenzao wanne ilhali wao waliobaki wakiwa hawaaminiani kabisa kutokana na hisia za kuweko msaliti miongoni wao; hisia ambayo pia ni yeye ndiye aliyeiweka wazi mbele ya wenzake.
Na sasa huu ugunduzi wa kuwepo mtu au watu wengine wanaotumia kifaa cha mawasiliano humu msituni ulizidi kumzidishia hofu ya kuwepo kwa jambo baya kuliko yale yaliyopita kichwani mwake wakati ule.Kwani pamoja na uwezekano kuwa ni ama mdunguaji ndiye aliyekuwa akijaribu kufanya mawasiliano na wenzake, au ni waasi wakiwa katika kambi yao ambayo wao ndiyo walikuwa wametumwa kuitafuta, pia kulikuwa kuna uwezekano mwingine...
Vampire alikiweka mfukoni kile kifaa cha mawasiliano na akiwa amejikunja kutokea kiunoni, aliuteremka kwa kasi ule mteremko mkali hadi nyuma ya mmoja kati ya miti iliyokuwa kule chini na kujibanza kwa kuuegemea kwa mgongo wake huku akihema kwa nguvu akiwa ameinua bastola yake mbele ya uso wake kwa mikono yake yote miwili.
Aliangalia kulia na kushoto kwake, kisha akachungulia nyuma ya ule mti aliokuwa ameuegemea. Kiasi cha hatua kama ishirini hivi kutoka pale alipokuwa kulikuwa kuna jabali kubwa. Muda huohuo aliona kundi la ndege wa mwituni likiruka kwa mkupuo kutoka nyuma ya lile jabali, naye alifinya macho kwa umakini. Alijilaza chini na kuweka darubini yake machoni kutazama kule walipotokea wale ndege.
“Well, well, well...ni nani aliyewakurupusha ghafla hivyo rafiki zangu, eeenh...?” Alijisemea mwenyewe kwa sauti ya chini kama kwamba wale ndege wangeweza kumsikia.
Alizidi kuangalia kule walipotokea wale ndege kwa darubini yake, lakini hakuona kitu kingine kisicho cha kawaida. Taratibu alianza kutambaa kwa tumbo kuelekea kule kwenye lile jabali, bunduki yake ikiwa mgongoni kwake, ile bastola yake ikiwa mkononi mwake. Ulikuwa ni mwendo wa taratibu na wa uangalifu sana, kwani hakutaka kabisa kufanya kosa ambalo lingesaliti uwepo wake eneo lile. Kufikia hapa hofu yake ya kibinadamu ilikuwa imemezwa
MDUNGUAJI
kabisa na ujasiri wake wa kijeshi, hivyo pamoja na kuwa moyo wake ulikuwa ukibondabonda kwa nguvu na kasi kubwa ndani ya kifua chake, akili yake haikuwa ikiutilia maanani hata kidogo. Badala yake ilikuwa ikizisikiliza njia zake zote za hisia ambazo zingemuwezesha kuhisi jambo lolote la hatari katika eneo lile na kumuwezesha kuchukua hatua muafaka katika mazingira yale.
Hizo zilikuwa ni mbinu za medani, naye alikuwa makini sana katika kuzitumia kwa usalama wake.
Mwendo mfupi baadaye alisikia mchakato hafifu wa majani kutokea hatua
chache kulia kwake, na harufu moja kali na mbaya sana ilizivamia pua zake. Hapohapo alijikausha akiwa amelalia tumbo huku bastola yake ikiwa makini mkononi mwake. Bila kugeuza kichwa chake, alizungusha mboni za macho yake kuelekea kule ulipotokea ule mchakato na ile harufu mbaya, akiwa tayari kukabiliana na lolote litakalofuatia.
Kwanza alianza kuona majani yakitikisika, kisha macho yalimtoka na mwili ulimfa ganzi. Alijikausha kama alivyokuwa na kuendelea kukikodolea macho kile kilichokuwa kikielekea pale alipokuwako. Nyoka mkubwa sana ambaye hajawahi kumuona hata siku moja maishani mwake alikuwa akimwendea kwa mwendo wa taratibu, kichwa kikiwa wima. Jasho lilimtoka Vampire, na moyo ulimwingia ubaridi wa ghafla. Akili yake ilifanya kazi haraka sana. Angeweza kumlipua kwa bastola yake na kumuua yule nyoka, lakini kwa kufanya hivyo pia angekuwa akiwashitua wale adui waliokuwa wakitumia kifaa cha mawasiliano eneo lile. Lakini pia, kama angejaribu kumpiga risasi halafu akamkosa, basi hakuwa na shaka kabisa kuwa lile joka lingemuua mara moja kwani alijua kuwa pamoja na ukubwa wa umbo lake, bado lile joka lilikuwa na wepesi wa ajabu, kama jinsi nyoka wengine walivyo.
Sasa nifanye nini Mungu wangu!
Mbinu za medani zilimwambia kuwa kama akitulia kama alivyokuwa bila ya kumchokoza yule mnyama mkali, alikuwa na nafasi kubwa ya kuishi. Kufikia hapo lile joka lilikuwa limeshafika karibu sana na pale alipokuwa.Oh, My Goodness! Oh, My Goodness...!
Taratibu alishusha mboni za macho yake na kuzielekeza eneo la chini ya kichwa cha yule nyoka mkubwa ambaye kufikia wakati ule alikuwa kiasi cha mita zipatazo mbili tu kutoka kwake. Alijua kuwa kukutanisha macho na mnyama yule kutakuwa ni kujithibitishia umauti. Hivyo ndivyo alivyofundishwa na maafande wake katika mbinu za medani, na hivyo ndivyo alivyoamini. Lakini moyo wake utaweza kumruhusu afanye hivyo bila kumshawishi kutimua mabio au kumshambulia yule mnyama kwa nia ya kujilinda?
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Sasa kulikuwa kuna nusu mita tu baina yao, na ile harufu kali iliyokuwa
ikitoka mwilini mwa yule mnyama ilimletea kichefucheu kikali na akahisi kutapika.Hapohapo wazo baya lilipita kichwani mwake, kuwa huenda ile ndiyo njia ya yule mnyama kuwakurupusha maadui zake kabla ya kuwadhuru kwa sumu yake kali. Ile harufu ilikuwa haivumiliki hata kidogo!
Oh, Mungu wangu! Nimeshachelewa...!
Vampire alijikausha na kubana pumzi zote, akiifungia ile harufu mbaya isizidi kumshambulia na kumletea hali ya kutapika ambayo moja kwa moja ingemjulisha yule nyoka juu ya kuwepo kwake eneo lile.
Alijikausha kama gogo.
Joka lilimpita kiasi cha sentimeta kumi mbele ya uso wake kama vile alikuwa ni jiti tu la porini na si binadamu mwenye uwezo wa kujaribu kulidhuru. Lilipopita, liliupanda mkono wa Vampire uliokuwa umelazwa mbele yake kama kwamba ni kijiti miongoni mwa vijiti vilivyotapakaa mle msituni huku likitoa sauti mithili ya mbinja ndogondogo na kuendelea na safari yake taratibu mno. Vampire alifumbua macho na kukodolea sehemu ya mwisho ya lile joka ikimalizia kutambaa juu ya mkono wake,akijitahidi kadiri awezavyo kutokuukurupua mkono wake kutoka chini ya mwili wa lile joka. Ilikuwa ni dakika moja ya kuogofya sana katika maisha yake.
Lilipopita na kumwachia uhai wake, Vampire alishusha pumzi ndefu na kulaza kichwa chake juu ya mkono wake na kumshukuru Mungu, akiwa amelowa mwili mzima kwa jasho lililombubujika kwa wingi mno ndani ya ile dakika moja kuliko muda wote ule aliokuwa mle msituni.
Kwa muda wa kama dakika tano zilizofuata Vampire alibaki akiwa amejilaza palepale, akitapatapa kuvuta pumzi katika mapafu yake baada ya kuzibana kwa muda mrefu na wakati huohuo akikusanya upya ujasiri wa kuendelea na lile jambo alilolianzisha huku moyoni akijilaumu kwa kuwaacha wenzake na kwenda eneo lile peke yake. Hatimaye alianza kutambaa tena taratibu na kwa tahadhari kubwa kuliendea lile jabali.
Ulikuwa ni mwendo uliojaa hofu kubwa, kwani sasa alijua kuwa alikuwa anakabiliana na hatari zaidi ya moja. Kulikuwa kuna uwezekano wa mdunguaji kumuona na kumuondoa duniani mara moja, tena akiwa peke yake bila ya wenzake kujua. Hili lilimtia hofu, kwani angalau wale wenzao waliouawa hapo awali miili yao ilijulikana ilipo. Yeye angeweza kuozea kule porini bila ya wenzake kujua alipopotelea. Lakini pia kulikuwa na hofu ya kushtukiwa na wale watu au mtu aliyekuwa akijaribu kutumia kifaa cha mawasiliano mle msituni na kushambuliwa bila ya yeye kuwa na hadhari ya kutosha;
MDUNGUAJI
jambo ambalo matokeo yake yasingekuwa tofauti sana na kushambuliwa na mdunguaji mwenyewe. Hatari nyingine ni ya kukutana na mnyama mwingine wa hatari mle msituni kama lile joka na kushambuliwa.
Mawazo haya yalikuwa yakipita kichwani mwake huku akitambaa kuliendea
lile jabali. Mara alisikia kishindo hafifu kutokea nyuma ya lile jabali alilokuwa akiliendea, na moyo wake ukapiga tiki-taka ndani ya kifua chake. Alitulia na kusikiliza kwa umakini zaidi, sasa akiwa amebakiza takriban hatua kumi kutoka kwenye lile jabali. Alisikia tena kile kishindo na mara moja akaelewa kuwa zilikuwa ni hatua za mtu aliyekuwa akitembea kwenye mawe, na kwa jinsi ilivyosikika, huyo mtu alikuwa akielekea pale alipokuwa. Haraka sana alijiinua na kukimbia kwa kasi huku akijitahidi kutotoa vishindo kuliendea lile jabali.
Huku nyuma Black Mamba naye alikuwa ameshajawa wasiwasi.Muda
mrefu ulikwishapita tangu Vampire apotelee msituni kutafuta sehemu iliyoweza kutuma mawimbi ya mawasiliano baina yao kwa urahisi.Hakuwa amesikia lolote kutoka kwake kupitia kwenye ile redio yao.Alipojaribu kuwasiliana na Vampire kwa kutumia ile redio aliyobebeshwa hakuwa akipata kitu. Jasho lilimtiririka na alishukuru kuwa naye, kama Vampire, aliamua kuvua lile gwanda lake la juu na kubaki na ile fulana ya kijeshi ambayo kidogo ilimletea unafuu dhidi ya joto lilitokana na hewa iliyojaa unyevunyevu wa mvua ya siku iliyopita.
“Hallo, Hallo Vampire unanisikia? Mimi sisikii lolote kutoka kwako! Narudia sisikii lolote kutoka kwako!” Aliongea kwa mara nyingine tena kwenye ile redio bila matarajio ya kusikia chochote kutoka upande wa pili wa chombo kile.
Kimya.
Kutoka pale alipokuwa aliweza kusikia harakati za wapiganaji wenzake waliokuwa wakishughulika kuihifadhi miili ya wale wenzao waliouawa.
Sasa kwa nini Vampire harudi?
Kama mawasiliano hayapatikani na walikuwa wameshakubaliana kuwa wanarudi kambini kwao, hakukuwa na sababu ya kuendelea kuhangaika kule msituni wakati angeweza kupata nafasi ya kuitengeneza vizuri ile redio kule kambini.
Au tayari naye ameshauawa na mdunguaji huko alipo? Bunduki aliyokuwa akitumia mdunguaji ilikuwa haitoi sauti, hivyo Vampire angeweza
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
kuwa ameuawa huko alipokwenda nao wasijue lolote juu ya hilo. Wazo hili lilimzidishia mashaka na akajikuta akitafuta hatua muafaka ya kuchukua asiipate.
Alitaka ajaribu kumfuata Vampire kule alipoelekea, lakini hili aliliona gumu kutokana na uwezekano mkubwa wa wao kupoteana na kuleta kizaazaa kingine. Wazo jingine lililomjia ni kurudi kule walipowaacha wenzao ili akawajulishe juu ya hali hiyo na labda watakubaliana kumsaka pamoja.
Lakini mbona hata Alpha aliyetumwa kuchunguza njia yao mpya ya kurudia kambini hajarudi? Isingekuwa rahisi kwa wao kuondoka eneo lile mpaka Alpha atakaporudi, na kwa hali hiyo basi, hata yeye kutoka pale ingekuwa ni kumchuuza Vampire pindi atakaporudi na kumkosa. Huenda kwa kufanya hivyo ndiyo atakuwa anampoteza kabisa mwenzake...kama bado yuko hai.
Black Mamba alijibanza chini ya mti mkubwa akihofia risasi za mdunguaji, huku akiendelea kumsubiri Vampire. Angalau vile vishindo kutoka kwa wale
wenzake waliokuwa wakishughulika kule walipowaacha wakati yeye na Vampire wanakuja eneo hili, vilimpa matumaini kuwa hakuwa mbali na wenzake.
Mara akasikia mayowe na kelele kutoka kule kwa wale wenzao zikiambatana na milio ya bunduki, naye bila kufikiri zaidi alijitupa pembeni na kujisokomeza katikati ya kichaka huku akiangaza kule walipokuwa wenzake, mtutu wa bunduki yake ukiwa tayari mikononi mwake.
Oh, My God! Mdunguaji ameshambulila tena...!?
Stealth na Swordfish walikuwa wanamalizia kuifunika kwa magogo ya miti ile miili ya wale wenzao waliouawa kwa risasi haramu za mdunguaji huku Honey-Bee akiwa makini na bunduki yake akitafuta mtikisiko wowote ambao ungeweza kumjulisha kama mdunguaji alikuwa karibu yao amuondoe duniani.
“Safari hii namuua huyu mwanaharamu, nakwambia! Yaani we’ mwache ajitikise kidogo tu na huo ndiyo utakuwa mwisho wake!” Honey-Bee alisema kwa hasira huku akiwa amejibanza vizuri nyuma ya mti akiwakinga wenzake waliokuwa wakiifunika ile miili ya wenzao ili isije kutafunwa na wanyama wa porini.
Stealth alisogeza vizuri gogo la mwisho kuifunika ile miili ya wale wenzao na kumgeukia Honey-Bee. Alimtazama kwa muda yule mwanamke jasiri na hatari kwa shabaha, kisha akamgeukia Swordfish kutoka Tanzania, halafu akamgeukia tena Honey-Bee kutoka Senegal.
MDUNGUAJI
“Nadhani hatashambulia tena. Si unajua kuwa umemjeruhi?” Alimwambia.
“Hapana! Hawezi kunidanganya mimi, bwana! Huyu mwanaharamu bado anasubiri, anataka tujisahau halafu ashambulie...kama wadunguaji wote!”
Honey-Bee alimjibu Stealth kwa jazba kubwa. Stealth alitazama eneo lile, na kugundua kuwa wenzao hawakuwepo eneo lile.
“Oi! Najua Alpha anachunguza njia yetu mpya, lakini wengine wako wapi?” Aliuliza.
Swordfish na Honey-Bee walitazamana. Swordfish, aliyekuwa nyuma ya shina kubwa la mti ambao chini yake ndiyo waliwahifadhi wale wenzao waliouawa kwa kuwafunika kwa matawi na magogo ya miti, alitoka nyuma ya ule mti na kutazama huku na huko. Hapo hapo, kwa pembe ya jicho lake, Honey-Bee aliona mwanga uliotokana na mwale wa jua kupiga kwenye kitu kama kioo au chuma, kutokea sehemu juu ya miti iliyokuwa kulia kwake.
“Lala chini!” Alipiga yowe na kujitupa chini huku akigeukia ule upande alioona ule mwanga ukiakisiwa na kumimina risasi. Wakati huohuo Swordfish aliachia yowe kubwa la uchungu na kutupwa nyuma ya lile shina la ule mti mkubwa na kutumbukia mtaroni.
“Swordfish amedunguliwa!”Stealth alipiga kelele huku akijitupa chini.
Kwa mara nyingine tena msitu ulirindima kwa milio ya bunduki wakati Honey-Bee na Stealth wakimimina risasi upande ule ilipotokea risasi ya Mdunguaji. Kutokea ndani ya ule mtaro, Swordfish alisikika akipiga mayowe ya uchungu.
“Swordfish! Swordfish...Umejeruhiwa vibaya?” Stealth alipiga kelele huku akizidi kumimina risasi kule walipohisi kuwa mdunguaji alikuwako.
“AAAAAAKH! mwanaharamu kanipiga risasi begani! Aaaaw! Inauma vibaya sana AAAYYYYAA!” Swordfish alilia kwa uchungu.
Kule alipokuwa, Black Mamba aliamua kukimbilia kule alipoelekea Vampire, kwani alijua kama mdunguaji alikuwa kule walipokuwa wenzake, basi uwezekano ni kwamba Vampire alikuwa hai huko aliko.
Kule alikokuwa, Vampire aliegemeza mgongo wake nyuma ya lile jabali huku bastola yake ikiwa makini katika mikono yake yote miwili, na moyo ukimpiga kwa nguvu sana. Alijiweka sawa na kutulia, akisikiliza vile vishindo vilivyokuwa vikitokea upande wa pili wa lile jabali, na hata pale alipokuwa anajiweka sawa nyuma ya lile jabali aliisikia waziwazi sauti ya yule mtu.
“...as earlier notified, the route is now south-south west. Zero-Six-Five degrees north of the hill...(...kama nilivyokueleza awali, njia sasa imekuwa ni kusinikusini-mashariki. Nyuzi Sifuri-Sita-Tano mashariki ya mlima...)”
Pumzi zilimbana na ghadhabu zikampanda. Alijizatiti na bastola yake akimsubiri yule mtu aliyekuwa akiongea kwenye kifaa cha kutuma mawasiliano ajitokeze.
Na hapo yule mtu alitokea akiwa amekishikilia kifaa chake cha mwasiliano kwenye sikio lake kwa mkono mmoja ilhali kwa mkono mwingine akiwa ameshikilia bunduki.
“Stay right where you are!” Vampire alibwata huku akiwa amemnyooshea bastola kichwani yule mtu. Jamaa aliruka kwa mshituko na kugeukia upande ilipotokea sauti ya Vampire huku mkono wake wenye bunduki akiuelekezea kule alipokuwapo Vampire tayari kwa kushambulia, lakini Vampire alikuwa makini. Aliruka kwa hatua moja kubwa na kuipiga teke ile bunduki huku bado akiwa ameielekeza bastola yake kichwani kwa yule mtu aliyekuwa amevaa magwanda ya kijeshi. Bunduki ilitupwa pembeni, na yule mtu aliduwaa huku ameshikilia kile kifaa chake cha mawsiliano.
“Heh!” Vampire alitoa mguno wa mshangao baada ya kumtambua yule mtu, na hapo ndipo ile milio ya bunduki za akina Honey-Bee na Stealth iliposikika kutokea kule alipowaacha wenzake. Akili yake ilishindwa kuhimili matukio yale yaliyotokea kwa haraka namna ile na kidogo alitetereka. Alijaribu kugeuza kichwa chake kuangalia kule ile milio ilipokuwa ikitokea huku bado akiwa amemuelekezea bastola yule adui yake.
Hilo lilikuwa ni kosa, kwani hapohapo adui yake aliirushia teke ile bastola iliyokuwa mikononi mwake. Vampire aligundua kosa lake mapema. Aliruka nyuma haraka na hivyo lile teke halikumpata.Hapo hapo alimshidilia teke la kifua lililomtupa nyuma kwa nguvu yule adui na kumbiringisha nyuma ya lile jabali kulikokuwa na mteremko mkali. Vampire hakumuacha, alimuendea kwa kasi kule alipokuwa akiporomokea huku bastola yake ikiwa makini mkononi mwake. Jamaa alijibamiza kwenye shina la mti na kuanza kujiinua huku akigumia kwa uchungu, lakini Vampire alimvamia na kumbabatiza kwa mkono wake wa kushoto pale kwenye mti huku akiwa amemuwekea bastola kwenye paji la uso na akimtazama kwa macho yaliyojaa ghadhabu.
“Wewe! Unatusaliti sisi!Why?” Vampire alimkemea adui yake.
Kanali Nathan Mwombeki, au jina la uficho Alpha wa kikosi maalum cha umoja wa mataifa cha kulinda amani nchini Sierra Leone, mpiganaji kutoka
Tanzania, alimtazama Vampire kwa jicho la ghadhabu huku akijaribu bila
mafanikio kujinasua kutoka kwenye ile kabali iliyombana pale kwenye mti. Walibaki wakitazamana kwa hasira na muda huo Vampire alisikia ukimya kutoka kule ambapo awali ilisikika milio ya bunduki. Akili ilimtembea, asijue achukue hatua gani.
Alimuachilia yule Mtanzania mwenzake na kurudi hatua tatu nyuma huku akiendelea kumnyooshea bastola na kumtazama kwa ghadhabu. Kanali Nathan Mwombeki alijishika shingo sehemu iliyokuwa imebabatizwa kwenye mti huku akimtazama yule mpiganaji mwenzake kwa hasira.
“Nilijua tu kuwa kuna msaliti miongoni mwetu, lakini sikutegemea kabisa kama ungekuwa wewe Nathan...kwa nini? Ili iweje? Wenzetu wameuawa, na bila shaka sasa hivi kuna mwenzetu mwingine ameuawa huko. Kumbe ni wewe ndiye unayetuuza kwa mdunguaji? Kwa lengo gani Nathan, eeenh? Kwa lengo gani....”
“Hebu acha kulalama kama mtoto wa kike wewe! Huu ni uwanja wa mapambano bwana! Unaona ajabu gani watu kufa kwenye uwanja wa mapambano?” Kanali Nathan Mwombeki alimjibu kwa jeuri huku bado akiwa ameegemea ule mti na mikono yake ikiwa imeinuliwa juu na kile kifaa chake cha mawasiliano kikiwa bado mkononi mwake.
“Khah! Nathan! Unatuuza kwa mdunguaji aliye upande wa adui halafu unatarajia nisishangae? Ina maana wewe uko upande wa waasi Nathan? Yaani Jeshi letu la Tanzania limekuteua uje uliwakilishe katika mpango huu wa kulinda amani halafu wewe unalisaliti kwa kuingia upande wa waasi? Hii inakuwaje lakini?” Vampire alimuuliza kwa mshangao uliochanganyika na hasira. Kwa kweli ilimuwia vigumu sana kuielewa hali ile. Kama msaliti wao angekuwa ni m-Sierra Leone Vampire angeelewa, lakini Mtanzania! Hapana, ilikuwa ni vigumu sana kuelewa.
Alpha alimtazama kwa kebehi huku akifuta mchirizi wa damu iliyokuwa ikimtiririka kutoka kwenye upande wa sura yake, baada ya kujigonga kwenye mawe wakati akiporomoka baada ya kushindiliwa teke la kifua na Vampire.
“Ni dhahiri kuwa huwezi kuelewa Vampire, kwa hiyo naomba uniache nawe hutajuta kwa hilo.Lakini kama unataka kujitia ushujaa, basi ujue ni wewe ndiye utakayeathirika na si mimi!” Kanali Nathan Mwombeki alimwambia Vampire kwa kujiamini. Vampire alimshangaa.
“Nathan, sielewi ni nini unachosema na naamini si kazi yangu kuelewa. Tumekuja huku kwa lengo moja lakini mwenzetu umeamua kutunga malengo yako mwenyewe. Nakuweka chini ya ulinzi na nitahakikisha nakufikisha kambini, ambako nina hakika Court Marshall ndiyo itakayoamua mwisho
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI wako!”
Hapo Nathan alikurupuka kumsogelea Vampire huku akitaka kupingana naye, lakini hapohapo bastola ya Vampire ilikohoa, na Nathan aliachia yowe la mshituko. Risasi iliuchimba ule mti milimita chache sana kutoka kilipokuwa kichwa chake.
“Tulia hapo hapo Nathan! Sijakukosa kwa bahati mbaya. Mara ya pili nakukongoroa goti, pumbavu!” Vampire alifoka na Nathan alirudi kwenye ule mti huku macho yamemtoka pima.
Kule alipokuwa, Black Mamba aliusikia ule mlio wa bastola ya Vampire. Alisita kidogo, kisha alianza kunyata kuelekea kule ulipotokea ule mlio, ile redio ya Vampire ikiwa mgongoni mwake.
Huku kwa akina Vampire, Alpha alimjia juu Mtanzania mwenzake.
“Sikiliza we’ mjinga-mjinga! Kaa ukijua kuwa mimi sitaenda kwenye Court Marshall hata kidogo, labda uipeleke maiti yangu. Ni kweli kuwa tumekuja huku kwa malengo, lakini si kwa lengo moja kama unavyojidanganya kuamini.
Mimi nina lengo langu, na kama utataka, mimi na wewe tunaweza kushirikiana katika hili na tutaondoka hapa na utajiri mkubwa sana ndugu yangu. Sasa acha
huo upumbavu wako wa uzalendo, kwani hautakufikisha popote, na usikilize ninachokuambia...”
“Ni nini unachoongea wewe?” Vampire alimuuliza kwa mshangao huku
akijaribu kuelewa kile alichokuwa akielezwa na Kanali Nathan Mwombeki.
Nathan Mwombeki aliketi chini ya shina la ule mti taratibu huku akimtazama
Vampire kwa umakini mkubwa.
“Nisikilize kwa makini Vampire, na weka pembeni hiyo bastola yako, kwani ukinilengeshea bastola namna hiyo itakubidi uitumie, kama huitumii basi weka pembeni!”
“Huna mamlaka ya kunishurutisha chochote wewe! Wewe ni msaliti na hivi sasa uko chini ya ulinzi wangu...utafanya kile ninachokuambia.”
“Hivi unadhani hapa tumekuja kupigana na hawa waasi kwa ajili gani?” Nathan alimuuliza Vampire, na kabla Vampire hajajibu, aliendelea, “Kwa ajili ya hizi almasi Vampire! Ahmed Tejan Kabbah na serikali yake wanabunya utajiri wa almasi uliozagaa katika nchi hii kama hawana akili vizuri, bila kuwaachia na wenzao wanufaike. Ndiyo kisa waasi wakaingia msituni, ili na wao watawale nchi wazibunye hizo almasi kama wanavyofanya wenzao waliopo madarakani hivi sasa. Na sisi kama mabwege tunakuja hapa kupigana ili kuwatetea akina Tejan Kabbah waendelee kujitajirisha huku asilimia zaidi ya sabini ya wananchi wa Sierra Leone, na sisi wenyewe huko tutokako, tukiwa kwenye umasikini
MDUNGUAJI uliokithiri!”
Vampire alimtazama kwa mshangao.
“Sasa...wewe ndiyo umeamua kuungana na waasi ili na wewe upate huu utajiri wa wa-Sierra Leone? Mbona sikuelewi?” Nathan alitikisa kichwa kwa huzuni na kuguna kabla ya kumjibu.
“Vampire huelewi bado, lakini nitakufahamisha.” Alitulia kwa muda huku akimtazama Vampire kwa macho makali. “Kadiri hii vita inavyoendelea, ndivyo nafasi ya kujipatia mgao katika hizi almasi inavyozidi kuwa kubwa. Mimi nimekuwa huku kwa muda mrefu kuliko wewe Vampire, na siku ulipokuja tu kuungana nasi nilijua kuwa utatuletea matatizo. Ukweli ni kwamba hatukutakiwa kabisa kuigundua hii kambi ya waasi, kwani kuigundua ni kuwaangamiza waasi na vita itakwisha. Na haitakiwi iwe hivyo! Mimi nina mpango wa utajiri mkubwa sana Vampire, na sasa uko katika hatua za mwisho. Ni almasi nyingi mno za kuniwezesha kuishi kifahari kwa maisha yangu yote yaliyobaki. Lakini wewe ulitaka kuuharibu kwa kunasa mawasiliano ya waasi...”
“Kwa hiyo ndiyo ukaamua kutuangamiza kwa kushirikiana na mdunguaji?” Vampire aliuliza kwa hasira.
“Sasa ulitakaje? Unajua...we’ uko kama siagi wewe! Laini sana, na sijui ilikuwaje hata ukaingia jeshini. Yaani kama ni rangi wewe ungekuwa njano, rangi ya upendo na ulaini-laini hivi...kama siagi!. Mimi nataka kujiwekea maisha yangu sawa bwana! Hebu nitazame, sasa nina miaka arobaini na minne. Kule nyumbani Tanzania huwa naona watoto wadogo, tena wengine wa kike, wanaendesha magari ya kifahari huku wanasikiliza miziki kwa sauti za juu na kutikisa vichwa! Na mimi? Mimi natembea kwa miguu bloody fool, kwa miguu!” Nathan alikuwa amepandisha jazba huku Vampire akimshangaa.
“Khah, sasa huo ni wivu usio na msingi...” Vampire alidakia kwa hasira lakini Nathan alimkatisha.
“Ita vyovyote utakavyo! Mimi na wewe ni watumishi wa kuwatumikia watoto kama hao ninaokwambia, na baba zao kama hawa akina Ahmed Tejan
Kabbah na marais wengine wa Kiafrika. Sifa yetu? Wapiganaji! Eti Kanali wa jeshi! Gari napanda lenye namba za jeshi! Naishi kwenye nyumba ya jeshi
iliyoandikwa namba ukutani. Nikistaafu au nikifa basi! Utasikia mijitu minafiki
kuliko yote duniani ikisema eti hoooh, marehemu ameacha pengo lisilozibika
kabisa kwa taifa!(akasonya) Kwa taifa? Pengo naacha kwa mke na familia yangu tu bwana! Mwisho wa taarifa ya habari! Sina kitu cha kumuachia mke wala
wanangu. Wanabaki kufukuzwa kwenye nyumba ya jeshi iliyoandikwa namba
ukutani na kupita wakihangaika na kumangamanga mitaani! Halafu wananileta
huku eti kumtetea Ahmed Tejan Kabbah na wapuuzi wenzake waendelee kubunya utajiri. Nikitoka salama nirudi kutembea kwa miguu nyumbani, au nirudi nikiwa maiti ndani ya boksi la mbao! No way bwana, sina uzalendo wa hivyo mimi! Kwangu mimi hii ni kampeni ya kunitoa kwenye umasikini kama utakubali kuacha ujinga na kushirikiana na mimi...sasa uko tayari?” Nathan alimueleza kwa kirefu na kumuacha na swali. Vampire alichanganyikiwa.
Ingawa maneno ya Nathan yalimuingia sana kichwani, bado hakuweza kuamini kuwa yule Mtanzania mwenzake aliweza kuwa na mtazamo potofu namna ile.
“Vipi kama siko tayari kushirikiana nawe?” Vampire alimuuliza huku akimtazama kwa makini.
“Basi itabidi nife na siri yangu Vampire. Siri ya sehemu zilipo almasi zenye thamani ya mabilioni, ambayo niko tayari kugawana nawe!”
Ukimya ulitawala baina yao na walibaki wakitazamana. Nathan akisubiri kusikia uamuzi wa Vampire, na Vampire akijaribu kuyachuja yote aliyoyasikia kutoka kwa yule mpiganaji na mtaifa mwenzake aliyemshangaza sana.
Mungu wangu! Hivi inawezekana haya anayoyasema yakawa ya ukweli? Almasi! Zenye thamani ya mabilioni...!
“Amua upesi Vampire! Hatuna muda wa kupoteza! Aidha uko nami ufaidi utajiri na uachane na jeshi, au...au vinginevyo!” Kanali Nathan Mwombeki alimhimiza huku akiinuka, na hapohapo bastola ya Vampire ilizidi kumsogelea.
“Shut-UpNathan!”
“Muda hautoshi Vampire! Ni lazima tufanye haraka. Sasa hivi wenzetu watakuwa wanatutafuta...”
“Tangu saa ngapi wale wameanza kuwa wenzako Nathan? Acha unafiki!”
“Suala ni wewe kufanya maamuzi ya haraka Vampire! Kwa nini unakuwa...”
“Sikuungi mkono katika hili Nathan! Nakuburuza moja kwa moja hadi kwenye Court Marshall. Wewe ni msaliti Nathan, na unajua kuwa wasaliti huwa tunawaua bila kujadili! Shukuru mimi nakupeleka kwenye sheria ambako labda utaambulia kifungo cha maisha au cha miaka kadhaa.” Vampire alimwambia kwa msisitizo huku akionesha wazi kuwa alikuwa amedhamiria kutekeleza yale aliyokuwa akiyasema. Kanali Nathan Mwombeki, pia akijulikana kama (p.a.k.) Alpha, alimtazama kwa mshangao mkubwa. Alifunua mdomo kisha akaufumba, halafu ule mshangao ukabadilika na kuwa fadhaa, ambayo haraka sana ikabadilika na kuwa ghadhabu kubwa kabisa.
“Pumbavu! Yaani mi’ nakupa utajiri wa maisha halafu unakataa? We’ fala sana wewe, na utakufa masikini...” Alisema kwa hasira na hisia kali, lakini
MDUNGUAJI
Vampire alikuwa amekwisha pitisha uamuzi.
“Hebu kelele wewe! Ujue ni mimi ndiye mwenye bastola hapa na usilisahau hilo hata dakika moja! Nahitaji kubonyeza kidogo tu kwa kidole changu na wewe utakuwa historia! Wewe ni aibu kwa jeshi na taifa letu kwa ujumla, na utafia jela kama siyo kwenye kitanzi. Inuka na uongoze njia upesi! Tunarudi nilipowaacha wenzangu na tunaelekea kambini! Twende!” Alimkemea kwa hasira iliyodhihiri.
“Then you will have to kill me Vampire, mi’ siendi popote!” Kanali Nathan Mwombeki alimjibu kwa jeuri iliyochanganyika na kukata tamaa; na kabla Vampire hajatanabahi, alijirusha pembeni huku mkono wake wa kulia ukichomoa bastola kwa uharaka wa ajabu. Vampire alishtukia akiikodolea bastola ya Nathan ambayo sasa ilikuwa ikimuelekea moja kwa moja usoni.
“Na kama ni kufa Vampire, basi nitakufa kwa mtindo niutakao mimi, nao ni kufa kiume...Nitakufa nikipambana. Sasa wote tuna bastola Vampire, na ukumbuke nilikwambia kuwa ni wewe ndiye utakayekufa hapa na sio mimi!”
Nathan alisema huku akiachia tabasamu baya kwa pembe ya mdomo wake, ilhali hasira na chuki vikionekana dhahiri machoni mwake.
Vampire alibaki akimtazama kwa ghadhabu huku naye akiwa amemuelekezea
ile bastola yake. Sasa wote walikuwa wamesimama huku wamenyoosheana bastola, Nathan bado akiwa na kile kifaa chake cha mawasiliano kilichokuwa kimeinuliwa kando ya uso wake kwa mkono wake wa kushoto.
Pagumu hapo!
Watanzania wawili waliokuwa katika jeshi muhimu kabisa la Umoja wa Mataifa kuliwakilisha taifa lao katika nchi ngeni walikuwa wakitazama kama majogoo yaliyokuwa tayari kupambana mpaka kufa. Mmoja akisimamia haki na utii kwa nchi yake, mwingine akisimamia ubinafsi na udhalimu bila kujali maslahi na heshima ya nchi yake.
“Usinifanye nilazimike kukuua Nathan. Tupa chini hiyo bastola na...”
Vampire alianza kumwambia.
“Shoot when you are ready!” Nathan aliropoka ghafla huku bado akiwa
amemuelekezea Vampire bastola na kichwa chake akiwa amekilaza kidogo
kushoto kwake, karibu na kile kifaa chake cha mawasiliano kilichokuwa
kwenye mkono wake wa kushoto ulioinuliwa usawa wa bega lake. Kidogo
Vampire alibabaika kutokana na ile kauli ya Nathan ambayo ilionekana kama
kwamba haikuwa imemkusudia yeye.
Lakini hapa tuko mimi na yeye tu...
Halafu hapohapo ikawa kama kwamba Nathan ameamua kurudi kuongea
naye.
“Nini Vampire, hujiamini? Basi bora ukubali kuchukua mgao wa almasi zangu...”
“Kelele! Almasi zako tangu lini? Hizo ni Almasi za damu na sina haja nazo...
kama ziko kweli. Inakubidi uelewe kuwa utajiri huu wa almasi unaounyemelea ni haki ya wa-Sierra Leone na wala haukuhusu wewe wala hao waasi ulioamua kujihusisha nao!Sijui umewezaje kuunda hujuma nzito kama hii ndani ya nchi ngeni Nathan, lakini hayo yote utayaeleza mbele ya mahakama ya kijeshi. Tupa chini hiyo bastola yako Nathan...”
“You have to shoot now!” Nathan aliropoka tena huku kwa mara nyingine tena akilaza kichwa chake kilipokuwa kile kifaa chake cha mawasiliano huku
akimtazama Vampire kwa makini,wote bado wakiwa wameelekezeana bastola.
“Khah...?!” Akili ya Vampire ilimzunguka kwa kasi.
Kuna kitu hakiko sawa. Kwa nini ananishurutisha nimuue? Ni kama...ni
kama anamuambia mtu mwingine...lakini itawezekana...?
“Kwa nini unanilazimisha Nathan? Na kwa nini unaongea kiingereza wakati hapa tupo wabongo tu? Ni kwa nini Nathan, eenh?” Alimuuliza huku akianza kumzunguka akiwa amemnyooshea bastola. Sasa walianza kuzungukana huku wakiendelea kuelekezeana bastola zao, Nathan akiendelea kushikilia kile kifaa chake cha mawasiliano. Kila mmoja akimtazama mwenzake kwa makini.
“Nitaongea lugha yoyote niitakayo. Na nilishakwambia mapema kuwa iwapo utanielekezea hiyo bastola yako basi ni sharti uitumie; kama huwezi itupe chini tuongee biashara. Hutaki kuongea biashara, basi unanilazimisha nikuue ingawa sitaki kufanya hivyo, kwa sababu naona unanipotezea muda bure!” Nathan alimjibu kwa jeuri. Sasa Vampire alikuwa amezunguka na kufikia sehemu yenye mteremko mkali na alihisi akizidi kuzunguka namna ile, huenda angeanguka kule bondeni ambako alihisi kuwa kulikuwa na mporomoko mrefu.
Alisimama.
“Mimi pia sitaki kukuua Nathan, lakini...”
“SHOOT, GODDAMMIT, SHOOT!!” Nathan alifoka kwa sauti, huku kwa mara nyingine tena akilaza kichwa chake kushoto kwake. Na kwa mara nyingine Vampire alipata hisia kuwa ile kauli haikuwa imemkusudia yeye. Lakini itawezekanaje...?
“Tulia hivyohivyo!”
Wote wawili waligeuka kwa mshituko kutazama kule sauti ilipotokea huku bado wakiwa wameelekezeana bastola.
MDUNGUAJI
Black Mamba, akiwa amevaa ile fulana yake ya kijeshi kama ya Vampire na mgongoni akiwa amebeba ile redio ya mawasiliano aliyopewa na Vampire, alikuwa amewaelekezea bunduki yake wale wapiganaji kutoka Tanzania ambao sasa walikuwa mahasimu wakubwa; ilhali uso wake ukiwa na mchanganyiko wa mshangao na hasira.
Wale Watanzania waliendelea kuelekezeana bastola huku kila mmoja akitembeza macho baina ya Black Mamba na hasimu wake.
“Ni upumbavu gani unaoendelea hapa?” Aliwauliza huku akiendelea kuwatazama kwa mshangao.
“Kinachoendelea hapa Mamba ni...” Vampire alianza kumjibu, lakini Alpha alimkatisha.
“Nimemkamata msaliti wetu! Huyu ndiye msaliti wetu Mamba...!”
“Khah!” Vampire alijikuta akitoa mguno wa mshangao.
Hii ni kali kuliko! Ama kweli huyu jamaa msaliti! Yaani mimi ndiyo nimekuwa msaliti tena?
Black Mamba alimgeukia Vampire kwa mshangao.
“Vampire...? Msaliti...!?”
“Yes Mamba! Huyu ndiye haswa msaliti wetu!” Nathan alimgeuzia kibao Vampire bila haya wala woga.
“Shut up Nathan! Usimsikilize huyu Black Mamba! We’ unajua kuwa mimi si msaliti! Nilikuwa nanyi muda wote, wakati yeye...” Vampire alimkatisha
Nathan, na kumwambia Black Mamba taratibu huku akimtazama Nathan kwa hasira, wote bado wakiwa wameelekezeana bastola, lakini Nathan aliingilia kati.
“Yeye ndiye msaliti, Mamba...!” Halafu hapohapo alifoka, “TAKE THE GODDAMN SHOT NOW! “Ni nini unachoongea Alpha?” Black Mamba
alimuuliza kwa mshangao, kwani ilionekana kama kwamba Alpha alikuwa anaongea vitu visivyoeleweka, na kabla hajajibiwa, Black Mamba alimtupia swali jingine huku akimtazama kwa makini.
“Na kwa nini umeshika kifaa cha mawasiliano mkononi mwako Alpha...?”
Vampire alimtazama Alpha na kumgeukia Black Mamba, kisha akamgeukia tena Alpha. Akili yake ilikuwa ikifanya kazi kwa kasi sana na wakati Black
Mamba alipouliza lile swali, alihisi kama kitu kikizibuka kichwani mwake na mara moja alielewa ni nini kilichokuwa kikiendelea. Moyo ulianza kumuenda
mbio na akilini mwake ilimjia ile hisia iliyokuwa ikimjia mara kwa mara
kuwa huenda Nathan alikuwa akiongea na watu wawili kwa wakati mmoja...
kuwa alipokuwa akiongea na yeye wakati huohuo alikuwa akiongea na mtu
mwingine...kwa kutumia kile kifaa cha mawasiliano...na ndiye ambaye muda
wote amekuwa akimsisitiza apige risasi...kuniua mimi!
Na sasa tuko mimi na Black Mamba!
“
Oh, Shit...!”
Nathan aliona kuwa Vampire alikuwa amegundua kitu. Alihamanika na kughadhibika kwa wakati mmoja. Black Mamba hakuwa ameelewa kitu na alikuwa akiwatazama wale Watanzania wawili mmoja baada ya mwingine.
“TAKE HIM OUT NOW...!” Nathan alifoka kwenye kile kifaa chake cha mawasiliano na wakati huohuo mkono wake wenye bastola ukianza kugeukia taratibu kule alipokuwa Black Mamba.
Black Mamba alikuwa ameachwa njia panda, lakini Vampire mara moja alielewa nia ya Nathan.
Ah! Yaani huyo anayewasiliana naye anipige mimi risasi, wakati yeye akimpiga risasi Black Mamba...watumalize! Yaani kumbe muda wote ule Nathan alikuwa akijaribu kuwasiliana na...na...mdunguaji!
Pumbavu!
Alijua kuwa pale alitakiwa achukue uamuzi wa haraka ama sivyo ataiaga dunia...yeye na Black Mamba.
Hakusita.
Alifyatua risasi huku akijitupa pembeni.Wakati huohuo alihisi maumivu makali upande wa kulia wa kifua chake, huku akihisi kitu kama msumari wa moto ukiuingia mwili wake na kutembeza ganzi upande wake wote wa kulia. Alitupwa hewani, ile ganzi ikitoweka haraka na maumivu makali yakiutawala mwili wake. Alipigiza mgongo wake kwenye jiwe kubwa lililokuwa karibu yake na kuserereka kuangukia kule kwenye mporomoko mkali...
Honey-Bee na Stealth walitazamana huku wakiwa wamelalia matumbo
kila mmoja upande wake wote wakiwa wamechukua tahadhari ya kujificha nyuma ya mashina ya miti. Baada ya kumimina risasi mfululizo kule walipohisi mdunguaji alikuwepo, hawakuona dalili zozote iwapo risasi zao zilikuwa zimefanikiwa kumpata mdunguaji.Baada ya kuchunguza mle msituni kwa muda bila ya kuona dalili yoyote, walibaki wakitazamana. Miguno ya maumivu kutoka kwa Swordfish iliendelea kusikika kutokea nyuma ya shina la mti alikoangukia baada ya kupigwa risasi na mdunguaji hatari. Stealth alielewa kuwa alitakiwa afanye maamuzi ya kudumu, kwani ilikuwa wazi kuwa wasipomuua yule mdunguaji, wangeendelea kuwa roho juu mle msituni kwa masiku au
MDUNGUAJI
hata mawiki,mpaka wamuue. Na sasa mwenzao alikuwa amejeruhiwa na wasingeweza kuendelea kuwa naye mle msituni kwa muda usiojulikana bila kumpatia matibabu.
“Hey Swordfish, utaweza kutembea?” Aliita kwa sauti kali lakini ya chini ambayo alijua kuwa ingemfikia Swordfish.
“Ndiii...yo! Nadhani n’taweza...lakini natokwa na damu nyingi sana bwana!”
Stealth alimgeukia Honey-Bee na kumpa ishara za kijeshi kwa kutumia vidole vyake, ambazo zilimwagiza Honey-Bee amkinge wakati yeye anaenda kumtazama Swordfish.Honey-Bee aliafiki kwa kichwa na Stealth alitambaa hadi pale kwa Swordfish. Kwa muda wa kama dakika kumi hivi alijitahidi kumfunga lile jeraha na kumpa dawa maalum ambazo zilikuwa kwenye mkoba wa kila mmoja wao,kwa ajili ya kutuliza maumivu na kuzuia damu. Muda mfupi baadaye Honey-Bee aliwafikia pale walipokuwa.
“Hii ni mbaya sana bwana...mbaya sana! Sasa tumebaki watatu tu... hatuna hakika iwapo wenzetu ni wazima au wameuawa...” Stealth alisema kwa uchungu huku akimalizia kumfunga Swordfish lile jeraha.
“Kwa hiyo tunafanyaje sasa? Hii hali si nzuri kabisa! Hatuwezi kuendelea kuwa katika hali hii...” Honey-Bee alimwambia kiongozi wao wa msafara huku akitazama huku na huko, bunduki yake ikiwa imara mikononi mwake. Stealth alitikisa kichwa kuafikiana naye.
“Uko sahihi Honey...wacha tubahatishe kuondoka eneo hili. Twendeni tukawasake wenzetu halafu tuondoke.” Akamgeukia Swordfish, “Itakubidi utembee Swordfish, sawa?”
“Usiwe na wasiwasi nami mshirika! Nitaimudu hii hali...” Swordfish alimjibu na msafara ukaanza. Stealth akiwa mbele, Swordfish katikati, HoneyBee nyuma. Honey-Bee alikuwa akitembea huku akiwa amegeukia kule walipokuwa wametokea. Stealth alikuwa akiita majina ya wale wapiganaji wenzao kwa sauti kali ya kunong’ona kila baada ya muda fulani. Walikuwa wanajaribu kufuata sehemu ambazo walihisi wenzao walipitia.
“Simama! Hebu angalieni hii!” Stealth alisema huku akiwaonesha wenzake hatua kadhaa mbele yake.Wote walitazama kile walichokuwa wakioneshwa na mwenzao. Yalikuwa ni yale magwanda mawili ya juu ya kijeshi yaliyolaliana chini ya shina la mti. Honey-Bee aliyakimbilia na kuyapekua harakaharaka huku wale wengine wakimtazama kwa wasiwasi.
“Ni magwanda ya Vampire na Black Mamba!” Honey-Bee aliwajibu wenzake baada ya kusoma majina ya uficho yaliyoandikwa kwa kufumiwa
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
kwenye mifuko ya kulia vifuani mwa yale magwanda, na wote wakabaki wamepigwa na butwaa. Hakuna hata mmoja kati yao aliyeweza kuelewa ni nini kilichowatokea wenzao. Kwa pamoja walifikia uamuzi kuwa huenda wenzao wametekwa. Hii iliwaletea hofu nyingine kubwa, ya kwamba sasa hawakuwa wakikabiliana na mdunguaji tu, bali pia kuna wengine, bila shaka ni haohao waasi, waliowateka wenzao. Uchunguzi wa eneo lile uliwaonesha alama za njia ambayo watu walipita.Hawakuwa na namna ya kujua ni nani aliyepita hapo, lakini waliamua kuifuata kwa tahadhari kubwa. Hawakuwa na namna nyingine, kwani sasa iliwajia wazi kuwa walikuwa wamepotea kwenye msitu ndani ya eneo linaloshikiliwa na waasi.Na hawakuwa na namna yoyote ya kuweza kuwasiliana na kambi yao.
Na ni hapo ndipo waliposikia mlio wa bastola ya Vampire, na mara moja
walianza kukimbia kwa tahadhari kubwa kuelekea kule mlio wa bastola ulipotokea, Swordfish akijitahidi kwa taabu sana kuwa pamoja na wenzake.
Kama wenzao walikuwa kwenye hatari,ulikuwa ni wajibu wao kuwasaidia.
Hiyo ndiyo kanuni yao kuu ya makabiliano katika mpango ule wa hatari.
Mmoja kwa ajili ya wote, na wote kwa ajili ya mmoja.
Sasa vita ilikuwa imepamba moto. Angalau ndivyo wao walivyodhani...
Huku kwa akina Vampire, Black Mamba alipiga kelele huku akishuhudia
kwa kihoro wakati kichwa cha mpiganaji kutoka Tanzania aliyemtambua kwa jina la uficho Alpha kikitawanywa vibaya sana na risasi kutoka kwenye bastola ya Vampire na kuanguka chini kama gunia huku bastola yake ikimtoka bila ya kufyatua risasi hata moja. Alijitupa chini na kugeukia kule alipoangukia Vampire na kumuona akiwa ametapakaa damu kifuani huku akijitahidi kujishikilia kwenye jiwe kubwa kwa mkono wake wa kushoto.Sehemu kubwa ya mwili wake ilikuwa inaelekea kuporomokea kule kwenye lile korongo refu ilhali mkono wake wa kulia ukiwa umekamata ile bastola yake tayari kwa kushambulia.
Black Mamba kutoka Sierra Leone alichanganyikiwa. Alpha hakufyatua risasi, sasa mbona Vampire naye anatokwa damu...? Ni nini kimetokea...?
Pale alipokuwa ameling’ang’ania lile jiwe, Vampire alikuwa katika maumivu
makali, damu nyingi ilikuwa ikimtoka na alihisi fahamu zikimpotea, lakini hakukubali kuziruhusu zimpotee. Alikuwa akitembeza macho kule ilipotokea ile risasi iliyompata kifuani. Akimtafuta adui yao aliyebakia. Akimtafuta
MDUNGUAJI mdunguaji.
“Jishikilie hivyo hivyo Vampire! jishikilie! Nakuja kukusaidia komredi...!”
Black Mamba alimpigia kelele huku akijiinua na kuanza kumuendea, lakini Vampire wala hakuwa akimsikiliza, alikuwa akimtafuta mdunguaji ambaye
alijua kuwa yuko karibu kabisa na pale walipokuwapo.
Na mara hiyo alimuona.
Alikuwa juu ya mti mmoja mita chache kutoka pale alipokuwa amesimama
msaliti Nathan dakika chache zilizopita.Walitazamana...Macho kwa macho!
Aliona mtu aliyejipaka rangi nyeusi usoni, lakini aliliona waziwazi jeraha kubwa na bichi lililotambaa upandewa jicho lake la kulia, damu ikiwa imegandia upande ule wa uso wake. Na hata pale alipokuwa akimkodolea
macho kwa taabu na mastaajabu, Vampire alimshuhudia yule muuaji wa kuvizia akiongeza risasi kwenye bunduki yake kubwa iliyokuwa na lenzi yenye nguvu na kumtazama kwa muda kisha alianza kuiinua ile bunduki taratibu
kumlenga huku akiwa amekenua meno kwa ghadhabu. Vampire alijaribu
kuinua bastola yake kumuelekezea yule muuaji lakini mkono ulimuwia mzito
sana. Alimtazama yule muuaji kwa kukata tamaa huku akipingana na fahamu
zilizokuwa zinaelekea kumpotea kwa kasi. Alisikia vishindo vya Black Mamba
akielekea kwa kasi pale alipokuwapo na akamkumbuka yule muuaji hatari.
Hapana! Haiwezekani atuue sote! Black Mamba hastahili kufa...
“Black Mamba usije! Mdunguaji! Mdunguaji yuko hapa! Kule...kule… huo mti mkubwa kulia kwako!” Vampire alipiga kelele kwa kadiri alivyoweza huku akielekeza bastola yake kule kwenye ule mti ambao mdunguaji alikuwa amejificha kwenye matawi yake.
Black Mamba alisita kidogo na kubaki akiwa ameduwaa, kisha alianza
kugeuka taratibu, huku akichutama, kuelekea kule alipokuwa akielekezwa na Vampire, ilhali akiwa ameshikilia vizuri bunduki yake.
Vampire alijaribu kujivuta juu ili asianguke kule kwenye korongo na ndipo kwa kihoro kingine alishuhudia lile jiwe alilokuwa akilitegemea likianza kung’oka na hapo alijua kuwa alikuwa hana namna ya kujiokoa. Aliinua uso wake kwa woga na kutaka kumpigia kelele Black Mamba lakini alipigwa na butwaa na kihoro kikubwa zaidi pale alipoona kichwa cha Black Mamba kikitawanyika vibaya sana na kiwiliwili chake kikianguka chini kama mzigo.
Mdunguaji alimuwahi.
Kutokana na ukaribu aliokuwako mdunguaji, ile risasi iliking’oa kabisa kichwa cha Black Mamba kutoka kwenye kiwiliwili chake na kukitawanya vipande vipande, damu,mapande ya nyama na ubongo vikitupwa kila upande.
“Black-Aaaayyyaaaaaa!” Yowe lilimtoka Vampire na hapohapo alimuona mdunguaji akimgeuzia ile bunduki yake kubwa iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti naye aliinamisha kichwa chake kwa kukata tamaa huku akihisi macho yake yakipoteza nuru na fahamu zikimhama. Alijua kuwa kifo kilikuwa kimemkabili na hakuwa tena na nguvu ya kufanya jambo lolote. Wazo la mwisho kumpitia kichwani mwake ni sura ya mkewe, kisha mikono ikamuisha nguvu, bastola ikamuanguka na mkono wake wa kushoto ukalichia lile jiwe ulilokuwa umelishikilia.
Mwili wake uliporomoka kwenye lile korongo refu sana ambalo chini yake kulikuwa kuna msitu mnene zaidi.
Hakuhisi chochote. Kote kulikuwa kiza...
Kiasi cha kama dakika kumi hivi baada ya shambulio la mdunguaji, na mpambano baina ya Vampire na Alpha, Stealth na Honey-Bee walifika eneo la maafa kwa usiri mkubwa na kupigwa butwaa kutokana na kile walichokikuta eneo lile.
Swordfish alikuwa amezidiwa na walifanikiwa kumshawishi abaki nyuma, sehemu ambapo alitakiwa awasubiri wenzake mpaka watakapomrudia baada ya wao kuwapata, kuwakosa au kugundua kilichowapata akina Vampire. Na katika hili, walimuachia Swordfish maelekezo fasaha kuwa iwapo itapita nusu saa bila wao kurejea, ajitahidi kurudi kambini akiwa peke yake, awaache wenzake watafute wenyewe njia yao ya kurudia...kama bado watakuwa hai.
Mdunguaji alikuwa amewasambaratisha vibaya sana wapiganaji wa kikosi hiki cha jeshi maalum la umoja wa mataifa kiasi kwamba hawakuwa na budi ila kubadili mbinu na kuamua kuvunja mshikamano wao ili angalau baadhi yao wafike kambini kwao salama na kutoa taarifa.Na sasa ilionekana kama kwamba Stealth na Honey-Bee walikuwa wameshagundua ni nini kilichowapata wenzao, nacho kilikuwa ni umauti!
Miili ya wenzao wawili ilikuwa imetawanyika kila upande, mmoja ukiwa na tundu la risasi katikati ya paji la uso, mwingine ukiwa hauna kichwa kabisa! Ilhali mwingine hakujulikana alipo...
“Oh! Mungu wangu! Ooh Mungu wangu...” Stealth alikuwa akibwabwaja peke yake huku akiangalia mauaji yaliyotendeka pale hali akitazama huku na huko, akiwa makini sana.
“Ni mdunguaji huyu!” Honey-Bee alinongóna kwa hasira huku naye akilikagua kwa makini eneo lile. Stealth aliuendea ule mwili usio na kichwa uliolala bila uhai pale chini,kifaa chao cha mawasiliano kilichokufa bado kikiwa kimebebwa mgongoni mwa mwili ule, damu nyingi iliyochanganyika na ubongo ikiwa imetapakaa eneo lote kuuzunguka. Aliutazama kwa fadhaa na hasira kisha akauendea ule mwili mwingine uliokuwa na jeraha la risasi kwenye
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
paji la uso, na kuhakikisha kuwa na Alpha naye alikuwa umekufa.
“Huyu mwanaharamu atatumaliza wote sasa, pumbavu!” Stealth alisema kwa hasira huku akizidi kutazama huku na huko.
“Hebu na ajitokeze basi pumbavu zake! Hapo ndipo tutaona nani atammaliza nani...!” Honey-Bee alisema kwa hasira.Na kabla Stealth hajajibu lolote wote wawili walishtushwa na mtikisiko hafifu kutokea kwenye kichaka kilichokua jirani na pale walipokuwapo,na haraka sana walijitupa pembeni huku Honey-Bee akimpigia Stealth kelele za tahadhari na wakati huohuo
akiachia risasi kuelekea kule ulipotokea ule mtikisiko na hapohapo yowe kubwa la maumivu lilisikika kutokea kule kichakani.
Wote walijigeuza kutazama kilichotokea na walijikuta wakikodolea mitutu minne ya bunduki zilizokuwa mikononi mwa wapiganaji wenye sura za kikatili za waasi wa jeshi la RUF (Revolutionary United Front) lililokuwa likipingana na vikosi vya jeshi la serikali halali ya Ahmed Tejjan Kabbah.Hatua chache
kutoka pale walipokuwa wamesimama wale waasi, kulikukwa kuna mwili wa muasi wa tano ambaye alikuwa amekufa, risasi kutoka kwenye bunduki ya Honey-Bee ikiwa imefanya makazi katikati ya koo lake!
Ama kwa hakika Honey-Bee alikuwa mwanamama hatari mno.
Wale waasi waliendelea kuwatazama kwa utulivu wa kutisha huku wakiwa wamewaelekezea bunduki zao, kisha kila mmoja kwa wakati wake akamtazama yule mwenzao aliyetandikwa risasi na Honey-Bee, akiwa amelala bila ya kutikisika,damu ikitirirka kutoka pale risasi ilipouingia mwili wake.
Stealth na Honey-Bee walitazamana, na taratibu walianza kujiinua kutoka kule walipojitupia hapo awali huku wakiwa wameshika silaha zao.
“Tulia hivyo hivyo!” Sauti kali iliwafokea, nao wakatulia pale chini wakiwatazama wale waasi huku bado mikono yao ikiwa kwenye silaha zao.
“Inukeni taratibu...na acheni silaha zenu hapohapo chini.” Mmoja wa wale waasi, ambaye alionekana kuwa ndiye kiongozi wao alifoka kwa mara ya pili, huku akimtazama Honey-Bee kwa macho yenye mchanganyiko wa mastaajabu, kutoamini na hasira.
Bila shaka alishuhudia kile kitendo cha wepesi wa ajabu na umakini wa hali ya juu alichofanya mwanamama yule, na hakutaka kuamini alichokiona. Mara moja alijua kuwa mbele yake kulikuwa kuna mwanamama hatari sana, na hiyo ilimzidishia ghadhabu. Kwake wanawake ni viumbe dhaifu na dhalili, sasa huyu aliye mbele yake alionekana kuwa hatari kuliko hata yeye mwenyewe, na hili hakulipenda kabisa!
Stealth na Honey-Bee waliziacha chini silaha zao na kusimama huku
MDUNGUAJI
wakiinua mikono yao juu, mioyo ikiwaenda mbio na akili zikiwatembea kila mmoja kwa kasi yake.
Walikuwa mikononi mwa waasi!
Wakiwa bado wamewaelekezea mitutu ya bunduki mateka wao, yule kiongozi wa kile kikundi kidogo cha waasi aliamrisha kwa lugha ambayo Stealth na Honey-Bee hawakuielewa, na hapohapo mmoja wa wale wafuasi wake aliukimbilia ule mwili wa yule mwenzao aliyepigwa risasi na kuugeuza kwa mguu wake, kisha akasema neno kwa lugha kama ile aliyotumia yule msemaji wa kwanza, bila shaka akitoa ripoti kuwa mwenzao alikuwa amekufa.
Jamaa aliwatazama kwa ghadhabu wale mateka wao wawili, kisha akapiga hatua moja kubwa na kumzaba kofi zito la uso Honey-Bee. Stealth alijikurupusha kutaka kumkabili, lakini hapohapo mmoja wa wale waasi alifyatua risasi iliyotoa mlio mkubwa na kuchimba ardhi hatua chache kutoka pale alipokuwa.
“Hatua nyingine moja tu ewe mamluki...na utakuwa mfu...!” Yule muasi aliyemfyatulia risasi alimkemea kwa hasira huku akimtazama kwa macho mekundu yaliyojaa wehu, na Stealth alibaki akifura kwa hasira.
Lile kofi liliusukuma kwa nguvu uso wa Honey-Bee, naye haraka sana aliugeuza kuendelea kumtazama yule muasi kwa hasira na wala halikuonesha kumteteresha hata kidogo, ingawa kwa hakika lilimuuma.Hakukubali kabisa kumpa faraja yule muasi kwa kuonesha kuwa ameumizwa na pigo lile. Badala yake alimtazama kwa jeuri na ghadabu yule muasi, ambaye naye alikuwa akimtazama kwa hasira.
“Nyie ni nani?” Yule mkuu wa kile kikosi aliwauliza kwa hamaki. Hawakumjibu.
Kwa hasira yule kiongozi wa kile kikosi alimsogelea Honey-Bee na kukamata sehemu ya mbele ya gwanda alilovaa na kulitazama kwa muda huku akisoma jina la uficho la yule mwanamama hatari lililoshonewa kwenye mfuko wa kifuani wa gwanda lile. Stealth alibaki akitazama hali ile kwa hasira, asiwe na la kufanya.
“Ni jeshi la Umoja wa Mataifa eenh? Hili ndilo haswa tulilokuwa tukilitaka! Kwa hiyo sasa Umoja wa Mataifa umevamia nchi yetu?” Yule kiongozi wa kile kikundi cha waasi alisema kwa kejeli.
“Tumekuja kulinda amani na sio kuvamia...!” Honey-Bee alimjibu kwa hasira, lakini hapohapo jamaa akamtwanga ngumi kali ya taya iliyomyumbisha yule mwanamama na kumtoa damu mdomoni.
“Mmekuja kumlinda kibaraka wenu Ahmed Tejjan Kabbah...!” Yule muasi
alimkemea Honey-Bee kwa hasira, ni wazi alikuwa ameamua kuwa Honey-Bee ndiye mbaya wake kati ya wale mateka wao wawili.
“Na nyie ni vibaraka wa nani... Forday Sanko, eenh?” Stealth alimtupia swali kwa hasira.
“Kelele wewe!” Yule muasi alimgeukia kwa hasira, huku na wale waasi wenzake wakiropoka maneno ya hasira kwa ile lugha ya kikwao, bila shaka wakimhimiza yule kiongozi wao atoe idhini wawaue wale wapiganaji waliotekwa. Yule muasi aliinua mkono wake kuwanyamazisha wenzake huku akiwatazama Stealth na Honey-Bee kwa hasira. Kisha aliwaambia wenzake kwa lugha ileile ya kikwao jambo fulani, na kuwageukia tena akina Stealth.
“Tunawapeleka kambini kwetu nyinyi...na dunia nzima itashuhudia jinsi tunavyowaua...hilo litaupelekea ujumbe wetu Umoja wa Mataifa na kwa kibaraka wao Tejjan Kabbah!”Yule muasi aliwaambia huku akiwatazama kwa macho yaliyoonesha wazi kuwa alikuwa amewehuka kwa hasira na bangi.
“Mnadhani mnaweza kupigana na Umoja wa Mataifa?”Honey-Bee alimuuliza kwa kejeli.
Jamaa alimtazama kwa hasira. Alimsogelea na kumuwekea mtutu wa bunduki yake kifuani na kumtazama moja kwa moja machoni.
“Mnadiriki vipi kuja nchini kwetu na kuua askari wetu,halafu mtarajie tusipambane nanyi, eenh?” Yule kiongozi wa waasi waliokuwa wamevaa nguo zisizo rasmi, wengine wakiwa wamevaa fulana za kawaida tu, na viatu kila mmoja cha aina yake, alimuuliza kwa hisia kali.
“Mnajiita askari nyie? Kwangu nyie ni kundi la wahuni tu...,” HoneyBee alimjibu kwa kejeli, lakini kabla hajamalizia jamaa alimzaba kofi jingine kali zaidi la uso. Honey-Bee alipepesuka vibaya kwa nguvu ya kofi lile na hakika aliona nyota zikielea mbele ya macho yake huku akiuhisi uso wake ukimtutumka na kuwa mkubwa sana. Kwa muda alijiinamia huku akitikisa kichwa huku na huko, kisha aliinuka na kumuinulia tena uso wake yule muasi kwa jeuri na kumtazama kwa ghadhabu huku chozi likimtiririka na midomo ikimcheza...
Hapo Stealth hakuweza kuvumilia zaidi.
“Wewee! Kwa nini usichague mtu aliyekuwa sawa yako eenh? ” Alimfokea yule muasi kwa hasira.Hapohapo mmoja wa wale waasi alimrukia huku akiwa ameinua juu kitako cha bunduki yake kwa lengo la kumpiga nacho.
Hilo lilikuwa ni kosa kubwa!
Kwa wepesi usiotarajiwa Stealth alijitupa chini na kujibiringisha kuelekea miguuni kwa yule muasi ambaye alishangaa akijikwaa kwenye kiwiliwili
MDUNGUAJI
cha Stealth na kupiga mweleka mzito huku risasi ikifyatuka kutoka kwenye bunduki yake.
Wakati huu wenzake walioona tendo lile walipayuka kwa kelele zisizo na mpangilio huku wakielekeza bunduki zao kule kwa Stealth, ambaye alijiinua haraka na hapohapo alimtupia kisu alichochomoa kutoka kwenye kiatu chake yule muasi aliyekuwa akimwendea tayari kumshambulia kwa bunduki yake.
Kisu kilijikita shingoni kwa yule muasi aliyeachia yowe kubwa, bunduki ikimtoka bila kujijua na kujikuta akipeleka mikono yake yote miwili shingoni akijaribu kukichomoa kile kisu huku akitumbua macho na miguu ikimlegea .
Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana, na mambo yote yalitokea kwa wakati mmoja.
Mmoja wa wale waasi waliobaki alitoa mguno wa mshangao kwa kitendo kile na yule kiongozi wao aligeuka kule alipokuwa Stealth ambako kulitokea ile purukushani, lakini hapohapo aligundua kuwa hilo lilikuwa ni kosa na aligeuka haraka kumuwahi Honey-Bee.
Tatizo ni kwamba alichelewa...
Haraka sana Honey-Bee alipiga msamba na kubonyea chini kwa wepesi wa ajabu,kisha akampiga ngumi nzito kwa mtindo wa upper cut iliyotua sawia kwenye korodani zake.
Yowe la maumivu lilimtoka yule muasi huku akijipinda bila kupenda, na hapohapo Honey-Bee alijigeuza pale chini na kulalia mgongo huku akitupa teke kali sana lililompata yule muasi aliyeinama vizuri sana kwenye upande wa uso wake mbaya na kumtupa pembeni, naye akajirusha kule ilipokuwa bunduki yake. Alichelewa kidogo, kwani muda huo alimuona muasi mwingine akimgeuzia bunduki yake tayari kwa kuachia risasi, huku akijitahidi kutompiga yule kiongozi wao aliyekuwa akijizoazoa baina yake na Honey-Bee...
Wakati huo huo, huku kwa Stealth, baada ya kumtupia kisu yule muasi wa tatu, akili yake ilirudi haraka kwa yule muasi wa pili aliyepiga mweleka baada ya yeye kumrukia miguuni na kumpoteza lengo. Aligeuka akiwa amepiga goti moja na wakati huohuo yule muasi naye akiwa anainua tena bunduki yake kumlenga. Kabla hajatanabahi, alishuhudia kisu kikijikita kifuani kwa yule muasi kutokea nyuma yake. Muasi alipiga yowe la uchungu na kujishika kifuani, bunduki ikimtoka. Stealth alijitupa pembeni akiwa amechanganyikiwa, akijiuliza ni nani aliyetupa kile kisu na kugeuka kule kisu kilipotokea.
Na hata pale alipogeuka, alimshuhudia kwa kutoamini Swordfish, mwamba wa makabiliano ya uso kwa uso katika medani ya vita, akiwa amefungwa bandeji mkono mmoja, akimrukia kwa miguu yake yote miwili yule muasi
aliyekuwa amemuelekezea bunduki Honey-Bee na kumbabatiza kwa kishindo eneo la kiunoni na kumtupa pembeni huku ile bunduki yake ikifyatuka na wakati huohuo ikimtoka mikononi.
“Swordfish!”Stealth aliropoka kwa mshangao uliojaa furaha.
Swordfish na yule muasi walipiga mweleka mzito, huku Honey-Bee akijibingirisha pembeni. Sasa yule muasi aliyekuwa akiwaongoza wenzake aliyekuwa na hasira na Honey- Bee naye alikuwa ameshasimama wima na akimwendea kasi Honey-Bee huku akipeleka mkono wake kiunoni kutoa kisu kikubwa na kikali, lakini Swordfish alikuwa ameshainuka na tayari kupambana. Yule muasi alikuwa akimwendea kasi Honey-Bee huku akiwa ametanguliza kisu chake kistadi.Muda huo Honey-Bee alikuwa akijiandaa kumkabili yule muasi aliyebabatizwa na Swordfish, lakini kwa pembe ya jicho lake alimuona yule muasi aliyekuwa akiliongoza lile kundi dogo la waasi akimwendea mbio huku akiwa na kisu mkononi, tendo ambalo Stealth pia aliliona na kumpigia ukelele wa tahadhari. Sasa Honey-Bee alibabaika kidogo, kwani hakujua akabiliane na yupi kati ya wale waasi wawili.
“Honey-Bee kaa pembeniii!” Swordfish aliruka mbele ya yule muasi aliyetanguliza kisu kwa kushambulia huku akimpigia ukelele Honey-Bee. Kilichotokea kilikuwa ni kitendo cha haraka sana. Honey-Bee hakusita tena, alijirusha pembeni na kumkabili yule muasi aliyeangushwa na Swordfish hapo awali.
Yule kiongozi wa wale waasi wachache alishtukia akikabiliana na Swordfish badala ya Honey-Bee aliyekuwa amemdhamiria. Haraka sana akabadili shambulio na kulielekeza kwa Swordfish aliyekuwa akitumia mkono mmoja tu.
Muasi alipeleka shambulio la kisu kwa nguvu zote, akiwa amekishika kwa mtindo wa kuchoma, ambao ni mtindo hatari sana na vigumu kwa mtu wa kawaida kuukwepa. Lakini Swordfish hakuwa mtu wa kawaida...
Alipiga hatua moja kubwa kumwendea mpinzani wake na wakati huohuo
akijigeuza huku akiruka juu kidogo na kutanua mkono wake wa kulia kama mtu anayetaka kupaa. Kisu cha muasi kilichokuwa kimemlenga tumboni kilipita
chini ya kwapa lake na wakati huohuo yule muasi alijikuta akijibamiza kwa tumbo lake mgongoni kwa Swordfish, ambaye haraka sana aliubana ule mkono wa muasi uliokuwa umeshika kisu kwa kwapa lake. Hapohapo alikamata
kiganja cha yule muasi kilichokuwa kimefumbata kile kisu. Muasi alipiga
ukelele wa ghadhabu huku akijirusha kujaribu kujinasua kutoka kwenye kabali ile maridhawa, lakini hilo Swordfish alilitarajia,na ndilo alilokuwa akilisubiri.
Haraka sana aliuzungusha mkono wa yule muasi na kuupitisha juu ya bega lake
MDUNGUAJI na kuuvuta chini kwa nguvu.
Yowe kubwa la maumivu lilimtoka yule muasi likiambatana na sauti ya mkono wake ukivunjika kama kipande cha muwa, na kisu chake kikianguka chini.
Huku bado akiwa amemkamata ule mkono uliovunjika, Swordfish alipiga hatua moja kubwa mbele huku akigeuka na kuwa uso kwa uso na yule muasi aliyekuwa akibweka kama mbwa kwa maumivu. Alimvuta mbele kwa nguvu na hapohapo akauachia ule mkono na kumuinulia teke zito lilitua sawia kidevuni kwa yule muasi na kuusukuma nyuma ghafla uso wake kwa nguvu na hapo sauti nyingine ya kitu kama gome la mti likivunjika ilisikika, na yule muasi alirembua macho huku akibwagika chini kama gunia tupu lililoachiwa lisimame lenyewe; shingo yake ikigeukia katika upande usiowezekana. Lile teke lilikisukuma nyuma kichwa chake kwa nguvu wakati mwili wake ukiwa kwenye kasi,na kumvunja shingo.Mwili wake ulipoigusa ardhi ile ya msituni tayari alikuwa ameshakata roho!
Yote hii ndani ya muda usiozidi nusu dakika.
Huku damu ikimvuja upya kutoka kwenye jeraha lake lililofungwa bandeji, Swordfish aligeuka kule alipokuwa Honey-Bee tayari kuendelea na makabiliano, na kuona kuwa yule mwanamama jasiri alikuwa amemuwekea bunduki kichwani yule muasi aliyebaki, ambaye alikuwa ametumbua macho kwa woga huku akiwa amepiga magoti na midomo ikimcheza.
Mchezo ulikuwa umekwisha.
Swordfish alihisi kichwa kikimuwia chepesi na akayumba kidogo. Stealth alimkibilia na kumdaka.
“Swordfish! Uliambiwa usije huku!”Alimwambia huku akimkalisha chini yule mpiganaji shujaa aliyewaokoa kutoka mikononi mwa waasi.
“Ndiyo! Lakini niliposikia milio ya bunduki nilijua kuwa mko matatani...” Swordfish alijibu kwa taabu.
“Lakini ulikuwa umejeruhiwa bwana...ungeweza kutumia bunduki yako tu badala ya kuamua kupambana kwa mikono na miguu yako...!” Stealth alimwambia.Swordfish alitabasamu kwa taabu.
“Milio ya bunduki ingeweza kuwashitua maadui zaidi...ni vyema kuwaua kwa ukimya kadiri iwezekanavyo bwana!”
“Ndiyo! Swordfish yuko sahihi Stealth...,”Honey-Bee alimjibu Stealth, kisha akamgeukia Swordfish na kumshukuru kwa heshima kubwa, “ Ahsante sana mzee...umeokoa maisha yetu.” Stealth aliafikiana naye kwa kichwa huku akimtazama Swordfish kwa macho yaliyojaa shukurani.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Kwa hakika aliamini kuwa yule alikukwa ni mpiganaji mahiri.
“Aaah...unajua, mmoja kwa ajili ya wote...” Swordfish alisema huku akihisi fahamu zikimpotea.
“...na wote kwa ajili ya mmoja...!” Stealth na Honey-Bee walimalizia ile kanuni yao ya makabiliano katika uwanja wa vita kwa pamoja.Lakini Swordfish alikuwa ameshapoteza fahamu.
Stealth na Honey-Bee walitazamana, Honey-Bee bado akiwa amemuwekea bunduki yake kichwani yule muasi aliyebaki. Walipeana ishara kwa macho yao.
Honey-Bee alimuamrisha yule muasi aongoze njia kuelekea nyuma ya lile jabali kubwa lililokuwa eneo lile.Muasi alitii bila kupinga na Stealth alimvutia Swordfish nyuma ya lile jabali kubwa ili kujikinga na shambulizi lolote ambalo lingeweza kutokea, hususan kutoka kwa mgunduaji ambaye hawakuweza kabisa kudiriki kumsahau akilini mwao.
Wakiwa wamejikinga nyuma ya lile jabali, Stealth na Honey-Bee walitazamana tena, kisha Stealth alimuacha Swordfish akiwa amelala chini bila fahamu na kumuendea yule mateka wao.
“Kambi yenu iko umbali gani kutoka hapa?” Alimuuliza, Honey-Bee akiwa amesimama nyuma ya yule muasi akiwa amemuwekea mtutu wa bunduki yake kisogoni. Badala ya kumjibu, yule muasi alimtamkia neno kwa ile lugha wasiyoielewa, ingawa haikuwa na shaka kuwa alikuwa amemtukana, kuonesha kuwa alikuwa tayari kufa kuliko kutoa majibu. Muda huohuo kitako cha bunduki ya Honey-Bee kilimshukia kwa nguvu kisogoni. Muasi alitoa mguno hafifu huku macho yakimrembuka na kujibwaga chini akiwa amepoteza fahamu.
Haraka haraka, bila ya kuongea wale wapiganaji wawili walianza kufanya kazi. Honey-Bee alimchomoa mkanda wa suruali yule muasi na kuutummia kumfunga mikono yake kwa nyuma, wakati Stealth alikimbia haraka hadi kwenye ukingo wa lile jabali na kuchungulia kule walipokuwa muda mfupi uliopita kwa darubini yake.
Hakuona mtikisiko wowote.Kote kulionekana kimya, kama kwamba hapakuwa na mapambano makali muda mfupi tu uliopita. Miili ya wale waasi wanne waliouawa ilikuwa imezagaa eneo lile sambamba na ile miili ya wenzao wawili waliyoikuta pale.
Darubini yake alitulia kwenye mwili wa hayati Nathan Mwombeki, au Alpha, na kushuka kwenye mkono wake wa kushoto na kutazama kile kifaa cha mawasiliano kilichokuwa bado kimekamatwa na mkono ule usiokuwa na uhai. Stealth alikunja uso na maswali kadhaa yakapita kichwani mwake, maswali
MDUNGUAJI
ambayo yalianza kujijenga akilini mwake mara moja baada ya kulifikia lile eneo la maafa na kuutazama kwa karibu ule mwili wa mpiganaji mwenzao kutoka
Tanzania, kabla ya kukurupushwa na wale waasi.
Nyuma yake, Honey-Bee alichomoa kamba za viatu vya yule muasi haraka haraka na kuziunganisha pamoja kisha akamfunga nazo miguuni kwa nguvu. Sasa yule mateka hakuwa tatizo tena kwao.Alimgeukia Stealth.
“Hali ikoje Stealth?” Alimuuliza.
“Kuko shwari.” Stealth alijibu huku bado akitazama eneo lile kwa kutumia darubini yake,kisha akaendelea, “Yanipasa nirudi tena kule...nikinge!”
“Sawa...kuwa mwangalifu...” Honey-Bee alikubaliana naye huku akiiweka sawa bunduki yake na kwenda kupiga goti kando yake.
Stealth alitoa glovu za mpira zilizokuwa mfukoni mwake ambazo wote walikuwa nazo kwa ajili ya kutumia wakati wa kutoa huduma ya kwanza pindi mmoja wao anapojeruhiwa, na kuzivaa. Kitendo hiki kilionekana kumshangaza
Honey-Bee, lakini hakusema lolote na badala yake alikuwa makini kutazama usalama wa eneo ambalo Stealth alikuwa anajiandaa kuliendea.
Stealth alichomoka mbio kwa mtindo wa zigi-zaga huku akiwa amejikunja
kutokea kiunoni hadi pale ilipokuwa ile miili ya wale waasi na wapiganaji wenzao. Alipiga goti kando ya mwili wa marehemu Alpha ambao bado ulikuwa na joto na hakupata taabu kukitoa kile kifaa mkononi mwa marehemu yule.
Alijibanza nyuma ya mti akiwa amechutama na kukiangalia kwa karibu zaidi kile kifaa, na mara moja aliona kuwa kilikuwa tofauti kabisa na kile alichokuwa akitumia mpiganaji Vampire, ambacho ndicho kilikuwa maalumu kwa vikosi vyote vya jeshi la Umoja wa Mataifa.
Sasa hiki kimetokea wapi? Na iweje kikawa mkononi kwa Alpha? Kwanza kwa nini Alpha awe na kifaa cha mawasiliano na si Vampire?
Alizidi kuchanganyikiwa.Aliutazama ule mwili usio na kichwa ukiwa na ile redio yao ya mawasiliano mgongoni, kisha akaugeukia mwili wa mpiganaji Alpha uliokuwa kando yake. Alikitazama tena kile kifaa cha mawsiliano kilichokuwa mkononi mwake, ambacho hakutaka kabisa kukishika bila zile glovu alizovaa kwa kuhofia kuacha alama zake za vidole kwenye kile kifaa.Ni
nini kilichotokea hata kifaa hiki kikawa mikononi mwa Alpha?Aliugeukia tena mwili wa mpiganaji Alpha.
“Alpha komredi wetu...umekuwa ukijihusisha na vitu gani wewe, eenh?”Alinong’ona peke yake huku akikitazama tena kile kifaa cha mawasiliano.
Kisha bila kupoteza muda zaidi aliinama na kutimua mbio kwa mtindo ule ule wa zigi-zaga kurudi kule alipomuacha Honey-Bee, huku mwili ukimsisimka
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
akihofia muda ambao risasi haramu ya mdunguaji itakapouingia mwili wake.
Alijitupa kando ya Honey-Bee nyuma ya lile jabali na haraka sana akageuka kule alipotokea huku akitweta. Amefika salama. Inaelekea Mdunguaji alikuwa ametoweka eneo lile. Honey-Bee alimgeukia na kukitazama kile kifaa kilichokuwa mkononi mwake.
“Umekichukua kutoka kwa Alpha?” Alimuuliza. Stealth aliafiki kwa kichwa huku akikitazama kwa makini kile kifaa, akijaribu kukitumia.
“Na kwa nini kikawa mikononi mwa Alpha?”Honey-Bee alizidi kuuliza.
“Hilo ndilo nililokuwa nikijiuliza muda wote, Honey...” Stealth alimjibu. Honey-Bee aliguna.
“Vampire alikuwa sahihi kabisa...huyu mshenzi alikuwa akitusaliti...yeye ndiye alikuwa msaliti!”Alisema kwa hasira.
“Ni masikitiko kuwa wote sasa wamekufa...hakuna namna ya kujua ni nini hasa kilichotokea!” Stealth alisema kwa huzuni huku akizidi kukitomasatomasa kile kifaa, na hapohapo kilikoroma, na wote wakawa makini sana.
“Nipe namba ya utambulisho ya dharura, haraka!” Stealth alimwambia Honey-Bee.
Katika kampeni za kijeshi kama ile, wapiganaji wote wa kikosi husika hupewa namba za mawasiliano ya dharura ambazo pindi zikitumiwa kwenye kifaa cha mawasiliano kama kile kilichokuwa mikononi mwake wakati ule, huwa zinapeleka mawasiliano ya moja kwa moja kwenye kambi yao.
Hii ni kwa sababu pamoja na kwamba kila kikosi huwa kina mtaalamu wake wa mawasiliano ambaye ndiye alikuwa na njia zote za kuweza kupeleka mawasiliano kambini, huenda mtaalamu huyo wa mawasiliano akauawa
katika mapambano. Na inapotokea hali hiyo, basi wale wapiganaji wanaobakia
hutumia kile kifaa cha mawasiliiano kwa kutumia namba hiyo ya dharura kuwasiliana na kambi yao. Kila mpiganaji alikuwa na hii namba kwenye sehemu wa uficho katika nguo zake. Haraka Honey-Bee alibinua mfuniko wa mfuko wa kifuani kwenye gwanda lake la kijeshi na kumsomea namba zilizokuwa zimeandikwa kwa ndani ya mfuniko ule,ambazo haraka Stealth aliziingiza
kwenye kile kifaa, kisha akabonyeza sehemu iliyoashiria kutuma mawasiliano.
Kifaa kilipiga mbinja hafifu na kukoroma kwa muda kisha kikawa kimya. Stealth alianza kuongea huku akimtazama Honey-Bee.
“Stealth naiita kambi, Stealth naiita kambi...unanisikia kambi?”
Kimya. Mkoromo tu, na sauti kama za mawimbi ya redio wakati mtu anajaribu kutafuta mitabendi. Walitazamana, Stealth akamtikisia kichwa
Honey-Bee kumjulisha kuwa hakuna majibu yoyote. Alijaribu tena kuita
MDUNGUAJI
mawasiliano na kambi yao, na mambo yakawa ni yale yale.
“Una hakika umeingiza namba sahihi?” Honey-Bee alimuuliza. Stealth alitazama tena zile namba alizotumia kutuma mawasiliano kwenye kile kifaa.
“Hakika nimeingiza namba sahihi…lakini haielekei kuleta majibu yoyote!” Stealth alimjibu.
Wapiganaji walichanganyikiwa.
Honey-Bee alisogea ukingoni mwa lile jabali na kuchungulia tena kule walikotoka kujaribu kuona kama bado walikuwa salama. Hakuona kitu kisicho kawaida, lakini bado hakuwa na amani. Aliinua darubini yake na kutembeza tena macho eneo lile kama alivyofanya Stealth hapo awali. Wakati Honey-Bee akihakiki usalama wa eneo lile, Stealth aliendelea kutafuta mawasiliano na kambi bila mafanikio.
“Bado hakuna majibu yoyote?” Honey-Bee alimuuliza, akirudi kutoka kule alipokuwa akichungulia nyuma ya lile jabali.
“Ndiyo…hamna kitu bwana! Hii ni mbaya…hii ni mbaya sana!” Stealth alijibu, huku dalili za kuhamanika zikijidhihirisha katika sauti yake, kisha akaendelea, “…tumo ndani ya eneo la waasi, na haitachukua muda kabla hawajaanza kuwatafuta hao wenzao…” Alisema huku akioneshea nyuma yake kwa kidole chake cha gumba kule ilipokuwa ile miili ya wale waasi waliowaua.
“Basi inatubidi tuchukue hakua za haraka…nini kinafuata sasa Stealth?”
Honey-Bee alimuuliza kiongozi wake. Stealth alitazama kulia na kushoto, kile kifaa kikiwa bado mkononi mwake, kisha akamgeukia Honey-Bee.
“Hebu mtazame Swordfish anaendeleaje…yatupasa turudi kambini mara moja! Tutaendelea kujaribu kuwasiliana na kambi wakati tukisonga mbele!”
Stealth alipitisha uamuzi, na haraka Honey-Bee alienda na kupiga goti kando ya mpiganaji pekee kutoka Tanzania aliyebakia katika kikosi chao. Bunduki yake ikiwa karibu na tayari kabisa kwa kuinyakua pindi ikibidi, alianza kumtikisa, lakini ilikuwa ni kama anatikisa gogo. Swordfish hakuwa na fahamu kabisa.
Akamtikisa tena kwa nguvu zaidi huku akiita jina lake kwa uharaka
ulioashiria kuwa hakukuwa na muda zaidi wa kupoteza, na akimchapa makofi
madogo madogo mashavuni.Swordfish alitoa mguno hafifu na kujitikisa
kidogo huku akibwabwaja maneno yasiyoeleweka.
“Anaelekea kuzinduka!” Honey-Bee alisema kwa furaha huku akimgeukia
Stealth aliyekuwa akiendelea kucheza na kile kifaa cha mawasiliano, akijaribu
kugeukia pande tofauti za dira kwa matarajio labda angeweza kupata
mawasiliano kwa urahisi zaidi kutokea upande moja kuliko mwingine.
“Ni bora azinduke! Vinginevyo itatubidi tumbebe njia nzima kutoka
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
hapa…hili eneo si salama kabisa kwetu!” Stealth alisema huku akisogea hatua
kadhaa kulia kwake, akiwa ameshughulika zaidi na kile kifaa cha mawasiliano.
Honey-Bee alimimina maji kwenye kiganja chake kutoka kwenye chupa yake ya maji na kumnyunyizia Swordfish usoni. Swordfish alitoa mguno
kwa sauti ya juu zaidi kuliko hapo mwanzo, na kugeuza uso wake pembeni
huku akitikisa miguu yake. Honey-Bee alirudia tena kitendo kile, safari hii akimmwagia maji mengi zaidi usoni na kifuani.
Mara Stealth alisikia kama sauti ya mtu ikimuongelesha kutokea kwenye
kile kifaa. Ilikuwa hafifu sana na wala hakuweza kusikia kilichosemwa.
Alihamanika na kukimbia hatua chache kushoto kwake, akitaraji kusikia vizuri zaidi kutokea upande ule huku akiongea haraka na kwa sauti kwenye kile kifaa.
“Eh-Hey! Kambi ya Umoja wa Mataifa mpango wa ReCAMP Sierra Leone! Mimi ni Stealth, nawasiliana na kambi… mnanisikia?”
Mkoromo mkali, na sauti ndogo sana ikiambatana na mbinja kali.
Stealth alizidi kuhamanika, kiherehere kikimpanda.Huenda ile ilikuwa ni nafasi ya kupeleka mawasiliano kambini kwao na kuokolewa kutoka kule msituni.
“Huyu ni Kamanda Stealth nawasiliana na kambi! Stealth nawasiliana na kambi! Operesheni safisha waasi Sierra Leone, mnanisoma?”
Bado alipokewa na mbinja kali na sauti ya mtu akimjibu au akimuuliza vitu
lakini kwa mbali sana kiasi cha kutoweza kuelewa neno hata moja, kiasi akatilia mashaka iwapo ni kweli amesikia hiyo sauti au ni mawazo yake tu.
Stealth alipagawa! Alijua kuwa hata wakiamua kuondoka eneo lile kurudi kambini, mwendo utakuwa ni wa kubahatisha tu na inawezekana kabisa wakazidi kupotea na kujiingiza zaidi ndani ya maeneo ya waasi. Mawasiliano na kambi yao kilikuwa ni kitu cha muhimu sana, kwani iwapo wenzao watajua walipo, itakuwa rahisi kwao kuja kuwaokoa kuliko wao kujaribu kurudi kule kambini kwa kubahatisha.
Kifaa kilikoroma tena naye haraka akakiweka sikioni, lakini bado ilikuwa ni mbinja, mikoromo na sauti mithili ya mvumo wa upepo mkali, huku vikiingiliana na sauti hafifu sana ya mtu akiongea.
“Stealth nawasiliana na kambi! Operesheni safisha waasi Sierra Leone, mnanisoma? Thibitisha tafadhali kambi, thibitisha! Mnanipata?”
Mambo yalikuwa ni yale yale.
Stealth aliwageukia akina Honey-Bee, akamtazama na yule muasi aliyepoteza fahamu. Mawazo mengi yalipita kichwani mwake, na kila lililopita lilikuwa zito. Na pamoja na uzito wa hayo yaliyopita kichwani mwake, jambo moja
MDUNGUAJI
lilibaki kuwa juu kuliko yote. Nalo ni kwamba yeye kama kiongozi wa kampeni
ile, alitakiwa atoe maamuzi ya busara, na usalama wa wale wapiganaji wenzake
ulikuwa mikononi mwake. Sasa walikuwa wamebaki watatu tu, na bado
alikuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa anafanya maamuzi yatakayowafikisha
salama kambini kwao wale wapiganaji wawili waliobaki naye,pamoja na yule
mateka wao.
Alihisi kukata tamaa, lakini hilo kwake kama mpiganaji mahiri hakukubali
kulipa nafasi, ingawa mazingira yote aliyokumbana nayo akiwa na wale wenzake
mpaka wakati ule yalikuwa ni ya kukatisha tamaa sana.Aliifikiria ile operesheni
yao iliyowafikisha pale msituni wakati ule na akaona kuwa ilikuwa ni vigumu
sana wazo la kukata tamaa kutopita kichwani mwake.
Operation Rebel Cleanse Sierra Leone!Operesheni Safisha Waasi Sierra Leone!
Sasa imegeuka na kuwa operesheni ya wao kusafishwa na mdunguaji!
Mdunguaji ambaye hakuwa na shaka kabisa kuwa alikuwa ni mmoja wale
waasi waliokuja “kuwasafisha” na hatimaye kuleta amani nchini Sierra Leone.
Na Alpha alikuwa akishirikiana naye! Alikuwa akishirikiana na waasi, na kwa kufanya hivyo, akiwasaliti wao wote na kuchangia kwa asilimia mia moja
katika vifo vyote vya wale wenzao. Alisonya kwa ghadhabu na hapohapo alianza
kurudi kwa akina Honey-Bee, akilini mwake tayari akiwa amejithibitishia
kuwa kilichobaki ni kuanza msafara wa kuitafuta kambi yao.
Na hapo kile kifaa kikakoroma tena kwa sauti ya juu zaidi. Alijaribu tena kuongea na kambi yao lakini bado hali ilikuwa ile ile, na hata pale alipokuwa akihangaika kusema peke yake kwenye kile kifaa, wazo jingine lilimjia.
Vipi iwapo mtu wa upande wa pili alikuwa akimsikia, lakini yeye (Stealth) ndiye ambaye kwa sababu moja au nyingine alikuwa hamsikii?
Ni jambo linalowezekana, hivyo akapitisha uamuzi.
“Jamani huyu ni Kamanda wa Kitengo wa Operesheni Safisha Waasi Sierra Leone! Tumekwama ndani ya eneo la waasi. Redio yetu imekufa na tunashambuliwa na Mdunguaji.Narudia, tunashambuliwa na Mdunguaji!”
Stealth aliongea kwenye kile kifaa, safari hii bila ya kujali iwapo kulikuwa kuna mtu anayemsikia upande wa pili au vinginevyo.
Alitazama dira yake, kisha akaendelea kuongea kwenye kile kifaa kwa ufasaha kadiri alivyoweza.
“Sehemu tulipo ni kiasi cha nyuzi sifuri-sita-sifuri, kusini-kusini-mashariki.
Wapiganaji sita tayari wameuawa, mmoja amepotea katika harakati,mmoja
amejeruhiwa.Wawili tu ndiyo walio katika hali nzuri kimapambano.
Tunamshikilia mateka muasi mmoja…tunajaribu kurudi kambini.Tunahitaji
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
msaada haraka sana. Narudia, tunahitaji msaada haraka sana! Tuko ndani ya eneo la waasi!Narudia, tuko ndani ya eneo la waasi! Sehemu tulipo ni kiasi cha nyuzi sifuri-sita -sifuri, kusini-kusini-mashariki! Narudia, sehemu tulipo ni kiasi cha nyuzi sifuri-sita-sifuri, kusini-kusini-mashariki. Mwisho wa ujumbe!”
Alikiweka kile kifaa cha mawasiliano kwenye mfuko wa kifuani wa gwanda lake na kuanza kurudi kule kwa akina Honey-Bee.
Kule kwa akina Honey-Bee, Swordfish alifumbua macho na kuona uso wa mpiganaji Honey-Bee ukiwa umemuinamia.“Aaanh…Uh! Ni…nini… kimetokea…?Waasi…?” Alibwabwaja.
“Ulizimia, lakini sasa inabidi tuondoke hapa, unadhani utamudu?” Swordfish alimtazama kwa muda, kama kwamba alikuwa akijaribu kuelewa ni kitu gani alichoambiwa,kisha aliguna huku akijaribu kuinuka.Maumivu makali yalimtambaa na alijikuta akiuma meno. Haraka sana Honey-Bee alimdaka na kumuegemeza kwenye lile jabali. Swordfish aliguna kwa maumivu na kushusha pumzi ndefu. Aligeuza shingo yake na kulitazama lile jeraha lililokuwa begani kwake, ile bendeji nyeupe iliyofungwa juu ya jeraha lile ikiwa imebadilika rangi na kuwa nyekundu kwa damu iliyokaukia, ikiwa imechanganyika na mchanga na vumbi.
“Nitaweza tu Honey…usijali.Vipi kuhusu wenzetu?” Swordfish alisema huku akisimama kwa kujishikilia kwenye uso wa lile habali.
“Wamekufa. Mwenzetu mmoja hajulikani alipo, lakini wengine wote wamekufa…”
Habari hii ilionekana kumchoma sana Swordfish, na mara moja akili yake ikaenda kwa Watanzania wenzake. “Una maana Vampire na Alpha nao wamekufa?” Aliuliza kwa kiherehere.
“Nasikitika hiyo ndiyo hali Swordfish. Tuliobaki ni sisi na Stealth tu. Hatujauona mwili wa Black Mamba, hivyo tunaweza kusema amepotea katika harakati, lakini kwa hali ilivyo, naye anaweza kuwa ameshauawa na mdunguaji bila ya sisi kujua…”
Uso wa Swordfish alionyesha huzuni kubwa, lakini mara moja huzuni ikapokewa na ghadhabu.
“Lau huyu mdunguaji angejitokeza kidogo tu…” Alisema kwa hasira, na muda huo Stealth alifika eneo lile na kuwapa habari ya hali ya mawasiliano ilivyokuwa, na kuwaambia kuwa walitakiwa waanze safari mara moja. Swordfish alianza kuongea kitu, lakini akahisi maumivu makali begani kwake, na akageuza uso wake huku akiinamisha kichwa chake kutazama pale kwenye jeraha, na hilo ndilo jambo lililookoa maisha yake.
MDUNGUAJI
Kwani hapohapo alisikia mlio wa bunduki ukiambatana na kishindo cha risasi ikichimba uso wa lile jabali milimita chache kutoka kichwani kwake, ambapo sekunde moja tu iliyopita ndipo uso wake ulipokuwa, na maumivu makali yakilipata jicho lake la kulia. Risasi ilimkosa kwa milimita chache sana na kuchimba lile jabali, kipande cha risasi kilichopasuka baada ya kujikita kwenye uso wa lile jabali gumu kikimchimba jichoni.
Yowe kubwa lilimtoka huku akianguka chini akiwa amejishika jicho lake la kulia na hapohapo akiwasikia Honey-Bee na Stealth wakipiga kelele.Msitu uliamshwa na milio mingi ya risasi kutokea pande mbili tofauti na wapiganaji walijikuta wamezingirwa
“AAAAAKH, Mdunguajiii…!”Stealth alibwata huku akijitupa kulia kwake akijaribu kujikinga nyuma ya mti uliokuwa karibu naye, lakini alichelewa, kwani Honey-Bee alimshuhudia kwa kihoro akitupwa nyuma huku akiachia yowe kubwa, na kubabatizwa kwenye lile jabali, damu ikiruka kama bomba
kutoka sehemu moja katika mwili wake, lakini hakujua ni wapi hasa.
“Sio Mdunguaji! Ni waasi pumbavu zao…!” Honey-Bee alibwata huku akijibiringisha na bunduki yake mikononi na kujilaza nyuma ya jiwe kubwa chini ya lile jabali. Alizungusha macho eneo lile na kupata uelekeo ambao risasi zilikuwa zikitokea.
Waasi wamewakuta!
Alimimina risasi za mfululizo kuelekea ule upande zilipotokea zile risasi na alishuhudia waasi wawili wakiporomoka kutoka kwenye jiwe kubwa lililokuwa kiasi cha mita kumi na tano hivi kutoka pale walipokuwa, ule upande ambao hapo awali wale waasi wa kwanza walitokea.
Swordfish alitoa mkono jichoni na kuona damu nyingi kiganjani kwake. Alikamata bastola yake kwa mkono wa kushoto na kujitupa kule alipokuwa Honey-Bee huku akigumia kwa uchungu.
“Stealth!Are you Okay?” Honey-Bee aliita huku akiangalia kule risasi zilipokuwa zimetokea, ambapo zilisikika sauti na kelele nyingi za waasi zikielekea pale walipokuwa.
Balaa!
“Nimepigwa shingoni! Tukimbie…” Stealth alipiga kelele huku akijiinua na kuwakimbilia, lakini alijikwaa na kupiga mweleka mzito, kile kifaa cha mawasiliano kikichomoka mfukoni mwake na kujipigiza chini kwa nguvu.
Aliinuka na kukiwapua huku akiendelea kutimua mbio, hali amejishika upande wa shingo yake kwa mkono wake wa kushoto, sehemu ambapo shingo ilikuwa ikiungana na kiwiliwili chake, damu nyingi ikimchuruzika vidoleni mwake.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Risasi ilikuwa imepita upande wa kulia wa shingo yake,kwa mbele, juu kidogo ya bega na kutokea nyuma ya shingo ile, ambapo ilikata mshipa wa damu. Na hata pale alipokuwa akikimbia alihisi miguu ikimuisha nguvuna ikigongana, macho yake yakipoteza nuru, ukungu mkubwa ukitanda mbele yake,lakini aliweza kuwaona wenzake wakiwa kiasi cha hatua zipatazo kumi mbele yake…
Swordfish alihisi maumivu makali jichoni, maumivu yaliyopeleka miale ya uchungu mpaka ndani kabisa ya moyo wake. Alifinya jicho lake lililojeruhiwa huku akiuma meno. Kelele za waasi zikiambatana na milio ya risasi kutoka kila upande zilizidi kuwakaribia. Alijitahidi kutazama kwa jicho lake moja lililobakia na alimuona Stealth akitetereka na akielekea kuanguka kwa mara nyingine na alijua kuwa naye alikuwa amejeruhiwa vibaya.
“Kimbia Stealth! Kimbia…utaweza tu, tunakungoja!”Alimpigia kelele.
Muda wote huo Honey-Bee alikuwa akijishughulisha kuongeza risasi kwenye bunduki yake haraka haraka, na sasa aliinua uso wake kutazama kule
alipokuwa akitokea Stealth, bunduki yake ikiwa imekamatwa kwa mikono yake yote miwili akisubiri muasi mwingine atakayejitokeza baada ya wale wawili aliowaangamiza ili amuondoe duniani.
“Vipi jicho lako Swordfish…unaweza kuona?” Alimpigia kelele Swordfish huku akimtazama Stealth akijitahidi kukimbia kwa taabu huku zile kelele za waasi zikizidi kuwakurubia.
“Kwa taabu…” Swordfish alijibu.
“Nikinge!” Honey-Bee alisema huku akitimua mbio kutoka pale nyuma ya jiwe lililowakinga na kumkimbilia Stealth. Alimkamata mkono wake na kuupitisha begani kwake na kuanza kurudi naye mbio nyuma ya lile jabali. Nyuma yao kelele za waasi,sasa zikiambatana na milio ya mbwa, zilizidi kuwa kubwa.
“Twendeni! Tusisimame mpaka pale kwenye ule mwinuko, tutapambana nao tukiwa pale juu!” Stealth alipiga kelele huku akisaidiwa kukimbia na Honey-Bee, ambaye naye aliloweshwa na damu nyingi iliyokuwa ikitoka kwenye jeraha la Stealth.
“Hapana! Unatokwa damu nyingi…tuisimamishe kwanza!” HoneyBee alimjibu huku akimbwaga chini kando ya Swordfish nyuma ya lile jiwe walilokuwa wamejificha hapo awali.
“Hatuna muda! Tutauawa sote…basi nyie nendeni!”Stealth alisema kwa taabu. Haraka, bila ya kumjibu, Honey-Bee alilirarua gwanda la Stealth kwa kutumia kisu chake kikali cha mapambano na kutazama lile jeraha. Akamgeukia
MDUNGUAJI
Swordfish na kumtazama jeraha lake. Yeye alikuwa akilia taratibu kwa uchungu na maumivu huku akijitahidi kutazama kwa taabu kule walipotarajia waasi watokee, akiwa amekamata bastola kwa mkono wake wa kushoto, ilhali mkono wake wa kulia uliojeruhiwa hapo awali ukiwa hauna uwezo wa kufanya lolote.
Honey-Bee alihamanika.
Wenzake wote walikuwa wamejeruhiwa, waasi walikuwa wanawajia kwa wingi, na hawakuwa na namna yoyote ile ya kuweza kuokoka kutoka eneo lile.
“Unasubiri nini sasa mwanajeshi? Fanya litakiwalo!” Stealth alimkemea akiwa amelala pale chini akivujwa damu. Honey-Bee alizinduka na haraka haraka alitoa kimkoba chake cha huduma ya kwanza na kuanza kumfunga lile jeraha kuzuia damu kutoka.
Kutoka pale alipokuwa Swordfish alianza kuwaona mbwa watatu wakija mbio kutokea kwenye msitu wa miti mirefu iliyokuwa umbali wa mita zipatazo mia moja kutoka pale walipokuwa, kisha likafuata kundi kubwa la waasi waliokuwa wakipiga kelele za jazba.
“Wajinga wanakuja na mbwa! Fanya haraka Honey-Bee, wanatukaribia!”Swordfish alihimiza na haraka Honey-Bee alimalizia kulifunga jeraha la Stealth kwa bandeji na plasta maalum zilizoweza kuzuia damu isiendelee kutoka, akijua kuwa haitaweza kuzuia damu ile kwa muda mrefu.
“Hiyo itasaidia kwa sasa!” Honey-Bee alimwambia Stealth na kuinua uso wake kutazama kule walipokuwa wakitokea wale waasi, na kuona walikuwa wakiwakaribia kwa kasi, wakiwa na mchanganyiko wa silaha. Mbwa wao walikuwa wameshawaona wale wapiganaji na walikuwa wakiwaendea kwa kasi huku wakibweka kwa hasira. Aliikwapua bunduki yake na kwenda pale alipokuwa Swordfish.
“Pumbavu! Wajinga wanakuja na mbwa!” Alisema kwa hasira huku akiinua bunduki yake.
“Tusipoteze muda…wako wengi sana…tujaribu kukifikia kile kichuguu, tuwashambulie tukiwa juu!”Stealth alisema kwa taabu.
“Hawa mbwa watatuletea taabu Stealth, inabidi tuwaondoe kwanza!”HoneyBee alijibu, na hata pale aliposema vile, risasi za waasi zilianza kuelekezwa pale walipokuwa. Honey-Bee atuma risasi mbili na mbwa mmoja alianguka huku akibweka yowe lake la mwisho hapa duniani. Waasi walizidisha kasi na kelele huku wakitupa risasi bila mpangilio.
Honey-Bee alituma risasi nyingine za mfululizo na wale mbwa wawili waliobaki walipiga mieleka kila mmoja kwa namna yake, wakipishana si zaidi ya sekunde kumi baina yao.
Kitendo hiki kilionekana kuwababaisha kidogo wale waasi, na baadhi yao
walijitupa chini kujaribu kuokoa maisha yao ilhali wengine walizidi kusonga
mbele bila kujali iwapo watapoteza maisha katika mapambano yale.
Muda huohuo wapiganaji waligeuka na kuanza kutimua mbio kukiendea
kile kichuguu ambacho hapo awali mpiganaji Vampire alikiteremka na kulifikia
lile jabali kabla ya kumkurupusha msaliti Alpha.Sasa wapiganaji walikuwa wakikimbizwa huku wakipigiwa kelele kama wezi na wakitupiwa risasi ovyo na kundi la waasi wapatao thelathini hivi.
Patashika!
Wapinaganaji walikimbia kwa kadiri walivyoweza, wakihema na kutweta, jasho likiwatiririka, risasi zikiwakosa-kosa na kupiga miti iliyotapakaa eneo
lile. Honey-Bee alikuwa amemshika mkono Swordfish aliyekuwa haoni vizuri wakati Stealth alikuwa akijitahidi kukimbia mwenyewe. Mwinuko waliokuwa wakiukimbilia ulikuwa kiasi cha mita zipatazo hamsini hivi kutoka pale walipofika, lakini waasi walikuwa wakiwafikia kwa kasi huku wakiwatupia
risasi na silaha nyingine zisizo rasmi.
“Pita kushoto!” Stealth alimpigia kelele Honey-Bee aliyekuwa mbele akimkokota Swordfish. Honey-Bee aliinua uso wake na kutazama kushoto kwake na alielewa ni kwa nini Stealth alitaka wapite kushoto. Kwa kukimbilia upande ule, wangeweza kuukwea ule mwinuko kutokea ubavuni na sio moja
kwa moja usoni ambapo wangekuwa ndiyo wamejianika ili wadunguliwe kwa urahisi na wale waasi.
Alifuata maelekezo ya kamanda wake. Swordfish alitetereka na kujipamia kwenye mti uliokuwa karibu yake na kuanguka huku akitoa mguno wa uchungu. Honey-Bee alianza kumrudia huku akilaani hali ile.
“Songa mbele…usirudi nyumaa!” Stealth alimpigia kelele Honey-Bee, ambaye aligeuka na kutimua mbio akimuacha Swordfish pale chini akijitahidi kujiinua. Stealth alikuja na kumnyakua Swordfish na kuendelea kutimua naye mbio, huku Swordfish naye akijitahidi kwenda naye sambamba. Jicho lilikuwa alikimuuma vibaya sana na hakuweza kabisa kuangalia sawasawa kwa kutumia jicho moja.
Mara mlio wa kitu kama mbinja nzito ulisikika kutokea nyuma yao, na wote walijiitupa chini kila mmoja kutokea mahala alipokuwa huku akiropoka neno la kuhamanika. Kishindo kikubwa kilisikika na miti kadhaa iliyokuwa mbele yao ilipasuka na kukatika ovyo, ikitawanyika vibaya na kutupa matawi
huku na huko. Wapiganaji walipiga kelele huku wakijibiringisha huku na huko pale chini walipojitupia, wakihangaika kujikinga na vipande vya matawi
MDUNGUAJI ya ile miti iliyotawanywa na lile kombora hatari lililofyatuliwa na wale waasi kwa lengo la kuwaangamiza, na sekunde moja baadaye, Stealth na Honey-Bee walishuhudia sehemu ya ule mlima waliokuwa wakiukimbilia ikimeguka kama pande la udongo lililomwagiwa maji. Mapande makubwa makubwa ya mawe
yalitupwa huku na huko kutoka kwenye mlima ule mdogo na kuanguka kwa
kishindo kikubwa kabisa!
Mayowe yaliwatoka Stealth na Honey-Bee bila kutarajia, na Swordfish aliyekuwa akihangaika na jicho moja alichelewa kushuhudia jinsi sehemu ya ule mlima ilivyotawanywa na lile kombora, ila kile kishindo tu kilitosha kumjulisha kilichotokea. Alihangaika kugeuka huku na huko akiwa amejilaza chini, bastola yake ikiwa mkononi na bunduki yake ikiwa imeshikiliwa kwa mkanda maaluum mgongoni kwake.
“Nini…wapi…?” Alimaka huku akihangaika kugeuza uso wake ili aweze kuona vizuri kwa jicho lake lililobaki.
“Wajinga wanatumia RPG!” Stealth alimjiibu huku akijigeuza kutazama kule kwa wale waasi.“Aakh…!RPG!? Pumbavu! Hivi ni nani huyu anayewapa hizi silaha hawa?”Swordfish alilaani huku akijirusha nyuma ya shina la mti mkubwa uliokuwa karibu yake na muda huo Stealth aliachia sauti ya mshituko baada ya risasi moja kupiga upande wa pili wa ule mti aliokuwa amejificha nyuma yake.
Honey-Bee alikuwa ameshajiweka sawa nyuma ya mti na sasa alikuwa amegeukia kule walipokuwa wakitokea wale waasi. Ndipo kwa mara ya kwanza alipouona wingi wao, wakiwakimbilia kwa kasi, wakiwa na silaha za kila aina, yakiwemo mapanga na marungu, mawe pamoja na zile silaha za moto walizokuwa wakizitumia.
Aliwaangalia wenzake na akaona kuwa walikuwa wameelemewa. Alitazama umbali uliobakia hadi kuufikia ule mwinuko waliokuwa wameukusudia na akaona kuwa ingawa haukuwa umbali mrefu, matarajio ya kuufikia
salama yalikuwa madogo, kwani baina ya pale walipokuwa na ule mwinuko, ilikuwa ni sehemu tambarare iliyokuwa na mawe mengi makubwa-makubwa
yaliyotapakaa kila upande. Ilikuwa ni sehemu ya wazi ambayo walitakiwa waipite wakati wale waasi wako mbali, lakini sasa walikuwa wamewafikia.
Aligeuka tena kule walipokuwa wale waasi.
“Hawa wako wengi sana Stealth…!Na wanazidi kutukaribia, itabidi…”
Honey-Bee alisema, lakini hata wakati maneno hayo yanamtoka, aliweza
kumuona muuasi mmoja akiliweka sawa begani mwake lile guruneti aina ya
RPG(Rocket Propelled Grenade) tayari kwa kuwashambulia tena, kitendo
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
ambacho pia kilionwa na wenzake, ambapo kila mmoja alizidi kujibanza zaidi sehemu aliyokuwepo kwani hawakuwa na la kufanya.
Honey-Bee hakusita wala kufikiri zaidi.
Aliinua bunduki yake na kumdungua yule muasi aliyekuwa akiwaelekezea lile kombora, na kabla kombora halijafyatuka waasi walimshuhudia mwenzao akitupwa nyuma huku akiachia yowe kubwa, lile kombora likimtoka mikononi.
“Safi sana Honey…!” Stealth aliropoka na kuchomoka kutoka pale alipokuwa amejificha na kuanza kukimbia kuelekea kule kwenye ule mwinuko, huku akimburura Swordfish.
“Twendenii!” Alipiga kelele na Honey-Bee alianza kugeuka kuungana na wenzake, lakini hapo alimuona muasi mwingine akiliokota lile kombora lililoangushwa na yule muasi wa kwanza ambaye sasa alikuwa akinyang’anyiana roho yake mbaya na ziraili pale chini huku wenzake wakiendelea na harakati zao bila kumjali.
“Wanachukua tena kombora Stealth!” Honey-Bee aliwapigia kelele wenzake, nao wakajitupa tena chini huku wakilaani hali ile. Kule kwa waasi Honey-Bee aliwashuhudia waasi wawili wakisaidiana kuliweka sawa lile kombora begani kwa mmoja wao, kisha yule mmoja akaanza kulielekeza kwao.Hakufanya kosa.
Alitupa risasi nyingine, na yule muasi alichia yowe kubwa huku akitupwa chini na lile kombora likimtoka mikononi kama mwenzake wa hapo awali. Haraka sana yule mwenzake aliyebaki alilirukia lile kombora na kuanza kugeuka nalo akiwa amepiga goti moja pale chini, lakini hapo ndipo alipoishia, kwani Honey-Bee alimtandika risasi ya kichwa naye akapiga mweleka, roho na kombora vikimtoka kwa pamoja.
Loh!
Stealth aliiona hali ile na alijua kuwa muda wa kufanya maamuzi ulikuwa umefika.
“Sasa itabidi tupambane nao hapa hapa! Hatuwezi kuufikia ule mlima bila kuuawa!” Alibwata huku akijiweka sawa nyuma ya mti na kuanza kuwatupia risasi za mfululizo wale waasi ambao nao walikuwa wakitupa risasi nyingi, zilizobanjua magome ya miti iliyokuwa karibu na wale wapiganaji, nyingine zikichimba ardhi eneo lote lile.
“Aaakh…Stealth! Sioni sawasawa bwana! Siwezi kabisa kupiga shabaha!”
Swordfish, shujaa wa makabiliano ya ana kwa ana alipiga kelele akiwa amehamanika.
“We’ elekeza bunduki yako kule kwa waasi halafu mwaga risasi! Usijali kitu!
Tumezidiwa kwa kila hali, lakini ni lazima tupambane!” Stealth alimjibu huku
MDUNGUAJI
akiwamiminia risasi wale waasi.
Basi ndani ya dakika kumi zilizofuata msitu ulirindima kwa majibizano ya risasi na kelele za waasi. Wapiganaji walikuwa wakiwaangusha waasi kwa kadiri walivyoweza huku wao wakinusuriwa na miti waliyokuwa wamejificha nyuma yake. Lakini wale waasi walikuwa wengi na walizidi kuwasogelea. Honey-Bee aliamua kucheza na muasi yeyote atakayelishika lile kombora kwani alijua kuwa lile kombora liliweza kuwaangamiza wote kwa pigo moja tu. Basi ikawa kila muasi anayelishika tu, anachukua risasi.
“Tunaishiwa risasi sasa…! Pumbavu!” Honey-Bee alipiga kelele.
Muda huo alimuona muasi mwingine akiliinua tena lile kombora, na akajua kuwa hatoweza kumuua kila atakaelishika lile kombora, kwani risasi zilikuwa zinawaishia. Aliamua kukata mzizi wa fitina. Huku milio ya risasi ikiwa imeshamiri masikioni mwake, alimlenga sawasawa yule muasi aliyeshika lile kombora, kisha aliteremsha bunduki yake usawa wa lile kombora na kufyatua risasi. Kombora lilipasuliwa kwa risasi na kumjeruhi vibaya mikononi yule muuasi aliyepiga yowe huku lile kombora likitupwa pembeni likiwa limeparaganyika vibaya sana.
Kwisha habari yake!
“Safi sana Honey…! Turudi nyuma sasa…wanazidi kuja!” Stealth alipiga kelele huku akirudi kimgongo-mgongo na akiendelea kuwamwagia risasi wale waasi. Lakini sasa wale waasi walimgeukia Honey-Bee na kuanza kum-miminia risasi kwa wingi.Ni wazi kuwa walishajua kuwa hatari kubwa kwao ilitokea kwake, na sasa alikuwa amewaharibia kombora lao, walikuwa na hasira naye.
Honey-Bee alikimbia kimgongo-mgongo huku akiwajibisha kwa risasi wale waasi waliokuwa wamepungua idadi. Eneo lote lile lilinuka baruti na kutawaliwa na milio ya risasi. Sasa waasi walianza kuwazingira wale wapiganaji kwa mtindo wa nusu-duara.
Ilikuwa ni hekaheka si kidogo!
Honey-Bee alijigonga kwenye mti uliokuwa nyuma yake. Akajisogeza pembeni kidogo na kujaribu kuuzunguka ule mti na kujificha nyuma yake, na kwa sekunde moja aliwageuzia mgongo wale waasi na hapo alihisi maumivu makali mguuni mwake huku akitupwa hewani kama mtu aliyepigwa ngwara kali, yowe kubwa likimtoka.
“Honey-Bee amepigwa!” Stealth alibwata huku akimshuhudia yule mwanamke shujaa akianguka chini na bunduki yake ikimtoka mikononi. Risasi ilimpata mguuni, nyuma ya paja lake na Honey-Bee aliuhisi mguu ukimfa ganzi.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Swordfish alijibanza nyuma ya mti, akiendelea kuwatupia risasi za mfululizo wale waasi ili kuwapoteza lengo kwani kwa hakika hakuweza kabisa kulenga shabaha sawasawa. Stealth alimkimbilia Honey-Bee huku akitupa risasi na akiwatukana matusi ya nguoni wale waasi kwa hasira. Honey-Bee aliendelea kulala pale chini huku akiwaangalia wale waasi walimkurubia, na hakudiriki kuinuka kwani alijua hapo ndiyo angekuwa anajianika vizuri zaidi kwa wale waasi.Risasi zilichimba michanga karibu na pale alipokuwa ameangukia na alikuwa hana la kufanya, mayowe yakimtoka huku akijaribu kuinyakua bunduki yake pale ilipoangukia, lakini hakuweza kuifikia.
Stealth alimruka na kusimama mbele yake huku akiwamwagia risasi wale waasi, sasa Honey-Bee akiwa mgongoni mwake.
“Inuka Honey-Bee! Jaribu kujificha nyuma ya mti!” Alimpigia kelele, na Honey-Bee alijitahidi kuinuka lakini alianguka tena kwani mguu wake haukumruhusu kufanya hivyo. Alilia kwa uchungu na maumivu na kutambaa hadi nyuma ya mti uliokuwa karibu yake, akiikwapua bunduki yake wakati akifanya hivyo. Stealth alikuwa akirudi nyuma huku akimimina risasi, wakati zile za waasi zikimkosa kwa bahati tu.
Mara risasi zikawa hazitoki kwenye bunduki yake.
“Aaaah…! Nimeishiwa risasi! Bloody hell!”Alipiga kelele huku akiitupa pembeni ile bunduki na na kuanza kutupa risasi moja moja kwa bastola yake huku akirudi nyuma. Sasa waasi walikuwa wamebakisha kiasi cha mita zisizozidi ishirini na tano kuwafikia, na zile kelele zao za mori na jazba zilizidi kuwachanganya wapiganaji.
“Na mimi nimeishiwa bwana…!” Swordfish naye alipiga kelele kutoka pale alipokuwa.Sasa Stealth alikuwa katikati ya wale waasi na wale wenzake wawili, mkononi akiwa na bastola tu! Alirudi nyuma na kujigonga kwenye mti, kisogo chake kikijipigiza vibaya kwenye mti ule. Kichwa kikamzunguka, macho yakaanza kumuingia kiza. Alijitahidi kuinua bastola yake kuwaelekezea wale waasi lakini hakuwa akiwaona vizuri.
Risasi za waasi zilikuwa zikipiga kwenye miti jirani yake na nyingine zikichimba ardhi na kumtupia michanga na majani, naye alionekana kuzongwa na mashaka. Ni wazi kuwa muda wowote moja au baadhi ya zile risasi ingempata, na wenzake waliiona hali ile.
“Stealth lala chini!” Honey-Bee alipiga kelele, na Stealth alijitupa chini. Alisota kinyume-nyume kuelekea kule kwa Honey-Bee ilhali macho yake yakiwa kule zilipokuwa zikitokea zile risasi za waasi, lakini cha ajabu ni kwamba alikuwa akiona ukungu mzito ukiwa umetanda mbele yake na kwa mara ya
MDUNGUAJI
kwanza akihisi kitu kama maji ya uvugu-vugu yakimtambaa kutokea shingoni kwake. Alifinya macho na kupeleka mkono shingoni kwake pale alipojeruhiwa hapo awali, na alipoutazama mkono wake uliovikwa glovu ya mpira aliona ukiwa umetapakaa damu. Damu ilikuwa imeanza kumtoka upya baada ya ile bandeji aliyofungwa na Honey-Bee kufumuka kutokana na hekaheka alizokuwa akikabiliana nazo na. Alihisi kupotewa na fahamu lakini alijitahidi kuinua bastola yake kuwaelekezea wale waasi.Bastola ilimuwia nzito sana, na matumaini yakampotea kabisa.
Alisikia muungurumo mpya ambao hapo awali haukuwapo, lakini hakuweza kuutilia maanani. Alikuwa akisubiri risasi za wale waasi zianze kuutoboa-toboa mwili wake.
“Stealth tulia hapohapo chini!” Honey-Bee alipigia kelele na kuanza kuwatupia risasi wale waasi kutokea nyuma ya mti alipokuwa amejilaza huku akibubujikwa na machozi kutokana na maumivu makali yaliyoutawala mguu wake, damu nyingi ikimbubujika.
Sasa waasi walikuwa karibu sana na walizidi kuwasogelea huku kila mmoja wao akitupa risasi kuelekea kule walipokuwa wale mashujaa watatu waliobaki, wengine wakiwatupia, pamoja na zile risasi, mawe na marungu! Yaani walikuwa ni kama watu waliopagawishwa kwa bangi au madawa ya kulevya.Wakati baadhi ya wenzao walikuwa wakiangushwa mmoja baada ya mwingine kwa risasi za Honey-Bee, wale wengine walikuwa wakija tu kama vichaa!
Ilikuwa ni hali moja ya kutisha sana, hata kwa wapiganaji mashujaa na mahiri kama wale wa jeshi la umoja wa mataifa.
Swordfish na wenzake walikiona kifo kikiwa kimewakabili, lakini HoneyBee aliendelea kuwamiminia risasi wale waasi waliopandisha mori huku akilia kwa sauti.
Sasa wapiganaji walikuwa wakipigana vita inayoelekea kwenye kushindwa, na msitu ulitawaliwa na milio ya risasi, sasa sauti nyingine ya ngurumo ikizidi
kudhihirika masikioni mwa wapiganaji wale, bila shaka na masikioni mwa wale waasi vile vile.
Mara risasi zikawa hazitoki kwenye bunduki ya Honey-Bee! Alibonyeza
kifyatulio, hamna kitu! Akabonyeza tena, patupu!
Muda huo risasi za mfululizo zikaumiminikia uso wa ule mti aliokuwa amejificha nyuma yake, naye akazidi kujikunyata nyuma ya ule mti, akiiachia ile bunduki isiyo na faida tena kwake ikianguka chini.
“Na mimi nimeishiwa risasi jamani…!” Honey-Bee naye aliripoti kwa hamaniko. Swordfish alitazama kule kwa Honey-Bee, akaona kuwa kweli
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Honey-Bee alikuwa ameelemewa. Akamgeukia Stealth, na hapo alimuona
Yule mwenzao akijiwekea alama ya msalaba kusali sala yake ya mwisho kisha
akaangusha uso wake chini kama mtu aliyepoteza fahamu.
Hapo akajua kuwa mwisho wao ulikuwa umefika.
Hakutaka kukubali.
“Laleni hapo hapo chiniiiii!” Alipiga kelele akiwa ameshatoa bomu lake la mkono, akavuta pini ya kutunza usalama wa bomu lile kwa meno yake na kulitupa kule kwa waasi.Mlipuko mkubwa ulisikika na waasi walitupwa
huku na huko, wakipiga mayowe ya maumivu, wengine wakifa pale pale ilhali wengine wakijeruhiwa kila mmoja kwa kiwango chake.
“Aaaakh! Swordfish! Na wao wana mabomu! Watatumaliza sasa hivi!”
Honey-Bee alipiga kelele, lakini hapo alishuhudia wale waasi walionusurika na bomu la Swordfish wakianguka mmoja baada ya mwingine, na mvumo mkubwa ukisikika kutokea juu. Waasi walianza kukimbia kurudi walikotoka huku wakipukutika kama maembe kutoka kwenye mti.
“Heh! Ni nini…?” Swordfish alimaka na hapo ngurumo za helikopta maalum za kijeshi zilitawala eneo lote lile. Swordfish na Honey-Bee walizidi kujificha nyuma ya miti huku wakitazama juu kwa taharuki. Helikopta mbili za kijeshi zilikuwa zikiwamiminia risasi wale waasi kutokea kule kwenye ule mwinuko waliokuwa wakiukimbilia hapo awali na mioyo ikawapasuka kwa furaha.
Zilikuwa ni helikopota za jeshi la umoja wa mataifa!
“AHHH! Mungu mkubwa! Mungu mkubwa!” Swordfish alipiga kelele kwa hamasa kubwa. Zile helikopta zilikuwa zikiwachabanga risasi wale waasi na wala hazikuonesha kuwa zilikuwa zimekuja kuwaokoa wale wapiganaji. Lengo lao lilikuwa ni kuwaangamiza wale waasi tu.
Stealth alizisikia zile ngurumo za helikopta zikiwa kubwa masikioni mwake. Alijilazimisha kurudi kwenye fahamu, na aliinua uso wake kutazama zilipotokea zile ngurumo, na ndipo alipoziona zile helikopta zikimimina risasi kwa wingi kutokea hewani. Akihisi nguvu zikimrejea, alijiinua na kuyumba kwa taabu kuelekea kule kwa wenzake.
“Sweepers! Hizo ni “Sweepers”, twendeni!” Aliwapigia kelele wenzake, na, wakiwa na matumaini mapya wale wapiganaji waliinuana na kuanza kukimbilia
kule mlimani wakiwa wameshikana mabega, Honey-Bee akiwa katikati ya wale
wenzake wawili, wakisaidiana kujisogeza mbali na lile eneo la maangamizo.
Katika kampeni za uokozi, au Rescue Missions, kama ile, huwa kuna helikopta
zinazotangulia mbele kwa lengo la kuwaweka mbali adui na wapiganajai
MDUNGUAJI
wanaotakiwa kuokolewa kwa kuwaangamiza kwa risasi kadiri iwezekanavyo.
Hizi huitwa “Sweepers”, yaani vifyagio. Jukumu lake ni kujiweka katikati ya wapiganaji wanaotakiwa kuokolewa na maadui zao. Ikifikia hapo, wapiganaji
walitakiwa wasonge mbele na kujiweka mbali zaidi na eneo la mashambulizi, ndilo jambo ambalo Stealth alikuwa akilifanya alipowashauri wenzake
wakimbilie kule mlimani zilipotokea zile helikopta.
“Wamejuaje kuwa tuko huku na tumo matatani? Eeeh! Hakika Mungu
mkubwa!” Swordfish alipiga kelele huku akisaidiana na wenzake kuelekea kule
kwenye ule mwinuko ulioparaganyishwa na guruneti la waasi hapo awali. Stealth alihisi fahamu zikimpotea tena.
“Watakuwa wamesikia ujumbe wangu wa redio! Kumbe nilikuwa sahihi! Wao walikuwa wananisikia wakati mimi nilikuwa siwasikii...!” Stealth alibwabwaja, ingawa ilikuwa kama kwamba anajisemea mwenyewe, kwani fahamu zilikuwa zikimhama kwa kasi sana. Miguu ilimlegea na ghafla akashindwa kutembea.Alianguka na kuwavuta wenzake pamoja naye. Haraka Honey-Bee na Swordfish waliinuka na kumuinua. Wakaendelea kuufuata ule mwinuko, sasa Stealth akibururwa katikati yao, Honey-Bee akichechemea kwa taabu.
Muda huo mvumo wa helikopta nyingine ulisikika kutokea nyuma ya ule mwinuko waliokuwa wakiukimbilia na wale wapiganaji wawili waliobakiwa na fahamu waliishuhudia helikopta ya tatu ikiibuka kutokea nyuma ya mwinuko ule, wapiganaji wengine wanne wenye silaha wakining’inia, wawili kila upande wa helikopta ile.
Kwa kufuata maelekezo ya mafunzo yao ya kijeshi, Swordfish na Honey-Bee walimlaza chini Stealth aliyepoteza fahamu na wao walilala chini wakiitazama ile helikopta ikishuka taratibu mita chache kutoka pale walipokuwa.
Kabla haijagusa ardhi, wale wapiganaji waliokuwa wakining’inia kila upande wa ile helikopta waliruka chini na kujibiringisha kiufundi na silaha zao mikononi. Waliwakimbilia wale wapiganaji waliojilaza pale chini na kuwazingira kwa kila mmoja kupiga goti huku akiwa amegeukia upande mmoja wa dira, bunduki zikiwa makini mikononi mwao na hivyo kuwawekea ukuta wenzao. Sasa jukumu la usalama wa wale wenzao lilikuwa mikononi mwao.
Hii ndiyo nidhamu ya kijeshi iliyotekelezwa kimya kimya na wale makomando wanne, kila mmoja akilijua jukumu lake na akilitekeza ipaswavyo.
Huku nyuma ile helikopta ilitua ardhini na hapo ndipo walipoteremka matabibu wa kijeshi na kuwakimbilia wale wenzao huku wakiwa wamebeba
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
machela maaluum za kubebea majeruhi katika kampeni za uokozi kama ile. Nyuma yao, makomando wengine wawili kutoka kwenye ile helikopta walibaki wakiwa wamepiga goti kila upande wa ile helikopta wakiwa tayari na bunduki zao. Hawa kazi yao ilikuwa ni kuwakinga wale matabibu waliokuwa wakikimbilia kuwaokoa wale majeruhi na pia kuilinda ile helikopta na rubani wake.
Matabibu walibwaga chini zile machela zao na kuanza kufanya kazi haraka haraka huku wakiwauliza wale mashujaa waliokuja kuwaokoa juu ya majeraha yao wakati wakiwachunguza sehemu ambazo waliweza kuziona kuwa zilikuwa zimejeruhiwa. Mara moja Honey-Bee alichukua jukumu la kutoa maelezo juu ya hali ya yake na za wenzake.
“Stealth amepigwa risasi upande wa kulia wa shingo yake…ametokwa damu nyingi na sasa amezirai!”
Kiongozi wa wale matabibu watatu wa kijeshi, ambaye alikuwa ni raia wa Uganda, alimtazama Stealth, na kuwaamrisha wale wasaidizi wake wawili ambao walimnyanyua kwa tahadhari kubwa na kumlaza juu ya moja kati ya machela walizokuja nazo. Waliinyanyua ile machela na kukimbia naye kule kwenye helikopta, wakiwa wamekingwa na wawili kati ya wale makomandoo wanne waliokuwa wamewawekea ukuta wale majeruhi na matabibu wao. Wale makomandoo wawili waliobaki kule kwenye helikopta walikuwa makini kuwatazama wale matabibu wakati wakiikimbilia ile helikopta wakiwa na majeruhi wao,nao wakiwa tayari kwa lolote ambalo lingeweza kutishia usalama.
Matabibu wengine wawili waliokuwa wakisubiri ndani ya ile helikopta kubwa walimpokea Stealth kutoka kwa wenzao huku mmoja wa wale waliombeba na kumfikisha pale akiwapa maelezo ya awali juu ya hali ya majeruhi wao.
“Amepoteza fahamu! Ana jeraha la risasi upande wa kulia wa shingo na ametokwa na damu nyingi!”
“Roger!” Mmoja wa wale matabibu waliobaki ndani ya ile helikopta iliyokuwa na zana zote za kitabibu na huduma ya kwanza zihitajikazo katika medani ya vita, alimjibu kwa kutumia lugha yao ya kijeshi kumaanisha kuwa alikuwa amemuelewa, uhalisi hasa wa neno lile ukiwa ni “Read You ”, yaani “Nimekusoma”, kwa maana ileile kuwa alikuwa amemuelewa.
Haraka sana wale matabibu wasaidizi wawili walirudi mbio kule kwa akina
Honey-Bee, ambako walimkuta tabibu mkuu akiwa anampatia huduma ya kwanza Swordfish kwa kumuosha jicho lake kwa dawa maalum, na alikuwa akifanya mambo hayo huku akiripoti hali ya majeruhi waliyoikuta pale kule
MDUNGUAJI
kambini kwao kwa kutumia kifaa maalum cha mawasiliano alichokuwa
amekivaa kichwani mwake, kikiwa na visikilizio vilivyobana masikioni mwake na kisemeo kilichochomoza mbele ya mdomo wake.
“…ni watatu tu ndiyo waliobaki…wote wamejeruhiwa vibaya, na tutahitaji kufanya operesheni mara moja pindi tukifika hivyo fanyeni maandalizi ipaswavyo!” Aliongea kwa ufasaha kwenye kifaa kile huku mikono yake ikifanya kazi haraka na kwa ufanisi mkubwa, sasa akimfunga bandeji ya dharura Swordfish kwenye lile jicho lake lililojeruhiwa vibaya.
Kule kwa wale waasi,zile helikopta mbili za mwanzo zilizokuwa na jukumu la kutawanya adui, au “sweepers”, ziliendelea kuwasambaratisha wale waasi, ambao sasa walikuwa wakikimbia ovyo, kila mmoja na njia yake mle msituni, wengine wakijaribu kuzitupia risasi zile helikopta bila ya kuziletea athari yoyote, ilhali wao wakizidi kuangamia.
Na sasa, kiasi cha kama mita mia mbili hivi kutoka lile eneo la maafa, rubani na wapiganaji wanne waliokuwa wakiwamiminia risasi wale waasi kutokea kwenye helikopta ya kwanza kati ya zile mbili, walishuhudia kundi jingine kubwa la waasi likielekea kule yalipokuwa yakiendelea yale mashambulizi kwa tahadhari kubwa.
“Wako wengi…wengine wanakuja na wana silaha kubwa zaidi!” Rubani wa ile helikopta alimpasha habari mwenzake aliyekuwa kwenye ile helikopta nyingine. Waasi wa lile kundi jingine, ambalo lilikuwa kubwa kuliko lile lililokuwa likiwaandama akina Swordfish walikuwa na makombora ambayo yangeweza kuziangusha zile helikopta kama jinsi tetere anavyoweza kudunguliwa kwa manati ya muwindaji kutoka juu ya mti.
“Nawaona! Twende tukawaangamize kabla hawajatufikia…!” Rubani wa helikopta ya pili alimjibu mwenzake.
“Nakanusha! Hii ni kampeni ya uokozi na si vinginevyo! Tumeshawatawanya adui sasa tunarudi kambini na wenzetu tuliokuja kuwaokoa!” Rubani wa helikopta ya kwanza alimjibu mwenzake, muda wote wakiwasiliana kwa vifaa maalum vya mawasiliano walivyovivaa kwenye kofia zao.
Muda wote huo wapiganaji wenye shabaha waliokuwa wamewabeba
kwenye helikopta zao walikuwa wakiendelea kuwaangamiza wale waasi waliokuwa kwenye lile kundi la kwanza mmoja mmoja kwa kadiri walivyoweza
kuwaona, kwani sasa walikuwa wametawanyika msituni, wengi kati yao wakiwa wamejificha chini ya miti iliyotapakaa eneo lile.
“Kwa hiyo turudi kambini hivi hivi tu?” Rubani wa helikopta ya pili, mpiganaji kutoka Sierra Leone, aliuliza huku akiilaza helikopta yake kulia na
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
kulitazama lile kundi jipya la waasi.
“Nawasiliana na helikopta ya matabibu kujua hali kwao ikoje.Kama ni shwari tunageuza, na tutatoa taarifa kambini wakati tukiwa hewani kurejea huko!”Rubani wa helikopta ya kwanza, mpiganaji kutoka Ghana alijibu.
Huku kwa akina Honey-Bee, wale matabibu wasaidizi walisogeza karibu machela nyingine iliyokuwa pale chini na kwa kufuata maelekezo kutoka kwa kiongozi wao walimpakia Swordfish na kukimbia naye kule kwenye ile helikopta, wakimuacha kiongozi wao akiugeukia mguu uliojeruhiwa wa Honey-Bee.
Aliichana suruali ya yule mwanamama jasiri katika ule mguu uliopigwa risasi kwa mkasi maalum wa kitabibu na kulitazama lile jeraha lililokuwa likivuja damu.Risasi mbili zilijikita nyuma ya paja jeupe lililojaa vizuri la yule mwanamama wa ki-Senegali, na zote mbili bado zilikuwa ndani ya mwili ule.
Haraka sana alitoa sindano kutoka kwenye mkoba aliokuja nao, akaweka kiasi cha dawa ya maji maji ndani ya bomba la sindano ile na kumchoma kando ya jeraha, sehemu ambapo risasi ililiingia paja lake na Honey-Bee aliguna kwa maumivu...
Rubani wa helikopta ya kwanza aliwasiliana na ile helikopta ya matabibu, na kupewa taarifa kuwa tayari walikuwa wameshaokoa wapiganaji wawili na sasa alikuwa akisubiriwa mpiganaji wa mwisho kati ya wale waliokuja kuwaokoa na wao watakuwa hewani kurudi kambini.
Hapo rubani wa helikopta ya kwanza alipitisha maamuzi, akiwa ndiye kiongozi wa zoezi lile la uokozi.
“Okay…! Nyie rudini moja kwa moja kambini. Kuna kundi kubwa la waasi linakuja eneo hili.Sisi tutafanya uchunguzi wa mwisho na tutawawahi wakati mkiwa hewani kurudi kambini, tumeelewana?”
“
Roger!”
Hapo tena aliwasiliana na rubani wa helikopta ya pili.“Rescue Mission II! Rescue Mission II…!” Alimwita yule rubani wa helikopta ya pili, ambayo katika mpago ule wa uokozi ilitambuliwa kama “Rescue Mission II”, wakati ile ya kwake ilikuwa ni “Rescue Mission I”, na ile ya matabibu ikiwa ni “Rescue Mission III”.
“Roger Rescue Mission I! Nakusikiliza!”
“Tutafanya mzunguko mmoja wa kutafiti eneo wanalotokea waasi, kisha
MDUNGUAJI
tutaungana na wenzetu kurudi kambini, umenipata?”
“Yiiiiih-Haaaah! Nimekupata loud and clear Rescue Mission I! Loud and Clear!” Rubani wa helikopta ya pili alipiga kelele kwa furaha na kuongeza kasi ya helikopta yake kuelekea kule lilipokuwa likitokea lile kundi jipya la waasi.
Zile helikopta mbili zilielekea kule walipokuwa wakitokea wale waasi, na walipokuwa wamefika usawa wa kuweza kushambulia tu walitupiwa kombora na wale waasi huku wengine wakizitupia risasi za rashasha.
Kombora lilikuwa linaiendea ile helikopta ya pili na rubani machachari wa ile helikopta aliiyumbisha kushoto helikopta yake huku tusi zito la kikwao likimtoka na kombora likamkosa. Hapo wale wapiganaji waliokuwa ndani ya ile helikopta walianza kuwamiminia risasi wale waasi ambao walianza kukimbia ovyo huku wakipukutika kama kuku mdondo.
Kama hiyo haitoshi, rubani wa Rescue Mission II aliilaza helikopta kushoto zaidi huku akiipeleka juu, na kuigeuza kulia huku akiiteremsha akiwa ameelekeza pua ya lile dege kubwa chini akiwaelekezea wale waasi mitutu miwili minene yenye tundu sita za kutolea risasi, mmoja kila upande wa helikopta ile. Akaweka vidole gumba vya mikono yake yote miwili kwenye vifyatulio maalum vya risasi vilivyokuwa kila upande wa usukani na kuvididimiza kwenye vifyatulio vile.Ile mitutu ilianza kuzunguka kama feni huku tundu zote sita kutoka katika kila mtutu zikitema risasi bila kituo.
Si kizaazaa hicho! Mvua ya risasi iliwanyeshea wale waasi kutoka angani, na hawakuwa na mwamvuli wowote wa kuwakinga na mvua ile ya kifo. Walikuwa wamefikwa…
Huku kwa akina Honey-Bee, yule tabibu mkuu alikitupa kile kibomba cha sindano na sindano yake, kisha akatoa sindano na bomba jingine, akanyonyea tena kiwango kile kile cha ile dawa ya maji maji ndani ya bomba lile, kabla ya kumdunga tena sindano yule dada kando ya sehemu ambapo risasi ya pili ililiingia paja lake, na Honey-Bee aliguna tena kwa maumivu akiwa amelalia tumbo pale chini.
Dakika mbili baadaye, naye alikuwa amebebwa kwenye machela akikimbizwa kwenye ile helikopta ya matabibu, akihisi macho yakimuwia mazito, usingizi mzito ukimuelemea. Wale makomando wanne waliokuwa wamewawekea ukuta wenzao walikuwa wakikimbia kimgongo-mgongo nyuma yao, bunduki zao zikiwa makini mikononi mwao. Honey-Bee aliingizwa haraka haraka ndani
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI ya ile helikopta, wale makomando wanne wakipanda baada ya wale matabibu, wakati wale makomandoo wawili waliobaki nyuma na ile helikopta hapo awali wakipanda mwisho.
Helikopta iliiacha ardhi taratibu na kuelea hewani.Iliyumba kulia kwa
muda, kisha ikalala kushoto na kuzidi kupanda hewani, kabla ya kugeukia kule
ilipotokea na kuchukua usawa wa kuelekea kambini kwao.
Wapiganaji watatu waliobaki wa kile kikosi maalum cha umoja wa mataifa
walikuwa wameokolewa, na sasa walikuwa hewani kurejeshwa kambini kwao
huku wakiendelea kuhudumiwa na wale matabibu.
Na ndipo kwa mara ya kwanza wale makomandoo walipokiona kile kifaa cha mawasiliano alichokuwa akikitumia msaliti Alpha kuwasiliana na mdunguaji
dhalimu. Kifaa ambacho baadaye kilitumiwa kwa taabu kubwa na mpiganaji
Stealth kufanya mawasiliano ya upande mmoja na kambi yao. Mawasiliano ambayo hatimaye yaliwezesha kutimia kwa zoezi lile muhimu la uokozi.
Wakati “Rescue Mission II” ikiwateketeza wale waasi, rubani wa “Rescue
Mission I” ilipitiliza mbele zaidi kiasi cha mita hamsini hivi kutoka pale walipokuwa wale waasi, na akiwa kule juu aliweza kuiona kambi kubwa sana ya waasi ikiwa nyuma ya milima miwili mikubwa.
Kutokea kule hewani, yeye na wapiganaji wengine wanne aliokuwa nao ndani ya ile helikopta, waliona mabanda marefu yakiwa yamejengwa kwa unadhifu yakiwa yamezungukwa na majabali makubwa. Upande mmoja kulikuwa na mto mkubwa uliozingirwa na miti mirefu. Alipotazama kwa makini, aligundua kuwa ile kambi ilikuwa chini kabisa ya korongo refu.
Bila ya rubani wa ile helikopta kujua, ile kambi ilikuwa umbali wa mita zipatazo mia tatu tu kulia kwa lile jabali ambalo muda si mrefu uliopita, mpiganaji Vampire alimkuta msaliti Alpha akituma mawasiliano kwa mdunguaji.
Akiwa kule hewani, aliweza kuona harakati kubwa za kijeshi zikiendelea kwenye uwanja wa ile kambi, na hapohapo alianza kutupiwa makombora ya mfululizo.Aliipandisha juu zaidi helikopta yake na kugeuza kurudi kule alipotokea.
“Rescue Mission II! Rescue Mission II! Nimeigundua kambi ya waasi na n’nashambuliwa kwa makombora! Turudi kambini mara moja! Wapiganaji wenzetu walikuwa wamebakisha mwendo mfupi sana kabla ya kuifikia! Turudi
MDUNGUAJI kambini!” Alimtaarifu mwenzake.
“Yuuu-Hhuuu! Safi sana Rescue Mission I! Kampeni imefanikiwa hatimaye! Wenzetu wameuawa, lakini walikuwa wamekaribia kutimiza lengo!” Rubani wa ile helikopta ya pili alimjibu huku akizidi kuwateketeza waasi. Aliirusha juu zaidi helikopta yake, akaipundua na kuchukua uelekeo wa kambini, akijumuika na yule mwenzake muda mfupi baadaye.
Zile Helikopta mbili za jeshi la Umoja wa Mataifa ziliruka hewani zikiwa zimeiweka katikati yao ile helikopta ya tatu iliyokuwa imewabeba wale wapiganaji watatu waliobaki katika kile kikosi maalum cha watu kumi kilichotumwa kupeleleza eneo ilipokuwa ile kambi ya waasi. Rubani wa “Rescue Mission I” alipeleka taarifa kambini kwao, akitoa maelekezo juu ya sehemu ilipokuwa ile kambi kubwa ya waasi waliyokuwa wakiisaka kwa muda mrefu.
“Rescue Mission I natoa taarifa Kambini! Rescue Mission I natoa taarifa Kambini! Mpango umekamilika! Tumewaokoa wapiganaji wetu watatu waliobakia na sasa tuko hewani kurudi kambini, umenipata kambi?”
“Kambi inapokea taarifa! Kazi nzuri kamanda!”
“Tumegundua sehemu ilipo kambi ya waasi, narudia, tumegundua sehemu ilipo kambi ya waasi!”
“Roger Rescue MissionI! Tupe mustakabali na tathmini tafadhali!”
“Kambi iko katika usawa wa nyuzi Sifuri-Sita-Tano, Kusini-KusiniMashariki ya eneo la mawasiliano ya mwanzo na wapiganaji wenzetu!”
“Roger Rescue Mission I, Roger!”
“Adui wako wengi na wana makombora makubwa! Nashauri mashambulizi ya anga yafanywe mara moja, kwani nahisi baada ya kuona tumeigundua kambi yao, waasi watavunja kambi na kuzidi kupotelea misituni!”
“Roger that Rescue Mission I! Kazi Nzuri! Kuna tathmini zaidi?”
“Mwisho wa kuripoti Kamanda!”
“Roger and out!”
Muda huohuo, kilometa kadhaa kutoka pale zilipokuwa zile helikopta, harakati za mashambulizi ya anga zilianza kutokea kule kwenye kambi ya wale wapiganaji wa jeshi la Umoja wa Mataifa.Ndege nne maalum za mashambulizi ya anga ziliruka kuelekea usawa wa ile kambi ya waasi.
Muda wa waasi kuendelea kuisumbua serikali halali ya Ahmed Tejjan
Kabbah na lile jeshi la Umoja wa Mataifa kwa kutumainia maficho yao yasiyojulikana katika misitu minene ya nchi ile ya Afrika ya magharibi sasa ulikuwa umefikia mwisho.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Marubani wa ndege zile walikuwa wanaliendea kwa kasi sana eneo la kambi ya waasi wakiwa na maelekezo ya kuangamiza kabisa kila watakachokikuta huko.
Zile ndege zilianza kuporomosha mabomu kule kwenye ile kambi ya waasi, na waasi waliokuwa wakijiandaa kuvunja kambi ile na kuingia msituni zaidi, walianza kukimbia ovyo.Mabomu yaliisambaratisha kambi ile huku waasi wakiuawa kwa mafungu wakati baadhi yao wakijitahidi kuzitupia makombora zile ndege. Lakini hivi sasa ilikuwa ni waasi ndiyo walikuwa wakipigana vita inayoshindwa.
Ndege nne za jeshi la Umoja wa Mataifa zilikuwa zikiwaangushia mabomu mfululizo, tena kutokea kila upande. Kwa mara nyingine tena, msitu ule ulirindima kwa milipuko ya mabomu, mayowe ya kihoro na woga kutoka kwa waasi, na milio ya bunduki na makombora yaliyokuwa yakitupwa angani kujaribu bila mafanikio kuziangusha ndege za jeshi la umoja wa mataifa.
Vita vilikuwa vimedumu kwa muda mrefu na vimeigharimu serikali ya Sierra Leone na Umoja wa Mataifa fedha na roho nyingi za wapiganaji wazuri; na hivyo kuongeza idadi ya wajane na watoto wanaolazimika kuishi na mzazi mmoja au bila ya mzazi hata mmoja barani Afrika.Na kuzidisha umasikini na kurudisha maendeleo nyuma.Sasa ulikuwa umefika muda wa vita vile kuisha kabisa.
Mabomu yaliendelea kuporomoshwa kama mvua...
Nusu saa baada ya zile ndege kutekeleza jukumu lao katika kambi ile, ndege nyingine ikiwa na askari wa miavuli iliruka kuelekea kule ilipokuwa ile kambi ya waasi. Askari wa miamvuli walishuka katika eneo la waasi kwa lengo la kumalizia waasi wote watakaokuwa wamenusurika katika shambulizi la anga na kuwakamata mateka wengi kadiri watakavyoweza.
Vilevile, wale askari wa miavuli walikuwa na kazi ya kuichukua miili ya wale wapiganaji wenzao waliouawa na kuirudisha kambini ili wapatiwe mazishi yanayostahili, kila mmoja nchini kwake.
Swordfish alisikia mvumo wa feni yake kwa mbali sana, na akajua kuwa alikuwa ameshafika nyumbani kwake, eneo la Jang’ombe, mjini magharibi, kisiwani Zanzibar. Alijaribu kufumbua macho lakini bado usingizi ulikuwa umemuelemea. Macho hayakutaka kufumbuka. Na feni ilizidi kuvuma tu.
Ah! Kila siku huwa nasema nitakuja kuitengeneza hii feni na halafu nafanya
MDUNGUAJI
ajizi! Safari hii nikiamka tu, naipeleka kwa fundi! Feni inapiga kelele kama... kama...
Helikopta!
Alifumbua macho ghafla na kugundua kuwa ni jicho moja tu ndilo lililofumbuka. Aligeuza kichwa kwa taabu na kutazama eneo alilokuwapo, na kugundua kuwa hakuwa nyumbani kwake Jang’ombe bali alikuwa akielea angani. Ndipo alipogundua kuwa mvumo aliokuwa akiusikia haukuwa wa ile feni yake ambayo mkewe huwa akimpigia kelele kila siku aitengeneze, bali ulikuwa ni mvumo wa mapangaboi ya ile helikopta aliyokuwa ndani yake wakati ule.
Na hapo kumbukumbu ya matukio yote aliyopambana nayo kule msituni akiwa na wale wenzake ikamjia na akajikuta akiachia mguno wa fadhaa.
Alijaribu kuinua mkono wake kujishika jicho lake kuona kama bado lipo, lakini mkono ulikuwa mzito sana.
Alisikia watu wakiongea kwa sauti za chini na kugeuza uso wake kule zilipotokea, na kuwaona wale matabibu watatu wakiwa wamemuinamia Stealth, ambaye alikuwa amelazwa kwenye machela maalum kama aliyolalia yeye, bila shaka akiwa hana fahamu. Wale matabibu walikuwa wakishughulika kwenye mwili wa Stealth huku wakiongea haraka haraka, na Swordfish hakuhitaji kuambiwa kuwa hali ya Stealth ilikuwa mbaya sana na wale matabibu walikuwa wanafanya kazi ya ziada kuokoa maisha yake.
Aligeuka upande wa pili na kumuona Honey-Bee naye akiwa amelala kwenye machela. Alimtazama yule mwanamama jasiri na shujaa kabisa aliyepata kukutana naye maishani mwake. Mguu wa kulia wa suruali yake ya kijeshi ulikuwa umekatwa na kubaki kama kaputura, sehemu iliyokuwa imejeruhiwa ikiwa imefungwa bandeji. Kwa jinsi alivyokuwa amelala, sura yake ilionekana kuwa na amani sana, na urembo wake kama mwanamke ulijidhihirisha.
Mrembo mwenye shabaha.
Kichwa kilianza kumuwia chepesi huku mvumo wa ile helikopta ukizidi kuyasumbua masikio yake.Alitazama nje ya ile helikopta na aliona helikopta
nyingine ikiruka sambamba na ile waliyokuwamo. Hapo akaelewa kwa nini ule mvumo wa helikopta ulikuwa kubwa sana, kwani haukuwa mvumo wa helikopta moja. Akageuka upande mwingine na akaona, japo kwa taabu
kutokana na kutumia jicho moja tu, kuwa huko pia kulikuwa kuna helikopta
nyingine iliyokuwa ikiruka sambamba na ile ya kwao.
Tumeokolewa kutoka mikononi mwa kundi la waasi waliopagawa...katika dakika za mwisho kabisa! Tulijitahidi sana...lakini tulikuwa tumeshaelemewa...
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Alimkumbuka mdunguaji...na jinsi alivyowataabisha na kuwajaza hofu na kutoaminiana miongoni mwao. Na jinsi alivyoweza kuwadungua na kuwaangamiza wenzao mmoja baada ya mwingine, naye akimuachia jeraha la risasi begani kwake.
Sijui ile risasi bado iko mwilini mwangu...?.
Mdunguaji...Khabbiith-L- A’mal!
Kwanza jina la uficho Cheetah kutoka Sierra Leone.
Halafu jina la uficho Glimmer kutoka Naijeria.
Akaja Eagle kutoka Sierra Leone...halafu Black Angel naye kutoka Sierra Leone, ambaye kwa ghadhabu alijianika mbele ya mdunguaji dhalimu, akaishia kudunguliwa kama wengine...
Na sasa naambiwa kuwa Black Mamba amepotea katika harakati...Missing in Action, lakini inawezekana kabisa kuwa naye amedunguliwa huko porini na huyo huyo mdunguaji. Aliwafikiria watanzania wenzake, Vampire na Alpha. Nao wameuawa kwa risasi haramu za mdunguaji...Shaitwaani-L-Rajiim!
Oh, Mungu wangu...! Tumekuja watatu kutoka nyumbani, japo kila mmoja kwa wakati wake...sasa n’tarudi peke yangu...
Wiki mbili baadaye, viongozi watatu wa ngazi za juu na wajumbe wa kudumu katika jeshi la Umoja wa Mataifa lililokuwa na jukumu la kulinda amani nchini Sierra Leone walikuwa wameketi nyuma ya meza kubwa na safi, ndani ya chumba kimoja kipana katika kambi ya jeshi lile nchini Sierra Leone, wakiwatazama wapiganaji wengine waliokuwa nao mle ndani. Hewa ya ndani ya chumba kile ilikuwa
ikipozwa kwa kiyoyozi mwanana.Hawa walikuwa ni wapiganaji waliobobea na wasio na masikhara hata kidogo. Wamekuwako nchini Sierra Leone tangu kuanza kwa kampeni ile. Hawa jamaa watatu waliweza kumfanya mtu yeyote atiririkwe na jasho mfululizo pamoja na kile kiyoyozi kilichokuwa mle ndani.
Wao ndiyo waliobeba dhamana ya wapiganaji wote waliokuwa katika Operesheni ile, na jukumu la harakati zote za jeshi lile la Umoja wa Mataifa nchini Sierra Leone lilikuwa mikononi mwao. Hivyo hawakusita hata kidogo katika kufanya lolote lililohitajika ili kuhakikisha kuwa jukumu lililokuwa mbele yao linatekelezwa bila ya kosa wala upungufu wowote.
Walikuwa ni watu wa kazi.
Hawa walikuwa ni Meja Jenerali Bartazar Swandoh kutoka Sierra Leone, Meja Jenerali Basil Kufoh kutoka Ghana na Meja Jenerali Fabiola Oluoch kutoka Kenya, mwanamama wa kwanza katika jeshi la nchi ile kufikia wadhifa ule wa kijeshi.
Pamoja nao ndani ya chumba kile, kulikuwa kuna wapiganaji wengine sita wa ngazi za juu katika majeshi ya nchi zao, ambao walikuwa ni wawakilishi kutoka majeshi ya nchi tatu za kiafrika zilizotuma wapiganaji katika jeshi lile la Umoja wa Mataifa nchini Sierra Leone.
Katika hawa sita, kulikuwa kuna Brigedia Mohammed Awolowo na Meja
Emeka Askia kutoka Naijeria. Aidha walikuwapo Brigedia Stanslaus Kahemela na Luteni Kanali Athanas Marwa Chacha, kutoka Tanzania; na Kanali Olga Tbage, mwanamke mweusi, mrefu na mnene, kutoka Senegali, aliyeambatana
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI na Luteni Kanali Mete Djiatete.
Wote hawa walikuwa wameingia Sierra Leone siku tatu nyuma kwa lengo la kuungana na wale viongozi wengine watatu wa ngazi za juu katika jeshi lile ili kuunda jopo la kijeshi la watu tisa. Jukumu la jopo lile lililokuwa ni kupitia ripoti ya matukio yaliyokikuta kile kikosi maaluumu kilichotumwa kupeleleza sehemu ilipokuwa kambi kubwa ya waasi katika msitu wa Tumbudu, mashariki mwa nchi ile.
Kikosi ambacho wapiganaji wake sita kati ya kumi waliokuwa wakikiunda, waliangamizwa kwa mashambulizi ya kuvizia yaliyoaminika kuwa yalifanywa na mdunguaji aliyejificha katika msitu waliokuwamo, wakati mmoja kati ya wapiganaji hao akisadikika kuwa amepotea katika harakati za kijeshi kule msituni.
Ukuta mmoja wa chumba kile, uliokuwa kulia kwa meza ile kubwa, ulikuwa una dirisha pana la kioo kizito chenye kiza au “Tinted”, na nyuma kioo kile kulikuwa kuna chumba kingine kidogo ambamo ndani yake alikuwa ameketi mpiganaji mwingine wa jeshi lile la Umoja wa Mataifa mwenye cheo cha Kepteni. Mbele yake kulikuwa kuna mitambo ya redio kama jinsi inavyokuwa katika studio za vituo vya redio. Kazi yake ilikuwa ni kurekodi kila kilichokuwa
kikiongelewa katika kile chumba ambamo lile jopo la kijeshi lilikuwa limeketi. Mbele ya kila mmoja wa viongozi wale wa kijeshi kulikuwa kuna faili jembamba lililokuwa na ripoti ya kampeni ile ya kuisaka kambi ya waasi, na matukio yote yaliyotokea kule msituni kama jinsi yalivyoelezewa kimaandishi na kiongozi wa kampeni ile, Stealth.
Kiasi cha hatua zipatazo kumi kutoka pale ilipokuwa ile meza kubwa ambayo nyuma yake ndiyo walikuwa wameketi wale viongozi tisa wenye nyadhifa za juu kijeshi kulikuwa kuna kiti kimoja cha mbao.
Kile kiti kilikuwa kimeielekea ile meza na kwenye ile sehemu ambayo mtu alitakiwa akalie, kulikuwa kuna faili jingine jembamba kama yale yaliyokuwa mbele wale wajumbe wa jopo lile la kijeshi. Meja Jenerali Basil Kufoh, kiongozi wa jopo aliwageukia wenzake.“Naamini sote tumeisoma hii ripoti...”
Vichwa vilitikiswa ndani ya chumba kile kuafikiana naye.
“Sasa tumekutana hapa ili kuanza hatua ya pili ya kuitathmini hii ripoti na hatimaye tutoe ripoti ya pamoja na kuweka hitimisho juu ya swala hili, naamini tuko tayari.” Meja Jenerali Basil Kufoh aliendelea. Kwa mara ya pili vichwa vilitikiswa kuafikiana na kauli yake.
“Vizuri. Tutaanza na kiongozi wa kampeni.” Alisema huku akibonyeza kitufe maalum kilichokuwa kulia kwake, chini ya uso wa meza ile.
MDUNGUAJI
Kanali Essaiyyah Okoronkwo p.a.k. “Stealth”, akiwa katika sare nadhifu za kijeshi aliongozwa ndani ya chumba kile na polisi wa kijeshi (Millitary Police) wa kike. Upande wa kulia wa shingo yake, alikuwa amebandikwa plasta kubwa nyeupe ambayo ilichomoza juu ya ukosi wa shati lake la kijeshi, ambalo katika mazingira ya kawaida angetakiwa awe amelifunga hadi kifungo cha mwisho kabisa shingoni kwake na kufunga tai maalum ya kijeshi iliyoambatana na sare ile. Lakini jeraha lililokuwa shingoni kwake halikumruhusu kufanya hivyo.
Alisimama hatua mbili ndani ya chumba kile wakati yule polisi wa kijeshi akitoka na kuufunga ule mlango taratibu nyuma yake, akimuacha peke yake mbele ya lile jopo. Aliwatazama wale wakuu wa kijeshi waliokuwa mbele yake kisha akatembea kikakamavu hadi kando ya kile kiti kilichokuwa mbele ya ile meza kubwa,kiatu chake kilichong’ara kwa rangi sawia kikipiga sakafu kwa kishindo kikali. Alisaluti kikakamavu na kubaki akiwa amekakamaa kama ubao mbele ya wale wakuu wake.
“Chukua hilo faili na ukae kwenye kiti Kanali!” Meja Jenerali Basil Kufoh alimwambia bila yeye wala wale wenzake kujishughulisha kuijibu ile salamu ya kijeshi.
Kanali Essaiyyah Okoronkwo alishusha saluti yake kikamavu, akachukua lile faili kutoka juu ya kile kiti na kuketi huku akiliweka lile faili mapajani kwake.Alishusha pumzi ndefu na kuwatazama wale wakuu wake, na mara moja akawatambua Brigedia Mohammed Awolowo na Meja Emeka Askia, kutoka nchini kwake. Pia aliwatambua wale viongozi watatu wa jeshi lile la Umoja wa Mataifa pale Sierra Leone, ila akashindwa kuwatambua wale wawakilishi wanne kutoka Tanzania na Senegali.
Akatulia.
Meja Jenerali Basil Kufoh aliwatambulisha wale wakuu wenzake na kumueleza kwa kifupi sababu ya kuitwa kwake mbele ya jopo lile.
“Kanali Okoronkwo, hiyo uliyoshika ni ripoti uliyoandika juu ya matukio yaliyokikuta kikosi chako cha wapiganaji kumi mlipokuwa katika kampeni ya uchunguzi mashariki mwa nchi hii, sawa?” Meja Jenerali Basil Kufoh alimuuliza. Kanali Okoronkwo alifunua baadhi ya kurasa za ripoti ile kwa muda, kisha akainua uso wake na kumjibu.
“Ndiyo Afande!”
Meja Jenerali Basil Kufoh alitikisa kichwa kuridhishwa na jibu lile, kabla ya kuongea tena, “Sasa wajumbe wa jopo hili tulio mbele yako, tutakuwa na maswali machache kuhusiana na ripoti hiyo, Okay?”
“Yes Sir!”
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Kanali Okworonkwo, katika ukurasa wa sita wa ripoti yako, aya ya nne hadi ya saba, unaeleza kuwa kuna sababu za kuamini kwamba mpiganaji Alpha alikuwa akiwasaliti kwa kutoa habari za nyendo za kikosi chenu kwa mdunguaji aliyekuwa akiwavizia na ambaye pia amefanikiwa kuwaua wapiganaji wetu sita...” Meja Jenerali Fabiola Oluoch alimuuliza, wakati wale wawakilishi kutoka Tanzania, Brigedia Stanslaus Kahemela na Lut. Kan. Athanas Chacha wakiwa makini sana kusikiliza maelezo ya kipengele hiki, ambacho kwa kweli kilikuwa kigumu sana kwao kukubaliana nacho.
“Ndiyo afande, hivyo ndivyo!” Brigedia Okoronkwo alijibu.
“Unaweza kulifafanulia jopo hili juu ya kipengele hicho?”
“Ndiyo Afande, ninaweza kufafanua kwa kadiri nijuavyo...” Kanali Essaiyyah Okoronkwo alijibu huku akiwa ameketi kwa nidhamu ya hali ya juu, kisha akalielezea lile jopo mazingira yote waliyokumbana nayo kule msituni, tangu jinsi mdunguaji alivyokuwa akiwadungua kila walipokuwa wakipitia, hadi jinsi mpiganaji Vampire alipoanza kutoa hisia zake kuwa kuna msaliti miongoni mwao. Alieleza jinsi mpiganaji Alpha alivyokuwa mstari wa mbele kupingana na ile hoja ya Vampire bila ya kutoa hoja mbadala. Akahitimisha kwa maelezo ya kile kifaa cha mawasiliano alichokikuta mkononi mwa mpiganaji Alpha, mwenyewe akiwa amekufa, kifaa ambacho sio tu kilikuwa tofauti kabisa na vile vilivyokuwa vikitumiwa na jeshi la Umoja wa Mataifa, bali pia hakikutakiwa kabisa kuwa mikononi mwake.
Wajumbe wa jopo hawakuwa na maswali zaidi kwake juu ya kipengele kile, na ingawa Lut. Kan. Athanas Chacha alitamani kummbana kwa maswali zaidi, hakufanya hivyo kwani alikwisha thibitishiwa kuwa alama za vidole zilizokutwa kwenye kile kifaa cha mawasiliano alichokuwa akikiongelea Stealth zilikuwa ni za mpiganaji Alpha, au Kanali Nathan Mwombeki, kutoka Tanzania.
“Kanali Okoronkwo, ukurasa wa tisa wa ripoti yako unaeleza kuwa ukiwa na mpiganaji Honey-Bee mlisikia mlipuko wa bastola, na mlipokimbilia eneo ambapo mlipuko ulitokea mlikuta miili ya wapiganaji wenzenu Alpha na Vampire wakiwa wamekufa, hali Vampire akiwa amelipuliwa kichwa chote, na kubaki kiwiliwili tu,ndivyo?” Meja Jenerali Bartazar Swandoh alimuuliza na Stealth aliafiki.
“Sasa unawezaje kujua kwa hakika kuwa ule mwili ulikuwa ni wa mpiganaji Vampire na si wa mtu mwingine?”
“Vitu viwili Afande ndivyo vilivyonijulisha kuwa yule alikuwa Vampire... cha kwanza, ambacho ndio kikubwa zaidi, ni ile redio ya mawasiliano aliyobeba mgongoni. Cha pili ni kuwa naye, kama mpiganaji mwenzetu tunayeamini
MDUNGUAJI
kuwa amepotea katika harakati, alikuwa amevua gwanda lake la kijeshi na kubaki na fulana yake ya ndani tu. Magwanda yote mawili ya wapiganaji hawa tuliyaokota mle msituni yakiwa na vithibitisho vyao vyote kama namba zao za kijeshi na majina yao ya uficho.” Stealth alijibu kwa kirefu.
“Kwani haiwezekani ikawa ule ni mwili wa mpiganaji Black Mamba, na sio wa mpiganaji Vampire?” Brigedia Stanslaus Kahemela kutoka Tanzania alidakia.
“Black Mamba hakuwa akibeba redio ya mawasiliano mgongoni afande.”
Stealth alijibu kwa kujiamini, na kimya kikatawala kwa muda mle ndani. Wale wajumbe wa jopo waliandika vitu kwenye karatasi walizokuwa nazo pale mezani kisha Kanali Olga Tbage aliinua uso wake na kumtazama yule mpiganaji jasiri
kutoka Naijeria.
“Nadhani unaelewa Kanali kuwa kwa sasa hatuna namna yoyote ya kuweza kuutambua vinginevyo ule mwili usiokuwa na kichwa isipokuwa kutokana na maelezo yako?” Alimuuliza yule Kanali mwenzake, na Kanali Okoronkwo aliafiki kwa kichwa kabla kuthibitisha kwa kauli.
“Naelewa Afande!” Akilini mwake akikumbuka tukio la siku tatu zilizopita
wakati alipotakiwa kwenda kuitambua miili ya wapiganaji wenzake waliouawa
kule msituni baada ya kufikishwa pale kambini.
Aliukumbuka ule mwili uliokuwa umeungua kiasi cha kutoweza kutambulika kwa namna yoyote ile. Kitu pekee alichoweza kukitambua katika
mwili ule ni ile hali ya kutokuwa na kichwa, na yale mabaki ya kifaa cha redio ya mawasiliano yaliyoungua kung’ang’aniana na ngozi iliyoungua ya mwili ule. Yule mtu alikuwa ameungua vibaya sana kiasi hata alama zake za vidole zilikuwa zimebabuka na kutoweza kabisa kutumika kama njia ya utambulisho. Stealth alikumbuka jinsi alivyoshituka baada ya kuoneshwa mwili ule, kwani vile sivyo alivyoukuta ukiwa hatua chache kutoka pale ulipokuwa mwili wa mpiganaji Alpha pale chini ya jabali kule msituni.
Alikumbuka jinsi alivyowageukia wale askari wa kijeshi waliomuonesha ule mwili pale mochwari, na jinsi alivyowabishia kabisa kuwa ule haukuwa mwili aliouacha kule msituni kabla ya kuanza kufurushwa na kundi la waasi. Na alikumbuka jibu alilopewa.Jibu ambalo kwa wakati ule lilimfanya ajihisi koo likimkauka na baridi ikimtambaa mwili mzima.
Akilini mwake, alirejewa na kumbukumbu ya majibizano baina yake na yule kiongozi wa wale askari wa miavuli waliotekeleza zoezi la kuirudisha kambini ile miili ya wale wenzao. Na kwa muda aliwasahau kabisa wale wakuu wake wa kazi...
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“No! Huyu siye Vampire bwana...hiki kitu gani mnaniambia nikitambue? Hii si..si....siye bwana! Mwili niliouacha pale chini ya jabali, na ambao niliutambua kuwa ni wa mpiganaji Vampire...haukuwa hivi bwana!”
“Inaweza kuwa usemayo ni kweli afande kuwa huu mwili haukuwa katika hali hii wakati ulipouacha pale kando ya jabali, lakini hivi ndivyo ulivyo sasa!”
“Kwa nini...? Ni nini kilichotokea...?”
“Eneo lote lililokuwa jirani na lile jabali mlilokuwa mmejificha nyuma yake, na ambapo miili ya wenzetu hawa ilikuwepo, lilishika moto mkubwa, na mpaka askari wetu wa miavuli waliposhuka eneo lile kuokoa miili yao, sehemu kubwa ya miili yao ilikuwa imeungua, lakini huu...huyu...ndiye aliyeungua vibaya zaidi, kwani ule moto ulikuwa umeanzia kule alipokuwako na kuelekea kule ilipokuwa ile miili mingine....”
“Ah! Siwaelewi! Moto? Moto umetokea wapi tena....?”
Yule mpiganaji mwenzao kutoka Ghana alimtazama moja kwa moja machoni kwa muda, kabla ya kumjibu.
“Afande, lile jabali lilikuwa umbali mdogo sana kutoka pale ilipokuwa kambi ya waasi mliyotumwa kuisaka. Ndege zetu za kivita zilipokuwa zikiiangushia makomora kambi ile, waasi nao walikuwa wakijibu mashambulizi kwa makombora ya kuangushia ndege, nayo ndiyo yaliyoangukia eneo lile na kusababisha moto mkubwa...”
Stealth alikumbuka jinsi alivyopigwa na butwaa.
Aliomba kuoneshwa mwili wa mpiganaji Alpha, na kweli kabisa, nao ulikuwa umeungua. Lakini hakupata ugumu wowote kumtambua kwani
Alpha alikuwa ameanza kuungua sehemu za miguu mpaka eneo la kiunoni kabla mwili wake haujaokolewa na wale askari wa kikosi cha miavuli.
“Kanali Okoronkwo!”
Alizinduka kutoka kwenye mawazo yale na kuwatazama wale wakuu wake.
“Jaribu kuzingatia lililokuleta hapa Afande, ebbo!” Brigedia Mohammed Awolowo alimkemea kwa ukali baada ya kuona kuwa amekuwa kimya ghafla huku akionekana wazi kuwa akili yake ilikuwa imehama kabisa kutoka eneo lile.
“Samahani! Samahani Afande...lakini sikuweza kuizuia akili yangu kurudi kwenye lile tukio la utambuzi wa miili ile...hasa wa...wa hayati Vampire!”
Alijitetea kwa nidhamu huku akionekana wazi kuwa alijikuta katika hali ile bila ya kupenda.
“Imeeleweka Afande” Kanali Olga Tbage alimwambia, kisha akaendelea, “na sasa nikirudi kwenye swali langu la hapo awali... unaelewa kuwa sisi hapa
MDUNGUAJI hatutakuwa na namna ya kuutambua vinginevyo ule mwili usio na kichwa isipokuwa kwa maelezo yako?”
Mwili usio na kichwa....sasa Vampire ndiyo amekuwa “mwili usio na kichwa”!
Stealth alikohoa kidogo kabla ya kuafiki.
“Naelewa afande”.
Kimya kilitawala mle ndani wakati wale wajumbe wa lile jopo la kijeshi wakimtazama kwa muda bila ya kusema neno, wakimpa muda aelewe uzito wa lile jibu lake. Baada ya muda ulioonekana kama milele kwa Kanali Okoronkwo, Lut. Kan. Athanas Chacha alikohoa kidogo.
“Kanali...” Aliita.
“Afande...!”Stealth alimuitikia na kuelekeza uso wake pale alipokuwapo.
“Unakumbuka kuona alama zozote za mwili... kovu, sunzua, au kitu kama hicho, mwilini mwa mpiganaji kutoka Tanzania aliyejulikana kwa jina la uficho Vampire?” Alimuuliza, na hili swali lilionekana kumshangaza kidogo Stealth. Lut. Kan. Athanas Chacha akafafanua haraka.
“Wakati wa uhai wake...”
“Oh...! Yeah...” Brigedia Okoronkwo alimjibu na kujiweka sawa huku akikunja uso wake kwa kuvuta kumbukumbu kisha akaendelea, “...alikuwa na alama ya mshono kwenye paji la uso....kutokea juu kidogo ya jicho lake la kushoto hadi karibu na zinapoanzia nywele zake. Halafu alikuwa na alama ya tojo...tatoo...ya nge upande wa kulia wa kifua chake...hizo ndizo alama pekee nilizopata kuziona mwilini mwake.”
“Huyo ndiye hasa mpiganaji Vampire,” Lut. Kan. Chacha alimwambia, kisha akaendelea, “...sasa je, uliona yoyote kati ya alama hizo kwenye ule mwili uliooneshwa na ambao hatimaye umekuja kuutambua kuwa ni wa mpiganaji Vampire?”
“Hapana afande, sikuziona.Wakati huo ule mwili haukuwa na kichwa tena, hivyo kovu la mshono lililokuwa usoni haikuwezekana kuliona...”
Kanali Okoronkwo alimjibu yule Mtanzania, kabla ya kuendelea, “...na mwili wake ulikuwa umebabuka vibaya sana kwa moto kiasi cha kubaki nyama tu iliyoshikamana na vipande vya chuma na plastiki kutoka kwenye ile redio ya mawasiliano iliyokuwa mgongoni kwake...ngozi yake yote ilikuwa imebabuka na kunyambuka vibaya kiasi cha kuipoteza kabisa sio tu ile alama ya tojo
iliyokuwa kifuani kwake, bali pia alama zake za vidole...” Ingawa Stealth alikuwa na cheo kikubwa kuliko yule mtanzania, kwa muda ule alikuwa chini ya wajumbe wote wa jopo lile.
Wajumbe wa jopo walibaki kimya kwa muda, wakiandika kwenye
makaratasi waliyokuwa nayo pale mezani.
“Kwa hiyo unalithibitishia jopo hili kuwa ule mwili ulioungua vibaya kwa moto uliotokana na makombora ya waasi,mwili usio na kichwa, ni mwili wa mpiganaji kutoka Tanzania aliyejulikana kwa jina la uficho Vampire?”Brigedia Stansalus Kahemela alimuuliza.
“Eeem...kutokana na picha nilizooneshwa za eneo ambalo mwili ule ulikutwa ukiwa umeungua, na ile redio ya mawasiliano iliyokuwa imegandamana na mwili ule, halikadhalika na mabaki ya fulana yake ya kijeshi iliyogandamana na mwili ule, nina kila sababu za kuamini na kulithibitishia jopo hili, japo kwa masikitiko makubwa, kuwa ule ni mwili wa mpiganaji Vampire!” Kanali Okoronkwo alijibu, na kwa mara nyingine chumba kiligubikwa na ukimya mzito, wale wakuu wa kijeshi wakiandika katika makaratasi waliyokuwa nayo pale mezani.
Wajumbe wote mle ndani walijua kuwa vipimo vya vinasaba (DNA)
vilivyotolewa kwenye mwili ule havikuwa na msaada wowote kwao katika
kumtambulisha mtu mwenye mwili ule kutokana na ukweli kwamba hakukukwa na kumbukumbu ya vipimo vya vinasaba vya mpiganaji
Vampire vilivyochukuliwa kabla ya kifo chake, ambavyo ndivyo vingetumika
kulinganishwa na vile vilivyotolewa kwenye ule mwili ulioungua na kuleta ufumbuzi katika swala lile.
Na sasa hakukuwa na namna isipokuwa kutegemea uthibitisho wa Kanali
Essaiyyah Okoronkwo p.a.k. Stealth, na mpiganaji mwingine aliyejulikana kwa jina la uficho Honey-Bee, ambao ndiwo pekee waliouona ule mwili ukiwa pale chini ya jabali kabla ya kuunguzwa vibaya kwa moto. Na wajumbe wote wa jopo lile la kijeshi walilijua hilo.
Sasa Meja Jenerali Bartazar Swandoh aliinua uso wake na kumtazama yule shujaa kabla ya kumtupia swali jingine muhimu sana kwa jopo lile.
“Kanali Okoronkwo, ukurasa wa mwisho wa ripoti yako, kwenye sehemu ya hitimisho, umeandika kuwa unaamini kwamba vifo vya wapiganaji kutoka Tanzania, Alpha na Vampire vinahusiana, kwamba unaamini kuwa Alpha aliuawa na Vampire, na Vampire ameuawa na mdunguaji aliyekuwa amejificha mle msituni na ambaye mpaka muda ulipokuwa ukiandika ripoti hii, siku mbili zilizopita, alikuwa hajapatikana.”
“Ndiyo Afande, ninaamini hivyo!”
“Fafanua tafadhali!” Brigedia Kahemela kutoka Tanzania alimwambia kwa jazba, wazi kuwa hakuyapenda kabisa mambo aliyokuwa akiyasikia juu ya wapiganaji kutoka nchini kwake. Wapiganaji waliouawa walikuwa ni kutoka
MDUNGUAJI
Tanzania, kama jinsi wale wengine kutoka Naijeria walivyouawa na kusababisha
Brigedia Mohammed Awolowo na Meja Emeka Askia kutoka Naijeria nao
kuwa sehemu ya jopo lile maalum.
“Afande, kanuni za makabiliano katika harakati za kijeshi kama ile
tuliyokuwa tukiiendesha kule msituni ziko wazi juu ya wasaliti....shoot on the spot!” Kanali Okoronkwo alijibu huku akimtazama yule Brigedia moja kwa
moja machoni, kisha akaendelea kwa jazba huku ghadhabu zikijionesha usoni
mwake, “Alpha alikuwa akitusaliti kwa mdunguaji kwa sababu ambazo bahati
mbaya sana ametangulia nazo kuzimu. Vampire ndiye alikuwa wa kwanza
kuhisi juu ya uwepo wa msaliti miongoni mwetu, hivyo, nahisi kuwa alimkuta
Alpha akituma mawasiliano kwa mdunguaji kwa kutumia kile kifaa chake kisicho rasmi, na akampiga risasi kama jinsi itakiwavyo!”
Wakuu wake wa kazi walimtazama kwa utulivu, Brigedia Kahemela akiwa makini sana.
“Bahati mbaya na yeye akalipuliwa na Mdunguaji, na kutokana na madhara ya risasi ya mdunguaji katika kichwa chake, inaonekana kuwa mdunguaji hakuwa mbali na eneo walilokuwepo.” Kanali Okoronkwo alimalizia. Kimya kilitanda kwa muda, kisha Meja Jenerali Basil Kufoh alimruhusu.
“Ahsante sana Kanali Okoronkwo,unaweza kwenda.”
Kanali Essaiyyah Okoronkwo, p.a.k. Stealth, aliinuka, akaweka lile faili juu ya kikalio cha kile kiti, na kusaluti kikakamavu. Kisha aligeuka na kutoka nje ya chumba kile kwa mwendo wa kijeshi.
Dakika kumi baadaye mlango wa kuingilia ndani ya chumba kile ulifunguliwa tena na Luteni Jeannette Tulaye-Bgayo, pia akijulikana kama (p.a.k.) Honey-Bee, aliingia mle ndani kwa mwendo wa kikakamavu kadiri alivyoweza, ingawa alionekana wazi kuwa alikuwa akichechemea na bado akihisi maumivu wakati akitembea.Baada ya kusaluti naye alikaribishwa kwenye kile kiti. Alichukua lile faili lililokuwa juu ya kile kiti,akaketi na kubaki akiwatazama wale vigogo wa kijeshi waliokuwa mbele yake.
Baada ya kutambulishwa kwa wajumbe wa lile jopo na kupewa sababu za yeye kuwepo pale, Meja Jenerali Fabiola Oluoch alimtupia swali.
“Luteni Jeannette, umepata kuiona na kuisoma hiyo ripoti iliyopo mikononi mwako hivi sasa kabla ya hapa?”
Luteni Jeanette Tulaye-Bgayo aliifunua ile ripoti iliyoandikwa na
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Stealth na ambayo yeye na mpiganaji Swordfish walipewa na kuipitia, kabla haijawasilishwa kwa wakuu wa jeshi lile la Umoja wa Mataifa pale Siera Leone. Aliiinua uso wake na kumtazama yule mwanamke mwenzake aliyefikia moja kati ya ngazi za juu kabisa za kijeshi, kisha akatembeza macho yake mazuri na makini kwa wale wajumbe wengine mle ndani na kumjibu.
“Ndiyo Afande. Nilipewa nakala ili nione kilichoandikwa na mkuu wetu wa kampeni ya upelelezi tuliyokuwa tukiiendesha katika msitu wa Tumbudu, mashariki mwa nchi hii.”
“Unakubaliana na yaliyoandikwa humo? Au kuna kipengele chochote unachodhani kuwa hakikuripotiwa ipaswavyo, au kimesahauliwa, au kimeingizwa wakati hakikuwepo?” Meja Jenerali Bartazar Swandoh alimuuliza mwanajeshi wake.
“Nimeisoma kwa makini ripoti hii afande, na nakubaliana na maelezo yote yaliyoripotiwa humu ndani!”
Kimya kifupi kilipita mle ndani, kisha Brigedia Mete Djiatete alimuuliza juu ya usaliti wa mpiganaji Alpha kama ulivyoelezewa kwenye ripoti ile. Luteni Jeannette Tulaye-Bgayo, p.a.k. “Honey-Bee”,alilielezea jopo lile mawazo yake juu ya usaliti wa mpiganaji Alpha, na alipomaliza, sehemu kubwa ya wajumbe wa lile jopo ilikubali kuwa hakika Alpha alikuwa akiwasaliti wenzake kwani aliongea kwa hisia na uwazi kwa kadiri alivyoona yeye, kwani yeye alikuwa ndiye mpiganaji wa kwanza kabisa kukubaliana na hoja ya mpiganaji Vampire kuwa kulikuwa kuna msaliti miongoni mwao.
Brigedia Kahemela akamuuliza juu ya ule mwili usio na kichwa, naye kama Kanali Okoronkwo, p.a.k Stealth, alithibitisha kuwa alipelekwa kuitambua miili yote ya wapiganaji wenzao waliouawa kule msituni, na kwamba naye anaamini kuwa ule mwili usio na kichwa na ulioharibiwa vibaya kwa moto ni wa mpiganaji Vampire.
“Una uhakika usio shaka kabisa Luteni kuwa ule ni mwili wa mpiganaji Vampire?” Luteni Kanali Chacha alimuuliza. Luteni Jeannette Tulaye-Bgayo alimtazama kwa muda na kushusha pumzi ndefu.
“Afande...mara ya mwisho kumuona Vampire akiwa hai alikuwa amebeba ile redio yake ya mawasiliano mgongoni. Nilichokuja kukiona baada ya hapo ni gwanda lake la juu likiwa na vitambulisho vyake vyote mifukoni, hivyo nikatarajia kumuona tena akiwa na ile fulana yake ya ndani tu, akiwa na ile redio yake mgongoni. Sasa nilipokuja kumuona tena, alikuwa marehemu asiye na kichwa, lakini akiwa na kila kitu kingine nilichotarajia awe nacho, yaani akiwa na ile fulana yake ya kijeshi inayovaliwa ndani ya gwanda, na akiwa na ile
redio yake mgongoni. Na pale nilikuwa na uhakika usio na shaka kabisa kuwa ni yeye.” Jeannette alimjibu kwa upole, huku macho yake makini yakionesha ni jinsi gani anavyoamini kile alichokuwa akikisema. Wajumbe wote walikuwa kimya wakimsikiliza kwa makini.
“Na nilipokuja kuuona tena ule mwili ukiwa umeungua vibaya sana hapa mochwari,kitu cha kwanza kilichoniwezesha kuutambua ni ile picha niliyooneshwa ya sehemu ambapo mwili ule ulichukuliwa na askari wetu wa miavuli...picha ambayo ililionesha wazi wazi lile jabali huku ule mwili ukiwa
tayari umeungua pale chini kabla haujaondolewa na kuletwa hapa kambini. Kitu cha pili ni yale mabaki ya ile redio yake ya mawasiliano yaliyogandamana na mwili wake. Kwa hiyo jibu ni ndiyo afande. Nina uhakika kuwa ule ni mwili wa mpiganaji Vampire!” Jeannette alijibu kwa kirefu.
Wajumbe waliandika kwenye makaratasi yao, wakamshukuru mpiganaji yule hatari sana kwa shabaha, na kumruhusu. Ilikuwa wazi kuwa maelezo ya ripoti ya Kanali Essaiyyah Okoronkwo yalikuwa sahihi. Angalau hivyo ndivyo walivyoanza kudhani hadi wakati mpiganaji kutoka Tanzania, Meja Abdul-Hameed Babu, p.a.k. Swordfish, alipoingia mle ndani. Baada ya kusikia maelezo yake, wajumbe wa jopo lile walijikuta njia panda juu ya swala la ule mwili usio na kichwa.
Meja Abdul-Hameed Babu aliwatazama wale wajumbe wa jopo waliokuwa mbele yake kutokea nyuma ya miwani myeusi aliyovaa na kama wale wenzake wa hapo awali, aliweza kuwatambua mara moja wale wawakilishi kutoka nchini kwake, Brigedia Stanslaus Kahemela na Luteni Kanali Athanas Chacha.
“Ni kweli nimeisoma hii ripoti iliyoandaliwa na kiongozi wa ile operesheni yetu kule msituni...” Alijibu swali la kwanza la wale wajumbe na kutulia kidogo kabla ya kumalizia, “...na kuna baadhi ya maeneo katika ripoti hii ambayo sikubaliani nayo!”
Wajumbe wa jopo walimtumbulia macho ya udadisi.
“Ni vipengele gani usivyokubaliana navyo Meja...?” Brigedia Mohammed Awolowo kutoka Naijeria alimuuliza kwa upole.
“Na kwa sababu gani?” Brigedia Stanslaus Kahemela kutoka Tanzania aliongezea. Swordfish alikaa vizuri kitini, akafunua ukurasa ambao tayari alikuwa akiujua kwa kichwa kisha akainua uso wake na kuongea.
“Ni kwamba siwezi kusema lolote juu ya kipengele kilichopo katika ukurasa
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
wa sita kisemacho kuwa mpiganaji mwenzetu kutoka Tanzania aliyejulikana
kwa jina la uficho Alpha alikuwa akitusaliti kwa kuwasiliana na mdunguaji aliyejificha mle msituni.”
“Kwa hiyo hukubaliani kuwa kulikuwa kuna msalitimiongoni mwenu na kuwa Alpha ndiye alikuwa huyo msaliti?” Brigedia Stanslaus Kahemela alimuuliza kwa udadisi mkubwa kabisa.
“Kwamba kulikuwa kuna msaliti katika kundi letu hilo linawezekana kabisa kwani ilitufunukia wazi kuwa yule mdunguaji alikuwa akijua kabisa nyendo zetu, na ndivyo alivyofanikiwa kuwadungua wenzetu. Ila sijaona ushahidi wa kunishawishi kuwa ni Alpha ndiye alikuwa msaliti...kwangu mimi inaleta maana zaidi kwa mpiganaji Black Mamba, ambaye mpaka sasa inasemekana kuwa amepotea katika harakati, kuwa ndiye msaliti!”
Wajumbe walitazamana, kimya kikatawala.
“Je, huu ushahidi kuwa Alpha alikutwa na kifaa cha mawasiliano mkononi mwake, kifaa ambacho ni tofauti kabisa na vile vitumikavyo na jeshi letu, hautoshi kukuthibitishia kuwa alikuwa msaliti?”Meja Jenerali Fabiola Oluoch alimuuliza.
“Ndiyo maana nikasema hapo awali kuwa kipengele hiki siwezi kusema lolote kwacho, kwa sababu mimi binafsi sikukiona hicho kifaa kikiwa mkononi mwa Alpha. Nilipofika eneo la tukio, niliwakuta Honey-Bee na Stealth wakiwa wamezingirwa na kundi dogo la waasi, nami nikaanzisha makabiliano. Baada ya makabiliano, nilipoteza fahamu, kwani muda huo tayari nilikuwa nimeshajeruhiwa na mdunguaji na nilishatokwa damu nyingi. Niliporejewa na fahamu, Honey-Bee aliniambia kuwa Alpha na Vampire wameuawa, na kwamba Black Mamba amepotea kwenye harakati... na kuwa huenda naye akawa tayari ameuawa ila tu mwili wake haujaonekana. Muda huohuo tukaanza kushambuliwa na kundi jingine la waasi, tukaanza kukimbia.
“Sasa katika mazingira kama hayo, naona si haki kwangu kuthibitisha moja kwa moja kuwa Alpha ndiye aliyekuwa akitusaliti...ingawa nakiri kuwa alikuwa mstari wa mbele kuipinga hoja ya Vampire ya kuwepo msaliti miongoni mwetu, bado sioni kuwa hiyo ni sababu ya kutosha kunishawishi kuikubali au kuikana moja kwa moja.” Meja Abdul-Hameed Babu alijieleza kwa kirefu.Wajumbe wa jopo walikuwa wakiandika maelezo yake, na kule kwenye kile chumba cha pili, maelezo yake yaliendelea kurekodiwa kwenye mikanda maalum ya kuhifadhia sauti. Mitambo ile iliweza kunasa mtikisiko hata mdogo sana katika sauti ya msemaji na kuweza kugundua iwapo alikuwa akiongea ukweli au vinginevyo.
Baada ya kimya kifupi, Meja Generali Basil Kufoh kutoka Ghana aliongea.
MDUNGUAJI
“Sawa Meja...maoni yako yamezingatiwa. Kama wote tujuavyo msako juu ya mpiganaji wetu Black Mamba bado unaendelea,hivyo nadhani iwapo atapatikana, au mwili wake ukipatikana, tutakuwa katika nafasi nzuri ya kupitisha maamuzi juu ya swala la nani alikuwa msaliti, lakini nadhani wajumbe wa jopo hili wanakubaliana zaidi na maelezo ya ripoti hii juu ya kipengele hicho, hasa ushahidi uliopatikana juu yake.”
Vichwa vya wale wajumbe wengine vilitikiswa kukubaliana na kauli ile, isipokuwa vya Brigedia Kahemela na Lut. Kan. Chacha. Meja Abdul-Hameed Babu, p.a.k. Swordfish, shujaa wa makabiliano ya ana kwa ana katika medani za vita alibaki kimya tu akiwatazama kutokea nyuma ya ile miwani yake.
“Je, kuna sehemu yoyote nyingine katika ripoti hii ambayo hukubaliani nayo Meja?” Meja Jenerali Bartazar Swandoh kutoka Sierra Leone alimuuliza.
“Kifo cha Vampire!” Meja Babu alijibu mara moja, na wale wajumbe wa jopo walimkodolea macho kwa mara ya pili ndani ya muda ule mfupi aliokuwamo mle ndani.
“Kifo cha mpiganaji Vampire? Una mawazo tofauti juu ya kifo cha mpiganaji Vampire?” Kanali Olga Tbage alimuuliza kwa udadisi.
“Ndiyo Afande...”
“Fafanua Meja...!” Lut. Kan. Athanas Chacha alidakia, wakati Brigedia Kahemela akimtazama Meja Babu kwa macho madogo yaliyofinywa kwa umakini.
“Siamini kuwa ule mwili ulioungua moto na kuharibika vibaya niliooneshwa pale mochwari ni wa mpiganaji Vampire wakuu wangu!”Swordfish alijiibu, na kimya kipya kikatanda mle ndani.
“Sasa unaamini kuwa ule ni mwili wa nani Meja?” Meja Emeka Askia alimuuliza kwa utulivu mkubwa.
“Sijui! Lakini najua kuwa yule siyo Vampire...”
“Na una nini la kusema juu ya ile redio ya mawasiliano iliyokuwa imegandamana na mwili ule?”
“Wakuu sijui ni nini hasa kilichotokea pale, lakini nadhani kutakuwa kumetokea mkanganyiko mkubwa sana...nafsi yangu haikubali kuwa ule ni mwili wa Vampire wazee!”
“Sasa hiyo haitoshi Meja! Tupe vigezo...sababu za wazi na za msingi kutilia nguvu hiyo hoja yako...” Meja Jenerali Fabiola Oluoch alimwambia kwa ukali.
“Itakuwa ni hisia tu niliyo nayo wazee...a...a..gut feeling of some kind...lakini unaponiambia kuwa yule mtu asiye na kichwa, aliyeungua kiasi cha kutoweza kutambulika kabisa, ambaye hata vipimo vyake vya vinasaba havituwezeshi
kumtambua kuwa ni Tom, Dick au...au...nani tu sijui huko, eti kuwa ni Vampire!” Meja Abdul-Hameed Babu alitulia kidogo huku akiwatazama wale wakuu wake mmoja baada ya mwingine kutokea nyuma ya miwani yake myeusi, kisha akaendelea, “...eti kwa vile tu mwili ule umebebeshwa redio ya mawasiliano kama jinsi ambavyo Vampire alivyokuwa akibeba?” Alinyamaza tena huku akiendelea kuwatazama wale waku wake, kisha akamalizia kwa sauti ya chini iliyokaribia kuwa mnong’ono,“...hapana wazee. Mimi hainiingii akilini kabisa!”
Ukimya uliofuata ulidhihirisha kuwa alikuwa amewachanganya vibaya sana wale wajumbe wa jopo.
“Akh! Sasa...kama yule si Vampire, basi Vampire yuko wapi?” Brigedia Stanslaus Kahemela alimuuliza taratibu.
“Yeah...Vampire yuko wapi?” Meja Jenerali Bartazar Swandoh alirudia swali la Brigedia Kahemela.
“Na kama hivyo ndivyo, basi ule mwili uliolala pale mochwari bila kichwa ni wa nani?” Meja Emeka Askia naye alisaili. Meja Babu alibaki kimya. Alishatoa mawazo yake, sasa ni juu ya lile jopo kuamua cha kufanya.
“Tunakuuliza wewe Meja!” Meja Jenerali Bartazar Swandor alimfokea huku akipiga meza. Meja Babu aliketi wima kwenye kiti chake.“Sina jibu lolote kwa maswali hayo wakuu wangu, nilichofanya ni kutoa mawazo yangu tu...”
“Ulichofanya ni kutuchanganya tu Meja! Hicho ndicho kitu pekee ulichokifanya!” Meja Jenerali Basil Kufoh, ambaye kwa kawaida huwa mpole kuliko wengine alifoka kwa hasira.
“Samahani sana wakuu wangu, lakini huo ndiyo mtazamo wangu.”
Wajumbe wa jopo walimtazama kwa muda mrefu, vichwa vikiwachemka. Kisha Meja Jenerali Fabiola Oluoch aliegemeza kifua chake kwenye ukingo wa ile meza na huku akimnyooshea ncha ya kalamu iliyokuwa mkononi mwake kutilia mkazo akamuuliza, “Hivi unaelewa Meja kuwa huo mtazamo wako unamtia mpiganaji Vampire kwenye tuhuma ya usaliti? Kuwa kama ule si mwili wake, ni kwamba inawezekana kuwa ni yeye ndiye alikuwa msaliti, na akamuua Alpha baada ya kugundulika, na akamuua na Black Mamba, kisha akamvisha ile redio yake ili aonekane kuwa ni Vampire, naye akatoweka msituni?”
Swordfish alimtazama yule mkuu wake wa kike, kisha akatikisa kichwa.
“Halafu akamtawanya kichwa makusudi na kumchoma moto? Hapana
Meja Jenerali. Nielewavyo mimi ule moto uliwaka baadaye sana tena kwa bahati mbaya tu. Ninachoweza kusema ni kwamba hili swala zima linatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina...!”
MDUNGUAJI
Wale wajumbe wa lile jopo walibaki kimya wakimtazama yule shujaa wa mapambano kutoka Tanzania aliyeweza kutoa hoja zake bila woga na kujibu maswali na shutuma zao bila ya kutetereka.Alikuwa ni mpiganaji halisi.
“Ahsante Meja Babu. Tunashukuru kwa maelezo yako, na tumeyazingatia. Sasa unaweza kwenda. Baada ya jopo hili kupitisha maamuzi, nyote mtajulishwa na kupewa maelekezo.”Hatimaye Meja Jenerali Basil Kufoh alimwambia.
Swordfish, aliinuka, akaliweka lile faili juu ya kile kiti alichokuwa amekalia, akasaluti kikakamavu, akazunguka kwa visigino vyake na kugeuka nyuma. Akatoka nje ya chumba kile akiyahisi kabisa macho kumi na manane ya wale wakuu tisa yakiwa mgongoni kwake.
Potelea mbali! Nimetoa mawazo yangu, watakachoamua ni juu yao.
Siku mbili baadaye ripoti ya kuridhia mapendekezo ya lile jopo maalum la kijeshi kutoka Umoja wa Mataifa iliingia,na wale wapiganaji watatu walionusurika katika kadhia ile ya mdunguaji waliitwa mbele ya jopo lile.Safari hii mbele ya ile meza kubwa ya wajumbe wa jopo kulikuwa kuna viti vitatu, na Kanali Essaiyyah Okoronkwo p.a.k. Stealth aliketi kwenye kiti cha mwisho kulia mbele ya ile meza, Luteni Jeannette Tulaye-Bgayo, p.a.k. Honey-Bee aliketi kwenye kiti kilichokuwa katikati, na Meja Abdul-Hameed Babu, p.a.k. Swordfish, aliketi kwenye kiti kilichokuwa kushoto kabisa. Mashujaa wale walitulia kimya na kuwatazama wale wajumbe wa jopo.
Safari hii mbele ya wale wajumbe waliokuwa nyuma ya ile meza kubwa iliyong’ara hakukuwa na makaratasi mengi wala mafaili kama wakati uliopita. Isipokuwa mbele ya mwenyekiti wa jopo lile, Meja Jenerali Basil Kufoh, ambaye mbele yake kulikuwa kuna faili moja tu jembamba.Ulikuwa umefika muda wa kupitisha maamuzi juu ya kadhia ile kama jinsi ilivyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa.
Meja Jenerali Basil Kufoh alikohoa kidogo na kuanza kuwaeleza wale mashujaa waliokuwa mbele yao, “Tumepokea majibu ya mapendekezo yetu kama jopo la kijeshi kutoka kwenye kamati ya usalama ya Umoja wa Mataifa, juu ya matukio yaliyotokea kule msituni.”
Wapiganaji walitulia kimya wakimsikiliza kwa makini.
“Mapendekezo yetu tuliyapeleka huko kutokana na ripoti iliyoandikwa na Kanali Essaiyyah Okoronkwo kama kiongozi wa kampeni ile, na pia kutokana na mahojiano tuliyoyafanya na kila mmoja wenu, kila mmoja kwa wakati
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
wake, juu ya ripoti ile, na mawazo yenu binafsi juu ya matukio ya kule msituni.
Sasa nina furaha kusema kuwa mapendekezo yetu yameidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, na hivyo kutuwajibikia sisi kutekeleza kama tulivyopendekeza.”
Meja Jenerali Basil Kufoh alitulia huku akiwatembezea macho yake makubwa wale wapiganaji watatu ambao waliendelea kutulia kimya kabisa, wote wakiwa wamevaa mavazi ya kijeshi maalumu kwa matukio ya kiofisa na sio kwa ajili ya mapambano msituni.
“Sasa nitawasomea maamuzi ya jeshi letu juu ya matukio mliyokutana nayo kule msituni kama ifuatavyo...” Meja Jenerali Basil Kufoh aliinama na kufunua lile faili jembamba lililokuwa mbele yake, na kuendelea, “...kutokana na ushahidi uliolizunguka swala lote la mauaji yaliyokuwa yakifanywa na mdunguaji aliyejificha kule msituni, baraza la usalama limeridhishwa kuwa mpiganaji aliyejulikana kwa jina la uficho Alpha kutoka Tanzania, ambaye hivi sasa ni marehemu, alikuwa akiwasaliti wenzake kwa kushirikiana na mdunguaji.
Alpha ameuawa akiwa katika harakati za kulisaliti jeshi sio tu la Umoja wa Mataifa, bali hata la nchi yake iliyomuamini na kumtuma kuja kuiwakilisha
kijeshi hapa Sierra Leone. Kutokana na kitendo chake hiki, mpiganaji huyu hatakuwa na heshima yoyote ya kijeshi.” Meja Jenerali Basil Kufoh alimalizia.
Meja Abdul-Hameed Babu aliuma meno baada ya kusikia maamuzi yale na alijikuta akipeleka macho yake yaliyofichwa na miwani myeusi kwa Brigedia
Stanslaus Kahemela na Lut. Kan. Athanas Chacha.
Wapiganaji walibaki kimya, na Mej. Jen. Kufoh aliendelea, “Kuhusu mdunguaji, ni msimamo wa jeshi la Umoja wa Mataifa kwamba kwa kuwa hakuna uthibitisho wowote kuwa naye ni miongoni mwa waasi waliouawa katika shambulio letu la anga kwenye eneo la kambi ya waasi, basi bado anahesabika kuwa yu hai na hatari na ataendelea kusakwa.”
Meja Basil Kufoh aliinua glasi ya maji iliyokuwa kando yake pale mezani na kunywa kidogo.
“Vile vile, jopo na baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa pamoja vimekubaliana na ripoti ya Kanali Okoronkwo kuwa kifo cha Alpha kilitokana na kuuawa na mpiganaji mwingine kutoka Tanzania aliyejulikana kwa jina la Vampire.
“Sanjari na hili, jopo na baraza pia vinakubaliana na ripoti ya Kanali Essaiyyah Okoronkwo kuwa mpiganaji Vampire kutoka Tanzania aliuawa na mdunguaji aliyejificha mle msituni baada ya kulipuliwa kichwa kwa bunduki yenye nguvu, akiwa karibu sana na muuaji na hivyo kumtawanya kichwa
MDUNGUAJI
chake kiasi cha kukitenganisha kabisa na mwili wake.”
Meja Abdul-Hameed Babu aliachia pumzi ndefu ya kukata tamaa na kukunja ngumi kwa nguvu juu ya mapaja yake, moyoni akitaka kusimama na kuipinga tena hoja ile, lakini nidhamu ya kijeshi ilimzuia.
“Na hivyo, jopo na kamati vinakubaliana kuwa mwili usio na kichwa na ambao ulikuwa umeunguzwa vibaya, ni wa mpiganaji kutoka Tanzania, aliyejulikana kama Vampire. Hivyo basi, pamoja na kutambua maoni tofauti ya mpiganaji kutoka Tanzania ajulikanaye kwa jina la Swordfish juu ya swala hili,jopo na kamati ya usalama vinasisitiza kuwa huu ndiyo uamuzi wa jeshi na ni wa mwisho hadi pale itakapothibitishwa vinginevyo.”
Meja Abdul-Hameed Babu alikunjua ngumi alizokuwa amezikunja na kutulia. Mwenyekiti wa jopo aliendelea kusoma kutoka kwenye lile faili lake.
“Mpiganaji Vampire anahesabika kuwa amekufa kijeshi, akiwa mzalendo na mwaminifu sio tu kwa jeshi la nchi yake, bali pia kwa jeshi la Umoja wa Mataifa.”
Aliendelea kwa kuwasomea maamuzi ya jeshi juu ya hatima ya mpiganaji Black Mamba, kwamba bado anahesabika kuwa amepotea kwenye harakati mpaka hapo itakapothibitika vinginevyo. Pia aliwafahamisha kuwa kwa sababu ile kambi ya waasi imeshagundulika na kuangamizwa, msako dhidi ya waasi waliofanikiwa kutoroka kwenye shambulizi lile bado unaendelea, sawia na msako wa mdunguaji, ili akipatikana atoe sababu za Alpha kushirikiana naye katika kuwaangamiza wenzake.Hivyo mpaka hilo litakapofanikishwa, msako wa mdunguaji bado uko wazi.
“Na mwisho napenda kuwafahamisha kuwa nyie nyote mtatunukiwa nishani za ushujaa na ujasiri katika medani ya vita, na kuanzia muda mtakapotoka nje ya chumba hiki, ziara yenu ya kijeshi hapa Sierra Leone, yaani Tour of Duty, itakuwa imekwisha na mtarudi kwenye nchi zenu kuendelea na majukumu mengine ya kijeshi mkiwa huko...mkiwa ni wapiganaji mliojibebea sifa kubwa kabisa, na mlioziweka nchi zenu katika nafasi ya kujivunia kabisa mbele ya Umoja wa Mataifa, na hususan bara letu la Afrika!” Basil Kufoh alisema kwa majigambo halisi ya kijeshi, huku wale wajumbe wengine wa jopo wakitikisa vichwa kwa nguvu kuafikiana naye.
Wapiganaji waliendelea kuwatazama tu wale wakuu wao kwa utulivu, mioyoni kila mmoja akiwa na hisia zake juu ya taarifa ile. Hapo Meja Jenerali Basil Kufoh alimgeukia Meja Jenerali Fabiola Oluoch.“Sasa kwa taarifa nyingine juu ya mafao yenu, Meja Jenerali Fabiola ataeleza juu hilo.”
Meja Jenerali Fabiola Oluoch kutoka Kenya alikohoa kidogo na kuongea
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
moja kwa moja.
“Kwa kuwa sasa ziara yenu ya kijeshi hapa Sierra Leone imekwisha, nyote mtarudi katika nchi zenu kama jinsi mwenyekiti alivyoeleza. Na huko, kila mmoja wenu tayari ameshawekewa kiasi cha dola za kimarekani elfu telathini
katika akaunti yake ikiwa ni mafao yenu kwa muda wote mliolitumikia bara lenu na Umoja wa Mataifa kwa ujumla, hapa Sierra Leone...”
Kimya kizito kuliko vyote vilivyowahi kutawala chumba kile kilitanda mle ndani, wakati wale wapiganaji wakizamisha akilini mwao taarifa ile.
Dola elfu thelathini!
Taarifa hii iliwaacha wale wapiganaji wakibadili mikao pale walipokuwa na ilikuwa ni ile nidhamu ya kijeshi tu ndiyo iliyowazuia kushangilia kwa sauti, lakini faraja za wazi zilijionesha katika nyuso zao.Wale wakuu wao wa kazi waliliona hilo na walionesha kuridhika na jinsi wale mashujaa walivyoipokea taarifa ile.
“Zaidi ya hapo, kama jinsi ilivyo kawaida ya jeshi letu, kiasi kama hicho cha fedha kimeshaingizwa kwenye akaunti za wenzetu waliouawa kule msituni.”
Meja Jenerali Fabiola Oluoch alimalizia.Ukimya ulitawala kwa muda mle ndani na Meja Jenerali Basil Kufoh aliingilia kati kuvunja ukimya ule.
“Sasa natangaza rasmi kuwa taarifa hii imezuiliwa. Je kuna lolote ambalo yeyote kati yenu anataka kulieleza jopo hili kabla hatujawaruhusu?”
Kimya kingine kifupi sana kilitanda mle ndani, kisha Luteni Jeannette Tulaye-Bgayo alikohoa na kusema, “Eem...ninaomba kuongea kidogo afande!”
Meja Jenerali Basil Kufoh alimuashiria aendelee kwa kutumia mkono wake.
“Nashukuru sana kwa maamuzi ya jopo na baraza letu la usalama la Umoja wa Mataifa, nami kama mpiganaji mtiifu nakubaliana nayo moja kwa moja...”
“Haya maamuzi yamezuiliwa afande! Kukubaliana nayo sio hiari!” Mej. Jen. Bartazar Swandoh alimkatisha.
“Ndiyo afande...ila mimi nilikuwa naomba kitu kimoja tu...” Luteni Jeannette Tulaye-Bgayo, p.a.k. Honey-Bee, alisema na kuendelea, “...naomba jopo hili liniidhinishe kuwa miongoni mwa watakaoendeleza msako dhidi ya mdunguaji aliyekuwa akitushambulia kule msituni. Naamini nina wajibu wa aidha kumtia mbaroni au kumuangamiza kabisa afande...”
Wajumbe wa jopo walibaki wakimkodolea macho yule mwanamama jasiri.
“Eemm...ni kwa nini unadhani kuwa una wajibu wa kumtia mbaroni au kumuangamiza kabisa huyu Mdunguaji Luteni...?” Hatimaye Brigedia Mete Djiatete kutoka Senegali alimuuliza huku akimtazama kwa udadisi mkubwa. Luteni Jeannette Tulaye-Bgayo hakusita.
MDUNGUAJI
“Afande, kama kuna askari anayeweza kumdondosha na kumuangamiza yule mdunguaji katika mchezo wake mwenyewe, basi askari huyo ni mimi! Panahitajika mtu mwenye shabaha makini na hisia kali sana kuweza kumdhibiti mdunguaji yule. Shabaha na hisia hizo mi’ n’nazo!”
Na hata wakati Honey-Bee akitoa maelezo yale, wale wajumbe wa lile jopo maalum la kijeshi waliwaona wale wapiganaji wenzake wakitikisa vichwa vyao kwa uhakika kabisa kumuunga mkono.
“Hapana afande. Tunaamini kuwa ulichokifanya na wenzako mpaka sasa kinatosha. Tuwape na wengine nafasi ya kupigania amani ya bara letu. Uzoefu mtakaotoka nao huku utahitajika sana katika nchi zenu, ambako mnapaswa mrejee mara moja.” Meja Jenerali Basil Kufoh alimjibu kwa upole uliojaa ithibati. Uso wake ukionesha kutoridhishwa na jibu lile Honey-Bee alifungua mdomo kutaka kujenga hoja zaidi, lakini akajizuia. Ile ilikuwa ni amri ya kijeshi na haikuwa na mjadala.
Muda mfupi baadaye, wale wapiganaji watatu waliinuka na Stealth akapiga saluti kikakamavu mbele ya ile meza, kisha wakageuka na kutoka nje ya chumba kila mmoja akiwa ameongezeka thamani kwa dola elfu thelathini za kimarekani.
Wiki mmoja baadaye:
Ndege ndogo ya kijeshi ilitua kwenye uwanja wa ndege wa jeshi ulioko kilometa chache kutoka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam, nchini Tanzania. Ilikuwa ni majira ya saa nne za asubuhi na pale uwanjani kulikuwa kuna kikosi kidogo cha wanajeshi waliojipanga kwa ajili ya gwaride maalumu. Nyuma yao kulikuwa kuna meza kubwa ambayo nyuma yake walikuwa wameketi viongozi wa ngazi za juu katika majeshi ya Tanzania.
Pamoja nao alikuwapo Waziri wa Ulinzi na baadhi ya viongozi wengine wa kiserikali. Hawa walikuwa wamekaa juu ya membari iliyojengwa maalum kwa
tukio lililokuwa likiendelea pale uwanjani muda ule, membari ambayo ilikuwa
imefunikwa kwa paa la turubai zuri la kijeshi.
Mlango uliokuwa ubavuni mwa ile ndege ulifunguka na ngazi ikateremshwa.
Muda huohuo, gari maalumu la wazi la kijeshi aina ya Land Rover liliiendea ile ndege kwa mwendo wa pole huku likisindikizwa na askari wanane waliovalia mavazi maalumu kwa tukio lile, wanne kila upande, na kusimama hatua chache usawa wa lango la nyuma la ndege ile. Lile lango lilifunguka taratibu na kulala
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
chini pale uwanjani likiiacha wazi sehemu ya nyuma ya ile ndege.
Huku kwenye ule mlango wa ubavuni wa ile ndege, Brigedia Stanslaus
Kahemela na Luteni Kanali Athanas Chacha waliteremka kwa mwendo wa kijeshi. Chini ya zile ngazi walilakiwa na kiongozi wa kijeshi aliyeandaliwa kwa
jukumu lile ambaye aliwaongoza hadi pale kwa Mkuu wa Majeshi na Waziri wa Ulinzi ambako salamu za kijeshi zilipitishwa.
Kisha wote walisimama na kugeukia kule ilipokuwa ile ndege.Bendi ya jeshi ilianza kupiga ala maalumu wakati wale askari wanane wakiingia ndani ya ile ndege kupitia kwenye ule mlango mkubwa wa nyuma.
Muda mfupi baadaye, Meja Abdul-Hameed Babu, akiwa amevaa suti yake ya kijeshi iliyomkaa vizuri sana, na ile nishani yake ya ushujaa na ujasiri aliyotunukiwa na jeshi la Umoja wa Mataifa kule Sierra Leone ikiwa inaning’inia upande wa kushoto wa kifua chake, alitoka kwenye ndege ile kupitia ule mlango wa nyuma, akiwaongoza wale wanajeshi wanane waliokuwa
wamebeba majeneza mawili yaliyofunikwa kwa bendera ya Taifa, kila jeneza
moja likiwa limebebwa na wanajeshi wanne.
Walipandisha yale majeneza sehemu ya nyuma ya ile Land Rover iliyokuwa wazi na Meja Abdul-Hameed Babu,p.a.k. Swordfish, akapanda kule nyuma pamoja nayo. Lile gari ilianza kuondoka taratibu kuelekea kule walipokuwa wamesimama wale viongozi wa kijeshi na kitaifa, huku wale askari wanane wakitembea kwa mwendo maalumu, wanne kila upande wa lile gari. Matarumbeta ya kijeshi yaliendelea kupigwa huku Meja Babu akiwa amesaluti kikakamavu nyuma ya lile gari hali amesimama katikati ya yale majeneza mawili. Safari hii hakuwa amevaa ile miwani yake myeusi, na jicho lake la kulia lilikuwa limefunikwa kwa kipande maalum cha ngozi au eye patch, kilichoshikiliwa jichoni pale kwa kamba maalum iliyopita kukizunguka kichwa chake.
Miili ya wapiganaji Alpha na Vampire ilikuwa imerejeshwa nyumbani.
Ndugu na jamaa wa wanapiganaji wale waliofika pale uwanjani walisikika wakiwalilia wale wapendwa wao walioondoka wazima miezi kadhaa iliyopita, na sasa wanarudi wakiwa maiti...na mwingine akiwa amebakiwa na jicho moja tu.
Lile gari lilisimama sehemu iliyoandaliwa mapema na yale majeneza yaliteremshwa na kuwekwa juu meza maalum. Gwaride maalum la mazishi
lilifanyika na Meja Abdul-Hameed Babu alitembea kikakamavu hadi mbele ya Mkuu wa Majeshi na kukabidhi nishani ya ushujaa ya mpiganaji Vampire, ambaye iliaminika kuwa mwili wake ulikuwa katika moja ya yale majeneza
MDUNGUAJI
mawili. Alipiga saluti ya heshima na kwenda kuketi kwenye kiti maalum kilichotengwa kwa ajili yake. Alitembeza jicho lake moja lililobakia na kuona sehemu ambapo familia yake ilikuwa imeketi kwenye sehemu iliyotengwa kwa ajili ya wanafamilia wa wale wanajeshi aliowarejesha nchini. Jicho lake liligongana na macho ya mkewe aliyekuwa amejitanda hijabu na baibui kama kama desturi yake, na alimuona mkewe pamoja na watoto wake na jamaa zake wa karibu wakilia wazi wazi. Donge lilimkaba na moyo ulimuuma, akijua kuwa walikuwa wakililia jicho alilopoteza vitani. Akajikaza kijeshi na kugeuza uso wake kutazama mbele ambako yale majeneza mawili yalikuwa yamewekwa.
Viongozi wa kijeshi walitoa hutuba zao juu ya wapiganaji wale wa kitanzania waliorudi kutoka kuiwakilisha nchi katika kampeni muhimu kabisa kwa amani na usalama wa bara la Afrika. Katika hutuba hizo, wapiganaji Alpha na Vampire walitajwa kuwa ni mashujaa watakaozikwa kishujaa.Naye akatajwa kuwa ni shujaa na jasiri aliyerejesha nyumbani miili ya wenzake akiwa na nishani ya ushujaa ya Umoja wa Mataifa, kama jinsi alivyotunukiwa mpiganaji aliyetambulika kwa jina la uficho Vampire. Hakikusemwa chochote juu ya Alpha kupewa au kutopewa nishani.
Wakati hotuba zikiendelea, Meja Babu alizungusha jicho lake hadi pale zilipokuwa zimeketi familia za wale wapiganaji wenzake marehemu, na hakupata taabu kuitambua familia ya Luteni Kanali Nathan Mwombeki, p.a.k.
Alpha, na aligundua mara moja kuwa mpiganaji Alpha alikuwa na familia kubwa sana na akajikuta akijiuliza wataishije bila ya yule kiongozi wao wa familia. Au ndiyo sababu Alpha aliamua kutusaliti kule Sierra Leone, kama kweli alikuwa akitusaliti...?
Alikuwa ameahidiwa pesa kufanya vile? Na kama ni pesa, ni pesa ngapi hizo za kumfanya akubali kulisaliti taifa lake namna ile? Itakuwa ni pesa nyingi kuliko hizi tulizopata kama mafao yetu?
Aliguna.
Angalau sasa familia yake itapata zile pesa za mafao ambazo naye, japo alisemekana msaliti,aliwekewa kwenye akaunti yake...dola elfu thelathini!
Mawazo yake yalikatishwa na maparapanda ya kijeshi baada ya hotuba kumalizika.
Msemaji wa kijeshi alisimama na kutangaza kuwa kutokana na kwamba ile
miili ilikuwa imekaa sana huko ilipotoka, ndugu na jamaa watapewa nafasi ya kuwaaga wapendwa wao pale pale uwanjani, na baada ya hapo moja kwa moja marehemu wataenda kuzikwa, jijini Dar es Salaam.
Kwa kuwa taarifa hii ilikuwa imeshaletwa nyumbani kabla hata ile miili
haijarejeshwa nyumbani, ndugu na jamaa wa marehemu hawakushitushwa na
taarifa ile, na badala yake waliendelea kulia tu kama walivyokuwa tangu miili
ile ifike nchini, wakiwa tayari wamejiandaa kwa maziko.Baada ya kuaga miili
Waziri wa Ulinzi pamoja na Mkuu wa Majeshi, waliandamana na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa kijeshi, na yeye akijumuishwa, kwenda kuwapa
pole wafiwa, hasa wake na watoto wa wale marehemu.
Vilio vilishamiri maradufu wakati wale viongozi wa kijeshi na kitaifa
wakiwapa pole jamaa wa Kanali Nathan Mwombeki. Muda wote yeye alikuwa
kimya, akishuhudia yote yale kwa jicho lake moja.
Hatimaye msafara ulihamia kwenye familia ya watu watatu tu ya mpiganaji
Vampire. Na hapo ndipo alipopata kumuona mke wa mpiganaji yule, na kwa mara nyingine akahisi koo likimkauka na donge likimkaba.
Alikuwapo mzee mtu mzima aliyepata kiasi cha miaka kama sitini na tano hivi aliyekuwa amevaa kaunda-suti nyeusi. Bila hata ya kuambiwa Swordfish
alimtambua kuwa ni baba wa yule mpiganaji shujaa ambaye yeye binafsi
hakuamini kabisa kuwa ndiye aliyelala ndani ya lile jeneza. Na ingawa yule mzee alikuwa amevaa miwani myeusi ya jua, bado mshabihiano wake na Vampire ulionekana waziwazi. Alikuwa akitembelea mkongojo ingawa bado alionekana kuwa na nguvu.
Wakati Mkuu wa Majeshi anasalimiana na yule mzee kwa heshima na unyenyekevu, Meja Babu alipeleka jicho lake kwa mke waVampire. Ingawa alikuwa amejitanda khanga mwili mzima, na kichwani alikuwa amejifunga kitambaa cheusi. Swordfish aliweza kuona kuwa alikuwa ni mwanamke wa kuvutia.Kama mkwewe, alikuwa amevaa miwani myeusi ambayo tofauti na ile ya mkwewe, ilikuwa ya kisasa na ki-ana mitindo zaidi.Alikuwa ni mwanadada aliyeonekana kujitunza na msomi. Na hata pale alipokuwa akimtazama yule mwanamke, Meja Babu alishuhudia michirizi ya machozi ikitiririka kutokea chini ya miwani ile.
Alimeza funda la mate na kushusha jicho lake kumtazama binti mdogo aliyepata umri wa miaka mitano hivi aliyekuwa ameketi kando ya yule mwanadada na ambaye ndiye aliyekamilisha familia ya mpiganaji Vampire iliyofika pale uwanjani siku ile. Meja Babu alitambua kuwa yule ni mtoto wa Vampire, baada ya kuona mshabihiano wa macho ya yule mtoto na yale ya Vampire. Akamtazama tena mke wa Vampire na moyo ukamuingia baridi.
Mungu wangu! Hivi nitaweza kweli kumwambia kwa yakini kabisa huyu mama kuwa mume wake amekufa na ndiye aliyelala ndani ya lile jeneza...?
Hatimaye zamu yake ilifika na alimpa mkono yule mzee aliyeonekana
MDUNGUAJI
kuwa mnyonge na aliyeishiwa nguvu kabisa. Hakuwa na la kumwambia. Alimpa tu mkono naye alitikisa kichwa kidogo kwa ishara ya kumshukuru. Akamsogelea mke wa Vampire, na kumpa mkono wa pole, na alishindwa kujizuia kumkumbatia kwa kumliwaza. Yule mwanadada alimkumbatia kwa nguvu na kuachia kwikwi ya kilio cha uchungu.
“Pole sana shemeji...vita haina macho...na kifo ni kazi ya Mungu!” Alimnong’oneza kwa sauti ya chini.Yule mwanadada alimuachia na kutikisa kichwa kuafiki maneno yale huku akitoa miwani usoni mwake na kujipangusa
machozi kwa kitambaa alichokuwa nacho mkononi na kuirudisha tena usoni ile miwani.
“Mtoto wetu...Claudia...” Yule mwanadada alisema kwa sauti ya chini, akimtambulisha kwake yule mtoto wa kike aliyekuwa akilia mfululizo kando yake. Meja Abdul-Hameed alimtazama yule mtoto na kumshika kidevu, kisha akampapasa kichwani, bila ya kusema neno.
Aseme nini?
Donge kubwa lilikuwa limemkaa kooni na alihofu kuwa kama angefungua tu mdomo kujaribu kuongea naye angeishia kuangua kilio.
“Eem...hakuna jamaa wengine waliokuja zaidi yenu na...na...mzee?”
Hatimaye alipata jambo la kusema. Mke wa Vampire alitikisa kichwa kwa masikitiko.
“Sisi ndiyo familia yake iliyobaki! Hakuwa na ndugu zaidi ya baba yake na...na sisi. Sasa tumebaki peke yetu!” Yule mwanadada alijibu na kuanza kulia tena. Akili ilimzunguka Meja Babu na akataka aendelee kumuuliza ni kwa vipi Vampire asiwe na ndugu wengine zaidi yao.
Haya basi huyo Vampire hakuwa na ndugu, basi hata mkewe pia hakuwa na ndugu waliojitokeza kwenye msiba mzito kama huu wa kufiwa na mume?
Lakini ule haukuwa wakati wala mahala muafaka.“Pole sana shemeji...” Ndilo neno pekee lililomtoka. Kwa mara nyingine yule mwanadada alitikisa kichwa kisha akainua uso wake na kumtazama kutokea nyuma ya miwani yake myeusi. Meja Babu naye alimtazama na huku akiwa amebana midomo yake kwa nguvu kujizuia asiangue kilio, alimtikisia kichwa kumuaga na kuanza kuodoka.
“Shemeji...” Mke wa Vampire alimkamata mkono wake kwa nguvu huku akimwita.
“Naam, bibie...wasemaje?” Alimgeukia na kumuuliza kwa upole. Yule mwanadada alitoa miwani yake usoni na kumtazama kwa macho mekundu na yaliyovimba kwa kulia.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Ulikuwa vitani na mume wangu kule Sierra Leone...”Alimwambia, na kwa muda Swordfish hakuelewa iwapo lile lilikuwa ni swali au vinginevyo.
“Eem...ndiyo,tulikuwa pamoja...”
Kimya kifupi kilifuata, na Swordfish alianza kuuliza iwapo ni hicho ndicho alichotaka kumueleza wakati yule mwanadada alipoongea.
“Nime...” Alianza kwa sauti ya chini, kisha akafumba macho na kuinamisha kichwa chake huku akijishika paji la uso kwa muda, halafu akainua tena uso wake na kumtazama usoni yule shujaa wa makabiliano ya ana kwa ana katika medani za vita, “...nimeambiwa kuwa mume wangu ameharibika vibaya na hivyo siwezi kumuona wakati nikimuaga kwa mara ya mwisho....”
Halikuwa swali. Ilikuwa ni kauli, kama kwamba alikuwa anampa taarifa ambayo haifahamu.
“Ndiyo...ni kweli, kwani...”
“Alikufaje shemeji?” Yule mwanamke alimuuliza kwa upole bila ya kumtazama, na Meja Babu alibaki akimkodolea jicho kwa mshangao. Yule mwanamke aliinua uso wake na kumtazama usoni.“Mume wangu alikufaje huko shemeji, eenh? How did he die, hata iwe vigumu mimi kumuona, eenh? Ni kifo kibaya kiasi gani hata-”
“Shemeji!” Swordfish alimkemea kwa sauti ya chini, na yule mwanamama alimnyamaza ghafla. Swordfish alimtazama kwa jicho kali kwa muda.
“Mumeo amekufa kishujaa. Hicho ndicho kitu cha muhimu na cha faraja kubwa kwako na kwetu sote! Kuna wapiganaji wanaokwenda vitani na wanakufa vifo vya aibu, vifo vya woga au wanakufa wakiwa wasaliti! Na hicho ni kifo kibaya kabisa kwa mwanajeshi yoyote. Mumeo hakuwa miongoni mwa hao.Yeye amekufa akiwa mpiganaji jasiri aliyeliweka mbele taifa lake kabla ya kitu kingine chochote hapa duniani! Mumeo alikuwa mpiganaji! Na hilo ndilo unalotakiwa ukae nalo kichwani mwako maisha yako yote!”
Baada ya kusema hayo, alipiga hatua moja nyuma na kujikakamua kijeshi mbele ya yule mwanamke bila ya kusaluti, na kurudi mahala pake akimuacha yule mwanamke akilia kwa kwikwi. Muda mfupi baadaye, waziri wa ulinzi aliongoza msafara wa kwenda kutoa heshima za mwisho kwa wale marehemu wawili, na nusu saa baadaye, msafara uliondoka pale uwanjani kuelekea makaburini kwa mazishi.
Ndugu walilia huku wao na watanzania kwa ujumla, wakiamini wale walikuwa ni mashujaa waliokufa katika kulitumikia taifa lao. Jeshi likatoa heshima zote za maziko kwa wale wapiganaji wawili, mmoja akiwa msaliti aliyezikwa na siri yake. Mwingine akibaki kuwa mzalendo kwa taifa lake
MDUNGUAJI
daima. Ukweli wa matukio yaliyotokea kule msituni ukibaki kwenye mafaili yao yaliyoletwa nchini kutoka Sierra Leone na Brigedia Stanslaus Kahemela. Kesi imefungwa. Imezuiliwa.
SEHEMU YA PILI
DAR ES SALAAM, MIAKA MITATU BAADAYE
Ndege kubwa aina ya Boeing 767 ya shirika la ndege la Kenya ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam.Muda ulikuwa ni saa nne za asubuhi. Miongoni mwa abiria walioteremka kutoka kwenye ndege ile, walikuwamo mwanamume mmoja mrefu, mwenye mwili uliojengeka kimazoezi aliyetembea kwa kuchechemea kidogo, na mwanamke mmoja mzuri aliyeweza kufananishwa na binti wa urembo. Kila mmoja akiwa na begi moja tu mkononi mwake, wawili wale walitoka nje ya uwanja ule na kutazama huku na huko kutafuta teksi.
Yule mwanamume alikuwa na alama ya mshono iliyokuwa kama herufi “Y” kwenye paji lake la uso...kutokea juu kidogo ya jicho lake la kushoto hadi karibu na zinapoanzia nywele zake. Alikuwa amevaa miwani myeusi ya jua iliyoacha ile sehemu ya juu ya mshono ule ikichomoza juu ya kingo za miwani ile.
Walikuwa wamesafiri kutokea Liberia, wakapita Senegali na kwenda moja kwa moja hadi Uholanzi ambako baada ya kusubiri katika nchi ile kwa saa mbili waliunganisha kwa ndege ya shirika la KLM hadi Nairobi ambako walipitisha usiku. Asubuhi iliyofuata waliruka tena kwa Kenya Airways hadi Tanzania, ambapo ndipo lilikuwa kusudio la safari yao.
Yule msichana alikuwa mfupi kidogo kuliko ambavyo binti wa urembo alivyotakiwa awe, hasa kwa nchi za ulaya, ingawa kwa hapa nchini kwetu angeweza tu kuingia kwenye mashindano ya urembo na kushinda. Alikuwa na sura ya kuvutia, miguu iliyojazia kiasi cha kutosha bila kuchusha. Matiti yake ya wastani hayakuwa mzigo kwa kiuno chake chembamba kilichotulia vizuri sana juu ya mapaja yaliyoviringika ipaswavyo. Mapaja yale yaliweza kumletea mtazamaji hamu ya kuendelea kuyatazama, hasa kwa jinsi yalivyobanwa ndani ya suruali nyeusi ya jeans na kutanukia pembeni kiasi cha kuleta ile taswira ya kuvutia sana.
Yule mwanamke, naye akiwa amebandika miwani ya jua usoni, alikuwa amezungusha kiwiko cha mkono wake mkononi mwa yule mwanamume na
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
haikuwa na shaka kabisa kuwa wawili wale walikuwa ni aidha mume na mke, au mtu na mpenzi wake.
Kinyume na muonekano wao wa kujiamini,wawili wale walikuwa na wasiwasi mkubwa mioyoni mwao. Mioyo ilikuwa ikiwapiga kwa hofu iliyokuwa imewapungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na ilivyokuwa wakati wakianza safari yao kule Liberia, nchi iliyojaa machafuko ya kila aina. Hofu ile iliendelea kuwa nao walipokuwa Uholanzi wakisubiri kubadili ndege, ikapungua kidogo walipoweza kuingia Kenya na ikaendelea kuwepo wakiwa ndani ya uwanja ule wa kimataifa wa Dar es Salaam.
Wakiwa pale nje ya uwanja, ile hofu ilikuwa inaelekea kuisha, lakini hakika bado ilikuwapo.Hakuna aliyeongea hata kidogo, wote walikuwa wakisubiri kuingia ndani ya gari na kupotelea jijini kabla hawajaanza kuongea lolote.
Jamaa alimuongoza yule binti hadi kwenye moja ya teksi nyingi zilizoegeshwa pale nje ya uwanja, akidharau miito ya madereva wengi wa teksi waliokuwa wakiwaitia kwenye magari yao.
Alifungua mlango wa nyuma wa lile gari aina ya Toyota Mark II na kumuacha yule binti aingie, kisha naye akaingia kule nyuma na kuketi pamoja naye.
“
Eeeh...speak kiswahili...?” Dereva aliuliza kwa kiingereza kilichoonekana wazi kuwa ni cha kuombea maji. Alijua kuwa hakukosea kutumia lugha ile ya kigeni kwa wale watu, kwani hakika hawakuelekea kuwa ni watanzania. Walionekana kuwa ni raia wa nchi moja wapo ya Afrika, lakini sio Tanzania, kwa jinsi walivyoonekana, walivyotembea na walivyojiweka mbele za watu pale uwanjani.Walionekana wageni waliogubikwa woga wa kigeni katika nchi ngeni.Hivyo dereva wa teksi moja kwa moja alijua kuwa wale walikuwa wageni na alikuwa amejiandaa kuwapa bei ya wageni, tena ikiwezekana kwa dola!
“Endesha gari dereva! Kwa nini tusiongee kiswahili?” Yule mwanaume alimjibu kwa sauti nzito na tamaa ya kupata dola ikamyeyuka dereva wa teksi.
“Oh! Kumbe ni wabongo wenzetu? Mnaonekana kama wasauzi bwana! Ama kweli mtoni hakuongopi babaake! Mambo vipi lakini wazee?” Alijichangamsha huku akiliondoa lile gari kutoka pale uwanjani.Hakujibiwa.
Kule nyuma wale abiria wake walitazamana na yule mwanaume alimbinya goti yule mwanamke kama ishara ya kumpa moyo.Yule mwanamke alishusha
pumzi ndefu na kuegemeza kichwa chake begani kwa yule mwanamume, ambaye aligeuka nyuma na kutazama kule walipokuwa wakitokea kupitia
kwenye kioo cha nyuma cha lile gari. Hakuona gari lolote lililoonekana kuwafuata, na akaamini kuwa walikuwa wamefanikiwa kutoka salama pale
MDUNGUAJI
uwanjani.Akamzungushia mkono begani yule binti na kumkumbatia kwa namna ya kumliwaza zaidi.Sasa hofu ilipotea kabisa. Baada ya misukosuko mingi katika nchi ngeni,hatimaye walikuwa wamerejea nyumbani salama... kama jinsi alivyomuahidi yule binti.
Bila ya wao kujua, nyendo zao zote zilikuwa zikifuatiliwa kwa makini sana na mtu mmoja mfupi na mnene aliyekuwa kwenye gari dogo aina ya Toyota Corolla lililokuwa limeegeshwa miongoni mwa zile teksi zilizokuwa pale uwanja wa ndege.
Ile teksi waliyopanda ilipoanza kuondoka pale uwanjani, yule mtu mnene alitoa simu yake ya kiganjani na kupiga namba fulani kabla ya kuiweka sikioni kwake.
“Nipe habari!” Sauti kwenye simu ilisema.
“Taarifa zako zilikuwa sahihi...jamaa kaingia nchini!” Mtu mnene alisema kwenye ile simu akiwa ameibana sikioni kwake kwa kichwa na bega lake, ilhali kwa mkono wake wa kulia akiandika namba ya ile teksi iliyowabeba wale wasafiri wawili walioingia nchini punde.
Kimya kilitawala kutokea upande wa pili wa simu ile, na mtu mnene alitaka kumuuliza mtu aliyekuwa akiongea naye iwapo bado alikuwapo, wakati yule mtu alipouliza.
“U-una hakika?”
“Asilimia mia moja! Amebadilika kidogo sana, na anatembea kwa kuchechemea, lakini ndiye hasa!”
“Sh-hiiit! Hii sasa inaharibu kila kitu...!”
“Na kwa hilo pia uko sahihi mzee...maana hakika jamaa kaingia jijini...au labda niseme nyoka kaingia nyumbani?”
“Yeah! Nyoka...tena nyoka mwenyewe Koboko! Nyoka mkimya na mpole karibu ya bwege, lakini mwenye sumu kali sana...ndiyo huyo jamaa! Hatari sana! SHIIIIIIIIT!” Sauti ilimjibu na mtu mnene alisikia kishindo kikifuatia kauli ile na akafinya uso, akiijua kuwa upande wa pili wa simu ile, kuna meza iliyobondwa kwa hasira na yule mtu aliyekuwa akiongea naye.
Kimya kilitawala, na ile teksi waliyopanda wale wageni ikapotea kutoka kwenye upeo wa macho ya yule mtu mnene. Akaondoa gari lake taratibu na kwa hiyo kuiona tena ile teksi ikikunja kulia, kuelekea katikati ya jiji.
“Umepata uelekeo wao?”
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Yep! Ameambatana na binti mmoja ambaye simtambui, na wanaelekea mjini, wamo ndani ya teksi aina ya Toyota Mark II...” Mtu mnene alijibu na kuendelea kumtajia yule muongeaji wa kwenye simu namba za ile teksi waliyopanda wale watu.
“Okay...wenzetu wako huko mbele na nitawapa hii namba sasa hivi! Wewe kazi yako imekwisha.” Sauti ilijibu. Mtu mnene aliiweka pembeni simu yake na kuondoka eneo lile, akichukua uelekeo tofauti kabisa na ule uliochukuliwa na ile teksi iliyowabeba wale wasafiri wawili.
Wazazi wake walimpa jina la Badru, hivyo akawa anaitwa Badru Gobbos kwa sababu baba yake alikuwa akiitwa Gobbos. Hapo nyuma aliwahi kutumia muda mwingi kufikiri ilikuwaje hata baba yake akapata jina la Gobbos, lakini kadiri miaka ilivyokuwa ikipita, jina lile likawa la kawaida kwake, na hata akafikia hatua ya kulipenda sana, kwa sababu lilionekana tofauti na majina mengi ya kibantu na hivyo alijiona kuwa si wa kawaida.Utotoni mwake kote wenzake walipenda kumkata jina na kumwita Badi. Matokeo yake hata yeye mwenyewe akatokea kulipenda jina lile pindi litamkwapo–Badi Gobbos!Lilileta ladha fulani kinywani, na ndiyo sababu hata alipopelekwa kuandikishwa shule kwa mara ya kwanza na mjomba wake, na kuulizwa jina alijibu bila hofu.
“Badi Gobbos.”
Na mwalimu aliyekuwa akiandikisha majina siku ile aliliandikaa hivyo hivyo!Alipofika muda wa kujiunga sekondari, alijaribu kuandikisha jina lake halali kwa shinikizo la wazazi wake, lakini tayari cheti cha darasa la saba kilimtambulisha kama Badi Gobbos, hivyo haikuwezekana, na jina la Badi Gobbos likashamiri.
Alipofikia muda wa kujiunga na elimu ya juu katika chuo kikuu cha Makerere, alienda kubadilisha jina lake kisheria–kuwa Baddi Gobbos, akiongezea “d” moja kwenye jina lake la kwanza.Na tangu wakati huo hadi wakati akitoka nje ya ule uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam aliendelea kuwa Baddi Gobbos.Lakini hiyo ilikuwa kichwani na moyoni mwake, kwani mara kadhaa amejikuta akitumia majina mengine tofauti kutokana na kazi zilizokuwa zikimkabili.
Akiwa ndani ya ile teksi alijikuta akimshukuru sana Mungu kwa kuwavusha salama katika miji yote waliyolazimika kupitia hadi kufika Tanzania, na pia kuwapitisha pale uwanja wa ndege wa Dar es Salaam bila ya tatizo lolote.
MDUNGUAJI
Hii ilitokana na ukweli kwamba walisafiri kwa majina bandia, wakiwa kama mke na mume, bwana na bibi Lamaye Walo, raia wa Senegali, waliokuwa wakijishughulisha na biashara ya nguo za asili za kiafrika, na walikuwa wamekuja Tanzania kuangalia uwezekano wa kuanzisha biashara hiyo hapa nchini.
Kama mtu angetaka kuthibitisha hilo, angegundua kuwa ndani ya mabegi yao, kulikuwa kuna nguo kadhaa za kiasili za kiafrika, ambazo zilikuwa za mfano kwa biashara yao. Pasi za kusafiria walizotumia zilikuwa za kughushi na zilizogharimu pesa nyingi sana, na ndiyo kilikuwa kiini cha hofu yao muda wote wa safari ile ndefu na ya mashaka.
Lakini sasa waliona matunda ya pesa walizotumia kwa kutengeneza pasipoti zile. Kwani kila walipopita zilipitishwa bila shaka yoyote, na hatimaye walikuwa wamerudi nyumbani...ambako walipoteza kabisa matumaini ya kurejea.
Ingawa walikuwa wakisafiri kama mke na mume, na kulikuwa na kila dalili kwamba walikuwa wakihusiana kimapenzi, kuwa kwao pamoja kulitokana na kila mmoja kumhitaji mwenzake ili kutimiza lengo lao la kurudi Tanzania kutoka kwenye nchi ngeni walikokutana katika mazingira magumu kabisa.
Sasa kila mmoja alikuwa anafikiria jinsi atakavyoachana na mwenzake na kushika hamsini zake, ilhali ndani kabisa ya mioyo yao, wakijua kuwa waliyopitia wakiwa pamoja yalikuwa yamewafunga milele, na wasingeweza kuachana kirahisi kama ambavyo walikubaliana wakati wakianza mipango ya safari hii huko Liberia miezi mingi iliyopita.
Akiwa amemkumbatia yule binti ndani ya ile teksi, Baddi Gobbos aliifikiria familia yake, na moyo ulimwenda mbio kwa matarajio ya kuiona tena familia yake baada ya kutengana nayo kwa muda mrefu...
Kutokea kule mbele dereva aliwauliza uelekeo.
“Ubungo... nyumba za Shirika la simu...” Baddi Gobbos alijibu bila kusita kutokea kule nyuma, kisha akaongezea, “Itakuwa kiasi gani...?”
Kabla yule dereva hajajibu, yule binti alidakia,“Ayyaah...si tumesahau kuchenji pesa? Sasa tutamlipaje...?”
Dereva aliachia tabasamu pana kule mbele, kumbe bado alikuwa na nafasi ya kujivunia dola kutoka kwa hawa jamaa.
“Pesa ipo...tutamlipa,”Jamaa alimjibu yule binti kwa sauti ya chini, na kupaza sauti yake kwa yule dereva, “E bwaa’ tuambie basi...kiasi gani?”
“Elfu kumi na tano bosi!”
“Hiyo ina maana ni shilingi elfu nane, kwa kukusaidia tu, tutakupa elfu kumi!” Baddi Gobbos alijibu kutokea kule nyuma.Dereva alifunua kinywa
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
kutaka kupinga kauli ile, lakini hapo aliona mkono wa yule jamaa ukimpitishia dola ya kimarekani kutokea kule nyuma.
“Na kwa kuwa hatuna pesa ya Tanzania kwa sasa, tutakupa dola kumi, ambayo nina hakika ni zaidi ya hizo elfu kumi nilizosema...” Alimwambia. Dereva alimeza mate na kuinyakua ile pesa haraka, huku akiendelea kuendesha.
“Ah, lakini ujue unaniua hivyo bosi wangu...!”
“Ndiyo najua...”
“Sasa...nifikirie kidogo basi....ongeza kidogo bwana...”
Hakupata jibu lolote, na akajua hakutakuwa na ongezeko lolote. Akaamua kuendelea na safari, alichopata si haba.
Safari ikaendelea kimya kwa muda, kisha yule binti ambaye jina lake halisi lilikuwa ni Gilda Shehoza, ingawa alisafiri kwa pasi iliyomtambulisha kama
Olga Lamaye Walo, aliinua uso wake na kumtazama yule bwana kwa muda, kisha akamwambia, “Na...naona ndiyo tumefika... sasa itabidi tuachane...”
“Twende kwanza nyumbani kwangu...huko tutaongea vizuri...uonane na mke wangu na familia yangu kwa ujumla. Kisha tutaagana. Si ndivyo tulivyokubaliana bwana?” Baddi alimjibu.
“Ndiyo.Lakini...naogopa Baddi...mkeo!”
“Hakuna jinsi Gilda! Njia yoyote kinyume na hii itakuwa mbaya sana kwetu. Lazima afahamu kuwa tulikuwa pamoja huko na tulilazimika kuwa wote na ndiyo maana tumefika hapa leo hii. Tukijaribu kufanya siri italeta matatizo yasiyo ya msingi Gilda. Yaliyotokea baina yetu huko nyuma yamepita, sasa tunarudi tena kwenye maisha yetu kabla ya kukutana kwetu...” Baddi alimjibu taratibu lakini kwa msisitizo. Gilda alionekana kutoridhishwa kabisa na maneno yale. Alitaka kuongea kitu, akasita. Akajiinua kutoka begani kwa Baddi na kutazama nje ya dirisha. Baddi naye aligeukia dirisha lililokuwa upande wake na kutazama huko nje huku akiwa ameuma mdomo wake na uso ameukunja kwa mawazo mazito.
Mke wangu...familia yangu...Gilda...
“Tumefika bosi...”
Mawazo yake yalikatishwa na dereva wa teksi.Aligeuza uso wake na kuona ni kweli walikuwa wamefika. Alimuelekeza dereva hadi kwenye geti lililokuwa linaelekea kwenye jengo ambamo alikuwa akiishi kabla hajaenda kule ugenini alipokutana na yule binti wa aina yake.
Wakiwa wamesimama mbele ya lile geti Baddi alishangaa kukuta limefungwa kwa kufuli kubwa, na mara moja akajua hali haikuwa sawa.Eneo lote lile lilikuwa kimya sana, jambo ambalo si la kawaida.
MDUNGUAJI
“Vipi?” Gilda alimuuliza.
“Ajabu...mbona geti limefungwa?” Alisema, hisia zake zote za tahadhari zikiwa makini, akichungulia ndani ya lile geti kulikokuwa na majengo kadhaa ya ghorofa, mojawapo ndimo alimokuwa akiishi na familia yake.Hakuona mtu hata mmoja.
“Hey! Nini pale?” Sauti kali ya kiaskari iliwashitua kutokea nyuma yao. Waligeuka na kuona mlinzi wa mgambo akiwafuata hali ameshika bunduki aina ya SAR mkononi.
“Oh Shiit, what is this now...?” Baddi alisema kwa sauti ya chini huku akimtazama yule mgambo na moyo ukimwenda mbio. Gilda alijisogeza karibu yake na kubaki akimkodolea macho yule mgambo. Baddi alimeundea yule mgambo taratibu, akiliacha begi lake chini.
“Mna shida gani hapa nyie?” Mgambo aliuliza tena, sasa akiwa amemfikia Baddi pale alipokuwapo.
“Habari yako ndugu...” Baddi aliamsalimu na kuendelea bila ya kusubiri jibu la salamu yake, “...tunataka kuingia humu ndani, sasa tumekuta geti limefungwa!”.
Yule mgambo alimtazama kwa muda kama kwamba alikuwa anataka kujithibitishia kuwa yule mtu aliyesimama mbele hakuwa akifanya masikhara.
“Mnataka kuingia humu ndani? Ndani wapi hasa mnapokusudia kuingia?”
Mgambo alimuuliza huku akimkazia macho. Baddi Gobbos alimtazama kwa muda bila ya kusema neno huku akiuma meno kujaribu kudhibiti ghadhabu zilizoanza kumpanda, kwani hakuona sababu ya yule mgambo kuwahoji maswali mengi badala ya kuwasaidia. Gilda alisogea na kusimama tena kando yake, na macho ya yule mgambo yakahamia kwake kwa muda, na yakaonekana kuvutiwa sana na yalichokiona, kisha yakarudi tena kwa Baddi,dhahiri kwa kujilazimisha tu.
“Mimi ninaishi...familia yangu inaishi kwenye moja kati ya majengo hayo humo ndani...Block F, sasa nashangaa nimekuta geti limefungwa...na kuko kimya sana...!” Baddi alimueleza yule mgambo kwa utaratibu akijitahidi
kudhibiti jazba zilizokuwa zikimpanda kadiri muda ulivyokuwa ukienda.
Alikuwa amekuja kuonana na familia yake aliyotengana nayo kwa muda mrefu, sasa anakuta mazingira yasiyoeleweka, na huyu mgambo naye analeta kiswahili kirefu. Mgambo alimtazama kwa mashaka na kurudi nyuma hatua moja.
“Ee bwana unafanya masihara na mimi nini? Au unataka kuleta utapeli wa kizamani hapa?” Alimuuliza huku akiiweka sawa bunduki yake. Gilda
alimkamata Baddi mkono kwa hofu na kukunja uso akimtazama yule mgambo
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI kwa macho ya kuuliza. Baddi ndiyo alizidi kuchanganyikiwa.
“Akh...! Kwani vipi bwana, mbona na mi’ kama sikuelewi? Humo ndani kuna watu au hamna? Kwa nini geti limefungwa...? Na kwa nini...”
“We’ unajua hizi ni nyummba gani lakini? Isiwe umepotea njia...” Mgambo alimkatisha na Baddi alitupa mikono hewani kwa kuchoshwa na hali ile.
“Bwana, hizi ni nyumba za shirika la simu...na mimi ninaishi humo na familia yangu kwa sababu mke wangu ni mfanyakazi wa shirika hilo! Sasa unapotaka kuniambia kuwa nime-”
“Aaaah? We’ bwana unaonekana unatoka safari...siyo?” Mgambo alimkatisha na Baddi akazidi kughadhibika,lakini mara moja kengele ya hatari ikagonga kichwani mwake.
Mbona maswali yanazidi...? Kwa nini? Lazima kuna kitu hakipo sawa...
“Mmnh! Baddi...mbona hivi tena?” Gilda aliuliza kwa wasiwasi. Baddi alimuashiria kwa kiganja chake atulie bila ya kumuangalia, na kumjibu yule mgambo.
“Nimekuwa nje ya nchi kwa miaka kama mitatu hivi, na leo ndiyo narudi... ila mke wangu atakuwemo hum-”
“Ah! Basi nd’o maana ati!...Pole sana bosi, lakini hizi nyumba sasa hivi hazina wakaazi kabisa!” Mgambo alimjbu na Baddi aliachia kinywa wazi huku akimkodolea macho.
“Kwamba...?” Hatimaye aliuliza kwa mshangao, akili ikimtembea na moyo ukimwenda mbio.
“Ndiyo hivyo bosi...humo hamna tena watu siku hizi! Wote wamehamishwa...”:
“Wamehamishwa na nani wewe? Mi’ nakwambia hizi nyumba za shirika la simu na mi’ familia yangu...” Baddi alimjibu huku akirudi tena kule kwenye geti na kujaribu kuchungulia ndani ya ule uzio.Mgambo alimtazama kwa masikitiko, na kumtazama Gilda, ambaye alikuwa amehamanika kupita kiasi.
“Ah! Sasa hii inawezekana vipi lakini?” Alimuuliza yule mgambo kwa wasiwasi, na muda huo Baddi alirudi pale walipokuwa.
“Hebu niambie vizuri mzee...inakuwaje hii hali? Kwani kweli naona hakuna dalili ya watu humo ndani...”
“Ah, Mi sijui...Kampuni imeuzwa sijui, au sijui imebinafsishwa...nyumba zimeuzwa! Watu imebidi wahamishwe bwana...!” Mgambo alijibu kienyeji tu kama kwamba anaongelea jambo la kawaida sana, wakati anaongelea jambo la maisha ya watu kuharibika moja kwa moja.Baddi alimtazama kwa muda bila ya kusema neno, huku akili yake ikijaribu kuelewa maana ya maneno yale.
MDUNGUAJI
Nyumba zimeuzwa! Watu wamehamishwa!
Gilda alimtazama na kuona kuwa alikuwa amechanganyikiwa, hivyo akaamua kunyamaza kimya kwanza.
“Akkh! Sasa...Oke, sawa. Watu wamehamishwa. Watakua wamehamishiwa wapi sasa?” Hatimaye aliuliza kwa wahka mkubwa.
“Huyo hawezi kujua Baddi...” Gilda alidakia, na muda huohuo na yule mgambo naye akajibu.
“Ah! Sasa mi’ n’tajuaje mzee? Mi’ mlinzi tu hapa...”
Baddi alijua kuwa alikuwa amechanganyikiwa. Na pia alijua kuwa ni lazima atulie...ama sivyo atashindwa kabisa kufikiri.
“Hanma sehemu nyingine tunayoweza kuwapata Baddi?” Gilda alimuuliza taratibu huku akimshika mkono.
“Hakuna...si unajua?” Baddi alijibu huku akiinua begi lake na kuliweka begani.
“Yeah..lakini sasa, yaani hakuna hata jamaa yoyote ambaye anaweza kujua mahala ambapo...mkeo...atakuwa amekwenda baada ya kutoka hapa?”
Baddi alijaribu kufikiri kidogo, lakini bado akili ilikuwa kama iliyosinyaa.
Hakuna jina lolote lililomjia kichwani kwa muda ule.
“Ah, hapana...ni muda mrefu sana...” Hatimaye alijibu kwa fadhaa, na Gilda aliona kuwa Baddi alikuwa kwenye wakati mgumu. Alimtazama kwa muda, naye akinyanyua begi lake. Alikumbuka kuwa walipokuwa Liberia, Baddi alimueleza juu ya mkewe, ya kwamba hakuwa na ndugu hata mmoja, baada ya familia yao yote kuangamia kwenye ajali mbaya ya MV Bukoba miaka kadhaa huko nyuma wakati wakitoka kwenye msiba wa mama yao. Kilichomuokoa huyo dada ambaye baadaye alikuja kuwa mkewe ni kwamba muda huo yeye alikuwa nje ya nchi kimasomo na hakuweza kabisa kuja kuhudhuria msiba ule.
Moyo wake ulimuendea yule bwana na alitamani amkumbatie kumliwaza, lakini alijua hilo jambo halikuwepo tena baina yao.Walishakubaliana hivyo, na wote walikuwa wana wajibu wa kutimiza makubaliano yao.
“Sasa tunafanyaje Baddi?” Aliuliza.
“Twende zetu!” Baddi alijibu kwa mkato na wakaanza kuondoka eneo lile. Gilda alichukua jukumu la kumshukuru na kumuaga yule mgambo. Walitembea kwa muda kidogo kuielekea barabara ya Mandela kutokea kwenye ile njia ya vumbi iliyokuwa ikitokea kule kwenye geti la uzio wa zile nyumba.
“Nadhani itabidi twende hoteli kwanza Gilda...” Hatimaye Baddi alisema.
“Okay...” Gilda alijibu.
“Nadhani tukishatulia kidogo huko, tutajua nini cha kufanya...nitajua pa
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI kuanzia kuwatafuta...” Baddi aliongezea.
“Ah! Baddi...ina maana huwezi kabisa kufikiri ni wapi wanaweza kuwa wameenda...?”
“Nadhani sehemu ya kuanzia itakuwa kule ofisini kwake...bila shaka wanaweza kuwa na habari zake...lakini nadhani kwanza tutafute hoteli ya kufikia...”
“Sawa...kwa hiyo...tutaenda hoteli gani sasa?” Gilda aliuliza.
“Ah...nina kijarida vya mahoteli kadhaa ya Afrika mashariki nilichochukua ndani ya ndege...”
Sasa walikuwa wamesimama kando ya ile barabara kuu ya Mandela na kila mmoja alianza kutazama huku na huko kuona kama kuna teksi inakuja. Lakini walikuwa wakiona mabasi ya abiria tu. Baddi aligeuka upande wa kutokea Ubungo na kujaribu kutazama iwapo kulikuwa na teksi itokeayo upande ule ili aisimamashe, wakati Gilda alikuwa amegeukia upande wa kutokea Mwenge. Magari yalikuwa yakipita tu na hakuna hata moja lililoelekea kuwa ni teksi. Mara Gilda aliona gari dogo aina ya Toyota Corolla likitokea kule maeneo ya Mwenge na mara moja akaanza kulipungia. Lile gari lilianza kupunguza mwendo na kuoneshea taa ndogo kuwa lilikuwa linaelekea kuegesha ule upande waliokuwapo.
“Teksi hiyo Baddi...” Gilda alisema, na Baddi akageuka na kuliona lile gari. Aliweka begi lake chini na kuanza kufungua zipu ya pembeni akitaka kutoa kile kijarida kidogo cha utalii kilichokuwa na habari za mahoteli mazuri ya Afrika Mashariki. Wakati anafanya hivi, alikuwa ameinama huku bado kichwa chake kikiwa na mawazo mengi.
Ghafla, wakati ile teksi ikiwa kiasi cha kama hatua kumi na tano tu kutoka pale walipokuwa, gari jingine aina ya Toyota Starlet lilichomoka kwa kasi sana kutokea nyuma ya ile teksi na kuipita kwa upande wa kushoto, ikivunja taratibu za barabara na kuelekea pale ambapo Baddi Gobbos alikuwa ameinamia begi lake. Gilda aliona jambo lile na alibaki mdomo wazi kwa muda na kabla hajatanabahi lile gari lilimpitia kwa kasi kubwa kiasi cha hatua si zaidi ya mbili kutoka pale alipokuwa amesimama,naye akaruka nyuma huku akili yake ikimuendea Baddi.
Baddi alikuwa akiinuka kutoka pale alipokuwa amechutama huku
akijishughulisha kulifunga begi lake, mkononi akiwa ameshika kile kijarida alichokuwa akikitafuta na lile gari likielekea kumgonga.
Baddi anagongwa...!
“BADDIIIIIIIIIH!” Alipiga kelele huku akianguka kinyuma nyuma.
MDUNGUAJI
Baddi alishituka na kuona lile gari likimuendea kwa kasi sana, na alijua kuwa alikuwa anagongwa. Muda huo huo yule dereva wa ile teksi iliyokuwa
ikielekea kuwachukua akakanyaga breki kali na kupiga honi kubwa.
Baddi aliigeukia ile Starlet na huku akipiga kelele za woga na mshituko, alijitupa kando mbali kadiri alivyoweza kujaribu kujiokoa na kifo kile
kilichokuwa kikimuendea kwa kasi kubwa.Starlet ilimgonga mkono wake na kulitupa hewani begi lake. Alibwagwa chini kwa kishindo, maumivu makali yakimtambaa mwilini kutokea pale mkononi alipogongwa. Alijigeuza haraka pale chini na kulitazama lile gari lililomkosa kwa sekunde tu.Aliishuhudia ile Toyota Starlet ikiyumba huku na huko na kwenda kujikita kwa kishindo kwenye mti uliokuwa kando ya ile barabara.
Gilda aliinuka na kumkimbilia huku akipiga kelele za woga. Baddi alijiinua huku hisia zake zote zikiwa zimewamba, moyo ukimwenda mbio na damu ikimchemka, maumivu yaliyokuwa yakimpata mkononi mwake yakisahaulika kabisa.
Mayowe ya watu yalisikika kutokea kila upande na aliona watu wengi wakikimbilia eneo lile, hata hakujua walitokea wapi. Alimuona dereva wa ile
Starlet akifungua mlango na kuanguka nje, kisha bila hata ya kuangalia kama
kuna madhara yoyote aliyosababisha kwa wapita njia, alitimua mbio.
“Eh! HHEY! Heeeeeey...!” Baddi aliita kwa sauti huku akianza kumkimbiza, lakini hapohapo Gilda alikamkamata mkono na kumziuia.
“Mwache Baddi!Haina...”
“No! Niachie bwana! Yule mshen-”
“Haina haja Bad-”
Mara kishindo kingine kikubwa kilisikika,kikiambatana na mkwaruzo mkali wa tairi za gari zikisuguana na lami, na yowe kubwa la woga na uchungu. Kwa mduwao mkubwa kabisa walimshuhudia yule dereva mbaya akitupwa hewani baada ya kugongwa na gari jingine aina ya Toyota Land Cruiser!
“Ebwana we!” Baddi aliropoka bila ya kujitambua huku akimshuhudia yule dereva akianguka kwa kishido juu ya ile LandCruiser na kutupwa katikati ya barabara. Daladala aina ya Hiace kipanya lililokuwa nyuma ya ile Land Cruiser lilijitahidi kufunga breki, lakini likashindwa na kumkanyaga yule dereva aliyeangukia pale barabarani!
Gilda aliachia kilio cha woga huku akijiziba macho, na Baddi aliachia kauli nyingine ya mshangao huku akiishuhudia ile Land Cruiser ikiongeza kasi na kutoweka eneo lile.
Mtafuruku uliofuatia haukuwa mdogo.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Watu walikuwa wakikimbilia kule alipoangukia yule dereva mbaya aliyegongwa na dereva mwingine mbaya zaidi, kila mmoja akipiga kelele anazozijua. Msongamano mkubwa wa magari ukajitokeza.Baddi alimgeukia Gilda.
“Uko salama...?”
“Wewe! Wewe uko sala-”
“Mimi mzima...mkono wangu tu...” Alijibu huku akikusanya baadhi ya vitu vichache vilivyotupwa nje ya begi lile, kisha akasogea pale kwenye kundi la watu waliomzunguka yule jamaa aliyegongwa na ile Land Cruiser. Alijipenyeza kwenye lile kundi na kuchungulia kupitia juu ya mabega na vichwa vyao.
Hakuwa amepata kumuona yule mtu hata siku moja, lakini hakuhitaji kuambiwa kuwa yeyote aliyekuwa, yule mtu alikuwa amekufa.
Muda huo Gilda alifika na kumchomoa kutoka kwenye lile kundi.“Tuondoke hapa Baddi...teksi yetu bado iko pale...” Baddi alitaka kubisha, lakini alipoona jinsi uso wa yule binti ulivyokuwa na woga, akabadili mawazo.Alimfuata haraka kuelekea kwenye ile teksi huku akili yake ikizidi kufanya kazi kwa kasi kuliko uwezo wake, kwani hakuwa na shaka kabisa kuwa yale matukio hayakuwa bahati mbaya. Yule dereva wa mara ya kwanza alikuwa amedhamiria
kumgonga yeye...makusudi!
Kwa nini?
Lakini kibaya zaidi ni uhakika aliokuwa nao kuwa na ile ajali iliyomkuta
yule dereva pia haikuwa ya bahati mbaya.Ilikuwa ni ya makusudi vile vile...!
Kwa nini...?
Alichanganyikiwa kweli kweli.
Walimuomba dereva wa ile teksi awapeleke kwenye hoteli yoyote ya bei nafuu na nusu saa baadaye walikuwa ndani ya chumba cha hoteli moja iliyojificha maeneo ya magomeni jijini Dar.Baddi alikuwa amejiinamia kitandani, akili ikimzunguka kutokana na mambo waliyokutana nayo kule Ubungo, wakati Gilda alikuwa amejikunyata kwenye kochi lililokuwa mle chumbani.
“Yule mtu alitaka kukugonga makusudi!” Hatimaye Gilda alisema kwa sauti ya chini iliyojaa hofu.
“Najua...na yeye pia amegongwa makusudi na ile Land Cruiser!”
“Oh, Baddi...ni nini kinaendelea lakini sasa? Mambo haya yanamaanisha nini...?”
MDUNGUAJI
“Sijui Gilda...lakini...”
“Hawa watakuwa ni watu wanaokufahamu Baddi na...na wana kisa na wewe...”
“Haiwezekani Gilda. Mi’ nimekuwa nje ya nchi kwa miaka mitatu, na kabla ya hapo sikuwa na uhasama na mtu yeyote!” Baddi alikana.
“Lakini sasa itawezekanaje mtu ufike tu nchini baada ya kutokuwepo kwa muda wote huo halafu watu waanze kukuandama hivi? Lazima itakuwa...”
“Kwanza mke wangu yuko wapi?” Baddi alimkatisha ghafla. Alikuwa amehamanishwa na mchanganyiko wa matukio yale ya kushtusha. Gilda aliona jinsi alivyochanganyikiwa, hivyo alimuacha akiwa katika hali ile kwa muda, kisha akamwambia kwa upole, “Sasa Baddi, lazima tuiangalie hii hali kwa kituo. Kwanza kuna swala la mkeo, na pia kuna swala la hawa watu waliotaka kukuua leo hii...”
“Ni kweli...wewe unadhani kuwa hawa ni watu ambao nilikuwa na kisa nao tangu miaka mitatu iliyopita?”
“Ndiyo. Vinginevyo itakuwa haileti maana!”
Baddi alikaa kimya kwa muda, kisha akamwambia, “Hapana Gilda. Italeta maana iwapo lile tukio ni muendelezo wa mambo yaliyotokea kule ugenini nilipokuwa, kabla sijakutana na wewe!”
Gilda alibaki akimkodolea macho.
“Unataka kuniambia kuwa hawa watu wametufuata kutoka huko kote hadi hapa nchini? Kama ni hivyo kwa nini wasikushambulie tukiwa huko na waje wakushambulie hapa?”
“Hapana. Hawa watu wako hapa hapa. Nadhani wamenitambua baada ya kushuka pale uwanja wa ndege leo hii. Tatizo ni kwamba sijui ni akina nani na kwa nini watake kuniua!”
“Ila unajua kuwa watakuwa na uhusiano na mambo ya kule tulipotoka?”
“Ndiyo maana pekee inayopatikana kwenye tukio hili”
Kimya kilitawala kidogo.
“Sasa kama walitaka kukuua, kwa nini tena wakamuua yule mwenzao aliyekosa kukugonga?”
“Sijui...lakini huenda hiyo ni njia ya kupoteza ushahidi!”
Kimya kifupi kilichukua nafasi, kisha Gilda akauliza, “Okay, sasa tunafanyaje?”
Baddi alimtazama kwa muda kisha akashusha pumzi ndefu.
“Mimi najua cha kufanya. Lakini nataka sasa tugawane njia Gilda. Tayari umeshanifanyia mengi ya kutosha mpaka hapa. Kwa kuwa mambo yameenda
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
kinyume na nilivyotarajia hapa nyumbani, ni bora tuachanie hapa...hili sasa ni tatizo langu, na sitaki nikutumbukize na wewe...”
“No! Tulikuwa pamoja ugenini kwenye matatizo makubwa, sasa nitawezaje kukuacha peke yako kwenye matatizo ya hapa nyumbani? Tutaendelea kuwa pamoja mpaka mwisho wa matatizo, hapo ndipo tutakapogawana njia!”
“Hapana! Yale ya kule ugenini hatukuwa na namna ya kuepuka kuwa pamoja, lakini hili wewe unaweza kuliepuka! Hili ni tatizo langu peke yangu!We’ una jamaa zako hapa nchini...nenda ukawaone na uanze maisha mapya.” Baddi alisisitiza.
Gilda alianza kulia.
“Okay Gilda, basi tutaongea zaidi baadaye, mi’ natoka mara moja...”
“Unaenda wapi sasa...?”
“Naenda ofisini kwa mke wangu, naamini huko nitaonana naye na kujua alipohamia...”
“Kisha utarudi?”
“
Of course nitarudi. Si ndiyo maana nikakwambia tutaongea baadaye?”
Gilda aliinuka na kwenda kumkumbatia kwa nguvu.“Uwe makini sana huko uendako Baddi...please!”
“Nitakuwa makini Gilda...”
Alibadilisha pesa pale pale hotelini na kupata pesa za kitanzania kisha akachukua teksi na kumuamuru dereva ampeleke makao makuu ya Kampuni ya Simu. Ndani ya ile teksi hakuona gari lolote lililokuwa likiwafuata, kwani alikuwa makini sana na hilo.
Aliingia ndani ya jengo la ile kampuni kubwa ya mawasiliano na kuona lilikuwa limepitia mabadiliko makubwa katika ile miaka mitatu aliyokuwa nje ya nchi. Eneo la mapokezi lilikuwa na watu wengi wakiwa wameketi kwenye viti na wengine wakiwa wamesimama mbele ya kaunta ya pale mapokezi. Mara moja alimtambua mmoja wa wale akina dada wa pale mapokezi na kumwendea.
“Habari Anna...” Alimsalimia na yule dada aliinua uso wake kumtazama, “...nahitaji kuonana na Shani...” Aliendelea, lakini sauti yake ilififia pale alipoushuhudia uso wa yule mwanadada ukimbadilika ghafla baada ya kumtambua, woga mzito ukijidhihirisha usoni mwake. Kabla hajajua afanye nini, yule dada aliachia ukelele mkubwa wa woga huku akijishika kichwa na kumkodolea macho.
Ama!
Baddi alihamanika. Aligeuka huku na huko, lakini watu wote waliokuwapo pale nao walikuwa wamehamanika kama yeye.
MDUNGUAJI
“
What the...?”
Na hapo alishangaa kuona watu wote wakimtazama yeye, naye kwa mshangao akamgeukia tena yule dada aliyekuwa akipiga kelele. Yule dada alikuwa akipiga kelele huku akimnyooshea yeye kidole kilichokuwa kikitetemeka, na hapohapo yule mwanadada alianguka na kuzirai!
Sasa watu waliokuwepo pale walikuwa wakipiga kelele ovyo. Baddi aligeuka kushoto kwake na kuona askari mwenye silaha wa kampuni binafsi ya ulinzi akipangua watu kumfuata. Aligeuka haraka na kuanza kusukuma watu kuuelekea mlango mpana wa kioo wa kutokea nje ya lile eneo la mapokezi, lakini nako aliona askari mwingine akiingia na bunduki.
“Hee! Wewe! Simama...!” Yule askari wa kwanza alimpigia kelele kutokea nyuma yake. Baddi alitimua mbio kuuelekea ule mlango wakati yule askari aliyekuwa akiingia pale mapokezi akiinua bunduki yake kumuelekezea.
Aliruka na kumshindilia teke la kifua yule askari, akisikia mayowe ya watu waliokuwamo mle ndani. Askari alitupwa nyuma huku bunduki yake ikifyatuka, risasi ikichimba dari la zege la pale ndani naye akipigizwa kwenye kioo kipana cha ule mlango na kukipasua vipande vipande na kuangukia nje. Alimruka yule askari na kuangukia nje jengo lile.
Alitimua mbio huku akipigiwa kelele na watu waliozagaa eneo lile, akili yake ikimrudisha kwenye misitu minene ya nchi ngeni alipokuwa akikimbia kuokoa maisha yake. Kando ya barabara ya Samora iliyopakana na jengo lile alisita kidogo, asijue iwapo aende kulia au kushoto, na hapo teksi iliyokuwa imeegeshwa kando ya ile barabara ilichomoka kwa kasi na kusimama mbele yake huku mlango wa nyuma ukifunguliwa.
“Baddi ingiaa…!”
Alijitupa ndani ya ile teksi na hapohapo lile gari likajichanganya kwenye msafara wa magari mengine pale barabarani na kutokomea kwa kasi.
“Gilda! U…umefikaje huku wewe?”Alimuuliza yule dada aliyemkuta kule kwenye kiti cha nyuma ndani ya ile teksi. Lakini kabla hajajibiwa, dereva wa teksi aliuliza uelekeo.
“Tuache huo mtaa unaofuata!” Gilda alimjibu yule dereva, ambaye aliingia mtaa alioekezwa na kuegesha gari kando ya barabara. Gilda alimtupia noti ya shilingi elfu kumi na kuteremka haraka, Baddi akimfuatia huku akiwa amepigwa butwaa. Teksi iliondoka nao wakaanza kutembea
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI kando ya barabara kwa mwendo wa haraka.
“Gilda! Imekuwaje...?” Alimuuliza.
“Unataka kuniambia kuwa hujafurahi jinsi nilivyokuibukia namna ile pale?”
“Hapana, pale umecheza heko kweli kweli, thanks a lot …lakini si nilikuacha hotelini? Ina maana uIinifuata kwa gari mpaka pale kampuni ya simu?” Baddi alimuuliza na hapo akaona mgahawa mdogo kando ya barabara ile. Akamshika Gilda mkono na kumuongoza ndani ya ule mgahawa. Waliketi mle mgahawani na kuagiza vinywaji. Baddi alitembeza macho mle ndani kwa muda kabla hajatulia na kumgeukia yule mwanadada aliyeokoa maisha yake kwa mara nyingine, safari hii ndani ya nchi waliyozaliwa.
“Hebu niambie Baddi…ni nini kilichotokea pale? Nimekuona ukitoka kasi nje ya lile jengo huku watu wakikupigia kelele...nimeogopa!”
“Mnh, Gilda! Ni kitendawili…yaani hata mi’ mwenyewe sielewi kwa kweli. Lakini…we’ umefikaje huku?”
“Kwa kweli roho yangu ilikuwa nzito sana kukuacha uje huku peke yako Baddi...hivyo muda wa kama dakika tano tu baada ya we’ kutoka hotelini nami nikatoka. Nilibadili pesa pale hotelini na kuchukua teksi kujaribu kukufuata...”
“Sasa...ina maana uliweza kuiona teksi yangu baada ya muda huo?”
“ No ...Nilimwambia dereva anipeleke makao makuu ya kampuni ya simu tu. Sikujua ningekutana na hali gani huku, lakini inaonekana kuwa nilifanya la maana. Nilipofika nilimwambia dereva aegeshe pale pembeni na kabla sijajua la kufanya ndiyo nikakuona ukichomoka mbio kutoka kule ndani. Ni nini kilichotokea pale? Mkeo…?” Gilda alijibu na kuuliza.
Baddi akamuelezea mkasa wote kama jinsi ulivyomtokea.
Gilda alipigwa butwaa.“Khah! Sasa hiyo imaanisha nini? Kwa nini huyo dada alipiga mayowe hivyo?”
“Sijui...halafu tunafahamiana! Nina hakika kabisa kuwa alinitambua, kisha ndiyo akaanza kupiga mayowe...yaani alikuwa kama aliyeona jini bwana! Inatisha kwa kweli...” Baddi alisema kwa mastaajabu makubwa.
“Kwa hiyo hatujui lolote juu ya mkeo?”
“Hakuna tujuacho...!”
“Nisubiri hapa hapa...” Gilda alisema huku akiinuka.
MDUNGUAJI
“Unaenda wapi sasa?”
“Narudi pale kampuni ya simu...kufanya uchunguzi.”
“ No! Ni hatari kwako. Kwa sasa mtu yoyote atakayekwenda kumuulizia mke wangu pale atatiliwa mashaka!”
“Siendi kumuulizia mkeo...nataka tu niende kupata maana ya tukio lile. Lazima bado kutakuwa kuna watu watakaokuwa wakilizungumzia...si unajua tena kawaida yetu waswahili?”
Baddi aliona kuwa ile hoja ilikuwa na uzito. “Uwe makini Gilda...na usichelewe!”
Gilda alibandika miwani yake ya jua usoni na kutoka.Alirejea dakika arobaini na tano baadaye, ambapo kufikia muda huo Baddi alikuwa ameshahamanika kiasi cha kuweza kuparamia kuta za mle mgahawani.
“Ah,umechelewa sana Gilda! Nilikuwa na wasi wasi sana…haya niambie...umegundua nini huko?”
“Wewe ni marehemu Baddi.” Gilda alimwambia huku akimtazama moja kwa moja usoni.
“Whaaat...? Marehemu? Unamaanisha nini hapo?”
Gilda`alitazama pembeni kwa muda kisha akamgeukia tena. “Ndio yale tuliyoyasikia Senegali, Baddi.” Alimwambia, na alivyoona Baddi hajaelewa, akaendelea, “Yule mwanamke…alipiga mayowe na kuzirai kwa sababu aliamini kuwa wewe ni mzuka…jini…mtu uliyekufa, ukafufuka.”
“Khah!”
“Ndivyo…!”
“Hebu nieleze kwa kirefu nielewe, mbona inakuwa hivi?”
Gilda alimueleza kuwa alipofika pale kwenye lile jengo alikuta kundi la watu waliokuwa wakizungumzia tukio lile. Alijipenyeza miongoni mwao na ndipo aliposikia mmoja wa wafanyakazi wa ile kampuni akitoa maelezo kwa wenzake kuwa yule mwanamke aliyezirai alipopatwa na fahamu alieleza kuwa alimuona mtu ambaye anamtambua kuwa ni mume wa mfanyakazi mmoja wa kampuni ile...ambaye hata hivyo
huyo jamaa alishafariki miaka mitatu iliyopita na kwamba hata
kwenye mazishi yake alihudhuria. Sasa jambo la kumuona mtu ambaye
alishahudhuria mazishi yake miaka mitatu iliyopita akimsimamia
mbele yake na kumwita kwa jina lake lilikuwa zito kabisa kwa yule mwanamke.
Baddi alibaki kimya huku uso wake ukiwa umeingia kiza kwa tafakuri na mduwao uliodhihiri.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Ina maana mimi hapa nchini najulikana kuwa nimekufa?”
“Kwa mujibu wa maelezo niliyoyanasa pale, hivyo ndivyo ilivyo.”
“Na nimezikwa hapa hapa nchini…?” Aliendelea kuuliza kwa fadhaa. Gilda hakujibu kitu.
“Nadhani sasa naanza kupata picha kamili…” Baddi alisema na kubaki kimya kwa muda, kisha akamuuliza, “Je, ulisikia lolote zaidi likisemwa kuhusu mke wangu?”
Gilda alitikisa kichwa. “Hili kwa kweli nilijikuta nikiliuliza moja kwa moja…kwamba ni wapi alipo huyo mke wa huyo jamaa anayesemekana alikufa miaka mitatu iliyopita...”
“Na...?” Baddi alizidi kusaili.
“Mkeo hafanyi tena kazi kwenye ile kampuni Baddi. Walisema kuwa baada ya kifo chako...I mean…cha mumewe, huyo dada aliamua kuacha kazi.”
“Hah…?” Baddi aliropoka kwa mshangao,“…yaani, Shani kaacha kazi? Sasa yuko wapi?” Gilda alimtazama bila kumjibu kitu.
“Oh, samahani Gilda...we’ huwezi kujua juu ya hilo. Ila...dah! Hizi habari zinanichanganya sana. Kwanza nafika hapa nakuta mke wangu hayupo nyumbani kwetu, sijakaa vizuri mtu anataka kunigonga makusudi kwa gari, halafu yule aliyetaka kunigonga naye anagongwa na kuuawa. Halafu napata habari kuwa kumbe nilishakufa na kuzikwa…na mke wangu hajulikani alipo!” Baddi alisema kwa kukata tamaa na kupiga meza kwa kiganja chake. Watu kadhaa mle mgahawani walishituka na kuwakodolea macho ya mshangao.
“Tuondoke hapa Baddi...” Gilda alimwambia naye bila kupinga aliinuka huku akitikisa kichwa, Gilda akichukua jukumu la kulipia vile vinywaji walivyoagiza.
Baddi alikuwa kimya njia nzima wakiwa ndani ya teksi kurejea hotelini kwao. Akili ilikuwa ikimzunguka kutokana na matukio yote ya siku ile. Walipofika hotelini walipita moja kwa moja hadi chumbani kwao.
“Sasa nini kinafuata?” Gilda aliuliza. Baddi aliketi kitandani na kufumbata kichwa chake kwenye viganja vya mikono yake. Alipoona hajibiwi, Gilda aliongeza swali jingine.
“Vipi kuhusu baba yako…? Si ulisema kuwa bado yuko hai…labda yeye anaweza kujua alipo mkeo...?”
“Ndiyo yu hai, lakini naye alikuwa akiishi kwenye nyumba ile ile!”
Baddi alijibu huku bado akiwa amejiinamia, na hapo hodi ilibishwa mlangonikwao.Baddi alimtupia Gilda jicho la kuuliza, ambaye
MDUNGUAJI alimrudishia mtazamo wa kuuliza. Hawakuwa wakitaraji mgeni yoyote.
“Na...nani?” Gilda aliita huku akisogea mlangoni. Wakati huo huo, sasa akiwa makini sana, Baddi aliruka kutoka kitandani na kusimama kando ya mlango ule. Sauti ilijibu kutokea nje ya chumba kile lakini kilichosemwa hakikuwa wazi.
“Nani...?” Gilda aliuliza tena huku akikunja uso na akisogeza sikio lake pale mlangoni ili asikie vizuri, na hapo ule mlango ulisukumwa kwa kishindo kutokea nje na kumbamiza kichwani. Gilda aliachia yowe la uchungu wakati akitupwa sakafuni kwa nguvu iliyousuma ule mlango.
Yaliyofuatia yalikuwa ni matendo ya haraka sana.
Watu wawili walivamia mle ndani wakiwa na bastola mikononi. Baddi alijitupa mzima mzima na kuubamiza tena ule mlango wakati mtu wa pili akimalizia kuingia mle ndani. Ule mlango ulimbabatiza kwenye goti yule jamaa ambaye aliachia mguno wa maumivu, na hapohapo Baddi alishusha mkono wake kwa nguvu na kuiputa bastola iliyokuwa mkononi kwa yule jamaa.Yule mvamizi wa kwanza ambaye alikuwa ameshaingia ndani, na ambaye alikuwa ameelekeza macho yake kwa Gilda, aligeuka baada ya kusikia kilio cha mwenzake na zile purukushani.
“HEY...!” Alianza kuropoka huku akiinua bastola yake, lakini Baddi alimrukia mzima mzima, akitanguliza miguu yake kwa mtindo wa “tandika reli”na kumbabatiza magotini. Jamaa alipoteza uelekeo na kuanguka, yowe likimtoka huku bastola yake ikifyatuka na kushindilia risasi ukutani, bila kutoa sauti. Baddi alijirusha wima haraka na kuipiga teke ile bastola iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti kutoka mkononi mwa yule adui yake.
Wakati huo huo, Gilda alijiinua haraka na kuirukia bastola ya yule mvamizi wa pili iliyokuwa sakafuni, lakini kabla hajaifikia yule mvamizi wa pili alimrukia na kumshindilia teke la uso lililomtupa pembeni yule dada.
“Gilda toka njeee!” Baddi alipiga ukelele huku akimwendea kasi yule mvamizi wa pili, akimuacha yule wa kwanza akigaagaa sakafuni. Jamaa alitaka kuiwahi ile bastola lakini aliona kuwa Baddi alikuwa akimkaribia, hivyo alimgeukia na hapohapo Baddi alimrushia ngumi kali. Jamaa alimkwepa na ngumi yake ikapita hewani, na wakati huohuo yule jamaa akamshindilia goti kwenye mbavu.
Baddi aliyumba kwa pigo lile, na hapohapo jamaa akamtwanga ngumi nzito ya taya iliyomsukumiza mlangoni na Baddi akabaki akitweta. Jamaa alijiweka sawa na kumrukia kwa mtindo wa “Flying Kick” kwa lengo la
kumbabatiza pale pale mlangoni, lakini Baddi aliruka pembeni na jamaa akaishia kuubamiza mlango kwa nguvu huku akitoa mguno wa kulaani jambo lile. Baddi akauchota ngwara kali ule mguu uliobaki, na jamaa akaenda chini mzima mzima.
“B addiii…!” Gilda alimpigia ukelele, na Baddi akaona kuwa yule jamaa mwingine alikuwa anaiendea ile bastola nyingine aliyoipiga teke hapo awali. Aliirukia ile bastola iliyokuwa karibu naye na kuinyakua huku akijibiringisha na kuinuka akiwa amepiga goti moja, bastola ikiwa mkononi mwake.
“
Don’t move, bloody swine!”Alifoka kwa hasira huku akiwa amemuelekezea bastola yule mvamizi wa kwanza. Jamaa alisita na kusimama akiwa amenyoosha mikono juu. Baddi alimtazama huku akitweta, pua zikimtanuka na akili ikimtembea. Alimtupia jicho yule mvamizi mwingine aliyekuwa akianza kujizoazoa pale chini, kisha akajiweka mbali nao huku akirudi nyuma.
“Okota hiyo bastola nyingine Gilda!”Aliamuru huku bado akiwa amewaelekezea bastola wale jamaa, akiwatazama kwa zamu. Hakuwa amepata kuwaona hata siku moja. Gilda alifanya alivyoamriwa na kujisogeza pale alipokuwa amesimama Baddi.
“Ninyi ni akina nani…na mna shida gani nami?” Baddi aliwafokea. Wale jamaa walibaki wakimtazama kwa ghadhabu, kisha yule aliyekuwa wa kwanza kuingia mle ndani alimjibu kwa hasira.
“Huna haja ya kutuuliza maswali fala wewe! Ni aidha utuue au utuachie tukuue!”
“Khah? Kwani...” Baddi alianza kuwauliza, lakini hapohapo vilisikika vishindo kutokea nje ya kile chumba huku wahudumu wa ile hoteli wakipiga kelele.
“Heeeh…! Kuna nini huko, mbona vishindo?”
Baddi aligeuka kidogo kule mlangoni na hilo lilikuwa kosa. Kwa kasi ya umeme jamaa alichomoa kisu na kumtupia kistadi sana.
“BAD-AAAAHHH...!” Gilda alipiga kelele huku akimsukuma Baddi pembeni, na hapohapo yule jamaa alijirusha mzima mzima kutoka pale alipokuwapo na kujitupa dirishani, akipasua kioo kipana cha dirisha lile na kupotelea nje ya chumba kile kilichokuwa ghorofa ya kwanza ya hoteli ile.Baddi alimtupia risasi lakini jamaa alikuwa ameshatoweka. Na ni muda huo ndipo wale wahudumu wa ile hoteli walipoingia mle ndani kwa vishindo.
Baddi alishangaa kumuona Gilda akianguka mbele yake na akamdaka,
MDUNGUAJI
wakati akimuona yule mvamizi wa pili akijipenyeza miongoni mwa wale wahudumu wa ile hoteli na kutoka nje ya chumba kile.
“WEZI! ANATOKA HUYOOO! Kamata!” Alimpigia kelele huku akiwa amemshika Gilda.
“Baddi!” Gilda aliita kwa uchungu, na ndipo kwa mara ya kwanza Baddi alipohisi unyevu mikononi mwake. Alimtazama yule binti na akahisi ubaridi ukimtambaa mwili mzima pale alipoona sehemu ya mbele ya nguo ya Gilda ikiwa imetapakaa damu hali mpini wa kisu ukiwa umechomoza kifuani kwa yule dada, upande wa kishoto!
Kile kisu kilikuwa kimemdhamiria yeye, na Gilda, katika kujaribu kumsukuma pembeni, akajiweka kwenye njia ya kisu kile na matokeo yake kimejikita kifuani kwake! Anakufa mtoto wa watu kwa ajili yangu!
Mwili ulimtetema na kichwa kilimuwia chepesi, lakini alijitahidi kwa nguvu zote kuishinda hali hiyo.Muda wote kulikuwa kuna kelele za wale wahudumu mle ndani lakini Baddi hakuwa akitilia maanani kelele na sauti zao.
“Gilda! Gilda…!” Aliita huku akimlaza kitandani yule dada. Gilda alimkamata ukosi wa shati lake na kumvutia karibu.
“Baddi...usini...ache tafadhali!”
“No way! Siwezi kukuacha Gilda! Sitokuacha kama jinsi ambavyo wewe hukuniacha huko nyuma...!” Kisha akawageukia wale wahudumu na kuwapigia kelele, “Ambyulensi! Ita Ambyulensi upesi! Kajeruhiwa huyu!”
“Kwani ni nini kimetokea jamani?”Mmoja wa wahudumu aliuliza.
“Majambazi bwana! Wamewavamia.” Mwingine alijibu.
Baddi alichanganyikiwa.
“Hebu keleleni bwana! Wapi ambyulensi?” Alifoka na hapohapo akamgeukia Gilda, kisha haraka alizunguka kitandani na kwenda kuchungulia pale dirishani alipotowekea yule mvamizi. Zaidi ya vipande vya vioo, kule chini hakukuwa na mtu. Alirudi pale kitandani na kumtazama yule dada. Uso wake uliovimba na kuchubuka kutokanana kipigo cha mvamizi wa pili, na kile kisu kilichokuwa kimechomoza kifuani kwake, vilimfanya atamani kulia.
“Duh, pole sana faza….lakini hapo mpaka upate PF 3 ya polisi ndiyo mpate matibabu.”
“Ah, sasa mtu kajeruhiwa huyu tusubiri PF ngapi-ngapi tu sijui huko? Hizi taratibu za wapi!”Baddi alimaka.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Ah, huo nd’o utaratibu.”
“Kwanza wale watu waliwezaje kupita huko chini hadi wakafika chumbani kwetu, eenh?” Baddi alimkemea yule mhudumu wa ile hoteli aliyekuwa akijitahidi kutoa maelezo.
“Ah, si wamekuja na kuwaulizia? Walijitambulisha kuwa ni jamaa zenu!”
“Wametuulizia kwa majina gani?”Baddi alimkemea, na hapo akamsikia Gilda akigumia kwa maumivu, akamgeukia. “Tunaenda hospitali Gilda…tunaenda sasa hivi!” Alimwambia, na kumgeukia tena yule jamaa, jamaa alipoona kageukiwa hakusubiri kukumbushwa tena lile swali.
“Wa...wao waliwaelezea tu jinsi mlivyo, wakisema kuwa mliwasiliana na mkawaambia kuwa mpo kwenye hii hoteli…”
“Wajinga wakubwa nyote nyie bloody fools! Humu chumbani si kuna simu humu? Sasa hii simu kazi yake nini bloody fucking fool wewe, eenh? Kwa nini msitupigie kututaarifu kuwa kuna wageni wetu halafu sisi wenyewe ndiyo tuamue iwapo waje au wasije? Ennh? Stupid individuals!”Alipomaliza kubwata alianza kumbeba Gilda kutoka pale kitandani.
“Naenda hospitali.Siwezi kuendelea kukaa hapa kusikiliza upumbavu!”
Alikuwa akisema wakati aliposikia vishindo vipya kutokea nje ya chumba kile, na hapo aliona askari wa jeshi la polisi wenye silaha wakiingia mle ndani.
“Ni nini kimetokea hapa?” Mmoja wa wale askari wanne walioingia mle ndani alisaili huku akitembeza macho mle ndani, akiona zile silaha zilizokuwa sakafuni, na kuyatuliza kwa muda kwa Gilda aliyekuwa mikononi mwa Baddi kabla ya kuyahamishia macho yake usoni kwa Baddi Gobbos.Taratibu Baddi alimlaza tena Gilda pale kitandani na kuwatazama wale askari mmoja baada ya mwingine.
“Tumevamiwa na watu wasiojulikana…mke wangu amejeruhiwa, na nilikuwa nampeleka hospitali...kwa kweli hakuna muda wa kupoteza, kwani anatokwa na damu nyingi!”
“Tulia ndugu…tunataka kujua kilichotokea, na pia kuna taratibu za kufuatwa katika hali kama hii.” Yule askari alimjibu wakati wale wenzake wakiziokota zile silaha na kuziweka kweye mifuko maalum ya plastiki waliyokuja nayo, ilhali askari mwingine akianza kuchukua maelezo kutoka kwa wale wahudumu wa mle hotelini.
Kwa kama dakika kumi zilizofuata Baddi alihojiwa na wale askari. Akikumbuka kuwa alikuwa amerejea nchini kwa pasi bandia za kusafiria, alijieleza kuwa yeye ni Mtanzania aliyezaliwa na kukulia nchini Senegali na hatimaye kuchukua uraia wa huko. Aliwafahamisha kwamba alikuwa
MDUNGUAJI
amekuja nchini kwa mapunziko mafupi na mkewe ikiwa ni pamoja na kutazama uwezekano wa kuanzisha biashara ya nguo hapa nchini, na kwamba wakiwa pale hotelini ndiyo wakajikuta. wakivamiwa.
Askari walitaka kuona ,pasi zao za kusafiria na akawaonesha huku moyo ukimwenda mbio, lakini wale askari hawakuzitoa kasoro yoyote.
Je, alishawahi kuwaona wale watu mahala popote kabla ya siku ile?
Hapana hajawahi kuwaona.
Je, akiwaona tena ataweza kuwakumbuka?
Bila shaka.
Yakafuata maswali ya hapa na pale na kisha yule askari akamwambia, “Pole sana bwana. Sasa hivi nchini kumeingia wimbi kubwa la ujambazi. Bila shaka hao watu waliwafuatilia tangu huko uwanja wa ndege.”
“Ah! Kweli aisee…Inawezekana kabisa!” Baddi alijitia kama kwamba ndiyo kwanza lile wazo linamjia akilini mwake, kisha akaongezea kwa wahka, “Sasa nahitaji kumfikisha mke wangu hospitali...”
“Okay, tutatoka pamoja hadi kituoni, utapata PF 3 kisha tutakupeleka mpaka hospitali ya Muhimbili halafu utarudi tena kituoni ili utupatie maelezo ya tukio zima hili kwenye maandishi.” Askari alimwambia.
Nusu saa baadaye, Baddi alikuwa akikimbizana na manesi kando ya kitanda cha magurudumu, Gilda akiwa amelala bila fahamu juu yake, wakielekea chumba cha upasuaji.
Na wakati akikimbia kando ya kitanda kile, Baddi Gobbos, mwanaume jasiri aliyekabiliana na misukosuko mingi huko nyuma, alikuwa akibubujikwa machozi waziwazi.
Eee, Mungu wangu, najua kuwa wewe ndiye mwenye mamlaka ya mwisho juu ya uhai wa viumbe wote hapa duniani, lakini tafadhali usimchukue kiumbe wako huyu sasa hivi…pleas e …!
Saa moja baadaye aliruhusiwa kuingia kwenye wodi alimolazwa Gilda. Kile kisu kilikuwa kimetolewa na lile jeraha lilikuwa limeshonwa. Huku uso ukiwa umemsawajika,alikisogelea kile kitanda na kumtazama yule binti aliyekuwa amelala kwa utulivu. Daktari alimwambia kuwa alikuwa amepigwa sindano ya usingizi na hatoweza kuamka kwa muda mrefu kidogo, ila alikuwa katika hali nzuri. Baddi aliketi kando ya kile kitanda huku akihisi koo likimkauka.
Alibaki akimtazama Gilda akiwa katika hali ile kwa muda mrefu, na hapo akili yake ilimrudisha miaka mitatu nyuma, kwenye nchi ngeni, ambako ndiko alipokutana kwa mara ya kwanza na yule binti. Alikumbuka jinsi
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
alivyojiona akiaga dunia katika nchi moja ilhali taswira ya mwisho akilini
mwake ikiwa ni sura ya mkewe…na jinsi alivyojikuta amerejeshwa tena duniani akiwa katika nchi nyingine; na sura ya kwanza aliyoiona baada ya kurejeshwa tena duniani, ikiwa ni ya yule dada aliyelala kwa amani kabisa pale kitandani.
Wingu la kumbukumbu lilimzingira na kuzigubika fahamu zake kama kwamba ndiyo kwanza alikuwa ndani ya ile siku, miaka mitatu nyuma,alipotokewa na tukio lililokuja kumkutanisha na yule binti aliyelala mbele yake wakati ule. Lile wingu la kumbukumbu lilimkumba kutoka pale alipokuwa na kumrejesha miaka mitatu nyuma hadi kwenye ile siku alipoonana jicho kwa jicho na Mdunguaji...
REJEA
MSITU WA TUMBUDU, SIERRA LEONE
Alifyatua risasi na kutawanya kichwa cha msaliti Nathan Mwombeki, au Alpha, na wakati huohuo maumivu makali yalipita upande wa kulia wa kifua chake, sawia na kitu kama msumari wa moto kikiuingia mwili wake na kutembeza ganzi upande wote wa kulia wa mwili wake. Alitupwa hewani na kupigiza mgongo kwenye jiwe kubwa lililokuwa karibu yake kisha alianza kuserereka kwenye mporomoko mkali. Alikamata jiwe kubwa ili kujizuia asiangukie kule korongoni, akitembeza macho kule ilipotokea ile risasi iliyompata kifuani, akimtafuta adui yao aliyebaki… akimtafuta mdunguaji.
“Jishikilie hivyo hivyo Vampire! Jishikilie! Nakuja kukusaidia komredi...!”
Black Mamba alimpigia kelele huku akijiinua na kuanza kumuendea, lakini yeye hakuwa akimsikiliza, kwani alikuwa akimtafuta mdunguaji ambaye alijua kuwa alikuwa karibu kabisa na pale walipokuwapo... na mara hiyo alimuona.
Alikuwa juu ya mti mmoja mita chache kutoka pale alipokuwa amesimama msaliti Nathan dakika chache zilizopita. Walitazamana. Macho kwa macho!
Alikuwa amejipaka rangi nyeusi usoni, lakini aliliona waziwazi jeraha kubwa lililotambaa kando ya jicho lake la kulia. Na hata pale alipokuwa akimkodolea macho kwa taabu na mastaajabu, alimshuhudia yule muuaji wa kuvizia akiongeza risasi kwenye bunduki kubwa iliyokuwa na lenzi yenye nguvu, kisha akiinua taratibu ile bunduki kumlengeshea huku akiwa amekenua meno yake kwa ghadhabu. Vampire alijaribu kuinua bastola yake kumuelekezea yule muuaji lakini mkono ulimuwia mzito sana. Alimtazama yule muuaji kwa kukata tamaa huku aking’ang’ania fahamu zake zilizokuwa zinaelekea kumpotea kwa kasi. Alisikia
vishindo vya Black Mamba akimkimbilia pale alipokuwapo, na akamkumbuka yule muuaji hatari.
Hapana! Haiwezekani atuue sote! Black Mamba hastahili kufa...!
MDUNGUAJI
Alimpigia kelele kumtahadharisha juu ya yule muuaji, lakini Black
Mamba hakumuelewa upesi, na badala yake alisita kidogo na kubaki akiwa ameduwaa, kisha alianza kugeuka taratibu, huku akichutama, kuelekea kule alipokuwa akimuelekezea, ilhali bunduki yake ikiwa makini mikononi mwake.
Vampire alikuwa akijaribu kujivuta juu ili asiangukie kule korongoni, na hapo
lile jiwe alilokuwa akilitegemea lilianza kung’oka na hakuwa na namna ya kujiokoa. Aliinua uso wake kwa woga na kutaka kumpigia kelele Black
Mamba lakini alipigwa na butwaa na kihoro kikubwa pale alipoona kichwa cha
Black Mamba kikitawanyika vibaya sana huku kiwiliwili chake kikianguka chini kama mzigo.
Mdunguaji alimuwahi.
“Black-Aaaayyyaaaaaa!” Yowe lilimtoka Vampire na hapohapo alimuona mdunguaji akimgeuzia ile bunduki yake kubwa iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti, naye aliinamisha kichwa chake kwa kukata tamaa huku akihisi macho yake yakipoteza nguvu na fahamu zikimhama. Alijua kuwa kifo kilikuwa kimemkabili na hakuwa tena na nguvu ya kufanya jambo lolote.
Lakini yule mtu...yule mdunguaji...mbona yale macho yake yanaonekana kama ambayo…kama ambayo...
Akili ilikuwa ikimhama kwa kasi, na akapoteza kabisa mtiririko wa mawazo kichwani mwake. Wazo la mwisho kumpitia kichwani mwake ni sura ya mkewe, kisha mikono ikamuisha nguvu, bastola ikamuanguka na mkono wake wa kushoto ukalichia lile jiwe alilokuwa amelishika. Hivi ndiyo nakufa Baddi mie...ndiyo mwisho wangu huu...!
Kote kukawa kiza.
Akiwa hana fahamu, alianguka kama mzigo kutoka kule korongoni, akijipigiza kwenye matawi ya miti iliyokuwa imeota kwenye kingo za lile korongo refu, akipigwa na mawe yaliyokuwa yakiporomoka pamoja naye kutoka kule juu.
Ghafla alihisi ubaridi ukimtambaa mwilini na kisha unyevu ukimtawala kila sehemu. Alijitahidi kufumbua macho, au kurejesha fahamu, lakini ilimuwia vigumu sana. Mapafu...! Mapafu yalikuwa yanamuuma…yanashindwa kufanya kazi? Yanapata moto…Pumzi! Pumzi hakuna kabisa...
0h My God...! Hivi ndivyo inavyokuwa roho inapotoka? Ah, Pumzi jamani, pumzi…!
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Yaani kama niko kwenye…niko kwenye…
Maji!
Alifumbua macho ghafla na kufunua kinywa chake kuvuta pumzi nyingi ili ayape nafuu mapafu yake, na badala yake alijikuta akibwia maji mengi na kutapatapa kwa namna halisi ya mfa maji huku akihisi kitu kizito kikimdidimiza kwenye kina kirefu cha maji.
Ameangukia mtoni!
Alikuwa amenasa kwenye kipago cha gogo kubwa lililokuwa limembana kifuani, na hakika hilo ndilo lililomzuia asizidi kupelekwa na yale maji ya mto yaliyokuwa yakitiririka kwa kasi. Aliinua uso wake na kutazama kule juu alipotokea. Hakuona kitu chochote zaidi ya matawi ya miti mikubwa na mikongwe yaliyoufunika ule mto kiasi kwamba hata mbingu zilizokuwa huko juu zilikuwa hazionekani. Kote kulikuwa kiza. Kikohozi cha mfululizo kilimshambulia huku maji yakimtoka puani na mdomoni, kisha akabaki akitweta huku akiwa amejishikillia kwenye lile gogo lililokuwa limekwama kwenye mawe makubwa yaliyokuwa kwenye kingo za mto ule. Mwili ulimuuma, nguvu zilimuishia na kila alipovuta pumzi alihisi kitu kikimchoma kwa nguvu sana kifuani. Nimepigwa risasi! Mdunguaji kanitwanga risasi, bloody coward!
Aliinamisha kichwa na kujitazama pale kifuani alipohisi kuwa.risasi ilikuwa imempata, na aliingiwa na woga mkubwa pale alipoona kuwa sehemu kubwa ya maji ya mto katika eneo Iile yalikuwa yamebadilika rangi na kuwa mekundu kwa damu iliyokuwa ikimtoka.
Ah, damu ni nyingi sana! Nitakufa tu...nitakufa...natokwa damu nyingi... ndiyo maana naishiwa nguvu.
Kwa taabu alijivuta na kujaribu kujichomoa kutoka kwenye kipago cha lile gogo ili ajitupe kwenye ukingo wa mto ule na atoke kwenye yale maji yaliyobadilishwa rangi na damu yake, lakini hapo alilitikisa lile gogo na likachomoka kutoka kwenye yale mawe yaliyolikwamisha. Kwa woga mkubwa Baddi Gobbos, p.a.k.Vampire, aliliona lile gogo likisombwa na yale maji yaendayo kasi naye akianza kuzama kwenye ule mto wenye kina kirefu. Kwa nguvu za mwisho alizokuwa nazo alijitahidi kulikamata lile gogo kwa mkono wake wa kushoto kabla halijamtoka kabisa, lakini bado lilikuwa likimchomoka huku likimvuta. Alijua
kuwa hakuwa kabisa na nguvu za kuweza kuogelea, hivyo alijitupa mzima
mzima juu ya lile gogo na kulilalia kifudifudi, akihisi maumivu makali
kabisa kifuani kwake.Aliling’ang’ania lile gogo kwa mikono yake yote
miwili, maji yakimsomba pamoja na gogo lile kufuata mkondo wa mto ule.
Woga ulimkumba wakati maji yakimpeleka kwa kasi ya ajabu, na alijitahidi
kulishika lile gogo huku akikwepa magogo mengine na mizoga ya wanyama
MDUNGUAJI
pori waliokufa kwa kusombwa na maji yale. Alikuwa akipumua kwa taabu na kila alipojitahidi kufunua kinywa ili avute hewa alijikuta akishindana na maji yaliyokuwa yakitaka kumuingia kinywani. Ilikuwa ni hekaheka mtoni.
Alipelekwa na maji yale kwa namna ile kwa muda mrefu bila hata dalili ya maji yale kupungua kasi, kisha kwa kihoro kikubwa aliona kuwa ule mto ulikuwa ukiishia kwenye maporomoko makubwa mithili ya yale ya Victoria Falls. Oh, My God...yaani ndiyo niangukie huko...?
Ukelele ulimtoka kwa woga na hakuwa na la kufanya zaidi ya kuzidi kuling’ang’ania lile gogo huku akiuona ule mporomoko ukizidi kumkaribia, ilhali mawe makubwa yakiwa yamechomoza kwenye ukingo wa mporomoko ule, asijue huko chini yale maji yalikuwa yanaanguka kwa umbali gani. Nifanyaje sasa pale…nifanyaje sasa pale...?
Hakika alikuwa amefikwa na salama yake ilikuwa ni iwapo lile gogo alilolalia litakwama kwenye yale mawe makubwa, lakini kwa jinsi lile gogo lilivyokuwa likienda ilibidi ajitahidi kuligeuza ili liende kule maporomokoni ki-ubavu-ubavu. Alijitahidi kujigeuza pamoja na lile gogo huku kingo ya maporomoko ikizidi kumkaribia, na mara alikuwa amefika.
“AAAAAAAYYYAAAAHHH…!” Alipiga ukelele peke yake huku macho yamemtoka pima, wakati lile gogo likijipiga kwenye jiwe moja kubwa, likakwama kidogo, naye akajinyoosha ili akamate jiwe lililokuwa karibu yake, lakini hapo lile gogo likasukumwa tena kwa nguvu na yale maji na kukatika katikati, naye akitupwa kwa nguvu huku akiachia ukelele mwingine mkubwa. Alipigiza kichwa chake vibaya sana kwenye moja ya yale mawe, na hapohapo kote kukaanza kuwa kweusi, kiza kikatanda machoni mwake, nguvu zikimhama taratibu.
Sasa hakika huu ndiyo mwisho wangu...
Alipoteza fahamu.
Wala hakujiona wakati akisombwa na yale maji yenye kasi na kutupwa kwenye mporomoko mkali wa ule mto uliokuwa ukianguka umbali wa mita
zipatazo mia na hamsini kutokea kule juu alipokuwapo.
Hakujua fahamu zilimrudia baada ya muda gani au baada siku ngapi. Wala hakujua iwapo fahamu zilimpotea, kwani akilini mwake alikuwa
akipitiwa na taswira nyingi za ajabu-ajabu ambazo zilifuatiwa na vipindi virefu
vya kiza na utupu mzito akilini. Miongoni mwa taswira zile ni pamoja na yale macho yaliyojaa chuki ya yule mdunguaji aliyoyaona sekunde chache
kabla hajaangukia korongoni na kutumbukia kule mtoni, na taswira za
kichwa cha Black Mamba kikitawanyika na kutandaza damu na mapande ya ubongo kila upande, wakati mara nyingine akisikia sauti za ajabu ambazo hakuwa amewahi kuzisikia maishani mwake. Zilikuwa ni sauti za mchanganyiko wa kike na kiume zikiongea lugha ngeni.
Lakini hisia kubwa aliyokuwa nayo katika vile vipindi vifupi vya mang’amung’amu ni hali ya kuelea...au kama kwamba amebebwa na kitu...watu...? Maji…? Naelea kwenye maji...? Hewani...? Pia alikuwa akipata hisia ya kusukwasukwa na watu...au viumbe asivyovifahamu... na maumivu makali yakikitawala kifua chake, lakini kila alipojitahidi kuinua mikono au miguu alishindwa.Kila alipojaribu kufumbua macho yalikuwa yanamuwia mazito sana. Kila alipojaribu kufunua kinywa kupiga kelele mdomo ulimuwia mzito sana.
Nimekufa. Harufu kali yenye kupalia ilizitawala pua zake na alijikuta akipiga chafya kubwa, ikifuatiwa na nyingine, na nyingine, na ghafla macho yakamfumbuka.
Mwanadada mrembo alikuwa amemuinamia huku akitabasamu, ilhali kwa mbali akisikia sauti za ndege wakiimba kwa mfumo uliopendeza masikioni. Niko peponi...Nimekufa...na Mungu ameniingiza peponi...
Alimtazama yule mwanamke aliyekuwa amemuinamia huku akitabasamu.
E bwana mtoto kaumbika huyu!
Yule mrembo mwenye tabasamu alikuwa akimsemesha lakini yeye hakusikia lolote.
Malaika huyu...Mungu kaniingiza peponi na kaniwekea na malaika wa kunilinda! Dah, Mungu bwana...!
“...nakuuliza unajisikiaje sasa...?” Yule malaika alimsemesha huku akitabasamu, na hapo Baddi akawa makini sana. Mnnh? Peponi huwa wanaongea kiswahili?
“Ni...niko wapi hapa?” Aliuliza kwa sauti iliyokwaruza, huku akihisi koo likimuuma. Alitazama huku na huko, na kuona kuwa alikuwa amelala juu ya kitanda cha miti na kamba, na kwamba yeye na yule mwanamke walikuwa ndani ya chumba kidogo chenye kuta za udongo na kuezekwa kwa nyasi. Hapa sio peponi hata kidogo!
Alimtazama yule dada kwa makini. Alikuwa ameketi kwenye kigoda
MDUNGUAJI
kilichokuwa kando ya kile kitanda alicholalia na alikuwa amevaa shati zito la kitambaa cha kombati lililoachwa wazi sehemu ya mbele na kufanya singlet nyekundu iliyokuwa chini ya shati lile ionekane. “We...wewe ni nani? Niko wapi hapa...?” Aliuliza tena.
“Naitwa Gilda...ni Mtanzania kama wewe. Hapa tuko kwenye kijiji kimoja kidogo nchini Liberia, na...”
“Liberia? Nimefikaje huku...?”
“Ni hadithi ndefu, lakini nashukuru kuwa hatimaye umeamka na umerejewa na fahamu. Nilipatwa na wasiwasi sana nilipoona kuwa siku zinapita nawe huamki sawasawa. Nimekunusisha huu unga niliopata kwa wenyeji hapa, na naona umesaidia kukuamsha...”
Wala Baddi hakuwa akimsikiliza tena. Akili yake ilikuwa ikimtembea kwa kasi sana. Liberia? Sio Sierra Leone...?
Alijaribu kujiinua lakini ilikuwa taabu, na akahisi maumivu hafifu kifuani kwake, ule upande aliopigwa risasi. Alihisi uzito kwenye mguu wake wa kushoto. Gilda alimsaidia kuinuka na kumketisha pale kitandani akiwa ameegemeza mgongo wake ukutani. Alibaki akitweta pale kitandani
kwa muda, akigundua kuwa alikuwa amefungwa bandeji pana na safi kifuani kulizunguka lile eneo ambalo alipigwa risasi hapo awali. Aliutazama mguu wake wa kushoto na kuona kuwa ulikuwa umefungwa kwa bandeji kubwa na zito, na pia ulikuwa umefungiwa vipande vya ubao kila upande.
Eh, na mguu umevunjika!
“Ni nini kimenitokea?” Aliuliza huku akiuangalia ule mguu wake.
“Hata sijui kaka’angu...ila ni kwamba umekuja hapa ukiwa umevunjika mguu na ukiwa na risasi mwilini mwako...” Yule dada alimjibu.
Oh, Shit!
“Umesema we’ ni Mtanzania kama mimi...?” Baddi aliuliza tena, kwa mara ya kwanza akigundua kuwa alikuwa akiumwa na njaa kali.
“Ndiyo...lakini nadhani we’ unahitaji kula kwanza. Subiri hapo hapo...”
Yule dada aliyejitambulisha kwa jina la Gilda alisema na kutoka mle ndani.
Baddi aliona kuwa chini ya lile kombati, yule dada alikuwa amevaa suruali ya jeans na viatu vya raba.
Ni nani huyu?
Gilda alirudi muda mfupi baadaye akiwa na bakuli la uji mzito wa ndizi na kuanza kumnywesha.
“Ni...ni vipi uliweza kujua kuwa mimi ni Mtanzania...mwenzako? Na wewe unafanya nini huku?” Baddi alimuuliza huku akimtazama kwa
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
makini yule dada.
“Kaka yangu hii ni hadithi ndefu sana. Ila tu kwa ufupi ni kwamba alfajiri moja kiasi cha mwezi mmoja uliopita nikiwa nimelala kwenye kibanda nilichokuwa nikijihifadhi katika kijiji kingine kilichokuwa kando ya ule mto mkubwa, nilikuja kugongewa na akina dada waliokuwa wameamka alfajiri kuwasubiri wavuvi ili wapate kununua samaki wa biashara huko mjini. Hawa ni akina dada ambao nilikuwa nikifahamiana nao pale kijijini.
“Wakaniambia kuwa wamekuta mtu kando ya ule mto, na kwamba huyo mtu alikuwa akiongea maneno ambayo wao walidhani kuwa ni kiswahili kwani hata mimi walikuwa wakinisikia nikitamka maneno yanayofanana na hayo uliyokuwa ukiyatamka...”
Baddi alishangaa, kwani hakuwa na kumbukumbu ya kutamka maneno yoyote, wala ya jinsi gani alifika kwenye kingo za huo mto.
“Ni maneno gani...?” Aliuliza, lakini Gilda aliendelea na maelezo yake kama kwamba hakulisikia lile swali.
“...basi nilikimbilia huko mtoni pamoja nao na kweli kabisa nikakukuta ukiwa kando ya ule mto, ukitapatapa na fahamu huku ukitamka neno “nakufa” mara kwa mara, na hili ndilo neno ambalo wale akina mama wa ki-Liberia walishawahi kunisikia nikilitamka. Mara moja nikajua kuwa wewe ni Mtanzania, na kutokana na mavazi yako sote pale tulijua kuwa wewe ni mwanajeshi wa jeshi la Umoja wa Mataifa...”
“Na hiyo ilikuwa mwezi mmoja uliopita...?” Baddi aliuliza.
“Ndiyo, na ulikuwa umejeruhiwa. Binafsi nilifurahi sana kuona mtu wa kwetu huku ugenini. Hivyo nikisaidiana na wale akina mama tulikubeba hadi pale nilipokuwa nikiishi, kisha nikachukua jukumu la kutafuta tabibu wa kukuhudumia ukiwa mle mle ndani kwangu.
“Ilikuwa ni taabu sana, na ulikaa kwa wiki nzima kabla sijaweza kupata tabibu. Liberia kuna machafuko makubwa sana hivi sasa, watu hawaaminiani hata kidogo...nililazimika kuwahonga pesa nyingi wale
akina mama ili wasiseme kuwa kuna askari wa umoja wa mataifa humu ndani, na pia nilimhonga pesa nyingi sana yule tabibu aliyekuja kukutibu, ingawa naye hakuwa na zana za kutosha…”
“Duh!”
“Ndiyo…alifanikiwa kuitoa risasi mwilini mwako na kulifunga hilo jeraha, kisha akaniachia dawa ya kukusafishia hicho kidonda na bandeji za kubadilisha. Hata hivyo sikupenda namna yule tabibu alivyokuwa
MDUNGUAJI akikutazama, na mara alipoondoka tu nikafanya taratibu za kukuhamisha
kutoka kile kijiji nilichokuwa naishi na kuja hapa tulipo sasa. Nimekuwa nikikuhudumia humu ndani tangu wakati huo, ingawa yule tabibu aliniambia kuwa hakuwa na matumaini sana nawe kutokana na damu uliyopoteza na kuwa risasi ilikuwa imekaa ndani ya mwili wako kwa muda mrefu...”
Gilda alimueleza kwa kirefu.
Baddi alichoka. Hakuwa na la kumlipa yule dada.
“Dah, Ahsante sana dada’angu...nadhani bila wewe ningekufa tu. Thamani yako kwangu ni ya malaika kabisa!”
“Usijali kaka’angu. Mimi nimefurahi sana kukutana na “mbongo” mwenzangu. Labda sasa na wewe ungenijulisha zaidi juu yako... jina lako...na... ilikuwaje hata ukakutwa pale kando ya mto ukiwa katika hali kama ile…”Baddi alishusha pumzi na kukaa kimya kwa muda.
“
Okay. Mi’ naitwa Baddi Gobbos, na kama ulivyohisi hapo awali, ni Mtanzania. Mimi ni mmoja wa wapiganaji wa jeshi la Umoja wa Mataifa tuliokuwa kwenye kampeni ya kulinda amani huko Sierra Leone... na ndiyo maana nashangaa unaponiambia kuwa leo niko Liberia.”
“Mnh, sijui ilikuwaje lakini hapa ni Liberia...” Gilda alisema, na kuongeza, “...inawezekana ulipoteza kumbukumbu fulani hapo kati kaka.Kwani… unakumbuka ulikuwa wapi mara ya mwisho kabla ya kujikuta ukiwa hapa?”
Kumbukumbu ya tukio zima la pale korongoni ilimrudia tena kichwani mwake.
“Yeah...nakumbuka. Nilikuwa kwenye msitu wa Tumbudu, nchini Sierra Leone…tulikuwa tunapambana na mdunguaji hatari, mwenzangu alipigwa risasi ya kichwa, nami nikapigwa kifuani, kisha nikaanguka kutoka kwenye korongo refu na kuangukia mtoni, nikapelekwa na mto hadi kwenye maporomoko makali...na baada ya hapo... hakuna kitu...sikumbuki kitu zaidi....” Baddi alimwambia.
Gilda alimtazama kwa muda, huku uso wake ukionesha mastaajabu makubwa.
“Mnh! Basi wewe ni mtu mmoja mwenye bahati kubwa. Msitu wa Tumbudu uko mpakani kabisa na Liberia, na huo mto unatambaa kutokea kwenye vilima vya katikati ya Sierra Leone na unakuja hadi Liberia. Kama jinsi mto Naili unavyosafiri baina ya Tanzania na Misri...”
“Alaa!”
“Ndiyo! Yale maporomoko ndiyo yanakuwa kama mpaka wa aina fulani...yaani maji ya mto ule yakianguka kutoka kwenye
maporomoko yale tayari yanakuwa kwenye ardhi ya Liberia na si Sierra
Leone tena....ni maporomoko makali sana yale na si rahisi mtu kupona! Wewe una bahati sana...!” Gilda alisema.
E bwana we!
Baddi alibaki kinywa wazi. Yaani...nimesafirishwa na ule mto tangu
Sierra Leone hadi Liberia? Alikumbuka jinsi alivyokuwa akipelekwa kwa kasi na yale maji yenye nguvu, na jinsi lile gogo alilokuwa ameling’ang’ania lilivyopasuka katikati pale kwenye mawe ya kwenye ule mporomoko. Inawezekana pale ndipo nilipovunja mguu...yale mawe...na ile kasi ya msukumo wa maji. Ni nini sasa hatima ya wenzangu kule Sierra Leone?
“Je umesikia lolote juu ya mapigano ya huko Sierra Leone? Unajua iwapo jeshi la Umoja wa Mataifa bado lipo huko?” Baddi alimuuliza Gilda.
“Hapana Baddi...Si unajua kuwa hapa Liberia sasa hivi kuna vita ya wenyewe kwa wenyewe? Hivyo kuna hali mbaya sana…redio hazitangazi chochote zaidi ya propaganda za mapigano yanayoendelea humu nchini. Na ukizingatia kuwa serikali ya hapa inawaunga mkono wale waasi wa Sierra Leone ndiyo kabisa!”
Baddi alikunja uso kuitafakari habari ile. Aliona ugumu wa kupata habari za kweli kuhusu wenzake kupitia vyombo vya habari vya Liberia.
“Je, kuna namna yoyote ya kupata mawasiliano ya simu? Nahitaji kuwajulisha wenzangu kuwa niko huku…au kuwasiliana moja kwa moja na nyumbani…”
“Simu ndiyo balaa kabisa huku brother. Yaani ukionekana na simu tu basi ujue ni kifo kwako, kwani moja kwa moja unaonekana kuwa ni msaliti unayetumia simu kutoa habari kwa majeshi pinzani...hapa ndugu yangu tumo shimoni. Mimi nimekuwa hapa kwa miezi tisa sasa, na nimejaribu kutafuta namna ya kurejea nyumbani nimeshindwa...hakuna namna ya kutoka mpaka hii vita iishe; na haina dalili za kuisha leo wala kesho...”
“Hapana, mi’lazima niondoke hapa. Siwezi kukaa miezi tisa huku...lazima niondoke!”Baddi alisema.
“Mimi pia nataka kuondoka huku kakaangu…na kama we’ utaweza kunisaidia kutoka kwenye shimo hili basi nitakushukuru sana. Labda tukiwa wawili tutaweza, lakini mimi peke yangu nimeshindwa!” Gilda alimjibu na kimya kilichukua nafasi kwa muda. Baddi alijisikia kuchoka sana.
“Nahitaji kurejesha nguvu kwanza…na hiki kidonda kipone, lakini lazima
MDUNGUAJI
tuondoke hapa. Lazima nirudi kwa wenzangu...na lazima turudi nyumbani!”
Alisema kwa dhamira. Gilda hakumjibu kitu.Alibaki akimtazama kwa simanzi, kisha akamwambia, “Nadhani inakubidi upumzike sasa…”
“No. Naomba unieleze ni jinsi gani wewe ulifika huku…na ni vipi uliweza kuwa na pesa za kuwahonga wale akina dada walionikuta kule mtoni na kumlipa yule tabibu aliyenitibu. Naona hilo ni jambo zito sana, hasa kwa huku ugenini...” Baddi alimwambia huku akimtazama kwa makini. Ndipo Gilda alipomuelezea kisa chake...
“Naitwa Gilda Shehoza, mzaliwa waTanga kule Tanzania,lakini nimekulia na kusomea jijini Dar. Nilimaliza kidato cha nne ila sikufaulu kwenda kidato cha tano. Baba alinitafutia shule ya kulipia na nikaanza kidato cha tano, lakini miezi sita tu tangu nianze kidato hicho cha tano, nikapata kijana aliyenilaghai na kunibebesha mimba. Baba akanitimua nyumbani kwake huko Mbagala, na jamaa nilipomfuata akaniruka futi mia! Nikabaki pekee nisiye na uelekeo. Shangazi yangu akanipa nauli nikarudi kwetu Korogwe, ambako nilijifungua kwa taabu sana, lakini bahati nzuri sana yule mtoto hakuwa riziki, alifia tumboni…”
Baddi alitupia jicho na kuuliza, “Bahati nzuri…?”
“...ndiyo, nasema bahati nzuri kwani kama asingekufa yule mtoto ningemleaje unadhani? Nashukuru kuwa sikumtupa chooni wala sikuitoa ile mimba, nilibeba mzigo kwa miezi yote tisa, sijui ni kitu gani lakini bila shaka matunzo duni ya mimba na utoto nao vilichangia kufanya mtoto yule afie tumboni. Anyway , nilirudi tena jijini baada ya kurudisha afya yangu na moja kwa moja nikaanza kazi ya kuuza baa, nikiwa nimepanga chumba maeneo ya Mwananyamala. Kwa miaka mitatu nimekuwa nikipitia misukosuko mbalimbali ya maisha pale Dar, na ndipo mwaka mmoja uliopita nilipokutana na mzungu mmoja raia wa Ufaransa ambaye alinipenda, na nikawa natoka naye. Yeye ndiye aliyeniachisha kazi ya kuuza baa na akanipatia ajira kwenye duka moja kubwa la nguo jijini Dar, duka ambalo lilikuwa linamilikiwa na dada mmoja raia wa ufaransa....”
Gilda alitulia kidogo, na kuendelea kumfahamisha kuwa ni huyo mpenzi wake wa kifaransa ndiye aliyemshawishi wasafiri pamoja hadi Liberia ambako alidai kuwa alikuwa ana mpango wa biashara kubwa ya almasi. Hapo Baddi akawa makini sana, akili yake ikarudi kule kwenye mzozo baina yake na
msaliti Nathan Mwombeki juu ya hizo hizo almasi. Almasi za damu.
“Almasi?”
“Yeah almasi...ndivyo alivyoniambia...”
“Enhe?”
“Tukaja bwana! Na kweli, almasi zilikuwepo. Tulifikia Monrovia, ambako aliniacha hotelini kwa muda naye akaenda kukutana na hao watu wenye hizo almasi, na jioni aliporudi alikuwa na rundo la almasi ambazo aliziweka
kwenye kifuko kidogo kirefu kilichokuwa kwenye muundo wa soksi, kisha akazificha juu ya dari kwenye bafu la mle chumbani....”
“Sasa hizo almasi, alizinunua au...?”
“Kwa kweli mi’ sijui...sikuwa nikimuuliza sana kuhusu biashara zake. Aliniambia kuwa tutasubiri kwa siku kama nne hivi ili “mzigo fulani” uingie, kisha tutaondoka kurudi zetu bongo. Mimi nilikuwa nafurahia tu kustarehe naye, na kwa kuwa wakati huo machafuko yalikuwa bado hayajashamiri, basi nilikuwa nimepumbazika tu na raha za kutembelea nchi ngeni…”
“Kwa hiyo sasa ye’ yuko wapi?” Baddi aliuliza.
“Ameuawa!”
“What?”
“Ndiyo...ameuawa na hawa wapiganaji wahumu nchini...”
“Sasa…ulijuaje kuwa hao waliomuua ni wapiganaji wanaoendeleza vita hapa Liberia…?”
“Ni kutokana na mavazi yao…magwanda yao…! Sijui Francois alikuwa na dili gani na hawa watu, lakini inaelekea kile alichokuwa amewaahidi kuwapatia hata wao wakampa zile almasi, hakuwapatia...”
“Silaha...” Baddi alisema.
“Nini...?”
“Itakuwa ni silaha tu. Hawa wapiganaji wa ukanda huu wote, Sierra Leone, Liberia...wanabadilishana almasi kwa silaha ili waweze kuendelea kupigana. Inaelekea jamaa yako, Francois, alikuwa akijihusisha na biashara ya kuingiza silaha haramu...akibadilishana na almasi.” Baddi alimwambia. Gilda alitikisa kichwa kwa masikitiko makubwa.“Inaweza kuwa hivyo Baddi, lakini kwangu mimi alikuwa ni mtu mzuri sana.Alinirejeshea heshima fulani niliyobaki nayo hapa duniani…alinijali na aliniamini sana.”
“Hiyo haina ubishi Gilda. Sasa aliuawa vipi…ilikuwaje hata ukawa na hakika kuwa ameuawa?”
MDUNGUAJI
“Siku hiyo tulikuwa tumejipumnzisha chumbani kwetu pale hotelini ndipo watu; wenye magwanda na silaha walipovamia na kuanza kumpiga huku wakimuuliza mambo fulani kwa lugha ya kifaransa ambayo mimi sikuwa nikiielewa vizuri...Francois alijitahidi kuwaeleza aliyokuwa akiwaeleza, lakini hawakumsikiliza hata kidogo. Wakanihoji na mimi huku wakinipiga, lakini mimi nikawa sielewi ile lugha, hivyo wakawa wananipiga bure tu. Francois hakuweza kuvumilia na akajaribu kupambana nao....” Hapo Gilda aligeuza uso wake pembeni na kuanza kulia.
“...wakamchabanga marisasi mbele ya macho yangu...!”Alisema huku akiangua kilio. “...wakamuua bwana...kama mbwa!”
“Pole sana...”.
Gilda alilia kwa muda, kisha akajifuta machozi na kumtazama tena Baddi.
“Milio ya bunduki ilileta mtafaruku mle hotelini, na wale watu walikimbia wakiniacha na maiti ya Francois mle ndani...”
“Loh!”
“Sikujua nifanye nini. Nilikuwa kwenye nchi ngeni, mwenyeji wangu ndiyo ameuawa, sikuwa na uelekeo. Nilijua kama askari wa nchi hii wangenikuta na maiti mle ndani, ningetupwa jela tu na kusahauliwa huko huko wakati wenyewe wanaendelea na mapambano yao...”
“Kweli kabisa!”
“Kwa hiyo nilichofanya ni kuchukua begi langu likiwa na pasi yangu ya kusafiria. Nikapanda pale juu ya dari nakuchukua kile kifuko cha almasi na kukishindilia kwenye sidiria yangu. Nilijua kuwa ningehitaji sana pesa nikiwa peke yangu mitaani, hivyo huku nikilia na nikimtaka radhi Francois aliyelala bila uhai sakafuni, nilifungua begi lake na kuchukua pesa zote alizokuwa nazo, ambazo zilikuwa nyingi tu, kisha nikatoka nje ya hoteli ile na kujichanganya mitaani ambako kulikuwa kumeanza kuchafuka kwa mapigano...
“...na kwa miezi tisa iliyofuata, nimekuwa nikikimbia kutoka mji mmoja kwenda mwingine ndani ya nchi hii, nikitafuta namna ya kurudi nyumbani
bila mafanikio. Pesa za Francois ndizo zilizokuwa zikinisaidia siku zote, na nilipoishiwa na pesa, niliuza almasi kidogo kwa bei nafuu na kuweza kuendelea kujikimu....na ni kwa pesa hizo ndivyo nilivyoweza kuwahonga
wale akina dada wasiseme juu ya kuwepo kwako kule kijijini, na pia niliweza
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
kumlipa yule tabibu...” Gilda alimalizia.
Baddi alishusha pumzi ndefu, akilini mwake akikiri kuwa kweli yule dada alikuwa amepitia misukosuko mizito.
“Sasa ilikuwaje hata ukawa kule kijijini...?” Alimuuliza.
“Ni katika kuhangaika tu...Monrovia, mji mkuu wa nchi hii, watu wanauawa kama kuku...yaani kule kifo kinakuja kirahisi sana. Huku vijijini ndiyo kuna usalama kidogo, lakini hasa kilichonipeleka kwenye kile kijiji ni kwamba kiasi cha meizi miwili iliyopita, nilipata habari kutoka kwa akina dada waliotoroka
kwenye kambi moja ya waasi kuwa kijiji kile ndiko ambako helikopta zinazoleta shehena ya silaha huwa zinashuka na kuondoka. Hivyo kama ukiwa na pesa, unaweza kupata usafiri kwa njia hiyo ya helikopta na kutoka nje ya nchi hii…lakini mpaka siku ile wewe unaokotwa pale kando ya mto, hakuna helikopta yoyote iliyoingia...” Baddi alimvulia kofia yule dada kwa ujasiri.
“Duh, e bwana pole sister. Sasa kwa kuhama kule kijijini huoni kuwa ndiyo utakuwa umepoteza kabisa nafasi ya kuipata hiyo helikopta pindi ikija?”
“Ni kweli, lakini pia nisingeweza kuacha maisha yangu na yako yawe hatarini kwa kuendelea kubaki kule. Iwapo yule tabibu angeenda kusema huko lazima waasi au wanajeshi wa serikali wangekuja kukufuata na wangetuangamiza sote. Bora hivi...tutapanga namna ya kujiokoa kutokea hapa tulipo sasa, kwani vichwa viwili ni bora kuliko kimoja...au siyo?” Baddi aliafiki kwa kichwa, uso akiwa ameukunja kwa tafakuri.
Miezi sita ilipita tangu wawili wale wakutane katika nchi ile ngeni iliyojaa machafuko, na bado hawakuwa wamepata namna ya kurejea nyumbani. Lile jeraha la risasi lilipona na kumuachia kovu baya kutokana na matibabu ya kulazimisha na yasiyo rasmi aliyopata. Mguu wake wa kushoto bado ulikuwa unamtatiza, kwani hakuweza.kuusimamia moja kwa moja na mara nyingi ulishindwa kufanya kazi kama ipaswavyo. Akawa anatembelea mkongojo pale kijijini huku akijitahidi kuupa mazoezi ya kutosha. Siku zote hizo Gilda alikuwa pamoja naye na walizidi kuzoeana na kuongea mambo mengi juu yao. Baddi akimueleza juu ya familia yake aliyoiacha Tanzania, na Gilda akimuelezea kwa undani zaidi juu ya jamaa zake walioko Tanzania.
Gilda alikuwa akitoka kwenda mjini mara moja moja na kurejea na baadhi ya mahitaji, na wakati huohuo alikuwa akiendelea kufuatilia habari kuhusu ujio wa zile helikopta za silaha za magendo, walizotegemea kuzitumia kutoka nje ya nchi ile iliyojaa machafuko, lakini hakukuwa na mafanikio
MDUNGUAJI
yoyote. Ilikuwa kama kwamba wale waasi wa Liberia walikuwa wamepata njia
nyingine ya kuingizia silaha zao.
Walikuwa wamekwama.
Akiwa amelala peke yake kitandani mle kibandani mwao, Baddi alikuwa akiitafakari ile hali iliyomchanganya sana. Miezi sita! Hapana, lazima afanye litakiwalo. Muda wa kuugulia majeraha sasa ulikuwa umekwisha!
Alijitahidi kuinuka kutoka pale kitandani na kujaribu kusimama
wima katikati ya chumba kile. Mguu ulimuuma sana, lakini alijilazimisha
kupiga hatua. Maumivu makali yalimtawala, lakini kama mpiganaji
aliyezoeshwa kupambana na majaribu ya kila hali, hakukubali kuendelea kukwazwa na mguu ule. Aliuma meno na kufinya uso kisha akapiga hatua nyingine, na moja kwa moja alienda chini kwa kishindo.
Alipiga ukelele wa hasira na kupiga ngumi sakafuni kabla ya kuinuka tena. Aliulazimisha mguu wake na kufanikiwa kutoka nje ya kibanda.Huko
alitembea kwa taabu sana kuuzuguka wigo wa kile kibanda cha matope. Jasho lilikuwa likimtoka, maumivu makali yakimtawala na mguu ukimuwia mzito kadiri alivyokuwa akisonga mbele.
Aliamua kurudi ndani, lakini lilikuwa ni zoezi zito sana. Hatua chache baada ya kuingia ndani ya nyumba ile alianguka na kubaki akitweta, moyo ukimpiga kwa nguvu na mguu ukimpwita vibaya sana. Alibaki akiwa amelala pale sakafuni bila msaada.
“Heh! Baddi...! Baddi...ni nini tena?” Gilda aliingia mle ndani na kumkuta akiwa amelala pale chini akitweta. Alipiga goti na kumtazama kwa karibu, uso wake ukionesha wasiwasi mkubwa.
“Umekuwaje Baddi?” Alimuuliza.
Baddi alikuwa akimtazama huku akiwa ameuma meno kwa kubana maumivu aliyokuwa nayo.
“Ah, huu mguu bwana....nilikuwa najaribu kutembea!”
“Oooh, Baddi jamani...bado hujapona wewe...usiwe na haraka...”
“Akh! Siwezi kuendelea kukaa hivi hivi tu Gilda wakati…wakati siku zina…kwenda!”
“Aaa, basi sio kwa namna hiyo Baadi jamani…hebu ona sasa...!” Gilda alimsema huku akianza kumuinua kutoka pale chini. Baddi alijitahidi kuinuka pamoja naye, na wakiwa wameshikana walijikongoja hadi kitandani ambapo Gilda alimlaza chali huku akiwa makini sana kutomuumiza tena mguu ule. Baddi alijikuta akimtazama kwa karibu zaidi yule dada na kwa mara nyingine alivutiwa na urembo wake.
Wakati Gilda akimlaza pale kitandani alizungusha macho yake na kumtazama usoni.
Macho yakagongana.
Wakabaki wakitazamana, nyuso zao zikiwa karibu sana, kiasi kwamba kila mmoja alipata joto la pumzi za mwenzake.Macho yao
yalizidi kushikana, na kila mmoja alipata ujumbe kutoka kwenye jicho la mwenzake.Taratibu Baddi aliinua mkono wake na kumpapasa shavuni yule dada.
“Thanks!” Alimwambia kwa sauti iliyojaa mikwaruzo, moyo ukimwenda mbio na pumzi zikimtoka kwa mikupuo mifupi mifupi.Badala ya kumjibu moja kwa moja Gilda alimparamia kwa busu kali la kinywani, na kama kwamba aliyekuwa akisubiri kuanzwa, Baddi Gobbos alilipokea busu lile kwa bashasha zote, ndimi zao zikikutana ndani ya vinywa vyao huku akimvutia kifuani kwake yule binti aliyekaa naye kule kijijini kwa miezi sita.
Kwa muda maumivu ya mguu, na vumbi la mchanga wa mle ndani lililomtapakaa baada ya kuanguka pale sakafuni vilisahaulika wakati wawili wale walipokuwa wakipeana mahaba mazito na yaliyojaa utashi mkubwa. Kisha ghafla, kama walivyoanza, Gilda alikatisha busu lile zito na refu.
Walibaki wakitazamana huku wakitweta. Kisha taratibu yule dada alianza kutoa viwalo vyake kimoja baada ya kingine, huku Baddi Gobbos akimtazama kwa uchu.Gilda akaanza kumtoa Baddi nguo zake moja baada ya nyingine. Hakuna aliyeongea.
Mioyo ilikuwa ikiwapiga kwa kasi ya ajabu. Kila mmoja alijua ni nini alikuwa anataka kutoka kwa mwenzake. Kisha Gilda alivuta begi lake na kutoa mpira wa kiume.
Na kuanzia hapo uhusiano wao uliingia kwenye hatua nyingine kabisa.
Miezi miwili baadaye, Baddi alikuwa amepona kabisa mguu wake, ingawa alilazimika kutembea kwa kuchechemea. Tayari alikuwa amemaliza miezi minane tangu alipoanguka korongoni kule kwenye msitu
MDUNGUAJI
wa Tumbudu, nchini Sierra Leone.
“Sasa nadhani tunaweza kuanza mikakati ya kuondoka nchi hii kwa njia nyingine Gilda...”Alimwambia Gilda wakiwa wamekalia gogo nyuma ya kibanda chao pale kijijini.Gilda aliafiki kwa kichwa, kabla ya kutaka kujua alikuwa amefikiria kuondoka kwa njia gani baada ya kushindikana ile ya kutumia helikopta ziletazo silaha za magendo.
“Kwanza ni muhimu tukapata mawasiliano na nyumbani au na wenzagu kule Sierra Leone, ingawa wao sijui nitawasiliana nao vipi...”
“Mnh! Baddi, simu ni hatari sana huku! Hakuna mtu anayekubali kuonekana na simu…”
“Sasa tutafanyaje? Si kuna shirika la simu la taifa? Tunaweza kwenda kujaribu kupiga Tanzania...”
“Mara ya mwisho nilipojaribu kufanya hivyo hakukuwa na hata simu moja ifanyayo kazi...mikonga ya simu yote ilikuwa imeng’olewa na waasi na nchi nzima haikuwa na mawasiliano...isipokuwa kwenye hizo kambi zao za kijeshi tu. Sasa nani ataweza kuingia kwenye kambi ya kijeshi na kuomba simu?” Gilda alisema na kumalizia na swali.Baddi alitulia kimya kwa muda.
“Ah, basi kama ndivyo, tukifanikiwa kuipata kambi ya jeshi la serikali, itakuwa rahisi Gilda...mimi ni mpiganaji wa jeshi la Umoja wa Mataifa, nikijitambulisha kwao kwa vyovyote nitapata msaada uhitajikao...tunaweza kurudishwa tu mpaka Sierra Leone, na tukifika huko tu tumeokoka!” Baddi alitoa hoja, na Gilda alitikisa kichwa kwa kukata tamaa.
“Baddi, mi’ nimekaa nchi hii zaidi ya mwaka sasa...nakwambia ni vigumu sana kujua ni yupi askari wa serikali na yupi wa waasi...lakini hilo si tatizo, tatizo la hapa ni kwamba hayo majeshi ya serikali ndiyo yanayowaunga mkono waasi wa Sierra Leone! Hivyo salama yako ni kwenda kwa waasi wanaoipinga serikali ya Liberia, ambao nao wamegawanyika kwenye vikundi tofauti-tofauti! Wala hutakiwi kabisa kujihusisha nao
Baddi, kwani huenda ukaishia kuwa mateka wao tu...kuna mashaka
mazito sana hapa!” Gilda alimwambia kwa msisitizo.Baddi aliuona ukweli katika maelezo yale.
Ngoma nzito!
“ All in all , bado tuna wajibu wa kujaribu kupata mawasiliano Gilda… naamini nikiweza kuwasiliana na mke wangu kule Dar, anaweza kwenda
makao makuu ya jeshi na kuwapa taarifa, kisha wao watawasiliana na kambi
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI ya umoja wa mataifa pale Sierra Leone na rescue mission itaandaliwa tu…”
Baddi alikazia hoja yake. Nusu saa baadaye walikuwa kwenye basi la abiria kuelekea mjini. Gilda alikuwa amempatia Baddi nguo za kiraia ambazo hazikumtofautisha na wanaume wengine watokao vijijini.
Jiji la Monrovia lilikuwa limechafuka vibaya sana. Baddi Gobbos alishuhudia mabaki ya magari yaliyoteketezwa, maiti wakiwa wamezagaa ovyo mitaani kama mizoga; magari yenye askari waliokuwa na silaha za moto na za hali ya juu sana, ambao hakuweza kabisa kujua iwapo ni wa serikali au waasi, yakizunguka kila kona mitaani. Ilikuwa ni mashaka makubwa.
Gilda alimuongoza hadi kwenye jengo la shirika la simu la nchi ile, ambamo walikuta msururu mrefu sana wa watu waliokuwa wakijaribu kutafuta mawasiliano kwa kutumia simu moja tu iliyokuwa ikifanya kazi.
“Eh! Hii si zahma tena hii jamani!” Gilda alimaka kwa hamaniko.
“Yeah, lakini hatuna namna…tutasubiri tu mpaka zamu yetu ifike…”
Zamu yao ilifika baada ya kusimama kwenye foleni kwa saa nne. Gilda
aliyekuwa akiifahamu kidogo lugha ya wenyeji aliongea na yule karani aliyekuwa akipigisha simu.
“Tunataka kupiga simu Tanzania…”
“Namba…?” Karani alimuuliza, na Gilda akamgeukia Baddi, ambaye bila hata ya kufikiri sana aliitamka namba ya simu ya nyumbani kwake huko Tanzania, na kusubiri wakati yule karani akiipiga ile namba. Alianza kujiuliza ni nani atakayepokea simu kule nyumbani kwake muda ule. Bila shaka atapokea baba, kwani mke wangu atakuwa kazini...
Ghafla mawazo yake yalikatishwa kwa vishindo na sauti za taharuki kutokea kila upande mle ndani.
What the...?
Kundi la wapiganaji wenye silaha waliovalia sare za kijeshi lilikuwa limeingia mle ndani kwa mikiki. Watu wote waliokuwa mle ndani walikuwa wakipiga mayowe kwa woga huku wakijisogeza
pembeni kuwapisha. Baddi alimkamata Gilda kiunoni kwa namna ya kumlinda huku akimtupia macho yule dada aliyekuwa akiwapigia ile
simu.Dada alikuwa ameirudisha chini ile simu na badala yake alikuwa
akiwatazama wale wapiganaji kwa woga usio kifani. Na hata pale alipokuwa
akimtazama yule dada, mmoja wa wale wapiganaji alifika pale mbele na kumsukuma Baddi pembeni na kuanza kumuamuru yule dada kwa lugha
MDUNGUAJI
ambayo Baddi hakuielewa, lakini mara moja alijua kuwa alikuwa
akimshurutisha ampigie simu.
“Tusogee pembeni Baddi!” Gilda alimnong’oneza huku naye akijisogeza pembeni. Na ndipo Baddi alipogundua kuwa watu wote waliokuwa
wamefoleni nyuma yao walikuwa wametawanyika kuwapisha njia wale
wapiganaji, na kuwaacha yeye na Gilda tu pale kaunta. Taratibu
alianza kusogea pembeni lakini muda huohuo mmoja wa wale wapiganaji
walioingia mle ndani alimsogelea na kuanza kumkemea huku
akimtumbulia macho na kumuoneshea bunduki!
Baddi hakuelewa kitu na hivyo alizidi kurudi nyuma akiwa kimya.
Jamaa alizidi kumuuliza kwa ukali huku akimtumbulia macho
yake mekundu. Baddi alianza kufunua kinywa kutaka kumwambia kwa lugha ya kiingereza kuwa alikuwa hamuelewi wakati Gilda alipojitokeza mbele na kumueleza yule askari haraka haraka na kwa wasi wasi sana kwa ile lugha ya wenyeji wa pale huku akimuoneshea Baddi na akishiria kwa mikono yake.Mara moja Baddi alitambua kuwa alikuwa anamfahamisha yule askari kwamba yeye alikuwa bubu!
E bwana we! Yule mwanadada kiboko! Kwani iwapo Baddi angeongea jambo lolote tu kwa kiingereza au hata kiswahili, basi angejulikana kuwa yeye si mwenyeji wa pale na hapo kila kitu kingeharibika.
Alizungusha macho mle ndani kutafuta njia ya kutorokea iwapo hali
ingeelekea kuwa nzito.Wale wapiganaji wengine walikuwa makini na silaha zao. Yule kiongozi wao alikuwa akiongea kwenye simu kwa sauti ya juu huku akifoka kwa ile lugha ya kikwao. Alirudisha macho kwa yule askari aliyekuwa akimsemesha kwa ukali, ambaye sasa alibaki akimtazama Gilda kwa hasira hali watu wote mle ndani wakiwa kimya kabisa. Yule askari akamsogeza Gilda pembeni na kumfuata Baddi. Walitazamana kwa hasira kwa muda, kisha akamtemea neno moja kwa ukali, ambalo mara moja Baddi alijua kuwa lilikuwa ni tusi. Hakuelewa kwa nini ametukanwa, lakini alibaki akimtazama tu.
Baada ya hapo jamaa akatoa msonyo mrefu na mkali, halafu
akageuka na kumkamata Gilda mkono na kuanza kumvuta kuelekea upande mwingine wa chumba kile.Gilda alipiga kelele kupinga hali ile, akimuomba yule askari amwachie kwa lugha ya wenyeji wa pale huku
akijitahidi kujichomoa mikononi mwake. Jamaa alimgeukia na kumchapa kofi kali lililomsukuma mpaka chini. Yowe lilimtoka Gilda pamoja na akina mama wengine waliokuwamo mle ndani. Jamaa alimuinamia pale chini
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI na kumkemea kwa ukali huku akimnyooshea kidole.
Baddi alifura kwa hasira. Alitamani amrukie yule jamaa na ampe mapigo kadhaa, lakini alijua kuwa hilo lingekuwa ni kosa kubwa.Aliwatazama wale wapiganaji wengine na kuona kuwa walikuwa wakilitazama lile tukio kama kwamba lilikuwa la kawaida tu. Gilda alijaribu kuinuka na yule mpiganaji alimkamata shingoni na kuanza kumburura kuelekea nje ya ofisi ile.
“Nooo! Niachie bwana! Unaniumiz-Baddiii…!” Gilda alijikuta akipiga kelele kwa kiswahili. Yule jamaa alizubaa kidogo baada ya kusikia ile lugha ngeni masikioni kwake. Na hapo Baddi alijua kuwa hali ilikuwa imeharibika. Hakuiacha iharibike zaidi.
Alipiga hatua moja kubwa na kuchomoa bastola iliyokuwa ikining’inia kiunoni kwa yule mkuu wa wale wapiganaji aliyekuwa akiongea na simu, na wakati huohuo akimrukia na kumbabatiza uso juu ya ile kaunta kisha akamuwekea mdomo wa ile bastola kisogoni.
“STAY RIGHT THERE!” Alifoka kwa ukali huku akimtumbulia macho yule askari aliyemkamata Gilda. Kilichofuata ni kizaazaa kikubwa.
Wale wapiganaji wengine walikuwa wakimkemea kwa ukali huku wakimuoneshea bunduki zao, ilhali yule aliyemkamata Gilda alibaki akiwa amemng’ang’ania yule binti huku akimtazama kwa macho yaliyojaa mashaka, udadisi na chuki kubwa.
“I say let the girl go…NOW!” Baddi alimaka kwa kiingereza, akiwaamuru wamuachie yule binbti mara moja. Jamaa walizidi kumkodolea macho na kumuoneshea bunduki huku yule mwingine bado akiwa amemng’ang’ania Gilda.Baddi alimuinua kwa nguvu yule kiongozi wao kutoka pale kwenye uso wa ile kaunta na kumkaba kabali huku akiwa amemuwekea bastola kwenye upande wa kichwa chake.
“Waambie watu wako wakae mbali...na yule mpumbavu amuachie yule binti...upesi!” Alimwambia kwa lugha ya kiingereza,akitaraji tu kuwa yule jamaa atamuelewa.
“Unafanya, kosa kubwa sana wewe…sisi ni wapiganaji wa jeshi la serikali! Hutakiwi kabisa kupingana nasi! Umetoka wapi wewe? Unaonekana kuwa si raia wa hapa!” Yule kiongozi wa wapiganaji alimjibu kwa sauti ya kunong’ona iliyojaa ghadhabu kwa kiingereza kibovu.
“Fanya nililokwambia la si hivyo natawanya ubongo wako mchafu sasa hivi!” Baddi alimkoromea huku akiikandamiza ile bastola kichwani kwa yule jamaa ili kutia msisitizo. Kule alipokuwa, Gilda
MDUNGUAJI
alikuwa hajiwezi kwa taharuki. Ama kwa hakika sasa mambo yalikuwa yameharibika.
“Mwachie huyo binti...haraka!” Jamaa alimwamuru yule mfuasi wake, ambaye alitoa jibu la kumbishia, lakini hapohapo yule kiongozi wao alimkatisha kwa ukali.
“Nimesema muachie!”
Jamaa alimsukuma Gilda mbele kwa nguvu, ambaye alipiga mweleka mzito mle ndani, na hapohapo alijiinua na kuanza kukimbilia kule alipokuwa Baddi.
“NO! Usije kwangu Gilda! Ondoka humu ndani na ukimbie! Kimbia na wala usinifikirie mimi…Go!” Baddi alimkemea. Gilda alisita na kubaki akimkodolea macho.
“Baddi…!”
“GO! Gilda…GO!” Baddi alifoka, na hapohapo alifyatua risasi hewani mle ndani. Tafrani iliyofuatia hapo si ya kitoto! Raia waliokuwa mle ndani walipiga kelele za woga huku wakianza kukimbilia nje ya jengo lile. Wale wapiganaji walijaribu kuwazuia kwa kuwalengeshea bunduki zao, lakini Baddi alikoroma tena kwa sauti.
“Waacheni wote!” Kisha akamgeukia yule kiongozi wa wale wapiganaji aliyemkwida, “Waambie watulie!”
Jamaa alitoa amri na watu wake walibaki wakiwatazama wale raia wakitoka mbio nje ya jengo lile hali Gilda alibaki akiwa ameduwaa katikati ya chumba kile.
“Nenda wewe! Mi’ n’tasevu kivyangu-vyangu tu… usiwe na wasi!” Baddi alimhimiza. Raia walikuwa wakizidi kutoka mbio nje ya chumba kile, na Gilda aliona kuwa Baddi alikuwa amedhamiria. Huku akitokwa na machozi, alimtupia jicho lililojaa upendo na uchungu, kisha akatoka mbio nje ya jengo lile akijichanganya na wale raia wengine.
Akiwa amebaki peke yake na wale wapiganaji mle ndani, Baddi alimburura yule kiongozi wao kuelekea nje ya jengo lile huku akiwa amemuweka mbele yake kama ngao. Wale wapiganaji wengine walikuwa wakimfuata kimya kimya huku wakiwa wamemuelekezea bunduki zao.
“Si unajua kuwa wewe sasa ni mfu?” Yule mateka wake alimuuliza kwa hasira huku akisota kufuata kule alipokuwa akibururiwa.
“Kifo ndiyo jina langu la kati kwa taarifa yako bloody swine wewe! Tafuta jambo jingine la kunitishia lakini sio kifo!” Baddi alimkoromea huku akiwa makini sana.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Sasa walikuwa wamefika nje ya lile jengo. Akatupa macho huku na huko na kuona watu wengi wakikimbia ovyo mitaani. Kuongeza kizaazaa alifyatua risasi
nyingine tatu hewani, kisha kwa nguvu sana alimsukumia ndani ya lile jengo yule askari, naye akageuka na kutimua mbio kujichanganya na watu waliokuwa
wakikimbia ovyo pale nje, nyuma yake akisikia makelele ya jazba kutoka kwa
wale wapiganaji yakiambatana na milio ya bunduki.
Alikunja kona na kutokomea ubavuni mwa jengo lile. Akakutana uso kwa uso na mpiganaji mmoja ambaye aliruka dirishani kutoka ndani ya jengo lile.
Baddi alifyatua risasi na yule mpiganaji alianguka huku akitoa yowe la uchungu. Alizidi kutimua mbio kwa mtindo wa zigi-zaga, raia kadhaa wakianguka huku na huko na milio ya risasi ikirindima kutokea kila upande.
Kutokea mbele yake aliona gari aina ya LandRover 110 lililokuwa katika muundo wa pick-up likimwendea kwa kasi huku watu wenye silaha waliokuwa nyuma ya gari lile wakimtupia risasi.
Mungu wangu…!
Alijitupa pembeni na kujibanza kwenye kiwambaza cha jengo lililokuwa karibu yake na kugeuka kule alipokuwa ametokea. Huko aliona watu wakikimbia ovyo huku wale wapiganaji waliokuwa wakimkimbiza wakiwa wanaelekeza bunduki zao kule kwenye ile Land Rover. Ah, ni nini tena?
Aliligeukia lile Land Rover na kuona kuwa wale wau wenye silaha waliokuwa kwenye lile gari hawakuwa wamevaa sare maalum bali nguo za ovyo ovyo tu. Waasi!
Alichomoka mbio na kuingia mtaa mwingine, akiacha wale wapiganaji wakitupiana risasi na waasi naye akajichanganya na raia wengine pale mtaani. Alitoa shati alilokuwa amevaa na kulitupa, akabaki na fulana nyepesi ya ndani. Aliongeza mwendo huku akijaribu kutafuta sehemu yoyote ambayo angeweza kupata basi la kumrejesha kule kijijini alipokuwa akiishi na Gilda.
Ah, Gilda masikini. Sijui atafanikiwa kurudi kule kijijini...?
Muda huu alikuwa amechoka na amekata tamaa kabisa. Alitokea kwenye
kitongoji fulani ambako alikuta watu kadhaa wakiwa wamekaa kwa kukata
tamaa nje ya jengo moja naye akaenda kukaa kando yao akivuta pumzi na kujaribu kujipanga upya. Muda mfupi tu baadaye gari la askari wa doria liliingia
eneo lile. Baddi alihamanika na kuanza kutazama huku na huko, lakini aliona
kuwa wale watu aliokuwa amekaa nao pale hawakuwa na wasi wasi wowote, naye akatulia.Wale askari walitaka kila mmoja aoneshe kitambulisho au pasi ya kusafiria, na kwa kihoro kikubwa Baddi aliwashuhudia wale wenzake
MDUNGUAJI
wakitoa aina fulani ya vitambulisho ambavyo wale askari walivikagua na kuwarejeshea.
Yeye hakuwa na kitu chochote cha kumtambulisha, na hakuwa na namna yoyote ya kutoroka kutoka pale. Ilipofika zamu yake wale askari walimuuliza kwa lugha ambayo hakuielewa.
“Mimi ni mgeni…raia wa Tanzania. Nimepoteza kila kitu huko mjini…nimeporwa na watu nisiowajua. Sina kitu chochote hapa nilipo, na sijui nitarudi vipi nchini kwangu!” Baddi alijieleza kwa kiingereza.
Yule askari alimtazama kwa muda kisha akamwita mwenzake, ambaye bila shaka alikuwa anaelewa kiingereza na Baddi akajieleza tena kwa yule mwenzake. Hapo jamaa akawa makini na mdadisi zaidi.
“Sasa umeingia lini Liberia... na umeingiaje?”
“Ni zaidi ya mwaka mmoja sasa.Nilikuja kwa ndege tu ya kawaida...lakini sasa naona nchi imechafuka…”
“Ulikuja kwa nia gani?”
“Kutafuta madini...almasi...”
Yule askari alimcheka kwa jibu lile, na Baddi akaona huenda akapata unafuu fulani. Ni wazi kuwa habari za kizaazaa alichozusha kule kwenye jengo la shirika la posta hazikuwa zimewafikia wale askari.
“Na ni nani aliyekwambia kuwa huku kuna almasi za kuokota wewe?”
Baddi hakujibu.
“Sasa sisi tunadhani wewe ni muongo…na mpaka tutakapothibitisha hayo maelezo yako, tutakuweka chini ya ulinzi. Simama!” Yule askari alimwambia na kumuamuru huku akiwa makini sana. Baddi alitii na mmoja wa wale askari akaanza kumsachi.
Ndipo walipomkuta na ile bastola!
Kilichofuata hapo ni makofi, kusukwa-sukwa na maswali ya mfululizo, kubwa kuliko yote likiwa ni wapi ameipata ile bastola.
“Jamani…hii nchi yenu haina amani kabisa! Mi’ nimeiokota! Kila nikipita watu wanauawa kama mbwa, sasa kwa nini nisiiokote wakati nimeikuta imezagaa tu barabarani? Labda na mimi ingenisaidia kujiokoa! Mi’ nimeporwa vitu vyangu vyote, kama ningekuwa na hii bastola si ningejitetea?” Baddi alijitahidi kujitetea kwa kusema uongo.
“Hakuna! Wewe ni muasi tu…!”
“Khah! Sasa nitakuwa muasi wa upande gani wakati mi’ nawaambia ni raia wa Tanzania? Nipelekeni kwenye ubalozi basi!”
“Unajua kabisa kuwa balozi zote zimeondoka Liberia halafu unasema
tukupeleke ubalozini? Wewe ni mamluki wa waasi! Tunakupeleka gerezani, huko ndiko mahala pekee panapokufaa kwa sasa!” Jamaa alimkemea.
Alizolewa na kutupwa kwenye gari la wale askari na kupelekwa moja kwa moja hadi kwenye gereza lililokuwa nje ya jiji la Monrovia
ambako alijikuta akitumikia kifungo bila ya hukumu kwa muda wa mwaka mzima.
Ndani ya mwaka mmoja huo hakusikia habari yoyote juu ya Gilda wala juu ya harakati za jeshi la Umoja wa Mataifa katika eneo lile la Afrika ya Magharibi. Baddi Gobbos alikata tamaa kabisa ya kuonana tena na yule mrembo mwenye mapenzi mazito, na alikata tamaa ya kurudi tena nyumbani kuungana na mke na familia yake.
Alikuwa amepotelea ughaibuni.
Ndivyo alivyoamini mpaka pale alipokutana na Ghudia Al-Haddad.
Miezi michache kabla ya kutimiza mwaka mle gerezani, Baddi alipata mshituko mkubwa pale alipojikuta akiitwa na askari wa pale gerezani.
“Hey, Tanzanie!” Mahabusu wenzake na askari wote wa mle gerezani walizoea kumwita kwa jina la “Tanzanie”, kutokana na habari ya kuwa alikuwa ametokea Tanzania kuzagaa mle gerezani. Mwanzoni hii ilimpa wasi wasi sana, kwa hofu kuwa huenda habari hii ingewafikia wale wanajeshi aliowazushia kizaazaa hapo awali, lakini haikuwa hivyo. Nchi ilikuwa imechafuka, na wao walikuwa wamekazana kupigana na waasi wao kiasi waliwasahau kabisa mahabusu waliowasweka magerezani.
Alipoitikia wito ule aliambiwa kuwa alikuwa ana mgeni. Kufikia hapa sasa naye alikuwa ameshakamata baadhi ya maneno ya lugha ya wenyeji, ingawa wengi wa wenyeji walikuwa wakiongea kiingereza pia. Alishangaa sana kwani hakuwa amepata kutembelewa kule gerezani hata siku moja.
Ni nani?
Alikuwa akijiuliza lile swali tena na tena kichwani mwake wakati akimfuata yule askari wa magereza aliyekuwa akimuongoza kuelekea sehemu ambapo mahabusu walikuwa wanakutana na wageni wao.Huko alikuta mwanamke asiyemfahamu kabisa akimsubiri, akiwa amejitanda mavazi ya wenyeji wa kule Liberia ambayo yalikuwa kama khanga wavaazo akina mama wa ki-tanzania.
Alibaki akimtazama yule mama aliyejiinamia, akijishauri aongee naye kwa lugha gani, wakati kwa mshituko mkubwa kabisa aliposhuhudia yule mwanamke akiinua uso taratibu huku akijifunua ule ushungi.
“Gilda!” Alimaka kwa mshangao na kubaki akimkodolea macho yule mwanadada aliyekuwa ameketi mbele yake.
“Baddi...” Gilda alisema huku akiinuka, na bila ya kujali mazingira
waliyokuwamo walikumbatiana kwa muda kabla ya kuketi na kutazamana.
“Heh, Gilda…! Vipi bado uko nchi hii muda wote huu? Uko salama wewe? Mi’ nilidhani umeshaondoka kitambo!” Baddi alimtupia maswali mfululizo.
Gilda alimhakikishia kuwa yuko salama, na kwamba muda wote ule hakuweza kuondoka katika nchi ile kutokana na matatizo yale yale yaliyowakwaza hapo awali. Aidha alimjuza kuwa baada ya ile tafrani ya pale kwenye jengo la shirika la simu, alilazimika kurudi tena kule kijijini walipokuwa wakiishi na kujificha huko kwa miezi kama mitatu bila ya kwenda mjini kabisa, na kwamba muda wote huo alikuwa na mashaka mazito juu yake.
“Hakika nilijua kuwa nimeshakupoteza kabisa hapa duniani Baddi... nilikuwa kwenye majonzi mazito!”
“Sasa...imekuwaje leo uko hapa?”
Gilda aliguna kabla ya kumjibu, “yaani ni baada ya miezi hiyo kupita ndipo nilipoanza tena kutoka na kutafuta namna ya kurejea nyumbani. Nilikuwa nimeshakubali kabisa kuwa wewe haupo tena hapa duniani wakati kwa bahati tu, kiasi cha wiki moja iliyopita, nilipokutana na mwanamke niliyefahamiana naye kutoka kwenye kile kijiji nilichokuwa nikiishi kabla ya wewe kufika hapa Liberia. Aliniambia kuwa alikuja hapa gerezani kumuona mjomba wake, na ndipo huyo mjomba wake alipotamka kuwa kuna raia wa Tanzania humu gerezani. Yule dada kwa kujua kuwa nami nimetokea Tanzania akaja kuniambia…basi tangu siku hiyo sikuweza kupata usingizi kabisa Baddi...nilikuwa nikiomba
Mungu Mtanzania huyo awe wewe...na nashukuru kuwa Mungu ameitikia dua zangu! Nimefurahi sana kuonana tena nawe...”
Baddi alibaki kinywa wazi.
“Mi’ nashauri ufanye bidii uondoke Gilda. Mimi kutoka humu gerezani ni vigumu sana. Fanya uondoke na ukifika nyumbani ukatoe taarifa...hiyo ndiyo njia pekee!”
“Baddi Liberia ni sawa na shimo miongoni mwa mashimo ya jehanamu...hakutokeki kabisa…Nimejaribu!”
“Endelea kujaribu! Kwani kadiri nizijuavyo hizi serikali za kijeshi, ni kwamba wakiona tumesongamana sana humu gerezani wataanza kutuua kama kuku!”
“Yaani nimekuona uko hapa halafu niondoke kweli Baddi…?” Gilda alisaili kwa simanzi huku akilengwa machozi.
MDUNGUAJI
“Hamna jinsi Gilda…”
Hatimaye walikubaliana kuwa Gilda angekuwa anakwenda kumtembelea
angalau mara moja kila mwezi na kumpa habari za maendeleo yake katika bidii zake za kuitoka nchi ile. Na kiasi cha miezi miwili baada ya ule ujio wa Gilda, ndipo mtu aitwaye Ghudia Al-Haddaad alipoletwa pale gerezani.
Alikuwa na asili ya kiarabu na aliletwa akiwa ametapakaa damu kwa kipigo alichopata kutoka kwa askari wa kijeshi waliomkamata. Alibwagwa kama mzigo mahala ambapo Baddi alikuwa amejibanza mle gerezani. Baddi alimsaidia
kumuweka sawa pale alipoangukia na kumfuta damu huku akimpa pole.
“Asante sana jamaa...” Yule mtu alimshukuru kwa kimombo huku akimtazama kwa mashaka.
“Usijali...” Baddi alimjibu. Huo ndiyo ukawa mwanzo wa ujamaa wao mle gerezani na ndipo Baddi alipolijua jina lake. Kadiri siku zilivyokuwa zikipita, ndivyo walivyozidi kuwa karibu.
“Ni kweli nisikiavyo kuwa wewe umetokea Tanzania?” Ghudia alimuuliza na Baddi akaafiki. Ghudia alimtazama kwa muda, kisha akasema, “Nadhani mimi na wewe tunaweza kuaminiana, kwa kuwa sote tu-wageni hapa, sivyo?”
“Yeah...inawezekana...kwani wewe ulikuwa na lolote linalohitaji kuaminiana?”
“Labda tuseme nina jambo ambalo naamini wewe pia unalitaka…” Ghudia alimjibu, na alipoona Baddi anamtazama kwa macho ya kuuliza, alimfafanulia, “...kutoka humu gerezani. Naamini wewe pia unataka kutoka humu ndani, sivyo?”
“Hakika! Lakini sioni ni kwa jinsi gani...”
“Hata mimi sijui kwa sasa, lakini huenda kadiri siku ziendavyo tukapata namna. Hebu nieleze juu yako… ulifikaje hapa Liberia na imekuwaje hata ukaingia humu gerezani?”
Baddi alimueleza hadithi ya kuja Liberia kujaribu kutafuta almasi na kujikuta akiporwa vitu vyake vyote na kuanza kutangatanga ovyo mitaani mpaka akaangukia mikononi mwa wapiganaji wa jeshi la serikali waliomsweka rumande.
“Vipi wewe...ni kipi kisa chako?” Hatimaye alimuuliza, na ndipo Ghudia alipomwambia kuwa yeye ni raia wa Lebanoni na kwamba
alikuwa amekwenda pale Liberia kufanya makubaliano ya kubadilishana silaha kwa almasi na kundi moja la waasi, lakini kabla hajakutana na hao wenyeji wake alivamiwa na doria ya majeshi ya serikali na kukamatwa.
“Sasa uliingiaje humu nchini Ghudia?” Baddi alimuuliza kwa udadisi, moyo ukimwenda mbio.
“Ah, tuna njia zetu...” Ghudia alijibu kwa mkato, na Baddi akawa makini sana. Ndiyo zile njia za waletaji silaha haramu ambazo Gilda alikuwa akizitafuta?
Na kabla Baddi hajasema kitu zaidi, Ghudia aliendelea, “...lakini nitatoka tu humu Baddi...jamaa yangu akijua nilipo tu nitatoka!”
Baddi alishangaa.
“Kivipi Ghudia? Mi nimekaa mwaka mzima humu, na sijaona mtu akitoka akiwa hai...”
“Ni kweli, lakini kwa huyu jamaa yangu hilo si tatizo...tatizo ni yeye kujua mimi niko wapi!”
Baddi alipandwa udadisi.
“Niambie zaidi Ghudia, huenda tukasaidiana kutoka humu ndani!”
Ghudia alimtazama kwa muda mrefu bila ya kusema kitu, kisha akashusha pumzi na kumwambia kwa usiri mkubwa.
“Hivi unajua ni nani anayewapatia hawa askari wa serikali silaha?” Alimuuliza, lakini hapohapo alimjibu, “...huwezi kujua...lakini ukweli ni kwamba jumuia nzima ya kimataifa imesusa kabisa kuwauzia silaha wa-Liberia, kama ilivyosusa kununua Almasi zao na za jirani zao Sierra Leone...”
“Hiyo ni kweli...” Baddi aliafiki.
“Yeah...sasa sisi ndiyo tunaowapatia silaha...huyo mwenzangu ndiye anayewapatia silaha zao zote!”
Baddi alibaki kinywa wazi.
“Mwenzako?”
“Yeah...M-Lebanoni mwenzangu. Tajiri wa kutupwa!”
E Bwana we!
“Sasa...mbona wewe umesema ulikuwa umekuja kuwauzia silaha waasi wa serikali hii?”
Ghudia alicheka kidogo.
“Brother,siku zote biashara ya vita ni biashara ya kugeukana na kuzungukana tu!” Alimwambia, na kuendelea, “waasi pia wanataka silaha, na kwa kuwa huyu tajiri yangu anahitaji almasi zao pia, basi na wao pia huwauzia silaha, ila
MDUNGUAJI
kwa usiri mkubwa, na kwa kutumia watu kama mimi...serikali ya Liberia
haijui kabisa juu ya hilo na haitakiwi kujua, na ndiyo maana nakwambia kuwa akijua tu nilipo, basi nimetoka humu ndani...hata yeye hataki niseme haya nikuambiayo kwa mtu asiyepaswa...”
Baddi alitikisa kichwa kwa mstaajabu.
“Sasa...ina maana akijua ulipo utatoka...au tutatoka?” Baddi alimuuliza.
“Ala! Unadhani nitakuacha humu Baddi? No way...tunatoka sote brother...! Itakuwaje bwana, kwani mimi si m-Lebanoni halisi? Lazima nikuchukue swahiba wangu bwana!” Ghudia alimjibu.
Kimya kilitawala kwa muda, wakati akili ya Baddi ikifanya marathon.
“Kwa hiyo tukipata wa kuwasiliana na huyo jamaa yako tunatoka humu ndani...” Baddi alisema kwa sauti ya chini.
“Kabisa! Yaani tukipata mtu wa kumfikishia ujumbe tu kuwa nipo hapa, mara moja tunatolewa...yeye anaongea na wakuu wa nchi wenyewe!”
Baddi alisisimkwa na mwili.
“U...una hakika?”
“Kama jinsi nilivyokuwa na hakika kuwa Ghudia Al-Haddaad ni jina langu na Lebanoni ni nchi yangu! Kwani vipi?”
Baddi alimtazama kwa muda, kisha akatazama pembeni kidogo, halafu akamtazama moja kwa moja usoni.
“Nadhani naweza kukupatia huyo mtu wa kumfikishia ujumbe jamaa yako.”
Ilikuwa ni zamu ya Ghudia kubaki kinywa wazi.Alibaki akimtazama kwa muda, akiwa amefinya macho kwa hisia kali.
“Inaelekea hukunieleza yote yanayokuhusu hapo awali rafiki...kuna mambo umenificha.”
“Sikukuficha, bali sikuona umuhimu wa kukueleza kwa wakati ule...”
Baddi alimjibu, na kimya kilichukua nafasi kwa muda.
“Sasa unadhani tutaweza kuaminiana iwapo tutakuwa tunafichana mambo patna?” Ghudia alimuuliza huku sura yake ikionesha kuumizwa na jambo lile.
“Hapana...sikukuficha Ghudia, ni kwamba sikuona kama kulikuwa kuna haja ya kukwambia kwa wakati ule! Ni hivyo tu...”
Ghudia alimtazama kwa muda, na Baddi alimrudishia mtazamo usiotetereka. Kisha Ghudia aliachia tabasamu pana na Baddi akatabasamu pia.
“Okay, bado nakuamini patna…hebu nieleze juu ya huyo mtu sasa...”
Ndipo Baddi alipomueleza juu ya Gilda. Moja kwa moja hoja ya
Baddi kuwa Gilda ndiye angeweza kuwasaidia ilikubalika. Wakajiandaa kama walivyoona inafaa, kisha walibaki wakisubiri kwa hamu ujio wa Gilda, ambaye kama kawaida aliwasili mwezi uliofuata.
Baddi alienda kuonana naye akiwa na maelekezo kamili kutoka kwa
Ghudia. “Inabidi uende kwenye jimbo liitwalo Fassana, unalifahamu?”
Baddi alimuuliza Gilda baada ya kusalimiana na kumpasha habari juu ya Ghudia na mpango wao wa kutoka mle gerezani na hatimaye nje ya nchi ile. Gilda alichanganyikiwa si kidogo.
“Nalijua jimbo hilo...ni eneo la watu wazito...ambako nadhani wengi wa viongozi wa nchi hii wanaishi...”
“Sawa. Basi kamtafute mtu aitwaye Twalal Ghailani...” Baddi alisema, kisha akatembeza kwa wizi mle ndani, na wakati huohuo akiingiza mkono wake ndani ya suruali yake na kuchomoa kipande cha karatasi alichokuwa amekificha kwenye nguo yake ya ndani.
“...ukionana naye, mwambie kuwa una salamu zake kutoka kwa Ghudia...lishike sana hilo jina, Ghudia Al-Haddad...na umpe hii karatasi...” Alimwambia huku akipitisha mkono wake chini ya meza na akimtazama moja kwa moja usoni. Gilda alipitisha mkono wake chini ya ile meza iliyokuwa kati yao na kukipokea kile kipande cha karatasi na kukifutika kwenye mfuko wa suruali aliyovaa chini ya khanga alizojitanda.
“Nimekuelewa vizuri...ila nitampataje sasa huyo Twalal...yaani hakuna jina la mtaa au namba ya nyumba ambapo naweza kumpata kwa urahisi?”
“Jamaa ni tajiri maarufu sana hapa… na kama jina lake lilivyo, ana asili ya kiarabu...haitakuwa ngumu kwako kumpata. Kwa maelezo ya Ghudia, ni kwamba ana kituo cha mafuta katika jimbo lile...ni kituo pekee cha mafuta kilichobaki eneo hilo, vingine vyote vilishafungwa na wenyewe wamekimbia...hapo mwenyewe utaona ni jinsi gani huyo mtu alivyokuwa na nguvu katika huu utawala uliopo.
“Yeye huwa anafika pale kwenye hicho kituo, ambacho hakika ni kama geresha tu ya namna anavyopata utajiri wake…biashara ya mafuta haina faida yoyote hapa Liberia sasa hivi. Nani anaendesha magari katika jiji hili
MDUNGUAJI
zaidi ya hao wanajeshi tu? Biashara yake kubwa ni hizo silaha!”Baddi alimfahamisha kwa kirefu.
“Mnh! Kweli aisee…Inaleta maana. Sasa huyu Twalal…nd’o n’tampata hapo kwenye hicho kituo cha mafuta?”
“Huwa anafika pale, ila hana ratiba maalum. Itabidi umvizie tu. Mtu mfupi mnene, anapenda kuvaa mavazi ya khaki na kofia pana ya pama... anatembelea magari ya kifahari sana. Ukimuona utamjua tu.”
Dakika kumi baadaye Gilda aliondoka kwa makubaliano kuwa muda atakapopata habari juu ya Twalal tu atarudi tena pale , gerezani kumpasha habari. Alirudi wiki moja baadaye akiwa na taarifa ambayo si Baddi wala Ghudia aliifurahia. Twalal Ghailani alikuwa nje ya Liberia kwa muda, na haikujulikana angerejea lini.
Haikuwa mpaka miezi mitano baadaye ndipo Gilda alipokuja na habari kuwa hatimaye amefanikiwa kuonana na Twalal Ghailani.
“Amekuelewa? Amekuamini…?” Baddi alimuuliza kwa bashasha.
“Oh, Baddi! Huwezi kuamini! Kwanza alikuwa na mashaka sana na mimi, lakini nilipomkabidhi kile kijikaratasi…Ah, jamaa alilia bwana!
Alisema amekuwa akimtafuta kisiri siri ndugu yake huyo bila mafanikio. Alijua ameshauawa kwa sababu alikuwa anakuja kwa usiri mkubwa sana hapa Liberia…”
Baddi alifurahi!
“Kwa hiyo ule ujumbe alioandika Ghudia ulikuwa mzuri sana…”
“Hiyo wala haina shaka! Ingawa alikuwa ameandika kwa kiarabu, ni wazi kuwa kwenye ile barua Ghudia alitutaja, kwani Twalal aliniuliza iwapo nakufahamu vizuri...”
“Wacha bwana!”
“Oh Yes! Na siku ileile akanihamishia kwenye ya jumba lake...ilinibidi nirudi kule kijijini kuchukua baadhi ya vitu vyangu muhimu...”
“Sasa...nini kinafuata?”
“Kwanza kanituma nije kuhakikisha tena iwapo huyu Ghudia bado yuko nawe humu gerezani...”
“Yupo...”
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Gilda alibaki kimya kwa muda. Baddi akaanza kuwa na wasi wasi. “Vipi?
Mbona kimya tena?” Gilda aliinua uso wake na kumtazama.“Nahisi leo ndiyo itakuwa siku yenu ya mwisho kukaa humu gerezani Baddi...”
“
Whaaat? Si...sikuelewi...”
“Nimeletwa hapa gerezani na gari la Twalal...ameniambia nikihakikisha kuwa nyote mpo salama humu ndani, nirudi kwenye lile gari, dereva wake ambaye ana simu atampigia ili nimjulishe hivyo...kisha yeye amesema atapiga simu moja tu na muda si mrefu mtatolewa...”
“E bwana we!”
“Ndivyo alivyoniambia Baddi...na kwa namna fulani naamini kabisa ndivyo itakavyokuwa. Yule mtu ana nguvu na mamlaka makubwa sana hapa
Liberia...hilo nimeliona wazi wazi ndani ya muda huu mfupi niliokutana naye...”
Baddi hakuamini. Lakini ndivyo ilivyokuwa.
Dakika arobaini na tano baada ya Gilda kutoka mle gerezani, Baddi Gobbos na mlanguzi wa biashara ya silaha na almasi haramu Ghudia Al-Haddad, walitolewa haraka haraka mle gerezani. Walipakiwa kwenye
gari la kifahari la Twalal Ghailani na kuondolewa kwa kasi kutoka eneo lile.
Hatimaye Baddi Gobbos Vampire alikuwa huru...
Waliishi pamoja na Ghudia ndani ya jumba la kifahari la mlanguzi mkubwa wa silaha na almasi za damu Twalal Ghailani kwa wiki mbili. Ndani ya wiki mbili zile walisahau madhila yote waliyokumbana nayo katika nchi ile iliyojaa machafuko. Baddi alinyoa nywele na ndevu zake vizuri na kurudisha ile haiba yake ya hapo awali. Twalal aliwapatia vyakula bora na vizuri kiasi cha kuwasahaulisha taabu zote za hapo nyuma. Aidha zilikuwa ni wiki mbili zilizosheheni mahaba na mapenzi moto moto baina yao wakati Twalal akifanya utaratibu wa kuwaondoa mle nchini. Akiwa katika jumba lile, Baddi alijaribu bila mafanikio kupiga simu nyumbani kwake na kule makao makuu ya jeshi la Tanzania. Namba zote hazikupatikana kabisa. Ujumbe uliokuja kutoka kwenye simu ni kwamba namba zote za
Tanzania zilikuwa zimebadilika, na kwa maelekezo zaidi alitakiwa aangalie kitabu kipya cha namba za simu. Kitabu hicho hakikuwepo kabisa Liberia.
Baddi alichanganyikiwa. Aliandika barua pepe kwa mkewe kumuelezea kwa kifupi juu ya mambo yaliyomkuta na kumuagiza apeleke taarifa makao
MDUNGUAJI makuu ya jeshi la Tanzania. Hakupokea majibu kabisa kutoka kwa mkewe. Alibakia akitazama anuani yake ya barua pepe kila siku akitaraji majibu pasina mafanikio. Hakuelewa ni nini kilichosababisha hali ile.
“Kazi yangu hapa imeshaharibika Baddi...nimekamatwa kabla hata sijafanya lililonileta. Twalal ameniambia kuwa nisirudi tena Liberia, tayari nimeshakuwa mtu hatari kwa usalama wa biashara yetu, nami nakubaliana naye kabisa...” Ghudia alimwambia Baddi siku moja.
“Yote ni kheri tu Ghudia...hii si biashara nzuri kabisa! Ni vyema kuachana nayo...”
“Na bila biashara hii leo tusingekuwa nje ya lile gereza tukila vyakula vizuri nawe ukijinafasi na mpenzi wako humu ndani huku mkila viyoyozi Baddi, usisahau hilo hata siku moja!” Ghudia alimwambia huku akitabasamu. Baddi aliitafakari kwa muda kauli ile.
“Ni kweli usemayo, lakini pia ni lazima tukubali kuwa maisha ya watu wengi yanaangamia...”
“Patna, suala sio kuacha kuuza silaha…suala ni kuacha vita! Na sioni dalili ya vita kuisha duniani ndugu yangu…kama si Liberia basi Sierra Leone, kama si Sierra Leone basi ni Afghanistan...orodha ni ndefu mno...! Achana na hayo bwana...angalia maisha yako. Kama mimi maisha yangu yanakuwa mazuri kwa kuwa waafrika fulani huku Afrika ya Magharibi wana hamu ya kuuana, basi hivyo ndivyo itakavyokuwa. Wao wauane, mimi maisha yangu yawe mazuri, basi! Hata ndugu yangu na bosi wangu Twalal aliyetutoa gerezani ndiyo mtazamo wake huo!”
Baddi alikaa kimya, akilini mwake akikumbuka maneno ya msaliti Nathan Mwombeki p.a.k. Alpha.
…kadiri hii vita inavyoendelea, ndivyo nafasi ya kujipatia mgao katika hizi almasi inavyozidi kuwa kubwa....
Ama kweli dunia imefika pabaya.
“Nitawatoa nje ya nchi hii bila gharama yoyote, ila suala la pasi za kuwasafirisha hadi nchini kwenu litahitaji muda kidogo.” Twalal Ghailani aliwaambia baada ya kukamilisha taratibu za kuwatoa nje ya Liberia
“Tatizo kubwa ni kuwa hamuwezi kuondoka kutokea hapa Liberia moja kwa moja, kutokana na hali ya kiusalama ilivyo. Vyovyote iwavyo, itabidi niwatoe kiwizi nje ya Liberia hadi kwenye moja ya nchi za
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
hapa jirani ambako nina watu wangu, huko ndiyo mchukue ndege ya kuwarudisha kwenu. Sasa…mi’ n’na watu Mali, Mauritania, Gabon na Senegali…naweza kuwapatia pasi za yoyote katika nchi hizo…”Twalal Ghailani aliwaambia.
“Basi tutengenezee pasi za uraia wa Senegali…” Baddi alimwambia.
“ Okay, no problem. Basi nitaongea na watu wangu wa Senegali na naamini pasipoti zitapatikana tu.”
“Tuna kiasi kidogo cha pesa ambacho labda kitasaidia kukamilisha zoezi hilo...” Gilda alimwambia, lakini Twalal alimkatisha kwa mkono wake.
“Pesa si tatizo, rafiki yoyote wa ndugu yangu Ghudia, ni rafiki yangu pia. Hilo suala nitalimaliza mimi. Nina hakika kuwa hizo pesa zetu mtazihitaji sana huko muendako.” Twalal alimjibu. Wiki mbili baadaye aliwaletea pasipoti zilizowatambulisha kama raia wa Senegali na bado Baddi hakuwa amepata majibu kutoka kwa mkewe.
“Helikopta ya watu wangu itawafikisha Senegali, na si zaidi ya hapo...kutokea hapo mtakuwa peke yenu. Itakuwa ni juu yenu kufanya taratibu za kuwarudisha Tanzania.” Twalal aliwaambia.
“Ah, hiyo ni habari nzuri sana brother. Je, hiyo helikopta itatushushia sehemu gani ya Senegali…?” Baddi alimuuliza. Hapohapo Twalal aliwasiliana na mtu wake kwa simu, na kuwajibu kuwa itawateremsha eneo lililokuwa kiasi cha kilometa mia mbili nje ya jiji la Dakkar.
“Basi nasi tutakuwa na maombi mawili zaidi kwako Twalal…” Baddi alimwambia.
“Not a problem…”
“Tunaomba utufanyie utaratibu tupate simu tutakayoweza kuitumia tukiwa Senegali…ni muhimu kwetu…tunaweza kukupa pesa za kununulia…”
“Ah, achana na hizo bwana! Simu ni kitu kidogo sana Baddi…hilo umepata rafiki. Tena kuna mtandao unaounganisha karibu nchi tano za afrika magharibi. Sema jingine…”
“Tutahitaji kiasi fulani cha pesa za kisenegali…unaweza kutubadilishia sehemu ya pesa zetu kwa fedha ya huko?”
“Pia si tatizo. Kingine…?”
“Hakuna Twalal…hakika msaada wako hauna mfano. Tunakushukuru sana, tena sana!” Baddi alimjibu. Twalal alitabasamu kwa furaha na kuridhika. Siku mbili baadaye, usiku wa manane, Baddi na Gilda walimuaga Ghudia na nduguye Twalal, kisha wakapanda helikopta iliyokuwa
MDUNGUAJI
ikiendeshwa na rubani wanaolipwa na Twalal kuingiza silaha haramu
nchini Liberia. Waliiacha ardhi ya nchi ile iliyojaa machafuko, wakapaa hewani na kutokomea kizani.
Helikopta iliwashusha kwenye uwazi mpana katikati ya msitu mnene na wenye kiza, kisha hapohapo ikapaa tena hewani na kuwaacha. Bila kupoteza muda walianza safari kwa miguu, wakifuata usawa wa mashariki mle msituni
ambao, kwa mujibu wa maelekezo ya yule rubani aliyewashusha pale msituni, ungewafikisha kwenye barabara kubwa iliyokuwa ikielekea Dakkar.Baada ya kukata mbuga kwa saa nne bila ya kukutana na barabara kuu waliamua kulala mle msituni, Gilda akitumia begi lake kama mto. Baddi ambaye hakuwa na mzigo wowote, alijiegemeza kwenye mti kando yake huku akiwa makini kutazama usalama wao. Kulipopambazuka waliendelea na safari, na saa mbili baadaye walikutana na barabara kubwa sana ya lami.
“Sasa nadhani hii ndiyo barabara kubwa ya kuelekea Dakkar…” Gilda alisema kwa matumaini.
“ Yeah …nadhani tukiifuata tutakuta kibao kitakachotujulisha tuko sehemu gani hasa…” Baddi alimjibu. Mwendo mfupi baadaye walifanikiwa kupata lifti kwenye lori la mizigo. Gilda aliongea na dereva kwa lugha ya kifaransa kibovu na dereva alimfahamisha kuwa alikuwa anaishia mji mdogo uliokuwa kilomita tatu kutoka pale walipokuwa.
Wakajipakia nyuma ya lile lori hadi kwenye ule mji mdogo, ambapo kwa pesa za ki-Senegali walizopewa na Twalal, walipanga chumba kwenye nyumba ndogo ya wageni.
Wakiwa chumbani mwao Baddi alitumia simu aliyopewa na Twalal kupiga namba ambazo kwa wiki nzima iliyopita zilikuwa zikirindima kichwani mwake.
Aliisikiliza ile simu ikiita kwa muda wakati Gilda akimtazama kwa sura yenye utashi mkubwa wa kujua matokeo ya simu ile.
“Nani…?” Sauti iliyopekea simu ile iliuliza kwa mashaka, na moyo wa Baddi ukapiga samasoti ndani ya kifua chake.
“Vampire.” Alisema, na alimsikia mtu aliyepokea ile simu akivuta pumzi ghafla kwa mshituko, kisha kukawa kimya kabisa. Baddi aliitazama kwa muda ile simu kisha akaiweka tena sikioni. Hakika mtu aliyepokea ile simu bado alikuwa hewani, ingawa hakuwa amesema neno zaidi.
“Honey-Bee…?” Aliita kwa mashaka kwenye ile simu.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Oh, mon dieu! Vampire…? FromTanzania…? Ni wewe…?” Sasa sauti ya Honey-Bee ilimjia wazi wazi masikioni mwake na akaachia tabasamu la ushindi huku akimtupia jicho Gilda, ambaye alifinyanga ngumi zake na kuzipiga magotini kwake kwa ishara ya kufurahia ushindi.
“Yes Honey-Bee, ni mimi…Vampire! Kumbe uko okay…ulinusurika na Mdunguaji? Basi hakika maneno yangu yalienda moja kwa moja hadi kwenye sikio la Mungu…ennh?” Alimwambia kwa hamasa.
“Vampire…I don’t understand….uko hai wewe?” Honey-Bee aliuliza kwa sauti iliyojaa mastaajabu.
“Sio tu niko hai bali niko Senegali hapa…na…nahitaji sana msaada wako…”
“Ah. Vampire…I don’t believe it…unajua its been three years…na nilijua umekufa!” Honey-Bee bado alikuwa ameshikwa na mastaajabu.
“Sijafa bali nina shida…I need your help Honey-Bee…”
Kimya kilichukua nafasi, kisha Honey-Bee alishusha pumzi ndefu. “Okay… umesema uko Senegali…sehemu gani?”
Baddi akamtajia jina la ile nyumba ya wageni waliyofikia, na jina la ule mji mdogo.
“Nipe saa mbili nitakuwa hapo komredi…usiende popote mpaka nifike!”
Saa mbili na nusu baadaye ile simu iliita na Baddi alipoipokea Honey-Bee alimpa maelekezo mengine.
“Hivi tuongeavyo, dereva wangu yuko hapo nje ya hiyo nyumba ya wageni ulofikia. Yuko kwenye gari dogo jeusi aina ya BMW… amevaa suti nyeusi na miwani myeusi. Rudisha hicho chumba, chukua vitu vyako vyote ingia kwenye hilo gari. Dereva wangu atakuleta hapa nilipo jijini Dakkar. Kama huna pesa ya kulipia hicho chumba, mwambie dereva wangu…yeye atakamilisha kila kitu, okay?”
“Okay komredi thanks. Chumba nilishalipia, kwa hiyo mi natoka tu…”
“Good…tutaonana muda si mrefu.” Honey-Bee alimjibu na akakata simu. Baddi na Gilda walifanya kama jinsi Honey-Bee alivyoelekeza. Waliikuta ile BMW nyeusi nje ya ile nyuma ya wageni, na walipotokeza tu nje ya jengo lile, mlango wa dereva wa gari lile ulifunguliwa na Baddi alishangaa kuona mwanadada mkakamavu aliyekuwa amevaa suti kali sana ya kike na miwani myeusi, akiteremka na kuwafungulia mlango wa nyuma wa gari lile. Huku akisita kidogo Baddi alimsalimia yule dereva wao ambaye badala ya kumjibu salamu yake, aliguna tu na kuwafungia mlango baada ya wao kuwa wameshaketi kwenye kiti cha nyuma cha lile gari la kifahari. Kisha yule mwanadada aliingia
MDUNGUAJI
nyuma ya usukani na kuliondoa lile gari kwa kasi. Kule nyuma Baddi na Gilda walitazamana, kisha Baddi akambinya kiganja cha mkono wake kwa kumtia moyo.
“Usiwe na shaka…Honey-Bee ni mpiganaji wa kuaminika…tuko salama tu!” Alimwambia. Gilda alitikisa kichwa kuafiki maneno yale. Kwa saa mbili na nusu zilizofuata, walibaki kimya kule nyuma wakiendeshwa kwa mwendo wa kasi sana na yule dereva aliyekuwa kimya njia nzima.
Ni baada ya saa mbili na nusu zile ndipo hatimaye, Baddi Gobbos p.a.k Vampire alipokutana tena na mpiganaji mwenye shabaha zisizosemekana, Honey-Bee.
Walifikishwa kwenye hoteli kubwa na ya kifahari jijini Dakkar, ambapo yule dereva wao aliwapitisha moja kwa moja hadi kwenye chumba kimoja kikubwa na kizuri sana katika hoteli ile kisha akatoka. Dakika kumi baadaye, mlango wa chumba kile ulifunguliwa na Honey-Bee aliingia.
“Vampire!”
“Honey-Bee!”
Walikumbatiana kwa nguvu, kisha wakabaki wakitazamana huku wakiwa wameshikana mikono. Honey-Bee alikuwa kwenye mavazi ya kiraia na alionekana kung’aa na kuvutia kweli kweli…sio tena yule mwanadada aliyekuwa kwenye magwanda ya kijeshi, akivujwa jasho huku akiwa ametapakaa vumbi na tope la msitu wa tumbudu kule Sierra Leone.
“Kweli uko hai Vampire…hiki ni kituko kikubwa kabisa…sote tuliamini kuwa umeuawa na mdunguaji kule msituni…!”
“Hapana…labda niseme nilipotea nikiwa katika harakati za kijeshi… ingawa nusura mdunguaji aniue. Hata hivyo sishangai iwapo mliamini kuwa nimeuawa…”
“Hapana Vampire huelewi…yaani huu ni utata mzito nakwambia! Kama wewe u-hai..basi hakika tulikosea…na mtu mwingine atakuwa amezikwa akiaminika kuwa ni wewe! Kumbe Swordfish alikuwa sahihi…!”
“Sikuelewi Honey…unamanisha nini Swordfish alikuwa sahihi? Naye alinusurika na mdunguaji?”
Badala ya kumjibu Honey-Bee alimtupia jicho Gilda, na kumgeukia tena Baddi, swali lake likiwa wazi machoni mwake.
“Ah…huyu ni Gilda…hana matatizo. Ni Mtanzania mwenzagu tuliyekutana katika mazingira ya mashaka kabisa huku ughaibuni…”
Bado Honey-Bee alionekana kutokuwa na imani kuongea mbele ya Gilda. Alikohoa kidogo na kwenda kuketi kwenye moja ya makochi yaliyokuwa ndani
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI ya chumba kile.
“Okay, ukweli ni kwamba nasikitika kwamba sina muda mrefu sana wa kuwa na wewe hapa hotelini kwa sasa Vampire…ningependa iwe hivyo lakini nina majukumu mazito na natakiwa nisafiri ndani ya saa mbili kutoka sasa. Hivi niongeavyo mizigo yangu tayari iko kwenye gari, na yumkini nikitoka hapa nitakuwa naelekea moja kwa moja uwanja wa ndege…”
“Hah…!”
“Yes…lakini labda nisikie unahitaji msaada gani kutoka kwangu, na nione iwapo nitaweza kufanya lolote ndani ya muda huu mfupi uliobakia…”
Baddi akamueleza.
Honey-Bee aliuma midomo kwa tafakuri kubwa huku akitazama ukuta uliokuwa mbele yake. Baddi na Gilda walitazamana, Gilda akionesha wasiwasi mkubwa. Honey-Bee alimtazama Baddi usoni.
“Vampire, unajua kuwa kitu ulichofanya hapa ni kumuomba naibu waziri wa ulinzi wa nchi hii, akusaidie kutoka nje ya nchi hii kwa kutumia pasi bandia za kusafiria, ilhali ukiwa umeingia humu nchini kinyume cha sheria?”
“Whaat…?” Baddi aliuliza huku akiwa amekodoa macho.
“Yes Vampire. Baada ya ile kampeni ya kule Sierra Leone miaka mitatu iliyopita, kwa namna ambayo hata mimi siielewi mpaka sasa, niliteuliwa kuwa mwambata wa kijeshi nchini Ujerumani, na miaka miwili baadaye nikaitwa tena nchini na kuambiwa kuwa nimeteuliwa katika baraza jipya la mawaziri kama naibu waziri wa ulinzi.”
Ebwana we!
“Wow, Honey-Bee…hiyo ni habari nzuri sana kwako. Nafurahi kusikia kuwa umepata mafanikio makubwa namna hiyo hapa nchini kwako…sasa… dah! Ina maana hutaweza kutusaidia? Utatuweka chini ya ulinzi?” Alimuuliza huku akimtazama kwa mashaka. Gilda alimshika Baddi mkono kwa nguvu huku naye akimtazama Honey-Bee kwa macho yenye kushutumu. Naibu waziri wa ulinzi wa Senegali Jeanette Tulaye-Bgayo, kwa Baddi Honey-Bee, alimtazama kwa muda huku akiwa amefinya macho kwa tafakuri, kisha alikunja nne pale kwenye kochi na kumjibu.
“Hivyo ndivyo ambavyo ningefanya iwapo ombi hilo lingetoka kwa mtu mwingine yeyote asiyekuwa wewe Vampire…”
“Oh, kwa hiyo utatusaidia?” Baddi aliuliza huku akiachia tabasamu.
“Of Course nitakusaidia Vampire, why not comrade? Tumepigana bega kwa bega kule msituni…sote tukiwa na mashaka ya kutoka hai katika msitu ule wa kifo, halafu leo nishindwe kukusidia kwa kuwa nimekuwa naibu waziri? No
MDUNGUAJI
way partner…baina yetu siku zote itakuwa ni one for all…all for one, right?”
Honey-Bee alimjibu huku akitabasamu.
“Oh, Honey-Bee!Hakika wewe ni mpiganaji halisi. Ahsante sana!” Baddi alimshukuru huku akimwona Gilda akishusha pumzi za faraja.
“No problem. Sasa muda ni kipingamizi kikubwa. Inanibidi niweke mazingira ya nyie kuondoka hapa haraka sana kabla sijapanda ndege leo hii…” Alisema, kisha akainuka hadi mlangoni na kumwita yule mwanadada aliyewafikisha pale hotelini kutoka kule kwenye nyumba ya wageni. Yule dada alipoingia mle ndani alimtambulisha kwao kama mlinzi na msaidizi wake binafsi kama naibu waziri wa ulinzi wa Senegali. Kisha akaongea haraka haraka na yule dada kwa lugha yao ya kienyeji. Yule dada aliiendea simu ya mle hotelini na kupiga simu kisha akaanza kuongea taratibu na mtu mwingine wa upande wa pili wa simu ile. Kisha akampa simu Honey-Bee naye akaongea na huyo mtu wa upande wa pili kwa muda. Alionekana kubishana kwa muda na mtu wa upande wa pili, na mara moja au mbili alifoka kidogo. Hatimaye alianza kutabasamu na kucheka na huyo mtu aliyekuwa akiongea naye, kisha akaweka simu chini.
“Sawa. Nadhani tutaweza kuwasaidia...mkabidhini Yvonne pasi zenu za kusafiria…” Honey-Bee aliwaambia huku akimuelekezea yule mlinzi wake, na akina Baddi wakatekeleza.
“Yvonne ataenda kuwawekea viza za kuonesha kuwa mliingia nchini kihalali siku mbili zilizopita kwa kupitia kwenye moja ya mipaka yetu ya barabara, kisha atawapatia tiketi za ndege za kuondoka Sengeali ikiwezekana leo hii hii, ikishindikana kesho mapema sana…hamtokaa humu nchini zaidi ya saa ishirini na nne, okay?”
“Dah! Hiyo ni sawa kabisa!”
“Okay…sasa mna pesa za kununulia tiketi? Au mtahitaji msaada…”
“Tunazo…tunazo ahsante sana…” Baddi alimjibu huku Gilda akifungua begi lake na kutoa rundo la pesa za ki-Senegali walizopewa na Twalal. Vyonne alizipokea zile pesa na kuzihesabu haraka haraka, kisha akamrudishia alizoona kuwa zimezidi. Aliongea na Honey-Bee kidogo kisha akatoka nje ya chumba kile.
“Okay, Vampire hebu sasa niambie ni nini hasa kilichotokea kule msituni…?” Honey-Bee alimwambia baada ya Vyonne kutoka mle ndani. Baddi alimuelezea kisa chote kama kilivyomtokea kule msituni kwa ufupi kadiri alivyoweza. Honey-Bee alichoka. “Kwa hiyo kumbe aliyekufa akiwa na kile kifaa cha mawasiliano mgongoni ni Black Mamba?”
“Oh yes! Nimemshuhudia kwa macho yangu! Ndipo nami nilipopigwa
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
risasi kifuani na kuangukia korongoni…huko ndipo nilipokutana na Gilda na kupitisha miaka yote mitatu Liberia…”
“Swordfish alibisha sana kuwa ule mwili sio wako…nasi tukadhani yeye anakosea…kumbe alikuwa sahihi maskini…” Honey-Bee alisema. Baddi hakuwa na la kusema juu ya hilo. Muda huo simu ya Honey-Bee iliita, naye aliinuka na kuingia bafuni kuongea nayo. Baada ya muda alitoka na kuwaambia.
“Kuna mtu nahitaji kuonana naye, na nimemwambia aje hapa hotelini… nitakutana naye hapo kwenye mgahawa wa hapa hotelini, kisha nitarudi…
nisubirini tu” Aliwaambia huku akitoka. Baddi na Gilda walitazamana.
“Mnh, unadhani tutafanikiwa…?” Gilda alimuuliza.
“Yeah, Honey-Bee ni mpiganaji wa kweli.Hawezi kutugeuka.”
Dakika arobaini na tano baadaye Yvonne aliingia mle ndani akiwa na pasi zao za kusafiria na tiketi za ndege mkononi.
“Ndege yenu itaondoka leo saa kumi jioni…naibu waziri bado yuko hapo chini na ameniambia niwakabidhi…” Yvonne alisema huku akimkabidhi Baddi vile vitu muhimu kabisa kwa mustakbali wa maisha yao kwa wakati ule.
“Yuu-huu!” Gilda alijisahau na kuruka juu huku akitupa ngumi hewani kwa ishara ya ushindi, na kwa mara ya kwanza tangu akutane na mwanadada yule Baddi alimuona Yvonne akitabasamu.
“Oh, ahsante sana, sana, sana, dada yangu! Hakika thamani yako leo hii ni ya dhahabu…!” Baddi alimshukuru. Yvonne aliachia tabasamu pana zaidi. “Sio mimi…nadhani mwenye thamani hiyo kwako leo hii ni naibu waziri…mimi ni mtumishi tu!” Alimjibu, na wote walibaki wakicheka.
Muda huo Honey-Bee aliingia mle ndani. “Okay Baddi, kwamba vicheko vimetawala humu ndani inamaanisha kuwa kila kitu kimeenda sawa. Sasa mimi sina tena muda wa kuendelea kuwa nanyi hapa ndugu zangu…yanipasa niende…”
“Honey-Bee…najua ni jinsi gani ulivyoweka madaraka yako rehani kwa kutusaidia, na hili sitalisahau kamwe. Nakushukuru sana komredi, kwa hakika hapa ulipotufikisha panatosha sana!”
“Oh, come on Vampire…najua hata wewe ungekuwa kwenye nafasi yangu ungenifanyia hivyo hivyo…” Honey-Bee alimjibu, na wapiganaji wale waliokubuhu walikumbatiana kwa nguvu. Kisha Honey- Bee akamgeukia Gilda.
“Mwende kwa amani dada…” Alimwambia.
“Yes, dada…nami nakushukuru pia. Umekuwa rafiki wa kweli kwa Baddi, na kwa hilo nami pia nimenufaika!” Gilda alimwambia huku akimpa mkono.
MDUNGUAJI
Honey-Bee aliupokea ule mkono huku akitabasamu.
“No big deal, okay?” Alisema, halafu akamgeukia Baddi.
“Nahitaji kuongea nawe faragha Vampire…”
Walisogea kwenye kona ya chumba kile mbali na wale wenzao wawili, na kwa sauti ya chini Honey-Bee alimwambia.
“Nina ombi moja tu kwako Vampire…”
“Baddi…”
“What…?”
“Jina langu halisi ni Baddi…Baddi Gobbos!”
“Ah, okay. Lakini kwangu siku zote utakuwa Vampire tu. Ila kwa kuwa umenipa jina lako, si vibaya nawe ukijua kuwa mimi naitwa Jeanette…Jeanette
Tulaye-Bgayo...”
“Okay...”
“Ninachokuomba ni kwamba ukifika huko nchini kwako, tafadhali sana tena sana, usiseme kabisa jinsi nilivyokusaidia leo hii hapa Senegali. Hiyo haitakuwa vizuri kwa wadhifa nilio nao sasa, please!”
“Hiyo haina tatizo Honey-Bee. Kwanza nitamueleza nani?”
“Amini usiamini ukifika Tanzania utawekwa mbele ya jopo zima la vigogo wa kijeshi, nao watahitaji kujua kile kilichokutokea tangu ulipopotea kule msituni Sierra Leone hadi ulipofanikiwa kurejea tena nchini kwako...na hapo ndipo ambapo nisingependa kabisa kuhusika kwangu kukutorosha hapa Senegali kuwekwe wazi. Hii iwe siri yako na Gilda tu! Unadhani unaweza kuniahidi hilo?”
“Bila shaka komredi...hii ni ahadi ya mpiganaji wa kweli!”
“Good!”
Walipeana mikono kwa mara ya mwisho na yule mpiganaji wa kike mwenye shabaha za pekee alitoka mle ndani akifuatiwa na Yvonne, wakiwaacha Baddi na Gilda wakitazamana kwa kutoamini.
Saa nane baadaye, wawili wale walipanda ndege na kuanza safari ya kurudi nyumbani, Tanzania.
“Sasa ndiyo tunaelekea nyumbani Gilda...” Baddi alimwambia yule dada wakiwa nchini Senegali.
“Ndiyo...na najua kuwa huko utarudi kwenye familia yako.” Gilda alisema kwa huzuni.
“Ni kweli. Lakini tuliyopitia mimi na wewe ni mazito na hatuwezi kuyaacha yapotee hivi hivi tu...” Baddi alisema.Gilda alikaa kimya kwa muda. “Unadhani tutafanyaje Baddi...?”
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Ni wazi kuwa tukifika salama nyumbani itabidi tugawane njia, ila itabidi tu nikukutanishe na mke wangu...”
“Ili iweje Baddi...ni bora tukifika kila mtu ashike hamsini zake, vinginevyo italeta matatizo...”
Baddi hakukubaliana kabisa na hoja hiyo. Kuna kitu kilikuwa kinamsukuma kutaka kuendelea kuwa na yule dada mpaka dakika ya mwisho. Hatimaye walikubaliana iwe hivyo wakiwa angani kurejea nchini.
Wingu la kumbukumbu liliyeyuka, na Baddi Gobbos alihamisha mawazo yake kutoka Liberia na Senegali, miaka mitatu iliyopita, na kuyarudisha kwenye wakati uliopo.
Hospitali ya Muhimbili…
WAKATI ULIOPO
DAR ES SALAAM,
Alimtazama Gilda aliyelala bila fahamu pale kitandani huku akijaribu kutathmini yale matukio aliyokumbana nayo tangu aliposhuka uwanja wa ndege asubuhi ile.
Alikumbuka jinsi wale watu wawili walipowavamia pale hotelini na ile kauli iliyomshangaza zaidi kuliko kumtisha, ya yule mvamizi aliyeishia
kujitupa dirishani na kutokomea baada ya mambo kuwawia magumu.
Huna haja ya kutuuliza maswali fala we! Ni aidha utuue au utuachie tukuue! Eti niwaachie waniue! Ni watu gani wale? Wametoka wapi? Wametumwa na nani?
Kuwa wanataka kuniua haina shaka kabisa, lakini...ni kwa sababu gani?
Maswali yalikuwa ni mengi kuliko majibu.
Na sasa suala la mke wangu…Yuko wapi? Kwa nini ameacha kazi...? Na baba naye…? Ghafla, wazo jipya likaingia akilini mwake.
Iwapo hapa nchini ninaaminika kuwa nimeshakufa na nimezikwa, basi ni wazi kuwa mke wangu, mama Claudia, atakuwa amelipwa mafao yangu yote! Hivyo ni wazi kuwa anaweza kuamua kuacha kazi baada ya kupata pesa zile...
Sasa yuko wapi? Baddi alijikuta anarudi pale pale…hana jibu.
Alimtazama Gilda kwa muda mrefu, kisha kwa sauti ya chini sana alimwambia kama kwamba yule mwanadada alikuwa akimsikia, “Samahani sana Gilda, lakini itabidi nikuache peke yako hapa hospitali kwa muda...
naamini hapa uko kwenye mikono salama. Nadhani sasa natakiwa nitafute majibu ya haya maswali yanayonizonga na kuniletea utata mzito…na nadhani najua ni wapi pa kuanzia...” alitulia kwa muda na kuzidi kumtazama yule dada, kisha akamalizia, “…pale ambapo mambo yote haya yalianzia!”
Aliinama na kumbusu kwenye paji la uso, na muda huohuo nesi aliyekuwa
akimhudumia Gilda aliinigia mle ndani.
“Nasikitika itabidi utoke sasa kaka...mkeo yuko kwenye mikono salama tu wala usiwe na wasi...” Nesi alimwambia.
MDUNGUAJI
“Its Okay. Nami ndiyo nilikuwa natoka hata hivyo...” Baddi alisema, kisha akatoa noti ya shilingi elfu kumi na kumpa yule dada.
“Naomba umuangalie vizuri mke wangu dada...nakuomba sana!”
Kama muujiza ile elfu kumi ilipotelea kifuani kwa yule nesi.“Hakuna wasi kaka...nitakuwa naye kwa karibu sana...na ahsante sana!”
“Usijali…na…utakuwa hapa mpaka saa ngapi?” Baddi alimuuliza, na nesi akamjuza kuwa ndiyo ameingia mchana ule, hivyo angekuwa pale mpaka saa nne usiku. Baddi aliitupia jicho saa iliyokuwa ikining’inia kwenye moja ya kuta za wodi ile ndogo. Ilikuwa ni saa nane kasoro dakika kumi za mchana. Alimuomba namba yake ya simu, na bila kusita nesi akamuandikia kwenye kipande cha karatasi na kumpa. Baddi alichukua mabegi yaoaliyokuja nayo pale hospitali kutoka kule hotelini na kutoka nayo nje ya jengo lile. Huko alichukua teksi na kumuagiza dereva ampeleke kwenye hoteli iliyo karibu na ile hospitali. Baada ya kupata chumba na kuhifadhi mabegi yao alitoka tena na kuchukua teksi nyingine.
“Nipeleke makao makuu ya Jeshi...haraka!” Alimuagiza dereva.
“Jeshi la Wananchi au la Kujenga Taifa?” Dereva aliuliza.
“La Wananchi!”
Ndiyo. Huko ndiko mambo yalipoanzia...na ndiko nitakapoanzia kutafuta majibu... Aliingia sehemu ya mapokezi ya makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kumuendea moja kwa moja afisa wa kike aliyekuwa pale mapokezi.
“Jambo!”
“Jambo...nikusaidie?”
“Ndiyo. Nahitaji kuonana na Meja Jenerali Gaudence Amani.” Baddi alimwambia. Yule dada alimtazama kwa muda, uso wake ukionesha mashaka, na mara moja Baddi akawa makini.
“Meja Jenerali Gaudence Amani...?” Yule dada alimuuliza kama kwamba alikuwa ameenda pale makao makuu ya jeshi kuulizia bei ya kilo ya sukari.
“Ndiyo kuruta! Kwani hukunisikia au...?” Baddi alimkemea, sauti yake ya kijeshi ikichukua nafasi bila kujitambua. Yule dada, ambaye kwa hakika alikuwa kuruta, aliingiwa na woga mkubwa.
“Ha...hapana Afande...ila simjui mtu wa jina hilo...hakuna mtu wa jina hilo!”
Baddi alimtazama kwa muda kama kwamba yule dada alikuwa mwehu.
“Hakuna mtu wa jina hilo au humjui mtu wa jina hilo kuruta?” Alimkemea kwa ukali.
“Meja Jenerali Gaudence Amani amestaafu jeshi miaka mitatu iliyopita!” Sauti nyingine ilimjibu kutokea nyuma yake na Baddi Gobbos alihisi mwiliukimwingia baridi.Taratibu aligeukia kule ilipotokea ile sauti.
Mtu mrefu aliyevaa mavazi ya kijeshi yaliyomkaa vema alikuwa akimtazama moja kwa moja usoni. Lakini si namna yule mtu alivyokuwa ndicho kilichomfanya Baddi achanganyikiwe, bali ni lile jibu alilotoa kwa swali alilokuwa amemuuliza yule kuruta.
“Meja Gaudence amestaafu...?” Alimuuliza huku akiegemea ile kaunta ya mapokezi, miguu ikimuisha nguvu. Hakika Meja Gaudence alikuwa mtu muhimu sana kwake, na sasa anaambiwa hayupo!
“Yep...! Una tatizo na hilo?” Mtu mrefu alimuuliza huku akizidi kumtazama kwa makini.
“No! Yaani, ndiyo! Je...unaweza kunifahamisha nitampata wapi...sasa baada ya kuwa amestaafu...?” Baddi alimuuliza.
“Bahati mbaya sijui anapoishi kwa sasa...lakini wewe ni nani? Ni mpiganaji? Na unamtakia nini Meja Gaudence...?” Jamaa aliuliza. Muda huo mtu mwingine mfupi na mnene aliyekuwa kwenye mavazi ya kijeshi alifika pale mapokezi akitokea ndani ya jengo lile. Alisita kidogo sana pale macho yake yalipokutana na yale ya Baddi, kisha akaendelea na mwendo wake, akisalimiana kijeshi na yule mtu mrefu, na kutoka nje ya jengo lile.
Lakini Baddi alishaona jinsi alivyosita, na mara moja kengele za hatari zikaanza kugonga mfululizo kichwani mwake. Amesita! Kwa nini? Amenitambua? Ni nani yule...?
“Na...shukuru sana...” Alimwambia yule mtu mrefu, “…nadhani nahitaji kwenda sasa...nitamtafuta Meja Jenerali Gaundence mahala pengine!” Aligeuka na kuanza kuondoka. Yule jamaa hakufanya bidii yoyote ya kumzuia wala kujaribu kuendelea kumuongelesha. Alimtazama Baddi akitoka nje ya ofisi ile kwa mwendo wa haraka, huku uso wake ukiachia tabasamu dogo...
Yule mtu mnene hakuwepo kabisa pale nje, na Baddi alishangaa. Hata
MDUNGUAJI
dakika tano zilikuwa hazijaisha tangu yule mwanajeshi mfupi na mnene atoke nje ya jengo, sasa vipi asimuone? Alitazama huku na huko, lakini hakumuona yule mtu wala gari lolote likiondoka eneo lile. Vipi hii?
Alianza kuondoka taratibu eneo lile, akili ikiwa imemchanganyika vibaya sana.
Meja Gaudence Amani amestaafu miaka mitatu iliyopita! Mke wangu ameacha kazi na kutoweka miaka mitatu iliyopita! Na mimi nimekufa na kuzikwa miaka mitatu iliyopita...!
What’s going on…?
Alikuwa akitembea huku akiwa amezongwa na mawazo yale wakati alipojihisi kuwa akitembea katikati ya watu wawili. Alitazama kulia kwake na kuona mtu mmoja mwembamba akitembea sambamba naye, na wakati huohuo akihisi akiwekewa kitu kigumu kwenye ubavu wake wa kushoto. Oh, Shit...bastola!
“Tembea hivyo hivyo Baddi Gobbos...!” Yule mtu mwembamba aliyekuwa kulia kwake alimwambia bila hata ya kumgeukia. Muda huo gari dogo aina ya Toyota Corolla liliwapita na kusimama kiasi cha hatua kumi mbele yao, na Baddi aliona mlango wa nyuma wa lile gari ukifunguka.
“Utaenda taratibu na kuingia ndani ya lile gari mbele yetu Baddi, na hutaleta ujinga wowote, kwani kuna bastola ubavuni kwako!” Mtu aliyekuwa kushoto kwake aliongea. Alikuwa ni yule jamaa aliyemvamia kule hotelini asubuhi ile...na kutorokea dirishani mambo yalipomzidi!
Baddi Gobbos alisita katika hatua zake. “Mnataka nini kwangu nyie lakini?” Aliuliza huku akimtazama yule mvamizi aliyewahi kukutana naye mapema siku ile.
“Tembea na uingie kwenye lile gari Baddi! Na usilete vurugu hata kidogo!” Jamaa alimkoromea huku akimgandamizia mdomo wa bastola ubavuni na akiwa amemshika mkono kwa nguvu, akiwa karibu sana naye kiasi kwamba hata wapita njia wengine hawakuweza kuiona ile bastola.
Baddi alienda hadi kwenye lile gari. Mbele alikuwako dereva na kwenye kiti cha nyuma kulikuwa kuna mtu mwingine ambaye alikuwa akimuashiria aingie mle ndani kwa bastola iliyokuwa mkononi kwake. Aligeuka nyuma na kuona kuwa yule jamaa aliyekuwa amemuwekea bastola hapo mwanzo alikuwa amerudi kama hatua tatu nyuma, sasa mkono wake mmoja ukiwa kwenye mfuko wa koti alilokuwa amevaa.
“Ingia Baddi! Bastola iliyomo humu mfukoni imekuelekea wewe…
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI na sitaona haya kukutia shaba hapa hapa kama utaleta ujuvi...!” Jamaa alizidi kumkoromea.
Baddi aliingia ndani ya lile gari na yule jamaa naye akawa anamfuata taratibu nyuma yake ili naye aingie kule nyuma ili Baddi awe katikati yake na yule mwenzake aliyekuwa mle ndani. Alipoufikia ule mlango tu, Baddi aliusukuma kwa nguvu sana ule mlango kutokea ndani ya lile gari. Mlango ulimbabatiza yule jamaa akiwa kule nje ambaye alitoa yowe la mshituko huku akipepesuka na kuangukia nje. Muda
huohuo Baddi aliinua mkono wake wa kulia na kumshindilia
kiwiko cha mwamba wa pua yule jamaa aliyekuwa naye mle ndani ya gari na jamaa alibweka kwa mshituko na mauminvu. Hapohapo
Baddi aliubana chini ya kwapa lake mkono wa yule jamaa uliokuwa na bastola na kwa mkono wake wa kushoto alikizungusha kwa nguvu kiganja kilichokamata ile bastola na ilisikika sauti mithili ya ujiti
mkavu ukivunjika, sambamba na kilio kikubwa cha uchungu kutoka
kwa yule jamaa ambaye aliiachia ile bastola ikianguka ndani ya lile gari.
Baddi alimvunja mkono!
vi...” Dereva aliyekuwa kule mbele alipiga ukelele huku akijikurupusha kugeuka kule nyuma, lakini Baddi alikuwa ameshajirusha nje ya lile gari na kuangukia barabarani kwenye vumbi.
Wapita njia wachache waliokuwa eneo lile walishituka na kusimama
kwa mshangao, lakini Baddi hakujali. Akili yake ilikuwa kwa yule mjinga aliyemsukumizia nje ya lile gari hapo awali, ambaye sasa alimuona akijiinua kutoka alipoangukia huku akihangaika kuutoa mkono wake ulionasa ndani ya mfuko wa koti lake ilhali uso wake ukiwa na mchanganyiko wa ghadhabu na hamaniko dhahiri.
Alimtandika teke kali la uso na jamaa alitupwa nyuma na wakati huohuo ile bastola iliyokuwa ndani ya mfuko wa koti lake ambamo mkono wake bado ulikuwa umeng’ang’ania ilifyatuka kwa mlipuko mkubwa, risasi ikichimba mchanga sentimita chache kutoka kwenye mguu wake mwenyewe.
Si tafrani hiyo!
Watu walianza kupiga kelele huku wakikimbia ovyo. Sasa Baddi alikuwa akimfikiria yule mtu mwembamba mrefu aliyetoroka kule hotelini asubuhi ile, na alimuona akimwendea kwa kasi kutokea mbele ya lile gari, uso ukiwa umemkunjamana kwa dhamira mbaya.
Baddi aliukamata ule mlango wa nyuma wa lile gari uliokuwa wazi na
“Hey...kwani
kumsukumia kwa nguvu. Jamaa aliuparamia ule mlango na kupoteza uelekeo, akiyumba huku akitukana.
Sasa hali ilikuwa ni ya taharuki kila upande. Wapita njia walizidi kupiga mayowe huku wakikimbia bila mpangilio.
“Majambazi…! Majambaziii…Wanauaaa…!”
Baddi alitoka mbio na kujichanganya kwenye lile kundi la wakimbiaji ovyo pale barabarani huku akiona wanajeshi wa jeshi la wananchi wenye silaha wakikimbilia eneo lile kutokea kule makao makuu ya jeshi.
Oh Shit…balaa…!
Wale watekaji nyara wake walioshindwa walijirundika haraka kwenye gari lao na kuondoka kasi kutoka eneo lile, gari lao likiyumba huku na huko, likigonga baadhi ya wananchi waliokuwa wakikimbia ovyo eneo lile. Wale wanajeshi kutoka makao makuu ya jeshi walitaka kulitupia risasi lakini walishindwa kwa kuhofia kuumiza raia waliokuwa wamezagaa eneo lile.
Baddi alizidi kujichanganya miongoni mwa raia waliokuwa wakikimbia huku na huko kwa kiwewe, yeye akitumia mojawapo ya mbinu za medani alizojifunza jeshini…ya kutimua mbio katikati ya kundi la watu huku akipunguza kasi kidogokidogo, na hatimaye kubaki akitembea kwa mwendo wa haraka, muda wote akihakikisha kuwa yuko katikati ya kundi la watu waliokuwa wakikimbia bila mpangilio. Mwishowe alianza kutembea taratibu na kuchukua uelekeo wa kituo cha mabasi kilichokuwa karibu na pale makao makuu ya jeshi. Alipokuwa karibu kabisa na kile kituo cha mabasi, alibadili tena uelekeo na kuziendea teksi zilizokuwa zimeegeshwa kando ya kile kituo cha mabasi.
Mtu mrefu aliyevaa sare za jeshi la wananchi alikuwa akifuatilia harakati zake zote tangu akiwasambaratisha wale watekaji nyara hadi alipokuwa akielekea pale kwenye kituo cha teksi, na kwa mara nyingine uso wake ulionesha tabasamu dogo. Lakini tabasamu lile lilipotea pale alipomshuhudia Baddi Gobbos akibadili tena uelekeo na kutoka kasi ghafla kulikimbilia daladala dogo aina ya Toyota Hiace lililokuwa likianza kutoka pale kituoni na kujitosa ndani yake.
Mtu mrefu mwenye mavazi ya kijeshi alibaki akilitazama lile daladala la kutoka posta kuelekea Kawe likiingia barabarani na kuondoka, Baddi Gobbos akiwa ndani yake.
Ndani ya daladala Baddi alikuwa amesimama akitweta taratibu. Alijua kuwa alichofanya ndicho alichopaswa kufanya katika mazingira yale, kwani alitambua kwamba ilikuwa ni rahisi kwa mtu yeyote aliyekuwa
akifuatilia nyendo zake kumfuata akiwa ndani ya teksi kuliko akiwa ndani ya daladala.
Vituo viwili mbele alibahatika kupata kiti. Aliketi huku bado akili ikimzunguka kutokana na yale mambo aliyokutana nayo kule ndani na nje ya makao makuu ya jeshi.
Meja Jenerali Gaudence Amani amestaafu jeshi miaka mitatu iliyopita! Lakini mbona hata umri wake wa kustaafu bado haujatimia?
Kwa jinsi alivyofahamu, umri wake ulimruhusu yule Meja Jenerali aliyemrudisha tena jeshini aendelee kuwa jeshini muda ule na aendelee kuwepo miaka kama mitatu zaidi kutokea pale. Sasa kwa nini amestaafu miaka sita kabla?
Na yule mtu mfupi niliyemuona pale makao makuu...ni wazi kuwa alisita kidogo aliponiona. Kwa nini? Na wale jamaa walionivamia kule hotelini...mbona wameniibukia tena na huku…what the hell is going on?
Kadiri alivyozidi kuwaza juu ya mambo yale, ndivyo alivyozidi kupata hisia kuwa vituko vyote vile alivyokutana navyo hapa nchini vinahusiana kwa kiasi kikubwa sana na mambo yaliyotokea kule Sierra
Leone... lakini kivipi?
Laiti msaliti Nathan angeniachia nimfikishe kwenye mahakama ya kijeshi mambo mengi yangekuwa wazi bloody hell...lakini yule mshenzi alitaka kujitia ubabe na ubishi ili yule mshirika wake... mdunguaji... aniue, shenzi taipu! Matokeo yake nimemuua na pamoja naye kila alichokuwa anakijua kuhusiana na hujuma ile ya usaliti wa almasi za damu kimepotea...isipokuwa kama ningeweza kumpata yule mdunguaji...
Baddi alikunja uso kwa tafakari nzito, na moyo ukaanza kumuenda mbio.
Mdunguaji!
Ni nini nilichokiona kutoka kwa yule mdunguaji muda ule kabla sijaangukia kule korongoni? Niliona kitu kilichokuwa kinanikumbusha kitu kingine hivi...lakini ni kitu gani?
Shit! Pale nilikuwa najiona nakufa! Sikuweza kuunganisha kila kitu kama ambavyo ningepaswa...lakini...
“Oyaa! Vipi pale...? Tukuwekee chandarua nini, mzee?”
Mawazo yake yalikatishwa na konda wa daladala aliyekuwa anadai nauli yake.
Shit! Shit! Shiiit...! Alikuwa akiwaza huku amefumba macho. Na wala
MDUNGUAJI
hakujua nauli ilikuwa kiasi gani tena sasa! Alitoa noti ya shilingi elfu tano na kumpa yule konda bila ya kusema neno, akiwapuuzia abiria wenzake waliokuwa wakimcheka.
Laiti mngejua yanayopita kichwani mwangu muda huu wala msingecheka, pumbavu wakubwa nyie!
Konda alimrudishia chenji naye akaiweka mfukoni bila hata kuhesabu. Aliona kuwa basi lilizidi kwenda naye hakujua ile safari ingemfikisha wapi. Alitaka kurudi hotelini kwake.
“Nishushe hapo wewe!” Alimpigia kelele konda.
“Aaaah, siyo baskeli hii babu…vipi? Subiri kituo hicho hapo mbele mtu wangu...” Konda alimwambia, na kwa mara nyingine abiria wenzake wakamcheka. Aliteremkia , kituo cha Shopper’s Plaza. Upande ule ule aliona teksi zimeegeshwa na alianza kuziendea ili achukue moja itakayomrudisha hotelini kwake. Alikuwa na hakika kabisa kuwa hakuna mtu aliyemfuata kutoka kule makao makuu ya jeshi mpaka pale, hivyo alikuwa na hakika hakuna atakayeifuata teksi yake wakati akirudi hotelini kwake.
Na ni hapo ndipo alipomuona.
Alihisi kitu kama mwale mkali wa moto kikiupenya moyo wake, na alibaki akiwa amepigwa na butwaa.
Alikuwa akiziendea zile teksi wakati gari aina ya Mitsubishi Pajero Short Chasis lenye rangi ya kijivu lililokuwa likiendeshwa na mwanadada aliyesuka rasta nene lilipotoka kwa kasi nje ya uzio wa pale Shopper’s Plaza na kuingia barabarani, likichukua uelekeo wa mjini.
Baddi Gobbos alibaki kinywa wazi akimtazama yule mwanadada wakati akiendesha kwa kasi lile gari hadi lile gari lilipofichwa kwenye upeo wa macho yake na magari mengine yaliyokuwa yakipita pale barabarani.
Alibaki akiwa amesimama kando ya barabara kama mjinga.
Baddi Gobbos alimtambua yule mwanadada aliyekuwa akiendesha lile gari, na alimtambua kwa sababu yule mwanadada alikuwa ni mkewe.
Nusu saa baadaye alikuwa kwenye chumba cha ile hoteli aliyopanga na bado alikuwa amechangayikiwa vibaya sana. Alikuwa na hakika kabisa kuwa Shani, mkewe, hakuwa amemuona pale Shopper’s Plaza, kwani angemuona lazima angesimama.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Muda alipoweza kufikiri vizuri baada ya mkewe kumpita aliwaendea wale madereva wa teksi na kuwauliza iwapo walikuwa wanamfahamu yule mwanamke aliyekuwa akiendesha ile Mitsubishi Pajero muda mfupi uliopita. Na alipokuwa anawauliza alijua kuwa alikuwa anapoteza muda tu. Lakini kinyume na matarajio yake, kuuliza kwake kulizaa matunda.
“Ile Pajero mbegu fupi ya rangi ya kijivu-jivu, sio?” Mmoja wa wale madereva wa teksi alimuuliza naye akaafiki kwa kichwa huku moyo ukimwenda mbio.
Yule dereva wa teksi alimgeukia dereva mwenzake. “Huyu anamsema yule dada mwenye duka la nguo hapo juu…yule rasta mwenye ile Pajero matata sana!”
Baddi alipigwa butwaa.
“Anhaa, yuuule…” mwenzake alijibu kisha akamgeukia Baddi na kumwambia, “...yule dada ana duka lake la nguo hapo juu. Anaendesha gari kwa kasi sana yule, ndiyo maana sote hapa tunamfahamu kwa hilo!”
Duh!
“Kwa...kwa hiyo mnaweza kunionesha duka lake?” Baddi aliwauliza.
Jamaa walimuonesha. Claudia Gobbos Boutique. Duka lilikuwa ghorofa ya kwanza ya jengo lile la biashara na kwa muda ule lilikuwa limefungwa. Alilitazama lile duka kwa muda mrefu, nguo za kisasa zikining’inia nyuma ya dirisha pana la kioo. Mke wake amefungua duka kubwa namna ile, na akaliita jina la binti yao pekee, Claudia. Chozi lilimtoka.
Akiwa mle hotelini mwake alijua kuwa siku iliyofuata angeonana tena na mkewe, na hapo angejua kila kitu kilichotokea tangu aondoke nchini kwenda kulinda amani nchini Sierra Leone.
Sasa tatizo la wapi mkewe alipo lilikuwa limekwisha,ingawa siku iliyofuata aliiona iko mbali sana. Bado alikuwa ana matatizo mengine.
Aliwaza kwa muda, kisha kama aliyeingiwa na wazo jipya, alikiendea kitabu cha simu kilichokuwa mle ndani na kuanza kufunua kurasa
kadhaa mpaka alipoupata ukurasa aliokuwa ameukusudia. Alitafuta
jina moja alilodhani kuwa alitakiwa alikute kwenye kitabu kile, ingawa
hakuwa na hakika. Aliona majina matatu yanayofanana.
Aliketi kitandani na kuanza kutumia simu iliyokuwa mle chumbani.
Mtu wa kwanza hakuwa aliyemkusudia, ingawa jina lilikuwa linafanana, lakini mtu wa pili alikuwa ndiye haswa aliyemkusudia.
MDUNGUAJI
“Je naweza kuongea na baba yako sasa hivi?” Alimuuliza binti aliyepokea simu ile, ambaye alijitambulisha kuwa ni mtoto wa mtu aliyemkusudia. Moyo ulikuwa ukimdunda kweli kweli!
“Subiri kidogo basi…” Binti alimjibu kisha Baddi alisikia ile simu ikiwekwa pembeni. Alibaki akisubiri huku moyo ukimuenda mbio. Hatimaye alisikia ile simu ikiinuliwa na sauti aliyoitambua iliongea.
“Meja mstaafu Abdul-Hameed Babu hapa, nani mwenzangu?”
E bwana we!
“Vampire!” Baddi alisema kwenye simu ile, na kimya kizito kilichukua nafasi.
“Va....Vampire? Baddi? Ni weye huyu?” Meja Abdul-Hameed Babu, p.a.k. Swordfish, aliuliza kwa sauti iliyojaa wahka na kitetemeshi.
“Ni mimi meja. Nimerudi…”
“Wallahi huu mtihani! Tena mtihani mkubwa!” Swordfish alisema kwa sauti ya chini.
“Ni kweli, kwani naamini kuwa kwenu nyote mimi ni marehemu.”
“Hakika mimi si miongoni mwao Vampire! Siku zote nilikuwa nahofia kuwa siku hii itafika...na sasa imefika! Vampire umekuwa Vampire kweli…umekuja kutoka kwenye ulimwengu wa wafu! Uko wapi weye hivi sasa? Kuna mengi yametokea.” Swordfish alimwambia.
“Ni kweli. Na nadhani sasa nimefikia mahala ambapo nahitaji msaada wako.” Baddi alimwambia.
“Niambie uliko Baddi, nami nitakuja mara moja!”
“Niko Dar.”
“Okay… Inshallah kesho naingia chomboni kuja huko partner . Saa nne nitakuwa jijini. Nitafikia hoteli ya Al-Uruba. Niulizie pale muda wowote kuanzia saa nne na nusu. Usifanye jambo lolote, usijaribu kuonana na mtu yoyote mpaka tuonanane!” Alipokwisha kusema hivyo, Meja mstaafu Abdul-Hameed Babu, p.a.k. Swordfish, shujaa wa mapigano ya ana kwa ana, alikata simu. Baddi Gobbos alibaki akiwa ameishikilia ile simu kwa muda mrefu, uso wake ukiwa umejaa tafakari zito.
Kisha alitoa kile kipande cha karatasi alichopewa na yule nesi wa kule Muhimbili na kumpigia simu. Nesi alimwambia kuwa “mkewe” aliamka kiasi cha saa moja baada ya yeye kuondoka pale hospitali, ila kwa muda ule alikuwa amelala. Alipomuuliza iwapo anaweza kwenda kumuona nesi alimwambia kuwa muda ulikuwa umekwisha,hivyo
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI aende asubuhi ya siku itakayofuata. Ilikuwa ni saa kumi na mbili na robo za jioni.
Ndipo kwa mara ya kwanza alipokumbuka kuwa hakuwa amekula kitu chochote cha maana tangu ameingia nchini.
Aliagiza chakula kutoka kwenye mgahawa wa mle hotelini akiwa mle mle chumbani. Alipoambiwa kuwa chakula alichoagiza kingekuwa tayari baada ya dakika ishirini, aliamua kupitisha muda huo kwa kuingia bafuni kuoga. Baada ya mlo alijitupa kitandani akiwa mchovu sana. Alipitiwa na usingizi mzito...
Wakati Baddi Gobbos anachapa usingizi mzito usiku ule, mtu mfupi aliyemuona kule makao makuu ya jeshi mchana ule alikuwa kwenye wakati mgumu sana.
“Una maana gani kuwa wameshindwa kumdhibiti...si ulisema walishafanikiwa kumuingiza ndani ya gari?” Sauti iliyokuwa upande wa pili wa simu aliyokuwa akiongea nayo ilimkemea. Jamaa alifinya uso na kuuma meno.
“Ndivyo ilivyokuwa mzee...lakini...dah! hata wao wenyewe hawajui ilikuwaje...Baddi aliwatoka kwa namna ambayo hawakuitarajia...”
“Wewe nilikuambiaje kuhusu Baddi?” Sauti iliuliza. Mtu mfupi alibaki kimya.
“Si nilikwambia kuwa huyo mtu ni hatari kuliko nyoka?”
“Ndi...ndiyo...hatari kama koboko...!” Mtu mfupi alijibu.
“Sasa kama ulijua hivyo kwa nini hukuwaasa mapema hao wajinga wako wewe?” Sauti ya kwenye simu ilimfokea, na mtu mfupi alijikuta akiiweka mbali na sikio lake ile simu huku akiikodolea macho kwa hasira.
“Niliwaambia hilo mkuu, ila tu ni kwamba Baddi ni mkali kuliko hata huyo koboko...sasa tutajipanga vizuri zaidi!”
“Hatuna muda wa kupoteza wewe! Hilo lifanyike haraka sana. Nataka Baddi adhibitiwe haraka sana...kabla mwenzetu hajaonana naye!” Sauti ilifoka tena.
“Ndi...”
Simu ilikuwa imeshakatwa kutokea upande wa pili.
MDUNGUAJI
Mtu mfupi alipiga ukelele wa ghadhabu na kumtupia mmoja wa wale vibaraka wake ile simu kwa hasira huku tusi zito la nguoni likimtoka. Yule mtu mwembamba mrefu aliikwepa ile simu huku akiwa ametumbua macho. Simu ilijipiga ukutani na kusambaratika vipande vipande.
Asubuhi ya siku iliyofuata Baddi Gobbos aliamka akiwa na nguvu mpya na wahka mkubwa wa kuonana tena na mkewe. Alianzia Muhimbili ambako bado Gilda alikuwa na uchovu wa dawa alizopewa siku iliyopita.
“Heeeey...mrembo fulani, hujambo leo?” Alijitahidi kumsalimia kwa uchangamfu na mbinu hiyo ilisaidia kwani Gilda aliachia tabasamu pana pamoja na kwamba bado macho yake yalionekana mazito.
“Baddi...”
“Vipi hali yako, umelala unono?”
“Mnnh! Nimechoka sana...sijui ni madawa niliyopewa? Yaani nimelala kama mzigo.” Gilda alimjibu, kisha uso wake ukiwa makini sana alimuuliza, “...vipi wewe...uko salama? Wale majambazi hawajakusumbua tena...?”
“ Yeah , niko salama...nadhani hilo ndilo la msingi kwa sasa. Vipi huduma za hapa ziko sawia?” Baddi hakutaka kumuongezea mashaka kwa kumueleza juu ya misukosuko aliyopambana nayo siku iliyopita.
“Ah, karibu muda wote nilikuwa nimelala, sasa siwezi kujua kwa kweli, ila katika muda ambao nimekuwa macho, nimepata huduma nzuri mno...huyu nesi anayenihudumia ni safi sana.”
“Okay, that’s good...” Baddi alisema kisha akabaki kimya kwa muda, uso wake ukionesha mawazo mazito. Gilda aliliona hilo mara moja.
“Ni nini Baddi...kuna tatizo...?” Alimuuliza huku akijitahidi kujiinua kutoka pale kitandani. Baddi alimzuia kwa kumuwekea mikono yake kifuani na kumlaza tena pale kitandani.
“Hakuna tatizo lolote Gilda, ila tu...nimemuona mke wangu.” Baddi alimwambia huku akimtazama kwa makini, mdomo wake ukifanya tabasamu dogo.
Gilda alionesha kuchomwa sana na kauli ile na kidogo uso wake ulidhihirisha fadhaa kubwa kabisa, kisha hapohapo ule uso ulichanua kwa
tabasamu pana na yale macho yaliyochoka yakaonekana kupata nuru mpya.
“Heeh, hiyo ni habari nzuri sana Baddi! Ulionana naye vipi? Wapi? Ilikuwaje? Hebu nielezee…umemuonaje, amebadilika eenh?”
Gilda alimuuliza kwa bashasha, na Baddi alichanganyikiwa. Hivi ni kweli niliona kama Gilda amefadhaishwa na habari hii au ni fikra zangu tu?
Akamuelezea namna alivyomuona mkewe siku iliyopita, kisha wote walibaki kimya kwa muda. Gilda aligeuza uso wake pembeni. “Kwa hiyo kumbe hamkuonana...ni wewe ndiye uliyemuona.” Alisema.
“Yeah…”
“Utaenda kumuona leo?”
“Yeah…nitaenda kuonana naye, nijue yaliyotokea muda wote ambao sikuwepo…nijue hali ya mwanangu Claudia.”
“Yeah Baddi.” Gilda alisema kwa sauti ya chini. Baddi alijua kuwa ile habari ilimtia unyonge Gilda, lakini hakujua afanye nini.
“Unaonekana kufadhaika Gilda.”
“Hapana Baddi nenda tu. Hilo si ndilo tulilotaka kulifanya mara tulipofika hapa?” Alimjibu, kisha akapangusa machozi na kumgeukia. Baddi aliona kuwa yule binti alikuwa analia.
“Oh, Gilda…” Alisema na kumkumbatia, akiwa makini kutomtonesha kidonda chake. Walikumbatiana namna ile kwa muda, kisha waliachiana na kubaki kimya, kila mmoja akiwa na mawazo yake. Muda huo nesi aliingia na kuwaarifu kuwa dokta angekuja kumuona Gilda baada ya muda mfupi na kumuomba Baddi awape nafasi. Baddi alimuaga Gilda kwa ahadi kuwa angerudi baadaye.
“Baddi...” Gilda aliita, na Baddi aligeuka.
“Uwe makini huko uendako...” Alimwambia.
Baddi aliafiki kwa kichwa, kisha akageuka na kutoka. Ilikuwa ni saa moja na nusu za asubuh, hivyo aliamua kurudi hotelini kusubiri muda wa kwenda kuonana Swordfish.
Meja Babu ameniambia nisionane na mtu yeyote kabla sijaonana naye...ni wazi kuwa ana jambo la kuniambia.
Lakini...
Moyo wake ulikuwa ukitekenyeka kwa wahka na kiherehere cha kumuona tena mkewe. Wakati akipitiwa na mawazo hayo, simu iliyokuwa mle chumbani iliita. Aliinua ile simu na kuiweka sikioni kwake akijua ni kutoka mapokezi, lakini sivyo ilivyokuwa.
MDUNGUAJI
“Eeeh, bwana Baddi Gobbos?” Sauti ya kike iliuliza na moyo ukampiga mshindo. Alikuwa ni yule nesi wa kule hospitali na mara moja Baddi alihisi kuwa hali ya Gilda imekuwa mbaya.
“Eh, yes...?” Alijibu kwa mashaka, “...Gilda yuko salama...?”
“Eh, ndiyo kaka...namba ya hii simu ilibaki kwenye simu yangu uliponipigia jana...”
“Ah, Okay...ku...kuna nini...”
“Nilitaka kukufahamisha kuwa dokta amesema Gilda anaweza kutoka leo, kwani kilichobaki ni kuwa anakuja kufunga kidonda tu na kama kuna mtu wa kumhudumia nyumbani, anaweza kuwa anasafishwa na kubadilishwa bandeji huko huko...” Nesi alimwambia.
“Alaa...hiyo ni habari nzuri...kwa hiyo naweza kuja kumchukua?”
“Ndiyo…yeye mwenyewe anataka kutoka…”
Dakika ishirini baadaye, Baddi alimkaribisha Gilda kwenye chumba cha ile hoteli aliyopanga. Walikuwa na dawa ambazo Gilda alitakiwa awe anameza kila baada ya saa kadhaa, na pia walipewa bandeji na dawa ya kuoshea kile kidonda kila jioni.
“Sasa si utaenda kuonana na mkeo leo...?” Gilda alimuuliza mara baada ya kutulia mle chumbani. Baddi alimueleza juu ya maongezi yake na Swordfish. “Sasa sijui...nadhani itanibidi nisubiri kuonana na Swordfish kwanza...” Alimalizia.
“Ah, kwani unadhani hilo analotaka kukuambia litakuwa linamhusu mkeo Baddi? Mi’ naona litakuwa linahusiana na wale wauaji zaidi kuliko.... kuliko vinginevyo...”
“Hata mimi pia nilikuwa nahisi hivyo.”
“Anyway, basi mi’ naomba unifanyie kazi moja asubuhi hii Baddi...” Gilda alimwambia. “Okay...what is it...?”
“Si unajua kuwa niliondoka hapa nchini na Francois...yule mpenzi wangu wa kifaransa...”
“Eeem...ndiyo...”
Gilda alibana mdomo wake na kufumba macho kwa muda, kisha akamwambia; “...naomba uende ukamfahamishe jamaa yake aliyeko hapa jijini juu ya uwepo wangu...yule dada wa kifaransa mwenye duka la nguo nililokuwa
nikifanyia kazi. Akiweza uje naye ili nimpe habari za kifo cha Francois... hakuna ndugu yake yeyote anayejua yaliyompata kule Liberia... can you do that for me? ”
“Of course Gilda...sasa...hilo duka lake liko wapi...?”
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Mnh, sijui kama bado litakuwa pale pale au vipi...au sijui hata kama bado lipo, kwani miaka mitatu ni mingi sana...ila lilikuwa maeneo ya Namanga...njia ya Msasani. Duka lenyewe lilikuwa linaitwa French Ellegance...”
“Okay, na huyo dada...? Nitamjuaje...?”
“Ulizia mmiliki wa hilo duka tu. Anaitwa, Mademoiselle Rachelle... mwanadada mrefu mwenye macho makubwa ya buluu...utamtambua tu...”
“
Okay...Gilda, nitafanya hivyo....na nikirudi huko muda wa kuonana na Swordfish utakuwa umefika. We’ utakuwa okay hapa peke yako?”
“Ndiyo...sina wasi wasi...”
Baddi alitoka. Na pale alipotoka tu Gilda aliinuka na kuufunga ule mlango kwa ndani, kisha akaliendea begi lake...
Duka lililoitwa French Ellegance bado lilikuwa ni miongoni mwa maduka mengi ya pale Namanga jijini Dar. Lakini Baddi Gobbos hakuweza kujua iwapo Mademoiselle Rachelle bado alikuwa akilimiliki lile duka au vinginevyo, na hakuweza kujua kwa kuwa lile duka lilikuwa limefungwa au lilikuwa bado halijafunguliwa asubuhi ile.
Alibaki akiwa amesimama nje ya duka lile kwa muda mawazo yakigongana kichwani mwake. Lile duka halikuwa mbali na eneo la Shopper’s Plaza lilipokuwa duka la mkewe.
Sasa niende, au nisubiri kuonana na Swordfish kwanza...?
Moyo ulizidi kumtekenyeka na wahka ukazidi kumpanda.
Sijamuona mke wangu na mwanangu kwa miaka mitatu...miaka mitatu...!
Alichukua teksi hadi Shopper’s Plaza, ambako nako alikuta duka la nguo la Claudia Gobbos Boutique likiwa halijafunguliwa. Aliamua kuondoka, kwani alihofia kukutwa na wale wauaji eneo lile.
Angalau nimejaribu kuonana naye...nitarudi baada ya kuonana na Swordfish...
Alikuwa anaanza kuondoka eneo lile wakati alipoliona gari la mkewe
likiingia kwa kasi sana ndani ya wigo wa eneo lile na kuegeshwa huku tairi zake zikitoa sauti za msuguano. Alibaki akiikodolea macho hali ile akiwa amejificha nyuma ya moja ya nguzo za jengo lile.
Huyu ni Shani kweli? Mbona anaendesha kwa fujo hivi...!
Hata pale wazo lile lilipokuwa likipita kichwani kwake, Shani Gobbos aliteremka kutoka kwenye lile gari na kuingia ndani ya jengo
MDUNGUAJI
lile huku akibonyeza komeo maalum ya gari iliyokuwa kwenye ufunguo wake. Lile gari lilitoa mlio mkali mithili ya mbinja kumaanisha kuwa tayari ile milango ilikuwa imejikomea.
Baddi alibaki akiwa amesimama nyuma ya ile nguzo huku moyo ukimwenda mbio. Hakika yule alikuwa ni mkewe Shani...lakini alionekana kuwa ni mwanamke mwenye ghadhabu kubwa... kwa nini?
Alisubiri kwa kama dakika tano hivi, kisha taratibu alianza kukwea ngazi kuelekea kule ghorofani lilipokuwa duka la mkewe. Aliufikia ule mlango wa kioo na kuona kibao kilichoandikwa “Closed”. Kwa ndani aliweza kumuona Shani akijishughulisha kupanga-panga vitu mle dukani. Alipoujaribu ule mlango ulifunguka, naye akaingia na kubaki akiwa amesimama mle ndani. Shani alikuwa hajamuona, akiendelea na harakati zake haraka haraka mle ndani.
“Shani...” Aliita taratibu.
Shani aligeuka huku akitoa sauti ya mshituko, kisha akabaki akiwa amepigwa na butwaa, akimkodolea macho ya kutoamini, kisha Baddi aliishuhudia midomo ya yule mwanamama ikimcheza kwa muda, kabla ya hofu kubwa kuutawala uso wake.
“Shani mke wangu...” Aliita tena huku akianza kumsogelea, na hapo ndipo Shani alipozinduka. Yowe kubwa lilimtoka huku akijishika kichwa na miguu ikimwisha nguvu, alianza kuanguka chini.
“Shani NOOO!” Baddi aliruka kwa hatua kubwa na kuwahi kumdaka kabla hajafika chini. Alimvutia kwenye kiti kilichokuwa karibu yao mle ndani na kumketisha.
“WEWE! We...we ni nan...toka! Tokaaa! Niachieeee!” Shani alipiga kelele huku akijitupa huku na huko.
“Tulia Shani...tulia...ni mimi mumeo Baddi...Badi Gobbos, eenh...? Baba Claudia mimi!” Baddi alijitahidi kumtuliza huku akimbana pale kwenye kiti.
“NO! Mume wangu amekufa... amekufa...! Wewe ni jini...niachie! Niachieeee...!”
“Hapana Shani sijafa...ni makosa tu yalifanyika, nikadhaniwa nimekufa!
Mimi ni mzima, na nime...”
“Wewe ni Mzuka!”
Vampire?
“...sio mtu wewe...!”
“Shani...”
“...ulikuwa ukinijia kwenye ndoto...!”
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“SHANI!”
“...sasa naona umeamua kunijia moja kwa mo...”
Kibao!
Shani alibweka kama mbwa kwa kofi alilochapwa, na kubaki akiwa anamkodolea macho kwa mshangao mkubwa huku akijipapasa shavuni pale kofi la Baddi lilipotua.
Lile kofi lilimzindua Shani Gobbos. Sasa alikuwa akimtazama yule mtu aliyepiga goti mbele yake kama kwamba ndiyo kwanza akili yake inaanza kumtambua. Midomo ilikuwa ikimcheza na mikono ilikuwa ikimtetema, hali machozi yakimbubujika.
“Oh, Shani mke wangu! I am so sorry! Lakini inabidi utulie. Umeshituka sana, inakubidi utulie mke wangu...nimerudi mumeo... nimekuja kuungana nawe...na mwanetu Claudia...yu hali gani yeye?” Baddi alimbembeleza huku naye akitokwa na machozi.
“Baddi...? U...um...uh..u-hai...?” Alimuuliza huku akimtazama kwa kutoamini. Baddi Gobbos alimtazama kwa uchungu, upendo na hisia kali. Alitaka kumwambia kuwa ni kweli yu-hai, lakini donge lililomkaba kooni lilikuwa ni kubwa sana, naye alihisi midomo yake ikianza kumcheza. Alibana midomo yake na kumuafikia kwa kichwa huku akimtazama usoni.
Doh! Ilikuwa kama kwamba Shani alikuwa anasubiri ile ishara tu.
Aliangua kilio kizito, huku akijiangusha kutoka pale kwenye kiti na kupiga magoti mbele ya mumewe na kumkumbatia kwa nguvu, akiuzamisha uso wa yule mwanamume aliyempenda kwa dhati katikati ya kifua chake.
“Oooh, Baddi mume wangu! Waliniambia umeuawa kule ughaibuni! Waliniambia kuwa ulikufa kishujaa...” Shani alikuwa akibwabwaja huku akilia.
“Najua Shani...najua mke wangu....” Baddi naye alibwabwaja huku akilia. Lakini Shani aliendelea na maombolezo yake kama kwamba Baddi hakuwa akiongea lolote.
“OOOH Baddi wangu jamani Baba Claudia! Ni jinsi gani nilivyobisha! Sikutaka kuamini kuwa umekufa mume wangu...sikutaka kuamini kabisa…
“Oh, Shani…”
“…lakini miaka ikazidi kukatika Baddi! Miwili…na sasa imekuwa mitatu...nikakubali kuwa mume wangu umekufa...sasa tena leo...ah,
MDUNGUAJI
Baddi! Kwa nini umekuja,eeenh...? Kwa nini Baddi...?” Shani alikuwa akilia huku akibwabwaja kwa uchungu. Baddi alijichomoa kutoka kifuani kwa mkewe na kumtazama kwa huzuni iliyochanganyika na mshangao.
“Nimerudi kwa kuwa tangu awali nilitakiwa nirudi kwako Shani...nirudi kwenu...wewe na mwanetu Claudia...nimerudi kwa sababu sijafa mke wangu...”
“Oh, Baddi! Laiti ungejua ulilolifanya...! Kwa nini unayafanya maisha yangu yazidi kuwa magumu kuliko yalivyo sasa Baddi?” Shani alizidi kulia huku akitikisa kichwa kwa huzuni.
“Ni nini unachoongea Shani...?” Baddi alimuuliza huku akisimama na kumtazama kwa wasiwasi mkubwa.
“Oh, Baddi...” Shani alilalama na kujiinamia huku akilaza kichwa chake kwenye viganja vya mikono yake.
“Shani...”
Shani alibaki akiwa katika hali ile kwa muda mrefu, akilia kwa uchungu. Baddi alichanganyikiwa.
“Mbona sikuelewi Shani...?”
Hatimaye Shani aliinua uso wake uliokuwa ukibubujikwa na machozi.
“Naomba ukaukomee kwa ndani ule mlango Baddi. Sitaki wahudumu wa hapa dukani watukute katika hali hii humu ndani...” Alimwambia kwa huzuni. Akiwa amechanganyikiwa pasina kifani, Baddi alitekeleza, kisha akarudi na kusimama mbele ya mkewe. Kuna jambo halikuwa likimkalia sawa kichwani mwake, na hakuelewa ni jambo gani.
“Vipi Shani...najua kuwa hii ni hali ya kushitua sana kwako, lakini...ina maana hukufurahi kuwa niko mzima na nimerudi...?” Alimuuliza. Shani alichia kicheko hafifu.
“Baddi, nimefurahi kuwa umzima...lakini...ningefurahi zaidi kama ungerudi angalau mwaka mmoja uliopita baba Claudia...” Alimjibu kwa huzuni huku akimtazama usoni.
“Ni kweli Shani...lakini sioni kuwa hilo ni tatizo...cha msingi ni kwamba nimeru...”
“Mimi sasa ni mke wa mtu Baddi...!” Shani alimkatisha kwa huzuni na hisia kali.
E bwana we!
Baddi Gobbos alihisi moyo wake ukipiga chogo chemba ndani ya kifua chake, halafu akahisi ile sakafu ya mle ndani ikididimia naye ikimuacha akielea hewani kwa sekunde kadhaa. Kichwa kilimuwia chepesi na akahisi
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI alikuwa anakaribia kupoteza fahamu.
“Eti… whaat ...?” Hatimaye alifanikiwa kutoa sauti iliyokwaruza kumuuliza yule mwanamke aliyekuwa mkewe na ambaye kumbe si mkewe tena. Shani alibaki akimtazama kwa huzuni huku akilia kwa simanzi.
“Ni kweli Baddi...mimi sasa nimeolewa na mtu mwingine...”
“ No way Shani! Utaolewaje wakati wewe ni mke wa mtu tayari…?” Baddi alikuja juu.
“Tulijua wewe umekufa Baddi...na...kwa namna fulani ilinibidi mimi niendelee na maisha yangu...”
“No way! Sasa si mimi hapa mumeo nimerudi Shani...? Yaani kusikia tu kuwa nimekufa unakimbilia kuolewa? Mwanangu yuko wapi sasa? Analelewa na baba wa kambo? No way, bwana! No way! No waaaaaay!”Jamaa alikuja mbogo. Alikuwa amechanganyikiwa. Si jambo alilolitarajia asilani.
“Baddi...! Usiseme hivyo jamani. Nimekaa kwa miaka miwili kabla sijaolewa mume wangu, na...”
“Mume wako nani sasa? Mimi au huyo...huyo...nani sijui huko?”
“Oh, Baddi jamani...” Shani aliangua kilio upya.
Alilia! Alilia sana!
Baddi alibaki akimtazama yule mkewe ambaye si mkewe tena kwa kutoamini. Na kadiri alivyokuwa akimtazama ndivyo alivyozidi kutulia na akili yake ikianza kufanya kazi kama ilivyotakiwa.
“Okay, Shani. Samahani kwa kukukemea.”
Shani aliinua uso wake na kumtazama kwa huzuni, “Unajua kuwa wewe ndiye mwanamume pekee niliyempenda kwa moyo wangu wote Baddi na siwezi kulibadili hilo hata kama nikitaka.”
“Acha Shani. Usiseme mambo hayo sasa, kwani tayari imeshakuwa tofauti.”
Shani alianza kulia tena.
“Okay. Sasa, dah! Si...sijui...yaani, ni nani huyu ambaye sasa ni mumeo Shani? Anakupenda? Anampenda binti yetu...?” Hatimaye Baddi aliuliza.
Ni bora hata asingeuliza.
Shani alimtazama kwa muda huku akibubujikwa na machozi. “Naomba unisamehe sana Baddi. Lakini miaka mitatu ni mingi. Nilifikia hatua nami nikaamini kuwa umekufa mume wangu.”
MDUNGUAJI
“Ni nani?” Baddi alisisitiza kumuuliza.
“Ni...ni Gaudence Baddi. Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani.”
Heh!
Baddi alimtumbulia macho kwa kutoamini.
Meja Jenerali Gaudence Amani!
Kizunguzungu kilimkumba na alijikuta akiwa ameketi sakafuni mle ndani.
Meja Jenerali Gaudence Amani!
“Baddi...” Shani aliita huku akimsogelea pale alipokuwa amekaa, lakini Baddi alimkatisha.
“Niache, Shani…! Naomba uniache tafadhali...!” Alimwambia huku akimnyooshea kiganja chake, uso wake akiwa ameugeuzia pembeni.
“Oh, Baddi jamani, sasa mimi...”
“Niache Shani....niache...!” Baddi alisisitiza kwa sauti iliyovunjika kwa uchungu uliodhihiri. Shani alibaki akiwa amesimama katikati ya duka lake akimtazama yule mwanamume mpiganaji shujaa wa vita vya msituni ambaye sasa alielekea kuwa mateka wa vita vya moyoni.
“Kwa nini Gaudence, Shani?” Hatimaye Baddi aliuliza. Kimya kilipita kabla Shani hajamjibu.
“Si...sidhani kama kuwa ni Gaudence au si Gaudence ni suala la msingi sana Baddi, suala ni kwamb...”
“WHY HIM?” Baddi alifoka, na Shani alitoa kilio kikali cha mshituko na woga. Hakuwa na jibu lolote kwa swali lile, badala yake alibaki akilia taratibu huku akifinyanga vidole vya mikono yake. Baddi alitikisa kichwa kwa kukata tamaa.
“Okay, vipi hali ya baba...yu hali gani...na yuko wapi ? Usiniambie kuwa unaishi naye hapo kwa huyo mumeo!”
“Ah! Baddi. Hakika leo umeniweka katika wakati mgumu sana... mi’ naona...”
“BABA YANGU YUKO WAPI?”
“Am...Ame...f...f....fariki, Baddi...!”
La Haula!
Baddi alimtazama yule mwanamke kama kwamba alikuwa ndiyo anamuona kwa mara ya kwanza.
“Ba...baba amefariki?”
“Ndiyo Baddi...I am so sorry!”
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Kwa mara nyingine Baddi alitikisa kichwa kwa kukata tamaa. Alihisi kusalitika kwa kiasi kikubwa kabisa. Yaani siku zote alivyokuwa akikabiliana na mashaka mazito huko ughaibuni ilikuwa ni kwa ajili aendelee kuishi ili hatimaye aje akutane tena na familia yake, sasa tena anaporejea hapa nchini anagundua kuwa kumbe vyote alivyokuwa akivipagania akiwa huko ughaibuni havipo tena kwa ajili yake.
Jamaa alilia!
Alilia kwa uchungu na fadhaa, Shani akilia pamoja naye.
“Alikufaje?” Hatimaye aliuliza huku akiwa amejiinamia pale chini.
“Eenh..?”
“Nauliza baba yangu alikufaje?”
“A...aligongwa na gari...ilikuwa ni ajali. Alikuwa anatoka kuchukua pesa zake za pensheni ambazo huwa anapata kila mwezi na...na...ndiyo alipopatwa na hiyo ajali...”
“Oh, My God...”
“Pole sana Baddi...”
Baddi alitaka kumuuliza mambo mengi zaidi, lakini muda huo mlango wa kuingilia pale dukani ulisukumwa kutokea nje, kisha mtu aliyeusukuma alianza kubisha hodi kwa kuugonga ule mlango.
“Oh, mhudumu wangu wa dukani huyo…” Shani alisema huku akiwa amechanganyikiwa na akijipangusa machozi.
Taratibu Baddi aliinuka na kusimama. Alivuta pumzi ndefu na kuzishusha huku akijifuta machozi. Alibaki akimtazama kwa muda yule mrembo aliyewahi kuwa mkewe hapo nyuma, kisha bila ya kusema neno aligeuka na kuuendea ule mlango.
“Baddi…” Shani alimwita kwa sauti iliyofadhaika. Bila ya kugeuka Baddi alimuinulia mkono wake kwa ishara ya kumuaga.
“Baddi please...sasa unaenda wapi? Sasa...sasa unaondokaje namna hiyo jamani...?”
Baddi alifungua ule mlango na kutoka nje ya duka lile, akimpuuza yule msichana aliyekuwa akibisha hodi nje ya mlango ule, ambaye alikuwa akimtazama kwa mshangao mkubwa.
Sauti ya kilio ilisikika kutokea ndani ya duka lile na yule binti alikimbilia mle ndani huku akiwa ametaharuki. Baddi hakugeuka. Wala hakujali tena. Aliteremka ngazi taratibu huku akiwa amezongwa na mawazo mazito.
Baba amekufa! Shani kaolewa na Gaudence Amani…!
MDUNGUAJI
Alimfikiria Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani, na kadiri alimvyofikiria
ndivyo alivyozidi kuchanganyikiwa.
Alifungua mlango wa moja ya teksi zilizoegeshwa nje ya jengo lile na kujibwaga kwenye kiti cha nyuma bila hata ya kuongea au kupatana na dereva.
“Wapi mzee...?” Dereva alimuuliza.
“Twende tu...”
“Ndiyo, lakini wapi sasa bosi?” Jamaa alimuuliza huku akipiga stati.
“Nizungushe tu mjini kwanza, kisha n’takwambia ni wapi uniteremshe...”
Baddi alimwambia huku akimtupia noti mbili za shilingi elfu kumi.
“Okay Boss....” Jamaa alisema huku akishindilia mfukoni zile pesa.
Lakini Baddi hakuwa akimsikia tena.
Akili yake ilirudi kwa mtu aitwaye Gaudence Amani...
Walikutana jeshini, yeye akiwa ameingia jeshini baada ya kuhitimu kidato cha sita wakati tayari Gaudence Amani akiwa na cheo cha Kepteni. Alipojiunga tu na jeshi alipewa nyota mbili. Kepteni Gaudence Amani, ambaye ndio alikuwa mkuu wa kombania yao, alimpokea yeye pamoja na wanajeshi wengine wapya kama yeye wakati huo, mmoja wao akiwa Nathan Mwombeki, p.a.k. Alpha, pale jeshini. Akiwa jeshini alijenga urafiki na Nathan na mara nyingi walijikuta wakiwa pamoja katika mambo mengi pale jeshini. Baadaye yeye alienda Cuba kusomea shahada ya juu katika fani ya mawasiliano ya kijeshi, akimuacha Nathan akiendelea kulitumikia jeshi hapa nchini. Aliporejea na shahada yake, alipandishwa cheo na kupewa u-Kepteni, Nathan akiwa na nyota zake mbili, na kwa namna fulani aliona kuwa Nathan hakupendezewa, lakini hakuwa na namna. Urafiki wao ukaanza kulegalega ingawa waliendelea kuonana mara kwa mara. Alipopelekwa kufundisha mawasiliano ya kijeshi katika chuo cha jeshi Monduli, ndipo walipoachana kabisa na Nathan, ambaye alibaki akilitumikia jeshi katika nyanja nyingine jijini Dar. Hata hivyo, wote waliendelea kuwa karibu sana na mkuu wao Gaudence Amani, japo kila mmoja kwa wakati wake.
Baddi alilitumikia jeshi kwa miaka mitano. Ndani ya miaka mitano hiyo, wote watatu, kila mmoja kwa wakati wake, walipanda ngazi za kijeshi. Ilikuwa ni miaka mitano ya harakati kali za kijeshi kwa Kepteni Baddi Gobbos, kwani alipata nafasi ya kulitumikia jeshi katika kampeni nyingi nje ya nchi kama vile Msumbiji, Namibia na Ethiopia, ambako kote huko alihatarisha sana maisha yake. Kutokana na umahiri wake katika mawasiliano ya kijeshi ulioudhihirisha katika kampeni hizo, wakuu wake wa kijeshi walimpandisha cheo na kufikia wadhifa wa Kanali. Ni katika mwaka wake wa tano jeshini ndipo alipooa.
MDUNGUAJI
Hapa Baddi alikumbuka kuwa katika miaka yote ile walipokuwa
jeshini, Meja Jenerali Gaudence Amani hakuwahi kuoa kabisa!
Miaka yote yeye alikuwa ni kapera tu, jambo ambalo hata wao, wapiganaji wenzake, liliwashangaza, na ambalo Gaudence hakutaka kabisa kulitolea maelezo. Sasa kwa nini aamue kuoa wakati huu?
Na kwa nini amuoe Shani?
Baddi alitoa mguno wa kuchanganyikiwa mle ndani ya gari na kurudisha mawazo yake huko nyuma...
Baada ya kutumikia jeshi kwa miaka sita, aliamua kustaafu na kuanzisha kampuni yake binafsi ya mawasiliano. Alikumbuka wazi wazi ushauri aliopewa na Meja Jenerali Gaudence Amani wakati huo.
“Wewe ni mpiganaji Baddi...a soldier! Na soldier siku zote huwa hafi, si unajua hiyo? A soldier never dies...! Ulikuwa mwanajeshi, u-mwanajeshi na utaendelea kuwa mwanajeshi tu Kanali...usisahau hilo kabisa...!”
“Ndiyo afande…nafahamu hilo”
“Sasa kwa nini unataka kuacha upiganaji Kanali Gobbos?...?”
“Nadhani nimeshatoa mchango wa kutosha kwa nchi yangu sasa afande...hivyo nataka nitumie muda wangu uliobaki kuitengenezea familia yangu mazingira mazuri zaidi...”
“Sasa unadhani ukiacha kazi ndiyo utakuwa unawatengenezea mazingira bora zaidi...?”
“Hapana, na ndiyo afande...” Baddi alimjibu, na kuendelea, “…ni kwamba nahitaji kutumia muda zaidi kwenye kampuni yangu ya mawasiliano kuliko jeshini, na siwezi kutumikia mabwana wawili... isitoshe, kuna kazi binafsi ambazo zitanilazimu kusafiri nje ya mkoa na hata nje ya nchi, sasa nikiwa jeshini sitaweza kusafiri kama nitakavyo...”
Kimya kilitawala.
“Sasa kama mkuu wako wa kazi, niliyekupokea jeshini na kukupa mafunzo yote muhimu jeshini, nakushauri usiache kazi. Badala yake mimi nitaidhinisha likizo bila malipo kwa muda wa hata miaka miwili. Nadhani baada ya muda huo utakuwa umeshaona iwapo hiyo kampuni yako inaweza kukutimizia malengo yako au la, na hapo utaweza kufanya uamuzi muafaka, unasemaje?”
Ulikuwa ni ushauri mzuri, na Baddi aliafikiana nao. Isipokuwa miezi saba tu baada ya kuanza kwa hiyo likizo yake ya bila malipo, Meja
Jenerali Gaudence alimwita ofisini kwake pale makao makuu ya jeshi
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
jijini Dar.
“Nimepewa jukumu la kusimamia wapiganaji wetu waliokwenda kulinda amani nchini Sierra Leone, Kanali.” Alimwambia.
“Ah, huo ni wajibu mkubwa sana Meja Jenerali, na nakupongeza kwa hilo. Lakini ndiyo umeniita kuja kuniambia hilo?” Baddi alimjibu na kumtupia swali, akiwa katika nguo zake za kiraia.
“Hapana. Nataka ukanisaidie kule Sierra Leone Baddi. Waasi wanawasumbua sana wapiganaji wa Umoja wa Mataifa. Wanawazunguka katika kila kona, wana mawasiliano makali ambayo hayapenyeki. Hata haijulikani wanatumia mitambo gani!”
Baddi alimtazama kwa mshangao yule mkuu wake wa kazi wa zamani.
“Sasa…?”
“Najua iwapo kuna mtu anayeweza kupenya mitandao ya mawasiliano ya wale waasi kule Sierra Leone, basi mtu huyo ni wewe Baddi. Na hata jeshi letu la Umoja wa Mataifa linatambua hilo. Mambo uliyofanya Namibia, Ethiopia, Msumbiji na Angola yanajulikana Baddi. Nahitaji taaluma yako kule Sierra Leone.”
“Ah, afande! Lakini mi’ niko likizo bila malipo bwana. Itawezekana vipi?”
“Likizo inaweza kuvunjwa wakati wowote Baddi...”
“Kwa hiyo ndiyo kusema…?”
“No! Uamuzi ni wako Baddi. Hii operesheni haitazidi miezi mitatu. Mimi sitaivunja likizo yako. Nataka uende ukapenye mitandao ya mawasiliano ya wale waasi tu, Baddi, kisha baada ya hapo unarudi kuendelea na likizo yako. Lakini wakati huohuo utalipwa posho kamili sawa na wapiganaji wetu wengine kule Sierra Leone.”
Akiwa ndani ya ile teksi Baddi alitikisa kichwa kusitikishwa na kumbukumbu ile. Kwani ni baada ya majadiliano marefu na Meja Jenerali
Gaudence Amani siku ile, ndipo alipoondoka nchini kwenda Sierra Leone akiwa kama mshauri maalum wa mawasiliano, na wakati huo huo, huku nyumbani bado akiwa kwenye likizo bila malipo. Malipo ambayo angelipwa kwa ile kazi ya Sierra Leone yalikuwa ni mazuri na tofauti kabisa na mafao yake ya kustaafu jeshi pindi muda huo utakapofika.
Baddi alikubali kwenda Sierra Leone kwa makubaliano yale, ambacho hakuwa akikijua wakati ule ni kuwa Nathan Mwombeki alikuwa ni miongoni mwa wapiganaji wa kitanzania waliotangulia
MDUNGUAJI
huko muda mrefu.
Alikumbuka maneno ya mwisho aliyoongea na Meja Jenerali
Gaudence Amani kabla hajaondoka kwenda Sierra Leone.
“Afande, sasa hii ndiyo itakuwa kazi yangu ya mwisho jeshini. Nadhani nikirudi huko sitahitaji tena likizo bila malipo. Nitahitaji kustaafu.”
“Umri wako bado mdogo kustaafu jeshi Kanali. Lakini kama ndivyo utakavyo siwezi kukulazimisha, ila ujue utakuwa unalinyima msaada mkubwa sana jeshi la nchi yako.”
Sasa mbona hapa naambiwa kuwa yeye ndiye aliyestaafu kabla ya muda wake? Vipi hii?
Alikatisha mawazo yake na kuitupia jicho saa iliyokuwa mle ndani ya gari. Ilikuwa ni tatu na nusu za asubuhi. Bado saa nzima kabla
Swordfish hajaingia jijini. Alimuamuru dereva ampeleke hotelini kwake, ambako alikuta mlango wa chumbani kwao ukiwa umefungwa. Alibisha hodi huku akimwita Gilda.
Kimya.
Aliita tena huku akibisha hodi kwa nguvu zaidi, lakini bado ukimya ulitawala. Moyo ukaanza kumwenda mbio. Ni nini tena? Gilda kazidiwa humo ndani akapoteza fahamu? Au…?
Muda huo mhudumu wa pale mapokezi alimjia mbio na kumpa ufunguo.
“Samahani kaka. Yule dada ametoka...aliacha ufunguo pale mapokezi.”
“Ametoka? Ameenda wapi?” Baddi aliuliza huku akili ikimzunguka.
“Sijui. Hakuniambia!”
“Okay. Asante.”
Aliingia mle ndani kusimama ghafla huku akiachia mguno wa fadhaa. Kile chumba kilikuwa kimehamwa ghafla sana. Begi lake la safari aliloliacha ndani ya kabati la nguo sasa lilikuwa juu ya kitanda. Baadhi ya nguo zake ambazo zilikuwa ndani ya lile begi sasa zilikuwa zimetokeza nje kama kwamba kuna mtu alikuwa akitafuta kitu ndani ya begi lile, tena akitafuta kwa haraka sana.
“Oh, Mungu wangu hii nini sasa...!” Alijisemea huku akiliendea kabati la nguo na kulifungua. Begi la Gilda halikuwepo, naye alichanganyikiwa maradufu. Mishipa ya kichwa ilikuwa ikimpiga na alihisi nguvu zikimkauka. Aliketi kitandani akijaribu kujituliza ili angalau aweze kufikiri kwa kituo.
Shani ameolewa na Gaudence!
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Baba amefariki!
Gilda ndiyo lilikuwa kimbilio lake pekee kwa muda ule. Gilda ambaye alipata naye taabu na misukosuko mingi sana katika nchi ngeni na ambaye upendo wake hakuwa na shaka nao kabisa.
Sasa tena naye hayupo!
Kaenda wapi? Na kwa nini aondoke kabla sijarudi wakati anajua kuwa aliniagiza kwenda kumtafutia rafiki yake wa muda mrefu? Kwanza Gilda ana hali kweli ya kuweza kutoka na kutembea siku ileile aliyotoka hospitali…?
Wazo la kuogofya lilipita kichwani mwake.
Au ametekwa na wale watu wabaya...?
Inawezekana kuwa wale watu wamegundua kuwa tupo hapa wakaja kumteka huyu binti? Wakamshurutisha aage pale hotelini kama kwamba hakukuwa na tatizo lolote?
Oh, My God!
Alikurupuka mbio hadi pale mapokezi.
“Dada...” Aliita na kubaki akitweta kwa muda, yule dada akimtazama kwa mashangao. “...yule dada niliyekuwa naye...ameondoka na nani?” Alimuuliza.
“Kwani vipi kaka, kuna tatizo...?” Mhudumu alimuuliza huku akimtazama kwa macho yaliyojaa mashaka.
“Nakuuliza swali. Yule dada niliyekuja naye leo asubuhi... ameondoka na nani?”
“Aliondoka peke yake…kwani vipi?”
“Una hakika binti...? Hakuwa ameongozana na mtu mwingine yeyote?” Baddi alizidi kusaili. Yule dada alimtazama kwa macho yaliyoonesha kuwa hakuwa akipenda kuendelea kuulizwa maswali namna lie, kisha akamwambia kwa utulivu wa kujilazimisha.
“Ndugu yangu, mimi nakwambia kuwa huyo dada ameondoka peke yake hapa. Amekuja na begi lake, akanikabidhi ufunguo, akaniambia kuwa ukija nikwambie kwamba yeye ametangulia kama mlivyoongea....”
“Whaaat...?”
“Ndivyo alivyoniambia! Nami nikajua wenyewe mlikuwa mmeshapanga kuwa yeye atangulie huko mlikokubaliana! Sasa tena unapokuja kuniuliza kama kwamba hakukuwa na mpango wa aina hiyo baina yenu mimi naanza kupata mashaka...!” Dada alimjibu kwa kirefu, tena sasa akionekana kuwa na wasi wasi mkubwa. Baddi alibaki akimkodolea macho.
MDUNGUAJI
Gilda kasema yeye anatangulia…? Anatangulia wapi sasa…?
Haikumuingia akilini.
“Kaka vipi...kakuibia nini...? Kwani si unamfahamu vizuri lakini, au...?” Dada alimuuliza akiwa makini sana sasa.
Oh, Shit...
“Ha...hapana...na…nadhani ni sawa tu...labda hakutukuelewana. Ilikuwa anisubiri tutoke pamoja, sasa yeye naona alielewa vibaya. Si kitu...ahsante na samahani kwa usumbufu.” Alijitutumua kumjibu, kisha akageuza na kurudi kule chumbani akiwa amevurugikiwa vibaya sana.
Aliketi kitandani akitafakari mambo yote ya siku ile na hakika alijiona kuwa sasa alikuwa anaelekea kupata wazimu. Alilisogeza pembeni begi lake lililokuwa pale kitandani ili ajilaze kidogo, ndipo aliposikia mchakacho wa karatasi ikiwa inafinyangwa na msukumo wa begi lile. Ilikuwa ni karatasi iliyokunjwa mara moja na kuwekwa chini ya lile begi lililokuwa pale kitandani. Aliichukua kwa pupa na kuikunjua. Ilikuwa ni barua ndefu kutoka kwa Gilda. Barua ambayo iligongelea msumari wa mwisho katika madhila yake ya siku ile.
Mpenzi Baddi, Samahani sana kwa huu uamuzi niliochukua. Pia nakupa pole iwapo uamuzi wangu utakuumiza na kukukwaza kama jinsi unavyoniumiza na kunikwaza mimi. Ila naomba uelewe kuwa kwa hali ilivyo, huu ni uamuzi bora na wa busara zaidi kwetu sote. Baddi mimi nimeamua kuondoka na naomba sana usinitafute.
Nilipokutuma uende kule Namanga nilitaka tu unipe nafasi kwani najua kuwa usingekubali niondoke. Na najua usingeniruhusu kwa kuwa nawe unanipenda Baddi. Lakini pia kuna mwenzangu ambaye naye bila shaka anakupenda vile vile na anakupenda kwa haki iliyo halali kabisa kwake.
Sijui iwapo lile duka bado lipo, lakini hata kama bado lipo mmiliki wake wala si huyo niliyekutajia. Hakuna kabisa mtu aitwaye Mademoiselle Rachelle Baddi, hivyo usihangaike kabisa kumtafuta kwa matumaini ya kunipata mimi. Nimechukua uamuzi huu ili nikuachie nafasi ya wewe kuendelea kuwa na mkeo mliyetengana kwa miaka mingi bila ya yeyote kati yenu kutaka wala kutarajia.
Hakika kwa muda tuliokuwa pamoja nimeondokea kukupenda sana, na
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
inaniuma moyoni kuwa siwezi kuwa na wewe kama ambavyo ningetaka kwa
kuwa wewe tayari ni mume wa mtu. Kuendeleza uhusiano baina yetu ni sawa na kujenga msingi wa kuvunja ndoa yako makusudi, jambo ambalo siwezi kujisamehe maishani iwapo litatokea. Hivyo nimeamua kuondoka na nakuomba sana, tena sana Baddi, usijaribu kabisa kunitafuta kwani ukifanya hivyo utakuwa hunitendei haki kabisa.
Najua kuwa sasa hivi una matatizio mengi na najua kuwa unajua kwamba nisingesita kuwa nawe kwenye misukosuko hii yote mpaka mwisho. Lakini sasa kwa kuwa tayari umeshaonana na mkeo, nikiendelea kuwepo, nitakuwa nakuingiza kwenye msukosuko na vita kubwa kuliko hii iliyopo hivi sasa. Vita vya mapenzi ni vibaya sana Baddi.
Baddi, sijui ni kwa nini hao watu wanakutafuta kwa nia mbaya namna hii, na ningekuwa tayari kuwa nawe mpaka mwisho, lakini naamini kuwa wewe ni mpiganaji mahiri na jasiri, hivyo utaishinda tu vita hiyo.
Nimebaki na kumbukumbu ya penzi tulilopeana Liberia na naamini kuwa nitabaki na kumbukumbu hii daima moyoni na akilini mwangu. Hilo tu ni tosha sana kwangu.
Baddi, mimi najua msimamo wako juu ya almasi za damu zilizosababisha vifo vingi huko Liberia na Sierra Leone, lakini pia najua kufikia sasa, unajua kuwa ni hizo hizo almasi za damu ndizo zilizotufanya tuishi kule ugenini na ndizo zilizotuwezesha kugharamia safari yetu kurudi hapa nyumbani. Kwa hiyo utakapofungua begi lako na kukuta ujumbe mwingine zaidi ya huu niliokuandikia hapa usishangae.
Naamini kuwa una haki ya kupata sehemu ya ujumbe huo, kwani bila wewe mimi nisingekuwa hapa nchini leo hii. Wewe una haki ya kufanya chochote na ujumbe huo, lakini naamini kuwa hutachukua uamuzi wa kijinga juu ya ujumbe huo Baddi. Kwa heri na kila heri mpenzi.
Akupendaye daima, Gilda Shehoza.
Nguvu zilimwisha. Aliinuka kutoka pale kitandani, lakini alijikuta akikaa tena, miguu yake ikimsaliti. Shujaa Baddi Gobbos aliangua kilio kikubwa. Alilia kwa fadhaa zaidi kuliko uchungu. Alifadhaika kutokana na matukio yale ya kukatisha tamaa yaliyomuandama mfululizo.
“Oh, Gilda…kwa nini umechukua uamuzi wa haraka namna hiyo
MDUNGUAJI
lakini?” Alilalama peke yake mle ndani. Alisikitika pasina kifani. Alibaki akilia kimya kimya, sasa akijumuisha msiba wa kifo cha baba yake katika kilio kile.
Hakika alijihisi kuwa amesalitika kweli kweli.
Kwa nini inakuwa hivi? Yaani laiti Gilda angefanya subira japo kidogo tu angejua juu ya mambo yaliyotokea baina yangu na aliyekuwa mke wangu Shani....lakini naye kwa sababu ambazo ameziona za msingi kwake, na si kwangu, ameamua kuondoka na kupotelea kusipojulikana!
“Eti nisimtafute na wala nisijaribu kumtafuta! Na nitaanzia wapi kumtafuta?” Alisema peke yake. Yaani Gilda amekuja maishani mwangu kama malaika wa ukombozi wakati nikiwa kwenye kizingiti cha umauti katika nchi ngeni. Yeye akanivutia upande wa uhai na kuniweka mbali na umauti. Tukapambana na vikwazo vya kila aina huko ugenini hadi tukafanikiwa kurejea hapa nchini. Tena tukapambana na maadui wengine hata alifikia hatua ya kujiingiza katikati ya matatizo yangu na kuchomwa kisu kilichokuwa kimenikusudia mimi...yote haya kwake hayakuwa tatizo...lakini suala la mimi kukutana tena na mke wangu...
Baddi alisonya kwa hasira.
...suala la mimi kukutana tena na Shani limekuwa ni zito sana kwake kiasi akaamua kuondoka na kuniacha namna hii? Eti mwenyewe akiamini kuwa anaokoa ndoa yangu!
“Ndoa gani Gilda, eeenh? ndoa gani...???” Alipiga kelele peke yake mle chumbani na kujiinamia akibubujikwa na machozi kama mtoto. Hakuwa na ndoa tena. Mke wake ameenda kuolewa na mkuu wake wa kazi wa zamani, mkuu ambaye hakuwa amewahi kuonesha haja ya kuwa na mke kwa miaka yote aliyojuana naye mpaka pale alipothibitika kuwa yeye amekufa, ndipo alipopata wahka wa kuwa na mke...na mke huyo asiwe mwingine isipokuwa Shani, mke wake yeye.
“Ni wazi kabisa kuwa Meja Jenerali Gaudence alitaka zile pesa za mafao alizopewa Shani kutoka na “kifo” changu...” Alijisemea.
“Lakini Shani naye pamoja na usomi na ujanja wake wote ameshindwa kuliona hilo...?”
Haikumuingia akilini.
Au walikuwa na uhusiano wa siri tangu hapo awali?
Moyo ulimuingia baridi.
Inawezekana...?
Alikumbuka miaka ile alipokuwa akienda kwenye kampeni za kijeshi
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
nje ya nchi, akimuacha mkewe hapa nchini. Meja Jenerali Gaudence Amani alikuwa akibaki nchini siku zote.
Je, kuna kitu kilichokuwa kikiendelea bila ya yeye, Baddi Gobbos, kujua…?
Alikuwa amefikishwa katika ukingo kabisa wa uvumilivu na sasa alikuwa anaelekea kuporomoka kwenye korongo la mfadhaiko wa mapenzi na kusalitika. Mawazo yalikuwa yakiruka kutoka kwenye usaliti mmoja kwenda mwingine.
Sasa na Gilda naye...
Aliisoma tena ile sehemu ya mwisho ya barua ile.
…Kwa hiyo utakapofungua begi lako na kukuta ujumbe mwingine zaidi ya huu niliokuandikia hapa usishangae….
Anamaanisha nini? Aliinuka na kulifungua begi lake kwa pupa, akitupa nguo zake huku na huko, na kubaki akiwa mdomo wazi. Chini kabisa ya lile begi aliona ujumbe mwingine kutoka kwa Gilda, na alipouona tu, kabla hata hajaufungua, alijua ni nini maana ya ujumbe ule. Kilikuwa ni kifurushi kidogo cha karatasi kilichofinyangwa katika umbo la mviringo.
“ Oh, No... Gilda...”
Alikichukua kile kifurushi na kukifungua, kisha akashusha pumzi ndefu na kutikisa kichwa kwa kutoamini. Almasi!
Almasi za damu.
Aliketi tena pale kitandani na kujiinamia, kile kifurushi cha almasi kikiwa juu ya mapaja yake. Ilikuwa kama kwamba akili yake imesimama kufanya kazi kwa muda, na alibaki katika hali ile kwa muda mrefu, akibubujikwa machozi...
Hakujua alikaa vile kwa muda gani, ila alipoinua tena uso wake saa ya ukutani ilimwambia kuwa muda ulikuwa ni saa nne na dakika kumi na tano za asubuhi.
Swordfish!
Hakutaka kuendelea kukaa pale akiijutia bahati yake mbaya. Alishasikitika na kulia vya kutosha. Gilda kaondoka, na badala yake kaniachia hizi almasi.
Hivi hajui kama ningetakiwa kuchagua baina yake na hizi almasi ningemchagua yeye? Alisonya.
“No Sweat...!” Alijisemea huku akiinuka kutoka pale kitandani na kuelekea bafuni ambako alinawa uso na kujiweka sawa. Sasa Baddi Gobbos alikuwa ni mtu mwenye hasira sana.
MDUNGUAJI
“
Okay , Baddi...muda wa kuendelea kujutia madhila yako sasa umefikia kikomo...na muda wa kuanza kuyapatia ufumbuzi madhila hayo umeanza...”
Alijisemea huku akizihifadhi zile almasi na kutoka mle chumbani.
Alipoingia hoteli ya Al-Uruba na kumuulizia Meja Abdul-Hameed Babu aliambiwa kuwa ameshafika. Aliongea naye kwa simu akiwa pale pale mapokezi.
“Habari Meja...nipo hapa mapokezi.” Alimwambia.
“Ah...Va...vampire! Karibu...njoo tu huku chumbani kwangu! Niko namba 201...” Meja Babu alisema. Baddi alipanda ngazi hadi ghorofa ya pili ambako alikwenda hadi chumba namba 201. Alibisha hodi na aliposikia sauti ya Meja Babu ikimkaribisha alisukuma mlango na kuingia mle ndani. La Haula!
“Hallo Baddi Gobbos…au niseme Vampire? Anyway, pita ndani kwa upole zaidi!” Mtu mfupi aliyemuona kule makao makuu ya jeshi alimwambia, akiwa amesimama nyuma ya kiti alichokalia Meja Babu, huku amemuwekea bastola kichwani.
“Swordfish…!” Baddi alimaka kwa mshituko, akili ikimtembea.
“Oh, Vampire…I am sorry partner…jamaa wamenishtukiza vibaya sana…!” Meja Babu alisema kwa uchungu, uso wake ukiwa umevimba kwa kipigo, mdomo wake ukiwa umetutumka upande mmoja, mikono yake ikiwa imefungwa kwa nyuma ya mgongo wa kile kiti alichokuwa amekalia.
Baddi alipigwa bumbuwazi. Muda huo mtu mwingine aliyekuwa kando ya ule mlango alimsukumia ndani na hapohapo akaufunga ule mlango.
“Taratibu sana Baddi…usijitie machinoo kabisa hapo, ama sivyo tunapasua bichwa la shoga’ako hapa sasa hivi!” Mtu mfupi alimkemea.
Baddi alimtupia jicho la ghadhabu. “Wewe ni nani lakini….na…unataka nini kwangu?” Hapohapo yule jamaa aliyekuwa nyuma yake alimpiga teke nyuma ya goti naye akaenda chini bila kupenda.
“Kelele wewe!” Yule jamaa alimkoromea na kumuwekea bastola kisogoni huku akiwa amemkwida ukosi wa shati lake kutokea nyuma.
“Hapa kuna mgawanyo wa kazi Baddi…na katika mgawanyo huu ni
MDUNGUAJI
kwamba mimi ndiye muulizaji maswali, nawe utakuwa unatoa majibu…kuuliza maswali sio sehemu ya job description yako kabisa!” Mtu mfupi alimwambia kwa kebehi. Baddi alimtazama Meja Babu, na pamoja na mazingira yale mazito aliyokuwamo, hakukosa kuona kuwa mwenzake sasa alikuwa amepoteza jicho moja.
“Ah, Swordfish…pole san…”
“Kelele!” Jamaa aliyekuwa nyuma yake alimkemea huku akimpiga kwa mdomo wa ile bastola kichwani.
“Utajuta sana kwa hili ulifanyalo hivi sasa wewe!” Baddi alimwambia yule mtu mfupi kwa hasira.
“Mi’ nadhani ni wewe ndiye utakayejuta pindi tukikufikisha tunapotaka, fisi we!” Mtu mfupi alimjibu.
“Na ni wapi hapo?”
“Hapa si mahala pake…tutatoka pamoja kwa utulivu na upole zaidi Baddi!” Mtu mfupi alimwambia huku akimtazama kwa makini, macho yake madogo na mekundu yakionesha kuwa alikuwa hatanii kabisa, kisha akaendelea; “… na ninaposema kwa upole namaanisha kwa upole kweli kweli! Usijitie ujanja wala ushujaa wowote ambao hauna manufaa hapa! Ulifanikiwa mara moja sasa usidhani kuwa utafanikiwa mara ya pili…”
“Na mnadhani tukitoka hapa tutakuwa tunaelekea wapi?” Baddi aliuliza, bado akiwa amepiga goti moja pale chini na akiwa ameshikwa ukosi na yule mvamizi mwingine. Akilini mwake alikuwa anapiga hesabu namna ya kuwasambaratisha wale watu.
“Tutaenda tunapotaka sisi…ambako tutaongea kwa kituo zaidi.” Cha ufupi alimjibu.
“Sasa itabidi mumuachie rafiki yangu aende kwanza ndipo nami nitaongozana nanyi…nyie si mnanitaka mimi? Basi muachieni swordfish aendelee na hamsini zak…”
Alipokea kipigo kingine cha kichwa kwa mdomo wa bastola kutoka kwa yule jamaa aliyemkwida ukosi. “Huna mamlaka ya kutoa masharti hapa wewe!”
Baddi aligumia kwa maumivu na kuachia tusi zito la nguoni kwa ghadhabu.
“Basi mi’ sitoki hata kidogo humu ndani, fanyeni mtakalo…”
“No Baddi…” Swordfish alimwambia kwa sauti ya chini, kisha akaendelea, “…usibishane nao bwana…”
“Unaona mawazo ya wenye busara hayo?” Cha ufupi alidakia.
“Hakuna! Mi’ siendi nanyi popote mpaka mumuachie Swordfish kwanza…”
Baddi alishikilia msimamo wake.
“No Baddi! Hii ni sehemu ya ile operesheni yetu ya kule Sierra Leone bwana, huoni?” Swordfish alimwambia kwa ukali huku akiwa amemkazia lile jicho lake moja lililobakia.
“Whaa…at…?”
“Unaongea nini wewe?” Mtu mfupi alimuuliza Swordfish kwa mashaka, lakini Swordfish alikuwa amemkazia jicho Baddi.
“Sierra Leone Baddi…umesahau ile operesheni yetu? Ilikuwa ikiitwaje?”
Swordfish alizidi kumuuliza huku akimkazia jicho. Baddi alichanganyikiwa. Hakujua ni nini mwenzake alikuwa akisema na wala hakuona uhusiano wowote kati ya yale aliyokuwa akiyasema na hali ile waliyokuwamo muda ule.
“Eeenh…? Umesahau…Iliitwaje?” Swordfish alizidi kumuuliza. Hapohapo mtu mfupi alimpiga kofi la kisogoni.
“Hebu acha kutuchanganya wewe!” Alimkemea. Swordfish hakulijali lile kofi, badala yake alizidi kumkazia jicho Baddi.
“Operesheni Rebel Cleanse Sierra Leone….?” Baddi alisema kwa mshangao na kutoelewa, na wale jamaa wawili nao walikuwa wamepigwa bumbuwazi.
“Yeah, ndiyo hivyo…kama ilivyokuwa kule, ndivyo ilivyo hapa…”
Swordfish alisema huku akimtazama kwa lile jicho lake kali.
Walitazamana.
“Hebu msituletee ujinga-ujinga wenu hapa! Tunatoka nanyi taratibu hadi nje na hakuna atakayeleta ujuvi baina yenu, kwani yeyote atakayejitia ujuvi tu haki ya mungu namuwasha on the spot!” Mtu mfupi alisema kwa hasira.
“Simama!” Yule jamaa mwingine aliamrisha, na mara moja meja mstaafu Abdul-Hameed Babu alisimama kutoka pale kwenye kiti. Alipepesuka kidogo na kusimama wima, mikono yake ikiwa imefungwa kwa nyuma.
“Nenda kamnawishe uso mwenzako hapo bafuni!” Baddi aliamriwa, na wakati akijivuta kutekeleza amri ile huku kichwa kikimzunguka, mtu mfupi alimwambia. “…uwe mtaratibu sana Baddi, ukileta ujanja kweli nawawasha nyote hapo hapo!”
Baddi hakujibu. Alianza kumnawisha Swordfish kwenye beseni maalum la kunawia lililokuwa bafuni mle ndani huku wale watu wawili wakiwa wamewaelekezea bastola hatua chache nyuma yao.
Dakika tano baadaye wote wanne walitoka nje ya hoteli ile. Baddi alitangulizwa mbele akiwa ameshikwa mkono na yule mtu mfupi ilihali mdomo wa bastola ukiwa umedidimizwa kwa nguvu ubavuni kwake, bastola ambayo ilikuwa imefichwa ndani ya mfuko wa koti alilovaa mtu yule.
Meja Babu naye alikuwa akifuatia nyuma akiongozwa kwa mtindo ule ule
MDUNGUAJI na yule kibaraka wa yule mtu mfupi.
Walielekezwa kuingia ndani ya gari moja kubwa aina ya Toyota Prado lenye vioo vilivyopigwa weusi mzito, yaani tinted. Ndani ya lile gari kulikuwa kuna watu wengine wawili pamoja na dereva.
Waliwekwa katikati ya watu wawili kwenye kiti kirefu cha nyuma, na muda walipoketi tu, kila mmoja alihisi mdomo wa bastola ukididimia ubavuni mwake.
Walikuwa wamenaswa.
Mtu mfupi alipita mbele na kuketi kwenye kiti kilichokuwa kando ya dereva, ilhali yule mwenzake aliingia kwa kutumia mlango wa nyuma kabisa wa lile gari na kuketi kwenye moja ya viti vidogo kule nyuma. Taratibu lile gari liliondoka eneo lile, wale wapiganaji wawili jasiri wakiwa mateka ndani yake.
Kutoka upande wa pili wa barabara yule mtu mrefu aliyemshuhudia Baddi akiwatoka wale wavamizi pale nje ya makao makuu ya jeshi siku iliyopita, alikuwa akiangalia kila kilichokuwa kikitokea eneo lile kutokea kwenye gari dogo aina ya Toyota Corolla. Alibaki katika hali ile kwa muda baada ya ile Prado kuondoka, kisha akaachia tabasamu dogo na kuliondoa gari lake kutoka eneo lile…
Ndani ya Prado Baddi Gobbos alikuwa amezongwa na mawazo mazito juu ya ile kauli ya Swordfish.
...umesahau ile operesheni yetu...? Kama ilivyokuwa kule, ndivyo ilivyo hapa...
Alimaanisha nini huyu? Ile ilikuwa Sierra Leone, hapa tupo Tanzania, na hakuna operesheni yoyote ifananayo na ile ya kule Sierra Leone! Ile ilikuwa Operation Rebel Cleanse Sierra Leone…Operesheni safisha waasi Sierra Leone!
Alitaka aendelee kumsaili juu ya kauli ile lakini mazingira hayakuruhusu.
Alijua kuwa Swordfish ni mpiganaji mzuri sana…hawa jamaa wamewezaje
kumnasa mapema hivi? Hakuweza kupata jibu muda ule, lakini bado imani yake kwa rafiki yake yule ilikuwa pale pale. Ile kauli ya Swordfish iliirudisha akili yake kwenye ile kampeni yao kule Sierra Leone.
All for one, One for all, .
Au ndicho alichomaanisha? Kwamba wote kwa ajili ya mmoja na mmoja kwa ajili ya wote? Kwamba kutokana na kanuni ile ndiyo maana ilibidi
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
wawe pamoja katika matatizo yale kinyume na jinsi yeye alivyowataka wale wavamizi wamuachie Swordfish?
Ilileta maana kidogo.
Kidogo.
Bado kuna namna ya jinsi Swordfish alivyomkazia jicho iliyomfanya ahisi kuwa ile kauli ilikuwa na maana zaidi ya ile aliyojaribu kuielewa. Alizungusha jicho na kumtazama Swordfish. Yule Mzanzibari alikuwa amelaza kidevu chake kifuani kwake akiwa amejiinamia.
Aligeuza uso wake na kutazama nje ya gari na kuona kuwa sasa walikuwa wakienda kwa kasi sana, hivyo hakuweza kuikariri vizuri mitaa waliyokuwa wanaikatisha muda ule. Alizungusha macho yake mle ndani ya gari.
Kutokea pale alipokuwa alikuwa na uwezo wa kumsambaratisha yule jamaa aliyekuwa ubavuni kwake, na kumvunja shingo yule mbegu fupi aliyekuwa mbele yake kwa kumbana kichwa na kukivutia nyuma kwa nguvu. Tatizo hakujua iwapo Swordfish angekuwa tayari kumsambaratisha yule jamaa aliyekuwa kule kwake na yule mjinga mwingine aliyekuwa nyuma yao. Alimzungushia tena jicho Swordfish, na kuona kuwa bado alikuwa amejiinamia vile vile.
Swordfish hakuonesha nia ya kuanzisha mpambano wowote!
Lakini hata hivyo, alifikiria kuwa hata kama wangeamua kuanzisha vurumai ya kujiokoa katika hali ile, bado kulikuwa kuna nafasi kubwa ya wao wenyewe kuumia vibaya au hata kufa katika kufanya hivyo kwani ambacho
kingefuata kingekuwa ni ajali mbaya ya gari.
Aliamua kutulia kama Swordfish.
Baada ya mwendo mrefu gari lilisimama mbele ya geti la uzio mmoja mkubwa. Ndani ya uzio ule kulikuwa kuna jumba kubwa ambalo bado lilikuwa likiendelezwa ki-ujenzi, likiwa limesimama ghorofa mbili kwenda juu.
Baada kupigwa honi mara mbili geti lilifunguliwa na mlinzi mmoja wa kimasai na gari liliingia ndani ya uzio ule. Sasa Baddi na Swordfish walikuwa makini sana kutazama pale mahala walipofikishwa.
Sehemu ya chini ya jengo lile kulikuwa kuna lango jingine la chuma ambalo moja kwa moja lilijidhihirisha kuwa ni la kuingilia kwenye gereji ya kuhifadhia magari. Lango la pili nalo lilifunguliwa na gari likaingia ndani. Kinyume na matarajio yao kuwa ile sehemu ilikuwa ni gereji, Vampire na Swordfish walishuhudia lile gari likiendelea na safari kwa umbali mfupi mle ndani, likifuata ujia mwembamba uliosakafiwa kwa zege ambao ulikuwa ukishuka chini ya jumba lile.
MDUNGUAJI
Gari lilisimama kwenye uwanja mdogo wa maegesho ya magari uliokuwa chini kabisa ya jumba lile. Mbegu fupi aliteremka haraka na kusimama hatua
kadhaa kutoka kwenye lile gari na kuwanyooshea bastola.
“Kwa upole zaidi, Baddi…kwa upole zaidi!” Aliamuru huku akiwaashiria kwa ile bastola yake kuwa watelemke. Muda huo yule jamaa aliyekuwa nyuma ya lile gari naye alikuwa ameshateremka na alikuwa amewaelekezea bastola.
Wale jamaa waliokuwa wamewaweka kati nao waliteremka kwa mtindo ule ule huku wakiwa wamewaelekezea bastola.
Swordfish alitokea upande wa kulia wa lile gari na Baddi akatokea upande wa kushoto, muda wote wale watekaji wao wakiwa wamewaelekezea bastola. Baddi alitembeza macho mle ndani na kuona kuwa eneo lote lilikuwa liking’aa kwa taa kubwa za mianzi. Kwenye kona moja ya eneo lile kulikuwa kuna ngazi fupi zilizoishia kwenye mlango ambao ulikuwa umejengewa geti la chuma.
Mara moja Baddi alimaizi kuwa ule mlango ndiyo uliokuwa ukielekea
kwenye gorofa ya chini ya jengo lile, kwani hakuwa na shaka kabisa kuwa pale walipokuwa ni chini ya ardhi. Katikati ya eneo lile kulikuwa kuna viti viwili vya mbao vilivyokuwa vikiangazwa na mwanga mkali wa taa.
“Kaa kwenye viti hapo…upesi!” Mbegu fupi aliwaamuru.
Baddi alimtazama kwa kiburi. “Mnhu! Inaelekea mlikuwa mmejiandaa sana kwa siku hii, sivyo?” Alimuuliza kwa hasira.
“Hebu fanya uambiwavyo huko!” Cha ufupi p.a.k. mbegu fupi alimkaripia.
Baddi na Swordfish waliketi kwenye vile viti na muda huohuo wale jamaa wawili waliokuwa wamewaweka kati kule kwenye gari waliwaendea na kuanza kuwafunga kwenye vile viti kwa kamba za nailoni walizotoa kwenye mifuko ya makoti yao.
“Yaani pamoja na mabastola yenu bado hamjiamini mpaka mtufunge kwa kamba? Ama kweli nyie mnatuogopa!” Baddi aliwaambia, na hapohapo yule jamaa aliyekuwa kule nyuma ya lile gari wakati wakitoka kule hotelini alimtandika kofi kali la uso.
“Hebu nyamaza wewe! Ebbo!” Alimkemea.
Baddi alisukumwa nyuma pamoja na kiti chake kwa kichapo kile, na yule mtu aliyekuwa akimfunga kamba kwenye kile kiti alimdaka na kumzuia asianguke chini. Mguno wa maumivu ulimtoka Baddi, nyota zikitambaa mbele ya macho yake.
“Halafu we’ n’lishakwambia kuwa utajuta sana kwa tabia yako hiyo, lakini huamini…! We’ subiri tu!” Baddi alimwambia kwa hasira.
“Alaa…? Basi ngoja…” Jamaa alimjibu kwa jeuri huku akimsogelea tena,
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
lakini hapo Cha ufupi alifoka.
“Waccha!”
Jamaa akatulia akimtumbulia macho yule mtu mfupi, ambaye sasa alikuwa akimtazama Baddi kwa kejeli. Muda wote huu Swordfish alikuwa akitazama kila kilichokuwa kikitokea mle ndani akiwa kimya kabisa.
“Baddi Gobbos!” Cha ufupi aliita kwa kejeli nzito, na Baddi akamgeukia, “…hivi kweli uliamini kuwa tumekuleta huku mafichoni ili tuongee tu?” Jamaa alimuuliza, na Baddi akamshangaa. Lakini kabla hajauliza maana ya kauli ile, kilisikika kishindo kutoka kona moja ya ukumbi ule, na wote waligeukia kule kwenye zile ngazi fupi zilizoishia kwenye mlango wa chuma. Ule mlango wa chuma ulisukumwa kutokea ndani ya jengo lile na mtu mmoja mrefu na mnene ambaye hajapata kumuona hata siku moja alitokeza pale ukumbini.
Hapohapo aliona sura ya yule mtu mfupi ikiingiwa mshangao mkubwa na macho yakimtembea kwa kukosa maamuzi. Baddi na Swordfish walizidisha udadisi. Yule mtu mnene mrefu alikuwa amesimama kwenye ngazi ya mwisho akiwa amefumbata mikono yake kifuani, akitazama kilichokuwa kikiendelea pale ndani.
“Akh! Huyu kajia nini tena huku?” Mbegu fupi alisema kwa sauti ya chini iliyosikika wazi wazi na akina Baddi, kisha akamfuata yule mtu mrefu kwa mwendo wa haraka. Baddi na Swordfish walitazamana, kisha wakageuka
kutazama kilichokuwa kikendelea baina ya mbegu fupi na yule mtu mnene.
Sasa mbegu fupi alikuwa akiongea na yule mtu mkubwa kwa sauti ya chini, lakini ilikuwa wazi kwamba alikuwa akipinga uwepo wa mtu yule eneo lile. Yule mtu naye alikuwa akimsisitizia jambo mbegu fupi. Walibishana kwa muda, sauti zao zikiwafikia akina Swordfish, ingawa hawakuweza kunasa maneno waliyokuwa wakiyatamka. Kisha mtu mfupi alirudi pale kwa akina Baddi akiwa amehamanika, ile jeuri yake ya awali ikiwa imeyeyuka. Alimtazama Baddi kwa muda, wazi kabisa alikuwa hajui aseme nini, na Baddi alizidi kuishangaa hali ile.
Yule mtu mnene ni nani? Anaweza kuwa ndiyo kiongozi wa hawa watu? Kama ndivyo, kwa nini mbegu fupi amebadilika baada ya ujio wake?
“Okay Baddi, sasa tunaweza kuongea kwa kituo.” Hatimaye Cha ufupi alimwambia kwa sauti huku akimtazama kwa hasira. Alifyatua vidole vyake kwa kusugua kidole chake cha kati na kile cha gumba, na hapohapo mmoja wa wale vibaraka wake alimletea kiti kingine ambacho alikiweka mbele ya akina Baddi waliokuwa wamefungwa kwenye viti. Aliketi kwenye kile kiti na kukunja nne kwa viji-guu vyake vifupi na vinene, yule kibaraka
MDUNGUAJI
wake mkorofi alikuwa amesimama kando yake. Baddi alibaki alimtazama kwa ghadhabu. Hakuweza kuwaona wale vibaraka wengine wawili kwani walikuwa wamesimama nyuma ya kiti chake. Yule mtu mnene alikuwa amesimama vile vile kule ngazini.
“Hivi unataka nini kwangu lakini wewe? Na yule ni nani, eenh?” Alimuuliza huku akimuoneshea yule mtu mnene kwa kichwa. Mtu mfupi alimtazama kwa muda mrefu bila ya kusema neno.
“Almasi ziko wapi Baddi?” Hatimaye alimuuliza kwa sauti ya chini huku bado akimtazama kwa uso ulioficha hisia zote. Si hasira, si tabasamu, si kejeli.
E bwana we!
Baddi alibaki akimkodolea macho kwa mshangao na kutoamini, hali ambayo pia ilikuwa ikijionesha usoni kwa Meja Babu.
Almasi?
Yaani kumbe misukosuko yote hii ni kwa ajili ya almasi? Almasi gani haswa?
“Almasi…? Mbona sikuelewi? Almasi gani?” Hatimaye Baddi alimuuliza. Lilikuwa kosa.
Kwa wepesi wa ajabu mtu mfupi alikurupuka na kumshidilia teke kali sana la uso. Baddi alitupwa nyuma mzima mzima ilhali bado akiwa amefungwa kwenye kile kiti. Yowe la uchungu lilimtoka na damu iliruka kutoka kinywani kwake. Swordfish aliachia tusi zito la nguoni huku akijaribu kujiinua lakini mmoja wa wale wafuasi wa Mbegu Fupi aliyekuwa nyuma yake alimkandamiza
kitini kwa kudidimiza mdomo wa bastola kwenye upande wa shingo yake.
Baddi alibaki akigaagaa sakafuni kabla mfuasi mwingine wa yule mtu mfupi hajamuinua pamoja na kiti chake na kumuweka sawa.
Mtu mfupi tayari alikuwa ameshaketi kitini kwake kwa mtindo ule ule wa kukunja nne akimtazama kwa ule uso wake uliofuta hisia zote, kama kwamba si yeye aliyekurukupuka na kumtandika teke sekunde chache tu zilizopita. Jamaa alikuwa mwepesi kuliko jinsi umbo lake lilivyoashiria.
“Hapa tupo kwenye chumba cha chini ya ardhi Baddi, hakuna ukelele wowote utakaopiga ambao utasikika huko nje. Hata yule mmasai aliyetufungulia geti hapo juu hasikii chochote. Kwa hiyo ukijitia hamnazo ni bora ujiandae kupiga mayowe sana leo manaake tutakufanyia mambo mabaya sana ambayo hujawahi kukutana nayo maisha…!” Mtu mfupi alimwambia, kisha akamgeukia yule kibaraka wake mkorofi, “…au naongopa mzee?”
“Hiyo ni sahihi kabisa!” Jinga lilijibu huku likichekelea.
“Sasa nakuuliza kwa mara nyingine tena Baddi Gobbos.” Mtu mfupi alimwambia na kutulia kwa muda huku akimtazama kwa uso ule ule
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
uliofuta hisia, “...almasi zetu ziko wapi?”
“Almasi zenu?” Baddi alijikuta akiuliza tena kwa mshangao. Mtu mfupi alikurupuka na kumshindilia kisigino kwenye korodani, na pamoja na ujasiri wake wote Baddi Gobbos aliachia yowe kubwa sana huku akijikunja, kile kiti kikimfuata mpaka chini ambapo aliangukia uso na kubaki akiwa amepiga magoti pale chini.
“Ni almasi gani hizo ninyi...?” Swordfish alimfokea yule jamaa.
“Kelele wewe!” Kibaraka wa mtu mfupi alimkemea huku kwa mara nyingine Baddi akiinuliwa mzima mzima na kuketishwa tena pale kwenye kiti. Alijikuta akitazamana na yule mtu mfupi aliyekuwa ameketi tena kwenye kiti chake ilhali akiwa amekunja nne na akimtazama kwa uso mkavu.
Lakini safari hii Baddi Gobbos aliona kitu kipya mkononi kwa yule mtu mfupi na moyo ukamsinyaa kwa muda, kisha ukaanza kumpiga kwa nguvu. Mtu mfupi alikuwa ameshika kifaa maalum cha kutobolea matundu kwenye kuta za nyumba au hata vyuma, ambacho hutumika sana na mafundi wa ujenzi. Aliukodolea macho msumari mrefu wenye ncha kali uliotokeza mbele ya kifaa kile. Kwa mara ya kwanza alianza kupata picha halisi ni watu gani haswa alikuwa akikabiliana nao. Alimtazama yule mtu mfupi kwa jicho lililojaa hasira na woga, akiuma meno ili kuzuia midomo isimtetemeke.
“Hii drill ina uwezo wa kutoboa ukuta wa zege kwa ufanisi mkubwa ndani ya muda mfupi sana Baddi....” Cha Ufupi alimwambia, kisha akabaki kimya kwa muda huku akimtazama, safari hii uso wake ukionesha hasira ya dhahiri, “...sitasita kutoboa sehemu yoyote ya mwili wako kwa drill hii iwapo utaendelea kujitia hamnazo, na nadhani nitaanza kwa kutengeneza tundu kwenye hilo goti lako!” Aliinyooshea ile drill kwenye goti la kulia la Baddi.
“Mimi sijui ni nini hasa mnachoongelea ndugu zangu! Sina tabia ya kupenda-penda almasi kama nyie, hivyo kama ningejua hizo almasi zenu zilipo ningewaambia tu!” Baddi alimjibu.
“Yaani matatizo yote haya ni kwa ajili ya almasi za kufikirika tu yakhe?” Swordfish alidakia kwa hasira. Mtu mfupi aliruka na kumzaba kofi kali, kisha haraka sana akarudi tena pale kwenye kiti chake na kuketi, kama si yeye aliyekuwa wima muda mfupi tu uliopita. Jamaa alikuwa anapenda sana kuonesha wepesi wake na alikuwa akifanya hivyo kwa mbwembwe za hali ya juu.
“Tena wewe ndiyo unyamaze kabisa yahe! Nisije nikakuchimbua hilo jicho lako lililobaki ukazikwa kipofu. Kaa kimya!” Cha Ufupi alimkemea Swordfish.
“Ni nani aliyewaambia kuwa mi’ n’na almasi zenu...? Na kama ni zenu,
MDUNGUAJI zimefikaje mikononi mwangu?” Baddi alimtupia swali yule mtu mfupi. Jamaa alimtazama kwa muda, kisha akamgeukia yule kibaraka wake mkorofi.
“Mista Baddi Gobbos bado anajitia haelewi...anaamini kuwa anaweza kutucheza shere kirahisi na kubaki na almasi zetu. Hebu mlegeze kidogo kabla sijaendelea kuongea naye kwa kituo...”
Kuambiwa hivyo yule jamaa alimsogelea Baddi taratibu huku akiwa ameachia tabasamu baya sana usoni mwake. Baddi alibaki akimtazama kwa kiburi. Jamaa alimtandika ngumi nzito ya uso. Baddi aliguna na kuyumba pale kwenye kiti, kisha akapewa ngumi nyingine kwa upande mwingine wa uso, na nyingine na nyingine. Alihisi maumivu makubwa na alielekea kushindwa kuvumilia. Jamaa alirudi nyuma hatua kadhaa na kumrukia teke la kubabatiza kifuani. Alitupwa nyuma na kiti chake, yowe kubwa likimtoka. Meja Babu alipiga kelele za kulaani kitendo kile, na hapohapo yule jamaa alimgeukia kwa teke kali la kichwa lililompeleka na yeye moja kwa moja mpaka chini.
“Inatosha!” Mbegu Fupi alibwata na jamaa alirudi nyuma na kusimama akiwa ameweka mikono yake nyuma. Alibaki akiwatazama wale mateka wao wakiinuliwa huku wakitweta, uso wake ukionesha kuwa hakuwa ametosheka na kipigo alichotoa.
Mtu mfupi alimsogelea Baddi na kupiga goti mbele yake, akimuwekea ncha ya ile mashine ya kutobolea kuta gotini. Baddi alimeza funda la mate na kuteremsha macho yake kwenye ile mashine, akijitahidi kutokwepesha goti lake.
“Nitakuuliza kwa mara nyingine moja tu Baddi...”
“Hebu acha upumbavu wewe!” Baddi alimkatisha kwa ghadhabu.
“Whaat...
“Nimeshakwambia kuwa sina almasi! Hebu niambie ni jinsi gani unadhani kuwa hizo almasi zenu zilifika mikononi mwangu, kwani sina kumbukumbu kabisa ya kukabidhiwa almasi na yeyote kati yenu ...kwanza mi’ ndiyo kwanza naingia nchini...wala sija...”
“Sierra Leone Baddi! Ulichukua almasi zetu kule Sierra Leone wewe, usitake kujitia ujuaji hapa!”
Duh! Hii kali!
“Whaat?” Ilikuwa ni zamu ya Baddi kupiga mshangao.
“Sierra...?” Swordfish naye alimaka kwa butwaa. Muda huo simu ya Mtu Mfupi iliita naye aliinuka na kwenda kuongea na simu ile pembeni.
“Ndiyo boss, tunao wote wawili hapa...”
Baddi alisikiliza kwa makini.
“Ndiyo...” Mtu mfupi alizidi kuongea na ile simu.
“Ah, bado...lakini kila kitu kitakuwa sawa....kuna jambo kidogo limejitokeza, lakini leo tunamaliza kazi, hilo nakuahidi!”
Alisikiliza maelekezo kwa muda, Baddi akifuatilia maongezi yake kwa makini. Hapo yule jamaa alikata simu na bila kuitoa ile simu sikioni kwake akasema, “Okay, don’t worry, leo tutapata almasi zetu!” Akarudisha simu mfukoni na kubaki akiwa amesimama kwa muda huku uso wake ameugeuzia pembeni. Aligeuka na kumwendea yule mtu mrefu na mnene aliyekuwa amesimama kule kwenye kona. Walianza kuongea kwa sauti za chini na Baddi akawa amepigwa butwaa. Cha Ufupi alikuwa akiongea na nani wakati ule? Na kwa nini ile kauli yake ya mwisho ameitoa baada ya kuwa ameshakata simu, huku akijitia bado anaongea na ile simu?
Muda huo Cha Ufupi alirudi pale alipokuwa na kumwambia, “Okay, Baddi…hatuna muda wa kuendelea kupoteza...”
“Unamaanisha bosi wako hana muda wa kuendelea kupoteza! Ni nani huyo bosi wako, eenh?” Baddi alimkatisha kwa kejeli.
“Usilete ujinga! Tueleze ni wapi zilipo almasi zetu ulizodhulumu kule Sierra Leone...!”
“Mnhu! Yaani wewe ungekuwa Sierra Leone ungekuwa marehemu saa hizi, kwa sababu wote wanaoenda kule kwa uroho wa mali huishia pabaya!”
“Kama jinsi ulivyohakikisha kuwa Nathan anaishia pabaya?” Mtu mfupi alimuuliza kwa upole na ghadhabu. Baddi na Swordfish walijikuta wakiachia miguno ya mshangao kwa kauli ile.
“U...unajua nini kuhusu Nathan wewe...?” Baddi alimuuliza kwa mshangao.
“Ninajua kila kitu kuhusu Nathan, Baddi...na ninajua kila kilichotokea baina ya Nathan Mwombeki...au Alpha…na mjinga aliyekuwa akijulikana kama Vampire, ambaye kama ataendelea na ujinga wake muda si muda atakuwa marehemu!”
“Na ndiyo mtakuwa hamzipati kabisa hizo almasi!” Swordfish alidakia na kumalizia kwa tusi kali. Mtu mfupi aligeuka na kumuendea kwa kwa kasi, uso wake ukiwa umejawa ghadhabu, ile mashine ikiunguruma mkononi mwake. Hilo lilikuwa ni kosa ambalo Swordfish alikuwa amelitarajia.
Ghafla Swordfish aliruka wima, kile kiti kikiwa kimefungwa pamoja naye, kisha akajirusha mzima mzima huku akijigeuza hewani na kumbabatiza mtu mfupi na kile kiti. Wote wawili walipiga mweleka mzito, kile kiti kikivunjika vipande vipande.
Kilikuwa ni kitendo cha haraka na kisichotarajiwa na wote, isipokuwa
MDUNGUAJI
Baddi, ambaye muda huohuo alijirusha juu pamoja na kile kiti na kujiachia, akijibwaga sakafuni kwa kishindo, kiti kikitawanyika, mbao zikiruka kila upande. Haraka sana alijibiringisha sakafuni na kumpamia yule kibaraka mkorofi aliyekuwa akimwendea mbio, ambaye alipiga mweleka huku bastola iliyokuwa mkononi mwake ikimtoka.
Ndiyo wale wafuasi wengine wawili wa mbegu fupi walipozinduka na kuanza kupiga kelele za wahka huku wakimwendea Baddi aliyekuwa akizikung’uta kamba zilizokuwa zimemfunga kwenye kile kiti kutoka mikononi mwake.
Haraka Baddi alijitupa wima kutoka pale sakafuni, na kugeukia kule alipokuwa yule mtu mrefu mnene na kushangaa kuona kuwa jamaa hakuwepo, ule mlango wa chuma ukiwa umefungwa.
Alimtandika teke la kichwa yule kibaraka mkorofi ambaye alikuwa ameshainuka na jamaa akatoa yowe huku akirudi chini. Sasa Baddi alikuwa ameshapandwa na jazba ya makabiliano. Alikuwa anaanza kumsogelea tena yule kibaraka mjinga wakati alipojikuta akikabiliana na mtutu wa bastola ya mmoja wa wale wafuasi wawili wa mtu mfupi.
“Tulia wewe!” Jamaa alimkemea na Baddi akasita, lakini kabla hajatanabahi
Swordfish aliunguruma.
“Wote tulieni hivyo hivyo!”
Swordfish alikuwa amemkandamiza mtu mfupi sakafuni kwa kumuwekea goti shingoni, huku kwa mkono wake wa kushoto akiwa amemuwekea ile drill kichwani, na kwa mkono mwingine akiwa amewaelekezea bastola wale vibaraka wa mbegu fupi.
E bwana we!
“Tupa chini bastola hizo la sivyo natoboa bichwa la huyu mtwana mwenzenu hapa!” Mzanzibari aliunguruma tena, na wale vibaraka wakagwaya. Baddi alimpokonya bastola kibaraka aliyekuwa karibu naye kisha akamshindilia ngumi ya tumbo. Jamaa aligumia huku akiinama, na hapohapo akamtwanga kwa kitako cha ile bastola kisogoni. Jamaa akatoa mguno hafifu huku akienda chini kama gunia tupu.
Kibaraka wa pili alitupa chini bastola yake na kubaki akiwa ameduwaa huku macho yakimtembea. Bila ya tahadhari Swordfish alimpiga risasi ya mguu na kumtawanya goti vibaya sana. Jamaa aliachia yowe la uchungu huku akigaragara chini kama mwehu, damu ikitapakaa kila upande.
Yule mtwana aliyepigwa kisogoni kwa kitako cha bastola alianza kuinuka huku akigumia kwa maumivu, na hapo tena bastola ya Swordfish ilikohoa na kumvunja paja kwa risasi. Jamaa alibweka kama mbwa huku akijibwaga chini,
akijishika paja huku akilalama kwa uchungu, kelele zake zikiungana na zile za yule mwenzake aliyetawanywa goti.
Sasa alibaki yule kibaraka mkorofi tu, na Baddi alikuwa akimsogelea taratibu. “Si unakumbuka nilikwambia kuwa nikikutia mkononi utajuta wewe?” Alimuuliza kwa hasira. Jamaa alijirusha mzima mzima huku akipiga ukelele wa ghadhabu, lakini Baddi aliruka pembeni na wakati huohuo mguu wake wa kulia ukichomoka kwa teke kali lililotua maridhawa chini ya kitovu cha yule jamaa. Jamaa aliyumba huku akipiga yowe la uchungu. Baddi alimgeukia kwa teke jingine la kisogoni kwa mguu wake wa kushoto na jamaa akaenda chini kifudifudi na kubamiza uso wake sakafuni, akivunja meno kadhaa na kinywa kikimtepweta.
Huku kwake, Swordfish alimnyayua mbegu fupi kimabavu na kumsukumia kwa nguvu kwenye kile kiti chake alichokuwa akikikalia kwa mbwembwe hapo awali.
“Kaa hapo sasa weye!” Alimkemea na Cha Ufupi alienda chini na kile kiti huku akiguna kwa mshituko na woga.
Baddi Gobbos alimshindilia teke la mbavu yule kibaraka mkorofi aliyekuwa akigaragara pale sakafuni akitema udenda uliosheheni damu na vipande vya meno na jamaa alitoa yowe jingine la maumivu. Wale vibaraka wengine waliovunjwa miguu kwa risasi za Swordfish sasa walikuwa wakilia kwa sauti zilizonywea na walikuwa wanaelekea kupoteza fahamu.
Swordfish alimuinua mbegu fupi kwa vurugu na kumketisha tena pale kitini. Alimzungushia shingoni ile kamba aliyokuwa amefungwa nayo kwenye kiti hapo awali na kumkaba nayo kwenye mgongo wa kile kiti. Mbegu fupi alifurukuta huku akiwa ametumbua macho lakini hapohapo Swordfish alimuwekea mdomo wa bastola utosini.
“Tulia, Mbilikimo!” Alimkemea, na hapohapo akamgeukia Baddi aliyekuwa akimshindilia mateke yule mkorofi aliyekuwa akigaagaa sakafuni huku akicheua damu.
“Baddi…njoo umdhibiti huyu kibushuti hapa…huyo khanithi niachie mimi sasa!” Alimwambia kwa sauti ya kuogofya. Baddi alimuacha yule kibaraka mkorofi akitapatapa pale sakafuni na kwenda hadi pale kwa Swordfish. Alimuwekea cha ufupi bastola yake utosini na Swordfish akaenda kwa yule mkorofi aliyekuwa akijizoazoa kutoka pale sakafuni. Jamaa alikuwa hoi kutokana na kipondo cha Baddi.
Swordfish alimshindilia teke la kifua na jamaa akarudi sakafuni kwa kishindo. Hapohapo akamuinua na kumkaba huku akimuwekea mdomo wa
MDUNGUAJI
bastola yake kichwani, halafu akamgeukia Cha Ufupi aliyekuwa amedhibitiwa na Baddi.
“Sasa utajibu maswali yote utakayoulizwa na Baddi, na utayajibu kwa ukweli…kwa kila jibu la uongo utakalotoa n’takuwa natoboa mwili wa huyu kibaraka wako kwa risasi…umeshaona jinsi nilivyowafanya wale wenzake!”
Swordfish aliunguruma, na kibaraka akaachia mguno wa fadhaa.
“Wewe hukutuleta huku kwa ajili ya kuniuliza juu ya almasi…ni nini hasa ulichotaka kuja kutufanya?” Baddi alimuuliza Mbegu Fupi huku akimpigapiga kichwani kwa mdomo wa bastola yake ilhali kwa mkono wake mwingine akiwa ameikamata ile kamba iliyomkaba shingoni.
“Ah…eeenh…ni almasi tu…!” Cha ufupi alibwabwaja na hapohapo bastola ya Swordfish ililipuka na kibaraka wake aliachia yowe kubwa, damu ikimbubujika kutoka upande wa kichwa chake, risasi ikiondoka na kipande cha sikio lake la kushoto.
“Nilikwambia ukisema uongo natoboa hii takataka yako kwa risasi!”
Swordfish alimkemea huku bado akimbana yule kibaraka aliyekuwa akipiga mayowe huku akijitupatupa ovyo pale chini.
“Kweli jamani…!” Cha Ufupi alijibu huku akitetemeka, jicho likiwa limemtoka pima.
“Inaelekea hajali iwapo kibaraka wake atakufa huyu!” Baddi alisema huku alimtomasa-tomasa kichwani kwa bastola yake. Swordfish alimuwekea bastola kwenye paji la uso yule kibaraka mkorofi.
“Bosi wako hana habari nawe…je nawe huna habari na maisha yako?” Alimuuliza kwa ukali.
“Si…si…sijui chochote mimi wazee…ningejua ningesema tu!” Kibaraka alibwabwaja huku akilia.
“Basi huna faida nasi!” Swordfish alimwambia na hapohapo aliielekeza juu bastola yake na kufyatua risasi nyingine, jamaa alipiga yowe na kujitupa chini, akiamini kuwa amelipuliwa kichwa kwa risasi, sambamba na yowe lake likisikika yowe la woga kutoka kwa Mbegu Fupi. Swordfish akamuinua kwa nguvu yule kibaraka kutoka pale chini na kumkalisha tena.
“Bado hujafa weye...tulia!” Alimwambia huku alimchapa makofi. Jamaa alitumbua macho huku akitoa mlio uliotetema kwa woga, mkojo ukampita bila kujitambua, kisha mboni zake zikapotelea ndani ya macho yake na kujibwaga chini, fahamu zikimhama.
“Kwisha habari yake, khanithi mkubwa!” Swordfish alisema na kuinuka, lakini hapohapo Mbegu Fupi alijikurupusha kutoka pale kwenye kiti, akikivuta
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
kile kiti pamoja naye huku akipiga kelele za ghadhabu kumrukia Swordfish.
Baddi Gobbos alimfyeka ngwala kali kutokea nyuma, na wakati huohuo
Swordfish akijirusha pembeni. Cha Ufupi alitupwa hewani pamoja na kile kiti na kujibwaga chini kwa kishindo, kile kiti kikitawanyika vipande-vipande naye akisota vibaya sakafuni, akijichubua sehemu za mwili wake.
Alijikurupusha na kutaka kuinuka lakini alijikuta akiwa amesimamiwa na wale mashababi wawili, mitutu ya bastola zao ikiwa imemuelekea usoni. Alitembeza macho yake kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine. Akameza funda kubwa la mate, pua yake bapa ikitanuka na kusinyaa haraka haraka.
“Sasa utajibu maswali yetu au vipi?” Baddi alimkoromea. Cha Ufupi alimtazama kwa kukata tamaa, kisha kwa unyonge akaafiki kwa kichwa.
“
Good! Sasa nitaacha lile swali langu la kwanza, na badala yake nataka utueleze juu ya lile bonge la mtu lililotoweka baada ya kuona mkong’oto umewageukia…ni nani lile?” Baddi alimuuliza.
“Na linahusika vipi na mambo yote haya?” Swordfish aliongezea.
“Anaitwa Kabwe wazee. Jairos Kabwe!” Cha Ufupi alijibu kwa kusitasita. Baddi na Swordfish walitazamana. Hili lilikuwa ni jina jipya kabisa kwao.
“Naye ni nani katika kundi lenu?” Baddi alimuuliza, huku akili ikimzunguka.
“Yeye nd’o bosi wetu…ni mfanyabiashara mkubwa wa madini nchini… hususan almasi.” Cha Ufupi alijibu. Hakika alikuwa amefikwa. Kimya kilitawala mle ndani.
“Sasa kama yule ndiye bosi wenu, na yule uliyeongea naye kwa simu ni nani?” Baddi alimuuliza. Jamaa akapepesa macho kwa muda.
“Ah, yule ni…mwenzake…lakini lile bonge la mtu ndiyo bosi…”
“Mnh! Jongo hili…hapo limeongopa. Hebu sema ukweli weye!” Swordfish alidakia huku akimshindilia teke la kifua. Mbegu Fupi aligaragara sakafuni huku akigumia kwa maumivu.
“Okay, tutaujua ukweli tu…sasa tueleze kwa kituo ni nini hasa unachojua kuhusu ya mambo yaliyotokea baina yangu na Nathan kule Sierra Leone, na umeyajuaje?” Baddi alimuuliza.
“Sijui chochote juu ya hayo wazee…ni bosi Kabwe ndiye aliyeniambia kuwa nikikutana nawe nikwambie maneno hayo. Alisema kuwa nikikwambia hivyo utajua kuwa tunasema kitu cha kweli na kwamba huna cha kutuficha.”
Cha ufupi alijibu, kisha akaendelea, “...na naona ni kweli.”
Swordfish na Vampire walitazamana. Kimya kilichukua nafasi kwa muda. Akili ilikuwa ikimzunguka Baddi, kwani kuna kitu hakikuwa kikimkalia sawa
MDUNGUAJI
katika maelezo yale. Vipi huyu Kabwe awe anajua yaliyotokea kule Sierra Leone? Ni kwamba naye alikuwepo huko?
“Je, huyo Kabwe ni mwanajeshi kama wewe? Ana uhusiano wa aina yoyote na jeshi letu la Tanzania?” Alizidi kuuliza.
“Mtu nimeshakwambia kuwa yeye ni mfanyabiashara ya madini! Huyu sio mwanaj...”
Swordfish alimtandika kofi kali la uso lililompeleka chini mzima mzima.
“Hebu jibu maswali yetu kwa nidhamu weye, aka! Waleta kibri sio?” Alimkemea. Cha Ufupi alijizoazoa kutoka pale sakafuni na kubaki akipepesuka huku akikohoa mfululizo na akimtupia Swordfish jicho la hasira.
“Kaa kwenye kiti hapo!” Baddi alimkemea. Jamaa alitii huku akijipapasa uso wake pale alipozabwa kibao.
“Nahitaji maji tafadhali…! N’na kiu…”
“Baadaye! Jibu maswali yetu kwanza!’ Swordfish alimkemea, na jamaa akagwaya.
“ Okay kwa hiyo huyo mtu si mwanajeshi na hana uhusiano na jeshi lolote ulijualo?” Baddi alizidi kumuuliza.
“Ndivyo!”
“Mbona napata hisia kuwa unatudanganya wewe?” Baddi alimuuliza huku akimkandamiza tumboni kwa mguu wake. Cha ufupi alitweta kwa taabu na kumjibu kwa kugumia, “Ni kweli kabisa niwaambiayo jamani! Sina sababu ya kuwadanganya sasa…naombeni maji basi!”
“Maji tutayatoa wapi saa hizi wewe?” Baddi alimkemea.
“Yamo kwenye gari mle…!” Jamaa alimjibu kwa kuomboleza.
“Utakunywa maji tutakapoamua sisi!” Swordfish alimfokea.
“Sasa mimi sina cha kuwaeleza zaidi. Niacheni niende basi!”
“Una wazimu mkubwa sana wewe! Tukuachie? Itabidi utupeleke kwa huyo Kabwe sasa! Nadhani yumo ndani ya hili jengo somewhere!” Baddi alimkemea.
Jamaa alionesha woga mkubwa kabisa.
“Mnh! Nyi’ nendeni tu mkamtafute humo ndani, nikiwapeleka ataniua…”
Baddi alimtandika ngumi ya uso. “Acha kutufanya wajinga sisi wewe!
Twende hadi hapo kwa bosi wako, akikuua poa tu kwani hata sisi tuna mpango wa kukuua fala we…twende!” Alimkoromea kwa hasira. Jamaa alijaribu
kusema neno lakini hapohapo Swordfish alifyatua risasi nyingine iliyochimba
sakafu katikati ya miguu ya yule mtu mfupi. Jamaa aliruka kwa mshituko huku
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
akibweka kama mbwa.
“Nyanyuka!” Alimkemea.
Walimuongoza hadi pale kwenye ule mlango wa chuma na kukuta ukiwa umefungwa kwa ndani. Bila mjadala Swordfish alirudi nyuma na kukitawanya kwa risasi kitasa cha mlango ule na mlango ukaachia. Walifuata ngazi zilizowatoa kule chini ya ardhi na kuwafikisha sehemu ya juu ya jengo lile ambako walikuta mlango mwingine uliokuwa wazi. Walimsukuma ndani mateka wao huku wakiwa makini na bastola zao. Walitokea kwenye ukumbi mrefu uliokuwa na vyumba kadhaa kila upande. Msako katika vyumba vile haukuzaa matunda yoyote, kwani bonge la mtu halikuwemo kabisa mle ndani. Waliendelea kupekua vyumba vyote vilivyokamilika katika jumba lile, na hali ikawa ni ile ile.
“Yu wapi yule mtu wewe?” Swordfish alimkemea Cha Ufupi kwa hasira.
“Sa’ mi’ n’tajuaje wazee? Sote tumeona kuwa hayupo!” Mbegu Fupi alijitetea kwa woga mkubwa. Walitoka nje ya jengo lile, na huko wakagundua geti jingine dogo lililokuwa sehemu ya nyuma ya uzio uliolizunguka lile jengo. Baddi alibaki na yule mateka wao wakati Swordfish akiliendea lile geti na kulisukuma. Alitazama nje ya uzio ule na kuona alama za matairi ya gari zilizoelekea kwenye ujia mwembamba uliopotelea kwenye msitu uliokuwa nyuma ya uzio ule. Mara moja akajua kuwa bonge la mtu lilikuwa limetoroka kutumia ujia ule.
“Jamaa katoweka!” Swordfish alirudi na kumjuza mwenzake.
“Okay, no problem…tunarudi kule chini na hii mbegu fupi itatupeleka mpaka nyumbani kwake, bloody fool!” Baddi alisema kwa hasira. Akiwa amegwaya vibaya sana, Cha Ufupi aliongozwa kurudi kule chini ya jengo.
Aliwekwa kwenye kiti cha abiria ndani ya ile Prado. Baddi akaketi nyuma ya usukani. Swordfish aliketi kwenye kiti kilichokuwa moja kwa moja nyuma ya kile cha mbegu fupi na kumuwekea bastola kisogoni huku akimbana pale kwenye kiti kwa mkanda wa kile kiti ili asifurukute, na kumwamuru atoe maelekezo ya kuwafikisha huko lilipokimbilia lile bonge la mtu.
“Naomba ninywe maji kidogo ndugu zangu. Nina kiu sana kwa kweli!”
Cha ufupi alisema huku akiwa amejibweteka kwa kukata tamaa pale kitini.
“Hebu lipe hayo maji linywe lisije likatufia hapa!” Swordfish alisema
kutokea kule nyuma.
“Haya, yako wapi hayo maji wewe?” Baddi alimuuliza yule mtu mfupi.
“Ah, ahsante sana. Yamo humo…” Cha Ufupi alisema huku akimuoneshea
kwenye droo maalumu mle ndani ya gari. Baddi alifungua droo na kutoa
MDUNGUAJI chupa ya maji ambayo ilikuwa bado haijafunguliwa na kumtupia. Jamaa aliichukua ile chupa na kuifungua kwa papara kisha akagugumia yale maji kwa pupa. Aliichia ile chupa ikianguka mapajani mwake na kupitiliza hadi kwenye sakafu ya lile gari, maji yaliyobaki ndani ya ile chupa yakimmwagikia.
“Hah, we vipi…?” Baddi aliuliza huku akimtazama yule jamaa kwa mshangao. Swordfish alididimiza mdomo wa bastola yake kisogoni kwa yule jamaa ambaye alibaki akiweweseka huku amejishika koo kwa muda, kasha hapohapo alijipinda kwa nyuma huku akifinya uso kwa uchungu mwingi, sauti za mikoromo zikimtoka.
“Ama! Nini tena…?” Swordfish aliuliza kutokea kule nyuma.
“Ah! Sijui…” Baddi alimjibu huku akimtazama yule mtu, akiwa amemuelekezea bastola, lakini yule mtu mfupi wala hakuwa na haja ya kutishiwa bastola wakati ule.
“Nini Vampire?” Swordfish aliruka kutoka kule nyuma na kufungua ule mlango wa abiria kule mbele. Muda huo yule mtu mfupi aliangukia ubavu, kiwiliwili chake kikiangukia nje ya gari. Swordfish alimdaka na kumtazama kwa kihoro.
“Nimekula kiapo cha usiri…na nimekitimiza...!” Cha Ufupi alisema kwa taabu.
“Ati?” Swordfish aliuliza.
“Ah, ina maana...” Baddi alianza kusema kwa mshangao.
“Maji Vampire! Ni haya maji aliyokunywa!” Swordfish alimkatisha kwa wahka.
“Lah! Yaani mjinga katunywea sumu hapa hapa!” Baddi alimaka.
“…ndiyo…bora kufa kuliko…” Mtu mfupi alisema kwa taabu.
“Wapi?” Swordfish aliuliza kwa kiherehere, “...ni wapi alipo huyo mkuu wako? Ni wapi alipo Kabwe weye, eenh? Sema upesi bloody fucking bastard weye…sema!” Alimkemea kwa kiherere. Mtu mfupi alimcheka kidogo kabla hajaanza kukohoa kwa nguvu, povu lililochanganyika na damu likimtoka kinywani.
“
Oh, my God...hii si kweli kabisa! Haiwezekani!” Baddi alimaka huku akimparamia kifuani yule mtu na kumkwida ukosi wa shati. “Ni wapi alipo huyu Kabwe wewe?”
Mtu mfupi alimzungushia jicho lililowiva kwa maumivu, akakohoa na kumrushia usoni povu lililotoka kinywani mwake, kisha akasema maneno yake ya mwisho, maneno ambayo yaliwatia ubaridi wale wapiganaji wawili.
“...ha...hamtompata tena m...mtu huyo! Nime...nim...aaaargh!” Cha Ufupi alisema kwa taabu lakini machungu ya sumu aliyokunywa yalimzidi na akaishia kupiga kelele za uchungu. Baddi alimzaba kofi yule mtu, na hapohapo akamnyanyua kwa ukosi wa shati lake na kukurubisha uso wake na ule wa yule jamaa.
“Unasema nini wewe? Hatutompata tena...? Una maanisha nin...”
“...too late!” Mtu mfupi alisema na kubaki akitweta, macho yakimlegea.
“Acha ujinga! Yu wapi Jairos Kabwe wewe?” Baddi alimkemea kwa hasira.
“Baddi...” Swordfish aliita kwa upole, akili yake ilikuwa imeshaanza kufikiri ni nini kifuate katika hali ile.
“No! Atasema tu huyu bloody fool, atasema tu...”
“…niliwalaghaiiii…!” Mtu mfupi alimalizia kwa taabu, kisha hapohapo mwili wake ulijipinda kwa nguvu na uso wake ukajikunja kwa uchungu mkubwa kabisa, akiwa ameuma meno na akitoa sauti za kukoroma. Kisha
akajibweteka kama mzigo, mwili wake ukimuelemea Swordfish, ambaye aliuachia na ukabaki ukining’inia nusu nje ya gari ilhali nusu ya chini ya mwili ule ikiwa ndani. Cha Ufupi akaaga dunia.
Jamaa walitazamana kwa mshangao na kutoamini.
“Khah! Ndiyo nini hii...!” Baddi alijikuta akiuliza kwa fadhaa. Swordfish alimkamata mkono yule mtu mfupi na kusikilizia msukumo wa damu. Kisha akamuwekea sikio lake kifuani na kusikiliza kwa muda. Kama haitoshi alimtandika makofi ya haraka haraka mashavuni yule mtu, lakini hakukuwa na dalili zozote kuwa yule mtu alikuwa hai.
“Mjinga kajiua bwana, khab-bithi mkubwa!” Swordfish alisema kwa hasira, na kumtemea mate usoni yule marehemu.
Duh! Baddi alichoka.
“Sasa...sasa...” Alijaribu kupata neno la kusema asilipate.
“Tuondoke hapa Baddi...!”
“Akh! Yaani huyu mjinga ndiyo katulaghai namna hii huyu?”
“Hawa si watu wa mchezo Baddi...lets just get out of here partner. Hapa tumeshinda pambano, lakini hii vita bado mbichi kabisa!” Swordfish alisema huku akiuvutia sakafuni ule mwili wa yule kibushuti aliyewacheza shere mbaya.
“Sasa unafanya nini?” Baddi alimuuliza.
“Tutahitaji hili gari kuturudisha hotelini kwetu, ama sivyo tutalazimika kutembea umbali mrefu sana.” Alipokwisha kusema hivyo, Swordfish alizungukia upande wa abiria na kujibwaga kwenye kiti cha upande ule.
“Endesha gari Baddi. We’ ndiye mwenyeji zaidi huku bara kuliko mimi,
MDUNGUAJI
lakini pia mimi siku hizi siruhusiwi kuendesha gari...si unaona nimebakiwa na jicho moja bwana?”
“Dah, Swordfish...nasikitika kwa hali hiyo, lakini pia nakushukuru sana bwana...”
“Achana na hayo kwa sasa, tuondoke hapa. Bado tuna mengi ya kuongea na kuwekana sawa...”
Baddi alitikisa kichwa huku akiliondoa lile gari kutoka eneo lile, wakiwaacha wale majambazi wawili waliovunjwa miguu nao wakiwa wamepoteza fahamu kama yule mwenzao mkorofi aliyetishwa vibaya sana na Swordfish. Baada ya mwendo mfupi mle ndani Baddi alisimamisha gari ghafla.
“Vipi…?” Swordfish alimuuliza kwa mashangao. Baddi alifungua mlango wa lile gari na kuruka nje. “Narudi sasa hivi!” Alimwambia huku akikimbia kurudi kule walipokuwa wale majeruhi watatu na marehemu mmoja. Alipiga goti kando ya ule mwili mnene na mfupi, kisha kwa haraka sana akaanza kusachi mifuko yote ya nguo za yule mtu. Alipopata alichokuwa akikitafuta aliinuka na kurudi mbio kwenye lile gari.
“Nini…?” Swordfish alimuuliza.
Baddi Gobbos alimuonesha ile simu ya yule mtu mfupi huku akitabasamu.
“Tulitaka kusahau kitu muhimu sana patna…” Alisema na kuitupia ile simu mapajani mwa Swordfish. Swordfish aliitazama ile simu kwa muda, kisha uso wake ukafanya tabasamu moja pana sana.
“Safi sana Vampire! Safi sana!!”
“Yeah, muda si muda bosi atapiga simu tu…na labda kutokea hapo tutajua tunamnasa vipi, au sio?”
“Yeah…” Swordfish alijibu kisha akamuuliza, “...kwa hiyo yule jamaa hakuwa na kitu kingine zaidi mfukoni mwake?”
“Hakuna bwana! Nilikuwa nataraji kupata kitambulisho ili angalau tumjue lakini wapi! Alikuwa na pakiti ya kondomu na hiyo simu tu!”
“Mzinzi mkubwa!” Swordfish alisema na kuishia kumsonya yule marehemu mfupi. Baddi aliliongoza lile gari kuelekea kwenye lile lango waliloingilia. Yule mmasai alikuja kuwafungulia lile geti.
“Rafiki, tunatoka mara moja, lakini wenzetu bado wamo humo ndani sawa?” Swordfish alimwambia.
“Sawasawa tu.” Mmasai alijibu nao wakatoka nje ya uzio wa lile jengo na kutazama huku na huko kujaribu kujua ni wapi walipokuwa. Lilikuwa ni eneo lenye mikorosho mingi sana, na nyumba moja moja ambazo bado zilikuwa zikiendelezwa
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI kiujenzi.
“Mnh! Sijui tuko wapi kwa kweli. Lakini nadhani naweza kuona alama za njia tuliyopitia wakati wa kuja.” Baddi alisema huku akizidi kutazama huku na huko. Kote kulikuwa kimya sana.
“Yeah...tuifuate tu hiyo njia mpaka tutakapotokea barabara kubwa, kisha tutajua uelekeo.” Swordfish alimwambia, na Baddi alitekeleza. Hawakuiona Toyota Corolla iliyokuwa imechomekwa katikati ya kichaka kilichokuwa kiasi cha kama mita kumi na tano kutoka pale kwenye lile jengo.
Aidha hawakuweza kumuona yule mtu mrefu mwenye tabasamu jepesi aliyekuwa amejilaza kwenye muinuko mdogo hatua chache kutoka pale alipoficha lile gari lake. Yeye alikuwa amefichwa na miti iliyotapakaa eneo lile na kwa kutumia darubini kubwa, alikuwa akifuatilia mwenendo wa lile gari tangu likitoka nje ya geti hadi lilipokunja kona na kuanza kuufuata ule ujia wa kuelekea barabara kubwa.
Na sasa, wakati akiiangalia ile Prado ikitokomea taratibu kutoka eneo lile, ule uso wake wenye mazoea ya kuachia tabasamu jepesi kila mara ulikuwa makini na wenye mashaka makubwa. Aliielekeza darubini yake kule kwenye lile jengo. Kote kulikuwa kimya. Alitoa simu ya kiganjani na kupiga namba fulani kabla ya kuiweka sikioni.
“Yeah hello!” Aliongea kwenye ile simu, kisha akaendelea, “…naona gari limetoka, lakini sasa linaendeshwa na Baddi akiwa na Meja Babu tu. Jamaa zetu hawamo!” Alisema kwa wasiwasi, kisha akasikiliza maelezo kutoka upande wa pili kwa muda kabla ya kuongea tena.
“Sasa namba za hilo gari si bado mnazo? Basi tuma vijana walisubiri barabara kuu, kisha walifuatilie mpaka watakapoishia…sawa?” Aliongea tena kwenye ile simu na kumsikiliza mtu wa upande wa pili kwa muda kabla naye hajaongea; “Mh! Sidhani kama itakuwa wamewapa wakitacho ndiyo wakawaachia mzee...sasa ndiyo wawape na gari? Mimi nadhani kule akina Baddi wameacha maafa makubwa!”
Alisikiliza kwa muda kisha akasema, “Okay, mi’ nazama mle ndani!”
Alikata simu na kuirudisha ile darubini yake kwenye gari lake. Akaaza kuliendea lile jengo taratibu.
Baada ya kuendesha gari kwa muda fulani, Baddi na Swordfish walianza kusikia milio ya magari kutokea pale walipokuwa.
“Okay, Baddi...nadhani hapa hatuko mbali na barabara kubwa.” Swordfish
MDUNGUAJI alisema.
“Yes. Na ndipo tunapoliacha hili gari, au siyo? Sidhani kama ni salama kuingia nalo mjini...hatujui hawa watu wamelitumia kufanya nini zaidi huko walikotoka.”
“True. Madhali limetufikisha karibu na barabara kubwa, tutapata usafiri tu.”
Baddi alilichomeka katikati ya kichaka ile gari, kisha wale wapiganaji wawili walifuta kila mahala waliposhika ndani ya gari lile kwa kadiri walivyoweza, kabla ya kukomea milango yote ya lile gari na kutembea kwa miguu kufuata kule sauti za magari zilipokuwa zikitokea. Dakika tano baadaye walitokea kwenye barabara kubwa ya lami, na ndipo walipogundua kuwa walikuwa maeneo ya Pugu. Walifanikiwa kukodi Land Rover la kuwarudisha mjini. Njia nzima walikuwa kimya, kila mmoja akitafakari yale matukio ya siku ile kwa namna yake.
Nusu saa baadaye waliingia chumbani kwa Swordfish ndani ya ile hoteli ya Al-Uruba. Swordfish alipita moja kwa moja hadi bafuni na kunawa uso na mikono, kisha akatoka, na Baddi naye akaenda kufanya hivyo.
Alipotoka bafuni alisimama akimtazama yule shujaa mwenzake kwa muda, na Meja Abdul-Hameed Babu aliinuka kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia na kwenda kumkumbatia rafiki yake.
“Karibu nyumbani Baddi...na pole na masahibu yote!”
“Oh, ahsante sana meja...ahsante sana.” Waliachiana na kubaki wakitazamana, kisha Baddi akamwambia, “Pole na wewe Meja…kwa kila kitu...”
“Usijali kamanda...madhali bado tunapumua kila kitu kitakuwa sawa tu.”
Baddi aliketi kitandani.
“Enhe, hebu nieleze Meja...ilikuwaje tena hata wale jamaa wakakudhibiti namna ile wakati nafika hapa?” Baddi alimuuliza.
Meja Babu alitikisa kichwa kwa masikitiko. “Dah, hata sielewi Baddi. Lakini nadhani kuwa simu yangu ya nyumbani ilikuwa imetegewa kitu kwa namna fulani ambacho kiliwawezesha kusikiliza maongezi yote yapitiayo kwenye simu ile. Nadhani...kwa sababu nilipofika hapa muda si muda nikagongewa mlango. Nami nilijua ni wewe tu, lakini kabla sijauliza nikasikia sauti ikiita jina langu kutokea nje, nilipouliza ni nani, ile sauti ilinijibu kwa wahka na wasiwasi mkubwa kuwa ni wewe. Basi nikajua kuwa ulikuwa umefikwa na tatizo, nikafanya haraka kufungua mlango...kosa!”
“Nini kilitokea?”
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Ah, ile nafungua tu nilibamizwa kwa nguvu na ule mlango, nikasukumwa ndani na wale jamaa wakaingia wote wakiwa wamenielekezea bastola, wakaniambia kuwa tutaketi sote humu ndani kukusubiri wewe, unaona maajabu hayo?”
“Duh!”
“Ndiyo! Si nd’o maana nakwambia hawa watu si mchezo! Basi kama kawaida yangu nikalianzisha, lakini nilijua kuwa walikuwa wamenizidi idadi na pia walikuwa na faida ya kunishtukiza namna ile…basi wakanidhibiti bwana. Sikuwa na budi ila kukusubiri tu...”
“Yeah...lakini...ni nini ulimaanisha pale uliposema kuwa...kama ilivyokuwa kule Sierra Leone, ndivyo ilivyo hapa...? Ulimanisha ile kanuni yetu ya kule Sierra Leone, One for all , and all for one... au...? Manaake ulinichanganya kidogo pale!”
“Ni hivyo na zaidi ya hivyo...”
“Yeah...nilihisi kuwa kuna zaidi, lakini haikuniingia sawasawa, ni nini haswa...?”
“Zaidi nilimaanisha lile lengo zima la ile operesheni yetu ya kule Sierra Leone Vampire,unakumbuka? Tulitakiwa tuitafute kambi ya waasi kwa kutumia utaalamu wako wa kunasa mawasiliano, sio?”
“Yeah...!”
“Tuliagizwa kuwa tukiitambua ile kambi tusifanye kitu chochote bali tuwajulishe wenzetu kule makao makuu ya kambi yetu mahala ilipo ili kikosi cha mashambulizi kije kutusaidia kuwaangamiza...”
Kufikia hapo Baddi alianza kuachia tabasamu la ufahamu.
“Na ndicho nilikichotaka pale! Nilitaka twende mpaka tufahamu makazi ya wale watu, kwa matumaini kuwa huenda huko tutamkuta huyo kiongozi wao...”
“Hakika ulitumia akili Swordfish...”
“Yeah...na...nadhani kwa namna fulani tulifanikiwa, ila tu huyo mkuu wao hakuwepo pale...”
“Ndiyo! Lakini sasa nadhani tunaweza kumfanya huyu mkuu wao aje kwetu sisi kwa kutumia hii simu.” Baddi alisema huku akiioneshea ile simu ambayo Swordfish alikuwa ameitupia pale kitandani hapo awali.
“ Exactly ...lakini yatupasa tuwe makini sana. Hii ni nafasi nzuri sana ya kumpata huyu mtu. Lakini tukikosea kidogo tu na akahisi kuwa kuna kitu kisicho sawa ndiyo hatutampata tena...”
“Yeah, sasa tufanyaje? Manake mambo yaliyonitokea leo hii ni mazito sana nashindwa hata kufikiri! Unadhani tumpigie sasa hivi?” Baddi alisema.
“Hapana, nadhani tusubiri atupigie...”
MDUNGUAJI
“Halafu tunamwambia nini sasa akitupigia? Definitely atajua kuwa aliyepokea simu si mtu mfupi, na unadhani itakuwaje?”
“Mnh! Kweli...sasa hapo tuta-tatizika kidogo...”
“Basi naona hiyo simu tuizime kwa muda...ili tujipange. Tukishajua namna ya kumvutia kwetu, tunaiwasha, unaonaje?” Baddi alitoa wazo.
“Ni wazo zuri! Pia hiyo itasaidia kumuweka kwenye kiti moto huyo mkuu, kwani kila akijaribu kupiga na kukuta kuwa simu imefungwa atazidi kujaa wahka...”
Baddi alicheka kidogo.
“
Yeah...ye’ atajua kuwa kibushuti kimepata almasi na kimeamua kumtosa!” Alisema.
“Haswa! Na atakapopata simu kutoka kwetu atakuwa ameshachanganyikiwa kiasi cha kushindwa kufikiri zaidi, na atafanya kile tutakachomwambia, na ndipo tutakapomnasa!”
Baddi aliizima ile simu, kisha akamgeukia yule shujaa wa makabiliano ya ana kwa ana katika medani za vita.
“Sasa hebu niambie kwa kina rafiki yangu...what really happened tangu tulipopoteana kule Sierra Leone...? Na nini kilitokea baada ya kurudi hapa nchini...manaake naona mambo hayako sawasawa kabisa, we’ mwenyewe umejionea leo!”
Swordfish alitikisa kichwa kwa masikitiko na kubaki kimya kwa muda kabla ya kumjibu.
“Wallahi...hata sijui nianzie wapi sheikh! Mambo yameenda ndivyo-sivyo tangu kule Sierra Leone...na yakazidi kwenda mrama hapa nyumbani. Siku zote mimi nilikuwa na mashaka yangu, na pale uliponipigia simu kuwa upo hapa nchini, mashaka yangu yalithibitika.”
“Hebu na tuanzie kule Sierra Leone...nini kilitokea? Nahisi hamkufanikiwa kumnasa yule Mdunguaji kule msituni...lakini...vipi Stealth...alinusurika...?”
Baddi alimuuliza, na kabla hajajibiwa akaendelea, “...najua nawe una wahka wa kujua yaliyonikuta...ambayo si madogo kwa kweli, lakini naomba kwanza nijue kisa cha upande wako....”
Swordfish alitabasamu na kutazama chini kwa muda. Alipoinua tena uso wake, alianza kuongea. Akamuelezea mambo yote yaliyotokea kule Sierra Leone. Tangu walipoanza kuwatafuta yeye (Baddi) na Black Mamba, hadi yeye alipofika pale chini ya jabali na kuwakuta Stealth na Honey-Bee wakiwa wamezingirwa na waasi na jinsi alivyoweza kuwaokoa.
“Sasa baada ya hapo ndipo utata ulipoanza Baddi, kwani baada ya
makabiliano ya pale chini ya jabali nilipoteza fahamu, na niliporejewa na fahamu na kuulizia juu yenu, Stealth na Honey-Bee wakaniambia kuwa nyote mmekufa...yaani wewe na Alpha!”
“Hah!”
“Ndiyo...iliniwia ngumu sana kukubali na kuelewa, lakini ndivyo ilivyokuwa!” Swordfish alisema, na kuendelea kuelezea mambo yote yaliyofuatia hadi pale walipoenda kutoa ushuhuda kule kwenye lile jopo maalum la kijeshi kuhusiana na matukio ya kule msituni.
“Na hata pale mbele ya lile jopo, niliwaeleza wazi kuwa siamini kwamba Vampire amekufa...kwamba wewe umekufa...Sikuwa na mashaka kuhusu Alpha, kwani mwili wake niliuona.”
Baddi aliguswa sana na maelezo yale. “Kwa hiyo jopo liliamua kwamba Alpha alikuwa amekufa na alikuwa msaliti?”
“Ndivyo...”
“Na kwamba, mimi ndiye yule askari aliyekutwa amekufa bila kichwa akiwa na ile redio ya mawasiliano mgongoni...ambaye baadaye aliunguzwa vibaya na moto kule msituni?”
“Ndivyo...”
“Na kwamba Black Mamba alitoweka kwenye makabiliano kule msituni... Missing in Action..?”
“Yaani hivyo ndivyo ilivyohitimishwa na ndiyo taarifa iliyorudi hapa nyumbani Baddi. Wewe ulishakufa!”
“Duh!”
Baddi aliinuka na kusimama nyuma ya dirisha la mle hotelini huku akitikisa kichwa kwa masikitiko. Ingawa alishasikia juu ya “kufa” kwake hapo awali, lakini kusikia tena habari ile kama ilivyoelezwa na Swordfish bado kulimletea masikitiko yale yale kama kwamba ndiyo anaisikia kwa mara ya kwanza habari ile.
“Nilijua kuwa kuna kosa limefanyika hata mimi nikasemekana kuwa nimekufa, lakini sikutaraji kuwa kosa lenyewe linaweza kuwa dogo kiasi hiki!” Alisema.
“Sijakuelewa.” Swordfish alimwambia. Baddi alimgeukia na kubaki akiwa ameegemea ukuta pale kando ya dirisha.
“Yeah...lakini utaelewa tu baada ya kusikia maelezo yangu Swordfish...na nadhani hata viongozi wetu wa kijeshi wanatakiwa wasikie maelezo yangu ili hili suala liwekwe wazi na lifungwe kama jinsi ipaswavyo...”
Swordfish alibaki akimtazama. Sura yake ikionesha kuwa alikuwa anataka
MDUNGUAJI
kusikia zaidi.
“Kwa ufupi Swordfish, ni kweli Alpha alikuwa akitusaliti, na yule mtu mliyemzika hapa nchini mkiamini kuwa ni mimi...ni Black Mamba!”
“La Haula!”
“Ndiyo. Mtu pekee ambaye alikuwa missing in action, ni mimi. Ni kosa dogo sana, lakini hakika madhara yake ni makubwa mno!” Baddi alisema kwa upole.
“Oh, My God...ama hakika huu ni utata mzito! Lakini nadhani mimi niliuliza juu ya uwezekano wa jambo hilo kutokea…kwamba vipi iwapo wewe ndiye uliyepotea, lakini uamuzi wa tume ulikuwa wa mwisho...” Swordfish alisema, kisha akaendelea, “Hebu nieleze kwa kirefu komredi, maana kwa miaka mitatu mfululizo hili suala la kifo chako limekuwa likiniamsha usiku wa manane huku nikivujwa jasho kwa taharuki!”
Ndipo Baddi alipomueleza kisa chake, tangu pale alipomkabidhi Black Mamba ile redio yake ya mawasiliano, jinsi alivyokuwa akijaribu kufuatilia mawimbi ya sauti za redio kule msituni hadi alipomfumania Alpha akiwa katikati ya mwasiliano na Mdunguaji; na jinsi hatimaye alipogundua mchezo ambao Alpha alikuwa akitaka kumchezea naye akamuua.
Akamuelezea jinsi Mdunguaji alivyomtandika risasi ya kifua kabla ya kumtawanya kichwa Black Mamba...na jinsi alivyoonana naye macho kwa macho kabla hajaporomokea kule korongoni.
Swordfish alichoka!
“Hah! Wajua Baddi haya unielezayo ni mambo mazito sana yakhe! Waniambia kuwa ulionana uso kwa uso na Mdunguaji?”
“Kabisa bwana! Na yale macho...sijui tu…lakini yaliniletea hisia ambayo hakika siku zote huwa siwezi kuieleza...hisia ambayo inanifanya nipate picha ya kuwa...sijui bwana...lakini...napata hisia kama kwamba ni macho ambayo nitakutana nayo tena baadaye...sijui kwa nini lakini ni hisia ambayo imenikaa sana kichwani siku zote!”
Kimya kilitwala mle ndani kwa muda.
“Dah, Wallahi hii kesi ngumu shekhe wangu…tena ngumu kwel’kweli!”
Hatimaye Swordfish alisema, kisha akaendelea, “...haya, sasa ilikuwaje tena hata ukarejea hapa nchini baada ya muda wote huo? Ulikuwa wapi muda wote wa hapo kati?”
Ndipo Baddi alipomuelezea namna alivyofika Liberia na jinsi alivyokutana na Gilda, na Ghudia Al-Haddaad, na Twalal Ghailani...na jinsi wale walanguzi wa silaha haramu na almasi za damu walivyowasaidia hadi wakaweza kurejea
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
hapa nchini. Swordfish ndiyo alichoka zaidi!
“Loh! Hakika Baddi wewe ni mpiganaji haswa! Haya unielezayo ni mambo mazito sana na yanahitaji mtu mwenye ujasiri na dhamira ngumu kama wewe. Pole sana kaka!”
Baddi alitikisa kichwa taratibu kuafikiana naye, lakini hakusema kitu. Kule kusimulia yale matukio aliyokumbana nayo kulimkumbusha juu ya Gilda na unyonge ukamtawala upya.
“Anyway, hayo ndiyo mambo yaliyonikuta hadi nilipofika hapa nyumbani Swordfish. Na sasa nilipofika hapa ndipo nilipokutana na mashaka mengine… kwanza kuhusu mke wangu na halafu mashaka ya hawa jamaa tuliotoka kuwasambaratisha leo hii...”
“Dah! Kweli hali ni ngumu Baddi. Kwa upande wangu nilikuwa na taarifa za baadhi ya mambo ya hapa nyumbani ambayo mara tu uliponipigia nikataka tuonane ili nikueleze...”
“Najua. Uliniambia nisiwasiliane na mtu yeyote mpaka tuonane...”
“Ndiyo...”
“Lakini nasikitika wahka ulinishika nikashindwa kufanya hivyo rafiki yangu…hasa pale nilipomuona Shani...”
“Umeonana na Shani?” Swordfish alidakia kwa wahka.
“Ndiyo...” Baddi alimjibu huku akimtazama kwa macho ya kuuliza.
“Na umeongea naye...?” Swordfish aliuliza tena. Baddi aliafiki kwa kichwa.
“Aaa Patna! Si...n’likwambia usubiri bwana?” Swordfish alisema huku akiinama na kujishika kichwa. Baddi alizidi kushangaa.
“Kwani vipi...kuna...”
“Nieleze kwa ukamilifu Baddi, ni vipi ilikuwa mpaka ukaonana naye na mliongea nini!”
Baddi akamweleza kila kitu, na alipomaliza akamueleza jinsi aliporudi hotelini kwake na kukuta kuwa Gilda naye ametoweka.
“Na ni baada ya kupata ule waraka wa Gilda, ndipo nilipokuja hapa kuonana nawe, na kukutana na yale ya Mbegu Fupi na wenzake.” Baddi alimalizia.
Swordfish alishusha pumzi ndefu. “Hakika umepatwa na mitihani ya mfululizo ndugu yangu...pole sana.”
“Ah, ahsante bwana. Lakini…ni kipi kilichokufanya umake sana nilipokwambia kuwa nilishaonana na Shani? Kuna kitu maalum ambacho ningepaswa kukijua kabla sijaonana naye...?”
Swordfish alimtazama kwa muda, kabla hajamjibu.
MDUNGUAJI
sasa naona hakuna namna tena, mwenyewe umeshajionea na umeshajua...”
“Ndiyo
“Nimejua nini...kwamba kaolewa na Gaudence Amani?”
“Hapana Baddi...ni hilo...na kwamba siku hizi Shani amekuwa mwanamke mwenye ghadhabu sana!”
Baddi alibaki akimkodolea macho kwa mshangao. Alikumbuka kuwa hata yeye alipata wazo hilo pale alipomuona Shani akiegesha gari lake pale Shopper’s Plaza asubuhi ya siku ile.
“Kwa hiyo ndiyo ulitaka kuniambia kuwa siku hizi Shani ana ghadhabu sana? Hilo ndilo ulilotaka nilijue kabla sijaenda kuonana na naye? Hainiingii akilini!” Alimwambia mwenzake huku akimtazama kwa mashaka. Lakini kabla
Swordfish hajaongea, Baddi aliongezea, “Hii inamaanisha kuwa ulishawahi kuonana naye hata ukajua kuwa siku hizi ana ghadhabu, sio? Hebu nieleze zaidi, vipi ulionana naye tena baada ya pale kwenye “mazishi” yangu?”
Ndipo Meja Babu alipomwambia kuwa alipata kuongea na Shani kiasi cha siku tatu baada ya maziko yale, ambapo alikwenda nyumbani kwao kumuaga kabla ya kurejea Zanzibar kula pensheni yake.
“Wakati huo alikuwa okay, ingawa mwenye huzuni. Alinisihi nimueleze iwapo nilikuwa na imani kuwa kweli umekufa. Nilipata wakati mgumu kidogo, kwani sikuwa na namna isipokuwa kusisitiza msimamo wa jeshi kuwa umekufa, ingawa mwenyewe nilikuwa na mashaka sana juu ya hilo.” Swordfish alimwambia.
Akazidi kumpasha kuwa baada ya siku hiyo walikuwa wakiwasiliana kwa simu, na kila alipopata safari za kuja Dar alikuwa akimtembelea.
“So…ilikuwaje hata akaolewa na Meja Jenerali Gaudence? Ulikuwa wapi wakati hili likitokea? Mi’ sielewi kabisa Swordfish, kwani Gaudence nimjuaye mimi hajawahi kuwa na mke hata siku moja. Vipi aanze kuoa wakati huo?”
Baddi alihoji.
“Wallahi hilo ndilo kwangu lilikuwa na linabaki kuwa mtihani hadi leo Baddi!” Swordfish alimjibu, na kuendelea kumwambia kuwa kiasi cha kama mwaka mmoja tangu Baddi asemekane kuwa amekufa, Shani alimpigia simu na kumtaka ushauri juu ya ndoa yake na Gaudence.
“Mwaka mmoja?”
“Ndiyo. Nami nikapanda boti siku ileile jioni nikaja Dar kuonana naye. Niliogopa sana rafiki yangu, kwani ndani kabisa ya moyo wangu nilijua kuwa we’ hujafa Baddi…lakini ningemueleweshaje?”
Baddi alikuwa makini kusikiliza maelezo ya uhusiano baina ya aliyekuwa
Baddi...lakini
mkewe na aliyekuwa mkuu wake wa kazi. Swordfish alimwambia kuwa Shani
alimjuza kwamba Mej. Jen. Gaudence Amani amemuomba uchumba kwa lengo la kumuoa, naye hakuwa akijua afanye nini.
“Ah, atamuombaje uchumba ghafla tu? Walikuwa na uhusiano kabla?” Baddi alidakia.
“Nilimuuliza hilo swali na nikamtaka awe muwazi lakini alinijibu kuwa hakuwahi kuwa na uhusiano na Gaudence zaidi ya kwamba alikuwa akimtambua kama mkuu wako wa kazi... na kwamba alikuwa akimheshimu sana. Kwamba hata yeye mwenyewe alikuwa ameshangazwa sana na jambo lile.”
“Oh, Come ooon!” Baddi alisema huku akitupa mikono yake hewani kuonesha kuwa haamini maelezo yale.
“Ni kweli Baddi, Shani hakuwa akiongopa aliponiambia vile. Mi’ najua. Alikuwa akisema ukweli!” Swordfish alimwambia kwa uhakika, na kuendelea kumueleza kuwa baada ya hapo alimshauri asifanye haraka kabisa kufunga ndoa yoyote kwa kipindi kile, akimwambia kuwa ni mapema mno.
“Na hapo ndipo aliponibana kwa maswali iwapo nilikuwa najua kwamba mumewe, yaani wewe, hajafa na sitaki kusema! Ilikuwa ni hali moja ngumu sana kwangu Baddi. Yule mwanamke alikuwa akilia akitaka nimthibitishie kuwa mumewe hajafa, nami nikishindwa kufanya hivyo…alimuradi hali haikuwa nzuri kabisa. Mwisho nikamshauri amtake ushauri mkwewe pia, yaani marehemu baba yako.”
“Ikawaje?”
“Kilipita kipindi kirefu bila kuwa na mawasiliano, kisha nikampigia kumuuliza iwapo alipata kuongea na mkwewe juu ya hilo, na akaniambia kuwa baba alikataa kabisa suala hilo, na kwamba naye pia amekubaliana naye, hivyo amemkatalia Meja Jenerali Gaudence ombi lake la ndoa.”
“Ah…sasa ikawaje wakaona tena?” Baddi akauliza.
Swordfish akamwambia kwamba hakukuwa na mawasiliano mengine baina yao mpaka pale alipopata habari kuwa baba yake Baddi amepatwa na ajali na amefariki. Alikuja kuhudhuria mazishi, na akaonana na Shani, wakati huo tayari alikuwa ameshahama kutoka pale kwenye zile nyumba za shirika la simu na kuhamia kwenye nyumba aliyonunua baada ya kupata yale mafao ya “marehemu” mumewe.
“Miezi minne baadaye nikasikia Shani na Mej. Jen. Gaudence Amani wameoana!”
“Aaanh?”
“Ndiyo bwana! Hakika nilishangaa sana. Nikampigia simu kumuuliza
MDUNGUAJI kulikoni.”
“Enhe?”
“Akaniambia kuwa imebidi iwe vile. Miaka miwili imepita na alishakubali kuwa hakika mumewe amekufa. Hakuwa na sababu ya kumkataa mtu ambaye ameonesha kumpenda na kumjali kwa dhati.”
Baddi alitikisa kichwa kwa masikitiko.
“Nikamsisitiza awe makini na fedha zake, isije kuwa huyo bwana ananyemelea hizo pesa, lakini akanijibu kuwa Gaudence ana pesa zake na hana shida ya fedha.”
“Hilo ni kweli…nijuavyo jamaa yuko safi kidogo kifedha.” Baddi alisema.
“Ah, basi sikumfuatilia tena. Nikabaki na hofu yangu tu kuwa itakuwaje siku utakapoibuka, kwani mimi nilikuwa na imani kuwa hujafa Baddi. Lakini miezi mitatu tu baadaye nilikuja Dar kwa mambo yangu na nikakutana na Shani kwa bahati tu.” Swordfish alisema na kutulia kwa muda, Baddi akahisi kuna kitu kizito anachotaka kumwambia.
“Yule mwanamke alikuwa mtu tofauti kabisa Baddi! Alikuwa mwingi wa ghadhabu, alinijibu kimkato-mkato tu, kisha akaniaga harakaharaka na kuniacha nikiwa nimepigwa butwaa katikati ya barabara, yeye akiingia kwenye gari lake la kifahari na kutimua maresi kwa fujo!”
“Hah?”
“Ndiyo bwana! Sikuamini. Niliporudi Zenji, nikampigia simu. Majibu yake hayakuwa mazuri sana, na nikahisi hakupenda nilivyompigia simu. Sikuelewa kwa nini, lakini nilipojaribu mara nyingine mbili na kukutana na hali ile ile, ndipo nilipoanza kupata hisia kuwa kuna kitu hakikuwa sawa. Na ndiyo maana nilitaka kuongea nawe kabla…kukutahadharisha juu ya hali hii kabla hujaonana naye.”
“Kwamba ana ghadhabu sana siku hizi? Swordfish sikuelewi ujue!”
“Hapana. Si hilo. Nililotaka kukujulisha ni kuwa nina hakika kwamba chochote ambacho Shani alikitarajia kwenye ndoa yake na Meja Jenerali
Gaudence, hakukipata... au hakipo tena, na kwamba sasa hawezi tena
kutoka kwenye ile ndoa. Na hicho ndicho kinachomfanya awe mwingi wa ghadhabu namna ile!”
Baddi alitafakari hali ile kwa muda akiwa amefumbata kichwa chake kwenye viganja vya mikono yake.
“Dah, Swordfish! Haya mambo ni mazito sana kwangu. Sasa hata sijui nifanyeje katika hali hii. Vyovyote iwavyo Shani si mke wangu tena, na
Gilda sinaye tena, na...”
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“La, Baddi! Ya Shani na Gaudence si ndoa tena hivyo! Madhali weye umethibitika kuwa u-hai basi ile ndoa mara moja inabatilika. Shani anabaki kuwa mkeo tu! Kuna taratibu tu itabidi zifuatwe, lakini Gaudence ni lazima amuachie Shani arejee kwako! Na labda baada ya hapo wewe ukiamua kumuacha, au wenyewe mkiamua muachane, ndipo Shani atakuwa huru kuolewa na mtu mwingine!” Swordfish alimwambia.
“Alaa!”
“Ndivyo ati!”
Baddi alikaa kimya kwa muda akiitafakari habari ile. Kisha alimtazama Swordfish kwa makini.
“Au ni Meja Jenerali Gaudence ndiye aliyetuma watu wa kuja kuniua kwa kunigonga na gari siku ile nilipoingia nchini? Ili nife naye aendelee kuwa na Shani?”
Swordfish alimtazama kwa muda.
“Sasa kama ni hivyo, inamaanisha kuna pande mbili zinazosigana juu yako Baddi.” Swordfish alisema, na Baddi alipozidi kumtazama kwa macho ya kuuliza, akaendelea, “Upande mmoja ndiyo huo unaotaka ufe.”
“Na ndiyo wale waliotaka kunigonga kwa gari siku ile!” Baddi alidakia.
“Ndiyo! Na upande mwingine ndiyo huu unaotaka usife ili wakudai almasi zao.”
“Na ndiyo wale waliomgonga kwa gari yule aliyetaka kunigonga mimi siku ile na kumuua?” Baddi alidakia tena.
“Yeah, nadhani ni hivyo, ingawa ni dhana ngumu sana kuithibitisha kwa hapa tulipo.”
Kimya kilitawala tena mle ndani, kisha Swordfish akakivunja.
“Baddi...najua sasa hivi uko kwenye wakati mgumu sana. Mi’ nashauri kuwa hili jambo la mkeo tuliache kwa sasa. Tutalishughulikia tukiwa tumetulia. Kwa sasa nadhani tungeshughulika na hawa watu wanaokudai almasi ambazo sidhani kuwa unazo, kwani nina hakika almasi wanazodai si zile ambazo umeachiwa na Gilda.”
“No, si zile! Wale wanamaanisha zile almasi ambazo msaliti Alpha alikuwa akizizungumzia kule msituni!”
“ Exactly. Na hawa ndiyo wa hatari zaidi. Unadhani ni kwa nini wao wanaamini kuwa wewe utakuwa na zile almasi?”
Baddi alikaa kimya kwa muda. “Unajua nini? Alpha alikuwa anajua alichokuwa akikiongea siku ile kule msituni. Ni kweli yule mtu alikuwa ana almasi nyingi na kwamba kutokana na maelezo yake alikuwa ana
MDUNGUAJI ushirika na watu au mtu fulani katika jambo lile. Sasa huyu aliyekuwa akishirikiana naye, ndiye ambaye anadhani kuwa mimi ninazo au najua ni wapi zilipo zile almasi.”
“Kwa nini adhanie hivyo?”
“Sijui. Labda anadhani kuwa nilimuua Alpha ili nizichukue mimi zile almasi... na kutokana na jinsi akina Mbegu Fupi walivyokuwa wakinihoji, nadhani hivyo ndivyo haswa wanavyoamini. Mbegu Fupi alisema kuwa mimi najaribu kuwacheza shere na almasi zao, unakumbuka?”
“Naam, halafu akasema kuwa anajua ni nini kilitokea baina yako na Alpha.”
“Enheee, unaona bwana? Na baadaye alisema kuwa ni huyo bosi wake ndiye aliyemwambia aseme vile.”
“Lah! Wajua hii yaniletea picha gani Baddi?” Swordfish alisema kwa jazba.
“Nadhani najua, lakini hebu niambie…inakuletea picha gani?”
“Inaniletea picha ya kwamba wakati wewe na Alpha mnatupiana maneno kule msituni, pamoja na yule Mdunguaji, pia kulikuwa kuna mtu mwingine aliyekuwa akiyasikia yale majibizano yenu!”
“Hapana Swordfish. Mimi nadhani kuwa mtu pekee aliyekuwa akisikia maongezi yetu ni yule Mdunguaji haramu…na nadhani ndiye huyu ambaye sasa ananisaka akiamini ninajua kitu kuhusiana na mahala ambapo msaliti Alpha alificha hizo almasi.”
Kimya kilitawala kwa muda wakati wale watu waliosumbuliwa sana na Mdunguaji katika msitu wa Tumbudu nchini Sierra Leone miaka mitatu iliyopita wakitazamana huku ile kauli ya Baddi ikirindima vichwani mwao.
“Mnh! Baddi, yaani wataka kusema...”
“Sitaki kusema Meja...ninasema! Ninasema kuwa Mdunguaji tunaye humu nchini! Huyu Jairos Kabwe, au yeyote awaye ambaye alimtuma kibushuti aje anihoji juu ya hizo almasi anazoamini kuwa ninazo, huyo ndiye Mdunguaji wetu Swordfish...ndiye aliyeua wenzetu kama njiwa kule msituni, akiongozwa na msaliti Nathan!”
Swordfish alijikuta akiuma meno kwa hasira, lakini alijitahidi kudhibiti hasira zake na kuipa nafasi akili yake ifanye kazi.
“Hapana Baddi, hebu tufikiri kidogo. Nakumbuka kuwa ulisema kwamba wakati unaongea na Alpha kule msituni, yeye alikuwa akijaribu kuwasiliana na Mdunguaji kwa kiingereza kuwa akushambulie, au siyo?”
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Baddi aliafiki kwa kichwa.
“Sasa ina maana kuwa huyo Mdunguaji alikuwa ana uwezo wa kusikia kila mlichoongea kwa kutumia kifaa cha mawasiliano alichokuwa akitumia kuwasiliana na Alpha...” Swordfish alisema, na kuendelea, “...na kwa maana hiyo tayari atakuwa anajua kwamba Alpha hajakutajia mahala almasi zilipokuwa, na pia atakuwa anajua mazingira ya wewe kumuua msaliti yule!”
Baddi alikunja uso kwa tafakuri.
“Mnh! Unalosema lina uzito Swordfish…na sasa swali linalobaki ni kwa nini Mdunguaji alinipiga risasi kule msituni? Kama angekuwa anaamini kuwa Alpha alinitajia mahala almasi zilipo, si ningekuwa na faida kwake nikiwa hai kuliko mfu? Nadhani angetaka anipate nikiwa hai ili nimtajie zilipo…”
“Hakika kabisa! Na ndicho ambacho Cha Ufupi alichokuwa anajaribu kukuuliza kule mafichoni kwao…”
“Ah, Cha ufupi alitupeleka kule mafichoni ili kutuua Swordfish… wala hakutaka almasi!”
“ What?”
“Kabisa bwana…yule alianza kujitia kuulizia almasi pale tu lile bonge la mtu lilipofika eneo lile, naye hakutaka kabisa yule mtu mnene afike eneo lile!”
“Ah, we wajuaje yote hayo?” Swordfish alimuuliza, na Baddi akamulezea jinsi Cha Ufupi alivyosema pale yule mtu mrefu mnene alipotokea, na namna alivyoonekana kukosa uelekeo kwa muda kabla hajaanza kumuuliza kuhusu almasi.
“Duh, sasa hii inamaanisha nini yakhe? Mbona ni vigumu kuelewa?”
“Nahisi ni mtu mnene ndiye anayetaka almasi…na Cha Ufupi na bosi wake ambaye aliongea naye kwa simu pale mafichoni ndiyo wanaotaka kuniua…”
“Ah, lakni hata pale alipoongea na simu na huyo bosi wake… nilimsikia kabisa akisema ‘ Okay, don’t worry, leo tutapata almasi zetu...’
Sasa hapo utasema hakuwa akitaka almasi huyo?”
“Basi wakati anatamka maneno hayo alikuwa ameshakata simu… alikuwa anageresha tu pale…”
“Hah!” Swordfish alistaajabu.
“Ndiyo! Na nahisi alisema maneno yale kwa faida ya lile bonge la mtu lililoibuka pale bila ya matarajio yake! Cha ufupi alitupeleka kule
MDUNGUAJI
ili atuue tu, mtu mnene ndiye aliyeharibu mipango yake nakwambia!”
Jibu hili lilimjaza umakini Swordfish. “Mnh! Kwa mtazamo huo hoja yako inaweza kuleta maana…kwa hivi nadhani kumpata huyu mtu mnene na kumsaili vilivyo ni muhimu sana kwetu!”
“Nakubaliana na hilo…”
“Lakini…haiwezekani kuwa mtu mfupi ndiye alikuwa Mdunguaji kule msituni? Yule ni mpiganaji pia ujue...!” Swordfish alisema.
“No! Sio yule...” Baddi alikana kwa uhakika kabisa.
“Sawa, lakini bado sioni sababu ya huyu anayekusaka awe ndiye Mdunguaji wetu! Nadhani huyu ndiye aliyemtuma Mdunguaji...Mdunguaji ambaye mpaka sasa hatujui hatma yake!”
“Unachosema chaweza kuwa sawa Swordfish...lakini ukweli ni kwamba huyo mtu aliyetarajia kugawana na Alpha hizo almasi, hakupata mgao wake na hajui almasi zilipo. Mtu pekee ambaye anajua mahala zilipokuwa ni msaliti Alpha ambaye amekufa. Mimi ndiye nilikuwa mtu wa mwisho kuongea na Alpha kabla hajafa Swordfish, kwa hiyo kwa vyovyote huyu mtu anaamini kuwa mimi, kwa namna moja au nyingine ninafahamu mahala zilipo!”
“Lakini hiyo bado haimfanyi yeye awe ndiye Mdunguaji...anaweza kuwa ni mtu aliyemtuma Mdunguaji pia!” Swordfish alimwambia. Baddi alishusha pumzi ndefu na kufikicha macho kwa uchovu.
“Okay Swordfish, unaweza kuwa sahihi pia...lakini mimi nina imani kuwa huyu ndiye Mdunguaji. Sijui kwa nini lakini nina hisia hiyo... kama jinsi nilivyopata hisia kuwa nitakuja kuonana tena...au nilishaonana... na Mdunguaji yule siku ile nilipokuwa nikianguka korongoni nikiwa na risasi yake mwilini mwangu...”
“Hiyo inaitwa gut feeling...”
“ Yeah , nasi kama askari na wapiganaji wazoefu tumefundishwa kutodharau kabisa gut feeling... hisia zetu za mwanzo…juu ya kila kitu tunachokutana nacho katika medani za vita, siyo?”
“Kabisa partner...!”
“Basi hebu ifungue hiyo simu Swordfish, nadhani sasa najua ni nini cha kuongea na huyu mtu, yeyote awaye...yeye ndiye Mdunguaji wetu.”
Swordfish alimtazama mwenzake kwa macho ya kuuliza iwapo alikuwa na hakika na kile akisemacho, na Vampire alimthibitishia kwa kichwa. Swordfish akaiwasha ile simu.
Kule kwenye ile kambi ya wale watu wabaya, mtu mrefu mwenye tabasamu jepesi alikuwa amesimama katikati ya ule ukumbi wa chini ya ardhi ilhali ule uso wake ukiwa umekunjamana kwa tafakuri na mastaajabu wakati akiangalia maafa yaliyoachwa mle ndani na wale wapiganaji wawili hatari.
Aliwaangalia wale wafuasi wawili waliovunjwa miguu kwa risasi za Swordfish wakiwa wametawanyika sakafuni bila fahamu baada ya kuvujwa na damu nyingi, akapeleka macho yake kwa yule kibaraka mkorofi aliyepoteza fahamu, kisha akayarudisha macho yake kwenye ule mwili wa yule mtu mfupi uliolala bila uhai pale sakafuni. Alichutama na kupekua mifuko ya yule mtu mfupi aliyekuwa akimfuatilia kwa muda mrefu, na kukuta kuwa alikuwa na kondomu tu. Alisonya na kusimama wima huku akitikisa kichwa kwa masikitiko. Alitoa simu yake na kupiga tena ile namba aliyopiga hapo awali na baada ya muda alianza kuongea.
“Yes, hello…sasa mzee, hapa hali si nzuri…Baddi na mwenzake wameacha maafa makubwa, infact, mmoja wa hawa jamaa zetu muhimu kabisa ameuawa… yes, huyu namba mbili…mfupi huyu…jamaa sasa marehemu...na bila shaka ndiyo hatorefuka tena!”
Alisikiliza kwa muda, kisha akaongea, “…sasa ndiyo hivyo bosi, jamaa wamewaangamiza vibaya sana, na sasa wameondoka. Hii hali si nzuri kabisa, mi’ nadhani sasa muda wa kumdhibiti Baddi umefika mzee, aliyofanya mpaka hapa yanatosha…watu wanakufa!”
Alisikiliza kwa muda maelezo ya upande wa pili, akataka kusema neno, lakini mtu wa upande wa pili akawa bado anaongea, kisha naye akapata nafasi ya kuongea tena.
“Ni sawa kabisa usemayo mzee, lakini kwa hali hii, inaonekana kuwa hawa jamaa sasa wamepoteza subira, hatujui ni maafa gani zaidi yatatokea! We need to move in now!”
Alisikiliza tena maelezo au majibu ya upande wa pili kwa muda.
“Okay…sasa in that case, mi’ nashauri muda wa kuendelea kucheza kombolela na Baddi umekwisha…sasa tuingie in full force tuumalize huu mchezo…”
Lakini inaelekea mtu wa upande wa pili alimkata kauli kabla hajamaliza maelezo yake, na mtu mwenye tabasamu jepesi alibaki kinywa wazi akisikiliza kwa muda mrefu, kisha kwa unyonge kidogo alijibu, “Ah, Okay boss, okay…nilikuwa natoa ushauri tu, lakini kama hivyo ndivyo uonavyo that’s fine!
MDUNGUAJI
So…nini kifuate sasa?”
Baada ya kusikiliza kwa muda, akasema, “Okay…sasa basi mi’ ntatoka hapa, inabidi watumwe watu kuja kusafisha huu uchafu, nitatoa maelekezo jinsi ya kufika hapa nikiwa kwenye gari…huyu mmasai watakayemkuta huko nje hana ajualo wanaweza kumuacha tu…natumai kuna mtu anayeitazama ile hoteli ya Swordfish sasa hivi, sio?”
Alitulia kidogo na kusikiliza, kisha akamalizia. “Okay, sawa. Mi’ najua lazima watarudi pale, kwa hiyo nataka mtu mmoja awe pale, asifanye lolote. Aangalie tu! Nikifika ataniachia mwenyewe…”
Alikata simu na kuirudisha mfukoni huku akitukana peke yake kwa sauti ya chini. Ni wazi kuwa hakukubaliana na maelekezo ya huyo mtu aliyekuwa akiongea naye muda mfupi uliopita, na hakuwa na namna isipokuwa kufuata maelekezo yake.
Alimuendea yule kibaraka mkorofi na kujaribu kumzindua kwa kumchapa makofi mepesi mashavuni. Jamaa aligumia na kujitikisa kidogo lakini hakuonesha dalili za kuzinduka haraka kama alivyotaka.
“Sasa we’ mjinga itabidi utulie hapa hapa mpaka jamaa waje wakukute… halafu utaona cha moto!” Mtu mrefu alimwambia bila kujali kuwa hakuwa akimsikia, na wakati huohuo alitoa kamba ya nailoni kutoka kwenye mfuko wa suruali yake na kumfunga mikono na miguu. Baada ya kufanya hivyo aliwageukia wale waliovunjwa miguu na kuwatazama kwa muda.
“Nyie hamuwezi kwenda popote…” Aliwaambia kwa sauti yake nzito.
Alitoka nje ya ukumbi ule na bila kusita aliliendelea lile geti kubwa la kutokea nje ya wigo ule, akimpuuzia yule mmasai aliyejirundika kwenye kona ya ukuta ule akiwa hana fahamu. Pigo moja tu la nguvu alilomshushia shingoni kwa ubapa wa kiganja chake lilitosha kumpotezea fahamu mmasai yule kwa muda wa zaidi ya nusu saa. Alisukuma lile geti na kutoka nje, kisha akalifunga taratibu, na kutembea pole pole kuelekea pale alipoficha gari lake.
Chumbani kwa Swordfish pale hoteli ya Al-Uruba ile simu iliita. Baddi na Swordfish walitazamana kwa muda, kisha Baddi aliinua ile simu na kuitazama.
Private Number Calling.
“Jamaa yuko makini…namba yake haionekani, bloody kenges!” Baddi
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI alisema.
“Alaa? Sasa…?” Swordfish aliuliza kwa wahka.
“Si tatizo…huyu tumeshamnasa, we tulia tu…” Baddi alisema huku akibonyeza kipokeleo cha simu ile.
“Vipi wewe? Mbona simu imekuwa haipatikani kwa muda mrefu…is every thing okay…?” Sauti iliyokuwa upande wa pili wa simu ile iliongea kwa wahka, na Baddi alifinya sura kujaribu kuiweka sawa sauti ile fahamuni mwake na kujaribu kukumbuka iwapo alikuwa amepata kuisikia kabla ya siku ile. Lakini hilo lilikuwa gumu kutokana na kwamba simu ya yule mtu wa upande wa pili ilikuwa imewekwa kwenye mfumo wa spika, kiasi kwamba ile sauti ilikuwa ikisikika kama kwamba ilikuwa ikitokea mbali kidogo na wakati huo huo ikiingiliana na mvumo wa upepo na mawimbi mengine ya sauti.
“Everything is under control boss…” Baddi alimjibu yule mtu kwa utulivu mkubwa, huku akijaribu kuiweka sawa akilini mwake ile sauti bila mafanikio.
Mtu wa upande wa pili alisita, kidogo.
“Ka…Kabwe…ni wewe…?” Sauti iliuliza, na Baddi aliingiwa ubaridi kidogo kwa jina lile.
Kabwe!
Mtu mfupi aliwaambia lile bonge la mtu linaitwa Kabwe…Jairos Kabwe. Sasa hii nini tena? Lakini haraka sana akili yake ikaweza kugundua mchezo aliowafanyia yule mzinzi mfupi, hivyo akamjibu kwa utulivu ule ule.
“Hapana…Kabwe nimemdhibiti mahala salama kwa sasa, kwa hiyo kama shida yako ni Kabwe…” Baddi alimjibu yule mtu huku akimuona Swordfish akimtolea macho ya kuuliza huku akiwa amekunja sura kwa kutoelewa. Akamuashiria atulie huku akiendelea kuongea na yule mtu aliyekuwa upande wa pili wa simu ile. “…basi nakushauri ungeanza kufanya maandalizi ya jeneza moja fupi na nene, kwani muda si muda atakuwa marehemu…”
“Who…who are you…?” Sauti iliuliza. Lakini badala ya kumjibu Baddi aliendelea kuongea kwa sauti ile ile ya upole, “…lakini kama unataka kile ulichomtuma kibushuti wako aje kukifuata kwangu, basi mi’ n’nacho… tuongee biashara kistaarabu tu na sote tutafurahi, au unaonaje?”
E bwana we!
Ukimya ulitawala kutokea upande wa pili, kisha kwa sauti isiyo thabiti yule mtu wa upande wa pili aliuliza, “Ba…Baddi…? Ni Baddi Gobbos unaongea…?”
“The one and only!”
Jamaa akakata simu.
MDUNGUAJI
Baddi aliitupia kitandani ile simu na kubaki akimtazama Swordfish huku akitabasamu.
“Vipi…imekuwaje tena…?”
“Jamaa kakata simu...”
“Ama! Sasa…ndio basi tena!”
“Atapiga tu huyu…tena muda si mrefu!” Baddi alimwambia huku akipiga miayo na akijinyoosha, kisha akaendelea, “Sasa tumembana sehemu nzuri, hana ujanja…kama ni kweli anataka almasi kwangu, au anataka kuniua tu, atatufuata popote tutakapotaka.”
“Baddi unajiamini ghafla sana bwana! Unajua ulilofanya ni janga kubwa hili? Huyu mtu keshajua kuwa una simu ya mtu wake, halafu simu yenyewe haioneshi namba yake…tukimpoteza…”
“Hatumpotezi swahiba…mjinga atapiga tu huyu!” Baddi alimsisitizia rafikiye.
“Sasa…unadhani huyu ndio lile bonge la mtu?”
“No…huyu siye. Nadhani ni yule aliyempigia cha ufupi tukiwa kule mafichoni kwao…ambaye mbegu fupi alikiri kuwa ni mshirika wa lile bonge la mtu!”
Swordfish alitaka kusema kitu lakini muda huo huo ile simu ikaanza kuita tena. Baddi akamtazama Swordfish huku akitabasamu.
“Si nilikwambia?” Alimwambia rafikiye huku akiichukua tena ile simu na kuipeleka sikioni kwake.
“Vipi boss, simu iliishiwa pesa?” Alimuuliza yule mtu wa upande wa pili, akimaizi kuwa bado yule mtu alikuwa ameiweka simu yake kwenye mfumo wa spika.
“Nahitaji kuongea na Kabwe. Mpe simu niongee naye sasa hivi!” Sauti ilimwambia.
“La, hatuendi hivyo mzee! Tunazungumzia biashara, biashara ikikamilika nakupatia Kabwe wako, kama biashara haikamiliki basi namuua!”
“Sasa mi’ n’taamini vipi kama bado hujamuua?” Sauti iliuliza.
“Itabidi uamini nikuambiacho tu, vinginevyo huna namna ya kujua.”
Baddi alimjibu. Jamaa alibaki kimya kwa muda na Baddi aliweza kuhisi ni jinsi gani alivyomchanganya yule mtu, na aliifurahia hali hiyo.
“Mi’ nadhani unanilaghai...hauko wazi wewe!” Jamaa alifoka.
“Uko huru kudhani utakacho…” Baddi alimjibu kwa upole na hapo akabadili sauti na kumueleza kwa mkazo, “Sikiliza wewe. Mimi sina muda wa kutongozana hapa. Mali ninayo, sababu pekee ya kutaka kuongea nawe
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI ni kwa vile umeonesha nia na utashi mkubwa wa kuupata huu mzigo nilio nao, lakini kama unadhani huyu kibaraka wako ni muhimu kuliko hii mali basi endelea kumsubiri nami nifanye biashara na watu wengine ambao sasa najua kuwa wako wengi tu!”
Alikata simu na kumgeukia Swordfish.
“Okay Sword, nadhani huyu mtu anajaribu kupoteza muda huku akijiandaa kufanya lolote analodhani anaweza kulifanya kutuzidi kete.”
“Swadakta..! Au anajaribu kuhakikisha iwapo kweli tunaye huyo Kabwe... na kama kweli Kabwe ndiye yule mzinzi aliyetunywea sumu kule, basi muda si muda atajua kuwa tayari ameshakufa.”
“Hilo si tatizo. Huyu ananitaka mimi...iwe ni kuniua au kunidai almasi, hivyo kibushuti awe hai au amekufa si muhimu kwake…huyu anapoteza muda tu…sijui kwa nini!”
“Unadhani huyo Kabwe ndiye yule mtu mfupi mtembea na kondomu?”
Swordfish aliuliza.
“Inaweza kuwa hivyo…nahisi kuwa jamaa alituchezea mchezo tu pale. Badala ya kututajia jina la bosi wake akatutajia jina lake, akijua kuwa sisi hatulijui. Ndio maana akasema hatutampata tena huyo Kabwe!”
Swordfish alitikisa kichwa kwa mastaajabu. “Kama atakuwa amefanya hivyo basi jamaa atakuwa maluuni kweli kweli!”
“Na sasa ni marehemu...”
“Yeah...” Swordfish alisema na kimya kilitawala kwa muda mle ndani. Baddi alionekana kuzama kwenye tafakari nzito, kisha akamgeukia Swordfish.
“Huyu jamaa anajaribu kututega kwa namna fulani...tusimpe nafasi kabisa!
Mpaka hapa tayari tumemdhibiti, kwa sababu yeye ndiye anayetuhitaji, na si vinginevyo…na hiyo ndio sumu itakayomuangamiza.”
“Ni kweli kabisa, kwa hiyo mi’ naona hapa cha kufanya ni kuua kambi… tuihame hii hoteli, kwani haifai tena!”
“Wazo zuri meja. Huyu tutacheza naye kwa simu tu, kwa sasa lets get out of here!”
Swordfish alipiga simu mapokezi na kuwaomba wamtayarishie bili yake kwa maelezo kuwa alikuwa amepata mwenyeji hivyo anahamia kwa mwenyeji wake. Alirejesha simu mahala pake na kumuoneshea Baddi alama ya dole gumba.
“Okay, sasa hapa Sword, ujue tunapambana na mtaalamu wa mambo haya…bado nina hisia kuwa huyu niliyeongea naye kwenye hii simu ndiye Mdunguaji wetu, na kama ni hivyo, lazima naye atakuwa anazijua
MDUNGUAJI
mbinu za medani, hivyo yatupasa tuwe makini maradufu kuanzia sasa.”
“Okay, sasa wataka tufanyaje? Mi’ ni-tayari kwa safari.”
“Sawa, hivi ndivyo ninavyoshauri tufanye...” Baddi alisema, na kwa dakika kumi zilizofuata walipanga mikakati yao juu ya namna ya kumdhibiti yule adui yao asiye na sura mpaka kufikia muda ule. Na wakati wakiendelea kupanga jinsi ya kumdhibiti adui yule hatari, ile simu ilianza kuita tena.
Baddi hakuipokea.
Dakika tano baada ya kukamilisha mipango yao, mtu aliyekuwa ndani Suzuki Escudo iliyokuwa imeegeshwa nje ya hoteli ya Al-Uruba alimwona Swordfish akitoka nje ya ile hoteli akiwa na begi lake la safari. Yule mtu alikaa vyema kwenye gari lake na kuzidi kuongeza umakini kwenye gazeti alilokuwa akilisoma, gazeti ambalo alikuwa amelitoboa kidogo na alikuwa akimchungulia Swordfish kupitia kwenye tundu lile. Alitoa simu na kumpigia tabasamu jepesi.
“E bwana hapa kuna jambo ambalo silo. Swordfish anatoka hotelini peke yake akiwa na begi lake la safari…bila shaka anahama hoteli...”
“Unamaanisha nini anatoka hotelini peke yake?” Sauti nzito ya tabasamu jepesi ilivuma kwenye simu yake.
“Namaanisha Baddi hayuko pamoja naye.” Na hata pale alipokuwa akijibu swali lile alimuona Swordfish akiingia kwenye moja ya teksi zilizokuwa nje ya ile hoteli.
“Na sasa ameingia kwenye teksi!” Jamaa aliripoti.
“Na bado Baddi hajatoka humo hotelini?”
“Yeah! Baddi hajatoka. Sasa naona teksi ya Swordfish inaondoka. Niifuatilie?”
“No! Baddi ndiyo wa muhimu zaidi. Hao jamaa ni wapiganaji mahiri, hiyo ni mbinu tu wanatumia.”
“Jamaa anaondoka hivyo! Kwa hiyo nimuache?” Mwenzake alimkatisha kwa uharaka.
“Muache! Mfuatilie Baddi tu, nina hakika atatoka muda si mrefu... huyo ndiye atakayetufikisha mwisho wa mchezo huu.” Tabasamu jepesi alijibu.
“Okay boss!” Jamaa alijibu na kujiweka sawa kwenye gari lake akitazama kule hotelini. Jambo ambalo hakulijua ni kuwa wakati yeye akiongea na mwenzake huku akimfuatilia Swordfish, Baddi Gobbos alikuwa
akitokea kwenye mlango mdogo wa ubavuni mwa hoteli ile akiwa amevaa
MDUNGUAJI
nguo alizoazima kutoka kwa Swordfish ilhali zile alizokuwa amevaa hapo awali, zikiwa kwenye begi la Swordfish.
Dakika ishirini na tano baadaye ile simu iliita tena. Wakati huu Baddi alikuwa ameketi kwenye mgahawa maarufu jijini uliopo mtaa wa Lumumba. Huku uso wake ukiwa umefanya tabasamu dogo aliipokea ile simu.
“Unanichezea Baddi.” Ile sauti ilisema.
“Narudisha kile ambacho wewe umekuwa ukinifanyia tangu nirejee hapa nchini.”
“Unazo Almasi hapo?”
“Zipo mahala salama. Kama unazitaka tunaweza kukubaliana na kumalizana bila kulazimika kumwaga damu. Tatizo la rafiki yako Kabwe ni kwamba alikuwa anataka nimpe bure!”
“Kwa hiyo ndio ukamuua?”
“Hapana, sijamuua… nimemdhibiti tu. Lakini kama na wewe unazitaka bure pia nitakudhibiti kama nilivyomdhibiti yeye!”
“How much?”
“Nini sasa?”
“Eenh?”
“How much nini? Almasi au bei ya almasi?”
“Oh, nilikuwa namaanisha bei ya hizo almasi…unataka kuniuzia kwa kiasi gani?”
“Mi’ nilidhani wewe ni mfanyabiashara mkubwa wa almasi, kumbe sivyo? Kabwe muongo sana!”
“Stop playing games with me Baddi!” Jamaa alifoka.
“Sifanyi maskhara hata kidogo! Utaulizaje bei wakati mzigo hujauona? Kama nina kijiwe kimoja tu cha almasi halafu nikataka milioni mia mbili utanipa?” Baddi alimuuliza.
Kimya kilitawala.
“Okay, you are right. Of course nahitaji kuuona huo mzigo, lakini kwanza nataka nisikie bei yako angalau nitakapouona niweze kupima iwapo bei inaendana na mali yenyewe!” Sauti ya upande wa pili ilijibu.
“Okay, tutafanya hivi…tuonane nikuoneshe mali. Kisha tutawasiliana tena na kupatana bei, tukikubaliana tunapeana maelekezo juu ya sehemu ambapo mali na pesa zitabadilishana mikono, unasemaje?”
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Kimya kifupi kilichukua nafasi, kisha jamaa akamjibu.
“Okay. Sasa nataka uje...”
“Hatuendi hivyo mzee! Mimi ndiye ninayepanga mahala pa kukutania bwana siyo wewe! Na naomba nikusisitizie jambo moja… wewe umeshaonesha nia mbaya kwangu, kwa hiyo nataka uje peke yako na kusiwe na ujanjaujanja wowote wa kijinga, upo?” Baddi alisema.
“Unadhani nitamtuma mtu kuja kuona mali kama hiyo? Nitakuja mwenyewe.”
“Okay good. Sasa si unaijua Motel Agip?” Baddi alimuuliza.
“Mo...Motel Agip…? Ndiyo naifahamu…unataka tukutane hapo?”
“Ndio. Pale kuna sehemu ya maegesho ya magari iliyokuwa juu ya jengo lile. Tukutane pale ndani ya saa moja kutoka sasa, si zaidi ya hapo na si kabla ya hapo. Ukikosa hii biashara imefutwa…na uje peke yako. Ukifika pale utanipigia simu na nitakuelekeza utaniona vipi!” Baddi alimjibu na kukata simu. Alishusha pumzi kwa muda, kisha akapiga namba nyingine ambayo aliihifadhi kwenye simu ile kabla hajatoka pale Al-Uruba.
“Swordfish!” Sauti iliyopokea upande wa pili ilisema.
“Mtego tayari. Uko eneo la tukio?”
“Yeah...”
“Good. Nakuja!” Baddi Gobbos p.a.k. Vampire alikata simu na kuizima kabisa.
Nusu saa baada ya Swordfish kutoka pale Al-Uruba, tabasamu jepesi aliegesha gari lake nje ya ile hoteli na kwenda moja kwa moja hadi pale kwa yule jamaa aliyekuwa ndani ya Escudo. “Vipi?”Alimuuliza.
“Baddi hajatoka bado.”
“Mpaka sasa?” Tabasamu jepesi aliuliza, jamaa akaafiki kwa kichwa. Mtu mrefu alimtazama kwa muda kisha akaenda kule hotelini. Aliingia ndani na kuangalia mazingira ya pale mapokezi ambapo pia kulikuwa kuna sehemu ya watu kupata maakuli. Baddi hakuwepo. Aliona ujia mwembamba ulioelekea upenuni mwa hoteli ile naye akaufuata. Ule ujia ulikuwa unaelekea nyuma ya hoteli ile na pia ulikuwa ukitokea kwenye kijigeti chembamba. Alikisukuma kile kijigeti na kutokea tena kule barabarani nje ya ile hoteli. Kutokea pale alipokuwa aliweza kuliona lile gari la mtu wake kutokea kwa nyuma.
“Bloody fool!” Alijisemea mwenyewe na kurudi pale kwenye lile gari.
MDUNGUAJI
“Umempoteza Baddi wewe, shenzi taipu!”Alimkemea.
“Ha! Kivipi wakati mi’ n’likuwa na...”
“Kuna mlango wa pembeni kule ambao wewe umeupa kisogo kabisa… sasa jamaa katoweka!Si nilikwambia kuwa hawa watu sio wajinga wewe!”
Jamaa alibaki akigwaya tu.
“Okay, ondoka hapa, huna lolote la maana ulilofanyal” Tabasamu jepesi alimfukuza yule jamaa na kusonya. Alirudi pale mapokezi na kumuonesha yule mtu wa mapokezi picha ya Baddi Gobbos.
“Huyu jamaa alikuwa hapa hotelini leo hii. Unajua yuko chumba gani?”Alimuuliza. Mhudumu aliitazama ile picha na kutokana na uso wake, tabasamu jepesi alijua kuwa ameitambua ile sura.
“Kwa kawaida huwa hatutoi habari za wapangaji wetu kwa mtindo huo, lakini kwa kuwa huyu si mpangaji wetu nitakwambia. Jamaa kaondoka kama nusu saa iliyopita. Alikuja kumtembelea mwenzake ambaye ndiye alikuwa mpangaji wetu, lakini naye amerudisha chumba na kuondoka.” Mhudumu alimjibu kwa kirefu. Tabasamu Jepesi alitoka nje ya hoteli ile akiwa amefura. Siku hizi tabasamu lake limekuwa kilisalitiwa sana na vituko vya Baddi Gobbos.
Aliingia kwenye gari lake na kuondoka. Kwa muda wa kama dakika kumi na tano hivi alikuwa akijiendeshea ovyo tu jijini, bila uelekeo maalum.
Baddi katoweka!
Hatimaye aliegesha gari kando ya barabara na kutulia nyuma ya usukani, akitazama kila apitaye na kila gari lipitalo, kama kwamba kwa kufanya vile angeweza kumuona tena Baddi Gobbos.
Baddi hakuonekana.
Alitaka kumpigia simu mkuu wake wa kazi lakini alihofia kuwa angeshindwa kuongea naye vizuri kutokana na ghadhabu alizokuwa nazo wakati ule. Yeye alishauri vizuri kabisa kuwa wamdhibiti Baddi muda ule mauaji ya yule mtu mfupi yalipotokea, lakini hoja yake haikutiliwa maanani, na sasa mambo yameharibika…ni vipi wataweza kumpata tena kirahisi kama wakati ule?
Baddi alijipeleka mwenyewe pale makao makuu ya jeshi kama jinsi ambavyo wao walitaraji pindi walipogundua kuwa yu hai na amerejea nchini, lakini sasa baada ya matukio yote tangu pale nje ya makao makuu ya jeshi hadi kule Pugu, ni wazi kuwa Baddi hatojipeleka tena pale makao makuu ya jeshi kama alivyofanya wakati ule.
Sasa tunaanzia kumpata wapi?
Muda huo simu yake ya kiganjani iliita. Bila hata ya kutazama ile simu alijua kuwa aliyekuwa akipiga ni mkuu wake wa kazi kutokana na muito aliouteua
maalum kwenda sambamba na namba ya simu ya mkuu wake. Alikunja uso maradufu na kuipeleka ile simu sikioni kwake.
“Yes boss.”
Alisikiliza maelezo ya upande wa pili akiwa kimya, kisha ilipomdhihirikia kuwa hakuwa na budi naye kuongea baada ya mkuu wake kumaliza ya kwake, alisema, “Sasa hilo halitawezekana tena kwa sasa mkuu, na halitawezekana kwa sababu hivi tuongeavyo Baddi Gobbos ametoweka!”
“What do you mean ametoweka?” Mkuu wake alimuuliza.
“Niliacha maelekezo kuwa hoteli aliyofikia Swordfish iangaliwe mpaka nitakapofika jijini kutoka kule Pugu boss…actually nilikuachia wewe maelekezo hayo.” Tabasamu Jepesi alisema, akishindwa kabisa kuficha kukereka kwake na namna mambo yalivyokuwa yakienda.
“Nami nikatuma kijana aende huko haraka sana, pamoja na maelekezo kamili juu ya nini cha kufanya akiwa huko!” Mkuu alijibu.
“Ni sawa…tatizo yule fala kaenda kule kuangalia mlango wa mbele tu, na kumuacha Baddi akimtoka kwa mlango wa kichochoroni!Hawa watu sijui watajifunza lini kuwa makini mzee!” Mzee wa matabasamu alisema, ingawa sasa ingeleta maana zaidi kama angeitwa mzee wa kununa. Kimya kilitawala kwa muda.
“Lah!” Hatimaye mkuu wake alimaka, na kuendelea, “...lakini kwa Baddi hilo ni la kutarajiwa. Hakupewa jina la Vampire hivi hivi tu…jamaa ni karibu ya mzuka kweli ujue!”
“Na hiyo ndio ilikuwa moja ya sababu za kumdhibiti pale tulipoweza kufanya hivyo boss! Sasa mzuka ndio umeshayeyuka hivi...sijui utaibukia wapi na lini tena!” Tabasamu jepesi, bila ya uso wa tabasamu, alisema. Kimya kilichukua nafasi tena, kisha mkuu wake wa kazi akamwambia jambo ambalo lilirejesha tabasamu usoni kwake.
“Anyway, hilo sasa si tatizo tena. Nadhani najua ni wapi ambapo Baddi atapatikana leo hii, na ndio maana nimekupigia.”
“E bwana we!” Tabasamu jepesi alimaka huku uso wake ukichanika kwa tabasamu dogo. “Yes! Na ndio maana ulipopokea simu nilikwambia kuwa sasa nataka suala la Baddi lifikie tamati.”
Tabasamu liliongezeka kidogo. “Kwa hiyo unamaanisha kuwa sasa tunaingia in full force?”
“Inaweza kuwa hivyo, ila sina hakika...ndio maana nataka uje haraka, hatuna muda wa kupoteza!”
“Niko njiani boss!” Tabasamu jepesi alisema na kukata simu, muda huo
MDUNGUAJI
huo akiwasha gari na kuingia barabarani kwa kasi, akisababisha honi na breki za ghafla nyuma yake. Huku uso wake ukiwa umetapakaa na tabasamu jepesi, mtu mrefu aliendesha gari kwa kasi, akipuuzia nyuso za mshangao kutoka kwa madereva wenzake.
Baddi Gobbos alikwea ngazi kuelekea kwenye maegesho ya magari yaliyo juu ya jengo lililoungana na lile la Motel Agip. Ingawa amekuwa nje ya nchi kwa muda mrefu, Swordfish aliweza kumhakikishia kuwa lile jengo bado lilikuwepo na kwamba halikuwa na mabadiliko makubwa katika ile miaka mitatu aliyokuwa nje ya nchi, ukachilia mbali badiliko la rangi na mandhari yaliyolizunguka.
Moyo ulikuwa ukimwenda mbio na msisimko wa ajabu ulimtambaa mwilini, msisimko ambao huwa unampata pindi awapo katika medani za vita, katika misitu minene yenye kila aina ya mashaka. Msisimko aliokuwa nao siku zote alizokuwa akihaha na wenzake katika ule msitu wa Tumbudu nchini Sierra Leone miaka mitatu iliyopita. Msisimko uliotokana na hofu ya risasi isiyo hadhari kutoka kwenye bunduki ya muuaji hatari mwenye kuvizia. Msisimko uliotokana na hofu ya kifo kutokana na risasi ya mdunguaji.
Ni msisimko ule ule ndio aliokuwa akiuhisi wakati akizikwea zile ngazi, akiwa sio msituni tena, bali katikati ya jiji la Dar es salaam nchini Tanzania. Kadiri alivyokuwa akizikwea zile ngazi ndivyo ule msisimko ulivyozidi na ndivyo hisia zake za hapo awali kuhusu yule mdunguaji zilivyozidi kumuwia sahihi…kuwa iko siku atakuja kuyaona tena
(au alishawahi kuyaona?) yale macho ya yule mdunguaji aliyoyaona siku ile kabla hajaangukia korongoni, kule Sierra Leone.
Alifika katika eneo la maegesho la kati na kutulia kwa muda akiwa amejibanza kwenye ngazi nyembamba zilizowawezesha wale walioegesha magari yao kule juu kuteremka na kuingia ndani ya jengo lile lenye shughuli nyingi. Kote kulikuwa kimya kabisa, na hakukuwa na magari mengi kwa muda ule. Alipapasa bastola iliyokuwa kiunoni kwake, ambayo aliwapora wale majambazi waliojaribu kuwateka hapo awali, na akahisi kujiamini.
Leo ni leo.
Zilikuwa zimebaki dakika ishirini itimie saa moja tangu aongee na yule
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI hasimu wake.
Alikuwa amemwambia yule mtu aliyeongea naye kwenye simu kwamba wakutane kwenye eneo la juu kabisa la maegesho yale, na zile ngazi ndizo zingemfikisha kwenye eneo la miadi, lakini alitaka kuhakikisha usalama wa mazingira yote ya eneo lile kabla hajafika kule alipotakiwa kukutana na adui yake. Alichutama nyuma ya moja ya nguzo nyingi zilizokuwa eneo lile akiwa ameiegemea kwa mgongo wake. Mkono wake ukiwa umetulia kwenye kishikio cha bastola aliyoichomeka kiunoni kwake, alichungulia kule kwenye lile eneo la maegesho, na hakuona mtikisiko wala dalili zozote za uhai. Aliamua kusubiri pale kwa dakika tano zaidi. Mara alisikia mvumo wa gari lililokuwa likipanda eneo lile na aliona gari aina ya Mitsubiri RVR likiegeshwa, kisha mwanadada mmoja aliyekuwa amevaa nguo za kiofisi aliteremka na kuingia kwenye mlango uliomuingiza ndani ya jengo lile.
Alisubiri mpaka zile dakika tano zitimie, na alipoona kuwa hakukuwa na harakati nyingine yoyote eneo lile, aliinuka na kukwea ngazi kuelekea kule juu. Huko alikuta magari mawili tu yaliyokuwa yameegeshwa kwenye eneo lile, moja likiwa ni Landrover Discovery, jingine likiwa ni aina ya Benz. Eneo Iote lilikuwa kimya kabisa. Upepo mwanana ulikuwa ukipiga eneo lile lililozungukwa na ukingo mfupi ilhali sehemu ya juu ya uzio ule ikiwa wazi.
Sasa zilikuwa zimebaki dakika kumi kabla muda wa kukutana na adui yake haujawadia. Kutoka pale alipokuwa, alijilaza chini na kuchungulia chini ya vungu za yale magari mawili na kuona kuwa kulikuwa salama.
Kwa usiri mkubwa, aliisogelea ile Landrover Discovery na kuchungulia ndani yake. Hamna mtu. Aliisogelea ile Benzi na kuchungulia ndani yake kwa usiri mkubwa. Nayo haikuwa na mtu ndani.
Kwenye kona moja iliyokuwa imeelekezana moja kwa moja na njia itumiwayo na magari yote yapandayo pale juu, kulikuwa kuna mapipa mawili ya taka, naye akaenda kujibanza nyuma ya mapipa yale. Kutokea pale alikuwa na uwezo wa kuona kila gari litakalopandisha pale juu na wakati huo huo aliweza kuona kila aliyeingia kwenye eneo lile kutokea kule kwenye zile ngazi alizotumia kufika pale juu. Aidha aliweza kumuona mtu yeyote atakayetoka ndani ya jengo lile na kuingia pale kwenye lile eneo la maegesho kutokea
kwenye mlango kama ule aliotumia yule mwanadada kule chini.
Dakika saba kabla ya muda wa kukutana na adui yake.
Sasa ule msisimko aliokuwa nao ulikuwa umemezwa na utulivu mkubwa. Hakuwa na papara hata kidogo, kwani sasa alikuwa amefikia kwenye ile saa ya ukweli. Saa ya kumjua mbaya wake na kufikisha tamati kisa kile
MDUNGUAJI
kilichomuandama tangu Sierra Leone hadi hapa nchini.
Dakika tano kabla ya muda wa kukutana.
Aliitoa ile simu iliyokuwa mfukoni mwake na kuiwasha, kisha hapo hapo akabadili muito wa simu kwa kutoa sauti na kuweka mzizimo. Hakutaka kabisa kelele ambazo zingeweza kusaliti mahala alipo pindi lie simu ikiita...kama itaita.
Mara akasikia mvumo wa gari likipandisha pale juu. Akiwa makini na bastola yake mkononi huku ameshika ile simu kwa mkono wake wa kushoto, aliishuhudia Toyota Mark II Baloon nyeusi ikiingia na kuegeshwa katikati ya ule uwanja, mbali na yale magari mengine mawili yaliyokuwa pale. Umakini ukimzidi, Baddi alibaki akiwa amejibanza nyuma ya yale mapipa, akitaka kuona ni nani atakayetoka ndani ya lile gari.
Je, ndiye mtu aliyekuja kuonana naye?
Alihamisha macho yake kutoka kwenye lile gari na kuitazama ile simu iliyokuwa mkononi mwake. Simu ilikuwa kimya.Alirudisha macho yake kule kwenye ile Baloon. Hakuna mtu yeyote aliyeteremka.
Simu ikaanza kuzizima.
Moyo ukimpiga, macho akiwa ameyakaza kwenye ile Baloon, aliipeleka ile simu sikioni kwake.
“Ongea!” Alisema, na wakati huo huo aliona mlango wa dereva wa lile gari ukifunguliwa na mguu mmoja uliokuwa umevaa suruali nyeusi na kiatu ghali sana cha ngozi uliteremshwa na kukanyaga sakafu ya maegesho yale.
“Umeshafika eneo la tukio?” Sauti iliuliza kupitia kwenye ile simu, bado simu ya muongeaji yule ikiwa katika ule ule mfumo wa spika kama ilivyokuwa mara zote alizowahi kuongea naye. Hapo aliliona lile bonge la mtu lililowatoroka kule mafichoni walipopelekwa na hayati mbegu fupi likiteremka kutoka kwenye ile Baloon na kutazama huku na huko ndani ya eneo lile. Baddi alifinya uso kwa umakini wakati akimtazama yule mtu, moyo ukimuenda mbio.
Lakini mbona hana simu?
“Wewe ndiye unayetakiwa ufike mahala nilipokuelekeza, na maelekezo yangu yalikuwa ni kwamba ukifika eneo la tukio ndipo nitakuelekeza ni jinsi gani tutaonana, sasa umeshafika?” Baddi aliuliza huku akimuona yule mtu mnene akiufunga mlango wa ile Baloon, na akiweka mkoba maalumu wa kiofisi , juu ya paa la lile gari. Kisha kwa mwendo wa haraka yule mtu aliondoka na kupotelea ndani ya lile jengo, akiuacha ule mkoba pale juu ya gari.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Ala! Hii nini sasa?
Ndani ya nukta ile alijikuta katikati ya maamuzi mawili, aidha alifuate lile bonge la mtu, na kwa kufanya hivyo asaliti uwepo waje mahala pale, au aendelee kujificha pale nyuma ya mapipa akiongea na yule mtu wa kwenye simu.
“Mimi nimeshafika, ndio maana nakuuliza iwapo nawe umeshafika!” Sauti ilimwambia. Baddi alijitahidi kutazama eneo lile akiwa amejawa wahka. Hamna mtu. Kimya kabisa!
“Aam, Okay…sawa. Sasa nataka usimame katikati ya huo ukumbi wa maegesho ya magari, na nataka mikono yako yote miwili iwe mahala inapoweza kuonekana kirahisi, ama si hivyo...” Baddi alianza kusema lakini sauti ya kwenye simu ilimkatisha.
“Hapana Baddi, mi’ nimeshafanya kila ulilotaka, sasa naona umefika wakati na wewe kufanya vile nitakavyo mimi ili twende sawa...”
“Usin’letee mchezo wewe, unasikia? Ni wewe ndiye mwenye shida na hii mali niliyo nayo, kwa hiyo...”
“Una hakika Baddi?” Sauti ilimkatisha tena. Baddi hakuelewa.
“Whaat?”
“Nakuuliza una hakika kuwa ni mimi tu ndiye mwenye kuhitaji kutoka kwako?”
“Unaongea vitu gani wewe sasa?” Baddi alimjia juu, muda wote akitembeza macho eneo lile akijaribu kumtafuta.
Hamna mtu.
Taratibu alijitoa nyuma ya yale mapipa na kuanza kuinyatia ile Baloon .
“Nakuuliza unaongea vitu gani?” Alimuuliza tena yule mtu huku akizidi kuisogelea ile Baloon.
“Hapo ulipo kuna Baloon nyeusi. Juu yake nimeacha Briefcase...”
Sauti iliongea na Baddi aliuma meno kwa hasira. Yaani kumbe hawa jamaa wananichezea mchezo!
“Lakini wewe siye uliyeacha ile briefcase!” Baddi alimaka.
“ No big deal! Huyo ni patna wangu na usipoteze muda…”
Jamaa alimng’akia, kisha akaendelea, “…ndani ya hiyo Briefcase nimekuwekea thamani inayotosha kukushawishi kunifanyia lolote nitakalo!”
Sauti iliendelea kusema.
“Whaat?” Baddi alimuuliza kwa kutoamini.
“Ndio. Sasa iendee ile Baloon, na uone kiasi nilichokutangulizia ndani
MDUNGUAJI ya hiyo briefcase…naamini kitatosha sana kuanzia mazungumzo.” Jamaa alimwambia na hapo hapo akakata simu.
Baddi alichanganyikiwa. Mtego wake sasa ulikuwa unamgeukia yeye mwenyewe. Kwa nini huyu mtu anaonekana kujiamini namna hii? Ndio vitimbi alivyokuwa akivihofia kutoka kwa huyu adui yake hivi!
Kutokea pale alipokuwapo, alijaribu kuona iwapo ndani ya lile gari kulikuwa kuna mtu yeyote lakini vioo vya lile gari vilikuwa vimewekwa weusi, yaani tinted .
Alitazama tena huku na kule ndani ya eneo lile. Bado eneo . lilikuwa pweke. Alirejesha ile simu mfukoni, na kuikamata vizuri bastola yake. Alipiga hatua moja kubwa na kuukamata mlango wa nyuma wa ile Baloon, na huku akiombea ule mlango usiwe umekomewa kwa ndani, aliuvuta kwa nguvu. Mlango ulifunguka alielekeza bastola yake mle ndani tayari kumshurutisha yeyote atakayekuwemo atulie kama alivyo.
Patupu!
Alisita kidogo tu, kisha akajitupa kwenye kiti cha nyuma ndani ya lile gari. Kiti cha abiria kule mbele kilikuwa kimelazwa nyuma na mtu mmoja aliyevaa kofia pana ya pama alikuwa amelala chali kwenye kile kiti.
“Tulia hivyo hivyo!” Alifoka huku akiwa ameweka mdomo wa bastola utosini kwa mtu yule. Yule mtu hakutikisika wala kutoa sauti yoyote.
“Oyaa! Naongea na wewe...!” Alifoka tena na alipoona hapati jibu, mwili ulimuingia baridi.
Jamaa kanitegea maiti!
Alitoka haraka nje ya lile gari huku akitaraji kusikia ving’ora vya gari za polisi vikielekea eneo lile muda wowote. Jamaa kampakazia kesi ya mauaji, bloody coward! Alichukua ule mkoba ulioachwa juu ya lile gari na kuchutama kando ya lile gari huku akitazama pande zote na kuona bado kulikuwa kimya. Aliufungua ule mkoba na kutazama kile kilichokuwa mle ndani.
Hah!
Alijikuta akiachia mguno pasi kupenda. Hakuamini kile alichokiona ndani ya ule mkoba, kwani badala ya pesa, kulikuwa kuna picha moja ya ukubwa wa kama inchi tano kwa saba hivi. Ile picha ilimuonesha aliyekuwa mkewe Shani, akiwa amegusanisha sura na mtoto wa kike apataye miaka minane hivi, wote wakiwa wanaichekea kamera. Hakuwa na shaka kabisa kuwa yule mtoto alikuwa ni binti yake Claudia.
E Bwana we!
Aliikwapua ile picha na kuitazama kwa kihoro. Na hata pale alipoishika ile
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI picha, aligundua kuwa ilikuwa imebandikwa picha nyingine kwa nyuma, hivyo akaigeuza. Sura ya Gilda ilikuwa ikimtazama kutoka kwenye ile picha ya pili iliyobandikwa mgongo kwa mgongo na ile ya mkewe na mwanawe.
Loh!
Alichanganyikiwa, kwani mara moja alielewa ni nini yule adui yake alikuwa akimfanyia. Aliziweka zile picha mbili zilizobandikwa pamoja mfukoni mwake na kufungua mlango wa dereva wa ile baloon.
Akasita.
Mtu aliyelala kwenye kile kiti cha abiria alikuwa mwanamke, sura yake ikiwa imefunikwa na lile kofia kubwa la pama. Baddi alihisi koo likimkauka na moyo ukimbamiza kwa fujo ndani ya kifua chake. Kwa mkono uliojaa kitetemeshi aliifunua ile kofia na kubaki akimkodolea macho mkewe wa zamani.
“Sha...Shani...?” Aliita kwa kitetemeshi kikubwa huku akihisi dunia ikimzonga.
Shani ameuawa! Wamemuua Shani..!
Lakini kwa nini…kwa nia ya kutekeleza nini hasa?
Alijaribu kumtikisa ili kujihakikishia kile alichokuwa akikidhania.
Muda huo gari jingine liliingia eneo lile, naye alijigeuza haraka na kubaki akiwa ameketi nyuma ya usukani wa ile baloon, mkono wake mmoja ukiwa umekamata bastola yake tayari kwa mpambano ilhali mwingine ukiwa umeegeshwa kwenye usukani.
Alilitazama gari aina ya Toyota double cabin likimpita na kwa kupitia kwenye kioo cha kuonea nyuma cha ile Baloon aliliona likiegeshwa sehemu nyuma zaidi ya eneo lile. Watu wawili waliteremka kutoka kwenye ile double cabin na kuingia ndani ya lile jengo. Alishusha pumzi za ahueni na kumgeukia Shani.
Ee Mungu wangu…tafadhali usiache wamuue mama wa mwanangu!
Alimkamata mkono na kubonyeza mshipa wa damu pale mkononi ili kusikiliza kama kulikuwa na msukumo wowote wa damu. Hamna kitu, ingawa mwili wake bado ulikuwa na joto.
Alimuwekea sikio lake kifuani kusikiliza mapigo ya moyo na kusikia mapigo hafifu sana. Alimuwekea Shani kidole kwenye mshipa uliokuwa shingoni kwake, na hapo aliweza kupata mapigo hafifu ya msukumo wa damu.
“Oh, yu-hai! Shani yu-hai!” Alisema kwa faraja huku akiachia pumzi ndefu.
“Shani!” Alimwita huku akimtikisa lakini Shani hakuitika. Aliita mara nyingine tatu bila mafanikio yoyote. Akiwa amezidi kuhamanika, alitoka nje ya
MDUNGUAJI
lile gari na kutazama huku na huko. Ni nini maana ya jambo hili?
Ni wazi kabisa kuwa sasa ule mtego wake haukufanikiwa. Aliitazama
ile simu kwa hasira, ambayo nayo iliendelea kuwa kimya kama kwamba haijawahi kuita hata siku moja. Alienda hadi kwenye uzio wa eneo lile kule juu na kuchungulia chini, na hapo kwa mshangao mkubwa aliweza
kumuona yule mtu mrefu na mnene akivuka barabara na kuingia kwenye gari jingine jeupe lililokuwa limeegeshwa upande wa pili wa barabara mbele ya jengo lile. Kwa mduwao mkubwa kabisa aliliona lile gari likiondoka taratibu kutoka eneo lile.
Sasa ni vipi tena?
Alirudi kwenye ile Baloon huku akili ikimzunguka. Hakuweza kumpigia simu yule adui yake mwenye vitimbi, ambaye hutumia namba iliyojificha. Na alijua kuwa baada ya kumchezea mchezo ule, yule adui yake sasa alikuwa akimuacha achemke kwanza kabla hajampigia tena na kumpa maelekezo ambayo kwa vyovyote itabidi ayatekeleze.
Bloody Swine!
Alilipekua lile gari kujaribu kuona kama angeweza kupata kitu chochote cha kumjulisha juu ya mmiliki wa lile gari au kitu kama hicho. Hakukuwa na hata kadi ya gari. Ni vipi-hawa watu wameweza kumpata Shani na kuja naye mpaka hapa? Vipi kuhusu huyo mumewe? Wamepataje picha ya Gilda, na kwa nini imewekwa pamoja na ile ya Shani na bintiye? Ina maana hawa watu wanajua mahala Gilda alipo?
Sio siri Baddi Gobbos alikuwa amefikwa, naye alilijua hilo. Aliitoa ile simu na kupiga namba ya Swordfish.
“Mission aborted partner. Mambo yameharibika, mpango wote tunausitisha mara moja!” Alimwambia.
“Imekuwaje tena?” Swordfisha aliuliza kwa wasiwasi.
“Ni utata! Hapa niko na Shani ambaye hana fahamu. Jamaa kaacha gari na picha za Shani, mwanangu Claudia na Gilda...”
“Na Gilda!?” Swordfish aliuliza.
“Kabisa bwana, na Gilda! Si utata huu?”
“Okay, so…nije hapo sasa hivi?” Swordfish aliuliza baada ya kuachia tusi zito la ghadhabu, lakini kabla hajamjibu, Baddi alisikia mvumo kwenye ile simu uliomjulisha kuwa kuna simu ilikuwa inataka kuingia.
“No! Tulia hapohapo kwanza. Nadhani mjinga anapiga...kata simu yako!” Baddi alimjibu. Akapokea ile simu na kubaki akisikiliza bila ya kusema neno.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Vipi, hujui nini cha kusema?” Jamaa aliuliza. Donge kubwa lilimkaa kooni kiasi alijikuta akijilazimisha kumeza funda la mate kabla hajamjibu.
“Nimeshaona ulichotaka nione, sasa nakusikiliza!” Baddi alisema huku chuki yake dhidi ya mtu yule ikiongezeka maradufu. Jamaa aliangua kicheko kikubwa cha kebehi.
“Nadhani sasa utakuwa na adabu wakati unatekeleza maelekezo yangu, au sivyo?”
Baddi aliuma meno kwa hasira.
“Okay, naona huna ari ya masikhara tena leo hii, ajabu jinsi watu wanavyoweza kubadili ari kama kinyonga siku hizi.” Jamaa alisema, kisha hapo hapo, sauti yake ikapoteza mzaha kabisa na kuendelea, “Oke…nadhani hicho nilichokutangulizia kinatosha kukufanya uniletee huo mwili wako mahala nitakapo bila bila masharti Baddi. Ningeweza kukuletea maiti ya huyo mkeo kama ningetaka kwani nina uwezo huo.”
“Sio mke wangu huyu! Ana mumewe…” Baddi alimkatisha.
“Oke, si mkeo…mzazi mwenzako. Kwa hiyo ningemuua tu siyo? Mi’ nimekuonesha ni jinsi gani nilivyokuwa na uwezo wa kufanya nitakalo kwako. Sasa ninaye mwanao, na pia kimada wako, pumbavu mkubwa we!”
Jamaa alimtemea maneno kwa ukali. Moyo wa Baddi ulipiga tikitaka ndani ya kifua chake.
Jamaa wamempata Gilda na wanaye mwanangu!
“Sielewi unachoongelea, ila nakuahidi kitu kimoja rafiki yangu...” Baddi alimwambia kwa utaratibu sana, akitamka neno moja baada ya jingine kwa ufasaha mkubwa.
“Enhe? Nakusikiliza rafiki yangu.” Jamaa alisema huku sauti yake ikiwa imejaa kejeli.
“…gusa unywele mmoja tu wa mwanangu…mmoja tu…! Na nakuahidi kuwa nitakuwinda kila kona hadi nitakupata…” Baddi aliweka kituo kidogo, na kumalizia, “na nikikupata nasikitika kuwa hutakuwa na muda wa kujuta kwa nini ulizaliwa hapa duniani!”
Ilikuwa ni ahadi iliyotolewa kwa ufasaha na kuogofya kwa hali ya juu, kiasi kwamba ukimya mzito ulimgubika yule mtu wa upande wa pili, kwani hakika sauti ya Baddi Gobbos wakati ule iliahidi kutimiza kile ilichokuwa ikikisema.
“Okay. Basi nadhani hutanifanya nilazimike kugusa unywele mmoja wa mwanao Baddi, au siyo?” Hatimaye jamaa alisema kwa upole uliojaa kejeli. Baddi aliuma tena meno kwa hasira.
MDUNGUAJI
“Sema utakacho!”
Kando yake, Shani alitoa sauti hafifu na kujitikisa kidogo.
“Unajua nitakacho Baddi...!”
Na wakati huohuo Shani alifumbua macho na kuyazungusha kwa mashaka mpaka yakakutana na yale ya Baddi. Hapo alifunua kinywa kwa mshangao huku macho yake yakisajili taharuki isiyosemekana, huku akijaribu kujiinua kutoka pale kwenye kiti alichokuwa amelalia na kuanza kusema neno la mshangao lakini haraka sana Baddi akamziba mdomo huku akimlaza pale pale kwenye kiti.
“Mwanzo nilidhani ninajua ukitakacho, lakini sasa baada ya kuniletea mke wa mtu hapa najikuta sina hakika kabisa ni kitu gani haswa ukitakacho!”
Baddi alisema huku akimtazama Shani, ambaye alibaki akimkodolea macho ya kuuliza huku akiwa amebanwa mdomo pale kwenye kiti. Hakuwa kabisa na nguvu ya kubishana na mtu yule ambaye mara ya mwisho alimuona akitoka nje ya duka lake huku akimuacha akilia kwa uchungu.
“Nataka almasi zangu zote Baddi! Nataka uziwasilishe kwangu bila mizengwe yoyote. Ukifanya hivyo, sitagusa nywele moja ya mwanao, na pia Gilda wako hatodhurika, kama humjali huyo mzazi mwenzako!” Sauti ilimjibu, ingawa sasa kidogo sauti ile ilisikika tofauti. Naongea na watu wawili tofauti kwa simu hii hii?
Jasho lilimtoka Baddi Gobbos. Ama hakika alikuwa amefikwa.
Ni wazi kuwa yule mtu alikuwa anadai almasi zilizotamkwa kwake na msaliti Alpha miaka mitatu iliyopita kule Sierra Leone, na sio zile za Gilda. Kwa uelewa wake, almasi za Alpha zilikuwa nyingi na hivyo zenye thamani kubwa kuliko zile za Gilda. Tatizo ni kwamba yeye hakuwa na hizo almasi alizokuwa akijinadi kuwa anazo!
“Okay, sasa unataka nikuwasilishie wapi hizo almasi?”
Jamaa akakata simu.
“Khah!” Baddi alijikuta akitoa mguno wa mshangao na kuitoa ile simu sikioni kwake na kuitazama kama kwamba ile simu ilikuwa ina wazimu.
Ama hakika alikuwa amefikwa, kwani sasa yule hasimu wake alikuwa anadai almasi alizojinadi kuwa anazo kwa kiokosi cha maisha ya Gilda na Claudia!
“Baddi…” Shani aliita baada ya Baddi kuutoa mkono wake kinywani kwake, “…ni nini kinaendelea hapa? Mbona sielewi nimefikaje huku? Hili gari… ni la nani?”
“Mnh! Ni hadithi ndefu Shani, kwani mimi pia nilikuwa nataraji kusikia kutoka kwako juu ya mazingira ya wewe kufika hapa, sasa tena…” Baddi alisema, na hapo Shani akamkatisha na kumueleza kwa wahka mkubwa kuwa akiwa
dukani kwake siku ile, aliingia mtu mmoja mnene na mrefu aliyemuwekea bastola kwa uficho kiasi hata mhudumu wake wa dukani hakuweza kuelewa kitu. Yule mtu alimuamuru atoke naye nje kwa ukimya kabisa, vinginevyo angemuua. Jamaa alimuongoza hadi kwenye lile baloon, ambamo kulikuwa kuna mtu mwingine mmoja ambaye pia hakumtambua. Wakaanza kumuuliza maswali ambayo hakuyaelewa, lakini wakati akitafakari yale maswali yao, walimnusisha unga fulani na ghafia kote kukawa kiza. Alipoamka alijikuta yuko na Baddi ndani ya lile gari.
“Kwa hiyo hao watu huwajui kabisa?” Baddi aliuliza.
“Si...siwajui! Baddi, ni nini kinachotokea? Ni nani huyo uliyekuwa ukiongea naye? Kwa nini na wewe uko hapa?” Shani aliuliza lakini Baddi hakuwa akimsikiliza tena. Alikuwa akipiga simu kwa Swordfish.
“Naona sasa inabidi uje hapa patna!” Alimwambia.
“Ni nani huyo unayempigia? Baddi mbona unanitisha lakini? Umekuwaje wewe?” Shani alimuuliza kwa woga mkubwa huku akimtazama kwa mashaka yule shababi aliyekuwa mumewe. Baddi hakujisumbua kumjibu.
Kutokea pale walipokuwa hawakuweza kabisa kuona wakati buti la ile Benzi iliyokuwa imeegeshwa katika eneo lile likifunguka taratibu na kwa usiri mkubwa.
Baddi hakujua iwapo alitakiwa amuamini Shani au vinginevyo, na kibaya zaidi ni kwamba kwa hali ilivyokuwa, hakuwa na muda tena wa kupoteza kwenye kulitafakari jambo lile. Akili yake ilikuwa imezongwa na mawazo juu ya habari aliyopewa na yule mtu wa kwenye simu kwamba binti yake Claudia na mpenzi wake Gilda wako mikononi mwa adui yule mwenye visa.
Inawezekana? Au ananivunga tu kunibabaisha?
“Claudia yuko wapi sasa hivi…?” Alimgeukia Shani na kumuuliza.
Badala ya kumjibu Shani alimkodolea macho na kumwemwesa kama kwamba hakuelewa msingi wa swali lile kwa wakati ule. Baddi alirejea swali lile kwa mara ya pili.
“Shu…le. Yuko shule. Kwani vipi…?”
“Anatoka saa ngapi…anarudi vipi nyumbani?” Baddi alimuuliza tena, akijitahidi kuficha wasiwasi aliokuwa nao.
“Ah, kuna basi la shule ndilo huwa linamrejesha, kwa nini?”
Kwa sababu kuna uwezekano kuwa atakuwa ametekwa na mwendawazimu mmoja anayetaka kuniondoa duniani na anamtumia Claudia kama chambo!
Baddi alitamani amjibu vile, lakini hakufanya hivyo. Bado hakuwa na imani na yule mkewe wa zamani kiasi cha kumueleza kila kitu muda ule…pia
MDUNGUAJI
kwa namna fulani alikuwa na hasira sana dhidi yake. Na bila shaka yule adui yake alilijua hilo, ndiyo maana akamleta Shani hapa kwa nia ya kumchanganya zaidi!
Akili yake ikarudi kwa yule adui yake…kwa nini amekata simu ghafla vile? Kuna nini anakiandaa dhidi yangu hapa?
“Hebu piga simu shuleni kuulizia iwapo mtoto yupo, na kama ndivyo waambie kuwa utaenda kumfuata wewe mweny….”Baddi alimwambia, huku akijitahidi kuficha wasiwasi uliomgubika iwapo atasikia kuwa binti yake ambaye alimuacha mdogo sana na hajamuona tangu ameingia nchini, atakuwa ametekwa na yule khabithi asiye sura.
“Sasa mbona simu yenyewe sina! Nimeiacha kule dukani…nakwambia mi’ nimetekwa kijambazi! Kuna nini kinachotokea lakini? Kwa nini umekuwa na hamu ya kujua habari za mtoto ghafla hivi?” Shani aliuliza na Baddi alizidi kuchanganyikiwa.
“Nitakufahamisha baadaye, lakini sasa…hebu chukua hii simu basi uwapigie huko shuleni…”
“Namba yao siijui kwa kichwa! Iko kwenye ile simu yangu….kwani vipi?”
“Ok. Basi mpigie mumeo aje akufuate hapa…muelezee yote yaliyotokea. Mi’ yanipasa niondoke hapa mara moja, siwezi kuendelea kubaki nawe hapa!”
Shani alimtazama kwa mashaka.“Kuna nini Baddi…?”
“Hapa kuna mambo yasiyo sawa Shani, nawe unajua hilo! Sina muda wa kujibishana saa hizi. Fanya nikwambiavyo….chukua hii simu umpigie mumeo sasa hivi. Aje akuchukue hapa. Mi’ yanipasa niondoke!”
Kwa mashaka Shani aliichukua ile simu na kuanza kupiga namba za mumewe, ambazo alikuwa amezishika kichwani.
“Ha…haloo!” Shani alianza kuongea na ile simu, baada ya mtu aliyempigia kupokea ile simu. Baddi alikuwa makini kusikiliza kile kilichokuwa kikiongewa.
“Kuna tatizo limetokea hapa…mimi niko…nimetekwa na majambazi…”
Shani aliongea, kisha akatulia kidogo kabla ya kuendelea, “...ndiyo, majambazi! Sasa nimeletwa hapa…hapa…” Shani alibabaika kutaja ni wapi alipokuwa. Akamgeukia Baddi kwa fadhaa. Baddi alichukua ile simu.
“Habari mzee…” Alianza kuongea.
“Who…who is this…nani wewe?” Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani aliuliza kwa ukali, moja kwa moja Baddi Gobbos akiitambua sauti ya yule bosi wake wa zamani.
Ambaye sasa ni mume wa mkewe.
“Ni hadithi ndefu mzee, ila kwa ufupi ni kwamba mkeo alitekwa na watu
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
wasiojulikana na kuja kuachwa hapa Motel Agip…”
“Motel Agip…? Sasa…sasa wewe ni nani? Na…na kwa nini uko hapo sasa hivi, na…” Mume mtu alikuja juu kwa jazba.
“Sikiliza mzee, mimi pia nimekutwa na madhila mazito! Najitolea tu kuongea nawe ili uje kumchukua mkeo hapa nami niweze kuendelea na hamsini zangu…” Kwa namna fulani Baddi hakutaka kujitambulisha moja kwa moja kwa Meja Jenerali Gaundence. Kwani pia alikuwa na ghadhabu dhidi yake, na alijichukia sana alipokuwa akiongea naye muda ule, tena akiongea naye kama mume wa mkewe.
“…lakini madhali umeshajua…” Baddi alikuwa akiongea, lakini hapo aliona gari aina ya Nissan Patrol likiingia eneo lile kwa kasi sana na kusimama hatua chache mbele ya lile gari walilokuwamo. Akawa makini huku akiendelea kuongea, “…mahala alipo, mi’ naweza kumuacha ili uje umkute hapa!”
Hakuna aliyeteremka kutoka kwenye lile gari lililosimama mbele yao. Na huku nyuma buti la ile Benzi lilijifunga taratibu.
“No! Hapana…aammm…samahani sana ndugu…umesema ni Motel Agip?” Meja Jenerali mstaafu Gaudence alikuwa akisema, sasa akiwa amejawa hofu zaidi kuliko hasira.
“Ndiyo…kwenye hii sehemu ya juu kabisa ya kuegeshea magari…ndipo alipo sasa…”
“Basi mwambie asubiri hapo hapo! Au nipe niongee naye…Mi’ siko mbali sana na hapo…bahati nilikuwa nimekuja benki hapa Masdo, hivyo nitafika muda si mrefu…Oh! Mungu wangu! Hajadhurika?” Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani alisema haraka haraka.
Baddi alimtupia Shani ile simu, akili yake ikiwa kwenye ile Nissan Patrol ambako sasa aliona watu watatu wakiteremka, mmoja wao akiwa ni yule mtu mwembamba na mrefu, ambaye alikuwa pamoja na wale watu waliojaribu kumteka nyara pale nje ya makao makuu ya jeshi siku alipokwenda kumtafuta
Meja Jenerali Gaudence Amani!
“Tulia humu humu!” Alimwambia wakati akisukuma mlango na kutoka nje ya gari, bastola yake ikiwa mkononi.
“Tupa chini hiyo bastola Baddi Gobbos!” Sauti nzito ilimkemea, lakini si kutoka kwa wale watu aliokuwa akiwatazama kule mbele yake, bali kutokea nyuma yake.
E bwana we!
Aligeuka na kujikuta uso kwa uso na yule jamaa aliyemtupia kisu
kilichomkosa na kumchoma Gilda kule hotelini ile siku ya kwanza
MDUNGUAJI
alipoingia nchini, ambaye alikuwa amemuelekezea bastola ndogo. Baddi alijisogeza pembeni na kusimama kuielekea ile Baloon, na kwa kufanya hivyo alijiweka pembeni, badala ya katikati, ya wale adui waliomzonga. Wale jamaa walioteremka kutoka kwenye ile Nissan Patrol sasa walikuwa kulia kwake, na yule aliyetokea ndani ya lile jengo, kwa nyuma yake, sasa alikuwa kushoto kwake.
Muda huo, mmoja wa wale watu waliokuwa kulia kwake alifungua mlango wa ile Baloon na kumvutia nje mkewe wa zamani, ambaye alipiga mayowe ya woga.
“Mnataka nini sasa?” Baddi aliuliza huku akitembeza macho kutoka kwa mmoja wa wale watu kwenda kwa mwingine.
“Umeambiwa tupa chini bastola Baddi, huelewi nini sasa hapo?” Yule mtu mrefu alimkaripia. Jamaa alikuwa na sauti nzuri sana ambayo ingependeza iwapo angekuwa muimbaji badala ya kujitia kwenye mambo ya kijasusi kama yale.
“Baddi…!” Shani aliita kwa woga. Baddi alitupa jicho upande wa pili wa ile Baloon na kuona kuwa yule mtu aliyemtoa Shani kutoka kwenye lile gari alikuwa amemkaba mkewe wa zamani huku amemuwekea ncha ya kisu shingoni.
“Okay! Nitafanya mtakalo wandugu! Muacheni huyo mama tafadhali…”
Baddi alisema huku akianza kuinama.
“A-a-aaa!” Jamaa aliyemuibukia kwa nyuma alimkemea kutokea kushoto kwake, na Baddi akatulia akiwa katika hali ileile ya kuinama.
“Naweka chini bastola kama mlivyoagiza…” Alijieleza hali bado akiwa ameinama vile vile, huku kwa pembe ya jicho lake akipima umbali baina yake na yule mtu aliyemtokea nyuma yake hapo awali.
“Iweke juu ya gari!” Jamaa alimuamuru.
Lilikuwa kosa la kwanza.
Baddi aliinuka na kupiga hatua mbili kuliendea lile gari, halafu ghafla sana alijigeuza huku akibonyea na kumtupia ile bastola yule jamaa kama jiwe na kujibiringisha uvunguni mwa ile Baloon.
Kilikuwa ni kitendo kisichotarajiwa na wote pale, kwani yule jamaa mwenye bastola alitoa yowe fupi huku akiikwepa ile bastola aliyotupiwa, ambayo alimpata kifuani na kumchanganya vilivyo. Hapohapo wale watu wawili waliobaki mbele ya ile Nissan Patrol walipayuka kila mmoja na neno lake huku wakikurupuka kumuendea Baddi, bastola zikiwa mikononi mwao, lakini muda huohuo walimshuhudia Baddi akipotelea chini ya uvungu wa ile Baloon.
Mtu mwembamba mwenye sauti nzuri alipiga hatua kumuwahi lakini
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
hapohapo alijikuta akipigwa butwaa pale aliposhuhudia buti la ile Mercedes Benz likitupwa juu kwa nguvu na mtu mmoja akijitupa nje ya lile buti.
“Cheki ‘uyooo!” Sauti nzuri alimpigia kelele yule mwenzao aliyetupiwa bastola na Baddi huku akimuoneshea kidole kule kwenye ile Benzi iliyokuwa nyuma yake.
“Whaaa...?” Jamaa aliuliza kwa hamaniko huku akigeuka nyuma wakati bastola iliyokuwa mkononi mwa Swordfish ilipotoa sauti kama chafya ya mtoto mchanga, na kuzamisha risasi kwenye paja la yule jamaa ambaye alienda chini kwa kishindo, bastola ikimtoka huku akiachia yowe la woga zaidi kuliko uchungu.
Wakati huo huo, upande wa pili wa ile Baloon, yule jamaa aliyekuwa amemkaba Shani akimvutia pembeni ili aone ni wapi Baddi alipopotelea wakati aliposhitukia Baddi akimuibukia kutoka uvunguni mwa ile Baloon na kusimama wima mbele yake. Jamaa akamsukuma Shani pembeni na kumtupia Baddi pigo la kuchanja kwa kisu chake.
Kosa la pili.
Baddi alitaraji ujinga kama huo hivyo akajigeuza haraka, akamdaka ule mkono wake wenye kisu naye akapiga goti moja haraka huku akimtupa jamaa hewani kwa mtindo wa judo. Jamaa aliangukia kwenye kioo cha mbele cha ile Baloon huku yowe kubwa likimtoka, kisha akasawajika sakafuni kama gunia tupu.
Muda huo Baddi alikuwa ameshajiinua wima na kumgeukia yule jamaa aliyebaki. Swordfish naye aliinuka kutoka pale sakafuni alipokuwa amepiga goti, jasho likimvuja mwili mzima kutokana na kukaa kwa muda mrefu ndani ya buti la ile Benzi ya binamu yake aliyotangulia nayo pale eneo la tukio, akamuelekea yule mtu mwenye sauti nzuri huku jicho lake moja likitoa mng’ao wa ghadhabu.
“Tulia hivyo hivyo weye!” Alimkoromea yule jamaa huku akimuoneshea mdomo mrefu wa bastola yake maalum iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti. Kilichofuatia hakuna yeyote kati ya wote waliokuwapo pale aliyekitarajia.
Wakati Baddi akimsogelea yule mtu wa tatu aliyekuwa mbele ya ile Nissan Patrol, na Swordfish akimwendea sauti nzuri huku wote wakiwa
wameelekezeana bastola, ghafla vilisikika vishindo kutokea nyuma yao, na wakati huohuo ilisikika sauti ikiita jina la Shani kwa wahka na pupa. Ndani ya nukta ile Swordfish alimuona sauti nzuri akitumbua
macho kwa mshituko na taharuki kutazama kule vilipotokea vile vishindo,
MDUNGUAJI
naye aliruka pembeni huku akigeuka kule ilipotokea ile sauti.
Baddi naye alisita kwenye hatua zake na hapohapo alibonyea kando ya ile Baloon akitaraji mashambulizi mapya dhidi yao kutokea kule viliposikika vile vishindo.
Ndipo wote kwa pamoja walipomuona Meja Jenerali mstaafu Gaudance
Amani akiingia eneo lile kwa wahka mzito, akitembeza uso wake uliofunikwa kwa miwani myeusi huku na huko. Na hata pale Baddi alipokuwa akimaizi kuwa yule aliyeingia ni bosi wake wa zamani, Shani alipiga yowe jingine la woga. Baddi aliachua tusi la kulaani kitendo kile kilichowapotezea umakini na hapohapo aligeuka kumkabili yule adui yake aliyekuwa amemdhamiria hapo mwanzo, lakini kosa lilikuwa limeshafanyika.
“Wote tulia hivyo hivyo, pumbavu!” Yule adui wa tatu alifoka kwa hasira, akiwa amembana Shani kwa kabali kali na akiwa amemuwekea bastola shingoni. Yaani ndani ya ile sekunde ambapo wapiganaji wale walipoteza mwelekeo kutokana na vishindo vya Meja Jenerali mstaafu
Gaudence Amani, wale adui walitumia nafasi hiyo kujiweka sawa na kuwazidi kete, kwani yule jamaa aliwahi kuruka na kumkwapua Shani aliyekuwa bado akijizoazoa kutoka pale alipoangukia na kumdhibiti tena.
“Heeh! Ni…kuna nini tena…?” Meja Jenerali Gaudance Amani aliuliza kwa mshangao huku akitembeza uso wake kwa wote waliokuwapo pale.
“Nasema wote tulieni hivyo hivyo! La sivyo mchumba anaaga dunia hapa hapa!” Jamaa aliyemkwida Shani alikoroma tena, na Shani aliachia kilio cha woga.
“Jamani mbo…mbona hivi...? Nimefanya nini mimi lakini...?”
Shani alilalama na hapohapo jamaa alimpiga kichwani kwa kichwa chake huku bado akiwa amemkandamizia mdomo wa bastola shingoni.
“Kelele mwanamama!”
Baddi alimgeukia Meja Jenerali Gaudence, ambaye alionekana
kuwa bado mwenye nguvu na aliyenawiri vizuri sana. Alikuwa amevaa miwani ya jua uliyoficha sehemu kubwa ya uso wake. Walitazamana.
“Ba...Baddi...? Baddi Gobbos...? U-hai...?” Meja Jenerali mstaafu
Gaudence Amani aliuliza kwa mshangao dhahiri, na kabla Baddi hajasema lolote, Gaudence alimgeukia Swordfish.
“Meja Babu! Wha... what is going on here jamani, mbona...”
Baddi na Swordfish walitazamana, kisha kwa pamoja wakamgeukia yule jambazi aliyekuwa amemkwida Shani.
“Weka chini bomba hilo wewe!” Jamaa aliyemkwida Shani alimkemea
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Swordfish, akimaanisha aweke chini ile bastola iliyokuwa mkononi mwake.
“Sawa...lakini huoni kuwa wamuonea bure huyo mama...?” Swordfish alimjibu huku akimtazama kwa makini, akilini akijaribu kupiga hesabu ni jinsi gani watajikwamua kutoka pale.
“Mmeambiwa wote mtulie! Na tupa chini hiyo bastola wewe ama si hivyo mchumba anaondoka duniani yule, ebbo!” Sauti nzuri alimkemea Swordfish huku bado akiwa amemuelekezea bastola yake. Ukiondoa ile bastola aliyokuwa nayo, ile sauti yake haikumtisha yoyote mle ndani, sana sana iliwaburudisha tu. Meja Jenerali Gaudence alipiga hatua tatu za haraka kuelekea pale alipokuwa Shani.
“Eeeeh! mwache huyo mama wewe!” Alimkemea yule jamaa.
“Heeeey!” Jamaa aliyemkwida Shani alipigia ukelele huku akizidi kumkodoela macho na akikandamiza ile bastola kwa nguvu zaidi shingoni kwa Shani.
“Bad...Gaudence!” Shani aliita kwa woga, macho yamemtoka pima. Gaudence alisimama, mikono ikiwa juu akionesha kuwa hakuwa na silaha yoyote.
“Oke...Oke...Basi!” Alisema huku akitweta, kisha akaendelea, “...mimi ndiyo mume wa huyo mama jamani...sijui mtakacho, lakini niko tayari kuwapatia mradi tu mniachie mke wangu…”
“Huna tukitakacho wewe! Umejileta kwa kiherehere chako tu hapa!”
Jamaa aliyemkwida Shani alimjibu kwa hasira. Sasa Shani alikuwa akilia wazi wazi.
Muda huo yule jamaa aliyetupwa hewani na Baddi hapo awali na kuangukia kwenye kioo cha ile Baloon alijizoazoa kutoka pale chini na kutikisa kichwa kama kwamba alikuwa akiweka akili yake sawa. Alimtazama Baddi kwa ghadhabu, kisha akaachia tusi zito na kumtandika konde zito la mbavu. Baddi aliguna kwa maumivu na hapohapo jamaa akamshika kichwa na kumshindilia bichwa la uso, kisha akamsukuma nyuma kwa nguvu. Baddi alitoa miguno ya maumivu wakati akipokea mapigo yale, na kujibabatiza kwenye ubavu wa ile Baloon, damu ikimvuja
puani kutokana na bichwa alilotoswa na yule adui mwenye ghadhabu.
Jamaa aliokota kisu chake na kwenda moja kwa moja hadi pale
alipokuwa ameshikiliwa Shani, na kwa pigo moja la haraka sana alikipitisha
kile kisu shingoni kwa Shani na kumchanja kwa nguvu. Shani
aliachia yowe kubwa la woga na maumivu. Baddi na Mej. Jen. Gaudence
walitoa sauti za mshituko kwa kitendo kile na kubaki wakitazama kwa
MDUNGUAJI
woga jinsi Shani alivyokuwa akivujwa damu. Jamaa akawageukia kwa hasira, akiwaoneshea kisu kilichokuwa kinachuruzika damu.
“Mara ya pili nacharanga reception ya kimada wenu hapa bloody fools! Weka chini bastola wewe!” Aliwakemea, akimaanisha kuwa mara ya pili atamchanja Shani usoni. Hakika jamaa alikuwa na roho mbaya sana. Swordfish alitupa chini ile bastola huku akimtazama yule jamaa kwa jicho lake moja lililojaa chuki mbaya. Sasa Shani alikuwa akilia kama mtoto huku damu ikimtoka kwenye lile jeraha lake na kulowesha nguo yake sehemu ya kifuani.
“Sasa jamani kwani…” Meja Jenerali Gaudance alianza kulalama.
“Kelele wewe!” Sauti nzuri alizidi kuwaburudisha.
“Wewe!” Jamaa mwenye kisu alimwita Baddi huku akimnyooshea kisu chake. Baddi alimtazama kwa chuki kubwa.
“Na wewe!” Jamaa akamnyooshea kisu Meja Jenerali Gaudence, ambaye alibaki akimtazama kwa taharuki zaidi kuliko chuki.
“Mbebeni yule mwenzetu mmuingize ndani ya gari...upesi!” Aliwaamuru, akimuoneshea yule mwenzao aliyepigwa risasi ya paja na Swordfish.
Baddi na Meja Jenerali Gaudance walitekeleza. Na hapo simu ya Baddi ikaanza kuzizima tena. Aliwaangalia wale jamaa wawili waliokuwa wakifuatilia kwa makini jinsi walivyokuwa wakimhamishia kwenye gari yule mwenzao wakati sauti nzuri akiwa amemdhibiti Swordfish kwa bastola yake.
“Nahitaji kupokea simu ya muhimu sana…” Aliwaambia huku akioneshea kwenye mfuko wake wa suruali ambamo simu yake ilikuwamo.
“Hakuna cha muhimu kuliko hili tulilo nalo sasa!” Mmoja wa wale jamaa alimjibu.
“Kwani ninyi ni nani na mnataka nini? Kwa sababu huenda huyu akawa ndiye bosi wenu...nimekuwa nikiwasiliana naye...” Aliwaambia. Jamaa mwenye kisu alimuamuru aitoe ile simu taratibu sana na aiweke juu ya boneti la ile Nissan Patrol. Baddi alitii huku ile simu bado ikiita na hata pale alipokuwa akiiweka juu ya ile boneti aliona kuwa ile namba iliyokuwa ikiita ilikuwa ni Private Number.
Jamaa aliichukua ile simu na kuipeleka sikioni kwake huku akimtazama Baddi kwa makini, lakini muda huo ile simu ikaacha kuita.
“Jamaa yako kakata. Lakini kama ndiye huyo bosi wetu umsemaye basi atapiga tena tu, na ndiye aliyetutuma tuje tukuchukue tukupeleke kwake, ukiwa na mzigo aliokuagiza…je unao?”
“Tulikubaliana kuwa nitamuonesha yeye tu, na si mtu mwingine
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI yeyote!” Baddi alijibu.
“Naye hajasema utupe au utuoneshe sisi...amesema tukupeleke huko alipo...sasa ole wako usiwe na huo mzigo!” Jamaa alimjibu huku akiitia mfukoni ile simu.
“Jamani ni nini kinachoendelea lakini? Mbona sielewi?” Meja Jenerali Gaudence aliuliza.
“Si kazi yako wewe!” Sauti nzuri alimkemea.
“Si kazi yangu wakati mmemchukua mke wangu bila ridhaa yake?” Gaudence alimjia juu.
“Hatuna muda wa mabishano hapa! Kama huyu mkeo basi subiri mkirudi nyumbani mkaulizane vizuri. Kwa sasa tuna kazi naye kwa sababu inaelekea mkeo pia ana mume mwingine hapa!” Jamaa alimjibu.
“Eti nini?” Gaudence alimaka.
“Ebbo!” Baddi naye alimaka kivyake, kushangaa ile kauli ya yule mtu mnafiki. Baddi na Gaudence walitazamana. Swordfish aliingilia kati hali ile.
“Saa tunafanya nini hapa...nini kinaendelea?”
“Hebu nyamaza we’ kijicho! Sisi ndiyo tunajua kinachofuata na tutakwambia muda ukifika! Kaa kimya!” Sauti nzuri alimkemea.
“Halafu wajua we’ ungependeza sana kama ungeimba taarabu weye! Ajabu wajiingiza kwenye mambo ya kishababi kama haya, wayaweza kweli?”
Swordfish alimjibu sauti nzuri huku akimtazama kwa dharau. Lengo likiwa ni kumkera ili afanye jambo la jazba apate kumtia adabu. Lakini jamaa alinusurika.
“Tutaona nani shababi kati yetu muda mfupi tu ujao...ingia kwenye gari kule!” Sauti nzuri alimkemea huku akimuelekezea kwa bastola yake kwenye ile Nissan Patrol. Swordfish alisita kidogo, kisha akatii.
“Na wewe…” Mwenye kisu alimwamuru Baddi, na kuendelea, “...pita kiti cha mbele kule!”
Baddi alitii. Jamaa aliziokota haraka haraka zile bastola zilizokuwa pale chini.
“Hey...sasa…vipi mke wangu? Mnaenda naye wapi…?” Meja Jenerali Gaudence alimaka huku akiwafuata. Jamaa alimgeukia na kofi kali la uso na kumsukuma nyuma.
“Kaa chonjo mzee!” Alimwambia huku naye akiingia ndani ya gari.
Baddi aliingia kwenye kiti cha mbele, jamaa aliyemkaba Shani aliingia kwenye kiti cha nyuma huku akiwa bado amemkwida Shani
aliyekuwa akilia huku akivujwa damu. Sauti nzuri alikaa na Swordfish
MDUNGUAJI
kule nyuma, Swordfish na Shani wakiwa wamebanwa kati kati ya wale jamaa wawili.
“Shani! Shani...!” Meja Jenerali mstaafu Gaudence alimwita mkewe kwa fadhaa na taharuki kubwa. Jamaa mwenye kisu aliingia nyuma ya usukani.
“Shani! Shani, mke wangu! Usihofu...nitajitahidi kukuokoa! Nakuahidi! Nakuahidi!” Gaudence alimwambia mkewe huku akimchungulia kule nyuma alipokuwa kupitia kwenye dirisha la dereva. Shani aliacha kulia na kubaki akimtazama mumewe, si kwa huzuni, si kwa simanzi, si kwa woga, bali kwa mshangao mkubwa kabisa!
“Mzee mkeo atarudi salama kama ukitulia...ukijitia kupiga simu polisi au kufanya ushujaa wowote wa kijinga, tunamuua nasi hutotuona tena! Upo?”
Jamaa mwenye kisu alimwambia kutokea dirishani.
“No! Hamuwezi kumchukua mke wangu namna hii! Baddi, ni nini kinatokea? Kuna nini?” Meja Gaudence alikuwa akisema kwa wahka huku akilifuata lile gari wakati likianza kuondoka taratibu eneo lile.
Jamaa alimsukuma kupitia pale dirishani na kuliondoa lile gari kwa kasi.
Kupitia kwenye kioo cha kuonea magari yatokayo nyuma, Baddi
Gobbos aliweza kumuona Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani akiwa
amesimama katikati ya eneo lile akilitazama lile gari likitoweka, bado miwani yake ya jua ikiwa usoni kwake.
Muda huo alishtukia kamba ikipitishwa haraka kichwani kwake na kumkaba shingoni kutokea kule nyuma. Alitoa sauti ya maumivu na kujaribu kujinasua, lakini Jamaa aliyekuwa nyuma yake alizidi kukaza kitanzi kile kwa kuivuta nyuma kwa nguvu ile kamba.
“Una tabia ya ukorofi Baddi Gobbos! Safari hii inabidi tukudhibiti ipaswavyo!” Jamaa alimkoromea kutoka kule nyuma. Baddi hakuweza kusema kitu, kamba ilikuwa imemkaba sana, na alihisi koo likimkauka.
“Sasa mnatupeleka wapi?” Swordfish aliuliza.
“Kuonana na bosi!”
Shani alianza kulia upya.
Kiasi cha kama dakika kumi baada ya kutoka pale Motel Agip, simu ya Baddi ilianza kuita tena. Jamaa aliyekuwa akiendesha gari na ambaye ndiye aliyebaki na ile simu aliitazama na kuipeleka sikioni.
“Yes?” Aliitika kwenye ile simu na kusikiliza kidogo, kisha akaendelea, “Aaah, Bosi! Ndiyo…kazi imekamilika, nilitaraji ungepiga kwenye simu yangu!”
Baddi akawa makini sana.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“ Okay , sawa.” Jamaa alisema, kisha akampa Baddi simu, “Ongea na bosi sasa!”
Baddi aliichukua ile simu wakati yule mtu wa kule nyuma akilegeza ile kamba iliyokuwa imemkaba pale kwenye kiti. Badala ya kuanza kuongea alikohoa kwa muda kisha akaiweka ile simu sikioni.
“Vipi wewe! Umepatwa na TB ghafla?” Sauti ya adui yake iliuliza kwa kebehi, bado simu ya mtu yule ilikuwa kwenye mfumo ule ule wa spika, na hivyo ikawa imeingiliwa na mawibi na mivumo mingi.
“Unata...taka nini sasa? Siyo makubaliano yetu haya…!” Baddi alisema kwa kutweta. Jamaa alimcheka kwa kebehi.
“Hatuna makubaliano zaidi ya kwamba uniletee mali yangu nikuachie mwanao na kimada wako!” Jamaa alimjibu.
“Sasa mbona mnamchukua na Shani? Muacheni aende basi!”
Jamaa akamcheka tena. “Vipi, unaogopa fumanizi? Hutaki Shani ajue kuwa una kimada pembeni?”
“Sio hivyo fala wewe! Hii haitakusaidia lolote! Mimi si tayari umenipata? Hakuna haja ya kumuingiza na mtu asiyehusika katika mambo haya!”
“Una hakika kama Shani hahusiki Baddi?”
Baddi alipigwa butwaa.
“Sikuelewi...”
“Na ndo hutaelewa mpaka utakaponipa mzigo wangu…na labda hapo utaelewa kuwa huenda Shani alikuwa akihusika tangu mwanzo.”
Jamaa alimjibu.
“Khah! Unamaanisha nini wewe?” Baddi alikuja juu.
“Nakusubiri Baddi Gobbos. Njoo na mzigo wangu, na utajua kila kitu!”
Jamaa alimjibu na kukata simu. Baddi alichanganyikiwa kweli kweli!
Safari iliendelea bila kituko chochote kikubwa, zaidi ya vilio
hafifu vya Shani aliyekuwa akilalama na kuomboleza njia nzima, huku akitukanwa matusi mfululizo na wale watekaji nyara wenye nia mbaya.
Swordfish na Baddi Gobbos walikuwa kimya tu, kila mmoja akiwa
amezama kwenye fikra nzito, ingawa kwa ukimya wao ule, walipelekeana
ujumbe wa kimya kimya kuwa pindi itakapofika wakati wa kufanya
lolote litakiwalo, watakuwa upande mmoja dhidi ya wale adui zao.
Kamba iliyokuwa imembana koo Baddi Gobbos pale kwenye kiti
kutokea nyuma yake ilikuwa ikimuumiza sana, na kwake ile safari
ilikuwa ya taabu mno. Pamoja na hivyo, alikuwa akitafakari hatima ya
MDUNGUAJI
utata ule aliojizonga ndani yake, kwani hakuwa na almasi ambazo yule adui yake alikuwa anazitaka, na ambaye kama ameziona almasi za Gilda, moja kwa moja ataamini kuwa amepewa na Baddi.
Na sasa yule adui anamwambia kuwa Shani anahusika kwa kiwango kikubwa na mkasa wote ule.
Kivipi?
Baddi alikuwa kwenye mgawanyiko mkubwa wa imani juu ya nani amuamini katika utata ule. Je amuamini Shani au yule adui yake, pindi itakapofika wakati wa kubaini juu ya kuhusika kwa Shani katika mkasa ule?
Alijikuta akizidi kumchukia yule adui yake ambaye mpaka muda ule hakuwa amemtia machoni, zaidi ya kumsikia kwenye simu tu, tena akiwa ameikoroga sauti yake kwa kuweka simu yake kwenye mfumo wa spika. Ni nani huyu mtu lakini?
Bado alikuwa na imani kubwa kabisa kuwa yule adui yake ndiye haswa yule mdunguaji wa kule msituni... Lakini inawezekana kweli?
Aliwezaje kumsubiri miaka yote hiyo iliyopita tangu yeye akiwa amedhaniwa mfu hadi alipokuja kuibuka tena hapa nchini? Je, ina maana alijua kuwa hakuwa amekufa muda wote huo? Alizidi kupata hamu ya kumuona huyo adui yake.
Swordfish naye alikuwa kimya akitafakari mambo kama yale yaliyokuwa
yakipita kichwani kwa Baddi lakini kutokea kwenye pembe nyingine kabisa. Yeye alikuwa akitafakari jinsi gani yule mke wa zamani wa rafikiye, ambaye kwa uelewa wake bado ni mke halali wa Baddi kwa kuwa mwenyewe yu-hai, anahusika katika kizaazaa kile. Kwa nini wale jamaa walimpeleka Shani pale Motel Agip, halafu tena waondoke naye pamoja nao?
Kama wangemuacha angeelewa kuwa alikuwa amefanywa chambo cha kupoteza malengo, lakini tena wameamua kumchukua naye pia… vipi hii inakuwa?
Na kwa nini Shani alimtazama mumewe Gaudence kwa mshangao namna ile wakati yule bwana akimlilia kwa upendo huku akimuahidi kuwa atafanya kila awezalo kumuokoa?
Swordfish alikuwa na hakika kuwa Baddi hakuona mshangao uliokuwa
usoni kwa Shani wakati ule, lakini alijua kuwa kama angeuona, basi naye angekuwa akijiuliza swali lile muda ule.
Shani ana nini?
Kwanza alikuwa akimuona kuwa ni mtu mwenye ghadhabu tangu
aolewe na Gaudence Amani, na sasa leo ule mshangao aliomtolea Gaudence
ulizidi kumchanganya Swordsfish. Aliamua kuvunja ukimya baina yake na Baddi.
“One for All Kanali...”
“Kelele wewe!” Sauti nzuri alimkemea huku akimsukuma kichwa chake kwa mdomo wa bastola yake.
“...All for one Meja!” Baddi alijibu kwa taabu kutokea kule mbele.
“Hebu msituzingue nyinyi saa hizi, ebbo!” Yule jamaa aliyemkwida Shani aliwabwatukia. Swordfish alishusha pumzi ndefu na kujiegemeza vizuri pale kwenye kiti, akisubiri hatima ya safari...
Safari iliishia ndani ya wigo mmoja mpana na mrefu maeneo ya Vingunguti, wigo ambao ulikuwa umehifadhi majengo matatu makubwa na marefu kwa mlalo, ambayo moja kwa moja yalionekana kuwa ni mabohari ya aina fulani.
Gari lilipita moja kwa moja hadi mbele ya moja ya yale majengo matatu ambapo dereva alipiga honi mara tatu, na geti kubwa la chuma lilisukumwa upande mmoja kutokea ndani na kuruhusu lile gari kuingia.
Vampire na Swordfish waliteremshwa chini ya uangalizi mkali na kuamriwa wasimame kando ya gari lile. Shani aliteremshwa na kusukumwa chini kwa nguvu, na kuachwa akigaragara. Baddi aliuma meno kwa hasira, lakini alikuwa akijitahidi kutuliza wahka mpaka atakapoonana na huyo adui yake.
Alitembeza macho kwa umakini sana ndani ya lile jengo lililomkumbusha ma-hanga ya kuhifadhia ndege. Mbele yao, ndani ya jengo lile kubwa lenye paa lililo juu sana, kulikuwa kuna mlango mwingine ambao ungewawezesha kuingia ndani zaidi ya jengo lile.
“Songa mbele huko!” Sauti nzuri aliwaburudisha tena wale wapiganaji, na wote watatu waliingizwa kwenye ule mlango uliokuwa mbele yao.
Walijikuta wameingia kwenye ofisi pana iliyokamilika, kinyume na hali waliyoiona kule nje. Moja kwa moja mbele yao kulikuwa kuna meza kubwa ikiwa na kiti kimoja cha kifahari nyuma yake, na viti vingine viwili mbele yake. Nyuma ya kile kiti cha kifahari kulikuwa kuna dirisha pana lililofunikwa kwa pazia kubwa, na juu ya kiti kile, mtu mnene na mrefu alikuwa ameketi ilhali akiwa amewageuzia mgongo. Mle ndani kulikuwa kuna watu wengine wawili walioshiba na ambao walikuwa wameshika bunduki fupi aina ya AK 47 mikononi mwao. Kushoto kwao mle ndani, kulikuwa kuna mlango mwingine ambao bila shaka ulikuwa ukielekea kwenye chumba kingine ndani zaidi ya jengo lile kubwa.
“Umekuja na mzigo wangu Baddi Gobbos?” Jamaa aliyekuwa kwenye kile kiti aliuliza kwa sauti nzito bila hata ya kugeuka.
“Baddi...ni nini kinaendele...” Shani alianza kusaili, lakini kabla hajamaliza, yule jamaa aliyemchanja kwa kisu kule Motel Agip alimzaba kofi la uso lililompeleka moja kwa moja mpaka chini.
“Kelele wewe!”
Hapohapo Swordfish alimrukia yule jamaa akiwa ametanguliza mikono yake kwa nia ya kumuadabisha, lakini kwa wepesi wa ajabu mmoja wa wale watu wawili waliokuwa mle ndani aliruka mbele yake na kumuwekea mtutu wa AK 47 kifuani.
“Tulia wewe! Muda wako wa kufa bado!” Jamaa alimkoromea, na Swordfish alibaki akimtazama yule jamaa mwenye kisu kwa ghadhabu, akimpuuzia kabisa yule baunsa aliyemsimamia na bunduki mbele yake. Muda wote Baddi Gobbos alikuwa akiikodolea macho sehemu ya kisogo cha yule mtu aliyemsemesha bila kumgeuzia uso, moyo ukimwenda mbio hali akihisi pumzi zikielekea kumuelemea.
Huyu ndiye mdunguaji kweli?
Na hata pale lile wazo lilipokuwa likipita kichwani mwake, yule mtu alijizungusha kwenye kile kiti na kuwageukia, akipandisha miguu yake juu ya ile meza.
“Nauliza umekuja na mzigo wangu Baddi Gobbos?” Jamaa aliuliza tena huku akimtazama moja kwa moja usoni.
“Wewe ni nani?” Baddi alimuuliza kwa hasira. Hapohapo jamaa mwenye AK 47 alimbamiza ubavuni kwa kitako cha bunduki ile huku akimkemea.
“Jibu swali uliloulizwa wewe!”
Baddi aliguna na kujipinda kwa maumivu.
“Hu...huyu ndiye aliyeniteka kule dukani huyu…ndiye!” Shani alipayuka kwa woga huku akimnyooshea kidole yule mtu na hapo mmoja wa wale mabaunsa wawili wenye bunduki alimuokoa na kipigo kingine kutoka kwa jamaa mwenye kisu kwa kuwahi kumzuia yule jambazi asimfikie.
“Kaa kimya bibie...utaumia bure!” Baunsa alimkoromea. Shani alibaki akimtazama yule jamaa mwenye kisu huku akitetemeka kwa woga mkubwa.
“Umekuja na mzigo wangu nakuuliza?” Mnene aliuliza tena, na Baddi alibaki akimkodolea macho ya kuuliza. Swordfish alikuwa akitembeza jicho mle ndani. Pamoja na wale watu wawili wakubwa wenye bunduki, wengine waliokuwamo mle ndani ni Sauti Nzuri na yule mwenzake mwenye
MDUNGUAJI
kisu. Wale majambazi wengine walibaki nje ya chumba kile.
“Makubaliano niliyokubaliana na mtu niliyekuwa nikiwasiliana naye, ambaye si wewe, ni kwamba nije nioneshe mali, kisha tukubaliane bei! Sasa wewe ni nani?” Baddi alijibu huku akimtazama kwa hasira.
“Hilo si la msingi! La msingi ni kwamba bei ulishapewa Baddi…aidha nipate mali au uwapendao waangamie…ambao ni wengi, sijui hata kama huyu mkeo anajua hilo!” Jamaa alimwambia huku bado akiwa amening’iniza miguu yake juu ya meza.
“Nilishakwambia huyu si mke wangu!” Baddi alimwambia.
“Na Claudia naye si mwanao?” Jamaa aliuliza.
“Hah! Unajua nini kuhusu Clau...” Shani alikuja juu huku akijaribu kumsogelea yule jamaa, lakini yule baunsa mmoja alimdaka shingo na kumsukumia ukutani kwa nguvu.”Kaa kimya mwanamke!” Alimfokea, na wakati huohuo bonge la mtu naye akawa anamkemea Baddi; “Mali yangu iko wapi wewe?”
“Kama umegusa unywele tu wa mwanangu…unywele tu narudia tena… ujue kuwa mali hupati na uhai wako halali yangu!” Baddi alimkoromea kwa hasira.
“Mikwara hiyo nimeanza kuisikia zamani hadi nimeizoea sasa Baddi…where are the diamonds?” Mnene alimkemea. Muda huo simu ya Sauti Nzuri iliita, naye alianza kuongea nayo, lakini bonge la mtu likamkemea naye akatoka nje.
“Ziko sehemu salama mpaka nitakapopata watu wangu wote!” Baddi alimjibu kwa jeuri. Jamaa alitikisa kichwa huku akitabasamu.
“Unajitia hamnazo sio?”
“Najaribu kuwa makini tu mzee. Mali nimeificha sehemu salama… inabidi niende kuifuata!” Baddi alimjibu huku akimtazama kwa makini, akilini mwake akijaribu kunasibisha umbo la yule mtu na Mdunguaji aliyekuwa akimsaka muda mrefu.
Ndiye?
Kwa wepesi wa ajabu, mnene alirukia upande wa pili wa ile meza, akamtandika Shani kofi kali sana la uso lililomsukuma na kumbabatiza tena ukutani. Shani aliachia yowe la uchungu kabla ya kuanguka sakafuni na kutulia kama mzigo, fahamu zikiwa zimemhama. Baddi aliachia ukelele wa ghadhabu huku akimrukia yule mtu mnene lakini alikutana na kitako kingine cha bunduki kilichotua sawia kwenye upande wa uso wake na kumpeleka chini kwa kishindo. Na wakati Baddi akipokea pigo
lile, Swordfish aliona nafasi ambayo angeweza kuitumia kuwasambaratisha wale adui zao, lakini yule jamaa mrefu na mnene alikuwa mwepesi kuliko aliyoonekana, kwani hapohapo alimtandika Swordfish teke zito la kifua na kumtupa chali mle ndani.
Kisha mnene akaketi kwenye moja wa vile viti viwili vilivyokuwa mbele ya meza yake, akiwaangalia wale mashujaa wa vita wakijizoazoa kutoka sakafuni huku kila mmoja akitweta kivyake.
“Usiniletee kabisa huo ujanja wako wa kubak’shiwa hapa Baddi, umesikia wewe?” Mnene aliunguruma na kuendelea, “Nilishaanza kuamini kuwa hiyo mali imepotea miaka mitatu iliyopita, sasa leo iko mbele ya pua yangu siwezi kabisa kuiachia!”
Baddi aliinua uso wake kumtazama. “Mimi nimetekeleza sehemu ya ahadi yangu, wewe bado…kwa sababu tayari nimeshakupatia ushahidi kuwa almasi ninazo, nawe sasa yakupasa unioneshe ushahidi kuwa watu wangu wako salama.” Alimjibu huku akijiinua kutoka pale chini, mmoja kati ya wale wafuasi wawili wenye bunduki akimfuatilia kwa makini.
“Unaongea nini wewe? Ni ushahidi gani wa almasi ulionipatia?” Mnene alisaili kwa jazba.
“Khah! Wewe umeagiza kuwa zile almasi nilizokuwa nazo nimkabidhi msaidizi wako, halafu yeye akikupigia simu kuwa anazo, ndiyo tuje huku sio?” Baddi alimuuliza kwa mshangao, na kumalizia, “Na ndivyo ilivyokuwa!”
“Khah! msaidizi wangu? Msaidizi wangu gani huyo?” Mtu mrefu mnene alimuuliza kwa utulivu huku akiwa amefinya macho.
“Khah! Kwani we’ si ulituma vijana wako waje watuchukue pale Motel Agip…?”
“Hatukuwa na makubaliano hayo!” Jamaa alifoka kwa hasira.
“Mnhu! Look who’s talking now…” Baddi aliguna na kusema kwa kebehi, kisha akaendelea, “…basi mi’ nimempa zile almasi za kuoneshea kama ulivyoagiza…na sehemu iliyobaki ya mzigo ndiyo iko mahala salama kwa sasa!”
“Ni nani huyo uliyempa pumbavu wewe?” Jamaa alifoka huku akiinuka kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia. Sasa hali ya mle ndani ilikuwa ikifukuta kweli kweli. Baddi na Swordfish walitazamana, kisha kwa pamoja, wakamuoneshea kidole yule mkorofi mwenye kisu.
E bwana we!
Mnene alimgeukia yule mfuasi wake kwa mshangao uliochanganyika na ghadhabu. Na hata pale alipokuwa anageukiwa, yule jamaa naye akawa ame -
MDUNGUAJI
finyanga uso wake kwa mchanganyiko wa mshangao, mshituko, hasira na tanabahi ya kufikwa kwa namna ambayo hakuitarajia kabisa.
“Ah! Waongo wakubwa hawa, hebu kwanza...” Alimaka huku akipiga hatua kumuendea Baddi huku akiwa ametanguliza mbele kisu chake.
“Hapo hapo!” Mnene alifoka na yule jamaa akasita kwenye hatua zake.
“Hah! Mbona sielewi? Mi’ nimemkabidhi mzigo wote niliokuwa nao huyu jamaa…!” Baddi alijitia kusema kwa taharuki kubwa.
“Muongo mzandiki! Anataka kutuchanganya tu huyu saa hizi...!” Jamaa mwenye kisu alimaka.
“Hebu kelele!” Mnene alifoka na kumgeukia Baddi “Unasema ulimpa huyu almasi zangu?”
“Ndivyo! Alisema kuwa wewe uliagiza hivyo...” Baddi alijibu, lakini hapohapo yule jamaa mwenye kisu alimrukia huku akipiga ukelele wa ghadhabu.
“Muongoooo…!”
Kosa kubwa sana.
Hapohapo mmoja wa wale mabaunsa wenye bunduki alijirusha pembeni
akijaribu kumzuia, au kumpisha, haijulikani, ila kwa kufanya vile alimpa Swordfish nafasi aliyokuwa akiisubiri. Mzanzibari yule alirudi nyuma hatua moja na kutupa teke la nguvu lililompita katikati ya miguu yule baunsa kutokea nyuma na kutua kwenye korodani zake. Jamaa aliachia yowe kubwa huku akienda chini mzima mzima.
“Hhheh!” Mnene alipiga ukelele na kugeuka kule kwa Swordfish. Yule baunsa wa pili aliachia mguno na kuanza kujifaragua, lakini hapo Baddi Gobbos naye akafanya vitu vyake. Alikikwapua kiti kilichokuwa mbele yake na kumtupia, na hapohapo akaruka juu na kukanyaga ile meza ya kifahari iliyokuwa pale ofisini kwa mguu wake wa kushoto, na kujirusha tena hewani huku akikunjua mguu wake wa kulia na kumtandika teke zito la kichwa yule mtu mnene. Jamaa akaenda chini kwa kishindo huku yowe la mshituko likimtoka.
Huku nyuma, Swordfish alimkanyaga mgongoni yule baunsa aliyekuwa akiangukia uso mbele yake, na kujirusha hewani kama jinsi Baddi alivyotumia ile meza kujirusha hewani, na kumshindilia teke la mtindo wa “Flying Kick” yule mjinga-mjinga mwenye kisu, teke ambalo lilimpata nyuma ya shingo na kumbabatiza ukutani, kile kisu kikimtoka mkononi.
Baddi Gobbos alirudi chini, akadunda, kisha akaenda tena hewani, safari hii akitanguliza miguu yake yote miwili na kuishindilia kifuani kwa
yule baunsa aliyemtupia kiti hapo awali ambaye ndiyo alikuwa akijaribu kujiweka sawa ili ashambulie kwa ile bunduki yake. Wote wawili wakaenda chini kwa kishindo, bunduki ikimtoka yule baunsa. Baddi alijigeuza haraka kutoka pale chini, na alimuona yule mtu mnene akimwendea mbio huku akiwa amekenua meno kwa hasira. Alijitahidi kujiinua lakini baunsa akamvuta mguu na kumrudisha chini kwa kishindo. Alijitahidi kuinuka tena lakini yule mtu mnene alikuwa amemkaribia sana naye hakuwa na namna ya kumkwepa.
Hapo alimshuhudia Swordfish akiwaruka yeye na lile baunsa pale chini kutokea nyuma yao huku akipiga ukelele wa ghadhabu na kuliparamia lile bonge la mtu kwa nguvu, bega lake la kushoto likijibabatiza tumboni kwa yule mtu mkubwa huku kwa mkono wake wa kulia akimkumbamtia kiunoni. Bonge la mtu liliachia mguno wa mshituko huku likiyumba vibaya na kupoteza muelekeo.
Baddi alimgeukia yule baunsa aliyekuwa naye pale chini na kumshindilia kiwiko cha uso, baunsa akaguna kwa uchungu huku akiangukia pembeni. Baddi alijirusha wima na kumuwahi kwa teke zito la shingo yule baunsa aliyeanza kuinuka, na baunsa alitupwa chini kwa msukumo wa teke lile na kupigiza vibaya kichwa chake sakafuni. Alifurukuta kidogo kisha akatulia kama gogo, fahamu zikimhama. Na hapo Baddi alisikia kishindo kikubwa kutokea nyuma yake. Aligeuka kule kilipotokea kile kishindo na kuona kuwa Swordfish na lile bonge la mtu walikuwa wameangukia kwenye ile meza kubwa ya kifahari, bonge la mtu likipigiza mgongo kwenye ile meza huku Swordfish akiwa amemuangukia kifudifudi juu yake.
Na hata pale alipokuwa akiona kitendo kile, Baddi Gobbos aliushuhudia mkono wa kulia wa Swordfish ukienda hewani na kushuka kwa nguvu na kushindilia bisu lililokuwa kwenye mkono ule pale mezani, na hapohapo bonge la mtu liliachia yowe kubwa na refu sana la uchungu. Alimuona Swordfish alijibwaga chini kutoka pale mezani huku lile bonge la mtu likiwa bado limelalia mgongo pale mezani likipiga mayowe, mkono wake wa kushoto ukiwa umelala mezani juu ya kichwa chake.
Bila ya kusubiri zaidi aliiwahi ile bunduki iliyokuwa mikononi mwa yule baunsa aliyepoteza fahamu na kuwaguekia wale wafuasi wengine wa yule mtu mnene na kuwalengeshea ile bunduki.
“Wote tulia…Bloody fools!” Aliwafokea, na jamaa wakasita. Kutokea pale
MDUNGUAJI
aliposimama aliona mpini wa lile bisu lililokuwa mkononi kwa Swordfish ukiwa umechomoza kwenye kiganja cha mkono wa kushoto wa lile bonge la mtu, lile bisu likiwa limekishindilia kile kiganja pale mezani na kumfanya bonge la mtu ashindwe kujinasua na abaki akilia kwa uchungu huku damu ikitambaa pale mezani.
Swordfish kiboko!
Hata pale wazo lile lilipokuwa likipita kichwani mwake, alimuona yule shababi wa ki-zanzibari akijiinua kutoka pale sakafuni huku akiokota bunduki iliyokuwa karibu naye na kumuelekezea yule mtu mnene aliyekuwa akihangaika huku akigumia kwa uchungu pale mezani.
Wafuasi wa bonge la mtu walibaki wakiwa wamepigwa butwaa mle ndani, wakishindwa kabisa kuamini jinsi ule mchezo ulivyowageukia. Baddi alimuendea yule jamaa aliyekuwa na kisu hapo awali, ambaye sasa alikuwa amejibweteka sakafuni bila kuamini kilichompata, akiukodolea macho mpini wa kisu chake ukiwa umekikandamiza mezani kiganja cha bosi wake.
“Toa bastola yetu uliyochukua kule Motel Agip wewe!” Baddi Gobbos alimfokea huku akiwa amemuwekea mtutu wa ile bunduki. Kwa kitetemeshi kikubwa jamaa aliichomoa ile bastola na kuiweka sakafuni. Baddi alimtwanga kichwani kwa kitako cha ile bunduki na jamaa akatikisika kidogo kisha akapoteza fahamu. Aliichukua ile bastola na kuining’iniza begani ile bunduki ya baunsa, kisha bila hata ya tahadhari, aliwatandika risasi za miguu wale mabaunsa wawili kwa ile bastola ya Swordfish iliyokuwa imefungwa kiwambo cha kuzuia sauti. Jamaa waliachia mayowe makubwa huku wakijitupa huku na huko pale sakafuni wakati mlango wa kuingilia mle ndani ukisukumwa kwa nguvu na Sauti Nzuri akiingia.
“Oyaaa...vipi huk…?” Alipigwa butwaa pale alipokutana na jicho kali la Swordfish aliyekuwa amemuwekea mtutu wa ile AK 47 bonge la mtu pale mezani.
“Ingia ndani taratibu swahiba, na mikono yako iwe juu!” Swordfish alimkoromea kwa hasira. Sauti Nzuri alisita, akitembeza macho huku na huko mle ndani, kisha akamtulizia Swordfish macho ya ghadhabu, na hapohapo alikenua meno kwa hasira huku mkono wake ukiinuka ukiwa na bastola.
AK 47 ilibanja kutokea mkononi kwa Swordfish, na Sauti Nzuri alitupwa nyuma kwa msukumo wa risasi, yowe la taharuki likimtoka na kujipigiza ukutani kabla ya kutawanyika sakafuni akiwa na baka kubwa la damu kifuani.
“Mnaambiwa mkaimbe taarabu hamtaki, khabbiithi-l-amal!” Swordsfish aliisimanga maiti ya Sauti Nzuri, tayari akiwa ameurudisha mtutu wa ile bun-
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
duki kichwani kwa bonge la mtu lililobanwa pale mezani. Baddi alipiga hatua za haraka hadi pale mezani.
“Dhibiti usalama wa hapa Swordfish, nahitaji kuongea na huyu fala sasa!” Alisema huku akimtazama yule adui yake kwa macho ya hasira. Mnene alibaki akimtazama huku akitweta kwa taabu. Swordfish aliufunga kwa ndani ule mlango na kusimama kando yake, bunduki yake ikiwa makini mkononi mwake.
Baddi Gobbos aliweka mkono wake kwenye mpini wa kile kisu na jamaa alilia kwa uchungu kutokana na maumivu aliyoyapata.
“Yu wapi mwanangu Claudia, eeenh!?” Baddi alimuuliza kwa ukali huku akiwa amemuinamia pale mezani. Jamaa alizidi kupiga mayowe ya uchungu, na Baddi alizidi kukididimiza kile kisu. Mnene alilia kama mbwa!
Baddi aliuachia ule mpini na kumkemea, “Nahitaji majibu paka shume wewe! Na nahitaji majibu upesi….la si hivyo mtindo utakuwa ni huo huo… nakandamiza kisu mpaka mpini wote upotelee ndani ya hii meza. Now tell me, yu wapi mwanangu?”
Jamaa alibaki akitweta kwa maumivu huku akimtazama kwa macho yaliyojaa chuki huku akiwa amebana meno kwa uchungu.
“Yu wapi Gilda?” Baddi alimbandika swali jingine.
“Al…masi! Toa Almasi…kwanza!” Jamaa alisema kwa kutweta.
“Ebbo!” Swordfish alimaka kutokea kule alipokuwa, wakati Baddi Gobbos
akimtazama yule mtu mroho wa mali isiyo yake kwa mshangao na hamaki kubwa. Yaani hata katika wakati mgumu kama huu bado mjinga anaulizia almasi!
Alimzaba kofi la uso.
“Acha ujinga wewe! Yu wapi mwanangu nakuuliza?”
Jamaa alimtemea mate mazito yenye mchanganyiko ya damu usoni kwa hasira, kisha akamtupia na tusi zito la nguoni. Baddi alimaka kwa hasira naye hapohapo akamtemea mate usoni yule jamaa kisha akaukamata ule mpini na kuusukuma mbele na nyuma kama anayeingiza gia ya gari. “AAAAAAAAYYYAAAAA….AAAA!” Jamaa alilia kwa sauti huku akitupatupa miguu huku na huko, na hapo aliivuta ile meza na kusambaratika nayo hadi sakafuni kwa kishindo. Baddi aliruka pembeni na kumtazama yule jamaa aliyebaki akiwa ameketi sakafuni huku ameegemea ile meza kwa mgongo wake ilhali ule mkono wake wa kushoto bado ukiwa umebanwa na kile kisu kwenye uso wa meza ile, na hivyo kubaki ukiwa umeinuliwa juu ya kichwa chake, damu ikichuruzika kwa wingi kutoka kwenye lile jeraha.
“Sema upesi Paka wewe...yu wapi mwanangu…?”
MDUNGUAJI
“AAAARGH…”
“Sema!”
“Mama weee..”
“Mamaako hayupo hapa shaitwani weye! Tuambie tukubakshie huo uhai wako mbovu ulobakia!” Swordfish alimkemea kutokea kule mlangoni.
“Ah! Si…Sijui! Sijui jamani….”
“Hu...whaat? Unajitia ujanja wakati kifo kimekukabili fala wewe? Where is my daughter?” Baddi alimkemea yule mtu.
“Nasema…kweli jamani…sivyo mnavyodhani…” Jamaa aligumia kwa taabu. Sasa alikuwa akilia kama mtoto. Hapohapo vilisikika vishindo kutokea nje ya ule mlango. Baddi alijirusha haraka kutoka pale alipokuwa na kujibanza kando ya ule mlango, hivyo yeye akawa amejibanza upande mmoja wa mlango na Swordfish akiwa amejibanza upande mwingine. Muda huo alishuhudia ule mlango ukibutuliwa kwa kishindo kutokea kule nje, na mmoja wa wale watekaji nyara wao wa kule Motel Agip akibingirika mle ndani na kulala sakafuni.
Mbinu za medani ziliwatuma watulie pale pale walipokuwa, wakimuangalia yule mtu aliyeangukia mle ndani namna ile, wote wakiwa wamemuelekezea silaha zao. Jamaa alibaki akiwa amelalala vile vile pale chini, hakuinuka wala hakutikisika.
Mtu wa kawaida angeweza kukurupuka na kwenda kumsogelea pale chini kutaka kuona kilichomsibu, lakini Kanali Baddi Gobbos p.a.k. Vampire, na Meja Abdul Hameed Babu p.a.k. Swordfish, hawakuwa watu wa kawaida. Walitulia kimya, wakiwa makini sana.
Baada ya muda kupita bila tukio lolote kutokea, jamaa alijiinua kutoka pale sakafuni akiwa makini na bastola mkononi, na alipogeuka alikutana na mitutu miwili ya silaha zilizokuwa mikononi mwa wale wapiganaji mahiri naye akabaki akiwa amepigwa butwaa. Lolote alilolitarajia kwa kujirusha mle ndani namna ile halikuwa.
“Tupa chini hiyo bastola wewe!” Swordfish alimkoromea kwa hasira. Jamaa alimtazama kwa wasiwasi, akahamishia macho yake kwa Baddi na kuyarudisha tena kwa Swordfish.
“Mi...mi’ niko upande wenu jamani...” Alisema kwa wahka huku akiwatazama kwa zamu wale wapiganaji.
“Tupa chini hiyo bastola mwanakwetu! Uko upande wetu tangu lini baradhuli mkubwa wewe?” Baddi alimjia juu. Jamaa aliona kuwa alikuwa amezidiwa. Alitii ile amri na kubaki akiwa ameduwaa.
“Kaa chini kwenye kona kule!” Baddi alimkoromea huku akimuoneshea
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
kona moja ya chumba kile. Jamaa alitekeleza amri ile huku akiwa amekunja uso kwa hasira.
Na hapo Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani aliingia mle ndani kwa tahadhari kubwa, bastola ikiwa imetangulizwa mbele yake, na haraka sana akajirusha pembeni na kugeukia kule mlangoni. Akakutana uso kwa uso na wale wanafunzi wake katika medani za kijeshi.
“Meja Jenerali!” Swordfish alimaka.
“Baddi…Meja Babu!” Gaudence Amani alisema kwa hamasa, bado uso wake ukiwa amebandikwa ile miwani yake ya jua, ambayo hata pale alipokuwa akimtazama kwa mshangao, Baddi Gobbos alibaini kuwa ilikuwa ni ile miwani ambayo iliweza kuvaliwa ndani na nje ya nyumba, ambapo ikiwa nje inakuwa ya jua, lakini ikiwa ndani inakuwa ya kawaida japo vioo vyake vinaendelea kuwa na muonekano wa kiza.
Taratibu za kijeshi zilichukua nafasi wakati wale wapiganaji wawili walipobana silaha zao na kukauka kwa saluti kali kwa mkuu wao wa zamani, na Meja Jenerali aliijibu ile saluti haraka, kisha akaligeukia lile bonge la mtu lililojibweteka pale sakafuni likiwa limebanwa kwenye meza na kile kisu.
Bonge la mtu lilimtazama Gaudence kwa matumaini, na lilikuwa linataka kufunua kinywa kusema kitu wakati Gaudence alipowageukia akina Baddi.
“Ni nini kinaendelea hapa! Nimekuwa nikilifuatilia lile gari lililowachukua kutoka pale Motel…” Na hata pale alipokuwa akisema vile, macho yake yakaangukia kwa Shani aliyepotezakuwa amelala bila fahamu sakafuni.
“Oooh, Shani….” Alisema huku akimkimbilia pale chini. Baddi na Swordfish walitazamana, kisha wakamgeukia yule mkuu wao wa kazi wa zamani aliyekuwa amemuinamia Shani aliyepoteza fahamu.
“Baddi, I am sorry, lakini sote tuliamini kuwa umekufa nd’o maana imekuwa hivi. Lakini...ni nini kinaendelea hapa…?” Gaudence aliwageukia na kumuuliza Baddi. Baddi alibaki akimtazama kwa kutoamini, Swordfish akachukua nafasi ya kumjibu yule Meja Jenerali mstaafu.
“Ni hadithi ndefu Meja Jenerali…” alimwambia, “...ila kwa ufupi ni kwamba hawa watu walimteka Shani, na pia tunaamini kuwa wamemteka Claudia…”
“Sasa kwa nini wawateke …?” Gaudence aliuliza kwa mshangao.
“Kwa sababu wanaamini kuwa nina almasi nilizotoka nazo huko Sierra Leone…wao wanazitaka. Kwa hiyo wamewaweka rehani mpaka niwape hizo almasi…” Baddi alidakia huku akimtazama Gaudence kwa makini.
“Ah! Is it possible? Wape basi hicho watakacho waturejeshee mtoto…hebu
MDUNGUAJI ona sasa mambo kama haya…!” Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani alisema kwa kiherehere.
“No! Hatuwezi kuwapa kwa sababu sasa sisi ndiyo tumewadhibiti Meja Jenerali! Huyu shaitwani atasema tu ni wapi Claudia alipo, Bloody fool!” Baddi alisema na kumrudia tena yule mtu mnene aliyebaki akiwa ametumbua macho kwa woga usio kifani. Alimkwida kwa nguvu huku kwa mkono wake mwingine ukiukandamiza ule mpini wa kisu kilichobabatiza kiganja cha yule mtu pale mezani. Jamaa alilia kwa uchungu na maumivu.
“Sema ni wapi walipo watu wangu wewe!” Alimkemea kwa hasira. Jamaa alibaki akilia kwa uchungu na maumivu makubwa kabisa. Meja Jenerali Gaudence alimsogelea pale mezani.
“Baddi…una hakika hii ni njia sahihi? Je huyu mtu akifa kabla hajasema, tutajuaje alipo mtoto? Naona tutumie busara….”
“Hakuna busara hapa!” Baddi alifoka huku akididimiza mdomo wa bastola yake usoni kwa yule jamaa aliyekuwa katika maumivu makubwa.
“Ni wapi walipo watu wangu wewe?” Alizidi kumkemea yule adui yake.
“All...masi…!” Jamaa aligumia.
“Unaona? Huyu mtu anaweweseka na kifo! Atakufa sasa hivi na tutakosa kila kitu! Hebu mpe hizo almasi ili angalau atutajie…” Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Amani alimnong’oneza Baddi kwa msisitizo. Baddi alijikuta akishindwa kudhibiti hisia zake na kumgeukia mkuu wake wa kazi wa zamani na kumsukuma kwa nguvu.
“Hebu nipishe wewe!” Alimkemea, kisha akamgeukia yule mtu mnene na kumzaba kofi la uso, halafu akamkamata kichwa chake na kukibamiza kwa nguvu kwenye uso wa ile meza.
“Utasema tu wewe, kwa sababu nitahakikisha haufi mpaka useme, na ukishasema nakuua kwa mikono yangu, kimburu wee! Ni wapi walipo watu wangu, eenh? Wapi mwanangu?” Baddi alimkemea yule adui mnene ambaye sasa alikuwa hajiwezi kabisa. Alikuwa akibwabwaja maneno yasiyoeleweka, lililosikika likiwa ni “almasi” tu.
Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani alimsogelea Swordfish na kumuoneshea Baddi kidole.
“Hebu mshauri rafikiyo Meja! Afanyacho ni jazba badala ya kutumia akili! Hii hali ni tete sana! Hatuko mahala pa kutumia ubabe tena sasa…ampe tu hizo almasi! Angalau amuoneshe tu ili aone kuwa kweli zipo, akitaja tunaachana naye, sio lazima ampe hizo almasi kama anazo!”
“Baddi anajua afanyacho Meja Jenerali!” Swordfish alimjibu.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Lakini sio kwa hiki nikionacho hapa Meja! Hapa inaonekana kabisa kuwa hajui afanyacho…yule mtu anaweza kufa muda wowote…”
“Swordfish!” Baddi aliita kutokea pale alipokuwa, kisha bila kugeuka akasema, “Huyu mjinga atasema tu, na wakati mimi nahakikisha kuwa anasema, wewe fanya upekuzi wa jengo hili…” Kisha akamgeukia Meja Jenerali mstaafu
Gaudence Amani.
“Gaudence umempata mkeo, hivyo pamoja na heshima zote nakuomba uchukue mkeo uende! Tuachie sisi tumalize matatizo yetu kwa namna tuijuayo sisi mzee, sawa?”
Kimya kizito kilitanda mle ndani wakati Gaudence Amani na Baddi Gobbos wakitazamana kwa hasira, Baddi akiishia kujiona taswira yake tu kwenye miwani ya yule mkuu wake wa kazi aliyegeuka mume mwenza.
Swordfish aliona hisia kali zilizokuwa zikipita baina yao wakati ule, na alitafuta namna ya kuondoa mtafaruku uliokuwa unaelekea kutokea.
“Mimi pia nina haki ya kuhakikisha kuwa Claudia yuko salama Baddi!”
Gaudence alijibu kwa hasira, na kumalizia, “na ndiyo maana nataka utumie akili badala ya jazba…”
“Nimekwambia chukua mkeo uondoke! Claudia ni mwanangu na ni mimi ndiye mwenye uchungu naye kuliko yoyote yule hapa duniani! Umeshachukua mke wangu haikutoshi?” Baddi alimjia juu.
“Alaa, kumbe hilo ndilo tatizo sio? Si ulikuwa umekufa bwana…yaani wivu wa kijinga kuhusu mkeo kuolewa ndiyo unakufanya uache kutumia akili…” Meja Jenerali mstaafu Gaudence alisema.
“Gaudence!” Swordfish alifoka kunyamazisha hali ile, lakini Gaudence Amani alikuwa amedhamiria kusema aliyotaka kuyasema, alikuwa ameghadhibika ghafla. “ …yaani we’ kwa mapenzi hujiwezi kabisa Baddi. Ndiyo maana siku zote nilikuwa nadhani kuwa huwezi kuwa mpiganaji mzuri!”
“Hukuwahi kuniambia hivyo hata siku moja!” Baddi naye alimjia juu.
“Jamani hebu acheni ujinga hapa, ebbo!” Swordfish alimaka.
“Nakupa ukweli wa mambo Baddi! Unaachia wivu wako wa mapenzi ya kitoto uhatarishe maisha ya mtoto ambaye yuko mikononi mwa hao watu… au niseme kuwa huna lolote ila umeweka mbele tamaa ya utajiri tu! Kama ungekuwa una upendo wa dhati ungewapa hawa watu vitu wanavyotaka ili umpate mwanao…” Gaudence alimwambia kwa hasira.
“Nimpe marehemu mtarajiwa huyu?” Baddi alimjia juu.
“Jamani hapa tuko ndani ya eneo la adui! Huu si muda wa kuanza kukorofishana, nyie vipi?” Swordfish aliwakemea.
MDUNGUAJI
“Si huyu rafiki yako! Hana ajualo…ama kweli kama angekuwa rangi basi angekuwa njano huyu! Rangi ya mapenzi-mapenzi tu, kama siagi! Yaani ye’ kwa sababu ya mapenzi yu-radhi mtoto apotee…”
Baddi Gobbos alihisi ganzi ikimtembea mwili mzima, na wala hakusikia sehemu ya mwisho ya ile kauli ya Meja Jenerali mstaafu Gaudence, kwani yale maneno yalimgonga ndani kabisa ya ubongo.
Wewe ni laini sana Baddi...kama ungekuwa rangi basi ungekuwa njano, rangi ya upendo na ulaini-laini…kama siagi…
Maneno ya hayati Nathan Mwombeki, p.a.k. Alpha, kule msituni, miaka mitatu iliyopita!
Alihisi dunia ikijigeuza nje ndani, naye akifinyangwa ndani yake. Alimtazama kwa makini yule mkuu wake wa kazi wa zamani, na aliona midomo ikimtembea wakati akiongea, lakini hakusikia lolote zaidi ya ile kauli ya hayati Nathan ikijirudia tena na tena kichwani mwake. Akili yake ilirudi kule msituni alipokuwa akiongea na msaliti Nathan kabla hajapigwa risasi na kuangukia korongoni. Maneno yale aliyeyajua ni yeye na Nathan tu…na Mdunguaji… ambaye bila shaka alikuwa akisikia kila walichokuwa wakikiongea kupitia kwenye redio iliyokuwa ikitupiana mawasiliano na ile ya msaliti Nathan!
Mdunguaji!
“Ni wewe!” Baddi alifoka ghafla huku akimrukia Meja Jenerali mstaafu Gaudence na kumsukuma kwa nguvu. Swordfish alipiga ukelele wa kuasa tukio lile, wakati Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani akisukumwa nyuma na kujipigiza ukutani, miwani ikimtoka usoni na kuanguka chini. Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani aliinua uso wake na kumtazama Baddi kwa hasira iliyokothiri.
Wakakutana uso kwa uso.
Macho! Oh My God…!
Yale macho…La Haula! Yale macho…
Kovu baya lilikuwa limetambaa pembeni ya jicho la kulia la Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani, kovu ambalo hakuwa nalo kabisa hapo awali.
Je ni risasi ya Honey-Bee iliyomjerushi kule msituni?
Alikumbuka jinsi alivyokutana macho kwa macho na Mdunguaji siku ile alipopigwa risasi ya kifua kule msituni miaka mitatu iliyopita. Aliiona ghadhabu halisi iliyokuwa machoni kwa Mdunguaji wakati ule…
Ni macho haya haya…
Na ghadhabu ile ile…
Duh!
Swordfish aliona badiliko lililokuwa likipita usoni kwa Baddi wakati ule na mara moja akabaini kuwa kuna jambo limejiri.
“Whaat…?” Alianza kusema lakini Baddi alimuwahi.
“Wewe ndiye mdunguaji Gaudence…ni wewe!” Alimwambia yule mtu aliyekuwa mbele yake huku akimnyooshea bastola iliyokuwa mkononi mwake.
“Ama!” Swordfish alimaka.
“Mdunguaji…? Hujui ukiongeacho wewe…!” Gaudence Amani alianza kusema, lakini Baddi akamkatisha.
“Why?”
Meja Jenerali Gaudence alijaribu kufumbua kinywa lakini akaghairi.
“Na ni wewe ndiye uliyekuwa ukiongea kwenye simu ukiiweka simu kwenye mfumo wa spika!” Baddi alimkemea tena huku akimsogelea.
“Kwa hiyo yeye na huyu khabbith wote lao moja?” Swordfish alimaka kwa mshangao huku akimuoneshea kidole yule mtu mnene aliyebanwa na kisu pale mezani.
“Why…?” Baddi alimuuliza tena Gaudence kwa uchungu.
“Jibu unalo Baddi…” Gaudence alimjibu huku akimtazama kwa ghadhabu.
“Nataka uniambie wewe sababu ya yote haya! Umenipeleka mwenyewe kule msituni…”
Meja Jenerali Gaudence alitupa teke la ghafla lililoipangusa ile bastola kutoka mkononi kwa Baddi na hapohapo alijirusha mzima mzima akitanguliza miguu yake mbele kwa mtindo wa tandika reli na kumkumba Swordfish katika pigo lile lisilotarajiwa na kumgaragaraza chini yule mzanzibari, bunduki iliyokuwa mkononi mwake ikimtoka.
Muda huo yule jamaa aliyeamriwa akakae kwenye kona ya kile chumba hapo awali alijirusha wima na kumtandika Baddi teke la mbavu. Baddi alijikunja kwa pigo lile lakini hapohapo akaukamata ule mguu uliompiga teke na kumchota ngwara kali yule jamaa aliyeenda chini kama gogo. Baddi alijirusha juu na kumdondokea kifuani yule adui yake kwa magoti yake na akasikia jinsi mbavu na mifupa ya kifua ya yule mtu vikivunjika, jamaa akipiga kelele za uchungu. Alijirusha tena wima na kumgeukia Gaudence Amani, na kuona akiwa amekabiliana uso kwa uso na Swordfish.
“Kumbe mdunguaji ni weye Gaudence?” Swordfish alimuuliza kwa mshangao na hasira, lakini Gaudence hakuwa na muda wa maongezi. Alimrushia teke zito lakini Swordfish aliliona na kuruka pembeni na hapohapo alirusha pigo kwa mkono wake wa kulia ambalo lilimpata Gaudence kwenye koo. Gaudence
MDUNGUAJI
alitoa sauti ya maumivu huku akiyumba wakati Swordfish alipojigeuza kwa teke la kuzunguka lililompata Gaudence kisogoni na kumsukuma mbele kwa nguvu. Baddi Gobbos alimdaka koo kwa nguvu na kwenda naye juu mzima mzima kisha akambwaga chini kwa kishindo huku bado akiwa amemkamata koo.
“Wewe ndiye mdunguaji Gaudence…na wewe ndiye utakayejibu maswali yetu sasa!” Baddi Gobbos alimkemea akiwa amembana pale sakafuni. Gaudence akijikurupusha na kumsukuma pembeni huku akiunguruma kwa ghadhabu, kisha akajiinua na kugeukia mlangoni lakini hapo alikutana na Swordfish ambaye alimtandika teke zito la mbavu. Gaudence aliyumba kwa pigo lile na Swordfish akamrukia kwa teke jingine lakini safari hii Gaudence alilizuia kwa mikono yake, kisha naye akamrushia teke kali. Swordfish aliruka nyuma na lile teke likamkosa. Walitazamana kwa hasira kisha wakarukiana kwa ghadhabu na kuanza kutupiana mapigo ya haraka haraka kwa mikono yao, mapigo yale yakipanguana kwa ustadi mkubwa bila ya hata pigo moja kutua mahala lilipokusudiwa.
“No, Baddi! Huyu niachie mimi!” Swordfish alimzuga kwa kuropoka ghafla huku bado akishambuliana na Gaudence. Gaudence alijigeuza kujaribu kufuata uelekeo wa jicho la Swordfish nalo likawa kosa. Swordfish alimpiga shingoni kwa nguvu kwa ubapa wa kiganja chake. Gaudence aliyumba huku akigumia, na hapohapo Baddi Gobbos akaenda hewani na kumshindilia kichwa kilichotua katikati ya mwamba wa pua. Gaudence alijibamiza ukutani huku akihisi nyota nyingi zikitanda mbele ya macho yake. Alirusha ngumi kali bila hata ya kuangalia na kuishia kupiga hewa. Akageuka upande wa pili kwa ngumi nyingine kali, lakini nako alijikuta akipiga hewa. Bado nyota zikiwa zimetanda mbele ya macho yake aliinua uso kwa hasira kujaribu kutafuta ni wapi walipo wale wapinzani wake, na alijikuta akipokea ngumi nzito ya uso kutoka kwa Baddi. “Hiyo ni kwa ajili ya marehemu Cheetah, nyang’au wee!”
Ile ngumi ilimsukuma pembeni, ambako alikutana na Swordfish, ambaye alimrukia teke zito la kifua lililombabatiza ukutani. “Na hiyo ni kwa ajili ya Glimmer, hayawani wee!”
Gaudence Amani alijibwaga chini kwa kishindo huku akikohoa na damu ikimtiririka. Baddi alimkamata mabega kutokea nyuma na kumuinua kimabavu kisha akamsukuma mbele kwa nguvu.
Swordfish alimdaka shingo na kumshililia kichwa cha uso. “Na hiyo ni kwa ajili ya Black Angel!” Alimwambia, kisha hapohapo akamtwanga kichwa kingine, “Na hiyo ni kwa ajili ya Eagle!” Alimwambia na kumsukuma nyuma
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
kwa nguvu wakati Meja Jenerali Gaudence akilia kwa uchungu huku akipepesuka. Baddi alimchota ngwara kali kutokea nyuma na Gaudence alijibwaga kama mzigo. Hapohapo alijigeuza na kujaribu kuinuka lakini aliishia kupiga magoti huku akiwa ameshika sakafuni kwa mikono yake miwili kama mbuzi, kichwa kikimuelemea.
Baddi alirudi nyuma na kumtandika teke kali sana la kichwa. “Na hiyo ni kwa ajili ya Black Mamba, khanithi mkubwa wee!”
Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani alitupwa kando na kusambaratika hadi ukutani, kisha kwa nguvu alizobakia nazo alijiinua na kumrukia Swordfish mzima mzima huku akipiga kelele za ghadhabu. Swordfish aliruka pembeni na Gaudence alipitiliza moja moja na kujibamiza ukutani, kisha hapohapo akatimua mbio na kupotelea nje ya ule mlango wa kutokea nje ya chumba kile.
“Swordfiiish!!!” Baddi alipiga ukelele huku akijaribu kumrukia mbaya wake. Na hata pale alipokuwa akiruka kuelekea kule mlangoni alipopotelea
Gaudence Amani, alisikia milipuko miwili ya bastola na sauti nzito ikitoa amri kwa sauti kubwa kutokea kule nje.
Oh Shit!
Baddi alijitupa nje ya chumba kile tayari kukabiliana na lolote liwalo, lakini hapo alijikuta akipigwa na butwaa.
Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani alikuwa amesimama kwenye ule ukumbi mpana huku akiwa ameinua mikono yake juu hali ameelekezewa bastola na yule mtu mrefu ambaye kwa mara ya kwanza Baddi alimuona pale makao makuu ya jeshi akiwa kwenye mavazi ya kijeshi.
“Uko chini ya ulinzi Meja jenerali! Tulia hivyo hivyo…!” Tabasamu Jepesi alisema huku akimtazama Gaudence Amani kwa hasira, na bila kuondoa macho yake kwa Gaudence, akaendelea, “Alright Baddi…mchaka mchaka wako sasa umekwisha, kuanzia hapa ni kazi yetu!”
“Whaaat…wewe ni nani…?” Baddi aliuliza kwa mshangao.
“Natoka kwenye kitengo cha upelelezi ndani ya Jeshi…niko upande wako. Tumekuwa tukimfuatilia Meja Jenerali hapa tangu alipochukua likizo ya dharura siku chache baada ya wewe kwenda Sierra Leone na kutoweka kabisa nchini, kisha akaibuka ghafla na kutangaza kustaafu…kabla hata ya muda wake…” Tabasamu Jepesi alimwambia.
Muda huo Swordfish naye alifika eneo lile, naye akishangazwa kwa hali ile. Na hata pale alipokuwa akishangaa, kundi la askari polisi wa kijeshi liliingia mle ndani kwa mikiki.
“Okay, mfunge pingu Meja Jenerali hapa, na awe chini ya ulinzi mkali!”
Tabasamu jepesi aliamuru.
“What? Hujui usemacho wewe! Mimi ni Meja Jenerali mstaafu bwana, ebbo!” Gaudence alimaka huku akianza kushusha mikono yake na hapo
Tabasamu Jepesi alimkemea kwa ukali.
“Mikono Juu Meja Jenerali!”
Gaudence alisita, hakutaka kuamini kuwa alikuwa amenaswa kirahisi namna ile. “Huna mamlaka ya kunidhibiti mimi wewe!” Alimkemea kwa ukali.
“Mamlaka hayo anayo Gaudence, na kama hutaki basi mimi pia nakuweka chini ya ulinzi as of this moment!” Sauti nyingine ilifoka na wote wakageukia ilipotokea ile sauti.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Baddi, Swordfish na Gaudence Amani walibaki wakimkodolea macho
Meja Jenerali Athanas Chacha aliyekuwa akiingia mle ndani taratibu. Mara moja Swordfish alimkumbuka kuwa alikuwa ni mmoja kati ya wale wakuu wa kijeshi kutoka Tanzania waliounda lile jopo la kijeshi lililowasaili baada ya matukio ya vifo vya msituni kule Sierra Leone. Wakati huo alikuwa na cheo cha Luteni Kanali. Saluti zilitembea mle ndani, kisha Meja Jenerali Athanas Chacha akawageukia wale askari wa kijeshi.
“Piga pingu huyu!” Aliwafokea, na mara moja wale askari walimdhibiti
Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani, ambaye kwa mshangao mkubwa alijikuta akifungwa pingu na kuwekwa chini ya ulinzi.
“Wengine fanyeni upekuzi humu ndani!” Tabasamu jepesi aliamuru na wale askari waliingia ndani ya jengo lile.
“Kazi nzuri sana kamanda!” Meja Jenerali Chacha alimwambia Tabasamu Jepesi, kisha akamgeukia Swordfish. “Meja Babu…inaelekea ulikuwa sahihi muda wote kule Sierra Leone…Baddi Gobbos hakufa kule msituni, au sivyo?”
Kisha bila kusubiri jibu la Swordfish akamgeukia Baddi. “Kanali Baddi Gobbos Vampire! Karibu tena katika ulimwengu wa walio hai kamanda! Tuna hamu ya kujua kisa chako, na kuelewa juu ya ule mwili tuliouzika miaka mitatu iliyopita tukiamini ni wewe…”
“Ndiyo afande…nami nina maswali mengi sana…”
“Okay, lakini first things first kama wasemavyo wazungu…tunahitaji kumaliza kituko kilichopo hapa kwanza.” Meja Jenerali Athanas Chacha alisema huku akizidi kuingia mle ndani. Swordfish na Vampire hawakuwa na la kusema, bado walikuwa wamepigwa mshituko kwa jinsi mambo yalivyobadilika haraka namna ile. Walichomeka bastola zao viunoni na kumtazama Meja Jenerali Athanas Chacha ambaye alikuwa akiifurahia kila dakika ya hali ile. Muda huo wale askari waliokuwa wakifanya upekuzi mle ndani walirudi tena eneo lile, pamoja nao alikuwapo Gilda na Claudia Gobbos.
“Hawa walikuwa wamefungiwa kwenye moja ya vyumba vya humu ndani kamanda!” Mmoja wa wale askari aliripoti.
Baddi na Gilda walikumbatiana kwa furaha, huku Gilda akibubujikwa na machozi. Lakini furaha kubwa ilikuwa ni pale Baddi Gobbos alipokutana tena na bintiye aliyemuacha akiwa na miaka mitano, lakini ambaye hata hivyo hakuwa amemsahau baba yake.
“Sielewi kinachoendelea jamani” Swordfish alisema kwa wahka.
“Ni hadithi ndefu Meja, lakini ufupi wake ni kwamba tulikuwa tukimpeleleza Gaudence kwa muda mrefu. Wacha tudhibiti hii hali hapa
kwanza halafu kesho asubuhi tutakutana ofisini kwangu ili mpate ufafanuzi
kamili…” Yule Meja Jenerali mpya alisema.
“No jamani…kesho ni mbali sana afande! Can we talk about this now please? Ningependa kulimaliza hili swala here and now!” Baddi alidakia huku akiwa amembeba binti yake.
“Naelewa wahka wako kamanda, lakini kuna taratibu za kufuatwa… nadhani tunaweza kuwekana sawa kwa kiasi fulani hapa hapa, kisha mambo mengine yatafuata taratibu zilizopo, okay?” Meja Jenerali Chacha alisema, kisha akaamuru wote warudi kule ofisini kwa mtu mnene, ambako walikuta maafa yaliyoachwa na akina Baddi, akiwamo yule mtu mrefu na mnene aliyekuwa amejibweteka sakafuni huku kiganja cha mkono wake kikiwa kimeshindiliwa pale mezani kwa kile kisu kikubwa, damu nyingi ikiwa imemtapakaa.
“Ama hakika hapa palikuwa na wapiganaji mahiri…mmefanya kazi nzuri sana Vampire!” Meja Jenerali Chacha alisema huku akitazama hali aliyoikuta mle ndani. Muda huo, kwa kufuata maelekezo ya Tabasamu Jepesi wale polisi wa kijeshi walianza kuwaondoa kutoka mle ndani wale mabaunsa na vibaraka wengine wa mtu mnene waliokuwa wamesambaratika huku na huko. Walipoanza kumchukua yule mtu mnene Meja Jenerali Athanas Chacha aliwazuia. “Huyo muacheni kwanza…chomoeni hicho kisu halafu mumdhibiti hapa…tutaondoka naye pamoja na Gaudence…”
“Huyu jamaa ni nani?” Baddi alishindwa kuendelea kusubiri.
“Willy Ngoma. Mfanyabiashara mkubwa wa madini nchini…tumekuwa tukitilia sana mashaka urafiki wake na Gaudence…na naona mashaka yetu leo yamethibitika.” Tabasamu Jepesi alimjibu.
Mmoja wa wale askari wa kijeshi alikichomoa kile kisu kutoka kwenye kiganja cha Willy kwa nguvu na jamaa alilia kwa uchungu. Hakuna aliyejali kelele zake wakati akiinuliwa kutoka pale chini na kuketishwa kwenye moja ya viti viliyokuwamo mle ndani. Askari mwingine alikamata shati lake na kulichana kwa fujo, kisha akatumia kipande cha shati lile kumfunga lile jeraha lililotokana na kile kisu alichoshindiliwa na Swordfish. Askari wengine wawili waliinua ile meza na kuiweka sawa kisha Meja Jenerali Athanas Chacha akaketi kwenye kiti nyuma ya meza ile. Kwa amri ya Tabasamu Jepesi, Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani aliketishwa kwenye kiti kingine kando ya kile
alichokalia Jairos Kabwe, mikono yake iliyofungwa pingu ikiwa juu ya mapaja yake. Askari wanne wenye silaha waliwazingira wale washirika wawili katika kadhia ile ya almasi za damu.
“Haya, sasa kabla hatujaongea lolote, nadhani mk…Shani…angehitaji
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI uangalizi wa kitabibu…” Baddi alisema na Meja Jenerali Chacha alimjibu.
“Actually, Bi. Shani pamoja na hawa mateka wengine tuliowakuta humu wote wataondolewa eneo hili sasa hivi. Shani atapelekwa Lugalo kwa matibabu, na huyu binti pamoja na mwanao watakuwa kwenye moja ya nyumba zetu salama kwa ajili ya usalama wao…hawa ni mashahidi muhimu katika kesi hii…”
“Hakuna kesi hapa jamani…ni misunderstanding ndogo tu imetokea…” Meja Jenerali mstaafu Gaudence alidakia, lakini Meja Jenerali Athanas Chacha alimtupia jicho kali. “Shut up Gaudence!”
Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani alimtazama kwa hasira lakini alifunga mdomo wake.
Ilikuwa taabu kidogo kumshawishi Claudia kuachana na babaye, lakini baada ya Baddi kumhakikishia kuwa watakuwa pamoja baada ya muda mfupi ujao alikubali.
“Bado tuna mengi ya kuwekana sawa Gilda…natumai tutapata nafasi hiyo baada ya kumaliza haya mambo yaliyopo hapa, sawa?” Baddi alimwambia Gilda. Gilda aliafiki kwa kichwa na kufuatana na askari wa kijeshi waliowaongoza yeye na Claudia kutoka nje ya chumba kile.
Shani alibebwa kwenye machela na kuondolewa eneo lile kwa gari maalum la kubebea majeruhi na wagonjwa, bado akiwa hana fahamu kabisa.
Sasa mle ndani walibaki Meja Jenerali Athanas Chacha, Baddi, Swordfish, Tabasamu Jepesi, pamoja na wale washirika wawili wabaya, Gaudence Amani na Willy Ngoma. Aidha kulikuwa kuna askari wa kijeshi sita wenye silaha.
“Naam, sasa tueleze juu ya hii uiitayo misunderstanding ndogo, Gaudence”. Meja Jenerali Chacha alimwambia Meja Jenerali mstaafu Gaudence. Baddi na Swordfish walikuwa wameketi kwenye viti vilivyokuwa kila upande wake. Tabasamu Jepesi alikuwa ameketi kwenye pembe ya ile meza kubwa. Nyuma viti walivyokalia Gaudence na Jairos kulikuwa kuna askari wawili wenye silaha waliokuwa wamewaelekezea wale wahalifu mitutu ya bunduki zao.
“Nahitaji wakili…siongei chochote bila wakili wangu kuwepo!” Gaudence alijibu kwa kiburi.
“Kama unadhani utashitakiwa katika mahakama ya kiraia basi umepotea sana Gaudence! Unakwenda kwenye mahakama ya kijeshi Gaudence…court marshall…kwa hiyo usifikiri utajiiokoa kwa kuhonga hizo almasi zako za damu!” Meja Jenerali Athanas Chacha alimjia juu. Ile kauli ilileta mtafaruku mkubwa mle ndani.
“Almasi…? Almasi gani alizo nazo?” Willy Ngoma alimaka kwa mshangao
MDUNGUAJI
huku akimtazama Gaudence na kumgeukia Meja Jenerali Athanas. Baddi na Swordfish walitazamana. Meja Jenerali Chacha alimgeukia Tabasamu Jepesi.
“Willy hajui kuwa mwenzake ana almasi…unaona hiyo?”
“Yeah…Sasa naona picha yote inaanza kukaa sawa hapa.” Tabasamu Jepesi alimjibu huku akimtazama Gaudence moja kwa moja usoni. Baddi na Swordfish walitazamana tena.
“What are you talking about jamani? Gaudence ana almasi?” Willy Ngoma aliuliza kwa jazba.
“Shut up Willy! Huoni kuwa hawa wanataka kututega hapa?” Gaudence alimkemea.
“Tuwatege wakati tayari tumeshawanasa Gaudence? Sema ukweli tu, kwani kama hutasema hapa utaenda kusema kwenye court marshall…huna ujanja tena!” Meja Jenerali Athanas Chacha alimjibu kwa utulivu. Gaudence alisonya na kugeuza uso wake pembeni.
“Sasa wewe ni almasi gani hizo ulizokuwa ukinidai mimi?” Baddi alimuuliza Willy kwa ukali, ambaye alimgeukia Gaudence. “Ni kweli una almasi Gaudence…?”
“Nyamaza Willy, usiwe mjinga! Hawa wanataka kutuchanganya tu hapa!”
“Tuwachanganyie nini wakati tumeshawadhibiti Gaudence?” Meja Jenerali Athanas alimuuliza, kisha akamgeukia yule mtu mnene na mrefu. “Willy, sisi tunajua kuwa wewe ni mfanyabiashara mkubwa wa madini…hebu tuambie ni kipi hasa ulichokuwa ukikitaka kutoka kwa Baddi?”
“Almasi! Jamaa alikuwa anataka almasi anazodai kuwa nilitoweka nazo kule Sierra Leone! Si nd’o kisa hata akawateka nyara watu wangu hapa!” Baddi alidakia kwa jazba.
“Ni kweli Willy?” Meja Jenerali Athanas alimuuliza.
Willy Ngoma alihamanika. Alimgeukia Gaudence kwa mashaka, kisha akamtazama Athanas. “Mi’ nili…I was just…nilikuwa nataka haki yangu tu!”
“Kwani kulikuwa kuna makubaliano yoyote ya awali juu ya hilo kati yako na Baddi?” Tabasamu Jepesi alimuuliza. Willy Ngoma alimtazama Gaudence, ambaye aligeuza uso wake pembeni kwa kiburi.
“Si…sikuwa na makubaliano naye…ye’ alimpora na kumuua mtu tuliyekuwa na makubaliano naye kisha akatoweka.”
“Nathan Mwombeki?” Athanas Chacha aliuliza.
Badala ya kujibu Willy alibaki akitikisa kichwa kwa masikitiko, wazi kabisa alikuwa amechanganyikiwa kwa namna mambo yalivyokuwa yakimfunukia mle ndani. “Mi’ nilikuwa nataka mali yangu tu…Mimi ni mfanyabiashara
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
jamani, na nilishatoa pesa nyingi…!”
“Sasa mbona mlikuwa mnataka kumuua Baddi? Kama kweli ulikuwa
unaamini ana hizo mali zako, why did you try to kill him? Tena mara tatu!”
Swordfish alidakia kwa ghadhabu.
Bonge la mtu lilizidi kuhamanika. “Kumuua! Mimi? Sikuwahi kabisa
kujaribu kumuua! Mtu nataka anipe changu, sasa nikimuua ningekipataje?”
Alimaka, kisha akamgeukia Gaudence. “What’s going on Gaudence? Ni nini hii ninayosikia…unajua lolote wewe?”
“Siongei kitu hapa mimi! Kama we’ unataka kujikaanga, jikaange tu!”
Gaudence alimjibu kwa ghadhabu. Bwana Ngoma akamgeukia Meja Jenerali
Athanas kwa macho yaliyochanganyikiwa. Baddi alitikisa kichwa kwa mastaajabu.
“Okay, kama Gaudence haongei, wacha mimi niseme kilichopo hapa, na nadhani na wewe Baddi utapata majibu kwa kiasi fulani…” Meja Jenerali
Athanas Chacha alisema huku akijiweka vizuri kitini.
“Miezi miwili baada ya kufanikiwa kutushawishi tukurudishe kazini ili uende kusaidia kule Sierra Leone, Gaudence aliomba kustaafu kwa sababu za kiafya.
“Hili lilitushangaza kidogo kwani Gaudence bado alikuwa na muda wa kuendelea kulitumikia jeshi letu, nasi huwa tunaangalia sana mambo kama haya. Tukamkubalia ombi lake, lakini hatukumuacha hivi hivi tu…ndipo hapo
ambapo kamanda Mnama hapa alipoingia kwenye picha…” Meja Jenerali
Athanas Chacha alimwoneshea Tabasamu Jepesi kwa gumba lake.
“Kamanda Mnama…?” Swordfish aliuliza.
“That’s me!” Tabasamu Jepesi alisema huku akitabasamu.
“Yes, Kamanda Mnama yuko kwenye kitengo cha usalama wa taifa ndani ya jeshi la wananchi wa Tanzania. Sisi humwita James Bond wa jeshi, naye tukampa kazi ya kufuatilia nyendo zote za Gaudence…”
Gaudence Amani alitumbua macho kwa mshangao, wazi kuwa hii ni habari mpya kwake.
“Does it mean mlikuwa mnamtilia mashaka tangu mwanzo?” Baddi aliuliza.
“Of Course! Lakini sio kwa kadhia hii ya almasi. Ni kwamba hatukutaka kushtukizwa…na ndiyo maana unaona hatuna matukio ya kijinga-jinga hapa nchini kuhusiana na jeshi. Tulijifunza sana kwenye lile tukio la miaka ya nyuma pale wapiganaji wetu walipojaribu kupindua serikali…tangu wakati huo tukajenga kikosi maalum ndani ya jeshi na kukiunganisha na usalama wa taifa, specifically kwa ajili ya kuchunguza nyendo za maafisa wa jeshi watakaoonesha
MDUNGUAJI
tabia za mashaka…”
“Ama!” Swordfish alimaka.
“Ndiyo. Si taarifa ijulikanayo na wengi ndani ya jeshi, lakini ndivyo ilivyo. Anyway, Kamanda Mnama alimfuatilia mpaka alipopanda ndege kwenda India kwa mapumziko mafupi kama mwenyewe alivyodai, na mpaka hapo hatukuona ajabu…na ni katika kipindi hicho ndipo uswahiba wake na Jairos ulipobainika. Hatukushangaa kwani tulidhani labda alikuwa anataka kuwekeza pensheni yake kwenye biashara ya madini. Sasa tulikuja kushangaa aliporejea nchini miezi michache baadaye akiwa anasukumwa na kiti cha wagonjwa akiwa na hogo kubwa mguuni na miwani myeusi usoni.”
“Sasa ni nini cha kushangaza katika hilo?” Gaudence aliuliza kwa hasira.
“Cha kushangaza ni kwamba kwanza ulipokuwa India, ulitoweka kwa muda wa mwezi mzima pasina yeyote kujua ulipopotelea huko India, na pili lile hogo uliloingia nalo nchini lilitoweka siku tatu tu baadaye na ukawa unatembea kama kawaida. Hapo tulipata mashaka zaidi.” Meja Jenerali Athanas Chacha alimjibu kwa utulivu. Gaudence alitikisa kichwa kama kwamba alichokuwa akikisikia kilikuwa ni upuuzi uliopindukia.
“Sasa ulipokuja kutangaza ndoa na Shani, mke wa Baddi ambaye wakati huo tuliamini amekufa, kengele zote za tahadhari zilianza kurindima vichwani mwetu. Tulijua kuna mchezo unachezwa…”
“Cha ajabu ni nini hapo? Yule si alikuwa mjane bwana…”
“Gaudence unaweza kudanganya wengine katika hilo lakini si mimi!” Athanas Chacha alimkatisha kwa ukali.
Wote mle ndani wakawa wamebutwaika kwa kutoelewa.
“What do you mean…?” Gaudence alimjia juu. Mej. Jen. Athanas alitikisa kichwa kwa masikitiko. “Gaudence kumbuka tulikuwa pamoja kwenye vita ya Kagera…na kumbuka kuwa ninajua ni nini kilichokukuta ulipotekwa na askari wa Amin kule, hivyo usitake nitoe siri zako binafisi hapa! Kufunga ndoa na Shani lilikuwa ni kosa kubwa sana kwako Gaudence kwani hilo ndilo lililofanya tuzidi kukufuatilia kwa karibu.”
Gaudence alihamanika vibaya sana. Alifunua kinywa lakini hakuna sauti iliyotoka. Baddi na Swordfish walitazamana kwa mshangao, kama jinsi Willy, Kamanda Mnama na wale askari waliokuwemo mle ndani walivyoshangwazwa na kauli ile.
“Lakini hiyo ndoa ilikuja baadae. Kabla ya hapo tuligundua kuwa baada ya kurejea tena nchini ulianza kukutana na wachuuzi kadhaa wa madini, hasa wahindi, pamoja na kuendelea kukutana na Willy…”
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Ama!” Willy alimaka.
“Ulikuwa hujui?” Mej. Jen. Athanas Chacha alimuuliza, kisha akaendelea, “Basi nd’o hivyo…na Kamanda Mnama alimbana mmoja wa hao wachuuzi wa kihindi, na ndipo mhindi alipobainisha kuwa Gaudence alikuwa anauza almasi zenye thamani ya mabilioni, lakini kwa usiri mkubwa.”.
“Hah!” Willy alimaka tena.
“Ndiyo! Na tunahisi kuwa hizo almasi aliziingiza nchini kwa kuzificha kwenye lile hogo alilojifunga.” Kamanda Mnama alibainisha.
“Mwanaharaaaaamm!” Willy Ngoma alibwata huku akimrukia Gaudence kwa hasira, lakini kwa wepesi wa ajabu Kamanda Mnama aliruka na kumdaka koo, kisha akamsukumia kitini kwa nguvu.
“Tulia usikilize habari za swahiba yako unayemtunzia siri hapo!” Alimkemea.
“Kwa hiyo kumbe siku zote almasi unazo wewe!” Bwana Ngoma alimuuliza Gaudence kwa wahka mkubwa kabisa.
“Usisikilize huu upuuzi wewe!” Gaudence alimjia juu, “Hawana ushahidi wowote hawa!”
“Sasa hizo almasi ziko wapi? Baddi nd’o huyu na inaonekana wazi kuwa hanazo, nawe uliniambia kuwa Baddi amezipora kule Sierra Leone, na kwamba ndiye aliyekujeruhi upande wa jicho lako naye akatowekea huko huko!” Willy alimjia juu.
“Ah! Unaona uongo wake huyu…?” Baddi alimaka huku akimnyooshea kidole Gaudence.
“Hilo jicho alipunyuliwa na risasi ya mpiganaji mmoja wa kike mahiri sana kule msituni shaitwani huyu!” Swordfish alidakia.
“…ndiyo maana nilipoibuka hapa nchini alituma watu kuja kuniua ili uongo wake usigundulike, shenzi taipu!” Baddi alisema kwa hasira. Willy Ngoma alitikisa kichwa kwa masikitiko huku akimtazama Gaudence.
“Kwa hiyo mpaka usawa huu pamoja na makosa mengine yote aliyonayo Gaudence, pia ana kosa la jaribio la kuua…na wewe ndugu yangu Ngoma kama mshirika wake pia unajumuishwa kwenye kosa hilo!” Kamanda Mnama alisema. Willy alitikisa kichwa kwa nguvu kukana hoja ile.
“Mi’ sijui kabisa kuhusu hizo njama jamani!”
“Na si hivyo tu. Gaudence amedungua na kuua wapiganaji sita kule Sierra Leone kwa ajili ya hizo almasi! Kwa hiyo pamoja na kesi ya jaribio la kuua hapa nchini, mwenzio ana kesi sita za mauaji halisi Willy...na wewe ni mshirika wake katika hilo!” Mej. Jen. Athanas alimwambia.
Willy Ngoma alichanganyikiwa. “Jamani mimi kwenye hilo swala la mauaji
MDUNGUAJI
simo kabisa…nilikuwa nafatilia haki yangu niliyoigharamia, na niliamini Baddi kaniibia…!”
“Sasa labda utueleze uhusiano wako na Gaudence unakomea wapi katika hili, labda tunaweza kupata namna ya kukuvua baadhi ya makosa…hasa hayo ya mauaji.” Mej. Jen. Athanas alimwambia.
“Usiwe mjinga Ngoma! Utajitia kitanzi mwenyewe hapo!” Gaudence alibwata. Mwenzake alimtazama kwa hasira iliyochanganyika na kukata tamaa.
“Ulishanitia kitanzi siku ulipofanikiwa kunishawishi nigharamie safari yako ili uende kuleta almasi kutoka Sierra Leone, Gaudence…” Alimwambia kwa masikitiko. Wote mle ndani walimakinika kwa kauli ile, na hivyo kilichofuatia hakuna aliyekitarajia hata kidogo.
Gaudence Amani alipiga ukelele wa ghadhabu na wakati huohuo akifanya kama anayemrukia Willy. Wale askari wawili waliokuwa nyuma yake walikurupuka kutaka kumzuia, wakati Kamanda Mnama akipiga ukelele wa tahadhari, na hapo Gaudence alidunda sakafuni kwa miguu yake yote miwili na kujirusha nyuma mzima mzima kwa sarakasi moja kali sana huku akijipindua hewani na kumwangukia mmoja wa wale askari waliokuwa nyuma yake na kusambaratika naye hadi sakafuni kwa kishindo.
Baddi Gobbos alijirusha pembeni huku akichomoa bastola, wakati Swordfish akijitupa chini huku naye akichomoa ya kwake.
Gaudence Amani alimuinua kimabavu kutoka pale chini yule askari aliyemparamia huku akirudi nyuma. Mikono yake iliyokuwa imefungwa pingu kwa mbele ikiwa imembana kabali kali yule askari, viganja vyake vikiwa vimeikamata ile bunduki iliyokuwa mikononi mwa yule askari hapo awali, ambaye sasa alikuwa amemuweka mbele yake kama ngao.
“Wote tulieni bloody bastards!” Alifoka huku akiwa ametumbua macho hali ile bunduki ameielekeza kwa Meja Jenerali Athanas Chacha, ambaye alikuwa ametulia pale pale alipokuwa ameketi, mikono yake ikiwa juu ya meza.
“Najua kuna askari wenye bunduki nyuma yangu…!” Gaudence alifoka huku akizidi kujisogeza pembeni. “…nataka muelewe kuwa bunduki yangu imemuelekea Athanas pale, na mkinipiga risasi kwa nyuma mjue kuna nafasi kubwa ya risasi zangu kumcharanga mkubwa wenu pale!”
“Unataraji kufanya nini hapo Gaudence?” Mej. Jen. Athanas Chacha alimuuliza kwa utulivu.
Askari wote waliokuwa mle ndani walikuwa wamemuelekezea Gaudence bunduki zao. Willy Ngoma alibaki akiwa amekodoa macho kwa woga mkubwa kabisa pale kitini. Kamanda Mnama alikuwa amesimama huku mguu wake
HUSSEIN ISSA TUWA
MDUNGUAJI
mmoja akiwa ameuegesha juu ya ile meza, mkono wake wenye bastola akiwa ameulaza juu ya paja lake, mdomo wa bastola ile ukiwa umemuelekea Gaudence aliyejificha nyuma ya yule askari aliyekuwa akikukuruka kwa taabu.
Baddi aliiona hali ile akiwa amesimama kando ya ile meza kubwa ilhali amemuelekezea Gaudence bastola yake. Swordfish naye aliiona hali ile akiwa amepiga goti baina ya ubavu wa ile meza na Baddi Gobbos, bastola yake akiwa amemuelekezea Gaudence.
“Kelele! Unadhani mnaweza kunichukua kirahisi mimi? Kwanza we’ unaelewa nini Athanas? Unaelewa nini kuhusu maisha niliyoishi miaka yote hii tangu vita vya Kagera?” Gaudence alifoka.
“Tupa chini hiyo bunduki Gaudence, umezingirwa na mitutu ya bunduki kutoka kila kona…”
“Never! Waambie watu wako watupe chini bunduki zao ama sivyo nakutandika risasi…!”
Akiwa amesimama huku amemuelekezea bastola Gaudence, Baddi alishusha jicho na kumuona Swordfish akiwa amepiga goti kando ya mguu wake wa kushoto. Aliinua macho yake na kumtazama Gaudence.
“Tupa chini hiyo bunduki Gaudence, usiwe mjinga!” Alimkemea.
“Funga bakuli lako Baddi! Una bahati sikukupa risasi ya kichwa siku ile kule msituni!” Gaudence alifoka bila ya kumgeukia, macho yake akiwa ameyaelekeza kwa Mej. Jen. Athanas Chacha.
“Kama jinsi ulivyompa Black Mamba?” Baddi alimuuliza kwa utulivu, bado akiwa amemuelekezea bastola.
“Nimesema bunduki zote zitupwe chini!” Gaudence alifoka.
“Mjumbe huwa hauwawi Swordfish…” Baddi alisema kwa sauti ya chini huku bado akiwa amemlengeshea Gaudence bastola yake.
“Yeah…kwa hiyo…?” Swordfish alimjibu kwa sauti ya chini kutokea pale alipokuwa amepiga goti. Bado Gaudence na Mej. Jen. Chacha walikuwa wakijibizana, lakini sasa Baddi na Swordfish hawakuwa wakitilia maanani majibizano yao.
“Kwa hiyo tunafanyaje iwapo mjumbe anakuwa kipingamizi katika kumfikia mlengwa?” Baddi aliuliza kwa sauti ya chini, bado akiwa amemlenga Gaudence.
“Na…nadhani…itabidi mjumbe awekwe pembeni Baddi…aondolewe…”
“Right! Sio auawe Swordfish…aondolewe njiani tu, ili tumpate mlengwa moja kwa moja…nataka umuondoe njiani mjumbe Swordfish.” Baddi alisema kwa sauti ya chini. Swordfish alikaa kimya, kisha Baddi akauliza, “Think you
MDUNGUAJI can do that, Partner?”
“Yeah, I can do that…” Sworfish alinong’ona.
“N’tahesbu mpaka tatu Athanas...kama hujaamuru watu wako waweke chini silaha zao nakuwasha!” Gaudence alifoka. Sasa hali ya mle ndani ilikuwa inafukuta kwa taharuki na mashaka makubwa.
“Asifikishe tatu Swordfish…!”
“Halafu ukishaniwasha unadhani watu wangu watakuacha hivi hivi tu?” Mej. Jen. Athanas Chacha alimuuliza kwa utulivu.
“Subiri uone basi…MOJA!” Gaudence alisema na kuanza kuhesabu kwa sauti. Alitulia kwa muda huku akitembeza macho mle ndani hali bado akiwa amamemkaba yule askari mbele yake na bunduki akiwa ameielekeza kwa Meja Jenerali Chacha. “MBIL…!”
Bastola ya Swordfish ilikohoa mle ndani, na yule askari aliyekuwa amekabwa na Gaudence aliachia yowe kubwa pale risasi ya Swordfish ilipompiga pajani. Mguu uliachia na jamaa akaenda chini kama mzigo, uzito wake ukimuelemea Gaudence.
Gaudence Amani hakuelewa kilichotokea wakati akivutwa chini na uzito wa yule askari. Alimuachia haraka na kujaribu kumuelekezea tena bunduki yake Athanas Chacha, lakini hapo hapo alijishtukia akitupwa nyuma kwa nguvu huku maumivu makali yakimtambaa kifuani, bunduki ikimdondoka na yowe kubwa likimtoka.
Alibwagwa chini kwa kishindo na hapohapo alizingirwa na mitutu ya bunduki za wale askari wa kijeshi. Alijaribu kuinuka lakini alishindwa, damu ilikuwa imemtapakaa kifuani, na nyingine ilikuwa ikimtoka puani na mdomoni. Alibaki akitweta pale chini, mikono yake yote miwili iliyokuwa imefungwa pingu ikimuwia mizito sana. Mabega yake yote mawili yalikuwa yamepigwa risasi. Aligeuza uso wake kuelekea kule ambako Baddi alikuwapo na kumtazama kwa macho mazito, koo lake likatoa sauti ya kikohozi.
Walitazamana.
Bado Baddi alikuwa amemuelekezea bastola iliyokuwa ikifuka moshi. Gaudence alibaki akitweta huku akimtazama kwa kukata tamaa.
“Hiyo ni pamoja na salamu kutoka kwa Honey-Bee, ewe mdunguaji uliye laaniwa!” Baddi alimkemea kwa hasira.
Mej. Jen. Athanas Chacha na Kamanda Mnama walimgeukia Baddi na kuona bado ile bastola yake yenye kiwambo cha kuzuia sauti ikiendelea kufuka moshi mwepesi, harufu ya baruti ikiwa imezagaa mle ndani. Muda huo
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Swordfish naye aliinuka na kusimama kando ya rafiki yake.
“Safi sana patna!” Alimwambia taratibu. Upande moja wa chumba kile, vilio vya yule askari wa kijeshi aliyempiga risasi ya mguu ili Baddi apate nafasi ya kumdungua mdunguaji vilisikika.
“Yeah, nawe ulimuondoa vizuri sana yule askari…hukumuua. Nice Shot!”
“Aaah, Baddi! Si…si u…ung…geniua tu…? Why?” Gaudence alisema kwa taabu.
“Kwa sababu nilijua hivyo ndivyo ulivyotaka Gaudence, nami sikuwa tayari kukupa njia ya mkato kutoka kwenye haya madhila uliojiletea…!” Baddi alimjibu.
“Huyu anahitaji uangalizi wa matabibu haraka, asije akatufia hapa. Bado ana kesi nyingi tu za kujibu!” Mej. Jen. Athanas Chacha alisema.
“Yeah, itabidi tumpeleke Lugalo hosp…” Kamanda Mnama alijibu.
“No! Tutaenda naye kule kule kwenye nyumba yetu salama! Pale kuna hospitali ya usalama wa kijeshi. Wapigie simu tu matabibu wa pale wajiandae…”
Mej. Jen. Athanas Chacha alisema, na kuwageukia akina Baddi.
“Mmecheza vizuri sana pale vijana…big up!” Aliwaambia huku akiinuka
kutoka kwenye kiti chake. Kamanda Mnama alimtazama Baddi huku tabasamu
jepesi likiwa limetanda usoni kwake na kumpa ishara ya saluti.
“Good move komredi…ungempa ya kichwa tungekosa mambo mengi sana kutoka kwake…Gaudence ni muhimu sana kwetu akiwa hai.” Alimwambia.
Baddi alitabasamu huku akimrudishia ishara ya saluti.
“Sasa nini kinafuata…?” Baddi aliuliza.
“Tutaenda sote na hawa jamaa kwenye nyumba yetu ya usalama wa kijeshi…huko mtakuwa salama mpaka pale hili swala litakapofungwa rasmi.”
Meja Jenerali Athanas Chacha alijibu.
“Okay, basi naomba kwanza tupitie kwenye hoteli tulizokuwa tumepanga tukachukue mabegi yetu…” Baddi alimwambia.
“Not a problem…lets go!” Mej. Jen. Chacha alimjibu, na dakika tano baadaye, Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani na Willy Ngoma waliingizwa kwenye moja ya magari ya kijeshi yaliyokuwa nje ya jengo lile wakiwa chini ya ulinzi mkali na kuondolewa kwa kasi kutoka eneo lile.
Kamanda Mnama p.a.k. Tabasamu Jepesi, Kanali Baddi Gobbos p.a.k.
Vampire, na Meja Abdul-Hameed Babu p.a.k. Swordfish walilifuata gari
lililowabeba washirika wale wawili kwa gari jingine lililokuwa likiendeshwa
na Kamanda Mnama, wakati gari alilopanda Meja Jenerali Athanas Chacha
lilikuwa likiongoza msafara ule.
Saa tatu baadaye, Baddi Gobbos alisimama nje ya mlango wa chumba alichoelekezwa ndani ya nyumba maalum ya jeshi na kubaki akiwa ameshikilia kitasa cha mlango ule kwa muda. Mambo mengi yalikuwa yametokea ndani ya saa tatu zilizopita, na sasa hakuwa na hakika kama alikuwa tayari kisaikolojia, kwa kile kilichokuwa nyuma ya mlango ule. Hatimaye aliusukuma ule mlango na kuingia ndani ya chumba kile.
“Baddi! Oh, Baddi…” Gilda aliita kwa bashasha huku akiinuka kutoka kwenye kochi alilokuwa amekalia na wakakumbatiana.
“Uko salama wewe?” Alimuuliza kwa sauti iliyokwaruza.
“Niko salama sasa…vipi wewe? Nilikuwa na wasiwasi sana juu yako…”
“Kwa nini ulinitoroka namna ile Gilda? Kwa nini hukutaka angalau tuagane kistaarabu, baada ya yote tuliyopitia tukiwa pamoja?”
“Oh, Baddi…naomba unisamehe tu.Hakika iliniwia vigumu sana kwangu kuagana nawe, na nd’o maana nilifanya vile…naomba unielewe. Ninakupenda sana, lakini najua kuwa siwezi kuwa nawe tena baada ya kuwa umekutana na mkeo!” Gilda alimwambia huku akimtazama usoni, machozi yakimlengalenga. Baddi alihisi donge kubwa likimkaa kooni.
“Kwa hiyo nd’o ukaamua kuniachia zile almasi ili ziniliwaze? Hivi hujui kuwa iwapo ningeambiwa nichague kati yako na zile almasi mi’ ningekuchagua wewe?”
“Sina shaka kabisa juu ya hilo Baddi, lakini nimekupa zile almasi kwa kuwa nawe unazistahili na si vinginevyo…”
“Lakini mi’ sikuwa na haja nazo tangu hapo mwanzo. Haja yangu ilikuwa wewe!”
“Najua, lakini sasa hatuwezi kuwa kama ilivyokuwa kule Liberia. Una familia inayokuhitaji sana hapa Baddi.”
“Lakini hayo si tuliyajua tangu wakati tunakuja hapa nchini Gilda…? Mi’ sitaki tupoteze mawasiliano sasa baada ya yote tuliyopitia kule ugenini!”
Gilda alikaa kimya kwa muda, kisha akamwambia huku akiwa ameinamisha uso wake.
“Okay, juu ya hilo ondoa shaka. Sitapoteza mawasiliano baina yetu. Ila mimi inanibidi niangalie maisha yangu sasa Baddi. Hizi almasi ndio njia pekee ya kuniwezesha kuanza maisha upya hapa nchini. Kwa hiyo naomba sana unapoongea na wakuu wako wa kazi, swala la almasi zangu lisizungumziwe
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI kabisa. Niahidi hilo!”
“Ah, hilo nakuahidi. Na nitahakikisha hatupotezi mawasiliano kabisa.”
Gilda aliafiki kwa kichwa bila ya kusema neno. Baddi alimtazama kwa muda, kisha akashusha pumzi ndefu na kumketisha kwenye kochi alilokuwa amekalia hapo awali naye akaketi kando yake.
“Okay, hebu sasa niambie ilikuwaje hata ukawa mikononi mwa wale watu Gilda…wamekupora almasi zako? Maana kwa kauli zao inaelekea wanajua kuwa wewe una almasi…”
Gilda alimfahamisha kuwa baada ya kumtoroka, alienda kupanga chumba katika hoteli nyingine maeneo ya kariakoo. Huko alificha almasi alizokuwa nazo na kutoka kwenda kuanza kutembelea maduka kadhaa ya wanunuzi wa madini. “Ilinibidi niuze japo almasi moja niweze kupata pesa ya kuanzia maisha Baddi…”
“Ulifanikiwa?”
“Ah, nilikuwa na kijiwe kimoja kidogo, na wale jamaa walikuwa wanataka kunilalia sana kwenye manunuzi…tulishindwana bei.”
Na alipokuwa akitoka kwenye moja ya maduka hayo ndipo aliposhtukizwa na watu wawili waliomuweka kati huku wamemuwekea mdomo wa bastola ubavuni, na kumuamuru aingie kwenye gari lililokuwa kando ya barabara.
“Niliogopa sana Baddi…!”
“Najua…lazima uogope. So, nini kilifuata?”
Gilda alitikisa kichwa kwa masikitiko na kushusha pumzi ndefu, kisha akamfahamisha kuwa alipelekwa hadi kwa Willy Ngoma.
“Jamaa akaanza kunihoji kuhusu mahala ulipo na ulipoficha almasi zake… mi’ nilishangaa sana. Nikamwambia sijui ulipo na kwamba huna almasi kabisa!”
“Ina maana hawakujua ni wapi tulikuwa tunakaa kabla hujaenda kwenye hiyo hoteli nyingine?”
“Ndivyo inavyoelekea…nadhani hata ile hoteli niliyohamia hawaifahamu. Wao waliniona nikiwa mitaani tu nikitembelea maeneo ya wanunuzi wa madini…bila shaka walikuwa wakituvizia sehemu hizo”
Gilda alizidi kumjuza kuwa bwana Ngoma alipoliona lile jiwe moja la almasi alilokuwa nalo ndio alizidi kuja juu, akiamini kuwa Gilda alikuwa ametumwa na Baddi kuliuza. Alimpora ile almasi na kumtaka ataje nyingine zilipo, au ataje mahala Baddi alipo. Lakini pamoja na vitisho na vipigo vyote, hakutaja.
“Nilijua kuwa ningewatajia almasi zangu zilipo wangeniua, na ningewatajia mahala ulipo, wangetuua sote…kwa hiyo nikasema liwalo na liwe!” Alimalizia.
Baddi alimtazama kwa huruma na masikitiko. “Dah, Pole sana Gilda…”
MDUNGUAJI
“Ndio hivyo bwana…” Alisema, na kuzidi kumfahamisha kuwa baada ya kuona kuwa hatosema, wale jamaa walimfungia kwenye chumba kimoja kule mafichoni kwao na kuondoka, na waliporudi ndipo walipomleta mtoto ambaye baadaye alikuja kumtambua kuwa ni Claudia Gobbos, akiingizwa mle ndani alimofungiwa.
“Willy Ngoma alitukemea, ‘Kaeni humo msubiri hatima yenu! Kama Baddi haleti mali zangu haki ya Mungu vichwa vyenu halali yangu…mtaona!’. Kisha akabamiza mlango na kutufungia kwa nje. Tulilia! Mwanao alikuwa analia, nami nikawa najaribu kumbembeleza huku mwenyewe nikilia…ilikuwa ni hali moja ya kuogopesha sana Baddi!”
“Pole sana. Lakini sasa kila kitu kimekaa sawa….Mdunguaji na Willy si tishio tena sasa… its over now.”
“Yeah…”
Kimya kilitanda kwa muda, kisha Baddi akaongea, “Okay Gilda…sasa turudi kwenye swala letu mimi na wewe…”
Kabla hajaendelea zaidi Gilda alidakia haraka.“Ni kweli nilichukua uamuzi wa haraka pale Baddi. Lakini sioni kama kuna badiliko lolote…”
“Lakini hujui ukweli wa mambo kuhusu mimi na Shani Gilda!”
“No, Baddi najua. Najua kuwa mkeo ameolewa na mtu mwingine… nilikuwa nikiongea na mwanao tulipokuwa tumefungiwa mle ndani. Hiyo ilinipa matumaini kidogo, lakini baadaye nimeona kuwa haibadili lolote.”
“Kivipi…?”
“Yule bado ni mkeo Baddi! Aliolewa akiamini wewe umekufa…lakini sasa umebainika kuwa uko hai! Kwa hiyo automatically hiyo ndoa yake inafutika, ya kwako inachukua nafasi. Shani is still your wife, na hivyo msimamo wangu juu ya swala hili unabaki pale pale Baddi, japo unaniuma sana. Ni uamuzi mgumu sana kwangu!”
Baddi alimtazama kwa mshangao.
“Ah, you may be right Gilda. Lakini ukweli ni kwamba nami napata taabu sana kuachana nawe…na pia sijui Shani ana mtazamo gani juu ya ndoa yetu baada ya muda wote huu, na baada ya yeye kuwa na Gaudence ki-ndoa. Bado nina maswali kadhaa kwake, na mpaka nitakapopata majibu ya kuniridhisha, nisingependa unipotee Gilda.”
“No problem Baddi, nakuelewa. Nimeambiwa kuwa kwa sasa nitakuwa kwenye hii nyumba ya usalama mpaka watakapoona inafaa mimi kuondoka. Hivyo utanipata tu nikiwa hapa…” Alimjibu kijasiri.
Walikumbatiana kwa muda mrefu, kisha Baddi aliinuka na kutoka nje ya
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
chumba kile. Gilda alijibwaga kitandani na kuangua kilio cha uchungu.
Baada ya kutoka kwa Gilda alirudi sebuleni na kumkuta Swordfish akiwa amepitiwa usingizi kwenye kochi, runinga ikiwa inacheza peke yake mbele yake. Alijibwaga kwenye kochi jingine na kuachia mwayo mrefu, uchovu ukimtambaa mwili mzima. Alijishika kichwa na kujiinamia, akili yake ikirudi
kwenye matukio ya saa tatu zilizopita…
Walipofika kwenye ile nyumba salama ya jeshi ambayo pia ilikuwa na kitengo kizima cha utabibu, walikuta matabibu watatu bingwa wa kijeshi wakiwasubiri. Moja kwa moja Mdunguaji Gaudence Amani aliingizwa kwenye
chumba cha utabibu. Willy Ngoma aliingizwa kwenye chumba kingine na kuachwa humo peke yake bila kupewa maelezo yoyote. Kamanda Mnama aliwaongoza akina Baddi kwenye chumba kingine ambamo kutokea kwenye dirisha la kioo maalumu lililokuwa kwenye ukuta mmoja wa chumba kile, waliweza kumuona yule mshirika wa Gaudence kule alipokuwa ingawa yeye hakuweza kuwaona.
“Sasa yule nd’o vipi kamanda?” Baddi aliluza huku akiashiria kwa kichwa chake kule kwa Willy.
“Tunamuacha achemke kwanza…tunamtazama tu. Akikaa vile peke yake kwa muda bila ya kuulizwa kitu, ataanza kujiuliza mwenyewe maswali kichwani mwake, kubwa kati ya hayo likiwa ni nini hatima yake…tutakapoanza kumhoji atasema kila kitu!” Kamanda Mnama alimjibu huku akijibwaga kwenye kochi na akimtazama Jairos kupitia kwenye lile dirisha maalumu. Swordfish na Baddi walitazamana huku wakitikisa vichwa kuafikiana na mbinu ile.
“Na kwa muda huu ambao tunamtazama bwana Ngoma, nini kingine kitakuwa kinaendelea? Yu wapi Meja Jenerali…?” Swordfish alisaili.
“Anawasiliana na wakuu wengine katika jeshi kuwapa hali halisi, na baada ya muda ataungana nasi hapa, pia anataka ajue mustakbali wa hali ya Gaudence baada ya kuangaliwa na matabibu wetu…” Kamanda Mnama alimjibu, na kwa nusu saa iliyofuata walibaki mle ndani wakimtazama Willy.
Jamaa alikuwa akihamanika kila dakika zilivyokuwa zikisonga. Aliinuka na kutembea huku na huko ndani ya kile chumba, kisha alirudi tena kwenye kiti. Alianza kuhangaika ovyo mle ndani. Mara ajishike kichwa, mara ajishike tumbo kama anayeumwa ugonjwa wa kuhara. Hatimaye alitoka kwenye kiti na kwenda kujikunyata kwenye kona moja ya chumba kile. Dakika ishirini
MDUNGUAJI
baadaye, Meja Jenerali Athanas Chacha aliingia mle ndani akiwa ameongozana na wanajeshi wengine wawili, mwanaume na mwanamke. Katika wawili wale alikuwako Luteni Kanali Damas Mvutakamba, ambaye Meja Jenerali Chacha aliwafahamisha kuwa ni wakili wa kijeshi aliyeteuliwa kumtetea
Gaudence pindi shauri lake litakapofikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi; na mwingine alikuwa ni Kanali Mwanamkasi Palangyo, wakili wa upande wa mashitaka katika mahakama ya kijeshi, aliyeteuliwa kuendesha mashtaka dhidi ya Gaudence baada ya taratibu zote za kisheria na kipelelezi ndani ya jeshi kukamilika.
“Taratibu zinahitaji mawakili wa pande za utetezi na mashitaka wawepo katika mahojiano yoyote yatakayofanyika baina yetu na watuhumiwa ili kuondoa utata wowote wa kisheria hapo baadaye, hivyo ndiyo maana hawa waheshimiwa wako hapa…” Meja Jenerali aliwaarifu.
“Vipi hali ya Gaudence?” Baddi alisaili.
“Matabibu wanasema ataishi…” Aliwafahamisha huku akijibwaga kwenye kochi mojawapo mle ndani.
“Good!”
“Tunaweza kuongea naye baada ya saa moja kutoka sasa. Mkuu wa Majeshi amehamaki sana. Ameagiza Court Marshal ifanyike haraka sana…na ndo maana Damas na Mwanamkasi wako hapa…”
Kauli yake ilikatishwa na kelele kutoka kule kwa Willy ambaye alianza kupiga-piga kile kioo kinachoona upande mmoja huku akilia, sauti yake ikiwafikia pale walipokuwa kupitia kwenye spika maalum zilizokuwa juu ya dari la chumba walichokuwamo.
“Sasa mbona siambiwi chochote jamani!? Nitoeni bwana…! Mi’ sihusiki na mauaji yoyote…! Labda ni Gaudence…mimi ni mfanyabiashara niliyedhulumiwa jamani…! Nilikuwa nadai changu tu…AH!”
“Inaelekea jamaa yuko tayari kusema yote sasa…!” Kamanda Mnama alisema, kisha akamgeukia Meja Jenerali Chacha, “Ruksa mkuu?”
Meja Jenerali Chacha alimtazama yule jamaa akipayuka ovyo kule chumbani, kisha akawageukia wale wanasheria wawili.
“Huyu ndiye mshirika wa mtuhumiwa Gaudence niliyewapa habari zake hapo awali…tunahitaji kuongea naye sasa.”
“Ina maana hamkuwa mmemhoji chochote hapo kabla?” Lut. Kan. Damas Mvutakamba aliuliza.
“Hapana…tulichofanya ni kumuweka chini ya ulinzi hapa…tunadhani anaweza kuwa na taarifa za msingi juu ya uhusika wa Gaudence katika sakata
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI hili…taarifa ambazo Gaudence mwenyewe hawezi kutupatia kamwe…”
Willy Ngoma alikuwa akiendelea kubwabwaja peke yake kule ndani, mara akitukana matusi, mara akitoa vitisho vya kutumia wakili wake kuwashitaki watu wote, mwisho akaishia kulia kama mtoto. Wale wanasheria wawili walisogea pembeni na kuongea kwa muda, kisha wakarudi pale walipokuwa akina Mnama.
“Okay…mnaweza kuongea naye. Sisi tutakuwa tunaangalia tu na tutaingilia pale tutakapoona inapaswa kufanya hivyo…” Kanali Mwanamkasi Palangyo alimwambia Mej. Jen. Chacha.
“Great! Lets do it then, kamanda!” Mej Jen. Chacha alisema huku akiinuka, na ndipo Baddi Gobbos na Swordfish walipopata majibu ya maswali mengi yaliyokuwa yakiwasumbua tangu kuanza kwa mkasa ule mzito.
Walipoingia mle ndani Willy Ngoma alimkimbilia Mej. Jen. Chacha kwa pupa, akiwa ametanguliza mbele mikono yake.
“Afande! Afande nisikilize tafadhali…!”
Kamanda Mnama alimdaka koo na kumsukumia kwenye kiti alichokuwa amekalia hapo awali. “Tulia hapo wewe!”
“Sawa, wazee, sawa! Natulia…natulia…!” Alibwabwaja huku akiwatazama kwa zamu, macho yakiwa yamemwiva kwa kulia na woga. Ubabe na mikogo aliyokuwa akiwatolea akina Baddi hapo awali vyote sasa vilikuwa vimetoweka.
“Sisi tutakuuliza maswali, nawe utatujibu kwa ukweli na ufasaha, sawa?”
Mej Jen. Chacha alimkoromea huku akiketi kwenye moja ya makochi yaliyokuwa mle ndani.
“Nitasema tu wazee…mradi tu msinipe kesi ya mauaji…!”
“Iwapo umeshiriki kwenye mauaji au hujashiriki yote yatajulikana hapa, na kwa taarifa yako kila kinachoongelewa hapa sasa hivi kinarekodiwa, tuko pamoja mpaka hapo?” Mej. Jen. Chacha alimwambia na kumuuliza.
“Good!”
Akawageukia akina Baddi. “Hii ndiyo nafasi ya kupata majibu, tutapima lipi jibu la ukweli na lipi la uwongo, na mjisikie huru kudakia kwa maswali yenu muda wowote wakati mimi na Kamanda Mnama tunamhoji, okay?”
Baddi na Swordifish walikubali kwa vichwa.
“Tuambie juu ya uhusiano wako na Meja Jenerali Gaudence…eleza kila
“Ndiyo mzee…ndiyo!”
MDUNGUAJI kitu tafadhali.”
Bila ubishi aliwaeleza kuwa alikuwa akifahamiana na Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani kwa muda mrefu, na kwamba miezi kadhaa kabla ya kustaafu kwake, Gaudence alifanikiwa kumshawishi washirikiane katika mpango wa kupata almasi zenye thamani ya mabilioni iwapo atagharamia safari yake kwenda Sierra Leone. Kwa vile alijua kuwa Gaudence amekuwa akienda na kurudi Sierra Leone katika harakati zake za kijeshi mara kadhaa, yeye hakushangaa pale Gaudence alipomwambia kuwa katika safari zake hizo, alikuwa amefanikiwa kujenga mahusiano ya siri na baadhi ya waasi waliokuwa wameshikilia maeneo yenye utajiri mkubwa wa almasi kiasi cha kuweza kumpatia kiasi chochote akitakacho kwa gharama kidogo tu.
Kamanda Mnama na Mej. Jen. Chacha walitazamana. Ni kweli Gaudence amekuwa akienda na kurudi Sierra Leone kikazi mara kwa mara, na kwamba ndiye aliyekuwa na mamlaka ya kuteua askari wa Tanzania waliokuwa wakipelekwa kuiwakilisha nchi katika kampeni mbalimbali za kijeshi barani afrika.
“Alikwambia ni jinsi gani angeweza kuzipata hizo almasi?” Mej. Jen. Chacha alimuuliza.
“Kwanza hakutaka kuniambia, lakini nilisisitiza kuwa iwapo ninatoa pesa zangu katika swala hili nilipaswa nijue…akasisitiza nimpe pesa kwanza ndiyo aseme. Nilipokubali kutoa pesa ndipo aliponiambia kuwa kwa kushirikiana na kiongozi mmoja wa ngazi ya juu ndani ya jeshi la Sierra Leone, walifanikiwa kutengeneza mtandao wa siri ambapo kwa namna fulani waasi walikuwa wakiwalipa almasi nyingi nao walikuwa wakiwapa habari za mipango ya majeshi ya kulinda amani kule Sierra Leone…au kutoa habari za kuwapoteza malengo wapiganaji wa umoja wa mataifa ili wasiwafikie waasi. Hata hivyo yeye alikuwa anapata mgao mdogo sana. Lakini pale yule mshirika wake wa kiSierra Leone alipotaka kujitoa katika usaliti ule, yeye aliona nafasi ya kujipatia mgao wote wa zile almasi za waasi. Hivyo aliwahi kuwahabarisha waasi juu ya nia ya yule M-Sierra Leone mwenzao, nao wakamuua naye akabaki kuwa mshirika pekee wa wale waasi kule Sierra Leone…mkimuuliza vizuri Gaudence atawaeleza zaidi, mi’ sikutaka kujua zaidi ya hapo …”.
Baddi alikumbuka kauli za msaliti Nathan kule msituni.
...Ukweli ni kwamba hatukutakiwa kabisa kuigundua hii kambi ya waasi, kwani kuigundua ni kuwaangamiza waasi...
Alimtazama Swordfish, ambaye alitikisa kichwa kuonesha kuwa alielewa ni nini kilikuwa kinapita kichwani mwake muda ule.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Una uhakika na hilo wewe?” Lut. Kan. Mvutakamba alimuuliza.
“Kabisa…sa’ mi’ si nd’o nawaambia hapa?” Willy alimjibu kwa msisitizo.
“Unadhani unaweza kutoa ushahidi huo mbele ya mahakama?” Kanali Mwanamkasi alidakia.
“Hata sasa hivi! Mi’ sikujua alikuwa anapataje hizo almasi mpaka baada ya kuwa nimeshatoa pesa kugharamia safari zake…na hapo sikuwa na namna ya kurudi nyuma, na nilitaka pesa yangu irudi…mimi ni mfanyabiashara jamani!”
“Hayo yataamuliwa mahakamani! Je, baada ya kuuawa huyo mshirika wake wa ki-Sierra Leone alikwambia ni nani mwingine aliyekuwa akishirikiana naye kule Sierra Leone katika hujuma yenu hiyo?”
“Am…aliniambia kwa ana kijana wake huko, Nathan Mwombeki…na kwamba yeye atakapofika Sierra Leone Nathan atakuwa ameshakusanya mali, yeye anaichukua na kurudi nayo…”
“Haya sasa mimi nimeingiaje hapo…nahusikaje?” Baddi alidakia. Willy alitikisa kichwa kwa masikitiko.
“Sasa hapo ndipo kidogo kulitokea mtafaruku…Gaudence aliporejea nchini aliniambia kuwa kidogo hali iliharibika kule Sierra Leone. Kwamba wewe uligundua juu ya njama hii. Ukadai nawe ujumuishwe kwenye mgao. Kwa namna fulani ulifanikiwa kumpora Nathan ule mzigo na kumuua…na ukamjeruhi Gaudence kwa kumvunja mguu, kisha ukapotelea huko huko na mali yote…baadaye nikasikia kuwa nawe umeuawa na waasi huko Sierra Leone. Nami nilihudhuria maziko yako hapa Dar…ulipozikwa hapo niliamini kuwa ndoto zote za kuzitia mikononi zile almasi zilikuwa zimezikwa pamoja nawe. Nikakubali hasara ile chungu.”
“Uongo mkubwa!” Baddi alimaka.
“Sasa ndiyo naelewa hivyo wazee, lakini kwa wakati ule niliamini yote niliyoelezwa na Gaudence…sasa kumbe mtu uko hai na Gaudence alikuwa na zile almasi siku zote hizi!”
“Sasa kama hivyo ndivyo, kwa nini nilipoingia nchini bado mlikuwa mkiniwinda kuniua?” Baddi alisaili, ingawa tayari alihisi kuwa jibu la swali hilo alikuwa nalo. Willy alishangaa waziwazi kwa kauli ile.
“Kukuua? Halafu iweje? Mi’ niliposikia kuwa upo hai nilijua kuwa angalau nitapata sehemu iliyobaki ya almasi ulizompora Nathan…nilitaka sana kukutia mkononi. Kwangu ulikuwa na thamani zaidi ukiwa hai kuliko mfu…sijui lolote juu ya kutaka kukuua. Nilipoona Gaudence na vijana wake wanazidi kupoteza muda katika kukutia mikononi, ndipo nilipoamua kuingilia kati mwenyewe…”
MDUNGUAJI
“Of course…kama Gaudence alikuwa amemzunguka mwenzake kwenye mgao wa mali ile, ni wazi angetaka Baddi aendelee kuwa mfu kama jinsi bwana Ngoma alivyokuwa akiamini…” Kamanda Mnama alithibitisha wazo lililokuwa kichwani kwa Baddi.
“Yeah…ni Gaudence alright…ni Gaudence!” Swordfish aliafiki.
Nusu saa baadaye Willy Ngoma hakuwa tena na jipya la kuwaeleza. Aliwaeleza kila alilojua, na katika mahojiano yale, Mej. Jen. Athanas Chacha na wenzake walielewa kuwa Gaudence ndiye alikuwa kinara wa njama ile chafu ya mauaji na hujuma. Willy alitumika tu kwa uwezo wake wa kifedha, ingawa naye alikuwa na mashitaka mazito ya kujibu kutokana na kuhusika kwake katika kadhia ile.
Mej. Jen. Chacha aliwageukia wenzake.“Naona hapa tumemaliza…unless kuna la ziada kabla hatujaendelea na taratibu nyingine…”
“Labda kitu kimoja tu zaidi…” Baddi alisema, na kumgeukia Willy, “… uliniambia kuwa nikikupatia mzigo wako labda nitaelewa kuwa huenda Shani alikuwa akihusika kwenye kadhia hii tangu mwanzo…ulimaanisha nini pale?”
Jairos alimtazama kwa mashaka. “Nilisema hivyo mimi?”
“Ndiyo ulisema! Wakati tukiwasiliana kwa simu nikiwa njiani kutoka kule Motel Agip kuelekea kule kwenye kambi yako. Ulimaanisha nini kwa kauli ile?” Baddi alimkemea.
“Ah, ni kwamba…baada ya we’ kusemekana kuwa umekufa, Gaudence aliniambia kuwa labda unaweza kuwa umemtumia mkeo ile mali…au maelekezo kuhusu ni wapi ile mali ilipo, kabla ya kifo chako. Ndipo alipokuja na wazo la kumuoa…ili awe karibu naye. By then niliamini kuwa ilikuwa ni mbinu nzuri na kwamba Gaudence alikuwa pamoja nami katika kuifuatilia mali yetu iliyopotea…lakini sasa…baada ya kugundua kuwa muda wote huo alikuwa akinizunguka tu, sielewi kwa nini aliona umuhimu wa kuwa karibu na Shani kiasi cha kumuoa…” Jairos alijibu kwa kirefu. Wote mle ndani walibaki kimya wakilitafakari lile jibu.
“Gaudence ametuzunguka sote kwa kweli…!” Swordfish alisema. Ukimya uliofuatia mle ndani uliashiria kuwa kauli ile ilikuwa sahihi.
“Sasa wazee mimi hatma yangu ni nini? Nimetoa ushirikiano wote jamani…” Willy alisema kwa kuomboleza. Mej. Jen. Chacha aliwageukia wale wanasheria wawili.
“Nakushauri utafute wakili…tena utafute wakili mzuri kweli kweli! Sisi tutakukabidhi kwenye mikono ya polisi kwa kuwa wewe ni raia…huko ndiko itaamuliwa ni kesi gani ujibu. Ila kwa hili la Gaudence, tutakuita kutoa ushahidi
HUSSEIN ISSA TUWA
MDUNGUAJI
kwenye mahakama yetu ya kijeshi, halafu tutakusalimisha tena kwenye mikono ya sheria ya kiraia…Gaudence atashugulikiwa kijeshi…” Kanali Mwanamkasi alimjibu huku akimtazama kwa macho makavu, na Luteni Kanali Damas Mvutakamba aliafiki kwa kichwa.
“Ah, sasa wazee…hayo hayawezi kuzungumzwa na kumalizwa hapa hapa tu jamani…?”
“Tafuta wakili Ngoma, usitake kujiongezea kosa la kujaribu kuzuia haki isitendeke kwa rushwa hapa!” Mej. Jen. Chacha alimkemea, kisha wote walitoka na kumuacha akilia kwa uchungu.
Baada ya kuachana na Willy Ngoma walienda moja kwa moja hadi kwenye wodi maalumu ndani ya lile jengo la usalama wa kijeshi ambamo Gaudence Amani alikuwa amelazwa. Mle ndani walikuwamo askari wa kijeshi wawili wenye silaha waliokuwa wamesimama kila upande wa mlango, wakati wengine wawili walikuwa nje ya mlango ule.
Kilikuwa ni chumba kikubwa kilichokuwa kwenye ghorofa ya kwanza ya jengo lile la ghorofa mbili. Dirisha pana la kioo lilikuwa likitazamana moja kwa moja na mlango wa kuingilia kwenye wodi ile ya mtu mmoja, na chini ya dirisha lile kulikuwa kuna kitanda. Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani alikuwa amelala kidari wazi pale kitandani kwa namna ambayo mgongo wake ulikuwa umeegemea mito kadhaa iliyokuwa imepangwa kwenye kitakizo cha kitanda kile, hivyo alikuwa nusu amelala-nusu amekaa. Mikono yake yote miwili alikuwa ameitandaza kila upande wa mwili wake. Risasi zilizotoka kwenye bastola ya Baddi Gobbos zilishatolewa mwilini mwake na sasa mabega yake yalikuwa yamefungwa bandeji nzito zilizoishia sehemu juu kidogo ya viwiko vya mikono yake.
Aliinua uso wake na kuwatazama wakati wakiingia mle ndani, athari za kipigo alichopokea kutoka kwa akina Baddi zikijidhihirisha wazi usoni kwake. Uso ulikuwa umemvimba, mdomo ulikuwa umemuumuka vibaya upande
mmoja, jicho lake la kulia lilikuwa limemvimba kiasi cha kulifunika kabisa, wakati chini ya jicho lake la kushoto alikuwa amebandikwa plasta nyeupe mahala ambapo bila shaka palikuwa pameshonwa. Zaidi ya hapo uso ule ulikuwa umetapakaa michubuko na manundu kadhaa.
Aliwachungulia mmoja baada ya mwingine kwa jicho lake zima, na kulituliza jicho lile kwa Baddi Gobbos, likimtupia miale ya ghadhabu kali
MDUNGUAJI kabisa.
“Unajisikiaje sasa Gaudence…?” Mej Jen. Chacha alimuuliza, lakini Gaudence alimtupia jicho la kiburi na kugeuka pembeni pasina kumjibu. Wote mle ndani walitazamana.
“Okay…” Mej. Jen. Chacha alisema huku akiketi kwenye moja ya viti vilivyowekwa kila upande wa kile kitanda maalum kwa ajili ya jopo lile dogo. Wengine nao waliketi.
“…unajua hiyo haitakusaidia lolote sasa Gaudence…you are in deep shit comrade...real deep shit! Cha msingi kwako kwa sasa ni kutoa ushirikiano tu, si vinginevyo…” Alimwambia, na bila kusubiri jibu, akaendelea kuwatambulisha wale wanasheria wa kijeshi waliojumuika na akina Baddi mle ndani.
“Nawajua wote hao…nisichojua ni kwa nini wako hapa…na usitake kuniambia kuwa eti hii ndiyo Court Marshall mliyokuwa mkiinadi kutwa nzima!” Gaudence alimkatisha kwa kiburi, ingawa alionekana wazi kuwa kule kuongea tu kulikuwa kunamletea maumivu makali.
“Hapana, hii sio court marshall, ila ni moja kati ya taratibu za mwanzo kuelekea kwenye court marshall, nayo ni kukutambulisha kwa wakili wa kijeshi atakayekutetea kwenye mahakama ya kijeshi, ambaye ni mimi…”
Luteni Kanali Damas Mvutakamba alimjibu kwa kirefu, na kumgeukia Kanali Mwanamkasi Palangyo, “…na kwa mwendesha mashtaka hapa kujionea hali yako kiafya, pamoja na kupata ripoti ya kitabibu, ili kumuwezesha kupanga muda wa kuanza kusikilizwa kwa shauri hili.”
“Mnapoteza muda…mimi nilishastaafu jeshi kitambo, hivyo siwezi kuhukumiwa kijeshi. Nahitaji wakili wangu binafsi awepo hapa, ama sivyo kila kitakachoongelewa hapa ni porojo msojo tu…hakitakuwa na nguvu yoyote kisheria…” Gaudence aliwaambia kwa kiburi, na Baddi akamjia juu.
“Acha ujinga Gaudence…si wewe uliyekuwa ukitufundisha miaka yote kuwa soldier never dies? Na kwamba once a soldier always a soldier…?”
“Tena wewe ndiyo usiseme lolote hapa shenzi taipu!” Gaudence alimjia juu.
“Huna ujanja Gaudence umenasa, muuaji mkubwa we! Mahakama yoyote utakayokwenda kitanzi halali yako!”
“Kwa ushahidi gani, eenh? Kwa ushahidi gani?” Gaudence naye alimjia juu.
“Aan-aa, sasa hakuna haja ya malumbano wazee…si mahala pake hapa!”
Wakili Damas Mvutakamba alidakia. Mej. Jen. Athanas Chacha alikuwa akifuatilia malumbano yale kwa udadisi mkubwa. Muda huo sauti ya Willy Ngoma ilisikika mle ndani ikielezea jinsi ambavyo Gaudence alivyoweza kujipatia almasi kutoka kwa waasi kwa kubadilishana nao na siri za harakati za
HUSSEIN ISSA TUWA
jeshi la umoja wa mataifa kule Sierra Leone.
MDUNGUAJI
Wote mle ndani walipiga kimya, Damas Mvutakamba na Mwanamkasi
Palangyo wakimgeukia Kamanda Mnama aliyekuwa ameshika kile kijiredio kidogo kilichorekodi mahojiano baina yao na Willy Ngoma muda mfupi uliopita; wakati Mej. Jen. Chacha, Baddi Gobbos, Swordfish na Kamanda Mnama mwenyewe wakimtazama Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani kwa makini.
Sasa Gaudence Amani alikuwa kama mtu aliyeona jini. Alikuwa amekitumbulia jicho kile kijiredio kilichokuwa kikitoa sauti ya Willy Ngoma huku mdomo wake ulioumuka ukimuanguka pasina kujitambua. Kamanda Mnama aliizima ile redio na ndipo Gaudence alipozinduka.
“No! Si kweli…hamuwezi kuamini maneno yake…yule ni mzushi tu!” Alibwata.
“Enh, nadhani hapa ndipo kama wakili wako ninapopaswa nikushauri ukae kimya Meja Jenerali, kwani…” Damas Mvutakamba alimwambia kwa wahka.
“Kwenda zako huko wewe! Mi’ sikutambui hata kidogo…nyie wote lenu si moja tu!” Gaudence alimjia juu, kisha akamgeukia Kamanda Mnama.
“Huo ni uzushi mtupu! Nyie mmemtesa Willy na kumlazimisha aseme hivyo…hamna ukweli wala ushahidi wowote hapo!”
“Jamaa yuko tayari kutoa maelezo haya mahakamani…mbele ya mahakama ya kijeshi…” Mej. Jen. Athanas Chacha alidakia kwa upole. Gaudence alimgeukia kwa mshangao na kutoamini. Alijaribu kumjibu lakini hakupata jibu muafaka.
“Umenasa Gaudence…huna kimbilio sasa.” Swordfish alimwambia.
“Si…sikubali! Nitahakikisha nina…”
“Keep quiet Meja Jenerali!” Damas Mvutakamba alimsahuri huku akiwatazama Kamanda Mnama na Mej Jen. Chacha.
“Hukubali nini? Umeua wapiganaji sita Gaudence…in cold blood! Wapiganaji sita kutoka nchi mbali mbali…ina maana una kesi za mauaji katika nchi zote hizo.” Mej Jen. Chacha alimwambia kwa msisitizo. Sasa Gaudence alikuwa na mchanganyiko wa hisia za kutoamini kilichokuwa kikitokea na wakati huohuo akionekana kuzidiwa na uzito wa tuhuma zilizokuwa mbele yake.
“…umelisaliti sio tu jeshi la nchi yako, bali pia la umoja wa mataifa kwa kuuza siri za harakati za kijeshi kwa waasi, Gaudence…”
“No, hujui unachosema wewe…” Gaudence alimbishia, lakini hata yeye mwenyewe alionekana kuwa haamini kuwa ana dalili za kushinda mkabala ule.
MDUNGUAJI
“Na kama hayo yote hayatoshi, bado una tuhuma za kupanga njama za kumuua Baddi Gobbos mara kadhaa! Hakika uko kwenye hali ngumu sana Gaudence, na hukumu itakayokufaa ni kifo tu, kilichobakia ni kuamuliwa ufe lini na kwa namna gani tu…”
“Meja Jenerali!” Lt. Kan. Damas Mvutakamba alimaka, “Hiyo sio namna ya kuongea na mtuhumiwa! Kumbuka kuwa ili sheria ifanye kazi yake ni lazima haki zote za mtuhumiwa zizingatiwe!”
“Wewe hukusikia alivyokwambia kuwa hakutambui?” Swordfish naye alimjia juu wakili Mvutakamba. Muda wote huo Baddi alikuwa akimtazama Gaudence kwa hasira kubwa. Shida zote alizopitia sasa akizinasibisha moja kwa moja na yule mtu aliyelala mbele yao mle ndani.
“Hivi ni kwa nini ulifanya yote hayo Gaudence, eenh?” Hatimaye alimuuliza kwa hasira. Gaudence alimrudishia jicho la hasira.
“Ni kwa ajili ya utajiri?” Baddi aliendelea kumuuliza, na bila ya kusubiri jibu akaendelea, “Kwa ajili ya almasi za damu?” Sasa Baddi alikuwa akionesha dharau ya hali ya juu kwa mtu yule aliyekuwa akimheshimu sana hapo nyuma. Gaudence alimtazama kwa muda, kisha akainamisha uso wake. Wote mle ndani wakabaki wakimtazama. Muda mrefu ulipita wakiwa katika hali ile, kisha Baddi akazidi kumvurumishia shutuma kwa hisia kali.
“Na hizo almasi zenyewe umeziiba kutoka Sierra Leone Gaudence…yaani ni kwamba umehujumu uchumi wa nchi ile, kosa ambalo hukumu yake ni kifo…! Sa’ utaponea wapi Gaudence? Ni bora utoe ushirikiano tu labda utapata unafuu wa adhabu…”
Lt. Kan. Damas Mvutakamba alitupa mikono hewani kwa kukata tamaa huku akitikisa kichwa kwa masikitiko. Gaudence alibaki akiwa amejiinamia tu. Hakika sasa ilimfunukia kwamba amefikwa.
Mej. Jen. Athanas Chacha alikuwa akimtazama Gaudence kwa makini. Baddi alimtazama Swordfish, ambaye alibetua mabega tu. Akamgeukia Mej. Jen. Chacha, ambaye alimtikisia kichwa mara moja kwa ishara ya kukubali kile alichokuwa akikifanya.
“Na kama bado kuna almasi ambazo hujaziuza basi itabidi uzisalimishe mara moja ili zirudishwe Sierra Leone…labda kwa kufanya hivyo utanusurika na adhabu ya kifo…” Baddi alizidi kumpasha.
“Ili iwe adhabu gani…kifungo cha maisha?” Hatimaye Gaudence aliuliza kwa sauti ya chini, bado akiwa amejiinamia.
“It doesn’t matter…sheria ndiyo itaamua. Cha msingi utoe ushirikiano tu, Gaudence…”
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Nyie hamuwezi kuelewa hata kidogo…” Gaudence alimkatisha kwa sauti ya chini, na wote mle ndani wakatazamana. Luteni Kanali Damas Mvutakamba alifunua kinywa kutaka kumuasa asiendelee kuongea kabla ya kufika kwenye taratibu za mahakama, lakini Mej. Jen. Chacha alimtupia jicho kali huku akimwashiria anyamaze.
“…sina nitakalowaeleza ambalo mtalielewa ndugu zangu. Sishangai nyinyi kuniona msaliti kwa jeshi na taifa, kwa sababu hamjui ni kwa kiasi gani mimi nimejitolea kwa jeshi na nchi yangu, na jinsi gani hilo jeshi lilivyonisaliti baada ya hapo. Kwa hiyo yote niliyofanya ilikuwa ni hatua za kujisaidia mwenyewe kutokana na athari nilizopata kwa kulitumikia jeshi la nchi yangu, jeshi ambalo liliamua kunitema kama jinsi mtu anavyotema makapi ya muwa baada ya kufyonza utamu wote…!”
Heh!
“
What is he talking about? Wallahi mi’ simuelewi…!” Swordfish aliuliza huku akimgeukia Mej. Jen. Athanas Chacha kwa macho ya kuuliza, kama jinsi ambavyo Baddi alivyofanya.
“Acha uongo Gaudence! Umeponzeka na tamaa ya utajiri wa haraka haraka, ukisahau kuwa uhalifu haulipi!” Mej Jen. Chacha alimjia juu, na hapo
Gaudence akamuinulia uso uliokunjamana kwa ghadhabu.
“Wacha unafiki Athanas! Unajua exactly ninaongelea nini ninaposema kuwa jeshi limenisaliti…!”
“Sasa wale wapiganaji shupavu uliowaua kule Sierra Leone wanahusika vipi na mambo hayo, eenh?” Swordfish alidakia kwa jazba.
“Keep quiet Gaudence!” Damas Mvutakamba alifoka.
“They were just collateral damage, that’s all…ni vipingamizi tu vilivyokuwa vikitishia lengo langu kutimia na ilibidi viondoke!” Gaudence alimjibu Swordfish kwa hasira.
“Hah!” Baddi alimaka.
“Kwa hiyo unakiri kuwa wewe ndiye uliyefanya yale mauaji ya kule msituni… Sierra Leone?” Kanali Mwanamkasi Palangyo alidakia kwa kiherehere.
“No, bwana! Unajua kuwa yote yanayoongelewa hapa hayana nguvu mbele ya mahakama…si ushahidi halali huu, kwa kuwa hapa sio mahakamani na Gaudence hajashitakiwa bado!” Lt. Kan. Damas Mvutakamba alimwambia wakili mwenzake, kisha akamgeukia Gaudence, “Meja Jenerali...nakushauri ukae kimya kwa sasa…”
“It doesn’t matter anymore now…” Gaudence alimjibu kwa kukata tamaa, na Baddi aliona nyuso za Mej. Jen. Chacha na Kamanda Mnama zikichanua kwa
MDUNGUAJI matabasamu ya ushindi.
“Sasa na Shani naye…? Kwa nini ulidhani ni lazima umuoe baada ya kuamini kuwa umeniua kule msituni…naye ni collateral damage pia…?” Baddi alimuuliza huku akimtazama kwa kutoamini. Gaudence alicheka kwa dharau na kukata tamaa.
“Yaani bado huamini kuwa mkeo ameweza kukubali kuolewa na mimi Baddi?” Alimuuliza.
“Jibu swali Gaudence! Umekuwa kapera miaka yote mpaka ulipoamini kuwa Baddi amekufa ndipo ulipoamua kumuoa mkewe…why?” Swordfish alimkoromea. Sasa wakili wa kijeshi Damas Mvutakamba aliamua kujinyamazia tu, akishuhudia yale yaliyokuwa yakiendelea mle ndani.
“That’s the problem. Sikuwahi hata siku moja kuamini kuwa Baddi alikufa siku ile kule msituni…ukiwa mpiga shabaha makini huwa unajua vitu kama hivyo…na kwa jinsi nilivyomjua Baddi, nilijua tu kuwa siku moja angeibuka. Na kwa jinsi yoyote ile, jambo lake la kwanza lingekuwa ni kuwasiliana na mkewe…na mnaona kuwa nilikuwa sahihi…” Gaudence alimjibu huku akimtazama moja kwa moja usoni.
Baddi aliachia kinywa wazi kwa kutoamini. Gaudence aliuona mshangao wake, na akamwambia huku akimtolea tabasamu la kejeli, “…Oh, yeah! Na nikiwa kama mumewe Shani hakusita kunipa password ya anuani yake ya barua pepe, na nilihakikisha kuwa naifungua anuani ile kila siku…”
“Oh, My God…! Kwa hiyo ulisoma barua pepe niliyomwandikia Shani nikiwa Liberia?”
“Kisha nikaifuta kabla yeye hajaiona…” Gaudence alimwambia kwa majigambo yenye kukera. Sasa Baddi alielewa ni kwa nini wale watu wabaya walikuwa wakimsubiri uwanja wa ndege siku alipoingia hapa nchini. Alitikisa kichwa kwa masikitiko.
“U-mtu mbaya sana Gaudence…mbaya sana! Na natumai adhabu utakayopewa itautafuna moyo wako kwa kiwango kikubwa kabisa, shetani mkubwa we!” Alimwambia kwa hasira. Gaudence hakuonekana kutikiswa hata kidogo na kauli ile. Alifumba macho na kujilaza vizuri pale kitandani.
“Nahitaji kupumzika sasa wazee. Siongei neno lolote zaidi…nimechoka.”
Alisema kwa upole.
“La! Tuambie ni wapi ulipoficha almasi ulizoiba kule Sierra Leone…tunajua hujaziuza zote…ziko wapi?” Kamanda Mnama alimjia juu.
“Tukutane mahakamani wazee…sina la kuongea zaidi kwa sasa…mnajua kuwa mimi ni mgonjwa hapa, na nimechoka.”
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Kamanda Mnama alimtazama kwa uso uliochanganyikiwa. Alimgeukia
Mej Jen. Chacha, ambaye alibetua tu mabega yake.
“Sema almasi zilipo wewe! Ujue usiposema hapa utasemea kwenye Court Marshall…” Kamanda Mnama alimkemea.
“Hizo ndiyo turufu yangu wazee…mnaninyonga, hamzipati kabisa… mnataka kuzipata ili zirudi zilipotoka na Tanzania isafishiwe jina, itabidi tupitishe makubaliano maalum juu ya hatma yangu!”
“Whaat…?” Kanali Mwanamkasi Palangyo alimaka. Gaudence aliachia kicheko cha dharau huku akiwa amefumba macho pale kitandani.
“Una wazimu wewe!” Mej Jen. Athanas Chacha alimaka kwa hasira.
“We’ ndo unagundua sasa?” Gaudence alimuuliza huku bado akiwa amefumba macho pale kitandani. Wote mle ndani walibaki wakimtazama, kila mmoja kwa hisia yake, kisha Mej Jen. Athanas Chacha aliinuka.
“See you in court Gaudence!” Alisema na kuanza kutoka nje ya ile wodi, akina Swordfish na wale wanasheria wa kijeshi nao wakimfuata, Baddi akiwa wa mwisho katika msafara ule wa kuelekea nje wodi. Akili ilimzunguka vibaya sana. Aliyoyasikia kutoka kwa Meja Jenerali Gaudence Amani Mdunguaji yalikuwa ni mazito na yalimuongezea maswali zaidi. Akilini mwake alikuwa akihisi kuna kitu hakikuwa sawa lakini kwa muda ule hakuweza kukitambua. Aliinua uso wake na kuwatazama wale askari wawili wa kijeshi waliosimama kila upande wa mlango wa kutokea nje ya wodi ile, na hapo alishtuka kuona nyuso za wale askari zikisajili mshangao mkubwa huku wakitumbua macho kuelekea kule alipokuwa akitokea. Na hata pale alipokuwa akishuhudia mshangao ule, wale askari walianza kupiga hatua kuelekea kule kilipokuwa kitanda cha Meja Jenerali mstaafu Gaudence Amani.
“What the…?” Alipayuka huku akigeukia kule kitandani wakati huohuo akimsikia mmoja wa wale askari akipiga ukelele wa tahadhari, na hapo alimshuhudia Meja Jenerali mstaafu Gauence Amani akiwa amesimama kitandani huku amepinda magoti yake kwa mbele kama mtu aliyekuwa kwenye hatua ya kuchutama, mikono yake isiyo na kazi ikimning’inia kila upande wa mwili wake, dirisha pana la kioo likiwa nyuma yake.
Baddi alisikia vishindo na sauti za mishangao kutoka kwa wale wenzake ambao sasa walikuwa nyuma yake, lakini akili yake ilikuwa kwa Gaudence. Sasa wale askari wawili walikuwa wamemuelekezea Gaudence bunduki zao huku wakikimbilia pale kitandani na kumpigia kelele.
Oh, My God!
Gaudence Amani alijirusha nyuma kwa nguvu, akiusukuma mwili wake
MDUNGUAJI
kwa miguu yake aliyoikunjua kutoka katika ile hali ya kuchutama, akisaidiwa na mtupo wa springi za kile kitanda alichokuwa amesimama juu yake.
“
Gaudence NOOOOOO…!”
Kishindo kikubwa kilisikika pale kisogo na mabega yake vilipojibamiza kwenye kile kioo kipana cha dirisha la wodi ile, kishindo kile kikiambatana na sauti kali ya mpasuko wa kile kioo.
Kwa kihoro aliishuhudia miguu ya Gaudence Amani ikipotelea nje ya dirisha la ile wodi iliyokuwa kwenye ghorofa ya kwanza ya jengo lile la usalama wa kijeshi.
Wote walijirundika kwa pupa pale dirishani na kuchungulia kule chini.
Gaudence Amani aliamua kuchukua njia ya mkato kuikimbia mikono imara ya sheria, na hata kwa umbali ule, hakukuwa na shaka kabisa kwao kuwa Mdunguaji alikuwa amekufa. Mwili wake ulikuwa umelala chali kwenye ujia wa lami uliokuwa kule chini. Kichwa chake kilikuwa kimegeukia katika pembe isiyowezekana kabisa kibinadamu, dimbwi kubwa la damu likiwa limetapakaa eneo aliloangukia.
“Hanithi kajiua, bloody swine!” Mej. Jen. Athanas Chacha alisema kwa hasira. Kule chini, baadhi ya askari waliokuwa ndani ya eneo la jengo lile walikimbilia pale mwili wa Gaudence Amani ulipoangukia. Mej Jen. Chacha aliwageukia wale askari wawili waliokuwa mle ndani.
“Nendeni mkadhibiti usalama kule chini, na mhakikishe ile takataka inaondolewa mara moja!” Aliwaamuru.
Jamaa walisaluti na kutoka mbio nje ya wodi ile.
“Dah! Ama sasa haki nd’o haitatendeka tena wallah…maana ushahidi wa mshenzi yule ulikuwa muhimu sana katika kuihitimisha kadhia hii!” Swordfish alilalama.
“Not to worry. Maelezo yake yote nimeyanasa kwenye mkanda…muda wote aliokuwa akijitapa hapa mimi nilikuwa namrekodi kwa hiki kifaa changu!” Kamanda Mnama, p.a.k. Tabasamu Jepesi alisema huku akiwaoneshea ile redio ndogo ya kurekodia maongezi ambayo aliitumia kumrekodi Willy Ngoma hapo awali.
“E bwana we! Safi sana!” Baddi alisema.
“Good job, kamanda!” Mej Jen. Chacha alimsifu kamanda wake, kisha akawageukia akina Baddi.
“Tuondokeni hapa…”
Wote walitoka nje ya wodi ile. Walipofika sehemu ya sebule ndani ya jengo lile, Mej Jen. Chacha aliwageukia Baddi na Swordfish.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
“Hii kesi imekwisha…lakini bado tunahitaji kupata maelezo yako Baddi kuhusu matukio ya kule msituni miaka mitatu iliyopita…Kamanda Mnama atawaonesha vyumba vyenu vya mapumziko na kuwapa maelekezo ya nini kitafuata.”
Waliagana na wale wanasheria wa kijeshi kisha wale wanasheria wakaongozana na Mej Jen. Chacha kutoka nje ya eneo lile.
“Meja Jenerali…” Baddi aliita. Meja Jenerali Athanas Chacha alisimama na kumgeukia.
“Kuna vitu sijavielewa…ulimaanisha nini pale ulipomwambia Gaudence kuwa unajua kilichomkuta alipotekwa na askari wa Iddi Amin katika vita vya Kagera…? Na vipi hilo lilisababisha yeye kumuoa Shani kuwe ni kosa kubwa?” Alimuuliza.
“Yes boss, na pia ni vipi juu ya hii habari ya jeshi la Tanzania kumsaliti hata akaamua kujiingiza kwenye utata huu wa almasi za damu?” Swordfish naye aliongezea swali lake.
Yule Meja Jenerali mtanashati aliwatazama kwa macho makavu kwa muda mrefu akiwa amesimama kwenye mlango wa kutokea nje ya sebule ile.
“Nilipomwita Gaudence hanithi sikuwa nimekosea…jamaa alikatwa uume wake kwenye mateso alipotekwa kwa muda na askari wa Amini…” Alisema, akiielekeza kauli yake moja kwa moja kwa Baddi.
“Aaa…?” Baddi na Swordfish walimaka kwa pamoja.
“Oh, yes! Jamaa walimkata uume wake na kuutupia kwenye moto…”
“Duh!”
“Yap! Alikuwa na hali mbaya sana…jeshi lilimshughulikia kwa matibabu ya kila hali mpaka akapona. Tatizo, kile kiungo chake kilichokatwa hakikuweza kurudishiwa tena…kwani hakikuwepo… na hivyo hakukuwa na jinsi…ilibidi akubaliane na hali halisi…”
“Mungu wangu!”
“Ndiyo…baadaye alikuja na habari kuwa huko India kuna watu mafukara waliokuwa tayari kukatwa uume wao ili kuwauzia wenye matatizo kama yake ili wafanyiwe upandikizwaji wa kiungo kile kitaalamu, na akaomba jeshi letu ligharamie tiba ile…ombi lake halikukubaliwa.”
“Why?” Baddi aliuliza.
“Jibu liko wazi. Utaratibu mzima wa kupata hao masikini waliokata tamaa kabisa maishani, wanaojitolea kukatwa hivyo viungo vyao, ni wa haramu. Unafanyika kinyume cha sheria, na hata hizo hospitali huko India zinazofanya upandikizwaji wa hivyo viungo…wenyewe wanaita transplant…zinafanya
MDUNGUAJI
jambo hilo kwa uficho mkubwa. Serikali ya India imekuwa ikipigia kelele sana
swala hilo. Uongozi wa jeshi letu haukuwa tayari kujiingiza kwenye jambo tata kama hilo…”
“Na ndipo Gaudence alipoona kuwa jeshi limemsaliti!” Swordfish alisema.
Mej Jen. Chacha aliafiki kwa kichwa, kisha akageuka na kutoka nje ya sebule ile, akiwaacha Baddi na Swordfish wakitazamana.
“Yakupasa uongee na mkeo patna…huenda hali sio mbaya kama ulivyodhani…” Swordfish alimwambia rafikiye, na Baddi alitikisa kichwa tu huku akiwa ameuma midomo yake kwa tafakuri. Alimgeukia Kamanda Mnama.
“Vipi kuhusu Shani Kamanda…unadhani naweza kuonana naye leo?”
“Aam…wacha niwasiliane na hospitali yetu ya Lugalo…” Kamanda Mnama alimjibu huku akitoa simu yake ya kiganjani. Aliongea na tabibu aliyekuwa akimhudumia Shani kule Lugalo, na kutokana na maongezi yake ambayo
Baddi na Swordfish walikuwa wakiyafuatilia kwa makini, walielewa kuwa
Shani alikuwa ameshaamka na hakuwa na hali mbaya ila alikuwa akimuulizia sana mwanae na mumewe Baddi…
“Okay, basi kama ni hivyo tuma dereva amlete sasa hivi…” Kamanda Mnama alimaliza na kukata simu, kisha akawaonesha vyumba vyao vya kulala.
“Ni usiku sasa…sote twahitaji kupumzika. Mi’ n’takuwa humu humu ndani. Mkinihitaji mtanyanyua simu iliyopo pale sebuleni na mtamwambia opareta naye atanijuza. Kwa sasa naenda kujimwagia maji kidogo…” Aliwaambia.
Walipobaki peke yao, waliongea kidogo juu ya kile kisa cha hayati Gaudence Amani mdunguaji, kisha Swordfish akapiga mwayo mrefu. “Mnh, naona na mimi nikajimwagie maji kidogo patna, kisha nijaribu kupata lepe japo kidogo yakhe…”
“Okay, wacha mi’ nikamuone Claudia…nadhani atakuwa amelala, kisha nikamuone Gilda…” Baddi alimjibu. Opareta aliyepokea ile simu ya pale sebuleni alimuelekeza vyumba ambamo Claudia na Gilda walikuwamo. Hiyo ilikuwa ni ndani ya saa tatu zilizopita…
Alimtazama Swordfish aliyekuwa amelala pale kwenye kochi lililokuwa mbele yake, naye akahisi usingizi ukimuelemea. Alipiga mwayo na kujinyoosha, na hapo alisikia vishindo vikitokea nje ya mlango wa kuingilia pale sebuleni. Shani aliingia kwa wahka mkubwa mle ndani, akifuatiwa na Kamanda Mnama.
Baddi aliinuka na kubaki akiwa amesimama akimtazama yule mwanamama
aliyewahi kuwa mjane, kisha akaolewa, halafu akagundua kuwa kumbe hakuwa
mjane wakati anaolewa kwa mara ya pili, na sasa amekuwa mjane tena katika
ndoa yake ya pili, ilhali ndoa yake ya kwanza bado ikiwa inaelea hewani. Wazo
lile lilipita kichwani mwake mara tu alipomuona Shani akiingia mle ndani
kwa wahka namna ile, na akahisi moyo wake ukimyeyuka kwa huruma isiyo semekana.
Walibaki wakitazamana namna ile kwa muda, Kamanda Mnama
akiwatazama kwa makini.
“Baddi…” Hatimaye Shani aliita, uso wake ukiwa umesajili mchanganyiko wa hisia.
“Shani…” Baddi aliita, na hapo Swordfish alikurupuka kutoka usingizini. Baddi alipiga hatua kumsogelea mzazi mwenzake, na mara moja Shani alimkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu.
“Oh, Baddi my love…Baddi my one and only love…!” Shani alibwabwaja huku akitiririkwa machozi. Ile kauli ilimtoa Baddi mashaka yote aliyokuwa nayo kuhusu mtazamo wa Shani juu yake baada ya mkasa ule wa maisha yao.
“Shani…my love…pole sana…pole bibie…” Baddi alijikuta akibwabwaja huku akihisi myeyuko wa ajabu ndani ya kifua chake, donge likimkaba na macho yakimchonyota kwa machozi. Swordfish aliwatazama huku akitabasamu.
“No, pole wewe Baddi…Claudia yu wapi…?” Shani alimjibu huku akiinua uso wake na kumtazama mumewe wa kwanza usoni.
“Claudia yuko salama tu…yuko humu humu ndani. Amelala…vipi wewe, uko salama?” Baddi alimjibu na kumuuliza. Kamanda Mnama alijikohoza, na hapo ndipo Baddi alipokumbuka kuwa hawakuwa peke yao mle ndani.
“Enh, nadhani sasa umemuona mkeo Baddi…na bila shaka mnahitaji faragha…kwa hiyo mi’ n’takuwa chumbani kwangu. Iwapo mtanihitaji basi unajua cha kufanya.” Kamanda Mnama alisema huku akiondoka eneo lile.
“Okay, yes…ahsante sana Kamanda…” Baddi alimjibu. Bila kugeuka
Kamanda Mnama alimuinulia mkono kwa ishara kumuaga na kutowekea sehemu ndani ya jumba lile la kijeshi.
“Hali kadhalika na mimi Baddi…nitakuwa chumbani kwangu…”
Swordfish alisema huku akianza kuondoka.
“No, please…!” Shani alisema kwa wahka.
Baddi na Swordfish walitazamana.
Shani alijichomoa kifuani kwa Baddi na kumgeukia Swordfish. “Naomba uwepo shemeji…” Akamgeukia Baddi, “…kuna mambo naomba niyaongee
MDUNGUAJI
mbele ya shemeji yangu hapa Baddi, kwani nahisi naye anastahili kujua…”
Akina Baddi walitazamana tena, kisha Baddi akaafiki kwa kichwa na wote watatu wakaketi kwenye makochi yaliyokuwa pale sebuleni, Shani akichagua kochi lililokuwa likitazamana na yale waliyokalia akina Baddi. Aliinama kwa muda kisha akainua uso wake kuwatazama na kuanza kuongea.
“Baddi mume wangu…shemeji Babu…naomba sana mnisamehe, kwani najua kuwa nimewakosea nyote…kila mmoja kwa namna na wakati wake…”
Swordfish alitaka kusema kitu aidha kupinga usemi ule au kutaka
ufafanuzi, lakini Shani alimwashiria kuwa anyamaze, naye akaendelea, “… mume wangu Baddi nakuomba sana msamaha kwa namna nilivyokujibu pale dukani kwangu…hakika sikupaswa kukwambia kuwa mimi ni mke wa mtu… wa Gaudence…muda ambao nimekuona kuwa uko hai. Nilipaswa nielewe
kuwa baada tu ya wewe kudhihirika kuwa uko hai basi sikuwa tena na ndoa na Gaudence...”
Baddi na Swordfish walitazamana tena, na Swordfish alimtikisia
Baddi kichwa chake mara moja kuafikiana na kauli ile. “…lakini nilikuwa nimechanganyikiwa sana Baddi, sikuwa nikijua nisemacho wala nifanyacho…
zaidi ya hapo, kilichonichanganya zaidi ni kwamba siku zote nilikuwa na imani kuwa bado uko hai…sasa vile kutokea kwako mbele yangu namna ile kulikuwa ni sawa na kunisuta kwa kukubali kuolewa na Gaudence wakati tayari moyoni nilikuwa na imani kuwa wewe…mume wangu…bado uko hai somewhere… ilinichanganya sana…naomba unisamehe sana juu ya hilo my love…”
“Ah Shani…sina kinyongo kabisa juu ya hilo. Liliniuma sana kwa kweli, lakini nikijiweka katika nafasi yako katika mazingira yale, siwezi kukulaumu hata kidogo. Hilo limepita Shani…”
“Ah…ahsante sana my love…ahsante…” Shani alimjibu, kisha akamgeukia Swordfish.
“Meja Babu…shemeji… we’ naomba nikutake msamaha kwa namna nilivyokubadilikia baada ya kuolewa na Gaudence…ukweli ni kwamba ulinishauri nisifanye haraka ya kuolewa naye, lakini miaka ilizidi kupita naye akawa anazidi kunishawishi. Hatimaye nilikubaliana naye, kinyume na ushauri wako…”
“Ah, sasa miaka ilikuwa imepita Shani…ilibidi ufike wakati uolewe tu, mi sioni kama unahitaji kunitaka msamaha kwa hilo…”
“La, si kwa hilo…bali kwa jinsi nilivyokuwa nikikujibu kijeuri na kimkato baada ya ndoa ile…”
Kwa mara nyingine wale wapiganaji wawili walitazamana. “Aam, ni kweli
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
hilo lilinishangaza sana bibie, na kama kuna kitu moyoni mwangu dhidi ya hilo, basi si kinyongo bali ni udadisi tu. Udadisi wa kutaka kujua sababu… maana ulibadilika sana Shani…ulikuwa mtu wa ghadabu moja kwa moja… nilipata wasiwasi sana juu yako, lakini ndo sikuwa na namna!” Swordfish alimjibu. Shani aliuma midomo na uso wake uliingia fadhaa kubwa kabla ya kumjibu.
“Na hili ndilo haswa nililotaka kuongea mbele yenu. Sikutaka kuliongea hili nikiwa na Baddi tu…” Shani alisema na kutulia kwa muda, akiangalia viganja vya mikono yake. Kisha aliinua uso wake na kuwatazama.
“Ndoa yangu na Gaudence haikuwa ndoa bali mchezo wa kuigiza tu. Hata sijui ni kwa nini yule bwana alitaka kunioa…”
“Kwa nini wasema hivyo shem…?” Swordfish alimuuliza huku tayari jibu akiwa nalo. Baddi alibaki akimtazama mzazi mwenzie huku moyo ukimwenda mbio.
“Ndoa gani isiyo na unyumba shemeji?” Shani alimuuliza kwa hisia kali.
“Ama?” Ingawa naye alihisi anaijua sababu, bado kusikia kauli ile ikitoka kinywani kwa Shani kulimfanya Baddi agune kwa mshangao.
“Ndiyo! Yaani tangu anioe bwana yule hakuwahi kukutana nami kimwili hata siku moja! Yaani ilikuwa kama aliyenifunga kifungo fulani ili nisiolewe na mtu mwingine yeyote. Halafu hakuwa na sababu iliyoeleweka…alikuwa msiri mno! Kibaya zaidi alifikia hatua ya kuniachia chumba naye akahamia chumba cha wageni, can you believe that?” Shani alisema kwa fadhaa.
“Loh, ama hakika huo mtihani…”
“Mtihani? Adhabu! Adhabu kubwa kabisa shemeji yangu sikufichi! Mimi nimeishi na Baddi miaka yote sijatoka nje ya ndoa hata siku moja. Na nilipojikubalisha kuwa sasa Baddi wangu amekufa, sikutaka kuolewa tena maishani mwangu, na hivyo mambo ya unyumba nikayafuta kabisa akilini mwangu. Gaudence aliponioa nilijua kuwa niliwajibika kukutana naye kiunyumba sio? Sasa nakuja kukutana na hali kama hiyo! Sio siri nilichanganyikiwa sana.
Bora ningebaki mpweke ningevumilia, lakini nimeolewa! Ananiweka ndani halafu muda wa kulala anahamia chumba cha pili? Aliniweka kwenye majaribu makubwa sana. Nikafikiria kutoka nje ya ndoa, nikashindwa, nikafikiria kunywa pombe kujipoteza mawazo nikashindwa…nikafikiria hata kuvuta bangi for God’s Sake! Sio siri nilikuwa na hasira…nilikuwa na hasira na maisha yangu, na nilikuwa n’na hasira na Baddi kwa kukubali kurudi jeshini na hatimaye kuuawa huko…yaani nilikuwa n’na hasira muda wote!” Shani
MDUNGUAJI aliongea kwa jazba na kubaki akihema.
“Sasa…hukupata kumuuliza kwa nini alikuwa hivyo…yaani, lazima mlikaa na kulizungumzia swala hilo, right?” Hatimaye Swordfish alimuuliza. Shani alitikisa kichwa kwa masikitiko.
“Nilijaribu sana. Lakini hakuwa muwazi hata kidogo. Aliniambia kuwa iwapo mimi nilikuwa tayari kuishi bila mume baada ya Baddi kufariki, isingekuwa vigumu kuishi naye bila unyumba…aliniambia kuwa alikuwa anapitia kipindi kigumu sana katika maisha yake na alinihitaji sana, na kwamba akivuka kipindi hicho, basi tutaishi kama wanandoa wengine waishivyo… alinichanganya sana kwa kweli.”
Ukimya ulitanda kwa muda, kisha Shani akamgeukia Baddi.
“Sasa Baddi mume wangu…naomba uelewe kuwa pamoja na kuwa niliolewa na Gaudence, kwa shani zake mwenyezi mungu sikuwahi kukutana naye kimwili asilani. Niko kama ulivyoniacha…na niko tayari kuendelea kuwa mkeo kuanzia sasa, iwapo utakuwa tayari kunisamehe na kunipokea…”
Baddi alijikuta akiinuka na kwenda kumkumbatia mkewe kwa upendo na hisia kali.
“Oh, Shani my wife…sina cha kukusamehe kwani huna makosa na…of course niko tayari kuendelea kuwa mumeo, kwani nimepambana na vigingi vingi sana ili niweze kurudi tena mikononi mwako na tulee mwanetu my love.”
“Ah, thank you my love! Thank you so much my hero…umerudi kuja kunikomboa kutoka kwenye gereza la ndoa ya Gaudence! Aah, Mungu na ashukuriwe jamani. Yaani kesho tu tunaanza taratibu za kuifuta kabisa ndoa ile tata…Gaudence akatafute mtu mwingine wa kumnyanyasa…”
“Gaudence is dead…”
“Gau…whaaat?” Shani alimaka kwa mshangao huku akijichomoa mikononi mwa Baddi na kumtazama usoni. Alikuwa ameshituka vibaya sana.
“Yes Shani…Gaudence hakuwa mtu mzuri kama sote tulivyomdhania…na sasa amekufa.” Baddi alimwambia kwa upole. Shani hakumuelewa, akamgeukia Swordfish kwa macho ya kuuliza.
“Khabari nd’o hiyo hiyo shemeji yangu…yule bwana keshatangulia mbele ya haki wallahi…hatunaye tena hapa duniani!” Swordfish alimthibitishia. Shani alimtazama kwa muda, kisha akamgeukia Baddi na kushusha pumzi ndefu.
“Siwezi kusema kuwa habari hii imenisikitisha jamani, la hasha. Ila imenishtua sana…how did it happen?” Alisema, akiwatazama mmoja baada ya mwingine.
“Hiyo ni hadithi ndefu Shani. Na kwa kuwa nyie mna mambo mengi
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI ya kuelezana, naamini hilo litakuwa moja wapo…mi’ naenda kulala sasa.”
Swordfish alimjibu huku akiondoka, akiwaacha mtu na mkewe pale sebuleni.
Usiku ule Baddi Gobbos na Shani hawakulala kabisa. Ulikuwa ni usiku wa kuelezana yote yaliyotokea tangu walipoachana, zaidi Baddi akimuelezea mkewe mambo yaliyomsibu kule Sierra Leone, Liberia na Senegal. Waliongea usiku kucha, na katika usiku ule Baddi alimueleza Shani kuhusu jinsi alivyokutana na Gilda na masahibu waliyopitia wakiwa pamoja kule ugenini hadi walipofanikiwa kufika pale nchini, na mambo waliyokutana nayo.
Shani aliumia sana alipogundua kuwa ndoa yake na Gaudence ilikuwa ni mbinu tu ya Gaudence kutaka kujua harakati za Baddi, na aliumia zaidi alipogundua kuwa Gaudence aliweza kujua juu ya mipango ya Baddi kurejea nchini kupitia kwenye anuani yake ya barua pepe.
Pamoja na kuwa hakumueleza mkewe kuhusu uhusiano wa kimapenzi uliojengeka baina yake na Gilda, kwa namna fulani aliona kuwa Shani alihisi uwezekano wa jambo hilo kutokea.
“Kuhusu huyo Gilda…kuna uwezekano wowote kuwa anaweza kuwa na ujauzito wako hivi sasa? Au aliwahi kuwa na hali hiyo mkiwa huko Liberia…?”
Shani alimuuliza huku akimtazama moja kwa moja usoni. Baddi hakusita hata kidogo.
“Hapana Shani. Hakuna kitu kama hicho…ninakuhakikishia kabisa, na ningependa kukutanisha naye…”
“Okay…It doesn’t matter now Baddi, madhali umerudi tena kwangu mkeo… mi sitataka kufuatilia sana juu ya yaliyokea baina yenu mlipokuwa huko. Miaka mitatu ni mingi sana Baddi, na kama si kwa kadari yake muumba, nadhani mimi ningeweza hata kuzaa na Gaudence, hebu niambie sasa tungekuwa kwenye njia panda ya aina gani…”
“Kweli…ungekuwa utata mkubwa…”
“Lakini madhali mungu ameweza kutuepusha na hilo kutokea kwangu, basi naamini atatuepusha na mengine kama hayo pia kutokea kwako, sio?” Shani alimwambia huku akimtazama machoni, macho yake yakimtupia ujumbe ambao Baddi aliuelewa vizuri sana.
Anataka kujua iwapo sitakuwa na uhusiano zaidi na Gilda wakati niko naye kama mke wangu…
Alimtazama mkewe kwa muda, akili yake ikijaribu kutafuta jibu la kweli kabisa kwa swali lile, na hapo maneno aliyoyasoma kwenye ile barua ya Gilda yalimrudia kichwani…
… mimi nimeondokea kukupenda sana Baddi, na inaniuma sana moyoni
MDUNGUAJI
kuwa siwezi kuwa na wewe kama ambavyo ningetaka kwa kuwa wewe tayari ni mume wa mtu. Kuendeleza uhusiano baina yetu ni sawa na kujenga msingi wa kuvunja ndoa yako makusudi, jambo ambalo siwezi kujisamehe maishani iwapo litatokea…
“Hatuna la kuhofia juu ya hilo my love…” Alimjibu mkewe na walibaki wakitazamana namna ile kwa muda, kisha Shani akamwambia huku akimtazama machoni.
“Okay, nakuamini my love…as always…”Kisha akajilaza kifuani kwake na kumkumbatia kwa muda mrefu. Na pale Baddi alikuwa ameshapitisha uamuzi juu ya mustakbali wake na Gilda.
Walibaki namna ile hadi walipopitiwa na usingizi. Huko nje majogoo yalikuwa yameshaanza kuwika. Waliamka saa nne na nusu za asubuhi na bado walikuwa na usingizi mzito. Furaha yao ilikamilika pale walipokutana na binti yao Claudia. Familia ilikuwa imeungana tena baada ya kutengana kwa muda mrefu.
Walikubaliana kuwa Shani afanye taratibu za kuhama kutoka kwenye nyumba ya hayati Gaudence Amani na wahamie kwenye nyumba yao ambayo
Shani aliinunua baada ya kupata “mafao” ya Baddi. Akiwa na hamu na wahka wa kuijenga upya familia yake, Shani aliuliza iwapo ataruhusiwa kutoka kwenye ile nyumba ya kijeshi ili aende kufanya taratibu za kuhamia kwenye nyumba yao.
Kamanda Mnama aliwaambia hilo linawezekana ila walitakiwa waongozane na askari wa kijeshi ili kwenda kufanya upekuzi katika nyumba ya Gaudence. Shani alikubali kuongozana nao ili baada ya upekuzi kukamilika, yeye ahamishe vitu vyake siku hiyo hiyo kuvipeleka kwenye nyumba yao.
Haikuwa mpaka Shani alipoondoka kuelekea nyumbani kwa Gaudence akiwa na wana usalama pamoja na Kanali Mwanamkasi, ndipo Baddi alipopata nafasi ya kwenda kuonana na Gilda. Alibisha hodi mlangoni kwake hakukuwa na jibu. Aligonga kwa mara nyingine na kuusukuma ndani ule mlango ambao ulifunguka naye akaingia kwenye kile chumba kitupu.
Hakukuwa na dalili ya uhai kabisa mle ndani.
E bwana we!
“Gilda…!” Aliita, lakini hata pale alipokuwa akiita alijua kuwa hakutakuwa na sauti yoyote itakayomuitikia. Ilikuwa ni ileile hali ya kule hotelini ikijirudia tena. Aliingia bafuni na kuona hakukuwa na mtu, alifungua kabati kubwa la nguo lililojengewa kwenye ukuta mmoja wa chumba kile, nalo lilikuwa tupu.
“Gilda…” Aliita tena bila matumaini.
HUSSEIN ISSA TUWA MDUNGUAJI
Ukimya ulikuwa umetanda.
Alijibwaga kitandani na kujiinamia. Alijua kuwa safari hii Gilda alikuwa
ameenda moja kwa moja na hatomuona tena. Pamoja na kwamba alikuwa ameshapitisha uamuzi juu ya hatima yake na binti yule usiku uliopita huku mkewe akiwa amelala kifuani kwake, bado alihisi uzito mkubwa moyoni kwa kutoonana tena na binti yule kwa mara ya mwisho.
Alienda kumuuliza Kamanda Mnama juu ya mahala alipo Gilda.
“Tumemuachia aende zake…”
“Kwa nini? Nilidhani yeye ni shahidi muhimu kwenye kesi ya Gaudence…?”
“Yeah, lakini baada ya kifo cha Gaudence hatukuwa na sababu ya kuendelea kumshikilia zaidi, na ukizingatia kuwa kimsingi Willy Ngoma amekiri makosa yake, ushahidi wa huyu binti haukuwa na nguvu sana. Hivyo tulichukua maelezo yake ya maandishi na kumuachia…”
“Ah, sasa…muda gani mambo haya yametokea lakini? Kwani jana tu alikuwepo hapa…”
“Jana usiku aliomba kuonana nami na ndipo aliponieleza nia yake ya kuondoka. Niliwasiliana na wanasheria wetu nao hawakuwa na pingamizi… yeye hakutaka kumfungulia Willy mashtaka ya utekaji nyara. Alitaka aendelee na maisha yake tu. Hatukuwa na sababu ya kuendelea kumshikilia kwa kweli…”
“Kwa hiyo ameondoka jana usiku?”
“Hapana…leo asubuhi sana. Wakati nyie mmelala. Ila jana usiku tulimpatia askari waliomsindikiza hadi kwenye hoteli aliyokuwa amepanga na kuchukua begi lake, kisha akarudi hapa, na alfajiri ya leo ndiyo ameondoka…”
“But…si mnajua alipoenda? Vipi iwapo atahitajika tena kwa sababu moja au nyingine huko mbeleni?”
Kamanda Mnama alimtazama kwa muda. “Inaweza kuwa hivyo, lakini aliniomba nisimfahamishe mtu yeyote mahala atakapokuwa…hata wewe! Yaani alinisisitizia sana juu ya hilo…nami nilimkubalia.”
Walibaki wakitazamana kwa muda, kisha Baddi aligeuka na kuondoka.
“Baddi…”
Aligeuka.
“Najua kuwa kuna kitu kilikuwa kikiendelea baina yako na yule binti. Niliweza kuona upendo wa hali ya juu kwako machoni mwake…lakini elewa kuwa amepitisha uamuzi mzito kwa faida yenu nyote...yeye, wewe, Shani, na Claudia. Ningekuwa wewe ningeheshimu uamuzi wake…angalia familia yako sasa Baddi. Ni wazi kuwa Mungu ana mipango mikubwa kwako na Shani… hivyo usimbeze.”
MDUNGUAJI
Baddi alibaki akimtazama kwa muda mrefu, kisha bila ya kujibu kitu alishindilia mikono yake kwenye mifuko ya suruali yake na kuondoka, akimuacha Kamanda Mnama p.a.k. Tabasamu Jepesi akimtazama.
KIHITIMISHO
Askari wa kijeshi waliofanya upekuzi nyumbani kwa Gaudence Amani walikuta kifurushi chenye rundo la almasi kikiwa kimefukiwa kwenye kona moja ya chumba cha wageni, kilichokuwa kikitumiwa na Gaudence. Ugunduzi ule ulikuwa ni matunda ya jitihada ya kupita wakigonga
kigae kimoja baada ya kingine katika nyumba ile, mpaka walipogonga moja ya vigae vilivyosakafia chumba kile na kusikia sauti ya mrindimo kama kwamba
kuna uwazi chini ya kigae kile, na walipokivunja wakaukuta mzigo ule.
Siku tatu baada ya kifo cha Gaudence, Baddi Gobbos akiwa katika mavazi
kamili ya kijeshi, aliingia kwenye chumba maalum ndani ya jengo la makao
makuu ya jeshi la wananchi wa Tanzania na kukutana na lile jopo la kijeshi
lililowasaili akina Swordfish kule Sierra Leone, miaka mitatu iliyopita. Jopo
lile sasa likiwa limehamia Tanzania kusikiliza ushuhuda wa Baddi Gobbos, p.a.k Vampire, juu ya matukio ya kule msituni miaka mitatu iliyopita. Wakati
huu lile jopo lilikuwa likiongozwa na Meja Jenerali Fabiola Oluoch kutoka
Kenya, akichukua nafasi ya Meja Jenerali Balthazar Swandoh wa Sierra Leone, aliyefariki dunia mwaka mmoja baada ya jopo lile kukutana kule Sierra Leone, kutokana na sababu za kawaida. Jenerali mwingine aliiwakilisha Sierra Loene
katika kikao hiki cha Tanzania. Kutoka Tanzania, pamoja na Brigedia Jenerali
Stanslaus Kahemela, ambaye wakati jopo lile lilipokutana kwa mara ya kwanza
kule Sierra Leone alikuwa na cheo cha Brigedia, na Meja Jenerali Athanas Chacha, safari hii aliongezeka mnadhimu wa jeshi la wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Gharib Panza.
Baddi alieleza kisa chake chote mbele ya jopo lile, huku akirekodiwa kama jinsi wenzake walivyorekodiwa miaka mitatu iliyopita kule Sierra Leone. Tangu alipomkabidhi Black Mamba redio yake ya mawasiliano, mpaka alipomuibukia msaliti Nathan Mwombeki kule msituni hadi jinsi alivyolazimika kumuua, na jinsi alivyomshuhudia mpiganaji Black Mamba kutoka jeshi la Sierra Leone
akitawanya kichwa na risasi ya Mdunguaji, na namna alivyoonana macho kwa macho na muuaji yule hatari.
Wajumbe wa jopo lile walimuuliza maswali mengi sana kutaka kupata uhakika juu ya ule mwili uliozikwa nchini Tanzania ukiaminika ni yeye. Alielezea kwa ufasaha kabisa kila kitu kama jinsi kilivyotokea, na alipomaliza, hakukuwa na shaka kabisa miongoni mwa wajumbe wa jopo lile kuwa yule
aliyezikwa Tanzania alikuwa ni Black Mamba kutoka Sierra Leone.
Wajumbe wa jopo walitaka kujua alikuwa wapi kwa miaka ile mitatu
MDUNGUAJI
baina ya tukio la kule msituni hadi alipokuja kuibuka ghafla hapa nchini, naye
aliendelea kuelezea namna alivyoweza kusota nchini Liberia kwa miaka mitatu na jinsi alivyoweza kutoroshwa kutoka kwenye nchini ile na mlanguzi wa silaha haramu wa ki-lebanoni Twalal Ghailani, akiacha kabisa kuelezea uhusika wa Honey-Bee kule Senegal.
Saa tatu baadaye, alitoka nje ya chumba kile akiwaacha wajumbe wa jopo lile wafanye maamuzi yao, mwenyewe akiwa amechoka sana. Swordfish na Kamanda Mnama walikuwa wakimsubiri nje ya chumba kile. Alikumbatiana na rafiki yake, na kupeana mikono na Kamanda Mnama.
“Nimemaliza…sasa naweza kuendelea na maisha yangu bila ya dukuduku lolote moyoni…nimesema yote niliyodhani nilitakiwa kuyasema…nadhani sasa jopo litaweza kufanya maamuzi sahihi juu ya ile kadhia ya Mdunguaji.”
“
Yeah…hatimaye Black Mamba atapata heshima itakiwayo…” Swordfish alisema. Baddi na Kamanda Mnama walitikisa vichwa kukubaliana naye.
Waliingia kwenye chumba kingine kilichokuwa na vinywaji mbalimbali na baadhi ya vitafunio. Waliketi wakisubiri kusikia maamuzi ya jopo. Nusu saa
baadaye jopo lilitoa tamko rasmi kuwa Gaudence Amani kutoka Tanzania
ndiye aliyekuwa akifanya hujuma ya kuwadungua wapiganaji wa jeshi lile miaka
mitatu iliyopita huko Sierra Leone, na kwamba ule mwili uliozikwa Tanzania
ukiaminika kuwa ni wa mpiganaji Vampire, kwa hakika ni wa mpiganaji Black
Mamba kutoka Sierra Leone. Aidha, jopo liliamua kwamba almasi zilizokutwa nyumbani kwa hayati Gaudence Amani, zirudishwe nchini Sierra Leone na kukabidhiwa serikali ya nchi hiyo.
Vile vile, jopo liliamua kuwa mwili wa Black Mamba ufukuliwe ili akazikwe tena katika ardhi ya nchi yake na ndugu zake wapate kuweka hitimisho katika utata wa ndugu yao kupotea katika harakati.
Mwisho wa yote, jopo liliagiza Kanali Baddi Gobbos p.a.k. Vampire, apatiwe nishani ya juu ya jeshi la umoja wa mataifa kwa ushujaa, uvumilivu na uaminifu kwa jeshi na taifa lake. Jeshi la Tanzania litaandaa sherehe maalum ya kukabidhiwa nishani hiyo mara itakapowasilishwa nchini kutoka makao makuu ya jeshi la umoja wa mataifa.
Hii ilikuwa habari njema na isiyotarajiwa kabisa kwa Baddi, naye aliifurahia sana. Swordfish na Kamanda Mnama walimkumbatia kwa furaha na pongezi.
Brigedia Kahemela, Meja Jenerali Athanas Chacha na mnadhimu Gharib Panza walikuja kumpa mikono ya pongezi, kisha akapeana mikono wajumbe wote wa jopo lile.
Baddi, Swordfish na Kamanda Mnama walitoka nje ya jengo la makao
makuu ya jeshi la wananchi wa Tanzania na kuingia kwenye LandRover
Freelander ya jeshi, Kamanda Mnama akiwa nyuma ya usukani, Swordfish akiketi kwenye kiti cha abiria kule mbele wakati Baddi akiketi kwenye kiti cha nyuma.
“Okay guys…wapi sasa? Najua leo tuna mwaliko wa lanchi sehemu fulani… je?” Tabasamu Jepesi alisema huku akiliondoa lile gari kutoka eneo lile.
“Of course tunaelekea kwenye mwaliko…mke wangu leo ameacha shughuli zote ili atuandalie chakula cha mchana kuhitimisha kadhia hii iliyotukumba… unadhani atatusamehe tukichelewa?” Baddi alijibu kwa bashasha kutokea kule nyuma. Swordfish na Tabasamu Jepesi waliangua kicheko kutokea kule mbele.
“Hih! Naona mtwana kaja juu kweli kweli huko nyuma…haya basi na twende huko kwenye maakuli yakhe…” Swordfish alimwambia Kamanda Mnama, ambaye aliendelea kuendesha huku tabasamu jepesi likiwa limeupamba uso wake. Kule nyuma Baddi Gobbos alitikisa kichwa huku akitabasamu. Safari iliendelea kwa ukimya.
“All for one, partner…” Hatimaye Swordfish alisema taratibu.“One for all, partner…!” Baddi na Tabasamu Jepesi walimalizia kwa pamoja, kisha wote walicheka kwa sauti... Siku mbili baadaye, Baddi Gobbos alikuwa amesimama juu ya jabali kubwa kando ya bahari ya hindi jijini Dar. Bahari ilikuwa imejaa na mawimbi yenye ghadhabu yalikuwa yakijipigiza kwa nguvu kwenye kingo za bahari ile, yakirusha rasha za maji ya chumvi kila upande. Mkononi alikuwa ameshika soksi ambayo ndani yake kulikuwa kuna rundo la zile almasi alizopewa na Gilda, pamoja na ile barua aliyoandikiwa na binti yule aliyepata naye taabu sana kwenye nchi ngeni. Aliongezea uzito kwa kuongezea jiwe kubwa ndani ya soksi ile na kuufunga vizuri mdomo wa ile soksi.
Alisimama pale juu ya jabali kwa muda mrefu, kisha kwa nguvu zake zote aliitupia baharini ile soksi pamoja na vyote vilivyokuwa ndani yake. Aliitazama ile soksi ikisafiri hewani kwa umbali mrefu kabla haijapotelea baharini.
Aligeuka na kuelekea pale alipoegesha Mitsubishi Pajero ya mkewe kando ya ile bahari ya hindi huku akiwa ameshindilia mikono yake kwenye mifuko ya suruali yake… *