Page 1

Lazima kusomwa na kila mtu anayefanya kazi na ng’ombe wa maziwa na kuwekeza kwenye ng’ombe wa maziwa. Unavutiwa na ng’ombe wa maziwa na labda unawahudumia mara kwa mara? Je unataka kuelewa vyema jinsi ya kuwahudumia ng’ombe? Kuhakikisha wana afya njema, wanazalisha, na kukua vyema au kutoa maziwa mengi? Basi kitabu cha Mambo ya Msingi ya Ng’ombe ni lazima kukisoma. Hiki kitabu kimeandikwa kwa lugha rahisi ya kusoma. Kina zaidi ya picha 200 na michoro ambayo inafanya taarifa kuwa wazi na za uhalisia. Mambo ya Msingi ya Ng’ombe hufanya mfugaji yeyote wa ng’ombe wa maziwa kuelewa usanifu wa kuhudumia ng’ombe wa maziwa na mifugo wadogo, kwa taswira ya ng’ombe mwenyewe. Jan Hulsen, mhariri na mtaalamu wa ng’ombe

Wahariri wa maudhui ya cow signals - msingi –wahariri wa toleo la afrika mashariki: Profesa Bockline Omedo Bebe, Chuo Kikuu cha Egerton Profesa Charles K. Gachuri, Chuo Kikuu cha Nairobi

Cow Signals Msingi Toleo la Afrika Mashariki

C o pr py ot ri ec gh te t d

Toleo la Afrika Mashariki

Cow Signals Msingi Toleo la Afrika Mashariki

Cow Signals Msingi

David Maina, Perfometer Agribusiness Ltd Peter Ngure, Kampuni ya Mauzo na Uchapishaji ya The Olive

www.cowsignals.co.ke

www.roodbont.com

www.vetvice.com

www.cowsignals.com

Kuelewa ng’ombe wanahitaji nini kuwa na afya na kuzalisha Jan Hulsen


YA L IYO M O

KUMFAHAMU NGOMBE

Almasi ya Ishara za Ng’ombe Angalia – Fikiria – Tenda Ishara za ng’ombe kwa jumla Chaguo la mbegu Hewa Mapumziko Utunzaji wa ng’ombe

4 5 6 8 10 12 16

UKAMUAJI

C o pr py ot ri ec gh te t d

Ukamuaji kwa usafi Usafi wa ng’ombe Ukamuaji kwa kutumia mikono Ukamuaji kwa kutumia mashine

20 22 24 26

LISHE NA MAJI

Lishe Usiagaji wa lishe kwa tumbo Lishe iletayo nguvu mwilini Protini Kulisha ng’ombe Ujazo wa tumbo Hali ya mwili Kinyesi Maji

28 30 32 35 37 39 42 44 46

Dalili za ng’ombe mgonjwa Ulinzi wa kibailojia Wadudu Afya ya kwato Dalili za joto/hari

48 50 52 55 56

AFYA

UZAZI NA MIFUGO WADOGO

Kuzaa ndama Kumudu fedha Kulea mifugo wadogo Hali ya mwili ya ndama

58 59 60 63 64

MAELEZO YA MANENO

3


ANGALIA-FIKIRIA-TENDA

Elewa ng’ombe walivyo, tenda ipasavyo Ng’ombe mara kwa mara huonyesha wanachofikiria na jinsi wanavyohisi. Unaweza kujifunza jinsi ya kuelewa vyema lugha ya mwili ya ng’ombe na mifugo wadogo. Taarifa iliyo ndani ya hiki kitabu inakusaidia kusoma, kuelewa na kuzingatia ishara za ng’ombe: angalia, fikiria, tenda.

Kuna maswali matatu ambayo unapaswa kujiuliza kila wakati unapojishughulisha na ng’ombe: ANGALIA Naona nini? Elezea kwa undani.

2

FIKIRIA Kwanini hili linajitokeza? Tambua sababu za mambo unayoona.

3

TENDA Vitu viko Sawa na, kama sivyo, ninafaa nifanye nini?

C o pr py ot ri ec gh te t d

1

Kwa ishara na dalili aina zote, ng’ombe hutoa taarifa kuhusu makao yao, virutubisho, afya yao, na mengineyo. Ni lazima usome ishara hizi na uhakikishe kwamba ng’ombe anapata anachohitaji, ili wawe na afya, wapate mimba na kutoa maziwa.

K U M FA H A M U N G O M B E

5


H E WA

Hewa safi Ng’ombe, mifugo wadogo na ndume wanahitaji hewa wakati wote. Wakati hali ya joto ni zaidi ya nyuzi joto 25 mpaka 27, ng’ombe wa maziwa hupata joto sana: hii inaitwa msongo wa joto.

C o pr py ot ri ec gh te t d

JINSI INAVYOTAKIWA KUWA: Kusiwe na ukuta au kipingamizi chochote kinachokinga uwepo wa hewa safi. Hakikisha upepo na hewa ya nje zinaingia kupitia kwenye banda na katikati ya ng’ombe kwa wingi iwezekanavyo. Weka sakafu na sehemu ya kulala safi kutokuwa na mikojo na kinyesi, na kukauke. (Inatarajiwa kwamba utakinga ng’ombe wako kutokana na hali mbaya ya hewa, kama kimbunga na mvua kubwa).

Joto kali sana Joto kali Joto jingi

Jenga paa juu, mbali na ng’ombe. Kwasababu kwenye paa la juu, hewa ya joto inayokaa upande wa chini wa paa hauwezi kuathiri ngombe.

Tumia vikingo vya mvua kutoa kivuli zaidi, kukinga mvua kuingia kwenye banda na kukusanya maji ya mvua.

10

CO W S I G N A L S - M S I N G I


H E WA

C o pr py ot ri ec gh te t d

HALI ISIYO YA AFYA: Kama ng’ombe wakivuta hewa chafu na ya kuzizima, wanaweza kuugua. Hewa chafu inaweza kuwa na mzizimo kutoka kwenye kinyesi, mkojo na maeneo ya maji maji. Inatengeneza hatari ya homa ya mapafu. Hewa ng’ombe wanayotoa nje pia ni ya mzizimo na ina oksijeni kidogo.

Jenga kuta chache iwezekanavyo. Kuta zina gharama kujenga, huzuia mzunguko wa hewa na kupunguza nafasi. Na kuta hufanya ndani ya banda kusiwe kupana: ni vigumu kubadili ukubwa au udogo wa vijichumba na kadhalika.

Weka banda sehemu ya juu mbali na miti, vichaka na majengo mengine ili upepo uweze kupiga ndani na kutoa hewa safi kwaajili ya ng’ombe. K U M FA H A M U N G O M B E

11


K U M T U N Z A N G’O M B E

Lugha ya mwili wa ng’ombe unayemkaribia Ng’ombe amechangamka, ametulia

C o pr py ot ri ec gh te t d

Ng’ombe ametulia

Ng’ombe ameinamisha kichwa, anaangalia anachokula, na ng’ombe wengine na mazingira. Masikio yake yanasikiza eneo linalomzunguka. Huyu ng’ombe hana wasiwasi na wewe, uko nje ya eneo lake la hatari.

Masikio yanalenga macho yanakoangalia. Macho yote yanaangalia sehemu moja. Ng’ombe ametulia na amechangamka.

Ng’ombe aliechonjo, kusita

Ng’ombe ana wasiwasi: kichwa kimeinuka

Ameinua kichwa, kuangalia pande zote, na masikio yanalenga kinyume na kule ng’ombe anakoangalia.

Ng’ombe ameinua kichwa chake juu, na masikio yake yanalenga nyuma. Hizi ni ishara za wazi za msongo na mshtuko.

18

CO W S I G N A L S - M S I N G I


K U M T U N Z A N G’O M B E

C o pr py ot ri ec gh te t d

Kumfanya ng’ombe asonge na kusimama

Unapotembea sambamba na ng’ombe anayetembea, lakini ukielekea upande mmoja na yeye, kwa kasi sawa na yake au haraka kidogo ngo’mbe atasimama.

Unapotembea sambamba na ng’ombe anayetembea, lakini ukielekea kinyume na yeye, ng’ombe atasonga mbele.

Ng’ombe anafaa, agutuke na azidi kutembee kwa kasi yake mwenyewe

Usiwapige ng’ombe au kuwapigia kelele. Hii itawashtua. Ng’ombe wanaojiskia hatarini ni wagumu kuwahudumia na wanaweza kuwa hatari sana.

Usimfanye ng’ombe ashtuke. Wafanye watembee polepole, tena kwa utulivu. Au wafanye wasimame, ili uweze kuwahudumia. Ng’ombe anafaa ajiandae na kutembea kwa kasi yake mwenyewe. Kitu wanachokosea wengi ni kumtia wasiwasi sana ng’ombe. Hii inafanya ng’ombe ashtuke. Ataruka uzio au kuwatoroka watu, au hatasongea kabisa.

K U M FA H A M U N G O M B E

19


U K A M UA J I K WA U S A F I

Usafi wa ukamuaji Usafi katika shughuli ya kukamua ni muhimu. Usafi wa kiwele, mtu anayekamua, na vifaa husababisha afya kwa ng’ombe, kiwango kizuri cha maziwa na walaji wenye afya.

C o pr py ot ri ec gh te t d

Kila kitu lazima kiwe safi

Ng’ombe mwenye afya

Viwele safi

Maziwa bora

Mikono safi

Vyombo safi Walaji wenye afya

Maziwa bora husababisha afya na huleta mapato zaidi yanapouzwa. 20

CO W S I G N A L S - M S I N G I


K U K A M UA K WA M I KO N O

Maelezo: jinsi ya kumkamua ng’ombe kwa mikono

2 Ongeza kidole chako cha kati na halafu ukamue taratibu kutoa maziwa kwenye njia ya chuchu.

3 Ongeza kidole chako cha pete na ukamue taratibu.

4 Ongeza kidole chako cha mwisho na ukamue kwa mara ya mwisho. Katika shughuli yote ya kukamua, usivute chuchu.

C o pr py ot ri ec gh te t d

1 Kamata chuchu vizuri kwa kuzungusha kiganja chako na kidole gumba pale chuchu inapoanza ili hupata maziwa yote kwenye chuchu.

5

Rudia hili mpaka kiwele kiwe kitupu.

Kukanda mara nyingi hutumika kama njia ya kukamua, inamaanisha kuvuta maziwa ndani ya chuchu na kidole gumba na kidole cha shahada. Hii husababisha uchungu kwa ng’ombe na huenda akaonyesha kwa kupiga teke. Usitumie njia hii. 24

CO W S I G N A L S - M S I N G I


U S I AG A J I N D A N I YA T U M B O

Usiagaji ndani ya tumbo ya ng’ombe Anza kusoma upande wa mkono wa kulia na soma kuanzia 1 hadi 6, hivyo ufuate chakula kinavyopita kwa ng’ombe. 5 Bakteria/kubuni tena

Utumbo ni chumba cha kuchachua. Hii ina maanisha kwamba mabilioni ya bakteria huponda na kula chakula, na hivo kuzalisha bakteria zaidi na zaidi. Kwa ng’ombe mkubwa utumbo una ukubwa kati ya lita 100 hadi 150 (ndoo 9 mpaka 15 za maji).

1 K  uchagua na kula malisho Kwa pua yake (harufu) na ulimi (ladha), ng’ombe anachagua atakachokula. Anakula chakula kibichi, laini na kitamu kwanza. Hapendi kula malisho ambayo yameganda au ambayo ni magumu. Ng’ombe atakula hii pekee wakati ana njaa au wakati hamna lishe mbadala.

C o pr py ot ri ec gh te t d

Kwenye utumbo mkubwa, kuna bakteria ambao huchachua chakula baada ya kutoka kwenye utumbo mdogo. Ng’ombe anatumia mabaki ya hawa bakteria ili kujipatia nguvu mwilini.

3 Bakteria za kuchachua lishe hukua na kutoa nguvu

6 Kupokea maji

4 Kusiaga bakteria

2 Kutafuna na kutafuna tena

Sehemu ya utumbo mkumbwa inayoitwa mjiko, hunyonya maji kutoka kwenye kinyesi.

Kubini au bakteria na chakula iliyobaki hisiagiwa kwenye sehemu ya mwisho ya utumbo na kwenye utumbo mdogo. Kila dakika utumbo hupanuka kuchanganya lishe iliyomo, na kusukuma baadhi yake kwenye sehemu ya mwisho ya utumbo.

Baada ya kutafuna kiasi, ng’ombe humeza chakula kwenye utumbo. Baadaye, utumbo hurudisha chakula juu ambacho ng’ombe hutafuna zaidi na kwa bidii sana. Hii inaitwa kucheua. Anatumia masaa 9 hadi 10 kwa siku katika jambo hili.

30

CO W S I G N A L S - M S I N G I


MAJI

Unywaji wa maji Maji safi

Kila ng’ombe anatakiwa kupata maji safi bila kipimo, siku nzima. Maji yawepo kwenye sehemu ya maji. Hakikisha kisiwe juu sana, kuhakiksha kwamba kila ng’ombe anaweza kunywa kwa urahisi.

Safi = bila uchafu, hayana harufu, hayana ladha

C o pr py ot ri ec gh te t d

Kielelezo cha unywaji wa maji kwa siku ya kawaida (nyuzi joto 30), kwa siku:

+

Ndoo moja = lita 10

Ng’ombe anayekamuliwa: ndoo 10-14 za maji

+

Ndama wa umri wa mwaka 1: ndoo 2-4 za maji

Ng’ombe ambaye hakamuliwi: ndoo 5-7 za maji

+

+

Ndama wa siku 14: lita 1-2

Dume: ndoo 5-7 za maji

LISHE NA MAJI

+

47


Toleo la Afrika Mashariki

Lazima kusomwa na kila mtu anayefanya kazi na ng’ombe wa maziwa na kuwekeza kwenye ng’ombe wa maziwa. Unavutiwa na ng’ombe wa maziwa na labda unawahudumia mara kwa mara? Je unataka kuelewa vyema jinsi ya kuwahudumia ng’ombe? Kuhakikisha wana afya njema, wanazalisha, na kukua vyema au kutoa maziwa mengi?

C o pr py ot ri ec gh te t d

Basi kitabu cha Mambo ya Msingi ya Ng’ombe ni lazima kukisoma. Hiki kitabu kimeandikwa kwa lugha rahisi ya kusoma. Kina zaidi ya picha 200 na michoro ambayo inafanya taarifa kuwa wazi na za uhalisia.

Cow Signals Msingi Toleo la Afrika Mashariki

Cow Signals Msingi

Cow Signals Msingi Toleo la Afrika Mashariki

Mambo ya Msingi ya Ng’ombe hufanya mfugaji yeyote wa ng’ombe wa maziwa kuelewa usanifu wa kuhudumia ng’ombe wa maziwa na mifugo wadogo, kwa taswira ya ng’ombe mwenyewe. Jan Hulsen, mhariri na mtaalamu wa ng’ombe

Wahariri wa maudhui ya cow signals - msingi –wahariri wa toleo la afrika mashariki: Profesa Bockline Omedo Bebe, Chuo Kikuu cha Egerton Profesa Charles K. Gachuri, Chuo Kikuu cha Nairobi David Maina, Perfometer Agribusiness Ltd Peter Ngure, Kampuni ya Mauzo na Uchapishaji ya The Olive

www.cowsignals.co.ke

www.roodbont.com

www.vetvice.com

www.cowsignals.com

Kuelewa ng’ombe wanahitaji nini kuwa na afya na kuzalisha Jan Hulsen

Cow Signals Msingi  
Cow Signals Msingi