KNH NEWSLINE ED 6 2022

Page 15

25/3/2022

Tiba ya mwili: Yote unayohitaji kujua kuihusu Na Melody Ajiambo na Elly Makanga Kila mmoja wetu amehisi maumivu ya kimwili kwa njia moja au nyingine. Ajali ni moja wapo ya kisababishi kikubwa zaidi cha maumivu haya. Ikiwa mgonjwa anahisi maumivu mwilini, ni jambo la kawaida kutafuta ushauri wa daktari. Baada ya kupata matibabu na kupewa dawa, daktari anaweza kukutuma kwa mtaalamu wa idara ya tiba ya mwili (physiotherapy). Newsline iliketi na Bw. Anthony Ndiema, mtaalamu wa tiba ya mwili hapa katika Hospitali Kuu ya Kenyatta ili kupata kujibu maswali makuu yanayohusu taaluma hii. Tueleze kuhusu tiba ya mwili. Bw. Anthony: Tiba ya mwili ni taaluma ya kusaidia mgonjwa arejelee hali yake ya kawaida bila kutumia dawa ama upasuaji wa kimwili. Isipokua mtu kuzaliwa akiwa mlemavu, kwa kawaida mwili haufai kuwa na maumivu yoyote.

kuenda msalani bila kutegemea mtu. Ijapokuwa kuna tofauti, taaluma hizi mbili zinaambatana.

Ni nani anahitaji tiba ya mwili? Bw. Anthony: Mtu yeyote anaweza kupata tiba ya kimwili haswa wafanyikazi wanaoketi kwenye ofisi siku nzima au kufanya kazi inayotumia nguvu nyingi. Lakini wale wanaohitaji tiba ya mwili kwa kawaida ni wale ambao wamepatwa na majeraha kutokana na ajali au wale wanaozaliwa na ulemavu fulani wa kimwili. Kama ilivyotajwa hapo awali, tiba ya mwili inamsaidia mgonjwa kurejelea halia yake ya kawaida, ikiwemo kutembea kwa ukawaida na kupungua kwa uchungu. Kuna tofauti gani baina ya tiba ya mwili na tiba ya kazi? Bw. Anthony: Kama nilivyosema hapo awali, tiba ya mwili humsadia mgonjwa kurejelea hali yake ya kawaida baada ya kupata matatizo ya viungo vya mwili, kwa kupitia ajali au njia nyingine, bila kutumia dawa au upasuaji. Ilhali tiba ya kazi humsaidia au kumfunza mgonjwa kutekeleza majukumu yake ya kila siku baada ya ajali au ugonjwa, bila kutegemea usaidizi wowote. Kwa mfano mgonjwa wa kiharusi anahitaji tiba ya kazi ili aweze kutekeleza majukumu kama kujilisha, kuoga,

Je taaluma hii ina mbinu tofauti? Tafadhali eleza kwa utendeti Bw. Anthony: Ikitegemea kiwango cha maumivu na jeraha, mtaalamu anaweza kutumia mbinu tofauti tofauti. Mojawapo ni mazoezi ya mwili,

PHOTO | MELODY AJIAMBO Mtaalamu wa tiba ya mwili, Anthony Ndiema

ISSUE 6 | Kenyatta National Hospital Newsline

PICHA | MELODY AJIAMBO Mtaalamu wa tiba ya mwili, Anthony Ndiema akimshughulikia mmoja wa wagonjwa wake katika kituo cha matibabu, KNH.

Kuna aina ngapi za tiba ya mwili? Bw. Anthony: Kuna aina mbalimbali za tiba ya mwili, kuna tiba ya watoto (paediatric physical therapy) ambayo hutambua, kuzuia, na kutibu matatizo yanayoathiri watoto na vijana. Matatizo hayo ni kama matatizo ya uti wa mgongo (spina bifida), ugonjwa wa kupooza kwa ubongo (cerebral palsy), kudhoofika kwa misuli, kasoro za kuzaliwa na ukuaji wa pole pole. Kuna tiba ya mifupa (orthopaedic physiotherapy) ambayo hushughulikia mifupa iliyotokana au kuvunjika. Tiba ya michezo (sports physical therapy) hutumiwa na wanamichezo kuzuia majeraha, kuboresha utendaji wao katika michezo, na kadhalika. Mwisho kuna tiba ya mwili kwa wazee (geriatric physiotherapy). Aina hii ya tiba husaidia kutibu magonjwa kama ‘alzheimer’ kutoweza kujizuia haja,

15


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.
KNH NEWSLINE ED 6 2022 by Kenyatta National Hospital - Issuu