7 minute read

Tiba ya mwili: Yote unayohitaji kujua kuihusu

Na Melody Ajiambo na Elly Makanga

Kila mmoja wetu amehisi maumivu ya kimwili kwa njia moja au nyingine. Ajali ni moja wapo ya kisababishi kikubwa zaidi cha maumivu haya. Ikiwa mgonjwa anahisi maumivu mwilini, ni jambo la kawaida kutafuta ushauri wa daktari. Baada ya kupata matibabu na kupewa dawa, daktari anaweza kukutuma kwa mtaalamu wa idara ya tiba ya mwili (physiotherapy). Newsline iliketi na Bw. Anthony Ndiema, mtaalamu wa tiba ya mwili hapa katika Hospitali Kuu ya Kenyatta ili kupata kujibu maswali makuu yanayohusu taaluma hii.

Advertisement

Tueleze kuhusu tiba ya mwili.

Bw. Anthony: Tiba ya mwili ni taaluma ya kusaidia mgonjwa arejelee hali yake ya kawaida bila kutumia dawa ama upasuaji wa kimwili. Isipokua mtu kuzaliwa akiwa mlemavu, kwa kawaida mwili haufai kuwa na maumivu yoyote.

Ni nani anahitaji tiba ya mwili?

Bw. Anthony: Mtu yeyote anaweza kupata tiba ya kimwili haswa wafanyikazi wanaoketi kwenye ofisi siku nzima au kufanya kazi inayotumia nguvu nyingi. Lakini wale wanaohitaji tiba ya mwili kwa kawaida ni wale ambao wamepatwa na majeraha kutokana na ajali au wale wanaozaliwa na ulemavu fulani wa kimwili. Kama ilivyotajwa hapo awali, tiba ya mwili inamsaidia mgonjwa kurejelea halia yake ya kawaida, ikiwemo kutembea kwa ukawaida na kupungua kwa uchungu.

Kuna tofauti gani baina ya tiba ya mwili na tiba ya kazi?

Bw. Anthony: Kama nilivyosema hapo awali, tiba ya mwili humsadia mgonjwa kurejelea hali yake ya kawaida baada ya kupata matatizo ya viungo vya mwili, kwa kupitia ajali au njia nyingine, bila kutumia dawa au upasuaji. Ilhali tiba ya kazi humsaidia au kumfunza mgonjwa kutekeleza majukumu yake ya kila siku baada ya ajali au ugonjwa, bila kutegemea usaidizi wowote. Kwa mfano mgonjwa wa kiharusi anahitaji tiba ya kazi ili aweze kutekeleza majukumu kama kujilisha, kuoga, kuenda msalani bila kutegemea mtu. Ijapokuwa kuna tofauti, taaluma hizi mbili zinaambatana.

Je taaluma hii ina mbinu tofauti? Tafadhali eleza kwa utendeti

Bw. Anthony: Ikitegemea kiwango cha maumivu na jeraha, mtaalamu anaweza kutumia mbinu tofauti tofauti. Mojawapo ni mazoezi ya mwili,

Kuna aina ngapi za tiba ya mwili?

Bw. Anthony: Kuna aina mbalimbali za tiba ya mwili, kuna tiba ya watoto (paediatric physical therapy) ambayo hutambua, kuzuia, na kutibu matatizo yanayoathiri watoto na vijana. Matatizo hayo ni kama matatizo ya uti wa mgongo (spina bifida), ugonjwa wa kupooza kwa ubongo (cerebral palsy), kudhoofika kwa misuli, kasoro za kuzaliwa na ukuaji wa pole pole.

Kuna tiba ya mifupa (orthopaedic physiotherapy) ambayo hushughulikia mifupa iliyotokana au kuvunjika. Tiba ya michezo (sports physical therapy) hutumiwa na wanamichezo kuzuia majeraha, kuboresha utendaji wao katika michezo, na kadhalika. Mwisho kuna tiba ya mwili kwa wazee (geriatric physiotherapy). Aina hii ya tiba husaidia kutibu magonjwa kama ‘alzheimer’ kutoweza kujizuia haja, ugonjwa wa yabisi, miongoni mwa magonjwa mengine.

Je mpango wa kimatibabu huchukuwa muda gani?

Bw. Anthony: Kuna wagonjwa ambao hutumwa kutoka kliniki mbalimbali kama vile za matibabu, za mifupa na hata za kliniki za watoto. Cha msingi ni kutambua tatizo la mgonjwa. Kuna wagonjwa ambao hutumwa huku na ukiwafanyia uchunguzi zaidi, unapata kuwa hawako kwenye hali ya kupewa tiba ya mwili wakati huo. Wagonjwa kama hawa huhitaji matibabu zaidi kabla ya kupewa tiba ya mwili. Kwa mfano wagonjwa ambao huletwa kutoka kwa kliniki za mifupa; labda wamepata ajali na kuvunjika miguu, hufanyiwa ukaguzi wa kutosha kama kupigwa picha ya x-ray au kuwekewa chuma. Hivyo, kilichobaki huwa ni tiba ya mwili ili kuipa miguu nguvu na kujifunza kutembea. Hii ni tofauti na ugonjwa wa kiharusi ambao huhitaji tiba ya hatua kwa hatua na huchukuwa muda mwingi Zaidi. Kwa hivyo mpango wa matibabu hutegemea hali na tatizo la mgonjwa.

Tiba ya mwili inauhusiano wowote na chakula anachofaa kutumia mgonjwa?

Bw. Anthony: Sisi hufanya kazi kwa pamoja na idara ya lishe bora. Iwapo mgonjwa atahitajika kuzingatia chakula anachofaa kula, basi idara hii hutoa ushauri kikamilifu na kiwango kinachohitajika. Vyakula vinavyopendekezwa husaidia mgonjwa kupata nguvu, kupunguza uzito wa mwili na kuboresha afya.

Kwa siku moja wewe hutarajia kuhudumia wagonjwa wangapi?

Bw. Anthony: Mara nyingi kipindi kimoja kinafaa kuchukuwa dakika 45 au 60. Lakini pia inategemea tatizo la mgonjwa, kuna yule atachukuwa dakika 30, 45 au 60. Mimi huchukuwa dakika 15 za kwanza kumfanyia mgonjwa uchunguzi. Kwa siku hapa Hospitali Kuu Ya Kenyatta kila mmoja wetu anafaa kuwaona takriban wagonjwa 12, wakati mwingine idadi hii huongezeka hadi 18. Kwa hivyo unaweza kuanza na wagonjwa watatu kwa wakati mmoja. Iwapo utatumia saa moja kwa mgonjwa mmoja pekee, huenda usitimize malengo ya idara. Usimamizi wa idara umetenga vyumba vya kutosha kwa shughuli hii. Tuseme kwa siku tunaweza kuhudumia wagonjwa zaidi ya 70.

Taaluma hii ina changamoto zipi?

Bw. Anthony: Wagonjwa tunaopata kwa kawaida hapa hospitalini hawana ufahamu zaidi kuhusu tiba hii ya mwili. Hivyo basi, wengi wao wanapata taabu kubwa kuelewa mambo tunayowaagiza kufanya. Kuongezea, wengine wana matatizo ya kifedha na jambo hilo hufanya watumie muda mwingi kurudi hospitalini wakitafuta pesa za kupata matibabu. Hatima yake ni kuwa mgonjwa atachukua muda mrefu zaidi kupona. Zaidi ya hayo, kutokua na vifaa vinavyofaa na wataalamu wa kutosha hufanya kazi kuwa ngumu zaidi. Hata hivyo, sisi hufaya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa tunawapa wagonjwa huduma ya hali ya juu. Pia kuna changamoto ya wagonjwa kutofwata maagizo. Wakati mwingine huwa tunapeana maagizo kwa wagonjwa wetu kufanya jambo hili au lile wanapokuwa nyumbani. Utampata mgonjwa hajafwata maagizo aliyopewa hivyo basi kufanya kipindi kizima cha matibabu kiwe na ugumu. Jamaa na marafiki wa wagonjwa pia huchangia pakubwa hali hii, wao huambatana na mgonjwa na kushuhudia kinachotendeka huku. Wanaporejea nyumbani wanajifanya wataalam wa tiba ya mwili, kwa vile hawana ujuzi katika nyanza hii matokeo yake ni kuzidisha tatizo la mgonjwa.

Je, umepata uradhi wowote katika taaluma hii?

Bw. Anthony: Nilipokua mchanga, nilitaka sana kuwa daktari baada ya masomo. Lakini nilipokosa alama zinazofaa kusomea udaktari, nilichagua kusomea tiba ya kimwili. Taaluma hii imenipa uradhi usio na kifani. Ninaweza kusaidia wagonjwa ili waeze kurejelea hali yao ya kawaida bila kutumia dawa. Nimepata wagonjwa wengi kutoka tabaka, maeneo na hata wenye vikundi tofauti vya umri. Jambo la kawaida kwa wote, licha ya kwamba wanatumia muda tofauti kupona, ni furaha ninayopata ninapoona mpito wa taratibu wa kurejelea hali ya kawaida na tabasamu yao wanapopata nafuu.

Je wewe hutimiza aje muda wako kazini na majukumu ya familia? Bw. Anthony: Familia yangu huishi mbali sana. Hospitali ilikuja na mpango wa siku za mapumziko, ambapo ukifanya kazi wikendi unapewa siku za mapumziko. Kwa hivyo mimi hutumia siku hizi kutangamana na jamii yangu, ningependa kuishukuru hospitali kwa mpango huo.

POSITIVE MENTIONS FROM KNH OFFICIAL FACEBOOK PAGE

By Luke Kung’u

Francis Ndwiga: KNH has the best brains to save lives in Kenya and has done wonders in the recent past, let lower lever hospitals do their part and not refer every patient.

Lucia Lucille Wairimu: We value your service continue in that spirit

Maryanne Njoki Waweru: KNH ilijali mtoto wangu. I almost lost her thanks to this team’s work

Gakii Muthee: I wish to give credit where it’s due. Through my assessments in the last 4 months that I have visited KNH, I can attest that there is a lot of professionalism at the facility. Timely and effective clientcentered services. Kudos to the catering department I think you deserved to be ISO certified.

Zainab Hussein: My mom was dying of heart disease. KNH squeezed out all the water that was in her heart in a day and she was admitted to a nursing home elsewhere for a week. Her oxygen levels normalized.

This article is from: