waandishi ebook 1688116620.8550842

Page 1

NOVEL.................... MY VALENTINE- 01 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ _________________________________ _____


Baada ya kuhitimu shahada yake ya uzamili (Master's degree) nchini Uturuki, Hatimaye kijana Owen alirejea kwa mara nyingine katika ardhi ya nyumbani kwao Tanzania. Familia nzima ya Mr & Mrs James ilikuwa kwenye wimbi zito la furaha baada ya kumpokea kijana wao aliyekuwa masomoni kwa takribani miaka miwili. Familia hiyo ilikuwa ni miongoni mwa familia zilizobarikiwa kuwa na kipato kikubwa sana yani ilikuwa ni familia ya kitajiri mno. Mr James


na mkewe walikuwa ni miongoni mwa viongozi wakubwa wa siasa nchini. Familia hiyo ilifanikiwa kupata watoto wanne. Wa kwanza alifahamika kwa jina la Robyson, wa pili ni Owen, wa tatu ni Catherine na wa mwisho ni Sharon. Robyson alikuwa tayari ameshahitimu shahada yake ya uzamili miaka takribani mitano nyuma hivyo aliamua kujikita kwenye siasa na ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuwa kiongozi mkubwa wa siasa ndani ya nchi. Owen yeye hakutaka kabisa kujihusisha na siasa japo wazazi


wake walimsisitiza ajikite zaidi kwenye masomo ya siasa ili afuate nyayo za wazazi. Owen alikuwa ni mtoto mwenye upeo mkubwa zaidi kuliko watoto wote wa Mr James hivyo wazazi waliamini kama Owen angeamua kujikita kwenye siasa basi angekuja kuwa hata Rais wa nchi hapo baadae. Kwa bahati mbaya ni kwamba Owen alikuwa na mtazamo tofauti juu ya siasa. Yeye aliamini kwamba siasa ni mchezo mchafu unaoweza kuchafua roho ya mtu mbele ya Mwenyezi Mungu. Siasa inaweza


kubadili roho na imani ya mtu kutoka kwenye uzuri kwenda kwenye ubaya. Owen alijua kabisa roho yake ni nyepesi hivyo asingeweza kuhimili mikiki mikiki ya siasa. Alichokifanya ni kujikita zaidi kwenye masomo ya teknolojia ya mawasiliano pamoja na biashara. Catherine alikuwa mwanafunzi wa sekondari na ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuwa Daktari na Sharon bado alikuwa mtoto wa shule ya msingi ambaye hakujua utofauti kati ya ndoto ya maisha na ndoto ya kitandani. Ndoto


yake ilikuwa ni ile ya kitandani tu. Baada ya Owen kurejea nchini, Siku hiyo familia nzima ya Mr James ilijumuika kumpokea kijana wao. Tafrija ndogo iliandaliwa kwa ajili ya kumpongeza Owen kwa kufikia kiwango kikubwa cha elimu. "Hongera sana mwanangu kwa kufikia ndoto zako katika elimu. Sasa ni wakati sahihi wa kuanza kuishi kwenye zile ndoto ulizokuwa unaota. Kwa elimu na ujuzi ulionao nafikiri ni wakati wako wa kufurahia matunda ya


ndoto zako. Kwa sasa sina ninachokudai zaidi ya mkwe wangu na mjukuu tu. Nataka kumuona mjukuu wangu anafananaje kabla sijafa mama yako.!" Mama mzazi wa Owen aliongea kauli hiyo kumpongeza mwanae na kumkumbusha kwamba kuna maisha mengine baada ya kusoma ambayo ni kuanzisha familia. "Hahah! Mjukuu tena? Sawa Mama Owen nimekuelewa. Mjukuu utamuona na mkweo nitakuletea muda si mrefu.!"


Owen alimjibu Mama yake huku akiwa katika hali ya furaha iliyopitiliza. "Owen kijana wangu, hapa una wiki mbili tu za kupumzika kwa kuwa tayari kuna kampuni inakusubiri ukafanye kazi. Hapa ni kazi tu usitegemee kubaki nyumbani kwangu kama mzigo. Ni lazima ukapambane mtoto wa kiume.!" Hiyo ilikuwa kauli ya Mr James ambaye ndo alikuwa baba mzazi wa kijana Owen. "Sawa mzee nipo tayari kwa ajili


ya kazi lakini sihitaji kazi yoyote inayohusiana na masuala ya kisiasa. Hiyo sio taaluma yangu mzee. Ni bora hata nikauze machungwa barabarani kuliko kujihusisha na siasa.!" "Hahaha! Tulia wewe acha uoga siwezi kukuingiza kwenye siasa maana una roho nyepesi sana. Nimekuunganisha kwenye kampuni inayomilikiwa na wakwe zako watarajiwa kwahiyo jiandae kwa ajili ya kazi.!" "Wakwe zangu? Wakwe zangu wa


wapi tena mzee? Kwani unamjua mchumba wangu?" "Hahah! Namjulia wapi mchumba wako wakati hujawahi hata kututambulisha. Mimi namaanisha wakwe zake kaka yako. Kaka yako Robyson tayari amepata mchumba na anataka kuoa. Hivi Robyson, hujamwambia mdogo wako kwamba unataka kuoa?" Mr James alimuuliza mwanae Robyson. "Hapana mzee nilikuwa


sijamwambia bado. Sikutaka kumwambia kwenye simu kwa kuwa nilijua siku si nyingi atarudi nchini.!" Robyson alijibu swali la baba yake. Taarifa ya Robyson kuoa ilikuwa mpya kabisa kwa Owen. Owen alijikuta anatabasamu kisha akamfuata kaka yake na kumkumbatia. "Hongera sana kaka mkubwa. Kwa hakika umeamua kufanya jambo kubwa sana mbele ya Mungu wetu. Hayo ni maamuzi


ya kiutuuzima na unatufungulia darasa sisi ndugu zako tunaokufuatia. Ndoa inakujengea heshima mbele ya jamii na ukizingatia upo kwenye mchakato wa kutaka kuwa kiongozi mkubwa katika serikali ya nchi. Ni lazima ujitoe kwenye ujana na kuingia kwenye utu uzima. Utu uzima ni majukumu, na ndoa huleteleza hayo majukumu. Kiukweli kabisa, kama ungechelewa kidogo tu basi mimi ningewahi kuoa kabla yako.!" Owen aliongea kauli hiyo na kuwafanya Wanafamilia


kucheka. Baada ya Owen kuzungumza maneno hayo, familia ilimgeukia na kumtaka na yeye aoe kwa sababu umri tayari ulikiwa unaruhusu. Owen aliwajibu kwamba ndoa ni miongoni mwa vitu alivyokuwa anaviwaza kwa wakati ule. Wakati yupo masomoni nje ya nchi alikuwa na mchumba na tayari walishaweka ahadi ya kuoana pindi atakapohitimu shahada yake ya uzamili na kurejea nchini. Owen aliongeza kwa kusema kwamba


siku ambayo kaka yake amepanga kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake basi na yeye angewatambulisha rasmi mpenzi wake. Familia nzima ilifurahi kusikia Owen nae alitaka kuwatambulisha mwanamke wa ndoto zake. Hakuna kati yao aliyeweka mashaka juu ya Owen kwa kuwa alikuwa kijana makini na anayejitambua kwa marefu na mapana. Walisubiri siku ifike ili wamuone huyo mchumba. Na uzuri ni kwamba hiyo siku haikuwa mbali yani zilikuwa zimebaki siku tatu tu Robyson


amvishe pete ya uchumba mpenzi wake. Kuhusu mchumba wa Robyson tayari alishajulikana na kukubalika kwa wazazi. Hakukuwa na kipingamizi kwani penzi hilo lilitengenezwa kwa shinikizo kubwa la wazazi wa pande zote mbili. Baba mzazi wa mpenzi wa Robyson alikuwa mfanyabiashara mkubwa na maarufu nchini. Alikuwa tajiri aliyekuwa anamiliki makampuni ya bidhaa mbalimbali nchini. Tajiri huyo alifahamika kwa jina la Mr Jay Calvin. Mr Jay Calvin alikuwa na urafiki mkubwa sana


na Mr James ambaye alikuwa kiongozi wa siasa nchini. Kwa masilahi mapana ya pande mbili, Mr James na Mr Jay Calvin walikubaliana kujenga mahusiano ya ukaribu kupitia vijana wao. Mr James alitaka mwanae Robyson aje kuwa kiongozi mkubwa wa siasa ikibidi aongoze nchi kwa siku zijazo hivyo alijua mchakato mzima ulikuwa unahitaji kiasi kikubwa cha pesa hivyo alihitaji msaada kutoka kwa Bilionea Mr Jay Calvin. Lakini pia Mr Jay Calvin aliona masilahi makubwa


yangekuwa upande wake kama angefanikiwa kupata nguvu kutoka serikalini. Biashara zake zingeenda vyema bila vizuizi vyovyote maana tayari angekuwa Baba mkwe wa Mheshimiwa Rais au Waziri wa nchi. *** Miongoni mwa vitu vilivyokuwa vinampa furaha Owen kurejea nchini ni pamoja na kuonana na mwanamke wa ndoto zake. Mwanamke aliyetokea kumpenda kuliko kitu chochote kile kwenye


uso wa dunia. Ni mwanamke pekee aliyekuwa anatembea na moyo wa mtoto wa Mama Owen. Hakuwa mwingine bali ni Diana. Ni takribani miaka miwili ilishapita tangu Owen alipoonana na Diana. Mara ya mwisho kuonana ilikuwa nchini Marekani walipokuwa masomoni na huko ndiko walipokutanaga kwa mara ya kwanza na kuanzisha mahusiano yao. Haikuwa ngumu kwao kujenga mahusiano kwa kuwa wote walikuwa ni raia wa Tanzania na walikuwa wanasomea kozi inayofanana.


Wote kwa pamoja walifanikiwa kuhitimu mwaka mmoja shahada yao ya kwanza (Bachelor's degree). Mara baada ya kuhitimu shahada zao za kwanza, Diana aliamua kurudi Tanzania kuendelea na maisha mengine huku Owen akisafiri kuelekea nchini Uturuki kuendelea na masomo kwa ngazi inayofuata yaani shahada ya uzamili (Master's degree). Katika kipindi chote cha maisha ya chuo nchini Marekani, Owen na Diana waliishi pamoja kama mke na mume. Waliishi pamoja kwa


takribani miaka miwili na nusu na walifanikiwa kujenga nguzo imara katika penzi lao. Kwa hakika walipendana sana na kuweka ahadi kwamba baada ya kufunga kurasa zote za masomo basi wangetambulishana kwa wazazi na kuoana kabisa. Kwa uhalisia wote walikuwa wanatoka kwenye familia za kitajiri hivyo hakuna mtu aliyempenda mwenzake kwa kufuata masilahi ya pesa. Ile siku ambayo Diana alirudi nchini Tanzania na kumuacha Owen akisafiri kuelekea nchini Uturuki


ilikuwa ni siku ya majonzi mazito kwa wapendanao. Ingawa haikuwa rahisi kwao kuishi mbali mbali lakini hawakuwa na namna zaidi ya kukubaliana na hali. Walipeana ahadi na matumaini kwamba wangeoana mara baada ya Owen kuhitimu shahada yake ya uzamili na kurejea nchini. "Owen mpenzi wangu, haijalishi itakuchukua muda gani kurudi Tanzania lakini mimi nitakusubiri babaa.! Kiukweli kabisa nitakusubiri kwa gharama yoyote ile mpenzi wangu. Wewe ndo


mume wangu Owen. Haijawahi kuisha siku kwangu bila kumshukuru Mungu kwa kunipa mwanaume bora kama wewe. Mwanaume handsome, mtanashati, unajitambua, unanijali, unanithamini, unaniheshimu, unanipenda na kubwa zaidi hujawahi kuwa bize kila ninapokuhitaji. Nakupenda sana Owen wangu. Nakuahidi kwamba nitakusubiri babaa. Nitakusubiri uje kunioa ili tuishi pamoja.I" "My dearest Diana, Thanks so


much for your unconditional love. Nakupenda sana Diana wangu. Popote utakapokuwa kumbuka kwamba unatembea na moyo ya mtoto wa Mama Owen. Nakuomba utunze heshima, na unililinde na jina. Nimekukabidhi mtima, alionipa Karma. Siku zote nitafanya maombi kwa Mungu wangu ili akutunze kwa ajili yangu. Palipo na upendo wa dhati, miaka miwili wala sio mingi kuisubiri. Nakuahidi Diana, nikisharudi nchini basi jambo la kwanza kulifanya litakuwa ni kukutambulisha rasmi nyumbani


na kwenda kujitambulisha kwa wazazi wako ili tupewe idhini ya kufunga ndoa. Kiukweli kabisa, Nakupenda sana Diana. Sijajua nitawezaje kuishi huko ugenini ninapokwenda bila uwepo wako. Nilikuzoe sana Diana wangu. Licha ya kuwa wapenzi lakini pia ulikuwa kama rafiki kwangu. Nitawezaje sasa ku-survive peke yangu ndani ya Taifa la watu? Nakumbuka nilipoingia chuoni hapa Marekani kwa mara ya kwanza, wewe ndo ulinipokea Diana. Nawaza sasa, Je huko Uturuki nani ataenda kunipokea?


Nitakuwa mgeni wa nani mimi? Na nitawezaje kuishi bila wewe Diana?" "Owen, hakuna namna baba itabidi ujikaze tu baada ya muda utazoea kuishi bila mimi. Hata mimi kwa upande wangu najua itakuwa ngumu sana kuishi bila wewe lakini naamini nitazoea hiyo hali. Uzuri ni kwamba bado tutaendelea kuwasiliana hiyo itapunguza maumivu kwenye mioyo yetu.!" "Lakini Diana, hivi utaweza kweli


kunisubiri katika kipindi chote utakachokuwa mbali nami?" "Owen, kwani una wasiwasi na mimi? Eti, Huniamini babaa?" "Kukuamini nakuamini sana mpenzi wangu. Lakini wasiwasi ndo akili mama'angu.!"

"Basi ondoa shaka katika hilo babaa. Diana amezaliwa kwa ajili yako na ni mwanamke wako peke yako. Owen my dear, No matter how long it takes, I will wait for you till the day you will ask me,


Will you marry me?" "Thanks alot My Diana. I will wait for you too till the day you will say, Yes! You are the one and only. I will marry you Owen.!" Hivyo ndivyo Owen na Diana walivyotengana nchini Marekani. Kwa hakika wawili hao walipendana sana na hawakuwahi kufikiria kama siku moja wangekuja kuachana. Katika kipindi chote cha miaka miwili walichotenganishwa na umbali, hawakuacha kuwasiliana


mara kwa mara. Waliwasiliana huku wakiendelea kuvuta subira mpaka ikafika ile siku iliyokuwa inasubiriwa. Ni siku ambayo Owen alirejea rasmi nchini. Shauku kubwa ya Owen ilikuwa ni kuonana na Diana wake ambaye hakumtia machoni kwa takribani miaka miwili. Mara baada ya kumaliza ile sherehe ndogo ya mapokezi aliyoandaliwa na familia yake, Owen aliamua kumtafuta Diana kwenye simu na kumtaka waonane. Diana hakuamini kama ni kweli Owen alikuwa katika


ardhi ya Tanzania. Alihisi pengine alikuwa anamfanyia utani tu kama ambavyo walivyozoeshana. Siku iliyofuata walipanga kukutana kwenye hoteli moja kubwa na maarufu pale pale ndani ya jiji. Mpaka anatoka nyumbani kwao, Diana hakuwa na uhakika kama ni kweli alikuwa anaenda kukutana na Owen. Alikuja kuamini mara baada ya kufika hotelini na kumuona Owen mbele ya macho yake. Diana alimkimbilia Owen kisha akamkumbatia kwa mahaba mazito. Hawakutaka


kuketi kwenye viti badala yake waliamua kulipia chumba kabisa ili wapate muda na nafasi nzuri ya kuzungumza mambo yao. Kuanzia majira ya saa nne asubuhi mpaka kufikia saa kumi jioni walishinda pale hotelini. Kwa namna walivyokuwa wame-miss-ana basi walijikuta wanakumbushia enzi kwa kupeana penzi la moto. Kwa namna kila mmoja alivyokuwa na kiu na mwenzake, wote kwa pamoja walijikuta wanafurahia maji ya uzima. Baada ya kumaliza kupeana mahaba ya


kitandani, stori zilifuata. Waliongea mengi sana siku hiyo ila kubwa zaidi lilikuwa hili; "Diana mpenzi wangu, nafikiri leo ndo siku ya mwisho kwetu kuendelea kufanya dhambi ya uzinzi. Huu ni muda sahihi wa kuomba kibali cha kuhalalisha penzi letu kwa yule aliyetuumba. Nilikuahidi kwamba nikirudi nchini nitakuoa na sasa nimerudi hivyo naomba nitimize ahadi yangu kwako. Tayari nimeshaongea na wazazi wangu kuhusu uwepo wako hivyo


wamenitaka nikakutambulishe kwanza kisha nawe unipeleke kwenu. Baada ya hapo zitafuata taratibu za kuvishana pete alafu ndoa ifuate. By the way, Siku ya kesho kutwa kaka yangu atakuwa na jambo lake kubwa na lenye kufurahisha hivyo wanafamilia wote watakuwepo kwenye hilo tukio. Naomba nitumie siku hiyo nikakutambulishe kwa wazazi na ndugu zangu. Na kama itakupendeza zaidi basi nipo tayari kukuvisha pete kabisa siku hiyo. Sihitaji tena kukuchezea


Diana. Nataka nikuoe uwe mke wangu halali.!" "Mmmh! Owen.! Hapana. Hapana Owen ni mapema mno. Ni mapema mno baba mbona una haraka hivyo? Kwanini tusikae chini na kujadili kwanza hili suala kabla hatujalipeleka kwa wazazi?" "Diana, tukae chini na kujadili kitu gani tena? Kwahiyo siku zote tulivyokuwa tunajadili hii mada tulikuwa tumesimama? Kitu gani tena unataka tujadili Diana. Au


Wakati tunapeana ahadi mwenzangu ulikuwa unafurahisha tu maongezi? Diana, em niambie basi kitu gani kipya ambacho mimi na wewe bado hatujakijadili?" "Owen, ujue kuna mambo mengi sana yamejitokeza upande wangu na kwa wazazi hivyo kwa kipindi hiki siwezi kulipeleka jambo hili nyumbani. Kwa sasa naomba tuendelee kuwa wapenzi hivi hivi na pia nataka penzi letu liwe la siri mno. Hata mawasiliano kati yetu itabidi


tupunguze mpaka nitakapoweka sawa mambo yangu. Mambo yakiwa freshi tutaliweka wazi penzi letu kwa wazazi.!" "Kama tatizo ni wazazi wako basi acha mimi nikakutambulishe kwanza nyumbani kwetu alafu tuanze kuangalia namna ya kulifikisha jambo letu kwa wazazi wako. Naomba tufanye hivyo mpenzi wangu. Wazazi wangu tayari wanakusubiri kwani nimeshawaahidi nitakupeleka kukutambulisha kesho kutwa.!"


"Owen, Kwa hilo utanisamehe tu babaa.! Kwa sasa hilo halitawezekana. Tuendelee kuvuta subira au kama kuna ulazima wa kumpeleka mwanamke kwa wazazi wako basi tufanye trick, nitaongea na rafiki yangu Vaileth kisha utampeleka yeye kwa wazazi wako kumtambulisha badala yangu. Baadae tutatengeneza tukio ionekane kwamba umeachana na Vaileth alafu utanivisha pete mimi na kunioa kabisa.!"


"Diana eeh, Hebu kuwa serious basi.! Hivi ni kweli una uhakika bado unanipenda mimi?" "Owen jamani.! Sasa swali gani hilo unaniuliza babaa.!" "Naomba unijibu tafadhali. Hivi ni kweli bado unanipenda Diana?" "Yes, why not.! Nakupenda sana Owen wangu.!" "Je una uhakika kwamba unanipenda peke yangu?"


"Owen, mbona una maswali ya ajabu sana siku hizi. Au marafiki zako wapya wa Uturuki ndo wamekubadilisha hivyo.!" "Diana eeh, Kwa mara ya kwanza kabisa leo ndo nimeanza kukuogopa. Nakuogopa Diana. Kiukweli kabisa naogopa mimi. Nahisi joto la Dar es salaam limekubadilisha ngozi na mpaka tabia. Nahisi kabisa kuna kitu hakipo sawa mpenzi wangu.!" "Hahah! Hayo ni mawazo yako tu Owen. Mimi sijabadilika babaa.


Nipo vile vile na kila kitu kipo sawa kama ilivyokuwa awali.! "Ok, Sawa Diana nimekubali wazo lako mpenzi wangu. Nitavuta subira mpaka mambo yatakapokuwa sawa. Lakini pia nitavumilia hali ya uwepo mdogo wa mawasiliano kati yetu. Najua wewe ni muajiriwa kwa sasa ndo maana unakuaga busy na kazi na hata ukirudi kwenu unakuwa umechoka kutokana na uchovu wa kazi. Diana, kwa hilo ondoa shaka sitokusumbua mamaa.!"


Hayo ndo yalikuwa makubaliano ya mwisho kabisa kati ya Owen na mpenzi wake Diana. **** Ile siku iliyokuwa inasubiriwa hamu na wanafamilia ili kushuhudia tukio la Robyson kumvisha pete mchumba wake, hatimaye iliwadia. Familia ya Mr James ilikuwa ya kwanza kabisa kufika ndani ya ukumbi wakiwa sambamba na ndugu wengine pamoja na marafiki. Waliendelea kuburudika na vinywaji


mbalimbali huku wakimsubiri mwali pamoja na familia yake. Lilikuwa ni tamasha lililoandaliwa kwa gharama kubwa sana ukizingatia familia zote mbili za wahusika wa ile sherehe walikuwa na uwezo mkubwa kifedha. Hazikupita dakika nyingi, familia ya Mr Jay Calvin iliwasili na binti yao kwenye eneo la tukio. Shangwe zilikuwa nyingi sana ndani ya ukumbi. Zoezi la kwanza kabisa kufanyika ndani ya ukumbi lilikuwa ni utambulisho baina ya familia hizo. Bwana harusi


mtarajiwa alianza kuwatambulisha ndugu zake kwa mke wake mtarajiwa na Bi harusi mtarajiwa alifanya vile vile kwa mume wake mtarajiwa. Lakini sasa, wakati zoezi la utambulisho likiendelea, Owen hakuwemo ndani ya ukumbi kwa wakati ule. Kuna mzigo wa baba yake alienda kuupokea bandarini hivyo alichelewa kufika ndani ya ukumbi. Baada ya zoezi la utambulisho kumalizika, sasa kilifuata kipengele cha Bwana harusi mtarajiwa kupeleka ombi lake la ndoa kwa Bi harusi wake


mtarajiwa. Robyson alijiandaa kutoa pete ya uchumba mfuko kisha aombe ridhaa kwa bibie akubali kuivaa mbele ya mashahidi. Lakini sasa, kabla hajafanya chochote, Owen aliingia ndani ya ukumbi. Watu wote waligeuka kumtazama Owen ambaye alionekana kuwa mtanashati na mwenye sifa za kipekee mwilini mwake ambazo wanawake wengi huvutiwa nazo kwa mwanaume. Owen alitupa macho mbele walipokuwa wahusika wakuu wa ile sherehe, Pale pale alijikuta anapata


mshtuko wa moyo. Mwili wote ulitetemeka na mapigo ya moyo yalianza kwenda spidi baada ya kuona sura ya mtu ambaye hakutarajia kama angemuona. "DIANA!" Owen alilitaja jina hilo mara baada ya kumuona yule mwanamke aliyekuwa mbele ya jukwaa kuu pamoja na kaka yake. Ni yule yule mwanamke wa ndoto zake ndo alikuwa mbele ya jukwaa kuu akisubiri kuvishwa pete na Robyson ambaye ni kaka yake. Owen hakuamini macho kwa kile alichokuwa anakiona.


Alipiga hatua kuelekea kule jukwaani kujidhihirishia kama ni kweli yule aliyemuona alikuwa Diana wake au alimfananisha. Wakati anapiga hatua kuelekea jukwaani, Diana nae alijikuta anashtuka mara baada ya kumuona Owen. Mapigo ya moyo yalimuenda mbio kwani hakutarajia kabisa kama Owen angekuwepo kwenye lile tukio. Hakuwahi kujua kama Robyson na Owen walikuwa na undugu. Robyson, wazazi wa pande zote mbili pamoja na marafiki waliohudhuria ile sherehe


walishangaa sana kuona Owen na Diana wanatazamana kana kwamba walikuwa wanafahamiana tangu siku nyingi au walikuwa wanadaiana. Yote kwa yote Robyson hakuwa na Shaka juu ya mpenzi wake wala mdogo wake. Alijua kwamba Owen alikuwa anasogea mbele ya jukwaa kwa ajili ya kutambulishwa maana wakati wenzake wakitambulishwa yeye hakuwepo. Mara baada ya Owen kufika mbele ya jukwaa alimtazama kwa umakini Diana na akagundua kwamba ndo yule


yule Diana wake. Mtaalam alimtazama kaka yake kisha akasema, "Brother, Nilikuahidi lazima niwahi sherehe yako, nadhani nimetimiza ahadi yangu.!" Owen alimwambia Robyson huku akitoa tabasamu la kutengeneza kwenye sura yake. "Ni kweli Bwana mdogo umewahi na naomba nichukue fursa hii kukutambulisha maana wengine tayari nimeshawatambulisha na umebaki wewe tu.!" Robyson


alimjibu Owen kisha akamshika bega Diana na kumwambia, "Dear, Nilikuambia bado sijamaliza kukutambulisha na huyu ndo mtu ambaye alibakia ili kukamilisha timu nzima ya Mr & Mrs James. Huyu unayemuona mbele yako ni mdogo wangu ambaye nilimuacha ziwa la mama yangu. Anaitwa Owen, Ni mtoto wa pili wa Mr James. Kwa miaka ya hivi karibuni hakuwepo hapa nchini na ana siku chache tu tangu aliporejea. Ni vile tu kuna mambo kadhaa yaliingiliana


ila na yeye alipanga kumtambulisha mke wake mtarajiwa siku ya leo.!" Robyson aliongea maneno hayo na kufanya mapigo ya moyo wa Diana kuongeza spidi mara dufu. Baada ya kumaliza kumtambulisha Owen, Robyson alimsogelea Diana kisha akamkamata mkono na kumgeukia Owen. "Owen bwana mdogo, huyu unayemuona mbele yako ni shemeji yako. Anaitwa Diana,


Yeye ndo mwanamke pekee aliyetokea kuuteka moyo wangu kwenye hii dunia. Yeye ndo mwanamke wa kwanza kabisa anayekwenda kubadilisha status ya maisha yangu kutoka kwenye maisha ya ubachela mpaka kwenye maisha ya ndoa. Yeye ndo mke wangu mtarajiwa hivyo naomba tumpokee kwa mikono miwili na tumkaribishe katika familia yetu. Owen mdogo wangu, Ukweli kutoka moyoni nampenda sana shemeji yako Diana.!"


Aisee! Machozi ya kiutu uzima yalianza kutiririka mashavuni mwa mtaalam Owen kuashiria kwamba moyo wake ulishindwa kuhimili kiasi cha maumivu aliyokuwa anapitia kwa wakati ule. NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu} EPISODE: 02 AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller) Ni Robyson na Diana tu ndo


walikuwa wanayaona machozi ya Owen kwa wakati ule kwa kuwa wengine walikuwa wamepewa mgongo. Robyson alishindwa kuelewa sababu kuu iliyokuwa inamfanya mdogo wake adondoshe machozi mbele yao. Hakujua kama machozi ya Owen yalikuwa ya furaha au huzuni. Ni Diana tu ndiye aliyekuwa anafahamu tafsiri halisi ya machozi ya Owen. Owen aliwaza na kuwazua chap chap ndipo akapata wazo la kiume lenye lengo la kutoharibu sherehe ya kaka yake. Alichokifanya ni


kumsogelea kaka yake kisha akamkumbatia na kumwambia, "Kaka Robby, Kiukweli kabisa mimi nina furaha kubwa sana siku ya leo. Furaha yangu imepitiliza ukomo ndo maana najikuta nadondosha machozi kaka. Nilikuwa naumia sana nilipokuwa nakuona huwazi chochote kuhusu ndoa na ndo maana nilikuwa nakusisitiza uoe. Hii siku nilikuwa naisubiria kwa hamu kubwa sana na ndo maana nimekuwa na furaha kiasi hiki. Kwa hakika hii ni hatua kubwa


sana unaenda kuifikia kwenye maisha yako. Hongera sana kwa kuchagua chombo kaka. Sio siri shemeji yangu ameumbwa na kuumbika.!" Owen alizungumza kauli hiyo kisha akafuta machozi na kujitoa kwenye kumbatio. Mtaalam alimgeukia Diana kisha akamwambia, "Diana! Mimi naitwa Owen James. Ni mdogo wake na Robyson James. Karibu sana kwenye familia yetu shemeji yangu.!" Owen alizungumza kauli


hiyo kwenda kwa Diana huku akiwa na tabasamu lenye maumivu mazito moyoni. Kidogo sasa pumzi ilimshuka Diana kwani hakutarajia kama Owen angechukua maamuzi ya kutoharibu sherehe ile. Fikra zake ni kwamba Owen angeharibu kila kitu. Kwa kuwa Owen aliamua kubaki na jambo lile moyoni mwake, Diana nae aliamua kubaki nalo. Alichokifanya ni kumjibu Owen maneno ya shukrani baada ya kumkaribisha kwenye familia yao. Owen alipiga


hatua kurudi nyuma kisha akaenda kuketi kwenye kiti pamoja na watu wengine waliohudhuria ile sherehe. Baada ya zoezi hilo kukamilika, sasa ulifika ule wakati wa Robyson kuomba ridhaa kutoka kwa Diana ili akubali kumvisha pete ya uchumba. Robyson aliingiza mkono mfukoni kisha akatoa kiboksi kidogo chenye pete ya dhahabu. Mwanaume alienda chini na kupiga goti moja mbele ya mrembo Diana kisha akasema,


"DIANA! WILL YOU MARRY ME?" Robyson alimuuliza Diana swali hilo lililobeba ombi la ndoa kwa wawili wapendanao. Robyson pamoja na ndugu na marafiki waliohudhuria ile sherehe walihisi labda swali lile lilikuwa jepesi sana kwa Diana. Vile walivyokuwa wanahisi ilikuwa tofauti kabisa na uhalisia uliopo akilini mwa Diana. Swali la Robyson lilimfanya Diana akumbuke miaka miwili nyuma alipokuwa Marekani pamoja na Owen. Alikumbuka Ile siku ya


mwisho walipokuwa wanaagana na kupeana ahadi za maisha,

"Basi ondoa shaka katika hilo babaa. Diana amezaliwa kwa ajili yako na ni mwanamke wako peke yako. Owen my dear, No matter how long it takes, I will wait for you till the day you will ask me, Will you marry me?" Diana alikumbuka maneno hayo ambayo aliongeaga siku za nyuma akimwambia Owen. Kauli yake ilimaanisha mwamba haijalishi itachukua muda gani lakini atamsubiri Owen mpaka


siku atakayomuuliza, Je upo tayari kuolewa na mimi? Mtoto wa kike alijikuta anadondosha machozi kwa kushindwa kutimiza ahadi yake kwa Owen. Swali lile lile ambalo alikuwa analisubiri kutoka kwa Owen hatimaye aliulizwa na Robyson kutokana na kushindwa kuvuta subira kumsubiri Owen. Diana aliangaza macho yake kule walipokaa watu na alifanikiwa kuona sura ya Owen. Owen alikuwa anamtazama Diana huku akiwa na tabasamu lililobeba


maumivu ndani ya moyo wake. Diana alijua maumivu aliyokuwa anapitia Owen kwa wakati ule. Mtoto wa kike alijikuta anazidi kudondosha machozi ambayo watu waliyatafsiri kama machozi ya furaha. Diana alishindwa kuendelea kumtazama Owen, aligeuza macho upande wa pili akakutana na sura za wazazi wake. Wazazi walitoa ishara ya kumtaka binti yao akubali ombi la kuolewa na Robyson. Lakini pia hata marafiki waliohudhuria ile sherehe walimsisitiza Diana akubali ombi la kuolewa na


Robyson. Diana alimgeukia Robyson kwa mara nyingine kisha akasema, "Yes! You are the one and only. I will marry you Robyson.!" Diana alizungumza maneno hayo kujibu ombi la Robyson akiwa na maana ya kwamba yupo tayari kuolewa na Robyson kwa kuwa yeye ndo mtu pekee anaempenda. Jibu la Diana lilimshtua sana Owen ingawa alitarajia kulisikia. Mtaalam alijikuta anakumbuka


kauli aliyowahi kumwambia Diana siku ya mwisho walipotengana kule Marekani, "Thanks alot My Diana. I will wait for you too till the day you will say, Yes! You are the one and only. I will marry you Owen.!" Hiyo ilikuwa ni kauli aliyozungumza Owen kumwambia Diana walipokuwaga nchini Marekani. Kauli hiyo ilikuwa na tafsiri ya kwamba 'Shukrani sana Diana wangu. Nitakusubiri pia mpaka siku utakayosema, Ndio! Wewe ni


mmoja na wapekee kwangu. Nipo tayari kuolewa na wewe Owen.' Owen alijikuta anaumia sana baada ya kukumbuka kauli hiyo. Yani jibu ambalo alikuwa analisubiria kutoka kwa Diana hatimaye alipatiwa mtu mwingine ambaye ni kaka yake wa tumbo moja. Yani Diana alijibu vile vile na utofauti ulikuwa kwenye jina tu, badala ya kutaja jina la Owen akataja Robyson. Shangwe na vifijo vilisikika ndani ya ukumbi. Watu walifurahi


kusikia Diana amekubali ombi la kuolewa na Robyson. Owen hakuona sababu ya kuonesha hisia zake kwa watu hivyo alitengeneza tabasamu kwenye uso wake kisha akaungana na watu kupiga makofi na kufurahia jibu la Diana. Baada ya Diana kukubali ombi la kuolewa na Robyson, Robyson aliinua pete kisha akamvisha Diana katika kidole cha uchumba. Owen alishuhudia mbele ya macho yake mwanamke wa ndoto zake akivishwa pete ya uchumba na mwanaume mwingine. Zile ahadi


zote walizokuwa wameziweka kwa miaka yote hatimaye zilizikwa mazima muda ule. Mtaalamu alitamani lile tukio lingekuwa ndoto lakini hakiwa kama alivyokuwa anatamani. Owen alijikuta anadondosha machozi kwa mara nyingine licha ya kujaribu kujikaza na kuzuia. Kilichokuwa kinamuumiza zaidi ni kumbukumbu za matukio aliyokuwa ameyafanya na mwanadada huyo. Shangwe ziliendelea kuwa nyingi, burudani ya mziki wenye nyimbo za kitajiri ikafuata. Watu walikunywa


vinywaji mbalimbali ukumbini. Walevi walikunywa pombe na wasiokuwa walevi walikunywa vinywaji visivyokuwa na vilevi. Wakati watu wanaendelea kunywa, Owen alishindwa kuhimili maumivu hivyo akatoka ndani ya ukumbi na kwenda kwenye gari lake. Alipofika ndani ya gari alitoa kitambaa chake mfukoni kisha akaanza kulia kama mtoto. Mtaalamu alimwaga machozi kama mtoto aliyeachwa na mama safarini. Alilia sana mpaka alipotosheka akaamua kunyamaza. Alitaka


kurudi ukumbini lakini macho yake tayari yalishakuwa mekundu. Alihisi kama angerudi tena ukumbini basi watu wangepata mashaka juu yake. Alichokifanya ni kuondoka kabisa eneo lile bila kumuaga mtu yoyote yule. Aliwasha gari na kutokomea mahala asipopajua. Pale ukumbini sherehe iliendelea kama kawaida kuanzia majira ya saa kumi na mbili jioni na ilipofika saa nne usiku waliamua kuhitimisha. Kila mmoja alienda mahala alipokuwa amepaki usafiri wake na kurudi nyumbani


kwake. Mr James alikamata usukani wa gari lililobeba familia yake isipokuwa Robyson na Owen tu. Robyson aliondoka na usafiri wake binafsi. Lakini pia Mr Jay Calvin alipanda gari moja na familia yake yote akiwemo binti yake Diana. Hakutaka kumwacha binti yake mikononi mwa Robyson ile siku kwa kuwa bado ndoa ilikuwa haijapita. Siku hiyo walikuwa wamelewa sana kama unavyojua familia za kitajiri zinapokuwa kwenye sherehe zao. Kwa bahati nzuri familia zote zilifanikiwa kufika salama


majumbani mwao. Tukio la mwanamke kuvishwa pete ya uchumba mara nyingi humpa furaha mtoto wa kike lakini kwa Diana ilikuwa ni tofauti kabisa. Diana alijikuta anapata huzuni baada ya kuvishwa pete na Robyson. Kilichomuhuzunisha zaidi ni baada ya kukumbuka dhambi aliyomtendea Owen. Akiwa kitandani amejilaza alianza kuikumbuka vyema sura ya Owen ilivyokuwa inamtazama kipindi alichokuwa anavishwa pete. Hakujua ni kwanini alimtenda vile mtoto wa watu


ilihali hakuna baya lolote alilowahi kumfanyia. Kila alilolikumbuka kutoka kwa Owen lilikuwa ni zuri kwake. "Kiukweli kabisa hakustahili adhabu niliyompa lakini kwa masilahi mapana ya familia ilibidi tu yeye awe mbuzi wa kafara. Sikuwa na namna nyingine ya kuilinda ahadi yangu kwake. Lakini kwanini hawa watu wawe ndugu? Ni bora hata wasingekuwa ndugu maana naweza kuharibu ndoa yangu kwa Robyson. Lazima nifanye


kitu ili kila kitu kiwe sawa.!" Diana alijisemea peke yake kauli hiyo alipokuwa chumbani kwake. Muda ule ule alivuta simu kisha akaanza kuitafuta namba ya Owen ili ampigie. Upande wa pili alionekana Owen akiwa ndani ya gari ameegemea usukani. Yalikuwa majira ya saa sita usiku na alikuwa amepaki gari lake katikati ya kiwanja cha mpira huku akiwa amelewa tilalila. Owen hakuwahi kabisa kunywa pombe katika maisha


yake wala hakuwahi kudhania kama kuna siku angeweka chupa ya pombe mdomoni mwake lakini kwa mara ya kwanza alijikuta anakunywa na kulewa. Ni stress za mapenzi ndizo zilimfanya atumie pombe akiamini zingeweza kumpunguzia mawazo. Ndani ya gari kulikuwa na chupa za kutosha zenye bia na nyingine tayari alishazinywa. Owen alikuwa amelewa chakari hata njia ya kurudi nyumbani kwao alikuwa haijui. Wakati ameegemea usukani wa gari,


Ghafla alisikia simu ikiita. 'MY LIFE PARTNER' ndo jina ambalo lilisomeka kwenye kioo cha simu ya Owen. Owen alitambua kwamba Diana ndo alikuwa mpigaji wa ile simu. Alitaka kuipotezea lakini akaona ni bora amsikilize kwa kuwa hakuwa adui yake na hata huyo adui anakuwa na haki ya kusikilizwa. "Owen, naomba unisamehe kwa kushindwa kutimiza ahadi yangu kwako. Naomba unisamehe sana


kwa hilo.!" Hiyo ilikuwa kauli ya kwanza kabisa ya Diana mara baada Owen kupokea simu yake. "Ok, umesamehewa shemeji Diana. Na je ukiachana na hilo kuna lingine unalotaka kuniambia muda huu?" "Mbona kama umelewa pombe Owen? Tangu lini umeanza kunywa pombe? Kwanza upo wapi muda huu?" "Diana, kujua kuhusu maisha yangu kwa sasa sio biashara


yako. Kama huna kingine cha kuongea niambie nikate simu.!" "Owen, kuna kitu nataka kukuambia ila kwa sasa nahisi umelewa hautaweza kunielewa. Naomba kesho tukutane kwenye ile hoteli tuliyokutana juzi ili tuzungumze vizuri.!" "Tuzungumze vizuri? Tuzungumze kitu gani Diana? Kipi sijakisia kutoka kwako? Tayari nimeshasikia kila kitu na kujionea kwa macho yangu kwahiyo huna haja ya kujieleza


tena. Hata ukijieleza hiyo haitabadilisha kitu chochote. Maumivu niliyoyapata hayawezi kufutika. Lakini pia sihitaji kaka yangu apitie maumivu kama haya ninayoyapitia mimi kwa sababu yangu. Hakuna haja ya kuniambia kitu chochote kwa sababu sihitaji kubadilisha uhalisia uliopo sasa hivi. Nimekubali kwamba wewe ni shemeji yangu Diana. Baki na kaka yangu na umpende kama ulivyokuwa unanipenda mimi hapo awali.!"


"Ni sawa Owen lakini mimi sina lengo la kubadilisha msimamo wangu juu ya ndoa yangu na Robyson. Nina ombi moja tu kwako. Nafikiri hili ndo litakuwa ombi langu la mwisho kwako Owen.!" "Sawa omba nakusikiliza shemeji.!" "Owen, naomba ufiche na utunze siri ya mahusiano yetu ya awali. Fanya kama hatujawahi kuonana wala kukutana mahala popote pale kwenye uso wa hii dunia.


Naomba kaka yako na wazazi wako wasijue chochote kuhusu hili. Nahitaji kuishi kwenye maisha ya ndoa na Robyson. Nahitaji kufurahia ndoa yangu. Sihitaji kabisa kumpoteza Robyson kwa masilahi mapana ya maisha yangu ya baadae. Owen, Subira ni kitu ambacho sio kila mwanadamu ameumbiwa. Subira ni zawadi ya pekee ambayo Mola wetu amewatunuku wanadamu wachache sana. Ukweli ni kwamba mimi nilikupenda sana Owen, lakini kwa bahati mbaya


Mungu hakuniumba na subra. Nilikosa subira kwako hivyo nikajikuta nashindwa kukwepa mtego wa wazazi juu ya Robyson. Ndoa yangu na Robyson imetokana na shinikizo la wazazi wetu. Mwanzo nilikuwa mgumu kukubali lakini umbali uliopo kati yetu ulisababisha niwe karibu na Robyson na nikajikuta nazama mazima kwenye penzi lake. Ukweli ni kwamba, kwa sasa nampenda sana Robyson. Naomba uitunze siri ya mahusiano yetu ya awali ili nisipoteze nafasi ya kuolewa na


kaka yako.!" "Diana! Maneno yako yanaumiza sana moyo wangu. Kiukweli kabisa naumia kuliko kawaida. Naumia kuliko hata unavyofikiria Diana. Ila ni sawa hakuna namna inabidi niishi nayo tu na kuyazoea. Lakini Diana, naomba nikuulize kitu. Hivi una uhakika unampenda kwa dhati kaka yangu?" "Yeah! Nina uhakika Owen, Nampenda sana Robby.!"


"Sawa.! Lakini kama unampenda Robyson kwanini ulikuwa unaendelea kuwasiliana na mimi kama mpenzi wako? Kwanini ulinivulia nguo na kunipa penzi siku mbili kabla ya kuvishwa pete na kaka yangu? Yapo wapi mapenzi ya dhati uliyonayo kwa kaka yangu? Natamani kukuita malaya lakini nashindwa kwa sababu nitakuwa namvunjia heshima kaka yangu. Anyway, naomba nikuulize swali moja la mwisho nahitaji jibu lililonyooka.!"


"Swali gani hilo Owen.!" "Mimi na Robyson nani unampenda?" "Swali lako ni gumu sana Owen lakini mwisho wa siku jibu ni Robyson tu. Of course ni Robyson kwa sababu the second choice is the best choice. If I would real love the first one, I wouldn't fall for the second one.!" "Anha! I see.! I see it Diana. Ni kweli kabisa upo sahihi kwa sababu kama ungekuwa


unanipenda mimi basi usingetoa nafasi ya upendo kwa mtu mwingine. Ni wazi kabisa kuna mahala nilikuwa navujisha pakacha. Kuna sehemu nilikuwa nafeli kwako. Of course nimelipenda jibu lako Diana. Sio mbaya kwa sababu uliyemchagua pia ni kaka yangu. Kwa sasa sina budi kuheshimu maamuzi yako mrembo. Daima nitaitunza siri ya mahusiano yetu ya awali kama ulivyoniomba nifanye. Nitahakikisha hakuna atakaefahamu siri hii ili kulinda furaha yako. Ni rasmi sasa


naenda kufuta picha zako zote na kumbukumbu za matukio yote tuliyoyafanya. Lakini pia nitakuheshimu kama shemeji yangu kuanzia muda huu. Nilipokuwa nchini Uturuki nilinunua pete ya uchumba na ndoa kwa ajili yako ila nayo nitaipoteza ili nianze upya kabisa. Kwa moyo mkunjufu kabisa nakutakia kila la kheri katika ndoa yako. Namuomba Mola akupe subra ili usije kuyafanya kwa kaka yangu yale uliyonifanyia mimi. Inauma sana Diana, tafadhali usije ukamfanyia


mtu mwingine hiki ulichonifanyia mimi. Kwa sasa sina ninachokudai Diana, nimekusamehe hivyo kuwa huru na maisha yako. Maadam hakuna mkamilifu kwenye hii dunia, basi naomba unisamehe kwa mabaya yote niliyowahi kukufanyia hapo awali. Nakupenda sana Diana, Nakupenda kama shemeji yangu. Karibu sana nyumbani kwetu, karibu kwenye familia yetu. Ni mimi Ex-boyfriend wako, Owen James.!"


NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu} EPISODE: 03 AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller) Mawasiliano ya simu kati ya Owen na Diana yalifikia tamati. Licha ya kuzungumza kauli ya kijasiri lakini mwanaume alianza kuugulia maumivu kwa mara nyingine. Alivuta chupa nyingine ya bia na kuanza kuinywa kwa mkupuo ili alewe kiasi cha kushindwa kukumbuka jina la


Diana. Mwanaume alikunywa pombe nyingi sana ule usiku na hakuwa na wazo la kurudi nyumbani kwao. Simu yake ilianza kupigwa na wazazi wake pamoja na kaka yake lakini hakupokea. Hakutaka kabisa wajue kama alikuwa amelewa. Mpaka kufikia majira ya saa saba usiku bado Owen alikuwa haonekani nyumbani kwao. Familia ilipata hofu na mashaka juu ya kijana wao. Na kwa kipindi hiko watoto wa Mr James wote walikuwa wanaishi nyumbani kwa wazazi wao. Sio Robyson


wala Owen ambaye alihama kwa wazazi. Ilikuwa ni kawaida sana kwa familia za kitajiri kuishi nyumba moja. Hata ikifikia kipindi mtoto akaoa basi yule mke atahamia pale pale kwa wakwe zake. Uzuri ni kwamba nyumba inakuwa kubwa na yenye nafasi ya kutosha kwa kuishi watu zaidi ya ishirini. Nyumba ya Mr James ilikuwa kubwa sana na ilikuwa ya ghorofa moja. Lakini pia kila mwanafamilia alikuwa na gari lake isipokuwa Catherine na Sharon ambao bado walikuwa wanasoma. Lakini sasa, kwenye


kile kiwanja cha mpira ambacho Owen alipaki gari lake, kumbe usiku kilikuwa kinatumika kama sehemu ya biashara. Kuna wadada walikuwa wanauza miili yao katika eneo lile kila yafikapo majira ya saa saa sita au saba usiku. Kulikuwa na takribani wanawake kumi na tano katika eneo hilo ambao walivaa nguo fupi zenye kukiuka maadili katika jamii. Zilikuwa ni nguo maalumu kwa ajili ya shughuli ya ukahaba. Magari tofauti tofauti yaliyokuwa na wanaume yalionekana kufika eneo lile na kuondoka na baadhi


ya wanawake walioonekana kuwa na mvuto zaidi. Akiwa hana hili wala lile huku akiwa na mipombe kichwani, Owen alisikia kwa mbali sauti za wadada zikisema; "Kaka, nichukue mimi. Em angalia mali hii, Mtoto nipo fiti fotati, English figure, mtoto ki-potable yani mali safi kabisa haina kipengele. Ukitaka show time au one night stand huduma zote utazipata.!" "Bae wangu em achana nae


huyo. Chukua hili zigo la kuvunja chaga. Wanasema uzuri wa nyumba choo. Hebu chukua mzigo huu ni double line na network inapanda vizuri kabisa kwenye laini zote mbili. Maamuzi ni yako kutumia laini one au two kwa gharama ile ile.!" Hizo zilikuwa sauti za wadada waliokuwa wanatangaza biashara zao za miili kuwavutia wateja wao waliofika kwenye lile eneo kwa ajili ya kuwanunua. Owen aliposikia sauti hizo hakuelewa vizuri zilikuwa


zinamaanisha nini. Akili ya pombe ilimtuma asogee kule walipokuwa wale wadada na ikibidi awaulize mahali ilipo Guest house ya karibu ili akapumzike. Aliwasha gari kisha akasogea mpaka pale walipokuwa wale madada poa. Alipofika tu, Gari lake lilizungukwa na wale wanawake. Kila mmoja alianza kunadi biashara yake kwa Owen. Licha ya kwamba alikuwa amelewa lakini alijua kwamba pale alikuwa kwenye danguro au chimbo la makahaba wa mjini. Kwa kuwa


hakujua mtaa aliokuwa kwa wakati huo na alihitaji hifadhi ya kwenda kupumzika, Owen aliona ni bora aondoke na kahaba mmoja ili amtumie kama njia ya kufika kwenye nyumba ya wageni yani Guest house. Zile kaka nichague mimi zilikuwa nyingi sana maskioni mwa Owen. Alishusha kioo cha gari na kuangaza macho kumtafuta kahaba mwenye chembe chembe za utulivu na uaminifu kidogo. Wakati anaangaza angaza macho alifanikiwa kumuona mtoto wa kike aliyeonekana


kuwa na umri mdogo kuliko wote kwenye lile danguro. Binti huyo alikuwa amejitenga pembeni akiwa na mavazi yake ya kikahaba vile vile. Owen alimtazama sana yule Binti na alionekana kutokuwa na furaha kama walivyokuwa wenzake. "Namtaka yule mdada aliesimama kwenye ule mti.!" Owen aliongea kauli hiyo akitaka aitiwe yule Binti aliyeonekana kuwa tofauti na wenzake. "Aah! Jamani handsome boy,


sasa unachukuaje dogo dogo hata hana nyama za kutosha? Hebu chukua zigo hili ni steki tupu. Kwanza ushawahi kula vya mijimama ukaonja ladha yake? Hebu jaribu leo ili ujue kwanini wanasema ng'ombe hazeeki maini.!" Hiyo ilikuwa kauli ya mmoja kati ya wale makahaba. Kahaba huyo alionekana kuwa na umri mkubwa sana kiasi kwamba alikuwa na uwezo wa kuwa na mtoto mwenye makamo ya Owen. "Nimesema namtaka yule malaya


mdogo dogo ndo saizi nazopendaga.!" Owen alirudia kuongea kauli yake kwa msisitizo zaidi. Yule Binti aliyechaguliwa na Owen aliitwa kisha akasogea karibu na kioo cha gari la Owen. Owen alifungua mlango wa mbele kushoto na kumtaka binti aingie ndani. "Kaka, naingiaje ndani ya gari bila kufikia makubaliano?" "Kwani wewe unataka


makubaliano au unataka pesa?" "Nataka pesa lakini pesa huja baada ya makubaliano.!" "Ok, kwani shi ngapi?" "Elfu kumi kwa show time na Elfu thelathini ni one night stand. Chumba ni juu yako ila isiwe nyumbani kwako. Ni gesti, hotelini au lodge.!" "Ok, Pesa sio tatizo kwangu hata elfu hamsini utapata. Panda kwenye gari tuondoke.!"


Yule Binti alipanda kwenye gari kisha Owen akaliwasha na kuondoka. Hawakufika mbali Owen alimwambia yule Binti ampe mwongozo wa mahali palipokuwa na Guest au lodge ya karibu kwa sababu kwa namna alivyokuwa amelewa asingeweza kumudu kuendesha gari. Baada ya kuzungumza vile Binti alimtaka Owen akunje kona kisha aingie kwenye barabara fulani ya vumbi. Owen alifanya vile na haikuchukua hata dakika mbili walifika kwenye lodge moja


maarufu ndani jiji. Owen alikuwa hajiwezi hivyo alimkabidhi Binti jukumu la kuulizia chumba kwa mhudumu wa ile lodge. Binti aliteremka kwenye gari kisha akaenda mapokezi kuulizia huduma ya chumba. Bahati ilikuwa upande wao kwa sababu kilibaki chumba kimoja tu hivyo alitajiwa bei kisha akaenda kumwambia Owen. Pesa haikuwa tatizo kwa Owen, alichomoa wallet yake na kumkabidhi yule Binti atoe kiasi kinachohitajika kisha akalipie. Kwanza kabisa mtoto wa kike


alishangaa kuona ameaminiwa kirahisi na mtu ambaye afahamiani nae kabisa. Ile wallet ilikuwa na pesa nyingi sana na Owen alilewa kiasi kwamba hata kuhesabu pesa kwake ulikuwa mtihani. Kadri dakika zilivyozidi kwenda ndivyo pombe ilivyozidi kumchanganya kichwani. Kwa tabia za makahaba na wadada wa mijini wenye njaa ya pesa, ilikuwa vigumu sana kwa Owen kukwepa kuibiwa ile siku. Lakini sasa, ajabu ni kwamba yule Binti alijikuta anamuhurumia Owen kwa hali aliyokuwa nayo.


Alichokifanya ni kutoa kwenye wallet pesa iliyokuwa inahitajika kulipia gharama ya chumba kisha akaenda kumpa mhudumu wa lodge. Baada ya kufanya vile alirudi kwenye gari kisha akamchukua Owen, akatoa funguo ya gari, akafunga milango na kuanza kumkokota Owen kuelekea kwenye chumba walicholipia. Walipofika, Owen alijitupa kitandani kama mzigo. Akili za pombe zilianza kumfanya aanze kuongea kwa uchungu yale yaliyo moyoni mwake. Owen alijikuta anamfungukia yule Binti


mkasa wa mapenzi uliomfanya awe kwenye ile hali. Mtaalam alishindwa kuzuia machozi yake kwa yule Binti. Mtoto wa kike alijikuta anamuhurumia Owen mpaka machozi yakaanza kumtiririka. Alishajua kwamba jamaa alikuwa anapitia kipindi kigumu sana kwa ajili ya mapenzi. Alishagundua pia hata pombe haikuwa starehe ya Owen ila alikunywa kwa kuamini angepunguza mawazo. Alichokifanya yule Binti ni kumsogelea Owen kisha akaanza kumfariji kwa kumpiga taratibu


begani. Owen alikuwa analia kutokana na maumivu ya mapenzi kujumlisha pombe. "Kaka yangu, kwanza kabisa pole sana kwa kusalitiwa mwanamke wa ndoto zako. Najua ulimpenda sana Diana wako ndo maana umepata pigo zito sana baada ya kumpoteza. Lakini naomba usitumie muda wako kujilaumu kwa kumpoteza huyo mwanamke kwa sababu sio kila unachokipoteza ni hasara. Lakini pia hata hayo maumivu uliyonayo sasa hivi hayataishi moyoni


mwako milele. Tuliza akili, na omba sana kwa Mungu atakuletea mwanamke sahihi kwako.!" "Lakini dadaa, Najua wewe ni mwanamke kama Diana. Hivi unaweza kuniibia siri moja tu kwenye jinsia yenu? Siri moja tu dada! Yani moja tuu.!" "Siri gani hiyo?" "Hivi unaweza kuniambia nyie wanawake huwa munataka kitu gani hasa kutoka kwa


mwanaume munaempenda?" "Dah! Kiukweli kabisa kwa upande wangu sijui jibu sahihi la swali lako. Sijui jibu kwa sababu katika maisha yangu sijawahi kupenda wala kupendwa na mwanaume yeyote yule licha ya kwamba kila siku nalala na wanaume tofauti tofauti.!" "Hebu tuanzie hapo kwenye kulala na wanaume tofauti tofauti. Hivi ni kitu gani hasa kinachokufanya uwe mwanamke wa kila mwanaume? Kwanini


umechagua kuwa kahaba mdogo wangu? Kwa umri wako ulitakiwa uwe hata shule sasa hivi unajiandalia maisha yako ya kesho badala ya kukaa barabarani kujiuza. Mungu amekubariki kwa kukupa sura na shepu nzuri sana hivyo kama ungeamua kujitunza basi ungepata mtu wa kukuoa. Kwanini umeingiwa na tamaa dada yangu? Kwanini umeamua kujikatia tamaa ilihali bado una umri mdogo kabisa. Ni bora hata ungejishughulisha na biashara ya kuuza mboga mboga mtaani


kuliko kuuza mwili wako. Hivi unahisi hii njia uliyoichagua ni sahihi mdogo wangu?" Owen alizungumza maneno hayo kwa hasira kumwambia yule Binti. Baada ya Owen kumaliza kuongea maneno makali kwa Binti, Cha ajabu yule Binti alianza kulia. Owen alishangaa kuona Binti analia kufuatia maneno yake. Alimsogelea yule Binti kisha akamuuliza ni kipi hasa kilichokuwa kinamliza. Binti alijifuta machozi kwa kitambaa chake kisha akamgeukia Owen.


"Kakaa, Kwenye hii dunia hakuna mtu ambaye alikuwa na ndoto ya kufanya kazi haramu. Kila mtu anapokuwa utotoni anakuwa na ndoto ya kufanya mambo chanya ndani ya jamii. Ni ndoto ya kila mtoto kuja kuishi maisha mazuri pindi afikapo ukubwani. Tulipokuwa watoto tulikuwa na ndoto za kuja kuwa marubani, walimu, mainjinia na madaktari. Lakini kwenye hii dunia ni watu wachache sana wanaopataga bahati ya kuishi katika ndoto zao. Ndoto za watoto wengi


zinapotea na kuyeyuka kwa dakika moja tu. Kaka eeh, hata wewe ulikuwa na ndoto ya kuja kuishi na Diana lakini dakika moja tu imetosha kuyeyuka ndoto yako. Ipo hivyo kaka, hata mimi nilikuwa na ndoto ya kusoma kama nyie. Nilikuwa na ndoto ya kuja kufanya kazi halali na nzuri kama nyie. Nilikuwa na ndoto ya kuwa na maisha mazuri kama nyie. Na nilikuwa na ndoto ya kuja kuwatunza wazazi wangu kama nyie. Lakini sasa, zile ndoto zote ziliyeyuka kama mshumaa unaowaka moto. Ile


siku niliyompoteza mama yangu ndo siku ambayo ilibadilisha taswira nzima ya maisha yangu. Kiukweli kabisa, hii kazi ninayoifanya sasa hivi sio chaguo langu wala sipendi kuifanya. Ni changamoto tu za maisha ndo zimenifanya nitafute ugali kwa hii njia isiyompendeza Mungu.!" Yule Binti aliongea maneno hayo huku akizidisha kilio. Kwa namna alivyokuwa anaongea, Owen alijikuta anamuhurumia. Alimshika bega


na kumtaka nae anyamaze kulia. "Mdogo wangu, inaonesha kuna mambo mengi magumu yapo upande wako. Tafadhali sana naomba unisimulie historia kwa ufupi kuhusu maisha yako. Yani japo nimelewa lakini maneno na machozi yako yameugusa sana moyo wangu. Naomba unihadithie yaliyokusibu kwenye maisha yako mpaka ukajikuta unaangukia kwenye kazi usiyoifurahia.!" "Kaka eeh, Wewe ndo


mwanaume wa kwanza kabisa kunihurumia na kuguswa na maisha haya ninayoyaishi. Nimekutana na wanaume wengi sana lakini hakuna hata mmoja aliewahi kuguswa na maisha yangu. Kila mmoja alinitumia kwa starehe zake bila kutaka kujua kwanini nimechagua kuwa kahaba. Hakuna aliewahi kugundua kwamba kwa makamo yangu nilitakiwa kuwa shule na sio kuwa kwenye danguro la wanawake wanaojiuza. Kaka, Ahsante sana kwa kutaka kujua kuhusu maisha yangu. Kuna


mambo mengi mazito yapo nyuma yangu pengine nisingekuwa na roho ya kijasiri basi mpaka kufikia leo hii ningekuwa nimeshakufa iwe kwa kuuawa au kujiua mwenyewe. Kaka eeh, Mimi naitwa Laurine Laurence, Ni mtoto pekee wa baba na mama yangu. Historia ya maisha yangu ilianzia katika.....!" NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu} EPISODE: 04


AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller) Mtoto wa kike alianza kumsimulia Owen stori kuhusu maisha yake. Hadithi ya maisha ya Binti ilIanzia jijini Mwanza ambako ndiko alipozaliwa. Anaitwa Laurine Laurence. Ni mtoto pekee wa Bwana Laurence na mkewe aliyefahamika kwa jina la Zuwena. Ndoa ya Bwana Laurence na Zuwena ilikithiri upendo na furaha licha ya kwamba walikuwa na kipato cha kawaida. Walifanikiwa kupata


mtoto mmoja tu wa kike ambaye walimuita kwa jina la Laurine. Uzuri na urembo wa Laurine uliweza kuonekana tangu alipokuwa mdogo. Yani kuna wadada wazuri alafu kuna Laurine Laurence. Bwana Laurence na mkewe walihakikisha mtoto wao anapata malezi bora na kumpeleka shule kwa ajili ya kutengeneza maisha ya kesho. Laurine alikuwa mtoto mwenye nidhamu na bidii kubwa hivyo taaluma yake ilikuwa nzuri sana. Alikuwa ni miongoni mwa


wanafunzi waliokuwa wanafaulu vizuri katika masomo ya darasani. Alipofikisha miaka kumi na nne alifanikiwa kuhitimu shule ya msingi na alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliofaulu mitihani yao. Wazazi wake walifurahi na kuanza kumpigania mtoto wao ili aweze kufikia ndoto zake za maisha kupitia masomo. Laurine alikuwa na ndoto ya kuja kuwa Daktari na hata alipofika sekondari alichagua kusoma masomo ya sayansi ili kukamilisha ndoto zake. Laurine aliendeleza juhudi


zake katika masomo na aliendelea kuwa bora kwenye nidhamu na taaluma. Hiyo ilifanya hata baadhi ya walimu kumpenda sana mtoto huyo. Misukosuko na vikwazo kwa Laurine ilianza punde tu Laurine alipofika kidato cha tatu. Jinamizi baya liliibuka ndani ya familia yao na kuanza kupandikiza miiba kwenye njia ya Laurine kuelekea dunia ya ndoto. Misukosuko hiyo ilianza mara baada ya Bwana Laurence kuwa na Mwanamke nje ya ndoa yani mchepuko. Mchepuko huo


ulimfanya Bwana Laurence asahau kila kitu kuhusu familia yake. Yale majukumu yake kama baba katika familia alishindwa kuyatimiza. Zile pesa za ada na matumizi ya Laurine shuleni, mchepuko alikuwa ananywea bia. Ilifikia hatua hata mahitaji ya nyumbani Bwana Laurence alishindwa kuyatimiza. Familia ilianza kupitia wakati mgumu huku mchepuko akininepeana pesa za Bwana Laurence. Ile furaha iliyodumu kwa miaka mingi ndani ya familia hatimaye ilitoweka mazima. Bwana


Laurence hakuwa na mapenzi tena na mke wake baada ya kubebewa ujauzito na mchepuko. Mwaka ulivyopinduka tu Bwana Laurence na mchepuko wake walifanikiwa kupata mtoto wa kiume. Hapo sasa Bwana Laurence aliamua kuhamia mazima kwa mchepuko wake na kumtelekeza mke wake wa ndoa pamoja na mtoto ambaye ni Laurine. Laurine na mama yake walianza kupitia wakati mgumu kwani Baba yake ndo alikuwaga muhimili mkubwa katika familia. Kula yao ilikuwa ya tabu na hata


maudhurio yake shuleni yakaanza kupungua. Mama yake Laurine hakuacha kumpa moyo Binti yake huku akiendelea kumpambania ili aweze kuhitimu elimu ya sekondari na ikibidi asonge mbele zaidi. Mama alimpanbania mwanae na kwa uwezo wa Mungu Laurine alifanikiwa kuhitimu kidato cha nne licha ya kukumbana na changamoto nyingi za maisha. Kipindi ambacho Laurine alikuwa anasubiri matokeo ya mitihani ndo kipindi ambacho alikutana na pigo kubwa kabisa katika


maisha yake. Laurine aliweza kumpoteza mama yake kipenzi kabla hajashuhudia matokeo yake ya mtihani wa kidato cha nne. Katika kipindi hiko, Laurine alikuwa ni Binti wa miaka kumi na saba tu. Kifo cha mama yake Laurine kilikuwa cha ghafla sana kwani hakuwahi kuumwa wala ugua. Siku moja kabla ya kifo chake, Bwana Laurence na mchepuko wake walienda kwa mganga wa kienyeji na mara baada ya kufika walieleza shida yao. Shida yao ilikuwa ni kufunga ndoa lakini kuna mtu alionekana


kuwa kikwazo kwa wao kuweza kuoana. Mtu huyo alikuwa ni Mama yake Laurine yake mke wake Bwana Laurence. Mama Laurine alikuwa kikwazo kwa sababu tayari alikuwa na ndoa ya kanisa na Bwana Laurence hivyo kwa mujibu wa sheria ya dini ya Kikristo, Bwana Laurence alikuwa haruhusuwi kuoa mwanamke mwingine mpaka mkewe wa awali afariki. Bwana Laurence na mchepuko wake walimlipa mganga pesa na kumtaka akatishe uhai wa Mama Laurine ili wao waweze kupata


kibali cha kufunga ndoa. Licha ya kwamba ripoti ya Daktari ilionesha Mama yake Laurine alifariki kwa mshtuko wa moyo lakini ukweli ni kwamba nguvu za giza ndo zilitumika kuzima pumzi yake. Bwana Laurence na mchepuko walihusika kumuua Zuwena ili waweze kufunga ndoa. Kifo cha Mama yake Laurine kilizika kabisa matumaini na ndoto zote za mwanae Laurine katika masomo. Licha ya kwamba alifaulu mtihani wake wa kidato cha nne na kupata nafasi ya kuendelea na kidato


cha tano lakini Bwana Laurence hakuwa tayari kumsomesha mwanae. Bwana Laurence hakuwa tayari kutumia pesa zake kwa ajili ya kumpeleka shule mwanae hivyo alimtaka abaki nyumbani amsaidie kazi na malezi mama yake wa kambo ambaye tayari alikuwa na mtoto mchanga. Laurine alianza maisha mapya chini ya mama wa kambo. Maisha ambayo aliishi Laurine yalikuwa yanamfanya amkumbuke mama yake siku zote. Hakuna aina ya manyanyaso, tabu na mateso


ambayo Laurine hakuyapitia chini ya Baba yake na mama wa kambo. Licha ya kufanyishwa kazi kama punda lakini pia kunyimwa chakula ilikuwa ni sehemu ya maisha yake. Mara nyingi mlo wa usiku alikuwa anaupata kwenye njozi. Bwana Laurence ni kama alirogwa kichwani kwa sababu alisahau kabisa kama Laurine alikuwa ni mtoto wake wa damu. Hakuwahi kumtetea kwa chochote kile zaidi ya kumshushia vipigo vya mara kwa mara. Laurine hakuwa na haki wala uhuru wa kutembea.


Unyonge na upweke ulikuwa sehemu ya maisha yake. Binti alikonda, ule uzuri wa asili wote ulipotea. Hakuwa na sehemu yoyote ya kukimbilia kwani tangu alipozaliwa alikuwa hamjui ndugu wala jamaa yake mwingine isipokuwa mama na baba yake tu. Siku moja Laurine alipokea taarifa nzuri kutoka kwa Baba yake. Aliambiwa kwamba ajiandae kwa ajili ya safari kuelekea jijini Dar es salaam kimasomo. Bwana Laurence alimwambia Binti yake huko Dar es salaam ataenda kuishi kwa


shangazi yake na tayari ametafutiwa shule ya kusoma kidato cha tano. Kwa hakika Laurine alifurahi sana kusikia taarifa Ile kwani alijua Ile ndoto yake iliyokuwa imefifia hatimaye inaenda kuchanua upya. Binti alifurahi sana. Hakujua atumie neno gani kumshukuru Baba yake. Kupitia lile jema moja tu alijikuta anasahau mabaya yote aliyotendewa na Baba yake huyo. Licha ya furaha alivyokuwa nayo Laurine lakini kuna swali alijiuliza kichwani mwake. Huyo shangazi yake anayeishi Dar es salaam


ametokea wapi tena maana tangu alipozaliwa mpaka kufikia umri ule hakuwahi kuambiwa kuhusu kuwa na shangazi Dar es salaam. Lakini pia Baba yake hakuwaga na dada wala mdogo wake wa kike katika uzao wa mama yao. Laurine alimuuliza kwa upole Baba yake juu ya huyo shangazi yake lakini aliambiwa akae kimya asihoji chochote. Kwa namna Laurine alivyokuwa anamuogopa Baba yake, aliamua kukaa kimya na kuacha mambo yaende kama yalivyopangwa. Moyoni alijikuta anafarijika


baada ya kuona anatoka rasmi kwenye mikono ya watu wakatili. Alijua kabisa kama angeendelea kuishi pale siku zote basi angekufa kutokana na tabu na mateso aliyokuwa anapewa na wazazi wake. Siku iliyofuata Laurine alipandishwa kwenye Bus na kuanza rasmi safari kutoka Mwanza kwenda Dar es salaam. Safari ilianza mnamo majira ya saa kumi na mbili alfajiri na kufanikiwa kufika ndani ya jiji la Dar es salaam majira ya sita usiku. Ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa Laurine


kufika ndani ya jiji la Dar es salaam. Jiji mashuhuri na maarufu zaidi nchini Tanzania. Baada ya kufanikiwa kufika aliweza kupokelewa na mwenyeji wake ambaye aliamini kuwa ni shangazi yake. Shangazi yake Laurine alikuwa anaishi kwenye jumba kubwa na mume wake pamoja na watoto. Alikuwa mtu mwenye kipato kikubwa kwa sababu mume wake alikuwa anafanya kazi bandarini. Laurine alijihisi kama yupo peponi mara baada ya kuingia ndani ya ule mjengo. Usiku ule alikaribishwa


vizuri, alikula, alioga kisha akaoneshwa chumba cha kulala. Mpaka wiki mbili zinakatika akiwa ndani ya jiji la Dar es salaam, Laurine hakusikia taarifa yoyote kuhusu kupelekwa shule. Kila siku alikuwa anaamshwa mapema na kufanya usafi ndani ya nyumba, kumuandaa mtoto aende shule, kupika na kufua nguo za shangazi na mjomba ambaye ni mume wa shangazi yake. Zile kazi zilikuwa nyingi sana kwa Laurine kiasi kwamba kila iitwayo leo alikuwa hapati kabisa muda wa kupumzika.


Alikuwa anafanya kazi kama punda wa mizigo. Utofauti wa maisha yake kule Mwanza na Dar es salaam ulikuwa kwenye chakula tu na vipigo. Kule Mwanza chini ya Baba yake na mama wa kambo alikuwa anapigwa na kunyimwa chakula. Ila pale Dar es salaam kwa shangazi yake alikuwa anakula vizuri tu Ila kazi ni masaa kumi na nane kati ya ishirini na nne kila siku. Siku moja Laurine aliamua kumuuliza shangazi yake juu ya suala lake la kupelekwa shule. Shangazi yake


alimjibu Laurine, "Laurine! Kwa sasa sahau kila kitu kuhusu shule kwani elimu haipo kwa ajili ya kila mtu. Kama kila mtu akienda shule nani atafanya kazi za ndani kwenye nyumba zetu? Wewe sio wa kusoma Laurine. Haya maisha unayoishi ndo hatima yako Binti yangu. Ngoja nikuambie kitu Laurine, Baba yako alikudanganya unakuja Dar kwa ajili ya masomo lakini sio kweli. Umekuja hapa kwa ajili ya kunisaidia kufanya kazi ndani.


Kule Mwanza Baba yako hakutaki kabisa ndo maana ameamua kunitupia mimi mzigo. Ukweli ni kwamba Baba yako amekufukuza. Kama huamini basi chukua hii simu ongea na Baba yako alafu muulize atakuambia ukweli halisi.!" Shangazi yake Laurine alizungumza maneno hayo kisha akampigia simu Bwana Laurence ili kumthibitishia Laurine kauli aliyozungumza. Simu iliita na Bwana Laurence alipokea upande wa pili.


Shangazi alimpa simu Laurine ili azungumze na Baba yake. "Baba eeh, Hivi ni kweli sikuja Dar es salaam kwa ajili ya masomo? Ni kweli baba?" "Sikiliza wewe mpumbavu, naomba iwe mwanzo na mwisho kunipigia simu na kuniuliza maswali ya kijinga. Tangu awali nilishakuambia wewe sio wa kusoma. Subiri upate mume huko Dar na uolewe kabisa. Nakupa onyo, Ishi huko huko na usirudi tena nyumbani kwangu.


Kama Ukithubutu kuja nitakufanyia kitu kibaya kabla kitu kibaya hakijatokea kwenye ndoa yangu. Kiufupi ni kwamba mimi na wewe tulishamalizana.!" "Baba eeh, Hivi mimi ulinizaa ili nije kuteseka hapa duniani? Mbona mimi sipati furaha kama ilivyo kwa watu wengine? Hivi ni wapi haswa nakosea nikiwa kama mtoto kwako Baba yangu? Nikiwa kama mwanao, ni kitu gani haswa sikuwahi kutimiza kwako baba yangu. Mbona sijawahi kukuvunjia heshima


babaa? Mbona sijawahi kupingana na amri yako babaa? Mbona nilikuwa nafanya kazi zote za nyumbani bila kusukumwa na mtu yoyote? Baba hukuwa hivyo Baba yangu, ni kitu gani haswa kimekupata mzee wangu mpaka umesahau maisha ya upendo na furaha tuliyoishi miaka ya nyuma. Siku zote nilikuwa najivunia uwepo wako Baba yangu. Ulikuwa unapigania elimu yangu na nikakuahidi nitasoma kwa bidii ili siku moja nije niwatunze wazazi wangu. Hivi babaa, umesahau


yote yale? Mbona mimi sikuwahi kuwa na ugomvi na wewe Baba yangu. Kama ulikuwa na ugomvi na mama sasa kwanini unanijumlisha na mimi mtoto nisiekuwa na hatia yoyote? Baba eeh, hivi kosa langu mimi ni lipi kwako? Naomba uniambie ili nijue babaa.!" Laurine alizungumza kauli hiyo huku akitiririkwa na machozi mazito kwenye mboni za macho yake. "Laurine! Kwahiyo unataka kujua kwanini nimebadili mwenendo wangu juu yako si ndio? Ok ngoja


sasa nikuambie ukweli. Nimebadilika ghafla kwa sababu wewe sio mwanangu wa damu. Mama yako alikuwa ananisaliti mpaka akabeba ujauzito nje ya ndoa. Kwahiyo kuanzia sasa, elewa kwamba mimi sio baba yako mzazi.!" Bwana Laurence alizungumza kauli hiyo iliyoenda kutengeneza sintomfahamu nzito kichwani mwa Laurine. Kabla Laurine hujazungumza chochote, Bwana Laurence alikata simu. Laurine alijikuta anazidi kulia baada ya kukanwa


na Baba yake mzazi. "Laurine, nadhani sasa umeshajijua wewe ni nani kwa kaka yangu. Kwahiyo basi kuanzia sasa utaishi hapa kama upo kwa bosi wako na sio shangazi yako. Majukumu yako ndani ya nyumba yangu ni kuhakikisha nyumba inakuwa safi kila dakika. Kila siku utakuwa unamuandaa mwanangu kabla hajaenda shule. Kama hutaki basi ni ruksa kuondoka, geti lipo wazi kwa ajili yako. Na kama utachagua kubaki


basi tambua kwamba mimi ni bosi wako na sio shangazi yako tena. Umesikia wewe mpumbavu?" NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu} EPISODE: 05 AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller) "Ndio shangazi nimekusikia.!" "Pumbavu! Usiniite shangazi,


Niite bosi.!" "Sawa Bosi nimekuelewa lakini vipi kuhusu mshahara wangu kwa mwezi?" "Mbona una tamaa wewe binti? Fanya kazi mshahara utapata kulingana na ufanisi wako wa kazi.!" Mpaka kufikia hapo ndoto za Laurine kuhusu kusoma zilififia kwa mara nyingine. Hatimaye Binti wa miaka takribani kumi na nane alianza maisha mapya


ndani ya jiji la Dar es salaam. Maisha hayo hayakuwa na utofauti kabisa na maisha aliyoishi jijini Mwanza. Kila aina ya mateso Laurine alikumbana nayo ndani ya nyumba aliyokuwa anaishi. Kitu pekee kilichokuwa kinampa faraja na matumaini ya kuishi ni kwa kuwa alikuwa anakula jikoni. Maisha aliyokuwa anapitia mtoto wa kike yalikuwa ya manyanyaso kila kukicha. Neno furaha kwake halikuwahi kutumiki kabisa tangu mama yake alipofariki. Siku zote alikuwa anamkumbuka sana


marehemu mama yake. Moyoni alikuwa anajisemea pengine kama mama yake angelikuwa hai basi yale yote yasingetokea. Kazi alikuwa anafanya lakini cha ajabu alikuwa halipwi mshahara. Kila alipodai mshahara wake mwisho wa mwezi ulipofika aliambiwa atapewa siku atakayokuwa tayari kuondoka na kwenda kuanza maisha yake. Laurine hakuwa na sauti mbele ya bosi wake. Siku zote alikuwa mnyonge na ukizingatia hakuwa na mtu wa kumtetea kwenye uso wa dunia. Alishajua kwenye uso


wa dunia yeye ni yatima na nusu. Hakuwa na wazazi wala ndugu. Aliamua kupiga moyo konde huku akiamini yale maisha yatapita. Yale maisha ya manyanyaso, tabu na mateso aliamua kuishi nayo kwa moyo mmoja na kuyapenda. Hakutaka tena kuupa nafasi moyo wake na kutafakari namna anavyofanyiwa na walimwengu. Nafsi yake ilikunjuka na kuamini kwamba yale ndo maisha yake na anastahili kuishi vile. Baada ya kuikunjua nafsi yake ilifikia hatua akayazoea kabisa yale maisha.


Wakati walimwengu wanahisi wanamtesa Laurine, Laurine yeye alichukulia yale mateso kama ni kitu alichokuwa anastahili. Ni kama mtuhumiwa ambaye amekubali kosa lake bila kupindisha maelezo mbele ya mahakama na kwenda kutumikia kifungo. Mara nyingi mtuhumiwa kama huyo hawezi kuwa na manunug'uniko wala hisia kwamba ameonewa. Lile jambo hata kama linatakuwa la kuumiza ila kwake maumivu yatadunda. Hivyo ndivyo Laurine alivyochagua kuishi. Na tangu


alivyoamua kuishi vile alijikuta ananepa na kujengeka vizuri kimwili licha kupitia mazingira magumu. Laurine aliweza kuishi pale kwa shangazi yake kwa takribani mwaka mmoja. Kwa muda wote alioishi alibadilika sana mtoto wa kike. Kwa hakika alinawiri na kujengeka vizuri kimwili. Uzuri wake wa asili ulirudi kama ulivyokuwa hapo awali. Umbo lake lilikuwa maridhawa kiasi kwamba lilimsababishia misukosuko kwa mara nyingine. Yule mume wa shangazi yake alijikuta anaingiwa


na tamaa ya kimapenzi dhidi ya Laurine. Alianza kumjali Laurine tofauti na ilivyokuwa hapo awali. Kila alipotoka kazini alikuwa anamletea vizawadi vidogo vidogo pamoja na kumpa vijisenti vya matumizi. Suala lile lilimchanganya sana Laurine na alishajua kwamba ule ulikuwa mtego. Aliwaza ni namna gani angeweza kukwepa lakini hakufanikiwa kupata jibu. Siku moja mume wa shangazi yake Laurine yani baba mwenye nyumba alitoka kazini mapema na kurudi nyumbani. Muda na


wakati ambao alifika mkewe alikuwa bado hajarudi kutoka kazini. Pale nyumbani kulikuwa na mtoto mdogo pamoja na Laurine tu. Yule mtoto ambaye alikuwa anaandaliwa na Laurine kila siku kwenda shule alikuwa bado hajarudi kutoka shule. Baba mwenye nyumba alipofika nyumbani kwake alimkuta Laurine sebuleni akitazama televisheni. Laurine alimsalimia bosi wake kwa kumwamkia lakini bosi hakuitikia. Hakuitikia kwa sababu mara nyingi alikuwa anamkataza Laurine


asimwamkie kwa kudai kwamba bado hajazeeka. Bosi alienda chumbani kwake huku Laurine akiendelea kutazama televisheni pale sebuleni. Dakika chache badae Laurine alisikia akiitwa na mara baada ya kuitika alisikia sauti ya baba mwenye nyumba akimuagiza ampelekee maji ya kunywa kule chumbani. Laurine alipata hofu na mashaka makubwa sana juu kuingia chumbani kwa bosi wake. Tayari alishajua ule ulikuwa mtego kwa sababu alishaonaga dalili za kutamaniwa na yule mwanaume.


Lakini sasa, licha ya kujua kwamba ulikuwa ni mtego lakini alishindwa kukwepa kwani hakuwa na nguvu ya kukataa kumpelekea maji bosi wake. Ilibidi atii amri kwa kuchukua maji na kupeleka chumbani alipokuwa bosi wake. Ile kufika tu akadakwa na kusukumwa kitandani. Bosi akafunga mlango kisha akamwambia Laurine endapo atathubutu kupiga kelele pale chumbani basi angemuua. Alimfuata Laurine pale kitandani kisha akaanza kumshika ili amvue nguo. Laurine alianza


kulia huku akijaribu kujitoa mikononi mwa boss wake ambaye ni mume wa shangazi yake. Jamaa alimtishia Laurine kama angekataa kumpa penzi basi angemfukuza pale ndani lakini bado Laurine hakuwa tayari kuvua nguo. Mtoto wa kike alikuwa tayari kufukuzwa kuliko kudondosha usichana wake mikononi kwa yule mtu mwenye makamo ya baba yake. Purukushani zikaanza, vuta nikuvute zilifuata. Mtu mzima alidhamiria kumbaka mtoto kike hivyo alitumia nguvu zake mpaka


akafanikiwa kumdhibiti. Kwa mara ya kwanza kabisa Laurine alijikuta anaingiliwa kimwili na mwanaume kwa kubakwa. Laurine alikutana na maumivu makali sana katika sehemu zake za siri kwani aliingiliwa bila kuandaliwa. Baada ya kumaliza zoezi la ubakaji, Mjomba alimtishia maisha Laurine endapo angethubutu kutoa ile siri. Laurine aliumia sana kuona usichana wake ukidondokea mikononi mwa yule mtu mzima. Alitamani kuondoka pale ndani lakini hakujua ni wapi angeenda.


Mbaya zaidi hakuna na senti yoyote mfukoni mwake. Siku zote alikuwa anafanya kazi lakini mshahara alikuwa halipwi. Mwezi mmoja baadae, Laurine alianza kuhisi kichefu chefu cha mara kwa mara pamoja na utofauti katika tumbo lake. Alihisi kuwa na dalili za ujauzito hivyo akamfahamisha Mjomba suala lile kwa kuwa yeye ndo alikuwa muhusika. Mjomba alishtuka sana baada ya Laurine kumwambia anajihisi mjamzito. Kwanza kabisa Mjomba aliamua kwenda kununua kipimo cha


mimba kisha akampa Laurine apime mimba kwa njia ya mkojo ili wapate uhakika na uthibitisho wa kina. Baada ya kupima mkojo, kipimo kilionesha kwamba Laurine alikuwa mjamzito. Wahusika wote wawili walijikuta wanachanganikiwa. Mume wa shangazi yake Laurine alimtaka Laurine atoe ile mimba ili kunusuru ndoa yake. Suala lile lilikuwa tata sana kwa Laurine kutokana na woga wa kutoa mimba. Mtoto wa kike hakuwa tayari kutoa mimba kwani aliogopa kuhatarisha maisha


yake au kizazi chake. Mtu mzima alimshawishi Laurine kwa kumwambia kwamba kuna dawa za kisasa zinazotumika kutoa mimba bila kuhatarisha maisha wala kuharibu kizazi. licha ya kuambiwa maneno hayo lakini Laurine bado alihofia sana suala la kutoa mimba. Alichokifanya Laurine ni kumuomba pesa kidogo yule mume wa shangazi yake ili aondoke pale nyumbani kwao na akaanze maisha sehemu nyingine huku akimlea mtoto wake. Laurine hakuwa tayari kukiangamiza kiumbe


kisichokuwa na hatia. Mjombaa alimuahidi Laurine angempatia kiasi cha pesa alichoomba ndani ya siku tatu hivyo avute subira na aendelee kujificha ili shangazi yake asijue Ile siri. Laurine alikubaliana na kauli ya Mjomba hivyo aliamua kubaki huku akiwa na matumaini kwamba baada ya siku tatu angeenda kuanza maisha nje ya ile nyumba. Lakini sasa, kile alichokuwa ameahidiwa sicho alichokuja kufanyiwa. Mjomba alihisi hata kama Laurine angeondoka pale ndani na kwenda kuishi mtaani


bado ingeleta hatari kwenye ndoa yake huko mbeleni. Alichokifanya jamaa ni kumtegeshea Laurine dawa za kuharibu mimba kwenye juisi. Maskini Laurine alikunywa dawa za kuharibu mimba pasipo kujua. Mjomba aliamini kwamba vidonge vile vingeharibu mimba kimya kimya bila kumletea madhara yoyote Laurine kwa kuwa aliambiwa hivyo na Mfamasia. Lakini sasa, dawa zilifanya kazi tofauti na matarajio ya Mjomba. Siku nzima Laurine aliteseka sana kwa maumivu ya


tumbo. Kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo maumivu yalivyozidi kuwa makali katika tumbo lake. Laurine alilia kama mtoto. Hakujua sababu iliyokuwa inafanya tumbo lake kuuma kiasi kile. Mwanzo shangazi alichukulia wepesi suala lile na hakuguswa kabisa kwa kuwa hakuwahi kumthamini wala kumpenda Laurine. Lakini sasa baada ya kuona sketi ya Laurine imelowa na kutapakaa damu, hapo sasa akashtuka. Sasa aliamini kwamba ni kweli Laurine alikuwa mgonjwa na kama


wangeendelea kumtazama basi pengine angelipoteza maisha. Chap chap alifanya mpango wa usafiri kisha akampeleka hospitali. Baada ya kufika hospitali madaktari walifanya kazi yao kwa ufasaha wakati huo Laurine alikuwa amepoteza fahamu. Baada ya muda fulani kupita Laurine alizinduka na alipoangalia pembeni kushoto alimuona Mjomba yani mume wa shangazi yake. Laurine hakutaka kabisa kumtazama mtu huyo. Aligeuza shingo upande wa pili akakutana na sura ya ngumu ya


shangazi yake akimtazama kwa hasira kali sana. "Laurine! Laurine! Laurine! Naomba uniambie. Nani amekupa mimba, nani alikununulia vidonge vya kutoa mimba na kwanini umetoa mimba?" Shangazi alimuuliza Laurine maswali hayo na kumfanya ashtuke baada ya kusikia taarifa mpya ya kutoa mimba. Laurine alimtazama Mjomba kisha akafumba macho kwa hisia


kali za uchungu huku machozi yakitiririka mashavuni mwake. NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu} EPISODE: 06 AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller) "Laurine! Nakuuliza kwa mara nyingine, Naomba uniambie, Nani amekupa mimba, nani alikununulia vidonge vya kuharibu mimba na kwanini umetoa mimba?" Shangazi


alimuuliza Laurine kwa mara nyingine tena kwa msisitizo wa hali ya juu. Bado Laurine aliendelea kufumba macho huku machozi yakiendelea kumtiririka kwa wingi mashavuni. Alishindwa kabisa kufumbua macho na kuwatazama wanandoa waliokuwa mbele yake. "Kwahiyo unataka unavyotoa machozi unataka nikuonee huruma sio? Sasa kama wewe mwenyewe umeshindwa


kujihurumia unadhani nani atakuhurumia? Hivi unajua kwamba ilikuwa alimanusura ufe kwa ushenzi wako ulioufanya? Yani kama ningejua umekunywa vidonge vya kutoa mimba nisingejisumbua kabisa kuinua mguu wangu na kukuleta hospitali. Ningekuacha ufe tu muuaji mkubwa wewe. Umeona raha kuua sio? Yani Binti mdogo umekuwa katili mpaka nakuogopa sasa. Kwanza niambie nani alikupa mimba maana naona kama kuna mchezo mchafu umefanyika


ndani ya nyumba yangu.!" Shangazi alizidi kuongea kwa hasira na jazba kubwa kwani alianza kuhisi kitu pengine ile mimba ilipatikana ndani ya nyumba yake. Kama sio mlinzi basi mume wake ndo atakuwa muhusika wa jambo hilo. Pale pale mume aliingilia kati suala hilo maana alishaanza kunusa hatari, "Mke wangu, Hebu tulia kwanza hapa sio sehemu sahihi ya kujadili hayo mambo. Bado tupo


hospitali hivyo tusubiri turudi nyumbani tutaenda kumuuliza vizuri Binti yetu na atatueleza kila kitu.!" Mume wa shangazi yake Laurine alizungumza kauli hiyo ili kumtuliza mke wake asiendelee kumhoji Laurine. Baada ya kusikia sauti ya mume wa shangazi yake, Laurine alipata machungu mara mbili zaidi ya hapo awali. Machozi yalizidi kumtiririka Laurine. Alikumbuka vyema ile siku aliyobakwa na mjomba yake huyo. Lakini pia alikumbuka mara


ya mwisho mjomba alipompa juisi na kumwambia ni juisi nzuri ya matunda kwa ajili ya afya ya kiumbe kilichopo tumboni mwake. Kumbe ile juisi iliwekwa za kuharibu mimba na ndo maana alipokunywa tu ndipo maumivu ya tumbo yalipomuanzia. Laurine aliumia sana baada ya kukumbuka matukio hayo. Hakuwa na hamu tena ya kuendelea kumtazama mume wa shangazi yake. Alishajua kwamba yule mwanaume alikuwa na roho ya kinyama hivyo hakuona sababu


ya kuendelea kufumbia macho suala lile. Hakuona sababu ya kuendelea kuficha uovu wa yule mwanaume hivyo akaona ni bora amueleze kila kitu shangazi yake. Laurine alifumbua macho kisha akazungumza, "Shangazi eeh, Naomba unisamehe sana. Nisamehe kwa hiki ninachoenda kukizungumza muda huu. Shangazi! Ukweli ni kwamba aliyenipa mimba na kunipa vidonge vya kutoa mimba ni Mume wako huyu hapa anaenitazama muda huu. Ukweli


ni kwamba, mimi...!" "Basi! Basi inatosha usiendelee kuzungumza kitu wewe mtoto. Hilo suala ndo lilikuwa kichwani mwangu muda wote. Kumbe siku zote migogoro ilikuwa haiishi ndani ya nyumba yangu kwa kuwa nilikuwa naishi na mke mwenzangu ndani ya nyumba moja? Ooh! My God.! Naomba unipe uvumilivu nisije nikatenda dhambi ya mauaji.!" Shangazi alinyong'onyea kisha akajikuta anakaa chini bila


kutarajia. Nguvu mwilini zilimuishia kabisa. Aliwaza na kuwazua baadhi ya matukio kadhaa aliyokuwa anayafanya mume wake kwa Laurine. Akili yake ilimwambia kwamba mume wake na Laurine walikuwa na mahusiano ya siri kwa muda mrefu. Kiufupi ujio wa Laurine ulikuwa na madhara makubwa kwenye ndoa yake. Shangazi alimtazama kwa hasira mume wake ambaye kwa wakati huo alikuwa amejiinamia chini kwa aibu. Alipotosheka kumtazama mume wake alimgeukia Laurine.


Alimtazama sana Laurine kisha akamwambia, "Laurine! Sijui na sitaki kujua utaenda kuishi wapi lakini nakuomba usitie tena mguu wako nyumbani kwangu. Kwa usalama wa maisha yako naomba uondoke kabisa vinginevyo nitakuua. Nguo zako utaletewa hapa hapa hospitali hivyo ukiamka nenda popote ukaishi ila usirudi nyumbani kwangu. Kwa maisha ya sasa, ndoa sio rahisi kuipata. Nilitumia nguvu na akili nyingi kupata na


kuijenga ndoa hivyo siwezi kuvumilia kuishi na haini wa ndoa yangu. Kwa hakika umenikosea sana wewe Binti.!" Shangazi alizungumza maneno hayo kisha akainuka pale chini na kuondoka kwa hasira. Mume nae aliamua kumfuata mkewe kwa lengo la kubembeleza ndoa yake. Laurine alibaki pale kitandani huku akiendelea kumwaga machozi kutokana na mfululizo wa mitihani ya maisha iliyokuwa inamuandama kila kukicha.


Masaa mawili baadae shangazi alimrudja Laurine kwenye kile chumba alichokuwa amelazwa kisha akamtaka waondoke kwani ruhusa ilishatolewa kutokana na hali kutokuwa mbaya. Walipewa dawa ambazo Laurine angetumia akiwa nyumbani. Walipotoka tu nje ya jengo la hospitali, shangazi alifungua mlango wa gari kisha akatoa begi dogo la mgongoni na kumkabidhi Laurine. Laurine alipolitazama lile begi alilitambua vyema. Lilikuwa begi lake la nguo alilitoka nalo mkoani Mwanza.


Shangazi alimkabidhi Laurine begi kisha akamwambia apotee kabisa kwenye mboni za macho yake. Kitu cha kusikitisha ni kwamba hakumpa hata senti moja ya kwenda kuanzia maisha huko aendako. Kwa hakika watu wamekosa mioyo ya huruma kwenye hii dunia. Yani zile kazi zote alizokuwa anafanya Laurine mshahara wake ulikuwa chakula tu. Zile pesa alizoahidiwa angepewa siku ya kuondoka hakupewa pia. Laurine alianza kutokwa na machozi kwenye mboni za macho yake. Shangazi


hakutaka kutazama tena machozi ya Laurine badala yake akapanda kwenye gari na kuondoka zake. Kwa hakika kilikuwa kipindi kigumu sana kwa Laurine kwani hakujua ni wapi aelekee kwa wakati ule. Dar es salaam ni jiji kubwa lenye watu wengi na mitaa mingi lakini Laurine alikuwa hajui mtaa wowote ule. Mbaya zaidi ni kwamba hakuwa hata na senti moja katika mfuko wake. Kwanza kabisa alipata wazo la kuwasiliana na baba yake Bwana Laurence licha ya kwamba


alishamkana. Aliomba simu kwa kijana mmoja aliyekuwa karibu yake kisha akampigia baba yake kwa kuwa alihifadhi kichwani namba yake. Kwa bahati nzuri simu iliita na kupokelewa. Lakini sasa, Bwana Laurence aliposikia sauti ya mwanae Laurine aliwaka kama moto wa vifuu. Laurine alijuta hata kumpigia baba yake kwani alichoambiwa kilizidi kudidimiza matumaini yake ya kuendelea kuishi. Kumbe tayari shangazi alimwambia kila kitu Bwana Laurence kuhusu kile kilichotokea kati ya Laurine na


mume wake. Bwana Laurence alimwambia Laurine asithubutu kumpigia tena simu wala kurudi Mwanza. Alimuita Laurine kahaba na kumwambia abaki Dar es salaam mpaka atakapokufa. Lakini pia alimkumbusha kwamba yeye sio baba yake mzazi hivyo amtafute baba yake mzazi. Baada ya kuambiwa kauli hiyo kwa mara ya pili, Laurine alikubali kufunga rasmi ukurasa wa mahusiano na baba yake. Ni rasmi sasa aliamini kwenye dunia hakuwa na wazazi wala ndugu. Huo ndo ulikuwa mwanzo


wa maisha mengine kwa Laurine ndani ya jiji la Dar es salaam. Mtoto wa kike alianza kutanga tanga huku na kule ilimradi kutafuta hifadhi ukizingatia hata afya yake haikuwa nzuri. Alizunguka huku na kule kutafuta msaada lakini kila mtu aliyemtazama alionekana kuwa bize na mambo yake. Mpaka kufikia majira ya saa tatu usiku, Laurine alikuwa hajapata msaada wa hifadhi wala kutia chochote tumboni mwake. Njaa ilimuuma sana mtoto wa kike. Kuna baadhi ya watu alijaribu


kuwagusa na kuwaomba msaada wa hifadhi na chakula lakini hakufanikiwa kupata. Msaada pekee alipatiwa ulikuwa ni ushauri tu kwamba aende kituo cha polisi akaombe msaada wa kusafirishwa mpaka nyumbani kwao Mwanza. Laurine hakuwa na lengo la kurudi Mwanza kwani tayari alishakanwa na baba yake hivyo hakuona tena sababu ya kurudi. Alijipa matumaini ya kubaki Dar es salaam na kuamini kwamba ipo siku angekuwa na maisha kama watu wengine. Baada ya


kukosa kabisa msaada, Laurine aliliona jumba fulani lililokuwa halijakamilika kiujenzi hivyo alisogelea na kuzama ndani. Baada ya kufika ndani alifungua begi lake na kutoa baadhi ya nguo zake na kuzitandika chini kisha akajilaza. Kwa hakika ilikuwa ni siku ya mateso sana kwa Laurine kwani aling'atwa na mbu, akapigwa na baridi na njaa pia ilikuwa inamuuma sana. Lakini sasa kwa bahati mbaya, watoto wa mjini wapatao tano walimuotea Laurine ndani ya ile nyumba aliyokuwa amelala. Wote


kwa pamoja walimvamia mtoto wa kike ule usiku kisha wakambaka bila huruma. Baada ya vijana kumaliza zoezi la ubakaji, Laurine aliachwa akiwa na hali mbaya sana. Licha ya kupata maumivu makali kwenye uke lakini pia tumbo lilianza kumuuma ukizingatia kuna kijusi kiliharibiwa. Sio hivyo tu, hata njaa ilikuwa inamuuma sana kwani hakula chakula cha mchana wala usiku. Kwa hali aliyokuwa nayo alijua kabisa kama angeendelea kubaki pale usiku ule bila kupata msaada


basi uhakika wa kufika asubuhi akiwa hai ungekuwa mdogo. Alijikongoja taratibu mpaka pembezoni mwa barabara. Alisimama kisha akaanza kusimamisha magari ili aweze kusaidiwa. Kwa bahati mbaya hakuna binadamu aliyethubutu kusimamisha gari lake ili kujua ni kitu gani haswa kilikuwa kinamsibu binadamu mwenzao. Hiyo ndo picha halisi ya jiji la Dar es salaam. Jiji lenye watu wengi Ila binadamu wake ni wachache. Laurine alijikuta anakata tamaa ya kupata msaada. Pale pale


alijikuta anakosa nguvu, akadondoka chini na kupoteza fahamu. Saa moja baadae alikuja kuzinduka na kujikuta ndani ya chumba akipatiwa huduma ya kukandwa kwa maji ya moto na wanawake wawili. Neno la kwanza kwa Laurine lilikuwa ni ombi la chakula. Aliomba asaidiwe chakula kwanza maana tumbo lake halikuwa na kitu kabisa. Mwanamke mmoja kati ya wale alivuta mfuko fulani mezani kisha akafungua na kumkabidhi Laurine. Mfuko huo ulikuwa na chakula aina ya


chipsi. Kutokana na njaa aliyokuwa nayo, Laurine alikula kwa pupa chipsi hizo na kuzimaliza ndani ya muda mfupi tu. Baada ya kumaliza kula aliomba apewe kibegi chake cha mgongoni. Bila kuchelewa alipatiwa kisha akafungua na kutoa zile dawa za hospitali alizopewa kwa ajili ya maumivu ya tumbo. Alikunywa dawa zake huku wale wadada wakiendelea kumtazama tu kwa macho ya huruma. Kutokana na hali aliyokuwa nayo Laurine, hakuna mtu aliyetaka kumuuliza usiku


ule kitu gani kilimsibu mpaka akawa kwenye hali ile. Walimuacha apumzike kwanza ili wamuulize vizuri siku inayofuata. Laurine alilala pale usiku ule na alikuja kuamka mnamo majira ya saa nne asubuhi. Alipoamka alikuta listi ya wadada imeongezeka pale ndani. Usiku walikuwa wawili ila asubuhi waliongezeka watatu na kufanya idadi yao kufikia tano. Wadada wote walimjulia hali Laurine. Laurine aliwajibu kwamba bado hakuwa vizuri kimwili. Walimpa pole kisha wakamtaka aende


bafuni akaoge kwanza ili wafanyie taratibu zingine. Laurine alijikaza na kuelekea bafuni kuoga. Alipomaliza kuoga alipewa chai akanywa kisha akatulia baada ya kumaliza. Hapo sasa wale wadada walipata wasaa mzuri wa kukaa chini na kumuuliza Laurine kipi kimemsibu mpaka walimuokota kwenye hali ile. Laurine alianza kwa kulia kisha akawasimulia wale wadada mkasa mzima wa maisha yake mpaka kufikia muda ule. Kwa hakika mkasa wa Laurine uliwahuzunisha na


kuwatoa machozi wale wadada. Kila mmoja alimpa pole Laurine na kumfariji kwa mazito aliyopitia. Walimwambia kwamba sio yeye tu bali hata wao wamepitia changamoto nzito ndo maana wapo pale muda ule wanaishi chumba kimoja wasichana tano. Chumba hakina kitanda ila kuna godoro tu limetandikwa chini. Kazi kubwa inayowaweka mjini ni kuuza miili yao ili wapate ridhiki. Kila mmoja alimsimulia Laurine historia ya maisha yake kabla hajajiingiza kwenye ile biashara ya kishenzi.


Laurine alijikuta anatokwa na machozi baada ya kusikia mikasa ya maisha waliyopitia wenzake. Wakati anaamini yeye ndo binadamu wa kwanza kuseka zaidi duniani kumbe kuna watu waliteseka zaidi yake. Wale wadada walimwambia Laurine kwamba walipata nguvu ya kumsaidia kwa sababu hali aliyokuwa nayo hata wao walishaipitiaga. Walimpa moyo na kumwambia watamsaidia kadri wawezavyo mpaka afya yake itakapokuwa sawa. Laurine aliwashukuru sana wale wadada.


Kwa mara nyingine alijikuta anapata tumaini la kuishi kwenye dunia yenye watu wengi na binadamu wachache. Inasikitisha sana kuona yule Daktari tuliepewa dhamana ya kutibu na kuokoa maisha ya watu akimkuta mgonjwa barabarani anahitaji msaada wa matibabu basi anampita kama kivuli. Laurine alianza maisha mapya kwenye kile chumba cha wadada wanaouza miili yao. Walimpa mahitaji yote ya msingi katika kipindi chote alichokuwa anaugua. Baada ya mwezi


mmoja kupita, hatimaye afya yake ilirudi kama ilivyokuwa hapo awali. Sasa alishakuwa na nguvu ya kujitafutia ridhiki yake mwenyewe. Kwa kuwa rafiki wa mwizi ni mwizi, Laurine alijikuta anajiunga na wale wadada kwenye biashara ya ukahaba. Hiyo ndo ilikuwa njia pekee ya Laurine kuendelea kuishi pale ndani. Naam! Hiyo ndo ilikuwa historia ya maisha aliyopitia Laurine mpaka kufikia hatua ya kuwa kahaba. Laurine alimsimulia Owen mkasa huo bila kupindisha maelezo. Kwa


hakika mkasa wa Laurine ulimpa huzuni kubwa sana Owen. Mtaalam alijikuta anamuhurumia mtoto wa kike kwa maisha aliyopitia. Alijikuta anakosa nguvu na kushindwa kujua aongee nini hivyo akaamua kulala usingizi. Ile stori ni kama ilitonesha kidonda kwa Laurine. Mtoto wa kike alianza kulia taratibu pale chumbani. Baada ya dakika chache kupita, Laurine alihitaji kulala. Alimtazama Owen namna alivyolala pale kitandani. Owen alikuwa amelala na viatu huku akiwa amevaa shati la


mikono mirefu. Laurine alimsogelea Owen kisha akamvua viatu na kumfungua kifungo cha juu kabisa cha shati ili kisimkabe koo wakati wa kugeuka. Baada ya kufanya hivyo, akimlaza vizuri Owen kisha akamfunika shuka. Laurine nae alichukua blanketi kitandani kisha akalitandika sakafuni na kujilaza hapo. Laurine aliendelea kukumbuka matukio kadhaa yaliyopita kwenye maisha yake huku akigugumia kilio. Kumbe wakati ule Owen alikuwa bado hajalala. Kila kitu kilichokuwa


kinaendelea alikuwa anakielewa. Licha ya kumuonea huruma mtoto wa kike, lakini pia aliweza kugundua uwepo wa moyo msafi ndani ya mwili mchafu wa Laurine. NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu} EPISODE: 07 AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller) Mnamo majira ya saa nne na nusu asubuhi, Owen aliamka


kutoka usingizi. Baada ya kuamka alishangaa kujikuta peke yake ndani ya chumba cha Lodge. Yule binti hakuwepo na tayari alishaondoka. Owen alikagua wallet yake na alizikuta pesa zake kama alivyotarajia. Mezani kulikuwa na simu pamoja na funguo ya gari lake. Kiufupi hakuna kitu chake ambacho kilikosekana. Laiti kama Owen angekuwa na mwanamke mwingine tofauti na Laurine basi ile siku angeibiwa kila kitu. Lakini pia pale mezani kulikuwa na hotpot nyekundu pamoja na


kipande cha karatasi. Owen hakujua ile karatasi ilikuwa na ujumbe gani na ile hotpot ilikuwa na nini ndani yake. Kwanza kabisa alianza kukagua simu yake ili ajue ni kitu gani kilijiri nyumbani kwao. Alipoangalia simu yake alikuta missed calls na meseji nyingi sana kutoka nyumbani kwao. Owen alimpigia simu mama yake na kumwambia kwamba yupo salama kabisa hivyo aondoe hofu muda si mrefu angerudi nyumbani. Roho ya mama ilipoa na hakutaka kumuuliza maswali mengi kwani


alijua mwanae ni mwanaume na tayari alishakuwa mtu mzima. Baada ya kuwatoa hofu nyumbani kwao, Owen aliteremka kitandani kisha akasogea pale mezani na kufungua ile hotpot. Alipofungua alishangaa kukuta supu safi ya kongoro ikimrembulia. Alipoangalia kile kipande cha karatasi aliona ujumbe wa maandishi. Owen alikichukua na kuanza kukisoma. "Ukiamka kunywa hiyo supu itakusaidia kukupa nguvu na


kukata kabisa pombe ulizokunywa usiku. Pombe haziwezi kumaliza matatizo bali zitakuongezea matatizo. Chukulia funzo jana yako ili kuboresha kesho yako. Siku imebadilika anza maisha mapya. Kumbuka kwamba sio kila unachokipoteza ni hasara, vingine ni faida.!" Huo ulikuwa ujumbe wa maandishi ulioandikwa kwenye kile kikaratasi. Owen aliposoma ujumbe ule alijikuta anatabasamu bila


kutarajia. Alishajua ule ujumbe uliandikwa na Laurine kwa ajili yake. Ujumbe ule uliweza kumpa Owen kitu chanya kichwani mwake. Mtaalamu aliiweka ile karatasi kwenye mfuko wake wa suruali kisha akaingia bafuni kuoga. Alipomaliza kuoga alirudi mezani na kuanza kunywa supu aliyonunuliwa na Laurine. Owen aliifurahia sana ile supu kwa kuwa ilikuwa na ladha nzuri sana mdomoni mwake. Katika maisha yake hakuwahigi kabisa kunywa supu ya kongoro hivyo kwa ladha aliyokutana nayo alijikuta


anaifurahia ile supu na kutamani kuinywa tena na tena. Alitamani pia kumshukuru Laurine kwa mazuri yote aliyomfanyia lakini tayari mtoto wa kike alishaondoka tena bila kudai hata fidia za kupotezewa muda wake usiku kucha. Kwa muda ambao Owen alikaa na Laurine aliweza kutambua kwamba Laurine alikuwa msafi wa roho licha ya kuwa mchafu kimwili. Baada ya kumaliza kunywa supu, Owen aliondoka pale Lodge na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwao.


*** Wiki nzima Owen hakuonekana kuwa na furaha kabisa pale nyumbani kwao. Familia nzima ilitambua ile hali. Owen aliulizwa ni kipi haswa kilichokuwa kinamsibu lakini alishindwa kuzungumza ukweli uliopo ndani ya moyo wake. Kwa namna mama alivyokuwa anampenda mwanae Owen, alijikuta anaumia sana kuona mtoto wake anakosa furaha. Alimbana kila kona na kumtaka amwambie kipi


kilichokuwa kinamsibu. Owen alimwambia mama yake asiwe na wasiwasi ni mambo ya ujana tu ndo yalikuwa yanamsumbua. Mpaka hapo mama wa kidigitali alishaelewa kile kilichokuwa kinamsumbua mwanae. Alijua masuala ya mahusiano ndo yalikuwa yanamtatiza Owen. Hata Robyson alikaa na mdogo wake na kumdadisi kwa kina kuhusiana na jambo hilo. Kwa kuwa Robyson ni mwanaume, Owen alimueleza tu kaka yake kwamba mapenzi ndo yalikuwa yanamsumbua. Yule mwanamke


wa ndoto zake ni kwamba tayari alishaachana nae na amepata mwanaume mwingine. "Bwana mdogo, Cool down.! Hebu tuliza akili ndugu yangu mbona hilo ni jambo dogo sana kulikabili. Hii dunia ina idadi kubwa ya wanawake kuliko hata sisi wanaume. Na cha kufurahisha zaidi ni kwamba kila siku watoto wazuri wanazidi kuzaliwa. Bado ujapoteza mdogo wangu! Bado ujachelewa kabisa hivyo una muda na nafasi nyingine ya kumpata mwanamke


mwingine mzuri kuliko hata huyo wa awali. Uzuri ni kwamba pesa zipo katika mikono yako na elimu pia unayo ya kutosha kwahiyo unaweza kumpata mwanamke yeyote umtakae.!" Robyson aliongea kauli hiyo kumtia moyo mdogo wake Owen "Sasa Kaka, kama wanawake wapo wengi na kila siku wanazidi kuzaliwa kwanini umemchukua Diana wangu? Kwanini usiwachukue hao wengi kaka. Inauma sana kaka! Ni bora hata angeenda kwa mtu mwingine


nisingepata nafasi ya kumuona hivyo ingekuwa rahisi kumsahau. Lakini kuja kwako maana yake nitakuwa namuona kila siku. Itanichukua muda mrefu kumsahau Diana kaka. Kwanini ni wewe kaka? Je siku ukijua kwamba Diana ndo alikuwa mwanamke wa ndoto zangu utafanyaje? Kipi kitafuata ndani ya familia yetu?" Owen alijisemea kimoyo moyo maneno hayo huku akimtazama Robyson. Alitamani kumwambia ukweli kaka yake lakini alisita. Alihisi


pengine angempa stress nzito sana kaka yake ambaye tayari alionesha kuzama mzima mzima kwenye penzi la Diana. Robyson alionekana kumpenda Diana kuliko kawaida. Alichokifanya Owen ni kukubaliana na ushauri wa kaka yake wa kutafuta mwanamke mwingine. Alimuahidi kwamba atavuta subira mpaka pale atakapompata mwanamke sahihi kwa ajili yake. Maongezi hayo Robyson aliyafikisha kwa wazazi na kuwaeleza kile kilichokuwa kinamsibu Owen. Wazazi wao


waliona kuna kila sababu ya kumsaidia kijana wao kutafuta mwanamke mzuri na anaeendana na hadhi ya familia yao kama walivyomtafutiaga Robyson. Wakati wao wanawaza kumtafutia Owen mwanamke, Owen yeye alijiwekea msimamo mpya moyoni wake. Mtaalamu alijiapiza kukaa kando na mahusiano kuanzia muda ule. Akili na nguvu zake aliamua kuzielekeza kwenye kufanya kazi tu. Wiki ile ile Owen alipokea simu ya kuhitajika kwenye Interview ya kazi katika Kampuni


iliyokuwa inamilikiwa na Mr Jay Calvin yani baba yake Diana. Wito huo ulimfikirisha sana Owen kwani alishajua Diana pia alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ile ile ya baba yake. Kitendo cha Owen kwenda kufanya kazi kwenye ile kampuni maana yake ni Kwamba angekuwa karibu sana na Diana hivyo ingempa tabu kumsahau mwanamke huyo. Yote kwa yote Owen hakutaka kuyapa nafasi mapenzi yaendeshe maisha yake badala yake aliamua kuweka kazi kama kipaumbele chake. Owen


aliamua kwenda kwenye interview. Alipofika kwenye ile kampuni alipokelewa na sekretari kisha akapewa maelezo ya kufika kwenye ofisi ya Meneja mwajiri ambako interview zilikuwa zinafanyika. Owen alipiga hatua kuelekea kwenye ofisi aliyoelekezwa na alipofika tu, alijikuta anashtuka. Mtaalamu alishtuka baada ya kukutana uso kwa uso na Diana ndani ya chumba cha Meneja mwajiri. Diana ndo alikuwa amekaa kwenye kiti na meza ya Meneja mwajiri wa kampuni ile. Kwa


tafsiri rahisi ni kwamba Diana ndo alikuwa Meneja mwajiri kwenye ile kampuni ya baba yake. Diana ndo alikuwa mtu wa mwisho kuamua nani anastahili kuajiriwa na nani hastahili. Mara ya baada ya kukutana uso kwa uso, Diana na Owen walibaki wanatazamana tu kwa mshangao. Owen alishindwa kuendelea kupiga hatua hivyo alisimama tu huku akimtazama Diana. Walitazama vile vile kwa takribani dakika mbili pasipo kusikika sauti yoyote ile. Wakati wameganda kwenye lile pozi,


Ghafla mlango uligongwa. Hapo sasa Owen aliamua kupiga hatua na kwenda kukaa kwenye kiti huku akiwa na bahasha yake mkononi. Diana alimruhusu kuingia yule aliyekuwa anagonga mlango. Dakika zile zile yule mgongaji aliingia. Alikuwa ni mfanyakazi mmoja hivi wa kike aliyejaliwa uzuri na urembo. "Boss, kuna zile documents za jana tayari nimeshazifanyia kazi kwahiyo nimekuletea uzipitie na utie saini ili zifike kwa Mkurugenzi.!" Yule mwanadada


alizungumza kauli hiyo huku akimkabidhi Diana bahasha yenye karatasi ndani yake. Diana alipokea ile bahasha, akatoa zile karatasi na kuanza kuzisoma. Baada ya dakika kadhaa alizisaini na kupiga mhuri. Alipomaliza kufanya hivyo alimkabidhi yule mwanadada kisha akamruhusu kuondoka. Muda wote Owen alikuwa anamtazama yule mwanadada kwa namna alivyokuwa mrembo. Mtaalamu alijikuta anakumbuka maneno ya kaka yake Robyson


kwamba dunia ina wanawake wengi sana na kila siku wazuri wanazidi kuzaliwa. Hapo sasa Owen aliamini kauli ya kaka yake kupitia muonekano wa mwanadada yule. "Owen! Umekuja kwenye interview ya kazi au umekuja kutazama na kuwatamani wafanyakazi wa kike?" Hiyo ilikuwa kauli ya Diana baada ya kumuona Owen amehamishia akili na macho yake kwa yule mfanyakazi wa kike aliyetoka.


Diana alizungumza kauli hiyo kwa hasira kwa maana ya kwamba hakufurahishwa kabisa na suala la Owen kumtamani yule mfanyakazi wa kike. Ni dhahiri kabisa kulikuwa na taswira ya wivu wa kimapenzi iliyojichora ndani ya moyo wa Diana juu ya Owen. NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu} EPISODE: 08 AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller)


Owen hakujibu chochote badala yake aliendelea kumtazama Diana. Diana alimtaka Owen amkabidhi vyeti vya taaluma pamoja na CV zake. Owen akamkabidhi bahasha yenye vyeti Diana. "Owen, Sina mashaka juu ya taaluma yako hivyo kesho asubuhi na mapema utafika hapa na kuanza kazi rasmi. Lakini nakukumbusha tu Owen unakuja hapa kufanya kazi sio mapenzi. Kampuni yetu ina wanawake


wengi wazuri lakini usije ukatumia uhensamu wako kama silaha ya kuwavuruga wasichana. Nikiwa kama Mwajiri wako sitovumilia kuona masuala hayo hivyo nitakufukuza kazi bila kujali status yako.!" "Diana kwani bado unanipenda?" "Kha! Swali gani hilo unaniuliza Owen? Kwanini nikupende wakati wewe ni shemeji yangu.!" "Sasa kwanini unaongea kauli za wivu kwangu?"


"Kauli za wivu? Wivu upi huo unaouzungumzia? Kwahiyo mimi kukupa utaratibu wa kampuni ni wivu? Au hujui mimi ni nani kwenye hii kampuni? Ok ngoja utaelewa kesho ukishaanza kazi. Yani kuanzia kesho utanisalimia na kuniita jina langu kwa heshima na adabu.!" "Sawa nitakuheshimu Madam Diana.! Lakini kaa ukijua kwamba nilikuwa na maswali mengi sana ya kukuuliza lakini yote nimeyafuata. Sihitaji tena


kukuuliza swali lolote linalohusu mahusiano yako. Namshukuru Mungu amenipa ujasiri wa kuvumilia maumivu hivyo kwa sasa akili na moyo wangu upo kwenye kazi tu. Nimekuja hapa kufanya kazi na sio kufuata mapenzi. Sina nia wala lengo la kurudisha tena mahusiano na wewe. Kaka yangu mimi anakupenda sana hivyo nitakuheshimu kama shemeji yangu ukiwa kwenye mazingira ya nyumbani. Lakini pia ukiwa kazini nitakutii na kukuheshimu kama boss wangu. Usiwe na


wasiwasi wowote kuhusu hilo.!" Owen aliongea kauli hiyo huku akimtazama Diana machoni. Hakukuwa na interview nyingine kwa Owen zaidi ya mazungumzo hayo. Owen aliondoka kwenye ile kampuni na kurudi nyumbani kwao. Siku iliyofuata aliamka asubuhi na mapema na kwenda kuanza kazi rasmi. Alifika mapema kwenye kampuni na kukabidhiwa mwenyeji wake kwa ajili ya kumpa muongozo katika kitengo chake. Owen aliajiriwa katika kitengo cha teknolojia ya


habari na mawasiliano ndani ya kampuni hiyo. Mtaalamu alianza kazi rasmi huku akiwa na uhakika wa kuingiza kiasi kikubwa cha pesa kila ifikapo mwisho wa mwezi. Alifanya kazi kwa weledi mkubwa sana hivyo mambo yakawa yanaenda vyema sana kwenye kitengo chake. Kila siku alikuwa anabuni vitu vipya vilivyopelekea mabadiliko chanya kwenye kampuni ile. Viongozi wakubwa wa kampuni ile walijikuta wanamkubali sana na kumwagia sifa nyingi nyingi. Owen alishirikiana vyema na


wafanyakazi wenzake kwenye masuala mbalimbali. Ndani ya muda mfupi tu aliofanya kazi ndani ya ile kampuni, Owen aliweza kuwa na marafiki wengi sana kutokana na upendo, ukarimu, busara na ucheshi wake. Hakuwa na maringo wala majivuno kwa wale aliowazidi cheo. Lakini siku zote kwenye maisha hakuna mtu anayeweza kupendwa na watu wote duniani hata awe mwema kiasi gani. Na siku zote ili ing'ae na kutoa mwanga basi ni lazima giza litande. Wakati nyota ya Owen


iking'aa ndani ya kampuni, kuna watu walikuwa wanachukizwa na mwanga huo. Wivu uliwatesa sana juu ya Owen. Miaka yote walikuwa pale kwenye kampuni lakini hawakuwahi kupewa sifa kama alivyokuwa anapewa Owen. Wafanyakazi wengi wa kike walionekana kumshobokea na kumpenda sana Owen kitu ambacho kiliwachukiza wafanyakazi wengi wa kiume. Wakati Owen anaongeza marafiki, lakini pia idadi ya maadui ilikuwa inaongezeka upande wake. Baadhi yao


walikuwa wanapanga njama na mikakati ya kumuharibia kazi ili afukuzwe kabisa kwa kuwa alizima kabisa majina yao kila sehemu. Mwezi mmoja ulikatika na tayari Owen alishayazoea mazingira na watu wote kwenye ile kampuni. Hakuna kitu kilichokuwa kigeni tena kwake. Tayari alishaonja matunda ya elimu yake kwa mara ya kwanza kabisa. Ule mshahara wake wa kwanza aliutumia kama sadaka kwa Mungu wake. Alinunua chakula na kupeleka kwenye vituo vya kulelea watoto yatima


na hiyo ilikuwaga ahadi yake tangu alipokuwa anasoma. Katika kipindi chote cha mwezi mmoja alichokuwa kwenye kampuni, Owen aliendelea kukumbuka matukio mbalimbali aliyoyapitiaga na Diana siku za nyuma. Haikuwa rahisi kwake kusahau kwa kuwa kila siku alikuwa anaonana na Diana. Lakini pia kuna muda Robyson alikuwa anafika pale kwenye kampuni kwa ajili ya kumchukua Diana baada ya muda wa kazi kumalizika. Owen alikuwa anaumia sana alipokuwa


anawaona Diana na Robyson wakiwa wamepakizana kwenye gari na kuondoka zao. Wafanyakazi wa ile kampuni walikuwa wanamjua Robyson kama ni mchumba wa Diana na walikuwa wanasubiri tarehe ifike ili wafunge pingu za maisha. Diana alikuwa anafurahia sana ile hali bila kujali maumivu aliyokuwa anapitia Owen kwa wakati ule. Kitu pekee kilichokuwa kinampa nguvu na amani kijana Owen ni kauli moja tu aliyowahi kuambiwa na binti mmoja ambaye alionana nae


mara moja tu katika maisha. Alikumbuka aliwahi kuambiwa na Laurine "Sio kila unachokipoteza ni hasara, vingine ni faida". Kauli hiyo ilikuwa inampa nguvu kubwa sana ya kuamini pengine kumpoteza Diana kuna faida kubwa kuliko hasara kwa upande wake. Siku zote taswira ya Laurine ilikuwa inamjia sana Owen kichwani mwake. Owen alipanga kumtafuta Laurine ili amlipe japo theluthi ya wema aliomtendea ile siku. Owen aliamini kwamba Laurine hakustahili kabisa kuishi kwenye


maisha aliyokuwa anaishi. Mtaalamu aliamua kupanga safari na kwenda kwenye lile danguro alilokutanaga na Laurine kwa mara ya kwanza kabisa. Mnamo majira ya usiku wa saa sita Owen aliendesha gari lake mpaka kwenye lile danguro la wadada wanaouza miili yao. Alipofika tu madada poa walilizunguka gari lake na kuanza kujipigia mnada kama ilivyokuwa kawaida yao. Owen hakuzungumza chochote zaidi ya kuanza kuangaza macho kwenye sura za wale wadada ili


kumtafuta mtu wake. Alipitisha macho kwenye nyuso zote lakini hakufanikiwa kabisa kuona sura ya Laurine. Kwa kuwa alikuwa analijua jina la Laurine, aliamua kumuulizia kwa wale wenzake. Hilo jibu alilopewa lilimchoma sana moyoni. Aliambiwa kwamba Laurine ametoka na mteja mwingine muda mfupi uliopita. Owen aliwasha gari na kuondoka kwa hasira baada ya kupewa taarifa ile. Ni kama vile aliumia baada ya kujua Laurine amechukuliwa na mwanaume mwingine. Kwa namna


alivyoumia moyoni, yeye mwenyewe hakujua ni kwanini aliumizwa na taarifa ile ilihali hakuwa na mahusiano ya kimapenzi wala undugu na Laurine. Kwa hasira alizozipata alijikuta tu anajisemea moyoni kuwa hatorudi tena kwenye lile danguro kumtafuta Laurine. Alikaa takribani siku tatu bila kwenda tena kwenye lile danguro. Msimamo aliouweka akilini mwake ulikuwa ni kuachana kabisa na wazo la kumtafuta Laurine lakini moyo wake ukaenda kinyume na akili.


Moyo ulimtaka Owen amtafute Laurine. Ile stori ya maisha ya Laurine na namna alivyoonesha upendo na uaminifu ile siku walipokuwa Lodge ni kama aliugusa moyo wa Owen. Owen aliamua kwenda tena kwenye lile danguro la makahaba kwa ajili ya kuonana na Laurine. Lakini sasa, alipofika alikuta lile eneo limepooza na hakukuwa na kahaba yeyote ile siku. Aliganda eneo lile kwa takribani lisaa zima lakini hakufanikiwa kumuona mdada yeyote katika eneo lile. Mpaka kufikia majira ya saa saba


na nusu usiku aliamua kurudi nyumbani kwao huku akiwa na mawazo mengi juu ya Laurine. Siku iliyofuata alienda kazini kama kawaida yake na yalipofika majira ya usiku akaenda tena kwenye lile danguro lakini hakufanikiwa kabisa kumuona kahaba yeyote kwenye eneo lile. Alijiuliza kulikoni tena wale wadada hawaonekani kwenye lile eneo. Alianza kupata hisia pengine labda walikuwa wamehamisha ofisi yao. Alijikuta ananyong'onyea kwani hakujua ni wapi angempata Laurine.


Pembezoni mwa lile eneo la danguro kulikuwa na kibanda cha chipsi hivyo Owen aliamini yule muuzaji anaweza kumfahamisha chochote kuhusu wale makahaba kutokana na kuwa mwenyeji sana katika eneo lile. Owen aliteremka kwenye gari na kwenda kwenye kile kibanda cha biashara ya chipsi. Kwanza kabisa alimuomba muuza chipsi amtengenezee chipsi yai moja pamoja na mishikaki miwili. Yule kijana akaanza kutengeneza chipsi yai kama alivyoagizwa. Wakati anaendelea kutengeneza,


Owen alimsogelea yule kijana na kumuuliza kama kijana mwenzake kuhusu wale makahaba. "Oya mwanangu, hivi hawa malaya mbona sijawaona siku mbili hizi? Au wamehamisha ofisi zao kimya kimya bila kutujuza sisi wateja wao?" Owen alimuuliza yule muuza chipsi. "Hahah! Hawajahama braza ila juzi ilikuja difenda ikawazoa malaya wote na kuondoka nao. Mpaka sasa wapo kituo cha


polisi, Oysterbay.!" Muuza chipsi alimjibu Owen kauli hiyo na kumfanya ashtuke kwa marefu na mapana. Taarifa ya kukamatwa kwa wale makahaba ilimfikirisha sana Owen. Mtaalamu alijiuliza kitu gani afanye kwa ajili ya kumsaidia Laurine. Wakati anaendelea kuwaza, alikabidhiwa chipsi alizoagiza kisha akaanza kupiga hatua kulifuata gari lake. "Oya braza, haujanilipa pesa yangu bado.!" Yule muuza chipsi


alizungumza kauli hiyo baada ya kumuona Owen anaondoka bila kulipia chipsi alizoagiza. Owen alisimama kisha akatoa noti ya shilingi elfu tano kwenye wallet yake kisha akamkabidhi yule muuza chipsi na kuondoka pasipo kusubiri chenji. Kiufupi Owen ni kama alichanganikiwa baada ya kuambiwa Laurine alikuwa chini ya jeshi la polisi. Usiku ule ule aliamua kukanyaga mafuta na kuanza safari kuelekea kwenye kile kituo cha polisi kilichowashikilia wale


wadada poa. Alifanikiwa kufika kwenye kituo cha polisi kisha akaenda moja kwa moja kwa askari waliokuwa zamu usiku ule. Alipofika aliwasalimia na kujieleza kwamba yeye ni kaka wa mmoja kati ya makahaba waliokuwa wamewakamata wakiuza miili yao barabarani. Alieleza pia dhamira yake kuu iliyompeleka pale ni kumtolea dhamana au kumlipia faini mdogo wake ili awe huru. Wale askari walivyosikia habari ya dhamana na faini wakajua kwamba kijana alikuwa na pesa


hivyo wakaamua kumsikiliza na kwenda nae taratibu ili wavune mapene. "Kijana, ni kweli tuliwakamata Machangudoa juzi usiku na idadi yao ilikuwa kama watu saba hivi. Lakini mpaka sasa tumebaki na mtuhumiwa mmoja tu hapa ndani. Tumewaachia huru watuhumiwa sita baada ya kulipa faini kulingana na makosa yao. Sasa hapa sijui aliyebakia ndani ndo ndugu yako au laa! Kwani wewe ndugu yako anaitwa nani?" Mmoja kati ya wale askari wa


zamu aliongea kauli hiyo alimuuliza swali Owen. Owen hakupata tabu kujibu swali la afande kwani alikuwa analifahamu vyema jina la Laurine mpaka la baba yake kwa kuwa tayari alishasimuliwa hadithi fupi kuhusu mtoto wa kike. Baada ya Owen kulitaja lile jina wale askari walimwambia kwamba jina alilolitaja ndo lilikuwa jina la mtuhumiwa aliyebaki ndani ya kituo cha polisi. Ni kweli, Laurine ndo kahaba pekee aliyekuwa amebaki


ndani ya kituo cha polisi mara baada ya kukosa ndugu au jamaa wa kumlipia faini ili awe huru. Owen alizungumza kiutu uzima na wale askari kisha akaambiwa amlipie faini Laurine. Kiasi cha shilingi laki tano za kitanzania kilihitajika ili kumfanya Laurine kuwa huru. Suala la pesa kwa Owen halikuwa tatizo kabisa hivyo alilipa pesa yote pale pale. Mmoja kati ya wale askari alienda sero kisha akamtoa Laurine. Baada ya kutolewa sero, Laurine alishtuka kumuona Owen


mbele yake. Hakutarajia kabisa kama siku moja angekuja kuonana au kusaidiwa na mtu huyo. Zile siku mbili alizokaa sero zilimdhoofisha sana Laurine. Sio kudhoofika tu bali hata kuchakaa. Owen alimtazama mtoto wa kike na kujikuta anamuonea huruma. Alimsogelea na kumwambia kwamba waondoke eneo lile kwani yupo huru kuanzia muda ule. Wakati wanaondoka askari aliongea na kumkumbusha Laurine kwamba ukahaba na uchangudoa sio ajira inayoakisi


maadili ya nchi hivyo atafute kazi nyingine ya kufanya. Akampa na onyo kabisa kama akikamatwa tena na hatia ya kosa la ukahaba basi hatolipishwa tena faini badala yake atapelekwa jela moja kwa moja. Owen alimfungulia Laurine mlango wa gari akaingia kisha nae akaenda kuingilia mlango wa upande wa pili. "Laurine! Kuwa huru kuanzia sasa upo kwenye mikono salama. Chukua hizi chipsi ule alafu nipe maelezo nikufikishe


mahala unapoishi ukapumzike.!" Owen alizungumza kauli hiyo huku akimtazama Laurine Kabla Laurine hajafanya chochote alianza kuhisi kizunguzungu kisha akafumba macho na kudondokea begani kwa Owen. Owen alimtingisha mtoto wa kike ili aamke ila akagundua kuwa alipoteza fahamu. Owen alichanganikiwa ghafla. Alimgusa kifuani akagundua kwamba bado mapigo ya moyo yalikuwa yanadunda. Akampima joto la


mwili kwa viganga vya mikono na akagundua joto la mwili wa Laurine lilikuwa kubwa kuliko kawaida. Owen alijua kabisa Laurine alikuwa mgonjwa hivyo aliwasha gari na kuanza kuitafuta hospitali ili kuokoa maisha ya mtoto wa kike. Hakuchukua muda mrefu aliweza kufika hospitalini. Bila kuchelewa mgonjwa wake alipokelewa na kuingizwa kwenye chumba cha matibabu. Madaktari walimfanyia vipimo Laurine na kubaini kwamba alikuwa na ugonjwa wa Malaria.


Walimdunga sindano kisha wakamtundika dripu ya maji usiku ule ule kwani hali yake haikuwa nzuri kabisa. Daktari alimpongeza sana Owen kwa kumuwahisha mgonjwa hospitali kwani Laurine angechelewa kupatiwa matibabu basi angeweza kupoteza maisha. Usiku ule Owen alilazimika kubaki kule kule hospitalini kwa ajili ya uangalizi wa mgonjwa wake. Alitamani kupiga simu kwa watu wa karibu wa Laurine ili kuwapa taarifa kuhusu ndugu yao lakini hakuwa na namba zao.


Mbaya zaidi ni kwamba Laurine mwenyewe hakuwa na simu kwa wakati ule. Simu yake ilidondokaga kwenye purukushani ile siku waliyokamatwa na askari polisi. Owen alilazimika kubaki na mgonjwa kwa kuwa yeye ndo alikuwa ndugu pekee wa Laurine kwa wakati ule. Uzuri ni kwamba siku iliyokuwa inafuata ilikuwa ni weekend ya mapumziko hivyo Owen hakuwa na ratiba ya kwenda kazini. Alichokifanya mtaalamu ni kupiga simu nyumbani kwao na


kuwafahamisha kwamba yupo salama kabisa Ila hatorudi ile siku. Kwa kuwa Owen alishafikisha umri wa utu uzima, wazazi hawakumuuliza kijana wao mahala alipokuwa na kitu alichokuwa anafanya. Kwa mara ya kwanza kabisa katika maisha yake, Owen alijikuta anakesha akiwa amekaa. Alikaa pembezoni mwa kitandani cha mgonjwa wake usiku kucha huku akiomba dua kwa Mungu wake ili amponye mtoto wa kike. NOVEL: MY VALENTINE (MV14)


{Kipenzi Changu} EPISODE: 09 AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller) Asubuhi ilipofika Laurine alirudisha fahamu na kufumbua macho yake. Alimuona Owen akiwa amekaa pembeni yake. Wakati huo bado alikuwa ametundikiwa dripu ya maji mwilini mwake. Laurine hakushangaa kujikuta hospitali kwa sababu mara ya mwisho alipata homa alipokuwa sero.


"Wow! Hatimaye umeamka sasa Laurine! Vipi unajisikiaje lakini?" Owen alizungumza kauli hiyo mara baada ya Laurine kuamka. Laurine hakujibu chochote badala yake alianza kujiinua ili akae. Owen alimsogelea Laurine na kumsaidia kuinuka pale kitandani kisha akamkalisha kitako. "Laurine, unajisikiaje" Owen alimuuliza Laurine kwa mara nyingine.


"Nahisi kukosa nguvu na maumivu ya kichwa kwa mbali.!" Laurine alijibu kwa sauti ya chini kabisa. "Ok, usijali utakuwa sawa tu ila kwa sasa tusubiri umalizie hiyo dripu ya maji kisha ule na umeze dawa. Nilikuleta hapa hospitali tangu jana usiku ulipopoteza fahamu. Dokta amekupima na alibaini kuwa una vijidudu vya Malaria mwilini mwako. Kwahiyo kuwa na amani kabisa maana tumefanikiwa kuwahi matibabu.!"


"Kaka eeh! Basi mimi hapa mimi, nakushukuru sana wewe. Asante sana kwa wema wako kakaa.!" Laurine alizungumza kauli hiyo huku akitokwa na machozi "Laurine! Kwa sasa tuangalie kuhusu afya yako hizo asante tutazijadili baadae. Sawa eeh?" "Sawa kakaa lakini asante sana kwa kunijali mimi. Jana nilipokuwa sero nilikata kabisa tamaa ya kuishi. Kwa namna nilivyokuwa naumwa nilijua


kabisa kama ningelala pale usiku basi nisingeiona hii leo. Tayari nilishakosa tumaini la kuishi ila ukajitokeza wewe na kuja kunisaidia. Kiukweli kabisa sikuwahi kufikiria kama siku moja ungekuja kunitafuta mimi mshezi wa tabia. Nashukuru sana kaka. Lakini pia naomba unisamehe kwa kukupotezea muda wako kakaa.!" "Laurine! Kwanza kabisa naomba unisamehe mimi kwa kuchelewa kuja kukutafuta. Yani ilikuwa ni lazima tu mimi nije kukutafuta ili


nikupe shukrani kwa yote uliyonitendea ile siku tuliyokutana kwa mara ya kwanza. Ulionesha huruma na upendo mkubwa sana kwangu. Niliifurahia na kuipenda sana ile supu uliyoniachia. Kubwa zaidi uliniachia ujumbe ulionisaidia kwa kiasi fulani kujenga saikolojia yangu. Nilitamani sana kukushukuru lakini sikukuona tena.!" Hayo yalikuwa mazungumzo machache baina ya Owen na Laurine. Baada ya muda fulani


kupita, dripu ya maji aliyotundikiwa Laurine iliisha. Owen alikuwa tayari ameshamnunulia mgonjwa chakula hivyo alihakikisha anakula na kushiba. Laurine alikula chakula cha asubuhi kisha akanywa dawa. "Laurine, Una namba ya simu ya mtu wako wa karibu ili tumfahamishe kuhusu hali yako na wapi ulipo kwa sasa?" Owen alimuuliza Laurine "Hapana kaka sina namba zao


marafiki zangu kichwani. Lakini usijali kaka, kwa sasa hali yangu sio mbaya hivyo naweza kurudi tu nyumbani. Najua una mambo mengi ya kufanya hivyo sihitaji kuendelea kukupotezea muda wako. Mpaka sasa umenisaidia kwa kiasi kikubwa sana kaka yangu.!" "Laurine! Bado hali yako haijakaa sawa hivyo huwezi kutoka hospitali siku ya leo. Hapo ulipo umeandikiwa sindano nne na mpaka sasa umeshachoma sindano moja tu. Saa nane


mchana baadae itabidi uchome sindano ya pili. Sindano ya tatu utachoma saa nne usiku na sindano ya mwisho utachoma kesho saa kumi na mbili alfajiri. Kiufupi ni kila baada ya masaa nane utachoma sindano. Baada ya hapo afya yako itakuwa imeimarika hivyo utakuwa huru kurudi nyumbani. Usijali kuhusu muda wangu. Mimi nipo hapa kwa ajili ya kukusaidia wewe. Nitakuwa nawe bega kwa bega mpaka afya yako itakapoimarika.!" Owen alizungumza maneno hayo huku


akim'miminia maji ya kunywa Laurine kwenye glasi "Kaka eeh, Asante sana kaka yangu. Kiukweli kabisa nakushukuru sana kwa kunijali mimi.!" Laurine alizungumza kauli hiyo huku akifuta machozi yaliyokuwa yanatiririka mashavuni mwake. Ratiba ya Owen muda ule ilikuwa ni kurudi nyumbani kwao kwanza. Alimuaga Laurine kwamba anaondoka ila atarudi majira ya mchana.


"Laurine, Mimi ndo naondoka muda huu ila zingatia sana mambo niliyokuambia. Maagizo yote nimeacha kwa Nesi. Ukiwa na tatizo lolote usisite kumwambia yeye. Mimi sitochelewa lakini, nitarudi kabla ya saa nane, Umenielewa Laurine?" "Ndio kakaa nimekuelewa.!" "Haya niambie basi nikuletee chakula gani mchana?"


"Chochote kile kaka mimi nitakula.!"

"Hahah! Mimi nataka uchague chakula kizuri ukipendacho wewe mgonjwa wangu.!" "Kakaa eeh! Chochote utakachoweza kukipata mimi nitakula. Ukileta magimbi, ugali, wali, pilau, mihogo hata mlenda nitakula mimi.!" "Hahah! Basi sawa nakuletea chi..chi..chiiipsiii. Najua hiko ndo chakula kinachopendwa zaidi na


nyie wadada wa kibongo. Bila shaka hata wewe unapenda. Si eti eeh? Au hupendi nisilete?" "Mmh! Napenda mnoo.!" "Basi sawa nakuletea chipsi yai na kuku mzima. Sasa ole wako usimalize, Yani tutagombana hapa hapa hospitali.!" "Mmh! Jamani kaka, Ndo kuku mzima? Hapo utanionea bure kaka.!" "Hahah! Mimi nataka ule vizuri na


ushibe mgonjwa wangu.!" Owen aliondoka na baadae alirudi pale hospitali kama alivyoahidi. Siku ile alishinda pale hospitalini pamoja na Laurine. Yalipofika majira ya usiku Owen alitakiwa kuondoka na kurudi nyumbani kwao. Siku ile alitakiwa kulala nyumbani kwao kwani siku iliyokuwa inafuata alitakiwa kuripoti kazini. Uzuri ni kwamba hali ya Laurine haikuwa mbaya mpaka kufikia muda ule. Owen alimlipa pesa Nesi mmoja ili amuangalie Laurine kwa


ukaribu na kumpa chakula kwa wakati. Ilibidi iwe hivyo kwa kuwa Laurine hakuwa na mtu yeyote wa karibu wa kuweza kumuuguza. "Laurine! Mimi narudi nyumbani muda huu. Kesho jioni nikitoka kazini nitapitia hapa. Daktari amesema kama hali yako itakuwa vizuri basi tutaruhusiwa kuondoka. Majukumu yangu kwako nimemwachia yule Nesi. Hakikisha unakula vizuri na kushiba na pia unywe dawa kwa wakati.!" Owen alizungumza


maneno hayo kisha akaondoka pale hospitalini. **** Siku iliyofuata Owen aliripoti kazini asubuhi na mapema. Aliwajibika kama kawaida yake na mpaka kufikia majira ya saa 10 jioni, muda wa kazi ulikuwa umetamatika. Owen alipanda gari lake na kuondoka bila kupoteza muda. Kabla hajafika nyumbani kwao alienda moja kwa moja hospitalini alipokuwa Laurine. Alipofika alifurahi sana


kumkuta Laurine akiwa amepata afueni ya kutosha. Hali yake ilikuwa nzuri kwa kiasi fulani. Daktari aliweza kuwaruhusu waondoke ila kabla hawajatoka aliwataka waende wakalipie gharama zote za matibabu. Aliwatajiwa kiasi chote cha pesa walichokuwa wanadaiwa pale hospitalini. Kiasi cha pesa kilichokuwa kinahitajika kilikuwa kikubwa kiasi kwamba kilimshtua Laurine. Owen yeye hakushtuka kabisa. Alienda kwenye dirisha la malipo kisha akalipia kiasi chote cha pesa kilichokuwa


kinahitajika. Ukweli usiopingika ni kwamba suala la pesa kwa Owen halikuwa tatizo kabisa. Nyumbani kwao kulikuwa na pesa na hata yeye mwenyewe alishapata ajira iliyokuwa inamlipa mshahara mkubwa na marupurupu pembeni. Owen alilipa deni lote kisha akamchukua Laurine, wakapanda gari na kuondoka zao. Walianza safari kuelekea uswahilini alipokuwa anaishi Laurine. Laurine alijikuta anamtazama sana Owen huku akijiuliza maswali yaliyokosa majibu juu ya


mwanaume huyo. Alishindwa kujua Owen ni mtu wa aina gani na kwanini alikuwa mwema kwake kwa kiasi kile. Ilikuwa vigumu sana kwa Laurine kuamini kwamba Owen alifanya vile kwa kuwa alikuwa na pesa nyingi. Katika maisha yake alikutana na watu wengi sana wenye pesa zaidi ya Owen lakini hakuna hata mmoja aliyediriki kumsaidia licha ya kuwaomba msaada. Hata wale waliompatia pesa walimpa kwa kuhitaji malipo ya ngono. Lakini kwa namna alivyokuwa anaonekana


Owen, Laurine aliamini kabisa jamaa hakuwa na lengo la kuhitaji penzi kutoka kwake. Owen alionekana kuwa smart sana kiakili hivyo isingekuwa rahisi kwake kumuhitaji kimapenzi mwanamke malaya, kahaba na anayeuza mwili wake. Baada ya kuwaza hivyo, Laurine aliona ni bora amuulize tu Owen ni kwanini ameamua kuwa mwema kwake. "Kaka eeh, lakini kwanini wewe apo umeamua kuwa mwema kwangu kiasi hiki? Kwanini


umenisaidia sana mimi?" Laurine alimuuliza Owen swali hilo kwa upole na unyenyekevu wa hali ya juu. "Hahah! Laurine, Kwahiyo muda wote umekaa kimya ulikuwa unawaza hilo swali Laurine?" "Ndio Kaka, naomba kujua sababu iliyokupa msukumo wa kunitafuta na kunipa msaada ambao umeacha deni zito kwenye moyo wangu. Kwanini umefanya hivyo kakaa?"


"Laurine, hili nililolifanya kwako halijafikia hata theluthi ya wema uliowahi kunitendea mimi. Wema wako wewe siwezi kuulipa ila nilikutafuta nilipe japo theluthi yake na kukupa shukrani kwa wema ulionitendea mimi.!" "Mmh! Wema niliokutendea? Wema gani niliokutendea mimi kaka? Mbona sikumbuki kama nilishawahi kukufanyia jambo kubwa kwenye maisha yako? Tulikutana siku moja na hakuna chochote cha ajabu nilichokifanyaga kwako.!"


"Laurine, wewe ndo mtu wa kwanza kabisa kuguswa na maumivu niliyokuwa nayapitia mimi. Ulinifariji na kuniachia kikaratasi chenye maneno ya kumtia mtu moyo. Ule ujumbe ulioniachia umeweza kunisaidia kwa kiasi kikubwa sana. Ulinihurumia sana ulivyoona pombe zimenikamata kichwani kwangu na ulijua kabisa sikuwa mlevi. Ulionesha uaminifu mkubwa sana dhidi ya mali zangu kwani ulizilinda licha ya kwamba ulikuwa na uwezo wa


kuniibia. Ukaenda mbali zaidi, uliamua kuninunulia supu kwa pesa yako ili niondoe arosto ya pombe na nipate nguvu mwilini. Unaweza kuhisi kile ulichokifanya ni kidogo lakini kwangu mimi kimebeba tafsiri kubwa sana ya upendo na moyo wa kujali. Lakini pia ile hadithi ya maisha yako ilinigusa sana moyoni mwangu ndo maana nikaamua kukutafuta. Wewe ni kahaba Laurine lakini nimeshajua kwamba ni changamoto tu za maisha ndo zimekufanya ujiingize kwenye hiyo kazi. Wewe


hustahili wala hufanani kabisa kufanya kazi unayofanya. Ninachotaka kukifanya sasa hivi ni kukusaidia kubadilisha taswira nzima ya maisha yako. Laurine! Sikuwahi kukuambia jina langu hapo awali. Mimi naitwa Owen James, kuanzia sasa unaweza kunichukulia kama kaka yako.!" NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu} EPISODE: 10 AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller)


Kauli ya Owen ilimfanya Laurine aanze kutokwa na machozi kwenye mboni za macho yake. Kila alipotamani kuzungumza ni kama alishikwa na kigugumizi kizito. Aliendelea kutokwa na machozi mpaka sauti ya kilio ikaanza kusikika. Owen alivyoona vile alitoa kitambaa mfukoni mwake kisha akaanza kumfuata machozi mtoto wa kike. "Laurine, unalia nini sasa? Huoni kama utajiongezea homa mwilini? Hebu nyamaza kulia


basi dada'angu. Au hupendi niingilie maisha yako?" Owen alimuuliza Laurine. "Kaka Owen! Asante sa.. sa.. sana. Asante sana kaka'angu. Nalia sio kwa sababu nahuzunika ila nalia kwa sababu nina furaha mimi. Kaka eeh, kwa kipindi chote nilichoishi ndani ya hili jiji nimekutana na watu wengi sana wenye pesa lakini hakuna hata mmoja aliyewahi kusikiliza shida zangu licha ya kuwatangazia. Ni wewe Tu ndo umeonesha moyo wa huruma na kunisaidia licha ya


kwamba sikukuomba msaada. Asante sana kaka Owen, siku zote nitaukumbuka wema wako kwangu.!" "Usijali kwa hilo Laurine, haya futa machozi basi. Huu ni muda wa kuanza kufurahia maisha sio kulia lia tena.!" Owen alizungumza maneno hayo huku safari yao ikizidi kusonga mbele. Baada ya mwendo wa takribani dakika thelathini, hatimaye walifika kule alipokuwa anaishi Laurine. Kwa kuwa hakukuwa na


njia pana ya kupita gari mpaka uwanjani kwa akina Laurine, walipaki gari njiani kisha wakaanza kutembea kwa miguu vichochoroni mpaka walipofika pale alipokuwa anaishi Laurine. Yalikuwa mazingira ya uswahilini kweli kweli. Nyumba ilikuwa imechoka na kuchakaa na wapangaji wote walikuwa wanawake ambao hawakuolewa. Ni wale wale makahaba waliokuwa wanajiuza kule barabarani. Picha linaanza walikutana na bonge moja la timbwili. Wadada walikuwa


wanatoleana matusi mazito kufuatia ugomvi wao. Kulikuwa na makundi mawili yaliyokuwa yanagombana na walichokuwa wanagombania ni mabwana. Owen alipowatazama aliweza kuzikumbuka baadhi ya sura za wadada wale kwani aliwaonaga kule kwenye danguro. Mavazi ya wale wadada yalikuwa nusu uchi mpaka Owen aliona aibu kuwatazama. Hata Laurine nae alimuonea aibu Owen baada ya kuona ule ugomvi. Aliona aibu kwa kuwa ile ndo ilikuwa kama familia yake na yale ndo yalikuwa


maisha yao ya kila siku. "Kaka Owen, hapa ndo mahali ninapoishi mimi siku zote. Kile chumba cha nje ndicho ninachoishi na wenzangu. Hizo vurugu na ugomvi unaouona hapo ndo maisha yetu ya kila siku. Naomba unisamehe mimi kwa kukuleta kwenye eneo kama hili. Najua ulichokiona hakijakufurahisha na ndio maana sikutaka ufike mpaka hapa. Mazingira ya watu ninaoishi nao nayajua vyema ndo maana nilitaka uishie kule ulipopaki gari.


Nisamehe mimi kaka Owen.!" Laurine alizungumza kauli hiyo baada ya kukuta machafuko pale kwao. Wanawake wazuri kabisa walivaa nguo fupi na zenye kuonesha maungo yao ya ndani. Owen alisikitika sana kuona taifa linahangamia kwa kuwa na watu waliokosa maadili. Owen aliamini asilimia kubwa ya wale wadada walikuwa wanajiuza kutokana na ukosefu wa ajira na ugumu wa maisha. Laiti kama serikali na wadau mbalimbali


wangejitolea kuwawezesha kiuchumi wale wadada basi zile biashara zingepotea kabisa kwenye sura ya nchi. Ukiwakamata makahaba ukawaweka sero na kisha kuwatoza faini haisaidii kutokomeza biashara ya ngono bali inajaza matumbo ya askari polisi wanaoenda kuwakamata. Kesho kahaba anarudi tena mtaani, hana ajira, hana elimu na pesa ambayo angeweza kuitumia kama mtaji wa biashara alishalipia faini kituo cha polisi. Unategemea atafanya kazi gani?


Ni ngumu sana kuzuia biashara ya ngono kwa njia ya kama hiyo. Owen alimtazama Laurine kisha akamjibu, "Laurine, usijali kabisa kuhusu mimi. Wewe nenda ukapumzike ndani muda huu. Kwa kuwa tayari nimeshapafahamu hapa unapoishi basi kesho majira kama haya nitakuja kukujulia hali baada ya kutoka kazini.!" "Kaka Owen, usiwe na mashaka tena kuhusu mimi. Wewe endelea tu kufanya shughuli zako mimi


nitakuwa salama kabisa hiyo kesho. Mpaka hapa ulipofikia umenisaidia kwa kiasi kikubwa sana kaka. Umetumia pesa zako nyingi kunitoa kituo cha polisi na kugharamia matibabu yangu hospitali. Sio hivyo tu, umepoteza mpaka muda wako kwa ajili yangu. Huna haja ya kupoteza tena muda wako kaka yangu. Mpaka kufikia hapa inatosha sana mimi kukushukuru wewe.!" "Laurine, Yani hapa bado kabisa sijafanya kitu chochote kwako.


Kila nikikutazama naona kabisa nina deni kubwa kwako na napaswa kulilipa. Nisikilize kwa umakini Laurine, kesho jioni nitakuja hapa majira kama haya. Tafadhali sana naomba nikukute usitoke kwenda mahala popote pale. Shika hiki kiasi kidogo cha pesa. Utafanya matumizi yako ya leo na kesho. Naomba usidiriki tena kwenda kwenye lile danguro.!" Owen alizungumza kauli hiyo huku akimkabidhi Laurine kiasi cha pesa. Laurine alipokea ile pesa kisha


akamshukuru Owen kwa mara nyingine. Wakati Owen akimkabidhi Laurine pesa, wale wadada wengine walikuwa wanatazama lile tukio. "Heheheee! Raha ya danga ulipate na ulichune bibi weee.... Chezea Queen Lau wewee.!" Wale wadada waliongea kwa pamoja maneno hayo kwa sauti ya juu huku wakigongeana mikono juu juu. Laurine alijisikia vibaya kwa mara nyingine. Aliona kama


wenzake walikuwa wanamuharibia kabisa kwa Owen. "Kaka Owen, naomba unisamehe mimi kwa niaba ya wenzangu. Fanya kama haujasikia kabisa kile walichoongea.!" "Laurine, ondoa hofu na mashaka juu yangu. Sio kusikia tu, hata kuona nitafanya kama sijawaona hao wenzako. Mimi nimekusikia wewe na kukuona wewe tu. Hata kesho nikija nitakusikia wewe na kukuona


wewe. Naomba ifikapo kesho muda kama huu basi ukae nje ili nisipate tabu kukuulizia. Nina imani kabisa Mungu atakuamsha salama siku ya kesho. Hakikisha unakula vizuri, kunywa maji mengi na uzingatie kunywa dawa kwa wakati. Sina kingine cha kuzungumza, Nakutakia jioni njema na ifikapo usiku ulale salama.!" Owen alizungumza kauli hiyo kisha akamruhusu Laurine aondoke. Laurine alianza kupiga hatua kuelekea kwenye nyumba


aliyokuwa anaishi. Owen aliona sio busara kuwadharau kabisa wale wadada wengine, aliwapungia mkono wa salamu kisha akageuka na kuondoka. Wale wadada kwa umalaya wao walijikuta wanamtamani Owen na vile alivyokuwa mtanashati na handsome. Kila mmoja alianza kumuonea wivu Laurine kwa kupata bonge la bwana. Yote kwa yote walimpokea mwenzao Laurine ambaye walimuachaga sero baada ya kukosa mtu wa kumlipia faini. Walifurahi tu mwenzao kurudi tena uraiani


huku akiwa na pesa mkononi. Walijua kabisa usiku wa ile siku wangekula na kushiba hata kama wasingeenda kwenye danguro. **** Siku iliyofuata Owen alienda kazini kama kawaida yake. Siku hiyo alikuwa na zoezi zito sana la kufanya kwenye kitengo chake. Lilikuwa ni zoezi la kutengeneza programu fulani yeye pamoja na wafanyakazi wenzake katika kitengo chao. Tangu asubuhi mpaka kufikia majira ya saa nane


mchana, zoezi lilikuwa bado halijakamilika. Chakula cha mchana kilipotayarika wafanyakazi walienda kwenye kantini yao maalumu kupata chakula. Ni Owen tu ndie hakuonekana kabisa kantini kuanzia kwenye chakula cha asubuhi mpaka kile cha mchana. Mtaalamu alikuwa bize na kazi kiasi kwamba hakuhisi njaa kabisa tumboni. Alidhamiria kufanikisha kwanza zoezi lake kisha awaze kuhusu chakula. Wakati anaendelea kupangilia data kwenye kompyuta yake ya


kazi, Ghafla alitokea mfanyakazi mmoja wa kike kwenye ofisi ya Owen. "Owen, kwahiyo leo hauna kabisa ratiba ya kula? Tangu asubuhi mpaka sasa ujala chochote kile. Sasa unafanyaje kazi bila kula?" Yule mwanamke alimuuliza Owen. Owen alisikia vyema lile swali lakini aliendelea kufanya kazi yake bila kujibu au kuzungumza neno lolote lile. Alifanya kama hakusikia ile kauli ya mtoto wa


kike. "Owen, mbona umenikalia kimya hivyo? Mimi nimekupitia ili tukapate chakula kwa pamoja.!" Yule mwanamke aliendelea kuongea kwa mara nyingine lakini bado Owen alikaa kimya. "Sasa jamani si unijibu tu kuliko kunikalia kimya kama tumegombana. Nijibu basi jamani.!" Kwa mara nyingine tena mtoto wa kike alizungumza maneno hayo.


Maneno yalikuwa mengi kiasi kwamba yalimpa kero Owen. "Salma.! Naomba uniache tafadhali. Kwani siku zote unaendaga kula na mimi? Em deal na mambo yako basi.!" Owen alimjibu yule mwanamke kauli hiyo huku akiendelea kufanya kazi yake bila kumtazama. "Ok, Sawa nimekuelewa lakini naomba unipe lile jibu langu basi nitaondoka.!"


"Jibu gani?" "Kuhusu ombi langu la kukupenda Owen.!" "Hivi Salma, nikupe jibu mara ngapi lakini? Si nilishakuambia sihitaji mahusiano na wewe Salma. Hebu niache nifanye mambo yaliyonileta kwenye Kampuni. Mimi sikuhitaji wewe na wala sihitaji vizawadi zawadi vyako unavyonileteaga.!" "Lakini Owen, hivi kwanini unapenda kunitenga mimi? Nina


kasoro gani mimi mpaka unashindwa kuelewa hisia zangu? Kitu gani nifanye kwa ajili yako ili uamini kwamba nakupenda? Hebu niambie, nini nikufanyie nini ili uamini kwamba nakupenda? Niambie Owen, nipo tayari kufanya chochote kwa ajili yako.!" "Ok, Ni hivi Salma kama kweli unanipenda basi naomba uniache huru na maisha yangu. Acha kunisumbua basi mbona wanaume tupo wengi kwenye hii kampuni. Kwanini unang'ang'ana


na mimi tu!" "Owen, tatizo moyo baba. Ni kweli wanaume wapo wengi na wananipenda na kunitongoza kila siku. Lakini tatizo babaa, Moyo wangu mimi unakupenda wewe tu. Kila siku nakufikiria wewe mpaka nashindwa kufanya kazi zangu kwa ufanisi. Nakupenda sana Owen. Au labda uvumi unaosambaa chini chini kuhusu mahusiano yako na Linda una ukweli ndani yake?" "Eti.! Mahusiano yangu na Linda?


Mbona hizo ni habari mpya kwangu. Ujue nyie watu sijui munanitafutia kitu gani haswa. Kwanza nani anasambaza huo uvumi?" "Awe nani sasa! Ni Linda mwenyewe ndo anasema na anafanya hivyo kumuumiza Ex-boyfriend wake ambaye ndo yule muhasibu wa hii kampuni. Si unaona siku hizi unachukiwa na Mr Kaysimat? Hivi ujajiuliza sababu ni nini mpaka akuchukie?!"


"Dah! Hii nchi ina watu wa hovyo sana. Yani mtu hujamtekenya ila anacheka. Je ukimtekenya, si atalala chali kabisa. Kwahiyo Linda anawaambia watu mimi ni mpenzi wake sio?" "Yeah! Anasema hivyo.!" "Sawa bhana, Ila naomba unisikilize kwa umakini Salma. Mimi sina mahusiano na mtu yeyote kwenye hii kampuni. Simuhitaji Linda wala sikuhitaji wewe. Kwa sasa nataka kuishi maisha yangu kivyangu vyangu.


Kwa sasa nimeamua kupumzisha moyo wangu maana niliupa mzigo mzito sana wa maumivu.!" "Lakini Owen, Mimi Nakupenda. Nakupenda sa...!" Salma alizungumza kauli hiyo lakini kabla hajamalizia maneno ya mwisho aliingia Bosi Diana. "Haya malizia kauli yako sasa. Unaogopa nini Salma? Malizia kwamba unampenda sana.!" Diana alizungumza kauli hiyo kisha akamkata jicho kali Salma.


NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu} EPISODE: 11 AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller) Salma aliamua kuondoka pale ofisini na kuwaacha Owen na Diana. Diana alianza kumtazama Owen kwa hasira mno. "Owen, kwahiyo umeamua kubadili ofisi na kuwa darasa la mapenzi sio?" Diana alimuuliza


Owen kwa hasira. "Me naona ni bora uzungumze kile kilichokuleta na sio kuzungumzia hiki ulichokikuta kwa kuwa hakikuhusu boss wangu.!" Owen alimjibu Diana. "Au sio? Naona umenizoea sana Owen ndo maana unanijibu kwa jeuri. Mimi ni boss wako kwa sasa hivyo nina haki ya kukuambia chochote ndani na nje ya ofisi.!" "Sikiliza Diana, Una haki ya


kuongea chochote kuhusu majukumu yangu ya kazi lakini sio mambo yangu binafsi. Mbona wafanyakazi wengi humu ndani wanazungumziaga masuala mapenzi? Mbona wafanyakazi wengi wanatongozana na kuoana kabisa kwenye hii kampuni? Ngoja nikutoe tu wasiwasi bosi wangu, Mimi najua wajibu wangu ndani ya hii kampuni kwahiyo usiwe na mashaka kabisa. Mapenzi ni kitu cha ziada hivyo hayawezi kuniharibia majukumu yangu ya kazi. Nitapiga kazi kama kawaida hata kama nikiwa


kwenye mahusiano.!" "Owen! Nimesema sitaki kusikia chochote kuhusu mapenzi. Fanya kazi iliyokuleta hapa.!" Diana aliongea kwa hasira. "Nilipataga nafasi ya kusoma vizuri mkataba wangu wa kazi na hii kampuni kabla sijausaini. Sikumbuki kama kuna kipengele kimepiga marufuku mahusiano ya kimapenzi baina ya wafanyakazi wa hii kampuni. Kikubwa nilichokiona ni kwamba kampuni huwa inatoaga bonus


maalumu kwa wafanyakazi waliokuwa kwenye ndoa. Lakini pia kampuni ina utaratibu wa kuandaa tafrija maalumu kwa wafanyakazi wake kila ifikapo Mei mosi na Februari 14 kila mwaka. Kwa ninavyofahamu mimi, Mei mosi ni sikukuu ya wafanyakazi na Februari 14 ni siku ya wapendanao. Kwahiyo basi kwa mujibu wa maelezo ya mkataba wa hii kampuni ni kwamba inatoa haki kwa watu kupendana na kuoana. Hata wewe ulivyovishwa pete siku chache zilizopita, wafanyakazi


wa hii kampuni ndo walijaa pale ukumbini.!" Owen alizungumza maneno hayo kwa kujiamini mbele ya bosi wake Diana. "Kwahiyo maelezo yako yanamaanisha kwamba huwezi kufanya kazi kwa kufuata maelekezo na matwakwa yangu sio?" Diana alimuuliza Owen "Nafikiri jibu ni ndio. Nimeajiriwa na kampuni na nitafanya kazi kwa kufuata matakwa ya kampuni. Siwezi kufuata sheria zako bali nitazifuata sheria za


kampuni. Diana, kazi yako wewe ni kutusainisha mikataba na ukiona tumeenda kinyume na matakwa ya mikataba basi unaweza kuandika ripoti kwenda kwa wakuu wako ili tufukuzwe kazi au kusimamishwa. Maamuzi ni yako sasa, kama nimekosea basi ni ruksa kunifukuza kazi au kunisimamisha.!" "Dah! Najua unapata ujasiri wa kuzungumza maneno hayo kwa kuwa unajua siwezi kufanya hivyo. Ushajua tayari udhaifu wangu ndo maana unanijibu kwa


jeuri hivyo. Haya sawa tuyaache hayo. Kwanini unafanya kazi mpaka unashindwa kwenda kula Owen?" "Ni kawaida tu nitakula muda wowote. Hii programu ninayoitengeneza ina mambo mengi sana ndo maana imenifanya nisahau kula. Ila nakuhakikishia Boss wangu, hii programu nikiikamilisha italeta matunda makubwa sana kwenye kampuni yetu. Nyie subirini na mtulie mtakuja kuelewa baada ya siku tatu nikishamaliza kila kitu.


Hapo ndo mutajua kwanini nimekaa na njaa kutwa nzima.!" "Ni sawa lakini bado unafanya kosa kubwa kufanya kazi na njaa. Huoni kama unajitesa Owen? Unatakiwa ule na ushibe ili akili iweze kufanya kazi vizuri.!" "Wala usijali bosi, kuna nukta nataka kuifikia kwanza kwa siku ya leo alafu baada ya hapo nitafikiria kuhusu kula. Ondoa shaka kabisa mimi nipo freshi kabisa.!"


"Mmh! Haya Mr labda siku hizi umebadilika maana kipindi kile ulikuwa huwezi kufanya jambo kwa ufanisi ukiwaga na njaa.!" Hayo yalikuwa maongezi kati ya Owen na Diana. Baada ya maongezi hayo, Diana aliondoka ofisini kwa Owen na kumwacha mtaalamu akiendelea kufanya zoezi la kutengeneza programu maalumu ya kuhifadhi na kuendesha taarifa za kampuni kwa ujumla. Hazikupita dakika tano wafanyakazi wenzake


kwenye kile kitengo walirudi kutoka kantini. Walikuwa vijana wakiume wawili na wakike mmoja. Walimkuta Owen bado anacheza na kompyuta huku kijasho kikiwa kinamtoka. Kila mtu alienda kukaa kwenye kiti chake na kuendelea na shughuli yake. Dakika zile zile aliingia muhudumu wa kampuni akiwa na chakula mkononi. Alienda moja kwa moja mpaka mezani kwa Owen kisha akakiacha kile chakula. Lilikuwa ni tukio la ajabu kidogo kwani hakukuwa na sheria ya kulia chakula ndani ya


ofisi isipokuwa vinywaji tu. Owen na wafanyakazi wenzake wakashangaa. Ilibidi Owen amuulize yule mhudumu ni nani aliyemruhusu na kumwambia ampelekee chakula. Yule mhudumu alijibu kwamba alipokea maagizo kutoka kwa Boss Diana. Diana ndo alimuagiza apeleke chakula kwa Owen. Owen alishtuka huku wafanyakazi wenzake wakibaki wanashangaa. Mwisho wa yote kila mtu aliacha lile lipite kwani wote walikuwa wanafahamu mahusiano yaliyokuwa kati ya


Diana na Owen. Kila mtu alikuwa anafahamu Diana na Owen ni mtu na shemeji yake. Kila mtu aliendelea kupiga kazi yake mpaka ulipofikia muda wa kufunga ofisi zao. Owen tayari alikuwa amefikia ile point aliyokuwa anaikusudia kuifikia kwa siku ile. Kilichokuwa kinafuata ni wafanyakazi kurejea kwenye makazi yao. Kabla hajaondoka, Owen alikumbuka ule muda alikuwa na appointment na watu wawili. Mtu wa kwanza ni Laurine ambaye alimuahidi angeenda kumjulia


hali na wa pili ni mwanadada mmoja aliyefahamika kwa jina la Linda. Linda ndo yule mfanyakazi ambaye inasadikika alikuwa anawatangazia wafanyakazi wenzake kwamba Owen ni mpenzi wake. Owen aliamua kuipiga chini appointment yake na Linda. Hakutaka kabisa kukutana na mwanadada huyo kwani alijua dhamira yake. Ukiachana na Salma, Linda pia alikuwa miongoni mwa wadada waliokuwa wanampenda sana Owen. Muonekano wa Owen ulikuwa unawachanganya


wafanyakazi wa kike kwenye ile kampuni. Kila mwanadada alijikuta anapata ndoto ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mtaalamu. Hata wale waliokuwa kwenye mahusiano, walikuwa na utayari wa kusaliti wanaume wao kisa Owen. Wadada walikuwa wanamshobokea sana mtaalamu. Suala lile lilifanya wafanyakazi wengi wa kiume kumchukia Owen. Kiufupi Owen alikuwa gumzo na super nyota kwenye ile kampuni. Baada ya kuipiga chini appointment baina


yake na Linda, Owen alipanda gari lake kisha akaanza safari kuelekea uswahilini kwa akina Laurine. Alitumia takribani dakika thelathini kufika mpaka uwanjani kwa akina Laurine. Owen alifanikiwa kumkuta Laurine nje akiwa amekaa kwenye kigoda akimsubiri. Alifurahia sana kumuona Laurine akiwa mzima wa afya kabisa. Hata Laurine alifurahi pia kumuona Owen ametimiza ahadi yake ya kumtembelea. Ilibidi tu watoke eneo lile na kwenda kule alipokuwa amepaki gari ili


wapate wasaa mzuri wa kuzungumza. Hawakutaka wambea wasikilize kabisa maongezi yao. Owen alimuuliza Laurine kuhusu afya yake kwa ujumla na Laurine alijibu kwamba anaendelea vizuri kabisa. Mtaalamu alifurahi na kushukuru sana baada ya kusikia hivyo. "Sasa Laurine, Mimi sijaja kukaa sana kwa sababu kuna kazi yangu ya kiofisi nataka nikaimalizie nyumbani. Ila kabla sijaondoka nataka tuzungumze jambo muhimu na la msingi


kabisa. Naomba unisikilize kwa umakini na kunielewa.!" "Sawa Kaka Owen mimi nakusikiliza wewe tu kaka 'angu.!" "Ok, Ni hivi Laurine, Kwa sasa nataka kukusaidia kubadilisha mfumo mzima wa maisha yako. Nahitaji kukutoa kwenye giza na kukurudisha kwenye. Nataka nikupambanie ili utimize zile ndoto zako ulizokuwa unaota tangu ulipokuwa mdogo. Nitahakikisha unarudi darasani


lakini sio sekondari. Nitakutafutia chuo ili ukasomee fani kwa kuanza na ngazi ya diploma alafu baadae utafute degree yako. Je upo tayari kubadilika Laurine? Au umeridhika kuishi kwenye maisha unayoishi sasa?" Owen alizungumza kauli hiyo na kumuuliza swali Laurine. "Kaka Owen eeh, maisha ya kujiuza barabari hayakuwa chaguo langu kaka. Nipo tayari kubadilika hata kwa kuivua ngozi ilimradi tu niishi kwenye dunia ya


ndoto zangu. Nahitaji kuwa mtu mpya kaka yangu.!" "Ok, Sasa ni hivi Laurine, Kwa sasa sitaki tena uendelee kuishi pale unapoishi. Nataka nikuchukue tukaishi wote kwa wazazi wangu huku nikiendelea kuweka mambo sawa kwa ajili yako.!" "Kaka Owen, Sijakuelewa vizuri. Unamaanisha kwamba mimi nije kuishi nyumbani kwa wazazi wako?"


"Yes, Twende nyumbani kwetu ukaishi na sisi. Wazazi wangu mimi hawana shida watakupokea na kukuchukulia kama mtoto wao wa damu.!" "Mmh! Lakini kaka itawezekana vipi wazazi wako wakubali kuishi na mtu kama mimi? Sijulikani natokea familia gani hivyo sio rahisi wao kunipokea kaka. Lakini pia usisahau kwamba mimi ni kahaba hivyo itakuja kuwa tatizo kama wazazi wako watagundua hili. Utawaeleza nini kuhusu mimi mpaka


wakuelewe?" "Laurine, Ninachokitaka kutoka kwako Ni jibu tu kwamba upo tayari kwenda kuishi kwenye familia yetu au laa! Kuhusu wazazi wangu niache mimi, Mimi ndo nitajua namna ya kuwaambia na kuwaeleza wazazi wangu kuhusu wewe.!" Owen aliongea kauli hiyo. "Ila Kaka Owen, mwezako nina wasiwasi mimi. Nahisi kabisa nitakuharibia status yako mbele ya wazazi wako pamoja na watu


waliokuzunguka. Mimi ni kahaba na changudoa wa hili jiji na watu wengi wananifahamu mimi.!" Laurine alizungumza kauli hiyo kwa unyonge sana. "Nisikilize mimi Laurine, Wewe sio kahaba ila ulikuwa kahaba. Nakupa onyo, ole wako urudi tena kwenye lile danguro. Nakupa hii pesa najua itatosha kukidhi mahitaji yako ndani ya hii wiki. Mimi naondoka muda huu ila nakupa siku tano tu za kufikiria maneno yangu. Leo ni jumanne, mpaka kufikia


jumamosi uwe umepata jibu kamili. Siku ya jumapili jioni nitakuja na nataka nikute jibu lililonyooka. Kama jibu litakuwa ndio yani umekubali kwenda kuishi nyumbani kwetu basi nikukute umepaki kabisa vitu vyako kisha tutaondoka. Na kama jibu litakuwa hapana basi sitokulazimisha katika hilo. Nitayaheshimu maamuzi yako.!" NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu} EPISODE: 12


AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller) Takribani siku tatu zilitosha kwa Owen kukamilisha zoezi la kutengeneza programu. Programu ilianza kufanya kazi na kila mfanyakazi aliikubali kwa asilimia mia. Viongozi wa juu wa ile kampuni walimkubali sana Owen kutokana na kipawa chake. Kwa namna ile programu ilivyokuwa inafanya kazi, mabosi wa kampuni waliipenda sana. Programu ile ilizidi kumfanya Owen kuwa maarufu zaidi


kwenye ile kampuni. Siku hiyo Owen aliruhusiwa kurudi nyumbani mapema ili akapumzike. Owen alipanda gari na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwao. Upande wa pili nyumbani kwa akina Owen kulikuwa na wageni wawili ndani ya nyumba ya Mr James. Wageni hao ni mfanyabiashara mmoja tajiri pamoja na Binti yake. Mfanyabiashara huyo alikuwa anafahamika kwa jina la Mr Evrat Gonzalo. Binti yake alikuwa anafahamika kwa jina la Juliette. Juliette alikuwa msichana


mmoja mzuri na mrembo kweli kweli. Makamo yake kiumri yalikuwa yanalingana kwa kiasi kikubwa na makamo ya Owen. Alikuwa ni mhitimu wa shahada ya biashara na alichagua kufanya biashara pamoja na Baba yake. Miradi yote ya Mr Evrat Gonzalo ilikuwa chini ya usimamizi wa Binti yake Juliette. Mr Evrat Gonzalo na Mr James walikuwa na urafiki wa karibu kutokana na itikadi zao za maisha kutegemeana. Mmoja alikuwa mwanasiasa na mwingine alikuwa mfanyabiashara. Kila


mmoja alikuwa ananufaika kupitia mwenzake. Kwa nia thabiti ya kuboresha urafiki wao, Mr James pamoja na Mr Evrat Gonzalo walikubaliana kuwafungisha ndoa vijana wao. Kwa mara nyingi tena Mr James na mkewe walimtafuta mwanamke wa kuolewa na kijana wao. Baada ya Robyson kutafutiwa mwanamke, sasa ilikuwa ni zamu ya Owen. Tangu Owen aonekane kuteswa na mahusiano, wazazi wake walibeba jukumu la kumtafutia mwanamke kijana wao. Kwa


kuwa walikuwa wanafahamiana vyema na Mr Evrat, waliamini kabisa Binti wa tajiri huyo angekuwa mke bora kwa kijana wao. Uzuri ni kwamba Juliette alikuwa na muonekano mzuri, msomi na tayari alikuwa na kipande cha utajiri mkononi mwake. Lengo kuu la Mr Evrat kwenda na mwanae nyumbani kwa Mr James lilikuwa ni kwenda kumkutanisha Juliette na Owen. Lakini sasa, wakati mipango yote ikiandaliwa, Juliette na Owen walikuwa hawafahamu chochote kuhusu


jambo lile. Kwa mara ya kwanza kabisa Juliette alishtuka baada ya kusikia Baba yake akiongea na Mr James na mkewe kuhusu ndoa ya vijana wao. Juliette alipiga hesabu za haraka haraka aligundua kwamba yale maongezi yalikuwa yanamuhusu yeye kwani Baba yake hakuwa na mtoto mwingine zaidi yake. Ilibidi sasa Juliette aulizie ukweli wa mambo. Jibu alilopewa lilimshtua sana kwani lilikuwa ni lile lile alilokuwa analiwaza. "Baba eeh, Mimi sipo tayari


kuolewa. Kwanini unapanga mikakati ya kuniozesha bila kunishirikisha mwenyewe? Kwanini unitafutie mchumba baba? Mimi sipo tayari kuolewa na mtu nisiyempenda Baba.!" Juliette alizungumza maneno hayo kisha akatoka kwa hasira pale sebuleni walipokuwa wamekaa na kwenda kukaa pekeake nyuma ya jengo lile. "Mr James, Naomba musijali kuhusu Binti yangu. Mimi ndo namjua vizuri hajawahi na hawezi kunipinga hata siku moja.


Najua atanielewa tu ndo maana sikuona sababu ya kumwambia mapema.!" Mr Evrat alimwambia Mr James na mkewe hiyo kauli. Watu wazima waliendelea kupanga mikakati huku Juliette akiwa peke yake nyuma ya jengo la Mr James. Nyumba ya Mr James ilikuwa kubwa kweli kweli. Ndani ya geti kulikuwa na vibustani pamoja na bwawa la kuogelea (swimming pool). Muda huo mwanadada Juliette alikuwa na stress sana hivyo akaanza kutembea tembea kwenye


vibustani ndani ya lile jengo. Muda ule ule honi ya gari ilisikika na mlinzi akafungua geti. Owen ndo alikuwa anawasili nyumbani kwao muda ule akitokea kazini. Aliteremka kwenye gari kisha akazama ndani ya mjengo. Alipofika sebuleni aliwakuta wazazi wake wakiwa na mgeni ambaye ni Mr Evrat Gonzalo. Owen aliwasalimia wote kwa pamoja kisha akaanza kupiga hatua kuelekea chumbani kwake. "Imekuwa vizuri sana leo umerudi mapema babaa. Hiki


kikao kinakuhusu kwahiyo njoo uketi mara moja tuongee.!" Hiyo ilikuwa kauli ya mama yake Owen. Baada ya kusikia kauli hiyo, Owen alipiga hatua kurudi nyuma kisha akakaa kwenye sofa ili kusikiliza ajenda kuu ya kikao kile. Kwanza kabisa Owen alipewa utambulisho wa kina kuhusu Mr Evrat Gonzalo na shughuli zake kwa ujumla. Mwisho kabisa aliambiwa ajenda kuu ya kikao kile kwamba anatakiwa kumuoa Binti wa Mr


Evrat Gonzalo. Owen aliambiwa kila sifa ya kupendeza kuhusu Binti wa Mr Evrat Gonzalo. Pale sebuleni Juliette hakuwepo kwa wakati ule hivyo Owen hakuijua kabisa sura ya msichana aliyeambiwa amuoe. "Wazee wangu, munajua kwamba sijawahi kabisa kwenda kinyume na kauli zenu lakini kwa hili mutanisamehe. Kwa suala kama hili mulitakiwa munishirikishe kwanza mimi mwenyewe kabla hamjafikia makubaliano. Kwanini hamkunishirikisha kwanza ili


mukajua kipi kipo moyoni mwangu? Mulianza na kaka Robyson na sasa mumehamia kwangu. Hizi ndoa za family friend zipo kwa ajili ya kulinda masilahi yenu binafsi bila kuzingatia furaha za vijana wenu. Kiukweli kabisa, nazichukia sana hizi ndoa za family friend. Nachukia kwa sababu zimenifanya nipoteze mwanamke wa ndoto zangu. Wazee wangu, kwa hili sihitaji mjadala wala kikao. Mimi sipo tayari kumuoa huyo mwanamke muliyenichagulia. Kama ni


msomi, ana pesa na Baba yake ni tajiri hiyo ni juu yake, mimi hainihusu.!" Owen alizungumza kauli hiyo kisha akainuka kwa hasira na kuanza kupiga hatua kuelekea chumbani kwake. "Owen...! Owen...! Owen..!" Mama Owen alijaribu kumsimamisha mwanae Owen lakini mtaalamu hakusimama. Alipandisha ngazi kuelekea juu ghorofani kulipokuwa na chumba chake. Alipofika alijitupa kitandani kwa hasira. Aliwaza na kuwazua kitu gani afanye ili kulimaliza jambo


lile bila kuwakwaza wazazi wake. Wakati amejilaza kitandani alisikia sauti ya mdogo wake wa mwisho (Sharon) ikiomba msaada kutokea chini. Owen aliinuka haraka kitandani kisha akasogea dirishani na kutazama kule chini ilipokuwa inatokea sauti. Alipoangaza macho vizuri alimuona mdogo wake Sharon akipiga kelele huku akinyosha mkono kwenye bwawa la kuogelea yani swimming pool. Owen alitazama kwenye lile bwawa akamuona mtu anatapa tapa kwenye maji na alionekana


kuhitaji msaada. Owen alichomoka kwa spidi chumbani kwake na kuelekea chini kutoa msaada. Alifika kwenye lile bwawa kisha akajitosa mzima mzima na kwenda kumuibua mtu aliyekuwa anatapa tapa. Alifanikiwa kumchomoa ndani ya swimming pool na aligundua bado alikuwa hai. Alipomtazama usoni alikutana na sura nzuri ya mtoto wa kike. Alikuwa ni Juliette, Binti wa Mr Evrat Gonzalo. Ilibidi kwanza ampe haraka huduma ya kwanza kwa kum'minya tumboni kisha


akaanza kumpa pumzi kupitia mdomo wake. Dakika zile zile Binti alifumbua macho na kukuta lipsi za mwanaume zikiwa mdomoni mwake. Yule Binti alishtuka sana kuona anapigwa busu na mwanaume. Alichokifanya ni kumsukuma pembeni Owen.kisha akainuka pale chini. "Kwahiyo hiyo ndo shukrani yako Binti? Yani nimekuokoa alafu unaanza kuleta nyodo?" Owen alimuuliza yule Binti.


Juliette hakuzungumza chochote badala yake alianza kumtazama Owen na kumkagua kwa umakini. Aise, baada ya Juliette kumtazama Owen ni kama alipigwa na shoti ya umeme hivi. Pale pale alijikuta anavutiwa na muonekano wa Owen. Alihisi kabisa tumboni mwake kuna mtoto wa Owen ameanza kucheza cheza. Kiufupi alijikuta anampenda mwanaume bila kutarajia. Na kitu ambacho hakujua ni kwamba yule ndo alikuwa mwanaume ambaye alichaguliwa kuolewa nae. Owen


yeye hakuwa na hisia zozote juu ya Juliette licha ya uzuri aliokuwa nao. Dakika zile zile walikuja wazazi wao maana Sharon alishaenda kutoa taarifa juu ya ajali iliyotokea kwenye swimming pool. Baada ya wale wazee kufika, Owen alipiga hatua na kuondoka kabisa eneo lile. Juliette alibaki mdomo wazi huku akimsindikiza Owen kwa macho. Wazee walimuuliza Juliette ni kipi kilitokea mpaka akatumbukia kwenye lile bwawa. Juliette alijibu kwamba alikuwa anatembea tembea pembezoni


mwa bwawa ila ghafla akahisi kizunguzungu na ndipo akadondokea bwawani. Walimuuliza Juliette kuhusu hali yake ili ikibidi wamuite daktari. Juliette alijibu kwamba yupo salama kabisa kwani Owen aliwahi kutoa msaada kwake. Kiukweli kabisa tukio lile lilimfanya Mr Evrat Gonzalo kumshukuru na kumkubali sana Owen. Aliamini kabisa Owen ndo kijana pekee anayestahili kumuoa mwanae kwani tayari alishaonesha uwezo wa kumlinda. Walitoka kwenye kile


kibwawa na kurudi sebuleni walipokuwa wamekaa. Wakati huo Juliette alikuwa amebadilisha nguo zake zilizoloa na alipewa nguo za Catherine (mtoto wa tatu wa Mr James) kwani miili yao ilikuwa inafanana. Wakiwa wameketi pale sebuleni, Owen alifika akiwa na glass ya maziwa mkononi. Alienda kuketi kwenye sofa alilokaa mama yake. Juliette alianza kumtazama Owen kwa macho ya aibu kwani lile busu alilopigwa wakati anapewa pumzi lilimchanganya sana.


Juliette aliomba utambulisho wa yule kijana (Owen) aliyemuokoa ili amfahamu zaidi. "Juliette mwanangu, Huyu kijana anaitwa Owen. Ni mtoto wa pili wa Mr James. Huyu sasa ndo kijana ambaye mimi Baba yako nimechagua uolewe nae.!" Mr Evrat Gonzalo alizungumza kauli hiyo kumwambia mwanae Juliette. Juliette alishtuka na kusisimka vilivyo baada ya kusikia kauli hiyo. Hakujua kabisa kama kijana


aliyekuwa anamkataa alikuwa na shupavu na mwenye mvuto kiasi kile. Ghafla mtoto wa kike alifanya maamuzi ya kushangaza mbele ya watu wazima. Pale pale alibadili maamuzi yake, "Baba eeh, Nimekubali kuolewa Owen. Nahisi kabisa moyo wangu umependa kwa mara ya kwanza. Nipo tayari kuwa mke wa Owen.!" Juliette alizungumza maneno hayo na kuwafanya wazee wafurahi. Wazazi walimgeukia Owen na


kumwambia yule Binti ndo aliandaliwa kwa ajili yake. Owen alipewa utambulisho wa kina juu ya Juliette. Mwisho wa yote wakampa nafasi ya kuzungumza baada ya Juliette kukubali kuolewa. Wao waliamini kabisa Owen lazima abadili maamuzi yake ya awali baada ya kuona uzuri wa Juliette. Owen alimtazama sana Juliette, akawatazama wazazi wake kisha akasema, "Wazee wangu, Mimi nipo tayari kuoa.!" Owen alizungumza kauli


hiyo na kufanya watu wote pale sebuleni waanze kufurahia. Wakati wanaendelea kufurahia, kumbe Owen bado alikuwa hajamaliza kuongea. Aliendelea kuongea na kusema, "Kiukweli kabisa nipo tayari kuoa lakini nitamuoa mwanamke ninayempenda mimi na sio munayempenda nyie. Juliette ni mwanamke mzuri sana lakini mimi sina hisia za kimapenzi juu yake. I'm sorry Dad, am sorry Mum, am sorry Mr Evrat Gonzalo


as well as my dearest Juliette. Nitaoa lakini nitamuoa yule nitakaempenda mimi.!" NOVEL.................... MY VALENTINE- 13 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................... 0699470521/0713601762 INSTAGRAM..............


@realsilentkiller_ "Owen mwanangu, Sisi wazazi wako ndo watu pekee tunaokutakia mema hapa duniani. Hakuna jambo tunaloweza kulifanya kwa lengo la kukuharibia maisha yako. Hiki tulichokifanya ni kwa faida yako mwanangu. Huyu Binti anaendana kabisa na hadhi yetu sisi. Lakini pia anatoka kwenye familia ambayo tuna urafiki nayo tangu miaka mingi. Kiufupi tunamjua ni Binti mzuri mwenye akili na maadili mema hivyo


atakufaa wewe na hata sisi.!" Mama Owen alizungumza kauli hiyo. "Mama eeh, Mimi nafikiri munipe muda wa kutosha ili nitafakari kuhusu hili. Kwa sasa hata nikisema nampenda Juliette bado nitakuwa naudanganya moyo wangu na pia nitakuwa namdanganya yeye. Kiukweli kabisa, kwa sasa sina hisia za mapenzi kwa Juliette. Naomba nipeni muda labda kwa siku za mbeleni nitakuwa na hisia nae.! Owen alimjibu Mama yake kauli


hiyo kisha akainuka na kuanza kupiga hatua kuondoka. "Owen!" Mr James alimuita Owen kwa hasira. Owen alisimama baada ya kusikia sauti ya baba yake. Alitega masikio kwa umakini na kuanza kumsikiliza Baba yake. "Owen, Sikiliza kwa umakini kijana wangu. Umetaka utamuoa na hata usipotaka utamuoa tu.!" Mr James alizungumza kauli hiyo kama kwa hasira mno.


Owen hakumjibu kabisa Baba yake badala yake alipiga hatua na kwenda moja kwa moja chumbani kwake. "Lakini wazee mwenzangu, mimi naona kama kijana yupo sahihi. Ni bora tuvunje hii ndoa maana hakutakuwa na upendo ndani ya ndoa yao endapo tutalazimisha waoane. Nafikiri kabisa mwanangu Juliette ataenda kuteseka kwenye hiyo ndoa kwa kuwa Owen ameonesha kutovutiwa na mwanangu.!" Mr


Evrat Gonzalo alizungumza kauli hiyo akiwataka wazazi wenzake wasitishe mpango wa kuwaozesha vijana wao. "Baba eeh, tafadhali sana musisitishe hii ndoa. Kiukweli kabisa nampenda sana Owen. Japo imekuwa ghafla lakini nimejikuta nampenda kweli yule kijana. Hata kama sasa hivi hanipendi lakini nitafanya kila niwezalo ili kumfanya Owen anipende. Mimi nitajua namna ya kufanya mpaka Owen anikubali. Kikubwa tuvute subira kwa


sasa.!" Juliette alizungumza kauli hiyo kuonesha wazi wazi ni jinsi gani alivyokuwa anampenda Owen. "Juliette, hautakuwa peke yako katika hilo. Yule Owen mimi ndo mama yake hivyo hanisumbui kwa chochote kile. Tulia mkwe wangu, Owen ndo mume wako mtarajiwa.!" Mama yake Owen alizungumza kauli hiyo kumfariji Juliette. Kwa ufupi ni kwamba upande wa Juliette mambo yalikuwa freshi


kabisa. Tatizo lilibaki kwa Owen tu kuweza kumkubali Juliette kisha wafungishwe ndoa. Mkakati uliokuwa umebaki ni kumshawishi Owen akubali kumuoa Juliette. *** Upande wa bibie Laureen tayari alishafanya maamuzi juu ya mahala pa kuishi kabla hata haijafika ile jumapili. Mtoto wa kike hakupenda kabisa kuendelea kuishi na makahaba huku akiendelea kufanya


biashara ya kuuza mwili wake. Tayari alishaona mwanga umeanza kujitokeza kwenye maisha. Alikubali kwenda kuishi maisha yoyote yale nyumbani kwa akina Owen kuliko kuendelea kuishi pale alipokuwa anaishi. Tayari alishawapa mkono wa kwa kheri wasichana wenzake na kuwakumbusha kwamba ukahaba sio kazi halali hivyo zinapotokea fursa zingine za maisha basi wazichangamkie ili wabadilishe status zao. Lakini pia Laureen aliwashukuru sana wale wadada kwa kumpokea na


kumsaidia katika kipindi chote alichoishi pale. Aliwaahidi siku zote atawakumbuka kwa wema wao na kama angefanikiwa kwenye safari yake ya maisha basi siku moja angerudi kuja kulipa japo theluthi ya wema waliomtendea wale wadada. Kwa hakika kilikuwa kipindi cha huzuni kubwa sana kwa wale wadada kwani walimzoea sana Laureen. Ni takribani miezi sita waliishi pamoja kule uswahilini. Wakati wengine wakihuzunika, kuna watu wengine walimuonea wivu Laureen. Walitamani sana


ile nafasi wangeipata wao. Waliumia sana kuona Laureen aliyedumu kwenye danguro kwa miezi sita amepata bahati ya kupata mwanaume wa kumtunza wakati wao walidumu kwa miaka zaidi ya miwili. Ni ukweli usiopingika kwamba Laureen aliwazidi nyota makahaba wote kwenye lile danguro. Hata walipokuwa barabarani wanajiuza wateja wengi walikuwa wanamuona yeye kwanza alafu wengine ndo wanafuata. Ile jumapili ilipofika Owen alienda kweli kule


uswahilini kwa akina Laureen. Alimkuta Laureen ameshajiandaa tayari kwa ajili ya kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya. Owen hakutaka tena kumuuliza Laureen kuhusu maamuzi yake kwani picha tayari lilishajionesha wazi kwamba Laureen alikubali kwenda kuanza maisha mapya nyumbani kwao. Laureen aliwaaga kwa huzuni marafiki zake kwa mara nyingine. Aliwaambia tu ule haukuwa mwisho wa wao kuonana. Ipo siku angewatafuta na kulipa fadhila alizotendewa. Licha ya


kwamba walimfundisha tabia ovu ya kuuza mwili, lakini aliwashukuru sana kwa kuwa wao ndo walimsaidia na kumpa tumaini la kuendelea kuishi ndani ya jiji. Ile tabia ovu ya kuuza mwili walimfundisha ili ajisaidie mwenyewe. Laureen aliwashukuru sana na kuwasihi wamuombe Mungu ili wapate fursa zingine za maisha tofauti na ukahaba. Lakini pia Owen nae aliwashukuru wale wadada kwa kumuokota Laureen barabarani na kuishi nae kama ndugu au rafiki. Pengine bila wale wadada


basi Laureen angepoteza maisha usiku ule. Owen alitoa kiasi cha pesa kisha akawapa wale wadada kama shukrani kwa wema wao. Kulikuwa na wadada takribani tano hivi na kila mmoja alimpatia kiasi cha shilingi laki moja ya kitanzania. Aliwapa zile pesa kisha akawaambia kwamba wazitumie kama mtaji wa kubadilishia staili zao za maisha kwa kufanya biashara ndogo ndogo kama vile kuuza mboga mboga, vitafunwa, matunda na biashara nyinginezo. Baada ya kusema hivyo Owen na Laureen


wakaanza kupiga hatua kuondoka eneo lile. Wale wadada walibaki na pesa zao mikononi huku wakiwasindikiza kwa macho Owen na Laureen. Kwa ule moyo aliyoonesha Owen mbele ya wale wadada, ilibidi tu wale wadada watamani kuwa Laureen. Walijikuta wanapata wivu baada ya kuona mwenzao amepata mwanaume mwenye kila sifa ya kuwa mwanaume kuanzia kimwili mpaka kiroho. Roho nzuri, muonekano wa sura mzuri na kuhusu pesa wala sio kitu cha kuuliza. Kiufupi Laureen


alipata bahati ambayo kila mwanamke anatamani kuipata. Wale wadada walichokuwa wanajua ni kwamba Owen alitokea kumpenda kimapenzi Laureen na si vinginevyo. Laureen yeye alikuwa anajua Owen ameamua kumsaidia kwa kuwa aliguswa na stori ya maisha yake na sio kwamba anampenda yeye kahaba aliyelala na wanaume wa kila aina. Owen yeye alikuwa hana uhakika na moyo wake juu ya mwanadada Laureen. Hakujua kabisa kama anamjali na


kumthamini kwa kuwa anampenda au analipa fadhila za wema aliotendewa ile siku ya kwanza walipokuwa Lodge. Kwanza kabisa kabla hawajaanza safari kuelekea nyumbani kwa akina Owen, Owen alimpitisha Laurine kwenye duka la nguo kisha akamnunulia nguo za heshima. Laureen alivaa mavazi ya heshima na kujiona mtu wa tofauti kabisa. Alijikuta amependeza kuliko siku zote. Owen alimtazama Laureen akajikuta anatabasamu tu. Hakuwa na namna nyingine zaidi


ya kukiri moyoni kwamba Laureen alikuwa ni zaidi ya utalii. Ni vile tu alikosa matunzo lakini mtoto wa kike alikuwa na mvuto kuliko hata mbuga za wanyama. Kumtazama Laureen ilikuwa ni zaidi ya burudani kutoka Azam tv. Baada ya kumaliza kufanya manunuzi walitoka dukani kisha wakaanza safari kuelekea nyumbani kwa akina Owen. Baada ya mwendo wa takribani nusu saa, walifanikiwa kuingia mjengoni. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Laureen kuingia kwenye jengo kubwa kama lile.


Mtoto wa kike alibaki kushangaa tu kwani jengo kama lile alikuwa anaishia kuliona kwa macho tu na ile ndo ilikuwa mara yake ya kwanza kuingia. Walipofika sebuleni, waliwakuta wanafamilia wote wakiwa kwenye maongezi yao. Siku ile ilikuwa ni jumapili ya mapumziko hivyo Mr James na mkewe hawakwenda kazini. Lakini pia Robyson nae hakwenda kazini alikuwa pale pale nyumbani. Hata Catherine na Sharon nao hawakwenda shule ile siku. Ukiachana na wanafamilia tu,


siku hiyo hata Diana alikuwa pale kwa Mr James aliwatembelea wakwe zake watarajiwa. Owen na Laureen walipofika tu waliwakuta watu sebuleni wakipiga stori huku wakifurahi na kucheka. Lakini sasa, zile furaha na vicheko vilikatika ghafla baada ya kumuona Owen akiwa na mwanamke mbele yao. Owen alijikuta anashtua mioyo ya watu na kukatisha furaha zao ndani ya sekunde moja tu. Ghafla kimya kikatawala ndani ya nyumba huku macho ya kila mtu yakimtazama na kumkagua


Laureen kwa marefu na mapana. NOVEL.................... MY VALENTINE- 14 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_


Macho ya wanafamilia yalimfanya Laureen kukosa ujasiri ndani ya ile nyumba. Alijikuta anapata wasiwasi na mashaka juu ya uwepo wake. Owen alimgusa bega Laureen na kumuonesha ishara kuwa wasogee kwenye kiti fulani kisha waketi. Wote kwa pamoja walipiga hatua na kwenda kuketi kwenye sofa lililokuwa wazi. Owen alimshtua mdogo wake Catherine kisha akamkabidhi begi dogo la Laureen na kumwambia apeleke chumbani kwake. Catherine alitii amri ya


Owen bila kuhoji. Alilichukua begi kisha akapeleka chumbani kwake. Bado watu wazima waliendelea kustaajabu matukio hayo. Owen alimfungulia njia Laureen ili aweze kuwasalimia watu pale ndani. Kwa hekima na utii Laureen alitoa salamu kwa watu wote waliokuwa ndani ya nyumba. Salamu yake ilipokelewa vizuri tu japo bado watu walionekana kuendelea kumshangaa. "Owen mwanangu, Huyu Binti ni nani tena maana naona


umetuletea mgeni bila taarifa.!" Mama yake Owen amuuliza mwanae swali hilo. Swali hilo lilimfanya Laureen ashtuke maana hakujua kabisa kama Owen alikuwa hajawaelezaga wazazi wake juu ya uwepo wake. Alichokuwa anafahamu ni kwamba Owen alishawashirikisha wazazi wake juu ya ujuo wake tangu hapo awali. "Wazazi wangu, ondoeni shaka kabisa. Baada ya chakula cha


usiku nitawaeleza kila kitu kuhusu huyu Binti. Kwa sasa tuendelee na stori nilizozikuta muda huu.!" "Aah! Shemeji Owen, Tuambie sasa hivi maana hiyo baadae wengine hatutakuwepo hapa.!" Diana aliongea kauli hiyo. Owen alimtazama Diana kisha akasema, "Shemeji, Kama utambulisho huu ni muhimu sana kwako basi subiri usiondoke, Lakini pia kama


hauna umuhimu wowote kwako basi unaweza kuondoka. Kaka Robyson yupo atakuelewesha kila kitu kesho.!" Owen alizungumza kauli hiyo kumjibu Diana. "Oya Bwana mdogo hebu tuondolee siasa zako kwenye ishu za kifamilia. Tutambulishe mgeni wetu ili tujue namna ya kuzungumza nae.!" Robyson alimwambia Owen kauli hiyo akimtaka atoe utambulisho juu ya Laureen.


"Owen.! Huyu Binti ni nani?" Mr James aliamua kumuuliza swali lililonyooka Owen. Baada ya Mr James kutia sauti kwenye lile suala, Owen hakutaka tena kupindisha pindisha maelezo. Aliona ni bora awape utambulisho wa kina juu ya Laureen. "Ok, Huyu Binti munaemuona mbele yenu anaitwa Laureen. Ni Binti anayekabiliwa na changamoto nyingi za maisha baada ya wazazi wake kufariki.


Kuna mtu alimchukua kutoka Mwanza mpaka hapa Dar es salaam kwa ajili ya kufanya kazi za ndani. Lakini kilichotokea ni kwamba alimtelekeza katikati ya jiji bila msaada wowote. Kwa sasa hana makazi wala ndugu yeyote kwenye hii dunia. Nilikutana nae mtaani kwa mara ya kwanza na aliniomba nimsaidie kupata kazi yoyote ile. Kutokana na nidhamu aliyokuwa nayo Binti huyu nikaona nimchukue tuje kuishi nae hapa nyumbani ili asaidiane na Munira kufanya kazi za hapa ndani.


Nawaomba sana wazazi wangu, mpokeeni Binti huyu na aishi hapa na sisi kama familia moja. Kuhusu mshahara na malipo mimi ndo nitajua namna ya kumlipa. Binti anahitaji msaada, naomba tumsaidie kwa moyo mmoja ili Mungu azidi kutuinua. Ni hayo tu wazazi wangu.!" Owen alizungumza maneno hayo na kufanya kimya kitawale kwa sekunde kadhaa pale sebuleni. Baada ya kimya kidogo kupita, Mr James alifungua mdomo wake na kizungumza,


"Owen! Owen! Owen! Oops..! Mbona unajitafutia matatizo kijana wangu? Huyu Binti hujui chimbuko lake, hujui tabia yake na pia huwajui ndugu zake. Je ikitokea akatufia hapa ndani tutampeleka wapi sisi?" Mr James alimuuliza Owen. "Mzee wangu, Huyu Binti kwa sasa hana familia hivyo tutamjumuisha kwenye familia yetu. Chochote kitakachomkuta basi sisi ndo tutawajibika nae. Ikiwa atakutwa na umauti basi


sisi tutawajibika kumzika. Tafadhali sana mzee wangu, naomba tumsaidie huyu Binti. Ameteseka sana huko mtaani hivyo anahitaji kusaidiwa.!" Owen alimjibu Baba yake. "Mmh! Hivi Owen, unataka kutuambia kwamba huko mtaani anayeteseka ni huyu Binti pekee? Kwanini umewaacha mamia ya watu wanaoteseka na kumchukua huyu Binti tu? Kwanini hujawakusanya watu wote wanaoteseka ukawaleta hapa tuishi nao? Kwanini


umemuona huyu Binti tu? Au kuna kitu kinaendelea kati yenu? Usitake kutuletea wakwe wakuokota okota huko mtaani. Sisi tunataka wakwe wanaoendana na hadhi yetu ya maisha kama Diana.!" Mama Owen alizungumza kauli hiyo. "Lakini mama unachozungumza ni kweli. Si ajabu kesho ukasikia unatambulishwa huyu Binti kama mkwe wako. Usikute Owen na huyu Binti wanapendana. Ni bora uzuie mapema hili jambo kabla aibu ya mwaka haijatokea. Huyu


Binti hana hadhi ya kuolewa na shemeji Owen.!" Diana aliamua kuvamia mada ya wanafamilia kwa kuzungumza kauli hiyo. Kauli ya Diana ilimchukiza sana Owen. Mtaalamu alijikuta anapandwa na hasira kuliko kawaida. Alimtazama Diana kisha akasema, "Shemeji Diana, Usiwe unachangia mada kwenye mijadala isiyokuhusu. Semea mahusiano yako sio kujipa usemaji kwenye mahusiano ya


watu wengine. Aliyekuumba wewe na kukupa hadhi ya juu ndo huyo huyo aliyemuumba huyu Binti na kumpa hadhi ya chini. Huyu Binti amenyimwa hadhi ya juu lakini inawezekana amebarikiwa subra ambayo pengine wewe hauna.!" Owen alimjibu Diana kauli hiyo na kufanya watu washangae kidogo kwa kuwa ilikuwa na chembe chembe za dharau ndani yake. Robyson hakufurahishwa kabisa na kauli ya mdogo wake Owen. Ilibidi aingilie kati maongezi yale


ili kumtetea mke wake mtarajiwa. "Dah! Bwana mdogo naona leo umeamua kunivunjia heshima kaka yako. Yani unamjibu shemeji yako kama adui yako. Anyway sitaki kuzungumzia sana jambo hilo pengine muna uadui nje ya ushemeji. Ila nataka tu kuchangia mada kuhusu hili suala la huyu Binti uliyemleta ndani. Kiukweli kabisa naweza kusema hujafanya jambo baya kutaka kumsaidia binadamu anayehitaji msaada. Lakini kosa lako ni kushindwa kujadili na


wazazi jambo hili. Hivi umesahau ulichokifanya juzi Bwana mdogo? Wewe si ndo umekataa kumuoa Juliette kisa wazazi hawakukushirikisha wewe mwenyewe? Sasa kwanini na wewe unarudia kosa lile lile ulilolikataaga? Kwanza kabisa ulitakiwa uwashirikishe wazazi juu ya suala hili kabla hujamleta huyo Binti. Ujue hii ni nyumba ya Mr James sio nyumba yako kwahiyo huna mamlaka ya kumuingiza mtu bila kumtaarifu mwenye nyumba.!" Hiyo ilikuwa kauli ya Robyson kuhusu sakata


lililokuwa linaendelea pale ndani. "Baba na Mama, Mimi pia namuunga mkono Kaka Owen. Naomba tumsaidie tu Laureen na tuishi nae hapa nyumbani ili tuzidi kuongeza familia yetu. Huyu Laureen anaonekana ni mdada mzuri wa nafsi. Hii nyumba ni kubwa sana na kuna shughuli nyingi sana za usafi zinahitajika. Nafikiri itapendeza sana kama ataishi hapa na sisi ili asaidiane na Munira kufanya kazi za hapa ndani.!" Hiyo ilikuwa kauli ya Catherine akimuunga


mkono kaka yake Owen. Catherine na Sharon walikuwa wanampenda sana kaka yao Owen kuliko hata Robyson. Hata Owen nae alikuwa anawapenda sana ndugu zake kuliko kitu chochote kile. Ajenda kuhusu sakata la Laureen liliendelea pale ndani. Mr James na mkewe hawakuwa tayari kumpokea Laureen kwenye nyumba yao. Wao waliwaza mbali sana. Walihisi kama Laureen angeishi pale ndani huenda siku moja wangeshuhudia akiamka


chumbani kwa Owen na khanga au taulo. Wao walitaka kijana wao Owen amuoe Juliette ili kupanua zaidi wigo wao wa uchumi. Endapo uchumi ungekuwa mkubwa basi ingekuwa rahisi kwao kupata nafasi za juu zaidi kwenye uongozi wa nchi. Ndoto ya Mr James ilikuwa ni kumfanya mwanae Robyson kuja kuwa kiongozi wa nchi kwa miaka ya baadae. Lakini pia hata yeye alikuwa anapigania nafasi za juu zaidi kwenye uongozi hivyo pesa ndo ilikuwa inaongea kuliko


maneno. Hiyo ndo ilikuwa sababu ya Mr James kutaka kuwa na ukaribu na wafanyabiashara wakubwa na matajiri ili iwe rahisi kwake kupata misaada ya kifedha. Baada ya Mr James na mkewe kukataa kumpokea Laureen, Ilibidi Laureen ainuke kwenye kiti na kwenda kupiga magoti mbele ya kiti walichokuwa Mr James na mkewe. Laureen alianza kuongea kwa hisia akionesha dhahiri kuhitaji msaada wa watu hao. Owen nae hakutaka kumwacha Laureen peke yake. Aliinuka nae


kwenye kiti kisha akaungana na Laureen kupiga magoti huku akiwaaomba wazazi wake wakubali kumsaidia Laureen. Hata Catherine nae hakuwa tayari kumwacha kaka yake, alisogea mbele ya wazazi wake kisha akapiga magoti kumuombea makazi Laureen. Sharon aliwatazama na kusema 'hapana kwa kweli, japo mimi ni mdogo sielewi kitu lakini hili nimelielewa, alipo kaka Owen nami nipo'. Pale pale Sharon nae akaenda kupiga magoti na kusema,


"Baba na Mama, muacheni dada Laureen aishi hapa na sisi.!" Mr James na mkewe walibaki wanatazamana tu maana watoto wao waliungana kumuombea Laureen aishi pale kwao. Ukweli ni kwamba Owen alikuwa na uwezo wa kumpangia chumba Laureen kwa gharama yoyote ile lakini hakutaka kufanya hivyo na alikuwa na sababu zake za msingi za kushindwa kufanya hivyo. Mtaalamu alikuwa na mahesabu makali sana ndo


maana alitaka Laureen aanze kuishi pale kwao. "Ok, Owen.! Sisi tunaweza kumpokea Laureen na kuishi nae hapa nyumbani kama mtoto wetu ila kwa sharti moja tu. Kama utaweza kutekeleza hilo basi Laureen atakuwa mwanafamilia yetu kuanza muda huu.!" Mr James alizungumza kauli hiyo baada ya kuona watoto wake wametaka Laureen aishi kwao. "Ok, Niambie Mzee wangu. Ni sharti gani hilo?" Owen


alimuuliza Baba yake "Sharti lenyewe ni wewe kumuoa Juliette. Kubali kumuoa Juliette, na sisi tukubali kumpokea Laureen.!" Mr James alizungumza kauli hiyo na kumfanya Owen aanze kuhisi kizunguzungu kizito huku moyo wa shemeji Diana ukilia 'PAAH.!' NOVEL.................... MY VALENTINE- 15 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY


DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ Owen alijikuta anavuta pumzi ya moto kufuatia kauli ya Baba yake. Aliwaza na kuwazua ni kipi afanye ili kuikwepa ndoa baina yake na Juliette na pia amsaidie Laureen kuishi nyumbani kwao. Mtaalamu hakuwa tayari kumuoa


Juliette na pia hakuwa tayari kuona Laureen anakosa nafasi ya kuishi pale kwao. Alimtazama Laureen akajikuta anamuhurumia sana Binti huyo. Ilibidi sasa mtaalamu afanye maamuzi magumu ili atimize lengo lake la kumsaidia mtoto wa kike. "Mzee wangu, Mimi nipo tayari kufanya kama munavyotaka nyie. Nitamuoa Juliette lakini kabla sijamuoa naomba munipe muda wa kujenga hisia za mapenzi juu yake. Nikishafanikisha hilo basi nitamuoa maadam nitakuwa


tayari nampenda.!" Owen alizungumza kauli hiyo huku moyoni akiwa anaumia. Kauli ya Owen ilipokelewa vyema kabisa na wazazi wake. Kwa kiasi fulani wazazi walipata matumaini juu ya mpango wao wa kumfungisha ndoa mtoto wao pamoja na mtoto wa rafiki yao Mr Evrat Gonzalo. Mr James na mkewe hawakutaka tena mgogoro na kijana wao Owen. Waliamua kukubaliana na ombi lake hivyo Laureen alipata rasmi idhini ya kuishi pale mjengoni.


Kwa mara nyingine tena Laureen alifungua ukurasa mpya wa maisha ndani ya jiji la Dar es salaam. Kwa mara ya kwanza kabisa alianza kufurahia maisha baada ya mateso ya muda mrefu. Ndani ya ile nyumba alikuwa anapata mahitaji yote ya msingi huku jukumu lake kuu likiwa kuhakikisha nyumba inakuwa safi pamoja na kupika vyakula. Uzuri ni kwamba alikuwa anafanya kazi hizo kwa kushirikiana na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Munira. Hawakuwa na kazi ngumu


kwenye kufua nguo za wenye nyumba kwa sababu kulikuwa na mashine maalumu ya kufulia nguo. Kiufupi Laureen na Munira walikuwa wanapata muda mwingi wa kupumzika na sio kufanya kazi kama Punda. Ndani ya ile nyumba Laureen alipendwa na wanafamilia wote isipokuwa mama Owen tu. Ukweli ni kwamba Mama Owen alikuwa hampendi Laureen kutokana na ukaribu wake na Owen. Kuna namna fulani mama alipata wasiwasi juu ya wawili hao. Kwa namna Owen alivyokuwa


anamjali na kumthamini Laureen ilikuwa vigumu sana kwa mtu wa kawaida kuamini hakukuwa na chembe chembe za mapenzi katika yao. Kila alipokuwa anarudi kazini kauli yake ya kwanza ilikuwa ni kujua kuhusu Laureen tu. Kuna namna fulani Owen alibadilika baada ya ujio wa Laureen ndani ya nyumba yao. Siku zote alizokuwa haendi kazini alikuwa anajumuika kufanya kazi za ndani pamoja na Laureen na Munira. Mtaalamu alikuwa anakaa jikoni kupika pamoja na kufua nguo huku


akipiga stori mbalimbali za maisha pamoja na Laureen. Suala lile lilifanya wazoeane kuliko kawaida. Sio tu Owen ndo alibadilika baada ya ujio wa Laureen, hata Catherine na Sharon walibadilika kwa kiasi kikubwa sana. Kila siku walikuwa wanaamka mapema na kuwasaidia Laureen na Munira kufanya kazi za ndani kama vile kuosha vyombo kabla hawajaenda shuleni. Mama yao alikuwa hapendi kabisa kuona wanae wanafanya zile kazi ilihali wafanyakazi wapo. Alijaribu


kugomba sana lakini watoto hawakuelewa kabisa. Walifanya zile kazi kwa furaha kutokana na upendo waliokuwa nao kwa Laureen. Huyo Sharon ulikuwa haambiwi kitu chochote kibaya kuhusu Laureen alafu akakubali. Alihama mpaka chumba alichokuwa analala na dada yake Catherine na kuhamia chumbani kwa Laureen wakawa wanalala kitanda kimoja. Sharon alimpenda na kumzoea Laureen ndani ya muda mfupi sana. Laureen na Catherine wao walijikuta wanakuwa mtu na


shoga yake walioshibana na kutunziana siri kabisa. Kuna mchoro fulani wenye umbo la kopa ulizunguka katikati ya Owen, Laureen, Catherine na Sharon . Kwa hakika kulikuwa na upendo mkubwa sana katikati yao. Kuna muda walikuwa wanacheza michezo mbalimbali iliyowafanya kufurahi pamoja ndani ya mjengo. Waliogelea pamoja kwenye swimming pool huku wakirushiana maji kama watoto. Tayari Owen alishamfundisha Laureen namna ya kuogelea. Sio siri Laureen


aliongeza furaha ndani ya ile familia. Lakini sasa yale matukio hayakumpendeza kabisa Mama mwenye nyumba. Hayakumpendeza kwa kuwa hakutaka kuona ukaribu kati ya Owen na Laureen. Alichokuwa anakitaka ni kuona Owen anakuwa karibu na Juliette tu. Ule uzurii wa Laureen ulimchanganya sana Mama yake Owen. Alihisi kabisa suala la Owen kumuoa Juliette linaweza kuwa gumu kutokana na uwepo wa Laureen. Mpaka kufikia muda ule, tayari ulishakatika mwezi


mmoja tangu Laureen alipoingia ndani ya nyumba ya Mr James kwa dhamana ya Owen. Lakini sasa licha ya mwezi mmoja kupita lakini bado Owen hakuwa na hisia zozote za mapenzi kwa mwanadada Juliette. Kwanza kabisa Juliette alipata muda mchache sana wa kuutumia na Owen. Lakini pia ndani ya huo muda hakuweza kubadilisha chochote kile ndani ya moyo wa Owen. Owen alikuwa hapati furaha yoyote alipokuwa na Juliette. Juliette alishahisi kwamba furaha ya Owen tayari


ilikuwa kwa mtu mwingine kabisa. Licha ya kuhisi hivyo lakini bado Juliette hakukatia tamaa moyo wake kwa Owen. Alijiapiza kumpata Owen kwa gharama yoyote ile. Mara kwa mara alikuwa anampigia simu Owen na hata kumfuata nyumbani kwao kuongea nae ili kumshawishi tu ampende. "Owen Baba! Moyo wangu mimi unauma sana. Moyo wangu unauma sio kwa sababu hunipendi bali unauma kwa sababu sijui moyo wako unataka


kitu gani kutoka kwangu mimi. Mengi nimeyafanya kwako lakini bado unashindwa kuelewa hisia zangu. Kila siku nimekuwa mtu wa kuwaza nikupe kitu gani ili unipende Baba. Hebu niambie Baba, nikufanyie nini ili unipende mimi? Nikujengee nyumba? Nikununulie gari? Nikupe kipande changu cha urithi? Au nikupe ATM card yangu ya Benki? Nijibu Owen, nipo tayari kukufanyia chochote kile.!" "Juliette, mimi nashukuru sana kwa kuonesha moyo wa upendo


kwangu. Ninachoweza kusema ni kwamba usitumie nguvu kubwa ya pesa ili kumfanya mtu akupende. Kamwe huwezi kutumia pesa kununua upendo kwa mtu mwenye pesa. Ili ufanikiwe kununua moyo wa mtu mwenye pesa basi tumia utu na utulivu tu. Lakini pia huwezi kutumia utu na utulivu kununua upendo kwa mtu asiyekuwa na pesa. Juliette, Ni vigumu sana kwako kununua upendo kwangu kwa kutumia pesa zako. Jaribu kutumia njia nyingine lakini sio pesa.!"


"Owen! Lakini mimi sifanyi hivi kwa kuwa nina pesa baba. Nafanya hivi kwa sababu nakupenda sana Owen.!" "Juliette, wewe ni mwanamke mzuri sana hivyo siwezi kusema kwamba kamwe siwezi kuwa na wewe. Ukweli ni kwamba una vigezo vyote vya kuolewa na mtu kama mimi ila kwa sasa bado sina hisia zozote juu yako. Sali sana my dear, kama Mungu amekupangia mimi basi nitakuwa wako tu. Ni suala la


muda tu kila kitu kitakuwa sawa bila hata kutumia nguvu ya pesa. Siku zote wakati wa Mungu ndo wakati sahihi, vuta subra usilazimishe vitu kufanyika kwenye wakati wako mwanadamu.!" Siku zote Owen alikuwa anampa Juliette majibu ya kumpa matumaini juu yake. Alikuwa anafanya hivyo ilimradi asiende kuharibu kwa wazazi ambao tayari alishawaahidi kumuoa Juliette. Wazazi wao walikuwa wanajua taratibu mambo


yalikuwa yanaenda vizuri kati ya Owen na Juliette kwa kuwa kuna muda waliwaona wakicheka pamoja. Lakini pia hata walivyokuwa wanawauliza kuhusu hatua waliyofikia kila mtu alijibu kwamba muda si mrefu mambo yangekuwa sawa na wangeweza kuoana. Hilo liliwapa faraja wazazi japo Mama Owen alikuwa na mashaka na kauli zao. Alihisi kabisa moyo wa Owen ulikuwa kwa Laureen na sio kwa Juliette. EPISODE 16


Tukirudi upande wa pili kule kwenye kampuni, Owen aliendelea kufanya kazi licha ya kukutana na changamoto mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa kike. Mwanadada Linda na Salma ndo walikuwa mstari wa mbele kuonesha wazi wazi hisia zao juu ya Owen. Lakini pia kuna namna fulani Diana alikuwa anaonesha bado alikuwa na chembe chembe za mapenzi kwa Owen. Mara nyingi alikuwa anamfanyia Owen matukio yaliyokuwa yanaashiria


bado alikuwa anampenda. Alikuwa hapendi kabisa kumuona mfanyakazi yeyote wa kike anakuwa karibu na Owen. Akiwa kwenye majukumu yake ya kazi, Owen alisikia mlio wa meseji kwenye simu yake ya mkononi. Alifungua simu yake na kukutana na ujumbe kutoka kwa Diana. "Hongera sana babaa.!" Huo ndo ulikuwa ujumbe aliotumiwa Owen na Diana. Owen aliitazama ile meseji kisha akajiuliza sana kuhusu ile


hongera maana hakuna jambo lolote zuri alilokuwa amelifanya kwa kipindi kile. Owen nae aliandika ujumbe kumuuliza Diana kuhusiana na zile pongezi. Lakini sasa kabla hajatuma alihisi kitu fulani hivyo akaghairisha zoezi la kutuma ule ujumbe. Aliisogeza simu yake pembeni kisha akaendelea na kazi. Hazikupita dakika nyingi alipokea ujumbe mwingine na mtumaji alikuwa yule yule Diana. "Kwahiyo hutaki kupokea pongezi zangu sio?"


Owen hakuona sababu ya kuhangaika na meseji za Diana. Aliisogeza tena simu pembeni kisha akaendelea kufanya kazi. Baada ya kimya cha dakika kadhaa, simu ilipigwa. Owen alitazama juu ya kioo akaona mpigaji alikuwa ni Diana. Ilibidi sasa apokee na amsikilize, "Owen, mbona haujibu meseji zangu?" "Nijibu nini sasa?"


"Si nimekupa pongezi au ujaona?" "Nimeona ila sijui hizo pongezi unazonipa nimefanya jambo gani zuri?" "Khaa! Jamani! Hujui kwamba ndoa ni jambo la kheri? Hongera sana kwa kufikia maamuzi ya kutaka kumuoa mwanamke wa ndoto zako. Kwa hakika Juliette ni mzuri sana alafu ni Bosslady.!" "Ok shukrani sana shemeji yangu. Je kuna kingine


unachotaka kuniambia ukiachana na hizo pongezi?" "Kwahiyo ni kweli Owen unamuoa Juliette?" "Dah! Kweli mnafiki ni mnafiki tu. Kwahiyo wewe ulikuwa unanipongeza kwa kitu usichokifahamu wala kuwa na uhakika nacho?" "Nataka unithibitishie tu kwa mdomo wako Owen.!" "Sasa nikikuthibitishia


itakusaidia nini? Au kitu gani kitaongezeka kwangu?" "Nataka kujua tu, kwani kuna ubaya gani jamani.!" "Sikia Shemeji Boss, Nina kazi nyingi sana za kufanya muda huu. Nakutakia mchana mwema.!" Owen alimaliza kwa kuongea maneno hayo kisha akakata simu. Baada ya Owen kukata simu, Diana aliendelea kupiga. Alipiga simu ya Owen mara mbili lakini


Owen hakupokea. Alichokifanya Diana ni kumpigia Owen kwenye simu ya kiofisi sasa. Hapo sasa Owen hakuwa na ujanja wa kukwepa kupokea simu ya Boss. Alipokea kisha akatega sikioni kumsikiliza Boss Diana. "Owen, Leo sijisikii vizuri kabisa. Muda wa kuondoka ukifika nipeleke nyumbani kwa gari lako. Mimi sitoweza kabisa kumudu usukani kuendesha gari hivyo nitaliacha hapa kazini. Hili sio ombi Owen, Hii ni amri kutoka kwa Boss wako.!" Diana


alizungumza maneno hayo kisha akakata simu. Owen alijikuta anachukizwa sana na usumbufu wa Diana. Hisia zake ni kwamba Diana alikuwa na jambo lake na sio kwamba alikuwa hajisikii vizuri. Ila ukweli ni kwamba siku ile Diana alikuwa hajisikii vizuri kimwili. Tangu asubuhi alipofika kazini alikuwa anajisikia uchovu, kichefu chefu na maumivu ya kichwa kwa mbali. Muda wa kazi ulipoishia Owen alikuwa wa kwanza kutoka ofisi na kwenda kwenye parking


ya magari ili amkimbie Diana. Lakini sasa, alipofika tu kwenye parking akimkuta Diana ameegemea gari lake kana kwamba alikuwa anamsubiri. Owen alivuta pumzi ndefu sana maana mpango wake ni kama ulishafeli tayari. "Hahah! Mbona umeshtuka Owen? Ulijua utanikimbia eeh?" Diana alimuuliza Owen "Hivi Diana unataka nini kutoka kwangu?" Owen alimuuliza Diana


"Mimi sitaki chochote zaidi ya msaada tu unipeleke nyumbani. Leo sijisikii vizuri kabisa.!" "Diana, Lakini mbona wafanyakazi wapo wengi kwenye hii kampuni. Kwanini usingewaomba wao wakuendeshe? Kwani ni lazima nikuendeshe mimi?" "Yeah! Lazima uniendeshe wewe kwa sababu wewe ni Shem-darling hivyo nitakuwa salama zaidi mikononi mwako.!"


"Kwanini usingempigia simu Kaka Roby akakufuata kama unavyofanyaga siku zingine?" Owen alimuuliza Diana "Kiukweli kabisa hali yangu ilivyo siku ya leo nashindwa kuielewa kabisa. Yani najikuta natamani kuwa karibu na wewe tu Owen. Lakini hata hivyo leo Robyson yupo kwenye mkutano mkubwa wa chama chao.!" Diana alimjibu Owen Owen hakutaka tena kuendelea kujibizana na Diana.


Alichokifanya ni kumfungulia Diana mlango wa gari kisha akaingia. Na yeye pia akazunguka upande wa pili kisha akaingia kwenye gari. Mtaalamu aliendesha gari kwa spidi ili amfikishe Diana nyumbani kwao. Njiani hakutaka kabisa stori na Diana. Lakini sasa wakati safari ikiendelea Diana alimwambia Owen ampitishe hospitali akacheki afya yake maana alihisi homa inazidi kuchachama mwilini mwake. "Sikiliza Diana nikikupitisha


hospitali mimi naondoka siwezi kubaki nikikusubiri. Mpigie simu Kaka Roby au mtu yeyote akufuate. Na kama huwezi basi utapanda taxi kurudi kwenu.!" "Sawa! Nimekuelewa My dear. Endesha gari ukaniache hospitali kisha endelea na safari yako.!" Owen aliendesha gari mpaka hospitalini kisha akamtaka Diana ateremke ili aendelee na safari yake. Diana aliteremka kwenye gari na kuanza kupiga hatua kuelekea kwenye geti la hospitali.


Lakini sasa, hakufikisha hatua tatu, alihisi kizunguzungu na kudondoka chini. Ilibidi Owen ateremke kwenye gari kisha akaenda kumuinua Diana pale chini. Owen aligundua Diana alikuwa ameshapoteza fahamu. Hapo sasa akaamini ni kweli mtoto wa kike alikuwa mgonjwa. Ilibidi amuinue na kumbeba chap chap kisha akaingia nae ndani ya geti la hospitali. Walipokelewa kisha Diana akaingizwa kwenye chumba cha matibabu. Owen alichanganikiwa ghafla. Alitoa simu yake mfukoni kisha


akampigia kaka yake Robyson ili ampe taarifa kuhusu mwanamke wake. Kwa bahati mbaya simu ya Robyson ilikuwa inaita tu bila kupokelewa.Muda huo Robyson alikuwa kwenye kikao cha masuala ya kisiasa. Owen hakuwa na namba nyingine ya mtu wa karibu wa Diana. Ilibidi tu abaki pale hospitalini kumpa uangalizi Diana. Alimpigia simu Laureen na kumjulisha kwamba atachelewa kurudi nyumbani Kutokana na suala lile. Ukweli ni kwamba ilifikia hatua Owen alikuwa hawezi kufanya kitu au


kuwa mahali alafu Laureen asijue. Ratiba zote za Owen, Laureen alikuwa anazifahamu. Wakati Diana amepoteza fahamu alikuwa ameshafanyiwa vipimo na kwa wakati huo alitundikiwa dripu ya maji. Ilichukua lisaa zima kwa Diana kuzinduka. Alipozinduka tu alikuwa vizuri kabisa. Daktari aliwaomba Owen na Diana kwenye chumba chake ili awape mrejesho wa tatizo la Diana na hali yake kwa ujumla. "Ok, Unajisikiaje sasa hivi bibie?" Daktari alimuuliza Diana


"Najisikia vizuri kwa sasa Dokta.!" Diana alijibu "Ok, vipi kichwa hakiumi?" "Ndio Dokta hakiumi kabisa.!" "Ok, Sasa ni hivi nilishakufanyia vipimo katika mwili wako na majibu yanaonesha kwamba hauna ugonjwa wowote mwilini. Lakini pia naomba nikupe hongera Binti kwa kuwa hapo ulipo wewe ni mjamzito. Una ujauzito wa miezi miwili Binti.!"


"What.! Ujauzito? Dokta, Mimi nina ujauzito wa miezi miwili?" Diana aliongea kwa mshangao mkubwa Kwa hakika ilikuwa ni taarifa ya kushtua sana kwa mwanadada Diana. Kilichokuwa kimemshtua sio suala la yeye kupata mimba bali ni kuwa na mimba yenye miezi miwili. King'ora kilichoashiria hali ya hatari kilianza kugonga kichwani mwake huku akimtazama Owen aliyekuwa pembeni yake.


Alilitazama kwa umakini tumbo lake huku akilishika shika taratibu. Dakika zile zile mawazo yalimpeleka mbali sana Diana. Ni kama alisikia sauti ya mtoto mdogo ikimuita 'Mama', Diana aliangalia mbele yake akakutana na sura ya mtoto anayefanana Robyson kwa kila kitu. Diana alijikuta anainuka kwenye kiti ili amfuate yule mtoto. Lakini sasa, ghafla alishikwa shati na alipogeuza macho kumtazama aliyemshika alijikuta anashtuka sana. Alikutana na sura ya mtoto mwingine aliyefanana kwa kila


kitu na Owen. Yule mtoto alimwambia Diana, "Mama! Mimi ndo mwanao.!" Diana alijikuta anachanganikiwa kwani hakujua mwanae halali ni yupi kati ya wale. Yale mawazo yalikuwa mazito kiasi kwamba Diana alidondokea kwenye meza ya Daktari na kupoteza fahamu. NOVEL.................... MY VALENTINE- 17 {Kipenzi Changu}


AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ Diana alichukuliwa na kupelekwa kitandani mara baada ya kupoteza fahamu. Owen alishindwa kuelewa ni kwanini Diana alipokea kwa mshtuko mkubwa sana le taarifa.


Alikumbuka namna Diana alivyokuwa anamtazama baada ya kupewa taarifa ya kuwa mjamzito. Wakati Owen anaendelea kuwaza ghafla simu yake iliita na alipoangalia namba na jina la mpigaji aligundua kwamba ni kaka yake Robyson. Owen alishukuru sana baada ya Robyson kupiga simu kwani alihitaji kutua ule mzigo kwa muhusika. Na pia alitaka kurudi nyumbani kwao kwani kuna mtu alikuwa amem'miss sana. Owen alipokea simu ya Robyson kisha akampa taarifa kuhusu hali ya


Diana kwa wakati ule. Robyson hakutaka tena kusubiri tena badala yake alianza safari kuelekea kule hospitali. Uzuri ni kwamba muda huo hakuwa mbali na pale hospitalini hivyo alitumia muda mfupi tu kufika. Baada ya Robyson kufika pale hospitali alikabidhiwa majukumu yote kuhusu Diana. Owen hakutaka kusubiri Diana azinduke hivyo aliondoka na kumuacha Robyson pale hospitali. Ukweli ni kwamba mpaka kufikia kipindi hiko Owen hakuwa na mapenzi kabisa na


Diana. Zile kumbukumbu za maisha yote waliyoishi miaka ya nyuma alishazifutaga kabisa kichwani mwake. Yale maumivu ya kusalitiwa na Diana tayari yalishapoa. Diana hakuwa na nafasi tena kwenye moyo wa Owen. Owen alifanikiwa kumtoa Diana moyoni mwake mara baada ya kuwa na ukaribu wa kina na Laureen. Ni kama vile moyo wa Owen ulishahifadhi jina la Laureen japo hakuweka wazi hisia zake. Tukirudi pale hospitalini, Robyson alimuuliza Daktari kuhusiana na hali ya


Diana kwa ujumla. Daktari alimwambia Robyson kwamba asiwe na wasiwasi kuhusu Diana kwani hana ugonjwa wowote mwilini na pindi atakapoamka basi atakuwa sawa kabisa. Lakini pia Robyson alijikuta anafurahi sana baada ya kupokea taarifa njema kuhusu Diana kuwa ni mjamzito. Kwa hakika Robyson alifurahi baada ya kujua miezi kadhaa ijayo ataenda kuitwa Baba. Alitamani kupiga simu nyumbani kwa akina Diana ili awajulishe hali ya mtoto wao lakini alisita. Hakuona sababu ya


msingi ya kuwapa taarifa kwani Daktari alisema Diana hakuwa na maradhi yoyote mwilini hivyo akizinduka atakuwa sawa na wataruhusiwa kuondoka. Robyson aliamua kumsubiri Diana azinduke huku muda wote akikenua meno kwa furaha isiyo na kifani. Baada ya kusubiri kwa muda fulani, hatimaye Diana alizinduka. Baada ya kuzinduka tu neno lake la kwanza kutamka lilikuwa ni jina la Owen. "Diana mpenzi wangu, Mimi sio Owen. Mimi ni mpenzi wako


Robby nipo hapa kwa ajili yako.!" Robyson alizungumza maneno hayo baada ya kuhisi Diana bado alijua Owen ndo yupo pale hospitali. Diana alifumbua macho akakutana na sura ya tabasamu ya Robyson. Robyson alishindwa kuvumilia hivyo alimkumbatia kwanza Diana kwa hisia kali za mapenzi huku akitokwa na machozi ya furaha. "Asante sana Diana wangu. Asante sana kwa kuniheshimisha


mamaa. Nakuahidi nitakuwa Baba bora kwa mwanangu na kuwa mume bora kwako. Nitakulinda wewe na mwanangu kwa gharama yoyote ile. Asante sana kipenzi changu.!" Robyson alizungumza maneno hayo kwa hisia kali huku akitokwa na machozi ya furaha. Ni kweli mara baada ya kuzinduka Diana alikuwa sawa kabisa kimwili. Waliruhusiwa kutoka pale hospitali na tayari yalishafikia majira ya saa moja usiku. Robyson alimpakiza Diana


kwenye gari lake na kuanza safari ya kumpeleka nyumbani kwao. Lakini sasa walipokuwa njiani walijadili jambo moja muhimu sana kwa ajili ya kulinda wadhifa wao kwenye jamii. Kutokana na status zao, lilikuwa ni jambo la aibu sana upande wao hasa hasa kwa Diana kupata mtoto bila kuolewa. Walikubaliana kurudisha nyuma tarehe na mwezi uliopangwa kwa ajili ya ndoa yao ili kuharakisha jambo hilo kabla ujauzito haujawa mkubwa. Wote kwa pamoja walikubaliana kila mtu


aende akazungumze na wazazi wake kuhusu mabadiliko hayo. **** Hatimaye suala la mabadiliko ya tarehe na mwezi wa ndoa ya Robyson na Diana lilifikishwa kwa wazazi wa pande zote mbili. Ilibidi wafanye kikao cha dharura kujadili upya siku maalumu ya kufanya sherehe yao. Walitumia muda mfupi tu kumaliza kikao chao na hatimaye tarehe maalumu ya ndoa ilipangwa. Kulikuwa na mwezi mmoja tu wa


maandalizi kabla ya siku maalumu ya harusi. Ndugu, jamaa na marafiki wote walitangaziwa kuhusu tukio hilo. Ndoa ya Robyson na Diana ilifufua upya kesi ya Owen dhidi ya wazazi wake juu ya mwanadada Juliette. Wazazi walimgeukia tena Owen na kumtaka awe tayari kumuoa Juliette. Walichokuwa wanakitaka Mr James na mkewe ni kuunganisha ndoa zote mbili kwa siku moja. Walitaka kuandaa sherehe moja kubwa sana kwa ajili ya vijana wao. Lakini sasa,


suala lile kwa Owen bado lilibaki kuwa kipengele. Owen aliendelea kubaki na msimamo wake ule ule kwamba hakuwa tayari kumuoa Juliette. Vuta nikuvute ilikuwa kubwa sana ndani ya nyumba ya Mr James. Siku hiyo familia nzima ilikuwa pamoja majira ya saa tatu usiku na lengo likiwa ni kuhakikisha Owen anakubali kumuoa Juliette. Alianza Mr James kuzungumza, akafuata mke wa Mr James na mwisho kabisa akaongea Robyson akimsihi Owen akubali kumuoa Juliette. Walitumia aina zote za


maneno lakini jibu la Owen lilikuwa ni lile lile kwamba hayupo tayari kumuoa Juliette. Catherine na Sharon wao walikuwa upande wa kaka yao Owen. Hawakutaka kabisa kaka yao amuoe mwanamke asiyempenda. Tayari walikuwa wanajua vyema mahali ilipokuwa furaha ya kaka yao. Wao wenyewe walishamtengeneza wifi yao na walikuwa wanampenda sana kama alivyokuwa anampenda kaka yao. Kiufupi Catherine na Sharon walikuwa wanajua Owen alikuwa


anampenda sana Laureen na hata Laureen alikuwa anampenda sana Owen. Walilitambua hilo ila waliamua kukaa kimya maana hakuna ambaye alishaweka wazi hisia zake. Wakati zile vuta nikukute zikiendelea pale sebuleni, Laureen alikuwa jikoni akiendelea na mapishi. Alikuwa hafahamu chochote kilichokuwa kinaendelea kwa wanafamilia mpaka pale Sharon alipoenda jikoni kumpa umbea. Sharon alimwambia Laureen juu ya ajenda ya kikao kilichokuwa


kinaendelea kule sebuleni. Mtoto wa kike alijikuta tu anaumia moyoni baada ya kusikia Owen analazimishwa kumuoa Juliette. Kiukweli kabisa Laureen alijikuta amesahau status yake ya maisha ya awali na kumpenda Owen. Ilikuwa vigumu sana kwa Laureen kukwepa hisia za mapenzi kwa Owen kwani mambo aliyoyafanya Owen kwake yalikuwa nadra sana kufanywa na mwanadamu wa kwenye huu ulimwengu. Laureen hakuwa na ujanja wa kulizuia jina la Owen ndani ya moyo wake.


Kiukweli kabisa alimpenda sana Owen na kutamani kuwa mke wake. Alimpenda Owen sio kwa sababu ya pesa zake bali ni ule moyo wake ulioweza kuugusa moyo mwanadada huyo katika kipindi kigumu cha maisha. Kwa hakika Laureen alijikuta anapata wakati mgumu sana kila aliposikia suala la Owen kumuoa Juliette. "Dada Laureen, usiwe na mawazo basi. Kaka Owen hawezi kumuoa Juliette.!"


"Sharon kwanini unaniambia hivyo? Kwani kuna ubaya gani kaka Owen akimuoa Juliette?" "Dada, Mimi najua wewe hapo na Kaka Owen munapenda sana. Najua unampenda sana kaka ndo maana nakuambia hivyo.!" "Sharon, Naomba usiwaze hivyo mdogo wangu. Usiwaze tena hivyo na hata usijaribu kuzungumza hivyo mbele ya mama. Umenielewa mdogo wangu?"


"Sawa Dada lakini najua Kaka anakupenda sana wewe. Hata mimi na Dada Cathe tunakupenda sana wewe.!" Hayo yalikuwa mazungumzo kati ya Sharon na Laureen kule jikoni. Kule sebuleni bado vuta nikuvute iliendelea. Owen aligoma kabisa kukubali kumuoa Juliette. "Hivi Owen, unaweza kuniambia sababu ya mwisho ya msingi kabisa inayokufanya ukatae kumuoa Juliette? Hebu niambie mimi mama yako huenda


nitakuelewa.!" Mama Owen alimuuliza mwanae Owen. "Mama eeh, sababu ni moja tu. Sina hisia zozote za mapenzi kwa Juliette. Kiufupi ni kwamba simpendi Juliette hivyo siwezi kumuoa mwanamke nisiyempenda.!" Owen alizungumza kauli hiyo kwa kujiamini. "Dah! Owen mwanangu, mbona unakuwa mpumbavu kiasi hiko lakini. Hivi unajua ni wanaume wangapi wanatamani kupata


nafasi ya kumuoa Juliette? Kwanini unakataa bahati ambayo vijana wenzako wanaililia?" "Mama eeh, hata kwa upande wangu kuna wanawake wengi sana wanatamani kupata nafasi ya kuolewa na mimi. Lakini nimeshindwa kuwapa nafasi kwa kuwa kwenye safari yangu ya mahusiano nimeshapigwa tukio baya ambalo sitamani tena lijirudie katika maisha yangu. Sifa za mwanamke aliyenipiga hilo tukio hazina utofauti kabisa na sifa za Juliette. Wazazi wangu


pamoja na Kaka Robby, kamwe musisifu uzuri wa kitabu kwa muonekano wa jalada. Jaribuni kusoma mpaka ndani ili ujue maudhui yake. Vipo vitabu vyenye majalada mazuri lakini hadithi zake hazisomeki kabisa. Lakini pia vipo vitabu vyenye majalada mabaya ila hadithi zake ni tiba tosha kwenye moyo wa kila mwenye pumzi. Mimi niwatoe tu wasiwasi wazazi wangu, Mimi nitaoa ila nitamuoa mwanamke atakaekuwa tiba ndani ya moyo wangu bila kujali status yake ya maisha.


Nashukuru Mungu nimeshampata hivyo muda ukifika nitawatambulisha wazazi wangu. Yeye ndo chaguo langu na nampenda sana.!" "Anha! Sasa nishaelewa kila kitu kupitia mafumbo yako. Nahisi kabisa kile nilichokuwa nafikiria ndo hiki kinaenda kutokea. Bila shaka hisia zangu zilikuwa sahihi kabisa. Naona kabisa Owen anaenda kutuletea doa na kuitia aibu familia. Ok, Kwahiyo mwanangu Owen kuna mwanamke unampenda si ndio?"


"Ndio Mama, Yupo mwanamke ninayempenda kwa dhati.!" "Bila shaka ni Laureen si ndio? Nakuuliza Owen naomba unijibu. Ni Laureen ndo anauburuza moyo wako si ndio baba? Ni Laureen huyu huyu kijakazi uliyemuokota mtaani ndo anakufanya umkatae Juliette si ndio? Sikiliza Owen, Kama utaniletea mwanamke anayeendana na hadhi yetu labda kidogo naweza kukuelewa. Lakini kama mwanamke


unayemzungumzia ni Laureen basi futa kabisa hiyo. Nikiwa kama mama yako niliyekutunza katika tumbo langu kwa miezi tisa na kukulea, Nasema kamwe sitokubali wala kuruhusu umuoe Laureen.!" Mama Owen alizungumza kauli hiyo kwa hasira na jazba kubwa sana. NOVEL.................... MY VALENTINE- 18 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER


{Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ _________________________________ _____ Owen alijikuta anakosa ujasiri wa kuzungumza kufuatia kauli ya mama yake. Alibaki tu akimtazama huku akimeza mafunda ya mate kwa uchungu.


"Lakini mama unakosea sana kuzungumza maneno hayo. Kiukweli kabisa umefika mbali sana mama'angu. Kwanza kabisa huna uhakika kama Laureen ndo mwanamke anayependwa na kaka. Lakini pia hata kama ni Laureen ndo anapendwa bado sioni tatizo lolote katika hilo. Laureen ni mwanamke mzuri na mrembo kuliko hata Juliette. Lakini pia kwa kipindi chote tulichoishi nae hapa nafikiri kila mtu amejionea sifa zake. Ni Binti mmoja mwenye sifa ya upole,


ukarimu, usikivu, hekima, busara, unyenyekevu, huruma, utii, mchapa kazi na bado Mungu amembariki uzuri wa kipekee kabisa. Tangu alipoingia ndani ya nyumba yetu kuna mabadiliko chanya yametokea hapa ndani. Kuna furaha na upendo umeongezeka kwa kiasi kikubwa hapa ndani. Tangu nizaliwe sikuwahi kujua kama kaka Owen anajua kupika ila nimekuja kujua baada ya ujio wa Laureen. Mimi kama mtoto wa hii familia nitakuwa mtu wa mwisho kabisa kuamini kwamba Laureen


hastahili kuwa mke wa Kaka Owen. Hivi Laureen ana kasoro gani mpaka asiwe na haki ya kupendwa kama wanawake wengine? Japo sina upeo mkubwa katika mahusiano na ndoa lakini naamini kwa hili wazazi wangu munakosea sana. Muacheni kaka amuoe mwanamke anayempenda kutoka moyoni mwake.!" Hayo yalikuwa maneno mazito kutoka kwa Catherine ambaye ni mdogo wake Owen. Catherine alizungumza maneno


hayo akijaribu kumtetea Owen kwa wazazi wake. "Cathe, Wewe ni mtoto mdogo sana kwahiyo unapaswa kutulia pindi wakubwa wanapozungumza.!" Hiyo ilikuwa kauli ya Robyson kwenda kwa mdogo wake Catherine. Owen alimtazama sana Robyson baada ya kuongea kauli hiyo. Alitegemea labda kaka yake angeunga mkono kauli ya Catherine ili kupiga vita fikra potofu za wazazi wao. Lakini


yote kwa yote hakushangaa kuona Robyson anasimama upande wa wazazi wake kwa kuwa wote walikuwa na falsafa za maisha zinazofanana. Robyson alikuwa anafuata kila hatua wanayopita wazazi wake na ndo maana alichagua kuingia kwenye siasa kama wazazi wake. Lakini pia Robyson alikuwa na upendo mdogo sana kwa ndugu yake Owen na ndio maana hata kile kipindi Owen alipokuwa masomoni hakupewa taarifa na Robyson kwamba anataka kufanya engagement na kumuoa


mchumba wake. Ndugu hao hawakuwa watu wa kuwasiliana mara kwa mara na hata kushirikishana kwenye masuala yao binafsi. Kuwasiliana kwao ilikuwa ni mpaka Owen aanze kumtafuta Robyson vinginevyo inapita mpaka miezi bila wawili hao kuongea. Mawasiliano finyu na kutoshirikishana kwenye masuala yao binafsi kama kutambulishana wachumba zao ndo yalipelekea ndugu hao kujikuta kwenye mahusiano na mwanamke mmoja. Laiti kama Owen angemtambulishaga Diana


kwa Robyson basi pengine Robyson asingemchumbia Diana. Lakini yote tisa, kumi ni kwamba Owen alikuwa anampenda sana Kaka yake Robyson. Siku zote alimpenda na kumthamini kama alivyokuwa anawathamini wazazi wake na ndugu zake wakike. Tukirudi kwenye sintomfahamu iliyokuwa inaendelea pale sebuleni baina ya wanafamilia. Mama Owen nae alimtuliza mwanae Catherine na kumwambia aache kumtetea Owen kwa kila jambo linalotokea pale ndani. Owen bado alikuwa


kimya hakuzungumza chochote juu ya kauli ya mama yake. Mr James ambaye ndo Baba wa familia aliingilia kati maongezi yale, "Owen, Hebu tolea maelezo juu ya kauli ya mama yako ili tupate ukweli kutoka kwako. Hivi ni kweli Laureen ndo mwanamke unayempenda au kuna mwingine?" Mr James alimuuliza Owen swali hilo. Owen alilisikia na kulielewa vizuri swali la baba yake lakini alihitaji


sekunde kadhaa za kutafakari jibu la kumpa. Alilidadavua kwa umakini lile swali akagundua kwamba ule ulikuwa mtego. Alijua kabisa kama angetoa jibu la kumkubali Laureen kwa muda ule basi angempa wakati mgumu mtoto wa kike. Aliwaza namna ya kujibu ili kurejesha amani pale ndani. "Owen! Nasubiri jibu lako. Je ni kweli mwanamke unayempenda ni huyu kijakazi wetu Laureen?" Mr James alimuuliza Owen swali hilo kwa mara ya pili.


Owen alivuta pumzi ndefu kisha akaiachia na kuanza kuzungumza, "Mzee wangu, Hiyo ni kauli ya mama sio kauli yangu. Mimi bado sijamtaja wala kumleta kwenu mwanamke ninayempenda. Kwahiyo hiyo kauli uliyoisikia isikuchanganye kabisa mzee wangu. Hiyo ni kauli ya kusadikika wala haina ukweli wowote.!" Owen alijibu swali la baba yake kwa staili hiyo.


"Kwahiyo unataka kututhibitishia kwamba hauna mahusiano yoyote na Laureen?" Mr James alimuuliza Owen swali lingine. "Mzee wangu, Zaidi ya Kaka na dada basi hakuna mahusiano mengine kati yangu na Laureen.!" Owen alijibu kwa ujasiri. "Cathe! Nenda kaniitie Laureen aje hapa sasa hivi.!" Mr James alimwambia mwanae Catherine akamuite Laureen kule jikoni alipokuwa.


Kauli hiyo ilimshtua sana Owen. Hakutaka kabisa Laureen ahusishwe kwenye yale masuala. "Sasa Mzee wangu, Laureen unayemuita wa nini tena mzee. Mbona hakuna sababu ya msingi ya kumuhusisha Laureen kwenye haya maongezi. Naomba mumuache Binti wa watu tafadhali. Nakuomba sana mzee wangu muacheni Binti aendelee na shughuli zake.!" Owen alizungumza akimuomba Baba yake asimuhusishe Laureen kwenye zile mada.


"Tulia basi kijana wangu, mbona hujiamini? Mimi ndo namtaka Laureen kuna maswali nataka kumuuliza.!" Mr James alimjibu Owen. "Mzee wangu, Hebu niulize mimi hayo maswali nipo tayari kuyajibu yote tena kwa ufasaha kabisa. Naomba tu Binti asiguswe kwa chochote maana atakosa amani na furaha ya kuishi hapa ndani. Naomba musimuhusishe kabisa kwenye huu mgogoro wa familia.!" Owen


alizungumza kauli hiyo lakini haikusaidia chochote maana tayari Laureen alishafika kabla hata hajamaliza kuzungumza kauli yake. Laureen alifika pale sebuleni akiwa tayari anaelewa kila kitu kilichokuwa kinaendelea. Alimtazama Owen akagundua kabisa mtaalamu hakuwa na furaha kabisa moyoni mwake. "Laureen!" "Abee babaa!"


"Unaweza kuniambia mahusiano yaliyopo kati yako na Owen?" Mr James alimuuliza Laureen kwa ukali na kumfanya Laureen ashtuke kidogo. "Ndi..ndi..ndio Baba.! Owen ni kaka yangu mimi.!" Laureen alimjibu Mr James kwa woga na wasiwasi mkubwa sana "Ni kaka yako tu hakuna kitu chochote kinachoendelea kati yenu?"


"Ndio Baba hakuna kitu chochote kinachoendelea kati yetu. Mimi hapa namuita Owen kaka na hata yeye ananiita mimi dada.!" "Mbona Owen ametuambia nyie ni wachumba na anataka kukuoa.!" Mr James aliongea kauli hiyo na kumfanya Laureen ashtuke tena. Laureen alimtazama Owen machoni akagundua kitu kwa kuwa tu alishamzoea sana. Mtoto wa kike alijua kauli ya Mr James haikuwa na ukweli


wowote isipokuwa ulikuwa mtego. Laureen alimtazama Mr James kisha akasema, "Baba eeh, Kaka Owen hawezi kusema hivyo Baba. Kama kweli amesema basi amedanganya ili akwepe kumuoa Juliette. Mimi sina sifa wala vigezo vyoyote vya kuolewe na mtu kama Kaka Owen.!" Laureen alizungumza kauli hiyo kinyonge sana huku moyoni akiumia. Hata Owen pia alijikuta anapitia maumivu mazito baada ya


kusikia kauli ya Laureen akijivua thamani yake kwa ajili ya kufurahisha nafsi ya mtu mwingine. Owen aliumia sana, hakujua afanye kitu gani kwa ajili ya mtoto wa kike. "Laureen, nakuuliza swali la mwisho. Naomba unipe jibu la kweli kutoka moyoni mwako. Umesema kwamba huna sifa na vigezo vya kupendwa na Owen lakini je wewe unampenda Owen? Naomba uzungumze ukweli wa moyo wako. Kama unampenda basi nitaruhusu


uolewe na kijana wangu.!" Mr James alimuuliza Laureen swali hilo kisha akakaa kusubiri jibu. Laureen alimtazama Owen akajikuta anapata furaha na faraja kubwa moyoni. Kiukweli kabisa mtoto wa kike alikuwa anampenda sana Owen. Moyo wake ulikuwa unamwambia amjibu Mr James kwamba anampenda sana Owen. Lakini sasa, akili yake ilikuwa inamwambia ule ulikuwa mtego wa Mr James hivyo asithubutu kusema ukweli wa moyo wake.


Laureen alikumbuka siku moja Owen alimwambia kwamba kama ikitokea akili na moyo wako vikawa kinyume katika suala zima la kutoa maamuzi basi fuata kile ambacho akili yako inataka. Kwa asilimia kubwa moyo ndo unaongoza kuumiza viungo vingine vya mwili. Baada ya kukumbuka hivyo Laureen alikubali kuusaliti moyo wake. "Baba eeh! Ukweli ni kwamba, Mimi hapa.. mimi hapa.. Sina kabisa hisia za mapenzi kwa


Owen. Mimi nampenda na kumuheshimu Owen kama Kaka yangu. Namshukuru sana kwa kunitoa kwenye giza na kunileta kwenye mwanga. Kiukweli kabisa mimi hapa nahisi si.. si.. simpe.. simpe..ndi Kaka Owen. Nitafurahi sana kama Owen atamuoa.. atamuoa.. atamuoa.. Juliette.!" Laureen alizungumza maneno hayo kwa kigugumizi ndani yake huku akijikaza ki kike kike ili tu asidondoshe machozi mbele ya watu wazima. Owen alishindwa kumtazama


usoni Laureen kwa sababu sauti pekee ilimpa tafsiri juu ya kile kilichokuwa moyoni mwa mtoto wa kike huyo. Siku ile Owen aliamini kwamba alikuwa anapendwa sana na Laureen japo Laureen alimkana mbele ya wazazi wake. "Owen, Nadhani umemsikia vyema Laureen. Sasa hivi nakuuliza swali kwa mara nyingine, Je wewe kwa upande wako. Unahisia zozote za mapenzi kwa Laureen?" Mr James alimuuliza Owen swali


hilo. Kila mtu alitulia ili asikie jibu atakalotoa Owen mbele ya mwanadada Laureen. Laureen mwenyewe alikuwa na shauku kubwa ya kujua ipi nafasi yake ndani ya moyo wa Owen licha ya kwamba aliulizwa swali la mtego. Owen alitoa kitambaa chake mfukoni kisha akapangusa uso wake. Baada ya kupungusa uso aliwatazama wazazi wake, akamtazama Kaka yake Robyson, akawatazama ndugu zake na mwisho kabisa


akamtazama Laureen. Mtaalamu alijisemea moyoni 'Siku zote wanaadamu hasa hasa wanasiasa wanapenda kusikia kile wanachokitaka wao na sio kile unachotaka kuwaambia'. Baada ya kujisemea moyoni maneno hayo Owen aliamua kutoa jibu walilotaka kulisikia wanaadamu na sio alilotaka kulisema yeye. "Wazazi wangu eeh, Mimi hapa... Mimi hapa... Yani mimi hapa.. Kiukweli kabisa... Kiukweli kabisa, Laureen sio mpenzi


wangu wala sina hisia za mapenzi kwake. Kiukweli kabisa mpo sahihi kusema kwamba mimi na Laureen hatuendani. Status yangu ya elimu na maisha kwa ujumla haiendani na kabisa na huyu kijakazi. Hebu tazameni macho yangu, Nadhani munaona haya machozi yanayotiririka muda huu machoni mwangu. Hivi munajua ni kwanini machozi haya yananitoka? Najua hamjui ila ngoja niwajuze. Haya machozi ni ya huzuni kwa kuwa mumenikosea sana kunihusisha kwenye skendo ya mapenzi na


huyu kijakazi. Kwa hakika mumenikosea sana wazazi wangu. Mimi sio wakutoka kimapenzi na kijakazi wakati kuna wanawake wasomi na mastaa wengi wanaopenda. Yote kwa yote naomba.. naomba.. naomba kwa msisitizo muniache kwanza nitulize akili kwa kipindi hiki kifupi. Nadhani munakumbuka kwamba Februari 14 ya mwezi ujao kutakuwa na sherehe ya siku yangu ya kuzaliwa. Imekuwa desturi kwenu kila ifikapo tarehe hiyo kila mwaka huwa munanifanyiaga


surprise ya kunipa zawadi mbalimbali. Lakini pia kama munavyojua siku yangu hiyo ya mfanano wa kuzaliwa ndo siku ambayo dunia nzima huwa inasherehekea sikukuu ya wapendanao yani Valentine's Day. Basi mimi nawaahidi kwamba hiyo siku nitakuwa na suprise kubwa sana kwenu nyie wazazi pamoja na ndugu zangu. Ni siku maalumu kwa ajili ya wapendanao hivyo nami nitamtambulisha na kumvisha pete yule nimpendae. Hii ni suprise hivyo sitaki kuwaambia


Valentine wangu ni nani. Yeyote anaweza kuwa pengine hata chaguo lenu Juliette. Baba yangu, Mama yangu, Kaka yangu na ndugu zangu, naomba mukae tayari namleta kwenu MY... MY... MY VALENTINE.!" Owen alizungumza maneno hayo na kuacha viulizo kwenye kichwa cha kila mwanafamilia. NOVEL.................... MY VALENTINE- 19 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY


DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ _________________________________ _____ Licha ya kauli ya Owen kuacha maswali kwenye vichwa vya wanafamilia lakini kila mtu alimuelewa vyema. Mr James na


mkewe waliona ni bora wavute subira kumsubiri huyo mkwe wao kisha watoe maamuzi yao. Kwa maelezo ya Owen wao waliamini pengine mchumba atakayetambulishwa anaweza kuwa Juliette au mwingine yeyote mwenye status kubwa kama ya Juliette. Waliamini hivyo kwa sababu Owen alitembea sehemu mbalimbali mpaka nje ya nchi na alikutana na wanawake wenye hadhi za juu kabisa na sio wale wa uswahilini waliozoea vigodoro. Walihisi pengine labda mwanamke anayempenda ni


mfanyakazi mwenzake wa kwenye kampuni au ni mfanyabiashara mwenye degree zake. Wazazi walisubiri kwa hamu hiyo siku ya wapendanao yani Valentine Day ili wamuone huyo Valentine wa kijana wao. Kwa upande wa Robyson yeye alimgusa bega Owen na kumkumbusha kwamba hadhi yake sio ya kuokota okota wanawake kwa sababu atachafua brand ama chapa ya familia yao. Familia ya Mr James ilikuwa na maadui wengi sana hasa hasa wale wapinzani wao


kwenye masuala ya siasa. Siku zote mpinzani anakesha kutafuta udhaifu wako kisha anakupiga hapo hapo kwenye mshono. Kama ingetokea Owen akamuoa Laureen alafu ile siri ya Laureen kuwa kahaba ingefichuka basi suala lile lingeichafua sana familia ya Mr James. Ingekuwa aibu kubwa sana kwa mtoto wa kiongozi mkubwa wa siasa kumuoa kahaba. Wapinzani wa Mr James wangetumia ule mwanya kumchafua yeye pamoja na chama chake kwa ujumla. Upande wa Catherine na Sharon


wao walihuzunishwa sana na masuala yote yaliyokuwa yanaongelewa muda ule. Walihuzunishwa kwa kuwa walijua mtoto wa watu Laureen alikuwa anapitia wakati mgumu sana kwa yale yaliyotokea. Walijua kabisa majibu aliyotoa Laureen mbele ya wazazi hayakutoka ndani ya moyo wake. Walijua kabisa Laureen anampenda sana Kaka yao. Lakini pia hata majibu ya Owen yalimuumiza sana Laureen. Kwa kiasi kikubwa Owen alionesha kumdharau Laureen ili tu


kuwafurahisha wazazi wake. Mpaka kikao kile kinaisha Laureen alitoka na jibu kwamba Owen hakuwa na hisia zozote za mapenzi juu yake. Mtoto wa kike aliamini kwamba kumbe tayari Owen alikuwa na mchumba na aliahidi kumtambulisha na kumvisha pete siku ya Birthday yake ambayo iliambatana na sikukuu ya watu wanaopendana duniani yani Februari 14. Laureen aliumia sana moyoni huku akitamani ile siku isifike. Kiukweli kabisa mtoto wa kike alishindwa kukaza moyo wake kwa Owen.


"Kaka Owen eeh, Mimi sijawahi kabisa kukupenda. Sina hisia zozote kwa.. kwa.. kwa.a..ko kaka.!" Laureen alijisemea peke yake maneno hayo ili kujifariji na kujitia nguvu. Lakini sasa cha ajabu ni kwamba alijikuta tu analia kwani maneno yake yalikuwa kinyume na moyo wake. Moyo wa mtoto wa kike ulishakuwa mwepesi na mlegevu kabisa kwa Owen. Yani Owen alimzamisha mtoto wa watu kwenye kina kirefu cha bahari ya


mapenzi. Kwa wakati huo Laureen alikuwa chumbani kwake amejilaza kitandani huku akilia. Siku ile alikosa kabisa hamu ya kula hivyo kile kikao kilipomalizika tu aliwaandalia chakula wanafamilia kisha akaenda zake chumbani kuugulia maumivu. Lakini pia sio Laureen pekee ndo alikosa hamu ya kula, hata Catherine na Sharon walisusa kabisa kula. Hawakupendezwa kabisa na kitendo cha wazazi wao kuingiza siasa zao kwenye masuala binafsi ya watoto. Owen yeye


hakutaka kuonesha uhalisia wa moyo wake kwa wakati ule. Licha ya kwamba alikuwa na maumivu lakini alikaza roho kiume kisha akala chakula cha pamoja na wazazi wake. Hakutaka kabisa kuonesha kwamba alikuwa ameumia kwa ajili ya Laureen. Ilibidi afanye vile ili kumlinda mtoto wa watu dhidi ya wazazi wake ambao walikusudia kuivunja amani aliyokuwa nayo. Punde tu baada ya kumaliza kula Owen nae alienda chumbani kwake kujipumzisha. Huko sasa ndo alipata wasaa mzuri wa


kuugulia maumivu. Mwanaume alijikuta anakuwa na usiku mrefu sana. Kila alivyoikumbuka sura ya Laureen alijihisi kuwa gaidi kwa mtoto wa kike. "Laureen! Naomba unisamehe mimi. Nisamehe sana Laureen kwa mabaya yote niliyokutendea siku ya leo. Nilikuahidi kukupa furaha siku zote lakini leo kwa mara ya kwanza kabisa nimekupa huzuni. Halikuwa lengo langu Laureen. Nisamehe sana mimi.!" Owen alijisemea maneno hayo huku akijipangusa


machozi kwenye mto wake wa kulalia. Mpaka kufikia majira ya saa saba usiku, sio Owen wala Laureen ambaye alipata usingizi. Owen aliona kuna kila sababu ya kumrudishia furaha Laureen. Alishajua kabisa kwa wakati ule mtoto wa kike alikuwa anapitia kipindi kigumu sana. Mtaalamu alishika simu yake kisha akamtumia meseji Laureen, "Vipi umeshalala?" Owen alituma meseji hiyo kisha akasikilizia jibu


kutoka kwa Laureen. Baada ya dakika kadhaa meseji iliingia kwenye simu ya Owen. Owen alijua ni Laureen ndo alikuwa amemtumia. Chap chap alifungua na kweli alikutana na ujumbe uliotoka kwa Laureen "Hapana bado sijalala mimi.!" "Kwanini mpaka sasa haujalala wewe?" "Nipo zangu mtandaoni tu.!"


"Unafanya nini huko mtandaoni?" "Nipo tu nasoma Hadithi za Silentkiller.!" "Hadithi gani hiyo unayoisoma?" "Hii inaitwa CRAZY FOR YOU.!" "Je nayo ni nzuri kama ile I MISS YOU YOU, BORA UNGESEMA, NASUBIRI NINI na IF I DIE ulizowahigi kunisimulia?" "Eeh! Ni nzuri sana. Kiukweli kabisa kazi ya Silentkiller kwenye


uandishi ni sawa na kazi ya Mungu kwa mwanadamu. Kazi zao huwa hazina makosa.!" "Hahah! Naona umeamua kunichekesha sasa Laureen.!" "Hahah! Nakuambia ukweli kabisa. Yani huyu mtunzi anastahili maua yake kwa kweli. Kiukweli kabisa anajua alafu anajua tena.!" "Laureen! Kwani wewe hapo hauna njaa? Kwanini umelala bila kula?"


"Kiukweli kabisa sina njaa kaka Owen. Nilishiba sana chakula cha mchana.!" "Najua unanidanganya Laureen. Sijawahi kukuona hata siku moja ukiacha kula usiku kisa tu ulishiba chakula cha mchana.!" "Kaka Owen, Naomba usijali sana kuhusu mimi. Hapa nilipo sina njaa wala sina hamu ya kula. Panapo uhai basi nitakula tu kesho asubuhi.!"


"Vipi umelala na Sharon?" "Hapana nipo peke yangu. Sharon amesema hawezi kunitazama leo hivyo amehama chumba.!" "Ok, Basi naomba nije nikuone kidogo tu. Yani kidogo tu huenda nitaweza kupata usingizi usiku huu.!" "Hapana Kaka Owen huu sio muda mzuri wa sisi kuonana. Kama wazazi wako watagundua hili basi tutaibua tena matatizo


mengine. Nahisi kabisa kuna matatizo mazito yatanikuta mimi kaka Owen.!" "Laureen, Hakuna kitu chochote kibaya kinachoweza kukukuta ikiwa mimi nipo hai. Nakuomba tu nikuone japo kidogo ili nikuambie kitu muhimu ambacho sipaswi kulala kabla sijakuambia. Naomba uniruhusu nije chumbani kwako nikuone tafadhali.!" "Lakini kaka si uniambie tu hata kwa meseji hiko kitu. Mbona


hapa nakuelewa tu vizuri.!" "Laureen, Sio kila kitu kinapaswa kuzungumzwa kwa njia ya simu. Hiki ninachotaka kukuambia hutoweza kunielewa kwa njia ya simu. Nahitaji kukuambia nikiwa nakutazama ili uamini kwamba namaanisha kauli yangu. Lakini hii sio amri bali ni ombi. Kama hutaki nije kukuona basi ni sawa.!" "Kaka Owen, Hivi mimi napata wapi ujasiri wa kukataa ombi lako? Kiukweli kabisa, wewe ndo


dereva wangu Kaka. Maisha yangu mimi yapo mikononi mwako wewe. Kwa sasa naishi kwa kukusikiliza na kufanya kile unachotaka nifanye. Nipo hapa nakusubiri uje uniambie hiko kitu ulichonacho. Mlango upo wazi ukifika tu sukuma then ingia ndani.!" "Ok, Nakuja hapo dakika si nyingi. Asante sana kwa kunielewa Laureen.!" Hayo yalikuwa mazungumzo baina ya Owen na Laureen kwa


njia ya meseji. Baada ya mazungumzo hayo Owen alitoka chumbani kwake usiku ule na kwenda kwenye chumba cha Laureen kama walivyokuwa wamekubaliana. Owen alifika chumbani kwa Laureen na alimkuta mtoto wa kike amekaa tu kitandani akimsubiri. Mtaalamu aliamua kuvuta kiti kisha akakaa na kuanza kumtazama Laureen aliyekuwa anajaribu kutengeneza tabasamu ilihali alikuwa na maumivu mazito moyoni.


"Laureen my dearest, Kitu pekee kilichonipa msukumo wa kuja hapa ni kukuomba msamaha tu kwa yale yote yaliyotokea masaa kadhaa yaliyopita. Najua nimekukosea sana Laureen. Kiukweli kabisa halikuwa lengo langu kuzungumza maneno ya kukudharau na kukushusha thamani yako Laureen. Nilifanya vile ili kuzifurahisha nyoyo za wanaadamu hasa hasa wanasiasa wanaopenda kusikia kile wanachokitaka wao na sio kile unachotaka kuwaambia. Naomba unisamehe sana


Laureen. Maumivu uliyoyapata pale ni mara mbili zaidi ya maumivu niliyoyapata mimi. Sincerely, I feel your pain Laureen.!" Owen alizungumza kauli hiyo kwa hisia kali za upendo. "Kaka Owen, Mimi sidhani kama kuna kosa lolote ulilolifanya juu yangu muda ule. Yote uliyoyaongea yalikuwa na ukweli ndani yake hivyo sioni kosa lako kaka. Ni ukweli usiopingika kwamba status yangu ya maisha ni ya chini sana. Sina elimu na


nimekuwa kijakazi tu wa ndani. Ulikuwa sahihi kabisa kusema huna hisia zozote za mapenzi kwangu na huwezi kuwa kwenye mahusiano na mtu kama mimi. Kwa hilo siwezi kukulaumu kwa sababu unalinda brand yako na familia yenu kwa ujumla. Ukiachana na status yangu ya maisha lakini pia kuna siri nzito unaijua kuhusu mimi hivyo ni vigumu sana kwako kunipenda. Utapata wapi hisia za kunipenda wakati unajua nimeshatumika na wanaume tofauti tofauti? Ni mwanaume gani anayeweza


kumuoa kahaba kwenye haya maisha ya sasa? Mimi sina hadhi ya kupendwa na mtu kama wewe kaka Owen. Kwa hilo siwezi kukulaumu hata kidogo.!" "Laureen naomba usirudie tena kusema wewe ni kahaba. Nilishakuambiaga Laureen, sahau kabisa kama ulishawahi kuishi kwenye lile danguro. Nakuomba tena na tena, usirudie kuzungumza kauli hiyo mbele yangu au mtu yeyote yule. Naomba ufanye hivyo kwa ajili yangu mimi. Wewe hapo sio


kahaba Laureen.!" "Sawa Kaka nimekuelewa na sitorudia tena kuzungumza kauli hiyo. Ila Kaka Owen naomba nitumie nafasi hii kukuomba msamaha kwa magumu yote unayopitia kwa ajili yangu. Naomba unisamehe kwa kukusababishia mgogoro na wazazi wako. Kiukweli kabisa umejitoa sana kwa ajili yangu kaka Owen. Mambo uliyonitendea mimi ni makubwa sana ndo maana kila siku ninaposali huwa nakuombea kwa


mola akutangulie kwa kila jambo unalotaka kulifanya. Lakini pia nakuombeaga pia Mungu akupe hitaji la moyo wako.!" "Laureen, Hitaji la moyo wangu mimi ni wewe hapo. Mwanamke pekee ninayempenda kwa dhati ni wewe hapo Laureen. Hata hiyo tarehe 14 inayosubiriwa na wazazi, mwanamke nitakayemtambulisha ni wewe hapo. Laureen eeh, May you be My valentine?" "Hahah! Kaka Owen, Yani


umeamua kuleta utani wako wa siku zote kwenye mambo ya msingi. Me sipendi utani wa hivyo bwana. Kuna muda wa kutaniana na kuna muda wa kuwa serious.!" "Laureen, Ninachokisema muda huu namaanisha wala sio utani. Yale yote niliyoyaongea mbele ya wazazi masaa yaliyopita hayakuwa na ukweli ndani yake. Najua Laureen najua! Najua kwamba hata wewe unahisia kama zangu. Najua kabisa unanipenda japo unajidharau na


kujiona hustahili. Lakini kwangu mimi, wewe ni wathamani sana. Nakupenda sana Laureen. Wewe ndo mwanamke uliyefanikiwa kuziteka hisia zangu. Naomba ukubali kuwa mke wangu mtarajiwa.!" "Lakini Kaka Owen, wewe unastahili mwanamke bora kaka. Mwanamke anayeendana na hadhi yako kama alivyokuwa Juliette. Hivi Kaka, umesahau kule uliponitoa kaka? Sihitaji kukuaibisha na kuishusha hadhi yako Kaka Owen.!"


"Laureen, haijalishi nimekutoa wapi lakini mimi nakupenda hivyo hivyo. Kama watu wataniambia wewe ni malaya unajiuza basi nitawajibu kwamba mimi ndo nakununua.!" "Lakini Kaka Owen, kumbuka wazazi wako hawanitaki mimi. Hadhi yangu mimi ni ya chini sana kaka. Sina status ya kuridhisha nafsi za wazazi wako hivyo sidhani kama naweza kuwa Mrs wako..!"


"Laureen, Status inategenezwa hivyo ondoa shaka kabisa kuhusu hilo. Hata hao akina Julliete wanaoonekana kuwa bora, Status zao zilitengenezwa na watu. Nitahakikisha nakutengenezea status nzuri ili kukufanya uwe bora kwa wanaokudharau. Ile ahadi yangu ya kukutafutia chuo bado ipo pale pale wala sijasahau. Kwa sasa naomba uvumilie tu hizi changamoto za muda mfupi unazopitia. Lakini pia naomba uelewe kwamba moyo wangu mimi umekuchagua wewe


Laureen. Amini kwamba kwenye maisha kila kitu kinatokea kwa sababu. Naamini kabisa hatima ndo imetukutanisha mimi na wewe. Nakupenda sana Laureen, Naomba nitumie usiku wa leo kudhihirisha upendo wangu kwako. Leo nitalala hapa na wewe ili kukuthibitisha kwamba una sifa na vigezo vyote vya kugusa sehemu yoyote ile ya mwili wangu. Plizi Laureen, naomba tuufanye usiku wa leo kuwa usiku wetu wa kwanza kabisa wa kukumbukwa.!"


"Kaka Owen eeh, Maisha yangu mimi tayari nilishayakabidhi mikononi mwako. Moyo wangu mimi ulikuwa wa kwanza kukupenda wewe kabla yako. Miongoni mwa vitu vigumu kwa sasa kwenye maisha yangu ni kuzuia kile unachotaka kukifanya kwangu. Moyo wangu mimi umekuwa dhaifu sana kwako. Naanzaje kusema sitaki Kaka? Huo ujasiri wa kukuambia sitaki napata wapi wakati wewe ndo My super commando. You are my soldier Owen. Fanya chochote unachoona kitakupa


furaha kwenye mwili wangu. Do Babaa do, Do whatever you want to me. I'm yours Babaa.! Kiukweli kabisa hata mie nakupenda sana wewe.!" NOVEL.................... MY VALENTINE- 20 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................


0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ _________________________________ _____ Kwa hakika ulikuwa ni usiku wa kipekee kabisa kwa mtaalamu Owen pamoja na Laureen. Ni rasmi sasa Owen na Laureen walipigilia msumari penzi lao kwa kushiriki tendo la ndoa. Wote kwa pamoja walifurahia tendo na kuonesha nia thabiti ya kutaka kurudia tena na tena. Kwa


mara ya kwanza kabisa Laureen alijikuta anafurahia tendo la ndoa licha ya kukutana na wanaume kadhaa hapo awali. Ilikuwa hivyo kwa sababu siku zote mwanamke hufurahia tendo la ndoa endapo tu atalifanya na mwanaume mwenye hisia nae, mwanaume anayempenda kwa dhati. Hisia za mwanamke zipo tofauti sana na hisia za mwanaume. Mwanaume anaweza kupata raha ya tendo la ndoa kwa mwanamke yeyote yule, awe anampenda au hampendi. Lakini kwa


mwanamke raha ya tendo hawezi kuipata kwa mwanaume asiyempenda. Kwa hakika ule ulikuwa usiku usiosahaulika. Ulikuwa ni usiku ulioweka rekodi zake za kipekee kabisa kwa wawili wapendanao. "Laureen, asante sana kwa kuniamini na kunipa penzi tamu. Kuanzia leo naomba utambue kabisa wewe ni mwanamke wangu mimi. Wewe ndo mwanamke pekee ninayekuhitaji kwenye maisha yangu. Kwa gharama yoyote ile nitakufanya


ufurahi na kukulinda kwa sababu wewe ndo Valentine wangu.!" "My me, mpaka kufikia muda huu sina chochote nachoweza kusema kwako zaidi ya asante tu. Kiukweli kabisa wewe ndo unayetembea na moyo wangu My me. Kila raha anayostahili kupata mtu, kwako nimeipata. Hata raha ya tendo la ndoa sikuwahi kuipata kwa wanaume wote niliolala nao ila kwa mara ya kwanza nimeipata kwako. Sikupata raha kwao kwa kuwa sikuwa na hisia zozote juu yao.


Kwako nina hisia za dhati My me. Nilikuwa tu nasikia kwa watu mapenzi matamu ila sasa ndo nimethibitisha kauli yao. Kumbe ni kweli mapenzi matamu lakini ni pale tu unapompata mtu unayem'feel in real. Kaka Owen eeh, Nakupenda sana mimi. In deed, Nakupenda sana My me.!" Huo ndo ulikuwa mwanzo wa penzi jipya kati ya Owen na Laureen. Lakini bado waliamua kufanya siri na kusubiri wakati sahihi wa kulipua bomu ufike.


**** Naam! Naam! Habari mpya mjini ilikuwa ni ndoa ya Mr Robyson James pamoja na Madam Diana Calvin. Wazazi wa pande zote mbili walifanya maandalizi kikamilifu kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa ili kufanikisha harusi ya vijana wao. Kadi za ndoa zilisambaa kwa ndugu na marafiki wa familia hizo. Kule kwenye kampuni ya akina Diana, wafanyakazi waliandaa zawadi nyingi nyingi kwa ajili ya kumpa Diana siku yake ya harusi.


Familia ya Mr James na familia ya Mr Jay Calvin zilipania kufanya kufuru ya pesa kuelekea harusi ya vijana wao. Kila mtu alikuwa anasubiri kwa hamu sana harusi hiyo. Maadam siku hazigandi, hatimaye ile siku ilifika. Ilikuwa ni siku ya kipekee kabisa kwa Robyson na mwanadada Diana kuweza kufunga pingu za maisha. Watu wengi walienda katika kanisa la katoliki kushuhudia wapendanao wakihalalisha mahusiano yao kwa maandiko matakatifu yenye saini ya muumba wa mbingu na


ardhi. Familia nzima ya Mr James na Mr Jay Calvin zilikuwa ndani ya kanisa kushuhudia harusi hiyo. Laureen pia alikuwa mmoja wa watu waliokuwemo ndani ya kanisa. Muda sahihi ulipowadia, sauti ya kiongozi wa kanisa aliyekuwa na dhamana ya kufungisha ndoa ilisikika ikisema, "Bwana Robyson James, Je upo tayari kumuoa Bi Diana Calvin?" Kiongozi wa kanisa alimuuliza Robyson swali hilo.


Robyson alimtazama Diana kwa tabasamu pana kisha akajibu kauli ya kiongozi wa kanisa kwa kusema, "Ndio, nipo tayari kumuoa Bi Diana Calvin.!" Kufuatilia kauli ya Robyson kukubali kumuoa Diana, watu walifurahi sana ndani ya kanisa. "Bi Diana Calvin, Je upo tayari kuolewa na Bwana Robyson James?" Kiongozi wa kanisa alimgeukia Diana na kumuuliza


swali lile lile alilomuuliza Robyson. Swali la kiongozi wa kanisa lilimfanya Diana ashtuke kana kwamba taarifa ya kufunga ndoa alikuwa haijui. Diana alishtuka baada ya kusikia jina la Robyson James likitajwa kama ndo mtu anayetaka kumuoa. Kiukweli kabisa, swali lile lilimfanya awaze mbali sana. Alijikuta anaanza kukumbuka matukio kadhaa ya nyuma aliyopitia kwenye maisha yake ya mahusiano. Alikumbuka siku


moja akiwa na Owen nchini Marekani walikuwa wanajiigizia sauti za viongozi wa kanisa kuulizana swali kama lile aliloulizwa na kiongozi wa kanisa. "Hahah! Bwana eeh, Em niache basi usinichekeshe babaa. Nijibu swali hata kama siwezi kugezea sauti ya kiume.!" "Hahah! Yani natamani nisicheke lakini najikuta tu nacheka. Ujue una vituko sana Diana? Bora utumie tu sauti yako kuniuliza


hilo swali kuliko kulazimisha sauti ya kiume.!" "Hahah! Sawa natumia sauti yangu nijibu sasa mme wangu.!" "Sawa anza basi kuniuliza Pastor wa mchongo.!" "Ok, Bwana Owen James! Upo tayari kumuoa Bi Diana Calvin?" "Ndio, Nipo tayari kumuoa Bi Diana Calvin.!" "Hahah! Yani Owen wewe.!


Unavyokaza sura utadhani umelazimishwa kuoa. Kwahiyo siku ya ndoa yetu ndo utanikazia sura hivyo jamani?" "Sasa unataka nirembue kama mimi ndo Bi harusi. Hiyo ni kazi yako mtoto wa kike. Kwanza ni zamu yako ngoja nikuulize swali na wewe.!" "Hahah! Haya uliza nikuoneshe namna mtoto wa kike mie nitakavyokuwa siku ya harusi yetu.!"


"Ok, Bi Diana Calvin! Je upo tayari kuolewa na Bwana Owen James?" "Ndio, Nipo tayari kuolewa na Bwana Owen James kwa shida na raha.!" "Diana mpenzi wangu, Kiukweli kabisa naisubiri sana hiyo siku. Nataka kufunga pingu za maisha na wewe Diana. Nataka kuzeeka na kufa na wewe tu Diana.!" Hiyo ilikuwa ni kumbukumbu ya siku za nyuma za mahusiano kati


ya Owen na Diana. Wakati Diana anawaza hivyo, hata Owen nae alikuwa anawaza vile vile. Diana aliangaza macho kule walipokuwa wamekaa watu na akafanikiwa kumuona Owen. Muda wote Owen alikuwa anamtazama Diana na hapo wakajikuta wanakutanisha nyuso zao. Diana alijikuta anatokwa na machozi tu kila alipomtazama Owen. Kitendo cha Diana kushindwa kujibu swali la kiongozi wa kanisa kiliwachanganya sana watu. Kila mtu alishindwa kujua ni kwanini


Diana ameshindwa kujibu lile swali. Sio wazazi wala Robyson ambaye alielewa kilichokuwa kinamsibu Diana. Walishangaa tu kuona machozi yakimtiririka huku akiwa ametupa macho kule walipokaa watu. Hawakujua kwanini amekuwa vile wakati ile ndoa aliiridhiaga kutoka moyoni. Hata kwenye maandalizi ya ile ndoa alishiriki kwa asilimia zote. Hata marafiki zake pamoja na wafanyakazi wenzake aliwaalika yeye mwenyewe akiwa na furaha isiyo na kifani. Wazazi, Ndugu, jamaa na marafiki walishangaa


kuona Diana hana furaha ya ndoa kwenye sekunde za mwisho kabisa. Pengine ni Owen tu ndo alikuwa anajua sababu ya Diana kuwa vile. "Bi Diana Calvin, Upo tayari kuolewa na Bwana Robyson James?" Kiongozi wa kanisa alimuuliza Diana kwa mara ya pili baada ya kuona Diana ameshindwa kujibu swali la awali. Baada ya kiongozi wa kanisa kumuuliza Diana swali lile kwa


mara ya pili ndipo sasa Diana akashtuka kutoka kwenye dimbwi la mawazo na kukumbuka kwamba yupo kanisani kwa ajili ya kuolewa. Alitazama mbele yake akamuona Robyson akiwa ndani ya suti nzuri na pengine ndo alikuwa mwanaume aliyependeza kuliko wanaume wote pale kanisani. Diana aliwatazama wazazi wake akajua kabisa nini wazazi wake wanachokitaka. Mtoto wa kike alifumba macho kisha akafumbua na kusema,


"Ndio, Nimekubali kuolewa na Bwana Robyson James kwa shida na raha.!" Diana alizungumza kauli hiyo kwa sauti ya chini kabisa akijibu swali la kiongozi wa kanisa. Ilibidi kiongozi wa kanisa amuulize Diana kwa mara nyingine ili kuthibitisha lile jibu alilitoa. Mara ya tatu Diana alipoulizwa alijibu kwa sauti ya juu kwamba amekubali kuolewa na Mr Robyson. Watu walifurahi sana ndani ya kanisa. Hata Owen pia alionesha kufurahi kwa kuwa


kaka yake alipata mke. Lakini akiwa kama binadamu aliyeumbwa na moyo wa nyama, alijikuta anaumia kwa kiasi fulani. Aliumia kwa kuwa alishuhudia kwa macho yake ndoa ya mwanamke aliyewahi kumpenda na kudhania kwamba angekuja kuwa mke wake. Licha ya kwamba aliumia lakini maumivu yale hayakumuathiri kabisa kwani tayari alikuwa amepata tiba sahihi ndani ya moyo wake. Tiba yenyewe ni mwanadada Laureen ambaye alikaa pembeni yake kwa wakati


ule. Hatimaye kiongozi wa kanisa aliwafunga mbingu za maisha Bwana Robyson na Bi Diana na kuwaambia kwamba wapo kwenye hatima na kitu pekee kinachoweza kuwatenganisha ni kifo tu. Ni rasmi sasa zile ndoto za Owen na Diana zilizikwa mazima. Zile ahadi zote walizopanga kutimiziana zilibaki tu kwenye vitabu vya kumbukumbu za hadithi za kusadikika. Diana alifunga ndoa ile kwa maumivu mno kwani zile ahadi alizowekaga na Owen zilikuwa zinamfunga vifundo


ndani ya moyo wake. Kwa kuwa Owen hakuwa chanzo cha kuachana na Diana, alijikuta tu hana kifundo chochote moyoni wala kuwa na mgogoro wa nafsi. Roho yake ilikuwa nyeupe kabisa kwa sababu hakuwa na kitu cha kujilaumu baada ya kuyeyuka kwa ahadi zake kwa Diana. Kwa moyo mkunjufu kabisa, Owen aliikubali na kuifurahia ndoa ya Kaka yake na Diana. Mtaalamu alimtazama Diana kisha akajisemea tu moyoni, "Diana! Nitajitahidi kuitunza siri


yangu ili kulinda heshima ya ndoa yako. Hata nikisema nimwambie kaka bado sijui nitaanzia mstari gani ili anielewe. Bado sipati picha itakuwaje kuhusu ndoa yenu? Vipi kaka ataniruhusu kuja kwenu kuona familia?Kwa sasa nimechelewa. Itabidi tu nibaki nalo moyoni mpaka nitakapoingia kaburini. Lakini Diana, I thought and expect you could be my wife but the history choose a different path. I wish you all the best.!" Owen alijisemea moyoni maneno hayo na kumalizia kwa maneno


ya kiingereza yaliyokuwa na maana ya kwamba alifikiri na kutarajia kwamba Diana angekuja kuwa mke wake lakini historia imechagua njia tofauti. Yote kwa yote anamtakia kila la kheri kwenye maisha yake. NOVEL.................... MY VALENTINE- 21 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY......


SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ _________________________________ _____ Pale kanisani shughuli ilimalizika mapema tu. Wanandoa pamoja na marafiki waliojitokeza walielekea ukumbini ambako sherehe ilipangwa kufanyika. Liliandaliwa bonge moja la tafrija ndani ya ukumbi mmoja mkubwa


na maarufu zaidi ndani ya jiji. Ndani ya ukumbi kulikuwa na watu wenye nyadhifa tofauti tofauti kuanzia serikalini mpaka uraiani. Mr James aliwaalika viongozi wenzake wa siasa, Mr Jay Calvin aliwaalika wafanyabiashara wenzake, Robyson nae aliwaalika marafiki zake na Diana pia aliwaalika wafanyakazi wenzake pamoja na marafiki zake aliokuwa amesoma nao. Sherehe ilihudhuriwa na mamia ya watu. Juliette alikuwa miongoni mwa watu waliopata mwaliko wa kuhudhuria sherehe


ile. Mama yake Owen ndo alimpa mwaliko Juliette na lengo lake lilikuwa kumfanya Julliete awe karibu na Owen ile siku. Lakini pia, familia nzima ya Mr James ilikuwa ndani ya ukumbi. Ni Laureen na Munira tu ndo walibaki nyumbani baada ya kuzuiliwa kwenda ukumbini. Walizuiliwa kuhudhuria kwa sababu status zao zilikuwa ndogo na sherehe ilikuwa maalumu kwa ajili ya watu wenye nyadhifa kubwa nchini. Suala lile halikumfurahisha kabisa Owen. Alichokifanya ni kurudi nyumbani


wakati sherehe inaendelea na alipofika aliwaambia Laureen na Munira wajiandae kisha waende wote kwenye ile sherehe. Ilikuwa vigumu sana kwa Laureen na Munira kukubaliana na Owen kwa kuhofia kuvunja amri ya Mama mwenye nyumba ambaye aliwazuia kutoka. Lakini mwisho kabisa walikubali kuongozana na Owen mpaka kwenye ule ukumbi wa sherehe. Mama Owen alichukia sana kumuona Laureen na Munira pale ukumbini. Alijua kabisa Owen ndo aliwapeleka pale vijakazi wake. Ilibidi tu


Mama awe mpole kwa wakati ule ili asiharibu sherehe ya mwanae. Alichokifanya ni kumfuata Owen na kumwambia akae karibu na Julliete ili ampe kampani. Owen alimjibu Mama yake kwamba haitaji kampani yoyote pale ukumbini zaidi ya Laureen tu. Sio Julliete tu ndo alihitaji kampani ya Owen, hata baadhi ya wafanyakazi wa kike kwenye ile kampuni aliyokuwa anafanya kazi walitaka kampani ya Owen ile siku. Miongoni mwa wadada hao ni Salma na Linda. Kumbe ule mpango wa Owen kwenda


kumchukua Laureen na Munira ulikuwa ni kwa ajili ya kuwakwepa wanawake waliokuwa wanataka kampani yake. Zawadi mbalimbali zilitolewa kwa wanandoa. Siku hiyo Mr & Mrs Robyson walikusanya mali na pesa nyingi sana kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki. Mr James aliwazawadia wanandoa gari la kutembelea huku Mr Jay Calvin akiwapatia zawadi ya nyumba ya kuishi. Watu walifanya kufuru ya pesa pale ukumbini. Owen alitoa zawadi ya maua kwa shemeji


yake Diana ambaye alikuwa mpenzi wake hapo awali. Diana alijikuta anapokea maua yale kwa uchungu sana moyoni. Tukio hilo lilimtonesha kidonda kwa mara nyingine. Kwa namna hali ya Diana ilivyokuwa inabadilika kila alipokuwa anamtazama Owen, Robyson alikuwa anapata mashaka kidogo. Mara kadhaa alishuhudia hiyo hali lakini alishindwa kuelewa sababu ilikuwa ni nini haswa. Baada ya Owen kumkabidhi Diana maua alimgeukia Robyson na kumkabidhi zawadi ya saa moja


ya dhahabu. Zoezi la kutoa zawadi lilifungwa, na ratiba zingine zikafuata pale ukumbini. Kwa hakika siku hiyo watu walikula, wakanywa kadri wawezavyo na kufurahia burudani ya mziki laini kabisa. Watu walikaa kwenye meza kulingana na mahusiano waliyokuwa nayo. Kuna watu walikaa kifamilia, kuna watu walikaa kulingana na urafiki wao na kuna watu walikaa kulingana na uchumba na ndoa zao. Kiufupi kila mtu alikuwa na kampani yake. Hakuna mtu aliyekuwa


kwenye meza ya pekee yake. Meza nyingi zilitapakaa pombe huku meza chache tu ndo zilikuwa na vinywaji visivyokuwa na kilevi. Kulikuwa na meza za watu wawili, wanne mpaka watu kumi. Wakati Julliete anahangaika kumtafuta Owen ili wakae meza moja, alijikuta tayari amechelewa. Owen alikuwa amekaa na Laureen kwenye meza ya watu wawili tu. Juliette aliumia sana kuona tukio hilo. Lakini pia wazazi wa Owen hawakufurahishwa kabisa na kile kitendo. Walitamani kuchafua


hali ya hewa lakini wakahofia kuharibu sherehe. Ilibidi tu waache mambo kama yalivyo. Juliette alienda kujichanganya kwenye meza moja iliyokuwa na wafanyakazi wa kampuni aliyokuwa anafanya kazi Owen. Aliketi hapo na akina Mr Kaysimat kisha akaanza kunywa pombe kwa hasira. Kwa hakika siku hiyo watu walikunywa pombe. Kadri dakika zilivyokuwa zinakwenda ndivyo watu walivyokuwa wanalewa. Lakini sasa, wakati watu wanaendelea kunywa, Ghafla mfanyakazi


mmoja wa kampuni aliyokuwa anafanya kazi Owen alishtuka sana baada ya kumuona Owen na Laureen. Kilichomshtua ni baada ya kuona sura ya Laureen akiwa pale ukumbini. Jamaa alimtazama Laureen mara mbili mbili ili kujithibitishia kama ni yeye anayemkusudia au amemfananisha. Alimtazama bila kupepesa macho kisha akaanza kukumbuka tukio fulani lililotokeaga nyuma kati yake na mtoto wa kike. Kumbukumbu zake zilimpeleka mpaka kwenye lile danguro la makahaba.


Alikumbuka kwamba alikuwa mteja mkubwa sana wa mwanadada Laureen. Ilikuwa kila akienda kwenye lile danguro ni lazima amnunue Laureen tu. Zile siku alizokuwa anachelewa na kukuta Laureen amempata mteja mwingine, jamaa alikuwa anaondoka huku akiwa amechukia sana. Baada ya Laureen kuondoka kwenye lile danguro, hata wenzake nao waliacha ile kazi na kuanza kufanya biashara ndogo ndogo hivyo danguro lilifungwa. Yule jamaa aliendelea kutembelea


kwenye lile danguro kwa zaidi ya wiki mbili kwa ajili ya kumtafuta Laureen. Kila alipoenda hakuwaona tena wale makahaba. Lengo la jamaa lilikuwa kuonana na Laureen ili amnunue moja kwa moja kwa matumizi yake binafsi. Kiukweli kabisa alikolezwa mazima na penzi la mtoto wa kike. Baada ya kumtafuta Laureen kwa muda mrefu hatimaye alikata tamaa ya kumpata. Kwa hakika ilikuwa ni bahati sasa upande wake kuonana tena na Laureen pale ukumbini.


"Nipo sahihi ndo yeye mwenyewe.!" Yule jamaa alisemea moyoni maneno hayo kisha akainuka kwenye kiti na kuanzia kupiga hatua kuelekea kwenye meza aliyokuwa Owen na Laureen. Alipofika tu, Laureen alishtuka mara baada ya kumuona jamaa. "Bila shaka unanikumbuka mrembo.!" Jamaa aliongea kauli hiyo huku akiwa anamtazama Laureen.


"Oya Sule, mbona unafika sehemu na kuanza kuwavamia watu bila kutoa salamu?" Owen alizungumza kauli hiyo kwa yule jamaa aliyemfahamu mpaka jina lake. Alimfahamu kwa kuwa wote walikuwa wafanyakazi kazi kwenye kampuni moja. "Tulia Owen nazungumza na huyu demu kwahiyo wewe kaa kimya.!" "Sule, Naona leo umekunywa pombe nyingi sana. Fanya utaratibu uende nyumbani kwako


ukapumzike tu.!" "Owen nisikilize, Mimi sijalewa kama unavyofikiria wewe. Yani hapa nipo very understanding kwa kila kitu na kila mtu aliyekuwa mbele yangu. Naelewa nini nachokifanya. Huyu mwanamke ndo namuhitaji mimi. Nimetumia muda mrefu sana kumtafuta.!" Mr Sule aliongea kauli hiyo "Laureen unamjua huyu jamaa?" Owen alimuuliza Laureen.


"Hapana! Mimi simfahamu kabisa.!" Laureen alijibu. "Wewe malaya, hunifahamu mimi? Kwahiyo hunifahamu kisa upo na mteja mwingine?" Mr Sule alimuuliza Laureen kwa hasira. "Mr Sule, chunga maneno yako tafadhali. Binti ameshasema hakufahami wala hakujui kwahiyo ondoka tu kistaarabu tusiharibiane starehe.!" "Sikiliza Owen, huyo demu ananifahamu vizuri sana ila


ananikana ili kuficha maovu yake. Ngoja nikuambie kitu sasa, Kama unahisi umepata demu basi umepotea kabisa ndugu yangu. Huyo demu ni malaya tena wakujiuza barabarani. Achana na huyo demu Mr. Mimi nakuambia hivyo kwa sababu namfahamu vyema na nataka kukuonesha ushahidi wa picha kwenye simu yangu.!" Mr Sule alizungumza kauli hiyo kwa sauti ya juu na kufanya baadhi ya watu kusikia. Kauli ya Mr Sule ilimshtua sana


Owen na Laureen. Ile siri ya Laureen kuwa kahaba hatimaye ilikuwa ukingoni kufichuka. Bado Mr Sule alitaka kuonesha uthibitisho juu ya kauli yake ila Owen aliona ni bora afanye jambo ili kuzuia fedhea iliyokuwa inafuata. Pale pale Owen aliinuka na kumpiga teke Mr Sule kwenye ule mkono alioshika simu. Lengo lilikuwa kudondosha simu ili iharibike na kweli simu ilidondoka. Kwa hasira Owen alimkwida shingoni Mr Sule na kumwambia aache kufuatilia mambo yasiyomuhusu. Watu


walisogea karibu na kumtaka Owen amwachie Mr Sule. Owen alimwacha Mr Sule kwa kumsukuma na kumdondosha chini kwa hasira. Watu wote ndani ya ukumbi walishangaa sana juu ya ule ugomvi. Kila mtu alitaka kujua chanzo cha ule ugomvi. Mr Sule aliinuliwa chini na rafiki yake Mr Kaysimat kisha akarudishwa kwenye meza aliyokuwa awali. Owen nae alirudi kuketi mahala alipokuwa amekaa na Laureen tangu mwanzo. Wazazi wa Owen walimfuata Owen na kumuuliza


sababu ya ule mgogoro. Kule kwenye meza aliyokuwa Mr Sule na wafanyakazi wenzake mambo yalishaanza kuharibika. Mr Sule alipoulizwa kuhusu chanzo cha ugomvi aliwaeleza kila kitu kuhusu Laureen. Alikosa tu ushahidi wa picha kwa kuwa simu yake iligoma kuwaka. Ile stori ya Mr Sule, Juliette aliisikia vyema pale pale kwenye meza waliyokaa. Stori ya Laureen kuwa kahaba haikuwashtua kabisa akina Mr Kaysimat, Salma, Linda na wafanyakazi wengine. Lakini sasa, kilichokuja kutingisha


vichwa vya watu ni baada ya Juliette kuwaambia kwamba huyo kahaba ndo mwanamke anayependwa na Owen. Hapo sasa kila mtu alipata shauku ya kumuharibia Owen. Kwanza kabisa Linda na Salma walikuwa wanampenda Owen hivyo ile taarifa ya Owen kuwa na mahusiano na Laureen iliwaumiza. Pili, Mr Kaysimat alikuwa anamchukia sana Owen kwa kuwa alikuwa anapendwa na Linda ambaye ni mpenzi wake. Lakini pia baadhi ya wafanyakazi waliozimwa nyota zao baada ya


ujio wa Owen kwenye Kampuni, waliona ile ndo ilikuwa fursa ya kumuharibia Owen. Kila mtu alikuwa anasubiri simu ya Mr Sule iwake ili waanze kusambaza picha chafu za mchumba wa Owen. Juliette alimwambia Mr Sule akawaeleze wazazi wa Owen suala lile bila kupoteza muda. Mr Sule kwa kuwa alikuwa na hasira za kupigwa na kuharibiwa simu yake ya gharama, aliona ni bora akamueleze Mr James ukweli wote. Alitupa macho akamuona Mr James na mkewe


wanazungumza na Owen pamoja na Laureen muda ule. Jamaa akaenda pale pale kwa lengo la kufichua siri ya Laureen kwa wazazi wa Owen. "Wazee wangu, Kwanza kabisa naomba munisamehe kwa kusababisha fujo kwenye sherehe ya kijana wenu Robyson. Kuna kitu kikubwa sana kipo nyuma ya mgogoro uliotokea. Halikuwa lengo langu kusababisha fujo lakini nilikuwa namuokoa kijana wenu dhidi ya huyu Binti. Nyie hamumfahamu


vizuri huyu mwanamke ila mimi ndo namjua vyema kabisa. Kwa hekima na tahadhima naomba munipe idhini ya kuwaeleza uchafu wa huyu mwanamke.!" Mr Sule alizungumza kauli hiyo kwenda kwa wazazi wa Owen. Kauli ya Mr Sule ilitetemesha viungo vyote vya mwili wa Owen na Laureen wake. Pengine ni miujiza tu ya Mungu ndo ilikuwa inahitajika ili kuificha siri ya Laureen dhidi ya wazazi wa Owen. Lakini mpaka kufikia dakika zile, Laureen alikuwa


anawaza tu namna ya kwenda kuanza maisha mapya mtaani..... ITAENDELEA..... NYIE... NYIE... NYIEEE.. THIS_IS_MV14 INSTAGRAM: @realsilentkiller_ WHATSAPP 0713601762 #MV14 #Herrydesouzer #InsanityGenius #Silentkiller #MrIG #Sk97



Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.