Kitini cha Ufahamu wa Sheria ya Baraza la Vijana la Taifa katika Lugha Nyepesi

Page 7

SURA YA

01

UTANGULIZI NA MATUMIZI YA KITINI

(a) Utangulizi Tanzania ni moja ya nchi za kidemokrasia inayofuata misingi ya utawala bora ambapo mojawapo ni ushiriki wa wananchi. Vijana ni moja ya kundi muhimu nchini ambalo linakadiriwa kuchangia asilimia 65 ya nguvu kazi ya nchi. Ushiriki wa vijana kwenye mchakato wa maendeleo ni jambo la muhimu na la wakati hata kupelekea Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Bunge lake kupitisha Sheria ya Baraza la Vijana la Taifa Namba 12 ya mwaka, 2015. Kitini hiki kinalenga kuelezea masuala muhimu yaliyomo kwenye Sheria husika yahusuyo uanzishwaji na uendeshaji wa Baraza la Vijana la Taifa. Kitini kimegawanyika katika sura tisa. Sura ya Kwanza imeanza na Utangulizi na Matumizi ya Kitini, Sura ya Pili imebainisha Madhumuni ya Baraza la Vijana la Taifa, Sura ya Tatu imefafanua Muundo wa Baraza, Uanachama na Kazi za Baraza, Sura ya Nne imejikita kwenye Taratibu za Uendeshaji wa Baraza la Vijana la Taifa ikijielekeza kwenye Uteuzi wa viongozi, Muda wa Kukaa Madarakani na Mikutano ya Baraza. Sura ya Tano inahusu Bodi ya Ushauri ya Baraza, Sura ya Sita inabainisha Kamati za Vijana za Kata, Wilaya na Mikoa, Sura ya Saba imeelezea Fedha na Mali za Baraza, Sura ya Nane imeainisha Masuala Mengine Muhimu ya Kuzingatia na hatimaye Sura ya Tisa ni Hitimisho. (b) Chapisho hili litatumika:  Kuwahamasisha vijana na wadau ili waweze kushiriki kwenye mchakato wa kuunda Baraza la Vijana la Taifa.  Kuelimisha jamii hususan wazazi na walezi waweze kuruhusu vijana kushiriki mchakato wa uundwaji wa Baraza la Vijana nchini  Kuwa kisaidizi cha Kamati ya Kitaifa inayoratibu na kusimamia uundaji wa Baraza la Vijana la Taifa kuanzia ngazi ya Kata hadi Taifa  Kama nyenzo ya wawezeshaji, waelimishaji na wahamasishaji wa maendeleo ya vijana ili kurahisisha kazi zao.  Kuendelea kuwa kisaidizi kwa viongozi na watendaji ngazi zote za Baraza mara baada ya kuchaguliwa au kuteuliwa.

1


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.