{' '} {' '}
Limited time offer
SAVE % on your upgrade.

Page 1

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017

Novemba 2017


YALIYOMO VIFUPISHO.................................................................................. ii SHUKRANI...................................................................................iii MUHTASARI................................................................................ iv UTANGULIZI................................................................................ 1 MTAZAMO WA JUMLA WA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGS)..... 2 KUTOKA MALENGO YA MILENIA (MDGs) HADI MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs)..................................................... 3 KWA NINI TUNAHITAJI MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs)?.... 4 MPANGO WA PILI WA MAENDELEO WA MIAKA MITANO TANZANIA....... 4 UTEKELEZAJI WA SDGs NA FYDP II NCHINI TANZANIA...................... 5 WAJIBU WA WATENDAJI MBALIMBALI KATIKA UTEKELEZAJI WA SDGs.... 7 1. (i) VYOMBO VYA SERIKALI7 OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI)................................................................. 7 WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO.............................................. 7 KITENGO CHA TAKWIMU CHA TAIFA (NBS)................................ 8 TUME YA MIPANGO................................................................. 9 POVERTY ERADICATION DEPARTMENT (PED).............................. 9 (ii) BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.............. 10 Kikundi Kazi Cha Bunge Cha Maendeleo Endelevu Katika Bunge la Tanzania................................................................ 11 Wajibu wa Kikundi Kazi cha Bunge Kuhusu SDGs...................... 11 2. ASASI ZA KIRAIA................................................................. 12 (i) JUKWAA LA MAENDELEO ENDELEVU TANZANIA.................... 12 3. USHIRIKI WA SEKTA BINAFSI................................................ 14 HATUA MUHIMU ZILIZOFIKIWA KATIKA UTEKELEZAJI WA SDGs NCHINI..................................................................................... 15 CHANGAMOTO ZINAZOJITOKEZA KATIKA UTEKELEZAJI WA SDGs TANZANIA......................................................................... 17 MAPENDEKEZO NA HATUA ZA MBELENI......................................... 18 ii

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017


VIFUPISHO AFRICA PHILANTHROPIC FOUNDATION APF AZAKI (CSOs) ASASI ZA KIRAIA AWAMU YA II YA MPANGO WA MAENDELEO FYDP II WA MIAKA MITANO UKATILI WA KIJINSIA GBV MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU SDGs OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU NBS MPANGO WA MAENDELEO WA UMOJA WA UNDP MATAIFA POLICY FORUM PF OFISI YA RAISI - TAWALA ZA MIKOA NA PO-RALG SERIKALI ZA MITAA UMOJA WA MATAIFA UN UMOJA WA AFRIKA AU UNITED NATIONS ASSOCIATION OF UNA TANZANIA MALENGO YA MAENDELEO YA MILENIA MDG’S MBUNGE MB (MP) LA MAENDELEO ENDELEVU THE PLAT- JUKWAA TANZANIA FORM KIKUNDI KAZI CHA TAWALA ZA MITAA LGWG KIKUNDI KAZI CHA BAJETI YA SERIKALI ZA LGBG MITAA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO MoFP

iii


SHUKRANI Policy Forum inapenda kushukuru United Nations Association of Tanzania na African Philanthropic (APF) kwa uandishi wa kitabu hiki. Tunapenda kushukuru jitihada kubwa zilizowekwa kuhakikisha kuwa, kiitabu hiki kinaelezea kwa undani ni wadau gani wanahusika katika usimamizi na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu yaani Sustainable Development Goals (SDGs) nchini. Policy Forum, kipekee inapenda kuwashukuru wanachama wa kikundi kazi cha Tawala za Mitaa yaani Local Governance Working Group (LGWG) kwa kutoa ushirikiano na utaalamu wao katika uandishi wa kitabu hiki. Si rahisi kumtaja kila mmoja kwa majina, Ila kwa dhati kabisa, tunapenda kutoa shukrani kwa kila mmoja aliyetoa mchango na ushauri wa kitaalamu katika uandishi wa kiitabu hiki.

iv

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017


MUHTASARI Ni miaka 2 sasa tangu kukubalika na kuanza kwa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania. Ripoti ya Malengo ya Maendeleo Endelevu nchini Tanzania ya mwaka 2017 inachimbua kwa undani mchakato mzima tangu uzinduzi, mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji hapa nchini. Inaonyesha wajibu na michango ya Serikali, Asasi za Kiraia na wadau wengine katika kuhakikisha kuwa ajenda inadhihirika na hivyo kufanikiwa.

IDADI YA WATU: 51 MILIONI (2015) MJI MKUU: DODOMA MFUMO WA UTAWALA: RAISI / YA KIDEMOKRASIA NA MUUNGANO PRESIDENTIAL DEMOCRATIC REPUBLIC)

JAMHURI (UNITARY

PATO LA TAIFA: $44.9 BILLION (2015) UKUAJI WA PATO LA TAIFA: 7 % (2014) KIWANGO CHA MAPATO: CHINI (OECD) UMRI WA KUISHI: 61.7 YEARS KUSOMA NA KUANDIKA: 70.6 % KIPIMO CHA MAENDELEO YA WATU: 0.521 (2014) GINI COEFFICIENT: 0.37 (2013)

v


Katika kusherehekea kumbukumbu ya miaka miwili tangu kuridhiwa kwa malengo haya, kikao cha AZAKI kilifanyika Dar es Salaam kushirikishana uzoefu, waliyojifunza na kubunga bongo (brainstorm) ili kupata njia bora zaidi za jinsi wadau mbali mbali watakavyoweza kutimiza wajibu wao kwa ufanisi katika utekelezaji, ufuatiliaji wa mara kwa mara wa SDGs nchini Tanzania hasa katika ngazi za Mikoa na Wilaya. Zaidi ya hayo inachambua uwajibikaji wa wahusika mbali mbali katika utekelezaji wa ajenda nchini, kuanzia Serikali kuu hadi chini kwenye wizara, mashirika yake na Asasi za Kiraia. Ripoti hii inaonyesha msingi wa ufuatiliaji na mapitio ya SDGs ikionyesha mchango kwa kila mhusika katika mchakato mzima. Dira ya Maendeleo ya Tanzania (TDV) 2025 inataka Tanzania igeuzwe kuwa ya uchumi wa kati na nusu-viwanda ifikapo mwaka 2025. Mafanikio yaliyopatikana yalijadiliwa kwa uwazi na mapendekezo kutolewa ya jinsi ya kusonga mbele zaidi ili kufikia dira ya Malengo ya Maendeleo Endelevu nchini Tanzania. Ni kwa kujitoa kwa dhati na kwa ushirikiano, Malengo ya Maendeleo Endelevu yanayotekelezwa kupitia Awamu ya Pili ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP II) yatafikiwa na kufikika.

vi

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017


UTANGULIZI Mwaka 2015 ulikuwa mwaka wa mafanikio katika maendeleo ya ulimwengu kwa kuwa Malengo ya Milenia yaliyowekewa sahihi mwaka 2000 yakiwa na malengo makuu 8, malengo madogo 21, na viashiria 60 yalifikia mwisho wake. Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa waliwekeana mkataba wa kihistoria kuunda ajenda za kimataifa kuongoza vipaumbele vya maendeleo kwa kizazi, na kwa kudhamiria kwa dhati kuondoa UMASKINI, KUPAMBANA NA UKOSEFU WA USAWA, KUJENGA JAMII ZENYE AMANI, UMOJA ZISIZOTETEREKA, na KUHAKIKISHA UWEPO WA SAYARI SALAMA KWA SIKU ZIJAZO na HALI NZURI YA VIZAZI VIJAVYO. Ajenda hizi zinajumuisha: Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030; Mfumo wa Sendai wa Kupunguza Uwezekano wa Majanga; Ajenda ya Utendaji ya Addis Ababba kwa Utoaji Fedha za Maendeleo na Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa. Pamoja na kwamba mikataba hii ni ya kimataifa, utekelezaji wake ni wa ndani ya nchi na matokeo yao yataonekana na kufahamika kwanza ndani ya nchi kabla ya kujulikana kama matokeo ya kimataifa. Nchi mbali mbali duniani ikiwa ni pamoja na Tanzania ziko katika hatua tofauti tofauti za utekelezaji na ufuatiliaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu. Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu nchini Tanzania ulianza katika muda muafaka wakati serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani na kuanza kazi, awamu ya pili ya Mpango Mkakati wa Taifa wa miaka mitano (2016-2020) na awamu ya tatu ya Mpango Mkakati wa Kuondoa Umaskini Zanzibar (MKUZA 2016-2020) ulipozinduliwa, Mpango wa Pili wa Misaada ya Umoja wa Mataifa (UNDAP II) kwa Tanzania ulipotiwa sahihi, na Tume ya Mipango ilipounganishwa na Wizara ya Fedha. 1


MTAZAMO WA JUMLA WA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGS) Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ni seti ya malengo ya kimataifa yaliyoridhiwa Septemba 2015 na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa. Malengo haya ya Maendeleo Endelevu yameorodheshwa katika Ajenda 2030, pamoja na Malengo Endelevu ya Maendeleo 17; na malengo madogo 169; yaliwekewa sahihi na Wakuu wa Nchi na Serikali katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo Endelevu, mwezi Septemba mwaka 2015. Ajenda ya mwaka 2030 kwa Maendeleo Endelevu inaeleza kwa kifupi mpango wa utekelezaji kwa sayari yetu ambapo “hakuna anayeachwa nyuma” Ajenda hiyo itatumika kama mpango mkuu wa kuongoza mpango wa maendeleo wa kimataifa na kitaifa kwa miaka 15 ijayo.

2

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017


KUTOKA MALENGO YA MILENIA (MDGs) HADI MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) Malengo ya Milenia yalikuwa na dhamira ya dhati ya kufanikisha malengo makuu nane (8) yenye kupimika ambayo yanajumuisha kupunguza umaskini wa hali ya juu na njaa kwa nusu ya kiwango kilichokuwepo, kuhamasisha usawa wa kijinsia na kupunguza vifo vya watoto ifikapo 2015. Malengo ya Milenia yalikuwa ya kimapinduzi katika kutoa lugha inayoeleweka na wote kufikia mkataba wa kimataifa. Malengo

hayo 8 yalikuwa halisi na rahisi kuelezea, yenye vipimo vya wazi na taratibu za ufuatiliaji. Mafanikio kadha wa kadha yalipatikana kutokana na utekelezaji wa MDGs ingawa mafanikio haya hayakulingana katika nchi zote duniani. Katika ngazi ya kidunia ilifanikiwa kufikia lengo la kwanza la kupunguza umaskini mkubwa kwa nusu ilipofika mwaka 2015. Kwa dhamira ya kuandaa ajenda mpya ya maendeleo yenye kujali watu, ushauri wa kimataifa ulifanyika mtandaoni (online 3


consultation) na nje ya mkondo (offline consultation). Asasi za kiraia, wananchi, wataalamu wa sayansi, wanazuoni na sekta binafsi kutoka ulimwenguni kote walishiriki kikamilifu katika mchakato huu. Mkutano wa Rio+20 (Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo Endelevu) uliofanyika Rio de Janeiro, Juni 2012, uliamsha ari ya kuanza mchakato wa kuandaa seti mpya ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo yataendeleza mwendo (momenta) ulioanzishwa na MDGs na kuingia katika mfumo wa maendeleo wa kimataifa zaidi ya mwaka 2015. Hali hii yenye nguvu zaidi ya umiliki sharti iwezeshe malengo haya kuwa chombo cha kuleta mabadiliko kwa ufanisi zaidi katika miaka 15 ijayo.

4

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017


KWA NINI TUNAHITAJI MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs)?

Malengo ya Maendeleo Endelevu ni ya kimataifa na kila nchi ina wajibu wa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa malengo haya. Hatua hii inavunja kabisa dhana iliyokuwepo kwamba mabadiliko makuu ya kiutendaji sharti yatekelezwe na nchi maskini peke yake. Serikali nyingi zilichangia kwa kiwango kidogo sana wakati MDGs zikiandaliwa mwaka 2000, ilhali watu wa ngazi za chini 5


ambao walitakiwa wanufaike nayo hawakuhusishwa kabisa. Hali hii ilichelewesha mno hatua za utekelezaji wake na kupunguza matokeo yake kwa ujumla. Mchakato wa kuandaa SDGs umekuwa wa wazi zaidi, na majadiliano ya kitaifa na mashauriano ya vikundi kazi yakijumuisha watu wengi ulimwenguni kote. Wakati wa utekelezaji wa Malengo ya Milenia (MDGs), kinadharia, yalionekana kutekelezeka kwa nchi zote lakini kiuhalisia yalichukuliwa kama malengo madogo ambayo nchi maskini pekee ndizo zilitakiwa ziyafanikishe kwa kutegemea fedha kutoka kwa mataifa tajiri. Hali hii ni tofauti katika kipindi hichi cha utekelezaji wa SDGs, ambapo kila nchi inategemewa kufanya kazi kuwezesha ufanikishaji wa malengo haya mapya.

6

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017


MPANGO WA PILI WA MAENDELEO WA MIAKA MITANO TANZANIA Kauli mbiu ya FYDP II “Kukuza Viwanda kwa Mageuzi ya Uchumi na Maendeleo ya Watu” inajumuisha mkazo wa mifumo miwili, yaani Ukuzaji na Mageuzi (FYDP I) na Upunguzaji Umaskini (MKUKUTA II). FYDP II unaeleza kwa kifupi miradi/shughuli mpya zitakazowezesha Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa namna itakayogeuza uchumi na jamii yake. Pia unajumuisha miradi/ shughuli ambazo hazijakamilika kutoka Mpango Mpango Mkakati ulioisha, ambazo ni za muhimu kwa mafanikio ya FYDP II. Muhimu zaidi, na sambamba na mipango hiyo miwili iliyopita, FYDP II pia inatekeleza vipengele vya Dira ya Maendeleo Tanzania (TDV) 2025 ambayo inadhamiria Tanzania igeuzwe kuwa nchi ya uchumi wa kati na nusu-viwanda ifikapo mwaka 2025, yenye sifa zifuatazo: (i) Maisha Bora naEndelevu yanayokidhi mahitaji ya msingi (ii) Amani, kutoyumba na umoja (iii) Utawala bora na wa kufuata sharia (iv) Jamii iliyoelimika na inayojifunza; na (v) Uchumi wenye nguvu na wa ushindani (Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21)

7


UTEKELEZAJI WA SDGs NA FYDP II NCHINI TANZANIA Tanzania imeendelea kupiga hatua katika utekelezaji wa makubaliano ya kimataifa kuhusu maendeleo endelevu ikiwa ni pamoja na Ajenda 2030 ya Maendeleo Endelevu. Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yanaendelea kutekelezwa katika mfumo wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 na mpango wake wa kati wa maendeleo wa miaka mitano (FYDP II (2016/172020/21) ambao hivi sasa, unafanyiwa kazi. Moja kati ya malengo ya FYDP II ni kuhakikisha kuwa mikataba ya kikanda na kimataifa (ikiwemo Ajenda ya Afrika 2063 na SDGs) iwe imeingizwa vya kutosha katika upangaji wa mipango ya maendeleo ya taifa na mifumo ya utekelezaji kwa manufaa ya nchi. Vyombo muhimu kwa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu nchini Tanzania vinajumuisha; Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Tume ya Mipango na Ofisi ya Raisi -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (PO-RALG) na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu mwaka 2000, mchakato wa upangaji Mipango ya Maendeleo Tanzania umekuwa ukiongozwa na Dira ya Maendeleo ya Tanzania (TDV) 2025. Dira ya Maendeleo ya Tanzania ni mwongozo wa kitaifa kwa mageuzi ya kiuchumi kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025. Katika kipindi cha nyuma, dira imekuwa ikitekelezwa kupitia mipango mingi ya kati. Kuanzia 2016, mipango hii mingi ya kati (Mpango Mkakati wa Kukuza na Kupunguza Umaskini, Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ) imefungamanishwa katika Mpango mmoja na kuwa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano, FYDP-II (2016/17-2020/21) ili kunufaika na utekelezaji wa pamoja wa malengo yanayofanana.

8

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017


Mpango wa Pili wa maendeleo wa Miaka Mitano na kauli mbiu ya “Kukuza Viwanda kwa Mageuzi ya Uchumi na Maendeleo ya Watu� ulizinduliwa rasmi tarehe 7 Juni 2016. Michakato ya kuandaa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano ulitokana na matokeo ya Ajenda ya Maendeleo Endelevu 2030 na Ajenda ya Afrika 2063.

Utekelezaji wa FYDPII Tanzania unafanyika kwa kuoanisha na Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs). Kufuatia vipaumbele vya FYDPII malengo yafuatayo yalichaguliwa rasmi kwa utekelezaji; Lengo 1: Kuondoa umaskini Lengo 2: Kilimo na Uhakika wa Chakula Lengo 3: Afya Lengo 4: Elimu Lengo 5: Usawa wa Kijinsia 9


Lengo 6: Maji na Usafi Lengo 7: Ugavi wa Nishati Lengo 9: Miundombinu na viwanda Lengo 17: Kuimarisha mbinu za utekelezaji na kuchochea ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo endelevu

10

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017


WAJIBU WA WATENDAJI MBALIMBALI KATIKA UTEKELEZAJI WA SDGs

1. (i) VYOMBO VYA SERIKALI OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) Kama sehemu ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (PORALG) imeanzisha mipango mikakati ambayo ni nyongeza kwa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano kwa ngazi za mikoa na wilaya. WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO Kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Wizara ya Fedha na Mipango inaandaa mfumo wa kitaifa wa utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya Ajenda 2030. Mpango huu pia umeipa Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP) wajibu wa kutoa ripoti za utendaji wa SDGs zitakazosaidia katika mchakato mzima wa utekelezaji, ufuatiliaji na mapitio katika ngazi ya nchi. 11


Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP) kupitia Kitengo cha Kupunguza Umasikini (PED) imeanza kuandaa Ripoti ya Awali ya Nchi (Baseline) ya Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs). Ripoti hii ndiyo inatoa msingi wa ripoti nyingine zote zitakazoandaliwa baadaye kuhusu maendeleo ya SDGs. Ripoti hii itakuwa na taarifa kuhusu hali na mwenendo wa viashiria vya kitaifa kwa kila lengo dogo na malengo makubwa. Pia itaainisha mapengo ya takwimu pamoja na mapengo ya kisera na kitaasisi katika kufanikisha malengo makuu yaliyokusudiwa nchini Tanzania. Ripoti ya Awali miongoni mwa mengine inakusudia:  Kuandaa taarifa ya awali itakayotumika katika utoaji wa ripoti ya SDGs. Mapengo katika data yataainishwa na taratibu za kujaza hayo mapengo.  Kuwezesha utoaji wa ripoti za muda / vipindi fulani kuhusu SDGs kwa wadau wa taifa na wa kimataifa  Kuchambua mafanikio ya SDGs kwa nia ya kuamua hatua za baadaye.  Kuimarisha uelewa wa mwingiliano wa malengo ili kufahamu hatua stahiki za kuchukua wakati wa mchakato wa utekelezaji. KITENGO CHA TAKWIMU CHA TAIFA (NBS) Kwa mujibu wa FYDP II, wajibu wa NBS utakuwa kutoa takwimu za msingi na takwimu ambazo zinahitajika katika ufuatiliaji na tathmini ya malengo na shughuli za kimkakati za FYDP II. Katika, utekelezaji wa SDGs nchini, NBS kimekuwa ni chombo kikuu katika utoaji wa takwimu kitaifa kwa lengo la kuweka msingi wa kutegemewa kuhusu upatikanaji wa takwimu ili kuweza kufidia mapengo kwa upangaji na ufuatiliaji wenye uthibitisho wa mipango ya maendeleo Kitaifa na ya Kimataifa ikijumuisha Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Malengo ya Maendeleo Endelevu vilevile. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Shirika la Ulimwengu la Ushirikiano wa Takwimu za Maendeleo Endelevu 12

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017


(GPSDD), Benki ya Dunia na MCC-PEPFAR waliandaa Warsha ya Kitaifa hapa nchini kuhusu Ramani ya Takwimu za SDG kati ya tarehe 12 hadi 13 Agosti 2016. Warsha hiyo ilitangulia nyingine iliyofanyika mwezi Octoba, 2015 kuhusu kuzifanya SDGs ziendane na nchi husika. Washiriki 300 kutoka serikali, asasi za kiraia, asasi zisizo za serikali, sekta binafsi, na wabia wa maendeleo walijadili kuhusu masuala ya maendeleo na utekelezaji wa SDGs kwa kuhusisha matumizi bora zaidi ya takwimu kupima utekelezaji. Kamati ya pamoja ya muda mfupi iliundwa, NBS ikiwa Mwenyekiti, kusaidia NBS katika kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo na uandaaji wa ramani ya takwimu za SDG. Baadhi ya mapendekezo yamekwishatekelezwa, mengine yako katika utekelezaji na mengine yatatekelezwa katika miezi ijayo. TUME YA MIPANGO Tume ya Mipango tayari imeshaunganisha malengo ya FYDP II na SDGs. Kwa sasa Tume ya Mipango iko katika mchakato wa kukamilisha utaratibu wa utekelezaji na ufuatiliaji (monitoring framework). POVERTY ERADICATION DEPARTMENT (PED) Idara ya Kuondoa Umaskini (PED) imekuwa ikiandaa warsha za kuhamasisha maofisa wa serikali. Awamu ya kwanza ya hizi warsha za kuhamasisha zilijikita katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa (LGAs). Warsha ya hivi karibuni na ya mwisho kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa ilifanyika wakati wa juma la pili la mwezi Januari huko Dodoma, ambapo NBS nao walishiriki. Awamu nyingine ya warsha za kuhamasisha zitakazoendeshwa na PED itajikita katika Wizara, Idara na Wakala wa serikali (MDAs). Mipango ya kuwa na vipindi na Makatibu Wakuu imeanza kama sehemu ya vipindi vya uhamasishaji wa wizara, idara na wakala wa serikali kuu.

13


(ii) BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge wana wajibu muhimu wakati wa kuandaa sheria, bajeti na usimamizi wa shughuli za serikali kuhakikisha masharti/misimamo ya kisiasa na malengo ya Ajenda 2030 ya Maendeleo Endelevu na Ajenda ya Umoja wa Afrika 2063 yanatekelezwa kupitia mifumo ya sera maridhawa na mipango ya maendeleo ya taifa. Kama wawakilishi wa wananchi, wabunge wanao wajibu wa kuhakikisha kuwa hakuna anayebakizwa nyuma kwa kuwezesha maendeleo ya watu na upangaji shirikishi wa maendeleo na bajeti inayojali mahitaji ya makundi yaliyo katika mazingira magumu na hatari ya kuachwa nyuma kama vile watu wenye vilema, watoto, wazee, wanawake na vijana n.k Ofisi ya Karani wa Bunge la Taifa ilitambua uwezo na wajibu muhimu ambao Bunge la Tanzania linaweza kufanya kuhusu utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu mwanzoni mwa 2016. Mwezi Machi, 2016 Ofisi ya Karani wa Bunge la Taifa ilifadhili ushiriki wa wabunge watatu katika mkutano wa wabunge wa Kiafrika juu ya Maendeleo Endelevu huko Abuja, Nigeria. Tarehe 4 Juni 2016, Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa ushirikiano na Wizara ya Fedha na Mipango, na Bunge la Tanzania iliandaa semina ya uhamasishaji kuhusu SDG kwa ajili ya wabunge mjini Dodoma na ikiongozwa na Naibu Spika, Mh. Tulia Ackson (MB). Tangu Juni 2016, Ofisi ya Karani wa Bunge la Taifa ilikuwa imepeleka maombi ya uanzishwaji wa Kikundi cha Bunge cha Malengo ya Maendeleo Endelevu pamoja na Hati za awali na mapatano mengine ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia. Kwa hivi sasa, masuala ya maendeleo ikiwa ni pamoja na Maendeleo Endelevu yanafanyiwa kazi kupitia kamati 10 za sekta mbali mbali 14

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017


za bunge zilizopo, kamati mbili za sekta mtambuka na kamati 3 za kuchunguza masuala ya bunge (watchdog committee),

Kikundi Kazi Cha Bunge Cha Maendeleo Endelevu Katika Bunge la Tanzania Kwa kuzingatia jinsi Maendeleo Endelevu yanavyoweza kuleta mageuzi, na kwa kulingana na Azimio la Umoja wa Mabunge ya Afrika R.141/39/16 kuhusu wajibu wa Mabunge ya Afrika katika kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, tunaamini kwa dhati kwamba kikundi kazi cha wabunge kuhusu SDGs kitaimarisha nafasi ya bunge la Tanzania katika upangaji, utengaji rasilimali, usimamizi / uangalizi wa utekelezaji, ufuatiliaji na mapitio ya utekelezaji wa miradi na mipango ya maendeleo endelevu Tanzania. Wajibu wa Kikundi Kazi cha Bunge Kuhusu SDGs • Kuhakikisha utimizwaji wa misimamo ya kisiasa katika utungiaji sheria na utekelezaji wa hati za awali (protocols), mapatano (conventions), na misimamo (commitments) za kimataifa katika ngazi ya kibunge 15


• Usimamizi na uwajibikaji katika utekelezaji wa hati za awali, mapatano na misimamo ya kimataifa • Sera na sheria zioane na misimamo ya kimataifa • Kamati husika za bunge kuwezesha muunganiko, mfungamano, utendaji mpana wa miradi/shughuli zenye malengo yanayofanana na uelewa wa Maendeleo Endelevu na misimamo mengine ya kimataifa • Kuwezesha shughuli za wadau mbalimbali, ushirikiano na majadiliano kuhusu maendeleo endelevu na watendaji, wahisani / wabia wa maendeleo, asasi za kiraia, sekta binafsi, na wataalamu au wanazuoni. • Utengaji wa bajeti unaozingatia haki sawa na unaozingatia na kulandana na vipaumbele vya taifa na malengo ya misimamo/ makubaliano ya kimataifa ambayo serikali ya Tanzania imeridhia. • Kuhakikisha usawa na uwajibikaji katika maeneo matatu ya maendeleo endelevu (kijamii, kiuchumi, na kimazingira) • Kuhakikisha ushirikiano wa vyama mbali mbali katika suala la Maendeleo Endelevu • Kuhakikisha maendeleo endelevu yanayojali na kushirikisha watu, bila kumwacha mtu yeyote nyuma. • Kuunga mkono ukusanyaji wa rasilimali za ndani kwa maendeleo ya Tanzania. • Kuandaa ripoti ya mwaka kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu Tanzania, ambayo itachambua, maendeleo kwa ujumla, mafanikio makuu na changamoto katika kufikia maendeleo endelevu Tanzania. • Kuongoza mijadala bungeni kwa kuunga mkono maendeleo endelevu. • Ushirikiano wa Kimataifa na uwakilishi katika mikutano ya kimataifa. 2. ASASI ZA KIRAIA (i) JUKWAA LA MAENDELEO ENDELEVU TANZANIA Jukwaa la Taifa la Asasi za Kiraia kwa Maendeleo Endelevu liliundwa Aprili 2005 baada ya warsha ya wadau kuhusu mapito kutoka MDGs 16

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017


hadi SDGs iliyoandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Mataifa Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya Africa Philanthropic Foundation– APF). Moja kati ya matokeo muhimu ya warsha hiyo ilikua ni pendekezo la kuanzishwa kwa jukwaa la AZAKi kuwezesha uratibu wa shughuli za AZAKi Tanzania kuhusu masuala ya Maendeleo Endelevu, na kuwa na jukwaa la kushughulika na serikali, Umoja wa Mataifa, wadau na wabia wengine wa maendeleo. Taasisi ya Africa Philanthropic Foundation (APF) na United Nations Association of Tanzania (UNA-Tanzania) zilijitolea kuwa waasisi wenza na waratibu wa mwanzo wa shughuli za Jukwaa hili. Jukwaa ni la hiari na ni la wazi kwa asasi za kiraia kujikusanya, kujipanga na kuratibu shughuli zao ili kuhakikisha ushiriki wenye matunda na kuchangia katika utekelezaji, ufuatiliaji na ufuatiliaji wa mara kwa mara wa Maendeleo Endelevu Tanzania. Jukwaa la Maendeleo Endelevu Tanzania linaendelea kuwa mstari wa mbele kushirikiana na Serikali pamoja na wabia wengine wa maendeleo wanapotaka kushirikiana na Asasi za Kiraia katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu Tanzania. Jukwaa linaendelea na wajibu wake kama sehemu ya data ya Maendeleo Endelevu, na hivi karibuni iliombwa kuwadhamini wanasayansi wawili wa takwimu kushiriki katika kamati ya taifa ya kiufundi kwa kushirikiana na NBS kwa ajili ya kuwa mstari wa mbele kitaifa katika kupokea na kutoa taarifa za kiufundi. Jukwaa la Maendeleo Endelevu Tanzania kupitia AFP na UNA Tanzania inafanya kazi kwa kushirikiana na NBS, na shirika la Data Shift ili kuandaa mwongozo wa asasi za kiraia kuhusu sheria ya takwimu ya mwaka 2015 Tanzania. Lengo la mwongozo huu ni kuwezesha asasi za kiraia kuzalisha na kutumia takwimu kufuatana na Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2025 na miongozo yake. Zaidi ya hayo, hatua hii itaambatana na kuandika rasmi maoni na mapendekezo ya asasi za kiraia kwa ajili ya kuboresha Sheria ya Takwimu ya 2015 pamoja na miongozo yake. 17


Shughuli kati ya Jukwaa la Maendeleo Endelevu Tanzania na Bunge la Taifa kuhusu uanzishwaji wa Kikundi Kazi cha Bunge imekamilika. Hivi sasa Jukwaa linaendelea kushughulika na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kufungua nafasi za asasi za kiraia katika ngazi za mikoa, wilaya na jamii kushiriki katika maandalizi, utekelezaji, ufuatiliaji na mapitio ya mipango mikakati ya wilaya na mikoa. Vilevile Jukwaa la Maendeleo Endelevu Tanzania ilishirikishwa na shirika la UNDP Tanzania kuchangia katika ujenzi wa uwezo kwa ajili ya uandaaji wa mfumo Uratibu wa Maendeleo Endelevu (implementation framework) hapa Tanzania. Mfumo huu utakuwa pointi ya rejea kwa juhudi za UN katika kujenga uwezo wa Maendeleo Endelevu Tanzania. Jukwaa la Maendeleo Endelevu Tanzania hivi sasa linakamilisha zoezi la kukusanya taarifa ya mchango wa asasi za kiraia katika utekelezaji wa FYDPII, SDGs, na Ajenda 2063, na mchango wao katika ufuatiliaji na tathmini ya mipango tajwa. Hii ni pamoja na kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango katika mchakato wa kuandaa takwimu za awali (baseline) na maandalizi ya mfumo wa taifa wa ufuatiliaji na tathmini. Asasi za Kiraia na Wahusika Wasio wa Serikali wanaendelea kufanya kazi muhimu katika mfumo wa takwimu wa Tanzania kupitia kazi za Asasi / Mashirika kama vile “The Tanzania Data Lab (D-Lab), Data Zetu, na Data for Local Impact Innovation Challenge (DLI)�. 3. USHIRIKI WA SEKTA BINAFSI Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yamekuwa ni fursa kubwa kwa jamii inayojishughulisha na masuala ya maendeleo kujihusisha kimkakati na sekta binafsi. Sekta binafsi ina nguvu ya ubunifu na uwezo wa kutoa ufumbuzi kwa changamoto nyingi zilizoko katika ulimwengu wetu hivi leo. Kwa kuwa tumeshaanza hatua za utekelezaji, tunahitaji kampuni nyingi zaidi kuongeza 18

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017


uwekezaji na shughuli za biashara kuweza kufikia malengo ya kimataifa. Kwa mfano, Lengo la 12 la Matumizi na Uzalishaji wenye Uwajibikaji linawajibisha sekta binafsi kuwa waangalifu zaidi kwa matumizi ya rasilimali zilizopo ardhini. Lengo ni kuchochea matumizi ya ufanisi ya rasilimali na nishati, miundombinu endelevu, na kuwezesha ufikiaji wa huduma za msingi, kazi yenye heshima na maisha bora kwa wote. Mafanikio katika ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu kunahitaji upunguzwaji wa haraka wa athari za Kiikolojia zinazotokana na shughuli zetu kwa kubadilisha jinsi tunavyozalisha na kutumia bidhaa na rasilimali. Sekta binafsi inawajibu mkubwa kwa suala hili. Kupitia ubia wa Serikali na sekta binafsi, sekta binafsi inaweza kuwa na nguvu ya teknolojia mpya ambazo zinaweza kupanuliwa zaidi kwa matokeo mapana zaidi. Kwa mfano mitambo ya mawasiliano kwa njia ya simu za mkononi Tanzania imeonyesha mfano mzuri siyo tu wa ubunifu kwa maendeleo kupitia uhawilishaji wa fedha taslimu lakini pia matumizi ya teknolojia ya simu za mkononi kuendeleza huduma za afya na elimu. Wajibu wa sekta binafsi ukioanishwa na utekelezaji wa SDGs unaweza kuonekana kupitia shughuli za Wajibu wa Kampuni kwa Jamii (Corporate Social Responsibility-CSR) kwa lengo la kuhakikisha kuwa makampuni yanaendesha shughuli zao kwa njia ambayo ni ya kimaadili. Hii ina maana kwamba makampuni ni sharti yazingatie matokeo / athari ya shughuli zao kijamii, kiuchumi na kimazingira, pia kuzingatia haki za binadamu. Wajibu wa kampuni kwa jamii unaweza kuwa katika shughuli mbali mbali kama vile kuhifadhi mazingira na uendelevu.

19


HATUA MUHIMU ZILIZOFIKIWA KATIKA UTEKELEZAJI WA SDGs NCHINI Kutoka katika ripoti ya mwisho yenye kichwa cha habari “Champions To Be” iliyoainisha mafanikio kadha wa kadha ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu hapa nchini hadi leo, Tanzania imeshapiga hatua kubwa zifuatazo katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu kama ilivyoainishwa hapa chini: • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Partnership in Statistics for Development in the 21st Century - PARIS 21 walifanya tathmini ya mapengo ya takwimu hapa Tanzania kama inavyotakiwa na Malengo ya Maendeleo Endelevu na Mpango wa II wa Maendeleo wa Miaka Mitano Tanzania. • Mpango wa miezi sita na bajeti kwa ajili ya shughuli za ramani ya takwimu (data roadmap) nchini Tanzania uliandaliwa na unatekelezwa na NBS. • Kama sehemu ya shughuli za ramani ya takwimu (data roadmap) nchini Tanzania, NBS inafanya kazi na Wizara, Idara, Mashirika na Wakala wa Serikali (MDAs) kukusanya, kusafisha, kupanga vizuri na kuwezesha ushirikiano katika matumizi ya takwimu zilizopo baina ya wizara, idara na mashirika (MDAs). • Idara ya kuondoa Umaskini (PED) chini ya Wizara ya Fedha na Mipango imetengeneza viashiria vya umaskini na sasa wako katika mchakato wa kukamilisha takwimu za awali (baseline) kwa ajili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu. • Uandaaji wa Mipango Mikakati ya Wizara, Mikoa, na Wilaya kwa ajili ya utekelezaji wa FYDP II, Malengo ya Maendeleo Endelevu, na Ajenda 2063 ya Umoja wa Kiafrika. • Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeunda kamati ya kiteknolojia ya wadau wa sekta mbali mbali ikiwa ni pamoja na wataalamu 20

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017


wa takwimu kutoka NBS, MDAS, wabia wa maendeleo, wanataaluma mbali mbali na Asasi za Kiraia ili kumshauri Mkurugenzi Mkuu na Kamati ya Muungano wa Kitaifa kuhusu masuala ya kitaalamu na kuwa mstari wa mbele kama jukwaa la utoaji taarifa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu. • Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu na Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika yamepewa kipaumbele kama sehemu ya Mipango ya Wizara, Mikoa na Wilaya. Sehemu kubwa ya mipango hii bado iko katika hatua ya maandalizi. • Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na shirika la UN Women, CIVICUS Data Shift, na NBS kwa pamoja waliitisha Mkutano wa Taifa wa Jinsia ukijikita katika utekelezaji na ufuatiliaji na mapitio ya lengo namba 5 la SDGs. • Kikundi Kazi cha Bunge kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu ambacho mwanzoni kilijulikana kama “Parliamentary Caucus” kimeundwa ndani ya Bunge la Taifa.

21


CHANGAMOTO ZINAZOJITOKEZA KATIKA UTEKELEZAJI WA SDGs TANZANIA Ukosefu wa taratibu za kitaasisi kwa ajili ya uratibu wa vipengele vitatu vya uendelevu (kijamii, kiuchumi na kimazingira) unaendelea kuwa moja ya changamoto kuu kwa utekelezaji mkamilifu wa malengo ya maendeleo endelevu Tanzania. Hili linachangiwa kwa sehemu kubwa na ukosefu wa uongozi wa kisiasa kuhusu takwimu nchini Tanzania. Utaratibu au mfumo wa ushirikiano wa wadau wa sekta mbali mbali haujarasimishwa na kufuatwa kikamilifu. Hali hii imesababisha wakati mwingine Serikali kuamua kufanyia kazi peke yake kwenye baadhi ya maazimio na kuhusisha Asasi za Kiraia na wadau wengine hufanywa pale tu maazimio hayo yanapokuwa yamekamilika au yanapokuwa katika hatua za mwisho za utekelezaji/uzinduzi. Kuna mapengo mengi ya takwimu ambayo yanahitaji kujazwa ili kuweza kufuatilia maendeleo ya FYDPII, SDGs na Ajenda 2063 nchini Tanzania. Kujazwa kwa haya mapengo kunahitaji mbinu za ushirikiano na wadau wa sekta mbali mbali kati ya serikali, sekta binafsi, wanazuoni, mashirika ya uhisani na asasi za kiraia. Upatikanaji wa fedha kwa ujumla, na hasa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kazi ya takwimu bado ni kikwazo kikubwa kwa mafanikio ya hapa nchini. Hili linachangiwa na utaalamu mdogo katika sayansi ya takwimu na usimamizi wake.

22

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017


MAPENDEKEZO NA HATUA ZA MBELENI

Maadhimisho ya miaka miwili toka utekelezwaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu hapa nchini uanze kutekelezwa, ulikutanisha wawakilishi wa AZAKI, Serikali, wadau mbalimbali wa maendeleo ambapo mazungumzo kubadilishana uzoefu na mijadala iliibuka. Maoni na mapendekezo ya jinsi gani wadau mbali mbali wanaweza kutimiza wajibu wao katika utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya SDGs nchini Tanzania hasa katika ngazi zaMikoa na Wilaya. Matumizi ya data katika ufuatiliaji na upimaji wa utekelezaji ulisisitizwa sana. Uandaaji wa mwongozo wa Asasi za Kiraia kuhusu Sheria ya Takwimu Tanzania ya Mwaka 2015 itawezesha AZAKi kutumia kwa ufanisi fursa ambazo hiyo sheria na miongozo yake inatoa, kuendana na utekelezaji wa SDGs na pia kuandaa maoni ya AZAKi kuhusu sheria ya takwimu na mapendekezo ya uboreshaji. Shughuli hii imeshaanza kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Jukwaa la Maendeleo Endelevu Tanzania na kwa kushirikiana na taasisi ya Data Shift. Kuna haja ya kuvitumia vikundi kazi chini ya Jukwaa la Maendeleo Endelevu Tanzania kama njia ya kuratibu vizuri zaidi michango kuhusu mada mbali mbali, ufuatiliaji na mapitio yanayofanywa na Asasi za Kiraia. Kuna hitaji la kushirikiana zaidi, kuongeza na kuendeleza shughuli ambazo zimekwisha anzishwa na asasi za kiraia kuhusu utekelezaji, ufuatiliaji na mapitio ya Malengo ya Maendeleo Endelevu, kama vile ufuatiliaji wa bajeti unaoongozwa na taasisi ya Policy Forum. 23


Ushirikiano na majadiliano miongoni mwa wadau ni muhimu katika kuimarisha utekelezaji wa ufanisi, ufuatiliaji na mapitio ya SDGs. Pia, ilishauriwa kutokujikita kwenye Malengo ya Maendeleo Endelvu (SDGs) pekee, bali msisitizo kama huo uwekwe pia kwenye Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano. Asasi za kiraia wanajukumu kubwa katika kuhamasisha jamii na kuoanisha utekelezaji wa FYDP II, SDGs na Ajenda ya Umoja wa Afrika 2063. Ni muhimu kwa wadau mbali mbali kushirikishana taarifa mapema miongoni mwao ili kuondoa upotevu wa juhudi, kuimarisha ushirikiano miongoni mwa wadau mbali mbali, hivyo kupata matokeo mapana zaidi ya ushiriki wa asasi za kiraia katika utekelezaji, ufuatiliaji, na mapitio ya Malengo ya Maendeleo Endelevu. Ilishauriwa na kutiliwa mkazo umuhimu wa uandaaji wa taarifa za mwaka za Jukwaa la Maendeleo Endelevu zinazoeleza kwa kina mchango wa Asasi za Kiraia katika utekelezaji na ufuatiliaji na mapitio ya Mpango wa Pili wa Tanzania wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Malengo ya Maendeleo Endelevu na Ajenda ya Umoja Afrika 2063.

24

MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs) UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI NA MAPITIO, TANZANIA - 2017

Profile for una_tz

SDGs Report Tanzania 2017 (Swahili Version)  

SDGs Report Tanzania 2017 (Swahili Version)  

Profile for una_tz
Advertisement