Kujikita Mizizi Wala Si Ukimbizi - UHAI Ripoti ya Mwaka 2021

Page 1

KUJIKITA MIZIZI WALA SI UKIMBIZI

BARUA KUTOKA KWENYE OFISI YA WAKURUGENZI WAKUU WENZA Mwaka wa 2021, ukiwa ni mwaka wa pili wa tandavu la COVID19 (UVIKO19) ulimwenguni. Dunia ikitafuta kitovu chake, na kutafuta njia mpya ya kufanya shughuli na mwamko mpya wa kuishi, jamii zetu za msagaji, shoga, anayevutiwa na jinsia zote mbili kimapenzi, transijenda, huntha na jinsia tata na wale wanafanya kazi ya ngono kwa kutafuta riziki katika Afrika mashariki walijipata katika njiapanda.

Wakati huu jamii zetu zilikabiliwa na chuki zinazosababisha Mataifa na watengenezaji sera kubuni sheria na miongozo ambayo inaleta hali za uharamishaji, unyanyapaa wa kijamii na ubaguzi, kutengwa katika kupata haki za msingi kama vile utunzaji wa afya na elimu.

Audre Lorde alisema wakati mmoja “ Nimekuja kuamini mara kwa mara kuwa lile lililo muhimu lazima lizungumziwe, litamkwe na lishirikishwe, hata likiwa katika hatari ya kutiwa doa au kutoeleweka.”

UHAI EASHRI lilipaza sauti tena kwa jamii zetu ujumbe wa kunawiri katika vurugu, kama vile tu ndege aina ya Finiksi anayefufuka kutoka kwenye majivu. Tulifaulu kupitia njia zetu za kufanya kazi kishirika; kupitia shughuli zetu za kutengeneza ruzuku; shughuli zetu za kubuni vuguvugu; na shughuli zetu za uongozi wa fikra na kushiriki maarifa.

Kama jamii hatukukabiliwa tu na maswali sawa kama wengine wote duniani lakini pia tulikabiliwa na maswali ambayo yaliongezea matatizo hata kabla ya tandavu maisha yetu hayakuwa ya kawaida. Tulikuwa na upeo wa matatizo kuhusu maisha yetu na maswali kuhusu kazi zetu kama wanaharakati, asasi na mavuguvugu; maswali kuhusu mustakabali wetu kama watu binafsi na mustakabali wa vizazi vya jamii ya jinsia tata. Kama jamii iliyo katika njiapanda, uliwadia wakati wa kujikita mizizi, si wa kuepa.

Katika waraka huu wa moyo wa dhati tutakuongoza katika hatua tulizozichukua kama wanaharakati wenye hisani, kama mfadhili wa asili ambaye kazi yake inalenga na kuendeshwa na jamii zake, kama mfadhili aliyejikita katika maudhui yake katika Ulimwengu wa Kusini, katika Afrika, katika Janga la Sahara la Afrika hata hivyo, na katika nchi saba za Afrika Mashariki kama Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Tanzania, na Uganda.

Tunachohitaji ni rasilimali ili kuleta mabadiliko, kwa yatakavyofanyikanamna.

Tunachohitaji ni dunia ilivyo sasa kubadilika na kuweza kututambua katika uhalisia wetu Na kutupilia mbali mfumo dume, siasa duni na mamlaka kulingana na nguvu ya kifedha. Kwasababu kuna kazi inayopendeza ya kutekelezwa Lorna Dias

Katika mwaka huu wa fedha 2021, makisio ya bajeti ya ruzuku za UHAI yalikuwa USD4,682,974 kwa ruzuku ziizotolewa kupitia Kamati Simamizi ya Ruzuku (SGC) na Kamati ya Ruzuku Mahirimu (PGC). Ikilinganishwa na mahitaji mengi ya jamii zetu, ingawa haikukidhi mahitaji yote ilichangia katika kutekeleza kazi inayopendeza

ruzuku zifuatazo: Ruzuku Mikakati: Ruzuku Fursa: Ruzuku Uwezo: 998 264, 44 790 415, 04 365 538,72

Gharama ya maisha katika nchi za Afrika Mashariki ilikuwa juu sana ikizidishwa na mfumko wa bei katika kwota za pili na tatu.

Wanajamii zetu waliojikimu kimaisha kutoka sekta za burudani na huduma walikabiliwa na mateso yasiyosimulika, waliowategemea waliteseka pia na masuala ya afya ya akili kutokana na madhara ya tandavu yaliyokithiri. Zaidi ya hayo, hali ya kutojali kutoka kwa umma kama mbinu ya kukabiliana na hali hii kulikuwa na ongezeko la dhuluma kwa jamaa za UHAI zilizoathirika zaidi.

SGC ya UHAI ilishughulikia mahitaji haya yanayoongezeka na kuendelea, kuwa waaminifu kwa thamani yetu ya Kusikiliza kama Tendo la Siasa. Mielekeo hii na sauti za jamii zetu zilisukumwa hadi mwisho wa jamii ambazo zilikuwa katika mstari wa mbele wa mwitikio wetu endelevu na nyumbufu mwaka mzima wote. SGC ilitoa ruzuku 148 za jumla ya USD2,154,218.72 kupitia aina tatu za

Watu wa tabaka la wanasiasa na wahubiri walifaidika visivyo kutokana na hali hiyo- kupata mashabiki wa itikadi zao na wafuasi wa mahubiri yao. Jamii zetu zililaumiwa kwa kuwa chanzo cha Tandavu na wengi wao wamepoteza maisha yao kwa sababu ya chuki ya viongozi wetu ubainifu wa chuki ikiwa chuki ya wafanya biashara ya ngono, chuki ya jamii transijenda na chuki ya jamii ya upinde. Mashirika makuu ya kijamii yalilalamikia ubaguzi wa chanjo kwenye misingi wa rangi, jamii zetu na mavuguvugu yetu kwa muda, yaliendelea kupambana ili kupata utunzaji wa afya ya msingi kwa wengi wa watu wa LGBTIQ+ na Wafanyakazi wa Ngono pamoja na matibabu ya VVU na usaidizi wa akili jamii. Vituo vya utunzaji afya vinavyoongozwa na jamii vilitekeleza jukumu muhimu katika kuchangia matokeo chanya ya afya kwa jamii zetu na utafutaji wao wa mahitaji ulikuwa mkubwa zaidi.

Ruzuku SGC (Kamati Simamizi ya Ruzuku)

KAMATI YA RUZUKU MAHIRIMU (PGC) Katika K4 2021, awamu ya 16 ya PGC iliandaliwa kutoka 6

Oktoba hadi 11 Oktoba. Mwito wa mapendekezo ulipokea jumla ya mapendekezo 338 ambapo 196 yalikuwa ya Msingi, 118 ya Tujenge, 22 ya Imarisha na watumaji maombi 2 hawakuonyesha safu waliyotuma ombi. Baada ya siku tano za mkutano wa ukaguzi, na baada ya mgawo, awamu ya 16 ya PGC ilitoa USD3,021,607 kwa mashirika 117 miongoni mwa LGBTIQ+ na mavuguvugu ya Wafanyakazi wa ngono katika Afrika Mashariki. Matoleo ya PGC yalitolewa katika mazingira yaliyokumbwa na changamoto zilizozikabili jamii zetu katika kila moja ya nchi zetu tunakofanyia kazi.

Burundi Hapakuwa na mabadiliko makubwa katika hali ya kawaida ya haki za binadamu tangu utawala ubadilike karibu zaidi ya mwaka mmoja sasa. Jamii ya LGBTIQ ilikaa macho kutokana na jinsi mawimbi ya kisiasa yatakavyobadilika na athari ya haya katika maisha yao halisia. Wakimbizi waliotoroka nchi hii miaka ya nyuma walirejeshwa wengi kutoka nchi jirani ya Tanzania na kuliripotiwa ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa mchakato huo. PGC ilitoa ruzuku 6 yenye thamani ya USD252,500 kwa jamii zetu nchini Burundi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) The DRC is one of 10 Nchi ya DRC ni moja kati ya nchi 10 za Afrika ambayo haijaharamisha wazi wazi watu wa LGBTIQ+. Kufoka kwa Mlima Nyiragongo mwezi wa Mei 2021 kulizidisha hali ya kutoa misaada kwa watu katika nchi ambayo ilikuwa tayari inakumbwa na Tandavu la COVID19 (UVIKO19). Uhamisho, ukosefu wa kupata mahitaji ya msingi kama vile chakula, makao, utunzaji wa matibabu na mavazi ulizidi kuwa mbaya. Maandamano ya raia dhidi ya uwepo wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo pamoja na maandamano yaliyotokana na uchaguzi ikizidishwa na mashambulizi mawili katika miji ya Ituri na Bukavu zilikuwa sehemu ya jumla za hali zilizozikabili jamii zetu nchini DRC. Kamati ya Ruzuku Mahirimu (PGC) ilitoa ruzuku 5 za jumla ya USD75,000 kwa jamii zetu katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Ethiopia Ethiopa ni mojawapo za nchi ambayo ina vuguvugu la kiasili dhidi ya mashoga “Zim Anlem” ambalo mwasisi wake anahusishwa na kanisa la Orthodox Tewahedo. Kwa kushawishika na kanisa, mtazamo wa umma unaonyesha angalau 97% ya idadi ya watu ina mtazamo hasi dhidi ya watu wa LGBTIQ+. Vita katika eneo la Tigray, masimulizi kuhusu uhalifu dhidi ya ubinadamu, msukosuko jijini Adis Ababa ulikuwa halimseto ambao ulizikabili jamii zetu nchini Ethiopia mwaka wa 2021. Serikali ilikimbilia kuwanyamazisha watetezi wa haki za binadamu ili wasizungumzie dhuluma na ikaanza kuzipeleleza jamii zetu. Hali hii iliyopo ilibuni kizuizi kingine katika kupeleka usaidizi wetu nchini kwa jamii zetu ambazo zilikuwa tayari zinakabiliwa na uharamishaji wa mtu wao kama watu wa LGBTIQ na wafanyakazi wa ngono pamoja na uharamishaji wa kazi ya ngono kama chanzo cha kupata riziki yao. Kamati ya Ruzuku Mahirimu ilitoa ruzuku mbili na jumla ya USD 40,000 kwa jamii zetu nchini Ethiopia.

Mwezi wa Septemba bodi ya serikali, Bodi ya Uanishaji Filamu ya Kenya (KFCB) ilipiga marufuku makala ya filamu “Iam Samwel” na sababu iliyotolewa na mkurugenzi wa bodi ni kuwa filamu hiyo ilikuwa ni ya “kufukuru”. Kauli hizo za mkurugenzi wa KFCB zilikuwa taswira ya ubaguzi wa jamii ambayo imeendelea kuwatenga watu wa jamii ya upinde(LGBTIQ) na wafanyakazi wa ngono kutoka mahitaji ya binadamu kimsingi kama vile utunzaji wa afya, elimu, makazi na fursa za ajira. Katika mwezi wa Oktoba 2021, Baraza la Pwani la Wachungaji wa Imani mseto lilisihi watu wa Lamu kutoajiri watu transijenda kwa huduma za harusi na pia wakaongoza maandamano ambayo ilipelekea kufungwa kwa kliniki inayofikiwa na jamii ya transijenda. Kenya inakabiliwa na uwepo amilifu na uliopangwa wa vuguvugu la uliwenguni dhidi ya haki na jinsia ambalo linaweza kushawishi sera hata katika kiwango cha EAC Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katika mwezi wa Machi 2021 serikali ya Kenya ilitoa makataa ya siku 14 kwa Kamishena mkuu wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa (UNHCR) kuandaa mpango wa kufungwa kwa kambi za wakimbizi za Kakuma na Dadaab. Wakimbizi wa LGBTIQ katika kambi hizi wangali katika hali ya taharuki na agizo hili halijabatilishwa.

Jamii za LGBTIQ zilijipata katika hali tatanishi kati ya kuchagua uchunguni makinikatika majiji ya Kenya kwa upande mmoja na uwezekano wa vurugu kutoka kwa jamii wafahidhina kutoka mashambani. PGC ya UHAI ilitoa ruzuku 52 yenye jumla ya thamani USD 1,279,852 kwa jamii zetu nchini Kenya. Rwanda Rwanda ni mojawapo ya nchi za Afrika ambapo watu wa LGBTIQ hawajaharamishwa na sheria. Hata hivyo, nafasi ya mashirika ya jamii zimeendelea kudidimia kutokana na ongezeko la kuchunguzwa kwa makini na serikali ikiwa imejificha katika taratibu za kufuatwa kwa makini ambazo ziliwafanya iwe vigumu kwa wanaharakati kukutana ana kwa ana mkutanoni. Mambo ya kipaumbele yalibadilika na kuelekezwa katika kudhibiti msambao wa COVID19 nchini na vitisho kwa Watetezi wa Haki za Binadamu, na vyombo vya habari vimesababisha masuala ya haki za binadamu kusahaulika. Cha kufurahisha, katika mwezi wa Oktoba 2021 kiwanda cha Ujerumani cha kutengeneza chanjo kiitwacho BioNTech kilitangaza mipango ya kusimika kitengo kimoja cha kutengeneza chanjo nchini Rwanda. Kwa kuweka hatua hizo chanya za kiuchumi na kisiasa, Upuuzaji wa upatikanaji wa haki za jamii na Rwanda huenda ukaendelea kutupwa katika kaburi la sahau. PGC ilitoa ruzuku 8 yenye jumla ya thamani USD122,356

Kenya

“Wasenge wanaudhi”, Rais aliendelea kutumia hofu ya usenge ili kuongeza chuki na kushutumu mpinzani wake kuwa mwenye jinsia tata na akadai ni kibaraka wa nchi za Magharibi. Wabunge wa Uganda waliendeleza mashambulizi haya baada ya uchaguzi kwa kutumia Mswada wa Dhuluma ya Kijinsia kama fursa ili kuharamisha zaidi watu wa LGBTIQ+ kwa kutoa kifungo cha miaka 11 katika sheria ambayo ilikuwa wazi kuliko Kanuni ya Adhabu ya sasa. Katika haya yote, unyumbukaji wa jamii ya Uganda ulileta ushindi kadhaa.. Rais hakutia sahihi Mswada wa Dhuluma za Kijinsia kuwa sheria; jamii hii ilifaulu kutetea kutotiwa mbaroni kwa watu wenye jinsia tata 44 kwa kusingizia ukiukaji wa miongozo ya COVID; Mwezi wa Agosti mahakama ya kikatiba ilitangaza kifungu cha 2 na 13 cha sheria Dhidi ya Ponografia kama kinyume cha katiba iliyoweka alama ya ushindi kwa Wafanyakazi wa Ngono; na hatimaye ushindi wa kibinafsi kwa Cleopatra Kambugu Mkurugenzi wa UHAI wa Mipango ulimfanya kuwa mtu wa kwanza wa transijenda ambaye jinsia yake ilitambuliwa kwenye kitambulisho chake cha taifa cha Uganda. Cleo anatumai kuwa ushindi wake wa binafsi kuwa utaleta mabadiliko ya uraia. Kamati yetu ya PGC ilitoa ruzuku 27 yenye jumla ya USD 869,899 kwa jamii ya Uganda.

Kanda hii ilisubiri kwa hamu wakati ambapo Rais Suluhu aliposhika hatamu za uongozi nchini baada ya hayati Dkt John Pombe Magufuli kufariki. Matumaini yoyote ya serikali ambayo inaheshimu haki za binadamu za raia wake yalififia wakati ambapo serikali ya Rais Suluhu ilipotoa amri tarehe 25 Novemba 2021 kuwa hali ya usagaji, ushoga, na kazi za ngono zilienda kinyume na tamaduni na desturi. Isitoshe, ilitangaza hatua kali kuchukuliwa dhidi ya yeyote anayetetea, anayepata raha kutoka kwa au anasaidia kueneza shughuli hizi. Jamii ya LGBTIQ na Wafanyakazi wa Ngono wanaishi kwa hofu ya kila mara hali isiyotabirika kwa vile hawajui ni nini serikali itafanya kuhakikisha kuwa uhuru wao na kuishi kwao kwa hadhi kukatizwa hata zaidi. Vile vile, mikutano katika maeneo ya miji na jamii zetu ilichunguzwa sana na hili lilipelekea kuratibu mikutano endelevu mashambani ili kukwepa uchunguzi huu. Tanzania imeendelea kuwarudisha wakimbizi kutoka Burundi na hii inafanyika katika hali ambayo inakiuka haki za binadamu ikiwemo mateso na kupotea kwa lazima kwa wakimbizi raia wa Burundi kutoka kwenye kambi za wakimbizi. PGC ilitoa ruzuku 16 yenye jumla ya USD374,500 kwa jamii zetu nchini Tanzania.. Uganda Mwaka wa 2021 ulikuwa mwaka wa uchaguzi ambapo Rais anayetawala alianza kuzisuta jamii za LGBTIQ+ kwa kusema

Tanzania

cisjendaNgono Jamii

kazi

PGC pia ilitilia maanani utofauti wa jamii zinazohudumiwa na UHAI na ikatoa ruzuku kama zifuatazo. Kutokana na mafunzo ya PGC 2020 palikuwa na haja ya tendo la usawazishaji kwa makundi anuwai na LBQ.

Mikakati ya Usawazishaji kwa jamii zetu

UHAI pia lilipokea usaidizi maalum kutoka kwa washirika wetu kuhusu utengenezaji ruzuku ulio na uamilifu, utofauti na usawa. ya (LGBTIQ+)Upinde Wafanyi Kazi ya TransijendayanaJamiiyaWalioghairiuwilli Wafanyi wa

Jamii hunthaya LBQ Jamii

waWakimbizijamiiyaupinde GBMSM

transijendaNgono TOTAL: 117

Ruzuku Mwaka Anuwai na Kazi ya Afrika yote

2Burundi:Tujenge,2Msingi=4 Kenya : 9 Tujenge, 1 Msingi = 10 Uganda: 7 Tujenge, 2 Msingi = 9 Kwa Jumla 23

Wanachama wa PGC ilihisi kuwa ruzuku za Mwaka-Anuwai (MYG) zilikuwa fursa kuu za ubia, mitandao na mashirika yanayofanya kazi katika kiwango cha kitaifa kwa vile itawezesha mavuguvugu kukua na kudumishwa kama mbinu ya unyumbukaji. Ruzuku mpya ya mwaka Anuwai ziliyavutia mashirika 10, 4 kutoka Kenya, 3 Uganda, 1 Tanzania, 2 kutoka Burundi kwa kikomo cha juu cha USD 60,000. Kamati ya PGC ilitoa USD7,500 kwa mashirika yanayofanya kazi ya Afrika yote katika nchi zote. Utengenezaji Ruzuku Unaozingatia Umoja na Wingi wa Uwepo Baada ya kiiniasili cha uchunguzi UHAI EASHRI liliamua kufanya majaribio ya programu kwa Watu wanaotumia dawa (PWUDs) katika nchi tatu tunazofanyia kazi zinazoitwa Burundi, Kenya na Uganda.PGC ilitoa ruzuku 5 Msingi na 18 Tujenge ambayo ni jumla ya USD 257,800 kwa waruzukiwa 23 katika nchi hizo tatu.

Idadi ya Awamu ya 1 ya ruzuku za PGC PWUDkwa kila jamii zilikuwa kama zifuatazo: Ugavu kwa kila nchi katika USD: Idadi ya Awamu ya 1 ya ruzuku za PGC PWUD kwa kila jamii zilikuwa kama zifuatazo: Wafanya kazi ya Ngono PWUDs (5) LGBT PWUDs (4) LGBT (4)PWUDsWakimbizi PWUDs Jamii za (7)KawaidaJamii za UHAI

USHAIRI KAMA UTENDAJI JINSI TULIVYOZISAIDIA JAMII ZETU KUKITA MIZIZI ”… ushairi si starehe. Ni nguzo ya uwepo wetu. Unaboresha mwangaza ulio msingi wa matumaini yetu na ndoto zetu katika kuendelea kuishi na mabadiliko, kwanza linatungwa katika lugha, kisha katika wazo, kisha katika matendo yaliyo dhairi…Ushairi ni jinsi tunavyoipa jina kwa lisilo na jina ili lifikiriwe. Upeo wa mbali zaidi wa matumaini yetu na hofu zetu zinakarabatiwa na mashairi zimechongwayetu, kutoka kwenye matukio magumu kama jabali ya maisha yetu ya kila siku.” - Audre Lorde

UTAFITI KUHUSU TANDAVU LA COVID

UHAI lilitoa zaidi USD46,000 kwa mradi huu mpya na likafanya kazi na INEND na MOLI. Mashirika 4 ya LBQ yalisajiliwa katika programu ya mwaka wa kwanza huku washirika 10 walishiriki katika utathmini wa uwezo na kukuza mtaala kwa kazi ya kujenga asasi na MOLI.

Kama sehemu ya kujikita mizizi tuliitambua wakala wa jamii zetu kama ajenti wa mabadiliko yao wenyewe. Tukitilia maanani nguvu iliyomo katika ushiriki wa pamoja katika maisha ya kipekee ya jamii zetu tulibuni nafasi ya kazi inayoongozwa na kushughulikiwa kikamilifu na mahirimu kando na utaratibu wa Ruzuku ya Mahirimu.

Changamoto zote pamoja na fursa zote ambazo zilizokumba jamii zetu zilitokea katika sawira ya COVID 19. Kwa hivyo UHAI iliamrisha utafiti ambayo ilichapishwa katika ripoti ya “AFYA! Ripoti Nyingine Kuhusu Maisha Ambayo Hayakupata Ukawaida ”. Hii ripoti ilikuwa muhimu katika ushawishi wa mwelekeo wa msimamo wa jamii zetu wa kukita mizizi na si kuepa na ilijumuisha mapendekezo ya kuanzisha hazina ya dharura itakayokabiliana na matandavu ya siku za usoni; ilijumuisha utathmini wa uhusiano wa jamii zetu na teknonojia ya kidijitali, kufanya kazi mtandaoni, na uvumbuzi kwa kutumia mitandao ya kijamii, gharama na ufikiaji wa teknolojia.

UHAI ikishirkiana na mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na vikundi kutoka sekta ya kibanafsi, ilitatua mianya ya uwezo katika uongozi na makuzi ya asasi, uwajibikaji wa fedha, kubuni na kuendesha programu yenye ufanisi, miundo ya kukuza maarifa na kutathmini (KEL) kwa mashirika yetu ya jamii.

UIMARISHAJI UWEZO UNAOLENGA MAKUNDI YA MAIRIMU

KUKUZA MAARIFA, PROGRAMU ZA UBADILISHANAJI WA UJUZI KWA MAHIRIMU Kwa kutambua kuwa jamii zetu ziliweza tu kukita mizizi na kuwa na unyumbukaji kama zilikuwa na uelevu wa matukio katika mazingara yao. UHAI ilifanya hili kwa njia mbili, kwanza ilizindua utafiti na pili kwa kubuni programu za kubadilishana ujuzi kwa mahirimu katika mashirika ya jamii zetu

Tulifanya kazi na washauri wa utafiti kutimiza malengo 2 ambayo ni: (i) Kuhakiki nguvu, changamoto na masuala ya kipaumbele ya Jamii ya Upinde (LGBTIQ) na Mavuguvugu ya Wafanyakazi wa Ngono, na mikakati muhimu katika kujielekeza kwenye mazingira yanayobadilika kila mara; (ii) Kuzingatia upeo wa mafunzo ambayo ni muhimu katika kuendeleza ahadi zetu za kudumu katika kukuza vuguvugu nchini

Uganda. PROGRAMU ZA UBADILISHANAJI WA UJUZI KWA MAHIRIMU Moja kati ya mapendekezo ya AFYA COVID 19 lilikuwa pia masomo na programu za kubadilishana kwa mahirimu. Uamuzi huu pia uliungwa mkono na michakato ya uhakiki wa usaidizi wa uwezo na waruzukiwa. UHAI liliamua kusaidia michakato miwili ya mafunzo na programu za kubadilishana kwa mahirimu katika mashirika yanachipuka ili kupata mbinu na maarifa katika sehemu mbalimbali. Mruzukiwa wetu wa kwanza linalongozwa na wafanyakazi ya ngono nchini Burundi ameshirikiana kwa pamoja na shirika linaloongozwa na LGBTIQ kuanzisha mchakato wa ushauriano wa mahirimu, kuwawezesha kuweka msingi wa kukuza muundomsingi wa kiasasi kama vile usimamizi wa fedha usimamizi wa miradi na utendakazi wa wafanyakazi katika kuratibu mipango. Upande mwingine, shirika la LGBTIQ linatumia fursa hii kutambua uwiano wa kazi ya ngono na Shirika linaongozwa na jamii trasijenda linalofanya kazi nchini Burundi, lilishirikiana na shirika la jamii transijenda ambalo linafanya kazi Tanzania kuanzisha programu ya masomo na programu za kubadilishana ambayo italiwezesha kuimarisha asasi zake, kukuza mfumo wa usimamizi wa fedha na kujifunza kutoka kwa lile shirika lililo

KUTATHMINI UWEZO WA VUGUVUGU NA KUAKISI UGANDA (MCAR UGANDA)

NAFSI KAMA MWONGOZO WA FIKRA YA KISIASA: JINSI TULIVYOTUMIA UHALISIA WA MAISHA YETU KWA UTETEZI WA UFADHILI NA KATIKA USHIRIKIANO WETU

” Kila mtu anafahamu kaulimbiu “Nafsi yako pia ni mada ya Kisiasa” --si tu kuwa tunayopitia katika kiwango cha nafsi yana athari kubwa kisiasa, lakini kuwa maisha yetu ya ndani, maisha yetu ya kihisia huongozwa sana na aidiolojia. Mara nyingi sisi hufanya kazi ya kitaifa kindani na kupitia maisha yetu ya -Angelandani.”Davis

UHAI imehadithia uhalisia wa kazi yetu kama shirika asili la ufadhili katika Afrika Mashariki pamoja na uhalisia wa maisha wa jamii zetu katika miungano inayoshiriki. Kulingana na maadili yetu ya upamoja na kufanya kazi miongoni mwa mavuguvugu pamoja na kutafuta usaidizi na ubia kutoka kwa mavuguvugu mengine tulishiriki katika nafasi zifuatazo:

ICASA ( Awamu ya 21 ya Kongamano la Kimataifa la Ukimwi na Magonjwa ya Zinaa) Desemba 2021, Durban South Africa:

Kongamano la Kikanda la 5 katika Muungano wa Afrika wa ILGA lenye kaulimbiu “Kurejesha hali Yetu ya Zamani- Kubainisha Mustakabali Wetu” Mijadala inayonuiwa kulenga hali ya uanaharakati ya sasa ya LGBTIQ+ katika muktadha unaoendelea wa Tandavu la COVID19 kama fursa ya sasa kwa makundi yaliyo katika hatari na yaliyotengwa ili kubainisha mustakabali wao. Mchango wa UHAI kwa mazungumzo husishi uliweka msingi thabiti wa kuzisaidia jamii zetu kurejesha hali mpya ya ukawaida. GiveOut 2021 Tumekuwa na hafla tatu na GiveOut mwaka huu ambazo ni: 1)Hafla ya Upeo wa Hatari na Jamii 2 Disemba 2021, 2) Hafla ya kuchangisha pesa tarehe 13 na 3) Adhimisho la “Fahari ya Jamii ya Upinde lenye azimio” tarehe 2 Juni 2021. Uhusiano unaoendelea wa UHAI na GiveOut umesaidia hasa katika kukuza wafadhili wa kibinafsi. Mkutano mkuu wa "Ubia Unaong’aa" (Shimmering Solidarity) wa Haki za Ulimwenguni GPP: UHAI lilichangia katika kupangia maarifa yaliyoshirikishwa katika mkutano mkuu. Tulishiriki katika majopo na Heath Gap na Dignity Consortium ambayo yalizungumzia matumizi ya uanaharakati katika ufadhili wa uhisani na feministi kama mwitikio wa usalama mtawalia. Tuliwasaidia wanaharakati kutoka Uganda na Burundi ili washiriki kama wazungumzaji katika jopo na Health Gap.

MAKONGAMANO

UHAI lilishiriki na kuziwezesha jamii zake kushiriki katika ICASA 2021. Hakika, tulishiriki katika makongamano ya awali ambayo moja kati yazo lilihusisha Accountability International kuhusu “Jinsi Washirika Wafadhili wanaweza kuwa wabunifu ili kuwajibika zaidi katika mwitikio wa Haki za Binadamu”; Kongamano la awali la GBMSM ambalo lilianzisha mjadala kuhusu programu endelevu na huru ya VVU kwa wanaume wa GBMSM barani Afrika. UHAI lilikuwa mmoja wa watetezi wa Azimio la Durban ambapo makundi maalum katika Afrika walidai hatua si ahadi tupu kutoka kwa wafadhili wakuu wa programu za VVU barani.

UHAI lilishiriki katika mahojiano na wanahabari mtandaoni pamoja na wataalam na wanaharakati wa afya ulimwenguni---washirika wa sasa na wa zamani wa Aspen Insitute New Voices Fellowship- (Ushirika wa Sauti Mpya wa Taasisi ya Aspen)- waliitwa kwa mabadiliko ya kimsingi kuhusu jinsi mataifa mfadhili na wahisani wanavyofadhili upatikanaji wa haki ya afya ya ngono na uzazi na uanaharakati. Wafadhili Wanaojali Kuhusu UKIMWI (FCAA)

UHAI lilishiriki katika jopo la FCAA lililokuzwa kwa pamoja na GPPlenye mada “Acha tuwe halisi- kuongeza ufadhili kwa wafadhili waliojikita na kuongozwa na jamii”. Tulizungumza na njia ya utengenezaji ruzuku shirikishi ya UHAI huku tukiongezea zaidi uwekezaji kwa waamuzi wanaohusika na VVU, hususan washauri waliojikita na kuongozwa na jamii.

Majadiliano yalichunguza kwa ndani jukumu la uhisani katika kusaidia vuguvugu kuhamisha mamlaka katika afya ya ulimwengu. Mamlaka nyingi kupindukia zipo katika uwanja na kuna haja ya kulenga sauti mbalimbali hususan ya wanawake, idadi ya watu iliyotengwa, na wanachama wa jamii zilizo katika mstari wa mbele na mashirika.

UHAI ilishiriki katika jopo lenye mada “Kuhamisha Mamlaka : Kufikiria tena Uhisani wa Kutafutiza Usawa wa Afya ya Ulimwenguni”.

2021 Viongozi Wanawake katika Kongamano la Afya Ulimwenguni

Kutoonekana hakupo tena (Invisible no More), Tamasha ya Upatikanaji wa haki za Afya ya Uzazi kwa wote:

UONGOZI WA MAONO kubuniKamasehemuyamaadiliyetuyafikrabadilivunaendelevuzilizoelekewzakwayasiyojulikananaupyapamojanachangamotokwanjiazakuratibuzilizojikitailinjiampyazakuratibu,zautendajinazakuishi.UHAIilishirikishaifuatavyo; MtandaowaTransijendaWaafrika TuliendeleakusaidiamaendeleoyaMtandaowakwanzabaraniwaTransijendawamuunganowaAfrikawakatihuutunapokabiliananaongezekolachukiulimwengunidhidiyamavuguvuguyanayoteteajinsianahaki. MuunganowaLoveAlliance programuunajumuishamabadilikoKupitiamuunganowaLoveAlliancetulichangiakatikakufahamikakwayenyenguvuyamfumowautengenezajiruzukushirikishiambaojukumulajamiikatikakufanyauamuzikuhusuufadhilikamailivyokatikaConsortium.Mchakatohuuumehakikishakuwakunamafunzoyamahirimumiongonimwawatengenezajiruzukuwalioshirikishwakwapamojawakiwawazoefunawanaochipuka.MkingamanonikipengelemuhimuyahiiambapokupitiaprogramuhiilimeliwezeshaUHAIkufikiamakundiyaWatuWanaotumiaDawa(PWUDs)ndaniyajamiizake.

AWID: Uchunguzi wa Mifumo ya Uongozi Shirikishi na Desturi Katika Mashirika Feministi: UHAI lilishiriki pamoja na mashirika feministi kuchunguza zaidi uongozi mwenza kama njia ya uongozi. Mradi huo bado unaundwa ili kufungua nafasi nyingi za mazungumzo kwa kutumia mifumo mitatu muhimu: Mahojiano ya pamoja na viongozi wenza, Hafla yenye mtindo wa warsha kuhusu maudhui na Mijadala ya Jopo.

Alkemia ya Kifeministi: Kujenga Ulimwengu baada ya Janga Hii ni jumuia ya hazina 14 feministi ulimwenguni, kwa usaidizi wa mtandao wa kimataifa wa hazina za wanawake, Prospera. Ujumuia huu wa hazina feministi umejikita katika mavuguvugu feministi, zikilenga sana wale ambao wameathirika na janga si tu kuitika wito wa na kuponya jamii zao lakini pia kufikiria na kubuni ulimwengu upya. Kongamano la Viongozi Wanawake katika Afya ya Ulimwengu (WLGH) COVID19 iliwaadhiri wanawake zaidi, haswa wanawake wa jamii za ueusi na rangi. Kongamano lilishughulikia maudhui ya “Kufikiria tena Uongozi,” kuangalia jinsi ambavyo uongozi utabadilishwa ili kuimarisha uwakilishi wa wanawake katika viwango vyote vya nyanja ya afya ulimwenguni na kufanikisha matokeo bora ya afya kwa wote.

WO=MEN liliandaa mahojiano na watetezi wa haki za binadanu za wanawake (WHRDs) katika kipindi cha siku 16 za uanaharakati na UHAI lilihakikisha jamii zake zimewakilishwa.

UTETEZI WA KIFADHILI

Kulingana na kiini cha maadili yetu ya kushirikiana ambayo inahusu kufanya kazi na wahisani wenye malengo sawa- watu binafsi, mashirika and mavuguvugu ya jamii endelevu. UHAI lilitekeleza utetezi wa kifadhili ulioelekezwa kwa wafadhili wa haki za binadamu, hususan pande mbili ambazo zinapatana na mwingiliano wa ndani, kuwekeza zaidi katika kurekebisha masanduku ya fedha katika utengenezaji wa ruzuku ili kutoa ufadhili usio na masharti ambayo yanachangia kuimarisha na kuendeleza mavuguvugu yetu ya mwanaharakati. Kongamano ya Wafadhili Weusi 2021 Kongamano liliadhimisha utamaduni wa Waafrika kihisani. Mazungumzo yalilenga umuhimu wa jinsi watu Weusi wanavyotekeleza chapa yao ya upekeeupekee ya uhisani, na kusisitiza kuwa ni sehemu ya mfumo wa utamaduni wa Kiafrika.

Mradi wa Ufadhili Ulimwenguni (GPP)

Ambao ulisaidia UHAI kushiriki katika mijadala muhimu ya kimataifa na pia kiserikali na fursa za ufikiaji kwa jamii zake. Muungano wa Wafadhili Wafanyakazi wa Ngono (SWDC) Ambao ulilenga matokeo bora kwa jamii za wafanyakazi wa ngono katika kanda zetu. SWDC linatoa jukwaa ambapo wafanyakazi wa ngono na wafadhili wanaweza kushiriki taarifa na mafunzo na ambapo wafanyakazi wa ngono wanaweza kuwahusisha wafadhili kama washirika marafiki katika jitihada zao za utetezi wa kisiasa. Muungano wa Ubia wa Sauti Zetu Mustakabali Wetu (OVOF)

UWEPO WETU KAMA UKWELI WETU KUKITA MIZIZI WALA SI UKIMBIZI

“Waridi la upinzani huchipuka kwenye lami.Tunapokea mawaridi, lakini tutakuwa na ngumi zetu zimekunjwa, kuzungumzia uwepo wetu dhidi ya msukumo na mvutano ambao huathiri maisha yetu.” - Marielle Franco

Hatuna majibu yote ya masuala ambayo yametufikisha hapa katika njia panda hii na kuchukua msimamo huu wa “Kujikita Mizizi wala si ukimbizi” lakini tunakualika uje utafute majibu na mwelekeo pamoja nasi. Tutaratibu mkutano wa CFCS 2023, kongamano la VIII la Kubadilisha Sura Kubadilisha Nafasi (CFCS), mwezi wa Mei 2023 kwetu sote kuhudhuria ili tutafakari pamoja na tuchague hatua tutakayochukua pamoja. Kama UHAI tulizinduliwa katika CFCS 2007, miaka 15 baadaye tunahisi tuna fursa kutungwa na kuzaliwa upya katika maisha yetu, katika jamii zetu na mavuguvugu yetu.

Kama ilivyo kawaida ujumbe wetu una wingi wa kusherehekea yale yote tumefanikisha pamoja- hata ikiwa katika kurasa hizi chache tulizoandika si kamilifu, lakini ujumbe wetu pia ni ushawishaji kama asemavyo ”Mtakatifu, mwanamke aliye na mapenzi kwa jinsia ya kike, mfeministi mweusi” Marielle Franco, “… ngumi zetu zikiwa zimekunjwa tukizungumzia kuhusu uwepo wetu…” sasa ndio wakati wa kutia bidii tuwe na ghadhabu na mapenzi ili kukabiliana na upinzani uliopangwa dhidi ya uwepo Njiawetu.yetu

Lorna Dias “kuna kazi maridadi ya kufanywa” na kama UHAI tumejitolea kutafuta rasilimali kwa jamii zetu ili kufanya kazi hii inayopendeza. Kama mwelekezi feministi wetu

pekee ya kukita mizizi na si ukimbizi, ni kuheshimu uwepo wetu kama ukweli wetu.

Kama anavyosema

Mwaka wa 2022 upo nasi sasa, asante kwa kusoma masimulizi yetu yote - yako na yetu pamoja- kama yalivyosimuliwa nasi.

Audre Lorde anasema tunawahimiza nyinyi jamii zetu ili kutimiza ndoto zenu, matumaini na fikra kuwa hai..Ndoto kwa ndoto , tumaini kwa tumaini, na fikra kwa fikra tutaangazia yote haya na kuyabadilisha kuwa kazi maridadi. “nafsi yako pia ni mada ya kisiasa” kama Dkt Angela Davis anavyosisitiza , tunaomba dhana yetu ya kisosiolojia ili kutuelekeza kuona uhusiano kati ya kila dhuluma za kunyimwa haki na kila mfumo ulio na dosari na jinsi zinavyoyaathiri maisha yetu, na jinsi zinavyoathiri nafsi zetu. Kwa zamu acha mwamko huu utupe changamoto ili tusitumaini tu kuwa na mabadiliko katika maisha ya kibinafsi na hali yetu ya kibinafsi lakini pia kuwa na mabadiliko katika jamii na kufanya mabadiliko ya kimfumo. Mabadiliko ambayo yatahakikisha kuwa kizazi kipya cha watu wa jamii ya upinde (LGBTIQ) wachanga wanaishi maisha yenye hadhi. Bora zaidi kama anavyosema Cleopatra Kambuga wetu <<Isiwe kuwa kazi ngumu tuliyofanya na miili yetu na maisha yaliyopotezwa yatupiliwe mbali…>>

Mukami Marete - Mkurugenzi Mwenza UHAI EASHRI Shamim Omar Salim Mwenyekiti Mwenza wa Bodi ya UHAI Katika Upendo wa Kimapinduzi Daima

Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.