Ua hai kama kizuizi

Page 1

Ua hai kama kizuizi Huu ni ua wa kizuizi ulio bora kwa mazingira unaotengenezwa kwa mimea na miti iliyo hai ambao huwazuia ndovu na wanyama wengine wa pori kuingia shambani na kwenye eneo la kaya.

“Hakuna njia kwenye miti hii mingi”

Kuweka aina yoyote ya mpaka, kama ua hai, fuo, au ua wa umeme kunapaswa kuamuliwa kwa uangalifu ili kutoongeza mgogoro kwa kukata njia za kutembelea, kugawanya idadi ya wanyama, na kuwafanya ndovu kukata tama na kuwa na fujo zaidi. (Fernando et al., 2008; Gunaryadi et al., 2017).

Kando na jukumu lao la ulinzi, ua hai huchukua sehemu muhimu katika udhibiti wa mazingira, uthabiti wa mchanga, uwiano wa virutubisho na kuongeza mapato.

Uchaguaji wa spishi za mimea, muundo wa ua na udhibiti yote hutegemea hali ya hewa. Kwa ua hai, Badala ya kukata miti ili kupata nyenzo za kujenga ua, tunaweza kuishi kwa amani na mazingira kwa kupanda miti na vichaka zaidi.

1.

Mishra, S., Vasudevan, P., & Prasad, S. (2011, June). Ua hai- ukuta wa mpaka unaofaa kwa mazingira.


Muundo wa Ua hai

a) Ua hai wenye fremu za mbao/nguzo hai za ua Nguzo hai za ua ni miti iliyopandwa kwa mstari mmoja iliyotumiwa badala ya chuma au nguzo za mbao za kuimarisha seng’enge, mianzi au au nyenzo zingine za ua. Vijiti na matawi mengi yaliyokauka pia yanaweza kufungiwa kwenye ua hai.

Huku miti inapokua, matawi hufungiwa kwenye fremu.

Ua ukitumiwa pamoja na ua wa kichaka wa pilipili upande wa nje unaweza kufukuza ndovu.

Kwa mimea inayotambaa, kuunda jengo kunaweza kusaidia mimea kukua ikizunguka fremu na mwishowe kuunda ua ua mnene imara wa kuzui.

b) Viunga Ua hai ni nene, nyingi na hupandwa pamoja na spishi mbalimbali. Huwa mara nyingi hujumuisha spishi zenye miiba na zinaweza kuunganishwa au kutounganishwa na waya. Miti hupandwa katika muundo wa zigizaga, ikiwa na nafasi ya sentimita 30- 40 kati ya safu 3 hadi 4.

Kuchimba fuo kwa Ua hai Mfumo wa fuo huboresha kupenya kwa maji na kuongeza ukuaji wa mizizi. Fuo husaidia katika urejeshaji wa mimea huku kukipinguza kazi.

30 40 sm

Fuo za mpaka zinapaswa kuwa na kipimo chaupana wa sentimita 50 kwa safu moja, sentimita 80. Angalia fuo kwa maelezo zaidi.

2.


Mifano ya miti ya kawaida inayotumika Eneo: Sri Lanka

Spishi za mimea yenye miiba hufaa zaidi kwa vizuizi hai na ua kwa kuwa miiba inaweza kusababisha uchungu kwa ndovu.

1. Mitende ya Palmyra

Palmyra huwafukuza ndovu kwa ncha zenye makali zinazomea kwenye shina. Huhusisha kupanda safu nne za mbegu katika muundo wa zigi-zaga zikiwa na futi 5-6 kati ya kila mti uliopandwa na takribani futi 8 kati ya safu.

Futi 5-6

Huchukua takribani miaka nane kwa mimea ya palmyra kukomaa kikamilifu na kufikia kiwango ambapo zinaweza kufanya kazi kama ua mnene wenye miiba. (Stearns, 2014). Ua mwingine wa kizuio wa muda mrefu lazima utumike kwa muda huku miti inapoendelea kukua. Ua wa Palmyra unaweza kustahimili hali kali za hewa kama kiangazi, mioto ya misitu, na kukua katika aina yoyote ya mchanga.

Aina hii ya spishi za miti huzaa matunda yanayoweza kuuzwa na kuongeza mapato kwa mkulima.

Angalia Ulinzi Wa Miti kwa mengi

Wakulima wanaweza kutumia majani kama kuni na kuezeka paa, kuta na mikeka, na vikapu vya kufuma.

kidokezo kikuu

Soma mengi kwenye: Ua hai wa Palmyra: suluhisho endelevu la mgogoro wa binadamu na ndovu jijini Sri Lanka. Hatua ya Vitendo Sri Lanka. Viungo vya YouTube: - https://www.youtube.com/watch?v=aoASL_IqGAE

3.

- https://www.youtube.com/watch?v=oLN3RVCFQzg

Ili kuhakikisha kuwa ndovu hawali matunda, funika mashina ya miti kwa kinyesi au ujenge kizuizi chenye ncha kali kikizunguka miti.


2. Mwanzi wenye miiba Hukua haraka na ina matumizi mengine kama ujenzi wa nyumba, kuezeka paa, kufuma vikapu, samani n.k, vitu vinavyoweza kuuzwa na kuongeza mapato. Ngozi za mwanzi pia hufumwa na kuwa vizuizi, ambavyo baadaye hufunikwa kwa pilipili na kinyesi cha ng’ombe.

Angalia Vizuio vya pilipili na Ulinzi wa miti na mengi kuhusu kinyesi.

3. Aina za Acacia Spishi kama Acacia brevispica, Acacia nilotica, Acacia tortilis zinaweza kupandwa kama ua hai. Acacia tortilis Ndovu hupenda kula majani ya miti ya Acacia Acacia. Unaweza kulinda miti yako kwa kutumia mbinu tofauti kama kutundika mizinga au kupaka kinyesi cha ng’ombe. Acacia brevispica

Angalia Ulinzi Wa Miti kwa mengi

4.

Acacia nilotica


4. Commiphora spp Miti kama vile Commiphora africana humea vyema katika mashamba kavu, ikitoa dawa, chakula na matumizi mengine mbalimbali. Nguzo iliyokatwa kutoka kwa mti uliokomaa inaweza kupandwa katika mchanga na itakua tena na kuwa mti mkubwa. Baadhi ya spishi za Commiphora kama Commiphora Jacq hupendelewa na ndovu na katika baadhi ya maeneo miti hii huharibiwa kwa idadi kubwa, hivyo hakikisha kuwa unaelewa ni spishi gani unayotumia. Kwa mfano, katika Mbuga ya Wanyama ya Kitaifa ya Mapungubwe, katika Mkoa wa Limpompo Kaskazini, Afrika Kusini, ndovu wameharibu miti hii mara nyingi. Mara kwa mara hulenga miti ya zamani zaidi na kuharibiwa sana. Holscher, B. (2011). Commiphora. Plantz Africa. http://www.plantzafrica.com/plantcd/commiphora.html

5. Matunda ya sitrasi- ndimu na machungwa Vizuizi vya Mti wa Machungwa: Nchini Sri Lanka, Project Orange Elephant Project Orange Elephant ni mpango wa kibunifu uliotolewa na Sri Lanka Wildlife Conservation Society (SLWCS) katika mwaka wa 1995. Walitoa nadharia kwamba Ndovu wa Kiasia hujiepusha na matunda ya sitrasi. Walienda kwenye Bustani ya Dehiwala na kufanya majaribio ya kulisha ndovu kwa kuwapa aina nyingi za chakula kama karoti, ndizi, tango na machungwa. Ndovu walijiepusha na matawi ya machungwa, huku wakila vyakula vingine. Miti ya machungwa huficha harufu ya mimea na kuwa kizuio asilia cha kuzuia ndovu kuvamia mashamba hivyo, kupunguza uwezekano wa mgogoro. Mitunda iliyokomaa ya sitrasi ni mirefu kiasi kwamba ndovu hawawezi kuwakanyanga. Matunda ya sitrasii yanaweza kutumiwa kutengeneza kachumbari, au kuuzwa soskoni na mkulima.

5.

Mkonge Agave ni mumea unaoweza kustahimili kiangazi ambao unaotengeneza nyuzi ambao hustawi katika maeneo kavu. Ndungusikakati na mimea sawa ni bora kwenye hali ya hewa kavu, yenye jua nyingi ambapo aina zingine za mimea haziwezi kustahimili.


Faida

+

hasara

-

Ua hai hufanya kazi kama kizuia upepo, ukilinda mchanga kutokana na mmomonyoko wa udongo, ambayo huongeza mavuno.

Lazima ujue ni spishi gani ya mti itakayostawi katika hali ya hewa ya mazingira yako.

Hufaa kwa mazingira.

Huchukua muda mrefu kwa miti kukomaa na kufaa.

Hakikisha kuwa hauzibi njia muhimu za wanyamapori. Hii itaongeza mgogoro na kuwalazimisha ndovu kuingia shambani mwako. umia mbinu zingine za kizuizi cha ua huku miche inapoendelea kukomaa.

Angalia Kulinda shule na Mazingira kwa maelezo zaidi kuhusu Ua hai.

Linda miti yako isiharibiwe na ndovuangalia Ulinzi wa Miti.

Ni ya gharama ya chini, ikilinganishwa na kuta zingine kama nyua za umeme na za mawe.

Mchwa huwezi kuvamia miti hai.

VIDOKEZO

Uapotegemea ua hai kama vizuizi vya shamba, lazima kuwe na uzingatiaji wa mpango wa matumizi ya shamba wa muda mrefu na ushauri kutoka kwa watetezi na wahifadhi wa wanyamapori ili kuweka ua katika maeneo yanayofaa. Lazima ulimie ua mara mbili au tatu katika mwaka wa kwanza baada ya kupanda, ili kupunguza ushindani wa magugu.

Miche huhitaji utunzaji na uangalifu mwingi.

Mimea ya dawa kama vile Mwarobaini na Mcheri wa Kiafrika inaweza kupandwa katika ua hai (Elevitch and Wilkinson 2000). Baadhi ya spishi za miti hutoa harufu ambayo ndovu hawapendi, ambayo inaweza kutumika kuficha harufu ya mazao mazuri. Daima zingatia kutumia udhibiti wa kikaboni/asili wa wadudu, inapohitajika. Kuwa mwangalifu unapochagua spishi za kama mwanzi za kutumia kama ua hai, kwa kuwa zinaweza kuenea bila kudhibitika haraka ikiwa haitunzwi vyema.

Huimarisha na kurutubisha udongo.

Utunzaji wa wastani unahitajika ili kuondoa mbegu.

Gua hai wa Ndovu wa Giribawa. Regenerative Organic Sri Lanka.

Angalia Chaguo Za Mazao Na Shughuli Za Bustani Ya Jikoni

Miche isipotunzwa vyema, itakauka mapema.

Sifa na Katao la Haki: Tumekusanya maelezo yaliyo hapo juu kutoka kwa vyanzo vingi vilivyopatikana katika hati hii. Mwongozo huu sio wa kina. Kujifunza zaidi na kujua kuhusu Ua hai na Kuta/Vizuizi, angalia Marejeleo. Baadhi ya majina halisi yaliyotumiwa sana yamefanywa kuwa rahisi ili uelewe haraka. Save the Elephants inashauri kuwepo kwa uangalifu kwa maelezo yote yaliyokusanywa na kupeanwa katika kijisanduku hiki cha vifaa. Huenda utafiti zaidi ukahitajika kabla ya utekelezaji wowote ,maalumu wa eneo. * Save the Elephants haiwajibikii gharama, uharibifu au majeraha yoyote, yanayotokana na matumizi ya mbinu au maelezo haya.

6. Imetengenezwa Kenya 2022

Imeandaliwa na Save the Elephants

www.savetheelephants.org

Michoro na Nicola Heath


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.