Mitaro

Page 1

Mitaro Mitaro ni nini?

Uchunguzi Kifani

Hii ni aina ya vizuizi vinavyoonekana vya ndovu na wanyama wengine wa pori. Vizuizi hivi hutumika kuzuia ndovu kutoka nje ya maeneo ya hifadhi ya misitu au kuingia katika mashamba yaliyolimwa au maeneo wanakoishi binadamu. Vinaweza kutumika kuwaongoza ndovu kupitia juu ya daraja au njia za chini. Huhitaji uzingatiaji, udumishaji na udhibiti mpana wa mazingira.

Kwa nini husaidia?

Karibu na Mbuga ya Kitaifa ya Wanyama ya Kibale (Uganda) mitaro imechimbwa ili kuzuia mwendo wa ndovu kwenye mashamba jirani. Chanzo: Gross, E. M., Lahkar, B. P., Subedi, N., Nyirenda, V. R., Lichtenfield, L.L., Jakoby, O. (2019) Je, ulinzi wa jadi na ulioboreshwa hupunguza hasara kutokana na wanyama wa pori? Uchanganuzi linganishi kutoka Afrika na Asia, Journal for Nature Conservation, Volume 50, August 2019, 125712.

Uganda

Mitaro huchimbwa mita mbili kwenda chini na upana wa mita mbili, na mchanga huwekwa pamoja ili kuunda ngome kando ya mitaro hiyo.

Ndovu hawawezi kuruka, hivyo mitaro iliyo pana sana na mirefu kwenda chini inaweza kufaa kuwa kizuizi kinachofaa. Hii inafaa kama mifumo ya kudumu ambapo mchanga ni imara vyakutosha kuruhusu uchimbaji na ambapo mmomonyoko wa udongo ni mdogo. Zinaweza kuchimbwa kwenye ardhi kavu na tambare. Haiwezi kuchimbwa kwenye maeneo yenye mwinamo au yanayokumbwa na mafuriko kwa kuwa mitaro itajaa maji, na kuwaruhusu ndovu kuvuka.

1.

Usijaribu kukata miti, vichaka au mimea ili kuunda mitaro. Hii itaathiri usawa wa eneo wa kiikolojia na kusababisha mmomonyoko zaidi wa udongo.

Mitaro mpya iliyochimbwa na iliyodumishwa vyema imethibitishwa kufanikiwa kufukuza ndovu. Kulingana na Gross (2019) Wakulima wanaoishi karibu na Mbuga ya Kitaifa ya Kibale huheshimu mitaro kuwa muhimu sana, ambayo mara nyingi ulipiwa na mapato ya Nationa Park. Chanzo: Gross, E. M. (2019) kufuatilia njia za kuishi pamoja kwa amani, Migogoro ya Binadamu na Ndovu Afrika kufuatilia mwa Jangwa la Sahara.


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.