Vizuio vya pilipili

Page 1

Vizuio vya Pilipili Pilipili ni kizuizi cha asilia. Huwa na kemikali iitwayo kapsaisini ambayo huwasha mapua na macho ya ndovu. Pilipili zinaweza kutumika kwa njia mbalimbali na kama mbinu inayohitaji teknolojia ya chini na isiyo hatari ya kuwafukuza ndovu.

Mbinu ya vizuio MBINU YA 1:

MBINU YA 2: Ua wa pilipili

Vizuizi vya mimea ya pilipili + KUPAMNDA PILIPILI MBALIMBALI

Pipili hoho ndicho kiungo kifanyacho pilipili kukolea.

Hii inapoathiriwa na unyevu (k.v ndani ya mkonga wa ndovu)- itasababisha mchomo unaosumbua.

Ndovu wana hisia nzuri sana za kunusa na wanaweza kunusa pilipili kutoka mbali.

MBINU YA 3:

Mbinu za moshi wa pilipili

MBINU YA 4:

Kelele ya pilipili/fataki tofauti

.Chanzo: Osborn F.V., Rasmussen L.E.L. 1995.

Ushahisi wa ufanisi wa erosoli ya pilipili hoho ya oleoresini kama dawa ya kufukuza ndovu wa porini Nchini Zimbabwe. Pachyderm 20:55–64.

MBINU YA 1: KUPANDA VIZUIZI VYA MIMEA YA PILIPILI Tumia hii kukuongeza mapato

Panda pilipili kali kama mimea ya kuzuia au kuimarisha mbinu zingine za vizuio. Pipili huwasha ndovu na kumfanya kuhisi vibaya na hii huwalazimu ndovu kuhamia kwenye maeneo mengine.

Vipande vya pilipili kavu

Pipili mbichi ni bidhaa ya thamani ya juu na ukulima wa pilipili hutoa chaguo zingine za kiuchumi. Pilipili zinaweza kusaidia kuongeza mapato kutoka kwa kilimo na zinaweza kuuzwa kama zao la biashara. Ndovu ni werevu sana na watajifunza kuzoea muda unavyosonga, hivyo ni bora kutumia vizuio vingi na kutumia mbinu hizi tu inapohitajika ili kuepuka kuwafanya ndovu kuzizoea.

1.

Sosi ya pilipili

Pilipili kachumbari


MBINU YA 2: UA WA PILIPILI

Ua wa pilipili huundwa kwa mchanganyiko wa pilipili, mafuta, na nguo.

AINA YA 1: Ua wa matambara wa pilipili

Unaweza pia kutumia mafuta ya mboga. Kamba mbili za makonge hutundikwa kwa mlalo kutoka kwa nguzo ikizunguka shamba. Vipande vya nguo hunyoshwa na kufungwa kwenye kamba za makonge kwa umbali tofauti. Ni muhimu kuwa ua uundwe jinsi ambavyo ndovu hawawezi kuvuka bila kuingia karibu na matambara yenye pilipili. Unaweza kukata shuka au nguo za zamani ili kutumika kama vipande vya nguo. Ikiwa huna hii, unaweza kutumia kamba zenye pilipili zilizowekwa katika mchanganyiko huu. Mara ndovu anapoathiriwa na pilipili kwenye mkonga wake, ndovu wengine pia watakuwa waangalifu.

ORODHA YA VIFAA

njia:

(ya ekari 1)

1.

Takribani lita 10 za mafuta ya mboga

Pilipili ya Ardhini Huchanganywa na mafuta ya mboga.

Vipande 32 vya nguo (60x40sentimita)

3.

Mita 7 - 10 Kilo 5 za kamba ya mkonge

2.

2.

Kisha kamba ya mkonge na nguo zinawekwa katika mchanganyiko huu.

5.

Mita1

4.

Mita 2.5

Umbali kati ya nguzo zinazofuata unapaswa kuwa umbali wa mita 7 hadi 10.

Kilo 2.5 za pilipili ya ardhi

Nguzo 36, angalau urefu wa mita 3 (inchi 118) na kipenyo cha inchi 3 hadi 4

Chanzo: Mwongozo wa Ushirikiano wa Chang’a et al. 2015. Ua wa pilipili huwafukuza ndovu kwenye mimea! Jinsi ya kuunda na kuimarisha ua wa pilipili.

Mkulima anaweza kuamua kuongeza kamba nyingine mita 1 juu ya ardhi, ikiwa kutakuwa na watoto katika kundi la ndovu.

Mita1.5-2

Urefu wa kamba ya chini na ya juu unapaswa kuwa mita 2.5 na 1.5 hadi mita 2 juu ya ardhi mtawalia.

6.

Nguzo hai zinazoweza kumea tena zinaweza kutumika badala ya nduzo zingine.


Aina ya 2: Ua wa kamba wa pilipili

FAIDA

Hii ni dhana sawa, bila kutumia vitambaa. Saga kilo 1 ya pilipili ya kijani katika mchanganyiko mzito bila kuongeza maji. Ongeza kilo 1 ya tumbaku, na 1/2 kilo ya grisi na 1/2kilo ya mafuta taka ya injini. Paka mchanganyiko huu kwenye kamba na uitundike kwenye eneo unalotaka kulinda. Tumia pamoja na mbinu zingine.

VIDOKEZO VYA UDHIBITI

Ua unaobadilika (ni rahisi kuweka na kutoa). Sio ya gharama ya juu sana kwa wakulima wanaoiunda na huchukua siku chache tu kuunda.

Lazima uchunguze ua mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa vipengele vyote viko sawa.

Gharama ya chini na vifaa vinaweza kupatikana kwa urahisi, hasa pilipili inayopandwa kama mumea wa kawaida.

Tambua wakati unaofaa wa kuweka ua na wakati wa kuuondoa. Weka ua mimea inapokomaa na karibu na wakati wa kuvuna na uuondoe baada ya mavuno ili kuzuia ndovu kuzoea.

hasara

Kuwepo kwa matawi ya miiba ya mshita (ua hai) kwenye ua kunaweza kufukuza ndama na wanyama wengine wadogo.

Tazama Kulinda Shule na Viwanga kwa Nyua hai

Wakulima wanapaswa kuwa na njia endelevu za kupata vifaa ili ua upakwe mara kwa mara.

Joto litapungua muda unavyosonga (baada ya siku 20 ikiwa kulikuwa kumekauka, siku 7 ikiwa kulikuwa kunanyesha sana).

Kuna vifaa vichache vya ua vilivyotumika vinavyofaa kwa mazingira na vinavyoweza kutupwa (k.m mafuta ya injini).

Tumia glavu za mpira na nguo ya kujikinga unapogusa mchanganyiko wapilipili.

Utunzaji wa ua ni muhimu. Ua wa pilipili huenda usiwe na ufanisi ikiwa wakulima hawako tayari au hawawezi kifedha kutunza ua.

Usiguse macho au uso wako unapotumia pilipili. Jiepushe na kugusa ngozi. Huu ni mkakati wa muda mfupi na unapaswa kutumia pamoja na vizuio vingine.

kidokezo: Unaweza kuweka nyua za pilipili na vizuio vingine vya kelele kimkakati kwenye njia za kutoka

kwa kichaka hadi kwa shamba lako. Ndovu huogopa kuvuka vikwazo au vizuio wasivyotarajia na wanapaswa kuogopa kukaribia sana shamba/kijiji chako. Jumuisha nyua za pilipili na ubadilishe na nyua za mtego wa ving’ora ili kuzuia uzoeaji.

Elimumwendo ya Ua usioonekana: Mafanikio kwa Upunguzaji wa Gharama ya chini na Endelevu wa Mgogoro wa Binadamu na Ndovu katika kilimo cha kujikimu

3.

-

Hii inaweza kuhitaji kazi nyingi hasa wakati wa mvua ambapo pilipili huhitaji kupakwa tena.

Chunguza upande wanakotoka ndovu na utundike matambara. Ni muhimu kutunza ua wako wa pilipili na kupaka tena pilipili inapohitajika.

+

Hii hufaa kwa mashamba madogo na wakati wa msimu wa jua.

Ua wa pilipili unaweza kuwa na changamoto kuu wakati wa kupaka. Nguvu ya pilipili huisha muda unavyosonga.

Imarisha ua wowote kwa pilipili ili kusaidia kufukuza ndovu.

Maelezo zaidi: www.connectedconservation.com, www.honeyguide.org, www.ecoexistproject.org , www.maraelephantproject.org


MBINU YA 3: MBINU ZA MOSHI WA PILIPILI

Chanzo: Ecoexist Project, Okovango delta, www.ecoexistproject.org

AINA YA 1: VIUNGO VYA KUTENGENEZA MATOFALI orodha ya vifaa

Kuchoma pilipili ni njia nzuri ya kufukuza ndovu. Huchukia harufu hii, na moshi wa pilipili huficha harufu ya mazao yaliyokomaa.

Pilipili ya ardhini

Kinyesi cha ndovu au ng’ombe

Maji

njia Kuchoma pilipili ni njia bora ya kufukuza ndovu.

Hii imeundwa kwa mchanganyiko wa kinyesi cha ndovu au ng’ombe, pilipili ya ardhini na maji. Hii hufinywa na kuwa tofali na kuachwa likauke.

1.

2. 1:2

Changanya pilipili ya ardhini na kinyesi cha ndovu/ng’ombe kilichopondwa kwa kiwango cha 1:2.

3.

15 sm 20 sm Finya hii iwe vipande vya sentimita 20 kwa upana na 15 urefu. Tumia kitu kama kopo la zamani au kisanduku cha plastiki.

4. Tofali linapokauka, unaweza kulichoma ili kutoa moshi mkali wa pilipili ambao ndovu wanaweza kunusa kutoka mbali.

Choma ukielekeza upande wa chini wa upepo kwenye upande wa njia ya ndovu, ili majirani wako wasipatwe na moshi kali.

4.

5. Mimea inapokomaa na ndovu wanatembea, anzisha sehemu ndogo za moto zinazodhibitiwa zikizunguka shamba.

Geuza matofali baada ya siku mbili ili kuhakikisha kuwa yamekauka kabisa.

Ongeza matofali haya ili kutoa moshi kali wenye harufu utakaoelekea kwenye upande wanakotokea ndovu.

Ondoa vipande hivi mchanganyiko unapokuwa tayari na uviache vikauke.

6.

7.

Kuwa mwangalifu chunguza upande ambapo upepo unatokea.

8. Usiache moto bila mtu wa kuushughulikia.


Aina ya 2: MIPIRA YA PILIPILI

njia

1.

Orodha ya vifaa

2.

Chanzo: Hifadhi ya wanyamapori ya Dinokeng Kisanduku cha vifaa cha Upunguzaji cha HEC 4.0, Antoinette van de Water.

3.

4. Chukua chupa ya wastani ya mafuta ya alizeti. Mwaga kidogo kuliko robo ya mafuta na ujaze pilipili kwa chupa.

Kwanza okota kinyesi cha ndovu. Kausha kinyesi kiwe kama mipira na uweke kwenye upande mmoja.

Kinyesi cha ndovu au ng’ombe

5.

6.

7.

Tikisa vizuri!

8.

Mafuta ya alizeti au mboga Hii ni dawa kali sana ya kufukuza, hivyo tumia mavazi yafaayo ya kukulinda wakati wa utaratibu huu. Kijiti chenye ncha kali nafaneli

Kopo safi na tupu la rangi

9. Kwa matumizi bora na salama – weka mipira katika kopo. Kabla ya kuiwasha moto, ongeza matone machache ya kerosini au mafuta ya taa kwenye mipira na uiweke kwenye kopo ili kuzuia moto.

Tumia kijiti kudunga shimo katika mpira na utumie faneli kuingiza kiowevu cha pilipili.

Chukua makopo ya nusu lita yaliyo tupu na yaliyo safi ya rangi.

10.

11.

Mipira inapowaka, igeuze polepole katika kopo ili kuufanya moto utoe moshi tu

13.

Mipira huchomeka polepole na kutoa wingu kali lenye harufu ya moshi wa pilipili.

Tengeneza mashimo madogo ya inchi 3 juu ya sehemu ya chini ya kopo.

12.

Funika kopo kwa kifuniko ili maji yaingie ndani.

14.

Kerosini/ Mafuta ya taa Moshi unapaswa kutoka kwenye mashimo katika kopo na kuenea kwenye eneo lililo karibu.

Poda ya pilipili ya ardhini

5.

Tundika hii kwenye maeneo kadhaa salama karibu na shamba.

Ikiwa ndovu wanakaribia shamba, harufu ya moshi wa chili inayochomeka itawafukuza.


faida

+

Research has shown that even the smallest amount of chilli smoke causes elephants to react and leave! Chilli briquettes are a more affordable option for small scale farmers. Hakikisha uko karibu ili kuyalinda makopo yanayotoa moshi.

Installation is very flexible and easy to implement. Materials are locally available, especially when chilli is grown as a buffer crop. Can be effective in helping change elephant movements.

Chunga usalama wako na usisimame upande ambao upepo unaelekea. Moshi wa pilipili ni mbaya sana kwa binadamu!

hasara

-

Wakati mwingine ndovu hubadilisha mwendo wao na kuzunguka maeneo yenye pilipili kabla au baada ya pilipili kuchomwa. Hutegemea upande wa upepo. Moshi ukielekea kwenye upande usiofaa, hii inaweza kumsumbua mkulima ikiwa kaya yake iko karibu. Pilipili nyingi sana huhitajika kwa uzalishaji. Matofali mengi ya pilipili yanahitajika ili kulinda shamba (matofali 5 kila mita 100). Wakati wa mvua, mbinu hii huwa haifai sana. Baadhi ya aina za paa huenda zikahitaji kufikiriwa endapo kutakuwa na mvua nyingi. Mbinu hii haiwafukuzi ndovu kwa muda mrefu. Matofali ya pilipili ni bora kama mkakati wa muda mfupi, lakini sio mkakati wa muda mrefu.

Wasiliana na majirani wako na uwe mwangalifu wa unapoelekea upepo ili kuepuka mwingiliano hatari wa moshi.

6.

Chanzo: Wildlife, Research and Conservation Society

AINA YA 3: MOSHI WA KOPO LA PILIPILI

Wakati wa mvua, huenda ikawa vigumu kutengeneza moshi wa pilipili hivyo tunapendekeza matumizi ya kopo la moshi wa pilipili. Chukua makopo ya 1/2 lita yaliyo tupu na yenye kifuniko k.m makopo ya zamani ya rangi. Tengeneza mashimo madogo inchi 3 juu ya sehemu ya chini yakizunguka kopo. Weka makaa ya mawe, nyasi iliyokauka, maganda ya pilipili nyekundu, mbegu za pilipili, n.k. ndani ya kopo. Washa moto ndani ya kopo ili moshi utokee kwenye mashimo. Funika kopo kwa kifuniko ili maji yasiingie ndani. Tundika makopo kadhaaa kama hayo karibu na sehemu ya kuingia.


MBINU YA 4: MABOMU YA PILIPILI, FATAKI AU EROSOLI Tumia njia zaidi ya moja kwa ulinzi bora zaidi wa shamba. Ikiwa mwanga na upulizaji pembe haujafaulu, unaweza kurusha fataki nyingi zikifuatana. Huenda fataki moja isitoshe kufukuza kundi la ndovu shambani.

orodha ya vifaa Chanzo:Mwongozo wa kupunguza mgogoro wa Mradi wa AMANI wa Elimu nafunzo ya ndovu www.ehranamibia.org

Hii hutumika bora kuzuia ndovu na wanyama wengine kuingia shambani.

Mawe/mchanga

Poda ya pilipili

1.

Njia

Hizi hutengenezwa kwa poda ya pilipili na fataki, zote zikiwa zimefungwa pamoja katika kondomu, ili kutengeneza fataki ya pilipili. Chembe ndogo za mawe huchanganywa na pilipili ili kuongeza uzito kwa kondomu ili kuongeza umbali itakaofika ikirushwa. (Vijiko 3 vidogo vikiwa vimejaa poda ya pilipil, vijiko 3 vidogo vikiwa vimejaa mawe/mchanga).

za pilipili kisha huwashwa na 2. Fataki kurushwa ju ya vichwa vya ndovu, kwa

kuzingatia upande ambao upepo unaelekea.

ya mlipuko wa kifaa na mwasho wa 3. Sauti poda ya pilipili huungana kuunda

Muda unavyosonga, ufanisi wake unaweza kupungua kwa kuwa ndovu wengine wa kiume wanaweza kuizoea.

Kondomu au puto

Huenda ikafukuza ndovu ambao tayari wako shambani.

kizuio imara cha ndovu.

mwangalifu unapotumia 4. Kuwa fataki au vifaa vinavyolipuka.

faida

Kuwa mwangalifu usiwaelekeze ndovu kwenye mashamba jirani.

AINA YA 1: MABOMU YA PILIPILI au FATAKI

Fataki

+

Huchanganya vizuio viwili vinavyojulikana na kuwa kimoja, kutumia vizuio vya harufu na sauti. Sauti ya juu husaidia kuwafukuza ndovu wanaokuja. Mawasiliano mema ni muhimu

Mabomu ya pilipili ni mchanganyiko wa pilipili na fataki, katika kondomu au puto kubwa. Lengo ni kuweka pilipili kwenye kondomu na kisha kuijaza na fataki. Kisha huwashwa na kurushwa karibu na ndovu, ikisababisha mlipuko wenye mwanga, harufu ya pilipili na kelele. Fataki hujumuisha sauti na vizuio vinavyoonekana kwa kutumia poda ya pilipili na fataki.

Nafuu na rahisi kwa yeyote kutengeneza akipewa mafunzo ya kimsingi. Hufaa katika kufukuza kikundi cha ndovu ikitumika mfululizo.

hasara

-

Kunaweza kuwa na hatari kubwa kwa mtumiaji na ndovu isipotumiwa vyema.

Baadhi ya ndovu wa kiume huenda wakarudi tena shambani muda mfupi baada ya kufukuzwa. Mafunzo yanahitajika ili kuhakikisha inatumika vyema.

Chanzo: Uvumbuzi wa Honeyguide. Honeyguide wakishirikiana na The Nature Conservancy walijaribu ili kwenye eneo linalozunguka Tarangire. www.honeyguide.org

7.

Usitumie hii katika eneo ambapo mabomu ya pilipili yanaweza kutumiwa vibaya.


aiNA YA 2: EROSOLI ZA PILIPILI Mbinu hii huenda ikatumia kifaa kinachochochewa na mwendo kinachoweza kuwekwa kwenye ua (kimiminio otomatiki cha kisafishaji hewa). Ndovu anapokaribia kwenye ua, kifaa hiki kitanyunyiza ukungu mwepesi wa pilipili kwenye upande walipo ndovu.

AINA YA 3: KINYUNYIZI CHA GESI YA PILIPILI/UTUPAJI MABOMU YA PILIPILi

faida

+

hasara

-

Hii ni nzuri kwa kuwa ndovu wanaweza kuzuiwa bila uingiliaji kati wa moja kwa moja wa binadamu.

Ina gharama ya juu kiasi na gharama ya juu ya utunzaji.

Ikitumiwa ipasavyo hii inaweza kuwa njia ya kufaa sana (matokeo bora nchini Zimbabwe).

Upande wa kunyunyizia unaweza kuathiriwa na upepo.

Nta ya nyuki ya kusugua ya pilipili Chanzo to Loki Osborn na Malvern Karidozo kutoka Connected Conservation waliounda hii.

Nta ya nyuki ya kusugua ni uvumbuzi mpya unaotumia pilipili iliyoyeyushwa katika nta ya nyuki ambayo huisaidia kushikamana kwenye maeneo tofauti.

www.connectedconservation.com

Itumike tu na wataalamu wakati wa operesheni!

Mafunzo na tajriba inahitajika

Hiki ni kifaa cha kurusha mpira wa meza uliojaa mafuta ya pilipili dhidi ya ndovu.

Ndovu

Mijengo ya nje

Mipira ya meza inapaswa kurushwa kwa nguvu nyingi, ili iwafikie Ndovu na kuvunjika inapogonga ngozi ya ndovu.

Huhifadhi mafuta ya pilipili ikiifanya kuwa kizuio kinachofaa cha ndovu kwa wiki nyingi.

Ingawa hii haipendezi, haiwezi kuua. Chanzo: Kuwafukuza ndovu kwa kinyunyizi cha gesi ya pilipili: majaribio ya shambani matumizi ya vitendo nchini Mozambique, Zambia na Zimbabwe kutoka 2009 hadi 2013.

8.

Usitumie kifaa hiki vibaya, na tumia vizuio vingine kwanza!

Miche ya miti

Mabomba ya maji

Nguzo za ua


HATUA ZA KUCHUKUA: MASOKO YA PILIPILI

UZALISHAJI WA PILIPILI

Ua wa pilipili na matofali ya pilipili yanaweza kuunda chanzo kipya cha mapato kwa wakulima, wanapopanda pilipili, ya kutumia na kama mazao ya fedha. Inayosalia inaweza kuuzwa sokoni.

Ikiwa pilipili itatumiwa kama kizuio kikuu, uzalishaji wa ndani unahitaji kuongezwa.

Vitu vilivyoongezewa thamana vinaweza kutengenezwa kwa kutumia pilipili, ikijumuisha mafuta ya pilipili, sosi, jamu, poda na vipande vya chakula.

Wakati mwingine hufanisi wa mbinu hupungua huku ndovu wanapozidi kuzoea mbinu hizi. Tumia vizuio hivi vyenye viungo pamoja na mbinu zingine.

UPEPO NA USALAMA

NZURI KWA ARDHI KAVU

Upepo ni suala kuu la kuzingatia unapotumia mbinu za moshi na erosoli. Kuwa mwangalifu wa watoto na watu wazee.

MAFUNZO Mafunzo na Tajriba inahitajika kwa mbinu fulani, hasa mbinu zilizo za kiufundi za ziada.

Vidokezo vya tahadhari:

Ndovu ni werevu sana na wanaweza kuzoea mbinu.

Jaribu uongeze uzalishaji wa pilipili, kupitia kuanzisha bustani za miche au nyumba za vioo za mimea.

Huku kukiwa na maendeleo mapya ya biashara, husaidia wakati ambapo tayari kuna soko lililopo la pilipili!

Pilipili ina nguvu sana na inaweza kuwa chungu sana pia kwa wanadamu!

KUZOEA

Pilipili hustahimili ukame kuliko spishi za mazao kama mahindi na hufaa zaidi kwenye maeneo kavu yasiyo na mvua ya kutegemewa (humea vyema katika maeneo yenye mvua kidogo).

Osha mikono vizuri unapogusa pilipili. Angalia Chaguzi za Mazao kwa maelezo zaidi kuhusu mazao yasiyoliwa na ndovu.

Unapotumia pilipili, usiguse macho, mdomo na sehemu zako nyeti. Tumia mavazi ya kujikinga na kifaa cha usalama. Inashauriwa kutumia glavu za mpira unapotumia pilipili. Tumia mbinu kimkakati ili kuwazuia ndovu kuzoea. Unapotumia mbinu za moto wa mipakani au moshi wa pilipili–kuwa mwangalifu usichome shamba! Chunguza kwa makini unapoelekea upepo. Mbinu hizi hufaa tu ikiwa upepo unaelekea mbali na mashamba na nyumbani kuelekea kwa ndovu wanaokuja. Baadhi ya mbinu huhitaji mafunzo na taaluma. Hakikisha kuwa una tajriba inayofaa ya mafunzo. Kuwa mwangalifu wa mifugo na watoto. Kwa mbinu zote upe usalama kipaumbele.

MAZAO MBADALA

Badala ya kupanda mimea inayowavutia ndovu, wakulima wanahimizwa kupanda mazao ambayo hayapendwi na ndovu – k.m alizeti, tangawizi, nyasi ya limau, pilipili, kitunguu saumu, kitunguu, tumbaku, miti ya kitropiki, pamba au biringanya kwenye ua. Hii inaweza kupunguza mvuto wa uvamizi wa mazao na inaweza kusaidia kuzuia uvunjaji wa ua.

Sifa na katao la haki:

Tumekusanya maelezo yaliyo hapo juu kutoka kwa miradi mingi. Vyanzo vikuu ni pamoja na: www.connectedconservation.com, www.honeyguide.org, www.wrcsindia.org, www.ecoexistproject.org, na www.maraelephantproject. org. Mwongozo huu sio wa kina. Kujifunza zaidi kuhusu kutumia chili na kusoma makala zaidi , angalia Marejeleo. Save the Elephants inashauri kuwa mwangalifu kwa mbinu zote zilizokusanywa na kupeanwa katika kijisanduku hiki cha vifaa. Utafiti zaidi huenda ukahitajika kabla ya kila utekelezaji maalumu wa eneo. *Save the Elephants haiwajibikii gharama yoyote, uharibifu au majeraha yanayotokana na matumizi ya mbinu hizi.

9. Imetengenezwa Kenya 2021

Imeandaliwa na Save the Elephants

www.savetheelephants.org

Michoro na Nicola Heath


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.