Vizuio vya Kelele “Vizuio vya kele ni kelele zinazotumika kuwazuia ndovu, kwa mshtuko wa kelele ya juu isiyotarajiwa, au kwa kelele maalumu zinazojulikana kuwashtua ndovu” (Parker et al., 2007).
VIZUIO VYA JADI Hivi mara kwa mara huundwa kutoka kwa vifaa rahisi na vinavyopatikana kote. Wakulima wanaweza kutumia aina mbalimbali za kelele, kama kupiga ngoma na makopo, ‘kupasua’ viboko, kupiga mayowe na kupiga miluzi ili kufukuza ndovu.
Kelele za juu ni kizuio kinachofaa cha muda mfupi dhidi ya ndovu. Ndovu ni werevu sana na wanaweza kuzoea mbinu zilizorudiwa au tabia ya kujifunza. Kwa muda, ndovu wanaweza kupuuza vizuio, mara wanapogundua kuwa haviwadhuru. Hivi vinaweza kuwa rahisi kutumika, vya gharama ya chini na vinaweza kutumiwa pamoja na mipango ya kijamii.
Aina ya vizuio vya kelele:
Wakulima wanaweza kutumia vifaa vinavyopatikana kwa urahisi kupiga kelele ya juu (Mabati ya chuma, chungu, ngoma). Kupiga ngoma
Kupiga risasi hewani
1.
Kupasua viboko
Kugonganisha mapipa, makopo, mabati, miti n.k kwa sauti ya juu
Mbweko
Kelele, mayowe, na kupiga miluzi
Fataki
Pembe/Vuvuzela
Kucheza sauti za nyuki na za wanyama kama (simba na chui)
Hizi hutumika vyema zikitumiwa pamoja na njia zingine za vizuio na ulinzi wa usiku.
Jiepushe na pombe/ulevi wakati wa msimu wa uvamizi wa mimea, kuwa mwangalifu. Vizuio vya jadi vya kufukuza ndovu shambani huonekana kutofaa vinapoendelea kutumika.