Umuhimu wa muunganiko kupitia ushoroba za wanyama pori

Page 1

umuhimu wa muunganiko kupitia ushoroba za wanyama pori Ushoroba wa wanyama pori ni maeneo ya makazi ambayo wanyama, ikiwa ni pamoja na ndovu, hutumia kusafiri baina ya maeneo mawili ya makazi yaliyounganishwa, lakini mara nyingi huwa yamegawanyika. Kuwa na ushoroba wenye manufaa ni mkakati wa muda mrefu ili kuzuia migogoro kati ya ndovu na binadamu, kurahisisha harakati za ndovu na jeni zao, na kuwaruhusu kuchangamana na kuzaliana. Ushoroba unawawezesha ndovu kuhamia kwenye makazi mapya na mahali kwenye chakula/maji nyakati za ukame kitu kinachowezesha nyasi na mimea kuota tena kwa ajili ya spishi nyingine.

Ikiwa imeasisiwa na Mwanafalsafa E.O. Wilson, Mradi wa Half-Earth umewekeza nguvu katika kulinda nusu ya ardhi na nusu ya bahari kuhakikisha afya ya muda mrefu ya sayari yetu na rasilimali tunazozitegemea. Pia inazingatia katika kuhifadhi ardhi iliyo muhimu kwa bioanuai na kutumia ushoroba asilia za wanyamapori katika juhudi za kulinda viumbe vilivyo hatarini kutoweka. Soma zaidi kuhusu Mradi wa Half-Earth https://www.youtube.com/ EOWilsonBiodiversity

Ushoroba sio lazima ziwe makazi ya ndovu kuishi. Ushoroba zinawezesha uhamaji kati na baina ya maeneo mawili yanayolindwa. Kutokufanya shuguli za kibinadamu kwenye ushoroba kunaweza kuwa na faida zingine kwenye jamii kama vile rasilimali za kuni na dawa za kienyeji/asili, asali au matunda kwa ajili ya kula.

Ushoroba za Wanyama Pori Unatoa Njia Baina ya Mbuga kwa Ndovu Walio Hatarini Kutoweka.

1.

“Ni kwa kuhifadhi nusu ya sayari tu, au zaidi, ndipo tutakapoweza kuokoa sehemu hai ya mazingira na kufikia uwiano unaotakiwa kwa ajili ya suatwi wetu wenyewe” - E.O. Wilson (1929-2021)


Vitisho kwa Ushoroba Uwepo wa makazi ya watu, mashamba na majengo huweza kusababisha vizuizi baina ya makazi ya wanyama pori. Ndovu hawapendi usumbufu unaotokana na shughuli za kibinadamu, hivyo kuwafanya wasite kuvuka au kuzunguka kwenye njia zilizofungwa au zenye kelele. Shughuli za kibinadamu zinapofunga ushoroba au njia, wanyama ni lazima watafute njia zingine za kupata rasilimali, hali inayoweza kuwalazimisha kuingia kwenye makazi ya watu na mashamba. Soma zaidi kuhusu: Kufuatilia uhamaji wa ndovu kumevumbua ushoroba za ndani ya mipaka, Ushoroba Muhimu kwa Wanyama Pori Unaunganisha Hifadhi za Wanyama.

Uanzishwaji wa makazi ya watu ndani au juu ya njia wanazotumia wanyama kuhama huongeza migongano baina ya binadamu na wanyama. Fikiria kubananisha nyumba na makazi kuwa katika maeneo madogo ili kuziachia nafasi ushoroba na kushiriki pamoja gharama za vizuizi vyamipaka ya shamba.

Sababu zinazosababisha kuzibwa kwa ushoroba

Ujenzi

Maendeleo

Kilimo

Majengo

Ukataji miti

Gara, T. W., Wang, T., Dube, T., Ngene, S. M., & Mpakairi, K. S. (2020). Ndovu wa Kiafrika huchagua maeneo ambayo hayajagawanyika sana ili kuungana na makazi makuu kwenye ardhi iluyotawaliwa na mwanadamu.. Green, S. E., Davidson, Z., Kaaria, T., & Doncaster, C. P. (2018). Je ushoroba za wanyama pori huunganisha au huongeza makazi?Mafunzo kutokana na ndovu kutumia ushoroba wa wanyama pori wa Kenya.

2.


Uhamaji wa Ndovu na Maamuzi ya Makazi Spishi zote 3 za ndovu (wa Kiafrika, wa Misituni & wa Kiasia) wanaongozwa na hitaji lao la kila siku la kunywa maji na hivyo huhama wakitafuta maji ya kutosha wakati wa kiangazi. Mvua zinaporudi, makundi ya ndovu hurudi kwenye makazi yao. Ndovu jike viongozi (kiongozi wa kundi) hutumia kumbukumbu yao ya ajabu kuongoza familia zao kwenda kwenye chakula na maji, na kisha kurudi nyumbani. Makundi ya ndovu yanayohama yanazidi kukabiliana na vitisho vipya kama vile majengo yaliyojengwa hivi karibuni, uzio na mashamba. Jamii zinabidi zielewe kuwa kubadili makazi asilia kuwa ardhi ya mashamba/miundombinu, mara nyingi huwa ni sababu kwa nini migogoro na ndovu inaendelea kuongezeka.

Hakikisha kuwa athari za upotevu na ugawanyikaji wa makazi asilia zinapunguzwa kwa kuhamasisha muunganiko wa makazi asilia kupitia ushoroba zinazolindwa ambazo zinahifadhi uoto asilia.

Tazama Kuelewa Ushoroba za Wanyama Pori-Nature Conservation Foundation

3.

Njia ya juu ya wanyama pori inawawezesha wanyama kuvuka barabara kuu 3 kwa wakati mmoja © Centre for Large Land Conservation. https://largelandscapes.org/news/invest-act/

Ushoroba zinaweza kupita juu au chini ya barabara kubwa. Faida ya njia zinazopita juu ni kwamba wanyama hawatagundua mabadiliko ya makazi yao na haina usumbufu kwa ndovu wenye ndama.


Mifano Hai 1. Ushoroba wa Ndovu wa Mlima Kenya-Njia ya chini

2. Bonde la Okavango, Botswana EcoExist imesaidia kulinda na kurejesha njia za uhamaji pembezoni mwa Bonde la Okavango.

Ushoroba wa Ndovu wa Mlima Kenya (Mount Kenya Elephant Corridor- MKEC) umeanzishwa ili kuwasaidia ndovu kupita kwa usalama chini ya barabara kuu ili kutumia njia zao za asili, ambazo zilitoweka kutokana na kilimo na ujangiri. MKEC inaunganisha kilomita 14 za njia ya kihistoria ya uhamaji wa ndovu baina ya Mlima Kenya na Samburu, hivyo kuwezesha upitaji salama wa ndovu.

An Ecoexist Elephant Corridor in the Northern Okavango Delta © EcoExist

Jamii ilishirikiana kikamilifu na timu ili kuachia wazi ushoroba kadhaa katika makazi ya watu na mashamba, baina ya maji na pori. Ushoroba zote 14 zimewekwa alama. Ardhi ya kilimo baina ya ushoroba sasa zinalindwa kwa ulinzi mkali kwa kutumia uzio za sola na uzio za mizinga ya nyuki ili kuhakikisha ndovu hawatangitangi nje ya ushoroba na kuingia kwenye mashamba. https://mountkenyatrust.org/wildlife/

Uzio kwenye pande zote mbili za ushoroba zinahakikisha kuwa jamii zinalindwa vyema zaidi na ndovu wako salama zaidi na wana uhuru wa kuhama bila usumbufu wowote. Njia za chini ya barabara kuu zinazopita maeneo ya hifadhi ni nyenzo ya thamani ya kupunguza malumbano kwa kuhakikisha wanyama wanavuka baina ya makazi bila kuuliwa kutokana na kugongwa na magari au kujeruhiwa na watu.

Jamii zimejifunza kuishi na ndovu kwa kuheshimu tabia za ndovu na kutambua tabia zao za kila siku, za kuhitaji kutembea baina ya maji na pori ili kupata malisho. Wakulima sasa wanawavuta watalii wanaopenda mbinu yao ya kuishi pamoja na ndovu na hii imeongeza zaidi ajira na fursa zenye kujali ndovu.

Angalia hii video kuhusu ushoroba wa Mlima Kenyahttps://www.youtube.com/watch?v=aoCs3aw4E5E

Ndovu wakitumia njia ya chini kupita eneo kwenda jingine © Mount Kenya Trust

4.

https://www.sanparks.org/assets/docs/conservation/scientific_new/savanna/ssnm2017/land-use-planning.pdf


3. Ushoroba wa Wanyama Pori wa Kasigau

Ndovu wakipita katikati ya Ushoroba wa Wanyama pori wa Kasigau © Fillip/Wildlife Works https://www.wildlifeworks.com/kenya

Eneo la Hifadhi ya Tsavo ndio eneo kubwa zaidi la wanyama pori linalolindwa nchini Kenya likiwa na idadi kubwa zaidi ya ndovu nchini. Ikiunganisha hifadhi za taifa za Tsavo Mashariki na Tsavo Magharibi ni Mradi wa Ushoroba wa Wanyama Pori wa Kasigau ukijumuisha jamii za ndani katika upatikanaji ajira na shughuli endelevu za kimaendeleo. Ushoroba huu wenye uwanda mpana unawezesha upitaji salama wa spishi zilizo hatarini kutoweka kama vile ndovu, pundamilia wa Grevy, duma, simba na mbwa pori wa Kiafrika, zikiwemo na spishi zaidi ya 300 za ndege. Vibali vya Kutoa Hewa ya Ukaa vinasaidia kufadhili usimamizi wa ushoroba na kusaidia jamii ambazo zinaishi kando ya wanyama pori wanaolindwa.

4. Mama Tembo, Kenya Kaskazini

Mama Tembo wakiwa kazini© Jane Wynyard/Save the Elephants

Akina Mama Tembo ni kikundi cha wanawake kutoka makabila ya Wasamburu na Waturkana wanaofanya kazi na Save The Elephants na Chama cha uhifadhi cha jamii ya Kalama ili kulinda ushoroba wa wanyama pori na mifugo Kaskazini mwa Kenya. Kwa kutumia vifaa vya GPS, akina Mama Tembo wamekusanya data za harakati za wanyama pori. Wamezitaarifu mamlaka juu ya ujenzi haramu wa maboma na makazi ambayo yanaweza kuzuia wanyama pori na mifugo kupita kwenye ushoroba. Kwa kuziweka wazi ushoroba hizi, ndovu wanaweza kuendelea kuhama baina ya mbuga za wanyama bila kuhitaji kuingia kwenye vijiji au mashamba. Wanawake hawa pia wanashugulika na jamii na familia zao kuhusu umuhimu wa upitaji salama kwa wanyama pori ili kupunguza migogoro kwenye kaya zao. Miaka zaidi ya ishirini ya kuwafuatilia ndovu na kutathmini mienendo yao imesaidia STE kutambua ushoroba muhimu kwa harakati za ndovu. Kaskazini mwa Kenya, ikiwemo ushoroba nne za wanyama pori zinazovuka barabara kuu ya kutoka Cape kwenda Cairo.

Soma zaidi kuhusu Ushoroba wa Wanyamapori wa Kasigau – Kenya https://www.youtube.com/watch?v=XkyhhdaV_KM

5.

Soma zaidi kuhusu: Namna akina Mama Tembo wanabadili mioyo na akili Kaskazini mwa Kenya.


Vidokezo vya Tahadhari Angalia mabango yoyote ya ishara yakiashiria ushoroba Muhimu wa Wanyama Pori.

Hakikisha hujengi nyumba yako au kulima shamba ndani ya ushoroba wa wanyama pori.

Ishara zinazoashiria vyombo vya moto kupunguza mwendo kwani wanyama wanaweza kuwa wanavuka © Wildlife Works

TAHADHARI,

USHOROBA WA WANYAMA PORI

KUWA MAKINI

WANYAMA WANAVUKA

Usikate miti au kulisha mifugo kupitiliza kwenye ushoroba wa wanyama pori — kama ndovu hawana chakula ndani ya ushoroba, watakuja kutafuta chakula kwenye mashamba yenu au nyumbani.

http://tsavoconservancy.com/visit-us/maps-directions/

Kama utaamua kulima shamba pembeni na ushoroba wa ndovu, elewa hatari zake na kuwa tayari kuwekeza katika vizuizi madhubuti kulinda shamba lako. Usishangae kuwaona ndovu kama umechagua kulima pembezoni mwa makazi yao.

Jizoeze na elimisha familia yako na marafiki kuhusu umuhimu wa ushoroba na namna gani, kwa kuzilinda, jamii yenu itaweza kuishi kwa amani na ndovu.

6.


Kama kuna ndovu wanatumia ushoroba, kuna uwezekano wa wanyama pori wengine (kama vile nyani na swala) kuiba mazao.

Ndovu pia watavutiwa na matangi na mabomba yako ya maji hivyo hakikisha umeyalinda vizuri ili kuepusha migogoro kutokea.

Angalia Kulinda Matangi ya Maji kwa taarifa zaidi.

Ndovu wanaweza kutoka nje ya ushoroba kuingia kwenye mashamba wakitafuta chakula na maji. Usipande mazao ambayo ndovu wanapenda kula karibu na ushoroba wa ndovu au kwenye mbuga ya wanyama.

Hamia kwenye kilimo cha kiwango kidogo chenye kuzingatia uhifadhi kwani kinahitaji ardhi ndogo ya kilimo, kinatumia maji kidogo, hakihitaji matumizi ya gharama ya viuatilifu hatari, ni rahisi na nafuu kulinda dhidi ya ndovu wavamizi wa mazao na kinaweza kutoa mavuno mengi.

Tumia njia mbalimbali za vizuizi ili kulinda mashamba yako ikiwemo kupanda mazao yasiyopendwa ndovu.

Vitunguu Swaumu

Alizeti

Angalia Aina za Mazao na Shuguli za Jikoni kwa taarifa zaidi.

Ginger Pilipili Manga Biringanya Binzari

Bamia

Pilipili Kichaa Ufuta

Viungo

7.

Imetengenezwa Kenya 2022

Mchaichai

Mpira Matunda Jamii ya ndimu

Imeandaliwa na Save the Elephants

Marejeleo na Angalizo: Tumekusanya taarifa hizi hapo juu kutoka kwa vyanzo mbalimbali vilivyofanyiwa marejeleo kote kwenye kijtiabu. Vyanzo vikuu ni Save the Elephants, EcoExist na Wildlife Works. Mwongozo huu hautoshelezi. Kujifunza zaidi na kuchunguza kuhusu Umuhimu wa Ushoroba, angalia Marejeleo. Save the Elephants inashauri tahadhari kwa taarifa zote zilizokusanywa na kuwasilishwa kwenye kitabu hiki. Utafiti zaidi unaweza kuhitajika kabla ya utekelezaji wa mbinu husika. *Save the Elephants haihusiki na gharama, uharibifu au majeraha yoyote yatokanayo na matumizi ya njia hizi.

www.savetheelephants.org

Michoro na Nicola Heath


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.