NDOVU KAMA WAHANDISI WA MFUMO IKOLOJIA Wahandisi wa mfumo ikolojia ni wanyama ambao huunda, kubadilisha au kuharibu makazi. Ni muhimu kwa kudumisha afya na uthabiti wa mazingira wanapoishi.
WAHANDISI WA MFUMO IKOLOJIA 1. Kusukuma miti na mimea
SPISHI KUU Spishi kuu ni kiumbe anayesaidia kushikilia mfumo pamoja na ni muhimu katika mfumo ikolojia.
Ndovu ni spishi muhimu sana
Ndovu ni spishi wenye athari kuu kwa mazingira.
Spishi nyingine hutegemea spishi kuu. Kuondoa spishi kuu kutoka kwa mfumo ikolojia kutasababisha ukosefu hatari wa usawa katika mfumo mzima. Utafiti unaonyesha kuwa ndovu ni mkulima, kontrakta, barabara na msawazishaji wa jumla katika mfumo ikolojia!
1.
Usukumaji wa miti wa ndovu unaweza kusaidia kudumisha Mifumo ikolojia ya Savana. Hii pia husaidia kuunda njia mpya ili kuwaruhusu wanyama wandogo kusonga bila tatizo. Hii huruhusu mwanga mwingi kwenye sakafu, ikiisaidia mimea mingine kustawi. Kupogoa miti pia husaidia kuboresha ukuaji na kupeana chakula.