Kulinda Shule na Viwanga

Page 1

kulinda shule na Viwanga Mjumuisho wa njia mbalimbali zinazoweza kutumika mashuleni na kwenye maeneo mengine ili kuwaweka mbali ndovu katika hali ya usalama.

6

7

2

8

4 5

1 1.

3


1

Uzio wa umeme

Uzio wa umeme unaochajiwa na sola unaweza kuwa kizuizi chenye ufanisi dhidi ya ndovu. Uzio wa umeme unaochajiwa na sola unaweza kuwa aina ya uzio unaodumu kwa muda mrefu na ambao u naweza kusimamiwa vizuri kukiwa na mafunzo.

faida

+

Inafaa katika kupunguza idadi ya ziara za ndovu kwenye eneo lililozungushiwa. Kama ukitunzwa vizuri, unaweza kudumu kwa muda mrefu. Hakuna madhara yoyote ya kimwili yanayoweza kusababishwa kwa binadamu na wanyama. Unaweza kutumia sola.

Yanahitajika matunzo ya mara kwa mara, ikiwemo kupunguza mimea inayozunguka uzio.

hasara

-

Gharama za awali zinaweza kuwa juu. Baadhi ya ndovu wamekuwa ‘wavunja uzio.’

unavyofanya kazi Paneli ya sola inakusanya nishati ya jua na kuibadili kuwa nishati inayohifadhiwa ndani ya betri. Ndovu anapogusa uzio, atasikia mshtuko mkali, wa muda mfupi, ambao ni salama na haumuui ndovu. Mshtuko huu utaleta hali ya kizuizi huku ikihakikisha hakuna maisha yaliyopotea. Paneli na betri za sola kwa ajili ya uzio wa umeme unaweza kuhifadhiwa mahali salama juu ya mnara wa ulinzi unaotazamana na njia ya kwenda shule inayopendelewa kupitwa na ndovu.

vyanzo: Sinha, A. (2020, June).). Namna uzio unaotumia sola umepunguza migogoro ya binadamu na ndovu. Down To Earth. Kutunza Uzio wa Umeme (WWF).

2.

vidokezo vya tahadhari Kujenga kizuizi cha mawe ndani ya uzio wa umeme kunaweza kuzuia wanafunzi wa shule kugusa umeme na kushtuliwa. Matunzo hafifu yatasababisha ndovu wauguse uzio mara kwa mara, na kusababisha uzio kuvunjika na kuharibika. Tafuta msaada wa kitaalam ili kuweka mifumo ya umeme kwenye uzio. Weka kibao cha onyo kuonyesha kuwa uzio ni wa umeme. Usiunganishe uzio wa umeme katika waya unaopitisha umeme mkubwa au kwenye laini za nyumbani, kwani hii inaweza kuwa hatari kwa wote bindamu na wanyama pori.


1a) Mchanganyiko wa pilipili kwenye nguzo za uzio

Ndovu wana akili na wanaweza kujifunza jinsi ya kuangusha nguzo. Nguzo zote zinazotumiwa kwenye uzio wa umeme lazima zipakwe unga/ mchangayiko wa pilipili katika msimu wa ndovu. Mchanganyiko wa pilipili na kinyesi cha ng’ombe na matambaa ya pilipili pia vinaweza kutumia kupaka kwenye mabomba ya maji.

Angalia Vizuizi vya Pilipili kwa maelezo zaidi

vidokezo

2

Taa za sola zinazomulika pamoja na mawe meupe na kengele za kushtua

Kwa vile ndovu hawapendi taa za kumulika, uzio huu ni kizuizi fanisi sana.

Kuna taa mbalimbali za LED, huku baadhi zikiwaka pale panapokuwa na mwendo. Taa zingine za LED zinamulika kwa rangi tofauti na kwa mpangilio tofauti usiku kucha, na hujizima zenyewe wakati wa mchana. Pale ndovu wanapoona taa za kumulika kwa mbali, huwa wanafikiri kuwa ni watu wameshikilia tochi, hivyo hawakaribii eneo.

Paka pilipili mara kwa mara kwenye nguzo na kuanika matambala, ili kutunza ufanisi wake. Angalia Vihisishi vya Infrared au Vya Mwendo

Pia unaweza kupanda mipilipili nje ya uzio wa umeme. Hakikisha nguzo zimepakwa vizuri mchanganyiko wa pilipili. Unga wa pilipili utafutika wakati wa mvua, hivyo tumia kama tu ni msimu wa ndovu ili kuokoa rasilimali.

vyanzo:

Soma zaidi kuhusu: Kupunguza Athari za Migogoro Baina ya Ndovu na Binadamu, Namibia. (2020).

3.

Kila taa ya LED ina chaja yake ya sola. Taa zinaunganishwa na nyaya na kubandikwa juu ya nguzo moja moja zilizosimikwa uwanjani.


VIDOKEZO VYA MATUNZO

Nguzo ndefu zinatumika ili ndovu wazione kwa mbali kabla ya kufika kwenye majengo. Taa za kumulika zina uwezo wa kujichaji wakati wa mchana ili ziweze kutumika usiku ambapo kuna uwezekano mkubwa wa ndovu kutembelea.

Tengeneza kivuli ili kuilinda kutokana na mvua, endapo kama haina kitu cha kuzuia mvua. Hakikisha taa ipo usawa wa macho au kifua cha ndovu aliyepevuka. Nguzo ni lazima zisimikwe ardhini kwa uimara ili kuepusha kuangushwa.

vyanzo:

Tumia pamoja na njia zingine za vizuizi (k.m mawe meupe yenye ncha kali au uzio wa mabati) utakaosaidia kuwazuia ndovu wakati wa mchana.

Jaribio lilifanywa kwa mafaniko katika Wilaya ya Chobe, Botswana. Soma zaidi kuhusu Zana mpya ya HEC: Uzio wa Taa za Kumulika. Mara Elephant Project.

faida

KIDOKEZO MUHIMU

+

Uzio unahama, kwani taa zinawekwa juu ya nguzo moja moja. Njia nzuri ya kuwazuia ndovu. Hakuna umeme unaohitajika kwani taa zinatumia sola. Gharama & matunzo ya wastani yanahitajika kuhakikisha nguzo haziangushwi na ndovu. Taa za kumulika pia zimegundulika kuwa zinawafukuza wanyama pori wengine kama vile simba.

hasara Kuna hatari ya wizi.

-

Ili kuepuka kuzoea, taa za rangi mbalimbali zinaweza kutumiwa na mpangilio wa rangi unapaswa kubadilishwa kila wiki.

Angalia Uzio wa Mabati

2a) VIZUIZI VYA MAWE MEUPE Hiki ni kizuizi cha mawe yenye ncha kali yanayopakwa rangi nyeupe. Mita 2 za mawe meupe yenye ncha kali pembezoni mwa nje ya uwanja yanaweza kuzuia ndovu kuingia ndani.

Inafaa zaidi usiku; haifai sana wakati wa mchana. Lazima iweze kuhimili hali za hewa. Tofauti na hapo inahitaji kufunikwa ili kuilinda dhidi ya mvua. Kuna hatari ya ndovu kuzoea.

4.

Ukali wa mawe ni kero na wenye maumivu kwa ndovu wakitembea. Changanya na taa za kumulika ili kutoa ulinzi wa ziada.

Angalia Matangi ya Maji kwa taarifa zaidi kuhusu kizuizi cha mawe meupe.


2b) KENGELE ZA KUSHTUA Angalia Kengele za Kushtua kwa taarifa zaidi

Hii inaweza kuwa njia nyepesi, isiyohitaji teknolojia kubwa ya kusaidia kwenye ulinzi wa shamba, kwa kuwashtua wakulima pale ambapo ndovu wanaingia kwenye majengo.

3

Mitaro ya kuzuia ndovu pamoja na Uzio wa Miti

Angalia Mitaro kwa maelezo zaidi.

Kwa nini zinafaa?

Mitaro inatengeneza kizuizi thabiti dhidi ya ndovu na wanyama pori wengine. Ndovu hawawezi kuruka, hivyo mtaro ambao ni mpana sana au wenye kina kirefu unaweza kuwa kizuizi muafaka.

Inaweza ikatumiwa na nini kingine

Pale waya unaposhtuliwa na ndovu, utatoa kelele kubwa ambazo zitawashtua wanafunzi na walimu shuleni. Ndovu wanaweza kuwa wakimya sana, na si rahisi kuwaona wakiingia ndani ya uwanja. Inasaidia kuwashtua watu kuwa kuna ndovu wanakaribia, na kuwawezesha kutafuta mahali salama, au kutumia njia zingine kuwafukuza ndovu.

kidokezo 5.

Tumia pamoja na njia zingine za vizuizi, kama vile taa za kumulika za sola kwa ufanisi zaidi.

Uzio Wa Miti

kidokezo

Taa za kumulika za sola

Taa za kutambua mwendo

Mitaro pamoja na Uzio wa Miti pembezoni mwa kiwanja inaweza kuwa njia muafaka ya kuzuia.

Mitaro ina hatari ya kumomonyoka udongo, hasa kwenye maeneo ya mlalo na mvua nyingi. Uwepo wa miti (uzio wa miti) husaidia kuimarisha na kuzuia mmomonyoko wa udongo.


faida Inaweza kujengwa bila vifaa vingi.

+

Mbinu inahusisha kupanda spishi imara za miti kama vile mianzi kwa kuzunguka mipaka ya jengo ili kuwazuia ndovu kuingia ndani.

Inaweza ikawa chaguzi yenye gharama ndogo au ya wastani. Inafaa kama kizuizi thabiti dhidi ya ndovu. Mkakati wa muda mrefu wa kusaidia kuzuia ndovu kuingia au kutoka.

KIDOKEZO CHA USALAMA

Mitaro pembeni mwa majengo ya shule lazima ichimbwe nje ya uzio, ili kutoa ulinzi kwa wanafunzi.

hasara

-

Kuta za mitaro zinahitaji matunzo, ambayo yanahitaji nguvu kazi na yana gharama, hasa baada ya mvua nyingi.

VIDOKEZO VYA UZIO MZURI WA MITI

Inaanzishwa kwa kupanda mstari wa miti na/au vichaka vya miiba/vinene kwa karibu karibu. Mijiti mikavu inaweza kufungwa na waya kuwekwa kwenye miti. Tumia njia mbalimbali kulinda miti yenye matunda dhidi ya ndovu kama vile kuchimba mifereji kwa nje.

Binadamu, mifugo na wanyama wengine wanaweza kujeruhiwa kwa kuanguka ndani ya mitaro yenye kina kirefu.

Mifano ya miti unayoweza kupanda

Ndovu watoto ndio hasa walio kwenye hatari ya kuanguka/kukwama mitaroni.

3a) Uzio wa Miti Hii ni mistari ya miti/vichaka inayopandwa kuzunguka mipaka ya shule na majengo ili kutoa ulinzi dhidi ya ndovu na wanyama pori wengine. Uzio wa miti unatumika kama kizuizi cha kushikika, kikiwazuia ndovu kuingia mahali.

6.

Commiphora spp.

Acacia nilotica: kwa ajili ya dawa

Mauritius thorn sp.

Mchaichai Ziziphus mauritiana: ina maunda yanayoliwa

Mkonge Mianzi ya miiba Nile Tulip – maua yanayovutia wachavushaji

vyanzo:

Physic Nut: inaleta kichaka kizito Palymra palm: unapandwa sana Sri Lanka

Soma zaidi kuhusu Kuweka Uzio kwenye Ardhi ya Kilimo Nigeria kwa Spishi Nyingi Zaidi za Miti, Uzio wa miti huko Segou, Mali: Tathmini ya watumiaji wake wa awali.


faida

+

4

imara za mawe Kutumia kuta imara za mawe kutatengeneza kizuizi imara dhidi ya ndovu.

Uzio wa miti unajali mazingira. Una gharama nafuu. Ni nafuu zaidi kuliko kujenga ukuta wa tofali au uzio wa umeme.

Angalia Njia ya Ulinzi wa Matangi ya Maji.

Inafaa sana katika kuwazuia ndovu wasiingie kwenye majengo yako. Miti itoayo matunda inatoa virutubisho vya ziada kwa wanafunzi. Miti inavutia wachavushaji kama nyuki, ambao pia ni vizuizi kwa ndovu.

hasara

-

Miti inaweza kuchukua muda mrefu kukua na kuwa fanisi. Njia zingine za kuzuia zinatakiwa zitumiwe wakati miti inakua.

Ndovu hawawezi kupanda, hivyo kuta za mawe zinawazuia wasipande juu yake.

faida

+

Inaweza kuhitaji matunzo ya mara kwa mara.

Kama ukijengwa vizuri, ukuta unaweza kuwa suluhu ya muda mrefu.

Hatari ya kuliwa na mifugo katika hatua za awali.

Unalinda vyema shule na viwanja dhidi ya ndovu.

KIDOKEZO CHA TAHADHARI

Usipande mikaktasi ya Cholla, kwani matunda yaotayo huwa na miiba inayoweza kuwadhuru ndovu na pia ni spishi vamizi.

Epuka kupanda miti ambayo itawavutia ndovu kuila (k.m miti ya akeshia).

Hauhitaji matunzo makubwa ili kuhakikisha ukuta bado ni imara.

VIDOKEZO VYA HATARI Kuta zinatakiwa ziwe umbali wa 3m kutoka kwenye matangi ili ndovu wasiweze kufikia na mikonga yao. Kuwa makini kuhakikisha watoto hawapandi juu ya kuta. Ndovu bado wanaweza kukubali maumivu ili tu wapate mazao matamu/ vyanzo vya maji, hasa wakati wa majira ya kiangazi, hivyo kutumia njia jumuishi kutaongeza ufanisi wa vizuizi. Soma zaidi kuhusu kuta za mawe: Kuta imara za mawe- EHRA

7.


5

6

Bustani za Mboga Mboga

Bustani za mboga mboga ni muhimu kwani zinatoa virutubishi, muhimu hasa kwa watoto mashuleni. Njia hizi zinasaidia kuhakikisha ulinzi wa ziada wa vizuizi kwenye bustani yako, ndani ya majengo, kuhakikisha ndovu hawavamii mazao yako.

5a) Uzio wa miti

Angalia Ulinzi wa Matangi ya Maji

Uzio wa miti hutumika kama vizuia upepo na pia vinapunguza mmomonyoko wa udongo.

Ndovu wanajulikana kwa kuvunja matangi ya maji na mabomba ili kupata maji ya kunywa. Kupaka mchanganyiko wa pilipili kwenye matangi au kupanda mipilipili kwa kuzunguka mabomba ya maji kunaweza kuzuia hii.

Hii inahakikisha kuwa mazao yanatosha na ni mengi.

kidokezo

Angalia vizuizi vya pilipili kwa taarifa zaidi

Pia unaweza kupanda mipilipili kama uzio wa mipaka.

ULINZI WA MATANGI YA MAJI

Inashauriwa kujenga kuta za ulinzi kuzunguka mfumo mzima wa maji, ikiwemo mabomba ya maji.

7

WATOTO WAKIWA WANAENDA SHULE NA KURUDI NYUMBANI

5b) Taa za Sola Zinazomulika

Taa za Sola zakuzuia Wanyama Kenya

8.

Mara zote wanafunzi wa shule wanakuwa katika hatari ya kukutana na ndovu wakiwa wanatembea njiani kati ya nyumbani na shuleni. Kuupa usalama wao kipaumbele inahakikisha hawakosi shule kwa kuogopa ndovu na wanakuwa salama.


7a) Elimu ya Kuelewa Tabia ya Ndovu

7b) Majukwaa ya miti Majukwaa rahisi ya miti yanaweza kujengwa kwenye njia za kila siku zinazotumiwa na wanafunzi.

Elimu kuhusu tembo ni muhimu katika kuhamasisha mahusiano mazuri baina ya binadamu na ndovu.

Ni salama kwa watoto kuweza kupanda haraka endapo ndovu wanakaribia ili kuepuka migogoro.

Ni muhimu kujua jinsi ya kutenda mbele ya ndovu, ili usiwachokoze hadi wakushambilie/waghafirike na ili kuzuia malumbano hatarishi.

Zingatia Uzito na Uimara

Kuelimisha wanafunzi kutawasaidia kufahamu kuhusu tabia mbalimbali za ndovu na muda gani wachukue tahadhari zaidi.

kidokezo

Tumia picha kutoa elimu kwa wanafunzi. Picha zinatengeneza taswira akilini ambazo hurahisisha watoto kuelewa.

Elimu ya wanyama pori ni muhimu zaidi kwa vijana ili waweze kuelewa umuhimu wa ndovu. Angalia ‘Ndovu kama Wahandisi wa Mfumo wa Ikolojia’ na ‘Utangulizi wa Ndovu’ kwa maelezo zaidi

9.

Chagua spishi ya miti iliyo imara yenye matawi yenye nguvu na yenye mizizi iliyoshika vizuri ili kuhakikisha jukwaa linadumu hata wakati wa mvua nyingi na upepo mkali. Tumia nguzo zilizochimbiwa kulipa jukwaa uimara zaidi. Weka kamba za kupanda zenye mafundo kwa njia nyingine za kupanda jukwaa.

faida

+

Watoto wakikaa juu ya jukwaa wanaweza kuwaona ndovu wakiwa mbali na kujituliza mpaka itakapokuwa salama kwao kuendelea kutembea. Kama ndovu wamesikika wapo karibu, watoto wanaweza kukaa juu ya jukwaa la mti katika usalama mpaka itakapokuwa salama kutembea tena. Kama yakisimamiwa vizuri, yanaweza kudumu kwa muda mrefu. Kuna gharama za wastani za kuanzia.


Vidokezo vya Tahadhari

Mavuvuzela hutumika kwa sababu hayawatishii ndovu. Hii ni muhimu kwa sababu ndovu anayehisi kutishwa ana uwezekano mkubwa wa kushambuliwa.

Ongezea wavu kwa kuzunguka mti ili kuhakikisha ndovu habandui magome ya mti na kuudhoofisha.

Vyanzo:

Usijenge kwenye miti yenye matawi machache/madhaifu.

https://nation.africa/kenya/ counties/kilifi/farmers-resort-to-drums-vuvuzelasto-fend-off-ravenous-elephants-3741868 https://learningenglish. voanews.com/a/vuvuzelaskeep-people-safe-from-elephants-attack/2703535.html

Angalia Ulinzi wa Miti kwa maelezo zaidi.

Ongeza paa la makuti, endapo matawi ya mti hayatoshi kutoa kivuli. Matunzo ya wastani yanahitajika ili kuhakikisha ni salama muda wote kwa watoto kupanda. Kama jukwaa si imara, kuna hatari ya majeraha.

faida

+

Sauti kubwa huwaogopesha tembo. Haiwatishi, hivyo ni salama kwa watoto kutumia.

7c) Mbiu ya mgambo/Mavuvuzela

Vifaa hivi ni vyepesi, rahisi kubeba na rahisi kwa wanafunzi kutumia.

Mlio mkali wa ajabu na usioacha kutoka kwenye Vuvuzela huweza kumkimbiza hata ndovu aliyekomaa. Mbiu za mgambo zikipulizwa pamoja katika kikundi, inaweza kuwa na athari zaidi ya kuwakimbiza ndovu.

Vidokezo vya Tahadhari Epuka kupiga kelele mpaka ukishajua mahali hasa alipo ndovu. Usipulize mbiu ndani ya sikio la mtu. Inaweza kuharibu usikivu wa mtu. Angalia Elimu ya Kuelewa Tabia za Ndovu ili wajue cha kufanya wanapokuwa karibu na ndovu. Angalia makala ya Vizuizi vya Sauti kwa njia nyingi zaidi.

10.


7d) Mabasi ya jamii/shule

faida

+

Mabasi yanasaidia kuimarisha ubora wa elimu, kwani wanafunzi hawakosi shule kwa sababu ya kuwaogopa ndovu na pia hali ya hewa mbaya. Wazazi wanakuwa na amani wakijua kuwa watoto wao wanasafiri kwenda shule kwa usalama, bila hatari ya kupondwa na ndovu. Inaboresha uhusiano uliopo kati ya jamii na ndovu. Mafanikio ya basi yanaonekana katika mtazamo chanya wa wanavijiji kwa ndovu.

Mabasi ya Jamii yanaweza kutoa mkakati wa kupunguza migogoro ambao utapunguza kwa kiasi kikubwa migogoro baina ya binadamu na tembo, kwa kutoa usalama wa kutosha kwa wanafunzi.

Sri Lanka

Mabasi haya yameanzishwa kwa mafanikio huko Sri Lanka na Botswana.

Botswana

Mabasi ya EleFriendly yalioundwa na Shirika la Uhifadhi Wanyama Pori la Sri Lanka (SLWCS) yameonyesha kuwa migogoro imepungua kwa 80% tangu mabasi yaanze kutumika.

Inawaruhusu ndovu kutembea kwa uhuru zaidi kwenye ushoroba ambapo wanaweza kula na kukutana, kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa karne na karne. Wakati wa shule kufungwa, mabasi yanaweza kuwasaidia watu kwenda katika vituo vya afya.

vidokezo: Matunzo ya mara kwa mara na huduma ya gari inahitajika kuhakikisha matumizi ya muda mrefu ya basi.

Mabasi ya Elephant Express nchini Botswana yanatoa usafiri kwenye ushoroba wa ndovu kwa wanafunzi ili kuongeza usalama wao kwa ndovu. Mabasi yamepambwa na michoro mizuri ya ndovu na kuwekewa vifaa vya kielimu, hivyo yanatuma ujumbe muhimu kuwa tunaweza kupata namna ya kuishi na wanyama pori.

Vyanzo:

Soma zaidi kuhusu -Basi la Kwanza Rafiki kwa Ndovu Duniani: Simulizi ya mafanikio.

-Kuhamasisha kuishi pamoja kwa usalama baina ya wanyama pori na binadamu huko Kavango Zambezi.

11.

Usitumie vibaya basi, kwani hii itapunguza urefu wa matumizi na inaweza ikapata uharibifu hivyo kuongeza gharama za matengenezo. Weka vitini vya kuelimisha ndani ya basi ili kuongeza elimu kuhusu ndovu kwa watoto. Wanafunzi wanatakiwa kusafiri bure, huku wengine wakulipa nauli kiasi kuhakikisha kuna fedha kwa ajili ya matunzo ya basi.


8

Minara ya Ulinzi

Angalia Minara ya Ulinzi maelezo zaidi.

Minara ya ulinzi inayojengwa mwanzoni mwa uwanja wa shule kuelekea njia zinazotumiwa sana na ndovu, inaweza kusaidia kutoa onyo mapema pale ndovu wanapokuwa karibu. Inaweza kutumiwa asubuhi ambapo watoto wanakwenda shule na jioni ambapo wanarudi nyumbani. Watu waliojitolea kutoka kwenye shule au kijiji wanaweza kusaidia kufanya lindo kwenye mnara. Minara ya ulinzi kwenye njia zinazotumiwa mara kwa mara inaweza kutengenezwa kwa usawa wa chini ili kuruhusu watoto kuupanda mnara kwa usalama endapo ndovu wapo karibu.

Angalia Vizuizi vya Sauti kwa maelezo zaidi.

Ndovu wanapoonekana kukaribia shule/watoto wanaotembea, wanaweza kutumia mbiu ya mgambo/mavuvuzela na filimbi kuwashtua watoto kutafuta mahali salama.

KIDOKEZO CHA USALAMA

Weka geti lenye komeo/kitasa kati ya urefu wa juu na urefu wa chini ili kuhakikisha watoto hawapandi mpaka mwisho.

Sifa na Katao la haki:

Tumekusanya rasilimali kutoka vyanzo mbalimbali. Baadhi ya njia zilizowasilishwa ni za majaribio na utafiti zaidi unahitajika. Angalia Marejeleo kwa maelezo zaidi. Save the Elephants inashauri tahadhari kwa njia zote na taarifa zitakazokusanywa na kuwasilishwa kwenye kitabu hiki kilichochorwa. Utafiti zaidi unaweza kuhitajika kabla ya utekelezezaji wa eneo husika. * Save the Elephants haihusiki kwa namna yoyote na gharama, uharibifu au majeraha yatakayosababishwa matumizi ya njia hizi.

12.

Imetengenezwa Kenya 2022

Imeandaliwa na Save the Elephants

www.savetheelephants.org

Michoro na Nicola Heath


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.