Kipato mbadala kutokana na biashara zinazojali ndovu

Page 1

KIPATO MBADALA KUTOKANA NA BIASHARA zinazojali ndovu Shughuli mbadala za kupata kipato zinatoa fursa kwa kwa wakulima kupata pesa ya ziada kwa namna nyinginezo, kuliko kutegemea moja kwa moja katika kilimo. Bidhaa zinazojali ndovu hutengenezwa kutokana na malighafi ambazo hazitishii maisha ya ndovu au kuwanyonya.

Jamii zinazoishi pamoja na wanyama pori pia wanakuwa na faida zingine zinazohusiana na uhifadhi wanyama pori uzingatiao maadili. Hii hupelekea kuimarika kwa hali ya kuishi pamoja baina ya watu na wanyama pori. Kwa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi, ukame umekuwa ukitokea mara kwa mara, hivyo kupelekea mazao kutofikia ubora unaohitajika sokoni au hayapandwi kutokana na kukosekana kwa mvua. Kuwa na vyanzo vingine vya mapato tofauti na kuvuna mazao pia inapunguza mzigo kwa familia endapo ndovu wanafanikiwa kuvamia shamba na kuharibu/kula mazao.

1.

Afya Moja: watu, wanyama, na mazingira, vyote vinahitaji kuwa na afya ili jamii na ikolojia yetu istawi.


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.