Chaguzi za mazao na shughuli za bustani ya jikoni endapo unaishi na ndovu

Page 1

CHAGUZI ZA MAZAO & SHUGHULI ZA BUSTANI ZA JIKONI ENDAPO UNAISHI NA Ndovu Ndovu wanahitaji kiasi kikubwa sana cha chakula kuweza kuishi; hadi 450kg kwa siku. Panapokuwa na vipindi virefu vya ukame, chakula cha ndovu kinakuwa adimu na wanalazimika kutafuta chakula mashambani.

kidokezo

Inashauriwa kupanda mazao kwenye mashamba madogo, hasa kwenye maeneo waliopo ndovu, kwani ni gharama nafuu na fanisi Zaidi kulinda mazao machache dhidi ya ndovu kwa kutumia njia mbalimbali za kulinda mipaka.

Mashamba madogo huhitaji kiasi kidogo cha maji. Udongo huweza kushuka ubora endapo utakuwa unapanda mazao yale yale kila msimu (Kilimo cha zao moja). Ili kulima kwa mafanikio kwenye shamba la hekari 1-3, jaribu kutumia Mbinu za Kilimo-Hifadhi ili kulinda rutuba ya udongo na kuhifadhi maji.

Kama unaishi karibu na hifadhi ya taifa/mbuga za wanyama, panda mazao ambayo ndovu hawali ili kuhakikisha hawavutiwi na shamba lako. Haya yanaitwa mazao yasiyolika. Mazao hayo yanaweza kuwa mazao ya biashara na yanaweza kuwa chanzo mbadala cha kipato yatakaposindikwa. Ukiwa na kipato chako cha ziada unaweza kununua mazao ya chakula kama vile mahindi na maharagwe kutoka kwa wakulima ambao hawaishi karibu na maeneo walipo ndovu. Tumia mipaka ya ziada au njia za awali za kutoa maonyo kwenye shamba lako kulinda mazao yako yasivamiwe.

1.

kidokezo

Epuka kulima zao moja kwenye shamba moja kwa zaidi ya msimu mmoja wa kilimo. Lima kwa mzunguko mazao yasiyopendwa na ndovu kwa kila msimu na lima kwa kuchanganya ina mazao yanayozalisha nitrojeni kama vile maharagwe/na mazao jamii ya maharagwe ili kuipa afya ardhi.


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.