DRONI NA NJIA ZA ANGA Droni ni vifaa vya kuruka vinavyoweza kudhibitiwa kutokea ardhini kwa kutumia remoti kuwafukuza ndovu kutoka kwenye shamba kwenda kwenye usalama. Ni mbinu ya gharama kubwa, ya teknolojia ya hali ya juu inayoruhusu maafisa wanyamapori/watu walioruhusiwa kutoa muitikio wa haraka kupunguza migogoro ili kuwalinda wote binadamu na ndovu.
Droni za kuruka zinatoa mlio kama wa kundi la nyuki. Pale ndovu wanapokabiliana na droni inayoruka na kusogea yenye mlio kama wa kundi la nyuki, wataondoka kwenye eneo husika haraka mbali na muelekeo wa sauti. Kwa miaka mingi sasa wanasayansi wamekuwa wakijua kuwa droni zinazoruka karibu sana na wanyama, wakiwemo ndovu, zina uwezo mkubwa wa kuwasumbua na hata kuwaelekeza katika eneo fulani. Hahn na wenzie wamethibitisha hili kwenye mfano hai wao wa mwaka 2017, ukionyesha mafanikio ya 100% kwamba ndovu wanaweza wakafukuzwa kabisa kwenye maeneo yenye migogoro baina ya binadamu na ndovu kwa kutumia droni. Droni zinaweza pia kutumiwa kurekodi video na picha, inayoruhusu watafiti kuelewa harakati na tabia za ndovu, hivyo kusaidia kupunguza migongano.
https://www.pbs.org/newshour/show/drones-keep-elephants-away-people-tanzania
1.
Soma zaidi kuhusu: Utafiti umefanywa kuthibitisha kuwa droni zina mlio kama wa nyuki
Njia zingine za anga ni pamoja na kutumia helikopta kuwafukuza ndovu kwa usalama waondoke kwenye makazi na mashamba.