Minara ya Ulinzi Mahali salama, palipo juu kunaweza kusaidia katika ulinzi wa usiku na katika kuwaona ndovu wanapokaribia. Kutumia minara ya ulinzi na ulinzi wa usiku kunasaidia kuwawezesha wakulima kuchukua hatua kwa haraka na kuwa na mfumo wa utoaji maonyo mapema pale ndovu wanapokuwa karibu.
Njia ya 2: Kubwa au inayosimamiwa na jamii Kutumia jukwaa zito la chuma au la mbao.
Hii inafaa kwa maeneo yenye migogoro na njia kuu ambazo ndovu hupita mara kwa mara.
Ushirikiano bora wa jamii unahitajika ili kuweza kusimamia minara mikubwa.
Lengo kuu ni kumpa mlinzi eneo salama, lililo juu, na lenye kuonyesha sehemu kubwa ya eneo ili kulinda na kuona maeneo yanayozunguka, na kutuma ishara salama.
Njia ya 1: Ndogo, ya shambani Majukwaa madogo ya ulinzi yanaweza kutengenezwa juu ya mti au juu ya nyumba. Inaweza kuwa hatari kutokana na urefu hivyo itumiwe kwa umakini na uzoefu.
Vifaa muhimu vya ulinzi wa usiku Taa za kumulika au tochi Simu za mkononi Vizuizi vinavyotoa kelele Vifaa na mahitaji ya kulalia
1.
Inafaa Zaidi kutumika na vizuizi vinavyotoa kelele na vya taa.
Hii inafaa Zaidi kwa ulinzi binafsi wa shamba.
Kupitia Ulinzi shirikishi wakulima wanaweza kusaidia kupunguza uvamizi wa ndovu kwenye mazao na mashambani.
Kengele za kushtua kwa ajili ya kuonya Kutumia mtandao wa kengele za ng’ombe au makopo yaliyojazwa mawe pia kunaweza kufaa kuwashtua wakulima.