Vihisishi vya Infrared au vya mwendo

Page 1

vihisishi vya infrared au vya mwendo Kihisishi cha infrared? Kihisishi cha infrared ni kihisishi cha umeme ambao hushtuliwa pale ambapo mnyama au kitu kinapopita mbele yako. Passive infrared sensor (PIR) ni kihisisi ambacho kinapima mwangaza wa infrared unaotoka kwenye mashamba ya mbali. Vifaa vya kifaa hiki kinaweza kuwa vinapatikana kwenye maduka ya umeme na vinaweza kutengenezwa na watu wenye uelewa wa umeme. Angalia zaidi kwenye Youtube kuhusu namna ya kutengeneza kihisishi cha infrared.

Mifumo ya kutoa maono ya kiotomatiki inaweza kusaidia kupunguza uhitaji wa ulinzi wa mara kwa mara kwa wakulima.

Kwa nini ni za muhimu? Mita10 - 15

Kihisishi cha mwendo kinatambua kufika kwa ndovu (ndani ya mita 10 hadi 15 ). Kifaa hiki kinatumia betri kidogo sana na hudumu kwa muda mrefu shambani kama kimetengenezwa vizuri. Mara baada ya kihisishi cha PIR kikishtuliwa, kinapiga kengele iliyowekwa kwenye banda la mlinzi.

vidokezo vya tahadhari: Nyaraka hii haijajitosheleza. Utafiti zaidi na uasili wa muundo unahitajika. Njia hii inategemea nguvu ya betri. Hakikisha vifaa vinajaa chaji vizuri ili kuvitumia vyema. Katika njia zote, kuna hatari ya hatari ya kuzoea. Ni vyema kuchanganya na kubadilisha mikakati.

Aina zingine: Baadhi ya vihisishi vinaweza kuwa na spika ndani yake. Kihisishi cha infrared kinashtua mfumo wa spika. Milio ya wanyama wawindao na nyuki inaweza kutumiwa kusaidia kuwafukuza ndovu. Mfano, Buzz Box na Wild Survivors.

Unaweza kuitumia na nini? Inafaa kutumiwa pamoja na vizuizi vingine vya mashambani.

Faida/Hasara

Upeo wa kifaa hiki unaweza usiwe mkubwa sana. Kifaa kinaweza kutoa muitikio kwa mnyama au gari lolote linalopita. Pia hakifai katika mazingira ya unyevunyevu. Vifaa hivi vinaweza kuwa vya gharama na vyenye changamoto za kiufundi. Kama vikifanya kazi, vinaweza kupunguza changamoto ya ulinzi wa mazao kwa wakulima.

Sifa na Katao la haki:

Tumekusanya taarifa kutoka vyanzo mbalimbali. Vyanzo vikuu ni pamoja na: Narayana, S. (2014),The Nature Conservation Foundation, Mongabay (2015) and Wild Survivors. Kwa taarifa, angalia Marejeleo. inashauriwa kuwa na tahadhari katika njia zote na taarifa zote zilizokusanywa na kuwasilishwa kwenye toolbox hii. Utafiti zaidi unaweza kuhitajika kabla ya utekelezaji wa eneo husika. * Save the Elephants haihusiki na gharama, hasara au majeraha yoyote yatokanayo na njia hizi.

1. Imetengenezwa Kenya 2021

Imeandaliwa na Save the Elephants

www.savetheelephants.org

Michoro na Nicola Heath


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.