Kengele za kushtua

Page 1

KENGELE ZA KUSHTUA Kengele ya kushtua ni nini?

Hii inaweza kuwa njia nyepesi, isiyohitaji teknolojia kubwa ya kusaidia kwenye ulinzi wa shamba, kwa kuwashtua wakulima pale ambapo ndovu wanaingia shambani.

Pale waya unaposogezwa na ndovu, utatoa mlio wa kengele utakaosaidia kwenye jitihada za ulinzi wa usiku. Mlio wa kengele ni muhimu sana katika kuwashtua wakulima kuhusu uwepo wa ndovu, na inaweza kusaidia kuwafukuza ndovu kabla hawajaanza kula. Waya unapoguswa, utavuta kengele na kuisababisha ilie, hivyo kuwataarifu walio karibu na kusaidia katika ulinzi wa mazao.

Aina mbalimbali? Njia za kawaida na za kisasa zaidi Uzio wa waya za kushtua zinazoamsha ving’ora vya umeme. Vishtukizi vilivyozoeleka kama vile baruti, kengele au makopo yaliyojazwa mawe. Njia moja rahisi inayoweza ikatumiwa ni ya waya wa kujikwaa. Hii itaamsha kengele endapo itawekwa njiani wanapopita ndovu. Aina za kengele za kushtua zinazotumiwa mara kwa mara ni pamoja na mabomu na makopo yaliyojazwa mawe.

Kwa nini zinafaa? Kengele za kushtua zinafaa sana kwa utambuzi wa mapema wa ndovu na kuwaonya wengine. Wakati mwingine ndovu wanaweza kuwa wakimya sana, na si rahisi mara zote kuwaona wakiingia mashambani. Hii inaweza kusaidia kuepusha kukutana kwa bahati mbaya.

Tambua: hiki pia ni kizuizi kizuri cha sauti.

1.

Unaweza kuwa mbunifu zaidi na kutumia chochote ulichonacho ili kutengeneza kengele ya kupiga kelele.

Unaweza kuzitumia na kitu gani kingine? Kengele za kushtua zinakuwa na ufanisi mkubwa endapo zitatumiwa pamoja na njia za ulinzi wa usiku na vizuizi/mjumuisho wa vizuizi. Njia zingine za ulinzi wa usiku ni pamoja na; majukwaa ya mti, vibanda vya ulinzi, tochi, mifumo ya utambuzi wa mapema, taa kali, redio au simu za mkononi. Inasaidia kujua njia zinazotumiwa mara za kwa mara za ndovu kuingia na kutoka– ili kuelekeza jitihada za ulinzi hapo.


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.
Kengele za kushtua by Save The Elephants - Issuu