uLINZI WA USIKU KWA KUTUMIA TAA NA MOTO Ndovu wanajulikana kwa kuvamia mashamba wakati wa usiku. Ili kupunguza ulinzi wa usiku, njia ya vizuizi vya taa na moto inaonekana kuwa inafaa zaidi kuwafukuza ndovu kutoka kwenye mashamba na maboma.
kidokezo
Kuwa na kisanduku cha kuwashtua ndovu kinaweza kuongeza ufanisi katika kuwazuia ndovu.
Kisanduku kinatakiwa kiwe na: Simu ya mkononi ili kutuma jumbe za SMS kwa jamii husika
Tochi/Taa yenye uwezo mkubwa
Ndovu wana akili na wanaweza kuingia kenye shamba bila kutoa sauti yoyote. Shirikiana na jirani yako kuwafukuza ndovu kabla hawajaingia kwenye shamba/eneo lako. Vizuizi vya taa na moto pamoja na kelele, vimekuwa vikitumika tangu zamani kufukuza ndovu. Watafiti wamegundua kuwa ndovu wanashtuliwa zaidi na taa za kumulika kuliko kubweka kwa mbwa. Angalia Kengele za Kushtua na Vizuizi vya kelele kwa maelezo zaidi
1.
Vuvuzela/mbiu ya mgambo, au kitu chochote kitakachoweza kutoa sauti kubwa pale kitakapotumika. Ni vyema kutotegemea taa na moto peke yake ili kulinda mazao yenu na nyumba zenu. Tumia pamoja na njia zingine za vizuizi na vikwazo shambani.
Mabomu ya Pilipili ambayo yameshaandaliwa kabisa kabla ya ulinzi wa usiku.
Kidokezo cha Tahadhari Mara zote tafakari kuhusu njia ya vizuizi unayotaka kutumia, ili usiwaweke watu wengine hatarini. Soma zaidi kuhusu: Kutumia Baruti Kuokoa Ndovu