1 minute read

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

MASAWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA

1. Nitafanyaje ikiwa nimelipia credits kutumia M-PESA lakini Kontrola yangu haionyeshi malipo niliyofanya?

Advertisement

Ikiwa umelipia angalau credit ya siku moja kwa M-KOPA kutumia M-PESA, Kontrola inafaa kusahihisha idadi ya credits yenyewe katika muda wa masaa 12. La sivyo, tafadhali hakikisha kwamba umepokea ujumbe unaothibitisha malipo kutoka M-KOPA na pia M-PESA, na kwamba maarifa yote ya malipo yalikuwa sawa. Unaweza bonyeza kidude cha M-KOPA utakapopata ujumbe kutoka M-KOPA ili Kontrola lionyeshe salio la credits sahihi. Usipofaulu, pigia Customer Care simu.

2. Niko na salio ya credits kwenye Kontrola yangu lakini mtambo wa kuchemsha maji haufanyi kazi.

Hakikisha kwamba Kontrola yako ina chaji ya kutosha, ilichaji kamili kwa muda wa masaa 8 (icon ya betri ni laini kamili wala sio kuvunjikavunjika), salio ya credit inaonekana kwenye skrini ya Kontrola na solar panel imaunganishwa. Iwapo bado kuna tatizo, pigia customer care kwa nambari 0707 333 222.

3. Kontrola yangu itapokea credits kutoka kwa nyumba?

Kontrola yako ya M-KOPA inafaa iwe na mwunganisho kwa mtandao mahali popote simu ya kawaida inaweza kushika mtandao. Ikiwa mtandao wa Safaricom ni duni mahali ulipo, tafadhali piga simu kwa agenti wetu wa customer care ili usaidiwe.

4. Nitafanya nini maji yakiwacha kuchemshwa?

Kwanza, chunguza hali ya hewa. Pia, hakikisha kwamba Kontrola yako ina idadi ya angalau credit moja. Iwapo shida haitatatulika, piga simu kwa nambari ya customer care ama utume ujumbe kwa nambari ya SMS ya customer care na utahudumiwa..

5. Je, mtambo wangu una udhamini?

Ndio. Vipengele kuu vina udhamini wa muda wa miaka 3. Kontrola na solar panel zina udhamini wa muda wa miaka 2. 20

This article is from: