
1 minute read
Maarifa ya Udhamini
Sehemu hii inaelezea kuhusu sharti na sheria za udhamini wa bidhaa.
Sheria za Udhamini
Advertisement
Kwa madai ya udhamini, lazima: ●• Bidhaa zikaguliwe na BOSCH kuhakikisha kwamba hitilafu ya mtambo imesababishwa na makosa katika kuundwa au vifaa vilivyotumika, katika muda wa udhamini. • Hakuna jambo lolote limefanyika ambalo limeondolewa kwa udhamini.
Muda wa Udhamini

Muda wa udhamini ni MIAKA TATU (3) kutoka siku ya kununua bidhaa kwa vipengele hivi vya mtambo wa kuchemsha maji kutumia nishai ya jua: 1. Kikusanyo cha nishai ya jua 2. Tenki ya maji moto 3. Lango la kupitihsa maji 4. Thermo-mixing valve 5. Fremu 6. Mabomba ya maji na viunganishi
Muda wa udhamini ni MIAKA MBILI (2) kutoka siku ya kununua bidhaa kwa vipengele hivi vya mtambo wa kuchemsha maji kutumia nishai ya jua: 1. Waya zote 2. Kontrola ya M-KOPA 3. Solar panel
6
Mwisho wa Dhima

Udhamini ulioelezwa hapo juu ndio dhima yetu kamili. Kuongezea, BOSCH inakataa kukubali dhima yoyote kwa ajili ya uharibifu wa mali au majeraha yoyote yatakayotokea.
Yasiyokuwepo katika Udhamini

Yafuatayo hayapo kwenye udhamini wa bidhaa: 1. Uharibifu wowote unaosababishwa na: • ‘Matendo ya Mungu’ au sababu lolte ambalo BOSCH haliwezi tawala. • Utumizi vibaya wa vipengele vya mtambo, pamoja na matumizi ya mtambo kwa kusudi lolote lisilo la kawaida kulingana na maagizo ya BOSCH. • Uhifadhi au utumizi vibaya wa vifaa vya mtambo. • Kuunganisha kwa nguvu za umeme isiyostahili. • Kujaribu kutengeneza au kufanyia ukarabati na mtu yeyote isipokuwa fundi waliothibitishwa na BOSCH. 2. Vifaa au vipengele vya mtambo vinavyoonyesha dalili za kufanyiwa ukarabati isiyostahili. 3. Vipengele vya mtambo ambavyo nambari ya serial imebadilishwa, imetolewa au kuharibiwa kiwango cha kukosa kusomeka. 4. Kusiha na kuzeeka kwa vipengele vya mtambo ya kawaida kwa muda, isipokuwa vipengele vinavyoonyesha dalili ya hitilafu katika uundaji.
7