
1 minute read
Mwongozo
Asante kwa kununua mtambo wa kuchemsha maji kwa nishati ya jua ya ComIN iliyoundwa na BOSCH. Kielekezo hiki kinaelezea vipengele vikuu vya mtambo huu, jinsi ya utumizi, uwekaji na utatuzi wa shida unazoweza kuambatana nazo.
Kwa maarifa zaidi, tafadhali piga simu kwa nambari ya Customer Care ya M-KOPA 0707 333 222 ama utume ujumbe bure wa SMS kwa 22363. Nambari ya Customer Care inapatikana 24/7.
Advertisement
Tafadhali soma kijitabu hiki chote kabla ya kutumia kipengele chochote.
Yalitomo katika Mtambo wa Kuchemsha Maji kutumia Nishai ya Jua
4 5
3
6
1 2 8
7
1 2 3
4
3 Tenki ya maji baridi Pampu Kikusanyo cha nishai ya jua Tenki ya maji moto 5 6 7
8 Lango la kuthibiti maji Kontrola ya M-KOPA Solar panel Fremu
Ujumbe za Usalama

Kukosa kufuata maagizo yaliyomo katika kijitabu hiki kunaweza kusababisha uharibifu wa mali, kuumia au kuondolewa kwa udhamini wa bidhaa.
Usiwahi kubali Kontrola ya M-KOPA kugusa maji au itaharibika na kuweza kusababisha kuumia.
Ikiwa Kontrola ya M-KOPA itashika maji, izime mara moja, toa maji yoyote na uiwache ikauke kabisa kabla ya kutumia tena.
Usichaji Kontrola ya M-KOPA bila kuikinga kutoka kwa jua kwa sababu betri inaweza kuharibika.
Usiwahi fungua au kujaribu kufanyia kipengele chochote ukarabati kwa sababu inaweza kusababisha kuumia, kuharibu mtambo na kuondolewa kwa udhamini wa bidhaa.
4
5
Maarifa ya Usalama
Ikiwa Kontrola ya M-KOPA itapata joto jingi zaidi inapochaji, itoe kwa chaja mara moja na pigia Customer Care simu kwa 0707 333 222 au tuma UJUMBE BURE kwa 22363.
Unganisha Kontrola ya M-KOPA kwa solar panel iliyothibitishwa na M-KOPA pekee. Kukosa kufuata maagizo haya kunaweza sababisha kuumia au kuharibika kwa Kontrola ya M-KOPA.
Utakapogundua hitilafu kwa bidhaa, tafadhali pigia Customer Care simu kwa 0707 333 222 au tuma UJUMBE BURE kwa 22363.
TAHADHARI!
Sehemu zifuatazo zinaweza kupata joto sana na huenda zikasababisha majeraha zikiguswa: - Kikusanyo cha nishai ya jua. - Tenki ya maji moto. - Maji moto kwenye mabomba na mfereji. - Mabomba amabayo hayajafunikwa na insulation.