I
PAMBAZUKO
Wahengawalisema,shangwehuwasikuyakuzaliwa, duniahuchekelea.Mtotoawapohadharani,ulimwengu humpokeanakumtiaakilini.Katikatiyamsituwa walimwengu,mtotohuchipukanakustawikwanasabana haiba.Kwakimohujitangazambeleyakilamzaliwa.Lakini upowakatihujapasipohiari,akuayehuchaguawa kuambatananaye.Kwausuhubaauhuba,nihiariyamoyo wamtuumtumavyo,kuchaguaaukuchaguliwa.Lakini mwishowayote,moyondiohumuongozamtu,kumpata wakewasirinimmeaumke.Hiyondiyosifayamaishaya muumbwakwadamunanyama.
Vilevileulimwenguuliwakutanishawatuwawilikutoka katikafamiliambili;Majaliwaakiwamtotowapekeekwa mamayake,BiLolaMuksin,mwenyejiwaPwaniiliyp mwambaowaBahirayaHindi;naMauabintiwaJackson, alikuwamzaliwawabara.Kukutanakwawawilihawa kulikuwakamapambazukolakuyatimizayasiyohiari mwilinimwao;walipendana.Niayaoiliwafanya wachaguaneilikuyaishimaishayauchumbahatimaye ndoa,walichukuana.Ilikuwafaharikubwakwaulimwengu kuwapokeawawilihaokamamkenammewalioshibana.
Hatimayewaliokotananakuvutanahadibara,niaikiwa nikujitafutiarizikiwaliyopangiwanaMaulana.Wakiwa barailipitamisimukuminamitanoyamasikanakiangazi wakiwanafuraha.Furahawaliyokuwanayo,ilifukuzaila zotekutokakwawatuwenyeinda.Walichekanakufurahi
pamoja.Msibaniwaliombolezapamojanahataharusini walikuwachandanapete.Hawakuachanahatahatuamoja kamakumbikumbi.Walistahilikuwababanamamawa mfano.Lakinije,lingewezekanajehilopasipokutokewana uzao?Hivyoiliwapasakukazanakumwomba aliyewaunganishawakimtakamzaliwawaowakwanza.
NdoayaMajaliwanaMauakatikatiyakijijicha Hamanikoilikuwayamfano.Mauaalikuwabadiijamali kwasura,umbonasauti.Majaliwanafsiilimsifuna kumpandishakwafaharinakujionaakiwakilelenimwa mlimamgumukuukwea.Kilaalipokuwaakimtazama Maua,hakuishahamuyakutakakumsogeleajapo amtekenyenakuisikiasautiyakenyembambatamukama kinanda.Walishibananakushabikiana.Mauaalijua mmewealikuwamtanashatikulikowaumewotealiopata kuwatiamachoni,vilevileMajaliwaalijuafikakuwa,ahali yakealikuwahanawakufanananayekwakilakitu. Walisifiana!
Sikuzilikatika,miezihatimayemiakaikawaimewapa kisogo,kitandachaohakikuwahikumbebamwanahata bintimchangawakumzaa.Walikuwabadowakibarizi kamawachumba.Wahengawalisema;juhudihaishindi kudra,hatimayendoayaMajaliwanamkeweilijibubaada yamiakamingi.Wakatiambaojiranizaowalikazana kuwanyosheavidolevyalawana,Rabanaalijazafuraha chumbanimwao.Mauaalishikaujauzito.
ShaukuyakumpatamwanakwaMajaliwailikomaa moyoni.Mauayeyehakutakakutabiriwalakutangaza tamaayajinsiayamtotoalomtakakuwanaye.Alitaka mtoto,awayeyeyote,mwanahatabintikwakeilikuwa zawadinatunukatikandoayake.Mauahakuishakudeka nayealidekezwa.Majaliwaalimtunzamkewezaidiya bustanimbeleyakasrilakifalme.Hakunaalichokitaka MauaambachoMajaliwaalishindwakumtimizia.Hata
kamailimlazimuMajaliwakumwagajashojingikwa kwendambalikwamiguukutafutalimau,hianahakuwa nayo,alitii.HatakamaMauaingefikasikuakahitajimzizi wamlima,Majaliwaangejipigakifuaakitakakuung’oa mlimaKilimanjaro.Hakutakamkeweaingiwehuzunihata kwasekundemojakutokananayeyekushindwajambo. Alitakamkeawenasihanjemanaakilitulivuiliamzalie mwana,mrithiwaamalinafaharizake.
MiezikendahaikuwamudamfupikwaMauaaliyepitia kilaainayachangamoto.Kwakuwahakuwahikuwana haliiletangukuzaliwa,ilimpasakuwaulizarafikize waliokuwawakifikakumjuliahali.Kunawakatimiguu ilimvimbanawakatimwinginehasirazilimchukuabila sababunakuhisikumchukiammewake.Kunawakati Mauaalitamaniharufuyamauamabichinakumlazimu Majaliwakuyatafutakondeniasubuhihatamchanawajua kali.KwaMajaliwamiezikendaaliyoipitiaMauailikuwasi chochote.Mudakwakeuliendakamakonokonotofautina hamuyakeiliyokuwaikiendakwakasikamamshalewa msasimawindoni.Alitakakumwonamzaliwawakewa kwanza.Sikumwonatu,balialitakakumwonamwana ambayealifanananayekwahaibananasaba.Halihiyo ingewezakumwondolealaananafununuzamajirani ambaowalikuwawakimbandikasifayakutokuwamme. Walikuwahawaishikumzushiakuwaalikuwachapapunga.
Hayawihayawimwishoweikawa.Usikuwasaatisa Mauaalishikwanauchungu.Majaliwaaliikupuaakiba yakeyoteyafedhanakumpelekaMauakwamkungawa kijijihicho.Alijifunguasalamausikuuleulebaadatuya Majaliwakuipakisogonyumbayamkunga.Majaliwa ambayealikuwanashaukuyakuitwababa,hakupatwana usingizi.Hakuwaakijitambuanaasingewezakufanya lolotebilakumfikiriaMaua.Hamuyakenimwana,mrithi wakekutokakwaubavuwake.
Mapemaalfajirihapajakuchwa,Majaliwaaliwasilikwa mkunga.HapakuwanasiritenayakumfanyaMajaliwa asitambueukweli.Sautiyamtotoilimpokeaangaliakiwa hatuachachekablahatahajafikauganikwamkunga.
FurahailibishahodinafsinimwaMajaliwa,mwili ulimsisimkahadivinyweleovilisimamawimabaadaya sautiyakichangakuisikia.Alitakakupayukakwafuraha kutangazaujiowadamuyake,lakinialijipamuda.
Aliharakishakutembeailiawahi,hatimayealifika mlangoninakubishahodiiliafunguliwe.
“AmejifunguaMaua,kipenzichangu?”Majaliwaaliuliza baadayakufunguliwa.Akiwanashaukuyakujibiwa, mkungaalisitakidogokumjibulakinibaadayakuona Majaliwaalitakakumpitamlangonibilaadabu,alimpatia ushuhuda.
“Ndiyobaba,amejifungua.Hongerasana,Mungu awakuzie,”alisemamkunga.Majaliwaalikuwatayari kaingiandani.Alikuwakasimamasebuleni.Koroboi iliyokuwainawakahaikutoamwangawakutoshana kumfanyaawezekuonachumbanialimokuwaMaua. BaadayaMajaliwakumpitakamamshalepalemlangoni, mkunganayealiingia.Alipitilizamojakwamojahadikwa Mauaaliyekuwakapumzikabaadayakazinzitoyakumleta shuhudawakizazichake.
“Mama,mtotogani?”AliulizaMajaliwa.Alitamani mkungaamjibupapokwahapokablahatahajamaliza kumezafundalamatealilokuwatayarikulimezabaadaya manenokumtoka.Masikioyalimsimamawimakama mbwamwituasikiayemilioyamnyamaaliyempoteza katikawindo.Moyouligonganakuripukakwakasiikiwa hamuyakujuaimeuzidimwilimzima.Mkungabado aliendeleakuwakimyakwasekundechache,akiwakama hakulisikiaswalikutokakwaMajaliwa.
Baadayaukimyandipoaliamuakumjibuilikumtoa wasiwasi.“Mrembokamamamayake,mrefukamababa yake,mkemwenzanguhuyo,”alijibumkunga.Majaliwa hakujibukituwalahakuulizatena.Jotolamwilililizimana baridikalililiuvamiamoyo,ukapoakamanofulililotiwa jokofuni.Aligeukabubu,machoakiyakodoakamamaarasi akichekurakwenyejaalauchafu.Ukimyawakehaukuweza kutabirikawalakubainika,lakinialiamuakuuvunjabaada yakutafakarisana.
“Mauahaliyeikoje,maanasimsikiiakinena. Anaendeleaje,mkewangu?”AliulizaMajaliwa.
“Hajambo,lakiniamelalatukwauchovu.Nataka apumzikekwanza.Nakuombakaninunuliemafutaya kugonga,yanaziauyakukama,yakarangaingalimapema. Kamakunanguozakubadilisha,nendakanileteevitenge dotimojanakangadotimbili.Hivisasa,navihitajiili akiamkaniendeleekumhudumia.Yakupasapiakumpeleka hospitalini,”alielezamkunga.
KunajambolilimchokonoaMajaliwaakilini.Alitaka kusemalakinialiishiakupanuamidomokamamamba aliyekosakumlasamakinakuparamiamziziautawilamti. Lakinikwakuwakilichofikranihusemwakwamdomo, hatimayealinenamashakayake.“Hospitalinikwalipitena mama?Kamakajifunguasalamasimamboyamekwisha!” AlisemaMajaliwaakiwakajaatanziko.Jambolakwenda hospitalinitenalilikuwakamahabarimpyakwake.Kutaja hospitaliniilikuwakamakumtajiakwendamahaliambako hajawahikuwazakwendakwahiariyake.Hakutakana walahakuwanawazolakwendahospitalinikabisa.Fikrani alijuanaalikuwanauhakikakuwa,kufikakwamkunga ilitoshakwanimamboyoteyaliishiapale.
Mkungaalilazimikakumfahamishasababuyakwenda hospitaliniakisema,“Mwanangu,duniayazamazenuni
tofautinayasasa.Mambohuendayakibadilikakizazihadi kizazi.Ukiendahospitali,hukowatamchunguzahaliyake kiafya,piawatampatiamtotokaratasiiliawezekupata chetichakuzaliwa.Sikuhizikilakitunimpakakaratasi.Ni nyarakamuhimusanausipuuzie,”mkungaalieleza.
KijashokatikatiyabaridikilimmiminikaMajaliwa. Ilimpasakukubaliananaagizolamkungaakiitikakwa unyongeuliojaabaridi,“Sawamama.Lakinimambohaya yachetikilauendako,yananisumbuasanahatamimi. Kamamarambiliautatunakosakupatiwastahikizangu nyingi,nikidaiwachetichakuzaliwaaukitambulishocha uraia.Sasamiminawashangaasanawatuhawa,tangulini mtualiyezaliwachiniyamwembekamamimiakawana chetichakuzaliwa?Kamamwembeulikuwanauwezowa kutoachetibasisikunitawapatiawaendeleekungoja. Lakinikwahuyu,nijambojemaumenifumbuamacho. Achanifuatenguokwanzandiponitarudiilitwendehuko hospitalini,”alisemaMajaliwa.Alitokanakutokomea alikokuwaakiishinamkewekwaajiliyakuchukua alivyokuwaameagizwa.
Baadayakuwawamempatabintikatikauzaowaowa kwanza,Majaliwaalipendekezajina.Ilipaswamtoto kuitwaLola.Jinahilolilikuwalamamayakeambaye alikuwaakipendasanakujitazamakwenyekioo.Tabiahiyo ndiyoilipelekeawazaziwamamayakeMajaliwa kumbandikamamayakejinahiloambalolilikuwana maanayampendakioo.Wakatiuliendeleakuyoyoma,Lola alikuanakuchipukakamamchewamgombakwenye rutuba.Alikuwanaafyanjemailiyowafurahishawazazi wakewote.
Majaliwaambayealikuwaakitegemeakumpatamwana badalayabintihatimayemoyowakealiushauri kukubaliananaukweli.Alijuafika,uzaouleungefuatwana uzaowakiumekamamatamanioyake.Alijipaimanihiyo baadayakudodosandaniyaukooalimozaliwa,hapakuwa nauzaomkubwawawatotowakike.AlimpendaLolana kumfanyamwanayenakumtukuza.
BaadayaLolakufikishaumriwakwendashule, Majaliwaalianzakumtiliamashakamkewe.Hakukuwana daliliyoyoteyakushikaujauzitozaidiyaMauakuongezeka kwaunene.Mauaalinenepanakuwanauzitomkubwa. Majaliwahakukomakulalamaakimlaumumkewekuwa alikuwaamefanyahilailiasiwezetenakujipatiamtoto aliyemhitaji.Mauayeyehakuwanawasiwasi,fikaalijua sikuingefikaambayoangempatamtotowapilikumfuata kifunguamimbawao.
WakatiLolaakianzadarasalakwanzahadianahitimu darasalasaba,MauanaMajaliwawalikuwawakiwa. HawakuwatenanamtotozaidiyaLolajamboambalo Majaliwalilimvurugaakili.Hakuwaakishindanyumbani walahakuwaakimgandamkewekamahapoawali.Kutwa alikuwaakihangaikanakazizakezajuakali.Mapenzi aliyokuwaakiyaoneshakwaMauahapoawaliyalipungua. Tabasamulakelilikuwanadrasanakuliona.Lolaililazimu kulelewakwakiasikikubwanasautiyamamaye.
Kwakuwamiongonimwasifazamama,nikumlea mwanayeiliawezekuwamfanowakuigwakwamema, Mauaalikuwamzazimwema.Pamojanasadfaya kumfanyamtotokuwajuuyakilelechatabianjemana vuruguzammekutakamwana,Mauaalibakikuwanguzo muhimu.Isingewezakuwafamiliaborabilauwepowa mamabora.Hiisawanaujenziwanyumba,haiwezikuwa nyumbapasipokuwananguzoimarayenyekuinyanyua. Kwauhitajihuo,babayeyehuwakamachumvi,hukoleza
uhainaladhakwakusimamiamiikonamisingiimara. Hivyokatikanyumba,Majaliwaalikuwamsingiwanguzo kusimamajapoalikuwakasongwanafadhaiko.
Mauahakuishakumnasihibintiyekwamanenoyakila aina.Ilipolazimikakuchekanayewalichekanailipobidi kumkanyakwamanenomakalialifanya.Palipohitaji kumpatiaperemendealimpatianapalipokuwapakihitaji mshubirinapohakusitakumjazia.Hakutakamtotowake akuenakuwakamachazaajianikayemwambani.Alitaka LolaawemfanomwemailikumwaminishaMajaliwakuwa, Lolaalikuwamtotosahihikwake.
SikuyakumnasihitenaLolailifika.Umriwakeulihitaji kukumbushwakilawakatikwakemeonaushauriiliakue nakukivukakipindikigumuchausichanawakebaadaya kuvunjaungo.Lingalijualimefifia,likichomozakwashida, MamaLolaalitokashambanialikokwendakuchuma kisamvu.Alimwitamwanayenakumtakawasaidizane angaliakisemanaye.
“Lolamwanangu,sasaweweniembebivumtini.Kama halikuliwachangakwachumvinapilipili,sasawatakiwa kuishitofauti.Kilaapitayekaribuyakoanalitamanitunda ilikuitulizanjaayake,”alisemamamaLolaangali akiendeleakuchambuakisamvu.
“Abee!”Lolaaliitikia.Alioneshakutoelewakilemama yakealisema.
“Nisikilizemwanangu.Maishasikuzoteniutukwa watu,endapowatageukaafriti,ubayawaohuuzidiulewa mnyama.Tanguutoketumbonimwangu,Molaamekujalia afya,waishisalama.Unapaswakumshukurukwakilahali. Ninachokusisitizanikimojaufahamu;ulimwenguhauna mgumu,kwakewotelainimithiliyamkatekwachai. HalahalabintiwaMajaliwa,ichungehaibayakonayetu pia,usituvuenguo.Ushakuamwanangu,kotekusinakasi
vijanawakutazama,”alisemaMamaLola.Alikisogezakinu alichokuwaamekiandaakwaajiliyakulitwangasamvu lililokuwalimejaatelekwenyekapu.
“Mama,huishimafumbo.Kilakukichakuniasakama miekiziwinisiyewezakusikia.Ninajitambuamama’ngu, kamwesitawezakuwavuanguo.Njiayangunyoofunajua waifahamu,namtumainiMungupekee.Mwalimuwangu wasomolaKiswahilialishasemamaranyingikuwa,miluzi mingihumpotezambwa.Nakuombauamininauniamini mwanao.Najitunzailindotozanguzisiendenamwezi,” alijibuLolawakatiakimnyang’anyamamayemchina kuanzakukitwangakisamvu.Mamayealimtazamakwa makiniusoni.Aliupelekamkonowakemmojashavunina kuubandikakishakuuegeshakwenyegotilake.Aliendelea kumpekuaLolakwamacho,tanguunyayohadinchaya unyewe.
“HiviLola,upitapomitaanisikuhizihaliikoje?”Aliuliza mamaLola.
“Mama,ushaanza,maswaliyakokamampelelezi. Mitaaninikawaidatu.Hakunaubaya,lakini……..”
“Hapoishia….Hiyolakininaitaka,hasandipo nikaamuakukuuliza.Nishalionajualikichomozakabla yakomiakamingiiliyopita.Niulizapomaanayanguni kubwa.Hebunieleze,lakiniinaninindaniyake?”Aliuliza mamaLola.
“Mama’nguweachatu,kilanikatizapombeleya wanaume,vijanahatawazee,haweshikuziachahamsini zaonakunikaziamacho.Tena,hunitazamatanguchiniya miguuhadiunywele.Basihunisindikizakwamachona utawasikiatuwakirushamanenoyachinichini,niaibu hatakuyasema,”alielezaLola.
“Aibueemama!Aibukaburilanafsi,sirisemana mamayo,kijakaziusimsiri.Ushakuanimesema.Enhee,
wanasemaje?Maanahapondipopaliponalileninalotaka kukuasa,”aliendeleamamaLola.
“Mamanitakwambia,achakwanzanimalizekutwanga kisamvuniinjike.Wauonawakatiwakimbiakamamshale wamsasi.Natakababa’nguarudipokutokakondeni ajipatiemlomapema,”alielezaLola.
“Kumbewamjuavemababayako.Tanguakiwa barobaronaukokoshingoni,yeyechakulakwanza menginehungoja.Hasirazakezamkiziakikosamlokwa wakatindipoutazijua,”alisemamamaLolakishakuangua kicheko.JichotenaliliendeleakumtazamaLolawakati akitingishikakilaalipousukumamchikwendakwenyekinu.
“Mashallah!”AlistaajabumamaLola.
“Mamajamani,wanitazamajekamasanamula maonesho,kwamakininamnaile?Hadinaogopa,aukuna jambomama’nguwalijuawatakakunijuza.Basiniume sikiounitoewasiwasi,”alisemaLola.
“Nikutazamaponayakumbukamengimwanangu. Nazikumbukaenzi,wakatinilikuwanikimwagamaji kichwani,yaliendaharakachinikumwagika.Mwili ulikuwamororonaulikuwaukimeremetakamaembe dodobivu.Kilamwanaumealitakajaponimpemkono kablayasalamu.Chaajabunakionasasa,baadayababa yakokunioa,hatimayekukuzaawewe,mamboyapotofauti. Mwiliushakuwakamagunialamkonge,ukitiamaji kichwanipengineyawezayasifikechini,huishia pasipojulikana.Salamutenazavijananawababa zishakoma,”alisemamamaLola.
“Mamanawe,mpakauzungukekamatiara.Najua unachotakakusema,weniambiemwanaonakusikiliza,” alisemaLola.
“Haya,pakuahilosamvu,litiekwenyechungu,nenda kaliinjikenaurudihapa.Kablababayakohajarudinikupe
yanguyamoyoni.Bintinamamaye,mwananababaye, hivyonisiposemautanilaaniuzeeni,”alisemamamaLola.
MamaLolaalibakikimyakajiegeshakwenyemtiwa kivuli.Ulikuwamtimkubwawamzambarau.Dusumali lakekichwanililipepeakwaupepouliokuwaukivumahasa baadayadaliliyamvuakutakakunyesha.Alikuwaakiwaza jinsiyakusemanamwanayekuhusumaisha,hasawakati ulewausichanaulioiva.Lolahakukawiakuinjikakisamvu alichokuwaamekiandaa.Alipomaliza,alitiakuniiliapate motowakutosha,kishaalipigahatuakurudikwamamaye aliyekuwaakimngoja.
“Ushatiakunizakutoshajikoni?”AliulizamamaLola.
“Ndiyomama,tenanaonaleozitawahishakisamvu kuiva,”alijibuLola.
“Hayasikioteganausikie.Niyasemayohutayasikia popotempakautaendakaburini,”aliongeamamaLola. Usonitayarialiuvaaumamaambaohaukuwanachembe yamasihara.Lolaalibakikimya,moyoulimdundakwa shaukuyakujuakilemamayealitakakumjuza.
“Nianuliekangayanguhapokambanindipouje tuendelee,”MamaLolaalimwagizamwanaye.Lola alinyanyukanakuivutakangailiyokuwaimekauka.Mji wakeulikuwaumepambwakwasamakiwadogowengi wakiwawamemzungukasamakimkubwaambayealipanua domo.Lolaaliketikwenyekigodakumsikilizamamaye.
“Watotowaleokwakutakalaana!Unajuamaanaya kuketijuuyakigodawakatiunazungumzanamamayako? Teremkajikaliehapomsalani.Mwikokwamsichana asiyeolewakuketijuuyakigodaangaliakizungumzana wazaziwake,”MamaLolaalifoka.Lolaalinyanyukakisha kuketimkekani.“Usipozingatiahilo,nakwambia hutaolewa,zaidiutakaliwavikaovyakusutwakwa ushankupe,”aliongezamamaLola.
“Nishaelewamamangu,nisamehe,”alisemaLolakwa unyenyekevu.
“Haya,ukotayarikunisikiliza?”
“Ndiyomama.”
“Naombanielezebilakuficha,ushaanzishausuhubana mvulanaaumwanaumeyeyotetangunikuzae?”
“Aka!Sijawahimama.Mbonawaulizauna…”
“Shhhhhhi!Taratibu.Nijibuhatuakwahatua.”
“Sijawahimama,”alijibuLola.”
“Vizuri!Umehitimudarasalasaba,sasawangojea matokeo.Je,watakakuendeleanashuleamaumefika kikomo?”
“Mamaaa!Kikomond’owapi?”
“Umefikiamwishowandotozako?”
“He!Mama,mienatakakusomahadimadarasa yasiwepohukombeleni.Ndotoyangunikusoma–kusomakusoma,mpakanitamanichonikifikie,”alijibuLola.
“Vizuri.Nakuulizahayakwamaanakubwa.Tazama, rafikizowotesasawanaelekamabegimgongoni,tena mapemabaadayakuzivuasarezashule.Wamezalishwa naowanalea.Waopiahawaitakishulekabisa,wanasema kuketidarasanikwabintiniutumwa.Waowanasema kuwa,wanasomewanabwanazao.Wanaringiamakalio yaokuwa,wakikaliasanaviti,watapigwapasikama wachina.Isiwenawewasomewanabwana’ko,”alieleza mamaLola.
“Mama,natakakusomakwajuhudizangumwenyewe. Natakakupatakilakituchangukwaakilinanguvu alizonijaliaMaulana.Sihitajiupendeleowalakumtegemea mtukamadhamanayamaishayangu,”alielezaLola.
“Isomehiikanga,imeandikwanini?”MamaLola alisemakishaalimpatiaLolakanga.Lolaaliizungusha kangakuiwekavemailiaisome.
“Imeandikwa;avumayebaharininipapa,dagaa mjichunge.”
“E-waaa!Haya,niambieinamaanagani?”
“Inamaanakuwa,papanikiumbemkubwaambaye anapaswakuogopekabaharini.Kwamba,dagaa wajihadhariwasijekuingiahatarinikwenyedomolake maanaatawalabilahuruma,”alijibuLola.
“YaoneshamwalimualokufundishaKiswahilihajambo. Safikabisa.”MamaLolaalifurahi.Alikenuahadimeno yakemdomoniyoteyalihesabika.“Hongerakwahilo Mwanambee!”
“Ahsantemama.”
“Je,katiyapapanahaodagaa,weweunajifananishana kipi?”AliulizamamaLola.
“Heemama!Miedagaatu,tenamdogokabisa.”
“Haya,nadhanisasautaelewamanenoyangukwani akiliyakoyaoneshakupevuka.Hapadunianinisawana bahari,papaniwanaumewenyehila.Niwalewatumiao vipawavyao,malizaonamionekanoyaokuwahadaa mabinti.Jichungedhidiyawanaumelaghai,watakao kuonekanakatikatiyadagaa,”alielezamamaLola.“Hivi kangaul’oivaaunajuaimeandikwaje?”MamaLola aliendeleakumdadisimwanaye.Lolaaliikaguakangayake kishakutoajibu.
“Imeandikwa;mbuzinang’ombewamoja,mtumbalini kondoo,”alisemaLola.
“Waelewanininapo?”AliulizamamaLola.
“Mamamiesielewi.Niambiewewe,”alijibuLola.
“Asiyejuamaanahaambiwimaana.Lakiniukae ukifahamukuwa,huwezikuwamwerevunamjuvikwakila jambo.Umewezakujibuvemamafumbonil’okuuliza, yumkinihilidogolimekuachaugenini.Namaanishakuwa, wenyemalinakaulindiohushirikiana;naoning’ombena mbuzi.Humkandamizakondooambayenisawanamtu mjingaamampole,kichwamajiasiyewezakujielezana kujitetea.Sasaukaeukijuamwanangu,dunianikuwa mwemakiasi,wemaukizidisanahuwaupumbavu. MsabihiMunguwako,kwakudraatazinyanyuajuhudi zakouifikiepepo.”
“Ahsantemama.Ndotozangumienatakakusomatu, hakunakingine.Sihitajikuolewakatikamaishayangu kablasijakamilishamatakwayanafsiyangu.Kwanimama, kutoolewanidhambi?”AlihojiLola.
“Nisingeolewaungetokawapi?”MamaLolaalijibukwa swali.
“Penginenisingelizaliwa.”
“Usiwembumbumbu.Kuolewasidhambi,lakininamna yakuolewanamtuwakuolewanayendichohuzaadhambi. Jitunze,somanafikiamalengoyakokishaMolaatakupa mumeumtakaye.Ulimwenguunaoupokeausichanawako umejaamashaka.Usiuharakieujananakuupakisogoutu wema, ”alielezamamaLola.“Nakumbukaulisemawataka kuwahakimu,badounaotakuwahivyoamaushageuka kamamlevikitandani?”AlihojimamaLola.
“Hapanamama.Ndotozanguhazitabadilikamaana ndilochaguolangu,”alijibuLola.
“HayabintiwaMajaliwa,nitakapopatawasaa nitakujuzamengi,lakinileonimekumbukashairila malengammoja.AnaitwaSudiBinHamoodAkwaay, alikuwaakiimbatungaliPwaniminazini.Nivema
nikuimbieupatekujitwaliaujumbeal’otakawasichana wajuejuuyanikuusiacho.”
“Mama,napendasanamashairi.Hebuniimbie.Naona Pwaniuliikaanapwaniilikaandaniyako,”Lolaalisema kishaalitabasamuakimtazamamamayake.
“Hayashairisikia,laitwaKIPEPEO:
Kipepeowempole,maishayoyashakani
Humjuimwendapole,kinyongaakutamani
Yakeniaakupole,furahayokichakani
Onawalalakodole,kipepeokwenyejani
Harakaguuchepusha,kinyongaatafutani
Yakeshidakukurusha,yakondotokufitini
Sijifanyekumrusha,yajasikukichakani
Zakondototazikosha,fahamukuziruhani
Ndefusafarimeenda,heshimayodarasani
Ngazinnekuzipanda,kujifunzakwahisani
Utelezinjiapanda,sisahaukurehani
Kwavitabuutapanda,safariyotokapwani
Kipepeobintiyangu,nakusihisijizini
Kinyongananyungunyungu,takukunakwathumuni
Barobarokamajungu,hakinaikukutani
Ujichungekwamajungu,kwazawaditakubani
Takuleteanikama,tamaayokwakidani Kingayowimasimama,kuupingaushetwani
Ilimuhimanimama,babayoaweilani Hishimayokwaulama,uombetenasirini
Sijifanyewechuchunge,taliwatenadomoni
Utajipatianunge,duniaitakuzini
Shaurilangukinange,himakijazisizini
Saharaninakinange,waombeekwaimani
Nachokajipendekeza,harusisimsibani
Ujingaotakutweza,kwaindanabaniani
Kwetumienijinaza,siyendikwaoMazini
Takutiakwajeneza,ndotoyakoukutani
Takushikakwaupaja,njaakendasebuleni
Nimechokakubwabwaja,piranatiakwapani
Kipepeowewemja,simtukuzeshetwani
Sasavaliapambaja,kinyongamwachechakani
“Mamaaaaa!Kipepeondiyenanikatikashairihilo?”
AliulizaLola
“Kipepeoasiliyakenimaua,mauaasiliyakeniurembo. Katikashairi,BinHamoodalimlengasanamsichana mbichianayechipuka.Sawakabisanawewebintiyangu. Wewenikipepeoambayewapaswakukaamachodhidiya maaduiwengi.Wapaswakujilindadhidiyao,”alieleza mamaLola.
“Kipepeokwahiyonimsichana!Amakwelisikuwa nafahamuhilo.Ahsantemama,nimelipendasanashairi hilo,”Lolaalisema.Mudahuoalifikababayeakitokea kondeni.
“Karibubaba’ngu.Shikamoo!”Lolaalimkaribishana kumsabahibabayake.
“Marahabamwanambee!Kunaherihapa?”Mzee Majaliwaaliitikianakudadisi.Alikuwaakihemakwashida kwanialifikapaleakiwambiombio.
“Baba,naonaumekujambimbio,kunausalama utokako?”AlihojiLola.
“Nawebabayakohatahajapumuaushamjazamaswali yamkimbizimpakani.Mwacheapumzikekwanzandipo maswaliyakomuulize,”mamaLolaalifoka.
“Achakisiranimkewangu.Hakiyakemtotokutaka kujuasihayababaye.Amakafanyakosa?”Aliuliza Majaliwa.Alimsogeleamkewakealiyekuwaakiutandua mkekailikuingiandani.Wingunaupepovilishindana. Upepoulipotuliawingunalolilisimamawima,upepo ulipovumanakufanyafujo,wingunalolilikimbiakwakasi angani.
“Wewewaonaje,nisawaafanyavyo?Anapaswa akukaribishe,akupokeekishauketipokitakondipoajekwa adabuakusabahi.Sasawamdekezakamayai,siku akikengeukautanigeukanajua,”mamaLolaaliendelea kunung’unika.
“Mkewanguyeshe!Minajuamtotonihakiyake,” alijibuMajaliwa.
“Haya,mkeohujaniona?Maanatanguuniache kitandanialfajiri,hunahatahamuyakunijuliahali.Jicho lakokwahuyomamayako,mwanambeemjawaVuga,” alilalamamamaLola.
“Mauamkewangu,achagubu.Huyunimwanetusote. Kusemasijakutakiaherinalolinatokawapi?Usikukuchwa tumelalawote,nilijidamkanik’endakondeninikitaka uendeleekupumzika,sasaimekuwanongwa?Kwelihila imekosapakwenda.Kibuyuakitiwakundehulalama kavimbiwa,akitiwamajihutapikayashamkinai,toshekana penzinikupalomkewangu,”alijibuMajaliwa.
“Majaliwamumewangu,sikuhizisikamazamani. Nilikuwakamayaikwakokablasijamzaahuyumrembo wako.Hukuwaukibandukahapanyumbaninawala hukuwahikuniachakitandani.Hatauk’endakokote, hujawahikurudibilakunibebeakijizawadinakuniuzia manenomatamu.Tena,niliyapokeambalikablahata hujafikanilipo.Mahabayashakwendanamajiyamoto sasawanionakamakibuyuchasiagi.Sawenibwana, mpendemwanao,”MamaLolaalilalama.
“He!Mkewangunisamehe.Sikudhanikamautawaza yotehayo.Nyakatihazifanani,nitakuwamwemabasi yaishe,”alijibuMajaliwa.
“Mienakubaliyaishelakiniyanaishajehapondipo unapaswaujirekebishe.Fahariyamumenimke,nafahari yamkenimume,”alielezamamaLola.
“MamaLolausitakekuamshayaliyolala.Tenanaomba yaishekwawematu,”alisemaMajaliwaangaliakiwa kaingiwanakijibarohoni.
“Hebuyaamsheyaliyolalaniyasikie.Yepihayoyalolala nisiyajueyakufanyehadiunisahaumkeo.Mapenziyote sasatangunimzaeLolayashakwishakabisa.Hutulii mwanaumekwamkeo,kutwakiguunanjiawalahujali kamanahitajihatatuchezebaokamazamani.Auwataka niendemtaanikukaakitakonawanawakemakuwadi,si utakatakauliweye?”AlisemamamaLola.
“Makuwadi,kinananihao?”AlihojiMajaliwa.
“KinamamaKoinahaovijusowengine,walewamtaa wamaduka.Huwajuimashambenganamakuwadi!Hadi midomoishawaendaupandekwakuwasemawatukwa mabaya.Kilammojaanawanyosheakidolewalejini walivyonamidomomirefu?”AlifafanuamamaLola.
“Usitakenichekeningalinauguliamoyoni.Unawaitaje mashambenganamakuwadi?Naonaakilizakozote
ushaziachaPwanijuuyamnaziungaliukijakatikakijiji hiki.Unapaswakuwaheshimu.Tenaunatakiwaukikutana naonjiani,unawapishawapitenakuwasabahikwa heshima.Uwapokisimaniwakifikaunawapishakwanza wachotemajinaweweuwatwishe.Waleniwakezawatu, wakewanaostahilikusalimiwaasubuhinawaumezao.Si weweMaua,hustahilikabisasalamunamatunzo ninayokupatiahadiunakuwakamafaruumenenepahumu kwangu,”alielezaMajaliwa.MamaLolaalikuwakasimama kwenyekizingitichamlangoangalimumeweakiwandani. Lolaalikuwajikoniakiendeleanamaandaliziyachakula. Mvuailikuwaimeanzakudondoshamatoneyarasharasha.
“Majaliwa,kosaganinililokutendahadiwanitusinamna hiyo?UlitakamtotonikakuzaliaLola,tenakwashida nusuraniupotezeuhaiwangu.Hiyohaitoshi,nimekuwa nikitiikilaagizolakolakutoubanduamguuwanguhapana kwendakwenyemagengeyawanawakenavikundivya upatu.Badowanionahayawaninastahilimatusi.Sibure bwanaweye!Utakuwaumeshapatabibimwinginezaidi yangu,naonaanakuzuzua.Hatahukukutokahapaalfajiri ninapatashakasasa,siajabuunaendakumaliziausingizi hukokwabimdogo.Mletebasituhangaikenayehapa,” alielezamamaLola.
“Mauashidayangunimojatu….”
“Ipi?Looh,hunahatahayaMajaliwa.Ushakuaachana natabiazabarobaro.”
“Badohujazaa.Kabisahujazaahatafamiliayangu naionaikipaparikakwaukiwa,haiheshimiki.Tunaonekana wotekamawanawake.”
“UnasemaniniMajaliwa?”
“Umesikia.Usijitiekiziwietihujasikia.Natakadume humundani.Ningetakamwanamkesiweweunatosha, yanininingeoasasa.Nizaliemshikafimbosimwiko,hapo
ndipoutajuaMajaliwaalizaliwaPwaninakulelewabara kwabahatimbaya.”
“Munguwangu!Majaliwakumbesikuzoteukimya wakoumefichahayo!NikwasababuyakukuzaliaLola, msichananasimvulana.Sasaleonimeelewa.Hatahiyo elimuyakoyadarasalannehaijakusaidiakabisa.Mtotoni mtototu,jinsianimaumbile,”alisemamamaLola.
“Tokambwa!Ukiwanarununuyatochinawe utajilinganishanamwenyerununuyavideonapicha? Utafananishajemtotowakiumenawakike.Haunazo kabisaMaua,leondonimefahamu.Mtotowakiumendiye mshikafimbonamkuki.Ndiyemshikasandakunitwaa kaburini.Sasahuyumshikamwikowakoanawezakunizika? Anawezakuniteteakwakuushikamkukinafimbodhidiya maadui!”alifokaMajaliwa.
“Kinywachanguumekitiashubiri.Usemayohatasielewi kamawayasemaweye.”
“Lione,usinisimamiewimakamanyonyadamu.Keti hapokitiniuipishemvuainyeshejapotupatekulima,” alisemaMajaliwa.
“Hayanaketi,lakiniMajaliwaleoumenikatakauli,” alilalamamamaLolaangaliakiingiandani.Alikivutakiti tayarikukikalia.Alipokifikiailikuketi,kitikilivunjika akajibwagasakafuni.
“Hayaumeona,kwadhambizakohukumuishaanza kukupataingaliasubuhi.Mauaniliyekuwanimeoaalikuwa mrembo.Alikuwamwembamba,kiunokimekatikakama dondola,umbolakibuyuchamaziwa.Shingoyakeilikuwa ndefukamatwiga.Kifuachakekipana,kiwiliwilikilikuwa kimeumbikanakuvutia.Mdomonialikuwaamejaameno meupenatabasamu.Ibarayanywelezakesasa,lainikama hariri.Midomokamakaswiba,waridikasingiziwa.Kula kwakekidogoalishibanakwausowenuruilichezana
kumfanyaanighuri.Hayondiyoyalinifanyaniachekazi zangunakukimbiambiokwendakumkumbatiakila wakati.Tazama,sasaushakuwadubwanakamamcheza mieleka.Mdomonind’okabisa,menoyoteyashapuruka kamamuuzaugoro.Hujulikanakichwaninamiguuniwapi. Umenenepampakaunachukiza.Sasaunadhaniwewe ndiyenilikuoamiakailiyopita.Umeharibikasanana umejisahau,kisatutayarinishakuoanasinalakukufanya.
Ujitunzekamavileulivyokuwakwababayako,naweza kukuonatena.Punguzakula,utanilaumubure,”Majaliwa alieza.
MamaLolaalikuwaamejizoazoanakuketi.Kifuakilijaa kwahasira.AlimtazamaMajaliwaakitamanijapo kumraruanakumfanyavipandevipande.Chozililianza kumtiririkawakatiakiliakwauchungu.Majaliwaalikuwa kaelezayafikranimwake.Mauaalipaswakuyasikiana aliyasikianakuyajibukwakilio.
“Majaliwamumewangu,leoumeniambiamaneno ambayosikutegemeakuyasikiatokakwako.Nisamehena Munguatasikiakiliochangu.Kamayotehayanisababuya kumzaaLola,basiatafanyanamnanitakupatiamtotowa kiume.HakikaMunguhanachoyo,”alisemaMauakwa uchungu.
“Mauaulishachelewakuamua.Lolandiyefunguana fungamimbakwauzaowetumiminawewe.Sitegemei kamakutakujamuujizawakwenu,labdautokekwa shetani.Hatakamavitabuvyadinivinawatajawatuwengi kuwawalizaawatotowakatiwamachweo,kwako haiwezekani,”alisemaMajaliwa.
“SawaMajaliwa.Hatahivyo,Lolaatakufaanajuaipo siku.Hatakamasiyeye,uzaowakeutakufaawakatiwa uzeewako.AminiMunguanayomakusudi.Tumpendena
kumleabilakuonyeshakuwahakustahilikuzaliwahapa.
Tuwazaziwakeujue,”Mauaalieleza.
“Haya,manenoyakonisawanakelelezamlango. Nishakuzoea,mwambiealetechakulanilehapamaana kazizashambazimenifanyakurudimbioniipozenjaa yangu, ”alisemaMajaliwa.
Lolaalikuwatayarikaivishachakula.Aliandaakama kawaidayaalivyolelewa.Alimtengeababayakechakula. Baadayababayakekutosheka,yeyenamamayewalitenga chakulawakala.MamaLolaalikuwamnyongejambo ambaloLolaalilazimikakulihoji.Sikuhiyoilikuwa ikiondokaifuatiwenasikuyamkeshawaNoeli.
“Mama,keshonitafanyakazizahapanyumbani mapema.NitakwendakwenyemkeshawaNoelikama nilivyozoeailinaweupatenafasiyakwendaasubuhi.Muda huomiminitakuwanaandaachakulachasiku,”alieleza Lolaakimjuzamamaye.
“Nishakuzoeabintiyangu,ibadanawewehamkwepani. Jitahidikuamkamapemailiuyakamilisheyotekwawakati tenakwaufanisizaidi,”alijibumamaLola.“Utaendana nanisafarihiikanisaniwakatihuowausiku?Nakumbuka Pasaka,uliendanaakinaJoyceambaosasahawapo.”
“Nitaendamwenyewemama.Siwezikuogopakitu maanambalamwezisasahuchomozamapema. Nitatembeaharakaharakabilashakanitafikanakurudi. Wakatiwakurudindokabisaa,watuwengisana nitaongozananao,”alisemaLola.
“Hayamwanambee,kuwamakinimaanausiwena mazoeanabinadamu.KilasikuiendayokwaMolakuna visangavingi.Huwezikuotananianakuwaziayepi,Mungu tuakuongoze.”
“Sawamama.”
Hatimayewalimalizakulachakulachamchana.Lola aliviokotavyomboiliapatekuviosha.Mvuailiyokuwa imesheheniwinguzitonaupepoilinyesha.Haliyamchana wasaananeilikuwakamajioniyasaakuminambili.Kila mmojaalijifungiandaniakitafakariyaliyotokeasikuile. Hakikailinyeshahadijimbilakwanzakuwikausikuule.