Ebook tanzania tanzanian islam imân na uislam

Page 71

kulingana na hadith hiyo. Pamoja na hayo, inamruhusu pia kutekeleza kulingana na madhehebu yake, kwasababu hakuna wasiwasi kwamba imam huyu katekeleza kulingana na ijtihadi yake. Mukallid kutojua delil hizi uislam unampa udhur. Kwasababu maimam wote hakuna aliyekwenda kinyume na kitabu na sunna wakati anafanya ijtihad. Madhihabu yao ni ufafanuzi wa kitabu na sunna. Walifafanua maana na sheria katika kitbu na sunna kwa waislam. Waliyafafanua kwa njia kwamba waislam wanaweza kuelewa, na wakayaandika kwenye vitabu. Kazi hi ya a’immat almadhâhib ‘rahmahum-Allâhu ta’âlâ ilikuwa kazi kubwa kwa uislam kiasi ambacho nguvu za binadamu hazingetosha kutekeleza Aallahu ta’âla angekuwa hajawasaidia. Upatikanaji wa madhehebu haya ni ushahidi kamili kuhakikisha kwamba Rasûlullah ‘sall-Allahu ta’âla alaih wasallam’ ni mtume wa kweli na Uislam ni dini ya kweli. Kutofautiana kwa ijtihad ya a’immat al*madhâhib wetu kuhusu masuala ya dini ipo katika furû’ ad-dîn tu, kwa kusema masuala yanayohusiana na fiqh. Hakujatokea tofauti kati yao kulingana na usûl ad-dîn, kwa mfano; kuhusu elimu ya itiqâd au imân. Wala hawajatofautiana kwenye mafunzo ya furû’ ambayo inajulikana kuwa ya msingi katika dini na inayotolewa kwenye hadithambazo dalil zake zililetwa kwa njia ya tawatûr. Walitofautiana tu kwenye badhi ya masuala ya elimu kuhusu furû’ ad-dîn. Hili liltokea kutokana na tofauti zao kwenye kufahamu dalil za kuhusu mambo haya. Na tofauti ndogo hi miongoni mwao ni rehema ya Allahu ta’âla juu ya umma; inaruhusiwa kwa kila muislam kufuata moja kati ya madhehebu manne anayopenda na kuona ni rahisi kwake. Rasulu ‘sallallahu alaih wa sallam’ alitabiri tofauti hizi kama habari njema, na zimetokea kama alivyotabiri. Hairuhusiwi kutumia ijthadi katika masuala ya itqâdi kwamfano masuala yanayohusiana na iman. Hi inasababisha kupotea kutoka kwenye njia sahih na uzushi. Tena ni dhambi kubwa mno. Kuna njia moja ilio sahih kuhusiana na masuala ya itqad nayo ni: ahl asSunnat wa’l-jamâ’a. Tofuauti ambazo zilielezwa kuwa huruma ya Mungu kwenye hadith sharif zilikuwa tofauti kwenye furû’ au ahkâm. Katika suala ambalo madhehebu manne yametofautiyana kwenye hukumu yake, basi hukumu moja tu ni sahih. Wale wanaotekeleza kulingana na hukumu hi iliosahih watapewa – 71 –


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.