KUMBUKA
Mwandishi wa kitabu I’tiqad-nama, Mawlana Diya’ad-din Khalid
al Baghdadi al-Uthman (alizaliwa mwaka 1192 hijiri sawa na 1778
miladi katika mji wa Shahrazur kaskazini mwa Baghdad, na alifariki
dunia mwaka 1242 hijiri sawa na 1826 katika mji wa Damascus
(syria) quddisa sirruh), Aliitwa Uthman kwasababu anatokana na
ukoo wa Uthman Dhu’nurain radiya-Allahu ta’ala anh ambaye ni
khalifa wa tatu. Alipokuwa anamfundisha ndugu yake Hadrat
Mawlana Mahmud Sahib hadith ambayo ni maarufu sana kama
Hadith al-Jibril, na ndio ya pili ndani ya kitabu Al-ahadith al-arba’un
zilizotolewa na mwanachuoni marufu an-Nawawi, Hadrat Sahib
alimuomba kaka yake mkubwa kuifafanua zaidi hadith hiyo.
Mawlana Khalid, ili kuridhisha moyo wa mdogo wake na kutimiza
ombi lake alikubali kufafanua hadith as-sharifu hiyo na akatunga
kitabu kwa lugha ya ki faris kwa jina la I’tiqad-nama. Tafsiir yake
kwa lugha ya kituruki kinaitwa “Herkese Lazim Olan Iman”, na pia
kilitafsiriwa kwa lugha ya kingereza na kuitwa Belief