Ebook tanzania tanzanian islam imân na uislam

Page 50

Muhammad ‘alaihi salâm’ ambaye ndie sababu ya kuumbwa kwa viumbe wote na mwenye cheo cha juu, ndie maaruf zaidi, mwenye heshima kubwa miongoni mwa binadamu, ni HabîbuAllah(kipenzi cha Mungu). Kulikuwa na ushahidi mwingi kuthitisha ukubwa wake na ndio maana kaitwa Habîbu-Allah. Kwa sababu hi, maneno kama ‘ka shidwa’ hayasemwi kwake. Katika siku ya kiyama atafufuka kutoka kwenye kaburi lake kabla ya watu wote. Atakuwa wa mwanzo kwenda kuhukumiwa. Ataingia pepo kabla ya watu wote. Ingawa miujiza yake tukihisabu haishi, na kuhisabu nguvu za mtu hazitoshi, acha tuandike mujiza wake wa Mirâj kwa kupamba mandishi yetu. Moja katika miujiza yake ni kwenda kwake Mi’râj: alipokuwa kitandani Makkat al-Mukarramat, aliamshwa na mwili wake mtukufu ulipelekwa masjid ya Aqsâ mji wa Jerusalem(Quds), na kuelekea mbinguni, na bada ya mbingu ya saba, kwenye maeneo abayo Allâhu ta’âla alikusudia. Tunapaswa kuamini Mi’râj hivyo.[1] Mi’râj ilitokea vipi imeandikwa kwa maelezo kwenye vitabu vyenye thamani vingi, hasa katika Shifâ’-sherîf.[2] yeye na Jibrîl alaih salam walikwenda kutoka Makka hadi Sidrat al-muntahâ, mti uliopo kwenye mbingu ya sita na saba. Zaidi ya hapo hakuna ndio kikomo cha maarifa na kupanda juu. Hapo kwenye Sidra, Mtume ‘alaih salam’ alimuona Jibrîl ‘alaih salam’ kwenye sura yake halisi akawa ana mbawa mia sita. Jibrîl ‘alaih salâm’ alibaki kwenye Sidra. Kutoka Makka kwenda Jerusalem, na kwelekea mbingu ya saba Rasûlullah ‘alaih salam’ alipanda Burâq, ambayo ni nyeupe, yenye kasi sana, haina jinsia sio dume wala jike na ni myama usiokuwa wa hapa duniani lakini kutoka peponi, ni mdogo kuliko nyumbu tena mkubwa kuliko farasi. Anakanyaga pale macho yake yanapoishia kuona. Kwenye masjid ya Aqsâ Rasûlullah ‘alaih salâm’ na mitume wengine walisali jamaat, Mtume ‘alaih salam’ akawa imamu; ilikuwa sala ya usiku au alfajir. Roho za mitume zilikuwepo pale [1] wazushi wenye madhehebu ya Ismâ’îlî na madui wa Uislamu waliojificha kama wanavyuoni wakiislamu, wanajaribu kuwadanganya vijana kwa kusema na kuandika kwamba Mi’râj Mtume hakupanda kimwili lakini kiroho(kama ndoto). Tunafaa kutonunua vitabu hivi vyenye uongo; tusiwape fursa ya kutudanganya. [2] Qâdî Iyâd al-Mâlikî, mtunzi wa kitabu Shifâ’, alifia Morocco mwaka 544 H.[1150 miladi].

– 50 –


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.