A3 brochure ukatili wa kijinsia

Page 1

Sheria ya makosa ya jinai sura ya 16 - Inakataza makosa mbalimbali ya ukatili wa kijinsia na kutoa adhabu kwa watuhumiwa wa makosa hayo kama vile ukatili wa kimwili, ukeketaji wa wanawake, kunajisi, kubaa, ulawiti, biashara ya binadamu, shambulio la aibu kwa wanawake, unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto n.k - Inakataza matumizi ya lugha chafu, matusi na vitisho Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 - Inaeleza haki ya mototo ya kupewa huduma muhimu kama vile chakula elimu, malazi, mavazi , afya n.k - Inatoa ulinzi wa jumla kwa watoto kwa kukataza ukeketaji wa watoto wa kike. Uchapishaji na utoaji wa machapisho au picha zenye kuathiri maslahi ya motto. - Inakataza ajira kwa watoto

-

chini ya umri wa miaka 18. Kwa maana hiyo ukeketaji wa wanawake walio na miaka 18 na kuendelea haujakatazwa.

Sheria ya kuzuia na kupambana na UKIMWI (2008) - Inamtaka mama mjamzito na mwanaume anayehusika na ujauzito kupima UKIMWI kwa hiari lakini mara nying ni wanaume wachache hupima. - Sheria imetilia mkazo matumizi ya kondomu laikin kuna shida ya upatikanaji wa kondomu za kike.

Sheria ya ardhi (1999) - Vifungu vilivyopo kwa ajili ya kumlinda mwanandoa kwenye kuweka rehani nyumba ya familia havitoshi - Ingawa inatoa haki kwa wanawake kumiliki ardhi, kwenye makabila mengi umiliki wa ardhi unarithishwa kwa watoto wa kiume. - Sheria inaruhusu kupata arhi kwa umiliki wa pamoja wa mume na mke lakini inaonekana kwamba hii hufanyika mara chache kutokana na mila na desturi.

Sheria ya arhi ya kijiji (1999) - Inafuata sana sheria ya kimila ambayo haizingatii umiliki wa ardhi kwa wanawake

Sheria ya kimila (1963) - Haitambui umiliki wa pamoja wa mali - Ina dhana ya kurithi wajane - Inanmyima mjane haki ya kurithi mali ya mume wake na watoto wa kike kurithi kidogo kuliko wa kiume.

Sheria ya elimu - Iko kimya kuhusu mwanafunzi wa kike aliyepata mimba kuendelea na shule.

Sheria za ardhi (1999) - Haki ya mwanamke kumiliki ardhi sawa na mwanaume - Mwanamke analindwa dhidi ya mila na desturi za kibaguzi zinazowazuia kumiliki, kupata na kutumia ardhi - Haki sawa katika maamuzi ya ardhi - Wajibu wa kupata ridhaa ya mwenza kwenye kuhamisha au kuuza ardhi ya wanandoa 10. CHANGAMOTO KATIKA UTEKELEZAJI WA SHERIA ZINAZOHUSU UKATILI WA KIJINSIA.

Sheria ya ajira na mahusiano kazini (2004) - Inakataza ajira kwa watoto wenye umri chini ya miaka kumi na minane - Wajibu wa mwajiri kuzingatia afya ya mama mjamzito na mototo - Haki ya kutokubaguliwa katika sehemu ya kazi - Mapumziko ya uzazi Sheria ya ndoa ya mwaka (1971) - Mwanamke anapewa haki ya kumiliki, kutumia na kuuza mali yake kama ilivyo kwa mwanaume - Haki ya kutoshurutishwa kuingia kwenye ndoa - Mgawanyo wa mali ya familia kwa kuzingatia mchango wa kila mwanandoa pale ndoa inapovunjika - Wajibu wa kuomba ridhaa ya mwanandoa katika kugawa, kuuza au kukodisha mali ya wanandoa - Haki ya mjane kuishi popote na haki ya

kuolewa tena au kutoolewa Haki ya kutoadhibiwa/kuteswa Haki ya mke na watoto kupata matunzo kwa kuzingatia uwezo wa kifedha wa mwanaume (mume/baba).

Sheria ya ndoa (1971) - Inaeleza mgawanyo wa mali pale ndoa inapovunjika, lakini kutokana na mila na desturi, wanawake wengi bado wanapata changamoto ya kutopata kabisa mgao wa mali walizochuma pamoja wakati wa ndoa au kutopata kabisa. - Sheria inaruhusu ndoa ya wake wengi, ingawa mke anatakiwa kufahamishwa na kuridhia lakini mara nyingi hili linakua halifanyiki. - Inaruhusu msichana wa miaka 15 au 14 kuolewa kwa ruhusa ya wazazi wake au mahakama. Hili linakinzana na sheria ya mototo ya mwaka 2009. (2008) ndani ya nchi

Sheria ya mototo (2009) - Haijaangalia suala la wasichana kuolewa wakiwa na umri mdogo, miaka 15 kama ilivyoelezewa na sheria ya ndoa.

Sheria ya makosa ya jinai sura ya 16 - Sheria inakataza ukeketaji wa wasichana


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.