Watu wataweka sheria zao kutenda kazi kinyume cha sheria ya Mungu, na katika juhudi zao kulazimisha utii kwa sheria hizi watawatesa wanadamu wenzao. Vita dhidi ya sheria za Mungu itaendelea mpaka mwisho wa dunia. Watu wote watatakiwa wachague baina ya sheria za Mungu na zile za wanadamu. Kutakuwa na makundi mawili tu. Kila tabia itadhihirika kikamilifu. Wote wataonyesha ikiwa wamechagua kuwa watii au kuwa waasi.