Pamoja Intellectuals Magazine

Page 31

31

wa sekta zilizotajwa hapo juu

UKUAJI WA ZA KIUCHUMI 2010/2011

SHUGHULI TANZANIA

Kwa upande mwingine tunaposema maendeleo ya kiuchumi tunamaanisha hali ya maisha ya wananchi katika nchi husika.tunapoongelea maendeleo ya kiuchumi upimwaji wake unaangaliwa kwa watu je watu wana maisha bora na ni vipi pato la taifa linagawanywa miongoni mwa watu. Hivyo maendeleo ya kiuchumi ya naangalia hali ya maisha ya watu je ni bora au sio bora na ni Idadi ngapi ya watu wana maisha bora . Tanzania ni kati ya nchi ambazo hazijaelekeza sana juhudi zake katika kuleta maendeleo ya kiuchumi yaani maisha bora kwa wananchi wake. Kwa Tanzania ukosefu wa ajira mwaka 2008/9 ulikuwa ni asilimia 2.5 na mwaka 2010/2011 ukosefu wa ajira uliongezeka hadi asilimia 3.5 . ukosefu wa ajira ulikua mkubwa Dar es salaam na hasa kwa vijana. Na wakulima wengi wa Tanzania, asilimia 85 wanamiliki mashamba chini ya heka nne hivyo uzalishaji wao ni mdogo. Na pia ajira kwa watoto wenye umri kati ya miaka 5 na 14 imeongezeka kutoka asilimia 14 mwaka 2008/09 na kufikia asilimia 25 mwaka 2010/2011 nba pia asilimia 96 ya watanzania wanategemea nishati ya kuni na mkaa. Na pia ukuaji wa kipato kwa mwananchi umekuwa ni wa asilimia 12 tu kwa mwaka. Mfumuko wa bei umeongezeka kufikia asilimia 18.7 mwaka

2012 ukilinganisha na asilimia 8.6 mwaka 2011. Mfumuko wa bei wa chakula ni asilimia 24.7, aprili 2012 wakati aprili 2011 ulikua ni asilimia 9.2 hivyo ni ongezeko la asilimia 15.5. na mfumuko wa bei katika nishati umeongezeka kutoka asilimia 22.1 mwezi wa nne 2011 hadi asilimia 24.9 mwezi wan ne mwaka 2012. Thamani ya shillingi imeshuka ambapo mwaka 2010 dola moja ya kimarekani ilikuwa sawa na shilingi 1,432/= na mwaka 2011 dola moja ilikua sawa na shilingi 1,579/= na mwaka 2012 ilikuwa shilingi 1600. Pia deni la taifa limeongezeka kutoka shilingi bil 17, 578.9 mwaka 2012 na kufikia shilingi bilioni 20,276.6 mwaka 2012. Na pia sekta ya afya ukuaji wake umeshuka. Hivyo haya matatizo yanayoikumba Tanzania yanaonyesha kwamba maisha kila siku gharama yake zinapanda na hivyo kupelekea umasikini kuongezeka na wakati ukuaji wa kiuchumi unakua kwa wastani wa asilimia sita. Je nini kifanyike? Ni wakati wa Tanzania kutambua kwamba ukuaji wa kiuchumi upimwe kwa kuangalia maisha ya watu yanaendeleaje hasa kuhusu mambo ya muhimu hasa afya, malazi, makazi na elimu. na ni lazima tuhakikishe tunapunguza utegemezi kutoka nje kwani deni la taifa linazidi kukua. Ni lazima pia kila mwananchi afanye kazi kwa bidii kwa ajili ya taifa lake la Tanzania ili tuweze kupata maendeleo ya kiuchumi na sio ukuaji wa kiuchumi tu. Pia serikali ni lazima ipendekeze na kufanyia kazi sera zitakaazoleta manufaa kwa jamii nzima na kuondokana na umasikini


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.