Lengo la kitabu hiki ni kuwasaidia wahadhiri wa fani ya sheria, mameneja wa kliniki za msaada wa kisheria na wanafunzi wa sheria nchini Tanzania kushiriki kikamilifu katika programu za mwitikio wa kitaifa juu ya UKIMWI. Mwitikio wa kitaifa unajumuisha kutoa ushauri wa kisheria unaohusiana na VVU, kuendesha mashauri yanayohusiana na uvunjifu wa haki za watu wenye VVU katika vyombo vya utoaji haki; kufanya tafiti zinazohusiana na masuala ya sheria, haki za bianadamu na VVU; na kuishauri serikali kuhusiana na uundwaji wa sheria zinazosimamia VVU pamoja na utekelezaji wa sheria zenyewe.